web viewhistoria yangu. naitwa jumanne gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika...

4
HISTORIA YANGU Naitwa Jumanne Gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi kielelezo no 1 JUMANNE GIDEON Wilaya ya maswa mkoani shinyaga .Nilizaliwa mtoto wa kwanza katika familia ya mzee Gideon yenye watoto watano, wadogo zangu wakiwa wakiume wawili na wa kike wawili Baba yangu na mama wote ni wakazi wa mkoa wa Shinyanga ninamaana ya kwamba ni Wasukuma Baada ya kufikisha miaka kumi na moja nilianza shule ya msingi Dodoma iliyoko kata ya Buchambi wilaya ya maswa na baaba ya kufika darasa la tano mwaka 2002 wazazi wangu waliamua kuhamia katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi iliyoko katika wilaya ya maswa kutokana na shughuki za uzalishaji mali kama kilimo na ufugaji

Upload: dinhquynh

Post on 02-Feb-2018

329 views

Category:

Documents


4 download

TRANSCRIPT

Page 1: Web viewHISTORIA YANGU. Naitwa Jumanne Gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi kielelezo no 1 JUMANNE GIDEON. Wilaya ya maswa mkoani

HISTORIA YANGU

Naitwa Jumanne Gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi

kielelezo no 1 JUMANNE GIDEON

Wilaya ya maswa mkoani shinyaga .Nilizaliwa mtoto wa kwanza katika familia ya mzee

Gideon yenye watoto watano, wadogo zangu wakiwa wakiume wawili na wa kike wawili

Baba yangu na mama wote ni wakazi wa mkoa wa Shinyanga ninamaana ya kwamba ni

Wasukuma

Baada ya kufikisha miaka kumi na moja nilianza shule ya msingi Dodoma iliyoko kata ya Buchambi wilaya ya

maswa na baaba ya kufika darasa la tano mwaka 2002 wazazi wangu waliamua kuhamia katika kijiji cha kulimi

kilichoko katika kata ya kulimi iliyoko katika wilaya ya maswa kutokana na shughuki za uzalishaji mali kama

kilimo na ufugaji

Baada ya kuhitimu Elimu ya msingi mwaka 2004, nilichaguliwa na kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2005

katika shule ya sekondari Malampaka ambapo mwaka 2008 ilihitimu mafunzo yangu ya kidato cha nne na

Mwaka2009 nilichaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya cheti katika chuo cha Ualimu Tarime

kilichoko Mkoa wa Mara ambapo mwaka 2011 nilihitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya cheti

Mwaka 2012 nilipangiwa Halmashauri ya Wilaya Bukombe ya iliyoko mkoa wa Geita katika shule ya msingi

Bulumbanga iliyoko kata ya Runzewe Magharibi ambapo mpaka sasa nipo nafanya kazi katika Halmashauri

hiyo

Page 2: Web viewHISTORIA YANGU. Naitwa Jumanne Gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi kielelezo no 1 JUMANNE GIDEON. Wilaya ya maswa mkoani

Mwaka 2014 nilichaguliwa na kujiunga na stashahanda ya elimu ya msingi katika chuo cha Ualimu

Marangu,Kilichopo wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro .Baada ya hapo nilianza kutafuta uwezekano wa

kupata fomu ya maelezo ya kujiunga na mafunzo hayo ambapo taarfa hizo zilinishikiza na nilianza michakato

ya kupata pesa na hatimaye nilifanikiwa kupata kiasi kidogo baada ya kukusanya nguvu kwa muda mrefu na

hatimaye niliweza kupata nwezekano wa kulipoti katika chuo cha ualimu marangu

Baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu mwaka 2011 nilirudi nyumbani kwetu wilaya maswa nilimkuta baba

yangu anaumwa sana kitu kilichonifanya niendelee kuungusa kwa muda mrefu kuanzia mwezi wa sita mwaka

2011 mpaka mwaka mwezi wa kumi na moja 2011,ambapo baba yangu kipenzi mungu alimpenda sana,kitu

kilichoniumwa sana baba yangu amnisomesha hata hajaonja mafanikio ya mwanae mpaka sasa nina mzazi

mmoja ambaye ni mama yangu anaishi katika kijiji cha kulimi kilichopo kata ya kulimi.

HALI YA NDOA

Mnamo mwaka 2008 baada kuhitimu mafunzo ya elimu ya sekondari baba mzazi alishauri nifanya maamuzi ya

busara kwani watumishi walio wengi wamekuwa na tabia ya kukaa muda mrefu .Nami nikaamua kutafuta

mchumba na nilipata mchumba wilaya ya shinyanga vijijini na mwaka 2011 nilifunga ndoa baada ya kuhitimu

Kama kielezo namba 2 na kwa sasa tuna watoto wawili wa kiume Godwin na Greyson

Page 3: Web viewHISTORIA YANGU. Naitwa Jumanne Gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi kielelezo no 1 JUMANNE GIDEON. Wilaya ya maswa mkoani

Mwaka 2014 mwezi wa tano niliomba kujiendeleza baada ya baraza la ufundi kutangaza nafasi za ualimu kwa

ngazi ya stahashahada ya elimu ya juu na nilifanya maombi hayo na baada ya hapo nilichanguiliwa na

stashahada ya elimu ya kawaida ya shule ya msingi katika chuo cha ualimu marangu kilichopo wilaya ya moshi

vijijini Mkoa wa Kilimanjaro kama kielelezo no 3 ni maeneo ya chuo cha Ualimu Marangu