document35

Upload: jackson-m-audiface

Post on 09-Oct-2015

12.806 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 35 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Septemba 26-Oktoba 2, 2014

    Helikopta, mitambo maalum kulinda bomba la gesi -Uk3

    nNi mfumo mpya wa kupata leseni za madini kwa mtandaonHakuna tena Urasimu, kila kitu sasa kwa uwazi Uk.2

    Kamishna Msaidizi wa Madini anayesimamia Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa akionyesha mfumo mpya wa utoaji huduma za leseni kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP) ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

    SEKTA YA MADINI YAZIDI KUBORESHA HUDUMA

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Uboreshaji Huduma Na Veronica Simba

    Dar es Salaam

    Sekta ya Madini nchini imeendelea kuboresha huduma zake kwa jamii ambapo sasa waombaji na wamiliki wote wa

    leseni za madini watapata hudu-ma kupitia njia ya mtandao, hali itakayoongeza uwazi, utawala bora na kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa ili-yotolewa hivi karibuni na Kam-ishna wa Madini Mhandisi Paul Masanja kwa vyombo vya habari, huduma zote za leseni zitatolewa kupitia mfumo huo mpya wa

    kielektroniki ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transac-tional Portal (OMCTP).

    Imeelezwa kuwa kupitia mfu-mo huo mpya, wateja ambao ni waombaji na wamiliki wa leseni wataweza kuingiza maombi ya leseni wao wenyewe na kuwa na uhakika na maombi yote yatakay-owasilishwa pamoja na malipo yote yatakayofanywa kupitia mfu-mo huo.

    Aidha, kwa kutumia mfumo huo, wateja wataweza kuhuisha taarifa za leseni zao kama vile anu-ani na namba za simu na watapata taarifa za leseni zao kila wakati ikiwa ni pamoja na kujua muda

    wanaotakiwa kufanya malipo ya leseni au kutuma taarifa zao za utendaji kazi.

    Pia, taarifa ya Kamishna Masanja inaeleza kuwa, kwa ku-tumia mfumo wa OMCTP, tatizo la mlundikano wa maombi kwe-nye ofisi za madini litakwisha kwani wateja watatuma maom-bi yao moja kwa moja kupitia mtandao.

    Kuhusu suala la usalama wa taarifa za wateja, imeelezwa kuwa mfumo huo umewezeshwa ku-hakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha, mathalan inapotokea mteja kaacha muamala ukiende-lea bila kuutumia, mfumo utaji-

    funga wenyewe. Vilevile, mteja anaweza kubadili anwani ya barua pepe, neno la siri, njia ya utambu-lisho wa ziada na taarifa nyingine binafsi.

    Kwa upande wa utaratibu wa usajili wa kutumia mfumo huo, imeelezwa kuwa mteja atapaswa kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya Wizara ya Nishati na Madini na kuiwasilisha pamoja na viambatisho vyake kwenye Ofisi ya Leseni za Madini zilizoko Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

    Taarifa inaendelea kueleza kuwa fomu zikishawasilishwa zitahakikiwa na Afisa wa Leseni

    na kumsajili mwombaji kwenye mfumo wa OMCTP na baada ya kukamilisha taratibu za usajili, mwombaji anaweza kuanza ku-tumia huduma za leseni kwa njia ya mtandao.

    Imeelezwa kuwa usajili utaan-za Makao Makuu ya Wizara ambapo wamiliki wa leseni za madaraja A na B watatangaziwa utaratibu wa kujisajili ifikapo Sep-temba 30 mwaka huu. Aidha, usa-jili wa leseni za madaraja C na D utaratibiwa kupitia ofisi za Madini za Kanda kwa utaratibu ambao utatangazwa ifikapo Oktoba 31 mwaka huu.

    SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

    TAARIFA KWA UMMA

    TPDC INAKANUSHA VIKALI UVUMI UNAOSAMBAA KUHUSU FURSA ZA KUWAPATIA MAFUNZO YA MUDA MFUPI NA AJIRA

    VIJANA 500 KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa: "Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!...Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014". TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.

    IMETOLEWA NA: MKURUGENZI MTENDAJI

    SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA BWM Pensions Towers, Tower A, Junction of Azikiwe /Jamhuri Streets

    P. O. Box 2774, Tel: +255 22 2200103/4 Dar-es-Salaam, Tanzania

    Ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi 1 unak-wenda sambamba na ujenzi wa majengo mbalimbali yatakayotu-mika kama Ofisi za wafanyakazi. Pichani ni Mafundi wakiende-lea na ujenzi wa Jengo la Utawala katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVE PILLARS OF REFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta, Mohamed Saif

    INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

    OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF

    THE CLIENTSATISFACTION OF

    BUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Flexi cadastre transactional Portal mfumo utakaoongeza ufanisi madini!!!

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Na Veronica Simba, Dar es Salaam

    Serikali inakusudia kuhakikisha mi-undombinu ya bomba la gesi asili linalojengwa kutoka Mt-wara hadi Dar es Salaam inalindwa kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kuepusha hasara inayoweza kujitokeza endapo miundombinu hiyo itahujumiwa.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Wa-jumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotembelea Mradi wa ku-zalisha umeme unaotokana na gesi wa Kinyerezi I na Kituo cha kupokea gesi mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Wataalamu wanao-simamia Miradi hiyo walisema njia kuu nne zitatumika kulinda miundombinu hiyo.

    Maswi alitaja njia mojawapo itakayotumiwa kulinda miun-dombinu ya bomba la gesi kuwa ni pamoja na kuwepo kituo maalum kitakachofungwa mi-tambo inayowezesha kufuatilia na kuliona bomba lote kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

    Chochote kitakachofanyika kulihusu bomba, ikiwa ni pamo-ja na vitendo vya kuthubutu kuhujumu miundombinu yake kitaonekana kutoka katika kituo chetu, alisema Maswi.

    Alifafanua kuwa kitendo cho-chote kitakachofanyika kuhusi-ana na bomba hilo na kutiliwa shaka na Walinzi watakaokuwa kwenye Kituo chenye mtambo huo maalum, kitaripotiwa sehe-mu husika kwa haraka na hatua zitachukuliwa mara moja kabla uharibifu wowote haujafanyika.

    Akizungumzia aina nyingine ya ulinzi itakayotumika kulinda bomba hilo, Katibu Mkuu Mas-wi alisema ni uimara wa bomba

    lenyewe ambalo chuma chake kitakuwa na unene wa milimita 19, hali inayodhihirisha uimara wake ambao ni vigumu kuhar-ibiwa kwa urahisi.

    Aidha, Maswi alisema bom-ba hilo litakuwa limechimbiwa chini kwa kina cha zaidi ya futi moja, hali itakayowezesha ku-toonekana au kufikiwa kwa ura-hisi isipokuwa kwa mtu ambaye amedhamiria ambapo atakay-ethubutu kufanya jitihada za kufukua ataonekana mara moja kupitia Kituo chenye mtambo maalum wa mawasiliano na hivyo kuzuiwa asifanye hujuma aliyoikusudia.

    Naye, Msimamizi wa Mra-di wa upokeaji wa gesi uliopo Kinyerezi, Mhandisi Kapuulya Msomba, alisema pamoja na aina za ulinzi zilizoelezwa na Ka-tibu Mkuu, pia kutakuwa na wal-inzi wa kuajiriwa ambao pamoja na mbinu nyingine, watatumia Helikopta na Magari kuzungukia eneo lote ambako bomba la gesi

    linapita.Mhandisi Msomba alisema

    njia nyingine muhimu itakayotu-mika katika ulinzi wa bomba hilo na miundombinu yake ni kuwa-shirikisha wananchi, hususan wanaoishi jirani na linakopita bomba.

    Kila baada ya Kilomita 20 mpaka 25 kutakuwa na walinzi walioajiriwa lakini utaratibu un-aandaliwa wa kuwashirikisha wananchi ili watusaidie pia ka-tika ulinzi wa bomba, alisema Msomba.

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meki Sadik aki-zungumza mara baada ya ku-kagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi I na Kituo cha kupokea gesi, alisisitiza umuhimu wa wananchi wote kujenga utamaduni wa kutunza miundombinu ya miradi mbal-imbali ya maendeleo inayojeng-wa kwa gharama kubwa ili iweze kuwanufaisha wananchi na Taifa zima kwa ujumla.

    Helikopta, mitambo maalum kulinda bomba la gesi

    Wiki hii Wizara ya Nishati na Madini iliutangazia umma kwamba imean-zisha utaratibu mpya wa kutoa hu-duma za leseni kwa njia mtandao yaani online Mining cadastre trans-

    actional portal mfumo ambao utawawezesha wateja waliosajiliwa kutuma maombi, kuhakiki taarifa za leseni wanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi za kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njia ya kielektroniki kupitia mitandao.

    Aidha, mfumo huu utawawezesha wateja kupata taarifa za kijiolojia zilizoandaliwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na GST.

    Shime Wadau wote wa sekta ya madini wakiwamo wachimbaji wadogo, wakubwa na hata wananchi wanao-taka kujua kwa undani masuala ya madini tunawaomba watumie Flexi Cadastre ili kufahamu mmasuala mbalim-bali kuhusu sekta ya madini na kuielewa sekta hii inavyo-fanya kazi na inavyochangia uchumi wa taifa letu.

    Huduma hii ya Cadastre kwa namna moja ama ny-ingine itasaidia kuongeza uwazi na kasi katika utoaji wa leseni na madini pamoja na kuondoa urasimu ambapo wa-teja watatakiwa kutuma maombi ya leseni wao wenyewe, hivyo kupunguza tatizo la mlundikano wa maombi kwe-nye ofisi za madini.

    Aidha, wateja na Serikali watakuwa na uhakika na maombo yote yatakayowasilishwa yakiwamo maombi ya uhamisho, maombi yanayoongezewa muda na yanayo-pandishwa daraja pamoja na kuwa na uhakika na malipo yote yanayofanya kupitia mfumo wa Online Mining Ca-dastre Transactional Portal. (OMCTP).

    Wateja watapata taarifa za leseni zao kila wakati na kujua wanapotakiwa kufanya malipo ya leseni au wataka-potakiwa kutuma taarifa za utendaji kazi. vilevile mfumo huo utarahisisha mawasiliano kati ya Wizara na wamiliki wa leseni.

    Wateja pia wataweza kuhuisha taarifa za leseni zao kama vile anuani na namba zao za simu kupitia mfumo wa OMCTP pindi taarifa hizo zitakapobadlishwa.

    Wizara ya Nishati na Madini inaamini kwamba mfu-mo huu utaongeza uwazi, utawala bora na kuimarisha usimamizi katika sekta ya Madini kwani huduma ya mfu-mo huo wa OMCTP itapatikana katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara na katika ofisi 21 za Madini mikoani.

    Shime wadau wote wa madini kuchangamkia huduma ya mfumo huu ili kuongeza ufanisi kwa pande zote.

    Na Veronica Simba Dar es Salaam

    Bomba la gesi

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    KAMERA YETU

    Mwanasheria wa mgodi wa Shanta Min-ing Limited David Rwechungura, (kulia) akielezea mchango wa mgodi huo katika ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Mangonyi mara timu ya majaji ilipofanya ziara katika mgodi huo.

    TUZO ZA RAIS

    Timu ya majaji ikielekea katika jengo la kituo cha polisi cha Mangonyi kilichojengwa kupitia ufadhili wa mgodi wa Shanta Mining Limited uliopo mkoani Singida

    Utoaji

    Mwanasheria wa mgodi wa Shanta Mining Limited David Rwechungura, (kushoto) akielezea mchango wa mgodi huo katika ujenzi wa kituo cha polisi cha Mangonyi.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    KAMERA YETU

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani akiongea na wafanyakazi (Hawapo pichani) katika mkutano wa pamoja na wafanyakazi uliofanyika mwishoni mwa wiki hii katika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Dar- es-Salaam.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa kwanza kulia) akiwaongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik (katikati), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kulia kwa Katibu Mkuu) na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, wakati wakitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi I na Kituo cha kupokea gesi jijini Dar es Salaam.

    Utoaji

    Na Leonard Mwakalebela, STAMICO

    Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza mchakato wa kuanzisha Baraza la Wafanyakazi ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha utendaji wa kazi wa Shirika.

    Akizungumza na wafanyakazi wa STAMICO, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Mhandisi Edwin Ngonyani amesema kuwa uund-

    waji wa Baraza hilo unafuatia ukamilikaji wa taratibu nyingine za kiutendaji.Alieleza kuwa, uwepo wa Baraza hilo utaongeza ushirikishwaji wa wafan-

    yakazi katika utendaji wa Shirika na hivyo kufanikisha azma ya Shirika ya kupaa.Mhandisi Ngonyani aliwaeleza wafanyakazi katika kikao kilichofanyika

    makao makuu ya STAMICO jijini Dar es Salaam kuwa, ushirikishwaji wa wafan-yakazi katika shughuli na miradi ya Shirika utakuwa wa wote kuanzia wale wa ngazi ya chini.

    Aidha, aliwaambia wafanyakazi wa STAMICO kuwa upangaji wa kazi au safari utafanywa kwa kufuata mfumo wa kazi na sio watu binafsi.

    Katika hatua nyingine, Mhandisi Ngonyani aliwataka wafanyakazi wa Shirika hilo kuwa waadilifu na waaminifu ili kutojiingiza katika vitendo vilivyo kinyume cha taratibu za kazi na Sheria za nchi.

    Alionya kuwa, kamwe hatavumilia vitendo vya kughushi nyaraka kwani vitendo hivyo ni vya kihalifu na lazima vishughulikiwe kisheria na si kiutawala.

    Katika ili mtanisamehe, suala lolote la kughushi sitalishughulikia kiutawala, nitalikabidhi Jamhuri kwa sababu ni criminal offence (ni kosa la kihalifu) na linashughulikiwa kisheria alisisitiza.

    Vilevile, Ngonyani alikiambia kikao hicho kuwa amepokea malalamiko mbal-imbali ya wafanyakazi yaliyopitia kwa viongozi wa juu Serikalini.

    Aliongeza kuwa, ameyafanyia kazi ya malalamiko hayo na tuhuma nyingine na kugundua nyingine hazina ushahidi.

    Mhandisi Ngonyani akawataka wafanyakazi wenye mawasiliano na viongozi wa juu Serikalini kuimarisha mawasiliano hayo kwa lengo la kulisaidia Shirika.

    Hata hivyo alitoa angalizo kuwa mawasiliano hayo yasiwe ya kubomoa au kukomoa bali yalenge kulisaidia Shirika kukabiliana na changamoto mbalimbali.

    Kuhusu maombi yaliyotolewa na baadhi ya wafanyakazi ya maboresho ya posho mbalimbali, Mhandisi Ngonyani alikiambia kikao hicho kuwa maombi hayo yatashughulikiwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Serikali.

    Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji na Masoko Aloyce Tesha alikiambia kikao hicho kuwa tayari STAMICO imeandaa Mpango Mkakati na Mpango Kazi wa Shirika, na kuongeza kuwa, STAMICO imeweza kushiriki katika maonesho ya kimataifa ya ndani na nje ya nchi kwa minajili ya kujitangaza na kwamba, hivi sasa Shirika linaangalia uwezekano wa kuingia katika biashara ya madini mengine yakiwemo gypsum.

    Naye Mkuu wa Kitengo cha Tehama cha STAMICO Raymond Rwehumbiza alieleza kuwa tayari Shirika limeunganishwa katika mkongo wa mawasiliano wa Taifa.

    Aidha Rwehumbiza aliongeza kuwa, maboresho ya tovuti ya Shirika yame-fikia hatua nzuri na majaribio ya tovuti mpya yataanza wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba, 2014.

    STAMICO mbioni kuanzisha Baraza la Wafanyakazi

    Wafanyakazi wa STAMICO wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Edwin Ngonyani (Hayupo pichani).

    Wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi. Wajumbe hao wanahudhuria mafunzo katika nchi za India na Thailand kujifunza namna nchi hizo zilivyofanikiwa katika sekta ya umeme kupitia Mashirika yao, Wengine katika picha wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava,anayefuatia ni Kamishna wa Nishati , Mhandisi Hosea Mbise , wajumbe wa Kamati hiyo na baadhi ya Maofisa wa Wizara.

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Na Asteria Muho-zya, Dar es Salaam

    Imeelezwa kuwa, matokeo ya Kongamano la tano (5) la Kimataifa la Jotoardhi linalotarajiwa kufanyika nchini kuanzia tarehe 27 Oktoba hadi Novemba 2, 2014 litainu-faisha Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo; kuhamasi-sha matumizi ya nishati jadidifu ili kuchangia katika upatikanaji wa nishati nchini; kubadilishana uzoefu na uelewa kwa wataalamu kutoka nchi mbalimbali duniani

    na kuharakisha uendelezaji wa jotoardhi;

    Aidha, mbali na mafani-kio hayo, mafanikio mengine yanatajwa kuwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano katika uen-delezaji wa nishati ya jotoardhi ; kujifunza utayarishaji wa Sera, Sheria na muundo wa kitaasisi katika uendelezaji wa Jotoardhi; kuhamasisha tafiti za uendelezaji wa Jotoardhi; kujifunza kuto-kana na maonesho ya teknolojia zilizopo katika tasnia ya Jotoar-dhi; na kukuza utalii, kilimo na mazingira.

    Jotoardhi ni mojawapo ya

    chanzo cha nishati kitokanacho na mvuke unaotoka ardhini, hususan katika maeneo yaliyo katika Bonde la Ufa (Rift Valley). Aidha nchi zilizo katika bonde la Ufa (African Rift Geothemal Facility ARGeo) ni pamoja na Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.

    Kongamano hilo la tano litakalofanyika Jijini Arusha litaongozwa na Kaulimbiu; Jotoardhi ni Suluhisho la Mahitaji ya Nishati katika Afrika (Geothermal: Solution to Africa Energy Needs).

    n Wanachama bonde la ufa kushiriki

    Kongamano Jotoardhi kuinufaisha TanzaniaKongamano Jotoardhi kuinufaisha Tanzania

    Power China yataka kuwekeza Mto Rufiji Na Mohamed Saif,

    Dar es Salaam

    Kampuni ya Kimataifa ya Power China yenye makao makuu yake nchini China imeonyesha nia ya kuwekeza katika umeme wa maji

    kwenye Bonde la Mto Rufiji. Hayo yalielezwa na ujumbe wa

    viongozi wa Kampuni hiyo ukion-gozwa na Makamu wa Rais wa kampuni hiyo, Wang Bin wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

    Ujumbe huo ulieleza kuri-dhishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo nchini na uli-bainisha kuwa upo tayari kufanya uwekezaji hususan katika eneo husika.

    Naye Katibu Mkuu Maswi, aliikaribisha Kampuni hiyo kwa ajili ya uwekezaji husika na aliahidi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo, Tumefurahishwa na ujio wenu na tupo tayari kushirikiana nanyi katika kuhakikisha tunafikia malengo ya kuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania alisema.

    Aidha, mbali na eneo hilo, Maswi ameikaribisha kampuni hiyo kuangalia maeneo mengine ya uwekezaji katika sekta ya Nishati ili kuweza kuwa na vyanzo mbal-imbali vya uzalishaji umeme.

    Makamu huyo wa Rais wa kampuni ya Power China ameeleza kuwa kampuni hiyo imewekeza katika maeneo mbalimbali barani Afrika na wana zaidi ya miaka 30 barani Afrika. Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (kulia) akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Kampuni

    ya Power China, Wang Bin (katikati) na mtendaji mwingine kutoka kampuni hiyo.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa kwanza kushoto), Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughuilikia Umeme, Mhandisi, Innocent Luoga (kushoto kwa Katibu Mkuu), na Mkurugenzi wa Sheria katika Wizara ya Nishati na Madini, Medard Kalemani (wa kwanza kulia), wakijadiliana jambo na watendaji kutoka Kampuni ya Power China, walioongozwa na Makamu wa Rais wa kampuni hiyo, Wang Bin (hawaonekani pichani) . Kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza katika umeme wa maji kwenye Bonde la Mto Rufiji.

    u

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akieleza jambo katika kikao cha kuagana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) wanaohudhuria mafunzo ya namna nchini India na Thailand zilivyoendelea kutokana na sekta ya umeme. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, anayefuatia ni Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise na wajumbe wa Kamati hiyo.

    TUICO CHANGIENI MABADILIKO TANESCO MASWI Na Asteria

    Muhozya, Dar es Salaam

    Katibu Mkuu Wiz-ara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, ameki-taka Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kuwa sehemu ya ma-badiliko ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufua-tia mpango wa Serikali wa kuli-badili shirika hilo.

    Hayo yalibainishwa wakati wa kikao kati yao na Katibu Mkuu Maswi, ambacho pia kilihudhuriwa na Naibu Ka-tibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ma-jadiliano ya TUICO, wakati wakiagwa ili kuhudhuria mafunzo ya namna ya kui-boresha shirika la TANESCO, yatakayofanyika katika nchi za India na Thailand.

    Maswi aliongeza kuwa, Wizara imeona ni muhimu kwa Kamati ya TUICO kuhudhuria mafunzo katika nchi hizo, kwa-sababu mbalimbali ikiwemo ya Chama cha wafanyakazi nchini India kusaidia kwa kiasi kikub-wa kuleta mabadiliko makub-wa ya nishati kupitia Shirika la Umeme nchini humo hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi hiyo.

    Akizungumzia kuhusu uzoefu wa nchi ya Thailand alieleza kuwa, nchi hiyo katika miaka ya 1978 ilikua ikizalisha umeme wa kiasi cha asilimia 10 tu lakini sasa inazalisha umeme kwa kiasi cha asilimia 98.8, pamoja na kwamba ni mion-goni mwa nchi maskini lakini imefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi jambo ambalo linaifanya nchi hiyo kuwa ya mfano kwa Tanzania.

    Shirika la Umeme India ni miongoni mwa mashirika makubwa duniani, wafanyaka-zi walichangia kwa kiasi kikub-wa kuleta mabadiliko. Thailand

    wanafanya mambo makubwa kupitia nishati, hata sisi tunata-ka kukimbia tutoke hapa tulipo, hivyo kujifunza kwa wenzetu na kuona wamefanya nini ni muhimu.

    Aidha, aliwataka kuy-achukua mafunzo hayo kwa uz-ito mkubwa ambapo anatarajia uzoefu watakaoupata usaidie na kuwa chachu ya mabadiliko bora na maendeleo ya Shirika la Umeme Tanzania kama ilivyo-tokea kwa nchi ya India.

    Ninyi kama TUICO tu-nataka muwe mabalozi wazuri katika jambo hili, leteni heshi-ma na matunda kwa manufaa ya sekta hii. Tafuteni namna ya kuiboresha TANESCO, Mtaona namna TANESCO Thailand na India wanavyofan-ya kazi, tunataka tutoke hapa, alisisitiza Maswi.

    Kwa upande wake Katibu Mkuu Msaidizi wa TUICO - Taifa Peles Jonathan, alieleza kuwa, mafunzo katika nchi za India na Thailand yatawaweze-sha kutoa maoni mazuri kutoka katika jumuiya hiyo ambayo yatasaidia katika maboresho ya shirika hilo ambalo mchango wake katika kuchangia uchumi wa Taifa ni mkubwa.

    Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano TUI-CO- (Tanesco) Abdul Mkama aliushukuru uongozi wa Wiz-ara kwa fursa hiyo ya kujifunza na kuahidi kwamba, wataitu-mia fursa hiyo kujifunza na kurudi na mwongozo ambao utakuwa na manufaa katika kuboresha shirika hilo.

    Hatuendi kutembea wala kufanya manunuzi. Tunak-wenda kufanya kazi. Tunataka kurudi na taarifa yenye kuleta mwongozo wa kuliboresha shirika letu, aliongeza Mkama.

    Wajumbe hao wa kamati ya majadiliano watatembelea sehemu mbalimbali ili kujio-nea maendeleo yalitokana na umeme nchini Thailand na namna Shirika la Umeme India kupitia Jumuiya ya Wafanyaka-zi lilivyoleta mabadiliko ndani ya shirika na kiuchumi kwa taifa hilo.

    HEMU kukagua Migodi Kanda ya Kusini

    Mohamed Saif- Dar es Salaam

    Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira katika Wizara ya Nishati na Madini kinatarajia ku-fanya ukaguzi wa maz-

    ingira katika migodi mbalimbali ka-tika Kanda ya Ziwa Nyasa na Kusini Magharibi ili kubainisha hali halisi ya utekelezaji wa Mpango wa Usimam-izi wa Mazingira (Environmental Management Plan) ya migodi husika.

    Ukaguzi huo unatarajia kufanyika katika mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka na migodi ya dhahabu ya Matundas na Shanta iliyopo katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

    Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Gidion Kasege ilieleza kuwa hii ni moja ya kaguzi zinazofanywa mara kwa mara na wataalamu kutoka Kitengo hicho ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji madini zinafanyika kwa kufuata uta-ratibu wa utunzaji mazingira ili kuto-leta athari.

    Mkuu wa kitengo cha Mazingira katika Wizara ya Nishati na Madini, Gideon Kasege.

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    PRESS RELEASE

    The Commissioner for Minerals wishes to inform holders of Mineral Rights and oth-er interested persons/entities to prepare for registration of clients for the purpose of operating the Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP). The OMCTP is a public facing mining cadastre geo-portal that will allow registered people to apply for mineral rights, maintain their existing rights, submit reports and produc-tion returns electronically and undertake online payments by using mobile phone money payment modalities (for example M-Pesa, Tigo-Pesa and Airtel Money) or VISA/MasterCard. In addition, the geo-portal will provide access to the vast geo- data repositories of the Ministry and the Geological Survey of Tanzania. Where appropriate, these datasets will be available for purchase and downloading.

    All holders of Division A Licences (Prospecting and Retention Licences); Division B Licences (Special Mining Licences, and Mining Licences); and Division C Licence (Primary Mining Licences) are required to register in order to continue to maintain their licences after December 2014. Other interested persons/entities are also en-couraged to register. The OMCTP will have the following benefits:

    Enabling the Ministry to speedily improve service delivery and transparency in the administration of the mineral sector; Allowing applications to be recorded by applicants directly, thereby reducing the existing application recording backlog especially those experienced in the Regional Mines Offices.

    Allowing mineral rights renewals, transfers and extensions to be managed through the online system;

    Allowing payments to be submitted and validated through the OMCTP with the funds deposited directly in Ministrys bank account;

    Facilitating all reports to be submitted electronically through the OMCTP;

    Giving the Cadastre Officers more time to process applications and follow-up on compliance issues; and

    Allowing registered clients to accurately and timely update their records, such as addresses and contact numbers.

    In order for Mineral Right holders to register, they will be required to present the following documents for validation at the Office where their Licences were issued or were last renewed:

    A fully completed OMCTP registration form which will become available from the Ministrys website;

    Mineral Right holders for Division A and B licences shall be required to submit the completed registration form at the Ministrys Headquarters with original licence documents and proof of payments since the last renewal. Licences acquired through transfers will require attachment of transfer certificate;

    Mineral Right holders for Division C and D licences shall be required to submit the completed registration form with required documentation to the

    relevant Zonal or Resident Mines Office. Original Licences must be presented to-gether with proof of payments since last renewal of licences; and transfer certifi-cates must be presented for transferred licences. Clients who will be represented by agents to operate the OMCTP, will require Power of Attorney authorising them to transact on the OMCTP; and the Power of Attorney must be presented in original form.

    Other individuals or entities not holding any mineral right at this time, but inter-ested to be registered for future use of the OMCTP will be required to submit the completed registration form together with their valid identification documents to the Ministrys Headquarters or at any nearby Zonal or Resident Mines Office.

    For the case of the Mineral Right Holders, upon presentation of the above men-tioned documentation, the validation process will involve the following:

    A Legal Entity History Report that will be generated by Licensing Offi cers, detailing particulars of licences held by the respective li cence holder. The report will cover information such as particulars of li cences held, overdue payments and overdue reports;

    The Licensing Officers will only proceed to capture the User Registration once the data is up-to-date and will inform the OMCTP applicant if more information is required;

    The Licensing Officers will create a user profile in the OMCTP on validating that the information is up-to-date;

    The Registered users will receive an email notifying that, user profile has been activated; and

    The Registered users will be required to create a password for the first time before access is enabled. Registration will start at MEM HQ, where holders of Division A and B li cences will be invited to come for registration in a pre-determined order to be published by 30 September, 2014. Registration of division C and D licences will be coordinated through Zonal Mines Offices, in a pre-de termined order to be announced by 31st October 2014.

    The introduction of Online Mining Cadastre Transactional Portal is a very important step in the Ministrys effort to enhance transparency and good governance in the mineral sector; as well as improving management of mineral licences in Tanzania. The portal will serve people at the Ministry Headquarters and at 21 regional offices, with new of Bariadi, Nachingwea, Njombe and Moshi expected to start using the OMCTP before 2016.

    For Further Information, you may contact: The Commissioner for Minerals,Ministry of Energy and Minerals,P.O. Box 2000,11474 DAR ES SALAAMEmail: [email protected] Or [email protected]

    THE LAUNCHING OF ONLINE SYSTEM FOR APPLICATION OF MINING LICENCES (ONLINE MINING CADASTRE TRANSACTIONAL PORTAL)

    18 September, 2014

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    Kamishna wa Madini anawataka wamiliki wote wa leseni za madini na wadau wa Sekta ya Madini kwa ujumla kujiandaa kwa usajili kwa ajili ya kutumia huduma za leseni kwa njia ya mtandao kupitia mfumo ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP). Mfumo wa kielektroniki wa OMCTP utawawezesha wateja waliosajiliwa kutuma maombi, kuhakiki taarifa za leseni wanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi na kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njia ya kielektroniki kupi-tia mitandao (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, VISA/Master card na kad-halika). Aidha, Mfumo wa OMCTP utawawezesha wateja kupata taarifa za kijiolojia zilizoandaliwa na Wakala wa Jiolojia wa Tanzania (GST), kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na GST.Wamiliki wote wa leseni za Daraja A (Prospecting Licence na Retention Licences); leseni za Daraja B (Special Mining Licence, na Mining Licence); na leseni za Daraja C (Primary Mining Licence) watatakiwa wawe wame-jisajili na mfumo huo wa kielektroniki ifikapo Disemba, 2014 ili waweze kuendelea kupata huduma ya leseni zao.

    Mfumo wa kielektroniki wa OTMCS utarahisisha mambo yafuatayo:- Kuongeza uwazi na kasi ya utoaji wa leseni za madini; Wateja wataingiza maombi ya leseni wao wenyewe, hivyo kupunguza tatizo la mlundikano wa maombi kwenye ofisi za madini; Wateja na Serikali watakuwa na uhakika na maombi yote yatakayowasilishwa (yakiwamo maombi ya sihia (transfer), extension, renewal n.k.), na pia kuwa na uhakika na malipo yote yatakayofanywa kupitia mfumo wa OMCTP; Wateja watapata taarifa za leseni zao kila wakati na kujua wanapotakiwa kufanya malipo ya leseni au watakapotaki wa kutuma taarifa za utendaji kazi. Mfumo huo utarahisha mawasiliano kati ya Wizara na wamimiki wa leseni; na Wateja wataweza kuhuisha taarifa za leseni zao kama vile anwani na namba za simu kupitia mfumo wa OMCTP pindi taarifa hizo zitakapobadilishwa. Ili kujisajili kwenye mfumo huo wa OMCTP, wamiliki wa leseni watatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi za madini zinazohusika na utoaji au uhuishaji wa lese ni husika:- Fomu ya kuomba usajili wa OTMCP iliyojazwa kikamimifu ambazo zitaweza kupatikana kwenye tovuti ya Wizara; Wamiliki wa leseni za madaraja A na B wawasilishe maombi yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara (MEM HQ) wakiambatisha leseni halisi pamoja na stakabadhi za malipo ya leseni husika kutokea leseni husika ilipohuishwa kwa mara ya mwisho hadi wakati wa kuomba usajili. Leseni zilizopatikana kwa njia ya sihia zi ambatishwe na hati halisi ya sihia (transfer certificate); Wamiliki wa leseni za madaraja C na D watahudumiwa kupitia ofisi za madini za mikoani (ZMO/RMO) zinazo-husika na usimamizi wa leseni husika. Maombi ya usajili yaambatane na leseni halisi pamoja na stakabadhi za malipo ya ada kutokea leseni husika ilipohuishwa kwa mara ya mwisho hadi wakati wa kuomba usajili. Leseni zilizopatikana kwa njia ya sihia ziambatishwe na hati halisi ya sihia; na

    Wamiliki wa leseni watakaotuma mawakala kwa ajili ya kujisajili na mfumo wa OTMCP, ni lazima wawape mawakala husika nguvu za uwakili (Power of Attorney) za kuwaruhusu mawakala husika kushughulikia leseni. Hati halisi ya Nguvu za Uwakili ziwasilishwe pamoja na fomu ya kuomba kujisajili kwenye mfumo wa OMCTP.Wadau wengine ambao hawamiliki leseni, na wangependa kusajiliwa, wa-wasilishe fomu a usajili pamoja na hati za utambulisho katika Ofisi ya Wiz-ara au Katika ofisi za Madini za Kanda au Ofisi za Madini za Wakazi.

    Uhakiki wa nyaraka za maombi ya usajili kwenye mfumo wa OMCTP uta-zingatia yafuatayo:- Afisa wa leseni atatayarisha muhtasari wa taarifa za leseni husika kutoka kwenye masjala ya leseni (MCIMS) utakaoonesha wamiliki wa leseni, mapungufu ya leseni husika (ada zinazodai wa, taarifa ambazo hazijawasilishwa n.k.) ili kuoanisha na ta arifa zilizowasilishwa na mwombaji; Afisa wa leseni atahakiki taarifa za leseni husika na kuhuisha taarifa ambazo zinahitajika ikiwa ni pamoja na taarifa za malipo ya ada; Pindi taarifa za leseni zote za mwombaji zitakapohuishwa kwenye masjala ya mfumo wa MCIMS, ombi husika la usajili lit ashughulikiwa. Aidha, mwombaji husika atajulishwa kama kuna mapungufu katika taarifa alizowasilisha na kutakiwa awasilishe upya; Afisa wa Leseni atamsajili mmiliki wa leseni kuwa mtumiaji wa OT MCP baada ya kuhakiki taarifa za leseni zote za mmiliki husika; Mwombaji aliyekamilisha usajili kwenye mfumo wa OMCTP ata pokea ujumbe wa barua pepe au ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuthibitisha usajili wake; na Kabla ya kuanza kutumia huduma ya leseni kupitia mfumo wa OMCTP, msajiliwa atatakiwa kubadilisha namba yake ya siri (password). Usajili utaanza kwenye ofisi za Wizara makao makuu ambapo wamiliki wa leseni za madaraja A na B watatangaziwa utaratibu wa kujisajili ifikapo tarehe 30 Septemba, 2014. Usajili wa leseni za madaraja C na D utaratibiwa kupitia ofisi za Madini za kanda kwa utaratibu ambao utatangazwa ifikapo Oktoba 31, 2014.

    Wizara ya Nishati na Madini inaanzisha mfumo wa OMCTP ili kuongeza uwazi, utawala bora na kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini. Hu-duma ya OMCTP itapatikana katika ofisi ya makao makuu ya wizara na kwenye ofisi 21 za mikoani (RMO na ZMO). Aidha, ofisi mpya nne zitaanza kutoa huduma hiyo katika kipindi cha miaka miwili ijayo. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia anwani zifuatazo:

    Kamisha wa Madini,Wizara ya Nishati na Madini,S.L.P. 2000,11474 Dar es Salaam.Baruapepe: [email protected] [email protected] www.mem.go.tz

    KUANZISHWA KWA HUDUMA ZA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO-ONLINE MINING CADASTRE TRANSACTIONAL PORTAL

    18 Septemba, 2014

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

    5 AFRICAN RIFT GEOTHERMAL CONFERENCE (ARGeo - C5)Geothermal: Solution to Africas Energy Needs

    29 -31 October, 2014 AICC Arusha, TanzaniaHosted and organized by the Government of the United Republic of Tanzania in collaboration with UNEP, GDC and other partners, Endorsed by the international Geothermal Association.

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Mwanasheria wa mgodi wa Shanta Mining Limited Bw. David Rwechungura, (kulia) akielezea mchango wa mgodi huo katika uwezeshaji wa vikundi vya wachimbaji wadogo mara timu ya majaji ilipotembelea kikundi cha wachimbaji wadogo kijulikana-cho kwa jina la Aminika Group

    Wadau wa madini wapongeza Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji

    Na Greyson Mwase

    Wadau kutoka katika makampuni mbalimbali ya madini nchini wamepongeza zoezi lililofanyi-ka katika mikoa mbalimbali la kumtafuta mshindi wa tuzo ya Rais ya huduma za jamii na uwezeshaji .

    Zoezi hilo lenye kuhusisha makampuni ya madini, mafuta na gesi nchini linalenga kuanga-lia mchango wa makampuni hayo katika utoaji wa huduma za jamii katika maeneo ya maji, miundombinu, elimu, afya, ajira, uwezeshaji wa vikundi vidogo na manunuzi ya ndani.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti walise-ma kuwa kupitia tuzo ya Rais Serikali inaonesha ni jinsi gani inathamini mchango wa wawekezaji nchini katika huduma za jamii.

    Afisa Mahusiano ya Jamii kutoka katika Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold, Manase Ndoloma alisema kuwa kuanzishwa kwa tuzo ya Rais katika makampuni ya madini yanay-ofanya vizuri katika utoaji wa huduma za jamii ni kichocheo kikubwa kwa makampuni hayo katika uboreshaji wa huduma zake.

    Hii tuzo ya Rais inatupa hamasa kama kampuni kuendelea kuchangia zaidi katika hu-duma za jamii na pia inaonesha ni jinsi gani Serikali inatambua mchango wa wawekezaji hu-susan makampuni ya madini katika huduma za jamii.

    Manase alieleza kuwa, kumekuwepo na mtizamo hasi kwa jamii kuwa makampuni ya madini hayana mchango wowote katika uboreshaji wa huduma za jamii katika maeneo

    ya wananchi wanayoyazunguka na kuongeza kuwa tuzo hii itakuwa kama njia ya kuonesha mchango wa makampuni hayo na wananchi ku-pata uelewa wa mchango wa makampuni hayo

    Vilevile Manase alisisitiza kuwa, lengo la mgodi wa GGM ni kuhakikisha kuwa un-achangia ipasavyo ukuaji wa uchumi wa mji wa Geita kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii ili mara baada ya kumalizika kwa shughuli za mgodi huo pawepo na alama ya miradi ya maen-deleo itakayonufaisha vizazi vijavyo.

    Naye Afisa Mahusiano wa Mgodi wa wa dhahabu wa Buzwagi Dorothy Bikurakule al-iongeza kuwa tuzo ya Rais inahamasisha wa-nanchi wanaozunguka migodi kuona uzito wa mchango wa migodi hiyo katika huduma za jamii na kuimarisha mahusiano

    Bikurakule alisisitiza kuwa, kupitia ushinda-ni katika tuzo ya Rais, makampuni ya madini yanaongeza kasi katika uboreshaji wa huduma za jamii hivyo kupelekea wananchi wanaozun-guka migodi hiyo kuendelea kuneemeka na hu-duma zake.

    Alisisitiza kuwa tuzo ya Rais inawezesha makampuni hayo kujitangaza zaidi duniani ka-tika ushiriki wake katika huduma za jamii kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo hivyo kujijengea heshima na kuvutia wawekezaji.

    Wakati huohuo wachimbaji wadogo waki-zungumzia tuzo ya Rais walisema kuwa kupitia tuzo ya Rais, makampuni ya madini yatahamasi-ka katika uboreshaji wa huduma za jamii kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya makam-puni hayo, ikiwemo wachimbaji wadogo.

    Kwa upande wake Abraham Meshack ambaye ni mmoja wa wachimbai wadogo wa-naonufaika kupitia ufadhili wa kiwanda cha

    TUZO kuyeyusha madini ya shaba cha TPM kilichopo Mpanda mkoani Katavi alise-ma kuwa tuzo ya Rais inaongeza kasi ya makampuni ya madini kuboresha utoaji wa huduma za jamii na uwezeshaji wa vikundi vya wachimbaji wadogo

    Tunaamini kupitia tuzo hii ya Rais yenye kulenga kuhamasisha makampuni kuchangia katika huduma za jamii pamoja na uwezeshaji wa vikundi vya wachim-baji wadogo, shughuli zetu za uchimbaji madini zitaboreshwa kwani makampuni yatatupatia vifaa vya kisasa. Alisema Bw. Meshack

    Meshack aliendelea kusema kuwa tuzo ya Rais imetoa mwamko mpya kwa makampuni ya madini katika huduma za jamii husan katika uwezeshaji wa vikundi vya wachimbaji wadogo.

    Alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa kiwanda cha TPM kinachukua tuzo katika uwezeshaji wa vikundi vidogo, kiwanda hi-cho kitaboresha mazingira yao ya kazi kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya uchimbaji pamoja na mitaji.

    Naye Pili Said ambaye ni mjumbe katika kikundi cha wachimbaji wadogo cha Aminika Group kinachofadhiliwa na mgodi wa Shanta Mining Limited

    uliopo mkoani Singida alisema kuwa shi-dano hili linatumika kama fursa ya kuwai-nua wachimbaji wadogo katika shughuli za uchimbaji na hivyo kuchangia katika ukuaji uchmi.

    Aliendelea kusema kuwa, baada ya makampuni ya madini kuhamasika kupi-tia tuzo ya Rais, makampuni hayo yat-aongeza kasi ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupitia mitaji na vifaa na kupele-kea wachimbaji hao kuzalisha zaidi na ku-changia katika ukuaji wa uchumi.

    Halikadhalika, Zacharia Mwita am-baye ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana cha Nyakegema Group kinachofadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa North Mara kupitia kilimo cha mboga alisema kuwa baada ya mgodi huo kushiriki katika awa-mu ya kwanza ya tuzo hiyo mwaka jana, mgodi huo uliongeza kasi katika uwez-eshaji wa vikundi vidogo ili kuhakikisha kuwa unanyakua tuzo

    Alipongeza kuanzishwa kwa tuzo hiyo na kuyataka makampuni ya madini yote nchini kushiriki na hivyo kupelekea uchumi wa nchi kukukua kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii.

    Taifa tunalojivunia ni lile lenye uchumi imara unatoa ajira na maisha bora kwa wote. Tanzania yenye amani, utulivu wa utaifa wa kudumu. Tumeingia kwenye uchumi wa gesi asilia wenye mapato makubwa yatakayoondoa umasikini nchini mwetu. Uongozi wa kizalendo na wenye umahiri mkubwa unahitajika. Tuchape kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu mkubwa sana. Kizazi chetu kitashinda na

    vizazi vijavyo navyo vitaushinda umasikini. Hii ndiyo Tanzania tuitakayo