alliance for change and transparency (act-wazalendo) …...kidemokrasia na falsafa ya unyerere...

67
1 Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Chama cha Wazalendo KATIBA TOLEO LA 2015 Kama ilivyoidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa ACT- Wazalendo, Jumamosi Tarehe 28 Machi 2015 Ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Dar es Salaam.

Upload: others

Post on 08-Jan-2020

2 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

1

Alliance for Change and Transparency

(ACT-Wazalendo)

Chama cha Wazalendo

KATIBA

TOLEO LA 2015

Kama ilivyoidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa ACT-

Wazalendo, Jumamosi Tarehe 28 Machi 2015

Ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Dar es Salaam.

Page 2: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

i

YALIYOMO

DIBAJI ................................................................................................................................... iv

SURA YA KWANZA ............................................................................................................. 1

JINA, MAKAO MAKUU, ALAMA, ITIKADI, LUGHA, MISINGI NA

MALENGO YA CHAMA ...................................................................................................... 1

SEHEMU YA I ........................................................................................................................ 1

1. Jina la Chama ................................................................................................................... 1

2. Makao Makuu ya Chama ................................................................................................. 1

3. Alama za Chama ........................................................................................................... 1

4. Itikadi na Falsafa ya ACT: ............................................................................................. 2

5. Lugha rasmi ya chama ................................................................................................... 2

SEHEMU YA II ...................................................................................................................... 3

MISINGI NA MALENGO YA CHAMA .............................................................................. 3

6. ACT itaongozwa .............................................................................................................. 3

7. ACT itapambana kuhakikisha kwamba inashinda uchaguzi ............................................ 3

SURA YA PILI ........................................................................................................................ 5

UANACHAMA NA UONGOZI ............................................................................................ 5

SEHEMU YA I ........................................................................................................................ 5

8. Uanachama wa ACT utakuwa wazi kwa raia wote.......................................................... 5

9. Ada ya Uanachama .......................................................................................................... 6

10. Haki za mwanachama wa ACT...................................................................................... 6

11. Kukoma Uanachama ...................................................................................................... 7

12. Orodha ya Uanachama ................................................................................................... 8

13. Ahadi tano za kila mwanachama wa ACT ..................................................................... 9

SEHEMU YA II .................................................................................................................... 10

14. Sifa za Kiongozi........................................................................................................... 10

15. Aina sita za Viongozi ................................................................................................... 10

Page 3: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

ii

16. Haki za Kiongozi ......................................................................................................... 11

17. Ukomo wa Uongozi ..................................................................................................... 11

18. Kukasimu Madaraka .................................................................................................... 12

SURA YA TATU ................................................................................................................... 13

19. Kuteuliwa kwa Kamati ya Uadilifu ............................................................................. 13

20. Mamlaka ya Kamati za Uadilifu .................................................................................. 14

21. Kazi ya Kamati za Uadilifu.......................................................................................... 15

22. Makosa Yanayoweza Kusababisha Hatua za Kinidhamu ............................................ 16

SURA NNE ............................................................................................................................ 18

23. ACT-Tanzania ni Chama cha kitaifa ........................................................................... 18

24. Ngazi ya ACT Tawi ..................................................................................................... 18

25. Ngazi ya ACT Kata/Wadi ............................................................................................ 21

26. ACT Jimbo ................................................................................................................... 27

27. Ngazi ya ACT Mkoa .................................................................................................... 32

28. ACT Zanziber .............................................................................................................. 37

29. ACT-Taifa .................................................................................................................... 39

30. Akidi katika vikao vyote .............................................................................................. 51

SURA YA TANO .................................................................................................................. 52

31. NGOME ni vitengo au jumuiya za Chama .................................................................. 52

32. Kutakuwa na jumuiya ya wabunge wa ACT ............................................................... 52

SURA YA SITA ..................................................................................................................... 53

33. Mapato ya Chama ........................................................................................................ 53

SURA YA SABA ................................................................................................................... 55

36. Marekebisho ya Katiba ................................................................................................ 55

37. Kanuni za Uendeshaji Chama ...................................................................................... 55

38. Kuvunjwa kwa Chama ................................................................................................. 55

Page 4: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

iii

NYONGEZA YA KWANZA ............................................................................................... 57

KANUNI ZA MWENENDO NA MAADILI YA VIONGOZI WA ACT ........................ 57

SEHEMU YA I: ..................................................................................................................... 57

MASHARTI YA JUMLA ..................................................................................................... 57

SEHEMU YA II: ............................................................................................................... 57

SIFA ZA KIONGOZI ........................................................................................................ 57

SEHEMU YA III: ................................................................................................................. 58

MAADILI YA VIONGOZI .................................................................................................. 58

SEHEMU YA IV: ................................................................................................................... 59

MWENENDO NA MATENDO YASIYORUHUSIWA ....................................................... 59

SEHEMU YA V: ................................................................................................................... 60

MASUALA KINZANI YANAYOHUSIANA NA KAZI ................................................... 60

SEHEMU YA VI: .................................................................................................................. 60

KUTANGAZA MALI BINAFSI ZA KIONGOZI ............................................................. 60

SEHEMU YA VII: ................................................................................................................ 61

ADHABU NA MAREJEO MENGINE ............................................................................... 61

SEHEMU YA VIII: ............................................................................................................... 62

MASHARTI MENGINEYO NA MASHARTI YA MPITO ............................................. 62

Page 5: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

iv

DIBAJI

KWA KUWA tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, ufisadi, uzembe na uvivu;

NA KWA KUWA tumeamua kuhakikisha kuwa maliasili ya Nchi yetu Tanzania ni

mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini

kwetu na kuleta maendeleo sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na

kisiasa;

NA KWA KUWA tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea

ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini,

kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na kwa kuzingatia misingi ya haki kwa watu

wake wote;

NA KWA KUWA tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili

kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Mwafrika na kujenga bara lenye sauti yenye

nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa ulimwenguni;

NA KWA KUWA tumeamua kupigania demokrasia, umoja, utu, uadilifu,

uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa;

NA KWA KUWA kwa nia moja tumeamua kujenga Chama chenye kufuata misingi

ya Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic Socialism), na misingi asili iliyoasisi Taifa

letu (Unyerere) ikiwemo Azimio la Arusha1; na

NA KWA wajibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na

utamaduni wa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania;

HIVYO BASI; Sisi Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha

Wazalendo (ACT) uliofanyika Dar es salaam leo tarehe 28 Machi 2015, tumepitisha

KATIBA MPYA ya Chama chetu itakayojulikana kama

KATIBA YA ACT YA MWAKA 2015.

1 Tamko la Azimio la Arusha lililotolewa na Chama cha TANU mnamo mwezi Februari mwaka 1967

. Tutazingatia misingi ya Azimio hili na hususani Miiko ya Uongozi kama itakavyofanyiwa marejeo

mara kwa mara, pamoja na Maazimio mengine yatakayotangazwa na chama kwa mujibu wa Katiba

hii yatakuwa ni marejeo halali ili kufikia maamuzi yeyote ya kisera ya Chama cha ACT – Tanzania.

Page 6: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

1

SURA YA KWANZA

JINA, MAKAO MAKUU, ALAMA, ITIKADI, LUGHA, MISINGI NA

MALENGO YA CHAMA

SEHEMU YA I

JINA, MAKAO MAKUU, ALAMA, ITIKADI NA LUGHA

1. Jina la Chama

Jina la Chama litakuwa ni ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY

(ACT) na chama kitajulikana kwa Kiswahili kama CHAMA CHA WAZALENDO.

2. Makao Makuu ya Chama

(1) Makao Makuu ya Chama yatakuwa ni Dar es Salaam

(2) Kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar na Mwanza.

3. Alama za Chama

(1) Alama za Chama zitakuwa ni:

i. Rangi za Chama ambazo ni Zambarau na Nyeupe;

ii. Bendera ya Chama ambayo itakuwa ni ya rangi ya Zambarau ama

Nyeupe ikiwa na nembo ya chama katikati ya bendera;

iii. Nembo ya Chama

iv. Wimbo rasmi wa Chama

v. Vazi rasmi la Chama.

(2) Halmashauri Kuu ya Chama itatengeneza na kufafanua muundo na yaliyomo

ndani ya Nembo ya Chama, Wimbo rasmi wa Chama na Vazi rasmi la Chama

kupitia Kanuni za uendeshaji Chama zitakazotungwa na Halmashauri Kuu ya

chama. Halmashauri Kuu itakuwa na uwezo wa kubadili alama za chama

kutokana na mahitaji ya wakati.

Page 7: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

2

4. Itikadi na Falsafa ya ACT:

(1) ACT inaamini katika msingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic Socialism).

Misingi mikuu ya ujamaa wa Kidemokrasia ni:

i. Undugu;

ii. Usawa;

iii. Uhuru;

iv. Heshima kwa kila mtu; na

v. Demokrasia

(2) Falsafa ya ACT ni UNYERERE, ikiwa ni dhamira ya kurudisha, kuhuisha na

kupigania misingi mama iliyoasisi Taifa la Tanzania, kama ilivyoainishwa katika

Azimio la Arusha na kwa mazingira ya Tanzania ya sasa.

(3) Shabaha kuu ya ACT ni kupigania na kusimamia uwajibikaji na uwazi nchini

Tanzania na Afrika kwa ujumla na kwamba mabadiliko ni ajenda ya kudumu.

(4) Chama kinazingatia elimu, uadilifu, uwajibikaji, kujitegemea na bidii katika

kazi kama njia kuu za kujikomboa dhidi ya umaskini, ujinga, maradhi na

rushwa, ambavyo ndio maadui wakuu wa Taifa la Tanzania na Afrika kwa

ujumla.

5. Lugha rasmi ya chama

(1) Lugha rasmi ya chama itakuwa ni Kiswahili.

(2) Bila kuathiri ibara ndogo ya (1) ya ibara hii hapo juu, lugha ya Kiingereza

inaweza kutumika sambamba na lugha ya Kiswahili inapobidi.

(3) Nyaraka zote muhimu, ikiwemo Katiba hii, zitaandikwa katika lugha ya

Kiswahili na kutafsiriwa katika lugha ya Kiingereza.

(4) Chama kitaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano

mbadala zikiwemo lugha za alama kwa kadri ya mahitaji.

Page 8: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

3

SEHEMU YA II

MISINGI NA MALENGO YA CHAMA

6. ACT itaongozwa

1) ACT itaongozwa na Misingi Kumi (10).

2) Misingi hii imewekwa kwa ajili ya kutekeleza Itikadi ya Ujamaa wa

Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake.

3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu ya chama na

hivyo kipengele chochote cha Katiba hii kitakachokiuka mmoja wa misingi

hii, kitakuwa batili.

4) Misingi kumi ya ACT ni:

i) Uzalendo

ii) Usawa

iii) Kupinga na Kupiga Vita ubaguzi

iv) Uadilifu

v) Uwazi

vi) Uwajibikaji

vii) Demokrasia

viii) Uhuru wa Mawazo na Matendo

ix) Utu

x) Umoja

5) Misingi hi itafafanuliwa katika nyaraka mbalimbali zitakazotolewa na Chama

kwa mujibu wa Katiba hii na Kanuni za uendeshaji wa Chama.

7. Malengo

ACT itapambana kuhakikisha kwamba inashinda uchaguzi na kuunda serikali ili

kutekeleza malengo yafuatayo:

i) Kuhakikisha kwamba serikali inatumia raslimali yote ya nchi kwa ajili ya

kuondosha umaskini, ujinga, maradhi, rushwa, na kuleta maendeleo ya nchi

kwa ujumla;

(ii) Kupigania na kulinda uongozi bora na Utawala wa Sheria;

(iii)Kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia raslimali na serikali

inayowajibika kwa umma wa Watanzania;

Page 9: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

4

(iv) Kuhakikisha usawa mbele ya Sheria kwa raia wote wanaume kwa wanawake

bila kujali kabila, rangi, imani za kidini, itikadi, utamaduni ama hadhi ya mtu

kiuchumi na kijamii;

(v) Kuendeleza na kudumisha Demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama

vingi vya siasa;

(vi) Kuchochea, kuimarisha na kulinda uzalendo, uadilifu, uwajibikaji na uwazi

kama misingi mikuu katika uongozi wa nchi;

(vii) Kuchochea na kuendeleza mapambano katika kulinda haki za watoto,

wanawake na watu wenye ulemavu;

(viii) Kupigania haki na heshima ya wafanyakazi, wakulima, wafugaji na

wajiasiliamali katika ngazi zote;

(ix) Kudhibiti soko huria ili kuhakikisha kuwa haliathiri haki za utu za

wafanyakazi na walaji wenye kipato cha chini;

(x) Kulinda na kuendeleza mazingira bora kwa vizazi vya leo na vijavyo;

(xi) Kuhakikisha kuwa idhini, mikataba na ushirikiano wa kikanda barani Afrika

ambavyo Tanzania ni mwanachama kama vile Umoja wa Afrika (AU),

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za

Kusini mwa Afrika (SADC) vinaendana na misingi mikuu ya kidemokrasia

na kuendeleza kuheshimu utawala wa sheria Afrika;

(xii) Kuhimiza ushirikiano na mahusiano na vyama vingine vinavyoamini katika

demokrasia jamii Afrika na duniani kote;na

(xiii) Kuunga mkono na kusukuma mbele juhudi za kuundwa kwa Shirikisho la

Kisiasa la Afrika Mashariki na kupigania umoja wa Afrika.

Page 10: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

5

SURA YA PILI

UANACHAMA NA UONGOZI

SEHEMU YA I

UANACHAMA

8. Uanachama wa ACT utakuwa wazi kwa raia wote

(1) Uanachama wa ACT utakuwa wazi kwa raia wote wenye umri wa kupiga kura

bila kubagua jinsia, kabila, dini, au hali yoyote.

a) Kila raia atakayekuwa ameandikishwa kuwa mwanachama wa ACT atapewa

kadi ya uanachama itakayoonyesha pamoja na habari nyingine, jina lake,

anuani, saini yake na saini ya afisa wa Chama aliyemwandikisha.

b) Kikundi cha watu kinaweza kujiunga na ACT kama kikundi kwa umoja wao,

na kwamba kikundi hicho kinakubali itikadi na misingi ya kuanzishwa kwa

ACT.

(2) Sifa mahsusi za mtu anayetaka kujiunga uanachama wa ACT:

i. Awe raia wa Tanzania;

ii. Awe ana umri wa kupiga kura kwa mujibu wa Sheria za Tanzania;

iii. Awe anakubaliana na itikadi, falsafa na misingi ya ACT;

iv. Awe na akili timamu;

v. Awe na moyo na utayari wa kukitumikia Chama na kueneza itikadi,

falsafa na misingi yake.

vi. Aonyeshe uzalendo na upendo wa kuitumikia nchi yake; na

vii. Asiwe Mwanachama wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na

ACT.

(3) ACT itakuwa na aina zifuatazo za wanachama:

i. Wanachama wa Kawaida

Ni wanachama wote waliojiandikisha na kulipa ada ya ACT na kuzingatia

masharti ya Katiba hii.

Page 11: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

6

ii. Wanachama Vikundi

Ni wanachama wanaotokana na jumuiya, taasisi, mashirika au vikundi

mbalimbali ambavyo vimeamua kujiunga na Chama kupitia umoja wao.

iii. Wanachama wanafunzi

Hawa ni wanachama ambao hawajatimiza umri wa kupiga kura na ambao

wanajiandaa kujiunga na Chama siku za usoni

9. Ada ya Uanachama

(1) Kila mwanachama atawajibika kulipa ada za uanachama kama itakavyoainishwa

kwenye Kanuni za Uendeshaji Chama zitakazotungwa na Halmashauri Kuu ya

Chama.

(2) Bila kuathiri Sheria zinazohusu vyama vya siasa nchini, pamoja na misingi na

masharti ya Katiba hii, kila mtu au kundi la watu wanaokubaliana na misingi,

malengo, sera na mipango ya Chama wanaweza kutoa ada ya kundi la

uanachama.

(3) Kutakuwa na kiingilio kwa kila mwanachama na kundi lolote litakalotaka

kujiunga na Chama itakavyoainishwa kwenye Kanuni za Uendeshaji Chama

zitakazotungwa na Halmashauri Kuu ya Chama

(4) Utaratibu wa ulipaji wa kiingilio na ada vitafafanuliwa katika kanuni za

Uendeshaji Chama.

10. Haki za mwanachama wa ACT

(1) Kila mwanachama wa ACT atakuwa na haki ya:

i. Kushiriki shughuli zote za Chama kwa mujibu wa kanuni na taratibu

zilizowekwa;

ii. Kusikilizwa na kuuliza maswali kuhusu maendeleo na mwenendo wa Chama;

iii. Kuchagua na kuchagliwa kuwa kiongozi ndani ya Chama;

iv. Kuwasilisha pendekezo au maelezo kwenye kikao chochote cha Chama, hadi

katika ngazi ya Halmashauri Kuu;

v. Kukosoa kiongozi yeyote ndani ya vikao vya Chama;

vi. Wajumbe wanaweza kuitisha kikao chochote endapo tu asilimia sabini na

tano ya wajumbe wa kikao hicho watatia saini kuhitaji kikao hicho kiitishwe;\

vii. Bila kuathiri yaliyomo katika kipengele (f) hapo juu, wajumbe wanaohitaji

kikao hicho lazima waonyeshe kuwa viongozi katika ngazi husika

Page 12: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

7

wameshindwa kuitisha vikao hivyo zaidi ya mara tatu kwa mujibu wa katiba

na utaratibu wa kuitisha vikao vya namna hiyo utafafanuliwa kwenye kanuni

za Chama.

(2) Kila mwanachama wa ACT atakuwa na wajibu wa:

a) Kujifunza na kupanua uelewa kuhusu itikadi, falsafa na misingi ya ACT;

b) Kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kwamba ACT inashinda katika

chaguzi mbalimbali zitakazoitishwa nchini kwa mujibu wa Katiba na Sheria

za Nchi;

c) Kuzingatia nidhamu ya ACT;

d) Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama na kutekeleza kwa vitendo

sera na maamuzi ya Chama;

e) Kushiriki kikamilifu katika kukomesha vitendo vyovyote ndani na nje ya

Chama vinavyoweza kuhatarisha uhai na maslahi ya Chama;

f) Kueneza itikadi, falsafa na misingi ya ACT kwa umma, na kujifunza mahitaji

ya umma kwa wakati na kuhakikisha kwamba yanazingatiwa katika sera za

Chama;

g) Kuwa mfano na sura ya ACT kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na umakini;

na

h) Kulipa ada na kuchangia mchango wowote kwa mipango maalumu na

shughuli za ACT kama itakavyokuwa imeamuliwa na vikao vya Chama.

11. Kukoma Uanachama

i. Mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa:

ii. Atajiuzulu mwenyewe kwa hiari yake kwa kuandika barua kwa Katibu wa

ngazi yake au Katibu Mkuu kwa kueleza kusudio la kuacha kuwa

mwanachama na kurudisha kadi ya uanachama;

iii. Kujiunga na chama kingine cha siasa;

iv. Kufukuzwa uanachama kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa katika Katiba

hii; au

v. Atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa katika Katiba hii.

(2) Mwanachama anaweza kusimamishwa uanachama ili kupisha uchunguzi

kuhusu mwenendo wake utakaofanywa na Kamati ya Uadilifu katika ngazi

husika.

Page 13: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

8

(3) Mwanachama anaweza kufukuzwa kwenye Chama kwa sababu zinazotokana

na mwenendo usiofaa kwa mujibu wa masharti na Kanuni za Katiba hii, na

mara baada ya kufukuzwa, uanachama wake utakoma.

(4) Pamoja na sababu nyingine kama zilivyoelezwa katika katiba hii na kanuni

zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia,

kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine

au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote

kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT.

(5) Hakuna mwanachama atakayesimamoshwa au kufukuzwa uanachama hadi

pale ambapo mashart yaliyoainishwa katika Katiba hii na Kanuni za

Uendeshaji Chama yatakapokuwa yamefuatwa.

(6) Uamuzi wa kumsimamisha uanachama ama kumfukuza mwanachama yeyote

hautakuwa na nguvu hadi pale uamuzi huo utakapokuwa umewasilishwa

kwa mwanachama husika kwa maandishi.

(7) Bila kuathiri ibara ndogo ya (6) ya ibara hii, mwanachama ambaye atakataa

kupokea taarifa ya maandishi juu ya uamuzi wa kusimamishwa au kufukuzwa

uanachama uliochukuliwa dhidi yake, atahesabika kwamba

ameshawasilishiwa taarifa hiyo kwa mujibu wa ibara ndogo ya (6) na uamuzi

wa kumsimamisha au kumfukuza uanachama utakuwa na nguvu.

(8) Kila mtu ambaye amekoma kuwa mwanachama atalazimika kurudisha mali

za Chama zilizo chini yake. Hata hivyo, ada, michango na mali zingine

ambazo atakuwa amechangia alipokuwa mwanachama hazitarudishwa

(9) Pale mwanachama atakapokuwa amepoteza uanachama wake kwa njia

yoyote ile anaweza kuomba tena uanachama wa ACT na anaweza

kukubaliwa kuwa mwanachama tena kwa mujibu wa Katiba hii, labda tu pale

ambapo Halmashauri Kuu ya ACT itakuwa imeamua vinginevyo.

12. Orodha ya Uanachama

(1) Kutakuwa na rejesta ya orodha ya wanachama wote katika kila Tawi,

Kata na katika kila Jimbo la Uchaguzi, na rejesta hii itahuishwa kila

baada ya miezi sita. Makatibu wa Chama katika ngazi husika

watatuma orodha ya wanachama kwa ngazi inayofuata kwa ajili ya

kumbukumbu za Chama katika kila ngazi.

Page 14: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

9

(2) Katibu wa Chama Mkoa atatunza orodha ya wanachama wote kwenye

mkoa wake na atapokea orodha ya wanachama wote walioandikishwa

kila jimbo katika mkoa wake.

(3) Sekretariati ya Chama Makao Makuu itatunza rejesta ya wanachama

wote nchi nzima.

13. Ahadi tano za kila mwanachama wa ACT

Kila mwanachama wa ACT atatoa ahadi tano zifuatazo:

i) Nitapambana dhidi ya dhuluma, fitina, unafiki uongo, rushwa na

ufisadi kwa uwezo wangu wote;

ii) Nitapambana dhidi ya umasikini na nitasimamia utajiri wa nchi yangu

kwa faida ya wote;

iii) Nitashiriki kujenga Taifa lenye kujitegemea, lisilo na unyonyaji,

ubaguzi na lenye misingi ya Haki;

iv) Nitashiriki kujenga Umoja wa Afrika; na

v) Nitapigania kuwepo kwa demokrasia ndani na nje ya Chama changu.

vi) Nitajielimisha kila mara na nitatumia elimu yangu kwa manufaa ya

jamii na Tanzania kwa ujumla

Page 15: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

10

SEHEMU YA II

UONGOZI

14. Sifa za Kiongozi

Sifa, mwenendo na maadili ya Kiongozi wa ACT

1) Sifa, mwenendo na maadili ya viongozi wa ACT vimeainishwa kwa kina

kwenye Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Viongozi wa ACT.

2) Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Viongozi zimeambatanishwa kama

Nyongeza ya kwanza na ni sehemu ya Katiba hii.

15. Aina za Viongozi

(1) Kutakuwa na aina zifuatazo za Viongozi ndani ya ACT:

i. Viongozi wa kuchaguliwa na mikutano mikuu ya kila ngazi;

ii. Viongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa na vikao vya uongozi katika

ngazi mbalimbali za Chama;

iii. Viongozi watakaoteuliwa na Kiongozi Mkuu wa chama kwa mujibu wa

Katiba hii

iv. Watendaji/waajiriwa/watumishi katika Chama;

v. Viongozi wa Ngome za Chama watakaochaguliwa au kuteuliwa kwa

mujibu wa katiba hii na kanuni za ngome zao; na

vi. Viongozi wanaotokana na nafasi zao kama zilivyoainishwa na Katiba

ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile Diwani, Mbunge,

Waziri, Waziri Mkuu, Rais, n.k.

(2) Kila kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa

Chama atashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka tano.

(3) Halmashauri Kuu inaweza kuitisha uchaguzi wakati wowote kabla ya muda

wa miaka mitano kwisha kama itaona inafaa na ni kwa manufaa ya Chama

na/au Taifa na viongozi ambao muda wao wa uongozi utafupishwa kwa

mujibu wa ibara ndogo hii watahesabika kwamba wamekaa madarakani kwa

kipindi cha miaka mitano

(4) Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, atashika

Page 16: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

11

wadhifa wake hadi kipindi cha Uchaguzi Mkuu alichochaguliwa/teuliwa

kwisha na anaweza kugombea au kuteuliwa kwa kipindi kingine cha miaka

mitano ambacho kitakuwa ndio ukomo wake wa kugombea au kuteuliwa

kushika nafasi hiyo.

(5) Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na

kuchaguliwa tena, mradi awe ametimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa

kiongozi. Isipokuwa mwanachama yeyote wa ACT atakuwa kiongozi kwa

vipindi visivyozidi viwili katika nafasi moja ya uongozi katika ngazi husika.

(6) Ibara hii itahusu pia viongozi wa NGOME za ACT-Vijana, Wazee na

Wanawake.

(7) Kwa muktadha wa ibara ndogo ya (5) ya ibara hii, Kiongozi

aliyechaguliwa/kuteuliwa kushika wadhifa kwa kuziba nafasi iliyoachwa

wazi atahesabiwa kwamba amekaa kwenye wadhifa wake kwa kipindi cha

miaka mitano ikiwa amedumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka

miwili au zaidi

16. Haki za Kiongozi

Pamoja na haki za mwanachama zilizoanishwa katika Katiba hii, Kiongozi wa

ACT pia ana haki zifuatazo:

i) Haki ya kukiwakilisha Chama katika shughuli mbalimbali za kijamii na

kiserikali;

ii) Kuandaa na kupendekeza programu mbalimbali za Chama ili kuleta ustawi

katika Chama;

iii) Haki ya kujitetea au kutoa taarifa juu ya jambo au mashtaka yoyote juu

yake na ana haki ya kukata rufaa kwenye vikao vya juu iwapo hajaridhika

na uamuzi uliotolewa na kikao cha chini; na

iv) Haki ya kupata habari au taarifa zote zilizojadiliwa na kutolewa uamuzi na

wanachama au uongozi wa juu katika kumbukumbu za vikao

vinavyomhusu.

17. Ukomo wa Uongozi

(1) Mwanachama wa ACT-Tanzania atakoma kuwa Kiongozi wa Chama:

i) Kwa kujiuzulu kwa hiari yake;

Page 17: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

12

ii) Kwa kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama;

iii) Kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya

Katiba; Kanuni au maadili ya Chama;

iv) Kwa kufariki dunia;

v) Kupatwa na matatizo ya akili;

vi) Muda wa uongozi kumalizika;

vii) Kupatikana na hatia mahakamani kwa kosa la jinai linalokidhalilisha

chama.

(2) Kamati ya Uongozi ya kila ngazi au Halmashauri Kuu kwa ngazi ya Taifa

itaziba kwa muda nafasi yoyote ya kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano

Mkuu wa ngazi husika.

(3) Nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa na vikao husika kwa kufanya

uteuzi mpya katika muda usiozidi miezi sita tangu nafasi kuwa wazi.

(4) Muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu ibara ndogo ya (2) hapo

juu hautazidi miezi kumi na miwili (12) na ndani ya kipindi hicho uchaguzi

mpya ufanyike kuziba nafasi iliyoachwa wazi.

(5) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (4) hapo juu, hakutafanyika

uchaguzi rasmi wa kuziba nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini ya

hapo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa kawaida wa Chama unaofuata kufanyika.

18. Kukasimu Madaraka

(i.) Kamati ya Uongozi ya kila ngazi au Kamati Kuu Taifa zinaweza kukasimu

baadhi ya madaraka kwa Sekretarieti yake kwa azimio la wingi wa kura za

wajumbe wa kikao

(ii.) Halmashauri Kuu inaweza kukasimu baadhi ya madaraka yake kwa Kamati

Kuu kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe

(iii.) Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Halmashauri Kuu baadhi ya

madaraka yake, lakini kwa azimio maalumu kwa ajili hiyo.

Page 18: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

13

SURA YA TATU

NIDHAMU NA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA CHAMA

19. Kuteuliwa kwa Kamati ya Uadilifu

(1) Kila Kata itakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Kata itakayoteuliwa na Mkutano

Mkuu wa Kata. Kamati ya Uadilifu ya Kata itaundwa na wajumbe

wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5), kwa kuzingatia kuwa

kutakuwa na angalau mjumbe mmoja (1) mwanamke kama Kamati itakuwa

na wajumbe watatu (3), au angalau wajumbe wawili (2) wa kike kama

Kamati itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa Chama

katika ngazi ya Kata atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu

ya Kata.

(2) Kila jimbo litakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itakayoteuliwa na

Mkutano Mkuu wa Jimbo. Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itaundwa na

wajumbe wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5), kwa kuzingatia

kuwa kutakuwa na angalau mjumbe mmoja (1) mwanamke kama Kamati

itakuwa na wajumbe watatu (3), au angalau wajumbe wawili (2) wa kike

kama Kamati itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa

Chama katika ngazi ya Jimbo atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya

Uadilifu ya Jimbo.

(3) Kila mkoa utakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itakayoteuliwa na

Mkutano Mkuu wa Mkoa. Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itaundwa na

wajumbe wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5), kwa kuzingatia

kuwa kutakuwa na angalau mjumbe mmoja (1) mwanamke kama Kamati

itakuwa na wajumbe watatu (3) au angalau wajumbe wawili (2) wa kike

kama Kamati itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa

Chama katika ngazi ya Mkoa atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya

Uadilifu ya Mkoa.

(4) Kutakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Taifa, ambayo itakuwa ni moja kati ya

Kamati za Kudumu za Chama, na itaundwa na wajumbe watakaochaguliwa

na Halmashauri Kuu ya Taifa ya ACT kwa mapendekezo ya Kamati Kuu.

Page 19: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

14

i) Kamati ya Uadilifu ya Taifa itakuwa na wajumbe wasiopungua

watano (5) na wasiozidi tisa (9).

ii) Mwanachama yeyote mwaminifu na mwenye uelewa wa

Chama na siasa za nchi na dunia anaweza kuomba ujumbe wa

Kamati ya Uadilifu.

iii) Halmashauri Kuu ya Taifa itateua wajumbe wa

Kamati ya Uadilifu wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa

(9), kwa kuzingatia kuwa kutakuwa na angalau wajumbe

wawili (2) wanawake kama Kamati itakuwa na wajumbe

watano (5), au angalau wajumbe watatu (3) wanawake kama

Kamati itakuwa na wajumbe wanaozidi watano (5). Hakuna

afisa au kiongozi wa Chama katika ngazi ya Taifa

atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu ya

Taifa.

iv) Halmashauri Kuu itachagua Mwenyekiti wa Kamati ya

Uadilifu ya Taifa kwa mapendekezo ya Kamati Kuu kwa

kuzingatia kuwa Mwenyekiti atakuwa mtu mwenye angalau

Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambulika na

mamlaka husika nchini.

(5) Hakuna chombo kitakachokuwa na mamlaka ya kuivunja Kamati ya Uadilifu

ya Taifa, isipokuwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa idadi ya zaidi ya nusu ya

kura zote za wajumbe waliohudhuria na kupiga kura.

(6) Muda wa wajumbe wa Kamati ya Uadilifu utakuwa miaka minne, lakini

wanaweza kuteuliwa tena baada ya muda wao kwisha na kuwepo kwake

kutazingatia masharti mengine ya Katiba hii.

20. Mamlaka ya Kamati za Uadilifu

(1) Kamati ya Uadilifu ya Kata itakuwa na mamlaka juu ya masuala yote ya

kinidhamu na kimaadili kwa wanachama na viongozi katika ngazi ya Kata na

ngazi za chini yake isipokuwa wale waliotajwa katika ibara ndogo za (2) na

(3).

(2) Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itakuwa na mamlaka kuhusu masuala yote ya

kinidhamu kwa viongozi katika ngazi ya Jimbo na wawakilishi wa chama

(wenyeviti na wajumbe) kwenye serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na

Page 20: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

15

halmashauri za miji midogo. Kamati hii haitakuwa na mamlaka kwa viongozi

waliotajwa katika ibara ya (3) na (4). Kamati ya uadilifu ya Jimbo kitakuwa

ndicho chombo cha rufaa na mapitio kwa masuala ya kinidhamu katika ngazi

ya Kata na uamuzi wake utakuwa ni wa mwisho.

(3) Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itakuwa na mamlaka ya masuala yote ya

kinidhamu yanayohusu viongozi wa ngazi ya Mkoa isipokuwa waliotajwa

kwenye ibara ndogo ya (4), pamoja na wawakilishi wa chama (madiwani)

kwenye Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya. Pia kitakuwa

chombo cha rufaa na mapitio kwa masuala ya kinidhamu katika ngazi ya

Jimbo na uamuzi wake utakuwa wa Mwisho.

(4) Kamati ya Uadilifu ya Taifa itakuwa na mamlaka ya kinidhamu kuhusu

maafisa na viongozi katika ngazi ya Taifa, pamoja na viongozi na

wanachama wengine waandamizi wakiwemo wabunge, wajumbe wa Kamati

za Kudumu na wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, pamoja na

masuala yote ya kinidhamu yatakayoelekezwa kwake na vikao vya Kamati

Kuu na Halmashauri Kuu.

(5) Kamati ya Uadilifu Taifa ndicho kitakachokuwa chombo cha Rufaa kwa

masuala ya kinidhamu kutoka ngazi ya Mkoa.

(6) Halmashauri Kuu itakuwa ndiyo ngazi ya rufaa ya kitaifa na uamuzi wake

utakuwa wa mwisho.

21. Kazi ya Kamati za Uadilifu

(1) Kamati za Uadilifu zitakuwa na kazi zifuatazo:

i) Kufanya uchunguzi kamili, kwa imani na weledi na bila upendeleo,

kuhusu tuhuma zilizowasilishwa dhidi ya mwanachama, mjumbe, afisa,

mwakilishi au kiongozi wa Chama katika ngazi husika;

ii) Kutoa taarifa kwa maandishi kuhusu matokeo ya uchunguzi na sababu na

mazingira yaliyosababisha kufikia hitimisho;

iii) Kutoa adhabu yeyote kwa mujibu wa Katiba hii isipokuwa kusimamisha

au kufukuza uanachama au uongozi;

iv) Kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa au Kamati ya

Uongozi kwa ngazi ya Mkoa na Jimbo kwa adhabu ambazo haina

mamlaka nazo;

Page 21: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

16

v) Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa au Kamati ya Uongozi kwa ngazi ya

Mkoa na Jimbo itayapitia mapendekezo ya Kamati ya Uadilifu na kutoa

mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu kwa ngazi ya Taifa au

Halmashauri ya Mkoa au Jimbo kwa ngazi hizo kwa maamuzi ya

mwisho;

vi) Kikao katika ngazi husika kitapokea na kutoa maamuzi ndani ya siku

kumi na nne (14) kuhusu mapendekezo ya Kamati ya Uadilifu kwa

kukubali mapendekezo yote, kurekebisha au kukataa na itatoa maamuzi

yake na sababu za maamuzi hayo kwa wote walioathirika; na

vii) Kikao katika ngazi husika kitatoa maelekezo na maamuzi yanayolenga

kuimarisha nidhamu ndani ya Chama, ikiwemo kusimamisha au kufukuza

uanachama.

viii) Uamuzi wa kikao husika utaanza kutekelezwa mara moja kama

hapatakuwa na rufaa ndani ya siku 14 tangu maamuzi yatolewe.

(2) Namna na mchakato wa Kushughulikia Mashauri ya Nidhamu na uadilifu

itaelezwa kwenye Kanuni za Uendeshaji Chama zitakazotungwa na

Halmashauri Kuu ya Chama.

(3)Mwanachama, mjumbe, mwakilishi au kiongozi yeyote ambaye hakuridhishwa

na maamuzi ya kikao kilichotoa maamuzi ya kinidhamu atakata rufaa kwa

mamlaka ya rufaa ndani ya siku kumi na nne (14) tangu maamuzi yatolewe.

(4) Maamuzi ya Mamlaka ya Rufaa yatakuwa ya mwisho.

22. Makosa Yanayoweza Kusababisha Hatua za Kinidhamu

(1) Makosa yafuatayo yanaweza kusababisha hatua za kinidhamu kwa

mwanachama, afisa, mjumbe, mwakilishi au kiongozi wa Chama:

i) Kukiuka miiko na maadili ya uongozi kama yalivyoainishwa katika

Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Viongozi ambazo

zimeambatanishwa kama Nyongeza ya Kwanza na ni sehemu ya Katiba

hii;

ii) Kukataa kutekeleza wajibu na/au majukumu ya kikatiba;

iii) Kufanya fujo au kutoa vitisho dhidi ya mwanachama au kiongozi

mwingine;

Page 22: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

17

iv) Kughushi au kutoa taarifa za uwongo kuhusu mahesabu au madai ya

uwongo kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali;

v) Kuharibu mali ya Chama kwa makusudi;

vi) Kupinga Itikadi, falsafa, misingi, katiba au sera za Chama katika

majukwaa ya kisiasa;

vii) Kusababisha mgawanyiko ndani ya Chama;

viii) Kufanya kitendo chochote ambacho kinagharimu na/au kuharibu taswira

ya Chama au taifa katika umma;

(2) Kuthibitika kutenda kosa lolote hapo juu au linalofanana na hayo

kutahesabiwa kuwa ni utovu wa nidhamu na kutasababisha kutolewa adhabu

stahiki zikiwemo:

i. Karipio;

ii. Karipio kali;

iii. Onyo;

iv. Onyo kali;

v. Faini;

vi. Kusimamishwa kugombea nafasi ya uongozi kwa kipindi

kisichopungua mwaka mmoja;

vii. Kusimamishwa uanachama; au

viii. Kufukuzwa uanachama.

Page 23: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

18

SURA NNE

MUUNDO WA CHAMA NA VIKAO

23. ACT-Tanzania ni Chama cha kitaifa

(1) ACT-Tanzania ni Chama cha kitaifa, na kitakuwa na uwakilishi katika kila

ngazi katika muundo wa uchaguzi wa nchi kama ifuatavyo:

a) ACT Tawi

b) ACT Kata

c) ACT Jimbo

d) ACT Mkoa

e) ACT Taifa

(2) Uundaji wa ngazi moja ya Chama utafanyika baada ya kuwa na muundo na

uongozi katika ngazi za chini kwa angalau asilimia 40 . Mfano, ili kuunda ngazi

ya Kata ni lazima kuwe na angalau asilimia 40 ya matawi yenye uongozi katika

kata husika.

(3) Kwa kuzingatia Ibara ndogo ya (1) hapo juu, ngazi ya juu ya Chama itateua

Kamati ya muda itakayokuwa na wajibu wa kuratibu shughuli za Chama na

kuwaunganisha wanachama katika eneo lisilo na uongozi wa kikatiba mpaka

wanapofikia uwezo wa kuwa na uongozi wa kikatiba.

24. Ngazi ya ACT Tawi

(1) Ngazi ya ACT Tawi itaundwa katika eneo la kijiji, Mtaa au Sheia kwa

Tanzania Zanzibar

(2) Idadi ya chini ya Wanachama wa ACT Tawi itakuwa ni watu ishirini (20)

(3) Viongozi wa ACT Tawi watakuwa ni:

(i.) Mwenyekiti wa ACT Tawi;

(ii.) Katibu wa ACT Tawi;

(iii.) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT Tawi;

(iv.) Mwekahazina wa ACT Tawi

(v.) Katibu wa Mipango na Chaguzi

(vi.) Wenyeviti wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee katika

Tawi;

Page 24: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

19

(vii.) Makatibu wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee katika

Tawi; na

(viii.) Wajumbe wanne wa Kamati ya Uongozi watakaochaguliwa na

Mkutano mkuu wa Tawi, wanaume wawili na wanawake wawili.

(4) Vikao vya ACT Tawi vitakuwa ni:

i. Mkutano Mkuu wa Tawi - Ndicho Kikao Kikuu kupita vyote kwenye

ngazi ya tawi na wajumbe wake ni viongozi wote wa ACT Tawi na

wanachama wote kwenye tawi;

ii. Kamati ya Uongozi – Ni chombo cha utendaji cha Mkutano Mkuu wa

Tawi na wajumbe wake ni viongozi wote waliotajwa kwenye ibara ndogo

ya (3) ya ibara hii pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa anayetokana na

ACT na mwakilishi wa wenyeviti wa vitongoji na mwakilishi wa

wajumbe wa serikali ya kijiji/Kamati ya Mtaa.

iii. Sektretarieti ya Tawi – Ni kikao cha utendaji wa kazi za siku kwa siku

kwenye ofisi ya tawi mwenyekiti wake akiwa ni Katibu wa tawi, katibu

wa kikao ni Katibu mwenezi wa tawi na wajumbe ni Mwekahazina wa

tawi, Katibu wa Mipango na chaguzi tawi na makatibu wa ngome za

vijana, wanawake na wazee kwenye tawi.

(5) Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT Tawi

i) Kuchagua viongozi wa ACT-Tawi kama walivyotajwa katika ibara

ndogo ya (3) hapo juu, isipokuwa kwamba viongozi wa ngome kwenye

tawi watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya ngome zao;

ii) Kupiga kura ya maoni na kupendekeza wagombea katika uchaguzi wa

Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji;

iii) Kujadili taarifa ya Kamati ya Uongozi ya ACT Tawi na kutoa maamuzi

au maelekezo ya utekelezaji;

iv) Kupokea maamuzi na maagizo ya vikao vya juu vya Chama na kutoa

maelekezo kwa Kamati ya Uongozi ya ACT Tawi kwa utekelezaji;

v) Kujadili utekelezaji wa itikadi, falsafa, sera na mipango ya Chama

inayohusu masuala ya jamii katika eneo la kijiji, mtaa ama Sheia;

vi) Kutoa mwongozo na maelekezo kwa wawakilishi wa Chama walio

kwenye Serikali ya Kijiji au Kamati ya Mtaa;

vii) Kujadili na kuzingatia taarifa za utendaji wa NGOME za ACT Vijana,

Page 25: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

20

Wanawake na Wazee katika Tawi na kutoa maelekezo; na

viii) Kuidhinisha programu za Chama katika eneo lao.

(6) Kazi za Kamati ya Uongozi ya ACT Tawi

i) Kuendesha shughuli za kila siku za Chama katika eneo lake;

ii) Kuandaa Mkutano Mkuu wa ACT Tawi na ajenda zake;

iii) Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi,

falsafa, sera na madhumuni ya Chama;

iv) Kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea kwenye serikali za

mitaa, vijiji na vitongoji;

v) Kuendesha na kusimamia Kampeni za Uchaguzi wa wagombea

wa Chama katika Uchaguzi wa Kiserikali;

vi) Kusimamia na kuweka kumbukumbu za mali, mapato na

matumizi ya ngazi husika;

vii) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama; na

viii) Kuhakikisha Chama kinashika hatamu kwenye uchaguzi wa Tawi

na kinapata kura nyingi za mwenyekiti wa kijiji/mtaa, Ubunge na

Urais katika ngazi ya Tawi.

(7) Kazi za Sekretarieti ya ACT Tawi:

i. Kuandaa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Tawi na agenda zake;

ii. Kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za Chama katika

Tawi;

iii. Kuandaa mikakati na kuishauri Kamati ya Uongozi ya Tawi juu ya

kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali;

iv. Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi,

falsafa, sera na madhumuni ya Chama;

v. Kutekeleza maamuzi ya vikao vya Tawi na ngazi za juu vya Chama;

vi. Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na wafuasi wa Chama

katika madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa

mujibu wa Kanuni za Chama;

vii. Kuandaa taarifa mbalimbali za Chama katika Tawi na kuziwasilisha

kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa Kanuni za Chama.

(8) Kazi za Mwenyekiti wa ACT Tawi

i) Atakuwa Mwenyekiti wa mikutano na vikao vyote vya ACT Tawi;

Page 26: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

21

ii) Atakuwa msemaji mkuu wa Chama katika ACT Tawi;

iii) Atakuwa ndiye mwenezi na mhamasishaji mkuu wa siasa ya Chama

katika eneo lake;

iv) Katika mikutano anayoongoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya

kawaida, atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura za wajumbe

wanaoafiki na wasiofiki zitalingana; na

v) Atahakikisha kuwa Chama kinashinda ngazi ya Tawi katika uchaguzi

wa serikali za mitaa.

(9) Kazi za Katibu wa ACT Tawi

i) Atakuwa Katibu wa mikutano na vikao vyote vya ACT Tawi;

ii) Atawajibika kuandaa na kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu utendaji

wa shughuli za Chama katika Tawi;

iii) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa ACT Tawi;

iv) Atakuwa Mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika Tawi;

v) Atatunza daftari la wanachama wote waliopo katika eneo lake;

vi) Ataitisha vikao vya tawi vya Kamati ya Uongozi na Mkutano Mkuu

kwa maelekezo ya Sekretariat na Kamati ya Uongozi;

vii) Atakuwa ndiye mwajibikaji mkuu wa masuala yote yahusuyo fedha

na mali za Chama katika eneo lake; na

viii) Kuhakikisha kuwa Chama kinashinda ngazi ya Tawi katika uchaguzi

wa kiserikali.

25. Ngazi ya ACT Kata/Wadi

(1) Ngazi ya ACT Kata/Wadi itaundwa katika eneo la kiutawala la Kata/Wadi

katika Serikali za Mitaa.

(2) Vikao vya Chama vya ACT Kata/Wadi vitakuwa ni:

i) Mkutano Mkuu wa ACT Kata/Wadi;

ii) Kamati ya Uongozi ya ACT Kata/Wadi; na

iii) Sekretariat ya Kata/Wadi.

(3) Viongozi wa Chama ngazi ya ACT- Kata/Wadi

i) Mwenyekiti wa Chama Kata/Wadi;

ii) Katibu wa Chama Kata/Wadi;

iii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama wa Kata/Wadi;

Page 27: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

22

iv) Mwekahazina wa Chama Kata/Wadi;

v) Katibu wa Mipango na Chaguzi wa Kata/Wadi;

vi) Wenyekiti NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee Kata/Wadi;

vii) Makatibu NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee Kata/Wadi; na

viii) Wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi ya ACT

Kata / Wadi watakaochaguliwa na mkutano mkuu wa Kata/Wadi, wanaume

wawili na wanawake wawili.

(4) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Kata/Wadi:

i) Wajumbe wote wa kamati ya uongozi ya ACT Kata/Wadi;

ii) Wenyeviti wote wa ACT Tawi kwenye Kata/Wadi;

iii) Makatibu wote wa ACT Tawi kwenye Kata/Wadi;

iv) Katibu Mawasiliano na Uenezi, Katibu wa Uchaguzi na Mwekahazina

wa kila tawi ndani ya Kata/Wadi;

v) Wenyeviti wote wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee wa

matawi kwenye kata/wadi;

vi) Makatibu wote wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee wa

matawi kwenye kata/wadi;

vii) Diwani, Diwani wa Viti Maalum, Mbunge/Mwakilishi anayeishi

katika Kata;

viii) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Wenyeviti wa Kamati za Mitaa

wanaotokana na ACT kwenye kata;

ix) Wawakilishi wawili wa kila ACT-Kijiji/mtaa waliochaguliwa na

Mkutano Mkuu.

(5) Kazi za Mkutano Mkuu wa Kata/Wadi

i) Kuchagua viongozi wa ACT Kata kama walivyoorodheshwa

kwenye ibara ndogo ya (3) ya ibara hii, isipokuwa viongozi wa

ngome watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya ngome zao;

ii) Kupiga kura ya maoni katika kuchagua mgombea udiwani katika

kata husika kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Kanuni za

ACT;

iii) Kujadili taarifa za Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi na kutoa

maamuzi au maelekezo kwa utekelezaji;

iv) Kupokea maamuzi na maagizo ya vikao vya juu na kutoa

Page 28: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

23

maelekezo ya utekelezaji kwa Kamati ya Uongozi;

v) Kuzingatia, kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa

Itikadi, Falsafa, Misingi na Sera za Chama katika Kata/Wadi;

vi) Kujadili na kutoa mapendekezo kwa ngazi za juu, kuhusu masuala

ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojitokeza katika Kata/Wadi,

ambayo yanahitaji hatua za kichama ngazi za juu;

vii) Kuidhinisha Programu ya Chama katika Kata/Wadi;

viii) Kuchagua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Kata; na

ix) Kujadili taarifa za utendaji wa NGOME za ACT Vijana,

Wanawake na Wazee katika Kata/Wadi.

(6) Mkutano Mkuu wa ACT Kata utakutana mara mbili (2) kwa mwaka.

Mikutano maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya

Utendaji kadri itakavyolazimu.

(7) Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi:

i) Mwenyekiti wa ACT-Kata/Wadi;

ii) Katibu wa ACT-Kata/Wadi;

iii) Katibu Mwenezi wa ACT-Kata/Wadi;

iv) Katibu wa Mipango na Chaguzi Kata/Wadi;

v) Mweka hazina wa Kata/Wadi

vi) Wenyeviti wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee

ngazi ya Kata/Wadi;

vii) Wajumbe wawili wa kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi ya

Kata/Wadi;

viii) Diwani wa kuchaguliwa na wa viti maalum wanaotokana na ACT

kwenye kata/wadi husika;

ix) Wawakilishi watatu (angalau mmoja awe mwanamke kama

yupo) wa wenyeviti wa Mitaa, vijiji na vitongoji na wajumbe wa

serikali na kamati za vijiji/mitaa.

(8) Kazi za Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi.

i) Kufanya uteuzi wa awali wa wagombea nafasi za uenyekiti, ujumbe na

ujumbe viti maalum wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji;

ii) Kupokea na kujadili majina ya wagombea wa Chama katika uchaguzi

wa Madiwani na kupeleka kwa Mkutano Mkuu wa ACT Kata/Wadi

Page 29: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

24

kwa kupigiwa kura ya maoni;

iii) Kuandaa Mkutano Mkuu wa Kata/Wadi na agenda zake;

iv) Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Chama

katika Kata;

v) Kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Chama katika matawi;

vi) Kuandaa mikakati na kusimamia kampeni za wagombea wa Chama

katika chaguzi za kiserikali ndani ya kati/wadi;

vii) Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi,

falsafa, sera na madhumuni ya Chama;

viii) Kutekeleza maamuzi ya vikao vya juu vya Chama;

ix) Kuweka kumbukumbu sahihi za uanachama na ufuasi wa Chama katika

madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa mujibu wa

kanuni za Chama;

x) Kuandaa taarifa mbali mbali za Chama Kata/Wadi na kuziwasilisha

kwenye ngazi ya Jimbo kwa mujibu wa Kanuni za Chama;

xi) Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu za vikao na nyaraka

nyingine za mawasiliano katika Chama;

xii) Kufuatilia utendaji kazi wa viongozi wa kiserikali katika Kata/Wadi

waliotokana na Chama na kutoa ushauri au maelekezo kwa kadri

inavyowezekana;

xiii) Kusimamia na kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya

Kata husika;

xiv) Kufuatilia utendaji na utekelezaji wa maelekezo ya Chama kwa

viongozi wawakilishi wa Chama katika mabaraza ya Serikali za Mitaa;

xv) Kutoa msaada kila inapobidi kwa viongozi wawakilishi wa Chama

katika mabaraza ya Serikali za Mitaa;

xvi) Kutayarisha na kusimamia programu za Chama katika ngazi husika;

xvii) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama; na

xviii) Kusimamia utendaji wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na

Wazee katika Kata.

(9) Kamati ya Uongozi ya ACT-Kata itakutana mara nne kwa mwaka yaani kila

baada ya miezi mitatu. Vikao maalum/dharula vinaweza kuitishwa kadri

itakavyolazimu.

Page 30: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

25

(10) Wajumbe wa Sekretariet ya Kata/Wadi watakuwa ni:

i) Katibu wa Kata /Wadi – Mwenyekiti;

ii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi Kata/Wadi – Katibu;

iii) Mweka hazina wa kata/wadi;

iv) Katibu mipango na chaguzi; na

v) Makatibu wa ngome za vijana, wanawake na wazee kwenye

kata/wadi.

(11) Kazi za Sekretarieti ya ACT Kata/Wadi:

(i) Kuandaa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi na agenda

zake;

(ii) Kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za Chama katika

kata/wadi;

(iii) Kuandaa mikakati na kuishauri Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi

juu ya kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za

kiserikali;

(iv) Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi,

falsafa, sera na madhumuni ya Chama;

(v) Kutekeleza maamuzi ya vikao vya Kata/Wadi na ngazi za juu vya

Chama;

(vi) Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na wafuasi wa

Chama katika madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa

Chama kwa mujibu wa Kanuni za Chama;

(vii) Kuandaa taarifa mbalimbali za Chama katika Tawi na

kuziwasilisha kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa Kanuni za

Chama.

(12) Kazi za Mwenyekiti wa Kata/Wadi:

i) Atakuwa na madaraka ya kuangalia mambo yote ya Chama katika

Kata/Wadi yake;

ii) Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama wa Kata au

Wadi na Kamati ya Uongozi ya Kata au Wadi;

iii) Katika Mikutano anayoiongoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya

kawaida, Mwenyekiti wa Chama wa Kata/Wadi pia atakuwa na

Page 31: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

26

kura ya uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na

wasioafiki zitalingana;

iv) Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa Chama katika

Kata/Wadi; na

v) Atahakikisha Chama kinashinda uchaguzi wa udiwani na kupata

kura nyingi za Urais na Ubunge katika eneo lake.

(13) Kazi za Katibu wa Kata/Wadi:

i) Atakuwa Katibu wa vikao vyote vya kikatiba vya Chama katika

Kata/Wadi;

ii) Atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama katika Kata/Wadi;

iii) Atakuwa ndiye Mkuu wa mipango ya Chama katika Kata /Wadi;

iv) Atatunza orodha ya ACT Matawi, idadi ya ACT Matawi na

wanachama waliopo kwa kila ACT Tawi lililoko katika

Kata/Wadi yake;

v) Atatunza kumbukumbu za mali za Chama zisizoondosheka na

zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya

Kata/Wadi hiyo;

vi) Atawajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa

shughuli za Chama katika Kata/Wadi kwa ngazi ya Jimbo;

vii) Atakuwa ndiye mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika

Kata/Wadi;

viii) Atawajibika kuandaa na kuitisha mikutano yote ya vikao halali

vya Chama vya Kata/Wadi kwa maelekezo ya secretariat na

Kamati ya Uongozi na kwa kushauriana na Mwenyekiti wake wa

Kata/Wadi;

ix) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wa Chama

katika Kata/Wadi yake;

x) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika

Katiba hii; na

xi) Atahakikisha Chama kinashinda ngazi zote za udiwani na kupata

kura nyingi za Urais na Ubunge.

Page 32: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

27

26. ACT Jimbo

ACT Jimbo itaundwa kwenye eneo la Jimbo la Uchaguzi wa Ubunge/Uwakilishi

katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwa kwa mujibu wa Katiba

na Kanuni za Chama.

(1) Vikao vya Chama vya ACT Jimbo vitakuwa ni:

i) Mkutano Mkuu wa ACT Jimbo;

ii) Kamati ya Uongozi ya ACT Jimbo; na

iii) Sekretarieti ya ACT Jimbo.

(2) Viongozi wa ACT-Jimbo

i) Mwenyekiti wa Jimbo;

ii) Katibu wa Jimbo;

iii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa Jimbo;

iv) Mweka Hazina wa Jimbo;

v) Katibu Mipango na Chaguzi Jimbo;

vi) Wenyeviti wa NGOME katika Jimbo;

vii) Makatibu wa NGOME katika Jimbo; na

viii) Wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi Jimbo

watakaochaguliwa na mkutano mkuu wa Jimbo, wanaume wawili na

wanawake wawili.

(3) Kwa wilaya zenye majimbo zaidi ya moja, Viongozi wa jimbo ambalo ndio

Makao Makuu ya wilaya watakuwa ndio wawakilishi wa Chama wilaya kwa

mambo yote ya kiserikali yanayohusu chama katika wilaya husika. Ikiwa

kiongozi yeyote wa jimbo la makao ya wilaya hayupo, atawakilishwa

kwenye shughuli za serikali ya wilaya na kiongozi mwenye cheo hicho hicho

kutoka kwenye jimbo lisilo makao makuu ya wilaya.

(4) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT Jimbo

i) Wajumbe wote wa Kamati ya Uongozi ya ACT Jimbo;

ii) Wenyeviti wote wa Kata/Wadi katika jimbo;

iii) Makatibu wote wa Kata/Wadi katika jimbo;

iv) Makatibu wa Uenezi, Makatibu wa Mipango na Wekahazina wote wa

Kata/Wadi katika Jimbo;

v) Wenyeviti wa Ngome zote za Kata/Wadi katika Jimbo;

vi) Makatibu wa Ngome zote za Kata/Wadi katika Jimbo;

Page 33: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

28

vii) Madiwani na Madiwani wa Viti maalum wanaotokana na ACT katika

Jimbo.

(5) Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT-Jimbo

i) Kuchagua Viongozi wa ACT Jimbo waliotajwa katika ibara ndogo

ya (2) hapo juu, isipokuwa katibu wa Jimbo atachaguliwa kwa

kupendekezwa kwa Kamati Kuu ambayo ndiyo itafanya uteuzi wa

mwisho;

ii) Bila kuathiri kipengele cha (i) hapo juu, viongozi wa ngome zote

watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya ngome husika;

iii) Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utendaji na mapato na

matumizi ya Jimbo;

iv) Kupokea na kuzingatia mikakati ya ushindi wa ACT katika chaguzi

za kiserikali ndani ya Jimbo;

v) Kuzingatia na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Kamati ya

Uongozi ya Jimbo juu ya maamuzi na maagizo ya vikao vya juu;

vi) Kujadili taarifa za Kamati ya Uongozi ya Jimbo na kutoa maamuzi

au maelekezo kwa utekelezaji;

vii) Kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa Itikadi, Falsafa,

Misingi na Sera za Chama katika Jimbo;

viii) Kutoa mwongozo na maelekezo kwa wawakilishi wa Chama katika

vyombo vya maamuzi vya kiserikali;

ix) Kuzingatia na kutoa mapendekezo kwa ngazi za juu, juu ya masuala

ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojitokeza katika Jimbo na

yanayohitaji hatua za kichama ngazi za juu;

x) Kuidhinisha Programu ya Chama katika Jimbo;

xi) Kupiga kura ya maoni ya wagombea wa Ubunge/uwakilishi katika

Jimbo husika; na

xii) Kuchagua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Jimbo. (6) Mkutano

Mkuu wa Jimbo utafanyika mara mbili kwa mwaka. Mikutano

maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya

Uongozi ya Jimbo kadri itakavyolazimu.

(6) Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya ACT Jimbo:

(ii) Mwenyekiti wa Jimbo;

Page 34: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

29

(iii) Katibu wa Jimbo;

(iv) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa Jimbo;

(v) Mweka Hazina wa Jimbo;

(vi) Katibu Mipango na Chaguzi Jimbo;

(vii) Wenyeviti wa NGOME katika Jimbo;

(viii) Makatibu wa NGOME katika Jimbo;

(ix) Wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi Jimbo;

(x) Mbunge na/au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi katika jimbo husika;

(xi) Meya na/au Naibu Meya anayetokana na ACT ikiwa anaishi ndani jimbo

husika;

(xii) Mwakilishi wa Madiwani wote wanaotokana na ACT katika jimbo

(xiii) Wenyeviti na Makatibu wa Kamati mbalimbali zilizoundwa katika

ngazi ya jimbo;

(xiv) Wajumbe wote wa Kamati Kuu wanaoishi katika Jimbo watakaoingia

kama waalikwa lakini watakuwa hawana haki ya kupiga kura.

(7) Kazi za Kamati ya Uongozi ya ACT Jimbo

i. Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Jimbo;

ii. Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za

Chama katika Jimbo;

iii. Kusimamia misingi mikuu ya ACT katika jimbo husika;

iv. Kusimamia uchaguzi wa ndani ya chama katika kata/wadi;

v. Kupanga mipango ya kampeni za uchaguzi katika jimbo;

vi. Kuhakikisha chama kinaenea kwenye jimbo lote;

vii. Kupanga na kuandaa mkutano mkuu wa Chama jimbo;

viii. Kufanya uteuzi wa awali wa wagombea udiwani kwenye kata/wadi

zilizo katika jimbo;

ix. Kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi mbalimbali katika

ngazi ya Mitaa, vijiji na vitongoji;

x. Kuunda Kamati ndogo kadri itakavyoona inafaa; na

xi. Kujaza kwa muda nafasi za uongozi zilizowazi katika jimbo.

(8) Vikao vya Kamati ya Uongozi ya jimbo vitakutana angalau mara nne (4) kwa

mwaka na vinaweza kuitishwa kwa dharula pale panapokuwa na uhitaji

kufanya hivyo.

Page 35: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

30

(9) Wajumbe wa Sekretariati ya ACT Jimbo

i. Katibu wa ACT Jimbo (Mwenyekiti);

ii. Katibu wa Mawasiliano na Uenezi Jimbo (Katibu)

iii. Mweka Hazina wa ACT Jimbo;

iv. Katibu wa Mipango na Chaguzi Jimbo

v. Makatibu wa NGOME katika Jimbo; na

vi. Makatibu wa Kamati mbalimbali katika Jimbo;

vii. Makatibu wa NGOME katika Jimbo;

(10) Kazi za Sekretarieti ya Jimbo

i. Kupokea taarifa ya majina ya wagombea udiwani katika Kata zilizo

ndani ya Jimbo na kura walizopigiwa za maoni;

ii. Kuandaa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Jimbo na agenda zake;

iii. Kuandaa mikakati na kuendesha shughuli za kila siku za Chama katika

Jimbo;

iv. Kuandaa mikakati itakayopitishwa na Kamati ya Uongozi ya Jimbo

kwa ajili ya kusimamia kampeni za wagombea wa Chama katika

chaguzi za kiserikali;

v. Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi,

falsafa, sera na madhumuni ya Chama;

vi. Kutekeleza maamuzi ya vikao vya Kamati ya Uongozi na Mkutano

mkuu Jimbo;

vii. Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na wafuasi wa Chama

katika madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa

mujibu wa Kanuni za Chama;

viii. Kuandaa taarifa mbalimbali za Chama katika Jimbo na kuziwasilisha

kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa Kanuni za Chama;

ix. Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu za vikao na nyaraka

nyingine za mawasiliano katika Chama;

x. Kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya Jimbo; na

xi. Kazi nyingine zozote watakazoagizwa na Kamati ya Uongozi ya

Jimbo.

(11) Sekretariati ya Jimbo itakutana mara moja kila mwezi na inaweza

Page 36: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

31

kukutana kwa dharula au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au

kwa maagizo ya vikao vya juu.

(12) Kazi za Mwenyekiti wa ACT-Jimbo

i) Atakuwa na wajibu wa kusimamia mambo yote ya Chama katika

Jimbo;

ii) Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mikakati ya ushindi wa Chama

katika chaguzi za serikali ndani ya Jimbo, na utendaji wake utapimwa

kutokana na, pamoja na mambo mengine, ufanisi wa Chama katika

chaguzi za kiserikali ndani ya Jimbo;

iii) Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu na Kamati ya Uongozi ya

Jimbo;

iv) Katika mikutano anayoiongoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya

kawaida, Mwenyekiti wa Chama wa Jimbo atakuwa na kura ya

uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki

zitalingana;

v) Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa shughuli za kila siku za

Chama katika Jimbo; na

vi) Atahakikisha chama kinashinda uchaguzi wa Ubunge na kupata kura

nyingi za Urais.

(13) Kazi za Katibu wa Jimbo

i) Atakuwa Katibu wa mikutano na vikao vya Kamati ya Uongozi na

Mkutano Mkuu wa Jimbo;

ii) Atakuwa mwenyekiti wa vikao vya Sekretarieti ya Jimbo;

iii) Atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama katika Jimbo na atafanya kazi

chini ya Kamati ya uongozi ya Jimbo;

iv) Atakuwa ndiye Mkuu wa mipango ya Chama katika Jimbo;

v) Ataitisha na kuongoza vikao vya viongozi watendaji wakuu wa Chama

katika Jimbo kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda ya vikao

vya Jimbo na kuchukua hatua za utekelezaji wa maamuzi ya Chama;

vi) Ataitisha vikao vya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu wa Jimbo

kwa maelekezo ya Sekretariat na Kamati ya Uongozi na kwa

kushauriana na Mwenyekiti wa Jimbo;

vii) Atatunza orodha ya Kata/Wadi, Matawi na wanachama wa Jimbo lake;

Page 37: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

32

viii) Atatunza kumbukumbu za mali za chama zisizoondosheka na

zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya Jimbo

lake;

ix) Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama za Jimbo;

x) Atawajibika kutoa taarifa za utendaji wa shughuli za Chama katika

Jimbo kila mwezi kwa ngazi ya Mkoa;

xi) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wa Chama katika

Jimbo lake; na

xii) Kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba

hii.

27. Ngazi ya ACT Mkoa

Ngazi ya ACT Mkoa itaundwa katika kila eneo la Nchi la kiutawala la Mkoa.

(1) Vikao vya ACT-Mkoa

i) Mkutano Mkuu wa Mkoa;

ii) Kamati ya Uongozi ya Mkoa; na

iii) Sekretariet ya Mkoa.

(2) Viongozi wa ACT-mkoa

i. Mwenyekiti wa ACT Mkoa;

ii. Katibu wa ACT Mkoa;

iii. Mweka hazina wa ACT Mkoa;

iv. Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT Mkoa;

v. Katibu wa Mipango na Uchaguzi wa Mkoa;

vi. Wenyeviti wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee Mkoa;

vii. Wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi Mkoa

watakaochaguliwa na Mkutano mkuu wa Mkoa, wanaume wawili na

wanawake wawili.

(3) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT Mkoa:

i. Wajumbe wote wa Kamati ya Uongozi ya Mkoa;

ii. Wenyeviti na Makatibu wa majimbo yote yaliyomo kwenye mkoa;

iii. Makatibu wa uenezi, mipango na wekahazina wa majimbo yote

yaliyomo kwenye mkoa;

Page 38: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

33

iv. Wajumbe wanne wa kamati za uongozi za majimbo wa kuchaguliwa,

wanaume wawili na wanawake wawili;

v. Wabunge na wabunge wa viti maalum wanaotokana na ACT kwenye

mkoa; na

vi. Wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu

wanaoishi katika Mkoa.

(iv.) Mkutano Mkuu wa ACT Mkoa utafanyika mara moja kwa mwaka. Mkutano

Mkuu Maalumu au wa dharula unaweza kuitishwa wakati wowote kwa

mahitaji maalumu na/au ya dharula.

(v.) Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT Mkoa

i. Kuchagua Viongozi wa ACT Mkoa waliotajwa katika ibara ndogo ya

(2) hapo juu, isipokuwa katibu wa Mkoa atachaguliwa kwa

kupendekezwa kwa Kamati Kuu ambayo ndiyo itafanya uteuzi wa

mwisho;

ii. Bila kuathiri kipengele cha (i) hapo juu, viongozi wa ngome zote

watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya ngome husika;

iii. Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utendaji na mapato na

matumizi ya Mkoa;

iv. Kupokea na kuzingatia mikakati ya ushindi wa ACT katika chaguzi za

kiserikali ndani ya Mkoa;

v. Kuzingatia na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Kamati ya Uongozi

ya Mkoa juu ya maamuzi na maagizo ya vikao vya juu;

vi. Kujadili taarifa za Kamati ya Uongozi ya Mkoa na kutoa maamuzi au

maelekezo kwa utekelezaji;

vii. Kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa Itikadi, Falsafa,

Misingi na Sera za Chama katika Mkoa;

viii. Kutoa mwongozo na maelekezo kwa wawakilishi wa Chama katika

vyombo vya maamuzi vya kiserikali kwa mambo yanayohitaji

msimamo wa chama kimkoa;

ix. Kuzingatia na kutoa mapendekezo kwa ngazi za juu, juu ya masuala ya

kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojitokeza katika Jimbo na

yanayohitaji hatua za kichama ngazi za juu;

x. Kuidhinisha Programu ya Chama katika Mkoa;

Page 39: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

34

xi. Kuchagua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Mkoa.

(6) Mkutano Mkuu wa Mkoa utafanyika mara moja kwa mwaka. Mikutano

maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya

Mkoa kadri itakavyolazimu.

(7) Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya ACT Mkoa:

i. Mwenyekiti wa Mkoa;

ii. Katibu wa Mkoa;

iii. Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa Mkoa;

iv. Mweka Hazina wa Mkoa;

v. Katibu Mipango na Chaguzi Mkoa;

vi. Wenyeviti wa NGOME katika Mkoa;

vii. Makatibu wa NGOME katika Mkoa;

viii. Wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi Mkoa;

ix. Wawakilishi wawili wa wabunge na/au wajumbe wa Baraza la

Wawakilishi katika mkoa husika;

x. Mwakilishi wa mameya/wenyeviti na mwakilishi wa manaibu

Meya/makamu wenyeviti wa halmashauri wanaotokana na ACT

katika mkoa; na

xi. Wenyeviti na Makatibu wa Kamati mbalimbali zilizoundwa katika

ngazi ya Mkoa.

(8) Kazi za Kamati ya Utendaji ya Mkoa

i) Kuratibu shughuli za chama katika Mkoa;

ii) Kufanya uteuzi wa awali wa wagombea ubunge/uwakilishi katika

mkoa;

iii) Kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea udiwani kwenye mkoa;

iv) Kutoa ushauri na misaada ya kiutendaji kwa uongozi wa ACT-Jimbo

katika Mkoa;

v) Kuratibu shughuli za kampeni za wagombea Urais na Ubunge katika

mikoa na mgawanyo wa majukumu kijimbo;

vi) Kuratibu na kuunganisha shughuli za NGOME za Chama katika

Mkoa;

vii) Kuwa kiunganishi cha Chama na shughuli za kiserikali katika Mkoa;

viii) Kuratibu na kutoa taarifa kwa Chama ngazi ya Taifa juu ya hali ya

Page 40: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

35

kisiasa, kijamii na kiutawala ndani ya Mkoa;

ix) Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku

za Chama katika Mkoa;

x) Kusimamia misingi mikuu ya ACT katika Mkoa husika;

xi) Kusimamia uchaguzi wa ndani ya chama katika Majimbo;

xii) Kupanga mipango ya kampeni za uchaguzi katika Mkoa;

xiii) Kuhakikisha chama kinaenea kwenye Mkoa wote;

xiv) Kupanga na kuandaa mkutano mkuu wa Chama Mkoa na agenda

zake;

xv) Kuunda Kamati ndogo kadri itakavyoona inafaa; na

xvi) Kujaza kwa muda nafasi za uongozi zilizowazi katika Mkoa.

(9) Kikao cha kawaida cha Kamati ya Uongozi ya Mkoa kitafanyika mara nne

kwa mwaka. Vikao maalum / dharula vinaweza kuitishwa na Sekretariet

wakati wowote kadri itakavyohitajika.

(10) Wajumbe wa Sekretariati ya Mkoa

i) Katibu wa Mkoa (Mwenyekiti);

ii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi Mkoa;

iii) Mweka Hazina wa ACT Mkoa;

iv) Katibu wa mipango na uchaguzi;

v) Makatibu wa NGOME za ACT Mkoa; na

vi) Makatibu wa Kamati mbalimbali zilizoundwa katika mkoa.

(11) Kazi za Sekretariati ya Mkoa

i. Kupokea taarifa ya majina ya wagombea ubunge katika majimbo

yaliyo ndani ya Mkoa na kura walizopigiwa za maoni;

ii. Kuandaa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Mkoa na agenda zake;

iii. Kuandaa mikakati na kuendesha shughuli za kila siku za Chama

katika Mkoa;

iv. Kuandaa mikakati itakayopitishwa na Kamati ya Uongozi ya Mkoa

kwa ajili ya kusimamia kampeni za wagombea wa Chama katika

chaguzi za kiserikali;

v. Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi,

falsafa, sera na madhumuni ya Chama;

Page 41: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

36

vi. Kutekeleza maamuzi ya vikao vya Kamati ya Uongozi na Mkutano

mkuu Mkoa;

vii. Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na wafuasi wa Chama

katika madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa

mujibu wa Kanuni za Chama;

viii. Kuandaa taarifa mbalimbali za Chama katika Mkoa na kuziwasilisha

kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa Kanuni za Chama;

ix. Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu za vikao na nyaraka

nyingine za mawasiliano katika Chama;

x. Kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya Mkoa; na

xi. Kazi nyingine zozote watakazoagizwa na Kamati ya Uongozi ya

Mkoa.

(12) Sekretariati ya Mkoa itakutana mara moja kila mwezi na inaweza

kukutana kwa dharula au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au

kwa maagizo ya vikao vya juu.

(13) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Mkoa.

i) Atashughulikia au atakuwa na madaraka ya kuangalia mambo yote ya

Chama katika Mkoa;

ii) Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama wa Mkoa, na

Kamati ya Uongozi ya Mkoa;

iii) Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida,

Mwenyekiti wa Chama wa mkoa atakuwa pia na kura ya uamuzi

endapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana; na

iv) Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa Chama wa Mkoa.

(14) Kazi za Katibu wa Chama wa Mkoa:

ii) Atakuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote za Chama katika mkoa na

atafanya kazi chini ya uongozi wa Kamati ya Uongozi ya Chama mkoa;

iii) Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mipango ya Chama katika

Mkoa;

iv) Ataitisha na kuongoza vikao vya viongozi watendaji wakuu wa

Chama katika mkoa kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda

Page 42: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

37

za Kamati ya Uongozi ya Mkoa na kuchukua hatua za utekelezaji wa

maamuzi ya Chama;

v) Kutunza orodha ya Majimbo, Kata/Wadi, Matawi, na wanachama wa

mkoa wake;

vi) Kutunza kumbukumbu za mali za Chama zisizohamishika na

zinazohamishika zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya mkoa

huo;

vii) Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama wa mkoa;

viii) Atawajibika kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli

za Chama katika mkoa kwa ngazi ya Kamati Kuu Taifa;

ix) Atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano yote ya vikao

vya Chama mkoa kwa maelekezo ya sekretarieti na Kamati ya

Uongozi Mkoa kwa kushirikiana na Mwenyekiti wake;

(a) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wa Chama

katika mkoa wake; na

(b) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika

Katiba hii.

28. ACT Zanzibar

(1) Kutakuwa na Kamati Maalum ya Kamati Kuu kwa upande wa Zanzibar.

(2) Wajumbe wa Kamati Maalum ya Chama Zanzibar watakuwa ni:

i) Makamu Mwenyekiti Zanzibar (Mwenyekiti wa Kamati);

ii) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar (Katibu wa Kamati);

iii) Wajumbe wa Kamati Kuu watokao Zanzibar;

iv) Manaibu Katibu Taifa wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee;

v) Wenyeviti wa Mikoa Zanzibar ; na

vi) Maofisa katika idara mbalimbali za Ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar

watakuwa wajumbe wasio na kura.

(3) Kazi za Kamati Maalumu Zanzibar:

i) Kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu juu ya masuala mbalimbali

yahusuyo Zanzibar;

ii) Kusimamia utendaji wa Sekretarieti ya ofisi ya Makao Makuu Zanzibar;

iii) Kupendekeza mambo ya kisera yahusuyo Zanzibar;

Page 43: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

38

iv) Kuleta mapendekezo kwa Kamati Kuu juu ya uteuzi wa wagombea

ubunge na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar kabla ya Kamati Kuu

kufanya uteuzi wa mwisho;

v) Kuteua maafisa wa idara mbalimbali za Ofisi ndogo ya Makao Makuu

Zanzibar;

vi) Kuratibu shughuli za chama Tanzania visiwani;

vii) Kutoa ushauri na misaada ya kiutendaji kwa uongozi wa ACT katika

Mikoa ya Zanzibar;

viii) Kuratibu shughuli za kampeni za wagombea Urais na Urais wa Zanzibar

katika eneo lote la visiwani;

ix) Kuratibu na kuunganisha shughuli za NGOME za Chama Visiwani;

x) Kuwa kiunganishi cha Chama na shughuli za kiserikali katika Zanzibar;

xi) Kuratibu na kutoa taarifa kwa Chama ngazi za juu kuhusu hali ya kisiasa,

kijamii na kiutawala Zanzibar;

xii) Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za

Chama visiwani;

xiii) Kusimamia misingi mikuu ya ACT visiwani;

xiv) Kuhakikisha chama kinaenea Zanzibar yote;

xv) Kupendekeza majina ya wagombea urais na makamu wa Rais Zanzibar;

na

xvi) Kufanya uteuzi wa awali wa mgombea uspika na naibu spika wa Baraza

la Wawakilishi Zanzibar.

(4) Kwa shughuli za kiutendaji Zanzibar, patakuwa na Sekretarieti ya Ofisi ndogo

ya Makao Makuu Zanzibar yenye wajumbe wafuatao:

i) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar (Mwenyekiti);

ii) Manaibu Makatibu wa Taifa wa Ngome za Vijana, Wanawake na

wazee;

iii) Maofisa wa idara mbalimbali zilizopo Ofisi ndogo ya Makao Makuu

Zanzibar; na

(5) Kazi za Sekretarieti ndogo Zanzibar:

i) Utekelezaji wa kazi za kila siku za chama Zanzibar;

ii) Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu yanayohusu

Zanzibar; na

Page 44: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

39

iii) Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya Kamati Maalum

Zanzibar.

29. ACT-Taifa

(1) ACT-Taifa ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwa kwa

kuzingatia masharti ya Kanuni za Chama zilizotungwa na Halmashauri Kuu ya

Taifa.

(2) Viongozi Wakuu wa Chama Taifa watakuwa ni:

i) Kiongozi wa ACT Taifa;

ii) Mwenyekiti wa ACT Taifa;

iii) Makamu Mwenyekiti wa ACT Taifa upande wa Zanzibar;

iv) Makamu mwenyekiti ACT Taifa upande wa Bara;

v) Katibu Mkuu wa ACT Taifa;

vi) Naibu Katibu Mkuu ACT Taifa upande wa Zanzibar; na

vii) Naibu Katibu Mkuu ACT Taifa upande wa Bara.

(3) Vikao vya Chama Taifa:

i) Mkutano Mkuu Taifa – ndicho kikao cha juu kabisa katika ACT na

ndicho chenye maamuzi ya mwisho kuhusu jambo lolote ndani ya

chama;

ii) Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia Taifa;

iii) Halmashauri Kuu ya Taifa;

iv) Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa; na

v) Sekretarieti ya Kamati Kuu.

(4) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT watakuwa wafuatao:

i. Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa;

ii. Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo;

iii. Wawakilishi 15 wa ngome za chama taifa kwa wawakilishi watano kila

ngome;

iv. Wawakilishi 12 wa wanafunzi wa vyuo vikuu waliochaguliwa na

umoja wao kwa mujibu wa Kanuni zitakazowekwa na Ngome ya

Vijana, kwa masharti kwamba angalau theluthi moja ya wajumbe hawa

watakuwa wanawake;

v. Wawakilishi watatu wa ACT Nje watakaochaguliwa na wanachama

walio nje ya nchi kwa sharti kwamba angalau mmoja awe mwanamke;

Page 45: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

40

vi. Wawakilishi watano wa Wabunge na wawakilishi wanaotokana na

ACT;

vii. Wawakilishi watano wa Madiwani wanaotokana na ACT; na

viii. Mjumbe mmoja atakayewakilisha kila mwanachama kikundi.

(5) Kazi za Mkutano Mkuu wa Chama Taifa:

i) Kuchagua Kiongozi wa ACT Taifa;

ii) Kuchagua Mwenyekiti wa ACT Taifa;

iii) Kuchagua Makamu Mwenyekiti wa ACT Taifa (Tanzania Bara);

iv) Kuchagua Makamu Mwenyekiti wa ACT Taifa (Zanzibar);

v) Kujadili taarifa za Halmashauri Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo

kwa utekelezaji;

vi) Kuteua mgombea wa Urais na mgombea mwenza wake kwa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

vii) Kujadili na kuridhia Itikadi, Falsafa, Misingi na Sera za Chama

kisha kuweka mikakati na miongozo ya utekelezaji;

viii) Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa kuzingatia

mapendekezo ya Halmashauri Kuu;

ix) Kupokea na kujadili taarifa ya Bodi ya wadhamini wa Chama juu ya

mali na raslimali za Chama;

x) Kuidhinisha Ilani (Manifesto) ya Chama kwa ajili ya Uchaguzi

Mkuu;

xi) Kujadili na kuthibitisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya

Chama; na

xii) Kujadili na kufanyia maamuzi agenda nyingine yoyote iliyoletwa

kwake na Halmashauri Kuu au Kiongozi Mkuu wa chama.

(6) Mkutano Mkuu Taifa utakutana mara moja katika kipindi cha miaka mitano.

Mkutano Mkuu maalum/dharula unaweza kuitishwa wakati wowote ukiwepo

ulazima kwa utaratibu utakaowekwa na Kanuni

(7) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa Kidemokrasia (National Democratic

Congress) ambao ni mkutano wa Wanachama wa ACT. Mkutano huu:

i. Wajumbe wa mkutano huu ni wanachama wote wa ACT-Tanzania,

wadau, wafadhili na wananchi wote kwa ujumla watakaopenda

kuhudhuria;

Page 46: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

41

ii. Utafanyika mara moja kwa mwaka kwa mikoa kupokezana na unaweza

kuitishwa mara nyingi zaidi kama kuna hitaji la kufanya hivyo;

iii. Mkutano Mkuu wa Wanachama utakuwa ndio jukwaa la Kiongozi wa

Chama kutoa mwelekeo wa kisera wa Chama na jukwaa la wanachama

wote kuhoji utendaji wake.

iv. Mkutano Mkuu wa wanachama utajadili hali ya siasa na uchumi ya

Nchi, Afrika na dunia kwa kila mwaka.

v. Mkutano Mkuu wa Wanachama litakuwa jukwaa la majadiliano lakini

hautakuwa na maamuzi yoyote.

vi. Mambo yote yaliyojitokeza na kupendekezwa katika majadiliano ya

Mkutano Mkuu wa Wanachama yanayohitaji maamuzi ya vikao

mbalimbali yatawasilishwa katika vikao husika vya chama kwa maamuzi

na yanayohitaji utekelezaji tu, yatawasilishwa kwa vyombo vya

utekelezaji kwa ajili hiyo.

(8) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya ACT Taifa:

i. Wajumbe wote wa Kamati Kuu;

ii. Wenyeviti wote wa Mikoa;

iii. Makatibu wote wa Mikoa;

iv. Makatibu wa Ngome taifa

v. Wawakilishi tisa wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee kwa kila

ngome kuwakilishwa na wajumbe watatu;

vi. Wawakilishi watano wa wabunge na wawakilishi wanaotokana na

ACT;

vii. Wawakilishi watatu wa wanafunzi wa elimu ya juu watakaochaguliwa

kwa utaratibu utakaoelezwa kwenye mwongozo wa Ngome ya Vijana;

viii. Wawakilishi watatu wa madiwani wanaotokana na ACT; na

ix. Wajumbe kumi na tano (15), ambapo angalau wajumbe watano (5)

watakuwa wanawake, waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

(9) Kazi za Halmashauri Kuu ya Chama ya Taifa:

i. Kupendekeza wagombea wa Urais na Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania na kuwasilisha mapendekezo yake katika

Mkutano Mkuu wa Taifa;

ii. Kuteua mgombea Urais wa Zanzibar;

Page 47: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

42

iii. Kuchagua Katibu Mkuu wa Chama;

iv. Kuchagua wajumbe wanane kuingia kwenye Kamati Kuu;

v. Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu

kwa mujibu wa Katiba hii;

vi. Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati

ya Mkutano Mkuu na kuifanyia maamuzi panapostahili;

vii. Kuthibitisha mikakati na raslimali za kuendesha kampeni za wagombea

wa Chama katika chaguzi za Serikali hususani Uchaguzi Mkuu na

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa;

viii. Kuandaa ratiba na Kanuni za Uchaguzi wa ndani ya chama kwa mujibu

wa Katiba na Kanuni za Chama;

ix. Kutunga na kuzifanyia marekebisho Kanuni za kuendesha shughuli za

Chama;

x. Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa

utekelezaji;

xi. Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu;

xii. Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na

mabadiliko yake;

xiii. Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi

Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwasilisha mapendekezo

yake kwa Mkutano Mkuu kwa maamuzi;

xiv. Kuteua Wadhamini wa Chama;

xv. Kuthibitisha miongozo ya NGOME za Vijana, Wanawake na Wazee;

xvi. Kujadili na kuidhinisha majina ya wagombea wa nafasi za Kiongozi

Mkuu, Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti.

(10) Halmashauri Kuu ya Taifa itakutana angalau mara mbili kila mwaka.

Vikao maalum/dharula vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa

mujibu wa kanuni za Chama.

(11) Kiongozi wa Chama ataendesha vikao vya Kamati ya Uongozi wa

Kitaifa ambayo itakutana kadri inavyoona inafaa. Inapotokea Kiongozi wa

Chama hayupo, Mwenyekiti ataendesha vikao vya Kamati ya Uongozi wa

Kitaifa.

Page 48: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

43

(12) Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa watakuwa:

i. Kiongozi wa ACT;

ii. Naibu Kiongozi wa ACT, kama yupo;

iii. Mwenyekiti wa ACT Taifa;

iv. Makamu wenyeviti Taifa;

v. Katibu Mkuu Taifa;

vi. Manaibu Katibu wakuu Taifa;

vii. Wenyeviti wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee Taifa;

viii. Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Chama Taifa;

ix. Makatibu wa Kamati za Kudumu za Chama Taifa;

x. Wajumbe wanane waliochaguliwa na Halmashauri Kuu kuingia Kamati Kuu

kwa kuzingatia kuwa wajumbe sita watatoka bara na ambao angalau wawili

(2) watakuwa wanawake, na wajumbe wawili (2) watatoka Tanzania

Zanzibar na ambao angalau mjumbe mmoja (1) atakuwa mwanamke;

xi. Wajumbe watano walioteuliwa na Kiongozi wa Chama kwa mujibu wa

Katiba hii

xii. Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,

Rais wa Zanzibar au Makamu wa Rais wa Zanzibar aliyetokana na ACT;

xiii. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Spika wa Baraza la wawakilishi

waliotokana na ACT;

xiv. Waziri Mkuu au Kiongozi wa Kambi ya Upinzani katika Bunge la Jamhuri

ya Muungano na Kiongozi wa Kambi ya upinzani kwenye Baraza la

Wawakilishi Zanzibar;

xv. Washauri wa chama Taifa, na

xvi. Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini.

(13) Kazi za Kamati Kuu ya Chama Taifa:

i. Kuunda Kamati za kudumu Makao Makuu ya chama;

ii. Kuteua washauri wa chama wasiozidi 3 kwa mapendekezo ya Kiongozi

baada ya kushauriana na Mwenyekiti;

iii. Kuteua Wajumbe na Makatibu wa Kamati za kudumu za Chama Makao

Makuu;

Page 49: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

44

iv. Kuidhinisha wasemaji wa kisekta (wenyeviti wa kamati za kudumu za

chama) kama walivyopendekezwa na Kiongozi wa Chama;

v. Kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na

kinidhamu;

vi. Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Halmshauri Kuu, Mikakati ya

kuendesha shughuli za Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha miaka

mitano;

vii. Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu, Mikakati ya

kupata mahitaji ya raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa

Chama katika chaguzi za kiserikali;

viii. Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu juu ya ratiba na

maelekezo ya uchaguzi wa ndani ya chama;

ix. Kupitia na kutoa kwa Halmashauri Kuu mapendekezo ya haja ya

kuzifanyia marekebisho au maboresho Kanuni za Chama ama Katiba ya

Chama;

x. Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na

maelekezo kwa utekelezaji;

xi. Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu;

xii. Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa

Halmashauri Kuu kwa kuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na

Sekretarieti ya Kamati Kuu;

xiii. Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Halmashauri Kuu

na Mkutano Mkuu;

xiv. Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama

vingine vya siasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine;

xv. Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama

kwa muda maalum;

xvi. Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka;

xvii. Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Uwakilishi;

xviii. Kuandaa agenda za Halmashauri Kuu na Mapendekezo ya agenda za

Mkutano Mkuu;

xix. Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama;

xx. Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar;

Page 50: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

45

xxi. Kusimamia utendaji kazi wa NGOME za Vijana, Wanawake na Wazee;

na

xxii. Kuthibitisha Uteuzi wa Manaibu Katibu wakuu wa Tanzania bara na

visiwani kutokana na mapendekezo ya Kiongozi wa Chama

atakayependekeza majina ya manaibu katibu wakuu kwa kushauriana na

Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu Taifa.

(14) Kamati Kuu itakutana mara nne (4) kwa mwaka. Vikao maalum/dharula

vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.

(15) Kutakuwa na kamati za kudumu za Utendaji Makao Makuu ya Chama

zitakazoundwa na Kamati Kuu, ie.

i. Kamati ya Fedha na Raslimali;

ii. Kamati ya Mawasiliano na Uenezi;

iii. Kamati ya Mipango na Mikakati;

iv. Kamati ya Chaguzi na Kampeni;

v. Kamati ya Katiba na Sheria;

vi. Kamati ya Utafiti na Sera;

vii. Kamati ya Uadilifu ya Taifa;

viii. Kamati ya ACT - Amani

ix. Kamati ya Mambo ya Nje.

(16) Kamati Kuu inaweza kuunda Kamati zingine kama itakavyoona inafaa kwa

ufanisi wa Chama.

(17) Kutakuwa na Kikosi cha Amani cha Chama kitakachoitwa ACT-Amani kuanzia ngazi

ya Tawi hadi Taifa ambapo katika ngazi hii ya Taifa kitakuwa chini ya Kamati

ya ACT- Amani. Kazi ya kikosi itakuwa ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa

wanachama, viongozi na mali za Chama.

(18) Muundo na kazi za Kamati zitaainishwa katika Kanuni za uendeshaji

zitazotungwa na Halmashauri Kuu.

(19) Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama Taifa:

i. Katibu Mkuu – Mwenyekiti wa Sekretarieti;

ii. Naibu Katibu Mkuu Bara;

iii. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar;

iv. Makatibu wa Kamati zote Makao Makuu; na

v. Makatibu wa NGOME zote za Chama Taifa.

Page 51: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

46

(20) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi atakuwa ndiye msemaji wa Chama na ndiye

Katibu wa secretariet ya Kamati Kuu.

(21) Kazi za Sekretariati ya Kamati Kuu ya Chama Taifa

i) Utekelezaji wa kazi za kila siku za uendeshaji shughuli za Chama;

ii) Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu;

iii) Kuajiri watumishi wa makao makuu; na

iv) Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya Kamati Kuu,

Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.

(22) Kutakuwa na Kamati ya Uongozi ya Kitaifa itakayoundwa na:

a) Kiongozi wa Chama

b) Mwenyekiti wa Chama

c) Naibu Kiongozi wa Chama (kama yupo)

d) Makamu Wenyeviti wa Chama

e) Katibu Mkuu

f) Wajumbe wasiozidi wawili watakaoteuliwa na Kiongozi wa Chama

(23)Kazi ya Kamati ya Uongozi wa Kitaifa itakuwa ni kushauriana kuhusu mambo

mbalimbali ya chama lakini sio kikao cha maamuzi

(24)Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, Kamati ya Uongozi wa Kitaifa inaweza

kufanya maamuzi kwa jambo lolote ambalo ni la dharura na ambalo kusubiri

kwake vikao vya kawaida vya chama kunaweza kuathiri taswira, uhai na/au

ustawi wa chama.

(25) Kazi na sifa za Kiongozi wa Chama

i) Atakuwa kiongozi mkuu wa Chama na Mwenyekiti wa kikao cha Mkutano

Mkuu wa kidemokrasia

ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na

maafisa wa ACT pamoja na vikao vya chama;

iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu baada ya kushauriana na

kukubaliana na Mwenyekiti wa Chama Taifa na uteuzi kuthibitishwa na

Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii;

iv) Kuteua wasemaji wa kisekta ambao pia watakuwa ni wenyeviti wa Kamati

za Makao Makuu;

v) Kuteua Naibu Kiongozi wa Chama kwa kushauriana na Kamati ya

Uongozi atakapoona haja hiyo;

Page 52: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

47

vi) Kiongozi wa Chama anaweza kuteua mwanachama mwingine mwenye

mchango maalumu kuingia katika vikao vya chama kwa kushauriana na

Mwenyekiti na Katibu Mkuu kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo

kwa maslahi ya chama;

vii) Kupendekeza majina ya washauri wa chama baada ya kushauriana na

Mwenyikiti;

viii) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa

Chama katika mambo ya kitaifa na kimataifa;

ix) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu

na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya

kitaifa na kimataifa;

x) Ataendesha vikao vya Kamati za Kisekta ili kutengeneza misimamo ya

kisera ya chama na kuwasilisha mapendekezo ya kisera katika vikao vya

chama kwa maamuzi

xi) Iwapo Kiongozi wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile na pale ambapo

hakuna Naibu Kiongozi wa Chama, basi Mwenyekiti wa Chama atamteua

moja ya wasemaji wa kisekta kuwa Kaimu Kiongozi wa Chama;

xii) Iwapo kiti cha Kiongozi wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya

kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama,

maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, Naibu Kiongozi

wa Chama au kama na yeye hayupo basi aliyechaguliwa kutoka miongoni

mwa wasemaji wa kisekta, atashikilia nafasi yake kwa sharti kwamba

Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi

kumi na miwili tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua

Kiongozi wa Chama, mwingine.

xiii) Mtu atakayechaguliwa kuwa Kiongozi wa Chama lazima awe na sifa za

kuwa mbunge

xiv) Endapo Kiongozi wa Chama atashindwa katika uchaguzi wowote wa

kiserikali, Halmashauri Kuu ya Taifa itabidi ikutane katika kipindi

kisichozidi miezi sita tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ili kujadili

mazingira ya kushindwa kwake na kupiga kura ya siri ya kuamua kama

Kiongozi wa Chama anastahili kuendelea na nafasi yake au la. Kiongozi

Page 53: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

48

wa Chama ataendelea na nafasi yake endapo zaidi ya nusu ya wajumbe

watapiga kura ya kuwa na imani naye.

(26) Halmashauri Kuu ya Taifa inaweza kumsimamisha Kiongozi wa Chama kwa

kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote

zilizopigwa. Hata hivyo, kura ya imani haitapigwa hadi kuwe na hoja

maalumu kwa ajili hiyo na ambayo imeungwa mkono na zaidi ya theluthi

moja ya wajumbe wote wa Halmashauri Kuu.

(27) Kiongozi wa Chama ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya

mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu

wa Taifa litakaloungwa mkono na zaidi ya nusu ya kura za wajumbe halali

waliohudhuria na kupiga kura.

(28) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Taifa :

i) Atakuwa mlinzi mkuu wa sera zilizopendekezwa na kupitishwa au

jambo lolote litakaloamuliwa na kupitishwa na vikao vya chama;

ii) Atahakikisha kuwa ngazi zote za chama zinatekeleza maamuzi

yaliyotolewa na vikao;

iii) Atahakikisha kuwa ngazi zote zinafanya kazi ndani ya mipaka ya katiba,

kanuni, sera na maamuzi yoyote yaliyoagizwa na vikao vikuu vya

chama;

iv) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama katika Chama

Taifa;

v) Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya chama ya kitaifa isipokuwa

vikao vya utendaji na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa Wanachama;

vi) Atafanya shughuli nyingine za Chama kama atakavyoelekezwa na vikao

vya Chama

vii) Atapendekeza kwa Kamati Kuu majina ya watu wanaofaa kuteuliwa

kuwa Manaibu Katibu wakuu kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi ya

Kitaifa

viii) Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida

atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura ya wajumbe wanaoafiki na

wasioafika zitalingana

(29) Iwapo Mwenyekiti wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile basi Makamu

Mwenyekiti kutoka Bara atakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama kama

Page 54: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

49

Mwenyekiti anatoka Zanzibar, au Makamu Mwenyekiti kutoka Zanzibar kama

Mwenyekiti anatoka Bara. Na kama huyo Makamu Mwenyekiti aliyetajwa

kwanza naye hayupo, basi makamu mwenyekiti aliyebakia atakaimu nafasi ya

uenyekiti.

(30) Iwapo kiti cha mwenyekiti wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu,

kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye

kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, Mkutano Mkuu maalumu wa Taifa

utaitishwa katika muda usiozidi miezi kumi na mbili tangu kuwa wazi kwa kiti

hicho ili kuchagua Mwenyekiti mwingine. Katika muda huo, Halmashauri Kuu

ya chama itateua Mwenyekiti wa muda kuziba nafasi hiyo kwa muda.

(31) Halmashauri Kuu ya Taifa inaweza kumsimamisha Mwenyekiti wa Chama

kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura

zote zilizopigwa. Hata hivyo, kura ya imani haitapigwa hadi kuwe na hoja

maalumu kwa ajili hiyo na ambayo imeungwa mkono na zaidi ya theluthi

moja ya wajumbe wote wa Halmashauri Kuu.

(32) Mwenyekiti wa Chama ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya

mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu

wa Taifa litakaloungwa mkono na zaidi ya nusu ya kura za wajumbe halali

waliohudhuria na kupiga kura.

(33) Kazi za Makamu Wenyeviti wa Chama Taifa

a. Watakuwa wasaidizi wakuu wa Mwenyekiti wa Chama na watafanya

kazi zozote za Chama watakazopewa na Mwenyekiti wa Chama Taifa;

b. Watakuwa washauri wakuu wa Ngome za chama katika maeneo yao

(Bara na Zanzibar)

c. Watakuwa wajumbe maalumu katika vikao vyote vya Ngome za chama

kitaifa;

d. Makamu Mwenyekiti Zanzibar ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati

Maalumu ya Zanzibar;

e. Watamshauri Mwenyekiti katika majukumu yake ya kila siku kwa

maeneo yao;

f. Watakuwa wahamasishaji wa chama katika maeneo yao; na

g. Watakaimu nafasi ya mwenyekiti kama hayupo kwa mujibu wa Katiba

hii

Page 55: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

50

h. Halmashauri Kuu inaweza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti kwa

kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na ambayo itaungwa mkono na

zaidi ya nusu ya wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri

Kuu wakati hoja hiyo inatolewa.

(34) Kazi za Katibu Mkuu wa Chama Taifa

i) Atakuwa Katibu wa mikutano ya chama katika ngazi ya Taifa;

ii) Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za utendaji za

Chama;

iii) Ataitisha na kuongoza vikao vya sekretariet ya Kamati Kuu ya Chama

kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda za Kamati Kuu na

kuchukua hatua za utendaji wa maamuzi ya Chama;

iv) Atakuwa na uwezo wa kuajiri, kuachisha kazi na kusimamia nidhamu

ya watumishi wote wa kwa kushauriana na sekretarieti ya Chama kwa

mujibu wa Katiba, Kanuni, taratibu za Chama na sheria za nchi;

v) Atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano yote ya vikao

vya Chama katika ngazi ya Taifa kwa kushauriana na Kiongozi wa

Chama na Mwenyekiti wa Chama, na kuchukua hatua za utekelezaji

wa maamuzi ya Chama;

vi) Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama zinazohamishika na

zisizohamishika; na

vii) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba

hii na/au kwa maelekezo ya vikao vya Chama.

viii) Halmashauri Kuu itakuwa na uwezo wa kumuondoa Katibu Mkuu

kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na kama kura hiyo itaungwa

na zaidi ya nusu ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa Halmashauri

Kuu ambapo hoja hiyo imetolewa.

(35) Kazi za Manaibu Katibu Wakuu wa Chama Taifa

i) Kutakuwa na Naibu Katibu Mkuu atakayeishi na kufanya kazi zake

Zanzibar na mwingine ataishi na kukaa Tanzania Bara. Isipokuwa kwa

kuishi kwao hivyo hakutapunguza upeo wa madaraka yao ya

kushughulikia kazi za Chama kwa Tanzania nzima;

Page 56: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

51

ii) Naibu Katibu Mkuu wa Chama atakayefanya kazi Zanzibar ndiye

atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano ya Kamati

maalumu ya Halmashauri Kuu ya Chama Taifa Zanzibar;

iii) Mmoja wao atamsaidia Katibu Mkuu kukaimu kiti chake wakati

Katibu Mkuu hayupo;

iv) Manaibu Katibu Mkuu wa Chama watakuwa ndio wasaidizi wakuu

wa Katibu Mkuu wa Chama na watafanya kazi zozote za Chama

watakazopewa na Katibu Mkuu wa Chama;

v) Watakuwa Makatibu wasaidizi wa vikao vyote vya Chama

wakimsaidia Katibu Mkuu;

vi) Watamsaidia Katibu Mkuu kusimamia shughuli, taratibu na Kanuni

zote za Kiutawala za Chama za kila siku;

vii) Watakuwa wajumbe wa vikao vyote ambavyo Katibu Mkuu wa

Chama Taifa anashiriki kwa wadhifa wake;

viii) Naibu Katibu Mkuu Bara ndiye atakuwa mkuu wa utawala na itifaki

wa Chama;

ix) Watafanya kazi nyingine zozote za Chama zitakazokuwa zimetajwa

penginepo katika Katiba hii na/au kwa maelekezo ya Vikao vya

Chama.

(36). Akidi katika vikao vyote

1. Akidi katika vikao vyote itakuwa ni asilimia 50 ya wajumbe wote

wanaopaswa kuhudhuria kikao husika.

2. Bila kuathiri ibara ndogo ya (1) ibara hii, kamati kuu yaweza kupunguza

idadi ya wajumbe watakaopaswa kuhudhuria vikao mbalimbali kwa wakati

fulani kwa asilimia zisizozidi hamsini kwa azimio litakaloungwa mkono na

asilimia 75 ya wajumbe wa Kamati Kuu.

3. Ikiwa wajumbe walioalikwa wamealikwa kwa kupunguza idadi kwa mujibu

wa ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, basi akidi kwenye vikao hivyo itakuwa

asilimia 75 ya wajumbe wanaopaswa kuhudhuria.

Page 57: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

52

SURA YA TANO

NGOME ZA CHAMA NA JUMUIA YA WABUNGE WA ACT

31. NGOME ni vitengo au jumuiya za Chama

1) NGOME ni vitengo au jumuiya za Chama ambazo zitaundwa na vijana,

wanawake na wazee ambao ni wanachama wa ACT.

2) Kutakuwa na Ngome za Vijana, Wanawake na Walezi.

3) NGOME za chama zitakuwa na jukumu kuu la kueneza itikadi, falsafa,

misingi na sera za chama kwa makundi yao husika (Vijana, Wanawake na

Walezi).

4) Kanuni za uendeshaji wa Ngome zitatungwa na Ngome husika na

kuidhinishwa na Halmashauri Kuu kabla ya kuanza kutumika.

5) Kanuni na miongozo ya Ngome lazima zizingatie misingi ya Katiba hii. Pale

ambapo kuna mgongano wa kitafsiri kati ya Katiba hii na Kanuni za Ngome,

Tafsiri ya Katiba ndiyo itakayotamalaki.

32. Kutakuwa na jumuiya ya wabunge wa ACT

Kutakuwa na jumuiya ya wabunge wa ACT itakayoundwa na wabunge wote wa

ACT kwa mujibu wa Katiba hii na Kanuni za Chama. Jumuiya itaunda utaratibu

wake wa kuijiendesha bila kuathiri masharti ya Katiba hii na kanuni za uendeshaji

kazi za chama.

Page 58: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

53

SURA YA SITA

MAPATO NA MALI ZA CHAMA:

33. Mapato ya Chama

(1) Mapato ya Chama ni:

i) Ada na viingilio vya wanachama.

ii) Michango ya hiari ya wanachama na wafuasi wa Chama.

iii) Michango ya hiari ya watu wa ndani na nje wanaounga mkono Chama.

iv) Misaada kutoka kwa vyama rafiki vya kisiasa vya ndani na nje ya nchi.

v) Misaada na ruzuku kutoka ndani na nje ya nchi.

vi) Mapato yanayotokana na hisa na miradi halali ya Chama.

(2) Mali za Chama ni:

i) Mali zozote zinazohamishika na zisizohamishika.

ii) Hisa za Chama katika miradi ya kiuchumi.

iii) Mali za NGOME Taasisi zingine katika Chama.

34. Kutakuwa na bodi ya wadhamini wa Chama

1) Kutakuwa na bodi ya wadhamini wa Chama yenye wajumbe wasiopungua

saba (7) na wasiozidi tisa (9) itakayoteuliwa na Halmashauri Kuu.

2) Mali zote za kudumu, vitega uchumi na dhamana zote zitawekwa chini ya

jina lililosajiliwa la Bodi ya Wadhamini.

3) Bodi ya wadhamini itateuliwa kila baada ya miaka mitano ya Uchaguzi Mkuu

wa viongozi wa Chama.

4) Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini watateuliwa na Kamati Kuu na

kuidhinishwa na Halmashauri Kuu.

5) Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini watachaguliwa na wajumbe

wenyewe kutoka miongoni mwao.

6) Wajumbe wa Kamati Kuu hawatateuliwa katika Bodi ya Wadhamini,

isipokuwa Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini watakaoingia

kwenye kamati kuu kwa nafasi zao.

7) Kanuni za Chama zitaainisha taratibu za mikutano ya Bodi ya wadhamini.

35. Ukaguzi wa Hesabu za Chama

(1) Kutakuwa na Kanuni za Fedha za Chama zitakazoidhinishwa na Halmashauri

Page 59: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

54

Kuu. Kanuni hizi zitaainisha utaratibu wa fedha ndani ya Chama.

(2) Kutakuwa na Idara ya Ukaguzi wa ndani wa Hesabu za Chama.

(3) Hesabu za Chama zitakaguliwa kila mwaka na Kampuni ya Wakaguzi wa Nje

itakayoteuliwa na Kamati Kuu.

(4) Hesabu za Chama zitatawasilishwa katika vikao vya Chama na kwa Msajili wa

Vyama ili azifikishe kwa vyombo vingine kwa mujibu wa Sheria ikiwamo ofisi

ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali.

(5) Mweka Hazina atatoa taarifa kwa umma kuhusu taarifa ya fedha ya Chama kila

baada ya muda maalum kama itakavyoamriwa na Halmashauri Kuu.

Page 60: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

55

SURA YA SABA

MAMBO YA JUMLA KUHUSU KATIBA

36. Marekebisho ya Katiba

1) Mapendekezo ya mabadiliko yoyote ya Katiba yatafanywa na Hamashauri

Kuu ya Taifa kabla ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

2) Mapendekezo yoyote ya mabadiliko ya Katiba yatajadiliwa katika ngazi za

chini za Chama kabla ya Halmashauri Kuu kuandaa Rasimu ya mapendekezo

kwa Mkutano Mkuu.

3) Mkutano Mkuu ndio pekee wenye mamlaka ya kubadili Katiba.

4) Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba yatafikishwa katika ngazi ya Jimbo

si chini ya siku 60 kabla ya tarehe ya Mkutano Mkuu unaohusika kujadili

mabadiliko.

5) Kamati za Jimbo zitatakiwa kurejesha maoni yake na ya wanachama angalau

marekebisho ya katiba.

37. Kanuni za Uendeshaji Chama

(1) Halmashauri Kuu itatunga Kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Chama kwa

kuzingatia masharti ya Katiba hii.

(2) Kukitokea mgongano kati ya kipengele cha Katiba na kile cha Kanuni,

kipengele cha Katiba kitatamalaki.

(3) Halmashauri Kuu itakuwa na mamlaka ya kuzifanyia marekebisho Kanuni za

Chama ili kwenda na mahitaji na wakati.

(4) Kamati Kuu itatunga mwongozo wa uendeshaji wa vikao vya Chama.

38. Kuvunjwa kwa Chama

(1) Chama kitavunjwa rasmi endapo robo tatu (3/4) ya wajumbe wote

watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama wa Taifa ulioitishwa kwa

madhumuni ya kuvunjwa kwa Chama watapitisha hoja hiyo. Mkutano huo

utatangaza rasmi kuvunjwa kwa Chama na kusimamishwa kwa shughuli zote

za Chama.

(2) Katika tukio la kuvunjwa kwa Chama, Bodi ya Wadhamini wa Chama

Page 61: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

56

itahodhi mali zote za chama na kipaumbele kitakuwa ni kulipia madeni yote

ya Chama. Endapo kutakuwa na salio lolote la mali ya Chama baada ya

kulipa madeni yote, salio hilo litawasilishwa au kukabidhiwa kwa Taasisi

yoyote ambayo shughuli zake zinaakisa misingi iliyoanzisha chama hiki

kama itakavyoamuliwa na Bodi ya Wadhamini.

(3) Katika tukio la kuvunjwa kwa Chama kwa nia ya kuungana na Chama

kingine cha Siasa, Bodi ya Wadhamini wa Chama itahodhi mali yote ya

Chama na kuitumia mali hiyo kulipia madeni yote ya Chama. Endapo

kutakuwa na salio lolote la mali ya Chama baada ya kulipa madeni ya Chama

salio hilo litatumika kufuatana na azimio la kuvunja Chama ili kuungana na

Chama kingine.

Kuanza Kutumika kwa Katiba Hii:

Katiba hii itaanza kutumia Tarehe 28 Machi 2015, baada ya kupitishwa na

Mkutano Mkuu wa Chama Taifa.

Page 62: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

57

NYONGEZA YA KWANZA

KANUNI ZA MWENENDO NA MAADILI YA VIONGOZI WA ACT

SEHEMU YA I:

MASHARTI YA JUMLA

Ibaya ya 1: Dhumuni la Maadili ya Uongozi

Dhumuni la Kanuni hizi za mwenendo na maadili ya viongozi ni kuweka viwango

vya tabia na mienendo ya viongozi wa chama ili kuwafanya wawe na uwezo wa

kimaadili kuiongoza jamii katika namna ya utii wa sheria na misingi ya ACT.

Ibara ya 2: Wanaohusika na Kanuni hizi za Mwenendo na Maadili

Kanuni hizi zitawahusu viongozi wote wa chama ndani ya ACT katika ngazi zote,

wagombea katika uchaguzi wowote ule wanaogombea kwa tiketi ya ACT na

mwanachama yeyote wa ACT-Tanzania anayeshikilia nafasi ya uongozi katika

taasisi ya umma.

Kanuni hizi pia zitakuwa ni rejea na nyongeza ya Katiba ya ACT.

SEHEMU YA II:

SIFA ZA KIONGOZI

Ibara ya 3: Kiongozi wa ACT:

1) Awe Mzalendo;

2) Asiidhalilishe nchi yake Tanzania na Watanzania;

3) Awe na mtazamo wa kimaendeleo na mbunifu;

4) Awe mwadilifu;

5) Awe na maadili ya kiutamaduni, mwenendo na awe ni mtu wa kuchangamana

na watu;

6) Awe na mapenzi ya dhati kwa chama na mweledi;

7) Asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai linalohusiana na kukosa

uaminifu;

8) Asiwe amewahi kunyang’anywa haki ya kiraia na/au ya kisiasa, isipokuwa

kama alirudishiwa haki hiyo baada ya kuthibitika kutokuwa na kosa;

9) Awe na umri wa miaka 18 au zaidi;

Page 63: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

58

10) Ajue kusoma na kuandika; na

11) Asiwe amewahi kufungwa jela kwa kipindi kinachozidi miezi sita bila parole

kwa kosa linalohusiana na kukosa uaminifu.

SEHEMU YA III:

MAADILI YA VIONGOZI

Ibara ya 4: Sheria na Kanuni ambazo kiongozi wa ACT anapaswa kuzitii

Kiongozi wa ACT atatii Katiba ya Nchi, Sheria za Nchi, Katiba ya ACT na kanuni

zake pamoja na Nyongeza hii ya Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Viongozi.

Ibara ya 5: Mwenendo bora wa Kiongozi

Kiongozi wa ACT atapaswa kuwa na viwango vifuatavyo vya kiuongozi:

1) Uzalendo na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi;

2) Kuzijua na kuziheshimu haki za binadamu na kuwahimiza wanachama na

viongozi wengine kufanya hivyo;

3) Kujielimisha wakati wote

4) Kufanya kazi zake kwa kuzingatia misingi ya Demokrasia, Uwazi na

Mashauriano;

5) Kuwa tayari kupokea na kuwasikiliza wote wanaomuijia;

6) Kukuza utamaduni wa mashirikiano na kuwawezesha wanachama kutekeleza

wajibu wao;

7) Kuwataka wanachama kuheshimu maelekezo halali na kusimamia utekelezaji

wa shughuli zilizoainishwa;

8) Kuheshimu ratiba ya kazi, muda na kuwasilisha ripoti panapohitajika;

9) Kuchapa kazi kwa bidii, umakini na weledi

10) Kuwafanya wanachama watambue mipango na programu za chama na kwa

nafasi yake, kiongozi awe mfano wa kuigwa katika kutekeleza mipango na

programu hizo;

11) Awe mtetezi wa Umoja wa Taifa na Afrika;

12) Kupinga na kupigana dhidi ya ubaguzi wa aina zote;

13) Kutangaza mali zake kwa mujibu wa sheria hii ya miiko na maadili ya

Viongozi;

Page 64: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

59

14) Kujitahidi kuwa mkweli katika kutimiza wajibu wake na katika jambo lingine

lolote linalohusu mwenendo kwa hiari ama kwa kuombwa;

15) Asiwe mtu wa kujali maslahi yake binafsi dhidi ya maslahi ya umma;

SEHEMU YA IV:

MWENENDO NA MATENDO YASIYORUHUSIWA

Ibara ya 6: Matendo ya Ubaguzi na Utengano

Katika kutekeleza majukumu yake, kiongozi hataruhusiwa kumpendelea mtu yeyote

kwa misingi ya udugu/urafiki, ukabila, familia, ukoo, udini, jinsia, mkoa ama

kufanya tendo lolote litakalopelekea ubaguzi na kuwatenga watu katika madaraja.

Ibara ya 7: Makatazo mengineyo

Kiongozi pia hataruhusiwa kufanya yafuatayo:

1. Kushindwa kulipa deni linalotokana na dai ama mkataba halali; kutoa ama

kupokea rushwa, kutaka kuabudiwa na kupewa upendeleo, utapeli,

utakatishaji fedha na makosa mengine yanayohusiana na rushwa;

2. Kuweka maslahi ya mataifa ya nje mbele badala ya maslahi ya Tanzania;

3. Kutenda ama kuunga mkono tendo lolote linalolenga kukidhalilisha chama

na/au nchi yetu;

4. Kutumia vibaya mali za chama na za taifa yeye mwenyewe ama kwa

makusudi kuwaacha wanachama kufanya hivyo; kujibinafsisha mali au

mchango uliotolewa kwa ajili ya chama na/au taifa, mradi ama tawi

analosimamia;

5. Matumizi ya maneno na matendo yanayolenga kushusha hadhi, kudhalilisha

utu, kumsimamisha ama kumfukuza mwanachama ama kiongozi mwingine

kinyume na katiba ya chama na kanuni za uendeshaji chama;

6. Kutumia udikteta na ukandamizaji;

7. Kutumia madaraka vibaya kwa kuwanyanyasa watu na kuvunja sheria;

8. Kujimilikisha ngazi/idara/kitengo cha chama anachoongoza;

9. Na mwenendo wowote ambao unaweza kushusha uadilifu, kazi ama nafasi

Page 65: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

60

aliyonayo kama itakavyotafsiriwa na Halmashauri Kuu kwa mujibu wa

Katiba ya ACT, Katiba ya Tanzania na sheria za nchi.

SEHEMU YA V:

MASUALA KINZANI YANAYOHUSIANA NA KAZI

Ibara ya 8: Masuala Kinzani

Inapotokea kiongozi ana wajibu wa kufanya maamuzi kwenye jambo lolote ambalo

ana maslahi binafsi nalo, atatakiwa kuwataarifu viongozi wa juu yake ama mkuu wa

taasisi iliyomwajiri ama kumteua na kuwataka radhi kwamba hatafanya uamuzi huo.

Maslahi binafsi yaweza kutokana na nafasi yake au sababu nyingine yoyote iwe ni

mchango wake mwenyewe ama kitu alichochangia na wengine ama ni mshauri tu.

Ibara ya 9: Viongozi kutofanya biashara

Kiongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa kwenye vyombo vya serikali kuanzia ngazi

ya jimbo na kuendelea, hataruhusiwa kumiliki, kufanya ama kuendesha biashara ya

binafsi. Ikitokea kiongozi wa namna hiyo ana biashara ya binafsi, mbali ya

kuitangaza hadharani, atatakiwa kuiweka biashara yake chini ya menejimenti binafsi

na kutangaza hilo hadharani.

SEHEMU YA VI:

KUTANGAZA MALI BINAFSI ZA KIONGOZI

Ibara ya10: Tangazo la mali binafsi za kiongozi

Kila kiongozi wa ACT wa kuchaguliwa ama kuteuliwa kwenye ngazi ya Jimbo au

zaidi atawasilisha tangazo la mali zake binafsi, zilizo ndani ama nje ya nchi, kwenye

Ofisi ya Katibu Mkuu.

Fomu ya tangazo la mali ikionyesha mali halisi za kiongozi itawasilishwa ofisini kwa

Katibu Mkuu si zaidi ya tarehe 30 Juni ya kila mwaka, kwa viongozi ambao bado

wako madarakani na katika kipindi kisichozidi siku 15 tangu wamalize muda wao

kwa viongozi waliomaliza muda wao wa uongozi. Viongozi wapya waliochaguliwa

watatakiwa kuwasilisha tangazo la mali ofisini kwa Katibu Mkuu wa chama katika

Page 66: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

61

kipindi cha mwezi mmoja tangu walipoingia madarakani.

Kiongozi yeyote ambaye fomu yake ya tangazo la mali haikukubaliwa, atatakiwa

kuwasilisha nyingine ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Na kama fomu ya tangazo

la mali haikukubaliwa kwa mara ya pili na kwa sababu ambazo amefahamishwa yeye

mwenyewe, Ofisi ya Katibu Mkuu itaandaa taarifa na kuiwasilisha kwa

chombo/mamlaka iliyomchagua/kumteua huyo kiongozi kwa ajili ya hatua stahiki

dhidi ya kiongozi mhusika. Taarifa ya Mali na Madeni ya Viongozi itawekwa wazi

kwenye tovuti ya chama na daftari la mali na madeni litakuwa wazi kwenye ofisi ya

Katibu Mkuu.

Ibara ya 11. Viongozi kutangaza mali kabla hawajamaliza muda wao

Kila kiongozi aliyeko madarakani kwa kuchaguliwa ama kuteuliwa kwenye ngazi ya

Jimbo au zaidi na ambaye ametangaza mali zake kwa mujibu wa ibara ya 10 ya

nyongeza hii, atalazimika kutangaza mali zake miezi sita kabla ya kipindi chake cha

uongozi kumalizika. Baada ya hapo ofisi ya Katibu Mkuu itafanya uchunguzi juu ya

tangazo hilo na kuweka hadharani ripoti.

Ikiwa uchunguzi utaonyesha kwamba kuna uvunjifu wa maadili, mali ilinunuliwa

kwa njia haramu, rushwa ama wizi, kiongozi ataondolewa kwenye nafasi yake na

kupelekwa kwenye vyombo vya nidhamu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

SEHEMU YA VII:

ADHABU NA MAREJEO MENGINE

Ibara ya 12: Adhabu kwa kiongozi mwenye hatia

Bila kuathiri sheria nyingine za nchi, kiongozi yeyote atakayevunja masharti ya

nyongeza hii ya kanuni za mwenendo na maadili, atakabiliwa na mojawapo ya

adhabu zifuatazo:

1. Onyo kwa maandishi;

2. Karipio kwa maandishi;

3. Kuachishwa uongozi; na

4. Kuachishwa uongozi kutakakofuatiwa na uchapishaji wa sababu za

kuachishwa kwenye magazeti ikiwa ni kwa maslahi ya umma.

Kiongozi atakayeng’ang’ania kukaa kwenye nafasi ambayo ameondolewa ama

Page 67: Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) …...Kidemokrasia na Falsafa ya unyerere katika ubora wake. 3) Katiba hii ya ACT ipo kwa ajili ya kuilinda misingi hii muhimu

62

kusimamishwa, ataondolewa uanachama.

Ibara ya 13: Haki ya Kujitetea

Kiongozi yeyote aliyepatikana na hatia kwa mujibu wa Maadili na Miiko

iliyoainishwa katika nyongeza hii atakuwa na haki ya kusikilizwa.

Ibara ya 14: Rufaa

Kiongozi yeyote atakayeadhibiwa adhabu yoyote iliyomo kwenye nyongeza hii ya

mwenendo na maadili ya viongozi, anaweza kukata rufaa kwa ngazi ya juu

inayofuata kwa maandishi akielezea utetezi wake ama maelezo mengine kwenye

kosa ambalo kwalo uamuzi ulichukuliwa. Utetezi huo uifikie ngazi ya rufaa ndani ya

siku 14 baada ya kutaarifiwa.

Mchakato wa rufaa hautasimamisha utekelezaji wa uamuzi uliokwishachukuliwa

isipokuwa kama mrufani ameomba hivyo na baada ya mamlaka ya rufaa kujiridhisha

kwamba mamlaka ya chini ilikosea katika uamuzi wake ama kwamba ilipotoshwa

wakati ikichunguza na kuchukua uamuzi huo.

SEHEMU YA VIII:

MASHARTI MENGINEYO NA MASHARTI YA MPITO

Ibara ya 14: Chombo chenye wajibu wa utekelezaji wa kanuni hizi za

mwenendo na maadili

Kamati ya Uadilifu ya kila ngazi ndiyo itakuwa na wajibu wa kutekeleza kanuni hizi

za mwenendo na maadili ya viongozi isipokuwa pale itakapokuwa imeelezwa

vinginevyo. Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama itahakikisha kunakuwepo utengamano

katika utekelezaji wa kanuni hizi za mwenendo na maadili na Katiba ya Chama.

Kila ripoti ya mwaka ya Katibu Mkuu itaonyesha nini kimeonekana katika

utekelezaji wa kanuni hizi za mwenendo na maadili ya viongozi.

Masharti yote yaliyotangulia yanayokinzana na kanuni hizi za asili yanabatilishwa

rasmi.

Ibara ya 15: Kuanza kutumika kwa Kanuni hizi

Kanuni hizi za mwenendo na maadili ya viongozi zimepitishwa rasmi kuwa

nyongeza ya katiba ya chama na Mkutano Mkuu wa Taifa wa ACT jijini Dar es

salaam na kuanza kutumika leo tarehe 28 Machi 2015.