maagano mawili aliyetafsiri ni, daniel wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ......
Post on 10-Mar-2021
10 Views
Preview:
TRANSCRIPT
1
2
MAAGANO MAWILI
Aliyetafsiri ni,
Daniel Wikama.
@2019
3
YALIYOMO
UTANGULIZI .....................................................................................4
AHADI KWA IBRAHIMU (E.J.WAGGONER).................................8
MAAGANO MAWILI........................................................................15
MAISHA YA IBRAHIMU.................................................................16
HAJIRI NA SARA..............................................................................20
JE UPO AGANO GANI?....................................................................25
LITUPE MBALI AGANO LA KALE ................................................30
MWANZO WA “IKIWA” NA “NDIPO”...........................................34
AGANO LA KALE LIMETETA JIPYA............................................38
TOFAUTI YA MAAGANO ...............................................................43
NAFSI AU KRISTO...........................................................................48
KUKAMILIKA KWA AGANO LA MILELE....................................56
4
UTANGULIZI.
Somo la maagano mawili ni somo ambalo wengi hawana uelewa mzuri.
Lakini japokuwa wengi hawana uelewa mzuri kuhusu maagano mawili,
wapo wengi ambao hawafahamu kama hawana uelewa mzuri kuhusu
maagano mawili. Lakini kwa rehema za Mungu, mwaka 1888 Mungu
aliwatumia vijana wawili E.J.Waggoner na A.T.Jones kufunua ukweli
uliopo katika maagano mawili. Ellen White baadae alifunuliwa kuwa
ukweli ambao umefunuliwa na watu hawa wawili ulikuwa ni kweli na
ni muhimu kwa watu wote waufahamu kabla ya ujio wa Yesu Kristo
mara ya pili. Akasema,
Bwana katika rehema yake, ametuma ujumbe wake wa kipekee kupitia
Wazee Waggoner na Jones. Ujumbe huu unatakiwa utolewe
ulimwenguni kote kuhusu mwokozi aliyeinuliwa, aliyekafara kwaajili
ya dhambi za ulimwengu. Umewasilisha kuhesabiwa haki kwa imani
kwa hakika, na unawaalika watu wapokee haki ya Yesu Kristo, ambayo
inadhihirishwa katika kutii amri zote za Mungu. (Ellen White,
Testimonies to Ministers 91,92 1895).
Lakini cha kusikitisha ni kwamba ujumbe huu ulikataliwa na viongozi
wa kanisa la waadventista wasabato. Ni muhimu kila mmoja ajue nini
maana ya agano, na nini kilicho ndani ya agano ili iwe rahisi sana kwa
msomaji aweze kuelewa yale ambayo yanaelezwa na mwandishi. Nini
maana ya agano? E.J.Waggoner alisema,
“Agano na ahadi ni kitu kimoja na vyote ni sawa na inaonekana wazi
katika wagalatia 3:17, ambapo inaonekana kuwa kubatilisha agano ni
kubatilisha ahadi. Katika mwanzo 17 tunasoma kwamba Mungu
alifanya agano na Ibrahimu kumpa nchi ya kaanani—na kwahilo ni
dunia nzima—kwa ajili ya urithi wa milele, lakini wagalatia 3:18
inasema kuwa Mungu alimpa kwa njia ya ahadi. Agano la Mungu kwa
wanadamu haiwezi kuwa kitu kingine ila ahadi zake kwao. “Au ni nani
aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote
vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu
una yeye milele. Amina” (Warumi 11:35-36). Ni nadra sana kwa watu
ufanya jambo bila kutegemea malipo, ndio maana wanateolojia
wamechukulia ndivyo hivyo hivyo kwa Mungu. Ndio maana wameanza
maandiko yao kuhusu agano la Mungu wakiwa na kauli kuwa “ni
5
makubaliano kati watu wawili au zaidi, kwaajili ya kufanya au
kutokufanya jambo fulani” Lakini Mungu hafanyi makubaliano na
wanadamu,kwasababu anajua kuwa hawawezi kutimiza sehemu yao.
Baada ya gharika, Mungu alifanya agano na kila kiumbe chenye uhai,
lakini wanyama wala ndege hawakurejesha ahadi yoyote (Mwanzo 9:9-
16). Walipokea upendeleo kutoka katika mkono wa Mungu. Hilo ndilo
tunalotakiwa kulifanya. Mungu ameahidi kila kitu tunachohitaji, zaidi
ya tunavyoweza kusema au kufikiri kama zawadi. Sisi tunampa nafsi
zetu, ambayo haina kitu, na yeye anatupa yeye mwenyewe ambaye ni
kila kitu. Kitu kinachosababisha tatizo, hata pale wanadamu
wanapomtambua Mungu, wanataka kufanya makubaliano naye.
Wanataka iwe ni mahusiano ya pande mbili—wabadilishane ili wajione
wapo katika makubaliano na Mungu. Lakini yoyote anayetaka
makubaliano na Mungu lazima ajihusishe naye kwa mujibu wa vigezo
vyake, kwamba katika uhalisia—hatuna kitu na sisi si kitu na yeye
anakila kitu na yeye ni kila kitu na anatoa kila kitu” (Glad tidings 70-
71)
Hivyo tunagundua kuwa Agano ni ahadi ile ambayo Mungu ameitoa.
Kama jinsi waggoner alivyosema, kuwa agano na ahadi ni jambo moja
na ni kitu kimoja, ni muhimu kuelewa kuwa Mungu anapoahidi jambo
ni sawa na kuwa ameweka agano. Kama jinsi alipoahidi kuwa
hatoangamiza dunia kwa gharika, ni sawa na kusema kuwa Mungu
aliweka agano kuwa hatoangamiza dunia kwa gharika.
Mwanzo 9
9 Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa,
na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina,
hata kila kilicho hai katika nchi. 11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila
chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika,
baada ya hayo, kuiharibu nchi
Ahadi kuwa “Kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika
wala hakutakuwa tena gharika” hili ndilo agano la Mungu. Na hakuna
kiumbe chochote kilichoahidi chochote kwa Mungu, ni Mungu ndiye
anayeweka agano kwa maana yeye ndiye anayeweza kutimiza agano
lake. Japokuwa Mungu alitamka agano lake kwa viumbe wote kuwa
hatoangamiza tena dunia kwa gharika, agano hili halikuwa agano la
6
wokovu na la Kumhesabia haki mwanadamu lakini lilikuwa tu kuwa
hatoangamiza dunia kwa gharika sio zaidi ya hapo.
Lakini kuna agano ambalo Mungu aliahidi kumhesabia haki mdhambi.
Hili ni agano la milele ambalo haki inapatikana kwa kumuamini Kristo.
Na hili agano lilikuwa katika akili ya Mungu hata kabla dhambi
haijaingia. Ellen White anasema,
Mpango wa wokovu wetu haukuanza baadae, kwamba mpango
ulianzishwa baada ya anguko la Adamu. Ulikuwa ni ufunuo wa “ile siri
iliyositirika tangu zamani za milele” (Warumi 16:25). Ulikuwa ni
mafunuo ya kanuni ambazo tangu zamani za milele zilikuwa ni msingi
wa kiti cha enzi cha Mungu. Tangu mwanzo, Mungu na Kristo walijua
uasi wa Shetani, na kuhusu anguko la mwanadamu kupitia nguvu ya
muasi. Mungu hakutaka dhambi iwepo, lakini aliona ujio wake, na
akafanya maandalizi kwaajili ya kukabiliana na dharura hiyo ya
kutisha. Upendo wake ulikuwa mkubwa sana kwa ulimwengu, kiasi cha
kuweka agano kumtoa mwanae wa pekee “ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16) (Desire of Ages,
22)
Agano ambalo Mungu aliweka hata kabla dhambi haijaingia
ulimwenguni ni agano la kumtoa mwanae wa pekee. Hili ni agano
ambalo kwa Lugha nyingine tunaweza kuliita agano jipya. Kuna jambo
ambalo tunagundua hapa, ya kuwa agano jipya ndio agano la milele
lililowekwa hata kabla ya dhambi haingia ulimwenguni. Hili ni agano
la wokovu, kwamba haki inahesabiwa kupitia Yesu Kristo. Agano jipya
ndio agano la wokovu kwa mwanadamu, hili ndilo lilikuwa agano la
kwanza Mungu kulitoa hata kabla ulimwengu haujawa na dhambi.
Ellen White anasema,
“Japokuwa hili agano jipya lilifanywa na Adamu na kurudiwa kwa
Ibrahimu, halikuweza kuthibitishwa mpaka kifo cha Kristo. Lilikuwepo
kwa ahadi ya Mungu tangu mpango wa wokovu ulipotolewa kwa mara
ya kwanza, lilikubaliwa kwa imani, lakini lilipothibitishwa na Kristo,
liliitwa agano jipya. Sheria ya Mungu ilikuwa ndio msingi wa hili
agano, ambalo lilikuwa ni mpango wa kuwaleta wanadamu tena katika
amani na mapenzi ya Mungu, na kuwaweka sehemu ambayo wanaweza
kutii sheria ya Mungu. Jambo jingine linalotajwa katika Maandiko ni
7
“Agano la Kale” lililofanywa kati ya Mungu na Israel pale sinai,
ambalo lilithibitishwa kwa damu ya kafara. Agano la Ibrahimu
lilithibitishwa kwa damu ya Kristo, na ndilo lilipoitwa agano la “pili”
au “Jipya”,kwasababu muhuri wa damu iliyomwagwa baada ya damu
ya agano la kwanza. Kwamba agano jipya lilikuwa ni thabiti katika siku
za Ibrahimu ni wazi kutokana na kuwa lilithibitishwa kwa ahadi na
kiapo cha Mungu—“vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika
hivyo Mungu hawezi kusema uongo” Waebrania 6:18 (Partriach and
Prophets 370-371)
Wapo wengi wanaodhani kuwa Agano la sinai ndio lilikuwa la kwanza
kufanywa. Na kwamba pale lilipovunjwa ndio la pili lililetwa kupitia
Yesu Kristo. Lakini ukweli ni kwamba kati ya haya maagano mawili,
agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza
kufanywa na Mungu na lilikuwa halisi kutokana na kiapo cha Mungu,
lakini japokuwa lilikuwa la kwanza kufanywa, agano hili lilikuwa
linasubiri damu ya Kristo ambaye ndiye mzao wa agano Hilo. Agano
hili lilikuwa linasubiri msalaba wa Yesu. Wakati agano la pale sinai
lilipofanywa, damu ya kafara ilitumika kuthibitisha agano hilo.
Kwahiyo agano la sinai ni la kwanza kwasababu ndilo lililokuwa la
kwanza kuthibitishwa kwa damu, wakati lile la Ibrahimu lilikuwa
linasubiri damu ya Yesu Kristo, na damu ya Yesu ilipomwagwa agano
hilo japokuwa ndio lilikuwa la kwanza kufanywa likawa agano la Pili.
Katika kitabu hiki A.T.Jones anaeleza kwa undani zaidi kuhusu
maagano mawili na kwa nini agano la sinai lilifanywa wakati tayari
kulikuwa na agano tayari –agano la Ibrahimu? Ubarikiwe.
Daniel Wikama.
8
AHADI KWA IBRAHIMU.
Na,
E.J.WAGGONER.
Tunaposoma ahadi, sehemu mbili katika maandiko zinatakiwa
ziwekwe katika akili. Ya kwanza ipo katika maneno ya Yesu
Yohana 5
39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima
wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia 46 Kwa maana kama
mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari
zangu. 47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?
Maandiko pekee katika kipindi cha Kristo yalikuwa ni vitabu
vinavyojulikana kama ni agano la kale: haya ndio yanayomshuhudia.
Yalitolewa si kwa dhumuni jingine. Yalikuwa yanaweza
kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu
(2 Timotheo 3:15) na miongoni mwa hayo maandiko ni vitabu vya
Musa, kama jinsi vilivyotajwa na Bwana vilikuwa vinamdhihirisha.
Yoyote anayesoma vitabu vya Musa na agano la kale lote bila
kutegemea kumpata Kristo na njia ya uzima kupitia yeye atajikuta
anashindwa kuvielewa. Na kusoma kwake kutakuwa ni bure.
Andiko lingine ni,
2Wakorintho 1
19 Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi,
yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni
Ndiyo. 1.20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa
hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.
Hakuna ahadi ya Mungu iliyotolewa kwa mwanadamu isipokuwa
kupitia Kristo. Kuwa na imani katika Kristo ni kitu kimoja muhimu ili
kupata chochote kile ambacho Mungu ameahidi, Mungu hawaheshimu
wanadamu: Anatoa utajiri wake kwa kila mtu: lakini hakuna mtu
yoyote anaweza kuwa na sehemu katika hayo bila kumpokea Kristo.
9
Hii ni sawa kabisa, kwa maana kristo ametolewa kwa wote kama
wanataka wanaweza kuwa naye.
Kwa kuwa na hizi kanuni kichwani, tunasoma sehemu ya kwanza ya
ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu,
Mwanzo 12
1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na
nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya
wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa
zote za dunia watabarikiwa.
Kwa kuanza kabisa tunaweza kuona kuwa ahadi hii kwa Ibrahimu
ilikuwa ni ahadi katika Kristo.
Wagalatia 3
8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki
Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika
wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9 Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja
na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani
Katika hili tunajifunza kuwa katika Ibrahimu familia zote za dunia
zitabarikiwa, alikuwa anamuhubiria Injili. Baraka ambazo zilikuwa zije
kwa watu wa dunia kupitia yeye zitafurahiwa tu kupitia Imani.
Kuhubiri injili ni msalaba wa Kristo.Ndio maana mtume Paulo anasema
kuwa alitumwa ili ahubiri injili sio kwa hekima ya maneno, ili kwamba
msalaba wa kristo usiwe na manufaa yoyote. Na akaongeza kuwa
kuhubiri msalaba ni nguvu kwa wote waliookolewa (Angalia 1Kor
1:17,18). Hii ni njia nyingine ya kusema kuwa ni injili, kwa maana injili
ni nguvu ya Mungu kwaajili ya wokovu.
Hivyo kwa vile kuhubiri injili ni kuhubiri msalaba wa Kristo ( na
hakuna wokovu kwa namna yoyote ile) na Mungu alihubiri injili kwa
Ibrahimu pale aliposema “katika wewe jamaa zote za dunia
watabarikiwa.” Ni wazi kuwa katika ahadi hiyo, msalaba wa kristo
ulifunuliwa wazi kwa Ibrahimu, na ahadi iliyotolewa ilikuwa inaweza
kupatikana kupitia msalaba wa Yesu pekee.
Hili limewekwa wazi sana katika sura ya tatu ya kitabu cha wagalatia.
Baada ya kauli kuwa ahadi ya baraka ni kwa watu wote wa dunia
10
kupitia Ibrahimu na kwamba wote waliokatika imani wanabarikiwa
pamoja na Ibrahimu, maneno,
Wagalatia 3
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili
yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14 ili
kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea
ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Haya yanaeleza kwa uwazi kabisa kuwa baraka za Ibrahimu, ambazo
zinakuja kwa familia zote za dunia, zitakuja tu kupitia msalaba wa
Kristo.
Hili ni jambo ambalo linatakiwa liwe katika akili zetu mwanzoni
kabisa. Kushindwa kuelewa kote kuhusu ahadi za Mungu kwa Ibrahimu
na mzao wake zimesababisha kushindwa kuona injili ya msalaba ndani
yake. Kama itaendelea kukumbukwa kuwa ahadi zote za Mungu ni
katika Kristo, ili zifurahiwe kupitia msalaba wake pekee, na kwamba
ni za kiroho na za milele katika asili yake, hakutakuwa na ugumu na
somo la ahadi kwa mababa litakuwa ni la furaha na baraka.
Tunasoma kuwa Ibrahimu kwa kuitii sauti ya Mungu, alijitenga na
nyumba ya baba yake, na kutoka katika nchi yake ya asili.
Mwanzo 12
5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao
vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka
ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani. 6 Abramu
akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa
More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. 7 Bwana akamtokea
Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea
madhabahu Bwana aliyemtokea. 8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima
ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli
upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu
huko, akaliitia jina la Bwana.
Ni muhimu tuweze kuelewa maana halisi ya ahadi za Mungu na
alivyokuwa anajihusisha na Ibrahimu tokea mwanzo na ndipo somo
letu litakuwa rahisi kwasababu litakuwa linatumia hizo kanuni. Katika
mstari wa mwisho kuna vitu vimeletwa ambavyo vinachukua uzito
mkubwa katika somo hili, na hivyo tutaviainisha hapa, Kwanza
11
MZAO
Bwana alimwambia Ibrahimu, alipofika katika nchi ya kaanani
Wagalatia 3
16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao,
kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani,
Kristo
Hili linaweza milele kuweka sawa swala hili,ili kwamba kusiwe na
mkanganyiko wowote kuhusu hilo. Mzao wa Ibrahimu, ambaye ahadi
zilinenwa ni Kristo. Yeye ndiye mrithi.
Lakini sisi pia ni warithi sawa na Kristo.
Wagalatia 3
27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.28 Hapana
Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu
mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na kama ninyi
ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Isisahaulike kuwa kuna maelfu wengi wanajumuishwa katika mzao,
kuna mzao mmoja, kwa maana wote ni wamoja katika Kristo, ambaye
ndiye mzao.
Wote waliobatizwa katika Kristo wapo ndani ya Kristo, na hivyo ni
wamoja katika yeye. Hivyo inaposemwa kuwa Kristo ni mzao wa
Ibrahimu, ambaye ahadi zilinenwa, wote waliondani ya Kristo
wanajumuishwa. Kusema kwamba urithi ulioahidiwa kwa mzao wa
Ibrahimu utaweza kupatikana kwa njia yoyote isipokuwa wale
waliokatika Kristo kupitia Imani ni kuipuuzia Injili, na kukataa neno la
Mungu. Kama mtu yoyote aliyendani ya Kristo ni kiumbe kipya. Hivyo
kwa vile ahadi kuhusu nchi ilikuwa ni kwa Ibrahimu na mzao wake,
ambaye ni Kristo na wote waliondani yake kupitia ubatizo na hivyo ni
viumbe wapya inamaana kuwa ahadi za nchi ilikuwa ni kwa wote
walioviumbe wapya katika kristo—Wana wa Mungu kupitia imani kwa
Kristo Yesu.
Hii ni ushahidi wa ziada ahadi zote za Mungu ni katika kristo, na ahadi
zote za Mungu zinaweza kupatikana kupitia msalaba wa Kristo. Kanuni
12
hii isisahaulike katika kusoma kuhusu Ibrahimu na ahadi kwake na
mzao wake—Kwamba mzao ni Kristo na wote waliondani yake.
NCHI
Ibrahimu alikuwa katika nchi ya kaanani wakati Mungu
alipomwambia, “Kwa mzao wako nitampa nchi hii” Turudi kwa
maneno ya mfia dini stefano, akiwa amejazwa na roho mtakatifu na
sura yake ikiwa ikin’gaa kama malaika aliwaambia wale wanaomtesa
Matendo 7
2 Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu
alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa
Harani, 3 akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata
nchi nitakayokuonyesha. 4 Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa
Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii
mnayokaa ninyi sasa
Haya ni marudio ya yale tuliokwisha soma katika sura ya kumi na mbili
ya Mwanzo. Sasa soma mstari unaofata
5 Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba
atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.
Tunajifunza hapa kuwa japokuwa wakati mwingine ni nadra sana
kusema “Kwa mzao wako nitakupa nchi hii” Ibrahimu mwenyewe
alijumuishwa katika ahadi hiyo. Hii ni wazi kabisa katika marudio
yanayofata katika kitabu cha mwanzo.
Lakini tunajifunza zaidi kuwa Ibrahimu hakupata urithi wowote wa
nchi. Hakuwa na hata sehemu kiasi cha kuweka mguu wake, lakini bado
Mungu alimuahidi kwake na mzao wake baada yake. Je tutasemaje
kuhusu hili?—kwamba ahadi ya Mungu ilishindikana?—hapana.
Mungu hawezi “kudaganganya” “Yeye ni mwaminifu.” Ibrahimu
alikufa bila kupokea ahadi ya urithi, lakini bado alikufa akiwa na imani.
Tunatakiwa kujifunza katika hili somo ambalo Roho mtakatifu alitaka
wayahudi wajifunze, kwamba ahadi ya urithi itapokelewa kupitia Yesu
na ufufuo. Hili pia liliwekwa wazi kabisa kupitia maneno ya mtume
Petro
13
Matendo 3
25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu
aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za
ulimwengu zitabarikiwa. 26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu,
alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia
Ahadi za Ibrahimu kama jinsi tulivyojifunza, zinawafikia watu wa
mataifa na familia zote za dunia, kupitia Yesu kristo na msalaba, lakini
baraka za Ibrahimu zinaambatana na ahadi ya nchi ya kaanani. Ambayo
ilikuwa ipokelewe kupitia Kristo na ufufuo. Kama ingekuwa ni
kinyume, Ibrahimu angekuwa amekwazwa, badala ya kufa akiwa na
imani tele kuhusu ahadi. Lakini hili nalo litakuwa wazi zaidi
tutakapoendelea.
14
15
1. MAAGANO MAWILI.
Wagalatia 4
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa maana
imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja
kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana
kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano
mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri
ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa
anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye
mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti,
ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa
huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini
kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho,
ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa
maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31
Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye
mwungwana.
“Haya ni maagano mawili.” maagano mawili ni yapi?—Hawa
wanawake wawili, kwa vile agano la pale sinai linawakilishwa na
Hajiri, Hivyo agano jingine linawakilishwa na Sara. Tafsiri nyingine ya
mstari wa 24 unasomeka “Kwa maana hawa ni maagano wawili”
Hawa wanawake wawili ni mama wa watoto wawili wa Ibrahimu.
Mwana mmoja alizaliwa na mtumwa, mwingine kwa Mwanamke huru
(Mwungwana): Sara alikuwa ni mwanamke Huru. Wana wawili wa
hawa wanawake wawili wanawakilisha watoto wa maagano mawili.
“Hawa ndio maagano mawili” yoyote basi anayesome kuhusu
maagano mawili lazima asome kuhusu hawa.
“Hawa ndio maagano mawili” Kila somo basi kuhusu maagano mawili,
kama sio somo kuhusu hawa basi hilo sio somo kuhusu maagano
mawili.
“Hawa ndio maagano mawili” Kwa kupitia hawa basi somo la maagano
mawili linaanza na yoyote anayesoma kuhusu maagano mawili lazima
aanze pale ambapo somo linaanza. Hivyo hapa ndipo tunapoanzia somo
la maagano mawili. Na ili tuweze anza kwa manufaa yetu ni lazima pia
tusome Mwanzo 15, 16, 17, na 21: 1-21- angalau mara saba.
16
2. MAISHA YA IBRAHIMU.
Wagalatia
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri
Hivyo maagano mawili yalikuwa katika familia ya Ibrahimu. Kwa
maana “Hawa ndio maagano mawili” mstari wa 24
Kwa nini maagano mawili yaliingia katika familia ya Ibrahimu, na moja
kati ya hayo ni agano la sinai? “kwa maana Hawa ndio maagano mawili
moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri”
Kwa vile Hajiri ni moja kati ya maagano mawili—la Kutoka sinai, na
ambalo linalozaa utumwa,—hadithi ya Hajiri katika familia ya
Ibrahimu ni hadithi ya agano kutoka sinai.
Lakini Mungu alifanya agano na Ibrahimu mwenyewe, kabla hata
Hajiri hajasikika. Na hili agano lilithibitishwa katika Kristo, kabla hata
Hajiri hajatajwa.
Agano hili lilikuwa ni agano la ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na kwa
mzao wake—sio “wazao kama vile ni wengi: lakini kama vile ni
mmoja, na kwa mzao wake yani Kristo” Hili ni agano la Haki ya
Mungu—haki ya Mungu kwa imani—kwa maana Mungu alipofanya
agano na Ibrahimu, Ibrahimu alimwamini Bwana na alimuhesabia
kuwa ni haki” (Mwanzo 15:6)
Hii ahadi ilikuwa kwa Ibrahimu, kwamba kwa kupitia yeye Familia
zote za dunia zibarikiwe—Kwa kupitia mzao wake atampa Nchi ya
ahadi, ambayo ndio ulimwengu ujao, na kwamba mzao wake atakuwa
kama nyota za mbinguni.
Mzao huyu, ambaye kwa yeye ahadi ilifanywa, ndiye Kristo, agano hili
lilifanywa kupitia Kristo, na pale ambapo Ibrahimu alipomwamini
Mungu, ilihesabiwa kwake kuwa haki, agano hili lilithibitishwa katika
17
Kristo. Hili ndilo agano la milele, Jerusalem ya juu, kwa maana katika
agano hilo, kwasababu ya ahadi ile, Ibrahimu “akiutazamia mji wenye
misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu” (Waebrania
11:10).
Haya yote yalikuja kwa Ibrahimu kipindi hana mtoto na ahadi lazima
ingetimizwa kupitia mzao wake. Miaka mingi ilipita tokea Bwana wa
Mzao wa Ibrahimu aongelee hilo kwa mara ya kwanza kipindi hana
mtoto. Ibrahimu alikuwa tayari mzee wakati alipoambiwa kwa mara ya
kwanza jambo hilo kuhusu mzao wake, na alikuwa anaendelea kuzeeka
bila hata kuona mzao yeyote. Hivyo alisema,
Mwanzo 15
2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina
mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 3 Abramu
akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye
mrithi wangu. 4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali
atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. 5 Akamleta nje, akasema,
Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu.
Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6 Akamwamini Bwana, naye
akamhesabia jambo hili kuwa haki. 7 Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana,
niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
Na pale ambapo Ibrahimu alipouliza “Mungu, nitajuaje kama kweli
nitairithi?” Bwana “Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu,
na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na
hua, na mwana njiwa. 10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande
viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege
hakuwapasua.” Ndipo Bwana kwa kupita katikati ya vile vipande
“akafanya agano na Abramu” agano la damu, ambalo linahitaji
kutimizwa kwa kila ahadi ambayo iliahidiwa kwa Ibrahimu. (Mwanzo
15:8-10, 18)
Hapa ndilo, Agano lake mwenyewe la kimbingu la Mungu, agano la
milele lilipofanywa na kuthibitishwa kwa Ibrahimu, Kwa ahadi yake
mwenyewe Mungu kuwa kila kitu kilichoahidiwa lazima kitimizwe, ili
kwamba chochote kilichoahidiwa kikishindwa kutimizwa basi Mungu
ataacha kuwepo.
18
Lakini bado muda unaenda, na hakuna mtoto anayeonekana, kwa
maana “Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana.” Lakini Sara
“alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri” na Sara akamwambia
Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie
mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye” (Mwanzo 16:1,2). Hapo
ndipo Hajiri anapokuja katika tukio, na kuletwa katika hii hadithi.
Lakini kwa namna gani Hajiri analetwa katika hadithi hii? Je ilikuwa
kwa kuamini ahadi ya Mungu? –Hapana. Imeletwa kwasababu ya
kutokuwa na imani. Je ilikuwa kwasababu ya Imani?-Hapana. Ilikuwa
ni kwasababu kutokuwa na imani. Hii inathibitishwa kutokana na jinsi
huu mpango ulivyofanywa, ni lazima mzao aje kupitia Sara yeye
mwenyewe na “Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa
kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa
alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu” (Waebrania 11:11)
Kama hilo ndilo lilivyokuwa mwisho, kwanini hapo mwanzo “Sara
mke wa Abramu hakumzalia mwana”?-Ilikuwa ni kwasababu ya
kutokuwa na imani kwake na yeye kushindwa “kumhesabu yeye
aliyeahidi kuwa mwaminifu”
Ndipo kwa kutokuwa na imani na Mungu, kwa kutokuwa na imani
huku, Sarai alifanya mpango uliomleta Hajiri. Huu mpango ulifanywa
kwasababu ya kutokuwa na imani na Mungu, ulikuwa ni mpango wa
akili ya asili—ulioletwa na mwili—ilikutimiza ahadi ya Mungu.
Kitu cha muhimu zaidi cha kuzingatia kutoka katika mpango huu ni
kwamba ulikuwa upo kwaajili ya kutimiza ahadi ya Mungu. Sio tu
walidhani kuwa Mungu hajatimiza ahadi yake, lakini pia alikataa
kutimiza. Kwa maana Sarai alisema wazi “Bwana amenifunga tumbo
nisizae.” Hii ni tuhuma ya wazi kabisa ya kutokuwa na imani na upande
wa Bwana, kwa vile aliamini kuwa Bwana ameshindwa kutimiza ahadi
yake, wakahitimisha kuwa walitakiwa wao wenyewe kutimiza kwa
kuleta mpango wao wenyewe ambao uliotokana na kutokuwa na imani
na Mungu.
Hata Abram alitolewa kutoka katika Imani yake kwa Mungu, kutoka
katika Imani kwa Bwana na ahadi yake. Abram akaanguka katika
19
mpango huu wa kutokuwa na imani, ulioletwa na mwili “Abramu
akaisikiliza sauti ya Sarai”
“Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada
ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu
mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba.
Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni
machoni pake.... Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu
akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa”.
(Mwanzo 16:4,15)
“Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili,” Kwanini hakuzaliwa
kwa njia nyingine yoyote? Mpango wote, ambao umemfanya mpaka
amezaliwa, wote ulikuwa ni akili ya asili, Katika Kutokuwa na imani
na Mungu—ulioletwa na mwili.
“Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama
maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa,
ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni”
(Wagalatia 4:24,25)
Hivyo Agano ambalo Hajiri anasimama—agano kutoka sinai—ni
agano ambalo watu walikuwa hawana Imani na Mungu na kutoamini
ahadi zake, wakijua tu akili ya asili na kuzaliwa katika mwili na kuunda
mipango yao wenyewe, na juhudi zao wenyewe kupata haki ya Mungu
na urithi ambao unaambatana na haki.
Lakini Haki ya Mungu ikiambatana na urithi katika ukamilifu wake ni
zawadi ya Bure.
20
3. HAJIRI NA SARA
Wagalatia 4
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko
Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
watoto
Hajiri anawakilisha agano kutoka sinai. Hajiri alikuwa ni mtumwa na
mmisri. Hivyo na mwana wake alikuwa ni mtumwa. Alikuwa ni
mtumwa kwa namna yoyote ile. Kwasababu mama yake alikuwa ni
mtumwa. Kama jinsi tulivyoona kuwa mwana wa Hajiri alizaliwa
kwasababu ya kukosa imani na Mungu na kutokuwa na imani katika
ahadi yake—ulikuwa ni mpango wa mwili, kwa hiyo “yule wa mjakazi
alizaliwa kwa mwili” Lakini
Warumi 8
“.7...ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu,
wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu”
Hivyo hivyo agano ambalo Hajiri anasimama—agano kutoka mlima
sinai—ni agano ambalo watu wanajua tu mtu wa asili na kuzaliwa kwa
mwili, wakitafuta kwa mafumbuzi yao wenyewe na kwa juhudi zao
wenyewe kupata haki ya Mungu, na urithi unaoambatana na haki hiyo.
Hili, kama jinsi tulivyokwisha ona, Sara na Abram walikuwa na ahadi
ya Mungu kwa ukamilifu, na haki yake, katika agano la Mungu
lililothibishwa kupitia Kristo, kabla hata mpango unaomleta Hajiri
haujaundwa. Na mpango huu uliundwa na ungeundwa, kwa kuweka
mbali ahadi na agano. Na kutelekeza ahadi na agano ni kuwa na imani
katika mwili.
Je watu pale Sinai walikuwa na ahadi yoyote kutoka kwa Mungu, au
agano ambalo wangeweza kuwa na imani kwake, kabla hata
hawajaingia katika agano la sinai?—Walikuwa nalo. Walikuwa na
21
agano la Ibrahimu, kama jinsi Abramu na Sarai kabla hawajaingia
katika mpango wa kumleta Hajiri.
Si tu walikuwa na hili agano la Ibrahimu, kwa kulinganisha umbali wa
muda kati ya Ibrahimu na wao, lakini lilirudiwa kwao, moja kwa moja
na Bwana, na kufanya nao kama jinsi ilivyokuwa kwa Ibrahimu kabla
hata hawajaondoka Misri.
Kutoka 6
2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3 nami
nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina
langu YEHOVA sikujulikana kwao. 4 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la
kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.5 Na zaidi ya hayo,
nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami
nimelikumbuka agano langu. 6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA,
nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na
utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu
kubwa; 7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi
mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya
mizigo ya Wamisri. 8 Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono
wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni
YEHOVA.
Hapa tunaona lilitolewa kwa wana wa Israel huko Misri pia lilitolewa
kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Agano hilo hilo alilo “fanya na
Ibrahimu na kuapa kwa Isaka” na “lililothibitishwa” kwa Yakobo,
lilifanywa na Israel, wakati bado wapo Misri, wakati Mungu anashuka
ilikuwaokoa kutoka Misri.
Sasa kwa nini tena wana wa Israel waliingia katika agano la pale
Sinai?—Kama jinsi mpango uliomhusu Hajiri ulivyoletwa. Kwa nini
agano jingie lililetwa?—Ni kama vile Hajiri alivyoletwa—yote ni
kwasababu ya kukosa imani katika agano la Mungu, yote ni kwasababu
ni kutokuwa na imani kuhusu ahadi ya Mungu iliyothibitishwa kwa
Kiapo chake. Kwa maana kama wangeamini katika ahadi za Mungu
alizozitoa kwao huko Misri, wangepata yote ambayo Ibrahimu au mtu
mwingine yoyote angeyapata, wangepata haki ya Mungu, wokovu
wake wa milele, na urithi ulioahidiwa kwa Ibrahimu na yote haya yapo
katika Kristo; Hii ndio jinsi Ibrahimu alivyopata.
22
Ni kweli waliimba nyimbo za ushindi katika Bahari ya shamu, baada
ya kuvuka, na kama wangeendelea katika imani hiyo, wangeendelea
katika agano la milele la Mungu alilowapa wakiwa huko Misri:
kusingekuwepo na agano lingine pale sinai.
Lakini hawakuendelea katika Imani; kwa maana muda mfupi tu
baadaye katika safari walipofika Marah, wakaanza kulalamika dhidi ya
Mungu. Na Mungu alipowaokoa kutoka katika hofu zao, walifikapo
katika nyika ya dhambi na “Makusanyiko yote walianza kulalamika”
tena.
Kutoka 17
3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona
umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa
kiu?
Na baada Mungu kuwaondolea hafu zao katika muda huo na wakaipita
nyika ya dhambi, wakafika Rephidimu, tena wakaanza kunun’gunika
na kusema
Kutoka 17
3 .................Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na
wanyama wetu kwa kiu? 4 Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu
hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.
Haya yote wanathibitisha kutokuwa na imani na kukosa imani kwake,
kwa upande wa Israel. Kukosa imani huku na kutokuwa na imani huku
ulizuia baraka na nguvu iliyotolewa katika agano la Ibrahimu, ambalo
Mungu aliwapa kipindi wapo huko Misri.
Hawakumuamini Mungu kwa urithi ambao ulikuwa unakuja, wala kwa
haki, ambayo pekee ndio ungewapatia urithi. Hili walifikiri wao
wenyewe wanaweza kulipata, na ili waone kwa jinsi gani wasingeweza
kuipata, Bwana aliwapa fursa pana sana ya kujaribu. Alisema,
Kutoka 19
4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya
mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu
kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu
kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi
23
mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno
utakayowaambia wana wa Israeli
Lakini bado hawakusikia sauti yake, lakini walipoisikia, Amri kumi
zilipotamkwa, wakakubali kutii amri kumi. Na hata waliposikia sauti
na utukufu wake na wakaogopa na “wakajiondoa na kukaa mbali”
walisema
Kutoka 24
7.............. Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.
Na wakafanana na mwana wa Hajiri mtumwa, ambaye “alizaliwa kwa
mwili.” Walijua tu kuzaliwa kwa Mwili na ndipo akili ya mwili pekee
ambayo ni
Warumi 8
7 .......uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
Na hawakuweza kuitii sheria kama Ishmael, mwana wa mwilini katika
familia ya Ibrahimu, asingeweza kutimiza ahadi kwa Ibrahimu. Katika
hali kama hii wasingeweza kushika agano la Mungu kama mpango wa
Sarai katika kumleta Hajiri ndivyo katika kushika agano hilo.
Kwanini agano hilo lililetwa? Kwanini waliingia katika agano hilo?
“Walikuwa hawana uelewa kuhusu utakatifu wa Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo
yao na kutojiweza kwao kutoa utii wa sheria za Mungu na uhitaji wao wa mwokozi.
Haya yote ni lazima wafundishwe....... Watu hao hawakugundua uovu wa mioyo
yao na kwamba bila Kristo ilikuwa haiwezekani wao kutii sheria ya Mungu
wakaingia mara moja katika agano na Mungu. Walihisi kuwa wanaweza kuanzisha
haki yao wenyewe, wakasema “Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii” (Ellen
White Wazee na manabii uk. 371,372)
Walikuwa tayari katika kifungo cha dhambi na kujihesabia haki; na
katika kifungo hicho kwa “akili zisizotii sheria ya Mungu” na
zisizoweza kufanya hilo, waliahidi kutii sheria za Mungu. Lakini kwa
hali waliyokuwepo ilikuwa ni wazi kuwa wangevunja ahadi yao.
Ilikuwa haiwezekani kwao kufanya hilo. Hivyo katika agano hilo,
walikuwa ni wavunjaji wa Sheria na wavunjifu wa ahadi yao ya
kutovunja sheria ya Mungu.
24
Na hili ndilo lilikuwa katika agano hilo, au kwa mujibu wa chochote
katika agano hilo. Hivyo katika Agano hilo KAMA HAJIRI, alizaa
utumwa pekee. Na hii ni kwasababu ya kutokuwa na imani na kukosa
imani na Mungu katika ahadi zake kama jinsi zinavyooneshwa katika
agano la Ibrahimu, ambalo lilitolewa kwao moja kwa moja, kabla hata
hawajaanza kutoa Misri.
“maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai,
lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima
Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa
anatumika pamoja na watoto. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana,
naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe
uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana
watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na
mume. Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi”
25
4. JE UPO AGANO GANI?
Wagalatia 4
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko
Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
watoto.
Ishmael alikuwa ni mwana wa Ibrahimu aliyezaliwa mwilini. Je
alikuwa mtu wa aina gani? Kabla ya kuzaliwa Bwana alieleza kuwa
“Atakuwa ni kama punda pori.” Tafsiri ya marudio (Revised Version)
inatafsiri “Atakuwa kama punda poro kati ya wanadamu.” “Mkono
wake utakuwa kwa watu wote na mkono wa kila mtu kwake”.
Kumbuka kuwa mtoto huyu wa Hajiri, huyu mwana aliyezaliwa katika
mwili, huyu “punda pori kati wa wanadamu” alikuwa ni matunda ya
mpango wa Sarai, uliokuja baada ya kutokuwa na imani na Mungu, na
kukosa imani katika ahadi yake kuwa atampa mwana. Pia weka akilini
kuwa mtoto huyu alidhamiriwa na Sarai kuwa ndiye atakaye timiza
ahadi za Mungu. Ilidhamiriwa na Sarai, hata na Ibrahimu kuwa huyu
mwana wa mwilini, huyu mtu pori, akubaliwe na Mungu kuwa ndiye
mwana aliyemmaanisha katika ahadi zake, na kwamba ahadi ya
Ibrahimu itekelezwe ndani yake. Hii ni wazi kabisa pale Bwana
alipomwaambia Ibrahimu kwamba atampa mwana kwa kupitia Sarai,
Ibrahimu alijibu, “lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele
yako.”(Mwanzo 17:18)
Sasa kumbuka kuwa Hajiri, mama wa huyu “Punda pori” anawakilisha
agano kutoka sinai, na mtoto wake alizaliwa katika mwili—Huyu mtu
pori—anawakilisha wana wa agano la sinai. Na kama vile ule mpango
uliomleta Ishmael, ulifikiriwa kutimiza ahadi ya Mungu, na kwamba
agano la Mungu kwa Ibrahimu litimizwe katika yeye, ndivyo kwa wana
wa hilo agano la sinai, kama Ishmael, walizaliwa katika mwili, na
walifikiri watamiza Ahadi ya Mungu kupitia wao, hivyo kupitia mwili.
26
Lakini Ibrahimu alishika amri za Mungu. Haki ya Mungu ndio kitu cha
kwanza cha muhimu katika agano na Ibrahimu, kwa maana bila hiyo
hakuna anayeweza kupata urithi aliopewa Ibrahimu katika Agano.
Lakini Je Ishmael atazaliwaje katika mwili, kisha akashika amri za
Mungu, wakati akili ya mwili ni uadui kwa Mungu na wala haiwezi
nyenyekea sheria za Mungu? Je inawezekanaje kwa huyo Punda pori
kushika amri za Mungu, wakati mkono wake upo kwa kila mtu, hali
moja kati vitu viwili katika sheria yote ya Mungu ni “Mpende jirani
yako kama nafsi yako”?
Huyu mtoto wa Hajiri aliyemtumwa anafanana na watoto wa agano lile
la Sinai, lililozaa utumwa. Kama Ishmael, walikuwa wanajua tu
kuzaliwa kwa mwili,na “akili ya mwili pekee” ambayo ni uadui dhidi
ya Mungu, na wala haitii sheria ya Mungu, na wala haiwezi kuwa,
waliahidi kuwa watatunza sheria ya Mungu “Ni kweli”
Lakini Ishmael alikuwa sio mtoto aliyedhamiriwa na Bwana,
hawezitimiza ahadi ya Mungu, wala ahadi ya Mungu haiwezi
kutimizwa katika yeye. Kwa jinsi ahadi na Agano la Ibrahimu lilivyo,
Kuzaliwa kwa Ishmael ilikuwa ni kama vile hajazaliwa kabisa.
Hivyo pale Ibrahimu alipomwambia Bwana “ Oh Ishmael angeishi
mbele yako” Mungu alisema
Mwanzo 17
“19 Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake
Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya
uzao wake baada yake. 20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki,
nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili,
nami nitamfanya awe taifa kuu. 21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka,
ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao”
Katika wakati huu Sarai alikuwa tayari ameamini katika ahadi ya
Mungu na kumuamini Mungu pekee na Mungu akambadili Jina kuwa
Sarah. Na hivyo “Kwa imani “hata Sara mwenyewe alipokea uwezo
wa kuwa na mimba” na kwa mujibu wa ahadi Isaka akazaliwa.
Sasa Isaka alikuwa ni mtu wa aina gani? Mienendo yake inaoneshwa
katika kipindi cha Ibrahimu pale alipokuwa anatakiwa atolewe kama
Kafara. Alinyenyekea kama mwanakondoo aliyetakiwa kutolewa. Na
inaoneshwa zaidi katika mwanzo 26 Baada ya Ibrahimu Kufa na isaka
27
akawa ndio mrithi wa agano, aliishi katika sehemu ambayo wafilisti
nao walikuwepo
Mwanzo 26
15 Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu
babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi. 16 Abimeleki
akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi. 17 Basi
Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko. 18 Isaka
akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu
babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake
Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. 19 Watumwa
wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.
Hivi visima bila pingamizi ni kwa Isaka. Ibrahimu alivichimba, na
hivyo ni mali ya Ibrahimu. Na pale Isaka alipokuwa ni mrithi wa
Ibrahimu, visima hivi vikawa ni mali yake kwa urithi. Na sasa
anavichimba tena, ambavyo ni kama anavichimba tena upya. Hivyo
bila pingamizi vilikuwa ni vyake. Lakini japokuwa vilikuwa ni vyake
kwasababu ya wafilisti pale visima vilivyofunguliwa, kutoka katika
kuwa vimejazwa na kifusi, ni wazi inaonesha kuwa hawakuwa
wanavitaka hata kidogo.
Lakini wafilisti wakaja kwa Isaka na kuvitaka visima ambavyo
vimefunguliwa ambavyo kwa haki kabisa ni vyake. “Maji ni yetu”
(Mwanzo 26:20). Isaka aliwaachia wawe navyo. Lakini ishmael
angefanyaje? Je wewe ungefanyaje? Kati ya wana wawili wa Ibrahimu
wewe upo upande upi? “Haya ni maagano mawili” Je wewe upo agano
gani?
Isaka “alichimba tena kisima kingine” na wafilisti tena “wakakitaka
tena na hicho.” Lakini Isaka badala ya kushindana nao ambacho kwa
kiwango kikubwa sana kilikuwa ni haki yake, alijiondoa kutoka kwao
na “akachimba kisima kingine” Lakini Ishmael angefanyaje? Wewe
ungefanyaje? Kati ya wana wawili wa Ibrahimu wewe ni yupi? “Haya
ni maagano mawili” je agano lipi upo?
Isaka alipochimba kisima cha mwisho, wafilisti hawakukitaka, ndipo
akakiita Rohoboth na akasema,
28
Mwanzo 26
22 Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi
Lakini Bwana alimuwekeaje nafasi?—Ni kwasababu alikataa
kugombana na wafilisti, kwa kuwakubalia yote ambayo wao
waliyataka, japokuwa ilikuwa ni haki yake. Lakini Je Mungu
angeweka nafasi kwaajili ya Ishmael na wafilisti? Je Mungu anaweka
nafasi kwaajili yako na wanaokupinga? Wewe ni yupi kati ya hawa
wana wawili wa Ibrahimu? “Haya ni maagano mawili” Je upo agano
gani?
Mwanzo 26
23 Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba. 24 Bwana akamtokea usiku uleule,
akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni
pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu
mtumishi wangu. 25 Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga
hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko26 Ndipo
Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli,
jemadari wa jeshi lake. 27 Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi
mmenichukia, mkanifukuza kwenu? 28 Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba
Bwana alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya
mapatano nawe 29 ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe,
wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u
mbarikiwa wa Bwana.
Lakini ilikuwa ni kwasababu ya unyenyekevu endelevu wa Isaka ndiyo
kilichowafanya waone kuwa Bwana alikuwa ndani yake na kwamba
alikuwa ni mbarikiwa wa Bwana. Lakini Ishmael angefanya nini? Je
wewe ungefanya nini? Wewe unafanya nini? Wewe ni yupi kati ya
wana wawili wa Ibrahimu? “Haya ndio maagano mawili” je wewe upo
agano gani?
Na ndivyo
Wagalatia 4
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko
Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
29
watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe
usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo
aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.
Wewe upo wapi?
30
5. LITUPE MBALI AGANO LA KALE.
Wagalatia 4
Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa
maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko
Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe
usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo
aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29
Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule
aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze
mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na
mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali
tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
Mpango ulioanzishwa na Sarai na kukubaliwa na Abram, uliomleta
Ishmael mwana wa mtumwa, ambaye alizaliwa kwa mwili, ulionesha
kuwa haukuwa wa kuridhisha kwa wote kuanzia hatua ya kwanza ya
kuanza kwake.
Mwanzo 16
3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa
Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe
mkewe. 4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya
kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
Japokuwa kama kumbukumbu zinavyonesha kuwa Sarai ndiyo wa
kwanza kutoa mpango huo kwamba “Sarai mkewe Abramu akamtwaa
Hajiri Mmisri mjakazi wake”...... “Akampa Abramu mumewe, awe
mkewe” lakini mara tu alipojua kuwa Hajiri anamuona duni, hii ni
kwasababu ya mafanikio ya mpango wa Sarai, anamgeukia Abramu
na kusema
31
Mwanzo 16
5 Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako,
naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake.
Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe 6 Naye Abramu akamwambia Sarai,
Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako.
Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake
Japokuwa Bwana alimwambia Hajiri
Mwanzo 16
.... 9 Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
Ni wazi kuwa hakukuwa na amani katika maisha yaliyofata. Tunaona
kuwa baada Ishmael kuzaliwa. Abram alimwambia Bwana “Ishmael
angeishi mbele yako” hakusikilizwa, lakini Ishmael aliwekwa pembeni,
na Abram akamwambia Sarai mke wake kuwa atamzalia mwana, na
atamwita jina lake Isaka “Nami nitafanya agano langu imara kwake
kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake” (Mwanzo
17:19).
Mwanzo 21
2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake,
kwa muhula alioambiwa na Mungu..... 8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya;
Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. 9 Sara
akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya
dhihaka. 10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na
mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. 11
Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. 12
Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya
huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa
maana katika Isaka uzao wako utaitwa
Lakini bado rekodi haijawa wazi. Ibrahimu alitoka katika ahadi
zilizowazi za Mungu na kuweka tegemeo katika mwili. Na sio tu
mtumwa na mwana wake wafukuzwe, na pia kila kitu kilichoshikiri
katika mpango kilichomleta mtumwa na mwana wake lazima
vitelekezwe. Hivyo Mungu akamwambia Ibrahimu,
32
Mwanzo 22
2 Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako
mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima
mmojawapo nitakaokuambia
Isaka alikuwa ni mwana wa ahadi, hakukuwa na mwana mwingine wa
ahadi, hakukuwa na ahadi nyingine na hakukuwa na mwana mwingine
kwa ahadi nyingine. Na sasa kwa Ibrahimu kumtoa Isaka kama kafara
ilikuwa ni zaidi ya kudhania kuchukua yote ambayo Mungu aliahidi.
Lakini Ibrahimu alipoangalia, aliangalia mbali zaidi, hata katika
chimbuko la ahadi ya Mungu na akaamini na kutegemea atakapomtoa
Isaka, Mungu anatimiza ahadi yake kwa kumfufua kutoka katika wafu-
kwa kumrudisha kutoka katika majivu baada ya kuwa ameunguzwa na
moto wa kafara.
Muito huu wa Bwana kwa Ibrahimu kumtoa Isaka kama sadaka ya
kuteketezwa, ulimrudisha Ibrahimu katika usiku wa ahadi halisi,
wakati Mungu aliposema,
Mwanzo 15
5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza
kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6 Akamwamini
Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Hivyo Ibrahimu alirudishwa kuamini katika ahadi ya Mungu iliyowazi
pekee, na yote ambayo ahadi imejumuisha. Na kama Ibrahimu
angesimama na kukataa pendekezo la Sarai kuhusu Hajiri,
kusingekuwa na matatizo ya kifamilia yaliyokuja kati ya Sarai na
Hajiri, Ishmael asingezaliwa na Ibrahimu asingeambiwa amtoe Isaka
sadaka. Kama tokea mara ya kwanza asinge “sita kwa kutokuamini”
(Warumi 4:20) lakini angekuwa ni imara katika imani akimpa Mungu
utukufu, akiamini kile kilichoahidiwa kukifanya, angepewa haki siku
zote.
“Haya ni maagano mawili moja kutoka katika mlima sinai, linalozaa
utumwa ambalo ni Hajiri” Agano la sinai ni matunda ya mwili, wa
kutokuwa na imani na kutoamini katika Mungu. Kama jinsi ule mpango
uliomleta Hajiri na uliomleta Ishmael. Kama jinsi Hajiri na Ishmael
mtumwa na mwana wake, walivyofukuzwa na mpango wote ulioletwa
33
ulivyowekwa pembeni, ndivyo agano la sinai linavyotakiwa lifukuzwe,
na yote yaliyofanya kuwepo kwa hilo agano yanatakiwa yawekwe
pembeni.
“Kwa kuwatoa Misri Mungu alikuwa anataka kuwaonesha nguvu yake na huruma
yake, ili kwamba wamwamini na wampende. Aliwaleta mpaka bahari ya shamu—
hali wakiwa wanafukuzwa na wamisri, na kutoroka ilikuwa ni ngumu—ili waone
hali yao kuwa hawajiwezi, na kuhitaji msaada wa Mungu, ndipo alipowaokoa.
Ndipo walipojawa na upendo na shukurani kwa Mungu na wakiwa na ujasiri katika
nguvu ya Mungu aliwachukua kama ndiye mwokozi katika utumwa.
Lakini kulikuwa na ukweli mwingine mkubwa kwaajili ya kushangaza akili zao,
hali wakiishi katikati ya sanamu na uovu, walikuwa hawana uelewa kuhusu
utakatifu wa Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo yao na kutojiweza kwao kutoa utii
wa sheria za Mungu na uhitaji wao wa mwokozi. Haya yote ni lazima wafundishwe.
Mungu aliwaleta Sinai aliwadhihirishia ukuu wake, aliwapa sheria zake, akitoa
ahadi ya mibaraka kama watatii “Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli,
na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila
yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme
wa makuhani, na taifa takatifu” (Kutoka 19:5,6).Watu hao hawakugundua uovu wa
mioyoyao na kwamba bila Kristo ilikuwa haiwezekani wao kutii sheria ya Mungu
wakaingia mara moja katika agano na Mungu. Walihisi kuwa wanaweza kuanzisha
haki yao wenyewe, wakasema “Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii” (Kutoka
24:7)
Walishuhudia kutolewa kwa sheria katika ukuu unaotisha, na waliogopa na
kutetemeka mbele ya mlima, lakini baada ya wiki chache walivunja agano lao na
Mungu, na walisujudia sanamu. Hawakuwa na tumaini tena kuwa katika upendeleo
wa Mungu kwa kupitia agano, ambalo wamelivunja SASA kwa kuona dhambi yao
na haja yao kwa kusamehewa, walipelekwa kuona hitaji lao la kuwa na mwokozi
aliyefunuliwa katika agano la Ibrahimu aliyekivuli katika kafara. SASA kwa imani
na upendo walimshikilia Mungu kama ndiye mkombozi kutoka katika vifungo vya
dhambi. SASA walikuwa katika hali ya kukubali baraka zilizokuwa katika
AGANO JIPYA’ (Ellen White, Wazee na manabii uk. 371,372)
34
6. MWANZO WA “IKIWA” NA “NDIPO”
Wagalatia 4
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.
Agano la sinai ni agano ambalo Mungu alifanya na wana wa Israel
alipowachukua kutoka Misri. Agano hilo lilikuwa na makosa,
Waebrania 8
7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa
kwa lile la pili.
Agano hilo lilikuwa na makosa katika ahadi zake kwa maana agano la
pili ni bora zaidi kuliko hilo kuwa “lililoamriwa juu ya ahadi zilizo
bora” (Waebrania 8:6)
kosa katika agano hilo lilikuwa ni kwa upande wa watu,
Waebrania 8
8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami
nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya
Hivyo kwasababu kosa la agano hilo lipo katika ahadi zake, kosa
lilikuwa kwa watu wenyewe, maana yake ahadi zilizotumika kuanzisha
agano hilo zilikuwa ni ahadi za watu.
Sasa je hizo ahadi zilikuwa ni ahadi zipi?—zilikuwa katika agano,
lililofanywa na wao walipotoka Misri na hilo ndilo agano.
Kutoka 19
4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya
mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu
kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu
kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi
mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno
utakayowaambia wana wa Israeli.....8 Watu wote wakaitika pamoja wakisema,
35
Hayo yote aliyoyasema Bwana tutayatenda. Naye Musa akamwambia Bwana
maneno ya hao watu.
Katika haya makubaliano watu wote waliahidi kusikia sauti ya Bwana.
Hawakusikia hata sauti ambayo angeiongea. Lakini katika sura ya
ishirini walisikia hiyo sauti likiongea maneno ya amri kumi,ambazo
Bwana alizinena na “Hakuongeza chochote.” Na waliposikia haya,
walirudia ahadi yao “Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii”
Hili ndilo agano ambalo Bwana alifanya na wao alipowashika mkono
kutoka Misri, na linaoneshwa wazi katika maneno yafuatayo
Yeremia 7
22 Maana sikusema na baba zenu, wala sikuwaamuru kwa habari za sadaka za
kuteketezwa na dhabihu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri; 23 lakini
naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu
wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru
mpate kufanikiwa.
Na haya yanathibitishwa na maneno haya
Yeremia 11
3 ukawaambie, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu
asiyeyasikia maneno ya maagano haya, 4 niliyowaamuru baba zenu, siku ile
nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti
yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa
watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;
Kuwa makini kwa kila kauli ya agano hili nakuona mfululizo wa ahadi.
Ya kwanza inaanza kwa upande wa Mungu “IKIWA mtaisikia sauti
yangu na kushika agano langu, NDIPO..............nanyi mtakuwa kwangu
ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno
utakayowaambia wana wa Israeli” n.k Katika hili tunaona kuwa ahadi
ya Mungu itakuja pale watakapotimiza ahadi yao, kwa maana agano
limeanza na “ikiwa” “IKIWA utafanya hili na hili, NDIPO hili na hili.
Huu pia ni mpangilio katika kauli ya pili, “Tiini sauti yangu NA
nitakuwa Mungu wenu, NA mtakuwa watu wangu”. Kwa mujibu wa
haya makubaliano, hawezi kuwa Mungu wao au wao kuwa watu wake,
mpaka wafanye kile walichoahidi, mpaka watakapo sikia sauti yake
kama walivyoahidi.
36
Kauli ya tatu nayo inasema hivyo hivyo “Itiini sauti yangu, mkafanye
sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu
wangu.” Hii inaweka wazi sio tu kwanza hakuna chochote kutoka kwa
upande wa Mungu kinaweza kuja, ni mpaka wao watimize kile
ambacho wameahidi. Upande wa Mungu utakuja kwa kufanya kile
ambacho wameahidi “Tiini sauti yangu” na “mkafanye” Hivyo [Kwa
jinsi hiyo na kwamtindo huo] mtakuwa watu wangu na nitakuwa
Mungu wenu”
Kwa vile katika agano hili sehemu ya Bwana, kile ambacho Bwana
angekifanya, kile ambacho ameahidi, kinaweza kuja baada ya watu
kufanya kile ambacho wameahidi, hii ni wazi kabisa kuwa ndio
msimamo wa agano, lilivyofanywa, ni kwa ahadi za watu pekee.
Nini thamani ya ahadi za watu? Nini walichoahidi? Waliahidi kutii
sauti ya Bwana kabisa. Waliahidi kutii sheria zake-kushika amri kumi
kabisa.
Lakini walikuwa katika hali gani wakati wanatoa ahadi hiyo?—
inafanana na hali ya ishmael katika familia ya Ibrahimu. Walifanana
na Ishmael: walikuwa wamezaliwa mwilini na walijua tu kuzaliwa
mwilini, hivyo walikuwa na akili ya mwilini. Lakini “Akili ya mwilini
ni uadui dhidi ya Mungu kwa maana hainyenyekei sheria ya Mungu
wala haiwezi kuitii” “Waliomwilini hawawezi kumpendeza Mungu”
Kama hii ndio ilikuwa ndio hali zao, kulikuwa na maana gani kutoa
ahadi kwamba watashika amri za Mungu kabisa?—ahadi yoyote au
zote zilikuwa ni sawa na hakuna kitu kabisa.
Katika agano watu walikuwa wanaahidi kufanya kitu ambacho
hawaizekani wao kukifanya. Na kwavile Bwana pamoja na ahadi zake,
asingefanya chochote katika agano hilo, mpaka watimize ahadi zao,
mpaka wafanye kile ambacho wamekubaliana, ilikuwa ni kwamba
katika uhalisia kile ambacho watu walikigundua au walichokibuni, hilo
agano halikuwa na maana yoyote, kwa maana ahadi ambayo ilikuwa
imesimamishwa nalo zilikuwa hazina maana yoyote.
Kwa asili ya vitu lile agano lilikuwa linazaa utumwa, kwasababu watu
ambao walikuwa wametoa ahadi walikuwa katika utumwa wa mwili,
utumwa wa dhambi, na badala ya kutunza amri za Mungu kweli kweli,
37
walikuwa wanazivunja. Na sio tu walikuwa wanavunja amri, ambazo
waliahidi kutozivunja, lakini walikuwa wanavunja ahadi yao ambayo
waliitoa kuwa hawatovunja amri. Hii ni kwasababu walikuwa katika
hali ya kutotii sheria za Mungu na hawawezi kutii.
Na hili limeelezwa haraka. Kwa maana Musa alipoenda kwenye mlima
kupokea Nakala ya sheria, ambayo waliahidi kuitii, alitoweka kwa
muda wa siku arobaini waliposema
Kutoka 32
1............Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa
huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.
Na wakajifanyia ndama wa dhahabu-mungu wa misri- na
wakamwabudu, kwa mtindo wa kimisri, hii inaonesha katika mioyo yao
walikuwa bado katika utumwa wa kimisri na walikuwa kama Ishmael,
mwana wa Hajiri mmisri “Aliyezaliwa katika mwili”
Japokuwa haya yote yameandikwa kwaajili watu wote watakaokuja
baadae, na kwaajili yetu “Kwa ambao miisho ya ulimwengu itakuja” ni
wazi kabisa hata leo wapo wengi ambao wanajua tu kuzaliwa katika
mwili, ambao hawajazaliwa tena, ambao hawajui kuzaliwa katika roho,
na bado wataingia katika agano kama hilo na watataka kutii amri zote
za Mungu. Lakini tatizo la hawa ni kama tatizo la watu wa sinai, na
kama ilivyotatizo la watu wa sinai, “Walikuwa hawana uelewa kuhusu
utakatifu wa Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo yao...............Walihisi
kuwa walikuwa wanaweza kuanzisha haki yao wenyewe na wanasema
“Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii|”
Swali linakuja hapa, kwanini waliruhusiwa waingie katika agano kama
hilo? Kwanini Mungu alifanya nao agano kama hilo?
38
7. AGANO LA KALE LIMELETA JIPYA
Wagalatia 4
Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa
maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko
Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe
usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo
aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29
Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule
aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze
mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na
mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali
tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
Agano la kwanza lilikuwa na makosa. Lilikuwa na makosa kwasababu
lilitegemea ahadi za watu ambapo watu waliahidi kitu ambacho
ilikuwa haiwezekani kukitimiza.
Kwanini sasa waliruhusiwa waingie katika agano hilo? Je hakujua
kuwa watu wasingeweza kutimiza kile walichoahidi? Kwa uhakika
alijua.
Lakini watu ndio ambao hawakugundua. “hali wakiishi katikati ya
sanamu na mauovu, walikuwa hawana uelewa kuhusu utakatifu wa
Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo yao na kutojiweza kwao kutoa utii
wa sheria za Mungu na uhitaji wao wa mwokozi. Haya yote ni lazima
wafundishwe. Mungu aliwaleta Sinai aliwadhihirishia ukuu wake,
aliwapa sheria zake, akitoa ahadi ya baraka kama watatii “Sasa basi
ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo
ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana
dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa
makuhani, na taifa takatifu” (Kutoka 19:5,6).Watu hao hawakugundua
uovu wa mioyoyao na kwamba bila Kristo ilikuwa haiwezekani wao
39
kutii sheria ya Mungu wakaingia mara moja katika agano na Mungu.
Walihisi kuwa wanaweza kuanzisha haki yao wenyewe, wakasema
“Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii”
Kwa vile watu hawakugundua vitu vya msingi kuhusu wao-
kutokuweza kwao n.k—kwavile hawakuamini katika Mungu ili
waweze kujua –na kwavile kila kitu wanatakiwa wafundishwe—njia
pekee ambayo inaweza kuwafanya wajifunze hiki ambacho hawakuwa
wanajua ni kuwafanya wajaribu na kushindwa ili wajifunze kutokana
na hayo kwamba wao wenyewe hawawezi kuanzisha haki yao
wenyewe kama ni haki ya Mungu. Ndipo wanaweza kukubali kwa
imani haki ya Mungu, ambayo imejengwa na Imani. Haya yote yapo
wazi katika mambo hayo.
Kama jinsi tulivyoona katika somo lililopita, kabla ya kuondoka Misri
Bwana alisema
Kutoka 6
“7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua
ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya
Wamisri
Ilikuwa wazi sana kama wangeamini tayari, wangejua kuwa tayari
alikuwa ni Bwana Mungu wao na wasingeingia katika makubaliano ili
Mungu awe Mungu wao na wao kuwa watu wake.
Kama wangeamini neno lake, kwamba siku zote alikuwa ni Mungu
wao,na kwamba wao tayari walikuwa ni watu wake,na kama
wangeelewa kuwa tayari alikuwa ni Bwana Mungu wao, je wangeitaji
kuahidi kuwa wataitii sheria yake “kwelikweli” ili kwamba wawe watu
wake, na yeye awe Mungu wao? Ni wazi kabisa, hapana.
Kama wangeamini kuwa Bwana angewapa wao urithi aliyoahidi kwa
Ibrahimu kuwa atampa, na kwa Isaka, na kwa Yakobo (Kutoka 6:8),
je kungekuwa na sehemu yoyote ambayo kuna makubaliano ambayo
wangeingia?, na kwamujibu wa waliyofanya, je kwa matendo,
wangeweza kupata urithi huo? Ni wazi hapana.
Kwa maneno mengine, kama wangempokea Mungu kwa imani katika
vitu hivi, alivyowaahidi kabla hata hawajatoka Misri, je wangejaribu
40
kutafuta njia ya ushindi dhidi yake katika vitu hivyo, kwa matendo yao?
Ni wazi hapana.
Kwa maneno mengine, kama wangemjua na wangekuwa ndani ya
agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu, agano la milele, je
wangehitaji kumjua na kuingia katika agano hili la sinai, ambalo
lilianzishwa na wao, kwasababu lilitegemea ahadi zao wenyewe? Ni
wazi hapana.
Tukifatilia mtiririko wa mawazo na kurudi katika mwanzo wake, katika
mistari hii ya wagalatia swali ni Kama Sarai na Abram wangeamini
ahadi ya Mungu na wangeishikilia , je ishmael angeonekana katika
familia ya Ibrahimu? Je wana wawili wa Ibrahimu wangezaliwa na
Ibrahimu? Ni wazi hapana.
Ni wazi kuwa, hakukuwa na haja yoyote ya Ibrahimu kuwa na mwana
zaidi ya mmoja—zaidi ya mwana ambaye Bwana alimuahidi. Lakini
“haya ni maagano mawili” Moja kutoka Sinai, linalozaa utumwa,
ambalo ni Hajiri.
Na kama jinsi ilivyokuwa hakukuwa na haya Ibrahimu kuwa na wana
wawili ila mmoja—mwana ambaye Mungu ameahidi—Hivyo
hakukuwa na haya Israel kuwa na maagano mawili ila agano moja—
Agano la Mungu na Ibrahimu—agano la milele.
Kama jinsi ilivyokuwa hakukuwa na haya ya wana wawili, hakukuwa
na haja ya maagano mawili.
Kutokana na kutoamini na kukosa imani na Mungu, Hajiri na Ishmael
waliingia kama vile kutokana na kutokuwa na imani na Mungu, agano
la Sinai liliingia.
Na kama vile Hajiri na Ishmael hawakuwa wanatambuliwa kwa namna
yoyote ile katika ahadi ambayo Mungu alimuahidi Ibrahimu kuhusu
mwana, ndivyo ilivyo kwa agano la sinai halikuwa linatambuliwa kwa
namna yoyote ile katika ahadi za Mungu kuhusu wokovu kwa
Wanadamu.
Kama jinsi Hajiri na Ishmael walikuwa wafukuzwe na yote
yaliyowaleta yalitakiwa yawekwe pembeni, ili kwamba mwana
aliyeahidiwa na Mungu awe na nafasi anayostahili, ndivyo ilivyo kwa
41
agano la Sinai lazima lifukuzwe na yote ambayo yaliyoleta agano hilo
lazima yawekwe pembeni, kwa upande wa watu, ambapo ndio ahadi za
agano hilo lilipoelemea, ili kwamba agano halisi—agano la Ibrahimu—
agano la milele liwe na nafasi linalostahili, katika maisha na wokovu
wa watu.
Lakini kama kulivyokuwa na matatizo na kushindwa kwa Sarai na
Ibrahimu katika mpango uliowaleta Hajiri na Ishmael, ilikuwa ni
chombo ya kuwaleta katika sehemu ambayo wangeweza kumwamini
Mungu pekee, ndivyo hivyo matatizo na kushindwa kwa wana wa Israel
katika agano la kwanza liliwaleta katika sehemu ambayo walikubali na
waliamini katika, agano halisi la Mungu—agano la Ibrahimu—agano
lake la Milele—ambalo alilitoa kabla hawajatoka Misri.
Hivyo tumeona Israel walivunja sheria ya Mungu na agano lao kuwa
hawatoivunja. Na Musa aliposhuka kutoka katika mlima, akiwa katika
mkono wake mbao za Sheria, walizoahidi kuwa hawatozivunja,
alipoona walichokifanya “akazitupa zile mbao mikononi mwake,
akazivunja chini ya mlima” (Kutoka 32:19)
“Ikiwakilisha kuwa walikuwa wamevunja agano lao na Mungu, hivyo
Mungu amevunja agano lake na wao” (Ellen White, Wazee na manabii
uk, 320)
Hivyo wakajikuta hawana la kufanya na wasio na msaada, wakiwa
wamechoka. Kwa maana “Hawakuwa na tumaini tena kuwa katika
upendeleo wa Mungu kwa kupitia agano, ambalo wamelivunja SASA
kwa kuona dhambi yao na haja yao kwa kusamehewa, walipelekwa
kuona hitaji lao la kuwa na mwokozi aliyefunuliwa katika agano la
Ibrahimu aliyekivuli katika kafara. SASA kwa imani na upendo
walimshikilia Mungu kama ndiye mkombozi kutoka katika vifungo vya
dhambi. SASA walikuwa katika hali kukubali baraka zilizokuwa katika
AGANO JIPYA” (uk. 372)
Hivyo agano la Sinai lilileta Agano la Ibrahimu. Agano la kwanza
lilileta la agano la pili. Agano la kale lilileta agano jipya. Hivyo sheria
ambayo ndio msingi wa agano hilo—sheria iliyovunjwa—ilikuwa ni
kiongozi kuwaleta kwa kristo ili wahesabiwe haki kwa imani.
42
43
8. TOFAUTI YA MAAGANO
Wagalatia 4
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri......... 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu
watoto wa ahadi.
Kama Ishmael alizaliwa katika mwili, bila ahadi yoyote ya Mungu,
lakini kutokana na Kutokuwa na imani na Mungu na kukosa kuamini
ahadi zake, ndivyo ilivyokuwa kuhusu agano la kwanza—agano la
sinai.
Na kama ilivyokuwa kwa Isaka alivyozaliwa kwa ahadi ya Mungu,
kwa kutegemea ahadi za Mungu, ndivyo ilivyokuwa kwa agano jipya—
agano la milele.
Agano la kwanza lilitegemea ahadi za watu, na lilitegemea kabisa
juhudi za watu. Agano la pili linategemea kabisa ahadi ya Mungu, na
linategemea katika nguvu na kazi ya Mungu.
Agano la kwanza linamtindo “Ikiwa mtafanya” hili na hili. Agano jipya
halina “ikiwa” wala mtu kufanya jambo, lakini ni kufanya katika
Bwana. Angalia jinsi yalisimama pamoja.
Agano la Kale
Kutoka 19
5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo
ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote
pia ni mali yangu, 6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.
Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. (Kutoka 19:5,6 Jeremia
7:23, 11:4)
Agano Jipya
Waebrania 8
10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile,
asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao
44
nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. 11 Nao
hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,
Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Tuanze kusoma agano jipya, tukianza na neno “ikiwa mtafanya” n.k
“Ikiwa mtaweka sheria zangu katika akili zenu, na kuandika katika
mioyo yenu, ndipo nitakuwa Mungu wenu na mtakuwa watu wangu”
weka sheria zangu katika akili zenu na ziandike katika mioyo yenu, ili
kwamba niwe Mungu wenu na nyie muwe watu wangu”
Kama agano jipya linasomeka hivyo, ni watu wangapi wangeweza
kuwa watu wa Mungu? Na yeye angekuwa ni Mungu wa watu
wangapi?—hakuna hata mmoja; kwasababu hakuna mtu yoyote
anayeweza kuandika sheria ya Mungu katika moyo wake; hakuna mtu
anayeweza kuweka sheria ya Mungu katika akili yake. Kwa maana akili
ya asili ni uadui dhidi ya Mungu haiwezi nyenyekea sheria ya Mungu
na wala haiwezi itii.”Hakuna chochote kilichopungukiwa na nguvu ya
Mungu pekee, kupitia roho wa milele, anaweza kuweka sheria ya
Mungu katika akili ya mtu yoyote au kuandika katika moyo wake.
Lakini kufanya haya yote, ndio ambayo wana wa israel walikubali
kufanya pale Sinai, katika agano la kale. Kwa maana walikubali
kushika sheria za Mungu “kabisa” ambayo hakuna mtu anaweza
kufanya hilo kama sheria haijawekwa katika akili yake. Na kuandikwa
katika moyo wake. Walikubali kushika sheria ya Mungu “kabisa” ili
kwamba wawe watu wake na yeye awe Mungu wao. Makubaliano yao,
yalikuwa ni wazi kwamba wao wenyewe waweke sheria za Mungu
katika akili zao na kuandika katika mioyo yao wakati bado walikuwa
wanachojua ni kuzaliwa katika mwili, wakati bado walikuwa wana akili
ya asili, ambayo ni uadui dhidi ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya
Mungu na wala haiwezi kutii.
Hivyo ilikuwa ni juhudi zao wenyewe kwamba wawe wenye haki, na
kwa haki hii wajiweke kuwa ni watu wake. Na kushinda ili awe Mungu
wao.
Hivyo agano hilo lilikuwa ni la matendo, la haki kwa matendo, la
kushindania upendeleo wa Mungu kwa matendo, la wokovu kwa
matendo.
45
Ilikuwa ni agano ambalo kwasababu ya matendo, zawadi haikuwa ni
kama neema, lakini ni kama deni.
Ilikuwa ni agano halikuwa na kitu kama kusahemewa dhambi; ilikuwa
ni kifungo, na kuzaliwa kwa utumwa.
Ndio maana agano hili limeletwa katika waraka huu wa wagalatia.
Wagalatia walikuwa wanatafuta haki kwa matendo, kwa juhudi zao
wenyewe. Walikuwa wanatafuta kuwa “wakamilifu katika mwili.”
Lakini mkristo yoyote akitafuta haki au kuwa mkamilifu, kwa njia hii,
ameanguka nje ya neema. Atakuwa ameiacha neema; kwasababu
Warumi 4
4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa
ni deni
Na,
Warumi 11
6 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa
neema
Hii ndio ilikuwa ni nafasi na hali za “mafalisayo waliyoamini” ambao
ndio waliowafanya wagalatia waende nje ya njia. Katika mfumo wa
kuhesabiwa haki kwa matendo, na kujaribu kuwa wakamilifu katika
mwili, mafalisayo walioamini walibadili kila kitu ambacho alichowapa
kuwaokoa kutoka katika utumwa wa kujihesabia haki na matendo ya
mwili na wangeweza kuharibu kwa huo uongo kila injili ya Kristo
mwenyewe.
Kwa upande mwingine, agano jipya lote ni la neema,na la matendo ya
Mungu kwa neema.
Ni agano ambalo kazi yote ni kazi ya Mungu na haki ni haki ya Mungu.
Ni agano ambalo kila mmoja anayendani yake amezaliwa katika roho
na kila mmoja anayepokea akili mpya na Moyo mpya, katika akili hiyo
sheria ya Mungu inawekwa, na katika moyo huo sheria inaandikwa kwa
roho wa Mungu aliyehai.
Ni agano ambalo kwa nguvu ya ubunifu ya Mungu, kila mmoja
anayekubali ile ahadi anafanywa kuwa mwana na Mungu.
46
Waefeso 2
10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema,
ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Ni agano ambalo ni kwasababu ya Huruma ya Mungu, na kwa ahadi
yake, kuna kusamehewa dhambi, zote na Bure; dhambi na uovu
havitakumbukwa tena.
Ni agano ambalo kweli msamaha lazima upatikane kwaajili ya dhambi
za watu waliokuwa katika agano la kwanza. Kwamaana,
Waebrania 9
15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa
kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee
ahadi ya urithi wa milele.
Kumbuka tena, katika agano jipya hakujatajwa kokote kuhusu kazi ya
watu. Kazi yote ni ya Mungu
Waebrania 8
10.......... Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika
12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Katika agano jipya ni Mungu pekee ndiye anayefanya kazi.
Wafilipi 2
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda
kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema
Ni kwa kupitia “damu ya agano la milele” ndipo “Mungu wa amani”
anawafanya kuwa “wakamilifu katika kila tendo jema, mpate
kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele
zake, kwa Yesu Kristo” ambaye ndiye hakika kwa “agano lililo bora”
(Waebrania 13:20,21;7:22)
Njia pekee ya mtu kuja katika agano hili ni kwa unyenyekevu, ni lazima
wajinyenyekeze katika haki ya Mungu. (Warumi 10:3). Wamkubali
Mungu na miili yao “viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za
haki.”(Warumi 6;13)
47
Hivyo yoyote ambaye yupo katika agano hili kwa namna yoyote ile,
yupo kikamilifu katika ahadi za Mungu, na kuwa “Kama isaka” mwana
wa ahadi.
Hakuna njia nyingine kuwa mshiriki wa agano jipya bila ahadi ya
Mungu kwa maana hakuna chochote katika agano ila ahadi za Mungu
zilizowazi. Hakuna njia nyingine ya kuwa mwana wa Mungu, ila kwa
kupitia ahadi ya Mungu. Ahadi iliyopokelewa kwa imani. Dhambi zetu
zimesamehewa na kutokuwa na haki kwetu kumesamehewa,
kwasababu Mungu amesema hilo, na kwa neno hilo la ahadi tunalijua.
Yoyote anayepokea na kutegemea katika ahadi za Mungu pekee ni
moja kati ya watu wa Mungu kwasababu Mungu amesema. Mungu
ndiye Mungu wake, kwasababu Mungu amesema hilo. Sheria ya
Mungu ipo katika akili yake na imeandikwa katika moyo wake,
kwasababu Mungu ameahidi kuwa ataweka katika akili yake na
kuandika katika moyo wake na yeye amejinyenyekeza mbele za Mungu
na kuacha Mungu afanye kazi. Na baada ya kujinyenyekeza katika haki
ya Mungu, anapata pumziko na ulinzi katika ahadi ya Mungu katika
Kristo, ambaye ndiye mpatanishi na hakika ya agano jipya. Na
Yohana 6
29 Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye
Agano la kale linaahadi na matendo ya watu ambao wanajua tu
kuzaliwa na mwili na akili ya mwili. Agano jipya lina ahadi na matendo
ya haki ya Mungu kwa wale wanaojua kuzaliwa kwa Roho katika ahadi
ya Mungu.
48
9. NAFSI AU KRISTO?
Wagalatia 4
Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa maana
imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja
kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana
kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano
mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri
ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa
anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye
mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti,
ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa
huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini
kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho,
ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa
maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31
Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye
mwungwana.
Agano la kwanza lilitegemea ahadi za watu, ambao walikuwa wanajua
tu kuzaliwa katika mwili. Na ahadi hiyo ilikuwa ni kutunza amri kumi
za Mungu kikamilifu. Lakini kwa vile walikuwa wanajua tu kuzaliwa
katika mwili, katika muda huo walikuwa ni wavunjifu wa sheria ya
Mungu, na hivyo walikuwa katika kifungo cha dhambi. Na kwakujua
tu kuzaliwa kwa mwili na kwa kuwa tu na akili ya mwilini, ahadi yao
ya kushika sheria ya Mungu kikamilifu ilikuwa haina maana,
kwasababu
Warumi 8
7 ........nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu,
wala haiwezi kuitii”
Hata kama wasingeahidi chochote kuhusu kuitii sheria ya Mungu, bado
wangeivunja, kwasababu walikuwa wanajua tu kuzaliwa kwa mwili,
“na walio mwilini hawawezi kumpendeza Mungu”. Hivyo, bila ahadi
yoyote kushika sheria ya Mungu, bila kuzaliwa upya, wangeendelea
kuwa katika utumwa wa dhambi. Na walipoahidi kushika sheria, na
kisha wakavunja ahadi yao (ambayo, kwa kuwa na akili ya mwilini
ilikuwa ni lazima kuwa wangefanya hivyo), hili liliwafanya waingie
katika utumwa wenye kina kikubwa, kwasababu
49
Kumbukumbu 23
21 Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika
kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi
itakuwa dhambi kwako
Hivyo, agano hilo lililetwa na watu ambao walikuwa tayari wapo katika
utumwa, na ni agano ambalo, kwa jinsi lilivyo, lilizaa utumwa, lilikuwa
ni agano la utumwa—agano ambalo linategemea juhudi zao kujitoa
katika utumwa ambao tayari wamo, liliwafanya wawe katika utumwa
mkubwa zaidi, utumwa wa dhambi, utumwa wa matendo yao wenyewe
na ahadi zilizovunjika, ambazo ni dhambi tu.
Yote yaliyoonekana au yangeonekana, katika agano la kwanza ilikuwa
ni kuvunjwa kwa sheria. Na hii itakuwa ni wazi milele kiasi cha
kwamba hakuna ambaye atashindwa kuona pale Musa aliposhuka
kutoka katika mlima na akaona sanamu zao, japokuwa alikuwa na mbao
za mawe zenye sheria ya Mungu,
Kutoka 32
19 .......... akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
Wao ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja sheria. Waliahidi kutovunja
sheria. Lakini sasa walivunja vyote sheria na ahadi yao ya kutovunja
sheria. Na kwa hiyo, kwasababu hii, Musa alizitupa zile mbao za mawe
zenye sheria ya Mungu na kuzivunja, hii ni ili kuwapa watu wote somo
milele lenye mfano, kwamba katika agano la kwanza, katika juhudi zote
za kujihesabia haki, na katika ahadi zao zote za kutovunja sheria ya
Mungu, hakuna mtu yoyote anayeweza kuona chochote isipokuwa
KUVUNJWA KWA SHERIA.
Lakini lilikuwepo na hata sasa lipo agano la Ibrahimu, agano la imani,
agano la milele la Mungu, kuwaokoa kutoka katika vifungo vya
dhambi, ambao juu yao kwasababu ya agano la matendo, la kutokuwa
na imani,ambalo walikuwa wameingia, “Hawa kuwa na tumaini lolote
la upendeleo wa Mungu kupitia agano ambalo walikuwa
wamelivunja”—kupitia agano ambalo hakuna chochote kinachoweza
kuonekana isipokuwa sheria iliyovunjwa. “sasa kwa kuona dhambi yao
na haja yao ya kusamehewa, walipelekwa kuona hitaji lao la kuwa na
50
mwokozi aliyefunuliwa katika agano la Ibrahimu aliyekivuli katika
kafara”
Ilikuwa ni agano kupitia Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambalo Musa
alimsihi Mungu, rehema kwa watu waliokuwa wanaabudu sanamu ya
dhahabu ya ndama chini ya mlima, wakati bado akiwa mlimani, kabla
bado hajashuka kwa mara ya kwanza. Angalizo: Kutoka 32:1-6
imeonesha watu wakiwa wanatengeneza ndama wa dhahabu na
kumuabudu, katika mstari wa saba,
Kutoka 32
7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa
katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, 8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia
niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea
dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya
Misri. 9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama,
ni watu wenye shingo ngumu 10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao,
niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
Kutoka 32
11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira
zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu,
na kwa mkono wenye nguvu? 12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa
kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso
wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu
wako. 13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao
uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota
za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi
milele. 14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu
wake.
Hili lilikuwa ni agano la Ibrahimu, agano la milele la Mungu ndilo
lililowaokoa watu kutoka katika vifungo na laana ya dhambi zao, katika
agano la kwanza. Na ndivyo ilivyokuwa. (Waebrania 9:15)
Ndipo aliposhuka kutoka mlimani, akiwa na mbao za sheria ya Mungu
katika mikono yake, na akazitupa zile mbao za sheria ya Mungu, na
akazivunja,
“Ikiwakilisha kuwa walikuwa wamevunja agano lao na Mungu, hivyo
Mungu amevunja agano lake na wao,” na inawakilisha kuwa katika
agano hilo hakuna chochote isipokuwa sheria iliyovunjwa, na kwamba
51
“Hawa kuwa na tumaini lolote la upendeleo wa Mungu kupitia agano
ambalo walikuwa wamelivunja” na “sasa kwa kuona dhambi yao na
haja yao kwa kusamehewa, walipelekwa kuona hitaji lao la kuwa na
mwokozi aliyefunuliwa katika agano la Ibrahimu aliyekivuli katika
kafara. Sasa kwa imani na upendo walimshikilia Mungu kama ndiye
mkombozi kutoka katika vifungo vya dhambi. Sasa walikuwa katika
hali kukubali baraka zilizokuwa katika agano jipya” (Wazee na manabii
p.373).
Hivyo agano la Sinai liliwaleta katika agano la Ibrahimu. Agano la
kwanza liliwaletea la pili. Agano la kale liliwaletea agano jipya. Na sasa
sheria ambayo ndio msingi wa agano—sheria iliyovunjwa—ilikuwa ni
kiongozi kuwa leta kwa Kristo, ili wahesabiwe haki kwa imani.
Ndipo,
Kutoka 34
1 Kisha Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile
za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya
mbao za kwanza, hizo ulizozivunja
Na Musa akasema,
Kumbukumbu 10
3 Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano
wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu.
4 Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi,
alizowaambia Bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; Bwana
akanipa. 5 Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya
sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru Bwana.
Na kukaanzishwa kati ya watu huduma ya Hekalu, na mwokozi akiwa
ni kivuli cha “kafara” na Kristo “mjumbe wa agano jipya” na
mpatanishi pekee kati ya Mungu na mwanadamu” akiwakilishwa na
kuhani mkuu katika huduma ya Hekaluni. Katika hekalu hilo walileta
kwa imani na unyenyekevu sadaka zao na kutubu dhambi zao. Damu
ya sadaka zao ilichukuliwa na kuhani mkuu katika hekalu, na
upatanisho ulifanyika kwaajili yao, na dhambi ilisamehewa. Katika
sikukuu ya upatanisho damu ya kafara kwa watu wote ilinyunyuziwa
52
katika kiti cha rehema na mbele ya kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya
sanduku , juu ya zile mbao za mawe.
Hivyo kati ya mdhambi na sheria kulikuwa na kafara, ikiwakilisha
Kristo, ( na ambaye kwa imani alikuwa ni Kristo, hakika ya agano
lililobora), ambaye kwa yeye alimletea mdhambi msamaha wa dhambi,
na haki ya Mungu, ambayo inatosheleza matakwa yote ya sheria. Na
hivyo kupitia imani kwa Kristo, katika agano hili ambalo Kristo
alikuwa ni mpatanishi, na ambaye yeye ni hakika, kinachoonekana ni
sheria isiyokuwa imevunjwa.
Hivyo ndio jinsi na ndivyo ilivyo maana halisi ya utaratibu mpya pale
sinai, baada ya kuvunja mbao za mawe, na baada ya kuliacha kabisa
agano la kwanza. Ilikuwa ni kupitia imani, kupitia haki ya Mungu
iliyokatika imani ya Yesu Kristo kwa wote wanaoamii (Warumi 3:22)
Lakini tazama katika kutoamini kwao, baadaye Israel waligeukia
mfumo wa matendo, kama ilivyokuwa katika agano la kwanza. Na
kafara na sadaka, na ibada iliyokuwa inaambatana nazo, zilitolewa na
Mungu iwe kielelezo cha imani. Lakini Israel katika kukosa kwao
imani, walipoteza yote haya, na wakafanya kuwa mfumo wa matendo,
na wakimatambiko. Badala ya haki kuja kupitia imani, na sadaka na
kafara kuwa kama kielelezo cha imani, walitegemea haki kupitia kafara
yenyewe, na kwa matendo yao mema kwa kutoa kafara.
Ndivyo ilikuwa kipindi cha Yesu hapa duniani, na kipindi cha Paulo na
wagalatia. Ndivyo ilivyokuwa kwa “mafalisayo walioamini”
(Mafalisayo waliodai kuamini injili) waliowachanganya wagalatia na
kuwaendesha kurudi nyuma kutoka haki kwa imani kwenda kwenye
haki kwa matendo na matambiko. Na hivyo Paulo angeandika na
aliandika,
Wagalatia 4
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa
mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa
mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;
kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo
kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 4.25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko
Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
watoto.
53
Hivyo njia ambayo Mungu aliitoa kuwaokoa kutoka katika utumwa wa
agano la kale, kwasababu ya kutoamini kwao, waligeukia mfumo wa
utumwa, uliokuwa unafanana kabisa na utumwa wa agano la Kale.
Waliharibu agano jipya kama jinsi ilivyokuwa limeelezwa kwenda
katika kanuni za agano la kale—haki kwa matendo. Kile ambacho injili
imeleezea kupitia kafara, sadaka na huduma ya kipindi hicho,
walibadili kuwa utumwa wa haki kwa matendo na matambiko, vile vile
kama ilivyokuwa “mafalisayo walioamini” walikuwa wanabadilisha
injili iliyokuwa inaelezwa kupitia kafara na huduma ya Kristo
mwenyewe.
Na kama jinsi Hajiri na Ishmael walivyofukuzwa, ili kwamba agano la
Mungu pamoja na Ibrahimu lifurahiwe kikamilifu, na kama jinsi
lilivyowekwa pembeni na kutupwa ili kwamba baraka za agano la
Ibrahimu, agano jipya, ziweze kufurahiwa, Kristo alipokuja kwa
kupitia sadaka na kafara yake mwenyewe, na kwa huduma yake
mwenyewe alileta ukamilifu wa injili—ilikwamba hili liweze
kufurahiwa kikamilifu, lazima mfumo wa ibada na matambiko uwekwe
pembeni, mfumo wa haki kwa matendo ambao Israeli walibadilisha
ambao hapo awali ulikuwa ni kielelezo cha injili ya kweli, wa haki kwa
imani. “Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na
watoto.”.......... “Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na
mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na
mwana wa mwungwana” “Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana,
naye ndiye mama yetu sisi.”........... “Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi
tu watoto wa ahadi”
Na ndipo kanuni za matambiko ziliachwa milele—kanuni ambazo
zilikuwa ni utumwa wa haki kwa matendo katika mtindo wowote ule
utakaojidhihirisha, na kukaanzishwa katika nafasi yake kanuni za
kimbingu za uhuru, katika haki kwa imani.
Wagalatia 5
1 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe
tena chini ya kongwa la utumwa.
Agano la kale, agano la sinai, linaweza kuhitimishwa kwa neno
“NAFSI.” Agano jipya, agano la milele, linaweza kuhitimishwa kwa
neno “KRISTO”
54
Agano la kale ni nafsi na haki yake. Agano jipya ni Kristo na haki ya
Mungu. Agano la kale ni nafsi na utumwa wa dhambi na matendo ya
sheria. Agano jipya ni Kristo na uhuru wa haki, ambao ni imani.
Agano la kale—nafsi—lazima ziachwe na liwekwe pembeni, ili
kwamba agano jipya—Kristo—awezekuchukua nafasi yake na
kudhihirisha nguvu yake ya wokovu, kwa maana mwana wa mjakazi
hawezi kuwa mrithi pamoja na mwana wa mungwana.
55
UFUPI WA SOMO LINALOFATA.
Nimeona niweke na sura hii inayofata katika kitabu hiki ilikutoa
maelezo ya kina zaidi kuhusu agano jipya kutoka kwa E.J.Waggoner.
Sura hii ni sura ya mwisho kwenye kitabu chake cha Agano la milele
(Everlasting Covenant). Katika sura hii waggoner anajaribu kutanua
uelewa wetu kuhusu agano jipya kwa kueleza kuwa, agano la sinai sio
tu lilikuwa ni agano la kwanza kuthibitishwa kwa damu, na Agano la
Ibrahimu japokuwa lilikuwa la kwanza kuanzishwa likawa agano la pili
kwasababu lilikuwa linasubiri damu ya Yesu pale msalabani, lakini pia
Agano la sinai ndio pia lilikuwa ni agano la kwanza kufanywa na
nyumba yote ya Israeli.
Waggoner anaamini kuwa kama jinsi Mungu alivyokusanya Israeli ya
kale ndivyo atakavyokusanya Israeli ijayo. Mungu atakusanya watu
wake ambao ndio Israeli kama jinsi ilivyoelezwa katika ufunuo wa
yohana sura ya 7. Na baada ya kuwakusanya watu wake ambao ndio
taifa lake Israeli katika siku ya ufufuo na pale ambapo waovu
watakapoangamizwa, Katika siku ambayo Mungu atafanya kila kitu
kipya, ndipo Mungu atafanya agano na Israeli, taifa lake, taifa la wote
waliomkubali Kristo kama ni Bwana wao, agano Jipya. Waggoner
anaamini kuwa agano jipya bado halijafanywa kwa maana bado Israeli
ijayo haijakusanywa pamoja kama taifa, lakini agano la Ibrahimu halina
tofauti na agano jipya kwa maana halina chochote zaidi ya agano jipya.
Hivyo japokuwa agano jipya halijafanywa bado katika uhalisia wake,
yoyote aliyekatika agano la Ibrahimu, ni kama yupo katika agano jipya,
kwa maana atakuwa miongoni wa watu ambao Mungu atafanya nao
agano jipya. Kwa maelezo zaidi endelea kusoma Sura inayofata.
56
KUKAMILIKA KWA AGANO LA MILELE
Na,
E.J.WAGGONER
Matendo 15
18 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele
Matendo 3
20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na
uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. 21 Kwa maana tangu
zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji
husomwa kila sabato katika masinagogi
Matendo 10
43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila
amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.
Kazi ya mwisho ya kukusanya watu wa Mungu na kusimama kwao
katika dunia mpya, imekuwa ndio somo la manabii tokea anguko na
wote wamekuwa mashahidi kuwa wote walio ndani ya Kristo watapata
ondoleo la dhambi, kwa vile ni kwa kupitia tu ondoleo la dhambi ndipo
kukusanywa na marejesho yanaweza kufanyika. Tuangalie vitu
vichache katika unabii unaozungumzia vitu hivi, na vitasimama kama
viwakilishi kwa vitu vingine. Tuangalie kwanza sura ya kumi na moja
ya kitabu cha Isaya
Isaya 11
1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka
katika mizizi yake litazaa matunda. 2 Na roho ya Bwana atakaa juu
yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya
maarifa na ya kumcha Bwana; 3 na furaha yake itakuwa katika
kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa
57
macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio
yake; 4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya
wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya
kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. 5 Na
haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.
(Linganisha na 2Thess.2:8)
6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala
pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono
watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. 7 Ng'ombe na dubu
watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula
majani kama ng'ombe. 8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la
nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.
9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote
mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji
yanavyoifunika bahari.
Hapa tunamchanganuo wa historia ya injili, ikiwamo na kuondolewa
kwa dhambi na wadhambi na kusimamishwa kwa watakatifu katika
dunia iliyoumbwa upya, wakati ambapo “wenye upole watairithi nchi,
Watajifurahisha kwa wingi wa amani” (Zaburi 37:11)
Kama vile alivyotupa simulizi, ambayo tayari tumekwisha isoma, nabii
anaendelea mbele kutupa ujumbe zaidi. Tukirudi pale alipoanzia,
anaendelea—
Isaya 11
10 Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara
kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na
mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu. 11 Na itakuwa katika
siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu
wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka
Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na
kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. 12 Naye atawatwekea
mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa,
atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za
dunia.
58
Kwa kuwakusanya watakatifu kutoka pande nne za dunia, tunasoma pia
katika Mathayo 24:31. Nguvu ambayo itakayotumika kukusanya huku
itakuwa ni sawa na ile ambayo Bwana aliitumia kukusanya katika
mkono watu wake kwa mara ya kwanza, Tunasoma:
Isaya 11
16 Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki,
watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile
waliyotoka katika nchi ya Misri
Kuhusu kukusanya, mwanzo na mwisho tunasoma pia katika sura ya
arobaini ya isaya. Kuhubiri injili inahusu pia kusamehewa dhambi,
kumtoa msaidizi, Roho mtakatifu, kumuweka Mungu kama ndio nguvu
pekee katika ulimwengu, Muumbaji na mtetezi, na kutangaza kuhusu
ujio wa Bwana katika utukufu, yote yanapatiana humo. Hivyo ujumbe
ni
Isaya 40
10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake
ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara
yake i mbele zake. 11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji,
Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani
mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
Hapo mwanzo tulisoma kuhusu kukusanya kondoo waliopotea wa
nyumba ya Israeli katika zizi moja ili kuwe na “Zizi moja na Mchungaji
mmoja” hapa tunaona kukusanya kunaanza na kuhubiri injili, na
inakamilika pale ambapo Bwana anakuja katika utukufu, akiwa na
malaika zake, na zaidi ni kwamba nguvu na utukufu ya ujio wa Bwana
ni sawa nguvu iliyopo katika kuhubiri injili.
Katika mistari inayofata tunasoma hali ya kondoo waliopotea wa
nyumba ya israel, na jinsi wachungaji wasiokuwa waaminifu
walivyowatawanya badala ya kuwakusanya—
Ezekieli 34
2 Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii,
uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole
wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi
59
wachungaji kuwalisha kondoo? 3 Mnawala walionona, mnajivika
manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. 4
Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi,
wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha
waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na
kwa ukali mmewatawala. 5 Nao wakatawanyika, kwa sababu
hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyama- mwitu,
wakatawanyika. 6 Kondoo zangu walitanga-tanga katika milima yote,
na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu ya
uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala
kuwatafuta. 7 Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; 8 Kama
mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu
walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu
wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu
hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe
wala hawakuwalisha kondoo zangu; 9 kwa sababu hiyo, enyi
wachungaji, lisikieni neno la Bwana; 10 Bwana MUNGU asema hivi;
Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo zangu
mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo;
nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo
zangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. 11 Maana, Bwana
MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi,
nitawatafuta kondoo zangu, na kuwaulizia. 12 Kama vile mchungaji
atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake
waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami
nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya
mawingu na giza. 13 Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na
kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao
wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji
ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu.
“23 Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam,
mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji
wao. 24 Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu,
Daudi, atakuwa mkuu kati yao; mimi, Bwana, nimesema haya. 25 Nami
nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali
kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni. 26 Nami
60
nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa
baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako
manyunyu ya baraka. 27 Na mti wa kondeni utazaa matunda yake,
nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao;
nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya
kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale
waliowatumikisha. 28 Hawatakuwa mateka ya makafiri tena, wala
mnyama wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana
mtu atakayewatia hofu.
Jinsi kazi ya kukusanya itakavyofanyika tunaambiwa vizuri katika sura
ya 37
Ezekieli 37
1 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika
roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa
mifupa; 2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa
na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu
sana. 3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami
nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. 4 Akaniambia tena, Toa
unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno
la Bwana. 5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya;
Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. 6 Nami nitatia
mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika
ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa
mimi ndimi Bwana. 7 Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata
nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama,
tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa
mwenziwe. 8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake,
nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo
pumzi ndani yake. 9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo,
mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo,
kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa,
wapate kuishi. 10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi
ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.
11 Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya
Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu
61
yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa. 12 Basi tabiri, uwaambie,
Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na
kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami
nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. 13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi
ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi
katika makaburi yenu, enyi watu wangu. 14 Nami nitatia roho yangu
ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi
mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema
Bwana.
Hivyo tunaona kuwa ahadi ya Bwana kwa Daudi ni kwamba ataandaa
mahali kwaajili ya watu wake Israeli, na kuwaweka ili kwamba wakae
katika sehemu zao wenyewe na wasiondoke tena na wasiteseke tena
(2sam.7:10), litatimia katika ufufuo wa wafu. Kukusanya Israeli, watu
pekee walioahidiwa, inajumuisha watu wote wa zama zote, kwa maana
Bwana anaponena, “Wote walio katika makaburi watasikia sauti yake
na kutoka”
Tunaona kuwa kukusanya huku ni kwa “nyumba nzima ya Israeli”
mstari unaofuata unaonesha kuwa katika muda huo hakutakuwa na
mgawanyo wa falme, bali “zizi moja na mchungaji mmoja”
Ezekieli 37
15 Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 16 Na wewe mwanadamu,
twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa
Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa
Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake; 17
ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe
kimoja katika mkono wako. 18 Na wana wa watu wangu
watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonyesha maana ya mambo
hayo utendayo? 19 Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama,
nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila
za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na
kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja
mkononi mwangu. 20 Navyo vijiti, ambavyo uliandika juu yake,
vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao. 21 Ukawaambie,
Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka
kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na
62
kuwaleta katika nchi yao wenyewe; 22 nami nitawafanya kuwa taifa
moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja
atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili,
wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele. 23 Wala
hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao
vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na
kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani
yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa
Mungu wao. 24 Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao,
nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika
hukumu zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda. 25 Nao watakaa
katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi wangu, walimokaa baba zenu;
nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao,
milele; na Daudi, mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao milele.
Sasa angalia kile kinachofuata
26 Tena nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la
milele pamoja nao; nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu
pangu nitapaweka katikati yao milele. 27 Tena maskani yangu itakuwa
pamoja nao; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
28 Na mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, mimi niwatakasaye
Israeli, patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao milele
Ni pale ambapo mji mtakatifu utakaposhuka kutoka kwa Mungu kutoka
mbinguni, ndipo sauti ikasikika ikisema “ Maskani ya Mungu ni
pamoja na wanadamu na ataishi kati yao na Mungu mwenyewe
atakuwapamoja nao na kuwa Mungu wao” (Ufunuo 21:2,9)
..............
Katika uhusianisho huu, hatuwezi kuwa katika hali ya kusita kuwa ni
wakati gani ambao unamaanishwa hapa, ni wakati wa kuadhibiwa kwa
waovu na kupewa ujira wale waliowanyenyekevu; muda ambao watu
wa Mungu wataokolewa milele kutoka katika uovu na katika
manyanyaso, na kusimamishwa katika nchi, na kuitawala katika zama
zote katika amani na katika haki. Wakati tukiongelea kuhusu muda huo,
unabii unaendelea,
63
Yeremia 31
Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na
nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile
nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili
kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja,
ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo
nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana;
Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami
nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 34 Wala
hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake,
wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye
mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema
Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka
tena. 35 Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati
wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku,
aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi,
ndilo jina lake; 36 Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema
Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu
milele. 37 Bwana asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na
misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa
Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda,
asema Bwana
Hili ni hitimisho la kila kitu. Kwa kufanya agano jipya, siku za
uhamishoni na mateka yote yameisha, na watu wa Mungu wanaishi
katika uwepo wake usioisha milele. Agano hilo linasubiri lifanywe,
lakini kwa imani iliyohai baraka zake zinafurahiwa hata sasa, hata
nguvu ya ufufuo, ambayo katika hiyo watu wa Mungu
watasimamishwa katika nchi yao, ni nguvu ambayo iliwaandaa kwaajili
ya siku hiyo yenye utukufu.
Katika somo hili la ahadi kwa Israeli tumeona kwanini na kwa
mazingira yapi agano la kale lilifanywa, pale Israeli waliposimama
chini ya Mlima sinai.Hili linaitwa agano la “kwanza” au “agano la
kale”, sio kwamba kulikuwa hakuna agano kabla yake, lakini ni
kwasababu lilikuwa ni agano la kwanza “lililofanywa na nyumba ya
Israeli na nyumba ya yuda”—Lilifanywa na nyumba yote ya Israeli.
64
Agano la Ibrahimu lilikuwepo zaidi ya miaka mia nne kabla, na
lilikuwa na kila kitu ambacho Mungu angeweza kumpa mtu. Ni kwa
kupitia hilo agano la Ibrahimu, lililothibitishwa na kiapo cha Mungu,
ndipo sasa tunakuja kwa kujiamini katika kiti cha rehema na kupata
upatanisho wa makosa yetu (Waebrania 6:13-20). Watu wote wenye
imani ni watoto wa Ibrahimu.
Lakini Israeli ya kale walikuwa sio waaminifu na walisahau au
walipuuzia agano la milele lilifanywa na Ibrahimu. Walitaka kutembea
kwa kuona na sio kwa imani. Walijiamini wao wenyewe badala ya
Mungu. Na katika jaribio, ambapo Mungu aliwakumbusha agano lake
na Ibrahimu kama msaada ili waamini katika nguvu ya ahadi yake,
aliwakumbusha yale ambayo alikwisha kuwafanyia lakini walichukua
jukumu kuhusu wokovu wao wenyewe, na wakaingia katika agano
ambalo halikuwa lingine lolote ila utumwa na kifo kikifuata. Mungu
ambaye ni mwaminifu, japokuwa wanadamu hawamuamini, alitumia
hili kama mfano wa kijifunzia. Katika kivuli wajifunze uhalisia, hata
utumwa wao ulikuwa na unabii na ahadi ya uhuru.
Mungu hawezi kuwaacha watu wake sehemu ambayo ujinga wao ndio
uliowapeleka. Hivyo akaahidi agano jipya. Sio kwamba kuna kitu
chochote kinacho pungua katika agano alilofanya na Ibrahimu, lakini
kwamba afanye agano hilo hilo na nyumba yote ya Israeli, kama taifa.
Hii ahadi ya agano jipya bado inauzuri, kwa maana kwa kiapo cha
Mungu na kwa kafara yake Yesu alifanywa kuwa ni “uhakika wa agano
bora” Angalia neno “hakika.” Wanadamu hawahitaji kuwa na uhakika
wa vitu ambavyo tayari wanavimiliki. Kwa vile kristo ni “Hakika ya
agano bora” inaonesha kuwa agano hilo litakuja. Sisi ni watoto wa
Mungu kwa imani katika Kristo Yesu, na kama niwa kristo, hivyo sisi
ni mzao wa Ibrahimu, na warithi wa ahadi. Tunaenda kwa Yesu
kwasababu ya agano alilofanya na Ibrahimu. Hilo ndio tegemeo letu
kubwa la kukimbilia kwa Yesu kwaajili ya hifadhi. Hakuna mtu
“aliyekatika agano jipya”, kwa maana hilo bado halijafanywa, lakini
kila mtu anayetunza agano la Mungu na Ibrahimu atakuwa miongoni
mwa hao ambao agano litafanywa. Kwa yoyote ambaye atakuwa
mkristo kama Ibrahimu alivyokuwa, atakuwa na uhakika kuwepo
katika agano jipya kama vile tayari amefufuliwa kutoka katika wafu,
Israeli yote itakusanywa na agano jipya, agano la milele litafanywa
65
pamoja nao—taifa takatifu linaloshika ukweli. Agano halitafanywa na
mwingine yoyote isipokuwa Israeli, lakini mtu yoyote asiachwe, yoyote
anayetaka anaweza kuja.
Pale ambapo agano la kwanza lilipofanywa na Israeli. Mungu alikuja
na malaika zake wote; na tarumbeta za Mungu zilipigwa, na sauti yake
ilitikisa dunia wakati Sheria inatamkwa. Hivyo agano Jipya
litakapofanywa, Israeli yote itakuwepo—hakutakuwa na yoyote
ambaye hatakusanywa—na “Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza”
(zaburi 50:3) “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda
ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza”( 1Thess
4:16) katika utukufu wa Baba yake “pamoja na malaika zake”
(Mathayo 24:27) Sauti yake itaitikisa dunia lakini katika muda huu
hautaitikisa Dunia pekee lakini hata Mbingu pia. Kwa hiyo, ulimwengu
mzima utahusika, na Israeli itaungana na “familia yote ya Mbinguni”
kwa msalaba wa Yesu, “Damu ya agano la milele” kwa hii, kiti cha
ufalme cha Mungu kimethibitishwa, na kile kilichowaokoa waliopotea
wa duniani ndio kinga ya milele ya viumbe ambao hakuanguka. Wakati
agano la kwanza linafanywa na Israeli, sheria ilitangazwa. “Sheria ya
kutisha” ilikuwa mbele yao.Hivyo wakati Mungu anakuja na malaika
zake wote, kufanya agano jipya na nyumba yote ya Israeli, “mbingu
zitatangaza haki yake” (Zaburi 50:6). “Moto hutangulia mbele zake,
Nao huwateketeza watesi wake pande zote.Umeme wake uliuangaza
ulimwengu, Nchi ikaona ikatetemeka. Milima iliyeyuka kama nta
mbele za Bwana, Mbele za Bwana wa dunia yote.Mbingu zimetangaza
haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake.” (Zaburi 97:3-6)
Somo moja ambalo linaweza kutolewa tunapomaliza ni kwamba agano
jipya halileti chochote kipya, isipokuwa dunia mpya, na hiyo ndivyo
ilivyokuwa mwanzo. Watu ambao agano limefanywa tayari watakuwa
wamefanywa upya katika Kristo. Utawala wa kwanza utarudishwa.
Mtu yoyote asitoe kisingizio cha kutoshika amri za Mungu kwa kusema
kuwa yupo chini ya agano jipya. Kama yupo ndani ya Kristo, basi yupo
katika (sio chini) agano la Ibrahimu, na kama mtoto wa Ibrahimu, ni
mrithi pamoja na Kristo, atatumaini katika agano jipya ambalo Kristo
ni mjumbe. Yoyote ambaye hakubali kuwa yupo katika kizazi cha
Ibrahimu, Isaka, na Yakobo na katika ushirika na Musa, Daudi na
66
manabii, hawana sehemu katika tumaini la agano Jipya. Na yoyote
anayefurahi katika ahadi za agano jipya, baraka ambazo hata sasa Roho
mtakatifu anafanya ziwe halisi, inabidi akumbuke kuwa ni kwa kupitia
agano jipya, sheria za Mungu zinawekwa katika mioyo yetu. Agano la
Kale halikumleta mtu yoyote katika kuitii sheria hiyo, lakini agano
jipya inaifanya iwe ya ulimwengu, ili kwamba dunia ijae maarifa ya
Bwana, kama jinsi maji yanavyojaza bahari.
Ndipo “Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo
Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zak.14:9). Na watu
“yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga;
vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika” (Isaya
33:20)
Agano la amani litaondoa wanyama waovu katika nchi, kwa maana
simba atakula majani kama n’gombe, na mbweha atacheza na ndama
mtoto na “nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni” (Eze.
34:25) kwa maana “Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa
katika shamba lizaalo sana. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao
ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima” (Isaya 32: 16-17) Na
zaidi ya yote, tutakuwa na Bwana na tutamuona uso.Hivyo sasa na
hata milele, Shukrani ziende kwa Mungu, kwa zawadi yake
isiyoelezeka. Katika yeye na kupitia yeye na kwa yeye vitu vyote
vimtukuze milele. Amen.
top related