annuur 1031

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1031 SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Sensa ya Watu na Makazi 26 Agosti 2012: Serikali yalikoroga dakika za majeruhi Ni Sensa ya liwalo na liwe-Ponda Serikali, Waislamu bado ngoma nzito kesho Waazimia kukaa Itiqaf Misikitini. Bukoba wasema… Serikali isipate tabu itangaze waje wenyewe jela MCHUNGAJI amekasirika. Anahoji maamuzi yetu Wazanzibari kupitia Waziri wetu wa KATIBA na SHERIA, na WAZIRI wa Utamaduni Utalii na Michezo. Anataka ufutwe na utokemezwe kwa mbali ule ustaarabu wa Wazanzibari wa kuheshimu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Anafoka na kuhoji ni kwa nini ni marufuku kutembea nusu uchi, kula chakula hadharani, kuvuta sigara na kupigana mabusu ovyo barabarani, unywaji wa pombe Wachungaji ni kero Muungano Zanzibar Wanataka waingie Barazani Chukwani… Wakatoe hoja kuzika ustaarabu wa Kiislam Kama ndio gharama ya muungano, hatulipi kiholela kwa kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhani! Kuvunjika Muungano ni Jambo la hatari. Lakini Zanzibar kumezwa na kupoteza uwezo wa kujiamulia mambo yake kitaifa na kimataifa na kupotea katika ramani ya dunia, ni Jambo la hatari zaidi. Ni nani anaeridhia kuona mamlaka ya familia yake yanamilikiwa na ndugu yake alie jirani? Hiyo ni kashfa! Haikubaliki. (Soma Uk. 7) Mh. Waziri Mkuu hii nyumba ni yetu sote Kudhani Kelele za mpangaji…ni kujidanganya Sana mnachelewesha tu muda wa kulipuka bomu Tutahaha kutafuta mchawi wakati mchawi serikali WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda SHEIKH Alhad Mussa www.tawheedtz.org Unakuhimiza ufanye Ibada ya Hijja 2012 Fanyeni Haraka Kuhiji. Maana Hajui Mmoja Wenu Kitakachomtokea – Ibn Abbas Mkabala na Msikiti wa Makonde, Kariakoo, Dar es Salaam 022 2182068; 0776 070770; 0719 689528 Mtandao wa Tawheed WAISLAMU Mjini Arusha wakiwa katika swala ya pamoja ya Eid iliyofanyika Msikiti Mkuu Arusha Jumapili iliyopita. Mratibu azuiya Waislamu kuswali Idd Umati wakusanyika Polisi Tanga Wawatoa Masheikh waliokamatwa Kwa Waziri Mkuu Pinda futari yadoda Waislam kukaa Itqaf siku saba za sensa - Uk. 3

Upload: annurtanzania

Post on 18-Apr-2015

584 views

Category:

Documents


6 download

DESCRIPTION

Sensa ya Watu na Makazi 26 Agosti 2012: Serikali yalikoroga dakika za majeruhiNi Sensa ya liwalo na liwe-PondaSerikali, Waislamu bado ngoma nzito keshoWaazimia kukaa Itiqaf Misikitini. Bukoba wasema…Serikali isipate tabu itangaze waje wenyewe jela

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1031

ISSN 0856 - 3861 Na. 1031 SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Sensa ya Watu na Makazi 26 Agosti 2012:

Serikali yalikoroga dakika za majeruhi

Ni Sensa ya liwalo na liwe-PondaSerikali, Waislamu bado ngoma nzito keshoWaazimia kukaa Itiqaf Misikitini. Bukoba wasema…Serikali isipate tabu itangaze waje wenyewe jela

MCHUNGAJI amekasirika. A n a h o j i m a a m u z i y e t u Wazanzibari kupitia Waziri wetu wa KATIBA na SHERIA, na WAZIRI wa Utamaduni Utalii na Michezo.

A n a t a k a u f u t w e n a utokemezwe kwa mbali ule ustaarabu wa Wazanzibari wa kuheshimu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Anafoka na kuhoji ni kwa nini ni marufuku kutembea nusu uchi, kula chakula hadharani, kuvuta sigara na kupigana mabusu ovyo barabarani, unywaji wa pombe

Wachungaji ni kero Muungano Zanzibar

Wanataka waingie Barazani Chukwani…Wakatoe hoja kuzika ustaarabu wa KiislamKama ndio gharama ya muungano, hatulipi

kiholela kwa kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhani!

Kuvunjika Muungano ni Jambo la hatari. Lakini Zanzibar kumezwa na kupoteza uwezo wa kujiamulia mambo yake kitaifa na kimataifa na kupotea katika ramani ya dunia, ni Jambo la hatari zaidi.

Ni nani anaeridhia kuona mamlaka ya famil ia yake yanamilikiwa na ndugu yake alie jirani?

Hiyo ni kashfa! Haikubaliki. (Soma Uk. 7)

Mh. Waziri Mkuu hii nyumba ni yetu sote

Kudhani Kelele za mpangaji…ni kujidanganyaSana mnachelewesha tu muda wa kulipuka bomuTutahaha kutafuta mchawi wakati mchawi serikali

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda SHEIKH Alhad Mussa

www.tawheedtz.orgUnakuhimiza ufanye Ibada ya Hijja 2012Fanyeni Haraka Kuhiji. Maana Hajui Mmoja Wenu Kitakachomtokea – Ibn AbbasMkabala na Msikit i wa Makonde, Kariakoo, Dar es Salaam022 2182068; 0776 070770; 0719 689528

Mtandao wa Tawheed

WAISLAMU Mjini Arusha wakiwa katika swala ya pamoja ya Eid iliyofanyika Msikiti Mkuu Arusha Jumapili iliyopita.

Mratibu azuiya Waislamu kuswali IddUmati wakusanyika Polisi TangaWawatoa Masheikh waliokamatwaKwa Waziri Mkuu Pinda futari yadoda

Waislam kukaa Itqaf siku saba za sensa - Uk. 3

Page 2: ANNUUR 1031

2 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari

ULE mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa swaumu, mwez i w a t o b a , u m e p i t a . Waislamu kote duniani wamehitimisha nguzo hii ya nne ya Uislamu kwa kusherehekea Sikukuu ya Eid Fitr mwishoni mwa wiki.

Wakat i Ramadhani ikiondoka, tunaamini kuwa Waislamu watakuwa wameiva baada ya kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja ya ucha Mungu.

M w e n y e z i M u n g u ameeleza katika Qur’an, “ E n y i m l i o a m i n i i m e l a z i m i s h w a k w e n u f u n g a k a m a ilivyolazimishwa kwa wale ambao waliopita kabla yenu ili mpate ucha Mungu.” (Baqara: 183).

Hivyo tunataraji kwamba Umma wa Kiislamu kwa darsa lililopatikana ndani ya Ramadhani, utaendelea kumcha Mwenyezi Mungu kwa usah ih i na kwa taqwa zaidi hata katika miezi mingine iliyosalia. Na hili hasa ndio lengo l a R a m a d h a n i k w a Waislamu.

Wakati wa Ramadhani, b i l a y a s h a k a s o t e tulishuhudia jinsi misikiti ilivyokuwa ikijaa waumini katika muda wa swala.

Q u r ’ a n i T u k u f u ilikuwa ikisomwa kwa wingi Misikitini na hata majumbani, hali kadhalika na tasbihi, ibada za Tahajud, tarawehe, witir, kukesha usiku wa Lailatul Kadir nk. Ilimradi kilikuwa kipindi cha ibada zaidi.

Hofu yetu ni iwapo u m m a w a K i i s l a m u utadumu katika kumcha Mungu kama ilivyokuwa katika Ramadhani. Kuna hatari kwamba baada ya Waislamu kukamilisha Ramadhani, mambo yote mema na mazuri yataishia

Waliokuwa wakiabudu Ramadhani imeondoka

hapo. Ramadhani inaweza kuondoka na ucha Mungu wake.

U m e f i k a m u d a w a kuacha mazoea haya ya kuabudu Ramadhani badala ya Mwenyezi Mungu (sw). Kweli Ramadhani imekwisha hadi mwakani, lakini tuliyekuwa tunafunga na kuswali kwa ajili yake yu hai milele, hamaliziki na wala haishi kama ilivyokwisha Ramadhani.

Badala ya Muislamu kuharibu funga yake kwa kuasi baada ya Ramadhani, ni vyema akafungamana na marejeo ya mkufunzi Ramadhani (reference) ili kujiepusha na hasara kubwa inayoweza kupatikana.

Kufunga sita katika mfungo Mosi inaweza kuwa msaada mkubwa w a k u t o h a r i b u y a l e tuliyojifunza ndani ya Ramadhani na itamsaidia muumini kuzoea kudumu k a t i k a i b a d a s i k u zinazofuata.

K a m a M u i s l a m u kaweza kufunga mwezi mzima, ni aibu na fedheha kwamba Muislamu huyu atashindwa kulinda yale aliyokuwa akiyafanya ndani ya Ramadhani na kurejea kwenye uchafu aliokuwa akiishi nao kabla ya Ramadhani.

Tulilo na uhakika nalo sote ni kwamba, Muislamu atakayeshindwa kulinda ucha Mungu alioupata ndani ya Ramadhani kwa kuendelea nao katika muda unaoendelea, huyo ndiye aliyeshindwa vibaya kabisa katika mafunzo ya Chuo Kikuu Cha Ucha-Mungu, R a m a d a n i . A t a k u w a ameambulia sifuri.

M w e n y e z i M u n g u atuwezeshe tudumu katika ucha Mungu na kuujengea heshima Uislamu hapa ulimwenguni. Amiin.

Serikali yalikoroga dakika za majeruhiI K I WA n d i o s i k u y a sensa imewadia , bado hali si shwari Waislamu wakibaki na msimamo wa kutokuhesabiwa.

Katika kukabiliana na hali hiyo, kumekuwa na kamatakamata wakiandamwa w a l e w a n a o t u h u m i w a kusambaza v ipeperushi vinavyowakataza Waislamu kuhesabiwa au kuwashawishi kwa namna yoyote.

Habar i ku toa mikoa , wilaya na vijiji mbalimbali, zinaonyesha kuwa badala ya serikali kutafuta namna ya kutuliza mambo, imekuwa ikichukua hatua ambazo z inawafanya ha ta wale Waislamu ambao walikuwa hawana msimamo juu ya ususiaji huo, sasa waungane na wenzao.

Habar i kutoka Tanga zinafahamisha kuwa jana umati mkubwa wa Waislamu ulifurika katika kituo cha Polisi Chumbageni kujua hatma ya Masheikh waliokuwa wamekamatwa wakidaiwa kuhamasisha watu kususia sensa.

Waliokamatwa walikuwa ni Sheikh Chambuso, Ustadh H a m a d Ay o u b , F a d h i l Chambo, Hussein Idd na Mwalimu Kassim Amar.

“Mfumokristo upo kazini, Sheikh Chambuso na Mwalimu Kassim Amar wamekamatwa kwa kuwaeleza Waislamu wa Tanga vijijini dhulma iliyopo nchini dhidi ya Waislamu. Wameshikiliwa katika kituo cha Polisi Mtandikeni, Duga Maforoni toka jana usiku wa saa tatu. Waislamu simameni kuwahami Askari hawa wa Allah, Makamanda wa Mtume (s.a.w). Fikisha ujumbe huu kwa nduguzo Waislamu.”

Ujumbe huu wa maneno ulioanza kusambaa jana saa nne usiku, ndio uliowavuta mamia ya Waislamu jijini Tanga leo asubuhi baada ya kupata taarifa kuwa Masheikh hao walikuwa wameletwa Chumbageni.

Hadi tukienda mitamboni, Masheikh hao walikuwa wameachiwa na kusindikizwa kwa maandamano hadi Masjid Qubah ambapo Waislamu walikariri msimamo wao wa kususia sensa.

K a t i k a m a e l e z o y a o w a l i s e m a k u w a walimfahamisha wazi Mkuu wa Kituo cha Polisi kuwa si kweli kuwa serikali haina dini, bali dini ni ya serikali ipo na ndiyo hiyo ya watu ambao wao ndio wenye kusikilizwa, huku Waislamu

Na Mwandishi Wetu

wakipuuzwa, kubaguliwa na kudharauliwa.

Kwa mtindo huo ndio maana Waislamu wameona serikali iendelee na hao inaowathamini katika zoezi hili la sensa.

Kwa upande wa Wilayani Same, habari zinafahamisha kuwa Mratibu wa Sensa aliye katika kituo cha Kisiwani ‘amelikoroga’ baada ya kuwakosesha Walimu kuswali swala ya Idd.

Habari zinasema kuwa ilitolewa maelekezo kuwa hakuna cha kuswali Idd, bali semina kwa walimu wal iopangwa kuhesabu w a t u i t a e n d e l e a k a m a kawaida wakati swala ya Idd inaendelea.

Hata baada ya Walimu Waislamu kulalamika, bado Mratibu alisisitiza hakuna cha kuswali Idd.

Habari zilizokuwa zimevuja zilisema kuwa huo ulikuwa mkakati uliowekwa toka Wilayani kuwa wakikosa kuja katika semina hiyo iwe sababu ya kuondolewa.

Walimu hao walifika na kwa mshangao, Mratibu alipoita majina na kuona Waislamu wapo akasema hakuna semina watu warudi nyumbani wakale Idd.

Hata hivyo, wakati huo swala ilikuwa ishamalizika watu wanarejea kutoka misikitini.

Mpasha haba r i we tu anafahamisha kuwa walimu Waislamu walikuja juu na wakataka kuwa maadhali wamekoseshwa swala, basi semina iendelee.

Tukio hilo limewafanya Waislamu wengi kuona kuwa kuna njama dhidi ya Waislamu na hivi sasa gumzo ni jinsi idadi kubwa ya Walimu Waislamu mjini Same walioomba kuwa wahesabuji walivyoachwa na kuchukuliwa Wakristo watupu.

Kwa upande mwingine inafahamishwa kuwa hali si shwari Sumbawanga ambapo futari iliyoandaliwa na Mkuu

wa Mkoa il idoda baada kususiwa na Waislamu.

Tukio hilo lilitanguliwa na lile la futari iliyoandaliwa na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) 16 Agosti, 2012 ambapo baada ya watu kumaliza maakuli, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi alisimama na kuzungumza lakini akabaki akishangaa baada ya kujikuta akiachwa pweke baada ya kundi la Waislamu kunyanyuka na kuondoka mara tu alipoanza kuzungumzia sensa.

Habari za tukio hilo la Waislamu kugomea Sensa mbele ya Mkuu wa Wilaya na RAS katika hafla ya mwaliko wa futari, zilisambaa kwa kasi na kuwa mada ya Khutba za Ijumaa takribani kwa Misikiti yote Sumbawanga mjini msisitizo ukiwa Waislamu kukataa kuhesabiwa.

Khatibu wa Ijumaa Msikiti wa Qibla ta in , Abdi l lah Salim Kanazawa, alielekeza Waislamu nini umuhimu wa Shura na nini madhara ya kupinga Shura.

Baadhi ya Maimamu a k i w e m o I m a m R a j a b waliwasisitiza Waislamu kuwa kinachohitajika ni umoja na kupigania haki na heshima ya Uislamu na Waislamu.

Katika kuhakikisha wapo pamoja na wanasaidiana kwa lolote litakalotokea, kumetolewa namba za simu kwamba mahali popote mtu atakapobughudhiwa kwa kukataa kuhesabiwa apige ili ipigwe Adhana katika Misikiti mbalimbali Waislamu wakusanyike na kuamua la kufanya.

Ilikuwa ni baada ya tukio hilo Mkuu wa Mkoa naye akaandaa futari katika jitihada za kupoza mambo.

Hata hivyo pamoja na kuandaliwa watu wa TV na magazeti, futari ilidoda baada ya Waalikwa Waislamu walio wengi kususia kwa kujua kuwa agenda itakuwa sensa. Futari hiyo ilifanyika Agosti 18, 2012.

Katika tukio jingine kutoka Sumbawanga Mjini, mtoto mmoja wa chini ya miaka 10 aliwaacha hoi wahesabuji waliokuwa katika zoezi la majaribio baada ya kukataa kuhesabiwa na kusema kuwa akihesabiwa atakuwa kafiri.

“ B a b a k a s e m a s i s i Waislamu hatuhesabiwi! Baba kasema ambaye atahesabiwa atakuwa kafiri.”

Al i sema mto to huyo a l iyekutwa akiwa peke nyumbani na kutimua mbio akiwacha maofisa wa sensa wakishangaa.

WAZIRI Mkuu Pinda

Page 3: ANNUUR 1031

3 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Habari

Ni Sensa ya liwalo na liwe-PondaITAKUWA ni sensa ya liwalo na liwe, baada ya serikali kugoma kusikiliza madai ya waislamu.

Hiyo ni Kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda wakati akisoma risala ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu katika Baraza la Idd.

Ponda amesema kuwa, bado wanaishauri Serikali kuakhirisha Sensa mpaka mwakani ili iweze kufanya Sensa ya Kitaifa badala ya kufanya Sensa ya ‘Liwalo na lilwe’.

Kwa upande mwingine, kwa wanaokataa sensa msimamo umekuwa kuwa kama ni kuwafunga, serikali i s i p a t e t a b u , i t a n g a z e watakuja wenyewe katika vituo vya Polisi na magereza kama itaona kwa busara zake kuwa hiyo ndiyo stahiki ya wasiotaka kuhesabiwa.

Wa m e y a s e m a h a y o baadhi ya Waislamu kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiitaka Serikali kuacha kutumia vitisho kuhusu suala la Sensa ya watu na makazi na badala yake kujenga tabia ya kuwasikiliza Waislamu kama inavyofanya kwa maaskofu.

Katika tamko lililotolewa wakati wa sherehe za Baraza la Idd ambalo liliandaliwa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania na kufanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu limesisitiza kuwa Waislamu hawatashiriki zoezi hilo la Sensa na kwamba siku ya Sensa Waislamu wanatakiwa kubaki Misikitini katika Ibada ya Itiqaaf na hata ikiwa watafungwa jela watakuwa tayari , kul iko kukubali kuhesabiwa.

Akisoma tamko hilo mbele ya umati mkubwa wa Waislamu waliohudhuria s h e r e h e h i z o , S h e i k h Ponda Issa Ponda alisema ingawa Serikali kupitia vyombo vyake vya habari imeendeleza propaganda za kuwa wamekubaliana na Waislamu juu ya kushiriki Sensa, ukweli ni kwamba hawajakubaliana popote juu ya hilo.

K u h u s u t a a r i f a zilizochapishwa magazetini za Mkurugenzi wa TBC1 kuwaomba radhi Waislamu kwa kutoa takwimu za uwongo zinazowahujumu, na hiyo ndiyo kuwa sababu ya wao kuachana na madai yao, Sheikh Ponda alisema TBC1 ni kama mtoto, na hivyo malalamiko yao yalikuwa ni kwa Serikali inayomiliki chombo hicho cha habari.

“Madai ya mapendekezo

Na Bakari Mwakangwale

ya Waislamu kuhusu namna ya kuzuia hujuma katika Sensa ya watu na makazi hayakuelekezwa kwa wale w a l i o g h u s h i t a k w i m u (TBC1) na wenzake, bali ni kwa Serikali kupitia Idara ya Takwimu ya Taifa”, alisema.

A k a s e m a k u f u a t i a taarifa hizo zinazodaiwa kusambazwa kwamba eti muafaka baina ya Serikali na Waislamu umekwishapatikana na kwamba sasa Waislamu watashiriki Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kuanza Agosti 26, 2012, bado msimamo wa Waislamu wa kutoshiriki uko palepale.

“Tunatamka kuwa, pamoja na propaganda za TBC1 kuomba radhi na vitisho vya Serikali, msimamo wa Waislamu wa kutoshiriki zoezi la Sensa Agost 26, 2012 upo palepale”, lilisema tamko hilo la Waislamu lenye kurasa tatu.

Katika hatua nyingine mwandishi wa habari hizi alishuhudia mwamko wa umati huo wa Waislamu wa kususia zoezi hilo la Sensa kwa kugombania vipeperushi vilivyoandikwa kwa herufi kubwa kuwa, “NYUMBA HII NI YA WAISLAMU, H AT U A N D I K I S H W I

SENSA”.Mbali ya suala la Sensa

ya watu na makazi, jambo jingine ambalo lilivuta hisia za Waislamu mkutanoni hapo ni lile linalohusiana na mchakato wa maoni juu ya Katiba mpya ambayo ilihudhurishwa na Sheikh Kondo Juma Bungo.

Katika mkutano huo, Sheikh Bungo alisisitiza umuhimu wa Wais lamu kushir ik i vema katika kuhakikisha wanawasilisha maoni yao k u h u s i a n a n a m a s u a l a mbalimbali yanayowagusa.

“Katiba ndiyo sheria mama ambayo inaelekeza namna viongozi watakavyoongoza na

raia wanavyotakiwa kufuata sheria hizo. Sasa kanuni mojawapo ya sheria duniani kote ni kwamba haiwezi kufanya kazi mahala ambapo sheria zilizopo zinakinzana na sheria hiyo”, alisema huku akitoa mifano kadhaa kutoka kwenye Qur’an na Sunnah.

Habari kutoka Bukoba zinasema kuwa serikali imetakiwa kutokupata tabu kusambaza Polisi kukamata Muislamu mmoja mmoja, bali iseme wale wote wasiotaka kuhesabiwa waje jela gani na Waislamu watafika.

Maoni hayo yametolewa na Masheikh na Maimamu mbalimbali baada ya kutokea hali ya kusumbuliwa kwa baadhi ya viongozi wa K i i s l a m u w a k i d a i w a kuhamasisha waumini wao kukataa sensa.

WAISLAMU wametakiwa kufurika misikitini kwa ajili ya ibada ya Itiqaf na Dua kuanzia usiku wa Jumamosi ya Agosti 25 siku ya sensa na kufunga swaumu siku tatu kuanzia tarehe hiyo kumuomba Allah juu ya kadhia inazowakabili hivi sasa.

Wito huo umetolewa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu jana Agosti 24, 2012.

“ N d u g u Wa i s l a m u , tumuogope Allah na kamwe tusiogope vitisho. Sote kwa pamoja tutekeleze maazimio haya ili historia ituandike kuwa tulipigania haki za Waislamu Tanzania”. Ilieleza taarifa ya Jumuia hiyo.

Akizungumza katika kikao kilichoandaliwa na Jumuia hiyo na kuhudhuriwa na Maimamu kutoka misikiti mbalimbali ya jijini Dar es Salaam, kilichofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya TAMPRO Magomeni Mapipa jana, Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema Mashe ikh wa Jumuia na Taasisi 63 nchini kwa pamoja wamekubaliana Waislamu nchini kutekeleza ibada hizo kufuatia kitendo cha serikali kwa makusudi kupuuza madai ya Waislamu.

Ponda amesema hakuna

Waislam kukaa Itqaf siku saba za sensaWatafunga siku tatu, kusoma Kunuti Mufti, RC wapata wakati mgumu SongeaDC, Madiwani, Waziri Malima hoi Mkuranga

Na Shaaban Rajab, Bakari Mwakangale

kiongozi wa Jumuia na Taasisi ya Kiislamu aliyewahi kuhubiri kuwa sensa ni haramu, bali wametoa sababu zao za msingi za kususia zoezi hilo ambazo wamezieleza na kuzifafanua vizuri, ila serikali inapotosha kwa makusudi.

Akasema, Viongozi wa Jumuiya wametaja baadhi ya madai ya Waislamu kuwa ni suala la wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita kufelishwa kwa makusudi na Baraza la Mitihani la Taifa na hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.

Tukio j ingine ambao limepuuzwa ni Waislamu kuletewa Kadhi asiye na nguvu za kisheria.

Taarifa ya Jumuia hiyo imeeleza kuwa Waislamu wanataka Kadhi aliyeteuliwa na Jumuia zote za Kiislamu na ambaye anatambuliwa na Katiba ya nchi.

Suala la tatu limetajwa kuwa ni sensa ya watu na makazi ambapo Waislamu wanataka kiwepo kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa ili kujua idadi kamili ya watu na dini zao, lengo likiwa ni kuondoa takwimu potofu zinazoendelea kutumiwa na serikali na taasisi zisizo za kiserikali kwa maslahi yao na kwa hasara ya Uislamu.

Aidha, Waislamu kwa muda mrefu wametaka serikali kujiunga na Jumuia ya Kiuchumi ya Kiislamu ya OIC, lakini licha ya serikali yenyewe kukiri kuwa hakuna athar i mbaya kwa nchi kujiunga na jumuia hiyo, bado haitaki kwa sababu Maaskofu

hawataki.Al isema, inas iki t i sha

k w a m b a h a t a w a s o m i walishiriki kupotosha suala hili katika jitihada za kuzima hoja ya Waislamu kuitaka serikali kujinga na OIC.

Akakumbusha kuwa Prof. Mwesiga Baregu aliwahi kutetea hatua ya serikali kuz ima uwezekano wa kujiunga na Jumuia hiyo pale aliponukuliwa akisema kuwa moja ya kanuni na masharti ya OIC ya kujiunga mwanachama mpya, ni lazima mwanachama huyo (nchi) iwe na idadi kubwa ya Waislamu, kinyume na hapo mwanachama huyo atakuwa hajakidhi kigezo cha kujiunga na jumuia hiyo.

Alisema, umefika wakati Waislamu wa Tanzania kuwa na msimamo na kushikamana pamoja katika masuala ya msingi yanayohusu maslahi ya Waislamu na Uislamu.

“ N d u g u W a i s l a m u tumuogope Allah na kamwe tusiogope vitisho. Sote kwa pamoja tutekeleze maazimio haya ili historia ituandike kuwa tulipigania haki za Waislamu Tanzania, usiku wa terehe 25 kuamkia 26 Agosti sote tuelekee katika misikiti ya jirani kwa ajili ya ibada za itiqaf na kunut. Kwa pamoja tutekeleze maazimio haya ili historia idhihiri”, ilisema sehemu ya azimio hilo la Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini.

Aidha imefahamishwa kuwa Mufti wa Bakwata

Issa Shaaban Simba akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa w a R u v u m a B w. S a i d Kalembo, wametahayari mjini Songea pale Waislamu walipowahakikishia kwamba wao hawahesabiwi.

Mufti Simba amekuwa Songea akishirikiana na Mkuu wa mkoa kuhamasisha Waislamu kushiriki katika sensa.

Wakati Mufti na baadhi ya Masheikh wa Bakwata wakifanya ziara za mikoani k u s h i n i k i z a Wa i s l a m u k u s h i r i k i s e n s a , h u k o Mkuranga wamedhihirisha h a d h a r a n i k w a m b a hawatoshiriki zoezi hilo.

Hayo yamejir i kat ika mkutano uliohudhuriwa na Madiwani pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Bw. Adam Malima, ambao walihamasisha Waislamu kushiriki zoezi la sensa na kukemea vipeperushi vilivyokuwa vikielezea sababu za Waislamu kugomea sensa hiyo.

Tukio hilo lilikuja baada ya Ust. Abdulswamad kutoka Baraza Kuu kupewa nafasi ya kuhutubia katika mkutano huo huku wageni wengine wakidhani kuwa anatoka BAKWATA baada ya kusikia kuwa anatoka Baraza Kuu.

Ust. Abdulswamad baada ya kupata nafasi hiyo alibainisha kuwa yeye ni miongoni mwa walioandaa kipeperushi hicho na kuwataka Waislamu kupima yale waliyoelezwa katika kipeperushi na yale waliyoelezwa na mawakala wa serikali kujua ukweli.

Hata baaada ya kutoa nasaha zake Waislamu walisisitiza kwamba hawatashiriki zoezi la sensa mbele ya mawakala hao wa serikali.

Page 4: ANNUUR 1031

4 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Habari

TOKA jana Alhamisi, Waislamu jijini Arusha wapo katika swaumu hadi kesho Jumamosi wakiomba subra kwa Allah katika kukamilisha msimamo wao wa kususia sensa.

Aidha, imefahamika kuwa waumini wa Mkoa huo watakuwa kat ika ibada ya Itiqaaf ambayo itafanyika katika Misikiti yote usiku wa Jumamosi kuamkia sensa.

Habari zilizopatikana jana kutoka jijini Arusha zinafahamisha kuwa katika kuandaa It iqaaf hiyo, mipango inafanywa kupata ng’ombe 7 na mbuzi saba kwa ajili ya chakula kwa Waislamu watakaojitokeza kukaa Itqaaf katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa.

H a b a r i k a m a h i z o z imetangazwa pia na baadhi ya vyombo vya habari ambapo imehimizwa kuwa Waislamu wafunge siku tatu kuanzia jana kisha kufanya Itiqaaf na kuleta Dua maalum.

Wa k a t i h u o h u o , I m a m u w a M s i k i t i Mkuu, Sheikh Hambali amewataka Wais lamu kuendelea kupinga dhulma wanazofanyiwa wanafunzi wa Kiislamu na Baraza la Mitihani Tanzania.

Hanbal anasema dhulma

Mashirika ya Kiislamu yaungana kuwasaidia Waislamu Myanmar

Arusha wapo katika fungaMsikiti Mkuu Bondeni kuchinja ng’ombe 7Dr. Ndalichako hajaachwa kutajwa

Na Mwandishi Wetu.

hii wanafanyiwa watoto wa Kiislamu si kwa sababu nyingine, bali ni kule kusema kwao hapana Mola apasaye kuwabudiwa kwa

haki ila Allah.Akasema, jambo la

kusikitisha na kushangaza ni kuwa badala ya serikali kuchunguza na kutoa

majibu juu ya madai ya Waislamu, Waziri husika analisifia Baraza hilo ili kuficha uozo na dhulma.

“Hapa kuna maswali

mengi ya kujiuliza juu ya sifa hizo walizopewa Baraza la Mitihani, je sifa walizopewa zimetokana na kazi walizofanya kuwadhulumu wanafunzi wa Kiislamu kwenye mitihani yao? Au kazi waliofanya ya kupuuza malalamiko ya Waislamu kana kwamba hakuna kitu kilichotokea? Au sifa za kufuata maelekezo ya mfumokristo juu y a k u w a d h u l u m u Waislamu?” Amehoji Hanbal.

Akasema, kuajiriwa mchungaji kwa ajili ya kul inda maslahi y a Wa k i r i s t o n a kuwadhulumu wanafunzi Waislamu, ni uovu, upendeleo na dhulma iliyo wazi, lakini serikali imekaa kimyaa haijali.

Kuhusu Mahkama ya Kadhi, Imam Hanbal amesema kuwa Waislamu b a d o h a w a j a p a t a Mahkama ya Kadhi na kwa hivyo hakuna Kadhi Mkuu.

Akifafanua akasema kuwa kilichofanywa na Mufti wa Bakwata ni kiini macho ambacho kinadhihirisha tu jinsi baraza hilo linavyotumiwa kirahisi kuhujumu haki za Waislamu nchini.

KUALA LUMPARMashirika ya Kiislamu yasiyo ya serikali ya n c h i w a n a c h a m a katika Jumuiya ya ASEAN yameungano kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu wa Myanmar na kutatua matatizo yao.

Shirika la habari la Malays ia Barnama, l i m e r i p o t i k u w a Jumuiya ya Kimataifa ya Ush i r ik i ano wa Kiislamu ya Malaysia (Ikiam) imepewa jukumu la kubuni muundo wa muungano huo.

U a m u z i w a kuanzishwa muungano huo ulichukuliwa katika k ikao cha jumanne iliyopita cha Jumuiya za Kiislamu zisizo za serikali katika nchi za Kusini Mashariki mwa

Asia. Katika kikao hicho

i m e t a j w a l e n g o l a kuanzishwa muungano huo kuwa ni kufanya jitihada za kukomesha mgogoro wa Myanmar na ukatili unaofanyika nchini humo dhidi ya Waislamu katika jimbo la Arakan.

M y a n m a r p i a n i mwanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).

Naye Katibu Mkuu wa

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiis lamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu, ametaka hatua za haraka zichukuliwe kuwafikishia misaada Waislamu wa Myanmar wanaoendelea kuuawa na kunyanyaswa na serikali ya nchi hiyo.

A m e s e m a k u w a wakati sehemu kubwa ya Waislamu wakiwa katika shamrashamra za kusherehekea sikukuu ya Eid el fitr, sehemu nyingine za ulimwengu wa Kiislamu zinakabiliwa

na matatizo mengi. Ameongeza kuwa

Waislamu wa Myanmar w a n a k a b i l i w a n a matatizo yanayokwenda sambamba na vitendo vya mabavu ambavyo vinahatarisha maisha yao katika ardhi zao za jadi.

K w a m s i n g i h u o amewataka Waislamu w o t e u l i m w e n g u n i kujali na kuwazingatia wenzao wanaoteseka h u k o M y a n m a r n a kuwafikishia haraka misaada ya kibinadamu.

Katibu Mkuu huyo wa OIC ameutaka umma wa Kiislamu pia kuwajali ndugu zao wanaopata matatizo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel na kuchukua hatua za dharura kwa lengo la kulinda Quds Tukufu na utambulisho wake wa Kiislamu, vilevile kuilinda kutokana na hujuma ya Mayahudi na Wazayuni.

Ihsanoglu amewataka Waislamu wawaunge mkono Wapales t ina k a t i k a m a p a m b a n o yao dhidi ya utawala wa Israel hadi pale w a t a k a p o f a n i k i w a kuunda nchi huru mji mkuu wake ukiwa ni Quds Tukufu. (IQNA)

WAISLAMU Mjini Arusha wakiwa katika swala ya pamoja ya Eid iliyofanyika Msikiti Mkuu Arusha Jumapili iliyopita.

Page 5: ANNUUR 1031

5 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

RAIS Muhammad Mursi wa Misri amependekeza kuundwa timu maalumu itakayoundwa na nchi za Iran, Misri, Saudi Arabia na Uturuki kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi mgogoro wa Syria.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa pendekezo hilo linaweza kuzua shauku zaidi juu ya mtizamo iwapo pendekezo la Rais Mursi linatekelezeka au la.

Wachambuzi wengine wanasema kuwa, pendekezo h i lo l inaonyesha waz i misimamo ya Rais Mursi ya kutaka kuirejeshea Misri

Mursi ataka Iran, Saudia Uturuki kuisaidia Syria

nafasi yake katika masuala ya ulimwengu wa Kiislamu iliyoipoteza miaka mingi iliyopita, baada ya kutiwa saini mkataba wa Camp David kati ya nchi yake na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Huku hayo yakiripotiwa, jeshi la Syria limeendelea kuyasafisha magenge ya kigaidi katika miji mbalimbali ya nchi hiyo hasa mji wa Halab.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kuwa nchi hiyo haiwezi kupokea wakimbizi zaidi kutoka Syria, hivyo ameutaka Umoja wa Mataifa kutenga eneo

maalumu ndani ya Syria la kuweza kuwahudumia wakimbizi hao.

Hatua hiyo inahesabiwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni njama za Uturuki za kufanikisha lengo lake la kuingiza majeshi ya kigeni ndani ya ardhi ya Syria kwa madai ya kulinda raia.

Naye Walid al Muallim, Waziri wa Mambo ya Syria amesema kuwa ni wananchi wenyewe wa Syria ndio pekee wenye haki ya kuamua waongozwe na serikali gani na amezilaumu baadhi ya nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu kwa kuchochea machafuko na kuongoza uasi ndani ya Syria. (IRIB)

Saudia waandamana dhidi ya UfalmeRIYADHWananchi wa Saudi Arabia wamefanya maandamano katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ikiwa ni ishara ya kupinga serikali kuendelea kukumbatia utawala wa kifalme.

Duru za habari zinaeleza kuwa, wakazi wa mji wa Qatif wamefanya maandamano makubwa wakipinga utawala wa nchi hiyo na kumuunga

mkono Hassam Haddad, mkazi wa Bahrain ambaye aliuawa kwa kupigwa na kujeruhiwa na vikosi vya utawala wa Aal Khalifa vinavyosaidiwa na vikosi vya Saudia.

Wa a n d a m a n a j i h a o wa l i t angaza kuungana na shahidi huyo mkazi wa Bahrain na kusisitiza kuendelea na maandamano yao ya amani hadi matakwa

yao yatakapotekelezwa. Tangu mwezi Februari

mwaka jana, wapinzani wa utawala wa kifalme wa Al Saudi wamekuwa wakifanya mihahara na maandamano katika maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo, wakitaka kufanyiwa marekebisho muundo wa utawala.

Aidha wamekuwa wakitaka kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa na kuwepo usawa.

Botswana yatakiwa kukataa Kuwepo kambi ya Marekani Makundi ya kijamii nchini B o t s w a n a y a m e i t a k a Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuiwekea vikwazo ser ikal i ya Gaborone iwapo itaruhusu Marekani kuanzisha kituo cha kijeshi nchini humo.

Makundi hayo yamesema kuwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Botswana na Marekani yaliyokamilika s iku chache zi l izopita , huenda yakatoa mwanya kwa Washington kuweka kambi ya kijeshi kwa ajili ya Bara la Afrika (AFRICOM)

nchini humo. Jumuiya mbalimbali za

Afr ika ikiwemo SADC kwa muda mrefu sasa zimekuwa zikipinga kambi hiyo kuwekwa barani Afrika hivyo kuilazimisha Marekani kuendelea kuendesha kambi hiyo kutokea Ujerumani.

Wazo la kutaka AFRICOM iwe na makao makuu yake barani Afrika lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2006 na George W. Bush, Rais wa zamani wa Marekani lakini viongozi wa Afrika wakalikataa. (IRIB)

Odinga asema hajakiuka makubaliano na Waislamu MOMBASA Wa z i r i M k u u w a Kenya Raila Odinga, amesema kwamba wale wanaodai kuwa alivunja makubaliano a l i y o t i l i a n a s a i n i na Waislamu kabla ya uchaguzi mkuu uliopita nchini humo, wanamchafulia jina kwani alikuwa katika safu ya mbele kutetea Mahakama za Kadhi wakati wa kampeni za kura ya maoni kuhusu katiba mpya mwaka

2010. Odinga amekumbusha

k u w a v i o n g o z i w a Makanisa na baadhi ya wanasiasa walizunguka nchi nzima wakiwataka wafuasi wao kuikataa katiba mpya kwa madai kwamba inawapendelea Waislamu kwa kuwapa Mahakama za Kadhi.

K i o n g o z i h u y o a m e o n g e z a k u w a aliwashirikisha viongozi kadhaa wa Kiislamu katika serikali akiwemo mbunge maalum, Sheikh

Mohammad Dor. Raila Odinga aliyasema

hayo baada ya kukutana na Wais lamu mj in i Mombasa katika Pwani ya Kenya Jumatatu ya wiki hii ambapo amewataka kumuunga mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Viongozi wa Kiislamu huko nyuma walisema hawatomuunga mkono Bw. Odinga kwa kuwa alikiuka makubaliano aliyotiliana saini na Waislamu mwaka 2007. WAZIRI Mkuu wa Kenya, Raila Odinga

RAIS Muhammad Mursi wa Misri

Page 6: ANNUUR 1031

6 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala/Matangazo

Na Tony Cartalucci

July 14, 2012 - Mtandao wa Kupashana Habari -

KWA uhakika kama hakuna ambacho ‘wanaharakati’ wamesema had i sa sa k u h u s u k i n a c h o i t w a ‘mauaji makubwa’ ya Tremseh, Syria kinaweza kuhakikishwa, haiwezekani “kumlaumu” yeyote kwa vifo vinavyodaiwa kuwa vimetokea. Hata hivyo, mashirika ya habari hodhi kama Associated Press, Reuters, AFP na mengineyo yalikuwa na vichwa vya habari kama “Umoja wa Mataifa walaumu majeshi ya serikali kwa mauaji Syria” (AP), “Serikali ya Syria yalaaniwa kwa mauaji ya Tremseh” (Reuters), “Machafuko Syria: ‘Mauaji’ ya Tremseh” (Guardian), na “Machafuko Syria: Kofi Annan ashtushwa na ‘vitendo vya kutisha’ Tremseh” (BBC).

Picha: Raia wasio na silaha? Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na nje kupitia mtandao wake katika mashirika hodhi ya habari, wanaoitwa “Free Syrian Army” mara nyingi wanaitwa kwa kubadilisha, iwe ni ‘raia’ au ‘wanaharakati.’ Katika hali halisi wana silaha nzito, wanapata misaada mikubwa ya nje na wanao miongoni mwao makundi makubwa ya wapiganaji kutoka nje - wakisali t i jina hilo, la Jeshi Huru ‘la Syria.’ Hata kwa maelezo ya ‘wanaharakati,’ ‘mauaji’ ya hivi karibuni yanaelekea kuwa ni mapigano ambayo wapiganaji hao walipoteza, na wengi kati ya waliokufa ni wapiganaji wenye silaha, na siyo raia.

Na hata chini ya vichwa vya habari danganyifu, vikionyesha jinsi serikali ya Syria ilivyohusika na kile walichoelezea kama ni kitendo cha kinyama cha mauaji ya watu wengi wasio na silaha, kila taarifa i n a k i r i , k w a m a e l e z o yaliyochimbiwa karibu na mwisho, kuwa Tremseh ilikuwa eneo la mapambano

Hillary Clinton anapokuwa Joseph Goebbels wa leoMauaji makubwa ya hivi karibuni ya Syria kama propaganda ya ki-Goebbels

Dai “Umoja wa Mataifa walaumu majeshi ya serikali kwa mauaji mapya nchini Syria,” wakati “si madai ya wanaharakati au video yaliweza kuthibitishwa na watu wengine.”

makali kati ya askari wa ‘Jeshi Huru la Syria’ wenye silaha nzito wanaoungwa mkono na NATO, na majeshi ya Syria. Chini ya vichwa vya habari danganyifu na ukishapita aya kadhaa za kwanza ambazo kwa dhamira zimejazwa propaganda za ki-Goebbels, kile ambacho mashirika ya habari hodhi ya nchi za Magharibi yanaripoti n i ma jesh i ya k iga id i yakishindwa na majeshi ya Syria na mapigano kuendelea kwa sababu tu nchi za Magharibi zinaendelea kutoa fedha, silaha zenye ubora mkubwa, na hata wapiganaji wa nje nchini humo.

BBC ilifikia hata kukiri, na kuning’iniza maelezo mengine ya staili ya Houla (dai la mauaji ya watu wengi), kuwa “

......baadaye, wanaharakati waliliambia shirika la habari la AFP (la Ufaransa) kuwa wapiganaji waasi walikuwa wameshambulia msafara wa magari ya jeshi, lakini w a l i r u d i s h w a n y u m a na kuuawa wakati jeshi liliporudisha mashambulio.

“Katika hali hiyo, licha ya kuwa hatuna uhakika bado wa idadi kamili, raia waliokufa kwa mabomu yaliyorushwa hawakuwa zaidi ya saba,” alisema Jaafar, mwanaharakati wa mtandao wa habari wa Sham unaoipinga serikali.

“Waliobaki walikuwa ni wapiganaji wa Jeshi Huru la Syria,” alikiri.

H i v y o , l i c h a y a wanaharakati wenyewe kukiri kuwa walishambulia majeshi ya Syria kwanza na halafu wakapoteza mapambano y a l i y o f u a t i a , a m b a y o inaelekea yaliwasukuma hadi kwenye kambi yao ya mapambano huko Tremseh, vyombo vya habari vya Magharibi viliamua kuipa haiba ya mauaji ya kunuia dhidi ya raia, kama gazeti la Guardian lilivyosema, “yaliyopangwa kwa wakati unaofaa ili kuwapa pumzi washirika wa kijeshi wa Assad na kuvunja juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa,” likimnukuu mjumbe wa “Baraza la Kitaifa la Syria”

linaloungwa mkono kwa uwazi na nchi za Magharibi.

L a b d a a l i y e t i a f o r a katika ujuha huu alikuwa si mwingine ila Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ambaye alidai kuwa “maelezo kuhusu mashambulizi katika kijiji cha Tremseh, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mizinga, vifaru na helikopta, yanadhihirisha bila utata serikali hiyo imefanya mauaji ya raia kwa kudhamiria.” Clinton, bila kuzuiwa na kipengere k u w a a n a z u n g u m z i a ‘maelezo’ na siyo “ushahidi uliohakikishwa,” anadai kuwa tukio hilo, lililoelezwa hata na waasi kuwa ni mapigano makali kati ya majeshi ya Syria na wapiganaji wa FSA, ilikuwa ni mauaji ya kudhamiria ya raia.

Clinton anajaribu kutafuta kuungwa mkono katika nchi mbalimbali kuhusu kushindwa kwa washirika wake wa kigaidi wanaopewa fedha, silaha na kuwekwa mbele kama FSA. FSA inaundwa na wapiganaji wa kukodiwa kutoka Libya, wengine ndiyo wametoka kuua askari wa Marekani na Uingereza huko Irak na sasa wanatumia mbinu zao za kupiga mabomu dhidi ya watu wa Syria, na wanachama wa kundi la Muslim Brotherhood la Syria ambao walianza kutafutwa mwaka 2007 na Marekani chini ya utawala wa George W. Bush, kuanza kuunda mkondo wa mapigano kuweza kuipindua serikali ya Syria.

Hawa ni wapiganaji ambao walikutana na kamanda wa kundi la Libyan Islamic Fighting Group (LIFG) Abdul Hakim Behaj, na kupata kutoka kwake silaha, fedha na wapiganaji licha ya kuwa hata hivi leo LIFG imeorodheshwa na wizara ya Hillary Clinton ya Mambo ya Nje kama shirika la nje la kigaidi, hivyo kufanya upelekaji fedha na kuungwa mkono kwa FSA kuwe ni kuvunja sheria za Marekani yenyewe dhidi ya ugaidi.

Lengo ambalo Clinton anatumai kulifikia ni kupitisha kwa sokomoko azimio la

hivi karibuni la Umoja wa Mataifa linaloungwa mkono na Marekani na Uingereza kupitia Baraza la Usalama, kwa kuziaibisha Russia na China kwa kuitetea Syria kuhusu uha l i fu ambao haikuwahi kuutenda. Ujanja ni kuisukuma propaganda kabla ukweli wa kilichotokea Tremseh haujaibuka.

Hatari kwa amani duniani

Ni kweli kuna hatari kubwa kwa amani duniani. Siyo majeshi ya ulinzi ya Syria yanayojaribu kurudisha amani kwa walio wengi kati ya watu wa nchi hiyo ambao hawashiriki katika mapigano na hujuma inayofadhiliwa kutoka nje. Ni nchi za Magharibi. hasa serikali na mashirika makubwa ya biashara na fedha ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Saudia, Qatar na washirika wao siyo tu kuendesha kampeni ya udanganyifu wa kudhamiria kuvuruga watu wanachohisi, lakini kwa uwazi wanatoa silaha, fedha na uungwaji mkono kisiasa kwa magaidi a m b a o k w a m u o n g o wote uliopita wamekuwa w a k i w a t a k a w a n a n c h i wao kujitolea mhanga na kuthamini kupigana katika kile kilichoitwa “Vita dhidi ya Ugaidi.”

Kama ambavyo wengine wamesema na kurudia, siyo kwamba watu wa Syria, au watu wengine kokote duniani hawahitaji jema zaidi katika maisha, ni uhalisi kuwa mapigano yanayoendelea Syria kwa uhakika hayatafikia jema zaidi. Ni udanganyifu unaoendeshwa na mataifa ya kigeni yanayotafuta uhodhi katika eneo hilo kwa kujificha nyuma ya ukasuku wa ‘haki za binadamu,’ ‘uhuru’ na ‘demokrasia.’ Ni udanganyifu uliopangwa ambao unagharimu maelfu ya maisha katika kila upande, na kama ilivyoonekana Libya, utaiacha nchi imevunjika, imegawanyika, hohehahe na ikiwa tegemezi kwa hisani za makampuni ya biashara na fedha ya nchi za Magharibi.

Picha: Kielelezo makini ka t ika Makumusho ya Shoa mjini Washington DC. Rais Obama ametumia makumbusho hayo kuweka jukwaa la kuendeleza uhalifu dhidi ya binadamu wa Wall Street na London (maskani ya mabenki makubwa duniani). Wanafunzi wa historia hata hivyo wataelewa kuwa wafuasi wa Hitler, Nazi hawakuanza mauaji ya halaiki na udhibiti wa dunia nzima, lakini walikuwa waigizaji washamba waliohamasika na kile ambacho Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton

Page 7: ANNUUR 1031

7 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

KIMAUMBILE hakuna binadamu anaezaliwa na wazo, bali wazo ni zao la matukio, hivyo ni uhakika kwamba udhaifu wa mfumo wa muungano tulionao ambao umekosolewa na wataalam mbali mbali wa kisheria na kisiasa, ndio tukio ambalo ni msingi mkuu wa kuzaliwa kwa “KERO”, na kwa hilo ndio likawa ni sababu ya kupatikana kwa chanzo na kichocheo cha chimbuko la kuzaliwa kwa WAZO LA KIZAZI KIPYA.

Kwa kukosa s i fa za kujitosheleza kwa uadilifu na kujaa mapungufu makubwa ya kisheria pamoja na kukosa misingi ya uwezo imara wa kuweka sawa haki za Zanzibar ndani ya muungano huo, huku ikionekana Tanganyika i k imi l i k i na ku t awa la nguvu kubwa za mamlaka ya kiutawala na kuiweka Zanzinzibar katika kona ya malalamiko ya “WIMBO” maarufu wa “KERO” za Muungano.

Hivyo kadiri ya wingi wa matukio yanavyoibuka na kutokea katika jamii ya Wazanzibari ndivyo kwa upande wa pili kunavyoibua wazo kuwa Muungano wenyewe ndio “KERO” hivyo msingi wa kutaka m a b a d i l i k o u k a j i k i t a kutokana na hayo, itambulike kuwa kwa namna yoyote ya kulidhibiti au kulizuia wazo hilo lisitekelezeke ndivyo unavyolijengea uimara kwa kushamiri kwa wazo hilo, ambapo kadiri unapolijengea uimara wazo hilo ndivyo unavyolikuza kwa kulijengea uwezo wa hoja na ujazo wa nguvu kubwa za mripuko.

U k w e l i u t a b a k i n a kudumu kwamba kila kitu ni lazima kinahitaji haki yake, jambo hilo huenda na kujitokeza kwa wakati tofauti kwa mujibu wa mahitaji ya wakati unavyojieleza au unaokusudiwa, itakua ni kutenda kosa na dhambi kubwa ambayo mawili hayo yanaweza kutuadhibu katika kila maeneo muhimu ya nchi hizi mbili, endapo tutafanya juhudi za makusudi na mbinu tofauti za kuepuka kutoa haki kwa jamii inayolazimika kuipata haki hiyo, kwa mujibu wa mahitaji ya wakati tulionao na matakwa ya kizazi cha sasa.

U m e f i k a w a k a t i w a kulazimika kutekeleza wazo jipya la mfumo wa muungano kwa sababu wakati wenyewe unalazimisha kufanya hivyo, kwakua hivyo ndivyo ilivyo haki ya wakati, ni jambo la

Wazo la Kizazi kipya:

Kuruhusu kupotea Zanzibar ni dhambi kubwa

Na Suleiman Kindy

lazima upatikanaji wake, kwa kuepuka kutokutekeleza na kulazimika huko hakutokua na sababu ya kuepuka kwa kupata wazo la ziada ambalo litakwenda mbali zaidi ya hapo, kwa sababu huo ndio mwenendo wa tabia za kimaumile ya mwanadam, na huo utakuwa ndiyo mwanzo wa muendelezo wa historia isiyo na tija kwa kizazi cha Wazanzibari wa sasa, kwasababu hakuna binadamu atakaelazimishwa au kulazimika kwa kudumu k u f u a t a m w e n e n d o uliobuniwa na binadamu tena uliojaa mapungufu na kasoro kubwa, kwa kisingizio cha kufuata i t ikadi au sera za CHAMA fulani, au venginevyo kuwepo kwa dhamira nyengine iliyofichikana au kuwepo kwa mapungufu katika chanzo na uwezo wa kufikiri katika wazo hilo, pia hutoweza kuepuka kulazimika kuwaza hivyo kwasababu ya chanzo cha kutakiwa muendelezo wa wazo hilo lililokosa kutoa muelekeo wa ufumbuzi wa kudumu kwa kupatiwa majibu na utatuzi sahihi wa KERO iliyotuganda kwa miaka 48.

Tunapenda ifahamike na kueleweka kwamba maslahi ya Zanzibar kwanza, Vyama vya siasa baadae, hiyo ndiyo

busara pekee iliyo sahihi.

DHANA ILIYOGANDISHWAH a l i t o k u a j a m b o l a

ajabu ikiwa kutatokea baadhi ya Wazanzibari au Watanganyika wachache ambao hawatopendelea kuiona Zanzibar ikiwa na mamlaka kamili ya serikali kuwa na uwezo wa kujiamulia mambo yake yote ya kitaifa na kimataifa bila ya kuingiliwa na mamlaka nyengine, yaani (sovereignty)

“THE POWER OF A COUNTRY TO CONTROL ITS OWN GOVERNMENT,” lakini itakuwa ni jambo la kushangaza na kushtusha sana ikiwa hawatoweza kujiweka hadharani kwa kujieleza na kujenga hoja kwa kile wanachoamini katika wazo lao, ili jamii ikaelewa ubora wa wazo hilo, kwakutokutenda hilo hakutokua na sababu i t a y o o n d o a s h a k a y a k u t o k u a m a n i k w a m b a wana lengo na dhamira ya kuendelea na tabia ya kutamani kuwa, muasisi wa chama fulani ni lazima apewe upendeleo, kisha kulazimika kufuata misingi ya kale ya Chama kushika hatamu, ambapo jambo hilo ndio

lilitoa mchango mkubwa kwa kuidumaza Zanzibar katika zama ziliopita kwa kuifikisha katika jikwaa la wimbo wa “KERO” za muungano.

Muungano imara kifo cha Zanzibar

Ni ukweli utakaokuwa ni ajabu katika maajabu ya dunia kwamba, eti kutokana na umuhimu wa muungano basi ni bora Zanzibar ikose MAMLAKA ya kujiamulia mambo yake yote kitaifa na kimataifa kwa kisingizio cha kudumisha na kutetea kuendelezwa kwa mfumo huo wa muungano ambao kila kukicha uimara wake unakuwa bora zaidi iwapo tu Zanzibar itakuwa inavizwa nguvu zake taratibu na huku Tanganyika ikijitwalia nguvu za kisheria kwa kumiliki mambo muhimu yaliyomo ndani ya Zanzibar kwa kuyavuta ndani ya Muungano kwa kuyatolea maamuzi bila ya kujali kuwa Wazanzibari wanafaidika au wanaathirika kwa kiasi gani, ilimradi tu sheria ikishatamka kuwa jambo hilo ni la Muungano, basi kwa Mzanzibari itakuwa ni haramu kwake kujadili, kuhoji au kutokukubaliana na sheria hiyo!

Kuvunjika Muungano ni Jambo la hatari, lakini Zanz iba r kumezwa na kupoteza uwezo wa kujiamulia mambo yake kitaifa na kimataifa na kupotea katika ramani ya dunia ni Jambo la HATARI ZAIDI ieleweke hivyo, ni nani anaeridhia kuona mamlaka ya familia yake yanamilikiwa na ndugu yake alie jirani? Hiyo ni sawa na kashfa! HAIKUBALIKI.

Hivyo dhana hiyo inakosa ladha ya matumaini kwa kizazi cha leo, kwa sababu kwa kufuata dhana hiyo ni sawa na kumtaka mtu atembee kizani wakati kuna njia yenye mwanga wa kutosha, je itawezekanaje kuamini kuwa AKILI i l iyobuni mfumo TATIZO halafu iwe na uwezo wa kutatua TATIZO kwa kutumia mbinu ileile iliyozaa TATIZO? Hapo ndipo utapopata mwanga wa kutambua kuwa TATIZO linaweza kuzaa ziada ya TATIZO ikiwa tutaendelea kuiamini AKILI iliyozaa TATIZO itutatulie TATIZO! Nadhani dunia ataandika maajabu ya kichekesho hicho cha kuvunja mbavu kwa werevu na wengine wakibaki na mshangao, kinchohitajika ni maamuzi ya wananchi kwa kutumia akili zao juu ya matakwa yao, juu ya nchi yao sio sera au msimamo wa chama fulani, ya kale yatakuwa ni historia, ya sasa yanatakiwa yafanyiwe kazi.

Kwa uchambuzi huo tunapata uhakika wa ufahamu kwamba mabadiliko katika jamii ni jambo la lazima, n i w a z i k u w a n g u v u inayokwenda mbele ni kubwa kuliko nguvu inayotaka kurudi nyuma au kubaki kama ilivyo, kupingana na nguvu hiyo itakuwa ni sawa na kuzusha jambo kubwa lisilikubalika na wakati ndani ya jamii ya wazanzibari inayokusudia kujinasua kutoka ndani ya tundu la mtego wa “KERO” za Muungano.

M S I N G I WA D H A N A YA UBAGUZI

I takuwa ni jambo la mshangao iwapo jamii itakosa ufahamu wa kutambuwa kuwa kichocheo cha UBAGUZI ni UBAGUZI, haitowezekana kwamba uvumil ivu wa j a m i i K U B A G A L I WA imaanishe kwamba hakuna UBAGUZI kwa sababu ya ALIYEBAGULIWA alidumu katika uvumilivu wa KUBAGULIWA, hivyo ni sahihi kufikiri kwamba

Inaendelea Uk. 13

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheikh (wa pili kutoka kulia) akiwa na Makamu wa Rais Seif Sharif Hamad katika sherehe za Eid Mubaraka Zanzibar hivi karibuni.

Page 8: ANNUUR 1031

8 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

Dhambi hii aliyotenda Nyerere haisameheki

Kwa uzito wa kipekee k a b i s a , M w e n y e z i Mungu anasema kuwa kwa hakika hatasamehi dhambi ya shirki. Qur’an inasema:

“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi y a ) k u s h i r i k i s h w a na k i tu , lak in i Yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye . Na anayemshir ikisha M w e n y e z i M u n g u , basi bi la shaka yeye amekwishapotea upotofu ulio mbali (na haki.) (4:116)

Nchi ya Uingereza haina mfumo wa kuwa na Rais Mtendaji kama ilivyo hapa kwetu au japo wa heshma kama ilivyo Ujerumani. Sasa kama asubuhi moja wataamka Waingereza na kusikia Malikia akitangaza kuwa kamteuwa Rais wa Uingereza, watashangaa sana. Si ajabu wakawa na wasiwasi kwamba huenda Malikia wao kapata tatizo kidogo la kiakili. Lakini haitakuwa wepesi hivyo. Kwa sababu wanajua kuwa Kiti cha Malikia pamoja na serikali kuna watu wengi, watashangaa zaidi na kupigwa na bumbuwazi, nini kimejiri maana hata kama Malikia zimemruka kidogo, basi ndio serikali nzima imezubaa isiweze kuchukua hatua mpaka i n a m w a c h a M a l i k i a anageuka kituko mbele ya watu wake na dunia nzima!

Hebu jaaliya siku moja katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku unasikia i n a t a n g a z w a k u w a Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kamteuwa Alex Massawe kuwa ‘Mangi Mkuu’ (Chifu) wa Tanzania. Yakatajwa na majina mengine kuwa watakuwa Machifu wa mikoa.

Nchi h i i i l i shafuta Uchifu. Hakuna mahali popote katiba Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambapo inatajwa kuwa kutakuwa na Mangi Mkuu na ma-Mangi wa mikoa. Kwa hiyo kwa akili tu ya kawaida, wala haihitaji idadi ya vidato au kuhitajia mtu kuwa razini sana, ambacho kingefanyika kwanza ni kubadili katiba. Utaratibu wa Umangi ukaingizwa. Kazi za mangi

Na Omar Msangi

Bakwata ina kipengele cha kuwepo Mahakama ya Kadhi? Jibu ni kuwa hakuna. Mfumo uliopo ni wa kuwa na Masheikh wa Mikoa na Wilaya. Sasa huyu Kadhi Mkuu wa Sheikh Shaabani Simba, anafanya kazi katika utaratibu gani? Mamlaka gani katika katiba ya Bakwata imempa uwezo wa kuteuwa Kadhi Mkuu wa Bakwata?

Pigia mstari na zingatia angalizo hili: Kadhi Mkuu wa Bakwata kama ilivyo kwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Bakwata, Sheikh Shaaban Issa Simba. Walichotaka Waislamu ni Mahakama ya Kadhi Tanzania, sio Mahakama ya Kadhi ndani ya Bakwata.

Uislamu ni Dini ya watu wenye akili. Ndio maana hata imani ya Kiislamu sio ya kuamini kibubusa. Fal yandhur l-insaana minmaa khul iqa . Je , hawatazami chakula chao, hawatazami ngamia jinsi walivyoumbwa? Na milima jinsi ilivyothubutishwa? Na ardhi jinsi ilivyotandazwa? Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi,…na meli zinavyoelea na kutembea baharini ,…na rangi zao na lugha zao, na katika ishara za kuonyesha kuwepo kwake na uwezo wake…afalaa ya ta fakaruun , a fa laa ya’qiluun.

Zote hizi ni baadhi ya aya zinazoonyesha kuwa

suala la kuamini katika Uislamu ni la kutumia akili . Na ndio maana mahali pengine Qur’an imewataja Waumini kwa jina la “wenye akili”.

I n a s e m a : “ H a k i k a kuumbwa kwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonyesha kuwapo kwa Mwenyezi Mungu mmoja) kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa na wakilala. Na hufikiri umbo la mbingu na ardhi (wakasema:) “Mola wetu! Hukuviumba hivi bure. Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu ya moto.” (3:190-191)

Katika jumla ya mambo m a b a y a a l i y o f a n y a Nyerere katika kuuwa Jumuiya na taasisi zao h u r u n a k u w a u n d i a Bakwata, ni hii hali ya kuwafanya wanaoingia ndani ya Bakwata kuweka akili zao kando na kufuata ki la l inaloridhiwa na linalotakiwa na serikali hata kama linawatoa katika ile sifa ya kuwa ‘Ulil-albaab’.

Madhara makubwa yaliyowasibu Waislamu katika nchi hii ni kuwa na watu ndani ya Bakwata ambao ndio wanaosikilizwa na serikali, na si kwa sababu nyingine, ila kwa sababu wanachotizama ni serikali inataka nini, sio kuangalia na kujali masilahi ya Waislamu.

Juzi hapa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa alihoji ni kwa nini Zanzibar watu wanazuiwa kula hadharani mchana wa Ramadhani wakati serikali haina dini. Majibu ya Waziri Mkuu yalikuwa sahihi kabisa. Kwamba amri ile haikuwa ya Jamhuri ya Muungano, bali ya Zanzibar na kwa Zanzibar wao ni zaidi ya asilimia 99 Waislamu. Kwa hiyo kwa mazingira yao amri hiyo ni sawa na wamekuwa wakifanya hivyo miaka yote na hakujakuwa na tatizo.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ni Makatoliki. Lakini pamoja na majibu yake hayo mazuri, Maaskofu wake wa Kikatoliki wametoa tamko la kumpinga. Maadhali wao agenda yao ni kuimarisha Ukristo Zanzibar na wakati

zikaainishwa, sifa zake, atapatikana vipi na mambo mengine kama hayo. Ufupi wa maneno ule mfumo wa Kimangi ungeundwa kwanza ndio akatafutwa Mangi Mkuu na mangi wa mikoa au wa makabila.

N i v i v y o h i v y o tunapokuja katika hili suala la Mahakama ya Kadhi. Awali Mahakama hii ilikuwepo ikijulikana uwepo wake kisheria, kazi zake, sifa za makadhi, namna ya kuwapata na uhusiano wa Mahakama hii na mahakama nyingine nchini. Mahakama ya Kadhi haipo tena ilishafutwa. Sasa leo anaposimama mtu anatangaza kumteuwa Kadhi Mkuu, anamteuwa akafanyie kazi wapi? A n a y e t e u l i w a n a y e anajisikia amepata Ukadhi Mkuu! Hiyo mahakama anayokwenda kufanyia kazi ipo wapi! Imeundwa lini?

Tu n a j u a n d a n i y a Bakwata kuna maafisa wengi ukiacha Makatibu wa Mikoa na Masheikh wao na linaloitwa Jopo la Maulamaa la Kitaifa la Bakwata. Basi nao hili hawakuliona mpaka wanamuacha Mufti wao anakuwa kichekesho?

Mpaka ninapoandika makala hii, katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hazitambui kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi. Sasa huyu Kadhi

Mkuu, ni kadhi wa wapi?Kinachosikitisha na

kuhuzunisha ni kuwa viongozi wa serikali hii, wamekuwa na chuk i (prejudice) iliyopindukia mipaka kiasi kwamba wanafikiri kila ugoro watakaokuja nao utakuwa b a n g i m u j a r a b u l a kuwapumbaza na kuwalaza Waislamu wasipiganie haki zao. Na ndio maana kuna ambao hivi sasa wakiwemo na baadhi ya viongozi wa Makanisa ambao hupita mitaani wakisema kuwa suala la Mahakama ya Kadhi lishapatiwa ufumbuzi, kwa hiyo lisizungumzwe tena na kuletwa katika mjadala huu wa kuchukua maoni juu ya katiba mpya.

Mahakama ya Kadhi hai jaundwa na hivyo hapawezi kuwa na Kadhi Mkuu kabla ya Mahakama yenyewe kuwepo na kwa hiyo agenda hii haijafungwa na Waislamu wataendelea kuzungumza na kudai katika mchakato huu wa kutengeneza katiba mpya. Vinginevyo serikali iseme kuwa haitaki Waislamu washir iki au pengine inataka kufungua mjadala mpya kama ulivyokuwa huu wa sensa na dini.

Ukiacha utaratibu huu wa kiserikali, wapo wanaosema kuwa kilichofanyika ni kulirejesha suala hil i Bakwata. Lakini hata kama ukisema hivyo, swali la kujiuliza ni je, Katiba ya Inaendelea Uk. 11

MWL. Julius K. Nyerere RAIS Jakaya Kikwete WAZIRI Mkuu Pinda

Page 9: ANNUUR 1031

9 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

Mh. Waziri Mkuu hii nyumba ni yetu soteKATIKA kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania…Padiri John Sivalon anasema kuwa, “Viongozi wa Kanisa Katoliki walipewa vibali vya Rais kuingiza vitu kutoka Kenya bila ushuru ingawa mpaka kati ya nchi hizi mbili ulikuwa umefungwa. Maagizo haya ya Mwalimu Nyerere…ama kwa hakika ushirikiano huu uliruhusu viongozi wa Kanisa Katoliki kuwa na nguvu za kiuchumi wakati Taifa likiwa katika hali mbaya”.

Pengine mtu atajiuliza, wakati Mwalimu Nyerere akiwapa upendeleo huu Wakatoliki na akiwaacha wengine wakitaabika kwa njaa katika miaka ya 1970s/80s, alichokuwa akitizama ni Utanzania au Ukatoliki?

Viongozi wetu mnatuambia na tumewasikia mkisema kuwa mnapopanga mipango ya maendeleo hamuangalii dini ya mtu na Mwalimu Nyerere amekuwa kama ‘Mzimu’ wenu mkimsifia kwa uzalendo na kutokuwa mdini.

Je, alipokuwa akiwashibisha na kuwanenepesha Maaskofu bila kujali kabisa kwamba anavunja sheria za nchi alizoziweka yeye mwenyewe na serikali yake, alichokuwa akitizama nini? Tusaidie Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda!

Waswahili wana msemo wao, apewaye ndiye aongezwaye. Kabla ya kufikia mwaka 1965, serikali ilikuwa ikigharamia bajeti ya kuendesha shule na taasisi nyingine za Wakristo kwa asilimia 60. Haya hayasemwi na Sheikh Bassaleh wala Kundecha au hao mnaowaita Waislamu wachache waliotangaza kususia sensa ya idadi ya watu na makazi. Anayesema haya ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Father Robinson. Kama alivyonukuliwa katika vitabu mbalimbali Father Robinson anasema kuwa kufikia mwaka 1965, shule za seminari za Kikr i s to z i l ikuwa “ to ta l dependent on State aid for administration.” Na akaongeza akisema, “if this aid were withdrawn, the church would be forced to close its schools.”

K w a m b a , l a u s e r i k a l i ingesitisha utaratibu wake huu wa kuchota fedha kutoka Hazina ya Taifa na kuwapa Wakatoliki pekee, basi Kanisa lingelazimika kufunga shule zake.

Wa z i r i M k u u w e t u , Mheshimwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, umekariri sana na kurudia kwa juhudi kabisa na maarifa kauli yako kuwa serikali haipangi mambo yake kwa kutizama dini za watu. Swali hapa ni je, katika kuweka mpango huu wa maendeleo katika elimu ambao serikali kwa busara zake inaona ikusanye kodi kutoka kwa Waislamu, Wakristo, Wahindu, Baniani na watambika mizimu na makomunisti, lakini bi la kutangaza hadharani ichukue pesa hizo na kuwapa Wakristo pekee ili kuwaimarisha, ilizingatia jambo gani? Kwamba Wakatoliki ndio wenye nyumba yao Tanzania na Waislamu ni walipa kodi tu ya pango, bali

watafunaji wa kodi ni Wakristo wenye meno?

Kila Waislamu wanapodai k w a m b a k u n a d h u l m a , halikuwa jibu la serikali ila kuwakejeli Waislamu kwamba hawataki kusoma, mara waache kulalamika, mara wasome na dunia sio Akhera tu, bali wakija kwa Wakristo huwapongeza kwa kuisaidia serikali kutoa elimu na

kuahidi kuwaongezea. Labda niulize Mheshimiwa

Waziri Mkuu wetu Pinda, hivi serikali hii inawadhania Waislamu wa Tanzania wana ujinga kilo ngapi?

Toka serikali ilivyokuwa inachukua kodi za Waislamu k inyemela kuwaimar i sha Wakatoliki kama anavyosema F a t h e r R o b i n s o n m p a k a

ikafikia kurasimisha dhulma na upendeleo huo kwa ile MoU ya mwaka 1992, leo mnataka Waislamu waamini kwamba TEC na CCT ndio wanaoisaidia serikali katika kutoa huduma za elimu na afya. Qur’an ina msemo wake, inasema:

“Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawadanganyi

ila nafsi zao; nao hawatambui.” (2:9)

M n a y a s e m a h a y a n a mnapanga kuwadanganya Waislamu ili kuficha ile dhulma mnayowafanyia Waislamu. Mnawapongeza Wakristo ili mpate kuwaongeza. Mwisho m n a w a k e j e l i Wa i s l a m u kwamba hamuwapi kwa sababu walizubaa, hawakuomba wakati wenzao wakiomba!

Hivi ninapoandika maoni yangu haya, Waislamu wana kesi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Pamoja na matatizo ya sasa ya Baraza la Mitihani, Waislamu wameonyesha jinsi majina ya watoto wa Kiislamu waliofaulu kwenda sekondari yalivyokuwa yakikatwa na nafasi zao kupewa watoto wa Kikristo. Kama risala ya Waislamu serikalini juu ya suala hili haijafika mezani kwako, Mheshimiwa Waziri Mkuu, nainukuu tena hapa.

L a b d a M h e s h i m i w a Waziri Mkuu niulize, kwa nini ilianzishwa AMNUT? All Muslim National Union of Tanganyika ilianzishwa ili kupigania haki za Waislamu moja wapo ikiwa ni kupinga dhulma iliyokuwa ikifanywa na mkoloni akichukua kodi kutoka kwa Waislamu, lakini ruzuku kwa ajili ya elimu akiwapa Wakristo pekee.

Ukirejea katika kumbukumbu za Ikulu hutakosa kuona barua ya Mzee Salimu Kiangi aliyomwandikia Mwalimu Nyerere, barua kumbukumbu namna IB/SK/61/1 ya tarehe 13. 8. 1961 akisema, sasa uhuru unakuja isije tena ikawa serikali huru ya Tanganyika ikawadhulumu Waislamu kama alivyokuwa akifanya mkoloni.

““Mheshimiwa mtajika wa sifa Dr. J. K. Nyerere, mimi nikiwa mmoja wapo wa viongozi wa Kiislamu Tanganyika, nimesukumwa na mapenzi kuleta haya yafuatayo mbele yako, ulipofungua Chama cha TANU 1954 ukataja Tanganyika ipate uhuru…ukaahidi Tanganyika itakapokuwa huru, kazi ya kwanza ni kuwapatia Waislamu elimu sawa na madhehebu mengine. Sisi Waislamu kwa uchungu tuliokuwa nao juu ya kuzuiwa kupata el imu tulisimama imara pamoja nawe mheshimiwa mtajika mpaka tumefikia hatua ya mwisho ya kupata uhuru 9. 12. 1961.”

Mzee huyo ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa East Africa Muslim Welfare Society akaendelea k u m k u m b u s h a M w a l i m u akisema, “Serikali inayoondoka ujue shule za sekondari na T.T.C zinazoendeshwa na madhehebu (za Kikristo) ni marufuku kusoma Muislamu hali zapata msaada wa serikali. Katika wanafunzi wanaopata msaada (scholarship) kusoma Amerika, Uingereza n.k. karibu wote ni Wakristo, …kwa nini mambo hufanywa hivi?”

Katika barua hiyo Mzee Salim Kiangi anamwambia Mwalimu Nyerere kuwa, wakati Waislamu walipotaka kuanzisha shule sawa na Wakristo serikali

Ndugu Waziri,Kwa muda mrefu sasa , kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Swali na kitendawili hiki k i m e k u w e p o k w a m u d a mrefu bila kupatiwa majibu. Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.

Akihoj i juu hal i h iyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo. Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja

Risala ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu Kuunda Tume Huru kuchunguza Baraza la Mitihani Tanzania

kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.

Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili? Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.

Mheshimiwa Waziri,Ni wazi kuwa Waziri wa

Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.

Mheshimiwa Waziri, Mwaka 1987 aliyekuwa

Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa

kwenda kidato cha kwanza. Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.

Mheshimiwa Waziri,Hali kama hii hapana shaka

inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.

Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili. Mwaka 1983 mwanafunzi a l iyekuwa ak i i twa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari. Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote. Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni

Inaendelea Uk. 10Inaendelea Uk. 11

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda (kushoto), Joseph Simbakalia (kulia)

Na Omary Msangi

Page 10: ANNUUR 1031

10 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

HIVI karibuni nimebahatika kusoma gazet i la NIPE HABARI la tarehe 27-7-2012 na la tarehe 3-9 August, 2012, magazeti yote mawili mlikuwa mna mahojiano na Mzee Ali Ameir aliyewahi kuwa Mbunge wa Donge siku za nyuma. Kuna mambo mengi sana Mzee huyo aliyaeleza.

Mimi nilivutiwa na baadhi ya maneno yake, moja katika haya yaliyonivutia ni ile kauli alioitoa ndani ya gazeti hilo la tarehe 3-9, August, 2012. Mzee Ali Ameir anasema: “Labda niseme kitu kimoja, siri hasa ya Muungano hivi sasa hakuna anayeijua” Mzee Ali Ameir anayasema maneno haya mwezi wa August, 2012.

Ali Ameir: Mkaazi asiye mzalendo

Na Ibrahim Mohammed Hussein

“Hakuna anayejua”. Kwanza nilicheka sana, nikawaza, nikasema, amma kweli mjini ni shule. Hivi haya Mzee vipi anaweza kubeba dhima ya kusema “hakuna anayejua”. Nilipoendelea kusoma nikaona maneno mengi aliyoyasema nayo ni “Ukweli wa ndani na dhamira ya ndani” wanaijuwa hawa watu wawili. Halafu Bwana huyu amejisifia kwamba yeye ni muandishi. Kama Ali Ameir angalikuwa mfuatiliaji kama vile alivyolifuatil ia Baraza la Wawakilishi na ile semina yao ikamuwezesha kubaini kwamba kuna watu hawaelewi na wanapotosha, na akasema inawezekana wao wenyewe wamepotoshwa. Mzee, kama aliona hivyo kwa upande wake, basi ndio hivyo hivyo kwa wenzake wameona ukweli wa Muungano watu wengi wamepotoshwa ukweli wa matokeo mawili makubwa nchini mwetu: Mapinduzi na Muungano.

Hivyo bwana Muandishi hebu durusu maneno haya aliyoyasema Nyerere, halafu utupe tafsiri ya muono wako.

“Ningalikuwa na uwezo basi ningaliviburuta Visiwa vya Zanzibar na kuvitupa katika Bahari ya Hindi, ningalifanya hivyo.”

Maneno hayo ameyasema

kabla ya Uhuru. Bw. Ali Ameir kweli hakuwahi kuyasikia maneno haya ya Nyerere? Je! hiyo bado haikupi mwanga wakuelewa dhamira ya Nyerere juu ya Visiwa hivi?

Hivyo Al i Ameri hana kumbu kumbu ya barua ya Waafrika /African Association ya 1949 waliomuandikia Balozi wa Kiingereza Zanzibar na kwa Waziri wa Makoloni w a U i n g e r e z a i s e m a y o “Tunasikit ika sana kuona kwamba Serikali imemteuwa MSHIRAZI, Mwasia kwa ajili ya kumtumiliya, baada ya Waafrika wa Zanzibar. Inaeleweka wazi kwamba Mshirazi ni Mwasia katika rekodi ya Serikali ya Zanzibar. Tumeelewa kwamba tunanyimwa haki zetu za Uraia na hili imewabakiza Waafrika katika hali ya kukata tamaa.

Kwa jina la Demokrasi, Ukristo, na usawa wa Binadamu, tunapinga vikali hatua ya Serikali na tunaomba ufikirie na kutizama upya mwenendo huu wa Ubaguzi, ukandamizaji, kunyimwa haki na kunyanyaswa katika nchi yetu”.

Huo ni Ubaguzi uliodhahiri kwa Washirazi. Na kilele chake ni pale walipotaka viongozi waliotokea upande wa African Association na wakalazimisha wazee wetu wote wafute kabila la Shirazi hapa Zanzibar. Mbona

walitaka umoja na wakaunda chama cha Afro-shirazi Party, tena leo iweje muambiwe mfute kabila hilo? Basi Bw. Ali Ameri bado hukujua dhamira ya ndani ya watu hawa ambao tunadai ni ndugu zetu.

Nia ya Mwalimu Nyerere ya kupindua Zanzibar ilidhihirika pale alipokua akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola tarehe 27/2/1963 mwaka mmoja kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar. Alimwambia wazi wazi Sir N. Pritchard, kwamba: “Baada ya Uingereza kuondolewa Tanganyika , Waafrika wa Zanzibar huenda wakauondowa utawala wa Kisultani.”

Hio ndio dhamira ya Nyerere” hiyo ndio mikakati ya Waafrika/African Association au na Washirazi nao walikuwa nayo dhamira hiyo. Basi ikiwa na Shirazi nao waliku nayo dhamira hiyo ndio pale uliposema katika makala ya Nipe Habari kwamba:

“Kila mtu anaweza kua na lengo lake”

Nyerere alikua na lengo lake katika Mapinduzi Karume nae alikua na lengo lake. Babu na yeye alikua na lengo lake. Sijuwi kama na Washirazi nao walikuwa na lengo lao. Kifupi dhamira ni moja ya Mapinduzi, malengo ni tofauti.

Basi Ali Ameir bado hata hivi leo hukuweza kubaini lengo la Mapinguzi na maana ya Muungano huu, ambao Waafrika wanataka uwe hivi hivi ulivyo. Mimi nasema sio kweli ule usemi wake kwamba “hakuna anayejua”.

Mzee Ali Ameir ni miongoni mwa Front liners kundi kubwa lililokua pamoja kupambana na wahafidhina. Kumbe yeye huku nyuma alikua akipekecha wenzake na akipeleka taarifa zao kwingine. Hivi sasa anakiri kwamba Muungano umekuwa na kasoro za hapa na pale. Ameshindwa hata kusaidia kuona kasoro za hapa na pale ni kitu gani. Angalikuwa shupavu Angalisema bila ya woga kama alivyosema Mzee Moyo na Enzi.

E n z i a l i s e m a m a n e n o mafupi sana lakini yalikuwa na mashiko, alisema “hakuna kero za Muungano. Hapa tunataka Sovereignty yetu (mamlaka yetu ya kitaifa).”

Siku zote mimi husema, jamani weee kuna uraiya na uzalendo. Hivi ni vitu tofauti kabisa. Wengi wa viongozi wetu ni raiya ambao wamekosa uzalendo, wao Serikali na Chama ndio msingi wa maisha yao. Hapa ndipo alipo Ali Ameiri.

Mh. Waziri Mkuu hii nyumba ni yetu soteInatoka Uk. 9iliwakatalia. Wakapigania haki hiyo mpaka wakapata ruhusa, lakini kwa sharti wawe na shule mwisho darasa la 4 tu. Juu ya hapo wakaambiwa ni Wakristo pekee wanaruhusiwa. Heri nusu shari kuliko shari kamili. Waislamu wakaanzisha shule zao za darasa la kwanza hadi la nne na wakiziendesha kwa nguvu zao wenyewe huku Wakristo wakikomba fedha (za kodi za Waislamu kutoka) serikalini. Ilipokuja hoja hii kwamba Waislamu hawapewi scholarship kwa sababu hawana e l imu, hawana shule, Mzee Kiangi akahoji na kumtaka Mwalimu Nyerere awategulie Waislamu kitendawili hiki. Anasema:

“Tukitaka turuhusiwe kuendesha shule tunaambiwa serikali haina fedha za kuendesha shule za Waislamu ilihali Wakristo wao wanapewa na mpaka sasa shule za Waislamu huendeshwa kwa nguvu zao, na pamoja na hayo wanazuiwa kufanya hivyo. Mheshimiwa nitashukuru kunitambulia kitendawili hiki kilichotumiwa na serikali itakayoondoka, na kuwa haki za Waislamu zimekuwa zikichukuliwa na nani?”

Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu, hizi kauli kwamba

Waislamu hawapewi kwa sababu hawakuomba zinatoka wapi? Mbona wameomba Mahakama ya Kadhi hamtaki kuwapa! Mbona wameomba OIC mpaka sasa mmegoma. Au walitakiwa waombe kwa “Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu”? Au kabla ya kuomba wasali kwanza Rozari na “Sala ya Maria Mama wa Mungu?”

Na katika hili wenyewe mlisema kuwa baada ya kufanya utafiti mmeridhika kuwa OIC ina masilahi na Taifa wala hakuna tatizo na mpo tayari kujiunga. Lakini mara mlipoitwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo mkageuka. Msimamo wenu sasa ni ule wa Kanisa. Tuambieni, katika suala hili mlichotizama ni masilahi ya nchi au msimamo wa Pengo na Maaskofu wenziwe?

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, kwa nafasi yako una njia nyingi za kuhakikisha kila ninalosema hapa kuwa ni kweli au la. Lile jopo la kuteuwa wanafunzi wa kwenda kidato cha tano likiongozwa na Padiri kama Mwenyekiti ambalo lilificha

majina ya watoto wa Kiislamu waliofaulu wasichaguliwe au lile lililomuuliza Mzee Lila, “wewe mgeni hapa” kwa vile hakukata majina ya watoto wa Kiislamu waliofaulu kama wenzake walivyokuwa wakifanya naye akawajibu “mimi Muislamu”, lilikuwa likiangalia masilahi ya nchi au ya Kanisa? Aliyeteua jopo lile akaweka Wakristo watupu tena na asiamini kuwa kazi ya kuwabamiza watoto wa Kiislamu itafanyika vizuri, akawawekea Mwenyekiti Padiri, alikuwa anaangalia Utanzania au Ukristo?

Haya ameyasema Mzee Bori Lila akiwa hai mpaka akafa, serikali ikapiga kimyaa kama mkakati wa kuzima dhulma hiyo isiwe jambo la kuzungumzwa mitaani na ili ipate kuendelea na sera hiyo ya kuwabamiza Waislamu.

Wais lamu wanasema nchini hapa kuna udini. Kuna dhulma kwa misingi ya dini. Serikali inapendelea. Serikali kwa upande wake inasema hakuna udini. Serikali haifanyi mipango ya maendeleo ya nchi kwa kutizama dini. Na ni kwa hoja hii inasema kuwa

haishughulishwi na idadi ya Waislamu au Wakristo. Na hii imekuwa ndio hoja inasimamia katika kukataa kuweka kipengele cha dini katika sensa.

Katika mpango uleule a l i o z u n g u m z i a F a t h e r Robinson, kila mwaka serikali imekuwa ikitoa mabilioni ya fedha kuimarisha na kuboresha hospitali na zahanati za kanisa huku ikiziacha Mawenzi, Bombo na hospitali nyingine za mikoa na wilaya zikiwa hoi. Ikitokea mgomo wa madaktari au kukosa huduma nzuri katika hospitali hizi ‘zis izo’ na mwenyewe, wananchi hukimbilia hospitali za misheni wakatibiwe kwa ‘Jina la Yesu’. Kanisa linasifiwa serikali inapondwa na kudharaul iwa na la kushangaza hata Maaskofu wanaochotewa fedha kutoka Hazina ya Taifa kuboresha hospitali na shule zao nao wanakuwa mstari wa mbele na wanaharakati kuibamiza serikali!

Mzee mmoja, Afisa Mstaafu wa serikali lakini akiwa na kazi nyingine ambayo watu mitaani wanasema kuwa hakuna kustaafu aliwahi kunukuliwa akionyesha

wasiwasi wake juu ya hatma ya nchi hii. Alichohofia ni vurugu huko mbele ya safari ambayo huenda watu wakaona mwanzo wake tu lakini namna ya kumaliza ikawa tabu.

Af i s a huyo ms t aa fu anasema kuwa zamani angalau vijana wa Kiislamu na wazee wao walikuwa wakionekana katika kada ya udereva, utarishi, ufagiaji na kazi mbalimbali za kada ya chini katika ofisi za serikali na taasisi za umma. Lakini anasema kuwa hata huko sasa hawaonekani. Nini itakuwa hatma ya nchi hii ukiwa na kundi kubwa la vijana wa Kiislamu wasio na ajira rasmi na wasio na uwakilishi serikalini huku wakiona wenzao wakihodhi kila kitu? Alihoji.

“Sioni ila giza nene mbele, kama hazikuchukuliwa hatua za makusudi kubadili hali hii.” Alisema kwa kifupi.

N a m i m i n a s e m a , Mwenyezi Mungu aepushie m b a l i , k a m a s e r i k a l i itakwenda na mtindo wake huu wa kelele za mpangaji: Kwanza ijue kuwa Waislamu sio wapangaji. Hapa ni kwao. Pili, litakapotokewa la kutokea kwa ajili ya dhulma inayofanyika nchini, isije kusikika tena serikali ikihangaika kutafuta mchawi. Mchawi ni serikali.

Page 11: ANNUUR 1031

11 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

Dhambi hii aliyotenda Nyerere haisameheki

Inatoka Uk. 8huo huo kudhoofisha Uislamu, waliona kuwa msimamo wa Waziri Mkuu Pinda ni wa kuimarisha Uislamu. Wamepinga kwa tamko kali.

Sasa njoo kwa Masheikh wetu wa Bakwata. Hoja ya Waislamu ni kuwa na Mahakama ya Kadhi ambayo itakuwa na mmlaka kisheria na nguvu za kusimamia utekelezaji wa maamuzi yake. Mahakama a m b a y o i t a w a n a s u a Waislamu kutokana na zile sheria za kikafiri za ndoa kama ile ya mwaka 1972.

Lakini Serikali haitaki na haitaki kwa sababu maaskofu hawataki. Na maaskofu hawataki kwa sababu wanaona kwamba kuwa na Mahakama ya Kadhi n i kuimar isha Uislamu na kumpa haki Muislamu. Wamepinga na serikali imesimama katika msimamo wa maaskofu. K i n y u m e n a w a l e maaskofu wa Kikatoliki waliompinga Waziri Mkuu, Pinda, muumini mtiifu wa Kanisa lao, Masheikh wa Bakwata wanakuja na kiroja cha kutangaza Kadhi Mkuu asiye na Mahakama ilimuradi tu wauwe agenda ya Mahakama ya Kadhi wanayotaka Waislamu. Wanafanya hivyo kwa lengo gani? Kukidhi matakwa ya serikali na maslaha ya Maaskofu hata kama kufanya hivyo ni kuudhalilisha Uislamu na kujitukanisha wao wenyewe kwa kukubali jambo lisilo na kichwa wala miguu.

Hii ni dhambi ambayo sioni kama kuna namna a m b a y o Wa i s l a m u wanaweza kumsamehe Nyerere kwa kuwaundia ‘dudu’ hili Bakwata. Ila niseme jambo moja: Nyerere ana yake na yalianza kuonekana kutokana na kishindo kilichotokea siku aliyozikwa. Masheikh wa Bakwata nao wana yao.

Katika Vita ya Uhud, baada ya makafiri kuwapiga sana Waislamu mpaka wakamje ruh i Mtume (s.a.w), wapo Waislamu waliojisemea, nini itakuwa hali ya makafiri hawa! Walihisi kuwa hao ni kana kwamba washajihukumu wao wenyewe kukabili adhabu kali ya Allah.

Aya ikaja ikisema kuwa

hao ni waja wa Mwenyezi M u n g u . M w e n y e w e M w a m b a a n a h i y a r i yake, ama awaadhibu au awasamehe.

Sasa hakuna mwenye mamlaka ya kumhukumu m w e n z a k e . H a y o n i m a m l a k a y a A l l a h mwenyewe. Kama Bakwata wanadhani wanayofanya dhidi ya maslaha ya Waislamu na Uislamu ili wapendeze serikalini na kuwafurahisha maaskofu, ni sawa; hukumu yao ipo kwa Allah.

Ila la kuzingatia ni kuwa haitakuwa sababu

mbele ya Allah kwamba walidanganywa au kupewa maelekezo na warithi wa Nyerere mwenye Bakwata yake.

Q u r ’ a n i n a s e m a : “ ( W a k u m b u s h e wakat i ) Wal iofua twa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwisha kuiona adhabu, na yatakatika m a f u n g a m a n o y a o . ” (2:166)

“ Wa t a s e m a w a l e w a l i o f u a t a , “ L a i t i tungeweza kurudi (duniani) t u k a w a k a t a a k a m a wanavyotukataa.” Hivi

ndivyo Mwenyezi Mungu a t a k a v y o w a o n y e s h a vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” (2: 167)

Niseme kwa msisitizo hapa kwamba suala hapa sio kumhukumu mtu. Hoja ya msingi ni kuwa Bakwata mara nyingi wamekuwa wakifanya mambo yaliyo kinyume na masi lahi ya Uislamu. Ukianza na kukubali kutumiwa k u v u n j a E A M W S , kukubali kuvunjwa kwa seminari za Kiislamu, kuzuia usaj i l i taasis i

za Kiislamu wakati wa Nyerere, kuchanwa Qur’an Buzuruga, Masheikh wa Bakwata walivyotumiwa na Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, walivyosimama upande wa wale waliowapiga risasi na kuuwa Waislamu Mwembechai n.k na sasa wanavyohujumu juhudi za Waislamu kurejesha Mahakama ya Kadhi.

Sasa kwa mujibu wa aya hizi , i le kwamba wanatumiwa na serikali au wanapewa maelekezo na serikali, haitakuwa hoja mbele ya Allah. Hao wanaowapa maelekezo serikalini watawaruka siku hiyo.

Wataishia kusema, “Laiti tungeweza kurudi (duniani) tukamkataa Kikwete, Pinda, Wassira na kila aliyehusika kuwapa maelekezo kutoka serikalini.”

TangazoUngana na UWASAKITA katika huduma za jamii, toa mchango kwa kutuma neno UWASAKITA kwenda Namba 15533 Tigo na Zantel.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0715 125455

Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah. Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.

Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.

Hali kama hiyo ilimkuta p i a A d a m R a m a d h a n i aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.

Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.

Mheshimiwa Waziri, Mifano kama hii ni mingi

mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo

Risala ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu Kuunda Tume Huru kuchunguza Baraza la Mitihani Tanzania

Inatoka Uk. 9 Kikuu. Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu y a k i w e k w a p e m b e n i japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.

Mheshimiwa Waziri,Ukiacha hujuma katika

k u w a a c h a w a n a f u n z i Wa i s l a m u w e n y e s i f a kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli. Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu. Na hii ni kwa masomo yote.

Mheshimiwa Waziri,Kumekuwa na utamaduni

katika nchi hii wa kukataa ukweli. Kufuatia uchunguzi u l io fanywa na Kamat i za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.

Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi. Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena

imani na Baraza hilo.Mheshimiwa Waziri,I l ikupa ta ukwel i wa

malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo.

Tu m e h u r u i u n d w e kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani ( NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.

Watendaj i wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.

Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhindi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.

Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu z inaonyesha Maka t ibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.

Mheshimiwa Waziri,

Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote. Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.

Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.

Lakin i kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa. Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.

Ni imani ye tu kuwa u t a y a p o k e a m a d a i y a Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.

Tunaomba kuwasilisha,MwenyekitiBaraza Kuu la Jumuiya

na Taasisi za KiislamuJuni 8, 2012

Page 12: ANNUUR 1031

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie:Mhariri AN-NUUR,

S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe

E-mail: [email protected]

12 AN-NUURMashairi/Barua SHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012

MIGOMO HAINA TIJA1. Kwa jina lake Rabuka, shairi naliandika,Salam zipate fika, kwenu wote wasifikaMlio bara hakika, na visiwani kufikaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

2. Migomo haina tija, ndugu zangu nawambiaPokeeni yangu hoja, wazi nawasimuliaMuone tunavyofuja, neema katika duniaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

3. Mola katupa uzima, siha na nyingi hekimaIli tuweze pima, yaliyo bora kwa ummaTuyatende hima hima, pasi na kurudi nyumaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

4. Asili yake migomo, Mapambano ya wanyongeKudai chao kipimo, cha haki sio mazongeWatwana pia kuwemo, kundini kukosa dongeMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

5. Agomewae katili, hatoi haki kwa ummaHuzidumaza akili, kuwazuia kusemaVibarua na makuli, wasimtie lawmaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

6. Elfu ya tisa mia, kumin na tisa elewaKatika historia, nilipata kusomewaMgomo uliingia, Amerika ukatuwaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

7. Kina mama waligoma, kiwandani Amerika Jijini walinguruma, Newyoki kusikikaKushona kukasimama, mashati yakusifikaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

8. Hawa wote walikua, wahamiaji nchiniUkweli tuliujua, walikua wazayuniJasho lao lilikua lanufaisha kampuniMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

9. Mabepari siri yao, kukuza mtaji kwaoIli kupata mafao, yenye faida kibaoWatumishi wanyonywao, daima wana chaoMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

10. Sura ya kwetu nchini, kwa watumishi wa ummaWallahi haifanani, na zile tulizosomaKwengine ulimwenguni, migomo ikirindima.MIGOOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

11. Maslahi ni ya umma, hapa nchini tambuaTukigoma kina Juma, wenyewe twajiumbuaUchumi warudi nyuma, pasi na kujitambuaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

12. Watunishi wa taifa, nyote wajuzi wa sifaTumieni marifa, hekima na utaifaNa njia zinazofaa, kudai ya manufaaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

13. Kugomea serikali, ya kizalendo nchiniKwetu tawaona muhali, wananchi mwatuhiniHuduma za stahili, mijini na vijijiniMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

14. Yaa illahi yaa Rabana, twakuomba mola wetuJalia wetu vijana, pamwe na wazee wetuDaima kusikizana, isije vurugu kwetu.MIGOMO HAINA TIJA KWA TAFA NATAMKA

15. Zatosha kumi na tano, nimefika kaditamaNaomba mshikamano, kuandika nasimamaTudumu kua mfano, amani na uslamaMIGOMO HAINA TIJA KWA TAIFA NATAMKA

USTADH ABDUL MAJID NCHAHAGAUMMUSALAMA SHULE YA SEKONDARIS.L.P 1648, IRINGA

Ndugu Mhariri wa Gazeti la AN-NUUR.N a o m b a u s i w a c h e kuichapisha barua hii ambayo n imekusud ia kujibu barua iliyotoka katika Sauti ya Waislam- AN-NUUR la Julai 13 - 19, 2012.

Ndugu anayejitambulisha kwa jina Yusuph Abdallah Kokole wa Chamazi Islamic Seminary, ametoa maswali sita yanayomkera kuhusu Rais ambayo nanukuu: “Mimi najiuliza, kwa madaraka aliyo

Kikwete analipa fadhila kwa maaskofukuwaweka katika sehemu zote nyeti, na kuwapa kupitia MoU mabilioni ya pesa k i la mwaka ambazo ni za walipa kodi na zimeshapangiwa matumizi, na pia mabilioni mengine ya misamaha ya kodi wakati huo huo Wa i s l a m u h a w a p a t i chochote.

Z a i d i y a a s i l i m i a 50 ya bajet i ya nchi wanafadhiliwa Wakristo wajiendeleze, na kwa k i l a s h i l i n g i m o j a wanayosamehewa kodi

Waislamu, basi Wakristo w a n a s a m e h e w a k w a kumi. Na washauri wake ni Maaskofu na Mapadri wa nchi hii. Hivi kweli u ta ta ra j ia Rais a ja l i maslahi ya Waislamu zaidi ya kuwapuuzilia mbali?

Kwa kumalizia, kwa mujibu wa Kitabu Kitukufu cha Qur’an, aya ya 15 Sura AI-Hujurat: “Wenye kuamini kweli kweli ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ; k i sha wakawa si wenye shaka, na wakaipigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kweli.”

Ahsante.Amour Kibuda JechaChake Chake,Pemba.

nayo Rais wetu (kwa mujibu wa katiba)”, na yanafuatia maoni yake:-

1. Anashindwa kutoa maamuzi juu ya suala la O.l.C.

2. Mahakama ya Kadhi. 3. Wakuu wa vitengo

mbalimbali katika Taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali.

4. Huyo Dkt. Ndalichako -”hivi kweli mtu unaitwa ‘Dkt.’ halafu unachakachua matokeo ya watu (kisa dini), huoni aibu kweli jamani.

5. UAMSHO na KATIBA - anasema haoni aibu Rais kushindwa na kuogopa kuwaruhusu Wazanzibari kutoa maoni yao juu ya Muungano.

6. Kadhia ya sensa - kuwa linagusa maslahi ya umma wa Kiislamu. Anajiuliza: “Hivi kweli mfumo Kristo achakachue mpaka idadi ya viumbe walioumbwa na Mwenyezi Mungu (S.W).”

Masuala yote haya Ndugu Yusuph anaelekea ni Muumini hasa na yanamkera, majibu ya masuala haya ni kuwa Mara baada ya kupewa Urais tuliwasikia Maaskofu na Mapadri wakisifu uteuzi wake kuwa Kikwete ni ‘Chaguo la Kanisa’. Mwenyewe ameshasema mara kadhaa kuwa kama si Kanisa basi angalikuwa akiuza karanga pale Chalinze.

Kwa maana mafanikio aliyoyapata hadi akawa Rais leo ni kwa sababu kasoma katika skuli za misheni zilizomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa. Ndiyo anawalipa fadhili kwa

Sheikh Bakwata azomewa mbele ya DC SingidaInatoka Uk. 16

kimeeleza kuwa Ust. Madina alimkabili DC huyo akimtaka aeleze ni wapi amepata takwimu zinaeleza idadi ya Wapagani kuwa ni wengi kuliko dini zote nchini.

“DC, tueleze umejuaje idadi ya Wapagani mpaka useme kuwa wao ni wengi kuliko dini zote katika nchi kuliko dini zote.” Alinukuliwa Ust. Madina na chanzo chetu, akimhoji DC huyo.

Katika hali iliyowashangaza viongozi wa Jumuiya zingine za Ki i s l amu, to fau t i na walivyotarajia, ni pale Sheikh Wa Wilaya Bakwata, Issa Simba, alipopewa nafasi na kutoa masharti ili Waislamu waweze kushiriki katika Sensa.

Sheikh huyo alimweleza DC, kwamba ili Waislamu washiriki kwanza Serikali ikane takwimu zote ambazo zimezagaa mitaani, kisha wakamatwe kwa mujibu wa sheria kwa kutoa takwimu feki.

Alisema, ikiwa Muislamu amekamatwa kwa kosa la k u s a m b a z a k i p e p e r u s h i k inachosema ‘Wais l amu hawashiriki Sensa’ na hao w a l i o t o a t a k w i m u h i z o wafikishwe Mahakanani ikiwa Serikali itathibitisha kuwa takwimu si za kweli.

“Lakini zaidi hatuwezi kushiriki na wala kuhamasisha k u p i t i a M i s i k i t i n i k w a sababu hatujapewa majibu ya kujitosheleza juu ya madai ya Waislamu.” Kilisema chanzo chetu kikimnukuu Sheikh huyo wa Bakwata, Wilaya.

Naye Sheikh Abdulrahman Mtyuku, a l imueleza DC, kuwa msimamo wa Waislamu utaendelea kubakia hivyo hivyo, kama ambavyo yeye (DC)

anavyopokea maagizo kutoka ngazi za juu na kuyafikisha na kama ambavyo hawezi kuyatolea maamuzi maswala hayo mpaka afikishe kwa Mkuu wa Mkoa, na ndivyo hivyo hivyo na wao (Masheikh) hawezi kubali msimamo mpaka viongozi wa Juu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zitoe maelekezo mapya.

Awlai katika ufunguzi huo wa kikao hicho kilichofanyika katika ofisi zake, aliwaomba viongozi wa dini ya Kiislamu kutumia fursa ya ibada ya swala ya Ijumaa, na swala zingine kuhamasisha Waislamu kushiriki katika sensa ya watu na makazi.

DC, huyo alionyesha kupinga takwimu ambazo zimetolewa na TBC (Televisheni), Bodi ya Utalii pamoja na Tovuti ya Wakatoliki, akidai kuwa takwimu hizo hazijasema kweli, akidai kwamba idadi ya Wapagani ni kubwa kuliko Wakristo na Waislamu.

Chanzo chetu kilisema, DC, alidai kwamba kuna viongozi wa dini aliwaita wanaharakati, wanahamasisha watu wasishiriki Sensa huku akidai wanafanya hivyo bila kujali Serikali ishatoa fedha nyingi juu ya swala la Sensa.

“Tukio hili halipo hapa tu, kwa sababu kuna vipeperushi vimesambazwa nchi nzima, v i n a v y o s e m a ‘ U j u m b e wa Ramadhani, Waislamu hatushiriki Sensa’”alisema Mpashaji habari wetu kwa njia ya simu akimnukuu DC, huyo.

Kikao hicho kilitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini, kwa barua yenye kumbukumbu namba DC/SGD/M.30/17/A, ya tarehe 10, Agosti, 2012.

Page 13: ANNUUR 1031

13 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala/Tangazo

WANAWAKE wa Kiislamu wametakiwa kutafuta Elimu kwa nguvu zao zote kwani kufanya hivyo nikutafuta radhi za Allah s.w.

Hayo yamesemwa na ukhut Saada Ali, kutoka Buguruni wiki iliyopita katika kongamano lililofanyika katika madrasa ya kinamama ya Masjid Taqwa iliyopo Kawe Mji Mpya, jijini Dar es Salaam.

Ukhti Saada amesema kuwa lengo la kutafuta elimu ni ili wamjue Mola wao na kwa ajili ya maisha yao hapa duniani.

Aliongeza kuwa kutafuta elimu hakuna ukomo mpaka kuingia kaburini.

Kwa upande mwingine akawahimiza kupata elimu ya ndoa kwani ni muhimu kwao kwa kuwa inawawezesha kujua mambo ya msingi katika ndoa zao na jinsi ya kuilinda na kuiheshimu ili kudumu katika umoja wa familia.

Ukhut Saada pia alisisitiza juu ya umuhimu wa elimu ya malezi kwa watoto wa Kiislamu, ambapo alisema elimu hiyo itaweza kusaidia kupunguza

Akina mama tafuteni elimuNa Azza Ally Ahmed momonyoko wa maadili kwa

watoto. “Tuwafuate Maswahaba,

pamoja na utukufu waliokuwa nao waliacha utukufu wao na wakatafuta elimu, hivyo basi hakuna utukufu mbele ya elimu. Aidha hakuna ibada bila ya elimu ”. Alifafanua Ukhut Saada.

Aliwatahadharisha kina mama hao kuacha kufunga na kuswali kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani pekee, bali waendelee kutekeleza ibada walizokuwa wakifanya kwani Mwenyezi Mungu ambaye ndiye anayeabudiwa yupo siku zote za maisha.

Naye Ukhut Tatu kutoka Buguruni aliwataka kina mama kufanya jitihada kubwa katika suala la malezi kwa watoto kwani wao ndio walimu wakubwa na wa kwanza wa watoto wao.

Alisema tatizo la kuporomoka maadili chanzo chake ni kina mama kukosa elimu sahihi ya Uislamu.

Kwamba kina mama ndio walezi wakubwa na ndio wanaolengwa na makafiri ili kuwapoteza katika nafasi yao ya msingi katika ulezi.

Kuruhusu kupotea Zanzibar ni dhambi Inatoka Uk. 7A L I Y E B A G U L I W A anapodai haki yake ya KUTOBAGULIWA ndiyo anasababisha UBAGUZI? Au yule aliekuwa chanzo cha sababu ya UBAGUZI huyo ndiye MBAGUZI? Mazoeya hayo yakamfikisha MBAGUZI kuamini kuwa tabiya hiyo ndiyo haki yake, hivyo harakati zozote utapoanzisha dhidi ya dhulma hiyo, MBAGUZI hujenga dhana kwamba unadhamiria kumpora haki hiyo aliyodumu nayo kwa nusu KARNE sasa!

Dunia ya leo kila taifa hujitahidi kwa kiwango cha juu kwa kujiweka katika hali nzuri ya kujiamulia mambo yake yenyewe bila ya kuwepo kwa mamlaka nyengine ambayo itaweza kuingilia maamuzi yake, kwa kuzingatia mahitaji yake na kwa zama zake na kwa mujibu wa uchumi wake, siasa yake watu wake na utamaduni wao, mambo hayo hayapaswi kuwa katika mamlaka ya nguvu nyengine isiyokuwa ya Wazanzibari wenyewe, kwa sababu Wazanzibari ndiyo wana uwezo wa pekee wa kutambua mahitaji yao kwa mujibu wa matakwa ya jamiii yao kwa misingi ya utamaduni wao.

NDOTO ZA MCHUNGAJI

SIKU ya Tarehe 26 july 2012 katika BUNGE la Jamhuri ya muungano kuliibuka hoja dhaifu ya kuudhi na ni kashfa kubwa kwa jamii yetu Wazanzibari kwamba eti kuna MCHUNGAJI kutoka IRINGA anahoji maamuzi yetu Wazanzibari kupitia Waziri wetu wa KATIBA na SHERIA, na WAZIRI wa Utamaduni Utalii na Michezo kwa kup iga maru fuku kutembea nusu uchi, kula chakula hadharani, kuvuta sigara na kupigana mabusu ovyo barabarani, unywaji wa pombe kiholela kwa kipindi cha Mwezi mtukufu wa RAMADHANI, kwa NDOTO hiyo ya MCHUNGAJI ndio maana tunazidi kuthibitisha kuwa muungano huu ni KERO na mabadiliko ni jambo la lazima ili wazo kama hilo la MCHUNGAJI liishie kijijini kwao IRINGA, kwa sababu MCHUNGAJI ameshindwa kuthamani na kuheshimu utamaduni wa Mzanzibari kwa kujenga hoja inayoashiria kupinga au kutaka kufutwa kwa maamuzi yetu hayo tunayojipangia Katika nchi yetu!

Moja ya kazi ya Wabunge bungeni ni kuhoji au kujenga hoja dhidi ya Serikali kwa dhamira ya kuikosoa kwa kuijengea uimara Serikali k u t o k a n a n a k a s o r o zinavyojitokeza kwa lengo la kuimarika Serikali hiyo, kutokana na mapungufu yanayojitokeza, sasa Je MCHUNGAJI aliona kwa kujenga hoja hiyo anatusaidia kutujenga au anadhamiria ku tubomoa? Kwakuwa anajua uhalisi wa utamaduni wetu na isitoshe alisaidiwa kwa kuelimishwa na Waziri Mkuu kwa kumpatia majibu yanayoendana na uhalisi huo, na akasisitiza kutoridhishwa na majibu ya Waziri Mkuu, kwa hivyo ni kwa nini tusiamani kuwa MOJA YA KAZI ZA WACHUNGAJI w a g e n i w a n a o k u j a ZANZIBAR wana dhamira inayofanana na MCHUNGAJI HUYO? Nadhani Mchungaji al i tamani kujenga hoja i le ndani ya BARAZA LA WAWAKILISHI i l i akamilishe malengo ya kufanikisha kusudio lake!

Je, kwa nini tusiamini kuwa kuna dhamira ya

WACHUNGAJI ya kutaka kuingia katika BARAZA LA WAWAKILISHI na kujenga hoja za mfano huo kwa dhamira ya kutubomoa katika Mila na Utamaduni wetu? Je, inaingia akilini kuwa Wazanzibari wana hitajio la kukosolewa juu ya Utamaduni wetu na Mtaalam anaepinga Utamaduni huo tena ni mchungaji? Tunaposema Muungano ni KERO mfano wake ni huo.

W A Z A N Z I B A R I tunalazimika kutoa somo kupitia MCHAKATO wa KATIBA kwa kujenga misingi itakayoondoa na kufuta kabisa udhaifu wa Muungano ili kuondoa mwanya kwa wale wanaodhamiria kutuharibia Mila, Utamaduni na sheria za ndani ya Zanzibar, hilo ndiyo litakuwa jibu sahihi kwa wale wanaoota NDOTO za kijijini kwao na kutaka kuzihamishia ndani ya ZANZIBAR kwa kuficha dhamira zao kwa kutmia fursa ya kisingizio cha ndani ya Bunge la Jamhuriya Muungano.

DHANA YA KUTISHANAKuna watu hudanganya

watu, eti kudai haki ya nchi

yako kutasababisha kupotea haki ya nchi nyengine, eti kudai haki ya nchi yako kunatetewa na nchi ambayo imeikamata na kuizuiya haki hiyo!, eti kudai HAKI ya nchi yako kunahatarisha amani kwa upat ikanaj i wa HAKI hiyo!,ni ajabu kubwa kuwa Wazanzibari wanapoidai HAKI ya nchi yao kutasababisha kuzuka kubaguana kwa sababu w a l i o n y i m w a H A K I wanadai haki yao!, hivyo ubaguzi utakuja kwa sababu Wazanzibari wanadai HAKI yao? Au ni kwa sababu ubaguzi ulijengwa baada ya kuwabana na kuwanyima Wazanzibari HAKI yao? jitahidi kutulia na kutafakari uchambuzi huo.

Tiba pekee ya kutibu gonjwa la kubaguana ni watu kupatiwa haki yao, itawezekanaje kutibu gonjwa hilo sugu kwa kuepuka kutumia tiba hiyo?

W A Z A N Z I B A R I T U N A P A S W A N A KULAZIMIKA KUTOA D O Z I S A H I H I YA KUIREJESHEA SERIKALI Y A M A P I N D U Z I ZANZIBAR MAMLAKA YOTE YA KISHERIA NA KUWA NA MAAMUZI Y O T E YA K I TA I FA NA KIMATAIFA BILA

Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeandaa safari ya Hijja na Umra mwaka 2012 kwa dola (US) $ 3375 tu.Mambo yatakayogharamiwa.Semina za Hijja, Huduma za Afya, Airport charge na Tiketi za ndege, Nyumba za kulala Makka na Madina, Ihram na Kuchinja kwa ajili ya Tamaa-tuu, Chakula wakati wote, Usafiri na ziara Makka na Madina, Mahema Mina na Arafa. KUHIJIWA ni DOLA US $ 1450.Fomu zinapatikana.1 Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam- Magomeni Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba namba 26 Mkabala na Show Room ya Magari Tel: 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930 444 au 0773 930 444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar RahaLeo Tel: 0777 484982, 0777 413987.3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar Es salaam Tel: 0784 453838.4. Abdallah Salehe Mazrui ( Hoko) Dar es salaam Tell. 0715 72 4444.5. Salim Is-haq Dar es Salaam Tell: 0754 286010, 0774 786101.6. Dukani kwa Mohamed Hafidh Mazrui Wete Pemba Tel: 0777 482665.7. Sheikh Daudi Khamis Sheha Tel: 07776 79692.8. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel: 0777 417736.

Wahi mapema kulipia ili ushughulikiwe mapema, kama utalipia kwa Account No 048101000030 NBC piga simu kwanza 0774 412975.Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa ni cha Bei nafuu zaidi na huduma zake ni bora zaidi ya vikundi vingine.

Ahlul Daawa Hajj and Travel Agency

Page 14: ANNUUR 1031

14 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

UNAMKUMBUKA huyu jamaa, Jason Russel? Ndiye al iyekuwa mbele katika sinema iliyodumu muda mfupi na kupigiwa debe sana ya ‘Kony 2012,’ kampeni ya propaganda iliyoteka hisia za vijana kupendezesha u v a m i z i w a M a r e k a n i nchini Uganda. Baada ya uwongo wake kuonyeshwa wazi katika Internet alipata fadhaa akapatwa na kiwewe. Alikimbia uchi karibu na taa za kuongoza magari, akapiga ngumi kwenye kiambaza, na kupiga mayowe yasioeleweka. Pepo la Uwazimu liliishinda nafsi yake dhaifu.

Siku moja kabla ya kupatwa na kiwewe Russel alikuwa shujaa katika vyombo vya habari kama mtakatifu aliyejitolea kuwaokoa watoto wa Afrika. Mkanda wake wa propaganda ya vita kuhusu mshirika aliyekufa wa CIA Joseph Kony ulikuwa ukipendwa sana katika Facebook na maeneo mengine ya mtandao. Lakini uficho wake ulipoanguka na uwazimu wake ukanasa kwenye kamera, kunguru wa vyombo vya habari wakasahau vita yake takatifu na haraka wakakimbilia habari mpya inayosisimua.

H a b a r i m p y a a m b a y o i l ikamata hisia za walafi katika vyombo vya habari vya Magharibi ni Syria. Vita ilikuwa inapamba moto, na “jumuia ya kimataifa” ilikuwa inasukumwa kuchukua hatua dhidi ya nchi hiyo. “Assad anaua watu wake mwenyewe,” walisema, bila kuonyesha ushahidi wowote. “Hii ndiyo domino inayofuata itakayoanguka katika Uamsho wa Nchi za Kiarabu; waasi lazima wasaidiwe na Assad hana budi kuachia madaraka,” p ropaganda i l i s ema . Na mengine, mengine mengi tu. Uwongo wa kijinga wa vyombo vya habari ulirudiwa kwa miezi kadhaa. Vituo vikubwa vya televisheni vilikuwa katika vita ya propaganda ya saa 24 kwa siku kuteketeza nchi huru ya Syria na kuiweka Syria katika utumwa.

Lakini jambo l i s i lo la kawaida na lisilotazamiwa lilitokea. Baadhi ya waandishi wa habari wa nchi za Magharibi walianza kueleza ukweli kuhusu vyanzo vya mgogoro huo, kinachosukuma propaganda dhidi ya Syria katika nchi

Kukwama kwa propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu Syria

Kinachoandikwa katika magazeti ni uwongoKilichojificha wazi hadharani ndiyo ukweli

Na Saman Mohammadi (July 31, -Mtandao wa Kusambaza Habari) -

za Magharibi na undani wa upinzani usioungwa mkono nchini Syria.

Ujanja ukaisha. Mwezi Juni, gazeti la Ujerumani la Frankfurter Allgemeine Zeitung (FAZ) liliripoti kuwa mauaji ya kutisha ya Houla hayakufanywa na majeshi ya Assad, kama ilivyosemwa na vyombo vya habari vya Magharibi mwanzoni, ila na upinzani wa kigaidi unaofadhiliwa na NATO.

Maelezo rasmi kuhusu mzozo wa Syria yalianguka baada ya hapo. Hoja ya kimaadili ya kumwondoa Assad ilipotea kwa sababu i l i tokana na uwongo mtupu. Uchokozi wa wazi unaofanywa na washirika maharamia wa NATO dhidi ya raia wa Syria ulikuwa wazi kwa yeyote aliyekuwa akiangalia.

Kuzuka kwa upashanaji habari tofauti wa kimataifa: Mwisho wa propaganda za vyombo mashuhuri vya habari

Vyombo vya habari vikubwa vya nchi tofauti haviwezi tena kuhodhi nini kinatokea, Uwongo ulio rasmi unakosolewa, kweli zilizofukiwa zinafukuliwa, na uhalisia unahifadhiwa. Mbinu za mfanya mazingaombwe zimefichuliwa na waharibifu katika kadamnasi. Vyombo vya habari tofauti duniani vinainuka na vimekuwa injini ya amani, ukombozi , maelewano na umakini.

Hata baadhi ya watendaji katika vyombo vya habari vikubwa wanalazimika kukiri kuwa wamekuwa wakiidanganya dunia kuhusu karibu kila kitu, na kuwa mawazo yao ya kuchochea vita hayakubaliki kote. Wanapoteza uwezo wao wa kukamata mawazo ya walio wengi, na kama Russel wa maonyesho ya Kony 2012, nao pia wameanza kupoteza uwezo wa kutawala akili zao.

Kwa uhakika, waandishi wa habari wa vyombo vikubwa tayari wamekuwa vichaa na kushindwa kuishika hali halisi. Dunia yao inaanguka kote walipo na mamlaka yao ya muda mfupi yanapotea kila kukicha. Ukweli ni nguvu kubwa mno. Vyombo vikubwa vya habari vinakwenda kinyume cha nguvu za uvutano za hali halisi na vinapoteza mapambano hayo.

Lakini siyo kila mtu katika vyombo vya haba r i vya Magharibi amepoteza kichwa chake na moyo wake. Bado wako waandishi wa habari wenye heshima ambao wanaweka ukweli kuhusu historia juu

ya uwongo wa serikali zao. Mwandishi ‘B’ wa MoA (nchini Ujerumani) anaandika:

“Inaelekea kuna mabadiliko kidogo katika vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu habari za Syria. Hapa Ujerumani magazeti (na vyombo vingine) vimeanza kuonyesha ‘waasi’ hao jinsi walivyo: wapiganaji Jihad wanaosafiri nchi tofauti, kundi la wapiganaji linalipwa na nchi za nje. Wazungumzaji katika habari sasa wamekuwa wakionyesha ukinzani kuhusu habari za kawaida za propaganda na sera ya serikali ya Ujerumani kuunga mkono SNC (Baraza la Kitaifa la Syria). Pia kuna mabadiliko kidogo katika vyombo vya habari vya kimataifa.”

Wakati hadi hivi karibuni vyombo vikubwa vya habari vya nchi za Magharibi vilikuwa na nguvu sana na maelezo yake rasmi kwa pamoja yalikubalika kwa watu, hivi sasa uhalali wake unaporomoka na vinashindwa kuwafanya watu waamini uwongo wa serikali.

Vijana wanaohitaji habari wanafuatilia vyombo vya habari huru mbadala kupata ukweli wa masuala magumu na mizozo. Katika mwenendo huo, mtazamo wao kuhusu dunia unabadilika na imani zao zilizosukwa na serikali zinakufa.

Ukweli kuhusu Syria, kama ukweli kuhusu Septemba 11 (2001), unaweza kukandamizwa kwa kitambo tu lakini hauwezi kufutwa katika mtiririko wa his tor ia . Tony Cartalucci anasema kuwa propaganda ya Magharibi dhidi ya Syria imevuka mpaka na matokeo yake inaparaganyika. Uwongo uliosukwa unafichuliwa kabla manufaa yake hayajafikiwa. Ifuatayo ni sehemu ya makala ya Cartalucci: “Wizara ya Fedha ya Marekani: Al Qaeda inaendesha ‘uasi’ nchini Syria.”

“Sasa, inaelekea kuwa jeshi la kukodiwa la nchi za Magharibi, Al Qaeda, liko mbioni kupata pigo kubwa - siyo katika mikono ya wapiganaji dhidi ya ugaidi wa nchi za Magharibi ila kutoka askari wa Syria katika jiji la Aleppo. Katika juhudi kubwa ya kuzuia hilo, nchi za Magharibi zinatumia njia tofauti za kufa na kupona kuanzia kuwaonyesha wapiganaji wa nje walioingia mtegoni na kufanya mauaji ndani ya Aleppo kuwa ni “hatari ya mauaji ya watu wengi yanayokaribia,” hadi kutumia uwepo wa wapiganaji hawa wa nje kama ushahidi kuwa “Al

Qaeda” inaendesha shughuli nchini Syria na lazima “izuiliwe” kwa nchi za Magharibi kuingilia kati.

Ni muhimu kuelewa kwamba, kama jinsi himaya zinavyofanya siku zote, maslahi makubwa ya makampuni hodhi ya nchi za Magharibi yanataka uhodhi katika eneo la Mashariki ya Kati kama hatua mojawapo kuelekea uhodhi wa biashara duniani kote, na watasema au kufanya chochote kinachohitaj iwa k u f i k i a h a p o . U p i n z a n i unavyoongezeka, uwongo wa Magharibi unakuwa mgumu kuuza, uthabiti wa propaganda zao unaporomoka waziwazi. Nchi za Magharibi, kwa pumzi moja, sasa wanasema wapiganaji wa FSA (Free Syrian Army) kwa wakati mmoja ni “Al Qaeda” wanaohitaji kuondolewa, na hapo hapo “mauaji ya watu wengi” na majeshi ya Syria yanakaribia kama hakuna kitakachofanyika kuwaokoa.

Wakati Rais Obama wa Marekani alipozungumzia “unyama uliokithiri” kuhusu kinachofanywa na majeshi ya Syria huko Aleppo, yeye na waandishi wa hotuba zake wanafanya hivyo wakiamini kuwa Wamarekani, na dunia, ni wajinga na hawaujali sana ukweli, na wataruhusu kwa furaha sera za nchi za nje za Magharibi kuvizia na kudandia hisia zao na nia zao njema ili kuuza uingiliaji kati kijeshi

wa kujinufaisha pamoja na uteketezaji mkubwa.

Ni jambo la kushangaza kusikia kuwa Marekani iko vitani na Al Qaeda nchini Yemen; halafu, wakati huo huo, ni mshirika wa Al Qaeda nchini Syria, Ni mojawapo tu kati ya hayo mawili inaweza kuwa kweli. Ni kwamba Marekani inaweza kuwa vitani na Al Qaeda, au hapana.

Hisia ya mantiki ya Marekani inachekesha na imepinda, lakini si ya kipekee. Hivyo ndivyo dunia ilivyo. Katika historia, himaya kwanza zinaushinda ukweli, hali halisi, na ufahamu wa binadamu, halafu wanaenda katika nchi zenye raslimali nyingi.

U w e z o w a h i m a y a unategemea imani za vikundi maalum na viongozi wao ambazo zinaundwa kuhalalisha utawala dhalimu nyumbani na nje. Ni ishara ya matumaini kwa dunia na kwa maisha ya jumla ya wanadamu pale uhalisi wa ukweli unaposhinda himaya ya kifo, katika wakati wowote ule wa historia.

(Makala hii imeandikwa na Saman Mohammadi - Email: [email protected] na kichwa cha habari “Flipping The Script: The Western Media’s Syria Propaganda Is Falling Apart” na kufasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija)

RAIS wa Syria, Dk. Saad Al Bashar

Page 15: ANNUUR 1031

15 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012Makala

NIKIWA naingia katika kijiji cha Vietnam Kusini, niliwaona watoto wawili w a d o g o w a l i o k u w a mashuhuda wa vita virefu zaidi katika karne ya 20. Ulemavu wao wa kutisha ul ikuwa unaonekana sehemu nyingi . Eneo lote la Mto Mekong, ambako misitu ilikuwa imeteketezwa na kubaki kimya, watu waliobadilika vinasaba waliishi vyema kiasi walichoweza.

Leo, katika hospitali ya watoto ya Tu Du mjini Saigon, chumba cha upasuaji c h a z a m a n i k i n a i t w a ‘chumba cha makusanyo’, lakini lugha rasmi n i ‘chumba cha kihoro.’ Ina milolongo ya chupa kubwa zenye vitoto vya kutisha vilivyoharibikia tumboni. Wakati wa uvamizi wake wa Vietnam, Marekani ilitumia kemikali ya kupukutisha majani katika mapori na vijiji ‘kumfichua adui,’ Hii ilikuwa ‘Agent Orange,’ iliyokuwa na dioxin. sumu kali ambazo zinaeweza kusababisha kifo cha kitoto tumboni , ku toka kwa mimba, kudhurika vinasaba na saratani.

Mwaka 1970, Ripoti ya Senate ya Marekani ilifichua kuwa “Marekani imemwaga (juu ya Vietnam Kusini) kemikali za sumu kiasi cha ratili sita (karibu kilo tatu) kwa kila mkazi, wakiwemo wanawake na watoto.” Jina la siri la kumwaga silaha hiyo ya maangamizi iliitwa Operation Hades (yenye maana ya kuzimu au Jehanamu). Baadae i l i bad i l i shwa ika i twa ‘Operesheni Ranch Hand,’ (kama vile ni shamba la mifugo). Leo hii inakisiwa kuwa waathirika milioni 4.8 wa Agent Orange ni watoto.

Len Aldis, katibu wa chama cha urafiki wa Uingereza na Vietnam, hivi karibuni alirudi kutoka Vietnam akiwa na barua kwenda kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kutoka Umoja wa Wanawake wa Vietnam. Rais wa umoja huo Thi Thanh Hoa, alielezea “athari kubwa za kimaumbile (zilizosababishwa na Agent Organge) kutoka kizazi kimoja hadi kingine.” Aliitaka OIC kufikiria upya kukubali ufadhili wa Michezo ya Olimpiki ya London uliokuwa ufanywe na Kampun i ya Dow Chemical Corporation,

Uhalifu wa Marekani dhidi ya BinadamuHistoria ndiyo adui ‘wataalamu’ wa ubadilishaji fikra wanaposhika hatamu

Na John Pilger

m o j a y a m a k a m p u n i ambayo yal i tengeneza sumu hiyo na imekataa kuwaf id i a waa th i r ika wake. Aldis aliwasilisha barua hiyo katika ofisi ya Lord Coe (Sebastian Coe, mwanariadha mashuhuri wa Uingereza zamani), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki, London. Hajapata jibu lolote.

W a k a t i A m n e s t y International ilipokumbusha kuwa mwaka 2001 Dow Chemical ilinunua kampuni iliyohusika na uvujaji wa gesi huko Bhopal nchini India (mwaka 1984) ambayo iliua watu kati ya elfu saba na elfu kumi papo kwa papo na wengine 15,000 katika miaka 20 iliyofuata, David Cameron (Waziri Mkuu wa Uingereza) aliita Dow kuwa ni ‘kampuni yenye sifa.’ Hivyo ni furaha na vifijo wakati camera za televisheni zinapoonyesha pambo lenye thamani ya pauni (za Kiingereza) milioni saba linalofunika u w a n j a w a O l i m p i k i (London), linalotokana na mkataba wa miaka kumi kati ya OIC na mharibifu huyo aliyekubuhu.

Historia imezikwa na waliokufa na kuharibiwa wa Vietnam na Bhopal. Na historia ndiyo adui mpya. Mnamo Mei 28, Rais Obama a l iz indua kampeni ya kubatilisha historia ya vita vya Vietnam. Kwa Obama, hapakuwa na Agent Orange, wala maeneo ya kushindilia risasi bila kizuizi, hapakuwa na kuficha mauaji ya watu

weng i , wa l a ubaguz i uliokithiri, au kujiua (kwani Wamarekani walioj iua wenyewe wanalingana na wale waliokufa vitani), wala kushindwa na jeshi la kujihami la jamii masikini. Ilikuwa, kwa mujibu wa Bw. Hopey Changey (tumaini la mabadiliko, Change we can believe in) “moja ya matukio ya kushangaza ya ujasiri na uadilifu katika historia ya kijeshi (ya Marekani).”

Siku iliyofuata, gazeti l a N e w Yo r k Ti m e s lilichapisha makala ndefu iliyoonyesha jinsi Obama mwenyewe anavyochagua nani watakaouawa kwa mabomu ya drone, ndege za kivita zisizo na rubani, maeneo tofauti duniani. Anafanya hivyo katika ‘Jumanne za kigaidi , ’ ambako anaangalia picha ndogo ziliowekwa katika orodha ya wanaotakiwa kuuawa, baadhi yao wakiwa na umri chini ya miaka 20, mmojawapo akiwa msichana “ambaye alionekana mdogo kuliko hata miaka yake 17.” Wengi wao hawajulikani au wamefikia tu umri wa kuingia jeshini. Zikiwa zinaongozwa na ‘marubani’ walioketi mbele ya vioo v y a k o m p y u t a m j i n i Las Vegas (Marekani), d rone h izo z ina lenga makombora ya Hellfire (Moto wa Jahannamu) ambayo yananyonya hewa kutoka kwenye mapafu na kulipua watu wabaki vipande vipande. Mwezi Septemba (mwaka jana) Obama alimwua raia wa Marekani, Anwar al-Awlaki

kwa habari za kuvumishwa tu kuwa alikuwa akichochea ugaidi. “Huyu ni rahisi,” ananukuliwa na wasaidizi wake ak isema wakat i akitia saini kifo cha mtu huyo. Hapo Juni 6, drone iliua watu 18 katika kijiji Afghanistan, wakiwemo watoto, wanawake na wazee waliokuwa wakifurahia harusi.

Makala hiyo ya New York Times haikuwa imetokana na kuvuja kwa habari au kufichuliwa. Ilikuwa ni taarifa ya majigambo iliyoasisiwa na utawala wa Obama kuonyesha jinsi ‘amiri jeshi mkuu’ alivyo thabiti katika mwaka wa uchaguzi mkuu.

Ikiwa atachaguliwa tena, Brand Obama (bidhaa) i t a ende l ea k u tumik i a wenye fedha, kufuatilia wanaosema ukweli, kutishia nchi, kueneza virusi vya komputa na kuua watu kila Jumanne.

Vitisho dhidi ya Syria, vinavyoratibiwa Washington na London, vinafikia ngazi mpya ya unafiki. Tofauti na propaganda za wazi zinazotolewa kama habari, uandishi wa kichunguzi wa gazeti la Ujerumani, Frankfurter Allgemeine Zeitung zinawataja wahusika wa mauaji ya watu wengi mjini Houla kuwa ni waasi wanaosaidiwa na Obama na Cameron. Waliolihafamisha gazeti hilo ni pamoja na waasi wenyewe. Uthibitisho huo haujapuuzwa moja kwa moja nchini Uingereza. Akiandika katika blogu yake binafsi, kimya kabisa,

Jon Williams, mhariri wa habari za kimataifa wa BBC, anaongeza ufuatiliaji wake binafsi wa suala hilo, akiwanukuu maofisa wa nchi za Magharibi wakisema kuwa operesheni ya kiakili dhidi ya Syria i l ikuwa imefana sana. Ilifana kama kuvunjiliwa mbali kwa Libya, na Irak na Afghanistan.

Na pia ni ya kufana kama ubunifu wa gazeti la Guardian likimkuza Alastair Campbell, mshirika mkuu wa Tony Blair katika uvamizi hadisi wa Irak. Katika kumbukumbu zake za tarehe hizo, Campbell anajaribu kupaka damu ya Irak kwa pepo liitwalo Murdoch (mmiliki wa magazeti yaliyofikiwa na kashfa ya kusikiliza simu za watu binafsi). Ipo ya kutosha kuwalowesha wote. Lakini kukubali kuwa vyombo vya habari vyenye hadhi, vya kiliberali na vinavyompenda Blair vilikuwa na nafasi ya ziada muhimu katika uhalifu huo mkuu kumefichwa na kumebakia ni jaribio muhimu la kitaaluma na kimaadili nchini Uingereza.

Ni kwa kitambo gani tutaendelea kuwa chini ya ‘serikali kivuli’ ya aina hiyo? Kielelezo hicho cha propaganda ya kupotosha kil i tumiwa kwanza na Edward Bernays, mpwa wa Sigmund Freud (mwanzilishi w a p s y c h o a n a l y s i s ) aliyetunga fani ya mahusiano (public relations), haijawahi kuonekana bayana kiasi hicho. Kutunga uhalisi ambao haupo kunahitaji kusahau historia, kusema uwongo kwa kukwepa, na kuhamisha kilicho muhimu katika visivyo muhimu, Kwa njia hii, mifumo ya siasa inayodhamiria usalama na haki kijamii imedilishwa na uharamia, ‘kufunga mkanda’ na vita visivyoisha - ukereketwa wenye nia ya kuangamiza demokrasia. Ingekuwa ni mtu binafsi angeweza kuitwa mwendawazimu, Kwanini tunaikubali?

(Imefasiriwa na Anil Kija kutoka makala ya John Pilger yenye kichwa cha habari: “U.S. Crimes Against Humanity?

History is the Enemy as ‘Brilliant’ Psy-ops Become the News”. www.johnpilger.com)

RAIS George Bush. RAIS George W. Bush. RAIS Barack Obama

Page 16: ANNUUR 1031

16 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 SHAWWAL 1433, IJUMAA AGOSTI 24-30, 2012

WAISLAMU wametakiwa kuhakikisha kuwa jambo la kwanza kulisema na kulitaka liwe katika Katiba ni kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi yenye mamlaka, i l iyopo kisheria na inayogharamiwa na serikali.

Akitoa wito huo, Maalim Ally Bassaleh amesema kuwa kile kilichotangazwa na Mufti wa Bakwata sio walichotaka Waislamu hivyo waiache Bakwata na Kadhi wao wa kuwaridhisha maaskofu.

Akasisitiza kuwa Kadhi Mkuu aliyetangazwa na Mufti wa Bakwata, ni Kadhi wa Bakwata pekee.

Maal im Al ly Bassa leh ameyasema hayo ka t ika Baraza la Idd lililofanyika Mwembeyanga mwishoni mwa wiki siku ya Eid El Fitri..

Bassaleh amesema kuwa Mufti amedai kuwa hakumteuwa Kadhi Mkuu kwa utashi wake mwenyewe, bali alishinikizwa na tume ya dini ya Bakwata ambayo ina uwakilishi wa Masheikh wa Wilaya na Mikoa.

Bassaleh akasema, kwa kuwa Mufti Simba wa Bakwata amefuata shinikizo la Mashekh wake wa Wilaya na Mikoa,

Jambo la kwanza kwa Warioba ni Mahakama ya Kadhi-BassalehKadhi Mkuu wa Mufti ni wa Bakwata pekee Na Bakari Mwakangwale huyo Kadhi anakuwa ni wa

Bakwata na si wa Waislamu wa Tanzania.

“Sheikh Simba, uelewe huyo Kadhi uliye mteuwa ni Kadhi Mkuu wa Bakwata, sio wa Waislamu huo ndio ukweli na utaendelea kubaki hivyo hivyo.” Alisema Maalim Bassaleh.

Awali Maalim Bassaleh, aliweka wazi mchakato mzima ulivyoanza wa kumpata Kadhi atakaye kubalika na Waislamu wote kupitia Jumuiya na Taasisi zote hapa nchini, lakini akasema kuwa Bakwata imekengeuka na kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu.

Akinukuu gazeti la Majira la Agosti 12, 2012, alisema Jumuiya ya Makanisa, imetoa tamko kuhusiana na suala la Mahakama ya Kadhi mara tu baada ya Bakwata kutangaza Makadhi wake.

A l i s e m a u m o j a h u o wa Jumuiya za Kikristo, zimenukuliwa na gazeti hilo zikisema kwamba, kutokana na kuwa Serikali imeridhia Mahakama ya Kadhi iwe nje ya Katiba na tayari Kadhi Mkuu na baadhi ya Makadhi wa mikoa wamekwisha chagualiwa, hawaoni sababu kwa Tume ya Marekebisho ya Katiba kuendelea kuchukua maoni kwa suala ambalo limekwisha tolewa uamuzi, na dini inayohusika.

“Tume hivi sasa inakusanya maoni, miongoni mwa maoni hayo ni maoni ya Waislamu mimi na wewe na katika yale ambayo Waislamu wamejipanga kuyatolea maoni yetu ni pamoja na hili la Mahakama ya Kadhi kuwamo katika Katiba mpya.

Mahakama ya Kadhi inayotambulika kisheria katika nchi, sio ambayo inaelea hewani isiyo na mashiko, tunataka Mahakama hiyo igharamikiwe na Serikali, lakini sasa Bakwata imekubali Mahakama ambayo wanaitaka Maaskofu.” Alisema Maalim Bassaleh.

Alisema, hatua ya Mufti wa Bakwata kuteuwa Makadhi inatoa mwanya kwa Maaskofu na kuwachanganya Waislamu, wasiendelee kudai Mahakama ya Kadhi katika Katiba mpya.

M a a l i m a B a s s a l e h , aliwataka Waislamu kutoacha kutoa maoni na kuzungumzia Mahakama ya Kadhi pindi watakapotembelewa na Tume, aliwataka kuhakikisha katika maoni yao jambo la kwanza liwe ni kuhusu Mahakama hiyo kutambulika kikatiba.

MWENYEKITI wa Bakwata, Mkoa wa Singida, Alhaji Swaleh Msuri, amejikuta katika fedheha kubwa baada ya kuzomewa alipojaribu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini kuwa watahamasisha Sensa.

Hali hiyo ilitokea Jumanne wiki hii, mjini Singida katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kilichohusu uhamasishaji wa ushiriki katika sensa ya watu na makazi kilichowahusisha viongozi wa dini.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya kikao hicho, kilisema katika majumuisho yake mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza, Sheikh huyo wa Bakwata, Alhaj i Msuri , anaungana na wanasemina pamoja na DC, kuwa wao (Masheikh) watahamasisha zoezi la Sensa kwa waumini wao.

Chanzo hicho kinasema,

Sheikh Bakwata azomewa mbele ya DC SingidaNa Bakari Mwakangwale mara baada kauli hiyo, hali ya

ukumbi ilibadirika kutoka kwa viongozi wa Kiislamu kwa ujumla kwa kuanza kumzomea kisha kumuambia hiyo ni kauli yake binafsi na si yao.

“Baada ya hapo alipingwa kwa nguvu, mwisho aliambiwa kuwa hiyo ni kauli yako na kama upo tayari kuhamasisha Sensa, nje ya madai ya Waislamu hiyo ni kauli yako kama uko tayari kafanye wewe.” Kilisema chanzo hicho.

Imeelezwa kuwa kufatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya, i l imlazimu kusimama na kutuliza hadhira ndani ya kikao hicho, ambacho kilikuwa kinafika ukingoni, baada ya hoja na maswali mbalimbali kutolewa na washiriki wa kikao hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho kilisema kuwa Mkuu wa Wilaya alidai kuwa amebaini kwamba ndani ya kikao hicho wamegawanyika ambapo alidai awali alidai kuwa wapo pamoja.

L a k i n i p i a D C , h u y o alionyesha masikitiko yake juu ya tukio hilo akidai kwamba hakufurahishwa na kitendo cha kuzomewa kwa kiongozi huyo wa dini, pamoja na kudai kuwa amepokea hoja kwa ujumla katika kikao hicho na kuahidi kuzifikisha kwa Mkuu wa Mkoa, kwa kuwa yeye si msemaji wa mwisho.

Mpashaji wetu habari alisema, mara baada ya DC, kuhitimisha utangulizi wake aliruhusu mjadala na maswali ambapo Sheikh Muro, kutoka Jumiya ya Answar, aliuliza sababu za kipengele cha Dini hakipo katika Sensa ilihali katika senza za nyuma kilikuwepo.

“Ikifahamika Waislamu wangapi na Wakristo wangapi na wasio na dini wangapi itazuia nini Serikali kufanya kazi zake. Jawabu la DC lilikuwa hakuna nafasi ya kuliingiza susla hilo kwa kuwa muda umeshakwisha.” Kilisema chanzo hicho.

Naye Ust. Suleiman Madina, alimweleza DC, huyo kwamba

Serikali isiwafanye Waislamu kama zimamoto, kwa kuwahitaji pindi wanapoona mambo yao yanakwama.

Alisema, kama Serikali inaona kuna umuhimu wa kupata sapoti kutoka kwa Waislamu ni vyema wakawa wanawashir ik isha kat ika masuala yao ya kijamii mapema na si kwa mpango huu.

Ust. Madina, akizungumzia kuhusu madai ya Waislamu kupinga ama kuzuia sensa, ambapo katika kikao hicho, DC alikuwa na kopi yake na kuisoma kwa viongozi hao, alisema kipeperushi hicho hakizuii zoezi la Sensa.

Akikifanua kipeperushi hicho, Ust. Madina, alisema kipeperushi hicho kimetoa msimamo wa Waislamu kwa serikali ili washiriki Sensa, kwanza tume huru ya Sensa, pili wawakilishi wa dini mbili kubwa na tatu kipengele cha Dini kirejeshwe.

Lakini pia chanzo hicho Inaendelea Uk. 12

Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa.Kwa mawasiliano:+255 22 2181577, +25 22 2182370, 0717 000065, 0786383820, 0754 261910E-mail: [email protected], [email protected]: wwwhajjtrusttz.org

Safari ya Hijja Hijiria 1433

AMIRAT wa Baraza Kuu la Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Bi Fatma Mdidi (kulia) akiwa pamoja na viongozi wenzake Bi Halima Sumaye (katikati) muda mfupi baada ya kuwasilisha maoni yao katika tume ya Kuratibu Katiba mpya hivi karibuni.