barua pepe: [email protected] jarida la uqab...

24
BARUA PEPE: [email protected] JARIDA LA UQAB 1 Page1

Upload: others

Post on 21-Oct-2020

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • BARUA PEPE: [email protected] JARIDA LA UQAB 1

    Pag

    e1

  • 2

    بسم هللا الرحمن الرحيم

    Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (swt), baraka, rehema na amani zimwendee Nabii wa Mwenyezi Mungu, familia yake na maswahaba zake na wale wanaomfuata…

    Kwa Ummah wa Kiislamu, ummah bora ulioletewa wanadamu… na wabebaji Dawah wema na wazuri… na kwa wageni adhimu wanaozuru ukurasa,

    Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

    Zipo siku zinazong’aa katika historia za mataifa ambazo ni chanzo cha ufahari wa

    mataifa hayo. Kwa hiyo itakuwaje ikiwa siku hizo zitakuwa ni katika kutimia kwa bishara njema za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw)? Bila shaka zitakuwa ni nyota zenye

    kung’aa angani, bali ni jua linalotoa nuru kwa ulimwengu na kulinyanyua taifa hilo juu angani… Na katika siku hizo tukufu, zipo siku za ukumbusho wa ukombozi wa Konstantinopoli… Al-Fatih alianza kuivamia na kuizingira Konstantinopoli kuanzia

    tarehe ishirini na sita ya Rabii’ al-Awwal mpaka ilipofunguliwa alfajiri ya tarehe ishirini ya mwezi huu wa Jumada al-Awwal 857 H, ikimaanisha kuwa kuzingira kulichukua

    muda wa takribani miezi miwili. Kisha Muhammad al-Fatih aliingia mjini kwa ushindi na kushuka kutoka katika farasi wake na kumsujudia Mwenyezi Mungu, akimshuruku Mwenyezi Mungu kwa ushindi huo na kufaulu huko. Kisha akaelekea katika Kanisa la

    Hagia Sophia ambapo Wabaizantino na watawa wao walikuwa wamekusanyika, akawapa ulinzi. Akaagiza kubadilishwa kwa Kanisa la Hagia Sophia kuwa msikiti na

    kuamrisha kujengwa kwa msikiti katika sehemu ya swahaba mtukufu Abu Ayoub Al-Ansari, ambapo alikuwa ni mmoja katika waliokuwa safu za mwanzo katika kampeni ya kuifungua Konstantinopoli na ndipo alifariki, rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe

    juu yake… Al-Fatih, ambaye aliitwa hivyo baada ya ukombozi na kuamua kuifanya Konstantinopoli kuwa mji mkuu wa dola yake ambayo kabla hapo ilikuwa Edirne, na

    kuita Konstantinopoli [Kostantiniyye] baada ya ukombozi wake kuwa “Islambol,” ikimaanisha mji wa Uislamu [Dar al-Islam] na kujulikana maarufu kama “Istanbul”. Al-Fatih kisha akaingia mjini na kwenda Hagia Sophia ambapo aliswali ndani yake na

    kuwa msikiti kwa neema, baraka na sifa za Mwenyezi Mungu… Na ulibakia kuwa msikiti

  • 3

    uliotakasika na wenye taadhima, uliostawi chini ya waumini, mpaka zama za wahalifu, Mustafa Kamal alipofaulu kupiga marufuku kuswali ndani yake na kuutia najisi na kuwa

    makumbusho kwa wale wanaokuja na kuondoka!

    Hivi ndivyo bishara njema ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ilivyo timizwa; ambaye katika Hadith yake tukufu iliyopokewa kutoka kwa Abdullah ibn Amr ibn Al-As aliyesema: “Tulipokuwa na Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) tukiandika, Nabii wa

    Mwenyezi Mungu aliulizwa, ni upi kati ya miji miwili utakaofunguliwa kwanza, Konstantinopoli au Roma? Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:« َمِديَنُة ِهَرْقَل

    ,Mji wa Heraclius utafunguliwa kwanza“«تُْفَتُح أَوَّالً، يَْعنِي ُقْسطَْنِطينِيَّةَ ikimaanisha Konstantinopoli.” Imesimuliwa na Ahmad katika Musnad yake na Al-

    Hakim katika Al-Mustadrak na akasema: “Hadith hii ni sahih kwa masharti ya msheikh wawili, na hawakuivua wao. Az-Zahabi ameizungumzia: “kwa masharti ya Bukhari na Muslim”. Pia katika Hadith tukufu iliyopokewa kutoka kwa Abdullah bin Bishr Al-

    Khathami kutoka kwa babake kwamba alimsikia Mtume (saw) akisema: « َّلَُتْفَتَحن Mutaifungua“«اْلُقْسطَْنِطينِيَُّة َفلَِنْعَم اْْلَِميُر أَِميُرَها َولَنِْعَم اْلَجْيُش َذلَِك اْلَجْيشُ

    Konstantinopoli, Amiri wake ni Amiri bora, na jeshi bora ni jeshi hilo.” Alisema, Maslama bin Abdul Malik aliniita na kuniuliza, kwa hiyo nikamtajia hiyo Hadith na hivyo basi akaivamia Konstantinopoli, imesimuliwa na Ahmad. Katika Mujma’

    Az-Zawaa’id, aliizungumzia na kusema: “Imesimuliwa na Ahmad, Al-Bazzar, Al-Tabarani na wanaume wake ni waaminifu…”

    Bishara njema hii ilitimizwa kupitia mikono ya kijana mwanamume, Muhammad al-

    Fatih, ambaye alikuwa na miaka ishirini na moja, lakini alikuwa ameandaliwa vyema tokea utotoni mwake. Babake Sultan Murad II alimlea na kumjenga kupitia mikono ya walimu bora wa zama zake, wakijumuisha Ahmad bin Ismail al-Kurani ambaye alitajwa

    na al-Suyuti kuwa mwalimu wa kwanza wa al-Fatih na alimzungumzia: “Alikuwa mwanachuoni wa kisheria, ambaye wanachuoni wa zama zake walishuhudia ubora na

    ustadi wake wa hali ya juu. Bali walikuwa wakimuita: Abu Hanifa wa zama zake.” Vilevile Sheikh Akshamsaddin Sungkar ambaye alikuwa wa kwanza kupanda akilini mwake hadith za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) juu ya “ukombozi wa

    Konstantinopoli” tangu utotoni mwake. Kwa hiyo kijana alikulia akilenga kufaulisha ukombozi kwa mikono yake… Sheikh Akshamsaddin alimfunza Muhammad al-Fatih

    misingi ya sayansi ya Qur’an, Hadith na Sunnah ya Mtume na Fiqhi pamoja na lugha za Kiarabu, Kifursi na Kituruki, pamoja na sayansi za maisha kama hesabu, falaki, historia… kwa kuongezea ujasiri wake katika kuongoza farasi na sanaa ya kupigana…

    Mwenyezi Mungu (swt) akamfadhilisha na kumbariki, kustahiki sifa kutoka kwa Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw). Al-Fatih alikuwa kiongozi bora na wanajeshi wake

    walikuwa bora, kwa kuwa mioyo yao ilikuwa imejaa Imani na nafsi zao zilikuwa

  • 4

    zimejisalimisha katika maandalizi na kuwa na ikhlass kwa jihad, walimnusuru Mwenyezi Mungu na Yeye akampa ushindi kwa ukombozi mtukufu, sifa zote ni kwa Mwenyezi

    Mungu, Bwana wa Ulimwengu.

    Al-Fatih alikuwa mtu aliye na ruwaza na mwenye maono na utambuzi wa kina. Kila alipoona tatizo alilishughulikia kwa usahihi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kila kikwazo kinapomtokezea, alikiondosha kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Alikumbana

    na vikwazo vitatu ambavyo alivitatua kwa akili yake makini na werevu wa hali ya juu:

    1-Wanajeshi wake walimlalamikia kuhusu baridi kali walipokuwa katika sehemu za wazi zilizozunguka kuta, kwa hiyo akawajengea ngome ili waweze kujihifadhi kila

    kunapokuwa na dharura. Hakutaka wanajeshi wasitishe uzingiraji lau ungeliendelea kwa muda na hivyo kurudi kama ilivyokuwa kwa majeshi ya Waislamu ya awali ambayo yaliivamia Konstantinopoli, lakini badala yake hakutaka kurudi isipokuwa

    mpaka kufunguliwa kwa Konstantinopoli kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…

    2- Pia, kuta za Konstantinopoli zilikuwa kuta tatu; kila mita chache kulikuwa na kuta baina yake. Hivyo basi, al-Fatih alishangazwa na suala hilo. Katika zama zao, hakukuwa na silaha zenye nguvu za kuzivunja. Bali, yenye nguvu zaidi ya zote ilikuwa

    panda ya kutupa mawe, sio ndogo kiukubwa lakini haitoshi kutoboa tundu katika ukuta wa ukubwa huo. Na kwa sababu Muhammad al-Fatih alikuwa anafuatilia uwezo wa

    kijeshi duniani, alikuja kugundua kwamba mmoja miongoni mwa wahandisi (Urban) wa Hangaria alikuwa amekuwa na fikra za kutengeneza mizinga maalum yenye nguvu za kuweza kuvunja kuta na Urban akaomba kumfanyia kazi Mfalme wa Konstantinopoli,

    lakini hakumjibu, kwa hiyo al-Fatih akampokea kwa wema na kumpa mshahara mkubwa na kila kitu anachohitaji kukamilisha uvumbuzi wake,

    Urban alijenga mizinga kwa msaada wa wahandisi wa Kiuthmaniya na al-Fatih

    aliwasimamia mwenyewe. Kabla hata miezi mitatu kupita Urban tayari alikuwa ametengeneza mizinga mitatu mikubwa, uzito wa kombora la mzinga lilikuwa takribani tani moja na nusu, hakupendelea kujaribu mizinga hiyo kwa kuhofia kwamba majibu

    yasiridhishe. Na hivyo Waroma wangelishuhudia hili wakiwa nyuma ya kuta zao na hili lingeathiri nguvu za Waislamu, kwa hiyo akafanya majaribio huko Edirne na yakafaulu.

    Akamshukuru Mwenyezi Mungu, na kuihamisha kutoka Edirne na kuipeleka mizinga karibu na kuta za Konstantinopoli ili kuzivunja na Waroma wangelijisalimisha…

    3-Kisha kulikuwepo na jambo jingine ambalo lilikuwa linamshughulisha, kwa kuwa alijua kwamba kuta za eneo la Ghuba zilikuwa dhaifu pembezoni mwa Konstantinopoli

    na licha ya Waroma kufahamu udhaifu wa kuta za upande wa Ghuba, walikuwa na

  • 5

    uhakika kwamba meli za Waislamu zisingeliweza kuwafikia kwa sababu ya kufungwa kwa lango la Ghuba kwa minyororo ya chuma, lakini al-Fatih kwa msaada wa

    Mwenyezi Mungu alikuwa amekatikiwa kuzitiririsha meli kupitia uso wa kilima cha Galata sawia na ukuta wa upande wa Ghuba (Pembe ya Dhahabu). Aliweka bao katika

    uso wa kilima na kumwaga viwango vikubwa vya mafuta na vilainishaji juu yake, kisha akazivuta meli juu yake. Na kwa usiku mmoja alifaulu kushusha meli 70 kwenda Ghuba. Hili liliwashtusha Waroma, ilipofika asubuhi na wakaona meli za Waislamu

    katika Ghuba, wakajaa uoga katika mioyo yao. Ushindi na ukombozi ulikuwa umefaulu, sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wa ulimwengu.

    Ndugu zangu wapendwa, Nilitaka kuwakumbusha baadhi ya matukio ya

    ukombozi wa Konstantinopoli kwa sababu tatu:

    Ya kwanza ni kukumbuka utukufu wake ili kila mwenye macho ataona utukufu wa

    Uislamu na Waislamu pale ambapo Uislamu wao unatekelezwa kivitendo. Ukafiri hautokuwepo, bali ukweli utakuwa juu na utanyanyuliwa kama Adhana (mwito wa

    kuswali) kwa Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa). Wafursi na Wabaizantino wakajisalimisha mbele yao, na hivi karibuni wataunganishwa, kwa Uwezo wa Mwenyezi

    Mungu, na dada wa Baizantino, Roma kwa kuamini sehemu ya bishara njema ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), ukombozi wa Roma.

    Ama ya pili, itulizeni mioyo yenu kwa kujihakikishia kutimia kwa bishara tatu nyingine za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa kuwa ya kwanza ishatimia. Mtume (saw)

    alitoa bishara njema za ukombozi wa Konstantinopoli, ukombozi wa Roma, kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume na kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa nguvu kubwa… Mtume (saw) anazungumza kutokamana na Wahyi, bishara njema tatu

    zilizobakia za Nabii zitatimizwa kwa idhini Yake, utukufu ni wake Yeye Subhannahu; lakini, hazitotimia kwa kushuka kwa malaiki kutoka mbinguni, na kutukukabishi sisi. Badala yake ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kwamba tumnusuru Mwenyezi Mungu na Yeye atupe ushindi Wake ili tuweze kusimamisha sheria Yake na

    kuutukuza muundo wa Dola Yake na kuandaa tunachoweza katika nguvu na kisha kupambana katika njia Yake. Kisha dunia itang’ara kwa bishara njema tatu zilizobakia na dunia itanawiri kwa kuwepo Khilafah kwa mara nyingine tena.

    Ama ya tatu, Kafiri Mmagharibi, pamoja na makhaini wa Kiarabu na Kituruki waliweza

    kuivunja Khilafah mnamo 1342 H – 1924 M na kuzingatia kuwa kuvunjwa huku ni sambamba na ukombozi wa Konstantinopoli, na hili likampa tena nguvu Kafiri Mmagharibi ambazo alikuwa amezipoteza. Wasiwasi wa Magharibi ukawa ni kuweka

    juhudi kubwa ili kuzuia kurudi tena kwa Khilafah ili isiweze kupoteza tena nguvu

  • 6

    walizozirudisha hususan kwa kuwa wamekuwa wakoloni wa nchi za Waislamu. Wanafuatilia kwa makini harakati ndani ya nchi za Waislamu, kwa hiyo ilipotangazwa

    kusimama kwa Hizb ut Tahrir mnamo 1372 H – 1953 M na ikawa wazi kwa Magharibi kwamba nguzo ya kazi za chama na suala lake nyeti ni kurudisha Khilafah tena na

    kwamba kiko makini katika kazi yake, Magharibi ikaamrisha vibaraka na watawala wake kukipiga marufuku chama na kukifuatilia kwa kuwashika na kuwatesa mpaka kupata shahada ndani ya baadhi ya maeneo na kuwafunga vifungo virefu na katika

    maeneo mengine kufikia kuwafunga maisha… Kisha wakaongeza njia za kudanganya, kughushi na kubadilisha ukweli pasina aibu…

    Na kwa hiyo ili hawa wapotoshaji wawe na athari, wakawafanya watu wanaotekeleza

    hatua hizi kuwa na majina ya Waislamu na kuvaa kama wao, hawa walifuatiwa na upotoshaji huu, na baadhi yao walitoka, walivunja viapo (an-Nakitheen) na walioadhibiwa, kutoka miongoni mwa waliokuwa katika chama hapo awali…

    Hivyo basi, aina hii wakajumuika na kushiriki katika upotoshaji, kughushi na

    kubadilisha ukweli na kila mmoja wao ana dori yake: makafiri, wanafiki na wale wanaoeneza uvumi, kisha baadhi yao wakaondoka, wakaadhibiwa na wakavunja viapo,

    na wale walio na maradhi katika mioyo yao, wameshiriki katika upotoshaji na mashambulizi dhidi ya Hizb. Walifuatilia hili kwa hatua zilizojaa sumu na kudanganya katika kila hatua. Walipokuwa wamefeli kusambaza uongo, wakaja na jingine,

    wakisahau kwamba wanachama wa chama wana akili zilizo makini na utambuzi wa haraka unaowawezesha kutofautisha baina ya baya na zuri, kwa hiyo hawakuruhusu

    uongo kupenya katika njia yao… Hivyo basi, licha ya njia za kuupamba uongo waliouzua licha ya kukithirisha majaribio ya udanganyifu dhidi ya ukweli ambao wamejikita ndani yake, hawakupata sikio linalosikiza kutoka katika wanachama wa

    chama au kutoka katika kila Muislamu aliye timamu. Badala yake walikuwa

    [ُه َشْيئاً َْْكَسَرابٍ بِِقيَعٍة يَْحَسُبُه الظَّْمآُن َماًء َحتَّى إَِذا َجاَءُه لَْم يَجِد]

    “Vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani, Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote.” [An-Nur: 39]

    Na kwa njama, kashfa na uovu wote dhidi ya chama na uongozi wake, wakidhania kwamba watakishawishi chama lakini walifeli kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na

    wakakata tamaa na hawakupata lolote zuri licha ya kiwango cha uongo wao, njama zao na uhadaifu wao kilipofikia,

    ي ُِئ إاِلَّ بِأَْهلِهِ ] [َواَل يَِحيُق اْلَمْكُر السَّ

  • 7

    “…na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya.” [Fatir: 43]

    [ ِ َمْكُرُهْم َوإِْن َكاَن َمْكُرُهْم َوقَ لْد َمَكُروا َمْكَرُهْم َوِعْنَد َّللاَّ [ تَُزوَل ِمْنُه اْلجِبَالُ ِْ

    “Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibrahim: 46].

    Kwa kutamatisha, misimamo yenu ndugu zangu iliyokita katika ukweli, nguvu na uwazi mbele ya kampeni za kufuatana dhidi ya ujumbe wa haki, unatukumbusha misimamo

    ya Maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwa kufuata misimamo ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), mtukufu na mwenye busara alipokabiliana na shari…

    Hivyo ndivyo misimamo yenu, iliyo madhubuti isiyodhoofika kwa shari na haitingishiki katika kipindi cha fitnah. Badala yake, ukakamavu wenu ni wenye nguvu na sauti zenu

    zinatamka haki. Munaitizama dunia mara moja na Akhera mara nyingi, kwa hiyo pongezi kwa chama kwa sababu kimewapata nyinyi na pongezi kwenu kwa kuwa na chama.

    َكاِة يََخاُفوَن َيوْ ] ِ َوإَِقاِم الصَََّلِة َوإِيَتاِء الزَّ ماً رَِجاٌل اَل تُْلِهيِهْم تَِجاَرٌة َواَل بَْيٌع َعْن ِذْكِر َّللاَّ

    َتَقلَُّب فِيِه اْلُقلُوُب َواْْلَْبَصارُ تَ ُ أَْحَسَن َما َعِملُوا َويَزِيَدُهْم ِمْن َفْضلِِه * لِيَْجزِيَُهُم َّللاَُّ يَْرُزُق َمْن يََشاُء بَِغْيرِ ِحَسابٍ [َوَّللاَّ

    “[Ni] wanaume ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu

    Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka – Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi

    Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” [An-Nur: 37-38]

    Mwisho wa kutamatisha, namuomba Mwenyezi Mungu (swt) atuwezeshe kutimia kwa bishara njema za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ili Khilafah ya Ummah huu iweze kurudi na baada ya hapo kuikomboa Al-Quds, na Roma itakombolewa kama

    ilivyotanguliwa na dadake… kutimia kwa hadith za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw)… Na pia tunamuomba Yeye, Utukufu uwe Kwake, atupe msaada kutoka Kwake ili tuweze

    kuboresha na kukita katika kazi ili tuwe tunaostahiki kupata ushindi wa Mwenyezi Mungu, Al-Aziz Al-Rahim.

    [ ِ يَْنُصُر َمْن يََشاُء وَويَْوَمئٍِذ يَْفَرُح اْلُمْؤِمُنوَن * بِ َنْصرِ َّللاَّ ِحيمُ َْ [ُهَو اْلَعزِيُز الرَّ

  • 8

    “Na siku hiyo Waumini watafurahi* Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-

    Rum: 4-5]

    Wa Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh Ndugi yenu,

    Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

    Ameer wa Hizb ut Tahrir Alhamisi, 7 Jumada Al-Awwal 1441 H 2/1/2020 M

  • 9

    Habari:

    Jumatano 18 Januari, kiongozi wa Urusi, Vladamir Putin na kiongozi wa Uturuki, rais Receip Tayyib Erdogan kwa pamoja walianzisha bomba kwa Bahari Nyeusi ambalo lita

    safirisha gesi kutoka Urusi kupitia Uturuki hadi Europa. Viongozi hao wawili walizindua ‘TurkStream’ mjini Istambul ambayo itabeba gesi kutoka bomba la ndani ya bahari lilio na urefu wa kilomita 930 kutoka Anapa iliopo sehemu za pwani ya bahari ya Urusi hadi

    KKiyikai magharibi mwa Istambuli kwa minajili ya matumizi ya ndani ya Uturuki, ilhali sehemu ya pili ya mradi huo utabeba gesi ya Urusi hadi kusini mashariki ya Europa

    kupitia Bulgeria, Serbia na Hungari. Hii nayo itawezesha Urusi kutopitisha bomba hilo la gesi hadi Europa nchini Ukrain. Mradi huu unazidisha mbele mahusiano na matangamano baina Urusi na Uturuki.

    Maelezo:

    Kwa kupitia kitendo hichi Erdogan amekuwa akiendeleza urithi wake kwa aibu kwa kumkumbatia mchinjaji wa kutoka Moskow. Badala ya kumkabili muuwaji Putin, ambae ni muhusika wa umwagaji damu, mchinjaji wa waisilamu maelfu wa Syria na kwa

    kumhifadhi Assad aliena kiu ya damu, Kiongozi wa Uturuki atafuta kuzidisha nguvu mkono na uchumi wa Katili wa kirusi, kumsaidia aendeleze mauiwaji ya halaiki ya

    waisilamu wa Ash-Sham, na pia kufanya Uturuki kuwa ni ya kuathirika mbeleni na maslahi ya Urusi. Necdet Pamir, kiongozi wa sera za Nishati katika

    Turkish Chamber of Petroleum Engineers, aliwahi kusema ya kwamba,” ingawa TurkStream itaboresha usambazaji ulo makinika wa gesi, Lakini itakuwa imeiacha Uturuki ‘kufungishwa kwa Urusi kwa shingo yake’ ”

  • 10

    Si tu Erdogran amefanya kazi mkono kwa mkono na warusi na wa Irani pamoja na wamagharibi dhidi ya mapinduzi ya Kiislamu nchini Syria kupitia makongamano ya

    kipumbavu na miito itwayo njia za amani iliyo na malengo ya kugawanya na kubadilisha lengo la kumtoa mchinjaji Bashar,bali amefanya juhudi za kuimarisha

    mafungamano na taifa la kikomonisti lililo na chuki kali dhidi ya uisilam na waisilamu na kuwa adui wazi wa umma wa kiisilamu na dini yao.Ni taifa ambalo limekuwa likiendesha mashtaka na kuwafunga vifungo virefu waisilamu wa kutoka Urusi na

    maeneo ya Tatari huko Krimea ili iwahofishe waache imani yao ya kiisilamu. Lakini haya yote hayana mizani kwa macho ya Erdogan kwa kuwa amezidisha

    mahusiano ya kijeshi na Moskow ikiwemo kubadilishana akili za kijeshi, kukubali kupokea nidhamu ya mizinga ya kirusi S-400 mwaka jana, na kukubali ushirikiano wakupiga doria kwa pamoja na warusi katika mipakani mwake na Syria.

    Erdogan kwa mara hubainisha wazo la kujiamini kuwa yeye ni mwili wa viongozi wa

    kale wa Ottomani lakini ghuba ya utofauti baina yake ni kubwa mno. Mwezi huu ndio unao tamautisha kumbukumbu za ukombozi wa mji wa Konstantinopol katika mwaka

    wa 857H-1453M na kiongozi mkuu wa Ottomani Sultan, kamanda Muhammad Al-Fathi, al maaruf Sultan Memed II. Huyu ndio mtu kwa hakika aliyeonyesha sifa za kiongozi wa Kiisilamu-kwani alielekeza maisha yake kwa kusukuma mbele gurudumu la dini na

    kufungua na kupanua mipaka ya kiisilamu ulimwenguni

    Tangu akiwa kijana, ufungamano wake wa ndani na uislam ulimjega kuwa na shaksia ambayo ilimtamanisha kupeana maisha yake kwa huduma ya Mola wake , Na kutaka kuikomboa mji mkuu wa Konstantinopoli ili aweze kuwa ni yule alie elezwa na bwana

    wetu Mtume {saw} pindi alipo sema: «اْلَجْيشُ َذلِكَ اْلَجْيشُ لَُتْفَتَحنَّ اْلُقْسطَْنِطينِيَّةُ َفلَِنْعمَ اْْلَِميرُ أَِميُرهَ ا َولَنِْعمَ »

    “Mutaifungua Constantinople, Amir wake atakuwa amir bora zaidi na jeshi bora zaidi ni jeshi hilo”

    Mapenzi yake yalikuwa si kuwapendeza na kushirikiana na wabazantayni na maadui wengine wa waisilamu bali nikuwashinda ili dini ya isilamu iwe juu ya dini zote duniani.

    Baada ya kuikomboa Konstantinopoli, Muhammad Al-Fathi alielekeza macho yake kuikomboa Europa ikiwemo Romi, ili aweze kutimiza bishara nyengine tena ya Mtume {saw}.

    Hi ndio sifa ya kiongozi anae hitajika….yule ambae anawahifadhi waisilamu na dini yao

    na kuueneza nuru ya uisilamu ulimwenguni, wala si yule anaeshirikiana katika njama dhidi ya isilamu na waumini, mwenye kuiipa nguvu mikono ya muuwaji dhalimu,

    anaepigana kwa manufaa yake pekee na mwenye kufanyia kazi ajenda ya madola

  • 11

    mageni. Walakini, Kiongozi sampuli hii ataibuka tu chini ya nidhamu ya kikweli ambayo kikweli ndio itakayo wakilisha maslahi ya umma na Islamu; Khilafah

    iliofungamanishwa na njia ya utume. Kwa hivyo, iwapo kama umma tutataka kuregea kwa viongozi wa kuu mithili ya Muhammad Al-Fathi, na kama tungelipendelea kuona

    ushindi mtukufu wa dini yetu kwa mara nyengine tena sawia na ukombozi wa Konstantinopoli na iwapo tutakuwa na hamu ya kutaka kushuhudia mafanikio ya bishara zengine za Allah{swt} na Mtume wake {saw} basi hatuna budi kuekeza juhudi

    zetu zote na kuwa macho kwa kusimamisha nidhamu ambayo matumaini na ndoto zitabadilishwa kuwa ni za ukweli:Dola ya Khilafah tukufu.Mola asema

    ُ َوَعدَ تِ َوَعِملُواْ ِمنُكم َءاَمُنواْ ٱلَِّذينَ ٱّللَّ ـٰ لَِح ـٰ َتخ لَِفنَُّهم ٱلصَّ ضِ فِى لَيَس ر َ لَفَ َڪَما ٱْل َتخ ٱس

    لِِهم ِمن ٱلَِّذينَ تََضٰى ٱلَِّذى ِديَنُہمُ لَُهم َولَُيَمك َِننَّ َقب لَُهم ٱر لَنَُّہم ْ دِ م ِن َولَُيبَد ِ فِِهم بَع ا َخو ًنً۬ أَم ُبُدونَنِى ْ رِكُ ونَ اَل يَع اْ بِى ُيش ـ ً۬ دَ َڪَفرَ َوَمن َشي و َذٲلِكَ بَع

    ُٰٓٮِٕكَ َْْفأ ـٰ ِسُقونَ ُهمُ لَ ـٰ َف ٱل

    “Allah ame ahidi wale miongoni mwenu ambao wameamini na wakafanya amali njema ya kwamba kwa hakika atawaruzuku katika ardhi na

    kuwarithisha nguvu,kama alivyowafanyia wale waliokuwepo kabla yao; ya kuwa ataanzisha uwongozi kwa dini yao,ile ambayo amewachagulia wao,:

    na yakuwa atawabadilishia hali zao,baada ya hofu waliokuwa wameishi nayo kwa amani na utulivu: na wata niabudu Mie pekee na wala hawatanishirikisha mie kamwe,’ iwapo mmoja wenu atakana imani baada

    ya haya,basi hao ni waasi na waovu.”[ An-Nur:55]

    Dr. Nazreen Nawaz Msimamizi wa kitengo cha wanawake -Afisi kuu ya Kati ya Habari

    Hizb ut Tahrir

  • 12

    Muhammad Al-Fatih ni mwenye kutoa mfano mbora kati ya umma pindi tukumbukapo matukio matukufu yaliopita ya waume ambao walikuwa viongozi na wala si watawala

    ambao wengi leo wanawachukiwa. Kwa kusoma ayah za Quran, twapata kukutana na Ayah kama vile ahadi ya Mwenyezi

    Mungu ni hakika: هِ أَْفَواًجا * َفَسبِ حْ بَِحْمدِ

    هِ َواْلَفْتحُ * َوَرأَْيتَ النَّاسَ يَْدُخلُونَ فِي ِدينِ اللَـّ إَِذا َجاءَ نَْصرُ اللَـّ َربِ كَ َواْسَتْغِفْرهُ إِنَّهُ َكانَ تَوَّابًا

    ”Pindi itakapo kuja nusra ya Mwenyezi Mungu na ishinde. Na utaona watu wakiingia kwa dini ya Allah makundi kwa makundi.Basi msabihi Mola wako

    na umtake msamaha, Hakika yeye ni mwingi wakukubali toba.” [An-Nasr: 1-3]

    Ushindi ni kwa wale wanaoutafuta na wanaomsaidia Mwenyezi Mungu {swt} ْخَرٰىَُوأ

    رِ اْلُمْؤِمنِينَ هِ َوَفْتحٌ َقرِيبٌ َوبَِش تُِحبُّونََها نَْصرٌ ِم نَ اللَـّ

    “Na mtapata neema ambayo mnaipenda-Ushindi kutoka kwa Allah na

    ukombozi unaokaribia,na wape bishara njema kwa waumini.” [As-Saff: 13] Tuchukue kijana mdogo lakini mkuu Muhammad Al-Fatih kama mfano, babake na

    walezi wake walifahamu vipi kauli ya Allah{swt} ilivyokuwa na uzito…si tu kisomo cha ayah kuregelewa lakini kwa udadisi wa ndani wa kauli yake Mola {swt} wa baini kipi chakuhitajika ili kupata ushindi….Ushindi ulio na thamani kwa mwenyewe Mtume

    {saw} kwa kusema kuwa kiongozi kama huyo amebarikiwa. Mtume {saw} asema, «ْعمَ اْلَجْيشُ َذلِكَ اْلَجْيشُ ِْلَُتْفَتَحنَّ الْ ُقْسطَْنِطيِنيَّةُ َفلَنِْعمَ اْْلَِميرُ أَِميُرَها َولَن»

    “Kwa hakika mutaikomboa Konstantinopoli. Vipi bora alioje kiongozi wake, na bora lilioje jeshi hilo litakuwa.”

    http://tanzil.net/#trans/en.sahih/110:3

  • 13

    ه ُقوا ف ي َسب يل اللَـّ تُنف ح َوَما لَُكم أَّلَّ َفت

    َتو ي م نُكم مَّن أَنَفقَ م ن َقب ل ال َر ض ّلَ يَس َماَوات َواْل يَراثُ السَّ ه م َول لَـّ

    َملُونَ َخب ير هُ ب َما تَع َنى َواللَـّ ُحس

    هُ ال دُ َوَقاتَلُوا َوُكّلً َوَعدَ اللَـّ ينَ أَنَفُقوا م ن بَع ِّنَ الَّذ ظَمُ َدَرَجة م ئ كَ أَع ـ ولَُ َوَقاتَلَ أ

    “Na kwanini musiwe ni wenye kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ilhali kwake yeye ndio kulioko urithi wa mbinguni na ardhini? Hamuko sawa kati yenu, wako wale ambao walitoa katika ukombozi {wa Makka} na wakapigana {na wale walifanya hivyo baada

    yake}.Hao ni wakubwa kwa daraja kuliku wale waliotoa baadae na kupigana. Lakini kwa wote Allah amewaahidi ujira bora.Na Mola ni mjuzi wa kufahamu yale munayo yatenda.” [al-Hadid: 10]

    Aya ilio zungumzwa hapo juu, ni yakuamrisha kufanya maandalizi ya kila Nyanja, kuazia ya kijeshi ikiwemo vifaa, mikakati, nguvu kazi na uchaji mungu unao hitajika kuweza kufaulu kwa ajabu wakati huo

    َن َهارُ ت َها اْل ر ي م ن تَح مَ َجنَّات تَج يَو َراُكمُ ال ي َمان ه م ُبش

    يه م َوب أَ َعى نُوُرُهم بَي نَ أَي د َنات يَس م ُمؤ ن ينَ َوال م مَ تََرى ال ُمؤ يَو

    يمُ زُ ال َعظ ل كَ ُهوَ ال َفو ينَ ف يَها َذ َخال د

    “Katika siku utakayo ona waumini wa kiume na wakike, mwangaza wao ukiwatangulia, na ubavuni mwao wakulia [itasemwa},”Mazuri yapendezayo yenu leo ni mabustani ambayo chini yake ni mito ipitayo, ambayo kwayo mutaishi milele,”Uko ndio kufaulu

    kukubwa.”[al-Hadid: 12] Isitoshe aya hizi na zengine nyingi ni alama ya matumaini na mwangaza kwa waisilamu wa leo….

    Amerika, Uingereza, Urusi na au Uchina,.. uvamizi wao wa ardhi za waisilamu na eti uharibifu wa dhamana utokeyao kila mara ilhali hakuna anae hisabiwa kosa kama vile mara kwa mara ni vyenye kufanyika kwa maafisa wa Kiamerika pindi wanapo pasha habari ya amali zao… Maneno yasiyo

    tambuwa maisha ya wanadamu na uhai wao na kuwaumiza waliobaki baada ya kumaliza kutekeleza malengo ya dola.

    Wakimbizi waliotapakaa,vilema ambao maisha yao daima yamekuwa malemavu, wajane, wenye makovu ya kunajisiwa,kuteswa na kuachwa na njaa…haya ni natija za madola ya leo.Lakini je kipi

    kinawaweka waisilamu kuwa wakweli kwa dini yao na kwa aqida yao?

    Akida ya la illah illah Allah Muhammad Rasuul Allah’ ndio humsukuma mja kuangalia mbele ya hali iliopo na kujaribu kutafuta suluhu la kumaliza janga hili, Akida hii ambayo ndio nyuzi ya umma wa

    kiisilamu hutembea kupitia mishipa ya umma. Akida hii lazima ishibishwe na vitendo kama alivyo amrisha Mola {swt}.Na hili laonekana kwa wengi wa waisilamu hata kama majeshi yao yakawa

    yamebaki kuganda pambizoni mwao.

    Quran ya Mwenyezi Mungi na Bishara za Mtume{saw} lazima zitafakariwe kwa mapana ili umma uweze kubadili umaskini pasi na kuacha dini yao hivyo basi kupata thawabu za balaa na bila hata

    kukata tama kwa kuanguka bele ya madola. Je kipi kinahitajika? Vipi Muhammad Al-Fathi aliweza kufaulu kupata ushindi kwa kurasa za historia na kukumbukwa kwa maombi ya waisilamu hadi leo? Quran huwa ni yenye kuongea illa ikiwa basi

    tutakuwa ni watu wenyekusikia maneno yake…. َينَ م ن َعف َتض َوَما لَُكم ّلَ تَُقات لُونَ ف ي َسب يل ّللاَّ َوال ُمس َعل لََنا َعل لََنا م ن لَُدن كَ َول يًا َواج لَُها َواج يَة الظَّال م أَه ه ال َقر ذ َنا م ن َه ر ج ينَ يَُقولُونَ َربََّنا أَخ ذ

    و ل َدان الَّالرِّ َجال وَ النِّ َساء َوال

    ا ير م ن لَُدن كَ نَص “Vipi ukawa ni mwenye kukataa kupigana kwa ajili ya Allah na kwa wasiojiweza

  • 14

    wanaume,wanawake na watoto ambao husema,”Mola wetu.tuongoze hadi tupata uhuru, nje ya mji huu wa wadhalimu.kupitia neema zako,tupe atakae tuhifadhi na msaidizi “[An-

    Nisa 4:75] ي طَان إ نَّ َكي دَ ل يَاءَ الشَّ اُغوت َفَقات لُوا أَو

    ينَ كَ َفُروا ُيَقات لُونَ ف ي َسب يل الطَّ ذ ينَ آَمُنوا ُيَقات لُونَ ف ي َسب يل ّللاَّ َوالَّ ذ

    الَّا يف ي طَان َكانَ َضع الشَّ

    “Wale walioamini hupigana kwa njia ya Allah .Na wale wasio amini hupigana kwa njia ya shetani. Kwa hivyo nyinyi waumini piganeni na marafiki wa shetani.Kwa hakika kaida za shetani ni dhaifu.” [An-Nisa 4:76]

    Ushindi ni kwa wale wanao msaidia Allah ….na ni ahadi walioahidiwa waumini na Mola wao mwenyewe. Na ahadi hii kutoka kwa Muumba wetu ni Aqida, na ni imani yetu ya hakika. Sasa kile kinacho hitajika ni maadalizi…kumakinisha aqidah. kusoma hali halisi ya maisha ya sasa na

    zamani na kubuni elimu ya kivitendo na maandalizi ya kusimama mbele ya dola za leo bila uwoga wala shaka ya uweza. Ama Aqidah ni sehemu mojawapo ya maandalizi na bila kwayo hapana

    mafanikio wala ushindi. Kutafuta kuwa mpokezi wa bishara za Mtume {saw}. Mola {swt} atuamrisha لَُمونَُهمُ , ه َوَعُدوَُّكم َوآَخر ينَ م ن ُدون ه م ّلَ تَع

    ُبونَ ب ه َعُدوَّ اللَـّ ه َخي ل تُر ة َوم ن ر ِّبَاط ال ِّن ُقوَّ ُتم م َتطَع ا اس وا لَُهم مَّ

    دُّ َوأَع إ لَي ُكم َوأَنُتم ّلَ تُظ لَُمونَ

    ه يَُوفَّ ء ف ي َسب يل اللَـّ ُقوا م ن َشي لَُمُهم َوَما تُنف هُ يَع اللَـّ

    “Na waadalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari tayari ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu na wengineo ambao hamuwajui lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mukitoa chochote katika njia ya Mola wenu

    mutarudishiwa na wala nyie hamtadhulumiwa. [Al-Anfal: 60]

    Na kwa hio Muhammad Al –Fathi alifanikiwa kupata moja kati ya bishara za Mtume {saw] mwakani

    1453 M, na kuna mbili zengine ambazo bado zingali kufanikishwa. Nani ata tangazia ulimwengu kuwa dola la Khilafah kwa njia ya utume imesimama? Dola ambayo kwamba ndio itakayo poromosha vibanzi vya madola katika ulimwengu wa kiisilamu? Ninani atapata

    utukufu wa tendo kubwa hapa ulimwenguni na akhera? Mambo matatu ambayo Mtume {saw}..Mtume ambae, hasemi illa kwa wahyi, Thawban aeleza ya kwamba Mtume {saw} alisema: َزي ن » : َكن

    يتُ ال ط ع َُها َوأ ن ُكَها َما ُزو يَ ل ي م

    لُغُ ُمل ت ي َسيَب مََُّ َزَوى ل يَ اْلَر ضَ َفَرأَي تُ َمَشار َقَها َوَمَغار بَهَ ا َوإ نَّ أ ّللاَّ

    إ نَّ

    ه م َوى أَن ُفس طَ َعلَي ه م َعُدًوا م ن س ة َوأَنَّ ّلَ ُيَسلِّ ل َكَها ب َسَنة َعامَّ ت ي أَن ّلَ ُيه َفرَ َوإ نِّ ي َسأَل تُ َربِّ ي ْلُمَّ َمرَ َواْلَص اْلَح

    ل َكُهم ه ُت كَ أَن ّلَ أ طَي ُتكَ ْلُمَّ َوإ نِّ ي أَع

    َربِّ ي َقالَ يَا ُمَحمَّدُ إ نِّ ي إ َذا َقَضي تُ َقَضاء َفإ نَّهُ ّلَ ُيَردَُّتب يحَ بَي َضَتُهم َوإ نَّ َفيَس

    طَار َها أَو َتَمعَ َعلَي ه م َمن ب أَق تَ ب يحَ بَي َضَتُهم َولَو اج ه م َفيَس طَ َعلَي ه م َعُدًوا م ن س َوى أَن ُفس

    َسلُِّة َوأَن ّلَ أ ب َسَنة َعامَّ

    ا ض ُضُهم بَع ب ي بَع ا َويَس ض ل كُ بَع ُضُهم ُيه طَار َها َحتَّى يَُكونَ بَع «َقالَ َمن بَي نَ أَق

    “Kwa hakika Allah alinikunjulia dunia na nikaona mashariki yake na magharibi yake. Na kwakweli , uwongozi wa umma wangu utafikia hadi pale nilipoonyeshwa mimi. Na

    nimekabidhiwa hazina mbili,nyeupe na nyeusi. Na nilimuomba Mola wangu ya kwamba Umma wangu usiangamie kwa njaa, na wala asiwe ni wenye kuwaajalia wawe ni

    wenyekushindwa na maadui zao wan je,hadi wafika katika moyo wa nguvu zao. Mola wangu akasema: Ewe Muhammad! Pindi ninampo amrisha jambo haliregeshwi.Nimeamrisha kuutunuku umma wako ya kwamba hautaangamizwa na baa

    la njaa na wala hautakabiliwa na kushindwa na maadui nje ya wao hadi kufika katika moyo wao wa nguvu hata kama wataugama kutoka sehemu zote ,” Au akasema:” kwa baaadhi ya maeneo.Lakini wengine watawaharibu wengine na wengine watawashika

    mateka wengine,”

  • 15

    Wakati daawah ilipo kuwa katika hatua za mwanzo mjini Makka, Khabbab bin Al-Arat (ra) alimjia Mtume {saw} nyakati za udhaifu na mateso

    ، ُقل َنا . بَة لِّ ال َكع َدة لَهُ ف ي ظ د ُبر وَ ُمَتَوسِّ نَا إ لَى َرُسول ّللاَّ صلى هللا عليه وسلم َوه َعن َخبَّاب ب ن اْلََرتِّ ، َقالَ َشَكو رُ لََنا ص َتن َعلُ ف يه ، َفُيَجاءُ لَهُ أَّلَ تَس َفرُ لَهُ ف ي اْلَر ض َفُيج َ لََنا َقالَ «َكانَ الرَُّجلُ ف يَمن َقب لَُكم ُيح ُعو ّللاَّ أَّلَ تَد ه م ، َما ُدونَ لَح يد َشاط ال حَ د ب أَم

    َشطُ ، َوُيم ين ه هُ َذل كَ َعن د ، َوَما يَُصدُّ َنَتي ن ب اث

    ه َفُيَشقُّ س َشار ، َفُيوَضعُ َعلَى َرأ ن م

    ب ال

    ين ه هُ َذل كَ َعن د رَ ،م ن َعظ م أَو َعَصب ، َوَما يَُصدُّ َت، َوّللاَّ لَيُت مَّنَّ َهَذا اْلَم َرَمو َعاءَ إ لَى َحض يرَ الرَّاك بُ م ن َصن َحتَّى يَس ج لُونَ َتع ئ بَ َعلَى َغَنم ه ، َولَك نَّكُ م تَس َ أَو الذِّ ّللاَّ

    ّلَ يََخافُ إ ّلَّ“Tulilalama kwa Mtume {saw} dhidi ya mateso wakati alipokuwa amekaa kwa kivuli cha

    Ka’ba huku ametegemea .Tukasema kwake yeye,”Je utatuombea nusura sisi? Je utatuombea kwa Allah?” Akasema miongoni mwa waliopita kabla yenu,mwanamume muumini alikuwa akiwekwa shimoni alilochimbiwa yeye na msumeno ungeliwekwa kwa

    kichwa chake na kukatwa vipande viwili na hata hivyo bado adhabu hio haingelimfanya awache dini yake. Mwili wake ungelichanwa na kichanio cha chuma ambacho

    kingelidondoa ngozi yake kutoka mifupa na mishipa na hata hivyo asiwe ni mwenye kuacha dini yake.Naapa kwa Mola ,Dini hii itafaulu hadi pale msafiri atasafiri Sanaa Hadrarmaut pasi na hofu illa ya Allah, au mbwa mwitu kwa kondoo wake,lakini nyie watu

    mna haraka.” Kiapo ambacho Mtume {saw} aliapia: “Naapa kwa Allah Dini hii (i.e. Islam) ita faulu,” alisema, “Wallahi” kuhakikisha na kusisitiza ya kwamba ushindi utapatikana kwa

    waumini.Kwakeli waumini hushikwa na huzuni,kutosubiria,machovu: laikini kwa ayah na hadithi hizi,Mioyo yao ina jazika na kuhamasika kutimiza ahadi ya bishara ya pili ya Mtume {saw}…. َهاج النُُّبوَّة » , ن َّلَفة َعلَى م ثُمَّ تَُكونُ خ

    “…na kisha Itarudi Khilafah kwa njia ya Utume.” Maneno yalio tamkwa na ulimi ulio barikiwa. Hapa ayah na hadithi hizi za piga mawimbi pande zote akilini ili kujenga nyuzi kwa vijana wa leo

    ambao itawasababisha wao kutoka kwa kuvunja ganda la uzembe na kwa wanajeshi waisilamu kutoka nje ya hali ya kutojifahamu.

    Uisilamu utakuwa na ushindi bila shaka lakini kwa kupitia mikono ya nani ndio haya yatapatikana? Hii hapa ni mashindano ya kushindania kupata tuzo hilo. Hii itatupa matumaini –utulivu wa kuwa uisilamu utaregeshwa tena. Ili nusra ije…..sisi kama waisilamu lazima tucheze dori yetu kwa uwezo

    wa juu. Na hili tutahesabiwa nalo….kuajibika dhidi ya kutoajibika- ….na wala hatutahisabiwa juu ya lini itakuja kwani hilo lipo kwa mikono ya Mwenyezi Mungu {swt} pekee. Hivyo basi kupata uzoefu wa

    furaha ya nuru ya uisilamu ndani ya Dola yake. يمُ َعز يزُ الرَّح

    ه يَنُصرُ َمن يََشاءُ َوُهوَ ال ر اللَـّ ُنونَ * ب َنص م ُمؤ َرحُ ال َمئ ذ يَف َويَو

    “Na siku hio waumini watafurahia.Kwa ushindi wa Allah.Humpaushindi amtakae na yeye ni mwenye nguvu mwenye huruma.” [Ar-Rum 4-5]

    Manal Bade

  • 16

    Katika maidhinisho ya Hijri ya ukombozi wa mji wa Consatantinople na

    Sultan Muhammad Al-Fathi twapenda kubainisha dori ya chuma kwa jeshi. Mizinga ya chuma ilioundwa mahsusi ilikuwa na dori kubwa katika kuizingira na

    kuikomboa Konstantinople mnamo mtarehe 20th Jumada Al Awwal. Sultan Muhammad Al Fatih, ambae jeshi lake Mtume {saw} alisema kuwa ni ََولَِنْعم

    jeshi bora’ liliweza kutumia chuma ambacho kilitumiwa kujenga mizinga‘ اْلَجْيشُ bora kwa wakati ule kuishinda ngome bora kwa wakati huo hivyo basi kuwezesha kutimiza ahadi ya kwanza ya bishara ya Mtume{saw}, kwa uweza wa mungu,

    Kuanguka kwa Konstantinople ndio ilikuwa kiazilishi cha kusimamisha uisilamu bara Europa.

    Pindi Mola alipo umba ulimwengu kama makaazi ya mwanadamu, alijaalia riziki ndani yake ili ituwezeshe kuishi kwa mwenendo autakao Mwenyezi Mungu{swt]. Alitumakinisha duniani na akajaalia maisha ndani yake ili tuweze kuishi kwa wepesi na

    faraja. Mola {SWT} asema,” نَّاُكمْ فِي اْلَْرضِ َوَجَعْلَنا لَُكمْ فِيَها َمَعايِشَ َقلِيَل ,

    مَّا تَْشُكُرونَ ًَْولََقدْ َمكَّ

    “Na hakika tumekuekeni katika ardhi na kujaaliandani yake njia za kutafutia maisha:Ni kuchache kushukuru kwenu” [7:10]

    Katika njia za kutafutia maisha hapa duniani, zipo nyenginezo zinacheza dori kubwa zaidi katika kutuezesha sisi kuishi vyema. Na moja kati ya hizo ni utumizi wa vyuma.

    Mapambo tunayo vyaa, sarafu tuzitumiazo, vifaa, silaha, viwanda vya kisasa ambavyo kwayo tumeendelea kwa kiasi kikubwa, vyote hivi vimeonyesha umuhimu wa chuma.

  • 17

    Laiti matumizi ya chuma hayangejulikana, basi mwanadamu bado angelibaki katika zama za mawe bila hata kuendelea zaidi kwa mujibu wa swala la vitu vya kimadania.

    Zama za shaba,bronze na iron na kwasasa zama za kiviwanda, zote hizi hazinge shuhudiwa na mwanadamu iwapo matumizi ya chuma hayange julikana .Hii ni kwa

    upande wa kimada wa matumizi ya chuma. Ama katika upande wa nguvu ya chuma, taifa lililokuwa lamiliki chuma basi lilikuwa

    ndio liko juu ya wengine. Hatimae, uvumbuzi wa kila chuma na njia zake za uvunaji ilikuwa muhimu kwa majeshi katika uwanja wa vita.Taifa lililokuwa na ilimu ya

    utengezaji wa ironi lilikuwa liko juu ya lile lililokuwa na ilimu ya bronze, ..chuma hafifu kikilinganishwa na ironi. Wanajeshi wa Mwenyezi mungu walitumia nguvu hizi kwa kuwasaidia mitume na dini

    ya Mwenyezi Mungu kutawala. Nabii Daudi [as] alifunzwa matumizi ya chuma ambayo kutokamana kwayo alipata riziki yake na kuhami wanajeshi dhidi ya majeraha kwa

    utumizi wa bahasha ya koti.

    Hii hapa ni baadhi ya uchunguzi juu ya utumiaji na ilimu ya vyuma kwa mwanaadamu ambao ni muhimu ili kubaini majukumu ya wanajeshi wetu juu ya utumizi wa vyuma:

    Ironi ndio chuma chenye nguvu: Vyuma vingi vilivyohitajika kutengeza silaha vilikuwepo kwa umbile la madini au

    misombo iitwayo mitapo. Madini kama vile dhahabu na fedha ni ya zamani na kwakuwa ni laini mno kwa kutengezea vifaa yalifungika kutengeza mapambo pekee. Ama kuhusu shaba igawa ni ya zamani na chache iliweza kudumishwa kwa kupigwa na

    nyundo au kutengezwa basi ikawa ni nzuri kutumika kutengezea vifaa. Kwa namna hii ndio ilipelekea kujiwa kwa zama za shaba ambapo vifaa vilijengwa kwa shaba kwa

    matumizi ya kulimia na haja nyengine. Lakini kwa kuwa shaba ina ulaini mchache, ilikuwa na thamani chache kwa ujezi wa silaha. Lakini kile kilichoipa mataifa kusonga mbele kwa vipimo vya silaha ni kufua shaba na kuichnaganya na chuma cha mkebe

    kupata chuma cha bronzi. Hii ikawa ni yenye kuzalisha zama za bronzi. Kisha ilimu ya kuwa ironi ingeliwezekana kuchukuliwa kwa kuchomwa na madini kwa kuwepo makaa

    na kuiongeza nguvu kwa kuipiga na nyundo basi ndio kulileta athari kubwa katika silaha za zama za zamani. Ironi hii iliyopigwa manyundo inanguvu zaidi kuliko chuma cha bronzi. Mataifa yaliokuwa yamemiliki taaluma ya chuma cha ironi katika upande

    wa kivita yalikuwa na uhakika wa ushindi dhidi ya wale wasiokuwa na taaluma hio. Kinyume na chuma cha bronze ambacho kilihitaji kuwepo kwa chuma cha mkebe

    ambacho kilikuwa nadra kupatikana, Chuma cha ironi kilikuwa chapatikana kwa wingi hivyo basi kuongeza faida zaidi dhidi ya chuma cha bronzi. Isitoshe ilikuwa jambo

  • 18

    lisiloepukika kwa wale waliokuwa wamemiliki silaha zilizo tengezwa na bronze kubadilisha kwa zile za kutewngezwa na ironi hivyo baasi kuzalisha zama za ironi.

    Kwa nyakati hizi mataifa yalikuwa saa zote yapo vitani na yalikuwa ya kitengeza mifano tofauti ya kila silaha zilizokuwa zimetengezewa kwa miaka mingi mbeleni hadi

    pale kulipo vumbuliwa unga wa bunduki. Dawud (as) aliwahi tumia nguvu hii ya chuma pamoja na unabii wake na utawala wake katika kumsaidia Mwenyezi Mungu . Asema Mola {swt} َاْلُمْلكَ َواْلِحْكَمة ُ َوآتَاهُ َّللا

    َوَعلََّمهُ ِممَّا يََشاء“Allah alimpa yeye Daud utawala, hikima{unabii} na akamfunza kile Mola

    {swt} aridhishwa nacho.” [2:251] Moja kati ya vitu Mwenyezi Mungu alimfunza nacho Dudi{as} ni utumiaji wa chuma ili kutengeza Makoti ya bahasha ya chuma. Mola (swt) asema, َْوأَلَنَّا لَهُ اْلَحِديدَ * أَنِ اْعَمل

    ْردِ رْ فِي السَّ َواْعَملُوا َصالًِحا إِن ِي بَِما تَْعَملُونَ بَِصيرٌ َسابَِغاتٍ َوَقد ِ“…tengeneza nguo za chuma pana na kadiria sawa katika kuunganisha, na

    tendeni mema Hakika Mimi ninayaona vyema mnayo yatenda.” [34:10–11] Na katika ayah nyengine , Allah (swt) asema, ْمَناهُ َصنْ َعةَ لَُبوسٍ لَُّكمْ لُِتْحِصَنُكم

    َوَعلَّ

    م ِن بَْأِسُكمْ َفَهلْ أَنُتمْ َشاكُِرونَ “Na tukamfunza kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu, Je mtakuwa wenye kushukuru? ” [21:80]

    Jukumu la majeshi:

    Kulinda nchi na kuvamia ardhi zengine ni mojawapo ya athari za ghariza za kuhifadhi maisha hivyo basi kuwepo kwa majeshi. Lakini katika ayah ifuatayo, Mola {swt} afafanua ipi sababu kuu ya kuwepo kwa jeshi, ٍالنَّاسَ بَْعَضُهمْ بَِبْعض ِ َولَْوالَ َدْفعُ َّللا

    َ ُذو َفْضلٍ َعلَى اْلَعالَِمينَ لََّفَسَدتِ اْلَْرضُ َولَـكِنَّ َّللا “Na iwapo isingekuwa kwa Allah swt}kuangalia watu kwa wengine,dunia

    ingelikuwa imefisidika,lakini Mola ni mwingi wa fadhila kwa ulimwengu.” [2:251] Mwenyezi Mungu {swt} aeleza maneno haya baada ya kumtaja Daudi [as] na

    wanajeshi wake ambao walimshinda vita Thaluth na watu wake ambao walikuwa wafisadi kaika ardhi. Mwanachuoni bora Sheikh Ata Bin Abu Al Rashtah afafanua katika

    tafsir ya ayah hii kuwa , َّل فرض القتال في سبيل هللا لردع اهل الشرور والفس اداي َولَو “I.e.na laiti haingejuzishwa kupigana kwa njia ya Mola{swt} ili kuwazuia watu walio na madhara na wafisadi{ dunia ingelikuwa imefisidika}[Tayseer

    Fi Usuli Tafsir].

    Ibn Abbas (ra)asema: ن يَن م ُمؤ ر ُكوَن َفَقَتلُوا ال ُمش ل م يَن لََغلََب ال ُع ّللاَّ ال َعُدوَّ ب ُجُنود ال ُمس َّل َدف َولَو

    دَ ب َّلَد َوال َمَساج َوَخرَُّبوا ال

  • 19

    “Na laiti haige kuwa ni Allah kuwazuia maadui kwa majeshi ya kiisilamu,washirikina wangeli wauwa waisilamu na kuharibu ardhi zao na

    misikiti [Tafsir Qurtubi 3/260].

    Kwa hivyo, niwazi hapa Mola [swt} ame bainisha majukumu ya majeshi nayo ni kuondoa ufisadi wa aina yoyote katika ardhi na hii ni tofauti na majukumu waliokabidhiwa majeshi ya leo na dola zao, kwa kuwaamrisha waheshimu mipaka ya

    mataifa ambayo yana sababisha ufisadi na kwa kuzuia watu wasishikamane na uisilamu, kuwauwa na kuwafukuza. Bali wanaita majeshi yao kushirikiana na mataifa

    ambayo haswa ni yenye kusababisha ufisadi kwa kisingizio cha usalama wa kitaifa. Kwa kufanya hivyo, nawo pia wakawa wafisadi au sehemu ya ufisadi badala ya wao kuuondoa ufisadi

    Ama kuondoa ufisadi katika ardhi, hili lapatikana kwa kusimamisha haki juu yake nayo ni kwa kutabikisha kile alo leta Mtume wetu{saw}, Na Quran kutoka kwa Mwenyezi

    Mungu {swt}. Asema Mola (swt), َْرَسْلَنا ُرُسلََنا بِاْلبَي َِناتِ َوأَنَزْلَنا َمَعُهمُ اْلكَِتابلََقدْ أَ

    َوالْ ِميَزانَ لِيَُقومَ النَّاسُ بِاْلِقْسطِ

    “Tayari tusha watumiliza mitume yetu na hoja wazi pamoja na vitabu na usawa ili watu watabikishe haki.” [57:25] Hamna haki yaweza tabikishwa ima na illmania au tawala ya kifalme pasi na yale

    alioleta Mtume {saw] kutoka kwa Allah {swt]. Nabii Daud{as] alitabikisha haki ardhini kwa kupitia unabii wake, utawala wake na kile alichofunzwa na Mola wake ikiwemo

    ilimu ya chuma. Tunae Mtume {saw} ambae amekuja na hoja wazii kutoka kwa Mwenyezi Mungu [swt] na tunacho kitabu Al-Quran ambacho kwayo twaweza kusimamisha haki katika ardhi.

    Je haijakuwa ni wakati kwa wanajeshi waisilamu, ambao wanamiliki ilimu ya chuma kama nguvu ya kijeshi-kinyume na watu wakawaida ambao wao wanamiliki ilimu hii

    kwa manaufaa ya kibinafsi tu,.. Kumsaidia Mola wao na Mtume {saw} alie ghaibu kwasasa kwa kusimamisha Uisilamu ambao utaondo aina zote za ufisadi? Je haijakuwa ni kwa wanajeshi waisilamu kutanabahi kwa ayah ambazo

    zinawazungumzia wao na wala si maswahaba wa Mtume {saw} ambao wao tayari washa msaidia wakiwa mbele yake? ….Kama vile Allah (swt) asemavyo,

    ُ َمن يَنُصُرهُ َوُرُسلَهُ بِاْلَغْيبِ إِنَّ َوأَنَزْلَنا اْلَحِديدَ فِيهِ بَْأسٌ َشِديدٌ َوَمَنافِعُ لِلنَّاسِ َولَِيْعلَمَ َّللاَّ َعزِيزٌ

    َ َقِوي na tuliteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa…“ َّللاَّkwa watu na ili Mwenyezi Mungu amjue anae mnusuru Yeye na mitume

    yake kwa ghaibu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nngu Mwenye

    kushinda [57:25]

  • 20

    Imam Qurtubi asema katika maoni yake juu ya ayah hii ya kwamba, ” اَل يََرْونَُهمْ )بِاْلَغْيبِ( أَْي َوُهمْ “)kwa ghaibu( i.e. wale ambao kwamba hawaoni

    mitume” [Tafsir Qurtubi 261/17]

    Je haijakuwa ni wakati kwa wanajeshi waisilamu kutanabahi kwa ayah hizi na kumpa nguvu Allah{swt} na Mtume wake {saw] ..kwa kutokuwepo kwake ..basi kuipa nusra Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah kwa njia ya utume ambayo itatabikisha haki juu

    ya ardhi na kile alolexha Mtume wetu kutoka kwa Allah{swt}!

    َ يَُحول ِ َولِلرَُّسولِ إَِذا َدَعاكُ م لَِما ُيْحيِيُكمْ َواْعلَُمواْ أَنَّ َّللا ُْيَا أَيَُّها الَِّذينَ آَمُنواْ اْسَتجِيُبواْ ّلِل بَْينَ اْلَمْرءِ َوَقْلبِهِ َوأَنَّهُ إِلَْيهِ تُْحَشُرونَ “ Enyi mlio amini,itikieni mwito wa Allah na mtume wake pindi anapo

    muiteni nyinyi kwa yale ambayo yatakayo wapeni maisha.Najuweni kuwa Mola huingilia katui baina ya mja na Moyo wake na kwake yeye

    mutakusanywa.” [8:24]

    Muhammad ibn Farooq

  • 21

    Ijumaa, 22 Jumadal 1 1441 M

    Chini ya uwongozi wa Ameer wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni bora, Ata Bin Khalil Abu

    Al-Rashtah…Mola amuhifadhi, Afisi ya Kati ya Habari ya Hizb ut Tahrir imeanzisha

    kampeni ya kiulimwengu ya kuangazia hafla ya hijiria ya ukombozi wa Konstantinople

    {mji wa Heraclius} ambao ulizingirwa kuanzia 26 Rabiul Al- Awwal hadi 20 Jumadal Al-

    Alwwal 857H sawia na 5 Aprili hadi 29 May 1453 M na ndio kwahivyo bishara njema ya

    Hadithi ya Mtume[saw} ikatimia « َشُ ِميُرَها َولَنِْعَم اْلَجْيُش ذَِلَك اْلَجيْ لَتُْفتََحنَّ اْلقُْسَطْنِطينِيَّةُ فَلَنِْعَم اْْلَِميُر أ

    “Mutaifunguwa Konstatinople, Amir wake ndie Amir mbora, na jeshi bora ni

    jeshi hilo..”

    Hizb ut Tahrir / Kenya iliangazia hafla hii ya kiulimwengu mnamo January 13th, 2020

    Kwa kutekeleza kipindi cha redio kilicho andaliwa na idhaa ya Radio Rahma. Katika

    kipindi hicho, Shaban Mwalimu, Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Afisi ya Habari

    ya Hizb ut Tahrir / Kenya, pamoja na mwenzake Ali Omar,walijadili juu ya ukombozi wa

    Konstantinople; bishara njema ikatimia .na itafuatiliwa na bishara njema.

    Mnamo Jumatano 15 Januari 2020 M, sawia na 20 Jumada al-Awwal 1441H,

    wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Kenya waliandaa amali ya migomo baridi na

    mazungumzo katika sehemu za umma kote chini. Katika mji wa Mombasa, mgomo

    baridi uliandaliwa nje ya Masjid Al Aqsa-Kisauni, Masjid Khairat-Kilifi na Masjid

    LungaLunga. Na katika amali hio, wanaharakati walikuwa na bendera zilizoandikwa:

    " ukombozi wa Konstantinople; bishara njema ikatimia...na itafuatiliwa na

    Afisi ya Habari

    Hizb ut Tahrir

    Kenya

    REF: 1441 / 04 H 17/01/2020 M

  • 22

    bishara njema! Kuregea kwa Khi[afah kwa njia ya Mtume(Saw), Kuwapiga na

    kuwashinda mayahudi, na ukombozi wa Romi.”

    Katika siku hiyohiyo baada ya swalah ya magharibi, hotuba kwa umma zikiongozwa

    na mwakilishi wa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir / Kenya Shabani Mwalimu

    zilitolewa mjini Mombasa, Nairobi na Kilifi. Hotuba zilikuwa ni za kuwakumbusha umma

    wawe na uhakika ya kutimia bishara tatu za Mtume {saw} kwani ya kwanza tayari

    ilikuwa ishatimia tangu kuwa hakuwa Mtume {saw} akiongea illa ni wahyi.Kwa

    kuongezea, wanaharakati walisisitiza kuwa bishara njema hizo hazitatimia kwa

    kushuka malaika watukufu kutoka mbinguni ambao watawasimamishia wao kwa niaba

    yao. Bali njia ya mtume wa Allah {saw} ni kuwa pindi tutakapo msaidia Mwenyezi

    Mungu,i.e kufanya kazi kuregesha Khilafah Rashidah kwa njia ya utume basi bila

    shaka atatushushia ushindi kwetu sisi.

    ِ يَْنُصُر َمْن يََشاُء َوهُوَ َويَْوَمئٍِذ يَْفَرُح ﴿ ﴾ِحيمُ يُز الرَّ اْلعَزِ اْلُمْؤِمنُوَن * بِنَْصِر َّللاَّ

    “Na siku hiyo waumini watafurahia * Kwaushindi wa Allah.Apeana ushindi

    kwa amtakae,nay eye ni mwenye nguvu mwenye huruma.” [Ar-Rum: 4-5]

    Shabani Mwalimu

    Mwakilishi wa Vyombo vya Habari -Hizb ut Tahrir Kenya

  • 23

  • 24

    ERDOGAN NA MUHAMMAD AL-FAATIH:HADITHI YA VIONGOZI WAWILIVIPI KUTAFUTA NUSURA KAMA ILIVYO AHIDIWA NA ALLAH KWAKUFUATA NYAYO ZA WAKUU KAMA MUHAMMAD AL- FATHIMuhammad Al-Fatih ni mwenye kutoa mfano mbora kati ya umma pindi tukumbukapo matukio matukufu yaliopita ya waume ambao walikuwa viongozi na wala si watawala ambao wengi leo wanawachukiwa.Kwa kusoma ayah za Quran, twapata kukutana na Ayah kama vile ahadi ya Mwenyezi Mungu ni hakika:إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ * وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّـهِ أَفْوَاجًا * فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ”Pindi itakapo kuja nusra ya Mwenyezi Mungu na ishinde. Na utaona watu wakiin...Ushindi ni kwa wale wanaoutafuta na wanaomsaidia Mwenyezi Mungu {swt} وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ