belgian technical cooperation btc report

28
MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MRADI WA MAJARIBIO WA KUKUZA UELEWA KUHUSU VVU NA UKIMWI KATIKA SHULE ZA MISINGI TANZANIA Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi WATOTO CHANZO CHA MABADILIKO Shirika la Maendeleo la Ubelgiji Tanzania

Upload: arnold-njuki

Post on 01-Apr-2016

328 views

Category:

Documents


8 download

DESCRIPTION

 

TRANSCRIPT

Page 1: Belgian Technical Cooperation BTC Report

MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MRADI WA MAJARIBIO WA KUKUZA UELEWA KUHUSU VVU NA UKIMWI KATIKA SHULE ZA MISINGI TANZANIA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

WATOTO CHANZO CHA MABADILIKO

Shirika la Maendeleo la Ubelgiji Tanzania

Page 2: Belgian Technical Cooperation BTC Report

VIFUPISHO BTC Shirika la Maendeleo la Ubelgiji Tanzania (Belgian Technical Cooperation)KUEKUS Kamati ya Unasihi na Elimu ya Kuijkinga na UKIMW ya ShuleTACAIDS Tume ya Kuthibiti Ukimwi Tanzania (Tanzania Commis sion for AIDS)TDHS Uchunguzi kuhusu Takwimu na Afya Tanzania (Tanza nia Demographic and Health Survey)THMIS Uchunguzi kuhusu Viashiria vya UKIMWI na Malaria Tanzania (Tanzania HIV and Malaria Indicator Survey)UKIMWI Upungufu wa Kinga MwiliniVVU Virusi Vya UKIMWI

Ripoti hii imeandaliwa/imehaririwa na Marleen (Mtaalamu wa VVU / UKIMWI, BTC), Hyacintha Musaroche (Mratibu wa Taifa wa Mradi, WEMU), Anna Patton (Afisa Mawasiliano, BTC)Picha zote na: BTC/Anna Patton, isipokuwa ilipoonyeshwa vinginevyo .

Msanifu: Arnold Njuki

© WEMU/BTCDar es Salaam, October 2012

Kano /KanushoMaoni na mawazo yaliyomo humu ni ya waandishi wenyewe na si lazima yawakilishe Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (BTC) au Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU).

MTOTO, BALEHE AU KIJANA?

Umoja wa Mataifa unawaelezea

vijana kama watu wenye umri kati ya

miaka 15 na 24.

Kwa ujumla, vijana balehe au ni wale

wenye umri kati ya miaka 10 na 18.

Mtoto ni mtu yeyote mwenye umri

chini ya miaka 18.

Mradi huu uliwalenga wanafunzi wa

shule za msingi, yaani wale wenye

umri kati ya miaka 7 na 13.

Page 3: Belgian Technical Cooperation BTC Report

1

MAFUNZO YA LEO MAJUKUMU YA KESHO

Kijitabu hiki kinawasilisha matokeo ya mradi wa Kukuza Uelewa kuhu-su VVU na UKIMWI uliojaribiwa katika shule za msingi 28 Tanzania. Unasisitiza kuhusu mambo tuliyojifunza na kutoa mapendekezo kuhu-su namna ya kuzipanua zaidi shughuli za mradi ili kuzifikia shule nyingi zaidi.

Manufaa ya mradi huu yameshuhudiwa katika sehemu muhimu zilizolengwa na hii inadhihirisha kuwa, hata kwenye ngazi ya elimu ya msingi, watoto na vijana wadogo wanaweza kubadilisha sio tu tabia zao bali hata kusaidia ma-badiliko ya mitazamo na matendo ya wanarika wenzao, familia na jamii kwa ujumla. Sifa muhimu zilizochangia kuleta matokeo haya ni pamoja na:

• KufuatamifumoyaKitanzania

• Kujikitakwenyemazingirawezeshi

• Mafunzokamilifukwawalengwawote.

• Matumiziyasanaanamichezo

Mradi huu ambao ni wa aina yake katika Tanzania umefadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji na kutekelezwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU) ikisaidiwanaBTC–ShirikalaMaendeleolaUbelgiji.Kwanamnahii,uzoefuwatimuyamradi,walimu,wanafunzi,kamatizashulemaafisawaserikalizamitaaunaweza kutoa mambo muhimu ya kujifunza kwa wadau wa elimu Tanzania na kwingineko.

Inatarajiwa kuwa kijitabu hiki na ripoti* inayoambatana nacho vitahamasisha umuhimuwakufikiriakuwekezakwenyeelimuyaVVU&UKIMWIkatikashuleza msingi na kuijumuisha elimu hiyo kwenye sera ya taifa.

*KijitabuhikikinatokananatathminihuruyamradiwamajaribioiliyofanyikaJulai2012.Ripotikamili inaweza kupatikana kwa kutuma maombi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Page 4: Belgian Technical Cooperation BTC Report

2

TUMEJIFUNZA NINI?

1. Umuhimu wa kuwahusisha wadau wengi na ushirikiano • Mazingirawezeshiyanahitajikailikuwawezeshavijana • Mafunzokwamaofisawahalmashaurinakamatizashuleni

muhimu ili kuhakikisha umiliki na uendelevu wa mradi. • Rasilimalivitu,kamavitabu,zinasaidiakuhakikishamasualayana

pewa nafasi na umakini unaostahili. • Kazikubwabadoinahitajikakuhakikishakuwahudumarafikiza

afyazinafikiwanavijana

2. Kuwa wazi kunaongeza ufahamu, ujasiri na mabadiliko ya tabia • Muunganikowashughulizamradiumeoneshakuwaunawezaku

leta mabadiliko chanya ya tabia kwa wanafunzi • Mafunzoyakinanaendelevuyanayohusishawadauwotehuleta

uelewa halisi • Watuambaosiowalengwawakuuwamradiwameripotikuwana

ongezeko la ufahamu na mabadiliko ya tabia

3. Mbinu bunifu na shirikishi hufanya mafunzo kuwa na ufanisi zaidi • Sanaanamichezohuwawezeshavijanakuzungumziamaswalaya

afya ya uzazi na ujinsia kwa ujasiri zaidi • Mbinubunifunashirikishizinamanufaazaidi,yakiwanipamojana

kuboresha mahudhurio shuleni

Kuwekeza kwa watoto na vijana katika masuala ya VVU & UKIMWI na afya ya uzazi kuna manufaa makubwa katika mwitikio wa kitaifa dhidi ya janga hili. Hata hivyo, mara nyingi, vijana wa rika balehe wamewekwa kando katika jitihada za kitaifa dhidi ya VVU & UKIMWI, kwa sababu umri wao unaingizwa kwenye kundi la wenye miaka kati ya 15-49. Wanafunzi wengi wa shule za msingi wanaachwa waufikie umri wa balehe bila kujua ni nani wa kumwuliza, kwani mara nyingi, wazazi huona aibu na walimu wanadhani kuwa wanafunzi hawahitaji elimu ya uzazi. Kwa jinsi hii, wanafunzi wako hatarini kupotoshwa kiurahisi.

Kwa ujumla, kuwatelekeza watoto kunamaanisha pia kuwa taasisi za kielimu zimeachwa zishughulikie suala hili bila msaada wa kutosha kutoka mashirika ya kitaifa na kimataifa. Katika muongo wa nne wa kuwepo UKIMWI, imedhihirika kwamba janga hili linaendelea kubadilika; mara nyingi limeonekana kuwa la kawaida hali likijikita zaidi katika makundi ya wahanga kama vile vijana na watoto waliobalehe / kuvunja ungo

DRBENNETTFIMBO,MTAALAMUWAELIMUNAMAENDELEOYAAFYA,NDIYEMWANDISHIWATATHMINIYAMRADIHUU

Page 5: Belgian Technical Cooperation BTC Report

3

KWA NINI UWEPO MRADI KAMA HUU? KUMBUSHO LA MUKTADHA

VVU & UKIMWI KWA WATOTO NA VIJANA BALEHE

Pamoja na kushuka kwa kiwango cha maambukizi katika Tanzania (kutoka 7% mwaka 2004 hadi 5.7% mwaka 2008), inakadiriwa kuwa watu milioni 2.2 wana VVU na UKIMWI. Katika maeneo ya mijini na katika miji midogo, kiwango cha maambukizi kipo juu zaidi (zaidi ya 9%) hali kukiwa na ongezeko la maambukizi mapya katika maeneo ya vijijini. Kuna ukosefu mkubwa wa takwimu kuhusu watoto na vijana wa-dogo. Kwa ujumla, takiwimu huzungumzia makundi yaliyopo kati ya miaka 15-49 au chini ya miaka 5 bila tarakimu kwa makundi ya kati. Hata hivyo, inakadiriwa idadi ya watoto wa Tanzania wenye VVU & UKIMWI inafikia 10%. Shirika la UNICEF linaonyesha kuwa idadi ya watoto wenye umri wa miaka 15 wenye VVU na UKIMWI ni 160,000 (2009).Hata watoto ambao hawajapata maambukizi, ni wahanga wa mad-hara ya ugonjwa huu. Takwimu za awali zilizokusanywa mwanzoni mwa mradi zilionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi (22.8%) wamewahi kuishi au walikuwa wakiishi na mtu mwenye VVU. Ki-taifa, zaidi ya watoto milioni moja wamepoteza mzazi mmoja au wawili kwa sababu ya UKIMWI.

Vyanzo:TACAIDS;THMIS;UNAIDSetal.;Chediel&Rajabu

VIJANA WANAFAHAMU NINI ? WAKO HATARINI KIASI GANI ?

Pamoja na kuwepo kwa mkanganyiko, wanafunzi wa shule za msingi wana ufahamu wa mambo ya msingi kuhusu VVU & UKIMWI. Hata hivyo, hawautumii ufahamu huo moja kwa moja katika mazingira ya maisha halisi.

TafitizaawalizilizofanywakatikashulezamradizimeonyeshakuwawanafunziwanaufahamukuhusuVVUnaUKIMWI,ingawaufahamuhuounatofautiana:

Page 6: Belgian Technical Cooperation BTC Report

4

wanafunzi wa Dar es Salaam walionyesha kuwa na ufahamu zaidi ya wale wa wilayazavijijininakiwangochaimanipotofukuhusuVVU&UKIMWIkilikuwakikubwa kwa wasichana kuliko wavulana.

Wengi wa wanafunzi waliohojiwa (79%) walionekana kuwa na ufahamu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ingawa majibu waliyoyatoa kwa maswali men-gineyalionyeshamkanganyiko.Kwamfano,kaributheruthimojayawanafunziwalisemawalimuwenyeVVUhawatakiwikufundishakwasababuwanawezakuwaambukiza wengine.

Theluthi ya Watanzania wako katika umri wa miaka 10 -24, kundi rika ambalo huanzakujihusishanangono.Katikamojayautafiti(TDHS2010),ilidhihirikakuwa 11% ya vijana wa kike na 8% ya vijana wa kiume walifanya ngono kwa marayakwanzakablayamiakakufikiaumriwamiaka15;6%yawasichanawa shule (msingi na sekondari) huacha shule kila mwaka kutokana na mimba (WEMU). Takwimu za mwanzo wa mradi zilionyesha kuwa 4% ya wanafunzi waliokusudiwanamradiwalikuwawameshaanzakujihusishanangono.KatikaTanzania 80% ya maambukizi mapya hutokana na mahusiano ya kingono na vijana ndiyo walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa.

Ngono zisizo salama zimepungua kwa vijana – kwa mfano, idadi ya wasi-chanawenyeumrikatiya15-19wanaofanyamapenzinazaidiyawenziwawiliimeshukakutoka5%hadi2%kutoka2004–2010(TDHS2004/2010).Hatahivyo,matumiziyakondombadonimadogosana:katikatafitinyingineidadiya vijana wanaoripoti kutumia kondomu wakati wa tendo la kwanza la ngono nichiniyatheluthimoja(THMIS2007-8).

NI ELIMU NA HUDUMA GANI ZINATOLEWA KWA VIJANA ?

Sera za sasa za elimu zinajumuisha Afya ya Jinsia na Uzazi kwa Vi-jana (ASRH) ikiwa ni pamoja na ufahamu kuhusu VVU & UKIMWI. Hata hivyo, mamlaka husika hazina nyenzo na rasilimali fedha za kutosha kwa ajili ya masuala haya. Baadhi ya huduma za ushauri nasaha, kupi-ma na matunzo kwa wenye UKIMWI zinatolewa lakini hazitoshelezi, na inawezekana watoto na vijana wa rika hawazifahamu au wanasita kuzitumia.

ElimuyaVVU&UKIMWIimeingizwakwenyemtaalawaelimuyamsingikuan-ziamwaka2000.Kablayahapo,WizarayaElimuiliwekailishaanzishaafuazakutekelezwakatikashulezamsingiambazoni:UfundishajiwamadazaVVU&UKIMWIdarasani;elimurika;hudumazaunasihi;nakuanzishaKamatiyaUnasihinaElimuyaKujikinganaUKIMWIyaShule(KUEKUS)

Hatahivyo,uborawaelimuyaVVUnaUKIMWIbadounatofautianasana.Kwakutumiamasomochukuzi;yaSayansi,HaibanaMichezo,naUraia,Walimu

Utandawazi ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya wanafunzi wetu hususani wale wa darasa la III na IV, kwani wengi wao wameona mambo mengi na hata wameyajaribu… Unajua wanafunzi wanapenda kujaribu. Kwa hiyo, unapoongea nao wanafahamu tayari – baadhi yao wanafahamu kupitia vyombo vya habari. Kwa hiyo, mradi huu ni muhimu ili kuyaweka mambo katika mtazamo sahihi kuhakikisha watoto wetu wa shule za msingi na hata jamii zetu wanaweza kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na maambukizi mengine ya maradhi ya ngono

AFISAELIMUWAWILAYA,KARATU

79% ya wanafunzi waliohojiwa walionekana kuwa na ufahamu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi.

Page 7: Belgian Technical Cooperation BTC Report

5

wamasomohayawanatakiwakufundishamadazaVVUnaUKIMWIzilizoingi-zwakatikamasomohayo.Hatahivyo,maranyingimambohayafanyikihivyokwa sababu ya kutokuwepo kwa mafunzo maalumu. Mara nyingi, walimu wa-nasitakuyakabilimasualanyetiyaafyayauzazinaujinsia.Utafitiwaawaliwamradi ulionyesha kukosekana kwa walimu, na baadhi yao walilalamika kuwa vifaa vya kufundishia havitoshelezi. Elimu rika ilionyesha kuwa na manufaa fulani lakini, mara nyingi, haifahamiki vizuri.

Katikakilashulekunawalimuwanasihiwawili(wakiumenawakike)ambaowanaweza kuwaelekeza wanafunzi kwenye huduma za afya endapo zinahi-tajika.KUEKUSinajukumulakuhakikishajamiiinahusishwanainasaidiakatikautekelezajiwaelimuyaUKIMWIshuleni.

Takwimu za awali zilionyesha kuwa, katika shule husika, utoaji wa huduma zaunasihihazitoshelezi.Ni63%tuyawanafunziwaliohojiwawalikubalikuwahudumakamahizozilikuwepo.Katikabaadhiyamaeneo,wajumbewaKUE-KUSwaliteuliwabilakupewamafunzowalamajukumuyakueleweka,jambolinalowafanya wasiwajibike. Mbali na hayo, idadi kubwa ya wanafunzi (48%) walisema kuwa wasingeweza kwenda kwenye huduma ya ushauri nasaha wa hiari na kupima, kwa sababu ya kuogopa matokeo mabaya.

Hivi karibuni, baadhi ya shule za Tanzania zimekuwa zikiwatambulisha wa-nafunziwenyeUKIMWIkwakuwavishautepemwekundu,kitukinachoashiriakuwa miongoni mwa walimu na wazazi wana uelewa mdogo kuhusu namna yakuwahudumiawenyeUKIMWIkimwilinakisaikolojia.

SIFA YA MRADI | KUENDANA NA MIFUMO YA KITANZANIA

NINI Kwa kutumia miongozo, vitendea kazi, vifaa na wataalamu wa WEMU pamoja na kuongeza ubunifu wa ziada unapohitajika.

KWA NINI Wafadhili wa kimataifa, ikiwemo Ubelgiji, wamejitolea kutekeleza Azimio la Paris linalosema kwamba misaada ya maendeleo ni lazima ijikite katika kuimarisha sera na utekelezaji wake. Kwa kutumia njia ya mfungamano (critical alignment), BTC ilifanya kazi na WEMU , kwani Mratibu wa Mradi alitoka nda-ni ya wizara, badala ya kutengeneza vifaa vipya au kuajiri mtaalamu elekezi kutoka nje, tulifanya kazi ya kuendeleza na kuimarisha vifaa ambavyo tayari vilikuwepo. Kwa mfano, kuimarisha zaidi miongozo ya sera, au kuzihuisha na kuzipa mafunzo KUEKUS zilizowekwa na WEMU. Uzoefu kutoka programu nyingine na nchi nyingine (kama vile kuhakikisha uwepo wa mazingira wezeshi, utumiaji wa sanaa na michezo, kusaidia waelimisha rika) viliongezewa kwenye hazina ya nyenzo na sera za WEMU.

48% ya wanafunzi

walisema hawawezi kwenda kwenye

huduma ya ushauri na upimaji wa

VVU, kwa kuwa wanaogopa majibu

mabaya

Page 8: Belgian Technical Cooperation BTC Report

6

HALI HALISIYA MRADI

Wizara ya Elimu inatambua haja ya kuelekeza elimu ya VVU & UKIMWI kwa watoto wa umri mdogo kabisa kama ilivyobainishwa kwenye sera za sasa. Hata hivyo, mifumo na rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa sera hizo vinahitaji kuimarishwa ili viwe na ufanisi.

Mradi wa majaribio uliobuniwa na BTC-Shirika la Maendeleo la Ubelgiji kwa ushirikiano na WEMU ni matokeo ya moja kwa moja ya haja hiyo. Programu yaKukuzaUelewawaVVUnaUKIMWIinayowalengawatotonaVijanawarikabalehe katika shule za msingi ililenga kupunguza matatizo yanayohusiana na UKIMWI,afyayauzazinaujinsia,nakuwawezeshavijanakujilinda.

TUNAANZIA UMRI MDOGO ?MFANO WA PROGRAMU KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGIWatoto wa umri wa elimu ya msingi lazima watazamwe kama kundi lengwa katika masuala yahusuyo uelewa kuhusu VVU & UKIMWI na afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana balehe (ASRH). Kwanza kabisa, ni 36% ya wanafunzi wanaendelea na elimu ya sekondari (UNESCO, 2011); hivyo programu zozote zinazohusu elimu lazima zijikite katika ngazi ya elimu ya msingi ili ziwe na ufanisi. Kwa hakika, baadhi ya Watanzania wanahitimu elimu ya msingi wakiwa na umri mkubwa: katika shule zilizohusika na mradi, baadhi ya wanafunzi walikuwa na umri wa miaka 17. Pili, afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana balehe haina maana ya kutoa elimu ya ngono au mada za watu wazima kabla ya wakati. Vifaa na mitaala ya WEMU vimeandaliwa mahususi kwa kila rika (kwa mfano, watoto wadogo kabisa hujifunza jinsi ya kuwa wasafi na wenye afya). Elimu rika inatolewa na watoto wa umri mkubwa zaidi (darasa la 5-7) tu.

Mradi wa majaribio ulizilenga shule 28 katika wilaya saba za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Arusha na Kilimanjaro

Marko B

alenovic

Page 9: Belgian Technical Cooperation BTC Report

7

DAR ESSALAAM

BAGAMOYO

MKURANGA

ROMBO

KARATU

KIWALANI

TANDALE

MBAGALA KUU

KINONDONI

ILALA

TEMEKE

TAREHE : SEPTEMBA 2009 – DESEMBA 2012

SHULE 28, WILAYA 7DAR Es sAlAAM > Kinondoni, Ilala & TemekepwANI > Bagamoyo & MkurangaARUsHA > KaratuKIlIMANjARO > Rombo

HUTEKElEZwA NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI; MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

wAsHIRIKANI: WIZARA YA AFYA NA USITAWI WA JAMII, OFISI YA WAZIRI MKUU – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, WIZARA YA FEDHA NA TACAIDS.

BAjETI EURO 1,606,486

Page 10: Belgian Technical Cooperation BTC Report

8

TULIFANYA NINI?

Katika kila wilaya• KutoamafunzokwawafanyakaziwaHalmashauriilikuwajengeauwezo

na ari ya kusimamia shughuli zinazoendeshwa ndani ya shule.• KutoamafunzokwawafanyakaziwaHalmashauriiliwafanyekazina

vijana, na kujenga mfumo wa rufaa ili kuwasaidia vijana wapate huduma rafikizaafya.

• Kufanyamapitioyamihtasariyamasomoyasayansi,HaibanaMich-ezo,naUraiailikuzibainimadanamadandogozaVVU&UKIMWI.

• Kuandaamiongozoyakufundishianazanazaufuatiliajinausimamizi.

Katika kila shule• KutoamafunzokwawalimuwotejuuyaufahamukuhusuVVU&UKIM-

WI na stadi za maisha.• KuhuishanakutoamafunzokwaKUEKUS.• KutoamafunzokwawalimuwanasihikuhusustadizaunasihiVVUna

UKIMWI,stadizamaishanauwezeshajiwaelimurika.• Kutoamafunzokwawalimu,maafisanawanafunzikuhusuuelewawa

VVU&UKIMWIkupitiasanaanamichezo.• Kutoamafunzokwawanafunziiliwawewaelimishajirika.• Kujenga na kuweka samani katika vyumba vilivyotengwa kwa ajili ya

klabu za afya za shule.

MIONGOZO YA ELIMU YA VVU & UKIMWI KATIKA SHULE ZA MSINGIKAMA IlIVYOTOlEwA OKTOBA 2012

Mradi ulilenga kuisaidia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika utekelezaji wa sera zi-lizopo. Hivyo tuliitumia miongozo ya Wizara na kuiongeza mingine kama ifuatavyo:

• Mwongozo wa mafunzo kwa ajili ya Kamati za Unasihi na Elimu ya Kujikinga na UKIMWI za Shule (KUEKUS)• Mwongozo wa mafunzo kwa Walimu wanasihi kuhusu Uwezeshaji wa Elimu rika• Mwongozo wa utoaji wa elimu ya VVU /UKIMWI kwa madara ya 1,2,3,4,5,6 na 7• Mwongozo wa Mafunzo kwa wawezeshaji wa wawezeshaji (ToT)• Mwongozo wa mafunzo kwa Walimu kuhusu matumizi ya sanaa na michezo katika kutoa elimu ya VVU naUKIMWI.

Page 11: Belgian Technical Cooperation BTC Report

9

DAR ESSALAAM

BAGAMOYO

MKURANGA

ROMBO

KARATU

NANI TULIMFIKIA?

28wAlIMU wAKUU

113wAlIMU wANAsIHI wA sHUlE

182wAFANYAKAZI wA wIlAYA

476wAjUMBE wA KUEKUs

840wAElIMIsHAjI RIKA

879wAlIMU

wAsIOKUsUDIwA MOjA KwA MOjA : wAZAZI, VIjANA NjE YA sHUlE, wANAjAMII

36,523wANAFUNZI

700wANAFUNZI wA sANAA NA MICHEZO

Page 12: Belgian Technical Cooperation BTC Report

10

MAMBO TULIYOJIFUNZA

FUNDISHO LA 1 / UMUHIMU WA NJIA SHIRIKISHI INAYOHUSISHA WADAU WENGI

• Mazingira wezeshi ya jumla yanahitajika katika kuwajengea uwezo vijana• Mafunzo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na kamati za shule yanasaidia kuhakikisha umiliki na uendelevu wa mradi• Rasilimali vitu, vikiwemo vitabu husaidia kuhakikisha kuwa masuala yanapewa nafasi na umakini unaotakiwa• Jitahada zaidi zinahitajika kuhakikisha kuwepo kwa huduma rafiki za afya kwa vijana

Nikatikamuktadhaupivijanawanawezakujifunzavyemazaidikuhusuelimuyaujinsianaafyayauzazi?Nimamboganiwanahitajiiliwajisikiewamewez-eshwakujilinda?Hayayalikuwanimaswaliyamsingikatikakuubunimradi.Mradi ulilenga kujenga mazingira wezeshi ambayo yanafaa kwa kujifunza, kue-lewa na kujisikia kuweza kubadili tabia.

Mradiulijumuishashughulimbalimbalizaziada,ndaninanjeyadarasa;len-go lilikuwa kuhakikisha uwepo wa rasilimali na miundombinu ya kutosha na kutafuta njia ya kupata ushiriki na msaada wa watu wazima walio karibu au wanaofanya kazi na watoto.

SIFA YA MRADI | KUjIKITA KATIKA KUjENGA MAZINGIRA wEZEsHININI Kuhakikisha nyenzo na rasilimali bora zinapatikana.

KWA NINI

Raisilimali watu na vitu zinaimarisha mafunzo. Hivyo, kuwepo kwa vitabu kwa kila mwanafunzi lilikuwa ni sharti muhimu. Jengo maalumu la klabu ya afya lilijengwa katika kila shule ili kuweka mazingira sala-ma kwa ajili ya unasihi na pia kutumika kama muundombinu kwa ajili ya mikutano ya waelimishaji rika na makundi ya sanaa na michezo. Shule zilitakiwa kuandaa ratiba inayojulikana na ya kudumu kwa ajili ya shughuli zote. Mradi huu haukufanya kazi na walimu pekee bali pia ulitoa mafunzo kwa watu wazima wanaofanya kazi na vijana, wakiwemo maafisa afya wa wilaya. Kushirikiana zaidi KUEKUS kulisaidia katika kuhusisha jamii ili kupata msaada wao.

Page 13: Belgian Technical Cooperation BTC Report

11

Cha

nzo

cha

kiel

elez

ona

Pet

erL

eona

rd(2

012)

Kifaa cha kutolea habari kilichoandaliwa na mradi.

Page 14: Belgian Technical Cooperation BTC Report

12

WajumbewaKUEKUSwalikuwananafasikubwakatikakuhakikshamradiuna-milikiwa na kusaidiwa na wenyeji. Ingawa kamati hizi zilikuwa zimeundwa kabla, mradiuliongezawajumbehadikufikia17,ilikilakamatiiwenaviongoziwawiliwadini(mwislamnamkristo)nawawiliwenyeUKIMWI(wakiumenawakike)pamoja na viongozi wa kijiji, wanafunzi na walimu. Wajumbe walipata mafunzo kuhusumadazaVVU&UKIMWI;namajukumuyaoyamewekwawazi–kui-unganisha shule na jamii. Matokeo yake ni kwamba kamati hizi zilijihuisha zaidi na utoaji wa elimu, kusaidia kushughulikia dukuduku za baadhi ya wazazi na kuhakikisha kuwa watoto wanajisikia kuwa wanaweza kuwa wazi zaidi katika kuzizungumzia mada nyeti.

Lengomojawapolamradiilikuwakuundamfumowarufaaunaowaruhusuvijanakuwaona moja kwa moja wataalamu wa afya ambao pia wamepata mafunzo kuhusunamnayakufanyakazinavijana.Hatahivyo,hadimwishonimwa2012,mfumohuuulikuwabadohaufanyikazikama ilivyotarajiwa.Kwamfano,hatabaadayamafunzo,maafisawaafyahawakuwawakizitembeleashulekamaili-vyopangwa.Kuboreshamahusianokatiyawizarahusika(WizarayaElimunaMafunzoyaUfundi,WizarayaAfyanaUsitawiwaJamii,OfisiyaWaziriMkuuTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) kunaweza kusaidia kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya.

Masualamengineyahusuyomazingirawezeshiyalikuwanamafanikiozaidi.Ku-likuwanaripotizakuwepokwamsaadawakaribukwawaelimisharika.Kulin-gananamaafisanawakaguziwawilaya,halihaikuwahivyokatikamiradiyanjeyashule.Njiayakutumia«masomoyadarasani»iliyoanzishwanawizarailione-kanakuwanaufanisiendapokukiwanamazingiramuafakanawezezi.Kwamfano, kuwepo kwa vitabu na nyenzo nyingine za kujifunzia ni kigezo muhimu katika mafunzo. Ilithibitishwa na watathmini wa mradi kuwa vitabu vilivyogawiwa kwakilamwanafunziwadarasala5-7vilikuwavikitumikasana.Kusisitiza

Kupitia vitabu vyake, programu hii imeboresha ufaulu wa wanafunzi wangu. Wanafunzi wangu wana uwezo wa kuelezea vizuri walichokisoma na uelewa wao uko juu sana

MWALIMUMKUU,BAgAMOYO

uwepo wa vitabu kunatoa ujumbe kwa wanafunzi na walimu kuhusu umuhimu wa somo husika na wakati mwingine imeonekana kukuza utamaduni wa kuji-somea na uwezo wa kuelewa.

Ujenzi wa vyumba kwa ajili ya vyama vya afya katika kila shule pia umekuwa na manufaa makubwa. Mmoja wa walimu wakuu wa Mkuranga alisema, “Wa-najamiiwanaionaprogramuhiinimakinikwasababuinaofisi”.Vyamavyaafyaambavyo pia vinapokea wanachama kutoka nje ya shule vimewavutia sana wa-najamii ambao sasa wanakuja kwa hiari kupata huduma.

17 WANAKAMATI WA KUEKUSKATIKA KILA SHULE

Page 15: Belgian Technical Cooperation BTC Report

13

FUNDISHO LA 2 | KUWA MAKINI KUNACHANGIA KUONGEZA MAARIFA, UJASIRI NA MABADILIKO YA TABIA

• Utafiti unaonyesha kuwa mradi ulisababisha mabadiliko chanya ya tabia miongoni mwa wanafunzi.• Uelewa halisi hutokana na mafunzo ya kueleweka na endel evu ambayo yanawahusisha wadau wote.• Walengwa wasiokusudiwa wameripoti pia kuongezeka kwa uelewa na mabadiliko ya tabia

Nikwanamnagani tunawezakuhakikishauelewathabitiwaHIV&UKIMWIna masuala yahusuyo gonjwa hili miongoni mwa wanafunzi na watu wazima? Wakati sera ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yamekuwa ni kutoa mafunzo kwa idadi ndogo tu ya walimu katika kila shule, mradi ulisisitiza ku-wepokwaprogramuyamafunzo inayowajumuishawalimuwotenamaafisaafya na elimu katika kufanya kazi na vijana. Pia, mafunzo yalikuwa endelevu. Kwamfano,walimu,waleziwawanafunzi shuleni nawanasihiwalihudhuriavipindivyamafunzokuhusuVVUnaUKIMWInaAfyauzazinayaujinsiakwaVijanakatikamwakawapilinawatatuwamradi.

Jambolakufurahishanikuwa,pamojamafunzokuwayamudamrefu,hapa-kujitokeza tatizo la muda. Badala yake, mafunzo haya yaliongeza ari kwa wa-nafunzinakuhakikishauwepowawataalamumbalimbalikatikakilashule.Halihii ilileta manufaa makubwa kwenye ubora wa ufundishaji na mafunzo kwa ujumla.

Mwisho,mbinuchanyanayawazidhidiyaVVU&UKIMWIambayoimechangi-wa na shughuli nyingine zote za mradi imeboresha mitazamo kuhusu waathirika wa ugonjwa huu, katika baadhi ya maeneo. Mbali na kupungua kwa unyanya-paadhidiyawanaoishinaVVUnaUKIMWI,shulezikomstariwambelezaidikatikakuwasaidiawanafunzi.Kwamfano,wanawezakuwatakawazazi/waleziwa watoto waathirika kuwajulisha walimu hali yao ya afya ili waweze kuwasaidia kusimamia matumizi ya dawa, kuwapa kazi nyepesi na kuwapa chakula kwa wakati.

Mwanzoni, nilikuwa na uelewa mdogo kuhusu ugonjwa huu na nilikuwa nafundisha bila ujasiri. Nilikuwa nikitumia uelewa wa jumla, nilioupata chuoni lakini baada ya mfululizo wa mafunzo haya, ninaweza kusema kuwa mimi ni mtaalamu wa VVU & UKIMWI … ndivyo ilivyo kwa wanafunzi… ninawaambi-eni kuwa wana ufahamu na ujasiri. Wanaweza kusimama mbele ya kadam-nasi ya watu na kuzungumza kuhusu VVU na UKIMWI na mkashangaa

MWALIMU,BAgAMOYO

Page 16: Belgian Technical Cooperation BTC Report

14

SIFA YA MRADI | / MBINU YA KUTOA MAFUNZO YA KINANINI

Kutoa mafunzo ya kina kwa kutumia njia shirikishi kwa walimu wote, wakiwemo walimu wakuu; wa-nasihi kadhaa, waratibu elimu kata, mafunzo kwa wafanyakazi wa halmashauri, wakaguzi wa shule na waelimishaji rika.

KWA NINI Katika miongozo iliyopo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, mafunzo ya Elimu ya UKIMWI yametolewa kwa walimu wachache tu na kuna wanasihi wawili tu kwa kila shule. Mradi huu ulitambua umuhimu wa walimu wote kuwa na uelewa na ujasiri wa kufundisha mada zinazohusu Afya ya Uzazi na ujinsia kwa Vijana; na kuwashirikisha pia walimu wakuu ili waunge mkono shughuli za mradi. Kozi za kunoa ubongo inahitajika kwa ajili ya uendelevu wa mradi na kulikabili tatizo la mabadiliko ya wafan-yakazi. Utoaji wa mafunzo kwa maafisa wa wilaya wenye dhima ya kupanga na kusimamia sera za elimu ni muhimu katika kujenga mazingira wezeshi, kwa ajili ya kuzuia maambukizi na kutoa huduma kwa waathirika, na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa umakini.

Ingawa tulikuwa tunafundisha kuhusu VVU na UKIMWI kabla ya mradi, hatukuwa na ufanisi kwa sababu ya kutokulifahamu vizuri somo hili, na tulikuwa tukijisikia aibu kuwaambia wanafunzi masuala haya.

MWALIMU,ROMBO

Kutokana na elimu hii, tumejifunza kuheshimu via vyetu vya uzazi … tumefundishwa kwamba, katika umri huu tukiwa shuleni, tunatakiwa kutumia via vyetu vya uzazi kwa ajili ya kujisaidia tu na si vinginevyo … kwa sababu tukivitumia vinginevyo, tunaweza kupata mimba, virusi vya UKIMWI au magonjwa mengine ya ngono.

MWELIMISHARIKA,BAgAMOYO

Walimu walipata ujasiri zaidi wa kuzungumzia VVU na UKIMWI na Afyayauzazi naujinsia naUzazi kwaVijana, nawameeleza kuwasasawa-nawezakuyazungumziamasualahayabilashida;jamboambaloninadrakwa shule ambazo hazipo kwenye mradi.

Kuwepokwaratibamaalamukunasaidiakuletaumakiniwakutoshakatikamasualayakukuzauelewa.Mmojawamaafisakutokawilayanianaeleza:“Programu hii inaonekana kuwa makini kwa sababu inaitaka shule kuweka ratiba inayoonyeshasikuzamafunzokwawanafunzi”.Kwamfano,sikumoja katika juma inaweza kutumika kwa ajili ya waelimishaji rika na ny-ingine kwa ajili ya maonyesho ya vikundi vya sanaa na michezo.

UmakinimkubwaunaowekwakwenyeelimuyaVVU&UKIMWIunamanu-faakatikamasualambalimbaliyanayoambatananaelimuhiyo.Kuzuianakuukabili ugonjwa huu kunahitaji stadi za maisha ambazo pia zinashabihi-ana na masuala mengine ya maisha ya ujana: afya ya jinsia kwa ujumla, kubalehe / kuvunja ungo, kuwajibika, kusimamia haki, na kadhalika.

Page 17: Belgian Technical Cooperation BTC Report

15

Majibu ya papo kwa papo Jumla % (N=776) Me % (N=370) Ke% (N=388)

Jinsiyakujilinda 34.9 38.9 32.2

Kuepukavishawishi 33.8 33.8 34.3

Kuachaunyanyapaa 24.6 26.2 23.2

Uelewa wa magonjwa ya zinaa 15.7 15.9 15.7

Kuepukatabiahatarishi 15.2 14.6 21.4

UKIMWI 14.8 12.2 17.8

Epuka mashugar mammy /dadi 13.8 14.6 12.9

Kuachangono 8.9 7.6 10.3

Ujasiri na kujiamini 8.4 9.5 7.7

Kuepukautoro&makundihatarishi 5.9 8.1 3.9

Kuepukamimba&ndoazautotoni 5.5 5.1 6.2

Kuepukakutembeausiku 4.8 3.2 6.4

Kuepukapombe&madawayakulevya 3.6 3.8 3.6

Stadi za maisha 3.2 4.1 2.6

AfyayaUzazi 2.7 3.8 1.5

“MMEJIFUNZA NINI KUTOKANA NA MRADI HUU?”(IdadiyaSampuli=776)

Siku hizi mtu akin-iambia njoo nikupe pesa au lifti, ninam-jibu “Subiri kidogo nikavae nguo”, halafu sirudi tena

MWANAFUNzI,ROMBO

Majibu ya wanafunzi kwa maswali ya kujieleza yanaonyesha kuwa mbinu za kueleweka zi-lizoelezwa hapo juu zimekuwa na matokeo mazuri katika kukuza uelewa mahsusi miongoni mwawanafunzi.UelewahuounajumuishakujikinganavirusivyaUKIMWInamagonjwamen-gineyangonokwajumlanastadizamaisha.Haishangazikuwaufahamuhuuunaendananakuongezeka kwa ujasiri unaojidhirisha katika namna watoto na vijana wadogo wanavyozun-gumzia masuala kama hayo.

Inaonekana kuwa ufahamu walionao wanafunzi umewawezesha zaidi kutambua mazingira hatarishinakuwapanguvuyakutoshakuyaepuka.Kwamfano,tathminiyamwishoyamradiilionyeshakuwakatikawilayayaRombo,AfisaElimuwawilayahajawahikusikiamsichanayeyote amepewa ujauzito, tangu kuanza kwa mradi katika shule nne pamoja na yeye bin-afsikuuliziakuhususualahili.Piakatikamijadalayavikundi,walimuwaRombowalisemakwamba hawajamwona msichana yeyote akipata ujauzito tangu kuanza kwa mradi mwaka 2009.Kadhalika,walimuwakuuwaKaratunaMkurangawaliripotikupunguakwamimbakatikashulezao.Hayayanathibitishwanamajibuyawanafunziwenyewekuhusutabiazao.

Page 18: Belgian Technical Cooperation BTC Report

16

“JE, UELEWA ULIOUPATA UMEBADILISHA TABIA YAKO?” (Idadiyasampuli=776)

Mabadiliko ya tabia Idadi Asilimia

Ndiyo 752 96.91

Hapana 13 1.68

Hakunajibu 3 0.39

Sijui 8 1.03

Jumla 776 100

“NI TABIA GANI ULIYOBADILISHA?”(Nambayasampuli=776)

Aina ya mabadiliko Waliotaja % Wasiotaja %

Kuachangono 46.5 53.5

Kuchelewakuanzangono 58.9 41.1

Kufanyangononampenzimmoja

1.9 98.1

Kutumiakinga 0.8 99.2

Kuepukangomazausiku 7.7 92.3

Katika kipindi cha nyuma, wanafunzi wengi walikuwa wamezoea kwenda kwenye ngoma za utamaduni za usiku…………tatizo ni kwamba walipokwenda kule walikutana na watu wengine toka kijijini ambao waliwashawishi na kuwaingiza katika kufanya ngono…….wakati mwingine, mabinti wadogo wanabakwa na watu wazima hasa wakiwa wamelewa. Lakini baada ya elimu hi,i tunashukuru kwamba wengi wameelimika na hawaendi tena

MWELIMISHARIKA,MKURANgA

Ufahamu na ujasiri ulioonyeshwa na walimu pamoja na wanafunzi uko dhahiri piakatikajamiinjeyashule.Kwamfano,watuwaishionavirusiwaliohojiwawalisemawakonaujasirikuhusuhalizao;unyanyapaanakutengwasiotatizokubwa.KamaanavyoelezamwanamkemmojawaMkuranga,mjumbewaKUEKUS“Baadayakujihusishakatikakamatihii,tulipatamafunzojuuyaVVUnaUKIMWI.Nilishawishikakwambawatuwenginewanapaswakufahamukuhusuhaliyangu,kwambanimeathirikanaVVU.Awali,nilikuwanaogopa kufanya hivyo, lakini baada ya mafunzo, nimejua kwamba huu ni ugonjwakamaugonjwamwinginewowote.”

WajumbewaKUEKUSambaoniviongoziwadinipiawalionatofauti,kamammojawaokutokaKaratualivyoeleza:“IlikuwangumukuzungumziaVVUnaUKIMWIhadharani,hasakwetusisiwaislamu.Lakinibaadayakuhudhuriamafunzo,kwauhakikatumepatanguvuyakuongeanawatuwetu.”

KIJANAWAKIKEAISHIYENAVVUMKURANgA

Baada ya mafunzo, nilitambua kwamba UKIMWI ni kama ugonjwa mwingine wowote …….kwahiyo, nilianza kuwaelimisha wengine, hasa nilipowakuta wamekaa katika vijiwe bila kazi ambako mara nyingi wanauliza maswali.”

Page 19: Belgian Technical Cooperation BTC Report

17

FUNDISHO LA 3 | UBUNIFU, MBINU SHIRIKISHI ZA UFUNDISHAJI KUNA FANYA UJUZI KUWA WA KUFAA ZAIDI

• Shughuli za Sanaa na michezo zinawawezesha vijana wadogo kugundua na kujihusisha na mada za afya ya uzazi kwa kujiamini zaidi• Ubunifu na mbinu shirikishi unaweza kuchangia kukuza/kuimari sha mahudhurio

Kuwafundishavijanawadogokuhusumaswalayaafyayauzazinaujinsiakupi-tia maonesho ya kisanaa imeonesha kuwa njia ya kufaa kurudisha heshima ya wasomaji na kuboresha utambuzi wa haki zao ( Bosmans et al., 2012).

Mradi uliongeza njia shirikishi kupitia sanaa na michezo kwenye hazina ya pro-gramuzaelimuUKIMWIyaWizarani.Hii ilijumuishakuwaongozawanafunzikufanyautafitikuhusumatatizoyaoyaafyayauzazinaujinsia,kuyachambuana kupendekeza njia za utatuzi. Kwa kutumia maigizo, michezo au muziki,wanafunzi wanaweza kujielezea kwa uhuru katika mada nyeti, hata katika hadhara.Kupitiamaoneshowanayoyaandaa,vijanahuishirikishapiahadhira-wakiwauliza kupendekeza masuluhisho kwa walichokiona. Hii inamaanishakuwaujumbewaohuwafikiapiawazazi,majiraninavijananjeyashule.

Kwambinuhizizaufundishaji,wanafunziwanajifunzakwaharaka;wanajihusi-shanamajadilianokuhusuVVU&UKIMWIkwasababuwanasawirikinacho-tokea hasa katika jamii.

Kwa sababu wanafunzi wanapenda maigizo watakuja mara zote shule na hawatapenda kukosa vipindi – kwa sababu pia watakosa maigizo.

MWELIMISHAJIRIKA,TEMEKE

SIFA YA MRADI | KwA KUTUMIA sANAA NA MICHEZONINI Kutumia sanaa na michezo kufikisha ujumbe wa afya ya uzazi kwa vijana balehe.

KWA NINI

Miiko ya kiutamaduni inayoendelea kuwepo inaleta ugumu wa kujadili kwa uwazi mada nyeti kama ku-fanya ngono , lakini kwa kutumia maigizo au nyimbo walimu na wanafunzi wanaweza kujieleza. Mbinu shirikishi za kujifunza zinawawezesha vijana wadogo kuchukua nafasi za kuongoza – na wanafunzi wadogo wanalifurahia somo.

Kama ilivyomiongozo ya sanaanamichezo, elimu rika (kwadarasa la 5-7pekee) pia inawapa wanafunzi nafasi ya msingi katika mchakato wa mafunzo. Waelimishaji rika wa kike na wa kiume katika kila mkondo wanachaguliwa na wanadarasanakupewamafunzonawalimuwanasihi.Halafu,waelimishajirikahao wanaandaa vipindi wanavyowezesha mara kwa mara kwa wenzao kwa

Page 20: Belgian Technical Cooperation BTC Report

18

kutumia nyenzo wanazopewa na mwongozo wa wanasihi. Ujasiri waliouonye-shatangukuanzakwamradi(MmojawawahojiwawaKaratualisema“Sasatunawezakuzungumzanamtuyeyotekwauwazikuhusuugonjwahili”)un-aambatana na utayari wa kutaka kuwashirikisha wengine walichojifunza ndani nanje ya shule.MmojawawalimuwakuuRomboalisema: “Waelishaji rikawetuwamekuwanauwezowakuwaelimishawengine”.

Pia utumiaji wa mbinu hizi unaonekana kuwa umechangia kuongeza mahud-hurio, kwani wanafunzi wana ari zaidi ya kuhudhuria madarasa hayo na hivyo hawawezikukosashule.Maafisaelimuwawilayanawalimuwakuuwameripotikuwa kiwango cha utoro kimeshuka katika shule zilizohusika na mradi katika wilaya saba.

Kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na mimbaza utotoni kumeboresha mahudhurio; na hii inaweza kuwa ni sababu yakuongezeka kwa ufaulu. Kama ilivyoripotiwa na Afisa Elimu wa Wilaya yaRombonaMkaguziwaShulewaWilayayaKinondoni,kiwangochaufaulukimeongezeka katika shule lengwa, tangu kuanza kwa mradi. Maoni kama hayo yalitolewa pia na walimu wakuu wa Shule ya Msingi Kwangao (ShuleyenyeufauluwajuuzaidiWilayaniRombo)naShuleyaMsingiyaHekima(mojaya shule zenye ufaulu wa juu zaidi wilayani Kinondoni) na walimu wenginembali mbali.

Mradi huu umekuwa na manufaa ya aina mbili. Kwanza, umewapa uwezo wa kupambana na VVU & UKIMWI bila woga. Pili, umewapa uwezo wa kujibu / kujieleza vizuri na kwa usahihi katika masomo mengine ya taaluma

MWALIMUMKUU,BAgAMOYO

Page 21: Belgian Technical Cooperation BTC Report

19

HITIMISHO

Wazazi wengi wamekuwa na utayari zaidi kupimwa.

MWALIMU,MKURANgA

Pia wazazi wameelimika kuhusu shughuli za usiku na wamegun-dua kuwa si nzuri kwa watoto wao

MWALIMUW,MKURANgA

HATA WATOTO WA UMRI WA SHULE YA MSINGI WANAWEZA KUWA CHANZO CHA MABADILIKO

Tathmini ya mwisho ya mradi ya mwaka 2012 inathibitisha kuwa matokeo yal-iyoshuhudiwa katika baadhi ya shule yanaonyesha hali ilivyo katika takribani shule zotezilizohusika.Katikakilawilaya,shulezilizohusishwakatikamradizilionyeshamabadiliko chanya yanayozitofautisha na shule nyingine.

Mafunzo ya kina yaliyotolewa katika mazingira wezeshi, yameonyesha mafani-kio katika kuongeza ufahamu na ujasiri katika kuchangia mabadiliko ya tabia na katikakuwahusishavijananawalewanaofanyakazinaoilikukabiliananaVVU&UKIMWI,kwauwazinaujasirizaidi.Piaprogramuhii imeonyeshakuchangiakatika kuboresha mahudhurio na ufaulu.

Chanzochamabadilikohayaniwanafunziwaliohamasika.Kuongezekakwauja-siriwawanafunzikatikakuvikabiliVVUnaUKIMWIkumeshuhudiwamarakwamara na walimu na wafanyakazi wa serikali. Wakati wa kazi za darasani na nje ya darasa, vijana wanazungumza kwa uwazi na wanaweza kujieleza. Namnaambavyo wanafunzi walizungumza kuhusu hali ya maisha, katika tathmini yetu, ni ishara ya ukomavu na ujasiri walioujenga na unaowasaidia kuepuka tabia na mazingira hatarishi. Uwezeshaji wa aina hii unadhihirika hasa kwa wasichana wa-naoonekana kumudu vyema majukumu yao kama waelimishaji rika.

Mbali na wanafunzi kuonyesha uwezo wa kubadili tabia zao, wamedhihirisha kuwa wanao pia uwezo wa kuwaeleza na kuwashawishi wengine kufanya kama wao.WajumbewaKUEKUSwalielezakuwawanafunzikutokashulezilizohusikana mradi, hasa wale waliopata mafunzo ya uelimishaji rika, huwashirkisha ndugu zao na hata wazazi wao walichojifunza. Pia wazazi na majirani hujifunza kupitia maonyeshoshuleninatafitiambazowanafunziwanahamasishwakuzifanyakati-ka jamii zao. Matokeo yake ni mabadiliko ya tabia kwa watu wazima, kwa mfano, katikakutumiavyumbavyavyamavyaafyanakuamuakupimaVVU.

KujadilimadazaAfyayauzazinaujinsiakwaVijananaVVUnaUKIMWIbadokunaugumu, katika umri mdogo. Walimu wameripoti kuwa baadhi ya wazazi wame-kuwa wakilalamika kuwa watoto wao wanafundishwa mambo yasiyoendana na umriwao.Hatahivyo,malalamikoyaoyanaoneshauelewafinyunasiyokuikataaelimu kama hiyo. Mmoja wa walimu wakuu kutoka Bagamoyo alisema: “Tuli-waeleza (wazazi) kuhusu programu hii na umuhimu wake. Mwishoni walielewa na hata wanafunzi wanatueleza kuwa, sasa wazazi wao, wanaweza kuuzungumzia ugonjwahuukwauwazi”

Page 22: Belgian Technical Cooperation BTC Report

20

Uju

mbe

um

etol

ewa

nam

radi

.Cha

nzo

cha

kiel

elez

ona

Pet

erL

eona

rd(2

012)

NI JUKUMU LETU WAZAZI KUZUNGUMZA NA WATOTO WETU JUU YA AFYA YA UZAZI NA UKIMWI

Page 23: Belgian Technical Cooperation BTC Report

21

Waandaaji wa sera, wakiwemo viongozi wa juu wa Wizara ya Elimu na Mafun-zoyaUfundinawalewaTumeyaTaifayakudhibitiUKIMWITanzaniaambayoinaratibumwitikiowakitaifadhidiyaVVUnaUKIMWI,wapotayarikusaidiailimradi uendelee.

Pia wengi wa waliohusika katika mradi wameonyesha utayari wa kusaidia maendeleonaupanuziwamradi.Kwamfano,walimuwaTemekewametumianjia zao wenyewe kutoa mafunzo yasiyo rasmi kwa walimu wa shule za karibu ambazo hazikuhusishwa katika mradi. Pia wafanyakazi wa wilaya wanasema wanatumaini mradi utaendelea.

Hata hivyo, shughuli za mradi haziwezi kupanuliwa wala kuendelezwa kwamuda mrefu bila uwepo wa rasilimali endelevu. Wakati mradi ukikaribia mwisho, timu ya mradi inajitahidi kuhakikisha mambo mazuri ya mradi yanaendelezwa namradiwenyeweunapanuliwakuzifikiashulezaidiyazile28zamradiwamajaribio. Moja ya mafanikio ya mradi hadi sasa ni kukubaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa nyenzo na miongozo iliyoandaliwa na mradi (kwa mfano, Mwongozo wa Mafunzo kwa Walimu katika Matumizi ya Sanaa naMichezokatikakutoaelimuyaVVUnaUKIMWI)

KUTOKA KWENYE MAJARIBIO KUELEKEA KWENYE SERA: HATUA ZINAZOFUATA

Mradi huu umethibitisha uwezo wa vijana kubadilisha desturi hasi na kuleta mabadiliko ya tabia. Mwanzoni, sikuwa nimeshawishika kuhusu mbinu hii, bali sasa nimeona ufanisi wake. Lakini kama mradi hautaendelea, manufaa haya yatapotea baada ya muda. Kila kizazi kipya kinastahili kupata kile ambacho mradi umetoa kuhusu afya ya jinsia na uzazi kwa vijana na ninashauri kuwa waandaaji wa sera wa Tanzania watafute namna ya kuuendeleza mradi huu.

DR.BENNETFIMBO,BINgWAWAELIMUNAUKUzAJIWAAFYA.MWANDISHIWATATHMINIYAMWISHOYAMRADI

Nitajaribu kuzihamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga rasilimali kutoka bajeti ya Halimashauri ili mradi uendelee hata baada ya udhamini wa BTC kwishaAFISAELIMUWAWILAYA,KARATU

Page 24: Belgian Technical Cooperation BTC Report

22

1. KUTUMIA VIZURI KAsI NA ARI YA sAsA

• Kuwahusisha wadau wa mradi katika majadiliano kuhusu hatua zi-takazofuata na kuendelea kufanya kazi na washirika (ikiwemo Tume ya Kuthibiti Ukimwi Tanzania-TACAIDS)nataasisihusikazaWiz-arayaElimunaMafunzoyaUfundi(VikundivyaKiufundiVinavyohusi-sha wadau mbalimbali) ili kuandaa mpango kazi wa kueleweka.

• Kuongezamatumizinauzalishajiwanyenzonamiongozoinayotumi-wa na kuandaliwa na mradi.

• Kushirikishana uzoefu wa mradi miongoni mwa wadau ndani na nje ya Tanzania.

2. UpANUZI wA MRADI KUZIFIKIA sHUlE NYINGI ZAIDI KwA KUIN-GIZA MAMBO MAZURI KATIKA sERA YA TAIFA

• Kuwepokwamajadilianoyawazinawaundajiwaseranamamlakahusika (k.m. Taasisi ya Elimu Tanzania) kuhusu kuyaingiza mambo mazuri ya mradi kwenye sera na miongozo ya taifa. Mahali pa kuanzia panatakiwa kuwa Mpango unaokuja wa Maendeleo ya Elimu yaMsinginaMkakatiwaTaifawaSektambalimbaliwaKuzuiaVVU.

3. KUTAFUTA VYANZO NA NjIA MpYA ZA UFADHIlI

• Kutokananamaelewanobainayawafadhili,Ubelgiji inatoamisaadayake kwa sekta mbili tu (usimamizi wa maliasili na maboresho ya seri-kalizamitaa).Kwishakwamradiwasasandioutakuwamwishowamisaada ya Ubelgiji kwenye sekta ya Elimu, na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itatakiwa kutafuta misaada mahali pengine kwa ajili ya upanuzi wa mradi. Tanzania imeendelea kutegemea ufadhili wa nje katikashughulizaVVU&UKIMWI.97%yagharamazotehutokakwawafadhili.KutokananakupunguakwamisaadayaVVU&UKIMWIki-mataifa, kutakuwa na changamoto kubwa. Wizara italazimika kufanya yafuatayo:

• Kutafuta wafadhili wengine na / au washirika binafsi.

• Kubuni mbinu mpya za kupunguza gharama bila kupunguza manufaa ya mradi. Kwa mfano, inawezekana kuwatumia walimuwaliopata mafunzo katika shule zilizohusika na mradi kutoa mafunzo kwa wengine katika wilaya zao na kuangalia pia uwezekano wa wal-imuhaokutoaelimuyaVVUkwenyevyuovyawalimu.

Tume ya Taifa ya Ukimwi haiwezi kukamilika bila kuwahusisha watoto wa umri wa shule ya msingi. Katika umri huu, wana uwezekano mkubwa wa kujenga uelewa na maarifa yanayohitajika kuzuia sababu hatarishi na kuwashawishi wengine kuiga: wao ndiyo sababu ya mabadiliko na watu wa kuigwa. Nilipoangalia maonyesho yao mazuri, nilifurahishwa sana kwani wanonyesha uwezo na ujasiri katika kile wanachokifanya. Kuupanua mradi huu hadi ngazi ya kitaifa kutahitaji uwekezaji mkubwa lakini naamini itakuwa ni matumizi mazuri ya fedha, na ninaunga mkono uwekezaji huo

MORRISLEKULE,TACAIDSMJUMBEWAKAMATIYAUSHAURIYAMRADI

Page 25: Belgian Technical Cooperation BTC Report

23

4. KUsIMAMIA UTEKElEZAjI NA KUHAKIKIsHA MRADI UNAENDElEA KwA MUDA MREFU

• Kuhakikisha kuwa dhamana ya elimu ya UKIMWI kupitia shule za msingi inapewa kwa taasisi yenye uwezo wa kusimamia utekelezaji kwaufanisi.Kwasasa,TACAIDS(TumeyakudhibitiUKIMWIyaTaifa)na Wizara ya Elimu ndio wanaosimamia.

• Kutegemea na kutumia shughuli zitakazofuata katika kuendelea kuboresha mpango huu.

• Kuendeleakushirikishana na kubadilishana uzoefu na wadau nje ya Tanzania.

• KuendeleakusimamiamalengokuhusuVVUnaUKIMWIkatikamipa-ngo ya maendeleo ya taifa ya muda mrefu na wa kati.

Page 26: Belgian Technical Cooperation BTC Report

24

Mafunzo yaliyoelezwa katika kijitabu hiki yanatokana na tathmini huru iliyofanywa kwa kutumia dodoso, hojaji na mijadala yavikundimweziJulai2012.Wafanyatathmini,walizitembeleashulembilikatikakilawilaya2sabazilizohusikanamradinakuwahojijumlayawanafunzi776(darasala5-7waumrikatiyamiaka11-17).Katikashulehizo14,mwenyekitiwaKUE-KUS,viongoziwadiniambaoniwajumbewaKUEKUS,walimunawaelimishajirikawalihojiwapia.Walimuwakuu26,ku-tokashule28walihojiwa.Ingawashulezisizohusikanamradihazikulengwanatathminihii,maofisawawilayawalithibitishakuwepokwa“tofautikubwasana”katiyashulezilizohusikanazileambazohazikuhusikakwenyemradikatikawilayazao.

Katikangaziyaserikalizamitaa,MaafisawotewaElimuWilaya,WakaguziwaShule,WaratibuwaElimuKata,WaratibuwaVVUnaUKIMWIwaHalmashaurinaWatuHusikakatikaWilayawalihojiwa.Kwenyengaziyataifa,taasisizifuatazozilihusishwa:WizarayaElimunaMafunzoyaUfundi,BTC,TumeyaUKIMWIyaTaifa,naWizarayaAfyanaUsitawiwaJamiikupitiaMpangowaTaifawaKudhibitiUKIMWInaKitengochaElimuyaUzazi.

Ripotikamiliyatathmini(DrBennetFimbo,“MafunzonaMamboMazuriKutokakwenyeProgramuyaElimuyaVVU&UKIMWI”,Augusti2012)inapatikanakwakutumamaombiWizarayaElimu.

VYANZO VINGINE

• R.WChedielandA.SRajabu,ProjectBaselinereport:‘HIV-AIDSAwarenessCreationProgramme:AProgramme

• TargetingYouthsandAdolescentsinPrimarySchools’.April2011(Datagathered2010-11).

• BosmansM.,F.gonzalez,E.Brems&M.Temmerman(2012),‘Dignityandtherightofinternallydisplacedadoles-centsinColombiatosexualandreproductivehealth’inDisasters.October2012;36(4):617-34.

• MoEVT,BasicEducationStatisticsinTanzania(BEST)2011-2.

• TACAIDS,‘NationalMultisectoralHIVPreventionStrategy2009-2012’.November2009.

• TACAIDS,‘NationalHIVandAIDSResponseReport2010forTanzaniaMainland’.August2011.

• ‘TanzaniaDemographicandHealthSurvey2010’(TDHS),NationalBureauofStatisticsandICFMacro.2011.

• ‘TanzaniaHIV/AIDSandMalariaIndicatorSurvey2007-08’(THMIS).TACAIDS,zAC,NBS,OCgS,andMacroInter-national Inc. 2008.

• UNESCO,‘globalEducationDigest2011:ComparingEducationStatisticsAcrosstheWorld’.2011.

• UNAIDS,UNESCO,UNICEF,UNFPAandWHO,‘ChildrenandAIDS:FifthStocktakingReport2010’.November2010.

MAELEZO

Page 27: Belgian Technical Cooperation BTC Report
Page 28: Belgian Technical Cooperation BTC Report

MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING KIVUKONI FRONT, p.O BOx 9121, DAR Es sAlAAM (+255) 022 2122 [email protected] www.MOE.GO.TZ

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

BTC (Shirika la Maendeleo la Ubelgiji) ni wakala wa Utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya serikaliyaUbelgiji.Ubelgijiinafadhilimiradizaidiya300katikanchi20katikaAfrika,Asia,nanchizaAmerikayakusini.

BTC TANZANIA, PO BOX 23209, DAR ES SALAAM(+255) 022 266 [email protected] www.BTCCTB.ORG