biblia takatifu - downloads.dbs.org

210
Biblia Takatifu Swahili Bible 1850 Public Domain

Upload: others

Post on 29-Nov-2021

6 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

Biblia TakatifuSwahili Bible

1850

Public Domain

Page 2: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org
Page 3: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

Mathayo .......................................................................4Marko .........................................................................28Luka ............................................................................43Yohana........................................................................69Matendo.....................................................................89Warumi.....................................................................1161 Wakorintho...........................................................1282 Wakorintho...........................................................139Wagalatia .................................................................146Waefeso ...................................................................150Wafilipi......................................................................154Wakolosai.................................................................1571 Wathesalonike......................................................1602 Wathesalonike......................................................1631 Timotheo...............................................................1652 Timotheo...............................................................168Tito............................................................................171Filemoni....................................................................173Waraka kwa Waebrania..........................................174Yakobo......................................................................1831 Petro ......................................................................1862 Petro ......................................................................1901 Yohana ..................................................................1922 Yohana ..................................................................1953 Yohana ..................................................................196Yuda..........................................................................197Ufunuo .....................................................................198

Page 4: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

MATHAYO MTAKATIFU

Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi,mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo orodhaya ukoo wake: 2 Abrahamu alimzaa

Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaaYuda na ndugu zake, 3 Yuda alimzaa Faresi naZera (mama yao alikuwa Tamari), Faresialimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami, 4 Ramialimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaaNashoni, Nashoni alimzaa Salmoni, 5 Salmonialimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwaRahabu). Boazi na Ruthi walikuwa wazazi waObedi, Obedi alimzaa Yese, 6 naye Yesealimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaaSolomoni (mama yake Solomoni alikuwa mkewa Uria). 7 Solomoni alimzaa Rehoboamu,Rehoboamu alimzaa Abiya, Abiya alimzaa Asa,8 Asa alimzaa Yehoshafati, Yehoshafatialimzaa Yoramu, Yoramu alimzaa Uzia, 9 Uziaalimzaa Yothamu, Yothamu alimzaa Ahazi,Ahazi alimzaa Hezekia, 10 Hezekia alimzaaManase, Manase alimzaa Amoni, Amonialimzaa Yosia, 11 Yosia alimzaa Yekonia nandugu zake. Huo ulikuwa wakati Wayahudiwalipopelekwa uhamishoni Babuloni. 12 Baadaya Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni:Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli alimzaaZerobabeli, 13 Zerobabeli alimzaa Abiudi,Abiudi alimzaa Eliakimu, Eliakimu alimzaaAzori, 14 Azori alimzaa Zadoki, Zadoki alimzaaAkimu, Akimu alimzaa Eliudi, 15 Eliudi alimzaaEleazeri, Eleazeri alimzaa Mathani, Mathanialimzaa Yakobo, 16 Yakobo alimzaa Yosefu,aliyekuwa mume wake Maria, mama yakeYesu, aitwaye Kristo. 17 Basi, kulikuwa na vizazikumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi,vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpakaWayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni,na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwamateka mpaka wakati wa Kristo. 18 Basi, hivindivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mamayake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakinikabla hawajakaa pamoja kama mume na mke,alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo waRoho Mtakatifu. 19 Yosefu, mumewe, kwa vilealikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibishahadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwasiri. 20 Alipokuwa bado anawaza jambo hilo,malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto,akamwambia, “Yosefu, mwana wa Daudi,usiogope kumchukua Maria awe mke wako,maana amekuwa mja mzito kwa uwezo waRoho Mtakatifu. 21 Atajifungua mtoto wakiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye

atawaokoa watu wake kutoka katika dhambizao.” 22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lileneno Bwana alilosema kwa njia ya nabii: 23

“Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wakiume, naye ataitwa Emanueli” (maana yake,“Mungu yu pamoja nasi”). 24 Hivyo, Yosefualipoamka usingizini alifanya kama malaikahuyo alivyomwambia, akamchukua mke wakenyumbani. 25 Lakini hakumjua kamwe kimwilihata Maria alipojifungua mtoto wa kiume.Naye Yosefu akampa jina Yesu.

Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu,mkoani Yudea, wakati Herodealipokuwa mfalme. Punde tu baada ya

kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota kutokamashariki walifika Yerusalemu, 2 wakauliza,“Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi,aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokeamashariki, tukaja kumwabudu.” 3 MfalmeHerode aliposikia hayo, alifadhaika, yeyepamoja na wakazi wote wa Yerusalemu. 4 Basiakawaita pamoja makuhani wakuu wote nawalimu wa Sheria, akawauliza, “Kristoatazaliwa wapi?” 5 Nao wakamjibu, “MjiniBethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabiialivyoandika: 6 Ewe Bethlehemu katika nchi yaYuda, kwa vyovyote wewe si mdogo kabisa katiya viongozi wa Yuda; maana kwako atatokeakiongozi atakayewaongoza watu wangu,Israeli.” 7 Hapo, Herode aliwaita faraghani haowataalamu wa nyota, akawauliza wakati hasaile nyota ilipowatokea. 8 Kisha akawatumaBethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguzekwa makini habari za mtoto huyo. Mkishampata nileteeni habari ili nami niendenikamwabudu.” 9 Baada ya kumsikilizamfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda.Kumbe ile nyota waliyokuwa wameionaupande wa mashariki iliwatangulia hataikaenda kusimama juu ya mahali palealipokuwa mtoto. 10 Walipoiona hiyo nyota,walifurahi mno. 11 Basi, wakaingia nyumbani,wakamwona yule mtoto pamoja na Mariamama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia.Kisha wakafungua hazina zao, wakampazawadi: dhahabu, ubani na manemane. 12

Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudieHerode; hivyo wakarudi makwao kwa njianyingine. 13 Baada ya wale wageni kuondoka,malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katikandoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtotopamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaenihuko mpaka nitakapokwambia, maana Herode

4

Page 5: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

anakusudia kumwua huyu mtoto.” 14 Hivyo,Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja namama yake, akaondoka usiku, akaenda Misri.15 Akakaa huko mpaka Herode alipokufa.Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwanakwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangukutoka Misri.” 16 Herode alipogundua kwambawale wataalamu wa nyota walikuwawamemhadaa, alikasirika sana. Akaamuruwatoto wote wa kiume mjini Bethlehemu nakandokando yake wenye umri wa miaka miwilina chini yake wauawe. Alifanya hivyokufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwawale wataalamu wa nyota. 17 Ndivyoyalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia yanabii Yeremia: 18 “Sauti imesikika mjini Rama,kilio na maombolezo mengi. Raheli anawaliliawatoto wake, wala hataki kutulizwa, maanawote wamefariki.” 19 Baada ya kifo chaHerode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefukatika ndoto kule Misri, 20 akamwambia,“Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake,urudi tena katika nchi ya Israeli, maana walewaliotaka kumwua mtoto huyo wamekwishakufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukuamtoto pamoja na mama yake, akarejea katikanchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikiakwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwamfalme wa Yudea mahali pa baba yake,aliogopa kwenda huko. Naye baada yakuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoawa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwaoNazareti. Ndivyo yalivyotimia manenoyaliyonenwa kwa njia ya manabii: “AtaitwaMnazare.”

Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea,akaanza kuhubiri katika jangwa laYudea: 2 “Tubuni, maana Ufalme wa

mbinguni umekaribia.” 3 Huyu Yohane ndiyeyule ambaye nabii Isaya alinena juu yakealiposema: “Sauti ya mtu imesikika jangwani:Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijiavyake.” 4 Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwamanyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozikiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzigena asali ya mwituni. 5 Basi, watu kutokaYerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea nasehemu zote za kandokando ya mto Yordani,walimwendea, 6 wakaziungama dhambi zao,naye akawabatiza katika mto Yordani. 7 Lakinialipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayowanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazicha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwambamnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja? 8

Onyesheni basi kwa matendo, kwambammetubu kweli. 9 Msidhani kwamba mtawezakujitetea kwa kusema, Baba yetu ni Abrahamu!Nawaambieni hakika, Mungu anawezakuyafanya mawe haya yawe watoto waAbrahamu. 10 Basi, shoka liko tayari kuikatamizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matundamazuri, utakatwa na kutupwa motoni. 11 Mimininawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba

mmetubu. Lakini yule anayekuja baada yanguana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hatakubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwaRoho Mtakatifu na kwa moto. 12 Yeye anashikamkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipurenafaka yake; akusanye ngano ghalani, namakapi ayachome kwa moto usiozimika.” 13

Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katikamto Yordani, akamwendea Yohane ili abatizwenaye. 14 Lakini Yohane alijaribu kumzuiaakisema, “Je, wewe unakuja kwangu? Mimihasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe.” 15

Lakini Yesu akamjibu, “Acha tu iwe hivyo kwasasa, maana kwa namna hii inafaatuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka.”Hapo Yohane akakubali. 16 Mara tu Yesualipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghaflambingu zikafunguka, akaona Roho wa Munguakishuka kama njiwa na kutua juu yake. 17

Sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiyeMwanangu mpendwa, nimependezwa naye.”

Kisha Roho alimwongoza Yesu mpakajangwani ili ajaribiwe na Ibilisi. 2

Akafunga siku arubaini mchana nausiku, na mwishowe akaona njaa. 3 Basi,mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa weweni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawemikate.” 4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa katikaMaandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwamikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.”5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu,mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wahekalu, 6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwanawa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajiliyako; watakuchukua mikononi mwao, usijeukajikwaa kwenye jiwe.” 7 Yesu akamwambia,“Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Munguwako.” 8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juuya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote zaulimwengu na fahari zake, 9 akamwambia,“Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magotina kuniabudu.” 10 Hapo, Yesu akamwambia,“Nenda zako Shetani! Imeandikwa:Utamwabudu Bwana Mungu wako nakumtumikia yeye peke yake.” 11 Basi, Ibilisiakamwacha, na malaika wakaja,wakamhudumia. 12 Yesu aliposikia kwambaYohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.13 Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu,mji ulio kando ya bahari ya Genesareti,mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali,akakaa huko. 14 Ndivyo lilivyotimia lile nenolililosemwa kwa njia ya nabii Isaya: 15 “Nchi yaZabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharining'ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watuwa Mataifa! 16 Watu waliokaa gizani wameonamwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi yagiza na kivuli cha kifo, mwangaumewaangazia!” 17 Tangu wakati huo Yesualianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maanaufalme wa mbinguni umekaribia!” 18 Yesualipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya,

MATHAYO MTAKATIFU 4:18

5

Page 6: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaePetro) na Andrea, ndugu yake; walikuwawakivua samaki kwa nyavu ziwani. 19 Basi,akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanyaninyi wavuvi wa watu.” 20 Mara wakaziachanyavu zao, wakamfuata. 21 Alipokwendambele kidogo, aliwaona ndugu wenginewawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo.Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja nababa yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao.Basi Yesu akawaita, 22 nao mara wakaiachamashua pamoja na baba yao, wakamfuata. 23

Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayaniGalilaya, akifundisha katika masunagogi nakuhubiri Habari Njema juu ya ufalme waMungu. Aliponya kila namna ya maradhi namagonjwa waliyokuwa nayo watu. 24 Habarizake zikaenea katika mkoa wote wa Siria.Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namnana wale waliosumbuliwa na kila namna yataabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa nawatu waliokuwa wamelemaa, walipelekwakwake; naye akawaponya wote. 25 Makundimengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli,Yerusalemu, Yudea na ng'ambo ya mtoYordani, walimfuata.

Yesu alipoyaona makundi ya watu,alipanda mlimani, akaketi. Wanafunziwake wakamwendea, 2 naye akaanza

kuwafundisha: 3 “Heri walio maskini rohoni,maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4 Heriwalio na huzuni, maana watafarijiwa. 5 Heriwalio wapole, maana watairithi nchi. 6 Heriwenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu,maana watashibishwa. 7 Heri walio nahuruma, maana watahurumiwa. 8 Heri wenyemoyo safi, maana watamwona Mungu. 9 Heriwenye kuleta amani, maana wataitwa watotowa Mungu. 10 Heri wanaoteswa kwa sababuya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wambinguni ni wao. 11 “Heri yenu ninyi watuwakiwatukana, wakiwadhulumu nakuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.12 Furahini na kushangilia maana tuzo lenu nikubwa mbinguni. Hivyo ndivyowalivyowadhulumu manabii waliokuwakokabla yenu. 13 “Ninyi ni chumvi ya dunia!Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwana nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje nakukanyagwa na watu. 14 “Ninyi ni mwanga waulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlimahauwezi kufichika. 15 Wala watu hawawashitaa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juuya kinara ili iwaangazie wote waliomonyumbani. 16 Vivyo hivyo, ni lazima mwangawenu uangaze mbele ya watu, ili wayaonematendo yenu mema, wamtukuze Baba yenualiye mbinguni.” 17 “Msidhani ya kuwanimekuja kutangua Sheria ya Mose namafundisho ya manabii. Sikuja kutangua balikukamilisha. 18 Kweli nawaambieni, mpakahapo mbingu na dunia zitakapopita, hakunahata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya

Sheria itakayoondolewa, mpaka yoteyametimia. 19 Basi, yeyote atakayevunja hataamri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundishawengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogokabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yuleatakayezishika na kuwafundisha wengine,huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wambinguni. 20 Ndiyo maana nawaambieni,wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo nawalimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katikaUfalme wa mbinguni. 21 “Mmekwisha sikia yakuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue!Atakayeua lazima ahukumiwe. 22 Lakini miminawaambieni, yeyote anayemkasirikia nduguyake, lazima ahukumiwe. Anayemdharaundugu yake atapelekwa mahakamani.Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahilikuingia katika moto wa Jehanamu. 23 Basi,ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahuna hapo ukakumbuka kwamba ndugu yakoana ugomvi nawe, 24 iache sadaka yako mbeleya madhabahu, nenda kwanza ukapatane nandugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.25 “Patana na mshtaki wako upesi mkiwa badonjiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtakiwako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimuatakukabidhi kwa askari, nawe utafungwagerezani. 26 Kweli nakwambia, hutatoka humompaka umemaliza kulipa senti ya mwisho. 27

“Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!28 Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazamamwanamke kwa kumtamani, amekwisha zininaye moyoni mwake. 29 Basi, kama jicho lakola kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali.Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimojacha mwili wako, kuliko mwili wako wotekutupwa katika moto wa Jehanamu. 30 Nakama mkono wako wa kulia unakukosesha,ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupotezakiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wakowote uende katika moto wa Jehanamu. 31

“Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mkewake, yampasa ampe hati ya talaka. 32 Lakinimimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka,isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanyaazini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewatalaka, anazini. 33 “Tena mmesikia kuwa watuwa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, balini lazima utimize kiapo chako kwa Bwana. 34

Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe;wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi chaMungu; 35 wala kwa dunia, maana ni kiti chakecha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu,maana ni mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiapekwa kichwa chako, maana huwezi kuufanyahata unywele mmoja kuwa mweupe aumweusi. 37 Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo;ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochotekinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu. 38

“Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho,jino kwa jino. 39 Lakini mimi nawaambieni,usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupigakofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili. 40

MATHAYO MTAKATIFU 4:19

6

Page 7: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

7

Mtu akikupeleka mahakamani kutakakukuchukulia shati lako, mwache achukue piakoti lako. 41 Mtu akikulazimisha kubeba mzigowake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. 42

Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopakitu usimnyime. 43 “Mmesikia kwambailisemwa: Mpende jirani yako na kumchukiaadui yako. 44 Lakini mimi nawaambieni,wapendeni adui zenu na kuwaombea walewanaowadhulumu ninyi 45 ili mpate kuwawatoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwamaana yeye huwaangazia jua lake watuwabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watuwanyofu na waovu. 46 Je, mtapata tuzo ganikwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi?Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuruhufanya hivyo! 47 Kama mkiwasalimu nduguzenu tu, je, mmefanya kitu kisicho chakawaida? Hata watu wasiomjua Mungu naohufanya vivyo hivyo. 48 Basi, muwe wakamilifukama Baba yenu wa mbinguni alivyomkamilifu.

“Jihadharini msije mkafanya matendoyenu mema mbele ya watu kusudimwonekane nao. La sivyo, Baba yenu

aliye mbinguni hatawapeni tuzo. 2 “Basi,unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanyekama wanafiki wafanyavyo katika masunagogina njiani ili watu wawasifu. Kwelinawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.3 Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanyahivyo kwamba hata rafiki yako asijue ufanyalo.4 Toa msaada wako kwa siri, na Baba yakoaonaye yaliyofichika, atakutuza. 5 “Mnaposali,msifanye kama wanafiki. Wao hupendakusimama na kusali katika masunagogi nakatika pembe za njia ili watu wawaone. Kwelinawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.6 Lakini wewe unaposali, ingia chumbanimwako, funga mlango, kisha umwombe Babayako asiyeonekana. Naye Baba yako aonayeyaliyofichika, atakutuza. 7 “Mnaposali,msipayuke maneno kama watu wasiomjuaMungu. Wao hudhani kwamba Munguatawasikiliza ati kwa sababu ya manenomengi. 8 Msiwe kama wao. Baba yenu anajuamnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba. 9

Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: Babayetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe. 10

Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike dunianikama mbinguni. 11 Utupe leo chakula chetutunachohitaji. 12 Utusamehe makosa yetu,kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. 13

Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yuleMwovu. is Baadhi ya makala za zamani zina;Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, nautukufu, hata milele. Amina. 14 “Maanamkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenuwa mbinguni atawasamehe ninyi pia. 15 Lakinimsipowasamehe watu makosa yao, naye Babayenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. 16

“Mnapofunga, msiwe na huzuni kamawanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate

kuonekana na watu kuwa wanafunga.Nawaambieni hakika, hao wamekwisha patatuzo lao. 17 Wewe lakini unapofunga, pakakichwa chako mafuta, nawa uso wako, 18 ilimtu yeyote asijue kwamba unafunga, ilaujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana.Naye Baba yako aonaye yaliyofichikaatakutuza. 19 “Msijiwekee hazina hapa dunianiambako nondo na kutu huharibu, na wezihuingia na kuiba. 20 Jiwekeeni hazinambinguni ambako nondo na kutu hawawezikuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba. 21

Maana pale ilipo hazina yako, ndipo piautakapokuwa moyo wako. 22 “Jicho ni taa yamwili. Kama jicho lako ni zima, mwili wakowote utakuwa katika mwanga. 23 Lakini ikiwajicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwakatika giza. Basi, ikiwa mwanga ulioko ndaniyako ni giza, basi, hilo ni giza la kutisha mno.24 “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwanawawili. Maana atamchukia mmoja nakumpenda huyo wa pili; au ataambatana nammoja na kumdharau huyo mwingine.Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.25 “Ndiyo maana nawaambieni, msiwe nawasiwasi juu ya chakula na kinywajimnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazimnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha nichakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi yamavazi? 26 Waangalieni ndege wa mwituni:hawapandi, hawavuni, wala hawana ghalayoyoye. Hata hivyo, Baba yenu wa mbingunihuwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao?27 Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa nawasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wamaisha yake? 28 “Na kuhusu mavazi, ya ninikuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porinijinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi walahayasokoti. 29 Lakini nawaambieni, hataSolomoni mwenyewe na fahari zake zotehakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.30 Ikiwa basi Mungu hulivika hivyo jani lashambani ambalo leo liko na kesho latupwamotoni, je, hatafanya zaidi kwenu ninyi? Enyiwatu wenye imani haba! 31 “Basi, msiwe nawasiwasi: Tutakula nini, tutakunywa nini,tutavaa nini! 32 Maana hayo yoteyanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu.Baba yenu wa mbinguni anajua kwambamnahitaji vitu hivyo vyote. 33 Bali, zingatienikwanza Ufalme wa Mungu na matakwa yake,na hayo mengine yote mtapewa kwa ziada. 34

Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; keshoinayo yake. Matatizo ya siku mojayanawatosheni kwa siku hiyo.

“Msiwahukumu wengine, msije nanyimkahukumiwa na Mungu; 2 kwamaana jinsi mnavyowahukumu

wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; nakipimo kilekile mnachotumia kwa wenginendicho Mungu atakachotumia kwenu. 3 Kwanini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa nduguyako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni

MATHAYO MTAKATIFU 7:3

7

Page 8: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

mwako? 4 Au, wawezaje kumwambia nduguyako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichonimwako, wakati wewe mwenyewe unayo boritijichoni mwako? 5 Mnafiki wewe! Ondoakwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapondipo utaona waziwazi kiasi cha kuwezakuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa nduguyako. 6 “Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasijewakageuka na kuwararua ninyi; walamsiwatupie nguruwe lulu zenu wasijewakazikanyaga. 7 “Ombeni, nanyi mtapewa;tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyimtafunguliwa. 8 Maana, aombaye hupewa,atafutaye hupata, na abishaye hufunguliwa. 9

Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambayemtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe?10 Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka?11 Kama basi ninyi, ingawa ni waovu, mwajuakuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Babayenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapamema wale wanaomwomba. 12 “Watendeeniwengine yale mnayotaka wao wawatendeeninyi. Hii ndiyo maana ya Sheria ya Mose namafundisho ya manabii. 13 “Ingieni kwakupitia mlango mwembamba. Kwa maana njiainayoongoza kwenye maangamizi ni pana, namlango wa kuingilia humo ni mpana; waendaonjia hiyo ni wengi. 14 Lakini njia inayoongozakwenye uzima ni nyembamba, na mlango wakuingilia humo ni mwembamba; ni watuwachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.15 “Jihadharini na manabii wa uongo. Waohuja kwenu wakionekana kama kondoo kwanje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. 16

Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watuhuchuma zabibu katika miti ya miiba, au tinikatika mbigili? La! 17 Basi, mti mwema huzaamatunda mema, na mti mbaya huzaa matundamabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaamatunda mabaya, wala mti mbaya hauwezikuzaa matunda mema. 19 Kila mti usiozaamatunda mema utakatwa na kutupwa motoni.20 Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao.21 “Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, ataingiakatika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tuanayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliyembinguni. 22 Wengi wataniambia Siku ile yahukumu: Bwana, Bwana! kwa jina lakotulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lakotuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi. 23

Hapo nitawaambia: Sikuwajua ninyi kamwe;ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.24 “Kwa sababu hiyo, kila mtu anayeyasikiamaneno yangu na kuyazingatia, anafanana namtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yakejuu ya mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mitoikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiganyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababuilikuwa imejengwa juu ya mwamba. 26 “Lakiniyeyote anayesikia maneno yangu haya bilakuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavualiyejenga nyumba yake juu ya mchanga. 27

Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali

zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayoikaanguka; tena kwa kishindo kikubwa.” 28

Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umatiwa watu ukashangazwa na mafundisho yake.29 Hakuwa kama walimu wao wa Sheria, balialifundisha kwa mamlaka.

Yesu aliposhuka kutoka mlimani,makundi mengi ya watu yalimfuata. 2

Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma,akamsujudia akisema, “Bwana, ukitaka,waweza kunitakasa!” 3 Yesu akanyosha mkonowake, akamgusa na kusema, “Nataka!Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukomawake. 4 Kisha Yesu akamwambia, “Sikiliza,usimwambie mtu yeyote, ila nendaukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadakailiyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwambaumepona.” 5 Yesu alipokuwa anaingia mjiniKafarnaumu, ofisa mmoja Mroma alimwendea,akamsihi 6 akisema, “Mheshimiwa, mtumishiwangu amelala nyumbani, mgonjwa wakupooza na anaumwa sana.” 7 Yesuakamwambia, “Nitakuja kumponya.” 8 Huyoofisa akamwambia, “Mheshimiwa, sistahiliuingie nyumbani mwangu. Lakini sema tuneno, na mtumishi wangu atapona. 9 Maana,hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka yawengine, ninao askari chini yangu.Namwambia mmoja, Nenda! naye huenda; namwingine, Njoo! naye huja; na mtumishiwangu, Fanya kitu hiki! naye hufanya.” 10 Yesualiposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watuwaliokuwa wanamfuata, “Kweli nawaambieni,sijapata kumwona mtu yeyote katika Israelialiye na imani kama hii. 11 Basi, nawaambienikwamba watu wengi watakuja kutokamashariki na magharibi, nao wataketikaramuni pamoja na Abrahamu, Isaka naYakobo katika Ufalme wa mbinguni. 12 Lakiniwale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalmehuo watatupwa nje, gizani, ambako watalia nakusaga meno.” 13 Kisha Yesu akamwambiahuyo ofisa Mroma, “Nenda nyumbani; na iwekama ulivyoamini.” Na mtumishi wakeakapona saa ileile. 14 Yesu alifika nyumbanikwa Petro, akamkuta mama mkwe wa Petroamelala kitandani, ana homa kali. 15 Basi, Yesuakamgusa huyo mama mkono, na homaikamwacha; akasimama, akamtumikia. 16

Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengiwaliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwakusema neno tu, akawafukuza hao pepo.Aliwaponya pia watu wote waliokuwawagonjwa. 17 Alifanya hivyo ili yale aliyosemanabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyeweameondoa udhaifu wetu, ameyachukuamagonjwa yetu.” 18 Yesu alipoona kundi lawatu limemzunguka, aliwaamuru wanafunziwake waende ng'ambo ya ziwa. 19 Mwalimummoja wa Sheria akamwendea, akamwambia,“Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako.”20 Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango,na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu

MATHAYO MTAKATIFU 7:4

8

Page 9: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

hana mahali pa kupumzikia.” 21 Kisha mtumwingine miongoni mwa wanafunzi wakeakamwambia, “Bwana, niruhusu kwanzaniende nikamzike baba yangu.” 22 Lakini Yesuakamwambia, “Nifuate! Waache wafu wazikewafu wao.” 23 Yesu alipanda mashua, nawanafunzi wake wakaenda pamoja naye. 24

Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hatamawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesualikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunziwakamwendea, wakamwamsha wakisema,“Bwana, tuokoe, tunaangamia!” 26 Yesuakawaambia, “Enyi watu wenye imani haba;mbona mnaogopa?” Basi, akainuka,akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwarikabisa. 27 Watu wakashangaa, wakasema, “Nimtu wa namna gani huyu? Hata pepo namawimbi vinamtii!” 28 Yesu alifika katika nchiya Wagerasi, ng'ambo ya ziwa, na huko watuwawili waliopagawa na pepo wakakutana nayewakitokea makaburini. Watu hawa walikuwawenye kutisha mno, hata hakuna mtualiyethubutu kupita katika njia hiyo. 29 Naowakaanza kupiga kelele, “Una shauri gani nasi,wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesakabla ya wakati wake?” 30 Karibu na mahalihapo kulikuwa na nguruwe wengiwakichungwa. 31 Basi, hao pepo wakamsihi,“Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingienguruwe wale.” 32 Yesu akawaambia, “Haya,nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao,wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwelikaporomoka kwenye ule mteremko mkali,likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafamaji. 33 Wachungaji wa hao nguruwewalikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoahabari zote na mambo yaliyowapata wale watuwaliokuwa wamepagawa. 34 Basi, watu wotekatika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu;na walipomwona, wakamsihi aondoke katikanchi yao.

Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa nakufika katika mji wake. 2 Hapo watuwalimletea mtu mmoja aliyepooza

mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoonaimani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza,“Jipe moyo mwanangu! Umesamehewadhambi zako.” 3 Baadhi ya walimu wa Sheriawakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuruMungu!” 4 Yesu aliyajua mawazo yao,akasema, “Kwa nini mnawaza mabaya mioyonimwenu? 5 Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema,Umesamehewa dhambi zako, au kusema,Simama, utembee? 6 Basi, nataka mjuekwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wakuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapoakamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka,chukua kitanda chako, uende nyumbanikwako.” 7 Huyo mtu aliyekuwa amepoozaakainuka, akaenda nyumbani kwake. 8 Watuwote katika ule umati walipoona hayo,walishangaa na kuogopa; wakamtukuzaMungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna

hiyo. 9 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwaanakwenda zake, alimwona mtu mmojaaitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi yaushuru. Basi, Yesu akamwambia, “Nifuate.”Naye Mathayo akainuka, akamfuata. 10 Yesualipokuwa nyumbani ameketi kula chakula,watoza ushuru wengi na wahalifu walikujawakaketi pamoja naye na wanafunzi wake. 11

Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambiawanafunzi wake, “Mbona mwalimu wenuanakula pamoja na watoza ushuru na wenyedhambi?” 12 Yesu aliwasikia, akasema, “Watuwenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji niwale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watuwema, ila wenye dhambi. 13 Basi, kajifunzenimaana ya maneno haya: Nataka huruma, walasi dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, baliwenye dhambi.” 14 Kisha wanafunzi waYohane mbatizaji walimwendea Yesu,wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufungamara nyingi; mbona wanafunzi wakohawafungi?” 15 Yesu akawajibu, “Je,walioalikwa arusini wanaweza kuombolezawakati bwana arusi yupo pamoja nao? Lahasha! Lakini wakati utafika ambapo bwanaarusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipowatakapofunga. 16 “Hakuna mtu atiaye kirakacha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maanakiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na palepalipokuwa pameraruka pataongezeka. 17

Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katikaviriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viribahupasuka na divai ikamwagika, navyo viribavikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viribavipya, na vyote viwili, viriba na divai,vikahifadhiwa salama.” 18 Yesu alipokuwaakisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika,akamwinamia na kusema, “Binti yanguamekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njooumwekee mkono wako naye ataishi.” 19 Yesuakaondoka pamoja na wanafunzi wake,akamfuata. 20 Mama mmoja, mgonjwa wakutokwa damu kwa muda wa miaka kumi namiwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindola vazi lake. 21 Alifanya hivyo kwani alifikirimoyoni: “Nikigusa tu vazi lake, nitapona.” 22

Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia,“Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya.”Mama huyo akapona saa ileile. 23 Kisha Yesuakaingia nyumbani kwa yule ofisa. Naalipowaona wapiga filimbi na umati wa watuwanaofanya matanga, 24 akasema, “Ondokenihapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu.” Naowakamcheka. 25 Basi, umati wa watuulipoondolewa, Yesu aliingia ndani, akamshikahuyo msichana mkono, naye akasimama. 26

Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote.27 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwaanakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipigakelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!” 28

Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawiliwakamwendea, naye akawauliza, “Je,mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo

MATHAYO MTAKATIFU 9:28

9

Page 10: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

hilo?” Nao wakamjibu, “Naam, Mheshimiwa.”29 Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema,“Na iwe kwenu kama mnavyoamini.” 30 Machoyao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwaukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.” 31

Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari zaYesu katika nchi ile yote. 32 Watu walipokuwawanakwenda zao, wengine walimletea Yesumtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababualikuwa amepagawa na pepo. 33 Mara tu huyopepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubuakaanza kuongea tena. Watu wakashangaa nakusema, “Jambo kama hili halijapatakuonekana katika Israeli!” 34 Lakini Mafarisayowakawa wanasema, “Anawatoa pepo kwanguvu ya mkuu wa pepo wabaya.” 35 Yesualitembelea miji yote na vijiji, akafundishakatika masunagogi yao akihubiri Habari Njemaya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwayote na udhaifu wa kila namna. 36 Basi,alipowaona watu, makundi kwa makundi,aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoina wenye wasiwasi kama kondoo wasio namchungaji. 37 Hapo akawaambia wanafunziwake, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji niwachache. 38 Kwa hivyo mwombeni mwenyeshamba atume wavunaji shambani mwake.”

Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi nawawili, akawapa uwezo wa kutoapepo wachafu na kuponya magonjwa

na maradhi yote. 2 Majina ya hao mitumekumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoniaitwae Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobomwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;3 Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayoaliyekuwa mtoza ushuru; Yakobo mwana waAlfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkanaani, naYuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu. 5 Yesualiwatuma hao kumi na wawili na kuwapamaagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifamengine, wala msiingie katika mji waWasamaria. 6 Ila nendeni kwa watu wa Israeliwaliopotea kama kondoo. 7 Mnapokwendahubirini hivi: Ufalme wa mbinguni umekaribia.8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseniwenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure,toeni bure. 9 Msichukue mifukoni mwenudhahabu, wala fedha, wala sarafu za shaba. 10

Msichukue mkoba wa kuombea njiani, walakoti la ziada, wala viatu, wala fimbo. Maanamfanyakazi anastahili riziki yake. 11 “Mkiingiakatika mji wowote au kijiji, tafuteni humo mtuyeyote aliye tayari kuwakaribisheni, na kaeninaye mpaka mtakapoondoka mahali hapo. 12

Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyejiwake. 13 Kama wenyeji wa nyumba hiyowakiipokea salamu hiyo, basi, amani yenuitakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawaipokei,basi amani yenu itawarudia ninyi. 14 Kamamtu yeyote atakataa kuwakaribisheni aukuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumbahiyo au mji huo, yakung'uteni mavumbimiguuni mwenu kama onyo kwao. 15 Kweli

nawaambieni, Siku ya hukumu mji huo utapataadhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji yaSodoma na Gomora. 16 “Sasa, mimi nawatumaninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwena busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.17 Jihadharini na watu, maana watawapelekaninyi mahakamani na kuwapiga viboko katikamasunagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele yawatawala na wafalme kwa sababu yangu,mpate kutangaza Habari Njema kwao na kwamataifa. 19 Basi, watakapowapeleka ninyimahakamani, msiwe na wasiwasi mtasemanini au namna gani; wakati utakapofika,mtapewa la kusema. 20 Maana si ninyimtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenuasemaye ndani yenu. 21 “Ndugu atamsalitindugu yake auawe, na baba atamsalitimwanawe, nao watoto watawashambuliawazazi wao na kuwaua. 22 Watu wotewatawachukieni kwa sababu ya jina langu.Lakini atakayevumilia mpaka mwisho,ataokolewa. 23 “Watu wakiwadhulumu katikamji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kwelinawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katikamiji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtuhajafika. 24 “Mwanafunzi si mkuu kulikomwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kulikobwana wake. 25 Yatosha mwanafunzi kuwakama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kamabwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wajamaa Beelzebuli, je hawatawaita watuwengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?26 “Basi, msiwaogope watu hao. Kilakilichofunikwa kitafunuliwa, na kilakilichofichwa kitafichuliwa. 27

Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemenikatika mwanga; na jambo mlilosikialikinong'onezwa, litangazeni hadharani. 28

Msiwaogope wale wauao mwili, lakinihawawezi kuiua roho. Afadhali zaidikumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwilipamoja na roho katika moto wa Jehanamu. 29

Shomoro wawili huuzwa kwa senti tano. Lakinihata mmoja wao haanguki chini bila kibali chaBaba yenu. 30 Lakini kwa upande wenu, hatanywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. 31

Kwa hiyo msiogope; ninyi mu wa thamanikuliko shomoro wengi. 32 “Kila mtu anayekirihadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pianitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.33 Lakini yeyote atakayenikana hadharani,nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliyembinguni. 34 “Msidhani kwamba nimekujakuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani baliupanga. 35 Maana nimekuja kuletamafarakano kati ya mtu na baba yake, kati yabinti na mama yake, kati ya mkwe na mkwewake. 36 Na maadui wa mtu ni watu wanyumbani mwake. 37 “Ampendaye baba aumama yake kuliko anipendavyo mimi,hanistahili. Ampendaye mwana au binti kulikomimi, hanistahili. 38 Mtu asiyechukua msalabawake na kunifuata, hanistahili. 39

MATHAYO MTAKATIFU 9:29

10

Page 11: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

12

Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza;lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajiliyangu, atayapata. 40 “Anayewakaribisha ninyi,ananikaribisha mimi; na anayenikaribishamimi, anamkaribisha yule aliyenituma. 41

Anayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii,atapokea tuzo la nabii. Anayemkaribisha mtumwema kwa sababu ni mtu mwema, atapokeatuzo la mtu mwema. 42 Kweli nawaambieni,yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogohawa kikombe cha maji baridi kwa sababu nimfuasi wangu, hatakosa kamwe kupata tuzolake.”

Yesu alipomaliza kuwapa wanafunzikumi na wawili maagizo, alitoka hapo,akaenda kufundisha na kuhubiri

katika miji yao. 2 Yohane mbatizaji akiwagerezani alipata habari juu ya matendo yaKristo. Basi, Yohane akawatuma wanafunziwake, 3 wamwulize: “Je, wewe ni yuleanayekuja, au tumngoje mwingine?” 4 Yesuakawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohanemambo mnayoyasikia na kuyaona: 5 vipofuwanaona, viwete wanatembea, wenye ukomawanatakaswa na viziwi wanasikia, wafuwanafufuliwa na maskini wanahubiriwa HabariNjema. 6 Heri mtu yule asiyekuwa na mashakanami.” 7 Basi, hao wajumbe wa Yohanewalipokuwa wanakwenda zao, Yesu alianzakuyaambia makundi ya watu habari za Yohane:“Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je,mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?8 Lakini mlikwenda kuona nini? Mlikwendakumtazama mtu aliyevaa mavazi maridadi?Watu wanaovaa mavazi maridadi hukaa katikanyumba za wafalme. 9 Basi, mlikwenda kuonanini? Nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii. 10

“Huyu ndiye anayesemwa katika MaandikoMatakatifu: Tazama, hapa namtuma mjumbewangu, asema Bwana, akutangulie nakukutayarishia njia yako. 11 Kwelinawaambieni, miongoni mwa watoto wote wawatu, hajatokea aliye mkuu kuliko Yohanembatizaji. Hata hivyo, yule aliye mdogo kabisakatika Ufalme wa mbinguni, ni mkubwa kulikoyeye. 12 Tangu wakati wa Yohane mbatizajimpaka leo hii, Ufalme wa mbinguniunashambuliwa vikali, na watu wakaliwanajaribu kuunyakua kwa nguvu. 13

Mafundisho yote ya manabii na sheriayalibashiri juu ya nyakati hizi. 14 Kamamwaweza kukubali basi, Yohane ndiye Eliyaambaye angekuja. 15 Mwenye masikio naasikie! 16 “Basi, nitakifananisha kizazi hiki nakitu gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaauwanjani, wakawa wakiambiana kikundikimoja kwa kingine: 17 Tumewapigieni ngomalakini hamkucheza; tumeimba nyimbo zahuzuni lakini hamkulia! 18 Kwa maana Yohanealikuja, akafunga na wala hakunywa divai, naowakasema: Amepagawa na pepo. 19 Mwanawa Mtu akaja, anakula na kunywa, naowakasema: Mtazameni huyu, mlafi na mlevi,

rafiki yao watoza ushuru na wahalifu! Hatahivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwanjema kutokana na matendo yake.” 20 KishaYesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawajealifanya miujiza mingi humo, watu wakehawakutaka kubadili nia zao mbaya: 21 “Olewako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana,kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyikakule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwishavaa mavazi ya gunia na kujipaka majivuzamani, ili kuonyesha kwamba wametubu. 22

Hata hivyo nawaambieni, Siku ya hukumu,ninyi mtapata adhabu kubwa kuliko Tiro naSidoni. 23 Na wewe Kafarnaumu, je, utajikwezampaka mbinguni? Utaporomoshwa mpakaKuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyikakwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huoungalikuwako mpaka hivi leo. 24 Lakininawaambieni, Siku ya hukumu itakuwa nafuuzaidi kwa watu wa Sodoma, kuliko kwakowewe.” 25 Wakati huo Yesu alisema,“Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu nadunia, maana umewaficha wenye hekimamambo haya, ukawafumbulia watoto wadogo.26 Naam Baba, ndivyo ilivyokupendeza. 27

“Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakunaamjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Babaila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwanaatapenda kumjulisha. 28 Njoni kwangu ninyinyote msumbukao na kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu,mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole namnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwarohoni mwenu. 30 Maana, nira niwapayo mimini laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Wakati huo, Yesu alikuwa anapitakatika mashamba ya ngano siku yaSabato. Basi, wanafunzi wake

wakaona njaa, wakaanza kukwanyua masukeya ngano, wakala punje zake. 2 Mafarisayowalipoona hayo, wakamwambia Yesu,“Tazama, wanafunzi wako wanafanya jamboambalo si halali siku ya Sabato.” 3 Yesuakawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudipamoja na wenzake wakati walipokuwa nanjaa? 4 Yeye aliingia katika Nyumba ya Mungupamoja na wenzake, wakala ile mikateiliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala haowenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyoisipokuwa tu makuhani peke yao. 5 Au je,hamjasoma katika Sheria kwamba kila siku yaSabato makuhani huivunja Sheria Hekaluni,lakini hawafikiriwi kuwa na hatia? 6 Basi,nawaambieni kwamba hapa pana kikuu kulikoHekalu. 7 Kama tu mngejua maana ya manenohaya: Nataka huruma wala si dhabihu,hamngewahukumu watu wasio na hatia. 8

Maana Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato.” 9

Yesu alitoka hapo, akaenda katika sunagogilao. 10 Kulikuwa na mtu mmoja mwenyemkono uliopooza. Basi, watu wakamwulizaYesu, “Je, ni halali kumponya mtu siku yaSabato?” Walimwuliza hivyo wapate kisa cha

MATHAYO MTAKATIFU 12:10

11

Page 12: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

kumshtaki. 11 Lakini Yesu akawaambia,“Tuseme mmoja wenu ana kondoo wakeambaye ametumbukia shimoni; je, hatamshikana kumtoa humo siku ya Sabato? 12 Mtu anathamani kuliko kondoo! Basi, ni halali kutendamema siku ya Sabato.” 13 Kisha akamwambiayule mtu, “Nyosha mkono wako.” Akaunyosha,nao ukawa mzima kabisa kama ule mwingine.14 Basi, Mafarisayo wakatoka nje,wakashauriana jinsi watakavyomwangamizaYesu. 15 Lakini Yesu alipojua jambo hilo,akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata,akawaponya wagonjwa wote, 16 akawaamuruwasiwaambie watu habari zake, 17 ili yalealiyosema nabii Isaya yatimie: 18 “Hapa nimtumishi wangu niliyemteua, mpendwawangu anipendezaye moyoni. Nitaiweka Rohoyangu juu yake, naye atatangaza hukumuyangu kwa mataifa yote. 19 Hatakuwa naubishi wala kupiga kelele, wala sauti yakehaitasikika barabarani. 20 Mwanzi uliopondekahatauvunja, wala utambi ufukao moshihatauzima, mpaka atakapoifanya hukumu yahaki itawale. 21 Katika jina lake mataifayatakuwa na tumaini.” 22 Hapo watuwakamletea Yesu kipofu mmoja ambayealikuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawana pepo. Yesu akamponya hata, akawezakusema na kuona. 23 Umati wote wa watuulishangaa ukasema, “Je, huenda ikawa huyundiye Mwana wa Daudi?” 24 Lakini Mafarisayowaliposikia hayo, wakasema, “Mtu huyuanawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli,mkuu wa pepo.” 25 Yesu, akiwa anayajuamawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowoteuliogawanyika makundimakundiyanayopingana, hauwezi kudumu, na mjiwowote au jamaa yoyote iliyogawanyikamakundimakundi yanayopingana, itaanguka.26 Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani,anajipinga mwenyewe. Basi, ufalme wakeutasimamaje? 27 Ninyi mnasema atinawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli; je,watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani?Kwa sababu hiyo wao ndio watakaowahukumuninyi. 28 Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwanguvu ya Roho wa Mungu, basi jueni kwambaUfalme wa Mungu umekwisha fika kwenu. 29

“Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtumwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake,bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenyenguvu? Hapo ndipo atakapowezakumnyang'anya mali yake. 30 “Yeyoteasiyejiunga nami, anapingana nami; na yeyoteasiyekusanya pamoja nami, hutawanya. 31

Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watuwatasamehewa dhambi na kufuru zao zote,lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuruRoho Mtakatifu. 32 Tena, asemaye neno lakumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakiniyule asemaye neno la kumpinga RohoMtakatifu, hatasamehewa, wala katikaulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

33 “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yakeyatakuwa mema; ufanyeni kuwa mbaya namatunda yake yatakuwa mabaya. Mtihujulikana kwa matunda yake. 34 Enyi kizazicha nyoka! Mnawezaje kusema mambo memahali ninyi ni waovu? Maana mtu husemakutokana na yale yaliyojaa moyoni. 35 Mtumwema hutoa mambo mema katika hazinayake njema; na mtu mbaya hutoa mambomabaya katika hazina yake mbaya. 36 “Basi,nawaambieni, Siku ya hukumu watuwatapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaawanalosema. 37 Maana kwa maneno yako,utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa manenoyako, utahukumiwa kuwa na hatia.” 38 Kishabaadhi ya walimu wa Sheria na Mafarisayowakamwambia Yesu, “Mwalimu, tunatakakuona ishara kutoka kwako.” 39 Nayeakawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu!Mnataka ishara; hamtapewa ishara nyingine,ila tu ile ishara ya nabii Yona. 40 Jinsi Yonaalivyokaa siku tatu kutwa kucha tumboni mwanyangumi, ndivyo naye Mwana wa Mtuatakavyokaa ndani ya ardhi siku tatu kutwakucha. 41 Watu wa Ninewi watatokea siku yahukumu, nao watakihukumu kizazi hikikwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubukwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbehapa kuna kikuu kuliko Yona! 42 Malkia wakusini atatokea wakati kizazi hikikitakapohukumiwa, naye atakihukumukwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutokambali akaja kusikiliza maneno ya hekima yaSolomoni, na kumbe hapa kuna kikuu kulikoSolomoni. 43 “Pepo mchafu akifukuzwa kwamtu, huzururazurura jangwani akitafutamahali pa kupumzika asipate. 44 Hapohujisemea: Nitarudi nyumbani kwangunilikotoka. Lakini anaporudi na kuikuta tupu,imefagiwa na kupambwa, 45 huendakuwachukua pepo wengine saba, wabayakuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyomtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbayakuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwakwa watu hawa waovu.” 46 Yesu alikuwa badoanasema na umati wa watu wakati mama yakena ndugu zake walipofika na kusimama nje,wakitaka kusema naye. 47 Basi, mtu mmojaakamwambia, “Mama yako na ndugu zakowako nje, wanataka kusema nawe.” 48 LakiniYesu akamjibu mtu huyo, “Mama yangu ninani? Na ndugu zangu ni kina nani?” 49 Kishaakaunyosha mkono wake kuelekea wanafunziwake, akasema, “Hawa ndio mama yangu nandugu zangu! 50 Maana yeyote anayefanyaanavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyondiye ndugu yangu, dada yangu na mamayangu.”

Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ilenyumba, akaenda na kuketi kando yaziwa. 2 Makundi makubwa ya watu

yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua,akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo

MATHAYO MTAKATIFU 12:11

12

Page 13: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

wa ziwa, 3 naye Yesu akawaambia mambomengi kwa mifano. “Sikilizeni! Mpanzialikwenda kupanda mbegu. 4 Alipokuwaakipanda, nyingine zilianguka njiani, ndegewakaja wakazila. 5 Nyingine zilianguka penyemawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaotamara kwa kuwa udongo haukuwa na kina. 6

Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwamizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka. 7

Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba,nayo ikakua na kuzisonga. 8 Lakini nyinginezilianguka penye udongo mzuri, zikaota,zikazaa: nyingine punje mia moja, nyinginesitini na nyingine thelathini. 9 Mwenye masikiona asikie!” 10 Wanafunzi wake wakamwendea,wakamwuliza, “Kwa nini unasema na watu kwamifano?” 11 Yesu akawajibu, “Ninyi mmejaliwakuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini waohawakujaliwa. 12 Maana, aliye na kitu atapewana kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hatakile alicho nacho kitachukuliwa. 13 Ndiyomaana ninasema nao kwa mifano, kwa sababuwanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakinihawasikii, wala hawaelewi. 14 Kwao yametimiayale aliyosema nabii Isaya: Kusikia mtasikia,lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama,lakini hamtaona. 15 Maana akili za watu hawazimepumbaa, wameyaziba masikio yao,wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeonakwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao,wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia,asema Bwana, nami ningewaponya. 16 “Lakiniheri yenu ninyi, maana macho yenu yanaonana masikio yenu yanasikia. 17 Kwelinawaambieni, manabii na watu wengi wemawalitamani kuyaona yale mnayoyaona,wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia,wasiyasikie. 18 “Basi, ninyi sikilizeni maana yamfano huo wa mpanzi. 19 Yeyote asikiayeujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zilembegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu hujana kunyakua kile kilichopandwa moyonimwake. 20 Ile mbegu iliyopandwa penyemawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe huona mara akaupokea kwa furaha. 21 Lakinihaumwingii na kuwa na mizizi ndani yake;huendelea kuuzingatia ujumbe huo kwakitambo tu, na wakati taabu au udhalimuvinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo,anakata tamaa mara. 22 Ile mbegu iliyoangukakati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiayehuo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwenguhuu na anasa za mali huusonga ujumbe huo,naye hazai matunda. 23 Ile mbegu iliyopandwakatika udongo mzuri ni mfano wa mtuausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, nayehuzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitinina mwingine thelathini.” 24 Yesu akawaambiawatu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguniunafanana na mtu aliyepanda mbegu nzurikatika shamba lake. 25 Lakini watu wakiwawamelala, adui yake akaja akapanda magugukati ya ngano, akaenda zake. 26 Basi, mimea

ilipoota na kuanza kuchanua, magugu piayakaanza kuonekana. 27 Watumishi wa yulemwenye shamba wakamwendea,wakamwambia, Mheshimiwa, bila shakaulipanda mbegu nzuri katika shamba lako.Sasa magugu yametoka wapi? 28 Yeyeakawajibu, Adui ndiye aliyefanya hivyo. Basi,watumishi wake wakamwuliza, Je, unatakatwende tukayang'oe 29 Naye akawajibu, La,msije labda mnapokusanya magugu,mkang'oa na ngano pia. 30 Acheni vikuepamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huonitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanzamagugu mkayafunge mafungumafungu yakuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiwekeghalani mwangu.” 31 Yesu akawaambia watumfano mwingine: “Ufalme wa mbinguniunafanana na mbegu ya haradali aliyotwaamtu mmoja, akaipanda katika shamba lake. 32

Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakiniikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote.Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja nakujenga viota katika matawi yake.” 33 Yesuakawaambia mfano mwingine: “Ufalme wambinguni umefanana na chachu aliyotwaamama mmoja, akaichanganya na unga pishitatu, hata unga wote ukaumuka.” 34 Yesualiwaambia watu hayo yote kwa mifano.Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,35 ili jambo lililonenwa na nabii litimie:“Nitasema kwa mifano; nitawaambia mamboyaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.” 36

Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingianyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea,wakamwambia, “Tufafanulie ule mfano wamagugu shambani.” 37 Yesu akawaambia,“Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana waMtu. 38 Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegunzuri ni watu wale ambao Ufalme ni wao.Lakini yale magugu ni wale watu wa yuleMwovu. 39 Adui aliyepanda yale magugu niIbilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati nawavunaji ni malaika. 40 Kama vile maguguyanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyoitakavyokuwa mwishoni mwa nyakati; 41

Mwana wa Mtu atawatuma malaika wakewawakusanye kutoka katika Ufalme wake walewote wenye kusababisha dhambi, na wotewenye kutenda maovu, 42 na kuwatupa katikatanuru ya moto, na huko watalia na kusagameno. 43 Kisha, wale wema watang'ara kamajua katika Ufalme wa Baba yao. Sikieni basi,kama mna masikio! 44 “Ufalme wa mbinguniumefanana na hazina iliyofichika shambani.Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena.Alifurahi sana hata akaenda kuuza yotealiyokuwa nayo, akalinunua shamba lile. 45

“Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana namfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulunzuri. 46 Alipopata lulu moja ya thamanikubwa, alienda akauza yote aliyokuwa nayo,akainunua lulu ile. 47 “Tena, Ufalme wambinguni unafanana na wavu uliotupwa

MATHAYO MTAKATIFU 13:47

13

Page 14: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

14

15

baharini, ukanasa samaki wa kila aina. 48

Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi,wakachagua samaki wazuri wakawawekandani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa.49 Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwanyakati: malaika watatokea,watawatenganisha watu wabaya na watuwema, 50 na kuwatupa hao wabaya katikatanuru ya moto. Huko watalia na kusagameno.” 51 Yesu akawauliza, “Je, mmeelewamambo haya yote?” Wakamjibu, “Naam.” 52

Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimuwa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wambinguni anafanana na mwenye nyumbaatoaye katika hazina yake vitu vipya na vyakale.” 53 Yesu alipomaliza kusema mifano hiyoalitoka mahali hapo, 54 akaenda kijijini kwake.Huko akawa anawafundisha watu katikasunagogi hata wakashangaa, wakasema,“Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je,mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake sikina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Nadada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi?Basi amepata wapi haya yote?” 57 Basi,wakawa na mashaka naye. Lakini Yesuakawaambia, “Nabii hakosi kuheshimiwa,isipokuwa katika nchi yake na nyumbanimwake!” 58 Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingipale kwa sababu ya kutoamini kwao.

Wakati huo, mtawala Herode alisikiasifa za Yesu. 2 Basi, akawaambiawatumishi wake, “Mtu huyu ni Yohane

mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyomaana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndaniyake.” 3 Herode ndiye aliyekuwa amemtiaYohane nguvuni, akamfunga minyororo nakumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mkewa Filipo, ndugu yake. Sababu hasa ni 4

kwamba alikuwa amemwambia Herode, “Sihalali kwako kuishi na huyo mwanamke!” 5

Herode alitaka kumwua Yohane, lakinialiogopa watu kwa sababu kwao Yohanealikuwa nabii. 6 Katika sherehe za sikukuu yakuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodiaalicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa,7 hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyomsichana chochote atakachoomba. 8 Naye,huku akichochewa na mama yake, akaomba,“Nipe papahapa katika sinia kichwa chaYohane mbatizaji.” 9 Mfalme alihuzunika, lakinikwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababuya wale wageni karamuni, akaamuru apewe.10 Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkatekichwa Yohane. 11 Kichwa chake kikaletwakatika sinia, wakampa yule msichana, nayeakampelekea mama yake. 12 Wanafunzi waYohane wakaja, wakauchukua mwili wake,wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habariYesu. 13 Yesu alipopata habari hiyo, aliondokamahali pale kwa mashua, akaenda mahali pafaragha peke yake. Lakini watu walipatahabari, wakamfuata kwa miguu toka mijini. 14

Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwawa watu, akawaonea huruma, akawaponyawagonjwa wao. 15 Kulipokuwa jioni, wanafunziwake walimwendea wakamwambia, “Mahalihapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaagewatu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”16 Yesu akawaambia, “Si lazima waende,wapeni ninyi chakula.” 17 Lakini waowakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu nasamaki wawili.” 18 Yesu akawaambia,“Nileteeni hapa.” 19 Akawaamuru watu waketikatika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate mitanona wale samaki wawili, akatazama juumbinguni, akamshukuru Mungu. Halafuakaimega hiyo mikate, akawapa wanafunziwake, nao wakawapa watu. 20 Watu wotewakala, wakashiba. Kisha wanafunziwakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumina viwili. 21 Jumla ya waliokula ilikuwawanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabuwanawake na watoto. 22 Mara, Yesuakawaamuru wanafunzi wake wapandemashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakatiyeye anawaaga watu. 23 Baada ya kuwaaga,alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwajioni, yeye alikuwa huko peke yake, 24 nawakati huo ile mashua ilikwishafika karibukatikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwendamrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.25 Usiku, karibu na mapambazuko, Yesualiwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji.26 Wanafunzi wake walipomwona akitembeajuu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, “Nimzimu!” Wakapiga kelele kwa hofu. 27 Mara,Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi.Msiogope!” 28 Petro akamwambia, “Bwana,ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu yamaji nije kwako.” 29 Yesu akasema, “Haya,njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua,akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu. 30

Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanzakuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!” 31

Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake,akamshika na kumwambia, “Ewe mwenyeimani haba! Kwa nini uliona shaka?” 32 Basi,wakapanda mashuani, na upepo ukatulia. 33

Wote waliokuwa ndani ya mashuawalimsujudia, wakasema, “Hakika wewe niMwana wa Mungu.” 34 Walivuka ziwa,wakafika nchi ya Genesareti. 35 Watu wa hukowalipomtambua, wakaeneza habari potekatika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesuwagonjwa wote, 36 wakamwomba awaruhusuwaguse tu pindo la vazi lake; wote waliomgusawalipona.

Kisha Mafarisayo na walimu wa Sheriawakafika kutoka Yerusalemu,wakamwendea Yesu, wakamwuliza, 2

“Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeotuliyopokea kutoka kwa wazee wetu?Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla yakula!” 3 Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyimnapendelea mapokeo yenu wenyewe na

MATHAYO MTAKATIFU 13:48

14

Page 15: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

hamuijali Sheria ya Mungu? 4 Munguamesema: Waheshimu baba yako na mamayako, na Anayemkashifu baba yake au mamayake, lazima auawe. 5 Lakini ninyimwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambachoangeweza kuwasaidia nacho baba au mamayake, lakini akasema: Kitu hiki nimemtoleaMungu, 6 basi, hapaswi tena kumheshimubaba yake! Ndivyo mnavyodharau neno laMungu kwa kufuata mafundisho yenuwenyewe. 7 Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawakabisa juu yenu: 8 Watu hawa, asema Mungu,huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyonimwao wako mbali nami. 9 Kuniabudu kwaohakufai, maana mambo wanayofundisha nimaagizo ya kibinadamu tu.” 10 Yesu aliuita uleumati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni namuelewe! 11 Kitu kinachomtia mtu najisi si kilekiingiacho kinywani, bali kile kitokachokinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu najisi.”12 Kisha wanafunzi wakamwendea,wakamwambia, “Je, unajua kwambaMafarisayo walichukizwa waliposikia manenoyako?” 13 Lakini yeye akawajibu, “Kila mmeaambao Baba yangu aliye mbingunihakuupanda, utang'olewa. 14 Waacheniwenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu;na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawilihutumbukia shimoni.” 15 Petro akadakia,“Tufafanulie huo mfano.” 16 Yesu akasema,“Hata nyinyi hamwelewi? 17 Je, hamwelewikwamba kila kinachoingia kinywani huendatumboni na baadaye hutupwa nje chooni? 18

Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni,na hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi. 19

Maana moyoni hutoka mawazo maovuyanayosababisha uuaji, uzinzi, uasherati, wizi,ushahidi wa uongo na kashfa. 20 Hayo ndiyoyanayomtia mtu najisi. Lakini kula chakula bilakunawa mikono hakumtii mtu najisi.” 21 Yesualiondoka mahali hapo akaenda kukaa katikasehemu za Tiro na Sidoni. 22 Basi, mamammoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia,akapaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana waDaudi, nionee huruma! Binti yanguanasumbuliwa na pepo.” 23 Lakini Yesuhakumjibu neno. Basi, wanafunzi wakewakamwendea, wakamwambia, “Mwambieaende zake kwa maana anatufuatafuataakipiga kelele.” 24 Yesu akajibu, “Sikutumwa ilakwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo.”25 Hapo huyo mama akaja, akapiga magotimbele yake, akasema, “Mheshimiwa, nisaidie.”26 Yesu akamjibu, “Si sawa kuchukua chakulacha watoto na kuwatupia mbwa.” 27 Huyomama akajibu, “Ni kweli, Mheshimiwa; lakinihata mbwa hula makombo yanayoangukakutoka meza ya bwana wao.” 28 Hapo Yesuakamjibu, “Mama, imani yako ni kubwa; basi,ufanyiwe kama unavyotaka.” Yule binti yakeakapona tangu saa hiyo wakati huohuo. 29

Yesu alitoka hapo akaenda kando ya ziwaGalilaya, akapanda mlimani, akaketi. 30 Watu

wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema,vipofu, viwete, bubu na wengine wengiwaliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele yamiguu yake, naye Yesu akawaponya. 31 Umatiule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubuwakiongea, waliokuwa wamelemaawamepona, viwete wakitembea na vipofuwakiona; wakamsifu Mungu wa Israeli. 32 Basi,Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema,“Nawaonea watu hawa huruma kwa sababukwa siku tatu wamekuwa nami, wala hawanachakula. Sipendi kuwaacha waende bila kulawasije wakazimia njiani.” 33 Wanafunziwakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapatawapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?”34 Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?”Wakamjibu, “Saba na visamaki vichache.” 35

Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini. 36

Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki,akamshukuru Mungu, akavimega, akawapawanafunzi, nao wakawagawia watu. 37 Wotewakala, wakashiba. Kisha wakakusanyamakombo, wakajaza vikapu saba. 38 Haowaliokula walikuwa wanaume elfu nne, bilakuhesabu wanawake na watoto. 39 Basi, Yesuakawaaga watu, akapanda mashua, akaendakatika eneo la Magadani.

Mafarisayo na Masadukayowalimwendea Yesu, na kwakumjaribu, wakamwomba afanye

ishara itokayo mbinguni. 2 Lakini Yesuakawajibu, “Wakati wa jioni ukifika ninyihusema: Hali ya hewa itakuwa nzuri kwamaana anga ni jekundu! 3 Na alfajirimwasema: Leo hali ya hewa itakuwa yadhoruba, maana anga ni jekundu na tenamawingu yametanda! Basi, ninyi mnajua sanakusoma majira kwa kuangalia anga, lakinikutambua dalili za nyakati hizi hamjui. 4 Kizazikiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara,lakini hamtapewa ishara yoyote isipokuwa tuile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake. 5

Wanafunzi wake walipokwisha vukia upandewa pili wa ziwa, walijikuta wamesahaukuchukua mikate. 6 Yesu akawaambia, “Muwemacho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayona Masadukayo!” 7 Lakini wao wakawawanajadiliana: “Anasema hivyo kwa kuwahatukuchukua mikate.” 8 Yesu alijua mawazoyao, akawaambia, “Enyi watu wenye imanihaba! Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa namikate? 9 Je, hamjaelewa bado? Je,hamkumbuki nilipoimega ile mikate mitanokwa ajili ya wale watu elfu tano? Je, mlijazavikapu vingapi vya makombo? 10 Au, ile mikatesaba waliyogawiwa wale watu elfu nne, je,mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki? 11

Inawezekanaje hamwelewi ya kwamba sikuwanikisema juu ya mikate? Jihadharini na chachuya Mafarisayo na Masadukayo!” 12 Hapowanafunzi wakafahamu kwamba aliwaambiawajihadhari siyo na chachu ya mikate, bali namafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. 13

MATHAYO MTAKATIFU 16:13

15

Page 16: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

17

Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi,aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasemaMwana wa Mtu kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu,“Wengine wanasema kuwa ni Yohanembatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia aummojawapo wa manabii.” 15 Yesu akawauliza,“Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?” 16

Simoni Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo,Mwana wa Mungu aliye hai.” 17 Yesu akasema,“Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwamaana si binadamu aliyekufunulia ukweli huu,ila Baba yangu aliye mbinguni. 18 Naminakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwambahuu nitalijenga kanisa langu; wala kifochenyewe hakitaweza kulishinda. 19 Nitakupafunguo za Ufalme wa mbinguni; kilautakachofunga duniani, kitafungwa piambinguni; kila utakachofungua duniani,kitafunguliwa pia mbinguni.” 20 Kishaakawaonya wanafunzi wasimwambie mtuyeyote kwamba yeye ndiye Kristo. 21 Tanguwakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwaziwanafunzi wake: “Ni lazima mimi niendeYerusalemu, na huko nikapate mateso mengiyatakayosababishwa na wazee, makuhaniwakuu na walimu wa Sheria. Nitauawa, na sikuya tatu nitafufuliwa.” 22 Hapo Petroakamchukua kando, akaanza kumkemea:“Isiwe hivyo Bwana! Jambo hili halitakupata!”23 Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro,“Ondoka mbele yangu Shetani! Wewe nikikwazo kwangu. Mawazo yako si ya mungubali ni ya kibinadamu!” 24 Kisha Yesuakawaambia wanafunzi wake, “Kama mtuyeyote anataka kuwa mfuasi wangu, ni lazimaajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake,anifuate. 25 Maana, mtu anayetaka kuyaokoamaisha yake mwenyewe, atayapoteza; 26 lakinimtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajiliyangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupatautajiri wote wa ulimwengu na hali amepotezamaisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwebadala ya maisha yake? 27 Maana, Mwana waMtu atakuja katika utukufu wa Baba yakepamoja na malaika wake, na hapo ndipoatakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake.28 Kweli nawaambieni, wako wenginepapahapa ambao hawatakufa kabla yakumwona Mwana wa Mtu akija katika Ufalmewake.”

Baada ya siku sita, Yesu aliwachukuaPetro, Yakobo na Yohane nduguye,akaenda nao peke yao juu ya mlima

mrefu. 2 Huko, wakiwa wanamtazama,akageuka sura, uso wake ukang'aa kama juana mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3

Mose na Eliya wakawatokea, wakawawanazungumza naye. 4 Hapo Petroakamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sanakwamba tupo hapa! Ukipenda nitajengavibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mosena kimoja cha Eliya.” 5 Alipokuwa badoanasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na

sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyuni Mwanangu mpendwa, ninayependezwanaye, msikilizeni.” 6 Wanafunzi waliposikiahivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopasana. 7 Yesu akawaendea, akawagusa,akasema, “Simameni, msiogope!” 8 Walipoinuamacho yao hawakumwona mtu, ila Yesu pekeyake. 9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani,Yesu akawaonya: “Msimwambie mtu mambomliyoyaona mpaka Mwana wa Mtuatakapofufuliwa kutoka wafu.” 10 Kishawanafunzi wakamwuliza, “Mbona walimu waSheria wanasema ati ni lazima kwanza Eliyaaje?” 11 Yesu akawajibu, “Kweli, Eliya atakujakutayarisha mambo yote. 12 Lakininawaambieni, Eliya amekwisha kuja naohawakumtambua, bali walimtendea jinsiwalivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyohivyo mikononi mwao.” 13 Hapo haowanafunzi wakafahamu kwamba alikuwaakiwaambia juu ya Yohane mbatizaji. 14

Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtummoja alimwendea Yesu, akampigia magoti,15 akasema, “Mheshimiwa, mwonee hurumamwanangu kwa kuwa ana kifafa, tenaanateseka sana; mara nyingi yeye huangukamotoni na majini. 16 Nilimleta kwa wanafunziwako lakini hawakuweza kumponya.” 17 Yesuakajibu, “Enyi kizazi kisicho na imani,kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini?Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapahuyo mtoto.” 18 Basi, Yesu akamkemea huyopepo, naye akamtoka, na yule mtoto akaponawakati huohuo. 19 Kisha wanafunziwakamwendea Yesu kwa faragha,wakamwuliza, “Kwa nini sisi hatukuwezakumtoa yule pepo?” 20 Yesu akawajibu, “Kwasababu ya imani yenu haba. Nawaambienikweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwendogo kama mbegu ya haradali, mtawezakuuambia mlima huu: Toka hapa uende pale,nao utakwenda. Hakuna chochote ambachohakingewezekana kwenu.” 21 “Pepo wa namnahii hawezi kuondolewa ila kwa sala nakufunga.” 22 Walipokuwa pamoja hukoGalilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Mtuatakabidhiwa kwa watu. 23 Watamuua, lakinisiku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunziwakahuzunika mno. 24 Walipofika Kafarnaumuwatu wenye kukusanya fedha ya zaka yaHekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, “Je,mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?” 25 Petroakajibu, “Naam, hulipa.” Basi, Petro alipoingiandani ya nyumba, kabla hata hajasema neno,Yesu akamwuliza, “Simoni, wewe unaonaje?Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodikutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchiama kutoka kwa wageni?” 26 Petro akajibu,“Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia,“Haya basi, wananchi hawahusiki. 27 Lakinikusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupendoana; chukua samaki wa kwanzaatakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani

MATHAYO MTAKATIFU 16:14

16

Page 17: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

18

19

utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukueukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.”

Wakati ule wanafunzi walimwendeaYesu, wakamwuliza, “Ni nani aliyemkuu katika Ufalme wa mbinguni?” 2

Yesu akamwita mtoto mmoja, akamsimamishakati yao, 3 kisha akasema, “Nawaambienikweli, msipogeuka na kuwa kama watoto,hamtaingia kamwe katika Ufalme wambinguni. 4 Yeyote anayejinyenyekesha kamamtoto huyu, huyo ndiye aliye mkubwa katikaUfalme wa mbinguni. 5 Yeyoteanayemkaribisha mtoto mmoja kama huyukwa jina langu, ananikaribisha mimi. 6 “Yeyoteatakayemkosesha mmoja wa hawa wadogowanaoniamini, ingekuwa afadhali afungweshingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwakwenye kilindi cha bahari. 7 Ole wakeulimwengu kwa sababu ya vikwazovinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo nilazima vitokee lakini ole wake mtu yuleatakayevisababisha. 8 “Kama mkono au mguuwako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbalinawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzimabila mkono au mguu, kuliko kutupwa katikamoto wa milele ukiwa na mikono miwili namiguu yako miwili. 9 Na kama jicho lakolikikukosesha, ling'oe na kulitupa mbali nawe.Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwachongo, kuliko kutupwa katika moto waJehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.10 “Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wawadogo hawa. Nawaambieni, malaika waohuko mbinguni wako daima mbele ya Babayangu aliye mbinguni. 11 Maana Mwana waMtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea. 12

Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia,akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaachawale tisini na tisa mlimani, na huendakumtafuta yule aliyepotea. 13 Akimpata,nawaambieni kweli, humfurahia huyo kulikoawafurahiavyo wale tisini na tisa ambaohawakupotea. 14 Hali kadhalika, Baba yenu wambinguni hapendi hata mmoja wa hawawadogo apotee. 15 “Ndugu yako akikukosea,mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu.Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako. 16

Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawilipamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidiwawili au watatu, kila tatizo litatuliwe. 17

Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kamahatalisikia kanisa, na awe kwako kama watuwasiomjua Mungu na watoza ushuru. 18

“Nawaambieni kweli, mtakachofunga dunianikitafungwa mbinguni, na mtakachofunguaduniani kitafunguliwa mbinguni. 19 Tenanawaambieni, wawili miongoni mwenuwakikubaliana hapa duniani kuhusu jambololote la kuomba, Baba yangu wa mbinguniatawafanyia jambo hilo. 20 Kwa maana popotepale wanapokusanyika wawili au watatu kwajina langu, mimi nipo hapo kati yao.” 21 KishaPetro akamwendea Yesu, akamwuliza, “Je,

ndugu yangu akinikosea, nimsamehe marangapi? Mara saba?” 22 Yesu akamjibu, “Sisemimara saba tu, bali sabini mara saba. 23 Ndiyomaana Ufalme wa mbinguni umefanana namfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu zawatumishi wake. 24 Ukaguzi ulipoanza,akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni lafedha talanta elfu kumi. 25 Mtu huyo hakuwana chochote cha kulipa; hivyo bwana wakealiamuru wauzwe, yeye, mke wake, watotowake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili denililipwe. 26 Basi, huyo mtumishi akapiga magotimbele yake, akasema, Unisubiri naminitakulipa deni lote. 27 Yule bwana alimwoneahuruma, akamsamehe lile deni, akamwachaaende zake. 28 “Lakini huyo mtumishiakaondoka, akamkuta mmoja wa watumishiwenzake aliyekuwa na deni lake fedha denarimia moja. Akamkamata, akamkaba kooakisema, Lipa deni lako! 29 Huyo mtumishimwenzake akapiga magoti, akamwomba,Unisubiri nami nitalipa deni langu lote. 30

Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezanimpaka hapo atakapolipa lile deni. 31 “Basi,watumishi wenzake walipoona jambo hilowalisikitika sana, wakaenda kumpasha habaribwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia. 32

Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi,akamwambia, Wewe ni mtumishi mbaya sana!Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.33 Je, haikukupasa nawe kumhurumiamtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?34 “Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoahuyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapoatakapolipa deni lote. 35 Na baba yangu aliyembinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kilammoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwamoyo wake wote.”

Yesu alipomaliza kusema manenohayo, alitoka Galilaya, akaenda katikamkoa wa Yudea, ng'ambo ya mto

Yordani. 2 Watu wengi walimfuata huko, nayeakawaponya. 3 Mafarisayo kadhaa walimjia,wakamwuliza kwa kumtega, “Je, ni halali mumekumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?” 4

Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katikaMaandiko Matakatifu kwamba Mungualiyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanyamwanamume na mwanamke, 5 na akasema:Kwa sababu hiyo mwanamume atamwachababa yake na mama yake, ataungana na mkewake, nao wawili watakuwa mwili mmoja? 6

Kwa hiyo wao si wawili tena, bali mwili mmoja.Basi, alichounganisha Mungu, binadamuasikitenganishe.” 7 Lakini wao wakamwuliza,“Kwa nini basi, Mose alituagiza mwanamkeapewe hati ya talaka na kuachwa?” 8 Yesuakawajibu, “Mose aliwaruhusu kuwaacha wakezenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 9

Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basinawaambieni, yeyote atakayemwacha mkewake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoamke mwingine, anazini.” 10 Wanafunzi wake

MATHAYO MTAKATIFU 19:10

17

Page 18: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

20wakamwambia, “Ikiwa mambo ya mume namkewe ni hivyo, ni afadhali kutooa kabisa.” 11

Yesu akawaambia, “Si wote wanaowezakulipokea fundisho hili, isipokuwa tu walewaliojaliwa na Mungu. 12 Maana kuna sababukadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwasababu wamezaliwa hivyo, wengine kwasababu wamefanywa hivyo na watu, nawengine wameamua kutooa kwa ajili yaUfalme wa mbinguni. Awezaye kulipokeafundisho hili na alipokee.” 13 Kisha watuwakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekeemikono na kuwaombea. Lakini wanafunziwakawakemea. 14 Yesu akasema, “Waachenihao watoto waje kwangu, wala msiwazuie;maana Ufalme wa mbinguni ni wa watu waliokama watoto hawa.” 15 Basi, akawawekeamikono, kisha akaondoka mahali hapo. 16 Mtummoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu,nifanye kitu gani chema ili niupate uzima wamilele?” 17 Yesu akamwambia, “Mbonaunaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmojatu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uzima,shika amri.” 18 Yule mtu akamwuliza, “Amrizipi?” Yesu akasema, “Usiue, usizini, usiibe,usitoe ushahidi wa uongo, 19 waheshimu babayako na mama yako; na, mpende jirani yakokama unavyojipenda mwenyewe.” 20 Huyokijana akamwambia, “Hayo yotenimeyazingatia tangu utoto wangu; sasanifanye nini zaidi?” 21 Yesu akamwambia,“Kama unapenda kuwa mkamilifu, nendaukauze mali yako uwape maskini hiyo fedha,nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoounifuate.” 22 Huyo kijana aliposikia hayo,alienda zake akiwa mwenye huzuni, maanaalikuwa na mali nyingi. 23 Hapo Yesuakawaambia wanafunzi wake, “Kwelinawaambieni, itakuwa vigumu sana kwa tajirikuingia katika Ufalme wa mbinguni. 24 Tenanawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupitakatika tundu la sindano, kuliko kwa tajirikuingia katika Ufalme wa mbinguni.” 25 Walewanafunzi waliposikia hivyo walishangaa,wakamwuliza, “Ni nani basi, awezayekuokoka?” 26 Yesu akawatazama, akasema,“Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakinikwa Mungu mambo yote huwezekana.” 27

Kisha Petro akasema, “Na sisi je? Tumeachayote tukakufuata; tutapata nini basi?” 28 Yesuakawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana waMtu atakapoketi katika kiti cha enzi chautukufu wake katika ulimwengu mpya, ninyimlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwilimkiyahukumu makabila kumi na mawili yaIsraeli. 29 Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu,au dada, au baba, au mama, au watoto, aumashamba, kwa ajili yangu, atapokea maramia zaidi, na kupata uzima wa milele. 30 Lakiniwalio wa kwanza watakuwa wa mwisho, nawalio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

“Ufalme wa mbinguni unafanana namtu mwenye shamba la mizabibu,ambaye alitoka asubuhi na mapema

kuwaajiri wafanyakazi katika shamba lake. 2

Akapatana nao kuwalipa dinari moja kwa siku,kisha akawapeleka katika shamba lake lamizabibu. 3 Akatoka mnamo saa tatu asubuhi,akaona watu wengine wamesimama sokoni,hawana kazi. 4 Akawaambia, Nendeni nanyimkafanye kazi katika shamba la mizabibu,nami nitawapeni haki yenu. 5 Basi, wakaenda.Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamosaa sita na saa tisa, akafanya vivyo hivyo. 6

Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatokatena; akakuta watu wengine wamesimamapale sokoni. Basi, akawauliza, Mbonammesimama hapa mchana kutwa bila kazi? 7

Wakamjibu: Kwa sababu hakuna mtualiyetuajiri. Yeye akawaambia, Nendeni nanyimkafanye kazi katika shamba la mizabibu. 8

“Kulipokuchwa, huyo mwenye shambaalimwambia mtunza hazina wake, Waitewafanyakazi ukawalipe mshahara wao,ukianzia na wale walioajiriwa mwisho, nakumalizia na wale wa kwanza. 9 Basi, wakajawale walioajiriwa mnamo saa kumi na moja,wakapokea kila mmoja dinari moja. 10 Walewa kwanza walipofika, walikuwa wanadhaniwatapewa zaidi; lakini hata wao wakapewa kilammoja dinari moja. 11 Wakazipokea fedha zao,wakaanza kumnung'unikia yule bwana. 12

Wakasema, Watu hawa walioajiriwa mwishowalifanya kazi kwa muda wa saa moja tu,mbona umetutendea sawa na wao hali sisitumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali? 13

“Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao,Rafiki, sikukupunja kitu! Je, hukupatana namimshahara wa denari moja? 14 Chukua hakiyako, uende zako. Napenda kumpa huyu wamwisho sawa na wewe. 15 Je, sina haki yakufanya na mali yangu nipendavyo? Je, unaonakijicho kwa kuwa mimi ni mwema?” 16 Yesuakamaliza kwa kusema, “Hivyo, walio wamwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanzawatakuwa wa mwisho.” 17 Yesu alipokuwaanakwenda Yerusalemu, aliwachukua walewanafunzi kumi na wawili faraghani, na njianiakawaambia, 18 “Sikilizeni! TunakwendaYerusalemu, na huko Mwana wa Mtuatakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimuwa Sheria, nao watamhukumu auawe. 19

Watamkabidhi kwa watu wa mataifa mengineili adhihakiwe, apigwe viboko na kusulubiwa;lakini siku ya tatu atafufuliwa.” 20 Hapo mamayao wana wa Zebedayo alimjia Yesu pamoja nawanawe, akapiga magoti mbele yake nakumwomba kitu. 21 Yesu akamwuliza,“Unataka nini?” Huyo mama akamwambia,“Ahidi kwamba katika Ufalme wako, hawawanangu wawili watakaa mmoja upande wakowa kulia na mwingine upande wako wakushoto.” 22 Yesu akajibu, “Hamjui mnaombanini. Je, mnaweza kunywa kikombe

MATHAYO MTAKATIFU 19:11

18

Page 19: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

21

nitakachokunywa mimi?” Wakamjibu,“Tunaweza.” 23 Yesu akawaambia, “Kwelimtakunywa kikombe changu, lakini kuketikulia au kushoto kwangu si kazi yangukupanga; jambo hilo watapewa walewaliowekewa tayari na Baba yangu.” 24 Walewanafunzi wengine kumi waliposikia hayo,wakawakasirikia hao ndugu wawili. 25 HivyoYesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwambawatawala wa mataifa hutawala watu wao kwamabavu na wakuu hao huwamiliki watu wao.26 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila yeyoteanayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awemtumishi wa wote; 27 na anayetaka kuwa wakwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu.28 Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakujakutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maishayake kuwa fidia ya watu wengi.” 29 Yesualipokuwa anaondoka mjini Yeriko, umati wawatu ulimfuata. 30 Basi, kulikuwa na vipofuwawili wameketi kando ya njia, na waliposikiakwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaazasauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi,utuhurumie!” 31 Ule umati wa watuukawakemea na kuwaambia wanyamaze.Lakini wao wakazidi kupaaza sauti:“Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”32 Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza,“Mnataka niwafanyie nini?” 33 Wakamjibu,“Mheshimiwa, tunaomba macho yetuyafumbuliwe.” 34 Basi, Yesu akawaoneahuruma, akawagusa macho yao, na papo hapowakaweza kuona, wakamfuata.

Yesu na wanafunzi wake walipokaribiaYerusalemu na kufika Bethfage katikamlima wa Mizeituni, aliwatuma

wanafunzi wake wawili, 2 akawaambia,“Nendeni hadi kijiji kilicho mbele yenu namtamkuta punda amefungwa na mtoto wake.Wafungueni mkawalete kwangu. 3 Kama mtuakiwauliza sababu, mwambieni, Bwanaanawahitaji, naye atawaachieni mara.” 4

Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa nanabii yatimie: 5 “Uambieni mji wa Sioni:Tazama, Mfalme wako anakujia! Ni mpole naamepanda punda, mwana punda, mtoto wapunda.” 6 Hivyo, wale wanafunzi waliendawakafanya kama Yesu alivyowaagiza. 7

Wakamleta yule punda na mtoto wake,wakatandika nguo zao juu yao na Yesu akaketijuu yake. 8 Umati mkubwa wa watuukatandaza nguo zao barabarani, na watuwengine wakakata matawi ya mitiwakayatandaza barabarani. 9 Makundi yawatu waliomtangulia na wale waliomfuatawakapaaza sauti: “Hosana Mwana wa Daudi!Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!Hosana Mungu juu mbinguni!” 10 Yesualipokuwa anaingia Yerusalemu, mji woteukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza, “Huyuni nani?” 11 Watu katika ule umati wakasema,“Huyu ni nabii Yesu, kutoka Nazareti katikamkoa wa Galilaya.” 12 Basi, Yesu akaingia

Hekaluni, akawafukuza nje watu waliokuwawanauza na kununua vitu ndani ya Hekalu;akazipindua meza za wale waliokuwawanavunja fedha, na viti vya wale waliokuwawanauza njiwa. 13 Akawaambia, “Imeandikwakatika Maandiko Matakatifu: Nyumba yanguitaitwa nyumba ya sala. Lakini ninyi mmeifanyakuwa pango la wanyang'anyi.” 14 Vipofu navilema walimwendea huko Hekaluni, naye Yesuakawaponya. 15 Basi, makuhani wakuu nawalimu wa Sheria walipoyaona maajabualiyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwawanapaaza sauti zao Hekaluni wakisema: “Sifakwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika. 16 Hivyowakamwambia, “Je, husikii wanachosema?”Yesu akawajibu, “Naam, nasikia! Je hamjasomaMaandiko haya Matakatifu? Kwa vinywa vyawatoto wadogo na wanyonyao unajipatia sifakamilifu.” 17 Basi, akawaacha, akatoka nje yamji na kwenda Bethania, akalala huko. 18 Yesualipokuwa anarudi mjini asubuhi na mapema,aliona njaa. 19 Akauona mtini mmoja kando yanjia, akauendea; lakini aliukuta haumachochote ila majani matupu. Basi akauambia,“Usizae tena matunda milele!” Papo hapo huomtini ukanyauka. 20 Wanafunzi walipouonawalishangaa wakisema, “Kwa nini mtini huuumenyauka ghafla?” 21 Yesu akawajibu, “Kwelinawaambieni, kama mkiwa na imani bila kuwana mashaka, mnaweza si tu kufanya hivyo, balihata mkiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitosebaharini, itafanyika hivyo. 22 Na mkiwa naimani, chochote mtakachoomba katika sala,mtapata.” 23 Yesu aliingia Hekaluni, akawaanafundisha. Alipokuwa akifundisha,makuhani wakuu na wazee wa watuwakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwamamlaka gani? Nani amekupa mamlaka haya?”24 Yesu akawajibu, “Na mimi nitawaulizeniswali moja; mkinijibu, basi nami nitawaambienininafanya mambo haya kwa mamlaka gani. 25

Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitokakwa nani? Je, yalitoka mbinguni ama kwawatu?” Lakini wakajadiliana wao kwa wao hivi:“Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi,mbona hamkumsadiki? 26 Na tukisema,Yalitoka kwa watu, tunaogopa umati wa watumaana wote wanakubali kwamba Yohane ninabii.” 27 Basi, wakamjibu, “Hatujui!” NayeYesu akawaambia, “Nami pia sitawaambienininafanya mambo haya kwa mamlaka gani. 28

“Ninyi mnaonaje; mtu mmoja alikuwa na wanawawili. Akamwambia yule wa kwanza,Mwanangu, leo nenda ukafanye kazi katikashamba la mizabibu. 29 Yule kijanaakamwambia, Sitaki! Lakini baadaye akabadilinia, akaenda kufanya kazi. 30 Yule babaakamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo,naye akamjibu, Naam baba! Lakini hakwendakazini. 31 Je, ni nani kati ya hawa wawilialiyetimiza matakwa ya baba yake?”Wakamjibu, “Yule mtoto wa kwanza.” Basi,Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni,

MATHAYO MTAKATIFU 21:31

19

Page 20: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

22

watoza ushuru na waasherati wataingia katikaUfalme wa Mungu kabla yenu. 32 MaanaYohane alikuja kwenu akawaonyesha njianjema ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakiniwatoza ushuru na waasherati walimwamini.Hata baada ya kuona hayo yote ninyihamkubadili mioyo yenu, na hamkusadiki.” 33

Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine.Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shambala mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimbakisima cha kusindikia divai, akajenga humomnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima,akasafiri kwenda nchi ya mbali. 34 Wakati wamavuno ulipofika, aliwatuma watumishi wakekwa wale wakulima, ili wakachukue sehemu yamavuno yake. 35 Wale wakulimawakawakamata hao watumishi; mmojawakampiga, mwingine wakamwua namwingine wakampiga mawe. 36 Huyo mtuakawatuma tena watumishi wengine, wengikuliko wa safari ya kwanza. Wale wakulimawakawatendea namna ileile. 37 Mwishoweakamtuma mwanawe huku akifikiri:Watamheshimu mwanangu. 38 Lakini walewakulima walipomwona mwanawewakasemezana wao kwa wao: Huyu ndiyemrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake! 39

Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lileshamba la mizabibu, wakamwua. 40 “Sasa,huyo mwenye shamba la mizabibuatakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?” 41

Wao wakamjibu, “Atawaangamiza vibaya haowaovu, na lile shamba atawapa wakulimawengine ambao watampa sehemu ya mavunowakati wa mavuno.” 42 Hapo Yesuakawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katikaMaandiko Matakatifu? Jiwe walilokataa waashisasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiyealiyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sanakwetu! 43 “Kwa hiyo nawaambieni, Ufalme waMungu utaondolewa kwenu na kupewa watuwa mataifa mengine wenye kutoa matundayake.” 44 “Atakayeanguka juu ya jiwe hiloatavunjika vipandevipande; na likimwangukiamtu yeyote, litamponda.” 45 Makuhani wakuuna Mafarisayo waliposikia hiyo mifano yakewalitambua kwamba alikuwa anawasema wao.46 Kwa hiyo wakawa wanatafuta njia ya kumtianguvuni, lakini waliwaogopa watu kwa sababuwao walimtambua yeye kuwa nabii.

Yesu alisema nao tena kwa kutumiamifano: 2 “Ufalme wa mbinguniumefanana na mfalme

aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. 3

Basi, akawatuma watumishi kuwaitawalioalikwa waje arusini, lakini walioalikwahawakutaka kufika. 4 Akawatuma tenawatumishi wengine, akisema, Waambieni walewalioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa;fahali wangu na ng'ombe wanonowamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoniarusini. 5 Lakini wao hawakujali, wakaendazao; mmoja shambani kwake, mwingine

kwenye shughuli zake, 6 na wenginewakawakamata wale watumishiwakawatukana, wakawaua. 7 Yule mfalmeakakasirika, akawatuma askari wakewakawaangamize wauaji hao na kuuteketezamji wao. 8 Kisha akawaambia watumishi wake:Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakiniwalioalikwa hawakustahili. 9 Basi, nendenikwenye barabara na wowote walemtakaowakuta waiteni waje arusini. 10 Walewatumishi wakatoka, wakaenda njiani,wakawaleta watu wote, wabaya na wema.Nyumba ya arusi ikajaa wageni. 11 “Mfalmealipoingia kuwaona wageni, akamwona mtummoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi. 12

Mfalme akamwuliza, Rafiki, umeingiaje hapabila vazi la arusi? Lakini yeye akakaa kimya. 13

Hapo mfalme akawaambia watumishi,Mfungeni miguu na mikono mkamtupe njegizani; huko atalia na kusaga meno.” 14 Yesuakamaliza kwa kusema, “Wengi wamealikwa,lakini wachache wameteuliwa.” 15 Kisha,Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsiya kumnasa Yesu kwa maneno yake. 16 Basi,wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasiwa kikundi cha Herode. Wakamwuliza,“Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtumwaminifu, na kwamba wafundisha njia yaMungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote,maana cheo cha mtu si kitu kwako. 17 Haya,twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipaKaisari?” 18 Lakini Yesu alitambua uovu wao,akawaambia, “Enyi 19 Nionyesheni fedha yakulipia kodi.” Nao wakamtolea sarafu ya fedha.sarafu ya fedha. 20 Basi, Yesu akawauliza,“Sura na chapa hii ni ya nani?” 21 Wakamjibu,“Ni vya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi,mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Munguyaliyo yake Mungu.” 22 Waliposikia hivyowakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.23 Siku hiyo, baadhi ya Masadukayowalimwendea Yesu. Hao ndio wale wasemaokwamba wafu hawafufuki. 24 Basi,wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtualiyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima nduguyake amwoe huyo mama mjane, amzaliendugu yake watoto. 25 Sasa, hapa petupalikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioakisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachiandugu yake huyo mke wake mjane. 26 Ikawavivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu,mpaka wa saba. 27 Baada ya ndugu hao wotekufa, akafa pia yule mama. 28 Je, siku wafuwatakapofufuka mama huyo atakuwa mke wanani miongoni mwa wale ndugu saba? MaanaWote saba walimwoa.” 29 Yesu akawajibu,“Kweli mmekosea kwa sababu hamjuiMaandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu!30 Maana wafu watakapofufuliwa hawataoawala kuolewa, watakuwa kama malaikambinguni. 31 Lakini kuhusu suala la wafukufufuka, hamjasoma yale aliyowaambieniMungu? 32 Aliwaambia, Mimi ni Mungu wa

MATHAYO MTAKATIFU 21:32

20

Page 21: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

23

Abrahamu, Isaka na Yakobo! Basi, yeye siMungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”33 Ule umati wa watu uliposikia hivyoukayastaajabia mafundisho yake. 34

Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwaamewanyamazisha Masadukayo, wakakutanapamoja. 35 Mmoja wao, mwanasheria,akamwuliza Yesu kwa kumjaribu, 36 “Mwalimu,ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?” 37

Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wakokwa moyo wako wote, kwa roho yako yote nakwa akili yako yote. 38 Hii ndiyo amri kuu yakwanza. 39 Ya pili inafanana na hiyo: Mpendejirani yako kama unavyojipenda wewemwenyewe. 40 Sheria yote ya Mose namafundisho ya manabii vinategemea amri hizimbili.” 41 Mafarisayo walipokusanyika pamoja,Yesu aliwauliza, 42 “Ninyi mwaonaje juu yaKristo? Je, ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “WaDaudi.” 43 Yesu akawaambia, “Basi,inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya RohoMtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana?Maana alisema: 44 Bwana alimwambia Bwanawangu: keti upande wangu wa kulia, mpakaniwaweke adui zako chini ya miguu yako. 45

Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo Bwana,anawezaje kuwa mwanawe?” 46 Hakuna mtuyeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu sikuhiyo hakuna aliyethubutu tena kumwulizaswali.

Kisha Yesu akauambia umati wa watupamoja na wanafunzi wake, 2

“Walimu wa Sheria na Mafarisayowana mamlaka ya kufafanua Sheria ya Mose. 3

Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochotewatakachowaambieni. Lakini msiyaigematendo yao, maana hawatekelezi yalewanayoyahubiri. 4 Hufunga mizigo mizito nakuwatwika watu mabegani, lakini waowenyewe hawataki kunyosha hata kidolewapate kuibeba. 5 Wao hufanya matendo yaoyote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenyemaandishi ya Sheria juu ya panda la uso namikononi na hupanua pindo za makoti yao. 6

Hupenda nafasi za heshima katika karamu naviti vya heshima katika masunagogi. 7

Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni nakupendelea kuitwa na watu: Mwalimu. 8 Lakinininyi msiitwe kamwe Mwalimu, maanamwalimu wenu ni mmoja tu, nanyi nyote nindugu. 9 Wala msimwite mtu yeyote Babahapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tualiye mbinguni. 10 Wala msiitwe Viongozi,maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiyeKristo. 11 Aliye mkubwa miongoni mwenu nilazima awe mtumishi wenu. 12 Anayejikwezaatashushwa, na anayejishusha atakwezwa. 13

“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo,wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wambinguni mbele ya macho ya watu. Ninyiwenyewe hamwingii ndani, walahamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie. 14

Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo,

wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingiziakuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwasababu hiyo mtapata adhabu kali. 15 “Olewenu walimu wa Sheria na Mafarisayo,wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ilikumpata mtu mmoja afuate dini yenu.Mnapompata, mnamfanya astahili maradufukwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyiwenyewe. 16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyimwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapohicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu yaHekalu, kiapo hicho kinamshika. 17 Enyi vipofuwapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi:dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabukuwa takatifu? 18 Tena mwasema ati mtuakiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapakwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu,kiapo hicho humshika. 19 Enyi vipofu! Ni kipikilicho cha maana zaidi: ile zawadi, aumadhabahu ambayo hufanya hiyo zawadikuwa takatifu? 20 Anayeapa kwa madhabahuameapa kwa hiyo madhabahu, na kwachochote kilichowekwa juu yake. 21 Naanayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekaluna pia kwa yule akaaye ndani yake. 22 Naanayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti chaenzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake.23 Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo,wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu yamajani yenye harufu nzuri, bizari na jira, nahuku mnaacha mambo muhimu ya Sheriakama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyohasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahauyale mengine. 24 Viongozi vipofu! Mnatoa nzikatika kinywaji, lakini mnameza ngamia! 25

“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo,wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwanje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitumlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo. 26

Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndanikwanza na nje kutakuwa safi pia. 27 “Ole wenuwalimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki!Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaaambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri,lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kilanamna ya uchafu. 28 Hali kadhalika ninyimnaonekana na watu kwa nje kuwa wema,lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu. 29

“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo,wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii nakuyapamba makaburi ya watu wema. 30

Mwasema: Kama sisi tungaliishi nyakati zawazee wetu hatungalishirikiana nao katikamauaji ya manabii! 31 Hivyo mnathibitishaninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wawatu waliowaua manabii. 32 Haya, kamilisheniile kazi wazee wenu waliyoianza! 33 Enyi kizazicha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepahukumu ya moto wa Jehanamu? 34 Ndiyomaana mimi ninawapelekea ninyi manabii,watu wenye hekima na walimu; mtawaua nakuwasulubisha baadhi yao, na wenginemtawapiga viboko katika masunagogi yenu na

MATHAYO MTAKATIFU 23:34

21

Page 22: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

24

kuwasaka katika kila mji. 35 Hivyo lawama yoteitawapateni kwa ajili ya damu yote ya watuwema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangukuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia,mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana waBarakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati yapatakatifu na madhabahu. 36 Nawaambienikweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababuya mambo haya. 37 “Yerusalemu, EeYerusalemu! Unawaua manabii na kuwapigamawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapinimejaribu kuwakusanya watoto wakokwangu, kama vile kuku anavyokusanyavifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakinihukutaka. 38 Haya basi, nyumba yakoitaachwa mahame. 39 Nakwambia kweli,hutaniona tena mpaka wakati utakaposema:Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.”

Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwaakienda zake, wanafunzi wakewalimwendea, wakamwonyesha

majengo ya Hekalu. 2 Yesu akawaambia,“Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kwelinawaambieni, hakuna hata jiwe mojalitakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitukitaharibiwa.” 3 Yesu alipokuwa ameketi juu yamlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendeafaraghani, wakamwuliza, “Twambie mambohaya yatatukia lini? Ni ishara ganiitakayoonyesha kuja kwako na mwisho wanyakati?” 4 Yesu akawajibu, “Jihadharini msijemkadanganywa na mtu. 5 Maana wengiwatatokea na kulitumia jina langu wakisema:Mimi ndiye Kristo, nao watawapotosha watuwengi. 6 Mtasikia juu ya vita na fununu za vita;lakini msifadhaike, maana hayo hayana budikutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalmemmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapana pale patakuwa na njaa na mitetemeko yaardhi. 8 Yote hayo ni kama mwanzo wamaumivu ya kujifungua mtoto. 9 “Kishawatawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifayote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu. 10

Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitianana kuchukiana. 11 Watatokea manabii wengiwa uongo watakaowapotosha watu wengi. 12

Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendowa watu wengi utafifia. 13 Lakiniatakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka. 14

Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njemaya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwengunikote kama ushuhuda kwa mataifa yote. 15

“Basi, mtakapoona Chukizo Haribifulililonenwa na nabii Danieli limesimama mahalipatakatifu, (msomaji na atambue maana yake),16 hapo, walioko Yudea na wakimbiliemilimani. 17 Aliye juu ya paa la nyumba yakeasishuke kuchukua kitu nyumbani mwake. 18

Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazilake. 19 Ole wao kina mama waja wazito nawanaonyonyesha siku hizo! 20 Ombeni ilikukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku

ya Sabato! 21 Maana wakati huo kutakuwa nadhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangumwanzo wa ulimwengu mpaka leo, walahaitapata kutokea tena. 22 Kama siku hizohazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyoteambaye angeokoka; lakini siku hizozitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa. 23

“Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: Kristo yukohapa au Yuko pale, msimsadiki. 24 Maanawatatokea kina Kristo wa uongo na manabiiwa uongo. Watafanya ishara kubwa namaajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekanahata wateule wa Mungu. 25 Sikilizeni,nimekwisha kuwaonya kabla ya wakati. 26

Basi, wakiwaambieni, Tazameni, yukojangwani, msiende huko; au, Tazameni,amejificha ndani, msisadiki; 27 maana, kamavile umeme uangazavyo toka mashariki hadimagharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwakeMwana wa Mtu. 28 Pale ulipo mzoga, ndipowatakapokusanyika tai. 29 “Mara baada yadhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezihautaangaza, nyota zitaanguka kutoka angani,na nguvu za mbingu zitatikiswa. 30 Kisha,ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani,na hapo makabila yote duniani yatalalamika;watamwona Mwana wa Mtu akija juu yamawingu ya angani mwenye nguvu na utukufumwingi. 31 Naye atawatuma malaika wakewenye tarumbeta la kuvuma sana, naowatawakusanya wateule wake kutoka pandezote nne za dunia, toka mwisho huu wambingu hadi mwisho huu. 32 “Kwa mtinijifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yakeyanapoanza kuwa laini na kuchanua majani,mnajua kwamba wakati wa kiangaziumekaribia. 33 Hali kadhalika nanyimtakapoona mambo haya yote yakitendeka,jueni kwamba yuko karibu sana. 34

Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kablaya mambo hayo yote kutukia. 35 Naam,mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yanguhayatapita kamwe. 36 “Lakini, juu ya siku ausaa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; walamalaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Babapeke yake ndiye ajuaye. 37 Kwa maana kamailivyokuwa nyakati za Noa, ndivyoitakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. 38

Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu,watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa nakuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ilesafina. 39 Hawakujua kuna nini mpaka ilegharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyoitakavyokuwa wakati Mwana wa Mtuatakapokuja. 40 Wakati huo watu wawiliwatakuwa shambani; mmoja atachukuliwa namwingine ataachwa. 41 Kina mama wawiliwatakuwa wanasaga nafaka, mmojaatachukuliwa na mwingine ataachwa. 42 Basi,kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokujaBwana wenu. 43 Lakini kumbukeni jambo hili:kama mwenye nyumba angejua siku mwiziatakapofika, angekesha, wala hangeiacha

MATHAYO MTAKATIFU 23:35

22

Page 23: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

25

nyumba yake ivunjwe. 44 Kwa hiyo, nanyi piamuwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtuatakuja saa msiyoitazamia.” 45 Yesuakaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishimwaminifu na mwenye busara, ambaye bwanawake atamweka juu ya watu wake, awapechakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumishiyule ambaye bwana wake atakapokujaatamkuta akifanya hivyo. 47 Kwelinawaambieni, atamweka mtumishi huyoaisimamie mali yake yote. 48 Lakini kamamtumishi mbaya akijisemea moyoni: Bwanawangu anakawia kurudi, 49 kisha akaanzakuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula nakunywa pamoja na walevi, 50 bwana wakeatakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua. 51

Atamkatilia mbali na kumweka kundi moja nawanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusagameno.

“Wakati huo, Ufalme wa mbinguniutafanana na wasichana kumiwaliochukua taa zao, wakaenda

kumlaki bwana arusi. 2 Watano miongonimwao walikuwa wapumbavu na watanowalikuwa wenye busara. 3 Wale wapumbavuwalichukua taa zao, lakini hawakuchukua akibaya mafuta. 4 Lakini wale wenye busarawalichukua mafuta katika chupa pamoja na taazao. 5 Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja,wale wanawali wote wote walisinzia, wakalala.6 Usiku wa manane kukawa na kelele: Haya,haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki. 7

Hapo wale wanawali wote wakaamka,wakazitayarisha taa zao. 8 Wale wapumbavuwakawaambia wale wenye busara: Tupenimafuta yenu kidogo maana taa zetuzinazimika. 9 Lakini wale wenye busarawakawaambia, Hayatatutosha sisi na ninyi!Afadhali mwende dukani mkajinunuliewenyewe! 10 Basi, wale wanawali wapumbavuwalipokwenda kununua mafuta, bwana arusiakafika, na wale wanawali waliokuwa tayariwakaingia pamoja naye katika jumba la arusi,kisha mlango ukafungwa. 11 Baadaye walewanawali wengine wakaja, wakaita: Bwana,bwana, tufungulie! 12 Lakini yeye akawajibu,Nawaambieni kweli, siwajui ninyi.” 13 KishaYesu akasema, “Kesheni basi, kwa maanahamjui siku wala saa. 14 “Itakuwa kama mtummoja aliyetaka kusafiri ng'ambo: aliwaitawatumishi wake, akawakabidhi mali yake. 15

Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake:mmoja sarafu tano za fedha ziitwazo talanta,mwingine talanta mbili na mwingine talantamoja, kisha akasafiri. 16 Mara yulealiyekabidhiwa talanta tano akafanya kazi nazoakapata faida talanta tano. 17 Hali kadhalikana yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapatafaida talanta mbili. 18 Lakini yulealiyekabidhiwa talanta moja akaendaakachimba shimo ardhini, akaificha fedha yabwana wake. 19 “Baada ya muda mrefu, yulebwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya

matumizi na mapato ya fedha yake. 20

Mtumishi aliyekabidhiwa talanta tano akajaamechukua zile talanta tano faida,akamwambia, Bwana, ulinikabidhi talantatano, hapa pana talanta tano zaidi faidaniliyopata. 21 Bwana wake akamwambia,Vema, mtumishi mwema na mwaminifu.Umekuwa mwaminifu katika mambo madogonitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamojana bwana wako. 22 “Mtumishi aliyekabidhiwatalanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida,akisema, Bwana, ulinikabidhi talanta mbili.Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata. 23

Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishimwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifukatika mambo madogo, nitakukabidhimakubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwanawako. 24 “Lakini yule aliyekabidhiwa talantamoja akaja, akasema, Bwana, najua wewe nimtu mgumu; wewe huvuna pale ambapohukupanda, na kukusanya pale ambapohukutawanya. 25 Niliogopa, nikaificha fedhayako katika ardhi. Chukua basi mali yako. 26

“Bwana wake akamwambia, Wewe ni mtumishimwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvunamahali ambapo sikupanda, na hukusanya paleambapo sikutawanya. 27 Ilikupasa basi,kuiweka fedha yangu katika benki, naminingelichukua mtaji wangu na faida yake! 28

Basi, mnyang'anyeni hiyo fedha mkampe yulemwenye talanta kumi. 29 Maana, aliye na kituatapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye nakitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. 30

Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida,mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio nakusaga meno. 31 “Wakati Mwana wa Mtuatakapokuja katika utukufu wake na malaikawote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu yakiti chake cha enzi kitukufu, 32 na mataifa yoteyatakusanyika mbele yake, nayeatawatenganisha watu kama mchungajianavyotenganisha kondoo na mbuzi. 33

Atawaweka kondoo upande wake wa kulia nambuzi upande wake wa kushoto. 34 “KishaMfalme atawaambia wale walio upande wakewa kulia, Njoni enyi mliobarikiwa na Babayangu; pokeeni Ufalme mliotayarishiwa tangukuumbwa kwa ulimwengu. 35 Maana nilikuwana njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiunanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyimkanikaribisha; 36 nilikuwa uchi, mkanivika;nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama;nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.37 Hapo, hao watu wema watamjibu mfalmeBwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasitukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasitukakunywesha maji? 38 Ni lini tulikuona ukiwamgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasitukakuvika? 39 Ni lini tulikuona ukiwamgonjwa au mfungwa nasi tukajakukutazama? 40 Mfalme atawajibu, Kwelinawaambieni, kila kitu mlichomtendeammojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo,

MATHAYO MTAKATIFU 25:40

23

Page 24: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

26

mlinitendea mimi. 41 “Kisha atawaambia walewalio upande wake wa kushoto, Ondokenimbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katikamoto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi namalaika wake. 42 Maana nilikuwa na njaananyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiunanyi hamkunipa maji. 43 Nilikuwa mgeninanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa namfungwa nanyi hamkuja kunitazama. 44

“Hapo nao watajibu, Bwana, ni lini tulikuonaukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bilanguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasihatukuja kukuhudumia? 45 Naye atawajibu,Nawaambieni kweli, kila mlipokataakumtendea mambo haya mmojawapo wahawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi. 46

Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu yamilele, lakini wale waadilifu watakwendakwenye uzima wa milele.”

Yesu alipomaliza kusema hayo yote,aliwaambia wanafunzi wake, 2

“Mnajua kwamba baada ya siku mbilitutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana waMtu atatolewa ili asulubiwe.” 3 Wakati huomakuhani wakuu na wazee wa watuwalikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa,Kuhani Mkuu. 4 Wakashauriana jinsi ya kumtiaYesu nguvuni kwa hila wamuue. 5 Lakiniwakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wasikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.6 Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwaSimoni, aitwaye Mkoma, 7 mama mmojaaliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashiya thamani kubwa, alimjia pale mezanialipokuwa amekaa kula chakula, akammiminiahayo marashi kichwani. 8 Wanafunzi wakewalipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Yanini hasara hii? 9 Marashi haya yangaliwezakuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewahizo fedha.” 10 Yesu alitambua mawazo yao,akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyumama? Yeye amenitendea jambo jema. 11

Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimisitakuwapo pamoja nanyi daima. 12 Huyumama amenimiminia marashi ili kunitayarishakwa maziko. 13 Nawaambieni kweli, popoteambapo hii Habari Njema itahubiriwaulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mamahuyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.” 14

Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi nawawili, akaenda kwa makuhani wakuu, 15

akawaambia, “Mtanipa kitu gani kamanikimkabidhi Yesu kwenu?” Wakamhesabiasarafu thelathini za fedha; 16 na tangu wakatihuo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.17 Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya MikateIsiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendeaYesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapichakula cha Pasaka?” 18 Yeye akawajibu,“Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie:Mwalimu anasema, wakati wangu umefika;kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunziwangu.” 19 Wanafunzi wakafanya kama Yesu

alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka. 20

Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamojana wanafunzi wake kumi na wawili. 21

Walipokuwa wakila, Yesu akasema,“Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.”22 Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanzakuuliza mmojammoja, “Bwana! Je, ni mimi?” 23

Yesu akajibu, “Atakayechovya mkate pamojanami katika bakuli ndiye atakayenisaliti. 24

Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kamaMaandiko Matakatifu yasemavyo, lakini olewake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu!Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kamahangalizaliwa.” 25 Yuda, ambaye ndiyealiyetaka kumsaliti, akamwuliza, “Mwalimu! Je,ni mimi?” Yesu akamjibu, “Wewe umesema.” 26

Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate,akashukuru, akaumega, akawapa wanafunziwake akisema, “Twaeni mle; huu ni mwiliwangu.” 27 Kisha akatwaa kikombe,akamshukuru Mungu, akawapa akisema,“Nyweni nyote; 28 maana hii ni damu yanguinayothibitisha agano, damu inayomwagwakwa ajili ya watu wengi ili kuwaondoleadhambi. 29 Nawaambieni, sitakunywa tenadivai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywampya pamoja nanyi katika Ufalme wa Babayangu.” 30 Baada ya kuimba wimbo,wakaondoka, wakaenda katika mlima waMizeituni. 31 Kisha Yesu akawaambia, “Usikuhuu wa leo, ninyi nyote mtakuwa na mashakanami, maana Maandiko Matakatifu yasema:Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundiwatatawanyika. 32 Lakini baada ya kufufukakwangu, nitawatangulieni Galilaya.” 33 Petroakamwambia Yesu “Hata kama wote watakuwana mashaka nawe na kukuacha, mimisitakuacha kamwe.” 34 Yesu akamwambia,“Kweli nakwambia, usiku huu kabla jogoohajawika, utanikana mara tatu.” 35 Petroakamwambia, “Hata kama ni lazima nifepamoja nawe, sitakukana kamwe.” Walewanafunzi wengine wote wakasema vivyohivyo. 36 Kisha Yesu akaenda pamoja naobustanini Gethsemane, akawaambiawanafunzi wake, “Kaeni hapa nami niende palembele kusali.” 37 Akawachukua Petro na wanawawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzunina mahangaiko. 38 Hapo akawaambia, “Ninahuzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaenihapa mkeshe pamoja nami.” 39 Basi, akaendambele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali:“Baba yangu, kama inawezekana, aachakikombe hiki cha mateso kinipite; lakini isiwenitakavyo mimi, ila utakavyo wewe.” 40

Akawaendea wale wanafunzi, akawakutawamelala. Akamwambia Petro, “Ndiyo kusemahamkuweza kukesha pamoja nami hata saamoja? 41 Kesheni na kusali ili msije mkaingiakatika majaribu. Roho i tayari lakini mwili nidhaifu.” 42 Akaenda tena mara ya pili akasali:“Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hikikinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi

MATHAYO MTAKATIFU 25:41

24

Page 25: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

27

yako yafanyike.” 43 Akawaendea tena,akawakuta wamelala, maana macho yaoyalikuwa yamebanwa na usingizi. 44 Basi,akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatukwa maneno yaleyale. 45 Kisha akawaendeawale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngalimmelala na kupumzika? Tazameni! Saayenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewakwa watu wenye dhambi. 46 Amkeni, twendenizetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.”47 Basi, Yesu alipokuwa bado anasema nao,mara akaja Yuda, mmoja wa wale kumi nawawili. Pamoja naye walikuja watu wengiwenye mapanga na marungu ambaowalitumwa na makuhani wakuu na wazee wawatu. 48 Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu,alikuwa amekwisha wapa ishara akisema: “Yulenitakayembusu ndiye; mkamateni.” 49 Basi,Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia,“Shikamoo, Mwalimu!” Kisha akambusu. 50

Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya ulichokujakufanya.” Hapo wale watu wakaja,wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni. 51

Mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesuakanyosha mkono, akauchomoa upanga wake,akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu,akamkata sikio. 52 Hapo Yesu akamwambia,“Rudisha upanga wako alani, maana yeyoteanayeutumia upanga, atakufa kwa upanga. 53

Je, hamjui kwamba ningeweza kumwombaBaba yangu naye mara angeniletea zaidi yamajeshi kumi na mawili ya malaika? 54 Lakiniyatatimiaje Maandiko Matakatifu yasemayokwamba ndivyo inavyopaswa kuwa?” 55 Wakatihuohuo Yesu akauambia huo umati wa watuwaliokuja kumtia nguvuni, “Je, mmekujakunikamata kwa mapanga na marungu kamakwamba mimi ni mnyang'anyi? Kila sikunilikuwa Hekaluni nikifundisha, nahamkunikamata! 56 Lakini haya yoteyametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie.”Kisha wanafunzi wote wakamwacha,wakakimbia. 57 Basi, hao watu waliomkamataYesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa,Kuhani Mkuu, walikokusanyika walimu waSheria na wazee. 58 Petro alimfuata kwa mbalimpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia ndanipamoja na walinzi ili apate kuona mamboyatakavyokuwa. 59 Basi, makuhani wakuu naBaraza lote wakatafuta ushahidi wa uongodhidi ya Yesu wapate kumwua, 60 lakinihawakupata ushahidi wowote, ingawa walikujamashahidi wengi wa uongo. Mwishowe wakajamashahidi wawili, 61 wakasema, “Mtu huyualisema: Ninaweza kuliharibu Hekalu la Munguna kulijenga tena kwa siku tatu.” 62 KuhaniMkuu akasimama, akamwuliza Yesu, “Je, hujibuneno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidiyako?” 63 Lakini Yesu akakaa kimya. KuhaniMkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa Mungualiye hai, twambie kama wewe ndiwe Kristo,Mwana wa Mungu!” 64 Yesu akamwambia,“Wewe umesema! Lakini nawaambieni, tangu

sasa mtamwona Mwana wa Mtu ameketiupande wa kulia wa Mwenyezi, akija juu yamawingu ya mbinguni.” 65 Hapo, Kuhani Mkuuakararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru!Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasammesikia kufuru yake. 66 Ninyi mwaonaje?”Wao wakamjibu, “Anastahili kufa!” 67 Kishawakamtemea mate usoni, wakampiga makofi.Wengine wakiwa wanampiga makofi, 68

wakasema, “Haya Kristo, tutabirie; ni naniamekupiga!” 69 Petro alikuwa ameketi njeuani. Basi, mtumishi mmoja wa kikeakamwendea, akasema, “Wewe ulikuwapamoja na Yesu wa Galilaya.” 70 Petro akakanambele ya wote akisema, “Sijui hata unasemanini.” 71 Alipokuwa akitoka mlangoni,mtumishi mwingine wa kike akamwona,akawaambia wale waliokuwa pale, “Mtu huyualikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti.” 72 Petroakakana tena kwa kiapo: “Simjui mtu huyo.” 73

Baadaye kidogo, watu waliokuwa palewakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika,wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wakounakutambulisha.” 74 Hapo Petro akaanzakujilaani na kuapa akisema, “Simjui mtu huyo!”Mara jogoo akawika. 75 Petro akakumbukamaneno aliyoambiwa na Yesu: “Kabla jogoohajawika, utanikana mara tatu.” Basi, akatokanje akalia sana.

Kulipopambazuka, makuhani wakuuwote na wazee wa watu walifanyamashauri juu ya Yesu wapate

kumwua. 2 Wakamfunga pingu,wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato,mkuu wa mkoa. 3 Hapo, Yuda ambaye ndiyealiyemsaliti, alipoona kwamba wamekwishamhukumu Yesu, akajuta, akawarudishiamakuhani wakuu zile sarafu thelathini zafedha. 4 Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoamtu asiye na hatia auawe.” Lakini waowakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shaurilako.” 5 Naye akazitupa zile fedha Hekaluni,akatoka nje, akaenda akajinyonga. 6 Makuhaniwakuu wakazichukua zile fedha, wakasema,“Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwamaana ni fedha za damu.” 7 Basi,wakashauriana, wakazitumia kununua shambala mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni. 8

Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwaShamba la Damu. 9 Hivyo maneno ya nabiiYeremia yakatimia: “Walizichukua sarafuthelathini za fedha, thamani ya yule ambayewatu wa Israeli walipanga bei, 10 wakanunuanazo shamba la mfinyanzi, kama Bwanaalivyoniagiza.” 11 Yesu alisimamishwa mbeleya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoaakamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme waWayahudi?” Yesu akamwambia, “Weweumesema.” 12 Lakini makuhani wakuu nawazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibuneno. 13 Hivyo Pilato akamwuliza, “Je, husikiimashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?” 14

Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata

MATHAYO MTAKATIFU 27:14

25

Page 26: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana. 15

Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasakamkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudimfungwa mmoja waliyemtaka. 16 Wakati huokulikuwa na mfungwa mmoja, jina lakeBaraba. 17 Hivyo, watu walipokusanyikapamoja, Pilato akawauliza, “Mwatakanimfungue yupi kati ya wawili hawa, Barabaama Yesu aitwae Kristo?” 18 Alisema hivyomaana alijua wazi kwamba walimleta kwakekwa sababu ya wivu. 19 Pilato alipokuwaamekaa katika kiti cha hukumu, mke wakeakampelekea ujumbe: “Usijitie katika shauri lamtu huyu mwema, maana leo nimetesekasana katika ndoto kwa sababu yake.” 20 Lakinimakuhani wakuu na wazee wakawashawishiwatu waombe Baraba afunguliwe na Yesuauawe. 21 Mkuu wa mkoa akawauliza, “Ni yupikati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?”Wakamjibu, “Baraba!” 22 Pilato akawauliza,“Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?”Wote wakasema, “Asulubiwe!” 23 Pilatoakauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Waowakazidi kupaaza sauti: “Asulubiwe!” 24 Basi,Pilato alipotambua kwamba hafanikiwichochote na kwamba maasi yalikuwayanaanza, alichukua maji, akanawa mikonombele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimisina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shaurilenu wenyewe.” 25 Watu wote wakasema,“Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watotowetu!” 26 Hapo Pilato akawafungulia Barabakutoka gerezani, lakini akamtoa Yesuasulubiwe. 27 Kisha askari wa mkuu wa mkoawakamwingiza Yesu ndani ya ikulu,wakamkusanyikia kikosi kizima. 28 Wakamvuanguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.29 Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvikakichwani, wakamwekea pia mwanzi katikamkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbeleyake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoomfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate,wakauchukua ule mwanzi, wakampiga naokichwani. 31 Baada ya kumdhihaki, wakamvualile joho, wakamvika nguo zake, kishawakampeleka kumsulubisha. 32 Walipokuwawakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lakeSimoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimishakuuchukua msalaba wake Yesu. 33 Walipofikamahali paitwapo Golgotha, maana yake,“Mahali pa Fuvu la kichwa,” 34 wakampamchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesualipoonja akakataa kunywa. 35

Walimsulubisha, kisha wakagawana mavaziyake kwa kuyapigia kura. 36 Wakaketi, wakawawanamchunga. 37 Juu ya kichwa chakewakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa,“Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.” 38

Wanyang'anyi wawili walisulubishwa piapamoja naye, mmoja upande wa kushoto namwingine upande wa kulia. 39 Watuwaliokuwa wanapita mahali hapo walimtukanawakitikisa vichwa vyao na kusema, 40 “Wewe!

Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwasiku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama weweni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!”41 Hali kadhalika na makuhani wakuu pamojana walimu wa Sheria na wazee walimdhihakiwakisema, 42 “Aliwaokoa wengine, lakinikujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalmewa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani,nasi tutamwamini. 43 Alimtumainia Mungu nakusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi,Mungu na amwokoe kama anamtaka.” 44 Halikadhalika na wale waliosulubiwa pamoja nayewakamtukana. 45 Tangu saa sita mchanampaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza. 46

Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa,“Eli, Eli, lema sabakthani?” Maana yake,“Mungu wangu, Mungu wangu, mbonaumeniacha?” 47 Lakini wale waliosimama palewaliposikia hivyo wakasema, “Anamwita Eliya.”48 Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo,akaichovya katika siki, akaiweka juu yamwanzi, akampa anywe. 49 Wenginewakasema, “Acha tuone kama Eliya anakujakumwokoa.” 50 Basi, Yesu akalia tena kwasauti kubwa, akakata roho. 51 Hapo pazia laHekalu likapasuka vipande viwili, toka juumpaka chini; nchi ikatetemeka; miambaikapasuka; 52 makaburi yakafunguka na watuwengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa; 53

nao, baada ya kufufuka kwake, wakatokamakaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu,wakaonekana na watu wengi. 54 Basi,jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesuwalipoona tetemeko la ardhi na yale mamboyaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema,“Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengiwakitazama kwa mbali. Hao ndio walewaliomfuata Yesu kutoka Galilayawakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwaMaria Magdalene, Maria mama yao Yakobo naYosefu, pamoja na mama yao wana waZebedayo. 57 Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmojatajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu.Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58

Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili waYesu. Basi, Pilato akaamuru apewe. 59 Yosefuakauchukua ule mwili akauzungushia sandasafi ya kitani, 60 akauweka ndani ya kaburilake jipya alilokuwa amelichonga katikamwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwambele ya mlango wa kaburi, akaenda zake. 61

Maria Magdalene na yule Maria mwinginewalikuwa wameketi kulielekea kaburi. 62

Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile yaMaandalio, makuhani wakuu na Mafarisayowalimwendea Pilato, 63 Wakasema,“Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yulemdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, Baadaya siku tatu nitafufuka. 64 Kwa hiyo amurukaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunziwake wasije wakamwiba na kuwaambia watukwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho

MATHAYO MTAKATIFU 27:15

26

Page 27: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

28

utakuwa mbaya kuliko ule wa awali.” 65 Pilatoakawaambia, “Haya, mnao walinzi; nendenimkalinde kadiri mjuavyo.” 66 Basi, wakaenda,wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lilejiwe na kuacha hapo askari walinzi.

Baada ya Sabato, karibu namapambazuko ya siku ile ya Jumapili,Maria Magdalene na yule Maria

mwingine walikwenda kutazama lile kaburi. 2

Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi;malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni,akalivingirisha lile jiwe, akalikalia. 3 Alionekanakama umeme na mavazi yake yalikuwa meupekama theluji. 4 Walinzi wa lile kaburiwakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawakama wamekufa. 5 Lakini yule malaikaakawaambia wale wanawake, “Ninyi msiogope!Najua kwamba mnamtafuta Yesualiyesulubiwa. 6 Hayupo hapa maanaamefufuka kama alivyosema. Njoni mkaonemahali alipokuwa amelala. 7 Basi, nendeniupesi mkawaambie wanafunzi wake kwambaamefufuka kutoka wafu, na sasaanawatangulieni kule Galilaya; hukomtamwona. Haya, mimi nimekwishawaambieni.” 8 Wakiwa wenye hofu na furahakubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini,wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunziwake. 9 Mara, Yesu akakutana nao,akawasalimu: “Salamu.” Hao wanawakewakamwendea, wakapiga magoti mbele yake,

wakashika miguu yake. 10 Kisha Yesuakawaambia, “Msiogope! Nendenimkawaambie ndugu zangu waende Galilaya,na huko wataniona.” 11 Wale wanawakewalipokuwa wanakwenda zao, baadhi yawalinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoataarifa kwa makuhani wakuu juu ya mamboyote yaliyotukia. 12 Basi, wakakutana pamojana wazee, na baada ya kushauriana,wakawapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha13 wakisema, “Ninyi mtasema hivi: Wanafunziwake walikuja usiku, wakamwiba sisi tukiwatumelala. 14 Na kama mkuu wa mkoa akijuajambo hili, sisi tutasema naye na kuhakikishakuwa ninyi hamtapata matatizo.” 15 Walewalinzi wakazichukua zile fedha, wakafanyakama walivyofundishwa. Habari hiyo imeeneakati ya Wayahudi mpaka leo. 16 Walewanafunzi kumi na mmoja walikwendaGalilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu.17 Walipomwona, wakamwabudu, ingawawengine walikuwa na mashaka. 18 Yesu akajakaribu, akawaambia, “Nimepewa mamlakayote mbinguni na duniani. 19 Nendeni basi,mkawafanye watu wa mataifa yote wawewanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina laBaba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. 20

Wafundisheni kushika maagizo yoteniliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi sikuzote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”

MATHAYO MTAKATIFU 28:20

27

Page 28: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

MARKO MTAKATIFU

Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwanawa Mungu. 2 Ilianza kamailivyoandikwa katika kitabu cha nabii

Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wanguakutangulie; yeye atakutayarishia njia yako. 3

Sauti ya mtu imesikika jangwani: MtayarishieniBwana njia yake, nyoosheni mapito yake.” 4

Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubirikwamba ni lazima watu watubu na kubatizwaili Mungu awasamehe dhambi zao. 5 Watukutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wotewa Yerusalemu walimwendea, wakaziungamadhambi zao, naye akawabatiza katika mtoYordani. 6 Yohane alikuwa amevaa vazilililofumwa kwa manyoya ya ngamia, namkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakulachake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 7

Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakujamwenye uwezo zaidi kuliko mimi, ambayemimi sistahili hata kuinama na kufunguakamba za viatu vyake. 8 Mimi ninawabatizakwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa RohoMtakatifu.” 9 Siku hizo, Yesu alifika kutokaNazareti, mji wa Galilaya, akabatizwa naYohane katika mto Yordani. 10 Mara tualipotoka majini, aliona mbinguzimefunguliwa, na Roho akishuka juu yakekama njiwa. 11 Sauti ikasikika kutokambinguni: “Wewe ni Mwanangu mpendwa,nimependezwa nawe.” 12 Mara akaongozwana Roho kwenda jangwani, 13 akakaa hukosiku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwahuko pamoja na wanyama wa porini, naomalaika wakawa wanamtumikia. 14 Yohanealipokwisha fungwa gerezani, Yesu alikwendaGalilaya, akahubiri Habari Njema ya Mungu,akisema, 15 “Wakati umetimia, na Ufalme waMungu umekaribia. Tubuni na kuiamini HabariNjema!” 16 Alipokuwa anapita kando ya ziwaGalilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni naAndrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.17 Yesu akawaambia, “Nifuateni naminitawafanya ninyi wavuvi wa watu.” 18 Marawakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 19

Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona Yakobona Yohane, wana wa Zebedayo. Nao piawalikuwa ndani ya mashua yaowakizitengeneza nyavu zao. 20 Yesu akawaitamara, nao wakamwacha baba yao Zebedayokatika mashua pamoja na wafanyakazi,wakamfuata. 21 Wakafika mjini Kafarnaumu,na mara ilipofika Sabato, Yesu akaingia katikaSunagogi, akaanza kufundisha. 22 Watu wote

waliomsikia walishangazwa na mafundishoyake, maana hakuwa anafundisha kamawalimu wao wa Sheria, bali kama mtu mwenyemamlaka. 23 Mara akatokea mle ndani yasunagogi mtu mmoja mwenye pepo mchafu,24 akapaaza sauti, “Una nini nasi, wewe Yesuwa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najuawewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!”25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtuhuyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafuakamtikisatikisa mtu huyo, kisha akalia kwasauti kubwa, akamtoka. 27 Watu wotewakashangaa, wakaulizana, “Ni mambo ganihaya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyuanayo mamlaka ya kuamuru hata pepowachafu, nao wanamtii!” 28 Habari za Yesuzikaenea upesi kila mahali katika wilaya yaGalilaya. 29 Wakatoka katika sunagogi,wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwaSimoni na Andrea; Yakobo na Yohanewalikwenda pamoja nao. 30 Basi, mamammoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandaniana homa kali. Wakamwarifu Yesu maraalipowasili. 31 Yesu akamwendea huyo mama,akamshika mkono, akamwinua. Na ile homaikamwacha, akaanza kuwatumikia. 32 Jioni, jualilipokwisha tua, wakamletea Yesu wagonjwawote na watu waliopagawa na pepo. 33 Watuwote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango.34 Naye Yesu akawaponya watu wengiwaliokuwa na magonjwa mbalimbali;aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusukusema kitu maana walikuwa wanamjua yeyeni nani. 35 Kesho yake, kabla yamapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahalipa faragha kusali. 36 Simoni na wenzakewakaenda kumtafuta. 37 Walipomwonawakamwambia, “Kila mtu anakutafuta.” 38

Yesu akawaambia, “Twendeni katika mijimingine ya jirani nikahubiri huko pia, maananimekuja kwa sababu hiyo.” 39 Basi, akaendakila mahali Galilaya akihubiri katikamasunagogi na kufukuza pepo. 40 Mtu mmojamwenye ukoma alimwendea Yesu, akapigamagoti, akamwomba, “Ukitaka, wawezakunitakasa!” 41 Yesu akamwonea huruma,akanyosha mkono wake, akamgusa nakumwambia, “Nataka, takasika!” 42 Maraukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika. 43

Kisha Yesu akamwambia aende zake upesi nakumwonya vikali, 44 “Usimwambie mtu yeyotejambo hili, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani;kisha utoe sadaka kwa ajili ya kutakasika

MARKO MTAKATIFU 1:2

28

Page 29: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

2

3

kwako kama alivyoamuru Mose, iweuthibitisho kwao kwamba umepona.” 45 Lakinihuyo mtu akaenda, akaanza kueneza habarihiyo kila mahali na kusema mambo mengihata Yesu hakuweza tena kuingia katika mjiwowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje,mahali pa faragha. Hata hivyo, watuwakamwendea kutoka kila upande.

Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudiKafarnaumu, watu wakapata habarikwamba alikuwa nyumbani. 2 Basi,

wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyoteikakosekana mlangoni. Yesu alikuwaakiwahubiria ujumbe wake, 3 wakati mtummoja aliyepooza alipoletwa kwake akiwaamechukuliwa na watu wanne. 4 Kwa sababuya huo umati wa watu, hawakuwezakumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboasehemu ya dari iliyokuwa juu ya mahalialipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi,wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juuya mkeka. 5 Yesu alipoona imani yao,akamwambia huyo mtu aliyepooza,“Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.” 6

Baadhi ya walimu wa Sheria waliokuwawameketi hapo wakawaza mioyoni mwao, 7

“Anathubutuje kusema hivyo? AnamkufuruMungu! Hakuna mtu awezaye kusamehedhambi isipokuwa Mungu peke yake.” 8 Yesualitambua mara mawazo yao, akawaambia,“Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu? 9 Nilipi lililo rahisi zaidi: kumwambia mtu huyualiyepooza, Umesamehewa dhambi zako, aukumwambia, Inuka! Chukua mkeka wakoutembee? 10 Basi, nataka mjue kwambaMwana wa Mtu anayo mamlaka yakuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapoakamwambia huyo mtu aliyepooza, 11

“Nakwambia simama, chukua mkeka wakouende nyumbani!” 12 Mara, watu wote wakiwawanamtazama, huyo mtu akainuka,akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watuwote wakashangaa na kumtukuza Munguwakisema, “Hatujapata kamwe kuona jambokama hili.” 13 Yesu alikwenda tena kando yaziwa. Umati wa watu ukamwendea, nayeakaanza kuwafundisha. 14 Alipokuwa akipita,akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketikatika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia,“Nifuate!” Lawi akasimama, akamfuata. 15

Baadaye, Yesu alikuwa amekaa mezani,nyumbani kwa Lawi, kula chakula. Watozaushuru wengi na wenye dhambi walikuwawamemfuata Yesu na wengi wao wakawawamekaa mezani pamoja naye na wanafunziwake. 16 Basi, baadhi ya walimu wa Sheriaambao walikuwa Mafarisayo walipomwonaYesu akila pamoja na watu wenye dhambi nawatoza ushuru, wakawauliza wanafunzi wake,“Kwa nini anakula pamoja na watoza ushuruna wenye dhambi?” 17 Yesu alipowasikia,akawaambia, “Watu wenye afya hawahitajidaktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa.

Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.”18 Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane nawanafunzi wa Mafarisayo walikuwawanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwulizaYesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na waMafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wakohawafungi?” 19 Yesu akajibu, “Walioalikwaharusini wanawezaje kufunga kama bwanaharusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapopamoja na bwana harusi hawawezi kufunga.20 Lakini wakati utafika ambapo bwana harusiataondolewa kati yao; wakati huo ndipowatakapofunga. 21 “Hakuna mtu anayekatakiraka kutoka katika nguo mpya na kukishoneakatika nguo kuukuu. Kama akifanya hivyo,hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazikuukuu, nalo litaharibika zaidi. 22 Wala hakunamtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu.Kama akifanya hivyo, divai itavipasua hivyoviriba, nayo divai pamoja na hivyo viribavitaharibika. Divai mpya hutiwa katika viribavipya!” 23 Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwaanapita katika mashamba ya ngano.Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wakewakaanza kukwanyua masuke ya ngano. 24

Mafarisayo wakawaambia, “Tazama! Kwa niniwanafanya jambo ambalo si halali kufanyawakati wa Sabato?” 25 Yesu akawajibu, “Je,hamjapata kusoma juu ya kile alichofanyaDaudi wakati alipohitaji chakula? Yeye pamojana wenzake waliona njaa, 26 naye akaingiandani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikateiliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hilililifanyika wakati Abiathari alikuwa KuhaniMkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwawameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudialiila, tena akawapa na wenzake.” 27 Basi, Yesuakawaambia, “Sabato iliwekwa kwa ajili yabinadamu na si binadamu kwa ajili ya Sabato!28 Kwa hiyo, Mwana wa Mtu ni Bwana hata waSabato.”

Yesu aliingia tena katika sunagogi namle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwana mkono uliopooza. 2 Humo baadhi

ya watu walimngojea amponye mtu huyo sikuya sabato ili wapate kumshtaki. 3 Yesuakamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkonouliopooza, “Njoo hapa katikati.” 4 Kisha,akawauliza, “Je, ni halali siku ya Sabatokutenda jambo jema au kutenda jambo baya;kuokoa maisha au kuua?” Lakini waohawakusema neno. 5 Hapo akawatazamawote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababuya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambiahuyo mtu, “Nyosha mkono wako!” Nayeakaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.6 Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanyashauri pamoja na watu wa kikundi cha Herodejinsi ya kumwangamiza Yesu. 7 Yesu aliondokahapo pamoja na wanafunzi wake, akaendakando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata.Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu,Yudea, 8 Idumea, ng'ambo ya mto Yordani,

MARKO MTAKATIFU 3:8

29

Page 30: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendeaYesu kwa sababu ya kusikia mambo mengialiyokuwa ameyatenda. 9 Yesu akawaambiawanafunzi wake wamtayarishie mashua moja,ili umati wa watu usije ukamsonga. 10 Alikuwaamewaponya watu wengi, na wagonjwa wotewakawa wanamsonga ili wapate kumgusa. 11

Na watu waliokuwa wamepagawa na pepowachafu walipomwona, walijitupa chini mbeleyake na kupaaza sauti, “Wewe ni Mwana waMungu!” 12 Lakini Yesu akawaamuru kwa ukaliwasimjulishe kwa watu. 13 Yesu alipandakilimani, akawaita wale aliowataka. Basi,wakamwendea, 14 naye akawateua watu kumina wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye,awatume kuhubiri 15 na wawe na mamlaka yakuwafukuza pepo. 16 Basi, hao kumi na wawiliwalioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesualimpa jina, Petro), 17 Yakobo na Yohane, wanawa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawilijina Boanerge, maana yake “wanangurumo”),18 Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo,Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo,Simoni Mkanani na 19 Yuda Iskarioti ambayealimsaliti Yesu. 20 Kisha Yesu alikwendanyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena,hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupatanafasi ya kula chakula. 21 Basi, watu wa jamaayake walipopata habari hiyo wakatoka kwendakumchukua maana walikuwa wanasemakwamba amepatwa na wazimu. 22 Nao walimuwa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu,wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena,anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wapepo.” 23 Hapo Yesu akawaita, akawaambiakwa mifano, “Shetani anawezaje kumfukuzaShetani? 24 Ikiwa utawala mmojaumegawanyika makundimakundiyanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu.25 Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyikamakundimakundi yanayopingana, jamaa hiyoitaangamia. 26 Ikiwa basi, utawala wa Shetaniumegawanyika vikundivikundi hauwezikudumu, bali utaangamia kabisa. 27 “Hakunamtu awezaye kuivamia nyumba ya mtumwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake,isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtumwenye nguvu; hapo ndipo atakapowezakumnyang'anya mali yake. 28 “Kwelinawaambieni, watu watasamehewa dhambizao zote na kufuru zao zote; 29 lakinianayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu,hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambiya milele.” 30 (Yesu alisema hivyo kwa sababuwalikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”) 31

Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo,wakasimama nje, wakampelekea ujumbekutaka kumwona. 32 Umati wa watu ulikuwaumekaa hapo kumzunguka. Basi,wakamwambia, “Mama yako na ndugu zakowako nje, wanataka kukuona.” 33 Yesuakawaambia, “Mama yangu na ndugu zangu nikina nani?” 34 Hapo akawatazama watu

waliokuwa wamemzunguka, akasema,“Tazameni! Hawa ndio mama yangu na nduguzangu. 35 Mtu yeyote anayefanya anayotakaMungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yanguna mama yangu.”

Yesu alianza kufundisha tena akiwakando ya ziwa. Umati mkubwa wa watuulimzunguka hata ikambidi aingie

katika mashua na kuketi. Watu wakawawamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa. 2

Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, nakatika mafundisho yake aliwaambia, 3

“Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.4 Alipokuwa akipanda, nyingine ziliangukanjiani, ndege wakaja wakazila. 5 Nyinginezilianguka penye mawe pasipokuwa naudongo mwingi. Mbegu hizo ziliota mara kwakuwa udongo haukuwa na kina. 6 Jualilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwamizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka. 7

Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba,nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaanafaka. 8 Nyingine zilianguka katika udongomzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini,moja sitini na nyingine mia.” 9 Kishaakawaambia, “Mwenye masikio na asikie!” 10

Yesu alipokuwa peke yake, baadhi ya walewaliomsikia walimwendea pamoja na walekumi na wawili, wakamwuliza juu ya hiyomifano. 11 Naye akawaambia, “Ninyimmejaliwa kujua siri ya Utawala wa Mungu,lakini wale walio nje wataambiwa kila kitu kwamifano, 12 ili, Watazame kweli, lakini wasione.Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo,wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe.”13 Basi, Yesu akawauliza, “Je, ninyi hamwelewimfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfanowowote? 14 Mpanzi hupanda neno la Mungu.15 Watu wengine ni kama wale walio njianiambapo mbegu zilianguka. Hawa hulisikia hiloneno lakini mara Shetani huja na kuliondoaneno hilo lililopandwa ndani yao. 16 Watuwengine ni kama zile mbegu zilizopandwapenye mawe. Mara tu wanapolisikia hilo nenohulipokea kwa furaha. 17 Lakini haliwaingii nakuwa na mizizi ndani yao; huendeleakulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabuau udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hiloneno mara wanakata tamaa. 18 Watu wengineni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti yamiiba. Huo ni mfano wa wale wanaolisikia hiloneno, 19 lakini wasiwasi wa ulimwengu huu,anasa za mali na tamaa za kila namnahuwaingia na kulisonga hilo neno, naohawazai matunda. 20 Lakini wengine ni kamazile mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri.Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea,wakazaa matunda: wengine thelathini,wengine sitini na wengine mia moja.” 21 Yesuakaendelea kuwaambia, “Je, watu huwasha taawakaileta ndani na kuifunika kwa pishi aukuiweka mvunguni? La! Huiweka juu ya kinara.22 Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila

MARKO MTAKATIFU 3:9

30

Page 31: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

kilichofunikwa kitafunuliwa. 23 Mwenyemasikio na asikie!” 24 Akawaambia pia,“Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimokilekile mnachowapimia watu wengine, ndichomtakachopimiwa; tena mtazidishiwa. 25 Aliyena kitu atapewa zaidi; asiye na kitu, hata kilealicho nacho kitachukuliwa.” 26 Yesuakaendelea kusema, “Ufalme wa Mungu nikama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegushambani. 27 Usiku hulala, mchana yu machona wakati huo mbegu zinaota na kukua; yeyehajui inavyofanyika. 28 Udongo wenyewehuiwezesha mimea kukua na kuzaa matunda:kwanza huchipua jani changa, kisha suke, namwishowe nafaka ndani ya suke. 29 Nafakainapoiva, huyo mtu huanza kutumia munduwake, maana wakati wa mavuno umefika.” 30

Tena, Yesu akasema, “Tuufananishe Utawalawa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani?31 Ni kama mbegu ya haradali ambayo nindogo kuliko mbegu zote. 32 Lakini ikishapandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kulikomimea yote ya shambani. Matawi yake huwamakubwa hata ndege wa angani huwezakujenga viota vyao katika kivuli chake.” 33 Yesualiwahubiria ujumbe wake kwa mifanomingine mingi ya namna hiyo; aliongea naokadiri walivyoweza kusikia. 34 Hakuongea naochochote bila kutumia mifano; lakini alipokuwapamoja na wanafunzi wake peke yao alikuwaakiwafafanulia kila kitu. 35 Jioni, siku hiyohiyo,Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvukeziwa, twende ng'ambo.” 36 Basi, wakauachaule umati wa watu, wakamchukua Yesu katikamashua alimokuwa. Palikuwapo pia mashuanyingine hapo. 37 Basi, dhoruba kali ikaanzakuvuma, mawimbi yakaipiga ile mashua hataikaanza kujaa maji. 38 Yesu alikuwa sehemu yanyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi,wanafunzi wakamwamsha na kumwambia,“Mwalimu, je, hujali kwamba sisitunaangamia?” 39 Basi, akaamka, akaukemeaule upepo na kuyaamrisha mawimbi ya ziwa,“Kimya! Tulia!” Hapo upepo ukakoma, kukawashwari kabisa. 40 Kisha Yesu akawaambiawanafunzi wake, “Mbona mnaogopa? Je, badohamna imani?” 41 Nao wakaogopa sana,wakawa wanaulizana, “Huyu ni nani basi, hataupepo na mawimbi vinamtii?”

Basi, wakafika katika nchi ya Wagerase,ng'ambo ya ziwa. 2 Mara tu Yesualiposhuka mashuani, mtu mmoja

aliyepagawa na pepo mchafu alitokamakaburini, akakutana naye. 3 Mtu huyoalikuwa akiishi makaburini wala hakuna mtualiyeweza tena kumfunga kwa minyororo. 4

Mara nyingi walimfunga kwa pingu naminyororo lakini kila mara aliweza kuikata hiyominyororo na kuzivunja hizo pingu, walahakuna mtu aliyeweza kumzuia. 5 Mchana nausiku alikaa makaburini na milimani akipaazasauti na kujikatakata kwa mawe. 6

Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia,

akamwinamia 7 akisema kwa sauti kubwa,“Una shauri gani nami, wewe Yesu Mwana waMungu aliye juu? Kwa jina la Mungu, nakusihiusinitese!” 8 (Alisema hivyo kwa kuwa Yesualikuwa amemwambia, “Pepo mchafu, mtokemtu huyu.”) 9 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lakonani?” Naye akajibu, “Jina langu ni Jeshi, maanasisi tu wengi.” 10 Kisha akamsihi Yesuasiwafukuze hao pepo katika nchi ile. 11

Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwemalishoni kwenye mteremko wa mlima. 12

Basi, hao pepo wakamsihi, “Utupeleke kwa haonguruwe, tuwaingie.” 13 Naye akawaruhusu.Basi, hao pepo wachafu wakatoka,wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote languruwe wapatao elfu mbili likaporomokakwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani,likatumbukia majini. 14 Wachungaji wa haonguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilomjini na mashambani. Watu wakafika kuonayaliyotukia. 15 Wakamwendea Yesu,wakamwona na mtu yuleyule aliyekuwaamepagawa na jeshi la pepo ameketi chini,amevaa nguo na ana akili yake sawa,wakaogopa. 16 Watu walishuhudia tukio hilowakaeleza wengine mambo yaliyompata huyomtu aliyekuwa amepagawa na pepo na juu yawale nguruwe. 17 Basi, wakaanza kumwombaaondoke katika nchi yao. 18 Yesu alipokuwaanapanda mashuani, yule mtu aliyekuwaamepagawa na pepo akamwomba amruhusukwenda naye. 19 Lakini Yesu akamkatalia.Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbanikwa jamaa yako, ukawaambie mambo yoteBwana aliyokutendea na jinsi alivyokuoneahuruma.” 20 Basi, huyo mtu akaenda, akaanzakutangaza huko Dekapoli mambo yote Yesualiyomtendea; watu wote wakashangaa. 21

Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwamashua. Umati mkubwa wa watuukakusanyika mbele yake, naye akawaamesimama kando ya ziwa. 22 Hapo akajammojawapo wa maofisa wa sunagogi, jina lakeYairo. Alipomwona Yesu, akajitupa mbele yamiguu yake, 23 akamsihi akisema, “Binti yangumdogo ni mgonjwa karibu kufa. Twendetafadhali, ukamwekee mikono yako, apatekupona na kuishi.” 24 Basi, Yesu akaondokapamoja naye. Watu wengi sana wakamfuata,wakawa wanamsonga kila upande. 25

Mmojawapo alikuwa mwanamke mwenyeugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wamiaka kumi na miwili. 26 Mwanamke huyoalikuwa amekwisha sumbuka sana kuwaendeawaganga wengi. Na ingawa alikuwaamekwisha tumia mali yake yote, hakupatanafuu bali hali yake ilizidi kuwa mbaya. 27

Alikuwa amesikia habari za Yesu, na hivyoakaupenya msongamano wa watu kutokanyuma, akagusa vazi lake. 28 Alifanya hivyo,maana alijisemea, “Nikigusa tu vazi lake,nitapona.” 29 Mara chemchemi ya damu yakeikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba

MARKO MTAKATIFU 5:29

31

Page 32: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

ameponywa ugonjwa wake. 30 Yesu alitambuamara kwamba nguvu imemtoka. Basiakaugeukia ule umati wa watu, akauliza, “Nanialiyegusa mavazi yangu?” 31 Wanafunzi wakewakamjibu, “Unaona jinsi watuwanavyokusonga; mbona wauliza nanialiyekugusa?” 32 Lakini Yesu akaendeleakutazama amwone huyo aliyefanya hivyo. 33

Hapo huyo mwanamke, akifahamuyaliyompata, akajitokeza akitetemeka kwahofu, akajitupa chini mbele ya Yesu na kusemaukweli wote. 34 Yesu akamwambia, “Binti,imani yako imekuponya. Nenda kwa amani,upone kabisa ugonjwa wako.” 35 Yesualipokuwa bado anaongea, watu walifikakutoka nyumbani kwa yule ofisa wa sunagogi,wakamwambia, “Binti yako amekwisha kufa. Yanini kuendelea kumsumbua Mwalimu?” 36

Lakini, bila kujali walichosema, Yesuakamwambia mkuu wa sunagogi, “Usiogope,amini tu.” 37 Wala hakumruhusu mtu yeyotekufuatana naye ila Petro, Yakobo na Yohanenduguye Yakobo. 38 Wakafika nyumbani kwaofisa wa sunagogi naye Yesu akasikiamakelele, kilio na maombolezo mengi. 39

Akaingia ndani, akawaambia, “Mbona mnapigakelele na kulia? Msichana hakufa, amelala tu.”40 Lakini wao wakamcheka. Basi, akawaondoawote nje, akawachukua baba na mama yahuyo msichana na wale wanafunzi wake,wakaingia chumbani alimokuwa huyomsichana. 41 Kisha akamshika mkono,akamwambia, “Talitha, kumi,” maana yake,“Msichana, nakwambia, amka!” 42 Maramsichana akasimama, akaanza kutembea.(Alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili.)Hapo watu wakashangaa kupita kiasi. 43 Yesuakawakataza sana wasimjulishe mtu jambohilo. Kisha akawaambia wampe huyo msichanachakula.

Yesu aliondoka hapo akaenda katikakijiji chake, akifuatwa na wanafunziwake. 2 Siku ya Sabato ilipofika, alianza

kufundisha katika sunagogi. Wengiwaliomsikia walishangaa, wakasema, “Je,ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima ganihii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu hayaanayoyafanya? 3 Je, huyu si yule seremalamwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo,Yose, Yuda na Simoni; Je, dada zake si wanaishipapa hapa kwetu?” Basi, wakawa na mashakanaye. 4 Yesu akawaambia, “Nabii hakosiheshima isipokuwa katika nchi yake, kwajamaa zake na nyumbani mwake.” 5 Hakuwezakutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikonowagonjwa wachache, akawaponya. 6

Alishangaa sana kwa sababu ya kutoaminikwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji vya palekaribu akiwafundisha watu. 7 Aliwaita walewanafunzi kumi na wawili, akaanza kuwatumawawiliwawili. Aliwapa uwezo wa kuwatoa pepowachafu, 8 na kuwaamuru, “Msichukuechochote mnapokwenda isipokuwa fimbo tu.

Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedhakibindoni. 9 Vaeni viatu lakini msivae kanzumbili.” 10 Tena aliwaambia, “Popotemtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humompaka mtakapoondoka mahali hapo. 11

Mahali popote ambapo watu watakataakuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokenihapo na kuyakung'uta mavumbi miguunimwenu kama onyo kwao.” 12 Basi,wakaondoka, wakahubiri watu watubu. 13

Waliwafukuza pepo wengi wabaya;wakawapaka mafuta wagonjwa wengi,wakawaponya. 14 Basi, mfalme Herode alisikiajuu ya hayo yote, maana sifa za Yesu zilieneakila mahali. Baadhi ya watu walikuwawakisema, “Yohane Mbatizaji amefufukakutoka wafu, ndiyo maana nguvu za miujizazinafanya kazi ndani yake.” 15 Wenginewalisema, “Mtu huyu ni Eliya.” Wenginewalisema, “Huyu ni nabii kama mmojawapo wamanabii wa kale.” 16 Lakini Herode alipopatahabari hizi alisema, “Huyu ni Yohane! Nilimkatakichwa, lakini amefufuka.” 17 Hapo awaliHerode mwenyewe alikuwa ameamuru Yohaneatiwe nguvuni, akamfunga gerezani. Herodealifanya hivyo kwa sababu ya Herodia ambayeHerode alimwoa ingawaje alikuwa mke waFilipo, ndugu yake. 18 Yohane alikuwaamemwambia Herode, “Si halali kwakokumchukua mke wa ndugu yako.” 19 BasiHerodia alimchukia sana Yohane, akatakakumwua, asiweze. 20 Herode alimwogopaYohane kwa maana alijua kwamba yeye ni mtumwema na mtakatifu, na hivyo akamlinda.Herode alipenda kumsikiliza Yohane, ingawajebaada ya kumsikiliza, alifadhaika sana. 21

Ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu yakuzaliwa kwake Herode. Herode aliwafanyiakaramu wazee wa baraza lake, majemadari naviongozi wa Galilaya. 22 Basi, binti yakeHerodia aliingia, akacheza, akawafurahishasana Herode na wageni wake. Mfalmeakamwambia huyo msichana, “Niombechochote utakacho, nami nitakupa.” 23 Tenaakamwapia, “Chochote utakachoniomba,nitakupa: hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu.”24 Hapo huyo msichana akatoka, akamwulizamama yake, “Niombe nini?” Naye akamjibu,“Kichwa cha Yohane mbatizaji.” 25 Msichanaakamrudia mfalme mbio akamwomba,“Nataka unipe sasa hivi katika sinia kichwa chaYohane mbatizaji.” 26 Mfalme akahuzunikasana, lakini kwa sababu ya kiapo chake, na kwaajili ya wale wageni wake karamuni, hakutakakumkatalia. 27 Basi, mfalme akamwamuruaskari kukileta kichwa cha Yohane. Askariakaenda, akamkata kichwa Yohane mlegerezani, 28 akakileta katika sinia, akampamsichana naye msichana akampa mama yake.29 Wanafunzi wa Yohane walipopata habari,walikwenda wakachukua mwili wake,wakauzika kaburini. 30 Wale mitume walirudi,wakakusanyika mbele ya Yesu wakamwarifu

MARKO MTAKATIFU 5:30

32

Page 33: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

7

yote waliyotenda na kufundisha. 31 Alisemahivyo kwa kuwa kulikuwa na watu wengi mnowalikuwa wanafika hapo na kuondoka hataYesu na wanafunzi wake hawakuweza kupatanafasi ya kula chakula. Basi, Yesu akawaambia,“Twendeni peke yetu mahali pa faragha kulachakula, mkapumzike kidogo.” 32 Basi,Wakaondoka peke yao kwa mashua, wakaendamahali pa faragha. 33 Lakini watu wengiwaliwaona wakienda, wakawatambua. Hivyowengi wakatoka katika kila mji, wakakimbiliahuko Yesu na wanafunzi wake walikokuwawanakwenda, wakawatangulia kufika. 34

Waliposhuka pwani, Yesu aliona umatimkubwa wa watu, akawahurumia, kwa sababuwalikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.Akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35 Saaza mchana zilikwisha pita. Basi, wanafunziwakamwendea Yesu, wakamwambia, “Hapa ninyikani, na sasa kunakuchwa. 36 Afadhaliuwaage watu waende mashambani na katikavijiji vya jirani, wanunue chakula.” 37 LakiniYesu akawaambia, “Wapeni ninyi chakula.” Naowakamwuliza, “Je, twende kununua mikatekwa fedha dinari mia mbili, na kuwapachakula?” 38 Yesu akawauliza, “Mnayo mikatemingapi? Nendeni mkatazame.” Walipokwishatazama, wakamwambia, “Kuna mikate mitanona samaki wawili.” 39 Basi, Yesu akawaamuruwanafunzi wawaketishe watu wotemakundimakundi penye nyasi. 40 Naowakaketi makundimakundi ya watu mia mojana ya watu hamsini. 41 Kisha Yesu akaitwaa ilemikate mitano na wale samaki wawili,akatazama juu mbinguni, akamshukuruMungu, akaimega mikate, akawapa wanafunziwake wawagawie watu. Na wale samaki wawilipia akawagawia wote. 42 Watu wote wakala,wakashiba. 43 Wakaokota mabaki ya mikate nasamaki pia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 44

Nao waliokula hiyo mikate walikuwa wanaumeelfu tano. 45 Mara Yesu akawaamuruwanafunzi wake wapande mashua,wamtangulie kwenda Bethsaida, ng'ambo yaziwa, wakati yeye anauaga umati wa watu. 46

Baada ya kuwaaga watu alikwenda mlimanikusali. 47 Ilipokuwa jioni, mashua ilikuwakatikati ya ziwa, naye alikuwa peke yake katikanchi kavu. 48 Basi, akawaona wanafunzi wakewakitaabika kwa kupiga makasia, maanaupepo ulikuwa unawapinga. Karibu namapambazuko, Yesu aliwaendea akitembeajuu ya maji. Alitaka kuwapita. 49 Lakiniwalimwona akitembea juu ya maji, wakadhanini mzimu, wakapiga yowe. 50 Maana wotewalipomwona waliogopa sana. Mara Yesuakasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!” 51

Kisha akapanda mashuani walimokuwa, naupepo ukatulia. Nao wakashangaa sana. 52

maana hawakuwa bado wameelewa maana yaile mikate. Akili zao zilikuwa badozimepumbazika. 53 Walivuka ziwa, wakafikanchi ya Genesareti, wakatia nanga. 54

Walipotoka mashuani, mara watuwakamtambua Yesu. 55 Basi, kwa harakawakazunguka katika nchi ile yote, wakaanzakuwachukua wagonjwa wamelala juu yamikeka yao, wakawapeleka kila mahaliwaliposikia Yesu yupo. 56 Kila mahali Yesualipokwenda, vijijini, mijini, au mashambani,watu waliwaweka wagonjwa uwanjani,wakamsihi waguse walau pindo la vazi lake.Nao wote waliomgusa walipona.

Baadhi ya Mafarisayo na walimu waSheria waliokuwa wametokaYerusalemu walikusanyika mbele ya

Yesu. 2 Waliona kwamba baadhi ya wanafunziwake walikula mikate kwa mikono najisi, yaanibila kunawa. 3 Maana Mafarisayo naWayahudi wengine wote huzingatia mapokeoya wazee wao: hawali kitu kabla ya kunawamikono ipasavyo. 4 Tena hawali kitu chochotekutoka sokoni mpaka wamekiosha kwanza.Kuna pia desturi nyingine walizopokea kamavile namna ya kuosha vikombe, sufuria navyombo vya shaba. 5 Basi, Mafarisayo nawalimu wa Sheria wakamwuliza Yesu, “Mbonawanafunzi wako hawayajali mapokeotuliyopokea kwa wazee wetu, bali hula chakulakwa mikono najisi?” 6 Yesu akawajibu,“Wanafiki ninyi! Nabii Isaya alitabiri ukweli juuyenu alipoandika: Watu hawa, asema Mungu,huniheshimu kwa maneno matupu, lakinimioyoni mwao wako mbali nami. 7 Kuniabudukwao hakufai, maana mambo wanayofundishani maagizo ya kibinadamu tu. 8 Ninyimnaiacha amri ya Mungu na kushikiliamaagizo ya watu.” 9 Yesu akaendelea kusema,“Ninyi mnajua kuepa kwa ujanja sheria yaMungu kwa ajili ya kufuata mapokeo yenu. 10

Maana Mose aliamuru: Waheshimu baba yakona mama yako, na, Anayemlaani baba aumama, lazima afe. 11 Lakini ninyimwafundisha, Kama mtu anacho kitu ambachoangeweza kuwasaidia nacho baba au mamayake, lakini akasema kwamba kitu hicho niKorbani (yaani ni zawadi kwa Mungu), 12 basi,halazimiki tena kuwasaidia wazazi wake. 13

Hivyo ndivyo mnavyodharau neno la Mungukwa ajili ya mafundisho mnayopokezana. Tenamnafanya mambo mengi ya namna hiyo.” 14

Yesu aliuita tena ule umati wa watu,akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe. 15

Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu tokanje ambacho chaweza kumtia mtu najisi. Lakinikinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtiamtu najisi.” 16 Mwenye masikio na asikie! 17

Alipouacha umati wa watu na kuingianyumbani, wanafunzi wake walimwulizamaana ya huo mfano. 18 Naye akawaambia,“Je, hata ninyi hamwelewi? Je, hamwelewikwamba kitu kinachomwingia mtu toka njehakiwezi kumtia unajisi, 19 kwa maanahakimwingii moyoni, ila tumboni, na baadayehutolewa nje chooni?” (Kwa kusema hivyo,Yesu alivihalalisha vyakula vyote.) 20

MARKO MTAKATIFU 7:20

33

Page 34: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani yamtu ndicho kinachomtia najisi. 21 Kwa maanakutoka ndani, katika moyo wa mtu, hutokamawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, 22

uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi,wivu, kashfa, kiburi na upumbavu. 23 Maovuhayo yote yatoka ndani ya mtu, nayo humtiamtu najisi.” 24 Yesu aliondoka hapo, akaendahadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katikanyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakinihakuweza kujificha. 25 Mwanamke mmojaambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikiahabari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chinimbele ya miguu yake. 26 Mama huyo alikuwaMgiriki, mwenyeji wa Sirofoinike. Basi,akamwomba Yesu amtoe binti yake pepomchafu. 27 Yesu akamwambia, “Kwanzawatoto washibe; kwa maana si vizuri kuchukuachakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” 28

Lakini huyo mama akasema, “Sawa, Bwana,lakini hata mbwa walio chini ya meza hulamakombo ya watoto.” 29 Yesu akamwambia,“Kwa sababu ya neno hilo, nenda. Pepoamemtoka binti yako!” 30 Basi, akaendanyumbani kwake, akamkuta mtoto amelalakitandani, na pepo amekwisha mtoka. 31 KishaYesu aliondoka wilayani Tiro, akapitia Sidoni,akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi yaDekapoli. 32 Basi, wakamletea bubu-kiziwi,wakamwomba amwekee mikono. 33 Yesuakamtenga na umati wa watu, akamtia vidolemasikioni, akatema mate na kumgusa ulimi. 34

Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite,akamwambia, “Efatha,” maana yake,“Funguka.” 35 Mara masikio yake yakafungukana ulimi wake ukafunguliwa, akaanza kusemasawasawa. 36 Yesu akawaamuruwasimwambie mtu juu ya jambo hilo. Lakinikadiri alivyowakataza, ndivyo walivyozidikutangaza habari hiyo. 37 Watu walishangaasana, wakasema, “Amefanya yote vyema:amewajalia viziwi kusikia, na bubu kusema!”

Wakati huo umati mkubwa wa watuulikusanyika tena, na hawakuwa nachakula. Basi, Yesu akawaita wanafunzi

wake, akawaambia, 2 “Nawahurumia watuhawa kwa sababu wamekuwa nami kwa mudawa siku tatu, wala hawana chakula. 3

Nikiwaacha waende nyumbani wakiwa na njaawatazimia njiani, maana baadhi yao wametokambali.” 4 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Hapanyikani itapatikana wapi mikate yakuwashibisha watu hawa wote?” 5 Yesuakawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Naowakamjibu, “Saba.” 6 Basi, akawaamuru watuwakae chini. Akaitwaa ile mikate saba,akamshukuru Mungu, akaimega, akawapawanafunzi wake wawagawie watu, naowakawagawia. 7 Walikuwa pia na visamakivichache. Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwewatu vilevile. 8 Watu wakala, wakashiba.Wakaokota mabaki yaliyosalia wakajazamakapu saba. 9 Nao waliokula walikuwa watu

wapatao elfu nne. Yesu akawaaga, 10 na maraakapanda mashua pamoja na wanafunzi wake,akaenda wilaya ya Dalmanutha. 11 Mafarisayowalikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwakumjaribu, wakamtaka awafanyie isharakuonyesha anayo idhini kutoka mbinguni. 12

Yesu akahuzunika rohoni, akasema, “Mbonakizazi hiki kinataka ishara? Kweli nawaambieni,kizazi hiki hakitapewa ishara yoyote!” 13 Basi,akawaacha, akapanda tena mashua, akaanzasafari kwenda ng'ambo ya pili ya ziwa. 14

Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukuamikate; walikuwa na mkate mmoja tu katikamashua. 15 Yesu akawaonya, “Angalieni sana!Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachuya Herode.” 16 Wanafunzi wakaanzakujadiliana wao kwa wao, “Anasema hivyo kwakuwa hatuna mikate.” 17 Yesu alitambua hayo,akawaambia, “Mbona mnajadiliana juu yakutokuwa na mikate? Je, bado hamjafahamu,wala hamjaelewa? Je, mioyo yenu imeshupaa?18 Je, Mnayo macho na hamwoni? Mnayomasikio na hamsikii? Je, hamkumbuki 19

wakati ule nilipoimega ile mikate mitano nakuwapa watu elfu tano? Mlikusanya vikapuvingapi vya mabaki ya makombo?” Wakamjibu,“Kumi na viwili.” 20 “Na nilipoimega ile mikatesaba na kuwapa watu elfu nne, mlikusanyamakapu mangapi ya makombo?” Wakamjibu,“Saba.” 21 Basi, akawaambia, “Na badohamjaelewa?” 22 Yesu alifika Bethsaida pamojana wanafunzi wake. Huko watu wakamleteakipofu mmoja, wakamwomba amguse. 23 Yesuakamshika mkono huyo kipofu, akampelekanje ya kijiji. Akamtemea mate machoni,akamwekea mikono, akamwuliza, “Je, unawezakuona kitu?” 24 Huyo kipofu akatazama,akasema, “Ninawaona watu wanaoonekanakama miti inayotembea.” 25 Kisha Yesuakamwekea tena mikono machoni, nayeakakaza macho, uwezo wake wa kuonaukamrudia, akaona kila kitu sawasawa. 26 Yesuakamwambia aende zake nyumbani nakumwamuru, “Usirudi kijijini!” 27 Kisha Yesu nawanafunzi wake walikwenda katika vijiji vyaKaisarea Filipi. Walipokuwa njiani, Yesualiwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasemamimi ni nani?” 28 Wakamjibu, “Wenginewanasema wewe ni Yohane Mbatizaji, wengineEliya na wengine mmojawapo wa manabii.” 29

Naye akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimini nani?” Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo.”30 Kisha Yesu akawaonya wasimwambie mtuyeyote habari zake. 31 Yesu alianzakuwafundisha wanafunzi wake: “Ni lazimaMwana wa Mtu apatwe na mateso mengi nakukataliwa na wazee na makuhani wakuu nawalimu wa Sheria. Atauawa na baada ya sikutatu atafufuka.” 32 Yesu aliwaambia jambo hilowaziwazi. Basi, Petro akamchukua kando,akaanza kumkemea. 33 Lakini Yesu akageuka,akawatazama wanafunzi wake, akamkemeaPetro akisema, “Ondoka mbele yangu, Shetani!

MARKO MTAKATIFU 7:21

34

Page 35: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

Fikira zako si za kimungu ila ni za kibinadamu!”34 Kisha akauita umati wa watu pamoja nawanafunzi wake, akawaambia, “Mtu yeyoteakitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikanemwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.35 Maana mtu anayetaka kuyaokoa maishayake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtuatakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu nakwa ajili ya Habari Njema, atayaokoa. 36 Je,kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wotena kuyapoteza maisha yake? 37 Ama mtuatatoa kitu gani badala ya maisha yake? 38

Mtu yeyote katika kizazi hiki kiovu nakisichomjali Mungu anayenionea aibu mimi namafundisho yangu, Mwana wa Mtuatamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokujakatika utukufu wa Baba yake pamoja namalaika watakatifu.”

Yesu akaendelea kuwaambia, “Kwelinawaambieni, wako wengine papahapa ambao hawatakufa kabla ya

kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.” 2

Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro,Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu pekeyao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, 3

mavazi yake yakang'aa, yakawa meupe sana,jinsi dobi yeyote duniani asingewezakuyafanya meupe. 4 Eliya na Mosewakawatokea, wakazungumza na Yesu. 5

Petro akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vizurisana kwamba tuko hapa. Basi, afadhali tujengevibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mosena kimoja cha Eliya.” 6 Yeye na wenzakewaliogopa hata hakujua la kusema. 7 Kishalikatokea wingu likawafunika, na sauti ikasikikakutoka katika hilo wingu, “Huyu ni Mwanangumpendwa, msikilizeni.” 8 Mara wanafunzi haowakatazama tena, lakini hawakumwona mtumwingine, ila Yesu peke yake pamoja nao. 9

Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesualiwakataza wasimwambie mtu yeyote mambowaliyoyaona, mpaka Mwana wa Mtuatakapokuwa amefufuka kutoka wafu. 10 Basi,wakashika agizo hilo, lakini wakawawanajadiliana wao kwa wao maana yakufufuka kutoka wafu. 11 Wakamwuliza Yesu,“Mbona walimu wa Sheria wanasema kwambani lazima Eliya aje kwanza?” 12 Nayeakawajibu, “Naam, Eliya anakuja kwanzakutayarisha yote. Hata hivyo, kwa nini basiimeandikwa katika Maandiko Matakatifukwamba Mwana wa Mtu atapatwa na matesomengi na kudharauliwa? 13 Lakininawaambieni, Eliya amekwisha kuja, naowakamtendea walivyotaka kama ilivyoandikwajuu yake.” 14 Walipowafikia wale wanafunziwengine, waliona umati mkubwa wa watuhapo. Na baadhi ya walimu wa Sheriawalikuwa wanajadiliana nao. 15 Mara tu uleumati wa watu ulipomwona, wote walishangaasana, wakamkimbilia wamsalimu. 16 Yesuakawauliza, “Mnajadiliana nini nao?” 17 Hapomtu mmoja katika ule umati wa watu

akamjibu, “Mwalimu, nimemleta mwanangukwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu. 18

Kila mara anapomvamia, humwangusha chinina kumfanya atokwe na povu kinywani,akisaga meno na kuwa mkavu mwili wote.Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyopepo lakini hawakuweza.” 19 Yesuakawaambia, “Enyi kizazi kisicho na imani!Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumiliampaka lini? Mleteni kwangu.” 20

Wakampeleka. Mara tu huyo pepo alipomwonaYesu, alimtia mtoto kifafa, naye mtotoakaanguka chini, akagaagaa na kutoka povukinywani. Yesu akamwuliza baba yake huyomtoto, 21 “Amepatwa na mambo hayo tangulini?” Naye akamjibu, “Tangu utoto wake. 22 Namara nyingi pepo huyo amemwangushamotoni na majini, ili amwangamize kabisa.Basi, ikiwa waweza, utuhurumie nakutusaidia!” 23 Yesu akamwambia, “Eti ikiwawaweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtualiye na imani.” 24 Hapo, huyo baba akalia kwasauti, “Naamini! Lakini imani yangu haitoshi,nisaidie!” 25 Yesu alipouona umati wa watuunaongezeka upesi mbele yake, alimkemeayule pepo mchafu, “Pepo unayemfanya huyumtoto kuwa bubu-kiziwi, nakuamuru, mtokemtoto huyu wala usimwingie tena!” 26 Hapohuyo pepo alipaaza sauti, akamwangushahuyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtotoalionekana kama maiti, hata wenginewalisema, “Amekufa!” 27 Lakini Yesuakamshika mkono, akamwinua, nayeakasimama. 28 Yesu alipoingia nyumbani,wanafunzi wake walimwuliza kwa faragha,“Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa?” 29 Nayeakawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutokaisipokuwa kwa sala tu.” 30 Yesu na wanafunziwake waliondoka hapo, wakaendelea na safarikupitia wilaya ya Galilaya. Yesu hakupendawatu wajue alipokuwa, 31 kwa sababu alikuwaanawafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia,“Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watuambao watamuua; lakini siku ya tatu baada yakuuawa atafufuka.” 32 Wanafunzihawakufahamu jambo hilo. Wakaogopakumwuliza. 33 Basi, walifika Kafarnaumu. Naalipokuwa nyumbani, aliwauliza, “Mlikuwamnajadiliana nini njiani?” 34 Lakini waowakanyamaza, maana njiani walikuwawamebishana ni nani aliye mkuu kati yao. 35

Yesu akaketi chini, akawaita wale kumi nawawili, akawaambia, “Yeyote anayetaka kuwawa kwanza lazima awe wa mwisho na kuwamtumishi wa wote.” 36 Kisha akamchukuamtoto mdogo, akamsimamisha kati yao,akamku mbatia, halafu akawaambia, 37

“Anayempokea mtoto kama huyu kwa jinalangu, ananipokea mimi; na anayenipokeamimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yulealiyenituma.” 38 Yohane akamwambia,“Mwalimu, tumemwona mtu mmoja akitoapepo kwa kulitumia jina lako, nasi tukajaribu

MARKO MTAKATIFU 9:38

35

Page 36: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu.” 39

Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maanahakuna mtu anayefanya muujiza kwa jinalangu, na papo hapo akaweza kusema mabayajuu yangu. 40 Maana, asiyepingana nasi, yukoupande wetu. 41 Mtu yeyote atakeyewapenikikombe cha maji ya kunywa kwa sababu ninyini watu wake Kristo, hakika hatakosa kupatatuzo lake. 42 “Mtu yeyote atakayemfanyammoja wa hawa wadogo wanaoniaminiatende dhambi, ingekuwa afadhali kwa mtuhuyo kufungiwa shingoni mwake jiwe kubwa lakusagia na kutupwa baharini. 43 Mkono wakoukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia kwenyeuzima bila mkono mmoja, kuliko kuwa namikono miwili na kwenda katika moto waJehanamu. 44 Humo, wadudu wake hawafi namoto hauzimiki. 45 Na mguu wakoukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katikauzima bila mguu mmoja, kuliko kuwa namiguu yote miwili na kutupwa katika moto waJehanamu. 46 Humo, wadudu wake hawafi namoto hauzimiki. 47 Na jicho lako likikukosesha,ling'oe! Afadhali kuingia katika utawala waMungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa namacho yako yote mawili na kutupwa katikamoto wa Jehanamu. 48 Humo wadudu wakehawafi, na moto hauzimiki. 49 “Maana kilammoja atakolezwa kwa moto. 50 Chumvi ninzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa nanini? Muwe na chumvi ndani yenu nakudumisha amani kati yenu.”

Yesu alitoka hapo akaenda mkoaniYudea na hata ng'ambo ya mtoYordani. Umati wa watu ukamwendea

tena, naye akawafundisha tena kamailivyokuwa desturi yake. 2 Basi, Mafarisayowakamwendea, na kwa kumjaribuwakamwuliza, “Je, ni halali mtu kumpa talakamkewe?” 3 Yesu akawajibu, “Mose aliwapamaagizo gani?” 4 Nao wakasema, “Mosealiagiza mume kumpatia mkewe hati ya talakana kumwacha.” 5 Yesu akawaambia, “Mosealiwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumuwa mioyo yenu. 6 Lakini tangu kuumbwaulimwengu, Mungu aliumba mwanamume namwanamke. 7 Hivyo mwanamume atawaachababa yake na mama yake, ataungana namkewe, 8 nao wawili watakuwa mwili mmoja.Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja.9 Basi, alichounganisha Mungu, binadamuasitenganishe.” 10 Walipoingia tena ndani yanyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu yajambo hilo. 11 Naye akawaambia,“Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine,anazini dhidi ya mkewe. 12 Na mwanamkeanayemwacha mumewe na kuolewa namwingine anazini.” 13 Watu walimletea Yesuwatoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunziwakawakemea. 14 Yesu alipoona hivyo,alikasirika akawaambia, “Waacheni hao watotowaje kwangu, wala msiwazuie, kwa maanaUfalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio

kama watoto hawa. 15 Nawaambieni kweli,mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungukama mtoto mdogo hataingia katika Ufalmehuo.” 16 Kisha akawapokea watoto hao,akawawekea mikono, akawabariki. 17 Yesualipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjiambio, akapiga magoti mbele yake,akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje iliniupate uzima wa milele?” 18 Yesu akamjibu,“Mbona unaniita mwema? Hakuna aliyemwema ila Mungu peke yake. 19 Unazijuaamri: Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wauongo; Usidanganye; Waheshimu baba namama yako.” 20 Naye akamjibu, “Mwalimu,hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu.”21 Yesu akamtazama, akampenda,akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja:nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwapemaskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni;kisha njoo unifuate.” 22 Aliposikia hayo,alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwamaana alikuwa na mali nyingi. 23 Yesuakatazama pande zote, akawaambiawanafunzi wake, “Jinsi gani itakavyokuwavigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme waMungu!” 24 Wanafunzi walishangazwa namaneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watotowangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalmewa Mungu! 25 Ni rahisi zaidi ngamia kupenyakatika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingiakatika Ufalme wa Mungu.” 26 Wanafunzi wakewakashangaa sana wakaulizana, “Ni nani basi,atakayeweza kuokoka?” 27 Yesu akawatazama,akawaambia, “Kwa binadamu haiwezekani,lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungumambo yote huwezekana.” 28 Petroakamwambia, “Na sisi je? Tumeacha yote,tukakufuata!” 29 Yesu akasema, “Kwelinawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, aundugu, au dada, au mama, au baba, au watotoau mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili yaHabari Njema, 30 atapokea mara mia zaidiwakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada,mama, watoto na mashamba pamoja namateso; na katika wakati ujao atapokea uzimawa milele. 31 Lakini wengi walio wa kwanzawatakuwa wa mwisho, na walio wa mwishowatakuwa wa kwanza.” 32 Basi, walikuwa njianikwenda Yerusalemu, na Yesu alikuwaanawatangulia. Wanafunzi wake walijawa nahofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesuakawachukua tena kando wale kumi na wawili,akaanza kuwaambia yale yatakayompata: 33

“Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na hukoMwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhaniwakuu na walimu wa Sheria, naowatamhukumu auawe na kumkabidhi kwawatu wa mataifa. 34 Nao watamdhihaki;watamtemea mate, watampiga mijeledi nakumwua. Na baada ya siku tatu atafufuka.” 35

Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo,walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu,tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” 36

MARKO MTAKATIFU 9:39

36

Page 37: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

Yesu akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” 37

Wakamjibu, “Uturuhusu tuketi mmoja upandewako wa kulia na mwingine upande wako wakushoto katika utukufu wa Ufalme wako.” 38

Yesu akawaambia, “Hamjui mnachoomba! Je,mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa,au kubatizwa kama nitakavyobatizwa?” 39

Wakamjibu, “Tunaweza.” Yesu akawaambia,“Kikombe nitakachokunywa mtakinywa kweli,na mtabatizwa kama nitakavyobatizwa. 40

Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushotokwangu si wajibu wangu kupanga, bali nafasihizo watapewa wale waliotayarishiwa.” 41 Walewanafunzi wengine kumi waliposikia hayo,walianza kuchukizwa na Yakobo na Yohane. 42

Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwambawale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifahuwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuuhao huwamiliki watu wao. 43 Lakini kwenuisiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu katiyenu, sharti awe mtumishi wenu. 44 Anayetakakuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wawote. 45 Maana Mwana wa Mtu hakujakutumikiwa, ila alikuja kutumikia, na kutoamaisha yake kuwa fidia ya watu wengi.” 46

Basi, wakafika Yeriko, naye Yesu alipokuwaanatoka katika mji huo akiwa na wanafunziwake pamoja na umati mkubwa wa watu,kipofu mwombaji aitwaye Bartimayo mwanawa Timayo alikuwa ameketi kando yabarabara. 47 Aliposikia kwamba ni Yesu waNazareti aliyekuwa anapita mahali hapo,alianza kupaaza sauti, “Yesu, Mwana wa Daudi,nihurumie!” 48 Watu wengi walimkemea ilianyamaze, lakini yeye akazidi kupaaza sauti,“Mwana wa Daudi, nihurumie!” 49 Yesualisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi,wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipemoyo! Simama, anakuita.” 50 Naye akatupiliambali vazi lake, akaruka juu, akamwendeaYesu. 51 Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyienini?” Huyo kipofu akamwambia, “Mwalimu,naomba nipate kuona.” 52 Yesu akamwambia,“Nenda, imani yako imekuponya.” Mara huyokipofu akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.

Walipokuwa wanakaribia Yerusalemuwalifika Bethfage na Bethania, karibuna mlima wa Mizeituni. Hapo

aliwatuma wawili wa wanafunzi wake, 2

akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichombele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo,mtakuta mwana punda amefungwa ambayebado hajatumiwa na mtu. Mfunguenimkamlete. 3 Kama mtu akiwauliza, Mbonamnafanya hivyo? Mwambieni, Bwanaanamhitaji na atamrudisha hapa mara.” 4 Basi,wakaenda, wakamkuta mwana pundabarabarani amefungwa mlangoni. Walipokuwawakimfungua, 5 baadhi ya watu waliokuwawamesimama hapo wakawauliza “Kwa ninimnamfungua huyo mwana punda?” 6

Wanafunzi wakajibu kama Yesu alivyokuwaamewaambia; nao wakawaacha waende zao. 7

Wakampelekea Yesu huyo mwana punda.Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwanapunda, na Yesu akaketi juu yake. 8 Watu wengiwakatandaza mavazi yao barabarani; wenginewakatandaza matawi ya miti waliyoyakatamashambani. 9 Watu wote waliotangulia nawale waliofuata wakapaaza sauti zaowakisema, “Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwajina la Bwana! 10 Ubarikiwe Ufalme ujao wababa yetu Daudi. Hosana juu mbinguni!” 11

Yesu aliingia mjini Yerusalemu akaenda mojakwa moja mpaka Hekaluni, akatazama kila kitukwa makini. Lakini kwa vile ilikwisha kuwa jioni,akaenda Bethania pamoja na wale kumi nawawili. 12 Kesho yake, walipokuwa wanatokaBethania, Yesu aliona njaa. 13 Basi, akaonakwa mbali mtini wenye majani mengi.Akauendea ili aone kama ulikuwa na tundalolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ilamajani matupu, kwa vile hayakuwa majira yamtini kuzaa matunda. 14 Hapo akauambiamtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asilematunda kwako.” Nao wanafunzi wakewalisikia maneno hayo. 15 Basi, wakafikaYerusalemu. Yesu akaingia Hekaluni, akaanzakuwafukuza nje watu waliokuwa wanauza nakununua vitu humo ndani. Akazipindua mezaza wale waliokuwa wakibadilishana fedha naviti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 16

Hakumruhusu mtu yeyote kupitia Hekaluniakichukua kitu. 17 Kisha akawafundisha,“Imeandikwa: Nyumba yangu itaitwa nyumbaya sala kwa ajili ya mataifa yote! Lakini ninyimmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi!” 18

Makuhani wakuu na walimu wa Sheriawaliposikia hayo, walianza kutafuta njia yakumwangamiza. Lakini walimwogopa kwasababu umati wa watu ulishangazwa namafundisho yake. 19 Ilipokuwa jioni, Yesu nawanafunzi wake waliondoka mjini. 20 Asubuhina mapema, walipokuwa wanapita, waliuonaule mtini umenyauka wote, hata mizizi. 21

Petro aliukumbuka, akamwambia Yesu,“Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani,umenyauka!” 22 Yesu akawaambia,“Mwaminini Mungu. 23 Nawaambieni kweli,mtu akiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitosebaharini bila kuona shaka moyoni mwake, ilaakaamini kwamba mambo yote anayosemayanafanyika, atafanyiwa jambo hilo. 24 Kwahiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu,aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.25 Mnaposimama kusali, sameheni kila mtualiyewakosea chochote, ili Baba yenu aliyembinguni awasamehe ninyi makosa yenu. 26

Lakini msipowasamehe wengine, hata Babayenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyimakosa yenu.” 27 Basi, wakafika tenaYerusalemu. Yesu alipokuwa akitembeaHekaluni, makuhani wakuu, walimu wa Sheriana wazee walimwendea, 28 wakamwuliza,“Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?Nani aliyekupa mamlaka ya kufanya mambo

MARKO MTAKATIFU 11:28

37

Page 38: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

12

haya?” 29 Lakini Yesu akawaambia,“Nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, na pianitawaambieni ni kwa mamlaka gani ninafanyamambo haya. 30 Je, mamlaka ya Yohane yakubatiza yalitoka mbinguni ama kwa watu?Nijibuni.” 31 Wakaanza kujadiliana, “Tukisema,Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbonahamkumsadiki? 32 Na tukisema, Yalitoka kwawatu...” (Waliogopa umati wa watu maanawote waliamini kwamba Yohane alikuwa kwelinabii.) 33 Basi, wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.”Naye Yesu akawaambia, “Nami piasitawaambieni ninafanya mambo haya kwamamlaka gani.”

Yesu alianza kusema nao kwa mifano:“Mtu mmoja alilima shamba lamizabibu. Akalizungushia ukuta, na

katikati yake akachimba kisima cha kusindikiadivai, akajenga mnara pia. Akalikodishashamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchiya mbali. 2 Wakati wa mavuno, alimtumamtumishi wake kwa wale wakulima akamleteesehemu ya mazao ya shamba lake. 3 Walewakulima wakamkamata, wakampiga,wakamrudisha mikono mitupu. 4 Akatumatena mtumishi mwingine; huyu wakamuumizakichwa na kumtendea vibaya. 5 Mwenyeshamba akatuma mtumishi mwingine tena, nahuyo wakamuua. Wengine wengi waliotumwa,baadhi yao walipigwa, na wengi wakauawa. 6

Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaanimwanawe mpendwa. Mwishowe akamtumahuyo akisema, Watamheshimu mwanangu. 7

Lakini hao wakulima wakaambiana, Huyundiye mrithi, basi, tumuue ili urithi wake uwewetu! 8 Kwa hiyo wakamkamata, wakamuuana kumtupa nje ya lile shamba la mizabibu. 9

“Basi, mwenye shamba atafanya nini? Atakujakuwaangamiza hao wakulima na kulikodishahilo shamba la mizabibu kwa watu wengine. 10

Je, hamjasoma Maandiko haya? Jiwewalilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu lamsingi. 11 Bwana ndiye aliyefanya jambo hili,nalo ni la ajabu sana kwetu.” 12 Makuhaniwakuu, walimu wa Sheria na wazeewalifahamu ya kwamba mfano huo ulikuwaunawahusu. Kwa hiyo walijaribu kumtianguvuni, lakini waliogopa umati wa watu. Basi,wakamwacha wakaenda zao. 13 Basi, baadhiya Mafarisayo na wafuasi wa kikundi chaHerode walitumwa ili wamtege Yesu kwamaneno yake. 14 Wakamwendea,wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwambawewe ni mtu mwaminifu unayesema ukwelimtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheocha mtu si kitu kwako, lakini wafundishaukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halalikulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe autusilipe?” 15 Lakini Yesu alijua unafiki wao,akawaambia, “Mbona mnanijaribu?Nionyesheni sarafu.” 16 Wakamwonyesha.Naye akawauliza, “Sura na chapa hii ni yanani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 17 Basi, Yesu

akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisarina Mungu yaliyo yake Mungu.”Wakashangazwa sana naye. 18 Masadukayowasemao kwamba hakuna ufufuowalimwendea Yesu, wakamwuliza, 19

“Mwalimu, Mose alituagiza hivi: Mtu akifa nakuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazimaamchukue huyo mama mjane amzalie watotondugu yake marehemu. 20 Basi, kulikuwa nandugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bilakuacha mtoto. 21 Ndugu wa pili akamwoahuyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto;na ndugu watatu hali kadhalika. 22 Wote sabawalikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yulemama mjane naye akafa. 23 Basi, siku watuwatakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wanani? Maana wote saba walikuwawamemwoa.” 24 Yesu akawaambia, “Ninyimmekosea sana, kwa sababu hamjuiMaandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu.25 Maana wafu watakapofufuka, hawataoawala kuolewa; watakuwa kama malaika wambinguni. 26 Lakini kuhusu kufufuliwa kwawafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katikasehemu inayohusu kile kichaka kilichokuwakinawaka moto? Mungu alimwambia Mose,Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu waIsaka, na Mungu wa Yakobo. 27 Basi, yeye siMungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.Ninyi mmekosea sana!” 28 Mmojawapo wawalimu wa Sheria alifika, akasikia mabishanoyao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema,akajitokeza akamwuliza, “Katika amri zote ni ipiiliyo ya kwanza?” 29 Yesu akamjibu, “Ya kwanzandiyo hii: Sikiliza, Israeli! Bwana Mungu wetundiye peke yake Bwana. 30 Mpende BwanaMungu wako kwa moyo wako wote, kwa rohoyako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvuzako zote. 31 Na ya pili ndiyo hii: Mpende jiraniyako kama unavyojipenda mwenyewe. Hakunaamri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.” 32 Basi,yule mwalimu wa Sheria akamwambia, “VyemaMwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu nimmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye. 33

Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyowote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, nakumpenda jirani yake kama anavyojipendamwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kulikodhabihu na sadaka zote za kuteketezwa.” 34

Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwaujasiri, akamwambia, “Wewe huko mbali naUfalme wa Mungu.” Baada ya hayo, hakunamtu aliyethubutu tena kumwuliza kitu. 35

Wakati Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni,aliuliza, “Mbona walimu wa Sheria wanasemaya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 36

Daudi mwenyewe akiongozwa na RohoMtakatifu alisema: Bwana alimwambia Bwanawangu: Keti upande wangu wa kulia, Mpakanitakapowaweka adui zako chini ya miguuyako.” 37 “Daudi mwenyewe anamwita KristoBwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanae?”Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa

MARKO MTAKATIFU 11:29

38

Page 39: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

14

furaha. 38 Katika mafundisho yake, Yesualisema, “Jihadharini na walimu wa Sheriaambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzundefu na kusalimiwa na watu kwa heshimasokoni; hupenda kuketi mahali pa heshimakatika masunagogi, 39 na kuchukua nafasi zaheshima katika karamu. 40 Huwanyonyawajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu.Siku ya hukumu watapata adhabu kali!” 41

Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku lahazina. Akawa anatazama jinsi watu wengiwalivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katikahazina ya Hekalu. Matajiri wengi walitoa fedhanyingi. 42 Hapo akaja mama mmoja mjanemaskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha.43 Yesu akawaita wanafunzi wake,akawaambia, “Kweli nawaambieni, huyu mamamjane maskini ametoa zaidi kuliko wenginewote waliotia fedha katika sanduku la hazina.44 Maana wote walitoa kutokana na ziada yamali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini,ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitualichohitaji kwa kuishi.”

Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni,mmoja wa wanafunzi wakealimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi

mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”2 Yesu akamwambia, “Je, unayaona majengohaya makubwa? Hakuna hata jiwe mojalitakalosalia juu ya lingine; kila kitukitabomolewa.” 3 Yesu alipokuwa ameketi juuya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro,Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwafaragha, 4 “Twambie mambo haya yatatukialini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwambamambo haya karibu yatimizwe?” 5 Yesuakaanza kuwaambia, “Jihadharini msijemkadanganywa na mtu. 6 Maana wengiwatakuja wakilitumia jina langu, wakisema,Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.7 Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita,msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee,lakini mwisho wenyewe ungali bado. 8 Taifamoja litapigana na taifa lingine; utawalammoja utapigana na utawala mwingine; kilamahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi nanjaa. Mambo haya ni kama tu maumivu yakwanza ya kujifungua mtoto. 9 “Lakini ninyijihadharini. Maana watu watawapelekenimahakamani, na kuwapigeni katikamasunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawalana wafalme kwa sababu yangu ili mpatekunishuhudia kwao. 10 Lakini lazima kwanzaHabari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote. 11

Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapelekamahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yalemtakayosema; saa ile itakapofika, semenichochote mtakachopewa, maana si ninyimtakaosema, bali Roho Mtakatifu. 12 Nduguatamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsalitimwanae; watoto watawashambulia wazaziwao na kuwaua. 13 Watu wote watawachukienininyi kwa sababu ya jina langu. Lakini

atakayevumilia mpaka mwisho ndiyeatakayeokolewa. 14 “Mtakapoona ChukizoHaribifu limesimama mahali ambapo si pake,(msomaji na atambue maana yake!) Hapo watuwalioko Yudea wakimbilie milimani. 15 Mtualiye juu ya paa la nyumba asishuke kuingianyumbani mwake kuchukua kitu. 16 Aliyeshambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.17 Ole wao waja wazito na wanaonyonyeshasiku hizo! 18 Ombeni ili mambo hayo yasitukienyakati za baridi. 19 Maana wakati huokutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tanguMungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, walahaitatokea tena. 20 Kama Bwanaasingepunguza siku hizo, hakuna binadamuambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili yawateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.21 “Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristoyupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki. 22

Maana watatokea kina Kristo wa uongo namanabii wa uongo, watafanya ishara namaajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu,kama ikiwezekana. 23 Lakini ninyi jihadharini.Mimi nimewaambieni mambo yote kablahayajatokea. 24 “Basi, siku hizo baada ya dhikihiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.25 Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvuza mbingu zitatikiswa. 26 Hapo watamwonaMwana wa Mtu akija katika mawingu kwanguvu nyingi na utukufu. 27 Kisha atawatumamalaika wake; atawakusanya wateule wakekutoka pande zote nne za dunia, kutokamwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.28 “Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tumatawi yake yanapoanza kuwa laini nakuchanua majani, mnajua kwamba wakati wakiangazi umekaribia. 29 Hali kadhalika nanyimtakapoona mambo hayo yakitendeka, juenikwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana. 30

Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kablaya mambo hayo yote kutukia. 31 Mbingu nadunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapitakamwe. 32 “Lakini hakuna mtu ajuaye siku ausaa hiyo itakuja lini; wala malaika wambinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiyeajuaye. 33 Muwe waangalifu na kesheni,maana hamjui wakati huo utafika lini. 34

Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbanikwenda safari akiwaachia watumishi wakemadaraka, kila mmoja na kazi yake;akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35

Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenyenyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usikuwa manane, alfajiri au asubuhi. 36 Kesheni iliakija ghafla asije akawakuta mmelala. 37

Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote:Kesheni!”

Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuuya Pasaka na ya Mikate IsiyotiwaChachu. Makuhani wakuu na walimu

wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtiaYesu nguvuni kwa hila wamuue. 2 Lakiniwalisema, “Tusimtie nguvuni wakati wa

MARKO MTAKATIFU 14:2

39

Page 40: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.” 3

Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni,Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula,mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabastayenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwaalikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminiaYesu marashi hayo kichwani. 4 Baadhi ya watuwaliokuwa hapo walikasirika wakajisemea,“Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya? 5

Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi chadenari mia tatu, wakapewa maskini!”Wakamkemea huyo mama. 6 Lakini Yesuakawaambia, “Mwacheni; kwa ninimnamsumbua? Amenitendea jambo jema. 7

Maskini mnao daima pamoja nanyi; mnawezakuwasaidia wakati wowote mnaopenda. Lakinimimi sitakuwapo pamoja nanyi daima. 8 Yeyeamefanya alivyoweza; ameupaka mwili wangumarashi kuutayarisha kwa maziko. 9

Nawaambieni kweli, popote ulimwenguniHabari Njema itakapohubiriwa, kitendo hikialichofanya kitatajwa kwa ajili yakumkumbuka.” 10 Kisha Yuda Iskarioti, mmojawa wale kumi na wawili, alienda kwa makuhaniwakuu ili kumsaliti Yesu. 11 Makuhani wakuuwaliposikia habari hiyo, walifurahi, wakaahidikumpa fedha. Basi, Yuda akaanza kutafutanafasi ya kumsaliti Yesu. 12 Siku ya kwanza yasikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakatiambapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa,wanafunzi wake walimwuliza, “Watakatukuandalie wapi karamu ya Pasaka?” 13 BasiYesu akawatuma wawili wa wanafunzi wakeakiwaambia, “Nendeni mjini, nanyi mtakutanana mtu anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni14 mpaka katika nyumba atakayoingia,mkamwambie mwenye nyumba, Mwalimuanasema: wapi chumba changu ambamonitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?15 Naye atawaonyesha chumba kikubwaghorofani kilichotayarishwa na kupambwa.Tuandalieni humo.” 16 Wanafunziwakaondoka, wakaenda mjini, wakakuta kilakitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia.Wakaandaa karamu ya Pasaka. 17 Ilipokuwajioni, Yesu alifika pamoja na wanafunzi wakekumi na wawili. 18 Walipokuwa mezani wakila,Yesu alisema, “Kweli nawaambieni, mmojawenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.” 19

Hapo wanafunzi wake wakaanza kuhuzunika,wakamwuliza mmojammoja, “Je, ni mimi?” 20

Yesu akawaambia, “Ni mmoja wenu ninyi kumina wawili, anayechovya mkate pamoja namikatika bakuli. 21 Kweli Mwana wa Mtuanakwenda zake kama Maandiko Matakatifuyanavyosema juu yake; lakini, ole wake mtuyule anayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwaafadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa!”22 Walipokuwa wanakula, Yesu alitwaa mkate,akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunziwake akisema, “Twaeni; huu ni mwili wangu.”23 Kisha akatwaa kikombe, akamshukuruMungu, akawapa; nao wote wakanywa katika

kikombe hicho. 24 Akawaambia, “Hii ni damuyangu inayothibitisha agano la Mungu, damuinayomwagwa kwa ajili ya watu wengi. 25

Kweli nawaambieni, sitakunywa tena divai yazabibu mpaka siku ile nitakapoinywa upyakatika Ufalme wa Mungu.” 26 Kisha wakaimbawimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlimawa Mizeituni. 27 Yesu akawaambia wanafunziwake, “Ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami;maana Maandiko Matakatifu yasema:Nitampiga mchungaji nao kondoowatatawanyika. 28 Lakini nikisha fufuka,nitawatangulieni kule Galilaya.” 29 Petroakamwambia “Hata kama wote watakuwa namashaka nawe na kukuacha, mimi sitakukanakamwe!” 30 Yesu akamwambia, “Kwelinakwambia, usiku huu, kabla jogoo hajawikamara mbili, utanikana mara tatu.” 31 LakiniPetro akasisitiza, “Hata kama ni lazima nifepamoja nawe, sitakuacha kamwe.” Wanafunziwote pia wakasema vivyo hivyo. 32 Basi,wakafika katika bustani iitwayo Gethsemane.Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaenihapa wakati mimi nasali.” 33 Kishaakawachukua Petro, Yakobo na Yohane;akaanza kufadhaika sana na kuhangaika. 34

Akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hatakaribu kufa. Kaeni hapa mkeshe.” 35 Akaendambele kidogo, akajitupa chini kifudifudi,akasali kwamba, kama ingewezekana, asiipitiesaa hiyo ya mateso. 36 Akasema, “Baba yangu,kwako mambo yote yanawezekana.Uniondolee kikombe hiki; lakini isiwe kamanitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.” 37 Kishaakarudi kwa wanafunzi wale watatu,akawakuta wamelala. Basi, akamwuliza Petro,“Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hatasaa moja?” 38 Kisha akawaambia, “Kesheni nakusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho iradhi, lakini mwili ni dhaifu.” 39 Akaenda kusalitena akirudia maneno yaleyale. 40 Kishaakarudi tena, akawakuta wamelala. Macho yaoyalikuwa yamebanwa na usingizi. Hawakujuala kumjibu. 41 Alipowajia mara ya tatualiwaambia, “Mnalala bado na kupumzika?Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtuanakabidhiwa kwa watu waovu. 42 Amkeni,twendeni zetu. Tazameni, yule atakayenisalitiamekaribia.” 43 Yesu alipokuwa badoanasema, Yuda, mmoja wa wale kumi nawawili, akafika pamoja na umati wa watuwenye mapanga na marungu. Watu haowalikuwa wametumwa na makuhani wakuu,walimu wa Sheria na wazee. 44 Msaliti Yudaalikuwa amewapa ishara: “Yule nitakayembusundiye; mkamateni, mkampeleke chini yaulinzi.” 45 Yuda alipofika tu, alimwendea Yesumoja kwa moja, akasema, “Mwalimu!” Kishaakambusu. 46 Basi, hao watu wakamkamataYesu, wakamtia nguvuni. 47 Mmoja wa walewaliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesuakauchomoa upanga wake, akampigamtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. 48

MARKO MTAKATIFU 14:3

40

Page 41: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

15

Yesu akawaambia, “Je, mmekuja na mapangana marungu kunikamata kana kwamba mimini mnyang'anyi? 49 Kila siku nilikuwa pamojananyi nikifundisha Hekaluni, walahamkunikamata. Lakini sasa lazima MaandikoMatakatifu yatimie.” 50 Hapo wanafunzi wotewakamwacha, wakakimbia. 51 Kulikuwa nakijana mmoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwaamevaa shuka. Nao wakajaribu kumkamata.52 Lakini yeye akaponyoka, akaiachilia ileshuka, akakimbia uchi. 53 Basi, wakampelekaYesu kwa Kuhani Mkuu ambapo makuhaniwakuu wote, wazee na walimu wa Sheriawalikuwa wamekutanika. 54 Petro alimfuataYesu kwa mbali, akaingia ndani ya ya waKuhani Mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiotamoto. 55 Makuhani wakuu na Baraza lotewakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesuwapate kumwua, lakini hawakupata. 56 Watuwengi walitoa ushahidi wa uongo juu ya Yesu,lakini ushahidi wao haukupatana. 57 Kishawengine walisimama, wakatoa ushahidi wauongo wakisema: 58 “Tulimsikia mtu huyuakisema, Nitaliharibu Hekalu hili lililojengwakwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga linginelisilojengwa kwa mikono.” 59 Lakini hata hivyo,ushahidi wao haukupatana. 60 Basi, KuhaniMkuu akasimama katikati yao, akamwulizaYesu, “Je, hujibu neno? Watu hawawanashuhudia nini dhidi yako?” 61 Lakini yeyeakakaa kimya; hakusema hata neno moja.Kuhani Mkuu akamwuliza tena, “Je, wewendiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?” 62

Yesu akajibu, “Naam, mimi ndiye. Tena,mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upandewa kulia wa Mwenyezi, akija katika mawingu yambinguni.” 63 Hapo Kuhani Mkuu akararuajoho lake, akasema, “Tuna haja gani tena yamashahidi? 64 Mmesikia kufuru yake! Ninyimwaonaje?” Wote wakaamua kwambaanastahili kuuawa. 65 Basi, baadhi yaowakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso,wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nanialiyekupiga!” Hata watumishi wakamchukua,wakampiga makofi. 66 Petro alipokuwa badochini ukumbini, mmoja wa wajakazi wa kuhaniMkuu alikuja. 67 Alipomwona Petro akiotamoto, alimtazama, akamwambia, “Hata weweulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 LakiniPetro akakana, “Sijui, wala sielewi unayosema!”Kisha Petro akaondoka, akaenda nje uani.Hapo jogoo akawika. 69 Yule mjakazialipomwona tena Petro, akaanza tenakuwaambia watu waliokuwa wamesimamahapo, “Mtu huyu ni mmoja wao.” 70 Petroakakana tena. Baadaye kidogo, watuwaliokuwa wamesimama hapo wakamwambiaPetro, “Hakika wewe ni mmoja wao, maanawewe ni Mgalilaya.” 71 Lakini Petro akaanzakulaani na kuapa akisema, “Mimi simjui mtuhuyu mnayesema habari zake.” 72 Hapo jogooakawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbukajinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla

jogoo hajawika mara mbili, utanikana maratatu.” Petro akabubujika machozi.

Kulipopambazuka, makuhani wakuuwalifanya shauri pamoja na wazee,walimu wa Sheria na Baraza lote,

wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka nakumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwulizaYesu, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesuakajibu, “Wewe umesema.” 3 Makuhani wakuuwakamshtaki Yesu mambo mengi. 4 Pilatoakamwuliza tena Yesu, “Je, hujibu neno?Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juuyako.” 5 Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilatoakashangaa. 6 Kila wakati wa sikukuu yaPasaka, Pilato alikuwa na desturi yakuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka. 7

Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba,ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasiwengine kwa kusababisha uasi na mauaji. 8

Watu wengi wakamwendea Pilatowakamwomba awafanyie kama kawaida yake.9 Pilato akawauliza, “Je, mwatakaniwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?” 10

Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwambamakuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwakekwa sababu ya wivu. 11 Lakini makuhaniwakuu wakawachochea watu wamwombePilato awafungulie Baraba. 12 Pilatoakawauliza tena, “Basi, sasa mwataka nifanyenini na mtu huyu mnayemwita Mfalme waWayahudi?” 13 Watu wote wakapaaza sautitena: “Msulubishe!” 14 Lakini Pilato akawauliza,“Kwa nini! Amefanya kosa gani?” Lakini waowakazidi kupaaza sauti, “Msulubishe!” 15 Pilatoalitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi,akamwachilia Baraba kutoka gerezani.Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoaasulubiwe. 16 Kisha askari walimpeleka Yesundani ukumbini, katika ikulu, wakakusanyakikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika vazi larangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba,wakamwekea kichwani. 18 Wakaanzakumsalimu, “Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!”19 Wakampiga kichwani kwa mwanzi,wakamtemea mate; wakampigia magoti nakumsujudia. 20 Baada ya kumdhihaki,walimvua lile joho, wakamvika nguo zake,kisha wakampeleka kumsulubisha. 21

Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmojaaitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeyealikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakatihuo alikuwa akitoka shambani. Basi,wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahalipalipoitwa Golgotha, maana yake, “Mahali paFuvu la Kichwa.” 23 Wakampa divaiiliyochanganywa na manemane, lakini yeyeakaikataa. 24 Basi, wakamsulubisha,wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kurawaamue nani angepata nini. 25 Ilikuwa saatatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Namshtaka wake ulikuwa umeandikwa: “Mfalmewa Wayahudi.” 27 Pamoja naye

MARKO MTAKATIFU 15:27

41

Page 42: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

waliwasulubisha wanyang'anyi wawili, mmojaupande wake wa kulia na mwingine upandewake wa kushoto. 28 Hapo yakatimiaMaandiko Matakatifu yanayosema, “Aliwekwakundi moja na waovu.” 29 Watu waliokuwawanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisavichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe mwenyekuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu! 30

Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!” 31

Nao makuhani wakuu pamoja na walimu waSheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoawengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! 32

Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, naashuke msalabani ili tuone na kuamini.” Hatawatu wale waliosulubiwa pamoja nayewalimtukana. 33 Tangu saa sita mchanampaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote. 34

Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa,“Eloi, Eloi, lema sabakthani?” Maana yake,“Mungu wangu, Mungu wangu, mbonaumeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliosimamapale waliposikia hivyo, walisema, “Sikiliza!Anamwita Eliya!” 36 Mtu mmoja akakimbia,akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu yamwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuonekama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!”37 Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.38 Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipandeviwili toka juu mpaka chini. 39 Jemadari mmojaaliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsiYesu alivyolia kwa sauti na kukata roho,akasema, “Kweli mtu huyu alikuwa Mwana waMungu!” 40 Walikuwako pia wanawakewaliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwaMaria toka mji wa Magdala, Salome, na Mariamama wa kina Yakobo mdogo na Yose. 41

Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya nakumtumikia. Kulikuwa na wanawake wenginewengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye. 42

Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyoilikuwa siku ya Maandalio, yaani sikuinayotangulia Sabato. 43 Hapo akaja Yosefumwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa BarazaKuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwaanatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi,alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewemwili wa Yesu. 44 Pilato alishangaa kusikiakwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi,akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesualikuwa amekufa kitambo. 45 Pilatoalipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesualikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefuauchukue mwili wake. 46 Hapo Yosefuakanunua sanda ya kitani, akauteremsha chinihuo mwili, akauzungushia sanda. Akauwekakatika kaburi lililokuwa limechongwamwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwambele ya mlango. 47 Nao Maria Magdalene na

Maria mama yake Yose walipaona hapoalipolazwa.

Baada ya siku ya Sabato, MariaMagdalene, Salome na Maria mamayake Yakobo walinunua manukato ili

wakaupake mwili wa Yesu. 2 Basi, alfajiri namapema siku ya Jumapili, jua lilipoanzakuchomoza, walienda kaburini. 3 Nao wakawawanaambiana, “Nani atakayetuondolea lilejiwe mlangoni mwa kaburi?” 4 Lakiniwalipotazama, waliona jiwe limekwishaondolewa. (Nalo lilikuwa kubwa mno.) 5

Walipoingia kaburini, walimwona kijanammoja aliyevaa vazi jeupe, ameketi upande wakulia; wakashangaa sana. 6 Lakini huyo kijanaakawaambia, “Msishangae. Mnamtafuta Yesuwa Nazareti aliyesulubiwa. Amefufuka,hayumo hapa. Tazameni mahali walipokuwawamemlaza. 7 Nendeni mkawaambiewanafunzi wake pamoja na Petro ya kwambaanawatangulieni kule Galilaya. Hukomtamwona kama alivyowaambieni.” 8 Basi,wakatoka pale kaburini mbio, maanawalitetemeka kwa hofu na kushangaa.Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababuwaliogopa mno. 9 Yesu alipofufuka mapemaJumapili, alijionyesha kwanza kwa MariaMagdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoapepo saba. 10 Maria Magdalene akaenda,akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu,na wakati huo walikuwa wanaomboleza nakulia. 11 Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yuhai na kwamba Maria Magdalene amemwona,hawakuamini. 12 Baadaye Yesu aliwatokeawanafunzi wawili akiwa na sura nyingine.Wanafunzi hao walikuwa wanakwendashambani. 13 Nao pia wakaendawakawaambia wenzao. Hata hivyohawakuamini. 14 Mwishowe, Yesu aliwatokeawanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamojamezani. Akawakemea sana kwa sababu yakutoamini kwao na ukaidi wao, maanahawakuwaamini wale waliokuwa wamemwonabaada ya kufufuka. 15 Basi, akawaambia,“Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri HabariNjema kwa kila mtu. 16 Anayeamini nakubatizwa ataokolewa; asiyeaminiatahukumiwa. 17 Na ishara hizi zitaandamanana wale wanaoamini: kwa jina langu watatoapepo na watasema kwa lugha mpya. 18

Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochotechenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekeawagonjwa mikono, nao watapona.” 19 Basi,Bwana Yesu alipokwisha sema nao,akachukuliwa mbinguni, akaketi upande wakulia wa Mungu. 20 Wanafunzi wakaendawakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazipamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwaishara zilizoandamana nao.

MARKO MTAKATIFU 15:28

42

Page 43: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

LUKA MTAKATIFU

Mheshimiwa Theofilo: Watu wengiwamejitahidi kuandika juu ya mamboyale yaliyotendeka kati yetu. 2

Waliandika kama tulivyoelezwa na walewalioyaona kwa macho yao tangu mwanzo, nawaliotangaza ujumbe huo. 3 Inafaa nami pia,Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwamakini mambo yote tangu mwanzo,nikuandikie kwa mpango, 4 ili nawe uwezekujionea mwenyewe ukweli wa mambo yaleuliyofundishwa. 5 Wakati Herode alipokuwamfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmojajina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mkewake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwawa ukoo wa kuhani Aroni. 6 Wote wawiliwalikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishikwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwanabila lawama. 7 Lakini hawakuwa wamejaliwawatoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, naowote wawili walikuwa wazee sana. 8 Sikumoja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa hudumaya ukuhani mbele ya Mungu, 9 Zakariyaalichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwadesturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani. 10

Watu, umati mkubwa, walikuwawamekusanyika nje wanasali wakati huo wakufukiza ubani. 11 Malaika wa Bwanaakamtokea humo ndani, akasimama upandewa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani. 12

Zakariya alipomwona alifadhaika, hofuikamwingia. 13 Lakini malaika akamwambia,“Zakariya, usiogope, kwa maana sala yakoimesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzaliamtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane. 14

Utakuwa na furaha kubwa na watu wengiwatashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake.15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana.Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa RohoMtakatifu tangu tumboni mwa mama yake. 16

Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwaBwana Mungu wao. 17 Atamtangulia Bwanaakiongozwa na nguvu na roho kama Eliya.Atawapatanisha kina baba na watoto wao;atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu,na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.” 18

Zakariya akamwambia huyo malaika, “Ni kitugani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi nimzee, hali kadhalika na mke wangu.” 19

Malaika akamjibu, “Mimi ni Gabrieli,nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwaniseme nawe, nikuletee hii habari njema. 20

Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadikihaya maneno yatakayotimia kwa wakati wake.

Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambiayatakapotimia.” 21 Wakati huo, wale watuwalikuwa wanamngoja Zakariya hukuwakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.22 Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawadhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maonoHekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwamikono, akabaki bubu. 23 Zamu yake yakuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani. 24

Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba.Akajificha nyumbani kwa muda wa miezimitano, akisema: 25 “Hivi ndivyoalivyonitendea Bwana; ameniangalia nakuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele yawatu.” 26 Mnamo mwezi wa sita, malaikaGabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mjiuitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwamsichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wamtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo waDaudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia,“Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi!Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikiamaneno hayo alifadhaika sana, akawaza:maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaikaakamwambia, “Usiogope Maria, kwa maanaMungu amekujalia neema. 31 Utachukuamimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampajina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwaMwana wa Mungu Mkuu. Bwana Munguatampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33

Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele,na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34

Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, halimimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “RohoMtakatifu atakushukia, na uwezo wake MunguMkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo,mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwanawa Mungu. 36 Ujue pia kwamba hata Elisabeti,jamaa yako, naye amepata mimba ingawa nimzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeyeambaye watu walimfahamu kuwa tasa. 37 Kwamaana hakuna jambo lisilowezekana kwaMungu.” 38 Maria akasema, “Mimi ni mtumishiwa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kishayule malaika akaenda zake. 39 Siku kadhaabaadaye, Maria alifunga safari akaenda kwaharaka hadi mji mmoja ulioko katika milima yaYuda. 40 Huko, aliingia katika nyumba yaZakariya, akamsalimu Elisabeti. 41 Mara tuElisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtotomchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka.Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifiu, 42

akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa

LUKA MTAKATIFU 1:42

43

Page 44: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

2

kuliko wanawake wote, naye utakayemzaaamebarikiwa. 43 Mimi ni nani hata mama waBwana wangu afike kwangu? 44 Nakwambia,mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchangatumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45 Heriyako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yaleBwana aliyokwambia.” 46 Naye Mariaakasema, 47 “Moyo wangu wamtukuza Bwana,roho yangu inafurahi kwa sababu ya MunguMwokozi wangu. 48 Kwa kuwa amemwangaliakwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu.Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenyeheri. 49 Kwa kuwa Mwenyezi Munguamenitendea makuu, jina lake ni takatifu. 50

Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumukizazi hata kizazi. 51 Amefanya mambo makuukwa mkono wake: amewatawanya wenyekiburi katika mawazo ya mioyo yao; 52

amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyaovya enzi, akawakweza wanyenyekevu. 53

Wenye njaa amewashibisha mema, matajiriamewaacha waende mikono mitupu. 54

Amemsaidia Israeli mtumishi wake,akikumbuka huruma yake. 55 Kamaalivyowaahidia wazee wetu Abrahamu nawazawa wake hata milele.” 56 Maria alikaa naElisabeti kwa muda upatao miezi mitatu,halafu akarudi nyumbani kwake. 57 Wakati wakujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifunguamtoto wa kiume. 58 Jirani na watu wa jamaayake walipopata habari kwamba Bwanaamemwonea huruma kubwa, walifurahipamoja naye. 59 Halafu siku ya nane walifikakumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la babayake, Zakariya. 60 Lakini mama yake akasema,“La, sivyo, bali ataitwa Yohane.” 61

Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katikaukoo wake mwenye jina hilo?” 62 Basi,wakamwashiria baba yake wapate kujuaalitaka mtoto wake apewe jina gani. 63 Nayeakaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi:“Yohane ndilo jina lake.” Wote wakastaajabu.64 Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariyavikafunguliwa, akawa anaongea akimsifuMungu. 65 Hofu ikawaingia jirani wote, nahabari hizo zikaenea kila mahali katika milimaya Yudea. 66 Wote waliosikia mambo hayowaliyatafakari mioyoni mwao wakisema:“Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?”Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamojanaye. 67 Zakariya, baba yake mtoto, akajazwaRoho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu:68 “Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwaniamekuja kuwasaidia na kuwakomboa watuwake. 69 Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawawa Daudi mtumishi wake. 70 Aliahidi hapo kalekwa njia ya manabii wake watakatifu, 71

kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetuna kutoka mikononi mwa wotewanaotuchukia. 72 Alisema atawahurumiawazee wetu, na kukumbuka agano laketakatifu. 73 Kiapo alichomwapia Abrahamubaba yetu, ni kwamba atatujalia sisi 74

tukombolewe kutoka adui zetu, tupatekumtumikia bila hofu, 75 kwa unyofu nauadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.76 Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa MunguMkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njiayake; 77 kuwatangazia watu kwambawataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao. 78

Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma.Atasababisha pambazuko angavu la ukombozilitujie kutoka juu, 79 na kuwaangazia wotewanaokaa katika giza kuu la kifo, aongozehatua zetu katika njia ya amani.” 80 Mtotoakakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwanimpaka alipojionyesha rasmi kwa watu waIsraeli.

Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa naKaisari Augusto kuwataka watu wotechini ya utawala wake wajiandikishe. 2

Kuandikishwa huku kulikuwa mara ya kwanza,wakati Kirenio alipokuwa mkuu wa mkoa waSiria. 3 Basi, wote waliohusika walikwendakujiandikisha, kila mtu katika mji wake. 4

Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazaretimkoani Galilaya. Kwa kuwa alikuwa wa jamaana ukoo wa Daudi alikwenda mjini Bethlehemumkoani Yuda alikozaliwa Mfalme Daudi. 5

Alikwenda kujiandikisha pamoja na mchumbawake Maria ambaye alikuwa mja mzito. 6

Walipokuwa huko, siku yake ya kujifunguaikawadia, 7 akajifungua mtoto wake wakwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto,akamlaza horini kwa sababu hawakupatanafasi katika nyumba ya wageni. 8 Katikasehemu hizo, walikuwako wachungajiwakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, nautukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote.Wakaogopa sana. 10 Malaika akawaambia,“Msiogope! Nimewaleteeni habari njema yafuraha kuu kwa watu wote. 11 Kwa maana, leohii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozikwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana. 12 Na hikikitakuwa kitambulisho kwenu: mtamkutamtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto,amelazwa horini.” 13 Mara kundi kubwa lajeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika,wakamsifu Mungu wakisema: 14 “Utukufu kwaMungu juu mbinguni, na amani duniani kwawatu aliopendezwa nao!” 15 Baada ya haomalaika kuondoka na kurudi mbinguni,wachungaji wakaambiana: “Twendeni mojakwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukiohili Bwana alilotujulisha.” 16 Basi, wakaendambio, wakamkuta Maria na Yosefu na yulemtoto mchanga amelazwa horini. 17 Haowachungaji walipomwona mtoto huyowakawajulisha wote habari waliyokuwawamesikia juu yake. 18 Wote waliosikia hayowalishangaa juu ya habari walizoambiwa nawachungaji. 19 Lakini Maria aliyaweka nakuyatafakari mambo hayo yote moyonimwake. 20 Wale wachungaji walirudi makwaohuku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa

LUKA MTAKATIFU 1:43

44

Page 45: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yoteyalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa. 21

Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtotoulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambaloalikuwa amepewa na malaika kablahajachukuliwa mimba. 22 Siku zilipotimia zaYosefu na Maria kutakaswa kamawalivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi haowalimchukua mtoto, wakaenda nayeYerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana. 23

Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: “Kilamzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfukwa Bwana.” 24 Pia walikwenda ili watoesadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa,kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana. 25

Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtummoja, mwema na mcha Mungu, jina lakeSimeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamuukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwapamoja naye. 26 Roho Mtakatifu alikuwaamemhakikishia kwamba hatakufa kabla yakumwona Masiha wa Bwana. 27 Basi,akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeonialiingia Hekaluni; na wazazi wa Yesuwalipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyiekama ilivyotakiwa na Sheria, 28 Simeonialimpokea mtoto Yesu mikononi mwake hukuakimtukuza Mungu na kusema: 29 “SasaBwana, umetimiza ahadi yako, wawezakumruhusu mtumishi wako aende kwa amani.30 Maana kwa macho yangu nimeuonawokovu utokao kwako, 31 ambaoumeutayarisha mbele ya watu wote: 32

Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa,na utukufu kwa watu wako Israeli.” 33 Baba namama yake Yesu walikuwa wakistaajabiamaneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. 34

Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu yakupotea na kuokoka kwa watu wengi katikaIsraeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa nawatu; 35 na hivyo mawazo ya watu wengiyataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchunguulio kama upanga mkali utauchoma moyowako.” 36 Palikuwa na nabii mmojamwanamke, mzee sana, jina lake Ana, bintiFanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishina mumewe kwa miaka saba tangualipoolewa. 37 Halafu alibaki mjane hadiwakati huo akiwa mzee wa miaka themanini naminne. Wakati huo wote alikaa Hekaluniakifunga na kusali usiku na mchana. 38 Saahiyohiyo alijitokeza mbele, akamshukuruMungu, na akaeleza habari za huyo mtoto kwawatu wote waliokuwa wanatazamia ukomboziwa Yerusalemu. 39 Hao wazazi walipokwishafanya yote yaliyoamriwa na Sheria ya Bwana,walirudi makwao Nazareti, mkoani Galilaya. 40

Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaahekima, na neema ya Mungu ilikuwa pamojanaye. 41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturiya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wasikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na

umri wa miaka kumi na miwili, wotewalikwenda kwenye sikukuu hiyo kamailivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu,walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesualibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa nahabari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundila wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa,halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwajamaa na marafiki. 45 Kwa kuwahawakumwona, walirudi Yerusalemuwakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkutaHekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza nakuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia manenoyake walistaajabia akili yake na majibu yake yahekima. 48 Wazazi wake walipomwonawalishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza,“Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Babayako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwahuzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa ninimlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasakuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakiniwazazi wake hawakuelewa maana ya manenoaliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja naohadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yakeakaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52

Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima nakimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.

Mwaka wa kumi na tano wa utawala waKaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwaanatawala mkoa wa Yudea. Herode

alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo,ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Itureana Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoawa Abilene, 2 na Anasi na Kayafa walikuwamakuhani wakuu mjini Yerusalem. Wakati huondipo neno la Mungu lilipomjia Yohane,mwana wa Zakariya, kule jangwani. 3 Basi,Yohane akaenda katika sehemu zotezilizopakana na mto Yordani, akihubiri watuwatubu na kubatizwa ili Mungu awaondoleedhambi. 4 Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabucha nabii Isaya: “Sauti ya mtu imesikikajangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake;nyosheni mapito yake. 5 Kila bonde litafukiwa,kila mlima na kilima vitasawazishwa;palipopindika patanyooshwa, njia mbayazitatengenezwa. 6 Na, watu wote watauonawokovu utokao kwa Mungu.” 7 Basi, Yohaneakawa anawaambia watu wengi waliofika iliawabatize: “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nanialiyewadokezea kwamba mngeweza kuiepukaghadhabu inayokuja? 8 Basi, onyesheni kwamatendo kwamba mmetubu. Msianze sasakusema: Sisi ni watoto wa Abrahamu.Nawaambieni hakika, Mungu anawezakuyageuza mawe haya yawe watoto waAbrahamu! 9 Lakini, sasa hivi shokalimewekwa tayari kukata mizizi ya miti. Kila mtiusiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwamotoni.” 10 Umati wa watu ukamwuliza,“Tufanye nini basi?” 11 Akawajibu, “Aliye nanguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliyena chakula afanye vivyo hivyo.” 12 Nao watoza

LUKA MTAKATIFU 3:12

45

Page 46: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza,“Mwalimu, tufanye nini?” 13 Naye akawaambia,“Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa.”14 Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanyenini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vyamtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyotekwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.” 15

Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi,wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusuYohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo. 16 HapoYohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatizakwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo zaidikuliko mimi ambaye sistahili hata kumfunguliakamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwaRoho Mtakatifu na kwa moto. 17 Yeye ni kamamtu anayeshika mikononi mwake chombo chakupuria nafaka, aipure nafaka yake, akusanyengano ghalani mwake, na makapi ayachomekwa moto usiozimika.” 18 Hivyo, pamoja namawaidha mengine mengi, Yohanealiwahimiza watu akiwahubiria Habari Njema.19 Lakini Yohane alimgombeza Herode, mkuuwa mkoa, kwa sababu alikuwa amemchukuaHerodia, mke wa ndugu yake, na kumfanyamke wake; na pia kwa ajili ya mabaya yotealiyokuwa amefanya. 20 Kisha Herodeakazidisha ubaya wake kwa kumtia Yohanegerezani. 21 Watu wote walipokuwawamekwisha batizwa, Yesu naye alibatizwa. Naalipokuwa akisali, mbingu zilifunguka, 22 naRoho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbokama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni:“Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa,nimependezwa nawe.” 23 Yesu alipoanza kaziyake hadharani, alikuwa na umri upatao miakathelathini, na watu walidhani yeye ni mwanawa Yosefu, mwana wa Heli. 24 Heli alikuwamwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwanawa Melki, mwana wa Yanai, mwana wa Yosefu,25 mwana wa Matathia, mwana wa Amosi,mwana wa Nahumu, mwana wa Hesli, mwanawa Nagai, 26 mwana wa Maathi, mwana waMatathia, mwana wa Shemeni, mwana waYoseki, mwana wa Yuda, 27 mwana waYohanani, mwana wa Resa, mwana waZerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana waNeri, 28 mwana wa Melki, mwana wa Adi,mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu,mwana wa Eri, 29 mwana wa Yoshua, mwanawa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana waMathati, mwana wa Lawi, 30 mwana waSimeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yosefu,mwana wa Yonamu, mwana wa Eliakimu, 31

mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwanawa Matatha, mwana wa Nathani, mwana waDaudi, 32 mwana wa Yese, mwana wa Obedi,mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwanawa Nashoni, 33 mwana wa Aminadabu,mwana wa Admini, mwana wa Arni, mwana waHesroni, mwana wa Feresi, mwana wa Yuda,34 mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka,mwana wa Abrahamu, mwana wa Tera, mwanawa Nahori, 35 mwana wa Serugi, mwana wa

Reu, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi,mwana wa Sala, 36 mwana wa Kainani, mwanawa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana waNoa, mwana wa Lameki, 37 mwana waMathusala, mwana wa Henoki, mwana waYaredi, mwana wa Mahalaleli, mwana waKenani, 38 mwana wa Enosi, mwana wa Sethi,mwana wa Adamu, aliyekuwa wa Mungu.

Yesu alitoka katika mto Yordani akiwaamejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa naRoho mpaka jangwani. 2 Huko

alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa sikuarubaini. Wakati huo wote hakula chochote, nabaada ya siku hizo akasikia njaa. 3 Ndipo Ibilisiakamwambia, “Kama wewe ni Mwana waMungu, amuru jiwe hili liwe mkate.” 4 Yesuakamjibu, “Imeandikwa: Mtu haishi kwa mkatetu.” 5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pajuu, akamwonyesha kwa mara moja falme zoteza ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia, 6

“Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi nafahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote;nikitaka kumpa mtu ninaweza. 7 Hivi vyotevitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.”8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: UtamwabuduBwana Mungu wako, na utamtumikia yeyepeke yake.” 9 Ibilisi akamchukua mpakaYerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu,akamwambia, “Kama wewe ni Mwana waMungu, 10 kwa maana imeandikwa:Atawaamuru malaika wake wakulinde, 11 natena, Watakuchukua mikononi mwao usijeukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.” 12 LakiniYesu akamjibu, “Imeandikwa: UsimjaribuBwana Mungu wako.” 13 Ibilisialipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwachakwa muda. 14 Yesu alirudi Galilaya akiwaamejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habarizake zikaenea katika sehemu zote za jirani. 15

Naye akawa anawafundisha watu katikamasunagogi yao, akasifiwa na wote. 16 Basi,Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa,na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi,kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama iliasome Maandiko Matakatifu kwa sauti. 17

Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifunguana akakuta mahali palipoandikwa: 18 “Roho waBwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafutaniwahubirie maskini Habari Njema.Amenituma niwatangazie mateka watapatauhuru, vipofu watapata kuona tena;amenituma niwakomboe wanaoonewa, 19 nakutangaza mwaka wa neema ya Bwana.” 20

Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu,akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wotewakamkodolea macho. 21 Naye akaanzakuwaambia, “Andiko hili mlilosikia likisomwa,limetimia leo.” 22 Wote wakavutiwa sana naye,wakastaajabia maneno mazuri aliyosema.Wakanena, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?” 23

Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambiamsemo huu: Mganga jiponye mwenyewe, napia mtasema: Yote tuliyosikia umeyafanya kule

LUKA MTAKATIFU 3:13

46

Page 47: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijijichako.” 24 Akaendelea kusema, “Hakikanawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijijichake. 25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa nawajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati zaEliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwamuda wa miaka mitatu na nusu; kukawa nanjaa kubwa katika nchi yote. 26 Hata hivyo,Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwamwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni. 27 Tena,katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwana wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakunayeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyejiwa Siria.” 28 Wote waliokuwa katika lilesunagogi waliposikia hayo walikasirika sana.29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji waouliokuwa umejengwa juu ya kilima,wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilimahicho ili wamtupe chini. 30 Lakini Yesu akapitakatikati yao, akaenda zake. 31 Kisha Yesuakashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa waGalilaya, akawa anawafundisha watu siku yaSabato. 32 Wakastaajabia uwezo aliokuwa naokatika kufundisha. 33 Na katika lile sunagogikulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa naroho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wakuziba masikio: 34 “We! Yesu wa Nazareti! Kwanini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza?Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbeMtakatifu wa Mungu!” 35 Lakini Yesuakamkemea huyo pepo akisema: “Nyamaza!Mtoke mtu huyu!” Basi, huyo pepo baada yakumwangusha yule mtu chini, akamtoka bilakumdhuru hata kidogo. 36 Watu wotewakashangaa, wakawa wanaambiana, “Hili nijambo la ajabu, maana kwa uwezo na nguvuanawaamuru pepo wachafu watoke, naowanatoka!” 37 Habari zake zikaenea mahalipote katika mkoa ule. 38 Yesu alitoka katika lilesunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni.Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa nahoma kali; wakamwomba amponye. 39 Yesuakaenda akasimama karibu naye, akaikemeaile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mamaakainuka, akawatumikia. 40 Jua lilipokuwalinatua, wote waliokuwa na wagonjwa waombalimbali waliwaleta kwake; naye akawekamikono yake juu ya kila mmoja wao,akawaponya wote. 41 Pepo waliwatoka watuwengi, wakapiga kelele wakisema: “Wewe uMwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea,wala hakuwaruhusu kusema, maanawalimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo. 42

Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaendamahali pa faragha. Watu wakawawanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa,wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao. 43

Lakini yeye akawaambia, “Ninapaswa kuhubiriHabari Njema za Ufalme wa Mungu katika mijimingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo.”44 Akawa anahubiri katika masunagogi yaYudea.

Siku moja Yesu alikuwa amesimamakando ya ziwa Genesareti, na watuwengi walikuwa wamemzunguka

wakisongana wanalisikiliza neno la Mungu. 2

Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa;wavuvi wenyewe walikuwa wametoka,wanaosha nyavu zao. 3 Baada ya Yesu kuingiakatika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni,alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogona ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umatiwa watu akiwa ndani ya mashua. 4 Alipomalizakufundisha, akamwambia Simoni, “Pelekamashua mpaka kilindini, mkatupe nyavu zenumpate kuvua samaki.” 5 Simoni akamjibu,“Bwana, tumejitahidi kuvua samaki usikukucha bila kupata kitu, lakini kwa kuwaumesema, nitatupa nyavu.” 6 Baada yakufanya hivyo, wakavua samaki wengi, hatanyavu zao zikaanza kukatika. 7 Wakawaitawenzao waliokuwa katika mashua nyinginewaje kuwasaidia. Wakaja, wakazijaza mashuazote mbili samaki, hata karibu zingezama. 8

Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magotimbele ya Yesu akisema, “Ondoka mbele yangu,ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenyedhambi!” 9 Simoni pamoja na wenzake wotewalishangaa kwa kupata samaki wengi vile. 10

Hali kadhalika Yakobo na Yohane, wana waZebedayo, waliokuwa wavuvi wenzake Simoni.Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangusasa utakuwa ukivua watu.” 11 Basi, baada yakuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa,wakaacha yote, wakamfuata. 12 Ikawa, Yesualipokuwa katika mmojawapo wa miji ya huko,mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzimaakamwona. Basi, mtu huyo akaangukakifudifudi akamwomba Yesu: “Mheshimiwa,ukitaka, waweza kunitakasa.” 13 Yesuakaunyosha mkono wake, akamgusa nakusema, “Nataka, takasika!” Mara ule ukomaukamwacha. 14 Yesu akamwamuru:“Usimwambie mtu yeyote; bali nendaukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwaajili ya kutakasika kwako kama inavyotakiwa naSheria ya Mose, iwe uthibitisho kwao kwambaumepona.” 15 Lakini habari za Yesu zilizidikuenea kila mahali. Watu makundi mengiwakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywamagonjwa yao. 16 Lakini yeye alikwenda zakemahali pasipo na watu, akawa anasali huko. 17

Siku moja Yesu alikuwa akifundisha.Mafarisayo na walimu wa Sheria kutoka katikakila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu,walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwanailikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponyeawagonjwa. 18 Mara watu wakajawamemchukua mtu mmoja aliyepoozamaungo, amelala kitandani; wakajaribukumwingiza ndani wamweke mbele ya Yesu.19 Lakini kwa sababu ya wingi wa watu,hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapandajuu ya dari, wakaondoa vigae, wakamshushahuyo aliyepooza pamoja na kitanda chake,

LUKA MTAKATIFU 5:19

47

Page 48: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

wakamweka mbele ya Yesu. 20 Yesu alipoonajinsi walivyokuwa na imani kubwa,akamwambia huyo mtu, “Rafiki,umesamehewa dhambi zako.” 21 Walimu waSheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nanihuyu anayemkufuru Mungu kwa manenoyake? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambiila Mungu peke yake!” 22 Yesu alitambuamawazo yao, akawauliza, “Mnawaza ninimioyoni mwenu? 23 Ni lipi lililo rahisi zaidi:kusema, Umesamehewa dhambi, au kusema,Simama utembee? 24 Basi, nataka mjuekwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wakusamehe dhambi duniani.” Hapoakamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama,chukua kitanda chako uende zako nyumbani.”25 Mara, huyo mtu aliyepooza akasimamambele yao wote, akachukua kitanda chakeakaenda zake nyumbani huku akimtukuzaMungu. 26 Wote wakashangaa na kushikwa nahofu; wakamtukuza Mungu wakisema:“Tumeona maajabu leo.” 27 Baada ya hayo,Yesu akatoka nje, akamwona mtoza ushurummoja aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesuakamwambia, “Nifuate!” 28 Lawi akaacha yote,akamfuata. 29 Kisha Lawi akamwandalia Yesukaramu kubwa nyumbani mwake; na kundikubwa la watoza ushuru na watu wenginewalikuwa wameketi pamoja nao. 30

Mafarisayo na walimu wa Sheriawakawanung'unikia wafuasi wake wakisema:“Mbona mnakula na kunywa pamoja nawatoza ushuru na wenye dhambi?” 31 Yesuakawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari,lakini wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. 32

Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi,ili wapate kutubu.” 33 Watu wenginewakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohanembatizaji hufunga mara nyingi na kusali; hatawafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo.Lakini wafuasi wako hula na kunywa.” 34 Yesuakawajibu, “Je, mnaweza kuwataka walewalioalikwa arusini wafunge hali bwana arusiyuko pamoja nao? 35 Lakini wakati utafikaambapo bwana arusi ataondolewa kati yao, nawakati huo ndipo watakapofunga.” 36 Yesuakawaambia mfano huu: “Hakuna mtu akatayekiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazikuukuu; kama akifanya hivyo, atakuwaamelikata hilo vazi jipya, na hicho kirakahakitachukuana na hilo vazi kuukuu. 37 Walahakuna mtu atiaye divai mpya katika viribavikuukuu; kwani hiyo divai mpya itavipasuahivyo viriba, divai itamwagika, na viribavitaharibika. 38 Divai mpya hutiwa katika viribavipya! 39 Wala hakuna mtu ambaye hutamanikunywa divai mpya baada ya kunywa yazamani, kwani husema: Ile ya zamani ni nzurizaidi.”

Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwaanapita katika mashamba ya ngano, nawanafunzi wake wakaanza kukwanyua

masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa

mikono, wakala. 2 Baadhi ya Mafarisayowakawauliza, “Mbona mnafanya jambo ambalosi halali siku ya Sabato?” 3 Yesu akawajibu, “Je,hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja nawenzake wakati walipokuwa na njaa? 4 Yeyealiingia ndani ya nyumba ya Mungu,akachukua ile mikate iliyowekwa mbele yaMungu, akala na kuwapa wenzake. Kisheria, nimakuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kulamikate hiyo.” 5 Hivyo akawaambia, “Mwana waMtu ni Bwana wa Sabato.” 6 Siku nyingine yaSabato, Yesu aliingia katika sunagogi,akafundisha. Mle ndani mlikuwa na mtuambaye mkono wake wa kuume ulikuwaumepooza. 7 Walimu wa Sheria na Mafarisayowalitaka kupata kisingizio cha kumshtaki Yesuna hivyo wakawa wanangojea waone kamaangemponya mtu siku ya Sabato. 8 Lakini Yesualijua mawazo yao, akamwambia yule mwenyemkono uliopooza, “Inuka, simama katikati.”Yule mtu akaenda akasimama katikati. 9 KishaYesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halalisiku ya Sabato kutenda jambo jema aukutenda jambo baya; kuokoa maisha aukuyaangamiza?” 10 Baada ya kuwatazamawote waliokuwa pale, akamwambia yule mtu,“Nyosha mkono wako.” Naye akafanya hivyo,na mkono wake ukawa mzima tena. 11 Lakiniwao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi yakumtendea Yesu maovu. 12 Siku moja Yesualikwenda mlimani kusali, akakesha hukousiku kucha akimwomba Mungu. 13 Keshoyake aliwaita wanafunzi wake, na miongonimwao akachagua kumi na wawili ambaoaliwaita mitume: 14 Simoni (ambaye Yesualimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake,Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo, 15

Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo naSimoni (aliyeitwa Zelote), 16 Yuda wa Yakobona Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwamsaliti. 17 Baada ya kushuka mlimani pamojana mitume, Yesu alisimama mahali palipokuwatambarare. Hapo palikuwa na kundi kubwa lawanafunzi wake na umati wa watu waliotokapande zote za Yudea na Yerusalemu na pwaniya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikilizaYesu na kuponywa magonjwa yao. 18

Aliwaponya pia wote waliokuwawanasumbuliwa na pepo wachafu. 19 Watuwote walitaka kumgusa, kwa maana nguvuilikuwa inatoka ndani yake na kuwaponyawote. 20 Yesu akawageukia wanafunzi wake,akasema: “Heri ninyi mlio maskini, maanaUfalme wa Mungu ni wenu. 21 Heri ninyimnaosikia njaa sasa, maana baadayemtashiba. Heri ninyi mnaolia sasa, maanabaadaye mtacheka kwa furaha. 22 “Heri yenuninyi iwapo watu watawachukia, watawatenga,watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajiliya Mwana wa Mtu! 23 Wakati hayoyatakapotokea, furahini na kucheza, maanahakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwamaana wazee wao waliwatendea manabii vivyo

LUKA MTAKATIFU 5:20

48

Page 49: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

7

hivyo. 24 Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri,maana mmekwisha pata faraja yenu. 25 Olewenu ninyi mnaoshiba sasa, maana baadayemtasikia njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka kwafuraha sasa, maana baadaye mtaomboleza nakulia. 26 Ole wenu ninyi iwapo watu wotewanawasifu, maana wazee wao waliwafanyiamanabii wa uongo vivyo hivyo. 27 “Lakininawaambieni ninyi mnaonisikiliza: wapendeniadui zenu, watendeeni mema walewanaowachukieni. 28 Watakieni baraka walewanaowalaani, na waombeeni walewanaowatendea vibaya. 29 Mtu akikupigashavu moja mgeuzie na la pili. Mtuakikunyang'anya koti lako mwachie pia shatilako. 30 Yeyote anayekuomba mpe, na mtuakikunyang'anya mali yako usimtakeakurudishie. 31 Watendeeni wengine kamamnavyotaka wawatendee ninyi. 32 “Na ikiwamnawapenda tu wale wanaowapenda ninyi, je,mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hatawenye dhambi huwapenda walewanaowapenda wao. 33 Tena, kamamkiwatendea mema wale tuwanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani?Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo! 34 Nakama mnawakopesha wale tu mnaotumainiwatawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hatawenye dhambi huwakopesha wenye dhambiwenzao ili warudishiwe kima kilekile! 35 Ilanyinyi wapendeni adui zenu, na kuwatendeamema; kopesheni bila kutazamia malipo, natuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwawatoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeyeni mwema kwa wale wasio na shukrani nawalio wabaya. 36 Muwe na huruma kama Babayenu alivyo na huruma. 37 “Msiwahukumuwengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumuwengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheniwengine, nanyi mtasamehewa. 38 Wapeniwengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam,mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa,kikashindiliwa na kusukwasukwa hatakumwagika. Kwa maana kipimo kilekilemnachotumia kwa wengine ndicho ambachoMungu atatumia kwenu.” 39 Akawaambiamfano huu: “Je, kipofu anaweza kumwongozakipofu mwenzake? La! Wote wataangukashimoni. 40 Mwanafunzi hamshindi mwalimuwake, lakini kila mwanafunzi akisha hitimuhuwa kama mwalimu wake. 41 Unawezajekukiona kibanzi kilicho katika jicho la mwenzio,usione boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe?42 Au, unawezaje kumwambia mwenzako,Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicholako, na huku huioni boriti iliyoko katika jicholako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanzaboriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaonasawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzikilicho katika jicho la ndugu yako. 43 “Mtimwema hauzai matunda mabaya, wala mtimbaya hauzai matunda mazuri. 44 Watuhuutambua mti kutokana na matunda yake. Ni

wazi kwamba watu hawachumi tini katikamichongoma, wala hawachumi zabibu katikambigili. 45 Mtu mwema hutoa yaliyo memakutoka katika hazina bora iliyo moyoni mwake;na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya katikahazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maanamtu huongea kutokana na yale yaliyojaamoyoni mwake. 46 “Mbona mwaniita Bwana,Bwana, na huku hamtimizi yale ninayosema?47 Nitawapeni mfano unaofaa kuonyeshaalivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikiamaneno yangu na kuyatimiza: 48 Huyoanafanana na mtu ajengaye nyumba, ambayeamechimba chini na kuweka msingi wake juuya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto,mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakinihaukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwaimejengwa imara. 49 Lakini yeyote anayesikiamaneno yangu lakini asifanye chochote, huyoanafanana na mtu aliyejenga nyumba juu yaudongo, bila msingi. Mafuriko ya mtoyakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumbaile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”

Baada ya kusema yale aliyotaka watuwasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu. 2

Huko kulikuwa na jemadari mmojaMroma ambaye alikuwa na mtumishi wakealiyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwamgonjwa karibu kufa. 3 Yule jemadarialiposikia habari za Yesu, aliwatuma wazeefulani Wayahudi waende kumwomba ajeamponye mtumishi wake. 4 Walipofika kwaYesu, walimsihi sana, wakasema: “Huyuanastahili afanyiwe jambo hilo, 5 maanaanalipenda taifa letu, na ndiye aliyetujengealile sunagogi.” 6 Basi, Yesu akaenda pamojanao. Alipokuwa karibu kufika nyumbani kwayule jemadari Mroma, yule jemadari aliwatumamarafiki zake wamwambie Yesu: “Bwana,usijisumbue zaidi, maana mimi sistahili uingienyumbani mwangu. 7 Ndio maana sikujionanastahili hata kuja kwako; amuru tu, namtumishi wangu atapona. 8 Mimi pia ni mtuniliye chini ya mamlaka, na ninao askari chiniyangu. Namwambia mmoja, Nenda!, nayehuenda; namwambia mwingine, Njoo! nayehuja; na nikimwambia mtumishi wangu, Fanyahiki!, hufanya.” 9 Yesu aliposikia hayo,alishangaa; halafu akauelekea ule umati wawatu uliokuwa unamfuata, akasema, “Sijaonaimani kubwa namna hii hata katika Israeli.” 10

Wale watu walipowasili nyumbani walimkutayule mtumishi hajambo kabisa. 11 Baadayekidogo Yesu alikwenda katika mji mmojauitwao Naini, na wafuasi wake pamoja nakundi kubwa la watu waliandamana naye. 12

Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji,walitokea watu wamebeba maiti ya kijanammoja, mtoto wa pekee wa mama mjane.Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja nahuyo mama. 13 Bwana alipomwona mamahuyo, alimwonea huruma, akamwambia,“Usilie.” 14 Kisha akaenda, akaligusa lile jeneza,

LUKA MTAKATIFU 7:14

49

Page 50: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

na wale waliokuwa wanalichukuawakasimama. Halafu akasema, “Kijana!Nakuamuru, amka!” 15 Yule aliyekufa akaketi,akaanza kuongea. Na Yesu akamkabidhi kwamama yake. 16 Watu wote walishikwa na hofu,wakawa wanamtukuza Mungu wakisema:“Nabii mkuu ametokea kati yetu. Munguamekuja kuwakomboa watu wake.” 17 Habarihizo zikaenea kote katika Uyahudi na katikanchi za jirani. 18 Wanafunzi wa Yohanewalimpa habari Yohane juu ya mambo hayoyote. Naye Yohane, baada ya kuwaita wawilikati ya wanafunzi wake, 19 aliwatuma kwaBwana wamwulize: “Wewe ndiye yule ajaye, autumtazamie mwingine?” 20 Wale wanafunziwalipomfikia Yesu wakamwambia, “YohaneMbatizaji ametutuma kwako tukuulize: Wewendiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”21 Wakati huohuo, Yesu alikuwa anawaponyawatu wengi waliokuwa wanateseka kwamagonjwa na waliopagawa na pepo wabaya,akawawezesha vipofu wengi kuona tena. 22

Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambieYohane yale mliyojionea na kuyasikia: vipofuwanaona, viwete wanatembea, wenye ukomawanatakaswa, viziwi wanasikia, wafuwanafufuliwa, na maskini wanahubiriwaHabari njema. 23 Heri mtu yule ambaye hanamashaka nami!” 24 Hapo wajumbe wa Yohanewalipokwisha kwenda zao, Yesu alianzakuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane:“Mlikwenda kule jangwani, hivi mlitaka kuonakitu gani? Mlitaka kuona unyasi unaotikiswa naupepo? 25 Basi, mlikwenda kuona nini?Mlikwenda kumwona mtu aliyevalia mavazimaridadi? La hasha! Wanaovaa mavazimaridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaakatika majumba ya wafalme! 26 Basi,niambieni, mlikwenda kuona nini? Mlikwendakumwona nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii.27 Huyu Yohane ndiye anayesemwa katikaMaandiko Matakatifu: Hapa ni mtumishiwangu, asema Bwana; ninamtumaakutangulie, akutayarishie njia.” 28 Yesuakamalizia kwa kusema, “Nawaambieni, kati yabinadamu wote hakuna aliye mkubwa zaidikuliko Yohane Mbatizaji. Hata hivyo, yule aliyemdogo kabisa katika ufalme wa Mungu nimkubwa zaidi kuliko yeye.” 29 Waliposikia hayowatu wote na watoza ushuru waliusifu wemawa Mungu; hao ndio wale waliokuwawameupokea ubatizo wa Yohane. 30 LakiniMafarisayo na walimu wa Sheria walikataampango wa Mungu uliowahusu wakakataakubatizwa na Yohane. 31 Yesu akaendeleakusema, “Basi, nitawafananisha watu wa kizazihiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani? 32

Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni nakuambiana, kikundi kimoja na kingine:Tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza!Tumeomboleza, lakini hamkulia! 33 Kwamaana Yohane alikuja, yeye alifunga nahakunywa divai, nanyi mkasema: Amepagawa

na pepo! 34 Akaja Mwana wa Mtu; anakula nakunywa, mkasema: Mwangalieni mlafi huyu namlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenyedhambi! 35 Hata hivyo, hekima ya Munguimethibitishwa kuwa njema na wote walewanaoikubali.” 36 Mfarisayo mmoja alimwalikaYesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingianyumbani mwa huyo Mfarisayo, akakaa kulachakula. 37 Basi, katika mji ule kulikuwa namama mmoja aliyekuwa anaishi maishamabaya. Alipopata habari kwamba Yesu yukonyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukuachupa ya alabasta yenye marashi. 38 Akaja,akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia,na machozi yake yakamdondokea Yesumiguuni. Huyo mwanamke akaipangusamiguu ya Yesu kwa nywele zake. Kishaakaibusu na kuipaka yale marashi. 39 YuleMfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo,akawaza moyoni mwake, “Kama mtu huyuangekuwa kweli nabii angejua huyumwanamke ni wa namna gani, ya kwamba nimwenye dhambi.” 40 Yesu akamwambia huyoMfarisayo, “Simoni, ninacho kitu chakukwambia.” Naye Simoni akamwambia, “NdioMwalimu, sema.” Yesu akasema, 41 “Watuwawili walikuwa wamemkopa mtu fedha:mmoja alikuwa amekopa dinari mia tano, namwingine hamsini. 42 Waliposhindwa kulipamadeni yao, huyo mtu aliwasamehe wotewawili. Sasa ni yupi kati ya hao wawiliatampenda zaidi huyo bwana?” 43 Simoniakamjibu, “Ni dhahiri kwamba yulealiyesamehewa deni kubwa zaidi atampendazaidi yule bwana.” Yesu akamwambia, “Sawa.”44 Halafu akamgeukia yule mwanamke nakumwambia Simoni, “Unamwona huyumwanamke, sivyo? Basi, mimi nilipoingia hapanyumbani kwako hukunipa maji ya kunawamiguu yangu; lakini mwanamke huyuameniosha miguu yangu kwa machozi yake nakunipangusa kwa nywele zake. 45 Wewehukunisalimu kwa kunibusu, lakini huyumwanamke tangu nilipoingia hapa amekuwaakiibusu miguu yangu. 46 Wewehukunionyesha ukarimu wako kwa kunipakamafuta kichwani, lakini huyu mwanamkeamefanya hivyo kwa kunipaka mafuta miguuyangu. 47 Kwa hiyo nakwambia amesamehewadhambi zake nyingi kwa kuwa ameonyeshaupendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo,hupenda kidogo.” 48 Basi, Yesu akamwambiayule mwanamke, “Umesamehewa dhambizako.” 49 Na hapo wale waliokuwa pamojanaye mezani wakaulizana, “Ni mtu wa namnagani huyu awezaye kusamehe dhambi?” 50

Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,“Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”

Baada ya hayo, Yesu alipitia katika mijina vijiji akitangaza Habari Njema zaUfalme wa Mungu. Wale kumi na wawili

waliandamana naye. 2 Pia wanawake kadhaaambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya

LUKA MTAKATIFU 7:15

50

Page 51: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

na kuwaponya magonjwa, waliandamananaye. Hao ndio akina Maria (aitwayeMagdalene), ambaye alitolewa pepo wabayasaba; 3 Yoana, mke wa Kuza, mfanyakazimkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa.Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwamali yao wenyewe. 4 Kundi kubwa la watulilikuwa linakusanyika, na watu walikuwawanamjia Yesu kutoka kila mji. Nayeakawaambia mfano huu: 5 “Mpanzi alikwendakupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda zilembegu, nyingine zilianguka njiani, na wapitanjia wakazikanyaga, na ndege wakazila. 6

Nyingine zilianguka penye mawe, na baada yakuota zikanyauka kwa kukosa maji. 7 Nyinginezilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti yamiiba ilipoota ikazisonga. 8 Nyinginezilianguka katika udongo mzuri, zikaota nakuzaa asilimia mia.” Baada ya kusema hayo,akapaaza sauti, akasema, “Mwenye masikio naasikie!” 9 Wanafunzi wake wakamwuliza Yesumaana ya mfano huo. 10 Naye akajibu, “Ninyimmejaliwa kujua siri za Ufalme wa Mungu,lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwakwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona,na wakisikia wasifahamu. 11 “Basi, maana yamfano huu ni hii: mbegu ni neno la Mungu. 12

Zile zilizoanguka njiani zinaonyesha watu walewanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja nakuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini nahivyo wakaokoka. 13 Zile zilizoanguka penyemawe zinaonyesha watu wale ambaowanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwafuraha. Hata hivyo, kama zile mbegu, watu haohawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu,na wanapojaribiwa hukata tamaa. 14 Zilezilizoanguka kwenye miti ya miiba ni watu walewanaosikia lile neno, lakini muda si muda,wanapokwenda zao, husongwa na wasiwasi,mali na anasa za maisha, na hawazai matundayakakomaa. 15 Na zile zilizoanguka kwenyeudongo mzuri ndio watu wale wanaolisikia lileneno, wakalizingatia kwa moyo mwema na wautii. Hao huvumilia mpaka wakazaa matunda.16 “Watu hawawashi taa na kuifunika kwachombo au kuiweka mvunguni. Lakini huiwekajuu ya kinara ili watu wanapoingia ndaniwapate kuona mwanga. 17 “Chochotekilichofichwa kitafichuliwa na siri yoyoteitagunduliwa na kujulikana hadharani. 18 “Kwahiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliyena kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu,hata kile anachodhani kuwa anacho,kitachukuliwa.” 19 Hapo mama na ndugu zakeYesu wakamjia, lakini hawakuweza kumkaribiakwa sababu ya umati wa watu. 20 Yesuakapewa habari kwamba mama na ndugu zakewalikuwa nje, wanataka kumwona. 21 LakiniYesu akawaambia watu wote, “Mama yangu nandugu zangu ni wale wanaolisikia neno laMungu na kulishika.” 22 Siku moja, Yesualipanda mashua pamoja na wanafunzi wake,akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka

ng'ambo.” Basi, wakaanza safari. 23

Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesualishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kaliikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndaniya mashua, wakawa katika hatari. 24 Walewanafunzi wakamwendea Yesu,wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana!Tunaangamia!” Yesu akaamka, akaikemeadhoruba na mawimbi, navyo vikatulia, kukawashwari. 25 Kisha akawaambia, “Iko wapi imaniyenu?” Lakini wao walishangaa na kuogopahuku wakiambiana, “Huyu ni nani basi, hataanaamuru dhoruba na mawimbi, navyovinamtii?” 26 Wakaendelea na safari, wakafikapwani ya nchi ya Wagerase inayokabiliana naGalilaya, ng'ambo ya ziwa. 27 Alipokuwaanashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwaamepagawa na pepo alimjia kutoka mjini. Kwamuda mrefu mtu huyo, hakuwa anavaa nguo,wala hakuwa anaishi nyumbani balimakaburini. 28 Alipomwona Yesu, alipigakelele na kujitupa chini mbele yake, na kusemakwa sauti kubwa “We, Yesu Mwana wa MunguAliye Juu una shauri gani nami? Ninakusihiusinitese!” 29 Alisema hivyo kwa kuwa Yesualikwishamwambia huyo pepo mchafu amtokemtu huyo. Pepo huyo mchafu alikuwaanamvamia mtu huyo mara nyingi, na ingawawatu walimweka ndani na kumfunga kwaminyororo na pingu, lakini kila mara alivivunjavifungo hivyo, akakimbizwa na pepo huyomchafu hadi jangwani. 30 Basi, Yesuakamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jinalangu ni Jeshi” —kwa sababu pepo wengiwalikuwa wamempagaa. 31 Hao pepowakamsihi asiwaamuru wamtoke na kwendakwenye shimo lisilo na mwisho. 32 Kulikuwa nakundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani.Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusuwawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa. 33

Kwa hiyo pepo hao wakamtoka yule mtu,wakawaingia wale nguruwe, naowakaporomoka kwenye ule mteremko mkali,wakatumbukia ziwani, wakazama majini. 34

Wale wachungaji walipoona yote yaliyotokeawalikimbia, wakaenda kuwapa watu habari,mjini na mashambani. 35 Watu wakaja kuonayaliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwonayule mtu aliyetokwa na pepo ameketi karibuna Yesu, amevaa nguo, ana akili zake,wakaogopa. 36 Wale watu walioshuhudia tukiohilo waliwaeleza hao jinsi yule mtualivyoponywa. 37 Wakazi wa nchi ya Gerasewalishikwa na hofu kubwa. Kwa hiyowakamwomba Yesu aondoke, aende zake.Hivyo Yesu alipanda tena mashua, akaondoka.38 Yule mtu aliyetokwa na wale pepo akamsihiaende pamoja naye. Lakini Yesu hakumruhusu,bali akamwambia, 39 “Rudi nyumbani ukaelezeyote Mungu aliyokutendea.” Basi, yule mtuakaenda akitangaza kila mahali katika mji ulemambo yote Yesu aliyomtendea. 40 Yesualiporudi upande mwingine wa ziwa, kundi la

LUKA MTAKATIFU 8:40

51

Page 52: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

watu lilimkaribisha, kwa maana wote walikuwawanamngojea. 41 Hapo akaja mtu mmojaaitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupamiguuni pa Yesu, akamwomba aendenyumbani kwake, 42 kwa kuwa binti yake wapekee, mwana wa pekee mwenye umri wamiaka kumi na miwili, alikuwa mahututi. Yesualipokuwa akienda, watu wakawawanamsonga kila upande. 43 Kulikuwa namwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu,ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwadamu kwa muda wa miaka kumi na miwili,ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yakeyote kwa waganga, hakuna aliyefaulukumponya. 44 Huyo mwanamke alimfuataYesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake. Papohapo akaponywa ugonjwa wake wa kutokwadamu. 45 Yesu akasema, “Ni nani aliyenigusa?”Wote wakasema kwamba hapakuwa na mtualiyemgusa. Naye Petro akasema, “Mwalimu,umati wa watu umekuzunguka na kukusonga!”46 Lakini Yesu akasema, “Kuna mtualiyenigusa, maana nimehisi nguvu imenitoka.”47 Yule mwanamke alipoona kwamba hawezikujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu,akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbeleya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsialivyoponyeshwa mara moja. 48 Yesuakamwambia, “Binti, imani yako imekuponya.Nenda kwa amani.” 49 Alipokuwa badoakiongea, Yairo akaletewa habari kutokanyumbani: “Binti yako ameshakufa, ya ninikumsumbua Mwalimu zaidi?” 50 Yesualiposikia hayo akamwambia Yairo, “Usiogope;amini tu, naye atapona.” 51 Alipofikanyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndanipamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobona wazazi wa huyo msichana. 52 Watu wotewalikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili yake.Lakini Yesu akawaambia, “Msilie, kwa maanamtoto hajafa, amelala tu!” 53 Nao wakamchekakwa sababu walijua kwamba alikuwa amekufa.54 Lakini Yesu akamshika mkono akasema,“Mtoto amka!” 55 Roho yake ikamrudia,akaamka mara. Yesu akaamuru wampechakula. 56 Wazazi wake walishangaa, lakiniYesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyotehayo yaliyotendeka.

Yesu aliwaita wale kumi na wawili,akawapa uwezo juu ya pepo wote, nauwezo wa kuponya wagonjwa. 2 Halafu

akawatuma waende kuhubiri Ufalme waMungu na kuponya wagonjwa. 3 Akawaambia,“Mnaposafiri msichukue chochote: msichukuefimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha,wala hata koti la ziada. 4 Nyumba yoyotemtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humompaka mtakapoondoka katika kijiji hicho. 5

Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katikamji huo, nanyi mnapotoka kung'utenimavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”6 Basi, wakaanza safari, wakapitia vijijiniwakihubiri Habari Njema na kuponya

wagonjwa kila mahali. 7 Sasa, mtawalaHerode, alipata habari za mambo yoteyaliyokuwa yanatendeka, akawa na wasiwasikwa vile walikuwa wakisema: “Yohaneamefufuka kutoka wafu!” 8 Wengine walisemakwamba Eliya ametokea, na wengine walisemakwamba mmojawapo wa manabii wa kaleamerudi duniani. 9 Lakini Herode akasema,“Huyo Yohane nilimkata kichwa; sasa ni nanihuyu ninayesikia habari zake?” Akawa na hamuya kumwona. 10 Wale mitume waliporudi,walimweleza yote waliyoyafanya. Yesuakawachukua, wakaenda peke yao mjiniBethsaida. 11 Lakini wale watu walipojuaalikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribishaakawazungumzia juu ya Ufalme wa Mungu,akawaponya wale waliohitaji kuponywa. 12 Jualilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawiliwalimwendea wakamwambia, “Waage watuwaende kwenye vijiji na mashamba ya karibu,wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwamaana hapa tulipo ni nyikani.” 13 Lakini Yesuakawaambia, “Wapeni ninyi chakula.”Wakamjibu, “Hatuna chochote ila mikatemitano na samaki wawili. Labda twendewenyewe tukawanunulie chakula watu wotehawa!” 14 (Walikuwepo pale wanaumewapatao elfu tano.) Basi, Yesu akawaambiawanafunzi wake, “Waambieni watu waketikatika makundi ya watu hamsinihamsini.” 15

Wanafunzi wakafanya walivyoambiwa,wakawaketisha wote. 16 Kisha Yesu akaitwaaile mikate mitano na wale samaki wawili,akatazama juu mbinguni, akamshukuruMungu, akavimega, akawapa wanafunzi wakewawagawie watu. 17 Wakala wote, wakashiba;wakakusanya makombo ya chakula, wakajazavikapu kumi na viwili. 18 Siku moja, Yesualikuwa anasali peke yake, na wanafunzi wakewalikuwa karibu. Basi, akawauliza, “Eti watuwanasema mimi ni nani?” 19 Nao wakamjibu,“Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohanembatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya,hali wengine wanasema kuwa wewe ni mmojawa manabii wa kale ambaye amefufuka.” 20

Hapo akawauliza, “Na ninyi je, mwasema mimini nani?” Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo waMungu.” 21 Halafu Yesu akawaamuruwasimwambie mtu yeyote habari hiyo. 22

Akaendelea kusema: “Ni lazima Mwana wa Mtuapate mateso mengi na kukataliwa na wazeena makuhani wakuu na walimu wa Sheria;atauawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” 23

Kisha akawaambia watu wote, “Mtu yeyoteakitaka kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikanenafsi yake, auchukue msalaba wake kila siku,anifuate. 24 Maana, mtu anayetaka kuyaokoamaisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakiniatakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu,atayaokoa. 25 Je, kuna faida gani mtu kuupatautajiri wote wa dunia kwa kujipoteza aukujiangamiza yeye mwenyewe? 26 Mtuakinionea aibu mimi na mafundisho yangu,

LUKA MTAKATIFU 8:41

52

Page 53: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyowakati atakapokuja katika utukufu wake na waBaba na wa malaika watakatifu. 27

Nawaambieni kweli, kuna wengine papa hapaambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalmewa Mungu.” 28 Yapata siku nane baada yakusema hayo, Yesu aliwachukua Petro, Yohanena Yakobo, akaenda nao mlimani kusali. 29

Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavaziyake yakawa meupe na kung'aa sana. 30 Nawatu wawili wakaonekana wakizungumzanaye, nao ni Mose na Eliya, 31 ambaowalitokea wakiwa wenye utukufu,wakazungumza naye juu ya kifo chakeambacho angekikamilisha huko Yerusalemu.32 Petro na wenzake walikuwa wamelemewana usingizi mzito, hata hivyo waliamka,wakauona utukufu wake, wakawaona na walewatu wawili waliokuwa wamesimama pamojanaye. 33 Basi, watu hao wawili walipokuwawakiondoka, Petro alimwambia Yesu, “Bwana,ni vizuri kwamba tupo hapa: basi, tujengevibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mosena kimoja cha Eliya.” —Kwa kweli hakujuaanasema nini. 34 Petro alipokuwa akisemahayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; nawingu hilo lilipowajia, wale wanafunziwaliogopa sana. 35 Sauti ikasikika kutokakatika hilo wingu: “Huyu ndiye Mwananguniliyemchagua, msikilizeni.” 36 Baada ya hiyosauti kusikika, Yesu alionekana akiwa pekeyake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukiohilo, na wakati ule hawakumwambia mtuyeyote mambo hayo waliyoyaona. 37 Keshoyake walipokuwa wakishuka kutoka kulemlimani, kundi kubwa la watu lilikutana naYesu. 38 Hapo, mtu mmoja katika lile kundiakapaaza sauti, akasema, “Mwalimu!Ninakusihi umwangaliemwanangu—mwanangu wa pekee! 39 Pepohuwa anamshambulia, na mara humfanyaapige kelele; humtia kifafa, na povu likamtokakinywani. Huendelea kumtesa sana,asimwache upesi. 40 Niliwaomba wanafunziwako wamfukuze, lakini hawakuweza.” 41 Yesuakasema, “Enyi kizazi kisicho na imani,kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumiliampaka lini?” Kisha akamwambia huyo mtu,“Mlete mtoto wako hapa.” 42 Wakati mtotohuyo alipokuwa anamjia Yesu, yule pepoalimwangusha chini na kumtia kifafa. LakiniYesu akamkemea yule pepo mchafuakamponya mtoto na kumkabidhi kwa babayake. 43 Watu wote wakashangazwa na uwezomkuu wa Mungu. Wale watu walipokuwa badowanashangaa juu ya mambo yote aliyofanya,Yesu aliwaambia wanafunzi wake, 44 “Tegenimasikio, myasikie mambo haya: Mwana waMtu anakwenda kutiwa mikononi mwa watu.”45 Lakini wao hawakuelewa maana ya usemihuo. Jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao iliwasitambue; nao wakaogopa kumwuliza juu yamsemo huo. 46 Kukatokea majadiliano kati ya

wale wanafunzi kuhusu nani kati yao aliyekuwamkuu zaidi. 47 Yesu aliyajua mawazoyaliyokuwa mioyoni mwao; basi akamchukuamtoto mdogo akamweka karibu naye, 48

akawaambia, “Mtu yeyote anayempokea mtotohuyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi;na yeyote anayenipokea mimi, anampokeayule aliyenituma. Maana yule aliye mdogokuliko wote kati yenu ndiye aliye mkubwakuliko wote.” 49 Yohane alidakia na kusema,“Bwana, tumemwona mtu mmoja akitoa pepokwa kulitumia jina lako nasi tukajaribukumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu.” 50

Lakini Yesu akamwambia, “Msimkataze; kwaniasiyepingana nanyi yuko upande wenu.” 51

Wakati ulipokaribia ambapo Yesuangechukuliwa juu mbinguni, yeye alikatashauri kwenda Yerusalemu. 52 Basi,akawatuma wajumbe wamtangulie, naowakaenda wakaingia kijiji kimoja chaWasamaria ili wamtayarishie mahali. 53 Lakiniwenyeji wa hapo hawakutaka kumpokea kwasababu alikuwa anaelekea Yerusalemu. 54

Basi, wanafunzi wake, kina Yohane na Yakobo,walipoona hayo, wakasema, “Bwana, watakatuamuru moto ushuke kutoka mbinguniuwateketeze?” 55 Lakini yeye akawageukia,akawakemea akasema, “Hamjui ni roho yanamna gani mliyo nayo; 56 kwa maana Mwanawa Mtu hakuja kuyaangamiza maisha ya watu,bali kuyaokoa.” Wakatoka, wakaenda kijijikingine. 57 Walipokuwa wakisafiri njiani, mtummoja akamwambia Yesu, “Nitakufuatakokote utakakokwenda.” 58 Yesu akasema,“Mbweha wana mapango, na ndege wanaviota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pakupumzikia.” 59 Kisha akamwambia mtumwingine, “Nifuate.” Lakini huyo akasema,“Bwana, niruhusu kwanza niende kumzikababa yangu.” 60 Yesu akamwambia, “Waachewafu wazike wafu wao; bali wewe nendaukatangaze Ufalme wa Mungu.” 61 Na mtumwingine akamwambia, “Nitakufuata, lakininiruhusu kwanza nikawaage wale walionyumbani kwangu.” 62 Yesu akamwambia,“Yeyote anayeshika jembe tayari kulima nahuku anaangalia nyuma, hafai kwa Ufalme waMungu.”

Baada ya hayo, Bwana aliwachaguawengine sabini na wawili, akawatumawawiliwawili, wamtangulie katika kila

kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewealitaka kwenda. 2 Akawaambia, “Mavuno nimengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo,mwombeni mwenye shamba atume wavunajishambani mwake. 3 Sasa nendeni; fahamunikwamba ninawatuma ninyi kama kondoowanaokwenda kati ya mbwa mwitu. 4

Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, walaviatu; msimsalimu mtu yeyote njiani. 5

Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanzawasalimuni hivi: Amani iwe katika nyumba hii!6 Kama akiwako mwenye kupenda amani,

LUKA MTAKATIFU 10:6

53

Page 54: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.7 Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywawanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahilimshahara wake. Msiende mara nyumba hiimara nyumba ile. 8 Kama mkifika mji fulani nawatu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni.9 Ponyeni wagonjwa walioko huko, waambieniwatu: Ufalme wa Mungu umekaribia kwenu. 10

Lakini mkiingia katika mji wowote,wasipowakaribisheni, tokeni; nanyi mpitapokatika barabara zao semeni: 11 Hata mavumbiya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetutunawakung'utieni. Lakini, jueni kwambaUfalme wa Mungu umekaribia. 12 Hakikanawaambieni, siku ile mji huo utapata adhabukubwa zaidi kuliko ile ya watu wa Sodoma. 13

“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida!Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenuingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wakewangalikwishavaa mavazi ya gunia kitambo,na kukaa katika majivu kuonyesha kwambawametubu. 14 Hata hivyo, Siku ya Hukumuninyi mtapata adhabu kubwa zaidi kuliko ile yawatu wa Tiro na Sidoni. 15 Na weweKafarnaumu, unataka kujikweza mpakambinguni? La; utaporomoshwa mpakaKuzimu.” 16 Halafu akasema, “Anayewasikilizaninyi, ananisikiliza mimi; na anayekataakuwapokea ninyi, anakataa kunipokea mimi.Yeyote anayekataa kunipokea, anakataakumpokea yule aliyenituma.” 17 Baadaye, walesabini na wawili walirudi wamejaa furaha,wakisema, “Bwana, hata pepo wametutiitulipolitaja jina lako.” 18 Yeye akawaambia,“Nilimwona Shetani jinsi alivyokuwaanaporomoka kama umeme kutoka mbinguni.19 Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaganyoka na ng'e, na uwezo juu ya nguvu zote zayule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru.20 Hata hivyo, msifurahi kwa sababu pepowamewatii, bali furahini kwa sababu majinayenu yameandikwa mbinguni.” 21 Saa ileile,Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,akasema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wambingu na dunia, kwa kuwa umewafichawenye hekima na elimu mambo haya,ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyoilivyokupendeza.” 22 Kisha akasema, “Babayangu ameweka yote mikononi mwangu.Hakuna amjuaye Mwana ni nani ila Baba, walaamjuaye Baba ni nani ila Mwana, na yeyoteyule ambaye Mwana anataka kumfunuliahayo.” 23 Halafu akawaelekea wafuasi wakeakawaambia, “Heri wanaoona yalemnayoyaona ninyi! 24 Hakika, manabii nawafalme walitamani kuona yale mnayoyaonaninyi wasiyaone, na kusikia yale mnayoyasikiawasiyasikie.” 25 Baadaye mwalimu mmoja waSheria alisimama akamwuliza akitakakumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipateuzima wa milele?” 26 Yesu akamwuliza,“Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?”27 Akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako

kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote,kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote.Na, mpende jirani yako kama unavyojipendamwenyewe.” 28 Yesu akawaambia, “Vema!Fanya hivyo, nawe utaishi.” 29 Lakini yeyeakitaka kujihakikishia kuwa mwemaakamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?” 30

Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anashukakutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Alipokuwanjiani, alivamiwa na majambazi,wakamnyang'anya mali yake na kumpiga,wakamwacha amelala pale nusu mfu. 31

Kumbe, kuhani mmoja akawa anapitabarabara ileile, akamwona, akapita kando. 32

Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofikamahali akamwona, akapita kando. 33 LakiniMsamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifikapale yule mtu alipokuwa, naye alipomwona,alimwonea huruma. 34 Akamwendea,akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafutana divai; na kuyafunga halafu akampandishajuu ya punda wake akampeleka katika nyumbamoja ya wageni akamuuguza. 35 Kesho yakeakatoa fedha dinari mbili akampa yulemwenye nyumba, akamwambia, Muuguze mtuhuyu; na chochote utakachotumia zaidi,nitakulipa nitakaporudi.” 36 Kisha Yesuakauliza, “Kati ya hao watatu, ni yupialiyeonyesha kuwa jirani yake yule aliyevamiwana majambazi?” 37 Yule mwalimu wa Sheriaakamjibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesuakamwambia, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”38 Walipokuwa safarini, waliingia katika kijijikimoja na mwanamke mmoja, aitwaye Martha,alimkaribisha nyumbani kwake. 39 Marthaalikuwa na dada yake aitwaye Maria; huyualiketi karibu na Yesu akisikiliza mafundishoyake. 40 Lakini Martha alikuwa anashughulikana mambo mengi. Basi, akamwendea Yesu,akamwambia, “Bwana, hivi hujali kwambadada yangu ameniacha nishughulike pekeyangu? Mwambie basi, anisaidie.” 41 LakiniBwana akamjibu, “Martha, Martha,unahangaika na kusumbuka kwa mambomengi. 42 Kitu kimoja tu ni muhimu. Mariaamechagua kitu bora zaidi ambacho hakunamtu atakayemnyag'anya.”

Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulaniakisali. Alipomaliza kusali, mmoja wawanafunzi wake akamwambia,

“Bwana, tunakuomba utufundishe kusali kamaYohane mbatizaji alivyowafundisha wanafunziwake.” 2 Yesu akawaambia, “Mnaposali,semeni: Baba! Jina lako litukuzwe; Ufalmewako ufike. 3 Utupe daima chakula chetu chakila siku. 4 Utusamehe dhambi zetu, maanasisi tunawasamehe wote waliotukosea; walausitutie katika majaribu.” 5 Kisha akawaambia,“Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaendakwake usiku wa manane, akamwambia: Rafiki,tafadhali niazime mikate mitatu, 6 kwa kuwarafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarininami sina cha kumpa. 7 Naye, akiwa ndani

LUKA MTAKATIFU 10:7

54

Page 55: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

angemjibu: Usinisumbue! Nimekwisha fungamlango. Mimi na watoto wangu tumelala;siwezi kuamka nikupe! 8 Hakika, ingawahataamka ampe kwa sababu yeye ni rafikiyake, lakini, kwa sababu ya huyo mtukuendelea kumwomba, ataamka ampechochote anachohitaji. 9 Kwa hiyo, ombeni,nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtapata,bisheni nanyi mtafunguliwa. 10 Maana yeyoteaombaye hupewa, atafutaye hupata naabishaye hufunguliwa. 11 Mtoto akimwombababa yake samaki, je, atampa nyoka badala yasamaki? 12 Na kama akimwomba yai, je,atampa ng'e? 13 Ninyi, ingawa ni waovu,mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Basi,baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi;atawapa Roho Mtakatifu walewanaomwomba.” 14 Siku moja Yesu alikuwaanamfukuza pepo aliyemfanya mtu mmojakuwa bubu. Basi, huyo pepo alipomtoka, yulemtu akaweza kuongea hata umati wa watuukashangaa. 15 Lakini baadhi ya watu haowakasema, “Anamfukuza pepo kwa uwezo waBeelzebuli, mkuu wa pepo.” 16 Wengine,wakimjaribu, wakamtaka afanye isharakuonyesha kama alikuwa na idhini kutokambinguni. 17 Lakini yeye, akiwa anayajuamawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowoteuliofarakana wenyewe, hauwezi kudumu;kadhalika, jamaa yeyote inayofarakanahuangamia. 18 Kama Shetani anajipingamwenyewe, utawala wake utasimamaje?Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepokwa uwezo wa Beelzebuli? 19 Kama ninafukuzapepo kwa uwezo wa Beelzebuli, watoto wenuhuwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababuhiyo, wao ndio watakaowahukumu ninyi. 20

Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa uwezo waMungu, basi jueni kwamba Ufalme wa Munguumekwisha fika kwenu. 21 “Mtu mwenyenguvu anapolinda jumba lake kwa silaha, maliyake yote iko salama. 22 Lakini akija mwenyenguvu zaidi akamshambulia na kumshinda,huyo huziteka silaha zake alizotegemea nakugawanya nyara. 23 Yeyote asiyejiunga nami,ananipinga; na yeyote asiyekusanya pamojanami, hutawanya. 24 “Pepo mchafu akifukuzwakwa mtu fulani, huzururazurura jangwaniakitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata,hujisemea: Nitarudi kwenye makao yangunilikotoka. 25 Anaporudi, huikuta ile nyumbaimefagiwa na kupambwa. 26 Basi, huenda nakuwachukua pepo wengine saba waovu zaidikuliko yeye; wote huenda na kumwingia mtuyule. Hivyo, basi hali ya mtu huyo sasa huwambaya zaidi kuliko pale mwanzo.” 27

Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmojakatika lile kundi la watu, akasema kwa sautikubwa: “Heri tumbo lililokuzaa, na maziwayaliyokunyonyesha!” 28 Lakini Yesu akasema,“Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno laMungu na kulishika.” 29 Umati wa watuulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia,

“Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara,lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ileya Yona. 30 Jinsi Yona alivyokuwa ishara kwawatu wa Ninewi, ndivyo pia Mwana wa Mtuatakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki. 31 Malkiawa kusini atatokea wakati kizazi hikikitakapohukumiwa, naye atashuhudia kwambakina hatia. Yeye alisafiri kutoka mbali, akajakusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni;kumbe hapa pana mkuu zaidi kuliko Solomoni.32 Watu wa Ninewi watatokea wakati kizazihiki kitakapohukumiwa, na watashuhudiakwamba kizazi hiki kina hatia. Hao watu waNinewi walitubu kwa sababu ya mahubiri yaYona; na hapa pana mkuu zaidi kuliko Yona! 33

“Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunikakwa pishi, bali huiweka juu ya kinara ili watuwanaoingia ndani wapate kuona mwanga. 34

Jicho lako ni kama taa ya mwili wako; likiwazima, mwili wako wote utakuwa katikamwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wakopia utakuwa katika giza. 35 Uwe mwangalifubasi mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.36 Basi, kama mwili wako wote una mwanga,bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwilihuo utang'aa kikamilifu kama vile taainavyokuangazia kwa mwanga wake.” 37 Yesualipokuwa akiongea, Mfarisayo mmojaalimkaribisha chakula nyumbani kwake, nayeakaenda, akaketi kula chakula. 38 HuyoMfarisayo alistaajabu kuona kwamba alikulachakula bila kunawa. 39 Bwana akamwambia,“Ninyi Mafarisayo huosha kikombe na sahanikwa nje, lakini ndani mmejaa udhalimu nauovu. 40 Wapumbavu ninyi! Je, aliyetengenezanje si ndiye aliyetengeneza ndani pia? 41 Toenikwa maskini vile vitu vilivyomo ndani, navingine vyote vitakuwa halali kwenu. 42 “Lakiniole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatozawatu zaka hata juu ya majani ya kukolezeachakula, mchicha na majani mengine, na hukuhamjali juu ya haki na upendo kwa Mungu.Mambo haya iliwapasa muwe mmeyazingatiabila kuyasahau yale mengine. 43 “Ole wenuninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapendakuketi mbele mahali pa heshima katikamasunagogi, na kusalimiwa kwa heshimahadharani. 44 Ole wenu, kwa sababu mkokama makaburi yaliyofichika; watu hutembeajuu yake bila kufahamu.” 45 Mmoja wa walimuwa Sheria akamwambia, “Mwalimu, manenoyako yanatukashifu na sisi pia.” 46 Yesuakamjibu, “Na ninyi walimu wa Sheria, olewenu; maana mnawatwika watu mizigoisiyochukulika, huku ninyi wenyewe hamnyoshihata kidole kuwasaidia. 47 Ole wenu, kwakuwa mnajenga makaburi ya manabii waleambao wazee wenu waliwaua. 48 Kwa hiyomnashuhudia na kukubaliana na matendo yawazee wenu; maana wao waliwaua haomanabii, nanyi mnajenga makaburi yao. 49

Kwa hiyo, Hekima ya Mungu ilisema hivi:Nitawapelekea manabii na mitume, lakini

LUKA MTAKATIFU 11:49

55

Page 56: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

12

watawaua baadhi yao, na kuwatesa wengine.50 Matokeo yake ni kwamba kizazi hikikitaadhibiwa kwa sababu ya damu ya manabiiwote iliyomwagika tangu mwanzo waulimwengu; 51 tangu kumwagwa damu yaAbeli mpaka kifo cha Zakariya ambayewalimuua kati ya madhabahu na mahalipatakatifu. Naam, hakika kizazi hikikitaadhibiwa kwa matendo haya. 52 “Ole wenuninyi walimu wa Sheria, kwa sababummeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu;ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuiawaliokuwa wanaingia wasiingie.” 53 Alipokuwaakitoka pale, wale Mafarisayo na walimu waSheria wakaanza kumshambulia vikali nakumsonga kwa maswali mengi 54 ili wapatekumnasa kwa maneno yake.

Wakati watu kwa maelfu walipokuwawamekusanyika hata wakawawanakanyagana, Yesu aliwaambia

kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini nachachu ya Mafarisayo, yaani unafiki. 2 Kilakilichofunikwa kitafunuliwa, kila kilichofichikakitafichuliwa. 3 Kwa hiyo, kila mliyosemagizani, watu watayasikia katika mwanga, nakila mliyonong'ona faraghani milangoimefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba. 4

“Nawaambieni ninyi rafiki zangu: msiwaogopewale wanaoua mwili, wasiweze kufanya kitukingine zaidi. 5 Nitawaonyesheni yule ambayeni lazima kumwogopa: mwogopeni yuleambaye baada ya kuua ana uwezo wakumtupa mtu katika moto wa Jehanamu.Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo. 6

Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwakwa senti kumi, au sivyo? Lakini mbele yaMungu hasahauliki hata mmoja. 7 Lakini hatanywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.Msiogope, basi, ninyi mna thamani zaidi kulikoshomoro wengi! 8 “Nawaambieni kweli, kilamtu anayekiri hadharani kwamba yeye niwangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele yamalaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake.9 Lakini, mtu yeyote anayenikana mbele yawatu, naye atakanwa mbele ya malaika waMungu. 10 “Yeyote anayesema neno lakumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa; lakinianayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.11 “Watakapowapeleka ninyi mbele yamasunagogi na mbele ya wakuu na watawalamsiwe na wasiwasi juu ya jinsi mtakavyojiteteaau jinsi mtakavyosema. 12 Kwa maana wakatihuo Roho Mtakatifu atawafundisheni kilemnachopaswa kusema.” 13 Mtu mmoja katikaule umati wa watu akamwambia, “Mwalimu,mwambie ndugu yangu tugawane urithialiotuachia baba.” 14 Yesu akamjibu, “Rafiki, ninani aliyeniweka mimi mwamuzi au msuluhishikati yenu?” 15 Basi, akawaambia wote,“Jihadharini na kila aina ya tamaa; maanauzima wa mtu hautegemei wingi wa vitu alivyonavyo.” 16 Kisha akawaambia mfano:“Kulikuwa na tajiri mmoja ambaye shamba

lake lilizaa mavuno mengi. 17 Tajiri huyoakafikiri moyoni mwake: Nitafanyaje nami sinamahali pa kuhifadhia mavuno yangu? 18

Nitafanya hivi: nitabomoa ghala zangu nakujenga kubwa zaidi, na humo nitahifadhimavuno yangu yote na mali yangu. 19 Haponitaweza kuiambia roho yangu: sasa unayoakiba ya matumizi kwa miaka na miaka. Pondamali, ule, unywe na kufurahi. 20 Lakini Munguakamwambia: Mpumbavu wewe; leo usikuroho yako itachukuliwa. Na vitu vile vyoteulivyojilundikia vitakuwa vya nani?” 21 Yesuakamaliza kwa kusema “Ndivyo ilivyo kwa mtuanayejilundikia mali kwa ajili yake mwenyewe,lakini si tajiri mbele ya Mungu.” 22 Kisha Yesuakawaambia wanafunzi wake, “Kwa sababuhiyo nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu yachakula mnachohitaji ili kuishi, wala juu yamavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. 23

Kwa sababu uzima ni bora kuliko chakula, namwili ni bora kuliko mavazi. 24 Chukueni kwamfano, kunguru: hawapandi, hawavuni walahawana ghala yoyote. Hata hivyo, Munguhuwalisha. Ninyi mna thamani zaidi kulikondege! 25 Ni nani kati yenu kwa kuwa nawasiwasi anaweza kuongeza urefu wa maishayake? 26 Basi, kama hamwezi kufanya jambodogo kama hilo, kwa nini kuwa na wasiwasi juuya yale mengine? 27 Angalieni maua jinsiyanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayafumi.Hata hivyo, nawahakikishieni kwamba hataSolomoni mwenyewe na fahari zake zotehakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.28 Lakini, kama Mungu hulivika vizuri jani lashambani ambalo leo liko na kesho latupwamotoni, je, hatawafanyia ninyi zaidi? Enyi watuwenye imani haba! 29 “Basi, msivurugike akili,mkihangaika daima juu ya mtakachokula aumtakachokunywa. 30 Kwa maana hayo yotendiyo yanayohangaikiwa na watu wasiomjuaMungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitajivitu hivyo. 31 Shughulikieni kwanza Ufalme waMungu, na hayo yote mtapewa kwa ziada. 32

“Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenuamependa kuwapeni Ufalme. 33 Uzeni maliyenu mkawape maskini misaada. Jifanyienimifuko isiyochakaa, na jiwekeeni hazinambinguni ambako haitapungua. Huko wezihawakaribii, wala nondo hawaharibu. 34 Paleilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwamoyo wako. 35 “Muwe tayari! Jifungenimkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka;36 muwe kama watumishi wanaomngojeabwana wao arudi kutoka arusini, iliwamfungulie mara atakapobisha hodi. 37 Heriyao watumishi wale ambao bwana waoatakaporudi atawakuta wanakesha!Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifungamkanda kiunoni, atawaketisha mezani nakuwahudumia. 38 Heri yao watumishi haoikiwa bwana wao atawakuta wanakesha hataikiwa atarudi usiku wa manane au alfajiri. 39

Jueni kwamba, kama mwenye nyumba angejua

LUKA MTAKATIFU 11:50

56

Page 57: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

saa ambayo mwizi atakuja, angekesha, walahangeiacha nyumba yake ivunjwe. 40 Nanyi,kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtuatakuja saa msiyoitazamia.” 41 Petroakamwambia, “Bwana, mfano huo ni kwa ajiliyetu tu, au ni kwa ajili ya watu wote?” 42

Bwana akajibu, “Ni nani basi, mtumishi aliyemwaminifu na mwenye busara, ambaye bwanawake atamweka juu ya watumishi wake iliawape chakula wakati ufaao? 43 Heri yakemtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudiatamkuta akifanya hivyo. 44 Hakika atampamadaraka juu ya mali yake yote. 45 Lakini,kama mtumishi huyo atafikiri moyoni mwake:na kusema: Bwana wangu amekawia sanakurudi halafu aanze kuwapiga watumishiwenzake, wa kiume au wa kike, na kula,kunywa na kulewa, 46 bwana wake atarudisiku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamkatiliambali na kumweka fungu moja na wasioamini.47 Mtumishi ambaye anajua matakwa yabwana wake lakini hajiweki tayari kufanyaanavyotakiwa, atapigwa sana. 48 Lakini yuleafanyaye yanayostahili adhabu bila kujua,atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atatakiwavingi; aliyekabidhiwa vingi zaidi atatakiwakutoa vingi zaidi. 49 “Nimekuja kuwasha motoduniani, laiti ungekuwa umewaka tayari! 50

Ninao ubatizo ambao inanipasa niupokee; jinsigani ninavyohangaika mpaka ukamilike! 51

Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani?Hata kidogo; si amani bali utengano. 52 Natangu sasa, jamaa ya watu watanoitagawanyika; watatu dhidi ya wawili, na wawilidhidi ya watatu. 53 Baba atakuwa dhidi yamwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mamadhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake;mama mkwe dhidi ya mke wa mwanawe nahuyo dhidi ya mama mkwe wake.” 54 Yesuakayaambia tena makundi ya watu,“Mnapoona mawingu yakitokea upande wamagharibi, mara mwasema: Mvua itanyesha,na kweli hunyesha. 55 Mnapoona upepo wakusi unavuma, mwasema Kutakuwa na hali yajoto na ndivyo inavyokuwa. 56 Enyi wanafiki!Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangaliadunia na anga; kwa nini basi, hamwezi kujuamaana ya nyakati hizi? 57 “Na kwa ninihamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema lakufanya? 58 Maana kama mshtaki wakoanakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhalikwako kupatana naye mkiwa bado njiani, iliasije akakupeleka mbele ya hakimu, nayehakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutiandani. 59 Hakika hutatoka huko nakwambia,mpaka utakapomaliza kulipa senti ya mwisho.”

Wakati huo watu fulani walikuja,wakamweleza Yesu juu ya watu waGalilaya ambao Pilato alikuwa

amewaua wakati walipokuwa wanachinjawanyama wao wa tambiko. 2 Naye Yesuakawaambia, “Mnadhani Wagalilaya haowalikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya

wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo? 3

Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, halikadhalika, msipotubu, mtaangamia kama wao.4 Au wale kumi na wanane walioangukiwa namnara kule Siloamu wakafa; mnadhani waowalikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wotewalioishi Yerusalemu? 5 Nawaambieni sivyo;lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kamawao.” 6 Kisha, Yesu akawaambia mfano huu:“Mtu mmoja alikuwa na mtini katika shambalake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchumamatunda yake, lakini akaukuta haujazaa hatatunda moja. 7 Basi, akamwambia mfanyakaziwake: Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwanikija kuchuma matunda ya mtini huu, naminisiambulie kitu. Ukate! Kwa nini uitumie ardhibure? 8 Lakini naye akamjibu: Bwana, tuuachetena mwaka huu; nitauzungushia mtaro nakuutilia mbolea. 9 Kama ukizaa matundamwaka ujao, vema; la sivyo, basi utawezakuukata.” 10 Yesu alikuwa akifundisha katikasunagogi moja siku ya Sabato. 11 Na hapopalikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwamgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokanana pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababuhiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibayahata asiweze kusimama wima. 12 Yesualipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama,umeponywa ugonjwa wako.” 13 Akamwekeamikono, na mara mwili wake ukawa wimatena, akawa anamtukuza Mungu. 14 Lakinimkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababuYesu alikuwa amemponya siku ya Sabato.Hivyo akawaambia wale watu walikusanyikapale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi,fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu;lakini msije siku ya Sabato.” 15 Hapo Bwanaakamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenuhangemfungua ng'ombe au punda wakekutoka zizini ampeleke kunywa maji, hatakama siku hiyo ni ya Sabato? 16 Sasa, hapayupo binti wa Abrahamu ambaye Shetanialimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi naminane. Je, haikuwa vizuri kumfunguliavifungo vyake siku ya Sabato?” 17 Alipokwishasema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakiniwatu wengine wote wakajaa furaha kwasababu ya mambo yote aliyotenda. 18 Yesuakauliza: “Ufalme wa Mungu unafanana nanini? Nitaulinganisha na nini? 19 NI kamambegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja nakuipanda shambani mwake; ikaota hata ikawamti. Ndege wa angani wakajenga viota vyaokatika matawi yake.” 20 Tena akauliza:“Nitaulinganisha Ufalme wa Mungu na nini? 21

Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja nakuichanganya pamoja na unga debe mojakisha unga wote ukaumuka wote.” 22 Yesualindelea na safari yake kwenda Yerusalemuhuku akipitia mijini na vijijini, akihubiri. 23 Mtummoja akamwuliza, “Je, Mwalimu, watuwatakaookoka ni wachache?” 24 Yesuakawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia

LUKA MTAKATIFU 13:24

57

Page 58: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

14

mlango mwembamba; maana nawaambieni,wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.25 “Wakati utakuja ambapo mwenye nyumbaatainuka na kufunga mlango. Ninyimtasimama nje na kuanza kupiga hodimkisema: Bwana, tufungulie mlango. Lakiniyeye atawajibu: Sijui mmetoka wapi. 26 Nanyimtaanza kumwambia: Sisi ndio wale tuliokulana kunywa pamoja nawe; na wewe ulifundishakatika vijiji vyetu. 27 Lakini yeye atasema: Sijuininyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu,enyi nyote watenda maovu. 28 Ndipo mtakuwana kulia na kusaga meno, wakatimtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo,na manabii wote wapo katika Ufalme waMungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje!29 Watu watakuja kutoka mashariki namagharibi, kutoka kaskazini na kusini,watakuja na kukaa kwenye karamu katikaUfalme wa Mungu. 30 Naam, wale walio wamwisho watakuwa wa kwanza; na wale waliowa kwanza watakuwa wa mwisho.” 31 Wakatihuohuo, Mafarisayo na watu wenginewalimwendea Yesu wakamwambia, “Ondokahapa uende mahali pengine, kwa maanaHerode anataka kukuua.” 32 Yesu akawajibu,“Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi:Leo na kesho ninafukuza pepo na kuponyawagonjwa, na siku ya tatu nitakamilisha kaziyangu. 33 Hata hivyo, kwa leo, kesho na keshokutwa, ni lazima niendelee na safari yangu,kwa sababu si sawa nabii auawe nje yaYerusalemu. 34 “Yerusalemu! We Yerusalemu!Unawaua manabii na kuwapiga mawe walewaliotumwa kwako! Mara ngapi nimetakakuwakusanya watoto wako pamoja kama kukuanavyokusanya vifaranga vyake chini yamabawa yake, Lakini wewe umekataa. 35

Haya, utaachiwa mwenyewe nyumba yako.Naam, hakika nawaambieni, hamtanionampaka wakati utakapofika mseme: Abarikiwehuyo ajaye kwa jina la Bwana.”

Siku moja ya Sabato, Yesu alikwendakula chakula nyumbani kwa mmojawa viongozi wa Mafarisayo; watu

waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.2 Mbele yake Yesu palikuwa na mtu mmojaaliyekuwa na ugonjwa wa kuvimba mwili. 3

Yesu akawauliza walimu wa Sheria naMafarisayo, “Je, ni halali au la kumponya mtusiku ya sabato?” 4 Lakini wao wakakaa kimya.Yesu akamshika huyo mgonjwa, akamponya,akamwacha aende zake. 5 Halafuakawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtotowake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni,hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?” 6

Nao hawakuweza kumjibu swali hilo. 7 Yesualiona jinsi wale walioalikwa walivyokuwawanajichagulia nafasi za heshima, akawaambiamfano: 8 “Kama mtu akikualika arusini, usiketimahali pa heshima isije ikawa amealikwamwingine mheshimiwa kuliko wewe; 9 namwenyeji wenu ninyi wawili atakuja na

kukwambia: Mwachie huyu nafasi. Hapoutaaibika mbele ya wote na kulazimika kwendakuchukua nafasi ya mwisho. 10 Bali ukialikwakwenye karamu, keti mahali pa mwisho, ilimwenyeji wako atakapokuja akwambie: Rafiki,njoo hapa mbele, mahali pazuri zaidi. Hapoutakuwa umeheshimika mbele ya wotewanaoketi pamoja nawe. 11 Kwa maanayeyote anayejikweza atashushwa, naanayejishusha, atakwezwa.” 12 Halafuakamwambia na yule aliyemwalika, “Kamaukiwaandalia watu karamu mchana au jioni,usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jiranizako walio matajiri, wasije nao wakakualikanawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea. 13

Badala yake, unapofanya karamu, waalikemaskini, vilema viwete na vipofu, 14 naweutakuwa umepata baraka, kwa kuwa haohawana cha kukulipa. Maana Mungu atakupatuzo lako wakati watu wema watakapofufuka.”15 Mmoja wa wale waliokuwa wameketipamoja na Yesu akasema, “Ana heri mtu yuleatakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu.”16 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alifanyakaramu kubwa, akaalika watu wengi. 17 Wakatiwa karamu ulipofika alimtuma mtumishi wakeawaambie walioalikwa, Njoni, kila kitu ni tayari.18 Lakini wote, kwa namna moja, wakaanzakuomba radhi. Wa kwanza akamwambiamtumishi: Nimenunua shamba, kwa hiyo sinabudi kwenda kuliangalia; nakuomba uniwieradhi. 19 Mwingine akasema: Nimenunuang'ombe jozi tano wa kulima; sasa nimo njianikwenda kuwajaribu; nakuomba uniwie radhi.20 Na mwingine akasema: Nimeoa mke, kwahiyo siwezi kuja. 21 Mtumishi huyo akarudi nakumwarifu bwana wake jambo hilo. Yulemwenye nyumba alikasirika, akamwambiamtumishi wake: Nenda upesi kwenye barabarana vichochoro vya mji, uwalete hapa ndanimaskini, viwete, vipofu na waliolemaa. 22

Baadaye, mtumishi huyo akasema: Bwanamambo yamefanyika kama ulivyoamuru, lakinibado iko nafasi. 23 Yule bwana akamwambiamtumishi: Nenda katika barabara navichochoro vya mji uwashurutishe watukuingia ili nyumba yangu ijae. 24 Kwa maana,nawaambieni, hakuna hata mmoja wa walewalioalikwa atakayeonja karamu yangu.” 25

Hapo, makundi mengi yakawa yanaandamanapamoja na Yesu. Basi, akawageukiaakawaambia, 26 “Mtu yeyote akija kwangu,asipowachukia baba na mama yake, mkewake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hatana nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwamwanafunzi wangu. 27 Mtu asipochukuamsalaba wake na kunifuata hawezi kuwamwanafunzi wangu. 28 Kwa maana, ni nanimiongoni mwenu ambaye akitaka kujengamnara hataketi kwanza akadirie gharama zakeili ajue kama ana kiasi cha kutosha chakumalizia? 29 La sivyo, baada ya kuwekamsingi na kushindwa kumaliza, watu

LUKA MTAKATIFU 13:25

58

Page 59: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

15

16

watamcheka 30 wakisema: Mtu huyu alianzakujenga, lakini hakumalizia. 31 “Au, ni mfalmegani ambaye, akitaka kwenda kupigana namfalme mwingine, hataketi kwanza chini nakufikiri kama ataweza, kwa askari wake elfuishirini? 32 Kama anaona hataweza,atawatuma wajumbe kutaka masharti yaamani wakati mfalme huyo mwingine angalimbali. 33 Vivyo hivyo, basi, hakuna hatammoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangukama asipoachilia kila kitu alicho nacho. 34

“Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake,itakolezwa na nini? 35 Haifai kitu wala kwaudongo wala kwa mbolea. Watu huitupiliambali. Sikieni basi, kama mna masikio!”

Siku moja, watoza ushuru na wahalifuwengi walikwenda kumsikiliza Yesu. 2

Mafarisayo na walimu wa Sheriawakaanza kunung'unika: “Mtazameni mtuhuyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tenaanakula nao.” 3 Yesu akawajibu kwa mfano: 4

“Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigunduakwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini?Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, nakwenda kumtafuta yule aliyepotea mpakaampate. 5 Akimpata, atambeba mabegani kwafuraha. 6 Anapofika nyumbani, atawaita rafikizake akiwaambia, Furahini pamoja nami, kwasababu nimempata yule kondoo wangualiyepotea. 7 Kadhalika nawaambieni, ndivyokutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajiliya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kulikokwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwawema, wasiohitaji kutubu. 8 “Au mwaonaje?Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi zafedha, akipoteza moja, atafanya nini?Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafutakwa uangalifu mpaka aipate. 9 Akiipata,atawaita rafiki na jirani zake akisema, Furahinipamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafuyangu iliyopotea. 10 Kadhalika nawaambieni,ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungukwa sababu ya mwenye dhambi mmojaanayetubu.” 11 Yesu akaendelea kusema,“Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wanawawili. 12 Yule mdogo, alimwambia baba yake:Baba, nipe urithi wangu. Naye akawagawiamali yake. 13 Baada ya siku chache, yulemdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedhaaliyopata, akaenda nchi ya mbali ambakoaliitumia ovyo. 14 Alipomaliza kutumia kilakitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, nayeakaanza kuhangaika. 15 Akaomba kazi kwamwananchi mtu mmoja wa huko nayeakampeleka shambani mwake kulishanguruwe. 16 Alitamani kula magandawaliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtualiyempa kitu. 17 Alipoanza kupata akiliakafikiri: Mbona kuna wafanyakazi wengi wababa yangu wanaokula na kusaza, namininakufa njaa? 18 Nitarudi kwa baba yangu nakumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, nanimekukosea wewe pia. 19 Sistahili hata

kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wawafanyakazi wako. 20 Basi, akaanza safari yakurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yumbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wahuruma alimkimbilia, akamkumbatia nakumbusu. 21 “Mwanawe akamwambia: Baba,nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewepia. Sistahili hata kuitwa mwanao. 22 Lakinibaba yake akawaambia watumishi wake:Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvishenipete na viatu! 23 Mchinjeni ndama mnono; tulekusherehekea! 24 Kwa sababu huyumwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzimaalikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.Wakaanza kufanya sherehe. 25 “Wakati huokaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwaakirudi na kukaribia nyumbani akasikia vifijona ngoma. 26 Akamwita mmoja wa watumishi,akamwuliza: Kuna nini? 27 Huyo mtumishiakamwambia: Ndugu yako amerudi nyumbani,na baba yako amemchinjia ndama mnono kwakuwa amempata akiwa salama salimini. 28

Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hataakakataa kuingia nyumbani. Baba yakeakatoka nje na kumsihi aingie. 29 Lakini yeyeakamjibu: Kumbuka! Miaka yotenimekutumikia, sijavunja amri yako hata maramoja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja narafiki zangu! 30 Lakini mtoto wako huyualiyekula mali yako pamoja na makahaba,mara tu alipokuja umemchinjia yule ndamamnono. 31 Baba yake akamjibu: Mwanangu,wewe uko pamoja nami siku zote, na kilanilicho nacho ni chako. 32 Ilitubidi kufanyasherehe na kufurahi, kwa sababu huyu nduguyako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima;alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.”

Yesu aliwaambia wanafunzi wake:“Tajiri mmoja alikuwa na karani wake.Huyu karani alichongewa kwamba

alitumia ovyo mali ya tajiri wake. 2 Yule tajiriakamwita akamwambia: Ni mambo gani hayaninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapatona matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezikuwa karani tena. 3 Yule karani akafikiri:Bwana wangu amenifukuza kazi ya ukarani;nitafanya nini? Kwenda kulima siwezi; kwendakuombaomba kama maskini ni aibu. 4 Naam,najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi,watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao. 5

Basi, akawaita wadeni wa bwana wake, mmojammoja, akamwambia yule wa kwanza:Unadaiwa kiasi gani na bwana wangu? 6 Yeyeakamjibu: Mapipa mia ya mafuta ya zeituni.Yule karani akamwambia: Chukua hati yako yadeni, keti haraka, andika hamsini. 7 Kishaakamwuliza mdeni mwingine: Wewe unadaiwakiasi gani? Yeye akamjibu: Magunia mia yangano. Yule karani akamwambia: Chukua hatiyako ya deni, andika themanini. 8 “Basi, yulebwana akamsifu huyo karani asiye mwaminifu,kwa kuwa alitumia busara. Kwa maana watu

LUKA MTAKATIFU 16:8

59

Page 60: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

17

wa dunia hii wana busara zaidi na mambo yaokuliko watu wa mwanga.” 9 Naye Yesuakaendelea kusema, “Nami nawaambieni,jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia,ili zitakapowaishieni, mweze kupokewa naokatika makao ya milele. 10 Yeyote aliyemwaminifu katika mambo madogo, atakuwamwaminifu katika mambo makubwa; nayeyote asiye mwaminifu katika mambomadogo, hatakuwa mwaminifu katika mambomakubwa. 11 Kama basi, ninyi si hamjawawaaminifu mali mbaya za dunia, ni naniatakayewakabidhi zile mali za kweli? 12 Nakama hamjakuwa waaminifu katika mali yamtu mwingine, ni nani atakayewakabidhi maliyenu wenyewe? 13 “Hakuna mtumishi awezayekuwatumikia mabwana wawili; kwa maanaatamchukia mmoja na kumpenda mwingine,au ataambatana na mmoja na kumdharaumwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu namali.” 14 Lakini Mafarisayo waliposikia hayo,kwa vile wao walikuwa wanapenda sana fedha,wakamdharau Yesu. 15 Hapo akawaambia,“Ninyi mnajifanya wema mbele ya watu, lakiniMungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana kilekinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu,Mungu anakiona kuwa takataka. 16 “Sheria namaandishi ya manabii vilikuweko mpakawakati wa Yohane mbatizaji. Tangu hapo,Ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmojaanauingia kwa nguvu. 17 Lakini ni rahisi zaidimbingu na dunia kupita, kuliko hata herufimoja ya Sheria kufutwa. 18 “Yeyoteanayemwacha mke wake na kuoa mwingine,anazini; na yeyote anayemwoa mwanamkealiyepewa talaka, anazini. 19 “Palikuwa na mtummoja tajiri, ambaye alikuwa anavaa mavaziya bei kubwa sana ya rangi ya zambarau, na yakitani safi, na kufanya sherehe kila siku. 20

Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lakeLazaro, aliyekuwa amejaa vidonda na alikuwaanalazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri.21 Lazaro alitamani kula makomboyaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi yahayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulambavidonda vyake! 22 “Ikatokea kwamba huyomaskini akafa, malaika wakamchukua,wakamweka karibu na Abrahamu. Na yuletajiri pia akafa, akazikwa. 23 Huyo tajiri,alikuwa na mateso makali huko kuzimu,akainua macho yake, akamwona Abrahamukwa mbali na Lazaro karibu naye. 24 Basi,akaita kwa sauti: Baba Abrahamu, nioneehuruma; umtume Lazaro angalau achovyencha ya kidole chake katika maji, auburudisheulimi wangu, maana ninateseka mno katikamoto huu. 25 Lakini Abrahamu akamjibu:Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea memayako katika maisha, naye Lazaro akapokeamabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, naweunateswa. 26 Licha ya hayo, kati yetu na ninyikumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kujakwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka

kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze. 27 Huyoaliyekuwa tajiri akasema: Basi baba, nakuombaumtume aende nyumbani kwa baba yangu, 28

maana ninao ndugu watano, ili awaonyewasije wakaja huku kwenye mateso. 29 LakiniAbrahamu akamwambia: Ndugu zako wanaoMose na manabii; waache wawasikilize hao. 30

Lakini yeye akasema: Sivyo baba Abrahamu, ilakama mtu atafufuka kutoka wafu nakuwaendea, watatubu. 31 Naye Abrahamuakasema: Kama hawawasikilizi Mose namanabii, hawatajali hata kama mtu angefufukakutoka wafu.”

Kisha, Yesu akawaambia wanafunziwake, “Haiwezekani kabisa kusitokeevikwazo vinavyosababisha dhambi;

lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha. 2

Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingonijiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini,kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa. 3

Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea,mwonye; akitubu, msamehe. 4 Na kamaakikukosea mara saba kwa siku, na kila maraakarudi kwako akisema Nimetubu, lazimaumsamehe.” 5 Mitume wakamwambia Bwana,“Utuongezee imani.” 6 Naye Bwana akajibu,“Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kamachembe ndogo ya haradali, mngewezakuuambia mti huu wa mkuyu: Ng'okaukajipandikize baharini, nao ungewatii. 7

“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambayeanalima shambani au anachunga kondoo. Je,anaporudi kutoka shambani, atamwambia:Haraka, njoo ule chakula? 8 La! Atamwambia:Nitayarishie chakula, ujifunge tayarikunitumikia mpaka nitakapomaliza kula nakunywa, ndipo nawe ule na unywe. 9 Jeutamshukuru huyo mtumishi kwa sababuametimiza aliyoamriwa? 10 Hali kadhalika naninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni:Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tuyale tuliyotakiwa kufanya.” 11 Yesu akiwasafarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakanimwa Samaria na Galilaya. 12 Alipokuwaanaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenyeukoma walikutana naye, wakasimama kwambali. 13 Wakapaza sauti wakisema, “YesuMwalimu, tuonee huruma!” 14 Alipowaonaakawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwamakuhani.” Basi, ikawa walipokuwawanakwenda, wakatakasika. 15 Mmoja waoalipoona kwamba ameponywa alirudiakimtukuza Mungu kwa sauti kubwa. 16

Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu hukuakimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria. 17

Hapo Yesu akasema, “Je, si watu kumiwalitakaswa? Wale tisa wako wapi? 18

Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuzaMungu ila tu huyu mgeni?” 19 Halafuakamwambia huyo mtu, “Simama, uende zako;imani yako imekuponya.” 20 Wakati mmoja,Mafarisayo walimwuliza Yesu, “Ufalme waMungu utakuja lini?” Naye akawajibu, “Ufalme

LUKA MTAKATIFU 16:9

60

Page 61: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

18

wa Mungu hauji kwa namna itakayowezakuonekana. 21 Wala hakuna atakayewezakusema, Uko hapa, au Uko pale. Kwa kweliUfalme wa Mungu uko kati yenu.” 22 Halafuakawaambia wanafunzi wake, “Siku zinakujaambapo mtatamani kuona mojawapo ya sikuza Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona. 23 Nawatu watawaambieni: Tazameni yuko hapa;ninyi msitoke wala msiwafuate. 24 Kwa maanakama vile umeme unavyotokea ghafla nakuangaza anga upande mmoja hadi mwingine,ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa sikuyake. 25 Lakini kabla ya hayo, itambidi atesekesana na kukataliwa na kizazi hiki. 26 Kamailivyokuwa nyakati za Noa, ndivyoitakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu. 27

Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa nakuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingiakatika safina. Gharika ikatokea nakuwaangamiza wote. 28 Itakuwa kamailivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendeleakula na kunywa, kununua na kuuza, kupandambegu na kujenga. 29 Lakini siku ile Lotialipoondoka Sodoma, moto na kiberitivikanyesha kama mvua kutoka mbinguni nakuwaangamiza wote. 30 Ndivyo itakavyokuwasiku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa. 31

“Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paaasishuke nyumbani kuchukua mali yake.Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudinyuma. 32 Kumbukeni yaliyompata mke waLoti. 33 Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake,ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.34 Nawaambieni, siku ile usiku watu wawiliwatakuwa wanalala pamoja, mmojaatachukuliwa na yule mwingine ataachwa. 35

Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafakapamoja; mmoja atachukuliwa na mwingineataachwa.” 36 Watu wawili watakuwashambani; mmoja atachukuliwa na mwingineataachwa. 37 Hapo wakamwuliza, “Ni wapiBwana?” Naye akawaambia, “Ulipo mzoga,ndipo tai watakapokusanyikia.”

Basi, Yesu aliwasimulia mfanokuonyesha kwamba ni lazima kusalidaima bila kukata tamaa. 2 Alisema:

“Katika mji mmoja kulikuwa na hakimuambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjalibinadamu. 3 Katika mji huohuo, kulikuwa piana mama mmoja mjane, ambaye alimwendeahuyo hakimu mara nyingi akimwombaamtetee apate haki yake kutoka kwa adui yake.4 Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupendakumtetea huyo mjane; lakini, mwishoweakajisemea: Ingawa mimi simchi Mungu walasimjali binadamu, 5 lakini kwa vile huyu mjaneananisumbua, nitamtetea; la sivyo ataendeleakufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!” 6

Basi, Bwana akaendelea kusema, “Sikieni jinsialivyosema huyo hakimu mbaya. 7 Je, ndiokusema Mungu hatawatetea walealiowachagua, ambao wanamlilia mchana nausiku? Je, atakawia kuwasikiliza? 8

Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je,kutakuwako na imani duniani wakati Mwanawa Mtu atakapokuja?” 9 Halafu Yesualiwaambia pia mfano wa wale ambaowalijiona kuwa wema na kuwadharau wengine.10 “Watu wawili walipanda kwenda Hekalunikusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtozaushuru. 11 Huyo Mfarisayo akasimama, akasalikimoyomoyo: Ee Mungu, nakushukuru kwa vilemimi si kama watu wengine: walafi,wadanganyifu au wazinzi. Nakushukurukwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru. 12

Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zakasehemu ya kumi ya pato langu. 13 Lakini yulemtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbalibila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tuakijipiga kifua kwa huzuni, alisema: Ee Mungu,unionee huruma mimi mwenye dhambi. 14

Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudinyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yulemwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikwezaatashushwa, na kila anayejishushaatakwezwa.” 15 Watu walimletea Yesu watotowadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunziwalipowaona, wakawazuia kwa manenomakali. 16 Lakini Yesu akawaita kwakeakisema: “Waacheni hao watoto waje kwangu,wala msiwazuie, kwa maana Ufalme waMungu ni kwa ajili ya watu kama hawa. 17

Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokeaUfalme wa Mungu kama mtoto mdogo,hataingia katika Ufalme huo.” 18 Kiongozimmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, “Mwalimumwema, nifanye nini ili niweze kuupata uzimawa milele?” 19 Yesu akamwambia, “Mbonawaniita mwema? Hakuna aliye mwema ilaMungu peke yake. 20 Unazijua amri: Usizini;usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo;waheshimu baba yako na mama yako.” 21 Yeyeakasema, “Hayo yote nimeyazingatia tanguujana wangu.” 22 Yesu aliposikia hayoakamwambia, “Unatakiwa bado kufanya kitukimoja: uza kila ulicho nacho, wagawiemaskini, na hivyo utakuwa na hazina yakombinguni; halafu njoo unifuate.” 23 Lakinihuyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sanakwa sababu alikuwa tajiri sana. 24 Yesualipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsigani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katikaUfalme wa Mungu! 25 Naam, ni rahisi zaidikwa ngamia kupita katika tundu la sindano,kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”26 Wale watu waliposikia hayo, wakasema,“Nani basi, atakayeokolewa?” 27 Yesu akajibu,“Yasiyowezekana kwa binadamu,yanawezekana kwa Mungu.” 28 Naye Petroakamwuliza, “Na sisi je? Tumeacha vitu vyotetukakufuata!” 29 Yesu akawaambia, “Kwelinawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumbaau mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajiliya Ufalme wa Mungu, 30 atapokea mengi zaidiwakati huu wa sasa, na kupokea uzima wamilele wakati ujao.” 31 Yesu aliwachukua

LUKA MTAKATIFU 18:31

61

Page 62: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

19

kando wale kumi na wawili, akawaambia,“Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na hukokila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusuMwana wa Mtu kitakamilishwa. 32 Kwa maanaatakabidhiwa kwa watu wa mataifa naowatamtendea vibaya na kumtemea mate. 33

Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku yatatu atafufuka.” 34 Lakini wao hawakuelewahata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwamaana ya maneno hayo, na hawakutambuayaliyosemwa. 35 Wakati Yesu alipokaribiaYeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketinjiani akiomba. 36 Aliposikia umati wa watuukipita aliuliza, “Kuna nini?” 37 Wakamwambia,“Yesu wa Nazareti anapita.” 38 Naye akapazasauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi,nihurumie!” 39 Wale watu waliotanguliawakamkemea wakimwambia anyamaze; lakiniyeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi,nihurumie;” 40 Yesu alisimama, akaamuruwamlete mbele yake. Yule kipofu alipofikakaribu, Yesu akamwuliza, 41 “Unatakanikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana,naomba nipate kuona tena.” 42 Yesuakamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.”43 Na mara yule aliyekuwa kipofu akapatakuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu.Watu wote walipoona hayo, wakamsifuMungu.

Yesu aliingia mjini Yeriko, akawaanapita katika njia za mji huo. 2

Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jinalake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru tena mtu tajiri. 3 Alitaka kuona Yesualikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wawatu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. 4

Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu yamkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maanaalikuwa apitie hapo. 5 Basi, Yesu alipofikamahali pale, aliangalia juu akamwambia,“Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazimanishinde nyumbani mwako.” 6 Zakayoakashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. 7

Watu wote walipoona hayo, wakaanzakunung'unika wakisema, “Amekwenda kukaakwa mtu mwenye dhambi.” 8 Lakini Zakayoakasimama akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana!Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, nakama nimenyang'anya mtu yeyote kitu,nitamrudishia mara nne.” 9 Yesuakamwambia, “Leo wokovu umefika katikanyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo waAbrahamu. 10 Kwa maana Mwana wa Mtuamekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” 11

Wakati watu walipokuwa bado wanasikilizahayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwaanakaribia Yerusalemu, na watu walewalidhani kwamba muda si muda, Ufalme waMungu ungefika.) 12 Hivyo akawaambia,“Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalmealiyefanya safari kwenda nchi ya mbali iliapokee madaraka ya ufalme, halafu arudi. 13

Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi

wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kilammoja na kumwambia: Fanyeni nazo biasharampaka nitakaporudi. 14 Lakini wananchiwenzake walimchukia na hivyo wakatumawajumbe waende wakaseme: Hatumtaki huyuatutawale. 15 “Huyo mtu mashuhuri alirudinyumbani baada ya kufanywa mfalme, namara akaamuru wale watumishi aliowapa zilefedha waitwe ili aweze kujua kila mmojaamepata faida gani. 16 Mtumishi wa kwanzaakatokea, akasema: Mheshimiwa, faidailiyopatikana ni mara kumi ya zile fedhaulizonipa. 17 Naye akamwambia: Vema; weweni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwamwaminifu katika jambo dogo, utakuwa namadaraka juu ya miji kumi! 18 Mtumishi wa piliakaja, akasema: Mheshimiwa, faidailiyopatikana ni mara tano ya zile fedhaulizonipa. 19 Naye akamwambia pia: Naweutakuwa na madaraka juu ya miji mitano. 20

“Mtumishi mwingine akaja, akasema: Chukuafedha yako; niliificha salama katika kitambaa,21 kwa maana niliogopa kwa sababu wewe nimtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukuayasiyo yako, na huchuma ambachohukupanda. 22 Naye akamwambia:Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewemtumishi mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtumkali, ambaye huchukua yasiyo yangu nakuchuma nisichopanda. 23 Kwa nini basi,hukuiweka fedha yangu benki, naminingeichukua pamoja na faida baada ya kurudikwangu? 24 Hapo akawaambia walewaliokuwa pale: Mnyang'anyeni hizo fedha,mkampe yule aliyepata faida mara kumi. 25

Nao wakamwambia: Lakini Mheshimiwa, huyoana faida ya kiasi hicho mara kumi! 26 Nayeakawajibu: Kila aliye na kitu atapewa nakuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kilealicho nacho kitachukuliwa. 27 Na sasa,kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendiniwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawauepapa hapa mbele yangu.” 28 Yesu alisemahayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekeaYerusalemu. 29 Alipokaribia kufika Bethfage naBethania, karibu na mlima wa Mizeituni,aliwatuma wanafunzi wake wawili, 30

akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilichombele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini,mtamkuta mwana punda amefungwa ambayehajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamletehapa. 31 Kama mtu akiwauliza, kwa ninimnamfungua, mwambieni, Bwana ana hajanaye.” 32 Basi, wakaenda, wakakuta sawakama alivyowaambia. 33 Walipokuwawanamfungua yule mwana punda, wenyewewakawauliza, “Kwa nini mnamfungua mwanapunda huyu?” 34 Nao wakawajibu, “Bwanaanamhitaji.” 35 Basi, wakampelekea Yesu yulemwana punda. Kisha wakatandika mavazi yaojuu yake wakampandisha Yesu. 36 Yesuakaendelea na safari, na watu wakatandazamavazi yao barabarani. 37 Alipofika karibu na

LUKA MTAKATIFU 18:32

62

Page 63: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

20

Yerusalemu, katika mteremko wa mlima waMizeituni, umati wote na wanafunzi wake,wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungukwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambomakuu waliyoyaona; 38 wakawa wanasema:“Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana.Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!” 39

Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwakokatika lile kundi la watu, wakamwambia Yesu,“Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!” 40

Yesu akawajibu, “Nawaambieni, kama hawawakinyamaza, hakika hayo mawe yatapazasauti.” 41 Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji,Yesu aliulilia 42 akisema: “Laiti ungelijua leo hiiyale yaletayo amani! Lakini sasa yamefichikamachoni pako. 43 Maana siku zaja ambapoadui zako watakuzungushia maboma,watakuzingira na kukusonga pande zote. 44

Watakupondaponda wewe pamoja na watotowako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hatajiwe moja juu jingine, kwa sababuhukuutambua wakati Mungu alipokujiakukuokoa.” 45 Kisha, Yesu aliingia Hekaluni,akaanza kuwafukuzia nje wafanyabiashara 46

akisema, “Imeandikwa: Nyumba yanguitakuwa nyumba ya sala; lakini ninyimmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.” 47

Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni.Makuhani wakuu, walimu wa Sheria naviongozi wa watu walitaka kumwangamiza, 48

lakini hawakuwa na la kufanya, maana watuwote walikuwa wakimsikiliza kwa makinikabisa.

Siku moja, Yesu alipokuwaakiwafundisha watu Hekaluni nakuwahubiria juu ya Habari Njema,

makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamojana wazee walifika, 2 wakasema, “Tuambie!Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?” 3

Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeniswali: 4 mamlaka ya Yohane ya kubatizayalitoka kwa Mungu au kwa watu?” 5 Lakiniwao wakajadiliana hivi: “Tukisema yalitokambinguni, yeye atatuuliza: Mbonahamkumsadiki? 6 Na tukisema yalitoka kwabinadamu, watu wote hapa watatupiga mawe,maana wote wanaamini kwamba Yohanealikuwa nabii.” 7 Basi, wakamwambia, “Hatujuimamlaka hayo yalitoka wapi.” 8 Yesuakawaambia, “Hata mimi sitawaambianinafanya mambo haya kwa mamlaka gani.” 9

Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu:“Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu,akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafirihadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa mudamrefu. 10 Wakati wa mavuno, mtu huyoalimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima,akachukue sehemu ya matunda ya shamba lamizabibu. Lakini wale wakulima wakampigamtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.11 Yule bwana akamtuma tena mtumishimwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevilena kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono

mitupu. 12 Akamtuma tena wa tatu; huyunaye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza. 13

Yule mwenye shamba akafikiri: Nitafanya nini?Nitamtuma mwanangu mpenzi; labdawatamjali yeye. 14 Wale wakulimawalipomwona tu, wakasemezana: Huyu ndiyemrithi. Basi, tumwue ili urithi wake uwe wetu.15 Basi, wakamtoa nje ya lile shamba lamizabibu, wakamwua.” Yesu akauliza, “Yulemwenye shamba atawafanya nini haowakulima? 16 Atakuja kuwaangamizawakulima hao, na atawapa wakulima wenginehilo shamba la mizabibu.” Watu waliposikiamaneno hayo, walisema: “Hasha! Yasitukiehata kidogo!” 17 Lakini Yesu akawatazama,akawaambia, “Maandiko haya Matakatifu yanamaana gani basi? Jiwe walilokataa waashi, sasalimekuwa jiwe kuu la msingi! 18 Mtu yeyoteakianguka juu ya jiwe hilo, atavunjikavipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote,litamsaga kabisa.” 19 Walimu wa Sheria namakuhani wakuu walifahamu kwamba mfanohuo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitakakumkamata palepale, ila tu waliogopa watu. 20

Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa.Wakawahonga watu fulani wajisingizie kuwawema, wakawatuma wamnase Yesu kwamaswali, na hivyo waweze kumtia nguvuni nakumpeleka kwa wakuu wa serikali. 21 Haowapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajuakwamba unasema na kufundisha mambo yakweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi;wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.22 Basi, twambie kama ni halali, au la, kulipakodi kwa Kaisari!” 23 Yesu alitambua mtegowao, akawaambia, 24 “Nionyesheni sarafu. Je,sura na chapa ni vya nani?” 25 Nao wakamjibu,“Ni vya Kaisari.” Yesu akawaambia, “Basi,mpeni Kaisari vilivyo vyake Kaisari, na Munguvilivyo vyake Mungu.” 26 Hawakufaulukumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watuna hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibulake. 27 Kisha Masadukayo, ambao husemakwamba wafu hawafufuki, wakamjia Yesu,wakasema: 28 “Mwalimu, Mose alituandikiakwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa nakumwacha mjane wake bila watoto, ni lazimandugu yake amchukue huyo mama mjane,amzalie watoto ndugu yake marehemu. 29

Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba.Yule wa kwanza alioa na baadaye akafa bilakuacha mtoto. 30 Yule ndugu wa pili akamwoayule mjane, naye pia, akafa; 31 na ndugu watatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wotesaba—wote walikufa bila kuacha watoto. 32

Mwishowe akafa pia yule mwanamke. 33 Je,siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyoatakuwa mke wa nani? Alikuwa ameolewa nawote saba.” 34 Yesu akawaambia, “Watu wanyakati hizi huoa na kuolewa; 35 lakini waleambao Mungu atawawezesha kushiriki ulewakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa. 36

Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu

LUKA MTAKATIFU 20:36

63

Page 64: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

21

watakuwa kama malaika, na ni watoto waMungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu. 37

Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu,hata Mose alithibitisha jambo hilo katikaMaandiko Matakatifu. Katika sehemu yaMaandiko Matakatifu juu ya kile kichakakilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwanakama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.38 Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Munguwa wale walio hai; maana wale aliowaitakwake, wanaishi naye.” 39 Baadhi ya walewalimu wa Sheria wakasema, “Mwalimu,umejibu vema kabisa.” 40 Walisema hivyo kwasababu hawakuthubutu kumwuliza tenamaswali mengine. 41 Yesu akawauliza,“Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana waDaudi? 42 Maana Daudi mwenyewe anasemakatika Zaburi: Bwana alimwambia Bwanawangu: Keti upande wangu wa kulia 43 mpakaniwafanye adui zako kama kiti cha kuwekeamiguu yako. 44 Ikiwa Daudi anamwita yeye,Bwana, basi atakuwaje mwanawe?” 45 Yesualiwaambia wanafunzi wake mbele ya watuwote, 46 “Jihadharini na walimu wa Sheriaambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshimamasokoni, huketi mahali pa heshima katikamasunagogi na kuchukua nafasi za heshimakatika karamu. 47 Huwadhulumu wajane hukuwakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu.Hao watapata hukumu kali zaidi!”

Yesu alitazama kwa makini, akawaonamatajiri walivyokuwa wanatia sadakazao katika hazina ya Hekalu, 2

akamwona pia mama mmoja mjaneakitumbukiza humo sarafu mbili ndogo. 3

Basi, akasema, “Nawaambieni kweli, mamahuyu mjane ametia zaidi katika hazina kulikowote. 4 Kwa maana, wengine wote wametoasadaka zao kutokana na ziada ya mali zao,lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoakila kitu alichohitaji kwa kuishi.” 5 Baadhi yawanafunzi walikuwa wanazungumza juu yaHekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe yathamani, pamoja na sadaka zilizotolewa kwaMungu. Yesu akasema, 6 “Haya yotemnayoyaona—zitakuja siku ambapo hakunahata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kilakitu kitaharibiwa.” 7 Basi, wakamwuliza,“Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na niishara gani zitakazoonyesha kwamba karibumambo hayo yatokee?” 8 Yesu akawajibu,“Jihadharini, msije mkadanganyika. Maanawengi watatokea na kulitumia jina languwakisema: Mimi ndiye, na, Wakati uleumekaribia. Lakini ninyi msiwafuate! 9 Basi,mtakaposikia habari za vita na misukosuko,msitishike; maana ni lazima hayo yatokeekwanza, lakini mwisho wa yote, bado.” 10

Halafu akaendelea kusema: “Taifa mojalitapigana na taifa lingine, na ufalme mmojautapigana na ufalme mwingine. 11 Kila mahalikutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi,

kutakuwa na njaa na tauni. Kutakuwa navituko vya kutisha na ishara kubwa angani. 12

Lakini kabla ya kutokea hayo yote, watawatieninguvuni, watawatesa na kuwapelekeni katikamasunagogi na kuwatia gerezani; mtapelekwambele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jinalangu. 13 Hii itawapeni fursa ya kushuhudiaHabari Njema. 14 Muwe na msimamo huumioyoni mwenu: hakuna kufikiria kabla yawakati juu ya jinsi mtakavyojitetea, 15 kwasababu mimi mwenyewe nitawapeni ufasahawa maneno na hekima, hivyo kwamba zenuhawataweza kustahimili wala kupinga. 16

Wazazi wenu, ndugu, jamaa na rafiki zenuwatawasaliti ninyi; na baadhi yenu mtauawa.17 Watu wote watawachukieni kwa sababu yajina langu. 18 Lakini, hata unywele mmoja wavichwa vyenu hautapotea. 19 Kwa uvumilivuwenu, mtayaokoa maisha yenu. 20

“Mtakapoona mji wa Yerusalemuumezungukwa na majeshi, ndipo mtambue yakwamba wakati umefika ambapo mji huoutaharibiwa. 21 Hapo walioko Yudeawakimbilie milimani; wale walio mjini watoke;na wale walio mashambani wasirudi mjini. 22

Kwa maana siku hizo ni siku za adhabu, ili yoteyaliyoandikwa yatimie. 23 Ole wao waja wazitona wanyonyeshao siku hizo! Kwa maanakutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasiraya Mungu itawajia watu hawa. 24 Wenginewatauawa kwa upanga, wenginewatachukuliwa mateka katika nchi zote; na mjiwa Yerusalemu utakanyagwa na watu wamataifa mengine, hadi nyakati zaozitakapotimia. 25 “Kutakuwa na ishara katikajua na mwezi na nyota. Mataifa dunianiyatakuwa na dhiki kwa sababu ya wasiwasikutokana na mshindo wa mawimbi ya bahari.26 Watu watazirai kwa sababu ya uoga,wakitazamia mambo yatakayoupataulimwengu; kwa maana nguvu za mbinguzitatikiswa. 27 Halafu, watamwona Mwana waMtu akija katika wingu, mwenye nguvu nautukufu mwingi. 28 Wakati mambo hayoyatakapoanza kutukia, simameni na kuinuavichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenuumekaribia.” 29 Kisha akawaambia mfano:“Angalieni mtini na miti mingine yote. 30

Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani,mwatambua kwamba wakati wa kiangaziumekaribia. 31 Vivyo hivyo, mtakapoonamambo hayo yanatendeka, mtatambuakwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32

Nawaambieni hakika, kizazi hiki cha sasahakitapita kabla ya hayo yote kutendeka. 33

Mbingu na dunia vitapita, lakini maneno yanguhayatapita. 34 “Muwe macho, mioyo yenu isijeikalemewa na anasa, ulevi na shughuli zamaisha haya. La sivyo, Siku ile itawajienighafla. 35 Kwa maana itawajia kama mtego,wote wanaoishi duniani pote. 36 Muwewaangalifu basi, na salini daima ili muwezekupata nguvu ya kupita salama katika mambo

LUKA MTAKATIFU 20:37

64

Page 65: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

22

haya yote yatakayotokea, na kusimama mbeleya Mwana wa Mtu.” 37 Wakati wa mchana, sikuhizo, Yesu alikuwa akifundisha watu Hekaluni;lakini usiku alikuwa akienda katika mlima waMizeituni na kukaa huko. 38 Watu wotewalikuwa wanakwenda Hekaluni asubuhi namapema, wapate kumsikiliza.

Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu,iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia. 2

Makuhani wakuu na walimu wa Sheriawakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu,lakini waliwaogopa watu. 3 Basi, Shetaniakamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wawale mitume kumi na wawili. 4 Yuda akaendaakajadiliana na makuhani wakuu na walinzi waHekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao. 5

Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipafedha. 6 Yuda akakubali, na akawa anatafutanafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wawatu kujua. 7 Basi, siku ya Mikate Isiyotiwachachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa. 8 Hivyo Yesuakawatuma Petro na Yohane, akawaambia,“Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kulaPasaka.” 9 Nao wakamwuliza, “Unatakatuiandae wapi?” 10 Akawaambia, “Sikilizeni!Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutanana mwanamume anayebeba mtungi wa maji.Mfuateni mpaka ndani ya nyumbaatakayoingia. 11 Mwambieni mwenye nyumba:Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumbaambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunziwangu? 12 Naye atawaonyesheni chumbakikubwa ghorofani ambacho kimepambwa.Andalieni humo.” 13 Basi, wakaenda, wakakutakila kitu sawa kama Yesu alivyokuwaamewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.14 Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakulapamoja na mitume wake. 15 Akawaambia,“Nimetamani sana kula Pasaka hii pamojananyi kabla ya kuteswa kwangu. 16 Maananawaambieni, sitaila tena hadi hapoitakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.” 17

Kisha akatwaa kikombe, akashukuru akasema,“Pokeeni, mgawanye ninyi kwa ninyi. 18 Kwamaana nawaambieni, sitakunywa tena divai yazabibu mpaka Ufalme wa Munguutakapokuja.” 19 Halafu akatwaa mkate,akashukuru, akaumega, akawapa akisema,“Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajiliyenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” 20

Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada yachakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipyalinalothibitishwa kwa damu yanguinayomwagika kwa ajili yenu. 21 “Lakini,tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapamezani. 22 Kweli Mwana wa Mtu anakwendakuuawa kama ilivyopangwa, lakini ole wakemtu anayemsaliti.” 23 Hapo wakaanzakuulizana wao kwa wao ni nani kati yaoatakayefanya jambo hilo. 24 Kulitokea ubishikati ya hao mitume kuhusu nani miongonimwao anayefikiriwa kuwa mkuu zaidi kuliko

wengine. 25 Yesu akawaambia, “Wafalme wamataifa huwatawala watu wao kwa mabavu,nao huitwa wafadhili wa watu. 26 Lakini isiwehivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenuni lazima awe mdogo wa wote, na aliyekiongozi lazima awe kama mtumishi. 27 Kwamaana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketimezani kula chakula, ama yule anayetumikia?Bila shaka ni yule anayeketi mezani kulachakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenukama mtumishi. 28 “Ninyi ndio mliobaki namiwakati wote wa majaribu yangu; 29 na, kamavile Baba yangu alivyonikabidhi Ufalme, vivyohivyo nami nitawakabidhi ninyi Ufalme. 30

Mtakula na kunywa mezani pangu katikaufalme wangu, na mtaketi katika viti vya enzikuyahukumu makabila kumi na mawili yaIsraeli. 31 “Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetanialitaka kuwapepeta ninyi kama mtuanavyopepeta ngano. 32 Lakini miminimekuombea ili imani yako isipungue. Naweutakaponirudia, watie moyo ndugu zako.” 33

Naye Petro akamjibu, “Bwana, mimi niko tayarikwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa.”34 Yesu akamjibu, “Nakwambia wewe Petro,kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikanamara tatu.” 35 Kisha, Yesu akawaulizawanafunzi wake, “Wakati nilipowatuma bilamfuko wa fedha wala mkoba wala viatu,mlitindikiwa chochote?” Wakajibu, “La.” 36

Naye akawaambia, “Lakini sasa, yule aliye namfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba,hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga,auze koti lake anunue mmoja. 37 Maananawaambieni, haya maneno ya MaandikoMatakatifu: Aliwekwa kundi moja na wahalifu,ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusuyanafikia ukamilifu wake.” 38 Nao wakasema,“Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili.” Nayeakasema, “Basi!” 39 Yesu akatoka, na kamailivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlimawa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata. 40

Alipofika huko akawaambia, “Salini, msijemkaingia katika kishawishi.” 41 Kishaakawaacha, akaenda umbali wa mtu kuwezakutupa jiwe, akapiga magoti, akasali: 42 “Baba,kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombehiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, walasiyo yangu.” 43 Hapo, malaika kutokambinguni, akamtokea ili kumtia moyo. 44

Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwabidii zaidi; na jasho likamtoka, kama matone yadamu, likatiririka mpaka chini. 45 Baada yakusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakutawamelala, kwani walikuwa na huzuni. 46

Akawaambia, “Mbona mnalala? Amkeni msali,msije mkaingia katika kishawishi.” 47

Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likajalikiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wawale mitume kumi na wawili. Yuda akaendakumsalimu Yesu kwa kumbusu. 48 Lakini Yesuakamwambia, “Yuda! Je, unamsaliti Mwana waMtu kwa kumbusu?” 49 Wale wanafunzi wake

LUKA MTAKATIFU 22:49

65

Page 66: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

23

walipoona hayo wakasema, “Bwana, tutumiepanga zetu?” 50 Na mmoja wao akampigaupanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkatasikio lake la kulia. 51 Hapo, Yesu akasema,“Acha! Hii inatosha.” Akaligusa sikio la mtuhuyo akaliponya. 52 Kisha Yesu akawaambiamakuhani wakuu, wakubwa wa walinzi waHekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je,mmekuja na mapanga na marungukunikamata kana kwamba mimi nimnyang'anyi? 53 Nilipokuwa pamoja nanyi kilasiku Hekaluni hamkunitia nguvuni. Lakini, huundio wakati wenu hasa, ndio wakati wautawala wa giza.” 54 Basi, wakamkamata,wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwaKuhani Mkuu. Petro akawa anamfuata nyumakwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwakatikati ya ua, nao wakawa wameketi pamojaPetro akiwa miongoni mwao. 56 Mjakazimmoja alipomwona Petro ameketi karibu namoto, akamkodolea macho, akasema, “Mtuhuyu alikuwa pia pamoja na Yesu.” 57 LakiniPetro akakana akisema, “Wee! simjui mimi.” 58

Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwonaPetro, akasema, “Wewe ni mmoja wao.” LakiniPetro akajibu “Bwana we; si mimi!” 59 Kamasaa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza,“Hakika huyu alikuwa pamoja naye; ametokaGalilaya ati.” 60 Lakini Petro akasema, “Bwanawee; sijui hata unachosema!” Na papo hapo,akiwa bado anaongea, jogoo akawika. 61

Bwana akageuka na kumtazama Petro, nayePetro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwana Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika,utanikana mara tatu.” 62 Hapo akatoka nje,akalia sana. 63 Wale watu waliokuwawanamchunga Yesu, walimpiga nakumdhihaki. 64 Walimfunga kitambaa usoni,wakawa wanamwuliza, “Ni nani aliyekupiga?Hebu bashiri tuone!” 65 Wakamtolea manenomengi ya matusi. 66 Kulipokucha, kikao chawazee wa watu kilifanyika, ambachokilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimuwa Sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.67 Nao wakamwambia, “Twambie! Je, wewendiwe Kristo?” Lakini Yesu akawaambia, “Hatakama nikiwaambieni, hamtasadiki; 68 na hatakama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu. 69

Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwaameketi upande wa kulia wa MunguMwenyezi.” 70 Hapo wote wakasema, “Ndiyokusema wewe ni Mwana wa Mungu?” Nayeakasema, “Ninyi mnasema kwamba mimindiye.” 71 Nao wakasema, “Je, tunahitajiushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikiaakisema kwa mdomo wake mwenyewe.”

Kisha, wote kwa jumla, wakasimama,wakampeleka Yesu mbele ya Pilato. 2

Wakaanza kumshtaki wakisema:“Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha watu wetu,akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita atiyeye ni Kristo, Mfalme.” 3 Pilato akamwulizaYesu, “Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Yesu

akamjibu, “Wewe umesema.” 4 Pilatoakawaambia makuhani wakuu na umati wawatu, “Sioni kosa lolote katika mtu huyu.” 5

Lakini wao wakasisitiza wakisema:“Anawachochea watu kwa mafundisho yakekatika nchi yote ya Yudea; alianza Galilaya, nasasa yuko hapa.” 6 Pilato aliposikia hayo,akauliza, “Je, mtu huyu ni mwenyeji waGalilaya?” 7 Alipojua kwamba Yesu alikuwachini ya utawala wa Herode, akampeleka kwaHerode, ambaye wakati huo alikuwaYerusalemu. 8 Herode alifurahi sanaalipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikiahabari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwamuda mrefu kumwona kwa macho yakemwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumainikumwona Yesu akitenda mwujiza. 9 Basi,akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu,lakini Yesu hakumjibu neno. 10 Makuhaniwakuu na walimu wa Sheria wakajitokezambele, wakatoa mashtaka yao kwa nguvusana. 11 Basi, herode pamoja na maaskariwake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyiamzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme,wakamrudisha kwa Pilato. 12 Herode na Pilato,ambao hapo awali walikuwa maadui, tangusiku hiyo wakawa marafiki. 13 Basi, Pilatoakaitisha mkutano wa makuhani wakuu,viongozi na watu, 14 akawaambia, “Mmemletamtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwaanawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada yakuchunguza jambo hilo mbele yenu,sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtakayenu juu yake. 15 Wala si mimi tu, bali hataHerode hakuona kosa lolote, kwa maanaamemrudisha kwangu. Ni dhahiri kwamba mtuhuyu hakufanya chochote kinachostahiliadhabu ya kifo. 16 Hivyo, nitaamuru apigweviboko, halafu nitamwachilia.” 17 Kila sikukuuya Pasaka, ilimlazimu Pilato kuwafunguliamfungwa mmoja. 18 Lakini wote wakapigakelele pamoja: “Mwondoe huyo, utufungulieBaraba!” 19 (Baraba alikuwa ametiwa ndanikwa kusababisha uasi katika mji na pia kwasababu ya kuua.) 20 Pilato alitaka kumwachiliaYesu, hivyo akasema nao tena; 21 lakini waowakapiga kelele: “Msulubishe, msulubishe!” 22

Pilato akawaambia mara ya tatu, “Amefanyakosa gani? Sioni kosa lolote kwakelinalomstahili auawe; kwa hiyo nitampigaviboko, halafu nimwachilie.” 23 Lakini waowakazidi kupiga kelele kwa nguvu sana,kwamba Yesu ni lazima asulubiwe. Mwishowe,sauti zao zikashinda. 24 Basi, Pilato akaamuakwamba matakwa yao yatimizwe. 25

Akamfungua kutoka gerezani yulewaliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwagerezani kwa sababu ya uasi na kuua; akamtoaYesu kwao, wamfanyie walivyotaka. 26

Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtummoja, aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwaanatoka shambani. Basi, walimkamata,wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya

LUKA MTAKATIFU 22:50

66

Page 67: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

24

Yesu. 27 Watu, umati kwa umati, walimfuata;miongoni mwao wakiwemo wanawakewaliokuwa wanaomboleza na kumlilia. 28 Yesuakawageukia, akasema, “Enyi kina mama waYerusalemu! Msinililie mimi, ila lieni kwa ajiliyenu wenyewe na kwa ajili ya watoto wenu. 29

Maana, hakika siku zitakuja ambapowatasema: Heri yao wale walio tasa, ambaohawakupata kuzaa wala kunyonyesha watoto!30 Wakati huo, ndipo watu wataanza kuiambiamilima: Tuangukieni! na vilima, Tufunikeni! 31

Kwa maana, kama watu wanautendea mtimbichi namna hiyo, itakuwaje kwa mtimkavu?” 32 Waliwachukua pia watu wenginewawili, wahalifu, wauawe pamoja naye. 33

Walipofika mahali paitwapo, “Fuvu la Kichwa,”ndipo wakamsulubisha Yesu pamoja na walewahalifu wawili, mmoja upande wake wa kuliana mwingine upande wake wa kushoto. 34

Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maanahawajui wanalofanya.” Kisha wakagawanamavazi yake kwa kuyapigia kura. 35 Watuwakawa wamesimama pale wakitazama. Naoviongozi wakamdhihaki wakisema:“Amewaokoa wengine; sasa na ajiokoemwenyewe, kama yeye ndiye Kristo, mteule waMungu!” 36 Askari nao walimdhihaki pia;walimwendea wakampa siki 37 wakisema:“Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi,jiokoe mwenyewe.” 38 Vilevile maandishi hayayalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake:“Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.” 39 Mmojawa wale wahalifu waliotundikwa msalabani,alimtukana akisema: “Je, si kweli kwambawewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe,utuokoe na sisi pia.” 40 Lakini yule mhalifumwingine akamkemea mwenzake akisema:“Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Weweumepata adhabu hiyohiyo. 41 Wewe na mimitunastahili, maana haya ni malipo ya yaletuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanyachochote kibaya.” 42 Kisha akasema, “Ee Yesu!Unikumbuke wakati utakapoingia katikaufalme wako.” 43 Yesu akamwambia,“Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamojanami peponi.” 44 Ilikuwa yapata saa sitamchana; jua likaacha kuangaza, giza likafunikanchi yote mpaka saa tisa, 45 na pazia lililokuwalimetundikwa Hekaluni likapasuka vipandeviwili. 46 Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba,naiweka roho yangu mikononi mwako.”Alipokwisha sema hayo, akakata roho. 47

Hapo, yule jemadari alipoona yaliyotukiaakamsifu Mungu akisema: “Hakika huyualikuwa mtu mwema.” 48 Watu wale wotewaliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili yatukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudimakwao wakijipiga vifua kwa huzuni. 49

Marafiki zake wote pamoja na wale wanawakewalioandamana naye kutoka Galilaya,walisimama kwa mbali kutazama tukio hilo. 50

Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yosefu,mwenyeji wa kijiji kimoja cha Wayahudi

kiitwacho Armathaya. Alikuwa mtu mwemaanayeheshimika; 51 Alikuwa akitazamia kujakwa Ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwammoja wa Baraza kuu la Wayahudi, hakuwaamekubaliana nao katika kitendo chao. 52

Basi, yeye alikwenda kwa Pilato, akaombaapewe mwili wa Yesu. 53 Kisha, akaushushamwili huo kutoka msalabani, akauzungushiasanda ya kitani, akauweka katika kaburilililokuwa limechongwa kwenye mwamba,ambalo halikuwa limetumika. 54 Siku hiyoilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabatoyalikuwa yanaanza. 55 Wale wanawakewalioandamana na Yesu kutoka Galilayawalimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi najinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa 56 Halafu,walirudi nyumbani, wakatayarisha manukatona marashi kuyapaka mwili wa Yesu. Siku yaSabato walipumzika kama ilivyoamriwa nasheria.

Jumapili, alfajiri na mapema, walewanawake walikwenda kaburiniwakichukua yale manukato

waliyotayarisha. 2 Walikuta lile jiwelimeviringishwa mbali na kaburi. 3 Walipoingiandani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4

Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambohilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenyekung'aa sana, wakasimama karibu nao. 5 Haowanawake wakaingiwa na hofu, wakainamachini. Ndipo wale watu wakawaambia, “Kwanini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu? 6

Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukenialiyowaambieni alipokuwa kule Galilaya: 7 Nilazima Mwana wa Mtu atolewe kwa watuwaovu, nao watamsulubisha, na siku ya tatuatafufuka.” 8 Hapo wanawakewakayakumbuka maneno yake, 9 wakarudikutoka kaburini, wakawapa mitume wale kumina mmoja na wengine habari za mambo hayoyote. 10 Hao waliotoa habari hizo kwa mitumeni: Maria Magdalene, Yoana na Maria mamawa Yakobo, pamoja na wanawake wenginewalioandamana nao. 11 Mitume waliyachukuamaneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyohawakuamini. 12 Lakini Petro alitoka, akaendambio hadi kaburini. Alipoinama kuchunguliandani, akaiona tu ile sanda. Akarudi nyumbanihuku akiwa anashangaa juu ya hayoyaliyotokea. 13 Siku hiyohiyo, wawili kati yawafuasi wake Yesu wakawa wanakwendakatika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wakilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu. 14

Wakawa wanazungumza juu ya hayo yoteyaliyotukia. 15 Walipokuwa wakizungumza nakujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea,akatembea pamoja nao. 16 Walimwona kwamacho, lakini hawakumtambua. 17

Akawauliza, “Mnazungumza nini hukumnatembea?” Nao wakasimama kimya, nyusozao wamezikunja kwa huzuni. 18 Mmoja,aitwaye Kleopa, akamjibu, “Je, wewe ni mgenipeke yako Yerusalemu ambaye hujui

LUKA MTAKATIFU 24:18

67

Page 68: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

yaliyotukia huko siku hizi?” 19 Naye akawajibu,“Mambo gani?” Wao wakamjibu, “Mamboyaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwanabii mwenye uwezo wa kutenda nakufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watuwote. 20 Makuhani na watawala wetuwalimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha.21 Lakini sisi tulitumaini kwamba yeye ndiyeangeikomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo nisiku ya tatu tangu mambo hayo yalipotendeka.22 Tena, wanawake wengine wa kwetuwametushtua. Walikwenda kaburini mapemaasubuhi, 23 wasiukute mwili wake. Wakarudiwakasema kwamba walitokewa na malaikawaliowaambia kwamba alikuwa hai. 24

Wengine wetu walikwenda kaburiniwakashuhudia yale waliyosema haowanawake; ila yeye hawakumwona.” 25 KishaYesu akawaambia, “Mbona mu wapumbavukiasi hicho na mioyo yenu ni mizito hivyokusadiki yote yaliyonenwa na manabii? 26 Je,haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingiekatika utukufu wake?” 27 Akawafafanuliamambo yote yaliyomhusu yeye katikaMaandiko Matakatifu kuanzia Mose hadimanabii wote. 28 Walipokikaribia kile kijijiwalikokuwa wanakwenda, Yesu akafanya kanakwamba anaendelea na safari; 29 lakini waowakamsihi wakisema, “Kaa pamoja nasi,maana kunakuchwa, na usiku unakaribia.”Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao. 30

Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukuamkate, akaubariki, akaumega, akawapa. 31

Mara macho yao yakafumbuliwa,wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.32 Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwainawaka ndani yetu wakati alipokuwaanatufafanulia Maandiko Matakatifu kulenjiani?” 33 Wakaondoka saa ileile, wakarudiYerusalemu: wakawakuta wale mitume kumina mmoja na wale wengine waliokuwa pamojanao, wamekusanyika 34 wakisema, “HakikaBwana amefufuka, amemtokea Simoni.” 35

Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yaleyaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambuakatika kumega mkate. 36 Wanafunzi wotewawili walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesumwenyewe akasimama kati yao, akawaambia“Amani kwenu.” 37 Wakashtuka na kushikwana hofu wakidhani wameona mzimu. 38 Lakiniyeye akawaambia, “Kwa nini mnafadhaika?Mbona mnakuwa na mashaka mioyonimwenu? 39 Angalieni mikono na miguu yangu,ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapasenimkanione, maana mzimu hauna mwili namifupa kama mnionavyo.” 40 Baada yakusema hayo, akawaonyesha mikono namiguu. 41 Wakiwa bado katika hali yakutosadiki kwa sababu ya furaha yao, nawakiwa wanastaajabu, akawauliza, “Mnachochakula chochote hapa?” 42 Wakampa kipandecha samaki wa kuokwa. 43 Akakichukua, akala,wote wakimwona. 44 Halafu akawaambia, “Hiindiyo maana ya maneno niliyowaambianilipokuwa pamoja nanyi: kwamba ilikuwalazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juuyangu katika Sheria ya Mose na katika vitabuvya manabii na katika kitabu cha Zaburi.” 45

Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewaMaandiko Matakatifu. 46 Akawaambia, “Ndivyoilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na sikuya tatu atafufuka kutoka wafu, 47 na kwambani lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanziana Yerusalemu yahubiriwe juu ya kutubu nakusamehewa dhambi. 48 Ninyi ni mashahidiwa mambo hayo. 49 Nami mwenyewenitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidikumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpakamtakapopewa ile nguvu itokayo juu.” 50 Kishaakawaongoza nje ya mji hadi Bethania,akainua mikono yake juu, akawabariki. 51

Alipokuwa anawabariki, akawaacha;akachukuliwa mbinguni. 52 Waowakamwabudu, wakarudi Yerusalemu wakiwana furaha kubwa: 53 wakakaa muda woteHekaluni wakimsifu Mungu.

LUKA MTAKATIFU 24:19

68

Page 69: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

YOHANA MTAKATIFU

Hapo Mwanzo, Neno alikuwako; nayealikuwa na Mungu, naye alikuwaMungu. 2 Tangu mwanzo Neno alikuwa

na Mungu. 3 Kwa njia yake vitu vyoteviliumbwa; hakuna hata kiumbe kimojakilichoumbwa pasipo yeye. 4 Yeye alikuwachanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwangawa watu. 5 Na mwanga huo huangaza gizani,nalo giza halikuweza kuushinda. 6 Mungualimtuma mtu mmoja jina lake Yohane, 7

ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huomwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watuwote wapate kuamini. 8 Yeye hakuwa huomwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu yahuo mwanga. 9 Huu ndio mwanga halisi,mwanga unaokuja ulimwenguni, nakuwaangazia watu wote. 10 Basi, Nenoalikuwako ulimwenguni; na kwa njia yakeulimwengu uliumbwa, lakini ulimwenguhaukumtambua. 11 Alikuja katika nchi yakemwenyewe, nao walio wake hawakumpokea.12 Lakini wale wote waliompokea nakumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwawatoto wa Mungu. 13 Hawa wamekuwawatoto wa Mungu si kwa uwezo wakibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, walakwa mapenzi ya mtu, bali Mungu mwenyewendiye baba yao. 14 Naye Neno akawamwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuonautukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwanawa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli.15 Yohane aliwaambia watu habari zake,akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtajawakati niliposema: Anakuja mtu mmoja baadayangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maanaalikuwako kabla mimi sijazaliwa.” 16 Kutokanana ukamilifu wake sisi tumepokea neemamfululizo. 17 Maana Mungu alitoa Sheria kwanjia ya Mose, lakini neema na kweli vimekujakwa njia ya Kristo. 18 Hakuna mtu aliyemwonaMungu wakati wowote ule. Mwana wa pekeealiye sawa na Mungu ambaye ameungana naBaba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu. 19

Huu ndio ushahidi Yohane alioutoa wakativiongozi wa Wayahudi kule Yerusalemuwalipowatuma makuhani wa Walawi kwakewamwulize: “Wewe u nani?” 20 Yohanehakukataa kujibu swali hilo, bali alisemawaziwazi, “Mimi siye Kristo.” 21 Hapowakamwuliza, “Basi, wewe ni nani? Je, wewe niEliya?” Yohane akajibu, “La, mimi siye.”Wakamwuliza, “Je, wewe ni yule nabii?” Yohaneakawajibu, “La!” 22 Nao wakamwuliza, “Basi,

wewe ni nani? Wasema nini juu yakomwenyewe? Tuambie, ili tuwapelekee jibu walewaliotutuma.” 23 Yohane akawajibu, “Mimindiye yule ambaye nabii Isaya alisema habarizake: Sauti ya mtu imesikika jangwani:Nyoosheni njia ya Bwana.” 24 Hao watuwalikuwa wametumwa na Mafarisayo. 25 Basi,wakamwuliza Yohane, “Kama wewe si Kristo,wala Eliya, wala yule nabii, mbona wabatiza?”26 Yohane akawajibu, “Mimi nabatiza kwa maji,lakini yuko mmoja kati yenu, msiyemjua bado.27 Huyo anakuja baada yangu, lakini mimisistahili hata kumfungua kamba za viatuvyake.” 28 Mambo haya yalifanyika hukoBethania, ng'ambo ya mto Yordani ambakoYohane alikuwa anabatiza. 29 Kesho yake,Yohane alimwona Yesu akimjia, akasema,“Huyu ndiye Mwana-kondoo wa Munguaondoaye dhambi ya ulimwengu! 30 Huyundiye niliyesema juu yake: Baada yanguanakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kulikomimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakininimekuja kubatiza kwa maji ili watu wa Israeliwapate kumjua.” 32 Huu ndio ushahidi Yohanealioutoa: “Nilimwona Roho akishuka kamanjiwa kutoka mbinguni na kutua juu yake. 33

Mimi sikumjua, lakini yule aliyenitumanikabatize watu kwa maji alikuwa ameniambia:Mtu yule utakayemwona Roho akimshukiakutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyondiye anayebatiza kwa Roho Mtakatifu. 34

Mimi nimeona na ninawaambieni kwambahuyu ndiye Mwana wa Mungu.” 35 Kesho yake,Yohane alikuwa tena mahali hapo pamoja nawanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Yesuakipita akasema, “Tazameni! Huyu ndiyeMwana-kondoo wa Mungu.” 37 Hao wanafunziwalimsikia Yohane akisema maneno hayo,wakamfuata Yesu. 38 Basi, Yesu aligeuka, naalipowaona hao wanafunzi wanamfuata,akawauliza, “Mnatafuta nini?” Nao wakamjibu,“Rabi (yaani Mwalimu), unakaa wapi?” 39 Yesuakawaambia, “Njoni, nanyi mtaona.” Haowanafunzi wakamfuata, wakaona mahalialipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo.Ilikuwa yapata saa kumi jioni. 40 Andrea,nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa haowawili waliokuwa wamemsikia Yohaneakisema hivyo, wakamfuata Yesu. 41 Andreaalimkuta kwanza Simoni, ndugu yake,akamwambia, “Tumemwona Masiha” (maanayake Kristo). 42 Kisha akampeleka Simoni kwa

YOHANA MTAKATIFU 1:42

69

Page 70: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

23

Yesu. Naye Yesu akamtazama Simoni akasema,“Wewe ni Simoni mwana wa Yohane. Sasautaitwa Kefa.” (maana yake ni Petro, yaani,“Mwamba.”) 43 Kesho yake Yesu aliamuakwenda Galilaya. Basi, akamkuta Filipo,akamwambia, “Nifuate.” 44 Filipo alikuwamwenyeji wa Bethsaida, mji wa akina Andreana Petro. 45 Naye Filipo akamkuta Nathanieli,akamwambia, “Tumemwona yule ambayeMose aliandika juu yake katika kitabu chaSheria, na ambaye manabii waliandika habarizake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu, kutokaNazareti.” 46 Naye Nathanieli akamwulizaFilipo, “Je, kitu chema chaweza kutokaNazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.” 47

Yesu alipomwona Nathanieli akimjia alisemajuu yake, “Tazameni! Huyo ni Mwisraeli halisi:hamna hila ndani yake.” 48 Naye Nathanieliakamwuliza, “Umepataje kunijua?” Yesuakamwambia, “Ulipokuwa chini ya mtini hatakabla Filipo hajakuita, nilikuona.” 49 HapoNathanieli akamwambia, “Mwalimu, wewe niMwana wa Mungu. Wewe ni Mfalme waIsraeli!” 50 Yesu akamwambia, “Je, umeaminikwa kuwa nimekwambia kwamba nilikuonachini ya mtini? Utaona makubwa zaidi kulikohaya.” 51 Yesu akaendelea kusema,“Nawaambieni kweli, mtaona mbinguzinafunguka na malaika wa Mungu wakipandana kushuka juu ya Mwana wa Mtu.”

Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjiniKana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesualikuwapo, 2 naye Yesu alikuwa

amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.3 Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia,“Hawana divai!” 4 Yesu akamjibu, “Mama,usiniambie la kufanya. Saa yangu bado.” 5

Hapo mama yake akawaambia watumishi,“Lolote atakalowaambieni, fanyeni.” 6 Hapopalikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kilammoja uliweza kuchukua kiasi cha madebemawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapokufuatana na desturi ya Kiyahudi yakutawadha. 7 Yesu akawaambia, “Ijazenimitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu.8 Kisha akawaambia, “Sasa chotenimkampelekee mkuu wa karamu.” 9 Mkuu wakaramu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwayamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka,(lakini wale watumishi waliochota maji walijua).Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi, 10

akamwambia, “Kila mtu huandaa divai nzurikwanza hata wakisha tosheka huandaa ilehafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzurimpaka sasa!” 11 Yesu alifanya ishara hii yakwanza huko Kana, Galilaya, akaonyeshautukufu wake; nao wanafunzi wakewakamwamini. 12 Baada ya hayo, Yesualishuka pamoja na mama yake, ndugu zakena wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumuambako walikaa kwa siku chache. 13 Sikukuuya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia;hivyo Yesu akaenda Yerusalemu. 14 Hekaluni

aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo nanjiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaakwenye meza zao. 15 Akatengeneza mjelediwa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalupamoja na kondoo na ng'ombe wao,akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha nakupindua meza zao. 16 Akawaambia walewaliokuwa wanauza njiwa, “Ondoeni vitu hivihapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwasoko!” 17 Wanafunzi wake wakakumbukakwamba Maandiko yasema: “Upendo wangukwa nyumba yako waniua.” 18 Baadhi yaWayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanyamuujiza gani kuonyesha kwamba unayo hakikufanya mambo haya?” 19 Yesu akawaambia,“Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa sikutatu.” 20 Hapo Wayahudi wakasema, “Hekaluhili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini nasita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?” 21

Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya Hekaluambalo ni mwili wake. 22 Basi, alipofufuliwakutoka wafu, wanafunzi wake walikumbukakwamba alikuwa amesema hayo, wakaaminiMaandiko Matakatifu na yale manenoaliyokuwa akisema Yesu. 23 Yesu alipokuwaYerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watuwengi walimwamini walipoona isharaalizozifanya. 24 Lakini Yesu hakuwa na imaninao kwa sababu aliwajua wote. 25 Hakuhitajikuambiwa chochote juu ya watu, maanaaliyajua barabara mambo yote yaliyomomioyoni mwao.

Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi,wa kikundi cha Mafarisayo, jina lakeNikodemo. 2 Siku moja alimwendea

Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajuakwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa naMungu, maana hakuna mtu awezaye kufanyaishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamojanaye.” 3 Yesu akamwambia, “Kwelinakwambia, mtu asipozaliwa upya hatawezakuuona ufalme wa Mungu.” 4 Nikodemoakamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwatena? Hawezi kuingia tumboni mwa mamayake na kuzaliwa mara ya pili!” 5 Yesuakamjibu, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwakwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingiakatika ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwakimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwakiroho kwa Roho. 7 Usistaajabu kwambanimekwambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8

Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikiasauti yake, lakini hujui unakotoka walaunakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtualiyezaliwa kwa Roho.” 9 Nikodemoakamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”10 Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katikaIsrael na huyajui mambo haya? 11 Kwelinakwambia, sisi twasema tunayoyajua nakushuhudia tuliyoyaona, lakini ninyi hamkubaliujumbe wetu. 12 Ikiwa nimewaambienimambo ya kidunia nanyi hamniamini,mtawezaje kuamini nikiwaambieni mambo ya

YOHANA MTAKATIFU 1:43

70

Page 71: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

mbinguni? 13 Hakuna mtu aliyepata kwendajuu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtuambaye ameshuka kutoka mbinguni. 14 “Kamavile Mose alivyomwinua juu nyoka wa shabakule jangwani, naye Mwana wa Mtu atainuliwajuu vivyo hivyo, 15 ili kila anayemwamini awena uzima wa milele. 16 Maana Mungualiupenda ulimwengu hivi hata akamtoaMwana wake wa pekee, ili kila amwaminiyeasipotee, bali awe na uzima wa milele. 17

Maana Mungu hakumtuma Mwanaeulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, baliaukomboe ulimwengu. 18 “AnayemwaminiMwana hahukumiwi; asiyemwaminiamekwisha hukumiwa kwa sababuhakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu. 19

Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwangaumekuja ulimwenguni lakini watu wakapendagiza kuliko mwanga, kwani matendo yao nimaovu. 20 Kila mtu atendaye maovuanauchukia mwanga, wala haji kwenyemwanga, maana hapendi matendo yakemaovu yamulikwe. 21 Lakini mwenyekuuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ilimatendo yake yaonekane yametendwa kwakumtii Mungu.” 22 Baada ya hayo, Yesu alifikamkoani Yudea pamoja na wanafunzi wake.Alikaa huko pamoja nao kwa muda, akibatizawatu. 23 Yohane pia alikuwa akibatiza watuhuko Ainoni, karibu na Salemu, maana hukokulikuwa na maji mengi. Watu walimwendea,naye akawabatiza. 24 (Wakati huo Yohanealikuwa bado hajafungwa gerezani.) 25 Ubishiulitokea kati ya baadhi ya wanafunzi waYohane na Myahudi mmoja kuhusu desturi zakutawadha. 26 Basi, wanafunzi haowakamwendea Yohane na kumwambia,“Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja naweng'ambo ya Yordani na ambaye weweulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watuwote wanamwendea.” 27 Yohane akawaambia,“Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa naMungu. 28 Nanyi wenyewe mwawezakushuhudia kuwa nilisema: Mimi siye Kristo,lakini nimetumwa ili nimtangulie! 29 Bibiarusini wake bwanaarusi, lakini rafiki yake bwanaarusi, anayesimama na kusikiliza, hufurahisana anapomsikia bwana arusi akisema.Ndivyo furaha yangu ilivyokamilishwa. 30 Nilazima yeye azidi kuwa maarufu, na miminipungue. 31 “Anayekuja kutoka juu ni mkuukuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, nahuongea mambo ya kidunia. Lakini anayekujakutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. 32 Yeyehusema yale aliyoyaona na kuyasikia, lakinihakuna mtu anayekubali ujumbe wake. 33

Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wakeanathibitisha kwamba Mungu ni kweli. 34 Yulealiyetumwa na Mungu husema maneno yaMungu, maana Mungu humjalia mtu huyoRoho wake bila kipimo. 35 Baba anampendaMwana na amemkabidhi vitu vyote. 36

Anayemwamini Mwana anao uzima wa milele;

asiyemtii Mwana hatakuwa na uzima wamilele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juuyake.”

Mafarisayo walisikia kwamba Yesualikuwa anabatiza na kuwapatawanafunzi wengi kuliko Yohane. 2

(Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwaanabatiza ila wanafunzi wake.) 3 Basi, Yesualiposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;4 na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.5 Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria,karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwaamempa mwanawe, Yosefu. 6 Mahali hapopalikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu,kutokana na uchovu wa safari, akaketi kandoya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. 7

Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafikakuteka maji. Yesu akamwambia, “Nipatie majininywe.” 8 (Wakati huo wanafunzi wakewalikuwa wamekwenda mjini kununuachakula.) 9 Lakini huyo mwanamkeakamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi nimwanamke Msamaria! Unawezaje kuniombamaji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano naWasamaria katika matumizi ya vitu.) 10 Yesuakamjibu, “Kama tu ungalijua zawadi yaMungu na ni nani anayekwambia: Nipatie majininywe, ungalikwisha mwomba, nayeangekupa maji yaliyo hai.” 11 Huyo mamaakasema, “Mheshimiwa, wewe huna chombocha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu;utapata wapi maji yaliyo hai? 12 Au, labdawewe wajifanya mkuu kuliko babu yetuYakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeyemwenyewe, watoto wake na mifugo yakewalikunywa maji ya kisima hiki.” 13 Yesuakamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataonakiu tena. 14 Lakini atakayekunywa majinitakayompa mimi, hataona kiu milele. Majinitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemiya maji ya uzima na kumpatia uzima wamilele.” 15 Huyo mwanamke akamwambia,“Mheshimiwa, nipe maji hayo ili nisione kiutena; nisije tena mpaka hapa kuteka maji.” 16

Yesu akamwambia, “Nenda ukamwite mumeouje naye hapa.” 17 Huyo mwanamkeakamwambia, “Mimi sina mume.” Yesuakamwambia, “Umesema kweli, kwamba hunamume. 18 Maana umekuwa na waumewatano, na huyo unayeishi naye sasa si mumewako. Hapo umesema kweli.” 19 HuyoMwanamke akamwambia, “Mheshimiwa,naona ya kuwa wewe u nabii. 20 Babu zetuwaliabudu juu ya mlima huu, lakini ninyimwasema kwamba mahali pa kumwabuduMungu ni kule Yerusalemu.” 21 Yesuakamwambia, “Niamini; wakati unakujaambapo hamtamwabudu Baba juu ya mlimahuu, wala kule Yerusalemu. 22 NinyiWasamaria mnamwabudu yule msiyemjua,lakini sisi tunamjua huyo tunayemwabudu,kwa maana wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23

Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika,

YOHANA MTAKATIFU 4:23

71

Page 72: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

ambapo wanaoabudu kweli, watamwabuduBaba kwa nguvu ya Roho; watuwanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka. 24

Mungu ni Roho, na watu wataweza tukumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake.”25 Huyo mama akamwambia, “Najua kwambaMasiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokujaatatujulisha kila kitu.” 26 Yesu akamwambia,“Mimi ninayesema nawe, ndiye.” 27 Hapowanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sanakuona anaongea na mwanamke. Lakini hakunamtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa niniunaongea na mwanamke?” 28 Huyo mamaakauacha mtungi wake pale, akaenda mjini nakuwaambia watu, 29 “Njoni mkamwone mtualiyeniambia mambo yote niliyotenda! Je,yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?” 30 Watuwakatoka mjini, wakamwendea Yesu. 31

Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwawanamsihi Yesu: “Mwalimu, ule chakula.” 32

Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninachochakula msichokijua ninyi.” 33 Wanafunzi wakewakaulizana, “Je, kuna mtu aliyemleteachakula?” 34 Yesu akawaambia, “Chakulachangu ni kufanya anachotaka yulealiyenituma na kuitimiza kazi yake. 35 Ninyimwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wamavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni,yatazameni mashamba; mazao yako tayarikuvunwa. 36 Mvunaji anapata mshahara wake,na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wamilele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahipamoja. 37 Kwa sababu hiyo msemo huu nikweli: Mmoja hupanda na mwingine huvuna.38 Mimi nimewatuma mkavune mavunoambayo hamkuyatolea jasho, wenginewalifanya kazi, lakini ninyi mnafaidikakutokana na jasho lao.” 39 Wasamaria wengiwa kijiji kile waliamini kwa sababu ya manenoaliyosema huyo mama: “Ameniambia mamboyote niliyofanya.” 40 Wasamaria walimwendeaYesu wakamwomba akae nao; naye akakaahapo siku mbili. 41 Watu wengi zaidiwalimwamini kwa sababu ya ujumbe wake. 42

Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuamini tukwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewetumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiyekweli Mwokozi wa ulimwengu.” 43 Baada yasiku mbili Yesu aliondoka hapo, akaendaGalilaya. 44 Maana Yesu mwenyewe alisemawaziwazi kwamba, “Nabii hapati heshimakatika nchi yake.” 45 Basi, alipofika Galilaya,Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana naopia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka,wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda hukoYerusalemu wakati wa sikukuu hiyo. 46 Yesualifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya,mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwana ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwahuko Kafarnaumu. 47 Basi, huyo ofisaaliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudeana kufika Galilaya, alimwendea akamwombaaende kumponya mtoto wake aliyekuwa

mgonjwa mahututi. 48 Yesu akamwambia,“Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!” 49

Huyo ofisa akamwambia, “Mheshimiwa,tafadhali twende kabla mwanangu hajafa.” 50

Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao yumzima.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu,akaenda zake. 51 Alipokuwa bado njiani,watumishi wake walikutana naye,wakamwambia kwamba mwanawe alikuwamzima. 52 Naye akawauliza saa mtotoalipopata nafuu; nao wakamwambia, “Jana saasaba mchana, homa ilimwacha.” 53 Huyo babaakakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileileambapo Yesu alimwambia: “Mwanao yumzima.” Basi, yeye akaamini pamoja na jamaayake yote. 54 Hii ilikuwa ishara ya pilialiyoifanya Yesu alipokuwa anatoka Yudeakwenda Galilaya.

Baada ya hayo kulikuwa na sikukuu yaWayahudi, naye Yesu akaendaYerusalemu. 2 Huko Yerusalemu,

karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo,kulikuwa na bwawa la maji liitwalo kwaKiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa nabaraza tano zenye matao. 3 Humo barazanimlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: vipofu,viwete na waliopooza. Walikuwa wakingojeamaji yatibuliwe, 4 maana mara kwa maramalaika alishuka majini nyakati fulani nakuyatibua. Mtu yeyote aliyekuwa wa kwanzakuingia majini baada ya maji kutibuliwa,alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao. 5 Basi,hapo palikuwa na mtu mmoja aliyekuwamgonjwa kwa muda wa miaka thelathini naminane. 6 Naye alipomwona huyo mtuamelala hapo, akatambua kwamba alikuwaamekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza,“Je, wataka kupona?” 7 Naye akajibu,“Mheshimiwa, mimi sina mtu wa kunipelekamajini wakati yanapotibuliwa. Kila nikijaribukuingia, mtu mwingine hunitangulia.” 8 Yesuakamwambia, “Inuka, chukua mkeka wakoutembee.” 9 Mara huyo mtu akapona,akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hilililifanyika siku ya Sabato. 10 Kwa hiyo baadhiya Wayahudi wakamwambia huyo mtualiyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali kubebamkeka wako.” 11 Lakini yeye akawaambia,“Yule mtu aliyeniponya ndiye aliyeniambia:Chukua mkeka wako, tembea.” 12 Naowakamwuliza, “Huyo mtu aliyekwambia:Chukua mkeka wako, tembea, ni nani?” 13

Lakini yeye hakumjua huyo mtu aliyemponya,maana Yesu alikuwa amekwisha ondokamahali hapo, kwani palikuwa na umatimkubwa wa watu. 14 Basi, baadaye Yesualimkuta huyo aliyeponywa Hekaluni,akamwambia, “Sasa umepona; usitendedhambi tena, usije ukapatwa na jambo bayazaidi.” 15 Huyo mtu akaenda, akawaambiaviongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiyealiyemponya. 16 Kwa vile Yesu alifanya jambohilo siku ya Sabato, Wayahudi walianza

YOHANA MTAKATIFU 4:24

72

Page 73: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

kumdhulumu. 17 Basi, Yesu akawaambia,“Baba yangu anafanya kazi daima, nami pianafanya kazi.” 18 Kwa sababu ya maneno haya,viongozi wa Wayahudi walizidi kutafuta njia yakumwua Yesu: si kwa kuwa aliivunja Sheria yaSabato tu, bali pia kwa kuwa alisema kwambaMungu ni Baba yake, na hivyo akajifanya sawana Mungu. 19 Yesu akawaambia, “Kwelinawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitupeke yake; anaweza tu kufanya kileanachomwona Baba akikifanya. Maana kileanachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.20 Baba ampenda Mwana, na humwonyeshakila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tenaatamwonyesha mambo makuu kuliko haya,nanyi mtastaajabu. 21 Kama vile Babahuwafufua wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyonaye Mwana huwapa uzima wale anaopenda.22 Baba hamhukumu mtu yeyote; shughuliyote ya hukumu amemkabidhi Mwana, 23 iliwatu wote wamheshimu Mwana kama vilewanavyomheshimu Baba. AsiyemheshimuMwana hamheshimu Baba ambayeamemtuma. 24 “Kweli nawaambieni,anayesikia neno langu, na kumwamini yulealiyenituma, anao uzima wa milele.Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pitakutoka kifo na kuingia katika uzima. 25 Kwelinawaambieni, wakati unakuja, tenaumekwisha fika, ambapo wafu wataisikia sautiya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia,wataishi. 26 Kama vile Baba alivyo asili ya uhai,ndivyo pia alivyomjalia Mwanawe kuwa asili yauhai. 27 Tena amempa mamlaka ya kuhukumukwa sababu yeye ni Mwana wa Mtu. 28

Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakujaambapo wote waliomo makaburini wataisikiasauti yake, 29 nao watafufuka: wale waliotendamema watafufuka na kuishi, na walewaliotenda maovu watafufuka nakuhukumiwa. 30 “Mimi siwezi kufanya kitu kwauwezo wangu mwenyewe. Mimi nina hukumukama ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayohukumu yangu ni ya haki. Nia yangu si kufanyanipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yulealiyenituma. 31 Nikijishuhudia mimimwenyewe, ushahidi wangu hauwezikukubaliwa kuwa wa kweli. 32 Lakini yukomwingine ambaye hutoa ushahidi juu yangu,nami najua kwamba yote anayosema juuyangu ni ya kweli. 33 Ninyi mlituma ujumbekwa Yohane naye aliushuhudia ukweli. 34 Sikwamba mimi nautegemea ushahidi wawanadamu, lakini nasema mambo haya ilimpate kuokolewa. 35 Yohane alikuwa kamataa iliyokuwa ikiwaka na kuangaza, nanyimlikuwa tayari kufurahia mwanga huo kwakitambo. 36 Lakini mimi nina ushahidi juuyangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule waYohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazializonipa Baba nizifanye, ndizozinazonishuhudia kwamba Baba ndiyealiyenituma. 37 Naye Baba aliyenituma

hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikiasauti yake, wala kuuona uso wake, 38 naujumbe wake haukai ndani yenu maanahamkumwamini yule aliyemtuma. 39 Ninyihuyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhanikwamba ndani yake mtapata uzima wa milele;na kumbe maandiko hayohayoyananishuhudia! 40 Hata hivyo, ninyi hamtakikuja kwangu ili mpate uzima. 41 “Shabahayangu si kupata sifa kutoka kwa watu. 42

Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendokwa Mungu haumo mioyoni mwenu. 43 Miminimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakinihamnipokei; bali mtu mwingine akija kwamamlaka yake mwenyewe, mtampokea. 44

Mwawezaje kuamini, hali ninyi mnapendakupokea sifa kutoka kwenu ninyi wenyewe,wala hamtafuti sifa kutoka kwake yeye aliyepeke yake Mungu? 45 Msifikiri kwamba miminitawashtaki kwa Baba. Mose ambaye ninyimmemtumainia ndiye atakayewashtaki. 46

Kama kweli mngemwamini Mose,mngeniamini na mimi pia; maana Mosealiandika juu yangu. 47 Lakini hamuyaaminiyale aliyoandika, mtawezaje basi, kuaminimaneno yangu?”

Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwaGalilaya (au Ziwa Tiberia). 2 Umatimkubwa wa watu ulimfuata kwa

sababu watu hao walikuwa wameona isharaalizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa.3 Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja nawanafunzi wake. 4 Sikukuu ya Wayahudiiitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia. 5 Basi, Yesuna alipotazama na kuona umati wa watu ukijakwake, alimwambia Filipo, “Tununue wapimikate ili watu hawa wapate kula?” 6 (Alisemahivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijuamwenyewe atakalofanya.) 7 Filipo akamjibu,“Mikate ya denari mia mbili za fedhahaiwatoshi watu hawa hata kama ila mmojaatapata kipande kidogo tu!” 8 Mmoja wawanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguyeSimoni Petro, akamwambia, 9 “Yupo hapamtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayirina samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwawatu wengi kama hawa?” 10 Yesu akasema,“Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi telemahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumlayapata wanaume elfu tano. 11 Yesu akaitwaaile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawiawatu waliokuwa wameketi; akafanya vivyohivyo na wale samaki, kila mtu akapata kadirialivyotaka. 12 Watu waliposhiba Yesuakawaambia wanafunzi wake, “Kusanyenivipande vilivyobaki visipotee.” 13 Basi,wakakusanya vipande vya mikate ya shayiriwalivyobakiza wale watu waliokula, wakajazavikapu kumi na viwili. 14 Watu walipoionaishara hiyo aliyoifanya Yesu, wakasema,“Hakika huyu ndiye nabii anayekujaulimwenguni.” 15 Yesu akajua ya kuwa watuwalitaka kumchukua wamfanye mfalme,

YOHANA MTAKATIFU 6:15

73

Page 74: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

akaondoka tena, akaenda mlimani peke yake.16 Ilipokuwa jioni wanafunzi wake waliteremkahadi ziwani, 17 wakapanda mashua ili wavukekwenda Kafarnaumu. Giza lilikuwa limeingia,na Yesu alikuwa hajawafikia bado. 18 Ziwalikaanza kuchafuka kwa sababu upepo mkaliulikuwa unavuma. 19 Wanafunzi walipokuwawamekwenda umbali wa kilomita tano au sita,walimwona Yesu akitembea juu ya maji,anakaribia mashua; wakaogopa sana. 20 Yesuakawaambia, “Ni mimi, msiogope!” 21

Walifurahi kumchukua Yesu katika mashua; namara mashua ikawasili nchi kavu walipokuwawanakwenda. 22 Kesho yake umati wa watuwale waliobaki upande wa pili wa ziwawalitambua kwamba kulikuwa na mashuamoja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashuapamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi haowalikuwa wamekwenda zao peke yao. 23

Mashua nyingine kutoka Tiberia zilifika mahalihapo watu walipokula ile mikate, Bwanaalipokwisha mshukuru Mungu. 24 Basi, haowatu walipogundua kwamba Yesu nawanafunzi wake hawakuwapo mahali hapo,walipanda mashua, wakaenda Kafarnaumuwakimtafuta. 25 Wale watu walipomkuta Yesung'ambo ya pili wa ziwa walimwuliza,“Mwalimu, ulifika lini hapa?” 26 Yesuakawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta sikwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababumlikula ile mikate mkashiba. 27

Msikishughulikie chakula kiharibikacho;kishugulikieni chakula kidumucho kwa ajili yauzima wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Babaamemthibitisha atawapeni chakula hicho.” 28

Wao wakamwuliza, “Tufanye nini ili tuwezekuzitenda kazi za Mungu?” 29 Yesu akawajibu,“Hii ndiyo kazi anayotaka Mungu muifanye:kumwamini yule aliyemtuma.” 30 Hapowakamwambia, “Utafanya ishara gani ili tuionetupate kukuamini? Utafanya kitu gani? 31

Wazee wetu walikula mana kule jangwani,kama yasemavyo Maandiko: Aliwalisha mkatekutoka mbinguni.” 32 Yesu akawaambia, “Kwelinawaambieni, Mose hakuwapeni mkate kutokambinguni; Baba yangu ndiye awapaye ninyimkate halisi kutoka mbinguni. 33 Maanamkate wa Mungu ni yule ashukaye kutokambinguni na aupaye ulimwengu uzima.” 34

Basi, wakamwambia, “Mheshimiwa, tupedaima mkate huo.” 35 Yesu akawaambia,“Mimi ndimi mkate wa uzima. Anayekujakwangu hataona njaa; anayeniamini hataonakiu kamwe. 36 Lakini niliwaambieni kwambaingawa mmeniona hamniamini. 37 Woteanaonipa Baba watakuja kwangu; namisitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu, 38

kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajiliya kufanya matakwa yangu, ila kutimizamatakwa ya yule aliyenituma. 39 Na matakwaya yule aliyenituma ndiyo haya: nisimpotezehata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufuewote Siku ya mwisho. 40 Maana anachotaka

Baba yangu ndicho hiki: kila amwonayeMwana na kumwamini awe na uzima wamilele; nami nitamfufua Siku ya mwisho.” 41

Basi, Wayahudi wakaanza kunung'unika kwakuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshukakutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Je, huyu simwana wa Yosefu? Tunawajua baba yake namama yake! Basi, anawezaje kusema kwambaameshuka kutoka mbinguni?” 43 Yesuakawaambia, “Acheni kunung'unika ninyi kwaninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu,Baba aliyenituma asipomvuta kwangu; naminitamfufua mtu huyo Siku ya mwisho. 45

Manabii wameandika: Watu wotewatafundishwa na Mungu. Kila mtuanayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake,huja kwangu. 46 Hii haina maana kwambayupo mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yulealiyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwonaBaba. 47 Kweli, nawaambieni, anayeaminianao uzima wa milele. 48 Mimi ni mkate wauzima. 49 Wazee wenu walikula mana kulejangwani, lakini walikufa. 50 Huu ndio mkatekutoka mbinguni; mkate ambao anayekulahatakufa. 51 Mimi ni mkate hai ulioshukakutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huuataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwiliwangu ninaoutoa kwa ajili ya uzima waulimwengu.” 52 Ndipo Wayahudi wakaanzakubishana kati yao: 53 Yesu akawaambia,“Kweli nawaambieni, msipokula mwili waMwana wa Mtu na kunywa damu yake,hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54

Anayekula mwili wangu na kunywa damuyangu anao uzima wa milele nami nitamfufuasiku ya mwisho. 55 Maana mwili wangu nichakula cha kweli, na damu yangu ni kinywajicha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kunywadamu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaandani yake. 57 Baba aliye hai alinituma, naminaishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilayemimi ataishi pia kwa sababu yangu. 58 Basi,huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; sikama mana waliyokula babu zetu, wakafa.Aulaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesualisema hayo alipokuwa akifundisha katikasunagogi kule Kafarnaumu. 60 Basi, wengi wawafuasi wake waliposikia hayo, wakasema,“Haya ni mambo magumu! Nani awezayekuyasikiliza?” 61 Yesu alijua bila kuambiwa namtu kwamba wanafunzi wake walikuwawananung'unika juu ya jambo hilo, akawauliza,“Je, jambo hili linawafanya muwe na mashaka?62 Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana waMtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?63 Roho ndiye atiaye uzima; binadamu pekeyake hawezi. Maneno niliyowaambieni ni Roho,ni uzima. 64 Hata hivyo, wako baadhi yenuwasioamini.” (Yesu alisema hivyo kwani alijuatangu mwanzo ni kina nani wasioamini, na piani nani atakayemsaliti.) 65 Kisha akasema,“Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakunaawezaye kuja kwangu asipowezeshwa na Baba

YOHANA MTAKATIFU 6:16

74

Page 75: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

7

yangu.” 66 Kutokana na hayo, wengi wawafuasi wake walirudi nyuma wasiandamanenaye tena. 67 Basi, Yesu akawauliza wale kumina wawili, “Je, nanyi pia mwataka kwendazenu?” 68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana,tutakwenda kwa nani? Wewe unayo manenoyaletayo uzima wa milele. 69 Sisi tunaamini, natunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifuwa Mungu.” 70 Yesu akawaambia, “Je,sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Hatahivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!” 71 Yesu alisemahayo juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti;maana huyu alikuwa ndiye atakayemsaliti,ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi nawawili.

Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembeakatika Galilaya. Hakutaka kutembeamkoani Yudea kwa sababu viongozi wa

Wayahudi walikuwa wanataka kumwua. 2

Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwaimekaribia. 3 Basi ndugu zake wakamwambia,“Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wakowazione kazi unazozifanya. 4 Mtu hafanyimambo kwa siri kama anataka kujulikana kwawatu. Maadam unafanya mambo haya, basi,jidhihirishe kwa ulimwengu.” 5 (Hata nduguzake hawakumwamini!) 6 Basi, Yesuakawaambia, “Wakati wangu ufaao haujafikabado. Lakini kwenu ninyi kila wakati unafaa. 7

Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakinimimi wanichukia kwa sababu mimi nauambiawazi kwamba matendo yake ni maovu. 8 Ninyinendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendikwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayohaijafika.” 9 Alisema hayo kisha akabaki hukoGalilaya. 10 Baada ya ndugu zake kwendakwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakinihakuenda kwa hadhara bali kwa siri. 11

Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanamtafutakwenye sikukuu hiyo; Wakauliza: “Yuko wapi?”12 Kulikuwa na minong'ono mingi katika umatiwa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtumwema.” Wengine walisema, “La!Anawapotosha watu.” 13 Hata hivyo hakunamtu aliyethubutu kusema, habari zakehadharani kwa kuwaogopa viongozi waWayahudi. 14 Sikukuu hiyo ilipofikia katikati,Yesu naye alikwenda Hekaluni, akaanzakufundisha. 15 Basi, Wayahudi wakashangaana kusema “Mtu huyu amepataje elimu nayehakusoma shuleni?” 16 Hapo Yesu akawajibu,“Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali niyake yeye aliyenituma. 17 Mtu anayependakufanya yale anayotaka Mungu, atajua kamamafundisho yangu yametoka kwa Mungu, aumimi najisemea tu mwenyewe. 18 Yeyeanayejisemea tu mwenyewe anatafuta sifayake mwenyewe; lakini anayetafuta sifa ya yulealiyemtuma, huyo ni mwaminifu, na ndaniyake hamna uovu wowote. 19 Je, Mosehakuwapeni Sheria? Hata hivyo, hakuna hatammoja wenu anayeishika Sheria. Kwa ninimnataka kuniua?” 20 Hapo watu wakamjibu,

“Una wazimu wewe! Nani anataka kukuua?” 21

Yesu akawajibu, “Kuna jambo moja nililofanya,nanyi mnalistaajabia. 22 Mose aliwapeni iledesturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyoilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu).Sasa ninyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.23 Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku yaSabato kusudi Sheria ya Mose isivunjwe,mbona mnanikasirikia kwa sababunimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku yaSabato? 24 Msihukumu mambo kwa nje tu;toeni hukumu ya haki.” 25 Baadhi ya watu waYerusalemu walisema, “Je, yule mtuwanayemtafuta wamuue si huyu? 26 Tazamenisasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtuanayemwambia hata neno. Je, yawezekanakuwa viongozi wametambua kweli kwambahuyu ndiye Kristo? 27 Kristo atakapokujahakuna mtu atakayejua mahali alikotoka, lakinisisi tunajua alikotoka mtu huyu!” 28 Basi, Yesualipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sautina kusema, “Ati mnanijua; hata nilikotokamnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlakayangu mwenyewe; ila yeye aliyenituma mimi niwa kweli, nanyi hamumjui. 29 Lakini miminamjua kwa sababu nimetoka kwake, nayendiye aliyenituma.” 30 Basi, watu wakatakakumtia nguvuni, lakini hakuna mtualiyethubutu kumkamata kwa sababu saa yakeilikuwa haijafika bado. 31 Wengi katika uleumati wa watu walimwamini, wakasema, “Je,Kristo akija atafanya ishara kubwa zaidi kulikoalizozifanya huyu?” 32 Mafarisayo waliwasikiawatu wakinong'ona maneno hayo juu ya Yesu.Basi, wao pamoja na makuhani wakuuwakawatuma walinzi wamtie nguvuni. 33 Yesuakasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi,kisha nitamwendea yule aliyenituma. 34

Mtanitafuta lakini hamtaniona, maana palenitakapokuwa ninyi hamwezi kufika.” 35

Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwawao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapohatutaweza kumpata? Atakwenda kwaWayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, nakuwafundisha Wagiriki? 36 Ana maana ganianaposema: Mtanitafuta lakini hamtanipata,na mahali nitakapokuwa ninyi hamwezikufika?” 37 Siku ya mwisho ya sikukuu hiyoilikuwa siku maalum. Yesu alisimama, akasemakwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwanguanywe. 38 Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: Anayeniamini mimi, mito ya majiyenye uzima itatiririka kutoka moyoni mwake!”39 (Alisema hayo kumhusu Roho ambaye walewaliomwamini yeye watampokea. Wakati huoRoho alikuwa hajafika kwa sababu Yesualikuwa hajatukuzwa bado.) 40 Baadhi ya watukatika ule umati walisikia maneno hayo,wakasema, “Kweli mtu huyu ndiye yule nabii!”41 Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!”Lakini wengine walisema, “Je, yawezekanaKristo akatoka Galilaya? 42 MaandikoMatakatifu yasemaje? Yanasema: Kristo

YOHANA MTAKATIFU 7:42

75

Page 76: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

atatoka katika ukoo wa Daudi, na atazaliwaBethlehemu, mji wa Daudi!” 43 Basi, kukatokeamafarakano juu yake katika ule umati wa watu.44 Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvunilakini hakuna aliyejaribu kumkamata. 45 Kishawale walinzi wakarudi kwa makuhani wakuuna Mafarisayo; nao wakawauliza, “Kwa ninihamkumleta?” 46 Walinzi wakawajibu, “Hakunamtu aliyepata kamwe kusema kama asemavyomtu huyu!” 47 Mafarisayo wakawauliza, “Je,nanyi pia mmedanganyika? 48 Je, mmekwishamwona hata mmoja wa viongozi wa watu, aummoja wa Mafarisayo aliyemwamini? 49 Lakiniumati huu haujui Sheria ya Mose;umelaaniwa!” 50 Mmoja wao alikuwaNikodemo ambaye hapo awali alikuwaamemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia, 51

“Je, Sheria yetu humhukumu mtu kabla yakumsikia kwanza na kujua anafanya nini?” 52

Nao wakamjibu, “Je, wewe pia umetokaGalilaya? Haya, kayachunguze MaandikoMatakatifu nawe utaona kwamba Galilayahakutoki kamwe nabii!” 53 Basi, wotewakaondoka, kila mtu akaenda zake;

lakini Yesu akaenda kwenye mlima waMizeituni. 2 Kesho yake asubuhi namapema alikwenda tena Hekaluni.

Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawaanawafundisha. 3 Basi, walimu wa Sheria naMafarisayo wakamletea mwanamke mmojaaliyefumaniwa katika uzinzi. Wakamsimamishakatikati yao. 4 Kisha wakamwuliza Yesu,“Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwakatika uzinzi. 5 Katika Sheria yetu Mosealituamuru mwanamke kama huyu apigwemawe. Basi, wewe wasemaje?” 6 Walisemahivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki.Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhinikwa kidole. 7 Walipozidi kumwuliza, Yesuakainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambimiongoni mwenu na awe wa kwanza kumpigajiwe.” 8 Kisha akainama tena, akawaanaandika ardhini. 9 Waliposikia hivyo,wakaanza kutoweka mmojammoja,wakitanguliwa na wazee. Yesu akabaki pekeyake, na yule mwanamke amesimamapalepale. 10 Yesu alipoinuka akamwuliza huyomwanamke, “Wako wapi wale watu? Je, hakunahata mmoja aliyekuhukumu?” 11 Huyomwanamke akamjibu, “Mheshimiwa, hakunahata mmoja!” Naye Yesu akamwambia, “Walamimi sikuhukumu. Nenda zako; na tangu sasausitende dhambi tena.” 12 Yesualipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimindimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuatamimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa namwanga wa uzima.” 13 Basi, Mafarisayowakamwambia, “Wewe unajishuhudiamwenyewe; kwa hiyo ushahidi wako si halali.”14 Yesu akawajibu, “Hata kama ninajishuhudiamwenyewe, ushahidi wangu ni wa kweli kwasababu mimi najua nilikotoka naninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka

wala ninakokwenda. 15 Ninyi mnahukumu kwafikira za kibinadamu, lakini mimi simhukumumtu. 16 Hata nikihukumu, hukumu yangu ni yahaki kwa sababu mimi siko peke yangu; Babaaliyenituma yuko pamoja nami. 17

Imeandikwa katika Sheria yenu ya kwambaushahidi wa watu wawili ni halali. 18 Miminajishuhudia mwenyewe, naye Babaaliyenituma, ananishuhudia pia.” 19 Hapowakamwuliza, “Baba yako yuko wapi?” Yesuakawajibu “Ninyi hamnijui mimi walahamumjui Baba. Kama mngenijua mimi,mngemjua na Baba yangu pia.” 20 Yesualisema maneno hayo kwenye chumba chahazina alipokuwa anafundisha Hekaluni. Walahakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababusaa yake ilikuwa haijafika bado. 21 Yesuakawaambia tena, “Naenda zangu nanyimtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambizenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kufika.”22 Basi, viongozi wa Wayahudi wakasema, “Je,atajiua? Mbona anasema: Niendako ninyihamwezi kufika?” 23 Yesu akawaambia, “Ninyimmetoka papa hapa chini, mimi nimetoka juu;ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si waulimwengu huu. 24 Ndiyo maananiliwaambieni mtakufa katika dhambi zenu.Kama msipoamini kwamba Mimi ndimi,mtakufa katika dhambi zenu.” 25 Naowakamwuliza, “Wewe ni nani?” Yesu akawajibu,“Nimewaambieni tangu mwanzo! 26 Ninayomengi ya kusema na kuhukumu juu yenu.Lakini yule aliyenituma ni kweli; naminauambia ulimwengu mambo yale tuniliyoyasikia kutoka kwake.” 27 Hawakuelewakwamba Yesu alikuwa akisema nao juu yaBaba. 28 Basi, Yesu akawaambia,“Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu hapondipo mtakapojua kwamba Mimi ndimi, nakwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ilanasema tu yale Baba aliyonifundisha. 29 Yulealiyenituma yuko pamoja nami; yeyehakuniacha peke yangu kwani nafanya daimayale yanayompendeza.” 30 Baada ya kusemahayo watu wengi walimwamini. 31 Basi, Yesuakawaambia wale Wayahudi waliomwamini,“Kama mkiyazingatia mafundisho yangumtakuwa kweli wanafunzi wangu. 32 Mtaujuaukweli, nao ukweli utawapeni uhuru.” 33 Naowakamjibu, “Sisi ni wazawa wa Abrahamu, nahatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtuyeyote yule. Una maana gani unaposema:mtakuwa huru?” 34 Yesu akawajibu, “Kwelinawaambieni, kila mtu anayetenda dhambi nimtumwa wa dhambi. 35 Mtumwa hana makaoya kudumu nyumbani, lakini mwana anayomakao ya kudumu. 36 Kama mwana akiwapeniuhuru mtakuwa huru kweli. 37 Najua kwambaninyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo,mnataka kuniua kwa sababu hamuyakubalimafundisho yangu. 38 Mimi nasema yalealiyonionyesha Baba, lakini ninyi mwafanyayale aliyowaambieni baba yenu.” 39 Wao

YOHANA MTAKATIFU 7:43

76

Page 77: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

wakamjibu, “Baba yetu ni Abrahamu!” Yesuakawaambia, “Kama ninyi mngekuwa watotowa Abrahamu, mngefanya kama alivyofanyaAbrahamu, 40 Mimi nimewaambieni ukweliniliousikia kwa Mungu; hata hivyo, ninyimwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!41 Ninyi mnafanya mambo yaleyale aliyofanyababu yenu.” Wao wakamwambia, “Sisi siwatoto haramu! Tunaye baba mmoja tu, yaaniMungu.” 42 Yesu akawaambia, “Kama Munguangekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi,maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa nikohapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe,ila yeye alinituma. 43 Kwa nini hamwelewihayo ninayosema? Ni kwa kuwa hamwezikuusikiliza ujumbe wangu. 44 Ninyi ni watotowa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekelezatamaa za baba yenu. Yeye alikuwa muuajitangu mwanzo; hana msimamo katika ukweli,kwani ukweli haumo ndani yake. Kila asemapouongo, husema kutokana na hali yake yamaumbile, maana yeye ni mwongo na baba wauongo. 45 Mimi nasema ukweli, na ndiyomaana ninyi hamniamini. 46 Nani kati yenuawezaye kuthibitisha kuwa mimi nina dhambi?Ikiwa basi nasema ukweli, kwa ninihamniamini? 47 Aliye wa Mungu husikilizamaneno ya Mungu. Lakini ninyi hamsikilizi kwasababu ninyi si (watu wa) Mungu.” 48

Wayahudi wakamwambia, “Je, hatukusemakweli kwamba wewe ni Msamaria, na tena unapepo?” 49 Yesu akajibu, “Mimi sina pepo; miminamheshimu Baba yangu, lakini ninyihamniheshimu. 50 Mimi sijitafutii utukufuwangu mwenyewe; yuko mmoja mwenyekuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu. 51

Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbewangu hatakufa milele.” 52 Basi, Wayahudiwakasema, “Sasa tunajua kweli kwamba weweni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, namanabii pia walikufa, nawe wasema ati,Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufamilele! 53 Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko babayetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata namanabii walikufa. Wewe unajifanya kuwanani?” 54 Yesu akawajibu, “Nikijitukuzamwenyewe, utukufu wangu si kitu. Baba yanguambaye ninyi mwasema ni Baba yenu, ndiyeanayenitukuza. 55 Ninyi hamjapata kumjua,lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui,nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjuana ninashika neno lake. 56 Abrahamu, babayenu, alishangilia aione siku yangu; nayealiiona, akafurahi.” 57 Basi, Wayahudiwakamwambia, “Wewe hujatimiza miakahamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?”58 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni,kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko.” 59

Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakiniYesu akajificha, akatoka Hekaluni.

Yesu alipokuwa akipita alimwona mtummoja, kipofu tangu kuzaliwa. 2 Basi,wanafunzi wakamwuliza, “Mwalimu! Ni

nani aliyetenda dhambi: mtu huyu, ama wazaziwake, hata akazaliwa kipofu?” 3 Yesu akajibu,“Jambo hili halikutukia kwa sababu ya dhambizake yeye, wala dhambi za wazazi wake; ilaalizaliwa kipofu ili nguvu ya Mungu ionekaneikifanya kazi ndani yake. 4 Kukiwa badomchana yatupasa kuendelea kufanya kazi zayule aliyenituma; maana usiku unakujaambapo mtu hawezi kufanya kazi. 5 Wakatiningali ulimwenguni, mimi ni mwanga waulimwengu.” 6 Baada ya kusema hayo,akatema mate chini, akafanyiza tope,akampaka yule kipofu machoni, 7

akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawala Siloamu.” (maana ya jina hili ni“aliyetumwa”). Basi, huyo kipofu akaenda,akanawa, kisha akarudi akiwa anaona. 8 Basi,jirani zake na wale waliokuwa wanajuakwamba hapo awali alikuwa maskinimwombaji, wakasema, “Je, huyu siye yulemaskini aliyekuwa akiketi na kuomba?” 9

Baadhi yao wakasema, “Ndiye.” Wenginewakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakinihuyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi!” 10

Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yakoyalipataje kufumbuliwa?” 11 Naye akawajibu,“Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope,akanipaka machoni na kuniambia: Nendaukanawe katika bwawa la Siloamu. Basi, miminikaenda, nikanawa, nikapata kuona.” 12

Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?” Nayeakawajibu, “Mimi sijui!” 13 Kisha wakampelekahuyo mtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo. 14

Siku hiyo Yesu alipofanya tope na kumfumbuamacho mtu huyo, ilikuwa siku ya Sabato. 15

Basi, Mafarisayo wakamwuliza mtu huyo,“Umepataje kuona?” Naye akawaambia,“Alinipaka tope machoni, nami nikanawa nasasa naona.” 16 Baadhi ya Mafarisayowakasema, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu,maana hashiki sheria ya Sabato.” Lakiniwengine wakasema, “Mtu mwenye dhambiawezaje kufanya ishara za namna hii?” Kukawana mafarakano kati yao. 17 Wakamwuliza tenahuyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadam yeyeamekufungua macho, wasemaje juu yake?”Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!” 18 Viongoziwa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyoalikuwa kipofu hapo awali na sasa anaonampaka walipowaita wazazi wake. 19 Basi,wakawauliza hao wazazi, “Je, huyu ndiye mtotowenu ambaye ninyi mwasema alizaliwa kipofu?Sasa amepataje kuona?” 20 Wazazi wakewakajibu, “Tunajua kwamba huyu ni mtotowetu, na kwamba alizaliwa kipofu. 21 Lakiniamepataje kuona, hatujui; na wala hatumjuiyule aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeyemwenyewe; yeye ni mtu mzima, anawezakujitetea mwenyewe.” 22 Wazazi wakewalisema hivyo kwa sababu waliwaogopaviongozi wa Wayahudi kwani viongozi haowalikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyoteatakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa

YOHANA MTAKATIFU 9:22

77

Page 78: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

nje ya sunagogi. 23 Ndiyo maana wazazi wakewalisema: “Yeye ni mtu mzima, mwulizeni.” 24

Basi, wakamwita tena aliyekuwa kipofu,wakamwambia, “Sema ukweli mbele yaMungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu nimwenye dhambi.” 25 Yeye akajibu, “Kama nimwenye dhambi mimi sijui. Lakini kitu kimojanajua: Nilikuwa kipofu, na sasa naona.” 26

Basi, wakamwuliza, “Alikufanyia nini?Alikufumbuaje macho yako?” 27 Huyo mtuakawajibu, “Nimekwisha waambieni, nanyihamkusikiliza; kwa nini mwataka kusikia tena?Je, ninyi pia mnataka kuwa wafuasi wake?” 28

Lakini wao wakamtukana wakisema, “Wewe nimfuasi wake; sisi ni wafuasi wa Mose. 29 Sisitunajua kwamba Mungu alisema na Mose,lakini mtu huyu hatujui ametoka wapi!” 30

Naye akawajibu, “Hili ni jambo la kushangaza!Ninyi hamjui ametoka wapi, lakiniamenifumbua macho yangu! 31 Tunajuakwamba Mungu hawasikilizi watu wenyedhambi, ila humsikiliza yeyote mwenyekumcha na kutimiza mapenzi yake. 32 Tangumwanzo wa ulimwengu haijasikika kwambamtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwakipofu. 33 Kama mtu huyu hakutoka kwaMungu, hangeweza kufanya chochote!” 34

Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewakatika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?”Basi, wakamfukuzia mbali. 35 Yesu alisikiakwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, nayealipomkuta akamwuliza, “Je, weweunamwamini Mwana wa Mtu?” 36 Huyo mtuakajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ilinipate kumwamini.” 37 Yesu akamwambia,“Umekwisha mwona, naye ndiye anayesemanawe sasa.” 38 Basi, huyo mtu akasema,“Ninaamini Bwana!” Akamsujudia. 39 Yesuakasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoahukumu, kusudi wasioona wapate kuona, nawale wanaoona wawe vipofu.” 40 Baadhi yaMafarisayo waliokuwa pamoja naye walisikiamaneno hayo, wakamwuliza, “Je, sisi pia nivipofu?” 41 Yesu akawajibu, “Kama mngekuwavipofu, hamngekuwa na hatia; lakini sasa ninyimwasema: Sisi tunaona, na hiyo yaonyeshakwamba mna hatia bado.

Yesu alisema “Kweli nawaambieni,yeyote yule asiyeingia katika zizi lakondoo kwa kupitia mlangoni, bali

hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo nimwizi na mnyang'anyi. 2 Lakini anayeingiakwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungajiwa kondoo. 3 Mngoja mlango wa zizihumfungulia, na kondoo husikia sauti yake,naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwajina lake na kuwaongoza nje. 4 Akisha watoanje huwatangulia mbele nao kondoohumfuata, kwani wanaijua sauti yake. 5

Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, baliwatamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.”6 Yesu aliwaambia mfano huo, lakini waohawakuelewa alichotaka kuwaambia. 7 Basi,

akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi nimlango wa kondoo. 8 Wale wengine wotewaliokuja kabla yangu ni wezi nawanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.9 Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitiakwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, nakupata malisho. 10 Mwizi huja kwa shabaha yakuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekujampate kuwa na uzima—uzima kamili. 11 “Mimini mchungaji mwema. Mchungaji mwemahuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake. 12

Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, nawala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo nakukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata nakuwatawanya. 13 Yeye hajali kitu juu yakondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshaharatu. 14 Mimi ni mchungaji mwema. Nawajuawalio wangu, nao walio wangu wananijuamimi, 15 kama vile Baba anijuavyo, naminimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangukwa ajili yao. 16 Tena ninao kondoo wengineambao hawamo zizini humu. Inanibidikuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu,na kutakuwako kundi moja na mchungajimmoja. 17 “Baba ananipenda kwani nautoauhai wangu ili nipate kuupokea tena. 18

Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu;mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe.Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wakuuchukua tena. Hivi ndivyo Babaalivyoniamuru nifanye.” 19 Kukawa tena namafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu yamaneno haya. 20 Wengi wao wakasema, “Anapepo; tena ni mwendawazimu! Ya ninikumsikiliza?” 21 Wengine wakasema, “Haya simaneno ya mwenye pepo. Je, pepo anawezakuyafumbua macho ya vipofu?” 22 HukoYerusalemu kulikuwa na sikukuu yaKutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi. 23

Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katikaukumbi wa Solomoni. 24 Basi, Wayahudiwakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuachakatika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiyeKristo, basi, tuambie wazi.” 25 Yesu akawajibu,“Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazininazozifanya mimi kwa jina la Baba yanguzinanishuhudia. 26 Lakini ninyi hamsadiki kwasababu ninyi si kondoo wangu. 27 Kondoowangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua,nao hunifuata. 28 Mimi nawapa uzima wamilele; nao hawatapotea milele, wala hakunamtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.29 Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao nimkuu kuliko wote, wale hakuna awezayekuwatoa mikononi mwake Baba. 30 Mimi naBaba, tu mmoja.” 31 Basi, Wayahudiwakachukua mawe ili wamtupie. 32 Yesuakawaambia, “Nimewaonyesheni kazi nyingikutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizoinayowafanya mnipige mawe?” 33 Wayahudiwakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa ajili yatendo jema, ila kwa sababu ya kukufuru!

YOHANA MTAKATIFU 9:23

78

Page 79: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe nibinadamu tu.” 34 Yesu akawajibu, “Je,haikuandikwa katika Sheria yenu: Miminimesema, ninyi ni miungu? 35 Mungu aliwaitamiungu wale waliopewa neno lake; nasi twajuakwamba Maandiko Matakatifu yasema ukwelidaima. 36 Je, yeye ambaye Baba alimwekawakfu na kumtuma ulimwenguni,mnamwambia: Unakufuru, eti kwa sababunilisema: Mimi ni Mwana wa Mungu? 37 Kamasifanyi kazi za Baba yangu msiniamini. 38

Lakini ikiwa ninazifanya, hata kamahamniamini, walau ziaminini hizo kazi mpatekujua na kutambua kwamba Baba yuko ndaniyangu, nami niko ndani yake.” 39 Wakajaributena kumkamata lakini akachopoka mikononimwao. 40 Yesu akaenda tena ng'ambo ya mtoYordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza,akakaa huko. 41 Watu wengi walimwendeawakasema, “Yohane hakufanya ishara yoyote.Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtuhuyu ni kweli kabisa.” 42 Watu wengi mahalihapo wakamwamini.

Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyejiwa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijijicha Bethania kilikuwa mahali

walipokaa Maria na Martha, dada yake. 2

Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashina kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kakayake, ndiye aliyekuwa mgonjwa.) 3 Basi, haodada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu:“Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!” 4 Yesualiposikia hivyo akasema, “Ugonjwa huohautaleta kifo, ila ni kwa ajili ya kumtukuzaMungu; ameugua ili kwa njia hiyo Mwana waMungu atukuzwe.” 5 Yesu aliwapenda Martha,dada yake na Lazaro. 6 Alipopata habarikwamba Lazaro ni mgonjwa, Yesu aliendeleakukaa mahali hapo alipokuwa kwa siku mbilizaidi. 7 Kisha akawaambia wanafunzi wake,“Twendeni tena Yudea!” 8 Wanafunziwakamwambia, “Mwalimu! Muda mfupi tuumepita tangu Wayahudi walipotaka kukuuakwa mawe, nawe unataka kwenda huko tena?”9 Yesu akajibu, “Je, saa za mchana si kumi nambili? Basi, mtu akitembea mchana hawezikujikwaa kwa kuwa anauona mwanga waulimwengu huu. 10 Lakini mtu akitembeausiku atajikwaa kwa maana mwanga haumondani yake.” 11 Yesu alipomaliza kusemamaneno hayo, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaroamelala, lakini mimi nitakwenda kumwamsha.”12 Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana,ikiwa amelala, basi atapona.” 13 Wao walidhanikwamba alikuwa amesema juu ya kulalausingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifocha Lazaro. 14 Basi, Yesu akawaambiawaziwazi, “Lazaro amekufa; 15 Lakini nafurahikwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ilimpate kuamini. Haya, twendeni kwake.” 16

Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunziwenzake, “Twendeni nasi tukafe pamoja naye!”17 Yesu alipofika huko alikuta Lazaro

amekwisha kaa kaburini kwa siku nne. 18 Kijijicha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemuumbali upatao kilomita tatu. 19 Wayahudiwengi walikuwa wamefika kwa Martha naMaria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao. 20

Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwaanakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibakinyumbani. 21 Martha akamwambia Yesu,“Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yanguhangalikufa! 22 Lakini najua kwamba hata sasachochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”23 Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.”24 Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufukawakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” 25 Yesuakamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uzima.Anayeniamini mimi hata kama anakufa,ataishi: 26 na kila anayeishi na kuniamini,hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?” 27 Marthaakamwambia, “Ndiyo Bwana! Naamini kwambawewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yuleajaye ulimwenguni.” 28 Baada ya kusemahayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dadayake, akamwabia faraghani, “Mwalimu yukohapa, anakuita.” 29 Naye aliposikia hivyo,akainuka mara, akamwendea Yesu. 30 Yesualikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa badomahali palepale Martha alipomlaki. 31 Basi,Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja naMaria wakimfariji walipomwona ameinuka nakutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhanialikuwa anakwenda kaburini kuomboleza. 32

Basi, Maria alipofika mahali pale Yesualipokuwa na kumwona, alipiga magoti,akamwabia, “Bwana, kama ungalikuwa hapa,kaka yangu hangalikufa!” 33 Yesu alipomwonaanalia, na wale Wayahudi waliokuja pamojanaye wanalia pia, alijawa na huzuni nakufadhaika moyoni. 34 Kisha akawauliza,“Mlimweka wapi?” Wakamwambia, “Bwana,njoo uone.” 35 Yesu akalia machozi. 36 Basi,Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsialivyompenda!” 37 Lakini baadhi yaowakasema, “Je, huyu aliyemfumbua machoyule kipofu, hakuweza kumfanya Lazaro asife?”38 Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni,akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwapango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe. 39

Yesu akasema, “Ondoeni hilo jiwe!” Martha,dada yake huyo aliyekufa, akamwambia,“Bwana, amekwishaanza kunuka; amekaakaburini siku nne!” 40 Yesu akamwambia, “Je,sikukwambia kwamba ukiamini utaonautukufu wa Mungu?” 41 Basi, wakaliondoa lilejiwe. Yesu akatazama juu mbinguni, akasema,“Nakushukuru Baba kwa kuwa wewewanisikiliza. 42 Najua kwamba unanisikilizadaima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watuhawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwambawewe ndiwe uliyenituma.” 43 Alipokwishasema hayo, akaita kwa sauti kubwa: “Lazaro!Toka nje!” 44 Huyo aliyekuwa amekufa akatokanje, huku amefungwa sanda miguu na mikono,na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia,

YOHANA MTAKATIFU 11:44

79

Page 80: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

12

“Mfungueni, mkamwache aende zake.” 45 Basi,Wayahudi wengi waliokuwa wamefika kwaMaria walipoona kitendo hicho alichokifanyaYesu wakamwamini. 46 Lakini baadhi yaowalikwenda kwa Mafarisayo wakatoa taarifa yajambo hilo alilofanya Yesu. 47 kwa hiyomakuhani wakuu na Mafarisayo wakafanyakikao cha Baraza kuu, wakasema, “Tufanyenini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno. 48

Tukimwacha tu watu wote watamwamini, naoWaroma watakuja kuliharibu Hekalu letu nataifa letu!” 49 Hapo, mmoja wao aitwayeKayafa, ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwakahuo, akawaambia, “Ninyi hamjui kitu! 50 Je,hamwoni kwamba ni afadhali kwenu mtummoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa zimaliangamizwe?” 51 Yeye hakusema hivyo kwahiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwaKuhani Mkuu mwaka huo, alibashiri kwambaYesu atakufa kwa ajili ya taifa lao; 52 na wala sikwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamojawatoto wa Mungu waliotawanyika. 53 Basi,tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudiwalifanya mipango ya kumwua Yesu. 54 Kwahiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati yaWayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahalikaribu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu.Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. 55

Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa karibu,na watu wengi walikwenda Yerusalemu iliwajitakase kabla ya sikukuu hiyo. 56 Basi,wakawa wanamtafuta Yesu; naowalipokusanyika pamoja Hekaluniwakaulizana, “Mwaonaje? Yaonekana kwambahaji kabisa kwenye sikukuu, au sivyo?” 57

Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwawametoa amri kwamba mtu akijua mahalialiko Yesu awaarifu kusudi wamtie nguvuni.

Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka,Yesu alifika Bethania alikoishi Lazaroambaye Yesu alikuwa amemfufua

kutoka wafu. 2 Huko walimwandalia chakulacha jioni, naye Martha akawa anawatumikia.Lazaro alikuwa mmoja wa wale waliokuwamezani pamoja na Yesu. 3 Basi, Mariaalichukua chupa ya marashi ya nardo safi yathamani kubwa, akampaka Yesu miguu nakuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yoteikajaa harufu ya marashi. 4 Basi, YudaIskarioti, mmoja wa wale kumi na wawiliambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema, 5

“Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwafedha dinari mia tatu, wakapewa maskini?” 6

Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juuya maskini, bali kwa sababu alikuwa mwekahazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwamara aliiba kutoka katika hiyo hazina. 7 LakiniYesu akasema, “Msimsumbue huyu mama!Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishiyangu. 8 Maskini mtakuwa nao siku zote,lakini hamtakuwa nami siku zote.” 9 Wayahudiwengi walisikia kwamba Yesu alikuwaBethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya

kumwona Yesu, ila pia wapate kumwonaLazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka wafu. 10

Makuhani wakuu waliamua pia kumwuaLazaro, 11 Maana kwa sababu ya LazaroWayahudi wengi waliwaasi viongozi wao,wakamwamini Yesu. 12 Kesho yake, kundikubwa la watu waliokuja kwenye sikukuuwalisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kujaYerusalemu. 13 Basi, wakachukua matawi yamitende, wakatoka kwenda kumlaki;wakapaaza sauti wakisema: “Hosana!Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.Abarikiwe mfalme wa Israeli.” 14 Yesuakampata mwana punda mmoja akapanda juuyake kama yasemavyo Maandiko: 15

“Usiogope mji wa Sioni! Tazama, Mfalme wakoanakuja, Amepanda mwana punda.” 16 Wakatihuo wanafunzi wake hawakuelewa mambohayo, lakini Yesu alipokwisha tukuzwa, ndipowalipokumbuka kwamba hayo yalikuwayameandikwa juu yake, na kwamba watuwalikuwa wamemtendea hivyo. 17 Kundi lawatu wale waliokuwa pamoja naye wakatialipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufuakutoka wafu, walisema yaliyotukia. 18 Kwahiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wotewalisikia kwamba Yesu alikuwa amefanyaishara hiyo. 19 Basi, Mafarisayo wakaambiana,“Mnaona? Hatuwezi kufanya chochote!Tazameni, ulimwengu wote unamfuata.” 20

Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwawatu waliokuwa wamefika Yerusalemukuabudu wakati wa sikukuu hiyo. 21 Haowalimwendea Filipo, mwenyeji wa Bethsaidakatika Galilaya, wakasema, “Mheshimiwa,tunataka kumwona Yesu.” 22 Filipo akaendaakamwambia Andrea, nao wawili wakaendakumwambia Yesu. 23 Yesu akawaambia, “Saaya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika! 24

Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubakipunje tu isipokuwa ikianguka katika udongona kufa. Kama ikifa, basi huzaa matundamengi. 25 Anayependa maisha yake,atayapoteza; anayeyachukia maisha yakekatika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili yauzima wa milele. 26 Anayetaka kunitumikia nilazima anifuate, hivyo kwamba popote palenilipo mimi ndipo na mtumishi wanguatakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikiaBaba yangu atampa heshima. 27 “Sasa rohoyangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme:Baba, usiruhusu saa hii inifikie? Lakini ndiyomaana nimekuja—ili nipite katika saa hii. 28

Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasemakutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nanitalitukuza tena.” 29 Umati wa watuwaliokuwa wamesimama hapo walisikia sautihiyo, na baadhi yao walisema, “Malaikaameongea naye!” 30 Lakini Yesu akawaambia,“Sauti hiyo haikutokea kwa ajili yangu mimi, ilakwa ajili yenu. 31 Sasa ndio wakati waulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawalawa ulimwengu huu atapinduliwa. 32 Nami

YOHANA MTAKATIFU 11:45

80

Page 81: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kilammoja kwangu.” 33 (Kwa kusema hivyoalionyesha atakufa kifo gani). 34 Basi, umatihuo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na Sheria yetukwamba Kristo atadumu milele. Wawezajebasi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswakuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?” 35

Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyikwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huomwanga ili giza lisiwapate; maana atembeayegizani hajui aendako. 36 Basi, wakati mnaohuo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wamwanga.” Baada ya kusema maneno hayo,Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao. 37

Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbeleyao, wao hawakumwamini. 38 Hivyo manenoaliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nanialiyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo waBwana umedhihirishwa kwa nani?” 39 Hivyohawakuweza kuamini, kwani Isaya tenaalisema: 40 “Mungu ameyapofusha machoyao, amezipumbaza akili zao; wasione kwamacho yao, wasielewe kwa akili zao; walawasinigeukie, asema Bwana, ili nipatekuwaponya.” 41 Isaya alisema maneno hayakwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasemahabari zake. 42 Hata hivyo, wengi wa viongoziwa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwasababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharanikwa kuogopa kwamba watatengwa nasunagogi. 43 Walipendelea kusifiwa na watukuliko kusifiwa na Mungu 44 Kisha Yesuakasema kwa sauti kubwa, “Mtu aliyeniamini,haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yulealiyenituma. 45 Anayeniona mimi anamwonapia yule aliyenituma. 46 Mimi ni mwanga, naminimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniaminiwasibaki gizani. 47 Anayeyasikia manenoyangu lakini hayashiki mimi sitamhukumu;maana sikuja kuhukumu ulimwengu balikuuokoa. 48 Asiyeyashika maneno yanguanaye wa kumhukumu: neno lile nililosema nihakimu wake siku ya mwisho. 49 Mimisikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ilaBaba aliyenituma ndiye aliyeniamuru nisemenini na niongee nini. 50 Nami najua kuwa amriyake huleta uzima wa milele. Basi, miminasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme.”

Ilikuwa kabla ya sikukuu ya Pasaka.Yesu alijua kwamba saa yake yakuondoka ulimwenguni na kwenda

kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwaamewapenda daima watu wake waliokoduniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho! 2

Basi, Yesu na wanafunzi wake walikuwamezani kwa chakula cha jioni. Ibilisi alikwishamtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, nia yakumsaliti Yesu. 3 Yesu alijua kwamba Babaalikuwa amemkabidhi kila kitu, na kwambaalikuwa ametoka kwa Mungu na anarudi kwaMungu. 4 Basi, Yesu aliondoka mezani,akaweka kando vazi lake, akachukua kitambaana kujifunga kiunoni. 5 Kisha akatia maji katika

bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi wakemiguu na kuipangusa kwa kile kitambaaalichojifungia. 6 Basi, akamfikia Simoni Petro;naye Petro akasema, “Bwana, wewe utanioshamiguu mimi?” 7 Yesu akamjibu, “Huelewi sasaninachofanya lakini utaelewa baadaye.” 8

Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguukamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuoshahutakuwa na uhusiano nami tena.” 9 SimoniPetro akamwambia, “Bwana, nioshe, si miguutu, bali na mikono yangu na kichwa pia.” 10

Yesu akamwambia, “Aliyekwisha oga hanalazima ya kunawa isipokuwa miguu, maanaamekwisha takata mwili wote. Ninyimmetakata, lakini si nyote.” 11 (Yesu alimjuayule ambaye atamsaliti, ndiyo maana alisema:“Ninyi mmetakata, lakini si nyote.”) 12

Alipokwisha waosha miguu na kuvaa tena vazilake, aliketi mezani, akawaambia, “Je,mmeelewa hayo niliyowatendeeni? 13 Ninyimwaniita Mwalimu na Bwana, nanyi mwasemavyema, kwa kuwa ndimi. 14 Basi, ikiwa miminiliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha ninyimiguu, nanyi pia mnapaswa kuoshana miguu.15 Nimewapeni mfano, ili nanyi pia mfanyekama nilivyowafanyieni. 16 Kwelinawaambieni, mtumishi si mkuu zaidi kulikobwana wake, wala mtume si mkuu zaidi kulikoyule aliyemtuma. 17 Basi, ikiwa mwayajuahayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza. 18

“Haya nisemayo hayawahusu ninyi nyote. Miminawajua wale niliowachagua. Lakini lazimayatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: Yulealiyeshiriki chakula changu amegeukakunishambulia. 19 Mimi nimewaambienimambo haya sasa kabla hayajatokea, iliyatakapotokea mpate kuamini kuwa mimindimi. 20 Kweli nawaambieni anayempokeayule ninayemtuma anaponipokea mimi; naanayenipokea mimi, anampokea yulealiyenituma.” 21 Alipokwisha sema hayo, Yesualifadhaika sana rohoni, akasema wazi, “Kwelinawaambieni, mmoja wenu atanisaliti!” 22

Wanafunzi wakatazama wasiweze kabisa kujuaanasema nani. 23 Mmoja wa wanafunzi,ambaye Yesu alikuwa anampenda sana,alikuwa ameketi karibu na Yesu. 24 Basi,Simoni Petro akamwashiria na kusema:“Mwulize anasema juu ya nani.” 25

Mwanafunzi huyo akasogea karibu zaidi naYesu, akamwuliza, “Bwana, ni nani?” 26 Yesuakajibu, “Yule nitakayempa kipande cha mkatenilichochovya katika sahani, ndiye.” Basi,akatwaa kipande cha mkate, akakichovyakatika sahani, akampa Yuda, mwana wa SimoniIskarioti. 27 Yuda alipokwisha pokea kipandehicho, Shetani akamwingia. Basi Yesuakamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanyeharaka!” 28 Lakini hakuna hata mmoja wa walewaliokaa pale mezani aliyefahamu kwa ninialikuwa amemwambia hivyo. 29 Kwa kuwaYuda alikuwa na wajibu wa kuutunza mfuko wafedha, baadhi yao walidhani kwamba Yesu

YOHANA MTAKATIFU 13:29

81

Page 82: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

14

15

alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwakwa sikukuu, au kwamba alikuwaamemwambia akatoe chochote kwa maskini.30 Basi, Yuda alipokwisha twaa kile kipandecha mkate, akatoka nje mara. Na ilikuwa usiku.31 Baada ya Yuda kuondoka, Yesu akasema,“Sasa Mwana wa Mtu ametukuzwa, nayeMungu ametukuzwa ndani yake. 32 Na kamautukufu wa Mungu umefunuliwa ndani yaMwana, basi, naye Mungu ataudhihirishautukufu wa Mwana ndani yake mwenyewe, naatafanya hivyo mara. 33 “Watoto wangu, badoniko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta,lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambiaviongozi wa Wayahudi: Niendako ninyihamwezi kwenda! 34 Nawapeni amri mpya:pendaneni; pendaneni kama nilivyowapendaninyi. 35 Mkipendana, watu wote watajuakwamba ninyi ni wanafunzi wangu.” 36 SimoniPetro akamwuliza, “Bwana, unakwenda wapi?”Yesu akajibu, “Niendako huwezi kunifuatasasa, lakini utanifuata baadaye.” 37 Petroakamwambia “Bwana, kwa nini siwezikukufuata sasa? Niko tayari kufa kwa ajiliyako!” 38 Yesu akajibu, “Je, uko tayari kwelikufa kwa ajili yangu? Kweli nakwambia, kablajogoo hajawika utanikana mara tatu!”

Yesu aliwaambia, “Msifadhaikemioyoni mwenu. Mwaminini Mungu,niaminini na mimi pia. 2 Nyumbani

mwa Baba yangu mna makao mengi; la sivyoningalikwisha waambieni. Sasa nakwendakuwatayarishieni nafasi. 3 Na nikienda nakuwatayarishieni nafasi, nitarudi nakuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe palenilipo mimi. 4 Mnajua njia ya kwenda hukoninakokwenda.” 5 Thoma akamwuliza,“Bwana, hatujui unakokwenda, tutawezajebasi, kuijua hiyo njia?” 6 Yesu akamjibu, “Mimini njia, na ukweli na uzima. Hakuna awezayekwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu. 7

Ikiwa mnanijua mimi mnamjua na Baba yangupia. Na tangu sasa, mnamjua, tenammekwisha mwona.” 8 Filipo akamwambia,“Bwana, tuonyeshe Baba, nasi tutatosheka.” 9

Yesu akamwambia, “Filipo, nimekaa nanyimuda wote huu, nawe hujanijua? Aliyekwishaniona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi,kusema: Tuonyeshe Baba? 10 Je, huaminikwamba mimi niko ndani ya Baba, naye Babayuko ndani yangu? Maneno ninayowaambieninyote siyasemi kwa mamlaka yangu; Babaaliye ndani yangu anafanya kazi yake. 11

Mnapaswa kuniamini ninaposema kwambamimi niko ndani ya Baba naye Baba yukondani yangu. Ama sivyo, aminini kwa sababuya mambo ninayofanya. 12 Kwelinawaambieni, anayeniamini atafanya mamboninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuuzaidi, maana nakwenda kwa Baba. 13 Nachochote mtakachoomba kwa jina langunitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.14 Mkiniomba chochote kwa jina langu,

nitawafanyieni. 15 “Mkinipenda mtazishikaamri zangu. 16 Nami nitamwomba Baba nayeatawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaananyi milele. 17 Yeye ni Roho wa kweli.Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababuhauwezi kumwona wala kumjua. Lakini ninyimnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yundani yenu. 18 “Sitawaacha ninyi yatima;nitakuja tena kwenu. 19 Bado kidogo naoulimwengu hautaniona tena, lakini ninyimtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi piamtakuwa hai. 20 Siku ile itakapofika mtajuakwamba mimi niko ndani ya Baba, nanyi mkondani yangu, nami ndani yenu. 21 Azipokeayeamri zangu na kuzishika, yeye ndiyeanipendaye. Naye anipendaye mimiatapendwa na Baba yangu, nami nitampendana kujidhihirisha kwake.” 22 Yuda (si yuleIskarioti) akamwambia, “Bwana, itawezekanajewewe kujidhihirisha kwetu na si kwaulimwengu?” 23 Yesu akamjibu, “Mtuakinipenda atashika neno langu, na Babayangu atampenda, nasi tutakuja kwake nakukaa naye. 24 Asiyenipenda hashiki manenoyangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lakeBaba aliyenituma. 25 “Nimewaambieni mambohaya nikiwa bado pamoja nanyi 26 lakiniMsaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Babaatamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kilakitu na kuwakumbusheni yoteniliyowaambieni. 27 “Nawaachieni amani;nawapeni amani yangu. Siwapi ninyi kama vileulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi,wala msifadhaike. 28 Mlikwisha sikianikiwaambieni: Ninakwenda zangu, kishanitarudi tena kwenu. Kama mngalinipendamngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwaBaba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi. 29

Nimewaambieni haya sasa kabla hayajatokea,ili yatakapotokea mpate kuamini. 30 Sitasemananyi tena mambo mengi, maana mtawala waulimwengu huu anakuja. Kwangu mimi hawezikitu; 31 lakini ulimwengu unapaswa kujuakwamba nampenda Baba, na ndiyo maananafanya kila kitu kama Baba alivyoniamuru.Simameni, tutoke hapa!”

“Mimi ni mzabibu wa kweli, na Babayangu ndiye mkulima. 2 Yeyehuliondoa ndani yangu kila tawi

lisilozaa matunda, na kila tawi lizaalohulisafisha lipate kuzaa zaidi. 3 Ninyimmekwisha kuwa safi kwa sababu ya uleujumbe niliowaambieni. 4 Kaeni ndani yangu,nami nikae ndani yenu. Tawi haliwezi pekeyake kuzaa matunda lisipokaa katika mzabibuhali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matundamsipokaa ndani yangu. 5 “Mimi ni mzabibu,nanyi ni matawi yake. Akaaye ndani yangu,nami ndani yake, huyo atazaa matunda mengi,maana bila mimi hamwezi kufanya chochote. 6

Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa njekama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watuhuliokota tawi la namna hiyo na kulitupa

YOHANA MTAKATIFU 13:30

82

Page 83: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

motoni liungue. 7 Mkikaa ndani yangu namaneno yangu yakikaa ndani yenu, basi,ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa. 8

Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matundamengi na kuwa wanafunzi wangu. 9 Miminimewapenda ninyi kama vile Babaalivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu.10 Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendolangu, kama vile nami nilivyozishika amri zaBaba yangu na kukaa katika pendo lake. 11

Nimewaambieni mambo haya ili furaha yanguikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike. 12

Hii ndiyo amri yangu: pendaneni; pendanenikama nilivyowapenda ninyi. 13 Hakunaupendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtuatoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14

Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru.15 Ninyi siwaiti tena watumishi, maanamtumishi hajui anachofanya bwana wake.Lakini mimi nimewaita ninyi rafiki, kwa sababunimewajulisha yote ambayo nimeyasikiakutoka kwa Baba yangu. 16 Ninyihamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni nakuwatuma mwende mkazae matunda,matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapaninyi chochote mumwombacho kwa jina langu.17 Basi, amri yangu kwenu ndiyo hii:pendaneni. 18 “Kama ulimwengu ukiwachukianinyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimikabla haujawachukia ninyi. 19 Kamamngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwenguungaliwapenda ninyi kama watu wake. Lakinikwa vile ninyi si wa ulimwengu, ila miminimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwasababu hiyo ulimwengu unawachukieni. 20

Kumbukeni niliyowaambieni: mtumishi simkuu zaidi kuliko bwana wake. Ikiwawamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia;kama wameshika neno langu, watalishika nalenu pia. 21 Lakini hayo yote watawatendeenininyi kwa sababu ya jina langu, kwanihawamjui yeye aliyenituma. 22 Kamanisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa nahatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwambahawana dhambi. 23 Anayenichukia mimi,anamchukia na Baba yangu pia. 24 Kamanisingalifanya kwao mambo ambayo hakunamtu mwingine amekwisha yafanyawasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameonaniliyoyafanya wakinichukia mimi, wakamchukiana Baba yangu pia. 25 Na hivi ni lazima yatimieyale yaliyoandikwa katika Sheria yao:Wamenichukia bure! 26 “Atakapokuja huyoMsaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwaBaba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba,yeye atanishuhudia mimi. 27 Nanyi piamtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa namitangu mwanzo.

“Nimewaambieni hayo kusudimsiiache imani yenu. 2 Watuwatawatenga ninyi na masunagogi

yao. Tena, wakati unakuja ambapo kilaatakayewaua ninyi atadhani anamhudumia

Mungu. 3 Watawatendeeni mambo hayo kwasababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi.4 Basi, nimewaambieni mambo haya ili saayake itakapofika mkumbuke kwambaniliwaambieni. “Sikuwaambieni mambo hayatangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamojananyi. 5 Lakini sasa namwendea yulealiyenituma; na hakuna hata mmoja wenuanayeniuliza: Unakwenda wapi? 6 Kwa kuwanimewaambieni mambo hayo mmejaa huzunimioyoni mwenu. 7 Lakini, nawaambieniukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu,maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu.Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu. 8

Naye atakapokuja atawathibitishiawalimwengu kwamba wamekosea kuhusudhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu. 9

Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababuhawaniamini; 10 kuhusu uadilifu, kwa sababunaenda zangu kwa Baba, nanyi hamtanionatena; 11 kuhusu hukumu kwa sababu mkuuwa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa. 12

“Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwasasa hamwezi kuyastahimili. 13 Lakiniatakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongozakwenye ukweli wote; maana hatasema kwamamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieniyote atakayosikia, na atasema mamboyatakayokuwa yanakuja. 14 Yeye atanitukuzamimi kwa kuwa atawaambieni yaleatakayopata kutoka kwangu. 15 Vyote alivyonavyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesemakwamba huyo Roho Mtakatifu atawaambieniyale atakayopata kutoka kwangu. 16 “Badokitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baadaya kitambo kidogo tena mtaniona!” 17 Hapobaadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, “Anamaana gani anapotwambia: Bado kitambokidogo nanyi hamtaniona; na baada yakitambo kidogo tena mtaniona? Tenaanasema: Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!”18 Basi, wakawa wanaulizana, “Ana maanagani anaposema: Bado kitambo kidogo?Hatuelewi anaongelea nini.” 19 Yesu alijuakwamba walitaka kumwuliza, basiakawaambia, “Je, mnaulizana juu ya yaleniliyosema: Bado kitambo kidogo nanyihamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tenamtaniona? 20 Nawaambieni kweli, ninyi mtaliana kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi:mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageukakuwa furaha. 21 Wakati mama anapojifunguahuona huzuni kwa sababu saa ya maumivuimefika; lakini akisha jifungua hayakumbukitena maumivu hayo kwa sababu ya furahakwamba mtu amezaliwa duniani. 22 Ninyi piamna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyimtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyohakuna mtu atakayeiondoa kwenu. 23 Sikuhiyo hamtaniomba chochote. Kwelinawaambieni, chochote mtakachomwombaBaba kwa jina langu, atawapeni. 24 Mpakasasa hamjaomba chochote kwa jina langu.

YOHANA MTAKATIFU 16:24

83

Page 84: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

17

18

Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenuikamilike. 25 “Nimewaambieni mambo hayokwa mafumbo. Lakini wakati utakuja ambapositasema tena nanyi kwa mafumbo, balinitawaambieni waziwazi juu ya Baba. 26 Sikuhiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambiikwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;27 maana yeye mwenyewe anawapenda ninyi,kwa sababu ninyi mmenipenda mimi nammeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 28

Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni;na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwaBaba.” 29 Basi, wanafunzi wakewakamwambia, “Ahaa! Sasa unasema waziwazikabisa bila kutumia mafumbo. 30 Sasa tunajuakwamba wewe unajua kila kitu, na huna hajaya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyotunaamini kwamba umetoka kwa Mungu.” 31

Yesu akawajibu, “Je, mnaamini sasa? 32 Wakatiunakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyinyote mtatawanyika kila mtu kwake, naminitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimisiko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.33 Nimewaambieni mambo haya ili mpatekuwa na amani katika kuungana nami.Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakinijipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!”

Yesu alipokwisha sema hayo,alitazama juu mbinguni, akasema,“Baba, saa imefika! Mtukuze Mwanao

ili naye Mwana apate kukutukuza. 2 Maanaulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote iliawape uzima wa milele wote hao uliompa. 3

Na uzima wa milele ndio huu: kukujua weweuliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjuaYesu Kristo uliyemtuma. 4 Mimi nimekutukuzahapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipanifanye. 5 Sasa, Baba, nitukuze mbele yakokwa ule utukufu niliokuwa nao kabla yakuumbwa ulimwengu. 6 “Nimekufanyaujulikane kwa watu wale ulionipa kutokaduniani. Walikuwa watu wako, nawe ukanipawawe wangu; nao wamelishika neno lako. 7

Sasa wanajua kwamba kila ulichonipakimetoka kwako. 8 Mimi nimewapa uleujumbe ulionipa nao wameupokea; wanajuakwamba kweli nimetoka kwako, na wanaaminikwamba wewe ulinituma. 9 “Nawaombea hao;siuombei ulimwengu, ila nawaombea haoulionipa, maana ni wako. 10 Yote niliyo nayo niyako, na yako ni yangu; na utukufu wanguumeonekana ndani yao. 11 Na sasa najakwako; simo tena ulimwenguni, lakini waowamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwanguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwawekesalama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyommoja. 12 Nilipokuwa nao, mimi niliwawekasalama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Miminimewalinda, wala hakuna hata mmoja waoaliyepotea, isipokuwa yule aliyelazimikakupotea ili Maandiko Matakatifu yapatekutimia. 13 Basi, sasa naja kwako, nanimesema mambo haya ulimwenguni, ili

waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu. 14

Mimi nimewapa neno lako, nao ulimwenguukawachukia, kwa sababu wao si waulimwengu kama vile nami nisivyo waulimwengu. 15 Siombi uwatoe ulimwenguni,bali naomba uwakinge na yule Mwovu. 16 Waosi wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo waulimwengu. 17 Waweke wakfu kwa ukweli;neno lako ni ukweli. 18 Kama vile ulivyonitumaulimwenguni, nami pia nimewatuma waoulimwenguni; 19 na kwa ajili yao mimimwenyewe najiweka wakfu ili nao piawafanywe wakfu katika ukweli. 20 “Siwaombeihao tu, bali nawaombea pia wotewatakaoamini kutokana na ujumbe wao. 21

Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba!Naomba wawe ndani yetu kama vile weweulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naombawawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upatekuamini kwamba wewe ulinituma. 22 Miminimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, iliwawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja; 23

mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu;naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, iliulimwengu upate kujua kwamba weweulinituma, na kwamba unawapenda wao kamaunavyonipenda mimi. 24 “Baba! Nataka waoulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, iliwauone utukufu wangu ulionipa; kwa kuwaulinipenda kabla ya kuumbwa ulimwengu. 25

Baba Mwema! Ulimwengu haukujui, lakinimimi nakujua. Hawa nao wanajua kwambawewe ulinituma. 26 Nimekufanya ujulikanekwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendoulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwendani yao.”

Yesu alipokwisha sema hayo,alikwenda ng'ambo ya kijito Kedroni,pamoja na wanafunzi wake. Mahali

hapo palikuwa na bustani, naye Yesu akaingiahumo pamoja na wanafunzi wake. 2 Yuda,aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwanimara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wakehuko. 3 Basi, Yuda alichukua kikosi cha askarina walinzi kutoka kwa makuhani wakuu naMafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa,mienge na silaha. 4 Yesu, hali akijua yoteyatakayompata, akatokea, akawauliza,“Mnamtafuta nani?” 5 Nao wakamjibu, “Yesuwa Nazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.”Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamojanao. 6 Basi, Yesu alipowaambia: “Mimi ndiye”,wakarudi nyuma, wakaanguka chini. 7 Yesuakawauliza tena, “Mnamtafuta nani?”Wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!” 8 Yesuakawaambia, “Nimekwisha waambienikwamba mimi ndiye. Basi, kama mnanitafutamimi, waacheni hawa waende zao.” 9 (Alisemahayo ili yapate kutimia yale aliyosema: “Waleulionipa sikumpoteza hata mmoja.”) 10 SimoniPetro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa,akamkata sikio la kulia mtumishi wa KuhaniMkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko. 11 Basi,

YOHANA MTAKATIFU 16:25

84

Page 85: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

19

Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upangawako alani. Je, nisinywe kikombe alichonipaBaba?” 12 Kile kikosi cha askari, mkuu wake nawalinzi wa Wayahudi walimkamata Yesu,wakamfunga 13 na kumpeleka kwanza kwaAnasi; Anasi alikuwa baba mkwe wa Kayafaambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo. 14

Huyo Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauriWayahudi kwamba ni afadhali mtu mmoja afekwa ajili ya taifa. 15 Simoni Petro pamoja namwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyomwanafunzi mwingine alikuwa anajulikanakwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia pamoja naYesu ndani ya ukumbi wa Kuhani Mkuu. 16

Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu namlango. Basi, huyo mwanafunzi mwinginealiyekuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuualitoka nje akasema na mjakazi, mngojamlango, akamwingiza Petro ndani. 17 Huyomsichana mngoja mlango akamwuliza Petro,“Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtuhuyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!” 18

Watumishi na walinzi walikuwa wamewashamoto kwa sababu kulikuwa na baridi, wakawawanaota moto. Naye Petro alikuwaamesimama pamoja nao akiota moto. 19 Basi,Kuhani akamwuliza Yesu juu ya wanafunziwake na mafundisho yake. 20 Yesu akamjibu,“Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kilamara nimefundisha katika masunagogi naHekaluni, mahali wakutanikiapo Wayahudiwote; na wala sijasema chochote kwa siri. 21

Kwa nini waniuliza mimi? Waulize walewaliosikia nini niliwaambia. Wao wanajuanilivyosema.” 22 Alipokwisha sema hayo mlinzimmoja aliyekuwa amesimama hapo akampigakofi akisema, “Je, ndivyo unavyomjibu KuhaniMkuu?” 23 Yesu akamjibu, “Kama nimesemavibaya, onyesha huo ubaya; lakini ikiwanimesema vema, mbona wanipiga?” 24 Basi,Anasi akampeleka Yesu akiwa amefungwa,kwa Kuhani Mkuu Kayafa. 25 Petro alikuwahapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je,nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeyeakakana na kusema, “Si mimi!” 26 Mmoja wawatumishi wa Kuhani Mkuu, jamaa wa yulealiyekatwa sikio na Petro, akamwuliza, “Je,mimi sikukuona wewe bustanini pamojanaye?” 27 Petro akakana tena; mara jogooakawika. 28 Basi, walimchukua Yesu kutokakwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwaalfajiri, nao ili waweze kula Pasaka,hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwanajisi. 29 Kwa hiyo, Pilato aliwaendea nje,akasema, “Mna mashtaka gani juu ya mtuhuyu?” 30 Wakamjibu, “Kama huyuhangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.”31 Pilato akawaambia, “Haya, mchukueni ninyiwenyewe, mkamhukumu kufuatana na Sheriayenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi hatunamamlaka ya kumwua mtu yeyote.” 32

(Ilifanyika hivyo yapate kutimia manenoaliyosema Yesu kuonyesha atakufa kifo gani.)

33 Pilato akaingia tena ndani ya ikulu,akamwita Yesu na kumwuliza: “Ati wewe ndiyeMfalme wa Wayahudi?” 34 Yesu akamjibu, “Je,hayo ni maneno yako au wenginewamekwambia habari zangu?” 35 Pilatoakamjibu, “Je, ni Myahudi mimi? Taifa lako namakuhani wamekuleta kwangu. Umefanyanini?” 36 Yesu akamjibu, “Ufalme wangu si waulimwengu huu. Kama ufalme wanguungekuwa wa ulimwengu huu watumishiwangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwaWayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wahapa.” 37 Hapo Pilato akamwambia, “Basi,wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Weweumesema kwamba mimi ni Mfalme. Miminimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyonimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu yaukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.” 38

Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?”Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tenaWayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatiayoyote kwake. 39 Lakini, mnayo desturikwamba mimi niwafungulie mfungwa mmojawakati wa Pasaka. Basi, mwatakaniwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?” 40

Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!”Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.

Basi, Pilato akaamuru Yesuachukuliwe, apigwe viboko. 2 Naoaskari wakasokota taji ya miiba,

wakamtia kichwani, wakamvika na joho larangi ya zambarau. 3 Wakawa wanakujambele yake na kusema: “Shikamoo, Mfalme waWayahudi!” Wakampiga makofi. 4 Pilatoakatoka tena nje, akawaambia, “Tazameni,namleta nje kwenu, mpate kujua kwambamimi sikuona hatia yoyote kwake.” 5 Basi, Yesuakatoka nje amevaa taji ya miiba na joho larangi ya zambarau. Pilato akawaambia,“Tazameni! Mtu mwenyewe ni huyo.” 6

Makuhani wakuu na walinzi walipomwonawakapaaza sauti: “Msulubishe! Msulubishe!”Pilato akawaambia, “Mchukueni basi, ninyiwenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimisikuona hatia yoyote kwake.” 7 Wayahudiwakamjibu, “Sisi tunayo Sheria, na kufuatanana Sheria hiyo, ni lazima afe, kwa sababualijifanya kuwa Mwana wa Mungu.” 8 Pilatoaliposikia maneno hayo akazidi kuogopa. 9

Basi, akaingia tena ndani ya ikulu, akamwulizaYesu, “Umetoka wapi wewe?” Lakini Yesuhakumjibu neno. 10 Hivyo Pilato akamwambia,“Husemi nami? Je, hujui kwamba ninayomamlaka ya kukufungua na mamlaka yakukusulubisha?” 11 Yesu akamjibu,“Hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangukama hungepewa na Mungu. Kwa sababuhiyo, yule aliyenikabidhi kwako ana dhambikubwa zaidi.” 12 Tangu hapo, Pilato akawaanatafuta njia ya kumwachilia, lakini Wayahudiwakapiga kelele: “Ukimwachilia huyu mtu,wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtuanayejifanya kuwa Mfalme humpinga Kaisari!”

YOHANA MTAKATIFU 19:12

85

Page 86: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

20

13 Basi, Pilato aliposikia maneno hayoakamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti chahukumu, mahali paitwapo: “Sakafu ya Mawe”(kwa Kiebrania, Gabatha). 14 Ilikuwa yapatasaa sita mchana, siku ya maandalio ya Pasaka.Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni,Mfalme wenu!” 15 Wao wakapaaza sauti:“Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” Makuhaniwakuu wakajibu, “Sisi hatuna Mfalmeisipokuwa Kaisari!” 16 Basi, hapo Pilatoakamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe.Basi, wakamchukua Yesu. 17 Naye akatokaakiwa amejichukulia msalaba wake kwendamahali paitwapo “Fuvu la Kichwa”, (kwaKiebrania Golgotha). 18 Hapo ndipowalipomsulubisha, na pamoja nayewaliwasulubisha watu wengine wawili; mmojaupande wake wa kulia na mwingine upandewake wa kushoto, naye Yesu katikati. 19 Pilatoaliandika ilani akaiweka juu ya msalaba. Nayoilikuwa imeandikwa hivi: “Yesu wa Nazareti,Mfalme wa Wayahudi.” 20 Wayahudi wengiwaliisoma ilani hiyo, maana mahali hapoaliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji.Tena ilani hiyo ilikuwa imeandikwa kwaKiebrania, Kilatini, na Kigiriki. 21 Basi,makuhani wakuu wakamwambia Pilato,“Usiandike: Mfalme wa Wayahudi, ila Yeyealisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.” 22

Pilato akajibu, “Niliyoandika, nimeandika!” 23

Askari walipokwisha msulubisha Yesu,walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungumanne, fungu moja kwa kila askari.Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyoilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bilamshono. 24 Basi, hao askari wakashauriana:“Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.”Jambo hilo lilifanyika ili yatimie MaandikoMatakatifu yasemayo: “Waligawana mavaziyangu, na nguo yangu wakaipigia kura.” Basi,ndivyo walivyofanya hao askari. 25 Karibu namsalaba wake Yesu walikuwa wamesimamamama yake, na dada ya mama yake, Mariamke wa Kleopa, na Maria Magdalene. 26 Yesualipomwona mama yake, na karibu nayeamesimama yule mwanafunzi aliyempenda,akamwambia mama yake: “Mama! Tazama,huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambiayule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mamayako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzialimchukua akae nyumbani kwake. 28 Yesualijua kwamba yote yalikuwa yametimia; na, iliMaandiko Matakatifu yapate kutimia,akasema, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa nabakuli limejaa siki. Basi, wakachovya sifongokatika hiyo siki, wakaitia juu ya ufito wahusopo, wakamwekea mdomoni. 30 Yesualipokwisha pokea hiyo siki, akasema,“Yametimia!” Kisha akainama kichwa, akatoaroho. 31 Ilikuwa Ijumaa, siku ya Maandalio.Kwa hiyo, kusudi miili isikae msalabani siku yaSabato, maana siku hiyo ya Sabato ilikuwa sikukubwa, Wayahudi walimwomba Pilato miguu

ya hao waliosulubiwa ivunjwe na miili yaoiondolewe. 32 Basi, askari walikwenda,wakaivunja miguu ya yule mtu wa kwanza nayule wa pili ambao walikuwa wamesulubiwapamoja na Yesu. 33 Lakini walipomfikia Yesuwaliona kwamba alikwisha kufa, na hivyohawakumvunja miguu. 34 Lakini askari mmojaalimtoboa ubavuni kwa mkuki, na maraikatoka damu na maji. 35 (Naye aliyeona tukiohilo ametoa habari zake ili nanyi mpatekuamini. Na hayo aliyosema ni ukweli, tenayeye anajua kwamba anasema ukweli.) 36

Jambo hilo lilitendwa ili Maandiko Matakatifuyatimie: “Hapana hata mfupa wake mmojautakaovunjwa.” 37 Tena Maandiko mengineyanasema: “Watamtazama yulewaliyemtoboa.” 38 Baada ya hayo, Yosefu,mwenyeji wa Armathaya, alimwomba Pilatoruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. (Yosefualikuwa mfuasi wa Yesu, lakini kwa siri, maanaaliwaogopa viongozi wa Wayahudi). Basi, Pilatoakamruhusu. Hivyo Yosefu alikwenda,akauondoa mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemoambaye hapo awali alikuwa amemwendeaYesu usiku, akaja akiwa amechukuamchanganyiko wa manemane na ubani kiasicha kilo thelathini. 40 Basi, waliutwaa mwili waYesu, wakaufunga sanda pamoja na manukatokufuatana na desturi ya Wayahudi katikakuzika. 41 Mahali hapo aliposulubiwa Yesupalikuwa na bustani, na katika bustani hiyokulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwabado mtu yeyote ndani yake. 42 Basi, kwasababu ya shughuli za Wayahudi za maandalioya Sabato, na kwa vile kaburi hilo lilikuwakaribu, wakamweka Yesu humo.

Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwabado na giza, Maria Magdalenealikwenda kaburini, akaliona lile jiwe

limeondolewa mlangoni pa kaburi. 2 Basi,akaenda mbio hadi kwa Petro na yulemwanafunzi mwingine ambaye Yesualimpenda, akawaambia, “WamemwondoaBwana kaburini, na wala hatujuiwalikomweka.” 3 Petro pamoja na yulemwanafunzi mwingine wakaenda kaburini. 4

Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzimwingine alikimbia mbio zaidi kuliko Petro,akatangulia kufika kaburini. 5 Alipoinama nakuchungulia ndani, aliona sanda, lakinihakuingia ndani. 6 Simoni Petro naye akajaakimfuata, akaingia kaburini; humo akaonasanda, 7 na kile kitambaa alichofungwa Yesukichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwapamoja na hiyo sanda, bali kilikuwakimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake. 8

Kisha yule mwanafunzi mwinginealiyemtangulia kufika kaburini, akaingia piandani, akaona, akaaamini. 9 (Walikuwa badohawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosemakwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka wafu).10 Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani. 11

Maria alikuwa amesimama nje ya kaburi, akilia.

YOHANA MTAKATIFU 19:13

86

Page 87: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

21

Huku akiwa bado analia, aliinama nakuchungulia kaburini, 12 akawaona malaikawawili waliovaa mavazi meupe, wameketi palemwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmojakichwani na wa pili miguuni. 13 Hao malaikawakamwuliza, “Mama, kwa nini unalia?” Nayeakawaambia, “Wamemwondoa Bwana wangu,na wala sijui walikomweka!” 14 Baada yakusema hayo, aligeuka nyuma, akamwonaYesu amesimama hapo, lakini asitambue yakuwa ni Yesu. 15 Yesu akamwuliza, “Mama,kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Maria,akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani,akamwambia, “Mheshimiwa, kama ni weweumemwondoa, niambie ulikomweka, naminitamchukua.” 16 Yesu akamwambia, “Maria!”Naye Maria akageuka, akamwambia kwaKiebrania, “Raboni” (yaani “Mwalimu”). 17 Yesuakamwambia, “Usinishike; sijakwenda badojuu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zanguuwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu naBaba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”18 Hivyo Maria Magdalene akaenda akawapahabari wale wanafunzi kuwa amemwonaBwana, na kwamba alikuwa amemwambiahivyo. 19 Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili.Wanafunzi walikuwa wamekutana pamojandani ya nyumba, na milango ilikuwaimefungwa kwa sababu waliwaogopa viongoziwa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama katiyao, akawaambia, “Amani kwenu!” 20

Alipokwisha sema hayo, akawaonyeshamikono yake na ubavu wake. Basi, haowanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana.21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu!Kama vile Baba alivyonituma mimi, naminawatuma ninyi.” 22 Alipokwisha sema hayo,akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni RohoMtakatifu. 23 Mkiwasamehe watu dhambi zao,wamesamehewa; msipowaondolea,hawasamehewi.” 24 Thoma mmoja wa walekumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwapamoja nao wakati Yesu alipokuja. 25 Basi,wale wanafunzi wengine wakamwambia,“Tumemwona Bwana.” Thoma akawaambia,“Nisipoona mikononi mwake alama zamisumari, na kutia kidole changu katika kovuhizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake,sitasadiki.” 26 Basi, baada ya siku nane haowanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani,na Thoma alikuwa pamoja nao. Milangoilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja,akasimama kati yao, akasema, “Amani kwenu!”27 Kisha akamwambia Thoma, “Lete kidolechako hapa uitazame mikono yangu; letemkono wako ukautie ubavuni mwangu. Usiwena mashaka, ila amini!” 28 Thoma akamjibu,“Bwana wangu na Mungu wangu!” 29 Yesuakamwambia, “Je, unaamini kwa kuwaumeniona? Heri yao wale ambao hawajaona,lakini wameamini.” 30 Yesu alifanya mbele yawanafunzi wake ishara nyingine nyingi ambazohazikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi

zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesuni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuaminimpate kuwa na uzima kwa nguvu ya jina lake.

Baada ya hayo Yesu aliwatokea tenawanafunzi wake kando ya ziwaTiberia. Aliwatokea hivi: 2 Simoni

Petro, Thoma (aitwaye Pacha), na Nathanielimwenyeji wa Kana Galilaya, wana wawili waZebedayo na wanafunzi wake wengine wawili,walikuwa wote pamoja. 3 Simoni Petroaliwaambia, “Nakwenda kuvua samaki.” Naowakamwambia, “Nasi tutafuatana nawe.” Basi,wakaenda, wakapanda mashua, lakini usikuhuo hawakupata chochote. 4 Kulipoanzakupambazuka, Yesu alisimama kando ya ziwa,lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwayeye. 5 Basi, Yesu akawauliza, “Vijana,hamjapata samaki wowote sio?” Waowakamjibu, “La! Hatujapata kitu.” 6 Yesuakawaambia, “Tupeni wavu upande wa kuliawa mashua nanyi mtapata samaki.” Basi,wakatupa wavu lakini sasa hawakuwezakuuvuta tena kwa wingi wa samaki. 7 Hapoyule mwanafunzi aliyependwa na Yesuakamwambia Petro, “Ni Bwana!” Simoni Petroaliposikia ya kuwa ni Bwana, akajifunga vazilake (maana hakuwa amelivaa), akarukiamajini. 8 Lakini wale wanafunzi wenginewalikuja pwani kwa mashua huku wanauvutawavu uliojaa samaki; hawakuwa mbali na nchikavu, ila walikuwa yapata mita mia mojakutoka ukingoni. 9 Walipofika nchi kavuwaliona moto wa makaa umewashwa na juuyake pamewekwa samaki na mkate. 10 Yesuakawaambia, “Leteni hapa baadhi ya samakimliovua.” 11 Basi, Simoni Petro akapandamashuani, akavuta hadi nchi kavu ule wavuuliokuwa umejaa samaki wakubwa mia mojana hamsini na watatu. Na ingawa walikuwawengi hivyo wavu haukukatika. 12 Yesuakawaambia, “Njoni mkafungue kinywa.”Hakuna hata mmoja wao aliyethubutukumwuliza: “Wewe ni nani?” Maana walijuaalikuwa Bwana. 13 Yesu akaja, akatwaa mkateakawapa; akafanya vivyo hivyo na wale samaki.14 Hii ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokeawanafunzi wake baada ya kufufuka kutokawafu. 15 Walipokwisha kula, Yesu alimwulizaSimoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je,wanipenda mimi zaidi kuliko hawa?” Nayeakajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba miminakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza wanakondoo wangu.” 16 Kisha akamwambia maraya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je,wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana;wajua kwamba nakupenda.” Yesuakamwambia, “Tunza kondoo wangu.” 17

Akamwuliza mara ya tatu, “Simoni mwana waYohane! Je, wanipenda?” Hapo Petroakahuzunika kwa sababu alimwuliza mara yatatu: “Wanipenda?” akamwambia, “Bwana,wewe wajua yote; wewe wajua kwamba miminakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza

YOHANA MTAKATIFU 21:17

87

Page 88: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

kondoo wangu! 18 Kweli nakwambia,ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi nakwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwamzee utanyosha mikono yako, na mtumwingine atakufunga na kukupelekausikopenda kwenda.” 19 (Kwa kusema hivyo,alionyesha jinsi Petro atakavyokufa nakumtukuza Mungu.) Kisha akamwambia,“Nifuate.” 20 Hapo Petro akageuka, akamwonayule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda,anafuata (Huyu mwanafunzi ndiye yuleambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaakaribu sana na Yesu na kumwuliza: “Bwana ninani atakayekusaliti?”) 21 Basi, Petroalipomwona huyo akamwuliza Yesu, “Bwana,

na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “Kama natakaabaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini?Wewe nifuate mimi.” 23 Basi, habari hiyoikaenea miongoni mwa wale ndugu kwambamwanafunzi huyo hafi. Lakini Yesuhakumwambia kwamba mwanafunzi huyohafi, ila, “Kama nataka abaki mpakanitakapokuja, yakuhusu nini?” 24 Huyo ndiyeyule aliyeshuhudia mambo haya nakuyaandika. Nasi twajua kwamba aliyoyasemani kweli. 25 Kuna mambo mengine mengialiyofanya Yesu, ambayo kama yangeandikwayote, moja baada ya lingine, nadhani hataulimwengu wenyewe usingetosha kuviwekavitabu ambavyo vingeandikwa.

YOHANA MTAKATIFU 21:18

88

Page 89: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

MATENDO YA MITUME

Ndugu Theofilo, Katika kitabu chakwanza niliandika juu ya mambo yoteYesu aliyotenda na kufundisha tangu

mwanzo wa kazi yake 2 mpaka siku ilealipochukuliwa mbinguni. Kabla yakuchukuliwa mbinguni aliwapa maagizo kwanjia ya Roho Mtakatifu wale mitumealiowachagua. 3 Kwa muda wa siku arobainibaada ya kifo chake aliwatokea mara nyingikwa namna ambazo zilithibitisha kabisakwamba alikuwa hai. Walimwona, nayealiongea nao juu ya ufalme wa Mungu. 4

Wakati walipokutana pamoja aliwaamuru hivi:“Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeeni ilezawadi aliyoahidi Baba, zawadi ambayomlikwisha nisikia nikiongea juu yake. 5 KwaniYohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya sikuchache, ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”6 Basi, mitume walipokutana pamoja na Yesu,walimwuliza, “Je Bwana, wakati huu ndipoutakaporudisha ule ufalme kwa Israeli?” 7

Lakini Yesu akawaambia, “Nyakati na majira yamambo hayo viko chini ya mamlaka ya Babayangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.8 Lakini wakati Roho Mtakatifuatakapowashukieni ninyi, mtajazwa nguvu namtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu,katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hatamiisho ya dunia.” 9 Baada ya kusema hayo,wote wakiwa wanamtazama, alichukuliwambinguni; wingu likamficha wasimwone tena.10 Walipokuwa bado wanatazama juu angani,akiwa anakwenda zake, mara watu wawiliwaliokuwa wamevaa nguo nyeupe walisimamakaribu nao, 11 wakasema, “Enyi wananchi waGalilaya! Mbona mnasimama mkitazamaangani? Yesu huyu ambaye amechukuliwakutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tenanamna hiyohiyo mliivyomwona akiendambinguni.” 12 Kisha mitume wakarudiYerusalemu kutoka mlima wa Mizeituni uliokokaribu kilomita moja kutoka mjini. 13

Walipofika mjini waliingia katika chumbaghorofani ambamo walikuwa wanakaa; naowalikuwa Petro, Yohane, Yakobo, Andrea, Filipona Thoma, Bartholomayo na Mathayo, Yakobomwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yudamwana wa Yakobo. 14 Hawa wotewalikusanyika pamoja kusali, pamoja nawanawake kadha wa kadha, na Maria mamayake Yesu, na ndugu zake. 15 Siku chachebaadaye, kulikuwa na mkutano wa waumini,karibu watu mia moja na ishirini. Petro

alisimama mbele yao, 16 akasema, “Nduguzangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya MaandikoMatakatifu itimie, sehemu ambayo RohoMtakatifu, kwa maneno ya Daudi, alibashirihabari za Yuda ambaye aliwaongoza walewaliomtia Yesu nguvuni. 17 Yuda alikuwammoja wa kikundi chetu maana alichaguliwaashiriki huduma yetu. 18 (“Mnajua kwambayeye alinunua shamba kwa zile fedha alizopatakutokana na kitendo chake kiovu. Akaangukachini, akapasuka na matumbo yakeyakamwagika nje. 19 Kila mtu katikaYerusalemu alisikia habari za tukio hilo nahivyo, kwa lugha yao, wakaliita lile shambaHekeli Dama, maana yake, Shamba la Damu.)20 Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi:Nyumba yake ibaki mahame; mtu yeyoteasiishi ndani yake. Tena imeandikwa: Mtumwingine achukue nafasi yake katika hudumahiyo. 21 Kwa hiyo, ni lazima mtu mwingineajiunge nasi kama shahidi wa ufufuo wakeBwana Yesu. 22 Anapaswa kuwa mmoja wawale waliokuwa katika kundi letu wakati woteBwana alipokuwa anasafiri pamoja nasi, tanguwakati Yohane alipokuwa anabatiza mpakasiku ile Yesu alipochukuliwa kutoka kwetukwenda mbinguni.” 23 Basi, wakataja majinaya watu wawili; wa kwanza Yosefu aliyeitwaBarsaba (au pia Yusto), na wa pili Mathia. 24

Kisha wakasali: “Bwana, wewe unajua mioyo yawatu wote. Hivyo, utuonyeshe ni yupi kati yahawa wawili uliyemchagua 25 ili achukuenafasi hii ya huduma ya kitume aliyoacha Yudaakaenda mahali pake mwenyewe.” 26 Hapo,wakapiga kura; kura ikampata Mathia, nayeakaongezwa katika idadi ya wale mitumewengine kumi na mmoja.

Siku ya Pentekoste ilipofika, wauminiwote walikuwa wamekusanyika pamoja.2 Ghafla, sauti ikasikika kutoka angani;

sauti iliyokuwa kama ya upepo mkali, ikajazaile nyumba yote walimokuwa wamekaa. 3

Kisha, vikatokea vitu vilivyoonekana kamandimi za moto, vikagawanyika na kutua juu yakila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa RohoMtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbalikadiri Roho alivyowawezesha. 5 Na hukoYerusalemu walikuwako Wayahudi, watuwamchao Mungu, waliotoka katika kila nchiduniani. 6 Waliposikia sauti hiyo, kundi kubwala watu lilikusanyika. Wote walishtuka sanakwani kila mmoja wao aliwasikia hao wauminiwakisema kwa lugha yake mwenyewe. 7

MATENDO YA MITUME 2:7

89

Page 90: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

Walistaajabu na kushangaa, wakisema, “Je,hawa wote tunaowasikia wakisema hivi, siwenyeji wa Galilaya? 8 Imekuwaje, basi,kwamba kila mmoja wetu anawasikiawakisema kwa lugha yake mwenyewe? 9

Baadhi yetu ni Waparthi, Wamedi na Waelami;wengine ni wenyeji wa Mesopotamia, Yudea,Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frugia naPamfulia, Misri na sehemu za Libya karibu naKurene; wengine wetu ni wageni kutoka Roma,11 Wayahudi na watu walioongokea dini yaKiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia.Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetuwenyewe mambo makuu ya Mungu.” 12 Wotewalishangaa na kufadhaika huku wakiulizana,“Hii ina maana gani?” 13 Lakini wenginewakawadhihaki wakisema, “Watu hawawamelewa divai mpya!” 14 Lakini Petroalisimama pamoja na wale kumi na mmojaakaanza kuwahutubia watu kwa sauti kubwa:“Ndugu Wayahudi nanyi nyote mnaokaa hapaYerusalemu, sikilizeni kwa makini manenoyangu. 15 Watu hawa hawakulewa kamamnavyodhani; mbona ni saa tatu tu asubuhi?16 Ukweli ni kwamba jambo hili ni lilealilosema nabii Yoeli: 17 Katika siku zile zamwisho, asema Bwana, nitawamiminiabinadamu wote Roho wangu. Watoto wenu,wanaume kwa wanawake, watautangazaujumbe wangu; vijana wenu wataona maono,na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, hatawatumishi wangu, wanaume kwa wanawake,nitawamiminia Roho wangu, siku zile, naowatautangaza ujumbe wangu. 19 Nitatendamiujiza juu angani, na ishara chini duniani;kutakuwa na damu, moto na moshi mzito; 20

jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundukama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu natukufu ya Bwana. 21 Hapo, yeyoteatakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.22 “Wananchi wa Israeli, sikilizeni manenohaya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambayemamlaka yake ya kimungu yalithibitishwakwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungualizofanya kati yenu kwa njia yake, kamamnavyojua. 23 Kufuatana na mpango wakemwenyewe Mungu alikwisha amua kwambaYesu angetiwa mikononi mwenu; nanyimkamuua kwa kuwaachia watu wabayawamsulubishe. 24 Lakini Mungu alimfufuakutoka wafu akamwokoa katika maumivu yakifo kwa maana haingewezekana kabisa kifokimfunge. 25 Maana Daudi alisema juu yakehivi: Nilimwona Bwana mbele yangu daima;yuko nami upande wangu wa kulia, na hivyositatikisika. 26 Kwa hiyo, moyo wangu ulifurahi;tena nilipiga vigelegele vya furaha. Mwiliwangu utakaa katika tumaini; 27 kwa kuwahutaiacha roho yangu katika kuzimu, walakumruhusu mtakatifu wako aoze. 28

Umenionyesha njia za kuufikia uzima, kuwakokwako kwanijaza furaha! 29 “Ndugu zangu,napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo

yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa,akazikwa, tena kaburi lake liko papa hapa petumpaka leo. 30 Lakini kwa vile Daudi alikuwanabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapokwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wakekuwa mfalme mahali pake. 31 Daudi alionakabla mambo yatakayofanywa na Mungu nahivyo akasema juu ya ufufuo wa Kristo wakatialiposema: Hakuachwa kuzimu, mwili wakehaukuoza. 32 Basi, Mungu alimfufua huyoYesu na sisi sote ni mashahidi wa tukio hilo. 33

Yesu aliinuliwa juu mpaka upande wa kulia waMungu, akapokea kutoka kwa Baba ile zawadialiyoahidi yaani Roho Mtakatifu; namnachoona sasa na kusikia ni mmiminiko wahuyo Roho. 34 Maana Daudi mwenyewe,hakupanda mpaka mbinguni; ila yeye alisema:Bwana alimwambia Bwana wangu: Ketiupande wangu wa kulia, 35 hadinitakapowafanya adui zako kibao chakukanyagia miguu yako. 36 “Watu wote waIsraeli wanapaswa kufahamu kwa hakikakwamba huyo Yesu mliyemsulubisha ninyi,ndiye huyo ambaye Mungu amemfanya kuwaBwana na Kristo.” 37 Basi, watu waliposikiahayo, walichomwa moyo, wakawauliza Petrona wale mitume wenzake: “Ndugu zetu,tufanye nini?” 38 Petro akajibu, “Tubuni na kilammoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristoili mpate kuondolewa dhambi zenu nakupokea ile zawadi ya Roho Mtakatifu. 39

Maana, ahadi ile ilikuwa kwa ajili yenu, kwa ajiliya watoto wenu, kwa ajili ya wote wanaokaambali; na kwa ajili ya kila mtu ambaye BwanaMungu wetu atamwita kwake.” 40 Kwamaneno mengine mengi, Petro alisisitiza nakuwahimiza watu akisema, “Jiokoeni katikakizazi hiki kiovu.” 41 Wengi waliyakubalimaneno yake, wakabatizwa. Watu wapataoelfu tatu wakaongezeka katika kile kikundi sikuhiyo. 42 Hawa wote waliendelea kujifunzakutoka kwa mitume, kuishi pamoja kidugu,kumega mkate na kusali. 43 Miujiza namaajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitumehata kila mtu akajawa na hofu. 44 Wauminiwote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zaowaligawana pamoja. 45 Walikuwa wakiuza malina vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri yamahitaji ya kila mmoja. 46 Waliendeleakukutana pamoja kila siku Hekaluni. Lakiniwakati wa kumega mkate, walikutana katikanyumba zao na wakakishiriki chakula hichokwa furaha na moyo mkunjufu. 47

Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watuwote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi yawatu waliokuwa wakiokolewa.

Siku moja, saa tisa alasiri, Petro naYohane walikuwa wanakwendaHekaluni, wakati wa sala. 2 Na pale

karibu na mlango wa Hekalu uitwao “MlangoMzuri”, palikuwa na mtu mmoja, kiwete tangukuzaliwa. Watu walimbeba huyo mtu kila sikuna kumweka hapo ili aombe chochote kwa

MATENDO YA MITUME 2:8

90

Page 91: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

wale waliokuwa wakiingia Hekaluni. 3

Alipowaona Petro na Yohane wakiingiaHekaluni, aliwaomba wampe chochote. 4

Petro na Yohane walimkodolea macho, nayePetro akamwambia, “Tutazame!” 5 Nayeakawageukia, akitazamia kupata kitu kutokakwao. 6 Kisha Petro akamwambia, “Sina fedhawala dhahabu lakini kile nilicho nachonitakupa. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,tembea!” 7 Halafu, akamshika mkono wa kulia,akamwinua. Papo hapo miguu na magoti yakeyakapata nguvu. 8 Akaruka, akasimama nakuanza kutembea. Halafu akaingia pamoja naoHekaluni, akitembea na kurukaruka hukuakimtukuza Mungu. 9 Watu wote waliokuwahapo walimwona akitembea na kumsifuMungu. 10 Walipomtambua kuwa ndiye yulealiyekuwa anaombaomba karibu na ule“Mlango Mzuri” wa Hekalu, wakashangaa mnohata wasiweze kuelewa yaliyompata. 11 Watuwote, wakiwa na mshangao mkubwawakaanza kukimbilia mahali palipoitwa“Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtualikuwa bado anaandamana na Petro naYohane. 12 Basi, Petro alipowaona watu haoakawaambia, “Wananchi wa Israeli, kwa ninimnashangazwa na jambo hili? Mbonamnatukodolea macho kana kwamba ni kwanguvu zetu au utakatifu wetu sisi wenyewetumemfanya mtu huyu aweze kutembea? 13

Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo,Mungu wa baba zetu amemtukuza Yesumtumishi wake. Yeye ndiye yuleyule mliyemtiamikononi mwa wakuu na kumkataa mbele yaPilato hata baada ya Pilato kuamua kumwachahuru. 14 Alikuwa mtakatifu na mwema; lakinininyi mlimkataa, mkataka mtu mwinginealiyekuwa muuaji afunguliwe. 15 Basi,mlimuua yule ambaye ni chanzo cha uzima.Lakini Mungu alimfufua, na sisi ni mashahidiwa tukio hilo. 16 Jina la Yesu na imani katikajina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyumnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesundiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kamamnavyoona nyote. 17 “Sasa ndugu zangu,nafahamu kwamba ninyi na wakuu wenumlitenda hayo kwa sababu ya kutojua kwenu.18 Lakini ndivyo Mungu alivyotimiza yalealiyotangaza zamani kwa njia ya manabii wote,kwamba ilikuwa lazima Kristo wake ateseke. 19

Basi, tubuni mkamrudie Mungu ili afutedhambi zenu. 20 Fanyeni hivyo ili Bwanaawape nyakati za kuburudika rohoni nakuwaletea yule Kristo aliyemteua ambayendiye Yesu. 21 Ni lazima yeye abaki hukombinguni mpaka utakapofika wakati wakurekebishwa vitu vyote, kama Mungualivyosema kwa njia ya manabii wakewatakatifu wa tangu zamani. 22 Kwa maanaMose alisema, Bwana Mungu wenuatawapelekeeni nabii kama mimi kutoka katiyenu ninyi wenyewe. 23 Yeyote yule ambayehatamsikiliza nabii huyo atatengwa mbali na

watu wa Mungu na kuangamizwa. 24 Manabiiwote, kuanzia Samweli na wale waliomfuata,walitangaza habari za mambo haya ambayoyamekuwa yakitendeka siku hizi. 25 Ahadi zileMungu alizotoa kwa njia ya manabii ni kwa ajiliyenu; na mnashiriki lile agano Mungualilofanya na babu zenu, kama alivyomwambiaAbrahamu: Kwa njia ya wazawa wako, jamaazote za dunia zitabarikiwa. 26 Basi, ilikuwa kwaajili yenu kwanza kwamba Mungu alimfufuamtumishi wake, alimtuma awabariki kwakumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa namaovu yake.”

Petro na Yohane walipokuwa badowanawahutubia watu, makuhani namkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na

Masadukayo walifika. 2 Walikasirika sana,maana hao mitume walikuwa wanawahubiriawatu kwamba Yesu alifufuka, jambo ambalolinaonyesha wazi kwamba wafu watafufuka. 3

Basi, waliwatia nguvuni na kwa kuwa usikuulikuwa umekaribia, wakawaweka chini yaulinzi mpaka kesho yake. 4 Lakini wengi kati yawale waliosikia ujumbe wao waliamini, na idadiya waumini ikawa imefika karibu elfu tano. 5

Kesho yake, viongozi wa Wayahudi, wazee nawalimu wa Sheria, walikusanyika pamoja hukoYerusalemu. 6 Walikutana pamoja na Anasi,Kayafa, Yohane, Aleksanda na wenginewaliokuwa wa ukoo wa Kuhani Mkuu. 7

Waliwasimamisha mitume mbele yao,wakawauliza, “Ninyi mmefanya jambo hili kwanguvu gani na kwa jina la nani?” 8 Hapo, Petro,akiwa amejawa na Roho Mtakatifu,akawaambia, “Viongozi na wazee wa watu! 9

Ikiwa mnatuuliza leo juu ya kile kitendo chemaalichofanyiwa yule mtu aliyekuwa kiwete najinsi alivyopata kuwa mzima, 10 basi, ninyi nawatu wote wa Israeli mnapaswa kujua kwambamtu huyu anasimama mbele yenu leo, mzimakabisa, kwa nguvu ya jina lake Yesu waNazareti ambaye ninyi mlimsulubisha, lakiniMungu akamfufua kutoka wafu. 11 Huyu ndiyeambaye Maandiko Matakatifu yanasema: Jiwemlilokataa ninyi waashi, sasa limekuwa jiwekuu la msingi. 12 Wokovu haupatikani kwa mtumwingine yeyote, kwa maana duniani pote,binadamu hawakupewa jina la mtu mwingineambaye sisi tunaweza kuokolewa naye.” 13

Hao wazee wa baraza, wakiwa wanajuakwamba Petro na Yohane walikuwa watu wasiona kisomo wala elimu yoyote, walishangaa juuya jinsi walivyosema kwa uhodari.Wakatambua kwamba walikuwa wamejiungana Yesu. 14 Lakini walipomwona yule mtualiyeponywa amesimama pamoja nao,hawakuweza kusema kitu. 15 Hivyo,waliwaamuru watoke nje ya baraza, naowakabaki ndani wakizungumza kwa faragha.16 Wakaulizana, “Tufanye nini na watu hawa?Kila mtu anayeishi Yerusalemu anajua kwambamwujiza huu wa ajabu umefanyika, nasihatuwezi kukana jambo hilo. 17 Lakini ili

MATENDO YA MITUME 4:17

91

Page 92: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati yawatu, tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwajina la Yesu.” 18 Kwa hiyo wakawaita tenandani, wakawaonya wasiongee tenahadharani, wala kufundisha kwa jina la Yesu.19 Lakini Petro na Yohane wakawajibu,“Amueni ninyi wenyewe kama ni haki mbele yaMungu kuwatii ninyi kuliko kumtii yeye. 20 Kwamaana hatuwezi kuacha kusema juu yamambo yale tuliyoyaona na kuyasikia.” 21 Basi,hao wazee wa Baraza wakawaonya kwa ukalizaidi, halafu wakawaacha huru. Hawakuwezakuwapa adhabu kwa sababu watu wotewalikuwa wakimtukuza Mungu kwa sababu yatukio hilo. 22 Huyo mtu aliyeponywa alikuwana umri wa miaka zaidi ya arobaini. 23 Mara tuwalipoachwa huru, Petro na Yohane walirudikwa wenzao, wakawaeleza yale waliyoambiwana makuhani wakuu na wazee. 24 Waliposikiahabari hiyo waliungana pamoja katikakumwomba Mungu wakisema, “Bwana, weweni Muumba wa mbingu na nchi, bahari navyote vilivyomo! 25 Ndiwe uliyemfanyamtumishi wako, babu yetu Daudi, aseme kwanguvu ya Roho Mtakatifu: Kwa nini mataifayameghadhibika? Mbona watu wamefanyamipango ya bure? 26 Wafalme wa duniawalijiweka tayari, na watawala walikutanapamoja, ili kumwasi Bwana na Kristo wake. 27

“Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, PontioPilato, watu wa Israeli na watu wa mataifawalivyokutanika papa hapa mjini, kumpingaYesu Mtumishi wako Mtakatifu ambayeumemtia mafuta. 28 Naam, walikutana iliwafanye yale ambayo ulikusudia na kupangatangu mwanzo kwa uwezo wako na mapenziyako. 29 Lakini sasa, ee Bwana, angalia vitishovyao. Utuwezeshe sisi watumishi wakokuhubiri neno lako kwa uhodari. 30 Nyoshamkono wako uponye watu. Fanya ishara namaajabu kwa jina la Yesu Mtumishi wakoMtakatifu.” 31 Walipomaliza kusali, pale mahaliwalipokuwa wamekutanika pakatikiswa, naowote wakajazwa Roho Mtakatifu. Wotewakaanza kuhubiri neno la Mungu bila uoga.32 Jumuiya yote ya waumini ilikuwa moyommoja na roho moja. Hakuna hata mmojaaliyekuwa na kitu chochote akakiweka kuwamali yake binafsi, ila waligawana vyotewalivyokuwa navyo. 33 Mitume walishuhudiakwa nguvu nyingi kufufuka kwa Bwana Yesu,naye Mungu akawapa baraka nyingi. 34

Hakuna mtu yeyote aliyetindikiwa kitu, maanawaliokuwa na mashamba au nyumba walikuwawanaviuza 35 na kuwakabidhi mitume fedhahizo, zikagawiwa kila mmoja kadiri ya mahitajiyake. 36 Kulikuwa na Mlawi mmoja, mzaliwawa Kupro, jina lake Yosefu, ambaye mitumewalimwita jina Barnaba (maana yake, “Mtumwenye kutia moyo”). 37 Yeye pia alikuwa nashamba lake, akaliuza; akazichukua zile fedha,akawakabidhi mitume.

Mtu mmoja aitwaye Anania na mkeweSafira waliuza shamba lao vilevile. 2

Lakini, mkewe akiwa anajua, Ananiaakajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ilesehemu nyingine akawakabidhi mitume. 3

Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbonaShetani ameuingia moyo wako na kukufanyaumdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekeasehemu ya fedha ulizopata kutokana na lileshamba? 4 Kabla ya kuliuza lilikuwa mali yako,na baada ya kuliuza, bado hizo fedha zilikuwazako uzitumie utakavyo. Kwa nini basi, uliamuamoyoni mwako kufanya jambo la namna hii?Hukumdanganya mtu; umemdanganyaMungu!” 5 Anania aliposikia hayo, akaangukachini, akafa. Watu wote waliosikia habari yatukio hilo waliogopa sana. 6 Vijana wakafikawakaufunika mwili wake, wakamtoa nje,wakamzika. 7 Baada ya muda wa saa tatu hivi,mke wake, bila kufahamu mambo yaliyotukia,akaingia mle ndani. 8 Petro akamwambia,“Niambie! Je, kiasi hiki cha fedha ndichomlichopata kwa kuuza lile shamba?” Yeyeakamjibu, “Naam, ni kiasi hicho.” 9 Naye Petroakamwambia, “Mbona mmekula njamakumjaribu Roho wa Bwana? Sikiliza! Wale watuwaliokwenda kumzika mume wako, sasa wakomlangoni na watakuchukua wewe pia.” 10

Mara Safira akaanguka mbele ya miguu yaPetro, akafa. Wale vijana walipoingia,walimkuta amekwisha kufa; hivyo wakamtoanje, wakamzika karibu na mume wake. 11

Kanisa lote pamoja na wote waliosikia habariya tukio hilo, waliogopa sana. 12 Mitumewalifanya miujiza na maajabu mengi kati yawatu. Waumini walikuwa wakikutana pamojakatika ukumbi wa Solomoni. 13 Mtu yeyotemwingine ambaye hakuwa mwaminihakuthubutu kujiunga nao. Hata hivyo, watuwengine wasiokuwa wa imani hiyo waliwasifu.14 Idadi ya watu waliomwamini Bwana,wanaume kwa wanawake, iliongezeka zaidi nazaidi. 15 Kwa sababu hiyo, watu walikuwawakipeleka wagonjwa barabarani na kuwalazajuu ya vitanda na mikeka ili Petro akipita,walau kivuli chake kiwaguse baadhi yao. 16

Watu wengi walifika kutoka katika miji yakando kando ya Yerusalemu, wakiwaletawagonjwa wao na wale waliokuwa na pepowachafu, nao wote wakaponywa. 17 Kisha,Kuhani Mkuu na wenzake waliokuwa wakikundi cha Masadukayo wa mahali hapo,wakawaonea mitume wivu. 18 Basi, wakawatianguvuni, wakawafunga ndani ya gereza kuu.19 Lakini usiku malaika wa Bwana aliifunguamilango ya gereza, akawatoa nje, akawaambia,20 “Nendeni mkasimame Hekaluni nakuwaambia watu kila kitu kuhusu maisha hayamapya.” 21 Mitume walitii, wakaingia Hekaluniasubuhi na mapema, wakaanza kufundisha.Kuhani Mkuu na wenzake walipofika, waliitamkutano wa Baraza kuu, yaani halmashauriyote ya wazee wa Wayahudi halafu

MATENDO YA MITUME 4:18

92

Page 93: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

wakawatuma watu gerezani wawalete walemitume. 22 Lakini hao watumishi walipofikahuko hawakuwakuta mle gerezani. Hivyowalirudi, wakatoa taarifa mkutanoni, 23

wakisema, “Tulikuta gereza limefungwa kilaupande na walinzi wakilinda milango. Lakinitulipofungua hatukumkuta mtu yeyote ndani.”24 Mkuu wa walinzi wa Hekalu na makuhaniwakuu waliposikia habari hiyo wakawa nawasiwasi, wasijue yaliyowapata. 25 Akafikamtu mmoja, akawaambia, “Wale watumliowafunga gerezani, hivi sasa wamoHekaluni, wanawafundisha watu.” 26 Hapomkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na watuwake walikwenda Hekaluni, akawaleta. Lakinihawakuwakamata kwa kutumia nguvu, maanawaliogopa kwamba watu wangewapiga mawe.27 Basi, wakawapeleka, wakawasimamishambele ya Baraza. Kuhani Mkuu akawaambia,28 “Tuliwakatazeni waziwazi kufundisha kwajina la mtu huyu; sasa mmeyaenezamafundisho yenu pote katika Yerusalemu namnakusudia kutuwekea lawama ya kifo chamtu huyo.” 29 Hapo Petro, akiwa pamoja nawale mitume wengine, akajibu, “Lazima tumtiiMungu, na siyo binadamu. 30 Mungu wa babuzetu alimfufua Yesu baada ya ninyi kumwuakwa kumtundika msalabani. 31 Huyu ndiyeyule aliyekwezwa na Mungu mpaka upandewake wa kulia, akawa kiongozi na Mwokozi, iliawawezeshe watu wa Israeli watubu, wapatekusamehewa dhambi zao. 32 Sisi ni mashahidiwa tukio hilo, naye Roho Mtakatifu ambayeMungu amewapa wale wanaomtii,anashuhudia pia tukio hilo.” 33 Wajumbe wotewa lile Baraza waliposikia hayo, wakawakahasira, hata wakaamua kuwaua. 34 LakiniMfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambayealikuwa mwalimu wa Sheria na aliyeheshimikasana mbele ya watu wote, alisimama mbele yalile Baraza, akataka wale mitume watolewe njekwa muda mfupi. 35 Kisha akawaambia walewajumbe wa Baraza, “Wananchi wa Israeli,tahadhari kabla ya kutekeleza hichomnachotaka kuwatenda watu hawa! 36 Zamanikidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda,akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibumia nne wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kishawafuasi wake wote wakatawanyika na kikundichake kikafa. 37 Tena, baadaye, wakati ule wakuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya.Huyu naye, aliwavuta watu wakamfuata; lakininaye pia aliuawa, na wafuasi wakewakatawanyika. 38 Na sasa pia miminawaambieni, msiwachukulie watu hawahatua yoyote; waacheni! Kwa maana, ikiwampango huu au shughuli hii yao imeanzishwana binadamu, itatoweka yenyewe. 39 Lakinikama imeanzishwa na Mungu, siyo tu kwambahamtaweza kuwashinda, bali mtajikutamnapigana na Mungu.” Basi, wakakubaliananaye. 40 Hivyo wakawaita wale mitume,wakaamuru wachapwe viboko na kuwaonya

wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kishawakawaacha waende zao. 41 Basi, mitumewakatoka nje ya ule mkutano wa halmashauriwakiwa wamejaa furaha, kwani walistahilikuaibishwa kwa ajili ya jina la Yesu. 42

Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiriHabari Njema ya Kristo, Hekaluni na nyumbanimwa watu.

Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwainazidi kuongezeka, kulitokeamanung'uniko kati ya wanafunzi

waliosema Kigiriki na wale waliosemaKiebrania. Wale waliosema Kigirikiwalinung'unika kwamba wajane wao walikuwawanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji yakila siku. 2 Kwa hiyo, mitume kumi na wawiliwaliita jumuiya yote ya wanafunzi, wakasema,“Si vizuri sisi tuache kulihubiri neno la Munguili tushughulikie ugawaji wa mahitaji. 3 Hivyo,ndugu zetu, chagueni miongoni mwenu watusaba wenye sifa njema, waliojawa na Roho nawenye hekima; nasi tutawakabidhi jukumuhilo. 4 Sisi, lakini, tutashughulika na sala nakazi ya kuhubiri neno la Mungu.” 5 Jambo hilolikaipendeza jumuiya yote ya waumini.Wakawachagua Stefano, mtu mwenye imanikubwa na mwenye kujawa na Roho Mtakatifu,Filipo, Prokoro, Nikanora, Timona, Parmena naNikolao wa Antiokia ambaye hapo awalialikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi. 6

Wakawaweka mbele ya mitume, naowakawaombea na kuwawekea mikono. 7

Neno la Mungu likazidi kuenea na idadi yawaumini huko Yerusalemu ikaongezeka zaidi,na kundi kubwa la makuhani wakaipokeaimani. 8 Mungu alimjalia Stefano neema tele,akampa nguvu nyingi hata akawa anatendamiujiza na maajabu kati ya watu. 9 Lakini watufulani wakatokea ili wabishane na Stefano.Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogimoja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”, naowalitoka Kurene na Aleksandria; wenginewalitoka Kilikia na Asia. 10 Lakini hawakuwezakumshinda kwa sababu ya hekima yake nakwa sababu ya yule Roho aliyeongoza manenoyake. 11 Kwa hiyo waliwahonga watu kadhaawaseme: “Tumemsikia Stefano akisemamaneno ya kumkashifu Mose na kumkashifuMungu.” 12 Kwa namna hiyo, waliwachocheawatu, wazee na walimu wa Sheria. Basi,wakamjia Stefano, wakamkamata na kumletambele ya Baraza kuu. 13 Walileta Barazanimashahidi wa uongo ambao walisema, “Mtuhuyu haachi kamwe kusema maneno yakupakashifu mahali hapa patakatifu na Sheriaya Mose. 14 Kwa maana tulikwisha msikiaakisema eti huyo Yesu wa Nazaretiatapaharibu kabisa mahali hapa na kufutiliambali desturi zile tulizopokea kutoka kwaMose.” 15 Wote waliokuwa katika kile kikao chaBaraza walimkodolea macho Stefano,wakauona uso wake umekuwa kama wamalaika.

MATENDO YA MITUME 6:15

93

Page 94: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

7Basi, Kuhani Mkuu akamwuliza, “Je,mambo haya ni kweli?” 2 Naye Stefanoakasema, “Ndugu zangu na akina baba,

nisikilizeni! Mungu alimtokea baba yetuAbrahamu alipokuwa kule Mesopotamia kablahajaenda kukaa kule Harani. 3 Mungualimwambia: Ondoka katika nchi yako; waachewatu wa ukoo wako; nenda katika nchinitakayokuonyesha! 4 Kwa hivyo, Abrahamualihama nchi ya Kaldayo, akaenda kukaaHarani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungualimtoa tena Harani akaja kukaa katika nchi hiimnayokaa sasa. 5 Mungu hakumpa hatasehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hatahivyo, alimwahidia kumpa nchi hii iwe yake naya wazawa wake, ingawaje wakati huu hakuwana mtoto. 6 Mungu alimwambia hivi: Wazaowako watapelekwa katika nchi inayotawaliwana watu wengine, na huko watafanywawatumwa na kutendewa vibaya kwa muda wamiaka mia nne. 7 Lakini mimi nitalihukumutaifa hilo litakalowafanya watumwa. Kishanitawatoa katika nchi hiyo ili waje kuniabudumahali hapa. 8 Halafu Mungu aliifanya toharaiwe ishara ya agano. Hivyo, Abrahamualimtahiri mtoto wake Isaka, siku ya nanebaada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo,alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendeawale mababu kumi na wawili vivyo hivyo. 9

“Wale mababu walimwonea wivu Yosefu,wakamuuza utumwani Misri. Lakini Mungualikuwa pamoja naye, 10 akamwokoa katikataabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili nahekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hataFarao akamweka awe mkuu wa ile nchi nanyumba ya kifalme. 11 Kisha, kulizuka njaakubwa katika nchi yote ya Misri na Kanaani,ikasababisha dhiki kubwa. Babu zetuhawakuweza kupata chakula chochote. 12

Basi, Yakobo alipopata habari kwamba hukoMisri kulikuwa na nafaka, aliwatuma watotowake, yaani babu zetu, waende huko Misrimara ya kwanza. 13 Katika safari yao ya pili,Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, naFarao akaifahamu jamaa ya Yosefu. 14 Yosefualituma ujumbe kwa baba yake na jamaa yote,jumla watu sabini na tano, waje Misri. 15

Hivyo, Yakobo alikwenda Misri ambako yeye nababu zetu wengine walikufa. 16 Miili yaoililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katikakaburi Abrahamu alilonunua kutoka kwa kabilala Hamori kwa kiasi fulani cha fedha. 17

“Wakati ulipotimia Mungu aitimize ahadialiyompa Abrahamu, idadi ya wale watu kuleMisri ilikwisha ongezeka na kuwa kubwa zaidi.18 Mwishowe, mfalme mmoja ambayehakumtambua Yosefu alianza kutawala hukoMisri. 19 Alilifanyia taifa letu ukatili,akawatendea vibaya babu zetu kwakuwalazimisha waweke nje watoto waowachanga ili wafe. 20 Mose alizaliwa wakatihuo. Alikuwa mtoto mzuri sana. Alilelewanyumbani kwa muda wa miezi mitatu, 21 na

alipotolewa nje, binti wa Farao alimchukua,akamlea kama mtoto wake. 22 Mosealifundishwa mambo yote ya hekima yaWamisri akawa mashuhuri kwa maneno namatendo. 23 “Alipokuwa na umri wa miakaarobaini aliamua kwenda kuwaona ndugu zakeWaisraeli. 24 Huko alimwona mmoja waoakitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, nakulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri. 25

(Alidhani kwamba Waisraeli wenzakewangeelewa kwamba Mungu angemtumiayeye kuwakomboa, lakini hawakuelewa hivyo.)26 Kesho yake, aliwaona Waisraeli wawiliwakipigana, akajaribu kuwapatanisha,akisema: Ninyi ni ndugu; kwa nini basi,kutendeana vibaya ninyi kwa ninyi? 27 Yulealiyekuwa anampiga mwenzake alimsukumaMose kando akisema: Ni nani aliyekuwekawewe kuwa kiongozi na mwamuzi wa watu? 28

Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yuleMmisri jana? 29 Baada ya kusikia hayo Mosealikimbia, akaenda kukaa katika nchi yaMidiani na huko akapata watoto wawili. 30

“Miaka arobaini ilipotimia, malaika wa Bwanaalimtokea Mose katika kichaka kilichokuwakinawaka moto kule jangwani karibu na mlimaSinai. 31 Mose alistaajabu sana kuona jambohilo hata akasogea karibu ili achungulie; lakinialisikia sauti ya Bwana: 32 Mimi ni Mungu wababa zako, Mungu wa Abrahamu, Isaka naYakobo! Mose akatetemeka kwa hofu na walahakuthubutu kutazama zaidi. 33 Bwanaakamwambia: Vua viatu vyako maana hapaunaposimama ni mahali patakatifu. 34

Nimeyaona mabaya wanayotendewa watuwangu kule Misri. Nimesikia kilio chao, naminimekuja kuwaokoa. Basi sasa, nitakutumaMisri. 35 “Huyu Mose ndiye yule watu waIsraeli waliyemkataa waliposema: Ni nanialiyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuziwetu? Kwa njia ya yule malaika aliyemtokeakatika kichaka kilichokuwa kinawaka moto,Mungu alimtuma Mose huyo awe kiongozi namkombozi. 36 Ndiye aliyewaongoza wale watuwatoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabukatika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu najangwani kwa muda wa miaka arobaini. 37

Mose ndiye aliyewaambia watu wa Israeli:Mungu atawateulieni nabii kama mimi kutokakatika ndugu zenu ninyi wenyewe. 38 Wakatiwatu wa Israeli walipokutana pamoja kulejangwani, Mose ndiye aliyekuwako hukopamoja nao. Alikuwa huko pamoja na babuzetu na yule malaika aliyeongea naye mlimaniSinai; ndiye aliyekabidhiwa yale manenoyaletayo uzima atupe sisi. 39 “Lakini yeye ndiyebabu zetu waliyemkataa kumsikiliza;walimsukuma kando, wakatamani kurudiMisri. 40 Walimwambia Aroni: Tutengenezeemiungu itakayotuongoza njiani, maana hatujuiyaliyompata Mose huyu aliyetuongoza kutokaMisri! 41 Hapo ndipo walipojitengenezeasanamu ya ndama, wakaitambikia na

MATENDO YA MITUME 7:2

94

Page 95: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi yamikono yao wenyewe. 42 Lakini Mungualiondoka kati yao, akawaacha waabudu nyotaza anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu chamanabii: Enyi watu wa Israeli! Si mimimliyenitolea dhabihu na sadaka kwa muda wamiaka arobaini kule jangwani! 43 Ninyimlikibeba kibanda cha mungu Moloki, nasanamu ya nyota ya mungu wenu Refani.Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu. Kwasababu hiyo nitakupeleka mateka mbali kupitaBabuloni! 44 Kule jangwani babu zetuwalikuwa na lile hema lililoshuhudia kuwekokwa Mungu. Lilitengenezwa kama Mungualivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili yakile alichoonyeshwa. 45 Kisha babu zetuwalilipokezana wao kwa wao mpaka wakati waYoshua, walipoinyakua ile nchi kutoka kwamataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbeleyao. Hapo lilikaa mpaka nyakati za Daudi. 46

Daudi alipata upendeleo kwa Mungu,akamwomba Mungu ruhusa ya kumjengeamakao yeye aliye Mungu wa Yakobo. 47 LakiniSolomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba.48 “Hata hivyo, Mungu Mkuu haishi katikanyumba zilizojengwa na binadamu; kama nabiiasemavyo: 49 Bwana asema: Mbingu ni kitichangu cha enzi na dunia ni kiti changu chakuwekea miguu. 50 Ni nyumba ya namna ganibasi mnayoweza kunijengea, na ni mahali ganinitakapopumzika? Vitu hivi vyote ni miminimevifanya, au sivyo? 51 “Enyi wakaidi wakuu!Mioyo na masikio yenu ni kama ya watu wamataifa. Ninyi ni kama baba zenu. Siku zotemnampinga Roho Mtakatifu. 52 Je, yuko nabiiyeyote ambaye baba zenu hawakumtesa?Waliwaua hao Mungu aliowatuma watangazekuja kwake yule Mwenye Haki. Na sasa, ninyimmemsaliti, mkamuua. 53 Ninyi mliipokea ileSheria iliyoletwa kwenu na Malaika, lakinihamkuitii.” 54 Wale wazee wa Barazawaliposikia hayo, walighadhibika sana,wakamsagia meno kwa hasira. 55 LakiniStefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu,akatazama juu mbinguni, akauona utukufu waMungu na Yesu amekaa upande wa kulia waMungu. 56 Akasema, “Tazameni! Ninaonambingu zimefunuliwa na Mwana wa Mtuamesimama upande wa kulia wa Mungu.” 57

Hapo, watu wote katika kile kikao cha Baraza,wakapiga kelele na kuziba masikio yao kwamikono yao. Kisha wakamrukia wote kwapamoja, 58 wakamtoa nje ya mji, wakampigamawe. Wale mashahidi wakayaweka makotiyao chini ya ulinzi wa kijana mmoja jina lakeSaulo. 59 Waliendelea kumpiga mawe Stefano,huku akiwa anasali: “Bwana Yesu, ipokee rohoyangu!” 60 Akapiga magoti, akalia kwa sautikubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu yadhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.

Saulo naye alikiona kitendo hicho chakumwua Stefano kuwa sawa. Siku hiyokanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa

vibaya. Waumini wote, isipokuwa tu walemitume, walilazimika kutawanyika katikasehemu za mashambani za Yudea na Samaria.2 Watu wamchao Mungu, walimzika Stefanona kumfanyia maombolezo makubwa. 3

Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamizakanisa. Alikwenda katika kila nyumba,akawatoa nje waumini, wanaume kwawanawake, akawatia gerezani. 4 Wale wauminiwaliotawanyika, walikwenda kila mahaliwakihubiri ule ujumbe. 5 Naye Filipo aliingiakatika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwawenyeji wa hapo. 6 Watu walijiunga kusikilizakwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ilemiujiza aliyoifanya. 7 Maana pepo wachafuwaliokuwa wamewapagaa watu wengiwaliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watuwengi waliokuwa wamepooza viungo nawaliolemaa waliponywa. 8 Kukawa na furahakubwa katika mji ule. 9 Basi, kulikuwa na mtummoja aitwaye Simoni ambaye alikuwaamekwisha fanya uchawi wake katika mji huokwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria,akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu. 10 Watuwote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwamakini wakisema, “Simoni ndiye ile nguvu yakimungu inayoitwa Nguvu Kubwa.” 11

Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwaamewashangaza kwa uchawi wake kwa mudamrefu. 12 Lakini walipouamini ujumbe waFilipo juu ya Habari Njema ya Ufalme waMungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa,wanawake na wanaume. 13 Hata Simonialiamini; baada ya kubatizwa ilikuwaakiandamana na Filipo, akastaajabia maajabuna miujiza iliyokuwa inafanyika. 14 Walemitume waliokuwa kule Yerusalemuwalipopata habari kwamba wenyeji waSamaria nao wamelipokea neno la Mungu,waliwatuma kwao Petro na Yohane. 15

Walipofika waliwaombea hao waumini iliwampokee Roho Mtakatifu; 16 maana wakatihuo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyotekati yao; walikuwa wamebatizwa tu kwa jina laBwana Yesu. 17 Basi, Petro na Yohanewakawawekea mikono hao waumini, naowakampokea Roho Mtakatifu. 18 Hapo Simonialing'amua kwamba kwa kuwekewa mikono yamitume waumini walipewa Roho Mtakatifu.Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,19 “Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyotenitakayemwekea mikono, apokee RohoMtakatifu.” 20 Lakini Petro akamjibu, “Poteleambali na fedha zako kwa vile unafikiri kwambaunaweza kununua karama ya Mungu kwafedha! 21 Huna sehemu yoyote wala hakikatika kazi hiyo kwa maana moyo wako haukosawa mbele ya macho ya Mungu. 22 Kwa hiyo,tubu ubaya wako huu na umwombe Bwananaye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.23 Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivumkali na mfungwa wa dhambi!” 24 Simoniakajibu, “Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije

MATENDO YA MITUME 8:24

95

Page 96: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

likanipata lolote kati ya hayo mliyosema.” 25

Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhudawao na kuutangaza ujumbe wa Bwana,walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudiwalihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vyaSamaria. 26 Malaika wa Bwana alimwambiaFilipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njiainayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njiahiyo hupita jangwani.) 27 Basi, Filipo akajiwekatayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwana Mwethiopia mmoja, towashi, ambayealikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyomtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina yaKandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwaamekwenda huko Yerusalemu kuabudu nawakati huo alikuwa anarudi akiwa amepandagari la kukokotwa. 28 Alipokuwa anasafiri,alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya. 29

Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo,“Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.”30 Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikiahuyo mtu akisoma katika kitabu cha nabiiIsaya. Hapo Filipo akamwuliza, “Je, unaelewahayo unayosoma?” 31 Huyo mtu akamjibu,“Ninawezaje kuelewa bila mtu kunielewesha?”Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketipamoja naye. 32 Basi, sehemu ya MaandikoMatakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii:“Alikuwa kama kondoo anayepelekwakuchinjwa; kimya kama vile mwana kondooanaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoasauti hata kidogo. 33 Alifedheheshwa nakunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongeajuu ya kizazi chake, kwa maana maisha yakeyameondolewa duniani.” 34 Huyo Mwethiopiaakamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabiianasema juu ya nani? Anasema mambo hayajuu yake yeye mwenyewe au juu ya mtumwingine?” 35 Basi, Filipo akianzia na sehemuhiyo ya Maandiko Matakatifu, akamwelezaHabari Njema juu ya Yesu. 36 Walipokuwabado wanaendelea na safari walifika mahalipenye maji na huyo ofisa akasema, “Mahalihapa pana maji; je, kuna chochote chakunizuia nisibatizwe?” 37 Filipo akasema,“Kama unaamini kwa moyo wako woteunaweza kubatizwa.” Naye akajibu, “Naam,ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana waMungu.” 38 Basi, huyo ofisa akaamuru lile garilisimame; na wote wawili, Filipo na huyo ofisawakashuka majini, naye Filipo akambatiza. 39

Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanyaFilipo atoweke. Na huyo Mwethiopiahakumwona tena; lakini akaendelea na safariyake akiwa amejaa furaha. 40 Filipo akajikutayuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiriHabari Njema mpaka alipofika Kaisarea.

Wakati huo Saulo alikuwa akizidishavitisho vikali vya kuwaua wafuasi waBwana. Alikwenda kwa Kuhani Mkuu, 2

akaomba apatiwe barua za utambulisho kwamasunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, iliakikuta huko wanaume au wanawake

wanaofuata Njia ya Bwana, awakamate nakuwaleta Yerusalemu. 3 Lakini alipokuwanjiani karibu kufika Damasko, ghafla mwangakutoka angani ulimwangazia pande zote. 4

Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia:“Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?” 5 NayeSaulo akauliza, “Ni nani wewe Bwana?” Na ilesauti ikajibu, “Mimi ni Yesu ambaye weweunamtesa. 6 Lakini simama sasa, uingie mjinina huko utaambiwa unachopaswa kufanya.” 7

Wale watu waliokuwa wanasafiri pamoja naSaulo walisimama pale, wakiwa hawana lakusema; walisikia ile sauti lakinihawakumwona mtu. 8 Saulo aliinuka, naalipofumbua macho yake hakuweza kuonachochote; hivyo wale watu wakamwongozakwa kumshika mkono mpaka mjini Damasko.9 Saulo alikaa siku tatu bila kuona, na wakatihuo hakula au kunywa chochote. 10 Basi, hukoDamasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwayeAnania. Bwana akamwambia katika maono,“Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa, Bwana.”11 Naye Bwana akamwambia, “Jitayarisheuende kwenye barabara inayoitwa Barabara yaMoja kwa Moja, na katika nyumba ya Yudaumtake mtu mmoja kutoka Tarso aitwayeSaulo. Sasa anasali; 12 na katika maonoameona mtu aitwaye Anania akiingia ndani nakumwekea mikono ili apate kuona tena.” 13

Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikiahabari za mtu huyu kutoka kwa watu wengi;nimesikia juu ya mabaya aliyowatendea watuwako huko Yerusalemu. 14 Na amekuja hapaakiwa na mamlaka kutoka kwa makuhaniwakuu kuwatia nguvuni wote wanaoomba kwajina lako.” 15 Lakini Bwana akamwambia,“Nenda tu, kwa maana nimemchagua awechombo changu, alitangaze jina langu kwamataifa na wafalme wao na kwa watu waIsraeli. 16 Mimi mwenyewe nitamwonyeshamengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili yajina langu.” 17 Basi, Anania akaenda, akaingiakatika hiyo nyumba. Kisha akaweka mikonoyake juu ya Saulo, akasema, “Ndugu Saulo,Bwana ambaye ndiye Yesu mwenyewealiyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa,amenituma ili upate kuona tena na kujazwaRoho Mtakatifu.” 18 Mara vitu kama magambavikaanguka kutoka macho ya Saulo, akawezakuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Nabaada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia.Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasihuko Damasko. 20 Mara alianza kuhubirikatika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana waMungu. 21 Watu wote waliomsikiawalishangaa, wakasema, “Je, mtu huyu siyuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaombakwa jina hili kule Yerusalemu? Tena alikujahapa akiwa na madhumuni ya kuwatianguvuni watu hao na kuwapeleka kwamakuhani!” 22 Saulo alizidi kupata nguvu, nakwa jinsi alivyothibitisha wazi kwamba Yesundiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko

MATENDO YA MITUME 8:25

96

Page 97: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

walivurugika kabisa. 23 Baada ya siku nyingikupita, Wayahudi walikusanyika na kufanyampango wa kumwua Saulo. 24 Lakini Sauloalipata habari ya mpango huo. Usiku namchana walilinda milango ya kuingia mjini iliwapate kumwua. 25 Lakini wakati wa usikuwanafunzi wake walimchukua,wakamteremsha chini ndani ya kapu kubwakwa kupitia nafasi iliyokuwako ukutani. 26

Saulo alipofika Yerusalemu alijaribu kujiungana wale wanafunzi. Lakini wote walimwogopa,na hawakuweza kuamini kwamba yeyeamekuwa mfuasi. 27 Hapo, Barnaba alikujaakamchukua Saulo, akampeleka kwa mitumena kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwananjiani na jinsi Bwana alivyoongea naye.Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwaamehubiri bila uoga kule Damasko. 28 Basi,Saulo alikaa pamoja nao, akatembeleaYerusalemu yote akihubiri neno la Bwana bilahofu. 29 Pia aliongea na kubishana naWayahudi wasemao Kigiriki, lakini waowalijaribu kumwua. 30 Wale nduguwalipogundua jambo hilo walimchukua Saulo,wakampeleka Kaisarea, wakamwacha aendezake Tarso. 31 Wakati huo kanisa likawa naamani popote katika Yudea, Galilaya, naSamaria. Lilijengwa na kukua katika kumchaBwana, na kuongezeka likitiwa moyo na RohoMtakatifu. 32 Petro alipokuwa anasafirisafirikila mahali alifika pia kwa watu wa Munguwaliokuwa wanaishi Luda. 33 Huko alimkutamtu mmoja aitwaye Enea ambaye kwa mudawa miaka minane alikuwa amelala kitandanikwa sababu alikuwa amepooza. 34 Basi, Petroakamwambia, “Enea, Yesu Kristo anakuponya.Amka utandike kitanda chako.” Enea akaamkamara. 35 Wakazi wote wa Luda na Saroniwalimwona Enea, na wote wakamgeukiaBwana. 36 Kulikuwa na mfuasi mmojamwanamke mjini Yopa aitwaye Tabitha (kwaKigiriki ni Dorka, maana yake, Paa). Huyomwanamke alikuwa akitenda mema nakuwasaidia maskini daima. 37 Wakati huoikawa kwamba aliugua, akafa. Watuwakauosha mwili wake, wakauzika katikachumba ghorofani. 38 Yopa si mbali sana naLuda; kwa hiyo wafuasi waliposikia kwambaPetro alikuwa Luda, wakawatuma watu wawilikwake na ujumbe: “Njoo kwetu harakaiwezekanavyo.” 39 Basi, Petro akaenda pamojanao. Alipofika alipelekwa ghorofani katika kilechumba. Huko wajane wengi walimzungukaPetro wakilia na kumwonyesha makoti nanguo ambazo Dorka alikuwa akitengenezawakati alipokuwa hai. 40 Petro aliwatoa njewote, akapiga magoti, akasali. Kishaakamgeukia yule maiti, akasema, “Tabitha,amka” Naye akafumbua macho yake naalipomwona Petro, akaketi. 41 Petroakamsaidia kusimama, halafu akawaita walewatu wa Mungu na wale wajane, akamkabidhikwao akiwa mzima. 42 Habari ya tukio hili

ilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengiwakamwamini Bwana. 43 Petro alikaa sikukadhaa huko Yopa, akiishi kwa mtu mmojamtengenezaji wa ngozi aitwaye Simoni.

Kulikuwa na mtu mmoja hukoKaisarea aitwaye Kornelio, Jemadariwa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha

Italia.” 2 Alikuwa mtu mwema; naye pamoja najamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwaanafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudina alikuwa anasali daima. 3 Yapata saa tisamchana, aliona dhahiri katika maono malaikawa Mungu akiingia ndani na kumwambia,“Kornelio!” 4 Kornelio alimkodolea machohuyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kunanini Mheshimiwa?” Huyo malaikaakamwambia, “Mungu amezipokea sala nasadaka zako kwa maskini. 5 Sasa, watumewatu Yopa wakamwite mtu mmoja aitwayeSimoni, kwa jina lingine Petro. 6 Yeye yumonyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngoziambaye nyumba yake iko karibu na bahari.” 7

Huyo malaika aliyesema hayo alipokwishakwenda zake, Kornelio aliwaita watumishiwawili wa nyumbani na mmoja wa askari zakeambaye alikuwa mcha Mungu, 8 akawaelezayote yaliyotukia, akawatuma Yopa. 9 Keshoyake, hao watu watatu wakiwa bado safarini,lakini karibu kufika Yopa, Petro alipanda juu yapaa la nyumba yapata saa sita mchana ilikusali. 10 Aliona njaa, akatamani kupatachakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa,alipatwa na usingizi mzito akaona maono. 11

Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kamashuka kubwa inateremshwa chini ikiwaimeshikwa pembe zake nne. 12 Ndani ya shukahiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama:wanyama wenye miguu minne, wanyamawatambaao na ndege wa angani. 13 Akasikiasauti ikimwambia: “Petro, amka uchinje, ule!”14 Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonjakamwe chochote ambacho ni najisi aukichafu.” 15 Ile sauti ikasikika tenaikimwambia: “Usiviite najisi vitu ambavyoMungu amevitakasa!” 16 Jambo hili lilifanyikamara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juumbinguni. 17 Petro alipokuwa badoanashangaa juu ya maana ya hilo maonoalilokuwa ameliona, wale watu waliotumwa naKornelio, baada ya kuigundua nyumba yaSimoni, walifika mlangoni, 18 Wakaita kwasauti: “Je, kuna mgeni humu aitwaye SimoniPetro?” 19 Petro alikuwa bado anajaribukuelewa lile maono, na hapo Rohoakamwambia, “Sikiliza! kuna watu watatuhapa, wanakutafuta. 20 Shuka upesi na walausisite kwenda pamoja nao kwa maana nimimi niliyewatuma.” 21 Basi, Petro akateremkachini, akawaambia hao watu, “Mimi ndiyemnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?” 22 Waowakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtumwema, mcha Mungu na mwenyekuheshimika mbele ya Wayahudi wote

MATENDO YA MITUME 10:22

97

Page 98: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifuakualike nyumbani kwake ili asikilize chochoteulicho nacho cha kusema.” 23 Petro akawaalikandani, akawapa mahali pa kulala usiku ule.Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao,na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatananaye. 24 Siku ya pili yake, walifika Kaisarea nahuko Kornelio alikuwa anawangojea pamojana jamaa na marafiki aliokuwa amewaalika. 25

Petro alipokuwa anaingia, Kornelio alitoka njekumlaki, akapiga magoti mbele yake nakuinama chini kabisa. 26 Lakini Petroalimwinua, akamwambia, “Simama, kwamaana mimi ni binadamu tu.” 27 Petroaliendelea kuongea na Kornelio wakiwawanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watuwengi wamekusanyika. 28 Petro akawaambia,“Ninyi wenyewe mnajua kwamba Myahudiyeyote amekatazwa na Sheria yake ya dinikushirikiana na watu wa mataifa mengine.Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtuyeyote kuwa najisi au mchafu. 29 Kwa sababuhiyo, mliponiita nimekuja bila kusita. Basi,nawaulizeni: kwa nini mmeniita?” 30 Kornelioakasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saatisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbanimwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaamavazi yenye kun'gaa alisimama mbele yangu,31 akasema: Kornelio! Sala yako na sadakazako kwa maskini vimekubaliwa na Mungu. 32

Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmojaaitwaye Simoni, kwa jina lingine Petroi; yukonyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozikaribu na bahari. 33 Kwa hiyo nilikutumiaujumbe bila kuchelewa, nawe umefanyavyema kuja. Sasa, sisi tuko mbele ya Mungu,kusikiliza chochote ambacho bwanaamekuamuru kusema.” 34 Hapo Petro akaanzakusema: “Sasa nimetambua kwamba hakikaMungu hana ubaguzi. 35 Mtu wa taifa loloteanayemcha Mungu na kutenda hakianapokelewa naye. 36 Huu ndio ule ujumbeMungu alioupeleka kwa watu wa Israeli,akitangaza Habari Njema iletayo amani kwanjia ya Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote.37 Ninyi mnajua jambo lililotukia katika nchiyote ya Wayahudi kuanzia Galilaya baada yaule ubatizo aliohubiri Yohane. 38 Mnajua Yesuwa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwakummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungualikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko nahuko akitenda mema na kuwaponya wotewaliokuwa wamevamiwa na Ibilisi. 39 Sisi nimashahidi wa mambo yote aliyotenda katikanchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu.Walimuua kwa kumtundika msalabani; 40

lakini Mungu alimfufua siku ya tatu,akamfanya aonekane 41 si kwa watu wote ilakwa wale Mungu aliokwisha wachagua wawemashahidi wake, yaani sisi tuliokula na kunywapamoja naye baada ya kufufuka kwake kutokawafu. 42 Alituamuru kuihubiri Habari Njemakwa watu wote na kushuhudia kwamba yeye

ndiye aliyeteuliwa na Mungu awe Mwamuzi wawazima na wafu. 43 Manabii wote waliongeajuu yake kwamba kila mtu atakayemwaminiatasamehewa dhambi zake zote kwa jina lake.”44 Wakati Petro alipokuwa bado anasemamaneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukiawote waliokuwa wanasikiliza ujumbe huo. 45

Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja naPetro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwaMungu aliwamiminia zawadi ya RohoMtakatifu watu wa mataifa mengine pia; 46

maana waliwasikia wakiongea kwa lughambalimbali wakimtukuza Mungu. Hapo Petroakasema, 47 “Watu hawa wamempokea RohoMtakatifu kama sisi wenyewe tulivyompokea.Je, kuna yeyote atakayeweza kuwazuiawasibatizwe kwa maji?” 48 Basi, akaamuruwabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Kishawakamwomba akae nao kwa siku chache.

Mitume na ndugu kule Yudea walisikiakwamba watu wa mataifa menginepia walikuwa wamelipokea neno la

Mungu. 2 Basi, Petro aliporudi Yerusalemu,wale Wayahudi waumini waliopendelea watuwa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumuwakisema: 3 “Wewe umekwenda kukaa nawatu wasiotahiriwa na hata umekula pamojanao! 4 Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juuya yale yaliyotendeka tangu mwanzo: 5 “Sikumoja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono;niliona kitu kama shuka kubwa likishushwachini kutoka mbinguni likiwa limeshikwapembe zake nne, likawekwa kando yangu. 6

Nilichungulia ndani kwa makini nikaonawanyama wenye miguu minne, wanyama wamwituni, wanyama watambaao na ndege waangani. 7 Kisha nikasikia sauti ikiniambia:Petro amka, chinja, ule. 8 Lakini miminikasema: La, Bwana; maana chochote kilichonajisi au kichafu hakijapata kamwe kuingiakinywani mwangu. 9 Ile sauti ikasikika tenakutoka mbinguni: Usiviite najisi vitu ambavyoMungu amevitakasa. 10 Jambo hilo lilifanyikamara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juumbinguni. 11 Ghafla, watu watatu waliokuwawametumwa kwangu kutoka Kaisareawaliwasili kwenye nyumba niliyokuwa nakaa.12 Roho aliniambia niende pamoja nao bilakusita. Hawa ndugu sita waliandamana namipia kwenda Kaisarea na huko tuliingianyumbani mwa Kornelio. 13 Yeye alituelezajinsi alivyokuwa amemwona malaikaamesimama nyumbani mwake nakumwambia: Mtume mtu Yopa akamwite mtummoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.14 Yeye atakuambia maneno ambayo kwayowewe na jamaa yako yote mtaokolewa. 15 Nanilipoanza tu kuongea, Roho Mtakatifualiwashukia kama alivyotushukia sisi paleawali. 16 Hapo nilikumbuka yale manenoBwana aliyosema: Yohane alibatiza kwa maji,lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. 17

Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa

MATENDO YA MITUME 10:23

98

Page 99: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

12

mataifa mengine zawadi ileile aliyotupa sisitulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ninani hata nijaribu kumpinga Mungu?” 18

Waliposikia hayo, waliacha ubishi,wakamtukuza Mungu wakisema, “Munguamewapa watu wa mataifa mengine nafasi yakutubu na kuwa na uzima!” 19 Kutokana namateso yaliyotokea wakati Stefano alipouawa,waumini walitawanyika. Wengine walikwendampaka Foinike, Kupro na Antiokia wakihubiriule ujumbe kwa Wayahudi tu. 20 Lakini baadhiya waumini waliotoka Kupro na Kurene,walikwenda Antiokia wakautangaza huoujumbe kwa watu wa mataifa menginewakiwahubiria ile Habari Njema juu ya BwanaYesu. 21 Bwana aliwasaidia na idadi kubwa yawatu iliamini na kumgeukia Bwana. 22 Habariya jambo hilo ikasikika kwa lile kanisa laYerusalemu. Hivyo wakamtuma Barnabaaende Antiokia. 23 Alipofika huko na kuonajinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu,alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katikauaminifu wao kwa Bwana. 24 Barnaba alikuwamtu mwema na mwenye kujaa Roho Mtakatifuna imani. Kundi kubwa la watu lilivutwa kwaBwana. 25 Kisha, Barnaba alikwenda Tarsokumtafuta Saulo 26 Alipompata, alimletaAntiokia. Nao wote wawili walikaa na lile kanisakwa mwaka wote mzima wakifundisha kundikubwa la watu. Huko Antiokia, ndiko, kwamara ya kwanza, wafuasi waliitwa Wakristo. 27

Wakati huohuo, manabii kadhaa walikujaAntiokia kutoka Yerusalemu. 28 Basi, mmojawao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezowa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaakubwa katika nchi yote (Njaa hiyo ilitokeawakati Klaudio alipokuwa akitawala). 29 Walewanafunzi waliamua kila mmoja kwa kadiri yauwezo wake apeleke chochote ili kuwasaidiawale ndugu waliokuwa wanaishi Yudea. 30

Basi, wakafanya hivyo na kupeleka mchangowao kwa wazee wa kanisa kwa mikono yaBarnaba na Saulo.

Karibu wakati huohuo, mfalmeHerode alianza kuwatesa baadhi yaWakristo. 2 Alimwua kwa upanga

Yakobo ndugu yake Yohane. 3 Alipoona kuwakitendo hiki kiliwapendeza Wayahudi,aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyikawakati wa sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu.)4 Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwagerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundivinne vya askari wannewanne. Herodealikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuuya Pasaka. 5 Basi, Petro alipokuwa gerezani,kanisa lilikuwa linamwombea kwa Mungu kwamoyo. 6 Usiku, kabla ya siku ile ambayoHerode angemtoa Petro hadharani, Petroalikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwaamefungwa minyororo miwili, na walinziwalikuwa wanalinda lango la gereza. 7 Ghafla,malaika wa Bwana akasimama karibu naye namwanga ukaangaza kile chumba cha gereza.

Malaika akamgusa akisema, “Amka upesi!”Mara ile minyororo ikaanguka kutoka katikamikono yake. 8 Malaika akamwambia, “Jifungemshipi wako, vaa viatu vyako.” Akafanya hivyo.Kisha huyo malaika akamwambia, “Vaa kotilako, unifuate.” 9 Petro akamfuata nje lakinihakujua kama hayo yaliyofanywa na huyomalaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwaanaota ndoto. 10 Walipita kituo cha kwanzacha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenyemlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huomlango ukawafungukia wenyewe, naowakatoka nje. Wakawa wanatembea katikabarabara moja na mara yule malaikaakamwacha Petro peke yake. 11 Hapo ndipoPetro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasanajua kwa hakika kwamba Bwana amemtumamalaika wake akaniokoa kutoka katika mkonowa Herode na kutoka katika mambo yale yotewatu wa Israeli waliyotazamia.” 12

Alipotambua hivyo alikwenda moja kwa mojampaka nyumbani kwa Maria mama yakeYohane aitwaye Marko. Humo watu wengiwalikuwa wamekusanyika wakisali. 13 Petroalibisha mlango wa nje na mtumishi mmojamsichana aitwaye Roda, akaenda mlangonikuitikia. 14 Huyo msichana aliitambua sauti yaPetro akafurahi mno, hata badala yakuufungua ule mlango, akakimbilia ndani nakuwaambia kwamba Petro alikuwaamesimama nje mlangoni. 15 Wakamwambiayule msichana, “Una wazimu!” Lakini yeyeakasisitiza kwamba ilikuwa kweli. Naowakamwambia, “Huyo ni malaika wake.” 16

Wakati huo Petro alikuwa anaendelea kupigahodi. Mwishowe walifungua mlango,wakamwona, wakashangaa. 17 Petroaliwaashiria kwa mkono wakae kimya,akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani.Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilokwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafuakatoka akaenda mahali pengine. 18

Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati yawale askari kuhusu yaliyokuwa yamempataPetro. 19 Herode aliamuru ufanywe msakolakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuruwale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe.Halafu akatoka huko Yudea akaenda Kaisareaambako alikaa. 20 Herode alikasirishwa sanana watu wa Tiro na Sidoni. Lakini waowalimpelekea wajumbe. Nao wakafaulukwanza kumpata Blasto awe upande wao.Blasto alikuwa msimamizi mkuu wa ikulu yamfalme. Kisha, wakamwendea Herodewakamwomba kuwe na amani, kwa maananchi yao ilitegemea nchi ya mfalme kwachakula. 21 Siku moja iliyochaguliwa, Herodeakiwa amevaa mavazi rasmi na kuketi katikakiti cha kifalme aliwahutubia watu. 22 Walewatu walimpigia kelele za shangwe wakisema,“Hii ni sauti ya mungu, si ya mtu.” 23 Papohapo malaika wa Bwana akamwangushaHerode chini kwa sababu hakumpa Mungu

MATENDO YA MITUME 12:23

99

Page 100: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa. 24 Neno laMungu likazidi kuenea na kukua. 25 Baada yaBarnaba na Saulo kutekeleza shughuli zao,walitoka tena Yerusalemu wakamchukuaYohane aitwaye pia Marko.

Katika kanisa la Antiokia kulikuwa nawatu wengine waliokuwa manabii nawalimu; miongoni mwao akiwa

Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio waKurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewapamoja na mfalme Herode, na Saulo. 2

Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwanana kufunga, Roho Mtakatifu alisema:“Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kaziniliyowaitia.” 3 Basi, baada ya kusali nakufunga zaidi, wakawawekea mikono,wakawaacha waende zao. 4 Basi, Barnaba naSaulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu,walishuka hadi Seleukia, na kutoka hukowalipanda meli hadi kisiwa cha Kupro. 5

Walipofika Salami walihubiri neno la Mungukatika masunagogi ya Kiyahudi. Yohane(Marko) alikuwa msaidizi wao. 6 Walitembeatoka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafoupande wa pili, na huko walimkuta mchawimmoja Myahudi aitwaye Baryesu ambayealijisingizia kuwa nabii. 7 Huyu alikuwa pamojana Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambayealikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Pauloaliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno laMungu. 8 Lakini huyo mchawi Elima (kamaalivyokuwa anaitwa kwa Kigiriki), alijaribukuwapinga ili kumzuia huyo mkuu wa kisiwaasije akaigeukia imani ya Kikristo. 9 Basi, Sauloambaye aliitwa pia Paulo, akiwa amejaa RohoMtakatifu, alimkodolea macho huyo mchawi,10 akasema, “Mdanganyifu wa kupindukia namlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Weweni adui wa chochote kile kilicho cha kweli;hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotoshanjia za Bwana zilizonyoka. 11 Sasa, mkono waBwana utakuadhibu: utakuwa kipofu nahutaweza kuuona mwanga wa jua kwakitambo.” Mara kila kitu kikawa kama ukunguna giza kwake, akaanza kwenda huku na hukuakitafuta mtu wa kumshika mkonoamwongoze. 12 Yule mkuu wa kisiwa alipoonahayo, aliongoka akawa muumini; akastaajabiasana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana. 13

Kutoka Pafo, Paulo na wenzake walipanda meliwakaenda hadi Perga katika Pamfulia; lakiniYohane (Marko) aliwaacha, akarudiYerusalemu. 14 Lakini wao waliendelea nasafari toka Pisga hadi mjini Antiokia Pisidia.Siku ya Sabato waliingia ndani ya Sunagogi,wakakaa. 15 Baada ya masomo katika kitabucha Sheria ya Mose na katika maandiko yamanabii, wakuu wa lile sunagogiwaliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kamamnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapamoyo, semeni.” 16 Basi, Paulo alisimama,akatoa ishara kwa mkono, akaanza kuongea:“Wananchi wa Israeli na wengine wote

mnaomcha Mungu, sikilizeni! 17 Mungu wataifa hili la Israeli aliwateua babu zetu nakuwafanya wawe taifa kubwa walipokuwaugenini kule Misri. Mungu aliwatoa huko kwauwezo wake mkuu. 18 Aliwavumilia kwa mudawa miaka arobaini kule jangwani. 19

Aliyaangamiza mataifa ya nchi ya Kanaaniakawapa hao watu wake ile nchi kuwa maliyao. 20 Miaka mia nne na hamsini ilipita,halafu akawapatia waamuzi wawaongozempaka wakati wa nabii Samweli. 21 Hapowakapendelea kuwa na mfalme, na Munguakawapa Saulo, mtoto wa Kishi wa kabila laBenyamini, awe mfalme wao kwa muda wamiaka arobaini. 22 Baada ya kumwondoaSaulo, Mungu alimteua Daudi kuwa mfalmewao. Mungu alionyesha kibali chake kwakeakisema: Nimemwona Daudi mtoto wa Yese; nimtu anayepatana na moyo wangu; mtuambaye atatimiza yale yote ninayotakakuyatenda. 23 Kutokana na ukoo wake mtuhuyu, Mungu, kama alivyoahidi,amewapelekea watu wa Israeli Mwokozi, ndiyeYesu. 24 Kabla ya kuja kwake Yesu, Yohanealimtangulia akiwahubiria watu wote wa Israelikwamba ni lazima watubu na kubatizwa. 25

Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wakealiwaambia watu: Mnadhani mimi ni nani?Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakujabaada yangu na mimi sistahili hata kuzifunguakamba za viatu vyake. 26 “Ndugu, ninyi mliowatoto wa ukoo wa Abrahamu, na wenginewote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wawokovu umeletwa kwetu. 27 Kwa maanawenyeji wa Yerusalemu na wakuu waohawakumtambua yeye kuwa Mwokozi. Walahawakuelewa maneno ya manabiiyanayosomwa kila Sabato. Hata hivyo,waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwakumhukumu Yesu adhabu ya kifo. 28 Ingawahawakumpata na hatia inayostahili auawe,walimwomba Pilato amhukumu auawe. 29 Nabaada ya kutekeleza yote yaliyokuwayameandikwa kumhusu yeye, walimshushakutoka msalabani, wakamweka kaburini. 30

Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu. 31 Naye,kwa siku nyingi aliwatokea wale waliofuatananaye kutoka Galilaya mpaka Yerusalemu. Haondio walio sasa mashahidi wake kwa watu waIsraeli. 32 Sisi tumekuja hapa kuwaleteeniHabari Njema: jambo lile Mungu alilowaahidiababu zetu amelitimiza sasa kwa ajili yetu sisitulio wajukuu wao kwa kumfufua Yesu kutokawafu. 33 Kama ilivyoandikwa katika zaburi yapili: Wewe ni Mwanangu, mimi leo nimekuwababa yako. 34 Na juu ya kumfufua kutokawafu, asipate tena kurudi huko na kuoza,Mungu alisema hivi: Nitakupa baraka takatifuna za kweli nilizomwahidia Daudi. 35 Naam, nakatika sehemu nyingine za zaburi asema:Hutamwacha Mtakatifu wako aoze. 36 Sasa,Daudi mwenyewe alitimiza mapenzi ya Munguwakati wake; kisha akafa na kuzikwa karibu na

MATENDO YA MITUME 12:24

100

Page 101: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

14

wazee wake, na mwili wake ukaoza. 37 Lakiniyule ambaye Mungu alimfufua kutoka wafuhakupata kuoza. 38 Jueni wazi, ndugu zangu,kwamba ujumbe kuhusu kusamehewa dhambiunahubiriwa kwenu kwa njia ya Yesu Kristo; 39

na ya kwamba kila mmoja anayemwamini Yesuanasamehewa dhambi zote, jambo ambalohalingewezekana kwa njia ya Sheria ya Mose.40 Jihadharini basi, msije mkapatwa na yaleyaliyosemwa na manabii: 41 Sikilizeni enyiwenye madharau, shangaeni mpotee! Kwamaana kitu ninachofanya sasa, nyakati zenu, nikitu ambacho hamtakiamini hata kama mtuakiwaelezeni.” 42 Paulo na Barnabawalipokuwa wanatoka katika ile sunagogi,wale watu waliwaalika waje tena siku yaSabato iliyofuata, waongee zaidi juu ya mambohayo. 43 Mkutano huo ulipomalizika,Wayahudi wengi na watu wa mataifa menginewaliokuwa wameongokea dini ya Kiyahudiwaliwafuata Paulo na Barnaba. Hao mitumewaliongea nao, wakawatia moyo waendeleekuishi wakitegemea neema ya Mungu. 44 Sikuya Sabato iliyofuata, karibu kila mtu katika ulemji alikuja kusikiliza neno la Bwana. 45 LakiniWayahudi walipoliona hilo kundi la watuwalijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasemaPaulo na kumtukana. 46 Hata hivyo, Paulo naBarnaba waliongea kwa uhodari zaidi,wakasema, “Ilikuwa ni lazima neno la Munguliwafikieni ninyi kwanza; lakini kwa kuwammelikataa na kujiona hamstahili uzima wamilele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watuwa mataifa mengine. 47 Maana Bwanaalituagiza hivi: Nimekuteua wewe uwemwanga kwa mataifa, uwe njia ya wokovu kwaulimwengu wote.” 48 Watu wa mataifamengine waliposikia jambo hilo walifurahi,wakausifu ujumbe wa Mungu; na walewaliokuwa wamechaguliwa kupata uzima wamilele, wakawa waumini. 49 Neno la Bwanalikaenea kila mahali katika sehemu ile. 50

Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake watabaka ya juu wa mataifa mengine ambaowalikuwa wacha Mungu, na wanaumemaarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesaPaulo na Barnaba, wakawafukuza kutokakatika eneo lao. 51 Basi, mitumewakayakung'uta mavumbi yaliyokuwa katikamiguu yao kama onyo, kisha wakaenda Ikonio.52 Lakini hao wafuasi walikuwa wamejaafuraha na Roho Mtakatifu.

Kule Ikonio, mambo yalikuwa kamayalivyokuwa kule Antiokia; Paulo naBarnaba walikwenda katika sunagogi

la Wayahudi wakaongea kwa uhodari hataWayahudi wengi na Wagiriki wakawa waumini.2 Lakini Wayahudi wengine waliokataa kuwawaumini walichochea na kutia chuki katikamioyo ya watu wa mataifa mengine iliwawapinge hao ndugu. 3 Paulo na Barnabawaliendelea kukaa huko kwa muda mrefu.Waliongea kwa uhodari juu ya Bwana, naye

Bwana akathibitisha ukweli wa ujumbewalioutoa juu ya neema yake, kwakuwawezesha kutenda miujiza na maajabu. 4

Watu wa mji huo waligawanyika: wenginewaliwaunga mkono Wayahudi, na wenginewalikuwa upande wa mitume. 5 Mwishowe,baadhi ya watu wa mataifa mengine naWayahudi, wakishirikiana na wakuu wao,waliazimu kuwatendea vibaya hao mitume nakuwapiga mawe. 6 Mitume walipogunduajambo hilo, walikimbilia Lustra na Derbe, mijiya Lukaonia, na katika sehemu za jirani, 7

wakawa wanahubiri Habari Njema huko. 8

Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambayealikuwa amelemaa miguu tangu kuzaliwa, naalikuwa hajapata kutembea kamwe. 9 Mtuhuyo alikuwa anamsikiliza Paulo alipokuwaanahubiri. Paulo alimtazama kwa makini, naalipoona kuwa alikuwa na imani ya kuwezakuponywa, 10 akasema kwa sauti kubwa,“Simama wima kwa miguu yako!” Huyo mtualiyelemaa akainuka ghafla, akaanzakutembea. 11 Umati wa watu walipoonaalichofanya Paulo, ulianza kupiga kelele kwalugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katikasura za binadamu!” 12 Barnaba akaitwa Zeu,na Paulo, kwa vile yeye ndiye aliyekuwaanaongea, akaitwa Herme. 13 Naye kuhani wahekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaletafahali na shada za maua mbele ya mlangomkuu wa mji, na pamoja na ule umati wa watuakataka kuwatambikia mitume. 14 Barnaba naPaulo walipopata habari hiyo waliyararuamavazi yao na kukimbilia katika lile kundi lawatu wakisema kwa sauti kubwa: 15 “Ndugu,kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia nibinadamu kama ninyi. Na, tuko hapakuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziachahizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliyehai, Mungu aliyeumba mbingu na nchi, baharina vyote vilivyomo. 16 Zamani Mungualiruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda. 17 Hatahivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwamambo mema anayowatendea: huwanyesheamvua toka angani, huwapa mavuno kwawakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyoyenu furaha.” 18 Ingawa walisema hivyohaikuwa rahisi kuwazuia wale watuwasiwatambikie. 19 Lakini Wayahudi kadhaawalikuja kutoka Antiokia na Ikonio,wakawafanya watu wajiunge nao, wakampigamawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mjiwakidhani amekwisha kufa. 20 Lakini wauminiwalipokusanyika na kumzunguka, aliamkaakarudi mjini. Kesho yake, yeye pamoja naBarnaba walikwenda Derbe. 21 Baada ya Paulona Barnabas kuhubiri Habari Njema hukoDerbe na kupata wafuasi wengi, walifungasafari kwenda Antiokia kwa kupitia Lustra naIkonio. 22 Waliwaimarisha waumini wa mijihiyo na kuwatia moyo wabaki imara katikaimani. Wakawaambia, “Ni lazima sisi sotetupitie katika taabu nyingi ili tuingie katika

MATENDO YA MITUME 14:22

101

Page 102: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

15

ufalme wa Mungu.” 23 Waliteua wazee katikakila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada yakusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinziwa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.24 Baada ya kupitia katika nchi ya Pisidia,walifika Pamfulia. 25 Baada ya kuhubiri uleujumbe huko Perga, walikwenda Atalia. 26

Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudiAntiokia ambako hapo awali walikuwawamewekwa chini ya ulinzi wa neema yaMungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwawameitimiza. 27 Walipofika huko Antiokiawalifanya mkutano wa kanisa la mahali hapo,wakawapa taarifa juu ya mambo Mungualiyofanya pamoja nao, na jinsialivyowafungulia mlango watu wa mataifamengine mlango wa kuingia katika imani. 28

Wakakaa pamoja na wale waumini kwa mudamrefu.

Basi, watu wengine walifika Antiokiakutoka Yudea wakaanzakuwafundisha wale ndugu wakisema,

“Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeoya Sheria ya Mose, hamtaweza kuokolewa.” 2

Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, nabaada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao,ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja nawaumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokiawaende Yerusalemu kuwaona wale mitume nawazee kuhusu jambo hilo. 3 Basi, kanisaliliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinikena Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifamengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizozikawafurahisha sana ndugu hao wote. 4

Walipofika Yerusalemu walikaribishwa nakanisa, mitume na wazee; nao wakawapataarifa juu ya yote Mungu aliyoyafanya pamojanao. 5 Lakini waumini wengine waliokuwa wakikundi cha Mafarisayo walisimama,wakasema, “Ni lazima watu wa mataifamengine watahiriwe na kufundishwa kuifuataSheria ya Mose.” 6 Basi, mitume na wazeewalifanya mkutano maalum wa kuchunguzajambo hilo. 7 Baada ya majadiliano marefu,Petro alisimama, akasema, “Ndugu zangu,ninyi mnafahamu kwamba hapo awali Mungualipenda kunichagua mimi miongoni mwenuniihubiri Habari Njema, ili watu wa mataifawapate kusikia na kuamini. 8 Naye Munguanayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwambaamewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifukama alivyotupa sisi. 9 Hakufanya ubaguziwowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yaokwa imani. 10 Sasa basi, kwa nini kumjaribuMungu kwa kuwatwika hao waumini mzigoambao wala babu zetu, wala sisi hatukuwezakuubeba? 11 Isiwe hivyo, ila tunaaminikwamba, sisi kama vile wao, tunaokolewa kwanjia ya neema ya Bwana Yesu.” 12 Kikundichote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba naPaulo wakieleza miujiza na maajabu ambayoMungu alitenda kwa mikono yao kati ya watuwa mataifa mengine. 13 Walipomaliza

kuongea, Yakobo alianza kusema: “Nduguzangu, nisikilizeni! 14 Simoni ameeleza jinsiMungu hapo awali alivyojishughulisha na watuwa mataifa mengine, akachagua baadhi yaowawe watu wake. 15 Jambo hili ni sawa kabisana maneno ya manabii, kama MaandikoMatakatifu yasemavyo: 16 Baada ya mambohaya nitarudi. Nitaijenga tena ile nyumba yaDaudi iliyoanguka; nitayatengeneza magofuyake na kuijenga tena. 17 Hapo watu wenginewote, watu wa mataifa yote niliowaita wawewangu, watamtafuta Bwana. 18 Ndivyoasemavyo Bwana, aliyefanya jambo hililijulikane tangu kale. 19 “Kwa hiyo, uamuziwangu ni huu: tusiwataabishe watu wa mataifawanomgeukia Mungu. 20 Bali tuwapelekeebarua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwanajisi kwa kutambikiwa sanamu za miungu;wajiepushe na uasherati; wasile mnyamayeyote aliyenyongwa, na wasinywe damu. 21

Kwa maana kwa muda mrefu maneno ya Moseyamekuwa yakihubiriwa katika kila mji nakusomwa katika masunagogi yote kila siku yaSabato.” 22 Mitume, wazee na kanisa lotewaliamua kuwachagua watu fulani miongonimwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulona Barnaba. Basi, wakamchagua Yuda aitwayepia Barsaba, na Sila ambao wote walikuwawanajulikana zaidi kati ya ndugu. 23

Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee,ndugu zenu, tunawasalimuni ninyi ndugu wamataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siriana Kilikia. 24 Tumesikia kwamba watu wenginekutoka huku kwetu waliwavurugeni kwamaneno yao, wakaitia mioyo yenu katikawasiwasi. Lakini wamefanya hivyo bila ya idhiniyoyote kutoka kwetu. 25 Hivyo, tumeamua kwapamoja kuwachagua watu kadhaa nakuwatuma kwenu pamoja na wapenzi wetuBarnaba na Paulo, 26 ambao wamehatarishamaisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetuYesu Kristo. 27 Kwa hiyo, tunawatuma Yuda naSila kwenu; hawa watawaambieni waowenyewe haya tuliyoandika. 28 Basi, RohoMtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwikemzigo zaidi ya mambo haya muhimu: 29 Msilevyakula vilivyotambikiwa sanamu; msinywedamu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa;na mjiepushe na uasherati. Mtakuwammefanya vema kama mkiepa kufanyamambo hayo. Wasalaam!” 30 Baada yakuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokiaambako waliita mkutano wa waumini,wakawapa hiyo barua. 31 Walipoisoma hiyobarua, maneno yake yaliwatia moyo,wakafurahi sana. 32 Yuda na Sila, ambao naowalikuwa manabii, walizungumza na haondugu kwa muda mrefu wakiwatia moyo nakuwaimarisha. 33 Baada ya kukaa huko kwamuda fulani, ndugu wa Antiokia waliwaagawakiwatakia amani, kisha wakarudi kwa walewaliokuwa wamewatuma. 34 Lakini Silaaliamua kubaki. 35 Paulo na Barnaba walibaki

MATENDO YA MITUME 14:23

102

Page 103: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

huko Antiokia kwa muda; wakafundisha nakuhubiri neno la Bwana, pamoja na watuwengine wengi. 36 Baada ya siku kadhaa,Paulo alimwambia Barnaba, “Turuditukawatembelee wale ndugu katika kila mjitulikolihubiri neno la Bwana tukajionee jinsiwanavyoendelea.” 37 Barnaba alitakawamchukue pia Yohane aitwaye Marko. 38

Lakini Paulo hakupendelea kumchukua Marko,ambaye awali aliwaacha kule Pamfulia nakukataa kushiriki katika kazi yao. 39 Basikukatokea ubishi mkali kati yao, nawakaachana. Barnaba akamchukua Marko,wakapanda meli kwenda Kupro. 40 Naye Pauloakamchagua Sila, na baada ya ndugu wamahali hapo kumweka chini ya ulinzi waneema ya Bwana, akaondoka. 41 Katika safarihiyo alipitia Siria na Kilikia akiyaimarishamakanisa.

Paulo alifika Derbe na Lustra, ambakoaliishi mfuasi mmoja aitwayeTimotheo. Mama yake ambaye pia

alikuwa mfuasi, alikuwa Myahudi; lakini babayake alikuwa Mgiriki. 2 Timotheo alikuwa nasifa kubwa kati ya wale ndugu wa Lustra naIkonio. 3 Paulo alitaka Timotheo aandamanenaye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanyahivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishisehemu hizo walijua kwamba baba yakeTimotheo alikuwa Mgiriki. 4 Walipokuwawanapita katika ile miji waliwapa watu yalemaagizo yaliyotolewa na mitume na wazeekule Yerusalemu, wakawaambia wayazingatie.5 Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imarakatika imani, na idadi ya waumini ikaongezekakila siku. 6 Walipitia sehemu za Frugia naGalatia kwani Roho Mtakatifu hakuwaruhusukuhubiri huo ujumbe mkoani Asia. 7

Walipofika kwenye mipaka ya Musia, walijaribukuingia mkoani Bithunia, lakini Roho wa Yesuhakuwaruhusu. 8 Basi, walipitia Musia,wakaenda moja kwa moja mpaka Troa. 9 Usikuhuo, Paulo aliona ono ambalo alimwona mtummoja wa Makedonia amesimama pale nakumwomba: “Vuka, uje Makedoniaukatusaidie.” 10 Mara baada ya Paulo kuonaono hilo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bilakukawia, tukiwa na hakika kwamba Munguametuita tuwapelekee Habari Njema. 11

Kutoka Troa, tulisafiri kwa meli moja kwa mojampaka Samothrake, na kesho yake tukatiananga Neapoli. 12 Kutoka huko, tulikwendampaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza yaMakedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma.Tulikaa katika mji huo siku kadhaa. 13 Siku yaSabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando yamto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pakusali. Tuliketi, tukaongea na wanawakewaliokusanyika mahali hapo. 14 Miongonimwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamkemmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyejiwa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiasharaya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana

aliufungua moyo wake hata akayapokea yalemaneno Paulo aliyokuwa anasema. 15 Baadaya huyo mama pamoja na jamaa yakekubatizwa, alitualika akisema, “Kama kwelimmeona kwamba mimi namwamini Bwana,karibuni nyumbani kwangu mkakae.”Akatuhimiza twende. 16 Siku moja, tulipokuwatunakwenda mahali pa kusali, msichanammoja aliyekuwa na pepo mwenye uwezo wakuagua alikutana nasi. Msichana huyo alikuwaanawapatia matajiri wake fedha nyingi kwauaguzi wake. 17 Basi, huyo msichana alimfuataPaulo na sisi, akipiga kelele na kusema, “Hawawatu ni watumishi wa Mungu Mkuu.Wanawatangazieni njia ya wokovu.” 18 Akawaanafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku mojaPaulo alikasirika, akamgeukia na kumwambiahuyo pepo, “Nakuamuru kwa jina la YesuKristo, mtoke huyu!” Mara huyo pepoakamtoka. 19 Matajiri wa yule msichanawalipoona kwamba tumaini lao la kupata malilimekwisha, waliwakamata Paulo na Sila,wakawaburuta mpaka hadharani, mbele yawakuu. 20 Wakawashtaki kwa mahakimuwakisema, “Watu hawa ni Wayahudi nawanafanya fujo katika mji wetu. 21

Wanafundisha desturi ambazo sisi raia waRoma haturuhusiwi kuzikubali wala kuzifuata.”22 Kundi la watu likajiunga nao,likawashambulia. Wale mahakimuwakawatatulia Paulo na Sila mavazi yao,wakaamuru wapigwe viboko. 23 Baada yakupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wagereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzimkali. 24 Kutokana na maagizo hayo, huyoaskari aliwaweka katika chumba cha ndanikabisa cha gereza na kuifunga miguu yaokwenye nguzo. 25 Karibu na usiku wa mananePaulo na Sila walikuwa wakisali na kuimbanyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwawengine wakiwa wanasikiliza. 26 Ghafla,kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambaouliitikisa misingi ya gereza. Mara, milango yoteikafunguka na minyororo iliyowafunga haowafungwa ikaachana. 27 Askari wa gerezaalipoamka na kuiona milango ya gerezaimefunguliwa, alidhani kwamba wafungwawote walikuwa wametoroka na hivyoakauchomoa upanga wake, akataka kujiua. 28

Lakini Paulo akaita kwa sauti kubwa:“Usijidhuru mwenyewe kwa maana sisi sotetuko hapa.” 29 Baada ya kumwita mtu aletetaa, huyo askari wa gereza alikimbilia ndani,akajitupa mbele ya miguu ya Paulo na Silahuku akitetemeka kwa hofu. 30 Halafualiwaongoza nje, akawauliza, “Waheshimiwa,nifanye nini nipate kuokoka?” 31 Waowakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu naweutaokolewa pamoja na jamaa yako yote.” 32

Basi, wakamhubiria neno la Bwana yeyepamoja na jamaa yake. 33 Yule askarialiwachukua saa ileile ya usiku akawasafishamajeraha yao, kisha yeye na jamaa yake

MATENDO YA MITUME 16:33

103

Page 104: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

17

wakabatizwa papo hapo. 34 Halafuakawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake,akawapa chakula. Yeye na jamaa yake yotewakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwawanamwamini Mungu. 35 Kesho yake asubuhi,mahakimu waliwatuma maofisa waowakisema, “Wafungueni wale watu.” 36 Yuleaskari wa gereza alimpasha habari Paulo:“Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe.Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwaamani.” 37 Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini?Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga vibokohadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena,walitutia ndani na sasa wanataka kutufunguliakwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewewaje hapa watufungulie.” 38 Hao maofisawaliwapasha habari mahakimu juu ya jambohilo, nao waliposikia kwamba Paulo na Silawalikuwa raia wa Roma, waliogopa. 39 Hivyo,walikwenda kuwataka radhi na baada yakuwatoa ndani waliwaomba watoke katika mjiule. 40 Paulo na Sila walitoka gerezani,wakaenda nyumbani kwa Ludia. Hukowalionana na ndugu waumini na baada yakuwatia moyo wakaondoka.

Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia,walisafiri mpaka Thesalonika ambakokulikuwa na sunagogi la Wayahudi. 2

Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturiyake akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo,akatumia Maandiko Matakatifu. 3 Aliyaelezana kuonyesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswana kufufuka kutoka wafu. Akawaambia, “Yesuambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”4 Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulona Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagirikiwaliomcha Mungu pamoja na wanawakewengi wa tabaka la juu, walijiunga nao. 5

Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodiwafidhuli sokoni, wakafanya kikundi nakuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumbaya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulona Sila ili wawalete hadharani. 6 Lakinihawakuwapata na hivyo walimburuta Yasonipamoja na ndugu wengine mpaka kwa wakuuwa mji, wakapiga kelele: “Watu hawawamekuwa wakivuruga dunia yote na sasawako hapa mjini. 7 Yasoni amewakaribishanyumbani kwake. Wote wanafanya kinyumecha amri ya Kaisari wakisema eti Kuna mfalmemwingine aitwaye Yesu.” 8 Kwa maneno hayowaliwatia wasiwasi wakuu wa mji na kundi lawatu. 9 Wakawafanya Yasoni na wenzakewatoe dhamana, kisha wakawaacha waendezao. 10 Usiku, wale ndugu waliwahimiza Paulona Sila waende Berea. Mara tu walipofikahuko, walikwenda katika sunagogi laWayahudi. 11 Watu wa huko walikuwawasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonika.Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa,wakawa wanayachunguza MaandikoMatakatifu kila siku, ili kuona kama yalewaliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli. 12

Wengi wao waliamini na pia wanawake waKigiriki wa tabaka la juu na wanaume pia. 13

Lakini, Wayahudi wa Thesalonikawalipogundua kwamba Paulo alikuwaanahubiri neno la Mungu huko Berea,walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo nakuchochea makundi ya watu. 14 Wale nduguwakamsindikiza haraka aende pwani lakini Silana Timotheo walibaki Berea. 15 Wale nduguwaliomsindikiza Paulo walikwenda pamojanaye mpaka Athene. Kisha, wakarudi pamojana maagizo kutoka kwa Paulo kwamba Sila naTimotheo wamfuate upesi iwezekanavyo. 16

Paulo alipokuwa anawasubiri Sila na Timotheohuko Athene, moyo wake ulighadhibika sanaalipoona jinsi mji huo ulivyokuwa umejaasanamu za miungu. 17 Alijadiliana naWayahudi na watu wengine waliomcha Mungukatika sunagogi; na kila siku alikuwa namajadiliano sokoni pamoja na wowote walewaliojitokeza. 18 Wengine waliofuata falsafa yaEpikuro na Stoiki walibishana naye. Wenginewalisema, “Anataka kusema nini huyubwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwaanahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo,wengine walisema, “Inaonekana kamaanahubiri juu ya miungu ya kigeni.” 19 Hivyowalimchukua Paulo, wakampeleka Areopago,wakasema, “Tunataka kujua jambo hili jipyaulilokuwa unazungumzia. 20 Vitu vinginetulivyosikia kwa masikio yetu vinaonekanakuwa viroja kwetu. Tungependa kujua mambohaya yana maana gani.” 21 Wananchi waAthene na wakazi wengine wa huko walikuwawanatumia wakati wao wote kuhadithiana nakusikiliza habari mpyampya. 22 Basi, Pauloalisimama mbele ya baraza la Areopago,akasema, “Wananchi wa Athene! Ninaonakwamba ninyi, kwa vyovyote, ni watu wa dinisana. 23 Sababu yenyewe ni kwamba katikapitapita yangu niliangalia sanamu zenu zaibada nikakuta madhabahu moja ambayoimeandikwa: Kwa ajili ya Mungu yuleAsiyejulikana. Basi, huyo mnayemwabudu bilakujua, ndiye ninayemhubiri kwenu. 24 Mungu,aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, niBwana wa mbingu na nchi; yeye hakai katikahekalu zilizojengwa na watu. 25 Walahatumikiwi kwa mikono ya watu kana kwambaanahitaji chochote kile, kwa maana yeyemwenyewe ndiye anayewapa watu uhai,anawawezesha kupumua na anawapa kila kitu.26 Kutokana na mtu mmoja aliumba mataifayote na kuyawezesha kuishi duniani kote.Aliamua na kupanga kabla kabisa lini na wapimataifa hayo yangeishi. 27 Alifanya hivyo, ilimataifa hayo yapate kumfuata, na kama vilekwa kupapasapapasa, yapate kumfikia. Hatahivyo lakini, Mungu hayuko mbali na kilammoja wetu. 28 Kama alivyosema mtu mmoja:Ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu, natuko! Ni kama washairi wenu wenginewalivyosema: Sisi ni watoto wake. 29 Ikiwa

MATENDO YA MITUME 16:34

104

Page 105: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

18

19

basi, sisi ni watoto wa Mungu, haifai kumfikiriaMungu kuwa kama dhahabu, fedha au hatajiwe lililochongwa na kutiwa nakshi nabinadamu. 30 Mungu alifanya kama kwambahaoni nyakati zile watu walipokuwa wajinga.Lakini sasa, anaamuru watu wote kila mahaliwatubu. 31 Kwa maana amekwisha weka sikuambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki kwanjia ya mtu mmoja aliyemteua. Munguamewathibitishia wote jambo hili kwakumfufua mtu huyo kutoka wafu!” 32

Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo lakufufuka kwa wafu, wengine wao walianguakicheko; lakini wengine walisema, “Tunatakakukusikia tena juu ya jambo hili!” 33 Hivyo,Paulo aliwaacha, akatoka barazani. 34 Lakiniwatu kadhaa waliandamana naye, wakawawaumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisiowa Areopago, mwanamke mmoja aitwayeDamari na wengineo.

Baada ya hayo, Paulo aliondokaAthene, akaenda Korintho. 2 HukoKorintho, alimkuta Myahudi mmoja

aitwaye Akula, mzaliwa wa Ponto. Akulapamoja na mkewe aitwaye Priskila, walikuwawamerudi kutoka Italia siku hizohizo kwasababu Kaisari Klaudio alikuwa ameamuruWayahudi wote waondoke Roma. Pauloalikwenda kuwaona, 3 na kwa vile waowalikuwa mafundi wa kushona mahema kamaalivyokuwa yeye, Paulo alikaa nao akafanyakazi. 4 Kila Sabato alifanya majadiliano katikasunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi naWagiriki. 5 Baada ya Sila na Timotheo kuwasilikutoka Makedonia, Paulo alianza kutumiawakati wake wote kwa ajili ya kuhubiri,akawathibitishia Wayahudi kwamba Yesu ndiyeKristo. 6 Walipompinga na kuanza kumtukana,aliyakung'uta mavazi yake mbele yao akisema,“Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sinalawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangusasa nitawaendea watu na mataifa mengine.”7 Basi, akatoka hapo akaenda kukaanyumbani kwa mtu mmoja mcha Munguaitwaye Tito Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwakaribu na lile sunagogi. 8 Lakini Krispo, mkuuwa sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamojana jamaa yake yote. Wakorintho wengiwaliusikiliza ujumbe huo, wakaamini nakubatizwa. 9 Siku moja usiku, Bwanaalimwambia Paulo katika maono: “Usiogope,endelea kuhubiri tu bila kufa moyo, 10 maanamimi niko pamoja nawe. Hakuna mtuatakayejaribu kukudhuru maana hapa mjinipana watu wengi walio upande wangu.” 11

Basi, Paulo alikaa huko akifundisha neno laMungu kati yao kwa muda wa mwaka mmojana nusu. 12 Lakini wakati Galio alipokuwamkuu wa mkoa wa Akaya, Wayahudiwalimvamia Paulo kwa pamoja na kumpelekamahakamani. 13 Wakasema, “Tunamshtakimtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watuwamwabudu Mungu kwa namna inayopingana

na Sheria.” 14 Kabla tu Paulo hajaanza kusema,Galio aliwaambia Wayahudi, “Sikilizeni enyiWayahudi! Kama kweli jambo hili lingekuwajuu ya uhalifu au uovu ningekuwa tayarikuwasikilizeni. 15 Lakini kama ni shauri laubishi kuhusu maneno na majina ya Sheriayenu, amueni ninyi wenyewe. Mimi sitaki kuwahakimu wa mambo haya!” 16 Basi,akawafukuza kutoka mahakamani. 17 Naowote wakamkamata Sosthene ambaye alikuwakiongozi wa sunagogi, wakampiga palepalembele ya mahakama. Lakini Galio hakujalikitendo hicho hata kidogo. 18 Paulo alikaabado na wale ndugu huko Korintho kwa sikunyingi. Kisha aliwaaga, akapanda meli kwendaSiria pamoja na Priskila na Akula. HukoKenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu yanadhiri aliyokuwa ameweka. 19 Walifika Efesona hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula,akaenda katika sunagogi, akajadiliana naWayahudi. 20 Walimwomba akae nao mudamrefu zaidi, lakini hakupenda. 21 Balialipokuwa anaondoka, alisema, “Munguakipenda nitakuja kwenu tena.” AkaondokaEfeso kwa meli. 22 Meli ilitia nanga Kaisarea,naye Paulo akaenda Yerusalemu kulisalimia lilekanisa, kisha akaenda Antiokia. 23 Alikaa hukomuda mfupi, halafu akaendelea na safari kwakupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatiamoyo wafuasi wote. 24 Myahudi mmojaaitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifikaEfeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wakuongea na mwenye ujuzi mkubwa waMaandiko Matakatifu. 25 Alikuwaamefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, naakiwa motomoto, aliongea juu ya habari zaYesu. Akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwaamepata ubatizo wa Yohane tu. 26 Priskila naAkula walipomsikia akiongea kwa uhodarindani ya sunagogi, walimchukua kwaowakamfundisha hiyo Njia ya Mungu kwausahihi zaidi. 27 Apolo alipoamua kwendaAkaya, wale ndugu walimtia moyo kwakuwaandikia wafuasi kule Akaya wampokee.Alipofika huko, aliweza kwa msaada wa neemaya Mungu, kuwasaidia sana wale nduguwaliopata kuwa waumini; 28 kwa maanaaliendelea kwa uhodari kuwashinda Wayahudihadharani akithibitisha kwa MaandikoMatakatifu kuwa Yesu ni Kristo.

Wakati Apolo alipokuwa Korintho,Paulo alisafiri sehemu za bara, akafikaEfeso ambako aliwakuta wanafunzi

kadhaa. 2 Akauliza, “Je, mlipopata kuwawaumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Naowakamjibu, “La! Hata kusikia kwamba kunaRoho Mtakatifu hatujasikia.” 3 Naye akasema,“Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?”Wakamjibu, “Ubatizo wa Yohane.” 4 NayePaulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwawa kuonyesha kwamba watu wametubu.Yohane aliwaambia watu wamwamini yuleambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani

MATENDO YA MITUME 19:4

105

Page 106: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

Yesu.” 5 Baada ya kusikia hayo, walibatizwakwa jina la Bwana Yesu. 6 Basi, Pauloakawawekea mikono, na Roho Mtakatifuakawashukia, wakaanza kusema lughambalimbali na kutangaza ujumbe wa Mungu.7 Wote jumla, walikuwa watu wapatao kumina wawili. 8 Kwa muda wa miezi mitatu Pauloalikuwa akienda katika sunagogi, akawa namajadiliano ya kuvutia sana juu ya Ufalme waMungu. 9 Lakini wengine walikuwa wakaidi,wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibayahadharani juu ya Njia ya Bwana. Hapo Pauloalivunja uhusiano nao, akawachukua pembeniwale wanafunzi wake, akawa anazungumzanao kila siku katika jumba la masomo laTurano. 10 Aliendelea kufanya hivyo kwa mudawa miaka miwili hata wakazi wote wa Asia,Wayahudi na watu wa mataifa mengine,wakaweza kusikia neno la Bwana. 11 Mungualifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo.12 Watu walikuwa wakichukua leso na nguonyingine za kazi ambazo Paulo alikuwaamezitumia, wakazipeleka kwa wagonjwa, naowakaponywa magonjwa yao; na walewaliokuwa na pepo wabaya wakatokwa napepo hao. 13 Wayahudi kadhaa wenyekupunga pepo wabaya, walisafiri huko nahuko, wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesukwa wale waliokuwa wamepagawa na pepowabaya. Walikuwa wakisema: “Ninawaamurukwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.” 14

Watoto saba wa Skewa, Kuhani Mkuu waKiyahudi, walikuwa miongoni mwa haowaliokuwa wanafanya hivyo. 15 Lakini pepombaya aliwajibu, “Ninamfahamu Yesu,ninamjua pia Paulo, lakini ninyi ni nani?” 16

Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wotekwa kishindo, akawashinda nguvu. Na haowatoto wa Skewa wakakimbia kutoka ilenyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.17 Kila mtu huko Efeso, Myahudi na asiyeMyahudi, alisikia juu ya tukio hilo. Wotewaliingiwa na hofu, wakalitukuza jina la BwanaYesu. 18 Waumini wengi walijitokeza wakakirihadharani mambo waliyokuwa wametenda. 19

Wengine waliokuwa wameshughulikia mamboya uchawi hapo awali, walikusanya vitabuvyao, wakavichoma mbele ya wote. Walikisiagharama ya vitabu hivyo, wakaona yafikiavipande vya fedha elfu hamsini. 20 Kwa namnahiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa nanguvu zaidi. 21 Baada ya mambo hayo, Pauloaliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitiaMakedonia na Akaya. Alisema, “Baada yakufika huko, itanilazimu kuona Roma pia.” 22

Hivyo, aliwatuma wawili wa wasaidizi wake,Timotheo na Erasto, wamtangulie kwendaMakedonia, naye akabaki kwa muda huko Asia.23 Wakati huo ndipo kulipotokea ghasia kubwahuko Efeso kwa sababu ya hiyo Njia ya Bwana.24 Kulikuwa na mfua fedha mmoja aitwayeDemetrio, ambaye alikuwa na kazi yakutengeneza sanamu za nyumba ya mungu wa

kike aitwaye Artemi. Shughuli hiyo iliwapatiamafundi faida kubwa. 25 Demetrioaliwakusanya hao wafanyakazi pamoja nawengine waliokuwa na kazi kama hiyo,akawaambia, “Wananchi, mnafahamu kwambakipato chetu kinatokana na biashara hii. 26

Sasa, mnaweza kusikia na kujionea wenyewemambo Paulo anayofanya, si tu hapa Efeso, ilapia kote katika Asia. Yeye amewashawishi nakuwageuza watu wakakubali kwamba miunguile iliyotengenezwa na watu si miungu hatakidogo. 27 Hivyo iko hatari kwamba biasharayetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali piajambo hilo linaweza kuifanya nyumba yamungu Artemi kuwa si kitu cha maana.Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na duniayote inamwabudu, zitakwisha.” 28 Waliposikiahayo, waliwaka hasira, wakaanza kupigakelele: “Mkuu ni Artemi, wa Efeso!” 29 Mji woteukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo naAristarko, wenyeji wa Makedonia, ambaowalikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbianao mpaka kwenye ukumbi wa michezo. 30

Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umatiwa watu, lakini wale waumini walimzuia. 31

Maofisa wengine wa huo mkoa wa Asia,waliokuwa rafiki zake, walimtumia Pauloujumbe wakimsihi asijihatarishe kwa kwendakwenye ukumbi wa michezo. 32 Wakati huo,kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili nawengine lile, mpaka hata ule mkutanoukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu yakukutana kwao. 33 Kwa vile Wayahudiwalimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhiya watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye.Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkonoakitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi,wote kwa sauti moja walipiga kelele: “Mkuu niArtemi wa Efeso!” Wakaendeleakupayukapayuka hivyo kwa muda wa saambili. 35 Hatimaye karani wa mji alifaulukuwanyamazisha, akawaambia, “Wananchi waEfeso, kila mtu anajua kwamba mji huu waEfeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu Artemina mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutokambinguni. 36 Hakuna anayeweza kukanamambo haya. Hivyo basi, tulieni; msifanyechochote bila hadhari. 37 Mmewaita watuhawa hapa ingawaje hawakuikufuru nyumbaya mungu wala kumtukana mungu wetu wakike. 38 Kama, basi Demetrio na wafanyakaziwake wana mashtaka yao kuhusu watu hawa,yapo mahakama na wakuu wa mikoa;wanaweza kushtakiana huko. 39 Kama mnamatatizo mengine, yapelekeni katika kikaohalali. 40 Kwa maana tungaliweza kushtakiwakwa kusababisha ghasia kutokana na vitukovya leo. Ghasia hii haina msingi halali nahatungeweza kutoa sababu za kuridhisha zaghasia hiyo.” 41 Baada ya kusema hayoaliuvunja mkutano.

MATENDO YA MITUME 19:5

106

Page 107: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

20

21

Ile ghasia ya Efeso ilipokwisha tuliaPaulo aliwaita pamoja wale waumini,akawatia moyo. Kisha akawaaga,

akasafiri kwenda Makedonia. 2 Alipitiasehemu za nchi zile akiwatia watu moyo kwamaneno mengi. Halafu akafika Ugiriki. 3

ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwaanajitayarisha kwenda Siria, aligunduakwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyiampango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwakupitia Makedonia. 4 Sopatro, mwana waPirho kutoka Berea, aliandamana naye; piaAristarko na Sekundo kutoka Thesalonika,Gayo kutoka Derbe, Timotheo, Tukiko naTrofimo wa mkoa wa Asia. 5 Haowalitutangulia na kutungojea kule Troa. 6 Sisi,baada ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu,tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya sikutatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwamuda wa juma moja. 7 Jumamosi jioni,tulikutana ili kumega mkate. Kwa vile Pauloalikuwa amekusudia kuondoka kesho yake,aliwahutubia watu na kuendelea kuongea naohadi usiku wa manane. 8 Katika chumbatulimokuwa, ghorofani, kulikuwa na taa nyingizinawaka. 9 Kijana mmoja aitwaye Eutukoalikuwa ameketi dirishani wakati Pauloalipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutukoalianza kusinzia kidogokidogo na hatimayeusingizi ukambana, akaanguka chini kutokaghorofa ya tatu. Wakamwokota amekwishakufa. 10 Lakini Paulo alishuka chini, akainama,akamkumbatia na kusema, “Msiwe nawasiwasi maana kuna uhai bado ndani yake.”11 Kisha akapanda tena ghorofani, akamegamkate, akala. Aliendelea kuhubiri kwa mudamrefu hadi alfajiri, halafu akaondoka. 12 Walewatu walimchukua yule kijana nyumbani akiwamzima kabisa, wakapata kitulizo kikubwa. 13

Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Asoambako tungemchukua Paulo. Ndivyoalivyopanga; maana alitaka kufika huko kwakupitia nchi kavu. 14 Basi, alitukuta kule Aso,tukampandisha melini, tukaenda Mitulene. 15

Kutoka huko tulisafiri tukafika Kio kesho yake.Siku ya pili, tulitia nanga Samo na kesho yaketukafika Mileto. 16 Paulo alikuwa amekusudiakuendelea na safari kwa meli bila kupitia Efesoili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na harakaya kufika Yerusalemu kwa sikukuu yaPentekoste kama ingewezekana. 17 KutokaMileto Paulo alituma ujumbe kwa wazee waEfeso wakutane naye. 18 Walipofika kwakealiwaambia, “Mnajua jinsi nilivyotumia wakatiwote pamoja nanyi tangu siku ile ya kwanzanilipofika Asia. 19 Mnajua jinsi nilivyomtumikiaBwana kwa unyenyekevu wote, kwa machozina matatizo yaliyonipata kutokana na mipangoya hila ya Wayahudi. 20 Mnajua kwambasikusita hata kidogo kuwahubiria hadharani nanyumbani mwenu na kuwafundisha chochoteambacho kingewasaidieni. 21 Niliwaonyawote—Wayahudi kadhalika na watu wa

mataifa, wamgeukie Mungu na kumwaminiBwana wetu Yesu. 22 Sasa, sikilizeni! Mimi,nikiwa ninamtii Roho, nakwenda Yerusalemubila kufahamu yatakayonipata huko. 23

Ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifuananithibitishia katika kila mji kwamba vifungona mateso ndivyo vinavyoningojea. 24 Lakini,siuthamini uhai wangu kuwa ni kitu sanakwangu. Nataka tu nikamilishe ule utumewangu na kumaliza ile kazi aliyonipa BwanaYesu niifanye, yaani nitangaze Habari Njemaya neema ya Mungu. 25 “Nimekuwa nikiendahuko na huko kati yenu nikiuhubiri Ufalme waMungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmojawenu atakayeniona tena. 26 Hivyo, leo hiininawathibitishieni rasmi kwamba ikijatokeaakapotea mmoja wenu, mimi sina lawamayoyote. 27 Kwa maana sikusita hata kidogokuwatangazieni azimio lote la Mungu. 28

Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundiambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyimuwe walezi wake. Lichungeni kanisa laMungu ambalo amejipatia kwa damu yaMwanae. 29 Nafahamu vizuri sana kwambabaada ya kuondoka kwangu mbwa mwituwakali watawavamieni, na hawatakuwa nahuruma kwa kundi hilo. 30 Hata kutokamiongoni mwenu watatokea watu ambaowatasema mambo ya uongo ili kuwapotoshawatu na kuwafanya wawafuate wao tu. 31 Kwahiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwamuda wa miaka mitatu, usiku na mchana,sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwamachozi. 32 “Na sasa basi, ninawaweka ninyichini ya ulinzi wa Mungu na ujumbe wa neemayake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga ninyi nakuwawezesha mzipate zile barakaalizowawekea watu wake. 33 Mimi sikutamanihata mara moja fedha, wala dhahabu, walanguo za mtu yeyote. 34 Mnajua ninyi wenyewekwamba nimefanya kazi kwa mikono yangumwenyewe, ili kujipatia mahitaji yangu na yawenzangu. 35 Nimekuwa nikiwapeni daimamfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyotunapaswa kuwasaidia walio dhaifu,tukikumbuka maneno ya Bwana Yesumwenyewe: Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.”36 Baada ya kusema hayo, Paulo alipigamagoti pamoja nao wote, akasali. 37 Wotewalikuwa wanalia; wakamwaga kwakumkumbatia na kumbusu. 38 Jambolililowahuzunisha zaidi lilikuwa neno alilosemakwamba hawangemwona tena. Basi,wakamsindikiza hadi melini.

Tulipokwisha agana nao, tulipandameli tukaenda moja kwa moja mpakaKosi. Kesho yake tulifika Rodo, na

kutoka huko tulikwenda Patara. 2 Huko,tulikuta meli iliyokuwa inakwenda Foinike,hivyo tulipanda, tukasafiri. 3 Baada ya kufikamahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitiaupande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitiananga katika mji wa Tiro ambapo ile meli

MATENDO YA MITUME 21:3

107

Page 108: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

ilikuwa ipakuliwe shehena yake. 4 Tulikutawaumini huko, tukakaa pamoja nao kwa mudawa juma moja. Waumini hao wakawa waongeakwa nguvu ya Roho, wakamwambia Pauloasiende Yerusalemu. 5 Lakini muda wetuulipokwisha tuliondoka. Wote pamoja nawanawake na watoto wao walitusindikizampaka nje ya mji. Tulipofika pwani, sotetulipiga magoti tukasali. 6 Kisha tuliagana; sisitukapanda meli nao wakarudi makwao. 7 Sisituliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafikaTolemai ambapo tuliwasalimu ndugu zetu,tukakaa nao siku moja. 8 Kesho yaketuliondoka tukaenda Kaisarea. Huko Kaisareatulikwenda nyumbani kwa mhubiri Filipo. Yeyealikuwa mmoja wa wale saba waliochaguliwakule Yerusalemu. 9 Alikuwa na binti watatuambao walikuwa na kipaji cha unabii. 10 Baadaya kukaa huko siku kadhaa, nabii mmojaaitwaye Agabo alifika kutoka Yudea. 11 Alitujia,akachukua mkanda wa Paulo, akajifungamikono na miguu, akasema “Roho Mtakatifuasema hivi: Wayahudi kule Yerusalemuwatamfunga namna hii mtu mwenye ukandana kumtia mikononi mwa watu wa mataifa.” 12

Tuliposikia hayo, sisi na wale watu wenginewaliokuwa hapo tulimsihi Paulo asiendeYerusalemu. 13 Lakini yeye alijibu, “Mnatakakufanya nini? Mnataka kuvunja moyo wangukwa machozi? Niko tayari siyo tu kutiwa ndanikule Yerusalemu, ila hata kufa kwa ajili yaBwana Yesu.” 14 Tuliposhindwa kumshawishitulinyamaza, tukasema tu: “Mapenzi ya Bwanayafanyike” 15 Baada ya kukaa pale kwa muda,tulifunga mizigo yetu, tukaendelea na safarikwenda Yerusalemu. 16 Wengine kati ya walewafuasi wa Kaisarea walienda pamoja nasi,wakatupeleka nyumbani kwa Mnasoni ambayetulikuwa tunakwenda kukaa naye kwa muda.Mnasoni alikuwa mwenyeji wa Kupro naalikuwa amekuwa muumini kwa siku nyingi. 17

Tulipofika Yerusalemu, ndugu wauminiwalitupokea vizuri sana. 18 Kesho yake Pauloalikwenda pamoja nasi kumwamkia Yakobo, nawazee wote wa kanisa walikuwako pia. 19

Baada ya kuwasalimu, Paulo aliwapa taarifakamili kuhusu yote Mungu aliyokuwaametenda kati ya mataifa kwa njia ya utumishiwake. 20 Waliposikia hayo, walimtukuzaMungu. Kisha wakamwambia Paulo, “Ndugu,unaweza kuona kwamba kuna maelfu yaWayahudi ambao sasa wamekuwa waumini nawote hao wanashika kwa makini Sheria yaMose. 21 Wamepata habari zako kwambaumekuwa ukiwafundisha Wayahudi wanaoishikati ya mataifa mengine kuwa wasiijali Sheriaya Mose, wasiwatahiri watoto wao na kwambawasizifuate mila za Wayahudi. 22 Sasa, mamboyatakuwaje? Ni dhahiri kuwa watapata habarikwamba umekwisha wasili hapa. 23 Basi, fanyakama tunavyokushauri. Tunao hapa watuwanne ambao wameweka nadhiri. 24 Jiungenao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na

gharama zinazohusika, kisha wanyolewenywele zao. Hivyo watu wote watatambuakwamba habari zile walizoambiwa juu yakohazina msingi wowote, na kwamba wewebinafsi bado unaishi kufuatana na maagizo yaSheria za Mose. 25 Kuhusu wale watu wamataifa mengine ambao wamekuwa waumini,tumekwisha wapelekea barua tukiwaambiamambo tuliyoamua: wasile chochotekilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywedamu, wasile nyama ya mnyamaaliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.” 26

Basi, kesho yake Paulo aliwachukua wale watuakafanya ibada ya kujitakasa pamoja nao.Kisha akaingia Hekaluni kutoa taarifa kuhusumwisho wa siku za kujitakasa na kuhusudhabihu itakayotolewa kwa ajili ya kila mmojawao. 27 Wakati siku hizo saba zilipokaribiakuisha, Wayahudi waliokuwa wametoka katikamkoa wa Asia walimwona Paulo Hekaluni.Wakachochea hasira kati ya kundi lote la watu,wakamtia nguvuni 28 wakipiga kelele:“Wananchi wa Israeli, msaada, msaada! Huyundiye yule mtu anayewafundisha watu kilamahali mambo yanayopinga watu wa Israeli,yanayopinga Sheria ya Mose na mahali hapapatakatifu. Hata sasa amewaingiza watu wamataifa mengine Hekaluni na kupatia najisimahali hapa patakatifu.” 29 Sababu ya kusemahivyo ni kwamba walikuwa wamemwonaTrofimo mwenyeji, wa Efeso, akiwa pamoja naPaulo mjini, wakadhani kwamba Paulo alikuwaamemwingiza Hekaluni. 30 Mji wote ulieneaghasia; watu wakaja kutoka pande zote,wakamkamata Paulo, wakamburuta,wakamtoa nje ya Hekalu na papo hapomilango ya Hekalu ikafungwa. 31 Walikuwatayari kumuua, lakini habari zilimfikia mkuu wajeshi la Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwaimejaa ghasia. 32 Mara, mkuu wa jeshiakawachukua askari na jemadari, akalikabili lilekundi la watu. Nao walipomwona mkuu wajeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo. 33

Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtianguvuni na kuamuru afungwe minyororomiwili. Kisha akauliza, “Ni mtu gani huyu, naamefanya nini?” 34 Wengine katika lile kundi lawatu walikuwa wanapayuka kitu hiki nawengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasiahiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisakamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampelekePaulo ndani ya ngome. 35 Paulo alipofikakwenye ngazi, askari walilazimika kumbebakwa sababu ya fujo za watu. 36 Kwa maanakundi kubwa la watu walimfuata wakipigakelele, “Muulie mbali!” 37 Walipokuwawanamwingiza ndani ya ngome, Pauloalimwomba mkuu wa jeshi akisema, “Nawezakukwambia kitu?” Yule mkuu wa jeshiakamjibu, “Je unajua Kigiriki? 38 Kwani wewe siyule Mmisri ambaye hivi majuzi alianzisha uasina kuwaongoza majahili elfu nne hadijangwani?” 39 Paulo akajibu, “Mimi ni Myahudi,

MATENDO YA MITUME 21:4

108

Page 109: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

22

23

mzaliwa wa Tarso katika Kilikia; mimi ni raia wamji maarufu. Tafadhali, niruhusu niongee nawatu. 40 Yule mkuu wa jeshi akamruhusu.Hivyo Paulo alisimama juu ya ngazi,akawapungia mkono wale watu na walipokaakimya, akaanza kuongea nao kwa Kiebrania.

“Ndugu zangu na akina baba,nisikilizeni sasa nikijitetea mbeleyenu!” 2 Waliposikia akiongea nao

kwa Kiebrania wakazidi kukaa kimya zaidikuliko hapo awali. Naye Paulo akaendeleakusema, 3 “Mimi ni Myahudi, mzaliwa waTarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapamjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli.Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti Sheria yawazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwaMungu kama ninyi wenyewe mlivyo hivi leo. 4

Niliwatesa hata kuwaua wale watu waliofuataNjia hii. Niliwatia nguvuni wanaume kwawanawake na kuwafunga gerezani. 5 KuhaniMkuu na baraza lote la wazee wanawezakushuhudia jambo hilo. Kutoka kwao nilipokeabarua walioandikiwa wale ndugu Wayahudiwaliokuwa huko Damasko. NilikwendaDamasko ili niwatie nguvuni watu hao nakuwaleta wamefungwa mpaka Yerusalemu iliwaadhibiwe. 6 “Basi, nilipokuwa njiani karibukufika Damasko, yapata saa sita mchana,mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokeaghafla ukaniangazia pande zote. 7 Haponilianguka chini, nikasikia sauti ikiniambia:Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? 8 Naminikauliza: Nani wewe, Bwana? Nayeakaniambia: Mimi ni Yesu wa Nazareti ambayewewe unamtesa. 9 Wale wenzangu waliuonaule mwanga lakini hawakusikia sauti ya yulealiyeongea nami. 10 Basi, mimi nikauliza:Nifanye nini Bwana? Naye Bwana akaniambia:Simama, nenda Damasko na huko utaambiwayote ambayo umepangiwa kufanya. 11

Kutokana na ule mwanga mkali sikuwezakuona na hivyo iliwabidi wale wenzangukuniongoza kwa kunishika mkono mpakanikafika Damasko. 12 “Huko kulikuwa na mtummoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu,mwenye kuitii Sheria yetu na aliyeheshimikasana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishiDamasko. 13 Yeye alikuja kuniona, akasimamakaribu nami, akasema: Ndugu Saulo! Ona tena.Papo hapo nikaona tena, nikamwangalia. 14

Halafu Anania akasema: Mungu wa babu zetuamekuchagua upate kujua matakwa yake nakumwona yule mtumishi wake mwadilifu nakumsikia yeye mwenyewe akiongea. 15 Kwamaana utamshuhudia kwa watu woteukiwaambia yale uliyoyaona na kuyasikia. 16

Sasa basi, ya nini kukawia zaidi? Simamaubatizwe na uondolewe dhambi zako kwakuliungama jina lake. 17 “Basi, nilirudiYerusalemu, na nilipokuwa nikisali Hekaluni,niliona maono. 18 Nilimwona Bwanaakiniambia: Haraka! Ondoka Yerusalemu upesikwa maana watu wa hapa binadamu

hawataukubali ushuhuda wako juu yangu. 19

Nami nikamjibu: Bwana, wao wanajua wazikwamba mimi ni yule aliyekuwa anapitapitakatika masunagogi na kuwatia nguvuni nakuwapiga wale waliokuwa wanakuamini. 20 Nakwamba wakati shahidi wako Stefanoalipouawa, mimi binafsi nilikuwako palenikakubaliana na kitendo hicho na kuyalindamakoti ya wale waliokuwa wanamuua. 21 NayeBwana akaniambia: Nenda; ninakutuma mbalikwa mataifa mengine.” 22 Mpaka hapa, walewatu walikuwa wanamsikiza, lakini aliposemamaneno haya, walianza kusema kwa sautikubwa, “Mwondoe duniani! Mtu wa namnahiyo hastahili kuishi.” 23 Waliendeleakupayukapayuka huku wakitikisa makoti yaona kurusha vumbi angani. 24 Mkuu wa jeshialiwaamuru watu wake wampeleke Paulondani ya ngome, akawaambia wamchapeviboko ili wapate kujua kisa cha Wayahudikumpigia kelele. 25 Lakini walipokwishamfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwulizajemadari mmoja aliyesimama hapo, “Je, nihalali kwenu kumpiga viboko raia wa Romakabla hajahukumiwa?” 26 Yule jemadarialiposikia hayo, alimpasha habari mkuu wajeshi akisema, “Unataka kufanya nini? Mtuhuyu ni raia wa Roma!” 27 Basi, mkuu wa jeshialimwendea Paulo, akamwambia, “Niambie; je,wewe ni raia wa Roma?” Paulo akamjibu,“Naam.” 28 Mkuu wa jeshi akasema, “Miminami nimekuwa raia wa Roma kwa kulipagharama kubwa.” Paulo akasema, “Lakini mimini raia wa Roma kwa kuzaliwa.” 29 Wale watuambao walikuwa tayari kumchunguza Paulowalitoweka mara. Hata yule mkuu wa jeshialiogopa alipojua kwamba Paulo ni raia waRoma na kwamba alikuwa amekwisha mfungaminyororo. 30 Kesho yake, mkuu wa jeshialitaka kujua mashtaka kamili ambayoWayahudi walikuwa wamemwekea Paulo.Hivyo, alimfungua Paulo minyororo, akaamurumakuhani wakuu na Baraza lote wafanyekikao. Kisha alimleta Paulo, akamsimamishambele ya Baraza.

Paulo aliwakodolea macho walewanabaraza, halafu akaanza kusema,“Ndugu zangu, mpaka hivi leo

nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele yaMungu.” 2 Hapo Kuhani Mkuu Ananiaakaamuru wale waliokuwa wamesimamakaribu na Paulo wampige kofi mdomoni. 3

Basi, Paulo akamwambia, “Mungu mwenyeweatakupiga kofi wewe uliye kama ukutauliopakwa chokaa! Unawezaje kukaa hapo iliunihukumu kisheria na huku wewe mwenyeweunaivunja Sheria kwa kuamuru nipigwe?” 4

Watu waliokuwa wamesimama palewakamwambia Paulo, “Unamtukana KuhaniMkuu wa Mungu!” 5 Paulo akajibu, “Nduguzangu, sikujua kama yeye ni Kuhani Mkuu.Maana Maandiko yasema hivi: Usiseme vibayajuu ya mtawala wa watu wako.” 6 Wakati huo

MATENDO YA MITUME 23:6

109

Page 110: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

24

Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu mojaya wanabaraza wale ilikuwa ni Masadukayo nanyingine Mafarisayo. Basi, alipaaza sauti yakembele ya Baraza: “Ndugu zangu, mimi niMfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Miminimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumainikwamba wafu watafufuka.” 7 Baada yakusema hivyo, mzozo mkali ulitokea kati yaMafarisayo na Masadukayo na mkutanoukagawanyika sehemu mbili. 8 Kisa chenyewekilikuwa hiki: Masadukayo hushikilia kwambawafu hawafufuki, hakuna malaika, na rohonazo hazipo. Lakini Mafarisayo husadiki hayoyote matatu. 9 Kelele ziliongezeka na baadhiya walimu wa Sheria wa kikundi chaMafarisayo walisimama na kutoa malalamikoyao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilichokiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwambaroho au malaika ameongea naye.” 10 Mzozoulizidi kuwa mwingi hata mkuu wa jeshiakaogopa kwamba Paulo angeraruliwavipandevipande. Kwa hiyo, aliwaamuru askariwake kuingia kati ya lile kundi, wamtoe Paulona kumrudisha ndani ya ngome. 11 Usikuuliofuata, Bwana alisimama karibu na Paulo,akamwambia, “Jipe moyo! Umenishuhudiakatika Yerusalemu, utafanya vivyo hivyo mjiniRoma.” 12 Kulipokucha, Wayahudi walifanyakikao cha faragha. Wakala kiapo: “Hatutakulawala kunywa mpaka tutakapokuwatumekwisha muua Paulo.” 13 Watu zaidi yaarobaini ndio waliokula njama kufanya hivyo.14 Basi, walikwenda kwa makuhani wakuu nawazee, wakasema, “Sisi tumeapa kwambahatutaonja chochote kwa vinywa vyetu mpakahapo tutakapokuwa tumemuua Paulo. 15 Sasabasi, ninyi pamoja na Baraza tumeni ujumbekwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenumkijisingizia kwamba mnataka kupata habarikamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumuua hatakabla hajafika karibu.” 16 Lakini mtoto wakiume wa dada yake Paulo alisikia juu yampango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome,akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo. 17 HapoPaulo akamwita mmoja wa askari,akamwambia, “Mchukue kijana huyu kwamkuu wa jeshi; ana kitu cha kumwambia.” 18

Askari akamchukua huyo kijana,akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi,akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniitaakaniomba nimlete kijana huyu kwako kwamaana ana jambo la kukwambia.” 19 Mkuu wajeshi alimshika huyo kijana mkono,akampeleka mahali pa faragha, akamwuliza,“Una nini cha kuniambia?” 20 Yeye akasema,“Wayahudi wamepatana wakuombe umpelekePaulo Barazani wakijisingizia kwamba Barazalingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.21 Lakini wewe usikubali kwa maana kunawatu zaidi ya arobaini walio tayari kumvamia.Wameapa kutokula wala kunywa mpakawatakapokuwa wamemuua. Sasa wako tayari,wanangojea tu uamuzi wako.” 22 Mkuu wa

jeshi alimwacha aende zake akimwonyaasimwambie mtu yeyote kwamba amemleteahabari hizo. 23 Basi, mkuu wa jeshi aliwaitaaskari wawili akawaambia, “Wekeni tayariaskari mia mbili, wapanda farasi sabini naaskari mia mbili wa mikuki, waende Kaisarea;muwe tayari kuondoka kabla ya saa tatu leousiku. 24 Wekeni farasi kadhaa kwa ajili yaPaulo; mfikisheni salama kwa Felisi, mkuu wamkoa.” 25 Halafu mkuu huyo wa jeshiakaandika barua hivi: 26 “Mimi Klaudio Lusianinakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuuwa mkoa. Salamu! 27 “Wayahudi walimkamatamtu huyu na karibu wangemuua kamanisingalifahamishwa kwamba yeye ni raia waRoma na hivyo nikaenda pamoja na askarinikamwokoa. 28 Nilimpeleka mbele ya Barazalao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao.29 Niligundua kwamba mashtaka yenyeweyalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadhaza Sheria yao na hivyo sikuona kwambaamefanya chochote kinachostahili auawe auafungwe gerezani. 30 Nilipofahamishwakwamba Wayahudi walikuwa wamefanyanjama za kumuua, niliamua kumleta kwako.Nikamwambia washtaki wake walete mashtakayao mbele yako.” 31 Basi, hao askariwalimchukua Paulo kama walivyoamriwa;wakampeleka usiku uleule mpaka Antipatri. 32

Kesho yake askari wa miguu walirudi ngomeni,wakawaacha wale askari wapanda farasiwaendelee na safari pamoja na Paulo. 33

Walipofika Kaisarea walimpa mkuu wa mkoaile barua na kumweka Paulo chini ya mamlakayake. 34 Felisi alipoisoma hiyo barua aliwaulizaPaulo ametoka mkoa gani. Alipofahamishwakwamba alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia, 35

akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada yawashtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Pauloawekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi waHerode.

Baada ya siku tano, Kuhani MkuuAnania aliwasili Kaisarea pamoja nawazee kadhaa na wakili mmoja wa

sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yulemkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yaojuu ya Paulo. 2 Paulo aliitwa na Tertuloakafungua mashtaka hivi: “Mheshimiwa Felisi,uongozi wako bora umeleta amani kubwa namarekebisho ya lazima yanafanywa kwamanufaa ya taifa letu. 3 Tunalipokea jambo hilikwa furaha daima na kutoa shukrani nyingikwako kila mahali. 4 Lakini, bila kupotezawakati wako zaidi, tunakusihi kwa wema wako,usikilize taarifa yetu fupi. 5 Tumegunduakwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeyehuanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahaliduniani na pia ni kiongozi wa kile chama chaWanazareti. 6 Tena alijaribu kulikufuru Hekalunasi tukamtia nguvuni. Kama ukimhoji wewemwenyewe, utaweza kubainisha mambo hayayote tunayomshtaki kwayo.” Tulitakakumhukumu kufuatana na Sheria yetu. 7

MATENDO YA MITUME 23:7

110

Page 111: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

25

Lakini Lusia, mkuu wa jeshi, aliingilia kati,akamchukua kwa nguvu kutoka mikononimwetu. 8 Kisha akaamuru washtaki wake wajembele yako. 9 Nao Wayahudi waliunga mkonomashtaka hayo wakisema kwamba hayo yoteyalikuwa kweli. 10 Basi, mkuu wa mkoaalimwashiria Paulo aseme. Naye Pauloakasema, “Nafurahi kujitetea mbele yakonikijua kwamba umekuwa hakimu wa taifa hilikwa miaka mingi. 11 Unaweza kujihakikishiakwamba si zaidi ya siku kumi na mbili tuzimepita tangu nilipokwenda kuabuduYerusalemu. 12 Wayahudi hawakunikutanikijadiliana na mtu yeyote. Hawakunikutanikichochea watu Hekaluni wala katikamasunagogi yao, wala mahali pengine popotekatika mji huo. 13 Wala hawawezi kuthibitishamashtaka waliyotoa juu yangu. 14

Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimininamwabudu Mungu na wazee wetu nikiishikufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiitachama cha uzushi. Ninaamini mambo yoteyaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria namanabii. 15 Mimi namtumainia Mungu, nawao wanalo tumaini hilo, kwamba watu, wemana wabaya, watafufuka. 16 Kwa hiyoninajitahidi daima kuwa na dhamiri njemambele ya Mungu na mbele ya watu. 17 “Baadaya kukaa mbali kwa miaka kadhaa, nilirudiYerusalemu ili kuwapelekea wananchiwenzangu msaada na kutoa dhabihu. 18

Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipowaliponikuta Hekaluni, nilipokuwa nimekwishafanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwakokundi la watu wala ghasia. 19 Lakini kulikuwana Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia;hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yakona kutoa mashtaka yao kama wana chochotecha kusema dhidi yangu. 20 Au, waache hawawalio hapa waseme kosa waliloliona kwanguwakati niliposimama mbele ya Baraza lao kuu,21 isipokuwa tu maneno haya niliyosemaniliposimama mbele yao: Mnanihukumu leo hiikwa sababu ya kushikilia kwamba wafuwatafufuliwa!” 22 Hapo, Felisi, ambayemwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo Njiavizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia,“Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Luisa,mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.” 23 Kishaakamwamuru yule jemadari amweke Paulokizuizini, lakini awe na uhuru kiasi, na rafikizake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake. 24

Baada ya siku chache, Felisi alifika pamoja namkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi.Aliamuru Paulo aletwe, akamsikiliza akiongeajuu ya kumwamini Yesu Kristo. 25 Lakini wakatiPaulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu, juu yakuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumuinayokuja, Felisi aliogopa, akasema, “Kwa sasaunaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopatanafasi.” 26 Wakati huohuo alikuwa anatumainikwamba Paulo angempa fedha. Kwa sababuhii alimwita Paulo mara kwa mara na

kuzungumza naye. 27 Baada ya miaka miwili,Porkio Festo alichukua nafasi ya Felisi, akawamkuu wa Mkoa. Kwa kuwa alitakakujipendekeza kwa Wayahudi, Felisi alimwachaPaulo kizuizini.

Siku tatu baada ya kufika mkoani,Festo alitoka Kaisarea, akaendaYerusalemu. 2 Makuhani wakuu

pamoja na viongozi wa Wayahudi walimpahabari kuhusu mashtaka yaliyokuwayanamkabili Paulo. Walimsihi Festo 3

awafanyie fadhili kwa kumleta PauloYerusalemu; walikuwa wamekula njamawamuue akiwa njiani. 4 Lakini Festo alijibu,“Paulo atabaki kizuizini kule Kaisarea na miminitakwenda huko karibuni. 5 Waacheniviongozi wenu waende huko pamoja namiwakatoe mashtaka yao juu yake kamaamefanya chochote kiovu.” 6 Festo alikaa naokwa muda wa siku nane au kumi hivi, kishaakarudi Kaisarea. Kesho yake alikwendabarazani, akaamuru Paulo aletwe ndani. 7

Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwawametoka Yerusalemu walimzungukawakaanza kutoa mashtaka mengimazitomazito ambayo hawakuwezakuthibitisha. 8 Kwa kujitetea, Paulo alisema,“Mimi sikufanya kosa lolote kuhusu Sheria yaWayahudi, wala kuhusu Hekalu, wala kumhusuKaisari.” 9 Festo alitaka kujipendekeza kwaWayahudi na hivyo akamwuliza Paulo, “Je,ungependa kwenda Yerusalemu na hukoukahukumiwe mbele yangu kuhusu mashtakahaya?” 10 Paulo akajibu, “Nasimama mbele yamahakama ya Kaisari na papa hapa ndiponinapopaswa kupewa hukumu. Kamaunavyojua vizuri, sikuwatendea Wayahudiubaya wowote. 11 Basi, ikiwa nimepatikana nakosa linalostahili adhabu ya kifo, siombikusamehewa adhabu hiyo. Lakini kamahakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watuhawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao.Nakata rufani kwa Kaisari!” 12 Basi, baada yaFesto kuzungumza na washauri wake,akamwambia Paulo, “Umekata rufani kwaKaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari.” 13 Sikuchache baadaye, mfalme Agripa na Bernikewalifika Kaisarea ili kutoa heshima zao kwaFesto. 14 Walikuwa huko siku kadhaa nayeFesto akamweleza mfalme kesi ya Paulo: “Kunamtu mmoja hapa ambaye Felisi alimwachakizuizini. 15 Nilipokwenda Yerusalemumakuhani wakuu na wazee wa Wayahudiwalimshtaki na kuniomba nimhukumu. 16

Lakini mimi niliwajibu kwamba si desturi yaWaroma kumtoa mtu aadhibiwe kablamshtakiwa hajakutana na washtaki wake anakwa ana na kupewa fursa ya kujitetea kuhusuhayo mashtaka. 17 Basi, walipofika hapasikukawia, ila nilifanya kikao mahakamanikesho yake, nikaamuru mtu huyo aletwe. 18

Washtaki wake walisimama lakini hawakutoamashtaka maovu kama nilivyokuwa

MATENDO YA MITUME 25:18

111

Page 112: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

26

ninatazamia. 19 Ila tu walikuwa na mabishanokadhaa pamoja naye kuhusu dini yao nakuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambayealikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.20 Sikujua la kufanya kuhusu shauri hilo. Basi,nilimwuliza Paulo kama angependa kwendamahakamani kule Yerusalemu kwa ajili yamashtaka hayo. 21 Lakini Paulo alikata rufani,akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi washauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyoniliamua akae kizuizini mpaka nitakapowezakumpeleka kwa Kaisari.” 22 Basi Agripaakamwambia Festo, “Ningependa kumsikiamtu huyu mimi mwenyewe.” Festoakamwambia, “Utamsikia kesho.” 23 Hivyo,kesho yake, Agripa na Bernike walifika kwashangwe katika ukumbi wa mkutano wakiwawameandamana na wakuu wa majeshi naviongozi wa mji. Festo aliamuru Paulo aletwendani, 24 Kisha akasema, “Mfalme Agripa nawote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbeleyenu yuko mtu ambaye jumuiya yote yaWayahudi hapa na kule Yerusalemuwalinilalamikia wakipiga kelele kwambahastahili kuishi tena. 25 Lakini mimi sikuonakuwa alikuwa ametenda chochote kibaya hataastahili kupewa adhabu ya kifo. Lakini, kwa vilePaulo mwenyewe alikata rufani kwa Kaisari,niliamua kumpeleka. 26 Kwa upande wangusina habari kamili ambayo nawezakumwandikia Kaisari juu yake. Ndiyo maananimemleta hapa mbele yenu na mbele yakomfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza,niweze kuwa na la kuandika. 27 Kwa maananadhani itakuwa kichekesho kumpelekamfungwa bila kutaja wazi mashtakayanayomkabili.”

Basi, Agripa akamwambia Paulo,“Unaruhusiwa kujitetea.” Hapo Pauloalinyosha mkono wake akajitetea hivi:

2 “Mfalme Agripa, ninajiona mwenye bahatileo kujitetea mbele yako kuhusu yalemashtaka yote ambayo Wayahudi walikuwawamesema juu yangu. 3 Hasa kwa vile wewemwenyewe ni mtaalamu wa desturi zaWayahudi na migogoro yao, ninakuomba basiunisikilize kwa uvumilivu. 4 “Wayahudiwanajua habari za maisha yangu tangu utoto,jinsi nilivyoishi tangu mwanzo kati ya taifalangu huko Yerusalemu. 5 Wananifahamu kwamuda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kamawakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishikama mmoja wa kikundi chenye siasa kali zaidikatika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.6 Na sasa niko hapa nihukumiwe kwa sababuninaitumainia ile ahadi ambayo Mungualiwaahidia babu zetu. 7 Ahadi hiyo ndiyo ileileinayotumainiwa na makabila kumi na mawiliya taifa letu, wakimtumikia Mungu kwa dhatimchana na usiku. Mheshimiwa mfalme,Wayahudi wananishtaki kwa sababu yatumaini hilo! 8 Kwa nini ninyi mnaona shidasana kuamini kwamba Mungu huwafufua

wafu? 9 Kwa kweli mimi mwenyewe niliaminikwamba ni wajibu wangu kufanya mambomengi kulipinga jina la Yesu wa Nazareti. 10

Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya hukoYerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewamamlaka kutoka kwa makuhani wakuu,nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu waMungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipigakura ya kukubali. 11 Mara nyingi niliwafanyawaadhibiwe katika masunagogi yotenikiwashurutisha waikane imani yao. Hasirayangu kwao ilikuwa kubwa hata nikawasakampaka miji ya mbali. 12 “Kwa mujibu huohuo,nilikwenda Damasko wakati mmoja, nikiwa namamlaka na maagizo kutoka kwa makuhaniwakuu. 13 Mheshimiwa, wakati nilipokuwanjiani, saa sita mchana, niliona mwangamkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutokambinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiriwenzangu. 14 Sisi sote tulianguka chini, naminikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: Saulo,Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza burekama punda anayepiga teke fimbo ya bwanawake. 15 Mimi nikauliza: Ni nani wewe Bwana?Naye Bwana akajibu: Mimi ni Yesu ambayewewe unamtesa. 16 Haidhuru, inuka sasa;simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmikuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watuwengine mambo uliyoyaona leo na yaleambayo bado nitakuonyesha. 17 Nitakuokoana watu wa Israeli na watu wa mataifamengine ambao mimi ninakutuma kwao. 18

Utayafumbua macho yao na kuwawezeshawatoke gizani na kuingia katika mwanga;watoke katika utawala wa Shetani, wamgeukieMungu; ili kwa kuamini, wapate kusamehewadhambi na kuchukua nafasi yao kati ya waleambao wamepata kuwa watu wa Mungu. 19

“Hivyo, mfalme Agripa, sikuweza kuwa mkaidikwa maono hilo la mbinguni. 20 Ila nilianzakuhubiri kwanza kwa watu wa Damasko,halafu kwa wale wa Yerusalemu na nchi yoteya Yudea, na pia kwa watu wa mataifamengine. Niliwahimiza wamgeukie Mungu nakuonyesha kwa vitendo kwambawamebadilisha mioyo yao. 21 Kwa sababuhiyo, Wayahudi walinikamata nikiwa Hekaluni,wakajaribu kuniua. 22 Lakini Mungualinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leonimesimama imara nikitoa ushuhuda kwawote, wakubwa na wadogo. Ninayosema niyale ambayo manabii na Mose walisemayatatukia; 23 yaani ilimpasa Kristo ateseke nakuwa wa kwanza kufufuka kutoka wafu, iliatangaze kwamba mwanga wa ukomboziunawaangazia sasa watu wote, Wayahudi napia watu wa mataifa mengine.” 24 Pauloalipofika hapa katika kujitetea kwake, Festoalisema kwa sauti kubwa, “Paulo! Una wazimu!Kusoma kwako kwingi kunakutia wazimu!” 25

Lakini Paulo akasema, “Sina wazimumheshimiwa Festo: Ninachosema ni ukwelimtupu. 26 Wewe Mfalme unayafahamu

MATENDO YA MITUME 25:19

112

Page 113: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

27

mambo haya, kwa hiyo ninaweza kuongea bilauoga mbele yako. Sina mashaka kwambamatukio hayo yanajulikana kwako maanajambo hili halikutendeka mafichoni. 27 MfalmeAgripa, je, una imani na manabii? Najuakwamba unaamini.” 28 Agripa akamjibu Paulo,“Kidogo tu utanifanya Mkristo!” 29 Pauloakamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwamuda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wotewanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyomimi, lakini bila hii minyororo.” 30 Hapomfalme Agripa, mkuu wa mkoa, Bernike nawale wote waliokuwa pamoja nao,walisimama. 31 Walipokwisha ondoka,waliambiana, “Mtu huyu hakufanya chochotekinachostahili adhabu ya kifo au kifungo.” 32

Naye Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyuangeweza kufunguliwa kama asingalikuwaamekata rufani kwa Kaisari.”

Walipokwisha amua tusafiri mpakaItalia, walimweka Paulo pamoja nawafungwa wengine chini ya ulinzi wa

Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosikiitwacho “Kikosi cha Augusto.” 2 Tulipandameli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitiabandari kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanzasafari. Aristarko, mwenyeji wa Makedoniakutoka Thesalonika, alikuwa pamoja nasi. 3

Kesho yake tulitia nanga katika bandari yaSidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwakumruhusu awaone rafiki zake na kupatamahitaji yake. 4 Kutoka huko tuliendelea nasafari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwaunavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitiaupande wa kisiwa cha Kupro ambapo upepohaukuwa mwingi. 5 Halafu tulivuka bahari yaKilikia na Pamfulia, tukatia nanga Mura, mji waLukia. 6 Hapo yule ofisa alikuta meli moja yaAleksandria iliyokuwa inakwenda Italia, nahivyo akatupandisha ndani. 7 Kwa muda wasiku nyingi tulisafiri polepole, na kwa shidatulifika karibu na Nido. Kwa sababu upepoulikuwa bado unatupinga, tuliendelea mbelemoja kwa moja tukapitia upande wa Kretekaribu na rasi Salmone ambapo upepohaukuwa mwingi. 8 Tulipita kando yakepolepole tukafika mahali paitwapo “BandariNzuri”, karibu na mji wa Lasea. 9 Muda mrefuulikuwa umepita, na hata siku ya kufungailikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatarisana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapaonyo: 10 “Waheshimiwa, nahisi kwamba safarihii itakuwa ya shida na hasara nyingi si kwashehena na meli tu, bali pia kwa maisha yetu.”11 Lakini yule ofisa alivutiwa zaidi na maoni yanahodha na ya mwenye meli kuliko yalealiyosema Paulo. 12 Kwa kuwa bandari hiyohaikuwa mahali pazuri pa kukaa wakati wabaridi, wengi walipendelea kuendelea nasafari, ikiwezekana mpaka Foinike. Foinike nibandari ya Krete inayoelekea kusini-magharibina kaskazini-magharibi; na huko wangewezakukaa wakati wa baridi. 13 Basi, upepo mzuri

wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhaniwamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang'oananga, wakaiendesha meli karibu sana napwani ya Krete. 14 Lakini haukupita muda,upepo mkali uitwao “Upepo wa Kaskazi”ulianza kuvuma kutoka kisiwani. 15 Upepouliipiga ile meli, na kwa kuwa hatukuwezakuukabili, tukaiacha ikokotwe na huo upepo.16 Kisiwa kimoja kiitwacho Kanda kilitukingakidogo na ule upepo; na tulipopita kusinimwake tulifaulu, ingawa kwa shida,kuusalimisha ule mtumbwi wa meli. 17 Walewanamaji waliuvuta mtumbwi ndani, kishawakaizungushia meli kamba na kuifunga kwanguvu. Waliogopa kwamba wangewezakukwama kwenye ufuko wa bahari, pwani yaLibya. Kwa hiyo walishusha matanga nakuiacha meli ikokotwe na upepo. 18 Dhorubailiendelea kuvuma na kesho yake wakaanzakutupa nje shehena ya meli. 19 Siku ya tatu,wakaanza pia kutupa majini vifaa vya meli kwamikono yao wenyewe. 20 Kwa muda wa sikunyingi hatukuweza kuona jua wala nyota;dhoruba iliendelea kuvuma sana, hatamatumaini yote ya kuokoka yakatuishia. 21

Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula,Paulo alisimama kati yao, akasema,“Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kamamngalinisikiliza na kuacha kusafiri kutokaKrete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepukashida hii na hasara hizi zote. 22 Lakini sasaninawaombeni muwe na moyo; hakuna hatammoja wenu atakayepoteza maisha yake; melitu ndiyo itakayopotea. 23 Kwa maana janausiku malaika wa yule Mungu ambaye mimi niwake na ambaye mimi ninamwabudualinitokea, 24 akaniambia: Paulo usiogope! Nilazima utasimama mbele ya Kaisari; nayeMungu, kwa wema wake, amekufadhili kwakuwaokoa wote wanaosafiri nawewasiangamie. 25 Hivyo, waheshimiwa, jipenimoyo! Maana ninamwamini Mungu kwambaitakuwa sawa kama nilivyoambiwa. 26 Lakini nilazima tutatupwa ufukoni mwa kisiwa fulani.”27 Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwatunakokotwa huku na huku katika bahari yaAdria. Karibu na usiku wa manane wanamajiwalijihisi kuwa karibu na nchi kavu. 28 Hivyowalitafuta kina cha bahari kwa kuteremshakamba iliyokuwa imefungiwa kitu kizito,wakapata kina cha mita arobaini. Baadayewakapima tena wakapata mita thelathini. 29

Kwa sababu ya kuogopa kukwama kwenyemiamba, waliteremsha nanga nne nyuma yameli; wakaomba kuche upesi. 30 Wanamajiwalitaka kutoroka, na walikwisha kuteremshaule mtumbwi majini, wakijisingizia kwambawanakwenda kuteremsha nanga upande wambele wa meli. 31 Lakini Paulo alimwambiayule ofisa wa jeshi na askari wake, “Kamawanamaji hawa hawabaki ndani ya meli,hamtaokoka.” 32 Hapo wale askari walizikatakamba zilizokuwa zimeshikilia ule mtumbwi,

MATENDO YA MITUME 27:32

113

Page 114: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

28

wakauacha uchukuliwe na maji. 33 Karibu naalfajiri, Paulo aliwahimiza wote wale chakula:“Kwa siku kumi na nne sasa mmekuwa katikamashaka na bila kula; hamjala kitu chochote.34 Basi, ninawasihi mle chakula kwa maanamnakihitaji ili mweze kuendelea kuishi. Maanahata unywele mmoja wa vichwa vyenuhautapotea.” 35 Baada ya kusema hivyo, Pauloalichukua mkate, akamshukuru Mungu mbeleyao wote, akaumega, akaanza kula. 36 Hapowote wakapata moyo, nao pia wakala chakula.37 Jumla tulikuwa watu mia mbili na sabini nasita katika meli. 38 Baada ya kila mmoja kulachakula cha kutosha, walipunguza uzito wameli kwa kutupa nafaka baharini. 39

Kulipokucha, wanamaji hawakuwezakuitambua nchi ile, ila waliona ghuba mojayenye ufuko; wakaamua kutia nanga hukokama ikiwezekana. 40 Hivyo walikata nanga nakuziacha baharini, na wakati huohuowakazifungua kamba zilizokuwa zimeufungausukani, kisha wakatweka tanga moja mbelekushika upepo, wakaelekea ufukoni. 41 Lakiniwalifika mahali ambapo mikondo miwili yabahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemuya mbele ilikuwa imezama mchangani bilakutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianzakuvunjika vipandevipande kwa mapigo yanguvu ya mawimbi. 42 Askari walitaka kuwauawafungwa wote kwa kuogopa kwambawangeogelea hadi pwani na kutoroka. 43

Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitakakumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo.Aliamuru wale waliojua kuogelea warukekutoka melini na kuogelea hadi pwani, 44 nawengine wafuate wakijishikilia kwenye mbaoau kwenye vipande vya meli iliyovunjika.Ndivyo sisi sote tulivyofika salama pwani.

Tulipokwisha fika salama kwenye nchikavu, tuligundua kwamba kile kisiwakinaitwa Malta. 2 Wenyeji wa hapo

walikuwa wema sana kwetu. Mvua ilikuwainaanza kunyesha na kulikuwa na baridi, hivyowaliwasha moto, wakatukaribisha. 3 Pauloaliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitiamotoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto,nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulomkononi na kujishikilia hapo. 4 Wenyeji wapale walipokiona kile kiumbe kinaning'iniakwenye mkono wake waliambiana, “Bila shakamtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawaameokoka kuangamia baharini, Hakihaitamwacha aendelee kuishi!” 5 Lakini Pauloalikikung'utia kile kiumbe motoni nahakuumizwa hata kidogo. 6 Wale watuwalikuwa wakitazamia kwamba angevimba auhapohapo angeanguka chini na kufa. Baada yakungojea kwa muda mrefu bila kuona kwambaPaulo amepatwa na jambo lolote lisilo lakawaida, walibadilisha fikira zao juu yake,wakasema kuwa ni mungu. 7 Karibu na mahalipale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuuwa kile kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki,

tukawa wageni wake kwa siku tatu. 8 Basi,ikawa kwamba baba yake Publio alikuwaamelala kitandani, mgonjwa, ana homa nakuhara. Paulo alikwenda kumwona na baadaya kusali, akaweka mikono yake juu yamgonjwa, akamponya. 9 Kutokana na tukiohilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikujawakaponywa. 10 Watu walitupatia zawadimbalimbali na wakati tulipoanza tena safari,walitia ndani ya meli masurufu tuliyohitaji. 11

Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetukwa meli moja ya Aleksandria iitwayo “MiunguPacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwaniwakati wote wa baridi. 12 Tulifika katika mji waSirakusa, tukakaa hapo kwa siku tatu. 13 Tokahuko tuling'oa nanga, tukazunguka na kufikaRegio. Baada ya siku moja, upepo ulianzakuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbilitulifika bandari ya Potioli. 14 Huko tuliwakutandugu kadhaa ambao walituomba tukae naokwa juma moja. Hivi ndivyo tulivyopata kufikaRoma. 15 Ndugu wa kule Roma walipopatahabari zetu, wakaja kutulaki kwenye soko laApio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaonaalimshukuru Mungu, akapata moyo. 16

Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa pekeyake pamoja na askari mmoja wa kumlinda. 17

Baada ya siku tatu, Paulo aliwaita pamojaviongozi wa Kiyahudi wa mahali hapo.Walipokusanyika, Paulo aliwaambia,“Wananchi wenzangu, mimi, ingawa sikufanyachochote kibaya wala kupinga desturi zawazee wetu, nilitiwa nguvuni kule Yerusalemuna kutiwa mikononi mwa Waroma. 18

Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa nahatia yeyote, walitaka kuniacha. 19 LakiniWayahudi wengine walipinga jambo hilo, naminikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawasikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchiwenzangu. 20 Ni kwa sababu hiyo nimeombakuonana na kuongea nanyi, maananimefungwa minyororo hii kwa sababu yatumaini lile la Israeli.” 21 Wao wakamwambia,“Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea,wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa nakutoa habari rasmi au kusema chochote kibayajuu yako. 22 Lakini tunafikiri inafaa tusikiekutoka kwako mwenyewe mambo yaliyokichwani mwako. Kwa maana tujualo sisikuhusu hicho kikundi ni kwamba kinapingwakila mahali.” 23 Basi, walipanga naye sikukamili ya kukutana, na wengi wakafika hukoalikokuwa anakaa. Tangu asubuhi mpaka jioniPaulo aliwaeleza na kuwafafanulia juu yaUfalme wa Mungu akijaribu kuwafanyawakubali habari juu ya Yesu kwa kutumiaSheria ya Mose na maandiko ya manabii. 24

Baadhi yao walikubali maneno yake, lakiniwengine hawakuamini. 25 Basi, kukawa namtengano wa fikira kati yao. Walipokuwawanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili,“Kweli ni sawa yale aliyoyanena Roho Mtakatifukwa wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya 26

MATENDO YA MITUME 27:33

114

Page 115: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

akisema: Nenda kwa watu hawa ukawaambie:kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; kutazamamtatazama, lakini hamtaona. 27 Maana akili zawatu hawa zimepumbaa, wameziba masikioyao, wamefumba macho yao. La sivyo,wangeona kwa macho yao, wangesikia kwamasikio yao. Wangeelewa kwa akili zao, nakunigeukia, asema Bwana, naminingewaponya.” 28 Halafu Paulo akamaliza nakusema, “Jueni basi, kwamba ujumbe wa

Mungu juu ya wokovu umepelekwa kwa watuwa mataifa. Wao watasikiliza!” 29 Pauloalipokwisha sema hayo, Wayahudiwalijiondokea huku wakiwa wanabishana vikaliwao kwa wao. 30 Kwa muda wa miaka miwilimizima Paulo aliishi katika nyumba aliyoipangayeye mwenyewe; akawa anawakaribisha wotewaliofika kumsalimu. 31 Alikuwa akihubiriUfalme wa Mungu na kufundisha juu ya BwanaYesu Kristo kwa uhodari, bila kizuizi.

MATENDO YA MITUME 28:31

115

Page 116: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

WARUMI

Kutoka kwangu mimi Paulo, mtumishiwa Kristo Yesu, na mtume niliyeteuliwana kuitwa kwa ajili ya kuhubiri Habari

Njema ya Mungu. 2 Hapo kale, Mungualiwaahidia watu hii Habari Njema kwa njia yamanabii wake katika Maandiko Matakatifu. 3

Hii Habari Njema inamhusu Mwana waMungu, Bwana wetu Yesu Kristo, ambayemintarafu ubinadamu wake, alikuwa mzawawa Daudi; 4 mintarafu utakatifu wake wakimungu, alithibitishwa kwa uwezo mkuukwamba ni Mwana wa Mungu kwa kufufuliwakutoka wafu. 5 Kwa njia yake, mimi nimepewaneema ya kuwa mtume, ili kwa ajili yakeniwaongoze watu wa mataifa yote wapatekuamini na kutii. 6 Ninyi ni miongoni mwawatu hao; mmeitwa muwe watu wake YesuKristo. 7 Basi, ninawaandikia ninyi nyotemlioko Roma ambao Mungu anawapenda,akawateua muwe watu wake. Nawatakienineema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetuna Bwana Yesu Kristo. 8 Awali ya yote,namshukuru Mungu wangu kwa njia ya YesuKristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imaniyenu inasikika duniani kote. 9 Mungu, ambayeninamtumikia kwa moyo wangu wote katikakuhubiri Habari Njema ya Mwanae, ni shahidiwangu kwamba ninawakumbukeni 10 daimakatika sala zangu. Namwomba Munguakipenda, anipatie nafasi nzuri ya kuja kwenusasa. 11 Kwa maana ninatamani sanakuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi yakiroho na kuwaimarisha. 12 Ndiyo kusema,tutaimarishana: imani yenu itaniimarishamimi, na yangu itawaimarisha ninyi. 13 Nduguzangu, nataka mjue kwamba mara nyinginilikusudia kuwatembeleeni, lakini mpaka sasanimezuiwa. Ningependa kupata mafanikiomema kati yenu kama nilivyopata kati ya watuwa mataifa mengine. 14 Ninalo jukumu kwawatu wote, waliostaarabika nawasiostaarabika, wenye elimu na wasio naelimu. 15 Ndiyo maana ninatamani piakuihubiri Habari Njema kwenu ninyi mliokohuko Roma. 16 Sioni aibu kutangaza HabariNjema; yenyewe ni nguvu ya Munguinayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudikwanza, na wasio Wayahudi pia. 17 Kwamaana Habari Njema inaonyesha wazi jinsiMungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu;jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzompaka mwisho. Kama ilivyoandikwa:“Mwadilifu kwa imani ataishi.” 18 Ghadhabu ya

Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidiya uasi na uovu wote wa binadamu ambaokwa njia zao mbaya wanaupinga ukweliusijulikane. 19 Kwa maana, yote yanayowezakujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao; maanaMungu mwenyewe ameyadhirisha. 20 TanguMungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wamilele na uungu wake, ingawa havionekanikwa macho, vinafahamika wazi. Watuwanaweza kuyajua mambo hayo kutokana navitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyohawana njia yoyote ya kujitetea! 21 Ingawawanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshimaanayostahili, wala hawamshukuru. Badalayake, fikira zao zimekuwa batili na akili zaotupu zimejaa giza. 22 Wanajidai kuwa wenyehekima, kumbe ni wapumbavu. 23 Wanaachakumwabudu Mungu aishiye milele, na badalayake, wanaabudu sanamu zilizo mfano wabinadamu ambaye hufa, mfano wa wanyama,ndege, au wanyama watambaao. 24 Kwasababu hiyo, Mungu amewaacha wafuatetamaa mbaya za mioyo yao na kufanyianamambo ya aibu kwa miili yao. 25 Wanaubadiliukweli juu ya Mungu kwa uongo;wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala yaMuumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliyesifa milele! Amina. 26 Kwa hiyo, Munguamewaacha wafuate tamaa mbaya. Hatawanawake wanabadili matumizi yanayopatanana maumbile. 27 Nao wanaume hali kadhalika,wanaacha kufuata matumizi ya maumbile yamume na mke wakawakiana tamaa wao kwawao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu,na hivyo wanajiletea wenyewe adhabuwanayostahili kwa vitendo vyao viovu. 28 Kwavile watu walikataa kumtambua Mungu,Mungu amewaacha katika fikira zao potovu,wakafanya yale ambayo hawangestahilikufanya. 29 Wamejaa kila aina ya uovu,dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji,ugomvi, udanganyifu na nia mbaya;husengenya, 30 na kusingiziana; ni watu wakuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye kiburina majivuno; hodari sana katika kutendamabaya, na hawawatii wazazi wao; 31 hawanadhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wemawala huruma kwa wengine. 32 Wanajuakwamba Sheria ya Mungu yasema kwambawatu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo.Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanyamambo hayo wao wenyewe, bali hata

WARUMI 1:2

116

Page 117: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

2

3

huwapongeza wale wanaofanya mambohayohayo.

Basi, rafiki, kama unawahukumuwengine, huwezi kamwe kujiteteahaidhuru wewe ni nani. Kwa maana,

kwa kuwahukumu wengine, unajilaani wewemwenyewe kwa vile nawe unayafanya mamboyaleyale unayohukumu. 2 Tunajua kwambahukumu ya Mungu kwa wale wanaofanyamambo kama hayo ni hukumu ya haki. 3

Lakini wewe, rafiki, unayewahukumu walewanaofanya mambo kama hayo bali wewe piaunayafanya, je unadhani utaiepa hukumu yaMungu? 4 Au labda unaudharau wema wakemkuu, uvumilivu wake na saburi yake, bilakutambua kwamba wema wake huo unashabaha ya kukuongoza upate kutubu? 5

Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, nahivyo unajilundikia adhabu kwa Siku ileambayo ghadhabu ya Mungu na hukumu zakeza haki vitadhihirishwa. 6 Siku hiyo Munguatamlipa kila mmoja kufuatana na matendoyake. 7 Wale wanaozingatia kutenda mema,kutafuta utukufu na heshima ya Mungu nakutokufa, watapata uzima wa milele. 8 Lakiniwale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataamambo ya haki na kufuata uovu,wataangukiwa na ghadhabu na hasira yaMungu. 9 Mateso na maumivu yatampatabinadamu yeyote atendaye uovu. YatawapataWayahudi kwanza, na watu wa mataifamengine pia. 10 Lakini Mungu atawapautukufu, heshima na amani wale wanaotendamema; Wayahudi kwanza, na watu wa mataifamengine pia. 11 Maana Mungu hambagui mtuyeyote. 12 Wale wanaotenda dhambi bilakuijua Sheria ya Mose wataangamia ingawajehawajui Sheria. Na wale wanaotenda dhambiwakiwa wanaijua Sheria watahukumiwakisheria. 13 Mtu hafanywi kuwa mwadilifumbele yake Mungu kwa kuisikia Sheria, balikwa kuitii Sheria. 14 Mathalan: watu wamataifa mengine hawana Sheria ya Mose;lakini kila wanapotimiza matakwa ya Sheriawakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewewanakuwa kipimo cha Sheria ingawa hawaijuiSheria. 15 Mwenendo wao unaonyeshakwamba matakwa ya Sheria yameandikwamioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia piajambo hilo, maana fikira zao mara nyinginehuwashtaki, na mara nyingine huwatetea. 16

Hivyo, kufuatana na hii Habari Njemaninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakatiMungu atakapohukumu mambo ya siri yabinadamu kwa njia ya Yesu Kristo. 17 Na wewe,je? Wewe mwenyewe unajiita Myahudi;unaitumainia Sheria na kujivunia kuwa waMungu; 18 kwa njia ya Sheria unajua matakwaya Mungu na unaweza kuchagua jambo jema;19 wewe unajiona kuwa kiongozi wa vipofu namwanga kwa wale walio gizani; 20 unajionakuwa mkufunzi wa wajinga na mwalimu wawale wasiokomaa bado. Unayo katika Sheria

picha kamili ya elimu na ukweli. 21 Basi, weweunawafundisha wengine; kwa nini hujifundishiwewe mwenyewe? Unawahubiria wenginewasiibe, lakini kumbe wewe mwenyeweunaiba. 22 Unasema: “Msizini,” na huku weweunazini; unachukia sanamu za miungu haliwewe unajitajirisha kwa kuiba katika nyumbaza miungu. 23 Kwa kujigamba ati unayo Sheriaya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunjaSheria unamdharau Mungu? 24 Kama vileMaandiko Matakatifu yasemavyo: “Watu wamataifa mengine wamelikufuru jina la Mungukwa sababu yenu ninyi Wayahudi!” 25

Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kamaukiitii Sheria. Lakini kama unaivunja Sheria,basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa. 26

Kama mtu wa mataifa mengine ambayehakutahiriwa akitimiza matakwa ya Sheria,hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.27 Watu wa mataifa mengine watakuhukumuwewe Myahudi kama ukiivunja Sheria,ingawaje unayo maandishi ya Sheria naumetahiriwa, hali wao wanaitii Sheria ingawahawakutahiriwa. 28 Ndiyo kusema, si kilaanayeonekana kwa nje kuwa Myahudi niMyahudi wa kweli, wala mtu hawi Myahudi wakweli ati kwa kuwa ametahiriwa kimwili. 29

Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwandani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni.Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishiya Sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, sikutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.

Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watuwengine? Au kutahiriwa kuna faidagani? 2 Naam, iko faida kwa kila

upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhiWayahudi ujumbe wake. 3 Lakini itakuwajeiwapo baadhi yao hawakuwa waaminifu? Je,jambo hilo litaondoa uaminifu wa Mungu? 4

Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima,ingawaje kila binadamu ni mwongo. KamaMaandiko Matakatifu yasemavyo: “Kilausemapo, maneno yako ni ya haki; na katikahukumu, wewe hushinda.” 5 Lakini, ikiwa uovuwetu unathibitisha kwamba Mungu anatendakwa haki, tutasema nini? Je, tutasema kwambaanakosa haki akituadhibu? (Hapa naongeakibinadamu). 6 Hata kidogo! Ingekuwa hivyo,Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? 7

Labda utasema: “Ikiwa ukosefu wa uaminifukwa upande wangu unamdhihirisha Mungukuwa mwaminifu zaidi na hivyo kumpatiautukufu, basi singepaswa kuhukumiwa kuwamwenye dhambi!” 8 Ni sawa na kusema:tufanye maovu ili tupate mema! Ndivyowengine walivyotukashifu kwa kutushtakikwamba tumefundisha hivyo. Watahukumiwawanavyostahili! 9 Tuseme nini, basi? Je, sisiWayahudi ni bora zaidi kuliko wengine? Hatakidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapomwanzoni kwamba Wayahudi na watu wamataifa mengine wote wako chini ya utawalawa dhambi. 10 Kama Maandiko Matakatifu

WARUMI 3:10

117

Page 118: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

yasemavyo: “Hakuna hata mmoja aliyemwadilifu! 11 Hakuna mtu anayeelewa, walaanayemtafuta Mungu. 12 Wote wamepotokawote wamekosa; hakuna atendaye mema,hakuna hata mmoja. 13 Makoo yao ni kamakaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu,midomoni mwao mwatoka maneno yenyesumu kama ya nyoka. 14 Vinywa vyao vimejaalaana chungu. 15 Miguu yao iko mbionikumwaga damu, 16 popote waendapohusababisha maafa na mateso; 17 njia yaamani hawaijui. 18 Hawajali kabisa kumchaMungu.” 19 Tunajua kwamba Sheria huwahusuwalio chini ya Sheria hiyo, hata hawawezi kuwana kisingizio chochote, na ulimwengu woteuko chini ya hukumu ya Mungu. 20 Maanahakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwamwadilifu mbele yake Mungu kwa kuishikaSheria; kazi ya Sheria ni kumwonyesha tu mtukwamba ametenda dhambi. 21 Lakini sasa, njiaya Mungu ya kuwakubali watu kuwa waadilifuimekwisha dhihirishwa, tena bila kutegemeaSheria. Sheria na manabii hushuhudia jambohili. 22 Mungu huwakubali watu kuwawaadilifu kwa njia ya imani yao kwa YesuKristo; Mungu hufanya hivyo kwa wotewanaoamini; hakuna ubaguzi wowote. 23

Watu wote wametenda dhambi nawametindikiwa utukufu wa Mungu. 24 Lakinikwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wotehukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya YesuKristo anayewakomboa. 25 Mungu alimtoaYesu kusudi, kwa damu yake, awe njia yakuwaondolea watu dhambi zao kwa imani yaokwake. Alifanya hivyo ili apate kuonyeshakwamba yeye ni mwadilifu. Hapo zamaniMungu alikuwa mvumilivu bila kuzijali dhambiza watu; 26 lakini sasa, wakati huu, anazikabilidhambi za watu apate kuonyesha uadilifuwake. Kwa namna hiyo Mungu mwenyewehuonyesha kwamba yeye ni mwadilifu nakwamba humkubali kuwa mwadilifu mtuyeyote anayemwamini Yesu. 27 Basi, tunawezakujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwasababu ya kutimiza Sheria? La! Bali kwa sababutunaamini. 28 Maana mtu hukubaliwa kuwamwadilifu kwa imani, wala si kwa kutimizamatakwa ya Sheria. 29 Au je, Mungu nuMungu wa Wayahudi tu, ama pia wa watu wamataifa mengine? Naam, wa mataifa menginepia. 30 Mungu ni mmoja, naye atawakubaliWayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, nawatu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.31 Je, tunaitumia imani kuibatilisha Sheria?Hata kidogo; bali tunaipa Sheria thamani yakekamili.

Tuseme nini basi, juu ya Abrahamubaba yetu? 2 Kama Abrahamualikubaliwa kuwa mwadilifu kutokana

na matendo yake, basi, anacho kitu chakujivunia mbele ya Mungu. 3 Kwa maana,Maandiko Matakatifu yasema: “Abrahamualimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali

kuwa mwadilifu.” 4 Mfanyakazi hulipwamshahara; mshahara wake si zawadi bali nihaki yake. 5 Lakini mtu asiyetegemeamatendo yake mwenyewe, bali anamwaminiMungu ambaye huwasamehe waovu, basi,Mungu huijali imani ya mtu huyo, na hivihumkubali kuwa mwadilifu. 6 Naye Daudiasema hivi juu ya furaha ya mtu ambayeMungu amemkubali kuwa mwadilifu bilakuyajali matendo yake: 7 “Heri walewaliosamehewa makosa yao ambao makosayao yamefutwa. 8 Heri mtu yule ambayeBwana hataziweka dhambi zake katikakumbukumbu.” 9 Je, hiyo ni kwa walewaliotahiriwa tu, ama pia kwa walewasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia.Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamualiamini, naye Mungu akamkubali kuwamwadilifu.” 10 Je, Abrahamu alikubaliwa kablaya kutahiriwa ama baada ya kutahiriwa? Kablaya kutahiriwa, na si baada ya kutahiriwa. 11

Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwahuko kulikuwa alama iliyothibitisha kwambaMungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababuya imani yake aliyokuwa nayo kabla yakutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwababa wa wale wote ambao, ingawahawakutahiriwa, wamemwamini Mungu,wakafanywa waadilifu. 12 Vilevile yeye ni babawa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwawametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njiaileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuatakabla ya kutahiriwa. 13 Mungu alimwahidiAbrahamu na wazawa wake kwambaulimwengu ungekuwa mali yao. Ahadi hiyohaikufanywa kwa sababu Abrahamu aliitiiSheria, bali kwa kuwa aliamini, akakubaliwakuwa mwadilifu. 14 Maana kama watakaopewahayo aliyoahidi Mungu ni wale tu wanaoitiiSheria, basi, imani haina maana yoyote, nayoahadi ya Mungu si kitu. 15 Sheria husababishaghadhabu; lakini kama hakuna Sheria,haiwezekani kuivunja. 16 Kwa sababu hiyo,jambo hili lategemea imani, hivyo kwambaahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, nakwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajiliya wote: si kwa wale tu wanaoishika Sheria,bali pia kwa wale waishio kwa imani kamaAbrahamu. Yeye ni baba yetu sisi sote. 17

Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:“Nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.”Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambayeAbrahamu alimwamini—Mungu ambayehuwapa wafu uzima, na kwa amri yake, vituambavyo havikuwapo huwa. 18 Abrahamualiamini na kutumaini ingawa hali yenyeweilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwababa wa mataifa mengi kama MaandikoMatakatifu yasemavyo: “Wazao wakowatakuwa wengi kama nyota!” 19 Alikuwamzee wa karibu miaka mia moja, lakini imaniyake haikufifia ingawa alijua kwamba mwiliwake ulikuwa kama umekufa, na pia mkewe,

WARUMI 3:11

118

Page 119: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

6

Sara, alikuwa tasa. 20 Abrahamu hakuioneamashaka ile ahadi ya Mungu; alipata nguvukutokana na imani, akamtukuza Mungu. 21

Alijua kwamba Mungu anaweza kuyatekelezayale aliyoahidi. 22 Ndiyo maana Mungualimkubali kuwa mwadilifu. 23 Inaposemwa,“Alimkubali,” haisemwi kwa ajili yakemwenyewe tu. 24 Jambo hili linatuhusu sisi piaambao tunamwamini Mungu aliyemfufuaYesu, Bwana wetu, kutoka wafu. 25 Yeyealitolewa auawe kwa ajili ya dhambi zetu,akafufuka ili tupate kukubaliwa kuwa waadilifuna Mungu.

Sasa, kwa vile tumekubaliwa kuwawadilifu kwa imani, basi, tunayo amanina Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu

Kristo. 2 Kwa imani yetu, yeye ametuletakatika hali hii ya neema ya Mungu ambamosasa tunaishi. Basi, tunajivunia tumaini tulilonalo la kushiriki utukufu wa Mungu. 3 Naam,si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabutukijua kwamba taabu huleta saburi, 4 nayosaburi huleta uthabiti, na uthabiti huletatumaini. 5 Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa,maana Mungu amekwisha miminia mioyonimwetu upendo wake kwa njia ya RohoMtakatifu aliyetujalia. 6 Tulipokuwa badowanyonge, Kristo, wakati ulipotimia, alikufakwa ajili yetu sisi waovu. 7 Si rahisi mtu kufakwa ajili ya mtu mwadilifu; labda mtu anawezakuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. 8

Lakini Mungu amethibitisha kwambaanatupenda, maana wakati tulipokuwa badowenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. 9

Kwa kuwa sasa tumekubaliwa kuwa waadilifukwa damu ya Kristo, ni dhahiri zaidi kwambaatatuokoa katika ghadhabu ya Mungu. 10

Maana, tulipokuwa bado adui zake, Mungualitupatanisha naye kwa kifo cha Mwanae. Nakwa vile sasa tumepatanishwa naye, ni dhahirizaidi kwamba tutaokolewa kwa uzima waKristo. 11 Wala si hayo tu, ila tunafurahi piakatika Mungu kwa njia ya Bwana wetu YesuKristo ambaye ametupatanisha na Mungu. 12

Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingiaulimwenguni, nayo ikasababisha kifo. Hivyokifo kimeenea katika jumuiya yote yabinadamu, kwa maana wote wametendadhambi. 13 Kabla ya Sheria kuwako, dhambiilikuwako ulimwenguni; lakini dhambihaiwekwi katika kumbukumbu bila sheria. 14

Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakatiwa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambaohawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, yakumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo chayule ambaye atakuja baadaye. 15 Lakini ipotofauti: neema ya Mungu si kama dhambi yaAdamu. Maana, ingawa dhambi ya mtu mmojailisababisha kifo kwa wote, kwa fadhili ya mtummoja, yaani Yesu Kristo, Munguamewazidishia wote neema na zawadi zake. 16

Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu, nadhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya

kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu;lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungualiwapa zawadi yake kwa kuwasamehe. 17

Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja kifo kilianzakutawala kwa sababu ya huyo mtu mmoja;lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanyayule mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni borazaidi. Wote wanaopokea neema na zawadi hiyoya kukubaliwa kuwa waadilifu, watatawalakatika uzima kwa njia ya huyo mmoja, yaaniYesu Kristo. 18 Basi, kama vile kosa la mtummoja lilivyoleta hukumu kwa binadamuwote, kadhalika kitendo kimoja kiadilifukinawapa uhuru na uzima. 19 Na kama kwakutotii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywawenye dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmojakutawafanya wengi wakubaliwe kuwawaadilifu. 20 Sheria ilitokea, ikasababishakuongezeka kwa uhalifu; lakini pale dhambiilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi. 21

Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo,kadhalika neema inatawala kwa njia yauadilifu, na kuleta uzima wa milele kwa njia yaYesu Kristo Bwana wetu.

Tuseme nini basi? Je, twendelee kubakikatika dhambi ili neema ya Munguiongezeke? 2 Hata kidogo! Kuhusu

dhambi sisi tumekufa—tutaendeleaje kuishitena katika dhambi? 3 Maana, mnajuakwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na KristoYesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake. 4

Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake,tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristoalivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendokitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishimaisha mapya. 5 Maana, kama sisitumeungana naye katika kufa kama yeye, vivyohivyo tutaungana naye kwa kufufuliwa kutokawafu kama yeye. 6 Tunajua kwamba utu wetuwa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo, ili hali yadhambi iharibiwe, tusiwe tena watumwa wadhambi. 7 Kwa maana, mtu aliyekufa,amenasuliwa kutoka katika nguvu ya dhambi.8 Basi, ikiwa tumekufa pamoja na Kristo,tunaamini kwamba tutaishi pia pamoja naye. 9

Maana, tunajua kwamba Kristo amekwishafufuliwa kutoka wafu na hafi tena; kifohakimtawali tena. 10 Hivyo, kwa kuwaalikufa—mara moja tu—dhambi haina nguvutena juu yake; na sasa anaishi maisha yakekatika umoja na Mungu. 11 Hali kadhalikananyi lazima mjione kuwa mmekufa kuhusudhambi, lakini kama mnaoishi katika umoja naMungu kwa njia ya Kristo Yesu. 12 Kwa hiyo,dhambi isiitawale tena miili yenu ambayo hufa,na hivyo kuzitii tamaa zake. 13 Wala msitoehata sehemu moja ya miili yenu iwe chombocha kutenda uovu na dhambi. Badala yake,jitoleeni ninyi wenyewe kwa Mungu kama watuwaliofufuliwa kutoka wafu; toeni nafsi zenuzote kwa Mungu kwa ajili ya uadilifu. 14

Maana, dhambi haitawatawala ninyi tena,kwani hamko chini ya Sheria, bali chini ya

WARUMI 6:14

119

Page 120: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

7

8

neema. 15 Basi, tuseme nini? Je, tutendedhambi ati kwa sababu hatuko chini ya Sheriabali chini ya neema? Hata kidogo! 16 Mnajuakwamba mkijitolea ninyi wenyewe kamawatumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweliwatumwa wake mtu huyo—au watumwa wadhambi, na matokeo yake ni kifo, au wa utii, namatokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu.17 Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambizamani, sasa lakini—namshukuruMungu—mmetii kwa moyo wote yalemaazimio na mafundisho mliyopokea. 18

Mlikombolewa kutoka utumwa wa dhambi,mkawa watumwa wa uadilifu. 19 (Hapanatumia lugha ya kawaida ya watu kwa sababuya udhaifu wenu wenyewe.) Kama vile wakatifulani mlivyojitolea ninyi wenyewe kutumikiauchafu na uhalifu kwa ajili ya uovu, vivyo hivyosasa jitoleeni nafsi zenu wenyewe kutumikiauadilifu kwa ajili ya utakatifu. 20 Mlipokuwawatumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali nauadilifu. 21 Sasa, mlipata faida gani siku zilekutokana na mambo yale ambayo mnayaoneaaibu sasa? Maana, matokeo ya mambo haya nikifo! 22 Lakini sasa, mmekwisha kombolewakutoka utumwa wa dhambi na mmekuwawatumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa niutakatifu, na matokeo yake ni uzima wa milele.23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo;lakini zawadi anayotoa Mungu ni uzima wamilele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwanawetu.

Ndugu zangu, bila shaka mtaelewayafuatayo, maana ninawazungumziawatu wanaojua Sheria. Sheria

humtawala mtu wakati akiwa hai. 2 Mathalan:mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheriamuda wote mumewe anapokuw hai; lakinimumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tenahuyo mwanamke. 3 Hivyo mwanamke huyoakiishi na mwanamume mwingine wakatimumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakinimumewe akifa, mwanamke huyo yu hurukisheria, na akiolewa na mwanamumemwingine, yeye si mzinzi. 4 Hali kadhalikaninyi ndugu zangu: ninyi pia mmekufa kuhusuSheria kwa kuwa ninyi ni sehemu ya mwili waKristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwakutoka wafu ili tupate kuzaa matunda memakwa ajili ya Mungu. 5 Maana, tulipokuwatukiishi kimaumbile tu, tamaa mbayazikichochewa na Sheria, zilifanya kazi katikamiili yetu, na kuchuma pato la kifo. 6 Lakinisasa tumekuwa huru kutoka vifungo vyaSheria, kwa sababu tumekufa kuhusu lilejambo lililotufanya sisi watumwa. Sasatunatumikia kufuatana na maisha mapya yaRoho, na si kufuatana na hali ile ya kale yaSheria iliyoandikwa. 7 Je, tuseme basi,kwamba Sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakinibila Sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitugani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamanimabaya, kama Sheria isingalikuwa imesema:

“Usitamani.” 8 Kwa kuitumia hiyo amri,dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina yatamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila Sheriadhambi ni kitu kilichokufa. 9 Wakati mmojamimi nilikuwa hai mbali na Sheria; lakini amriilipokuja, dhambi ilifufuka, 10 nami nikafa.Hiyo amri ambayo shabaha yake ilikuwa kuletauhai, kwangu imeleta kifo. 11 Maana, dhambiilichukua fursa iliyopatiwa na amri hiyo,ikanidanganya na kuniua. 12 Basi, Sheriayenyewe ni takatifu, na amri yenyewe nitakatifu, ni ya haki na nzuri. 13 Je, hiiinamaanisha kwamba kile kilicho kizurikimesababisha kifo changu? Hata kidogo! Iliyoni kwamba, dhambi, ili ionekane dhahiri kuwani dhambi, imekitumia kile kilicho kizuri nakusababisha kifo changu. Hivyo dhambi, kwanjia ya ile amri, ilijionyesha kikamilifu jinsiilivyo mbaya mno. 14 Tunajua kwamba Sheriani ya kiroho, lakini mimi ni wa kidunia, miminimeuzwa kuwa mtumwa wa dhambi. 15

Sielewi nifanyacho, maana kile ninachotakasikifanyi, bali kile ninachochukia ndichonikifanyacho. 16 Ikiwa basi, ninatendakinyume cha matakwa yangu, hii inamaanishakwamba nakubali kuwa ile Sheria ni nzuri. 17

Basi, si mimi hasa ninayefanya kitu hicho, baliile dhambi iliyo ndani yangu. 18 Najuakwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi,kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana,ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezikulitekeleza. 19 Yaani, badala ya kufanya lilejambo jema ninalotaka, nafanya lile bayanisilotaka. 20 Basi, kama ninafanya kinyumecha matakwa yangu, hii inamaanisha kwambasi mimi ninayefanya hayo, bali ni ile dhambiiliyo ndani yangu. 21 Basi, nimegundua kanunihii: ninataka kufanya jema, lakini najikutakwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua. 22

Ndani kabisa katika moyo wangu naifurahiasheria ya Mungu. 23 Lakini naona kwambakuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilinimwangu, sheria ambayo inapingana na ileinayokubaliwa na akili yangu. Hiyo inanifanyaniwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayokazi mwilini mwangu. 24 Maskini miye! Naniatakayeniokoa kutoka katika mwili huuunaonipeleka kifoni? 25 Shukrani kwa Munguafanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu YesuKristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi,kwa akili yangu, ninaitumikia sheria yadhambi.

Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwawale ambao katika maisha yaowameungana na Kristo. 2 Maana,

sheria ya Roho iletayo uzima kwa kuungana naKristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheriaya dhambi na kifo. 3 Mungu ametekelezajambo lile ambalo Sheria haikuweza kutekelezakwa sababu ya udhaifu w binadamu. Mungualimtuma Mwanae akiwa mwenye mwili sawana miili yetu sisi wenye dhambi, ili aikabilidhambi, na kwa mwili huo akaiangamiza

WARUMI 6:15

120

Page 121: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

dhambi. 4 Mungu alifanya hivyo kusudimatakwa ya haki ya Sheria yatekelezwekikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, sikwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu yaRoho. 5 Maana, wale wanaoishi kufuatana namatakwa ya mwili, hutawaliwa na fikira zamwili. Lakini wale wanaoishi kufuatana namatakwa ya Roho Mtakatifu, hutawaliwa nafikira za Roho. 6 Fikira za mwili huleta kifo;fikira za Roho huleta uzima na amani. 7

Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwilini adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, walahawezi kuitii. 8 Watu wanaotii matakwa yamwili hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakinininyi hamuishi kufuatana na matakwa yamwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho,ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu.Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wakeKristo. 10 Lakini kama Kristo yumo ndani yenu,ingawa miili yenu itakufa kwa sababu yadhambi, kwenu Roho ndiye uhai kwa sababummekubaliwa kuwa waadilifu. 11 Ikiwa Rohowa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafuanaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufuaKristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenuyenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia yaRoho wake akaaye ndani yenu. 12 Hivyo basi,ndugu zangu, tunalo jukumu, lakini si la kuishikufuatana na maumbile ya kibinadamu. 13

Kwa maana, kama mkiishi kufuatana namatakwa ya maumbile ya kibinadamu, hakikamtakufa. Lakini, kama kwa njia ya Rohomnayaua matendo yenu maovu, basi, mtaishi.14 Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu niwatoto wa Mungu. 15 Kwa maana, Rohomliyempokea si Roho mwenye kuwafanyaninyi watumwa na kuwatia tena hofu; sivyo,bali mmempokea Roho mwenye kuwafanyaninyi watoto wa Mungu, na kwa nguvu ya huyoRoho, sisi tunaweza kumwita Mungu, “Aba,”yaani “Baba!” 16 Naye Roho mwenyeweanajiunga na roho zetu na kuthibitishakwamba sisi ni watoto wa Mungu. 17 Basi, kwavile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea barakazote Mungu alizowawekea watu wake, natutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana,tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushirikipia utukufu wake. 18 Naona kuwa mateso yawakati huu wa sasa si kitu kamwe kamatukiyafananisha na ule utukufuutakaodhihirishwa kwetu. 19 Viumbe vyotevinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishewatoto wake. 20 Kwa maana, viumbeviliwekwa katika hali ya kutojiweza kabisa, sikwa hiari yao, ila vilifanywa hivyo kwa mapenziya Mungu. Hata hivyo yapo matumaini, 21

maana hivyo viumbe navyo vitaokolewa kutokakatika utumwa wa uharibifu, vishiriki uhurumtukufu wa watoto wa Mungu. 22 Kwa maanatunajua kwamba mpaka hivi sasa, viumbevyote vinalia kwa maumivu kama yakujifungua mtoto. 23 Wala si hivyo viumbepeke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho,

aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi piatunalalamika ndani yetu, tukitazamia kufanywawatoto wa Mungu, nazo nafsi zenuzikombolewe. 24 Maana kwa matumaini hayosisi tumekombolewa; lakini tumaini halinamaana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia.Maana ni nani anayetumaini kile ambachotayari anakiona? 25 Kama tunakitumaini kileambacho hatujakiona bado, basi, tunakingojeakwa uvumilivu. 26 Hali kadhalika, naye Rohoanatusaidia katika udhaifu wetu. Maanahatujui inavyotupasa kuomba; lakini Rohomwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mliowa huzuni usioelezeka. 27 Naye Munguaonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajuafikira ya huyo Roho; kwani huyo Rohohuwaombea watu wa Mungu kufuatana namapenzi ya Mungu. 28 Tunajua kwamba,katika mambo yote, Mungu hufanya kazi nakuifanikisha pamoja na wote wampendao,yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake.29 Maana hao aliowachagua tangu mwanzo,ndio aliowateua wapate kufanana na Mwanae,ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwandugu wengi. 30 Basi, Mungu aliwaita walealiokuwa amewateua; na hao aliowaitaaliwakubali kuwa waadilifu; na haoaliowakubali kuwa waadilifu aliwashirikisha piautukufu wake. 31 Kutokana na hayo, tusemenini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu,nani awezaye kutupinga? 32 Munguhakumhurumia hata mwanae wa pekee, balialimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanyahivyo, je, hatatujalia pia mema yote? 33 Ni naniatakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungumwenyewe huwaondolea hatia! 34 Ni naniatakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristondiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka wafu naanakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeyeanatuombea! 35 Ni nani awezaye kututenga namapendo ya Kristo? Je, ni taabu, au dhiki, aumateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, auhatari, au kuuawa? 36 Kama MaandikoMatakatifu yasemavyo: “Kwa ajili yako,twakikabili kifo kutwa kucha: tunatendewakama kondoo wa kuchinjwa.” 37 Lakini, katikamambo haya yote, tumepata ushindi mkubwakwa msaada wake yeye aliyetupenda. 38

Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitukiwezacho kututenganisha na upendo wake:wala kifo, wala uhai; wala malaika, au nguvunyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa,wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka;39 Wala ulimwengu wa juu, wala wa chinikabisa. Hakuna kiumbe chochotekitakachoweza kututenga na upendo waMungu kwetu kwa njia ya Kristo Yesu Bwanawetu.

Nasema ukweli mtupu; nimeungana naKristo nami sisemi uongo. Dhamiriyangu ikiongozwa na Roho Mtakatifu

inanithibitishia jambo hili pia. 2 Natakakusema hivi: nina huzuni kubwa na maumivu

WARUMI 9:2

121

Page 122: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

yasiyopimika moyoni mwangu 3 kwa ajili yawatu wangu, walio damu moja nami! Kamaingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhikulaaniwa na kutengwa na Kristo. 4 Hao ndiowatu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawewatoto wake, akawashirikisha utukufu wake;aliagana nao, akawapa Sheria yake, imani yakweli na ahadi zake. 5 Wao ni wajukuu wamababu, naye Kristo, kadiri ya ubinadamuwake, ametoka katika ukoo wao. Munguatawalaye juu ya yote, na atukuzwe milele!Amina. 6 Sisemi kwamba ahadi ya Munguimebatilika; maana si watu wote wa Israeli niwateule wa Mungu. 7 Wala, si wazawa wotewa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila,kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Wazao wake watatokana na Isaka.” 8 Nidokusema, wale waliozaliwa kimaumbile ndiowatoto wa Mungu, bali wale waliozaliwakutokana na ahadi ya Mungu ndiowatakaoitwa watoto wake. 9 Maana ahadiyenyewe ni hii: “Nitakujia wakati maalum, nayeSara atapata mtoto.” 10 Tena si hayo tu ila piaRebeka naye alipata mapacha kwa babammoja, yaani Isaka, babu yetu. 11 Lakini, iliMungu aonekane kwamba anao uhuru wakuchagua, hata kabla wale nduguhawajazaliwa na kabla hawajawezakupambanua jema na baya, 12 Rebekaaliambiwa kwamba yule mtoto wa kwanzaatamtumikia yule wa nyuma. Hivyo uchaguziwa Mungu unategemea jinsi anavyoitamwenyewe, na si matendo ya binadamu. 13

Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:“Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia.”14 Basi, tuseme nini? Je, Mungu amekosa haki?Hata kidogo! 15 Maana alimwambia Mose:“Nitamhurumia mtu yeyote ninayetakakumhurumia; nitamwonea huruma mtu yeyoteninayetaka.” 16 Kwa hiyo, yote hutegemeahuruma ya Mungu, na si bidii au mapenzi yamtu. 17 Maana Maandiko Matakatifu yasemahivi kwa Farao: “Nilikufanya mfalme ili kwa njiayako, uwezo wangu ujulikane, na jina langulitangazwe popote duniani.” 18 Ni wazi, basi,kwamba Mungu humhurumia yeyoteanayetaka kumhurumia, na akipendakumfanya mtu awe mkaidi, hufanya hivyo. 19

Labda utaniuliza: “Ikiwa mambo yako hivyo,Mungu anawezaje kumlaumu mtu? Naniawezaye kuyapinga mapenzi yake?” 20 Lakini,ewe binadamu, u nani hata uthubutu kumhojiMungu? Je, chungu chaweza kumwulizamfinyanzi wake: “Kwa nini umenitengenezanamna hii?” 21 Mfinyanzi anaweza kuutumiaudongo apendavyo na kufinyanga vyunguviwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumiziya heshima, na kingine kwa matumizi yakawaida. 22 Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu.Alitaka kuonyesha ghadhabu yake na kujulishauwezo wake, Basi, alikuwa na saburi sana,akiwavumilia wale ambao walikuwa lengo laghadhabu yake, ambao walistahili

kuangamizwa. 23 Alitaka pia kudhihirishawingi wa utukufu wake ambao alitumiminiasisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambaoalikwisha kututayarisha kuupokea utukufuwake. 24 Maana sisi ndio hao aliowaita, si tukutoka miongoni mwa Wayahudi bali piakutoka kwa watu wa mataifa mengine. 25

Maana ndivyo asemavyo katika kitabu chaHosea: “Wale waliokuwa Si watu wangunitawaita: Watu wangu! Naye Sikupendiataitwa: Mpenzi wangu! 26 Na palewalipoambiwa: Ninyi si wangu hapo wataitwa:Watoto wa Mungu hai.” 27 Naye nabii Isaya,kuhusu Israeli anapaaza sauti: “Hata kamawatoto wa Israeli ni wengi kama mchanga wapwani, ni wachache tu watakaookolewa; 28

maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumuyake kamili juu ya ulimwengu wote.” 29 Nikama Isaya alivyosema hapo awali: “KamaBwana Mwenye Nguvu asingalituachia baadhiya watoto wa Israeli, tungalikwisha kuwa kamaSodoma, tungalikwisha kuwa ma Gomora.” 30

Basi, tuseme nini? Ni hivi: watu wa mataifaambao hawakutafuta kukubaliwa kuwawaadilifu, wamekubaliwa kuwa waadilifu kwanjia ya imani, 31 hali watu wa Israeli waliokuwawakitafuta Sheria iletayo kukubaliwa kuwawaadilifu, hawakuipata. 32 Kwa nini? Kwasababu walitegemea matendo yao badala yakutegemea imani. Walijikwaa juu ya jiwe lakujikwaa 33 kama yesemavyo MaandikoMatakatifu: “Tazama! Naweka huko Sioni jiwelikwazalo, mwamba utakaowafanya watuwaanguke. Mtu atakayemwamini yeye aliyehilo jiwe, hataaibishwa!”

Ndugu zangu, ninataka na kutazamiakwa moyo wangu wote hao wananchiwenzangu wakombolewe. Tena

nawaombea kwa Mungu daima. 2 Maananaweza kuthibitisha kwa niaba yao kwambawanayo bidii ya kumtafuta Mungu; lakini bidiihiyo haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli. 3

Maana hawakufahamu jinsi Munguanavyowafanya watu wawe waadilifu, nawamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe,na hivyo hawakuikubali njia hiyo ya Mungu yakuwafanya wawe waadilifu. 4 Maana kwa kujakwake Kristo, Sheria imefikia kikomo chake, ilikila mtu anayeamini akubaliwe kuwamwadilifu. 5 Kuhusu kukubaliwa kuwamwadilifu kwa kuitii Sheria, Mose aliandikahivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa yaSheria ataishi.” 6 Lakini, kuhusu kukubaliwakuwa mwadilifu kwa njia ya imani, yasemwahivi: “Usiseme moyoni mwako: Nani atapandampaka mbinguni? (yaani, kumleta Kristo chini);7 wala usiseme: Nani atashuka mpaka Kuzimu(yaani, kumleta Kristo kutoka kwa wafu).” 8

Maandiko Matakatifu yesema hivi, “Ujumbehuo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywanimwako na moyoni mwako” nao ndio ile imanitunayoihubiri. 9 Kama ukikiri kwa kinywachako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini

WARUMI 9:3

122

Page 123: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

moyoni mwako kwamba Mungu alimfufuakutoka wafu, utaokoka. 10 Maana tunaaminikwa moyo na kukubaliwa kuwa waadilifu; natunakiri kwa midomo yetu na kuokolewa. 11

Maandiko Matakatifu yasema: “Kilaamwaminiye hatakuwa na sababu yakuaibika.” 12 Jambo hili ni kwa wote, kwanihakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasioWayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye nimkarimu sana kwao wote wamwombao. 13

Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtuatakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.”14 Basi, watamwombaje yeye ambayehawamwamini? Tena, watamwaminije kamahawajapata kusikia habari zake? Na watasikiajehabari zake kama hakuna mhubiri? 15 Na watuwatahubirije kama hawakutumwa? Kamayasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni jambo lakupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiriHabari Njema!” 16 Lakini wote hawakuipokeahiyo Habari Njema. Maana Isaya alisema:“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17

Hivyo basi, imani inatokana na kuusikilizaujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno laKristo. 18 Lakini nauliza: je, hawakuusikia huoujumbe? Naam, waliusikia; kama MaandikoMatakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeeneaduniani kote; maneno yao yamefika mpakakingo za ulimwengu.” 19 Tena nauliza: je,yawezekana kwamba watu wa Israelihawakufahamu? Mose mwenyewe ni kwakwanza kujibu: “Nitawafanyeni mwaonee wivuwatu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe nahasira juu ya taifa la watu wapumbavu.” 20

Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Waleambao hawakunitafuta wamenipata;nimejionyesha kwao wasiouliza habari zangu.”21 Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchanakutwa niliwanyoshea mikono yangu watuwaasi na wasiotii.”

Basi, nauliza: je, Mungu amewakataawatu wake? Hata kidogo! Mini binafsini Mwisraeli mzawa wa Abrahamu, wa

kabila la Benyamini. 2 Mungu hakuwakataawatu wake aliowateua tangu mwanzo.Mnakumbuka yasemavyo MaandikoMatakatifu juu ya Eliya wakatialipomnung'unikia Mungu kuhusu Israeli: 3

“Bwana, wamewaua manabii wako nakubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu pekeyangu niliyebaki, nao wanataka kuniua?” 4 Je,Mungu alimjibu nini? Alimwambia:“Nimejiwekea elfu saba ambaohawakumwabudu Baali.” 5 Basi, ndivyo ilivyopia wakati huu wa sasa: ipo idadi ya waliobakiambao Mungu aliwateua kwa sababu yaneema yake. 6 Uteuzi wake unatokana naneema yake, na si kwa sababu ya matendoyao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemeamatendo ya watu, neema yake haingekuwaneema tena. 7 Sasa, je? Watu wa Israelihawakukipata kile walichokuwa wanakitafuta;lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine

walipumbazwa, 8 kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: “Mungu ameifanya mioyo yaokuwa mizito, na mpaka leo hii hawawezi kuonakwa macho yao wala kusikia kwa masikio yao.”9 Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwemtego wa kuwanasa, waanguke nakuadhibiwa. 10 Macho yao yatiwe gizawasiweze kuona. Migongo yao ipindike kwataabu daima!” 11 Basi, nauliza: je, Wayahudiwamejikwaa hata wakaangamia kabisa? Hatakidogo! Kutokana na kosa lao ukomboziumewajia watu wa mataifa mengine, iliWayahudi wapate kuwaonea wivu. 12 Kosa laWayahudi limesababisha baraka nyingi kwaulimwengu, na utovu wao kwa kiroho umeletabaraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine.Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu waoutasababisha baraka nyingi zaidi. 13 Basi, sasanawaambieni ninyi watu wa mataifa mengine:Maadamu mimi nimekuwa mtume kwa watuwa mataifa mengine, ninajivunia hudumayangu, 14 nipate kuwafanya wananchiwenzangu wawaonee ninyi wivu, na hivyonipate kuwaokoa baadhi yao. 15 Maana ikiwakukataliwa kwao kulisababisha ulimwenguupatanishwe na Mungu, itakuwaje wakatiwatakapokubaliwa na Mungu? Wafuwatafufuka! 16 Ikiwa kipande cha kwanza chamkate kimewekwa wakfu, mkate woteumewekwa wakfu; mizizi ya mti ikiwa mizuri,na matawi yake huwa mazuri pia. 17 Naam,baadhi ya matawi ya mzeituni bustaniniyalikatwa, na mahali pake tawi la mzeitunimwitu likapandikizwa. Ninyi watu wa mataifamengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; nasasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeitunibustanini. 18 Basi, msiwadharau walewaliokatwa kama matawi! Na, hata kama kunala kujivunia, kumbukeni kwamba si ninyimnaoitegemeza mizizi, bali mizizi ndiyoinayowategemeza ninyi. 19 Lakini utasema:“Matawi yalikatwa kusudi mimi nipandikizwemahali pake.” 20 Sawa! Yalikatwa kwa sababuya kukosa imani, bali wewe unasimama kwaimani yako. Lakini usijivune; ila uwe natahadhari. 21 Kwa maana, ikiwa Munguhakuwahurumia Wayahudi ambao ni kamamatawi ya asili, je, unadhani atakuhurumiawewe? 22 Kumbuka, basi, jinsi Mungu alivyomwema na mkali. Yeye ni mkali kwa walewalioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwautaendelea katika wema wake; la sivyo, nawepia utakatwa. 23 Nao Wayahudi, hali kadhalika;wakiacha utovu wao wa imani, watapandikizwatena. Maana Mungu anao uwezo wakuwapandikiza tena. 24 Ninyi watu wa mataifamengine, kwa asili ni kama tawi la mzeitunimwitu, lakini mmeondolewa huko,mkapandikizwa katika mzeituni bustaninimahali ambapo kwa asili si penu. Lakini,Wayahudi kwa asili ni kama mzeituni bustanini,na itakuwa jambo rahisi zaidi kwaokupandikizwa tena katika mti huohuo wao. 25

WARUMI 11:25

123

Page 124: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

12

13

Ndugu zangu, napenda mjue ukweli huuuliofichika msije mkajiona wenye akili sana.Ukaidi wa Wayahudi ulikuwa ni wa muda tu,mpaka watu wa mataifa menginewatakapokuwa wamemfikia Mungu. 26 Hapondipo taifa lote la Israeli litakapookolewa,kama yesemavyo Maandiko Matakatifu:“Mkombozi atakuja kutoka Sioni, atauondoauovu wa Yakobo. 27 Hili ndilo aganonitakalofanya nao wakati nitakapoziondoadhambi zao.” 28 Kwa sababu wanaikataaHabari Njema, Wayahudi wamekuwa adui waMungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wamataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado nirafiki wa Mungu kwa sababu ya baba zao. 29

Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zakena kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo.30 Hapo awali ninyi mlikuwa mmemwasiMungu, lakini sasa mmepata huruma yakekutokana na kuasi kwao. 31 Hali kadhalika,kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi,Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao piawapokee sasa huruma ya Mungu. 32 MaanaMungu amewafunga watu wote katika uasiwao ili wapate kuwahurumia wote. 33 Utajiri,hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno!Huruma zake hazichunguziki, na njia zakehazieleweki! Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: 34 “Nani aliyepata kuyajuamawazo ya Bwana? Nani awezaye kuwamshauri wake? 35 Au, nani aliyempa yeye kitukwanza hata aweze kulipwa tena kitu hicho?”36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyotevipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake.Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina.

Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamMungu ni mwenye huruma nyingi,nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni

nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai,takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njiayenu halisi ya kumwabudu. 2 Msiige mitindoya ulimwengu huu, bali Mungu afanyemabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikirazenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajuamapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililojema, linalompendeza na kamilifu. 3 Kutokanana neema aliyonijalia Mungu, nawaambienininyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kulikomnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe nakiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungualiyomgawia kila mmoja. 4 Mwili una viungovingi, kila kimoja na kazi yake. 5 Hali kadhalikaingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwakuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungocha mwenzake. 6 Basi, tunavyo vipajimbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa.Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri yaimani yake. 7 Mwenye kipaji cha utumishi naatumikie. mwenye kipaji cha kufundisha naafundishe. 8 Mwenye kipaji cha kuwafarijiwengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawiamwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwaukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii;

naye mwenye kutenda jambo la huruma naafanye hivyo kwa furaha. 9 Mapendo yenu nayawe bila unafiki wowote. Chukieni jambololote ovu, zingatieni jema. 10 Pendanenikidugu; kila mmoja amfikirie mwenzakekwanza kwa heshima. 11 Msilegee katika bidii,muwe wachangamfu rohoni katikakumtumikia Bwana. 12 Tumaini lenu liwawekedaima wenye furaha; muwe na saburi katikashida na kusali daima. 13 Wasaidieni watu waMungu katika mahitaji yao; wapokeeni wagenikwa ukarimu. 14 Watakieni baraka wotewanaowadhulumu ninyi; naam, watakienibaraka na wala msiwalaani. 15 Furahinipamoja na wanaofurahi, lieni pamoja nawanaolia. 16 Muwe na wema uleule kwa kilamtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni nawatu wadogo. Msijione kuwa wenye hekimasana. 17 Msilipe ovu kwa ovu. Zingatienimambo mema mbele ya wote. 18 Kadiriinavyowezekana kwa upande wenu, muwe naamani na watu wote. 19 Wapenzi wangu,msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambohilo; maana Maandiko Matakatifu yasema:“Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipizaasema Bwana.” 20 Tena, Maandiko yasema:“Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwana kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanyahivyo utamfanya apate aibu kali kama makaaya moto juu ya kichwa chake.” 21 Usikubalikushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwawema.

Kila mtu anapaswa kuwatii wenyemamlaka katika serikali; maanamamlaka yote hutoka kwa Mungu;

nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu.2 Anayepinga mamlaka ya viongozi anapingaagizo la Mungu; nao wafanyao hivyowanajiletea hukumu wenyewe, 3 Maana,watawala hawasababishi hofu kwa watuwema, ila kwa watu wabaya. Basi, watakausimwogope mtu mwenye mamlaka? Fanyamema naye atakusifu; 4 maana yeye nimtumishi wa Mungu anayefanya kazi kwafaida yako. Lakini ukifanya mabaya, basi, hunabudi kumwogopa, maana anao kweli uwezowa kutoa adhabu. Yeye ni mtumishi wa Munguna huitekeleza ghadhabu ya Mungu kwaowatendao maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kuwatiiwenye mamlaka, si tu kwa sababu ya kuogopaghadhabu ya Mungu, bali pia kwa sababudhamiri inadai hivyo. 6 Kwa sababu hiyohiyoninyi hulipa kodi; maana viongozi haohumtumikia Mungu ikiwa wanatimiza wajibuwao. 7 Mpeni kila mtu haki yake; mtu waushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliyeheshima, heshima. 8 Msiwe na deni kwa mtuyeyote, isipokuwa tu deni la kupendana.Ampendaye jirani yake ameitekeleza Sheria. 9

Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;”na nyingine zote, zimo katika amri hii moja:“Mpende jirani yako kama unavyojipendamwenyewe.” 10 Ampendaye jirani yake

WARUMI 11:26

124

Page 125: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

14

15

hamtendei vibaya. Basi, kwa mapendo Sheriayote hutimizwa. 11 Zaidi ya hayo, ninyi mnajuatumo katika wakati gani: sasa ndio wakati wakuamka usingizini; naam, wokovu wetu ukaribu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanzakuamini. 12 Usiku unakwisha na mchanaunakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yoteya giza, tukajitwalie silaha za mwanga. 13

Mwenendo wetu uwe wa adabu kamainavyostahili wakati wa mchana; tusiwe na ulafina ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu.14 Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu;msishughulikie tena tamaa zenu za maumbilena kuziridhisha.

Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu,lakini msibishane naye juu ya mawazoyake binafsi. 2 Watu huhitilafiana:

mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu;lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu,hula tu mboga za majani. 3 Mtu ambaye hulakila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kulakila kitu; naye ambaye hula tu mboga zamajani asimhukumu anayekula kila kitu,maana Mungu amemkubali. 4 Wewe ni nanihata uthubutu kumhukumu mtumishi wamwingine? Akisimama au akianguka ni shaurila Bwana wake; naam, atasimama imara,maana Bwana anaweza kumsimamisha. 5 Mtuanaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maanazaidi kuliko nyingine; mtu mwingine awezakuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja naafuate msimamo wa akili yake. 6

Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha sikuhiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; nayeanayekula chakula fulani anafanya hivyo kwakumtukuza Bwana maana anamshukuruMungu. Kadhalika naye anayeacha kulachakula fulani anafanya hivyo kwa ajili yakumtukuza Bwana, naye pia anamshukuruMungu. 7 Maana hakuna mtu yeyotemiongoni mwetu aishiye kwa ajili yakemwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajiliyake mwenyewe 8 maana tukiishi twaishi kwaajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili yaBwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi nimali yake Bwana. 9 Maana Kristo alikufa,akafufuka ili wapate kuwa Bwana wa wazimana wafu. 10 Kwa nini, basi wewe wamhukumundugu yako? Nawe, kwa nini wamdharaundugu yako? Sisi sote tutasimama mbele yakiti cha hukumu cha Mungu. 11 MaanaMaandiko yanasema: “Kama niishivyo, asemaBwana kila mtu atanipigia magoti, na kilammoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.” 12

Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja yakembele ya Mungu. 13 Basi, tuachekuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwekikwazo kwa ndugu yetu au kumsababishaaanguke katika dhambi. 14 Katika kuunganana Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakunakitu chochote kilicho najisi kwa asili yake;lakini, mtu akidhani kwamba kitu fulani ninajisi, basi, kwake huwa najisi. 15 Kama

ukimhuzunisha ndugu yako kwa sababu yachakula unachokula, basi mwenendo wakohauongozwi na mapendo. Usikubali hatakidogo chakula chako kiwe sababu ya kupoteakwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa kwaajili yake! 16 Basi, msikubalie kitumnachokiona kuwa kwenu ni kitu chemakidharauliwe. 17 Maana Utawala wa Mungu sishauri la kula na kunywa, bali unahusika nakuwa na uadilifu, amani na furaha iletwayo naRoho Mtakatifu. 18 Anayemtumikia Kristonamna hiyo humpendeza Mungu, nakukubaliwa na watu. 19 Kwa hiyo tuyazingatiedaima mambo yenye kuleta amani, nayanayotusaidia kujengana. 20 Basi, usiiharibukazi ya Mungu kwa sababu ya ubishi juu yachakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifaikula chakula ambacho kitamfanya mtuaanguke katika dhambi. 21 Afadhali kuachakula nyama, kunywa divai, au kufanyachochote ambacho chaweza kumsababishandugu yako aanguke. 22 Basi, shikiliaunachoamini kati yako na Mungu wako. Herimtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya,haipingi dhamiri yake. 23 Lakini mtu anayeonashaka juu ya chakula anachokula,anahukumiwa kama akila, kwa sababumsimamo wa kitendo chake haumo katikaimani. Na, chochote kisicho na msingi wakekatika imani ni dhambi.

Sisi tulio imara katika imanitunapaswa kuwasaidia wale waliodhaifu wayakabili matatizo yao.

Tusijipendelee sisi wenyewe tu. 2 Kila mmojawetu anapaswa kumpendeza jirani yake kwawema ili huyo apate kujijenga katika imani. 3

Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ilaalikuwa kama yasemavyo Maandiko: “Kashfazote walizokutolea wewe zimenipata mimi.” 4

Maana yote yalioandikwa yameandikwa kwaajili ya kutufundisha sisi ili kutokana na saburina faraja tupewayo na Maandiko hayoMatakatifu tupate kuwa na matumaini. 5

Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote,awajalieni ninyi kuwa na msimamo mmojakufuatana na mfano wake Kristo Yesu, 6 ilininyi nyote, kwa nia moja na sauti moja,mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetuYesu Kristo. 7 Basi, karibishaneni kwa ajili yautukufu wa Mungu kama naye Kristoalivyowakaribisheni. 8 Maana, nawaambieniKristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonyeshauaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungualizowapa babu zetu zipate kutimia; 9 ili naowatu wa mataifa mengine wapate kumtukuzaMungu kwa sababu ya huruma yake. Kamayasemavyo Maandiko Matakatifu: “Kwa sababuhiyo, nitakusifu miongoni mwa watu wamataifa. Nitaziimba sifa za jina lako.” 10 TenaMaandiko yasema: “Furahini, enyi watu wamataifa; furahini pamoja na watu wake.” 11 Natena: “Enyi mataifa yote, msifuni Bwana; enyiwatu wote, msifuni.” 12 Tena Isaya asema:

WARUMI 15:12

125

Page 126: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

“Atatokea mtu katika ukoo wa Yese, nayeatawatawala watu wa mataifa; naowatamtumainia.” 13 Basi, Mungu aliye msingiwa matumaini, awajazeni furaha yote naamani kutokana na imani yenu; tumaini lenulipate kuongezeka kwa nguvu ya RohoMtakatifu. 14 Ndugu zangu, mimi binafsi ninahakika kwamba ninyi pia mmejaa wema, elimuyote, na mnaweza kushauriana ninyi kwa ninyi.15 Lakini nimewaandikia hapa na pale katikabarua hii bila woga, nipate kuwakumbushenijuu ya mambo fulani. Nimefanya hivyo kwasababu ya neema aliyonijalia Mungu 16 yakuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wamataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiriHabari Njema ya Mungu ili watu wa mataifamengine wapate kuwa dhabihu inayokubaliwana Mungu, dhabihu iliyotakaswa na RohoMtakatifu. 17 Kwa hiyo, nikiwa nimeungana naKristo Yesu, naweza kujivunia huduma yangukwa ajili ya Mungu. 18 Sithubutu kusema kitukingine chochote isipokuwa tu kile ambachoKristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi iliwatu wa mataifa wapate kutii. Amefanya hivyokwa maneno na vitendo, 19 kwa nguvu yamiujiza na maajabu, na kwa nguvu ya Roho waMungu. Basi, kwa kusafiri kila mahali, tangukule Yerusalemu mpaka Iluriko, nimeihubirikikamilifu Habari Njema ya Kristo. 20 Niayangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njemapopote pale ambapo jina la Kristo halijapatakusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtumwingine. 21 Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: “Watu wote ambaohawakuambiwa habari zote wataona; nao waleambao hawajapata kusikia, wataelewa.” 22

Kwa sababu hiyo nilizuiwa mara nyingi kujakwenu. 23 Lakini maadam sasa nimemalizakazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miakamingi nimekuwa na nia kubwa ya kuja kwenu,24 natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependakuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania nakupata msaada wenu kwa safari hiyo baada yakufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi. 25

Lakini, kwa sasa nakwenda kuwahudumiawatu wa Mungu kule Yerusalem. 26 Maanamakanisa ya Makedonia na Akaya yemeamuakutoka mchango wao kuwasaidia watu waMungu walio maskini huko Yerusalem. 27 Waowenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini,kwa kweli, hilo ni jukumu lao kwa hao. Maana,ikiwa watu wa mataifa mengine wameshirikibaraka za kiroho za Wayahudi, wanapaswa naopia kuwahudumia Wayahudi katika mahitajiyao ya kidunia. 28 Nitakapokwisha tekelezakazi hiyo na kuwakabidhi mchango huouliokusanywa kwa ajili yao, nitawatembeleenininyi nikiwa safarini kwenda Spania. 29 Najuaya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wabaraka za Kristo. 30 Basi, ndugu zangu,nawasihi kwa kwa ajili ya Bwana wetu YesuKristo, na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho,mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.

31 Ombeni nipate kutoka salama miongonimwa wale wasioamini walioko Uyahudi, nayohuduma yangu huko Yerusalem ipatekukubaliwa na watu wa Mungu walioko huko.32 Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kujakwenu na moyo wa furaha, nikapumzikepamoja nanyi. 33 Mungu aliye chanzo chaamani na awe nanyi nyote! Amina!

Napenda kumjulisha kwenu dada yetuFoibe ambaye ni mtumishi katikakanisa la Kenkrea. 2 Mpokeeni kwa

ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu waMungu. Mpeni msaada wowote atakaohitajikutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwemasana kwa watu wengi na kwangu pia. 3

Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula,wafanyakazi wenzangu katika utumishi waKristo Yesu. 4 Wao walihatarisha maisha yaokwa ajili yangu. Wanastahili shukrani; si tukutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisayote ya watu wa mataifa mengine. 5 Salamuzangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbanikwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yanguEpaineto ambaye ni kwa kwanza katika mkoawa Asia kumwamini Kristo. 6 Nisalimieni Mariaambaye amefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.7 Salamu zangu kwa Androniko na Yunia,wananchi wenzangu waliofungwa gerezanipamoja nami; wao wanajulikana sana kati yamitume; tena walikuwa Wakristo kabla yangumimi. 8 Salamu zangu kwa Ampliato, rafikiyangu katika kuungana na Bwana. 9 Salamuzangu zimfikie Urbano, mfanyakazimwenzangu katika utumishi wa Kristo; salamuzangu pia kwa rafiki yangu Staku. 10

Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwaKristo umethibitishwa. Salamu zangu kwawote walio nyumbani mwa Aristobulo. 11

Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchimwenzangu; na kwa jamaa yote ya Narkisiiliyojiunga na Bwana. 12 Nisalimieni Trufenana Trufosa wanaofanya kazi katika utumishi waBwana, na rafiki yangu Persi ambayeamefanya mengi kwa ajili ya Bwana. 13

Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kaziya Bwana, na mama yake ambaye ni mamayangu pia. 14 Nisalimieni Asunkrito, Flegoni,Herme Patroba, Herma na ndugu wote waliopamoja nao. 15 Nisalimieni Filologo na Yulia,Nerea na dada yake, na Olumpa, pamoja nawatu wote wa Mungu walio pamoja nao. 16

Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa ishara yaupendo. Salamu kwenu kutoka kwa makanisayote ya Kristo. 17 Ndugu zangu, nawasihimuwafichue wote wanaosababishamafarakano na kuwafanya watu wenginewaanguke, kinyume cha mafundishomliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao, 18

maana watu wa namna hiyo hawamtumikiiKristo Bwana wetu, bali wanayatumikiamatumbo yao wenyewe. Kwa maneno yaomatamu na hotuba za kubembelezahupotosha mioyo ya watu wanyofu. 19 Kila

WARUMI 15:13

126

Page 127: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyommekuwa sababu ya furaha yangu.Nawatakeni muwe na hekima katika mambomema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.20 Naye Mungu aliye chanzo cha amanihatakawia kumponda Shetani chini ya miguuyenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwenanyi. 21 Timotheo, mfanyakazi mwenzangu,anawasalimu. Hali kadhalika Lukio, Yasoni, naSosipatro, wananchi wenzangu,wanawasalimu. 22 Nami Tertio, ninayeandikabarua hii nawasalimuni katika Bwana. 23 Gayo,mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lotelinalokutana kwake, anawasalimu. Erasto,mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto,

wanawasalimu. 24 Neema ya Bwana wetu YesuKristo iwe nanyi nyote. Amina. 25 Basi, sasa natumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarishenikatika ile Habari Njema niliyohubiri juu yaujumbe wa Yesu Kristo, na katika ile siriiliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichikakwa karne nyinyi zilizopita. 26 Lakini, sasaukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandikoya manabii; na kwa amri ya Mungu wa mileleumedhihirisha kwa mataifa yote ili wotewaweze kuamini na kutii. 27 Kwake Mungualiye peke yake mwenye hekima, uwe utukufukwa njia ya Yesu Kristo, milele na milele!Amina.

WARUMI 16:27

127

Page 128: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

1 WAKORINTHO

Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume waKristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, nandugu Sosthene, 2 tunawaandikia ninyi

mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Ninyimmefanywa watakatifu katika kuungana naKristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu,pamoja na watu wote popote wanaomwombaBwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao nawetu pia. 3 Nawatakieni neema na amanikutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetuYesu Kristo. 4 Ninamshukuru Mungu wangudaima kwa ajili yenu kwa sababuamewatunukia ninyi neema yake kwa njia yaKristo Yesu. 5 Maana, kwa kuungana na Kristommetajirishwa katika kila kitu. Mmejaliwaelimu yote na uwezo wote wa kuhubiri, 6

kwani, ujumbe juu ya Kristo umethibitishwandani yenu, 7 hata hampungukiwi kipajichochote cha kiroho mkiwa mnangojeakufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 8

Yeye atawaimarisha ninyi mpaka mwishompate kuonekana bila hatia Siku ile ya Bwanawetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu; yeyealiwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae YesuKristo Bwana wetu. 10 Ndugu, ninawasihi kwajina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni nyotekatika kila jambo msemalo; yasiwekomafarakano kati yenu; muwe na fikira moja nania moja. 11 Ndugu zangu, habari nilizopatakutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe,zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewanakati yenu. 12 Nataka kusema hivi: kila mmojaanasema chake: mmoja husema, “Mimi ni waPaulo,” mwingine: “Mimi ni wa Apolo,”mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine:“Mimi ni wa Kristo,”. 13 Je, Kristoamegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulubiwakwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina laPaulo? 14 Namshukuru Mungu kwambasikumbatiza mtu yeyote miongoni mwenuisipokuwa tu Krispo na Gayo. 15 Kwa hiyohakuna awezaye kusema amebatizwa kwa jinalangu. 16 (Samahani, nilibatiza pia jamaa yaStefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kamanilimbatiza mtu mwingine yeyote.) 17 Kristohakunituma kubatiza, bali kuhubiri HabariNjema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifaya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo chaKristo msalabani isibatilishwe. 18 Maanaujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani nijambo la kipumbavu kwa wale walio katikamkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tuliokatika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu ya

Mungu. 19 Maana Maandiko Matakatifuyasema: “Nitaiharibu hekima yao wenyehekima, na elimu ya wataalamu nitaitupiliambali.” 20 Yu wapi basi, mwenye hekima? Yuwapi basi, mwalimu wa Sheria? Naye bingwawa mabishano wa nyakati hizi yuko wapi?Mungu ameifanya hekima ya ulimwengu kuwaupumbavu. 21 Maana, kadiri ya hekima yaMungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwanjia ya hekima yao wenyewe. Badala yake,Mungu amependa kuwaokoa walewanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenyehekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaaniujumbe tunaohubiri. 22 Wayahudi wanatakaishara, na Wagiriki wanatafuta hekima; 23

lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa.Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwawatu wa mataifa ni upumbavu; 24 lakini kwawale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristoni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25

Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu waMungu, kina busara zaidi kuliko hekima yabinadamu; na kinachoonekana kuwa niudhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kulikonguvu za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeniwakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwawenye hekima hata kwa fikira za binadamu;wengi hawakuwa wenye nguvu au watu watabaka ya juu. 27 Ndiyo kusema, Mungualiyachagua yale ambayo ulimwengu huyaonani upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; naaliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaonani dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu. 28

Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikiraza dunia ni mambo yaliyo duni nayanayodharauliwa, mambo ambayo hatahayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yaleambayo kwa fikira za binadamu ni mambo yamaana. 29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivuniachochote mbele ya Mungu. 30 Mungumwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi naKristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awehekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwana Mungu, tunakuwa watu wake Mungu nakukombolewa. 31 Basi, kama yasemavyoMaandiko Matakatifu: “Mwenye kutakakujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana.”

Ndugu, mimi nilipokuja kwenusikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungukwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima

ya binadamu. 2 Nilipokuwa kwenu niliamuakutojua chochote kile isipokuwa tu kumjuaYesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa. 3

1 WAKORINTHO 1:2

128

Page 129: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu,natetemeka kwa hofu nyingi. 4 Hotuba zanguna mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno yakuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitishomwingi na nguvu ya Roho. 5 Nilifanya hivyokusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu yaMungu, na si hekima ya binadamu. 6 Hatahivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwawale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo siya hapa duniani, wala si ya watawala wa duniahii ambao wako katika mkumbo wa kupotea. 7

Hekima tunayotumia ni hekima ya siri yaMungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungualiiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufuwetu. 8 Ni hekima ambayo watawala wa duniahii hawakuielewa; maana wangalielewa,hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu. 9

Lakini, ni kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapatakuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayobinadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayondiyo Mungu aliyowatayarishia walewampendao.” 10 Hayo ndiyo mambo Mungualiyotufunulia kwa njia ya Roho wake. MaanaRoho huchunguza kila kitu hata mambo yandani kabisa ya Mungu. 11 Nani awezayekujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa rohoyake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuayemambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.12 Sasa sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu,bali tumepokea Roho atokaye kwa Mungu iliatuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu.13 Basi sisi twafundisha, si kwa manenotuliyofundishwa kwa hekima ya binadamu, balikwa maneno tuliyofundishwa na Roho,tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio nahuyo Roho. 14 Mtu wa kidunia hapokei mamboya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambohayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake;maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaadawa Roho. 15 Lakini mtu aliye na huyo Rohoanaweza kubainisha ubora wa kila kitu, nayemwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine. 16

Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamuakili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?”Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.

Ndugu, mimi sikuweza kusema nanyikama watu mlio na huyo Roho.Nilipaswa kusema nanyi kama watu wa

kidunia, kama watoto wachanga katika maishaya Kikristo. 2 Ilinibidi kuwalisheni kwa maziwa,na si kwa chakula kigumu, kwani hamkuwatayari kukipokea. Hata sasa hamko tayari. 3

Maana bado mu watu wa kidunia. Je, si kwelikwamba bado uko wivu na magombano katiyenu? Mambo hayo yanaonyesha wazikwamba ninyi bado ni watu wa kidunia,mnaishi mtindo wa kidunia. 4 Mmoja wenuanaposema, “Mimi ni wa Paulo”, na mwingine,“Mimi ni wa Apolo”, je, hiyo haionyeshikwamba mnaishi bado kama watu wa dunia hiitu? 5 Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Sisi niwatumishi tu ambao tuliwaleteeni ninyi imani.

Kila mmoja wetu anafanya kazi aliyopewa naBwana. 6 Mimi nilipanda mbegu, Apoloakamwagilia maji; lakini aliyeiotesha mbegu niMungu. 7 Wa maana si yule aliyepandambegu, au yule aliyemwagilia maji; wa maanani Mungu aliyeiwezesha mbegu kuota. 8 Yulealiyepanda na yule aliyemwagilia maji wote nisawa, ingawa kila mmoja atapokea tuzo lakekufuatana na jitihada yake mwenyewe. 9

Maana sisi ni ndugu, wafanyakazi pamoja naMungu; na ninyi ni shamba lake; ninyi ni jengolake. 10 Kwa msaada wa neema aliyonipaMungu, nimefaulu, kama mwashi stadimwenye busara, kuweka msingi ambao juuyake mtu mwingine anajenga. Basi, kila mmojaawe mwangalifu jinsi anavyojenga juu yake. 11

Hakuna mtu awezaye kuweka msingimwingine badala ya ule uliokwisha wekwa,yaani Yesu Kristo. 12 Juu ya msingi huo mtuanaweza kujenga kwa dhahabu, fedha aumawe ya thamani; anaweza kutumia miti,majani au nyasi. 13 Iwe iwavyo, ubora wa kaziya kila mmoja utaonekana wakati Siku ile yaKristo itakapoifichua. Maana, Siku hiyoitatokea na moto, na huo moto utaipima nakuonyesha ubora wake. 14 Ikiwa alichojengamtu juu ya huo msingi kitaustahimili huomoto, atapokea tuzo; 15 lakini kamaalichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzolake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kanakwamba ameponyoka kutoka motoni. 16 Je,hamjui kwamba ninyi ni hekalu la Mungu, nakwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?17 Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamharibu; maana hekalu la Munguni takatifu, na hekalu hilo ni ninyi wenyewe. 18

Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenuakijidhania mwenye hekima mtindo wakidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa nahekima ya kweli. 19 Maana, hekima ya kiduniani upumbavu mbele ya Mungu. KwaniMaandiko Matakatifu yasema: “Munguhuwanasa wenye hekima katika ujanja wao.”20 Na tena: “Bwana ajua kwamba mawazo yawenye hekima hayafai.” 21 Basi, mtu asijivuniewatu. Maana kila kitu ni chenu. 22 Paulo, Apolona Kefa, ulimwengu, maisha na kifo; mamboya sasa na ya baadaye, yote ni yenu. 23 Lakinininyi ni wa Kristo naye Kristo ni wa Mungu.

Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishiwa Kristo tuliokabidhiwa siri za mungu.2 Kinachotakiwa kwa yeyote yule

aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu. 3

Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na ninyi, auna mahakama ya kibinadamu; walasijihukumu. 4 Dhamiri yangu hainishtaki kwajambo lolote, lakini hiyo haionyeshi kwambasina lawama. Bwana ndiye anayenihukumu. 5

Basi, msihukumu kabla ya wakati wake achenimpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichuamambo ya giza yaliyofichika, na kuonyeshawazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mmojaatapata sifa anayostahili kutoka kwa Mungu. 6

1 WAKORINTHO 4:6

129

Page 130: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

6

Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo najuu yangu, ni kielelezo kwenu: kutokana namfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewemaana ya msemo huu: “Zingatieniyaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtuyeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharaumwingine. 7 Nani amekupendelea wewe? Unakitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwaumepewa, ya nini kujivunia kana kwambahukukipewa? 8 Haya, mmekwisha shiba!Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalmebila ya sisi! Naam, laiti mngekuwa kweliwatawala, ili nasi pia tuweze kutawala pamojananyi. 9 Nafikiri Mungu ametufanya sisimitume tuwe watu wa mwisho kabisa, kamawatu waliohukumiwa kuuawa, maanatumekuwa tamasha mbele ya ulimwenguwote, mbele ya malaika na watu. 10 Sisi niwapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi niwenye busara katika kuungana na Kristo! Sisini dhaifu, ninyi ni wenye nguvu. Ninyimnaheshimika, sisi tunadharauliwa. 11 Mpakadakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo,twapigwa makofi, hatuna malazi. 12 Tenatwataabika na kufanya kazi kwa mikono yetuwenyewe. Tukitukanwa, tunawatakia baraka;tukidhulumiwa, tunavumilia; 13 tukisingiziwa,tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewakama uchafu wa dunia; na kwa kila mtu sisi nitakataka! 14 Siandiki mambo haya kwa ajili yakuwaaibisha ninyi, bali kwa ajili yakuwafundisheni watoto wangu wapenzi. 15

Maana hata kama mnao maelfu ya walezikatika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu nimmoja tu, kwani katika maisha ya Kikristomimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri HabariNjema. 16 Kwa hiyo, nawasihi: fuateni mfanowangu. 17 Ndiyo maana nimemtuma Timetheokwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi namwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheninjia ninayofuata katika kuishi maisha yaKikristo; njia ninayofundisha kila mahali katikamakanisa yote. 18 Baadhi yenu wameanzakuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakujatena kwenu. 19 Lakini, Bwana akipenda,nitakuja kwenu upesi; na hapo ndiponitakapojionea mwenyewe, sio tu kilewanachoweza kusema hao wenye majivuno,bali pia kila wanachoweza kufanya. 20 MaanaUtawala wa Mungu si shauri la manenomatupu, bali ni nguvu. 21 Mnapendelea lipi?Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo waupendo na upole?

Ziko habari za kuaminika kwamba kunauzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzimbaya ambao haujapata kuwako hata

kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwaeti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!2 Mnawezaje kujivuna? Ingekuwa afadhalikwenu kuomboleza, na huyo aliyefanya kituhicho aondolewe miongoni mwenu. 3 Nami,kwa upande wangu, ingawa kwa mwili nikombali nanyi, hata hivyo kwa roho niko hapo

pamoja nanyi: na hivyo, kama vile nipo hapo,nimekwisha mhukumu huyo aliyefanya jambohilo la aibu. 4 Wakati mnapokusanyika pamojakwa jina la Bwana Yesu, nami nikiwa pamojananyi kwa roho, basi, kwa uwezo wa Bwanawetu Yesu, 5 mkabidhini mtu huyo kwaShetani ili mwili wake uharibiwe na roho yakeiweze kuokolewa Siku ile ya Bwana. 6 Majivunoyenu hayafai! Je, hamjui kwamba chachukidogo huchachusha donge lote la unga? 7

Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ilimpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachukama mnavyopaswa kuwa; maana, Kristo,Pasaka yetu, amekwisha tolewa tambiko. 8

Basi, tufanye karamu hiyo si kwa chachu ile yakale, chachu ya ubaya na uovu, bali kwa mkateusiotiwa chachu, mkate wa usafi na kweli. 9

Niliwaandikia katika barua yangu msishirikianena wazinzi. 10 Ukweli ni kwamba sikuwa namaana ya watu wote duniani walio wazinzi,wachoyo, walaghai na wenye kuabudusanamu. Maana, ili kuwaepa hao woteingewalazimu ninyi kuihama dunia hii kabisa!11 Nilichoandika ni hiki: msishirikiane nandugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenyekuabudu sanamu, mchongezi mlevi namlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msilenaye. 12 Je, ni shauri langu kuwahukumu watuwalio nje? Hao Mungu atawahukumu. Je, ninyihampaswi kuwahukumu wale walio katikajamii yenu ninyi wenyewe? 13 Mfukuzeni mbalinanyi huyo mwovu!

Anathubutuje mmoja wenu kumshtakindugu muumini mbele ya mahakamaya watu wasiomjua Mungu badala ya

kumshtaki mbele ya watu wa Mungu? 2 Je,hamjui kwamba watu wa Munguwatauhukumu ulimwengu? Ikiwa basi,ulimwengu utahukumiwa nanyi, kwa ninihamstahili kuhukumu hata katika mambomadogo? 3 Je, hamjui kwamba, licha yakuhukumu mambo ya kawaida ya kila siku,tutawahukumu hata malaika? 4 Mnapokuwana mizozo juu ya mambo ya kawaida, je,mnawaita wawe mahakimu watu ambao hatahawalijali kanisa? 5 Aibu kwenu! Ndiyo kusemahakuna hata mmoja miongoni mwenumwenye hekima kiasi cha kuweza kutatuatatizo kati ya ndugu waumini? 6 Badala yake,kweli imekuwa mtindo ndugu kumpelekandugu yake mahakamani, tena mbele yamahakimu wasioamini. 7 Kwa kweli hukokushtakiana tu wenyewe kwa wenyewekwabainisha kwamba mmeshindwa kabisa! Je,haingekuwa jambo bora zaidi kwenukudhulumiwa! Haingekuwa bora zaidi kwenukunyang'anywa mali yenu? 8 Lakini, badalayake, ninyi ndio mnaodhulumu nakunyang'anya; tena, hayo mnawafanyia nduguzenu! 9 Au je, hamjui kwamba watu wabayahawataurithi Utawala wa Mungu?Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha yauasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au

1 WAKORINTHO 4:7

130

Page 131: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

7

walawiti, 10 wevi, wachoyo, walevi,wasengenyaji, wanyang'anyi, hao wotehawatashiriki Utawala wa Mungu. 11 Baadhiyenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa,mkafanywa watakatifu, na kupatanishwa naMungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwaRoho wa Mungu wetu. 12 Mtu anawezakusema: “Kwangu mimi kila kitu ni halali.”Sawa; lakini si kila kitu kinafaa. Nakubalikwamba kila kitu ni halali kwangu lakini sitakikutawaliwa na kitu chochote. 13 Unawezakusema: “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, natumbo ni kwa ajili ya chakula.” Sawa; lakiniMungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mtu sikwa ajili ya uzinzi bali ni kwa ajili yakumtumikia Bwana, naye Bwana ni kwa ajili yamwili. 14 Basi, Mungu aliyemfufua Bwanakutoka wafu atatufufua nasi pia kwa nguvuyake. 15 Je, hamjui kwamba miili yenu niviungo vya mwili wa Kristo? Je, mnadhaninaweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristona kuifanya kuwa sehemu ya mwili wa kahaba?Hata kidogo! 16 Maana, kama mjuavyo,anayeungana na kahaba huwa mwili mmojanaye—kama ilivyoandikwa: “Nao wawiliwatakuwa mwili mmoja.” 17 Lakini aliyejiungana Bwana huwa roho moja naye. 18 Jiepushenikabisa na uzinzi. Dhambi nyingine zotehutendwa nje ya mwili lakini mzinzi hutendadhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe. 19 Je,hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la RohoMtakatifu aliye ndani yenu, ambayemlimpokea kutoka kwa Mungu? Ninyi basi, simali yenu wenyewe. 20 Mlinunuliwa kwa beikubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa ajiliya kumtukuza Mungu.

Yahusu sasa mambo yale mliyoandika:naam, ni vizuri kama mtu haoi; 2 lakinikwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi,

kila mwanamume na awe na mke wakemwenyewe, na kila mwanamke awe na mumewake mwenyewe. 3 Mume atimize wajibu alionao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alionao kwa mumewe. 4 Mke hana mamlaka juuya mwili wake, bali mumewe anayo; halikadhalika naye mume, hana mamlaka juu yamwili wake, bali mkewe anayo. 5 Msinyimanehaki zenu, isipokuwa kama mnaafikianakufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasinzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, iliShetani asije akawajaribu kwa sababu yaudhaifu wenu. 6 Ninayowaambieni sasa nimawaidha, si amri. 7 Ningependa watu wotewawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmojaanacho kipaji chake kutoka kwa Mungu;mmoja kipaji hiki na mwingine kile. 8 Basi,wale ambao hawajaoana na wale walio wajanenawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwakama mimi nilivyo. 9 Hata hivyo, kama mtuhawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhalizaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa. 10 Kwa walewaliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni yaBwana: mke asiachane na mumewe; 11 lakini

kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa;ama la, apatanishwe na mume wake. Mumenaye asimpe talaka mkewe. 12 Kwa walewengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi:Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mkeasiyeamini, na huyo mwanamke akakubalikuendelea kuishi naye, asimpe talaka. 13 Na,kama mwanamke Mkristo anaye mumeasiyeamini, na huyo mwanamume akakubalikuendelea kuishi naye, basi, asimpe talakamumewe. 14 Kwa maana huyo mumeasiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwakuungana na mkewe; na huyo mke asiyeaminihupokelewa kwa Mungu kwa kuungana namumewe. Vinginevyo watoto wao wangekuwasi wa Mungu; kumbe sasa ni watoto wakeMungu. 15 Hata hivyo, ikiwa yule asiyeaminianataka kumwacha mwenzake aliye Mkristo,basi, na amwache tu. Hapo huyo Mkristo,mume au mke, atakuwa huru. Maana Munguamewaiteni ninyi muishi kwa amani. 16 Wewemama Mkristo, unawezaje kuwa na hakikakwamba hutaweza kumwokoa mume wako?Au wewe mume Mkristo, unawezaje kuwa nahakika kwamba hutaweza kumwokoa mkeo?17 Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatanana vipaji alivyogawiwa na Bwana, na kamaalivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langukwa makanisa yote. 18 Kama mtu aliitwa akiwaametahiriwa, basi asijisingizie kwambahakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwaametahiriwa, basi na asitahiriwe. 19 Maanakutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilichomuhimu ni kuzishika amri za Mungu. 20 Basi,kila mmoja na abaki kama alivyokuwa wakatialipoitwa. 21 Je, wewe ulikuwa mtumwa wakatiulipoitwa? Sawa, usijali; lakini ukipata fursa yakuwa huru, itumie. 22 Maana yeye aliyeitwa naBwana akiwa mtumwa huyo huwa mtu huruwa Bwana. Hali kadhalika naye aliyeitwa akiwamtu huru, huwa mtumwa wa Kristo. 23 Nyotemmenunuliwa kwa bei; kwa hiyo msiwe tenawatumwa wa watu. 24 Ndugu zangu, kilammoja wenu basi, na abaki na Mungu kamaalivyokuwa wakati alipoitwa. 25 Sasa, kuhusumabikira na waseja, sina amri kutoka kwaBwana; lakini natoa maoni yangu mimiambaye kwa huruma yake Bwana nastahilikuaminiwa. 26 Basi, kutokana na shida iliyoposasa nadhani ingefaa mtu abaki kama alivyo.27 Je, umeoa? Basi, usitake kuachana na mkeo.Wewe hukuoa? Basi, usitake kuoa. 28 Lakiniikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; namsichana akiolewa hatakuwa ametendadhambi. Hao watakaooana watapatwa namatatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependahayo yasiwapate ninyi. 29 Ndugu, natakakusema hivi: muda uliobaki ni mfupi. Na tangusasa wale waliooa na waishi kama vilehawakuoa; 30 wenye kulia wawe kama hawalii,na wenye kufurahi wawe kama hawafurahi;wanaonunua wawe kama hawana kitu; 31 naowenye shughuli na dunia hii wawe kama vile

1 WAKORINTHO 7:31

131

Page 132: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

9

hawana shughuli sana nayo. Maanaulimwengu huu, kama tuujuavyo, unapita. 32

Ningependa ninyi msiwe na wasiwasi. Mtuasiye na mke hujishughulisha na kazi ya Bwanajinsi atakavyompendeza Bwana. 33 Mtu aliyeoahujishughulisha na mambo ya dunia jinsiatakavyompendeza mkewe, 34 nayeamegawanyika. Mwanamke asiyeolewa aubikira hujishughulisha na mambo ya Bwanaapate kujitolea mwili na roho kwa Bwana.Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulishana mambo ya dunia hii jinsiatakavyompendeza mumewe. 35

Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwakuwawekeeni kizuio. Nataka tu muwe nampango unaofaa, mpate kumtumikia Bwanakwa moyo na nia moja. 36 Kama mtu anaonakwamba hamtendei vyema mchumba wakeasipomwoa, na kama tamaa zake zinamshinda,na afanye atakavyo; waoane tu; hatakuwaametenda dhambi. 37 Lakini kama huyomwanamume akiamua kwa hiari moyonimwake kutooa na kama anaweza kuzitawalatamaa zake na kuamua namna ya kufanya,basi, anafanya vizuri zaidi asipomwoa huyomwenzake bikira. 38 Kwa maneno mengine:yule anayeamua kumwoa huyo mchumbawake anafanya vema; naye anayeamuakutomwoa anafanya vema zaidi. 39

Mwanamke huwa amefungwa na mumewekwa muda wote mumewe aishipo. Lakinimumewe akifa, mama huyo yuko huru, naakipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote,mradi tu iwe Kikristo. 40 Lakini, nionavyo mimi,atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyoalivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimipia ninaye Roho wa Mungu.

Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwasanamu: Tunajua kwamba sisi sote tunaujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu

wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga. 2

Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kwelihajui chochote kama inavyompasa. 3 Lakinianayempenda Mungu huyo anajulikana naye.4 Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwasanamu, twajua kwamba sanamu si kituduniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.5 Hata kama viko vitu viitwavyo miunguduniani au mbinguni, na hata kama wakomiungu na mabwana wengi, 6 hata hivyo,kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba,Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisituko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo,ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, nasisi twaishi kwa njia yake. 7 Lakini, si kila mtuanao ujuzi huu. Maana wako watu wenginewaliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpakahivi sasa wanapokula vyakula huviona badokama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Nakwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.8 Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibuzaidi na Mungu. Tukiacha kukilahatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi

kitu. 9 Lakini, jihadharini: huu uhuru wenuusiwafanye walio na imani dhaifu waangukekatika dhambi. 10 Maana, mtu ambayedhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewemwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani yahekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kulavyakula vilivyotambikiwa sanamu? 11 Hivyo,huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufakwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuziwako. 12 Kama mkiwakosesha ndugu zenujinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu,mtakuwa mmemkosea Kristo. 13 Kwa hiyo,ikiwa chakula husababisha kuanguka kwandugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisijenikamfanya ndugu yangu aanguke katikadhambi.

Je, mimi si mtu huru? Je, mimi simtume? Je, mimi sikumwona YesuBwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya

kazi yangu kwa ajili ya Bwana? 2 Hata kamakwa watu wengine mimi si mtume, lakini walaukwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi niuthibitisho wa mtume wangu kwa sababu yakuungana kwenu na Bwana. 3 Hoja yangu kwawale wanaonipinga ndiyo hii: 4 Je, hatuna hakiya kula na kunywa? 5 Je, hatuna ruhusakumchukua mke Mkristo katika ziara zetu,kama vile wafanyavyo mitume wengine, nduguzake Bwana, na pia Kefa? 6 Au ni mimi tu naBarnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahiyetu kwa kufanya kazi? 7 Je, mwanajeshi ganianayelipia utumishi wake jeshini? Mkulimagani asiyekula matunda ya shamba lake lamizabibu? Mchungaji gani asiyekunywamaziwa ya mifugo yake? 8 Je, nasema mambohaya kibinadamu tu? Je, Sheria nayo haisemihivyo? 9 Imeandikwa katika Sheria ya Mose:“Usimfunge kinywa ng'ombe anapoliwatanafaka.” Je, ndio kusema Munguanajishughulisha na ng'ombe? 10 Je, hakuwaanatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, hayayaliandikwa kwa ajili yetu; kwani yuleanayelima na yule anayevuna, wote wawiliwana haki ya kutumaini kupata sehemu yamavuno. 11 Ikiwa sisi tumepanda mbegu yakiroho kati yenu, je, ni jambo kubwa tukichumakwenu faida ya kidunia? 12 Ikiwa wenginewanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu,je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisihatukuitumia haki hiyo, Badala yake,tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizichochote Habari Njema ya Kristo. 13 Je, hamjuikwamba wanaotumikia Hekaluni hupatachakula chao Hekaluni, na kwambawanaotolea sadaka madhabahuni hupatasehemu ya hiyo sadaka? 14 Bwana aliagizavivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapateriziki zao kutokana nayo. 15 Lakini, mimisikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Nawala siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimini afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aonekwamba najisifu bure. 16 Ikiwa ninaihubiriHabari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni

1 WAKORINTHO 7:32

132

Page 133: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

jukumu nililopewa. Na, ole wangu kamasitaihubiri Habari Njema! 17 Ningekuwanimeichagua kazi hii kwa hiari, basi,ningetazamia malipo; lakini maadam naifanyaikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba nijukumu nililopewa nitekeleze. 18 Mshaharawangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu nifursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bilakudai haki ninazostahili kwa kuihubiri. 19 Kwahiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote,nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatieKristo watu wengi iwezekanavyo. 20 KwaWayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapateWayahudi; yaani, ingawa mimi siko chini yaSheria, nimejiweka chini ya Sheria kwao, iliniwapate hao walio chini ya Sheria. 21 Na kwawale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, njeya Sheria, ili niwapate hao walio nje ya Sheria.Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje yasheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria yaKristo. 22 Kwao walio dhaifu nimejifanyadhaifu ili niwapate hao walio dhaifu.Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipatekuwaokoa baadhi yao kwa kila njia. 23 Nafanyahaya yote kwa ajili ya Habari Njema, nipatekushiriki baraka zake. 24 Je, hamjui kwambakatika uwanja wa michezo, ingawa wapigambio wote hukimbia, ni mmoja tuanayejinyakulia zawadi? 25 Wanariadha hujipamazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo iliwajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanyahivyo tupate taji ya kudumu daima. 26 Ndivyobasi, ninavyopiga mbio nikiwa na nia yakushinda; ndivyo ninavyopigana, na si kamabondia anayetupa ngumi zake hewani. 27

Naupa mwili wangu mazoezi magumu nakuutia katika nidhamu kamili, nisije mimimwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiriawengine.

Ndugu, nataka mjue kwamba babuzetu wote walikuwa chini ya ulinzi walile wingu, na kwamba wote walivuka

salama ile bahari. 2 Wote walibatizwa katikaumoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari. 3

Wote walikula chakula kilekile cha kiroho, 4

wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho,maana walikunywa kutoka ule mwamba wakiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwaKristo mwenyewe. 5 Hata hivyo, wengi waohawakumpendeza Mungu, na maiti zaozilisambazwa jangwani. 6 Sasa, mambo hayoyote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisitusitamani ubaya kama wao walivyotamani. 7

Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yaowalivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko:“Watu waliketi kula na kunywa, wakasimamakucheza.” 8 Wala tusizini kama baadhi yaowalivyozini, wakaangamia siku moja watuishirini na tatu elfu. 9 Tusimjaribu Bwana kamabaadhi yao walivyomjaribu, wakauawa nanyoka. 10 Wala msinung'unike kama baadhiyao walivyonung'unika, wakaangamizwa naMwangamizi! 11 Basi, mambo hayo

yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, nayaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwishowa nyakati unatukabili. 12 Anayedhaniamesimama imara ajihadhari asianguke. 13

Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwabinadamu. Mungu ni mwaminifu, nayehataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ilapamoja na majaribu, yeye atawapeni pianguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humosalama. 14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeniibada za sanamu. 15 Naongea nanyi, watuwenye busara; jiamulieni wenyewe hayonisemayo. 16 Tunapomshukuru Mungu kwakikombe kile cha baraka, je, huwa hatushirikidamu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je,huwa hatushiriki mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwamkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tumwili mmoja; maana sote twashiriki mkatehuohuo. 18 Chukueni, kwa mfano, Wayahudiwenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwamadhabahuni waliungana na hiyomadhabahu. 19 Nataka kusema nini, basi?Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu nikitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, nikitu kweli zaidi ya sanamu? 20 Hata kidogo!Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoawatu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo,sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe naushirika na pepo. 21 Hamwezi kunywakikombe cha Bwana na kikombe cha pepo;hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana nakatika meza ya pepo. 22 Au je, tunatakakumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tunanguvu zaidi kuliko yeye? 23 Vitu vyote ni halali,lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakinisi vyote vinajenga. 24 Mtu asitafute faida yakemwenyewe, ila faida ya mwenzake. 25 Kulenichochote kile kiuzwacho sokoni bila yakuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu; 26

maana Maandiko yasema: “Dunia na vyotevilivyomo ni mali ya Bwana.” 27 Kama mtuambaye si muumini akiwaalikeni nanyimkakubali kwenda, basi, kuleni vyoteatakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwasababu ya dhamiri zenu. 28 Lakini mtuakiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwasanamu,” basi, kwa ajili ya huyoaliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri,msile. 29 Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” sidhamiri yenu, bali dhamiri yake huyoaliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwa nini uhuruwangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?30 Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho hukunamshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwachakula ambacho kwa ajili yakenimemshukuru Mungu?” 31 Basi, chochotemfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yotekwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwekikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwakanisa la Mungu. 33 Muwe kama mimi;najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bilakutafuta faida yangu mwenyewe ila faida yawote, wapate kuokolewa.

1 WAKORINTHO 10:33

133

Page 134: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

12

Niigeni mimi kama ninavyomwigaKristo. 2 Nawapeni hongera kwasababu mnanikumbuka na kwa

sababu mnayashikilia yale maagizoniliyowapeni. 3 Lakini napenda pia mjuekwamba Kristo ni kichwa cha kilamwanamume, na mwanamume ni kichwa chamkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. 4 Basi,kila mwanamume anayesali au anayetangazaujumbe wa Mungu huku amefunika kichwachake, huyo anamdharau Kristo. 5 Namwanamke akisali au kutangaza ujumbe waMungu bila kufunika kichwa chake,anamdharau mumewe; anayefanya hivyo nisawa tu na mwanamke aliyenyoa kichwachake. 6 Mwanamke asiyefunika kichwa chake,afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwamwanamke kukatwa nywele zake aukunyolewa; basi, afadhali afunike kichwachake. 7 Haifai mwanamume kufunika kichwachake, kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu nakioo cha utukufu wake Mungu; lakinimwanamke ni kioo cha utukufu wamwanamume. 8 Mwanamume hakutoka kwamwanamke, ila mwanamke alitoka kwamwanamume. 9 Mwanamume hakuumbwakwa ajili ya mwanamke, ila mwanamkealiumbwa kwa ajili ya mwanamume. 10 Ndiyomaana mwanamke hufunika kichwa chake, iweishara ya mamlaka yaliyo juu yake, na pia kwasababu ya malaika. 11 Hata hivyo, mbele yaBwana mwanamke si kitu bila mwanamume,naye mwanamume si kitu bila mwanamke. 12

Kama vile mwanamke alivyotokana namwanamume, vivyo hivyo mwanamumehuzaliwa na mwanamke; kila kitu hutoka kwaMungu. 13 Amueni wenyewe: Je, inafaamwanamke kumwomba Mungu bila kuvaa kitukichwani? 14 Hata maumbile yenyewehuonyesha wazi kwamba kwa mwanamumekuwa na nywele ndefu ni aibu kwakemwenyewe; 15 lakini kwa mwanamke kuwa nanywele ni heshima kwake; nywele zake ndefuamepewa ili zimfunike. 16 Kama mtu anatakakuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajuekwamba sisi hatuna desturi nyingine, walamakanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.17 Nikiwa bado nawapeni maagizo haya,siwezi hata kidogo kuwapa ninyi hongerakuhusu haya yafuatayo: mikutano yenu ninyiwaumini yaleta hasara zaidi kuliko faida. 18

Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutanapamoja hutokea mafarakano kati yenu. Naminaamini kiasi, 19 maana ni lazima fikira tofautiziweko miongoni mwenu, ili wale walio thabitiwapate kutambulikana. 20 Kweli mnakutana,lakini si kwa ajili ya kula chakula cha Bwana! 21

Maana mnapokula kila mmoja hukikaliachakula chake mwenyewe, hata hutokeakwamba baadhi yenu wana njaa, na wenginewamelewa! 22 Je, hamwezi kula na kunywanyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa laMungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu?

Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusujambo hili. 23 Maana mimi nilipokea kwaBwana yale maagizo niliyowaachieni: kwamba,usiku ule Bwana Yesu aliotolewa, alitwaamkate, 24 akamshukuru Mungu, akaumega,akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajiliyenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” 25 Vivyohivyo, baada ya kula, akatwaa kikombeakasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipyalinalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyenihivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”26 Maana kila mnapokula mkate huu nakunywa kikombe hiki, mwatangaza kifo chaBwana, mpaka atakapokuja. 27 Kwa hiyo, kilaaulaye mkate huo au kunywa kikombe chaBwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi yamwili na damu ya Bwana. 28 Basi, kila mtuajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo alemkate huo na anywe kikombe hicho; 29 maanaanayekula na kunywa bila kutambua maana yamwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumuyake yeye mwenyewe. 30 Ndiyo maana wengikati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wenginekadhaa wamekufa. 31 Kama tungejichunguzawenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo. 32

Lakini tunapohukumiwa na Bwana,tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusijetukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33 Kwahiyo, ndugu zangu, mnapokutana kula chakulacha Bwana, kila mmoja amngoje mwenzake.34 Na kama kuna yeyote aliye na njaa, na alenyumbani kwake, ili kukutana kwenukusisababishe hukumu. Lakini, kuhusu yalemambo mengine, nitawapeni maelezonitakapokuja.

Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho,napenda mfahamu vizuri mambohaya: 2 Mnajua kwamba, kabla ya

kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwana sanamu tupu. 3 Basi, jueni kwamba mtuyeyote anayeongozwa na Roho wa Munguhawezi kusema: “Yesu alaaniwe!” Halikadhalika, mtu yeyote hawezi kusema: “Yesu niBwana,” asipoongozwa na Roho Mtakatifu. 4

Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakiniRoho avitoaye ni mmoja. 5 Kuna namna nyingiza kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa nimmoja. 6 Kuna namna mbalimbali za kufanyakazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja,anayewezesha kazi zote katika wote. 7 Kilamtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida yawote. 8 Roho humpa mmoja ujumbe wahekima, na mwingine ujumbe wa elimuapendavyo Roho huyohuyo. 9 Roho huyohuyohumpa mmoja imani, na humpa mwinginekipaji cha kuponya; 10 humpa mmoja kipajicha kufanya miujiza, mwingine kipaji chakusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipajicha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho navisivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji chakusema lugha ngeni, na mwingine kipaji chakuzifafanua. 11 Hizo zote ni kazi za Rohohuyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu

1 WAKORINTHO 11:2

134

Page 135: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

14

kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe. 12

Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungovingi, na viungo hivyo vyote—ingawaje nivingi—hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo piakwa Kristo. 13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi auwatu wa mataifa mengine, watumwa au watuhuru, sote tumebatizwa kwa Roho mmojakatika mwili huo mmoja; na sotetukanyweshwa Roho huyo mmoja. 14 Mwilihauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.15 Kama mguu ungejisemea: “Kwa kuwa mimisi mkono, basi mimi si mali ya mwili”, je,ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!16 Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi sijicho, basi mimi si mali ya mwili”, je, kwa hojahiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La! 17

Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikiolingekuwa wapi? Na kama mwili woteungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa? 18

Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemuhizo tofauti katika mwili kama alivyopenda. 19

Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja,mwili ungekuwa wapi? 20 Ukweli ni kwamba,sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili nimmoja. 21 Basi, jicho haliwezi kuuambiamkono: “Sikuhitaji wewe”, wala kichwahakiwezi kuiambia miguu: “Siwahitaji ninyi.” 22

Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemuzile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifundizo zilizo muhimu zaidi. 23 Tena, viungo viletunavyovifikiria kuwa havistahili heshimakubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifuzaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekanikuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi, 24

ambapo viungo vingine havihitajikushughulikiwa. Mungu mwenyeweameuweka mwili katika mpango, akakipaheshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwaheshima, 25 ili kusiweko na utengano katikamwili bali viungo vyote vishughulikiane. 26

Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyotehuumia pamoja nacho. Kiungo kimojakikisifiwa viungo vingine vyote hufurahipamoja nacho. 27 Basi, ninyi nyote ni mwili waKristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwilihuo. 28 Mungu ameweka katika kanisa:kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu;kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanyamiujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenyekusema lugha ngeni. 29 Je, wote ni mitume?Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote niwenye kipaji cha kufanya miujiza? 30 Je, woteni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenyekipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wotehufafanua lugha? 31 Muwe basi, na tamaa yakupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasanitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizizote.

Hata kama nikinena lugha za watu nahata za malaika, lakini kama sinaupendo mimi nimekuwa tu kama

sauti ya debe tupu au kengele. 2 Tena, nawezakuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa

Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu;naweza kuwa na imani yote hata nikawezakuihamisha milima, lakini kama sina upendomimi si kitu. 3 Nikitoa mali yangu yote nakuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wanguuchomwe, kama sina upendo hiyo hainifaichochote. 4 Mwenye upendo huvumilia,hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai,wala hajivuni. 5 Mwenye upendo hakosiadabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hanawepesi wa hasira; haweki kumbukumbu yamabaya, 6 hafurahii uovu, bali hufurahiaukweli. 7 Mwenye upendo huvumilia yote,huamini yote, na hustahimili yote. 8 Upendohauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vyakutangaza ujumbe wa Mungu, hivyovitatoweka siku moja; kama ni vipaji vyakusema lugha ngeni, vitakoma; kama kunaelimu, nayo itapita. 9 Maana ujuzi wetu sikamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno laMungu si kamili. 10 Lakini kile kilicho kikamilifukitakapofika, vyote visivyo vikamilifuvitatoweka. 11 Nilipokuwa mtoto mchanganilisema kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikirikitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtumzima, mambo ya kitoto nimeyaacha. 12

Tunachoona sasa ni kama tu sura hafifu katikakioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwauso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapobaadaye nitajua yote kikamilifu, kama vileMungu anavyonijua mimi. 13 Sasa yanadumuhaya matatu: imani, tumaini na upendo; lakinilililo kuu kupita yote ni upendo.

Jitahidini kuwa na upendo. Vilevilefanyeni bidii ya kupata vipaji vinginevya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza

ujumbe wa Mungu. 2 Mwenye kunena lughangeni hasemi na watu bali anasema naMungu. Yeye hunena kwa nguvu ya Rohomambo yaliyofichika. 3 Lakini mwenye kipajicha kutangaza ujumbe wa Mungu, husema nawatu kwa ajili ya kuwajenga, kuwafariji nakuwatia moyo. 4 Mwenye kunena lugha ngenianajijenga mwenyewe. Lakini mwenye kipajicha kutangaza ujumbe wa Mungu, analijengakanisa. 5 Basi, ningependa ninyi nyote msemekwa lugha ngeni lakini ningependelea hasamuwe na kipaji cha kutangaza ujumbe waMungu, maana mtu mwenye kipaji chakutangaza ujumbe wa Mungu, ni wa maanazaidi kuliko yule mwenye kusema lugha ngeni,isipokuwa tu kama yupo hapo mtu awezayekuyafafanua hayo mambo asemayo, ili kanisalipate kujengwa. 6 Hivyo, ndugu zangu, kamanikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeniitawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwatu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu auujuzi fulani au ujumbe wa Mungu aumafundisho fulani. 7 Ndivyo ilivyo kwavyombo visivyo na uhai vyenye kutoa sautikama vile filimbi au kinanda. Je, mtu anawezajekuutambua wimbo unaochezwa kama vyombohivyo havitoi sauti waziwazi vinapopigwa? 8 La

1 WAKORINTHO 14:8

135

Page 136: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

15

mgambo likilia bila kufuata taratibu zake, naniatajiweka tayari kwa vita? 9 Hali kadhalika naninyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenyekueleweka, nani ataweza kufahamumnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.10 Zipo lugha mbalimbali ulimwenguni, nahakuna hata mojawapo isiyo na maana. 11

Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lughaasemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtuhuyo naye pia ni mgeni kwangu. 12 Halikadhalika na ninyi, maadam mna hamu yakupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatiavile vinavyosaidia kulijenga kanisa. 13 Kwahiyo, mwenye kunena lugha ngeni na aombeapate uwezo wa kuzifafanua. 14 Maana,nikisali kwa lugha ngeni roho yangu ndiyoinayosali, lakini akili yangu hubaki bure. 15

Nifanye nini, basi? Nitasali kwa roho yangu,nitasali pia kwa akili yangu; nitaimba kwa rohoyangu, nitaimba pia kwa akili yangu. 16

Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezajemtu wa kawaida aliye katika mkutano kuitikiasala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina,”kama haelewi unachosema? 17 Sala yako yashukrani yaweza kweli kuwa bora, lakini huyomwingine haitamfaidia. 18 NamshukuruMungu kwamba mimi nasema kwa lughangeni zaidi kuliko ninyi nyote. 19 Lakini katikamikutano ya waumini napendelea zaidikusema maneno matano yenye kueleweka iliniwafundishe wengine, kuliko kusema manenoelfu ya lugha ngeni. 20 Ndugu, msiwe kamawatoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu muwekama watoto wachanga lakini katika kufikiri nilazima muwe kama watu waliokomaa. 21

Imeandikwa katika Sheria: “Bwana asema hivi:Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwamidomo ya wageni, nitasema na watu hawa,hata hivyo, hawatanisikiliza.” 22 Hivyo basi,kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwaajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya walewasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbewa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini nasi kwa ajili ya wasioamini. 23 Basi, kanisa lotelinapokutana pamoja, na wote wakaanzakusema kwa lugha ngeni, kama wakija watuwa kawaida au wasioamini, je, hawatasemakwamba ninyi mna wazimu? 24 Lakini, wotewakiwa wanautangaza ujumbe wa Mungu,akija mtu wa kawaida au asiyeamini, yoteatakayosikia yatamhakikishia ubaya wakemwenyewe; yote atakayosikia yatamhukumu.25 Siri za moyo wake zitafichuliwa, nayeatapiga magoti na kumwabudu Munguakisema: “Kweli Mungu yupo pamoja nanyi.”26 Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutanapamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoemafundisho, mwingine awe na ufunuo kutokakwa Mungu, mwingine atumie kipaji chakusema kwa lugha ngeni na mwingineafafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili yakulijenga kanisa. 27 Wakiwepo watu wenyevipaji vya kusema kwa lugha ngeni, waseme

wawili au watatu, si zaidi, tena mmojammoja;na aweko mtu wa kufafanua yanayosemwa. 28

Lakini kama hakuna awezaye kufafanua, basi,mwenye kusema lugha ngeni anyamazemkutanoni, aseme na nafsi yake mwenyewe naMungu. 29 Kuhusu wale wenye kipaji chakutangaza ujumbe wa Mungu, waseme wawiliau watatu, na wengine wayapime maneno yao.30 Ikiwa mmoja anaposema mwingine wawasikilizaji amepata ufunuo kutoka kwaMungu, basi, yule anayesema anyamaze. 31

Maana nyote mwaweza kutangaza ujumbe waMungu, mmoja baada ya mwingine, ili nyotempate kujifunza na kutiwa moyo. 32 Kipaji chakutangaza ujumbe wa Mungu ni lazimakitawaliwe na huyo mwenye hicho kipaji. 33

Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani.34 Kama ilivyo desturi katika makanisa yote yawatu wa Mungu, wanawake wakae kimyakatika mikutano ya waumini. Hawana ruhusakusema; ila wawe watii kama isemavyo Sheria.35 Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza,wawaulize waume zao nyumbani, maana niaibu kwa mwanamke kusema katika mikutanoya waumini. 36 Je, mnadhani neno la Mungulimetoka kwenu ninyi au kwamba limewajienininyi peke yenu? 37 Kama mtu yeyoteanadhani kwamba yeye ni mjumbe wa Munguau kwamba anacho kipaji cha Roho, na ajuekwamba haya ninayowaandikia ninyi ni amri yaBwana. 38 Lakini mtu asiyetambua hayo, basi,mtu asimjali mtu huyo. 39 Hivyo basi, nduguzangu, mnapaswa kuwa na hamu yakutangaza ujumbe wa Mungu; lakinimsimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni. 40

Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwautaratibu.

Sasa ndugu, napenda kuwakumbushaile Habari Njema niliyowahubirieninanyi mkaipokea na kusimama imara

ndani yake. 2 Kwa njia yake mnaokolewa,ikiwa mnayazingatia manenoniliyowahubirieni, na kama kuamini kwenuhakukuwa bure. 3 Mimi niliwakabidhi ninyimambo muhimu sana ambayo miminiliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili yadhambi zetu kufuatana na MaandikoMatakatifu; 4 kwamba alizikwa, akafufuka sikuya tatu kama ilivyoandikwa; 5 kwambaalimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea walekumi na wawili. 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidiya mia tano kwa mara moja; wengi waowanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwishakufa. 7 Baadaye alimtokea Yakobo kishaakawatokea mitume wote. 8 Baada ya wote,akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kamamtu aliyezaliwa kabla ya wakati. 9 Maana mimini mdogo kabisa miongoni mwa mitume nawala sistahili kuitwa mtume, kwa sababunililidhulumu kanisa la Mungu. 10 Lakini, kwaneema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo.Na neema yake kwangu haikuwa bure. Miminimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni

1 WAKORINTHO 14:9

136

Page 137: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.11 Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirioau mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndichotunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini. 12

Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristoamefufuliwa kutoka wafu, baadhi yenuwanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuowa wafu? 13 Kama hakuna ufufuo wa wafu,basi, Kristo naye hakufufuka; 14 na kamaKristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayanamaana na imani yenu haina maana. 15 Zaidi yahayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongombele ya Mungu, maana tulisema kwambaMungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbeyeye hakumfufua—kama ni kweli kwambawafu hawafufuliwi. 16 Maana, ikiwa ni kwelikwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristohakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuliwa,basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katikadhambi zenu. 18 Zaidi ya hayo, wale wotewaliokufa wakiwa wameungana na Kristowamepotea kabisa. 19 Kama matumaini yetukatika Kristo yanahusu tu maisha haya ya sasa,basi, sisi ni watu wa kusikitikiwa zaidi kulikowengine wote duniani. 20 Lakini ukweli nikwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu,limbuko lao wale waliolala katika kifo. 21

Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani namtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutokawafu kumesababishwa na mtu mmoja. 22

Kama vile watu wote wanavyokufa kwakujiunga na Adamu, vivyo hivyo wotewatafufuliwa kwa kuungana na Kristo. 23

Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristokwanza, halafu wale walio wake Kristo wakatiKristo atakapokuja. 24 Baada ya hayo, mwishoutafika wakati ambapo Kristo atamkabidhiMungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbalikila tawala na mamlaka na nguvu. 25 MaanaKristo sharti atawale mpaka Munguatakapowashinda adui zake na kuwaweka chiniya miguu yake. 26 Adui wa mwishoatakayeangamizwa ni kifo. 27 Maana,Maandiko yasema: “Mungu ameweka vituvyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandikoyanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini yamiguu yake avitawale” ni dhahiri kwambaMungu haingii katika kundi hilo la vitu, maanayeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini yaKristo. 28 Lakini vitu vyote vitakapowekwachini ya Utawala wa Kristo, ndipo naye Mwanaatakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyotechini ya Utawala wake; ili Mungu atawale juuya vyote. 29 Kama hakuna ufufuo, je watu walewanaobatizwa kwa ajili ya wafu wanatumainiakupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya ninikubatizwa kwa ajili yao? 30 Na sisi, ya ninikujitia hatarini kila saa? 31 Ndugu, miminakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayo juuyenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwanawetu inanifanya nitangaze jambo hili. 32 Kamakusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu,kule kupigana kwangu na wanyama wakali

hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafuhawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maanakesho tutakufa.” 33 Msidanganyike! Urafikimbaya huharibu tabia njema. 34 Amkeni!Anzeni kuishi vema, na acheni kutendadhambi. Baadhi yenu hawamjui Mungu kabisa.Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu! 35

Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafuwatafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namnagani wakati watakapokuja tena?” 36 Hayo nimaswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufakwanza haitaota. 37 Unachopanda ni mbegutu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na simmea mzima ambao hutokea baadaye. 38

Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutakamwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wapekee. 39 Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili yabinadamu ni ya namna moja, ya wanyama niya namna nyingine, ya ndege ni ya namnanyingine na miili ya samaki pia ni ya namnanyingine. 40 Iko miili ya mbinguni na miili yaduniani; uzuri wa miili ya mbinguni nimwingine, na na uzuri wa miili ya duniani nimwingine. 41 Uko uzuri wa jua, wa mwezi nawa nyota; hata nyota nazo huhitilafiana kwauzuri. 42 Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu.Kama vile mbegu, mwili huzikwa ardhini ukiwakatika hali ya kuharibika, lakini hufufuliwakatika hali ya kutoharibika. 43 Huzikwa katikahali duni, hufufuliwa katika hali tukufu;huzikwa katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwawenye nguvu. 44 Unapozikwa ni mwili wakawaida, unapofufuliwa ni mwili wa kiroho.Kuna mwili wa kawaida na kutakuwa na mwiliwa kiroho. 45 Maana Maandiko yasema: “Mtuwa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe mwenyeuhai;” lakini adamu wa mwisho ni Rohoawapaye watu uzima. 46 Lakini unaotanguliakuwako si ule mwili wa kiroho, ila ule mwili wakawaida kisha ule mwili wa kiroho. 47 Adamuwa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitokaardhini; mtu wa pili alitoka mbinguni. 48 Wotewalio wa dunia wako kama huyo mtualiyeumbwa kwa udongo; wale walio wambinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni.49 Kama vile tulivyofanana na yule aliyeumbwakwa udongo, vivyo hivyo tutafanana nahuyohuyo aliyetoka mbinguni. 50 Basi, ndugu,nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili nadamu hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu;na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali yakutoharibika. 51 Sikilizeni, nawaambieni siri:sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa 52

wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja,kufumba na kufumbua. Maana mbiuitakapolia, wafu watafufuliwa katika hali yakutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa. 53

Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie haliya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie haliya kutokufa. 54 Basi, mwili huu wenyekuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika,na kile chenye kufa kitakapojivalia hali yakutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno

1 WAKORINTHO 15:54

137

Page 138: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa ushindiumekamilika!” 55 “Kifo, ushindi wako ukowapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?” 56

Ukali wa kifo hutokana na dhambi, nayodhambi hupata nguvu yake katika Sheria. 57

Lakini tumshukuru Mungu anayetupatiaushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 58

Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imarana thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidiikatika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazimnayofanya katika utumishi wa Bwanahaitapotea bure.

Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili yawatu wa Mungu: fanyeni kamanilivyoyaagiza makanisa ya Galatia. 2

Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi chafedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na hajaya kufanya mchango wakati nitakapokuja. 3

Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma walemtakaowachagua miongoni mwenu wapelekebarua na zawadi zenu Yerusalemu. 4 Kamaitafaa nami niende, basi, watakwenda pamojanami. 5 Nitakuja kwenu, baada ya kupitiaMakedonia—maana nataraji kupitiaMakedonia. 6 Labda nitakaa kwenu kwa mudafulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakatiwote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendeleena safari yangu kokote nitakakokwenda. 7

Sipendi kupita kwenu harakaharaka nakuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenukwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu. 8

Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku yaPentekoste. 9 Mlango uko wazi kabisa kwa ajiliya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzaninao ni wengi. 10 Timotheo akija, angalieni

asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu,kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi. 11

Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieniaendelee na safari yake kwa amani ili awezekurudi kwangu, maana mimi namngojeapamoja na ndugu zetu. 12 Kuhusu nduguApolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja nandugu wengine, lakini hapendelei kabisa kujasasa ila atakuja mara itakapowezekana. 13

Kesheni, simameni imara katika imani, muwehodari na wenye nguvu. 14 Kila mfanyachokifanyike kwa upendo. 15 Ndugu, mnaifahamujamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanzakabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya,na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu.Ninawasihi ninyi ndugu zangu, 16 muufuateuongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kilamtu afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao.17 Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunatona Akaiko wamefika; wamelijaza pengolililokuwako kwa kutokuwako kwenu. 18

Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwahiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii.19 Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni.Akula na Priskila pamoja na watu wote waMungu walio nyumbani mwaowanawasalimuni sana katika Bwana. 20 Nduguwote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwaishara ya mapendo ya Mungu. 21 Mimi Paulonawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangumwenyewe. 22 Yeyote asiyempenda Bwana, naalaaniwe. MARANA THA—BWANA, njoo! 23

Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. 24 Mapendoyangu yawe kwenu katika kuungana na KristoYesu.

1 WAKORINTHO 15:55

138

Page 139: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

2 WAKORINTHO

Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwamapenzi ya Mungu, na nduguTimotheo, tunawaandikia ninyi mlio

kanisa la Mungu huko Korintho, na watu wotewa Mungu kila mahali katika Akaya. 2

Tunawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. 3

Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetuYesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungumwenye kuleta faraja yote. 4 Yeye hutufarijisisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupatekuwafariji wengine katika kila taabu kwa farajahiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu. 5

Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidindani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidikufarijiwa naye. 6 Ikiwa tunapata taabu, basini kwa ajili ya faraja na wokovu wenu.Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji ninyi nakuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimilimateso yaleyale tunayoteseka sisi. 7 Tena,matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara;tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu,mtashiriki pia faraja yetu. 8 Ndugu, tunatakakuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia;taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hatatukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.9 Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwakuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungumwenye kuwafufua wafu, badala yakutegemea nguvu zetu sisi wenyewe. 10 Yeyealituokoa katika hatari kubwa ya kifo, naanaendelea kutuokoa; sisi tumemwekeatumaini letu kwamba atatuokoa tena, 11 ninyimkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea.Hivyo neema tutakazokuwa tumepatakutokana na maombi ya watu wengi hivyo,ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuruMungu kwa ajili yetu. 12 Sisi tunajivunia kitukimoja: dhamiri yetu inatuhakikishia kwambatumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu,kwa unyenyekevu na unyofu tuliojaliwa naMungu; hatukuongozwa na hekima yakibinadamu bali neema ya Mungu. 13

Tunawaandikia ninyi mambo mnayowezakuyasoma na kuyaelewa. Ninatumaini kwambamtaelewa vizuri kabisa, 14 maana mpaka sasammenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwambakatika ile Siku ya Bwana Yesu mtawezakutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaoneaninyi fahari. 15 Nikiwa na matumaini hayo,nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpatebaraka maradufu. 16 Nilikusudia kupita kwenunikiwa safarini kwenda Makedonia, na wakati

wa kurudi pia, ili nipate msaada wenu kwasafari yangu kwenda Yudea. 17 Je, mnadhaninilipopanga hivyo nimekuwa kama mtu asiyena msimamo? Je, mnadhani kwambaninafanya uamuzi wangu kwa fikira zakibinadamu na kwamba nasema “Ndiyo” na“Siyo” papo hapo? 18 Mungu ni ukweli mtupu;basi, kile tulichowaambia ninyi si jambo la“Ndiyo” na “Siyo”. 19 Maana Kristo Yesu,Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano naTimotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa“Ndiyo” na “Siyo”; bali yeye daima ni “Ndiyo” yaMungu. 20 Maana ndani yake ahadi zote zaMungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo,“Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwaajili ya kumtukuza Mungu. 21 Mungumwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi naninyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuwekawakfu; 22 ndiye aliyetutia mhuri wa kuwa maliyake yeye na kutujalia Roho mioyoni mwetukama dhamana ya mambo yote ambayoametuwekea. 23 Mungu ndiye shahidiwangu—yeye anajua moyo wangu! Mimi sikujatena Korintho, kwa sababu tu yakuwahurumieni. 24 Hatutaki kutumia mabavujuu ya imani yenu; ninyi mko imara katikaimani yenu. Wajibu wetu ni kufanya kazipamoja kwa ajili ya furaha yenu.

Basi nimeamua nisiwatembelee tenakuwatia huzuni. 2 Maananikiwahuzunisha ninyi, basi, ni nani

atakayenifariji? Ni walewale niliowahuzunisha!3 Ndiyo maana niliwaandikia—sikutaka kujakwenu na kuhuzunishwa na ninyi ambao ndiomngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakikakwamba, mimi nikifurahi, ninyi nyote piamnafurahi. 4 Nilipowaandikia hapo awalikatika hali ya huzuni na sikitiko moyoni na kwamachozi mengi, haikuwa kwa ajili yakuwahuzunisha ninyi, bali kwa ajili yakuwaonyesheni kwamba nawapenda mno. 5

Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine,hakunihuzunisha mimi—ila amewahuzunishaninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi. 6

Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengiwenu inamtosha. 7 Iliyobakia ni afadhalikwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyoili asije akahuzunika mno na kukata tamaakabisa. 8 Kwa hiyo nawasihi: mwonyeshenikwamba mnampenda. 9 Madhumuni yangukuandika ile barua yalikuwa kutaka kujua kamamko tayari kutii katika kila jambo. 10

Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe.

2 WAKORINTHO 2:10

139

Page 140: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

Maana ninaposamehe—kama kweli ninachocha kusamehe—nasamehe mbele ya Kristokwa ajili yenu, 11 ili tusimpe nafasi Shetaniatudanganye; maana twaijua mipango yakeilivyo. 12 Nilipofika Troa kuhubiri Habari Njemaya Kristo, nilikuta mlango u wazi kwa ajili yakazi ya Bwana. 13 Lakini nilifadhaika sana kwakutomkuta ndugu yetu Tito. Ndiyo maananiliwaaga wote pale nikaenda Makedonia. 14

Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongozadaima katika msafara wa ushindi wa Kristo.Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristokama harufu nzuri, kila mahali. 15 Maana sisini kama harufu nzuri ya ubani ambayo Kristoanamtolea Mungu, harufu nzuri inayofikiawote wanaookolewa na wanaopotea. 16 Kwawale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakinikwa wale wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai.Nani basi, awezaye kushiriki katika kazi yanamna hiyo? 17 Sisi si kama wengine ambaohufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisitunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kamawatu tuliotumwa na Mungu, tukiwatumeungana na Kristo.

Je, tunaanza tena kujipendekeza? Je,tunahitaji barua ya utambulisho kwenu,au kutoka kwenu, kama watu wengine?

2 Ninyi wenyewe ni barua yetu; baruailiyoandikwa mioyoni mwetu kila mtu aione nakuisoma. 3 Ni dhahiri kwamba ninyi ni baruaya Kristo aliyoipeleka kwa mikono yetu. Baruayenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwaRoho wa Mungu hai; imeandikwa si juu yakipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu. 4

Tunaweza kusema hayo kwa sababu yatumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia yaKristo. 5 Si kwamba sisi tunaweza kufanyachochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezowetu wote hutoka kwa Mungu: 6 maana yeyendiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipyaambalo si agano la sheria iliyoandikwa, baliAgano la Roho. Maana sheria iliyoandikwahuleta kifo, lakini Roho huleta uzima. 7 Sheriailiwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vyamawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo,utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wanawa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mosekwa sababu ya mng'ao wake. Tena mng'ao huoulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma yakile ambacho kimesababisha kifo imefanyikakwa utukufu mwingi kiasi hicho, 8 basi,huduma ya Roho ina utukufu mkuu zaidi. 9

Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika hudumaile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba hudumaile iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu itakuwana utukufu mkuu zaidi. 10 Sasa utukufu mkuuzaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokujahapo awali, ambao fahari yake imekwishatoweka. 11 Maana ikiwa kile kilichokuwa chamuda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shakakile chenye kudumu milele kitakuwa nautukufu mkuu zaidi. 12 Kwa vile hili ndilotumaini letu, sisi twasema kwa uhodari mkuu.

13 Sisi hatufanyi kama Mose ambayealilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaaili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wamng'ao uliokuwa unafifia. 14 Lakini akili zaozilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Aganola Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifunikohicho kitaondolewa tu mtu anapoungana naKristo. 15 Naam, mpaka hivi leo kila isomwapoSheria ya Mose akili zao huwa zimefunikwa. 16

Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana,kifuniko hicho huondolewa. 17 Hapa “Bwana”ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipoulipo uhuru. 18 Basi, sisi sote ambao nyusozetu hazikufunikwa, twaonyesha kama katikakioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwatufanane zaidi na huo mfano wake kwautukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Rohowa Bwana.

Basi, Mungu, kwa huruma yake,ametukabidhi kazi hii na hivyo hatufimoyo. 2 Tumeyaacha kabisa mambo

yote ya aibu na ya kisirisiri. Hatuishi tena kwaudanganyifu, wala kwa kulipotosha neno laMungu; bali tunaudhihirisha ukweli kwakuufanya ukweli, na hivyo kujiweka chini yauamuzi wa dhamiri za watu mbele ya Mungu.3 Maana, kama Habari Njema tunayohubiriimefichika, imefichika tu kwa walewanaopotea. 4 Hao hawaamini kwa sababuyule mungu wa ulimwengu huu amezitia gizaakili zao wasipate kuuona wazi mwanga waHabari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye nimfano kamili wa Mungu. 5 Maanahatujitangazi sisi wenyewe, ila tunamhubiriYesu Kristo aliye Bwana, sisi wenyewe tukiwawatumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6 Munguambaye alisema, “Mwanga na uangaze kutokagizani,” ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu,na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu waMungu uangazao katika uso wa Kristo. 7 Basi,sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombovya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvuhiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisiwenyewe. 8 Daima twapata taabu, lakinihatugandamizwi; twapata mashaka, lakinihatukati tamaa; 9 twateseka, lakini hatuachwibila msaada; na ingawa tumeangushwa chini,hatukuangamizwa. 10 Kila wakati tumekuwatukichukua mwilini mwetu kifo cha Kristo, iliuhai wake Yesu pia udhihirike katika miili yetu.11 Naam, katika maisha yetu yote tunakabiliwana kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uzima wakeYesu udhihirike katika miili yetu inayokufa. 12

Hii ina maana kwamba ndani yetu kifokinafanya kazi, lakini ndani yenu uhai unafanyakazi. 13 Maandiko Matakatifu yasema:“Niliamini, ndiyo maana nilinena.” Nasi pia,tukiwa na moyo huohuo wa imani, tunaamini,na kwa sababu hiyo twanena. 14 Tunajuakwamba yule aliyemfufua Bwana Yesuatatufufua sisi pia pamoja na Yesu nakutuweka mbele yake pamoja nanyi. 15 Yotehaya ni kwa faida yenu; ili kama vile neema ya

2 WAKORINTHO 2:11

140

Page 141: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

6

Mungu inavyoenea kwa watu wengi zaidi nazaidi vivyo hivyo watu wengi zaidi watoeshukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu. 16

Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kamamaumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndanitunafanywa wapya siku kwa siku. 17 Taabutunayopata ni kidogo, tena ya muda tu: lakiniitatupatia utukufu upitao matazamio yote,utukufu ambao hauna mwisho. 18 Hivyotunatazamia kwa makini si vituvinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maanavinavyoonekana ni vya muda tu; lakini vilevisivyoonekana ni vya milele.

Maana tunajua kwamba hema hiiambayo ndani yake tunaishi sasa hapaduniani, yaani mwili wetu,

itakapong'olewa, Mungu atatupa makaomengine mbinguni, nyumba ya mileleisiyotengenezwa kwa mikono. 2 Na sasa,katika hali hii, tunaugua, tukitazamia kwahamu kubwa kuvikwa makao yetu yaliyombinguni. 3 Naam, tunapaswa kuvikwanamna hiyo ili tusije tukasimama mbele yaMungu bila vazi. 4 Tukiwa bado katika hemahii ya duniani, tunalia kwa kukandamizwa; sikwamba tunataka kuuvua mwili huu wa kufa,ila tuna hamu ya kuvalishwa ule usiokufa, ilikile chenye kufa kimezwe kabisa na uhai. 5

Mungu mwenyewe alitutayarishia mabadilikohayo, naye ametupa Roho wake awe dhamanaya yote aliyotuwekea. 6 Tuko imara daima.Tunajua kwamba kuishi katika mwili huu tu nikukaa mbali na Bwana. 7 Maana tunaishi kwaimani, na si kwa kuona. 8 Lakini tuko imara natungependelea hata kuyahama makao haya,tukahamie kwa Bwana. 9 Lakini jambo lamaana zaidi, tunataka kumpendeza, iwetunaishi hapa duniani au huko. 10 Maana soteni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumucha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahilikwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwaanaishi duniani, mema au mabaya. 11 Basi, sisitunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyotunajitahidi kuwavuta watu. Mungu anatujuawaziwazi, nami natumaini kwamba nanyi piamnatujua kinaganaga. 12 Si kwambatunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ilatunataka kuwapa ninyi sababu zetu za kuonafahari juu yenu, ili mpate kuwajibu walewanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsiwalivyo moyoni. 13 Ikiwa tumeonekana kuwawendawazimu, hiyo ni kwa ajili ya Mungu; naikiwa tunazo akili zetu timamu, hiyo ni kwafaida yenu. 14 Maana mapendo ya Kristoyanatumiliki sisi ambao tunatambua yakwamba mtu mmoja tu amekufa kwa ajili yawote, na hiyo ina maana kwamba wotewanashiriki kifo chake. 15 Alikufa kwa ajili yawatu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili yaowenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa,akafufuliwa kwa ajili yao. 16 Basi, tangu sasa,sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hatakama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo

kibinadamu, sasa si hivyo tena. 17 Mtu yeyoteakiungana na Kristo huwa kiumbe kipya,mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.18 Yote ni kazi ya Mungu mwenyekutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo,akatupa nasi jukumu la kuwapatanisha watunaye. 19 Ndiyo kusema: Mungu, amekuwaakiupatanisha ulimwengu naye kwa njia yaKristo, bila kutia maanani dhambi zaobinadamu. Yeye ametupa ujumbe kuhusukuwapatanisha watu naye. 20 Basi, sisitunamwakilisha Kristo, naye Mungumwenyewe anatutumia sisi kuwasihi ninyi.Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo,mpatanishwe na Mungu. 21 Kristo hakuwa nadhambi, lakini Mungu alimfanya ahusike nadhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungananaye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu.

Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja naMungu, tunawasihi msikubali ile neemamliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee

bure. 2 Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaanimekusikiliza, wakati wa wokovunikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa,sasa ndiyo siku ya wokovu! 3 Kusudi tusiwe nalawama yoyote katika utumishi wetu,hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuiochochote. 4 Badala yake, tunajionyesha kuwakweli watumishi wa Mungu kwa kila kitu: kwauvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida nataabu. 5 Tumepigwa, tumetiwa gerezani nakuzomewa hadharani; tumefanya kazitukachoka; tumekesha na kukaa bila kula. 6

Tunajionyesha kuwa watumishi wa Mungu kwausafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwaRoho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki, 7

kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu.Uadilifu ndiyo silaha yetu upande wa kulia naupande wa kushoto. 8 Tuko tayari kupataheshima na kudharauliwa, kulaumiwa nakusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbetwasema kweli; 9 kama wasiojulikana, kumbetwajulikana kwa wote, kama waliokufa, lakinimwonavyo, sisi ni wazima kabisa. 10 Ingawatumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayohuzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskinihohehahe, lakini twatajirisha watu wengi;twaonekana kuwa watu tusio na chochote,kumbe tuna kila kitu. 11 Ndugu Wakorintho,tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetuiko wazi kabisa. 12 Kama mnaona kuna kizuizichochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu ninyiwenyewe, na si kwa upande wetu. 13 Sasanasema nanyi kama watoto wangu, wekenimioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya. 14

Msiambatane na watu wasioamini. Je, wemana uovu vyapatana kweli? Mwanga na gizavyawezaje kukaa pamoja? 15 Kristo anawezajekupatana na Shetani? Muumini ana uhusianogani na asiyeamini? 16 Hekalu la Mungu linauhusiano gani na sanamu za uongo? Maanasisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungumwenyewe alivyosema: “Nitafanya makao

2 WAKORINTHO 6:16

141

Page 142: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

78

yangu kwao, na kuishi kati yao; NitakuwaMungu wao, nao watakuwa watu wangu.” 17

Kwa hiyo Bwana asema pia: “Ondokeni katiyao, mkajitenge nao, msiguse kitu najisi, naminitawapokea. 18 Mimi nitakuwa Baba yenu,nanyi mtakuwa watoto wangu, waume kwawake, asema Bwana Mwenye Uwezo.”

Basi, wapenzi wangu, tukiwa tumepewaahadi hizi zote, na tujitakase nachochote kiwezacho kuchafua miili na

roho zetu, tuwe watakatifu kabisa, na tuishikwa kumcha Mungu. 2 Tunaomba mtupenafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtuyeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtuyeyote. 3 Sisemi mambo haya kwa ajili yakumhukumu mtu; maana, kama nilivyokwishasema, ninyi mko mioyoni mwetu, tufe pamoja,tuishi pamoja. 4 Nina imani kubwa sananinaposema nanyi; naona fahari kubwa juuyenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizokikubwa na kufurahi mno. 5 Hata baada yakufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kilaupande tulikabiliwa na taabu: nje ugomvi;ndani hofu. 6 Lakini Mungu, mwenye kuwapashime wanyonge alitupa moyo sisi pia kwakuja kwake Tito. 7 Si tu kwa kule kuja kwakeTito, bali pia kwa sababu ya moyo mliompaninyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamanikuniona, jinsi mlivyo na huzuni, namnavyotaka kunitetea. Jambo hililinanifurahisha sana. 8 Maana, hata kama kwabarua ile yangu nimewahuzunisha, sionisababu ya kujuta. Naam, naona kwamba baruahiyo iliwatia huzuni lakini kwa muda. 9 Sasanafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwakuwa huzuni yenu imewafanya mbadili niazenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri yampango wa Mungu, na kwa sababu hiyohatukuwadhuru ninyi kwa vyovyote. 10 Kuwana huzuni jinsi atakavyo Mungu, husababishabadiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu;hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuniya kidunia huleta kifo. 11 Sasa mnaweza kuonamatokeo ya kuona huzuni jinsi Munguatakavyo: ninyi mmepata kuwa sasa watuwenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka nakuogopa, mna bidii na mko tayari kuonakwamba haki yatekelezwa. Ninyimmethibitisha kwa kila njia kwamba hamnahatia kuhusu jambo hili. 12 Hivyo, ingawaniliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yulealiyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa.Niliandika kusudi ionekane wazi mbele yaMungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu. 13

Ndiyo maana sisi tulifarijika sana. Siyo kwambatulifarijika tu, ila pia Tito alitufurahisha kwafuraha aliyokuwa nayo kutokana na jinsimlivyomchangamsha moyo. 14 Miminimewasifu sana mbele yake, na katika jambohilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukwelidaima, na kule kuwasifia ninyi mbele ya Titokumekuwa jambo la ukweli mtupu. 15 Hivyoupendo wake wa moyo kwenu unaongezeka

zaidi akikumbuka jinsi ninyi nyote mlivyo tayarikutii, na jinsi mlivyomkaribisha kwa hofunyingi na kutetemeka. 16 Nafurahi sanakwamba naweza kuwategemea ninyi kabisakatika kila jambo.

Ndugu, tunapenda kuwapa habari juuya neema ambazo Mungu ameyajaliamakanisa ya Makedonia. 2 Waumini wa

huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakinifuraha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawawakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwamaskini sana. 3 Naweza kushuhudia kwambawalikuwa wakarimu kadiri ya nguvu zao nahata zaidi. Kwa hiari yao wenyewe, 4 walitusihisana wapewe nafasi ya kushiriki katikahuduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu. 5

Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamiakabisa! Kwanza walijitolea wao wenyewe kwaBwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia,kufuatana na mapenzi ya Mungu. 6 Kwasababu hiyo, tulimsihi Tito aliyeianza kazi hiyoawasaidieni pia muitekeleze huduma hii yaupendo miongoni mwenu. 7 Ninyi mna kilakitu: imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yoteya kutenda mema, na upendo wenu kwetu.Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu katikahuduma hii ya upendo. 8 Siwapi ninyi amri,lakini nataka tu kuonyesha jinsi wenginewalivyo na bidii ya kusaidia ili nipate kujua jinsiupendo wenu ulivyo wa kweli. 9 Maana, ninyimnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo:yeye, ingawa alikuwa na kila kitu, alijifanyamaskini kwa ajili yenu, ili kutokana na umaskiniwake, awatajirishe. 10 Kuhusu jambo hili, basi,nawapeni shauri hili: inafaa kwenu kutekelezasasa yale mliyoanza mwaka jana. Ninyimlikuwa wa kwanza kuchukua hatua nakuamua kufanya hivyo. 11 Basi, kamilishenishughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa nahamu kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidiivivyo hivyo, kadiri ya uwezo wenu,kuikamilisha. 12 Maana ikiwa mtu ana moyowa kusaidia, Mungu hupokea kila anachowezakutoa: hadai zaidi. 13 Ninyi hampaswikuongezewa taabu kusudi wenginewapunguziwe mzigo wao; sivyo, ila ni lazimatujali usawa na haki. 14 Kila mlicho nacho sasacha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili naowakati watakapokuwa na ziada, wawasaidieninyi katika mahitaji yenu, na hivyo kuwe nausawa. 15 Kama Maandiko yasemavyo:“Aliyekusanya kwa wingi hakuwa na ziada, nayule aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.” 16

Namshukuru Mungu aliyeweka ndani ya moyowa Tito hamu hiyo niliyo nayo mimi yakuwasaidia. 17 Si tu kwamba alikubali ombiletu, ila pia alikuwa na hamu kubwa yakusaidia, hata akaamua kwa hiari yakemwenyewe kuja kwenu. 18 Pamoja naye,tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zakekatika kueneza Habari Njema zimeenea katikamakanisa yote. 19 Zaidi ya hayo, yeyeamechaguliwa na makanisa awe mwenzetu

2 WAKORINTHO 6:17

142

Page 143: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

10

safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetuya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili yautukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetunjema. 20 Tunataka kuepa lawama zinazowezakutokea kuhusu usimamizi wetu juu ya zawadihii karimu. 21 Nia yetu ni kufanya vema, si tumbele ya Bwana, lakini pia mbele ya watu. 22

Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtumandugu yetu mwingine ambaye mara nyingitumempa majaribio mbalimbali, tukamwonakuwa ni mwenye hamu kubwa ya kusaidia;hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababuana imani sana nanyi. 23 Tito ni mwenzangu;tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakinikuhusu hawa ndugu zetu wengine, wanaokujapamoja nao, hao ni wajumbe wa makanisa, nautukufu kwa Kristo. 24 Basi, waonyesheniuthabiti wa upendo wenu, makanisa yapatekuona kweli kwamba fahari ninayoona juuyenu ni ya halali.

Si lazima kuandika zaidi kuhusuhuduma hiyo yenu kwa ajili ya watu waMungu. 2 Ninajua jinsi mlivyo na moyo

wa kusaidia, na nilijivuna juu yenu kuhusujambo hilo mbele ya watu wa Makedonia.Niliwaambia: “Ndugu zetu wa Akaya wakotayari tangu mwaka jana.” Hivyo, moto wenuumekwisha wahimiza watu wengi zaidi. 3 Basi,nimewatuma ndugu zetu hao, ili fahari yetujuu yenu ionekane kwamba si manenomatupu, na kwamba mko tayari kabisa namsaada wenu kama nilivyosema. 4 Isije ikawakwamba watu wa Makedonia watakapokujapamoja nami tukawakuta hamko tayari, haposisi tutaaibika—bila kutaja aibu mtakayopataninyi wenyewe—kwa sababu tutakuwatumewatumainia kupita kiasi. 5 Kwa hiyo,nimeona ni lazima kuwaomba hawa nduguwatutangulie kuja kwenu, wapate kuwekatayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayoionyeshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewakwa hiari na si kwa kulazimishwa. 6

Kumbukeni: “Apandaye kidogo huvuna kidogo;apandaye kwa wingi huvuna kwa wingi.” 7 Kilammoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwamoyo na wala si kwa huzuni au kwakulazimishwa, maana Mungu humpenda yulemwenye kutoa kwa furaha. 8 Mungu anawezakuwapeni ninyi zaidi ya yale mnayoyahitaji,mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji,na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.9 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Yeye hutoa kwa ukarimu, huwapa maskini,wema wahudumu milele.” 10 Na Munguampaye mkulima mbegu na mkate kwachakula, atawapa ninyi pia mbegu mnazohitaji,na atazifanya ziote, ziwe na kuwapa mavunomengi ya ukarimu wenu. 11 Yeyeatawatajirisha ninyi daima kwa kila kitu, iliwatu wapate kumshukuru Mungu kwa ajili yazawadi zenu wanazozipokea kwa mikono yetu.12 Maana huduma hii takatifu mnayoifanya situ kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa

Mungu, bali pia itasababisha watu wengiwamshukuru Mungu. 13 Kutokana nauthibitisho unaoonyeshwa kwa huduma hiiyetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababuya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristomnayoiungama, na pia kwa sababu yaukarimu mnaowapa wao na watu wote. 14 Kwahiyo watawaombea ninyi kwa moyo kwasababu ya neema ya pekee aliyowajalieniMungu. 15 Tumshukuru Mungu kwa ajili yazawadi yake isiyo na kifani!

Mimi Paulo mwenyewe ambayenaonekana kuwa mpole nikiwapamoja nanyi, lakini mkali wakati

nikiwa mbali nanyi, nawasihini kwa huruma nawema wake Kristo. 2 Nawaombenimsinisababishe kuwa mkali wakatinitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwamkali kwa wote wale wanaotudhania kwambatunaishi kidunia. 3 Kweli tunaishi duniani,lakini hatupigani vita kidunia. 4 Maana, silahatunazotumia katika vita vyetu si silaha zakidunia, ila ni nguvu za Mungu zenye kuharibungome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo, 5

na kubomoa kila kizuizi cha majivunokilichowekwa kuipinga elimu ya Mungu;tunaziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo.6 Mkisha kuwa wakamilifu katika kutii, sisituko tayari kuadhibu kila namna ya kutotii. 7

Ninyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupomtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni waKristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisipia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo. 8

Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangujuu ya ule uwezo aliotupa—uwezo wakuwajenga na sio wa kubomoa—hata hivyosijutii hata kidogo. 9 Sipendi mfikiri kwambanataka kuwatisha ninyi kwa barua zangu. 10

Mtu anaweza kusema: “Barua za Paulo ni kalina zenye maneno mazito, lakini yeyemwenyewe anapokuwa pamoja nasi ni mtudhaifu, na hata anapoongea maneno yake nikama si kitu.” 11 Mtu asemaye hivyo heriakumbuke kwamba hakuna tofauti ya yaletunayoandika katika barua wakati tuko mbali,na yale tutakayofanya wakati tutakapokuwananyi. 12 Kwa vyovyote hatungethubutukujiweka au kujilinganisha na wale watuwanaojisifia wenyewe. Watu wenye kujifanyawao kuwa kipimo cha kujipimia, na watuwanaojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, niwapumbavu. 13 Lakini sisi hatutajivuna kupitakiasi; kujivuna huko kutabaki katika kile kipimocha kazi aliyotukabidhi Mungu, kazi ambayotunaifanya pia kwenu. 14 Na kwa vile ninyi mukatika mipaka hiyo, hatukuipita tulipokujakwenu, tukiwaleteeni Habari Njema juu yaKristo. 15 Basi, hatujivunii kazi waliyofanyawengine zaidi ya kipimo tulichopewa; ilatunatumaini kwamba imani yenu itazidimiongoni mwenu kufuatana na kipimoalichotuwekea Mungu. 16 Hapo tutawezakuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine,

2 WAKORINTHO 10:16

143

Page 144: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

12

mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivuniakazi waliyofanya watu wengine mahalipengine. 17 Lakini kama yasemavyo Maandiko:“Mwenye kuona fahari na aone fahari juu yaalichofanya Bwana.” 18 Anayekubaliwa si yuleanayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwana Bwana.

Laiti mngenivumilia kidogo, hatakama mimi ni mjinga kiasi fulani!Naam, nivumilieni kidogo. 2

Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu;maana ninyi ni kama bikira safi niliyemposakwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiyeKristo. 3 Lakini naogopa kwamba, kama vileyule nyoka kwa hila zake za uongoalimdanganya Hawa, fikira zenu zawezakupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wakweli kwa Kristo. 4 Maana mtu yeyote ajaye nakumhubiri Yesu aliye tofauti na yuletuliyemhubiri, ninyi mwampokea kwa mikonomiwili; au mnakubali roho au habari njematofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!5 Sidhani kwamba mimi ni mdogo kuliko hao“mitume wakuu.” 6 Labda sina ufasaha walugha, lakini elimu ninayo; jambo hilitumelionyesha wazi kwenu, kila mahali na kilawakati. 7 Mimi niliihubiri kwenu Habari Njemaya Mungu bila kudai mshahara;nilijinyenyekeza ili nipate kuwakweza ninyi. Je,nilifanya vibaya? 8 Nilipofanya kazi kati yenu,mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisamengine. Kwa namna moja au nyingineniliwapokonya wao mali yao nipatekuwatumikia ninyi. 9 Nilipokuwa nanyisikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha;ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kilakitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sananisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, nanitaendelea kufanya hivyo. 10 Naahidi kwa uleukweli wa Kristo ulio ndani yangu, kwambahakuna kitakachoweza kunizuia kujivuniajambo hilo popote katika Akaya. 11 Kwa nininasema hivyo? Kwa sababu eti siwapendininyi? Mungu anajua kwamba nawapenda! 12

Nitaendelea kufanya kama ninavyofanya sasa,ili nisiwape nafasi wale wanaotafuta nafasi,nafasi ya kujivuna kwamba eti wanafanya kazikama sisi. 13 Maana, hao ni mitume wa uongo,wafanyakazi wadanganyifu wanojisingiziakuwa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu,maana hata Shetani mwenyewe hujisingiziakuwa malaika wa mwanga! 15 Kwa hiyo sijambo la kushangaza ikiwa na hao watumishiwake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki.Mwisho wao watapata kile wanachostahilikufuatana na matendo yao. 16 Tena nasema:Mtu asinifikirie kuwa mpumbavu. Lakini kamamkifikiri hivyo, basi, nichukueni kamampumbavu ili nami nipate kuwa na chakujivunia angaa kidogo. 17 Ninachosema sasasi kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hilila kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.18 Maadam wengi hujivuna kwa sababu za

kidunia, nami pia nitajivuna. 19 Ninyi ni wenyebusara, ndiyo maana hata mnawavumiliawapumbavu! 20 Mnamvumilia hata mtuanayewafanya ninyi watumwa, mtu mwenyekuwanyonya, mwenye kuwakandamiza,mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni! 21

Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwadhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtuyeyote anayethubutu kujivunia kitu—nasemakama mtu mpumbavu—mimi nathubutu pia.22 Je, wao ni Waebrania? Hata mimi. Je, wao niWaisraeli? Hata mimi. Wao ni wazawa waAbrahamu? Hata mimi. 23 Wao ni watumishiwa Kristo? Hata mimi—nanena hayokiwazimu—ni mtumishi wa Kristo zaidi kulikowao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi,nimekaa gerezani mara nyingi zaidi,nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribiakifo mara nyingi. 24 Mara tano nilichapwa vileviboko thelathini na tisa vya Wayahudi. 25

Nilipigwa viboko mara tatu, nilipigwa mawemara moja; mara tatu nilivunjikiwa melibaharini, na humo nikakesha usiku kucha nakushinda mchana kutwa. 26 Kila mara safarininimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, nahatari za wanyama; hatari kutoka kwawananchi wenzangu na kutoka kwa watu wamataifa mengine; hatari za mjini, hatari zaporini, hatari za baharini, hatari kutoka kwandugu wa uongo 27 Nimefanya kazi nakutaabika, nimekesha bila usingizi maranyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyinginimefunga na kukaa katika baridi bila nguo. 28

Na, licha ya mengine mengi, kila sikunakabiliwa na shughuli za makanisa yote. 29

Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu;mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa nawasiwasi. 30 Ikinilazimu kujivuna, basi,nitajivunia udhaifu wangu. 31 Mungu na Babawa Bwana Yesu—jina lake litukuzwemilele—yeye anajua kwamba sisemi uongo. 32

Nilipokuwa Damasko, mkuu wa mkoa,aliyekuwa chini ya mfalme Areta, alikuwaakiulinda mji wa Damasko ili apatekunikamata. 33 Lakini, ndani ya kapu kubwa,niliteremshwa nje kupitia katika nafasi ukutani,nikachopoka mikononi mwake.

Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakinisasa nitasema juu ya maono naufunuo alivyonijalia Bwana. 2 Namjua

mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi naminne iliyopita alinyakuliwa mpaka katikambingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwamwili au kwa roho; Mungu ajua.) 3 Narudia:najua kwamba mtu huyo alinyakuliwa mpakapeponi. (Lakini sijui kama alikuwa huko kwamwili au kwa roho; Mungu ajua.) 4 Hukoakasikia mambo ya siri ambayo binadamuhastahili kuyatamka. 5 Basi, nitajivunia juu yamtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimibinafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu. 6

Kama ningetaka kujivuna singekuwampumbavu hata kidogo, maana ningekuwa

2 WAKORINTHO 10:17

144

Page 145: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

nasema ukweli mtupu. Lakini sitajivuna;sipendi mtu anifikirie zaidi ya vile anavyoonana kusikia kutoka kwangu. 7 Lakini, kusudimambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanyenilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilinikama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenyekunipiga nisijivune kupita kiasi. 8 NilimsihiBwana mara tatu kuhusu jambo hili ili linitoke.9 Lakini akaniambia: “Neema yangu inatoshakwa ajili yako; maana uwezo wanguhukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, niradhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezowake Kristo ukae juu yangu. 10 Kwa hiyonakubali kwa radhi udhaifu, madharau, taabu,udhalimu na mateso, kwa ajili ya Kristo; maananinapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa nanguvu. 11 Nimekuwa kama mpumbavu, lakini,ninyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Ninyi ndiomngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi sikitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo zaidi kulikohao “mitume wakuu.” 12 Miujiza na maajabuyaonyeshayo wazi kwamba mimi ni mtumeyalifanyika miongoni mwenu kwa uvumilivuwote. 13 Je, mlipungukiwa nini zaidi kulikomakanisa mengine, isipokuwa tu kwambamimi kwa upande wangu sikuwasumbuenikupata msaada wenu? Samahani kwakuwakoseeni haki hiyo! 14 Sasa niko tayarikabisa kuja kwenu mara ya tatu, nasitawasumbua. Maana ninachotafuta si malizenu, bali ni ninyi wenyewe. Ni kawaida yawazazi kuwawekea watoto wao akiba, na siwatoto kuwawekea wazazi wao. 15 Mimi niradhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hatakujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida yaroho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwakuwa mimi nawapenda ninyi mno? 16 Basi,mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu.Lakini labda mtu mwingine atasema: “Kwa vilePaulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.” 17

Je, mimi niliwanyonyeni kwa njia ya mjumbeyeyote niliyemtuma kwenu? 18 Mimi nilimwitaTito, nikamtuma kwenu na ndugu yetumwingine. Je, Tito aliwanyonyeni? Je, hamjuikwamba sisi tumekuwa tukiongozwa na rohoyuleyule, na mwenendo wetu ni mmoja? 19

Labda mnafikiri kwamba mpaka sasatumekuwa tukijitetea wenyewe mbele yenu!Lakini, tunasema mambo haya mbele yaMungu, tukiwa tumeungana na Kristo. Mambohayo, yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili yakuwajenga ninyi. 20 Naogopa, huendanitakapokuja kwenu nitawakuta katika halinisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali

msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa naugomvi, wivu, uhasama, ubishi,masengenyano, kunong'ona, majivuno na fujokati yenu. 21 Naogopa huenda haponitakapokuja safari ijayo Mungu wanguatanifanya niaibike mbele yenu, naminitaomboleza kwa ajili ya wengi wa walewaliotenda dhambi lakini hawakujutia huouchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwawamefanya.

Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu.“Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidiwa watu wawili au watatu,” yasema

Maandiko. 2 Nilikwisha sema, na kamailivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tenanikiwa mbali: wale wote waliotenda uovu bilakutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja,watakiona cha mtema kuni. 3 Mtajioneawenyewe kwamba Kristo anasema ndaniyangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yakeyafanya kazi miongoni mwenu. 4 Maana hatakama alisulubiwa kwa sababu ya udhaifu,lakini sasa anaishi kwa uwezo wa Mungu. Sisipia tu dhaifu kwa kuungana naye lakini tutaishinaye kwa uwezo wa Mungu kwa ajili yenu. 5

Jichunguzeni ninyi wenyewe mpate kujuakama kweli mnayo imani. Jichunguzeni ninyiwenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumondani yenu? Kama sivyo, basi ninyimmeshindwa. 6 Lakini natumaini kwambaninyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa. 7

Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote,lakini si kusudi tuonekane kama watuwaliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema,hata kama sisi tunaonekana kuwatumeshindwa. 8 Maana hatuwezi kuupingaukweli; uwezo tulio nao ni wa kuuendelezaukweli. 9 Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu,lakini ninyi mna nguvu; kwa hiyo tunaombampate kuwa wakamilifu. 10 Basi, ninaandikabarua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenunisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumiaule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wakujenga na si wa kubomoa. 11 Kwa sasa,ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikenimashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwaamani. Naye Mungu wa mapendo na amaniatakuwa pamoja nanyi. 12 Salimianeni kwaishara ya upendo. 13 (G13-12) Watu wote waMungu huku wanawasalimuni. 14 (G13-13)Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo waMungu na umoja wa Roho Mtakatifu, viwenanyi nyote.

2 WAKORINTHO 13:14

145

Page 146: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

WAGALATIA

Mimi Paulo mtume, 2 na ndugu wotewalio pamoja nami, tunayaandikiamakanisa yaliyoko Galatia. Mimi

nimepata kuwa mtume si kutokana namamlaka ya binadamu, wala si kwa nguvu yamtu, bali kwa uwezo wa Yesu Kristo na waMungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka wafu. 3

Tunawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana YesuKristo. 4 Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili yadhambi zetu kufuatana na mapenzi ya Munguwetu na Baba, ili apate kutuokoa katikaulimwengu huu mbaya wa sasa. 5 Kwake yeyeuwe utukufu milele! Amina. 6 Nashangaakwamba muda mfupi tu umepita, nanyimnamwasi yule aliyewaita kwa neema yaKristo, mkafuata Habari Njema ya namnanyingine. 7 Lakini hakuna “Habari Njema”nyingine. Ukweli ni kwamba wako watuwanaowavurugeni, watu wanaotakakuipotosha Habari Njema ya Kristo. 8 Lakini,hata kama mmoja wetu au malaika kutokambinguni, atawahubirieni Habari Njematofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyona alaaniwe! 9 Tulikwisha sema, na sasanasema tena: kama mtu yeyoteanawahubirieni Habari Njema ya ainanyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea,huyo na alaaniwe! 10 Sasa nataka kibali chanani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je,nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanyahivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi waKristo. 11 Ndugu, napenda mfahamu kwambaile Habari Njema niliyoihubiri si ujumbe wakibinadamu. 12 Wala mimi sikuipokea kutokakwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu.Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia. 13

Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwaninaishi zamani kwa kuzingatia dini yaKiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungukupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa. 14

Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchiwenzangu wa rika langu katika kuizingatia diniya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashikamapokeo ya wazee wetu. 15 Lakini Mungu,kwa neema yake, alikuwa ameniteua hatakabla sijazaliwa, akaniita nimtumikie. 16 Maratu alipoamua kunifunulia Mwanae kusudiniihubiri Habari Njema yake kwa watu wamataifa mengine, bila kutafuta maoni yabinadamu, 17 na bila kwenda kwanzaYerusalemu kwa wale waliopata kuwa mitumekabla yangu, nilikwenda kwanza Arabia, kisha

nikarudi tena Damasko. 18 Ilikuwa tu baada yamiaka mitatu, ndipo nilipokwenda Yerusalemukuonana na Kefa; nilikaa kwake siku kumi natano. 19 Lakini sikuwaona mitume wengineisipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 20

Haya ninayowaandikieni, Mungu anajua;sisemi uongo. 21 Baadaye nilikwenda katikatarafa za Siria na Kilikia. 22 Wakati huo, mimibinafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristokule Yudea. 23 Walichokuwa wanajua ni kile tuwalichosikia: “Mtu yule aliyekuwa akitutesahapo awali, sasa anaihubiri imani ileilealiyokuwa anajaribu kuiangamiza.” 24 Basi,wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.

Baada ya miaka kumi na minne,nilikwenda tena Yerusalemu pamoja naBarnaba; nilimchukua pia Tito pamoja

nami. 2 Kwenda kwangu kulitokana na ufunuoalionipa Mungu. Katika kikao cha faraghaniliwaeleza hao viongozi ujumbe wa HabariNjema niliohubiri kwa watu wa mataifa.Nilifanya hivyo kusudi kazi yangu niliyokuwanimefanya, na ile ninayofanya sasa isije ikawabure. 3 Lakini, hata mwenzangu Tito, ambayeni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa, 4 ingawakulikuwa na ndugu wengine wa uongowaliotaka atahiriwe. Watu hawa walijiingizakwa ujanja na kupeleleza uhuru wetu tulio naokatika kuungana na Kristo Yesu, ili wapatekutufanya watumwa. 5 Hatukukubaliana naohata kidogo ili ukweli wa Habari Njema ubakinanyi daima. 6 Lakini watu hawawanaosemekana kuwa ni viongozi—kamakweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu,maana Mungu hahukumu kwa kuangaliamambo ya nje—watu hawa hawakuwa na kitucha kuongeza katika Habari hii Njema kamaniihubirivyo. 7 Badala yake, walitambuakwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiriHabari Njema kwa watu wa mataifa menginekama vile Petro alivyokuwa ametumwakuihubiri kwa Wayahudi. 8 Maana, yulealiyemwezesha Petro kuwa mtume kwaWayahudi, ndiye aliyeniwezesha nami piakuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine. 9

Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambaowaonekana kuwa viongozi wakuu, walitambuakwamba Mungu alinijalia neema hiyo,wakatushika sisi mkono, yaani Barnaba namimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasatukafanye kazi kati ya watu wa mataifamengine, na wao kati ya Wayahudi. 10

Wakatuomba lakini kitu kimoja: tuwakumbuke

WAGALATIA 1:2

146

Page 147: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

maskini; jambo ambalo nimekuwa nikijitahidikutekeleza. 11 Lakini Kefa alipofika Antiokianilimpinga waziwazi maana alikuwa amekosea.12 Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwawametumwa na Yakobo kuwasili hapo, Petroalikuwa akila pamoja na watu wa mataifamengine. Lakini, baada ya hao watu kufika,aliacha kabisa kula pamoja na watu wa mataifamengine, kwa kuogopa kikundi chawaliosisitiza tohara. 13 Hata ndugu wengineWayahudi walimuunga mkono Petro katikakitendo hiki cha unafiki, naye Barnabaakakumbwa na huo unafiki wao. 14 Basi,nilipoona kuwa msimamo wao kuhusu ukweliwa Habari Njema haukuwa umenyooka,nikamwambia Kefa mbele ya watu wote:“Ingawa wewe ni Myahudi, unaishi kama watuwa mataifa mengine na si kama Myahudi!Unawezaje, basi kujaribu kuwalazimisha watuwa mataifa mengine kuishi kama Wayahudi?”15 Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watuwa mataifa mengine hao wenye dhambi! 16

Lakini, tunajua kwa hakika kwamba mtuhawezi kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa kuitiiSheria, bali tu kwa kumwamini Yesu Kristo. Nasisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupatekukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imaniyetu kwa Kristo, na si kwa kuitii Sheria. 17

Sasa, ikiwa katika kutafuta kukubaliwa kuwawaadilifu kwa kuungana na Kristo sisitunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambohili lina maana kwamba Kristo anasaidiautendaji wa dhambi? Hata kidogo! 18 Lakiniikiwa ninajenga tena kile nilichokwisha bomoa,basi nahakikisha kwamba mimi ni mhalifu. 19

Maana, kuhusu Sheria hiyo, mimi nimekufa;Sheria yenyewe iliniua, nipate kuishi kwa ajiliya Mungu. Mimi nimeuawa pamoja na Kristomsalabani, 20 na sasa naishi, lakini si mimitena, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maishahaya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imanikatika Mwana wa Mungu aliyenipenda hataakayatoa maisha yake kwa ajili yangu. 21

Sipendi kuikataa neema ya Mungu. Kama mtuhuweza kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa njiaya Sheria, basi, Kristo alikufa bure!

Enyi Wagalatia, mmekuwa wajingakweli! Ni nani aliyewaloga? Habari juuya kusulubiwa kwake Yesu Kristo

ilielezwa waziwazi mbele ya macho yenu. 2

Napenda kujua tu kitu kimoja kutoka kwenu:Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa sababu yakutimiza matakwa ya Sheria ama kwa sababuya kuisikia na kuiamini Habari Njema? 3 Je, muwajinga kiasi hicho? Ninyi mlianza yote kwamsaada wa Roho je, mnataka sasa kumalizakwa nguvu zenu wenyewe? 4 Je, mambo yaleyote yaliyowapata ninyi yamekuwa bure tu?Haiwezekani! 5 Je, Mungu huwajalia Roho nakutenda miujiza kati yenu ati kwa sababumnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwasababu mnasikia Habari Njema na kuiamini? 6

Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu:

yeye alimwamini Mungu, naye Munguakamkubali kuwa mwadilifu. 7 Sasa basi juenikwamba watu wenye kumwamini ndio waliowatoto halisi wa Abrahamu. 8 MaandikoMatakatifu yalionyesha kabla kwamba Munguatawakubali watu wa mataifa kuwa waadilifukwa njia ya imani. Hivyo Maandiko Matakatifuyalitangulia kumtangazia Abrahamu HabariNjema: “Katika wewe mataifa yoteyatabarikiwa.” 9 Basi, wale walio na imaniwanabarikiwa pamoja na Abrahamualiyeamini. 10 Lakini wote wanaotegemea tukutimiza yanayotakiwa na Sheria, wako chiniya laana. Maana, Maandiko Matakatifuyasema: “Yeyote asiyeshika na kutimiza yoteyaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria, yukochini ya laana.” 11 Ni dhahiri kwamba Sheriahaiwezi kumfanya mtu akubaliwe kuwamwadilifu; maana Maandiko Matakatifuyasema: “Mwadilifu kwa imani ataishi.” 12

Lakini Sheria haitegemei imani, ila Maandikoyasema: “Mwenye kutimiza yanayotakiwa naSheria ataishi.” 13 Kristo alitukomboa kutokakatika laana ya Sheria kwa kujitwalia laana hiyokwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema:“Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”14 Jambo hili lilifanyika kusudi ile barakaaliyopewa Abrahamu iwashukie watu wamataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwaimani, tumpokee yule Roho ambaye Mungualituahidia. 15 Ndugu, nitawapeni mfanokutoka maisha yetu ya kila siku. Fikirini juu yamkataba kati ya watu wawili. Mkataba ukishafanyika na kutiwa sahihi hapana mtuanayeuweka kando au kuuongezea kitu. 16

Basi, Abrahamu alipewa ahadi, yeye pamoja namzawa wake. Maandiko hayasemi: “Na wazawawake,” yaani wengi, bali yasema, “Na mzawawake,” yaani mmoja, naye ndiye Kristo. 17

Ninachotaka kusema ni hiki: Mungu alifanyaagano lake akalithibitisha; Sheria ambayoilitokea miaka mia nne na thelathini baadaye,haiwezi kulitangua hilo agano wala kuibatilishahiyo ahadi. 18 Maana, kama urithi ya Munguinategemea Sheria, basi, haiwezi kutegemeatena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungualimkirimia Abrahamu kwa sababu aliahidi. 19

Ya nini basi, Sheria? Iliongezwa hapo ilikuonyesha uhalifu ni kitu gani, mpakaatakapokuja yule mzawa wa Abrahamualiyepewa ile ahadi. Sheria ililetwa na malaikakwa mkono wa mpatanishi. 20 Ama hakika,mpatanishi hahitajiwi ikiwa jambo lenyewelamhusu mtu mmoja; na Mungu ni mmoja. 21

Je, Sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hatakidogo! Maana, kama kungalitolewa sheriaambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi,tungeweza kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njiaya Sheria. 22 Lakini sivyo; Maandiko Matakatifuyamekwisha sema kwamba ulimwengu woteupo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, kwakumwamini Yesu Kristo, wenye kuaminiwatimiziwe ile ahadi. 23 Kabla ya kujaliwa

WAGALATIA 3:23

147

Page 148: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

5

imani, Sheria ilitufanya wafungwa mpakaimani hiyo iliyokuwa inakuja ifunuliwe. 24 Basi,hiyo Sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpakaalipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani,tukubaliwe kuwa waadilifu. 25 Tangu kufikakwa hiyo imani, Sheria si mlezi wetu tena. 26

Kwa njia ya imani, ninyi nyote mmekuwawatoto wa Mungu katika kuungana na Kristo.27 Ninyi nyote mliobatizwa mkaungana naKristo ni kama vile mmemvaa Kristo. 28 Hivyo,hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki,mtumwa na mtu huru, mwanamume namwanamke. Nyote ni kitu kimoja katikakuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni waKristo, basi ni wazawa wa Abrahamu, namtapokea yale aliyoahidi Mungu.

Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa badomtoto, hawi tofauti na mtumwaingawaje mali yote ni yake. 2 Wakati

huo wote yuko chini ya walezi na wadhaminimpaka wakati ule uliowekwa na baba yake. 3

Hali kadhalika na sisi tulipokuwa bado watoto,tulikuwa watumwa wa pepo watawala waulimwengu. 4 Lakini wakati ule maalumuulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawealiyezaliwa na mwanamke, akaishi chini yaSheria 5 apate kuwakomboa wale waliokuwachini ya Sheria ili sisi tufanywe wana waMungu. 6 Kwa vile sasa ninyi ni wana, Munguamemtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwenu,Roho ambaye hulia “Aba,” yaani “Baba.” 7 Basi,wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa nimwana, basi, wewe utapokea yote Mungualiyowawekea watoto wake. 8 Zamanihamkumjua Mungu na hivyo mkatumikiamiungu isiyo miungu kweli. 9 Lakini sasa, kwavile mnamjua Mungu, au tuseme mnajulikanana Mungu, mnawezaje tena kurudi kwa walepepo maskini na dhaifu hata kutakakuwatumikia tena? 10 Bado mnaadhimishasiku, miezi na miaka! 11 Nahofu kwamba labdakazi niliyoifanya kwa ajili yenu imepotea bure!12 Ndugu, nawasihi muwe kama mimi, kwavile hata mimi nimekuwa kama ninyi.Hamkunitendea ubaya wowote. 13 Mnajuakwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia fursaya kuwahubirieni Habari Njema kwa mara yakwanza. 14 Hata hivyo, wakati ulehamkunidharau wala kunikataa kwa sababu yaudhaifu wangu ingawa mlishawishiwa kufanyahivyo; lakini mlinipokea kama malaika waMungu, kama vile ningekuwa Kristo Yesumwenyewe. 15 Mlikuwa wenye furaha; sasakumetokea nini? Naapa kwamba wakati ulemngaliweza hata kuyang'oa macho yenu nakunipa mimi. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenukwa sababu ya kuwaambieni ukweli? 17 Haowatu wengine wanawahangaikia ninyi, lakininia zao si njema. Wanataka kuwatenganishanami ili ninyi muwahangaikie wao. 18 Kwakweli ni jambo jema daima kuwahangaikiawengine katika mambo mema, na si tu wakatimimi nipo pamoja nanyi. 19 Watoto wangu,

kama vile mama mja mzito anavyotaabikawakati wa kujifungua, mimi nataabika tenakwa ajili yenu mpaka hapo hali yake Kristoitakapoundwa ndani yenu. 20 Laiti ningekuwapamoja nanyi sasa, maana ningalipatamsimamo ufaao juu yenu! Nina wasiwasi sanananyi! 21 Niambieni, enyi mnaopendakutawaliwa na sheria: Je, mnasikia isemavyoSheria? 22 Imeandikwa katika MaandikoMatakatifu kwamba Abrahamu alikuwa nawatoto wawili: mmoja kwa mwanamkemtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru. 23

Yule wa mwanamke mtumwa alizaliwa kamakawaida, lakini yule wa mwanamke hurualizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu. 24

Mambo hayo yamekuwa mfano; mama haowawili ni mfano wa maagano mawili; la kwanzani lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishiwake ni Hagari, na watoto wake wanazaliwautumwani. 25 Hagari anawakilisha mlima Sinaiulioko Arabia, na ni mfano wa Yerusalemu yasasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake. 26

Lakini Yerusalemu ya juu mbinguni ni mji uliohuru, nao ni mama yetu. 27 Maanaimeandikwa: “Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa;paaza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto;maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengizaidi kuliko wa yule aliye na mume.” 28 Sasa,basi, ndugu zangu, ninyi ni watoto wa Mungukutokana na ahadi yake kama alivyokuwaIsaka. 29 Lakini kama vile siku zile yule mtotoaliyezaliwa kwa njia ya kawaida alimdhulumuyule aliyezaliwa kwa uwezo wa Roho waMungu, vivyo hivyo na siku hizi. 30 LakiniMaandiko Matakatifu yasemaje? Yasema:“Mfukuze mama mtumwa pamoja namwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithipamoja na mtoto wa mama huru.” 31 Kwahiyo, basi, ndugu, sisi si watoto wa mtumwabali wa mama huru.

Kristo alitupa uhuru akataka tubakihuru. Basi, simameni imara walamsikubali tena kuwa chini ya nira ya

utumwa. 2 Sikilizeni! Ni mimi Pauloninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa,Kristo hatawafaidia chochote. 3 Nasema tenawazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidikuishika Sheria yote. 4 Kama mnatazamiakukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria,basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje yaneema ya Mungu. 5 Kwa upande wetu, lakini,sisi tunatumaini kwamba kwa nguvu ya Rohotunakubaliwa kuwa waadilifu kwa njia yaimani. 6 Maana ikiwa tumeungana na KristoYesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakunamaana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwamapendo. 7 Mwenendo wenu ulikuwa mzuri!Nani, basi aliyewazuia kuuzingatia ukweli? 8

Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambayeamewaiteni. 9 “chachu kidogo tu huchachushadonge lote la unga!” 10 Kutokana na kuunganakwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwambaninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami.

WAGALATIA 3:24

148

Page 149: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

Tena yeyote huyo anayewavurugeni—awe naniau nani—hakika ataadhibiwa. 11 Na kwaupande wangu, ndugu zangu, kama badoninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwanini basi, bado ninadhulumiwa? Kamaingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu yamsalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote. 12

Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakatawenyewe! 13 Ninyi, ndugu, mliitwa muwe watuhuru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio chakutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswakutumikiana kwa upendo. 14 Maana Sheriayote hutimizwa katika kushika amri hii moja:“Mpende jirani yako kama unavyojipendamwenyewe.” 15 Lakini ikiwa mtaumana nakutafunana kama wanyama, jihadharini msijemkaangamizana wenyewe kwa wenyewe! 16

Basi, nasema hivi: mwenendo wenu nauongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tenatamaa za kidunia. 17 Maana, tamaa za kiduniahupingana na matakwa ya Roho; na matakwaya Roho hupingana na tamaa za kidunia.Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababuhiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyiwenyewe. 18 Kama mkiongozwa na Roho, basi,hamko tena chini ya Sheria. 19 Basi, matendoya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati,ufisadi; 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui,ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano,mafarakano; 21 husuda, ulevi, ulafi na mambomengine kama hayo. Nawaambieni tena kamanilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambohayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalmewa Mungu. 22 Lakini matokeo ya kuongozwana Roho ni mapendo, furaha, amani,uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upolena kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayowezakupinga mambo hayo. 24 Wale walio wa Kristowameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja namawazo yake mabaya na tamaa zake. 25

Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuatemwongozo wake. 26 Basi, tusijivune,tusichokozane wala kuoneana wivu.

Ndugu, kama mkimwona mtu fulaniamekosea, basi, ninyi mnaoongozwa naRoho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe;

lakini fanyeni hivyo kwa upole, mkiwa natahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa. 2

Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyomtatimiza sheria ya Kristo. 3 Mtu akijionakuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyoanajidanganya mwenyewe. 4 Lakini kilammoja na aupime vizuri mwenendo wakemwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anawezakuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa nasababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5

Maana kila mmoja anao mzigo wakemwenyewe wa kubeba. 6 Mwenyekufundishwa neno la Mungu na amshirikishemwalimu wake riziki zake. 7 Msidanganyike;Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtundicho atakachovuna. 8 Apandaye katikatamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu;lakini akipanda katika Roho, atavuna kutokakwa Roho uzima wa milele. 9 Basi, tusichokekutenda mema; maana tusipolegea tutavunamavuno kwa wakati wake. 10 Kwa hiyo, tukiwabado na wakati, tuwatendee watu wote mema,na hasa ndugu wa imani yetu. 11 Tazamenijinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwamkono wangu mwenyewe. 12 Wale wanaotakakuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndiowanaotaka kuwalazimisha ninyi mtahiriwe.Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudiwao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwasababu ya msalaba wa Kristo. 13 Maana, haowenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria;huwataka ninyi mtahiriwe wapate kujivuniaalama hiyo mwilini mwenu. 14 Lakini mimisitajivunia kamwe chochote isipokuwamsalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maanakwa njia ya msalaba huo ulimwenguumesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwakwa ulimwengu. 15 Kutahiriwa au kutotahiriwasi kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya. 16

Wanaoufuata mwongozo huo nawatakiaamani na huruma; amani na huruma kwaIsraeli—Wateule wa Mungu. 17 Basi, sasa mtuyeyote asinisumbue tena, maana alama nilizonazo mwilini mwangu ni zile za Yesu. 18

Ndugu, nawatakieni ninyi nyote neema yaBwana wetu Kristo. Amina.

WAGALATIA 6:18

149

Page 150: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

WAEFESO

Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwamapenzi ya Mungu, nawaandikia ninyiwatu wa Mungu huko Efeso, mlio

waaminifu katika kuungana na Kristo Yesu. 2

Nawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. 3

Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetuYesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristoametubariki kwa kutujalia zawadi zote zakiroho mbinguni. 4 Kabla ya kuumbwaulimwengu, Mungu alituteua tuwe wake katikakuungana na Kristo ili tuwe watakatifu na bilahitilafu mbele yake. Kwa sababu ya upendowake, 5 Mungu alikuwa ameazimia tanguzamani kutuleta kwake kama watoto wake kwanjia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda nakunuia. 6 Basi, tumsifu Mungu kwa sababu yaneema yake tukufu katika Mwanae mpenzi! 7

Maana kwa damu yake Kristo sisitunakombolewa, yaani dhambi zetuzinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neemayake 8 aliotukirimia bila kipimo! Kwa hekimana ujuzi wake wote 9 Mungu alitekeleza kilealichonuia, akatujulisha mpango wakeuliofichika, ambao alikuwa ameazimiakuutekeleza kwa njia ya Kristo. 10 Mpango huoambao angeutimiza wakati utimiapo nikukusanya pamoja viumbe vyote, kila kitumbinguni na duniani, chini ya Kristo. 11 Kilakitu hufanywa kufuatana na mpango nauamuzi wa Mungu; naye Mungu ametuteuasisi tuwe watu wake kwa mapenzi yake katikakuungana na Kristo, kufuatana na azimioalilofanya tangu mwanzo. 12 Basi, sisituliotangulia kumtumainia Kristo tunapaswakuusifu utukufu wa Mungu! 13 Nanyi pia watuwa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wakweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu,mkamwamini Kristo; naye Mungu, ilikuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapigamhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifualiyetuahidia. 14 Huyu Roho ni dhamana yakurithi yote yale Mungu aliyowaahidia watuwake, na jambo hili latuhakikishia kwambaMungu atawakomboa kabisa wote walio wake.Tuusifu utukufu wake! 15 Kwa sababu hiyo,tangu niliposikia juu ya imani yenu kwa BwanaYesu na mapendo yenu kwa watu wa Mungu,16 sijaacha kamwe kumshukuru Mungu kwaajili yenu. Ninawakumbuka katika sala zangu17 ili Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Babamtukufu, awajalieni Roho wake atakayewapahekima na kuwafunulieni Mungu mpate

kumjua. 18 Namwomba Mungu aifunue mioyoyenu iweze kuuona mwanga wake, mpatekutambua lile tumaini alilowaitieni na utukufumkuu wa zawadi alizowawekea watu wake, 19

mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyomkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini.Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawana nguvu ile kuu mno 20 aliyomfufua nayoKristo kutoka wafu, akamketisha kulia kwakembinguni. 21 Huko, Kristo anatawala juu yakila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawalajuu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katikaulimwengu huu na katika ulimwengu ujao. 22

Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguuyake, akamkabidhi kwa kanisa akiwa mkuu wavitu vyote. 23 Kanisa ni mwili wa Kristo, naukamilifu wake yeye anayekamilisha vitu vyotekila mahali.

Ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu yamakosa na dhambi zenu. 2 Wakati ulemliishi kufuatana na mtindo mbaya wa

ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wapepo wenye nguvu wa anga, pepo ambaohuwatawala sasa watu wasiomtii Mungu. 3 Nahata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishikufuatana na tamaa zetu za kidunia nakufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili naakili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao,tulistahili ghadhabu ya Mungu. 4 LakiniMungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupendakwa mapendo yasiyopimika, 5 hata, ingawatulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi,alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema yaMungu ninyi mmeokolewa. 6 Kwa kuunganana Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye,tukatawale pamoja naye mbinguni. 7 Ndivyoalivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakatiza baadaye, ukuu wa neema yake aliyotujaliakwa ukarimu katika kuungana kwetu na KristoYesu. 8 Maana, kwa neema ya Mungummekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hilisi matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi yaMungu. 9 Wala halitokani na matendo yenuwenyewe, asije mtu akajivunia kitu. 10 Sisi niviumbe vyake Mungu, na kwa kuungana naKristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishimaisha ya matendo mema aliyotutayarishiatuyatende. 11 Ninyi mlio kwa asili watu wamataifa mengine—mnaoitwa, “wasiotahiriwa”na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,”(kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao)—kumbukeni mlivyokuwa zamani. 12 Wakatiule ninyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya

WAEFESO 1:2

150

Page 151: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwana sehemu yoyote katika lile agano la zileahadi. Mlikuwa bila matumaini Mungu hapaduniani. 13 Lakini sasa, kwa kuungana naKristo Yesu, ninyi ambao hapo awali mlikuwambali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yakeKristo. 14 Maana Kristo mwenyewe ametuleteaamani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wamataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwiliwake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukutauliowatenganisha na kuwafanya maadui. 15

Aliiondoa ile Sheria ya Wayahudi pamoja naamri zake na kanuni zake, ili kutokana na jamiihizo mbili aumbe jamii moja mpya katikaumoja naye na hivyo kuleta amani. 16 Kwamwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao;kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizokuwa moja na kuzipatanisha na Mungu. 17

Basi, Kristo alikuja akahubiri Habari Njema yaamani kwenu ninyi watu wa mataifa menginemliokuwa mbali na Mungu, na pia kwaWayahudi ambao walikuwa karibu na Mungu.18 Hivyo, kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi nawatu wa mataifa mengine, tunawezakumwendea Baba katika Roho mmoja. 19 Basi,ninyi si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyini raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watuwa jamaa ya Mungu. 20 Mmejengwa juu yamsingi uliowekwa na mitume na manabii, nayeKristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. 21

Yeye ndiye mwenye kulitengeneza jengo lotena kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajiliya B wana. 22 Katika kuungana naye, ninyi piamnajengwa pamoja na wote wengine, muwemakao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.

Kutokana na hayo, mimi Paulo,mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu,namwomba Mungu. 2 Bila shaka

mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neemayake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faidayenu. 3 Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuompango wake uliofichika. (Nimeandika kwaufupi juu ya jambo hili, 4 nanyi mkiyasomamaneno yangu mtaweza kujua jinsininavyoielewa siri hiyo ya Kristo.) 5 Zamaniwatu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasaMungu amewajulisha mitume na manabiiwake watakatifu kwa njia ya Roho. 6 Siriyenyewe ni hii: kwa njia ya Habari Njema watuwa mataifa mengine wanapata sehemu yaopamoja na Wayahudi katika zile baraka zaMungu; wao ni viungo vya mwili uleule, nawanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwanjia ya Kristo Yesu. 7 Mimi nimefanywa kuwamtumishi wa Habari Njema kwa neema yapekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wakemkuu. 8 Mimi ni mdogo kuliko watu wote waMungu; lakini amenijalia neema yake, iliniwahubirie watu wa mataifa utajiri wakeKristo usiopimika, 9 tena niwaangazie watuwote waone jinsi mpango wa Munguuliofichika unavyotekelezwa. Mungu aliyeMuumba wa vitu vyote alificha siri hiyo yake

tangu milele, 10 kusudi, sasa kwa njia yakanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguniwapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo yanamna nyingi. 11 Mungu alifanya jambo hilokufuatana na azimio lake la milele ambaloamelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu. 12

Basi, katika kuungana na Kristo, na kwa njia yaimani katika Kristo, sisi tunathubutukumkaribia Mungu kwa uhodari. 13 Kwa hiyo,nawaombeni msife moyo kwa sababu yamateso ninayopata kwa ajili yenu, maana hayoni kwa ajili ya utukufu wenu. 14 Kwa sababuhiyo, nampigia magoti Baba, 15 aliye asili yajamaa zote duniani na mbinguni. 16

Namwomba Mungu, kadiri ya utajiri wautukufu wake, awajalieni kwa uwezo wa Rohowake, nguvu ya kuwa imara ndani yenu, 17

naye Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani.Namwomba mpate kuwa na mzizi na msingikatika mapendo 18 kusudi muweze kufahamupamoja na watu wote wa Mungu jinsi upendowa Kristo ueneavyo kwa mapana na marefu,kwa kimo na kina. 19 Naam, mpate kujuaupendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwekabisa utimilifu wote wa Mungu. 20 Kwakeyeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazindani yetu, aweza kufanya mambo makuuzaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria; 21

kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa nakatika Kristo Yesu, nyakati zote, milele namilele! Amina.

Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwanamtumikia Bwana, nawasihi muishimaisha yanayostahili wito mlioitiwa. 2

Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenyesaburi; vumilianeni ninyi kwa ninyi kwamapendo. 3 Fanyeni bidii ya kuhifadhi umojauletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyokati yenu. 4 Kuna mwili mmoja na Rohommoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Munguni moja. 5 Kuna Bwana mmoja, imani moja naubatizo mmoja; 6 kuna Mungu mmoja naBaba wa wote, ambaye yuko juu ya wote,afanya kazi katika yote na yuko katika yote. 7

Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri yakipimo alichojaliwa na Kristo. 8 Kamayasemavyo Maandiko: “Alipopaa mbinguni juukabisa, alichukua mateka; aliwapa watuzawadi.” 9 Basi, inaposemwa: “alipaa juu,” inamaana gani? Maana yake ni kwamba, kwanzaalishuka mpaka chini kabisa duniani. 10 Basi,huyo aliyeshuka hapa duniani, ndiye aliyepaajuu ya mbingu zote apate kuujaza ulimwengu.11 Ndiye aliyewapa watu zawadi: wenginealiwajalia wawe mitume, wengine manabii,wengine wawe waeneza Habari Njema,wengine wachungaji na walimu. 12 Alifanyahivyo apate kuwatayarisha watu wote waMungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristoili kuujenga mwili wa Kristo, 13 na hivyo sotetuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana waMungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikiautimilifu wake Kristo mwenyewe. 14 Basi,

WAEFESO 4:14

151

Page 152: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa nakupeperushwa huko na huko kwa kila upepowa mafundisho wanayozua watuwadanganyifu, ili wawapotoshe wengine kwahila. 15 Ila, sisi tukisema ukweli kwa moyo wamapendo tutakua zidi katika kila jambokulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa; 16

chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwilihushikamana pamoja, na mwili wotehutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake.Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yakeipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katikaupendo. 17 Basi, kwa jina la Bwana,nawaonyeni: msiishi tena kama watuwasiomjua Mungu, ambao fikira zao zimekuwaupuuzi mtupu, 18 na akili zao zimo gizani.Wako mbali na uzima wa Mungu, kwa sababuya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao. 19

Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosakatika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina yamambo ya aibu. 20 Lakini ninyi hamkujifunzahivyo juu ya Kristo. 21 Ni dhahiri kwambamlisikia barabara habari zake, na mkiwawafuasi wake mkafundishwa ukweli ulivyokatika Yesu. 22 Basi, acheni mwenendo wenuwa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwaunaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu.23 Jirekebisheni upya rohoni na katika fikirazenu. 24 Vaeni hali mpya ya utu ambayoimeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayohujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifuna utakatifu. 25 Kwa hiyo, acheni uongo. Kilammoja anapaswa kumwambia mwenzakeukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo chamwili wa Kristo. 26 Kama mkikasirika,msikubali hasira yenu iwafanye mtendedhambi, na wala msikae na hasira kutwanzima. 27 Msimpe Ibilisi nafasi. 28 Aliyekuwaakiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazinjema kwa mikono yake, apate kuwa na kitucha kumsaidia mtu aliye maskini. 29 Manenomabaya hata yasisikike kamwe miongonimwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaana ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, iliyawaneemeshe wasikilizaji wenu. 30

Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungumaana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenukwamba ninyi ni watu wake, na thibitishokwamba siku itakuja ambapo Munguatawakomboeni. 31 Basi, achaneni nauhasama, chuki, hasira, kelele, matusi!Achaneni na kila uovu! 32 Muwe na moyomwema na wenye kuhurumiana; kila mmojana amsamehe mwenzake kama naye Mungualivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.

Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyini watoto wake wapenzi. 2 Upendouongoze maisha yenu, kama vile Kristo

alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoamwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzurina tambiko impendezayo Mungu. 3 Kwa vileninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafuwowote ule au choyo visitajwe kamwe

miongoni mwenu. 4 Tena maneno ya aibu, yaupuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu;maneno ya kumshukuru Mungu ndiyoyanayofaa. 5 Jueni wazi kwamba mwasheratiyeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawana kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa ainahiyo hataambulia chochote katika Utawala waKristo na wa Mungu. 6 Msikubalikudanganywa na mtu kwa maneno matupu;maana, kwa sababu ya mambo kama hayoghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.7 Basi, msishirikiane nao. 8 Zamani ninyimlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katikamwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kamawatoto wa mwanga: 9 maana matokeo yamwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. 10

Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana.11 Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya gizabali yafichueni. 12 Mambo yanayotendwa kwasiri ni aibu hata kuyataja. 13 Lakini mamboyale yanayotendwa katika mwanga, ukweliwake hudhihirishwa; 14 na kilakilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyomaana Maandiko yasema: “Amka weweuliyelala, fufuka kutoka wafu, naye Kristoatakuangaza.” 15 Basi, muwe waangalifu jinsimnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, balikama wenye hekima. 16 Tumieni vizuri mudamlio nao maana siku hizi ni mbaya. 17 Kwahiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujuamatakwa ya Bwana. 18 Acheni kulewa divaimaana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe RohoMtakatifu. 19 Zungumzeni kwa maneno yaZaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieniBwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyonimwenu. 20 Mshukuruni Mungu Baba daimakwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu YesuKristo. 21 Kila mmoja amstahi mwenzake kwasababu ya kumcha Kristo. 22 Wake wawatiiwaume zao kama kumtii Bwana. 23 Maanamume anayo mamlaka juu ya mkewe, kamavile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa;naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa,mwili wake. 24 Kama vile kanisa linavyomtiiKristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zaokatika mambo yote. 25 Nanyi waume,wapendeni wake zenu kama Kristoalivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewesadaka kwa ajili yake. 26 Alifanya hivyo, ili kwaneno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baadaya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, 27

kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safukabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochotecha namna hiyo. 28 Basi, waume wanapaswakuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.29 (Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwiliwake; badala ya kuuchukia, huulisha nakuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunzakanisa, 30 maana sisi ni viungo vya mwiliwake.) 31 Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: “Kwa hiyo, mwanamumeatawaacha baba na mama yake, ataungana namkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.”

WAEFESO 4:15

152

Page 153: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

32 Kuna ukweli uliofichika katika manenohaya, nami naona kwamba yamhusu Kristo nakanisa lake. 33 Lakini yanawahusu ninyi pia:kila mume lazima ampende mkewe kama nafsiyake mwenyewe, naye mke anapaswakumstahi mumewe.

Enyi watoto, watiini wazazi wenuKikristo maana hili ni jambo jema. 2

“Waheshimu Baba na mama yako,” hiindiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewaahadi, yaani, 3 “Upate fanaka na miaka mingiduniani.” 4 Nanyi akina baba, msiwachukizewatoto wenu ila waleeni katika nidhamu namafundisho ya Kikristo. 5 Enyi watumwa,watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofuna tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wamoyo kana kwamba mnamtumikia Kristo. 6

Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ilimjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyokama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi niwatumishi wa Kristo. 7 Muwe radhi kutumikiakwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu. 8

Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutendamema, awe mtumwa au mtu huru, atapokeatuzo lake kutoka kwa Bwana. 9 Nanyimnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyowatumwa wenu, na acheni kutumia vitisho.Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao,mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheocha mtu si kitu. 10 Hatimaye, nawatakenimuwe imara katika kuungana na Bwana nakwa msaada wa nguvu yake kuu. 11 Vaenisilaha anazowapeni Mungu mpate kuzipingambinu mbaya za Ibilisi. 12 Maana vita vyenu sivita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi yajeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana

na watawala, wakuu na wenye nguvuwanaomiliki ulimwengu huu wa giza. 13 Kwasababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ileitakapofika muweze kuyapinga mashambulioya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho,muwe bado thabiti. 14 Basi, simameni imara!Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu,uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, 15

na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amaniiwe kama viatu miguuni mwenu. 16 Zaidi yahayo yote, imani iwe daima kama ngaomikononi mwenu, iwawezeshe kuizimamishale ya moto ya yule Mwovu. 17 Upokeeniwokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno laMungu kama upanga mnaopewa na RohoMtakatifu. 18 Salini daima, mkiomba msaadawa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu yaRoho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili yawatu wote wa Mungu. 19 Niombeeni nami piaili niongeapo Mungu anijalie cha kusema,niweze kuwajulisha watu fumbo la HabariNjema kwa uthabiti. 20 Mimi ni balozi kwa ajiliya Habari Njema hiyo ingawa sasa nikokifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodarikatika kuitangaza kama inipasavyo. 21 Tukiko,ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifuwa Bwana, atawapeni habari zangu zotempate kujua ninachofanya. 22 Namtumakwenu awapeni habari zetu mpate kuwa namoyo. 23 Ninawatakieni ninyi ndugu amani,upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba nakutoka kwa Bwana Yesu Kristo. 24 Nawatakianeema ya Mungu wote wanaompenda Bwanawetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo namwisho.

WAEFESO 6:24

153

Page 154: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

WAFILIPI

Mimi Paulo na Timotheo, watumishi waYesu Kristo, tunawaandikia nyinyi watuwa Mungu huko Filipi ambao

mmeunganishwa na Kristo Yesu, pamoja naviongozi na wasaidizi wa kanisa. 2

Tunawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana YesuKristo. 3 Namshukuru Mungu wangu kilaninapowakumbukeni; 4 na kilaninapowaombeeni nyote, nasali kwa furaha, 5

kwa sababu ya jinsi mlivyonisaidia katika kaziya Injili tangu siku ile ya kwanza mpaka leo. 6

Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanzakazi hii njema ndani yenu, ataiendeleza mpakaikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu. 7 Hivyondivyo ninavyopaswa kuwafikirieni, kwaninawakumbukeni daima moyoni mwangu. Kwamaana nyinyi nyote mmeshiriki katika fadhilialiyonijalia Mungu ya kutetea na kuithibitishaInjili, sasa niwapo kifungoni na pia pale awalinilipokuwa huru. 8 Mungu anajua kuwaninasema ukweli ninaposisitiza kwamba, kwaupendo uleule wa Yesu Kristo, natamani sanakuwaoneni. 9 Sala yangu ni hii: Naombaupendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidipamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kilanamna, 10 ili muweze kuchagua jambo lililobora. Hapo ndipo mtakuwa safi na bila lawamayoyote ile katika siku ile ya Kristo. 11 Maishayenu yatajazwa mambo yote yaliyo kweli bora,ambayo Yesu Kristo mwenyewe anawezakuwajalieni, kwa ajili ya utukufu na sifa yaMungu. 12 Ndugu zangu, napenda mfahamukwamba mambo yote yaliyonipata yamesaidiasana kuieneza Injili. 13 Kutokana na hayo,walinzi wote wa ikulu pamoja na wengine wotehapa wanafahamu kwamba niko kifungonikwa sababu mimi namtumikia Kristo. 14 Nahuku kuweko kwangu kifungoni kumewafanyandugu wengi kuwa na imani kwa Bwana, hatawanazidi kuwa hodari katika kuutangazaujumbe wa Mungu bila hofu. 15 Kweli, baadhiyao wanamhubiri Kristo kwa sababu wanawivu na ni watu wagomvi; lakini wenginewanamhubiri Kristo kwa nia nzuri. 16 Hawawanafanya hivyo kwa upendo, kwani wanajuakwamba Mungu amenipa jukumu hili lakuitetea Injili. 17 Hao wengine wanamtangazaKristo kwa mashindano na si kwa moyomnyofu, wakidhani kwamba wataniongezeamateso yangu kifungoni. 18 Haidhuru! Miminafurahi ikiwa tu watu wanamhubiri Kristo kwakila njia, iwe ni kwa nia nzuri au kwa nia

mbaya. Tena nitaendelea kufurahi, 19 kwaninajua kwamba kwa sala zenu na kwa msaadawa Roho wa Yesu Kristo, nitakombolewa. 20

Hamu yangu kubwa na tumaini langu nikwamba kwa vyovyote sitashindwa katikakutimiza wajibu wangu, bali nitakuwa na moyothabiti kila wakati na hasa wakati huu, ili kwamaisha yangu yote, niwapo hai au nikifa,nimpatie Kristo heshima. 21 Kwangu, kuishi niKristo, na kufa ni faida zaidi. 22 Lakini, kamakwa kuishi nitaweza kufanya kazi yenye faidazaidi, basi, sijui nichague lipi! 23 Nakabiliwa nahaya mawili yaliyo sawa. Natamani kuyaachamaisha haya nikakae pamoja na Kristo, jamboambalo ni bora zaidi; 24 lakini ni jambo lamaana zaidi kwenu kama nikiendelea kuishi.25 Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najuakwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyinyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu nafuraha katika imani. 26 Basi, nitakapokuwananyi tena mtakuwa na sababu ya kuonafahari juu yangu katika kuungana na KristoYesu. 27 Basi, jambo muhimu ni kwambamwenendo wenu uambatane na matakwa yaInjili ya Kristo, ili kama nikiweza kuja kwenu aunisipoweza, nipate walau kusikia kwambamnasimama imara mkiwa na lengo moja, nakwamba mnapigana vita kwa pamoja namnayo nia moja kwa ajili ya imani ya Injili. 28

Msiwaogope maadui zenu, bali muwe hodaridaima, na hiyo itawathibitishia kwamba waowatashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungumwenyewe ndiye anayewapeni ushindi. 29

Maana nyinyi mmepewa fadhili ya kumtumikiaKristo si tu kwa kumwamini bali pia kwakuteswa kwa ajili yake. 30 Sasa mwawezakushirikiana nami katika kupigana vita. Vitahivi ni vile mlivyoona nikipigana pale awali naambavyo bado napigana sasa kamamnavyosikia.

Je, maisha yenu katika Kristoyanawapeni nguvu? Je, upendo wakeunawafarijini? Je, mnao umoja na Roho

Mtakatifu na kuoneana huruma nakusikitikiana nyinyi kwa nyinyi? 2 Basi,ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikiramoja, upendo mmoja, moyo mmoja na niamoja. 3 Msifanye chochote kwa moyo wa fitinaau kwa majivuno ya bure; muwe naunyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmojaamwone mwenzake kuwa bora kuliko yeyemwenyewe. 4 Pasiwe na mtu anayetafutafaida yake mwenyewe tu bali faida ya

WAFILIPI 1:2

154

Page 155: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

mwenzake. 5 Muwe na msimamo uleulealiokuwa nao Kristo Yesu: 6 Yeye, kwa asilialikuwa daima Mungu; lakini hakufikirikwamba kule kuwa sawa na Mungu ni kitu chakungangania kwa nguvu. 7 Bali, kwa hiari yakemwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwaliahali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu,akaonekana kama wanadamu. 8

Alijinyenyekesha na kutii mpaka kufa, hatakufa msalabani. 9 Kwa sababu hiyo Mungualimkweza juu kabisa, akampa jina lililo kuukuliko majina yote. 10 Ili kwa heshima ya jinala Yesu, viumbe vyote mbinguni, duniani nakuzimu, vipige magoti mbele yake, 11 na kilamtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwautukufu wa Mungu Baba. Mwanga kwaulimwengu 12 Wapenzi wangu, nilipokuwananyi mlinitii daima, na hata sasa niwapombali nanyi endeleeni kutii. Fanyeni kazi kwahofu na tetemeko kwa ajili ya ukombozi wenu,13 kwani Mungu ndiye afanyaye kazi daimandani yenu, na kuwapeni uwezo wa kutaka nakutekeleza mambo yanayopatana na mpangowake mwenyewe. 14 Fanyeni kila kitu bilakunungunika na bila ubishi, 15 ili mpate kuwawatu safi, wasio na lawama, kama watotowanyofu wa Mungu wanaoishi katikaulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangarakati yao kama nyota zinavyoliangaza anga, 16

mkishika imara ujumbe wa uhai. Na hapondipo nami nitakapokuwa na sababu yakujivunia katika siku ile ya Kristo, kwaniitaonekana dhahiri kwamba bidii yangu na kaziyangu havikupotea bure. 17 Hata ikiwanitatolewa mhanga pamoja na imani yenu iliyotambiko kwa Mungu, basi, nafurahi sana nakuwashirikisha nyinyi nyote furaha hiyo. 18

Hali kadhalika nanyi mnapaswa kufurahi nakunishirikisha mimi furaha yenu. 19 Katikakuungana na Bwana Yesu ninalo tumainikwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenuhivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habarizenu. 20 Sina mtu mwingine kama yeyeambaye anawashughulikieni kwa moyo. 21

Wengine wanashughulikia tu mambo yaowenyewe badala ya kuyashughulikia mamboya Yesu Kristo. 22 Nyinyi wenyewemwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeyena mimi, kama vile mtoto na baba yake,tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili. 23

Kwa hiyo natumaini kumtuma kwenu maranitakapojua jinsi mambo yatakavyoniendea. 24

Na, ninatumaini katika Bwana kwamba namipia nitaweza kuja kwenu karibuni. 25 Nimeonasina budi kumtuma kwenu ndugu yetuEpafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini navitani na ambaye ni mjumbe wenualiyenisaidia katika mahitaji yangu. 26 Anayohamu kubwa ya kuwaoneni nyinyi nyote, naamesikitika sana kwani nyinyi mmepata habarikwamba alikuwa mgonjwa. 27 Naam, alikuwamgonjwa hata karibu ya kufa. Lakini Mungualimwonea huruma, na si yeye peke yake, ila

na mimi pia ili nisipate uchungu zaidi. 28 Basi,nataka sana kumtuma kwenu, ilimtakapomwona mpate kufurahi tena, nayohuzuni yangu itoweke. 29 Mpokeeni, basi, kwafuraha yote kama ndugu katika Bwana.Mnapaswa kuwastahi watu walio kama yeye,30 kwani yeye alikuwa hata karibu ya kufa kwaajili ya kazi ya Kristo, na kuhatarisha maishayake ili aweze kunipa mimi msaada ule ambaohamkuweza kuuleta nyinyi wenyewe.

Hatimaye, ndugu zangu, furahini katikakuungana na Bwana. Sichoki kurudiayale niliyokwisha andika pale awali,

maana yatawaongezeeni usalama. 2

Jihadharini na hao watendao maovu, haombwa, watu wanaosisitiza kujikata mwilini. 3

Watu waliotahiriwa kikweli ni sisi, si wao; kwanisisi twamwabudu Mungu kwa njia ya Rohowake, na kuona fahari katika kuungana naKristo Yesu. Mambo ya nje tu hatuyathamini. 4

Mimi pia ningeweza kuyathamini hayo mamboya nje; na kama yupo mtu anayefikiri kwambaanaweza kuyathamini hayo mambo ya nje,mimi ninayo sababu kubwa zaidi ya kufikirihivyo: 5 Mimi nilitahiriwa siku ya nane baadaya kuzaliwa kwangu; mimi ni wa taifa la Israeli,kabila la Benyamini, Mwebrania halisi. Kuhusukuizingatia sheria mimi nilikuwa Mfarisayo, 6

na nilikuwa na bidii sana hata nikalidhulumukanisa. Kuhusu uadilifu unaopatikana kwakuitii sheria, mimi nilikuwa bila hatia yoyote. 7

Lakini hayo yote ambayo ningeweza kuyafikiriakuwa ni faida, nimeyaona kuwa ni hasara, kwaajili ya Kristo. 8 Naam, wala si hayo tu; ilanaona kila kitu kuwa ni hasara tupu, kwa ajiliya jambo bora zaidi, yaani kumjua Kristo YesuBwana wangu. Kwa ajili yake nimekubalikutupilia mbali kila kitu; nimeyaona hayo yotekuwa ni takataka, ili nimpate Kristo 9 nakuunganishwa naye kabisa. Mimi sitaki tenauadilifu unaotokana na kuitii sheria. Sasaninao ule uadilifu unaopatikana katikakumwamini Kristo; uadilifu utokao kwa Munguna ambao unategemea imani. 10 Ninachotakatu ni kumjua Kristo na kuiona nguvu ya ufufuowake, kushiriki mateso yake na kufanana nayekatika kifo chake, 11 nikitumaini kwamba namipia nitafufuliwa kutoka kwa wafu. 12 Sijidaikwamba nimekwisha faulu au nimekwishakuwa mkamilifu. Naendelea kujitahidi kupatalile tuzo ambalo kwalo Kristo amekwishanipata mimi. 13 Ama kweli, ndugu zangu,sidhani kuwa nimekwisha pata tuzo hilo; lakinijambo moja nafanya: Nayasahau yaleyaliyopita na kufanya bidii kuyazingatia yaleyaliyo mbele. 14 Basi, nimo mbioni kuelekealengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo nimwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njiaya Kristo Yesu. 15 Sisi sote tuliokomaatunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakinikama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi,Mungu atawadhihirishieni jambo hilo. 16 Kwavyovyote, tusonge mbele katika njia hiyohiyo

WAFILIPI 3:16

155

Page 156: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

ambayo tumeifuata mpaka hivi sasa. 17 Nduguzangu, fuateni mfano wangu. Tumewapenimfano mwema, na hivyo wasikilizeni walewanaofuata mfano huo. 18 Nimekwishawaambieni jambo hili mara nyingi, na sasanarudia tena kwa machozi: Watu wengiwanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.19 Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbolao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu yamambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo yakidunia. 20 Lakini sisi ni raia wa mbinguni, natwatazamia kwa hamu kubwa Mwokozi ajekutoka mbinguni, Bwana Yesu Kristo. 21 Yeyeataibadili miili yetu dhaifu na kuifanya ifananena mwili wake mtukufu, kwa nguvu ile ambayokwayo anaweza kuviweka vitu vyote chini yautawala wake.

Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi,ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyimlio furaha yangu na taji ya ushindi

wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imarakatika kuungana na Bwana, enyi wapenziwangu. 2 Euodia na Suntike, nawaombeni nakuwasihi mpatane kama ndugu katika Bwana.3 Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutakauwasaidie akina mama hao, kwani wamefanyakazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami naKlementi na wafanyakazi wenzangu wenginewote ambao majina yao yameandikwa katikakitabu cha uhai. 4 Basi, furahini daima katikakuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! 5

Upole wenu ujulikane kwa watu wote. Bwanayu karibu. 6 Msiwe na wasiwasi juu ya kituchochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungukatika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani.7 Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote zawatu italinda salama mioyo na akili zenu katikakuungana na Kristo Yesu. 8 Hatimaye, nduguzangu, zingatieni mambo mema nayanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli nabora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na yaheshima. 9 Tekelezeni yale mliyojifunza nakupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia

nimesema na kuona nimeyatenda. NayeMungu anayetujalia amani atakuwa pamojananyi. 10 Katika kuungana na Bwana nimepatafuraha kubwa kwamba mwishoni mlipata tenafursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka.Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daimaila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambohilo. 11 Sisemi hivyo sasa kwa sababu nahitajikitu; maana nimejifunza kuridhika na vitunilivyo navyo. 12 Najua hali ya kutokuwa navitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoezakuridhika katika kila hali na mahali; niwe ninacha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada aunimepungukiwa. 13 Naweza kuikabili kila halikwani Kristo hunipa nguvu. 14 Hata hivyo,nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana namikatika taabu zangu. 15 Nyinyi Wafilipimwafahamu wenyewe kwamba mwanzonimwa kuhubiri Habari Njema, nilipokuwanaondoka Makedonia, nyinyi peke yenu ndiokanisa lililonisaidia; nyinyi peke yenu ndiomlioshirikiana nami katika kupokea na kuwapawengine mahitaji. 16 Nilipokuwa nahitajimsaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidiya mara moja. 17 Sio kwamba napenda tukupokea zawadi; ninachotaka ni faidaiongezwe katika hazina yenu. 18 Basi,nimekwisha pokea vitu vyote mlivyonipa, tenani zaidi kuliko nilivyohitaji. Nina kila kitu kwavile sasa Epafrodito amekwisha niletea zawadizenu. Zawadi hizi ni kama tambiko yenyeharufu nzuri, sadaka inayokubaliwa nakumpendeza Mungu. 19 Basi, Mungu wangu,kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo,atawapeni mahitaji yenu yote. 20 Utukufu uwekwa Mungu wetu na Baba yetu, milele namilele. Amina. 21 Nawasalimu watu wote waMungu walio wake Kristo Yesu. Ndugu waliopamoja nami hapa wanawasalimuni. 22 Watuwote wa Mungu hapa, na hasa wale waliokatika ikulu ya mfalme, wanawasalimuni. 23

Nawatakieni nyote neema ya Bwana wetu YesuKristo.

WAFILIPI 3:17

156

Page 157: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

WAKOLOSAI

Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwamapenzi ya Mungu, na nduguTimotheo, 2 tunawaandikia ninyi watu

wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetuwaaminifu katika kuungana na Kristo.Tunawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu. 3 Daima tunamshukuruMungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,wakati tunapowaombea. 4 Maana tumesikiajuu ya imani yenu katika Kristo Yesu na juu yaupendo wenu kwa watu wote wa Mungu. 5

Wakati ujumbe ule wa kweli, yaani HabariNjema, ilipowafikieni kwa mara ya kwanza,mlipata kusikia juu ya lile tumainilinalopatikana kwake. Kwa sababu hiyo imanina upendo wenu vinategemea jambo lilemnalotumainia ambalo mmewekewa salamambinguni. 6 Habari Njema inazidi kuzaamatunda na kuenea ulimwenguni kote kamavile ilivyofanya kwenu ninyi tangu siku ilemliposikia juu ya neema ya Mungu nakuitambua ilivyo kweli. 7 Mlijifunza juu yaneema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishimwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifuwa Kristo kwa niaba yetu. 8 Yeye alitupa habariza upendo wenu mliojaliwa na Roho. 9 Kwasababu hiyo tumekuwa tukiwaombeeni daimatangu tulipopata habari zenu. TunamwombaMungu awajazeni ujuzi kamili wa mapenziyake, awajazeni hekima yote na elimu iletwayona Roho wake. 10 Hapo mtaweza kuishi kamaanavyotaka Bwana na kutenda daimayanayompendeza. Maisha yenu yatakuwayenye matunda ya kila namna ya matendomema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.11 Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wakemtukufu ili mweze kustahimili kila kitu kwauvumilivu. 12 Na kwa furaha, mshukuruniBaba aliyewawezesha ninyi kuwa na sehemuyenu katika mambo yale Mungu aliyowawekeawatu wake katika utawala wa mwanga. 13 Yeyealituokoa katika nguvu ya giza, akatuletasalama katika ufalme wa Mwanae mpenzi, 14

ambaye kwa njia yake tunakombolewa, yaanidhambi zetu zinaondolewa. 15 Kristo ni mfanowa Mungu asiyeonekana; ni mzaliwa wakwanza wa viumbe vyote. 16 Maana kwa njiayake vitu vyote viliumbwa duniani nambinguni, vitu vinavyoonekana navisivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuuna wenye mamlaka. Vyote viliumbwa kwa njiayake na kwa ajili yake. 17 Kristo alikuwakokabla ya vitu vyote; kwa kuungana naye, vyote

vyadumu mahali pake. 18 Yeye ni kichwa chamwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo chauhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo,mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu,ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote. 19

Maana Mungu alipenda utimilifu wote uwendani yake. 20 Kwa njia yake Mungualivipatanisha naye vitu vyote naam, viumbevyote mbinguni na duniania; alileta amani kwadamu ya Kristo msalabani. 21 Hapo kwanzaninyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwaadui zake kwa sababu ya fikira zenu namatendo yenu maovu. 22 Lakini sasa, kwa kifocha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Munguamewapatanisha naye, kusudi awalete mbeleyake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama. 23

Mnapaswa, lakini kuendelea kuwa imara nathabiti katika imani hiyo, na msikubalikusukumwa mbali na tumaini lile mlilopatawakati mlipoisikia Habari Njema. Mimi Paulonimekuwa mtumishi wa hiyo Habari Njemaambayo imekwisha hubiriwa kila kiumbeduniani. 24 Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajiliyenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani,nasaidia kukamilisha kile kilichopungua badokatika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake,yaani kanisa. 25 Nami nimefanywa kuwamtumishi wa kanisa kufuatana na mpangowake Mungu ambao alinikabidhi kwa faidayenu. Mpango wenyewe ni kuutangaza kwaukamilifu ujumbe wake, 26 ambao ni sirialiyowaficha binadamu wote tangu milele,lakini sasa amewajulisha watu wake. 27

Mpango wa Mungu ni kuwajulisha watu wakesiri hii kuu na tukufu ambayo ni kwa ajili yawatu wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristoyuko ndani yenu, na jambo hilo lamaanishakwamba ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu.28 Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwawatu wote; tunawaonya na kuwafundisha wotekwa hekima yote, ili tuweze kumleta kilammoja mbele ya Mungu akiwa amekomaakatika kuungana na Kristo. 29 Kwamadhumuni hayo mimi nafanya kazi nakujitahidi nikiitumia nguvu kuu ya Kristoifanyayo kazi ndani yangu.

Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazikwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili yawatu wa Laodikea na kwa ajili ya wote

ambao hawajapata kuniona kwa macho. 2

Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe nakuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazweuthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli.

WAKOLOSAI 2:2

157

Page 158: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristomwenyewe. 3 Ndani yake zimefichika hazinazote za hekima na elimu. 4 Basi, nawaambieni,msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwamaneno ya uongo hata kama ni ya kuvutiasana. 5 Maana, ingawa mimi niko mbali nanyikwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho,na ninafurahi kuona uthabiti kamilimnaosimama nao pamoja katika imani yenukwa Kristo. 6 Maadamu ninyi mmemkubaliKristo Yesu kuwa Bwana, basi, ishini katikamuungano naye. 7 Mnapaswa kuwa na mizizindani yake, kujijenga juu yake na kuwa imarakatika imani yenu kama mlivyofundishwa.Muwe na shukrani tele. 8 Angalieni basi, mtuasiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wahekima ya kibinadamu, ambayo chanzo chakeni mafundisho ya mapokeo ya watu na ya pepowatawala, na wala si Kristo mwenyewe! 9

Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamuwake, umo ukamilifu wote wa Mungu, 10 nanyimmepewa uzima kamili katika kuungana naye.Yeye yuko juu ya pepo watawala wote nawakuu wote. 11 Katika kuungana na Kristoninyi mlitahiriwa, lakini si kwa toharaifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristomwenyewe, na ambayo inahusikana nakukombolewa kutoka katika utu wa dhambi. 12

Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja naKristo, na katika ubatizo, mlifufuliwa piapamoja naye kwa imani yenu katika nguvu yaMungu ambaye alimfufua Kristo kutoka wafu.13 Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwasababu ya makosa yenu na kwa sababu ninyimlikuwa watu wa mataifa mengine. LakiniMungu amewapa ninyi uzima pamoja naKristo. Mungu ametusamehe dhambi zetuzote; 14 alifutilia mbali ile hati ya deniiliyokuwa inatukabili na masharti yake, nakuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani. 15 Juuya msalaba Kristo aliwapokonya nguvu zaohao pepo watawala na wakuu; aliwafanyakuwa kitu cha fedheha hadharani kwakuwaburuta kama mateka katika msafara waushindi wake. 16 Kwa hiyo, basi, msikubalikupewa masharti na mtu yeyote kuhusuvyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuuya Mwezi mpya au Sabato. 17 Mambo ya ainahiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweliwenyewe ndiye Kristo. 18 Msikubalikuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwawa maana kwa sababu ya maono ya pekee naambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wauongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namnahiyo amepumbazika kwa fikira danganifu zakidunia 19 na amejitenga na Kristo aliyekichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi waKristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwapamoja kwa viungo na mishipa yake, naohukua kama atakavyo Mungu. 20 Ninyimmekufa pamoja na Kristo na kukombolewakutoka nguvu za pepo watawala waulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama

vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya ninikuwekewa masharti: 21 “Msishike hiki,”“Msionje kile,” “Msiguse kile!” 22 Mambo hayoyote yanahusika na vitu vyenye kuharibikamara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo namafundisho ya kibinadamu tu. 23 Kweli,masharti hayo yaonekana kuwa ya hekimakatika namna ya ibada ya kujitakia wenyewe,unyenyekevu wa uongo na kuutendea mwilikwa ukali; lakini kwa kweli, haifai chochotekuzuia tamaa za mwili.

Basi, ikiwa mmefufuka pamoja naKristo, panieni mambo ya juu, kuleKristo aliko, ameketi upande wa kulia

wa Mungu. 2 Muwe na hamu ya mambo yahuko juu, na siyo mambo ya hapa duniani. 3

Maana ninyi mmekufa na uzima wenuumefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4

Uzima wenu halisi ni Kristo, na wakatiatakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokeapamoja naye katika utukufu. 5 Basi,komesheni kabisa kila kitu kilicho ndani yenuambacho chahusika na mambo ya kidunia:uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya nauchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu). 6

Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Munguhuwajia wote wanaomwasi. 7 Wakati mmojaninyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo,mlipotawaliwa nayo. 8 Lakini sasa mnapaswakuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa,uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitokekamwe vinywani mwenu. 9 Msiambianeuongo, kwani ninyi mmekwisha vua ule utu wakale pamoja na matendo yake yote, 10 mkavaautu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa naMungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake,ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu. 11

Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati yaMgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa naasiyetahiriwa, msomi na asiye msomi,mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu,na yumo katika yote. 12 Ninyi ni watu wakeMungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwahiyo basi, vaeni moyo wa huruma, wema,unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13

Vumilianeni na kusameheana iwapo mmojawenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake.Mnapaswa kusameheana kama Bwanaalivyowasamehe ninyi. 14 Zaidi ya hayo yote,zingatieni upendo kwani upendo huunganishakila kitu katika umoja ulio kamili. 15 Nayoamani ya Kristo itawale mioyoni mwenu;maana kwa ajili hiyo ninyi mmeitwa katikamwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani! 16

Ujumbe wa Kristo ukae ndani yenu pamoja nautajiri wake wote. Fundishaneni nakushauriana kwa hekima yote. Imbeni zaburi,nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungumioyoni mwenu kwa shukrani. 17 Na, kilamfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyotekwa jina la Bwana Yesu na kumshukuru MunguBaba kwa njia yake. 18 Enyi akina mama,watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo

WAKOLOSAI 2:3

158

Page 159: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

Bwana. 19 Nanyi waume, wapendeni wakezenu, na msiwe wakali kwao. 20 Enyi watoto,watiini wazazi wenu daima maana hiyohumpendeza Bwana. 21 Nanyi wazazi,msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakatatamaa. 22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenuwa kidunia katika mambo yote, na si tu wakatiwanapowatazama kwa kuwa mnatakakujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwamoyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana. 23

Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote, kwasababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. 24

Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lilealilowawekea watu wake. Mtumikieni KristoBwana! 25 Atendaye mabaya atalipwakufuatana na ubaya wake; Mungu hanaubaguzi.

Nanyi wakuu, watendeeni watumwawenu kwa uadilifu na haki,mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye

Bwana mbinguni. 2 Dumuni katika sala, namnaposali muwe waangalifu, mkimshukuruMungu. 3 Vilevile, mtuombee sisi pia ili Munguatupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhususiri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasakifungoni. 4 Basi, ombeni ili niweze kusemakama inavyonipasa na kwa namnaitakayodhihirisha siri hiyo. 5 Muwe na hekimakatika uhusiano wenu na watu wasioamini,mkitumia vizuri kila nafasi mliyo nayo. 6

Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daimamema na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsiya kumjibu vizuri kila mmoja. 7 Ndugu yetumpenzi Tukiko, mfanyakazi mwaminifu namtumishi mwenzetu katika kazi ya Bwana,atawapeni habari zangu zote. 8 Ndiyo maana

namtuma, ili aichangamshe mioyo yenu kwakuwaambieni habari zetu. 9 Anakuja pamojana Onesimo, ndugu yetu mpenzi namwaminifu, ambaye ni mwananchi mwenzenu.Watawapeni habari za mambo yoteyanayofanyika hapa. 10 Aristarko, ambayeyuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni;hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba,(mmekwisha pata maagizo juu yake; akifikakwenu mkaribisheni). 11 Naye Yoshua aitwayeYusto, anawasalimuni. Miongoni mwaWayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tupeke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja namikwa ajili ya Utawala wa Mungu; naowamekuwa msaada mkubwa kwangu. 12

Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishiwa Kristo Yesu anawasalimuni. Daimaanawaombeeni ninyi kwa bidii ili mpatekusimama imara, mkomae na kuwa thabitikabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.13 Naweza kushuhudia kwamba anafanya kazikwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu waLaodikea na Hierapoli. 14 Luka, daktari wetumpenzi, na Dema, wanawasalimuni. 15 Salamuzetu kwa ndugu zetu wa Laodikea; msalimunidada Nimfa pamoja na jumuiya yote yawaumini inayokutana nyumbani kwake. 16

Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwambainasomwa na Wakristo wa Laodikea; na ninyifanyeni mpango mpate kuisoma baruawaliyoipata kwao. 17 Mwambieni Arkipoaitekeleze vizuri ile huduma aliyokabidhiwa naBwana. 18 Naandika haya kwa mkono wangumwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimiPaulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni.Neema ya Mungu iwe nanyi.

WAKOLOSAI 4:18

159

Page 160: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

1 WATHESALONIKE

Mimi Paulo, Silwano na Timotheotunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisala Thesalonike, ambao ni watu wake

Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. 2

Tunamshukuru Mungu daima kwa ajili yenuninyi nyote na kuwakumbukeni daima katikasala zetu. 3 Maana, mbele ya Mungu Babayetu, twakumbuka jinsi mnavyoonyesha imaniyenu kwa matendo, jinsi upendo wenuunavyowawezesha kufanya kazi kwa bidii, najinsi tumaini lenu katika Bwana wetu YesuKristo lilivyo thabiti. 4 Ndugu, twajua kwambaMungu anawapenda na kwamba amewateuamuwe watu wake, 5 maana wakatitulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwakwa maneno tu, bali pia kwa nguvu na kwaRoho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwambaujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsitulivyoishi pamoja nanyi; tuliishi kwa manufaayenu. 6 Ninyi mlifuata mfano wetu, nakumwiga Bwana. Ingawa mliteswa sana,mliupokea ujumbe huo kwa furaha itokayokwa Roho Mtakatifu. 7 Kwa hiyo ninyimmekuwa mfano mzuri kwa waumini wote waMakedonia na Akaya. 8 Maana, kutokana nabidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si tuhuko Makedonia na Akaya, bali imani yenukwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitajikusema zaidi. 9 Watu hao wanazungumza juuya ziara yetu kwenu: jinsi mlivyotukaribisha,jinsi mlivyoziacha sanamu mkamgeukiaMungu aliye hai na wa kweli, 10 na sasamwamngojea Mwanae ashuke kutokambinguni, Yesu, ambaye Mungu alimfufuakutoka wafu, na ambaye anatuokoa katikaghadhabu ya Mungu inayokuja.

Ndugu, ninyi wenyewe mnafahamukwamba ziara yetu kwenu haikuwabure. 2 Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa

na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenuThesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzanimwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wakuwahubirieni Habari Njema yake. 3 Jambotunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemeauongo au nia mbaya; wala hatupendikumdanganya mtu yeyote. 4 Sisi twanenadaima kama atakavyo Mungu kwani yeyealituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hiiHabari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watuhata kidogo, bali twataka kumpendeza Munguambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani. 5

Ninyi mnajua kwamba sisi hatukuja kwenu namaneno matamu ya kubembeleza wala

hatukutumia maneno ya kijanja ya kufichaubinafsi fulani; Mungu ni shahidi! 6

Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, walakutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote, 7

ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo,tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakinisisi tulikuwa Wapole kati yenu kama alivyomama kwa watoto wake. 8 Tuliwapenda ninyisana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tuHabari Njema ya Mungu, bali pia na maishayetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu! 9

Ndugu, mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi nakutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema yaMungu tulifanya kazi mchana na usiku kusuditusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongonimwenu. 10 Ninyi mnaweza kushuhudia, naMungu pia ni shahidi, jinsi mwenendo wetukati yenu ninyi mnaoamini ulivyokuwa mzuri,mwadilifu na usio na lawama. 11 Mnajuakwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenukama vile baba anavyowatendea watoto wakemwenyewe. 12 Tuliwapeni moyo, tuliwafarijinina kuwahimiza ili mpate kuishi maishayampendezayo Mungu ambaye aliwaitenimshiriki Utawala na utukufu wake. 13 Tenatunayo sababu nyingine ya kumshukuruMungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu,ninyi mliusikia mkaupokea, si kama vileujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe waMungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Munguanafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. 14

Ndugu, ninyi mmepatwa na mambo yaleyaleyaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea,mambo yaliyowapata watu walio wake KristoYesu. Ninyi mlidhulumiwa na wananchiwenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa nawenzao Wayahudi, 15 ambao walimuua BwanaYesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watuhao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kilamtu! 16 Hata walijaribu kutuzuia kuwahubiriawatu wa mataifa mengine ujumbeutakaowaletea wokovu. Ndivyowalivyokamilisha orodha ya dhambi zotewalizotenda siku zote. Lakini sasa hasira yaMungu imewaangukia. 17 Ndugu, kuachanakwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tenakuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na sikwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwana hamu kubwa ya kuwaoneni tena! 18 Kwahiyo tuliamua kuwatembeleeni tena. Nami,Paulo, nilijaribu kuja kwenu zaidi ya maramoja, lakini Shetani alituzuia. 19 Je,tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati

1 WATHESALONIKE 1:2

160

Page 161: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

5

atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwanini? Itakuwa ni ninyi wenyewe; ninyi ndiotumaini letu na furaha yetu. 20 Naam, ninyi niutukufu wetu na furaha yetu!

Mwishowe hatukuweza kuvumilia zaidi.Basi, tuliamua kubaki kule Athene pekeyetu, 2 na kumtuma kwenu ndugu yetu

Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetukwa ajili ya Mungu katika kuhubiri HabariNjema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarishenina kuwafarijini, 3 kusudi imani ya mtu yeyotemiongoni mwenu isije ikafifia kwa sababu yataabu hizo. Ninyi mnajua kwamba tunapaswakupata mateso. 4 Maana, tulipokuwa pamojananyi, tuliwaambieni kwamba tutateswa; nakama mjuavyo ndivyo ilivyotukia. 5 Ndiomaana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuwezakungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipatehabari za imani yenu. Isije ikawa labdaMshawishi aliwajaribuni na kazi yotetuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!6 Sasa Timotheo amekwisha rudi, nayeametupa habari za kufurahisha kuhusu imanina upendo wenu. Ametuarifu kwambamnatukumbuka daima, na kwamba mna hamuya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu yakuwaoneni. 7 Basi, habari za imani yenuzimetutia moyo katika taabu na mateso yetuyote, 8 kwani sasa tunaishi kweli ikiwa ninyimnasimama imara katika kuungana na Bwana.9 Sasa twaweza kumshukuru Mungu wetu kwaajili yenu. Tunamshukuru kwa furaha tuliyonayo mbele yake kwa sababu yenu. 10

Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchanakwa moyo wetu wote ili atupatie fursa yakuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebishachochote kilichopungua katika imani yenu. 11

Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe,na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kujakwenu. 12 Bwana awawezeshe ninyikupendana na kuwapenda watu wote zaidi nazaidi, kama vile sisi tunavyowapenda ninyi. 13

Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwawakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu naBaba yetu wakati Bwana wetu Yesuatakapokuja pamoja na wote walio wake.

Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunzakutoka kwetu namna mnavyopaswakuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli

mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombenina kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanyevema zaidi. 2 Maana mnayajua yale maagizotuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu. 3

Mungu anataka ninyi muwe watakatifu namjiepushe kabisa na maisha ya zinaa. 4 Kilamwanamume anapaswa kujua namna yakuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima, 5

na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifamengine wasiomjua Mungu. 6 Basi, mtuyeyote asimkosee au kumpunja mwenzakekuhusu jambo hili. Tulikwisha waambieni hayona kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibuwanaofanya mambo hayo. 7 Mungu hakutuita

tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katikautakatifu. 8 Kwa hiyo basi, anayedharaumafundisho hayo hamdharau mtu, baliamdharau Mungu mwenyewe anayewapeniRoho wake Mtakatifu. 9 Hakuna haja yakuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenuwaumini. Ninyi wenyewe mmefundishwa naMungu namna mnavyopaswa kupendana. 10

Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenuwote kila mahali katika Makedonia. Basi,ndugu tunawaombeni mfanye hata zaidi. 11

Muwe na nia ya kuishi maisha ya utulivu, kilammoja ashughulikie mambo yake mwenyewena afanye kazi kwa mikono yake mwenyewekama tulivyowaagiza pale awali. 12 Kwanamna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwawale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazimaya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.13 Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu waleambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwena huzuni kama watu wengine wasio namatumaini. 14 Sisi tunaamini kwamba Yesualikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaaminikwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesuwale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.15 Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana;sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki,wakati Bwana atakapokuja, hakikahatutawatangulia wale waliokwisha farikidunia. 16 Maana patatolewa amri, sauti yamalaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu,naye Bwana mwenyewe atashuka kutokambinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwawanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. 17

Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywapamoja nao katika mawingu kumlaki Bwanahewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja naBwana. 18 Basi, farijianeni kwa maneno haya.

Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikienijuu ya nyakati na majira yatakapotukiamambo haya. 2 Maana ninyi wenyewe

mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kamamwizi ajavyo usiku. 3 Watu watakapokuwawanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla!Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchunguwa uzazi unavyomjia mama anayejifungua,wala watu hawataweza kuepukana nayo. 4

Lakini ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyohaipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. 5

Ninyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga,watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, walawa giza. 6 Basi, tusilale usingizi kama wengine;tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi. 7

Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewausiku. 8 Lakini sisi ni watu wa mchana natunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaaimani na upendo kama vazi la kujikingakifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofiaya chuma. 9 Maana Mungu hakututeua ilituangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupatewokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi

1 WATHESALONIKE 5:10

161

Page 162: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. 11 Kwahiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyikama mnavyofanya sasa. 12 Ndugu,tunawaombeni muwastahi wale wanaofanyakazi kati yenu, wale wanaowaongoza nakuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo. 13

Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwasababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amanikati yenu. 14 Ndugu, tunawahimizenimuwaonye watu walio wavivu, muwatie moyowatu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu,muwe na subira kwa wote. 15 Angalieni mtuyeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu,ila nia yenu iwe kutendeana mema daima nakuwatendea mema watu wote. 16 Furahinidaima, 17 salini kila wakati 18 na muwe nashukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka

Mungu kwenu katika kuungana kwenu naKristo Yesu. 19 Msimpinge Roho Mtakatifu; 20

msidharau unabii. 21 Pimeni kila kitu:zingatieni kilicho chema, 22 na epukeni kilaaina ya uovu. 23 Mungu anayetupatia amaniawafanye ninyi watakatifu kwa kila namna nakuzilinda nafsi zenu—roho, mioyo na miiliyenu—mbali na hatia yoyote wakati wa kujakwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeyeanayewaita ninyi atafanya hivyo kwani nimwaminifu. 25 Ndugu, tuombeeni na sisi pia.26 Wasalimuni ndugu wote kwa ishara yaupendo. 27 Nawahimizeni kwa jina la Bwanamuwasomee ndugu zetu wote barua hii. 28

Tunawatakieni neema ya Bwana wetu YesuKristo.

1 WATHESALONIKE 5:11

162

Page 163: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

3

2 WATHESALONIKE

Mimi Paulo, Silwano na Timotheotunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisala Thesalonike, ambao ni watu wake

Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. 2

Tunawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. 3

Ndugu, tunapaswa kushukuru Mungu daimakwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyokwani imani yenu inakua sana na kupendanakwenu kunaongezeka sana. 4 Ndio maana sisitunajivunia ninyi katika makanisa ya Mungu.Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendeleakuamini na kustahimili katika udhalimu wotena mateso mnayopata. 5 Hayo yoteyanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu niya haki, na matokeo yake ninyi mtastahiliUtawala wake ambao kwa ajili yakemnateseka. 6 Mungu atafanya jambo la haki:atawalipa mateso wale wanaowatesa ninyi, 7

na kuwapeni nafuu ninyi mnaoteseka, na sisipia. Atafanya jambo hilo wakati Bwanaatakapotokea kutoka mbinguni pamoja namalaika wake na wakuu 8 na miali ya moto,kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu nawale wasiotii Habari Njema ya Bwana wetuYesu. 9 Adhabu yao itakuwa kuangamizwamilele na kutengwa mbali na utukufu wakemkuu, 10 wakati atakapokuja Siku ile kupokeautukufu kutoka kwa watu wake na heshimakutoka kwa wote wanaoamini. Ninyi piamtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuaminiule ujumbe tuliowaletea. 11 Ndiyo maanatunawaombeeni daima. Tunamwomba Munguwetu awawezeshe muyastahili maishaaliyowaitia myaishi. Tunamwomba, kwa uwezowake, atimize nia yenu ya kutenda mema nakukamilisha kazi yenu ya imani. 12 Kwa namnahiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufukutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutokakwake kwa neema ya Mungu wetu na yaBwana Yesu Kristo.

Sasa yahusu kuja kwake Bwana wetuYesu Kristo na kukusanywa kwetupamoja tukae naye. Ndugu,

tunawaombeni sana 2 msifadhaike upesimoyoni, na wala msitiwe wasiwasi kwa sababuya madai kwamba Siku ya Bwana imekwishafika. Labda inadhaniwa kwamba jambo hililimetokana na uaguzi fulani, mahubiri aubarua inayosemekana kuwa imetoka kwetu. 3

Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwanamna yoyote ile. Maana Siku hiyo haitakujampaka kwanza ule Uasi Mkuu utokee na yule

Mwovu aonekane ambaye mwisho wake nikuangamizwa kabisa. 4 Yeye atapinga kila kituwanachokiona watu kuwa ni mungu, auwanachokiabudu. Naam, hata ataingia nakuketi ndani ya Hekalu la Mungu akijidai kuwaMungu. 5 Je, hamkumbuki kwambaniliwaambieni haya yote wakati nilipokuwapamoja nanyi? 6 Lakini kuna kitukinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho.Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wakeufaao. 7 Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichikaanafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpakayule anayemzuia aondolewe. 8 Hapo ndipoMwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesuanapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywachake na kumwangamiza kwa mng'ao wa kujakwake. 9 Huyo Mwovu atakuja na nguvu zaShetani na kufanya kila namna ya miujiza namaajabu ya uongo, 10 na kutumiaudanganyifu wa kila namna kwa wale waliokatika mkumbo wa kupotea. Hao watapoteakwa sababu hawakuupokea na kuupenda uleukweli ili waokolewe. 11 Ndiyo maana Munguamewaweka chini ya nguvu ya upotovu,wauamini uongo. 12 Matokeo yake ni kwambawote wasioamini ukweli, ila wafurahia dhambi,watahukumiwa. 13 Tunapaswa kumshukuruMungu daima kwa ajili yenu ninyi ndugu, ninyimnaopendwa na Bwana, kwa maana Munguamewateua tangu mwanzo mpate kuokolewakwa nguvu ya Roho mfanywe watu wakewatakatifu kwa imani yenu katika ukweli. 14

Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya HabariNjema tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpatekupokea sehemu yenu katika utukufu waBwana wetu Yesu Kristo. 15 Basi, ndugu,simameni imara na zingatieni yale mafundishotuliyowafundisheni kwa mahubiri yetu nabarua zetu. 16 Tunamwomba Bwana wetuYesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetuambaye alitupenda, na kwa neema yakeakatujalia faraja ya milele na tumaini jema, 17

aifariji mioyo yenu na kuwaimarisheni ilimweze daima kutenda na kusema yaliyomema.

Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbewa Bwana uzidi kuenea upesi nakupokelewa kwa heshima kama vile

ulivyo kati yenu. 2 Ombeni pia ili Munguatuokoe na watu wapotovu na waovu, maanasi wote wanaoamini ujumbe huu. 3 LakiniBwana ni mwaminifu. Yeye atawaimarisheni nakuwalinda salama na yule Mwovu. 4 Naye

2 WATHESALONIKE 3:4

163

Page 164: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

Bwana anatupatia tumaini kubwa juu yenu, nahatuna shaka kwamba mnafanya namtaendelea kufanya yale tuliyowaambieni. 5

Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo waMungu na katika uvumilivu tunaopewa naKristo. 6 Ndugu, tunawaamuru kwa jina laBwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na nduguwote walio wavivu na ambao hawafuatimaagizo tuliyowapa. 7 Ninyi wenyewe mnajuakwamba mnapaswa kufuata mfano wetu. Sisitulipokuwa nanyi hatukuwa wavivu; 8 hatukulachakula kwa mtu yeyote bila ya kumlipa.Tulifanya kazi kwa bidii na taabu mchana nausiku ili tusiwe mzigo kwa mtu yeyote katiyenu. 9 Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatunahaki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababutunataka kuwapeni mfano. 10 Tulipokuwapamoja nanyi tulikuwa tukiwaambieni, “Mtuasiyefanya kazi, asile.” 11 Tunasema mambohayo kwa sababu tumesikia kwamba wakobaadhi yenu ambao ni wavivu na ambao

hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingizakatika mambo ya watu wengine. 12 Kwa jina laBwana wetu Yesu Kristo tunawaamuru nakuwaonya watu hao wawe na nidhamu nakufanya kazi ili wajipatie maslahi yao wenyewe.13 Lakini ninyi ndugu, msichoke kutendamema. 14 Huenda kwamba huko kuna mtuambaye hatautii huu ujumbetunaowapelekeeni katika barua hii. Ikiwahivyo, basi, mfichueni mtu huyo na msiwe nauhusiano wowote naye kusudi aone aibu. 15

Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, balimwonyeni kama ndugu. 16 Bwana mwenyewendiye chanzo cha amani, awajalieni amani sikuzote kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote.17 Kwa mkono wangu mwenyewe naandikahivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyoninavyotia sahihi kila barua; ndivyoninavyoandika. 18 Tunawatakieni nyote neemaya Bwana wetu Yesu Kristo.

2 WATHESALONIKE 3:5

164

Page 165: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

1 TIMOTHEO

Mimi Paulo, mtume wa Yesu Kristo kwaamri ya Mungu Mwokozi wetu na YesuKristo tumaini letu, 2 nakuandikia

Timotheo mwanangu halisi katika imani.Nakutakia neema, huruma na amani kutokakwa Mungu Baba yetu na Kristo Yesu Bwanawetu. 3 Napenda ukae huko Efeso, kamanilivyokuomba nilipokuwa ninakwendaMakedonia. Wako watu fulani hukowanaofundisha mafundisho ya uongo.Wakomeshe watu hao. 4 Waambie waachanena zile hadithi tupu na orodha ndefu zamababu, ambazo huleta tu ubishi, walahaviwajengi watu katika mpango ujulikanaokwa imani. 5 Shabaha ya amri hii ni kuhimizamapendo yatokayo katika moyo safi, dhamirinjema, na imani ya kweli. 6 Watu wenginewamepotoka na kugeukia majadiliano yasiyona maana. 7 Wanapenda kuwa walimu waSheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyeweau mambo wanayosisitiza. 8 Twajua kwambaSheria ni njema, kama ikitumiwa ipasavyo. 9

Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheriahaziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajiliya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu nawenye dhambi, watu wasio na dini na wakidunia. Watu wanaowaua baba na mama zao,au wauaji wowote wale; 10 sheria imewekwakwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaibawatu, waongo, na wanaoapa uongo auwanaofanya chochote ambacho ni kinyumecha mafundisho ya kweli. 11 Mafundisho hayohupatikana katika Habari Njema ambayo miminimekabidhiwa niihubiri, Habari Njema yaMungu mtukufu na mwenye heri. 12

Namshukuru Bwana wetu Yesu Kristo aliyenipanguvu kwa ajili ya kazi yangu. Namshukurukwa kuniona mimi kuwa ni mwaminifu,akaniteua nimtumikie, 13 ingawa pale awalimimi nilimtukana na kumtesa nakumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma,kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyosikujua nilichokuwa ninafanya. 14 LakiniBwana wetu alinijalia neema yake kwa wingi,akanipa imani na upendo katika kuungana naKristo Yesu. 15 Usemi huu ni wa kuaminika, natena unafaa kukubaliwa kabisa: Kristo Yesualikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi.Nami ni mkosefu zaidi kuliko hao wote, 16

lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristoaonyeshe uvumilivu wake wote kwangu mimi,kama mfano kwa wale wote ambao baadayewatamwamini na kupokea uzima wa milele. 17

Kwake yeye aliye Mfalme wa milele naasiyekufa, yeye aliye Mungu pekee—kwakeviwe heshima na utukufu milele na milele!Amina. 18 Mwanangu Timotheo, nakukabidhiamri hii kufuatana na maneno ya unabiiyaliyosemwa zamani juu yako. Yatumiemaneno hayo yawe silaha yako katikakupigana vita vizuri, 19 na ushike imani yakona dhamiri njema. Watu wenginehawakusikiliza dhamiri zao na hivyowakaiharibu imani yao. 20 Miongoni mwao niHumenayo na Aleksanda ambaonimewakabidhi kwa Shetani, ili wafundishwewasimtukane Mungu.

Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala,maombi na sala za shukrani zitolewekwa Mungu kwa ajili ya watu wote, 2

kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka,ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amanipamoja na uchaji wa Mungu na mwenendomwema. 3 Jambo hili ni jema na lampendezaMungu Mwokozi wetu, 4 ambaye anatakawatu wote waokolewe na wapate kuujuaukweli. 5 Maana yuko Mungu mmoja, na piayuko mmoja anayewapatanisha watu naMungu, binadamu Kristo Yesu, 6 ambayealijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote.Huo ulikuwa uthibitisho, wakati ufaaoulipowadia. 7 Kwa sababu hiyo mimi nilitumwaniwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa,niutangaze ujumbe wa imani na ukweli.Nasema ukweli; sisemi uongo! 8 Basi, popotemnapokutana kufanya ibada nataka wanaumewasali, watu waliojitolea kweli na ambaowanaweza kuinua mikono yao wakisali bilahasira wala ubishi. 9 Hali kadhalika, nawatakawanawake wawe wanyofu na wenye busarakuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwaurembo wa mitindo ya kusuka nywele,kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi yagharama kubwa, 10 bali kwa matendo memakama iwapasavyo wanawake wamchaoMungu. 11 Wanawake wanapaswa kukaakimya na kuwa wanyenyekevu wakati wakujifunza. 12 Mimi simruhusu mwanamkeamfundishe au amtawale mwanamume;anapaswa kukaa kimya. 13 Maana Adamualiumbwa kwanza, halafu Hawa. 14 Na wala siAdamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiyealiyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu.15 Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwakupata watoto, kama akidumu katika imani,upendo, utakatifu na unyofu.

1 TIMOTHEO 2:15

165

Page 166: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

5

Msemo huu ni wa kweli: mtu akitakakuwa kiongozi katika kanisa, huyoanatamani kazi nzuri. 2 Basi, kiongozi

wa kanisa anapaswa awe mtu asiye nalawama; anapaswa awe na mke mmoja tu, awemwenye kiasi, nidhamu na utaratibu; ni lazimaawe mkarimu na anayeweza kufundisha; 3

asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole,apendaye amani; asiwe mtu wa kupendafedha; 4 anapaswa awe mtu awezayekuongoza vema nyumba yake, na kuwafanyawatoto wake wawe watii kwa heshima yote. 5

Maana kama mtu hawezi kuongoza vemanyumba yake, atawezaje kulitunza kanisa laMungu? 6 Mtu ambaye hajakomaa bado katikaimani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa,asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kamavile Ibilisi alivyohukumiwa. 7 Anapaswa awemwenye sifa njema kati ya watu walio nje yakanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katikamtego wa Ibilisi. 8 Wasaidizi katika kanisawanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njemana wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai auwenye tamaa ya fedha; 9 wanapaswakuzingatia kwa dhamiri njema ukweli wa ndaniwa imani. 10 Ni lazima kwanza wathibitishwe,na wakionekana kuwa wanafaa, basi, watoehuduma yao. 11 Wake zao wanapaswa piakuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu,wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.12 Msaidizi katika kanisa lazima awe na mkemoja tu, na awezaye kuongoza vema watotowake na nyumba yake. 13 Maana wasaidiziwanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamomzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu yaimani yao katika Kristo Yesu. 14 Ninakuandikiabarua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwakohivi karibuni. 15 Lakini kama nikicheleweshwa,basi, barua hii itakufahamisha mwenendotunaopaswa kuwa nao katika nyumba yaMungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai,na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli. 16

Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri yadini yetu: Alionekana katika umbo lakibinadamu alithibitishwa na Roho kuwa nimwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwakati ya mataifa, aliaminiwa popoteulimwenguni, akachukuliwa juu mbingunikatika utukufu.

Roho asema waziwazi kwamba siku zabaadaye watu wengine wataitupiliambali imani; watazitii roho danganyifu

na kufuata mafundisho ya pepo. 2 Mafundishoya namna hiyo yanaenezwa na watu waongowadanganyifu, ambao dhamiri zao ziko kamazimechomwa kwa chuma cha moto. 3 Watuhao hufundisha kwamba ni makosa kuona napia kula vyakula fulani. Lakini Mungu aliviumbavyakula hivyo, ili wale walio waumini na ambaowanapata kuujua ukweli, wavitumie kwashukrani. 4 Kila kitu alichoumba Mungu nichema, wala hakuna kinachohitaji kukataliwa,bali vyote vipokelewe kwa sala ya shukrani, 5

kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanyakitu hicho kikubalike kwa Mungu. 6 Kamaukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwamtumishi mwema wa Kristo Yesu,ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani namafundisho ya kweli, ambayo weweumeyafuata. 7 Lakini achana na hadithi zilezisizo za kidini na ambazo hazina maana.Jizoeshe kuishi maisha ya uchaji wa Mungu. 8

Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakinimazoezi ya kiroho yana faida za kila namna,maana yanatuahidia uzima katika maisha yasasa, na pia hayo yanayokuja. 9 Usemi huo niwa kusadikika kabisa na unastahili kukubaliwa.10 Sisi tunajitahidi na kufanya kazi kwa bidiikwani tumemwekea tumaini letu Mungu aliyehai ambaye ni Mwokozi wa watu wote, na hasawale wanaoamini. 11 Wape maagizo hayo namafundisho hayo. 12 Usikubali mtu yeyoteakudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakinijitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katikausemi wako, mwenendo wako, upendo, imanina maisha safi. 13 Tumia wakati wako najuhudi yako katika kusoma hadharaniMaandiko Matakatifu, kuhubiri na kufundisha,mpaka nitakapokuja. 14 Usiache kukitumia kilekipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwamaneno ya manabii na kwa kuwekewa mikonona wazee. 15 Fikiri kwa makini juu ya hayo yotena kuyatekeleza kusudi maendeleo yakoyaonekane na wote. 16 Angalia sana mamboyako mwenyewe, na mafundisho yako. Endeleakufanya hayo maana ukifanya hivyo utajiokoamwenyewe na wale wanaokusikiliza.

Usimkemee mtu mzee, bali msihi kamavile angekuwa baba yako. Watendeevijana kama ndugu zako, 2 wanawake

wazee kama mama yako, na wasichana kamadada zako, kwa usafi wote. 3 Waheshimuwanawake wajane walio wajane kweli. 4 Lakinimjane aliye na watoto au wajukuu, haowanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wakidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyokuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hiloni jambo la kupendeza mbele ya Mungu. 5

Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wakumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lakena huendelea kusali na kumwomba msaadausiku na mchana. 6 Lakini mwanamke ambayehuishi maisha ya anasa, huyo amekufa, ingawayu hai. 7 Wape maagizo haya, wasije wakawana lawama. 8 Lakini kama mtu hawatunzi watuwa jamaa yake, hasa wale wa nyumbanikwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na nimbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini. 9 Usimtiekatika orodha ya wajane, mjane yeyoteambaye hajatimiza miaka sitini. Tena aweamepata kuolewa mara moja tu, 10 na awemwenye sifa nzuri: aliyewalea watoto wakevizuri, aliyewakaribisha wageni nyumbanikwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu,aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitoleakufanya mambo mema. 11 Usiwaandikishe

1 TIMOTHEO 3:2

166

Page 167: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

wajane vijana, kwani kama tamaa zao zamaumbile zikizidi kuwa na nguvu zaidi kulikokujitolea kwao kwa Kristo watataka kuolewatena, 12 na wataonekana kukosa uaminifukuhusu ahadi yao ya pale awali. 13 Wajanekama hao huanza kupoteza wakati waowakizurura nyumba hata nyumba; tena ubayazaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu,na kujitia katika mambo ya watu wengine,huku wakisema mambo ambayohawangepaswa kusema. 14 Kwa hiyoningependelea wajane vijana waolewe, wapatewatoto na kutunza nyumba zao ili adui zetuwasipewe nafasi ya kusema mambo maovu juuyetu. 15 Kwa maana wajane wenginewamekwisha potoka na kumfuata Shetani. 16

Lakini kama mama Mkristo anao wajane katikajamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na sikuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisa liwezekuwatunza wajane wale waliobaki peke yaokabisa. 17 Wazee wanaowaongoza watu vizuriwanastahili kupata riziki maradufu, hasa walewanaofanya bidii katika kuhubiri nakufundisha. 18 Maana Maandiko Matakatifuyasema: “Usimfunge ng'ombe kinywaanapopura nafaka.” na tena “Mfanyakaziastahili malipo yake.” 19 Usikubali kupokeamashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa namashahidi wawili au watatu. 20 Walewanaotenda dhambi waonye hadharani, iliwengine wapate kuogopa. 21 Nakuamurumbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, nambele ya malaika watakatifu uyazingatiemaagizo haya bila kuacha hata moja, walakumpendelea mtu yeyote katika kilaunachotenda. 22 Usiharakishe kumwekea mtuyeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia Bwana.Usishiriki dhambi za wengine; jiweke katikahali safi. 23 Usinywe maji tu, bali unywe divaikidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unauguamara kwa mara. 24 Dhambi za watu wenginehuonekana waziwazi, nazo zawatanguliakwenye hukumu; lakini dhambi za wenginehuonekana tu baadaye. 25 Vivyo hivyo,matendo mema huonekana waziwazi, na hatayale ambayo si dhahiri hayawezi kufichika.

Watumwa wote wanapaswakuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe nasababu ya watu kulitukana jina la

Mungu na mafundisho yetu. 2 Watumwaambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharaukwani ni ndugu zao. Badala yake, wanapaswakuwatumikia hata vizuri zaidi, maana haowanaopata faida kutokana na kazi yao niwaumini ambao wanawapenda. Unapaswakufundisha na kuhubiri mambo haya. 3 Mtuyeyote anayefundisha kinyume cha mambohaya, na ambaye hakubaliani na maneno yakweli ya Bwana wetu Yesu Kristo namafundisho ya dini, 4 huyo amejaa majivunona wala hajui chochote. Ni mtu wa kupenda

ubishi na magombano juu ya maneno matupu,na hiyo husababisha wivu, ugomvi, matusi,shuku mbaya, 5 na ubishi usio na kikomokutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika,na ambao hawana tena ukweli. Wanadhanidini ni njia ya kujipatia utajiri. 6 Kweli dinihumfanya mtu awe tajiri sana, ikiwaanatosheka na vitu alivyo navyo. 7 Maanahatukuleta kitu chochote hapa duniani, walahatutachukua chochote. 8 Kwa hiyo basi, kamatunacho chakula na mavazi, tunapaswakuridhika navyo. 9 Lakini wale wanaotakakutajirika huanguka katika majaribu, nakunaswa katika mtego wa tamaa nyingi mbayaza kipumbavu, ambazo huwavuta mpakakwenye uharibifu na maangamizi. 10 Kwamaana kupenda sana fedha ni chanzo chauovu wote. Watu wengine wametamani sanakupata fedha hata wakatangatanga mbali naimani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuninyingi. 11 Lakini wewe, mtu wa Mungu,jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu,uchaji wa Mungu, imani, mapendo, subira naunyenyekevu. 12 Piga mbio kadiri uwezavyokatika shindano la mbio za imani, ukajipatietuzo la uzima wa milele, uliloitiwa wakatiulipokiri imani yako mbele ya mashahidiwengi. 13 Mbele ya Mungu anayevipa vituvyote uhai, na mbele ya Yesu Kristo aliyetoaushahidi na kukiri ukweli mbele ya PontioPilato, 14 nakuamuru ushike maagizo yako nakuyatii kwa uaminifu mpaka Siku ileatakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo. 15

Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaaouliopangwa na Mungu mwenye heri na aliyeMtawala pekee, Mfalme wa wafalme, naBwana wa mabwana. 16 Yeye peke yakeanaishi milele, katika mwanga usiowezakukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepatakumwona au awezaye kumwona. Kwake iweheshima na uwezo wa milele! Amina. 17

Waamuru watu walio matajiri katika mambo yamaisha ya sasa, wasijivune, wasiweke tumainilao katika mali isiyoweza kutegemewa; baliwamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimuhutupatia vitu vyote tuvifurahie. 18 Waamuruwatende mema, wawe matajiri katika matendomema, na wawe wakarimu na walio tayarikuwashirikisha wengine mali zao. 19 Kwanamna hiyo watajiwekea hazina ambayoitakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao.Hapo wataweza kujipatia uzima ambao niuzima wa kweli. 20 Timotheo, tunza salamayote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe namajadiliano ya kidunia na ubishi wakipumbavu juu ya kile wanachokiita watuwengine: “Elimu”. 21 Maana wenginewamejidai kuwa na hiyo elimu, na matokeoyake wamepoteza imani. Nawatakieni nyoteneema!

1 TIMOTHEO 6:21

167

Page 168: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

2 TIMOTHEO

Mimi Paulo, ambaye Mungu alitakaniwe mtume wa Kristo Yesu iliniutangaze ule uzima tulioahidiwa

katika kuungana na Kristo Yesu, 2 nakuandikiawewe mwanangu mpenzi Timotheo. Nakutakianeema, huruma na amani kutoka kwa MunguBaba na Kristo Yesu Bwana wetu. 3

Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikiakwa dhamiri safi kama walivyofanya wazeewangu; namshukuru kila ninapokukumbukadaima katika sala zangu. 4 Nakumbukamachozi yako na ninatamani usiku na mchanakukuona, ili nijazwe furaha. 5 Naikumbukaimani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayonyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike.Nina hakika kwamba wewe pia unayo. 6 Ndiomaana nakukumbusha ukiweke motomoto kilekipaji ulichopewa na Mungu wakatinilipokuwekea mikono yangu. 7 Kwa maanaMungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwewaoga, bali alitupa Roho wa kutujalia nguvu,upendo na nidhamu. 8 Basi, usione hayakumshuhudia Bwana wetu, wala usione hayakwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwaajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajiliya Habari Njema, kadiri ya nguvu unazopewana Mungu. 9 Yeye alituokoa, akatuita tuwewatu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu yamatendo yetu wenyewe bali kwa sababu yakusudi lake na neema yake. Alitujalia neemahiyo katika Kristo Yesu kabla mwanzo wanyakati; 10 lakini sasa imefunuliwa kwetu kwakuja kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeyeamekomesha nguvu za kifo, na kwa njia yaHabari Njema akadhihirisha uzima usio kufa.11 Mungu amenichagua mimi niwe mtume namwalimu kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema,12 nami nateseka mambo haya kwa sababuhiyo. Lakini niko bado timamu kabisa kwaninamjua yule niliyemwamini, tena nina hakikakwamba yeye aweza kukilinda salama kilealichonikabidhi, mpaka Siku ile. 13 Shika kwamakini mafundisho yale ya kweliniliyokufundisha, na kubaki katika hiyo imanina huo upendo wetu katika kuungana naKristo Yesu. 14 Jambo lile bora ulilokabidhiwalilinde kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeishindani yetu. 15 Kama unavyojua, watu wotemkoani Asia wameniacha, miongoni mwaowakiwa Fugelo na Hermogene. 16 Bwanaaihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababualiniburudisha rohoni mara nyingi, walahakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni, 17

ila mara tu alipofika Roma, alianza kunitafutakwa bidii mpaka akanipata. 18 Bwana amjaliehuruma katika Siku ile! Nawe wajua vizurimengi aliyonifanyia huko Efeso.

Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvukatika neema tunayopata katikakuungana na Kristo Yesu. 2 Chukua

yale mafundisho uliyonisikia nikitangazambele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwawatu wanaoaminika, ambao watawezakuwafundisha wengine pia. 3 Shiriki katikamateso kama askari mwaminifu wa Kristoyesu. 4 Mwanajeshi vitani hujiepusha nashughuli za maisha ya kawaida ili awezekumpendeza mkuu wa jeshi. 5 Mwanariadhayeyote hawezi kushinda na kupata zawadi yaushindi kama asipozitii sheria za michezo. 6

Mkulima ambaye amefanya kazi ngumuanastahili kupata sehemu ya kwanza yamavuno. 7 Fikiria hayo ninayosema, kwaniBwana atakuwezesha uyaelewe yote. 8

Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutokawafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kamaisemavyo Habari Njema ninayoihubiri. 9 Kwasababu ya kuihubiri Habari Njema miminateseka na nimefungwa minyororo kamamhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezikufungwa minyororo, 10 na hivyo navumiliakila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili waopia wapate ukombozi upatikanao kwa njia yaYesu Kristo, na ambao huleta utukufu wamilele. 11 Usemi huu ni wa kweli: “Ikiwatulikufa pamoja naye, tutaishi pia pamojanaye. 12 Tukiendelea kuvumilia, tutatawala piapamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.13 Tukikosa kuwa waaminifu, yeye hubakimwaminifu daima, maana yeye hawezikujikana mwenyewe.” 14 Basi, wakumbushewatu wako mambo haya, na kuwaonya mbeleya Mungu waache ubishi juu ya maneno.Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuukwa wale wanaousikia. 15 Jitahidi kupata kibalikamili mbele ya Mungu kama mfanyakaziambaye haoni haya juu ya kazi yake, naambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.16 Jiepushe na majadiliano ya kidunia na yakipumbavu; kwani hayo huzidi kuwatengawatu mbali na Mungu. 17 Mafundisho ya ainahiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongonimwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo naFileto. 18 Hawa wamepotoka kabisa mbali naukweli, na wanatia imani ya watu wenginekatika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu

2 TIMOTHEO 1:2

168

Page 169: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

umekwisha fanyika. 19 Lakini msingi thabitiuliowekwa na Mungu uko imara, na juu yakeyameandikwa maneno haya: “Bwanaanawafahamu wale walio wake,” na “Kilaasemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachanena uovu.” 20 Katika nyumba kubwa kunamabakuli na vyombo vya kila namna: vingineni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao naudongo, vingine ni vya matumizi ya pekee navingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida. 21

Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitengambali na mambo hayo yote maovu, atakuwachombo cha matumizi ya pekee, kwa sababuamewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake nayupo tayari kwa kila kazi njema. 22 Jiepushe natamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo,amani, pamoja na watu wote ambaowanamwomba Bwana kwa moyo safi. 23

Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajuakwamba hayo huleta magomvi. 24 Mtumishiwa Bwana asigombane. Anapaswa kuwampole kwa watu wote, mwalimu mwema namvumilivu, 25 ambaye ni mpole anapowaonyawapinzani wake, kwani huenda Munguakawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujuaukweli. 26 Hapo fahamu zao zitawarudia tena,wakaponyoka katika mtego wa Ibilisialiyewanasa na kuwafanya wayatii matakwayake.

Kumbuka kwamba, katika siku zamwisho kutakuwa na nyakati za taabu.2 watu watakuwa na ubinafsi, wenye

tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenyekujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatiiwazazi wao, wasio na shukrani na waovu; 3

watatokea watu wasio na upendo moyoni,wasio na huruma, wachongezi, walafi nawakali; watachukia chochote kilicho chema; 4

watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi;watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. 5

Kwa nje wataonekana kama watu wenyekumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake.Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo. 6

Baadhi yao huenda katika nyumba za watu nahuwateka wanawake dhaifu waliolemewamizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa natamaa za kila aina; 7 wanawake ambaowanajaribu daima kujifunza lakini hawawezikuufikia ujuzi wa huo ukweli. 8 Watu haohuupinga ukweli kama vile Yane na Yambrewalivyompinga Mose. 9 Lakini hawatawezakuendelea zaidi kwa maana upumbavu waoutaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwakwa akina Yane na Yambre. 10 Wewe lakini,umeyafuata mafundisho yangu, mwenendowangu, makusudi yangu katika maisha, imaniyangu, uvumilivu wangu, upendo wangu,subira yangu, 11 udhalimu na mateso yangu.Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia,Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwamno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambohayo yote. 12 Kila mtu anayetaka kuishimaisha ya kumcha Mungu katika kuungana na

Kristo Yesu lazima adhulumiwe. 13 Watuwaovu na wadanyanyifu watazidi kuwa waovuzaidi na zaidi kwa kuwadanganya wengine nakudanganyika wao wenyewe. 14 Lakini wewedumu katika ukweli ule uliofundishwa,ukaukubali kabisa. Unawajua wale waliokuwawalimu wako. 15 Unakumbuka kwamba tanguutoto wako umeyajua Maandiko Matakatifuambayo yaweza kukupatia hekima iletayowokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu. 16

Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwauongozi wa Mungu, na yanafaa katikakufundishia ukweli, kuonya, kusahihishamakosa, na kuwaongoza watu waishi maishaadili, 17 ili mtu anayemtumikia Mungu awemkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila tendojema.

Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbeleya Kristo Yesu atakayewahukumu watuwalio hai na wafu, na kwa sababu

anakuja kutawala akiwa Mfalme: 2 hubiri huoujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wakufaa au wakati usiofaa), karipia, onya nahimiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivuwote. 3 Utakuja wakati ambapo watuhawatasikiliza mafundisho ya kweli, ilawatafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyiawalimu tele watakaowaambia mambo yale tuambayo masikio yao yako tayari kusikia. 4

Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithiza uongo. 5 Wewe, lakini, uwe macho katikakila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiriwa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishiwako. 6 Kwa upande wangu mimi, niko karibukabisa kutolewa dhabihu na wakati wa kufarikikwangu umefika. 7 Nimefanya bidii katikamashindano, nimemaliza safari yote na imaninimeitunza. 8 Na sasa imebakia tu kupewatuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzoambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimiSiku ile na wala si mimi tu, ila na wale wotewanaotazamia kwa upendo kutokea kwake. 9

Fanya bidii kuja kwangu karibuni. 10 Demaameupenda ulimwengu huu akaniacha nakwenda zake Thesalonike. Kreske amekwendaGalatia, na Tito amekwenda Dalmatia. 11 Lukapeke yake ndiye aliye hapa pamoja nami.Mpate Marko uje naye, kwa maana atawezakunisaidia katika kazi yangu. 12 NilimtumaTukiko kule Efeso. 13 Utakapokuja niletee kotilangu nililoacha kwa Karpo kule Troa; nileteepia vile vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwakwa ngozi. 14 Yule sonara aitwaye Aleksandaamenitendea maovu mengi; Bwana atamlipakufuatana na hayo matendo yake. 15 Jihadharinaye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwaukali. 16 Wakati nilipojitetea kwa mara yakwanza hakuna mtu aliyesimama upandewangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabiekosa hilo! 17 Lakini, Bwana alikaa pamojanami, akanipa nguvu, hata nikawezakuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifawausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya

2 TIMOTHEO 4:17

169

Page 170: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

kifo kama kinywani mwa simba. 18 Bwanaataniokoa na mambo yote maovu, nakunichukua salama mpaka katika Utawalawake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milelena milele! Amina. 19 Wasalimu Priska na Akula,pamoja na jamaa ya Onesiforo. 20 Erasto

alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwachaMileto kwa sababu alikuwa mgonjwa. 21 Fanyabidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo,Pude, Lino na Klaudia wanakusalimu; vilevilendugu wengine wote. 22 Bwana awe nawerohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.

2 TIMOTHEO 4:18

170

Page 171: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

TITO

Mimi Paulo, mtumishi wa Mungu namtume wa Yesu Kristo naandika. Miminimechaguliwa kuijenga imani ya

wateule wa Mungu na kuwaongozawaufahamu ukweli wa dini yetu, 2 ambayomsingi wake ni tumaini la kupata uzima wamilele. Mungu ambaye hasemi uongo,alituahidia uzima huo kabla ya mwanzo wanyakati, 3 na wakati ufaao ulipowadia,akaudhihirisha katika ujumbe wake. Miminilikabidhiwa ujumbe huo nuutangazekufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wakweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakianeema na amani kutoka kwa Mungu Baba, nakutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu. 5

Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mamboambayo hayakuwa yamekamilika bado, nakuwateua wazee wa kanisa katika kila mji.Kumbuka maagizo yangu: 6 mzee wa kanisaanapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye namke mmoja tu, na watoto wake wanapaswakuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofiau wakaidi. 7 Maana kwa vile kiongozi wakanisa ni mkurugenzi wa kazi ya Mungu,anapaswa kuwa mtu asiye na hatia. Asiwemwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi,mkorofi au mchoyo. 8 Anapaswa kuwamkarimu na anayependa mambo mema.Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu,mtakatifu na mwenye nidhamu. 9 Ni lazimaashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminikakama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyowezakuwatia wengine moyo kwa mafundisho yakweli na kuyafichua makosa ya walewanaoyapinga mafundisho hayo. 10 Maana,wako watu wengi, hasa wale walioongokakutoka dini ya Kiyahudi, ambao ni wakaidi,wanaowapotosha wengine kwa upumbavuwao. 11 Lazima kukomesha maneno yao,kwani wanavuruga jumuiya nzima kwakufundisha mambo ambayo hawapaswikufundisha; wanafanya hivyo kwa nia mbayaya kupata faida ya fedha. 12 Hata mmoja wamanabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete,alisema: “Wakrete, husema uongo daima; nikama wanyama wabaya, walafi na wavivu!” 13

Naye alitoboa ukweli kwa sababu hiyo,unapaswa kuwakaripia vikali, ili wawe na imanikamilifu. 14 Wasiendelee kushikilia hadithitupu za Kiyahudi na maagizo ya kibinadamuyanayozuka kwa watu walioukataa ukweli. 15

Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini

hakuna chochote kilicho safi kwa walewaliochafuliwa na wasioamini, maana dhamirina akili zao zimechafuliwa. 16 Watu kama haohujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwamatendo yao humkana. Ni watu wa kuchukizamno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolotejema.

Lakini wewe unapaswa kuhubirimafundisho safi. 2 Waambie wazeekwamba wanapaswa kuwa na kiasi,

wawe na busara na wataratibu; wanapaswakuwa timamu katika imani yao, upendo nauvumilivu. 3 Hali kadhalika waambiewanawake wazee wawe na mwenendo wauchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi, auwatumwa wa pombe. Wanapaswa kufundishamambo mema, 4 ili wawazoeze kina mamavijana kuwapenda waume zao na watoto, 5

wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mamboya nyumbani, na wawatii waume zao, iliujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa. 6

Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi. 7

Katika mambo yote wewe mwenyeweunapaswa kuwa mfano wa matendo mema.Uwe mnyofu na uwe na uzito katikamafundisho yako. 8 Maneno yako yasiwe nahitilafu yoyote ili adui zako waaibikewasipopata chochote kibaya cha kusema juuyetu. 9 Watumwa wanapaswa kuwatii wakuuwao na kuwapendeza katika mambo yote.Wasibishane nao, 10 au kuiba vitu vyao. Badalayake wanapaswa kuonyesha kwamba wao niwema na waaminifu daima, ili, kwa matendoyao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juuya Mungu, Mwokozi wetu. 11 Maana neema yaMungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wawatu wote. 12 Neema hiyo yatufunzakuachana na uovu wote na tamaa za kidunia;tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumchaMungu katika ulimwengu huu wa sasa, 13

tukiwa tunangojea siku ile ya heritunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufuwa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu iliatukomboe kutoka katika uovu wote nakutufanya watu safi walio wake yeyemwenyewe, watu walio na hamu ya kutendamema. 15 Basi, fundisha mambo hayo natumia mamlaka yako yote ukiwahimiza nakuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote naasikudharau.

TITO 2:15

171

Page 172: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3Wakumbushe watu kuwastahi watawalana wenye mamlaka, kuwatii na kuwatayari kwa kila namna kutenda mambo

yote mema. 2 Waambie wasimtukane mtuyeyote; bali waishi kwa amani na masikizano,wawe daima wapole kwa kila mtu. 3 Maana,wakati mmoja sisi tulikuwa wapumbavu,wakaidi na wapotovu. Tulikuwa watumwa watamaa na anasa za kila aina. Tuliishi maisha yauovu na wivu; watu walituchukia nasitukawachukia. 4 Lakini wakati wema naupendo wa Mungu, Mwokozi wetu,ulipofunuliwa, 5 alituokoa. alituokoa si kwasababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi,bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake,kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujaliatuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwakutuosha kwa maji. 6 Mungu alitumiminiaRoho Mtakatifu bila kipimo kwa njia ya YesuKristo, Mwokozi wetu, 7 ili kwa neema yaketupate kukubaliwa kuwa waadilifu nakuupokea uzima wa milele tunaoutumainia. 8

Jambo hili ni kweli. Ninakutaka uyatilie mkazomambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu,

wawe na hamu ya kuutumia wakati wao katikakutenda mema, ambayo ni mambo mazuri naya manufaa kwa watu. 9 Lakini jiepushe naubishi wa kipumbavu, ugomvi na mabishanojuu ya Sheria. Mambo hayo hayana faidayoyote na ni ya bure tu. 10 Mtuanayesababisha mafarakano mpe onyo lakwanza na la pili, kisha achana naye. 11 Wajuakwamba mtu wa namna hiyo amepotokakabisa, na dhambi zake zathibitisha kwambaamekosea. 12 Baada ya kumtuma kwakoArtema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoliunione, maana nimeamua kukaa huko wakatiwa majira ya baridi. 13 Jitahidi kumsaidiamwana sheria Zena na Apolo ili wawezekuanza ziara zao na uhakikishe kwamba wanakila kitu wanachohitaji. 14 Ni lazima watu wetuwajifunze kuutumia wakati wao katika kutendamema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, namaisha yao yawe ya kufaa. 15 Watu wote waliopamoja nami wanakusalimu. Wasalimu rafikizetu katika imani. Nawatakieni nyote neema yaMungu.

TITO 3:2

172

Page 173: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

FILEMONI

Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya KristoYesu, na ndugu Timotheo,ninakuandikia wewe Filemoni

mpendwa, mfanyakazi mwenzetu 2 na kanisalinalokutana nyumbani kwako, na wewe dadaAfia, na askari mwenzetu Arkupo. 3

Tunawatakieni neema na amani kutoka kwaMungu Baba yetu, na kwa Bwana yesu Kristo.4 Kila wakati ninaposali nakukumbuka weweFilemoni, na kumshukuru Mungu 5 maananasikia habari za imani yako kwa Bwana wetuYesu na upendo wako kwa watu wote waMungu. 6 Naomba ili imani hiyo unayoshirikipamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzimkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopatakatika kuungana kwetu na Kristo. 7 Ndugu,upendo wako yameniletea furaha kubwa nakunipa moyo sana! Nawe umeichangamshamioyo ya watu wa Mungu. 8 Kwa sababu hiyo,ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa nduguyako katika Kristo, kukuamuru ufanyeunachopaswa kufanya. 9 Lakini kwa sababu yaupendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanyahivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa KristoYesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake. 10

Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusumwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangukatika Kristo kwani nimekuwa baba yakenikiwa kifungoni. 11 Ni Onesimo yuleyuleambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu,lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia. 12 Sasanamrudisha kwako, naye ni kama moyo wangumimi mwenyewe. 13 Ningependa akae namihapa anisaidie badala yako wakati niwapo

kifungoni kwa sababu ya Habari Njema. 14

Lakini sitafanya chochote bila kibali chako.Sipendi kukulazimisha unisaidie, kwani wemawako unapaswa kutokana na hiari yako wewemwenyewe na si kwa kulazimika. 15 LabdaOnesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu,kusudi uweze tena kuwa naye daima. 16 Nasasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi yamtumwa: yeye ni ndugu yetu mpenzi. Na wamaana sana kwangu mimi, na kwako atakuwawa maana zaidi kama mtumwa na kamandugu katika Bwana. 17 Basi, ikiwawanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokeetena kama vile ungenipokea mimi mwenyewe.18 Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwana deni lako, basi, unidai mimi. 19 Naandikajambo hili kwa mkono wangu mwenyewe:Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusemakwamba wewe unalo deni kwangu la nafsiyako.) 20 Haya, basi, ndugu yangu, nifanyiejambo hilo kwa ajili ya jina la Bwana; burudishamoyo wangu kama ndugu katika Kristo. 21

Naandika nikitumaini kwamba utanikubaliaombi langu; tena najua kwamba utafanya hatazaidi ya haya ninayokuomba. 22 Pamoja nahayo, nitayarishie chumba kwani natumainikwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalianiwatembeleeni. 23 Epafra, mfungwamwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu,anakusalimu. 24 Nao akina Marko, Aristarko,Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu,wanakusalimu. 25 Nawatakieni ninyi nyoteneema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

FILEMONI 1:25

173

Page 174: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

WARAKA KWA WAEBRANIA

Hapo zamani, Mungu alisema na babuzetu mara nyingi kwa namna nyingikwa njia ya manabii, 2 lakini siku hizi za

mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae.Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungualiumba ulimwengu na akamteua avimiliki vituvyote. 3 Yeye ni mng'ao wa utukufu waMungu, na mfano kamili wa hali ya Mungumwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwaneno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatiabinadamu msamaha wa dhambi zao, aliketihuko juu mbinguni, upande wa kulia waMungu Mkuu. 4 Mwana ni mkuu zaidi kulikomalaika, kama vile jina alilopewa na Mungu nikuu zaidi kuliko jina lao. 5 Maana Munguhakumwambia kamwe hata mmoja wa malaikawake: “Wewe ni Mwanangu; Mimi leonimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu yamalaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake,naye atakuwa Mwanangu.” 6 Lakini Mungualipokuwa anamtuma Mwanae mzaliwa wakwanza ulimwenguni, alisema: “Malaika wotewa Mungu wanapaswa kumwabudu.” 7 Lakinikuhusu malaika, Mungu alisema: “Munguawafanya malaika wake kuwa pepo, nawatumishi wake kuwa ndimi za moto.” 8 Lakinikumhusu Mwana, Mungu alisema: “Utawalawako ee Mungu, wadumu milele na milele!Wewe wawatawala watu wako kwa haki. 9

Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu.Ndiyo maana Mungu, Mungu wakoamekuweka wakfu na kukumiminia furahakubwa zaidi kuliko wenzako.” 10 Pia alisema:“Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo,mbingu ni kazi ya mikono yako. 11 Hizozitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zotezitachakaa kama vazi. 12 Utazikunjakunjakama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi.Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yakohayatakoma.” 13 Mungu hakumwambiakamwe hata mmoja wa malaika wake: “Ketiupande wangu wa kulia, mpaka niwaweke aduizako chini ya miguu yako.” 14 Malaika ni rohotu wanaomtumikia Mungu, na Munguhuwatuma wawasaidie wale watakaopokeawokovu.

Kwa sababu hiyo tunapaswa kuzingatiakwa makini zaidi yote tuliyosikia, ilitusije tukapotoshwa. 2 Ujumbe ule

waliopewa wazee wetu na malaikaulionyeshwa kuwa kweli, hata mtu yeyoteambaye hakuufuata au hakuutii aliadhibiwakama alivyostahili. 3 Basi, sisi tutaokokaje

kama hatuujali wokovu mkuu kama huu?Kwanza Bwana mwenyewe aliutangazawokovu huu, na wale waliomsikiawalituthibitishia kwamba ni kweli. 4 Mungu piaaliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanyakila namna ya miujiza na maajabu, na kwakuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifukadiri ya mapenzi yake. 5 Mungu hakuwawekamalaika wautawale ulimwengu ujao, yaaniulimwengu ule tunaoongea habari zake. 6

Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko:“Mtu ni nini ee Mungu, hata umfikirie;mwanaadamu ni nini hata umjali? 7 Ulimfanyakwa kitambo kidogo kuwa chini zaidi kulikomalaika; ukamvika taji ya utukufu na heshima,8 ukaweka kila kitu chini ya miguu yake,avitawale.” Yasemwa kwamba Mungualimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyoteyaani bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo,hatuoni bado mtu akivitawala vitu vyote sasa.9 Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywakwa kitambo kidogo kuwa chini zaidi kulikomalaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajiliya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwakwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifoalichoteseka. 10 Ilikuwa haki tupu kwambaMungu, ambaye huumba na kutegemeza vituvyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisakwa njia ya mateso, ili awalete watoto wengiwaushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiyeanayewaongoza kwenye wokovu. 11 Yeyeanawatakasa watu dhambi zao, naye pamojana wale waliotakaswa, wote wanaye Babammoja. Ndiyo maana Yesu haoni aibu kuwaitahao ndugu zake; 12 kama asemavyo: “EeMungu, nitawatangazia ndugu zangu matendoyako. Nitakusifu katika kusanyiko lao.” 13 Tenaasema: “Nitamwekea Mungu tumaini langu.”Na tena: “Mimi niko hapa pamoja na watotoalionipa Mungu.” 14 Basi, kwa vile watoto hao,kama awaitavyo, ni watu wenye mwili nadamu, Yesu mwenyewe akawa kama wao nakushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili kwanjia ya kifo chake amwangamize Ibilisi,ambaye ana mamlaka juu ya kifo, 15 na hivyoawaokoe wale waliokuwa watumwa maishayao yote kwa sababu ya hofu yao ya kifo. 16

Maana ni wazi kwamba yeye hakuja kwa ajili yakuwasaidia malaika, bali kama yasemavyoMaandiko; “Anawasaidia wazawa waAbrahamu.” 17 Ndiyo maana ilimbidi awekama ndugu zake kwa kila namna, ili aweKuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye

WARAKA KWA WAEBRANIA 1:2

174

Page 175: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4huruma katika kumtumikia Mungu, ili dhambiza watu ziondolewe. 18 Na, anaweza sasakuwasaidia wale wanaojaribiwa na kuteswa.

Ndugu zangu watu wa Mungu ambaommeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesuambaye Mungu alimtuma awe Kuhani

Mkuu wa imani tunayoiungama. 2 Yeyealikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteuakufanya kazi yake kama vile Mose alivyokuwamwaminifu katika nyumba yote ya Mungu. 3

Mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidikuliko hiyo nyumba yenyewe. Hali kadhalikanaye Yesu anastahili heshima kubwa zaidikuliko Mose. 4 Kila nyumba hujengwa namjenzi fulani—na Mungu ndiye mjenzi wa vituvyote. 5 Mose alikuwa mwaminifu katikanyumba yote ya Bwana kama mtumishi, naalinena juu ya mambo ambayo Munguatayasema hapo baadaye. 6 Lakini Kristo nimwaminifu kama Mwana mwenye mamlakajuu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yakekama tukizingatia uhodari wetu na uthabitiwetu katika kile tunachotumainia. 7 Kwa hiyo,basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: “Kamamkisikia sauti ya Mungu leo, 8 msiifanyemioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenuwalivyokuwa wakati walipomwasi Mungu;kama walivyokuwa siku ile kule jangwani, 9

Huko wazee wenu walinijaribu nakunichunguza, asema Bwana, ingawawalikuwa wameyaona matendo yangu kwamiaka arobaini. 10 Kwa sababu hiyoniliwakasirikia watu hao nikasema, Fikira zawatu hawa zimepotoka, hawajapata kamwekuzijua njia zangu. 11 Basi, nilikasirika,nikaapa: Hawataingia huko ambakoningewapa pumziko.” 12 Basi ndugu,jihadharini asije akawako yeyote miongonimwenu aliye na moyo mbaya hivyo naasiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.13 Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katikaMaandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswakusaidiana daima, ili mtu yeyote miongonimwenu asidanganywe na dhambi na kuwamkaidi. 14 Maana sisi tunashirikiana na Kristoikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumainitulilokuwa nalo mwanzoni. 15 Maandikoyasema hivi: “Kama mkisikia sauti ya Munguleo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kamawazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasiMungu.” 16 Ni akina nani basi, waliosikia sautiya Mungu wakamwasi? Ni wale wotewalioongozwa na Mose kutoka Misri. 17

Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miakaarobaini? Aliwakasirikia wale waliotendadhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.18 Mungu alipoapa: “Hawataingia hukoambako ningewapa pumziko,” alikuwaanawasema akina nani? Alikuwa anasema juuya hao walioasi. 19 Basi, twaona kwambahawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.

Mungu alituahidia kwamba tutawezakupata pumziko hilo alilosema. Basi, natuogope ili yeyote kati yenu asije

akashindwa kupata pumziko hilo. 2 MaanaHabari Njema imehubiriwa kwetu kama vileilivyohubiriwa kwa hao watu wa kale. Lakiniujumbe huo haukuwafaa chochote, maanawaliusikia lakini hawakuupokea kwa imani. 3

Basi, sisi tunaoamini tunapata pumziko hiloaliloahidi Mungu. Kama alivyosema:“Nilikasirika, nikaapa: Hawataingia hukoambako ningewapa pumziko.” Mungu alisemahayo ingawa kazi yake ilikuwa imekwishamalizika tangu alipoumba ulimwengu. 4

Maana Maandiko yasema mahali fulani kuhususiku ya saba: “Mungu alipumzika siku ya saba,akaacha kazi zake zote.” 5 Tena jambo hililasemwa pia: “Hawataingia huko ambakoningewapa pumziko.” 6 Wale waliotanguliakuhubiriwa Habari Njema hawakupatapumziko hilo kwa sababu hawakuamini. Wapo,basi, wengine ambao wangejaliwa kulipata. 7

Jambo hili ni wazi, kwani Mungu aliweka sikunyingine ambayo inaitwa “Leo”. Miaka mingibaadaye Mungu alisema juu ya hiyo siku kwamaneno ya Daudi katika Maandikoyaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti yaMungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwamigumu.” 8 Kama Yoshua angaliwapa watuhao hilo pumziko, Mungu hangalisemabaadaye juu ya siku nyingine. 9 Kwa hiyo, basi,bado lipo pumziko kwa watu wa Mungu kamakule kupumzika kwake Mungu siku ya saba. 10

Maana, kila anayepata pumziko aliloahidiMungu atapumzika baada ya kazi yake kamavile pia Mungu alivyopumzika baada ya yake.11 Basi, tujitahidi kupata pumziko hilo, iliasiwepo yeyote miongoni mwenuatakayeshindwa, kama walivyofanya wao kwasababu ya ukosefu wao wa imani. 12 Neno laMungu ni hai na lina nguvu; ni kali zaidi kulikoupanga wenye makali kuwili. Hukata kabisampaka mahali ambapo moyo na rohohukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vyamwili na mafuta. Neno hilo huchambua nia nafikira za mioyo ya watu. 13 Hakuna kiumbechochote kilichofichika mbele ya Mungu; kilakitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake.Kwake, sisi sote tutapaswa kutoa hoja yamatendo yetu. 14 Basi, tunapaswa kuzingatiakwa uthabiti imani tunayoiungama. Maanatunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka kwaMungu mwenyewe—Yesu, Mwana wa Mungu.15 Huyu Kuhani Mkuu wetu si mmoja ambayehawezi kutuunga mkono katika unyonge wetu,ila ni Kuhani Mkuu ambaye alijaribiwa kamasisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi.16 Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzicha Mungu, palipo na neema, ili tukajipatiehuruma na neema ya kutusaidia wakati walazima.

WARAKA KWA WAEBRANIA 4:16

175

Page 176: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

6 7

Kila kuhani mkuu huchaguliwa kutokamiongoni mwa watu kwa ajili yakumtumikia Mungu kwa niaba yao,

kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambizao. 2 Maadamu yeye mwenyewe yu dhaifuanaweza kuwaonea huruma wale wasiojua kituna wanaofanya makosa. 3 Na kwa vile yeyemwenyewe ni dhaifu, anapaswa kutoleadhabihu si tu kwa ajili ya watu, bali pia kwa ajiliya dhambi zake. 4 Hakuna mtu awezayekujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhanimkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwakuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni. 5 Halikadhalika naye Kristo hakujitwalia mwenyeweheshima ya kuwa kuhani mkuu, bali Mungualimwambia: “Wewe ni Mwanangu; mimi leonimekuwa baba yako.” 6 Alisema pia mahalipengine: “Wewe ni kuhani milele, kufuatana nautaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.” 7 Yesualipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kiliokikuu na machozi, alisali na kumwombaMungu ambaye alikuwa na uwezo wakumwokoa kutoka kifo; naye alisikilizwa kwasababu ya kumcha Mungu. 8 Lakini, ingawaalikuwa Mwana wa Mungu, alijifunza kutii kwanjia ya mateso. 9 Na alipofanywa mkamilifu,akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa walewote wanaomtii, 10 naye Mungu akamteuakuwa kuhani mkuu kufuatana na utaratibu waukuhani wa Melkisedeki. 11 Tunayo Mengi yakusema juu ya jambo hili, lakini ni vigumukuwaelezeni, kwa sababu ninyi si wepesi wakuelewa. 12 Sasa mngalipaswa kuwa tayariwalimu, lakini mnahitaji bado mtu wakuwafundisheni mafundisho ya mwanzo yaujumbe wa Mungu. Badala ya kula chakulakigumu, mnapaswa bado kunywa maziwa. 13

Kila anayepaswa kunywa maziwa huyo nimtoto bado, hajui uadilifu ni nini. 14 Lakinichakula kigumu ni kwa ajili ya watuwaliokomaa, ambao wanaweza kubainishamema na mabaya.

Basi, tusonge mbele kwa yaleyaliyokomaa na kuyaacha nyuma yalemafundisho ya mwanzo ya Kikristo.

Hatuhitaji kuweka msingi tena kwa kurudiayale mafundisho ya mwanzo kama vilekuachana na matendo ya kifo, kumwaminiMungu; 2 mafundisho juu ya ubatizo nakuwekewa mikono; ufufuo wa wafu nahukumu ya milele. 3 tusonge mbele! Hayotutayafanya, Mungu akitujalia. 4 Maana watuwanaoiasi imani yao inawezekanajekuwarudisha watubu tena? Watu haowalikwisha kuwa katika mwanga wa Mungu,walikwisha onja zawadi ya mbinguni nakushirikishwa Roho Mtakatifu; 5 walikwishaonja wema wa neno la Mungu na nguvu zaulimwengu ujao, 6 kisha wakaiasi imani yao!Haiwezekani kuwarudisha watubu tena, kwasababu wanamsulubisha tena Mwana waMungu na kumwaibisha hadharani. 7 Munguhuibariki ardhi ambayo huipokea mvua

inayoinyeshea mara kwa mara, na kuoteshamimea ya faida kwa mkulima. 8 Lakini kamaardhi hiyo ikiota miti ya miiba na magugu,haina faida; karibu italaaniwa na Mungu namwisho wake ni kuchomwa moto. 9 Lakini,ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu,tunalo tumaini kubwa juu ya hali yenu. Tunajuakwamba mmepokea baraka zile bora zawokovu wenu. 10 Mungu hakosi haki; yeyehataisahau kazi mliyoifanya au upendomlioonyesha kwa ajili ya jina lake katikahuduma mliyowapa na mnayowapa sasa watuwake. 11 Hamu yetu ni kwamba kila mmojawenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho,ili yale mnayotumainia yapate kutimia. 12

Msiwe wavivu, bali muwe kama walewanaoamini na wenye uvumilivu na hivyowanapokea yake aliyoahidi Mungu. 13 Mungualipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lakemwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kulikoMungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa. 14

Mungu alisema: “Hakika nitakubariki nanitakupa wazawa wengi.” 15 Abrahamualisubiri kwa uvumilivu na hivyo alipokea kilealichoahidiwa na Mungu. 16 Watu wanapoapa,huapa kwa mmoja aliye mkuu zaidi kuliko wao,na kiapo hicho husuluhisha ubishi wote. 17

Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo;na kwa namna hiyo akawaonyesha wazi walealiowaahidia kwamba hatabadili nia yake. 18

Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo,ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu yahivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyosisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewamoyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwambele yetu. 19 Tunalo tumaini hilo kamananga ya maisha yetu. Tumaini hilo ni imara nathabiti, nalo lapenya lile pazia la hekalu lambinguni mpaka patakatifu ndani. 20 Yesuametangulia kuingia humo kwa niaba yetu, naamekuwa kuhani mkuu milele, kufuatana nautaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.

Melkisedeki alikuwa mfalme waSalemu, na kuhani wa Mungu Mkuu.Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka

vitani ambako aliwaua wafalme, Melkisedekialikutana naye akambariki, 2 naye Abrahamuakampa sehemu ya kumi ya vitu vyotealivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jinahili Melkisedeki ni “Mfalme wa Uadilifu”; na,kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jinalake pia lina maana ya “Mfalme wa Amani.”) 3

Baba yake na mama yake hawatajwi, walaukoo wake hautajwi; haisemwi alizaliwa lini aualikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu,na anaendelea kuwa kuhani daima. 4 Basi,mwaona jinsi mtu huyu alivyokuwa maarufu.Baba Abrahamu alimpa sehemu moja ya kumiya vitu vyote alivyoteka vitani. 5 Tunajuavilevile kwamba kufuatana na Sheria, wana waLawi ambao ni makuhani, wanayo haki yakuchukua sehemu ya kumi kutoka kwa watu,yaani ndugu zao, ingawaje nao ni watoto wa

WARAKA KWA WAEBRANIA 5:2

176

Page 177: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

Abrahamu. 6 Lakini huyo Melkisedeki hakuwawa ukoo wa Lawi, hata hivyo alipokea sehemuya kumi kutoka kwa Abrahamu; tenaakambariki yeye ambaye alikuwa amepewaahadi ya Mungu. 7 Hakuna mashaka hatakidogo kwamba anayebariki ni mkuu zaidikuliko yule anayebarikiwa. 8 Tena, haomakuhani wanaopokea sehemu ya kumi, niwatu ambao hufa; lakini hapa anayepokeasehemu ya kumi, yaani Melkisedeki,anasemekana kwamba hafi. 9 Twaweza, basi,kusema kwamba Abrahamu alipotoa sehemumoja ya kumi, Lawi (ambaye watoto wakehupokea sehemu moja ya kumi) alitoa sehemumoja ya kumi pia. 10 Maana Lawi hakuwaamezaliwa bado, bali ni kama alikuwa katikamwili wa baba yake, Abrahamu, wakatiMelkisedeki alipokutana naye. 11 Kutokana naukuhani wa Walawi, watu wa Israeli walipewaSheria. Sasa, kama huduma ya Walawiingalikuwa kamilifu hapangekuwa tena na hajaya kutokea ukuhani mwingine tofauti, ukuhaniambao umefuata utaratibu wa ukuhani waMelkisedeki, na si ule wa Aroni. 12 Maanaukuhani ukibadilika ni lazima Sheria nayoibadilike. 13 Naye Bwana wetu ambayemambo hayo yote yanasemwa juu yake,alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hatammoja wa kabila lake aliyepata kutumikiamadhabahuni akiwa kuhani. 14 Inafahamikawazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila laYuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwaanasema juu ya makuhani. 15 Tena jambo hilini dhahiri zaidi: kuhani mwingine anayefananana Melkisedeki amekwisha tokea. 16 Yeyehakufanywa kuwa kuhani kwa sheria namaagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu yauhai ambao hauna mwisho. 17 MaanaMaandiko yasema: “Wewe ni kuhani milele,kufuatana na utaratibu wa ukuhani waMelkisedeki.” 18 Basi, ile amri ya zamaniilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na isiyofaakitu. 19 Maana Sheria ya Mose haikuwezakukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahalipake pamewekwa tumaini lililo bora zaidiambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu.20 Zaidi ya hayo hapa pana kiapo cha Mungu.Wakati wale wengine walipofanywa makuhanihapakuwako kiapo. 21 Lakini Yesu alifanywakuhani kwa kiapo wakati Mungualipomwambia: “Bwana ameapa, walahataigeuza nia yake: Wewe ni kuhani milele.”22 Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwamdhamini wa agano lililo bora zaidi. 23 Kunatofauti nyingine pia: hao makuhani wenginewalikuwa wengi kwa sababu walikufa nahawakuweza kuendelea na kazi yao. 24 LakiniYesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhaniwake hauondoki kwake. 25 Hivyo, yeyeanaweza daima kuwaokoa kabisa wotewanaomwendea Mungu kwa njia yake, maanayeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.26 Basi, Yesu ndiye Kuhani Mkuu ambaye

anatufaa sana katika mahitaji yetu. Yeye nimtakatifu, hana hatia wala dhambi ndani yake;hayumo katika kundi la wenye dhambi naameinuliwa mpaka juu mbinguni. 27 Yeye sikama wale makuhani wakuu wengine; hanahaja ya kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwaajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajiliya dhambi za watu. Yeye alifanya hivyo maramoja tu wakati alipojitoa yeye mwenyewe, nahiyo yatosha kwa nyakati zote. 28 Sheria yaMose huwateua watu waliokuwa dhaifu kuwamakuhani wakuu; lakini ahadi ya Mungualiyoifanya kwa kiapo na ambayo imefikabaada ya sheria imemteua Mwana ambayeamefanywa mkamilifu milele.

Basi, jambo muhimu katika hayotunayosema ni hili: sisi tunaye KuhaniMkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi

upande wa kulia wa kiti cha enzi cha MwenyeziMungu mbinguni. 2 Yeye hutoa huduma yaKuhani Mkuu katika Mahali Patakatifu sana,yaani ndani ya ile hema ya kweli iliyojengwa naBwana, siyo na binadamu. 3 Kila Kuhani Mkuuameteuliwa kumtolea Mungu vipawa nadhabihu, na hivyo Kuhani Mkuu wetu lazimapia awe na kitu cha kutolea. 4 Kama yeyeangekuwa wa hapa duninani, asingekuwakamwe kuhani, kwani wako makuhani wenginewanaotoa sadaka kufuatana na Sheria. 5

Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivulicha yale yaliyoko mbinguni. Ndivyo piailivyokuwa kwa Mose. Wakati alipokuwa karibukuitengeneza ile hema, Mungu alimwambia:“Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfanoulioonyeshwa kule mlimani.” 6 Lakini sasaYesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo borazaidi kuliko yao, kama vile agano alilothibitishakati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani linamsingi wake katika ahadi za mambo yaliyobora zaidi. 7 Maana kama lile agano la kwanzahalingalikuwa na dosari, hakungalikuwa nahaja ya agano la pili. 8 Lakini Mungualiwalaumu watu wake aliposema: “Sikuzinakuja, asema Bwana, ambapo nitafanyaagano jipya na watu wa Israeli na kabila laYuda. 9 Agano hili halitakuwa kama lilenililofanya na babu zao siku ile nilipowaongozakwa mkono kutoka nchi ya Misri. Hawakuwawaaminifu kwa agano langu; na hivyo mimisikuwajali, asema Bwana. 10 Na hili ndiloagano nitakalofanya na watu wa Israeli sikuzijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zanguakilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao.Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwawatu wangu. 11 Hakuna mtuatakayemfundisha mwananchi mwenzake,wala atakayemwambia ndugu yake: MjueBwana. Maana watu wote, wadogo nawakubwa, watanijua mimi. 12 Nitawasamehemakosa yao, wala sitakumbuka tena dhambizao.” 13 Kwa kusema juu ya agano jipya,Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote

WARAKA KWA WAEBRANIA 8:13

177

Page 178: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

9

10

kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatowekakaribuni.

Agano la kwanza lilikuwa na taratibuzake za ibada na pia mahali patakatifupa ibada palipojengwa na watu. 2

Palitengenezwa hema ambayo sehemu yakeya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwana kinara cha taa, meza na mikate iliyotolewakwa Mungu. 3 Nyuma ya pazia la pili, kulikuwana hema iliyoitwa Mahali Patakatifu KupitaPote. 4 Humo mlikuwa na madhabahu yadhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, naSanduku la Agano, ambalo lilikuwa limepakwadhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwana chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana;fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, navile vibao viwili vilivyoandikwa agano. 5 Juu yahilo Sanduku kulikuwa na viumbevilivyodhihirisha kuweko kwa Mungu, namabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapodhambi huondolewa. Lakini sasa, hatuwezikusema kinaganaga juu ya mambo hayo. 6

Mipango hiyo ilitekelezwa kisha ikawa desturikwa makuhani kuingia kila siku katika hema yanje kutoa huduma zao. 7 Lakini kuhani Mkuupeke yake ndiye anayeingia katika lile hema lapili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwamwaka. Anapoingia ndani huwa amechukuadamu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yakemwenyewe na kwa ajili ya dhambi ambazowatu wamezitenda bila wao wenyewe kujua. 8

Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifuanafundisha wazi kwamba wakati ile hema yanje ingali ipo imesimama, njia ya kuingiaMahali Patakatifu haijafunguliwa. 9 Jambo hilini mfano wa nyakati za sasa. Linaonyeshakwamba zawadi na dhabihu zinazotolewa kwaMungu haziwezi kuifanya mioyo ya walewanaoabudu kuwa mikamilifu, 10 kwani hayayote yanahusika na vyakula, vinywaji nataratibu mbalimbali za kutawadha. Yote hayoni maagizo ya njenje tu; na nguvu yakehukoma wakati Mungu atakaporekebisha vituvyote. 11 Lakini Kristo amekwisha fika, akiwaKuhani Mkuu wa mambo yaliyo mema,ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoahuduma zake katika hema iliyo bora nakamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono yawatu, yaani isiyo ya ulimwengu huuulioumbwa. 12 Yeye aliingia Mahali Patakatifumara moja tu, tena hakuwa amechukua damuya mbuzi wala ng'ombe, bali aliingia kwa damuyake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wamilele. 13 Watu waliokuwa najisi kidiniwaliweza kutakasika na kuwa safiwaliponyunyiziwa damu ya mbuzi na yang'ombe pamoja na majivu ya ndama. 14

Lakini, kwa damu ya Kristo, mambo makuuzaidi hufanyika! Kwa nguvu za Roho wa milele,Kristo alijitolea mwenyewe dhabihu kamilifukwa Mungu. Damu yake itatutakasa dhamirizetu kutokana na matendo yaletayo kifo, ilitupate kumtumikia Mungu aliye hai. 15 Kwa

hiyo, Kristo ndiye aliyeratibisha agano jipya iliwale walioitwa na Mungu wazipokee baraka zamilele walizoahidiwa. Watazipata, kwani kifokimetokea ambacho huwakomboa watukutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lileagano la kale. 16 Kwa kawaida wosiahutambuliwa tu kama kifo cha yule aliyeufanyahuo wosia kimethibitishwa. 17 Wosia hauwezikutekelezwa mpaka kumetokea kifo, kwaniwosia hauna maana ikiwa mwenye kuufanyabado anaishi. 18 Ndiyo maana hata lile aganola kwanza halikuwekwa bila damu kumwagwa.19 Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amrizote kama ilivyokuwa katika Sheria; kishaakachukua damu ya ndama pamoja na maji,na kwa kutumia majani ya mti uitwao husopona pamba nyekundu, akakinyunyizia kilekitabu cha Sheria na hao watu wote. 20 Mosealisema: “Hii ni damu inayothibitisha aganomliloamriwa na Mungu mlitii.” 21 Vilevile Mosealiinyunyizia damu ile hema na vyombo vyaibada. 22 Naam, kadiri ya Sheria karibu kilakitu chaweza kutakaswa kwa damu, na dhambinazo zaondolewa tu ikiwa damu imemwagwa.23 Vitu hivi ambavyo ni mfano tu wa mambohalisi ya mbinguni, vililazimika kutakaswa kwanamna hiyo. Lakini vitu vya mbinguni huhitajidhabihu iliyo bora zaidi. 24 Maana Kristohakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwamikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kilekilicho halisi. yeye aliingia mbinguni kwenyeweambako sasa anasimama mbele ya Mungukwa ajili yetu. 25 Kuhani Mkuu wa Wayahudihuingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwaamechukua damu ya mnyama; lakini Kristohakuingia humo ili ajitoe mwenyewe maranyingi, 26 maana ingalikuwa hivyo, Kristoangalipaswa kuteswa mara nyingi tangukuumbwa ulimwengu. Lakini sasa nyakati hizizinapokaribia mwisho wake, yeye ametokeamara moja tu, kuondoa dhambi kwa kujitoayeye mwenyewe dhabihu. 27 Basi, kama vilekila mtu hufa mara moja tu, kisha husimamambele ya hukumu ya Mungu, 28 vivyo hivyoKristo naye alijitoa dhabihu mara moja tu kwaajili ya kuziondoa dhambi za wengi.Atakapotokea mara ya pili si kwa ajili yakupambana na dhambi, bali ni kwa ajili yakuwaokoa wale wanaomngojea.

Sheria ya Wayahudi si picha kamili yamambo yale halisi: ni kivuli tu chamema yanayokuja. Dhabihu zilezile

hutolewa daima, mwaka baada ya mwaka.Sheria yawezaje, basi, kwa njia ya dhabihuhizo, kuwafanya wale wanaoabudu wawewakamilifu? 2 Kama hao watuwanaomwabudu Mungu wangekuwawametakaswa dhambi zao kweli,hawangejisikia tena kuwa na dhambi, nadhabihu hizo zote zingekoma. 3 Lakinidhabihu hizo hufanyika kila mwakakuwakumbusha watu dhambi zao. 4 Maanadamu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe

WARAKA KWA WAEBRANIA 9:2

178

Page 179: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

11

kuondoa dhambi. 5 Ndiyo maana Kristoalipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambiaMungu: “Hukutaka dhabihu wala sadaka, lakiniumenitayarishia mwili. 6 Sadaka zakuteketezwa au za kuondoa dhambihazikupendezi. 7 Hapo nikasema: Niko hapaee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako kamailivyoandikwa juu yangu katika kitabu chaSheria.” 8 Kwanza alisema: “Hutaki, walahupendezwi na dhabihu na sadaka, sadaka zakuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisemahivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewakufuatana na Sheria. 9 Kisha akasema: “Nikohapa, ee Mungu, tayari kufanya mapenziyako.” Hivyo Mungu alibatilisha dhabihu zazamani na mahali pake akaweka dhabihunyingine moja. 10 Kwa kuwa Yesu Kristoalitimiza mapenzi ya Mungu, sisi tunatakaswadhambi zetu kwa ile dhabihu ya mwili wakealiyotoa mara moja tu, ikatosha. 11 Kila kuhaniMyahudi humhudumia Mungu kila siku, akitoadhabibu zilezile mara nyingi, dhabibu ambazohaziwezi kuondoa dhambi. 12 Lakini Kristoalitoa dhabihu moja tu kwa ajili ya dhambi,dhabihu ifaayo milele, kisha akaketi upandewa kulia wa Mungu. 13 Huko anangoja mpakaadui zake watakapowekwa kama kibao chini yamiguu yake. 14 Basi, kwa dhabihu yake mojatu, amewafanya kuwa wakamilifu milele walewanaotakaswa dhambi zao. 15 Naye RohoMtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanzaanasema: 16 “Hili ndilo agano nitakalofanyanao, katika siku zijazo, asema Bwana: Nitawekasheria zangu mioyoni mwao, na kuziandikaakilini mwao.” 17 Kisha akaongeza kusema:“Sitakumbuka tena dhambi zao, wala vitendovyao vya uhalifu.” 18 Basi, dhambi zikishaondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoadhabihu za kuondoa dhambi. 19 Basi, ndugu,kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wakuingia Mahali Patakatifu. 20 Yeyeametufungulia njia mpya na yenye uzimakupitia lile pazia, yaani kwa njia ya mwili wakemwenyewe. 21 Basi, tunaye kuhani maarufualiye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. 22

Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyomnyofu na imani timilifu, kwa mioyoiliyotakaswa dhamiri mbaya, na kwa miiliiliyosafishwa kwa maji safi. 23 Tushikilie imaratumaini lile tunalokiri, maana Mungualiyefanya ahadi zake ni mwaminifu. 24

Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili yakuongezeana bidii ya kupendana na kutendamema. 25 Tusiache ile desturi ya kukutanapamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Balitunapaswa kusaidiana kwani, kamamwonavyo, Siku ile ya Bwana inakaribia. 26

Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudibaada ya kufahamu ukweli, hakuna dhabihuiwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoadhambi. 27 Linalobaki ni kungojea tu kwa hofuhukumu ya Mungu na moto mkaliutakaowaangamiza wote wanaompinga. 28

Mtu yeyote asiyeitii Sheria ya Mose, huuawabila ya huruma kukiwa na ushahidi wa watuwawili au watatu. 29 Je, mtu yuleanayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharaudamu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtuanayemtukana Roho wa Mungu, anastahilikupata adhabu kali ya namna gani? 30 Maanatunamfahamu yule aliyesema, “Mimi nitalipizakisasi, mimi nitalipiza,” na ambaye alisema pia,“Bwana atawahukumu watu wake.” 31

Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai nijambo la kutisha mno! 32 Kumbukeniyaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwamwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwana mateso mengi, ninyi mlistahimili. 33 Maranyingine mlitukanwa na kufedheheshwahadharani; mara nyingine mlikuwa radhikuungana na wale walioteswa namnahiyohiyo. 34 Mlishiriki mateso ya wafungwa, namliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwafuraha, maana mlijua kwamba mnayo malibora zaidi na ya kudumu milele. 35 Basi,msipoteze uhodari wenu, maana utawapatienituzo kubwa. 36 Mnahitaji kuwa na uvumilivu, ilimweze kufanya anayotaka Mungu na kupokeakile alichoahidi. 37 Maana kama yasemavyoMaandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja,atakuja, wala hatakawia. 38 Lakini mtu wangualiye mwadilifu ataamini na kuishi; walakiniakirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye.” 39

Basi, sisi hatumo miongoni mwa walewanaorudi nyuma na kupotea, ila sisitunaamini na tunaokolewa.

Kuwa na imani ni kuwa na hakika yamambo tunayotumainia; kusadikikabisa mambo tusiyoyaona. 2 Maana

wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwasababu ya imani yao. 3 Kwa imani sisitunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwakwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekanakutoka vitu visivyoonekana. 4 Kwa imani Abelialimtolea Mungu dhabihu iliyokuwa bora zaidikuliko ile ya Kaini. Kwa imani yake alikubaliwana Mungu kuwa mwadilifu; Mungu mwenyewealizikubali sadaka zake. Kwa imani yake ingawaamekufa, bado ananena. 5 Kwa imani Henokialichukuliwa na Mungu, asipate kufa.Hakuonekana tena kwa sababu Mungualikuwa amemchukua. Maandiko yasemakwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeyealikuwa amempendeza Mungu. 6 Basi, pasipoimani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwamaana kila mtu anayemwendea Mungu nilazima aamini kwamba Mungu yuko, nakwamba huwatuza wale wanaomtafuta. 7 Kwaimani Noa alionywa na Mungu juu ya mamboya baadaye ambayo hakuweza kuyaona bado.Alimtii Mungu, akajenga ile safina ambamoaliokolewa yeye pamoja na jamaa yake.Kutokana na hayo ulimwengu ulihukumiwa,naye Noa akapokea uadilifu unaotokana naimani. 8 Kwa imani Abrahamu alimtii Mungualipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu

WARAKA KWA WAEBRANIA 11:8

179

Page 180: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

12

angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwaanakwenda, Abrahamu alihama. 9 Kwa imanialiishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa naMungu. Aliishi huko katika hema kamawalivyoishi Isaka na Yakobo, ambao piawalishiriki ahadi ileile. 10 Maana Abrahamualikuwa akingojea mji wenye misingi imara, mjiambao Mungu mwenyewe ndiye fundialiyeubuni na kuujenga. 11 Kwa imani hataSara aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadizake, kwa hiyo akajaliwa kuchukua mimbaingawaje alikuwa amepita umri. 12 Kwa hiyo,kutoka katika mtu huyo mmoja, Abrahamu,ambaye alikuwa kama amekufa, walitokeawatu wengi wasiohesabika kama vile nyota zambinguni na mchanga wa pwani. 13 Watuhawa wote walikufa wakiwa na imani. Walikufakabla ya kupokea mambo ambayo Mungualikuwa ameahidi, lakini kwa mbali waliyaona,wakashangilia, na kukiri wazi kwamba waowalikuwa wageni na wakimbizi duniani. 14

Watu wanaosema mambo kama hayo,huonyesha wazi kwamba wanaitafuta nchi yaowenyewe. 15 Kama wangalikuwa wanaifikirianchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi yakurudi huko. 16 Lakini sasa wanataka nchi iliyobora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndiyomaana Mungu haoni haya wakimwita yeyeMungu wao, kwa sababu yeye mwenyeweamekwisha watayarishia mji. 17 Kwa imani,Abrahamu alimtoa mwanae Isaka sadakawakati Mungu alipomjaribu. Huyo Abrahamundiye aliyekuwa amepokea ahadi ya Mungu,lakini, hata hivyo, alikubali kumtoa dhabihumwanae wa pekee, 18 ingawa Mungu alikuwaamemwambia: “Wazawa wako watatokana naIsaka.” 19 Abrahamu aliamini kwamba Munguanaweza kuwafufua wafu: na kwa namnafulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanaekutoka wafu. 20 Kwa imani Isaka aliwabarikiYakobo na Esau, wapate baraka zitakazokujabaadaye. 21 Kwa imani Yakobo alipokuwakaribu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wanawa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea ilefimbo yake. 22 Kwa imani Yosefu alipokuwakaribu kufa, alinena juu ya kutoka kwaWaisraeli katika nchi ya Misri, na piaakawaachia maagizo kuhusu mifupa yake. 23

Kwa imani wazazi wa Mose walimficha huyomtoto kwa muda wa miezi mitatu baada yakuzaliwa kwake. Walimwona kuwa ni mtotomzuri, wala hawakuiogopa amri ya mfalme. 24

Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima,alikataa kuitwa mwana wa binti Farao. 25

Aliona ni afadhali kuteseka pamoja na watu waMungu kuliko kufurahia raha ya dhambi kwakitambo kidogo. 26 Alitambua kwambakuteseka kwa ajili ya Masiha kuna faida kubwazaidi kuliko utajiri wote wa nchi ya Misri,maana alikuwa anatazamia tuzo la baadaye. 27

Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misribila kuogopa hasira ya mfalme; na walahakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu

aliyemwona yule Mungu asiyeonekana. 28 Kwaimani aliadhimisha siku ya Pasaka, akaamurudamu inyunyizwe juu ya milango, ili yuleMalaika Mwangamizi asiwaue wazaliwa wakwanza wa Israeli. 29 Kwa imani watu waIsraeli walivuka bahari ya Shamu, kanakwamba ilikuwa nchi kavu; lakini Wamisriwalipojaribu kufanya hivyo walikufa maji. 30

Kwa imani kuta za mji wa Yeriko ziliangukawatu wa Israeli walipokwisha zunguka kwamuda wa siku saba. 31 Kwa imani Rahabualiyekuwa malaya hakuangamia pamoja nawale waliomwasi Mungu, kwa sababualiwakaribisha wale wapelelezi. 32 Basi, nisemenini zaidi? Wakati hauniruhusu kueleza juu yaGedeoni, Baraki, Samsoni, Yeftha, Daudi,Samweli na manabii. 33 Kwa imani hawa wotewalipigana vita na wafalme, wakashinda.Walitenda mambo adili, wakapokea yalealiyoahidi Mungu. Walifunga vinywa vya simba,34 Walizima mioto mikali, waliepuka kuuawakwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini walipatanguvu. Walikuwa hodari katika vitawakashinda majeshi ya kigeni. 35 Na,wanawake walioamini walirudishiwa wafu waowakiwa wamefufuliwa. Baadhi yao walikataakufunguliwa, wakateswa mpaka kufa ili wapatekufufuliwa na kuingia katika maisha bora zaidi.36 Wengine walidhihakiwa na kupigwamijeledi, na wengine walifungwa minyororo nakutupwa gerezani. 37 Walipigwa mawe,walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwaupanga. Walizungukazunguka wakiwawamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi,walikuwa watu maskini, walioteswa nakudhulumiwa. 38 Ulimwengu haukustahilikuwa na watu hao. Walitangatanga jangwanina mlimani, wakaishi katika mashimo namapango ya ardhi. 39 Watu hawa wotewalionekana kuwa mashujaa kwa sababu yaimani yao. Hata hivyo, hawakupokea yaleambayo Mungu aliwaahidia, 40 maana Mungualikuwa ameazimia mpango ulio bora zaidi kwaajili yetu; yaani wao wangeufikia ukamilifuwakiwa pamoja nasi.

Sisi tunalo kundi hili kubwa lamashahidi mbele yetu. Kwa hiyotuondoe kila kizuizi kinachotuzuia, na

dhambi ile inayotung'ang'ania. Tupige mbiokwa uvumilivu katika mashindano yaliyowekwambele yetu. 2 Tumwelekee Yesu ambaye ndiyealiyeianzisha imani yetu na ambayeataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwainamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani,bila kujali juu ya aibu yake, na sasa anaketiupande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu. 3

Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsialivyostahimili upinzani mkubwa kwa watuwenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikatetamaa. 4 Maana katika kupambana nadhambi, ninyi hamjapigana mpaka kiasi chakumwaga damu yenu. 5 Je, mmesahau yalemaneno ya kutia moyo ambayo Mungu

WARAKA KWA WAEBRANIA 11:9

180

Page 181: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

anawataja ninyi kuwa wanawe? “Mwanangu,usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyoanapokukanya. 6 Maana Bwana humwadhibukila anayempenda, humpinga kila anayekubalikuwa mwanae.” 7 Vumilieni adhabu kwani nimafundisho; Mungu huwatendea ninyi kamawanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwana baba yake? 8 Lakini msipoadhibiwa kamawana wengine, basi, ninyi si wanawe, bali niwana haramu. 9 Zaidi ya hayo sisitunawaheshimu wazazi wetu waliotuzaa hatawanapotuadhibu. Basi, tunapaswa kumtii zaidiBaba yetu wa kiroho ili tupate kuishi. 10 Wazaziwetu hapa duniani walituadhibu kwa muda,kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema;lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faidayetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifuwake. 11 Kuadhibiwa si jambo la kufurahishabali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwakuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo laamani kutoka katika maisha adili! 12 Basi,inueni mikono yenu inayolegea na kuimarishamagoti yenu yaliyo dhaifu. 13 Endeleenikutembea katika njia iliyonyoka, ili kilekilicholemaa kisiumizwe, bali kiponywe. 14

Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishinimaisha ya utakatifu, kwa sababu hakuna mtuatakayemwona Bwana bila ya maisha kamahayo. 15 Jitahidini sana mtu yeyote asijeakapoteza neema ya Mungu. Muwe waangalifuili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwauawengi kwa sumu yake. 16 Jihadharini ilimiongoni mwenu pasiwe na mtu mwasheratiau mtu asiyemcha Mungu kama Esau, aliyeuzahaki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mlommoja. 17 Ninyi mnafahamu kwamba hataalipotaka kuipata tena ile baraka iliyokuwayake, alikataliwa, maana hakupata tena nafasiya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi. 18

Ninyi hamkuwasili mlimani Sinai, ambaounaweza kushikika kama walivyofanya watuwa Israeli, hamkufika kwenye moto uwakao,penye giza, tufani, 19 mvumo wa tarumbetana sauti ya maneno. Wale waliosikia sauti hiyowaliomba wasisikie tena neno jingine, 20

kwani hawakuweza kustahimili amriiliyotolewa: “Atakayegusa mlima huu, hatakama ni mnyama, atapigwa mawe.” 21 Hayoyote yalionekana ya kutisha mno, hata Moseakasema, “Naogopa na kutetemeka.” 22 Lakinininyi mmefika katika mlima wa Sioni, kwenyemji wa Mungu aliye hai. Mmefika Yerusalemu,mji wa mbinguni, ambapo wamekusanyikamalaika elfu nyingi wasiohesabika. 23 Mmefikakwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wakwanza wa Mungu, ambao majina yaoyameandikwa mbinguni. Mnasimama mbeleya Mungu aliye hakimu wa wote, na mbele yaroho za watu waadilifu waliofanywa kuwawakamilifu. 24 Mmefika kwa Yesu ambayeameratibisha agano jipya, na ambaye damuyake iliyomwagika inasema mambo memazaidi kuliko ile ya Abeli. 25 Basi, jihadharini

msije mkakataa kumsikiliza yeye ambayeanasema nanyi. Kama wale walikataakumsikiliza yule aliyewaonya hapa dunianihawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kamatukikataa kumsikiliza yule anayetuonya kutokambinguni? 26 Wakati ule sauti ilitetemeshanchi, lakini sasa ameahidi: “Nitatetemesha nchitena, lakini si nchi tu bali pia mbingu.” 27 Nenohili: “tena” linatuonyesha kwamba vitu vyotevilivyoumbwa vitatetemeshwa na kutoweka ilivibaki vile visivyotetemeshwa. 28 Sisi basi, natushukuru kwani tunapokea utawalausiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabuduMungu kwa namna itakayompendeza, kwaibada na hofu; 29 maana Mungu wetu kweli nimoto mkali unaoteketeza.

Endeleeni kupendana kidugu. 2

Msisahau kuwakaribisha wageni;maana kwa kufanya hivyo watu

wengine walipata kuwakaribisha malaika bilakujua. 3 Wakumbukeni wale waliofungwa kanakwamba mmefungwa pamoja nao.Wakumbukeni wale wanaoteseka kanakwamba nanyi mnateseka kama wao. 4 Ndoainapaswa kuheshimiwa na watu wote, na hakizake zitekelezwe kwa uaminifu. Munguatawahukumu waasherati na wazinzi. 5 Msiwewatu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitumlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema:“Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.” 6 Ndiyomaana tunathubutu kusema: “Bwana ndiyemsaada wangu, sitaogopa. Binadamuatanifanya nini?” 7 wakumbukeni viongoziwenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu.Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imaniyao. 8 Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo namilele. 9 Msipeperushwe huku na huku kwamafundisho tofauti ya kigeni. Neema yaMungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na walasi masharti juu ya chakula; masharti hayohayakumsaidia kamwe mtu yeyotealiyeyafuata. 10 Sisi tunayo madhabahuambayo wale wanaotumikia bado katika hemala Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake.11 Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu yawanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoadhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama zahao wanyama huteketezwa nje ya kambi. 12

Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apatekuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe,aliteswa na kufa nje ya mji. 13 Basi,tumwendee huko nje ya kambi tukajitwikelaana yake. 14 Maana hapa duniani hatuna mjiwa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja.15 Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungudhabihu ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewana midomo inayoliungama jina lake. 16

Msisahau kutenda mema na kusaidiana,maana hizi ndizo dhabihu zinazompendezaMungu. 17 Watiini viongozi wenu na kushikaamri zao; wao huchunga roho zenu usiku namchana, na watatoa ripoti ya utumishi waombele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya

WARAKA KWA WAEBRANIA 13:17

181

Page 182: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwahuzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu. 18

Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwambatunayo dhamiri safi, maana twataka kufanyalililo sawa daima. 19 Nawasihi sana mniombeeili Mungu anirudishe kwenu upesiiwezekanavyo. 20 Mungu amemfufua Bwanawetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuuwa kondoo kwa sababu ya kumwaga damuyake iliyothibitisha agano la milele. 21 Munguwa amani awakamilishe katika kila tendo jemaili mtekeleze mapenzi yake; yeye na afanyendani yetu kwa njia ya Kristo yale

yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwekwake, milele na milele! Amina. 22 Basi,ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbehuu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tuambayo nimewaandikieni. 23 Napendakuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheoamekwisha funguliwa gerezani. Kama akifikahapa mapema, nitakuja naye nitakapokujakwenu. 24 Wasalimieni viongozi wenu wotepamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italiawanawasalimuni. 25 Tunawatakieni nyoteneema ya Mungu.

WARAKA KWA WAEBRANIA 13:18

182

Page 183: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

WARAKA WA YAKOBO

Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu nawa Bwana Yesu Kristo, nawaandikianinyi, makabila kumi na mawili,

yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam! 2

Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwana majaribu mbalimbali, 3 kwani mwajuakwamba imani yenu ikisha stahimili,itawapatieni uvumilivu. 4 Muwe na hakikakwamba uvumilivu wenu utawategemezampaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu nawatimilifu, bila kupungukiwa chochote. 5

Lakini kama mmoja wenu ametindikiwahekima, basi, anapaswa kumwomba Munguambaye atampatia; kwani Mungu huwapawote kwa wingi na kwa ukarimu. 6 Lakinianapaswa kuomba kwa imani bila mashakayoyote. Mtu aliye na mashaka ni kamamawimbi ya bahari ambayo husukumwa nakutupwatupwa na upepo. 7 Mtu wa namnahiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamokatika mwenendo wake wote, 8 asidhani yakwamba atapata chochote kile kutoka kwaBwana. 9 Ndugu aliye maskini anapaswakufurahi wakati Mungu anapomkweza, 10

naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwana Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua laporini. 11 Jua huchomoza na kwa joto lake kalihukausha mimea, nayo maua yake huanguka,na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo,tajiri ataangamizwa katika shughuli zake. 12

Heri mtu anayebaki mwaminifu katikamajaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzola uzima ambalo Mungu aliwaahidia walewanaompenda. 13 Kama mtu akijaribiwa,asiseme: “Ninajaribiwa na Mungu.” MaanaMungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeyehamjaribu mtu yeyote. 14 Lakini mtuhujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaazake mbaya. 15 Tamaa ikiiva huzaa dhambi;nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo. 16 Nduguzangu wapenzi, msidanganyike! 17 Kila kipajichema na kila zawadi kamilifu hutokambinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wamianga, ambaye habadiliki wala hana alamayoyote ya ugeugeu. 18 Kwa kupenda kwakemwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ilituwe namna ya matunda ya kwanza miongonimwa viumbe vyake. 19 Ndugu zangu wapenzi,kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awemwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wakusema wala mwepesi wa kukasirika. 20

Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa yaMungu yaliyo ya haki. 21 Kwa hiyo, tupilieni

mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu;jiwekeni chini ya Mungu na kupokea uleujumbe uliopandwa mioyoni mwenu, ambaowaweza kuziokoa nafsi zenu. 22 Msijidanganyewenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, balilitekelezeni kwa vitendo. 23 Yeyoteanayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyoni kama mtu anayejiangalia sura yakemwenyewe katika kioo. 24 Hujiangaliamwenyewe, kisha huenda zake, na marahusahau jinsi alivyo. 25 Lakini mtuanayeangalia kwa makini sheria kamilifuambayo huwapa watu uhuru, mtuanayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu nakuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyoatabarikiwa katika kila kitu anachofanya. 26

Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini,lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yakehaifai kitu, na anajidanganya mwenyewe. 27

Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele yaMungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima nawajane katika shida zao, na kujilindamwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.

Ndugu zangu, mkiwa mnamwaminiBwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu,msiwabague watu kamwe. 2 Tuseme

mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabuna mavazi nadhifu anaingia katika mkutanowenu, na papo hapo akaingia mtu maskinialiyevaa mavazi machafu. 3 Ikiwa mtamstahizaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia nakumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” nakumwambia yule maskini: “Wewe, simamahuko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”4 je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huouamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya? 5

Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Munguamechagua watu ambao ni maskini katikaulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katikaimani na kupokea Utawala aliowaahidia walewanaompenda. 6 Lakini ninyi mnawadharauwatu maskini! Je, matajiri si ndiowanaowakandamizeni na kuwapelekamahakamani? 7 Je, si haohao wanaolitukanahilo jina lenu zuri mlilopewa? 8 Kamamnaitimiza ile sheria ya Utawala kamailivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu:“Mpende binadamu mwenzako kamaunavyojipenda wewe mwenyewe”, mtakuwamnafanya vema kabisa. 9 Lakini mkiwabaguawatu, basi, mwatenda dhambi, nayo Sheriainawahukumu ninyi kuwa mna hatia. 10

Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa

WARAKA WA YAKOBO 2:10

183

Page 184: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

na hatia ya kuivunja Sheria yote. 11 Maanayuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia“Usiue”. Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini lakiniumeua, wewe umeivunja Sheria. 12 Basi,semeni na kutenda kama watuwatakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.13 Maana, Mungu hatakuwa na hurumaatakapomhukumu mtu asiyekuwa na huruma.Lakini huruma hushinda hukumu. 14 Nduguzangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani,lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imaniyawezaje kumwokoa? 15 Tuseme kaka au dadahana nguo au chakula. 16 Yafaa kitu gani ninyikuwaambia hao: “Nendeni salama mkaotemoto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yaoya maisha? 17 Vivyo hivyo, imani peke yakebila matendo imekufa. 18 Lakini mtu anawezakusema: “Wewe unayo imani, mimi ninayomatendo!” Haya! Nionyeshe jinsi mtuanavyoweza kuwa na imani bila matendo,nami nitakuonyesha imani yangu kwamatendo yangu. 19 Je, wewe unaaminikwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakinihata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwahofu. 20 Mpumbavu wee! Je, watakakuonyeshwa kwamba imani bila matendoimekufa? 21 Je, Abrahamu baba yetu alipatajekukubalika mbele yake Mungu? Kwa matendoyake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadakajuu ya madhabahu. 22 Waona basi, kwambaimani yake iliandamana na matendo yake;imani yake ilikamilishwa kwa matendo yake. 23

Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifuyasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu nakwa imani yake akakubaliwa kuwa mtumwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafikiwa Mungu.” 24 Mnaona basi, kwamba mtuhukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendoyake na si kwa imani peke yake. 25 Ilikuwavivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeyealikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababualiwapokea wale wapelelezi na kuwasaidiawaende zao kwa kupitia njia nyingine. 26 Basi,kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyoimani bila matendo imekufa.

Ndugu zangu, wengi wenu msiwewalimu. Kama mjuavyo, sisi walimututapata hukumu kubwa zaidi kuliko

wengine. 2 Lakini kama mtu hakosi katikausemi wake, basi, huyo ni mkamilifu, naanaweza kutawala nafsi yake yote. 3 Sisihuwatia farasi lijamu kinywani mwao ili watutii;na kwa njia hiyo twaweza kuwaongoza kokotetunakotaka. 4 Meli nazo pia, ingawa ni kubwasana, na husukumwa na upepo mkali, huwezakugeuzwa kwa usukani mdogo sana,zikaelekea kokote nahodha anakotaka. 5 Vivyohivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo chamwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogowaweza kuteketeza msitu mkubwa. 6 Halikadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovuchungu nzima, unayo nafasi yake katika miiliyetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote.

Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokaoJehanamu kwenyewe. 7 Binadamu anawezakuwafuga wanyama, na amefaulu kufugaviumbe vyote—wanyama wa mwituni, ndege,nyoka na viumbe vya baharini. 8 Lakini hakunamtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitukiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.9 Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Babayetu. Kwa ulimi huohuo twawalaani watu, watuambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.10 Maneno ya laana na ya kusifia hutoka katikakinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo hayahayapaswi kuwa hivyo. 11 Je, chemchemi mojayaweza kutoa maji matamu na maji machungupamoja? 12 Ndugu zangu, je, mti wa mtiniwaweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu wawezakuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvihaiwezi kutoa maji matamu. 13 Je, ni nanimwenye hekima na akili miongoni mwenu?Basi, aonyeshe jambo hilo kwa mwenendowake mzuri na kwa matendo yake memayanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.14 Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chukina ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongodhidi ya ukweli. 15 Hekima ya namna hiyohaitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni yaulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.16 Maana popote palipo na wivu na ubinafsihapo pana fujo na kila aina ya uovu. 17 Lakinihekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi;inapenda amani, upole na huwajali watu;imejaa huruma na huzaa matunda ya matendomema; haina ubaguzi wala unafiki. 18 Uadilifuni mazao ya mbegu ambazo wapenda amanihupanda katika amani.

Mapigano na magombano yote katiyenu yanatoka wapi? Hutoka katikatamaa zenu mbaya ambazo hupigana

daima ndani yenu. 2 Mnatamani vitu na kwavile hamvipati mko tayari kuua; mwatamanisana kupata vitu, lakini hamvipati, hivyomnagombana na kupigana. Hampati kilemnachotaka kwa sababu hamkiombi kwaMungu. 3 Tena, mnapoomba hampati kwasababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaombaili mpate kutosheleza tamaa zenu. 4 Ninyi niwatu msio na uaminifu kama wazinzi. Je,hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu nikuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwarafiki wa ulimwengu anajifanya adui waMungu. 5 Msifikiri kwamba MaandikoMatakatifu yamesema maneno ya bure,yanaposema: “Roho ambaye Munguamemweka ndani yetu ana wivu mkubwa.” 6

Lakini, neema tunayopewa na Mungu inanguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko:“Mungu huwapinga wenye majivuno lakinihuwapa neema wanyenyekevu.” 7 Basi,jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi nayeatawakimbieni. 8 Mkaribieni Mungu, nayeatakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyiwakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!9 Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko

WARAKA WA YAKOBO 2:11

184

Page 185: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzunikubwa. 10 Nyenyekeeni mbele ya Bwana, nayeatawainueni. 11 Ndugu, msilaumiane ninyikwa ninyi. Anayemlaumu ndugu yake nakumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumuSheria. Kama ukiihukumu Sheria, basi, wewehuitii Sheria, bali waihukumu. 12 Mungu pekeyake ndiye mwenye kuweka Sheria nakuhukumu. Ni yeye peke yake anayewezakuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nanihata umhukumu binadamu mwenzako? 13

Basi, sasa sikilizeni ninyi mnaosema: “Leo aukesho tutakwenda katika mji fulani na kukaahuko mwaka mzima tukifanya biashara nakupata faida.” 14 Ninyi hamjui hata maishayenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kamaukungu unaotokea kwa muda mfupi tu nakutoweka tena. 15 Mngalipaswa kusema:“Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki aukile.” 16 Lakini sasa mwajivuna na kujigamba;majivuno ya namna hiyo ni mabaya. 17 Basi,mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojuakwamba anapaswa kulifanya, anatendadhambi.

Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni nakuomboleza kwa sababu ya taabuzitakazowajieni. 2 Mali zenu zimeoza,

na nguo zenu zimeliwa na nondo. 3 Dhahabuyenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyoitakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miiliyenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia malikatika siku hizi za mwisho! 4 Hamkuwalipamishahara watumishi waliofanya kazi katikamashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao!Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenukimefika masikioni mwa Bwana, MwenyeNguvu. 5 Mmeishi duniani maisha yakujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepeshatayari kwa siku ya kuchinjwa. 6 Mmemhukumuna kumwua mtu asiye na hatia, nayehakuwapigeni. 7 Basi, ndugu zangu, muwe nasubira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni

mkulima anavyongoja kwa subira mimea yakeitoe mavuno mazuri. Yeye hungojea kwa subiramvua za masika na za vuli. 8 Nanyi piamnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyoyenu, maana siku ya kuja kwake Bwanainakaribia. 9 Ndugu zangu, msinung'unikianeninyi kwa ninyi msije mkahukumiwa naMungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia. 10

Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira nauvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabiiambao walinena kwa jina la Bwana. 11

Tunawaita hao wenye heri kwa sababuwalivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu waYobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendeamwishoni. Maana Bwana amejaa huruma narehema. 12 Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu,msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwakitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kamamaana yenu ni ndiyo, na “La” kama maanayenu ni la, na hapo hamtahukumiwa naMungu. 13 Je, pana mtu yeyote miongonimwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je,yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimbanyimbo za sifa. 14 Je, yuko mgonjwa kati yenu?Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, naowatamwombea na kumpaka mafuta kwa jina laBwana. 15 Wakiomba kwa imani mgonjwaataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, nadhambi alizotenda zitaondolewa. 16 Basi,ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni,ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema inanguvu ya kutenda mengi. 17 Eliya alikuwabinadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvuaisinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa mudawa miaka mitatu na miezi sita. 18 Kishaakaomba tena, mvua ikanyesha kutoka anganina nchi ikatoa mazao yake. 19 Ndugu zangu,mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, namwingine akamrudisha, 20 fahamuni kwamba,huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutokanjia yake ya upotovu, ataiokoa roho yakekutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.

WARAKA WA YAKOBO 5:20

185

Page 186: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

1 PETRO

Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristonawaandikia ninyi wateule wa MunguBaba, ambao mmetawanyika na

mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia,Kapadokia, Asia na Bithunia. 2 Mungu Babaaliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, nammefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtiiYesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake.Nawatakieni neema na amani tele. 3 AsifiweMungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo!Kwa huruma yake kuu alitufanya tuzaliwe upyakwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Ametujaliatumaini lenye uzima, 4 na hivyo tunatazamiakupata baraka zile ambazo Mungu aliwawekeawatu wake. Mungu amewawekeeni barakahizo mbinguni ambako haziwezi kuoza aukuharibika au kufifia. 5 Hizo zitakuwa zenuninyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwanguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambaouko tayari kufunuliwa mwishoni mwa nyakati.6 Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa,kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunikakwa sababu ya majaribio mbalimbalimnayoteseka. 7 Shabaha yake ni kuthibitishaimani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayohuharibika, hujaribiwa kwa moto; halikadhalika na imani yenu ambayo ni ya thamanizaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipatekuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufuna heshima Siku ile Yesu Kristoatakapofunuliwa. 8 Ninyi mnampendaingawaje hamjamwona, na mnamwaminiingawa hamumwoni sasa. Hivyo, mnafurahikwa furaha tukufu isiyoelezeka, 9 kwa sababumnapokea wokovu wa roho zenu ambao nilengo la imani yenu. 10 Manabii walipelelezakwa makini na kufanya uchunguzi juu yawokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyoambayo ninyi mngepewa. 11 Walijaribu kujuanyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakatialioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndaniyao, akibashiri juu ya mateso yatakayompataKristo na utukufu utakaofuata. 12 Mungualiwafunulia kwamba wakati walipokuwawanasema juu ya hayo mambo ambayo ninyimmekwisha sikia sasa kutoka kwa walewajumbe waliowatangazieni Habari Njemakwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyetumwakutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwafaida yao wenyewe, bali kwa ajili yenu. Hayondiyo mambo ambayo hata malaikawangependa kuyafahamu. 13 Kwa hiyo, basi,muwe tayari kabisa kwa nia, na kukesha.

Wekeni tumaini lenu lote katika baraka ilemtakayopewa wakati Yesu Kristoatakapoonekana! 14 Kama watoto wa Munguwenye utii, msikubali kamwe kufuata tenatamaa mbaya mlizokuwa nazo wakatimlipokuwa wajinga. 15 Bali mnapaswa kuwawatakatifu katika mwenendo wenu wote, kamavile yule aliyewaiteni ni mtakatifu. 16 Maandikoyasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi nimtakatifu.” 17 Mnapomtaja Mungu ninyihumwita Baba. Basi, jueni kwamba yeyehumhukumu kila mmoja kadiri ya matendoyake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenuuliowabakia hapa ugenini katika kumchaMungu. 18 Maana mnajua kwamba ninyimlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaaambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, sikwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha nadhahabu; 19 bali mlikombolewa kwa damutukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwanakondoo asiye na dosari wala doa. 20 Yeyealikuwa ameteuliwa na Mungu kabla yaulimwengu kuumbwa, akafunuliwa siku hizi zamwisho kwa ajili yenu. 21 Kwa njia yake, ninyimnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafuna kumpa utukufu; na hivyo imani namatumaini yenu yako kwa Mungu. 22

Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyimmezitakasa roho zenu na kuwapendawenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwamoyo wote. 23 Maana kwa njia ya neno hai laMungu, ninyi mmezaliwa upya, si kama watotowa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufamilele. 24 Kama Maandiko yasemavyo: “Kilabinadamu ni kama nyasi, na utukufu wakewote ni kama maua ya porini. Nyasi hunyaukana maua huanguka. 25 Lakini neno la Bwanahudumu milele.” Neno hilo ni hiyo HabariNjema iliyohubiriwa kwenu.

Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki,wivu na maneno ya kashfa visiwekotena. 2 Kama vile watoto wachanga

wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswakuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ilikwa nguvu yake mpate kukua nakukombolewa. 3 Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana nimwema.” 4 Basi, mwendeeni Bwana! Yeyendiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakinimbele ya Mungu ni jiwe teule, na la thamanikubwa. 5 Mwendeeni yeye kama mawe haimkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho,ambamo mtatumikia kama makuhani

1 PETRO 1:2

186

Page 187: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

watakatifu, kutolea dhabihu za kiroho zenyekumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. 6

Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama!Naweka huko sioni jiwe kuu la msingi, jiwe lathamani kubwa nililoliteua. Mtuatakayemwamini yeye aliye hilo jiwe,hataaibishwa.” 7 Kwenu ninyi mnaoamini, jiwehilo ni la thamani kubwa; lakini kwa walewasioamini, “Jiwe walilokataa waashi, sasalimekuwa jiwe kuu la msingi.” 8 TenaMaandiko yasema: “Jiwe hilo ni jiwe lakujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu.”Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini uleujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangumwanzo. 9 Lakini ninyi ni ukoo mteule,makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watuwake Mungu mwenyewe, mlioteuliwakutangaza matendo makuu ya Mungualiyewaiteni kutoka gizani akawaingizeni katikamwanga wake mkuu. 10 Wakati mmoja ninyihamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa ninyi niwatu wake; wakati mmoja hamkupewahuruma ya Mungu, lakini sasa mmeipokea. 11

Wapenzi wangu, nawasihi ninyi kama wagenina wakimbizi hapa duniani! Achaneni na tamaaza mwili ambazo hupingana na roho. 12

Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjuaMungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ilihata watakapowasingizieni kwamba mnatendamabaya, waweze kutambua matendo yenumema na hivyo wamtukuze Mungu Siku yakuja kwake. 13 Basi, jiwekeni chini ya mamlakayote ya kibinadamu, kwa ajili ya Bwana: utiikwa mfalme aliye mtawala mkuu, 14 utii kwawakuu wa mikoa ambao wameteuliwa nayekuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendaomema. 15 Maana Mungu anataka mwezekuyakomesha maneno ya kijinga ya watuwasio na akili kwa matendo memamnayofanya. 16 Ishini kama watu huru; lakinimsiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya, baliishini kama watumishi wa Mungu. 17

Waheshimuni watu wote, wapendeni nduguzenu waumini, mcheni Mungu, mheshimunimfalme. 18 Enyi watumishi wa nyumbani,watiini wakuu wenu kwa heshima yote, wawewema na wapole au wenye kuchukiza. 19

Maana kama mnavumilia maumivu ya matesomsiyostahili kwa sababu mwajua kwambaMungu anataka hivyo, basi Munguatawafadhili. 20 Maana, mtapata tuzo ganimkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababuya makosa yenu? Lakini kama mnavumiliamateso hata ingawa mmetenda mema, Munguatawapeni baraka kwa ajili hiyo. 21 Hayo ndiyomliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe alitesekakwa ajili yenu, akawaachieni mfano, ilimuufuate mwenendo wake. 22 Yeyehakutenda dhambi, wala neno la udanganyifuhalikusikika mdomoni mwake. 23

Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano;alipoteseka yeye hakutoa vitisho, balialiyaweka matumaini yake kwa Mungu,

hakimu mwenye haki. 24 Yeye mwenyewealizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu yamsalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, nakuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa majeraha yake,ninyi mmeponywa. 25 Ninyi mlikuwa kamakondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasammemrudia Mchungaji na Mlinzi wa rohozenu.

Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlakaya waume zenu, ili kama wako waumewowote wasioamini neno la Mungu,

wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu.Haitakuwa lazima kwenu kusema neno, 2

kwani wataona jinsi mwenendo wenu ulivyosafi na wa kumcha Mungu. 3 Katika kujipambakwenu msitegemee mambo ya njenje, kamavile mitindo ya kusuka nywele, kujivalia vituvya dhahabu na nguo maridadi. 4 Bali, uzuriwenu unapaswa kutokana na hali ya ndani yautu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema nautulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwambele ya Mungu. 5 Ndivyo walivyojipambahapo kale wanawake waadilifuwaliomtumainia Mungu; walijiweka chini yamamlaka ya waume zao. 6 Sara kwa mfanoalimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana.Ninyi mmekuwa sasa binti zake kamamkitenda mema bila kuogopa tisho lolote. 7

Kadhalika nanyi waume, katika kuishi na wakezenu mnapaswa kutambua kwamba wao nidhaifu na hivyo muwatendee kwa heshima;maana nao pia watapokea pamoja nanyizawadi ya uzima anayowapeni Mungu. Hapondipo sala zenu hazitakataliwa. 8 Mwishonasema hivi: mnapaswa kuwa na moyommoja, na fikira moja; mnapaswa kupendanakidugu, kuwa wapole na wanyenyekevu ninyikwa ninyi. 9 Msiwalipe watu ovu kwa ovu, autusi kwa tusi; bali watakieni baraka, maananinyi mliitwa na Mungu mpate kupokeabaraka. 10 Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: “Anayetaka kufurahia maisha, nakuona siku za fanaka, anapaswa kuachakusema mabaya na kuacha kusema uongo. 11

Na ajiepushe na uovu, atende mema, atafuteamani na kuizingatia. 12 Maana Bwanahuwatazama kwa wema waadilifu nakuzisikiliza sala zao. Lakini huwapa kisogowatu watendao maovu.” 13 Ni naniatakayeweza kuwadhuru ninyi kamamkizingatia kutenda mema? 14 Lakini, hatakama itawapasa kuteseka kwa sababu yakutenda mema, basi, mna heri. Msimwogopemtu yeyote, wala msikubali kutiwa katikawasiwasi. 15 Lakini mtukuzeni Kristo kamaBwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibuyeyote atakayewaulizeni juu ya matumainiyaliyo ndani yenu, 16 lakini fanyeni hivyo kwaupole na heshima. Muwe na dhamiri njema,kusudi mnapotukanwa, wale wanaosemaubaya juu ya mwenendo wenu mwema kamaWakristo, waone aibu. 17 Maana ni afadhalikuteseka kwa sababu ya kutenda mema, kama

1 PETRO 3:17

187

Page 188: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

45

Mungu akipenda, kuliko kuteseka kwa sababuya kutenda uovu. 18 Kwa maana Kristomwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu;alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwemakwa ajili ya waovu, ili awapeleke ninyi kwaMungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa haikiroho; 19 na kwa maisha yake ya kirohoalikwenda kuwahubiria wale roho waliokuwakifungoni. 20 Hao ndio wale waliokataa kumtiiMungu alipowangoja kwa saburi wakati Noaalipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani yachombo hicho ni watu wachache tu, yaaniwatu wanane, waliookolewa majini, 21 ambayoyalikuwa mfano wa ubatizo unaowaokoa ninyisasa. Ubatizo si shauri la kuondoa uchafumwilini, bali ni ahadi kwa Mungu inayofanyikakatika dhamiri njema. Huwaokoeni kwa njia yaufufuo wa Yesu Kristo, 22 ambaye alikwendambinguni na sasa amekaa upande wa kulia waMungu, anatawala juu ya malaika, wakuu nawenye enzi.

Maadamu Kristo aliteseka kimwili,nanyi pia mnapaswa kujiimarisha kwania hiyo yake; maana mtu akisha teseka

kimwili hahusiki tena na dhambi. 2 Tangusasa, basi, maisha yaliowabakia kuishi hapaduniani yanapaswa kuongozwa na matakwa yaMungu, si na tamaa za kibinadamu. 3 Wakatiuliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanyamambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu.Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi,ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu zasanamu. 4 Sasa, watu hao wasiomjua Munguwanashangaa wanapoona kwambahamwandamani nao tena katika hali ya kuishivibaya, na hivyo wanawatukaneni. 5 Lakiniwatapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbeleyake Mungu aliye tayari kuwahukumu wazimana wafu! 6 Kwa sababu hiyo, hao waliokufaambao walikuwa wamehukumiwa katikamaisha yao ya kimwili kama anavyohukumiwakila mmoja, walihubiriwa Habari Njema kusudikatika maisha yao ya kiroho waishi kamaaishivyo Mungu. 7 Mwisho wa vitu vyoteumekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa nautaratibu na nidhamu, ili mweze kusali. 8 Zaidiya yote pendaneni kwa moyo wote, maanaupendo hufunika dhambi nyingi. 9 Muwe naukarimu ninyi kwa ninyi bila kunung'unika. 10

Kila mmoja anapaswa kutumia kipajialichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine,kama vile uwakili mwema wa zawadimbalimbali za Mungu. 11 Anayesema kitu,maneno yake na yawe kama maneno yaMungu; anayetumika anapaswa kutumikia kwanguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mamboyote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo,ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele namilele! Amina. 12 Wapenzi wangu, msishangaekuhusu majaribio makali mnayopata kanakwamba mnapatwa na kitu kisicho chakawaida. 13 Ila furahini kwamba mnashirikimateso ya Kristo ili mweze kuwa na furaha tele

wakati utukufu wake utakapofunuliwa. 14 Heriyenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina laKristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Rohomtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juuyetu. 15 Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenuambaye anapaswa kuteseka kwa sababu nimuuaji, mwizi, mhalifu au mwovu. 16 Lakinikama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo,basi asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwasababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo. 17

Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyoinaanza na watu wake Mungu mwenyewe.Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basimwisho wake utakuwa namna gani kwa walewasioamini Habari Njema ya Mungu? 18 Kamayasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni vigumukwa watu waadilifu kuokolewa; itakuwaje basikwa wasiomcha Mungu na wenye dhambi?” 19

Kwa hiyo, wale wanaoteseka kufuatana namatakwa ya Mungu, wanapaswa, kwamatendo yao mema, kujiweka chini yaMuumba wao ambaye ni wa kuaminika kabisa.

wazee! Mimi niliye mzee ninalo ombimoja kwenu wazee wenzangu. Mimimwenyewe nilishuhudia kwa macho

yangu mateso ya Kristo na natumainikuushiriki ule utukufu utakaofunuliwa. Miminawaombeni 2 mlichunge lile kundi la Mungumlilokabidhiwa, mlitunze si kwa kulazimika,bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyenikazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyowenu wote. 3 Msiwatawale kwa mabavu haowaliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali muwemfano kwa hilo kundi. 4 Na wakati MchungajiMkuu atakapotokea, ninyi mtapokea taji yautukufu isiyofifia. 5 Kadhalika nanyi vijanamnapaswa kujiweka chini ya mamlaka yawazee. Ninyi nyote mnapaswa kuwa naunyenyekevu mpate kutumikiana; maanaMaandiko Matakatifu yasema: “Munguhuwapinga wenye majivuno, lakini huwajalianeema wanyenyekevu.” 6 Basi, nyenyekeenichini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainuewakati ufaao. 7 Mwekeeni matatizo yenu yote,maana yeye anawatunzeni. 8 Muwe macho;kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi,huzungukazunguka kama simba angurumayeakitafuta mawindo. 9 Muwe imara katika imanina kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenupote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.10 Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungualiye asili ya neema yote na ambayeanawaiteni muushiriki utukufu wake wa milelekatika kuungana na Kristo, yeye mwenyeweatawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvuna msingi imara. 11 Kwake uwe uwezo milele!Amina. 12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwamsaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua nakumwamini. Nataka kuwapeni moyo nakushuhudia kwamba jambo hili ni neema yaMungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.13 Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa naMungu hapa Babuloni wanawasalimuni.

1 PETRO 3:18

188

Page 189: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni. 14

Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo.Nawatakieni amani ninyi mlio wake Kristo.

1 PETRO 5:14

189

Page 190: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

2 PETRO

Mimi Simoni Petro, mtumishi na mtumewa Yesu Kristo, nawaandikia ninyiambao, kwa wema wake Mungu wetu,

na Mwokozi Yesu Kristo, mmejaliwa imani ileileya thamani kuu tuliyojaliwa sisi. 2 Nawatakienineema na amani tele katika kumjua Mungu naYesu Bwana wetu. 3 Kwa uwezo wake wakimungu, Mungu ametujalia mambo yotetunayohitaji, ili tuishi maisha ya kumchaMungu kwa kumjua yeye aliyetuita tuushirikiutukufu na wema wake yeye mwenyewe. 4

Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na zathamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadihizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbayazilizomo duniani, na mpate kuishiriki hali yakeya kimungu. 5 Kwa sababu hiyo, fanyeni bidiiya kuongeza fadhila katika imani yenu:ongezeni elimu katika fadhila yenu, 6 kuwa nakiasi katika elimu yenu, uvumilivu katika kuwana kiasi, uchaji wa Mungu katika uvumilivuwenu, 7 udugu katika uchaji wenu, namapendo katika udugu wenu. 8 Mkiwa na sifahizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwawatendaji na kupata faida katika kumjuaBwana wetu Yesu Kristo. 9 Lakini mtu asiye nasifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahaukwamba alikwisha takaswa dhambi zake zazamani. 10 Kwa hiyo basi, ndugu zangu,fanyeni bidii zaidi kuufanya huo wito wenumlioitiwa na Mungu uwe jambo la kudumukatika maisha yenu; kama mkiishi namna hiyohamtaanguka kamwe. 11 Kwa namna hiyomtafaulu kupewa haki kamili ya kuingia katikaUtawala wa milele wa Bwana na Mwokozi wetuYesu Kristo. 12 Kwa hiyo nitaendeleakuwakumbusheni daima mambo haya, ingawammekwisha yafahamu, na mko imara katikaukweli mlioupokea. 13 Nadhani ni jambo jemakwangu, muda wote niishio hapa duniani,kuwapeni moyo na kuwakumbusheni juu yamambo haya. 14 Najua kwamba karibunitauweka kando mwili huu wenye kufa, kamaBwana alivyoniambia waziwazi. 15 Basi,nitajitahidi kuwapatieni njia ya kuyakumbukamambo haya kila wakati, baada ya kufarikikwangu. 16 Wakati tulipowafundisheni juu yaukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi.Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetuwenyewe. 17 Sisi tulikuwapo wakati alipopewaheshima na kutukuzwa na Mungu Baba, wakatisauti ilipomjia kutoka kwake yeye aliye UtukufuMkuu, ikisema: “Huyu ni Mwanangu mpenzi,

nimependezwa naye.” 18 Tena, sisi wenyewetulisikia sauti hiyo kutoka mbinguni wakatitulipokuwa pamoja naye juu ya ule mlimamtakatifu. 19 Tena, ujumbe wa manabiiwatuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanyavema kama mkiuzingatia, maana ni kama taainayoangaza mahali penye giza mpaka Siku ileitakapopambazuka na mwanga wa nyota yaasubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu. 20

Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwambahakuna mtu yeyote awezaye kufafanuamwenyewe unabii ulio katika MaandikoMatakatifu. 21 Maana hakuna ujumbe wakinabii unaotokana na matakwa ya binadamu,bali watu walinena ujumbe wa Munguwakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Palitokea manabii wa uongo kati yawatu, na vivyo hivyo walimu wa uongowatatokea kati yenu. Watu hao

wataingiza mafundisho maharibifu nakumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njiahiyo watasababisha ghafla maangamizi yaowenyewe. 2 Tena watu wengi watazifuata hizonjia zao mbaya, kwa sababu yao, wenginewataipuuza Njia ya ukweli. 3 Kwa tamaa yaombaya watajipatia faida kwa kuwaambienihadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasaHakimu wao yu tayari, na Mwangamizi wao yumacho! 4 Malaika walipotenda dhambi,Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katikamoto wa Jehanamu ambako wamefungwawakingojea Siku ile ya Hukumu. 5 Munguhakuihurumia dunia ya hapo kale, bali aliletagharika kuu juu ya nchi ile ya watu wasiomchaMungu; lakini Noa ambaye alihubiri uadilifu,Mungu alimwokoa pamoja na watu wenginesaba. 6 Mungu aliadhibu miji ya Sodoma naGomora, akaiteketeza kwa moto, akaifanya iwemfano wa mambo yatakayowapata watuwasiomcha Mungu. 7 Alimwokoa Loti, mtumwema, ambaye alisikitishwa sana namwenendo mbaya wa watu hao waasi. 8 Lotialiishi miongoni mwa watu hao, na kwa sikunyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasimkuu aliposikia matendo yao maovu. 9 Kwahiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoakatika majaribu watu wanaomcha Mungu, najinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadiSiku ile ya hukumu, 10 hasa wale wanaofuatatamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka.Watu hao ni washupavu na wenye majivuno,huvitukana na hawaviheshimu viumbevitukufu vya juu. 11 Lakini malaika, ambao

2 PETRO 1:2

190

Page 191: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

wana uwezo na nguvu zaidi kuliko hao walimuwa uongo, hawawashtaki na kuwatukana haombele ya Bwana. 12 Watu hao ambaohutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawana wanyama wasio na akili, ambao huzaliwa nabaadaye hukamatwa na kuchinjwa!Wataangamizwa kutokana na uharibifu waowenyewe, 13 na watalipwa mateso kwa matesoambayo wameyasababisha. Furaha yao nikufanya, tena mchana kabisa, chochotekinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao nifedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenuwakati wanapojiunga nanyi katika karamuzenu, bali wakifurahia njia zao za udanganyifu.14 Macho yao yamejaa uzinzi na uwezo waowa kutenda dhambi hauna kikomo.Huwaongoza watu walio dhaifu mpakamitegoni. Mioyo yao imezoea kuwa na tamaaya mali. Wapo chini ya laana ya Mungu! 15

Wameiacha njia iliyonyoka, wakapotoka nakuifuata njia aliyofuata Balaamu, mwana waBeori, ambaye alipendelea kupata faida kwakufanya udanganyifu, 16 akakaripiwa kwa ajiliya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinenakwa sauti ya binadamu, akaukomesha wazimuwa huyo nabii. 17 Watu hao ni kamachemchemi zilizokauka, kama mawinguyanayopeperushwa na tufani; makao yaowaliyowekewa ni mahali pa giza kuu. 18

Husema maneno ya majivuno na yasiyo namaana, na kutumia tamaa zao mbaya zakimwili kuwatega wale ambao wamejitengahivi karibuni na watu waishio katikaudanganyifu. 19 Huwaahidi watu wengine etiwatakuwa huru, kumbe wao wenyewe niwatumwa wa upotovu—maana mtu nimtumwa wa chochote kile kinachomtawala. 20

Watu waliokwisha ponyoka katika upotovu waulimwengu kwa kupata kumjua Bwana naMwokozi wetu Yesu Kristo, kisha wakakubalikunaswa na kutawaliwa tena na upotovu huo,hali yao itakuwa mbaya zaidi kuliko awali. 21

Ingalikuwa afadhali kwao kama wasingalijuakamwe njia hiyo ya uadilifu kuliko kujua nakisha kuiacha na kupoteza amri takatifuwaliyopokea. 22 Ipo mithali isemayo: “Mbwahuyarudia matapishi yake mwenyewe,” nanyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwishaoshwa hugaagaa tena katika matope!” Ndivyoilivyo kwao sasa.

Wapenzi wangu, hii ni barua ya pilininayowaandikia. Katika barua hizombili nimejaribu kufufua fikira safi

akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambohaya. 2 Napenda mkumbuke manenoyaliyosemwa na manabii watakatifu, na ileamri ya Bwana na Mwokozi mliyopewa namitume wenu. 3 Awali ya yote jueni kwambasiku za mwisho watakuja watu ambao

mienendo yao inatawaliwa na tamaa zaombaya. Watawadhihaki ninyi 4 na kusema:“Aliahidi kwamba atakuja! Je, sasa yuko wapi?Mambo ni yaleyale tangu babu zetuwalipokufa; hali ya vitu ni ileile kamailivyokuwa mwanzo wa ulimwengu!” 5 Watuhao, kwa makusudi, husahau kwamba zamaniMungu alinena, nazo mbingu na nchizikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika majina kwa maji; 6 na kwa maji hayo, yaani yalemaji ya gharika kuu, dunia ya wakati uleiliangamizwa. 7 Lakini mbingu na nchi za sasazahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili yakuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili yaSiku ile ambapo watu wasiomcha Munguwatahukumiwa na kuangamizwa. 8 Lakini,wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbeleya Bwana, hakuna tofauti kati ya siku moja namiaka elfu; kwake yote ni mamoja. 9 Bwanahakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watuwengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeyeana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hatammoja wenu apotee, bali huwavuta wotewapate kutubu. 10 Siku ya Bwana itakuja kamamwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwakishindo kikuu; vitu vyake vya asilivitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatowekapamoja na kila kitu kilichomo ndani yake. 11

Maadamu kila kitu kitaharibiwa namna hiyo, je,ninyi mnapaswa kuwa watu wa namna gani?Mnapaswa kuishi kitakatifu na kumcha Mungu,12 mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanyaije upesi—Siku ambayo mbingu zitateketezwakwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asilivitayeyushwa kwa joto. 13 Lakini sisi,kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingumpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu.14 Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwamnangojea Siku ile, fanyeni bidii kuwa safikabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa naamani naye. 15 Mnapaswa kuuona uvumilivuwa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni mpatekuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzialivyowaandikia akitumia hekima aliyopewa naMungu. 16 Hayo ndiyo asemayo katika baruazake zote anapozungumzia suala hilo. Yapomambo kadhaa katika barua zake yaliyomagumu kuyaelewa, mambo ambayo watuwajinga, wasio na msimamo, huyapotoshakama wanavyopotosha sehemu nyingine zaMaandiko Matakatifu. Hivyo wanasababishamaangamizi yao wenyewe. 17 Lakini ninyi,wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili.Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwana makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katikamsimamo wenu imara. 18 Lakini endeleenikukua katika neema na katika kumjua Bwanawetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwekwake, sasa na hata milele! Amina.

2 PETRO 3:18

191

Page 192: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

1 YOHANA

Habari hii ya yahusu Neno la uzimalililokuwako tangu mwanzo. Sisitumepata kulisikia na kuliona kwa

macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishikakwa mikono yetu wenyewe. 2 Uzima huoulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasemahabari zake na kuwaambieni juu ya uzima huowa milele uliokuwa kwa Baba nauliodhihirishwa kwetu. 3 Tulichokiona nakukisikia ndicho tunachowatangazieni ninyi piaili nanyi mpate kushirikiana nasi katika umojatulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo. 4

Tunawaandikia ninyi mambo haya kusudifuraha yetu ikamilike. 5 Basi, habari tuliyoisikiakwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii:Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndaniyake. 6 Tukisema kwamba tuna umoja naye,na papo hapo twaishi gizani, tutakuwatumesema uongo kwa maneno na matendo. 7

Lakini tukiishi katika mwanga, kama nayealivyo katika mwanga, basi tutakuwa na umojasisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo,Mwanae, inatutakasa dhambi zote. 8 Tukisemakwamba hatuna dhambi, tunajidanganyawenyewe na ukweli haumo ndani yetu. 9

Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Munguni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehedhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10

Tukisema kwamba hatujatenda dhambi,tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, naneno lake halimo ndani yetu.

Watoto wangu, ninawaandikienimambo haya, kusudi msitende dhambi.Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi,

tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba,ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa. 2

Kristo ndiye sadaka iondoayo dhambi zetu;wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi zaulimwengu wote. 3 Tukizitii amri za Mungu,basi, tunaweza kuwa na hakika kwambatunamjua. 4 Mtu akisema kwamba anamjua,lakini hazitii amri zake, basi mtu huyo nimwongo, na ukweli haumo ndani yake. 5

Lakini mtu yeyote anayeshika neno la Mungu,huyo ndiye aliye na upendo kamili wa Mungundani yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa nahakika kwamba tunaungana naye: 6 mtuyeyote anayesema kwamba ameungana naMungu, anapaswa kuishi kama alivyoishi YesuKristo. 7 Wapenzi wangu, amri hiininayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileileya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo.Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia.

8 Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni niamri mpya, na ukweli wake unaonekana ndaniya Kristo na ndani yenu pia. Maana gizalinatoweka, na mwanga wa ukweli umekwishaanza kuangaza. 9 Yeyote asemaye kwambayumo katika mwanga, lakini anamchukiandugu yake, mtu huyo bado yumo gizani. 10

Yeyote ampendaye ndugu yake, yuko katikamwanga, na hamna chochote ndani yakekiwezacho kumkwaza mtu mwingine. 11 Lakinianayemchukia ndugu yake, yumo gizani;anatembea gizani, na hajui anakokwenda,maana giza limempofusha. 12

Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa kuwadhambi zenu zimeondolewa kwa jina la Kristo.13 Nawaandikieni ninyi kina baba kwanimnamjua yeye ambaye amekuwako tangumwanzo, Nawaandikieni ninyi vijana kwasababu mmemshinda yule Mwovu. 14

Nawaandikieni ninyi watoto, kwa sababumnamjua Baba. Nawaandikieni ninyi kinababa, kwa kuwa mnamjua yeye ambayeamekuwako tangu mwanzo. Nawaandikienininyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno laMungu limo ndani yenu na mmemshinda yuleMwovu. 15 Msiupende ulimwengu, walachochote kilicho cha ulimwengu. Mtuanayeupenda ulimwengu, upendo wa Babahauwezi kuwamo ndani yake. 16 Vitu vyote vyaulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vituwanavyoviona watu na kuvitamani, majivunoyasababishwayo na mali-vyote hivyo havitokikwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu. 17

Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenyekutamanika unapita; lakini mtu atendayeatakalo Mungu, anaishi milele. 18 Watoto,mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba aduiwa Kristo anakuja, na sasa adui wengi waKristo wamekwisha fika, na hivyo twajuakwamba mwisho u karibu. 19 Watu haowametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wakwetu na ndiyo maana walituacha; Kamawangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi.Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudiionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wakwetu. 20 Ninyi, lakini, mlipata kumiminiwaRoho Mtakatifu na Kristo, na hivyo mnaujuaukweli. 21 Basi, nawaandikieni, si kwa kuwahamuujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; napia mnajua kwamba uongo wowotehaupatikani katika ukweli. 22 Mwongo ni nani?Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Masiha.Mtu wa namna hiyo ni adui wa

1 YOHANA 1:2

192

Page 193: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

4

Kristo—anamkana Baba na Mwana. 23 Maanayeyote anayemkana Mwana, anamkana piaBaba; na yeyote anayemkubali Mwana,anampata Baba pia. 24 Basi, ujumbe ulemliousikia tangu mwanzo na ukae mioyonimwenu. Kama ujumbe huo mliousikia tangumwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtaishidaima katika umoja na Mwana na Baba. 25 Naahadi aliyotuahidia sisi ndiyo hii: uzima wamilele. 26 Nimewaandikieni mambo hayakuhusu wale wanaotaka kuwapotosha ninyi. 27

Lakini, kwa upande wenu ninyi, Kristoaliwamiminieni Roho wake. Na kamaakiendelea kukaa ndani yenu, hamhitajikufundishwa na mtu yeyote. Maana Rohowake anawafundisheni kila kitu na mafundishoyake ni ya kweli, si ya uongo. Basi shikenimafundisho ya huyo Roho na kubaki katikamuungano na Kristo. 28 Naam, watoto, kaenindani yake kusudi wakati atakapotokea tuwehodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwaaibu Siku ya kuja kwake. 29 Mnajua kwambaKristo ni mwadilifu kabisa; basi, mnapaswakujua pia kwamba kila mtu atendaye mamboadili ni mtoto wa Mungu.

Oneni basi, jinsi Baba alivyotupendamno hata tunaitwa watoto wa Mungu!Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana

ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjuiMungu. 2 Wapenzi wangu, sisi ni watoto waMungu sasa, lakini bado haijaonekana wazijinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwambawakati Kristo atakapotokea, tutafanana nayekwani tutamwona vile alivyo. 3 Basi, kila mtualiye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safikama vile Kristo alivyo safi kabisa. 4 Kila mtuatendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu,maana dhambi ni uvunjaji wa sheria. 5 Mnajuakwamba Kristo alikuja kuziondoa dhambi zetu,na kwamba kwake hamna dhambi yoyote. 6

Basi, kila aishiye katika muungano na Kristohatendi dhambi; lakini kila mtu atendayedhambi hakupata kamwe kumwona, walakumjua Kristo. 7 Basi, watoto wangu,msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtuatendaye matendo maadilifu ni mwadilifukama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa. 8

Lakini atendaye dhambi ni wa Ibilisi, maanaIbilisi ametenda dhambi tangu mwanzo. LakiniMwana wa Mungu alikuja duniani kuiharibukazi ya Ibilisi. 9 Kila aliye mtoto wa Munguhatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungundani yake; hawezi kutenda dhambi kwasababu yeye ni mtoto wa Mungu. 10 Lakiniyeyote asiyetenda mambo maadilifu, auasiyempenda ndugu yake, huyo si mtoto waMungu. Hiyo ndiyo tofauti iliyoko kati yawatoto wa Mungu na watoto wa Ibilisi. 11 Na,ujumbe mliousikia tangu mwanzo ndio huu:Tunapaswa kupendana! 12 Tusiwe kama Kainiambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu,alimuua ndugu yake. Na, kwa nini alimuua?Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu,

lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema! 13

Basi, ndugu zangu, msishangae kamaulimwengu unawachukia ninyi. 14 Sisi tunajuakwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo nakuingia katika uzima kwa sababutunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye naupendo hubaki katika kifo. 15 Kilaanayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyimnajua kwamba muuaji yeyote yule hanauzima wa milele ndani yake. 16 Sisi tumepatakujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoamaisha yake kwa ajili yetu. Nasi vileviletunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili yandugu zetu. 17 Basi, mtu akiwa na mali zahapa duniani, halafu akamwona ndugu yakeana shida, lakini akawa na moyo mgumu bilakumwonea huruma, anawezaje kusemakwamba anampenda Mungu? 18 Watotowangu, upendo wetu usiwe maneno matupu,bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo. 19

Hivyo ndivyo tuwezavyo kuwa na hakikakwamba sisi ni watu wa ukweli; na hatutakuwana wasiwasi mbele ya Mungu. 20 Kwa maana,hata kama dhamiri yetu yatuhukumu, twajuakwamba Mungu ni mkuu zaidi kuliko dhamiri,na kwamba yeye ajua kila kitu. 21 Wapenziwangu, kama dhamiri yetu haina lawama juuyetu, basi, twaweza kuwa na uthabiti mbele yaMungu, 22 na twaweza kupokea kwakechochote tunachoomba, maana tunazitii amrizake na kufanya yale yanayompendeza. 23 Na,amri yake ndiyo hii: Kumwamini MwanaeKristo, na kupendana kama alivyotuamuru. 24

Anayezitii amri za Mungu anaishi katikamuungano na Mungu na Mungu anaishi katikamuungano naye. Kwa njia ya Roho ambayeMungu ametujalia, sisi twajua kwamba Munguanaishi katika muungano nasi.

Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtuasemaye kwamba ana Roho wa Mungu,bali chunguzeni kwa makini kama huyo

mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la,Maana manabii wengi wa uongo wamezukaulimwenguni. 2 Hii ndiyo njia ya kujua kamamtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kilaanayekiri kwamba Kristo alikuja, akawabinadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu. 3

Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hanahuyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo anaroho ambaye ni wa Adui wa Kristo; nanyimlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasatayari amekwisha wasili ulimwenguni! 4 Lakinininyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwishawashinda hao manabii wa uongo; maana Rohoaliye ndani yenu ana nguvu zaidi kuliko rohoaliye ndani ya hao walio wa ulimwengu. 5 Waohusema mambo ya ulimwengu, naoulimwengu huwasikiliza kwani wao ni waulimwengu. 6 Lakini sisi ni wake Mungu. Mtuanayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye waMungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyotunaweza kutambua tofauti kati ya Roho waukweli na roho wa uongo. 7 Wapenzi wangu,

1 YOHANA 4:7

193

Page 194: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

5

tupendane, maana upendo hutoka kwaMungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto waMungu, na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye naupendo hamjui Mungu, maana Mungu niupendo. 9 Na Mungu alionyesha upendo wakekwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekeeulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake.10 Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisitulikuwa tumempenda Mungu kwanza, balikwamba yeye alitupenda hata akamtumaMwanae awe sadaka ya kutuondolea dhambizetu. 11 Wapenzi wangu, ikiwa Mungualitupenda hivyo, basi, nasi tunapaswakupendana. 12 Hakuna mtu aliyekwishamwona Mungu kamwe; lakini kamatukipendana Mungu anaishi katika muunganonasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.13 Tunajua kwamba tunaishi katika umoja naMungu, naye Mungu anaishi katika umojanasi, kwani yeye ametupa Roho wake. 14 Sisitumeona na kuwaambia wengine kwambaBaba alimtuma Mwanae awe Mwokozi waulimwengu. 15 Kila mtu anayekiri kwambaYesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishikatika muungano na mtu huyo, naye anaishikatika muungano na Mungu. 16 Basi, sisitunajua na tunaamini upendo alio nao Mungukwetu sisi. Mungu ni upendo, na kila mtuaishiye katika upendo, anaishi katikamuungano na Mungu, na Mungu anaishikatika muungano naye. 17 Upendoumekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwana ujasiri Siku ile ya Hukumu; kwani maishayetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo. 18

Palipo na upendo hapana uoga; naam, upendokamili hufukuza uoga wote. Basi, mtu mwenyeuoga hajakamilika bado katika upendo, kwaniuoga huhusikana na adhabu. 19 Sisi tunaupendo kwa sababu Mungu alitupendakwanza. 20 Mtu akisema kwamba anampendaMungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo nimwongo. Maana mtu asiyempenda nduguyake ambaye anamwona, hawezi kumpendaMungu ambaye hamwoni. 21 Basi, hii ndiyoamri aliyotupa Kristo: Anayempenda Munguanapaswa pia kumpenda ndugu yake.

Kila mtu anayeamini kwamba Yesu niKristo, huyo ni mtoto wa Mungu; na,anayempenda mzazi humpenda pia

mtoto wa huyo mzazi. 2 Hivi ndivyotunavyojua kwamba tunawapenda watoto waMungu: Kwa kumpenda Mungu na kuzitii amrizake; 3 maana kumpenda Mungu ni kuzitiiamri zake. Na, amri zake si ngumu, 4 maanakila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda

ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushindaulimwengu: kwa imani yetu. 5 Nani, basi,awezaye kuushinda ulimwengu? Ni yuleanayeamini kwamba Yesu ni Mwana waMungu. 6 Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa majiya ubatizo wake na kwa damu ya kifo chake.Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwadamu. Naye Roho anashuhudia kwamba nikweli, kwani Roho ni ukweli. 7 Basi, wakomashahidi watatu: 8 Roho, maji na damu; naushahidi wa hawa watatu waafikiana. 9 Ikiwatwaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidiwa Mungu una uzito zaidi; na huu ndioushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu yaMwanae. 10 Anayemwamini mwana wa Munguanao ushahidi huo ndani yake; lakiniasiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwamwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoaMungu juu ya Mwanae. 11 Na, ushahidiwenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uzima wamilele, na uzima huo uko kwa Bwana. 12

Yeyote, aliye na Mwana wa Mungu anao uzimahuo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uzima.13 Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnaouzima wa milele ninyi mnaoamini kwa jina laMwana wa Mungu. 14 Na sisi tuko thabitimbele ya Mungu kwani tuna hakika kwambatukimwomba chochote kadiri ya mapenzi yake,yeye hutusikiliza. 15 Yeye hutusikiliza kilatunapomwomba; na kwa vile tunajua kwambayeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajuapia kwamba atupatia yote tunayomwomba. 16

Mtu akimwona ndugu yake ametenda dhambiisiyompeleka kwenye kifo anapaswakumwombea kwa Mungu, naye Munguatampatia uzima. Nasema jambo hili kuhusuwale waliotenda dhambi ambazo si za kifo.Lakini ipo dhambi yenye kumpeleka mtukwenye kifo nami sisemi kwamba mnapaswakumwomba Mungu kwa ajili ya hiyo. 17 Kilatendo lisilo adilifu ni dhambi, lakini kunadhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo. 18

Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Munguhatendi dhambi, kwa sababu Mwana waMungu humlinda salama, na yule Mwovuhawezi kumdhuru. 19 Tunajua kwamba sisi niwake Mungu ingawa ulimwengu woteunatawaliwa na yule Mwovu. 20 Twajua piakwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupaelimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katikamuungano na Mungu wa kweli—katikamuungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyundiye Mungu wa kweli, na huu ndio uzima wamilele. 21 Watoto wangu, epukaneni nasanamu za miungu.

1 YOHANA 4:8

194

Page 195: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2 YOHANA

Mimi Mzee nakuandikia weweBimkubwa mteule, pamoja na watotowako ninaowapenda kweli. Wala si

mimi tu ninayewapenda, bali pia wotewanaoujua ule ukweli wanawapenda ninyi, 2

kwa sababu ukweli unakaa nasi milele. 3

Neema na huruma na amani zitokazo kwaMungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwana waBaba, zitakuwa pamoja nasi katika ukweli naupendo. 4 Nilifurahi sana kuona kwambabaadhi ya watoto wako wanaishi katika ukwelikama Baba alivyotuamuru. 5 Basi, Bimkubwa,ninalo ombi moja kwako: tupendane. Ombi hilisi amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwanayo tangu mwanzo. 6 Upendo maana yake nikuishi kwa kuzitii amri zake Mungu. Amriniliyoisikia tangu mwanzo ndiyo hii: mnapaswanyote kuishi katika upendo. 7 Wadanganyifuwengi wamezuka duniani, watu ambao

hawakiri kwamba Yesu Kristo amekuja kwetuakawa binadamu. Mtu asemaye hivyo nimdanganyifu na ni Adui wa Kristo. 8 Basi,jihadharini ninyi wenyewe ili msije mkapotezakile mlichokishugulikia, bali mpate tuzo lenukamili. 9 Asiyezingatia na kudumu katikamafundisho ya Kristo, bali anayakiuka, hanaMungu. Lakini anayedumu katika mafundishohayo anaye Baba na Mwana. 10 Basi, kamamtu akija kwenu bila kuwaleteeni mafundishohayo, msimkaribishe nyumbani kwenu, walamsimsalimu. 11 Maana anayemsalimu mtuhuyo, anashirikiana naye katika matendo yakemaovu. 12 Ninayo mengi ya kuwaambienilakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi nawino; badala yake, natumaini kuwatembeleenina kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furahayetu ikamilike. 13 Watoto wa dada yako mteulewanakusalimu.

2 YOHANA 1:13

195

Page 196: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

3 YOHANA

Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo,rafiki yangu, ninayekupenda kweli. 2

Mpenzi wangu, nakutakia mafanikiomema ya kila aina; nakutakia afya njema yamwili kama ulivyo nayo rohoni. 3 Nimefurahisana ndugu kadhaa walipofika hapa,wakaiambia juu ya uaminifu wako kuhusuukweli; naam, wewe unaishi daima katikaukweli. 4 Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidikuliko kusikia kwamba watoto wangu wanaishikatika ukweli. 5 Mpenzi wangu, wewe nimwaminifu kila mara unapowahudumiandugu, hata kama ni wageni. 6 Ndugu haowamelieleza kanisa hapa habari za upendowako. Tafadhali uwasaidie waendelee na safariyao kwa namna itakayompendeza Mungu, 7

Maana wanaanza safari yao katika utumishi waKristo bila kupokea msaada wowote kutokakwa watu wasioamini. 8 Basi, sisi tunapaswakuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate kushirikikatika kazi yao kwa ajili ya ukweli. 9 Niliandikabarua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe,

ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hatakikabisa kunisikiliza. 10 Basi, nitakapokujanitayafichua mambo yote anayofanya, manenomabaya anayotutolea na uongo anaosema juuyetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha haondugu walio safarini, na hata huwazuia watuwengine wanaotaka kuwakaribisha, nahujaribu kuwafukuzia nje ya kanisa. 11 Mpenziwangu, usifuate mfano mbaya, bali mfanomwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu;lakini anayetenda mabaya hajapata kumwonaMungu. 12 Kila mtu anamsifu Demetrio; naam,ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoaushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwambatunachosema ni kweli. 13 Ninayo bado mengiya kukwambia, lakini sipendi kuyaandika kwakalamu na wino. 14 Natumaini kukuonakaribuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.(G1-15) Nakutakia amani. Rafiki zakowanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu wote kilammoja binafsi.

3 YOHANA 1:2

196

Page 197: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

WARAKA WA YUDA

Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo,ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyimlioitwa na Mungu na ambao mnaishi

katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinziwa Yesu Kristo. 2 Nawatakieni huruma, amanina upendo kwa wingi. 3 Ndugu wapenzi,wakati nimo katika jitihada ya kuwaandikienijuu ya ule wokovu tunaoshiriki sote, nimeonalazima ya kuwaandikieni na kuwahimizenimwendelee kupigana kwa ajili ya imaniambayo Mungu amewajalia watu wake maramoja tu kwa wakati wote. 4 Maana watuwasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwasiri miongoni mwetu, watu ambao, kwa faidaya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbewa neema ya Mungu wetu na kumkana YesuKristo aliye peke yake kiongozi na Bwana wetu.Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tanguawali hukumu inayowangojea watu hao. 5

Nataka kuwakumbusheni mambo fulaniambayo mmekwisha yajua: kumbukeni jinsiBwana alivyowaokoa watu wa Israeli nakuwatoa katika nchi ya Misri, lakini baadayealiwaangamiza wale ambao hawakuamini. 6

Na, malaika ambao hawakuridhika na cheochao, wakayaacha makao yao ya asili, Munguamewafunga gizani kwa minyororo ya milelewahukumiwe Siku ile kuu. 7 Kumbukeni piaSodoma na Gomora, na miji ya kandokandoyake; wenyeji wake walifanya kama walemalaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyokinyume cha maumbile, wakapewa hukumu yamoto wa milele, iwe onyo kwa watu wote. 8

Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. ndoto zaohuwaongoza katika kuichafua miili yaowenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu nakuvitukana viumbe vitukufu vya huko juu. 9

Hata Mikaeli, malaika mkuu, hakufanya hivyo.Katika ule ubishi kati yake na Ibilisiwaliobishana juu ya mwili wa Mose, Mikaelihakuthubutu kumhukumu Ibilisi kwa matusi;ila alisema: “Bwana mwenyewe na akukaripie.”10 Lakini watu hawa hutukana chochotewasichokielewa; mambo yaleyale wanayoyajuakwa silika kama vile wanyama wanayoyajuandiyo yanayowaangamiza. 11 Ole wao! Watuhao wamefuata mwenendo uleule wa Kaini.Kwa ajili ya fedha, wamejiingiza katika mkosiuleule wa Baalamu. Wameasi kama Koraalivyoasi na wameangamizwa kama yeyealivyoangamizwa. 12 Kwa makelele yao yasiyo

na adabu, watu hao ni kama madoa machafukatika mikutano yenu ya karamu ya Bwana.Hujipendelea wao wenyewe tu, na wako kamamawingu yanayopeperushwa huko na huko naupepo bila ya kuleta mvua. Wao ni kama mitiisiyozaa matunda hata wakati wa majira yake,wamekufa kabisa. 13 Watu hao ni kamamawimbi makali ya bahari, na matendo yao yaaibu yanaonekana dhahiri kama vile mapovuya mawimbi. Wao ni kama nyotazinazotangatanga, ambao Munguamewawekea mahali pao milele katika gizakuu. 14 Henoki, ambaye ni babu wa sabatangu Adamu, alibashiri hivi juu ya watu hawa:“Sikilizeni! Bwana atakuja pamoja na maelfu yamalaika wake watakatifu 15 kutoa hukumu juuya binadamu wote, kuwahukumu wote kwaajili ya matendo yao yote maovu waliyotendana kwa ajili ya maneno yote mabaya ambayowatu waovu walimkashifu nayo.” 16 Watuhawa wananung'unika daima na kuwalaumuwatu wengine. Hufuata tamaa zao mbaya,hujigamba na kuwasifu watu wengine mnokusudi wafaulu katika mipango yao. 17 Lakinininyi wapenzi wangu, kumbukeni yalemliyoambiwa hapo awali ni mitume wa Bwanawetu Yesu Kristo. 18 Waliwaambieni: “Siku zamwisho zitakapofika, watatokea watuwatakaowadhihaki ninyi, watu wafuatao tamaazao mbaya.” 19 Hao ndio watuwanaosababisha mafarakano, watuwanaotawaliwa na tamaa zao za kidunia, watuwasio na Roho wa Mungu. 20 Lakini ninyi,wapenzi wangu, endeleeni kujijenga kikamilifukatika imani yenu takatifu. Salini kwa nguvu yaRoho Mtakatifu, 21 na kubaki katika upendowa Mungu, mkiwa mnamngojea Bwana wetuYesu Kristo awapeni uzima wa milele kwahuruma yake. 22 Muwe na huruma kwa watuwalio na mashaka; 23 waokoeni kwakuwanyakua kutoka motoni; na kwa wenginemuwe na huruma pamoja na hofu, lakinichukieni hata mavazi yao ambayoyamechafuliwa na tamaa zao mbaya. 24 Kwakeyeye awezaye kuwalinda msije mkaanguka, nakuwaleta ninyi bila hatia mpaka mbele yautukufu wake, 25 kwake yeye aliye peke yakeMungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu,nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwanawetu, tangu zama zote, sasa na hata milele!Amina.

WARAKA WA YUDA 1:25

197

Page 198: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

1

2

UFUNUO WA YOHANA

Hizi ni habari za mambo ambayoyalifunuliwa na Yesu Kristo. Mungualimpa Kristo ufunuo huu ili

awaonyeshe watumishi wake mambo ambayoyanapaswa kutukia karibuni. Kristo alimtumamalaika wake amjulishe Yohane, mtumishiwake, mambo hayo, 2 naye Yohane,ameyasema yote aliyoyaona. Na hii ndiotaarifa yake kuhusu ujumbe wa Mungu naukweli uliofunuliwa na Yesu Kristo. 3 Heri yakemtu anayesoma kitabu hiki; heri yao walewanaosikiliza maneno ya ujumbe huu wakinabii na kushika yaliyoandikwa humu, maanawakati umekaribia ambapo mambo hayayatatukia. 4 Mimi Yohane nayaandikiamakanisa yaliyoko mkoani Asia. Nawatakienineema na amani kutoka kwake yeye aliyeko,aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa rohosaba walio mbele ya kiti chake cha enzi, 5 nakutoka kwa Yesu Kristo, shahidi mwaminifu,wa kwanza kufufuliwa kutoka wafu, na ambayeni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeyeanatupenda, na kwa damu yake ametufunguakutoka vifungo vya dhambi zetu, 6 akatufanyasisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikieMungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uweutukufu na nguvu, milele na milele! Amina. 7

Tazama! Anakuja katika mawingu! Kila mtuatamwona, hata wale waliomchoma. Makabilayote duniani yataomboleza juu yake. Naam!Amina. 8 “Mimi ni Alfa na Omega,” asemaBwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko,aliyekuwako na anayekuja. 9 Mimi ni Yohane,ndugu yenu; na kwa kuungana na Kristonashiriki pamoja nanyi katika kustahimilimateso yanayowapata wale walio wa Utawalawake. Mimi nilikuwa kisiwani Patmo kwasababu ya kuhubiri ujumbe wa Mungu naukweli wa Yesu. 10 Basi, wakati mmoja, siku yaBwana, nilikumbwa na Roho, nikasikia nyumayangu sauti kubwa kama sauti ya tarumbeta.11 Nayo ilisema, “Andika katika kitabu yoteunayoyaona, ukipeleke kwa makanisa hayasaba: Efeso, Smurna, Pergamoni, Thuatira,Sarde, Filadelfia na Laodikea.” 12 Basi,nikageuka nimwone huyo aliyesema nami,nikaona vinara vya taa saba vya dhahabu, 13

na katikati yake kulikuwa na kitu kama mtu,naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na ukandawa dhahabu kifuani. 14 Nywele zake zilikuwanyeupe kama pamba safi, kama theluji; machoyake yalimetameta kama moto; 15 miguu yakeiling'aa kama shaba iliyosafishwa katika tanuru

ya moto na kusuguliwa, na sauti yake ilikuwa,kama sauti ya poromoko la maji. 16 Katikamkono wake wa kulia, alikuwa na nyota saba,na kinywani mwake mlitoka upanga wenyemakali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali.17 Basi, nilipomwona tu, nilianguka mbele yamiguu yake kama maiti. Lakini yeye akawekamkono wake wa kulia juu yangu, akasema,“Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa mwisho.18 Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwa nimekufa,lakini, tazama, sasa ni mzima milele na milele.Ninazo funguo za kifo na Kuzimu. 19 Basi, sasaandika mambo haya unayoyaona, mamboyanayotukia sasa na yale yatakayotukiabaadaye. 20 Siri ya nyota zile saba ulizozionakatika mkono wangu wa kulia, na siri ya vilevinara saba vya taa hii: zile nyota saba nimalaika wa makanisa; na vile vinara saba vyataa ni makanisa saba.

“Kwa malaika wa kanisa la Efeso andikahivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwakeyeye ashikaye nyota saba katika mkono

wake wa kulia, na ambaye hutembea katikatiya vinara saba vya taa vya dhahabu. 2 Najuamambo yako yote; najua bidii yako nauvumilivu wako. Najua kwamba huwezikuwavumilia watu waovu, na kwambaumewapima wale wanaojisemea kuwa mitumena kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.3 Wewe unayo saburi, umestahimili taabunyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjikamoyo. 4 Lakini ninayo hoja moja juu yako:wewe hunipendi tena sasa kama pale awali. 5

Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla yakuanguka, ukayaache madhambi yako, nakufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo,naja kwako na kukiondoa kinara chako mahalipake. 6 Lakini nakusifu juu ya kitu kimoja:wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolaikama ninavyoyachukia mimi. 7 “Aliye namasikio, basi, na asikie yale Rohoanayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshindanitawapa haki ya kula matunda ya mti wauzima ulioko ndani ya bustani ya Mungu. 8

“Kwa malaika wa kanisa la Smurna andika hivi:“Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye wakwanza na wa mwisho, ambaye alikufa naakaishi tena. 9 Najua taabu zako; najua piaumaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe nitajiri; najua kashfa walizokufanyia walewanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi wakweli, bali ni kundi lake Shetani. 10 Usiogopehata kidogo yale ambayo itakulazimu

UFUNUO WA YOHANA 1:2

198

Page 199: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

3

kuteseka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribukwa kuwatia baadhi yenu gerezani; nanyimtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Muwewaaminifu hata mpaka kufa, nami nitawapenitaji ya uzima. 11 “Aliye na masikio, basi, naasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!“Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo chapili. 12 “Kwa malaika wa kanisa la Pergamoniandika hivi: “Huu ndio ujumbe wake yeye aliyena upanga mkali wenye kuwili. 13 Najuaunakoishi: Wewe unaishi kwenye makaomakuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jinalangu; hukuikana imani yako kwangu hata sikuzile Antipa shahidi wangu mwaminifu,alipouawa pale mahali anapoishi Shetani. 14

Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhiyenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundishaBalaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakulavilivyotambikiwa sanamu za kufanya uzinzi. 15

Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watuwanaofuata mafundisho ya Wanikolai. 16 Basi,achana na madhambi yako. La sivyo, nitakujakwako upesi na kupigana na watu hao kwaupanga utokao kinywani mwangu. 17 “Aliye namasikio, basi, na asikie yale Rohoanayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshindanitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa piajiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalohakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu walewanaolipokea. 18 “Kwa malaika wa kanisa laThuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe waMwana wa Mungu, ambaye macho yakeyametameta kama moto, na miguu yakeinang'aa kama shaba iliyosuguliwa. 19 Najuamambo yako yote. Najua upendo wako, imaniyako, utumishi wako na uvumilivu wako. Weweunafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali. 20

Lakini nina hoja moja juu yako: weweunamvumilia yule mwanamke Yezabelianayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundishana kuwapotosha watumishi wangu wafanyeuzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwasanamu. 21 Nimempa muda wa kutubudhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinziwake. 22 Sikiliza! Sasa namtupa kitandaniambapo yeye pamoja na wote waliofanyauzinzi naye watapatwa na mateso makali.Naam, nitafanya hivyo, kama wasipotubumatendo yao mabaya waliyotenda naye. 23

Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yoteyatambue kwamba mimi ndiyeninayechunguza mioyo na fikira za watu. 24

“Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatiraambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, naambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri yaShetani, nawaambieni kwamba sitawapenimzigo mwingine. 25 Lazima mzingatie yalemliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja. 26

“Wanaoshinda, na wale watakaozingatiampaka mwisho kutenda ninayotaka, nitawapamamlaka juu ya mataifa. 27 Naam, nitawapauwezo uleule nilioupokea kwa Baba: yaani,watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma na

kuyavunjavunja kama chombo cha udongo. 28

Tena nitawapa nyota ya asubuhi. 29 “Aliye namasikio, basi, na ayasikie yale Rohoanayoyaambia makanisa!

“Kwa malaika wa kanisa la Sarde andikahivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwakeyeye aliye na roho saba za Mungu na

nyota saba. Nayajua mambo yako yote; najuaunajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa! 2

Amka! Imarisha chochote chemakilichokubakia kabla nacho hakijatowekakabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaonamatendo yako kuwa ni makamilifu mbele yaMungu wangu. 3 Kumbuka, basi, yaleuliyofundishwa na jinsi ulivyoyasikia, uyatii naubadili nia yako mbaya. Usipokesha nitakujiaghafla kama mwizi, na wala hutaijua saanitakapokujia. 4 Lakini wako wachache hukoSarde ambao hawakuyachafua mavazi yao.Hao wanastahili kutembea pamoja namiwakiwa wamevaa mavazi meupe. 5 “Walewanaoshinda, watavikwa mavazi meupe kamahao. Nami sitayafuta majina yao kutoka katikakitabu cha uzima; tena nitawakiri kwamba niwangu mbele ya Baba yangu na mbele yamalaika wake. 6 “Aliye na masikio, basi, naayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa! 7

“Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andikahivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeyealiye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao uleufunguo wa Daudi, na ambaye hufungua nahakuna mtu awezaye kufungua. 8 Nayajuamambo yako yote! Sasa, nimefungua mbeleyako mlango ambao hakuna mtu awezayekuufunga; najua kwamba ingawa huna nguvusana, hata hivyo, umezishika amri zangu,umelitii neno langu wala hukulikana jina langu.9 Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundilake Shetani, watu ambao hujisema kuwa niWayahudi, kumbe ni wadanganyifu. Naam,nitawapeleka kwako na kuwafanya wapigemagoti mbele yako wapate kujua kwambakweli nakupenda wewe. 10 Kwa kuwa weweumezingatia agizo langu la kuwa na uvumilivu,nami pia nitakutegemeza salama wakati ule wadhiki inayoujia ulimwengu mzima kuwajaribuwote wanaoishi duniani. 11 Naja kwako upesi!Linda, basi, ulicho nacho sasa, ili usijeukanyang'anywa na mtu yeyote taji yako yaushindi. 12 “Wale wanaoshinda nitawafanyawawe minara katika Hekalu la Mungu wangu,na hawatatoka humo kamwe. Pia nitaandikajuu yao jina la Mungu wangu na jina la mji waMungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mjiambao utashuka kutoka juu mbinguni kwaMungu wangu. Tena nitaandika juu yao jinalangu jipya. 13 “Aliye na masikio, basi, naayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa! 14

“Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andikahivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeyeaitwaye Amina. Yeye ni shahidi mwaminifu nawa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyotealivyoumba Mungu. 15 Nayajua mambo yako

UFUNUO WA YOHANA 3:15

199

Page 200: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

4

5

yote! Najua kwamba wewe si baridi wala simoto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: baridiau moto. 16 Basi, kwa kuwa hali yako nivuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika!17 Wewe unajisema, Mimi ni tajiri;ninajitosheleza, sina haja ya kitu chochote.Kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge,unahitaji kuhurumiwa, maskini, kipofu tenauko uchi! 18 Nakushauri ununue kwangudhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwatajiri kweli. Tena afadhali ununue pia vazijeupe, uvae na kufunika aibu ya uchi wako.Nunua pia mafuta ukapake machoni pakoupate kuona. 19 Mimi ndiye mwenyekumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda.Kwa hiyo kaza moyo, achana na dhambi zako.20 Sikiliza! Mimi nasimama mlangoni nakubisha hodi. Mtu akisikia sauti yangu nakufungua mlango, nitaingia nyumbani kwakena kula chakula pamoja naye, naye atakulapamoja nami. 21 “Wale wanaoshindanitawaketisha pamoja nami juu ya kiti changucha enzi, kama vile mimi mwenyewenilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangujuu ya kiti chake cha enzi. 22 “Aliye na masikio,basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambiamakanisa!”

Baada ya hayo nilitazama nikaonamlango umefunguliwa mbinguni. Na ilesauti niliyoisikia pale awali ambayo

ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema,“Njoo hapa juu nami nitakuonyesha mamboyatakayotukia baadaye.” 2 Mara nikachukuliwana Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti chaenzi na juu yake ameketi mmoja. 3 Huyoaliyeketi juu yake alikuwa kama almasi na jiwezuri jekundu. Upinde wa mvua ulikuwaunang'aa kama zumaridi na ulikizunguka kiticha enzi pande zote. 4 Kulikuwa na duara laviti ishirini na vinne kukizunguka kiti cha enzi,na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wannewalikuwa wameketi wamevaa mavazi meupena taji za dhahabu vichwani. 5 Umeme, sautina ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hichokiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwazinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizoni roho saba za Mungu. 6 Mbele ya kiti chaenzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo,angavu kama jiwe linga'aalo sana. Katikapande zote za hicho kiti cha enzi nakukizunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne.Viumbe hivyo vilikuwa vimejaa macho mbelena nyuma. 7 Kiumbe cha kwanza kulikuwakama simba, cha pili kama ng'ombe, cha tatukilikuwa na sura kama mtu, na cha nnekilikuwa kama tai anayeruka. 8 Viumbe hivyovinne vilikuwa na mabawa sita kila kimoja, navilikuwa vimejaa macho, ndani na nje. Usiku namchana, bila kupumzika huimba: “Mtakatifu,mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, MunguMwenye Uwezo, aliyekuwako, aliyeko naanayekuja!” 9 Kila mara viumbe vinnevilipoimba nyimbo za kumtukuza,

kumheshimu na kumshukuru huyo aliyeketijuu ya kiti cha enzi, ambaye anaishi milele namilele, 10 wale wazee ishirini na wannehujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiticha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishimilele na milele; na huziweka taji zao mbele yakiti cha enzi wakisema: 11 “Wewe ni Bwana naMungu wetu, unastahili utukufu na heshimana nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote, nakwa matakwa yako kila kitu kimepewa uhai nauzima.”

Kisha katika mkono wa kulia wa huyoaliyeketi juu ya kiti cha enzi, nikaonakitabu; nacho kilikuwa kimeandikwa

ndani na nje na kufungwa na mihuri saba. 2

Tena nikamwona malaika mwenye nguvuakitangaza kwa sauti kubwa: “Nani anayestahilikuvunja hiyo mihuri na kukifungua kitabuhicho?” 3 Lakini hakupatikana mtu yeyotembinguni, wala duniani, wala chini Kuzimu,aliyeweza kukifungua hicho kitabu aukukitazama ndani. 4 Basi, mimi nikalia sanakwa sababu hakupatikana mtu aliyestahilikukifungua, au kukitazama ndani. 5 Kishammoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie!Tazama! Simba wa kabila la Yuda, mjukuumaarufu wa Daudi, ameshinda. Yeye anawezakuivunja mihuri yake saba na kukifungua hichokitabu.” 6 Kisha nikaona pale katikati ya kiticha enzi Mwana kondoo amesimama,akizungukwa kila upande na vile viumbe haivinne, na wale wazee. Huyo Mwanakondooalionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwana pembe saba na macho saba ambayo niroho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwakila mahali duniani. 7 Mwanakondoo akaenda,akakitwaa hicho kitabu kutoka mkono wa kuliawa yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi. 8 Mara tualipokwisha twaa hicho kitabu, vile viumbe haivinne pamoja na wale wazee ishirini na wannewalianguka kifudifudi mbele yaMwanakondoo. Kila mmoja, alikuwa na kinubina bakuli za dhahabu zilizojaa ubani, ambao nisala za watu wa Mungu. 9 Basi, wakaimbawimbo huu mpya: “Wewe unastahili kukitwaahicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwasababu wewe umechinjwa, na kwa damu yakoumemnunulia Mungu watu kutoka katika kilakabila, lugha, jamaa na taifa. 10 Weweumewafanya wawe ufalme wa makuhaniwamtumikie Mungu wetu nao watatawaladuniani.” 11 Kisha nikatazama, nikasikia sautiya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika,maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaakuzunguka kiti cha enzi, vile viumbe hai vinnena wale wazee; 12 wakasema kwa sauti kuu:“Mwanakondoo aliyechinjwa anastahilikupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu,utukufu na sifa.” 13 Nikasikia viumbe vyotembinguni, duniani, chini kuzimuni nabaharini—viumbe vyoteulimwenguni—vikisema: “Kwake yeye aketiyekatika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe

UFUNUO WA YOHANA 3:16

200

Page 201: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

6

7

sifa na heshima na utukufu na enzi milele namilele.” 14 Na vile viumbe vinne hai vikasema,“Amina!” Na wale wazee wakaangukakifudifudi, wakaabudu.

Kisha nikamwona Mwanakondooanavunja mhuri mmojawapo wa ilemihuri saba. Nikasikia kimoja cha vile

viumbe hai vinne kikisema kwa sauti kama yangurumo, “Njoo!” 2 Mimi nikatazama, nakumbe palikuwa na farasi mmoja mweupehapo. Na mpanda farasi wake alikuwa naupinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kamamshindi aendelee kushinda. 3 Kisha,Mwanakondoo akavunja mhuri wa pili.Nikamsikia yule kiumbe hai wa pili akisema,“Njoo!” 4 Nami nikatazama na kumbepalikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu.Mpanda farasi wake alikabidhiwa jukumu lakuondoa amani duniani, watu wauane,akapewa upanga mkubwa. 5 KishaMwanakondoo akavunja mhuri wa tatu.Nikamsikia yule kiumbe hai wa tatu akisema,“Njoo!” Nikatazama na kumbe palikuwapofarasi mmoja hapo, mweusi. Mpanda farasiwake alikuwa na vipimo viwili vya kupimiauzito mkononi mwake. 6 Nikasikia kitu kamasauti itokayo kwa vile viumbe hai vinne. Nayoilisema, “Kibaba kimoja cha unga wa ngano wakiasi cha fedha dinari moja, na vibaba vitatuvya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiharibumafuta wala divai!” 7 Kisha Mwanakondooakavunja mhuri wa nne. Nikamsikia yulekiumbe hai wa nne akisema, “Njoo!” 8 Naminikatazama, na kumbe alikuwapo farasi mmojahapo, rangi yake kijivu. Na jina la mpandafarasi wake lilikuwa kifo, na Kuzimu alimfuatanyuma. Hao walipewa mamlaka juu ya robomoja ya dunia, wawaue watu kwa upanga,njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.9 Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri watano. Nikaona pale chini ya madhabahu yakufukizia ubani roho za wale waliouawa kwasababu ya ujumbe wa Mungu, na kwa sababuya ushuhuda waliotoa. 10 Basi, wakalia kwasauti kubwa: “Ee Bwana, uliye mtakatifu namwaminifu, mpaka lini utakawia kulipiza kisasikwa wakazi wote wa dunia kwa ajili ya kuuawakwetu?” 11 Wakapewa kila mmoja vazi refujeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa mudamfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishiwenzao na ndugu ambao watawaua kama waowenyewe walivyouawa. 12 Kisha nikatazama,na wakati Mwanakondoo alipouvunja mhuriwa sita, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi;jua likawa jeusi kama gunia; mwezi woteukawa mwekundu kama damu; 13 nazo nyotaza mbingu zikaanguka juu ya ardhi kamamatunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyowakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali.14 Anga likatoweka kama vile karatasiinavyokunjwakunjwa; milima yote na visimavyote vikaondolewa mahali pake. 15 Kishawafalme wa duniani, wakuu, majemadari,

matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mtuhuru, wakajificha mapangoni na kwenyemajabali milimani. 16 Wakaiambia hiyo milimana hayo majabali, “Tuangukieni, mkatufichembali na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, nambali na ghadhabu ya Mwanakondoo! 17

Maana siku maalum ya ghadhabu yao imefika.Nani awezaye kuikabili?”

Baada ya hayo nikawaona malaikawanne wamesimama katika pembe nneza dunia wakishika pepo nne za dunia ili

upepo usivume hata kidogo: wala katika nchi,wala baharini, wala kwenye miti. 2 Kishanikamwona malaika mwingine akipanda juukutoka mashariki akiwa na mhuri wa Mungualiye hai. Akapaaza sauti na kuwaambia haomalaika wanne waliokabidhiwa jukumu lakuiharibu nchi na bahari, 3 “Msiharibu nchi,wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwishawapiga mhuri watumishi wa Mungu wetukatika paji la uso.” 4 Kisha nikasikia idadi yahao waliopigwa mhuri: Watu mia mojaarobaini na nne elfu wa makabila yote ya watuwa Israeli. 5 Kabila la Yuda walikuwa watukumi na mbili elfu; kabila la Reubeni, kumi nambili elfu, kabila la Gadi, kumi na mbili elfu; 6

Kabila la Asheri, kumi na mbili elfu; kabila laNaftali, kumi na mbili elfu; kabila la Manase,kumi na mbili elfu; 7 kabila la Simeoni, kumina mbili elfu, kabila la Lawi, kumi na mbili elfu,kabila la Isakari, kumi na mbili elfu; 8 kabila laZabuloni, kumi na mbili elfu; kabila la Yosefu,kumi na mbili elfu, na kabila la Benyamini,kumi na mbili elfu. 9 Kisha nikatazama,nikaona umati mkubwa wa watuwasiohesabika: watu wa kila taifa, ukoo, jamaana lugha. Nao walikuwa wamesimama mbeleya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo,wakiwa wamevaa mavazi meupe na kushikamatawi ya mitende mikononi mwao. 10

Wakapaaza sauti: “Ukombozi wetu watoka kwaMungu wetu aketiye juu ya kiti cha enzi, nakutoka kwa Mwanakondoo!” 11 Malaika wotewakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazeena vile viumbe hai vinne. Wakaangukakifudifudi mbele ya kiti cha enzi,wakamwabudu Mungu, 12 wakisema, “Amina!Sifa, utukufu, hekima, shukrani, heshima,uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu, milelena milele! Amina!” 13 Mmoja wa hao wazeeakaniuliza, “Hawa waliovaa mavazi meupe niwatu gani? Na wametoka wapi?” 14 Naminikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wajua!” Nayeakaniambia, “Hawa ni wale waliopita salamakatika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavaziyao katika damu ya Mwanakondoo, yakawameupe kabisa. 15 Ndiyo maana wako mbele yakiti cha enzi cha Mungu. Humtumikia Mungumchana na usiku katika Hekalu lake; nayeaketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hemalake juu yao kuwalinda. 16 Hawataona tenanjaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachomatena, 17 kwa sababu Mwanakondoo aliye

UFUNUO WA YOHANA 7:17

201

Page 202: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

8

9

katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungajiwao, naye atawaongoza kwenye chemchemi zamaji ya uzima. Naye Mungu atayafuta machoziyote machoni mwao.”

Na Mwanakondoo alipouvunja mhuriwa saba, kukawa kimya mbinguni kwamuda wa nusu saa. 2 Kisha nikawaona

wale malaika saba wanaosimama mbele yaMungu wamepewa tarumbeta saba. 3 Malaikamwingine akafika, akiwa anachukua chetezocha dhahabu, akasimama mbele yamadhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewaubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala zawatu wote wa Mungu, juu ya madhabahu yadhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4 Moshiwa ubani ukapanda juu, pamoja na sala zawatu wa Mungu, kutoka mikononi mwakehuyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu. 5

Kisha malaika akakichukua hicho chetezo,akakijaza moto wa madhabahuni akakitupaduniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umemena tetemeko la ardhi. 6 Kisha wale malaikasaba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayarikupiga mbiu ya mgambo. 7 Malaika wakwanza akapiga tarumbeta yake.Mchanganyiko wa mvua ya mawe na moto,pamoja na damu, ukamwagwa juu ya nchi.Theluthi moja ya nchi ikaungua, theluthi mojaya miti ikaungua, na majani yote mabichiyakaungua. 8 Malaika wa pili akapigatarumbeta yake. Na kitu kama mlima mkubwaunaowaka moto ukatupwa baharini. Theluthimoja ya bahari ikawa damu, 9 theluthi moja yaviumbe vya baharini vikafa na theluthi moja yameli zikaharibiwa. 10 Kisha malaika wa tatuakapiga tarumbeta yake. Na nyota kubwaikiwaka kama bonge la moto, ikaangukakutoka mbinguni, na kutua juu ya theluthimoja ya mito na chemchemi za maji. 11 (Nyotahiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja yamaji yakawa machungu; watu wengi wakafakutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeukakuwa machungu. 12 Kisha malaika wa nneakapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi mojaya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hatamwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng'aowake. Theluthi moja ya mchana ikakosamwanga, hali kadhalika na theluthi moja yausiku. 13 Kisha nikatazama, nikasikia taiakiruka juu kabisa angani anasema kwa sautikubwa, “Ole, ole, ole kwa wanaoishi dunianiwakati malaika watatu waliobaki watakapopigatarumbeta zao!”

Kisha malaika wa tano akapigatarumbeta yake. Nami nikaona nyotailiyokuwa imeanguka juu ya nchi kutoka

mbinguni. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo laKuzimu. 2 Basi, nyota hiyo ikafungua shimo laKuzimu, kukatoka moshi wa tanuru kubwa. Juana anga vikatiwa giza kwa moshi huo waKuzimu. 3 Nzige wakatoka katika moshi huo,wakaingia duniani wakapewa nguvu kama yang'e. 4 Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za

nchi wala majani wala miti yoyote, baliwawaharibu wale tu ambao hawakupigwamhuri wa Mungu katika paji la uso. 5 Nzigehao hawakuruhusiwa kuwaua watu, ilakuwatesa tu kwa muda wa miezi mitano.Maumivu watakayosababisha ni kamamaumivu yanayompata mtu wakatianapoumwa na ng'e. 6 Muda huo watuwatatafuta kifo lakini hawatakipata;watatamani kufa lakini kifo kitawakimbia. 7

Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kamafarasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu yavichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama zadhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama zabinadamu. 8 Nywele zao zilikuwa kama nyweleza wanawake, na meno yao yalikuwa kamameno ya simba. 9 Vifua vyao vilikuwavimefunikwa kitu kama ngao ya chuma. Sautiya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya msafarawa magari ya farasi wengi wanaokimbiliavitani. 10 Walikuwa na mikia na miiba kamang'e, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu yakuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.11 Tena wanaye mfalme anayewatawala, nayendiye malaika wa kuzimu; jina lake kwaKiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki niApolioni, yaani mwangamizi. 12 Maafa yakwanza yamepita; bado mengine mawiliyanafuata. 13 Kisha malaika wa sita akapigatarumbeta yake. Nami nikasikia sauti mojakutoka katika pembe nne za madhabahu yadhahabu iliyokuwa mbele ya Mungu. 14 Sautihiyo ikamwambia huyo malaika wa sitamwenye tarumbeta, “Wafungulie malaikawanne waliofungwa kwenye mto mkubwaEufrate!” 15 Naye akawafungulia malaika haowanne ambao walikuwa wametayarishwa kwaajili ya saa hiyo ya siku ya mwezi huo, wamwaka huohuo, kuua theluthi moja yawanaadamu. 16 Nilisikia idadi ya majeshiwapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili. 17

Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi nawapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwa nangao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenyerangi ya samawati na njano kama kiberiti.Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vyasimba; na moto, moshi, na kiberiti vilikuwavinatoka kinywani mwao. 18 Theluthi moja yawanaadamu waliuawa kwa mabaa hayomatatu yaani, moto, moshi na kiberiti,yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao; 19

maana nguvu ya farasi hao ilikuwa vinywanimwao na katika mikia yao. Mikia yao ilikuwa navichwa kama nyoka, na waliitumia hiyokuwadhuru watu. 20 Wanaadamu wenginewaliobaki ambao hawakuuawa na mabaahayo, hawakugeuka na kuviacha vituwalivyokuwa wametengeneza kwa mikono yaowenyewe; bali wakaendelea kuabudu pepo,sanamu za dhahabu, fedha, shaba, mawe namiti, vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikiawala kutembea. 21 Wala hawakutubu nakuacha kufanya mauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.

UFUNUO WA YOHANA 8:2

202

Page 203: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

10

11

12

Kisha nikamwona malaika mwinginemwenye nguvu akishuka kutokambinguni. Alikuwa amevikwa wingu,

na upinde wa mvua kichwani mwake. Usowake ulikuwa kama jua, na miguu yake ilikuwakama moto. 2 Mikononi mwake alishika kitabukidogo kimefunguliwa. Aliweka mguu wake wakulia juu ya bahari, na wa kushoto juu ya nchikavu, 3 na kuita kwa sauti kubwa kama yamngurumo wa simba. Alipopaaza sauti,ngurumo saba ziliitikia kwa kishindo. 4 Na hizongurumo saba ziliposema, mimi nikatakakuandika. Lakini nikasikia sauti kutokambinguni: “Maneno ya ngurumo hizo saba nisiri; usiyaandike!” 5 Kisha yule malaikaniliyemwona akisimama juu ya bahari na juuya nchi kavu akainua mkono wake wa kulia juumbinguni, 6 akaapa kwa jina la Mungu aishiyemilele na milele, Mungu aliyeumba mbingu navyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo,dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wakusubiri zaidi umekwisha! 7 Lakini wakati ulemalaika wa saba atakapotoa sauti yake, wakatiatakapopiga tarumbeta yake, Munguatakamilisha mpango wake wa siri kamaalivyowatangazia watumishi wake manabii.” 8

Kisha ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutokambinguni pale awali ikasema nami tena:“Nenda ukakichukue kile kitabukilichofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaikaasimamaye juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”9 Basi, nikamwendea huyo malaika,nikamwambia anipe hicho kitabu kidogo. Nayeakaniambia, “Kichukue, ukile; kinywani mwakokitakuwa kitamu kama asali, lakini tumbonikitakuwa kichungu!” 10 Basi, nikakichukuakitabu hicho kidogo kutoka mkononi mwahuyo malaika, nikakila; nacho kilikuwa kitamukinywani mwangu kama asali, lakininilipokimeza kikawa kichungu tumbonimwangu. 11 Kisha nikaambiwa, “Inakubiditena kutangaza ujumbe wa Mungu kuhusuwatu wengi, mataifa, watu wa lugha nyingi nawafalme!”

Kisha nikapewa mwanzi uliokuwakama kijiti cha kupimia, nikaambiwa,“Inuka, ukalipime Hekalu la Mungu,

madhabahu ya kufukizia ubani, naukawahesabu watu wanaoabudu ndani yaHekalu. 2 Lakini uache ukumbi ulio nje yaHekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwawatu wa mataifa mengine, ambaowataukanyanga mji Mtakatifu kwa muda wamiezi arobaini na miwili. 3 Nami nitawatumamashahidi wangu wawili ili watangaze ujumbewa Mungu kwa muda huo wa siku elfu mojamia mbili na sitini wakiwa wamevaa mavazi yamagunia.” 4 Hao mashahidi wawili ni mitimiwili ya Mizeituni na taa mbili zinazosimamambele ya Bwana wa dunia. 5 Kama mtuakijaribu kuwadhuru, moto hutoka kinywanimwao na kuwaangamiza adui zao; na kila mtuatakayejaribu kuwadhuru atakufa namna hiyo.

6 Hao wanayo mamlaka ya kufunga anga,mvua isinyeshe wakati wanapotangazaujumbe wa Mungu. Tena wanayo mamlaka yakuzigeuza chemchemi zote za maji ziwe damu,na ya kusababisha maafa ya kila namnaduniani kila mara wapendavyo. 7 Lakiniwakisha maliza kutangaza ujumbe huo,mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigananao, atawashinda na kuwaua. 8 Maiti zaozitabaki katika barabara za mji mkuu ambapoBwana wao alisulubiwa; jina la kupanga la mjihuo ni Sodoma au Misri. 9 Watu wa kila kabila,lugha, taifa na rangi wataziangalia maiti hizokwa muda wa siku tatu na nusu, nahawataruhusu zizikwe. 10 Watu waishioduniani watafurahia kifo cha hao wawili.Watafanya sherehe na kupelekeana zawadimaana manabii hawa wawili walikuwawamewasumbua mno watu wa dunia. 11

Lakini baada ya zile siku tatu na nusu pumzi yauhai kutoka kwa Mungu iliwaingia, naowakasimama; wote waliowaona wakaingiwa nahofu kuu. 12 Kisha hao manabii wawiliwakasikia sauti kubwa kutoka mbinguniikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapandajuu mbinguni katika wingu, maadui waowakiwa wanawatazama. 13 Wakati huohuo,kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemumoja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu elfusaba wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi.Watu waliosalia wakaogopa sana,wakamtukuza Mungu wa mbinguni. 14 Maafaya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatuyanafuata hima. 15 Kisha malaika wa sabaakapiga tarumbeta yake. Na sauti kuuzikasikika mbinguni zikisema, “Sasa utawalajuu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristowake. Naye atatawala milele na milele!” 16

Kisha wale wazee ishirini na wanne walioketimbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi,wakaanguka kifudifudi, wakamwabuduMungu, 17 wakisema: “Bwana Mungu Mwenyeuwezo, uliyeko na uliyekuwako!Tunakushukuru, maana umetumia nguvu yakokuu ukaanza kutawala! 18 Watu wa mataifawaliwaka hasira, maana wakati wa ghadhabuyako umefika, wakati wa kuwahukumu wafu.Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wakomanabii, watu wako na wote wanaolitukuzajina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wakuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia.”19 Hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa,na Sanduku la Agano lake likaonekanaHekaluni mwake. Kisha kukatokea umeme,sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvuakubwa ya mawe.

Kisha ishara kubwa ikaonekanambinguni. Palikuwa hapo mwanamkealiyevikwa jua, na mwezi chini ya

miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juuya kichwa chake! 2 Alikuwa mja mzito, naakapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wakujifungua mtoto. 3 Ishara nyingine ikatokea

UFUNUO WA YOHANA 12:3

203

Page 204: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

13

mbinguni: joka kubwa jekundu na lenyepembe kumi na vichwa saba; na kila kichwakilikuwa na taji. 4 Joka hilo liliburuta kwa mkiawake theluthi moja ya nyota za anga nakuzitupa duniani. Nalo lilisimama mbele yahuyo mama aliyekuwa karibu kujifunguamtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tuatakapozaliwa. 5 Kisha mama huyoakajifungua mtoto wa kiume, ambayeatayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma.Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwaMungu na kwenye kiti chake cha enzi. 6 Huyomama akakimbilia jangwani, ambako Mungualikuwa amemtayarishia mahali pa usalamaambapo angehifadhiwa kwa muda wa siku elfumoja mia mbili na sitini. 7 Kisha kukazuka vitambinguni: Mikaeli na malaika wake walipiganana hilo joka, nalo likawashambulia pamoja namalaika wake. 8 Lakini joka hilo halikuwezakuwashinda, na hatimaye hapakuwa tena nanafasi mbinguni kwa ajili yake na malaikawake. 9 Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Jokahilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwapia Ibilisi au Shetani. Ndiye anayeudanganyaulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, namalaika wake wote pamoja naye. 10 Kishanikasikia sauti kubwa kutoka mbinguniikisema: “Sasa ukombozi utokao kwa Munguumefika! Nguvu na Utawala wa Mungu wetuumedhihirika. Na Kristo wake ameonyeshamamlaka yake! Maana yule mdhalimu wandugu zetu, aliyesimama mbele ya Munguakiwashtaki usiku na mchana, sasa ametupwanje. 11 Ndugu zetu wameshinda kwa damu yaMwanakondoo na kwa nguvu ya ukweliwalioutangaza; maana hawakuyathaminimaisha yao kuwa kitu sana, wakawa tayarikufa. 12 Kwa sababu hiyo, furahini enyimbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini,ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisiamewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwasababu anajua kwamba siku zake zilizobakia nichache.” 13 Joka lilipotambua kwambalimetupwa chini duniani, likaanza kumwindayule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wakiume. 14 Lakini mama huyo akapewamabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sanana hilo joka, mpaka mahali, pake jangwaniambapo angehifadhiwa salama kwa muda wamiaka mitatu na nusu. 15 Basi, joka likatapikamaji mengi kama mto, yakamfuata huyomama nyuma ili yamchukue. 16 Lakini nchiikamsaidia huyo mama: ikajifunua kamamdomo na kuyameza maji hayo yaliyotokakinywani mwa hilo joka. 17 Basi, joka hilolikamkasirikia huyo mama, likajiondokea,likaenda kupigana na wazawa wengine wahuyo mama, yaani wote wanaotii amri zaMungu na kuuzingatia ukweli wa Yesu.

(G12-18) Na likajisimamia ukingonimwa bahari. (G13-1) Kisha nikaonamnyama mmoja akitoka baharini.

Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na

kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfalilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo. 2

Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui;miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na kinywachake kama cha simba. Lile joka likampa huyomnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi nauwezo mkuu. 3 Kichwa kimojawapo cha huyomnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwavibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwalimepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyomnyama na kumfuata. 4 Watu wotewakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyomnyama uwezo wake. Wakamwabudu piahuyo mnyama wakisema, “Nani aliye kamahuyu mnyama? Ni nani awezaye kupigananaye?” 5 Kisha huyo mnyama akaruhusiwakusema maneno ya kujigamba na kumkufuruMungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwamuda wa miezi arobaini na miwili. 6 Basi,akaanza kumtukana Mungu, kulitukana jinalake, makao yake, na wote wakaao mbinguni.7 Aliruhusiwa kuwapiga vita na kuwashindawatu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu ya watuwa kila kabila, ukoo, lugha na taifa. 8 Wotewaishio duniani watamwabudu isipokuwa tuwale ambao majina yao yameandikwa tangumwanzo wa ulimwengu katika kitabu chauzima cha Mwanakondoo aliyechinjwa. 9 “Aliyena masikio, na asikie! 10 Waliokusudiwakuchukuliwa mateka lazima watatekwa;waliokusudiwa kuuawa kwa upanga lazimawatauawa kwa upanga. Kutokana na hayo nilazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu naimani.” 11 Kisha nikamwona mnyamamwingine anatoka ardhini. Alikuwa na pembembili kama pembe za kondoo, na aliongeakama joka. 12 Alikuwa na mamlaka kamilikutoka kwa yule mnyama wa kwanza, naakautumia uwezo huo mbele ya huyomnyama. Akailazimisha dunia yote na wotewaliomo humo kumwabudu huyo mnyama wakwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifolililokuwa limepona. 13 Basi, huyu mnyama wapili akafanya miujiza mikubwa hataakasababisha moto kutoka mbinguni ushukeduniani mbele ya watu. 14 Aliwapotoshawakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwakutenda mbele ya mnyama wa kwanza.Aliwaambia wakazi wa dunia watengenezesanamu kwa heshima ya yule mnyamaaliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakiniakaishi tena. 15 Kisha alijaliwa kuipulizia uhaihiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hataikaweza kuongea na kuwaua watu woteambao hawakuiabudu. 16 Aliwalazimishawote, wadogo na wakubwa, matajiri namaskini, watu huru na watumwa, watiwealama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya pajiza nyuso zao. 17 Akapiga marufuku mtuyeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tumtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yulemnyama au tarakimu ya jina hilo. 18 Hapa nilazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza

UFUNUO WA YOHANA 12:4

204

Page 205: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

14

15

kufafanua maana ya tarakimu ya mnyamahuyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtufulani. Tarakimu hiyo ni mia sita sitini na sita.

Kisha nikaona mlima Sioni, naMwanakondoo amesimama juu yake;pamoja naye walikuwa watu mia moja

arobaini na nne elfu ambao juu ya paji zanyuso zao walikuwa wameandikwa jina laMwanakondoo na jina la Baba yake. 2 Basi,nikasikia sauti kutoka mbinguni, sautiiliyokuwa kama sauti ya maji mengi na kamasauti ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikiailikuwa kama sauti ya wachezaji muzikiwakipiga vinubi vyao. 3 Walikuwa wanaimbawimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbeleya wale viumbe hai wanne na wale wazee.Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huoisipokuwa hao watu mia moja arobaini na nneelfu waliokombolewa duniani. 4 Watu hao ndiowale waliojiweka safi kwa kutoonana kimwilina wanawake, nao ni mabikira. Wao humfuataMwanakondoo kokote aendako.Wamekombolewa kutoka miongoni mwabinadamu wengine, wakawa wa kwanzakutolewa kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.5 Hawakupata kamwe kuwa waongo; hawanahatia yoyote. 6 Kisha nikamwona malaikamwingine anaruka juu angani akiwa na HabariNjema ya milele ya Mungu, aitangaze kwawatu wote waishio duniani, kwa mataifa yote,makabila yote, watu wa lugha zote na rangizote. 7 Akasema kwa sauti kubwa, “McheniMungu na kumtukuza! Maana saa imefika yakutoa hukumu yake. Mwabuduni yeyealiyeumba mbingu na nchi, bahari nachemchemi za maji.” 8 Malaika wa pilialimfuata huyo wa kwanza akisema,“Ameanguka! Naam, Babuloni mkuuameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifayote wainywe divai yake—divai kali ya uzinziwake!” 9 Na malaika wa tatu aliwafuata haowawili akisema kwa sauti kubwa, “Yeyoteanayemwabudu yule mnyama na sanamu yakena kukubali kutiwa alama yake juu ya paji lauso wake au juu ya mkono wake, 10 yeyemwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu yaMungu, ambayo imemiminwa katika kikombecha ghadhabu yake bila kuchanganywa namaji. Mtu huyo atateseka ndani ya moto nakiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbeleya Mwanakondoo. 11 Moshi wa motounaowatesa kupanda juu milele na milele.Watu hao waliomwabudu huyo mnyama nasanamu yake, na kutiwa alama ya jina lake,hawatakuwa na nafuu yoyote usiku namchana.” 12 Kutokana na hayo, ni lazima watuwa Mungu, yaani watu wanaotii amri yaMungu na kumwamini Yesu, wawe nauvumilivu. 13 Kisha nikasikia sauti kutokambinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambaotangu sasa wanakufa wakiwa wameungana naBwana.” Naye Roho asema, “Naam!Watapumzika kutoka taabu zao; maana

matunda ya jasho lao yatawafuata.” 14 Kishanikatazama, na kumbe palikuwapo wingujeupe hapo. Na juu ya wingu hilo kulikuwa nakiumbe kama mtu. Alikuwa amevaa taji yadhahabu kichwani, na kushika mundumkononi mwake. 15 Kisha malaika mwingineakatoka Hekaluni, na kwa sauti kubwaakamwambia yule aliyekuwa amekaa juu yawingu, “Tafadhali, tumia mundu wako ukavunemavuno, maana wakati wa mavuno umefika;mavuno ya dunia yameiva.” 16 Basi, yulealiyekuwa amekaa juu ya wingu akautupamundu wake duniani, na mavuno ya duniayakavunwa. 17 Kisha malaika mwingineakatoka katika Hekalu mbinguni akiwa namundu wenye makali. 18 Kisha malaikamwingine msimamizi wa moto, akatokamadhabahuni akamwambia kwa sauti kubwayule malaika mwenye mundu wenye makali,“Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakatevichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibuzake zimeiva!” 19 Basi, malaika huyo akautupamundu wake duniani, akakata zabibu za dunia,akazitia ndani ya chombo kikubwa chakukamulia zabibu, chombo cha ghadhabu yaMungu. 20 Zabibu zikakamuliwa ndani ya hiloshinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatokakatika shinikizo hilo mtiririko mrefu kiasi chamita mia tatu na kina chake kiasi cha mita miambili.

Kisha nikaona ishara nyinginembinguni, kubwa na ya kushangaza.Palikuwa hapo malaika saba wenye

mabaa makubwa saba ya mwisho. Kwa mabaahayo makubwa saba, ghadhabu ya Munguimekamilishwa. 2 Kisha nikaona kitu kamabahari ya kioo, imechanganywa na moto.Nikawaona pia wale watu waliomshinda yulemnyama na sanamu yake na ambaye jina lakelilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwawamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo,wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu. 3

Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishiwa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo:“Bwana Mungu Mwenye Uwezo, matendo yakoni makuu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njiazako ni za haki na za kweli! 4 Bwana, ni naniasiyekucha wewe? Nani asiyelitukuza jina lako?Wewe peke yako ni Mtakatifu. Mataifa yoteyatakujia na kukuabudu maana matendo yakoya haki yameonekana na wote.” 5 Baada yahayo nikaona Hekalu limefunguliwa mbinguni,na ndani yake hema ionyeshayo kuwapo kwaMungu. 6 Basi, wale malaika saba wenyemabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwawamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa, nakanda za dhahabu vifuani mwao. 7 Kisha,mmojawapo wa vile viumbe vinne akawapahao malaika saba mabakuli ya dhahabuyaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milelena milele. 8 Hekalu likajaa moshiuliosababishwa na utukufu na nguvu yaMungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia

UFUNUO WA YOHANA 15:8

205

Page 206: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

16

17

Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwasaba ya wale malaika saba.

Kisha nikasikia sauti kubwa kutokaHekaluni ikiwaambia wale malaikasaba, “Nendeni mkamwage mabakuli

hayo saba ya ghadhabu ya Mungu duniani.” 2

Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwagabakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabayana ya kuumiza sana yakawapata wotewaliokuwa na alama ya yule mnyama, na walewalioiabudu sanamu yake. 3 Kisha malaika wapili akamwaga bakuli lake baharini. Nayobahari ikawa damu tupu kama damu ya mtualiyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa.4 Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katikamito na chemchemi za maji, navyo vikageukadamu. 5 Nikamsikia malaika msimamizi wamaji akisema, “Ewe mtakatifu, Uliyeko nauliyekuwako! Wewe ni mwenye haki katikahukumu hii uliyotoa. 6 Maana waliimwagadamu ya watu wako na ya manabii, naweumewapa damu wainywe; wamestahili hivyo!”7 Kisha nikasikia sauti madhabahuni ikisema,“Naam, Bwana Mungu Mwenye Uwezo!Hukumu zako ni za kweli na haki!” 8 Kishamalaika wa nne akamwaga bakuli lake juu yajua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watukwa moto wake. 9 Basi, watu wakaunguzwavibaya sana; wakamtukana Mungu aliye nauwezo juu ya mabaa hayo makubwa. Lakinihawakuziacha dhambi zao na kumtukuzaMungu. 10 Kisha malaika wa tano akamwagabakuli lake juu ya makao makuu ya yulemnyama. Giza likauvamia utawala wake, watuwakauma ndimi zao kwa sababu za maumivu,11 wakamtukana Mungu wa mbinguni kwasababu ya maumivu yao na madonda yao.Lakini hawakuyaacha matendo yao mabaya. 12

Kisha malaika wa sita akamwaga bakuli lakejuu ya mto mkubwa uitwao Eufrate. Maji yakeyakakauka, na hivyo njia ilitengenezwa kwa ajiliya wafalme wa mashariki. 13 Kisha nikaonapepo wabaya watatu walio kama vyura,wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywanimwa yule mnyama, na kinywani mwa yulenabii wa uongo. 14 Hawa ndio roho za pepowafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwawafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanyapamoja kwa ajili ya vita kuu Siku ile ya MunguMwenye Uwezo. 15 “Sikiliza! Mimi naja kamamwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaa nguo zakeili asije akaenda uchi huko na huko mbele yawatu.” 16 Basi, roho hao wakawakusanya haowafalme mahali paitwapo kwa KiebraniaHarmagedoni. 17 Kisha malaika wa sabaakamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwaikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, Hekaluni,ikisema, “Mwisho umefika!” 18 Kukatokeaumeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwala ardhi ambalo halijapata kutokea tanguMungu alipomuumba mtu. 19 Mji ule mkuuukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifaikateketea. Babuloni, mji mkuu,

haukusahauliwa na Mungu. Aliunyweshakikombe cha divai ya ghadhabu yake kuu. 20

Visiwa vyote vikatoweka, nayo milimahaikuonekena tena. 21 Mvua ya mawemakubwa yenye uzito wa kama kilo hamsinikila moja, ikawanyeshea watu. Naowakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigoya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvuahiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno.

Mmoja wa wale malaika sabawaliokuwa na bakuli akaja,akaniambia, “Njoo, mimi

nitakuonyesha adhabu aliyopewa yule mzinzimkuu, mji ule uliojengwa juu ya maji mengi. 2

Wafalme wa dunia wamefanya uzinzi pamojanaye; na wakazi wa dunia wamelewa divai yauzinzi wake.” 3 Kisha, Roho akanikumba,akaniongoza mpaka jangwani. Hukonikamwona mwanamke ameketi juu yamnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwaameandikwa kila mahali majina ya makufuru;alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. 4

Mwanamke huyo alikuwa amevaa vazi la rangiya zambarau na nyekundu; alikuwaamejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamanina lulu. Mkononi mwake alishika kikombe chadhahabu ambacho kilikuwa kimejaamachukizo na mambo machafuyanayoonyesha uzinzi wake. 5 Alikuwaameandikwa juu ya paji la uso wake jina lafumbo “Babuloni mkuu, mama wa wazinzi nawa mambo yote ya kuchukiza sana duniani.” 6

Nikamwona huyo mwanamke amelewa damuya watu wa Mungu, na damu ya watuwaliouawa kwa sababu ya kumtangaza Yesu.Nilipomwona nilishangaa mno. 7 Lakinimalaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa?Mimi nitakuambia maana iliyofichika yamwanamke huyu na mnyama huyoamchukuaye ambaye ana vichwa saba napembe kumi. 8 Huyo mnyama uliyemwonaalikuwa hai hapo awali, lakini sasa amekufa.Hata hivyo, karibu sana atapanda kutokashimoni kuzimu, lakini ataangamizwa.Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watuwote ambao majina yao hayakupatakuandikwa katika kitabu cha uzima tangumwanzo wa ulimwengu, watashangaakumwona huyo mnyama ambaye hapo awali,aliishi, kisha akafa na sasa anatokea tena! 9

“Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwasaba ni vilima saba, na huyo mwanamkeanaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalmesaba. 10 Kati ya hao wafalme saba, watanowamekwisha angamia, mmoja anatawalabado, na yule mwingine bado hajafika; naatakapofika atabaki kwa muda mfupi. 11 Huyomnyama ambaye alikuwa anaishi hapo awalilakini sasa haishi tena ni mfalme wa nane,naye pia ni miongoni mwa hao saba, naanakwenda zake kuharibiwa. 12 “Zile pembekumi ulizoziona ni wafalme ambao badohawajaanza kutawala. Lakini watapewa

UFUNUO WA YOHANA 16:2

206

Page 207: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

18

19

mamlaka ya kutawala kwa muda wa saa mojapamoja na yule mnyama. 13 Shabaha ya hawakumi ni moja, na watampa yule mnyamanguvu na mamlaka yao yote. 14 Watapiganana Mwanakondoo, lakini Mwanakondoopamoja na wale aliowaita na kuwachagua,ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababuyeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wawafalme.” 15 Malaika akaniambia pia, “Yalemaji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi, nimataifa, watu wa kila rangi na lugha. 16

Pembe zile kumi ulizoziona na yule mnyamawatamchukia huyo mzinzi. Watachukua kilakitu alicho nacho na kumwacha uchi; watakulanyama yake na kumteketeza kwa moto. 17

Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia yakutekeleza shabaha yake, yaani kwakukubaliana wao kwa wao na kumpa huyomnyama mamlaka yao ya kutawala, mpakahapo neno la Mungu litakapotimia. 18 “Na yulemwanamke uliyemwona ndio ule mji mkuuunaowatawala wafalme wa dunia.”

Baada ya hayo, nilimwona malaikamwingine akishuka kutoka mbinguni.Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia

ikamulikwa na mng'ao wake. 2 Basi, akapaazasauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka;Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwamakao ya mashetani na pepo wachafu;umekuwa makao ya ndege wachafu na wakuchukiza mno. 3 Maana mataifa yoteyalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, naowafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye.Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirikakutokana na anasa zake zisizo na kipimo.” 4

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguniikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ilimsishirikiane naye katika dhambi zake, msijemkaipata adhabu yake. 5 Kwa maana dhambizake zimekuwa nyingi mno, zimelundikanampaka mbinguni, na Mungu ameyakumbukamaovu yake. 6 Mtendeeni kamaalivyowatendea ninyi; mlipeni mara mbili kwayale aliyoyatenda. Jazeni kikombe chake kwakinywaji kikali mara mbili zaidi ya kilealichowapeni. 7 Mpeni mateso na uchungukadiri ya kujigamba kwake, na kuishi kwakekwa anasa. Maana anajisemea moyoni:Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane,wala sitapatwa na uchungu! 8 Kwa sababuhiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja:ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto,maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu niMwenye Uwezo.” 9 Wafalme wa Duniawaliofanya uzinzi naye na kuishi naye maishaya anasa wataomboleza na kulia wakatiwatakapoona moshi wa mji huo unaoteketea.10 Wanasimama kwa mbali kwa sababu yakuogopa mateso yake, na kusema, “Ole! Olekwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu!Kwa muda wa saa moja tu adhabu yakoimekupata.” 11 Wafanyabiashara wa duniawatalia na kumfanyia matanga, maana hakuna

mtu anayenunua tena bidhaa zao; 12 hakunatena wa kununua dhahabu yao, fedha, maweya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi yazambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombovya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vyapembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa,vya shaba, chuma na marmari; 13 mdalasini,viungo, ubani, manemane, udi, divai, mafuta,unga na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi namagari ya kukokotwa, watumwa wao na hatamaisha ya watu. 14 Wafanyabiasharawanamwambia: “Faida yote uliyotazamiaimetoweka, na utajiri na faharivimekuponyoka; hutaweza kuvipata tena!” 15

Wafanya biashara waliotajirika kutokana na mjihuo, watasimama mbali kwa sababu ya hofuya mateso yake, watalalamika na kuomboleza,16 wakisema, “Ole! Ole kwa mji huu mkuu.Ulizoea kuvalia nguo za kitani, za rangi yazambarau na nyekundu, na kujipamba kwadhahabu, mawe ya thamani na lulu! 17 Kwasaa moja tu utajiri wako umetoweka!” Halafumanahodha wote na wasafiri wao, wanamajina wote wanaofanya kazi baharini, walisimamakwa mbali, 18 na walipouona moshi wa motoule uliouteketeza, wakalia kwa sauti:“Hakujapata kuwako mji kama mji huu mkuu!”19 Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyaowakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Olekwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenyemeli zisafirizo baharini walitajirika kutokana nautajiri wake. Kwa muda wa saa moja tuumepoteza kila kitu!” 20 Furahi ee mbingu,kwa sababu ya uharibifu wake. Furahini watuwa Mungu, mitume na manabii! Kwa maanaMungu ameuhukumu kwa sababu ya mambouliyowatenda ninyi! 21 Kisha malaika mmojamwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wajiwe kubwa la kusagia, akalitupa bahariniakisema, “Ndivyo, Babuloni atakavyotupwa nakupotea kabisa. 22 Sauti za vinubi za muziki,sauti za wapiga filimbi na tarumbetahazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wanamna yoyote ile atakayepatikana tena ndaniyako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikikatena ndani yako. 23 Mwanga wa taahautaonekana tena ndani yako; sauti za bwanaarusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako.Wafanyabiashara wako walikuwa wakuuduniani, na kwa uchawi wako mataifa yoteyalipotoshwa!” 24 Mji huo uliadhibiwa kwanihumo mlipatikana damu ya manabii, damu yawatu wa Mungu na damu ya watu wotewaliouawa duniani.

Baada ya hayo nikasikia kitu kamasauti kubwa ya umati wa watu wengimbinguni ikisema, “Haleluya!

Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yakeMungu wetu! 2 Maana hukumu yake ni yakweli na ya haki. Amemhukumu yule mzinzimkuu ambaye alikuwa ameipotosha dunia kwauzinzi wake. Amemwadhibu kwa sababu yakumwaga damu ya watumishi wake!” 3

UFUNUO WA YOHANA 19:3

207

Page 208: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

20

Wakasema, “Asifiwe Mungu! Moshi wa motounaoteketeza mji huo utapanda juu milele namilele!” 4 Na wale wazee ishirini na wanne, navile viumbe hai vinne, wakajitupa chini,wakamwabudu Mungu aliyeketi juu ya kiti chaenzi wakisema, “Amina! Asifiwe Mungu!” 5

Kisha kukatokea sauti kwenye kiti cha enzi:“Msifuni Mungu enyi watumishi wake wote,nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.” 6

Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umatimkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na yangurumo kubwa, ikisema, “Haleluya! MaanaBwana Mungu wetu Mwenye Uwezo niMfalme! 7 Tufurahi na kushangilia; tumtukuze,kwani wakati wa arusi ya Mwanakondooumefika, na bibi arusi yuko tayari. 8 Amepewauwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi,iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo yakitani safi ni matendo mema ya watu waMungu.) 9 Kisha malaika akaniambia, “Andikahaya: Heri wale walioalikwa kwenye karamu yaarusi ya Mwanakondoo!” Tena akaniambia,“Hayo ni maneno ya kweli ya Mungu.” 10 Basi,mimi nikaanguka kifudifudi mbele ya miguuyake nikataka kumwabudu. Lakini yeyeakaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kamawewe na ndugu zako; sote tunauzingatiaukweli ule alioufunua Yesu. Mwabudu Mungu!Maana ukweli alioufunua Yesu ndiounaowaangazia manabii.” 11 Kisha nikaonambingu zimefunguliwa; na huko alikuwakofarasi mmoja mweupe, na mpanda farasi wakealiitwa “Mwaminifu” na “Kweli”. Huyohuhukumu na kupigana kwa ajili ya haki. 12

Macho yake ni kama mwali wa moto, naalikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwaameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuayeisipokuwa tu yeye mwenyewe. 13 Alikuwaamevaa vazi lililokuwa limelowekwa katikadamu. Na jina lake huyo ni “Neno la Mungu.”14 Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwayamepanda farasi weupe na walikuwawamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi. 15

Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwaupanga huo atawashinda mataifa. Yeye ndiyeatakayetawala kwa fimbo ya chuma nakuikamua divai katika chombo cha kukamuliazabibu za ghadhabu kuu ya Mungu MwenyeUwezo. 16 Juu ya vazi lake, na juu ya mguuwake, alikuwa ameandikwa jina: “Mfalme wawafalme na Bwana wa mabwana.” 17 Kishanikamwona malaika mmoja amesimama katikajua. Akapaaza sauti na kuwaambia ndege wotewaliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni!Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu yaMungu. 18 Njoni mkaitafune miili ya wafalme,ya majemadari, ya watu wenye nguvu, yafarasi na wapanda farasi wao; njonimkaitafune miili ya watu wote: walio huru nawatumwa, wadogo na wakubwa.” 19 Kishanikaona yule mnyama pamoja na mfalme wadunia na askari wao wamekusanyika pamojakusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi

juu ya farasi, pamoja na jeshi lake. 20 Lakinihuyo mnyama akachukuliwa mateka, pamojana nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujizambele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwaamewapotosha wale waliokuwa na chapa yahuyo mnyama, na ambao walikuwawameiabudu sanamu yake.) Huyo mnyamapamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili,wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwalinalowaka moto wa kiberiti. 21 Majeshi yaoyaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwayule anayepanda farasi. Ndege wotewakajishibisha kwa nyama zao.

Kisha nikamwona malaika mmojaanashuka kutoka mbinguni akiwa naufunguo wa kuzimu na mnyororo

mkubwa mkononi mwake. 2 Akalikamata lilejoka—nyoka wa kale, yaani Ibilisi auShetani—akalifunga kwa muda wa miaka elfumoja. 3 Malaika akalitupa Kuzimu, akaufungamlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ililisiweze tena kuyapotosha mataifa mpakahapo miaka elfu moja itakapotimia. Lakinibaada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena,lakini kwa muda mfupi tu. 4 Kisha nikaona vitivya enzi na watu walioketi juu yake; watu haowalipewa mamlaka ya hukumu. Niliona piaroho za wale waliokuwa wamenyongwa kwasababu ya kumtangaza Yesu na kwa sababu yaneno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yulemnyama na sanamu yake, wala hawakupigwaalama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu yamikono yao. Walipata tena uhai, wakatawalapamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfumoja. 5 (Wale wengine waliokufa hawakupatauhai mpaka miaka elfu moja itimie.) Huu ndioufufuo wa kwanza. 6 Wameneemeka sana,tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wakwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juuyao; watakuwa makuhani wa Mungu na waKristo, na watatawala pamoja naye kwa miakaelfu moja. 7 Wakati miaka elfu mia mojaitakapotimia, Shetani atafunguliwa kutokagerezani mwake. 8 Basi, atatoka nje, ataanzakuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kilamahali duniani, yaani Gogu na Magogu.Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita;nao watakuwa wengi kama mchanga wapwani. 9 Walitawanyika katika nchi yote,wakaizunguka kambi ya watu wa Mungu namji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishukakutoka mbinguni, ukawaangamiza. 10 Ibilisi,aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani yaziwa linalowaka moto wa kiberiti, walimo yulemnyama na yule nabii wa uongo, naowatateswa mchana na usiku, milele na milele.11 Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe,na yule aketiye juu yake. Dunia na mbinguvikatoweka mbele ya macho yake, nahavikuonekana tena. 12 Kisha nikawaona watuwakubwa na wadogo, wamesimama mbele yakiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafukitabu kingine, yaani kitabu cha uzima,

UFUNUO WA YOHANA 19:4

208

Page 209: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

21

22

kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiriya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani yavitabu hivyo. 13 Bahari ikawatoa nje wafuwaliokuwa ndani yake; kifo na kuzimuvikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao. Kilammoja akahukumiwa kufuatana na matendoyake. 14 Kisha kifo na kuzimu vikatupwa ndaniya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifocha pili. 15 Mtu yeyote ambaye jina lakehalikupatikana limeandikwa katika kitabu chauzima, alitupwa katika ziwa la moto.

Kisha nikaona mbingu mpya na duniampya. Mbingu ile ya kwanza na duniaile ya kwanza vilikuwa vimetoweka,

nayo bahari pia haikuweko tena. 2 Nikaona mjimtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutokakwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwavizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayarikukutana na mumewe. 3 Kisha nikasikia sautikubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema,“Tazama! Mungu amefanya makao yake kati yawatu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watuwake, naye atakuwa Mungu wao. 4 Yeyeatayafuta machozi yao yote; maanahakutakuwako tena na kifo, wala uchungu,wala kilio, wala maumivu; maana ile hali yakale imepita!” 5 Kisha yule aliyeketi juu ya kiticha enzi akasema, “Tazama, nafanya yotemapya.” Tena akaniambia, “Andika hili, maanamaneno haya ni ya kuaminika na ya kweli!” 6

Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa naOmega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiunitampa kinywaji cha bure kutoka katikachemchemi ya maji ya uzima. 7 Yeyoteatakayeshinda atapokea hiki, nami nitakuwaMungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8

Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu,wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu,na waongo wote, mahali pao patakuwa ndaniya lile ziwa linalowaka moto na kiberiti; hichondicho kifo cha pili.” 9 Kisha mmoja wa walemalaika saba waliokuwa na yale mabakuli sabayaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho,akaja na kuniambia, “Njoo! Miminitakuonyesha bibi arusi, mkeweMwanakondoo!” 10 Basi, Roho akanikumba,naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefusana. Akanionyesha mji mtakatifu, ukishukakutoka kwa Mungu mbinguni, 11 uking'aa kwautukufu wa Mungu. Mwangaza wake ulikuwakama wa jiwe la thamani kubwa kama yaspi,angavu kama kioo. 12 Ulikuwa na ukuta mrefuna mkubwa, wenye milango kumi na miwili, namalaika wanangojea kumi na wawili. Majina yawangoja milango kumi na mawili ya Israeliyalikuwa yameandikwa juu ya milango hiyo. 13

Kila upande ulikuwa na milango mitatu:upande wa mashariki, milango mitatu,kaskazini milango mitatu, kusini milangomitatu na magharibi milango mitatu. 14 Kutaza mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya maweya msingi kumi na mawili, na juu ya mawehayo yalikuwa yameandikwa majina na

mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo. 15

Basi, yule malaika aliyekuwa anasema namialikuwa na kijiti cha dhahabu cha kupimia, kwaajili ya kuupima huo mji, milango yake na kutazake. 16 Mji wenyewe ulikuwa wa mraba,upana na urefu wake sawa. Basi, malaikaakaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwa naurefu, upana na urefu wa kwenda juu, kamakilomita elfu mbili na mia nne. 17 Kishaakaupima ukuta wake pia; nao ulikuwa mitasitini kwa kipimo cha macho cha kibinadamuambacho malaika alitumia. 18 Ukuta huoulikuwa umejengwa kwa mawe mekundu yathamani, na mji wenyewe ulikuwa umejengwakwa dhahabu safi, angavu kama kioo. 19 Maweya msingi wa ukuta huo yalikuwayamepambwa kwa kila aina ya mawe yathamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwela thamani jekundu, la pili yakuti samawati, latatu kalkedoni, la nne zamaradi, 20 la tanosardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, la nanezabarijadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, lakumi na moja yasinto, na la kumi na mbiliamethisto. 21 Na ile milango kumi na miwiliilikuwa lulu kumi na mbili; kila mlango ulikuwaumetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuuya mji ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabusafi, angavu kama kioo. 22 Sikuona hekalukatika mji huo, maana Bwana Mungu MwenyeUwezo na yule Mwanakondoo ndio Hekalulake. 23 Mji huo hauhitaji jua wala mwezikuangazia, maana utukufu wa Munguhuuangazia, na taa yake ni yuleMwanakondoo. 24 Watu wa mataifawatatembea katika mwanga wake, na wafalmewa dunia watauletea utajiri wao. 25 Milango yamji huo itakuwa wazi mchana wote; maanahakutakuwa na usiku humo. 26 Fahari nautajiri wa watu wa mataifa utaletwa humondani. 27 Lakini hakuna chochote kilicho najisikitakachoingia humo; wala mtu yeyoteatendaye mambo ya kuchukiza au ya uongohataingia humo. Ni wale tu walioandikwakatika kitabu cha uzima cha Mwanakondoondio watakaoingia ndani.

Kisha malaika akanionyesha mto wamaji ya uzima maangavu kama kiooyakitoka kwenye kiti cha enzi cha

Mungu na Mwanakondoo. 2 Mto huo ulitiririkakupitia katikati ya barabara kuu ya mji.Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wauzima unaozaa matunda mara kumi na mbilikwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yakeni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa. 3

Hapana kitu chochote kilicholaaniwakitakachokuwa katika mji huo. Kiti cha enzi chaMungu na cha Mwanakondoo kitakuwa katikamji huo, na watumishi wake watamwabudu. 4

Watauona uso wake, na jina lake litaandikwajuu ya paji za nyuso zao. 5 Usiku hautakuwakotena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wajua, maana Bwana Mungu atawaangazia, naowatatawala milele na milele. 6 Kisha malaika

UFUNUO WA YOHANA 22:6

209

Page 210: Biblia Takatifu - downloads.dbs.org

akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na yakuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapamanabii Roho wake, alimtuma malaika wakeawaonyeshe watumishi wake mambo ambayolazima yatukie punde. 7 “Sikiliza! Naja upesi.Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabiiyaliyo katika kitabu hiki.” 8 Mimi Yohane,niliyaona na kusikia mambo haya. Nilipokwishasikia na kuona nikajitupa chini mbele ya miguuya huyo malaika aliyenionyesha mambo hayo,nikataka kumwabudu. 9 Lakini yeyeakaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kamawewe na ndugu zako manabii na wotewanaoyatii maagizo yaliyomo katika kitabuhiki. Mwabudu Mungu!” 10 Tena akaniambia,“Usiyafiche kama siri maneno ya unabiiyaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wakutimizwa kwake umekaribia. 11 Kwa sasaanayetenda mabaya na aendelee kutendamabaya, na aliye mchafu aendelee kuwamchafu. Mwenye kutenda mema na azidikutenda mema, na aliye mtakatifu na azidikuwa mtakatifu.” 12 “Sikiliza!” Asema Yesu,“Naja upesi, pamoja na tuzo nitakalompa kilammoja kufuatana na matendo yake. 13 Mimini Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wakwanza na wa mwisho.” 14 Heri yao walewanaoosha mavazi yao, kwani watakuwa na

haki ya kula tunda la mti wa uzima, na haki yakuingia mjini kwa kupitia milango yake. 15

Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji,waabudu sanamu na wote wanaopendakusema uongo, watakaa nje ya mji. 16 “Mimi,Yesu, nimemtuma malaika wanguawathibitishieni mambo haya katika makanisa.Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ninyota angavu ya asubuhi!” 17 Roho naBibiarusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili,na aseme, “Njoo!” Kisha, yeyote aliye na kiu naaje; anayetaka maji ya uzima na apokee bilamalipo yoyote. 18 Mimi Yohane nawapa onyowote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomokatika kitabu hiki: mtu yeyote akiongezachochote katika mambo haya, Munguatamwongezea mabaa yaliyoandikwa katikakitabu hiki. 19 Na mtu yeyote akipunguzachochote katika maneno ya unabii yaliyomokatika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anyasehemu yake katika ule mti wa uzima, nasehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyovimeelezwa katika kitabu hiki. 20 Nayeanayetoa ushahidi wake juu ya mambo hayaasema: “Naam! Naja upesi.” Amina. Na iwehivyo! Njoo Bwana Yesu! 21 Nawatakieni nyoteneema ya Bwana Yesu. Amen.

UFUNUO WA YOHANA 22:7

210