bunge la tanzania majadiliano ya bunge mkutano wa...

350
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Sita – Tarehe 3 Mei, 2017 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO (K.n.y. MHE. PETER J. SERUKAMBA - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu

Upload: others

Post on 08-Sep-2019

211 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Kumi na Sita – Tarehe 3 Mei, 2017

(Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu.

NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotokwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO (K.n.y. MHE. PETER J.SERUKAMBA - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZAMAENDELEO YA JAMII):

Taarifa ya Kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamiikuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwakawa Fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwakawa Fedha 2017/2018.

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. GODWIN O.MOLLEL - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI KWA WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusuWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotojuu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwaMwaka wa Fedha 2017/2018.

MWENYEKITI: Ahsante. Katibu.

NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, swali lakwanza ni la 130 ambalo linaulizwa na Mheshimiwa ZainabKatimba, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yakeMheshimiwa Peter Serukamba.

Na. 130

Kufanya Vibaya kwa Shule za Sekondari za Umma Nchini

MHE. PETER J. SERUKAMBA (K.n.y. MHE. ZAINAB A.KATIMBA) aliuliza:-

Shule za Sekondari za Umma zimeendelea kufanyavibaya katika mitihani ya kidato cha nne na sita, ambapokwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nnewatahiniwa waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa naasilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri ni 113,489 sawa naasilimia 32.09:-

(a) Je, Serikali ina mkakati gani mahsusi katikakuboresha mazingira ya kujifunzia katika Shule za Umma za

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Sekondari nchini ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati wamiundombinu ya majengo ya madarasa, mabweni namaabara?

(b) Je, kwa nini Serikali isione umuhimu wa kuifutakazi Bodi ya Menejimenti ya Mamlaka ya Elimu Tanzania nakuiunda upya kutokana na kushindwa kusimamia ubora waelimu nchini ambayo ni moja ya jukumu lake?

(c) Je, Serikali ina mpango gani wa kuzifufuazilizokuwa shule za vipaji maalum za Ilboru, Kilakala, Mzumbena Kibaha zilizowahi kufanya vizuri miaka ya 1990?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa VitiMaalum, lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Mpango waMaendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II) Serikaliimekamilisha uboreshaji wa Shule za Sekondari 792 kwakukarabati miundombinu na kuweka samani; shule 264ziliboreshwa katika awamu ya kwanza kwa gharama yashilingi bilioni 56; na shule 540 katika awamu ya pili kwagharama ya shilingi bilioni 67.8 na zote zimekamilika.Ukamilishaji wa ujenzi wa shule hizo, umesaidia katikakuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia katika Shuleza Sekondari za Serikali.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ubora waelimu linajumuisha mambo mengi ambayo yanahusishakuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia jamboambalo linatekelezwa kupitia mipango na bajeti kila mwaka.Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inasimamia udhibiti waubora wa elimu ikishirikiana na taasisi nyingine zinazotekelezaSera ya Elimu Tanzania. Kutokana na hatua zinazochukuliwana Serikali kuboresha elimu nchini, hatuoni sababu ya kuvunja

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Bodi hiyo, badala yake tutaendelea kuiwezesha kutekelezamajukumu yake vizuri zaidi kwa kushirikiana na taasisi nyingine.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendeleana ukarabati wa shule kongwe zote 89 nchini zikiwemo Ilboru,Kilakala, Mzumbe na Kibaha. Mwaka wa fedha 2013/2014Serikali ilitoa shilingi bilioni 12.8 kwa ajili ya ukarabati wamiundombinu ya shule kongwe na shilingi bilioni 3.5 zilitolewana kutumika kukarabati shule saba za ufundi za Iyunga, Moshi,Mtwara, Musoma, Bwiru Boys na Ifunda. Katika mwaka wafedha wa 2016/2017, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)itakarabati shule kongwe 11 zikiwemo za vipaji maalum zaMzumbe, Ilboru, Kilakala, Tabora Boys, Tabora Girls, Pugu,Nganza, Mwenge, Same na Msalato.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sina swali.

MWENYEKITI: Aah, huna swali. Mheshimiwa JamesMbatia.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Kwa kuwa swali la msingi linaulizia vitendea kazi vya elimu,ubora wa elimu, pamoja na mazingira yake yote ambayo nielimu kwa wote, shirikishi na yenye ubora; mwaka 2013 tarehe2 Machi siku ya Jumamosi, Mheshimiwa Rais aliunda Tumeya Sifuni Mchome ya kuangalia vigezo vyote hivi. Tarehe 31hoja binafsi ilikuwa Bungeni kuhusu vigezo vyote hivi. Je, nilini Serikali italeta ile ripoti ya Tume ya Sifuni Mchome hapaBungeni ili Wabunge tuweze tukaishauri vizuri Serikali kuhusuubora wa elimu Tanzania?

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Engineer Manyanya.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni kweli nafahamu kunahiyo Tume ilikuwa imeundwa na kuna baadhi ya mamboambayo yalikuwa yameelezwa kwenye ile Tume; lakini baadaya hapo kuna team mbalimbali ziliundwa ambazo pianyingine zilikuja kuona hata baadhi ya mapendekezopengine hayako sawa; yaani hayaendani sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Wizara tumekuwatukiendelea kufanya marekebisho kulingana na mahitaji, kwamfano katika suala la utoaji wa tuzo. Mwanzo zilikuwazinatumia GPA, sasa hivi tumerudi tena kwenye division. Kwahiyo, kuna mambo mengi tu ambayo yamekuwa yakifanyiwakazi kila wakati. Hata hivyo, siyo tatizo kuweza kuwaoneshaWaheshimiwa Wabunge nini kilikuwa kimezungumzwakwenye Tume, lakini pia mabadiliko yanayoendana nauhalisia wa sasa yaliyofanyika.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Khadija.

MHE. KHADIJA N. ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania,ni lini Wizara itaingiza mitaala ya masomo ya kilimo na ufugajikwenye Sekta ya Elimu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

MWENYEKITI: Ahsante. Naibu Waziri, Mheshimiwa Jafokwa kifupi twende mbele.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, concern hiyokweli imejitokeza wazi; na nakumbuka kipindi cha nyumawaliokuwa wanasoma sekondari, kulikuwa na somo mojalinaitwa Agricultural Science na mambo ya Nutrition, lakinihapa katikati lilipotea.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba kwanza mitihani ya Form Sixna ile ya Form ya Four mwaka 2016, somo hilo sasalimeshaanza kuingizwa. Utaratibu wa Serikali ni kuhakikishakwamba somo hili la Agricultural Science na masomomengine, kuhakikisha kwamba suala la kilimo linapatikanalimeweza kufanyika hivyo. Nashukuru sana Walimu ambaowamejitokeza, nami nilienda kuwatembelea wakati ule wapoHombolo wakifanya usahihishaji, wamesema vijanawametoa mwitikio mkubwa sana, inaonekana tunaendeleavizuri. Kwa hiyo, hilo tuondoe shaka, Serikali inalifanyia kazivizuri.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali namba131, linaulizwa na Mheshimiwa Dkt. Shukuru JumanneKawambwa, Mbunge wa Bagamoyo. Kwa niaba yake,Mheshimiwa Ulega. Aah, Mheshimiwa Dkt. samahani, karibu.

Na. 131

Huduma za Afya - Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA aliuliza:-

Kwa muda mrefu sasa, huduma za afya katikaHospitali ya Wilaya Bagamoyo zimekuwa dhaifu sanakutokana na upungufu mkubwa wa miundombinu, vitendeakazi, uhaba wa watumishi na ukosefu wa dawa:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha hudumaza afya katika Hospitali hiyo kwa kuhakikisha upatikanaji wamiundombinu bora, vitendea kazi, kuiongezea watumishi nadawa za kutosha?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa, Mbunge waBagamoyo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018, Serikali imetenga shilingi 1.4 kwa ajili ya kuboreshahuduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyoambapo itahusisha kuboresha miundombinu ya Hospitali naupatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile zimetengwa shilingi185,000,000/= kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kutokana naruzuku ya maendeleo kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wamiundombinu mbalimbali ya vituo vya kutolea huduma zaafya, shilingi 59,790,600/= kutokana na mapato ya ndani kwaajili ya upanuzi wa wodi ya wazazi, ukarabati wa kitengo chawagonjwa wa nje (OPD) na eneo la kuhudumia wagonjwawa dharura pamoja na kumaliza ukarabati wa wodi yawanaume. Aidha, Serikali imetoa kibali cha kuajiri Madaktarina watumishi wengine wa afya ambapo Halmashauri hiyopia itapewa kipaumbele. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Kawambwa.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya MheshimiwaWaziri, isipokuwa nina maswali mawili ya nyongeza yakuuliza. Moja, Mheshimiwa Waziri katika mwaka huu wafedha 2016/2017, tulitengewa fedha jumla ya sh. 82,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa wodi kwenye Hospitali ya Wilaya yaBagamoyo, lakini mpaka hapa tunapoongea fedha hizihazijapelekwa katika Halmashauri. Je, Mheshimiwa Waziriatatuhakikishia Bagamoyo kwamba fedha hizi zitawezakutolewa kabla ya mwaka huu kumalizika il i tuwezekuboresha huduma katika hospitali hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, MheshimiwaWaziri amenijibu kuhusu ujenzi wa OPD kwa kutumia fedhaza (own source) za kwetu wenyewe, lakini OPD hii ni mbovusana; haina uwezo wa kuhudumia wagonjwa kwa kadriambavyo ingeweza kutoa huduma ile ambayo wanasema

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

inafaa kwa wananchi wale wa Bagamoyo. Inahitaji ujenzimpya kabisa. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari ku-commitkiasi cha fedha ili angalau tuweze kuijenga upya OPD hiyo?

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Naibu Waziri,kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lacommitment ya Serikali katika bajeti ambayo mwaka huutunaondoka nayo, naomba nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba bado tuna mwezi mpaka tufike mwezi waSita. Lengo letu Serikali ni ile wodi iweze kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la OPD, nimhakikishieMheshimiwa Mbunge, kwanza Bagamoyo tumeingiza katikaprogram maalum ya RBF na hivi sasa tumewapelekeatakriban shilingi milioni 150 kutokana na kuwepo kwazahanati zao 15. Mpango huu utaenda takriban miaka mitatukwa sababu tume-site kama ni sehemu ya mfano kuanziana hiyo program.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba wakati tunaenda na hiziintervention, kwa sababu lengo letu ni kupandisha vituo vyetuviwe na star. Bahati nzuri Jimbo lake ni miongoni mwamaeneo yaliyofanya vema. Katika vituo 15, vituo 11 vilipatastar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wetu ni nini? Nikwamba tutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo, naminaifahamu OPD yaou pale Bagamoyo jinsi ilivyo, tutashirikianakwa pamoja nini kifanyike tuhakikishe tunafanya marekebishomakubwa katika OPD ile, kwa sababu wagonjwa wengi sanaukiangalia katika jiografia ya pale wanatibiwa pale. Kwahiyo, Serikali tutafanya kila liwezekano ili mradi tuwezekuweka mazingira yawe mazuri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Owenya na mwishoMheshimiwa Hawa Ghasia.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kuniona. Nina swali dogo la nyongeza kwaMheshimiwa Naibu Waziri. Tatizo la ukosefu wa dawa ni tatizokubwa katika mahospitali mengi nchini, kuanzia Zahanatina Vituo vya Afya. MSD imeshalipwa zaidi ya shilingi bilioni80. Sasa Mheshimiwa Waziri naomba atueleze ni kwa nini MSDinashindwa kuagiza dawa wakati wana fedha katika akauntizao? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisiya Rais (TAMISEMI).

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kwambasasa hivi tunapeleka fedha nyingi sana. Kama nilivyosemahapa mara kadhaa katika Bunge letu hili, kupitia ule mfuko(basket fund) peke yake, tuna fedha nyingi ambazotumezipeleka kule na nimekuwa nikihamasisha Halmashaurimbalimbali wafanye procurement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tumewekautaratibu kwamba endapo dawa zinakosekana, kuna primevendors ambao wanapatikana kwa ajili ya kuhakikisha dawazinapatikana. Kwa hiyo, endapo dawa zimeonekanamiongoni mwa dawa zil izoombwa kutoka MSDzimekosekana, basi tumewaelekeza wataalam wetu katikakanda kwamba waweze kutumia prime vendors ambaowamekuwa identified kabisa na Serikali, kuhakikisha kwambatuna-fast truck katika suala la upatikanaji wa dawa. Lengokubwa ni kwamba Hospitali zetu, Zahanati zetu na Vituo vyaAfya viweze kupata dawa kwa ajili ya wananchi wetu.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Hawa Ghasia.

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nami napenda niulize swali la nyongeza. Mikakatiya Serikali ni kuboresha afya katika maeneo yote nakupandisha hadhi baadhi ya Vituo vya Afya kuwa Hospitali.Katika Mkoa wa Mtwara tulikuwa tunapandisha hadhi Kituocha Afya Nanguruwe na Kituo cha Afya Nanyumbu,

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

kuhakikisha inakuwa Hospitali na tumefikia hatua nzuri yakufungua kuwa Hospitali. Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuukutoka TAMISEMI alipokuja alisema Vituo vya Afya viendeleekuwa Vituo vya Afya na tuanze ujenzi upya. Sasa natakakujua ile ni kauli yake au ni kauli ya Serikali? Kwa sababuSerikali siku zote imekuwa ikitusaidia kufikia hapo ili vituo hivyoviwe hospitali. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisiya Rais (TAMISEMI)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Kituo chaAfya cha Nanguruwe na Nanyumbu, Mheshimiwa Mbungeanakumbuka nilivyofika pale, Nanguruwe, Kituo cha Afyaambacho kina facilities nyingi sana, kilikuwa na suala zima laahadi ya Mheshimiwa Rais kuifanya kuwa Hospitali ya Wilaya.Maana yake nini? Naibu Katibu Mkuu wetu alizungumzatechnically kwamba nini tunatakiwa kufanya? Kwambatukiwa tuna upungufu wa mambo ya hospitali, lazimatujiwekeze katika suala zima la ujenzi wa hospitali zetu zaWilaya. Siyo kama ni kauli yake, isipokuwa ni kauli ya Serikalisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema kwamba tuvi-convert Vituo vya Afya kuwa Hospitali za Wilaya, maana yaketunafifisha baadhi ya juhudi, lakini kuna maeneo mengineyana special preferences. Kwa mfano, pale Nanguruwe,Nanyumbu au maeneo mengine niliyotembelea, unakutaVituo vya Afya vingine walikuwa katika program ya kufanyakuwa Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nimesematuna-treat maeneo mengine case by case. Kwa case kamapale Nanguruwe au Namyumbu ambapo hata MheshimiwaRais mstaafu alipopita pale alitoa ahadi, ahadi ile itaendeleakuwepo pale pale. Lengo kubwa ni kuwasaidia wananchiwale na kwa kiwango kikubwa Serikali imesha-invest vyakutosha kukodi na vifaa vingine kuwasaidia wananchi waeneo lile. (Makofi)

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Ofisi hiyo hiyoya Rais, TAMISEMI, swali namba 132, linaloulizwa naMheshimiwa Rose Kamili Sukum, Mbunge wa Viti Maalum.

Na. 132

Utaratibu wa Upelekaji Fedha katika Halmashauri

MHE. ROSE K. SUKUM aliuliza:-

Serikali hupeleka fedha kwenye Halmashauri baadaya kupokea mpango kazi wa maendeleo au matumizi yakawaida kwa Halmashauri husika. Kama ikitokea fedha zaidizimepelekwa katika Halmashauri, maana yake kunaHalmashauri imepelekewa kidogo:-

(a) Je, kwa nini fedha za ziada zisirudishwe Hazinana badala yake zinaombwa kutumiwa na Halmashauriambayo haikuwa na mahitaji nazo?

(b) Je, Halmashauri ambazo zinakuwazimepelekewa fedha kidogo zinafidiwa vipi ili kukidhi maombiya mpango kazi wake?

(c) Je, kwa Halmashauri inayotumia fedha hizobila ya kusubiri maelekezo kama ilivyo pale inapokuwa ziadakuwekwa kwenye Akaunti ya Amana kama Memorandumya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Kifungu Na. 9(2)(e)kinavyoelekeza, endapo itabainika, wanachukuliwa hatuagani?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali laMheshimiwa Rose Kamili Sukum, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, upelekaji wa fedhakatika Halmshauri huzingatia Mpango Kazi (Action Plan)ambao huandaliwa kwa kuzingatia bajeti iliyoidhinishwa naBunge. Fedha hizo hupelekwa na Hazina kila robo mwakazikiwa na maelekezo ya matumizi. Uzoefu unatuoneshaHalmashauri zimekuwa zikipokea pesa pungufu ikilinganishwana bajeti iliyoidhinishwa kwa sababu upelekaji wa fedha hizohuzingatia hali ya makusanyo kwa nchi nzima. Hata hivyo,pale inapobainika kuwa fedha zilizopokelewa zaidi ya bajetiiliyoidhinishwa na hakuna maelezo ya matumizi, ni wajibu waAfisa Masuhuli kuuliza matumizi ya fedha hizo Hazina au Ofisiya Rais (TAMISEMI) kabla ya kuzitumia.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoelezakatika sehemu (a) ya jibu langu, kila Halmashauri hupelekewafedha kulingana na bajeti iliyoidhinishwa na kwa kuzingatiampango kazi. Fedha hupelekwa katika Halmashauri kwakuzingatia hali ya makusanyo (Cash Budget). Kwa mantikihiyo, hakuna utaratibu wa kufidia bajeti ambayo haikutolewakwa mwaka husika. Mwongozo wa Bajeti huzitaka mamlakahusika kuzingatia maeneo ambayo hayakupata fedha katikavipaumbele vya bajeti inayofuata ili kupata fedha.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha zotezinazotumwa katika Halmashauri huambatana na maelezoya matumizi ya fedha hizo ambayo hupitia kwa Katibu Tawalawa Mkoa. Pale inapotokea maelezo yamechelewa kufika,ni wajibu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika kufuatiliaHazina au Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kabla ya kuzitumia. AfisaMasuhuli atakayetumia fedha za ziada bila idhini, anakiukasheria na taratibu za fedha na anastahili kuchukuliwa hatuakwa mujibu wa sheria.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Sukum.

MHE. ROSE K. SUKUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri waTAMISEMI, lakini nina maswai mawili ya nyongeza.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziriamekiri kwamba Afisa Masuhuli anayetumia fedha bila idhiniya TAMISEMI au ya Hazina, hastahili kutumia hizo fedha. Je,ni kwa nini ofisi yake haikutekeleza wajibu huo kwa MaafisaMasuhuli ambao wametumia hizo fedha bila idhini yake aubila idhini ya Ofisi yake pamoja na Hazina? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe mwenyewe umekirikwamba fedha endapo itabainika imeongezwa, lakini (b)yake umesema kwamba hakuna bajeti inayoidhinishwaikazidi kupelekwa kwenye Halmashauri: sasa ni ipi tuipokeekutoka kwako endapo fedha zimeongezeka? Unasemakwamba haziongezeki, nami nina uhakika kwamba fedhazinaongezeka; sasa naomba kuuliza. Je, kwa wale ambaowameongezewa fedha na wale ambao wamepunguziwawanafidiwaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa NaibuWaziri atupatie majibu ambayo yanastahili. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisiya Rais (TAMISEMI) majibu kwa kifupi tu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema hapakwamba kwa Afisa Masuhuli yeyote ambaye atakiukautaratibu wa fedha, maana yake atachukuliwa hatua. Kwasababu, Mheshimiwa Sukum hakunipa mfano halisi, lakininaomba nimhakikishie, kuna maamuzi mbalimbali yakinidhamu tumeyachukua kwa Watendaji mbalimbali. Hatabaadhi ya Wakurugenzi wengine ambao wameenda nje yasystem sasa kutokuwa Wakurugenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni kwa sababu mwanzokatika njia moja ama nyingine walikiuka utaratibu wa fedhana kufanya ufisadi mkubwa katika fedha hizo na ndiyomaana Serikali ilichukua hatua. Ni kwa sababu hatuwezi ku-publicize hapa kwamba nani na nani, lakini tumechukua

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

hatua mbalimbali kwa baadhi ya Wakurugenzi ambao niMaafisa Masuhuli, walioko katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake linginekwamba fedha sehemu nyingine zinaongezeka na nyinginezinapungua, nimezungumza wazi, hapa kila Mbungeakisimama anazungumza kwamba fedha haziji, fedha haziji.Ndiyo nimesema, kwa uzoefu tuliokuwa nao, mara nyingisana fedha zile tunazozipanga, ndiyo maana hataMheshimiwa Kawambwa hapa anaomba fedha za wodiyake hazijafika. Uzoefu uliokuwepo ni kwamba fedhazinazokwenda ni chache kuliko kile kilichopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kunatokea na specialcase kwamba kuna baadhi ya fedha zimeongezeka, nilazima utaratibu ufuatwe kama nilivyoelekeza katika maelezoyangu ya awali, kwamba lazima atoe taarifa aidha Hazinaau Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa Katibu Mkuu kwa ajili yaufuatiliaji, fedha hizo zirudishwe katika Mfuko Mkuu waHazina.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa SophiaMwakagenda.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa, Halmashauri mara nyingitatizo la fedha ni shida kubwa sana. Je, Mheshimiwa NaibuWaziri anaweza kutuambia ni jinsi gani atahakikisha Ofisi yakeinatimiza yale malengo ya fedha iliyoahidi kwenda kwenyeHalmashauri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuhusu usimamizi, asemekwa kina atazisimamiaje Halmashauri zake zisifanye ufisadikwa kuwa, imekuwa ikijirudia mara kwa mara na kutuleteamatatizo katika Halmashauri zetu?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapatunazungumzia suala zima la fedha na fedha hizi zinatafutwakwa gharama kubwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Naomba nimhakikishie, nilikuwa nikifanya ziara katikaHalmashauri zote na nashukuru Mungu sasa nimebakiza chiniya Halmashauri 10 kuzipitia Tanzania nzima. Ajenda yetu yakwanza ni suala la uadilifu katika usimamizi wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumewaambia na nimetoamaelekezo katika maeneo yote kwamba Wakurugenzi naWaweka Hazina sasa lazima wanapokwenda katika Kikaocha Kamati ya Fedha ambapo Madiwani na Wabunge niWajumbe hapo, lazima watoe taarifa ya transactions katikaHalmashauri zao, fedha zilizopokelewa na matumizi yakeyalikuwaje. Siyo kupokea lile kabrasha la mapato namatumizi ambapo Mbunge au Diwani anashindwa kujuandani kilichokuwemo. Kwa hiyo, tumetoa maelekezo hayavya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba sanaWaheshimiwa Wabunge ambao sisi ni Wajumbe wa Kamatiya Fedha kwamba tukiingia katika vikao vyetu, tuwezekuzisaidia Halmshauri hizi kwa sababu sisi ndio wafanyamaamuzi ambao tunawawakilisha wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwasihi Wabunge wotekwamba kwa moyo mkunjufu na moyo wa dhati tuzisimamieHalmashauri zetu, compliance iwepo na wananchi wetuwapate huduma na maendeleo.

MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea. Swali namba 133linaulizwa na Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko, Mbunge waBukombe.

Na. 133

Ujenzi wa Kilometa Tano Kwenye Mji wa Ushirombo

MHE. DOTO M. BITEKO aliuliza:-

Wakati wa Kampeni za Mwaka 2015, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania aliahidi kilometa tano kwenyeMji wa Ushirombo:-

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Je, ni lini ahadi hiyo itatekelezwa?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Doto Mashaka Biteko, Mbunge wa Bukombe,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara za Mji waUshirombo zinahudumiwa na Halmashauri ya Wilaya yaBukombe. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbungekuwa Serikali imekusanya ahadi zote za viongozi na kuwekautaratibu wa jinsi ya kuzitekeleza, ikiwemo ujenzi kwa kiwangocha lami wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa tanozilizoahidiwa na Mheshimiwa Rais mwaka 2015, MjiniUshirombo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msimamo wa Serikali yaAwamu hii ya Tano ni kuhakikisha kuwa inatekeleza ahadizake zote katika kipindi cha miaka mitano.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Biteko, swali la nyongeza.

MHE. DOTO M. BITEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa nafasi hii. Kwa kuwa, Serikali imesemakwamba imeshaweka utaratibu wa namna gani itatekelezaahadi za viongozi, ikiwemo ahadi ya Mheshimiwa Rais wakatiwa kampeni ya ujenzi wa kilometa tano za lami kwenye Mjiwa Ushirombo; wananchi wa Bukombe wanataka kujua tusasa kwamba ni lini? Kwa sababu amesema ndani ya miakamitano, basi waambiwe ni lini itaanza kutekelezwa katikakipindi cha miaka hii mitano, maana huu ni mwaka wa pilitayari tumeingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hicho ndicho wananchiwanataka kusikia. Nakushukuru. (Makofi)

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naombakumpongeza sana Mheshimiwa Biteko kwa kazi kubwaanayoifanya kufuatilia masuala ya miundombinu katikamaeneo yake. Namwomba tu, yale ambayo tuliongea ofisinina yale ambayo tuliongea mbele ya Mheshimiwa Waziriwangu ni kweli tutayatekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba utaratibu tuliopewa, kitu cha kwanza nikuhakikisha tunatekeleza ahadi zote, lakini wakati huo huozina Wakandarasi site ili kuondoa matatizo ya kulipa interestpamoja na idle time. Hicho ndicho kipaumbele cha kwanzaili tuweze kupata hela nyingi zaidi za kuwekeza kwenyemiundombinu badala ya kuwalipa watu ambao wanakaatu hawafanyi kazi. Kwa hiyo, hicho ni kipaumbele chakwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele cha pili nikuhakikisha ahadi zote za Mheshimiwa Rais na zilizoandikwakatika Ilani ya Uchaguzi tunazipangia ratiba. Sasatunakwenda miaka kwa miaka; mwaka wa kwanzatumemaliza, mwaka huu mmeona kwamba mambo mengitumeyaingiza ambayo ni mapya siyo yale ambayo tulikuwatunategemea wakati ule kwa sababu tumeshapunguza kwakiwango kikubwa yale madeni ambayo tulikuwa nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nimhakikishieMheshimiwa Mbunge na wananchi wa Ushirombo kwambaahadi zote katika miaka hii mitatu iliyobakia tutatekelezaahadi hii tuliyoitoa wakati wa uchaguzi.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa, janammejibiwa mambo mengi na Mheshimiwa Waziri.Tunaendelea na swali linalofuata. Swali namba 134 linaulizwana Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda.

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Na. 134

Barabara ya Masasi – Nachingwea Kujengwakwa Kiwango cha Lami

MHE. DAVID E. SILINDE (K.n.y. MHE. CECIL D. MWAMBE)aliuliza:-

Barabara ya Masasi – Nachingwea imekuwa namatatizo kwa muda mrefu ya kupitika kwa shida:-

Je, barabara hiyo itajengwa lini kwa kiwango chalami ili kufanya wananchi wa Jimbo la Ndanda waondoeimani kuwa wametengwa?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha kazi yaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Masasi– Nachingwea hadi Nanganga yenye urefu wa kilometa 91kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Katika mwaka wafedha 2017/2018, mradi huu umeombewa fedha za jumla yash. 3,515,394,000/= kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwangocha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya barabara yaMasasi – Nachingwea yenye urefu wa kilometa 45 imekuwaikifanyiwa matengenezo ya kawaida na matengenezo yamuda maalum kila mwaka na inapitika vizuri katika kipindicha mwaka mzima. Serikali itaendelea kuifanyiamatengenezo ya aina mbalimbali barabara hiyo ili iendeleekupitika majira yote ya mwaka wakati barabara hiiinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Silinde.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napendakuuliza maswali madogo ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutoka Masasi mpakaNachingwea ni kama kilometa 42 na kutoka Masasi mpakaNdanda ni kama kilometa 40; na kwenye bajeti iliyokuwaimeitengwa ambayo imeombwa mwaka 2017/2018 kamashilingi bilioni tatu, ni fedha ndogo ambayo haiwezi kukidhikumaliza barabara hiyo. Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadiyake ya kukamilisha barabara hiyo kwa kiwango cha lamikama ambavyo Mheshimiwa Mbunge alikuwa ameomba,kwa sababu fedha iliyotengwa ni ndogo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali dogo la pil i lanyongeza ni kwamba, matatizo ya Jimbo la Ndandayanafanana kabisa na Jimbo la Momba kule; sasa naombaniulize kwamba barabara ya kutoka Kakozi kwenda Kapelempaka Namchinka kilometa 50.1 imepandishwa hadhi naWizara yako, lakini mpaka sasa haijawahi kuhudumiwa nahiyo barabara ni mbovu. Ni kwa nini barabara hizimnazipandisha hadhi na hamzihudumii kwa wakati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri,majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu udogo wafedha, kitu ninachojaribu kumweleza ni kwamba katika ulempangilio wa kutekeleza ahadi sasa tumefikia kuanzautekelezaji wa ahadi ya barabara hii na tumeanzia na hizifedha ndogo kutokana na bajeti tuliyopata mwaka unaokujawa 2017/2018. Nimhakikishie, katika miaka yote inayofuata,barabara hii itakuwa inaendelea kupewa fedha za kutoshaili hatimaye katika kipindi chetu tulichoahidi, barabara hiiitakuwa imekamilika.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara ya Kakozi– Kapele na kuendelea ambayo imechukuliwa na TANROAD,nimhakikishie tu kwamba tutahakikisha TANROAD inapangafedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa barabara hiikama ilivyokusudiwa kwa kupandishwa hadhi.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Joseph Kakundana wa mwisho Mheshimiwa Risala Kabongo.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwambabarabara ya Sikonge – Mibono – Kipili ilipandishwa hadhitangu mwaka 2009 na hadi leo imetobolewa kwa kiwangocha kilometa 42 tu kati ya 282 ambayo ni kama kilometa tanokwa mwaka; ina maana kwamba hadi itakapokamilikabarabara hiyo tunahitaji miaka 44. Je, Serikali iko tayarikuwaambia wananchi wa Sikonge kwamba itajengabarabara hiyo kwa kipindi cha miaka 44 ijayo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri. Speed yaujenzi wa barabara hiyo.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utaratibu wafedha za Mfuko wa Barabara zinazogawiwa mikoani kwa ajiliya matengenezo, haturuhusiwi kutumia fedha nyingi sanakwa ajili ya kutoboa barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba ombi lake tunalichukua na tutatafutanamna ya kuhakikisha barabara hii kipande hiki kipya chakukitoboa tunakitoboa kwa haraka zaidi na naombawananchi wote wa Sikonge wachukue hiyo ndiyo kamacommitment ya Serikali.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Risala Kabongo.

MHE. RISALA S. KABONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Kwa kuwa Barabara ya kutoka Mlowo - Mbozi kwenda

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Kamsamba - Momba haipitiki wakati wa mvua, je, ni liniSerikali itatengeneza barabara hii kwa kiwango cha lami ilikuweza kusaidia uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Songwena Mkoa wa Katavi? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tunimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, yale ambayotumeshayasema kabla ni ya kweli na tutayatekeleza.Tulichokiahidi, kitu cha kwanza ni kukamilisha daraja,tukishamaliza kukamilisha daraja tutashughulikia hii barabarakatika kiwango cha lami. Tupeni fursa, hizo pesa ambazotumezitenga kwa ajili ya daraja kwanza tukamilishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina uhakika, maadamtunatenga fedha za utengenezaji wa hii barabarakuhakikisha inapitika karibu muda wote, naomba tupeni fursatutekeleze kwa namna tulivyopanga.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali namba135, linaulizwa na Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate,Mbunge wa Kyerwa. Linaelekezwa kwa Mheshimiwa Waziriwa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Na. 135

Fidia kwa Wananchi WaliopishaUjenzi wa Barabara

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Barabara ya kutoka Mgakorongo, Kigarama mpakaMurongo iliwekwa kwenye ilani kuwa itajengwa kwakiwango cha lami na wananchi waliokuwa ndani ya mradiwaliowekewa alama ya ‘X’ wanashindwa kuendelezamaeneo yao wakisubiri fidia zaidi ya miaka mitano sasa:-

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

(a) Je, ni l ini wananchi hawa watapewa fidia i l iwaendelee na mambo ya kimaendeleo?

(b) Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANOalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Innocent Sebba, Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa,lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara yaOmugakorongo – Kigarama hadi Murongo ni barabara kuuinayohudumiwa na Wakala wa Barabara Mkoa wa Kagerana ina jumla ya kilometa 111. Serikali inatambua umuhimuwa barabara hii kiuchumi na kijamii ndiyo maana imeiwekakwenye mpango wa kujenga kwa kiwango cha lami. Hivi sasaupembuzi yakinifu wa barabara hii umekamilika, kaziinayoendelea ni usanifu wa kina na uandaaji wa nyaraka zazabuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kupitiaWakala wa Barabara Tanzania inaendelea na uhakiki wa fidiaya mali zitakazoathiriwa na mradi kulingana na sheria, kanunina taratibu zilizopo. Wananchi wote wanaostahili kulipwa fidiakwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007watalipa fidia mara zoezi la uhakiki litakapokamilika naWizara yangu itahakikisha kuwa taratibu zote za malipo yafidia na sheria zinafuatwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kazi za ujenzi wabarabara ya Omugakorongo – Kigarama hadi Murongozitaanza mara baada ya usanifu wa kina kukamilika na fedhaza ujenzi kupatikana.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Bilakwate.MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa

Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

mawili ya nyongeza. Kwa kweli nasikitika sana kuona majibuambayo ametoa Mheshimiwa Waziri. Hii ni mara yangu yapili namwuliza hili swali. Mara ya kwanza alinijibu hapahapaBungeni, akasema kabla ya mwezi wa Sita barabara hiiitakuwa imeanza ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri, anapotujibu siyo kuwajibu Wabunge kuwafurahisha,haya ni majibu ambayo tunakuja kuuliza kwa ajili yawananchi wetu. Naomba Mheshimiwa Waziri atupe majibuambayo ni ya uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza; ni linibarabara hii ujenzi utaanza? Kwa sababu hii barabara ni yamuda mrefu tangu kipindi cha Mheshimiwa Rais Mkapaamestaafu; amekuja Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,sasa anakuja Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwenye bajetiya mwaka 2017/2018, je, imetengwa pesa kwa ajili ya ujenzihuu kuanza na wananchi wapewe fidia?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa EngineerNgonyani, kwa kifupi tu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanimhakikishie, tunapojibu hapa kwanza tunaonesha dhamiralakini pili, tunaonesha mipango ambayo ipo mbioni.Hatuwezi kuanza ujenzi wa barabara hii kabla ya upembuziyakinifu na usanifu wa kina kukamilika. Hakuna aina hiyo yaujenzi ya barabara kuu na muhimu kama hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba MheshimiwaMbunge atupe fursa tukamilishe upembuzi yakinifu na usanifuwa kina. Kwa mwaka huu tunakamilisha kazi hizo mbili. Kwahiyo, hatujatenga fedha za kuweza kujenga, tumetengafedha kwa ajili ya kukamilisha kazi hizo mbili. Nimhakikishiekwamba mara baada ya kazi hizo mbili kukamilika, ujenzi

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

utaanza, Serikali hii ya Awamu ya Tano inachosemainakusudia kukitekeleza na huwa inakitekeleza. (Makofi)

MWENYEKITI: Niangalie wa huko huko, MheshimiwaGashaza, Mbunge wa Ngara.

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Barabara ya Dar es Salaam – Isaka – Rusumo, inayojulikanakama central corridor ni barabara inayohudumia nchitakriban nne ambazo zipo kwenye Jumuiya ya Afrika yaMashariki, lakini kipo kipande cha kilometa 150 kutokaLusahunga kutoka Rusumo; Nyakasanza kwenda Kobelompaka Bujumbura. Kipande hiki kimekuwa ni kero kwa mudamrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana ambao ndiyohuu tunamalizia 2016/2017 barabara hii ilitengewa shilingibilioni tano, lakini mpaka sasa hivi ukarabati unaofanyika nimdogo na kwa bajeti hii ya 2017/2018 tumetengewa shilingibilioni 1.19 tu kiasi kwamba haiwezi kufanya ukarabatiunaoridhisha. Je, ni lini Serikali sasa itaweza kutenga fedhaza kutosha ili kukarabati kipande hiki ambacho ni kero kwaWatanzania wanaotumia barabara hii na wageniwanaotoka kwenye nchi za Burudi na Rwanda, Kongo naUganda ili barabara hii iweze kukidhi viwango na kukidhimahitaji?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, MheshimiwaGashaza kwa sababu anapita hii barabara, anafahamu kazikubwa inayofanywa kuirekebisha hiyo barabara kuanziaIsaka na kuendelea. Tunakwenda kwa hatua; mimimwenyewe nimeona ukarabati ulioanzia Rusahungakuelekea Rusumo. Nimeiona, nimepita hiyo barabara.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaMbunge, aridhike na hiki kinachofanyika na kwa vyovyotevile, baada ya kukamilisha hii, tutakwenda kukamilishakipande kilichobakia. Suala siyo rahisi kupata fedha zote zakutosha kuikamilisha barabara yote kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba tutaendelea kuikarabati barabara hiimpaka ikamilike. Tutafika Rusumo, tutafika hii njiainayokwenda Burundi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Savelina Mwijage.

MHE. SAVELINA S. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa kuwa ahadi za barabara ya Karagwekwenda mpaka Benako kutoka Nyakaanga zimekuwa kerokwa muda mrefu; nimeingia Bungeni mwaka 2005 barabaraya kwenda mpaka Mlongwe nimeiongea barabara yakutoka Nyakaanga kwenda Benako nimeiongea:-

Ni lini Serikali itachagua moja; kutengeneza upandena mmoja kuumaliza na kuingia wa pili? Mnatafuta ma-engineer na Wakandarasi ambao hawana viwango.Barabara unatengeneza siku mbili, tatu, barabarainaharibika. Lini mtatafuta ma-engineer wa uhakika wakutengeneza barabara zikawa za viwango? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikiaMheshimiwa Mbunge kwa makini anachokiongelea. Huwanaamini kwamba tunachagua Wakandarasi makini, ila kwakauli yake inaonekana tunatakiwa tuongeze nguvu zaidi namacho yaangalie zaidi ili kuhakikisha kweli tunapataWakandarasi wanaoweza kusaidia kufanya kazi bila kurudiarudia mara nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa ushauriwake.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali 136, linaulizwa na Mheshimiwa Yussuf Haji Khamis,Mbunge wa Nungwi, linaelekezwa kwa Waziri wa MamboKatiba na Sheria.

Na. 136

Kukamatwa kwa Meli ya Uvuvi MFV Tawariq

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS aliuliza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2009 Serikaliilikamata Meli ya Uvuvi MFV TAWARIQ, nahodha wake TsuChin Tai pamoja na watu wengine 36 walishtakiwaMahakama Kuu kwa kesi ya Jinai Na. 38 ya mwaka 2009.Kwa amri ya Mahakama samaki tani 296.3 wenye thamaniya sh. 2,074,000,000/= waligawiwa bure. Aidha, meli hiyoilizama ikiwa inashikiliwa kama kielelezo. Tarehe 23 Februari,2012 watuhumiwa wawili walihukumiwa kifungo na walikatarufaa Mahakama ya Rufaa ambapo tarehe 25 Machi, 2014waliachiwa huru na sasa ni miaka saba tangu meli hiyoikamatwe.

Je, Serikali itarudisha lini sh. 2,07,000,000/= ambazo nithamani ya samaki na fedha ambazo ni thamani ya melikwa Mawakili wa Nahodha wa Meli hiyo?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA (K.n.y. WAZIRI WAKATIBA NA SHERIA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Yussuf Haji Khamis, Mbunge wa Nungwi kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamo tarehe 8 Machi,2009 kikosi kazi kilichokuwa kikifanya doria katika ukanda wakiuchumi wa Bahari Kuu ya nchi yetu (Exclusive EconomicZone) katika Bahari ya Hindi kilifanikiwa kukamata meli yauvuvi iitwayo Na. 68 BU YOUNG ikivua katika bahari yetu bila

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

kibali. Meli hiyo ilikuwa ikiongozwa na nahodha aitwaye TSUCHIN TAI, raia wa Jamhuri ya Watu wa China na alikuwapamoja na wenzake 36. Pamoja na kuwa jina la meli hiyo niNo. 68 BU YOUNG, meli hiyo ilikuwa inatumia pia jina laTAWARQ 1 na TAWARIQ 2 ili kuficha jina halisi na kuendelezakufanya uvuvi haramu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nahodha wa meli hiyo, yaaniTSU CHIN TAI na wenzake walishtakiwa Mahakama Kuu katikakesi ya jinai Na. 38/2009 ambapo nahodha Tsu Chin Tai naZHAO HANQUING aliyekuwa wakala wa meli hiyo, walitiwahatiani. Wawili hawa waliomba rufaa Mahakama ya Rufaniambapo mwaka 2014 Mahakama hiyo ilibatilisha na kufutamwenendo mzima wa kesi baada ya kubaini kuwa kulikuwana kasoro katika taratibu za kuwafungulia mashtaka. Kwaufupi, hawakuwahi kushinda kesi na Mahakama ya Rufanihaikuwahi kutamka kuwa wako huru kwa sababu hawanahatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya uamuzi huo waMahakama ya Rufani, Mkurugenzi wa Mashtaka alifunguamashtaka upya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutuna baadaye kuondoa mashtaka dhidi yao tarehe 22/8/2014.Baada ya miaka miwili, yaani 2016 Wakili Captain Benderaalifanya maombi namba 108/2016 katika Mahakama Kuuakimwakilisha Bwana Said Ali Mohamed Al Araimi ambayehakuwa mmoja kati ya washtakiwa katika kesi ya msingiakiomba apewe meli au USD 2,300,000.00 kama thamani yameli hiyo na sh. 2,074,249,000/= kama thamani ya samaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama Kuu baada yakusikiliza hoja za pande zote mbili, ilikubaliana na hoja zaJamhuri na kutupilia mbali maombi hayo. Katika uamuziwake, Mahakama ilitamka yafuatayo, naomba kunukuu: “thisapplication was uncalled for, superfluous and amounts toabuse of court process, thus devoid of any merit.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni suala la kisheria nawahusika wanaweza kuendelea kulishughulikia kupitiaMahakamani.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Yussuf Haji Khamis.

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Pamoja na mlolongo mrefu wa majibu yaMheshimiwa Waziri, lakini naomba niulize maswali mawilimadogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mataifa mbalimbali dunianiwanapozikamata meli kama hizi wanazitaifisha kwa ajili yakujenga uchumi wa ndani ya nchi yao. Ajabu sisi meli iletumeiacha imezama mahali (bandarini) ambapo hapanaupepo, hapana wimbi wala hapana dhoruba yoyote nakupoteza thamani kubwa ya meli ile. Je, Serikali inatamkatamko gani kuhusu suala hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwawashtakiwa wameingizwa hatiani: Je, utaratibu ganiuliotumika kuwaachia huru mpaka muda huu wakawa wakonje? Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na UtawalaBora.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA (K.n.y. WAZIRI WASHERIA NA KATIBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisaametolea mifano au ameelezea uzoefu wa nchi nyinginewanapokamata vyombo vya baharini au meli kama hizi.Kwanza, napenda tu kusema kwamba kwa Tanzania kufanyauamuzi ule waliouchukua imesaidia sana kukemea au ku-deter uvuvi haramu katika bahari zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia matukio ya ainahii kuanzia mwaka 2009 tangu uamuzi huu ulipochukuliwa,kwa kweli hata Wizara ya Uvuvi itakuwa ni shahidi na vyombovyetu vinavyofanya doria katika bahari zetu, matukio ya ainahii yamepungua sana. Kwa hiyo, kwa kweli na sisi Tanzaniakama nchi tumeweka mfano, tumeweka precedent ili nchi

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

nyingine na watu wengine wenye masuala kama hayawasitumie bahari zetu kwa makosa na kuchezea rasilimalizetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la pili laMheshimiwa Mbunge, kwamba ni utaratibu gani uliotumikakatika kuwaachia huru watuhumiwa; kama nilivyoeleza,mwaka 2014 Mkurugenzi wa Mashtaka ali-enter nolle kupitiaKifungu cha 98 ambacho anayo mamlaka kwa mujibu waSheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na masualamengine yaliyofuata hapo ilikuwa ni masuala ya diplomasiana waliweza kuachiwa huru.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali 137,linaulizwa na Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge waKibaha Mjini, linaelekezwa kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Na.137

Ujenzi wa Bomba la Maji Ruvu Juu - Kimara

MHE.SILVESTRY F. KOKA aliuza:-

Kazi kubwa ya ujenzi wa Mradi wa Bomba la Majikutoka Ruvu Juu kupitia Kibaha Mkoani Pwani hadi KimaraJijini Dar es Salaam, imeshafanyika.

Je, ni lini mradi huo kwa upande wa Kibaha Mjiniutakamilika na wananchi waweze kupata maji ya uhakika?

NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Majina Umwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa SilvestryFrancis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutumia mkopowa masharti nafuu kutoka Serikali ya India, imetekeleza mradiwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu, ulazaji wa bomba kuula kutoka Mlandizi hadi Kimara na ujenzi wa tanki jipya la

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Kibamba. Upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu uliogharimuDola za Marekani milioni 39.7 umeongeza uwezo wa mtambowa kuzalisha maji kutoka lita milioni 82 hadi lita milioni 196kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukamilika kwa upanuzi wamtambo wa Ruvu Juu na Ujenzi wa bomba kuu kutokaMlandizi hadi Kimara kumeongeza uwezo wa kuzalisha majiya kutosha na hivyo maeneo yenye mtandao wa mabombaya usambazaji ya Mlandizi, Kibaha na Kiluvya pamoja namaeneo ya Kibamba, Mlonganzila, Mbezi kwa Yusufu, Mbezimwisho, Kimara, Kilungule, Mavurunza, Baruti, Kibo, Kibangu,Tabata, Segerea, Kinyerezi, Vingunguti, Kipawa, Airport naKarakata yameanza kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, DAWASCO wako katikakampeni ya siku 90 ya kuunganisha wateja wotewanaohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu na Ruvu chini.Kwa upande wa Kibaha, DAWASCO wamepangakuwaunganishia maji wateja wapya elfu 30. Ombi langu kwawananchi, wapeleke maombi ya kuunganishiwa maji katikaOfisi za DAWASCO iliyoko katika maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Wizara yanguitaendelea kutenga fedha kwenye programu ya Maendeleoya Sekta ya Maji, Awamu ya Pili, ili kupanua mtandao wamabomba ya kusambaza maji na kuweza kuwapatiawananchi huduma ya maji safi na salama. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Koka.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nachukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa kazinzuri ya mradi huu mkubwa kwa takriban shilingi bilioni 90ambao umekamilika. Pamoja na pongezi hizi, ninayomaswali mawili madogo ya nyongeza. Bado kuna tatizo lamsukumo wa maji kutoka Ruvu Juu ili yaweze kuwa napressure ya kutosha kuwafikia watejea, tatizo linalotokanana uhafifu wa umeme. Je, Serikali ina mpango gani wa

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

kurekebisha tatizo hili, ili mradi huu uweze kuwa na mafanikiomakubwa zaidi hususan kwa wananchi wa Kibaha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; pamoja na kazinzuri hii, lakini bado maeneo ya Kidenge, Muheza, Kidagulo,Kikalabaka, Mikongeni na Mbwawa hawajakamilishiwamradi wa usambazaji wa maji ili waweze kufaidi mradi huu.Je, kupitia bajeti hii tunayokwenda nayo Mheshimiwa Waziriyupo tayari kushughulikia na kuhakikisha miradi hii inakamilikaili wananchi waweze kupata huduma hii nzuri kwa mradihuu ulio bora ambao umeshakamilika. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri Majina Umwagiliaji, Mheshimiwa Eng. Isack Kamwelwe, majibu.

NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa nampongeza sana MheshimiwaKoka kwa jinsi ambayo anawapenda wananchi wake waKibaha Mjini. Kwa sababu mara zote anafuatilia kwa kupigasimu kwa kuja Ofisini moja kwa moja, kumwona MheshimiwaWaziri pamoja na mimi kuhusiana na tatizo la maji la Mji waKibaha, kwa sababu Mji wa Kibaha kwa sasa unapanukasana. Swali la kwanza, pressure ni kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maji tuligunduakwamba hakukuwa na umeme wa kutosha ili kuwezakuendesha mtambo ule kwa sababu ni mkubwa. Kwa sababuhiyo, tulitenga fedha na tayari sasa kazi inafanyika naimeanza kukamilika ili kuwa na umeme wa kutosha ambaoutaweza kuendesha mtambo uliojengwa ambao ni mtambomkubwa. Kwa hiyo, hili suala Mheshimiwa Koka ni kwambatunalimaliza muda wote wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pil i, kamanilivyozungumza katika swali letu la msingi kwamba kupitiaawamu ya pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji,tunatenga fedha kuhakikisha kwamba maeneo yote yaKibaha na maeneo yote yanayopitiwa na bomba kuu lakutoka Ruvu kwenda Dar es Salaam tutahakikisha kwamba

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

tunaweka miundombinu ya kutosha ili wananchi wawezekupata maji, umbali wa kilomita 12 kutoka eneo la bomba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba programu hiyo tunayoambayo imeanza kutekelezwa kwenye mwaka wa fedha.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Joseph Haule nawa mwisho Mheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Katika ziara yake Naibu Waziri pale WilayaniKilosa alitembelea bwawa la Kidete na alijionea jinsiambavyo limekuwa likileta madhara makubwa ya mafurikona kuharibu mpaka reli kwenye Wilaya yetu ya Kilosa. Je, nilini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa hili la Kidete ambaloni muhimu kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri,majibu.

NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza ni kweli kabisa nilitembelea hilo eneona nikaenda kuona shida iliyoko katika lile bwawa. Palikuwana mkataba lakini tayari Serikali imechukua hatua yakuhakikisha kwamba sasa unafanyika usanifu upya na fedhailishatengwa katika bajeti ya mwaka huu tunaokwenda nao.Kwa hiyo, wakati wowote tutatangaza tenda baada yakukamilisha usanifu mpya ili tuweze kulijenga lile bwawakatika standard ile inayotakiwa isilete madhara tena kwawananchi wa Kilosa.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swalimoja tu dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa, Mkoa wetu waIringa una mito kama Ruaha, Mto Lukosi na kadhalika, lakiniwananchi wamekuwa wakipata shida sana kwa suala lamaji hasa vijijini ikiwepo Kilolo na Mufindi. Ni kwa nini Serikali

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

sasa isitumie mito hii kuondoa huu upungufu ambao upokatika Mkoa wetu wa Iringa? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri waMaji na Umwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli Mkoa wa Iringa una utajiri mkubwa sanawa mito ikiwepo Ruaha Mkuu, lakini bado kuna RuahaMdogo, kuna Mto Lukosi ambao unatokea maeneo ya Kilolo.Kutokana na utajiri huo wa kuwa na mito mingi, kwanzakabisa Mto Ruaha Iringa Mjini tumeutumia, maji yanapatikanakwa asilimia 100 katika Mji wa Iringa. Sasa hivi tunaanzakusambaza maji kuyapeleka nje ya Mji wa Iringa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutumia Mto Lukosi,nimeenda kule Kilolo, sasa hivi tunafanya utaratibu wakuhakikisha tunasanifu mradi ili tuweze kutoa maji Mto Lukosikuyapeleka maeneo yanayopitiwa na huo mto kuhakikishakwamba maeneo mengi ya Iringa yanakuwa na maji yakutosha ambayo ni safi na salama.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea tuyamalize hayamaswali mawili yaliyobaki. Muda ndiyo huo. Swali namba138, linaulizwa na Mheshimiwa Oliver Daniel Semuguruka,Mbunge wa Viti Maalum, linaelekezwa kwa Waziri wa Afya.

Na. 138

Upungufu wa Dawa Katika Hospitali za Serikali

MHE. ILIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:-

Upungufu wa dawa katika Hospitali mbalimbali zaSerikali nchini umeleta athari kubwa kwa wananchi wa Mkoawa Kagera na Wilaya zake zote:-

Je, Serikali inakiri uwepo wa upungufu wa dawanchini? Kama inakiri hivyo, inawaambia nini wananchikuhusu tatizo hilo?

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba yaMheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, naomba kujibu swali la Mheshimiwa OliverDaniel Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kulitaarifu Bungelako Tukufu kuwa mojawapo ya vipaumbele vya Serikali yaAwamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituovya kutolea huduma za afya kwa umma hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza azma hii,Serikali ya Awamu ya Tano ilichukua juhudi za makusudi kwakuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi bilioni 31 katikamwaka wa fedha wa 2015/2016 hadi kufikia shilingi bilioni251.5 katika mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha, napendakuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi kufikia mwezi Aprili, 2017jumla ya sh. 112,198,920,456/= zilishatolewa na kupelekwaBohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolea huduma zaafya vya umma kupata mahitaji yake ya dawa, vifaa, vifaatiba na vitendanishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia ongezeko hilo lafedha, hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika nakumbukumbu zilizopo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto zinaonesha kuwa hali ya upatikanajiwa dawa nchini imeimarika kwa kufikia asilimia 83. Kadhalika,hadi kufikia tarehe 15 mwezi Januari, 2017 Mkoa wa Kagerapekee umepokea kiasi cha sh. 4,150,767,216/= kupitia FunguNamba 52, yaani Wizara ya Afya, kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa, vifaa tiba na vitendanishi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Semuguruka.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.Kwa sasa MSD ina Bohari Kikanda. Je, Serikali ina mpangogani wa kufungua Bohari ya MSD kila Mkoa ili kurahisishausambazaji wa madawa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; Serikaliimejiandaaje kudhibiti upotevu, wizi wa dawa kwawatumishi wasio waaminifu katika zahanati na vituo vyaafya? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri,majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Swali la kwanza kuhusu Serikali kujenga bohari zadawa kila mkoa; kwamba tuna mpango gani; kwa sasahatujawa na mpango wa kufanya hivyo kwa sababutunaamini utaratibu wa kuwa na bohari kwenye kila kandabado haujakwama. Ni kwamba tunahitaji kufanyamaboresho kidogo tu ili tuweze kuongeza tija na ufanisikwenye kuhakikisha vituo vya umma vinapata dawa kadriambavyo vinahitaji na kwa haraka kadri ambavyoinawezekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mfumo wetu wasasa hivi wa Supply Chain Management, tunaamini badohaujakwama na ndiyo maana tumeendelea kuuboresha.Tulikuwa na changamoto kidogo za kifedha, ambazo kamaambavyo sisi Wabunge ni mashahidi na naomba nitumienafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli, kwa azma yake thabiti ya kuongezaupatikanaji wa dawa kwa kutuongezea bajeti kwenye eneohili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, changamoto yakifedha tuliyokuwanayo ambayo ilikuwa inashusha tija na

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

ufanisi, sasa inaelekea kuondoka na mfumo wa upatikanajiwa dawa umeimarika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuhusu udhibiti,naomba nitumie Bunge lako Tukufu kuwaombaWaheshimiwa Wabunge wote, Madiwani wote na Viongoziwote kuanzia Viongozi wa Mikoa na Wilaya washirikikikamilifu katika kusimamia udhibiti wa mfumo waupatikanaji wa dawa kwenye vituo vyetu kwa sababu,jambo hili haliwezi kuwa ni la sisi tu tuliopo Fungu 52, kwamaana ya Wizara ya Afya pekee. Kwa sababu, mfumo wetuwa udhibiti upo, kwamba kwenye kila zahanati, kila Kituocha Afya na kwenye kila hospitali, kuna Kamati ya Udhibitiwa Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi ambapo ndaniyake kuna viongozi wa kuchaguliwa na kuna watendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni kwamba, mfumohuu hausimamiwi ipasavyo. Kama ungefanya kazi ipasavyo,kwa hakika, tungeweza kudhibiti wizi na ubadhirifu wamadawa ambao umekuwa ukitokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu, kama kuna mtuana taarifa yoyote ile ya mahali ambapo kuna wizi amaupotevu wa dawa ambao umejitokeza, atupe taarifa nasisi tutachukua hatua haraka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anna Gidarya naMheshimiwa Bulembo wa mwisho.

MHE. ANNA J. GIDARYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza. Ugonjwa wa fistula ni ugonjwa ambao umeeneakaribu Tanzania nzima. Ugonjwa huu unawadhalilishaakinamama, hususan mikoa yetu ambayo ina jamii yawafugaji, watu ambao hawahudhurii mara nyingi kliniki. Je,Wizara ina mpango mkakati gani wa kutoa elimu hii kwakila Wilaya, hasa kwa jamii hii ya wafugaji? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri,majibu.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwanza nakubaliana na Mheshimiwa Gidaryakwamba ugonjwa wa fistula unawadhalilisha sana mamazetu, shangazi zetu, dada zetu katika jamii. Ni jambo ambalomwanaume yeyote ambaye anawapenda mama zetu nadada zetu hawezi kukubaliana nalo. Nami kama Balozi waWanawake nimhakikishie tu kwamba tutaendelea kuboreshahuduma za uzazi kwa sababu ndiyo kisababishi kikubwa chaugonjwa wa fistula ili kupunguza cases za fistula ambazozimekuwa zikijitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango tulionao kwa sasani kutumia kliniki zetu za uzazi ambazo zipo kwenye kila kituocha kutolea huduma za afya, kuanzia ngazi ya zahanatikwenda ngazi ya kituo cha afya, ngazi ya hospitali ya wilayampaka ngazi ya hospitali za rufaa, kutoa elimu kwaakinamama wote na akinababa wote ambao wanafikakuhudhuria kliniki za uzazi salama katika vituo vyetu vyakutolea huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa changamotozinazojitokeza za tiba zimekuwepo na tunaendeleakuzipunguza kwa kuendelea kutoa ujuzi, lakini pia elimu kwaumma juu ya kuwahi kupata huduma za uzazi ili wasipatemadhara yanayotokana na mchakato wa uzazi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulembo.

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii nami niulize swali moja lanyongeza. Kwa kuwa, tatizo linalozikabili zahanati nyinginchini siyo upungufu wa dawa tu, bali pia huduma kwaakinamama wajawazito, hususan katika wodi zao hudumani mbaya, ni hafifu, vifaa stahiki hakuna: Je, ni lini Serikaliitahakikisha inaboresha afya kwa akinamama wajawazitokatika hospitali na zahanati zote za Mkoa wa Kagera?(Kicheko/Makofi)

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

MWENYEKITI: Eeh, leo! Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla, utoe majibu ya uhakika hapo, kama Balozi waWanawake. (Kicheko/Makofi)

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naomba nitoe majibu ya uhakika kwamba, kwanzanimkumbushe Mheshimiwa Halima Bulembo kwamba kwenyeIlani ya Uchaguzi ya CCM katika vipaumbele vitano kwenyeSekta ya Afya ambavyo vimeandikwa mle ni pamoja nakuboresha huduma za akinamama wajawazito na watoto.

Kwa maana hiyo, naye kama Mwana-CCMmwenzangu lazima anafahamu kwamba jitihada zakupunguza matatizo na changamoto mbalimbali zilizopokwenye huduma za akinamama wajawazito, zimekuwepo,zitaendelea kuwepo na ndiyo maana hata leotutakapowasilisha bajeti yetu ataona tuna mikakati mahususiambayo imejikita kwenye kuboresha huduma za uzazi kwaakinamama wajawazito. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli hili ni jamboambalo Mheshimiwa Rais mwenyewe alilizungumza pia hapaBungeni na sisi wakati anatukabidhi majukumu hayaalituagiza tulisimamie kwa nguvu za kutosha. Kwa hiyo, nijambo ambalo kwa hakika hatulifanyii mzaha hata kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu MheshimiwaMbunge kwamba huduma za uzazi zitakuwa bora na yeyeatajifungua salama kadiri Mungu atakavyomsaidia. (Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali letu lamwisho kwa leo. Swali namba 139, linaulizwa na MheshimiwaMary Pius Chatanda, Mbunge wa Korogwe Mjini,linaelekezwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Na. 139

Ujenzi wa Jengo la Maktaba Chuo cha Ualimu Korogwe

MHE. MARY P. CHATANDA aliuliza:-

Mwaka 2001, Chuo cha Ualimu Korogwe kwakushirikiana na wananchi, walianza ujenzi wa maktabaambayo bado haijakamilika; na kwa kuwa wanachuo nawananchi wa Korogwe wanahitaji sana maktaba hiyo:-

Je, Serikali itakuwa tayari kusaidia juhudizilizokwishaanza ili kukamilisha jengo hilo?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mary Pius Chatanda, Mbunge wa Korogwe Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu wamaktaba hiyo kwa Wanajumuiya wa Chuo cha UalimuKorogwe na wananchi kwa ujumla, Wizara yangu iko tayarikusaidia ujenzi wa maktaba hiyo na hivyo itatuma wataalamkwenda kufanya tathmini ya hatua iliyofikiwa na msaadaunaohitajika ili ujenzi huo uweze kukamilika katika mwakawa fedha wa 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kutokana na jinsiwananchi wa Korogwe wanavyoshirikiana vizuri na Mbungewao, Mheshimiwa Mary Pius Chatanda, kuunga mkono juhudiza Serikali katika kuboresha elimu.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mary Chatanda,swali la nyongeza.

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kwanza nampongeza Waziri wa Elimu na Naibu

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

wake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu kwa kazi nzuriambayo wanaifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa basi, Mheshimiwa NaibuWaziri atakuwa tayari kufuatana nami ili aweze kuangalialile jengo ili kusudi waweze kutoa kitu ambacho kinalinganana kazi ambayo inakusudiwa kumaliziwa?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu ni ndiyooo! (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Haya, tumemaliza kwa leo. Nisababu ya muda tu Waheshimiwa.

Matangazo ya wageni waliopo leo hapa Bungeni,kwenye Jukwaa la Spika, tunao wageni watatu waMheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu kutokaWizara yake ambao ni Ndugu Sihaba Nkinga, Katibu MkuuIdara Kuu ya Maendeleo ya Jamii. Tunaye pia Dkt. MpokiUlisubisya, Katibu Mkuu Idara Kuu ya Afya; na pia tunaye Dkt.Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI),anayeshughulikia afya. Pia hawa wageni watatuwameambatana na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi, Idarana Maafisa mbalimbali waliopo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Karibuni sana,leo ndiyo Wizara yetu. (Makofi)

Wageni wengine, sidhani kama wanamjumuisha naMheshimiwa Halima Bulembo, lakini ni wajawazito 12wanaowawakilisha wenzao Tanzania nzima. Nirudie? Eeh!(Kicheko/Makofi)

Wageni wengine ni wajawazito 12wanaowawakilisha wenzao Tanzania nzima. Karibuni sana.Pia Wameambatana na Wauguzi wao wawili na Wajumbewawili kutoka Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Salama, wakiongozwa na Ndugu Rose Mlay, Mratibu wa Taifawa The White Ribbon Alliance for Safe Motherhood in Tanzania.Karibuni sana. (Makofi)

Pia, tunao wageni mbalimbali wa WaheshimiwaWabunge pamoja na wanafunzi waliotembelea hapaBungeni kwa ajili ya mafunzo.

Mheshimiwa Joseph Selasini, Mwenyekiti wa Jumuiyaya St. Thomas More hapa Bungeni anawatangazia WakristoWakatoliki wote, leo Jumatano, terehe 3 Mei, 2017 kutakuwana Ibada ya Misa mara baada ya kuahirisha Bunge saa 7.00mchana katika Kanisa Dogo lililopo ghorofa ya pili, Ukumbiwa Msekwa.

Waheshimiwa Wabunge wengine pia mnakaribishwakushiriki katika ibada hii takatifu.

Hayo ndio matangazo niliyonayo. Katibu!

NDG. ZAINAB ISSA – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwaMwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MBUNGE FULANI: Kuhusu jambo la dharura.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Mwenyekiti.

MWONGOZO WA SPIKA

MWENYEKITI: Nitajie tu jina lako Mheshimiwa.

MHE. RHODA KUNCHELA: Rhoda Kunchela.

MWENYEKITI: Nitajie jina lako.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: InnocentBashungwa.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Rhoda Kunchela.

MWENYEKITI: Kwa hiyo, nina hawa WaheshimiwaYussuf Hussein, Rhoda Kunchela na Mheshimiwa Innocent.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Na Kakunda, hukuniona.

MWENYEKITI: Waheshimiwa, nikisema msimame, basimsimame. Mheshimiwa Joseph Kakunda.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesimama kwa Kanuni ya 68(7). Wakati nilipouliza swali lanyongeza kuhusu barabara ya Sikonge – Mibono – Kipili,Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba Serikalihairuhusiwi kuweka bajeti kubwa kwa ajili ya kutoboabarabara, lakini hapo hapo akaweka commitment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaridhika na jibu hilo, naonakama siyo sahihi kwa sababu Serikali ninavyojua jinsiinavyohudumia watu, inaruhusiwa kupanga bajeti kwa ajiliya kuwahudumia wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba utoemaelekezo tupate ufafanuzi wa kina jinsi Serikaliitakavyotekeleza ile commitment ambayo wameisema hapaili kusudi wananchi wangu wa Sikonge waweze kupatacommitment ambayo inaridhisha. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa InnocentBashungwa.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kutumiaKanuni ya 47(1) kuzungumzia jambo la dharura ambalolimetokea Jimboni kwangu Karagwe.

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kijiji cha Mguruka Kataya Bwelanyange Jimbo la Karagwe hivi ninavyozungumza,kaya zaidi ya 300 zimepewa Eviction Order na Wizara yaMaliasili na Utalii kupitia Game Officers wa Pori la Akiba laKimisi, kwamba wananchi ambao wanaishi kwenye Vitongojivya Mguruka, Rweizinga na Misenyi waondoke kwenyevitongoji hivyo ndani ya siku tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linasikitisha kwasababu Kijiji cha Mguruka kimekuwepo kabla hili Pori la Akibala Kimisi halijawa gazetted kisheria. Vitongoji hivi viko chiniya TAMISEMI kwa mujibu wa Sheria za TAMISEMI na vinapatahuduma kama kawaida.

Kwa hiyo, Eviction Order hii ambayo imetolewa naWizara ya Maliasili ni kandamizi, onevu na inawarudishawananchi kwenye umaskini. Kwa sababu hivininavyozungumza, wananchi hao wamelima, wana mifugona hivi sasa wameambiwa ndani ya siku tatu wawewameondoka kwenye hayo maeneo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hili jambo nimahususi na changamoto za migogoro kati ya Vijiji na Maporiya Akiba hayako Karagwe tu, ni nchi nzima, naomba kupitiaKanuni ya 47(1) nitoe hoja ili jambo hili lijadiliwe na Bunge nanaomba Waheshimiwa Wabunge wenzangu mniungemkono. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea. MheshimiwaYussuf Hussein.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Nina tatizo hapa na nimeshaliripoti kwa Watendajimara tatu. Watendaji walichukua hatua wakaniambiawameshindwa. Nimeshaliripoti kwenye kiti chako mara tatuakiwepo Spika, Naibu Spika na Mwenyekiti, MheshimiwaZungu, sijapata jibu. Jana nimeliripoti nikaambiwa nikiingiaBungeni jioni tatizo hilo litakuwa limerekebishwa.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi hivi sasaninapozungumza, tatizo hilo halijarekebishwa. Kiti changuninachokalia kimevuka hii cover, imekuwa kama teitei,inachafua nguo na kuharibu kila kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba mwongozowako, nitumie kanuni gani ili niweze kuingia na fundi humundani anitengenezee hiki kiti? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Rhoda Kunchela.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nasimama kwa Kanuni ya 68(7), kwa sababu yamuda sitaisoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyoongea katikaMkoa wa Katavi, Manispaa ya Mpanda kuna wafanyakaziwanne wamelazwa hospitali; wawili wana pressure lakiniwengine wametundikiwa drip. Hii ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni MheshimiwaRais alipokea ripoti ya majina ya watuhumiwa wanaotumiavyeti feki. Katika hao wagonjwa ambao wapo hospitaliwengine walikuwa masomoni wametuhumiwa kwambawana vyeti feki, lakini wengine ni wastaafu na wenginehawajamaliza wala hawajawahi kusoma sekondari lakini piawametuhumiwa wana vyeti feki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako,kama ni Serikali ilitoa ripoti hii bila kuhakiki vizuri haya majinana hawa watuhumiwa ambao sasa wapo hospitali wenginewamelazwa na wengine wamezimia; nini tamko la Serikalikwamba hawa watu waliotuhumiwa na kwambawameonewa na ikiwa kuna baadhi ya watu wanamzungukaMheshimiwa Rais lakini pia hawajaguswa: Sasa hawa watuambao wameonewa nini kifanyike ili wasafishwe na ninitamko la Serikali ili kuwanusuru hali yao ya kiafya. (Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

MWENYEKITI: Nianze na hili la Mheshimiwa YussufHussein. Niseme, kalieleza kwa uchungu, lakini naaminiWaheshimiwa Wabunge wengine wangesimama. Jiraniyangu hapo kwenye kiti changu ninapokaa Mheshimiwa Dkt.Kikwembe, kiti chenyewe; na jirani yangu Mheshimiwa Mussapale; naweza nikataja kule ambapo huwa napitia mimi kule.

Kwa hiyo, hili ni tatizo ambalo Ofisi ya Katibu waBunge wanalifanyia kazi. Wanaomba uvumilivu tuWaheshimiwa Wabunge; pia na Serikali watuelewe kwa hilikwa sababu Bunge liliahidi kulishughulikia suala hili nawalitegemea zile fedha ambazo zilipaswa kuwa zimefika sasakwamba washughulike, maana lilikuwa kwenye bajeti yamwaka huu. Kwa hiyo, bado ni matarajio yetu kwamba hilolitatekelezwa na upande wa Serikali ili turejeshe heshima yaWaheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Hussein huhitaji kuingia humu na fundiwako, hapana. Bunge litatekeleza hayo ili muweze kukaakwa staha, lakini pia nguo zenu ziendelee kuwa nadhifu namavazi yenu yaendelee kuwa nadhifu. Kwa hiyo, hilo limekaavizuri, tuvumiliane tu. Nami pia nitakwenda kumkumbushiaMheshimiwa Spika na Katibu wa Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Joseph Kakunda, nadhani kamahukujibiwa kikamilifu na Mheshimiwa Naibu Waziri,nisingependa sana nichukue muda wa Bunge hili kwendakusoma Hansard ya jibu lililotolewa. Kwa vile Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano na Naibu wake aliyejibu swali kwaniaba yake yupo, suala hili mwongozo wangu ni kwambahebu sasa wakupatie yale maelezo mazuri kuhusiana namatumizi ya fedha za barabara kwa wananchi wa Sikonge.Jana tu tumepitisha bajeti ya Wizara hii, nadhani ndiyo mudamuafaka kuweza kulisemea suala hili kama kweli kwenyebajeti ya mwaka ujao wa fedha sehemu ya barabaraambayo umeisemea imetengewa fedha.

Mheshimiwa Innocent Bashungwa, dharura.Nawavumilieni tu. Umesikika, lakini ni jambo ambalohalikutokea leo Bungeni hapa mapema, lakini Serikali imo

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

humu Bungeni na maeneo haya kama yanatambuliwakisheria na Wizara yenyewe, wewe unasema wananchi hawajana wamepewa Eviction Order waondoke ndani ya siku tatu,basi nadhani Serikali kwa ajili ya kuwapatia comfort wananchihawa katika maeneo unayowakilisha wewe, mwongozowangu ni kwamba Serikali i je itoe tu maelezo kwaWaheshimiwa Wabunge na Watanzania wa maeneo hayona mengine ambayo yataguswa na operesheni hiyo iliwaweze kujua ni nini ambacho kinaendelea. Hii operesheninaamini inaweza ikafika hata kwangu Bariadi kule Serengeti.(Makofi)

Kwa hiyo, tuwe na uelewa wa pamoja kama viongoziwa nchi hii na kwa faida ya wananchi wetu wa maeneohayo. Serikali itajipanga ni lini wanataka kutoa kauli hiyokatika Bunge hili. Kama Waziri anaweza akasimama baadayeakalisemea, itakuwa ni vyema tu.

Mheshimiwa Kunchela, hawa wagonjwa umesemani mshtuko wa moyo wa vyeti! Sasa nadhani mwongozowangu kwa hilo, Serikali hii ni makini sana, napenda kuaminihivyo na Waziri mwenye dhamana ya masuala haya yumoBungeni. Nadhani anaweza akalitolea taarifa kwa haoambao wameonewa au wanajiaminisha kwambawameonewa au wanadhani kwamba wameonewa ni niniwafanye; na utaratibu gani ufuatwe? Nadhani ndichokinachoweza kufanyika. (Makofi)

Kwa hiyo, huo ndiyo mwongozo wangu. Sasa kwaupande wa Serikali, kama Mheshimiwa Profesa Maghembeunataka kusema hapa, sawa. Mheshimiwa Angellah Kairuki.(Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, Serikali tumepokea miongozo hapa miwili,tunaona kwamba hiyo tunaweza tukaitolea maelezo. Kwamwongozo unaohusu Wizara ya Maliasili, Mheshimiwa Waziri

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

ameridhia Mheshimiwa Naibu Waziri atoe maelezo sasa hivi.Mwongozo unaohusu masuala ya utumishi na vyeti atafuatiaMheshimiwa Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ridhaa yako, basitunaomba Serikali i-respond kwenye mambo hayo. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Chief Whip .Mheshimiwa Dkt. Eng. Ramo Makani.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,napenda kutoa maelezo kwa ufupi kama ifuatavyo ili niwezekujenga mazingira ya kukuwezesha kutoa mwongozo kuhususuala lililoletwa mbele yako na Mheshimiwa InnocentBashungwa, Mbunge wa Karagwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongezaMheshimiwa Innocent Bashungwa pamoja na Wabungewote wa Mkoa wa Kagera, lakini pia hata Mkoa wa jirani waKigoma kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakifuatilia masualayanayohusiana na mahusiano baina ya wananchi na hifadhizilizopo kwenye maeneo yao na hususan wahifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala ambalo MheshimiwaMbunge amelileta mbele ya Bunge leo hii, liliwahi kuletwapia na Mheshimiwa Magdalena Sakaya na maelezoyaliyotolewa awali yalikuwa kama ifuatavyo; na nitayatoanikiwa nimeweka na nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwa upande waSerikali kwa sasa tunayo Kamati inayohusisha Wizara nne kwakuanzia; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) pamojana Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati hii inachokifanyasasa hivi, inaratibu kazi ya awali itakayotoa mwongozo juuya kuweza kutatua tatizo hili la mahusiano kati ya wananchiwanaoishi jirani ya hifadhi na hifadhi zenyewe. Sasa jambo

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

hili kama ambayo wewe na Wabunge wote kwa ujumlatunavyofahamu, kwanza ni la muda mrefu halafu ni kubwana limekuwa gumu kwa muda mrefu na kwa hiyo, kamaunaweka mfano wa ugonjwa ni kwamba na tiba yake pialazima itafuata mkondo huo huo kwamba itakuwa ni kubwana inahitaji pia muda wa kutosha kuweza kulishughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara ya mwisho Serikalitulisema kwamba Kamati hii imefika mahali ambapo kaziyake ya awali imeshakabidhiwa kwenye Kamati Maalum yaMakatibu Wakuu na kwamba baada ya hatua hiyo, kazi hiyoitakwenda kwenye ngazi ya Baraza la Mawaziri na baadayekwenye uongozi wa juu wa Serikali ili kuweza kutoa mwongozokamili wa kutatua tatizo hili la muda mrefu, kubwa na gumukatika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ieleweke kwamba matatizoau changamoto zinazohusiana na masuala ya uhifadhihayako sawa nchi nzima. Yako maeneo menginechangamoto hizi ni kubwa zaidi, maeneo mengine ni wastanina pengine kuna maeneo ambayo hayana kabisa matatizohaya. Kwa hiyo, ufumbuzi wake pia unataka kuangaliamaeneo kama yalivyo na kupata ufumbuzi mahususikulingana na eneo jinsi lilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto za Wilaya yaKaragwe na maeneo mengine yanayofanana nayo nikwamba sasa hivi zoezi linaloendelea kwa upande wa Serikalikupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, tunachokifanya ni kuwekamipaka kwenye hifadhi hizo. Zoezi la uwekaji wa mipaka niuwekaji wa alama. Mipaka ipo tangu siku nyingi kwa mujibuwa sheria, lakini ipo kitaalam GPS Coordinates zipo kwamujibu wa sheria na kwa mujibu wa GN zilizounda maeneohayo, lakini mipaka physically haikuwahi kuwekwa katikabaadhi ya maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi hili linaendelea nakatika baadhi ya maeneo uwekaji wa alama hizi ndiyouliokuja kuleta changamoto kwamba wananchi wanafikirikwamba alama hizo zinawekwa kwa mara ya kwanza na

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

kwa hiyo, wanaona kwamba pengine Serikali inawekamipaka kwenye maeneo ambayo siyo ya hifadhi.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.Huku nyuma!

MWENYEKITI: Kwa nini usimwachie amalize? EndeleaMheshimiwa.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na kazi yote hiyo ambayo inafanyikahivi sasa, nimesema kwamba kila eneo linakuwa nachangamoto zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hiki ambachokimetolewa taarifa sasa hivi ya kuomba mwongozo naMheshimiwa Bashungwa ni tukio ambalo linahitaji kupatahali halisi kama ilivyo hivi sasa ili tuweze kuwianisha kati yakazi ile ambayo ndiyo tulikuwa tunaifanya siku zote na hikiambacho kimejitokeza pengine suala la kuhamisha watukwa mtindo huu ambao ameuelezea ni suala ambalo sisikama Serikali tunatakiwa kwenda kupata first handinformation tulione jinsi lilivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa maelezomafupi yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI janawakati akiwa anafafanua jambo linalofanana na hili, nikwamba kama Serikali sasa jambo la kufanya katika kipindihiki cha Bunge haraka iwezekanavyo, tutakachokifanya nikukimbia kwenda kuona hali halisi jinsi ilivyo katika eneo hililinalotajwa kwa Mheshimiwa Bashungwa ili kuweza kuonanamna ya kuweza kupata suluhisho la haraka la sasa hiviwakati tukiwa tunaendelea na suluhisho lile la muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kufupisha,niseme tu kwamba ili kuweza kufahamu uhalisia, tutajipangakuweza kwenda kuona hali halisi jinsi ilivyo ili kuweza kwendakutatua yale matatizo ambayo yanawezekana kutatua sasahivi kwa haraka wakati tukiwa tunasubiri ufumbuzi wa mudamrefu. (Makofi)

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

MWENYEKITI: Ahsante. Fanyeni hivyo kwa haraka kwasababu suala hili siyo dogo. Maelezo ni mazuri sana kwambautatuzi wa suala hili utategemea hali halisi ya mahali tatizolenyewe lilipo, lakini kwa vile linajirudia rudia, Serikali ingefanyakupitia Wizara ya Maliasili na Utalii msiishie Karagwe tu,nendeni kwenye maeneo yote ambayo tunajua.

Nimeletewa message jana kwamba kuna operesheniinakuja kwenye maeneo ya mpaka wetu na Serengeti. Sasakwa vile Mheshimiwa Bashungwa amesema kuna EvictionOrder, sasa mimi sijui, siku nyingi sijaisoma sheria yetu hiyo,Eviction Order hiyo ni ya Mahakama? Kwa sababu kama niya Mahakama inachukua sura tofauti. Sasa ni vyematukalifahamu vizuri suala hili kwa uharaka. Hata hivyo,nashukuru kwa maelezo hayo na uharaka wa Serikali wakuweza kukubali kuelekea kwenye eneo la tukio. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii kuweza kutoaufafanuzi kuhusiana na mwongozo ulioombwa na Mbungewa Viti Maalum, kutoka Katavi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili liko katika pandenyingi. Toka tarehe 28 tulipokabidhi taarifa ya uhakiki kwaMheshimiwa Rais, wako wengi tu na hata wengine niWaheshimiwa Wabunge, siyo kwamba wana vyeti feki lakiniunakuta wamepiga wakifuatilia taarifa za ndugu zao nawengine wengi. Ila unapowabana kwa undani, unajua mtuanapopata taarifa kwa haraka wengine hawakubali, wakokwenye denial na obviously wengine, niseme baadhi maanayake bado nitakapoeleza utaratibu mwingine tutakujakuhitimisha; kwa ndugu zao wanawaeleza kwambawameonewa; lakini ukibana vizuri, MheshimiwaSimbachawene amepokea, mimi nimepokea wengi nawengi tu nina uhakika wamepokea, wanakuja ku-admitkwamba kweli somewhere somehow kuna cheti niligushi.

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa napenda kusema hivi,kwa kutambua hilo na kuweza kutoa fursa kwa haowaliolazwa na kwa wengine ambao wanaonahawajatendewa haki. Bahati nzuri leo hii Katibu Mkuu wanguatakuwa na Press Conference saa 5.00, ndani ya dakika 15zijazo kutoa utaratibu wa suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachotakiwa kufanyikasasa, Mheshimiwa Rais alishaelekeza by tarehe 15, Mei kwawale ambao watakuwa hawajajiondoa tunafuata taratibunyingine katika sheria na vyombo vya dola.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Naomba tusikilizane,mliomba mwongozo, kwa hiyo, tusikilizane.

Kwa wale ambao wanaona wana lolote la kuripotina kwamba wanaona taarifa za NECTA siyo sahihi,wanatakiwa kuandika barua ya kukata rufaa kwa KatibuMkuu wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma, nakala iendeBaraza la Mitihani na ipitishwe kwa mwajiri wao naiambatishe vyeti vilevile ambavyo viko katika jalada lakebinafsi la kiutumishi na ambavyo ndivyo vilihakikiwa kwamara ya kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwajiri akishavipitisha,atavipeleka moja kwa moja Baraza la Mitihani halafu seti hiyonyingine itapelekwa kwa Katibu Mkuu Utumishi. Tutavipitiakwa kina kuliko hata awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe tu kutoaangalizo, tusifanye nalo mzaha kwa wale ambaowanatusikiliza. Tunatoa ruhusa hiyo ya rufani lakini kweli iwemtu ana uhakika anaona ameonewa, kwa sababuitakapotokea mtu ametumia fursa hii ya rufani na anaujuaukweli na matokeo yakarudi vilevile, kwa kweli adhabuitakuwa ni kali zaidi. (Makofi)

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelezo yangu ni hayo.Tumetoa fursa hiyo na wafuatilie kwa karibu zaidi kupitia portalyetu ya Human Capital Management Information System auTaarifa za Kiutumishi na Mishahara maarufu kama Lawson,tangazo zima litakuwa limewekwa, waweze kufuatilia pia…

MBUNGE FULANI: Bashite!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: …kwa Maafisa waowa utumishi na wataweza kuona taarifa kamili na ninikinapaswa kufanyika lakini maelezo ya kina, saa 5.00 kamiliKatibu Mkuu wangu atafanya Press Conference hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naaminiwahusika hao wala wasipandishe pressure, wawe na utulivuwa hali ya juu. Kama wanaona wana haki, haki yaowataipata, lakini kama wanaona kuna kuzungushachochote, adhabu itakuwa kali zaidi.

MBUNGE FULANI: Daudi.

MWENYEKITI: Ahsante kwa ufafanuzi huo.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea…

MBUNGE FULANI: Kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Unanipa mimi utaratibu? Mheshimiwa,unanipa mimi utaratibu?

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuniinasema wakati wowote naweza kuomba kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Nakuuliza, unanipa mimi utaratibu?Nimekiuka nini?

MBUNGE FULANI: Mwongozo. (Kicheko)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Kiti.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nawavumiliatu.

MWENYEKITI: Sasa namwita Mtoa Hoja, MheshimiwaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto. (Makofi)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kablaya kuendelea, hotuba yangu yote iingie katika Hansard kamanilivyoiweka Mezani. La pili, nawaomba WaheshimiwaWabunge katika ukurasa wa 100 wa hotuba yangu, kichwacha habari cha jedwali lile ni Hali ya Upatikanaji wa Fedhaza Dawa kuanzia Mwaka 2015/2016 na Mwelekeo wa mwaka2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuwasilishwaTaarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaHuduma na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufuambayo imechambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, naomba sasa kutoa hojakwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifaya Utekelezaji wa Kazi za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka 2016/2017, vipaumbelevya Wizara kwa mwaka 2017/2018. Aidha, naliomba Bungelako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya kawaida na Mpango wa Maendeleo wa Wizarakwa Mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kumshukuruMwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezeshakusimama hapa, napenda kuchukua fursa hii kwa heshimana unyenyekevu mkubwa kumshukuru kwa dhati MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, kwa uongozi wake imara kwa nchi yetu namaelekezo yake ambayo yamekuwa dira sahihi katikautendaji wangu na katika kuimarisha huduma za afya, ustawiwa jamii na maendeleo ya jamii.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, nampongezaMheshimiwa Rais kwa kuweka chachu katika kudhibitimatumizi ya dawa za kulevya nchini ikiwa ni jitihada zake zakulinda afya za Watanzania hasa vijana ambao ndionguvukazi ya Taifa letu. Kwa hali hiyo, Wizara yanguitaendelea kuelimisha na kuhimiza umma wa Watanzaniakuhusu madhara yatokanayo na madawa ya kulevya lakinipia kuzingatia mfumo bora wa maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kutoashukurani zangu za dhati kwa Mheshimiwa mama SamiaSuluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa miongozo na ushauri wake wa dhati, hasakatika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto namasuala ya kuwawezesha wanawake kiuchumi. Wizarayangu itaendelea kutumia taswira yake, ushawishi wake nauzoefu wake ili kujenga jamii ya Watanzania inayowajali,kuheshimu na kuwaendeleza wanawake na wasichana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuchukua fursahii kumshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongoziwake ambao umesaidia kuongeza ufanisi katika utendajindani ya Wizara yangu. Pia nampongeza kwa hotuba yakealiyoiwasil isha ambayo imetoa dira ya jinsi Serikaliitakavyotekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedhawa 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakupongeza wewe naWenyeviti wote, Mheshimiwa Spika na Mheshimiwa NaibuSpika kwa kuendelea kulisimamia Bunge letu Tukufu. Nimalizepia kumpongeza Mheshimiwa George Simbachawene, Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kwa ushirikiano wakeanaonipatia katika kusimamia na kuboresha utoaji wahuduma za afya ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nawashukuru kwaheshima na unyenyekevu mkubwa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekitiwake, Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba na Makamu

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mwenyekiti, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu kwa ushauri namaelekezo yao. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wotekwa ushauri, maoni ambayo mmekuwa mkitupatia katikautendaji wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba yangunimepongeza Waheshimiwa Wabunge wote walioingiakatika Bunge letu Tukufu katika kipindi cha 2016/2017, lakinipia nimetoa pole kwa Wabunge wenzetu waliotanguliambele za haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pole pia kwawagonjwa na majeruhi wa ajali waliopo hospitalini namajumbani lakini pia wahanga wa vitendo vya ukatili naunyanyasaji wa kijinsia. Namwomba Mwenyezi Munguawaponye haraka ili waweze kuendelea na ujenzi wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, sasaniruhusu nizungumzie utekelezaji wa shughuli za Wizara kwamwaka 2016/2017, vipaumbele vya Wizara vya mwaka wa2017/2018 pamoja na maombi ya fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunatekelezamajukumu yetu tumezingatia sera, mipango na mikakatimbalimbali ya Kitaifa, lakini nitaje tu kwamba tumezingatiaSera ya Afya ya 2007, Mpango Mkakati wa Pili wa Sekta yaAfya wa 2016 - 2020, Mpango wa Maendeleo wa Afya yaMsingi, lakini pia tumezingatia Sera ya Taifa ya Wazee, Seraya Maendeleo ya Jamii, Sera ya Maendeleo ya Mtoto, Seraya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia na Sera ya Taifa yaMashirika Yasiyo ya Kiserikali. Tumezingatia pia malengoyaliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya chama changu,Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 - 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mapato na matumizikwa upande wa Fungu 52, hadi kufikia mwezi Machi, Wizaraimekusanya takriban shilingi bilioni 118.7 sawa na asilimia 75ya makadirio. Pia kwa upande wa mapokeo ya fedha,tumepokea shilingi bilioni 339.1 ambayo ni sawa na asilimia43 ya fedha zilizoidhinishwa.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kwa upande wafedha za maendeleo, Wizara imepokea shilingi bilioni 133.8sawa na asilimia 26 ya fedha zilizotengwa, lakini piatumepokea vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingibilioni 256.2 kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana naUKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu ikiwa ni sehemu ya utekelezajiwa miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Fungu 53, Wizaraimekusanya shilingi milioni 930.2 ambayo ni sawa na asilimia39 ya makusanyo yaliyotarajiwa. Hadi kufikia mwezi Machi,2017, fedha za matumizi mengineyo zilizopokelewa ni shilingibilioni 4.9 sawa na asilimia 28.4 ya bajeti iliyoidhinishwa napia kwa upande wa miradi ya maendeleo, Wizara imepokeashilingi milioni 204.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi sasanitazungumzia kazi maalum zil izotekelezwa, lakinisitazungumzia zote, nitajikita katika masuala muhimu. Sualala kwanza ni huduma za kinga. Lengo la kutoa huduma zakinga ni kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na magonjwayasiyo ya kuambukiza. Kwa hiyo, tumefanya kazi katikamaeneo ya chanjo, huduma za uzazi na mtoto, lishe pamojana utoaji elimu kwa afya ya umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu chanjo, nimeelezakatika aya ya 18 ya hotuba yangu. Kupitia Mpango wa Taifawa Chanjo tumehakikisha kuwepo kwa chanjo za kutoshakwa ajili ya huduma za chanjo kwa watoto na makundimengine. Chanjo tulizonunua nimeziainisha katika aya ya 18ya hotuba yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja ambalo natakaBunge lako litambue ni kwamba hatuna tatizo la uhaba wachanjo za watoto katika nchi yetu na nchi yetu imekuwa nimiongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika utoaji wahuduma za chanjo kwa mwaka 2016 ambapo tuliwezakuvuka lengo kwa kufikia kiwango cha asilimia 97. Tumenunua

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

magari tisa kwa ajili ya kuboresha huduma za usambazajiwa chanjo lakini pia tumenunua majokofu 317 ya kutunziachanjo kwa ajili ya Vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usafi wa mazingira;tumeendelea kuratibu kampeni ya Kitaifa ya usafi wamazingira na nafurahi kulitaarifu Bunge lako kwamba kupitiakampeni hii kaya 391,337 zimejenga vyoo bora. Kati ya hizi,kaya 320,894 zina sehemu ya kunawia mikono mara baadaya kutoka chooni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuongeza chachu yaushindani katika kuboresha huduma za usafi wa mazingira,tumeweza kuendesha mashindano na kuitunuku Halmashauriya Wilaya ya Njombe kwa kuwa mshindi wa jumla Kitaifaambapo tumeipatia gari aina ya Toyota Land Cruiser HardTop. Pia tumenunua pikipiki 100 na kuzigawa katikaHalmashauri 100 nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeendelea pia na jitihadaza kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele,kwa mfano matende, mabusha, usubi, trachoma, kichochona minyoo katika Halmashauri 71 zenye maambukizi.Tumefanya pia upasuaji wa matende na mabusha bilamalipo kwa wagonjwa takriban 805 katika Halmashauri zaTemeke na Ilala na wagonjwa 100 katika Mkoa wa Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malaria bado imeendeleakuwa ni changamoto katika nchi yetu, nimeeleza katika ayaza 27, 28 na 29 hatua ambazo Serikali imechukua ikiwemokusambaza dawa za kutibu malaria na vipimo vya kupimamalaria katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Tumegawavyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu lakini piatumepulizia dawa ukoka katika mikoa minne ya Kanda yaZiwa ambayo ina maambukizi makubwa ya ugonjwa wamalaria ambayo ni Kagera, Mwanza, Mara na Geita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifua Kikuu na Ukomatumeendelea na jitihada za kuimarisha huduma hizi. Kwa sasakiwango cha wagonjwa wanaotibiwa na kupona Kifua Kikuu

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

ni asilimia 90. Nitumie Bunge lako Tukufu kuwaomba tenawananchi wote wenye dalili za Kifua Kikuu kujitokeza iliwaweze kupata huduma za tiba kwa sababu Kifua Kikuukinatibika. Pia tumesogeza huduma za uchunguzi kutokahospitali moja hadi hospitali 18 katika maeneo ambayonimeyaainisha katika aya ya 31.

Mheshimiwa Mwenyekiti, udhibiti wa UKIMWI;tumeendelea kutoa huduma za kupima pamoja na ushaurinasaha wa virusi vya VVU na UKIMWI ambapo Watanzaniatakribani milioni 7.4 walipata ushauri nasaha katika kipindihiki. Pia jambo kubwa ambalo tumelifanya katika mwakahuu tunaoumaliza, tumeanza kutoa dawa za kupunguzamakali ya UKIMWI kwa Watanzania wanaozihitaji bila kujalikiwango cha CD4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia mwezi Oktoba mtuyeyote ambaye ana maambukizi ya VVU na UKIMWI naamepima, tumemwingiza katika mpango wa dawa. Piatumenunua mashine 14 kwa ajili ya kupima wingi wa virusivya damu na kuzisambaza katika mikoa mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeendelea pia na jitihadaya kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa kutumia toharakwa wanaume ambapo kuanzia Januari hadi Desemba, 2016wanaume takribani 374,411 wamefanyiwa tohara natunaendelea kuhamasisha tohara kwa wanaume katikamikoa ya kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, magonjwa yasiyo yakuambukiza kwa mfano magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizola damu, yameendelea kuongezeka katika nchi yetu, kwahiyo mwaka huu tumeandaa mkakati wa Kitaifa wakupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapopia tumezindua kampeni chini ya Mheshimiwa Makamu waRais, Mama Samia Suluhu Hassan na kampeni yetu tumeipajina la “Afya Yako, Mtaji Wako, Fanya Mazoezi, Linda AfyaYako.”

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe rai kwa WaheshimiwaWabunge na Watanzania kujenga utamaduni wa kufanyamazoezi mara kwa mara lakini pia kuzingatia ulaji wavyakula unaofaa kwa ajili ya kujikinga na magonjwa yasiyoya kuambukiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti katika hotuba yangu,Waheshimiwa Wabunge wataona karibu kurasa nyinginimezungumzia huduma za afya ya uzazi na mtoto kwasababu hicho ndiyo kimekuwa kipaumbele changu chakwanza toka nimeteuliwa kuwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ambazo tumezitoani huduma kabla ya uzazi ambapo tumetoa huduma za uzaziwa mpango na sasa hivi tumeongeza idadi ya Watanzaniawanaotumia huduma za uzazi wa mpango kutoka asilimia27 hadi asilimia 32. Lengo letu ni kwamba ifikapo mwaka 2020wanawake wanaotumia huduma za uzazi wa mpangowafikie asilimia 45. Pia tumeendelea kutoa huduma wakatiwa ujauzito ikiwemo huduma za kupima na kuelimishawanawake wajawazito kuhudhuria kliniki angalau mara nnekwa mwaka kama wataalam wanavyopendekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri, bado hatuko vizuri nchiyetu, ni asil imia 51 tu ya wanawake wajawazitowanaohudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi chaujauzito wao. Lengo letu ni kufikia asilimia 70 ifikapo mwaka2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma wakati wakujifungua, tumeendelea kushirikiana na wadau ikiwemo Ofisiya Rais (TAMISEMI) kuhamasisha na kuhimiza wanawakewajawazito kujifungulia katika Vituo vya Afya kwa sababutafiti zinaonesha ukijifungulia katika Vituo vya Afya unawezakupunguza changamoto za matatizo yanayokukabili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya ukarabati waVituo vya Afya nane katika Mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyuna Mara ili kusogeza huduma za dharura za uzazi ikiwemoupasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (SEMONC) lakini pia

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

tumeendelea kuhakikisha kwamba huduma za rufaa kwawanawake wajawazito zinaendelea kuboreshwa ambapoWizara imegawa magari ya kubebea wagonjwa(ambulance) 67 katika Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa ikiwemoKigoma, lakini pia tumegawa katika mikoa mingine nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumegawa magari nanekwa ajili ya kuratibu shughuli za afya ya mama na mtotokatika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa sababu ndiyo ina viashiriavya vifo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kupunguza vifovitokanavyo na uzazi, tumeanzisha utaratibu kuanzia mwakahuu; kila kifo kinatakiwa kujadiliwa ndani ya masaa 24 tokakilipotokea ili kubaini chimbuko la kifo hicho. Pia nimeelezakatika aya ya 50 hadi 51 hatua ambazo tumezichukua katikakupunguza vifo vya watoto wachanga ikiwemo watotowenye umri wa chini ya miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma za lishenimeongea katika aya ya 53 ya hotuba yangu na nafurahikuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kiwango cha udumavukwa watoto kimepungua kutoka asilimia 42 hadi asilimia 34lakini uzito pungufu pia umepungua kutoka asilimia 16 hadiasilimia 14 na hii ni kutokana na jitihada ambazo tumezifanyaikiwemo kuhakikisha virutubisho muhimu kwa ukuaji wa mwilivinaongezwa katika unga wa mahindi na usindikaji wamafuta ya alizeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumziabaadhi ya huduma za kinga tulizozitoa, napenda sasa kujikitakatika huduma za tiba na nimeeleza katika aya ya 55.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Mpango wa Taifa waDamu Salama, tumeendelea kukusanya damu na kuzipimaambapo tumekusanya chupa za damu 145,300 sawa naasilimia 63 ya mahitaji, lakini pia kwa kushirikiana na Ofisi yaRais (TAMISEMI), tumeanzisha Benki za Damu za Mikoa katikaMikoa saba; Dar es Salaam, Lindi, Morogoro, Dodoma, Iringa,Kigoma na Shinyanga. Lengo letu kila Mkoa uwe na Benki ya

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

damu ili kuweza kusaidiana na Benki za Damu za Kanda.Huduma za Maabara na uchunguzi wa magonjwanimezieleza katika hotuba yangu aya ya 56.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naibu Waziri asubuhi alielezasuala la hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba.Kati ya jambo kubwa ambalo tunajivunia katika kutekelezabajeti yetu ya 2016/2017, ni kuboresha upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba. Wakati tunaanza bajeti ya 2016/2017,hali ya upatikanaji wa dawa il ikuwa ni asil imia 36.Tunaangalia dawa 30 muhimu ambazo zinatakiwa kuwepokatika Vituo vya Afya. Hadi mwezi Machi, 2017, asilimia 81 yadawa muhimu sana (essential medicine) zinapatikana katikabohari ya dawa na vituo vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeonesha katika hotubayetu hali ya upatikanaji wa dawa katika Wilaya, katika Mikoana katika Halmashauri mbalimbali. Hili limefanikiwa kutokanana uamuzi wa dhati wa Mheshimiwa Rais, Dkt. John PombeMagufuli wa kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 hadibilioni 251.5 mwaka 2017 na hizi siyo fedha ambazo ziko katikamakaratasi; hadi mwezi Machi, Wizara imeshapokea shilingibilioni 112.1 kwa ajili ya dawa ukilinganisha na shilingi bilioni24 ambazo zilitolewa kwa ajili ya dawa kwa mwaka wa2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalotumefanikiwa ni kusambaza kwa kila Halmashauri vitanda vyakawaida 20, vitanda vya kujifungulia vitano, magodoro 25na mashuka 50 ikiwa ni kuhakikisha kila kituo cha afya nchinikinakuwa na vifaa vya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha hudumaza matibabu ya Kibingwa; hili ndiyo eneo la pili ambalotunajivunia sana kwamba tumefanikiwa. Tumepunguza rufaaza wagonjwa nje ya nchi kwa asilimia 35. Mwaka 2015/2016wagonjwa waliopewa rufaa kwenda nje ya nchi walikuwa553 hadi mwezi Machi tumetoa rufaa 357. Maana yake,hospitali zetu zimejenga uwezo wa kutibu magonjwaikiwemo yanayohitaji huduma za kibobezi.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Mwenyekiti, magonjwa ambayoyanaongoza kupeleka watu nje ya nchi ni saratani,magonjwa ya moyo na figo. Nitaeleza kwa ufupi kazizilizofanywa na hospitali yetu ya Taifa Muhimbili ambapo waowamekarabati wodi za wagonjwa mahututi na sasa hiviwatakuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 75 kutoka vitanda21. Pia Muhimbili imeshaanza kazi ya kukarabati jengo laupasuaji wa akinamama wajawazito ambapo vitandavitaongezeka kutoka vitanda sita hadi vitanda 19, lakini piazimeanza jitihada za kupanua jengo la kusafisha figo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali yetu ya MifupaMuhimbili (MOI) imeendelea na juhudi za kupanua wigo wahuduma ya upasuaji wa mifupa ikiwemo migongo ya watotoiliyopinda. MOI kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM Foundationimetoa huduma za upasuaji wa vichwa vikubwa vikubwa namgongo wazi kwa watoto takriban 2,020 na pia watoto 250walifanyiwa upasuaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya hospitali ambayoimefanikiwa sana na kuleta mabadiliko makubwa ni hospitaliya moyo ya Jakaya Kikwete. Sasa hivi ina uwezo wa kufanyiaupasuaji wagonjwa 30 kwa mwezi kutoka wagonjwa 15mwaka 2015/2016. Sasa hivi imejenga uwezo, wanapasuawagonjwa kwa kupitia tundu dogo, wagonjwa 608, mwakauliopita walikuwa ni wagonjwa 190. Kwa kupitia Taasisi yaJKCI tumeweza kupunguza gharama za kupeleka wagonjwanje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Saratani yaOcean Road imeendelea kutoa huduma na kubwatumeboresha jengo la kutolea tiba ya dawa (Chemotherapy)sasa hivi ina uwezo wa kuwaweka wagonjwa kwa pamoja100 kutoka wagonjwa 40. Lingine ambalo tumelifanyiamaboresho makubwa, muda wa kusubiri kuanza tiba yamionzi (Radiotherapy) tumepunguza kutoka miezi mitatu hadiwiki sita na lengo letu ni kuhakikisha ndani ya siku 14,mgonjwa anayetakiwa kupata matibabu ya mionzi yasaratani (Radiotherapy) anapata huduma hizo.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma za dawa zasaratani zimeboreshwa kutoka 5% mwaka 2015/2016 hadi 60%kufikia mwezi Machi, 2017. Kwa baadhi ya saratani dawazinapatikana kwa asilimia 100 ikiwemo saratani ya mlangowa kizazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza kazizilizotekelezwa na Hospitali Maalum ya Kibong’oto, Hospitaliyetu ya Mirembe, lakini pia na sambamba na Hospitali zaRufaa za Kanda za Juu Kusini, Mbeya; Hospitali yetu ya Kandaya Benjamin Mkapa, Dodoma; Hospitali yetu ya Rufaa yaKanda ya Ziwa, Bugando na Hospitali yetu ya Rufaa ya Kandaya Kaskazini, KCMC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa, hospitali hizizimeweza kutoa huduma za matibabu ya kibingwa ilikupunguza usumbufu wa wananchi kwenda Dar es Salaamkupata huduma hizi. Huduma za moyo, huduma za sarataniikiwemo tiba ya maji zinapatikana sasa hivi KCMC naBugando. Pia ikiwemo kusafisha damu. Sasa hivi kusafisha figohuduma zimeanza kupatikana katika hospitali zetu za rufaaza Kanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumzia pia katikahotuba yangu, kazi zinazofanywa na Wizara katika kusimamiaubora wa huduma za afya ambapo tumeendelea na zoezitunaliita la star rating, (kutoa nyota) kwa aili ya Vituo vyaAfya na zoezi hili limefanyika katika Mikoa sita ya Iringa,Njombe, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro na Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asil imia 52 ya vituotulivyovifanyia tathmini vimepata nyota sifuri. Ni asilimia 4.1tu ya vituo vilivyofanyiwa tathmini ndiyo vimepata nyota tatuna nyota nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, rasilimali watu katika Sektaya Afya; tumeendelea kuimarisha miundombinu katika Vyuovya Afya lakini pia tumeongeza udahili na upatikanaji warasilimali watu. Nimeonesha wataalam tuliozalisha katikamwaka 2016/2017 lakini pia tunamshukuru sana Mheshimiwa

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amewezeshakupatikana kwa Madaktari 258 na hadi ninavyosematumeshawagawa katika Mikoa na Halmashauri mbalimbalinchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara pia imekamilishamaandalizi ya mkakati wa kugharamia huduma za afya,lengo ni kuhakikisha tunapata rasilimali fedha za kutosha kwaajili ya huduma za afya na kupitia Mfuko wa Taifa wa Bimaya Afya tumeongeza idadi ya wanachama wa Bima kutokawanachama 702,598 hadi wanachama 792,986. Piawanachama wa CHF wameongezeka kutoka milioni 1.4 hadimilioni 1.5.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kushirikiana na Benki yaMaendeleo ya Ujerumani (KFW), tumetekeleza mpango wakuwapa Bima ya afya wanawake wajawazito kwa jina la“Tumaini la Mama” ambapo wanawake wajawazito 147tumewapa Bima na hivyo kupata huduma za afya bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite sasa katika kutekelezabajeti kwa upande wa Fungu 53 - Maendeleo ya Jamii.Kubwa ambalo tumelifanya ni kuwezesha na kuratibuutekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya jamii hususankatika kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katika shughulimbalimbali za maendeleo kupitia miongozo mbalimbali;lakini pia tumeendelea kutoa wataalam wa kada yaMaendeleo ya Jamii katika ngazi mbalimbali katika Vyuovyetu nane vya Maendeleo ya Jamii pamoja na Taasisi yaMaendeleo Tengeru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa maendeleoya jinsia tumeendelea na jitihada za kuwezesha wanawakekiuchumi kupitia Benki ya Wanawake na Mfuko waMaendeleo ya Wanawake. Kupitia Mfuko wa Maendeleo yaWanawake, shilingi milioni 156 zimekopeshwa katikaHalmashauri tano za Kisarawe, Busokelo, Gairo, IringaManispaa, Masasi na Mtwara Vijijini lakini pia tumeendelea

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

kushirikiana na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kuhamasishaHalmashauri kuchangia asilimia tano ya mapato yao ya ndanikwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutumia fursa hiikuzipongeza Halmashauri zote zilizotenga na kutoa asilimiatano ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya Mfuko waMaendeleo wa Wanawake; lakini nazilaani Halmashauri zoteambazo hazikuchangia Mfuko wa Maendeleo waWanawake na naamini Mheshimiwa Simbachaweneatachukua hatua kuziwajibisha Halmashauri zote ambazohazijatenga Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi hapa tuko Bungenikwa sababu ya kura za wanawake, lakini pia wote tunajuakwamba wanawake ndiyo msingi wa maendeleo ya familia,maendeleo ya Taifa na maendeleo ya jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Wanawake imetoamikopo kwa wajasiriamali 6,959 yenye thamani ya shilingibilioni 10, lakini pia tumeongeza vituo vya kutoa huduma.Benki ya wanawake imewasaidia wanawake 223 katikaMkoa wa Dar es Salaam na Pwani kumiliki ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeendelea na jitihada zakusimamia na kulinda haki za mtoto ambapo tumeendeleakupinga na kujenga hamasa kuhusu mimba na ndoa zautotoni; na katika hotuba yangu nimeonesha Mikoainayoongoza kwa ndoa za utotoni ambapo ni Shinyanga,Tabora, Mara, Dodoma na Lindi; lakini pia nimeonyesha Mikoainayoongoza kwa mimba za utotoni ikiwemo Katavi, Tabora,Simiyu, Geita na Shinyanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya utafiti wa kubainivyanzo vya ndoa na mimba za utotoni. Katikakumwendeleza mtoto wa kike, tumewezesha kuanzishwakwa Club za Wasichana na Wavulana 105. Tumetoa hudumaza ustawi wa jamii kwa ajili ya watoto walio katika mazingirahatarishi, watoto walio katika mkinzano na sheria, watuwenye ulemavu na wazee ikiwemo familia zenye migogoro.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa haki naustawi wa wazee; nimeeleza katika hotuba yangu hatuatulizochukua ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuwaheshimuna kuwathamini wazee, lakini pia tumefurahi kwamba kwamujibu wa taarifa za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,mauaji ya wazee yamepungua kutoka 190 mwaka 2015 hadi135 mwaka 2016. Tumeendelea kutoa huduma kwa wazee456 wasiojiweza katika Makazi 17 yanayoendeshwa naSerikali. Huduma hizi ni pamoja na chakula, malazi namatibabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hiikuwashukuru wadau wote waliochangia katika kuhakikishahuduma bora kwa wazee nchini. Kipekee namshukuru mkewa Rais, Mheshimiwa Mama Janet Magufuli kwa kuwa mstariwa mbele katika kuwasaidia wazee wanaotunzwa katikamakazi ya wazee hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito kwa jamii kuigamfano wa mama yetu, sote ni wazee watarajiwa tunahitajikuwaenzi, kuwaheshimu na kuwatunza wazee wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza pia wataalamwa ustawi wa jamii ambao wameendelea kuzalishwa naTaasisi yetu ya Ustawi wa Jamii katika ngazi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba yangunimeeleza pia kuanzia aya ya 164 kazi zilizotekelezwa naTaasisi za Wizara ikiwemo Taasisi ya Chakula na Lishe, Bohariya Dawa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mamlaka yaChakula na Dawa, Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuuwa Serikali, Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR). Naomba Waheshimiwa Wabunge wapitie kazi hizozilizofanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijikite katikasehemu ya tatu ya hotuba yangu ambayo nitazungumziavipaumbele vya Wizara na bajeti ya mapato na matumizikwa mwaka 2017/2018.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Mheshimimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa fungu 52;Wizara itakeleza vipaumbele vifuatavyo:-

(i) Kuimarisha huduma za kinga, tiba nakuongeza usawa katika kutoa huduma za afya.

(ii) Tutaimarsha huduma za afya ya uzazi namtoto ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito nawatoto. Lengo letu ni kupunguza vifo hivi kutoka 556 katikakila vizazi hai 100,000 na kufikia vifo 290 ifikapo mwaka 2020.

(iii) Tutaimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa,vifaa tiba na vitendanishi katika Vituo vya Umma.

(iv) Tutaimarisha miundombinu katika vituo vyamafunzo.

(v) Tutaimarisha matibabu ya kibingwa nchinikwa kuendeleza ujenzi, upanuzi na kununua vifaa vya kisasakatika Hospitali yetu ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya MifupaMuhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Hospitali yaBenjamin Mkapa, Hospitali zetu za Rufaa za KCMC, Bugandona Mbeya, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, HospitaliMaalum za Mirembe na Kibong’oto.

(vi) Tutaimarisha huduma za lishe na upatikanajiwake katika jamii na vituo.

(vii) Tutaimarisha matumizi ya teknolojia ya habarina mawasiliano katika kuboresha huduma za afya.

(viii) Tutahamasisha wananchi kwa nia yakuongeza idadi ya wanaojiunga na Mifuko ya Afya, badohatufanyi vizuri. Ni asilimia 27 tu takriban ya Watanzaniaambao wanatumia Bima ya Afya.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

(ix) Kwa upande wa maendeleo ya jamii kupitiaFungu 53, tutaendelea kuamsha ari ya wananchi kushirikikatika shughuli za kujiletea maendeleo.

(x) Tutawezesha utekelezaji wa mpango kazi waTaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watotokwa mwaka 2018 mpaka 2020/2021.

(xi) Tutaimarisha upatikanaji wa haki namaendeleo ya watoto.

(xii) Tutakuza usawa wa jinsia na uwezeshaji wawanawake kiuchumi.

(xiii) Tutaimarisha huduma za ustawi pamoja nahaki na ustawi wa wazee na watoto na ushiriki wa mashirikayasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya jamii.

(xiv) Vile vile tutaboresha mazingira ya kufundishiana kujifunzia katika Taasisi yetu ya maendeleo Tengeru, Vyuovya Maendeleo ya Jamii pamoja na Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili kufikia malengo hayo,nitaeleza tu masuala makubwa machache. MkiniulizaMheshimiwa Waziri wa Afya, bajeti yako ya 2017/2018 inajibuvitu gani? Bajeti yetu inajibu mambo makubwa matatu:-

Jambo la kwanza; tunataka kuimarisha huduma zamatibabu ya kibingwa ili kupunguza rufaa za wagonjwa njeya nchi ili tuweze kupunguza hizo gharama. Kupitia hospitaliyetu ya Taifa Muhimbili, itaanza kutoa huduma za kupandikizafigo (Renal transpant) ambapo tukipeleka Mtanzania mmojanje ya nchi kwa ajili ya kupandikizwa figo, tunatumia takribanShilingi milioni 80. Huduma hii ikianza kupatikana Muhimbili,gharama zitapungua hadi kufikia milioni 20.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Hospitali yaMuhimbili itaanza kutoa huduma za kupandikiza vifaa vyakusaidia kusikia, kwa kitaalamu inaitwa cochlear implants.Tunakimpeleka mgonjwa nje ya nchi tunatumia takribanimilioni 30. Huduma hii ikitolewa hapa nchini si tu Serikali lakiniwananchi wengi wataweza kumudu huduma hizi kwasababu gharama hizi zitapungu kwa zaidi ya asilimia 70.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafurahi kuliarifu Bunge lakoTukufu kwamba Watanzania wengi sasa hivi wana imani nahuduma zinazotolewa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Hivyotumeamua katika mwaka unaokuja tutajenga jengo lawagonjwa binafsi (private wing), tumetenga shilingi bilioni14.5 kwa sababu watu wengi wanataka kwenda Muhimbililakini wanashindwa kwenda kwa sababu pia ya mazingira.Kwa hiyo, nawapongeza sana Watanzania wote walioamuakutumia huduma za hospitali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesem sa tunajibu kero zakupunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pil i ambalotunawekeza kwa mwaka 2017/2018. Kupitia Taasisi yetu yaSaratani ya Ocean Road tunanunua mtambo wa kisasa kwaajili ya uchunguzi na matibabu ya saratani unaitwa PET Scanambapo tumetenga shilingi bilioni 14.5. Kifaa hiki hakipoKenya, hakipo Uganda, hakipo Malawi, hakipo Zambia, kwamara ya kwanza Tanzania itaanza kutoa huduma za vipimovya saratani (PET-Scan). Tunategemea kupitia uamuzi huututaokoa takribani shilingi bilioni tano kwa mwaka. Kwasababu kupeleka mgonjwa kwa ajili ya kipimo hiki inagharimumilioni 100. Huduma hii sasa itaweza kupatikana nchini kwatakribani shilingi milioni kumi na mbili. Hayo ndiyo maeneomakubwa ya kujibu hoja za kupeleka rufaa nje ya nchi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tutaendelea kuimarishahospitali yetu ya MOI, Hospitali ya Jakaya Kikwete ambayoimewekeza sana katika matibabu ya moyo. Sambamba nahayo tutajenga uwezo katika hospitali zetu za Rufaa za

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Kanda ya Benjamin Mkapa. Kama mnavyofahamu, Serikaliimehamia Dodoma, tumeshamaliza kusimika mitambo yakisasa. Kwa hiyo lengo letu huduma zote za kibingwa piazitapatikana katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea na ujenzi waHospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara ambapotumetenga shilingi bilioni mbili. Lakini pia tutawekeza katikaHospitali za Mbeya, Bugando na KCMC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa hudumaza tiba tutaendelea kutoa chanjo, na labda niliweke wazi,ukiangalia bajeti ya dawa ya mwaka jana na mwaka huu,mwaka huu ni shilingi bilioni 236, mwaka jana bajeti ya dawatuliweka shilingi bilioni 251. Vilevile kulikuwemo na fedha zachanjo. Kwa hiyo, katika kuhakikisha kwamba hatuteterekikatika kutoa huduma za chanjo hasa chanjo za watoto,tumeamua kutenganisha fedha za dawa na fedha za chanjo.Kwa hiyo tumetenga shilingi bilioni 33 kutoka vyanzo vyandani kwa ajili ya chanjo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wataalam wametuelekeza,kila dola moja inayowekezwa kwenye chanjo ya mtotomaana yake tunaokoa angalau dola nane mpaka dola 44katika kutibu magonjwa ya watoto hao. Kwa hiyo, bajeti yadawa haijapungua lakini tumetenga fedha za dawa, vifaana vifaa tiba na kuziweka tofauti na fedha za chanjo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma ya afya yauzazi na mtoto, tutaendelea kununua na kusambaza dawana vifaa vya uzazi wa mpango. Haya ni maboreshomakubwa, tumekuwa tukitegemea wafadhili wa nje kwa ajiliya huduma za uzazi wa mpango. Wataalam wanatuambiatukitumia huduma za uzazi wa mpango tunaweza kupunguzavifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 40. Kwa hiyo,tumetenga kwa mara ya kwanza shilingi bilioni 14 za ndanikwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutanunua, kusambaza nakutoa bila malipo, dawa kwa ajili ya uzazi salama katika

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

vituo vya umma. Nimeona wanawake wajawazito ambaompo hapa, nataka kuwathibitishia, chini ya Serikali ya Awamuya Tano kupitia bajeti hii hakuna mwanamke mjamzitoatafariki kwa kukosa dawa ya kuzuia kuvuja damu (oxytocin).(Makofi)

Nataka kupitia Bunge hili kuwathibitishia wajawazitowote kupitia bajeti hii hakuna mwanamke mjamzito atafarikikwa sababu amekosa dawa ya magnesium sulphate kwaajili ya kuzuia kifafa cha mimba. Kwa mara ya kwanza dawahizi tutazitoa bure na tutahakikisha kila mwanamke mjamzitoanayejifungua katika vituo vya umma anapata dawa;tumetenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya huduma hii.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tutaendeleakuboresha huduma za uchunguzi za uzazi salama kwakununua mashine za Ultra Sound 65, tutazipeleka katika vituovya afya ili viweze sasa kufanya huduma za uchunguzi.Kupitia bajeti hii tutawakatia Bima ya Afya wanawakewajawazito 150,000 ili kuweza kupata huduma za afya katikahospitali za umma. Lakini kwa kupitia bajeti hii tutaendeleakuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi za dharuraikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni ambapotutaboresha vituo vya afya 150.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshawasiliana nawenzetu wa TAMISEMI watuletee mapendekezo ya vituohivyo na tayari timu ya TAMISEMI na timu ya Wizara ya Afyaimepita katika Halmashauri mbalimbali kwa hiyo nasubirikuletewa orodha ya mwisho ya vituo hivyo. Ninachotakakuwathibitishia, tumesherehekea takriban miaka 50 ya Uhuruvituo vya afya vya Serikali vinavyotoa huduma za dharuraza uzazi ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto (CEMOC) nivituo vya afya 117 tu, ambayo ni sawa na asilimia 20.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia bajeti hii tutaongezavituo vya afya 150 ndani ya mwaka mmoja, vitaweza kutoahuduma za uzazi za dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoamtoto. Tutaboresha upatikanaji wa damu salama, ambapo

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

tutajenga benki za damu katika Mikoa ya Katavi, Rukwa,Ruvuma, Njombe na Manyara ambapo tumetenga shilingibilioni mbili. Hayo ndiyo mambo makubwa ambayotutayafanya kupitia sekta ya afya, na kama nilivyosemayanajibu kero kubwa tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia sekta ya maendeleoya jamii tutaendelea kuamsha ari ya wananchi kushiriki katikashughuli za kujiletea maendeleo, tutawezesha utekelezaji wampango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi yawanawake na watoto, tutaimarisha upatikanaji wa haki namaendeleo ya mtoto, kukuza usawa wa kij insia nauwezeshaji wanawake kiuchumi, kuimarisha huduma zaustawi wa jamii na wazee, lakini pia kuboresha mazingira yakujifunzia na kufundishia katika vituo vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri waKatiba na Sheria, juzi wakati anawasilisha hotuba yake,amezungumzia kuhusu Sheria ya Ndoa. Nikiwa mlezi namsimamizi mkuu wa haki na maendeleo ya wasichananataka kukiri mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba zipochangamoto mbalimbali zinazoleta mimba na ndoa zautotoni, lakini Sheria ya Ndoa nayo ni kikwazo. Kwa hiyo,tutaendelea kushirikiana na wenzetu wa Katiba na Sheriakuhakikisha kwamba tunafanyia marekebisho sheria ya ndoaili kuwawezesha wasichana waweze kuendelea na masomobadala ya kuwaoza mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika kushughulikiamasuala ya maendeleo ya jinsia tutaendelea kuwawezeshawanawake kiuchumi ili kutoa mikopo kupitia Benki yaWanawake katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Njombe,Iringa, Dodoma, Ruvuma na Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maendeleo ya mtotokama nilivyosema tutaendelea kuimarisha utendaji waKamati za Ulinzi na Usalama wa Mtoto, kwa huduma zaustawi wa jamii tutaendelea kuhakikisha tunatoa hudumaza wazee pamoja na wazee wanaokaa katika makazimaalum.

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ni mengi lakininaomba kwa sababu ya muda nitoe shukrani kwa wadauwetu wakubwa ambao wamewezesha kutekelezwa kwamiradi mbalimbali ya sekta ya afya. Kipekee niwashukuru sananchi rafiki na mashirika ya kimataifa yanayosaidia kuboreshahuduma za afya kupitia Mfuko wa Pamoja wa KugharamiaHuduma za Afya (Health Basket Fund) ambazo ni Denmark,Uswis, Ireland, Canada, Benki ya Dunia, UNICEF na Korea.Tunawashukuru sana kwa sababu mchango wenu ambaoumesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kuzishukurunchi za Canada, China, Cuba, Hispania, India, Italia, Japan,Marekani, Misri, Sweden, Uingereza, Ujerumani na Ufaransaambazo zimeendelea kusaidia Wizara ya Afya katika maeneomahsusi. Nayashukuru mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia,sekta binafsi, vyuo vikuu, taasisi za kitafiti na vyama vyakitaaluma, wadau wote nimewaainisha katika hotuba yangukuanzia aya ya 219 hadi 223. Pia ningependa kutamkakwamba Global Fund for HIV/AIDS , Malaria and TBtunawashukuru sana, African Development Bank, BADEA, EU,Global Aliance on Vaccine, US AID, PEPFAR, UN-Women naUNFPA tunawashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha utendajiwa kazi zangu, nikiwa Waziri nimepata ushirikiano mkubwakutoka kwa viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kipekeenamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Hamisi AndreaKigwangalla, Mbunge na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano anaonipakatika kutekeleza majukumu yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kuwashukuruDkt. Mpoki Ulusubisya - Katibu Mkuu Afya na Bibi Sihaba NkingaKatibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotokwa mchango wao. Ninamshukuru sana Profesa MohamedKambi Bakari - Mganga Mkuu wa Serikali kwa mchango wakemkubwa katika utendaji wa kazi zangu, nawashukuru

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Makamishna, Wakurugenzi na Viongozi wa vitengo vyaWizara. Nawashukuru Wakurugenzi wa Hospitali zetu ambazoni Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Museru tunakushukurusana, MOI, JKCI - Profesa Janabi, Ocean road, Mirembe,Kibong’oto na Hospitali za Rufaa ya Kanda ya Mbeya,Benjamini Mkapa - Dodoma, Bugando na KCMC na taasisizilizo chini ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikiri katika Bungelako Tukufu kwamba mimi si daktari lakini siku hizi nimekuwabush doctor kwa sababu ya msaada na mchango mkubwaambao nimekuwa nikiupata kutoka katika timu yangu yawataalam. Nawashukuru sana kwa kuniwezesha kusimamiaWizara vizuri. (Makofi)

Aidha niwashukuru Waganga Wakuu wa Mikoa wote,Waganga Wakuu wa Wilaya, Waganga Wafadhi waHospitali, Vituo vya Afya na Zahanati, Wakuu wa Vyuo vyaMafunzo vilivyo chini ya Wizara na Mashirika ya Dini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa watumishi wenzanguwa sekta ya afya, nawashukuru sana, sana sana kwa sababummeendelea kutoa huduma katika mazingira yenyechangamoto mbalimbali, lakini bado mmeendelea kutoahuduma, niendelea kuwasihi madaktari, wauguzi, wafamasia,watumishi wote wa sekta ya afya muendelee kutoa hudumakwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi ya kutoa huduma zaafya ili mwisho wa siku tuweze kulipeleka mbele Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenaishukuru sana familia yangu kwa uvumilivu na ustahimilivuwao mkubwa sana, bila wao nisingekuwa naendelea kuwavizuri katika kazi zangu kwa kujitoa na kujituma. Vilevilekwa wananchi hasa wanawake wa UWT wa Mkoa wa Tanga,ninawashukuru sana kwa kuendelea kunipa ushirikiano katikautendaji wa kazi zangu. Ninaahidi kwamba nitaendeleakuwaenzi na kuwatumikia kwa nguvu zangu zote ili kuletamabadiliko ya kweli na ya haraka katika Mkoa wetu waTanga. Tanga inapendeza na tumeamua kuwa iwe ni Tangaya viwanda. (Makofi)

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo sasanaomba ninywe maji sasa kusudi niombe fedha. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Fungu 52 - Afyakatika mwaka 2017/2018 Wizara imekadiria kukusanyamapato ya shilingi 225,038,495,525, kati ya fedha hizo shilingi207,472,729,612 zitakusanywa kutoka katika mashirika nataasisi zilizo chini ya Wizara na shilingi 17,565,765,913 ni kutokamakao makuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya kawaidakupitia Fungu 52 Wizara inakadiria kutumia kiasi cha shilingi291,895,940,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati yafedha hizo shilingi 64,063,937,000 zitatumika kwa ajili yamatumizi mengineyo na shilingi bilioni 227,823,003,000zitatumika kwa ajili ya mishahara ya watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya fedha zilizotengwakwa ajili ya mishahara shilingi 49,360,787,000 ni kwa ajili yawatumishi wa Wizara Makao Makuu na shilingi 178,795,217,000ni kwa ajili watumishi wa taasisi, mashirika na wakala zilizochini ya Wizara. Kwa upande wa miradi ya maendeleo Fungu52 linakadiria kutumia shilingi 785,805,952,000 kwa ajili yamiradi ya maendeleo kati ya fedha hizo fedha za ndani nishilingi 336,300,000,000 na fedha za nje ni shilingi bilioni449,505,952,278.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya makadirio ya bajetikwa mwaka 2017/2018 kwa Fungu 52 ni shil ingi1,077,701,892,000. Kwa upande wa Fungu 53 Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto, makadirio ya makusanyo yamaduhuli na matumizi kwa mwaka ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa makusanyoya maduhuli Wizara inatarajia kukusanya maduhuli yenyejumla ya shilingi 2,101,874,000 ambazo ni ada za wanafunzikutoka vyuo vinane kutoka maendeleo ya jamii, ada zamashirika yasiyo ya kiserikali na mauzo ya vitabu vya zabuni.(Makofi)

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Mheshimiwa Mwenyekiti, makadirio ya matumizi yakawaida kwa mwaka 2017/2018 ni shilingi 35,300,602,090ambapo mishahara ni shilingi 19,142,252,240, na shilingi16,158,449,850 ni matumizi mengineyo. Aidha, Fungu 53 kwaupande wa miradi ya maendeleo inakadiriwa kutumia kiasicha shil ingi 2,606,278,000 kati ya fedha hizo shil ingi2,000,000,000 ni fedha za ndani na shilingi 606,278,000 ni fedhaza nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhimajumla ya makadirio ya bajeti kwa Fungu 53 ni shilingi37,906,880,090. Jumla ya fedha zote ambazo ninaliombaBunge lako Tukufu lipitishe kwa Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni shilingi 1,115,680,772,090.

Mheshimiwa Mwenyekiti baada ya kusema hayonashukuru kwa kunipa fursa hii na ninaomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Ahsante! Hoja imetolewa na imeungwamkono, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa wasilisholako zuri.

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB),

KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHAKWA MWAKA 2017/18 – KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

I. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa naMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma naMaendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufu, ambayoimechambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, naomba kutoa hoja kwamba sasa

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Bunge lako likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezajiwa Kazi za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto kwa mwaka 2016/17 na Vipaumbele vya Wizarakwa mwaka 2017/18. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufulikubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Kawaida naMpango wa Maendeleo ya Wizara ya Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2017/18.

2. Mheshimiwa Spika, baada ya kumshukuru MwenyenziMungu kwa kuniwezesha kusimama hapa, napendakuchukua fursa hii kwa heshima na unyenyekevu mkubwakumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwauongozi wake imara kwa nchi yetu na maelekezo yakeambayo yamekuwa dira sahihi katika utendaji wangu nakatika kuimarisha huduma za Afya na ustawi ya jamii nchini.Aidha, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuweka msingiwa kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya nchini ikiwani katika jitihada zake za kulinda afya za Watanzania hasavijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa letu. Kwa jinsi hiyo,Wizara itaendelea kuelimisha na kuhimiza umma waWatanzania kuhusu madhara yatokanayo na matumizi yamadawa ya kulevya sambamba na kuzingatia mfumo borawa maisha.

3. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani za dhatikwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo naushauri wake wa dhati hasa katika kuboresha huduma zaafya ya mama na mtoto na masuala ya kuwawezeshawanawake kiuchumi. Wizara yangu itaendelea kutumiataswira, ushawishi na uzoefu wake ili kujenga jamii yawatanzania inayowajali, kuwaheshimu na kuwaendelezawanawake na wasichana kwa ajili ya kuwa na maendeleoya kweli na endelevu katika nchi yetu

4. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hiikumshukuru Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa (Mb),Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwauongozi wake ambao umesaidia kuongeza ufanisi katika

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

utendaji na kuimarisha huduma zinazotolewa na Wizarayangu. Aidha, naomba nimpongeze kwa hotuba yakealiyoiwasilisha kwenye Bunge hili ambayo imetoa dira ya jinsiSerikali itakavyotekeleza majukumu yake katika mwaka 2017/18.

5. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewebinafsi, kwa kuendelea kutekeleza majukumu yako kwaweledi katika kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania. Aidha, nampongeza Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson(Mb.) kwa ushirikiano wake kwako, katika kutekelezamajukumu yako. Vilevile, nichukue fursa hii kuwapongezaWenyeviti wa Bunge kwa kusimamia vyema mijadala ndaniya Bunge.

6. Mheshimiwa Spika, napenda nimshukuru MheshimiwaGeorge Boniface Simbachawene (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwa ushirikianowake uliowezesha kusimamia na kuboresha utoaji wahuduma za afya nchini hasa afya ya msingi. Pia, nawashukuruMawaziri wa Wizara nyingine zote ambazo ushirikiano waona Wizara yangu umechangia katika utoaji wa huduma zaafya na maendeleo ya jamii.

7. Mheshimiwa Spika, kipekee napenda kuishukuruKamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo yaJamii, chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Peter JosephSerukamba (Mb), na Makamu Mwenyekiti, MheshimiwaMussa Azzan Zungu (Mb) kwa ushauri na maelekezowaliyoyatoa wakati wa maandalizi ya Bajeti hii. Aidhanawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikianomzuri wanaonipatia ikiwemo kutoa ushauri na maonimbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma za afya naustawi wa jamii nchini. Ninawashukuru sana! Ninawaahidikwamba, Wizara yangu itazingatia ushauri wao nakuendelea kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumuna kazi zetu za kuwatumikia wananchi ndani na nje yaBunge.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

8. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi kwaMheshimiwa Abdallah Majura Bulembo (Mb), MheshimiwaAnna Kilango Malecela (Mb), Mheshimiwa Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb),Mheshimiwa Juma Ali Juma (Mb), Mheshimiwa Salma RashidKikwete (Mb) na Mheshimiwa Getrude Pangalile Rwakatare(Mb) kwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. Aidha nampongeza Prof. Kabudi kwa kuteuliwakuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Ninawaahidi kuwapaushirikiano ili tuendelee kuwatumikia wananchi kwa pamoja.

9. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa pole kwako,Bunge lako Tukufu, kwa familia na wananchi wa Jimbo laDimani kwa kifo cha Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir na Dkt.Elly Marko Macha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum,CHADEMA. Aidha, natoa pole kwako na watanzania wote,ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu na jamaa zaokutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja namagonjwa, ajali na majanga. Pia, natoa pole kwawagonjwa na majeruhi wa ajali waliopo hospitalini namajumbani pamoja na wahanga wa vitendo vya ukatili naunyanyasaji wa kijinsia. Namuomba Mwenyezi Munguawaponye haraka ili waweze kuendelea na ujenzi wa Taifa.

10. Mheshimiwa Spika, Baada ya kusema hayo,ninapenda sasa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji washughuli za Wizara kwa mwaka 2016/17, Vipaumbele vyaWizara kwa mwaka 2017/18 pamoja na maombi ya fedhaambazo zitaiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumuyetu.

II. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI NAMPANGO WA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17

11. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake,Wizara imeendelea kuzingatia Sera, Mipango na Mikakati

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja naMalengo ya Maendeleo Endelevu (2030), Dira ya Taifa yaMaendeleo (2025), Mpango wa II wa Taifa wa Maendeleowa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21), Sera ya Afya (2007),Mpango Mkakati wa IV wa Sekta ya Afya (2016 - 2020) naMpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM 2007 – 2017).Aidha tumezingatia Sera ya Taifa ya Wazee (2003), Sera yaMaendeleo ya Jamii (1996), Sera ya Maendeleo ya Mtoto(2008), Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000),Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (2001). Vilevile,Wizara imeendelea kutekeleza malengo yaliyoainishwa katikaIlani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

Mapato na Matumizi ya Fedha - Fungu 52 (Afya)

12. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Fungu 52(Afya) hukusanya mapato yake kupitia Bodi na Mabarazambalimbali, ada za uchangiaji wa gharama za mafunzo,marejesho ya masurufu, malipo ya ununuzi wa vitabu vyamaombi ya zabuni, pamoja na makusanyo yatokanayo nautoaji wa huduma katika Taasisi na Mashirika yaliyo chini yaWizara. Hadi kufikia mwezi Machi 2017, Wizara imekusanyajumla ya Shilingi 118,701,870,697.00 ikilinganishwa namakadirio ya Shilingi 157,786,384,366.00 yaliyoidhinishwa kwamwaka 2016/17. Makusanyo haya ni sawa na asilimia 75 yamakadirio ya makusanyo ambapo usimamizi thabiti pamojana matumizi ya mifumo ya Kielektroniki vimechangia kwakiasi kikubwa kupatikana kwa ufanisi huu.

13. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, jumla yaShilingi 796,115,856,780.00 ziliidhinishwa kwa ajili ya utekelezajiwa majukumu ya Wizara. Kati ya fedha hizo, Shilingi277,629,895,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida naShilingi 518,511,683,780.00 ikiwa ni kwa ajili ya kugharamiautekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Hadi kufikia mweziMachi, 2017, jumla ya Shilingi 339,194,232,240.85.00

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

zilipokelewa ikiwa ni asilimia 43 ya fedha zilizoidhinishwa.Kati ya fedha zilizopokelewa Shilingi 205,321,959,485.85 sawana asilimia 74 ni fedha za Matumizi ya Kawaida na Shilingi133,872,272,755.00 sawa na asilimia 26 ni fedha za Miradi yaMaendeleo. tumepokea vifaa, vifaa tiba na dawa vyenyethamani ya shilingi 256,238,088, 964 kutoka mfuko wa duniawa kupambana na UKIMWI, malaria na kifua kikuu ikiwa nisehemu ua utekelezaji wa bajeti ya miradi ya maendeleo.

Fungu 53 - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

14. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarakupitia Fungu 53, ilitarajia kukusanya jumla ya Shilingi2,382,679,000. Vyanzo vya mapato ikiwa ni ada za wanafunzikatika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ada za MashirikaYasio ya Kiserikali. Hadi kufikia mwezi Machi, 2017, makusanyoyalifikia Shilingi 930,281,152 sawa na asilimia 39.0.

15. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, jumla yaShilingi 49,857,955,920 ziliidhinishwa kwa ajili ya kutekelezamajukumu ya Wizara kupitia Fungu hili. Kati ya hizo, Matumiziya Kawaida ni Shilingi 41,009,372,644 yakijumuisha Shilingi18,669,129,000 kwa ajili ya mishahara na Shilingi 22,340,243,644kwa ajili ya Matumizi Mengineyo. Bajeti ya matumizi ya Miradiya Maendeleo iliyoidhinishwa ilikuwa Shilingi 8,848,583,276 katiya fedha hizo, Shilingi 5,365,400,000 ni fedha za ndani naShilingi 3,483,183,276 ni fedha za nje. Hadi kufikia mweziMachi, fedha za Matumizi Mengineyo Shilingi 4,950,097,864zilipokelewa sawa na asilimia 28.4 ya bajeti iliyoidhinishwana Shilingi 7,866,426,933 za Mishahara zilipokelewa sawa naasilimia 42.1 ya bajeti iliyoidhinishwa. Vilevile, katika bajetiya miradi ya Maendeleo, Shilingi 497,718,250 zilipokelewaambapo Shilingi 204,217,000 (3.8%) ni fedha za ndani naShilingi 293,501,250 (8.4%) ni fedha za nje.

16. Mheshimiwa Spika, ifuatayo ni taarifa kuhusumajukumu yaliyotekelezwa na Wizara katika kipindi cha Julai2016 hadi Machi 2017;

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA SEKTA YA AFYA

HUDUMA ZA KINGA

Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Yasiyo yakuambukiza

17. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoahuduma za kinga nchini ambazo zinajumuisha udhibiti wamagonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyo ya kuambukiza,huduma za uzazi na mtoto, lishe pamoja na utoaji wa elimuya afya kwa umma. Katika kipindi cha 2016/17 Wizarailitekeleza afua mbalimbali za huduma za kinga ikiwa nipamoja na;

Huduma za Chanjo

18. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoahuduma za Chanjo kulingana na Sera na Miongozo. Aidha,Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo, imehakikishakuwepo kwa chanjo za kutosha kwa ajili ya huduma zachanjo kwa watoto na makundi mengine kwa kununua nakusambaza chanjo katika Mikoa na Halmashauri zote nchini.Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 18 kununulia chanjona vifaa vya kutolea chanjo. Chanjo zilizonunuliwa kwamwaka 2016/2017 zilikuwa BCG (chanjo ya kifua kikuu) dozi6,000,000, Polio dozi 6,000,000, Penta (chanjo ya dondakoo,kifaduro, homa ya ini, Preumonia, homa ya uti wa mgongona kichomi) dozi 5,975,500, PCV (chanjo ya homa ya nimoniana homa ya uti wa mgongo) dozi 5,082,200, Rota (chanjodhidi ya ugonjwa wa kuharisha) dozi 3,303,400, TT (chanjo yaPepo punda kwa wajawazito) dozi 2,480,000, Surua Rubelladozi 4,797,600 na HPV (chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi)dozi 67,100. Hii imewezesha nchi yetu kuwa miongoni mwanchi zilizofanya vizuri katika utoaji wa huduma za chanjokwa mwaka 2016, ambapo tuliweza kuvuka lengo kwakufikia kiwango cha chanjo cha asilimia 97.

19. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wizarakwa kushirikiana na wadau wa chanjo imenunua magari 9

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

kwa ajili ya kuboresha huduma za usambazaji wa chanjo,usimamizi elekezi na ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilikakwa chanjo. Kati ya magari hayo, manne ni ya tani 3.5 nayana vyumba vya ubaridi. Aidha, Wizara ilinunua nakusambaza majokofu 317 ya kutunzia chanjo kwenye vituovya huduma za afya ambapo majokofu 70 yanatumia mionziya jua na 247 yanatumia gesi. Vilevile Wizara imeanzishamfumo wa kukusanya taarifa za chanjo ikiwa ni pamoja naufuatiliaji wa chanjo kutoka ngazi ya Taifa hadi kwenye vituovya kutolea chanjo (Vaccination Immunization ManagementSystem (VIMS)). Mfumo huu umeshapelekwa kwenye mikoasaba ambayo ni Dar es salaam, Lindi, Njombe, Arusha,Mtwara, Tabora na Mwanza.

Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko

20. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kufuatiliamwenendo na viashiria vya magonjwa yanayotolewa taarifakitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na magonjwa yamilipuko. Katika mwaka 2016/17 nchi yetu ilikumbwa naugonjwa unaosababishwa na sumu kuvu (Afflatoxicosis).Hata hivyo Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbaliilidhibiti ugonjwa huo. Aidha, Wizara iliendesha mafunzo kwawatumishi wa afya mipakani, bandarini, viwanja vya ndegena bandari kavu kuhusu namna ya kukabiliana na magonjwaya kuambukiza ikiwemo Ebola. Mafunzo haya yalishirikishawatumishi na wadau 110. Vilevile, Wizara imeandaa MpangoMkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Milipuko na Majangaili kulinda usalama wa nchi kiafya (National Health SecurityPlan, 2017-2021). Utekelezaji wa Mpango huo umeshaanza.

21. Mheshimiwa Spika, ugonjwa wa kipindupinduuliendelea kutolewa taarifa na kudhibitiwa kwa kiasikikubwa ambapo hadi Machi 2017, jumla ya wagonjwa 2,927waliripotiwa na vifo 46 viliripotiwa. Wizara inaendeleakushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kupanga mikakatiya kudhibiti ugonjwa huo na magonjwa yote ya milipukoambapo mafunzo yalitolewa kwa Mikoa na Halmashaurizilizoathiriwa na ugonjwa huo. Mafunzo hayo yalijielekezazaidi katika matumizi ya maji safi na salama, usafi wa

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

mazingira na usafi binafsi wa mwili. Aidha, jumla ya tani 50za dawa ya kutibu maji ya kunywa (Chlorine) ilisambazwakatika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani, Morogoro,Iringa, Mwanza, Mara, Kagera, Arusha, Kilimanjaro, Tanga,Dodoma, Mbeya, Rukwa, Singida, Kigoma na Manyaraambayo iliathiriwa zaidi na ugonjwa wa kipindupindu. Visimavirefu 18 vya maji vilichimbwa katika Mikoa ya Mara naMwanza kupitia msaada wa Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO).

22. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha udhibiti waugonjwa wa homa ya manjano, Wizara imeendeleakuhamasisha wananchi wanaotegemea kusafiri nje ya nchikuhusu umuhimu wa kupatiwa chanjo ya ugonjwa huo siku14 kabla hawajasafiri ambapo kati ya Julai 2016 hadi Machi2017 wananchi 26,045 wamepatiwa chanjo hiyo. Sambambana uhamasishaji huo, Wizara imezindua vyeti vipya vya Homaya Manjano vilivyoboreshwa vyenye alama maalum ya siriambayo itazuia kughushi vyeti hivyo, ambapo kuanzia mweziAgost 2016 mpaka sasa jumla ya vyeti 34,000 vimebadilishwakote nchini.

Usafi wa Mazingira

23. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kuratibu awamuya pili ya Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira (2016-2021) ambapo katika mwaka 2016/17, jumla ya kaya 391,937zimejenga vyoo bora, kati ya hizi, kaya 320,894 zina sehemumaalum ya kunawa mikono mara baada ya kutoka chooni.

24. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza chachu ya ushindanikatika kutekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira,Wizara iliendesha mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingirana kutoa zawadi mbalimbali kwa Halmashauri zilizofanyavyema. Katika mashindano hayo, Halmashauri ya Wilaya yaNjombe iliibuka mshindi wa jumla kitaifa na kukabidhiwazawadi ya gari jipya aina ya Toyota Hardtop 4WD. Zawadinyingine zilizotolewa kwa washindi ni pamoja na pikipiki 17,vyeti na vikombe. Aidha, katika kujenga uwezo waHalmashauri kusimamia na kufuatilia shughuli za afya

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

mazingira, Wizara ilinunua na kugawa jumla ya pikipiki kwaHalmashauri 100 nchini hususani za vijijini (Kiambatisho Na.1).

Udhibiti wa Magonjwa Yaliyokuwa HayapewiKipaumbele

25. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mpango wa Taifawa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbeleimeendelea kugawa dawa za kingatiba za matende,mabusha, usubi, trakoma, kichocho na minyoo ya tumbokatika Halmashauri zote zenye maambukizi haya . Katikakipindi cha Julai 2016 hadi Machi 2017, mpango umegawadawa katika Halmashauri 71 na kufikia watu millioni 14.3katika mikoa ya Dar Es Salaam, Pwani, Ruvuma, Rukwa,Mbeya, Dodoma, Singida, Tanga, Tabora, Manyara, Mtwara,Lindi na Morogoro. Katika zoezi hilo serikali imesambazavidonge milioni 54.5 vya dawa ya Mectizan kwa ajili ya kuzuiamaambukizi ya ugonjwa wa usubi na Matende, vidongemilioni 23.8 vya albendazole kwa ajili kuzuia maambukizi yaugonjwa waminyoo ya tumbo, vidonge milioni 13.3 vyadawa ya Prazquantel kwa ajili kuzuia maambukizi yaugonjwa wa kichocho na dozi million 8.7 ya dawa yaMectzan kwa ajili kuzuia maambukizi ya ugonjwa watrakoma.

26. Mheshimiwa Spika Serikali imefanya kambi za upasuajikwa wagonjwa 805 wa matende na mabusha bila malipoambapo 705 ni katika Halmashauri ya Temeke na Ilala jijiniDar es salaam na 100 katika mkoa wa Mtwara. Wizara ilifanyatathmini ya kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wamatende na mabusha katika Halmashauri 27 za mikoa yaDodoma, Katavi, Rukwa, Singida, Lindi, Mtwara, Ruvuma naPwani. Matokeo ya tathmini hii yameonesha kushuka kwakiwango cha maambukizi katika Halmashauri zote na hivyohazihitaji tena ugawaji dawa wa kingatiba; isipokuwa katikaHalmashauri ya Kondoa na Chemba.

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Udhibiti wa Malaria

27. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na juhudi zaudhibiti wa malaria nchini, kwa kutekeleza afua mbalimbalizinazopendekezwa kimataifa, ili kuhakikisha kuwa wananchiwanapata kinga na matibabu pale wanapothibitika kuwana vimelea vya malaria.

28. Mheshimiwa Spika, katika kuendelea namapambano dhidi ya Malaria, Wizara imesambaza dawaza kutibu malaria na vipimo vya kupima malaria (mRDT)kwenye mikoa 26 ya Tanzania Bara. Katika kipindi cha Julai2016 hadi Machi 2017, jumla ya dozi za ALU 12,530,040 naVitepe vya mRDT 15,511,500 vimenunuliwa na kusambazwakatika vituo vya huduma za afya nchini. Aidha, uhamasishajiwa jamii juu ya matumizi ya kipimo cha mRDT na matibabusahihi ya malaria kupitia kampeni ya “SIO KILA HOMA NIMALARIA NENDA UKAPIME” umeendelea kufanyika katikamikoa yote nchini.

29. Mheshimiwa Spika, unyunyiziaji wa dawa ukokaumefanyika katika mikoa minne ya Kanda ya Ziwa ambayoina maambukizi makubwa zaidi ya malaria hapa nchiniambayo ni (Kagera, Mwanza, Mara na Geita). Pia kampeniya ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefuimetekelezwa katika Halmashauri ya Kilombero Mkoa waMorogoro na Halmashauri zote za Mkoa wa DSM. Jumla yavyandarua 2,617,465 vilinunuliwa na kusambazwa katikaHalmashauri hizo. Hivyo kukamilisha jumla ya Mikoa 23 yaKigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe,Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Manyara, Tanga,Pwani, Dar es Salaam, Arusha, kilimanjaro, Mara, Simiyu,Mwanza, Geita, Kagera na Morogoro ambayo ilikuwaimelengwa na kampeni ambapo jumla ya vyandarua27,189,572 vimesambazwa kwa kipindi cha mwaka 2015/2016na 2016/2017.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Udhibiti wa Kifua Kikuu na Ukoma

30. Mheshimiwa Spika, huduma za kifua kikuu na Ukomazimeendelea kuimarika nchini ambapo mafanikio makubwayameendelea kupatikana. Kwa hivi sasa kiwango chawagonjwa wanaotibiwa na kupona ni asilimia 90 kati yawaliogunduliwa kuugua kifua kikuu. Wizara imeendeleakuboresha huduma za vipimo kwa kuimarisha maabara 4za Kanda ya Mbeya (Hospitali ya Rufaa Mbeya), Mwanza(Bugando Medical Centre), Dodoma (Hospitali ya Rufaa yaMkoa) na Kilimanjaro (Hospitali ya Kibong’oto) ambazozimeweza kufunguliwa na kuanza kutoa huduma zauchunguzi wa vimelea vya kifua kikuu. Hapo awali hudumahii ilikuwa inapatikana katika maabara moja tu iliyopo katikaHospitali ya Taifa Muhimbili.

31. Mheshimiwa Spika, huduma za uchunguzi namatibabu ya kifua kikuu sugu zimeimarishwa na kusogezwakaribu na wananchi. Awali huduma hizi zilikuwa zinatolewakatika hospitali ya Kibong’oto (Kilimanjaro) pekee, ambapokuanzia Mwezi Desemba 2016 jumla ya vituo 18 vimeanzakutoa huduma hiyo. Vituo hivyo ni Tambuka reli, Bukombe,Mbogwe (Geita), Hospitali Amana, Ukonga, Rangi tatu naSinza (Dar es salaam), Newala (Mtwara), Ifakara-Kibaoni(Morogoro), Bagamoyo (Pwani), Hospital ya Rufaa ya KandaMbeya, Ruanda, Mana (Mbeya), Hospitali ya Rufaa ya Mkoawa Kagera, Rubya, Kamachumu (Kagera), Tanga Mjini(Tanga) na Bariadi (Simiyu). Aidha, shughuli mbalimbali zauelimishaji na uhamasishaji jamii kuhusu Kifua Kikuuzilitekelezwa ikiwemo kuendesha Kampeni kupitia vyombovya habari (TV, Radio) yenye lengo la kuibua wagonjwawapya wa kifua kikuu kwa kuwa ni asilimia 39 tu kati yawagonjwa 162,000 waliopo nchini ndio waliopo katikamatibabu. Tunamshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza mapambanodhidi ya kifua kikuu.

32. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imeendesha Seminakwa Waheshimiwa Wabunge mwezi Novemba, 2016,ambayo iliwezesha kuanzishwa rasmi kwa Umoja/Mtandao

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

wa Wabunge wanaofuatilia masuala ya Kifua Kikuu,(Tanzania Parliamentary TB Caucus) ikiwa ni utekelezaji wamaazimio ya kimataifa. Nitumie fursa hii kumpongeza Dkt.Faustine Ndugulile kwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza waTanzania Parliamentary TB Caucus. Aidha, nawapongezawabunge wote kwa kuwa chachu ya mapambano dhidi yakifua kikuu. Napenda kutumia fursa hii kuwaombaWaheshimiwa Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu waWilaya, Viongozi wa Dini, Madiwani na jamii kwa ujumlakuhimiza wananchi wote wenye dalili za ugonjwa wa kifuakikuu kupata tiba mara moja. Tusipofanya hivyo tunaiwekanchi katika hatari zaidi ya kuwa na wagonjwa wengi wakifua kikuu kwa kuwa mtu mmoja anayeugua na hajanzatiba anauwezo wa kuambukiza hadi watu 20 kwa mwaka.Nisisitize kuwa Kifua Kikuu Kinatibika na Huduma za Kupimana Matibabu hutolewa bila Malipo.

33. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha tunaibuawagonjwa wapya wa kifua kikuu, Wizara kwa kushirikianana Sekta Binafsi inatekeleza Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuuna Ukoma wa 2015-2020 wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuukupitia sekta binafsi; ambapo mwaka 2016 jumla yawagonjwa 7,090 kati ya 65,785 sawa na asilimia 11 waliibuliwakupitia vituo vya afya vinavyomilikiwa na Sekta Binafsi. Aidha,Wizara ilishirikisha maduka ya dawa muhimu (ADDO) katikakuibua wagonjwa wa Kifua kikuu, jumla ya wauza dawa300 kutoka mikoa 10 walipatiwa mafunzo ya mfumo wautoaji wa rufaa za wahisiwa wa ugonjwa wa kifua kikuu.Vilevile, Wizara imeongeza wigo wa utoaji huduma za kifuakikuu katika vituo binafsi vya afya kutoka asilimia 10 mwaka2014 hadi asilimia 15 mwaka 2016.

34. Mheshimiwa Spika, kuhusu jitiada za kutokomezaugonjwa wa ukoma, Wizara imeendelea kufanya kampenimaalum ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu dalili za ukoma nanamna ya kutambua mapema wagonjwa katika hatua zaawali za ugonjwa. Kampeni hiyo imetekelezwa katika wilayaza Kilombero, Liwale na Nanyumbu ambapo jumla yawagonjwa 61 waligunduliwa. Hii inaonesha kuwa bado kunauwepo wa ugonjwa huu katika wilaya hizi.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Udhibiti wa UKIMWI

35. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2016/17, Wizaraimeendelea na juhudi za kudhibiti UKIMWI kwa kutoa ushaurinasaha na kupima virusi vya UKIMWI (VVU). Kuanzia mweziJanuari hadi Desemba, 2016 jumla ya wateja wapya 7,447,102walipata ushauri nasaha na kupima VVU. Aidha, Wizaraimepanua wigo wa utoaji huduma za tiba na matunzo kwawatu wanaoishi na VVU. Hadi kufikia Desemba 2016, vituo6,155 vilikuwa vinatoa huduma za tiba na matunzo kwa watuwanaoishi na VVU. Kati ya vituo hivyo vituo 5,690 (92%)vinatoa huduma za maambukizi ya VVU kutoka kwa mamakwenda kwa mtoto. Vilevile, Wizara imeanzisha mfumo waufuatiliaji wa watoto wachanga waliozaliwa na mama wenyemaambukizi ya VVU. Programu hii imeweza kufanyamajaribio ya mfumo mpya uitwao “Mother baby cohortmonitoring system” katika mikoa 5 ya Iringa, Mbeya, Pwani,Tanga na Tabora ambapo tathmini yake imeonyesha kuwamfumo huu unafaa kuanza kutumika katika mikoa yotenchini. Mpango huu utasaidia katika kubaini mapemawatoto walioathirika na VVU.

36. Mheshimiwa Spika, kuanzia mwezi Oktoba 2016,Wizara il ianza kutoa dawa za ARV kwa watu wenyemaambukizi ya Virusi vya VVU/UKIMWI (WAVIU) bila kujalikiwango cha CD4 ambapo hadi Machi 2017 jumla ya WAVIUwanaotumia ART/ARV ni 849,594 ambayo ni sawa na asilimia60 ya watu million 1.4 wanaokadiriwa kuwa na maambukiziya VVU nchini. Kati ya hao watoto 55,670 wako kwenyematibabu ya ARV ambayo ni asilimia 50% ya lengo. Aidha,huduma mkoba za UKIMWI na Kifua kikuu zimeendeleakutolewa, na hadi Desemba 2016 asilimia 96 ya WAVIUwanaohudhuria kliniki za Tiba na matunzo wamepimwa halizao za maambukizi ya kifua kikuu na dawa za Isonizidi yakuzuia maambukizi ya Kifua kikuu kwa WAVIU inatolewakatika vituo 512 sawa na asilimia 30 ya vituo vya matunzona Tiba kwa WAVIU. Pia, Wizara imefunga mashine mpya 14za kupima uwingi wa virusi vya UKIMWI {viral load} katikadamu katika hospitali za rufaa za mikoa ya Mtwara, Dodoma,Tabora, Iringa, Morogoro, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Hospitali za Rufaa za Kanda - Bugando, Mbeya, KCMC,Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Maabara ya Taifa yaViwango na Ubora.

37. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekelezaafua ya tohara kwa wanaume kama mojawapo ya afua yakupambana na maambukizi ya VVU. Kuanzia mwezi Januarihadi Desemba, 2016 jumla ya wanaume 374,411 kati ya lengola wanaume 492,844 wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi49 wamepata huduma ya Tohara kutoka mikoa 14 yakipaumbele (Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, RuvumaNjombe, Iringa, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu,Mara (Wilaya ya Rorya) na Kagera na kufikisha jumla yawanaume 2,203,230 waliokwisha kupata huduma hiyo tanguilipozinduliwa nchini mwaka 2010. Idadi hiyo ni sawa naasilimia 79 ya wanaume 2,800,000 wanaopaswa kufikiwaifikapo mwaka 2017.

38. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadauimebuni kifungashio kipya kwa kondom ya kiume ambayoimekuwa ikitolewa na serikali na kuipa jina la ZANA. Kondomya ZANA ilizinduliwa kitaifa katika mkoa wa Mbeya nakutambulishwa kwa umma na hali kadhalika, uzinduziulifanyika pia katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Tanga,Dodoma, Mtwara, Kigoma na Morogoro. Jumla ya kondomza ZANA 21, 000,000 ziliagizwa na kusambazwa katika mikoayote kupitia Bohari ya Dawa.

Udhibiti wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Nchini

39. Mheshimiwa Spika; kutokana na ongezeko kubwa laMagonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Kisukari, Shinikizola Damu na Magonjwa ya Moyo, Wizara imeandaa Mkakatiwa Kitaifa wa kupambana na magonjwa Yasiyo yaKuambukiza wa 2016 – 2020 ambao ulizinduliwa Dodomamwezi Novemba 2016. Hatua hiyo ilifuatiwa na kuanzishwakwa Kampeni ya Kitaifa inayolenga katika kuhamasishawananchi kufanya mazoezi na kupima afya mara kwa marana kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa. Kampeni hiyo

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

ilizinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia SuluhuHassan mwezi Desemba 2016 jijini Dar es Salaam, ambapopamoja na mambo mengine Mhe. Makamu wa Rais aliagizakuwa kila Jumamosi ya Pili ya Mwezi iwe ni Siku ya Hamasaya Kufanya Mazoezi.

40. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa agizo hilo umeanzamara moja ambapo Mikoa/Halmashauri mbalimbaliinaandaa mazoezi ya pamoja angalau mara moja kwamwezi lengo likiwa ni kujenga utamaduni kwa wananchihasa wanaoishi mijini na wanaofanya kazi za ofisini kufanyamazoezi ya mwili mara kwa mara na hivyo kupunguzamaradhi, ulemavu na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoya kuambukiza. Sambamba na kampeni ya mazoezi, Wizaraimeendelea kuhamasisha wananchi kuzingatia mfumo borawa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula unaofaa, kupunguzaunywaji wa pombe kupita kiasi, kujiepusha na matumizi yasigara na bidhaa za tumbaku pamoja na kujenga utamaduniwa kupima afya mara kwa mara. Inategemewa kuwa,kutekelezwa kikamilifu kwa mikakati hii kutapunguza kwakiasi kikubwa kasi ya kuongezeka kwa magonjwa haya nchini.

Udhibiti wa Matumizi ya Tumbaku na Kilevi

41. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na utekelezajiwa afua mbalimbali zenye lengo la kuelimisha wananchi juuya madhara ya Tumbaku, pamoja na kusimamia Sheria naKanuni zinazohusu Uvutaji Sigara na matumizi ya mazao yaTumbaku nchini kwa lengo la kulinda afya za wananchi.Katika kutekeleza hilo, Wizara imehakikisha kuwa Pakiti zaSigara zinazouzwa nchini hivi sasa zina maandishi ya onyo“Uvutaji wa Sigara una athari katika Afya” yanayoonekanakwa urahisi (yenye ukubwa wa asilimia 30). Aidha, kanuni zamwaka 2014 za kudhibiti matumizi ya tumbaku zilifanyiwamapitio na kuongeza suala la udhibiti wa matumizi ya Shisha.Kanuni hizi zinatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanziamwezi Julai 2017.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto

42. Mheshimiwa Spika, Upatikanaji wa hudumainayofikiwa na wanawake wote, kabla ya ujauzito, wakatiwa ujauzito, na wakati wa kujifungua hadi wiki sita baadaya kujifungua ni muhimili muhimu wa kupunguza vifovitokanavyo na uzazi. Hata hivyo, tatizo la vifo vitokanavyona uzazi bado ni changamoto. Tafiti zilizofanyika hapa nchinimwaka 2015 zinaonyesha kwamba vifo vitokanavyo na uzazihavijapungua, ambapo takwimu zinaonesha idadi ya vifoni 556 kwa kila vizazi hai 100,000. Katika kuimarisha hudumaza Afya ya Uzazi na Mtoto nchini, Wizara imeandaa MpangoMkakati unaotekelezwa kuanzia mwaka 2016 hadi 2020unaolenga kuboresha afya ya uzazi, watoto na vijanapamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kufikia 292kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2020. Katikakutekeleza mkakati huo, Wizara imezingatia maeneo makuumatatu: ambayo ni: huduma ya uzazi wa mpango, hudumawakati wa ujauzito na huduma wakati wa kujifungua.

43. Mheshimiwa Spika, uzazi wa mpango ni eneo muhimukatika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na kuhakikishaafya nzuri kwa mama na mtoto. Tafiti zinaonyesha kwambauzazi wa mpango ukitumiwa kikamilifu, unaweza kupunguzavifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 30. Hivyo, Wizarayangu imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali ili kuhakikishakwamba huduma hii inapatikana kwa wote wanaoihitaji.Katika kipindi cha Julai 2016 hadi Machi 2017, jumla ya wateja357,244 walifikiwa kupitia huduma za mkoba na 2,509,280walifikiwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya. Wizarakwa kushirikiana na wadau imetoa mafunzo kwa watoahuduma 3,233 ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma zaaina mbalimbali za uzazi wa mpango. Aidha, Wizaraimenunua na kusambaza dawa za uzazi wa mpango ikiwani pamoja na “Depo-provera” vichupa 4,973,811, “Microval”mizunguko (cycles) 743,615 na Kondomu za Kiume 13,096,916.Utekelezaji wa afua hizo umewezesha kiwango cha kutumiauzazi wa mpango kupanda kutoka asilimia 27 mwaka 2010hadi asilimia 32 mwaka 2015/16 (TDHS). Lengo ni kufikiaasilimia 45 mwaka 2020.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

44. Mheshimiwa Spika, kuhusu huduma wakati waujauzito imebainika kuwa matatizo mengi wakati wa ujauzitoyanaweza kuzuil ika, kugundulika na kutibiwa kamawanawake wajawazito watahudhuria kliniki ya wajawazitona kupimwa na wahudumu wenye ujuzi. Hudumazinazopaswa kutolewa katika kliniki za wajawazito ni pamojana; chanjo ya pepopunda, kupimwa wingi wa damu,kupimwa protini kwenye mkojo, kupimwa kamakunauambukizo wa VVU na vimelea vya kaswende nakupewa matibabu. Huduma nyingine zinazotolewa nikugundua dalili za hatari na kutoa matibabu mapema wakatiwa ujauzito. Katika kipindi cha 2016/17, Wizara kwakushirikiana na wadau iliendelea kuhakikisha huduma hizizinapatikana sambamba na kuelimisha wajawazitokuhudhuria kliniki. Kulingana na tafiti zilizofanyika mwaka2015/16 asilimia 98 ya wajawazito wote walihudhuria klinikiangalau mara moja na asilimia 51 walihudhuria angalaumara 4 ambacho ni kiwango cha chini cha mahudhuriokinachopendekezwa. Lengo ni kufikisha asilimia 70 yawanawake wajawazito kuhudhuria kliniki angalau mara 4katika kipindi cha ujauzito ifikapo mwaka 2020. Nitumie fursahii kuwahimiza akinamama wajawazito kuhudhuria klinikikama inavyoshauriwa.

45. Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma wakatiwa kujifungua ikiwemo huduma ya dharura wakati wakujifungua hadi wiki sita baada ya kujifungua, ni muhimusana ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi. Huduma kwamatatizo haya hupatikana tu kwenye vituo vya kutoleahuduma ya afya na mtoa huduma mwenye ujuzi. Katikamwaka 2016/17, Wizara kwa kushirikiana na wadauimeendelea kuhamasisha na kuhimiza wanawakewajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma.Idadi ya akinamama wanaojifungulia katika vituo vyakutolea huduma imeongezeka kutoka asilimia 51 mwaka2010 hadi kufikia asilimia 64 mwaka 2015/16. Napenda kutoawito kwa wanawake wajawazito wote nchini wajifunguliekwenye vituo vya kutolea huduma ya afya ili kupunguza vifona changamoto za uzazi kwa mama na mtoto. Aidha,Wizara imetoa mafunzo mbalimbali ya uzazi salama na

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

huduma za dharura wakati wa ujauzito na kujifungua kwawatoa huduma 1,300 nchini.

46. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kusogezahuduma karibu na wananchi, Wizara kwa kushirikiana na OR- TAMISEMI, imekamilisha ukarabati wa vituo vya afya 8 katikaMikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu na Mara ili viweze kutoahuduma za uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji wa kutoamtoto tumboni (CEmONC). Hadi sasa vituo vya Afya 171vinatoa huduma za upasuaji na kati ya hivyo, 117vinamilikiwa na Serikali ambapo ni sawa na asilimia 21 yavituo vya afya 473 vinavyomilikiwa na Serikali. Aidha vituovya afya 145 viko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ilikuweza kutoa huduma za dharura za uzazi ikiwemo upasuajiwa kutoa mtoto. Lengo la serikali ni kuhakikisha angalauasilimia 50 ya vituo vya afya nchini vinatoa huduma kamiliza uzazi wa dharura ifikapo mwaka 2020.

47. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kukabiliana natatizo la uhaba wa damu hasa kwa wanawake wajawazito.Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI imeanzisha utaratibuwa kuwa na vituo vya benki za damu kwenye ngazi ya mikoahapa ili visaidaine na benki za damu za kanda katikakuboresha upatikanaji wa damu salama. Hadi sasa Benki zadamu za Mikoa 7 zimeanzishwa katika mikoa ya Dar essalaam, Lindi, Morogoro, Dodoma, Iringa, Kigoma naShinyanga. Aidha, uanzishwaji wa benki hizo katika mikoaya Mara na Kagera upo katika hatua za mwisho. Lengo nikuhakikisha kila Mkoa una Benki ya Damu ikiwa ni jitihada zakupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

48. Mheshimiwa Spika, Huduma za Rufaa kwaWajawazito zimeendelea kuboreshwa ambapo Wizaraimegawa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 67katika Halmashauri za Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa naKigoma na mikoa mingine hapa nchini. Aidha, Wizaraimegawa magari 8 kwa ajili ya kuratibu shughuli za afya yamama na mtoto katika Kanda ya Ziwa, Kati, Magharibi, OR- TAMISEMI Dodoma, na magari 2 katika kitengo cha Afya yamama na Mtoto Wizarani. Hatua hiyo itatoa msukumo na

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

kuimarisha juhudi za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazikatika mikoa hiyo ambayo takwimu zimeonesha kuwa wanavifo vingi zaidi kuliko mikoa mingine nchini.

49. Mheshimiwa Spika, Wizara imechukua hatua kwa ajiliya kuongeza uwajibikaji kwa ngazi zote ili kupunguza vifovitokanavyo na uzazi kwa kutaka kila kifo cha mama namtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kijadiliwe ndaniya saa 24 katika kituo/hospitali husika kwa lengo la kubainichimbuko la kifo hicho na kuchukua hatua stahiki ikiwa nipamoja na kuboreshwa zaidi kwa huduma zinazotolewakatika kituo husika. Miongozo imeandaliwa na mafunzo yakujenga uwezo yamefanyika kwa mikoa yote nchini.Sambamba na hilo Wizara kuanzia mwezi Oktoba 2016imeanzisha utaratibu wa kutaka kila halmashauri na mikoanchini kutoa taarifa ya vifo vitokanavyo na uzazi kila mwezi.Taarifa hizi zinafanyiwa kazi na hatua stahiki zimekuwazikichukuliwa na mrejesho kutolewa kwa Mikoa naHalmashauri husika.

50. Mheshimiwa Spika, kuhusu vifo vya watoto, kupitiaMpango Mkakati wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa 2016-2020,Serikali imedhamiria kuwa ifikapo 2020 kupunguza vifo vyawatoto wa chini ya mwezi mmoja kutoka 21 hadi 16 katikakila vizazi hai 1,000; vifo vya watoto wa chini ya umri wamwaka mmoja kutoka 45 hadi 25 katika kila vizazi hai 1,000na vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano kutoka54 hadi 40 katika kila vizazi hai. Katika mwaka 2016/17,Wizara imeendelea kuwajengea uwezo watoa huduma yaafya 241 katika wilaya tano za mkoa wa Iringa. Aidha katikakupunguza vifo vya watoto waliozaliwa na uzito pungufu,Wizara ilitoa mafunzo kwa watoa huduma 143 jinsi yakumtunza mtoto mchanga kwa njia ya Kangaroo.

51. Mheshimiwa Spika, Jamii ni sehemu muhimu katikamikakati ya kuboresha afya ya uzazi na mtoto. Hivyo katikamwaka 2016/17 Wizara imetoa mafunzo ya afya ya uzazi namtoto kwa wahudumu 1,649 wa afya kwa ngazi ya jamii(Community Health care Workers program) ambaowanatumika kuhamasisha na kuelimisha jamii wanapoishi.

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Aidha Wizara imeanzisha mpango maalum wa kuwa nakada ya watoa huduma ngazi ya jamii watakaoajiriwabaada ya kupata mafunzo rasmi yaliyopitishwa na NACTE.Katika mwaka wa fedha 2016/17, jumla ya wahudumu 3,688walihitimu mafunzo yao.

52. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na juhudi zakudhibiti saratani za via vya uzazi (Reproductive cancers)ikiwemo saratani ya mlango ya kizazi, saratani ya matiti nasaratani ya Tezidume. Katika kuhakikisha kuhakikishaupatianaji wa huduma za kupima na matibabu yaMabadiliko ya awali ya Saratani ya Mlango wa kizazi nasaratani ya matiti ambazo ndizo zinazoongoza nchini, vituo360 vya kupima dalili za awali ya Saratani ya mlango wakizazi vimeanzishwa na kutoa huduma hiyo katika mwakawa fedha 2016/17. Aidha Taasisi za Serikali na mashirika yasiyoya kiserikali yameendesha kampeni za kuelimisha jamii juuya kudhibiti saratani za via vya uzazi sambamba na kuandaakambi na huduma za kupima saratani za uzazi katika maeneombalimbali nchchi.

Huduma za Lishe

53. Mheshimiwa Spika katika mwaka 2016/17, Wizarainaendelea kushirikiana na asasi mbalimbali za Serikali nazisizo za kiserikali kuhakikisha virutubishi muhimu kwa ukuajiwa mwili na akili vinaendelea kupatikana kote nchini. Kwasasa urutubishaji unaoendelea ni ule wa uongezaji wavirutubishi muhimu kwenye unga wa mahindi na unafanyikakatika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Dar es Salaamwakati mikoa ya Iringa (Kilolo na Iringa vijijini), Njombe(Njombe mjini) na Arusha (Monduli, Karatu na Meru)inaendelea na mradi wa urutubishaji vijijini. Aidha usindikajiwa mafuta ya alizeti kwa kuongeza vitamini A unaendeleakatika mikoa ya Singida na Manyara. Jumla ya mikoa 11(Dodoma, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi, Iringa,Mbeya, Tabora, Rukwa, Mara na Simiyu) imefikiwa kupitiampango wa urutubishaji chakula kwa kutumia virutubishinyongeza kwenye chakula cha kawaida kwa watoto wenyeumri wa miezi 6 hadi 59 katika ngazi ya jamii (Home food

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Fortification). Kwa mujibu wa takwimu za TDHS 2015/16 kayazinazotumia chumvi yenye madinijoto kwa viwangovilivyowekwa kisheria zimeongezeka na kufikia asilimia 61kutoka asilimia 47 mwaka 2010.

Elimu ya Afya kwa Umma

54. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2016/17, Wizarailiendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kutunza afya zaodhidi ya magonjwa na kufanya uchunguzi wa afya mara kwamara. Wizara iliendelea kuelimisha jamii kujikinga naugonjwa wa kipindupindu kupitia matangazo ya Radio,Runinga, simu za kiganjani kwa kupiga simu nambari 117 bilamalipo. Aidha Wizara ilitayarisha na kusambaza kupitiamitandao ya kijamii elimu kuhusu magonjwa ya kuambukizana yale yasiyo ya kuambukiza. Vilevile, Wizara ilihakikimatangazo na vielelezo mbalimbali vilivyotayarishwa nawadau, kuhusu ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja nakuzingatia Sera na Miongozo ya Wizara. Matangazo naVielelezo hivyo vilihusu uzazi wa mpango, afya ya uzazi namtoto, saratani ya mlango wa kizazi, lishe, chanjo, UKIMWI,kifua kikuu, afya ya mazingira, magonjwa yanayoambukizana yasiyo ya kuambukiza, magonjwa yaliyokuwa hayapewikipaumbele, malaria, afya ya kinywa na meno pamoja namacho. Wizara imekamilisha ujenzi wa studio ya radio naruninga ambazo zitaiwezesha Wizara kurekodi vipindi vyakuelimisha na kuhamasisha jamii.

HUDUMA ZA TIBA

Huduma za Damu Salama

55. Mheshimiwa Spika Wizara kupitia Mpango wa Taifawa Damu Salama imeendelea kutekeleza jukumu laukusanyaji na usambazaji wa Damu Salama nchini, ambapokatika kipindi cha Julai 2016 hadi Machi, 2017 jumla ya chupaza damu 145,300 zilikusanywa, sawa na asilimia 63 ya lengola kukusanya chupa 230,000 kwa mwaka. Chupa zote zadamu zilizokusanywa ziliweza kupimwa kwa ufasahamagonjwa yote manne ambayo ni VVU, kaswende, homa

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

ya ini aina B na C pamoja na kuangalia makundi ya damu,ambapo jumla ya chupa 130,408 sawa na asilimia 90zilionekana kutokuwa na maambukizi ya aina yoyote nahatimaye kusambazwa hospitalini kwa ajili ya kupewawagonjwa wahitaji.

Upatikanaji wa Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

56. Mheshimiwa Spika; Serikali imeendelea kutoakipaumbele katika kuboresha upatikanaji wa dawa kwakununua, kutunza na kusambaza dawa, vifaa, vifaa tiba navitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.Katika mwaka 2016/17, Wizara il itenga Shilingi251,500,000,000.00 kwa ajili ya kununua na kusambaza dawa,vifaa, vifaa tiba,na vitendanishi ikilinganishwa na kiasi chaShilingi 31,000,000,000.00 kilichotengwa mwaka 2015/16. Hadikufikia Machi 2017, jumla ya Shilingi 112,198,920,456zilipokelewa ambazo ni sawa na asilimia 45. Hadi kufikiamwezi Machi 2017 mikoa/halmashauri/hospitali zimepokeazaidi ya asilimia 95 ya fedha za dawa. (kiambatisho Na. 2)Upatikanaji wa fedha hizi umeboresha upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba nchini ikilinganishwa na kipindi kilichopita.Nitumie furusa hii kuzitaka mamlaka za halmashauri namikoa/hospitali kuhakikisha uwepo wa mifuko maalum yadawa (drung revolving fund) katika maeneo yao il ikuhakikisha upatikanaji endelevu wa fedha za dawa, vifaa,vifaa tiba na vitendanishi.

57. Mheshimiwa Spika; Hadi kufikia Machi, 2017, asilimia81 ya dawa muhimu zaidi (essential medical items)zinapatikana katika Bohari ya Dawa. Ongezeko hili laupatikanaji wa dawa kutoka asilimia 36 kipindi cha mweziJuni 2016 na kufikia asilimia 81 mwezi Machi, 2017 limetokanana uamuzi wa Serikali wa kuongeza bajeti ya dawa nakuhakikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya dawa, vifaa,vifaa tiba, na vitendanishi. Aidha, katika kuboreshaupatikanaji wa dawa, Wizara kupitia Bohari ya Dawa (MSD)imeanza kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo ununuziwa dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kwa lengola kupunguza gharama za dawa na kuongeza uwezo wa

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

MSD kununua dawa nyingi zaidi ambapo Zabuni 6 zawazalishaji zimekamilika. Kukamilika kwa zabuni hizi,kutawezesha upatikanaji wa dawa muhimu zaidi kutokamoja kwa moja kwa wazalishaji kwa asilimia 76. Lengo laWizara ni kuhakikisha hali ya upatikanaji wa dawa inafikiaasilimia 90 ifikapo mwishoni mwa mwaka wa fedha 2016/17.

58. Mheshimiwa Spika; kuimarika kwa hali ya upatikanajiwa dawa, vifaa, vifaa tiba, na vitendanishi katika Bohari yaDawa kumeongeza upatikanaji wa dawa kwenye vituo vyaumma vya kutolea huduma za Afya afya nchini. Kwa mujibuwa takwimu zil izokusanywa kutoka katika Mikoa naHalmashauri mbalimbali nchini, hali ya upatikanaji wa dawakwenye vituo inakadiriwa kuwa wastani wa asilimia 83kufikia mwishoni wa Machi 2017 (Kiambatisho Na. 3). Wizaraitaendelea kukusanya taarifa za upatikanaji wa dawa kutokaHalmashauri na Mikoa kila mwezi ili kujiridhisha zaidi juu yahali halisi ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutoleahuduma hasa ngazi ya zahanati na vituo vya afya. Hatahivyo, bado zipo changamoto mbalimbali katika upatikanajiwa dawa ikiwemo baadhi ya Halmashauri /Hospitalikutowasilisha mahitaji yao ya dawa kwa wakati na hivyokusababisha tatizo la upatikanaji wa dawa katika vituo.Vilevile, kuna usimamizi hafifu wa matumizi ya dawa,makusanyo na matumizi ya fedha zitokanazo na uchangiajiwa huduma za afya na matumizi ya mifumo na utunzajitaarifa za dawa na vifaa tiba. Wizara imejipanga kukabilianana changamoto hizi kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI. Mojaya hatua tulizochukua ni kuamua kuwa kuanzia Julai 2017fedha za dawa kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya (HealthBasket Fund) zitapelekwa moja kwa moja kwenye vituo vyakutolea huduma. Nitumie fursa hii kuzitaka mamlaka zahalmashauri na mikoa kuhakikisha wanasimamia fedha hizoikiwemo makusanyo na matumizi ya fedha zitokanazo nauchangiaji wa huduma za afya sambamba na kutoa taarifasahihi za hali ya upatikanaji wa dawa.

59. Mheshimiwa Spika; kwa kutambuachangamoto zilizopo katika mfumo wa ugavi na usambazaji

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

wa dawa, vifaa, vifaa tiba, vitendanishi na chanjo nchini,Wizara imefanya mapitio ya mfumo (Holistic Supply ChainReview) kwa lengo la kuandaa mpango mkakati wautekelezaji ili kuwa na mfumo madhubuti wenye kukidhimahitaji ya nchi.

60. Mheshimiwa Spika; Wizara pia imetekeleza ahadi yaMhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kila kituocha kutolea huduma za afya cha umma kinakuwa na vifaavya kutosha. Katika mwaka 2016/17, Wizara imenunua nakuanza kusambaza kwa kila Halmashauri vitanda vyakawaida 20, vitanda vya kujifungulia 5, magodoro 25 namashuka 50. Uzinduzi wa zoezi hili umefanyika mwezi Aprili2017 katika halmashauri ya Kongwa Dodoma. Jumla yavitanda vya kawaida (Hospital beds) 3,680, vitanda vyakujifungulia (delivery beds) 920, magodoro 4,600 na mashuka9,200 vimenunuliwa ambapo thamani yake ni Shilingi2,933,125,600.00

61. Mheshimiwa Spika, Usugu wa dawa aina ya antibiotikini tatizo kubwa ambalo linaikabili dunia kwa sasa. Hali yaDunia ya utumiaji wa dawa aina ya antibiotiki kwa mwaka2015 inaonyesha kwamba matumizi ya dawa hizo kwa ukuzajiwa kuku, ng’ombe na nguruwe, husababisha Usugu wa dawakwa vimelea vya bakteria ambavyo vinaenea kwabinadamu. Aidha, utafiti uliofanyika hapa nchini umeoneshakuongezeka kwa usugu wa dawa za antibiotiki katika kutibumagonjwa ya kuambukiza kwa binadamu, wanyama namazingira.

62. Mheshimiwa Spika, Katika kupambana na usugu wadawa hizo, Serikali imeitikia tamko la Mkutano Mkuu wa 68wa Shirika la Afya Duniani uliofanyika mwaka 2015 ambaponchi Wanachama walikubaliana kufanya juhudi za dhati zakupambana na usugu wa dawa hizo. Wizara yangu kwakushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na uvuvi na Wadauwengine imeandaa mpango wa miaka mitano wakupambana na usugu wa dawa hizo kwa binadamu, mifugona kilimo. Mpango huu umekamilika na kuzinduliwa mweziAprili, 2017.

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

63. Mheshimiwa Spika Mpango huo pamoja na mambomengine umelenga kuhamasisha na kuelimisha wataalamwa afya na wananchi kwa ujumla juu ya madharayatokanayo na utumiaji wa dawa za antibiotiki usio sahihikwa binadamu, mifugo na kwenye kilimo na jinsi ya kutatuachangamoto hizo. Aidha, Wizara itaendelea kusimamiautumiaji ulio sahihi wa dawa aina ya antibiotiki hasa kwakufuata sheria na kanuni zilizowekwa na inapobidi kuandaasheria mpya; Kuzuia maambukizi ya vimelea vya bakteria kwakuzingatia usafi wa mazingira hasa sehemu za kutoleahuduma na katika kukuza mifugo.

Uimarishaji wa Huduma za Matibabu ya kibingwa

64. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, moja yajukumu la kipaumbele kwa Wizara ilikuwa ni kuendeleakuboresha na kuimarisha huduma za kibingwa zitolewazonchini. Maboresho hayo, yanalenga katika kupunguza idadiya wagonjwa wanaopewa rufaa ya Matibabu nje ya nchi ilikupunguza gharama kubwa ambazo serikali inaingia katikakupeleka wagonjwa nje ya nchi. Hadi kufikia Machi 2017,idadi ya Wagonjwa waliopewa rufaa ya Matibabu nje yanchi ilipungua kwa asilimia 35 kutoka wagonjwa 553 mwaka2015/16 hadi Wagonjwa 357 mwaka 2016/17. Mafanikio hayani kutokana na maboresho yaliyofanyika katika Hospitali zilizochini ya Wizara zinazotoa huduma za Kibingwa ambazo niHospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo JakayaKikwete (JKCI), MOI na Ocean Road. Takwimu za mwaka2016/17 zinaonyesha kuwa magonjwa yanayoongozwa kwarufaa nje ya nchi ni Saratani (36%), Moyo (17%), Masikio, puana koo (15%), mishipa ya fahamu (8%), mifupa (4%) namengineyo (5%).

Hospitali ya Taifa Muhimbili

65. Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017, Hospitali ya Taifa Muhimbili imewahudumiajumla ya wagonjwa wa nje 317,660 ikilinganishwa nawagonjwa 357,343 waliopatiwa huduma mwaka 2015/2016.Aidha, hospitali ilihudumia jumla ya wagonjwa waliolazwa

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

39,418 ikilinganishwa na wagonjwa 51,698 mwaka 2015/2016.Pia, ukusanyaji wa mapato ya Hospitali umeongezeka nakufikia kiasi cha shilingi 39,793,000,000 kwa kipindi cha Julai2016 hadi Machi, 2017 ikilinganishwa na shilingi 30,145,000,000zilizokusanywa katika kipindi kama hicho 2015/16 ikiwa nisawa na ongezeko la asilimia 32.

66. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Taifa Muhimbiliimeendelea kuchukua hatua mbalimbali zenye lengo lakuboresha utoaji wa huduma za kibingwa. Hatua hizo nipamoja na kufanya ukarabati wa Wodi mbalimbali kwalengo la kuongeza uwezo wa kuhudumia wagonjwa wengi,ambapo jumla ya wadi 5 za ICU zimefanyiwa ukarabati.Ukarabati huo utaongeza vitanda vya ICU kutoka 21 nakufikia 75. Aidha, mashine 14 za upasuaji (DiathermyMachines), mashine kubwa mbili (2) za utakasishaji vifaa zenyethamani ya Shilingi milioni 717.6 zimenunuliwa. Vilevile,Hospitali imenunua mashine ya CT-Scan mpya yenye uwezowa “slice” 128, ambayo imegharimu Shilingi bilioni 3.9. PiaHospitali imefanya ukarabati wa mashine za ventilators,monitors na anaesthesia kwa jumla ya Shilingi milioni 213.Hospitali imeanza kukarabati jengo kuu la upasuaji wa kinamama wajawazito na jengo la upasuaji wa watoto;ukarabati huo utaongeza vyumba vya upasuaji 6 na kufanyaHospitali iwe na jumla ya vyumba 19. Upanuzi wa jengo lakusafisha figo unafanyika ambao utaongeza vitanda 27 nakufikia jumla ya vitanda 42 ambapo jumla ya Shilingi bilioni1.02 zitatumika. Aidha, Hospitali ya Taifa ya Muhimbiliimepeleka jumla ya wataalamu saba (7) nchini India kwaajili ya mafunzo ya upandikizaji wa vifaa vya kusaidia kusikia(Cochlear Implants) kwa wagonjwa wenye matatizo yakusikia. Jumla ya Shilingi milioni 75.8 zimetumika katikamafunzo haya. Vilevile katika kuhakikisha upatikanaji wahuduma za kubadilisha figo nchini, wataalamu ishirini (20)wakiwemo Madaktari, Wauguzi, Wataalamu wa Maabarawamepatiwa mafunzo nchini India kwa gharama ya Shilingimilioni 700.

67. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Taifa ya Muhimbil piaimepanua sehemu ya kutoa huduma za dharura ili kuendana

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

na ongezeko la wagonjwa sambamba na kuwa na sehemuya dharura kwa ajili ya watoto. Upanuzi huo umeshakamilikakwa asilimia 60 na utagharimu Shilingi bilioni 1. Aidha,Hospitali imekarabati Wadi ya Sewahaji namba 18 kwa ajiliya wagonjwa wa kulipia yenye vitanda 13 kwa kutumiaShilingi milioni 250 ambazo zimetokana na vyanzo vya ndani.Aidha, upatikanaji wa Dawa katika Hospitali ya TaifaMuhimbili umeongezeka na kufikia zaidi ya asilimia 95. VilevileHospitali imeanzisha mfuko wa fedha za kununulia dawa(Revolving Fund) ambao sasa umefikia Shilingi 1,000,000,000inayolipwa kila mwezi ili kukabiliana na changamoto zaupatikanaji wa dawa.

68. Mheshimiwa Spika, Hospitali kwa kushirikiana naMpango wa Damu Salama ilianzisha huduma za kuchangiadamu katika jamii zoezi ambalo limepunguza kwa kiasikikubwa sana ukosefu wa damu Hospitalini. Hospitaliimeanzisha mpango wa uchunguzi na tiba kwa ugonjwasugu wa homa ya ini ambao utatoa fursa kwa watanzaniakupata huduma hiyo. Mpango huo utawezesha vituo vinginekujifunza na kuweza kutoa huduma hiyo.

Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

69. Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017 Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)imewahudumia jumla ya wagonjwa wa nje 119,580ikilinganishwa na wagonjwa 79,927 waliopatiwa hudumamwaka 2015/2016. Aidha, hospitali ilihudumia jumla yawagonjwa waliolazwa 6,830 ikilinganishwa na wagonjwa8,355 mwaka 2015/2016. Pia, kutokana na matumizi yamfumo wa kieletroniki (HMIS) ukusanyaji wa mapato,umeongezeka kwa asil imia 8.5 na kufikiashilingi 6,707,172,559.43 kwa kipindi cha Julai 2016 hadiFebruari, 2017 ikilinganishwa na shilingi 6,134,667,970.65zilizokusanywa katika kipindi kama hicho 2015/16.

70. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya MOI imeendelea najuhudi za kupanua wigo wa huduma za kibingwa ambapokatika kipindi cha Julai 2016 - Machi 2017, imeanza kutoa

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

huduma ya upasuaji wa migongo ya watoto iliyopinda(paediatric scoliotic spine correction) ikishirikiana na Centreof Disease Excellence in Orthopaedics (COEDN) ya Marekanipamoja na kuanzisha mafunzo ya upasuaji huo. Aidha, Taasisihiyo imetoa huduma za upasuaji mkubwa kwa wagonjwa496, wakijumuisha wagonjwa 67 waliofanyiwa upasuaji wanyonga, 62 mgongo, 55 Ubongo, 262 watoto wenye vichwavikubwa na 50 watoto wenye mgongo wazi.

71. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya MOI kwa kushirikianana GSM Foundation imetoa huduma ya upasuaji wa vichwavikubwa na mgongo wazi kwa watoto kupitia kambi Tibakatika mikoa 18 ya Tanzania Bara na hospitali ya Mnazi Mmoja– Zanzibar. Katika kipindi cha Julai 2016 hadi Machi 2017, jumlaya watoto 2,200 walifanyiwa uchunguzi na watoto 250walifanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kutoa mafunzo kwaMadaktari wa upasuaji wa kawaida katika hospitali za rufaaza mikoa/kanda nchini. Kwa sasa Taasisi ipo kwenye mpangowa kuchukua madaktari wa upasuaji toka hospitali husikakuja Dar es Salaam kujifunza zaidi upasuaji huo. Aidha, Taasisikwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Weil Cornel na CaliforniaSan Francisco vya Marekani, inafanya utafiti wa kuboreshamatibabu kwa wagonjwa wa ajali ya Kichwa, mfupa wapaja na Ugoko.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

72. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai 2016 hadi2017, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKC) imewahudumiajumla ya wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na kurudinyumbani 37,199 ikilinganishwa na wagonjwa 24,570waliopatiwa huduma hiyo mwaka 2015/2016. Taasisi ilifanyaupasuaji wa moyo kwa wagonjwa 236 kwa gharama yashilingi 1,555,500,000.00 ambapo kama upasuaji huoungefanyika India ungegharimu takribani shilingi5,307,000,000.00, hivyo kuokoa kiasi cha shilingi3,751,500,000.00. Idadi hii ni sawa na wastani wa wagonjwa30 kwa mwezi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganishana wastani wa wagonjwa 15 kwa mwezi katika mwaka wafedha 2015/16. Kati ya wagonjwa 236 waliofanyiwa upasuaji,

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

watu wazima walikuwa 74 wakati watoto walikuwa 162.Asilimia 49 ya wagonjwa walifanyiwa upasuaji na madaktariwa JKCI na asilimia 51 walifanyiwa kwa kushirikana namadaktari kutoka nje ya nchi kupitia kambi za upasuaji wapamoja. Aidha jumla ya wagonjwa 608 walipatiwa matibabumaalum kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa kisasa- catheterization laboratory (stents, percutaneousintervention, device closure, pacemarker). Idadi hii niongezeko la asilimia 190 ukilinganisha na wagonjwa 290waliohudumiwa katika mwaka wa fedha 2015/16. Kati yawagonjwa hao, asilimia 82.6 walikuwa watu wazima naasilimia 17.4 walikuwa watoto. Asilimia 89 ya huduma yamatibabu maalum ya moyo kwa kutumia mtambo wa kisasa– catheterization laboratory zimefanywa na madaktari waTaasisi na asilimia 11 zilifanywa kwa kushirikiana na wataalamkutoka nje ya nchi.

73. Mheshimiwa Spika, Vilevile, JKCI ilifanya kambi 3 zaupasuaji kwa kushirikiana na mataifa rafiki (Israel, Germanyna Australia). Hatua hiyo imesaidia kujenga uwezo wamadaktari wazawa kwa kupata utaalam wa kupasuawagonjwa kutumia tundu dogo (hii inasaidia wagonjwakupona mapema na kuruhusiwa kurudi nyumbani ndani yasiku chache). Vilevile, JKCI kwa kushirikiana na Wizaraimeweza kupeleka madaktari 9 kwenye masomo ya juukatika fani ya moyo (2 Afrika ya Kusini, 2 Israel, 1 India, 1 Chinana 3 MUHAS). Pia imeweza kuchapisha matokeo ya chunguzizake kwenye majarida ya kimataifa machapisho 3 (3 peeredreviewed publications).

Taasisi ya Saratani Ocean Road

74. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2016 hadiMachi, 2017, Taasisi ya Saratani Ocean Road iliendelea kutoahuduma za uchunguzi, matibabu, kinga, mafunzo na utafitiwa saratani. Katika kipindi hicho, Taasisi imehudumia jumlaya wagonjwa 19,244 ambapo 3,982 ni wagonjwa wapya waSaratani, 13,109 ni wagonjwa wa marudio wa saratani, na2,133 ni wagonjwa wasio wa saratani ikilinganishwa na

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

wagonjwa 31,075 walipatiwa huduma na Taasisi katikamwaka 2015/2016. Aidha, jumla ya wanawake 6,717walifanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wakizazi na matiti na wanaume 534 walifanyiwa uchunguzi wasaratani ya tezi dume. Katika uchunguzi huo, jumla yawanawake 451 waligunduliwa kuwa na dalili za awali zasaratani ya mlango wa kizazi na 267 walikutwa na dalili zasaratani ya matiti. Vilevile, wananchi 1,204 walifanyiwauchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi, saratani yamatiti na saratani ya tezi dume katika kampeni ya mkoa waDar es Salaa iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmojapamoja iliyofanyika kwa Waheshimiwa wabunge, Dodomamwezi Februari 2017.

75. Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendelea kutoa hudumaza mkoba katika mikoa mbalimbali ambapo jumla yawagonjwa 3,215 walipatiwa matibabu na rufaa kufuatanana mwongozo wa huduma. Aidha, jumla ya wananchi 16,433walifanyiwa upimaji wa saratani katika mashirika mbalimbaliya serikali na yasiyo ya kiserikali katika huduma ya elimu naupimaji. Vilevile, Taasisi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu chaAfya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) iliendeleakutoa mafunzo kwa wanafunzi 43 wa Shahada ya Kwanzaya Tiba ya Saratani kwa Mionzi na wanafunzi 17 wa Shahadaya Uzamili katika Sayansi ya Tiba ya Saratani. Wanafunzi 2walihitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Tiba yaSaratani na wanafunzi 3 Shahada ya Kwanza ya Tiba yaSaratani kwa Mionzi. Pia, Taasisi imeendelea kushirikiana nawadau wa ndani na nje katika utafiti wa Saratani na katikakipindi husika jumla ya machapisho matatu (3) yalichapishwakatika majarida ya kisayansi duniani (peer-reviewed journals).

76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Taasisi yaSaratani Ocean Road imekamilisha ukarabati wa jengo lakutolea tiba ya dawa (chemotherapy) pamoja na kununuavifaa na vitanda ambapo idadi ya wagonjwawanaohudumiwa imeongezeka kutoka wastani wa wagonjwa40 hadi kufikia wagonjwa 100 kwa wakati mmoja. Aidha,Taasisi imeweza kupunguza muda wa kusubiri kuanza tibaza mionzi (radiotherapy) kutoka miezi 3 hadi wiki 6; kwa

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

kuhakikisha wagonjwa wanapata tiba mara mbili kwa wikina kufanya matengenezo ya mashine kwa haraka. Lengo laWiraza ni kupunguza muda huo uwe chini ya wiki 2 pindimashine mpya za LINAC zitakaposimikwa.

77. Mheshimiwa Spika, upatikanajii wa dawa za sarataniumeboreshwa kutoka asilimia 4 mwaka 2015/16 hadi kufikiaasilimia 60 mwezi Machi, 2017; na kwa baadhi ya saratanikama ya mlango wa kizazi, saratani ya koo, tezi dume nadawa za dripu (chemotherapy) zinapatikana kwa asilimia100. Aidha, upatikanaji wa dawa za mionzi hasa radioactiveiodine kwa sasa zinapatikana kwa asilimia 100 na ununuziwa dawa hizo unafanywa kutoka kiwandani nchini AfrikaKusini kupitia MSD. Taasisi imeanzisha duka la dawa la jamiiambalo limeongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwawagonjwa na hasa wale wa Bima na kuongeza mapato yadawa kutoka Milioni 30 kwa mwezi hadi kufikia Milioni 700kwa mwezi.

78. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Saratani Ocean Roadilikamilisha ujenzi wa jengo la ‘bunker’ ambapo mashine zamionzi za LINAC pamoja na CT Simulator zitasimikwa. Aidha,Taasisi inakamilisha taratibu za manunuzi ili kununua mashinehizo ambazo zinategemewa kusimikwa mwezi Juni 2017.

Hospitali ya Rufaa Benjamin Mkapa - DODOMA

79. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017, Hospitali ya Rufaa Benjamin Mkapa ilihudumiajumla ya wagonjwa 21,662 ambapo wagonjwa wa njewalikuwa 20,812 na waliolazwa 850 ikilinganishwa nawagojwa 6,450 waliohudumiwa mwaka 2015/2016. Aidha,uchunguzi wa matibabu ya Macho kwa ushirikiano na timuya wataalamu kutoka Marekani ulifanyika katika Hospitalikwa wagonjwa 3,500 na kati ya hao wagonjwa 500walifanyiwa upasuaji na waliobaki walipata matibabumengine ikiwemo utoaji wa miwani na ushauri mbalimbali.Vilevile, kulifanyika huduma za uchunguzi wa figo mweziMachi 2017 ambapo wagonjwa 754 walichunguzwa nakupewa ushauri. Pia, Hospitali imekabidhiwa gari la kubebea

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

wagonjwa na Wizara ili kukidhi mahitaji ya huduma kwawagonjwa.

80. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza na kuboreshautoaji wa huduma za afya, Hospitali imefunga mitambo yaUchunguzi wa magonjwa mbalimbali kama vile MRI, CT-Scan, Mammography, General Purpose X-ray, Fluoroscopy,Ultrasound na Dental Unit and Dental X-ray machine. Hudumazitaanza kutolewa baada ya Tume ya Taifa ya Mionzi kutoaleseni. Aidha, hospitali ipo katika hatua za mwisho zaukamilishwaji wa maabara ya kisasa Cath-lab kwa ajili yamatibabu ya moyo pamoja na Maabara yenye uwezo wakuchunguza vinasaba ambapo hadi mwezi Machi 2017baadhi ya vifaa vimenunuliwa ikiwemo DNA, Analyser,Dignator PCR na Conventional PCR. Vilevile, hospitaliimeboresha na kuimarisha miundombinu ya kutolea hudumaza afya katika Wodi za wagonjwa, jengo la huduma zakinywa na Meno, Vyumba vya upasuaji na Chumba chaWagonjwa mahututi.

Hospitali ya Mirembe

81. Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017 Hospitali ya Mirembe ilihudumia jumla yawagonjwa wa akili 2,111 kati yao wanaume 1,511 nawanawake 600 na pia ilihudumia wagonjwa wa magonjwaya kawaida 364. Aidha, hospitali ilihudumia wagonjwa waakili wa kutibiwa na kuondoka 8,363 ambao kati yaowanaume walikua 3,023 na wanawake 5,340. Wagonjwa wamagonjwa mengine 12,633 walihudumiwa katika mwaka2016/17; ikilinganishwa na wagonjwa 33,900 waliopewahuduma mwaka 2015/2016.

82. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria yaMwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 na Sheria yaAfya ya Akili ya mwaka 2008, Hospitali ilihudumia jumla yawagonjwa wa akili wahalifu 374 waliopokelewa katika Taasisiya Isanga ambapo wanaume walikuwa 297 na wanawake77. Aidha, Hospitali iliandaa ripoti za kisheria kwa wagonjwawa akili wahalifu 75 ambao walihisiwa kutenda makosa

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

wakati wakiwa na ugonjwa wa akili, kati yao wanaume 66na wanawake 9. Wagonjwa hao walichunguzwa na taarifaza kitaalamu zil itumwa katika Mahakama Kuu naMahakama za Wilaya ili kuzisaidia katika kufikia maamuzi yakisheria. Taasisi pia, ilipokea hati za ruhusa kwa wagonjwa62 wa kundi maalum (Category C) wakiwemo wanaume 53na wanawake 9. Wagonjwa hao ni wale waliopona nakumaliza muda wao wa matibabu wa miaka 3 kwa mujibuwa Sheria.

Hospitali Maalumu ya Kibong’oto

83. Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017, Hospitali i l iendelea kutoa huduma kwawagonjwa 18,441 wa nje na kati ya hao wagonjwa wa KifuaKikuu na UKIMWI ni 283, Kifua Kikuu Sugu waliolazwa 112, KifuaKikuu cha kawaida 159 na wagonjwa 17,887 wa magonjwamengine ikilinganishwa na wagojwa 22,348 kwa mwaka2015/2016. Katika kufuatilia mwenendo wa magonjwa yakuambukiza, Hospitali imeweza kupima sampuli za makohozikwa wagonjwa 1,961 na kupata wagonjwa 367 (asilimia 33.5)na kati yao wagonjwa 30 walikuwa na Kifua Kikuu Sugu.Aidha hospitali imepata mashine ya kupima usugu wavimelea vya Kifua Kikuu kwa dawa daraja la pili (Secondlineanti tuberculosis drug susceptibility testing) na kupunguzamuda wa uchunguzi wa Kifua Kikuu Sugu Zaidi (Extensive drugResistant TB) chini ya siku 90.

84. Mheshimiwa Spika, Hospitali pia iliendelea kutoa elimukwa watoa huduma kutoka Hospitali mbalimbali nchini kwalengo la kuwajengea uwezo wa kuanzisha matibabu ya KifuaKikuu Sugu nchini. Vituo 19 katika Mikoa 14 wamejengewauwezo wa kutibu wagonjwa na kuwafuatilia matibabu. Kwahivi sasa hospitali imeweza kufupisha muda wa kuanza Tibakutoka siku 14 mpaka siku 3 tangu mgonjwa kugundulikakuwa na kifua Kikuu Sugu hivyo kupunguza maambukizi kwajamii. Aidha, Hospitali ilifanya tafiti mbalimbali za kusaidiakujua changamoto zinazoikabili sekta ya afya katika mfumomzima wa ugunduzi na tiba ya Kifua Kikuu na UKIMWI kwakushirikiana na taasisi za utafiti nchini na nchi za nje. Vilevile,

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Hospitali imechapisha machapisho matatu ya kisayansi kifuakikuu na kifua kikuu sugu.

85. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa bajeti ya2016/17, Hospitali ya Kibong’oto kwa kushirikiana na ChuoKikuu cha Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela imeandaaandiko la kuanzisha mafunzo ya shahada za uzamili nauzamivu katika magonjwa ya kuambukiza ikiwa na lengo lakuongeza wataalam wabobezi wenye uwezo wa ugunduziwa vipimo kwa magonjwa haya nchini. Kwa makubalianohayo wafanyakazi wawili (Madaktari; 1 shahada ya uzamivuna 1 shahada ya uzamili) wamejiunga na Chuo cha NelsonMandela kusomea Sayansi ya Magonjwa ya Kuambukiza.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya)

86. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017 Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Mbeyaimewahudumia jumla ya wagonjwa wa nje 175,478ikilinganishwa na wagonjwa 198,219 waliopatiwa hudumamwaka 2015/2016. Aidha, Hospitali ilihudumia jumla yawagonjwa waliolazwa 24,927 ikilinganishwa na wagonjwa29,162 mwaka 2015/2016.

87. Mheshimiwa Spika, Hospitali imeendelea kuimarishahuduma za kibingwa, ambapo hadi kufikia Machi 2017, jumlaya wagonjwa 37 walifanyiwa upasuaji kwa kutumia tundudogo. Aidha, Hospitali kwa kushirikiana na Taasisi ya MifupaMuhimbili imefanya upasuaji kwa watoto wenye matatizoya mgongo wazi na vichwa vikubwa. Jumla ya Wagonjwa10 wamewekewa Arteriovenosus Fistula kwa ajili ya kuchujiadamu (dialysis).

88. Mheshimiwa Spika, Hospitali imeendelea kuboreshana kupanua wigo wa huduma zinazotolewa kwa kukarabatijengo la daraja la kwanza na kukamilisha ujenzi wa jengola watoto. Kukamilika kwa jengo jipya la Idara ya Watotokutatoa nafasi kwa Idara ya upasuaji (mifupa na ajali, njiaya mkojo na tezi dume pamoja na upasuaji wa jumla) na

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

hivyo kumaliza tatizo la wagonjwa kulala chini. Kukamilikakwa miradi hiyo miwili kutaongeza uwezo kwa hospitalikutoka vitanda 477 vya sasa mpaka vitanda 605.

89. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Hospitaliimeanzisha idara ya matibabu ya pua, koo na masikio (ENT)na hivyo kuwaondolea wananchi mzigo wa kusafiri kufuatahuduma hizo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Hadi kufikiamwezi Machi 2017 wagonjwa 883 wenye matatizo ya pua,koo na masikio wamehudumiwa. Aidha, Idara ya Mifupaimeimarishwa baada ya kupata vifaa kama sign nails setshivyo kupunguza sana muda wa wagonjwa walio vunjikakukaa wodini ambapo kwa sasa mgonjwa hukaa wodinikwa muda wa chini ya siku tatu ikilinganishwa na siku 42ilivyokuwa hapo awali. Vilevile, Huduma ya kusafisha figo(dialysis) imeimarishwa kwa kununua vitanda vipya 3 na hivyokufikisha idadi ya vitanda 6. Pia, hospitali imepata mashineza kisasa za maabara (cobas machine), histopathology namashine ya kutolea dawa ya usingizi, vyote vikiwa nathamani ya shilingi milioni 340, pamoja na kununua mashineya vipimo vya damu (Hematology) kupitia fedha zake zandani iliyogharimu kiasi cha shilingi milion 57. Aidha,mchakato wa kukamilisha ujenzi wa jengo la radiologiaunaendelea ambapo tayari shilingi bilioni 1.5 zimepokelewakutoka Hazina.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa – Bugando

90. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2016 hadiMachi 2017, Hospitali ya Bugando iliwahudumia jumla yawagonjwa 117,992 ambapo wagonjwa wa nje walikuwa89,091 na waliolazwa walikuwa 28,901 ikilinganishwa nawagonjwa 327,080 mwaka 2015/2016. Hospitali piaimeendelea kutoa huduma za kifua na moyo ambapo jumlaya wagonjwa 1,347 walihudumiwa na 26 walifanyiwaupasuaji mkubwa. Aidha, huduma za moyo kwa watotozimeanza kutolewa kuanzia mwezi Januari 2017 na hadi sasawatoto 250 wamepata huduma hizo. Hospitali imetoahuduma kwa akinamama 174 wenye fistula. Vilevile, Hospitaliimeendelea na ukarabati wa miundombinu ya kutolea

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

huduma ikiwa ni pamoja na kliniki za wagonjwa wa nje,jengo la Saratani, na kukamilisha ujenzi wa kliniki yawanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

91. Mheshimiwa Spika, Hospitali imekamilisha ufungajiwa CT-Scan simulator ambayo hutumika kupanga matibabuya mionzi ya saratani. Huduma zitaanza kutolewa baada yaTume ya Mionzi ya Taifa (TAEC) kutoa leseni. Kukamilika kwausimikaji wa mitambo hiyo na kuanza kutolewa kwamatibabu ya saratani kwa njia ya mionzi itakuwa ni ukombozina faraja kubwa kwa wagonjwa wa saratani wa Kanda yaZiwa ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri hadi Dar esSalaam ili kupata huduma hiyo katika Taasisi ya SarataniOcean Road. Hospitali ya Bugando pia imeweza kuanzishakituo cha kusafisha damu (Haemodialyis Unit) ambachokinaweza kutoa huduma kwa wagonjwa 10 kwa wakatimmoja. Kituo hiki ambacho kilianza mwezi Julai 2016 hadisasa kimeweza kuhudumia wagonjwa 30 katika mizunguko(sessions) 2,107.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC

92. Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha Julai 2016 hadikufikia Machi 2017, Hospitali ya KCMC ilihudumia jumla yawagonjwa 162,078 ikilinganishwa na wagonjwa 223,198waliohudumiwa mwaka 2015/16. Hospitali kwa kushirikikianana Taasisi za Foundation for Cancer Care in Tanzania (FCCT)na Tanzania Cancer Care Foundation (TCCF) ambao nimarafiki wa Shirika la Msamaria Mwema Tanzaniaimekamilisha ujenzi wa kituo cha tiba za saratani awamuya kwanza kati ya nne. Awamu hiyo ilijumuisha ujenzi wajengo la kliniki kwa ajili ya wagonjwa wa saratani na jengola tiba ya dawa (Chemotherapy). Utoaji wa huduma katikakituo hiki umerahisisha upatikanaji wa matibabu ya saratanikaribu na wananchi wa mikoa ya Tanga, Manyara, Singida,Arusha, na Kilimanjaro.

93. Mheshimiwa Spika, wagonjwa waliohudumiwa nakituo cha tiba za saratani ni 415, kati yao watu wazimawalikuwa ni 367 (wanawake 189 na wanaume 178) na watoto

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

ni 48. Watu wazima 160 na watoto 19 walikuwa wakiendeleana tiba ya dawa. Aidha Hospitali imekamilisha ujenzi waWodi mpya kwa ajili ya wagonjwa walioungua moto nakemikali. Wodi hizo zina uwezo wa kulaza wagonjwa 24 kwawakati mmoja. Vilevile, Kitengo cha ICU kwa ajili ya watotokimefunguliwa tangu Oktoba 2016 ambapo hadi kufikiamwezi Machi 2017, jumla ya watoto 91 wamepata huduma.Hospitali pia imeanza kutoa huduma za kusafisha figo tanguDesemba 2016 baada ya kufunga mashine nne za kusafishafigo. Kati ya Januari na Machi 2017, jumla ya wagonjwa 32wameshapata huduma hii.

Usimamizi wa utoaji wa Huduma za Tiba Nchini

94. Mheshimiwa Spika, Wizara ikiwa na dhamana yakusimamia utoaji wa huduma za afya nchini imeendeleakutoa miongozo na maelekezo yenye lengo la kuhakikishautoaji wa huduma bora kwa wananchi unazingatiwa. Wizarakwa kushirikiana na OR-TAMISEMI inaendelea kusisitiza kwavituo vyote vya umma vya kutolea huduma za afya nchinikuweka utaratibu mwepesi kwa wananchi kufikishamalalamiko yao pindi wanapoona kwamba hawakupatiwahuduma za afya kwa kiwango stahiki. Aidha, Wizaraimeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko na keroza wananchi juu ya huduma zinazotolewa. Kwa kipindi chaJulai 2016 hadi Machi 2017 malalamiko kuhusu utoaji wahuduma kwa vituo binafsi na huduma kwa vituo vya Ummayalipokelewa na kupatiwa ufumbuzi. Vilevile magari 10 yawagonjwa kutoka katika Serikali ya Qatar yalitolewa kwahospitali mbalimbali nchini ili kuimarisha huduma za rufaakwa wagonjwa.

95. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara piaimeendelea kuratibu utolewaji wa huduma ya matibabubure kwa wazee. Katika kutekeleza azma hiyo, Halmashauriziliendelea kuhimizwa kutenga fedha kwa ajili ya kulipiamatibabu ya wazee kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii nakuwanunulia dawa na vifaa tiba.

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

Huduma za Maabara za Uchunguzi wa Magonjwa

96. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizaraimeendelea kuboresha huduma za maabara ambapo hadikufikia mwezi Machi 2017, jumla ya maabara 66 ambazo zipokatika ngazi za Mikoa, Wilaya na Vituo vya Afya, zilishirikikwenye utaratibu wa Shirika la Afya Duniani wa kutoa Ithibatihatua kwa hatua, kwa kutoa nyota za viwango vya uborawa huduma za maabara. Maabara 33 zilipata kati ya nyotamoja (1) mpaka Tatu (3) za viwango vya ubora. Aidha,Maabara ya Taifa na zile za Kanda sita (6) zimepata ithibatiya SADCAS ya kiwango cha kimataifa yaani ISO 15189:2012.Maabara hizo ni Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii(NHLQATC), Hospitali ya Kanda Bugando (BMC), Hospitali yaKanda Mbeya (MRH), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) naKilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Pia, Wizarainaendelea na ujenzi wa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamiikatika eneo la Mabibo, Dar es salaam. Mradi huo hadikukamilika unatarajiwa kutumia kiasi cha Shilingi7,493,193,434.97.00.

Huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala

97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizaraimeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vyahabari kuhusu Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 yaMwaka 2002, kanuni zake na miongozo mbalimbali. Katikakutekeleza majukumu ya Kisheria, Wizara imeandaa nakuchapisha nakala 4,950 za mpango mkakati wa tiba asilina tiba mbadala 2016/17-2021/22. Vitabu hivyo vitatoamsaada kwa waganga wakuu wa mikoa na Halmashaurikuweza kupanga mipango itakayo husu tiba asili na tibambadala katika maeneo yao. Aidha, Wizara inaendeleakuwakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatiaSheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002,kanuni zake katika utoaji wa matangazo ya Tiba Asili na TibaMbadala. Vilevile, Wizara iliratibu mafunzo kwa waganga25 wa tiba asili yaliyofanyika mwezi Februari 2017 katika chuokikuu cha MUHAS na wanachuo 44 katika Chuo Kikuu chaKumbukumbu ya Sebastian Kolowa.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

HUDUMA ZA UUGUZI NA UKUNGA

98. Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha kuwa hudumaza Uuguzi na Ukunga zinaimarika, Wizara imezindua MpangoMkakati kwa ajili huduma za Uuguzi na Ukunga. Lengo laMpango huo ni kutoa dira inayolenga katika kuboreshahuduma za Uuguzi na Ukunga nchini. Aidha, Wizara imezinduamwongozo wa maabara ya mafunzo ya Uuguzi na Ukunganchini, mwongozo huo unalenga katika kuboresha mafunzoya vitendo yatolewayo katika vyuo vya uuguzi na ukunga, ilikuongeza weledi, maarifa, na stadi za kuhudumia wananchikwa ubora zaidi. Katika kuimarisha umahiri kwa wauguzi nawakunga, Wizara imetayarisha na kuzindua mwongozo wamafunzo sehemu za kazi kwa ajili ya kuwaongoza wakufunziwa vitendo katika kusimamia mafunzo yatolewayo kwawanafunzi sehemu za kazi. Vilevile, Wizara imeendeleakusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya Uuguzi naUkunga kwa kutumia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja nakufanya usimamizi shirikishi, mikutano ya wauguzi na ile yawasimamizi wao

UHAKIKI UBORA WA HUDUMA ZA AFYA

Uhakiki na Ukaguzi

99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizaraimekamilisha zoezi la kufanya tathmini ya awali ya Vituo vyaKutolea Huduma za Afya ya msingi (Zahanati, Vituo vya Afyana Hospitali) katika Halmashauri zote za mikoa 6 iliyosalia yaIringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro na Arusha. Vituovilipewa hadhi ya nyota kulingana na ubora wa hudumazinazotolewa. Jumla ya vituo 1,665 vimefanyiwa tathmini,ambapo kati ya vituo hivyo, 446 (27%) vilipata nyota sifuri,862 (52%) vilipata nyota moja, 272 (16.3%) vilipata nyota mbili,63 (4%) vilipata nyota tatu na 2 (0.12%) vilipata nyota nne.Mipango ya Uimarishaji Ubora wa huduma za afya kwa kilaKituo iliandaliwa na utekelezaji unaendelea kwa kushirikianana Timu za Uendeshaji Afya za Halmashauri. Aidha, katikautekelezaji na ufuatiliaji wa mipango ya uboreshaji wahuduma za afya, Wizara ilitoa kiasi cha 3,040,000,000 katika

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

mikoa 4 ambapo jumla ya vituo 304 (Dodoma 118, Kigoma135, Singida 32 na Tanga 19) vilivyokuwa na nyota sifurivilipatiwa Shilingi 10,000,000 kwa kila Kituo.

100. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya tathmini yamarudio kwa vituo 52 katika mkoa wa Shinyanga.Ukilinganisha matokeo ya awali na matokeo ya tathmini yamarudio, vituo vimeonyesha mabadiliko makubwa katikautekelezaji wa mipango ya uboreshaji wa huduma ambapokati ya vituo 40 vilivyokuwa na nyota sifuri, ni vituo 3 tu (7.5%)ndivyo vimebaki katika hadhi ya nyota sifuri.

Aidha, Wizara imefanya usimamizi shirikishi kwenye eneo laKukinga na Kudhibiti Maambukizi (infectious, prevention andcontrol) katika vituo vya kutolea huduma vya mikoa 22(Kiambatanisho Na. 4) ya Tanzania bara. Vilevile, Jitihada zaKukinga na Kudhibiti Maambukizi zimeimarishwa katika utoajihuduma za dharura na Maafa ili kuzuia kuenea kwamaambukizi wakati wa utoaji wa huduma hizo.

Dharura na Maafa

101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizaraimetekeleza mikakati ya kujenga utayari wa kisekta wakukabiliana na dharura kwa kuwapatia mafunzo yakukabiliana na dharura na maafa timu za dharura katikamikoa 23 ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma,Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi, Mtwara,Mbeya, Iringa, Rukwa, Tabora, Kigoma, Kagera, Mwanza,Mara, Geita, Simiyu Shinyanga na Katavi ambapo jumla yawatoa huduma 120 walipata mafunzo hayo. Aidha, Wizaraimeandaa na kuchapisha miongozo ya kutoa huduma zadharura pamoja na kufanya tathmini ya viashiria vya dharura“Vulnerability Risk Assessment and Mapping” kuhusu mlipukowa ugonjwa wa kipindupindu nchini ili kusaidia kuimarishamikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo.

102. Mheshimiwa Spika, Aidha, Wizara imeanzamaandalizi ya kuanzisha huduma za dharura katika barabarakuu kutoka Dar es Salaam hadi mpaka wa Tanzania na

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Malawi, kwa kupitia mradi wa South Africa Trade andTransport Facilitation (SATTF). Awamu ya kwanza ya mradi huoutaanzia Dar Es Salaam hadi mpakani mwa Morogoro naIringa katika eneo la Ruaha Mbuyuni. Aidha, Wizarainashirikiana na wadau wa usalama barabarani kutekelezamikakati ya kupunguza ajali za barabarani kwa kupitia Mradiwa “Bloomberg Initiative for Road Safety (2015-2019)”. KatikaMradi huo, Wizara inaratibu Wadau wa Usalama Barabarani,kuhamasisha uboreshaji wa sheria, utoaji wa taarifa zakuhamasisha masuala ya usalama barabarani na mafunzoya kujenga uwezo kwa wanasheria na waandishi wa habari.

103. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imeshiriki katikakukabiliana na dharura mbalimbali pamoja na kuratibuushiriki wa wadau katika kukabiliana na dharura. Kwa kupitiakituo cha uratibu wa Operesheni za Dharura na Maafa,Wizara imeratibu utoaji wa huduma za afya katika dharuraikiwemo matukio ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera,mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu na sumu kuvu.Shughuli hizo zimefanyika kwa njia ya kutuma wataalamu,kupeleka dawa, vifaa na vifaa tiba na kuratibu mikutano yawadau mbalimbali katika ngazi ya Taifa na Mikoa.

URATIBU, UFUATILIAJI NA UGHARAMIAJI HUDUMA ZAAFYA

Tathmini, Ufuatiliaji na Usimamizi wa huduma za Afya

104. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha ushirikishwaji wawananchi na uwajibikaji katika kutekeleza vipaumbele vyaSekta ya Afya, Wizara imeendelea kufanya tathmini shirikishikwa kutumia nyenzo ya kijamii (Community Score Card) ilikuongeza uwazi na uwajibikaji kwa lengo la kuboreshakiwango cha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.Tathmini hiyo imefanyika katika ngazi ya jamii inayohudumiwana vituo vya afya 227 vya umma katika Halmashauri 14 (Mkoawa Pwani halmashauri 8 na Kilimanjaro halmashauri 6).Matokeo ya tathmini hizo yametumika kuandaa mipangokabambe ya Halmashauri ya uboreshaji wa huduma za afyakatika vituo vya kutolea huduma.

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

105. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha dhana yaushirikishwaji wa wananchi katika mipango na utawala borakatika sekta ya afya, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMIimefanya usimamizi shirikishi katika mikoa yote na kubainiuwepo wa Bodi za Usimamizi wa Huduma za Afya zaHalmashauri katika Halmashauri 45 za mikoa ya Singida,Dodoma, Mbeya, Songwe, Tanga na Tabora ambazohazifanyi kazi vizuri. Katika kuhakikisha Bodi hizo zinatekelezamajukumu yake ipasavyo, Wizara kupitia zoezi la usimamizishirikishi ilitoa mafunzo elekezi, miongozo ya namna bora yakutatua changamoto za usimamizi wa shughuli za afya zaHalmashauri.

106. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imeendelea kuboreshaupatikanaji wa takwimu za afya kutoka katika vituo vyakutolea huduma za afya nchini. Uboreshaji huo unatokanana kuimarishwa kwa mfumo wa kielektroniki wa kutoa taarifaza vituo vya afya nchini yaani “Health Facility Registry” nauboreshaji wa mtandao wa kutoa taarifa za afya kupitiaanuani ya hmisportal.moh.go.tz

107. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kuimarishamfumo wake wa Takwimu za kila siku katika kila kituokinachotoa huduma za Afya unaoitwa “Mfumo wa Taarifaza Uendeshaji wa Huduma za Afya (MTUHA) na pia kusimamiamfumo wake wa kielektroniki unaoitwa “District HealthInformation System (DHIS2)”. Mfumo huu umezisaidiaHalmashauri, Mikoa pamoja na ngazi ya Taifa katikakuchambua na kutumia taarifa hizo katika kuandaa mipangoya utoaji wa huduma za afya. Aidha, Wizara imeingizaMafunzo ya MTUHA kwenye mitaala ya kufundishia katika Vyuovya Mafunzo ya Afya Nchini.

TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

108. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuelekezamatumizi ya mifumo ya kielektroniki kwa taasisi zilizo chiniyake ili kuondoa matumizi ya karatasi na kuimarisha taarifaza wagonjwa na mtoa huduma. Kupitia Mfuko wa Taifa waBima ya Afya (NHIF), Wizara imekamilisha kufunga mfumo wa

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

kielektroniki wa hospitali (paperless) ikiwa ni pamoja nakusimamia mapato katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili,Hospitali za Mikoa za Singida na Tabora, usimikaji unaendeleakatika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Kandaya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mirembe naHospitali ya Kibong’oto.

109. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikia na OR-TAMISEMI na wadau mbalimbali imetengeneza MpangoMkakati wa uwekezaji katika mifumo ya TEHAMA (InvestmentRecommendation Plan), mpango huu umewezesha Serikalina Wadau kubaini maeneo ya uwekezaji. Pamoja nakuharakisha uunganishaji wa mifumo katika sekta ya Afya.

110. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2016/17, Wizaraimeendelea na utekelezaji wa Mkakati wa TEHAMA katikaSekta ya Afya (ehealth Strategy 2013-2018). Katika kipindi chaJulai 2016 hadi Machi 2017, Wizara imefanya tathmini yamifumo ya kieletroniki iliyofungwa kwenye hospitali zote zarufaa katika ngazi ya Mkoa na hospitali za Wilaya ili kujuakama inakidhi miongozo na viwango vilivyotolewa naWizara pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao. Tathminiilionyesha kuwa mifumo iliyopo inakidhi vigezo kwa kati yaasilimia 18 hadi 92. Kufuatia matokeo ya tathimini hiyo, Wizarailielekeza kuwa, Mifumo ambayo haikufikia vigezo kwaasilimia 60 isitumike na ile iliyofikia zaidi ya asilimia 60 iboreshwekufikia asilimia 100. Aidha, Wizara inakamilisha mfumo wakupokea maoni ya wananchi juu ya ubora wa hudumazinazotolewa katika vituo vya Afya nchini, ambapomgonjwa ataweza kutoa taarifa kupitia code namba*152*05#.

RASILIMALI WATU KATIKA SEKTA YA AFYA

111. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia nakuratibu uzalishaji wa wataalamu kutoka vyuoni ambaowameendelea kuwa nguzo muhimu ya utoaji huduma zaafya nchini. Uzalishaji huu umeendelea kuimarika kutokanana ongezeko la wanafunzi watarajali wanaodahiliwa katikavyuo vya afya kutoka wanafunzi 13,002 mwaka 2015/16 hadi

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

wanafunzi 13,632 mwaka 2016/17. Serikali imevuka lengo laMpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) lakudahili wanafunzi 10,000 waliotarajiwa kudahiliwa ifikapomwaka 2017. Vilevile, kwa mwaka wa fedha 2016/17, Wizarainasimamia utoaji wa mafunzo kwa vitendo (internship) kwawahitimu 1,798 wa vyuo vikuu katika fani mbalimbali za afyaikiwemo madaktari (1,072), wafamasia (186), wauguzi (265),maafisa mazingira (46), Radiologia na Radiografia (9), namaabara (220). Wanafunzi hao wanatarajia kukamilishamafunzo hayo mwezi Oktoba, 2017.

112. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na jitihada zakupunguza uhaba wa wataalam wanaotoa huduma zakibingwa nchini kwa kutekeleza mpango wake wakugharamia masomo ya uzamili kwa wataalamu 404 waafya katika nyanja mbalimbali. Hadi Machi 2017, wanafunzi387 walikuwa wanaendelea na masomo katika vyuombalimbali ndani ya nchi na wanafunzi 17 katika vyuo vyanje ya nchi.

113. Mheshimiwa Spika, Aidha, Wizara inaendeleakuimarisha vyuo vyake vya Mafunzo kwa kuvifanyia ukarabatimkubwa pamoja na ujenzi wa majengo mapya. Katikamwaka 2016/17, vyuo 14 vimeboreshewa miundombinu yakekupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund) na kati yahivyo vyuo 12 vimekamilika na kukabidhiwa kwa watumiaji.Vyuo hivyo ni Lindi CATC, Songea CATC, Njombe NTC, PHIIringa, Rukwa CATC, Mpanda CATC, Kigoma CATC, MusomaNTC, Nzega NTC, PHN Morogoro, Tanga NTC na MtwaraCOTC. Vyuo viwili ambavyo havijakamilika ni Mirembe NTCna Mvumi TI ambavyo vinategemea kukamilika mwaka wafedha 2017/18. Wizara pia imenunua vifaa vya Maabara zavitendo kwa ajili ya kufundishia kwa vyuo 10 vya utabibu,uuguzi na ukunga.

114. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na kituocha kudhibiti magonjwa cha Marekani “Centre for DiseaseControl (CDC)” inatekeleza mpango wa uimarishaji mifumoya huduma za Afya. Katika mwaka 2016/17, Wizara imejengaKituo kipya cha Elimu kwa njia ya Masafa eneo la Mkundi

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Manispaa ya Morogoro kitakachoweza kutoa elimu kwaKada za Afya. Kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuchukuawanafunzi hadi 300 kwa wakati mmoja. Vilevile, Mpangohuo wa uimarishaji mifumo ya huduma za Afya umewezeshakutoa ajira za mkataba kwa wauguzi (97) na Tabibu wasaidizi(95) ambao wamesambazwa kwenda kutoa hudumakwenye vituo vya Afya na Zahanati katika Halmashauri 40hapa nchini.(Kiambatisho Na 5)

115. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na jitihada zakuajiri watumishi wa afya ambapo katika mwaka 2016/17,kibali cha kuajiri madaktari 258 kimepatikana. Hatua hiiitasaidia kupunguza pengo la watumishi hasa katika ngaziya vituo, Hospitali za wilaya na mikoa. Hata hivyo, Sekta yaafya bado inakabiliwa na upungufu wa watumishi wa afya,kwa takribani asilimia 49. Serikali inaendelea na jitihadambalimbali za kuhakikisha upungufu huu unaisha il ikuhakikisha huduma bora za afya kwa wananchi wotezinapatikana hasa kwenye zahanati, vituo vya afya, Hospitaliza Wilaya na Hospitali za Rufaa za Mikoa.

116. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarakwa kushirikiana na wadau wakiwemo Taasisi ya BenjaminiMkapa imeendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba200 za watumishi katika Mikoa 9 ya Kigoma, Mwanza,Shinyanga, Geita, Kagera, Tanga, Manyara, Pwani na Simiyu.Chini ya udhamini wa Mfuko wa Dunia (Global Fund), Ujenziwa nyumba 132 umekamilika na nyumba 68 ujenziunaendelea. Kukamilika kwa nyumba hizo kutaongeza idadiya nyumba za watumishi zilizojengwa kupitia mradi huu nakufika nyumba 480 katika maeneo yenye mazingira magumu.

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYAYA MSINGI

117. Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha utekelezaji waMpango wa miaka kumi wa Maendeleo wa Afya ya Msingiunaokamilika mwaka 2017. Katika utekelezaji wa mpangohuo, Vituo vya kutolea huduma vimeendelea kuongezekakutoka jumla ya vituo 5,172 mwaka 2005 na kufikia jumla ya

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

vituo 7,232 mwaka 2016. Hii ni ongezeko la vituo 2,060 sawana asilimia 40. Kati ya vituo vyote vilivyopo nchini, vituo 5,414sawa na asilimia 75 ni vya Serikali na 1,818 ni vya taasisi binafsi.Aidha kupitia MMAM, Serikali iliingia Mkataba na watoahuduma binafsi (Service Level Agreement) ili kupunguzaulazima wa Halmashauri kujenga vituo vipya vya hudumaza afya sehemu ambazo kuna vituo binafsi. Katikamakubaliano hayo jumla ya Halmashauri 39 zinatumiahospitali teule.

118. Mheshimiwa Spika, kutokana na kipindi chautekelezaji wa MMAM kufikia ukingoni, Wizara imeanzamaandalizi ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa mpangohuo ili kupima mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakatiwa utekelezaji wake na kutoa mapendekezo ya namna boraya kuandaa na kutekeleza mpango mwingine.

UGHARAMIAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

119. Mheshimiwa Spika, Utoaji wa huduma za afya nchiniunasimamiwa na Sera ya Afya ya mwaka 2007. Sera hii ni yamuda mrefu hivyo katika mwaka 2016/17 Wizara ilifanyamapitio ya Sera na kubaini kuwa kuna maeneo mengi yaSera ambayo yametekelezeka kwa ufanisi mkubwa namaeneo machache ambayo hayakutekelezeka kikamilifu.Kufuatia matokeo haya, Wizara imeanza maandalizi yakutunga Sera mpya ya Afya itakayokidhi mabadiliko katikaSekta ya Afya. Maandalizi ya Sera hiyo yanatarajiwa kukamilikakatika mwaka 2017/18. Maandalizi ya Sera hii yamekuwashirikishi na nichukue fursa hii kuwaomba WaheshimiwaWabunge na wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano wadhati kwa Wizara kwa kutoa maoni na ushauri katikaukamilishwaji wa Sera hiyo.

120. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilikamilisha maandaliziya Mkakati wa Ugharamiaji huduma za afya nchini. Lengokuu la Mkakati huu ni kutafuta vyanzo mbalimbali vya uhakikavya kuongeza rasilimali fedha katika Sekta ya afya. Mkakatihuo una maeneo mengi ya Kisera ambayo bado yanafanyiwakazi na wadau kabla ya kuanza kutekelezwa. Utekelezaji wa

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

mkakati huu utasaidia kuimarisha upatikanaji wa RasilimaliFedha katika Sekta ya Afya na kuwahakikishia wananchiupatikanaji wa huduma bora za Afya pindi wanapozihitajihasa wananchi wasio na uwezo na wenye mahitaji maalum.

121. Mheshimiwa Spika, kupitia Mfuko wa Bima ya Taifaya Afya na kwa kushirikiana na Benki ya Ujerumani (KfW)inatekeleza Mpango wa NHIF/CHF kwa WanawakeWajawazito na Watoto ujulikanao kama Tumaini la Mama.Mpango huo wenye lengo la kupunguza vifo vya akinamamana watoto ulianza kutekelezwa mwaka 2012 ambapo akinamama wajawazito hulipiwa kadi za NHIF/CHF ili kuwa nauhakika wa matibabu katika kipindi chote cha ujauzito namiezi sita baada ya kujifungua kwa mama na mtoto. Katikakipindi cha Julai 2016 hadi kufikia mwezi Machi 2017,wanawake wajawazito 147,615 walijisajiliwa na hivyo kufanyajumla ya wanufaika kufikia wanawake 572,576 katika mikoaya Mbeya, Tanga, Lindi, Mtwara na Songwe.

122. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana naOR-TAMISEMI pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afyaimepanga kutekeleza mpango wa Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa ili kuhakikisha watanzania wanapatahuduma bora na kwa urahisi kwa kuzingatia uwezo wakifedha wa mwanachama. Kupitia mpango huo,mwanachama ataweza kupata huduma kutoka ngazi yazahanati hadi ngazi ya mkoa bila kujali Kituo/Halmashaurialipojisajili tofauti na ilivyo sasa ambapo mwanachama waCHF hupata huduma kutoka ngazi ya zahanati hadi ngaziya Halmashauri aliyojisajili tu.

123. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza ufanisi, kupitiaMpango huu wa CHF iliyoboreshwa, Halmashauri zitabakina jukumu la kutoa huduma (service provider) na Mfuko/NHIF utakuwa na jukumu la kuandikisha wanufaika,kukusanya fedha za wanachama na kulipa watoa huduma(purchaser). Aidha, katika kuimarisha ushirikishwaji wawananchi, vikao vya kijiji vitapewa fursa ya kuteua maafisawatakaokuwa na jukumu la kusajili wananchama nakuwahamasisha pamoja na kukusanya michango. Mpango

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

huo utatekelezwa kwa kuanzia katika halmashauri 50 zamikoa ya Kagera, Mwanza, Singida, Mara, Tabora, Pwani,Ruvuma na baadae utasambazwa katika mikoa yote nchini.Uzinduzi rasmi wa mpango huu unatarajiwa kufanyika katikamkoa wa Singida kabla ya mwisho wa fedha 2016/17. Nitoerai kwa Waheshimiwa Wabunge, kwa nafasi zao na ushawishimkubwa walionao katika jamii tunayoishi, kuendeleakuwaelimisha wananchi wote umuhimu wa kujiunga nabima ya afya ili waweze kupata huduma za tiba bila kikwazocha fedha.

Uratibu wa Mfuko wa Pamoja wa Afya (Health BasketFund)

124. Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa na jukumu lakuratibu Mfuko wa Pamoja wa Afya (Health Basket Fund)ulioanzishwa mwaka 1996. Kupitia Sekretarieti ya Uratibu waMfuko, Vikao mbalimbali vya majadiliano kati ya Serikali naWadau vimekuwa vikifanywa ikiwa ni pamoja na kutoataarifa ya Serikali jinsi inavyotekeleza kazi zinazogharamiwana fedha za Wadau. Kwa hivi sasa Mfuko huo unachangiwana Wadau (8) ambao ni Denmark, Uswisi (SDC), Ireland,Canada, Benki ya Dunia, UNICEF, UNFPA na Korea Kusini.Wizara inaendelea na juhudi za kuwaleta pamoja wadauwengine zaidi ili wachangie katika Mfuko huo ili kuleta ufanisina matokea makubwa katika utekelezaji wa miradi ya afyanchini.

125. Mheshimiwa Spika, wanufaika wa Mfuko huu ni OR -TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazeena Watoto (Idara kuu ya Afya), Mikoa na Halmashauri zotenchini. Fedha hizo hugawiwa kwa fomula kwa kuzingatiamakubaliano kati ya Serikali na Wadau wanaochangiaMfuko. Asilimia 90 ya fedha zote hupelekwa katika Mamlakaya Serikali za Mitaa, asilimia 6 ya fedha hizo hutumika katikaWizara ya Afya kwa ajili ya masuala ya uratibu, usimamizi naufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Kiserakatika Sekta ya Afya. Aidha, asilimia 3 ya fedha hizohupelekekwa katika Mikoa kwa ajili ya kugharamia ufuatiliajikatika ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa na asilimia 1 ya

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

fedha zote hupelekwa Makao Makuu ya OR– TAMISEMI kwaajili ya kugharamia ufuatiliaji katika Mikoa na Mamlaka zaSerikali za Mitaa.

126. Mheshimiwa Spika, Hadi robo ya tatu ya mwaka wafedha 2016/17, kiasi cha shilingi bilioni 88.8 kimepokelewakupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya. Kati ya fedha hizo, shilingibilioni 5.6 zilipokelewa na Wizara ya Afya (Fungu 52), shilingimilioni 865.05 zilipokelewa na OR-TAMISEMI, shilingi bilioni 2.6zilipokelewa na Mikoa na kiasi cha shilingi bilioni 79.7zilipokelewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Fedha hizihutumika kadiri ya Mkataba wa Makubaliano kati ya Serikalina Wadau wa Maendeleo, ambapo asilimia 33 ya fedhazinazopelekwa katika Halmashauri zinatakiwa kutumikakama nyongeza ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa naasilimia 67 ni kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbaliambazo zinalenga kuboresha huduma za afya nchini ikiwani pamoja na kugharamia usambazaji na ufuatiliaji wachanjo kwa kuimarisha mnyororo baridi (cold chain),uimarishaji wa huduma za dharura za mama na mtoto(CEmOC), udhibiti wa magonjwa yanayoambukiza nayasiyoambukiza pamoja na yale yasiyopewa kipaumbele nakuwajengea uwezo watoa huduma za afya.

127. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuzingatia vigezo vyausawa katika kugawanya fedha za Mfuko, muelekeo waWadau kwa sasa ni kutoa umuhimu kwa ufanisi katikautekelezaji wa kazi zilizokubaliwa ili kuongeza ufanisi katikakazi zinazokubaliwa. Na ili kuviwezesha vituo vya kutoleahuduma za afya kupata fedha kwa wakati na kuwezakufanya maamuzi ya haraka ya kutumia fedha hizo kulinganana mahitaji ya kituo husika, Wizara imeandaa utaratibu wakuwezesha fedha za Mfuko kutumwa moja kwa moja kwavituo vya kutolea huduma za afya ili kuviwezesha vituokununua dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kulinganana mahitaji yao kwa haraka. Halmashauri zitabaki na jukumula kusimamia na kufuatil ia matumizi ya fedha hizo.Mheshimiwa Spika, ninapenda kutumia fursa hii kuwaombawaheshimiwa wabunge pia kufuatilia matumizi ya fedha hizi.

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO (FUNGU 53)

MAENDELEO YA JAMII

128. Mheshimiwa Spika, Sera ya Maendeleo ya Jamii ya1996 inasisitiza ushiriki wa wananchi katika shughuli zamaendeleo kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka kuletamabadiliko chanya katika jamii. Katika kutekeleza maelekezohayo, Wizara katika kipindi cha 2016/17 iliendelea kuwezeshana kuratibu utekelezaji wa majukumu ya Maendeleo ya Jamiihususan katika kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katikashughuli za maendeleo kupitia miongozo mbalimbali. Kazizilizofanyika ni pamoja na kuandaa Mwongozo wa Ufuatiliajina Tathmini wa shughuli za Maendeleo na Ustawi wa Jamiikwa ajili ya kuhakikisha shughuli za maendeleo na ustawiwa jamii zinatekelezwa kwa ufanisi na kuwanufaishawananchi ipasavyo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlakaza Serikali za Mitaa na hivyo kuharakisha kufikiwa kwamalengo mbalimbali ya maendeleo. Kazi hii ilifanyika kwakushirikiana na OR- TAMISEMI.

129. Mheshimiwa Spika, Wataalam wa Maendeleo yaJamii ni muhimu wakatumika ipasavyo katika kufanikishaMalengo ya Sera mbalimbali za Maendeleo ya nchi yetu.Wataalamu hawa ni muhimu katika kuwandaa wananchikushiriki katika kupanga na kutekeleza programu za Kilimo,Elimu, Maji, Barabara, Afya, Mifugo na Hifadhi ya Mazingira.Wizara ina jukumu la kuandaa wataalam wa kada yaMaendeleo ya Jamii katika ngazi mbalimbali za elimu kupitiaVyuo 8 vya Mafunzo ya Taaluma ya Maendeleo ya Jamii nataasisi moja ambayo ni Taasisi ya Maendeleo Tengeru. Katikamwaka 2016/17, Wizara kupitia Vyuo hivi imeendeleakuzalisha wataalamu hao ambapo jumla ya wataalam 1,685walihitimu na wanachuo 2,216 walidahiliwa katika ngazi zaAstashahada, Stashahada, Shahada na Stashahada yaUzamili. Aidha, katika kuboresha utoaji wa mafunzo katikachuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, Wizaraimewezesha kukirejeshea chuo eneo lenye ukubwa wa hekari

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

175 lililokuwa na mgogoro na wanakijiji wa Rungemba,ambapo jumla ya Shilingi milioni 193,384,000.00 zimelipwakwa wananchi 39. Hatua hii inatoa fursa ya kuhifadhi eneola chuo kwa ajili ya upanuzi.

MAENDELEO YA JINSIA

130. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizaraimeendelea kutekeleza afua mbalimbali kwa lengo la kufikiausawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake nchini.Utekelezaji huo ulizingatia maeneo manne ya kipaumbeleambayo ni Uwezeshaji wanawake kiuchumi; Kuzuia nakutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo Ukatili Dhidi yaWanawake na Watoto; Kuwawezesha wanawake kushirikikatika uongozi na ngazi za maamuzi; na uingizaji wa masualaya jinsia katika sera, mikakati na mipango ya kisekta nakitaifa.

Uwezeshaji Wanawake kiuchumi

131. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana nawadau mbalimbali imeendelea na jitihada za kuwawezeshawanawake kiuchumi kwa kuwapatia mikopo kupitia Benkiya Wanawake Tanzania na Mfuko wa Maendeleo yaWanawake ili waweze kushiriki na kunufaika na ukuaji wapato la kaya na taifa sawa na wanaume.

132. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Mfuko waMaendeleo wa Wanawake, Wizara imeendelea kuratibuMfuko huu kwa lengo la kuwawezesha wanawakewajasiriamali wadogo. Katika mwaka 2016/17, jumla yashilingi milioni 156 zilikopeshwa kwa Halmashauri tano zaKisarawe, Busokelo, Gairo, Iringa Manispaa, Masasi na Mtwaravijijini kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi 61 vyenyewanawake wajasiriamali 658.

133. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Mfuko waMaendeleo ya Wanawake unawafikia wanawake wengi,Wizara kwa kushirikiana na OR TAMISEMI imeendeleakuzihamasisha Halmashauri kuchangia asilimia tano (5%) ya

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

mapato yao ya ndani katika Mfuko huo. Katika kipindi chaJulai hadi Disemba 2016, jumla ya Halmashauri 147 zilichangiajumla ya Shilingi 7,826,722,946. Pamoja na kuongezeka kwamwamko wa Halmashauri kuchangia katika Mfuko waMaendeleo ya Wanawake, Halmashauri 39 hazikuchangia.Kiambatisho Na. 6 Napenda kutumia fursa hii kuzipongezaHalmashauri zote ambazo zimechangia katika Mfuko huu.Aidha, natoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijachangiazichangie Mfuko huu ili kuharakisha kufikiwa kwa malengoya maendeleo jumuishi ambayo nchi imejiwekea. Vilevile,natoa rai kwenu wabunge wenzangu kuhakikishaHalmashauri zetu zinachangia ipasavyo Mfuko huu.

134. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Benki yaWanawake Tanzania, mikopo kwa wajasiriamali 6,956 yenyethamani ya shilingi bilioni 10,469,282,000 (wanawake 4,596na wanaume 2,360) imetolewa. Hivyo, mikopo iliyotolewana Benki imeongezeka kutoka shilingi 112,473,600,000 mwaka2015/16 hadi kufikia shilingi 121,796,840,000 mwaka 2016/17.Aidha, idadi ya wajasiriamali walionufaika na mikopoinayotolewa na benki imeongezeka kutoka wajasiriamali79,983 mwaka 2015/16 hadi kufikia wajasiriamali 86,939mwaka 2016/17 ambapo asilimia 75 ya wanufaika niwanawake.

135. Mheshimiwa Spika, Aidha, Benki imeongeza vituo vyakutolea mikopo na mafunzo kutoka vituo 184 mwaka 2015/16 hadi kufikia vituo 252 mwaka 2016/17. Aidha, Benkiiliwezesha jumla ya wanawake 223 kati ya wanufaika 560kumiliki ardhi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Benkipia katika kumwezesha mwanamke wa kipato cha chinikupata huduma za mikopo yenye riba nafuu, Benki imeanzishaAkaunti ya Malaika ambayo ilizinduliwa na Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia SuluhuHassan. Lengo la akaunti hiyo ni kutoa mikopo yenye ribanafuu isiyozidi asilimia 10.

136. Mheshimiwa Spika, vile vile, Wizara kwa kushirikianana Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamojana Ofisi ya Rais TAMISEMI iliratibu uanzishwaji na uzinduzi wa

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoaya Kigoma, Singida na Dar es Salaam. Uanzishwaji wamajukwaa haya unalenga kuendeleza jitahada za Makamuwa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alizinduaJukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania kwangazi ya taifa.

137. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imeratibumaadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyikamwezi Machi, 2017 ambapo hapa nchini yalifanyika katikangazi ya mkoa kwa mikoa yote. Kaulimbiu ya maadhimishohayo ilikuwa ‘Tanzania ya Viwanda: Wanawake ni Msingiwa Mabadiliko ya Kiuchumi’. Maadhimisho hayo yametoafursa kwa wadau kutafakari, kubadilishana uzoefu kuhusumafanikio yaliyofikiwa na kuzitafutia ufumbuzi changamotombalimbali zinazowakabili wanawake katika kufikiaukombozi wa kiuchumi.Jitihada za Kuzuia na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia

138. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na ukatili wakijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Wizara kwakushirikiana na wadau imendaa Mpango wa Taifa waKutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18– 2021/22) ambao uliozinduliwa mwezi Disemba, 2016.Uzinduzi huo ulishirikisha Mawaziri 10 kutoka katika wizarambalimbali ambao waliahidi kuutekeleza Mpango huo kwamanufaa ya wanawake na Watoto wa Tanzania. KatikaAidha, yamefanyika maandalizi ya awali ya utekelezaji wampango huu ambayo yalihusisha: kutoa mafunzo kwaMaafisa Maendeleo ya Jamii wa mikoa 25, Maafisa waMadawati ya Jinsia 25 kutoka katika Wizara, Idarazinazojitegemea na Wakala za Serikali. Aidha, mwongozowa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto katika ngazimbalimbali umeandaliwa.

Ushiriki wa Wanawake katika Ngazi za Uongozi naMaamuzi

139. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhamasishawanawake kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

maamuzi. Katika kutekeleza hilo, wizara kwa kushirikana nashirika la TGNP imeandaa Kanzidata inayoonesha wasifu wawanawake kwa ajili ya kuwawezesha kushiriki katika fursaza uongozi, ngazi za maamuzi na ajira. Kanzidata hii piaitasaidia kuwatambua wanawake wajasiriamali. Katikakanzidata hii tumebainisha uwepo wa wanawake wasomi,wataalam wenye uwezo katika fani mbalimbali ikiwemoengineers, wahasibu, Madaktari, Wachumi na Wataalam waMaendeleo wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii. Wizaraitaendelea kuhimiza waajiri na mamlaka za uteuzi kutumiakanzidata hii.

Kuimarisha haki ya Mwanamke Kunyonyesha Wakatiya Kazi

140. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni moja kati ya nchizilizoridhia matamko na mikataba mbalimbali ya kimataifainayohusu haki ya unyonyeshaji wa Watoto. Miongoni mwamikataba na matamko ya kimataifa ambayo imeridhiwa naTanzania ni pamoja na ‘Innocent Declaration on theProtection, Promotion and Support of Breastfeeding naMaternity Protection Convention, 2000 (No. 183)’. Katikamwaka 2016/17, Serikali imefanya mapitio ya Sheria ya Kazina Mahusiano Kazini hususan kifungu cha 33(10) na kuifanyiamarekebisho kupitia Kanuni zake mpya zilizotangazwakwenye Gazeti la Serikali la Na. 47 la tarehe 24/2/2017 ambapokwa sasa imewekwa wazi haki ya mama kunyonyesha mudawa masaa mawili katika muda wa kazi kwa kipindi cha miezi6 baada likizo ya uzazi. Kabla ya marekebisho haya, haki yamama kunyonyesha baada ya likizo ya uzazi haikuwaimefafanuliwa ni kwa kipindi cha muda gani. Kifungu hikisasa kinasomeka ‘Where an employee is breast-feeding achild, the employer shall allow the employee to feed the childduring working hours up to a maximum of two hours per day,for a period of 6 months after maternity leave’, badala yakusomeka ‘Where an employee is breast-feeding a child, theemployer shall allow the employee to feed the child duringworking hours up to a maximum of two hours per day.’Marekebisho hayo yatasaidia kuimarisha upatikanaji wa hakiza wanawake katika uzazi na kuhakikisha haki na

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

maendeleo ya mtoto mchanga. Nitumie fursa hii kuwatakawaajiri wa sekta binafsi na wa umma kuzingatia matakwahaya ya kisheria. Aidha, pia ninapenda kuwahamasishawanawake kuitumia fursa hii kwa ajili ya kuweka msingi imarawa maendeleo ya awali ya watoto wao.

Uingizaji wa Masuala ya Jinsia Katika Sera Sheriana Mipango ya Kisekta na Taifa

141. Mheshimiwa Spika, kuhusu uingizaji wa masuala yajinsia katika Sera na Mipango, Wizara kwa kushirikiana nawadau imeandaa Taarifa ya Hali ya Jinsia Nchini ya mwaka2016. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa yaTakwimu pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN-Women imeandaa viashiria vya jinsia katika utekelezaji waMalengo ya Maendeleo Endelevu hapa nchini. Uwepo waviashiria hivi utasaidia kuhakikisha upangaji, utekelezaji naufuatiliaji wa malengo hayo unazingatia masuala ya jinsiana uwezeshaji wanawake.

MAENDELEO YA MTOTO

142. Mheshimiwa Spika, Maendeleo endelevu ya Taifalolote, yanategemea uwekezaji katika makuzi, malezi, namaendeleo ya mtoto. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu naMakazi ya mwaka 2012, idadi ya watoto ni asilimia 51.6 yawatanzania wote. Hali hii inaonesha umuhimu wa kulinda nakusimamia utekelezaji wa haki za msingi za mtoto ambazoni; kuishi, kuendelezwa, kulindwa, kushiriki na kutobaguliwa.

Ukatili dhidi ya watoto

143. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na ongezeko la taarifaza vitendo vya ukatili vinavyofanywa dhidi ya watoto. Kwamujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto kwa mwaka 2016vilivyoripotiwa ni 10,551 ikilinganisha na vitendo 9,541 mwaka2015 sawa na ongezeko la asilimia 9.6%. Vitendo hivyovinasababishwa kwa kiasi kikubwa na hali ya umaskini nauwepo wa mila na desturi zenye madhara. Utolewaji wa

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

taarifa za vitendo vya ukatili ni mojawapo ya mikakati yaKupunguza vitendo hivyo katika jamii. Hivyo, Wizara kwakushirikiana na wadau imeendelea kupokea taarifa juu yavitendo husika na kuchukua hatua. Taarifa kupitia mtandaowa huduma ya simu ya kusaidia kuripoti taarifa za ukatilidhidi ya watoto kupitia namba ya simu 116 (Child Helpnine)zimeongezeka kutoka 33,675 mwaka 2015/16 hadi kufikia simu37,888 mwaka 2016/17, ongezeko hili sawa na asilimia 12.5ya simu zilizopokelewa. Kuongezeka kwa idadi hii ya simu nimatokeo ya mwamko wa jamii katika kutoa taarifa zamasuala ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwemoulawiti na ubakaji. Nitumie fursa hii kutoa rai kwa jamii,wazazi, walezi na watoto kutosita kutoa taarifa kuhusuvitendo vya ukatili katika maeneo yao.

144. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imetoa mafunzo juuya mbinu za kushirikisha wazazi na walezi kubadili mitazamokuhusu mila na desturi zenye madhara kwa watoto naumuhimu wa kuwekeza katika malezi yenye mwelekeo wakumlinda na kumwendeleza mtoto hasa mtoto wa kike.Mafunzo hayo yalitolewa wa kipindi cha Julai 2016 mpakaMachi 2017 kwa maafisa maendeleo ya jamii 505, walimu 40na maafisa ustawi wa jamii 39 katika Halmashauri 72 nchini.

Mimba na ndoa za utotoni

145. Mheshimiwa Spika, mimba na ndoa za utotoni badoni kikwazo katika kufikia maendeleo endelevu ya nchi yetu.Kwa mujibu wa Utafiti wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa kiwangocha ndoa za utotoni nchini ni asilimia 37. Mikoa inayoongozakwa ndoa za utotoni ni Shinyanga (59%) Tabora (58%), Mara(34%), Dodoma (51%) na Lindi (48%). Aidha Takwimu hizo piazinaonesha kuwa asilimia 27 ya watoto wanaathirika namimba za utotoni nchini, mikoa inayoongoza ni Katavi (36.8%),Tabora (36.5%), Simiyu (32.1%), Geita (31.6%) na Shinyanga(31.2%). Katika kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni,Wizara kwa mwaka 2016/17 ilishirikiana na wadau kufanyautafiti katika mikoa 10 na halmashauri 20 na kubaini kuwavyanzo vikubwa vya ndoa na mimba za utotoni ni umaskinina mila potofu. Utafiti huu umesaidia Serikali na wadau

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

wengine kuendesha kampeni na programu za kupinga ndoaza utotoni ili kupunguza tatizo hili. Wizara kwa kushirikianana wadau iliendesha Kampeni maalum ya kupinga ndoa zautotoni mkoani Shinyanga ambayo iliwafikia wananchi zaidiya 800 na kuokoa Watoto wa kike 102 waliokuwa katikahatua za kuozeshwa.

Maendeleo ya Mtoto wa Kike

146. Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha kuwa mtotowa kike anapata fursa ya kujiendeleza, Wizara imeendeleakuhamasisha uanzishwaji wa klabu za wasichana shuleniambazo zinawapa fursa ya kujitambua, kujua haki zao nakutoa taarifa ya ukiukwaji wa haki zao. Vilevile, klabu hizi nisehemu ambayo watoto wanakutana na kubadilishanamawazo kuhusu maendeleo yao kielimu. Katika Mwaka 2016/17, Wizara imehamasisha na kuwezesha kuanzishwa kwaklabu 105 za watoto wa kike na kiume shuleni katika wilayaya Tarime, Shinyanga vijini na Kahama.

Ushiriki wa Mtoto katika Maendeleo

147. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kusimamiaupatikanaji wa haki ya ushiriki wa mtoto kupitia mabarazaya watoto. Katika mwaka 2016/17, Wizara iliwawezeshaviongozi wa Kamati Kuu ya Baraza la Watoto la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kufanya ziara ya mafunzo kwenyemabaraza yanayotekeleza majukumu yake vizuri. Mikoailiyotembelewa ni pamoja na Mwanza, Lindi, Iringa, MjiniMagharibi, Mkoa wa kusini na Mkoa wa Kaskazini. Lengo laziara hii ni kupata ujuzi, kuboresha mabaraza na ushiriki waWatoto katika shughuli za maendeleo. Hadi sasa, jumla zaHalmashauri zilizoanzisha Mabaraza ya Watoto ni 108 naMikoa yenye Mabaraza za Watoto ni 21 Kiambatisho Na. 7

HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII

148. Mheshimiwa Spika, huduma za ustawi wa jamiizinalenga kuyawezesha makundi maalum kupata hudumaza msingi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Makundi haya ni pamoja na watoto walio katika mazingirahatarishi, watoto walio katika mkinzano na sheria, watuwenye ulemavu na wazee. Makundi mengine ni yale ambayoyanakosa au yapo katika hatari ya kukosa fursa ya kushirikikikamlifu katika shughuli za maendeleo mfano familia zenyemigogoro, wakimbizi, waathirika wa matumizi mabaya yapombe na madawa ya kulevya.

Huduma za Ustawi kwa Watoto, Watoto Walio katikamazingira Hatarishi na Walio katika Mkinzano wa Sheria

149. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwekamifumo ya matunzo, malezi na ulinzi wa watoto yenye misingiya kijamii. Mwaka 2016/17, Wizara kwa kushirikiana na wadauimehamasisha na kuzijengea uwezo Halmashauri 18kuanzisha timu za ulinzi na usalama wa mtoto ambapo idadiya Halmashauri zenye timu za ulinzi na usalama imeongezekakutoka 33 mwaka 2015/16 hadi kufikia Halmashauri 51 mwaka2016/17. Vilevile, kwa kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi2017 Wizara imeendelea na zoezi la kuziwezesha Halmashaurikuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishiili kuwa na takwimu sahihi zitakazotumiwa na wadau kutoahuduma. Jumla ya watoto 131,304 (wavulana 66,965 nawasichana 64,339) walitambuliwa na kupatiwa hudumambalimbali ikiwemo chakula, mavazi, mahitaji ya shule namsaada wa kisaikolojia.

150. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2016/17, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI imeandaamwongozo wa mfumo wa kushughulikia masuala ya watotowalio katika mazingira hatarishi. Mfumo huu utawezeshakushughulikia masuala ya watoto kwa wakati. Vilevile, kwakushirikiana na wadau, wizara imewajengea uwezo watoahuduma za ustawi wa jamii na watoa huduma za kujitolea2,974, ili waweze kutoa huduma katika ngazi za kata na vijiji/mitaa.

151. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilitoa leseni 18 zauendeshaji wa makao ya watoto na kufanya Makao yaWatoto yaliyosajiliwa kufikia 195. Aidha, Wizara imeendelea

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

kutoa huduma za chakula, malazi na huduma za afya kwawatoto 115 waliotunzwa katika Makao ya Taifa ya WatotoKurasini.

152. Mheshimiwa Spika, Ili kuwezesha watoto wanaoishikatika mazingira hatarishi kulelewa katika familia, Wizarainatekeleza mpango wa kuwatumia walezi wa kuaminiwa,walezi mbadala, huduma ya malezi ya kambo na kuasili.Kwa mwaka 2016/17, jumla ya watoto 53 (Me 19, Ke 24)waliwekwa katika malezi ya kambo na watoto 20 (Me 7, Ke13) waliasiliwa. Katika kipindi hicho Wataalamu wa Ustawiwa Jamii 35 walijengewa uwezo kuhusu kuwatambua waleziwa kuaminika ambao watatoa huduma ya muda kwawatoto hao.

Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto

153. Mheshimiwa Spika, Malezi Changamshi ya awali kwamtoto yameendelea kuratibiwa. Kwa mwaka 2016/17, vituo75 vya kulelea watoto wadogo mchana vimesajiliwa nakufanya idadi ya vituo hivyo kuongezeka kutoka vituo 782mwaka 2015/16 hadi kufikia vituo 856 mwaka 2016/17. Aidha,jumla ya walezi wa watoto 1,211 walidahiliwa katika vyuo23 vya malezi ya watoto. Vilevile, Wizara iliwajengea uwezowa malezi na makuzi ya mtoto wataalam wa afya nawahudumu wa afya ngazi ya jamii 401 katika Manispaa yaTabora na Halmashauri ya Nzega na Igunga.

Huduma kwa Watoto walio katika Mkinzano na Sheriana Marekebisho ya Tabia.

154. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoamatunzo na maadilisho kwa watoto walio katika mkinzanona sheria katika mahabusu za watoto za Dar es Salaam,Arusha, Mbeya, Moshi na Tanga na Shule ya MaadilishoIrambo. Katika mwaka 2016/17, Wizara imetoa huduma zachakula, malazi, mavazi, huduma za matibabu na elimu kwawatoto 375 (wavulana 345, wasichana 30) walio katikamahabusu za watoto na waadiliwa (wavulana 72) katikashule ya Maadilisho Irambo. Aidha, Wizara imewachepusha

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

watoto 882 kutoka katika mfumo wa makosa ya jinai. Katiyao, watoto 353 wamepitia mpango wa jamii wamarekebisho ya tabia kwa watoto waliokinzana na sheriana watoto 529 waliotuhumiwa kufanya makosa ya jinaikutoka katika Vituo vya Polisi na kuunganishwa na familiazao.

155. Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara iliwajengea uwezomaafisa 228 wanaosimamia haki za Watoto. Mafunzoyalihusu utekelezaji na usimamizi wa amri za mahakama ilikuboresha upatikanaji wa haki kwa wakati. Kati ya hao,Mahakimu 46, Maafisa Ustawi wa Jamii 135 na WaendeshaMashtaka 47.

Maendeleo na Ustawi wa Familia

156. Mheshimiwa Spika, familia ni kitovu cha maendeleoya binadamu na Taifa kwa ujumla. Katika kuhakikisha utulivuna uimara wa familia ambao ni msingi wa jamii, Wizaraimeendelea kutoa huduma za unasihi na usuluhishi wamigogoro ya ndoa. Katika mwaka 2016/17, jumla ya mashauriya ndoa 6,819 yalipokelewa ambapo mashauri 2,727yalisuluhishwa na mengine 4,092 yalipelekwa mahakamanikwa utatuzi wa kisheria.

157. Mheshimiwa Spika, Wizara imewajengea uwezowataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii 402kuhusu elimu ya malezi bora katika ngazi ya familia. Mafunzohayo yalitolewa katika Halmashauri na Kata za Temeke,Mafinga na Mufindi. Mafunzo hayo yanatarajiwakuwawezesha wataalam hao kuwajengea uwezo wazazi nawalezi kuhusu malezi bora ya watoto.

HAKI NA USTAWI WA WAZEE

158. Mheshimiwa Spika, wazee ni rasilimali muhimu kwamaendeleo ya taifa kutokana na uzoefu na ujuzi walionaokatika nyanja mbalimbali. Kwa mwaka 2016/17, Wizara kwakushirikiana na wadau imeendelea kutoa elimu kwa jamiikuhusu haki na ustawi wa wazee kupitia vyombo vya habari

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

na maadhimisho ya siku ya wazee. Elimu hii imesaidiakuongezeka kwa idadi ya wazee wanaopata huduma zaafya na kupungua kwa vitendo vya ukatili. Kwa mujibu waTaarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mauaji yawazee yamepungua kutoka 190 (me 66, ke 124) mwaka 2015hadi 135 (me 44, ke 91) mwaka 2016.

159. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarakwa kushirikiana na OR - TAMISEMI imewezesha kuwatambuawazee 69,100 na kufanya idadi ya wazee waliotambuliwakufikia 367,889. Kati yao, wazee 16,990 walipatiwavitambulisho vya msamaha wa matibabu na kufanya idadiya wazee wenye vitambulisho hivyo kufikia 74,590. Vilevile,Wizara kwa kushirikiana na wadau imewezesha kufanyikakwa ukarabati katika makazi ya wazee ya Kailima. Wizarapia imeboresha miundombinu kwa kuanza ujenzi wa bwenikatika makazi ya Kolandoto (Mkoa wa 17)Vilevile, Wizaraimeendelea kutoa huduma kwa wazee 456 wasiojiwezakatika makazi 17 yanayoendeshwa na Serikali. Huduma hizini pamoja na chakula, malazi na matibabu.

160. Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kuwashukuruwadau mbalimbali waliochangia katika kuhakikisha hudumabora kwa wazee nchini. Kipekee napenda kumshukuru Mkewa Rais, Mhe, Mama Janet Magufuli kwa kuwa mstari wambele katika kuwasaidia wazee wanaotunzwa katikamakazi ya wazee hapa nchini. Natoa wito kwa jamii kuigamfano wa mama yetu huyu. Sote ni wazee watarajiwatunahitaji kuwaenzi, kuwaheshimu na kuwatunza wazeewetu.

Wataalam wa Ustawi wa Jamii

161. Mheshimiwa Spika, Wataalam wa Ustawi wa Jamiini muhimu katika kuhakikisha utengamano wa familia najamii. Katika kuhakikisha tunakua na wataalam hao katikangazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara kupitia Taasisiya Ustawi wa Jamii imeendelea kuzalisha wataalam haokupitia mafunzo katika fani za Ustawi wa Jamii na fani

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

nyingine ikiwemo Rasilimali Watu na Mahusiano Kazini kwangazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada, Stashahadaya Uzamili na Shahada ya Uzamili. Kwa kipindi cha mwaka2016/17, jumla ya wataalamu 1,164 walihitimu. Aidha, katikakuboresha mafunzo hayo, Taasisi imeendelea na ujenzi waMaktaba ya kisasa.

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

162. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwekamazingira wezeshi kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kushirikikikamilifu katika kuchangia kufikiwa kwa maendeleo naustawi wa jamii. Katika kutekeleza hilo, Wizara iliendeleakusajili, kufuatilia na kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo yaKiserikali nchini ambapo, katika kipindi cha 2016/17, jumlaya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 264 yalisajiliwa. Kati ya hayomashirika 26 ni ngazi ya Kimataifa, 218 ngazi ya Kitaifa, 5ngazi ya Mkoa na 15 ni ya ngazi ya Wilaya. Usajili huoumeongeza idadi ya mashirika kutoka 8,047 mwezi Julai, 2016hadi kufikia 8,144 mwezi Machi, 2017 (Kiambatisho Na.8 ).

163. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2016/17, Wizara ilifuatilia utendaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.Katika ufuatiliaji huo, jumla ya miradi 79 ya Mashirika Yasiyoya Kiserikali iliyopo katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Geita,Mara, Tanga na Mtwara ilitembelewa na kukaguliwa. Wizarapia ilifanya tathmini ya taarifa za utekelezaji kutoka katikamashirika 267. Matokeo ya tathmini yanaonesha kuwamchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali umezidi kuimarikahasa katika maeneo ya; afya, hifadhi ya mazingira, elimu,jinsia, utawala bora, utetezi wa haki za binadamu, hifadhiya jamii na kilimo.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya ufuatiliaji na tathmini piailibainisha kuwa, jumla ya Mashirika 100 hayakuzingatiamiongozo ya kisera, sheria, kanuni na katiba ya mashirikahusika na hivyo kufutiwa usajili.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2016/17 KWATAASISI NYINGINE ZILIZO CHINI YA WIZARA

TAASISI YA CHAKULA NA LISHE (TFNC)

164. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Chakula na lishe inajukumu la kuratibu, kutoa miongozo, kujenga uwezo kwawataalamu, kufanya tafiti na kuishauri Serikali na wananchikwa ujumla juu ya lishe bora na namna ya kuutokomezautapiamlo. Taasisi imeendelea na jitihada za kupambana nautapiamlo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitanona wanawake walioko kwenye umri wa kuzaa. Aidha, Utafitiwa Maendeleo ya Afya Nchini wa mwaka 2016 umebainikuwa tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka mitanolimepungua kutoka asilimia 42 hadi 34, uzito pungufuumepungua kutoka asilimia 16 hadi 14. Mafanikio hayayametokana na utekelezaji wa afua mbalimbali. Vilevile,Taasisi ilikamilisha maandalizi ya Mpango wa Taifa waUtekelezaji wa masuala ya lishe 2016/17 – 2020/21. Mpangohuo ni mbadala wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Lishe wamwaka 2011/12-2015/16 ambao umekwisha muda wake.

165. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Taasisiilifanya mafunzo kwa wakufunzi wa Taifa wa Afya na Lisheya watoto. Mafunzo yalihusisha wajumbe wa Timu zaUendeshaji wa Huduma za Afya za Halmashauri kwaHalmashauri zote 184 nchini. Mafunzo yalilenga kutathminizoezi la Afya na Lishe ya watoto la mwezi Juni 2016, kuangaliachangamoto zinazowakabili, ili kuwapa wajumbe wa Timuza Uendeshaji wa Huduma za Afya za Halmashauri ujuzi zaidina mbinu za utekelezaji wa afua za Afya na Lishe ya watoto.Aidha, Taasisi imeendelea kukusanya taarifa za ufanisi wautoaji huduma za mwezi wa Afya na Lishe ya Mtoto kwamwezi Desemba 2016 kutoka mikoa yote nchini ili kujua idadiya watoto waliofikiwa na huduma za matone ya vitamini A(miezi 6 – 59), utoaji wa dawa za kutibu maambukizi yaminyoo (miezi 12 – 59) na upimaji wa hali ya lishe ya watotowenye umri wa miezi 6 -59 pamoja na kutoa rufaa kwawatoto wenye utapiamlo.

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

BOHARI YA DAWA (MSD)

166. Mheshimiwa Spika, Bohari ya Dawa imetekelezamajukumu yake ya msingi ya ununuzi, uhifadhi na usambazajiwa Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba, Vitendanishi na chanjo ilikuwezesha upatikanaji endelevu katika vituo vya kutoleahuduma za afya zaidi ya vituo 5,414 nchini. Wastani waupatikanaji wa dawa muhimu katika Bohari ya Dawaumeimarika. Hali hiyo inatokana na ongezeko la bajeti yadawa kutoka Shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi kiasi chaShilingi bilioni 251.5 mwaka 2016/17. Aidha, Katika kipindi chaJulai 2015 mpaka Machi 2016, Bohari ilipokea ni Shilingi bilioni24 tu kwa ajili ya dawa. Kwa mwaka mzima ikilinganishwana kipindi cha 2016/17 hadi kufikia Machi 2017 ambapo Boharitayari imeshapokea kiasi cha shilingi bilioni 112.198.

167. Mheshimiwa Spika, MSD inaendelea kuimarishamfumo wa ugavi ambapo imefunga viambato vyakielektroniki (Barcode Scanners) katika maeneo yote yausambazaji dawa ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihiza dawa, vifaa na vifaa tiba katika maghala wakati wote.Aidha, Kwa upande wa miradi msonge, MSD imetunza nakusambaza dawa zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni202 katika kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi, 2017.Hali hiyo, imewezesha kuimarika kwa upatikanaji wa dawaza Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma nchi nzima. Vilevile,MSD imenunua, kutunza na kusambaza vifaa, vifaa tiba navitendanishi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 57kwa ajili ya kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwaya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma nchi nzima.

168. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha upatikanaji wadawa na vifaa tiba kwa kiwango cha kutosha nchini, Serikalikupitia mpango wa ushikirishwaji wa sekta binafsi imeanzakutekeleza mkakati wa ujenzi wa viwanda vitakavyozalishadawa na vifaa Tiba hapa nchini ambapo MSD imetengewaeneo la Ekari 100 Mkoani Pwani. Aidha, MSD imeendeleakupanua uwezo wa maghala katika kanda zake ambapokatika kipindi cha Julai 2016 hadi Machi, 2017, maandalizi yaujenzi wa ghala la Kanda ya Dar es Salaam ujenzi wake

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

unategemewa kuwa umekamilika ifikapo June 2018.Kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuondoa gharama yashilingi milioni 800 zinazotumika katika ukodishaji wamaghalaya kuhifadhia dawa kutoka sekta binafsi kwamwaka.

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

169. Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umeendelea kubuni na kutekeleza mikakatimbalimbali hususan kuongeza wigo wa wanufaika wa bimaya afya. Idadi ya wanachama wachangiaji wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya, imeongezeka kutoka wanachama702,598 waliokuwa wameandikishwa mwaka 2015/16 hadikufikia wanachama 792,987 mwezi Machi 2017. Aidha, idadiya wanufaika nayo iliongezeka kutoka 3,377,023 mwaka2015/16 hadi kufikia wanufaika 3,880,088 mwezi Machi 2017.Hii inaonyesha kuwa wanachama wa Mfuo wameongezekakwa wastani wa asilimia 11 na wanufaika wameongezekakwa wastani wa asilimia 8 katika kipindi cha miaka mitano(Kiambatisho Na.9). Mafanikio hayo yameweza kupatikanakutokana na juhudi zinazofanywa na Mfuko za kuelimishawatanzania pamoja na kubuni mbinu mbalimbali zakuongeza wigo wa wanachama, kama kuanzishwa kwampango wa KIKOA (unaojumuisha kundi la wajasiriamali,vikundi vya vikoba, saccos na wavuvi), TOTO AFYA KADI(unaojumuisha watoto chini ya miaka 18), Wanafunzi wa vyuovya Elimu ya Juu, Wastaafu na wanachama binafsi.

MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

170. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Machi 2017 Mfuko waAfya ya Jamii (CHF) ulikuwa na jumla ya kaya 1,595,651zilizojiunga ukilinganisha na kaya 1,452,855 zilizokuwazimejiunga mwaka 2015/16. Aidha, wanufaikawameongezeka kutoka 8,717,130 mwaka 2015/16 hadi kufikiawanufaika 9,573,906 Machi 2017. (Kiambatisho Na.10). Katikakuchangia juhudi za wananchi wanaochangia CHF nakuboresha huduma zitolewazo, Serikali hutoa malipo ya telekwa tele kwenye Halmashauri kulingana na kiwango cha

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

makusanyo ya CHF. Malipo yaliyofanyika kwa Halmashaurikwa kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi 2017 ni Shilingibilioni 3.5. na hivyo kuwezesha jumla ya Shilingi bilioni 12.3kulipwa kwa Halmashauri mbalimbali nchini tangu Mfukoulipokabidhiwa jukumu hili mwezi Julai 2009. Vilevile, Mfukoumefanya mapitio ya Tiba kwa Kadi (TIKA) ili Huduma hiyoiimarike Mijini, Utaratibu wa uanzishaji wa TIKA uko katikahatua mbalimbali za utekelezaji katika Manispaa za jiji laDar-es-salaam, Kibaha Mji na Babati Mjini. Matarajio ya Mfukoni kuwa Halmashauri zote za Miji zitajielekeza katikakutekeleza TIKA.

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA)

171. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka yaChakula na Dawa imeendelea na shughuli za udhibiti waubora na usalama wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tibaambapo Mamlaka inakamilisha utekelezaji wa MpangoMkakati wake wa miaka mitano wa 2012 – 2017. Aidha, katikakipindi cha mwaka 2016/17, Mamlaka ilipokea jumla yamaombi ya usajili wa viwanda vipya 767 (chakula 739, dawa1, vipodozi 27) na vyote vilitathminiwa na kukaguliwaambapo viwanda 635 (chakula 613, dawa 1 na vipodozi 21)sawa na asilimia 82.8 vilisajiliwa baada ya kukidhi vigezo.Vilevile, Mamlaka ilipokea jumla ya maombi 8,023 ya usajiliwa majengo na maeneo ya biashara ambapo maeneo 7,873sawa na asilimia 98.4 yalikidhi vigezo na kusajiliwa.

172. Mheshimiwa Spika;, Katika kujiridhisha na usalama naubora wa bidhaa katika soko, Mamlaka ilifanya ukaguzi wamajengo 13,461 (6,743 ya chakula, 2,553 dawa, 3,957 vipodozina 208 vifaa tiba) ambapo majengo 11,923 sawa na asilimia89 yalikidhi vigezo na hivyo kuhuishiwa vibali vyao vyabiashara kwa mwaka 2016/17. Aidha, kupitia mfumo waufuatiliaji wa ubora na usalama wa bidhaa katika soko, jumlaya sampuli 462 zilichukuliwa katika soko na kuchunguzwakatika maabara ambapo sampuli 451 sawa na asilimia 98zilifaulu na sampuli 11 hazikukidhi vigezo na hivyo bidhaahusika ziliondolewa katika soko. Aidha, Mamlaka ilipokeamaombi 5,802 kwa ajili ya usajili wa bidhaa za dawa,

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

chakula, vifaa tiba na vipodozi ambapo bidhaa 4,322 sawana asilimia 75 yalisajil iwa. Vilevile, Mamlaka ilifanyauchunguzi wa jumla ya sampuli 2,860. Kati ya sampulizilizochunguzwa, sampuli 2,396 sawa na asilimia 84 zilifauluvigezo vya ubora na usalama na asilimia 16 hazikukidhivigezo na hivyo bidhaa husika hazikusajiliwa na nyinginekuondolewa.

173. Mheshimiwa Spika; Mamlaka ilisimamia uteketezajiwa jumla ya tani 631.7 za bidhaa za chakula, dawa, vipodozina vifaa tiba, zenye thamani ya takriban Shilingi 797,312,103.15kutokana na kutofaa kwa matumizi ya binadamu. Aidha,vipodozi vyenye viambato sumu vya thamani ya takribanShilingi milioni 616 vilikamatwa katika maghala ya kificho naviwanda bubu jijini Dar es Salaam na matenka ya kubebeamafuta mkoani Njombe ambapo vipodozi hivyo vinasubirihatua za kisheria kukamilika kabla ya kuteketezwa. Vilevile,Mamlaka imetoa Elimu kwa Umma kwa makundi mbalimbaliya wananchi na mihadhara katika vyuo na shule za sekondariambapo wanafunzi na walimu 51,835 katika mikoa yaRuvuma, Lindi, Pwani, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mbeya,Rukwa, Tanga, Simiyu na Songwe walielimishwa.

174. Mheshimiwa Spika; Ili kusogeza huduma karibu nawananchi, Mamlaka imekamilisha ujenzi wa ofisi namaabara ya Kanda ya Ziwa katika eneo la Nyakato, jijiniMwanza. Kukamilika kwa ofisi na maabara hiyo kutaongezaufanisi wa utoaji huduma na hivyo kuimarisha udhibiti. Aidha,Mamlaka imeimarisha mfumo wa kielektroniki wa kupokeataarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwanjia ya simu ya kiganjani ili kurahisisha upatikanaji wa taarifaza madhara ya dawa kwa haraka. Kupitia mfumo huo jumlaya taarifa mpya 71 sawa na asilimia 44 ya taarifa zotezimepokelewa. Vilevile, Mamlaka imeanzisha mfumo wakuweka taarifa za bidhaa zote zilizosajiliwa nchini kwenyemtandao ambao unasaidia wananchi na wateja kwa ujumlakuona bidhaa zilizosajiliwa na tarehe za kuisha muda wausajili.

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WASERIKALI (GCLA)

175. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2016/17, Wizarakupitia Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali imenununuamtambo wa Liquid Chromatography Mass Spectrometer kwakiasi cha shilingi bilioni 1.6. Mtambo huo utatumika katikakufanya uchunguzi wa sampuli mbalimbali, zikiwemo zasumu, kilimo, uvuvi, mifugo, maji, dawa za binadamu, gesi,mafuta n.k. Aidha, mtambo utatumika kuchunguza dawaza kulevya na kutoa mchango katika juhudi za Serikalikupambana na matumizi ya dawa za kulevya. Vilevile, katikakuboresha huduma za uchunguzi wa kimaabara Wakalaimenunua na kusimika mtambo wa kisasa (ED–XRF) katikaMaabara ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya. Mtambohuo utatumika kutambua ubora na usalama wa bidhaambalimbali za viwandani na kilimo, kutambua uwepo wamadini ya thamani kwenye udongo na bidhaa za vito nasampuli zinazohusiana na usalama wa afya na mazingira.

176. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2016/17, Wakalailikagua na kusajili makampuni 261 yanayojihusisha na shughuliza kemikali nchini sawa na asilimia 70 ya lengo. Aidha, Wakalailikagua viwanda na maghala 346 ambayo ni sawa naasilimia 65 ya lengo hadi kufikia Machi, 2017. Vilevile, Wakalailifanya uchunguzi na kutoa taarifa ya sampuli 25,632, sawana asilimia 194 ya lengo la kuchunguza sampuli 13,170.Sampuli hizo ni za Vinasaba, Sumu, Dawa za Kulevya,Vyakula, Dawa asilia, Kemikali, Maji, Vilainishi vya Mitambona sampuli za mazingira. Pia, Wakala umeendelea na ujenziwa Maabara ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya ambao hadimwezi Machi jengo hilo l imeshapauliwa na Shilingi180,000,000.00 sawa na asilimia 60 ya gharama zotezimetumika.

TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YABINADAMU (NIMR)

177. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Taasisi yaUtafiti wa Magonjwa ya Binadamu imeendelea na utafiti wa

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

chanjo dhidi ya virusi vya HPV vinavyosababisha Saratani yamlango wa kizazi. Utafiti huo unalenga kubaini kama dozimoja ya chanjo hiyo inaweza kutoa kinga sawa na dozi mbiliau tatu. Utafiti unashirikisha wasichana walio na umri wamiaka kati ya 9 na 14 walio katika shule za umma za kutwaza msingi na sekondari zilizopo jijini Mwanza. Utafiti huoutashirikisha wasichana 900, watakaofuatiliwa kwa miezi 36tangu walipopata dozi ya kwanza na unategemewakukamilika mwaka 2021.

178. Mheshimiwa Spika; Taasisi kwa kushirikiana na Taasisikutoka nchi za Kenya, Uganda na Ghana zilishiriki katika utafitiwa awali wa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola. Madhumuniya utafiti huo ilikuwa ni kutathmini usalama, ubora na uwezowa kutengeneza kinga dhidi ya virusi vya Ebola. Aidha, utafitihuo ulifanyika katika jiji la Mwanza kwa kushirikisha watuwazima 25 wasiokuwa na matatizo ya kiafya waliohiarikushiriki, wakiwemo wanaume 23 na wanawake Wawili.Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa chanjo hiyo kuwani salama. Uchambuzi wa takwimu unaendelea ili kuwezakubaini ubora wa chanjo hiyo katika kufanya mwiliutengeneze kinga dhidi ya virusi vya Ebola. Matokeo hayayatawasil ishwa pale uchambuzi wa takwimuutakapokamilika.

179. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2016/17, Taasisiilifanya utafiti katika tiba asilia ili kubaini uwezo na usalamawa dawa za asili zinazotumiwa na jamii mbalimbali hapanchini. Aidha, Taasisi imefanya utafiti wa dawa za asilizinazotumika kwa ajili ya tiba ya magonjwa ya malaria,UKIMWI na magonjwa nyemelezi, ugonjwa wa ini, shinikizola damu, kisukari na kupunguza mafuta lehemu mwilinipamoja na uvimbe wa tezi dume kwa wanaume na dawainayoongeza nguvu za kiume. Taasisi iko katika hatua zamwisho za kukamilisha usajili wa dawa asilia 11 ili ziwezekuingizwa sokoni.

MABARAZA YA KITAALUMA180. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wataaluma mbalimbali zilizomo katika sekta ya afya. Kwa

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

kuzingatia hilo Serikali imetunga sheria mbalimbali zakusimamia wanataaluma wa taaluma hizo. Hadi Machi 2017,Wizara imetunga sheria nane zinazosimamia taaluma zaudaktari na udaktari wa meno; uuguzi na ukunga; ufamasia;wataalam wa maabara; wataalam wa afya; optometria;radiolojia na tiba asili. Aidha, Wizara inasimamia utoaji wahuduma kupitia hospitali na maabara binafsi nchini.

181. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2016/17, Baraza laUuguzi na Ukunga Tanzania limeendelea kusimamia uborawa huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchinina kuhakikisha jamii inapata huduma za uuguzi na ukungazilizo bora na salama. Aidha, awamu ya kwanza ya Ujenziwa Kituo cha kuwaendeleza Wauguzi na Wakunga kitaalumanchini katika eneo la mjini Kibaha (Pwani) kwa kutumiavyanzo vya mapato ya ndani umekamilika. Lengo la mradihuo ni kuwawezesha wauguzi na wakunga nchini kupatanafasi ya kujiendeleza kitaaluma kwa kupitia mafunzo yamasafa yatakayokuwa yakiratibiwa katika jengo hilo. Mradihuo umegharamiwa kwa mapato ya ndani ya Barazaambapo unatarajia kukamilika kabla ya Mwezi Juni, 2017 nakiasi cha Shilingi bilioni 2.674 kimetumika.

182. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2016/17, Baraza laFamasi liliendelea kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikalikufanya kaguzi katika maduka ya jumla na rejareja ya dawaambapo jumla ya maduka ya dawa 721 yalikaguliwa namaduka 396 asilimia 54.9 yalikutwa na makosa mbalimbali.Baadhi ya makosa yaliyobainika ni pamoja na utoaji hudumaikiwemo kuendesha biashara ya dawa pasipo usimamizi wamfamasia na uuzaji wa dawa zisizoruhusiwa kwa madukaya dawa muhimu. Aidha, Baraza limetoa vibali kwa famasi190 na maduka ya dawa muhimu 1,009 katika Halmashaurimbalimbali ambapo hadi kufikia Machi 2017 jumla ya famasi1,432 na maduka ya ADDO 11,517 yalikuwa yamesajiliwanchini kote.

183. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Baraza laTiba Asili na Tiba Mbadala kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,TAMISEMI imewasajili waganga wa tiba asili na tiba mbadala

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

5,298 kutoka mikoa yote nchini na hivyo kufikisha waganga15,960 waliosajiliwa, vituo vya kutolea huduma vilivyosajiliwani 45 na hivyo kufikisha jumla ya vituo 228. Aidha, Barazalilifanya ufuatiliaji wa huduma za tiba asili katika Mikoa yaRuvuma, Mbeya, Iringa na Songwe na kutoa elimu kuhusuSheria, Kanuni, Miongozo mbalimbali kwa waratibu 17 wamikoa hiyo pamoja na baadhi ya waganga 373 wa tiba asili.

184. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Bodi yaUshauri ya Hospitali Binafsi imesajili vituo 45, makampuni 13na kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Wateja. Aidha, Bodiya Maabara Binafsi za Afya ilifanya ukaguzi wa jumla yabidhaa 309 zilizoingizwa nchini.

III. VIPAUMBELE VYA WIZARA NA BAJETI YA MAPATO,MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEOKWA MWAKA WA FEDHA 2017/18

185. Mheshimiwa Spika Katika mwaka wa fedha 2017/18, Wizara kupitia fungu 52 itatekeleza vipaumbelevifuatavyo:

i. Kuimarisha Huduma za Kinga, Tiba, nakuongeza usawa katika kutoa huduma za afya

ii. Kuimarisha huduma za afya ya uzazi na mtotoili kupunguza vifo vya wanawake wajawazitona watoto,

iii. Kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaatiba na vitendanishi katika vituo vya umma vyakutolea huduma za afya,

iv. Kuimarisha miundombinu kwenye vyuo vyamafunzo ya afya kwa lengo la kuongezaudahili na upatikanaji wa rasilimali watu,

v. Kuimarisha matibabu ya kibigwa nchini kwakuendeleza ujenzi, upanuzi, ukarabati wamiundombinu na kufunga mitambo ya kisasa

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

ya kutolea huduma za afya katika Hospitaliya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),Hospitali ya Benjamini Mkapa - Dodoma,Taasisi ya Saratani Ocean Road, HospitaliMaalum za Mirembe na Kibong’oto; piaHospitali za Rufaa za Kanda za Bugando,KCMC, Mbeya na Mtwara.

vi. Kuimarisha mazingira ya ubia na ushirikianokati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP) katikautoaji wa huduma za afya,

vii. Kuimarisha huduma za lishe na upatikanajiwake katika jamii na vituo vya kutoleaHuduma za Afya,

viii. Uimarishaji wa matumizi ya Teknolojia yaHabari na Mawasiliano (TEHAMA) katikakuboresha huduma za afya.

ix. Kuhamasisha wananchi kwa nia ya kuongezaidadi ya wanaojiunga na Mifuko ya Bima zaAfya.

186. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Fungu 53imepanga kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatiamaeneo ya kipaumbele yafuatayo;

i. Kuamsha ari ya wananchi kushiriki katikashughuli za kujiletea maendeleo

ii. Kuwezesha utekelezaji wa Mpango Kazi waTaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi yaWanawake na Watoto wa mwaka 2017/18 –2021/22;

iii. Kuimarisha upatikanaji wa haki na maendeleoya Mtoto;

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

iv. Kukuza usawa wa jinsia na uwezeshaji wawanawake kiuchumi;

v. Kuimarisha huduma za ustawi wa Mtoto naWazee;

vi. Kuimarisha ushiriki wa Mashirika Yasiyo yaKiserikali katika maendeleo ya jamii kwakuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi;na

vii. Kuboresha mazingira ya kufundishia nakujifunzia katika Taasisi ya Maendeleo ya JamiiTengeru, Vyuo vya Maendeleo ya Jamiipamoja na Taasisi ya Ustawi wa Jamii

187. Mheshimiwa Spika, i l i kutekeleza vipaumbelevil ivyoainishwa katika mwaka 2017/18, kazizitakazotekelezwa ni pamoja na;

HUDUMA ZA KINGA

188. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha 2017/18, Wizaraitaendelea kutekeleza afua mbalimbali za huduma za kingaikiwa ni pamoja na;

i. Kununua na kusambaza chanjo kulingana namahitaji ya nchi ambapo jumla ya shilingibilioni 33 zimetengwa.

ii. kununua na kusambaza majokofu 1,710 yakutunzia chanjo yatakayotumika katika ngaziya wilaya na vituo vya huduma.

iii. Kuendelea kutekeleza Kampeni yauhamasishaji na uelimishaji umma (BehaviourChange and Communication-BCC) kuhusuusafi wa mazingira nchini.

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

iv. Kuendelea kugawa dawa kwa ajili ya kuzuiamaambukizi ya ugonjwa wa usubi naMatende, minyoo ya tumbo, kichocho naugonjwa wa trakoma katika Halmashauri zamikoa ambayo haikupatiwa dawa hizo kwamwaka 2016/2017.

v. Kuendela kugawa vyandarua kupitia kliniki zawajawazito na watoto (RCH) katika mikoa 9ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Geita, Mwanza,Kagera, Mara, Simiyu na Kigoma na baadaekujumuisha Mikoa mingine iliyobaki hadikukamilisha mikoa yote kwa awamu

vi. Kuendelea kuhakikisha upatikanaji wavitendanishi (mRDT) kwa ajili ya kupima uwepowa vimelea vya malaria na dawa mseto katikavituo vyote vya kutolea huduma za afyanchini.

vii. Kuongeza wigo na kasi ya uibuaji wawagonjwa wa kifua kikuu katika mikoa yotenchini.

viii. Kusambaza mashine 90 za GenXpertzitakazotumika kufanyia uchunguzi wavimelea vya Kifua kikuu nchini

ix. Kufanya kampeni maalum za uchunguzi nauibuaji wa wagonjwa wapya wa ukomakatika wilaya zenye viwango vikubwa vyamaambukizi zikiwemo wilaya za Liwale,Kilombero, Chato, Nanyumbu, Mkinga naMuheza.

x. Kuendelea kutoa dawa za kufubaza virusi vyaUKIMWI kwa jumla ya watu 2,253,836 nchini.

xi. Kufunga mashine mpya 80 za kupima uwingiwa virusi vya UKIMWI, TB na Utambuzi wa Virusi

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

vya UKIMWI kwa watoto wadogo wenye umrichini ya miezi 18 katika hospitali za mikoaambayo haijapatiwa huduma hii na hasakatika wilaya zenye idadi kubwa ya WAVIU.

xii. Kuendelea kuhamasisha wananchi kuzingatiamfumo bora wa maisha ikiwemo kufanyamazoezi mara kwa mara, kuzingatia ulaji wavyakula unaofaa, kupunguza unywaji wapombe kupita kiasi, kujiepusha na matumiziya sigara na bidhaa za tumbaku pamoja nakujenga utamaduni wa kupima afya marakwa mara.

xiii. Kuanza mchakato wa kutunga sheria mpyainayoendana na Framework of theconvention on tabacco control badala yasheria ya Tumbaku ya mwaka 2003inayotumika sasa.

Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto

i. Kuendelea kushirikiana na wadau wamaendeleo katika kununua na kusambazadawa na vifaa vya uzazi wa mpango nchiniambapo Serikali imetenga jumla ya shilingibilioni 14

ii. Kuendelea kununua, kusambaza na kutoa bilamalipo dawa kwa ajili ya uzazi salama katikavituo vya umma vya kutolea huduma ikiwemooxytocin (dawa ya kuzuia kutokwa na damubaada ya kujifungua), magnesium sulphate(kwa ajili ya kifafa cha mimba), Fefol (kwa ajiliya kuongeza damu) ambapo jumla ya shilingibilioni 7 zimetengwa.

iii. Kuendelea kuhamasisha jamii kuhusuumuhimu wa kuhudhuria kliniki kwaakinamama wajawazito nchini na kujifungulia

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

katika Vituo vya kutolea huduma badala yakujifungulia nyumbani.

iv. Kuendelea kushirikiana na wadau wamaendeleo kwa kulipia kadi za Bima ya Afyakwa wanawake wajawazito wa kipato chachini 150,000 kupitia Mradi wa Tumaini laMama ambapo jumla ya shilingi milioni 600zimetengwa

v. Kuboresha huduma za uchunguzi za uzazisalama kwa kununua mashine 65 zaultrasound kwa ajili ya vituo vya afya ilikuwezesha kutoa huduma maalum za dharurakwa kinamama wajawazito ambapo jumla yashilingi 5,412,500 zimetengwa

vi. Kuendelea kuboresha upatikanaji wa hudumaza uzazi za dharura ikiwemo upasuaji wakumtoa mtoto tumboni kwa kuboresha vituovya afya 150 ambapo jumla ya shilingi bilioni1.8 kutoka vyanzo vya ndani zimetengwa.

vii. Kuendelea kuboresha upatikanaji wa damusalama kwa kuongeza vituo 5 vya benki zadamu katika mikoa yenye takwimu za vifovingi vitokanavyo na uzazi ikiwemo mikoa yaKatavi, Rukwa, Ruvuma, Njombe na Manyarajumla ya shilingi bilioni 2 zimetengwa.

viii. Kuongeza upatikanaji wa huduma za kupimana matibabu ya mabadiliko ya awali yasaratani ya mlango wa kizazi na saratani yamatiti katika Vituo vya afya na zahanati 100nchini.

ix. Kuhakikisha wodi za watoto wachanga (neonatal ward) zinaanzishwa katika hospitali zoteza Rufaa za mikoa na wilaya nchini.

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

x. Kuendelea kutoa huduma za urutubishaji waunga, mafuta na uongezaji wa madinijotokatika chumvi kwa mikoa yote nchini.

xi. Kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamiikuhusu masuala mbalimbali ya kiafya kupitianjia zote za mawasiliano, ikiwemomachapisho, vyombo vya habari, simu za kiganjani na mitandao ya kijamii.

HUDUMA ZA TIBA

Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi.

189. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha 2017/18, Wizaraitaendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa Dawa, Vifaa,Vifaa Tiba na Vitendanishi nchini kwa kununua nakuvisambaza katika vituo vya kutolea huduma za afya. Jumlaya shilingi bilioni 236 zimetengwa.

Huduma za Damu Salama

190. Mheshimiwa Spika katika mwaka 2017/18, Wizaraimetenga jumla ya shilingi bilioni 3.5 ili kuendelea kukabilianana tatizo la uhaba wa damu salama kwa kutekelezayafuatayo:

i. Kukusanya chupa za damu salama 230,000kukidhi mahitaji ya damu salama nchini

ii. Kuendesha kampeni ya ukusanyaji wa damukutoka katika makundi mbalimbali katika jamii

Uimarishaji wa Huduma za kibingwa

191. Mheshimiwa Spika katika mwaka 2017/18, Wizaraitaendelea kuimarisha upatikanaji na utoaji wa huduma zakibingwa nchini. Kupitia Hospitali ya Taifa Muhimbili kazizitakazotekelezwa ni pamoja na:

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

i. Kuanzisha huduma za kubadilisha figo (renaltransplant)

ii. Kuanzisha huduma za upandikizaji wa vifaavya kusaidia kusikia ambapo jumla ya shilingimilioni 206.3 zimetengwa kwa ajili ya kununuavifaa vya kusaidia kusikia.( cochlear inplant)

iii. Kuanza ujenzi wa jengo maalum kwawagonjwa wanaolipia (private wing) ambapojumla ya shilingi bilioni 14.5 zimetengwa.

iv. Kununua Vifaa, Vitendanishi na Vifaa Tiba kwalengo la kuboresha huduma za kibingwaambapo jumla ya shilingi bilioni 4zimetengwa.

192. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Taasisi ya MifupaMuhimbili (MOI), katika mwaka 2017/18, Wizara itaendeleakutekeleza kazi zifuatazo:

i. Kuendelea kutoa matibabu kwa maradhi yoteya Mgongo, mishipa ya fahamu na mifupa.

ii. Kuwaongezea ujuzi wataalam wa upasuajiwa kubadilisha Nyonga na Goti.

iii. Kuanza upasuaji wa vivimbe kwenye mishipaya damu ya ubongo.

iv. Kuboresha utoaji wa huduma kwa kununuavifaa na vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya jengola MOI awamu ya tatu ambapo jumla yashilingi bilioni 2 zimetengwa, na

v. Kuendelea kurejesha Mkopo uliotumikakugharamia ujenzi wa jengo hilo ambapojumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetengwa.

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

193. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Taasisi yaMoyo Jakaya Kikwete itaendelea kuboresha huduma zamatibabu ya moyo kwa kutekeleza yafuatayo:

i. Kuboresha miundombinu ya kutolea hudumaikiwa ni pamoja kununua vifaa tiba kwa ajiliya chumba cha upasuaji ambapo jumla yashilingi bilioni 2 zimetengwa, na

ii. Kuendelea kuwajengea uwezo wataalam.iii. Kuandaa kambi mbalimbali za upasuaji kwa

kushirikiana na madaktari bigwa kutoka njeya nchi

194. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Taasisi yaSaratani Ocean Road itaendelea kuimarisha huduma zakinga, uchunguzi, mafunzo na tiba ya saratani kwa kutekelezakazi zifuatazo:

i. Kununua vifaa vya kisasa vya uchunguzi namatibabu ikiwa ni pamoja na PET Scanambapo kiasi cha shilingi bilioni 14.5zimetengwa. Hatua hii inatarajiwa kupunguzarufaa za wagonjwa nje ya nchi zaidi ya asilimia60 na hivyo kuokoa pesa za Serikali kiasi chashilingi billioni 5 kwa mwaka zinazotumikakulipia matibabu ya wagonjwa nje ya nchi

ii. Kuimarisha huduma za mkoba hasa katikamaeneo ambayo yanaonekana kuwa naidadi kubwa ya watu waliogundulika kuwana saratani.

iii. Kuimarisha upatikanaji wa dawa kwawagonjwa wa saratani ili kupunguza mzigokwa wagonjwa hasa wa kipato cha chini.

195. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuboreshaupatikanaji wa huduma za afya za kibingwa katika Hospitaliya Benjamin Mkapa Dodoma kwa kutekeleza yafuatayo:

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

i. Kununua vifaa na vifaa tiba ili kuboreshautoaji wa huduma za kibingwa ambapojumla ya shilingi bilioni 1 zimetengwa

ii. Kuongeza watalaam wa fani mbalimbali nakuwajengea uwezo waliopo.

iii. Kuanzisha maabara ya kisasa (cath lab) kwaajili ya matibabu ya moyo pamoja namaabara yenye uwezo wa kuchunguzavinasaba.

iv. Kuanzisha huduma ya matibabu yamagonjwa ya Figo na njia ya mkojo (Dialysis)na upandikizaji wa Figo (Renal Transplant)

196. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Wizara kupitia Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembeitaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya tiba ya afyaya akili katika kwa kutekeleza yafuatayo:

i. Kununua vifaa na vifaa tiba ambapo jumla yashilingi bilioni 1 zimetengwa.

ii. Kujenga uzio kuzunguka eneo la hospitali

iii. Kuendelea na ukarabati wa wodi zawagonjwa

197. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Rufaa ya Kanda yaNyanda za Juu Kusini Mbeya itatekeleza kazi zifuatazo:

i. Kuboresha na kupanua wigo wa hudumazinazotolewa kwa kufanya ukarabati jengo ladaraja la kwanza na kukamilisha ujenzi wajengo la watoto hivyo kuongeza uwezo kwahospitali kutoka vitanda 477 vya sasa mpakavitanda 605.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

ii. Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutoahuduma za radiolojia (Radiology) ambapojumla ya shilingi bilioni 2 zimetengwa.

198. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Rufaa ya Kanda yaZiwa Bugando itatekeleza kazi zifuatazo:

i. Kukarabati wa miundombinu ya kutoleahuduma ikiwa pamoja na kliniki za wagonjwawa nje, jengo la Saratani,

ii. Kukamilisha ujenzi wa kliniki ya wanachamawa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

iii. Kununua mashine ya Brachytherapy kwa ajiliya matibabu bora zaidi ya saratani.

199. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Hospitaliya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC, sambamba nakuendelea kutoa huduma itaendelea kutekeleza kazizifuatazo:

i. Kutekeleza awamu ya pili ya ujenzi wa wodina hosteli za wagonjwa wa sarataniutakaogharimu shilingi bilioni 2.

ii. Kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma zakusafisha figo.

200. Mheshimiwa Spika, Hospitali Maalumu ya Kibong’otoitaendelea kutekeleza kazi zifuatazo:

i. Kuboresha miundombinu ya kutolea hudumaikiwa ni pamoja na ukarabati wa wodi zawagonjwa na maabara. Jumla ya shilingibilioni 1 zitatumika kutekeleza kazi hizo

ii. Kutoa elimu kwa wataalam mbalimbali kwaajili ya kuwajengea uwezo wa kuanzishamatibabu ya kifua kikuu sungu.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

201. Mheshimiwa Spika, katika kuimalisha Huduma zauchunguzi wa magonjwa Wizara itaendelea na ujenzi wamaabara ya Taifa ya Afya ya Jamii katika eneo la Mabibo,Dar es salaam. Mradi huo hadi kukamilika unatarajiwakutumia kiasi cha Shilingi 7,493,193,434.97.00.

202. Mheshimiwa Spika, kuhusu Tiba Asili na Tiba MbadalaWizara itaendelea kutoa elimu kwa umma na wagangakupitia vyombo vya habari kuhusu usajili wa dawa za asilina maeneo ya kuzalishia dawa hizo.

203. Mheshimiwa Spika; katika mwaka, 2017/18, Wizarainakusudia kuboresha utoaji wa huduma za uuguzi naukunga unaozingatia maadili, utu, na heshima ya mteja“respective care”. Aidha, Wizara inapanga kuandaa mafunzoya muda mfupi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kurahisishaupatikanaji wa huduma muhimu zitolewazo na Wauguzi naWakunga.

204. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuboreshamfumo wa ufuatiliaji na upatikanaji wa takwimu za afyakutoka katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.kwakuimarisha mfumo wa kielektroniki wa kutoa taarifa za vituovya afya nchini yaani (HMIS/DHIS2) na uboreshaji wa mtandaowa kutoa taarifa za afya kupitia anuani yahmisportal.moh.go.tz

205. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizarakwa kushirikiana na OR-TAMISEMI inatarajia kuimarisha mfumowa mawasiliano kwa kutekeleza yafuatayo:

i. Kufunga awamu ya kwanza ya mfumo wakieletroniki wa kuhifadhi kumbukumbu zawagonjwa katika vituo vyote vya kutoleahuduma za Afya na kutoa mafunzo yamatumizi ya mfumo huo.

ii. Kuanza kutumia TEHAMA katika kufuatiliawagonjwa na taarifa zao katika ngazi ya jamiihususan taarifa za vifo, uzazi, magonjwa ya

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

mlipuko na magonjwa sugu kama kifua kikuuna UKIMWI (self-assessment) kwa kutumiamfumo wa simu za kiganjani.

iii. Kuanzisha mfumo wa CHF mobile app ambaoutarahisisha upatikanaji wa huduma za bimaya afya katika jamii.

RASILIMALI WATU KATIKA SEKTA YA AFYA

206. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kusimamiaeneo la raslimali watu katika sekta ya afya ambapo katikamwaka 2017/18 kazi zifuatazo zitatekelezwa:

i. Kudahili wanafunzi watarajari 13,632 katikavyuo vya afya vilivyoko chini ya Wizara

ii. Kuendelea kugharamia mafunzo ya uzamili nauzamivu kwa watalaam wa kada mbalimbaliza afya.

iii. Kuendelea kuboresha miundombinu katikaVyuo vya Afya kwa kufanya ukarabati naupanuzi wa vyuo ambapo jumla ya shilingibilioni 3 zimetengwa.

207. Mheshimiwa Spika, i l i kutekeleza vipaumbelevil ivyoainishwa katika mwaka 2017/18, kazizitakazotekelezwa na fungu 53 ni zifuatavyo;

MAENDELEO YA JAMII

208. Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha kufikiwa kwamalengo ya nchi ya kufikia Uchumi wa kati kupitia wataalamhawa, Wizara katika mwaka 2017/18 itatekeleza yafuatayo:

i. Kuendelea kuhamasisha Halmashauri naMikoa kuajiri watumishi wa fani ya Maendeleoya Jamii;

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

ii. Kuendelea kuboresha utekelezaji wa shughuliza Maendeleo ya Jamii ikiwemo kuimarishamfumo wa ufuatiliaji na tathmini wa shughuliza maendeleo na ustawi wa jamii katika ngaziza Sekretarieti za Mkoa na Mamlaka za Serikaliza Mtaa. Uimarishaji wa mfumo huuutawezesha serikali kupata taarifa sahihi zaushiriki wa Jamii katika kuleta maendeleo yanchi yetu;

iii. Kuendelea kuwajengea uwezo Wataalam waMaendeleo ya Jamii wa kusimamia sera namiongozo ya Wizara ili waweze kuishirikishajamii katika kujiletea maendeleo;

iv. Kuendelea kuwezesha vyuo kuandaa nakutoa wataalam wa maendeleo ya jamiikatika Vyuo 8 na Taasisi ya Maendeleo yaJamii Tengeru katika ngazi za Astashahada,Stashahada, Shahada na Stashahada yaUzamili.

v. Kuboresha miundombinu ya vyuo namazingira ya kujifunzia na kufundishia; na

vi. Kuimarisha ubora wa wataalam wamaendeleo ya jamii wanaozalishwa na Taasisikwa kuandaa mitaala ya NTA level 4 & 9itakayozingatia hali halisi ya mabadiliko namahitaji ya jamii.

MAENDELEO YA JINSIA

209. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Wizara itaendelea kusimamia maendeleo ya jinsia kwakutekeleza yafuatayo:-

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Kuwawezesha wanawake kiuchumi

i. Kupitia Benki ya Wanawake Tanzania kutoaMikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 12kwa wajasiriamali wanawake 9,650 katikamikoa ya Dares Salaam, Mbeya, Njombe,Iringa, Dodoma, Ruvuma, Pwani na Mwanza.

ii. Kuwezesha Akaunti ya Malaika kufanya kazikwa ufanisi na kuwafikia wanawakewajasiriamali walengwa;

iii. Kuhamasisha uanzishwaji wa majukwaa yauwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoayote ya Tanzania Bara kwa kushirikiana naBaraza la Taifa la Uwezeshaji WananchiKiuchumi pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

iv. Kuendelea kuhakikisha Mfuko wa Maendeleoya Wanawake unawafikia wanawake wengi.Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais –TAMISEMI katika mwaka 2017/18, itaendeleakuhamasisha Halmashauri kuchangia asilimiatano (5%) ya mapato yao ya ndani katikaMfuko.

v. Kuboresha mfumo wa taarifa za mikopo nawanufaika wa mfuko, kazi itafanyika kwakushirikiana na OR - TAMISEMI;

vi. Kusambaza mwongozo wa uendeshaji waMfuko ulioboreshwa kwa Sekretarieti za Mikoana Halmashauri zote nchini; na

vii. Kuzijengea uwezo Kamati za Mikopo za Mfukokatika Halmashauri 15 kuhusu uendeshaji nausimamizi wa Mfuko ili kuimarisha utendaji nausimamizi wake kwa kushirikiana na Ofisi yaRais – TAMISEMI.

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Kuzuia na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia

viii. Kusambaza na kuwezesha kuanza kutumikakwa Daftari la kutunza taarifa za ukatili wakijinsia katika Mamlaka za Serikali za Mitaa naSekretarieti za Mikoa ili kuimarisha upatikanajina ubora wa taarifa na takwimu za ukatiliDhidi ya Wanawake na Watoto;

ix. Kuimarisha Kamati 51 za Ulinzi wa Wanawakena Watoto; na

x. Kufuatilia utekelezaji wa afua za kuzuia ukatiliwa kijinsia hususan dhidi ya wanawake nawatoto.

Ushiriki wa Wanawake katika Ngazi za Uongozi naMaamuzi

xi. Kuendelea kuhuisha Kanzidata inayooneshawasifu wa wanawake kwa ajili yakuwawezesha kushiriki katika fursa za uongozi,ngazi za maamuzi na ajira; na

xii. Kuziwezesha taasisi mbalimbali kutumiataarifa katika kanzidata kuajiri, kufanya uteuzina maamuzi mbalimbali ya kisera.

Uingizaji wa Masuala ya Jinsia Katika Sera, Sheria naMipango ya Kisekta na Taifa

xiii. Kukamilisha mapitio ya Sera ya Maendeleo yaWanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamojana Mkakati wake. Mapitio ya Sera hiyoyatawezesha kuzingatiwa kwa masualamuhimu ikiwemo Malengo ya MaendeleoEndelevu, Agenda ya Afrika Tuitakayo 2063,Mpango wa Taifa wa Maendeleo MiakaMitano na kukidhi mahitaji ya sasa ya kufikia

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawakenchini.

xiv. Kupitia Mwongozo wa uingizaji wa masualaya jinsia katika Sekta zote pamoja nakuandaa Kanzidata kwa ajili ya kuhifadhitaarifa za hali ya jinsia nchini.

MAENDELEO YA MTOTO

Ukatili dhidi ya watoto

210. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, kupitiaMpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi yaWanawake na Watoto, Wizara itatekeleza yafuatayo katikakutokomeza ukatili dhidi ya mtoto

i. Kuimarisha utendaji wa kamati za ulinzi wamtoto katika Mamlaka za Serikali ya Mitaakuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Halmashauriza Wilaya;

ii. Kuendelea kutoa mafunzo kuhusu malezichanya na athari za ukatili dhidi ya watotokatika Halmashauri 12 za Mikoa ya Lindi naMtwara;

iii. Kuhamasisha kuanzishwa kwa mfumo wa ulinziwa mtoto katika shule za msingi kwa ajili yakukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi yamtoto katika mazingira ya shule;

iv. Kuendelea kuelimisha wazazi, walezi na jamiikutokomeza mila na desturi zinazoathiri afyana maendeleo ya mtoto wa kike na kumnyimahaki kuendelea na masomo na hivyo kufifishandoto zake;

v. Kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa klabukatika shule za msingi na sekondari; na

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

vi. Kuendelea kusimamia upatikanaji wa haki yaushiriki wa mtoto kupitia mabaraza ya watoto.Kwa mwaka 2017/18, Wizara itaendeleakuhamasisha Halmashauri kuanzishamabaraza ya Watoto ili kuongeza idadi kutoka108 iliyopo sasa hadi kufikia 140 nakuyawezesha kutekeleza wajibu wakeipasavyo.

HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII

211. Mheshimiwa Spika Wizara imeendelea kuwekamifumo ya matunzo, malezi na ulinzi wa watoto yenye misingiya kijamii. Kwa mwaka 2017/18, pamoja na mambo mengineitafanya yafuatayo:

i. Kuendelea kuzijengea uwezo Halmashauri nawadau wengine kuweka mifumo imara yamatunzo na ulinzi kwa watoto wanaoishikatika mazingira hatarishi;

ii. Kuhamasisha na kuelimisha waajiri kuzingatiamarekebisho ya Sheria ya Kazi na MahusianoKazini hususan kifungu cha 33(10) na kuzifanyiamarekebisho kupitia Kanuni zake mpya kwakutoa fursa kwa waajiriwa wanawake kupatahaki ya kunyonyesha watoto wao;

iii. Kuendelea kuratibu na kusimamia uanzishwajina uendeshaji wa vituo vya malezi ya watotopamoja na kuwajengea uwezo watoahuduma za malezi na makuzi ya awali yaWatoto;

iv. Kuendelea kuwajengea uwezo watoahuduma kwa watoto wanaokinzana na sheriaili kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wakati;

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

v. Kuendelea kuwezesha utoaji wa huduma zausuluhishi na ushauri nasaha ili kuleta utulivuna uimara katika ndoa kwa maendeleo naustawi wa taifa;

vi. Kuendelea kuwajengea uwezo wataalam waMaendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii katikaHalmashauri ili kuboresha makuzi na malezikatika familia kwa lengo la kupunguza vitendovya ukatili wa watoto kwenye jamii;

vii. Kuendelea kuongeza idadi ya wanafunziwanaodahiliwa katika fani mbalimbali; na

viii. kuboresha miundombinu ya kufundishia nakujifunzia na kuanzisha kituo cha utafiti naubunifu katika fani ya ustawi wa jamii ilikuongeza ufanisi katika kufundisha.

HAKI NA USTAWI WA WAZEE

212. Mheshimiwa Spika, wazee ni rasilimali muhimu kwamaendeleo ya taifa kutokana na uzoefu na ujuzi walionaokatika nyanja mbalimbali. Katika mwaka 2017/18, Wizaraitaendelea kuboresha huduma, makazi ya wazee nakuimarisha upatikanaji wa haki kwa wazee kote nchini nakutokomeza mauaji ya wazee.

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

213. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwekamazingira wezeshi kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kushirikikikamilifu katika kuchangia kufikiwa kwa maendeleo naustawi wa jamii. Kwa mwaka 2017/18, Wizara itaendeleakusajili na kuratibu utendaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikalikwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Aidha,Wizara itaendelea kufuatilia utendaji wa Mashirika Yasiyo yaKiserikali na kuhakikisha yanatoa mchango unaotarajiwa kwamaendeleo na ustawi wa jamii.

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

214. Mheshimiwa Spika, aidha Taasisi zilizo chini ya Wizarazitaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma kwakutekeleza na Mipango ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na:

i. Kupanua maghala ya MSD katika Kanda yaDar es Salaam

ii. Kufanya upanuzi wa maabara ya MakaoMakuu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa ilikuongeza ufanisi katika uchunguzi wa bidhaa,

iii. Kuanza udhibiti wa vitendanishi na vifaa vyamaabara, kukamilisha ununuzi wa vifaa vyamaabara ya kisasa ya TFDA Kanda ya Ziwa,Mwanza

iv. Kuanza ujenzi wa jengo la Maabara na ofisiza TFDA kwa ajili ya kanda ya Kati - Dodoma.

v. Kununua mitambo na vifaa mbalimbali vyamaabara ya Wakala wa Mkemia Mkuu waSerikali ambapo jumla ya shilingi bilioni 10zimetengwa.

vi. Kukamilisha ujenzi wa Maabara ya MkemiaMkuu na Ofisi ya Kanda ya Kaskazini - Arusha,

vii. Kukarabati maabara ya Vinasaba vyaBinadamu ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopoDar es Salaam

viii. Kuboresha utafiti na uzalishaji wa dawa za asilikatika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwaya Binadamu (NIMR) kwa kununua mashine zakisasa kwa ajili ya kiwanda cha kuzalisha dawaza asili Mabibo. Jumla ya shilingi milioni 800zimetengwa.

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

Taasisi za Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii

215. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizarakupitia Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru itaendeleakuongeza udahili wa wanafunzi katika fani mbalimbali.Aidha, Wizara itaboresha miundombinu ya vyuo; na mazingiraya kujifunzia na kufundishia. Vilevile, itaimarisha ubora wawataalam wa maendeleo ya jamii wanaozalishwa na Taasisikwa kuandaa mitaala ya NTA level 4 & 9 itakayozingatia halihalisi ya mabadiliko na mahitaji ya jamii.

Aidha, Wizara itaendelea kuratibu utoaji wa mafunzo yamaendeleo ya jamii kupitia Vyuo (8) vya Maendeleo ya Jamiipamoja na kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.Lengo ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga namafunzo katika vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na kudurusuMtaala wa Mafunzo kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ilikuendana na mahitaji ya soko la ajira na kuwawezeshawahitimu kujiajiri.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii

216. Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha tunakua nawataalam wa Ustawi wa Jamii katika ngazi za Mamlaka zaSerikali za Mitaa, Wizara kupitia Taasisi ya Ustawi wa Jamiiimeendelea kuzalisha wataalam hao kupitia mafunzo katikafani za Ustawi wa Jamii na fani nyingine ikiwemo RasilimaliWatu na Mahusiano Kazini kwa ngazi ya Astashahada,Stashahada, Shahada, Stashahada ya Uzamili na Shahadaya Uzamili. Katika mwaka 2017/18, Taasisi itaendeleakuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika fanimbalimbali, kuboresha miundombinu ya kufundishia nakujifunzia na kuanzisha kituo cha utafiti na ubunifu katikafani ya ustawi wa jamii ili kuongeza ufanisi katika kufundisha.Aidha, Taasisi inatarajia kukamilisha mchakato wa kuanzishashahada ya uzamili katika fani ya rasilimali watu na shahadaya maendeleo ya jamii.

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

MABARAZA YA KITAALUMA

217. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutambuaumuhimu wa taaluma mbalimbali zilizomo katika sekta yaafya; kwa kuzingatia hilo, Serikali itasimamia sheriambalimbali za wanataaluma wa taaluma hizo. Aidha, Wizaraitaendelea kusimamia utoaji wa huduma kupitia hospitalina maabara binafsi nchini.

USHIRIKIANO WA NDANI NA NJE YA NCHI

218. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kushirikiana nanchi rafiki katika kuimarisha Sekta ya Afya nchini. Aidha, Wizarailiratibu na kushiriki kwenye mikutano ya jumuiya za kikandaza SADC, EAC, ECSA-HC na mashirika mengine ya kitaifa nakimataifa na katika kutekeleza maamuzi ya pamoja yenyemanufaa kwa taifa. Katika mwaka 2017/18, Wizaraitaimarisha ushirikiano na nchi rafiki na Mashirika ya Kimataifayanayosaidia Wizara yangu. Aidha, itaimarisha ushirikiano nasekta nyingine ambazo zinachangia katika kutoa hudumaza afya na ustawi wa jamii nchini. Vilevile, Wizara kwakushirikiana na mikoa na wadau wa sekta itaendeleakuadhimisha siku mbalimbali za afya za kitaifa na kimataifakwa lengo la kuhamasisha na kufikisha ujumbe kwa umma.Baadhi ya siku hizo ni za Afya, Malaria Afrika, UKIMWI, KifuaKikuu, Ukoma, Wazee, Kutotumia Tumbaku, Tiba Asili yaMwafrika, Wachangia Damu, Utepe Mweupe, Siku yaWauguzi na Fimbo Nyeupe na Siku ya Mtoto Njiti duniani.

IV: SHUKRANI

219. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii yakipekee kuzishukuru nchi za Denmark (DANIDA), Uswisi (SDC),na Ireland (Irish Aid), Canada (DFATD) na Mashirika yaKimataifa yakiwemo Benki ya Dunia, UNICEF, na UNFPA kwakutoa misaada katika Mfuko wa Pamoja wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaoumesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afyanchini. Aidha, naishukuru na kuipongeza Korea Kusini kupitiashirika lake la Maendeleo (KOICA) kwa kuamua kujiunga na

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

nchi zinazochangia fedha katika Mfuko wa pamoja kwa ajiliya huduma za afya kuanzia mwaka 2016/17. Pia, napendakuzishukuru nchi za Canada, China, Cuba, Hispania, India,Italia, Japan, Marekani, Misri, Sweden, Uingereza, Ujerumanina Ufaransa na ambazo zimeendelea kuisaidia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa njiambalimbali.

220. Mheshimiwa Spika, vilevile nayashukuru mashirikamengine ya Kimataifa kwa ushirikiano wao waliotoa kwaWizara. Mashirika haya yanajumuisha Mfuko wa DuniaKupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (GFATM), Benkiya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Nchi za Kiarabu kwaajili ya Maendeleo ya Uchumi ya Nchi za Afrika (BADEA),Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU), Global Aliance on Vaccine(GAVI), Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Shirikala Umoja wa Mataifa la Kudhibiti UKIMWI (UNAIDS), Shirika laUmoja wa Kimataifa la Maendeleo (UNDP), UNFPA, UN-Women, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Benki ya Dunia (WB).Wengine ni Abbott Fund, BASIC NEED (UK), ACF – Canada,Baylor College of Medicine ya Marekani, Canadian BarAssociation, CDC, CORDAID (Netherlands), CUAMM, DANIDA,DFID, Engender Health (USA), EED, Elizabeth Glaser PaediatricAids Foundation (EGPAF), Family Health International (FHI360),FINIDA, GIZ, Good Samaritan Foundation (GSF), German TBand Leprosy Relief Association (GLRA), HelpAge International,ILO, Jane Adams School of Social Work ya Chuo Kikuu chaIllinois Marekani, John Snow Incorporation (JSI), JICA, KOICA,KfW,Global Partnership for Education (GPE), Madaktari Afrikana Madaktari Wasio na Mipaka (Medicins Sans Frontieres –MSF), MSERIOR, ORIO, P4H, SAREC, SDC, SIDA (Sweden), Shirikala Upasuaji la Spain, SIGN la Marekani, na Shirika la HumanResource Capacity Project, Touch Foundation, USAID na,Children Investment Foundation Fund (CIFF), World LungFoundation.

221. Mheshimiwa Spika, ninawashukuru pia Wadau waMaendeleo ambao ni African Programme for OrchorcerciasisControl, Africare, Axios International, Aids Relief Consortium,AIHA, ASCP, ASM, APHL, Balm and Gillead Foundation, Bill

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

and Melinda Gates Foundation, Clinton Health AccessInitiative, CLSI, CMB, Christoffel Blinden Mission (CBM), ChristianRelief Services (CRS), Citi Bank, Department of Defence yaMarekani, Community of Saint Egidio (DREAM), Duke University,ECSA, Futures Group, Glaxo Smith Kline (GSK), General Electric(GE – USA), Havard University na University of Maryland, HelenKeller International, Henry Jackson Foundation, IMA, ICAP,International Trachoma Initiative, Intrahealth, International EyeFoundation, I-TECH, Jhpiego, Johns Hopkins University,Labiofarm Industry, London School of Hygiene and TropicalMedicine, Management Science for Health (MSH), MEDA,Merck & Company, Malaria No More, Military Advancementfor Medical Research, NOVARTIS, Pathfinder, PATH, President’sEmergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), Pharm AccessInternational, PactWorld, Plan International, Pfizer, Qiagen,Research Triangle Institute (RTI), Regional Psychosocial SupportInitiatives (REPSSI), Saint Thomas Hospital- London, Save theChildren, SightSavers International, Supply Chain ManagementSystems (SCMS) na University of Columbia, URC, USA-Presidential Malaria Initiative (PMI), World Vision, FXB, WalterREED Army Institute of Research (WRAIR) na World EducationInc.

222. Mheshimiwa Spika, ninawashukuru watu binafsi,vyama vya hiari na mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani yanchi kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia uimarishajiwa huduma za afya. Mashirika hayo ni pamoja na AGOTA,Aga Khan Foundation, APHFTA, AMREF, AGPAHI, APT,BAKWATA, Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation,CCBRT, CSSC, CCT, Counsenuth, ELCT, Ifakara Health Institute,Lions Club, MAT, AFRICARE, Msalaba Mwekundu, MEHATA,MEWATA, MUKIKUTE, FAWETA, TAMWA, TAWLA, TGNP, MDH,MeLSAT, PASADA, PAT, PSI, PRINMAT, Rotary Club International,SIKIKA, Shree Hindu Mandal, TANNA, TPHA, TPRI, TanzaniaSurgical Assosciation (TSA), Tanzania Society of Anaethesiologistof Tanzania (SATA), Association of Gynaecologists andObstetricians of Tanzania (AGOTA), Association of Paedriciansof Tanzania (PAT),Tanzania Diabetic Association, TANESA, THPS,TUNAJALI, Tanzania Midwife Association, TDA, TAYOA, TISS, TEC,UMATI, USADEFU, White Ribbon Alliance, Mabaraza yote ya

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Kitaaluma, Mashirika, hospitali na vituo vya kutolea hudumaza afya na ustawi wa jamii nchini pamoja na vyama vyotevya kitaaluma vya sekta ya afya.

223. Mheshimiwa Spika, navishukuru Vyuo Vikuu vya Dares Salaam, Muhimbili, Sokoine, Ardhi, Mzumbe, Dodoma,Chuo Kikuu Huria, Kumbukumbu ya Hurbert Kairuki, IMTU,Tumaini, St. Agustino, CUHAS, Sebastian Kolowa, St. John, AgaKhan, Morogoro Muslim, Taasisi ya Teknolojia ya NelsonMandela, Arusha pamoja na Vyuo vyote vilivyo chini ya Wizaraya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwakuwa mstari wa mbele katika kuchangia uimarishaji wahuduma za afya na maendeleo ya jamii. Aidha, nawashukuruwadau wengine waliotoa huduma ya elimu kwa njia zaredio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii katikamasuala ya afya na maendeleo ya jamii.

224. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki cha utendajiwangu wa kazi nikiwa Waziri, nimepata ushirikiano mkubwakutoka kwa viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Napendakumshukuru Mheshimiwa Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla(Mb.), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa ushirikiano anaonipa katikakutekeleza majukumu yangu. Aidha naomba kuwashukuruDkt. Mpoki M. Ulisubisya Katibu Mkuu (Afya) na Bibi SihabaNkinga Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto) kwa mchango wao katika kuwezesha utekelezajiwa majukumu yangu. Vilevile, nawashukuru Prof.Muhammad Bakari Kambi, Mganga Mkuu wa SerikaliMakamishna, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Wizarayangu. Nawashukuru pia Wakurugenzi wa Hospitali ya TaifaMuhimbili, MOI, JKCI, ORCI, BMH, Mirembe, Kibongoto naWakurugenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda za Mbeya,Bugando, na KCMC na Taasisi zilizo chini ya Wizara, WagangaWakuu wa Mikoa na Wilaya, Waganga Wafawidhi waHospitali, Vituo vya Afya na Zahanati, Wakuu wa Taasisi,Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo vilivyo chini ya Wizara nawatumishi wote wa wizara, Mashirika ya Dini, Mashirika yaKujitolea na Mashirika Binafsi. Natoa shukrani kwa sekta zote

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

ambazo tunashirikiana nazo katika kutoa huduma za afyana ustawi wa jamii pamoja na wananchi wote kwaushirikiano wao. Kwa namna ya pekee napenda kuwashukuruwatumishi wote wa sekta ya afya, maendeleo na ustawi wajamii wakiwemo madaktari, wauguzi na wakunga kwakuendelea kutoa huduma kwa wananchi. Naombawaendelee kuzingatia misingi ya kutoa huduma bora, maadiliya kazi na kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya taifa letu

225. Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii pia kuishukurufamilia yangu, kwa uvumilivu wao na pia kwa kunitia moyokatika kutekeleza majukumu yangu ya Kitaifa. Kwa Viongozina Wananchi hasa wanawake wa Mkoa wa Tanganinawashukuru kwa ushirikiano wanaoendelea kunipatiakatika utekelezaji wa majukumu yangu. Naahidi kuwanitaendelea kuwaenzi na kuwatumikia kwa nguvu zanguzote ili kuleta mabadiliko ya haraka ya kimaendeleo katikaMkoa wetu.

V: MAOMBI YA FEDHA KWA KAZI ZILIZOPANGWAKUTEKELEZWA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2017/18

Fungu 52 – Afya

Mapato

226. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Wizaraimekadiria kukusanya mapato ya Shilingi 225,038,495,525.00Kati ya fedha hizo Shilingi 207,472,729,612.00 zitakusanywakatika mashirika na Taasisi zilizo chini ya Wizara na Shilingi17,565,765,913.00 ni kutoka katika vyanzo vya makao makuu.Vyanzo hivyo vinatokana na makusanyo ya uchangiaji wahuduma za afya, tozo na ada mbalimbali, usajili wa vituobinafsi vya kutolea huduma, maabara binafsi na Mabarazaya Kitaaluma.

Matumizi ya Kawaida

227. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizarainakadiria kutumia kiasi cha Shilingi 291,895,940,000.00 kwa

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi64,063,937,000.00 zitatumika kwa ajili ya Matumizi Mengineyona Shilingi 227,832,003,000.00 zitatumika kwa ajili ya Mishaharaya Watumishi. Kati ya fedha zilizotengwa kwa ajili yaMishahara Shilingi 49,036,786,000.00 ni kwa ajili ya watumishiwa Wizara, Makao Makuu na Shilingi 178,795,217,000.00 nikwa ajili ya watumishi wa Taasisi, Mashirika na Wakala zilizochini ya Wizara.

Miradi ya Maendeleo

228. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Wizarainakadiria kutumia Shilingi 785,805,952,000.00 kwa ajili yaMiradi ya Maendeleo. Kati ya hizo, fedha za ndani ni Shilingi336,300,000,000.00 na fedha za nje ni Shilingi449,505,952,278.00. Jumla ya Makadirio ya Bajeti kwa 2017/18kwa Fungu 52 ni Shilingi

Fungu 53 – Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

229. Mheshimiwa Spika, Makadirio ya Makusanyo yaMaduhuli na Matumizi kwa Mwaka 2017/18 kwa Fungu – 53ni kama ifuatavyo:

Makusanyo ya Maduhuli

Wizara inataraji kukusanya Maduhuli yenye jumla ya Shilingi2,101,874,000.00 ambazo ni kutokana na ada za wanafunzikutoka Vyuo 8 vya Maendeleo ya Jamii, ada za MashirikaYasiyo ya Kiserikali na mauzo ya vitabu vya zabuni.

Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo

Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa mwaka 2017/18, niShilingi 35,300,602,090.00 ambapo Mishahara ni Shilingi19,142,252,240.00 na Shilingi 16,158,349,850.00 ni MatumiziMengineyo. Aidha, Miradi ya Maendeleo inakadiriwa kutumiakiasi cha Shilingi 2,606,278,000. Kati ya fedha hizo, Shilingi2,000,000,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 606,278,000 nifedha za nje.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Jumla ya Makadirio ya ya Bajeti kwa 2017/18 kwaFungu 53 ni Shilingi 37,906,880,090

230. Mheshimiwa Spika, Jumla ya fedha zotezinazoombwa ni shilingi 1,115,608,772,090.

231. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii inapatikana piakatika tovuti za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto www.moh.go.tz. na www.mcdgc.go.tz.

232. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja

MWENYEKITI: Tunaendelea na mtiririko wetu, namwitasasa Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo yaJamii Mheshimiwa Mheshimiwa Peter Serukamba. (Makofi)

MHE. PETER J. SERUKAMBA – MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9) yaKanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMaendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu yaWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwamwaka 2016/2017, pamoja na maoni ya Kamati kuhusumakadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwamwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda ninaomba hotuba yangu yote ingie kwenye Hansard kama ilivyo,hapa nimefanya summary kubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili, uchambuzikatika masuala mbalimbali. Katika maoni ushauri namapendekezo yaliyo tolewa na Kamati iliyopita yapo maoniyaliyoweza kutekelezwa kikamilifu, yanayoendeleakutekelezwa na Wizara na ambayo hayajatekelezwa. Katikaushauri tulioutoa Kamati inaipongeza Serikali na Wizara kwajitihada hizo na yale ambayo yanaendelea kutekelezwaKamati inaiomba Wizara iendelee kusimamia ili yatekelezwekama tulivyoshauri na yale ambayo hayajatekelezwa kwa

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

sababu ya kutopata fedha kutoka Serikalini Kamati inaiagizaWizara kufuatilia fedha hizo na kuyatekeleza mara moja kablaya mwaka 2016/2017 haujaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchambuzi wamapitio ya utekelezaji wa mpango wa bajeti wa mwaka2016/2017; Kamati ilifanya mapitio na mwenendo wamakusanyo maduhuli ya Wizara hii kwa mwaka 2016/2017,na kufanya ulinganisho wa makadirio wa maduhuli wamwaka 2017/2018 na kuona mwenendo wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2016/2017 Wizara ilikadiria kukusanya kiasi cha shilingi bilioni170 kutoka Fungu 52 - Idara Kuu ya Afya na kufikia mweziMachi, 2017 Wizara imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingibilioni 157 sawa na asilimia 75.5

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upatikanaji wa fedhakutoka Hazina kwa mwaka 2016/2017; upatikanaji wa fedhakatika Wizara haujawa wa kuridhisha kwani fedhazilizotolewa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 ilikuwa haijafikaasilimia 50. Katika Fungu 52 hadi kufika mwezi Machi, 2017 nikiasi cha shilingi bilioni 314.67 sawa na asilimia 40 kati ya shilingibilioni 796.11 kilichokuwa kimeidhinishwa na Bunge lakoTukufu kilikuwa kimepatikana.

Mheshimwia Mwenyekiti, aidha, Fungu namba 53 hadikufika mwezi Machi, 2017 Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ilikuwa imepokea shilingi bilioni 16.23sawa na asilimia 39.57 kati ya shilingi 41,000,000,000kilichoidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Kamati inaonakwamba Serikali haijaamua kulipa kipaumbele suala la afya,kwanza kwa kutokutenga fedha za kutosha katika sekta hii,pili kutotoa fedha za utekelezaji wa shughuli zake kwa wakati.

Kamati inaona kwamba hata mafanikio yanayopataika katika Wizara hii, ni kutokana na uzalendomkubwa walionao Wizara, watendaji wakuu pamoja nawasaidizi wao katika kutafuta vyanzo vingine vya fedha nasi fedha za Serikali ambazo zimetengwa na bajeti yako.

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Mheshimiwa Mwenyekiti, aliyekuwa mpigania uhuruna baba wa taifa la India Mahatma Gandhi aliwahi kusema;“It is health that is real wealth and not pieces of gold andsilver.” Hivyo Serikali haina budi kuhakikisha afya zaWatanzania ndicho kipaumbele na ndio utajiri wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaisihi Serikali kuipakipaumbele cha pekee Wizara hii kwa kuhakikisha inatengafedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zikiwemoshughuli za kutoa huduma za kuzia magonjwa (preventionservices), matibabu (curative services), hata promotion service.Kwa kutekeleza haya hatuta lazimika kutenga fedha nyingikwa masuala ya dawa kwani magonjwa yatakayohitajidawa yatakuwa tayari ya mekwisha zuiliwa katika hudumaya kinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelezo kuhusu miradi yamaendeleo iliyokaguliwa ni kuwa mwaka 2016/2017 Fungu52 lilitengewa shilingi 518,000,000,000 kwa ajili ya kutekelezamiradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo shilingi 320,000,000sawa na asilimia 40.2 ni kutoka vyanzo vya ndani na kiasicha shilingi bilioni hizo ni vyanzo vya nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo ya ukaguzi wamiradi ni kuwa Kamati ilifanya ukaguzi wa miradi iliyotengewajumla ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya kununua mashinempya za kisasa za kutibia saratani. Gharama za mashine hizizilikuwa ni bilioni 9.5 ambapo katika mwaka wa fedha2015/2016 taasisi ilitengewa shilingi bilioni 4.5 ambazoimeshapokelewa.

Aidha, hadi kufikia siku Kamati inakagua mradi huu,Tasisi ilikuwa imeshapokea bilioni tano, sawa na asilimia 100,fedha il iyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Kamatiimejulishwa kuwa Taasisi imekamilisha kuandaa makabrashaya zabuni na mashine zinatarajiwa kufika mwezi Mei, 2017.

Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu,kwani utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwakatika Taasisi hii, wanaokwenda kupata matibabu ya

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

saratani. Kamati inasisitiza Taasisi chini ya usimamizi waWizara iharakishe mchakato wa manunuzi ya vifaa tiba hivyoili viweze kuanza kutoa huduma haraka kwa wagonjwa wasaratani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mradi wa ununuzi wamitambo ya vifaa tiba katika Taasisi ya Mifupa (MOI); Mradihuu ulitengewa kiasi cha shilingi bilioni 4.8 ambapo kati yafedha hizo shilingi bilioni 1.8 ni kwa ajili ya kulipa mkopo waNHIF na shilingi bilioni tatu ni kwa ajili ya ununuzi wa mitambona vifaa tiba. Hadi Kamati inatembelea MOI hakuna fedhailiyokuwa imetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwamba Taasisiya MOI ni Taasisi nyeti sana kutokana na utoaji wake wahuduma ya mifupa hususani kutokana na ongezeko kubwala wahitaji wa huduma ya mifupa katika Taasisi hiyo.Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa ajali hapanchini zikihusisha magari, pikipiki na vyombo vya motoambavyo hupelekea watu kuvunjika miguu ama mwisho wasiku huduma yake hupatikana katika Taasisi ya Moi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inasikitishwa sana nahali ya kutotolea kwa fedha kwani MOI ni moja ya Taasisimuhimu sana nchini na ndiyo Taasisi pekee inayotoa tiba yamifupa hapa nchini. Taasisi hii inatumia mapato yake yandani kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kutoa huduma kwaajili ya wananchi. Pia ikumbukwe kwamba kuna kundilinapewa msamaha katika gharama za matibabu, ikiwemowazee na watoto walio chini ya miaka mitano. Hawa wotewanategemea fedha za matibabu kutoka Serikalini ambazohaziletwi kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kuna mtotoaliyepata matibabu ya kunyooshwa mgongo wake kwasababu ulipinda. Mgonjwa huyu alipatiwa matibabu kwakuwekewa vifaa tiba 12 ambapo kila kimoja gharama yakeni dola 60 ambayo ni sawa sawa na 132,000, jumla ya vifaatu ni shilingi 1,584,000. Gharama hii ni vifaa tuu ambapo kwamujibu wa sera, mgonjwa huyu anatakiwa apewe matibabu

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

bila ya malipo yoyote. Sasa je ni wagonjwa wangapi wanamna hii wanaolipiwa na hawatalipiwa katika taasisi?Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha inapeleka fedha hizokatika Taasisi ya MOI kabla hatujamaliza bajeti ya mwakahuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vifaa tiba Muhimbili,mradi huu ulitengewa jumla ya shilingi 4,000,000,000. HadiKamati inatembelea kulikuwa hakuna fedha yoyoteiliyopokelewa kwa ajili ya kununua vifaa tiba kama ilivyokuwaimepangwa, hivyo kupelekea hospitali kushindwa kutekelezaununuzi wa vifaa tiba. Aidha, pamoja na kutopokea fedhahizo za maendeleo kutoka Serikalini bado hospitali hii ilihitajikuendelea kutoa huduma kwa wahitaji wagonjwa, hivyoilipelekea hospitali kutumia fedha zake za ndani, fedhakutoka kwa wahisani pamoja na mikopo kutoka NHIF zaidiya shilingi bilioni 7.8 yenye riba nafuu ili kuendesha shughuliza hospitali ikiwemo ukarabati wa wodi na vyumba vyaupasuaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inasikitishwa na halihii kwani Hospitali ya Taifa ya Muhimbilli ni hospitali kongwenchini na ndiyo hospitali inayotegemewa na Taifa.Wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali nchini wamekuwawakipelekwa kupata rufaa Muhimbili ili kupata huduma naidadi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfanomwaka 2015 wagonjwa 191,241 walihudumiwa Muhimbili,mwaka 2016 wagonjwa 238,000 walihudumiwa, sawa naongezeko la asilimia 20. Ongezeko hili la wagonjwawakiwemo wagonjwa wanaopata huduma bila malipo kwamujibu wa sera wa kiwemo Watoto chini ya umri wa miakamitano na Wazee lilihitaji uwepo wa rasilimali fedha zakutosha ili kuweza kuwa hudumia. Serikali lazima iamue kutoakipaumbele kwenye huduma za afya ili kulinda wananchiwake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mradi wa ununuzi wamitambo katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa (NIMRI); katikamajadiliano na uchambuzi wa bajeti ya mwaka 2016/2017Kamati ilikubaliana na Kamati ya Bajeti pamoja na Wizara

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

kwamba ifanye uhamisho wa fedha kutoka katika vifunguvingine, Fungu namba 52 (Re-allocation) ili iweza kuipatiaTaasisi ya utafiti ya magonjwa ya binadamu (NIMRI) kiasi chashilingi 800,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo. Hadisiku Kamati inakwenda kufanya ukaguzi wa maendeleo wamiradi hiyo hakuna fedha yoyote iliyokuwa imepelekwa kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo. Kamati inaishauri Serikaliihakikishe inapeleka fedha shilingi 800,000,000 kwa ajili yautekelezaji wa mradi huu ili Taasisi ianze utekelezaji wa dawaza asilia kabla mwaka huu haujaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa mpango wamakadirio 2017/2018; pamoja na malengo mengi ambayoWizara kupitia Fungu 52 na 53 imeyapanga malengo hayayanaonekana kuwa yana tija katika suala zima la uboreshajiwa sekta za afya kwa kuzingatia mipango mikakatimbalimbali pamoja na makubaliano ya kitaifa na kimataifayenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018 Wizara hii yenye mafungu mawili inatarajiakukusanya maduhuli yake kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Fungu 52inatarajia kukusanya shilingi bilioni 245.038 ikiwa ni ongezekola shilingi 87,000,000,000 sawa na asilimia 35 ya kiasi cha shilingi157,000,000,000 zilizokadiliwa kwa mwaka 2016/2017.Ongezeko hii ni kutokana na uimarishaji wa mifumo yaukusanyaji wa mapato yatokanayo na utoaji wa huduma zaafya katika vituo vyote vya kutolea huduma. Katika Fungu52 Wizara inakadiria kukusanya shilingi 2,000,000,000 ikiwa nipungufu ya shilingi 280,000,000, sawa na asilimia 11.8 kiasi chashilingi bilioni 2.3 kilichotakiwa kwa mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa fedha 2017/2018Wizara kupitia Fungu 52 imepanga kutumia shil ingi1,078,754,221,478 ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu yaWizara. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 291.9 sawa ya asilimia27 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikiwa ni pamoja namishahara na watumishi. Aidha, shilingi bilioni 786.8, sawa

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

na asilimia 73 kinachoombwa ni kwa ajili ya miradi yamaendeleo, na hapa tunawapongeza sana Wizara kwakutenga fedha nyingi kwa ajili ya fedha za maendeleo.

Kwa upande wa Fungu 53 Wizara imepanga kutumiashilingi 40,000,000,000, kati ya fedha hizo shilingi 4,000,000,000sawa na asilimia 12 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo,35,000,000,000 sawa na asilimia 88 ni kwa ajili ya matumizi yakawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makadirio haya ya matumiziya fedha yanaonyesha kuongezeka kwa asilimia 25.9 hasakwa Fungu 52 kwa mwaka 2017/2018 ikilinganishwa namakadirio ya matumizi ya mwaka 2017/2018. Pamoja nakuongezewa fedha, Kamati inajiuliza je, bajeti ya mwakawa fedha unaoisha iliyopokelewa mpaka sasa sawa naasilimia 50 je, asilimia hizi 73 zitaweza kupatikana kwa ajili yamwaka kesho?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya tatu ya taarifainahusu maoni, ushauri na mapendekezo ya Kamati. Mwaka2016/2017 Wizara ilitengewa kiasi cha shilingi 796,000,000,000kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake. Hata hivyo hadikufika mwezi Machi Wizara ilipokea kiasi cha shilingi314,000,000,000, sawa na asilimia 40 tu ya fedha ambazozilitakiwa kupokelewa na Wizara hii. Kamati inahoji ni lini sasaSerikali itatekeleza haya ambayo yalitakiwa yatekelezwa kwamwaka 2016/2017 kwani sasa tunaelekea mwaka mwinginewa fedha, ni vyema sasa Serikali ikajipanga na kuhakikishabajeti yote iliyoidhinishwa na Bunge inatolewa yote kwawakati ili Wizara iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya afya; katika bajetiya mwaka 2017/2018 iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji washughuli za Fungu 52 na 53 inaonekana kuongezeka kwaasilimia karibia 30. Hata hivyo bajeti hii bado haijafanikiwakufika asilimia 100 ya bajeti nzima ambayo imetengewa kwaasilimia 10 ya bajeti nzima ambayo imetengwa kwa ajili yautekelezaji wa shughuli za Wizara ya Afya. Bajeti ya mwakaya Wizara hii ni sawa na asilimia 3.5 tu ya bajeti ya Serikali ya

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

trilioni 31.9. Bajeti hii ni ndogo kwani bado hatujatekelezamakubalino ya Mkutano wa Azimio la Abuja (Abujadeclaration) ya mwaka 2001 ya kwamba nchi zipangeasilimia 15 ya Bajeti kwenye sekta ya afya. Kamati inaonaimefika wakati sasa Serikali ikaamua kwa dhati kulipakipaumbele suala afya na kutenga Bajeti ya kutosha, angalaukufika asilimia 10 ya Bajeti Kuu ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Bima ya Afya kwaMtanzania; katika kutekeleza ahadi kwa wananchi ni lazimakuangalia suala la afya katika mapana yake, hasa kwakuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na uhakika wakupata huduma za afya wakati wowote mahali popoteinapohitajika. Kutokana na hali hii, Kamati inatoa ushaurikwamba Serikali ilipe kipaumbele cha pekee suala zima labima ya afya kwa Watanzania ili ijiwekee malengo ambayoyanaambatana na mpango kazi wa kutekeleza azma hiyokwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupungua kwa fedha kutokakwa wahisani - Bajeti ya Wizara ya Afya imekuwa ikitegemeasana fedha kutoka kwa wahisani. Madhalani mwaka wafedha 2017/2018 Wizara ilitegema fedha kutoka kwa wahisanizaidi ya asilimia 59.8 ya Bajeti nzima ya maendeleo ambapohadi kufika mwezi Machi ni asilimia sita tu ya fedhailiyotengwa na wahisani ilikuwa imetolewa kwa ajili yashughuli hiyo. Pamoja na kutopatikana kwa fedha hizokutoka kwa wahisani bado Wizara imeendelea kutengaasilimia 94 ya bajeti ya maendeleo kwa mwaka wa fedha2017/2018 kwa kutegemea kwa wahisani, ambao ni sawana asilimia 57.2 ya bajeti nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imerejea baadhi yamiradi ya maendeleo ambayo inategemea wafadhili kutokanje kwa asilimia 100. Miradi hiyo ya maendeleo ni pamojaUdhibiti wa Virusi vya UKIMWI (HIV/Aids Control Programme)pamoja na Mradi wa Udhibiti wa Kifua Kikuu. Kwenye miradihii hakuna hata shilingi moja ya fedha za ndani zilizotengwakwa ajili ya usimamizi wa utekelezaji wa magonjwa haya.Kamati inajiuliza, je, magonjwa haya ni kipaumbele katika

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

kupambana nayo hapa nchini? Au je, Serikali imeamua kutoareheni ya afya za wananchi katika magonjwa haya ambayondiyo kati ya magonjwa yanayowasumbua wananchi waTanzania bila kujali umri, dini, cheo, itikadi wala siasa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaishauri Serikalikutenga fedha katika masuala haya pamoja na miradimingine ya maendeleo ili iache kutegemea fedha zawahisani na wafadhili wa nje kwa ajili ya kuokoa maisha yaWatanzania kama wafadhili hawataleta fedha hizo kwamwaka 2016/2017 basi tuwe na miradi endelevu katika Wizarahii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa vifaa tiba navilainishi; utoaji wa huduma bora nchini ni pamoja na uwepowa vitendea kazi katika vituo vya huduma za afya.Kumekuwa na malalamiko ya upungufu wa dawavitendanishi, vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma zaafya. Kamati inaishauri Serikali kutenga bajeti ya kutoshaitakayotosha kununua vifaa hivi na kuvisambaza katika vituovyote vya kutolea huduma hapa Nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jamii kumekuwa namakundi mbalimbali ambayo yapo katika mazingiramagumu likiwemo kundi la watoto yatima ambalo linatokanana sababu mbalimbali ikiwemo vifo vitokanavyo na ugonjwawa UKIMWI.

Katika kuhakikisha kwamba kundi hili linapatahuduma za afya kama walivyo watoto wengine, Kamatiinaishauri Serikali kuhakikisha leseni zinapatikana kwa urahisiili hawa wanaojitolea kutoa huduma hizi za watoto yatimawasikate tamaa, kwani juhudi hizi zote ni kwa ajili ya kuisaidiaSerikali pale ambapo inaonekana imeelemewa na jukumula kutunza watoto hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kutenga fungu kwaajili ya msamaha wa matibabu, nchi yetu imetengeneza seranzuri sana, sera ya mwaka 2007 ambapo katika sera hiyoimeanishwa bayana makundi ambayo yamepewa

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

msamaha wa gharama ya matibabu, likiwemo kundi lawatoto wa umri wa miaka tano, wajawazito pamoja nawazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera hii imegeuka kuwachangamoto kwa taasisi zinazotoa huduma za afya kwamakundi haya na kupelekea kuwa kero kwa makundi hayona hata kwa taasisi husika inayotoa huduma kwa kuwa nauhaba wa rasilimali fedha kwa ajili ya kununua dawa pamojana vifaa tiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilitembelea Hospitaliya Taifa ya Muhimbili na kupewa taarifa kwamba, kipindi chakuanzia Julai hadi Desemba 2015 zaidi ya shilingi bilioni 1.6ilitoka kwa ajili ya watoto hawa ambao ni kwa ajili yamsamaha. Mwaka wa fedha 2016/2017 Taasisi ya Mifupa -MOI ilitoa huduma kwenye zaidi ya Mikoa 18 Tanzania Barana Zanzibar kwa watoto 2,200 na kati ya watoto hao wenyevichwa vikubwa walipata huduma ya upasuaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaishauri Serikalikutenga fedha maalum (separate vote) ambayo ni kwa ajiliya kutoa huduma bora ya afya kwa ajili ya msamaha wagharama za matibabu ili kuweza kuwa na gharama endelefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bajeti ya Taasisi ya JakayaKikwete. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa ikitoahuduma ya matibabu ya moyo kwa Watanzania. Taasisi hiiimetoa huduma kwa mazingira magumu sana. Kamatiinashangazwa na kitendo cha taasisi inayookoa fedha nyingikwa kutopeleka wagonjwa nje lakini bado fedhazinazoombwa hazipelekwi katika Taasisi hiyo. Kamatiinaishauri bajeti ya JKCI itolewe yote na kwa wakati ili iwezekusaidia kuoko fedha nyingi ambazo zingetumika kupelekawagonjwa kwenye matibabu nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ripoti ya ukaguzi waBenki ya Wanawake, Kamati inaishauri Serikali kupitia MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali kuifanyia ukaguzi wa kimahesabubenki hii ili kubaini kiasi cha mtaji wake, nini kikwazo cha

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

benki hiyo kutokuwa kama benki nyingine, na kuna namnagani inaweza kuibuliwa kwa kukuzwa ili kuweza kushindanana benki nyingine kwa ajili ya kuwasaidia wanawakeWakitanzania lakini pamoja na wanaume kwa ajili yakujiinua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utoaji wa zabuni zautoaji huduma katika Taasisi ya Afya Muhimbili. Utoaji wahuduma ya afya katika taasisi kubwa kama vile Muhimbiliimekuwa ni changamoto kubwa kutokana na uhaba wavifaa, vifaa tiba, dawa na vitendanishi kama nilivyoelezahapo awali. Aidha, upungufu huo unapelekea kuwa namsongamano mkubwa katika sehemu ya vipimo vyawagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamotohiyo ya ugumu wa upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya vipimona dawa; kutokana na taasisi kukosa fedha za kununuliavifaa na dawa, Kamati inaishauri Serikali kuruhusu hudumahizo za vipimo na dawa zitolewe na mzabuni wa nje (TaasisiService Outsourcing) ambaye ataweza kuwekeza katikamaeneo hayo; ambapo mbia huyo ataleta vifaa vyake kwaajili ya upimaji wa wagonjwa mbalimbali lakini pia utoajiwa dawa kwa wagonjwa katika taasisi husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inashauri hivyo kwakuwa kuna faida kubwa katika kutekeleza hayo. Kwanzaitapungumza mzigo mkubwa wa Serikali na Taasisi hiyo katikasuala zima la ukarabati (maintenance) wa vifaa hivyo,itapunguza shughuli ya uagizaji wa dawa katika Taasisi hiyo,pia hata teknolojia ya vifaa itabadilika kwa kuwa jukumu lamzabuni huyo litakuwa ni hubadilisha na kwamba jukumuhalitakuwa la Serikali tena kama ilivyo sasa. Hii itaifanya nchiyetu kuendana na mabadiliko ya teknolojia yanayoendeleakatika ulimwengu wa suala zima la afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la kutopelekwakwa fedha zil izotengwa kwa mradi wa maendeleo,tunaomba sana Serikali fedha hizo zinazotengwa zamaendeleo ziweze kwenda kwa wakati. Vyuo vya Maendeleo

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

ya Jamii vipelekwe Wizara ya Elimu, Kamati inashauri vyuohivyo vyote vilivyo chini ya Fungu namba 53 vihamishiwe nakupelekwa chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojiakama ilivyo vyuo vikuu vingine hapa nchini. Kwa kufanyahivyo, kutasaidia kufuatilia ubora wa elimu itolewayo na vyuohivyo vya maendeleo ya jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Bohari Kuu ya Dawa,Kamati inashauri Bohari hiyo kufanyiwa ukaguzi wa kina kwaajil i ya kubaini, mafanikio (strength), changamoto(challenges) na mahitaji (demands) ili kuweze kubaini namnaya kuboresha usambazaji wa dawa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mabadiliko ya Sheriaya Ndoa na ndoa za utotoni, Kamati inaishauri Serikalipamoja na ugumu unaojaribu kuwekwa na taasisi za kidini,na mila na desturi za mahali husika, Kamati inaamini Serikaliina mamlaka juu ya kulinda haki na ustawi wa jamii zetu,hasa kulinda haki za watoto hapa nchini. Serikali ilinde hakiza watoto hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuongeza idadi yamakundi maalum; makundi maalum yanajumuisha watuwanaojidunga dawa za kulevya, wanaofanya biashara yangono, wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (men who sexwith the men; the women who sex with the women; and transgender). Makundi haya yamekuwa yakiongezeka siku hadisiku katika jamii yetu. Imekuwa ni tishio kubwa hasa katikasuala zima la ongezeko la virusi vya UKIMWI.

Ongezeko la kundi hili ni kutokana na mabadiliko yajamii yetu ikiwemo suala zima la malezi katika ngazi zafamilia, shuleni na katika jamii kwa ujumla. Matendo hayayamekuwa yakifanyika majumbani mwetu, shuleni kutwa,hata mabwenini kwetu. Kamati inaishauri Serikali kuhakikishakwamba inaajiri Maafisa Maendeleo ya Jamii, katika kila kata,ambao watasaidia kutekeleza mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vifo vya akina mama,Kamati inaishauri Serikali kuwanusuru akina mama hawa

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

katika matatizo ya uzazi na kuwatengea na kutoa fedha zakutosha katika bajeti yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma za Bima yaAfya (NHIF); Kamati inaishauri Serikali kuupa muda Mfuko waBima ya Afya ya Taifa kujiandaa vyema ili uweze kutoahuduma bora kwa wateja wake ili hata mashirika hayoyajiunge nayo, tofauti ya upatikanaji wa hudumawalizokuwa wanapata kabla ya kujiunga katika mifukomingine ya bima ya afya. Kwa kufanya hivyo kutaondoamalalamiko, pia kuwapa uwezo kuendana na soko la utoajiwa huduma za afya kama mifuko mingine inavyotoahuduma za afya hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa vituo vyaafya; Kamati inaishauri Serikali kwa ujumla wake kuhakikishavituo vya afya vinajengwa vya kutosha ili kusaidia kutoahuduma za afya hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la TFDA Kamatiinaishauri Serikali iziangalie Sheria zinazounda taasisi hiziambazo zinaainisha majukumu hayo pale kwenye tatizolinapotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vikwazo katikamsaada kwa wahisani, Kamati inaishauri Serikali kupitia TFDAifanye jukumu lake bila kutoza kiasi chochote kwa Wizarakwani hilo ndilo jukumu ambalo limepangiwa katika vajetiya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu magonjwayatokanayo na kukosekana kwa matumizi bora ya vyoo namaji na salama; Kamati inashauri Serikali ihimize ujengaji wavyoo nchini pamoja na kuhakikisha kwamba Wizara ya Afyainatoa maji katika vyoo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho; ninakushukuruwewe binafsi kwa kunipa muda kuwasilisha taarifa hii mbeleya Bunge lako Tukufu. Pia napenda kumshukuru sanaMheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu(Mbunge) pamoja na Naibu Waziri Mheshimiwa Dkt. HamisiKigwangalla kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoendeleakuutoa kwa Kamati wakati wote wa shughuli za Kamati hasaKamati ilipokuwa ikijadili makadirio ya mapato na matumiziya Wizara hii kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Vilevile napenda kuwashukuru Makatibu Wakuu waWizara, Idara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsiana Watoto, Wazee pamoja na Maafisa Waandamizi wao,Wizara na Taasisi zote kwa ushirikiano wanaotoa katikaKamati yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchukuwa nafasihii kuwashukuru wadau wetu wote wa sekta ya afya kwakazi nzuri wanayoifanya, kwa ushirikiano wao mkubwawanaoutoa kwa Serikali yetu katika kuendelea kutoa hudumabora za afya hapa nchini. Naomba kuwataja baadhi nawachache tu ambao wanatoa huduma hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni TGNP, Tanzania WomenLawyers (TAWLA), Shirika la Utepe Mwekundu, Tanzania HealthPromotion (HDT), Tanzania Water and Sanitation Network naMashirika mengine Yasiyo ya Kiserikali kwa juhudiwanazoendelea kufanya hapa Nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nafasi ya pekee kabisanaomba niwashukuru wajumbe wa Kamati ya Huduma naMaendeleo ya Jamii kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kujadilina kuchambua makadirio na mapato ya matumizi ya Wizarahii kwa mwaka 2017/2018. Pamoja na ufinyu wa mudawalikuwa tayari kutekeleza jukumu hili kubwa na hatimayekukamilisha uchambuzi wa bajeti hii kwa weledi mkubwana kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwashukuru kwadhati watumishi wa Ofisi ya Bunge wakiongozwa na Dkt.Thomas Kashililah Katibu wa Bunge, Ndugu Athumani HusseinMkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge na Dickson BisileMkurugenzi Msaidizi kwa kuiwezesha Kamati kufanya kazi zao

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

vizuri. Kipekee kabisa naomba niwashukuru Ndugu PamelaPallangyo na Ndugu Agnes Nkwela Makatibu wa Kamatiyangu na ndugu Gaitana Chima kwa msaada wao mkubwakatika Kamati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, sasanaomba Bunge lako Tukufu likubali na kuidhinisha makadirioya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na Maendeleo yaJamii, Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zake kwa mwaka2017/2018 kama yalivyowasilishwa na mtoa hoja. Fungu 52jumla ya shilingi 1,078,344,282,000; Fungu 53 jumla ya shilingibilioni 40,130,215,784.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha naninaunga mkono hoja hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana MheshimiwaMwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaHuduma na Maendeleo ya Jamii kwa taarifa uliyowasilishakwa niaba ya Kamati yako, tunakushukuru sana. (Makofi)

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NAMAENDELEO YA JAMII KUHUSU UTEKELEZAJI WA WIZARA YAAFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 PAMOJA NA MAONI YAKAMATI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAWIZARA HIYO KWAMWAKA WA FEDHA 2017/2018 – KAMA

ILIVYOWASILISHWA MEZANI___________

SEHEMU YA KWANZA____________

MAJUKUMU YA KAMATI NA MUUNDO WA TAARIFA

1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji waMajukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha2016/2017, pamojana Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara hiyo kwaMwaka wa Fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa Kanuni ya 6(5)(a) na 7(1)ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleola Januari, 2016, Kamati hii ina jukumu la kusimamiautekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Bajeti ya Wizara hii. Aidha,kwa mujibu wa Kanuni ya 7(1) ya Nyongeza ya Nane ya Kanunihizo, Kamati hii inao wajibu pia wa kushughulikia Bajeti yakila Mwaka ya Wizara hii.

Vile vile, Kanuni ya 98 (1) ya Kanuni za Bunge, imeweka shartila Kamati za Kisekta, ikiwemo Kamati hii, kufanya Ukaguziwa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyopo chini yausimamizi wa Kamati hii ambazo ni tatu (3) ikiwemo Wizarahii.

Naomba kutoa Taarifa kuwa Kamati ilifanya Ukaguzi waMiradi ya Maendeleo iliyotengewa Fedha chini ya Wizara hiikwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na kufanya Uchambuzi waMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 ambayo ni Fungu 52- Idara Kuu ya Afyana Fungu 53- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazeena Watoto.

Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo hayo, naomba kutoataarifa hii ambayo inafafanua mambo manne (4) yafuatayo:-

i. Hali halisi katika Utekelezaji wa Mapendekezoya Kamati kwa Mwaka unaoisha;

ii. Mapitio ya Taarifa ya Utekelezaji wa Mpangowa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017na Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

iii. Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha2017/2018; na

iv. Maoni na Ushauri wa Kamati kuhusu Makadirioya Mapato na Matumizi kwa Mwaka waFedha 2017/2018

SEHEMU YA PILI____________

2.0 UCHAMBUZI WA KAMATI KATIKA MASUALA MBALIMBALI2.1 Utekelezaji wa Ushauri wa Kamati

Mheshimiwa Spika, Katika kufanya Uchambuzi wa Taarifa yaUtekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017, Kamatiilifanya Mapitio ya Maoni na Mapendekezo yaliyotolewawakati wa kupitisha Bajeti ya Mwaka 2016/2017. Jumla yaMapendekezo Ishirini na mbili (22) yalitolewa.

Mheshimiwa Spika, Katika Maoni, Ushauri na Mapendekezoyaliyotolewa na Kamati iliyopita, yapo maoni yaliyowezakutekelezwa kikamilifu, yanayoendelea kutekelezwa naambayo hayajatekelezwa kabisa na Wizara. Katika ushauriuliotekelezwa, Kamati inaipongeza Serikali naWizara kwajitihada hizo na yale ambayo yanaendelea kutekelezwaKamati inaiomba Wizara kuendelea kusimamia il iyatekelezwe kama il ivyoshauriwa. Na yale ambayohayajatekelezwa kwa sababu ya kutopata Fedha tokaSerikalini Kamati inaiagiza Wizara kufuatilia Fedha hizo nakuyatekeleza mara moja kabla ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 haujamalizika.(Rejea Kiambatisho Namba 1).

3.0 UCHAMBUZI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGOWA BAJETI NA UZINGATIAJI WA MAONI YA KAMATI KWAMWAKA WA FEDHA 2016/2017.

3.1 Uchambuzi wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mpangowa Bajeti kwa MwakawaFedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya Uchambuzi wa Utekelezajiwa Mpango wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 kadiri

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

zilivyokuwa zimepangwa katika kutekeleza majukumu yake.Kamati ilijikita katika kufanya Uchambuzi wa Makusanyo yaMaduhuli kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 katika kikaokilichofanyika tarehe 31 Machi na 1 Aprili 2017 kwa kufanyamapitio katika taarifa za utekelezaji zilizowasilishwa naWizara mbele ya Kamati wakati wa kujadili taarifa zautekelezaji pamoja na taarifa zilizowasilishwa wakati wavikao vya Kamati katika kutekeleza shughuli za Kamati kwaMwaka wa Fedha wa 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya mapitio ya mwenendowa Makusanyo ya Maduhuli ya Wizara hii kwa Mwaka waFedha 2016/2017 na kufanya ulinganisho wa Makadirio yaMaduhuli kwa Mwaka wa Fedha unaofuata wa 2017/2018 ilikuona mwenendo wake.

3.1.1 Uchambuzi wa Taarifa kuhusu Ukusanyaji waMaduhuli

Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedhawa 2016/2017,Wizara il ikadiria kukusanya kiasi cha shil ingi Bilioni170.01kutoka Fungu 52 (Idara Kuu Afya), hadi kufikia mweziMachi 2017 Wizara imefanikiwa kukusanya kiasi chashilingiBilioni 157.801 sawa na asilimia 75.48.

Mheshimiwa Spika,kwa upande wa Fungu 53- Idara Kuu yaMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ilikadiriwakukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 2.38, hadi kufikia mweziMachi 2017 Idara hii imekusanya kiasi cha shilingi Milioni 930.28sawa na asilimia 39.04 ya lengo.

Mheshimiwa Spika,hadi Kamati inakutana na Wizara hakunahata Fungu moja ambalo limekamilisha ukusanyaji waMaduhuli kwa asilimia 100.Kamati inaamini kwamba kwamuda uliobaki Idara Kuu Afya (Fungu 52) itaweza kukamilishaMakadirio ya Makusanyo yao kadiri ilivyojiwekea malengoyake, kwani hadi kufikia mwezi Machi 2017 Idara Kuu hiiilifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 75.

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Aidha, kwa upande wa Fungu 53 Idara Kuu Maendeleo yaJamiimpaka wakati Kamati inapokea taarifa ya Utekelezajiwa Bajeti ya Mwaka 2016/2017, makusanyo hayajafika hatanusu ya lengo kwa maana ya asilimia 50. Hali hii imepelekeakupunguza makadirio ya makusanyo ya mapato kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 kwa asilimia 13 kwa sababu zilezilezilizoainishwa mwaka uliopita kwa maana ya kupungua kwamakusanyo ya ada kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vyaokama chanzo kikuu cha makusanyo ya mapato yake. Kamatiinaitaka Wizara kuangalia tena Idara Kuu hii ili kuwezakubuni vyanzo vingine vya mapato yake na kuwezakugundua sababu zinazoipelekea Idara kuporomoka kwakiwango cha Makadirio ya Mapato yake kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, Idara Kuu Afya inaendelea kufanya vizurikatika Makusanyo yake kwa kuweza kutekeleza Makadirioya Makusanyo ya Mapato yake na kuweza kuongezaMakadirio ya makusanyo kila mwaka na Kamati inatambuajuhudi hizo kubwa. Kamati inaipongeza Wizara na Idara KuuAfya kwa ufanisi huo mkubwa na kuiomba Wizara kutumiambinu hizo katika Idara Kuu Maendeleo ya Jamii ili nayoiweze kupiga hatua mbele kutoka pale ilipo na kuwezakufanya Makusanyo makubwa zaidi kwa Mwaka wa Fedha2017/2018 na hata miaka mingine ijayo.

3.1.2 Upatikanaji wa Fedha kutoka Hazina kwa Mwaka waFedha 2016/2017Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa shughuli za Wizara katikakuboresha Afya na Ustawishaji wa Jamii nzima ya Watanzaniaunategemea upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini kwa

Kielelezo Na. 1: Ukusanyaji wa Maduhuli kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Mwaka wa

2016/2017 Fedha Mwaka wa

2017/2018 Fedha

Fungu Makadirio Makusanyo % Makadirio % Tofauti

52 Bilioni 170.011 Bilioni 157.801 75.48 Bilioni 245.038 +36 53 Bilioni 2.382 Milioni

930.281 39.04 Bilioni 2.101 -13

Chanzo: Taarifa ya Wizara kuhusu utekeleaji wa Majukumu kwa Mwaka 2016/2017

 

 

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

asilimia 100. Kamati ilifanya Uchambuzi wa Taarifa zaUtekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 kwamafungu yote mawili (52 & 53) kabla ya kufanya Uchambuziwa Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, Upatikanaji wa fedha katika Wizarahaujawa wa kuridhisha kwani fedha zilizotolewa hadi kufikiamwezi Machi 2017 hazijafika hata asilimia 50. Katika Fungu52 hadi kufikia mwezi Machi 2017 ni kiasi cha shilingiBilioni314.67 sawa na asilimia 40 kati ya shilingi Bilioni796.11kilichokuwakimeidhinishwa na Bunge lako Tukufukilikuwa kimepatikana. Aidha, kuhusu Fungu 53, hadi kufikiamwezi Machi 2017 Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ilikuwa imepokea kiasi cha shilingi Bilioni16.23sawa na asilimia 39.57 kati ya kiasi cha shilingi Bilioni41.00kilichoidhinishwa na Bunge lako Tukufu.(Rejea KielelezoNa. 2)

Mheshimiwa Spika, Katika uchambuzi huo, Kamati inaonakwamba utoaji wa fedha kwa ajili ya Wizara hii ni wakusuasua kila mwaka licha ya kutengewa fedha kidogo kilalakini hata hicho kiasi kidogo kimekuwa hakitolewi hata kwaasilimia 50 kama siyo 75 kama ilivyo matarajio kwa watuwote ambao wanaona Afya ni kipaumbele katika nchiyoyote.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kwamba Serikalihaijaamua kulipa kipaumbele suala la Afya, kwanza kwakutotenga fedha za kutosha katika Sekta hii na pili kwakutotoa fedha za utekelezaji wa shughuli zake kwawakati.Kamati inaona pia kwamba, hata mafanikioyanayopatikana katika Wizara hii ni kutokana na Uzalendomkubwa walionao Watendaji Wakuu pamoja na wasaidiziwao kwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha na siyo fedhaau jitihada ambazo zinawekwa na Serikali kwa ajili yauboreshaji wa Afyaza Watanzania. Aliyekuwa Mpigania Uhuruna Baba wa Taifa la India Mahatma Gandhi aliwahi kusema“It is Health that is real Wealth and not pieces of gold andsilver”hivyo Serikali haina budi kuhakikisha afya zaWatanzania ndiyo kipaumbele kwani ndiyo utajiri wenyewe.

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mheshimiwa Spika, Kamati inaisihi Serikali kuipa kipaumbelecha pekee Wizara hii kwa kuhakikisha inatenga fedha zakutosha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake zikiwemoshughuli za kutoa huduma za kuzuia magonjwa (PreventionServices), Matibabu (Curative Services) na hata uraghabishaji(Promotion Services). Kwa kutekeleza haya hatutalazimikakutenga fedha nyingi katika masuala ya dawa kwanimagonjwa yatakayohitaji dawa yatakuwa tayari yamekwishazuiliwa na huduma za kinga.

Aidha, Kamati inashauri Serikali pia kuiangalia Idara KuuMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Fungu 53) iliIdara hii iweze kutimiza wajibu wake wa kuifanya jamii istawivilivyo ikiambatana na kutoa ajira ya kwa ajili ya MaafisaMaendeleo ya Jamii.

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoelezwa awaliKamati inaonakwamba Serikali kutokupeleka Fedha kwa wakatikunakwamisha Wizara katika kutekeleza majukumu yake.

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

3.2 Maelezo kuhusu Miradi ya Maendeleo iliyokaguliwa

Mheshimiwa Spika,kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Wizaraya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Fungu 52, i l itengewa kiasi chashilingi518,511,683,780/=kwa ajili ya kutekeleza Miradi yaMaendeleo, Kati ya fedha hizo shilingi 320,134,600,000/= sawana asilimia 40.2 ni kutoka vyanzo vya ndani na kiasi chashilingi 198,377,083,780/=kutoka vyanzo vya nje.

Kielelezo: Na.2: Ulinganishowa Bajeti iliyoidhinishwa na kiasi cha Fedha kilichopatikana

Chanzo: Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

 

 

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanikiwa kukagua jumla yaMiradi minne iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha2016/2017 licha ya ukweli kwamba Miradi iliyotengewa fedhailikuwa 28. Ukaguzi wa Miradi hii michache ulitokana na ufinyuwa muda lakini pia uwezo wa kifedha. Miradi iliyokaguliwana Kamati imeanishwa kwenye Taarifa hii.

3.2.1 Matokeo ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoelezwa awali, Kamati ilifanyaukaguzi wa jumla ya Miradi ya Maendeleo minne (4) iliyo chiniya Wizara hii ambayo ilitengewa fedha katika Mwaka waFedha 2017/2018. Miradi hiyo ni pamoja na:-

3.2.2 Mradi wa Ununuzi wa Mashine ya kupima ugonjwawa Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya Ziara ya Ukaguzi wa Mradihuu mnamo tarehe 20 Machi, 2017. Mradi hu ulitengewa jumlaya shilingi Bilioni 5kwa ajili ya kununua mashine mpya na zakisasa za kutibu Saratani (Linear Accelerator –LINAC na CTSimulator). Gharama za mashine hizi zilikuwa ni shilingi Bilioni9.5 ambapo katika Mwaka wa Fedha 2015/2016 Taasisiilitengewa shilingi Bilioni 4.5 na zilishapokelewa.

Aidha, katika Mwaka huu wa Fedha 2016/2017, hadi kufikiasiku Kamati inakagua mradi huu Taasisi ilikuwa imekwishakupokea fedha zilizokuwa zimetengewa kiasi cha shilingiBilioni 5 sawa na asilimia 100 ya fedha iliyoidhinishwa naBunge.Kamati imejulishwa kuwa Taasisi imekamilishakuandaa makabrasha ya Zabuni na mashine zinatarajiwakufika nchini ifikapo mwezi huu wa Mei, 2017.Kamatiimeridhishwa na utekelezaji wa Mradi huu kwani utasaidiakupunguza msongamano wa Wagonjwa katika Taasisi hiiwanaokwenda kupata matibabu ya Saratani, pamoja na hili,Kamati inasisitiza kuwa Taasisi chini ya usimamizi wa Wizarawaharakishe mchakato wa manunuzi wa vifaa tiba hivyo iliiweze kuanza kutoa huduma ya haraka kwa wagonjwa waSaratani.

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

3.3.2 Mradi wa Ununuzi wa Mitambo na Vifaa Tiba katikaTaasisi ya Mifupa (MOI) (Namba ya Mradi-5491)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitembelea Mradi huu siku yatarehe 23 Machi, 2017. Mradi huu ulitengewa kiasi cha shilingiBilioni 4.8 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 1.8nikwaajili ya kulipa mkopo NHIF na shilingi Bilioni 3 ni kwaajiliya manunuzi ya mitambo na vifaa tiba. Hadi Kamatiinatembelea MOI hakuna fedha iliyotolewa.

Mheshimiwa Spika, Ikumbukwe kwamba Taasisi ya MOI niTaasisi nyeti sana kutokana na utoaji wake wa huduma yamifupa na hususan kutokana na ongezeko kubwa la wahitajiwa huduma ya mifupa katika Taasisi hiyo. Ongezeko hililinatokana na kuongezeka kwa ajali kila siku hapa nchinizikihusisha magari, pikipiki na vyombo vingine vya motoambavyo hupelekea watu kuvunjika viungo ambapomwisho wa siku huduma yake hupatikana katika Taasisi yaMOI.

Mheshimiwa Spika, Kamati imesikitishwa sana na hali hii yakutotolewa fedha kwani MOI ni moja ya Taasisi muhimu sananchini na ndiyo Taasisi pekee inayotoa tiba ya mifupa hapanchini. Taasisi hii inatumia mapato yake ya ndani kwa ajili yakununua vifaa tiba na kutoa huduma kwa ajili ya wananchi.Pia ikumbukwe kwamba, kuna kundi ambalo limepewamsamaha katika gharama za matibabu wakiwemo wazeena watoto walio chini ya miaka mitano (5) hawa wotewanategemea fedha za matibabu kutoka Serikalini ambazohaziletwi kabisa. Mfano kuna mtoto aliyepata matibabu yakunyooshwa mgongo wake kwa sababu ulipinda, mgonjwahuyu alipatiwa matibabu kwa kuwekewa vifaa tiba 12ambapo kila kimoja grarama yake ni dola za Kimarekani 60(60 USD) ambayo ni sawa na shilingi 132,000/= na jumla yavifaa tu ni shilingi 1,584,000/=, gharama hii ni vifaa tu ambapokwa mujibu wa sera mgonjwa huyu anatakiwa apewematibabu bila ya malipo yoyote. Sasa je ni wagonjwawangapi wa namna hii hata wale wanaolipa wanatibiwakatika Taasisi.

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali kuhakikishainapeleka fedha hizo katika Taasisi ya MOI kabla ya Mwakawa Fedha wa 2016/2017 haujaisha.

3.3.3 Mradi wa Ununuzi wa Vifaa Tiba katika Hospitali yaTaifa Muhimbili (MNH)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitembelea Mradi huu mnamotarehe 23 Machi, 2017. Mradi huu ulitengewa jumla ya shilingiBilioni 4. Hadi Kamati inatembelea kulikuwa hakuna fedhayoyote iliyopokelewa kwa ajili ya kununua Vifaa tiba kamailivyokuwa imepangwa. Hivyo kupelekea Hospitali kushindwakutekeleza ununuzi wa vifaa tiba hivyo.

Aidha, pamoja na kutopokea fedha hizo za maendeleokutoka Serikalini bado Hospitali ilihitaji kuendelea kutoahuduma kwa wahitaji (Wagonjwa) hali iliyopelekea Hospitalikutumia fedha zake za ndani, fedha kutoka kwa Wahisani,pamoja na mkopo kutoka NHIF kiasi cha shilingi Bilioni 7.89(wenye riba nafuu) ili kuendesha shughuli za hospitali ikiwemoukarabati wa wodi na vyumba vya upasuaji.

Kamati imesikitishwa na hali hii kwani Hospitali ya Taifa yaMuhimbili ni Hospitali kongwe nchini na ndiyo Hospitali kubwainayotegemewa na Taifa. Wagonjwa kutoka sehemumbalimbali nchini wamekuwa wakipewa rufaa kuja Muhimbilikupata huduma na idadi yao imekuwa ikiongezeka mwakahadi mwaka. Kwa mfano Mwaka 2015 jumla ya wagonjwa191,241 walihudumiwa ikilinganishwa na Mwaka 2016 ambapowagonjwa 238,026 waliohudumiwa sawa na ongezeko lawagonjwa 46,785 sawa na asilimia 20. Ongezeko hili lawagonjwa wakiwemo wagonjwa wanaopata huduma bilamalipo kwa mujibu wa Sera wakiwemo watoto wenye umrichini ya miaka mitano (5) na wazee linahitaji uwepo warasilimali fedha za kutosha ili kuweza kuwahudumia. Serikalilazima iamue kutoa kipaumbele kwenye huduma za afyanchini ili kuwalinda wananchi wake.

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

3.3.4 Mradi wa Ununuzi wa Mitambo katika Taasisi yaUtafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)

Mheshimiwa Spika, Katika majadiliano ya Uchambuzi waBajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 Kamati ilikubaliana naKamati ya Bajeti pamoja na Wizara kwamba ifanye uhamishowa fedha kutoka katika vifungu vingine ndani ya Fungu 52(Re-allocation) ili iweze kuipatia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwaya Binadamu (NIMR) kiasi cha shilingi Milioni 800 kwa ajili yaununuzi na ufungaji wa mitambo ya kutengeneza dawazitokanazo na miti dawa.

Mheshimiwa Spika, Mpaka kufikia siku Kamati inakwendakufanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi, hakuna fedhayoyote iliyokuwa imepelekwa kwa ajili ya utekelezaji wamradi huu. Kamati inahoji Serikali, je kwanini hakuna fedhailiyopelekwa katika mradi huu? Je, ni kwa kuwa utengenezajiwa dawa asilia hauna umuhimu katika afya za wananchiwetu, au ni nini kinapelekea Serikali kutoupa kipaumbelemradi huu wa ununuzi wa mitambo ya utengenezaji wadawa asilia.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali ihakikisheinapeleka fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 800 kwa ajili yautekelezaji wa mradi huo ili Taasisi ianze utengenezaji wa dawahizo asilia kabla ya Mwaka huu wa Fedha 2016/2017haujaisha.

3.3 Matokeo na Maoni ya Jumla kuhusu Utekelezaji waMiradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoelezwa awali kwambaKamatiilifanikiwa kutembelea miradi minne kati ya Miradi 28iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2016/2017.Kutokana na hali iliyoikuta kwenye Miradi hiyo, Kamati inatoaUshauri ufuatao:-

i) Kamati inashauri Serikali itoe fedhazilizoidhinishwa kwaajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba katikaHospitali ya Taifa Muhimbili. Ikumbukwe kwamba hii ni Hospiali

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

ya Taifa ambayo Rufaa zote nchini zinaelekezwa katikaHospitali hii. Kutoipa fedha za maendeleo ni kuirudisha nyumakimaendeleo. Hadi siku Kamati inaitembelea Taasisi hiihakuna fedha iliyopelekwanakuilazimu Taasisi hii kutekelezashughuli zake kwa kutumia fedha zake za ndani.

ii) Kamati inashauri Serikali kuipa dhamanaHospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kukasimishahuduma nyingine kwa wadau wengine wa afya (ServicesOutsourcing) ikiwemo huduma za dawa pamoja na vipimo,ambapo ulimwengu wa sasa ndicho kinachofanyika katikaSekta ya afya. Kwa kufanya hivyo, Taasisi itaondokana namasuala mazima ya ukosekanaji wa Dawa na hata kufanyamatengenezo ya vifaa vya upimaji wa magonjwambalimbali.

iii) Kamati inashauri Serikali kupeleka fedha zamaendeleo kiasi cha shilingi Bilioni 4.8 kwa ajili ya ununuzi waVifaa Tiba katika Taasisi ya Mifupa MOI ili kuiwezesha Taasisihiyo kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi, kwani hadi Kamatiinaitembelea Taasisi hiyo hakuna hata shilingi moja iliyokuwaimekwisha pelekwa na Serikali. Ikumbukwe kwamba kunakundi kubwa la watu ambao wanatibiwa bila malipo kwamujibu wa Sera ya Afya (Wazee na Watoto) ambapounakuta vifaa vyake ni gharama kubwa sana haliinayopelekea Taasisi kubebe mzigo mkubwa ambaoungeweza kutekelezwa kwa fedha zilizotengwa na Serikalina kupitishwa na Bunge lako Tukufu.

iv) Kamati inashauri Serikali ihakikishe inasimamiavyema Taasisi ya Saratani ya Ocean Road katika uharakishajiwa mchakato wa ununuzi wa Vifaa Tiba ambavyovimepatiwa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 5 ili kuepukausumbufu utakaotokana na mabadiliko ya thamani ya fedha(Inflation). Aidha, kuharakisha kwa mchakato huokutapelekea upatikanaji wa vifaa tiba hivyo kwa harakaambako kutatatua msongamano wa wagonjwawanaohitaji huduma ya matibabu ya mionzi katika Taasisiya Ocean Road.

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

v) Kamati inashauri Serikali kupeleka fedha katikaTaasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu kiasi cha shilingiMilioni 800 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Ununuzi naUfungaji wa mitambo ya kutengeneza dawa zitokanazo naMiti Dawa ili Taasisi hiyo iendelee kuzalisha Dawa hizozinazogundulika kutokana na Utafiti wao. Aidha, Kamatiinashauri pia kuongeza eneo la kujenga kiwanda hicho chautengenezaji waDawa asilia kwani sasa hivi kipo katikati yamakazi ya watu (Mabibo External) ambapo Kamati inaonani eneo dogo na linaweza kuleta usumbufu hapo mbelenikama Taasisi hiyo itakua katika uzalishaji wa dawa asilia.

vi) Kutokana na Serikali kupeleka fedha zamaendeleo kiasi cha shilingi Bilioni 133.872 sawa na asilimia25.82 tu (Fungu 52) nakiasi cha shilingi Milioni 204.217 sawana asilimia 2 tu (Fungu 53) ya kiasi kilichopangwa, Kamatiinashauri Serikali kupeleka fedha katika miradi yoteiliyotengewa fedha kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017angalau kwa asilimia 50 hadi ifikapo tarehe 30 June, 2017 iliMiradi hiyo ianze kutekelezwa.

4.0 UCHAMBUZI WA MPANGO WA MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

4.1 Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato kwa Mwaka waFedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kutekeleza malengombalimbalikatika MwakawaFedha 2017/2018 kwa Fungu 52& 53. Kati yaMalengo hayo ni pamoja na;

1. Kukuza usawa wa jinsia na uwezeshaji wawanawake Kiuchumi

2. Kuimarisha upatikanaji wa haki na hudumaza Ustawi wa Jamii kwa Wazee na Watoto

3. Kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa Taifawa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawakena Watoto wa Mwaka 2017/2018-2021/2022

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

4. Kusimamia Sera ya Afya na kutoa huduma zaKinga na Tiba

5. Kuendesha ukaguzi wa wa huduma za afyazitolewazo katika ngazi mbalimbali

6. Kuandaa na kusimamia mpango wa mafunzoya wataalamu wa afya na kuwaendelezakitaaluma watumishi wa sekta ya Afya

7. Kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya Wizara,Sekta binafsi, Idara mbalimbali na kuimarishaubora wa huduma za Afya

8. Kuratibu, Kutekeleza na kusimamia masualaya lishe nchini

9. Kuendesha utafiti wa magonjwa ya binadamuna kutumia matokeo hayo kwa manufaa yawananchi

10. Kuongoza na kusimamia Wakala wa Serikali,Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyo chini yaWizara-Afya

Mheshimiwa Spika,Pamoja na malengo mengi ambayoWizara kupitia Fungu 52 na 53 imeyapanga, Malengo hayoyameonekana kuwa yana tija katika suala zima la uboreshajiwa Sekta ya Afya kwa kuzingatia Mipango Mikakatimbalimbali pamoja na makubaliano ya Kitaifa na Kimataifayenye lengo la kuimarisha utoaji wa Huduma ya Afya nchini.Malengo ambayo Wizara inatarajia kutekeleza ni yaleambayo yameainishwa katika miongozo mbalimbaliikiwemoDira ya Taifa ya Maendeleo (2025), Mpango waMaendeleo wa Muda Kati 2016/2017-2020/2021, Mpango waPili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017-2020/21),Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable DevelopmentGoals 2030), Sera ya Afya (2007) Mpango Mkakati wa IV waSekta ya Afya (2015-2020). Aidha, Malengo haya yoteyanalenga katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zenye

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

uwiano wa kijiografia, viwango vya ubora wa hali ya juu,gharama nafuu lakini pia huduma ambazo ni endelevu. Kwakutekeleza Malengo haya ya Afya kutapelekea kuwa na jamiiyenye afya bora na Ustawi wa Jamii ambao utachangiakupelekea Jamii iliyo bora katika Ustawi wa jamii kwa ujumla.

4.2 Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato kwa Mwaka waFedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha 2017/2018,Wizara hii ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto yenye mafungu mawili inataraji kukusanya maduhuliyake kama ifuatavyo:- Kwa upande wa Fungu 52 (Idara KuuAfya) inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi 245,038,495,525/= ikiwa ni ongezeko la shilingi 87,237,111,159/=, sawa naasilimia 35 ya kiasi cha shilingi 157,801,384,366/= zilizokadiriwakatika Mwaka wa Fedha 2016/2017. Ongezeko hilo nikutokana na uimarishaji wa mifumo ya ukusanyaji wa Mapatoyatokanayo na utoaji wa Huduma za afya katika vituo vyotevya kutolea huduma.

Mheshimiwa Spika, Katika Fungu 53 (Idara Kuu Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Wizara inakadiriakukusanya kiasi cha shilingi 2,101,874,000/= ikiwa ni pungufukwa shilingi 280,805,000/=, sawa na asilimia11.8 ya kiasi chashilingi 2,382,679,000/= kilichokadiriwa katika Mwaka waFedha 2016/2017.

4.3 Uchambuzi wa Makadirio ya Matumizi kwa Mwakawa Fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Wizarakupitia Fungu 52 (Idara Kuu Afya) imepanga kutumia kiasicha shilingi 1,078,754,221,478/= ili kuwezesha utekelezaji wamajukumu ya Wizara kwa Idara Kuu Afya. Kati ya fedha hizokiasi cha shilingi 291,932,052,000/= sawa na asilimia 27 nikwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ikiwa ni pamoja naMishahara ya Watumishi. Aidha, kiasi cha shilingi786,822,169,478.62/= sawa na asilimia 73 kinaombwa kwaajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Fungu 53 (Idara KuuMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), Wizaraimepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 40,130,215,784/=.Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi 4,829,613,784/= sawa naasilimia 12 ni kwa ajili Miradi ya Maendeleo na shilingi35,300,602,000/= sawa na asilimia 88 ni kwa ajili ya Matumiziya Kawaida.

Mheshimiwa Spika, Makadirio haya ya Matumizi ya Fedhayanaonesha kuongezekakwaasilimia 25.9 hasa kwa Fungu52 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 ikilinganishwa naMakadirio ya Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.Kamati inaona kwamba pamoja na Fungu hili kuongezewafedha, Kamat inaona haina tija sana kwani hata Bajeti ya

Kielelezo Na. 3: Makadirio ya Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Chanzo: Randama ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

 

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

Mwaka wa Fedha unaoisha imepelekwa chini ya asilimia50. Kamati inajiuliza kama kiasi kidogo cha mwaka uliopitahakikwenda, je kiasi hiki chenye ongezeko la asilimia 25.9kitakwenda?

SEHEMU YA TATU__________

5.0 MAONI, USHAURI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI

Mheshimiwa Spika, Napenda kuchukua fursa hii kutoa Maoni,Ushauri na Mapendekezo ya Kamati kuhusu utekelezaji wamajukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 katika maeneo yafuatayo:-

5.1 Bajeti ya 2016/2017 haijatekelezeka kwa asilimia 60

Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha 2016/2017Wizarailitengewa kiasi cha shilingi Bilioni 796.115 kwa ajili yautekelezaji wa shughuli zake. Hata hivyo, hadi kufikia tarehe30, Machi 2017 Wizara ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 314.673sawa na asilimia 40 tu ya fedha zote ambazo zilitakiwakuletwa katika Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, Kamati inahoji ni lini sasa Serikaliitatekeleza haya ambayo yalitakiwa kutekelezeka kwaMwaka wa Fedha unaoisha (2016/2017) kwani sasatunaelekea Mwaka wa Fedha mwingine? Ni vyema sasaSerikali ikajipanga na kuhakikisha Bajeti yote inayoidhinishwana Bunge inatolewa yote na kwa wakati ili Wizara iwezekutekeleza majukumu yake ipasavyo.

5.2 Bajeti ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shuguli za Wizarakwa Fungu 52 &53 inaonekana kuongezeka kwa asilimia 25.9.Hata hivyo, bajeti hii bado haijafanikiwa kufikia hata asilimia10 ya bajeti nzima ya nchi ambayo imetengwa kwa ajili ya

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

utekelezaji wa shughuli za Wizara. Bajeti ya Mwaka huu yaWizara hii ni sawa na asilimia 3.5 tu ya Bajeti nzima ya Serikaliya shilingi Trilioni 31.9. Bajeti hii ni ndogo kwani badohaijatekeleza makubaliano ya Mkutano wa Azimio la Abuja(Abuja Declaration, 2001) ya kwamba nchi zipange asilimia15ya Bajeti ya nchi kwenye Sekta ya Afya.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaona ni wakati sasa Serikaliikaamuakwa dhati kulipa kipaumbele suala la Afya kwakutenga Bajeti ya kutosha angalau kufikia asilimia 10 ya BajetiKuu ya Serikali.

5.3 Bima ya Afya kwa kila Mtanzania

Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza ahadi kwa Wananchiwa Tanzania ni lazima kuangalia suala la afya katikamapana yake hasa katika kuhahakikisha kuwa kilaMtanzania anakuwa na uhakika wa kupata huduma za afyawakati wowote na mahali popote anapohitaji kuzipata.

Mheshimiwa Spika, suala la bima ya afya kwa wote si sualageni katika nchi za Afrika Mashariki, jirani zetu Rwandawamefanikiwa katika suala hilo na hakuna mwananchiambaye ana wasiwasi na suala la kupata huduma ya Afyaiwapo atakosa fedha taslimu.

Kutokana na hali hii, Kamati inatoa ushauri kwamba Serikaliiipe kipaumbele cha kipekee suala la bima ya afya kwa kilamtanzania na ijiwekee malengo ambayo yataambatana naMpango kazi wa kutekeleza azma hiyo kwa Watanzania.5.4 Kupungua kwa Fedha kutoka kwa Wahisani

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Wizara ya Afya imekuwaikitegemea sana fedha kutoka kwa Wahisani. Mathlani,kwaMwaka wa Fedha 2016/2017 Wizara ilitegemea fedhakutoka kwa hisani kwaasilimia 59.8 ya bajeti nzima yaMaendeleo ambapo hadi kufikia mwezi Machi 2017, niasilimia 6 tu ya fedha iliyotegemewa na Wahisani ndiyoiliyotolewa kwa ajili ya kutekeleza shughuli zake.

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

Mheshimiwa Spika, pamoja na kutopatikana kwa fedha hizokutoka kwa Wahisani kwa asilimia 94, lakini bado bajeti yaWizara hii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 imeendeleakutegemea fedha kutoka kwa Wahisani hao hao kwaasilimia 57.2 ya bajeti nzima.

Mheshimiwa Spika, Kamati imerejea baadhi ya Miradi yaMaendeleo ambayo inategemea ufadhili wa nje kwa asilimia100, Miradi hiyo ya Maendeleo ni pamoja na Udhibiti wa Virusivya UKIMWI na UKIMWI (HIV/AIDS Control Programme), Mradiwa Udhibiti wa Kifua Kikuu na Ukoma (Support to TB/LeprosyControl Programme), katika Miradi hii hakuna hata shilingimoja ya fedha za ndani iliyotengwa kwa ajili ya usimamizina utekelezaji wa magonjwa haya. Kamati inajaribu kuhojiSerikali je, magonjwa haya si ya kipaumbele katikakukabiliana nayo hapa nchini? Au je, Serikali imeamua kutoarehani ya afya za wananchi katika magonjwa haya ambayondiyo kati ya magonjwa yanayosumbua wananchi waTanzania bila kujali umri, dini, cheo, itikadi za siasa wala zakidini.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali kutenga fedhakatika masuala haya pamoja na Miradi mingine yaMaendeleo ili itekelezeke kwa kutegemea fedha za ndanibadala ya kutegemea ufadhili wa nje kwa ajili ya kuokoamaisha ya watanzania hata kama Wafadhili hawataletafedha zao kama mwaka huu (2016/2017) basi tuwe na miradiendelevu katika Wizara hii.

5.5 Upungufu wa Vifaa, Vifaa Tiba,Vitendanishi na Dawanchini

Mheshimiwa Spika, Utoaji wa huduma bora nchini ni pamojana uwepo wa vitendea kazi katika vituo vya kutolea hudumaya afya. Kumekuwa na malalamiko ya upungufu wa dawa,vitendanishi, vifaa na vifaa tiba katika vituo vya kutoleahuduma za afya.Kamati inaishauri Serikali kutenga bajeti inayotoshelezakuweza kununua vifaa hivi na kuvisambaza katika vituo vyotevya kutolea huduma za afya nchini.

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

5.6 Urasimu wa Upatikanaji wa Leseni kwa ajili ya Vituovya kulelea Watoto Yatima

Mheshimiwa Spika, Katika jamii kumekuwa na makundimbalimbali ambayo yapo katika mazingira magumulikiwemo kundi la watoto yatima ambao wametokananasababu mbalimbali ikiwemo vifo vitokanavyo na ugonjwawa UKIMWI. Jamii katika kuhakikisha kundi hili linapatahuduma za jamii kama walivyo watoto wengine, kunaMashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa huduma hizi kwawatoto hao yatima. Changamoto kubwa ni katikaupatikanaji wa leseni za kuanzisha vituo vya kuwaleleawatoto hao ili wapate huduma umekuwa mgumu na wenyeurasimu mkubwa.

Kamati inashauri Serikali kuhahakikisha leseni hizizinapatikana kwa urahisi ili wanaojitolea kutoa huduma hizokwa watoto yatima wasipate kukata tamaa kwani juhudi hizizote ni kwa ajili ya kuisaidia Serikali pale ambapoinaonekana kuelemewa na jukumu la kuwatunza watoto hao.

5.7 Kutenga Fungu kwa ajili ya Msamaha wa Matibabu

Mheshimiwa Spika, Nchi yetu imetengeneza Sera nzurisana(Sera ya Afya 2007) ambayo katika Sera hiyo imeainishabayana makundi ambayo yamepewa msamaha wagharama za matibabu likiwemo kundi la Watoto wenye umrichini ya miaka mitano (5), Wajawazito pamoja na Wazeewenye umri zaidi ya miaka 60. Katika kutekeleza Sera hiiimegeuka kuwa changamoto kwa Taasisi zinazotoa hudumaza afya kwa makundi haya na kupelekea kuwa kero kwamakundi hayo na hata kwa taasisi husika inayotoa hudumakwa kuwa na uhaba wa rasilimali fedha kwa ajili ya kununuaDawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa ajili ya kuwapahuduma bora za afya kwa makundi husika.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitembelea Hospitali ya TaifaMuhimbili na kupewa taarifa kwamba kwa kipindi chakuanzia Julai hadi Disemba 2015 Taasisi ilitumia kiasi cha shilingiBilioni 1.640 kwa ajili ya kutoa huduma kwa msamaha na

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017 Taasisi hiyo kwa kipindicha kuanzia Julai hadi Disemba 2016 ilitumia kiasi cha shilingiBilioni 1.560 kwa wagonjwa walio na sifa za kupatamatibabu kwa msamaha. Hii ni kwa kipindi cha miezi sita (6)tu katika miaka hiyo miwili mfululizo Taasisi hiyo imekuwaikitumia fedha zake kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwamakundi ya msamaha ambazo zinakusanywa na Taasisihusika.

Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha 2016/2017 Taasisiya Mifupa ya Muhimbili (MOI) ilitoa huduma katika mikoa 18ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa watoto 2200 na kati haowatoto 202 wenye vichwa vikubwa walipata huduma yaupasuaji na katika huduma hiyo iliyotolewa fedha zilizotumikani kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya Taasisi. Kwamantiki hii, Taasisi hizi zimekuwa zikifanya kazi kubwa ambayoinalazimika kutumia mapato ya ndani na hata hivyokusababisha kufanya kazi kwa kiasi kidogo kutokana nauhaba wa rasilimali fedha ambazo kama Taasisi inahangaikakuzikusanya na kuzigawanya katika utoaji wa huduma kwamakundi yenye msamaha.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali, kutenga Fungulake maalumu (Separate Vote) ambalo litatengwa kwa ajiliya kutoa huduma bora za afya kwa makundi hayo yamsamaha wa gharama za matibabu ili kuweza kuwa nahuduma endelevu.

5.8 Bajeti ndogo ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikweteimekuwa ikitoa huduma ya matibabu ya Moyo kwaWatanzania. Taasisi hii imekuwa ikitoa huduma katikamazingira magumu sana kutokana na kuongezeka kwawagonjwa na upande mwingine Serikali kutopeleka fedhakama ilivyokuwa imepangwa kwa ajili ya kutekelezamajukumu yake. Mathlani, kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017Taasisi hii ilitengewa kiasi cha shilingi Bilioni 4 lakini mpakakufikia mwezi Machi 2017 Taasisi hii ilikuwa imepokea kiasi

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

cha shilingi Milioni 500 tu sawa na asilimia 12.5 ya fedhazote zilizotengwa. Wakati huo huo Taasisi hii imeokoa kiasicha shilingi Bilioni 3.75kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 iwapowagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi hasa India kwaajili ya matibabu hayo ya Moyo.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashangazwa na kitendo chaTaasisi inayookoa fedha nyingi kwa kutokupeleka wagonjwanje lakini bado fedha zinazoombwa hazipelekwi katika Taasisihiyo. Kamati inashauri bajeti ya JKCI itolewe yote na kwawakati ili iweze kuisaidia Serikali kuokoa fedha nyingi ambazoingetumia kupeleka wagonjwa kwenye matibabu nje ya nchi.

5.9 Ripoti ya Ukaguzi wa Benki ya Wanawake yaTanzania (TWB)

Mheshimiwa Spika, Benki ya Wanawake ya Tanzania(Tanzania Women Bank) ipo chini ya Wizara ya Afya na Benkihii imekuwa ikisuasua katika ukuaji wake na hata kutofikiamaeneo mengine ya nchi kwa maana ya mikoa yapembezoni na kujikuta imebakia katika mkoa wa Dar esSalaam peke yake.

Kamati inaishauri Serikali kupitia Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali, kuifanyia ukaguzi wa kimahesabu Benki hiyo ilikubaini kiasi cha mtaji wake, nini kikwazo cha Benki hiyokutokukua kama Benki nyingine na kuona namna ganiinaweza kuibuliwa na kukuzwa ili kuweza kushindana naBenki nyingine kwa ajili ya kuwasaidia Wanawake waKitanzania lakini pamoja na Wanaume kwa ajili ya kujiinuakiuchumi.

5.10 Utoaji wa zabuni za utoaji wa Huduma katika Taasisiza Afya.

Mheshimiwa Spika, Utoaji wa Huduma za Afya katika Taasisikubwa kama vile Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi yaMifupa (MOI) imekuwa ni changamoto kubwa kutokana nauhaba wa Vifaa, Vifaa Tiba, Dawa na Vitendanishi kamailivyoelezwa hapo awali. Aidha, upungufu huo unapelekea

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

kuwa na msongamano mkubwa katika sehemu ya vipimona hata kupelekea wagonjwa kwenda kununua dawa njeya Taasisi kwa gharama kubwa kwa kuwa hazijawezakupatikana ndani ya Taasisi ambayo mgonjwa amekuwaakipata matibabu yake. Hali hii inapelekea hata wagonjwawengine kurejea nyumbani wakiwa wamekosa vipimo, dawaau fedha za kupata huduma nje ya Taasisi hizo. Hili limekuwalinaleta usumbufu na hata kupoteza maisha yao kwamaradhi ambayo yamekuwa yakiwasumbua.

Mheshimiwa Spika,kutokana na changamoto hizo za ugumuwa upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya vipimo na dawa kutokanana Taasisi kukosa fedha za kununulia vifaa na dawa Kamatiinaishauri Serikali kuruhusu huduma hizo hasa za Vipimo nadawa zitolewe na Mzabuni wa nje ya Taasisi(ServicesOutsourcing) ambaye ataweza kuwekeza katika maeneohayo ambapo mbia huyo ataleta vifaa vyake kwa ajili yaupimaji wa magonjwa mbalimbali lakini pia utoaji wa dawakwa wagonjwa katika Taasisi husika.Kamati inashauri hivyokwakuwa kuna faida kubwa katika kutekeleza hayo,kwanza, itaipunguzia mzigo mkubwa kwa Serikali na Taasisihiyo katika suala zima la ukarabati (Maintanance) ya vifaahivyo, itapunguza shughuli ya uagizaji wa dawa katika Taasisilakini pia hata kama teknolojia ya vifaa itabadilika itabakikuwa jukumu la Mzabuni huyo kubadilisha na si jukumu laSerikali tena kama ilivyo sasa na zaidi tena kuifanya nchiyetu kuendana na mabadiliko ya teknolojia yanayoendeleakutokea ulimwengunikatika suala zima la afya.

5.11 Kutopelekwa kwa fedha zilizotengwa katika Miradiya Maendeleo

Mheshimiwa Spika, Miradi ya Maendeleo ya Afya ndiyo msingimkubwa wa kuwekeza katika Sekta ya Afya kwa mustakabliwa afya za wananchi wa Tanzania, ikiwemo miradi ya Lishe,Kifua Kikuu na UKIMWI, Maendeleo ya masuala ya Utafiti yaMagonjwa ya Binadamu. Kamati imesikitishwa kuona katikaMwaka huu wa Fedha wa 2016/2017 Wizara imepokeaasilimia 25 tu ya fedha za Miradi ya Maendeleo. Kuna Msemo

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

usemao “Nothing happens without Focus, Don’t try to doeverything at once, Take it one step at a time”.

Kamati inaona ni wakati sasa umefika Serikali iamuekuchagua Miradi michache ya Kipaumbele kulingana nauwezo wake wa kifedha ili iweze kuitekeleza.

5.12 Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vipelekwe Wizara yaElimu

Mheshimiwa Spika, Wizara hii katika Fungu 53 (Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) inasimamia Vyuovinavyotoa Elimu kwa ajili ya kupata Wataalamu waMaendeleo ya Jamii kikiwemo chuo cha Tengeru-Arusha,Rungemba-Iringa, Mondoli, Uyole, Misungwi na vingine vingi.Katika suala hili Taaluma hii imekuwa si katika ubora uleambao unatarajiwa kutolewa na vyuo hivyo.

Kamati inashauri vyuo hivi vyote vilivyoko chini ya Fungu 53vihamishwe na kupelekwa chini ya uangalizi wa Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia kama ilivyo vyuo vikuu vinginehapa nchini. Kwa kufanya hivi kutasaidia kufuatilia uborawa Elimu itolewayo na vyuo hivyo vya Maendeleo ya Jamii.

5.13 Bohari Kuu ya Dawa

Mheshimwa Spika, Bohari ya Dawa hapa nchini ndiyowanaohusika katika Uagizaji na Usambazaji wa Dawa hapanchini. Katika kutekeleza suala hili Bohari ya Dawa imekuwaikilalamikiwa sana katika kutotekeleza majukumu yake ikiwakutopeleka Dawa katika vituo kwa wakati hali inayopelekeawagonjwa kutopata matibabu yanayotakikana.

Kamati inashauri Bohari hiyo kufanyiwa ukaguzi wa kina kwaajili ya kubaini mafanikio (Strength), Changamoto(Challenges), Mahitaji (Demands) ili kuweza kubaini namnagani ya kuboresha usambazaji wa dawa nchini.

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

5.14 Mabadiliko ya Sheria ya ndoa na Ndoa za utotoni

Mheshimiwa Spika, Katika suala la ndoa kuna Sheriainayosimamia masuala ya ndoa ya Mwaka 1971. Sheria hiyoimeonekana kuwa namapungufu mengi hasa katika Kifungucha 13 na 17. Kifungu cha 17 kinahusu wanaotaka kufungandoa wawe wameridhiana na kama yupo chini ya miaka 18ridhaa itatoka kwa baba na kama baba amefariki ridhaaitatoka kwa mama na kama wazazi wote wamefariki basiridhaa hiyo itatoka kwa mlezi wa mtoto huyo.

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni nchi mojawapo ya nchiambazo zinaongoza kwa ndoa za utotoni duniani ambapokwa wastani kati ya watoto wakike watano (5) watoto wawili(2) huolewa kabla ya umri na takwimu za Utafiti wa Afya naWatu (Demographic Health Survey 2015/2016) inaoneshakuwa asilimia 30.5% ya wanawake kati ya umri wa miaka20-24 inaonesha waliolewa chini ya umri wa miaka 18.

Mheshimiwa Spika, Mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotonikwa zaidi ya asilimia 50 ni pamoja na Shinyanga (asilimia59), Tabora (asilimia 58), Mara (asilimia 55) na mkoa waDodoma (asilimia 51). Ndoa hizi za chini ya umri wa miaka 18zinapelekea watoto hao kupata athari nyingi zikiwemo zakiafya na hata kukosa haki yao ya kupata Elimu na hatakupata athari za kisaikolojia.

Kamati inashauri Serikali pamoja na ugumu unaojaribukuwekwa na Taasisi za kidini na mila na desturi za mahalihusika, Kamati inaamini Serikali ina mamlaka juu ya kulindahaki na ustawi wa jamii zetu hasa kulinda haki za watotohapa nchini Serikali ilinde haki hizo za watoto.

5.15 Kuongezeka kwa Idadi ya Makundi Maalum (KeyPopulations) katika Jamii

Mheshimiwa Spika, Makundi maalum (Key Populations)inajumuuisha watu wanaojidunga madawa ya kulevya(IDUs), Wanaofanya biashara ya ngono (wakike na kiume)na wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (Men who Sex with

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

Menand women who sex with women and Trans-Gender).Makundi haya yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku katikajamii zetu na imekuwa tishio kubwa hasa katika suala zimala ongezeko la Virusi vya UKIMWI. Ongezeko la kundi hili nikutokana na mabadiliko ya jamii zetu ikiwemo katika sualala malezi kuanzia katika ngazi ya familia, shuleni na hatakatika jamii kwa ujumla. Matendo haya yamekuwayakifanyika majumbani, shuleni za kutwa na hata bweni.

Mheshimiwa Spika, Kuna athari nyingi zitokanazo na makundihaya maalumu ikiwemo za maambukizi ya Virusi vya UKIMWI,Homa ya ini, kupoteza nguvu kazi ya Taifa katika jamii nahata watoto kukatisha masomo yao na kujiingiza katikamakundi hayo.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali kuhakikishainaajiri Maafisa maendeleo ya jamii, katika kila kata ambaowatasaidia katika kutekeleza afua mbalimbali na hatakuwapa miongozo wanajamii ya namna gani ya kuenendaili kudhibiti suala hili la makundi maalumu, kwani imethibitikakwamba katika maeneo mengi kuna upungufu mkubwa waWatumishi wa hao pamoja na Halmashauri nyingine lakinihata Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwako MheshimiwaSpika kuna upungufu wa Maafisa hao wa maendeleo yaJamii kwa asilimia 82, Kondoa asilimia 100, Ruangwa (WaziriMkuu) upungufu ni asilimia 100, Mji wa Bunda na Halmashaurinyingine nyingi hapa nchini. Kamati inaendelea kusisitizakuwa Serikali itimize wajibu wake wakuajiri Maafisa maendeleona Ustawi wa Jamii ili kuweza kupunguza ongezeko lamakundi haya.

5.16 Vifo vya akina Mama vitokanavyo na Uzazi

Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kwamba Serikalii badohaijatilia mkazo suala la vifo vya akina mama vitokanavyouzazi na akina mama hapa nchini. Suala hili lilielezwa naKamati katika Taarifa ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 kwamba, kumekuwa na vifo vingi vitokanavyo namasuala ya uzazi, ikiwemo wakati wakati wa ujauzito,

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

wakati wa kujifungia na hata ndani ya siku arobaini (40)baada ya kujifungua.

Mheshimiwa Spika, Takwimu zinazoonesha vifo vya akinamama zipo juu kila mwaka pamoja na jitihada zote zaSerikalikatika kupunguza au kumaliza tatizo hili. Vifo hivi vinatokanana sababu mbalimbali ikiwemo umbali wa vituo vya kutoleahuduma za afya ya uzazi, kukosekana kwa huduma za uzaziwa mpango takwimu zinaonesha kuwa katika kilawanawake Watano (5) wa Kitanzania mwanamke mmoja(1) ana mahitaji yasiyofikiwa. Aidha, kutokana nakutopatikana kwa huduma hizo za Uzazi wa Mpango kilamwaka wanawake wa Kitanzania Milioni moja (1,000,000)hupata mimba zisizotarajiwa ambazo kati ya hizo asilimia39 (Wanawake 390,000) huishia kwenye utoaji wa mimba hizotena kwa usiri mkubwa na kupelekea kupata matatizoambayo yanahitajimatibabu.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kuwanusuruakina mama hawa katika matatizo ya uzazi kwa kuwatengeana kutoa fedha za kutosha kwani Bajeti yao imekuwaikipungua mwaka hadi mwaka. Kwa mfano katikaMwakawa Fedha wa 2016/2017 Masuala ya kupunguza vifovitokanavyo na uzazi (Support to Maternal MortalityReduction) ilitengewa kiasi cha shilingi Bilioni 13 na Mwakawa Fedha 2017/2018 fedha zimetengwa shilingi ni shilingi Bilioni8.6. Upungufu huu ni sawa na asilimia 33.8.Kamati inaona hiisi sawa hata kidogo kwani inaonesha Serikali kukosa niathabiti ya kutatua tatizo hili.

5.17 Huduma za Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)ni Mfuko ambao unatumika kukusanya makato ya Watumishiwa Serikali na Taasisi zake kutoka katika mishahara yao nakukusanya fedha hizo katika kapu moja ili kutoa hudumabora za afya kwa Watumishi hao pamoja na wategemeziwao. Kabla Mfuko huu haujaanza kutoa huduma hizoMashirika ya umma yaliingia mikataba na Mifuko ya Bima

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

binafsi na walikuwa wanapata huduma bora kulingana natozo za makato yao. Kuna maelekezo ya kutaka Mashirikaya Umma kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afyawakati Mfuko huo haujajiandaa vya kutosha kutoa hudumahizo za afya kama mahitaji ya wachangiaji mfuko huo nandani na hata nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kuupa mudaMfuko wa Bima ya Afya ya Taifa kujiaandaa vyema ili uwezekutoa huduma bora kwa wateja wake ili hata Mashirika hayoyakijiunga wasione tofauti ya upatikanaji wa hudumawalizokuwa wanapata kabla ya kujiunga katika mifukomingine ya Bima ya Afya .Kwa kufanya hivyo kutaondoamalalamiko na pia kuwapa uwezo wa kuendana na soko lautoaji wa huduma bora za afya kama mifuko mingineinayotoa huduma ya Bima ya Afya hapa nchini na hata njeya nchi.

5.18 Ujenzi wa Vituo vya Afya

Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina upungufu mkubwa wa vituovya Afya kwani kwa mujibu wa Takwimu ni kuwa kunaupungufu wa vituo vya Afya kwa asilimia 85 Hali hii inasikitishakwani asilimian kubwa ya Watanzania wanaishi maeneo yavijijini ambako wanategemea vituo vya Afya kupatahuduma. Kamati inajiuliza je ni jukumu la nani kujenga vituohivi vya Afya?

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali kwaujumla wakekuhakikisha vituo vya Afya vinajengwa vya kutosha ilikusaidia kutoa huduma ya afya nchini.

5.19 Utenganishajiwa Majukumu ya Mamlaka ya Chakulana Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Mheshimiwa Spika, Katika Udhibiti waBidhaa nchini Serikaliiliamua kuunda Taasisi kwaajili ya usimamizi wa majukumuhaya kwa Mujibu wa Sheria. Katika utekelezaji wa majukumuya Taasisi hizo, Kamati imebaini kuwa kumekuwa namuingiliano wa majukumu siyo tu baina ya TFDA na TBS lakinipia na Taasisi nyingine kama Bodi ya Maabara Binafsi za Afya

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

(Private Health Laboratories). Muingiliano huu umekuwaukikiuka utaratibu wa kisheria na kuleta usumbufu katikautekelezaji wa majukumu ya kila Taasisi. Kutokana na halihii, Kamati inashauri Serikali iziangalie Sheria zinazoundaTaasisi hizi ambazo pia zimeainisha majukumu yao na palekwenye tatizo basi marekebisho yafanyike kuepushamuingiliano wa majukumu ya Taasisi moja kufanywa na Taasisinyingine.

5.20 Vikwazo katika uingizwaji wa Misaada kutoka kwaWahisani

Mheshimiwa Spika, Katika uboreshaji wa Sekta ya Afyakumekuwa na Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchiwakisaidiana na Serikali hasa katika upatikanaji wa dawana vifaa tiba.Kamati imebaini kuwa pamoja na nia njemaya wahisani ya kutupatia msaada wa dawa muhimu pamojana dawa za uzazi wa mpango, kumekuwa na vikwazombalimbali katika utekeleaji wa azma hii ikiwemo urasimuna gharama kubwa za kuhakikisha msaada huo unawafikiawananchi. Vikwazo hivyo ni pamoja na tozo za kutupatiamsaada ambazo Serikali imekuwa ikimtaka anayetoamsaada kulipa kodi ya kutupatia msaada huo, gharama zakupakua mzigo ufikapo bandarini, gharama ya kutunzamsaada huo ufikapo bandarini gharama za kuwalipaMamlaka ya kukagua msaada huo ambayo ni Mamlaka yaChakula na Dawa (TFDA) ipo chini ya Wizara ya Afya nainatengewa Bajeti ya kutekeleza majukumu yak echini yaWizara ya Afya na Serikali inaitengea fedha hizo.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na taratibu za kwambamsaada huo unatakiwa utolewe bandarini ndani ya siku saba(7) baada ya hapo gharama zinaongezeka kila siku, kodizimekuwa zikiongezeka kwa baadhi ya Misaada kutokanana kuchelewa kutolewa kwa msaada (Mzigo) kutokana naurasimu. Kwa Mfano imewahi kutokea msaada wa sindanozenye thamani ya shilingi milioni 800kutakiwa kulipiwa kodikiasi cha shilingi Bilioni 1.2 iliyopelekea Wahisani kushindwakutoa na hatimae msaada huo kuishia hewani.

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kupitia TFDAifanye jukumu lake bila kutoza kiasi chochote kwa Wizarakwani hayo ndiyo majukumu yake ambayo amepangiwaBajeti na haipaswi kulipwa vilevile, Kamati inaona hiki nikikwazo kikubwa kwa wafadhili na inaweza kuwa ni moja yasababu ya wao kuanza kupunguza msaada ambaowamekuwa wakiahidi. Pia Serikali itambue kwamba kodi natozo mbalimbali kunapelekea kuongezeka kwa gharama zamatibabu ya afya na anayeumia hapa ni mwananchiambaye ndiyo mlaji au mtumiaji wa mwisho wa huduma hiyo.

5.21 Magonjwa yatokanayo kwa kukosekana kwamatumizi bora ya vyoo, maji safi na salama

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la AfyaDuniani (WHO 2004) imeonesha kwamba kuboresha kwa Usafiwa mazingira kunaweza kupunguza magonjwa ya kuharakwa asilimia 32 na kuboresha Afya ya mazingira kunawezakupunguza magonjwa ya kuharisha kwa asilimia 45.Uboreshaji wa afya ya mazingira ni pamoja na ujengaji wavyoo bora, upatikanaji wa maji safi na salama pamoja nautoaji wa elimu kwa umma kuhusu matumizi bora ya vyoo.

Mheshimiwa Spika, Utunzaji wa usafi wa mazingira ni jukumula kila mmoja wetu kuanzia katika ngazi ya familia (ujenzina utumiaji bora wa vyoo) hata katika shule. Taarifa za utafitimbalimbali unaonesha kwamba ni asilimia 11 tu ya shule yamsingi nchini zilikuwa na namba ya vyoo vya kutosha naasilimia 1 ya sehemu zinazotumika kunawia mikono na sabuni(School WASH Mapping Report 2011). Kumekuwa na tabia awananchi kujisaidia kiholela (Open defecation) majumbani,shuleni na hata wakati wa safari ndefu (kuchimba dawa)ambao ni uchafuzi wa mazingira. Matumizi bora ya vyookutapelekea kulinda vyanzo vya maji ambayo yanatumikana wananchi wetu hivyo kulinda afya kwa kujikinga namagonjwa yatokanayo na maji kwani imebainika kwambaasilimia 70 ya wagonjwa kwa siku ni wagonjwa wenyemagonjwa yatokanayo na maji (Waterborne Diseases).

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

Mheshimiwa Spika, Hakuna siku ambayo itapitamwanadamu asitumie maji tumekuwa tusikia kila siku kuwamaji ni uhai na maji ni afya. Nchi yetu imekuwa na tatizokubwa sana la magonjwa yatokanayo na kukosekana kwamaji safi na salama (Waterborne diseases) yakiwemomagonjwa ya homa ya tumbo, Kichocho, kipindupindu,magonjwa ya kuhara na kuharisha na hata magonjwa yangozi .

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri Serikali ihimize ujengajina matumizi bora ya vyoo na kuhakikisha kupitia Wizara yaAfya inashirikiana na Wizara ya Maji katika kuhakikishawananchi wanapata maji safi na salama ili kuepukamagonjwa hayo.

6.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, nakushukuru wewe binafsi kwa kunipamuda wa kuwasilisha Taarifa hii mbele ya Bunge lako Tukufu.Pia napenda kumshukuru Waziri wa Afya na Maendeleo yaJamii, Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy A.Mwalimu (Mb) pamoja na Naibu Waziri Mheshimiwa HamisKigwangala(Mb) kwa ushirikiano wao mkubwawanaoendelea kuutoa kwa Kamati wakati wote wa shughuliza Kamati hasa Kamati ilipokuwa ikijadili Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha2017/2018. Vilevile napenda kuwashukuru Makatibu Wakuuwa Wizara Idara kuu Afya na Idara Kuu ya Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na MaafisaWaandamizi wao wa Wizara na Taasisi zake zote kwaushirikiano walioutoa kwa Kamati hii ya kutekelezamajukumu yake kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bungehili.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuruWadau wetu wote waSekta ya Afya kwa kazi nzuriwanayoifanya na kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoutoakwa Serikali yetu katika kuendelea kutoa huduma bora yaAfya kwa wananchi wetu.Naomba kuwataja kwa uchacheWadau hao ni pamoja na Wadau wote wa Kimataifa

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

wanaoendelea kutoa fedha za Maendeleo ya Afya, TanzaniaGender Networking Program (TGNP), Tanzania WomenLawyers Association (TAWLA), Shirika la Utepe Mweupe (WhiteRibbon Association), Tanzania Health Promotion (HDT),Tanzania Water and Sanitation Network (TaWaSaNet) naMashirika mengine yasiyo ya kiserikali kwa juhudi zaowanazoendelea kuzifanya katika kusaidia uboreshaji wa SektaAfya hapa nchini. Kamati inaiomba Serikali kuendeleakuwapa ushirikiano mkubwa ili waweze kuendelea kutimizamajukumu yao hasa katika utoaji wa Huduma za Afya kwaWananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, Kwa nafasi ya pekee kabisa naombaniwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma naMaendeleo ya Jamii, kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kujadilina kuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizarahii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na ufinyu wamuda lakini walikuwa tayari kutekeleza jukumu hili kubwana hatimaye kukamilisha Uchambuzi wa Bajeti hii kwa weledimkubwa na kwa wakati. Kwa heshima kubwa, naombakuwatambua kwa majina Waheshimiwa wafuatao:

1. Mhe. Peter Joseph Serukamba, Mb, -Mwenyekiti2. Mhe.Mussa Azzan Zungu, Mb - M/Mwenyekiti3. Mhe.Hussein Mohamed Bashe, Mb - Mjumbe4. Mhe. Grace Victor Tendega, Mb - Mjumbe5. Mhe.Peter Ambrose Paciece Lijualikali, Mb - Mjumbe6. Mhe.Joseph Osmund Mbilinyi, Mb - Mjumbe7. Mhe.Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, Mb Mjumbe8. Mhe.Kasuku Samson Bilago, Mb - Mjumbe9. Mhe.Juma A. Juma, Mb - Mjumbe10. Mhe.Lucia Ursula Michael Mlowe, Mb - Mjumbe11. Mhe.Dkt. Jasmine Tiisekwa, Mb - Mjumbe12. Mhe.Ahmed Ally Salum Mb - Mjumbe13. Mhe.Susan Anselm Lyimo, Mb - Mjumbe14. Mhe.Juma Selemani Nkamia, Mb - Mjumbe15. Mhe.Seleman Said Bungara, Mb - Mjumbe16. Mhe.Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe, - Mjumbe17. Mhe.Boniphace Mwita Getere, Mb - Mjumbe

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

18. Mhe.Bernadeta K. Mushashu,Mb - Mjumbe19. Mh.Hussein Nassor Amar, Mb - Mjumbe20. Sikudhani Yassin Chikambo, Mb - Mjumbe21. Savelina Sylvanus Mwijage, Mb - Mjumbe22. Jaku Hashim Ayoub, Mb -Mjumbe

Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru kwa dhatiWatumishi wa Ofisi ya Bunge, wakiongozwa na Dkt. ThomasD. Kashililah, Katibu wa Bunge, Ndugu Athman BrambathHussein Mkurugenzi Idara ya Kamati za Bunge na NduguDickson Bisile Mkurugenzi Msaidizi kwa kuisaidia na kuiwezeshaKamati hii kutekeleza majukumu yake kwa weledimkubwa.Kipekee nawashukuru Ndg. Pamela Pallangyo naNdg. Agnes Nkwera (Makatibu Kamati) na Ndg.GaitanaChima msaidizi wao kwa kuratibu vyema kazi za Kamati nakuhakikisha kuwa Taarifa hii inakamilika kwa wakatiuliopangwa.

Mheshimiwa Spika,baada ya kusema haya, sasa naliombaBunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha2017/2018, kama yalivyowasilishwa na mtoa hoja Fungu 52jumla ya shilingi Trilioni moja, Bilioni sabini na nane, Milionimia tatu arobaini na nne na Laki mbili na themanini na mbilielfu (1,078,344,282,000/=) na Fungu 53 jumla ya shilingi BilioniArobaini, Milioni Mia Moja na Thelathini, Laki Mbili na Kumina Tano na Mia Saba Themanini na Nne (40,130,215,784/=)

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na ninaunga mkonohoja.

Mh. Peter Joseph Serukamba (Mb),MWENYEKITI

KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII3 MEI, 2017

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

MWENYEKITI: Tunaendelea sasa namuita msemajiMkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, naonaMheshimiwa Ester Bulaya, karibu. (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA (K.n.y MSEMAJI MKUU WAUPINZANI KWA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana namuda naomba hotuba yote ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni iingie kwenye Hansard na nina furaha leo kusimamakwenye Bunge lako Tukufu nikiwa upinzani baada ya kuhamaCCM na sasa ni Mbunge wa Jimbo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Msemaji Mkuuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara yaMaendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, MheshimiwaGodwin Mollel, naomba kuwasilisha Maoni Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Wizara husikakwa mwaka wa fedha 2016/2017 na makadirio ya mapatona matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijawasilisha maonihayo, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kutujalia sisi sote afya njema na kutuwezesha kushirikimkutano wa Bunge la Bajeti tukiwa salama. Kipekeenamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kunilinda dhidiya njama na hila za shetani zenye lengo ovu la kudharirishajitihada zangu na Kambi nzima ya Upinzani katika kupiganiamisingi ya haki na demokrasia katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kutumia fursahii kumpongeza kwa dhati Kiongozi wa Kambi ya UpinzaniBungeni, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe kwa busarana moyo wake wa ujasiri ambao amefanikisha kuiunganishaKambi ya upinzani Bungeni, licha ya vikwazo na changamotonyingi zinazozikabiri siasa za upinzani hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongezaWaziri Kivuli wa Wizara hii, Mheshimiwa Godwin Mollel(Mbunge) na Naibu wake Mheshimiwa Zubeda Sakuru kwakazi kubwa waliyoifanya katika kuandaa hotuba hii.

Page 223: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa sina fadhila kamasitawashukuru sana wapiga kura wangu wa Jimbo la BundaMjini kwa kuendelea kuniamini na kunipatia ushirikianomkubwa katika kutekeleza majukumu yangu. Napendakuwaahidi utumishi uliotukuka na kamwe sitowaangushakatika kuhakikisha kwamba maendeleo ya Jimbo letuyanapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho lakini si kwaumuhimu, naishukuru sana familia yangu hasa mtoto wangumpendwa Brighton, kwanza kwa kunitia moyo lakini kwauvumilivu hasa pale ninapokuwa mbali nao kwa muda mrefukutokana na majukumu yangu ya Kibunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaanza kuzungumziamasuala ya afya naomba kumnukuu nguli wa Kiswahili namwanafalsafa mashuhuri Hayati Shaabani Robert, alisemahivi: “Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake, nikipatwa naajali kama hiyo sitawaonea wivu wale wanaodumu namarafiki zao siku zote, siweze kuikana kweli kwa kuhofiaupweke wa kitambo na kujinyima furaha ya mileleinayokaribia kutokea baada ya kushindwa kwa uoga.”(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno haya ni muhimu naya faraja sana kwa wote walioamua kusimama na kupingaunafiki mkubwa dhidi ya hofu, ubinafsi, ubabe, matisho,kujipendekeza, dhuluma na ufedhuli wowote juu ya haki.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika kutafakalimaneno haya ya Shaabani Robert ni vyema pia wenyemamlaka wakatambua ahadi namba nane ya TANUinayosema; “Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninadhani tafakari hiyoitatusaidia kusema ukweli na kutetea ukweli tunapojadili Bajetiya Wizara ya Afya, ambayo imebeba maisha ya Watanzaniawote. Tafakuri hiyo itatusaidia kuponya afya na nguvu yaTaifa hili. (Makofi)

Page 224: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Salamu hizo zautangulizi sasa naomba nianze kuzungumzia masualayaliyomo katika hotuba. Hotuba hii imebeba mambomuhimu yafuatayo; mkanganyiko wa kiutendaji ndani yaWizara ya Afya, hali ya sekta ya afya nchini, upungufu wavituo vya kutolea huduma ya afya nchini, ongezeko kubwala wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na vitengovyake, upungufu wa watumishi katika sekta ya afya, hudumaya afya ya mama na mtoto, uhaba wa chanjo nchini,changamoto za kibajeti katika utatuzi wa vifo vitokanavyona afya ya uzazi, kukabiliana na tatizo la akili nchini, lisheduni na ongezeko la utapiamlo na udumavu, kansa yashingo ya uzazi, udhibiti na upungufu wa dawa nchini,ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukizwa na atharizake, ongezeko kubwa la wagonjwa Hospitali ya TaifaMuhimbili na vitengo vyake, wanawake na usawa wa kijinsia,masuala ya watoto, ukatili dhidi ya watoto, Vyuo vyaMaendeleo ya Jamii na utekelezaji wa Bajeti ya Wizara yamwaka wa fedha 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na mkanganyikowa utekelezaji ndani ya Wizara ya Afya; kumekuwepo namkanganyiko mkubwa juu ya utendaji wa Wizara ya Afyahapa nchini. Wizara hii imekosa uhuru wa kiutendaji nautekelezaji wa shughuli zake kutokana na kuingiliana naWizara nyingine. Mkanganyiko huu umesababisha usumbufumkubwa kwa wananchi na wadau wa afya hususan katikamasuala ya kiutawala, masuala ya kutoa huduma nakupokea huduma kwenye hospitali za wilaya mpakazahanati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na mkanganyikohuu, Wizara imeshindwa kutoa majibu mahsusi kwenyechangamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya kwakigezo kuwa masuala mengine yako chini ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI na mengine chini ya Ofisi ya Rais - Manejimenti yaUtumishi wa Umma. Hivyo Wizara hizi huishia kutupiana mipirapale linapotokea suala la uwajibikaji. Tutambue kuwa nivigumu sana kwa Waheshimiwa Wabunge kuongelea Wizara

Page 225: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

ya Afya, bila kuongelea pale walipo wapiga kura wao auwanapoishi Watanzania walio wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Afya kwa mujibuwa hati idhini pamoja na mambo mengine inasimamia Seraya Afya na huduma za kinga na tiba, kusimamia na kudhibitiubora wa dawa, vifaa na vifaa tiba, kusimamia mpangowa afya ya uzazi na mtoto, kuendesha ukaguzi wa hudumaza afya katika ngazi mbalimbali, kuongoza na kusimamiataasisi zote zilizopo chini ya Wizara hii na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkawanyiko mkubwaunajitokeza pale ambapo Wizara ya Afya inapokaa pembenikatika kuhakikisha kuwa zahanati, vituo vya afya, na Hospitaliza Wilaya zinakuwa chini ya jukumu lake la msingi badala yakuiachia majukumu mengine Ofisi ya Rais – TAMISEMI napengine Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kuhakikisha Wizara hii inafanya kazi zake vizurikwa kuweka mfumo utakaoipa Wizara mamlaka kamili katikautekelezaji wa majukumu yake yote badala ya kutumiamuingiliano wa kimajukumu kama kichaka cha kukwepautekelezaji wa majukumu ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upungufu wa vituovya kutolea huduma za aya nchini; hali ya vituo vya kutoleahuduma ya afya nchini ni mbaya sana. Siku zote Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni imekuwa ikilisemea jambo hili, lakiniSerikali haijalichukulia kwa uzito wake. Upatikanaji na utoajiwa huduma za afya umekuwa na changamoto lukukiukiwemo ufinyi wa bajeti, upungufu wa watoa huduma zaafya, ukosefu wa mawasiliano, usafiri na uhaba wa vitendeakazi na zaidi uwepo wa mikakati isiyoendana na mabadilikoya kimaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ina maana kwambamikakati mingi tuliyonayo katika sekta ya afya nchini haiwezikutatua changamoto za afya, kutokana na kushindwakuzingatia mabadiliko ya kiuchumi na kiteknolojia. Tafiti

Page 226: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

zilizochapishwa na jarida la uchumi na fedha la nchiniCanada mwezi Julai, 2016 zilieleza kwa kina kwambamatokeo ya tafiti il iyofanywa nchini Tanzania juu yachangamoto ya upatikanaji wa huduma za afya nchinizinaonesha kuwa takribani asil imia 45 ya wananchiwanapata huduma za afya ndani ya kilometa moja hukuasilimia 93 wakilazimika kutembea kwa zaidi ya kilometa 10kufuata huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Shirika la SIKIKAlilibaini takribani asilimia 80 ya Watanzania waishio vijijinihutembea zaidi ya kilometa tano kufuata huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanalazimikakwenda mbali sana kutafuta huduma za afya, haliinayopelekea kuongezeka kwa vifo ambavyo vingewezakuepukika endapo huduma zingepatikana kwa urahisi katikamaeneo ya karibu. Maeneo mengi ya nchi bado hayanazahanati za kutosha, vituo vya afya na hata Hospitali za Wilayaambapo vituo hivyo vya kutolea huduma vinapaswa kuwakaribu zaidi na wananchi hususani maeneo ya vijijini. Pamojana hayo yapo maeneo ambayo Hospitali za Wilaya zinabebamajukumu makubwa ya Hospitali za Mikoa na vituo vya afyavinabeba majukumu ya Hospitali za Wilaya na kadhalika.Sisi Waheshimiwa Wabunge tumeyashuhudia hayo katikamaeneo yetu

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kwa mudamrefu sasa, Kituo cha Afya cha Manyamanyama kilichopoBunda Mjini, kimekuwa kikitumika kama Hospitali ya Wilayahuku mgao na vifaa tiba vikiendelea kutolewa kwa mgaowa vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwa kituo hikikimekuwa kikitoa huduma kubwa na muhimu kwa wananchiwa Bunda kutokana na umuhimu wake wa kijiografia badompaka leo kituo hiki cha afya hakina chumba cha kuhifadhiamaiti, jambo ambalo limesababisha kituo hiki kushindwakupandishwa hadhi kwa muda mrefu sana huku majukumuyake yakibeba hadhi ya Hospitali ya Wilaya. (Makofi)

Page 227: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo Hospitali yaMji wa Tarime ambayo inatumika kama Hospitali ya Wilayainahudumia idadi kubwa sana ya wananchi wanaotokamaeneo mbalimbali ndani na nje ya Mji wa Tarime. Baadaya Halmashauri kugawanywa Serikali ilishusha hadhi Hospitalihii ya Wilaya kuwa Hospitali ya Mji huku Mganga Mkuu wakeakiwa ni TMO. Bado mpaka leo kwenye vitabu hospitali hiiinasomeka kama Hospitali ya Wilaya ya Tarime. Hospitali hiiimekuwa ikielemewa na mzigo mkubwa ya kutoa hudumakuliko uwezo wake kwani watu wanaotoka nje ya Mji waTarime hutumia Hospitali hii pia. Tukumbuke kuwaHalmashauri ya Mji wa Tarime haina hata kituo kimoja chaafya, japo Serikali iliahidi kujenga vituo vinne katika mwakawa fedha 2016/2017. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo makubwayanayojidhihirisha hapa ni pamoja na Serikali kushindwakuweka mipango ya ufuatiliaji wa vituo vya kutolea hudumaya afya vinavyoendana na uhitaji wa huduma ya afya.Kugawa majimbo kisiasa bila kuzingatia huduma za msingiza eneo husika, idadi ya watu na rasilimali zilizopo, Serikalikukosa mpango wa uendelezaji na ufuatiliaji wa mipangoinayojiwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni, inaitaka Serikali kuacha kuwahadaa katika masualaya kimsingi ya afya za wananchi. Tabia ya Serikali ya kuwekapamba masikioni pale ambapo Waheshimiwa Wabungewanaleta kero hizi za msingi zinazohitaji ufumbuzi wa harakalakini inachukua takribani miaka kumi mpaka ishirini kutatuatatizo dogo inazidi kudhihirisha kuwa hatuwezi kupatasuluhisho la matatizo kwa kutegemea uwelewa ule uleuliotengeneza tatizo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upungufu wawatumishi katika sekta ya afya; hatuwezi kuizungumziaWizara ya Afya bila kugusia suala la watumishi ndani yaWizara hii. Uhaba wa wahudumu wa afya ni tatizo sugulinaloonekana kuielemea Serikali. Tatizo hili lipo kwenye ngazizote kuanzia kwenye zahanati, vituo vya afya, Hospitali za

Page 228: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

Wilaya, Mikoa, Hospitali ya Taifa na linalenga taaluma zoteza afya ambapo ni madaktari, wauguzi, mafundi sanifu,wataalamu wa miale, wafamasia, watoa dawa na maafisadawa wasaidizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa ripoti yamadaktari wenza wa Afrika Kusini, ukuaji wa rasilimali watukwa ajili ya afya katika Tanzania; Tanzania ina upungufu wawataalamu wa afya kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, madaktari bingwa ni kwaasilimia 58.1; wauguzi wa sekta ya umma ni kwa asilimia54.4; wataalamu wa miale ni kwa asilimia 50.8; maafisa klinikini kwa asilimia 50; waganga wasaidizi na waganga wasaidiziwa meno ni kwa asilimia 46.2; wafamasia ni kwa asilimia49.9; mabwana afya ni kwa asilimia 45.7; mafundi sanifu wamaabara ni kwa asilimia 41.5; maafisa kliniki wasaidizi ni kwaasilimia 40.7; madaktari kwa asilimia 37.3; maafisa wauguziasilimia 33.2 na makatibu wa afya ni kwa asilimi 27.1.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonesha pia,kwamba zaidi ya asilimia 74 ya madaktari waliopo nchini,wanafanya kazi maeneo ya mijini, hii ina maana kwambawafanyakazi walio wengi ambao wanaishi vij i j iniwanahudumiwa na asilimia 26 tu ya madaktari. Aidha,uwiano kati ya daktari mmoja na wagonjwa anaohudumiani wa kutisha, daktari mmoja anahudumia wagonjwa 77,880kwa maeneo ya vijijini kinyume kabisa na maelekezo ya Shirikala Afya Duniani ambapo daktari mmoja anatakiwakuhudumia wagonjwa elfu moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba huu mkubwa wawatumishi katika sekta ya afya umekuwa ni j ipulililoshindikana kutumbuka. Pamoja na uhaba huu mkubwawa watumishi, Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kuwekaafya za Watanzania rehani kwa kuruhusu hao hao madaktariwachache ambao ndio tegemeo la Watanzania kwendanchini Kenya kuwahudumia raia wa Kenya huku raia wakewakipata adha kubwa ya matibabu.(Makofi)

Page 229: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jambo hilolililokosa uzalendo, mwezi April mwaka huu wa 2017 Waziriwa Afya alitangaza kuwa Mheshimiwa Rais ameamurumadaktari 258 walioomba kufanya kazi Kenya waajiriwe maramoja. Jambo hili si tu limewashangaza Watanzania baliulimwengu kwa ujumla. Serikali hii imefanya maamuzi yaajabu ambayo hayakuwahi kutokea katika historia ya nchihii tangu uhuru. Kitendo cha Serikali kuwaajiri madaktariwalioomba ajira nje ya nchi na kuwatupia kapuni mamia yamadaktari ambao kwa namna moja au nyingine walioneshauzalendo wa kutamani kuitumikia nchi yao ni kitendo chakibaguzi na kikatili sana kwa wazalendo wa nchi hii.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinapata wasiwasi juu ya uwezo wa Serikali katika kuratibuna kupambana na vipaumbele vyake. Serikali imeshindwakabisa kujua kama Nchi hii ina huduma duni za afya nainakabiliwa na uhaba wa watendaji katika sekta ya afyakuliko Kenya. Katika ripoti ya Benki ya Dunia ya mwezi Mei,2016 inaonesha kuwa utendaji wa sekta ya afya namaendeleo ya sekta hii katika nchi mbalimbali, ikiwemoTanzania na Kenya, Serikali hii pengine itueleze na itoetakwimu sahihi juu ya watumishi katika sekta ya afya kwakuwa hali inaonesha dhahiri takwimu hizo hazikuwepoWizarani na ndiyo maana Serikali ikawa radhi kupelekamadaktari nje ya nchi ilhali hospitali nyingi majimbonizinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madaktari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wahenga wanasemamtu mzima akivuliwa nguo huchutama, hivyo basi Serikali nilazima ijue kuwa il ipotoka na ij isahihishe katika hil i.Hatuwezi kuendelea kuhubiri uzalendo kwa maneno bilavitendo. Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza mamboyafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Serikali itoe tamkokuhusu maamuzi yake ya kutaka madaktari waende nchiniKenya kutoa huduma kwa wananchi wa Kenya huku ikijuaTanzania tuna uhaba mkubwa wa watoa huduma wa afya.(Makofi)

Page 230: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

Pili, Serikali ieleza Bungeni mpaka sasa mwaka 2017Tanzania inakabiliwa na uhaba wa watumishi wa afya kwaasilimia ngapi na huku ikizingatia kuwa kwa muda mrefuilisitisha zoezi la kutoa ajira nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, Serikali ituambieimepanga kutoa ajira ngapi katika sekta ya afya kwa mwakahuu wa fedha 2017/2018 zenye uhakika katika utelekezaji?Katika hili Serikali izingatie imewaacha mamia ya madaktariwakikosa ajira nchini kwa sababu ya uzalendo wao wakutamani kuitumikia nchi zaidi kuliko kwenda nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitendo cha madaktari 258kujitokeza kwenda nchini Kenya kimeonesha kuwa kunamadaktari wengi nchini ambao wanapenda kufanya kazinje ya nchi kwa sababu mbalimbali. Je, Serikali ina mpangogani wa kuhakikisha maslahi ya watumishi katika sekta yaumma yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na kuhakikishawanapata call allowance, overtime na nyumba za watumishiwa afya hususan maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ustawi wa jamii,wanawake na usawa wa kijinsia; usawa wa kijinsia ni nyenzomuhimu katika kufikisha maendeleo endelevu ya Taifa.Changamoto kubwa inayowafanya wanawake washindwekukabiliana na usawa wa kijinsia ni pamoja na uwepo wamila na desturi zinazomkandamiza mwanamke. Hii nipamoja na changamoto ya Sheria kandamizi ya Ndoa yamwaka 1971 ambayo inaendelea kukandamiza watoto wakike na kuchochea ndoa za utotoni; Sheria ya Mirathi yaKimila, tohara kwa watoto wa kike, watoto wanaopataujauzito shuleni kukosa fursa ya kuendelea na masomo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa na tatizo kubwala kutisha la ongezeko la ndoa na mimba kwa watoto wenyeumri wa kwenda shule na wale walio mashulen nchini. Kwamujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani iliyotolewa mweziJanuari, 2016 inaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya tatu BaraniAfrika kwa matukio ya mimba na ndoa za utotoni ikiongozakwa takribani asilimia 28. Hii ina maana kwamba watoto

Page 231: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

wengi chini ya umri wa miaka 18 wanajihusisha na vitendovya ngono visivyo salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 Katibu Mkuuwa Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee naWatoto alithibitisha kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwala mimba kwa wasichana wenye umri kuanzia miaka 15mpaka 20, na ongezeko hili asilimia 28 ni kwa kipindi chamwaka 2015/2016 pekee ikilinganishwa na mwaka 2010ambapo tatizo hilo lilikuwa asilimia 10 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Idadi ya WatuDuniani lilibaini kuwa kila kwenye wasichana kumi wenye umrikati ya miaka 12 mpaka 16 kati yao wanne wamepatamimba. Pamoja na hilo lilibaini kuwa kwa wastani wasichanawawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka18 hususani kwa maeneo ya vijijini. Vilevile Shirika laKuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) katika ripoti ya mwaka2012 lilibaini kuwa mikoa ifuatayo inaongoza kwa tatizo lamimba na ndoa za utotoni, Shinyanga ni asilimia 59, Taboraasilimia 58, Mara asilimia 55, Dodoma asilimia 51 na Lindiasilimia 48.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mapitio ya tafitimbalimbali zilizofanywa kitaifa na kimataifa Kambi yaUpinzani imebaini kuwa ongezeko la mimba za utotonilinatokana na kushuka kwa kipato cha familia, kubadilikakwa mfumo wa maisha ambapo wazazi wengi wamekuwawakitumia muda mwingi katika shughuli za kujipatia kipatona hivyo kuwa na muda kidogo kwa malezi, kukua kwateknolojia hususan matumizi ya simu ya mkononi kwa mjiniambapo watoto wa kike hulaghaiwa na vijana kwakuahidiwa simu; kushuka kwa hali ya kujifunza na mfumowa elimu nchini, ukosefu wa ajira hususani kwa vijana wakiume, kubadilika kwa mfumo wa maisha ambapoutamaduni uliokuwa umejengeka katika jamii kuwa mtotowa jamii sasa unabakia na mtoto anaonekana kama ni wafamilia pekee na hivyo jamii kujiondoa katika ulinzi wa mtotowa kike.

Page 232: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili la ndoa na mimbaza utotoni limekuwa na mtazamo mkubwa kwani jamiiimekuwa na maoni tofauti kutokana na makundi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masuala ya watoto;watoto ni rasilimali muhimu ya maendeleo ya Taifa lolote, iliwatoto waweze kukua na kuwa raia wema, wanahitajikupewa haki zao za msingi ambapo ni pamoja na kuishi,kulindwa, kuendelezwa, kutobaguliwa na kushirikishwa. Hayayote yanaongozwa na Sera ya Mtoto ya mwaka 2008 nakutunga Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009. Aidha,uanzishwaji wa madawati ya jinsia na watoto katika vituovya polisi nchini pamoja na kutoa mafunzo kwa polisi hususanmasuala ya madawati hayo hayajaongeza ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukatili dhidi ya watoto.Vitendo vya kikatili dhidi ya watoto vimekuwa vikishamirinchini, mifano hai ni kama ifuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Juni 27, 2016 katika kitongojicha Moha, kijiji cha Ilugu, kata ya Nyigogo, tarafa ya ItumbiliWilayani ya Magu Mkoani Mwanza, Julius Leonard aliyekuwana umri wa miaka saba aliuawa kwa kupigwa fimbo nababa yake wa kambo Leonard Joseph kwa kuchelewa kurudinyumbani baada ya kutumwa kwenda kuchukua battery.Mtoto huyu alipigwa mpaka kifo na mwili wake baada yakuchunguzwa na madaktari ulionyeshwa kuvilia damu ndanikutokana na fimbo hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa bajeti yaWizara kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa Fungu 52 nikuwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti inaonesha kuwa hadimwezi Machi, 2017 Wizara ilikuwa imetengewa jumla yashilingi 319,000,000,000 sawa na asilimia 40 ya bajeti ya Wizaraikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida pamoja na miradiya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kuhusu fedhaza maendeleo, randama zinaonesha kuwa hadi mweziMachi, 2017 ni asilimia 37 tu ya fedha za ndani ndizo

Page 233: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

zilizotolewa Hazina, na kwa fedha za nje ni asilimia sita tu yafedha hizo zilizokuwa zimetengwa na Hazina kwa kipindihicho. Hii ina maana ya kwamba bajeti ya maendeo kwafedha za ndani haijatekelezwa kwa asilimia 63, na kwa fedhaza nje haijatekelezwa kwa asilimia 94. Kwa utekelezaji huuduni wa bajeti ya maendeleo katika fungu hili Kambi Rasmiya Upinzani ina mtazamo kwamba Serikali haiko makini kabisana afya ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Fungu 53 kwa mwakawa fedha 2016/2017 Bunge liliidhinisha jumla ya shilingi bilioni49.9. Kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida 41,000,000,000na shilingi 8,848,000,000 zikiwa ni fedha za maendeleo. Hatahivyo, fedha za maendeleo zilizotolewa hadi kufikia Machi,2017 ni shilingi 497,000,000 sawa na asilimia 5.62 tu ya shilingi8,000,000,000 zilizoidhinishwa na Bunge hili. Hii maana yakeni kwamba bajeti ya maendeleo katika fungu hili lamaendeleo ya jamii haikutekelezwa taktribani asilimia 95.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu hili ndilo linalohusikana vyuo vya maendeleo ya jamii, na kwa maana hiyoutekelezaji duni wa bajeti wa vyuo hivyo haviwezi kuwa nauwezo wa kujiendesha na kuzalisha wataalam wa kuzisaidiajamii zetu kujiletea maendeleo kwa kuweza kuibua fursa hizokatika jamii zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho; Serikali hii yaAwamu ya Tano imekuwa ikij igamba kuwa afya nimojawapo ya vipaumbele katika utekelezaji wa majukumuyake. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilitegemea hayoyaonekane katika utekelezaji wa bajeti ya maendeleo kwaangalau kwa kutenga asilimia 80 ili kuudhihirisha uhalisia wamajigambo ya hapa kazi tu. Tofauti na tegemeo hilo, Wizarahii ni miongozi mwa Wizara zinazoongoza kwa utekelezajiduni wa bajeti ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya Wizara hii kusemakwamba mojawapo ya vipaumbele vyake kwa mwaka wafedha 2016/2017 ni kusimamia upatikanaji wa huduma zaustawi wa jamii kwa wazee, imewasahau wazee kabisa.

Page 234: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

Ikumbukwe kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ilishatoauamuzi wa kuwapatia mafao ya uzeeni wazee wote lakiniSerikali hii ya Awamu ya Tano imeweka kapuni azimio hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatoa rai kwa Serikali kuacha kufanya mzaha na afya zaWatanzania. Serikali iache kuwahadaa wananchi kwakutenga bajeti kubwa ya kushindwa kuitekeleza. Ni vemaSerikali ikapanga mipango inayotekelezeka kuliko kupangamipango yenye lengo la kukidhi matakwa ya kisiasa nakuwaacha wananchi wakihangaika. Ili kukabiliana namaadui watatu yaani umaskini, ujinga na maradhi ni lazimauwekeze katika afya ya uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kuwasilisha.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Ester Bulayakwa niaba ya Kambi Rasmi humu Bungeni tunakushukurusana.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANIBUNGENI, MHESHIMIWA DR GODWIN OLOYCE MOLLEL (MB),

AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YAUPINZANI BUNGENI KUHUSU BAJETI YA WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WAZEE NA WATOTO KWA

MWAKA WA FEDHA WA 2017/2018 – KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

(Yanatolewa chini ya Kanuni za Bunge, Kanuni ya 99(9),toleo la mwaka 2016)

1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa GodwinOloyce Mollel (Mb), naomba kuwasilisha Maoni ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu utekelazaji wa bajeti yaWizara husika kwa mwaka wa fedha 2016/17 na makadirio

Page 235: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

ya mapato na matumizi ya wizara hiyo, kwa mwaka wafedha 2017/18.

Mheshimiwa Spika, kabla sijawasilisha maoni hayo, naombakutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujaliasisi sote afya njema, na kutuwezesha kushiriki Mkutano huuwa Bunge la Bajeti tukiwa salama. Kipekee namshukuruMwenyezi Mungu kwa kuendelea kunilinda dhidi ya njamana hila za shetani zenye lengo ovu la kudhoofisha jitihadazangu na jitihada za Kambi nzima ya upinzani katikakupigania misingi ya haki na demokrasia katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hii,kumpongeza kwa dhati Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Mb), kwa busara namoyo wake wa ujasiri, ambapo amefanikiwa kuiunganishaKambi ya Upinzani Bungeni, licha ya vikwazo na changamotonyingi zinazokabili siasa za upinzani hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa sina fadhila, kamasitawashukuru sana wapiga kura wangu wa Jimbo BundaMjini, kwa kuendelea kuniamini na kunipatia ushirikianomkubwa katika utekelezaji wa majukumu yangu. Napendakuwaahidi utumishi uliotukuka na kamwe sitawaangushakatika kuhakikisha kwamba maendeleo ya Jimbo letuyanapatikana. Mwisho lakini si kwa umuhimu, naishukuru sanafamilia yangu, kwanza kwa kunitia moyo, lakini pili, kwauvumilivu wao hasa pale ninapokuwa mbali nao kwa mudamrefu, kutokana na majukumu yangu ya kibunge.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuzungumzia masuala yaafya, naomba kumnukuu nguli wa Kiswahili, na mwanafasihimashuhuri Hayati Shaabani Robert. Alisema hivi: “Msemakweli hukimbiwa na rafiki zake, nikipatwa na ajali kama hiyositawaonea wivu wale wanaodumu na marafiki zao sikuzote.Siwezi kuikana kweli kwa kuhofia upweke wa kitambona kujinyima furaha ya milele inayokaribia kutokea baadaya kushindwa kwa uongo”.

Page 236: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

Mheshimiwa Spika, Maneno haya ni muhimu na ya farajasana kwa wote walioamua kusimama na kuupinga unafikimkubwa dhidi hofu, ubinafsi, ubabe, matisho, kujipendekeza,dhulma na ufedhuli wowote juu ya haki. Aidha, katikakutafakari maneno hayo ya Shaaba Robert ni vema piawenye mamlaka, wakakumbuka ahadi namba nane ya TANUinayosema: “nitasema kweli daima na fitina kwangu mwiko”.Ninadhani tafakari hiyo itatusaidia kusema ukweli nakuutetea ukweli tunapojadili bajeti ya Wizara ya afya ambayoimebeba maisha ya watanzania wote. Tafuakuri hiyo,itusaidie kuponya afya na nguvu kazi ya taifa hili.

Mheshimiwa Spika, baada ya salamu hizo za utangulizi, sasanaomba nianze kuzungumzia masuala yanayohusu wizarahii.

2. MKANGANYIKO WA KIUTENDAJI NDANI YA WIZARA YAAFYA

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na mkanganyiko mkubwajuu ya utendaji wa Wizara ya afya hapa nchini. Wizara hiiimekosa uhuru wa kiutendaji, na utekelezaji wa shughuli zakekutokana na kuingiliana na wizara nyingine. Mkanganyikohuu umesababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi nawadau wa afya hususani katika masuala ya kiutawala,masuala ya kutoa huduma na kupokea huduma kwenyehospitali za wilaya mpaka zahanati.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mkanganyiko huu, Wizaraimeshindwa kutoa majibu mahususi kwenye changamotombalimbali zinazoikabili sekta ya afya kwa kigezo kuwamasuala mengine yapo chini Ofisi ya Rais - TAMISEMI namengine chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi waUmma. Hivyo, Wizara hizi huishia kutupiana mpira palelinapotokea suala la uwajibikaji.

Mheshimiwa Spika, tutambue kuwa ni vigumu sana kwawaheshimiwa wabunge kuongelea wizara ya afya bila yakuongelea pale walipo wapiga kura wao, au wanapoishiwatanzania walio wengi. Wizara ya afya kwa mujibu wa hati

Page 237: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

Idhini pamoja na mambo mengine, inasimamia sera ya afyana huduma za kinga na tiba, kusimamia na kudhibiti uborawa dawa, vifaa na vifaa tiba, kusimamia mpango wa afyaya uzazi na mtoto, kuendesha ukaguzi wa huduma za afyakatika ngazi mbalimbali, kuongoza na kisimamia taasisi zotezilizopo chini ya Wizara hii n.k

Mheshimiwa Spika, mkanganyiko mkubwa unajitokeza paleambapo Wizara ya afya inapokuwa pembeni katikakuhakikisha kuwa zahanati, vituo vya afya, na hospitali zawilaya zinakuwa chini ya jukumu lake la msingi badala yakuiachia majukumu mengine Ofisi ya Rais TAMISEMI na pengineMenejimenti ya Utumishi wa umma. Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka serikali kuhakikisha Wizara hii inafanya kazi zake vizurikwa kuweka mfumo utakaoipa Wizara mamlaka kamilikatika kutekeleza majukumu yake yote badala ya kutumiamwingiliano wa kimajukumu kama kichaka cha kukwepautelekezaji wa majukumu ya Wizara hii.

3. HALI YA SEKTA YA AFYA NCHINI

Mheshimiwa Spika, Sote tunatambua suala la afya ni sualala ‘msingi’ katika ustawi wa taifa (primary concern). Ilikuhakikisha taifa linakuwa na watu wenye afya bora, serikaliina jukumu la kuhakikisha hali ya utoaji huduma ya afya mijinina vijijini inaboreshwa ili kupunguza maradhi, vifo na hivyokuongeza umri wa kuishi (life span).

Mheshimiwa Spika, katika azimio la Alma Ata la mwaka 1978,(Declaration of Alma Ata), liliazimia kuwa nchi zote dunianini lazima kuwa na huduma za afya ya msingi (Primary healthcare) mpaka mwaka 2000. Azimio hilo lilikwenda mbali zaidilikizitaka nchi zote kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma zaafya haziishii kwenye kupunguza magonjwa tu bali piakuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa katika utoajiwa huduma za afya na tiba.

Mheshimiwa Spika, Mpaka sasa Serikali hii ya CCM haijawezakutekeleza azimio hili la Alma Ata ipasavyo, kutokana nakushindwa kutoa huduma za afya za msingi zinapatikana

Page 238: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

kwa uhakika hususani maeneo ya vijijini, na pia imeshindwakutoa huduma hizo kwa ubora.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Tume ya Takwimu nchini(NBS) kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, jumla ya hospitaliza serikali na zile za binafsi ni 252 sawa na 3.4%, vituo vyaafya 718 sawa na 9.5%, na jumla ya zahanati 6549. Hii ikiwani jumla ya vituo 7,519 vinavyotoa huduma za afya nchinzima. Hii ina maana kwamba takribani wananchi milioni56 kwa mujibu wa tume ya Taifa ya takwimu ya mwezi March2016, wanategemea idadi hii ndogo ya vituo vya kutoahuduma ya afya nchi nzima ambapo kimsingi idadi hiihaikidhi hata nusu ya mahitaji yanayoendana na ongezekohili la watu nchini.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa idadi ya watu nchiniinakuwa kwa kasi sana huku miundo mbinu hii ya afyaikishindwa kuendana na kasi ya ukuaji huo. Kwa mujibu waTakwimu za Tanzania Demographic and Heath Survey (TDHS)2015/16, wastani wa kujifungua kwa wanawake wa Tanzaniani kuanzia watoto 5.2. Hii ina maana kwamba idadi ya watunchini itaendelea kuongezeka kwa kuwa mpaka sasawastani wa kujifungua kwa wanawake waishio vijijini nikuanzia watoto 6.

Mheshimiwa Spika, ongezeko hil i kubwa na la kasilinaonyesha kwamba, nchi ni lazima iwe na mpango waukuaji wa sekta ya afya unaoendana na kasi ya ukuaji wawatu na teknolojia. Ikiwa na maana ya kuongeza hospitaliza utoaji wa huduma maalum, hospitali za rufaa za Kanda,Mikoa, Wilaya, mpaka zahanati zenye uwezo wa kutoahuduma kwa wagojwa wengi zaidi ili kupunguza idadi yavifo vinavyotokana na magonjwa ambayo yangewezakupata tiba (Death due to illness)

Mheshimiwa Spika, Mpaka sasa takribani Kanda tatu hazinahospitali za Rufaa za Kanda kuacha hospitali za Rufaa zaMikoa. Mfano, Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Singida,na Dodoma ambapo ndipo Makao Makuu ya nchi hakunahospitali ya Rufaa ya Kanda ukiachilia mbali za mikoa na

Page 239: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

hospitali ya magonjwa maalum ya Mirembe. Hali kadhalikakwa kanda ya Kusini yenye mikoa ya Lindi na Mtwara naKanda ya Magharibi mikoa ya Katavi, Tabora na Kigoma.Mikoa yote hii imekuwa ikitegemea hospitali za mikoa pekeeambazo zinazidiwa na wingi wa wagonjwa na haziendanikabisa na ongezeko la idadi ya watu katika mikoa husika.

Mheshimiwa Spika, katika Mpango wa Maendeleo wa Taifawa miaka mitano (National Five Year Development Plan2016/17-2020/21 ukurasa wa 266; serikali ilikusudia kutengashilingi bilioni 80 kwa mwaka wa fedha 2016/17 na bilioni 80pia kwa mwaka 2017/18 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali zaKanda ya Kusini, Magharibi, Kaskazini na Kanda ya Ziwa ilikupunguza tatizo la uhaba wa hospitali nchini .

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujuaje, serikali imeanza kujenga hospitali hizo za Rufaa za Kandakama zinavyoonyeshwa katika Mpango wa Mandeleo wamiaka mitano? Na kama bado, serikali ina mpango ganiwa kuhakikisha kuwa hospitali hizo zinajengwa kamailivyokusudiwa katika mpango huo?

4. UPUNGUFU WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYANCHINI

Mheshimiwa Spika, hali ya vituo vya kutolea huduma za afyanchini ni mbaya sana. Siku zote Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni imekuwa ikilisema jambo lakini serikali haijalichukuliakwa uzito wake. Upatikanaji na utoaji wa huduma za afyaumekuwa na changamoto lukuki zikiwemo ufinyu wa bajeti,upungufu wa watoa huduma za afya,ukosefu wamawasiliano, usafiri na uhaba wa vitendea kazi na zaidiuwepo wa mikakati isiyoendana na mabadiliko yakimaendeleo.

Mheshimiwa Spika, hii ina maana kwamba mikakati mingituliyonayo katika sekta ya afya nchini haiwezi kutatuachangamoto za afya kutokana na kushindwa kuzingatiamabadiliko ya kiuchumi kijamii na kiteknolojia.

Page 240: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Mheshimiwa Spika, Katika tafiti zilizochapishwa na jarida lauchumi na fedha la nchini Canada Mwezi Juni 2016, lilielezakwa kina matokeo ya tafiti iliyofanywa nchini Tanzania juuya changamoto za upatikanaji wa huduma za afya nchini(Challenges hindering the accessibility of Tanzania’s healthservices) zinaonyesha kuwa takribani 45% ya wananchiwanapata huduma za afya ndani ya kilometa 1, huku 93%wakilazimika kutembea zaidi ya kilometa 10 kufuata hudumaza afya. Vilevile Shirika la Sikika lilibaini takribani 80% yaWatanzania waishio vijijini hutembea zaidi ya kilometa 5kupata huduma ya afya.

Mheshimiwa Spika, wananchi wanalazimika kwenda mbalisana kutafuta huduma za afya hali inayopeleka kuongezekakwa vifo ambavyo vingeweza kuepukika endapo hudumazingepatikana kwa urahisi katika maeneo ya karibu. Maeneomengi ya nchi bado hayana zahanati za kutosha, vituo vyaafya na hata hospitali za wilaya ambapo vituo hivi vyakutolea huduma vinapaswa kuwa karibu zaidi na wananchihususani maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, yapo maeneo ambayohospitali za wilaya zinabeba majukumu makubwa yahospitali za mikoa na vituo vya afya vikibeba majukumu yahospitali za wilaya n.k Sisi Waheshimiwa Wabungetumeyashuhudia hayo katika maeneo yetu. Mfano, kwamuda mrefu sasa, kituo cha afya cha Manyamanya kilichopoBunda mjini kimekuwa kikitumika kama hospitali ya Wilayahuku mgao wa bajeti na vifaa tiba vikiendelea kutolewakwa mgao wa vituo vya afya.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na kuwa kituo hiki kimekuwakikitoa huduma kubwa na muhimu kwa wananchi wa Bundakutokana na umuhimu wake kijografia, bado mpaka leokituo hiki cha afya hakina chumba cha kuhifadhia maitijambo ambalo limesababisha kituo hiki kushindwakupandishwa hadhi kwa muda mrefu sana huku majukumuyake yakibeba hadhi ya hospitali ya Wilaya.

Page 241: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

Mheshimiwa Spika, Pamoja na hilo, hospitali ya mji wa Tarimeambayo inatumika kama hospitali ya Wilaya inahudumiaidadi kubwa sana ya wananchi wakutoka maeneombalimbali ndani na nje ya mji wa Tarime.Baada yahalmashauri kugawanywa serikali iliishusha hadhi hospitalihii ya Wilaya kuwa hospitali ya mji, huku mganga mkuu wakeakiwa ni TMO. Bado mpaka leo kwenye vitabu hospitali hiiinasomeka kama hospitali ya Wilaya ya Tarime (Tarime DistrictHospital).Hospitali hii imekuwa ikielemewa na mzigo mkubwawa kutoa huduma kuliko uwezo wake kwani watuwanaotoka nje ya mji wa tarime hutumia hospitali hii pia.Tukumbuke kuwa halmashauri ya mji wa Tarime haina hatakituo kimoja cha afya japo serikali iliahidi kujenga vituo vinnekatika mwaka wa fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, matatatizo makubwa yanayojidhihirishahapa ni pamoja na:

· serikali kushindwa kuweka mipango yaufuatiliaji wa vituo vya kutolea huduma yaafya vinavyoendana na uhitaji wa huduma yaafya

· Kugawa majimbo kisiasa bila kuzingatiahuduma za msingi za eneo husika, idadi yawatu na rasilimali zilizopo

· Serikali kukosa mpango wa uendelezaji naufuatiliaji wa mipango inayojiwekea.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni,inaitaka serikali kuacha hadaa katika masuala ya kimsingiya afya za wananchi. Tabia ya serikali ya kuweka pambamasikioni pale ambapo waheshimiwa wabunge wanaletakero hizi za msingi zinazohitaji ufumbuzi wa haraka lakiniinachukua takribani miaka kumi mpaka ishirini kutatua tatizodogo inazidi kudhihirisha kuwa “hatuwezi kupata suluhishola matatizo kwa kutegemea uwelewa ule ule uliotengenezatatizo hilo”.

Page 242: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

5. UPUNGUFU WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA

Mheshimiwa Spika, uhaba wa wahudumu wa afya ni tatizosugu linaloonekana kuielemea serikali. Tatizo hili lipo kwenyengazi zote kuanzia kwenye zahanati, vituo vya afya,hospitaliza wilaya, mikoa mpaka hospitali ya Taifa na linalengataaluma zote za afya ambazo ni madaktari, wauguzi,mafundisanifu,wataalamu wa miali, wafamsia, watoa dawa,na maafisa dawa wasaidizi.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti ya madaktariwenza wa Afrika (Africa Cuamm) ‘Ukuaji wa rasilimali watukwa ajili ya afya katika Tanzania’ ;Tanzania ina upungufu wawataalamu wa afya kama ifuatavyo:

· Madaktari bingwa (Specialist doctors) kwa58.1 %

· Wauguzi wa sekta ya umma II (Public healthnurses II ) kwa 54.4%

· Wataalamu wa miale (Radiographers) kwa50.8%

· Maafisa kliniki (clinical officers) kwa 50.0%

· Waganga wasaidizi na waganga wasaidiziwa meno( assistant medical officer/assistantdental officer) kwa 46.2%

· Wafamasia(pharmacist) 49.9%

· Mabwana afya (health officers) kwa 45.7%

· Mafundisanifu wa maabara (laboratorytechnicians) kwa 41.5%

· Maafisa kliniki wasaidizi (assistant clinicalofficers) 40.7%

Page 243: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

· Madaktari (medical doctors) kwa 37.3%

· Maafisa wauguzi (nursing officers) 33.2%

· Makatibu wa afya (health secretaries) kwa27.1%

· Makatibu wa afya (health secretaries) kwa21.8%.

Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonyesha pia kwamba, zaidiya asilimia 74% ya madaktari waliopo nchini, wanafanyakazi maeneo ya mijini. Hii ina maana kwamba, wananchiwalio wengi ambao wanaishi vijijini wanahudumiwa naasilimia 26 tu ya madaktari. Aidha uwiano kati ya daktarimmoja na wagonjwa anaohudumia ni wa kutisha. Daktarimmoja anahudumia wagonjwa 78,880 kwa maeneo ya vijijinikinyume kabisa na maelekezo ya Shirika la afya dunianiambapo daktari mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwaelfu moja. (1:1,000).

Mheshimiwa Spika, uhaba huu mkubwa wa watumishi katikasekta ya afya umekuwa ni jipu lililoshindikana kutumbulika.Pamoja na uhaba huu mkubwa wa watumishi, serikali yaawamu ya tano iliamua kuweka afya ya watanzania rehanikwa kuruhusu hao hao madaktari wachache ambao ndiotegemeo la watanzania kwenda nchini Kenya kuwahudumiaraia wa Kenya huku raia wake wakipata adha kubwa yamatibabu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Chama cha MadaktariTanzania (MAT) kupinga uamuzi wa serikali kupelekamadaktari 500 nchini Kenya, bado Serikali ilipuuza maoni yaChama cha madaktari mpaka pale serikali ya Kenyailipositisha ombi la uhitaji wa madaktari. Kitendokilichofanywa na serikali cha kuipigia debe nchi ya Kenya nakujigamba kuwapa madaktari huku ikijua dhahiri Tanzaniainakabiliwa na uhaba wa wataalamu hao pengine kulikonchi ya Kenya ni kitendo kisicho cha kizalendo na

Page 244: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

kimedhihirisha nia mbaya ya serikali ya awamu ya tano kwawananchi wake wanaoteseka kwa kukosa huduma za afya.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jambo hilo l i l i lokosauzalendo, Mwezi April mwaka huu wa 2017 Waziri wa Afyaalitangaza kuwa Mheshimiwa Rais ameamuru madaktari 258walioomba kufanya kazi Kenya waajiriwe mara moja. Jambohili sio tu limewashangaza Watanzania bali Ulimwengu kwaujumla. Serikali hii imefanya maamuzi ya ajabu ambayohayakuwahi kutokea katika historia ya nchi hii tanguuhuru.Kitendo cha serikali kuwaajiri madaktari walioombaajira nje ya nchi na kuwatupia kapuni mamia ya madaktariambao kwa namna moja au nyingine walionyesha uzalendowa kutamani kuitumia nchi yao ni kitendo cha kibaguzi nakikatili sana kwa wazalendo wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya upinzani, inapatawasiwasi juu ya uwezo wa serikali katika kuratibu nakupambanua vipaumbele vyake (coordination andprioritization). Serikali imeshindwa kabisa kujua kama nchihii ina huduma duni za afya na inakabiliwa na uhaba wawatendaji katika sekta ya afya kuliko Kenya. Katika ripoti yaBenki ya Dunia ya mwezi Mei, 2016, “Tanzania Service DeliveryIndicators”inaonyesha kuwa, utendaji wa sekta ya afya namaendeleo ya sekta hii katika nchi mbalimbali IkiwemoTanzania na Kenya. Serikali hii pengine itueleze na itoetakwimu sahihi, juu ya watumishi katika sekta ya afya kwakuwa hali inaonyesha dhahiri takwimu hizo hazikuwepowizarani na ndio maana serikali ikawa radhi kupelekamadaktari nje ya nchi ilhali hospitali nyingi majimbonizinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madaktari.

Mheshimiwa Spika, wahenga wanasema “mtu mzimaakivuliwa nguo huchutama”. Hivyo basi, serikali ni lazima ijuekuwa ilipotoka na ijisahihishe katika hili. Hatuwezi kuendeleakuhubiri uzalendo kwa maneno bila vitendo. Kuna mithaliya kingereza inasema “one’s first responsibility is for the needsof one’s own family” kwa tafsiri isiyo rasmi ikiwa na maanakwamba ‘jukumu binafsi la kwanza ni kwa ajili ya mahitaji ya

Page 245: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

familia yako mwenyewe’. Hivyo basi, Kambi rasmi ya upinzaniinapendekeza mambo yafuatayo:

i. Serikali itoe tamko kuhusu maamuzi yake yakutaka madaktari waende nchini Kenya kutoa huduma kwawananchi wa Kenya huku ikijua Tanzania tuna uhabamkubwa wa watoa huduma wa afya.

ii. Serikali ilieleza Bunge, mpaka sasa mwaka2017 Tanzania inakabiliwa na uhaba wa watumishi wa afyakwa asilimia ngapi huku ikizingatia kuwa kwa muda mrefuilisitisha zoezi la kutoa ajira nchini?

iii. Serikali ituambie imepanga kutoa ajira ngapikatika sekta ya afya kwa mwaka huu wa fedha 2017/18 zenyeuhakika katika utelekezaji? Katika hili serikali izingatieimewaacha mamia ya madaktari wakikosa ajira nchini kwasababu ya uzalendo wao wa kutamani kuitumia nchi zaidikuliko kwenda nje.

iv. Kitendo cha madaktari 258 kujitokeza kwendanchini Kenya kimeonyesha kuwa kuna madaktari wenginchini ambao wanapenda kufanya kazi nje ya nchi kwasababu mbalimbali.Je, serikali ina mpango gani wakuhakikisha maslahi ya watumishi katika sekta ya ummayanaboreshwa ikiwa ni pamoja wa uhakika wa kupata callallowance, overtime, na nyumba za watumishi wa afyahususani maeneo ya vijijini?

6. KANSA YA SHINGO YA KIZAZI

Mheshimiwa Spika, saratani ni miongoni mwa maradhimengi yanayoisumbua jamii kubwa duniani. Zipo saratani zaaina nyingi, lakini saratani ya shingo ya kizazi ndiyoinayoongoza kwa vifo vya akina mama. Takwimuzinaonyesha kwamba saratani ya shingo ya kizazihusababisha vifo 274,000 duniani kote kila mwaka, ambapokila baada ya dakika mbili, mwanamke mmoja hufarikikutokana na saratani ya shingo ya kizazi. Katika kila

Page 246: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

wanawake wawili wanaofariki kwa saratani, mmoja hufarikikwa saratani ya shingo ya kizazi.

Mheshimiwa Spika, asilimia 85 ya vifo vinavyotokana nasaratani ya shingo ya kizazi hutokea katika nchi zinazoendelea.Barani Afrika, kwa ukanda wa mashariki asilimia 33.6 yawanawake wote wanasadikiwa kuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo, navyo vinaitwa human papillomavirus (HPV).

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Daktari Bingwa wamagonjwa ya Saratani hapa Tanzania Dr. Harrison Chuwa nikwamba, wagonjwa wanaokwenda kutibiwa katika Hospitaliya Ocean Road, takriban wagonjwa 22,000 kwa mwaka niwagonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi. Aidha saratanihiyo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa -takriban 40% ya wagonjwa wote wa saratani hapa nchini.Ugonjwa huu huwaathiri wanawake wengi wa rika zotewalio katika umri wa kuzaa, ikiwapata zaidi wanawakewenye umri wa miaka 45 na kuendelea.

Mheshimiwa Spika, Ugonjwa huu huchukua zaidi ya miaka15 mpaka 20 kugundulika lakini kabla ya kujitokeza bayanahutokea mabadiliko kadhaa yanayoweza kugundulikamapema na kufanikiwa kuzuilika katika hatua za mwanzoni.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kabisa hospitali ya Ocean Roadimezidiwa na wingi wa wagonjwa wanaokwenda kupatahuduma ya mionzi. Wagonjwa hawa hulazimika kutumiafedha nyingi sana kusafiri mpaka jijini Dar es Salaam, malazina huduma nyingine katika hali hii ngumu ya maisha ilikufuata huduma ya mionzi jambo ambalo linawaongezeamsongo wa mawazo na kuugua zaidi.

Mheshimiwa Spika, serikali ni lazima iangalie jambo hili kwakina, na iwe na huruma kwa wananchi wake.Ni wakati sasani kkuona namna bora ya kuboresha huduma kwenyehospitali za mikoa,wapate mashine hizi ili kuokoa maisha yakina mama wengi na hata kurefusha maisha yao kwa

Page 247: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

kuwapunguzia msongo wa mawazo ambao piaunachangiwa na hali ngumu ya kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ugonjwa huu wa saratani yashingo ya kizazi unazidi kushamiri hapa nchini; na kwa kuwaugonjwa huu umekuwa sababu kubwa ya vifo vingi vya kinamama wenye umri uliotajwa; Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inataka kujua Serikali imeweka mkakati gani wamakusudi katika bajeti hii ya 2017/18 kukabiliana na ugonjwahuu ambao umepoteza maisha ya mama zetu?

7. HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Mheshimiwa Spika, katika dira ya Maendeleo ya Taifa 2025,lengo kuu la dira hiyo ilikuwa ni kuhakikisha maisha borakwa Watanzania wote(high quality of life for all Tanzanians)na kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inapewakipaumbele ili kufikia lengo. Hii ni pamoja na kutoa kipaumbekwa kina mama wa kitanzania kupata huduma bora ya afyakwa kuwa wao ndio walezi wa kwanza wa Taifa letu. Kwahiyo, ni muhimu sana kuboresha afya ya mama na mtotokwa kutoa huduma bora ya afya ya uzazi.

Mheshimiwa Spika, Bado idadi ya vifo vinavyotokana nauzazi kwa kina mama ni kubwa. Kwa mujibu wa ripoti yashirika la tafiti za afya lisilo la kiserikali la Sikika kuhusu ‘Tafsirirahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM2007-2017’inaonyesha kuwa akina mama 578 kati ya vizazihai 100,000 hufariki dunia kutokana na matatizo ya uzazi.Takwimu za serikali zinaonyesha makadirio ya takribani kinamama 42 hufariki kila siku kutokana na changamoto za uzazi.Hii ikiwa na maana kwamba, kina mama 1,255 hufariki kilamwezi na kina mama 15,056 hufariki kila mwaka. Taarifa hiyoinaonyesha pia kwamba, ni asilimia 46 tu ya kina mamaambao wanaojifungua chini ya uangalizi wa wataalamu waafya.

Mheshimiwa Spika , Kutokana na hali hiyo, serikaliisipochukuwa hatua mahususi tutapoteza kina mama wengiambao huleta faraja katika hii dunia kwa kutuletea watoto

Page 248: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

.Kwa uhalisia ni kwamba ,serikali haitaweza kuyafikia malengoya kupunguza vifo vya kina mama kutokana na kukosaumakini katika kutelekeza sera za afya kutokana nachangamoto za kibajeti, changamoto za miundo mbinuikiwemo vyumba za kujifungulia,magari ya kubebeawagonjwa na vifaa vya kufanyia upasuaji, elimu ya uzaziwa mpango na uzembe wa baadhi ya watoa huduma yaafya.

7.1 Uhaba wa Chanjo nchini

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/2017wananchi na wadau wa sekta ya afya walieleza malalamikoyao kuhusu upungufu wa dawa pamoja na chanzombalimbali ikiwemo chanjo za watoto wachanga.

Mheshimiwa Spika, chanjo kwa watoto wachanga nimuhimu sana katika kuimarisha afya ya mama na mtoto.Katika hali isiyokuwa ya kawaida chanjo muhimu kwawatoto wachanga wanazopatiwa mara tu baada yakuzaliwa zilipungua na kusababisha usumbufu mkubwa kwaakina mama mara baada ya kujifungua. Kwa upande wamijini chanjo nyingi za watoto zilikuwa zinapatikana kwenyehospitali binafsi ambapo bei yake si chini ya laki moja.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mapungufu mengiyaliyojitokeza kwenye suala la chanjo, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inahoji ni sababu gani zilizopelekea uhabawa chanjo nchini na kuleta kadhia kwa wananchi? Serikaliimejipanga vipi kukabiliana na changamoto hiyo kwamwaka wa fedha 2017/2018?

Mheshimiwa Spika, ni hivi majuzi tu Shirika la Afya dunianilimezindua mradi wa chanjo ya malaria katika nchi zaGhana, Kenya na Malawi kwa ajili ya majaribio. Ikumbukwekuwa malaria bado ni tatizo kubwa ambalo linawaathirizaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inapenda kufahamu je, serikali imefanyajuhudi gani kuhakikisha kuwa nchi yetu inanufaika na chanjohiyo huko baadae?

Page 249: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

7.2 Changamoto za Kibajeti katika Utatuzi wa VifoVitokanavyo na Afya ya Uzazi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/2017serikali ilitoa asilimia 25 tu ya fedha iliyotengwa kwa ajili yaupatikanaji wa huduma ya uzazi wa mama na mtoto.Pamoja na hilo fedha zilizotengwa kwa mwaka huu ni shilingibilioni 12 tu, tofauti na bajeti iliyopita ya shilingi bilioni 13kwa mujibu wa mchanganuo wa fedha za miradi yamaendeleo kwa mwaka 2017/18 kwa Wizara hii fungu 52.Mara nyingi fedha hizi zimekuwa hazitolewi kamazilivyopangwa na hivyo kushindwa kabisa kumaliza matatizoya afya kwa mama na mtoto na hivyo kuendelea kuchangiaongezeko la vifo vya mama na mtoto.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Wizarailitengeneza mfumo wa tathimini ya vifo vinavyotokana nauzazi (Maternal and Prenatal Death Review). Mfumo huuilitengenezwa tangu mwaka 2006 ambapo uliwatakawataalamu wa afya kuhakikisha wanafanya kikao maalumcha kuzungumzia, kutathimini na kutoa taarifa juu ya kifochochote kinachotokana na uzazi (case management).Lengo kuu la Shirika la afya duniani (WHO) katika kuanzishampango huo, ni kuhakikisha uwajibikaji wa hali ya juu kwawatoa huduma ya afya. Hata pale ambapo kifo cha mamakimetokea katika mazingira ya nyumbani inahitajika kikaocha kujadili chanzo cha kifo hicho.

Mheshimiwa Spika, Tathimini ya kifo chochote cha uzaziinapaswa kufanyika ndani ya masaa 24 na taarifa ya kifoinapaswa kuhifadhiwa katika jalada la marehemu. Mfumohuu wa MPDR unasaidia kupata taarifa zote zinazopelekeavifo wakati na baada ya kujifungua. Taarifa hizi ni muhimukwani zinasaidia katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,kutatua changamoto za ucheleweshaji wa rufaa na tathiminiya uwepo wa vifaa vinavyohitajika katika masuala yote yauzazi, pamoja na uwepo wa damu ya akiba kwa kina mamawakati ya kujifungua.

Page 250: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaonauzembe mkubwa ndani ya wizara hii ambapo fedha nyingizinatumika katika kutengeneza program nyingi lakiniutekelezaji wake unakuwa hafifu sana. Kambi Rasmi yaUpinzani inataka kujua mpango wa serikali katika utekelezajiwenye tija wa mpango huu ili kupunguza vifo vinavyotokanana uzazi.

7. KUKABILIANA NA TATIZO LA AFYA YA AKILI NCHINI

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na ongezeko kubwa la watuwenye matatizo ya afya ya akili nchini.Katika hotuba yaKambi Rasmi ya Upinzani kwa mwaka wa fedha 2016/2017ilizungumzia ongezeko hili la watu wenye matatizo ya akili.Lakini kutokana na serikali kutokuchukulia tatizo hili kwa uzitowake, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeona ni vyemaikalirudisha jambo hili kwa upana ili serikali hii ya CCM iwezekutambua kuwa hakuna taifa linaloweza kuendelea endapoafya ya akili ya watu wake si salama.

Mheshimiwa Spika, magonjwa mengi ya akili kama vilehuzuni kupindukia(bipolar disorder),hali ya wasiwasi(schizopheria) na magonjwa ya akil i (mentaldisorders)yanachangiwa na mambo mengi kwani huletamabadiliko katika umbo la ubongo ambapo mabadilikohayo huathiri hisia na tabia za watu,mazingira yamtu,uhusiano wake na watu wengine n.k Japo, mapitiomengi ya taarifa yanaonyesha magonjwa ya akili nchiniTanzania hutokana na matatizo ya kurithi(inherited problem)

Mheshimiwa Spika, pamoja na ongezeko kubwa la watuwenye matatizo ya akili ambapo kwa mwaka 2013/2014takwimu zilionyesha kuna takribani watu 450,000 na wenyematatizo ya akili nchini. Vilevile, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni imebaini kuwa kwa sasa takribani wagonjwa 150mpaka 200 huudhuria kliniki za watu wenye magonjwa yaakili kwa wiki mkoa wa Dar es Salaam pekee.

Mheshimiwa Spika, ukubwa wa tatizo hili hauendani kabisana rasilimali zilizopo katika kukabiliana na tatizo.Katika sekta

Page 251: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

ya afya Idara ya kuhudumia wagonjwa wa akili ni Idarailiyosahauulika kabisa.Ni moja ya Idara inayopaswakuangaliwa kwa kina zaidi.

Mheshimiwa Spika, nchi nzima ina takribani madaktari 26 tuwanaoshughulikia matatizo ya afya ya akili nchini. Wengi wamadaktari hawa wanahudumia hospitali za Rufaa pekee.Mfano Kwa Dar es Salaam kuna madaktari takribani 8 tuwanaotoa huduma katika hospitali ya Muhimbili Idara ya afyaya akili, Mwananyama na Temeke, hospitali maaluminayoshughulikia masuala ya afya ya akili Milembe –Dodomaina jumla ya madaktari 5 tu,Bugando daktari 1, KCMC kwasasa haina daktari hata mmoja huku hospitali ya MawenziMoshi iliyokuwa inatoa huduma hiyo imebaki na nesi mmojatu ambae anauzoefu wa muda mrefu wa kutoa hudumahiyo baada ya kufariki kwa daktari bingwa Marehemu Dr.Ringo.

Mheshimiwa Spika, hospitali hizi zinazotoa huduma za afyaya akili zina hali mbaya kwani mpaka sasa hospitali yaMuhimbili ina vyumba viwili tu ambapo kimoja ni chawagonjwa wa kiume na kingine ni cha wagonjwa wa kike.Pamoja na hayo,kuna chumba kimoja tu cha wagonjwawenye matatizo makubwa kwani wengi wao hufanya fufanyafujo,kupiga kelele n.k(acute ward)Chumba hiki ni kwawagonjwa na kiume pekee .Pale inapotokea mgonjwa wakike wa aina hiyo basi inalazimu mgonjwa huyuachanganywe na wengine jambo ambalo ni hatari sanakwani ilishawahi kutokea mgonjwa wa aina hiyo kumuuamwezake.

Mheshimiwa Spika, kutokana na uhaba wa vyumba navitanda inalazimu wagonjwa ambao wamepata unafuukuruhusiwa haraka hata kama hawajapona vizuri ili kupishawengine wenye hali mbaya zaidi. Kwa kuwa wagonjwawengi wamepata tatizo kwa sababu ya kurithi unakuta nivigumu sana kuweza kumudu matibabu kwani kuna familiahujikuta zikiwa na wagonjwa zaidi ya watatu na hivyo kuathirihata wale wanaowategemea kuchumi.

Page 252: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

Mheshimiwa Spika, dawa za magonjwa ya akili nchini nichache sana na hazipatikani kwa urahisi. Dawa nyingihutengeneza usugu kwa wagonjwa kutokana na kwambawanalazimika kuzitumia kwa muda mrefu.Pale ambapoinalazimu kubadilishiwa inakuwa ni vigumu kwa kuwa dawazake ni za gharama kubwa, kwani dozi moja inawezakugharimu zaidi ya shil ingi laki mbili jambo ambaloWatanzania wengi hawawezi kuzimudu.

Mheshimiwa Spika,ni wa wakati muafaka sana kwa serikalikuanza kuchukua hatua za dharura. Mpaka sasa chuo chakutoa mafunzo ya udaktari cha Muhimbili kitengo chamagonjwa ya akili kina wanafunzi wachache sana. Kwamwaka wa kwanza kuna mwanafunzi mmoja, na kwamwaka wa tatu kuna mwanafunzi mmoja tu. Mpaka sasahospitali hii inategema madaktari ambao ni wanafunziwatano na mbobezi (Specialist) mmoja ambae amepewamajukumu mengine ya kufundisha pia. Japokuwa serikaliimefungua kitengo kipya cha wanasaikolojia badowanafunzi ni wachache sana na walimu ni wanne tu ambaoni wahadhiri wasaidizi pekee.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapendekeza yafuatayo

1. Serikali ilichukue tatizo hili kwa hali ya upekee kabisa

2. Kwa kuwa tatizo hili ni kubwa, na linapojitokezakatika familia lina madhara makubwa ya kiuchumi na kijamiikwani wengi wao hawawezi tena kumudu maisha yao napia hawawezi kumudu gharama za matibabu ambazo ninyingi sana kwani wengi hulazimika kusafiri kutoka mikoanimpaka Dar es Salaam au hospitali za Rufaa ambapo ndipohupata huduma za matibabu. Hivyo basi serikali iweze kutoaruzuku katika dawa hizi ili wagonjwa wengi zaidi wawezekunufaika.

3. Serikali ichukue jit ihada za makusudi zakuhamasisha watanzania kujiunga na taaluma hii ili kuokoamaisha ya Watanzania wengi.

Page 253: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

4. Kwa kuwa tatizo la magonjwa ya afya ya akilihuendana na unyanyapaa. Vilevile mara nyingi jamii imekuwaikihusisha tatizo hili na masuala ya ushirikina Ni vyema sasaserikali ianze kutoa elimu ya kutosha kwa jamii.

5. Serikali iangalie namna bora ya kuboresha hudumakatika vituo hivi vya kutolea huduma kwa wagonjwa waakili na ihakikishe hospitali za Wilaya, Vituo vya afya nazahanati zinaanza kutoa watu watakao jifunza kuhusumasuala ya afya ya akili ili kuanza kutoa huduma kule chinikwa wananchi. Na katika ameneo ambapo wataalamuhawa ni wachache basi wafanye kazi za kitaalamu badalaya kupewa majukumu mengine. Hili litapunguza mrundikanowa wagonjwa katika hospitali za Rufaa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi inasikitika sana kuonaWizara hii ikianza na unyanyapaa mkubwa kwa Idara hiikutokana na kutokutenga bajeti ya kusaidia vitengo vya afyaya akili nchini. Mwana falsafa mmoja aliwahi kusema“unexpressed emotions will never die,they are buried aliveand will come forth later in uglier ways”. Kwa tafsiri isiyo rasmiikiwa na maana kwamba hisia zilizofichika huwa hazipotei,hutulizwa tu katika uhai wake na siku moja zinaweza kuibukavibaya zaidi.Ni muhimu sasa serikali ikasikia kilio hiki chakugugumia cha vitengo na Idara zote zinazohusika nahuduma ya afya ya akili ili kuweza kutatua changamotozilizopo na kuwasaidia wale wote wanaokumbwa namatatizo ya akili nchini.

9. UDHIBITI WA UPUNGUFU WA DAWA NCHINI

Mheshimiwa Spika, upungufu wa dawa na vifaa tiba,umekuwa ni changamoto kubwa katika sekta ya afyaduniani. Hata hvivyo, kwa nyakati tofauti serikali imetoa kaulizinazokinzana kuhusu tatizo hilo. Kutokana na hali hiyo,Mheshimiwa Upendo Peneza – Mbunge wa Viti Maalumaliandaa hoja binafsi akiliomba bunge liazimie kuitaka serikalikubadili mfumo wa bajeti ya dawa ili kukabiliana na tatizola upungufu wa dawa nchini. Hata hivyo, hoja hiyo hoja hiyohaikupata nafasi ya kuingia bungeni kutokana na kukosa

Page 254: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

nafasi katika ratiba ya shughuli za bunge katika Mkutanowa Sita wa Bunge.

Mheshimiwa Spika, katika maelezo ya hoja yake, alirejeaRipoti ya utafiti uliofadhiliwa na Benki ya Dunia juu yaMabadiliko ya dawa na vifaa tiba (Pharmaceuticals Reform)ya mwaka 2011, ambayo inaeleza kwamba; licha ya ukwelikwamba dawa ni kiungo muhimu cha ufanisi wa mfumomzima wa afya, bado kumeendelea kuwa na upungufu wadawa muhimu katika nchi zinazoendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa utafiti huo, kila mwakawatoto zaidi ya milioni 10 hufariki katika nchi zinazoendeleakutokana na magonjwa ambayo yangeweza kuzuiliwa aukutibiwa na chanjo au dawa zilizopo. Aidha, inakadiriwakwamba wanawake 1,000 hufariki kila siku kutokana namatatizo wakati wa ujauzito au wakati wa kujifunguaambao wengi wao wangeweza kuokolewa kwa kupatauangalizi stahiki – ikiwemo kuwapatia dawa shahili.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Shirika la Global HealthTanzania, asilimia ya vifo vinavyosababishwa na magonjwaambayo yanaweza kutibiwa au kupunguzwa makali yakekwa dawa hapa nchini ni kama ifuatavyo:

i. UKIMWI – asilimia 17ii. Maambukizi ya Mfumo wa chini wa Upumuaji

(Lower Respiratory Infections) – asilimia 11iii. Malaria – asilimia 7iv. Kuhara – asilimia 6v. TB – asilimia 5vi. Kansa – asilimia 5 nk.

Mheshimiwa Spika, suala la ukosefu wa dawa hapa nchinipia halikuanza juzi wala jana. Utafiti uliofanywa na shirikalisilo la Kiserikali la Sikika mwaka 2011 ulibaini kwamba katiya wilaya 71 zilizofanyiwa utafiti, asilimia 48 ya wilaya hizohazikuwa kabisa na pamba (absorbent gauze) inayotumikahospitalini kama kifaa tiba kwa matumizi mbalimbali kama

Page 255: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

vile kusafisha vidonda na kwa akina mama wanaojifungua.Katika utafiti huo, ni asilimia 8 tu ya wilaya zilizofanyiwa utafitizilikuwa na pamba hizo kwa kiwango cha kutosha kukidhimahitaji.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa hospitali na vituo vyaafya, utafiti ulibaini kwamba, kati ya hospitali na vituo vyakutolea huduma za afya (health facilities) 30 vilivyofanyiwautafiti, asilimia 37 ya hospitali au vituo hivyo havikuwa kabisana pamba hizo. Ni asilimia 10 tu ya hospitali au vituo hivyovilikuwa na kiasi cha kutosha cha pamba hizo. Aidha, utafitiunaendelea kuonyesha kwamba; miongoni mwa sababuza upungufu ni kutokana na ukweli kwamba ; pamba hizozilikuwa hazifiki kwa wakati katika hospitali na vituo vya afya.Wakati mwingine hospitali na vituo vya afya vililazimikakusubiri kwa takriban miezi miwili kupokea pambawalizoagiza kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kupitia kwamaafisa afya wa wilaya (DMO’s). Utafiti unaonyesha piakwamba Maafisa afya wa Wilaya pamoja na wakuu wahospitali na vituo vya afya hawakuagiza pamba hizo kutokaMSD kwa viwango vinavyotosheleza kutokana na ukosefuwa fedha kwenye akaunti zao za MSD.

Mheshimiwa Spika, katika chapisho la “Policy Brief”lililotolewa na Shirika la Sikaka mwaka 2014 juu ya hitaji laSerikali kuongeza bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba ilikukabiliana na upungufu (Stock Outs) linaonyesha kwambaupungufu wa mara kwa mara wa dawa muhimu na vifaatiba hapa nchini ni tatizao sugu. Jambo hili limesababishautoaji duni wa huduma za afya na hivyo kuathiri afya zawananchi.

Mheshimiwa Spika, sababu kubwa iliyotolewa katikachapisho hilo inayosababisha upungufu wa dawa muhimuni bajeti ndogo inayotengwa kwa ajili ya dawa muhimuambayo haikidhi mahitaji. Kwa mfano, ukiangalia bajeti yaWizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha2013/14; bajeti hiyo iliongezeka kwa asilimia 30.8 kutokashilingi bilioni 581.7 mwaka 2012/13 hadi kufikia shilingi bilioni753.9 mwaka 2013/14.

Page 256: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

Mheshimiwa Spika, jambo la kushangaza ni kwamba,ongezeko la bajeti ya afya katika mwaka wa fedha 2013/14halikuwa na tija au maana yoyote katika bajeti ya dawamuhimu na vifaa tiba kwani bajeti ya dawa muhimu na vifaatiba ilishuka kwa asilimi 20.5 kutoka shilingi bilioni 80.5 mwaka2012/13 hadi kufikia shilingi bilioni 64 mwaka 2013/14.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Sikika unaonyesha piakwamba kwa mwaka wa fedha 2014/15 bajeti ya dawamuhimu na vifaa tiba ilishuka tena kwa asilimia 28.4 kutokashilingi bilioni 64 mwaka 2013/14 hadi kufikia shilingi bilioni45.8 mwaka 2014/15.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Hali yaUpatikanaji wa Dawa Nchini iliyowasilishwa na Wizara yaAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenyeKamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo yaJamii – Oktoba, 2016; bajeti ya dawa kwa mwaka wa fedha2016/17 imeongezeka karibu mara nane hadi kufikia shilingibilioni 251.5 ukilinganisha na bajeti ya dawa iliyotengwamwaka jana 2015/16 ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 29 tu.Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, fedha ambazozilikuwa zimeshatolewa hadi kufikia tarehe 30 Septemba(robo ya kwanza ya mzunguko wa bajeti) zilikuwa ni shilingibilioni 20 tu sawa na asilimia 7.95 tu ya bajeti iliyotengwakwa ajili ya dawa.

Mheshimiwa Spika, licha ya taarifa hiyo ya Wizara kuoneshakwamba bajeti ya dawa kwa mwaka wa fedha 2016/17 nikubwa (shilingi bilioni 251) lakini katika fedha hizo kunamatumizi ya miradi mingine ya maendeleo ambayohayahusiki na dawa kama vile ugharamiaji wa wa tafitimbalimbali, ugomboaji wa magari bandarini, ununuzi wavitanda, gharama za usambazaji wa dawa nk. Kwa sababuhiyo, kiasi halisi kitakachotumika kwenye dawa tu katika hiyoshilingi bilioni 251 hakijulikani.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba kwa mwenendo huuwa ufinyu wa bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba;sambamba na utekelezaji duni wa bajeti hiyo; tatizo la

Page 257: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

upungufu wa dawa na vifaa tiba katika hospitali, zahanatina vituo vyetu vya afya litaendelea kuwepo ikiwa Serikalihaitachukua hatua za makusudi za kuongeza bajeti ya dawaili kuondokana na tatizo hilo.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya tafiti nyingi zilizofanyikakuhusu ukosefu au upungufu wa dawa muhimu na vifaa tiba,yanaonyesha kwamba, sababu kubwa inayopelekeaukosefu au upungugu huo ni bajeti ndogo inayotengwa naSerikali kwa ajili ya ununuzi wa dawa. Hata hivyo, miongoinimwa mapendekezo yaliyotolewa na tafiti hizo ni kuongezabajeti ya afya angalau kufikia asilimia 15 ya Bajeti Kuu yaSerikali ikiwa ni utekelezaji wa Azimio la Abuja ambapo nchiza Afrika zilikubaliana kwa kauli moja kutenga asilimia 15 yaBajeti za Serikali zao kwenda kwenye huduma za afya.Itakumbukwa kwamba Tanzania iliridhia kwa kutia sainiazimio hilo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tafiti zinaonyesha kwamba,sababu kubwa ya upungufu wa dawa ni utekelezaji duni wabajeti ya maendeleo ambayo ndiyo inabeba fedha za dawa,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakubaliana na inaungamkono mapendekezo ya hoja ya Mheshimiwa Upenzo Peneza(Mb) kwamba; Serikali ibadili mfumo wake wa bajeti ilikutenga fedha za dawa katika kifungu maalum kwenyebajeti ya matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) nakuziwekea fedha hizo zuio (ring fence) kuanzia mwaka wafedha 2018/19 na kuendelea. Kinachopendekezwa nikwamba; matumizi ya fedha katika fungu la matumizi yakawaida kwenye wizara husika (kwa maana ya Wizara yaAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisiya Rais – TAMISEMI) yafuate vipaumbele katika mpangilioufuatao:

1. Mishahara2. Dawa za Binadamu na vifaa tiba (ring fenced)3. Matumizi Mengineyo (OC)

Mheshimiwa Spika, msingi wa pendekezo hili unatokana naukweli kwamba mahitaji ya dawa na vifaa tiba kwa

Page 258: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

wananchi wetu ni mahitaji ya kila siku na hayawezi kusubirikwa muda mrefu kama miradi mingine ya maendeleo kaitikasekta hiyo hiyo ya afya inavyoweza kusubiri. Kwa mfanoutekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la hospitali unawezakusubiri kwa muda fulani ukisubiria fedha, na pia utekelezajihuo unaweza kufanywa kwa awamu na hata ukachukuamiaka miwili mitatu kukamilika bila kuathiri maisha yamwananchi. Fedha za mradi wa namna hii kuwekwa kwenyebajeti ya maendeleo ni sahihi kabisa.

Lakini mgonjwa anayehitaji dawa sasa hivi ili apone, hawezikusubiri, vinginevyo atapoteza maisha. Kutokana naumuhimu wa kulinda afya na maisha ya wananchi KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inashauri na kupendekezakwamba, fedha za dawa ziwekewe zuio (ring fence) ilizisitumiwe kwa matumizi mengine yoyote isipokuwa tu kwamanunuzi ya dawa na vifaa tiba. Vifaa tibavinavyozungumziwa hapa ni vile vifaa vidogo vidogovinavyohitajika kila siku katika ‘administration’ ya dawakama vele pamba, sindano pamoja na vitendanishi(reagents). Vifaa tiba vikubwa kama vile mashine za mionzi(X-ray) MRI, CT Scan nk. viendelee kuwa chini ya fungu labajeti ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Tanzania haitakuwa nchi ya kwanzakutenga fedha za dawa na vifaa tiba na kuziweka kwenyebajeti ya matumizi ya kawaida. Afrika ya Kusini wanafanyahivyo, na hata nchi ya Zambia – jirani zetu wanafanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, l icha ya faida tutakayoipata yakupunguza tatizo la ukosefu wa dawa kwa wananchi wetukwa kuweka bajeti ya dawa kwenye bajeti ya matumizi yakawaida; faida nyingine tutakayoipata ni kwamba tutakuwatumeweza kutoa huduma za afya kwa wananchi wetu kwakutumia fedha za ndani kwa kuwa bajeti ya matumizi yakawaida ni ya fedha za ndani. Kwa kufanya hivyo; tutaingiakatika rekodi nzuri ya utekelezaji wa bajeti kwa vigezo vyaBenki ya dunia . Nchi inayotekeleza bajeti yake vizuri kwavigezo vya Benki ya dunia ni ile inayotekeleza bajeti yake ya

Page 259: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

matumizi ya kawaida katika kuwapatia wananchi wakehuduma za kijamii zinazokidhi mahitaji.

10. LISHE DUNI NA ONGEZEKO LA UTAPIAMLO NAUDUMAVU

Mheshimiwa Spika, katika bunge la bajeti lililopita 2016/2017Kambi Rasmi ya Upinzani ilizungumzia kwa kina tatizo laupungufu wa lishe na madhara ya utapiamlo kwa Taifa.Pamoja na hayo, bado tatizo la utapiamlo linazidikuongezeka hususani hivi karibuni ambapo nchi imekumbwana ukame na ukosefu wa chakula katika maeneo mengi yanchi.

Mheshimiwa Spika, tatizo la utapiamlo ni tatizo kubwa sanakwa nchi kwani ni tatizo lenye madhara ya muda mrefu kwataifa kwani lina athari kubwa katika ukuaji wa ubongo ikiwani pamoja na uwezo wa kufikiri na ukuaji wa maungo kwawatoto wadogo.

Mheshimiwa Spika, mwaka 1991 asilimia 49.7 (takriban nusu)ya watoto chini ya umri wa miaka mitano walikuwa naudumavu. Mwaka 2010, asilimia 42.5 ya watoto wote chiniya umri wa miaka mitano walipata udumavu .Ripoti iliyolewana taasisi ya utafiti ya REPOA ilionyesha mpaka mwaka 2014takribani watoto milioni 2.7 walikuwa na udumavu na katiyao watoto 100,000 walikuwa na udumavu uliokithiri. Tafitizi l izofanywa mwaka 2015 zil ionyesha kiwango hichokimepungua kwa mijini na kufikia asilimia 35 wakati vijijinibado tatizo likiwa kubwa kwa takribani asilimia 45. Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la Mtanzania latarehe 18 Machi,2015 mikoa inayoongoza kwa udumavu niDodoma 57.1%, Lindi 53.3%, Iringa 52%, Rukwa 51.4% na Mbeya51.3% huku mikoa yenye udumavu mdogo ikiwa ni Dar esSalaam 19.7% , Kilimanjaro 27.6% na Mara 30 %.

Mheshimiwa Spika, tatizo la udumavu, unyafuzi na utapiamloni tatizo linaloweza kuzuilika au kupunguzwa kabisa.Nchi yaHaiti ilikumbwa na tetemeko mwaka 2010 hivyo wananchiwengi walikumbwa na uhaba wa chakula pamoja na

Page 260: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

ongezeko kubwa la maradhi. Lakini pamoja na hilo walionaumuhimu mkubwa wa kuanza kukabiliana na tatizo laudumavu wa watoto kuanzia miezi 6 mpaka miezi 59 ilikuepusha jamii yao na matatizo ya uwezo mdogo wa kufikirina kudumaa kwa viungo siku za mbeleni. Katika tafitiilizonyesha ndani ya kipindi cha miaka miwili tatizo laudumavu lilipungua kutoka asilimia 29 mpaka 22.Hii nikutokana na mpango wa serikali kuongeza uzalishaji wachakula,virutubisho pamoja na kuhakikisha upatikanaji walishe bora kwa urahisi kwenye jamii.

Mheshimiwa Spika, halikadhalika, nchi ya India ilianzishampango maalum wa kukabiliana na tatizo la udumavulililokuwa limeikumba nchi hiyo ambapo watoto zaidi yamilioni 60 waliathirika.Katika mji wa Maharashtra ambao nimji tajiri bado tatizo hilo lilikuwa kubwa.Hii ni kwa sababuwatoto wanaweza kushiba lakini wakakosa lishe bora. Hivyoserikali ilianzisha program maalum ya “Mother-Child Healthand Nutrition Mission” iliyoanzia katika maeneo yaliyoathirikazaidi.Serikali ya India ikaanza usambazaji wa vyakula vyenyevirutubisho kwa bei rahisi ambapo kina mama wajawazitona wale wanaohudhuria kliniki baada ya kujifunguawaliweza kuimudu.

Mheshimiwa Spika, Serikali itambue kuwa, hakuna taifa loloteduniani, lililowahi kupata maendeleo huku wananchi wakewakikosa afya bora hasa afya ya akili. Hatuwezi kupataviongozi wa serikali wenye uwezo mkubwa wa kutafutasuluhu ya matatizo yanayolikabili Taifa kama utotoni waliwahikuugua tatizo la udumavu au hawakupata lishebora.Hatuwezi kupata usalama wa taifa wenye uwezo wakuwa tanuru la fikra (think tank) kama utotoni hawakupatalishe bora iliyojenga afya ya akili. Mwalimu Nyerere aliwahikusema maadui watatu wa taifa hili ni ujinga umaskini namaradhi. Matatizo haya yote yanachangiwa na tatizo kubwala kukosa lishe bora kwa wananchi wetu. Ili binadamu awena uwezo mzuri wa kufikiri hasa katika hali ya utupu (invacuum) ni lazima kuhakikisha anapata lishe yenye kujengaubongo na kinga imara za mwili.

Page 261: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

Mheshimiwa Spika, Hivyo basi Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka serikali kuhakikisha kuwa tatizo la udumavu, unyafuzina utapiamlo linapunguzwa. Hii ni kutokana na madharamakubwa yanayoweza kulikumba taifa endapo watoto auvijana watakumbwa na matatizo hayo. Kama taifatutapoteza kabisa kisima cha fikra cha taifa hili kutokana naukosefu wa lishe bora unaosababisha udumavu.

11. ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZANA ATHARI ZAKE

Mheshimiwa Spika, magonjwa yasio ya kuambukiza kamavile saratani za aina zote, magonjwa ya moyo, shinikizo ladamu, figo, matatizo ya upumuaji na kisukari yameendeleakuwa visababishi vya ongezeko la vifo nchini.Takwimuzinaonyesha watu wazima 9-11 kati ya 100wanaugua ugonjwa wa kisukari na kati ya watu wazima 3mmoja ana tatizo la shinikizo la juu la damu. Aidha, tatizo laMagonjwa yasiyo ya Kuambukiza linakua kwa kasi katika nchizinazoendelea, kama Tanzania. Inakisiwa kuwa mwaka 2020Magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia73% ya vifo vyote duniani na asilimia 60% ya ukubwa wa tatizola magonjwa duniani.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara kwakushirikiana na Tanzania Diabetes na World DiabetesAssociation ya mwaka 2013 ni kwamba, gharama yakukabiliana na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani koteni mabilioni ya dola na hivyo kusababisha upotevu mkubwawa rasilimali finyu zilizopo. Kwa mwaka 2010 Shirika la AfyaDuniani lilikadiria kuwa, jumla ya gharama za huduma zaafya zinazohusiana na kisukari zilifikia dola za kimarekanibilioni 378 duniani kote, na kiasi hiki cha fedha kinawezakufikia dola za kimarekani bilioni 490 ifikapo mwaka 2030.

Mheshimiwa Spika, tunatambua kuwa magonjwa hayayasiyo ya kuambukiza yanachangiwa sana namfumo wamaisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na ulaji na unywaji usiofaa,matumizi ya sigara na madawa ya kulevya tabia yakutokufanya mazoezi,shughuli za kimaendeleo zenye athari

Page 262: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

kwa miili yetu na matumizi mbalimbali ya vipodozi,msongowa mawazo n.k.

Mheshimiwa Spika, nchi nyingi duniani zimekuwa mstari wambele katika kupambana na magonjwa hayo kutokana naathari kubwa zinazosababishwa na magonjwa haya ikiwani pamoja na serikali kupoteza nguvu kazi ya taifa, familiakupotelewa na wapendwa wao hali inayopelekea ongezekola yatima na wajane katika jamii, ongezeko la umaskini ndaniya familia kutokana na vifo vya wategemezi wa familia,kuwa na taifa la watu wengi walio wagonjwa n.k

Mheshimiwa Spika, Kutokana na hali hiyo, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inataka kujua yafuatayo:

· Je, serikali ina mkakati gani wa kuhakikishaangalau vifo vinavyotokana na magonjwayasiyo ya kuambukiza nchini vinapungua?

· Je, ni fedha kisiasi gani ambazo mpaka sasazimekwisha tumika kupeleka wagonjwa njeya nchi kupata matibabu kutokana namagonjwa yasiyo ya kuambukiza?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaishauri Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kuweka mikakatiya kuzuia tatizo (preventive measures). Fedha hizo zitumikekatika uratibu wa kuamsha uelewa wa wananchi(awarenesscampaign) kwa kada zote, kurudisha michezo mashuleni kwania ya kujenga afya, kuimarisha michezo katika sekta zoteza umma,kuhakikisha serikali inakuja na mpango mahususiya kurudisha viwanja vya wazi vya umma kwa ajili yamatumizi ya mazoezi na michezo il i kuboresha afyakupunguza kodi katika vifaa vya kufanyia mazoezi,kuzuiakabisa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali, kuzuia kabisabiashara ya kuuza dawa kiholela bila cheti chadaktari,kushirikiana na taasisi mbalimbali yakiwemomashirika,taasisi za dini, wasanii na wanasiasa katika kutoaelimu kwa jamii juu ya tabia hatarishi.

Page 263: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

12. ONGEZEKO KUBWA LA WAGONJWA HOSPITALI YATAIFA MUHIMBILI NA VITENGO VYAKE

Mheshimiwa Spika, Kwa sasa hali ya hospitali ya Taifa yaMuhimbili inakabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa.Wapo wanaotoka mikoani bila hata ya rufaa yoyote nakulazimika kwenda hospitali hii ya Taifa. Tatizo hil ilinachangiwa sana na ukosefu wa huduma katika hospitaliza mikoa, wilaya na vituo vya afya.

Mheshimiwa Spika, Katika Taasisi ya Mifupa (MOI), hali yaongezeko la wagonjwa nayo ni ya kutisha sana. Kumekuwana idadi kubwa ya wagonjwa kuliko uwezo wa taasisi hii.Japokuwa jengo la taasisi hii hali jakamilika walakukabidhiwa limekuwa likitoa huduma kwa wagonjwa wengiwanaozidi uwezo wa jengo.Jambo hilo sio tu ni la hatarikwa wagonjwa na wale wanaowahudumia bali pialinaiweka serikali katika hatari kwani matatizo yoyoteyakitokea ndani ya jengo lile hakuna wa kuchukuliwa hatua.

Mheshimiwa Spika, tatizo la mrundikano wa wagonjwakwenye hospitali moja linaweza kuepukika kabisa endaposerikali itajikita kwenye kuhakikisha huduma za afya za msingizinapewa kipaumbele chini ya utekelezaji na usimamizi waWizara hii. Ni lazima Serikali ikatambua kuwa mahitaji yahuduma za afya yanaongezeka kwa kasi kwa kadiri idadi yawatu inavyoongezeka na changamoto za afya zinajitokeza

Mheshimiwa Spika, kusingekuwepo na sababu yoyote yawagonjwa wanaopata ajali au kuvunjika kukimbizwahospitali ya Taifa na hususan MOI, endapo serikali ingeboreshahuduma za afya katika vitengo mbalimbali kuanzia kwenyezahanati mpaka hospitali za Rufaa.

Mheshimiwa Spika, ongezeko hili kubwa la watumiaji wahuduma ya afya, linazikumba hospitali na zahanati nyinginchini. Mfano, Mwaka 2013 takribani watu 45,682,479walipata huduma za afya katika zahanati ikilinganishwa nawatu 39,917,117 walipata huduma za afya katika zahanatimwaka 2011. Kwa mujibu wa Sera ya Afya ya Taifa ya mwaka

Page 264: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

2004 ni kwamba; mwaka 2004 Tanzania ilikuwa na idadi yazahanati 4,400 na zahanati moja ilitoa huduma kwa takribaniwatu 8,020 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2003 ambayoilieleza kwamba zahanati moja ilitakiwa kutoa huduma kwatakribani watu 5,000. Hii ikionyesha kwamba kwa kipindi chamwaka mmoja tu kumekuwa na ongezeko la uhitaji kwatakribani 38%. Pamoja na hilo kuanzia mwaka 2012 mpakamwezi Machi 2017 kipindi cha miaka mitano pekeekumekuwa na ongezeko la idadi ya watu takribani milioni11.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haioni jitihadaza makusudi za serikali katika kutatua matatizo ya afya kamakipaumbele cha kwanza cha taifa. Serikali hii ya awamu yatano imeshindwa kabisa kuimarisha uchumi shirikishi kwa raiawake (economic inclusiveness) kwa kupitia huduma za afyaza msingi. Serikali imekuwa na tabia ya kuwekeza zaidi katikauchumi wa kibaguzi ambao unanufaisha kundi la watuwachache katika huduma kama za usafiri wa ndege na hukuikisahau kabisa kwamba afya ndio uchumi wa kwanzaunaoiunganisha jamii. Ni wakati muafaka sasa wa serikalikujitathimini kama bado inahitaji kukuza uchumi wa kwenyemakaratasi au uchumi shirikishi kwa maendeleo ya taifa.

USTAWI WA JAMII

13. ONGEZEKO LA KUTISHA LA MIMBA KWA WANAFUNZINCHINI.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo kubwa na la kutishala ongezeko la ndoa na mimba kwa watoto wenye umri wakwenda shule na wale walio mashuleni nchini. Kwa mujibuwa ripoti ya Shirika la Afya Duniani iliyotolewa mwezi Januari2016, ilionyesha kuwa Tanzania ni nchi ya tatu Barani Afrikakwa matukio ya mimba na ndoa za utotoni, ikiongoza kwatakribani asilimia 28.Hii ina maana kwamba, watoto wengichini ya umri wa mika 18 wanajihusisha na vitendo vya ngonozisizo salama.

Page 265: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016 Katibu Mkuu wa Wizara yaAfya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watotoalidhibitisha kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa lamimba kwa wasichana wenye umri kuanzia miaka 15 mpaka20 na ongezeko hili la 28% ni kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 pekee ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo tatizohilo lilikuwa ni asilimia 10 tu.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Idadi ya watu duniani (UNFPA)lilibaini kuwa kila kwenye wasichana kumi wenye umri katiya miaka 12 mpaka 16 kati yao wanne wamepata mimba.Pamoja na hilo lilibaini kuwa kwa wastani wasichana wawilikati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18hususani kwa maeneo ya vijijini.Vilevile, Shirika la watotoduniani (UNICEF) katika ripoti yao ya mwaka 2012 ilibaini kuwamkoa ifuatayo inaongoza kwa tatizo la mimba na ndoa zautotoni: Shinyanga 59%,Tabora 58%,Mara 55%,Dodoma 51%na Lindi 48%.

Mheshimiwa Spika, katika mapitio ya tafiti mbalimbalizilizofanywa kitaifa na kimataifa Kambi ya Upinzani imebainikuwa ongezeko la mimba za utotoni linatokana na kushukakwa kipato cha familia, kubadilika kwa mfumo wa maishaambapo wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda mwingikatika shughuli za kujipatia kipato na hivyo kuwa na mudakidogo kwa malezi, kukua kwa teknolojia hususani matumiziya mitandao ya simu kwa mijini ambapo watoto wa kikehulaghaiwa na vija kwa kuahidiwa simu,kushuka kwa ari yakujifunza na msukumo wa elimu nchini, ukosefu wa ajirahususani kwa vijana wa kiume, kubadilika kwa mfumo wamaisha ambapo utamaduni uliokuwa umejenga katika jamiikuwa mtoto ni wa jamii sasa unabadilika na mtotoanaonekana kama ni wa familia pekee na hivyo jamiikujiondoa katika ulinzi wa mtoto wa kike.

Mheshimiwa Spika, jambo hili la ndoa na mimba za utotonilimekuwa na mtanzuko mkubwa kwani jamii imekuwa namaoni tofauti kutoka kwenye makundi mbalimbali yakidini,tamaduni, wasomi, wanaharakati wa haki zabinadamu, wanaharakati wa kutetea haki za watoto wa

Page 266: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

kike, wanasiasa n.k Lakini pamoja na hayo ni lazima Serikaliitoe tamko ili watoto hawa wasiendee kuumizwa na sheriahii au pengine sheria hii iweze kuwa na manufaa kwao.Hivyobasi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujuamsimamo wa Wizara hii ya maendeleo ya jamii, jinsia ,wazeena watoto katika kusimamia, kulinda na kutetea haki zawatoto hususani watoto wa kike ambao ndio walengwawakubwa wa sheria hii.

14. VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kupanua maeneo yakiutawala nchini, bila kupanua uwezo wa kutoa hudumakwa wananchi. Ushahidi wa hili ni ongezeko la Mikoa, Wilaya,Kata na Vijiji ikiwa ni pamoja na ongezeko la Majimbo yauchaguzi.

Mheshimiwa Spika, ieleweke kuwa ili kujenga uwezo wa jamiikuibua miradi ya maendeleo ni lazima kama nchi kuwa nauwezo wa kuzalisha wataalam wa maendelo ya jamii ilikuisaidia jamii kuibua miradi na masuala yanayogusa jamiikwa ujumla.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaonakuwa serikali hii, haijaweka kipaumbele katika kuendelezavyuo vya maendeleo ya jamii. Hii inatokana na uzito auugumu wa Serikali kutoa fedha za maendeleo katika wizarahii. Nasema hivi kwa kuwa Serikali imetoa asilimia tano tuya fedha za maendeleo hadi kufikia Machi, 2017 kwa ajili yavyuo vya maendeleo ya Jamii. Ikumbukwe kuwa fedhazilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maendeleo kwa ajili yavyuo hivi ilikuwa ni bilioni 8.8 lakini mpaka Machi mwakafedha zilizotolewa zilikuwa takribani milioni 497 sawa naasilimia 5.6.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaserikali kulieleza Bunge lako tukufu sababu za kutoa fedhapungufu kwa ajili ya vyuo hivi huku ikijulikana wazi kuwa vyuohivi vinakabiliwa na uchakavu wa majengo pamoja namazingira duni ya kujifunzia.

Page 267: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

15. WANAWAKE NA USAWA WA KIJINSIA

Mheshimiwa Spika, usawa wa kijinsia, ni nyenzo muhimukatika kufikia maendeleo endelevu ya Taifa. Changamotokubwa inayowafanya wanawake washindwe kukabiliana nausawa wa kijinsia ni pamoja na uwepo wa mila na desturizinazomkandamiza mwanamke. Hii ni pamoja nachangamoto ya Sheria kandamizi ya Ndoa ya mwaka 1971,ambayo inaendelea kukandamiza watoto wa kike nakuchochea ndoa za utotoni, Sheria ya Mirathi ya kimila,tohara kwa watoto wa kike, watoto wanaopata ujauzitoshuleni kukosa fursa ya kuendelea na masomo n.k

16. MASUALA YA WATOTO

Mheshimiwa Spika, watoto ni rasil imali muhimu kwamaendeleo ya Taifa lolote. Ili watoto waweze kukua na kuwaraia wema, wanahitaji kupewa haki zao za msingi ambazoni pamoja na: kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kutobaguliwa,na kushirikishwa. Haya yote yanaongozwa na Sera ya Mtotoya mwaka 2008 na kutunga Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka2009. Aidha, uanzishwaji wa Madawati ya Jinsia na Watotokatika Vituo vya Polisi nchini pamoja na kutoa mafunzo kwaPolisi kuhusu kusimamia madawati haya hakujaongeza ufanisiwala kuleta tija katika kusimamia upatikanaji wa haki zawatoto na wanawake. Uanzishwaji wa Mabaraza ya Watotokatika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri haujawezakutekelezwa nchini na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwakudorora kwa utoaji na upatikanaji wa haki za watoto.Mabaraza hayo yanawezesha ushirikishwaji wa watoto katikamasuala yanayohusu maendeleo yao. Vilevile, Serikaliimeshindwa kuendeleza mipango yake iliyoanisha ikiwemoMpango wa Uhai, Ulinzi na Maendeleo ya Mtoto. Mpangohuu ulilenga kuhamasisha wazazi kuwapeleka watotokupata chanjo ya maradhi mbalimbali ya utotoni, lishe borana upatikanaji wa maji safi na salama.

16.1 Ukatili dhidi ya watotoMheshimiwa Spika, vitendo vya kikatili dhidi ya watotovimeendelea kushamiri nchini, mifano hai ni kama ifuatayo;

Page 268: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

i. Juni 27, 2016 katika kitongoji cha moha, kijijicha Ilungu Kata ya Nyigogo, tarafa ya Itumbili wilaya ya Magumkoani Mwanza, Julius Leonard aliyekuwa na umri wa miaka7 aliuawa kwa kupigwa fimbo na baba yake wa kamboLeonard Joseph kwa kuchelewa kurudi nyumbani baada yakutumwa kwenda kuchukua betri. Mtoto huyu alipigwampaka kifo na mwili wake baada ya uchunguzi wa daktariulionesha kuvuja kwa damu kwa ndani kutokana na fimbohizo.

ii. Julai 2016, mtoto John Kyando mwenye umriwa miaka miwili (2) aliuawa kikatili na baba yake wa Kambokwa kushirikiana na mama yake mzazi katika kitongoji chaMang’oto, kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani Makete kwakunyongwa mpaka kufa kasha kutupwa mtoni.

iii. Aprili, 2017 mtoto wa mwaka mmoja na miezisana aliuwawa kikatili kwa kuchomwa moto sehemu zamakalio na baba yake wa kambo anayejulikana kwa jina laPetro Bahatu huko kijiji cha Nyalubanga, kata ya Lwezerawilaya na mkoa wa Geita.

Mheshimiwa Spika, haya ni baadhi tu ya matuko ya ukatilidhidi ya watoto ambayo yameripotiwa. Bado watotowameendelea kukubwa na ukatili mkubwa na matukio hayomengi yanapita bila kufanyiwa kazi ipasavyo, ipo haja sasaya Serikali kupitia wizara hii kuhakikisha kesi za watotowanaofanyiwa ukatili wa kijinsia zinapewa uzito na adhabuyake iwe kali ili kufikisha ujumbe kwa jamii.

17. UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WAFEDHA 2016/17

a. Fungu 52

Mheshimiwa Spika, taarifa ya utekelezaji wa bajeti inaoneshakuwa hadi mwezi Machi, 2017 Wizara ilikuwa imepokea jumlaya shilingi 314,673,230,000.95 sawa na 40% ya bajeti ya Wizarazikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida pamoja na miradiya maendeleo.

Page 269: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kuhusu fedha za maendeleo,randama zinaonesha kuwa, hadi mwezi Machi, 2017 niasilimia 37 tu ya fedha za ndani ndizo zilizotolewa na Hazinana kwa fedha za nje ni asilimia 6 tu ya fedha hizo zilikuwazimetolewa na hazina kwa kipindi hicho. Hii ina maanakwamba bajeti ya maendeo kwa fedha za ndanihaijatekelezwa kwa asilimia 63, na kwa fedha za njehaijatekelezwa kwa asilimia 94. Kwa utekelezaji huu duni wabajeti ya maendeleo katika fungu hili, Kambi Rasmi yaUpinzani ina mtazamo kwamba Serikali haiko makini kabisana afya za watanzania.

b. Fungu 53

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeliliidhisha jumla ya shilingi bilioni 49.9 kati ya fedha hizo,matumizi ya kawaida shilingi bilioni 41 na shilingi bilioni 8.848zikiwa ni fedha za maendeleo. Hata hivyo, fedha zamaendeleo zilizotolewa hadi kufikia Machi, 2017 ni shilingi497,718,250/- sawa na asilimia 5.62 tu ya shilingi bilioni 8.8zilizoidhinishwa na Bunge. Hii maana yake ni kwamba, Bajetiya maendeleo katika fungu hili la maendeleo ya jamiihaikutekelezwa kwa taktriban asilimia 95. Fungu hili ndilolinahusika na vyuo vya maendeleo ya jamii, na kwa maanahiyo hiyo utekelezaji duni wa bajeti vyuo hivyo haviwezi kuwana uwezo wa kujiendesha na kuzalisha wataalam wakuzisaidia jamii zetu kujiletea maendeleo kwa kuweza kuibuafursa zilizo katika jamii zao.

18. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Serikali hii ya awamu ya tano imekuwaikijigamba kuwa afya ni mojawapo ya vipaumbele katikautekelezaji wa majukumu yake. Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni ilitegemea hayo yaonekane katika utekelezaji waBajeti ya maendele kwa angalau kwa asil imia 80 il ikudhihirisha uhalisia wa majigambo ya “hapa kazi tu”. Tofautina tegemeo hilo, wizara hii ni miongozi mwa wizarazinazoongoza kwa utekelezaji duni wa bajeti ya maendeleo.

Page 270: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

Mheshimiwa Spika, licha ya wizara hii kusema kwambamojawapo ya vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha2016/17 ni kusimamia upatikanaji wa huduma za ustawi wajamii kwa wazee, imewasahau wazee kabisa. Ikumbukwekwamba Serikali ya awamu ya nne ilishatoa uamuzi wakuwapatia mafao ya uzeeni (universal pension) wazee wotelakini Serikali hii ya awamu ya tano imeweka kapuni azimiohilo.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa rai kwaserikali kuacha kufanya mzaha na afya za watanzania. Serikaliiache kuwahadaa wananchi kwa kutenga bajeti kubwa nakushindwa kuitekeleza. Ni vema Serikali ikapanga mipangoinayotekelezeka kuliko kupanga mipango yenye lengo lakukidhi matakwa ya kisiasa na kuwaacha wananchiwakihangaika. Ili kukabiliana na maadui watatu yaani ujinga,umaskini na maradhi; ni lazima kuwekeza katika “Uchumiwa afya (health economy)”.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuwasilisha.

Esther Amos Bulaya (Mb)K.N.Y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI

BUNGENI KATIKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

3 Mei, 2017

MWENYEKITI: Kabla sijaitoa hoja hii kwenu muanzekuijadili nina tangazo moja lilisahaulika tu, linatoka Idara yaUtawala na Rasilimali Watu - Bunge na linahusu zoezi laupimaji na ushauri wa afya linaloratibiwa na Mfuko wa Taifawa Bima ya Afya. Tunaarifiwa kwamba zoezi la upimaji naushauri wa afya zetu kwa Wabunge, Watumishi na familiazao litaendelea hapa kwa wiki mbili kuanzia jana tarehe 02hadi 13 Mei, 2017. Huduma zitakazotolewa ni kama ifuatavyo;moja, upimaji wa magonjwa ya moyo, mbili, upimaji watezi dume, tatu, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,nne, uchunguzi wa saratani ya matiti na tano, uchunguziwa magonjwa ya kisukari. (Makofi)

Page 271: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

Zoezi hili litafanyika katika Kituo cha Afya cha Bungekuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kila siku,yaani kuanzia jana mpaka tarehe 13 Mei, zoezi hili linashirikishaMadaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwetena Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge tunakaribishwa,ni muhimu sana kwa ajili ya afya zetu, hivyo tuna mudakidogo ili tuanze kazi. Waheshimiwa Wabunge wawiliwanaweza, sasa nianze na Mheshimiwa Selemani Zediatafuatiwa na Mheshimiwa Abdallah Bulembo. (Makofi)

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kuwa naafya njema ili na mimi kwa niaba ya wananchi wa Jimbo laBukene niweze kuchangia hoja muhimu sana ya Wizara yaafya.

Mheshimiwa Mwenyekti, awali ya yote nimpongezesana Mheshimiwa Waziri wa Afya, Mheshimiwa UmmyMwalimu kwa uwasilishaji mzuri sana na hotuba nzuri sanaambayo imewasilishwa kwa weledi wa hali ya juu, hongerasana Mheshimiwa Ummy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kabisa kwa kusemakwamba naunga mkono hoja hii asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi waJimbo la Bukene, kwa dhati kabisa ya moyo wanguniipongeze Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetuMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhakikishakwamba Jimbo langu la Bukene kwa mara ya kwanzalinapata huduma ya upasuaji kwa vituo viwili vya afya.Huduma ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na nichukue fursa hiinimpongeze Naibu Waziri ya Afya Mheshimiwa Dkt. HamisiKigwangalla ambaye alifunga safari baada ya kufanyaufuatiliaji wa muda mrefu na kuja hadi kituo cha afya cha

Page 272: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

Itobo kufanya uzinduzi kwa niaba pia ya kituo cha afya chaBukene, hongera sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kazinzuri hiyo uliyoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo hivi vya upasuaji niazma ya Serikali ya Awamu ya Tano kupunguza vifo visivyovya lazima vya akina mama na watoto. Kabla ya vituo hiviakina mama waliokuwa wakihitaji huduma za upasuaji katikaJimbo la Bukene walikuwa wakilazimika kusafiri zaidi yakilometa 80 kutoka maeneo mengine hadi hospitali ya Wilayaili kupata huduma hii. Lakini sasa huduma hii imesogezwakaribu sana na niseme tu kwamba katika muda wa hii miezimiwili ambayo upasuaji umeanza muitikio ni mzuri sana natumeweza kufanya operesheni za kutosha na kuokoa maishaya akina mama na watoto wa ndani ya Jimbo la Bukene.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni moja tu,pamoja na kwamba huduma hii imeanza, lakini kunaupungufu mkubwa sana wa watumishi. Katika kituo cha afyacha Bukene mganga anayeweza kufanya upasuaji yukommoja tu na huyu anaifanya shughuli hiyo kwa muda wasaa 24. Kwa hiyo, inapotokea kwamba anakuwa kwenyemajukumu yasiyoweza kuzuilika mgonjwa akifika pale kamaanahitaji upasuaji anakosa hiyo huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hivyo hivyo kwenyekituo cha afya cha Itobo, mganga anayeweza kufanyaupasuaji kwa sasa tunaye mmoja tu na kwa Itobo ni mbayazaidi kwa sababu mganga huyu bado ana miezi michachetu ili astaafu. Kwa hiyo, kama hakutakuwa na jitihada zaziada ili kupata mganga basi huenda kituo hiki kikashindwakutoa huduma ya upasuaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya Halmashauri yaNzega tumejaribu kufanya re-allocation ya kuwatoawaganga kutoka Hospitali ya Wilaya kuwapeleka kwenyehivi vituo vya afya lakini re-allocation hii sasa imefika mwishokwa sababu hata Hospitali ya Wilaya nao wana upungufu.Hata hao wawili huyu aliyeko Bukene na aliyeko Itobotumewatoa pale Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Kwa hiyo, re-

Page 273: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

allocation ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imefikamwisho haiwezekani tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niombe kwa niabaya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Wizaraitufikirie kama ombi maalum ili tuweze kupata madaktariwanaoweza kupasua wapangwe katika Halmashauri yaWilaya ya Nzega na mmoja hususan apelekwe kituo cha afyacha Itobo na mmoja hususan apelekwe kwenye kituo chaafya cha Bukene ili huduma hizi muhimu na nzuri za upasuajiziendelee kupatikana ili wananchi wetu, na hasa akina mamana watoto waweze kuepukana na vifo ambavyo kimsingivinaweza kuzuilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kuzungumzia ni huduma za x-ray katika Hospitaliya Wilaya ya Nzega. Leo hii tunapozungumza hapa ni miezimitano sasa x-ray ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega imekufahaifanyi, kazi. Hoja yangu hapa ni kwamba tatizo sio kufakwa x-ray; x-ray ni kifaa ambacho kinafanya kazi kwa hiyokinaweza kufa. Lakini hoja yangu hapa ni uharaka wa namnaambavyo x-ray iliyokufa inaweza kushughulikiwa ikapona naikaendelea kutoa huduma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, x-ray ya Hospitali ya Wilayaya Nzega imekufa tangu tarehe 13 Desemba, 2016 na baadaya kufa tu Mkurugenzi wa Halmasauri ya Nzega aliandikabarua kwa Katibu Mkuu wa Wizara ili Wizara wai-engagekampuni ambayo ina mkataba wa kutengeneza hizi x-ray zaPhillips ili iweze kuja Nzega na kutengeneza. Lakini speedimekuwa ndogo mno, mpaka leo tunaongelea mwezi watano ni danadana tu. Hao mafundi walikuja mara mojawakaangalia vifaa, wakatoweka mpaka sasa hawajaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziriatakapokuja kufanya majumuisho tutataka tujue utaratibuau mkataba uliopo kati ya Wizara na hawa watoa hudumawa ku -service hizi x-ray aina ya Phillips ukoje na umekaa vipikwasababu kama utaratibu ni mbaya basi tupendekezakwamba Hospitali za Wilaya zenyewe zitafute mafundi au

Page 274: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

service provider wenye uwezo ili waweze kutengeneza x-ray.Kwa sababu ni jambo ambalo halikubaliki x-ray kukaa miezimitano imekufa na wagonjwa wanakwenda pale wanakosahuduma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linaleta usumbufumkubwa sana kwa wagonjwa wanaofika Hospitali ya Wilayaya Nzega na ambao matatizo yao yanahitaji huduma za x-ray wanapata taabu sana. Kwa hiyo, niombe kabisa kwambaMheshimiwa Waziri atakapokuja kutoa majumuisho atoeufumbuzi, kwamba x-ray ya Hospitali ya Wilaya ya Nzegaambayo miezi mitano sasa imekufa ni l ini itawezakushughulikiwa ili wananchi waweze kupata huduma hiyomuhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine nizungumzieupatikanaji wa dawa katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD).Kwanza niipongeze Serikali kwa dhati kabisa kwa kutengahela nyingi za kutosha kununua dawa. Hili kwa kweli ni jambola kupongezwa, haijawahi kutokea kiwango cha bajetikilichokwenda kwenye dawa mwaka huu ukilinganisha namiaka ya nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hoja hapa ni sasamadawa yapatikane, kwa sababu kupatikana kwa fedhaza kununua dawa ni jambo moja lakini kupatikana kwadawa pia ni jambo linguine. Kwa sababu utaona kwambafedha za dawa ambazo zinapelekwa kwenye akaunti zavituo vya afya au zahanati kule MSD kwa hiyo, unakuta vituovya afya au zahanati vikiomba dawa MSD kunakuwa naout of stock nyingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano waHalmashauri ya Wilaya ya Nzega. Taarifa za tarehe 28 mweziuliopita, ukijumlisha vituo vya afya na zahanati zote tuliombadawa za shilingi milioni 126 lakini tukapata dawa za shilingimilioni 24 tu, ambayo ni kama asilimia 20 tu. Kwa hiyo,utakuta kwamba sasa hivi tuna balance ya fedha za dawaambazo ziko MSD, karibu shilingi 503,000,000. Hata hivyoukiomba dawa sasa upatikanaji wa dawa unakuwa

Page 275: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

mdogo. Kwa hiyo upatikanaji wa fedha uendane sambambana upatikanaji wa dawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja asilimia100 na Wizara ya Afya wanafanya kazi nzuri sana. Ahsantesana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa AbdallahBulembo.

MHE. ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana na mimi niweze kuchangiakwenye hoja ya Wizara hii muhimu sana kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipendekumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwaanayoifanya katika Wizara hiyo, Naibu Waziri wake Dkt.Kigwangalla, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote waWizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka nianzie kwenyehili la madaktari. Mwezi uliopita tulikuwa na sherehe zetu zawazazi pale Kagera, mojawapo ya kazi yetu ni kwenda kutoahuduma katika hospitali. Hospitali ya Mkoa wa Kagerainahitaji Madaktari Bingwa 21, madaktari waliopo ni wawili.Sasa naiomba Wizara hii, nina imani hawa wakubwaniliyowapongeza ni wasikivu sana. Ukitafuta ratio ya 21 nambili pale watu wanapata shida sana. Nawaamini, lakininichukue nafasi hii kuomba kwamba kazi mnayofanya nikubwa lakini hao wenzetu hospitali inalemewa na hawanamahali pa kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba mbili tulikuta tatizolingine pale, kama alivyosema aliyemaliza kuongea sasa hivi.Tuipongeze Serikali kwa mara ya kwanza pesa ya dawa ipokatika Halmashauri. MSD inafanya kazi kubwa lakiniinawezekana imelemewa sasa. Isaidiwe, iongezewe nguvuili dawa zipatikane ziweze kwenda kwenye vituo vya afyana hospitali zetu. Kila unayemuuliza hapa kwenyeHalmashauri yake, pesa zipi, dawa hatujapata kutoka MSD.

Page 276: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

Kwa hiyo, nina uhakika Mheshimiwa Ummy na Naibu kwakazi mnayoifanya hebu elekezeni macho yenu kule kwenyeMSD, kwa sababu MSD ndiye anafikisha dawa kwaWatanzania waliokuwa wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru hichowanachokipata lakini kila mtu anakwambia nimeshapelekahela sijapata dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine niende kwenye hiyohiyo MSD. Tunaomba MSD ule utaratibu mliotengeneza kidogowa kuweka alama kwenye madawa ya Serikali, kila dawaya Serikali iwe na alama yake ya nembo inayojulikana ilituweze kuendelea kutunza dawa hizi zisiende kwenyemaduka ya watu binafsi. Katika hilo naipongeza sana Serikali,lakini sasa yale maeneo ambako hamjaanza kuweka zilenembo ni vizuri zile alama ziwepo ili mtu akienda kuuziwadukani anasema ile ni ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali yangukwa sababu bajeti iliyopita kwenye eneo la dawa ilikuwakama shilingi bilioni 50 au 65, lakini mwaka huu wameendazaidi ya shilingi bilioni 200 na mpaka leo Serikali yanguimeshaweza kutoa zaidi ya shilingi bilioni 120, ni kitu chakupongeza sana kwa maana kwamba Serikali hii inajali afyaya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nihamie kwenye maendeleoya jamii, ndugu zangu haya maendeleo ya jamii mbonawanyonge hivi? Kila Halmashauri utakayokwenda ukamkutamtu wa maendeleo ya jamii hana hamu na kazi yake. Hapewigari, hapewi huduma, haonekani kama ni mtumishi, kwanini ndugu zangu? Hawa ni watumishi na wana haki kamaidara zingine! Lakini wao wanakuwa ni watumwa fulanikatika ofisi, hakuna mtu utamkuta amechangamka kwenyekazi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niombe, Wizara hiini kubwa dawa zipo, mazuri yapo. Mheshimiwa Ummy hebuhamia hapo kwenye watu wa maendeleo ya jamii. Hawa ni

Page 277: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

watu muhimu sana katika taasisi yetu, shughuli zao ni nyetisana. Lakini unakuta Mkurugenzi akisema lazima “ah wewesubiri” akifanya hivi “wewe ngoja bado kasma haipo.” Kwanini hawa watu wawe wanyonge? Hebu tuwaongezeenguvu basi kama idara zingine zinavyofanya kazi ili na waowawe na afya katika meza zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine niongelee madaktari.Tunaipongeza Serikali, imesema inaajiri madaktari hao 258;mimi nafikiri tumpongeze Rais kwa uamuzi wa haraka. Hotubaya wenzangu huku wamesema kwa nini watu wanasikiahamu kwenda kufanya kazi nje. Unajua ajira ni nafasi, zamanitulikuwa kila mtu anaweza kuajiriwa kwa nafasi zilikuwachache, lakini leo lazima ikama iwepo, mshahara uwepo,na taratibu ziwepo ndiyo mtu aajiriwe. Sasa watuwameambiwa wanaenda Kenya na wanajua wanaendakulipwa dola, kuna mtu atabaki? Habaki mtu ukishatamkadola.

Sasa Rais wetu tumpongeze kwa maamuzi ya harakakwamba hawa waliokwishajitolea wanataka kwenda nchininyingine kufanya kazi hebu tuwape ajira moja kwa mojawatufanyie uzalengo katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nafikiri badala yakulaumu hebu tumpongeze Rais kwenye uamuzi huo. Raishata kama mtu unatakiwa kupinga akifanya jema basitumpongeze, na siamini kama kuna Mbunge yeyote waupinzani atasema madaktari wanaoajiriwa kesho kutwakwenye Jimbo langu wasije, yupo? Mtawapokea, sasakwenye kuwapongeza tumpongeze Rais anatakakutuondelea ile kero.

Kwa hiyo mimi nimeona niseme lakini watani wanguwa upande wa pil i kwamba hoja Rais akiajir i koteWatanzania tutapata faida ya wale wanaoajiriwa. Sasamsingi wa kubeza unapunguza nguvu ya wale watendajiwetu. Mimi niwaombe sana, mema anayofanya Rais wetutumpigie makofi, yakiwa mapungufu mna haki ya kusemakwa sababu kazi yenu ni kurekebisha. (Makofi)

Page 278: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naendelea kusemakwamba akifanya mema Rais tumpongeze wala hainatatizo. Hata hivyo ninyi kukosoa ni jukumu lenu ndiyo maanammekuja humu mkosoe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo mimi hojazangu zil ikuwa zinaishia hapo. Naunga mkono hoja,naendelea kuipongeza Wizara chapeni kazi, mko vizuri,fanyeni muungano, tuko nyuma yenu, Chama cha Mapinduzikitawaunga mkono. Nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, nakushukuru sanaMheshimiwa Bulembo kwa mchango wako mzuri.Wachangiaji wetu wa mchana tutakaoanza nao; tunaorodha ndefu lakini hawa wa kuanza nao tu, MheshimiwaInnocent Bilakwate, Mheshimiwa Sebastian Kapufi, MhesimiwaMartha Umbulla, sasa mnajua style yangu, nitachanganyabaadaye.

Baada ya kusema hayo, nasitisha shughuli za Bungehadi saa kumi na moja jioni.

(Saa 06.56 Mchana Bunge lilisitishwa hadi saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae.

Waheshimiwa Wabunge, niliwataja wachangiaji wetuwa kwanza, kwanza tuanze na Mheshimiwa InnocentBilakwate, atafuatiwa na Mheshimiwa Sebastian Kapufi naMheshimiwa Martha Umbulla ajiandae.

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuchangiaWizara hii muhimu. Kwanza nichukue nafasi hii kumshukuruMwenyezi Mungu ambaye amenipa afya na nguvu na kuwezakuendelea kuwatumikia wananchi wangu wa Jimbo laKyerwa. (Makofi)

Page 279: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

279

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kipekeekumpongeza Rais wetu, kwa kazi nzuri anayoifanya, hakikaimeonekana mbele ya Watanzania kuwa huyu ni Rais mteteziwa wanyonge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii piakumpongeza Waziri wetu Mheshimiwa Ummy, Naibu Waziri,Makatibu Wakuu na watendaji wote kwa kweli kazimnayoifanya ni nzuri, Mheshimiwa Ummy na timu yakoninasema msonge mbele na Mungu atawafanikisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia bajeti.Kwanza niipongeze Wizara ya Afya kwa kuboresha kituochetu cha afya cha Nkwenda. Kituo hiki sasa hivi akina mamawanapata huduma nzuri, kituo hiki kimeboreshwa,Mheshimiwa Ummy nakushukuru sana umetupatiaambulance, tulikuwa na hali mbaya. Sasa hivi kile kituo kwakweli ni cha kisasa ingawa bado wananchi wanahitajihuduma zaidi kwa sababu ukilinganisha na jiografia ya jimbolangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kwa upande wadawa. Kwa kweli Serikali inajitahidi lakini bado mahitaji nimengi na dawa bado haziwafikii wananchi wetu. NiombeSerikali iongeze nguvu na tumeona kwenye bajeti imetengahela nyingi lakini bado. Niiombe Serikali, Mheshimiwa Wazirihizi dawa mnazopeleka hebu zisimamiwe vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo menginemimi bado ninaamini pesa inayotengwa dawa zinanunuliwalakini zile dawa zinachakachuliwa zinauzwa mitaani. Miminitoe mfano kama kule kwangu Kyerwa. Ukimuuliza DMOatakwambia dawa zipo, lakini unapooenda kwa wananchiwanakwambia kila tunapoenda kituo cha afya hatupatidawa za uhakika. Kwa hiyo, mimi niombe Mheshimiwa Waziriuweke utaratibu ambao tunaweza kufuatilia hizo dawatukajua kwa siku ni watu wangapi, ikiwezekana hata majinayale waliotibiwa na kupewa dawa yawe yanabandikwa ilitupate uhakika hizi dawa zinaenda vizuri. (Makofi)

Page 280: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

280

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuiomba Serikaliyangu, bado wananchi wanahitaji sana kwa upande wavituo vya afya, Serikali inajitahidi kuboresha, lakini bado kunamaboma ambayo wananchi wameanzisha wao wenyewe,mengine yamekaa muda mrefu miaka mitano mpaka kumi.Niiombe sana Serikali, hawa wananchi tusije tukawakatishatamaa, tujitahidi kumalizia haya maboma ili wananchi wetuwaweze kupata huduma. Lakini kuna jambo ambalo miminishauri, kwenye ilani yetu ya Chama cha Mapinduzitunasema kituo cha afya kila kata na zahanati kila kijiji. Hilijambo ni zuri lakini mimi niishauri Serikali, kwa kipindi hikiambacho bado hatujaweza kufikia hapo hebu tupelekenguvu yetu kila kituo cha afya kila tarafa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano mimi nina tarafanne, katika tarafa nne nilizonazo mimi nina kituo cha afyakimoja ambacho kina uhakika. Tunaposema tunapelekakwenye kila kata nina uhakika hatutaweza kufikia hayomalengo kwa wakati tulioupanga; lakini tukipeleka kwenyekila tarafa ikapata kituo cha afya mimi ninaamini wananchiwetu tutaweza kuwasogezea huduma kwa ukaribu. Kwahiyo, huo ni ushauri Mheshimiwa Waziri uuchukue na iwe kwaWaheshimiwa Wabunge wote kwenye majimbo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala lawatumishi. Mheshimiwa Waziri bado watumishi ni wachache,wananchi wanakosa huduma kwa sababu ya watumishi. Kwamfano mimi kwenye kituo changu pale Nkwenda tunawatumishi wachache sana. Nimuombe Mheshimiwa WaziriUmmy, mmetangaza ajira kwa ajili ya madaktari, hebutuangalie haya majimbo ambayo yako pembezoni kamakwetu Kyerwa, kwa kweli hali ni mbaya sana. Tusiangaliemaeneo ya mijini hebu tuangalie na huku pembezoni iliWatanzania wote waweze kupata huduma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la bimaya afya. Suala la bima ya afya ni zuri sana, niombe sana Serikalituendelee kuwahamasisha wananchi ili kila mwananchiaweze kupata bima ya afya. Vilevile tuangalie hawa wazeewetu ambao tumesema wapate matibabu bure, bado

Page 281: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

281

huduma hii ni ngumu, wazee wetu bado hawapati hudumabure. Wanapokwenda kwenye zahanati au hospitaliwanahudumiwa na daktari lakini mwisho wanaambiwawaende kununua pharmacy.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wazee kamatumesema wapate huduma bure, Mheshimiwa Waziri hebutuweke utaratibu ili waweze kupata huduma bure ili na waowafurahie matunda ya taifa lao wakati wanaelekea jionikuaga dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi michango yangusehemu kubwa ni hiyo, lakini niombe sana MheshimiwaUmmy, kwa kweli umekuwa ukitoa ushirikiano paletunapokuja kwako kuleta matatizo ya wananchi wetu.Nikuombe sana Mheshimiwa Ummy na MheshimiwaKigwangalla moyo huo uendelee bado wananchi wetuwanayo mahitaji mengi, bado huduma za afya hazijawezakukidhi viwango vinavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayoninaunga mkono hoja, ninaishukuru sana Serikali yetu kwakazi zinazofanyika, ahsanteni sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, tunaendelea naMheshimiwa Sebastian Kapufi na Mheshimiwa MarthaUmbulla.

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nianze na neno la shukrani. Nashukuru kwa maanaya hotuba ya Mheshimiwa Waziri, taarifa ya kamati nikiaminivyote vimesheheni mambo ambayo macho yanapendakuona na masikio kusikia. Nikianza na nukuu kama ambavyowenzetu wa kamati waliitoa ya Mahatma Gandhi, waowaliitoa kwa kingereza lakini mimi nitaitoa kwa tafsiri yaKiswahili changu mwenyewe kwa maana ya afya ndio utajirihalisi na si vipande vya dhahabu na fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa misingi hiyo nakwendakuisemea Hospitali yetu ya Manispaa ya Mpanda. Hospitali

Page 282: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

282

ya Manispaa ya Mpanda ilianza mwaka 1957 ikiwa kituo chaafya. Leo hii inafanya kazi kama Hospitali ya Manispaa, nakwa misingi hiyo watu wote ndani ya mkoa wanaitegemeahospitali ile, na ndiyo maana sisiti kuishukuru Serikali yangukwa sababu najua tuko mbioni kutengeneza hospitali yamkoa na fedha zimekuwa zikitengwa na hivi karibunitumetengewa shilingi bilioni moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini, Serikali itaendeleakutuangalia kwa jicho la huruma nikiamini sisi tukopembezoni na tukikosa huduma muhimu za afya tunakuwapembezoni zaidi. Kwa hiyo, hilo nilikuwa napenda kuliwekakatika sura hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hospitali yetu hiyohiyo, mara ya mwisho alikuja Naibu Waziri. Katika kuitembeleahospitali, alipokwenda kwenye chumba cha upasuaji,nasikitika kusema alikifananisha chumba kile na machinjio;yaani kwa maana kwamba vifaa vilivyomo mle havifananina vifaa vya chumba cha upasuaji, kwa huduma zote, kamavile utoaji hewa na vinginevyo. Kwa hiyo, mahali ambapotunakusudia tuokoe maisha ya watu ukifananisha namachinjio Mheshimiwa Waziri unaona kabisa kwamba watuwale wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la huruma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua pia kunachangamoto ya upungufu wa dawa. Ni kweli mara yamwisho alikuja Mheshimiwa Waziri Mkuu akatusaidiatukaanzishiwa duka la MSD, hilo nashukuru maanausiposhukuru kwa kidogo hata kwa kikubwa unawezausishukuru. Hata hivyo pamoja na uwepo wa duka hilo badotuna tatizo kubwa la uhaba wa madawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nakumbuka MheshimiwaWaziri wetu mara ya mwisho aligusia habari ya kuiangaliamikoa ya pembezoni kwa maana ya kupeleka madaktaribingwa. Nilikuwa naomba wazo hilo muhimu, wazo hilo lauokoaji liendelee kuwa katika kichwa chako MheshimiwaWaziri. Nafahamu tuna ukosefu wa magari na katika hiliuungwana tu kama binadamu naomba niwapongeze wale

Page 283: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

283

wote waliobahatika kupata ambulance. Hata hivyo wakatinikiwapongeza hao Mheshimiwa Waziri maana yake na miminatoa shukrani in advance kwa maana najua mgaounafuata na sisi tutafikiriwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Mkoa wangu waKatavi napata aibu kuhusu suala la mimba za utotoni nikiwamwakilishi wa wananchi. Tunapozungumzia habari za mimbaza utotoni, na kwamba Mpanda ndio wa kwanza katika nchihii sisi wawakilishi wa wananchi tunayo kazi nzuri kubwa yakufanya. Nilikuwa naomba hiyo kazi kubwa ya kufanya, kwamaana ya kuwafikia vijana katika kuendelea kutoa elimukatika suala hili na tatizo la mimba za utotoni nahitaji msaadakutoka katika ofisi yako Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshazungumzia habariya ujenzi wa hospitali ya mkoa ambayo inahitaji msisitizo namsukumo. Tunacho chuo cha afya, miundombinu yote yakile chuo ambacho kilikuwa cha zamani imeshafufuliwa, kilakitu kipo katika hatua za mwisho. Rai yangu na ombi langukwako, Serikali ifanye jitihada kuhakikisha chuo kile kinaanza.Najua ni chuo kwa ajili ya matabibu, lakini ningeombatukibahatika pia katika chuo hicho hicho tukawa tunatoana wauguzi tafsiri yake ni nini? Kwanza habari ya mahitaji yawataalamu hawa itakuwa ni ndoto katika hospitali yetu,nilikuwa naomba hilo tusaidiwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipongeze, kwenyekitabu chako Mheshimiwa Waziri umeongelea habari yahuduma ya matabibu bingwa. Nafahamu kwa kupitiahuduma ya matabibu bingwa kwa Taasisi ya Jakaya Kikwetena kwa MOI, huu ni mwarobaini wa kutusaidia Watanzaniakwenda nje ya nchi, mimi hilo nalipongeza sana. Hata hivyo,pamoja na kulipongeza basi maeneo hayo yapewe fedha,na hapa si suala tu la kusema fedha zimetengwa ila ionekanefedha zikipelekwa, nilikuwa naomba kutoa rai hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayoniendelee tena kutoa pongezi kwa kupunguza rufaa nje yanchi. Suala hili ni la msingi, najua ni kwa maana ya kupunguza

Page 284: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

284

rufaa ya nje ya nchi kama vile kwa masuala ya kupandikizafigo. Tumeona pale ukizungumzia nje ya nchi ni shilingi milioni80 lakini kwa shughuli hiyo kufanywa ndani ya nchi inakuwani shilingi milioni 20, huu ni msaada mkubwa kwa wananchiwetu. Naamini nchi ya uchumi wa viwanda bila kuwekezakwenye afya ya watu, rasilimali watu, nguvu kazi ndoto yauchumi wa viwanda itakuwa mashakani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende kwenyeushauri, lakini wakati nikienda kwenye ushauri kuna suala ladharura...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Kapufi.Mheshimiwa Martha Umbulla atafuatiwa na MheshimiwaFaida Bakar na hawa sasa wajiandae dakika tano, tano kilammoja, Mheshimiwa Suzana Mgonokulima na MheshimiwaLucy Owenya. Mheshimiwa Martha Umbulla karibu.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hojailiyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote na miminimshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye amenijalia uzimana kunipa afya kuweza kusimama hapa ili kuchangia hojaya Wizara ya Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzangu kwakweli kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja naNaibu wake, na jopo zima la wataalam katika Wizara yaokwa kazi nzuri sana wanayoifanyia nchi yetu na kuitendeahaki sekta ya afya. (Makofi)

Page 285: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

285

Mheshimiwa Mweyekiti, kipekee pia nimshukuru sanaMheshimiwa Rais wetu kwa dhamira njema sana yakuhakikisha kwamba sekta ya afya hapa inakwendakuboresha afya za wananchi walio wengi wa vijijini na hasawale watu maskini ambao hawana uwezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mengi yamekwishafanyikana Mheshimiwa Rais wetu, kipekee naomba nilenge sektaya afya, ametenda mengi lakini kubwa ambalo katika sektahii naweza kulisema ameondoa tatizo sugu la uhaba wavitanda katika Hospitali ya Muhimbili; ameweza kutoa amrina kurekebisha vitendea kazi ambavyo vilikuwa havifanyi kazi,na zaidi sana dhamira yake njema ya kuboresha sekta yaafya kwa kuinua hadhi hospitali mbalimbali, vituo vya afyana zahanati katika vijiji katika kuboresha afya ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wananchi wa Mkoa waManyara hatuna la kusema, tunatoa pongezi na shukraninyingi sana kwa kuridhia kupandisha hadhi Hospitali yetu yaHaydom ambayo Mheshimiwa Waziri Mkuu alikujaakaitembelea, akaiona na akatoa pendekezo kwambaanakubali iwe Hospitali ya Rufaa ya Kanda, lakini vilevileakatoa jopo la wataalamu kuja kuangalia vigezo naninaamini kwamba vigezo vinakidhi. Kubwa la kushukuruamemtuma Mheshimiwa Waziri wa Afya hivi karibuni, hanahata siku tatu ametoka Manyara kuangalia Hospitali yaHaydom kama inakidhi vigezo vya kuwa Hospitali ya Rufaa.Hongera sana Mheshimiwa Rais wetu, hongera MheshimiwaWaziri Mkuu, hongera Mheshimiwa Ummy Mwalimu na timuyako nzima katika sekta hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ametupandishia hadhikituo chetu cha afya cha Dongobesh kuwa Hospitali yaWilaya na hilo nalo ni katika harakati za kuboresha afya katikaMkoa wetu wa Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatoa shukrani nyingi, kwaSerikali yetu ya Chama cha Mapinduzi. Lakini sambamba nakupandisha hadhi ya Hospitali ya Haydom kuwa ya Rufaaninatoa tahadhari na ombi kwa Serikali kwamba mara nyingi

Page 286: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

286

wakipandisha hadhi hospitali, huduma zinazotolewa kwenyehospitali hizo zinakwenda kupanda gharama. Tunaombakwa dhamira hiyo hiyo ya kuboresha afya katika vijijitunaomba wasimamie kwamba Hospitali ya Haydomitakapopanda hadhi kuwa ya rufaa, basi na hudumazitakazotolewa ziweze kuwa wananchi wetu wanazimudukwa maana ya kwamba kutopandisha gharama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na habari njema hizinilizotaja bado Mkoa wa Manyara una matatizo lukuki.Kubwa sana ni katika Wilaya za Simanjiro na Kiteto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na Kiteto, miminimekuwa Mkuu wa Wilaya katika Wilaya ya Kiteto kwa miakamitatu. Wilaya haina gari la wagonjwa. Miaka yote niliyokuwapale, gari ni moja iko garage kila wakati, miundombinu yaWilaya ile ni mibaya sana, bila gari wananchi wanafiabarabarani na sasa hivi tunasikia habari njema za kugawamagari kwenda katika Wilaya mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwa moyo wadhati Hospitali ya Kiteto iweze kupata gari ya kubebawagonjwa ili iweze kuondokana na tatizo la usafiri kwawagonjwa wetu. Tukizingatia Wilaya ile ni kubwa sana,miundombinu ni mibaya barabara ni za rough roads,tunakuomba Mheshimiwa Ummy iangalie Kiteto kwa jichola ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende katika Wilaya yaSimanjiro, hapo ndipo fungakazi. Wilaya ya ile ni ya siku nyingilakini hakuna Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba, leo, walivyosikiajina langu nachangia mchana, Mkurugenzi alinipigia simu.Akasema najua kwamba na Mbunge yupo mama tunaombautoe kilio chetu kwa Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Menyekiti, hakuna kituo cha afya paleau Wilaya yetu ya Simanjiro haina Hospitali ya Wilaya na hilini tatizo kubwa sana. Wagonjwa wanatoka Orkesment

Page 287: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

287

kwenda kupata huduma ya afya Seliani – Arusha, kilometakaribu 200. Wanatoka Orkesment kwenda Mererani kilometakaribu 122, wataoka hapa wanakwenda KCMC kwakilometa nyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Wazirininakuomba, najua kwamba Wilaya imeshakuandikia baruatoka Disemba, 2016 na ninadhani hapo nitashika shilingipamoja na mambo mazuri na sifa niliyokupa.

Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri, Wilaya yaSimanjiro iweze kupandisha hadhi Kituo cha Afya cha Urbancha Orkesment kuwa Hospitali ya Wilaya ili wananchi walewapate huduma ya afya kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasahivi ambapo hali ni ngumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka hapo niendeleekuchangia kwamba huduma za afya hasa zahanati zetu zavijijini, katika Wilaya hizo nilizotaja ni za duni sana. Hata hivyotumepata habari njema kwamba, Wizara ya Afya imetengashilingi bilioni 251, hizo zinakwenda kuboresha huduma zaafya. Pamoja na hayo, katika zahanati na vituo vya afyavingi vij i j ini hakuna madaktari, hakuna wahudumuwataalam wa afya kwa hiyo, hizo fedha zinakwendakutumika kwa jinsi ambavyo haitaboresha afya za wananchi.Tunaomba sambamba na kutoa fedha kwa ajili ya hudumaza afya, Serikali iangalie kupeleka wataalam, madaktari,wauguzi na wahudumu wenye taaluma katika Wizara yaAfya. Kituo kizima kinakuwa na mhudumu ambaye hana hataelimu yoyote na ndiye anayetegemewa kama daktari, kamamuuguzi. Haya ninayosema ni ya kweli, tufanye utafiti tusaidiewataalam waende katika wilaya zetu hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haraka haraka nije kwenyesekta ya maendeleo ya jamii na mimi nioneshe masikitikoyangu kidogo katika sekta hii. Najua kwamba umefanyamengi na tumesikiliza jinsi ambavyo umetueleza mengi katikasekta ya afya na hata katika sekta ya maendeleo ya jamii,lakini niseme mengi bado yanaonekana kama nadharia.Tutakwenda kuboresha, tutasimamia, bado hatujapata hasa

Page 288: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

288

hasa ni nini kimefanyika, hatujaona sheria zinazokandamizawanawake kuletwa hapa ili tuweze kuzirekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuoni mikakati madhubutiya kuondoa ajira haramu ya watoto wetu katika migodi nakadhalika. Hatujaona ni jinsi gani wazee wetu wanaendakunufaika na hizi shilingi 251,000,000,000 za sekta ya afya. Kwahiyo, mimi nitoe rai kwamba pengine ni vizuri Wizara ya Afyani giant ministry, sekta ya maendeleo ya jamii ni kamaimemezwa, nilikuwa nashauri na kwa kuzingatia kubanamatumizi, pengine sekta ya maendeleo ya jamii ingeendakwenye wizara ambayo si kubwa kama Wizara ya Afya iliiweze kutendewa haki na yenyewe iweze kuhudumiawananchi zaidi kwa jinsi ambavyo sasa hivi inahudumia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ni ombi ambalo nilionanilitoe na ni mawazo yangu, lakini ninazingatia suala lakubana matumizi. Ninaomba kwamba Waziri atakapokuwaana-wind up atueleze sasa sisi wananchi wa Mkoa waManyara, kwanza pamoja na shukrani tulizompa, na asituonekwamba hatuna shukrani, lakini atutendee haki katika Wilayazetu nyingine, hasa hizi za wafugaji za Simanjiro na Kiteto.Waheshimiwa Wabunge wa Wilaya nilizotaja, mimi niMbunge wa Viti Maalum, tunajenga nyumba moja,tusaidiane wala mtu asinielewe vibaya, lakini mimi pianimepata kura zangu kutoka kwa wananchi Wilaya hizo,naomba tusaidiane kuhakikisha kwamba na Wilaya hizizinapata huduma ambazo wananchi wengine wanapata.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa ni gari la kubebawagonjwa. Wilaya zetu hizi zina kilometa nyingi sana, hususanWilaya ya Simanjiro ina square kilometer zaidi ya 20,000;unaweza kuangalia kutoka kituo cha afya hadi makazi yawananchi ni zaidi ya kilometa 20, 30 hadi 50, nadhani utaonaumuhimu wa kupeleka gari katika maeneo haya.Tunakuomba Mheshimiwa Ummy na tunakuamini, weweunatosha na unatosha kabisa na chenji inabaki, naombaupeleke gari katika Hospitali za Kiteto na Simanjiro ili tuweze

Page 289: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

289

kuhudumia wananchi wetu na wenyewe wanufaike nahuduma za afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,hongera CCM, hongera Serikali yangu ya CCM kwa kufanyahaya, hasa Serikali ya Awamu ya Tano, wamefanya kazikubwa na tunampongeza Rais wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkonohoja, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya, ahsante sana MheshimiwaUmbulla, naelewa kwa nini umesema hivyo. Tunaendelea,Mheshimiwa Faida Bakar, atafuatiwa na Mheshimiwa SuzanaMgonokulima na Mheshimiwa Lucy Owenya wajiandae.Hawa ni dakika tano-tano tu.

MHE. FAIDA MOHAMMED BAKAR: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangiaHotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto. (Makofi)

Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwakutujalia pumzi hadi kufikia siku ya leo na tunawaombeamaghufira ambao wametangulia mbele ya haki, Inshallah.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi sana kwa Serikaliyangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwana chama changu kitukufu Chama cha Mapinduzi. Na pia,napenda kuipongeza Serikali yangu ya Mapinduzi Zanzibarinayoongozwa na Dkt. Shein, na vilevile kumpongeza Raiswangu Magufuli kwa jitihada kubwa ambazo anazichukuakatika nchi hii, na kwamba ametujali sisi wanawake kwakumteuwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongezajembe! Huyu ni jembe kabisa! Huyu ni Mheshimiwa dada yangu

Page 290: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

290

Ummy, napenda kumpongeza kwa kazi kubwa anayoifanyakwa kushirikiana na Naibu wake Dkt. Kigwangalla. Hawa niviongozi bora sana na wanaiweza Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi napenda kuongeleaBenki ya Wanawake. Hii Benki ya Wanawake kilaninaposimama ninaitetea. Kwanza naipongeza kwa sababuimefanya kazi kubwa sana. Mheshimiwa Waziri ameongeakwamba shilingi 12,000,000,000 zimetolewa kwa wajasiriamalimbalimbali 9,650 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya,Njombe, Iringa, Dodoma, Ruvuma, Pwani na Mwanza, lakinikila nikisimama najiuliza, napata wivu sana mimi nasema kwanini hii Benki ya Wanawake na Zanzibar isiwepo? Hii Benki niya Wanawake wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii benki si ya Dar es Salaamwala si ya Mwanza wala si ya Songea wala si ya sehemumoja tu, hii ni Benki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Naomba Mheshimiwa Ummy uniambie leo, kila nikikuulizaunaniambai sijui hazijatolewa pesa milioni ngapi, kwani hiikazi ya kutoa hii pesa ni ya nani? Si iko katika bajeti ya Wizarayako? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi naombamshirikiane na Serikali na Wizara ya Serikali ya MapinduziZanzibar kule, mshirikiane Mheshimiwa Ummy, mimi sitapendakusimama hapa tena kuiongelea Benki hii ya Wanawake waZanzibar.

Zanzibar kuna wanawake kama sehemu nyingineyoyote, Zanzibar kuna wanawake ambao niwafanyabiashara kama sehemu nyingine yoyote, Zanzibar niwapiga kura wakubwa wa Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba leo iwe mwisho,Mheshimiwa Ummy, naomba leo iwe mwisho wewe nimwanamke mwenzangu naomba unisikie. Nasema mwishoiwe leo, la kama mimi sitajibiwa leo hapa kama Benki yaWanawake itaanza shughuli zake Zanzibar, mimi na wewetutakuwa hatuelewani. (Makofi)

Page 291: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

291

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukatili dhidi ya watoto wakike na wa kiume. Wote hapa ni mashahidi juu ya mamboyanayotokea katika dunia yetu hii, si hapa tu dunia nzimawanawake, na watoto wanadhalilishwa, wengi wa watotowanadhalilika; wengi wa watoto jamani ni mashahidikwenye whatsApp siku hizi mengi. Utaona mtoto kakatwamkono, sijui kakatwa mguu, kakatwa kichwa; wanadhalilikawatoto; kwa nini watoto wanadhalilika Mheshimiwa UmmyAlly Mwalimu kwa nini watoto wadhalilike? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kama Wizara yakoinajitahidi katika kuwatetea watoto wa kike na wa kiume,lakini bado. Tunaomba watoto wa nchi wasidhalilishwe kwasababu watoto ndio Taifa letu la kesho. Mheshimiwa UmmyAlly nakuomba sana maafisa wako wafuatilie sana habarikama hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo linajitokezajamani, mimi naomba kusema tu ukweli, unanua sipendikufichaficha. Watoto wanadhalilishwa kijinsia jamani ninyihamjui wenzangu ninyi? Watoto wanadhalilishwa kijinsia,mimi nimekwenda kufanya ziara Mkoa wa Kusini Pemba, kilaninapokwenda wananiambia Mheshimiwa Mbungetunalalamika watoto wetu washaharibika, watotowameshaharibiwa, kwa nini baba mtu mzima uendekumharibu mtoto mchanga? Mtoto mdogo anayesomashule, wa kike na wa kiume, kwa nini jamani? Nililia watotowanadhalilishwa, wanaharibiwa maumbile yao jamani!(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, turudi kwa Mwenyezi Mungubinadamu, akina baba nawaomba hii si nzuri. Mheshimiwanasema kwa uchungu kwa sababu mimi ni mzaziMheshimiwa Ummy, watoto wanabakwa nawanadhalilishwa. Sitaki niseme mengi leo, nikisema nitalia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanawake wa KusiniPemba walinililia wakasema watoto wetu wanadhalilishwa

Page 292: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292

mpaka shule kule, na kuna baadhi ya walimuwanawadhalilisha watoto. (Makofi)

MBUNGE FULANI: (Hapa hakutumia kipaza sauti).

MHE. FAIDA MOHAMMED BAKAR: Sitaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu gani inakuwahivi? Watoto wetu tunawazaa wenyewe watoto, mtu babueti anakwenda kumfanyia ushenzi mjukuu wake! Eeh! Babaaliyemzaa mtoto anamgeuka, kwa nini? Turudi kwa MwenyeziMungu sisi binadamu, si nzuri, inatisha. Tanzania hii inatakiwaiwe ya amani na utulivu na upendo, kwa nini tunabadilika?Tumeacha dini sasa hivi tunahururika na dunia tunafanyamambo ya ajabu binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimba za utotoni. Baba mtumzima anakwenda kumjaza mimba mtoto; Sheria ya Ndoairekebishwe, iletwe Bungeni tuirekebishe sheria hii, haikubaliki,watoto wanadhalilika wanapigwa mimba na watu wazimawalio na madevu yao mengi tu, wanawadhalilisha watoto.Hii haikubaliki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wengine wanawaozesha watoto umri mdogo kwa sababuya visenti, kwa sababu ya ng’ombe. Kwa nini tunafanya hivibinadamu? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto tuwajali natuwatunze. Watoto ndio watakaokuja kutusaidia sisi, tusijionevijana kesho kutwa sisi tutakapozeeka na tutakapokuwahatujiwezi wao watatusaidia; kwa nini tunafanya hivi?

Mheshimiwa Waziri nakuomba ulisimamie, naanayepatikana na hatia hii achukuliwe hatua kali, naonabado hatua hazijachukuliwa kali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wazee wetu, mzee wamwenzako ni mzee wako, leo wewe mzee wa mwenzakounamdhalil isha. Kuna makabila mbalimbaliwanawanyanyasa wazee kwa sababu ya kuona kwamba niwashirikina, wazee wakiwa na macho mekundu wanawaua;nashukuru Serikali siku hizi inajitahidi sana katika hili; na kuwaua

Page 293: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

293

ma-albino; nashukuru sana sasahivi Serikali imejitahidi, lakinitusichoke na tuone kwamba wadhalilishaji wa wazee wamo.Tuwalinde wazee, wapewe vituo vyao, nyumba zao ziwe safi,wapewe lishe kwenye vyakula vyao na vile vile walindwe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mzee wa mwenzako nimzee wako tusijione leo vijana, sisi wenyewe tutakuwa wazeena tutataka kuhudumiwa. Ukiwaona saa nyingine unaliawazee nyumba wanazolala zile. Vituo vile Mheshimiwa Ummyjitahidi, vituo hata kama… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea!

MHE. FAIDA MOHAMMED BAKAR: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Suzana Mgonokulima,atafuatiwa na Mheshimiwa Lucy Owenya na MheshimiwaZuberi Kuchauka ajiandae kwa dakika tano na mwenzake.

MHE. SUZANA C. MGONOKULIMA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zanguza dhati kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia jioni ya leokwenye Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naombanianze na kundi la walemavu. Ninarudia tena kusemaMheshimiwa Ummy - Waziri wa Afya, matatizowanayoyapata wanawake wenye ulemavu wakati wakujifungua bado yako pale pale. Niliongea mwaka wa janakatika Bunge hili lakini wakati nikiwa field huko kwenyemajimbo nimekuta wauguzi wengi wanawanyanyapaa sanawanawake wenye ulemavu wakati wa kujifungua.

Page 294: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

294

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, kwa dhamanaya nafasi yako, hili ulichukue na ulifanyie kazi, walewatakaobainika wanaendeleza vitendo vyakuwanyanyapaa wanawake wenye ulemavu wakati wakujifungua wachukuliwe hatua za kinidhamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2011 mpaka mwaka2012 Hospitali ya Mkoa wa Iringa ilipata hadhi ya kuwaHospitali ya Rufaa. Tatizo ambalo linaikumba hospitali ile niukosefu wa madaktari bingwa. Hitaji la madaktari ni 24, hadisasa hivi hospitali yetu ile ya rufaa ina madaktari watano,hivyo kusababisha kazi ya kiutendaji ya kuokoa maisha yawananchi wa Mkoa wa Iringa kuwa ngumu sana.Mheshimiwa Waziri, naomba hili ulichukue kwenye mgawowako wa madaktari hao wanaopata ajira, basi MadaktariBingwa uwapeleke kwenye Mkoa wetu wa Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuja kwenye Mfuko waBima. Afya kwa wazee wetu wa Taifa hili imekuwa ni tatizo.Serikali imejikita kuwasaidia wazee hawa huduma yamagonjwa ya homa, tumbo, lakini si pale wanapopatamagonjwa yale ya moyo, ini, figo, vipimo hivi lazima walipie.Sasa kama Serikali inataka kusaidia kundi la wazee; hivivipimo nilivyovisema gharama yake ni kubwa; na Serikalihaitaki kuwekeza mkono wake, hii huduma ambayotunasema tunataka kuwasaidia wazee naona sio sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi Wizara ichukue jukumuhili kuhakikisha hawa wazee ambao Serikali imesemaitawatibia bure, iwe bure ya magonjwa yote hata hayoniliyoyaainisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Hospitali ya Mkoawa Iringa kupata hadhi ya kuwa Hospitali ya Rufaa, Manispaaya Iringa tulijenga Hospitali ya Wilaya ambayo iko maeneoya Frelimo na inaitwa Hospitali ya Frelimo. Hospitali hii inawauguzi wakutosha, madaktari wakutosha, kinachokujakuleta shida ni upungufu wa vifaa tiba.

Page 295: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

295

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi ninapozungumza sasahivi hospitali hiyo yenye wauguzi wa kutosha na madaktariwa kutosha haina vifaa vya uuguzi ambapo tumekosa kupatavipimo vya full blood picture, x-ray, ultra sound ambapoingekuwa vipimo hivi viko pale, hospitali hii ingepokeamsongamano wa wagonjwa ambao wanatakiwa kutibiwapale ili wasiende kutibiwa kwenye hospitali ya rufaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayoningependa nijikite kwenye unyanyasaji wa watoo wadogowa kike. Sipo sambamba na wachangiaji waliosema, mtotowa miaka chini ya miaka 18 kuozeshwa na kuwa mama wanyumba ni makosa makubwa sana kiafya. Kwanza nyongazake zenyewe hazijakomaa kuweza kuendeleza mambo yamipango mingine ya kiutu uzima na hivyo tunawafanyia hayomatendo kiunyama kwa sababu tendo la ndoa kwa mtotowa miaka chini ya 18 hana hisia nalo kwenye akili yake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba Wizara hiikama sheria inakingana, kuwa haiwezekani kutungwa sheriahiyo, basi tutalazimisha Wizara ya Elimu iweke kiwango chaelimu ya mtoto wa kike ni Kidato cha 12, ili kama itaonekenakuna mzazi yeyote yule ana binti yake ameolewa chini yamiaka 18 aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tutakuwatumewakwamua kundi la watoto wa kike ambao kwatamaa za wazazi wao… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. SUZANA C. MGONOKULIMA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja ya Kambi ya Upinzani kwamaana hii ndio inayo… (Makofi)

Page 296: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

296

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Lucy Owenya,atafuatiwa na Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka naMheshimiwa Mgeni Jadi Kadika ajiandae.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kupata nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ugonjwa wa saratani kwasasa hivi katika dunia ni ugonjwa hatari sana pamoja nasaratani ya shingo ya kizazi imekuwa ni tishio. Zaidi yawanawake 274,000 duniani wanafariki kwa ugonjwa huuna Tanzania ikiwa ni mojawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru hospitali yaOcean Road imekuwa ikitoa huduma ya mionzi na kusaidiawagonjwa wa saratani lakini hospitali ile wote tunashuhudiaimezidiwa na wagonjwa ni wengi. Nashukuru hospitali yarufaa KCMC ilipata wafadhili na wakafadhili jengo kwa ajiliya unit ya kansa, walijenga kwa shilingi bilioni 1.2 na wafadhilikwa sasa hivi wako tayari kununua vifaa kwa ajili ya mionzi,kutoa vifaa zaidi ya shilingi bilioni sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri, kwenye kitabu cha maendeleoumetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya KCMC, jengoambalo ni special kwa kitaalam linaitwa banker linahitajikakwa ajili ya kuweka vile vifaa vya mionzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, KCMC tunachoomba,Serikali itusaidie wanahitaji shilingi bilioni saba. TunamwombaWaziri wa Fedha na Kamati yako ya Bajeti mkae chinimuangalie ni kwa jinsi gani mnaweza mkaipatia KCMC hizishilingi bilioni saba ili waweze kujenga lile jengo. Kwa sababu,Kanda ya Kaskazini itapunguza msongamano katika Hospitaliya Ocean Road, inaweza ika-save zaidi watu milioni 15 nakwa kiasi kikubwa tunaweza tukapunguza ugonjwa wasaratani ya kizazi kwa wanawake na kutoa huduma yamionzi pale KCMC.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie

Page 297: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

297

kidogo magonjwa yasiyoambukiza (non-communicabledisease). Nimekuwa nikiongea mara nyingi hapa,ninamshukuru Mheshimiwa Waziri amesema wameanzishawatu kwenda mazoezi na kadhalika, nafikiri ni vizuri sasaWizara hizi zikashirikiana Wizara ya Miundombinu na Michezoili muweze kujenga pavement kwa ajili ya watu kutembeakwa miguu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pale Dar esSalaam kwa mfano, zile njia ya majitaka (sewage system)mnaweza mkazifunika na watu wakaweza kupita kwamiguu. Nchi zilizoendelea kwa sasa hivi wanahimiza watuwaende kazini kwa kutumia baiskeli, kwa sehemu kama Dares Salaam mtu atatembeaje na baiskeli? Kutembea tu kwamiguu unagongwa na bodaboda. Kwa hiyo, ni vizuri Serikalimkashirikiana kwa pamoja mkatengeneza pavement kwaajili ya watu wa kutembea kwa miguu na kwa kiasi kikubwasana tutapunguza magonja ya kisukari ambayo inasemekanaTanzania watu zaidi ya asilimia tisa wana ugonjwa wa kisukarimpaka watoto wadogo wana wanapata kisukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zi l izoendeleawameacha kabisa ku-serve hivi vyakula vya junk food, lakinisasa hivi ndiyo vimeanza kuletwa Tanzania kama Kentucky,Fried Chicken na kadhalika. Ni vizuri mkazidi kutupa elimu iliwatu waachane na hivyo vyakula ambavyo vinaongezamagonjwa ya shinikizo la damu ya kupanda na kushuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kidogo nizungumzie mimbaza utotoni. Mimba za utotoni imekuwa ni hatari kwa kweli.Pamoja na kusema watoto wadogo wanaweza kuolewachini ya miaka 18 mimi napinga jambo hili, kwa sababukwanza tunawakosesha watoto wale elimu, pili mtoto wakike akijifungua kabla ya umri wake anaweza akapatamagonjwa kama ya fistula, tatu anaweza kushindwakujifungua inabidi atumie scissor na wengine baada ya hapowanakuwa ni single parent, unakuta wazazi wenyewe wakatimwingine wana wanyanyapaa wanawaambia hukusoma,kwa hiyo watoto wale wanaishia kuwa watoto wa mtaani,wanashindwa kuendelea na masomo, wanaweza kwenda

Page 298: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

298

kuwa machangudoa na hii ni kumrudisha mtoto wa kikenyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna moja aunyingine naomba Wabunge tukubaliane na hili, tulionawenyewe juzi tulivyoongelea suala hili, Sheria ile ya Ndoa yamwaka 1971 ibadilishwe wengine walikuwa wanapingakutokana na imani zao za dini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja yaUpinzani naomba muichukue na muifanyie kazi kwa sababuina ushauri wa kutokasha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa ZuberiKuchauka atafuatiwa na Mheshimiwa Mgeni Kadika.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi hii nichangie Wizara hii ya Afya.

Awali ya yote nitoe shukrani zangu za dhati kwaMheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Katibu wa Wizara hii kwahaki walioyonitendea katika kipindi hiki. Mwaka jananilisimama hapa nikalalamika sana, nikalia sana, kwambahospitali yangu ile ya Wilaya ya Liwale haina wafanyakazikwa maana ya madaktari lakini nashukuru AlhamdulillahMheshimiwa Waziri ameisikia kil io changu amenipamadaktari wawili namshukuru sana nasema ahsante sana.(Makofi)

Pamoja na hilo bado nitaendelea kukuombakwamba katika zahanati 31 za Wilaya ya Liwale zinaongozwana enrolled nursing, kwa maana ya kwamba hatuna clinicalofficers. Wilaya mzima ile ina clinical officer wanne tu. Kwahiyo, bado tunaendelea kulia pengine kama utapata nafasihiyo utuongezee hao clinical officers.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile hospitali ile ya Wilayaya Liwale ina x-ray haina mtaalamu wa hiyo x-ray.

Page 299: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

299

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nijielekeze kwenyetaasisi moja muhumu sana ambayo ni taasisi ya Mirembe.Taasisi ya Mirembe kama ilivyo umuhimu wake, nimefanyautafiti huu kwa muda wa miezi sita, taasisi ya Mirembeinakabiliwa na matatizo lukuki. Kwanza kabisa ni Ikama yawafanyakazi, posho ya mazingira magumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoongea posho yamazingira magumu Hospitali ya Mirembe inafahamika. Piamadai ya watumishi mbalimbali waliopandishwa madarajapamoja likizo. Kikubwa zaidi katika taasisi ile ya hospitali yaMirembe sasa hivi imegubikwa na tatizo kubwa la rushwa.Kwa utafiti nilioufanya, tatizo hili na matatizo mengine yotelukuki niliyoyaorodhesha hapa, tatizo kubwa liko kwenyeuongozi wa Hospitali ya Mirembe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiongea na wafanyakaziwa Hospitali ya Mirembe morali ya kufanyakazi imeshuka.Hawana ushirikiano kutoka ngazi ya juu mpaka kwa mtu wachini. Naomba Mheshimiwa Waziri ufanye utafiti, nendaHospitali ya Mirembe, Mkurugenzi wa Hospitali Mirembe siyorafiki kwa wafanyakazi wa Mirembe, na hii inashusha hadhina morali ya wafanyakazi ya Hospitali ya Mirembe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuna wafanyakaziambao wameshushwa madaraja na wanashushwa namshahara, hivi mfanyakazi aliyeshushwa daraja, mkashushana mshahara halafu unamuacha kituo hicho hicho, huoufanisi wa kazi atautoa wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijielekeze sasa kwenyeHospitali ya Wilaya ya Liwale. Hospitali ya Wilaya ya Liwaleaina hadhi ya kuitwa Hospitali ya Wilaya, kama ambavyoKatibu wa Wizara ya TAMISEMI anayeshughulikia mambo yaafya alivyosema. Halmashauri pamoja na kwambatumeambiwa sisi wenyewe ndiyo tuanzishe vipaumbe, kwelisasa hivi tumeshatafuta kiwanja tumeshapata kiwanja, naInshaallah bajeti inayokuja tunaweza tukaanza ujenzi.Tunaomba Mheshimiwa Waziri support yako tujengee Hospitaliya Wilaya ya Liwale.

Page 300: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

300

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kama nilivyosemaawali Wilaya ya Liwale ina zahanati 31, ina kata 20 lakinituna kituo kimoja tu cha afya. Hapa napenda kutoa shukranizangu za dhati kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI amewezakutusaidia pesa kidogo kwa ajili ya kuboresha kile kituo chetukidogo cha afya, naye nasema Alhamdulillah MwenyeziMungu ampe umri mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa badonaendelea kusisitiza takwimu za ...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana, ninaunga mkono hotuba ya upinzani. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mgeni Kadika, atafutiwa naMheshimiwa Susan Lyimo.

MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza sina budi kumshukuru Mwenyenzi Mungu, kwakunijalia afya njema na leo hii kuweza kusimama kwa ajili yakuchangia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazeena Watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kunipatia nafasihii. Nampongeza Katibu Mkuu wa Chama changu CUFMaalim Seif Sharif Hamad, pamoja na uongozi wa Taifa kwakazi kubwa aliyonayo kupambana na wanafiki walioko ndaniya chama chetu, kututaka kutugawa na kusambaratishachama chetu. Nasema chama chetu kiko imara Maalim Seifchapa kazi tuko pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu uzazisalama. Takwimu za hivi karibuni zinaonesha wanawake 30wanafariki kila siku kwa kujifungua. Hii ni idadi tu ya walewanawake wanaofika kwenye vituo vya afya na wanaofika

Page 301: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

301

hospitali kwani wengi wanajifungulia majumbani, idadi nikubwa na hii hali inatisha. Wanawake wengi tunapotezamaisha kwa uzazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo changamoto nyingizinazo msababisha mwanamke kufariki. Kwanza ni kukosavifaa tiba na dawa; pili, lishe bora na umaskini unachangiapamoja vituo vya afya kujengwa mbali na wananchi, hivyo,inapelekea kupata matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naishauri Serikalibajeti ya Wizara ya Afya iongezwe na wale watuwanaofanyakazi kwenye sekta ya afya waboreshewe piamaslahi yao ili wapate kufanyakazi kwa weledi mkubwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naipongeza Serikalikwa kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya katikanchi hii vijijini na mijini. Waathirika wengi wanaopotezanguvukazi ni vijana walio chini ya umri wa miaka 18. Watotohawa wanatoroka shule na baadaye wanajiingiza katikavitendo vya kutumia dawa za kulevya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dawa za kulevyazinachangia kiasi kikubwa maambukizi ya UKIMWI namagonjwa ya akili, naishauri Serikali kupitia sober house nilazima akiingia mle walipie ada, wengi wao hawana uwezo,wazazi wao tayari wameshawatelekeza, kwa hiyo Serikaliiwatibu bure kupitia Wizara ya Afya kwa sababu hawanauwezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu ukatiliwa kijinsia. Wanawake wengi katika nchi hii wananyanyasika,wananyanyaswa na waume zao, kupigwa hata kuuawa,kwa sababu ya mapenzi tu. Wengine ni waume zao, wengineni wapenzi tu, hilo jambo lipo, mashuleni, vyuo vikuu watotowanajiingiza kwenye mapenzi na baadaye wanauawa. Hilijambo ni la kutiliwa nguvu sana kwa sababu linapotezavijana wetu wengi kwa ukatili. (Makofi)

Page 302: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

302

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Susan Lyimo atafuatiwa na Mheshimiwa GraceTendega na Mheshimiwa Devotha Minja ajiandae.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana kwa kunipatia fursa hii na mimi niwezekuchangia kwenye hoja muhimu sana ya afya za Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri tu kwamba na mimi niMjumbe wa Kamati hii, kwa hiyo mambo mengiyanayozungumzwa kwa kweli yananifurahisha na niseme tukwamba Wizara inajitahidi, lakini Serikali inashindwa kupelekafedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani kwa Taifakubwa kama Tanzania, lenye watu zaidi ya milioni 50, Wizaraya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto hiindiyo ambayo imeshika jamii nzima nazungumzia hasa Fungunamba 53.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kusikitisha kwamwaka unaoisha Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii nikiondoaFungu lile la Afya wametengewa fedha za maendeleo mpakasasa hivi zilizoenda ni asilimia 2.3. Hii ni aibu kubwa mno, hivituaacha kuwaona watoto wa mitaani, tuaacha kuwaonawatoto wadogo wenye mimba changa?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni Wizarainayoshughulikia wazee, niseme tu labda ndiyo sababu mvuahazinyeshi na zikinyesha zinanyesha za mafuriko, kwa sababunchi hii ni kwamba tumelaaniwa na wazee. (Makofi)

Nimepita hapo nje kuna bango la Wizara ya Afyalinasema “Mzee Kwanza,” na linasema “Mzee alikuwa kamawewe na wewe utakuwa kama huyo mzee.” Ajabuukiangalia hotuba nzima ya Waziri ameongelea kidogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi hapa ninahotuba ya Waziri ya mwaka jana alizungumza na alisemamwaka huu wa wataleta Sheria ya Wazee. Mwaka huu

Page 303: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

303

hakuna chochote kinachozungumzwa kuhusu Sheria yaWazee. Wakati Sera ya Wazee inapita toka mwaka 2003 leoni mwaka wa 14, hakuna Sheria ya Wazee na ndiyo sababuleo wazee wanauawa kwa sababu hakuna sheriainayowasimamia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwa kuwaMheshimiwa Waziri mwaka jana alisema na siyo mara moja,amekuwa akijibu maswali hapa kwamba sheria italetwa,leo kwenye kitabu chake chote hakuna jambo lolotelinalozungumzia kuhusu sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua wazee wa Taifa hiliwamelitumikia Taifa hili wametusaida kuleta uhuru, lakiniwazee hawa wametelekezwa. Makazi yao hayaeleweki,chakula wanachokula ni taabu, kubwa zaidi naomba Serikalisasa ituambie ni lini inaleta Sheria ya Wazee, ili wazee wanchi hii waweze kujua haki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye Wizara yaAfya. Wizara ya Afya, afya ndiyo jambo la msingi, afya ndiyoutajiri kama ambavyo Mahatma Gandhi amesema. Utajirinamba moja ni afya zetu wananchi. Unapokuwa na afyanjema ndiyo unaweze kujenga Taifa. Afya za Watanzania zikomashakani na ninasema hivi kwa sababu fedha hazijaenda.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali kama ya Muhimbilini hospitali ya Taifa, ilikuwa inaomba shilingi bilioni tano kwaajili ya vifaa tiba hawajapewa hata senti tano. Hospitali yaKCMC imeomba shilingi bilioni nne hawajapewa hata sentitano. Hospitali ya Bugando kwa ajili ya mashine ya Kansahaijapewa fedha, tunategemea nini? Kubwa zaidi Hospitaliya Jakaya Kikwete ambayo inafanya kazi kubwa sana yakutibu wagonjwa wa moyo, ambayo inasaidia sanakupunguza gharama za kwenda nje, lakini taasisi ilehaijapewa fedha. Pamoja na kwamba Mawaziriinawezekana wanajitahidi sana, lakini fedha hakuna.Tunafanyaje? (Makofi)

Page 304: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

304

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba kamamwaka jana tulitoa shilingi trilioni 28 zimeshindwa kwendajapo asilimia 50 za fedha za maendeleo, leo tunaongezatunasema shilingi trilioni 33 hizo hela zinatoka wapi. Kwa hiyo,jambo ambalo linashangaza hata zile fedha zetu za ndanibado haziendi tatizo liko wapi? Au mnatudanganya kwambamnakusanya sana lakini fedha hazipo. Hili jambo kwa kwelilinatutia wasiwasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambaloninapenda kuzungumza ni suala la madaktari walioajiriwajuzi. Hapa nina barua mbili kutoka TAMISEMI kwa ajili ya hawamadaktari. In fact, walikuwa waje Dodoma Chuo chaMipango kwa ajili ya semina elekezi na wafike kabla ya tarehenane, baadaye kuna barua nyingine inasema waende mojakwa moja. Hii imetoka juzi tarehe Mosi, waende moja kwamoja kwenye vituo, jana tena Dkt. Chaula ameandika baruanyingine waende moja kwa moja kwenye Halmashauri, hukokwenye Halmashauri watafutiwe sehemu za makazi na fedha.Hivi najiuliza hizo Halmashauri tayari zimetengewa hizo fedhaau mnataka hawa madaktari waende huko kama ambavyowalimu wanateseka, wanafika wanaolewa na Wenyeviti waMitaa au viongozi wa kata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri sana tunahitaji kwelimadaktari, kama ambavyo Kambi ya Upinzani imesema,sielewi inawezekanaje Rais tu ndiyo aseme baada ya haomadaktari kushindwa kupokelewa kule Kenya, leo anatoakibali kwa hawa madaktari 258. Je, hawa 3,000 waliokomitaani wanakwenda wapi? Ndiyo sababu Kambi yaUpinzani inasema je, huu siyo ubaguzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hawa wasingekuwawamejiandikisha kwenda Kenya ina maana leowasingeajiriwa, kwa hiyo kuna haja ya Serikali kuwa namipango thabiti ya ajira ya watu wake na siyo kusubiri watuwaende mahali fulani, wanatakiwa kwenda nchi fulaniwakikosa ndiyo Serikali inawapa ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni kwamba

Page 305: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

305

hawa madaktari wamesomeshwa kwa gharama kubwasana, kwa maana hiyo, ni lazima kama wanapelekwa mahalikwenda kufanya kazi maandalizi ya kina yawe yamefanyikaili wasije kuwa frustrated. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie nadhani hiyo nibado dakika tano. Pamoja na kwamba nia njemahaikuwepo ya kupeleka madaktari hawa, kwa sababu wotetunajua Kenya ina madaktari wengi kuliko Tanzania, WorldHealth Organization inasema kwamba daktari mmoja Kenyaanahudumia wagonjwa 16,000 wakati Tanzania daktarimmoja anahudumu watu 20,000. Kwa hiyo, hainiingii akilinini sawa na mgonjwa yuko ICU halafu na mwingine ana nafuuunasema daktari ampe dawa yule mwenye nafuu amwacheyule ambaye amezidiwa. Kwa hiyo, hili jambo halikubaliki.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niongelee suala landoa za utotoni. Pamoja na kwamba sheria yetu inakinzanalakini hatuwezi kuvumilia watoto wa kike wakiendeleakupata mimba za utotoni, maana yake ni kwamba Serikaliinaruhusu mimba za utotoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwambatunajua kuna watoto wengi wako mitaani, rai yangu nikwamba lazima tulete sheria hiyo, tuipitishe na nina hakikaMheshimiwa Ummy ulikuwa mstari wa mbele katika hilinaomba usirudi nyuma. Suala la imani kweli lipo, lakinituangalie madhara makubwa ambayo wanayapata watotowa kike na yameshazungumzwa mengi na weweunayafahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa kweliSerikali kupitia Wizara hii na Wizara ya Sheria na Katiba waletesheria hiyo ili tuibadilishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa ni kuhusuBenki ya Wanawake. Ukiangalia katika randama benki hiiilikuwa inatakiwa kila mwaka ipewe shilingi bilioni moja,bado Serikali imetoa kwa mwaka huu shilingi milioni 69.

Page 306: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

306

Jamani hivi kweli tunataka kuwawezesha wanawake mdogowangu Mheshimiwa Ummy? Kama hii benki kwanza mojaipo Dar es Salaam na sehemu chache sana, tunataka benkihii iende maeneo yote. Wanawake ni wengi sana nchi hii nawanaume. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana naungamkono hoja ya Kambi ya Upinzani pamoja na Kamati yanguya Maendeleo ya Jamii. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa GraceTendega, Mheshimiwa Devotha Minja ajiandae naMheshimiwa Halima Ali Mohammed atafuatia.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia katika Wizarahii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niweze kumshukuruMwenyenzi Mungu aliyenijalia afya na pia niwashukuru sanawote waliochangia kuhusu Wizara hii ya Afya kwa sababubila afya hatuna hiyo Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninazungumza kwa huzunisana kwa sababu bajeti ya Wizara hii kwa kipindi hikiambacho tumebakiza muda mfupi sana haijatekelezeka kwaasilimia 60; japokuwa tuna Mawaziri ambao kwa kweliwanajitajidi kufanya kazi, lakini hawapati fedha zakutosheleza bajeti yao, na tunaona afya za Watanzaniazinazidi kudorora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinga ni bora kuliko tiba,nilikuwa natengemea Mheshimiwa Waziri pia aje na jinsiambavyo tutazungumzia jinsi ya kuwakinga Watanzaniakutokupata maradhi mbalimbali, ukija ukaangalia katikamaendeleo ya jamii ambako ndiko wako vijana wetuwafanyakazi ambao wanaweza wakaenda nawakawasaida Watanzania, bajeti yao ni ndogo na hukotunakotoka kwenye Halmashauri hawajaliwi, wako kamawanyonge ukiwakuta kule utawaonea huruma. (Makofi)

Page 307: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

307

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri vijanawetu kule wananyanyasika hawako vizuri kabisa katika hiisector, ninaona kwa mfano, kuna masuala ya afya yamazingira ambayo unaweza ukashirikiana na Wizara yaMazingira, mkaanza kuona ni jinsi gani mnaweza kupunguzamasuala ya maabukizi mbalimbali. Kwa mfano, Dar esSalaam asilimia 90 ni vyoo vya shimo, asilimia tisa tu ndiyoina vyoo vya kuvuta, hizi ni takwimu ambazo zimetolewana mashirika mbalilmbali waliopita na kufanya tafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa utaona kipindi chamasika jinsi ambavyo mtiririko wa maji taka unavyosambaakatika Jiji lile. Hii inakwenda kuleta maambukizo mbalimbali.Tunaambiwa kwamba Watanzania asilimia kubwa tunakawaida ya kutonawa baada ya kwenda sehemu zakujisaidia na sehemu mbalimbali na hizi zinasababishamaradhi mbalimbali ambayo tunayapata na magonjwambalimbali. Kwa mfano, UTI ambao inafikia mahali sasaumekuwa ni ugonjwa wa kawaida lakini pia unaua.Mheshimiwa Waziri uweze kulitizama hilo na kulifanyia kazi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika makubalianoya Abuja (Abuja Declaration) makubaliano yalikuwa asilimia15 ya bajeti mzima inaweza kutatua changamoto za afya,lakini asilimia hii imekuwa haitolewi kwa muda wote wabajeti. Ukianzia mwaka 2015/2016 zilitengwa shilingi trilioninne zikaidhinishwa shilingi trilioni 1.5 tu. Ambayo ilikuwa niasilimia saba hatukuweza kufikia hata hapo. Kwa hiyo, hiiinaonesha jinsi ambavyo hatuwezi kutekeleza baadhi yamipango ambayo tumeipanga ili iweze kutekelezeka kwaWatanzania wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumziesuala hili la kutokupeleka fedha vizuri ambalo linaanzia ngaziya sera tunavyotunga sera katika Wizara ya Afyatunakwenda katika mikoa, halmashauri mpaka vijijini, jinsiambavyo mtirir iko mzima unavyochanganya. Huumchanganyiko wa kiutendaji katika Wizara hii unatuleteashida katika utekelezaji na ufuatiliaji. (Makofi)

Page 308: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

308

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kamatitumependekeza mara zote kwamba ingewezekana Wizaraya Afya kama ilivyo Wizara ya Elimu, kuwe na mtiririko kutokasera mpaka utendaji wake. Unakuta katika Halmashauribaadhi ya masuala hayatekelezeki tunaambiwa hii ikoTAMISEMI, hii iko Wizara ya Afya, basi unakuta ni mchanganyikona fedha zinakuwa hazifuatiliwi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Waziri awezekumshauri Rais j insi juu ya Wizara hii nyeti ambayoitatengeneza Watanzania ambao wenye akili timamu nanzuri, wenye afya bora wa kuweza kuendeleza na kuletamaendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Menyekiti, nizungumzie kule kwangujapokuwa kuna baadhi ya mambo ambayo yalitakiwayazungumzwe kwa TAMISEMI, kwa sababu sikupata nafasilakini pia kwa sera yakwenda. Kwa mfano, katikaHalmashauri ya Wilaya ya Iringa waliomba shilingi milioni 150waliidhinishiwa shilingi milioni 35 na hawakupata hata shilingimoja, unategemea hawa watafanyaje kazi zao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia OC ilikuwa nishilingi milioni 25 badala yake wamepelekewa shilingi milionisita tu. Ukija katika Halmashauri ya Kilolo kwanza Halmashauriile ina upungufu wa watumishi asilimia 51, waliopo ni asilimia49 na hao tumepata wenye vyeti fake 13 bado kunaupungufu wa watumishi katika Halmashauri hiyo ya Kilolo.Kwa hiyo, katika mgawanyo wenu wa watumishi wa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ndiyo hivyo muda umeisha,ahsante sana.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuunga mkono hoja ya Kambi ya Upinzani.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Devotha Minja,

Page 309: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

309

atafuatia Mheshimiwa Halima pacha wako simuoni wadakika tano, mimi naendelea.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niwezekuchangia Wizara hii muhimu kwa maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefuatilia sana hotubazote tatu ikiwemo ya Waziri, hotuba ya Kamati na hotubaya Kambi ya Upinzani. Katika hotuba zote hizi, kila hotubailigusa kuwapongeza madaktari kwa kazi kubwa ambayowanaifanya kwa Watanzania. Tunafahamu kazi yao ningumu kazi ya kutetea uhai wa wanadamu siyo kazi rahisi.Kazi ya kuahirisha kifo siyo kazi rahisi ni kazi ambayo kwakweli inatoka moyoni katika kuhudumia watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia madaktariwakifanyakazi katika mazingira magumu, tumeshuhudiawengine hata waki- risk kwenye kazi zao magonjwa, kupatamaambukizi, lakini madaktari hawa hawakati tamaawanaendelea kuwahudumia Watanzania. Kwa kweli,niwapongeze sana madaktari kwa kazi ngumuwanayoifanya. (Makofi)

Pamoja na kazi hii sasa wanayoifanya lakini kunamambo ambayo tukiyaangalia yanakatisha tamaa. Daktarianafanya afanyavyo kuhudumia wagonjwa walio wengi,lakini inatokea viongozi kama DC, RC anamtumbuahadharani Daktari - DMO akishasikiliza malalamiko yawananchi kwenye mkutano wa hadhara, anasema kuwanzialeo hana kazi. Nafikiri ifike mahali tuwape moyo watu hawaambao wanajitoa kwa ajili ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, madaktari wana madai yaoya msingi, kwa zaidi ya mwaka mmoja hivi sasa DaktariBigwa kwenye zile call allowance kwa maana mgonjwakazidiwa saa nane saa tisa ya usiku analipwa shilingi 25,000na dakitari wa kawaida analipwa shilingi 15,000. Madaktarihawa kwa zaidi ya mwaka hospitali nyingi hawajalipwa.(Makofi)

Page 310: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

310

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende kwa Mkoa waMorogoro. Hospitali ya Mkoa wa Morogoro inahudumiawagonjwa 500 kwa siku na hii ni baada ya hospitali ile kuwaya rufaa kwa maana inahudumia wagonjwawanaoshindikana katika Wilaya zake zote. Hospitali hiipamoja na ukubwa kuhudumia wagonjwa 500 ni sawa nawagonjwa 15,000 kwa mwezi, lakini hospitali hii haina x-raymachine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, x-ray machine iliyopo niambayo imenunuliwa tangu vita ya pili ya dunia, kwa sababuhospitali ile ilikuwa ya Jeshi. X-ray inagharimu siyo zaidi yashilingi milioni 100, hospitali hii haina. Wagonjwa wanatokana drip wanakwenda Mazimbu, wanakwenda hospitali yaJeshi kwenda kufanya x-ray. Hilo nimelishuhudia mwenyewena tumefuatilia na tumewahi hata kusema hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mortuary,hivi leo ndugu yako akipoteza maisha katika Mkoa waMorogoro utalazimika kumsitiri pasipo hata kusubiri ndugu,kwa sababu mortuary hazifanyi kazi. Kweli kwa hospitali hiiambayo ina hadhi ya kuwa ya rufaa inashindwa kutengenezatu mortuary kwa ajili ya kuwaifadhi wapendwa wetu ili basiwalau waweze kuagwa kwa heshima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee pia suala linginela Madaktari Bingwa. Tumekuwa na ajali nyingi sana Mkoawa Morogoro, Daktari Bingwa wa mifupa hakuna, theatrekwa ajil i mifupa hakuna, theatre i l iyopo ni moja nainategemewa kwa maana ya magonjwa yote, akina mamawanaojifungua ndiyo hiyo hiyo. Watu wenye vidonda ndiyohiyo watu wa ajali ndiyo hiyo. Nafiki Waziri alitizame kwanamna nyingine suala hili ili kuipa hadhi hospitali ya Mkoawa Morogoro iweze kuwa na theatre room.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala lasakata la madaktari. Serikali ya Awamu ya Nne, kipindi chanyuma ilikuwa ikihamasisha kwa maana ya ule mpango wabrain bridge kutoka nje, madaktari wetu ambaowamesomeshwa na kwa fedha za Tanzania watoke nje,

Page 311: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

311

waje nchini, tena nakumbuka Rais wa Awamu ya Nne, ndiyoulikuwa mkakati wake wa kuwaomba Watanzania waliokonje warudi hapa nchini watoe huduma kwa Watanzaniawenzao. Nakumbuka walikwenda Cuba, BotswanaUingereza na kwingineko na baadhi ya madaktari nafikiriwaliitika wito wa Rais wa Awamu ya Nne wakarudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii cha kushangazaTanzania ambayo ina upungufu wa madaktari, inawachukuamadaktari kwenda kutoa huduma kwa Wakenya.Tumeushangaza ulimwengu kwa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia daktari mmojakwa takwimu nimepitia hotuba ya Kambi ya Upinzani kwavijijini daktari mmoja anahudumia watu zaidi ya 78,000 nanane, kwa mjini anahudumia watu 25,000. Wenzetu Kenyadaktari mmoja anahudumia watu 15,000. Leo hii sisi ndiyowa kupeleka Madaktari Bingwa, madaktari wetu, watotowetu, waende wakahudumie kuwaponyesha Wakenyawakati wamesomeshwa na kodi za Watanzania! Kunamahali ambapo tunabidi kukubali kwamba tumefanyamakosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hayo tu, najaribukuwatizama wale ambao hawakujitokeza kwa maanawalikuwa na nia pengine ya kutoa matibatu kwaWatanzania, kuwaajiri madaktari 258 kati ya wale ambaowalitahiniwa na kuwaacha wale wazalendo ambaowalikuwa na nia ya uzalendo siyo sawa. Nafikiri priorityingekuwa kwa wale ambao walisema wana nia yakuwatumikia Watanzania zaidi, kubaki nchini na kusaidiaTaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera ya Serikali inasema nikuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya, hivi sasatuna kata zaidi ya 3,900, hospitali ambazo zinamejengwakatika kata hizi ni hospitali 448 ambayo ni sawa na asilimia11 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango huu unatekelezeka

Page 312: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

312

kwa namna hii? Yako mengi ambayo tunataka kuyajua,flyover ndiyo ni maendeleo, flyover moja ambayo ni shilingibilioni 100 ni sawa na kujenga hosptali ngapi za Kata? Nizaidi ya hospitali 250. Priority kwa Watanzania walio wengini flyover au ni kupata hospitali ili wapate huduma za afya?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu suala laupungufu wa vifaa. Ukienda kwenye hospitali kifaa chakupima wingi wa damu baadhi ya hospitali za privateunapata, siyo hospitali za government. Ukienda kupimahospitali za government itakuchukua siku tatu kufahamuwingi wa damu, private ndani ya saa kadhaa unapata jibu,kwa sababu hospitali za government zinazidiwa nawagonjwa, ni kwa nini vifaa hivi muhimu visiwepo kwenyehospitali za government zikaweza kuwasaidia wagonjwa?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwa naliangalia sana sualala….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kwamchango wako.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, naunga mkono hoja ya Kambi ya Upinzani.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Halima AliMohammed dakika tano na Mheshimiwa Riziki ShahariMngwali dakika tano.

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Awali ya yote nichukue nafasi hiinimshukuru Mwenyenzi Mungu mwingi wa rehema na utukufukwa kutujalia afya njema. Ninakushukuru wewe kwa kunipatianafasi hii ili na mimi niweze kutoa mchango wangu katikamada iliyoko mbele yetu. Namwomba Mwenyenzi Mungu

Page 313: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

313

amjalie maisha marefu Katibu Mkuu wa Chama cha CUFMaalim Seif Sharif Hamad ili aweze kuwatumikia Watanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuzungumziakuhusu hoja ya haki za watoto. Tanzania tumekuwa tukiridhiamikataba mbalimbali inayohusiana na haki za watoto, kamaMkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1989, vilevilekuna Mkataba wa Haki za Mtoto wa Afrika ambaoumeridhiwa mwaka 1979, lakini Tanzania tuna sheriainayomlenga mtoto wa Tanzania sheria hii imepitishwa katikamwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekusudiaKuna watotowengi wa Kitanzania watoto hawa aidha baba ama mamawamehukumiwa jela kifungo cha muda mrefu ama wazazihawa wako rumande kwa muda mrefu. Sasa watoto hawawanakosa haki zao za msingi kwa mujibu wa sheria ya nchiyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kuangalia sheria,sheria hii imekaa kimya kuhusiana na mtoto ambaye mzaziwake mmoja ma wote wawili wako gerezani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto wetu wanasoma,watoto wetu tunawatibia vizuri, watoto wetu wanachezawanafurahi lakini watoto wa Watanzania hawa wanakosahaki zao za msingi. Sasa nilikuwa naiuliza Serikali je, imefanyautafiti kwa kiasi gani kuhakikisha kwamba watoto hawa waKitanzania nao wanapatiwa haki zao za msingi kwa mujibuwa Katiba? (Makofi)

Je, kwa sasa Serikali watakubaliana na mimi ili watotohawa waweze kupatiwa haki zao za msingi kwa mujibu washeria za nchi hii? Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba nizungumziesuala la uzazi salama. Uzazi salama umeshazungumziwahapa kwa Wabunge waliotangulia na mimi nazungumzia,nawaomba na Wabunge wengine walizungumzie suala la

Page 314: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

314

uzazi salama. Takwimu zinaonyesha wanawake wengiwanapoteza maisha wakati wakitimiza jukumu lao la kuletawatoto duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu za hivi karibu nikwamba wazazi 30 wanapoteza maisha kila siku. Sasa idadihii ni idadi kubwa na inawezekana kwamba idadi hii ni waleambao wanajifungulia sehemu husika ambao ni zahanati,vituo vya afya na hospitali. Lakini kuna idadi kubwa ambayowanajifungulia vijiji, huko ambako wanakosa huduma halisia.(Makofi)

Kwa hiyo, napendekeza kwa Serikali yenye kusikiakwamba bajeti basi ya Wizara ya Afya iweze kuongezwa kwamaksudi ili kuokoa vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango wako.Tunaendelea na Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali dakikatano.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru kwa fursa na mimi kama ada nianzekumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi,aliyetujalia uhai, uzima na afya na akatuwezesha kuwa hapa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze hapoalipomalizia Mheshimiwa Halima kwa kuzungumzia suala lakunusuru akina mama na vifo wakati wa ujauzito. Miminimeogopa kweli labda kwanza nianze kusema naipongezaKamati ya Bunge husika kwenye Wizara hii kwa ripoti yao hiina naunga mkono hoja hii ya wao walichosema na pia ripotiya Kambi Rasmi ya Upinzani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 33 Kamatiinasema bajeti hii inayoitwa Support to Maternal MortalityReduction imepungua kutoka shilingi bilioni 13 mpaka shilingibilioni nane. Mheshimiwa mdogo wangu Ummy ana liletangazo lake anatoka sana kwenye televisheni “Kama

Page 315: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

315

Halmashauri zinataka kuona kipaumbele cha kunusuruwakina mama watatenga pesa.” Wizara yenyeweinapunguza bajeti, Halmashauri itatenga pesa za kutoshakutosha kutoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani tuishi yaletunayoyasema, kama kweli tunataka kunusuru akina mamahawa wanaotimiza jukumu la msingi, kweli tuwatengenezeemazingira ya kuwanusuru na tusiwanusuru kwa maneno tu.Hii inauma na haikubaliki, mdogo wangu Mheshimiwa Ummynakuelewa, nakufahamu na ninakuamini katika utendaji kaziwako, hili lirekebishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine linaloendana naHalmashauri kubebeshwa mzigo ambao hawauwezi ni hayamasuala ya kuhakikisha huduma za msingi kama afyazinatolewa ipasavyo. Ajira zinatangazwa Serikali Kuu, watuwanaomba halafu wanapangiwa kwenye Halmashauri, kishawatu hao wanatakiwa washughulikiwe na Halmashauri.Halmashauri hizi hazina uwezo, mbaya zaidi hii tofauti yauwezo wa Halmashauri inajenga matabaka ya watendajiwa kada moja katika sehemu mbalimbali za nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nani midwife professionalataenda kukaa Mafia ambako Halmashauri yenyewe hohe-hahe aache kukaa Kinondoni kwenye mabilioni huku?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali Kuu ishughulikiewafanyakazi wa kada hizi nchi nzima. Nurse wa Mafia, nursewa Kinondoni na nurse wa Ilolangulu huko wote wapatehadhi sawa, kwa maana ya mishahara na stahiki nyingine.Vinginevyo yale maeneo ya pembezoni yataendelea kuwaya pembezoni na watumishi watatukimbia kila siku. Hililirekebishwe watu wapate stahiki zinazostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafia in particular jamanini kisiwa, tena kisiwa kile kilichosahauliwa. Hatuna usafiri wakuaminika ambao watu wengi wangeweza kutumia wameli, Hospitali ya Wilaya x-ray hatuielewi na vipimo vingine

Page 316: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

316

sijui vitendanishi na vitu gani, mpaka kumpima mamamjamzito kuangalia tu mkojo wake, ile kama sijui kuna vidudegani vingine visivyotakiwa, sukari na vitu vingine hakuna vituvya kuwezesha kufanya hivyo. Sasa watu hawa wakipatadharura tunawapeleka wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafia huko hospitali hiyohaijiwezi, majeruhi chungu mzima wanaovunjika,tunawafanya nini? Hata tukimudu kuwatia kwenye ndege,ndege zetu zinazokwenda ni hivi vidogo vya privatecompanies vya eight seaters sijui 13 seaters; kumuingizamgonjwa mle aliyevunjika mguu au aliyevunjika ni mtihani,angalau maeneo kama haya yangepewa kipaumbele.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Serikali inayofanyamambo kwa jumla bila kuangalia specific case kama hizikwenye masuala kama haya ya afya na mengineyo naonasiyo sahihi lazima Serikali ibadilike katika kuweka mipangoyake na kutuambia wananchi kwamba kweli wanatakakutupa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema kwenye kikaokilichopita tubadilike kwenye budgeting process yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Riziki.Tunaendelea kwa dakika kumi sasa, Mheshimiwa AzzaHamad atafuatiwa na Mheshimiwa Kemilembe Lwota naMheshimiwa Juliana Shonza ajiandae.

MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Awali ya yote nianzekwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njemana hatimae niko ndani ya ukumbi huu wa Bunge nikiwa naafya ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuunga mkonobajeti ya Wizara ya Afya kwa asilimia mia moja. Kwa nini

Page 317: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

317

naunga mkono bajeti ya Wizara ya Afya? Nitumie fursa hiikuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa naMheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli, MheshimiwaMama Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Kassim MajaliwaMajaliwa, Waziri Mkuu na Baraza lote la Mawaziri bilakuwasahau Mheshimiwa Ummy na Naibu wake MheshimiwaDkt. Kigwangalla. Mmefanya kazi kubwa ambayoinaonekana kwa muda mfupi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mfupi mmewezakugawa ambulance 67 katika baadhi ya Halmashauri zetu.Kwa muda mfupi mmeweza kutoa vitanda 20 vya kulaliawagonjwa, vitanda vitano vya kujifungulia, magodoro yakena mashuka 50 kwa kila Halmashauri zetu. Kwa hilo,nawapongeza sana na nawatia moyo pigeni kazi tupopamoja na ninyi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nirudi katikaMkoa wangu wa Shinyanga, niwasemee wanawake waMkoa wa Shinyanga walionileta ndani ya ukumbi huu. NajuaWizara ya Afya hamjengi miundombinu katika hospitali zetu,lakini ndugu yangu Mheshimiwa Ummy wewe ni ndugu yangusana, kwa hili naomba unisamehe. Pamoja na yoteunayoyafanya na pamoja na jitihada zote za ambulance,sijui vitanda na nini kama hamtokaa sawa na TAMISEMIhakuna ambacho kitawezekana. Hivyo vitanda vitakuwahavina pahala pa kuviweka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hilo kwa sababugani? Miaka mitano iliyopita kila nikisimama ndani ya bajetihii huwa nasema ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilayaya Shinyanga na suala hili halijawahi kuchukuliwa hata sikumoja. Najua siyo la Wizara ya Afya lakini kwa sababuMheshimiwa Simbachawene yupo hapa na sikupata nafasikusema TAMISEMI naomba niliseme. Hamtutendei hakiHalmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, tumeanzisha ujenzi kwanguvu zetu wenyewe, lakini hakuna fedha ambayotunapewa kutoka Serikalini. Tukipewa fedha tunapewa fedhakidogo, tutamaliza lini ujenzi wa hospitali hii? (Makofi)

Page 318: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

318

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanzisha ujenzi waHospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, toka tumeanzakila mwaka tunapewa shilingi bilioni moja, ujenzi huuutakamilika lini? Ndiyo maana ninasema Mheshimiwa Ummyna Mheshimiwa Kigwangalla pamoja na jitihada zote bilakukaa sawasawa na TAMISEMI yote mnayoyafanyahayatakuwa na maana yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaomba pamoja nakwamba ni Wizara ya Afya nitaomba TAMISEMI watujibu nikwa nini Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kila mwakahatupewi pesa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Mkoa waShinyanga inahudumia wagonjwa wengi zaidi kwa sababuHalmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Manispaa yaShinyanga hatuna Hospitali za Wilaya. Kwa hiyo, inabebamzigo mkubwa ambao haikustahili kuubeba. Hospitali hii yaMkoa wa Shinyanga pamoja na kuhudumia wagonjwa wotehao x-ray machine ni mbovu, hazifanyi kazi, kilazikitengenezwa zinaharibika. Kuna kampuni inaitwa Phillipswala hawaonekani kwenda kutengeneza mashine hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapata taabu kidogo,kwa sababu nikienda Hospitali ya Kahama hawana x-raymachine, Hospitali ya Wilaya ya Kishapu hawana x-raymachine na nikienda Mkoani x-ray machine ni mbovu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanawake hawa nawananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga wanakwendakupata wapi huduma za x-ray? Namuomba MheshimiwaWaziri wa Afya akija atuambie wanaiangaliaje Hospitali yaMkoa wa Shinyanga kwa kuiletea x-ray machine mpya kwasababu hii ni ya muda mrefu na imekwishachoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali ya Mkoa waShinyanga haina vifaa vya upasuaji, ninaiomba Wizara yaAfya, kwa sababu hospitali hii inabeba Mkoa mzima na uzito

Page 319: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

319

mnauona, tunaomba Wizara ya Afya mtuletee vifaa vyaupasuaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali ya Mkoa waShinyanga inaitwa Hospitali ya Rufaa, inapaswa kuwa naMadaktari Bingwa 21, mpaka hivi ninavyoongea inaMadaktari Bingwa watatu tu. Sasa madaktari hawawanafanya kazi kwa kiasi gani? Ninakuomba sana Waziriutakaposimama utuambie, ni lini mtatuongezea MadaktariBingwa katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, kwa sababuhawa waliopo hawatoshelezi hata kidogo. Kinachonisikitishazaidi katika hawa watatu hakuna hata Daktari Bingwa waWanawake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusuvya vituo vya afya, Mkoa wa Shinyanga tuna vituo vya afya21, katika vituo hivi ni vituo vitano tu ambavyo vinatoahuduma ya upasuaji. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziriukurasa wa 76 nimeona amesema kwa mwaka huu wa fedhawataboresha vituo 150 vya afya kwa kuwa na majengo yaupasuaji. Nikupongeze Mheshimiwa Waziri na watendajiwako wote kwa jambo hili kubwa ambalo mnakwendakulifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu kubwa sasa nilini utekelezaji huu utaanza? Tunaposema tunakwendakupunguza vifo vya mama na mtoto ni kupeleka hudumaya upasuaji kwenye vituo vyetu vya afya. Bila kuwa nahuduma ya upasuaji kwenye vituo vyetu vya afya vifo vyamama na mtoto vitazidi kuongezeka. Ninakuomba Waziriutuambie hivi vituo 150 ambavyo umevisema kwenye hotubayako ni lini utekelezaji wake utaanza? Niwashukuru sana lakininiwaombe Serikali iangalie kila mwaka ijaribu kuboreshavituo vyetu vya afya tulivyonavyo ili viweze kutoa hudumazinazostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mgawanyo wawatumishi. Nasikitika kusema kwamba mgawanyo wawatumishi hauko sawasawa. Ukienda maeneo ya mijiniwatumishi unawakuta wako wengi, unakuta labda hospitali

Page 320: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

320

inahitaji watumishi labda 30 lakini wapo 50, kwa nini?Hamtutendei haki tunaoishi maeneo ya vijijini. NinaiombaWizara na wanaohusika mtuangalie hata tunaotokamaeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini watumishi wengiwanakwenda maeneo ya mjini na maeneo ya vijijini tunakosawatumishi. Naomba hili mliangalie kwa makini ili na sisiwananchi wetu waweze kupata huduma zinazostahili.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niongeleekuhusu maendeleo ya jamii. Katika Mkoa wa Shinyanga kunavituo vya wazee viwili, kituo cha Kolandoto na Usaanda.Bajeti iliyokwisha nakumbuka kuna fedha zilitengwa kwa ajiliya ujenzi wa vituo vya wazee ingawa hazikuainishwazinakwenda kujengwa wapi, naomba Waziri akija aniambie,kile Kituo cha Kolandoto ambacho hali yake ni mbaya sana,majengo karibu yanadondoka, Wizara inafikiria ninikuboresha majengo haya ya wazee ambao kwa kweliyanasikitisha na yanatia huruma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mtuambiemaendeleo ya jamii vituo hivi vya wazee mnafikiria lini nafedha zake zipo wapi kwa ajili ya kuwaweka wazee wetukatika mazingira mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kusema hayayote nirudi kwenye Mfuko wa Wanawake katika Halmashaurizetu. Fedha zinazotoka maendeleo ya jamii kwenda katikaHalmashauri zetu sielewi kidogo ni kwa nini usimamizi wakeunakuwa mgumu na mbaya. Kuna fedha zinazotoka Wizaranina kuna fedha zinazotoka Halmashauri, ninawaomba WizaraHalmashauri isipotoa fedha zake za asilimia kumi ya mapatoya ndani msiwape fedha za Wizarani. Kwa sababumnapokuwa mnawapa fedha kutoka Wizarani ndipowanapokuwa na jeuri ya kutokutoa ile asilimia kumi yamapato ya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga

Page 321: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

321

mkono hoja, Waheshimiwa Mawaziri pigeni kazi, MwenyeziMungu atawabariki. (Makofi)

MHE. KEMILEMBE J. LWOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote napenda kukushukuru kwa kuweza kunipanafasi ya kuweza kuchangia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa kabisaanayoifanya na Watanzania wote wanaona, ninampongezaMakamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri wote kwa kazikubwa wanazofanya na niwatie moyo ninawaambia wakazebuti, wapige kazi, hapa kazi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwapongeza piaMawaziri Dada yangu Mheshimiwa Ummy na Naibu wakeMheshimiwa Kigwangalla kwa kazi kubwa wanazofanya,wametuletea ambulance kwenye Mkoa wetu wa Mwanza,wametupatia fedha za dawa, lakini hizi fedha za dawamlizotupatia ni fedha ndogo hazitoshi, bado kuna baadhiya vituo vyetu vya afya vina upungufu wa dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalonapenda kuzungumzia ni suala la vifo vya akina mama nawatoto. Hili ni janga na naomba kama Serikali tulichukuliekwa umuhimu wake na tulipe kipaumbele. Kila siku ya Munguakina mama kati ya 24 mpaka 30 wanapoteza maisha yaokutokana na uzazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watoto kati ya 170mpaka 180 kila siku ya Mungu wanapoteza maisha kwasababu ya vifo vitokanavyo na uzazi. Ninashukuru katikahotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumza na amesematukimpitishia bajeti hii itakuwa ni muarobaini wa hayamasuala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa takwimu,mwaka 2000 kwa kila vizazi hai 100,000 vizazi 529 vilikuwavinapotea, mwaka 2005 kwa kila vizazi 100,000 vizazi 578vilikuwa vinapotea, mwaka 2010 vikapungua vikafika 454

Page 322: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

322

na sasa kwa bahati mbaya mwaka 2015/2016 vizazi hivivimeongezeka kwa kila vizazi 100,000 tunapoteza watu 556,hili ni janga na ninaomba sana Mheshimiwa dada yanguUmmy tulifanyie kazi hili ili tuweze kuepusha vifo hivi, akinamama hawa wakiwa wanatimiza wajibu wao wa msingikabisa wa kupata watoto, kwa bahati mbaya vifo hivivinatokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vifo vingi vya akina mamahawa vinatokana na mambo makuu manne, jambo lakwanza ni upungufu wa damu, damu salama ya kuongezaakina mama hawa inakosekana akina mama hawawanapoteza maisha. (Makofi)

Jambo la pili ni uzazi pingamizi, akina mama hawawanapotakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji zahanati wakatimwingine ziko mbali, zilizopo karibu hazitoi huduma yakupasua akina mama hawa wanapoteza maisha yao.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kifafa chamimba, Mheshimiwa Ummy ameongelea na tiba ni sindanoza magnesium sulphate. Ninaomba sana katika vituo vyetuvya afya mambo haya yawepo ili tuweze kuokoa vifo vyaakina mama. Mimba za utotoni na kuharibika kwa mimba,akina mama hawa mimba zinaharibika wanaenda kwenyezahanati zetu hatuna vifaa vya kusafisha hizi mimba na hiiinasababisha vifo kwa akina mama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la upungufu wawataalam kwenye sekta ya afya, Mheshimiwa Waziriamesema kuna ajira mpya kwenye sekta ya afya lakini nijanga kubwa kweli, hatuna wafanyakazi wa afya wakutosha. Naomba hili suala tuliangalie na tuajiri wafanyakaziwa afya ili tuweze kuokoa maisha ya Watanzania hawa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana nilisimamahapa na nikaongelea suala la vifaatiba. Hospitali yetu yaSekou Toure kubwa kabisa ya Mkoa wa Mwanza hatuna CT

Page 323: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

323

Scan, tumeomba hapa Mheshimiwa Waziri akaahidi akasemaCT Scan hii inakuja lakini mpaka sasa ninavyosimama nakuongea hapa CT Scan haipo. Hii inapelekea Watanzaniawa Mkoa wa Mwanza waende kufanya vipimo hivi kwenyeprivate clinics. Private clinics vipimo hivi ni kati ya shilingi300,000 mpaka 400,000, ni aghali na Watanzania wengihawawezi kumudu fedha hizi kuzilipa.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri tunaomba unapokujahapa kuhitimisha utuambie ni lini vifaatiba hivi vitaendakwenye Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la watoto njitisijaliona kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri. Watotowanaozaliwa njiti ni wengi katika wodi yao, nimetembeleawodi yao Mkoa wa Mwanza, wodi haina vifaa. Watoto njitihawa wanahitaji suction machines, wanahitaji blood pressuremonitors, wanahitaji incubators ili waweze kuwekwa nakuhifadhiwa ili waweze kufika siku zao za kuweza kuruhusiwana kwenda nyumbani, lakini inabidi watoto hawawaruhusiwe kwa sababu wodi ya watoto hawa haina vifaa.Mheshimiwa Waziri tunaomba sana uweze kutupatia vifaahivi, wananchi na akina mama hawa wanahangaika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la D by D, conceptyake ni nzuri kabisa haina tatizo, lakini inatokea mkanganyikokati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI. Naomba ifike mahali sasaWizara ya Afya isimame kama Wizara ya Afya. Tunapokuwakwenye Halmashauri zetu huko tunauliza hili suala la afyambona halifanyiki, mbona haliendi, tunaambiwa hili sualalipo TAMISEMI, ukienda TAMISEMI unauliza unaambiwa hili sualalipo Wizara ya Afya, sasa tufike mahali tuone ownership ikowapi na tujue Wizara ya Afya isimame kama Wizara ya Afyana tu-deal na Wizara ya Afya, peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba hii tumeonafedha zilizotengwa za dawa ni zaidi ya shilingi bilioni 230,kiuhalisia fedha za dawa zilizoenda ni shilingi bilioni 88 tu,nyingine zinaenda kwenye kusafirisha dawa, kwenye kujenga

Page 324: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

324

majengo, kwenye vifungashio, tungejua kabisa specific helaza dawa zimetumika...(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana kwa mchango wako.Tunaendelea, Mheshimiwa Juliana Shonza, atafuatiwa naMheshimiwa Taska Raphael Mbogo na Mheshimiwa SilafuMaufi ajiandae.

MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi hii nami kuweza kuchangiaWizara hii ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto. (Makofi)

Awali ya yote nichukue nafasi hii kuweza kumpongezaWaziri wa Wizara hii, kwa kweli anafanya kazi nzuri na kaziyake siyo ya kubeza hata kidogo anastahili pongezi pamojana Naibu Waziri wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba nijikite sasa katika kuelezea Idara ya Maendeleo yaJamii. Naomba nielezee kwanza historia, Idara hii yaMaendeleo ya Jamii ni zao la kihistoria la mapinduzi yaviwanda yaliyofanyika katika karne ya 19 katika Bara la Ulaya.Walipojenga viwanda yalijitokeza matatizo mengi ya kijamiihivyo wakaanzisha masomo ambayo yatazalisha wataalamambao watashughulika na masuala ya mabadiliko katikajamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababunchi za Afrika ikiwemo Tanzania haikufanya makosakuchukua funzo hili na hatimae kujenga na kuanzisha VyuoVikuu vya Maendeleo ya Jamii, pamoja na vyuo vya katiambavyo moja kwa moja vita-deal na mabadiliko ya kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hata ukisomahotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 87 ameelezeakabisa kwamba vyuo hivyo vitaendelea na udahili wa

Page 325: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

325

wanafunzi watakaojishughulisha na masuala ya maendeleoya jamii, ni vema tukaangalia kwamba tunapoendeleakudahili wanafunzi katika vyuo vya maendeleo ya jamiituangalie na wale ambao kwa sasa hivi wapo maofisini,hawa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mantiki hiyo, ni wazikwamba kwa sasa hivi ambapo nchi yetu inapiga hatuakuelekea kwenye uchumi wa viwanda hakuna namna yoyoteambayo tunaweza tukaiacha nyuma Idara hii ya Maendeleoya Jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kusikitisha sanaidara hii kwa kifupi imesahaulika. Mwaka jana wakatinachangia Wizara ya Afya, nilizungumzia Idara ya Maendeleoya Jamii, lakini ni wazi kwamba sijaona mabadiliko yoyoteambayo yamefanyika. Leo hii ukitembea katika Halmashaurizetu nyingi, siyo katika Mkoa wa Songwe tu nchi nzima Idarahizi za Maendeleo ya Jamii ziko hoi. Watumishi wa idara hiiya maendeleo ya jamii hawapelekewi fedha za oc, walahakuna vitendeakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenyeHalmashauri nyingine unakuta idara ya maendeleoimewekwa nyuma ya Halmashauri, nyingine ziko nje kabisaya Halmashauri kuonesha kwamba siyo part ya Halmashaurizetu. Suala hili linasikitisha sana. Hali hiyo imepelekea sasahata fedha ambazo zinapelekwa fedha za miradi, miradimingi katika Halmashauri zetu inakufa haizai matunda,haioneshi mafanikio kwa sababu tumeiacha nyuma idaraya maendeleo ya jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitolea mfano katikaHalmashauri yangu ya Wilaya ya Mbozi, kuna miradi mizurisana ambayo imeanzishwa na Serikali, lakini kwa sababuwananchi hawajashirikishwa, watu wa idara ya maendeleoya jamii hawajashirikishwa, inapelekea wananchi sasahawana ile sense of ownership, wanaona kwamba ile miradisiyo ya kwao, wanaona miradi ile ni ya Serikali, kumbe tatizohawajaelimishwa kuona kwamba ile miradi ina faida hivyo

Page 326: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

326

wanapaswa kuitunza, hii yote ni sababu Idara ya Maendeleoya Jamii imesahaulika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi utaratibuuliowekwa na Serikali wa kutenga asilimia tano ya vijanapamoja na asilimia tano ya wanawake, lengo lilikuwa ni zurilakini ukiangalia katika Halmashauri idara inayohusika mojakwa moja kufuatilia pesa hizi ni idara ya maendeleo ya jamiilakini hawashirikishwi ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda leo hii katikaHalmashauri zetu hususan Halmashauri ambazo zipo katikaMkoa wangu wa Songwe, wanawake hawana kabisauelewa wa asilimia tano ambayo inatengwa na Halmashauri.Ukienda kwenye makaratasi unaona kabisa kwamba fedhazinatengwa lakini impact kwenye jamii haionekani, swaliukijiuliza ni kwa sababu Idara hii ya Maendeleo ya Jamiiambayo ndiyo inategemewa kwenda kutoa mafunzo kwavijana pamoja na wanawake wajue namna gani ya kuwezakuzitumia hizo fedha za Halmashauri, wajue namna gani yakuweza kuzifuatilia fedha hizo ili ziweze kutumika kamailivyopangwa. Kwa sababu idara hii haishirikishwi, unaonakabisa kwamba fedha hizo hazijulikani zinaenda wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, Wabungewa Viti Maalum siyo Wajumbe wa Kamati ya Fedha, kwahiyo unaweza ukaona ni namna gani ambavyo hizi asilimiatano za wanawake na asilimia tano za vijana zinapoteakatika mazingira ambayo ni ya kutatanisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la bima ya afya.Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumziakwamba bado mwamko ni mdogo sana wananchi kuwezakujiunga na hii mifuko ya hifadhi ya hifadhi ya jamii, mifukoambayo ingeweza kuwasaidia pia wanawake ambao wakovijijini, ambao kimsingi wao ndiyo wana matatizo makubwasana ya kiafya, wanapata matatizo makubwa sanawanapoenda kujifungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanaojiunga na hii mifuko

Page 327: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

327

ukiangalia idadi ni ndogo kwa sababu wanachi badohawajaelimishwa, elimu bado haijawafikia kwa hiyohawaelewi umuhimu wa kujiunga na hii mifuko ya bima yaafya. Hii yote ni kwa sababu tumepuuza Idara hii yaMaendeleo ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ukiangalia hatakatika jamii zetu, masuala ya unyanyasaji wa kijinsia yawanawake na watoto yamekua kwa kasi kubwa sana. Dadayangu hapa ameongea kwa uchungu, ni masuala ambayohata katika Mkoa wangu wa Songwe yapo kwa kiasikikubwa, watoto wadogo wanaozeshwa, hivi ninavyosemanina mtoto ambaye namsomesha sekondari kwa sababu tumzazi wake alikwishakupokea ng’ombe 60 ili amuozeshehuyo mtoto. Masuala kama haya tunapaswa kama Taifakuyapinga… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nashukuru sana. Mheshimiwa RaphaelMbogo, atafuatiwa na Mheshimiwa Silafu Maufi naMheshimiwa Ester Mahawe ajiandae.

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naomba nirekebishe jina siitwi Raphael Mbogonaitwa Taska Restituta Mbogo.

MWENYEKITI: Ahsante Restituta Mbogo.

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,baada ya kusema hayo, naomba nikushukuru kwanza wewekwa kunipa nafasi hii kuchangia hoja hii ya Wizara ya Afyaambayo ni Wizara muhimu kwa sisi akina mama na ni Wizaramuhimu kwa nchi yetu.

Page 328: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

328

Napenda kwanza kuishukuru Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania chini ya uongozi thabiti waMheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufulikwa kasi yake ya hapa kazi. Ninasema hivi kwa sababu katikaMkoa wetu wa Katavi tulikuwa hatuna duka la dawa tangulabda niseme tangu Wilaya ile ianzishwe mwaka 1945.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipata Mkoa hapa juzi,Mheshimiwa Waziri Mkuu alipotembelea kule akatuahididuka la dawa na ndani ya miezi sita duka la dawa la MSDlilikuwa limejengwa na tukaenda kulizindua, naipongezasana Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimpongeze Waziriwa Afya, Mheshimiwa Ummy na Naibu wake MheshimiwaDkt. Kigwangalla kwa kazi nzuri, kwa sababu baada yauzinduzi tuliweza kupata pia vitanda, hivyo naishukuru sanaSerikali hii kwa kasi yake ya ufanyaji kazi maana yake ndaniya miezi sita duka la dawa lilijengwa. Hongera Serikali yote,hongera kwa Mawaziri wote na hongera sana kwaMheshimiwa Rais wetu na tunakupongeza sana endelea nakazi na hekima zako unazozitumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,napenda niende moja kwa moja kwenye hoja ya Wizara yaAfya. Ninampongeza Mheshimiwa Ummy na Naibu wake,naomba nitoe ushauri kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sihoji uwezo wao waWatendaji wanafanya kazi vizuri sana akiwepo mwenyeweMheshimiwa Ummy na Naibu wake, lakini naona Wizara hiini kubwa, naona kama vile upande wa maendeleo ya jamii,wazee, unasahaulika. Naomba kutoa ushauri kwa Serikaliiweze kuigawa Wizara hii, Wizara ya Afya ibaki peke yake,Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Wazee itenganishwe nahii Wizara, huu ni ushauri tu nautoa maana Wizara ya Afyaina mambo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye dawahospitalini Waziri na Naibu wake washughulikie, zahanati,

Page 329: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

329

vituo vya afya, hela za mgao kwenda kwenye Mikoa yotempaka Wilaya, vifaatiba kuangalia japokuwa ndiyotunasema viko TAMISEMI, lakini Waziri pia anatupia jicho, yotehayo yanamkabili Waziri wa Afya na Naibu wake, naonakama vile kazi inakuwa kubwa mno. Natoa ushauri tukuomba Wizara ya Afya ingeachwa peke yake ili iweze kutoahuduma vizuri kwa sababu kila Mtanzania bila kuwa na afyanjema sidhani kama kuna kitu ambacho mtu anawezaakafanya. Hata hapa tunakaa kwa sababu tuna afya, ukiwana afya iliyotetereka sidhani kama utaingia humu Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayoniongelee sakata la vyeti fake. Ninavyoongea hapa kuleMkoani kwangu Katavi kuna Halmashauri Tano, ndani ya hizoHalmashauri tano wafanyakazi 60 wa Wizara ya Afyawalikuwa na vyeti ambavyo vinasemekana kwambahavijakaa vizuri au ni vyeti fake. Sasa tuna uhaba wawafanyakazi 60 ghafla kwenye Mkoa wetu wa Katavi,tunaomba replacement. Uajiri wafanyakazi kamawafanyakazi wapya madaktari pamoja na wauguzi, hililimewakumba madaktari pamoja na wauguzi. Mkoa mzimakupoteza wafanyakazi wa sekta ya afya 60 ni wengi mno,utaangalia mwenyewe jinsi gani vituo vya afya, zahanati nahospitali zetu zitakavyokosa huduma na jinsi gani wananchiwa Mkoa wa Katavi watakavyokosa huduma. Naomba ajiraiharakishwe ya hawa madaktari, Serikali jinsi ambavyoimezungumzia suala la vyeti fake basi wakamilishe huoutaratibu na ajira mpya za wale madaktari pamoja nawauguzi wenye vyeti ambavyo ni genuine iweze kutangazwamapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie pia suala laKituo cha Afya cha Mkoani Katavi. Mheshimiwa Waziri kilekituo cha afya ambacho mwaka jana tulisimama hapatukaomba kirekebishwe na kifanyiwe ukarabati, napendakushukuru Serikali kituo cha afya kimefanyiwa ukarabatikimekwisha, tatizo hakijafunguliwa. Namuomba MheshimiwaWaziri atakapokuwa anafanya majumuisho yake atuambiekile kituo cha afya cha Mkoa wa Katavi ambacho kimekwishakitafunguliwa lini?

Page 330: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

330

Naomba pia kile chuo cha afya kiweze pia ku-trainwauguzi wasaidizi ili tuweze kuwa na ma-nurse wengi nahawa Medical Assistants wengi ambao watakuwawamekuwa trained Mkoani Katavi, kwa sababu ukiangaliajiografia kule kwetu ni Mikoa ambayo iko pembezoni lakinikama mtu atakuja atasoma kule ile miaka miwili atazoeamazingira kiasi kwamba hata kama atapangiwa kufanyakazi katika Mkoa wa Katavi atakaa. Ukimtoa mtu Mikoa yambali ukamleta kule anaweza akaona jiografia ni mbayana hiyo kazi yenyewe asiipende kwa hiyo naomba kile chuopia kiweze kuwa-train wauguzi wasaidizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualala ndoa za utotoni. Sheria zetu tulizojipangia wenyewe katikaJamhuri ya Muungano wa Tanzania unaweza ukasema kwaupande mwingine zinachangia ndoa za utotoni. Tunazosheria ambazo zinakinzana, tunayo Sheria ya Mtoto ya mwaka2009 ambayo ibara ya kwanza inasema kwamba mtu yeyoteambaye yuko chini ya umri wa miaka 18 ni mtoto. Ibara yakwanza hiyo ambayo ni ya Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009inasomeka hivyo. Ukienda kwenye Sheria za Kimataifaambazo tumeziridhia tunayo Sheria ya Kimataifa yaMwanamke ambayo inatoa tafsiri ya umri wa mtoto natunayo mikataba ambayo imeonesha umri wa mtoto nimiaka mingapi. Ukichukua zile sheria ambazo tumezisaini natuliziridhia ambazo tunatakiwa tuzifuate zinakuja zinakinzanana Sheria ya Ndoa ya mwaka 1970 ambayo inamruhusumtoto wa kiume kuoa akiwa na miaka 18 na mtoto wa kikekuolewa akiwa na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa unakuta kwambakunakuwa na discrimination, ukishaweka ile tofauti ya age,moja kwa moja umeweka utofauti wa mtu mmoja kuwasupreme na mwingine kuwa chini yake kwa ajili ya jinsia.Kama unataka kuwaweka watoto wote kuwa sawa,unatakiwa ule umri usiweke ile tofauti kati ya mtoto wa kikena mtoto wa kiume. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 331: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

331

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Taska Mbogo.

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuunga mkono hoja ya Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya tunaendelea na Mheshimiwa SilafuMaufi atafuatiwa na Mheshimiwa Ester Mahawe naMheshimiwa Neema Mgaya ajiandae.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kunipatiaafya nami kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kwa sikuya leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa ni mnyimi wafadhila kama nisipomshukuru Mheshimiwa Rais John PombeMagufuli. Kwa kweli amefanyakazi kubwa na kazi nzuri natarajio jema kwa wananchi wa Tanzania kwa maendeleoyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuwashukuruWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,wamefanya kazi nzuri ambayo sikutarajia kabisa katika kipindihiki kifupi kuweza kuifanya kazi kubwa hii ndani ya afya katikanchi yetu. Wakati akisoma mdogo wangu Mheshimiwa Ummytaarifa yake ya Wizara, kwa kweli ameni-impress na kujua yakwamba kumbe yeye ni bush doctor lakini kwa kweli nidaktari kamili, kwa jinsi anavyoifanya kazi yake kwa kuipendana kuifahamu Wizara ya Afya na kweli ameishika nakuhakikisha kwamba anaifanyia kazi njema katika kipindichake hiki cha uongozi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuzungumziasuala la maendeleo ya jamii. Kitengo cha Maendeleo ya Jamiikimesahaulika hivi sasa ndani ya utekelezaji wake wa kazi.Maendeleo ya jamii ilikuwa kila mwaka wanaketi MaafisaMaendeleo ya Jamii kukaa pamoja, kushauriana,kuelekezana na hatimaye kupeana ubunifu wa kuwezakuitekeleza Wizara yao, tatizo vikao hivi sasa hivi havifanyiki

Page 332: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

332

ikidaiwa kwamba bajeti ni finyu. Ninaomba vikao hivi virejeeili maendeleo ya jamii iweze kufufuka tena upya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya jamii nikitengo ambacho kinatoa elimu kwa akina Mama katikakuhamasisha ujasiriamali, kuwahamasisha akina mamakiuchumi, kuelekeza akina mama umuhimu wa kujiunga natiba, umuhimu wa kujiunga na bima, umuhimu wa mikopona namna ya utekelezaji wa mikopo hiyo ya vyombo vyafedha na SACCOS na kadhalika. Tatizo ni kwamba hawaMaafisa Maendeleo ya Jamii hawana vitendea kazi, hawanausafiri na hata alivyozungumza Mheshimiwa Waziri yakwamba wasitumie magari ya miradi ya UKIMWI na kadhalika,ajue wazi ya kwamba maendeleo ya jamii hawana usafiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Rukwa hatunausafiri, Wilaya zote hazina usafiri na hata ngazi ya Katahawana usafiri hata wa pikipiki. Mimi ninavyoelelwa nikwamba, Maafisa Maendeleo ya Jamii siyo desk officers, hawani field officers, wanahitaji kwenda kwenye maeneo,wanahitaji kupatiwa usafiri, vinginevyo watatumia nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri wana mambomengi, wanawapa usafiri kwa kubahatisha, lakini wakiwana usafiri wao watu wa maendeleo ya jamii watafanya kazinzuri kwa wananchi wetu wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninapendakuishukuru Serikali yangu kwa kutoa ajira takribani kwawananchi 52,000; ninaomba katika hawa 52,000 hebutuangalie ajira ya Maafisa Maendeleo ya Jamii. HatunaMaafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, katika Mkoawetu wa Rukwa ndani ya kata 97 ukiacha zile zilizoongezekatunao Maafisa 51 tu, tuna upungufu mkuwa wa MaafisaMaendeleo ngazi ya Kata, tuna upungufu mkubwa waMaafisa Maendeleo ngazi ya vijiji na tunao upungufu mkubwawa Maafisa Maendeleo wa Wilaya ya Nkasi na Wilaya yaKalambo bado wana kaimu.

Page 333: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

333

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba hawa MaafisaMaendeleo wa Jamii wa Wilaya ya Nkasi na Kalambowapatiwe uthibitisho kamili wa Maafisa Maendeleo waWilaya yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kulizungumzia ni kuhusu suala la afya. Mkoa waRukwa na Mkoa wa Katavi tuko mbali na Hospitali ya Rufaaya Kanda ambayo iko Mbeya. Tumekubaliana Mikoa hii miwilituweze kujenga hospitali ya rufaa kati ya Rukwa na Katavina tumeweza kupata eneo la hekari 97 kuijenga hospitalihiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishukuru Serikali kwaawamu ya awali imetupatia shilingi bilioni moja kwa maanaya kulipa fidia ya wananchi wetu waliokuwa katika lile eneo,ninashukuru sana kwa ngazi hiyo mliyoifikia. Kutokana naHalmashauri zetu kutokuwa na pato la kutosha, tunaombaSerikali Kuu iweze kuongeza hatua inayofuata ya uchorajiwa ramani na ujenzi wa hospitali ile iweze kuanzishwa katikaMkoa wetu wa Katavi na Mkoa wa Rukwa harakaiwezekanavyo ndani ya kipindi hiki tuweze kuifungua hiyoHospitali ya Kanda ambayo ni hospitali ya Rufaa kwa Mikoahii miwili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo linguine katikaupande wa afya ni upungufu wa madaktari. Katika Hospitaliya Mkoa tunao madaktari 20, kati ya madaktari 20tunaowahitaji tunao madaktari 12 tu ambao hawakidhimahitaji. Upande wa Madaktari Bingwa, tunao madaktariwatano lakini tuna uhitaji wa Madaktari Bingwa 15 wawezekukidhi pale. (Makofi)

Jambo lingine katika upande wa afya ni kuhusu vituovya afya na zahanati. Tunazo zahanati na vituo takribani 54ambavyo vimejengwa lakini bado havijakamilika. TunaombaSerikali iweze kuhakikisha ya kwamba haya majengo ambayohayajakamilishwa 54, zahanati zikiwa 48 na sita ikiwa ni vituovya afya viweze kukamilishwa ili viweze kutoa huduma kamilina hatimaye kuondoa msongamano katika hospitali ya

Page 334: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

334

Mkoa ambayo hivi sasa ndiyo inaifanya hiyo kazi ili akinamama na watoto vifo viwe vichache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa vifo vya akinamama na watoto kwa kweli vimekithiri na tuna kila sababuya kuweza kuhakikisha vinapungua kama siyo kuisha kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuzungumziasuala la 10 percent za Halmshauri; wakati TAMISEMIikizungumza, ilisema kwamba itatoa waraka kupelekakwenye Halmashauri kuhakikisha ya kwamba wanafunguamifuko na hizo fedha za asilimia 10 zinapatikana nazinagawiwa katika vikundi vinavyohitaji vya akina mamana vijana. Tunaomba waraka huo kutoka TAMISEMI utoke iliHalmashauri ziwe na uhakika wa kutoa hizi asilimia 10 naWabunge wa Viti Maalum tupate hizo nakala za waraka huoili tuweze kufuatilia hizi fedha kama zinatoka na kuwafikiawalengwa wanaohitajika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninalopendakulizungumzia ni kuhusu ziara ya Mheshimiwa Waziri. Wazirialikuja Mkoa wa Rukwa bahati mbaya jioni yake akapatadharura ikabidi arudi Dar es Salaam na ziara yake ikafutika,hivyo tunamuomba Mheshimiwa Waziri urejee tena katikaziara yako ya Mkoa wa Rukwa il i uweze kufahamuchangamoto za afya katika Mkoa wa Rukwa, kwa sababuMkoa wa Rukwa hatuna hata Wilaya moja yenye Hospitaliya Wilaya, tuna Hospitali Teule tu, tunahitaji kuwa na Hospitaliya Wilaya.

Katika kuhangaika kutafuta hospitali ya Wilaya,tuliweza kuomba majengo ambayo yako chini ya TANROADSyaliyokuwa kambi ya kujengea barabara bahati mbayainasemekana kwamba majengo yale ni madogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kutokana na juhudiuliyonayo Mheshimiwa Ummy na Mheshimiwa Kigwangalla,nina imani kwamba mtasimamia kuhakikisha Mkoa wetu waRukwa tunapata hospitali za Wilaya katika Wilaya zake zotenne ambazo kwa sasa hatuna hizo hospitali.

Page 335: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

335

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inaonekana ya kwambaMkoa wa Rukwa tuko mwisho, tuko pembezoni, bila ya kuwana afya bora itakuwa ni hatari, sisi ndiyo wazalishajitunaowalisha katika nchi hii ya Tanzania. Hivyo tunawaombakabisa kwamba tujaribu kuangalia hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho katika upande waafya ni huduma ya damu salama, akina mama na watotondiyo wanaohitaji kuhakikisha kwamba wanapata hudumasalama na huduma salama ni damu, damu kwetu kuna tatizola chupa za damu, sasa katika hizi chupa 250,000 sijui Mkoawa Rukwa una kiasi gani cha hizo chupa, hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine la pili ni kwamba,vituo vyetu vya afya havina majokofu ya kuhifadhi hiyo damusalama na wale wataalam wa kukusanya damu salamawengi wao hawajapata mafunzo, hivyo ni kwamba hawapoambao wanaweza kukusanya damu salama na kuhakikishakwamba wagonjwa wetu wanapata damu salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo tunawaomba mtoemafunzo kwa wale wataalam wanaoshughulika na damusalama...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima na taadhima napenda kuunga mkono hoja kwaasilimia mia moja na big up. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Ester Mahawe,Mheshimiwa Neema Mgaya na Mheshimiwa LolesiaBukwimba ajiandae.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii na mimi niweze kutoamawazo yangu katika Bunge lako Tukufu.

Page 336: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

336

Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani zangu za dhatina pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Ummy pamoja naMheshimiwa Kigwangalla. Amezungumza mwenzanguMheshimiwa Mama Martha Umbulla muda si mrefu yakwamba juzi tu tuna kama siku mbili, tatu alitoka katika Mkoawetu wa Manyara kwa sababu ya Hospitali ya Haydom, kwakweli tunamshukuru sana Mheshimiwa Ummy lakini kubwazaidi nimshukuru pia na Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayealisema atamtuma Waziri wake kwenda kuangalia jinsi ganiHospitali ya Haydom inaweza ikawa Hospitali ya Rufaa yaKikanda kwa sababu hospitali hii inahudumia watu wengisana, inahudumia Mikoa siyo chini ya mitano, ina Wabungewanaoweza kuisema humu ndani siyo chini ya 20, kwa hiyohili siyo jambo dogo. (Makofi)

Nimuombe sana sada yangu Mheshimiwa Ummykwamba ikiwezekana kwa vile ile hospitali iko kijijini, kunaumbali wa zaidi ya kilometa 900 kutoka Haydom mpakaMuhimbili, kuna umbali wa zaidi ya kilometa 400 kutokaHaydom mpaka KCMC, kuna umbali wa zaidi ya kilometa200 kutoka Haydom mpaka Hospitali ya Mkoa wa Manyara,tunakuomba sana Mheshimiwa Ummy kwa hili acha legacy.Watu wa Haydom, watu wa Mkoa wa Manyara, Arushakupitia Wilaya yake ya Karatu, Meatu, Simiyu upandemkubwa sana wa Simiyu hawatakusahau, Singida ndiyousiseme hata Dodoma.

Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri Ummy hospitalihii iweze sasa kufikiriwa kuwa Hospitali ya Kikanda ili kwaukanda huu tuwe tumepata hospitali ya rufaa ya kuwezakumaliza matatizo ya wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Baada yapongezi hiso naomba sasa nijielekeze katika pongezi hizo,nisisahau kumshukuru Rais wangu ametoa vitanda kwa kilaHalmashauri. Kwa kweli Mheshimiwa Rais Mungu ambarikisana jamani kazi inafanyika, tunaona kwa macho ya nyama,Mungu ambariki sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya yetu ya Babati

Page 337: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

337

tuna changamoto mbalimbali, ninaomba tu niongelee kwauchache hospitali yetu ya Mkoa wa Babati haina theatreinayoeleweka, haina x-ray inayoeleweka, haina haya ultra-sound inayoeleweka, haina wataalam wa radiology,tunaomba sana Mheshimiwa Ummy, tunajua kazi inafanyika,tunajua mnajitahidi sana, lakini penye changamoto lazimatuseme, tunaomba muikumbuke hospitali hii ya Mkoa waManyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna Hospitali yaMrara ambayo inatoa huduma kama Hospitali ya Wilayapale, tunakuomba sana Mheshimiwa Ummy changamotonilizozitaja zilizoko katika Hospitali ya Mkoa zipo na kwenyehospitali ya Mrara, tunaomba uikumbuke hospitali hii. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, pia nisisahau kuishukuru Wizarayako Mheshimiwa Ummy umepeleka vifaa vya kutosha nawataalam wa kutosha katika Kituo cha Afya cha Maguguhili lazima tukupongeze sana. Kwa kweli, tunakushukuru sana,tumeona juhudi zenu na pale kwa kweli sasa neno upungufuhakuna, ahsanteni sana kwa hili mlilolifanya pale Magugu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ninaishukuru Serikali kwasababu sasa inafanya sana kazi nzuri kupitia PPP, tayariimepeleka ruzuku katika Hospitali ya Dareda, hii ni Hospitaliya Mission ambayo inahudumia wananchi wengi sana waWilaya ya Babati Mji na Babati Vijijini Halmashauri zote hizizinasaidiwa sana na hospitali hii ya Dareda, kwa kwelinaishukuru Serikali imepeleka ruzuku pale ya kutosha lakinipia inasaidia kulipa watumishi wa kada hii ya afya wa hospitaliile. Kwa kweli kwa ujumla wake, niiombe Serikali iendeleekutoa ushirikiano kwa hospitali hizi za makanisa ambazo kwakweli ni hospitali teule katika maeneo yetu, zinafanya kazinzuri sana kutoa huduma kwa wananchi. Hivyo, niipongezeSerikali kwa kukubali kufanya kazi kupitia PPP na hizi hospitaliza makanisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Wilaya yetu yaBabati tuna mapungufu, tuna vituo saba na mahitaji yetu ni

Page 338: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

338

vituo 25, tuna zahanati 32 mahitaji ni zahanati 102; tunaombasana haya mapungufu yatazamwe kwa jicho la kipekee sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri kwamba badalaya kuhangaika kuja kuweka labda Hospitali ya Wilaya paleBabati, ningeshauri zile fedha ambazo zilipaswa kuelekezwakwenye ujenzi wa hospitali, vituo hivi vikiboreshwa vinawezavikachukua nafasi kubwa sana ya kumaliza tatizo kiasikwamba hata umuhimu wa kuwa na hospitali ya Wilaya paleunaweza usiwe wa lazima sana. Hivyo, naomba Kituo chaBashnet, Hospitali ya Dareda pamoja na Kituo cha Mrarahozpitali hizi zikiboreshwa ukweli ni kwamba taabu itakuwaimekwisha maana wananchi hawa watakapokuwawanahitaji huduma yoyote ya rufaa wataelekea Haydomambako siyo mbali. Naomba tuboreshe kwanza huku chiniili tuweze kusaidia wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa pia la hospitalizetu katika Mkoa mzima wa Manyara hatuna ambulance.Kwa mfano, Wilaya ya Simanjiro imesemwa tayari kwambatuna ambulance moja ambayo ni mbovu kila wakati ipogarage. Tunaomba jiografia ya Mkoa wa Manyara imekaakidogo ni tatizo. Kwa mfano, Wilaya ya Simanjiro kutoka katamoja kwenda kata nyingine unakuta siyo chini ya kilometa50 mpaka 80, kwa hiyo tunapokuwa na ambulance ambayokwa kweli haipo vizuri tunapata shida.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisahau pia kuishukuruSerikali, tayari pale Simanjiro tunapanua wodi sasa, hudumaya mama na mtoto inakwenda kupatikana vizuri sana paleOrkesment, ninaishukuru sana Serikali kwa kuliona hili. Pianisisahau kuishukuru hospitali ya Orkesment ya KKKT, hospitaliteule iliyoko pale Simanjiro inaendelea kutoa huduma nzurikwa wananchi wetu. Niiombe tu Serikali kama nilivyosemakwa sababu gharama kwa kiwango fulani ni kubwa katikahospitali hizi ambazo zina muundo wa hospitali binafsi,ninaomba ile Urban Orkesment itakapokuwa imeboreshwavizuri na kuwekwa vifaa vyote vinavyotakikana, kwa kweliwananchi wetu watapata huduma bora ya afya pasipokuwana tatizo.

Page 339: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

339

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nizungumze suala sasala afya ya mama na mtoto - uzazi salama. Uzazi salama nikitu muhimu sana, kama takwimu zinavyoonesha kwambaakina mama wasiopungua 30 wanakufa kila iitwapo leo. Hiiidadi siyo ndogo, tunaomba katika vituo hivi vya afyahuduma hii iboreshwe, katika zahanati zetu huduma hiziziboreshwe. Kwa mfano, katika Wilaya ya Simanjiro, kata yaNgorika pana umbali wa kilometa 60 kutoka Ngorika mpakaOrkesment. Nilikuwa naomba ikiwezekana ile zahanati iliyokopale iweze kupandishwa hadhi kidogo, iweze kukaa vizuri iliwale wananchi wa Ngorika waweze kupata huduma paleNgorika maana kutoka Ngorika mpaka Orkesment mtuanatembea kilometa 60 kwa kweli huu umbali ni mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema jiografiaya Simanjiro ni zaidi ya square kilometer 17,000 hiyo Wilaya nikubwa sana na sehemu kubwa ni pori, kwa hiyo tunaombamsaada wenu sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba nizungumziesuala la ndoa za utotoni; vifo vingi vimekuwa vikitokeakupitia ndoa hizi za utotoni. Ninaomba sana ikiwezekanaMheshimiwa Waziri sasa alete marekebisho ya sheria hii hukundani. Ninawaomba wakina baba mlioko humu ndani,ninawaomba sana akina mama watoto wetu wanateketea.Hii biashara ya kusema kwamba kigezo cha mtoto wa kikekuolewa ni baada ya kuvunja ungo hii siyo sahihi. Siku hiziwatoto kwa ajili ya hizi chips, corie na kadhalika wanavunjaungo wana miaka 10, wana miaka 11, wana miaka tisa, hivikweli mtoto huyo ame-qualify kuwa mke wa mtu?

Jamani akina baba tunaomba mtusaide, hawa niwatoto wenu kama siyo wa kwako ni wa mjomba wako,kama siyo wa mjomba wako ni wa kaka yako, kama siyowa kaka yako ni wa shangazi yako. Ninaomba katika hilituungane jamani, tuweke itikadi zetu pambeni, tunafahamumambo mengine ya kidini yapo humu na imani za watutunaziheshimu, lakini ili kuokoa nafsi hizi za watoto wa kiketunaomba basi tushirikiane kwa pamoja ili kwamba watotowetu waweze kupona. (Makofi)

Page 340: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

340

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante naomba niunge hoja kwa asilimia mia moja.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Neema Mgaya,Mheshimiwa Lolesia Bukwimba na kama muda utakuwepokwa dakika tano Mheshimiwa Bashe.

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi kuweza kuchangiahotuba hii ya Wizara ya Afya. Nianze kwa kumpongeza Raiswangu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihadakubwa ya kuimarisha upatikanaji wa dawa.

Ukiangalia kwenye bajeti ya mwaka 2015/2016 pesazilizopelekwa kwenye huduma ya upatikanaji wa dawailikuwa shilingi bilioni 24, hivi sasa ndani ya miezi tisa chini yaDkt. John Pombe Magufuli, pesa zilizopelekwa za dawa nishilingi bilioni 112. Kwa Mkoa wa Njombe mpaka dakika hiihospitali, zahanati, vituo vya afya tumeshapokea karibiaasilimia 80 mpaka 90 ya pesa za dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza Mawazirikwa usimamizi mzuri, Mheshimiwa Ummy Mwalimu naMheshimiwa Dkt. Kigwangalla kwa kweli wanasimamia vizurizoezi hili, pongezi sana kwao. Ombi langu moja kwa Serikali,Mheshimiwa Ummy ile hospitali yetu pale ya Makambako niHospitali ambayo ipo katikati inahudumia Mikoa ya karibukama Iringa, wengine wanatoka Mbeya maeneo yale yaMbarali kuja kupata huduma za matibabu pale Makambako.Hivyo basi, zile pesa mnazotupangia zinakuwa chache mno.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru tumepata pesakaribu asilimia 90 za dawa lakini mnazo tupangia ni ndogotunaomba muongeze bajeti katika pesa za dawa katikaHospitali ile ya Makambako.

Page 341: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

341

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee pia kuwapongezatena Mheshimiwa Ummy na Mheshimiwa Dkt. Kigwangallakwa kusimamia kikamilifu huduma ya matibabu ya kibingwa.Kwa kweli katika hili mmefanya vizuri, tumeona katika hotubayenu rufaa sasa hivi zimepungua za kwenda nje, hivyonaamini zile pesa ambazo zingetumika kwa ajili ya rufaa zawagonjwa kwenda nje zitatumika katika masuala mengineya maendeleo kama maji, umeme, barabara na kadhalika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitochoka kuendeleakupongeza, nawapongeza pia Mheshimiwa Rais, WaziriUmmy, Naibu Waziri Kigwangalla kwa kuweza kufanikishaupatikanaji wa vifaa vya hospitali kama magodoro, vitanda,mashuka, tumeona kwamba Wilaya zote ndani ya nchi yetuya Tanzania tumeweza kupata vifaa hivyo. Hongera sanakazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualala vifo vya mama wajawazito, kila mwanamke aliyesimamahapa amezungumzia tatizo hili la vifo vya akina mamawajawazito. Takwimu zinaonesha na kwenye hotuba yakeMheshimiwa Waziri ameonesha kabisa kwamba vifo vyaakina mama wajawazito vimeongezeka kutoka 430 mpaka556 katika vizazi hai 100,000, hali ni mbaya sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ummy wewendiye Waziri mwenye dhamana katika Wizara hii ya Afya,wewe ni mwanamke, wewe ni mzazi, wewe ni mama wawatoto. Mheshimiwa Ummy unatusaidiaje wanawake wenziokatika tatizo hili? Hakikisha unapambania tatizo hili kutusaidiawanawake wenzio ili uweze kuacha alama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mheshimiwa Ummykatika Wizara hii unaye kaka yetu Naibu Waziri Dkt.Kigwangalla yeye ni daktari kwa taaluma na Balozi waWanawake, shirikianeni katika kuhakikisha kwamba tatizohili la vifo vya wanawake linakwisha nchini kwetu Tanzania.(Makofi)

Page 342: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

342

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualapia la huduma za afya kwa watoto wachanga. Nataka nijueni lini Serikali itaweka utaratibu mzuri wa kuweza kusimamiaafya ya mtoto mchanga kwa maana ya siku 30 mpaka sikumoja. Nimesoma vijarida mbalimbali vya wataalamvinaonyesha kwamba tukiweza kudhibiti vifo vya watotokuanzia siku 30 mpaka siku moja kwa maana ya kuboreshaafya za watoto wao, tutaweza kupunguza vifo vya watotowadogo chini ya miaka mitano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ulaya wenzetu watotoambao wanazaliwa kwa gramu 500 mpaka gramu 600wanaishi tofauti na hapa kwetu. Naiomba Serikali sasa ioneumuhimu wa kuweza kuanzisha huduma ya afya za watotohawa wachanga wa siku 30 mpaka siku moja, waanzishewodi kwenye kila Wilaya ndani ya Tanzania kama ilivyopelekavifaa vile kila Wilaya na hizi wodi za watoto wachangazifunguliwe kila Wilaya il i kina mama wa Wilaya yaWanging’ombe waweze kupata huduma hiyo, Ludewa,Makete, Njombe na Wilaya zingine ndani ya Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ya matibabu yasaratani, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumzakwamba sasa hivi wanakwenda kununua mitambo ya kutoahuduma ya tiba kwa ajili ya saratani. Mheshimiwa Waziri nadada yangu Ummy, kwa nini Serikali msiwekeze zaidi kwenyekinga, ukizingatia kwamba saratani ambayo inauaWatanzania wengi ni saratani ya shingo ya uzazi. Wanawakewengi wanakufa, hebu wekezeni zaidi kwenye kinga, kwenyeWilaya zetu kule tunakotoka ili mwanamke wa Ludewa kuleaweze kupata huduma hiyo na kugundua hilo tatizomapema. Kwa sababu inaonekana kwamba wagonjwa wasaratani wanakuja kugundulika wana matatizo hayo wakatiimeshafika stage ya hali mbaya, matokeo yake Serikaliinatumia gharama kubwa kuwatibia, kuwafanyia hudumana matibabu ya mionzi, chemotherapy wakatitungezigundua mapema tungeweza kuokoa maisha yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina experience Mama

Page 343: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

343

yangu amekufa kwa pancreatic cancer, na tumekujakugundua muda umeshapita, kama kungekuwa na hudumahizi mapema hata akina mama wanapokwenda tu hospitalianaweza aka-check, akagundua mapema, mtu anawezaakakaa kwa muda mrefu zaidi ya miaka 15 mpaka 20, lakiniwagonjwa wengi wa kansa wanagundulika wakati haliimeshakuwa mbaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali ijikite zaidikwenye kinga na kushusha kule kwenye Wilaya zetu ili kilaWilaya tuweze kupata huduma hii ya kinga ili tuweze kuokoawanawake wengi, Kwa sababu kansa ya shingo ya uzazindiyo ambayo inaua wanawake wengi. Wengi wanaokufana kansa ni wanawake ukiangalia katika takwimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualala uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi. Mheshimiwa Waziri,Dada Ummy kwenye hotuba yako umejinasibu kwamba kuleDar es Salaam mmefungua Benki ya Wanawake, Pwaniwamefaidika, Dar es Salaam wamefaidika na mikopowamepatiwa viwanja. Mimi naomba kwenye majumuishoyako ukija kujumuisha hapa uniambie ni lini Benki yaWanawake itafunguliwa Mkoa wa Njombe ili sisi wa kinamama wa Njombe tuweze kufaidika na sisi na mikopo hiyo,lakini vilevile tuweze kufaidika tupate viwanja kamawalivyopata akina mama wa Dar es Salaam, kamawalivyopata akina mama wa Pwani. Hivyo, katikamajumuisho yako nitapenda unijibu kwamba ni lini benki hiyoitafunguliwa ndani ya Mkoa wa Njombe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimalizie kwakuzungumza suala la haki za watoto hasa watoto wa kike.Akina mama wenzangu Mheshimiwa Faida Bakar mpakaametoa machozi hapa kuhusiana na suala la watoto,nakubali kabisa sisi kama walezi, wazazi tunajitahidi sanakuwasaidia watoto wetu wasiingie kwenye ndoa za utotoni,lakini Sheria ya Ndoa ni kichocheo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua kabisa kuwa sualahili ni la Katiba na Sheria, lakini Mheshimiwa Waziri wa Afya,

Page 344: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

344

Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dada Ummywewe ndiye unayesimamia haki ya mtoto wa kike.Nakuomba sasa kushirikiana na Waziri wa Katiba na Sheria,mlilete suala hili mapema ndani ya Bunge ili tuweze kulifanyiamaboresho na tusibaki tu tunalalamika hapa.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa LolesiaBukwimba.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangiaWizara muhimu kabisa Wizara ya Afya.

Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa MheshimiwaRais John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ndaniya Taifa letu hasa katika suala la maendeleo kwa ujumla.Wote tunaona kazi inayofanyika ndani ya nchi yetu kwakipindi kifupi cha mwaka mmoja na tunaona mambomakubwa yanafanyika kwa namna ya kipekee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue nafasi hiikumshukuru sana Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu kwakutupatia gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya Katoro.Napenda kutoa salamu hizi kutoka kwa wananchi wa Jimbola Busanda hasa Katoro, salamu hizi kwa kweliwamekushukuru na wamekupongeza wamefurahia sana nawanasema hakika vifo vya akinamama vitakwisha sasa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nichukue nafasi hiikumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri Kigwangalla, kupitiawataalam wa taasisi ya AMREF walikuja kuzindua mradimkubwa sana wa kuweza kuboresha huduma za afya katikaKituo cha Afya Chikobe, Zahanati ya Nyamalimbe, Zahanati

Page 345: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

345

ya Rwamgwasa pamoja na Kituo cha Afya cha Kashishi. Kwahiyo, kipekee nitumie fursa hii kushukuru sana AMREF kwa kazikubwa kuweza kuungana pamoja na Serikali katikakuboresha huduma hizi kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nichukue nafasi hiikuwashukuru GGM kwa kuweza kujenga mochwari palekatika Kituo cha Afya Katoro. Hakika ushirikiano huu pamojana Serikali yetu inaonesha jinsi ambayo tutaweza kutatuachangamoto mbalimbali za afya katika sehemu mbalimbalikatika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo,napenda kuzungumzia suala la watumishi. Katika sekta yaafya kweli kuna upungufu mkubwa sana wa watumishi,nikiangalia katika Halmashauri yangu ya Wilaya ya Geita kunaupungufu mkubwa sana, mahitaji ni watumishi 824, walioponi watumishi 345, kwa hiyo upungufu ni mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kwa kuwaSerikali inakusudia kutoa ajira iangalie upungufu huu katikaHalmashauri ya Wilaya yangu ya Geita, ndiyo maanakunatokea hata hivi vifo, vilevile kunatokea changamotombalimbali kwa sababu kuna upungufu mkubwa sana wawataalam wa afya hasa katika sehemu za vijijini ambapokunakuwa na upungufu mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimesoma hii bajetiambayo Mheshimiwa Waziri ameiwasilisha, kipekee sijawezakuona ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.Ninaomba katika majumuisho Mheshimiwa Waziri uwezekutueleza wananchi wa Geita kwamba kuna mpango ganisasa wa kuanzisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa katika Mkoawa Geita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivyo kwa sababuhospitali ambayo sasa hivi imepewa hadhi kuwa ya rufaa niHospitali ya Wilaya ya Geita na sababu hiyo hatuna kabisahospitali ya Wilaya kwa sasa. Tunaomba Serikali ioneumuhimu sasa wa kuanzisha hospitali ya Mkoa ili kurahisisha

Page 346: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

346

huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Geita. Kumbuka Mkoawa Geita tuna watu wengi sana zaidi ya milioni moja, kwasababu hiyo tunahitaji huduma. Nichukue fursa hii kumuombaMheshimiwa Waziri muangalie uwezekano wa kipaumbelekatika kuhakikisha kwamba tunapata Hospitali ya Mkoa waGeita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika suala la mamana mtoto, nilikuwa nikiangalia bajeti, ninapenda kuungamkono hoja ya Kamati ya Bunge ambayo imezungumziakatika ukurasa wa 33, kutokana na kwamba bajetiimepunguzwa hasa katika kupunguza vifo vinavyotokanana uzazi kwa asilimia 33.8. Mimi naungana na Kamati, kuonakwamba Serikali iangalie umuhimu wa kuweza kuongezabajeti hii kwani akina mama wengi wanakufa kutokana nasuala la kujifungua. Kwa vile tunapunguza bajeti maana yakeni kwamba tatizo hili litashindwa kutatulika kwa sababubajeti imepunguzwa.

Kwa hiyo, niiombe Serikali iangalie uwezekanomkubwa wa kuendelea kuongeza bajeti hasa katika sualahili, ili kuwezesha kupunguza vifo vya kina mama hasa wakatiwa kujifungua na katika uzazi baada ya kujifungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya ni suala muhimusana. Serikali kupitia Sera ya Taifa inasema kwamba kila kijijituwe na zahanati, kila kata tuwe na kituo cha afya. Sualahili ukiangalia kiuhalisia hasa katika sehemu mbalimbaliTanzania na hasa nikiangalia kwenye Jimbo langu tunaupungufu mkubwa kabisa. Mimi ninazo kata 22, lakini katikakata hizo ninavyo vituo vya afya vinne tu, hivyo bado tatizoni kubwa. Naiomba Serikali iwekeze zaidi katika kuhakikishakwamba iweze kutekeleza sera yake ambayo ni kuwa nakituo cha afya kwenye kila kata na kila kijiji tuwe na zahanatiili kuweza kuboresha huduma hasa kwa akina mamawajawazito pamoja na watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuzungumziasuala la watoto wetu wa kike waliopo hasa katika sekondari.Wakati wa hedhi, tunaomba Serikali iwaangalie watoto

Page 347: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

347

hawa tuweze kutoa hivi vifaa vya kujihifadhi, kutokana nakwamba wengine wanashindwa hata kuendelea namasomo kwa sababu hiyo.

Kwa hiyo, niombe katika bajeti hii iangalie uwezekanokwenye shule zetu za sekondari watoto wapewe hudumahii, wapewe vifaa vya kujihifadhi, wengine wanashindwakuendelea na masomo hasa kipindi hicho wanashindwa ku-concentrate katika masomo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kuiombaSerikali kama bajeti haijapangwa basi waangalie namna yakuipanga ili kuweza kunusuru watoto wetu ili wawezekuendelea mbele zaidi hasa watoto wa kike ambao waposhuleni. Sambamba na hilo nilikuwa naomba pia Serikaliipunguze kodi, iondoe kodi kabisa zile pad ziwe zinaingiafree zisiwe na kodi zozote. Hii itawezesha pia akina mamapamoja na wasichana kuweza kupata vifaa hivi kwa beinafuu ili waweze kujihifadhi. Kwa sababu hali ya hedhi nihali ya kawaida tu ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka kwawanawake, ni nature, kwa hiyo Serikali inatakiwa ituangaliewanawake, iangalie namna yakutusaidia na kutu-support.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la maendeleoya jamii, ninapenda kuungana na wenzangu, kusemakwamba Halmashauri nyingi kwa kweli hazitilii mkazo sualala maendeleo ya jamii. Haiwezekani kama tutawezakushindwa kusimamia sekta ya maendeleo ya jamii,hatutaweza kufikia maendeleo ambayo tumekusudia katikanchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema nchi yetutunaelekea kwenye viwanda, tutafikaje kwenye viwandabila kuimarisha sekta ya maendeleo ya jamii? Hivyo nitumiefursa hii kuiomba Wizara iweke mkazo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 348: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

348

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Bukwimbakwa mchango wako. Mheshimiwa Hussein Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru nianze kabisa kwa kuunga mkono hoja.

Mimi nina mambo machache, jambo la kwanzaalilisema Mheshimiwa Selemani Zedi, tarehe 19 Januari,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega alimuandikiaKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuitaka kampuni inayoitwaMokasi Medical Systems and Electronics iliyopewa mkatabawa ku-service x-ray waje waifanyie marekebisho x-ray yaHospitali ya Wilaya ya Nzega. Mpaka leo ni miezi mitano,ninataka nimuombe Mheshimiwa Waziri anapokuja ku-windup atuambie kwa nini, kwa sababu nimemsikia hata nduguyangu wa Mafia amelalamika sana kuhusu hili suala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini hii kampuni kamaina mkataba na Serikali usivunjwe huu mkataba? Jambo lakwanza. Jambo la pili kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe?Hili ni jambo ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wananchi waHalmashauri ya Wilaya ya Nzega na Halmashauri ya Mji waNzega wanapata shida, x-ray ipo, hairuhusiwi kuguswa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe taarifa kwenyeBunge na nimpongeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Nzega, ninaamini kaka yangu Simbachawenehatamchukulia hatua kwa maamuzi aliyoyafanya huyuMkurugenzi. Mkurugenzi ameamua kuwasialiana na Hospitaliya Rufaa kwa ajili ya kumpata Biomedical Engineer anaitwaEmmanuel Nkusi kutoka Bugando ili aje aweze kwa sababuni mtaalamu kushughulikia suala la x-ray ya Hospitali yaWilaya ya Nzega. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwamba kwa

Page 349: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

349

kuwa mkataba ni Philips huyu mtu amefanya maamuzi kwakuangalia maslaha mapana ya nchi, nataka nisemekwamba maamuzi haya yamefanyika na mtaalamu amefikana ameshalipwa na amechukua kifaa kuondoka nacho.(Makofi)

Hoja yangu, Mheshimiwa Waziri anapokuja why huyuMokasi asifukuzwe kufanya hizi kazi, hili ni jambo moja. Jambola pili mimi ni mpongeze sana Mheshimiwa Rais, mimi nimjumbe wa Kamati, support aliyoitoa Mheshimiwa Raiskwenye suala la hospitali ya Ocean Road na tunafahamumatatizo ya cancer, na mimi nimpongeze sana MheshimiwaWaziri Ummy kwa sababu tupo kwenye Kamati yeye naMheshimiwa Kigwangalla tunaona tatizo la resource lililopona namna anavyoweka priority, nataka niombe kwa ushauri,mwaka huu tunamaliza ile Phase II pale Ocean Road natutakuwa kwenye nafasi nzuri sana kwenye Ocean Road.Niombe jitihada ziongezwe kwenye Hospitali ya Kikwete yaMoyo na Hospitali ya MOI ili ziweze kuongeza utoaji wahuduma katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho natakaniishauri Serikali, Ilani yetu ya uchaguzi it is very clear, kwambakila kijiji - zahanati na kila kata - kituo cha afya, hii ndiyocommentment yetu kwa Watanzania. Ningeomba kuwepona proper plan na kuwe kuna strategic unit kati ya Wizaraya TAMISEMI na Wizara ya Afya ni namna gani tunajenga kilamwaka vituo vya afya. Kama kila Halmashauri ikiwekewacondition kwamba kila mwaka wa fedha angalau vijengwevituo viwili, vitatu vya afya tuna uwezo wa kupata kwamwaka angalau vituo 200 vya afya. Hii itatusaidia sanakupunguza matatizo katika maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami niwapongeze sanaWizara ya Afya na TAMISEMI, kuwepo kwa Dkt. Chaula paleanayeshughulika na masuala ya afya, angalauanatupunguzia.

Nataka niwaombe Mheshimiwa Simbachawene naWaziri wa Afya, hebu ondoeni haka ka-condition kwa tofauli

Page 350: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1495705860-03 MEI 2017.pdf · kwa mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne watahiniwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

350

za nchi sita. Kule kwenye Halmashauri wananchitumewahamasisha, mfano kwangu sasa hivi tunavyoongeatuna zahanati 15 tunajenga sisi wananchi, zimefika kwenyelevel ya madirisha, lakini kuna kale ile condition ya kusemakwamba ili ujenge zahanati lazima iwe tofali ya nchi sita.Tofali ya nchi sita kwa kule kwetu Nzega ni 1200, mwaka huumimi nimegawa matofali 47,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua hiyo twentypercent ya incremental cost ni milioni tisa na laki nne,gharama additional cost. Hivyo, tuwe na flexibility kwenyehaya mambo ili angalau kama tulivyojenga madarasa katikakuanzishwa kwa shule za kata, wananchi walijitahidi sanakwa sababu tuliondoa zile condition za ki-engineer. Niombesana Serikali iangalie namna gani Serikali inaweza kufanyajambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kuwapongezakwa jitihada mnazofanya lakini Mheshimiwa Waziri usipokujana hoja ya huyu Mokasi Medical Systems.....

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: ….nitashika shilingi. AhsanteMheshimiwa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge, huyondiye mchangiaji wetu wa mwisho kwa jioni ya leo.Ninawashukuru sana kwa kazi nzuri mliyoifanya kwa hoja hii,tutaendelea nayo kesho ambapo ndiyo itahitimishwa. Kwahiyo, sina matangazo niliyoletewa hapa.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayonaahirisha shughuli za Bunge hadi kesho siku ya Alhamisi saatatu asubuhi.

(Saa 1.43 Usiku Bunge liliahirishwa Mpaka Siku ya Alhamisi,Tarehe 4 Mei, 2017 Saa Tatu Asubuhi)