chuo cha serikali za mitaamuki.lgti.ac.tz/documents/lgti_mwanafunzi_mwongozo... · 2018-10-23 · 6...
TRANSCRIPT
1
CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA
MWONGOZO WA MWANAFUNZI
Mwongozo huu wa Mwanafunzi umetayarishwa kwa ushirikiano kati ya Ofisiya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI), Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), uliopo Dar es Salaam, Tanzania © Chuo cha Serikali za Mitaa, 2018 ,Toleo la Kwanza ,(Elimu Masafa), 2018 . Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili au kutoa kwa njia yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Chuo cha Serikali za Mitaa.
2
Yaliyomo 1.0 Mpangilio wa mfumo ................................................................................................................... 3
2.0 Programu nyingine ...................................................................................................................... 3
3.0 Upatikanaji wa Mfumo ................................................................................................................ 3
4.0 Kuingia katika Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa ............... 3
5.0 Ukurasa wa mwanzo .................................................................................................................... 4
6.0 Kisanduku cha kutafuta kozi....................................................................................................... 5
7.0 Mwonekano wa kozi .................................................................................................................... 6
8.0 Kalenda ........................................................................................................................................ 8
9.0 Taarifa Binafsi ........................................................................................................................... 10
9.1 Wasifu Wangu ......................................................................................................................... 10
9.2 Hariri picha ya mtumiaji........................................................................................................... 12
10.0 Badilisha Nywila ...................................................................................................................... 13
11.0 Washiriki .................................................................................................................................. 14
12.0 Kutuma jumbe ......................................................................................................................... 16
13.0 Zoezi ................................................................................................................................... 19
13.1 Matini inayoandikwa mtandaoni ............................................................................................. 19
13.2 Ukusanyaji wa faili ................................................................................................................ 21
13.3 Kufuta faili lililoambatishwa .................................................................................................. 22
14.0 Zoezi la papo kwa papo ...................................................................................................... 24
15.0 Alama ....................................................................................................................................... 27
16.0 Jukwaa la majadiliano ...................................................................................................... 28
17.0 Soga ..................................................................................................................................... 31
18.0 Faharasa ................................................................................................................................... 32
19.0 Tathmini ya Kozi ..................................................................................................................... 33
20.0 Kupakua Mwongozo wa Mwanafunzi ..................................................................................... 35
21.0 Kutoka nje ya mfumo .............................................................................................................. 35
22.0 Msaada wa kiufundi na Kimaudhui ........................................................................................ 36
3
1.0 Mpangilio wa mfumo Kivinjari:Kabla ya kuingia kwenye mfumo wa ujifunzaji kielekroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa, unatakiwa kuhakikisha kwamba una moja kati yavivinjari vilivyopendekezwa hapo chini.
• Google Chrome • Firefox Internet explorer Microsoft Edge Opera-mini Web
2.0 Programu nyingine Ili kutazama baadhi ya mafaili, media au vitu vingine vinavyoweza kupatikana katika mfumo huu, unaweza kuhitaji baadhi ya programu zifuatazo:
• Adobe Flash
• Windows Media Player
• Adobe Reader
3.0 Upatikanaji wa Mfumo Mfumo unaweza kupatikana kwa kutumia vifaa mbalimbali kama vile kompyuta ya mezani, tabiti na simu janja.
4.0 Kuingia katika Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa Anuani ya Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa ni http://elms.lgti.ac.tz .Wakati ukurasa unafunguka, utakupeleka kwenye ukurasa wa ‘kuingia’ kama unavyoonekana hapa chini;
Bofya huu mshale kuangalia Video inayoelezea Umuhimu wa Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki
4
Kisha utatakiwa kuingiza jina lako la mtumiaji pamoja na nywila yako:
Jina la mtumiaji: (kwa mfano: Jina la kwanza. Jina la ukoo)
Nywila: kama uliyopewa na msimamizi wa MUKI/mfanyakazi aliyeidhinishwa
5.0 Ukurasa wa mwanzo Baada ya kufanikiwa kuingia katika mfumo wa ujifunzaji kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa “Ukurasa wa kwanza”utafunguka,Ukurasa huu utakupa uwezo wa kuzipata/kuzifikia kozi na huduma zingine zinazotolewa na Mfumo wa Ujifunzaji Kielekroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa.
Ingia kwenye kozi yako kwa kutumia eneo hili
5
6.0 Kisanduku cha kutafuta kozi
Unaweza kuifikia kozi yako kwa kuandika jina la kozi hapa
Msimbo wa kozi
Bofya hapa kutafuta kozi
Bofya hapa kuona maudhui ya kozi
Hawa ni wawezeshaji wa kozi uliyoitafuta
6
7.0 Mwonekano wa kozi Kozi yako katika Mfumo wa ujifunzaji kielekroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa itaonekana katika mtazamo wa safu ya 3 . Safu pana ya katikati ni mahali ambapo vifaa na shughuli nyingi za kozi zimewekwa, zimepangiliwa kwa kuzingatia mada, majuma au moduli. Hii Safu ya maudhui imegawanywa katika miraba mingi , au "sehemu," na inaweza kuhusisha shughuli mbalimbali za aina tofauti tofauti , rasilimali, na viungo vinavyowekwa na mwalimu wako
Eneo la juu ya Kozi likionyesha Msimbo na jina la Kozi, Maelezo na Malengo ya kozi Pamoja na Maelezo ya kina ya Kozi
7
Vifaa,nyenzo na Shughuli za kozi
Sehemu ya Chini ya Kozi inaonyesha Faharasa ,Marejeo na Tathmini ya Kozi
8
8.0 Kalenda Ili kuifikia kalenda tafadhali fuata mwongozo huu,
Baada ya kubofya neno kalenda ukurasa ufuatao utafunguka,
Bofya hapa kuifikia kalenda
Nukta hii inaonyesha kuna tukio katika tarehe hii
Ingiza tukio jipya Chagua kategoria unayotaka kuingiza
tukio
Bofya hapa kuona tukio
9
Bofya hapa kwenda kwenye kazi
10
9.0 Taarifa Binafsi 9.1 Wasifu Wangu Unaweza kutengeneza maelezo mafupi ya wasifu wako na baadhi ya mipangilio ya Mfumo wa ujifunzaji kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa kwa kutumia Mipangilio yakundi hili la taarifa.
Hatua ya 1: katika kona ya juu zaidi ya kushoto bofya pale unapoona jina lako ->alama ya mshalealama wa chini ->Maelezo mafupi ya wasifu
Hatua ya 2: Dirisha la taarifa za Mtumiaji litajitokeza kama ilivyooneshwa hapa chini
Mshale wa Alama wa chini
11
Hatua ya 3: Kisha dirisha linaloonesha taarifa zako binafsi litaonekana
Unaweza kuhariri taarifa zako binafsi hapa
Bofya hapa kuhariri wasifu wa mtumiaji
12
9.2 Hariri picha ya mtumiaji
Bofya hapa kusasisha taarifa zako
Unaweza kupakia picha yako kwa kutumia kisanduku hiki. Unaweza kukokota faili na kuliingiza kwenye kisanduku chenye alama ya mshale wa wa bluu, au bofya kitufe cha weka ili kulitafuta faili na kulipakia.
Weka majina yako mengine hapa
Pia unaweza kuhariri vitu unavyopendelea na taarifa zingine
Kitufe cha kuweka
13
10.0 Badilisha Nywila Unaweza kubadilisha nywila yako kwa kutumia mipangilio ya kundi la taarifa.
Hatua ya 1: Kwenye kona ya juu zaidi kulia bofya pale unapoona jina lako ->mshale wa alama chini->uteuzi.
Kisha dirisha la chaguzi litaonekana, katika chaguzi ulizopewa, bofya badili nywila
Mshale wa Alama chini
Bofya hapa kubadili nywila
14
Katika “badili nywila” kipengele kilichowekwa rangi nyekundu kinahitajika. Nywila lazima iwe na tarakimu zisizopungua 6.
11.0 Washiriki Hatua ya 1: Katika mwonekano wa kozi, bofya hapa ili kuwaona washiriki wa kozi hii ni akina nani.
Angalia washiriki hapa
Mara utakapokuwa tayari, bofya hapa
kuhifadhi mabadiliko
15
Hatua ya 2: Baada ya dirisha la washirki kufunguka, tumia kichujio kuchagua majukumu ya washiriki (Mwalimu, mwanafunzi )
Bofya mshale wa alama kuchagua
kundi la washiriki
16
12.0 Kutuma jumbe Kipengele hiki kinakusaidia kuwasiliana na washiriki (mwalimu, mwanafunzi,mratibu n.k) kwa kutumia ujumbe mfupi.
Katika orodha ya washiriki, Bofya washiriki unaotaka kuwatumia ujumbe
Chagua jukumu la mshiriki hapa
17
Bofya hapa kutuma ujumbe kwa Francis
Mashalla
Bofya hapa kufungua kisanduku cha ujumbe
18
Mara baada ya ujumbe kutumwa, utakuwa na chaguo la kuona kikasha chako na ujumbe uliotumwa.
Ili kuona ujumbe wako ona skrini hapa chini
Baada ya kubofya jumbe dirisha lifuatalo litafunguka
Andika ujumbe wako
hapa
Mara upokuwa tayari, bofya hapa kutuma ujumbe
Mshale wa alama chini
19
13.0 Zoezi
Mwalimu wako atakutaka upakie maudhui ya kidigitali na/ ama majibu ya mtandaoni kwa ajili ya kupewa alama/ kusahihishwa. Kwa mfano, insha, jedwali, mawasilisho, kurasa za tovuti, picha, video sauti au majibu ya aya zilizochapwa yanaweza kutakiwa.
Kuna njia mbili za kukusanya kazi;
Matini inayoandikwa mtandaoni Ukusanyaji wa faili (Mwanafunzi anatakiwa kukusanya faili kwa ajili ya kupewa alama)
13.1 Matini inayoandikwa mtandaoni Kukusanya Matini inayoandikwa mtandaoni, mwanafunzi anahitaji kukamilisha hatua zifuatazo:
Bofya kitufe cha ‘weka wasilisho’ ili kupata ukurasa wa mhariri wa matini inayoandikiwa mtandaoni :
Bofya hapa kuingia kwenye Zoezi Assignment
ujumbe uliotuma na uliotumiwa utaonekana hapa
Bofya hapa kutuma ujumbe
Bofya hapa kujibu ujumbe
20
Chapa matini inayohusika katika mhariri wa HTML, ama nakili kutoka katika faili lililokwisha andikwa kisha Bofya ‘Hifadhi mabadiliko’.
Weka matini yako hapa
Bofya hapa kuanza kufanya zoezi
21
Bofya ‘hifadhi mabadiliko’
13.2 Ukusanyaji wa faili Ili kukusanya faili, kamilisha hatua zifuatazo:
1. Bofya kitufe cha ‘Weka wasilisho’ ili kupata ukurasa wa kupakia faili.
2. Bofya katika ‘weka’ na chagua faili/mafaili yako kutoka katika kompyuta. Unaweza pia kuvuta na kutupia faili/ mafaili kwenye kisanduku cha uwasilishaji. Kisha bofya ‘hifadhi mabadiliko’
Vuta na tupia faili lako hapa
Matini yako itaonekana hapa
Weka faili
22
13.3 Kufuta faili lililoambatishwa Kama unataka kulifuta faili lililoambatishwa, unatakiwa kubofya mara mbili kwenye faili hilo .
Hili ni faili lililowekwa
Bofya mara mbili kwenye faili ili
kulifungua
23
Baada ya kutuma zoezi lako, hadihi ya uwasilsihaji itaonekana kama inavyoonekana katika ukurasa ufuatao .
Bofya hapa kufuta
Hii inaonyesha kuwa zoezi lako limekusanywa
Pia unaweza kuhariri wasilisho lako kabla ya tarehe ya makataa
24
14.0 Zoezi la papo kwa papo
Mara utakapoingiza zoezi la papo kwa papo, utaona maelekezo yaliyotolewa na mwalimu wako, kujibu maswali kunaruhusiwa, tarehe na wakati zoezi la papo kwa papo linapopatikana, na wakati zoezi la papo kw apapo litafungwa. Ili kuanza zoezi la papo kwa papo, chagua kitufe cha kuanza kufanya zoezi la papo sasa.
Ikiwa zoezi linaruhusu kufanyika kwa kurudiwa mara nyingi na umefanya, kitufe kitasomeka jaribu tena kufanya zoezi la papo kwa papo. Ikiwa zoezi la papo kwa papo inaruhusu kufanyika mara moja tu, dirisha litajitookeza likikuuliza endapo ungependa kendelea.
Bofya hapa kuingia kwenye zoezi la papo kwa papo
25
Mara unapoanza kufanya zoezi la papo kwa papo, hakikisha unalisoma kila swali kwa umakini. Unaweza kuyawekea alama maswali ambayo unataka kuyaruka na / au kuyahakiki baadaye.
Ubofyaji wa kitufe cha "maliza kufanya maswali" utakuhitimishia kujibu maswali. Papohapo itakuhitaji kuthibitisha. Mara itakapokubalika kuthibitisha haiwezi kurudishwa nyuma.
26
Wakati wa kumaliza zoezi la papo kwa papo, muhtasari wa kujibu maswali utatolewa kwa mwanafunzi na mfumo wa ujifunzaji Kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa kwa mawanafunzi.
NB: Jaribio jipya la kufanya zoezi linawezekana endapo tu MUDA haujaisha.
27
15.0 Alama Ikiwa mwalimu wako anatumia kipengele cha Kitabu cha Alama, utaweza kuziona alama zako kwa kuchagua Alama, zilizowekwa kwenye mfumo.
Bofya hapa kuona alama
28
16.0 Jukwaa la majadiliano Tuma- ujumbe wowote kwenye jukwaa la majadiliano ikiwa ni pamoja na mada za mjadala na majibu yoyote.
Mada– Mada ya wasilisho .
Ujumbe – inaweza kuwa mawazo ya mwanafunzi, maoni au majibu ya mada ya mjadala.
Kiambatisho – Mwanafunzi anaweza kuambatisha rasilimali mbalimbali ambazo zinahusiana na mada ya mjadala.
Mfululizo –Mfuatano wa majibu (au majibu ya jibu) kwenye wasilisho asilia.
Mada – Mada ya wasilisho asilia la mfululizo wa mawasilisho.
Mada mpya ya mjadala imewekwa
Kushiriki katika jukwaa la mjadala la jibu langu bofya hapa
Mada ya mjadala iliyowekwa
Bofya hapa kuingia kwenye jukwaa la majadiliano
Hapa unaweza kuweka mada kwa ajili ya mjadala
29
Bofya hapa kuingia kwenye jukwaa la majadiliano
Andika jibu lako hapa
30
Kuangalia jibu lako na jibu la watu wengine, tafadhali angalia skrini hapa chini
vuta na tupia faili lako hapa
Mara utakapokuwa tayari kukusanya, bofya ‘Tuma kwenye jukwaa la majadiliano ’
Bofya hapa kuona Majibu yako na ya washiriki wengine ’
31
17.0 Soga Moduli ya shughuli za mazungumzo inawawezesha washiriki kuwa na majadiliano ya maandishi ya ana kwa ana.
Gumzo inaweza kuwa shughuli ya wakati mmoja au inaweza kurudiwa kwa wakati mmoja kila siku au kila wiki. Vikao vya mazungumzo vinahifadhiwa na vinaweza kupatikana kwa kila mtu kuona au kuzuiwa kwa watumiaji wenye uwezo wa kuona kumbukumbu za kikao cha mazungumzo.
Kuingia kwenye Gumzo fanya yafuatayo;
Baada ya kuingia kwenye Soga dirisha la Soga litakuwa kama ilivyoonyeshwa hapo chini
Bofya hapa kuingia kwenye Gumzo la Madiwani
Haya ndiyo majibu uliyochangia wewe na washiriki wengine
32
18.0 Faharasa Moduli wa shughuli za Faharasa huwezesha washiriki kuunda na kudumisha orodha ya ufafanuzi, kama kamusi, au kukusanya na kupanga rasilimali au habari.
Kuweza kupata Faharasa ya kozi, fuata mwongozo hapo chini.
Baada ya kubofya sehemu elekezwa, orodha ya maneno na ufafanuzi wake vitaonekana kama hivo apo chini.
Bofya hapa kuingia kwenye Ufafanuzi wa maneno magumu yaliyotumika kwenye kozi
33
19.0 Tathmini ya Kozi Moduli ya shughuli za tathmini hutoa mwongozo na kuhamasisha kujifunza katika mazingira ya mtandaoni. Mwalimu anaweza kutumia haya kukusanya Takwimu kutoka kwa wanafunzi wao ambayo itawasaidia kujifunza kuhusu darasa lake na kutafakari juu ya mafundisho yao wenyewe.
Kushiriki kwenye kutathmini kozi, fuata mwongozo hapo chini.
Orodha ya maneno na ufafanuzi wake (Faharasa) vitaonekana hapa
Bofya hapa kushiriki kwenye tathmini ya kozi
34
Baada ya kubonyeza Tathmini ya Kozi, dirisha la tathmini litakuwa kama ilivyoonyeshwa hapa chini
Ukishamaliza kujaza, Bofya hapa kumaliza kushiriki
35
20.0 Kupakua Mwongozo wa Mwanafunzi
21.0 Kutoka nje ya mfumo Baada ya ukamilishaji wa kazi yoyote katika Mfumo wa ujifunzaji kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa, mwanafunzi anatakiwa Kutoka nje ya mfumo (Ni muhimu kutokana na taarifa za kiusalama)
Hatua: Kwenye kona ya juu zaidi kushoto Bofya pale ambapo unaona jina lako -> mshale wa alama chini -> toka nje.
Bofya hapa kupakua kiongozi cha
36
22.0 Msaada wa kiufundi na Kimaudhui Endapo utapata tatizo lolote wakati unatumia Mfumo wa Ujifunzaji wa Kielektroniki wa Chuo cha Serikali za Mitaa (muki.lgti.ac.tz), tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia taarifa za mawasiliano zifuatazo,
Simu: (255)262961101
Barua Pepe: [email protected]
Barua Pepe: [email protected]
Tovuti: www.lgti.ac.tz
Bofya hapa kutoka nje ya mfumo
Mshale wa alama chini