covid-19 vyombo vya habari vyahitaji · 2020. 6. 2. · waliomeremeta toleo la ptmbrktoba 1 na...

Click here to load reader

Upload: others

Post on 25-Jan-2021

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

    Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 153, Mei, 2020ISSN 0856-874X

    Uhuru wa habari wazidi kuporomoka -IPI

    EACJ kuamua kuhusu notisi ya serikali

    Mkongwe wa habari afariki

    Uk 5 Uk 11Uk 9

    Vyombo vya habari

    vyahitaji msaada

    COVID-19

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

    MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

    2

    TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

    Kusaidia vyombo vya habari ni muhimu Dhamira na wajibu wa vyombo vya habari kuhabarisha umma inaviweka katika majaribu. Hali ni mbaya katika kipindi cha majanga kama ilivyo sasa - kutokana na kusambaa kwa Covid-19.

    Baraza la Habari Tanzania linakiri kwamba “wanahabari ni watu wa kwanza kuitikia dharura na wako mstari wa mbele.

    Hata hivyo kutokana na kazi zao wanahabari wengi wanahatarisha maisha yao kwa kuandika habari za ugonjwa huo wakiwa mstari wa mbele au kuambukizwa wanapokutaa na vyanzo vya habari.

    Tofauti na wanataaluma wengine wanahabari hawawezi kufanyakazi wakiwa wamejitenga ama kujiweka katika karantini”.

    Hii inahitaji taratibu za kipekee na kwa msingi huu wanahabari wanahitaji kusaidiwa kwa dharura katika kipindi hiki.

    Wakati wengine wanaweza kuchukua hatua zote za usalama, kwa wanahabari nafasi yao ni finyu.

    Wanachanganyika na watu ili kuweza kupata habari stahiki ili nao waweze kuhabarisha kwa usahihi.

    Ili kuwawezesha kufanyakazi kwa ufanisi kuhakikisha umma unapata habari za uhakika, ni muhimu ombi lililotolea na Baraza la kutaka wapatiwe vitendea kazi na vifaa vya kujilinda litekelezwe.

    Wadhamini walioombwa kutoa msaada wazingatie maombi hayo kwa kuwa wanahabari kama watu wengine wanahitaji kuwa na afya na salama.

    Kwa ujumla umma wenye taarifa ni muhimu kwa kuhamasisha maendeleo ya jamii na taifa kwa jumla na ni muhimu kukubali ukweli umuhimu wa mchango wa wanahabari wenye afya nzuri.

    MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

    FREE MEDIA PIONEER

    Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye chumba cha habari.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    3

    Habari

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Na Mwandishi wa Barazani

    Kuna haja kubwa ya kuwa na utaratibu wa muda mrefu wa kuvipa-tia msaada vya viten-dea kazi vyombo vya habari kukabiliana na majanga kama Covid -19 na mengine yanay-oweza kutokea katika siku za mbele.

    Mwito huo umo katika ripoti iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) kwa ajili ya wadau na washirika wa maendeleo.

    MCT ilipewa jukumu na wadau wa habari kufanya utafiti kuhusu mahitaji ya vyombo vya habari kutokana na mlipuko wa Covid-19 katika mkutano ulioandaliwa na Internews.

    Kulingana na ripoti ya Baraza

    vyombo vya habari 120 vya Bara na Visiwani vikiwemo vikubwa kama – Mwananchi Communications Limited – wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi na The Citizen,Star TV, The Guardian na Clouds vilihusika katika utafiti.

    Matokeo ya utafiti huo umebaini kuwa vipaumbele vya mahitaji ya kujikinga ni pamoja

    Vyombo vya habari vyahitaji kusaidiwa kutokana na Covid-19

    Wanahabari wakiwa kazini

    Endelea Ukurasa wa 4

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    4

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    na barakoa, vitakasa mikono na vifaa vya usafi vya ofisi wakati vya kutendea kazi ni maikrofoni na kinga zake, vifurishi vya intaneti na kompyuta mpakato.

    Baada ya kubaini mahitaji , MCT imewandikia wahisani mbalimbali kwa lengo la kuvipatia msaada vyombo vya habari.

    Orodha ya wafadhili walioandikiwa na Baraza ni:-Airtel, Bakhresa, GSM, Sikika, Bank of Africa, Coca Cola, Costech, Freedom House, Geita Gold Mine, Halotel, HelpAge, Internews na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

    Wengine ni Marie Stopes, MIC Company, MISA-TAN, Multichoice, Pathfinders, Precision Air, Serengeti Breweries, TCC, TSN, UNISEF,

    USAID TULONGE AFYA, .VODACOM na WORLD LUNG FOUNDATION.

    Katika barua kwa wafadhali hao Baraza limeeleza kuwa ni kazi ya mwandishi kuwasilisha habari za uhakika kwa uwazi kabisa kwa umma na katika kipindi cha majanga, jukumu hili linakuwa muhimu zaidi.

    Limeeleza kuwa “ wanahabari ni watu wa kwanza kutikia dharura na wako mstari wa mbele.

    Hata hivyo kutokana na kazi zao wanahabari wengi wanahatarisha maisha yao kwa kuandika habari za ugonjwa huo wakiwa mstari wa mbele au kuambukizwa wanapokutaa na vyanzo vya habari.

    Tofauti na wanataaluma wengine wanahabari hawawezi kufanyakazi wakiwa

    wamejitenga ama kujiweka katika karantini”.

    Baraza kwa niaba ya wadau wengine wa habari, limewataka wahisani kusaidia ama kwa kutoa fedha ama vifaa vinavyohitajika kuwawezesha waandishi na vyombo habari kuendelea na majukumu yao muhimu ya kuupasha habari umma katika kipindi cha janga.

    Limeeleza katika barua yake kuwa Baraza litaratibu usambazaji wa vifaa kwa vyombo vya habari kwa Bara na Visiwani.

    Kulingana na takwimu za karibuni za Idara ya Habari iliyo kwenye tovuti yake http://www.maelezo.go.tz/ kuna majarida 229, vituo vya redio 186, Vituo vya Runinga 44 na runinga za mtandaoni 264 nchini.

    Vyombo vya habari vyahitaji kusaidiwa kutokana na Covid-19Inatoka Ukurasa wa 3

    Maikrofoni vifaa m muhimu katika ukusanyaji habari vinahitaji kuwa na vizuizi vya kinga.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Hali ya uhuru wa habari duni-ani kote imekuwa mbaya ku-tokana na kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19, kwa kuwa serikali zote za kidemokrasia na za kiimla zimekuwa zikichukua hatua za kubana vyombo vya habari.

    Taasisi ya Kimataifa (IPI) ya Habari katika taarifa iliyochapisha Mei mosi, 2020 imeeleza katika miezi michache ya kusambaa ugonjwa huo duniani, umeleta changamoto kwa wanahabari na vyombo vya habari na kwamba vitendo vya kukamatwa, kushambuliwa hata kimwili na kuwepo kanuni mbaya za usimamizi wa habari vimeongezeka na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

    Ikikariri taarifa yake ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ya mwaka 2020, IPI imesema kuwa serikali za kidemokrasia pamoja na zile za kiimla, tatizo hili la kiafya dunaini limezifanya kuzidi kubana vyombo vya habari kwa kisingizio cha kudhibiti upotoshaji.

    Serikali za kiimla ambazo tayari zilikuwa na sheria kandamizi za habari, zimekiuka hatua za dharura kwa kubana zaidi vyombo huru na kufanya uandishi kuwa uhalifu, taasisi hiyo yenye makao yake Vienna, Austria imeeleza katika taarifa yake.

    Aidha IPI imeeleza mataifa yenye demokrasia pia yamechukua hatua za kubana upatikanaji wa habari kuhusu ugonjwa huo.

    Hatua za kuzuia vyombo vya habari vinavyohoji kuhudhuria vikao vya kutoa taarifa za balaa hilo la afya na kuvifunga baadhi ya vyombo vya habari na kufanya uangalizi ambao matokeo yake yana athari za muda mrefu, serikali zinafanya kila mbinu kubinya mtiririko wa habari uhuru wa habari wakati ambapo mtiririko huo ni muhimu zaidi.katika kuhabarisha umma kuhusu hatua muhimu za kudhibiti virusi hivyo.

    Katika kipindi cha miezi miwili na nusu, IPI katika kufuatilia habari za Covid-19 imebaini ukiukaji tofauti 162 wa uhuru wa habari kuhusiana na virusi vya corona.

    Theluthi moja ya ukiukaji huo

    unahusisha kukamatwa, kuwekwa ndani ama kufunguliwa mashataka wanahabari kwa kuandika habari za janga hilo na kulingana na takwimu za IPI kumekuwa na matukio zaidi ya 50 ya mashambulizi ya kufokewa na ya mwili dhidi ya waandishi wa habari wakati wakiandika habari kuhusu virusi vya corona.

    Pia zaidi ya matukio 27 udhibiti na ubinyaji habari umerekodiwa na visa vingine 25 vya ubanaji habari wa kupitiliza.

    Mkurugenzi Mtendaji wa IPI, Barbara Trionfi, amesema taarifa zilizokusanywa na taasisi yake zinaonyesha hatari – ambayo katika baadhi ya maeneo imeshatokea - kwamba mataifa yatatumia janga hili

    la kiafya kudhibiti habari, bila kujali matakwa ya habari kwa umma.

    Hii imesababisha kuwepo mazingira mabaya zaidi kwa vyombo huru vya habari.

    “Ni muhimu” IPI imeeleza katika taarifa hiyo “ hatua hizi ziada za udhibiti wa vyombo vya habari zilizowekwa katika kipindi hiki zinaweza kugeuzwa kuwa za kawaida na kuendelezwa hasa pale inapotokea serikali kukosa uwazi, vyombo vya habari kutoweza kukutana na watoa maamuzi na hatua zozote za kubana vyombo hivyo.

    “Wakati huo huo, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa vyombo vya habari kutokana na tishio la kiuchumi ambalo

    5

    Habari

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Covid-19 yaathiri zaidi uhuru wa habari - IPI

    Endelea Ukurasa wa 10

    Mkurugenzi Mtendaji wa IPI, Barbara Trionfi.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    6

    Fursa

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    The Media and Journalism Days in Africa is a project led by Africa 21 and its partners aimed at annually convening journalists from the African continent, alongside experts from international Geneva and around the world, to review, exchange and debate on a selected theme related to the United Nations 2030 Agenda for Sustainable Development.

    The first edition took place in 2019 on the theme of climate change with journalists from French-speaking Africa, with a follow up edition in 2020 covering the same theme with journalists from English-speaking Africa. The objectives are two-fold. The event will strengthen the skills of journalists invited on this topic, offering participating journalists the opportunity to share their realities with the public and international experts. In addition, the event will integrate the Network of African journalists specializing in sustainable development and climate change, in order to create a strong link between international Geneva and the African media.

    Objectives

    The 2020 edition of the ‘Media and Journalism Days in Africa’ engages Journalists from Anglophone Africa to:• Raise awareness among African media on the 2030 Agenda, international Geneva and environmental

    and climate issues so that these subjects are adequately followed in the participating media;• Renew the appeal of international Geneva to the English-speaking African media by establishing a

    connection between African journalists and organizations in international Geneva;• Highlight to international Geneva, the realities, challenges and opportunities facing African Journalists,

    with a particular focus on the realities facing the participating Journalists• Expand the Network of African journalists specializing in sustainable development and climate change.

    What will be funded

    Africa 21 and partners cover all travel related and subsistence costs for Journalists attending the MJDA in Geneva, this includes travel allowance, flight ticket, on-site transport, hotel and allowances for food costs on site.

    Selection Criteria

    Participating Journalists must meet the following criteria :• Current Professional Journalist for the written press, radio or TV (press card);• Poses at least 5 years of professional experience in media;• Must be active in the field as well as in the newsroom;• Interest or specialization in sustainable development and climate change issues;• Valid passport until December 31, 2020 at least and availability to travel to participate in the MJDA

    event;• Female candidates strongly encouraged;• Eligible countries: Botswana, Egypt, Eswatini, Ethiopia, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Liberia,

    Malawi, Mauritius, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, South Africa, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia, Zimbabwe.

    Call for Applications "2020 Media and Journalism days in Africa"

    For more information, visithttp://www.africa21.org/call-for-applications-media-and-journalism-days-in-africa-2020-special-

    climate-change-october-12-16-2020-in-geneva/

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Kilele cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2019 am-bapo wanahabari waliotoa kazi nzuri watatambuliwa na kutun-ukiwa imepangwa kuwa Septemba 5, 2020.

    Ofisa Programmu, Paul Mallimbo, anayeratibu mashindano hayo katika Baraza la Habari Tanzania (MCT) ameeleza matumaini kwamba wakati huo utakuwa muafaka kwani tishio la Covid-19 litakuwa limepungua na

    wadhamini watakuwa tayari kuuunga mkono.

    “ Hivi sasa tumo katika mchakato wa kuwaandikia barua wadhamini watarajiwa “ alisema.

    Kutakuwa na makundi 21 katika EJAT 2019 ambayo ilizinduliwa rasmi Oktoba mwaka jana.

    Makundi mapya ni pamoja na Ubunifu Maendelo ya Binadamu, Hedhi Salama, Afya ya Uzazi na Athari za Afya na Mazingira.

    Makundi mengine ni Biashara na Fedha, Utamaduni na Michezo, Kilimo na Biashara ya Kilimo, Utalii na Uhifadhi, Elimu, Uandishi wa

    Habari za Uchunguzi, Uandishi wa Habari za Data, Utawala Bora, Mpiga Picha Bora , Mpiga Video Bora, Mchora Vibonzo Bora, Uandishi wa Jinsia, , Mafuta, Gesi na Usimamizi wa Madini, Usalama wa Barabara na kundi la wazi. Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindanisha ilikuwa Januari 31, 2020.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT, Kajubi Mukajanga alisema wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo kwa mwaka 2019, kuwa Tuzo hizo zimewainua wanahabari kutoka vyombo vikubwa na hata vidogo vya kijamii. Mashindano ya mwaka huu ni ya 11 ambapo washirika wanayoyasimamia ni Baraza la Habari Tanzania, Wakfu wa Habari (TMF) Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), HakiElimu, AMREF, SIKIKA, Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

    Shughuli za kufanikisha mashindano hayo zilipungua kwa kiasi kutokana na kuibuka mlipuko wa baa la Covid-19.

    7

    Habari

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Tuzo za EJAT kutolewa Septemba 5

    Washindi wa Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari (EJAT) 2018 wakionyesha tuzo walizotunukiwa.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    8

    Fursa

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Entries Open for 2020 Media Monitoring Africa lsuElihle Awards

    The Media Monitoring Africa (MMA) invites journalists within the African continent to apply for the lsuElihle Awards.

    MMA’s awards seek to give children a voice and highlight the status of children in the continent. Journalists are encouraged to submit their story ideas and these can be targeted at any mainstream news medium such as TV, Radio or Online.The top six story ideas will then be selected during an awards ceremony which will be held in September.

    Award InformationJournalists behind these ideas will each receive guaranteed financial support of ZAR 10 000. MMA will also offer support to the finalists to develop their concepts.The final stories will be ranked and the final cash prizes will be awarded as follows:• ZAR 25 000 (Overall Winner);• ZAR 15 000 (2nd place);• ZAR 10 000 (Third Place).

    The media can play an important role in protecting and promoting children’s rights and, in many instances, in exposing their abuses and triumphs. This is informed by the belief that children are not a homogenous group and deserve protection of their rights in all stages of their lives from early childhood development right up until they are legally considered to be adults. The IsuElihle Awards therefore aim to encourage alternative think-ing around reporting on children, and to contribute to an environment that enables journalists to expose and highlight issues affecting children in the country and the continent.

    For more information, visithttp://isuelihle.org.za/mma-opens-entries-for-the-isu-elihle-awards-2020/

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    9

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Habari

    Na Mwandishi wa Barazani

    Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha rufaa Juni 9, 2020 itatoa hukumu juu ya shauri la kuondoa hati ya rufaa dhidi ya Serikali ya Tanzania katika kesi ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari 2016.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mahakama hiyo kukubaliana na maelezo yaliyotolewa na pande zote mbili katika kesi hiyo.

    Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) walifungua kesi namba 2/2017 kupinga vipengele vya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambavyo vinakiuka baadhi ya vipengele vya mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

    na kukinzana na misingi ya utawala bora, demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu.

    Mahakama hiyo ilitoa hukumu juu ya kesi hiyo Machi 28, 2019 na kuiangusha Serikali. Hata hivyo, Serikali haikukubaliana na hukumu hiyo ambapo iliwasilisha hati ya maombi ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo Aprili 11, 2019.

    Akizungumza baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo iliyofanyika kwa njia ya video ya mtandao (teleconference), Wakili Fulgence Massawe ambaye ni mmoja wa mawakili wanaowawakilisha MCT, LHRC na THRDC alisema kwamba hata baada ya kuwasilisha hati yao ya kukata rufaa Serikali, mpaka kufikia mwezi Disemba 2019, ilikua bado haijakata rufaa hiyo.

    “Sasa kulingana na kanuni za Mahakama ndani ya siku 30 baada ya kuwasilisha hati ya kutaka kukata rufaa unatakiwa uwe

    umeshakata rufaa hiyo, lakini mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka 2019 ambapo tulipeleka maomba namba 5/2019 juu ya hati hiyo serikali ilikua bado haijakata rufaa.

    “Na sisi kila tulivyokua tunafuatilia utekelezaji wa hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo Machi 28, 2019 serikali imekua ikituambia kuwa kuna hati ya rufaa,” alisema Wakili Massawe akiongeza kuwa hati hiyo imekua kikwazo katika utekelezaji wa hukumu hiyo.

    Wakili Massawe aliongeza kuwa “kwa hiyo leo Mahakama ilikua inatusikiliza kuhusiana na maombi hayo na imekubaliana na maelezo ya pande zote mbili na hivyo imetaja kwamba ifikapo Juni 9, 2020 itatoa hukumu sasa juu ya maombi yetu”.

    Katika kesi ya msingi ambayo

    EACJ kuamua kuhusu notisi ya rufani ya serikali Juni 9

    Wadau wa habari na mawakili wao wakifuatilia kesi ya kupinga notisi ya rufaa ya serikali dhidi ya ushindi wa wadau katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

    Endelea Ukurasa wa 10

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    10

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Baraza pamoja na wadau wenzake waliyoifungua mwaka 2017, waliishtaki Serikali kwa kutunga Sheria ya Huduma za Vyombo Vya Habari ya mwaka 2016 na kupinga vifungu mbali mbali vya sheria, ambapo katika hukumu yake Mahakama hiyo iliiangusha Serikali na ilivitaja vifungu vya 7 (3) (a) (b) (c) (f) (g) (h) (i) na (j), 13, 19, 20, 21, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 50, 54, 52, 53, 58, na 59 vya sheria hiyo kuwa vinakinzana na misingi ya utawala

    bora, demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu.

    Mahakama hiyo ya EAC ilisema vifungu vya sheria hiyo vinaenda kinyume na vifungu vya 6(d), 7(2) na 8 (1) (c) vya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu kupitishwa

    kwake mwaka 2016, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari imekwishatumika kufungia magazeti matano kwa nyakati tofauti; Mawio (miaka miwili), Tanzania Daima (miezi mitatu), RaiaMwema (miezi mitatu), Mwanahalisi (miaka miwili) na The Citizen (siku saba).

    linavikumba vyombo vidogo , huru vya habari”, Trionfi ameongeza.

    “Katika nchi nyingi ambapo vyombo hivi ndiyo njia pekee ya habari huru, hali ya uchumi itakuwa mbaya zaidi kutokana na kubanwa na serikali na kuvifanya kushindwa kutimiza majukumu ya kihabari .

    Mauaji wa wanahabari yanaendelea

    Ingawa dunia kwa sasa inaangalia janga la corona, katika kipindi cha miezi 12 iliyopita umedhihirisha ni mwaka wa hatari kwa wanahabari, kulingana na taarifa ya IPI.

    Tangu Mei 2019, waandishi 53 wameuawa kutokana na kufanya kazi zao. 32 kati ya waandishi hao waliouawa, waliuliwa na vikundi vyenye silaha, maofisa wa usalama na makundi ya wahalifu.

    Amerika Kusini imeendelea kuwa eneo baya kwa wanahabari ambapo

    waandishi 20 wameuawa ambapo 10 kati yao wameuawa Mexico peke yake.

    Katika maeneo ya mapigano wanahabari 14 wameuawa. Kati ya maeneo hayo wanahabari saba wameuawa Syria, watatu Afghanistan,

    Chad na Yemen wakiwa wanaandika habari za migogoro hiyo. Waandishi wawili wameuawa Irak wakiandika habari za machafuko na wengine sita wameuawa wakifuatilia matukio waliyotumwa kuandika habari.

    Inatoka Ukurasa wa 5

    Inatoka Ukurasa wa 9

    Covid-19 yaathiri zaidi uhuru wa habari - IPI

    EACJ kuamua kuhusu notisi ya rufani ya serikali Juni 9

    Wanahabari wakiwa na bango lenye maandishi kuwa Unadhishi wa Habari siyo Uhalifu.

    Mawakili wa wadau wa habari wakifuatilia kesi ya kutaka kutupuliwa mbali notisi ya rufani ya serikali katika Mahakama ya Afrika Mashariki.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    11

    Tanzia

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Na Kajubi Mukajanga

    Saa sita na dakika ishirini na moja mchana wa Jumapili, Mei 10, 2020 nilizungumza na Kagina Karashani kuhusu maendeleo ya matibabu ya baba yake, Fili, na mipango ya kumtembelea hospitali katika mazingira ya homa kali ya mapafu (Covid-19) yaliyofanya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili (MNH) kuamua awe anaonwa na mtu mmoja tu kwa siku!

    Alikuwa amelazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda wa miaka kadhaa. Saa sita baadaye, saa kumi na mbili na dakika ishirini na tatu, nikapokea simu ya Kagina: “Habari ni mbaya. Mzee amefariki.”

    Nilimfahamu Fili Karugahale Karashani kama rafiki mcheshi, rafiki wa kifamilia, mtu wa masihara ambaye katika nyakati za furaha alinihakikishia kuwa ataandika wasifu wangu pindi nitakapofariki. Nilikuwa nikimjibu kuwa mimi ndiye nitakayeandika wa kwake. Na sasa nauandika.

    Nilimfahamu pia kama mwanataaluma mahiri wa uandishi wa habari, na mkufunzi bora. Kabla sijawa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) tulizunguka nchi nzima kufundisha maadili ya uandishi, stadi za uongozi katika klabu za waandishi, mbinu za uandishi wa uchunguzi, uandishi wa habari za

    uchaguzi na uandishi wa makala.Machi 30, 2012, Fili, kama

    anavyojulikana kwa wengi, alikuwa mtu wa kwanza kutunukiwa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari (Lifetime Achievement in Journalism Award) ambayo alikabidhiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Tuzo hizo huandaliwa na MCT na washirika wake, na hutolewa katika kilele cha Tuzo za Umahiri katika Uandishi wa Habari nchini, EJAT.

    Alikuwa mmoja wa wanahabari Watanzania ambao usingeweza kuongelea uandishi wa habari uliotukuka bila kuwataja. Nguli huyu alikuwa katika taaluma hii kwa miongo mitano kama ripota, mwandishi wa makala, mhariri, mkufunzi, mtafiti na

    mtaalamu mshauri wa

    masuala ya habari hapa nchi na ughaibuni. Kwa maneno yake mwenyewe, alijinasibu: “I am a child of the Media” (Mimi ni mtoto wa Tasnia ya Habari).

    Fili alianza maisha ya kazi kama msaidizi wa duka la vitabu mjini Dodoma mnamo mwaka wa 1960, ambapo alijenga tabia ya kujisomea, na baadaye, kuandika. Akahudhuria warsha ya uandishi wa habari huko Kiomboi, mkoani Singida, iliyoandaliwa na Christian African Writing Centre iliyokuwa na makao makuu Kitwe, Zambia, na kumaliza akiwa mwanafunzi bora darasani. Ushindi huo ulimwezesha kupata udhamini wa kusomea Cheti cha Uandishi huko Kitwe, akiwa mmoja wa vijana 30 waliokusanywa kutoka kusini, mashariki na magharibi mwa Afrika. Baada ya kupata cheti chake akaajiriwa kama ripota katika magazeti ya Target na Lengo, ambayo yalikuwa ndiyo kwanza yameanzishwa kwa ushirikiano kati ya mabaraza ya Kikristo ya Kenya na Tanzania.

    Miaka miwili baadaye mwajiri wake akampeleka kusomea Diploma ya Uandishi iliyoandaliwa na taasisi ya kimataifa ya wahariri, International Press Institute. Kwa mara nyingine, Fili akawa wa kwanza katika darasa la wanafunzi 30 toka kusini na mashariki mwa Afrika. Wakati wa sherehe za mahafali, Mhariri wa Taifa Leo, linalochapishwa na Nation Media Group (NMG) ya Kenya akamfuata na kumweleza kuwa angependa kumpa kazi. Fili akakubali. Hiyo ilikuwa mwaka 1964. Miezi mitatu tu baadaye,

    Mbuyu wa Uandishi, Fili Karashani, Umeanguka

    Hayati Fili Karashani.

    Endelea Ukurasa wa 14

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    12

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Fursa

    The National Geographic Society has launched an emergency fund for journalists all over the world who wish to cover Covid-19 within their own communities.This fund will place particular emphasis on delivering news to underserved populations, particularly where there is a dearth of evidence-based information getting to those who need it.The National Geographic Society is interested in local and even hyper-local distribution models. This fund is designed to quickly deliver support so that both individual stories and longer series of content may be created.Beyond reporting on medical and physical health related to Covid-19, they especially encourage reporting that covers social, emotional, economic, and equity issues. Narratives around the Pandemic necessarily include facts and numbers, but ultimately, must also go deeper—telling the stories of inequities that Covid-19 has brought to light.

    Reporting may cover any aspect of the virus and its fallout, including but not limited to:• Social consequences of Covid-19 and

    measures to contain it, particularly related to equity—such as its impact on immigrant communities, domestic violence, and early childhood education.

    • Stories of resilience and solutions that could be applied on a regional or global scale.

    • Novel forms of data visualization or science communication to help communities better understand how to protect themselves.

    • Lessons learned from local response(s) to Covid-19 that could be applied to other large-scale challenges, such as climate change or the refugee crisis.

    • Best practices of how educators, students, and schools are reacting to this crisis, particularly as they illuminate under-resourced schools.

    Priority communities include: Those at high risk or hit especially hard by the virus, indigenous communities, immigrant or refugee communities, underserved, urban, rural, elderly populations, and children.

    Funding InformationThe fund will distribute support ranging from $1,000–8,000 USD for local coverage of the preparation, response, and impact of this global pandemic as seen through evidence-based reporting.

    Eligibility Criteria• The National Geographic Society seeks

    writers, photographers, videographers, audio journalists, cartographers, filmmakers, and data visualization experts to apply for this funding.

    • Applicants must be at least 18 years old at the time they submit an application.

    • Journalists should seek placement of this work within their local media ecosystems and must attribute their support to the National Geographic Society’s Emergency Fund for Journalists.

    • National Geographic Society or National Geographic Partners may also choose to publish some of this work as part of its global coverage.

    • Applicants may use up to 100 percent of their budget as personal reimbursement for their reporting time. National Geographic Society asks that applicants estimate their standard fee for reporting on or creating such content.

    NATIONAL GEOGRAPHIC SOCIETY LAUNCHES COVID-19 EMERGENCY FUND FOR JOURNALISTS

    For more information, visit https://www.nationalgeographic.org/funding-opportunities/grants/what-we-fund/Covid-19-emergency-

    fund/

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    13

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Maoni

    Na Saidi Nguba.

    Unaweza ukawa unamfahamu Fili Karashani akiwa katika chumba cha habari au katika shughuli fulani ya kihabari kuwa ni mtu makini na mwanataaluma thabiti. Lakini huna uhakika wa mzee huyu kijamii na anavyokuwa baada ya kazi jioni na giza linapoingia.

    Alikuwa anafurahia kinywaji chake na kukinywa kikiwa safi na kwa uhakika na kwa njia ya kistaarabu. Huwezi kumkuta amekasirika au akijigamba na huwa ni mtu mzuri wa kuwa naye pamoja. Tulikuwa tunakutana mara kwa mara kwa kinywaji wakati fulani, lakini baadaye tulipokuwa hatufanyi kazi pamoja, tulikuwa hatukutani tena katika namna hiyo na ilikuwa ni mara chache tu. Na afya yake ilipoanza kuterereka, tukawa hatuonani tena. Sasa kwamba ametangulia mbele ya haki Mei 11, 2020, hakuna la zaidi ninaloweza kusema isipokuwa kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Kazini na katika jamii, alikuwa rafiki, kaka na kiongozi mshauri.

    Nilianza kumfahamu Fili akiwa mwandishi mwandamizi wa Daily News miaka ya mwisho ya 1970. Lakini kukutana kwetu Bukoba, mapema mwaka 1980 kulitufanya tuelewane vizuri zaidi. Kukutana kwetu Bukoba wala hakukupangwa, ilikuwa kama ajali. Wakati huo nilikuwa nafanyakazi ya uandishi wa habari katika chumba cha habari Radio Tanzania. Nilikwenda Bukoba katika mkoa wa Kagera kwa ajili ya ziara ya Rais Nyerere katika wilaya ya Ngara, inayopakana na Rwanda.

    Nilifika Bukoba, mji mkuu wa mkoa wa Kagera siku mbili kabla ya ziara ya Mwalimu. Na wakati nazururazurura mjini baada ya kujihakikishia usafiri wa kwenda Ngara, nikaingia katika baa moja. Kwa mshangao mkubwa nikamuona Fili amekaa kwenye kaunta akinywa pombe kali inayoitwa Duncan na chupa nzima ikiwa mbele yake.

    Nikaenda moja kwa moja alipoketi na baada ya kumuuliza kuna kinywaji kingine chohote kinachoweza kupatikana pale badala ya hiyo Duncan. Akanijibu: “huwezi kupata kingine chochote hapa Saidi…ndiyo maana nakunywa kitu hiki nilichokuja nacho…” Nikashiriki na kukaa naye pamoja.

    Hizo zilikuwa nyakati za uhaba mkubwa

    wa karibu kila kitu kutokana na vita ya kumuondoa Idi Amin wa Uganda, tena iliyoanzia mkoa wa Kagera.

    Fili aliniambia kuwa naye amekuja kwa ziara hiyo hiyo ya Rais. Baada ya kufanya mawasiliano mazuri na viongozi wa Bukoba nilifanikiwa kupata nafasi ya usafiri wa gari la mwenyekiti wa UWT wa mkoa ambaye naye alikuwa anakwenda Ngara kwa ajili ya ziara ya Mwalimu. Lilikuwa gari la kizamani aina ya Landrover 109.

    Nilimwambia Fili kuwa kuna nafasi katika gari hilo na kama yuko tayari tuambatane pamoja na akakubali. Mazungumzo yetu katika baa ile yalimalizika jioni ile. Mchana siku iliyofuata tulikuwa ndani ya gari hilo kwa nyuma tukiwa na abiria wengie wawili.

    Pamoja nasi ni pamoja na pipa la mafuta ya petroli ya akiba, gurudumumu la akiba na jeki. Ilikuwa ni safari ngumu kwenye barabara ya changarawe na tulikula vumbi la kutosha kiasi kwamba tuipofika kwenye kituo cha mpakani cha Rusumo, tukiwa njiani kwenda Ngara, tulikuwa hata hatuwezi kutambuana vizuri.

    Hata hivyo tulipata ahueni kidogo tuliofika hapo mpakani. Tukiwa na maofisa wa Uhamiaji wa Tanzania, tulivuka mpaka kuingia upande wa Rwanda kwenye baa moja ndogo kupata kinywaji. Bia ilikuja aina ya Primus, kwenye chupa ndefu na wahudumu wetu wasichana wa Kinyarwanda walikuwa wakipiga magoti wakati wakituhudumia. Nikamkonyeza Fili, ambaye alionekana dhahiri kufurahia takrima ile.

    Hata hivyo safari yetu ilikwenda vizuri. Tulifika salama Ngara na tukalala kwenye darasa la shule ya msingi ambako kulikuwa na matandiko yaliyowekwa kulalia sisi na baadhi ya wageni wengine. Kulipokucha asubuhi nilimuona Fili akiwa uwanjani kweupe akinyoa ndevu zake na kujiandaa kwa kazi siku hiyo.

    Tulianza kwa kwenda kwenye kiwanja cha ndege kidogo cha Ngara, kwa mapokezi ya Mwalimu Nyerere aliyewasili kwa ndege ya Caribou ya jeshi. Tulishiriki kwenye matukio mengi aliyoandaliwa Mwalimu. Alifungua tawi la benki, akatembelea shule ya sekondari ya Kanisa Katoliki Rulenge, miongoni mwa shughuli kadhaa. Tulipata habari nyingi za kupeleka kwenye vyombo vyetu.

    Siku iliyofuata Mwalimu alikwenda Kibondo kuendelea na ziara yake ya mikoa ya magharibi. Ila mimi na Fili iibidi tumalize ziara yetu Ngara kwa vile RTD na

    Daily News walikuwa na timu nyingine za waandishi kwa ajili ya kuandika habari za Kibondo. Kwa hiyo tukapa nafasi ya ndege ya jeshi hadi Mwanza ili tutafute njia nyingine za kurudi Dar es Salaam.

    Pakatokea na tukio jingine ambalo mimi na Fili tuliishi na kulikumbuka kwa muda mrefu. Tulipokuwa tumefunga mikanda tayari kuanza kuruka, tukaambiwa kwamba kuna uchelewesho kwa kuwa kuna zawadi ambayo Mwalimu amepewa inayotakiwa isafirishwe kwenda kijijini kwake Butiama kupitia Mwanza. Alikuwa nguruwe mkubwa. Alifungwa kwenye kasha lakini akiwa anaonekana wazi.

    Katika mfumo huo wa ndege ya jeshi, mzigo huo ulikuwa amepakiwa kwenye sehemu hiyo hiyo wanapokaa abiria. Kwa hiyo nguruwe huyo hapo.

    Akapandishwa na kuwekwa kati kati ndani ya ndege na kuwa amezungukwa na abiria. Ilikuwa safari ya bugudha sana iliyochukua zaidi ya saa moja kwenda Mwanza. Nguruwe huyo alikuwa akinusanusa na kupiga chafya mara kwa mara na kumfanya mhudumu wa ndege hiyo ya jeshi kulalamikalalamika mara kwa mara: “…oh huyu nguruwe, ni bughudha sana…” Usafiri wa ndege, hata kama ni ndege ya jeshi, huwa wa starehe, lakini kusafiri na mnyama kama nguruwe haivumiliki. Tuliendelea kucheka kwa muda mrefu na Fili tukiikumbuka safari hii, lakini ilikuwa ni kioja na ya ajabu.

    Fili pia aliwahi kunishauri kuhusu jambo ambalo sitomsahau katika maisha yangu. Nilipoteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi mwaka 2004, nilimkuta Fili hapo akiwa Mhariri Mshauri. Katika mazungumzo ya kirafiki tu nilimwambia Fili kuwa nataka kuchukua mafao yangu kutoka mfuko wa NSSF baada ya kuwa nimeuchangia kwa miaka kadhaa.

    Alinisihi sana nisifanye hivyo na badala yake niendelee kuchanga na nisubiri michango yangu ikifikia miezi 180 au jumla ya miaka 15 ambapo nitastahili kupata malipo ya pensheni kutoka katika mfuko huo, chini ya mfumo wake wa pensheni unaoweza kunipatia hadi asilimia 70 ya mshahara wa mwisho niliokuwa naupata. Na sasa nikiwa mstaafu, Napata pensheni hiyo, japo ndogo.

    Mwandishi ni mwanahabari na mhariri mkongwe nchini. Simu ya mkononi: 0754-388418. Barua-pepe:

    [email protected]

    FILI KARASHANI mwanahabari mahiri, makini lakini pia mcheshi

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    wahariri wa Daily Nation, gazeti jingine la NMG, “wakamwiba” toka gazeti lao dada. Akaingia chumba cha habari cha gazeti lao la Kiingereza akiwa Mtanzania pekee.

    Tangu hapo, Fili hakuwahi kutazama nyuma.

    Kwa Fili, ukweli na usahihi (truth and accuracy) ndiyo msingi wa uandishi wa habari. Mhariri wake wa habari pale Daily Nation, Mike Chester, alikuwa kati ya watu waliosaidia kumfinyanga Fili kuwa gwiji wa taaluma hiyo. Chester hakuwa na masihara kazini, na kwake, stori ilikuwa haijakamilka bila kujibu maswali “kwa nini” na “kwa jinsi gani”. Kati ya kazi alizofanya wakati huo ni pamoja na kuripoti machafuko ya kijamii, ukame na njaa huko Wajir, mpakani mwa Kenya na Somalia. Baadhi ya stori alizoandika zilimuudhi aliyekuwa Waziri wa Kilimo wa Kenya wakati huo, Jeremiah Nyagah. Lakini ukweli na usahihi ukamwokoa, hakufanywa chochote.

    Aliandika pia matatizo ya wananchi huko Baringo, jimboni kwa Daniel arap Moi, wakati huo akiwa Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani. Mzee Moi hakupendezwa sana na stori za Fili, na akaagiza aletwe kwake. Alipofika, akamtazama Fili kwa mshangao toka chini hadi juu na kumaka, “Oh, huyu ndiye Karachani – nilidhani ni Mhindi! Kwenda!” Awali, lengo lilikuwa kumsweka korokoroni. Ukweli na usahihi vikamwokoa.

    Tom Mboya alipouawa, Fili ndiye aliyeliandikia Daily Nation mkasa huo.

    Mwaka 1967 akahamishiwa Dar es Salaam kwa mwaka mmoja na kuendelea kupeleka Nairobi stori kemkem. Asilimia kubwa ya stori za Tanzania zilizochapishwa ukurasa wa mbele wa Daily Nation wakati huo ziliandikwa na Fili.

    Aliporudi Nairobi, Fili alikwea vidato toka ripota hadi mwandishi mkuu wa habari za Bunge, akawa pia mwanasafu, na baadaye Mhariri-usu/Msanifu Habari (Sub-editor). Alikuwa pia akiandika safu kuhusu masuala ya Tanzania katika gazeti hilo lililoongoza kwa mauzo Afrika Mashariki.

    Baadaye akaacha kazi na kujiunga Chuo Kikuu cha Dar e Salaam na kupata shahada yake ya kwanza mwaka 1978, kisha shahada ya uzamili toka Chuo Kikuu cha Queens, Canada, mwaka 1981.

    Baada ya chuo kikuu Fili akajiunga na gazeti la Daily News kabla ya kuwa

    mkufunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania, TSJ. Akiwa mkufunzi, akawa pia akiandikia majarida na taasisi za nje zikiwamo jarida maarufu la Africa Now na shirika la Inter Press News Agency (IPS). Kwa bahati mbaya, jambo hili lilitafsiriwa na wakubwa wake kuwa ni “kufanya kazi mbili”, japo kwake yeye aliona ni njia ya kuwaonyesha wanafunzi kwa vitendo jinsi uandishi bora ulivyo.

    Alipoona anasakamwa sana, akaacha kazi na mara moja IPS wakamchukua na kumpa kazi Roma, Italia, na baadaye wakampeleka Harare, Zimbabwe, kama Mkuu wa Kituo (Bureau Chief).

    Aliporudi Tanzania 1989 akawa Mhariri mwanzilishi wa Business Times, akiwa na kina Rashid Mbuguni, Narendra Joshi, Ali Chimbyangu na Richard Nyaulawa.

    Mwaka 1991 Fili Karashani aliajiriwa kama Mhariri wa Southern Africa Economist jijini Harare, kabla ya kurudi Dar es Salaam na kuwa Mhariri mwanzilishi wa The Guardian na baadae Sunday Observer.

    Mnamo 2004 hadi 2005 alikuwa The Citizen kama Mhariri wa Mafunzo.

    Katika miaka ya mwisho ya maisha yake, Fili Karashani , ambaye waandishi wengi wamepitia mikononi mwake akiwa mhariri na mwalimu, aliendelea kutoa mafunzo ya uandishi, hususan uandishi wa habari za uchunguzi, makala, na maadili. Alitoa pia huduma

    kama mtaalamu mshauri wa masuala ya habari, huku akichangia katika majarida ya kitaaluma yakiwamo Scribes la MCT na The Global Journalist la Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Missouri, Marekani.

    Vitabu alivyoandika au kushiriki kuandika ni pamoja na: To Write or Not to Write – Ethical Concerns in Journalism; Poverty Reporting – A Manual for Tanzanian Journalists; Media Ethics: Duties and Responsibilities; Feature Writing Manual na Investigative Journalism Practice in Tanzania.

    Fili Karashani alipata kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wanahabari wa Kenya (Kenya Union of Journalists) na katika miaka yake ya mwisho alikuwa mwenyekiti wa Kituo cha Habari, Tanzania Press Centre kabla ya kupatwa na matatizo ya kiafya.

    Fili Karashani alizaliwa Agosti 23, 1938 mjini Dodoma. Baba yake alikuwa Yakobo Kagina, mchungaji wa kanisa la Anglikana, na mama yake aliitwa Blandina.

    Fili na mkewe, Geraldina, walijaaliwa watoto watano: Magezi, Baraka, Kagina, Koku na Bahati. Baraka, aliyechukua kazi ya baba yake ya uanahabari, alishatangulia mbele ya haki. Fili pia ameacha wajukuu wanane.

    Mungu ailaze pema roho ya marehemu Fili Karugahale Karashani—Amina.

    14

    Tanzia

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Mbuyu wa Uandishi, Umeanguka

    Fili Karashani akipokea tuzo na cheti kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kuibuka mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Uandishi wa Habari (LAJA).

    Inatoka Ukurasa wa 11

  • 15

    Muongozo wa kuripoti Covid19

    Toleo la 153, Mei, 2020

    Utangulizi

    Ni jukumu la mwanahabari kutoa taarifa sahihi na kuwa makini katika kuiarifu jamii. Wakati wa kipindi hiki kigumu mitaarafu ya afya ya binadamu ambapo tunapambana na ugonjwa wa Covid-19 (ambao pia unajulikana kama ugonjwa mpya wa homa ya mapafu—novel Coronavirus au “Korona” kwa kifupi) jukumu hili la wanahabari linapata umuhimu mkubwa zaidi. Kirusi cha Covid-19 kimeshatinga Tanzania tayari, kwa mujibu wa uthibitisho uliotangazwa na Wizara ya Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Baraza la Habari Tanzania (MCT), pamoja na mambo mengine, linawajibika kuhakikisha kwamba wanahabari nchini wanazingatia viwango vya juu kabisa vya kitaaluma na kimaadili. Ili kuhakikisha vyombo vya habari nchini vinafanya kazi za kuarifu umma kwa usahihi katika kipindi cha majanga kama hiki tunachopitia sasa, MCT imetayarisha Mwongozo ufuatao kwa ajili ya wanahabari.

    Mwongozo• Pamoja na kwamba hutegemewi kupuuzia uzito wa

    janga lililo mbele yetu kwa sasa, unapaswa kuchangia katika kupunguza hofu na taharuki miongoni mwa jamii.

    • Jitahidi kuelewa mipango na mikakati ambayo inatekelezwa katika juhudi za kupambana na janga la Korona na athari zake kijamii na kiuchumi.

    • Ongea na kuhoji watu wengi iwezekanavyo na wa tabaka mbalimbali. Jaribu kupata mitazamo anuwai ya watu wanaopitia kipindi cha tukio la janga hili ili uweze kupata mrejesho utakaowezesha uongozi wa nchi kuwa na mipango sahihi ya kupambana na janga lililopo.

    • Zingatia kwa makini taratibu za kitaaluma, huku ukihakikisha unatumia vyanzo vya habari vya kuaminika kama vile Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO).

    • Jihadhari na taarifa potofu! Fanya juhudi ya kuthibitisha ukweli wa taarifa ulizopata ili usiwe sehemu ya mtandao wa kuzambaza habari zizizo za kweli.

    • Waheshimu waathirika wa Korona na jali haki yao ya faragha. Punguza mahojiano nao na waathirika wasipigwe picha na majina yao yasitajwe katika habari zinazowahusu, labda pale tu ambapo wangependa kutajwa ili kueleza uzoefu wao ili jamii ijue bayana juu ya kadhia iliyowasibu.

    • Kuripoti janga la Covid-19 kwa njia ya picha kuna umuhimu mkubwa, lakini panatakiwa umakini katika utumiaji wa njia hii ya kuripoti. Wanahabari wanapaswa kuhakikisha picha au vielelezo wanavyotumia katika taarifa zao ni sahihi na vinaakisi hali halisi iliyopo.

    • Jikite katika kuripoti na si kufanya uchambuzi, labda tu pale uchambuzi wako unapokuwa umegezwa katika maoni uliyopata kwa wataalamu.

    • Wahariri wawe makini katika uandishi wa vichwa vya habari. Kutokana na uwepo wa utitiri mkubwa wa taarifa, ikiwa ni pamoja na uharaka wa usambaaji habari kupitia mitandao ya kijamii, watu wengi wanatosheka na kile wanachokiona kwenye vichwa ya habari na kuchukulia kwamba hizo ndizo habari zenyewe.

    • Tumia takwimu na vielelezo kwa umakini na usahihi kulingana na muktadha husika ili kuepusha hofu miongoni mwa jamii.

    • Epuka matumizi ya viashiria vya ubaguzi wa rangi—usihamasishe mitazamo finyu ya kibaguzi au kutoa habari kwa namna ambayo inaweza kusababisha wengine kushadidia ubaguzi.

    • Chunguza kwa makini aina ya tukio ambalo umepanga kuhudhuria, ukizingatia kwamba pana amri ya Serikali inayokataza mikusanyiko ya idadi fulani ya watu.

    • Kuwa mwangalifu, ukijua kwamba pana uwezekano wa wewe kukwamishwa kwenye karantini ndani ya eneo lililozuiliwa kutokana na Korona.

    • Tafakari juu ya athari za kisaikolojia zitakazokutinga pale ambapo utakuwa umelazimika kuripoti ukiwa ndani ya eneo ambalo limeathiriwa na Korona, hasa pale ambapo utakuwa ukiripotia chombo chako cha habari huku ukiwa ndani na kituo cha afya, eneo lililotengwa au eneo lililo chini ya karantini.

    Mwongozo kutoka MCT:Uandishi wa Habari za Janga la Korona

  • 16

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania Muongozo wa kuripoti Covid19

    • Hakikisha umejipanga vizuri kwa ajili ya dharura, ukizingatia kwamba kuna uwezekano wa maeneo fulani, wilaya, mikoa na hata nchi nzima kutengwa kwa njia ya karantini au kufungwa kwa mipaka baada ya kutolewa taarifa ya muda mfupi au bila kutolewa tahadhari yoyote.

    • Epuka kukaa karibu na mtu yeyote mwenye kuonyesha dalili za kuwa na ugonjwa wa njia za hewa, kama vile kikohozi na kupiga chafya. Hakikisha unafunika mdomo na pua unapokohoa au kupiga chafya.

    • Nawa mikono yako mara kwa mara kwa kutumia maji moto na sabuni. Tumia jeli au vifutio vya kuua vijidudu iwapo hakuna maji moto na sabuni, lakini hakikisha kwamba baadaye, unanawa kwa maji moto na sabuni.

    • Usikaribiane sana na mtu unayemhoji iwapo anaonyesha dalili za kuumwa Korona. Umbali unaoshauriwa ni mita moja hadi mbili.

    • Kuwa mwangalifu na aina ya usafiri unaotumia wakati wa kwenda kukusanya habari na kurejea ofisini. Epuka kutumia usafiri wa umma (daladala) nyakati ambazo vyombo hivi vinakuwa vimejaza abiria mpaka pomoni; na hakikisha unatumia jeli yenye viua-vijidudu wakati unashuka kwenye daladala.

    • Tumia maikrofoni ya kushikilia (directional mic) ukiwa umeishika kwa mbali iwezekanavyo, badala ya kutumia maikrofoni inayoshikizwa kwenye mavazi (clip mic).

    • Tumia glavu ukiwa, ama unafanya kazi, unazuru eneo lenye maambukizi ya korona kama vile kwenye kituo, au ukiwa kwenye eneo la kutolea matibabu. Yawezekana pia ukahitaji mavazi ya kujikinga kiafya kama vile suti ya kitabibu (bodysuit) na barakoa inayofunika uso gubigubi (full face mask).

    • Vifaa vya kazi kama vile kamera, vinasa sauti na maikrofoni ambavyo vinatumiwa kwa kushirikiana, ni lazima vifutwe kwa vieuzi (sanitisers) vyenye uwezo wa kuondoa vijidudu kwa haraka kabla na baada ya kutumika, na watumiaji wa vyombo hivi wavae glavu.

    • Kwa muda wote, hakikisha unanawa mikono vizuri ukitumia maji moto na sabuni kabla ya kuingia eneo lililoathirika, uwapo kwenye eneo hilo, na baada ya kuondoka.

    • Iwapo utapatwa na dalili za maambukizo ya virusi vya Korona, hasa homa inayoambatana na shida

    wakati wa kupumua, wahi kumwona daktari. Zingatia kwamba, kama upo ndani ya eneo lililoathirika kwa kiwango kikubwa, unakuwa hatarini kukutana na wagonjwa wa Covid-19 kwenye vituo vya matibabu, na hivyo kuongeza uwezekano wa wewe kuambukizwa.

    • Zingatia miongozo na maelekezo ya wataalamu wa afya wa eneo unaloishi.

    • Shirila la Afya Duniani (WHO) na Wizara ya Afya Tanzania wanakubaliana kwamba si lazima kwa watu wasio na dalili za Korona kuvaa barakoa, labda tu pale utapoamriwa kufanya hivyo na mamlaka ya eneo ulipo, au kama upo katika eneo hatarishi kama vile hospitalini au pale ambapo wewe ni mwangalizi wa mtu ambaye anashukiwa ana maambukizi ya Covid-19.

    • Yawezekana wanahabari ambao wamekuwa wakiripoti kutoka kwenye maeneo yenye maambukizi yaliyoshamiri kutakiwa watengwe na wenzao maofisini, au wakatazwe kuchanganyika na vyanzo vya habari, familia zao au watu wengine, kwa kipindi cha siku 14.

    • Vipindi vinavyohusisha wageni studioni vyapasa kuepukwa. Kama ni lazima kuwa na washiriki ndani ya studio, basi pawe na umbali wa angalao mita moja kati ya mshiriki mmoja na mwingine. Waendesha vipindi sharti wanawe mikono kabla na baada ya kipindi na waepuke kugusa nyuso zao wakati wowote.

    • Vieuzi sharti viwekwe sehemu zote za kuingilia vyumba vya habari, msisitizo ukiwekwa zaidi kwenye milango ya kuingia studio. Waendesha vipindi na wageni wa studio sharti wanawe mikono kabla ya kuingia studioni. Wasaidizi wa vipindi sharti wanawe kwa maji na sabuni kabla na baada ya shughuli nzima ya kurusha kipindi na pale itakapoonekana ni lazima, wavae barakoa na glavu, na

    • Meza za kufanyia uhariri, kompyuta, vichanganyio (mixers) na vifaa vingine vya kazi lazima vifutwe na vitakasa kila baada ya kipindi au shughuli ya uhariri.

    Vipengele hivi vya mwongozo vimetokana na vianzo mbalimbali vya hapa nchini, vya kikanda na vya kimataifa vinavyohusu utendaji bora na salama kwa wanahabari ndani ya mazingira hatarishi.

    Dar es Salaam, Machi 20, 2020

  • 17

    Uchambuzi

    Toleo la 153, Mei, 2020

    By Gervas Moshiro

    Salaam kwa watendaji wa majukwaa yote ya habari kwa kutupatia habari na taarifa za yote yanayopangwa, kusemwa na kutendwa pamoja na hali ilivyo mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya Covid 19, ya kweli na ya kufikirika.

    ‘Kufikirika’ kwa sababu kuna taarifa duniani kote za wanahabari kupotosha ukweli kuhusu chanzo, maambukizo na matibabu, ambayo yanahalalishwa kwa kusingizia kuwa yanatoka vyanzo vya kitaalam. Tumekuwa wahanga wa upya wa maradhi hayo na kujikuta tunaogelea maji tusiyojua kina chake. Namna ya kuenenda kwa usalama ni jambo la kujadiliwa na wanataaluma wote.

    Kwa upande mwingine tuna uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu kipindi ambacho kwa kawaida huhitaji matumizi makubwa ya uweledi na juhudi katika kutafuta na kutoa habari na taarifa. Je, vyombo vya habari vitamudu hayo licha ya kibano kilichopo kutoka kwa watawala na njama za kisheria? Hali hizo za corona na uchaguzi mkuu zimenitafakarisha na kutaka nitoe maoni yangu kwa wanataaluma ili vyombo vya habari viweze kumudu majukumu yake katika nyanja hizo na nyingine kwa ufanisi.

    Mwezi Machi mwaka huu nchi ilitangaza rasmi kuwa maradhi ya Covid 19 yameingia nchini na kutangaza azma ya kuanzisha vita dhidi ya janga hilo.

    Tunasoma katika historia jinsi vita ilivyo na inavyovuruga taifa. Kila aina ya rasilimali na sekta zote – uzalishaji, huduma na utawala zinaelekezwa kuwezesha ushindi dhidi ya mvamizi, wakati huu ikiwa ni dhidi ya Covid 19. Mfano wa karibuni ni iliyokuwa vita dhidi ya Uganda, Oktoba 1978 hadi Aprili 1979 Iddi Amini alipovamia Tanzania. Mkuu wa Majeshi, Mwalimu Julius Nyerere alitangaza vita dhidi ya Uganda. Aliliarifu taifa nia hiyo na kuanza kuhamasisha watu. Wanajeshi pamoja na vikosi vingine, ikiwemo mgambo walihusika mstari wa mbele wa vita. Wananchi waliitikia wito na kujitolea kwa hali na mali kufanikisha mwendelezo wa vita hiyo.

    Mgambo waliandikishwa kutoka wilaya zote na kufanya vita hiyo iwe imepigwa na taifa zima.

    Vyombo vya habari, wakati ule ikiwemo redio, magazeti na filamu, waliunda vikosi maalum vya kutangaza vita ikiwa na kuwa

    mstari wa mbele wa mapigano ili kuhakikisha taarifa zinakuwa za kweli na uhalisia wa mambo. Kwa kuwa wanahabari walihusika mstari wa mbele, haikuweko haja ya kuandika habari za kukisia au kupotosha kwani walikuwa chini ya uangalizi wa kamanda mmoja.

    Wanahabari walioteuliwa kutangaza vita hiyo walikuwa ripota wenye ujuzi mkubwa na wabunifu. Matendo ya ubinadamu na ya kuhuzunisha yalisimuliwa kwa ustadi mkubwa uliovutia wasikilizaji na wasomaji wa magazeti.

    Hii inanikumbusha kuwa kuripoti vita si kazi unayoweza kumpa ripota asiye na ujuzi mkubwa. Inahitaji umahiri wa hali ya juu na uzalendo usio shaka.

    Kuripoti Covid 19 hakuna tofauti na kuripoti wakati wa vita. Ni kwa kiasi gani tunafahamu kuripoti vita? Mara baada ya taifa kuamua kuingia vitani dhidi ya Covid 19, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga aliharakisha kuwatahadharisha wanahabari juu ya umuhimu wa kuzingatia mbinu za kuripoti vita hiyo, lengo likiwa kuhakikisha taarifa za vyombo vya habari zinafuata misingi ya uandishi unaotakiwa wakati wa vita hiyo.

    Kwa kawaida katika hali ya dharura ya Covid 19, maudhui ya kila siku ya vyombo vya habari yangelikuwa yanachambua zaidi changamoto zilizoko kwa kutumia kila aina ya miundo ya mawasiliano kama vile taarifa za habari, ripoti, simulizi halisi, makala, mahojiano, majadiliano, barua, mijadala, hotuba, maoni, matangazo na pia hata kwa kutumia sanaa ya muziki, ngonjera, mashairi na tamthilia, na vyote vikijihusisha na masuala mbalimbali kuhusu Covid 19.

    Hatujawa na maudhui kama yale ninayoona katika vyombo vya kimataifa vya nchi nyingine ambavyo kwa kiwango kikubwa hadi Mei vilikuwa vinachapisha na kutangaza mambo mbalimbali yanayohusiana na Covid 19 tu siku nzima. Si dhambi kwa wanahabari wa nchini wakaiga mtindo huo ili mradi wazingatie hali halisi ya nchi yetu.

    Mwishoni mwa mwezi Mei, mamlaka zilitangaza kuruhusu shughuli za maisha kuendelea kama ilivyokuwa kabla ya Covid 19, ili mradi maelekezo ya tahadhari yaliyotolewa na mamlaka za afya yanazingatiwa kwa ukamilifu. Je, hii ina maana kuwa sasa tutaacha kuwa kwenye tahadhari ya kivita na kurejea mienendo yetu kawaida? Nadhani hapana. Hakuna ajuaye ni lini janga hili litatoka. Yaweza kuwa mwezi, mwaka au hata

    mwongo na zaidi. Kubwa ni kujizatiti kwa maisha yenye taratibu na utamaduni mpya.

    Haya ni maisha yasiyokuwa na baadhi ya mienendo na vitu tulivyozoea. Itabidi tuzoee kuvaa barakoa tuwapo maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kukaa mbali kidogo na wenzetu, hususan si chini ya mita moja, kuosha mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni, kutoshikana mikono, kukumbatiana au kubusiana, kutumia vitakasa na mengine kadri ya maelekezo ya wataalam wa afya.

    Huu ndio utakaokuwa utaratibu wetu wa maisha. Vyombo vya habari vina jukumu kubwa sana katika kufanikisha kuendeleza maisha haya mapya. Matangazo ya mara kwa mara, kukumbushana, taarifa za maendeleo ya maisha haya mapya na habari kuhusu Covid 19 ni maudhui yatakayotakiwa kutawala sana vyombo vya habari nchini ili kuzoea utamaduni huo.

    Japo hali ya Tanzania sio mfano madhubuti wa vita dhidi ya janga la corona kwa sababu Rais wa nchi alikataa kufungia shughuli zisifanyike na watu kujifungia ndani wakati wote au wa baadhi ya saa za siku, kama njia ya kuzuia maambukizi, hii haina maana kuwa wajibu wa vyombo vya habari nao umepungua. Badala yake mkakati huo wa Rais unahitaji vyombo vya habari kuhusika zaidi kwa kuhamasisha wananchi ili wakati wote waelewe na kutekeleza wajibu wao, wakati huo huo vyombo hivyo vikitekeleza majukumu yake ya kawaida.

    Kuongezeka huko kwa majukumu ya vyombo vya habari kunakuwa na changamoto moja kubwa, nayo ni kule kufanya kazi kukiwa na ukiritimba wa vyanzo vya habari kuhusu Covid 19. Data, hadi hii leo bado haipatikani na bila kufahamu ukweli wa hali ilivyo ni muhali kuweza kusaidia wananchi kujielewa ili wachukue hatua stahiki. Uzoefu umetuonesha kuwa kuchapisha data isiyotolewa na mamlaka rasmi ni kutafuta mgogoro na serikali, kama si kujiangamiza. Kuna haja ya vyombo vya habari kujadili kwa uwazi hadharani ili wananchi waelewe vikwazo vinavyozuia utekelezaji wa dhima ya habari.

    Wananchi wanatarajia vyombo vya habari kuripoti kwa uhuru maendeleo ya janga la corona, nje ya hapo inaweza kutafsiriwa kuwa vyombo hivyo vinaungana na serikali kuwadanganya. Kukosekana kuaminika ni kitu cha mwisho ambacho vyombo vya habari vingetaka kitokee. Ni hali ya kutatiza

    Corona na Uchaguzi 2020 ni changamoto kwa wanahabari

    Endelea Ukurasa wa 18

  • Uchambuzi

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    18

    kutokana na msimamo wa serikali kwa vyombo vya habari unaofanya kuwa vigumu vyombo hivyo kuungana na kukutana na serikali kudhihirisha haki na wajibu wake kwa wananchi. Ni kupitia vikao vya pamoja ndipo serikali inapoweza kupata ushirikiano wa dhati bila kulazimisha.

    Tofauti na vyombo vya umma vyenye mapato ya uhakika kuwezesha utafutaji kamilifu wa taarifa za Covid 19, vyombo binafsi vyenye wasomaji, wasikilizaji na watazamaji wengi zaidi vinajikongoja kuishi kutokana na sheria inayoweka ugawaji wa matangazo kwenye uhodhi wa mshindani wao.

    Kama kweli serikali inaamini kuwa mapambano dhidi ya corona ni ya raia na vyombo vyote nchini, haina budi kuviwezesha kuishi ili vitimize wajibu huo. Kanuni inayompa Mkurugenzi Mkuu wa Habari mamlaka ya kugawa matangazo haina budi kurekebishwa ili mgao ufuate vigezo vinavyokubaliwa na vyombo vyote vya habari.

    Asasi za kihabari hazina budi kutumia juhudi za ziada kushinikiza serikali kufanya mapitio ya sheria hiyo. Ikishindikana ni dhahiri baada ya muda mfupi nchi itarudia enzi zile za chama kimoja cha siasa zilizoruhusu uwepo wa vyombo vya habari vya umma tu nchini, kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini. Uhuru kidogo uliopo wa kutoa mawazo utatoweka kwa vile hakutakuwa na vyombo mbadala vya kutolea maoni hayo. Ni njia ya kijanja ya kudhibiti fikra za watu, kitu ambacho hakiendani na muktadha wa demokrasia ya aina yoyote.

    Kuhusu uwekaji wa vyombo vya habari chini ya utawala mmoja, huenda ikawa vigumu kutokana na wingi na uanuwai wa vyombo hivyo, isipokuwa wakati wa vita ambapo hilo hulazimishwa kuwa na hurejea kawaida mara baada ya dharura hiyo.

    Wengine wetu tuna wasi wasi kuwa hali ya dharura iliyotangazwa wakati wa Covid 19 kuhusu udhibiti wa taarifa za ugonjwa huo huenda ikaendelezwa hata baada ya ugonjwa kupita. Ni kama ilikwisha anza na dharura hiyo ni mwendelezo tu.

    Hapa pana mtanziko. Mamlaka zinaruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao lakini wakiwa wanatimiza taratibu za msingi kujikinga. Hii ina maana kuwa dharura imekwisha? Kama ndivyo, utafutaji wa habari nao uwe huru. Waandishi wa habari waweze kunukuu chanzo chochote chenye habari kuhusu ugonjwa huo, ikiwemo vifo vikitokea. Hili nalo lahitaji kufafanuliwa na mamlaka husika.

    Kufanya corona kuwa dharura imezuia jukumu kuu la vyombo vya habari ambalo ni uchambuzi na kutoa maoni ili taarifa zieleweke. Hili nalo ni eneo muhimu linalohitaji ufafanuzi.

    Vyombo vya habari vitakuwa na ufanisi katika Uchaguzi Mkuu?

    Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba ni jukumu jingine ambalo huhitaji werevu, weledi na ubunifu mkubwa wa wanahabari. Kwa kawaida kipindi hiki tayari tungelikwishaona jitihada zimeanza za maandalizi kama vile semina za mafunzo ya kuripoti uchaguzi, maadili yake, nafasi ya vyombo vya kijamii na mengine yanayohusika.

    Huko nyuma, vyombo vya habari vikitegemea sana wafadhili wa ndani na nje katika jitihada za mafunzo. Itakuwa vigumu sasa hivi kujua kama mwaka huu hali itakuaje, lakini kuna kila dalili kuwa huenda mambo yakawa magumu kupata wafadhili. Hata hivyo tunamwachia mungu.

    Inatia shaka sana kwetu sisi wengine tukiangalia mambo hasi yaliyotokea toka uchaguzi mkuu wa 2015. Vyombo vya habari, kama mlinzi mkuu wa wananchi vitakuwa timilifu na fanisi kuwezesha wananchi kufanya uamuzi wa busara wakati wa kuchagua wawakilishi wao? Kutokana na shinikizo mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza siku za karibuni, nahisi nguvu fulani ndani ya mamlaka za utawala zimenuia kufanya vyombo vya habari kuwa sehemu ya utawala kama ilivyokuwa kabla ya uhuria wa habari.

    Pigo la kwanza kubwa kwa wananchi na vyombo vya habari lilikuwa wakati Bunge lilipokataza matangazo mbashara ya vikao vyake mwanzoni 2016. Hii ilikuwa inawezesha wananchi kufuatilia wawakilishi wao na michango yao bungeni, kitu kilichokuwa kinawezesha kujua ufaaji wao katika kutetea maslahi yao. Kutokana na tathmini wananchi waliweza kujua nani wa kuchagua wakati wa uchaguzi.

    Katika miaka michache tumeona wanahabari wakistakiwa mahakamani, kutweshwa na hata kutoweka kwa kuandika habari zisozofurahisha baadhi ya watawala. Hii imefanya vyombo vya habari kuogopa na kuacha kufanya uchunguzi wa kuibua ubovu wa watendaji kwenye mamlaka mbalimbali. Matokeo yake ni kwamba wananchi wananyimwa uelewa muhimu wa kusaidia katika kutathimini ufaaji wa wawakilishi na watendaji wake.

    Nyenzo za vyombo vya habari binafsi zimekuwa duni kwa vile matangazo, ambayo ni tegemeo kubwa la mapato, yamehodhiwa na chombo cha serikali, na kugawiwa kwa kinachodaiwa kuwa ni wale wasiokosoa serikali. Itakua vigumu sana kwa vyombo huru vya habari kuweza kuandika na kutangaza uchaguzi unaohitaji kusafiri kwingi, vifaa na kujikimu kwa watendaji wake wakati wa kampeni. La sivyo itabidi wategemee taarifa kutoka kwa vitengo vya habari vya wahusika ambazo huwa za upande mmoja na hukosa uchambuzi.

    Ujumbe wa kampeni mwingi mwaka huu utatolewa kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni na vile vya kiserikali. Vyombo hivyo vina mwelekeo wa upendeleo na haviwezi kumfanya mwananchi akafanya uamuzi huru kutokana na elimu atakayopata, uamuzi ambao kwa kawaida hufanywa mtu akishapata maelezo ya pande mbili za jambo. Uchambuzi wa wagombea wawezekana tu kwa kutumia vyombo vya habari vyenye nyenzo na utaalam huo. Wagombea wengine watatumia uwezo wao kuzuia wasichambuliwe kwani huenda maovu yao yakawekwa hadharani. Hutumia njia za kutishia, kudhuru, kuhonga na hata kutokomeza.

    Wazo la kwamba wanahabari wanaweza kudhurika kwa kufanya uchambuzi wa mwenendo wa mtu, huzuia dhamira na nia ya kumchambua mgombeaji, hasa kama mtu huyo ana uwezo wa mali au tabia za kibabe. Ni uamuzi mgumu kufanya. Kushindwa kufanya uchambuzi wa wagombea ni kitu ambacho wahanabari itabidi waishi nacho, jambo ambalo ni kasoro kubwa katika kutimiza dhima yao kwa jamii.

    Hali zilizoelezwa hapo juu zitakabili vyombo vya habari wakati wa uchaguzi ujao miezi michache ijayo. Kushindwa kuchunguza hali kwa niaba ya jamii ni pigo kubwa kwa vyombo vya habari, kwani ni kupoteza uhalali wa kuwepo.

    Kwamba vyombo vya habari ni taasisi za huduma ya jamii halidhaminiwi na watawala. Wakati umefika wa kuweka wazi ukweli huu na wa kufanya kazi hii ni wanahabari wenyewe. Itabidi kuungana au kutumia asasi zilizopo – za kikazi au kitaaluma kuendeleza ajenda hiyo. Utafika wakati vyombo vya habari vitasema HAPANA kwa baadhi ya vitendo inavyofanyiwa na watawala. Huduma ya jamii hutolewa na vyombo vilivyo huru kitaaluma kwa kutumia vigezo vilivyowekwa na taaluma yenyewe kupitia watoa huduma walioidhinishwa na jamii.

    Watawala wanakosea kuchanganya uandishi wa habari kama taaluma, na habari kama mawasiliano ya kuwezesha taasisi kukubalika na kupendwa na jamii au wadau. Vyombo vya aina hiyo haviwajibiki kwa jamii bali kwa taasisi – ikiwemo serikali. Vinasaidia taasisi kutimiza azma au ahadi yake kwa jamii, ndiyo maana kuna tofauti kati ya vyombo vilivyoundwa kutekeleza mawasiliano ya kitaasisi na vyombo huru vya habari, au kati ya waandishi wa habari na maafisa mawasiliano (uhusiano).

    Wakati umefika wa kupigania taaluma ya uandishi wa habari nchini. Inaanza kwa majadiliano kati ya wanataaluma wa habari wenyewe kujitambua na kujua namna ya kusonga mbele.

    Covid 19 bado iko. Inaua. Tuwe na tahadhari.

    Corona na Uchaguzi 2020 ni changamotoInatoka Ukurasa wa 17

  • Habari

    Toleo la 153, Mei, 2020

    19

    Na Mwandishi wa Barazani

    Wadau wa habari wametakiwa kufungua kesi za kimkakati kwa ajili ya kutetea maslahi ya umma katika mahakama mbalimbali nchini, ili kuleta mabadiliko ya kisheria.

    Mwito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga na Mratibu wa Kitaifa wa Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Onesmo Olengurumwa. Viongozi hao ambao wako mstariwa mbele katika kupigania uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza wametoa mwito huo katika taarifa ya pamoja waliyoitoa kabla kusikilizwa ombi la taasisi zao kupinga notisi ya serikali kukata rufani dhidi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Afrika Mashariki Machi 28, 2019 kuhusu sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari.

    Mahakama hiyo katika hukumu yake ilisema vifungu vingi vya sheria hiyo vimekiuka haki za msingi za demokrasia na makubaliano ya Jumuia ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

    Kwa sababu ya vikwazo vya kiutendaji vilivyosababishwa na janga la Covid-19 nchini Tanzania na duniani kote, Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) iliendesha shauri hilo mubashara kwa

    njia ya mtandao Mei 21, 2020Katika tamko hilo la pamoja taasisi hizo pia zimeeleza:- • Kwa pamoja tunatoa wito kwa wadau

    wote wa habari, wadau wote wa Asasi za Kiraia na umma kwa ujumla, kufuatilia kesi hii kwa ukaribu siku ya kesho tarehe 21 Mei 2020 na pia hukumu yake ifikapo tarehe 9 Juni 2020.

    • Tunaviomba vyombo vyote vya habari kuungana pamoja kuihimiza Serikali ya Tanzania irekebishe sheria kandamizi zinazominya uhuru wa vyombo vya habari nchini.

    • Tunatoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania irekebishe vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari, 2016 vinavyopingwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki ili kulinda uhuru wa kujieleza kama ilivyoanishwa kwenye Katiba. Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge

    Novemba 5, 2016 na kuidhinisha rasmi na Rais John Pombe Magufuli Novemba 16 imepingwa na wadau waliofungua kesi kutokana na kuwa na vifungu na mambo kadhaa yalisiyokubalika yakiwemo :-1) Kuwepo kwa vifungu vipya kwenye

    sheria ambavyo havikuwepo awali katika mchakato wa uundwaji wa Muswada wa Huduma za Habari wa 2015. Kwa mfano, kuongezwa kwa kifungu cha 7 cha Sheria ya Huduma za Habari, kinachoeleza juu ya haki

    na wajibu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari na haswa kifungu cha 58 kinachompa Waziri wa Habari mamlaka ya kuzuia usambazwaji wa habari yeyote anayodhani inaweza kuhatarisha usalama wa taifa au umma.

    2) Katika kipindi chote cha utungwaji wa Muswada wa Huduma za Habari wa mwaka 2015, wadau wa vyombo vya habari nchini Tanzania hawakuhusishwa na hivyo hawakuweza kutoa mapendekezo yao kipindi cha utungaji wa Muswada.

    3) Inataka waandishi wote wa habari wawe na leseni.

    4) Inaelekeza kuundwa kwa Baraza la kisheria la Huduma za Habari kusimamia tasnia ya habari badala ya Baraza la Habari Tanzania lililopo.

    5) Imeainisha adhabu kali kwa baadhi ya makosa ya vyombo vya habari.

    6) Imempa Waziri wa Habari mamlaka makubwa ya kusitisha au kufungia vyombo vya habari.

    7) Imefanya makosa ya uchochezi na udhalilishaji kuwa makosa ya jinai.

    Tangu kupitishwa kwake mwaka 2016, Sheria ya Huduma za Habari wadau wameeleza katika tamko la pamoja kuwa imekwishatumika kufungia magazeti matano kwa nyakati tofauti; Mawio (miaka miwili), Tanzania Daima (miezi mitatu), Raia Mwema (miezi mitatu), Mwanahalisi (miaka miwili) na The Citizen (siku saba).

    Wadau wahimizwa kufungua kesi za kimkakati

    Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania(MCT), Kajubi Mukajanga.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Anna Henga.

    Mratibu wa Taifa wa Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa.