darubini ya uchaguzi toleo na. 1

12
Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania Magazeti feki mtandaoni yatikisa tasnia Toleo Na. 1 2015 Vyama vidogo vinapewa nafasi finyu katika vyombo ya habari 6-7

Upload: christopher-stephens

Post on 14-Jul-2016

213 views

Category:

Documents


10 download

DESCRIPTION

Magazeti Feki

TRANSCRIPT

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Magazeti fekimtandaoni yatikisa tasnia

Toleo Na. 1 2015

Vyama vidogo vinapewa nafasifinyu katika vyombo ya habari 6-7

Mbio za kuingia ikulu mwakahuu zimeibua mbinu nyingiza kufanya kampeni na hivi

karibuni nakala za kughushi zamagazeti maarufu zimekuwazikiwekwa kwenye mitandaozenye habari za uongo zenye niaya kumbomoa mgombe wa uraiskupitia Chadema, EdwardLowassa na wanasiasa wenginewa kambi ya upinzani.

Magazeti yaliyoghushiwa nipamoja na Mwananchi, Mtanzania,Nipashe na Rai na yamekuwayakisambazwa kupitia mitandao yakijamia ikiwa ni pamoja na facebook,

whatsApp na blogu mbalimbaliambayo hutumiwa sana na vijanakatika kukidhi haja zao za habari nakupata taarifa.

Kitendo hicho kimeleta mstukomkubwa kwenye tasnia ya habari nawahariri wa magazeti hayoyaliyoghushiwa wameandika taharirikali kulaani kitendo hicho ambachomhariri Nipashe amesema: “Nipashehalikubali uhuni huu, halitatishwa nawahuni hawa.”Katika tahriri yakegazeti la Mtanzania pia lilionyeshakuchukizwa kwa kughushiwa kwagazeti lake na kulaani matumizimabaya ya mtandao. Mhariri huyo

aliitaka Mamlaka ya Uthibiti waMawasiliano (TCRA) kutumia sheriatata ya Makosa ya Mtandaoniiliyopitishwa mapema mwaka huukuwatafuta na kuwapelekawaliofanya vitendo hivyo mbele yamamlaka za sheria.

Magazeti hayo yameghushiwa kwaustadi mkubwa na si rahisi sanakutambua si la kweli na msomajiunaweza ukawaza kwa nini nakalailikupita. Kichwa cha habari cha Raifeki kinasema:

Gwajima: Nina imani na Lowassakwenye kutimiza ndoto zangu

- Asema ni lazima misikiti iweSunday schools ndani ya siku 100Lowassa akiwa Rais

- Azungumzia juu ya nenomabadiliko na kusema hiyo ndiyoitakuwa Tanzania mpya

Gazeti la kughushi la Mwananchilina kichwa cha habari: Uchaguzi2015: Mbatia akamatwa na fuvu lamtoto mchanga kwenye ofisi za NECna lile feki la Nipashe lina kichwa chahabari: Lowassa ashinda kwawaganga wa kienyeji iliyoambatanana picha ambayo pia inaonyesha niya kughushi ikimuonyesha Lowassaamekaa na waganga wa kienyeji.Kitu kimoja ambacho walioghushiwalisahau ni kuwa Nipashewalibadilisha muonekano wa gazetilao na wao walitumia wa zamani.

Ustadi uliotumika katika kughushimagazeti hayo ambayo yanasomwasana na kuyasambaza kwenyemitandao ni wa hali ya juu nahuenda ukapeleka propaganda zauchaguzi katika upeo wa juu zaidi waudanganyifu.

Darubini ya Uchaguzi 20152

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Magazeti feki mtandaoniyatikisa tasnia ya habari

Baraza la Habari Tanzania (MCT)S.L.P 10160, Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255-22-2775728 / 2771947

+255-784-314880 Nukushi:+255-22-2700370Baruapepe: [email protected]: http://www.mct.or.tz

Bodi ya UhaririMwenyekiti: Kajubi MukajangaWajumbe: Pili Mtambalike

John MirenyAlpha NuhuAttilio Tagalile

Wasil iana nasi:

Darubini ya Uchaguzi 2015 3

Baraza la Habari Tanzania

Cha kushtusha zaidi kuhusuhabari feki zilizowekwa kwenyemagazeti hayo feki ni kuwa siomasihara ya kitoto yaliyofanywa navijana hodari wa teknohama. Habarihizo feki ni za hatari sana kama ileinayohusiana na Gwajima kusemakuwa Lowassa atamsaidia kutimizandoto yake ya kubadili misikiti yoteiwe shule za kufundishia ukristoyaani sunday schools.

Ni dhahiri kulikuwa na nia mbayaya kuleta mtafaruku wa kidini navilevile kuonyesha kuwa wapinzanini wadini. Hata zile habari zakugushi za uchawi ziliwekwamahsusi kuwashushia hadhi

viongozi wa upinzani kwa kutoataswira kuwa hawajiamini nawanategemea ushirikina kupatamadaraka.

Kinachobaki sasa ni kwa wenyemamlaka kufanya kilalinalowezekana kuwasaka nakuwachukulia hatua kali za kisheriawale wote walioshiriki katikakuishirikisha tasnia ya habari katikapropaganda zao za kichochezi nakwa kutumia vibaya mitandao yakijamii ili kuzua tafrani wakatiwatanzania wanapojitayarishakwenda kwenye uchaguzi wenyeupinzani mkali kuliko chaguzi zozotezilizopita.

PushObserverkusaidiaMCTufuatiliajiwa vyombovya habari

Baraza la Habari Tanzania(MCT) limeingia mkataba nakampuni ya Push Observer

ili kuongeza ufanisi katikaufuatiliaji wa vyombo vya habarikatika kuandika habari zauchaguzi.

Push Observer ambayo nikampuni yenye lengo la kufuatiliamienendo ya vyombo vya habarikatika nyanja tofauti tofauti,yakiwemo matangazo yanayorushwakwenye vyombo vya habari.

MCT imeanza kuvifuatilia vyombovya habari kwa kutumia utaalamuwa mitambo kutoka kampuni hiyolakini wakati huo huo ikiwatumiawataalamu wa habari kufanyatathmini za kitaaluma kulinganamwongozo wa maadili ya uandishiwa habari.

Vyombo vinavyofuatiliwa nipamoja na TBC1, ITV, Channel 10,Star TV, Azam TV, Radio one, RedioFree Africa, Clouds FM na TBC taifa.

Vingine ni magazeti ya ZanzibarLeo, Daily News, The Guardian, TheCitizen, Habari Leo, Nipashe,Mwananchi, Uhuru, Tanzania Daima,Mtanzania, Rai Tanzania, Jambo Leo,na Majira.

Kufuatia Baraza kuingia mkatabana Push Observer, limetoa ripoti zamwenendo wa vyombo vya habaritano na imekuwa ikizichapishakatika tovuti ya Baraza la HabariTanzania (MCT) na vilevilekuzisambaza kwa wadau mbalimbali.

Baraza linatarajia kuendeleakuvifuatilia vyombo vya habari hasajinsi vinavyoripoti habari zauchaguzi mpaka itakapofika Disembaya mwaka huu.

Magazeti yanayomilikiwa naserikali ya Daily News naHabari Leo yameonyesha

mwelekeo chanya kitaalumakatika kuandika habari zauchaguzi mwaka huu.

Tathmini hii ni kwa mujibu waRipoti ya Ufuatiliaji wa Habari zaUchaguzi ya Septemba 1 hadi 10iliyotolewa na Baraza la HabariTanzania.

Ripoti hiyo inaonyesha kwambamagazeti hayo mawili yaliandikahabari za uchaguzi kwa usahihi lichaya kutoa nafasi zaidi kwa wagombeawa Chama Cha Mapinduzi hukuyakiacha habari za vyama vyaupinzani.

Habari zinaonyesha kwambahabari za magazeti hayo amazilipewa nafasi katika ukurasa wakwanza au wa pili.

Ripoti hiyo inaonyesha kwambahabari za vyama vya upinzanizilipewa nafasi ukurasa wa kwanzazikiwa tu zina ujumbe wenyemaudhui hasi.

Mfano halisi wa taarifa za namnahiyo ni taarifa ya Daily News yaSeptemba 2 liliyokuwa na kichwacha habari: "Slaa amshutumuLowassa".

Gazeti la Jambo Leo pialilijidhihirisha bayana kuwapendeleawagombea wa CCM, hasa palelilipokuwa na vyanzo vya habari 43ikilinganishwa na vyanzo 14 vya vyawagombea wa Umoja wa Katiba yaWananchi (Ukawa) – vyama vya CUF,NCCR-Mageuzi na National Leaguefor Democracy (NLD).

Gazeti ya Uhuru, ambalolinamilikiwa na cha Chama ChaMapinduzi, na magazeti ya TanzaniaDaima na gazeti la Mtanzania kwakiwango kikubwa yaliyonyeshaupendeleo wa hali ya juu kwakuwaponda wapinzani wawagombea wa vyama vyao.

Hata kama haijulikani waziwazi,

magazeti ya Tanzania Daima naMtanzania yote yako chini ya milkiya kambi ya Umoja wa Katiba yaWananchi UKAWA).

Kwa mfano, gazeti la TanzaniaDaima la Septemba 6 lilikuwa nataarifa yenye kichwa cha habari: NECyaionya CCM. Habari hiyoilipotoshwa kwa sababu Tume yaTaifa ya Uchaguzi ilivionya vyamavyote vyenye wagombea katikaUchaguzi Mkuu kuheshimu muda wakufanya kampeni.

Kwa kuionyeshea kidole CCMpekee, gazeti hilo kitaaluma lilikiukamisingi ya usawa katika kuandikahabari zisizokuwa na upendeleo.

Nalo gazeti la Uhuru la Septemba 1

lilibeba kichwa cha habari: Nchihaiwezi kukabidhiwa wapiga dililikijenga taswira kwamba wagombeawa Chadema hawafai kuchaguliwakwa sababu watauza nchi.

Vichwa hivyo vya habarivilivyotajwa hapo juu vinaonyeshamfano halisi wa taarifa za uchochezikwa sababu mambo madogoyamekuzwa kupita kiasi badala yakutilia mkazo masuala ya msingiyaliyoelezwa na wagombea katikamikutano ya kampeni.

Kwa mujibu wa Ripoti yaUfuatiliaji, nyingi ya taarifazilizochunguzwa zilikuwa na chanzokimoja cha habari. Wananchiwaliohudhuria kampeni hizo

Darubini ya Uchaguzi 20154

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Daily News, Habari Leoyaonyesha mwelekeo chanya

kuhusu habari za uchaguzi

Darubini ya Uchaguzi 2015 5

hawakupewa nafasi angalau tu yakueleza kile walichokisikia kutokakwa wagombea walipokuwamajukwaani.

Magazeti ya Nipashe, Mwananchina The Citizen, kwa mujibu wa Ripotiya Ufuatiliaji wa Habari za Uchaguzi,yaliyoonyesha weledi wa hali juu wakitaaluma kwa kutoa nafasi sawakwa wagombea urais wa CCM naUKAWA.

Kwa mfano, Nipashe la Septemba7 lilionyesha mfano mzuri kwakuzingatia misingi ya kitaaluma palelilipoandika taarifa zenye vichwa vyahabari: Lowassa atikisa, kuteka Darleo na Moro gharika JK mshangao.Habari hizo zilikuwa zikiwahusuwagombea Edward Lowassa waChadema na Dk John Magufuli waCCM.

Jambo moja lililo dhahiri, kwamujibu wa taarifa za uchunguzi, nikwamba magazeti hayo matatu –Nipashe, Mwananchi na The Citizen –yaliandika habari chache zinazohusuwagombea wa urais wa vyamavingine kana kwamba Uchaguzi

Mkuu unahusu wagombea wa CCMna UKAWA tu.

Chama Cha Mapinduzi, ambachokwa asili kina mtandao mpana wamatawi nchi nzima, ndichokilichopewa nafasi kubwa namagazeti, nyingi ya habari zake(asilimia 65) zikitoka mkoa wa Dares Salaam.

Taarifa zinabainisha kwambakatika kipindi cha wiki moja yakufuatilia habari za uchaguzi, taarifanyingi ziliandikwa kuhusuwagombea urais wakati wagombeaubunge na udiwani walipewa nafasindogo au kutupwa kando.

Kwa kuzingatia miiko na misingiya uandishi habari, Radio Free Africailionyesha upendeleo wa wazi kwamgombea urais wa Chama ChaMapinduzi kuliko wapinzani wake,hasa mgombea wa Chadema.

Mfano halisi ni ule wa Septemba 1,ambapo taarifa ya dakika mbiliiliyosomwa katika redio hiyoilimshambulia mgombea waChadema Edward Lowassa kwakumwonyesha kwamba ni mlarushwa wa kupindukia.

Shambulizi hilo lilitoka kwaaliyekuwa Katibu Mkuu wa ChademaDk Wilbroad Slaa wakati wamkutano wake na waandishi wahabari mjini Dar es Salaam.

Zaidi ya hayo, Slaa alipewa nafasikwenye taarifa ya habari pamoja na

dakika tano zaidi baada ya taarifahizo katika kipindi cha Darubini yaLeo. Kulikuwa na chanzo kimoja tucha habari na kwa bahati mbaya mtualiyeshutumiwa hakupewa nafasi yakujibu.

Katika kipindi cha uchunguzi chaSeptemba 1 hadi 10, TBC Taifa ilitoanafasi sawa kwa wagombea wote wavyama vya siasa kwa kuzingatiamgombea mwenyewe na masualaanayoyazungumzia.

Wakati vyama vinane vinawagombea urais kwenye UchaguziMkuu, ni wagombea wawili tuwenye nguvu na mvuto wa CCM naCHADEMA ndio wanaopewa nafasikubwa huku wagombea ubunge naudiwani wakisahauliwa kabisa.

Kituo cha televisheni cha ITVkilitoa nafasi kubwa kwa mgombeawa UKAWA (CHADEMA). Kituohicho kilitangaza taarifa 18ikilinganishwa na taarifa 12 yataarifa zote zinazohusu uchaguzi.Vyama vya NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo vilipewa asilimia 8 yataarifa zote.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Ripotiya Ufuatialiaji wa Habari za Uchaguziya Septemba 1 hadi 10, hii hainamaana kwamba ITV ilifanyaupendeleo. Ukweli ni kwambaUKAWA-CHADEMA ilikuwa navuguvugu ya kampeni nyingi katikakipindi hicho.

Baraza la Habari Tanzania

Darubini ya Uchaguzi 20156

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Vyombo vya habari -magazeti, televisheni naredio – kwa ujumla

vimejitahidi kuandika habari zaUchaguzi Mkuu tangukuzinduliwa kwa kampenimwishoni mwa mwezi Agostimwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti za kilawiki za ufuatiliaji wa habari zauchaguzi zilizotolewa na Baraza laHabari Tanzania (MCT), vyamavinavyopewa nafasi kubwa zaidikatika vyombo hivyo ni chamatawala, CCM, Chama chaDemokrasia na Maendeleo na

Chama cha Wananchi (CUF)ambavyo katika chaguzi zilizopitavimekuwa vikishindana vikalikuchukua uongozi wa nchi.

Habari za vyama vingine vyenyewagombea wa urais, ubunge naudiwani katika Uchaguzi Mkuumwaka huu kama vile ACT-Wazalendo, Tanzania Labour Party,United People's Democratic Party(UPDP), Chama cha Ukombozi waUmma (CHAUMMA), NationalReconstruction Alliance (NRA) naAlliance for Democratic Change(ADC) zinapewa nafasi ndogokatika magazeti, redio natelevisheni.

Chini ya Mradi wa Ufuatiliaji waHabari za Uchaguzi unaoendeshwana Baraza la Habari Tanzania,magazeti yaliyochaguliwa kwauchunguzi ni Zanzibar Leo, DailyNews, The Guardian, The Citizen,habariLeo, Nipashe, Mwananchi,Tanzania Daima, Mtanzania, RaiaTanzania, Jambo Leo na Majira.Vituo vya televishenivilivyochaguliwa kwa uchunguzi niStar TV, TBC1 na ITV wakati vituovya redio ni Radio One, TBC Taifa,Clouds FM na Radio Free Africa.

Kwa upande wa Star TV, ITV,TBC1, Radio Free Africa na RadioOne vipindi vilivyofanyiwa

Vyama vidogo v finyu katika vyo

Darubini ya Uchaguzi 2015 7

Baraza la Habari Tanzania

uchunguzi ni taarifa za habari zasaa mbili usiku wakati kwa redio yataifa, TBC Taifa, ni taarifa za saasaba mchana.

Kwa upande wa Zanzibar, habarizilizochunguzwa ni za magazetiyaliyotajwa hapo juu pamoja na zileza ZBC TV, Radio Zenj FM na HitsFM.

Taarifa za ZBC TV za ZBC TV naZBC Radio ni za saa mbili na robousiku na saa tatu usiku. Kwaupande wa Hits FM uchunguziulifanywa kwa taarifa zake za saatatu usiku wakati kwa upande waZenj FM taarifa zilizofuatiliwa ni zasaa tisa alasiri.

Mambo mengine muhimuyanayochunguzwa kuhusuuandishi wa habari za uchaguzi nimasuala ya katiba, tatizo rushwa nausawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Ripoti yaUfuatiliaji wa Habari za Uchaguziya Septemba 1 hadi 10, magazetimachache yalionyeshakutopendelea upande wowote kwakutenga nafasi sawa kwa vyamavikubwa vya siasa.

Hata hivyo, kwa mujibu waRipoti hiyo, magazeti hayohayakuandika habari za vyamavingine zaidi ya CCM na vyamavilivyo chini ya mwavuli wa Umoja

wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),yaani Chadema, NCCR-Mageuzi,National League for Democracy naCivic United Front (CUF).

Ripoti ya Ufuatiliaji Habari zaUchaguzi ya Septemba 11 hadi 17kwa mfano, inaonyesha kwambajumla ya taarifa 332 ziliandikwa namagazeti ya Mwananchi, TanzaniaDaima, Jambo Leo na The Citizenambazo zilitoa nafasi kubwa kwavyama vya CCM na Chadema.

Vyama hivyo viwili ndivyovyenye upinzani mkubwa katikaUchaguzi Mkuu wa mwaka huuunawajumuisha wagombeawanane wa urais.

vinapewa nafasi ombo ya habari

Chifu Lutasola Yemba(aDC)

Hashim Rugwe(CHaUMMa)

Macmillan Lyimo(TLP)

Fahmi Dovutwa(UPDP)

Darubini ya Uchaguzi 20158

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Habari za uchochezizinazokiuka maadili yauandishi wa habari

zilijitokeza bayana kwenyemagazeti ya Raia Tanzania naUhuru ya Septemba 11 na 14wakati yalipotoa tuhuma nzitokwamba kuna kikosi cha vurugukinachoandaliwa kwa ajili yakuvuruga Uchaguzi Mkuu Oktoba25.

Gazeti la Raia Tanzania laSeptemba 11 lilichapisha taarifayenye kichwa: Kikosi cha vuruguOktoba 25 mafunzoni wakati gazetila Uhuru la Septemba 14 lilichapishataarifa yenye kichwa: Chademawaingiza msituni vijana 3,000.

Magazeti hayo mawili yalidai

kwamba Chama cha Demokrasia naMaendeleo kinatoa mafunzo kwavijana 3,000 kwa ajili yakusababisha vurugu wakati wauchaguzi.

Taarifa hiyo haikuwa na ukwelithabiti wa kuthibitisha madai hayoyanayogusa usalama wa taifa.

Kitu kibaya zaidi kitaaluma, gazetila Raia Tanzania lilikariri chanzoambacho halikuweza kukitajawakati gazeti la Uhuru lilidaikwamba lilipata habari hizo kutokakwa watu waliohama Chadema nakujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Madai hayo nyeti yalipaswakufanyiwa uchunguzi wa hali juu.Viongozi wa ngazi za juu waCHADEMA, vyombo vya usalama nawatu ambao mafunzo hayo yalikuwa

yakifanyika wangepaswa kuhojiwa.Kwa mantiki hiyo, taarifa hiyo

isingeweza kuchapisha bila yauchunguzi thabiti kufanyika.

Kitu kibaya zaidi, taarifa hiyo yapropaganda ingeweza kuharibuuhusiano wa kidiplomasia kati yaTanzania na nchi ambayo ilidaiwakwamba iliyabariki mafunzo hayokufanyika kwenye ardhi yake.

Isitoshe, hakuna hatua zozotezilizochukuliwa na vyombo vyausalama kuthibitisha ukweli wataarifa hiyo, ambayo kitaalumahaikuwa na vyanzo vya kuaminikavya habari.

Taarifa hiyo ni ushahidi wakutosha wa kukiukwa kwa miiko yauandishi wa habari ambayoinakataza habari za uchochezi.

Kama kuna chombo chahabari ambacho vyama vyaupinzani hususan Chadema

haitakisahau katika uchaguzi wamwaka huu ni Star TV ambachokilichukua jukumu lakuwashambulia katika taarifazake mbalimbali na matangazo.

Tangu kuanza kwa kampeni zauchaguzi Agosti 22, 2015, televishenihiyo hiyo ilianza mashambulizi dhidiya mgombe wa kiti cha urais kupitiaCHADEMA, Edward Lowassa, katikataarifa zake mbalimbali. Kituo hicho

pia kilirusha matangazo kadhaaambayo yalikuwa yakimshutumu nakumuelezea Lowassa kuwa ni fisadi,mwenye uchu wa madaraka naanatumia dini ili kutafuta urais.Matangazo hayo ya kisiasa piayalidai kuwa hizo ‘dhambi tatu’ zaLowassa’s ni tishio kwa umoja naamani ya taifa.

Hata hivyo mgombe wa urais waChama cha Mapinduzi (CCM), JohnPombe Magufuli na mgombeamwenza wake, Ms Samia Suluhu,walipewa nafasi kubwa na chanya

katika taarifa za habari na vipindivingine vya TV hiyo.

Vyama vingine vya upinzanivimekuwa vikipewa nafasi ndogo nani hapo tu kama taarifa zao ni zileambazo zinahusu kuishambuliaCHADEMA.

Katika kipindi cha TuongeaAsubuhi kilichoruka Septemba 4,2015, watangazaji waliopo Mwanzana Dar es Salaam walikiongozakipindi hicho kwa kupendelea zaidichama tawala na katikati ya kipinditangazo la kampeni ya CCM

Raia Tanzania, Uhuru yaingiakwenye mtego wa uchochezi

Star TV yatopea kuipigia debe CCM

Inaendelea Ukurasa 12

Darubini ya Uchaguzi 2015 9

Baraza la Habari Tanzania

Wakati Shirika la UtangazajiTanzania, hasa televisheniya taifa, TBC1,

imeonekana kutoa nafasi kubwakwa habari za kampeni za ChamaCha Mapinduzi, televisheni yabinafsi ya ITV imeonekanakufanya vizuri kwa kutoa nafasikwa wagombea na vyama vyote.

Kwa mujibu wa Ripoti yaUfuatiliaji wa Habari za Uchaguzi yaSeptemba 11 hadi 17, kati ya taarifa18 zilizotangazwa na kituo hicho, 14zilikuwa za CCM wakati Chama ChaDemokrasia na Maendeleo(CHADEMA), kilipewa taarifa mojatu.

Kutokana na televisheni hiyokuwa ya umma kinapaswa kisheriakuvipa nafasi sawa vyama vinginevya siasa vyenye wagombea katikaUchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wakati TBC1 kilitangaza kampeniza mgombea urais wa CCM akiwaTabora, Lindi, Nzega na Mtwara,

mgombea wa kambi ya UKAWA navyama vingine vya upinzanivilinyimwa haki ya kutangazwa kwakampeni zao. Mgombea urais waCCM na mgombea mwenza walipewanafasi kubwa katika matangazo yakituo hicho.

Ripoti ya ufuatiliaji inasemakwamba uzinduzi wa kampeni zamgombea urais wa Chama ChaMapinduzi kwa upande wa Zanzibar,Dk Ali Mohamed Shein zilipewamuda zaidi ya dakika tatu kwenyetaarifa ya habari.

Vyama vidogo vya UPDP, TLP naNRA vilipewa taarifa moja tu wakatimgombea urais wa chama na NRAJanken Mali Kasambala hapoSeptemba 13 alipewa nafasi yakutangazwa kwa habari zake kwazaidi ya dakika 2.

Pia katika kipindi hicho kituo chaITV kilifanya kazi nzuri kwa kutoanafasi sawa kwa wagombea. Kwamfano, kituo hicho kilitangaza habari

za kampeni wa wagombea urais wavyama mbalimbali, bila kujaliumaarufu wao au wa vyama vyao.

Mtitiriko huo wa usawa katikakutangaza habari za uchaguzi, piauliwahusu wagombea wenza wavyama mbalimbali ingawa vyamavikubwa vya CCM na CHADEMAndivyo vilivyotangazwa zaidi.

Hii inatokana na ukweli kwambavyama hivyo viwili ndivyo vyenyeshughuli nyingi za kampeniikilinganishwa na vyama vingine vyakwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Hali kadhalika, vyama hivyo katikauchaguzi wa mwaka huu ndivyovyenye kundi la waandishi wa habariwanaofuatilia wagombea yaani Dk.John Magufuli wa CCM na EdwardLowassa wa CHADEMA.

TBC 1 ni chombo cha umma nakinawajibika kisheria kutoa fursakwa vyama vyote vya siasakutangaza sera na ilani zauchaguzi.

TBC yaonyesha upendeleokwa CCM, ITV yafanya vizuri

Darubini ya Uchaguzi 201510

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Wakati habari zinazohusumasuala ya UchaguziMkuu nchini zimekuwa

zikiongezeka jinsi sikuzinavyokwenda, habarizinazohusu wanawake na masualaya jinsia hazipewi kipaumbelehuku baadhi ya vyombo vyahabari vikiacha kabisa kuandikahabari hizo.

Hili linatokea japokuwawanawake wengi wamejitokezakugombea nafasi za kuchaguliwamwaka huu na takriban zaidi yanusu ya waliojiandikisha kupiga kurani wanawake.

Changamoto kubwailiyojidhihirisha bayana katika Mradiwa Ufuatiliaji Habari za Uchaguziunaoendeshwa na Baraza la HabariTanzania ni kuandikwa kwa habarichache zinazohusu wanawake namasuala ya jinsia.

"Kukosekana kwa habari zamasuala ya kijinsia ni changamotokwa vyombo vya habari," inaelezaRipoti ya Ufuatiliaji wa Habari zaUchaguzi. Taarifa hiyo inaelezakwamba habari za masuala ya jinsiailikuwa ni bidhaa adimu katikataarifa nyingi zilizoandikwa katikakipindi cha kampeni.

Baadhi ya vyombo vya habari

ambavyo vimekuwa vikitoakipaumbele japo kidogoukilinganisha na vyombo vinginekatika masuala ya jinsia kwa upandewa magazeti ni pamoja na magazetiya Mwananchi , The Citizen, JamboLeo, Zanzibar Leo, Tanzania Daima,Daily News na Raia Tanzania.

Mgombea mwenza wa CCM, SamiaSuluhu Hassan na Mgombea uraisKupitia ACT- Wazalendo AnnaMgwira ndio ambao wamepatanafasi kwenye vyombo vyahabari.

Magazeti ambayo hayajaandikakwa uchache sana masuala ya jinsiakwenye habari za uchaguzi nipamoja na Nipashe, The Guardian naMtanzania kulingana na ufuatiliajiwa vyombo vya habari katikakuandika habari za uchaguziunaofanywa na Baraza la habariTanzania (MCT) kati ya septemba 1hadi 17, 2015.

Wakati ripoti ya MCT yaufuatiliaji wa vyombo vya habarikuhusu uchaguzi ya kati yaSeptemba 11na 17 mwaka huuinaonyesha kuwa magazeti yaliyotoahabari zinazohusu jinsia miongonimwake kulikuwa na magazeti yenyehabari zinazofikia 98 lakini hakunagazeti hata moja lililokuwa na habarizaidi ya nne zilizoandikwa kuhusu

jinsia isipokuwa gazeti la ZanzibarLeo.

Kwa upande wa radio natelevisheni vyombo ambavyovimetangaza walao kwa uchachemasuala ya jinsia ni pamoja na ITV,Radio One, Radio Free Africa, TBCOne, TBC Taifa, Clouds Star TV, ZBCRadio, ZBC TV, Zenj FM, Hits FM.

Wakati Radio Free Africa licha yakutangaza habari zinazohusumasuala ya jinsia imejihusisha piakutangaza habari za watu wenyeulemavu kuhusiana na masuala yauchaguzi.

Uandishi wa habari za makundiyaliyoko pembezoni , masuala yajinsia hasa habari zinazohusuwanawake ni muhimu kwa lengo lakuwainua wapate nafasi mbalimbaliza maamuzi pia kuwawezeshakushiriki katika mchakato mzima wauchaguzi.

Makundi mengine ya pembezoniambayo pia habari zao zinatakiwakupewa kipaumbele ni pamoja navijana, watu wenye ulemavu namakabila madogo ambayo badoyamejitenga na jamii kama jamii yaWahazabe na Watindiga.

Kwa kuandika habari za makundikama haya vyombo vya habarivitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuzademokrasia kwa kuwapa sauti.

Samia Suluhu Anna Mghwira

Habari zamasuala

ya jinsia nibidhaaadimu

kwenyevyombo

vya habari

Darubini ya Uchaguzi 2015 11

Baraza la Habari Tanzania

Taarifa zenye maudhui yakupanda mbegu za chuki,kinyongo na kupandikiza

kila aina ya kisirani zimejitokezakatika baadhi ya magazetiyanayoendelea kufuatiliwa chiniya Mradi wa Ufuatiliaji wa Habariza Uchaguzi.

Moja ya taarifa hizo ni ile yailiyochapishwa na gazeti la TanzaniaDaima la Septemba 12 iliyodaikwamba "baadhi ya wananchi wajimbo la Uchaguzi la Ilemelawaliangua kilio mkutanoniwaliposimuliwa na mmoja wawagombea wa jimbo hilo kwambaalinusurika kifo baada ya kutekwa nakukatwa mapanga na watuwanaodhaniwa kuwa wafuasi waChama Cha Mapinduzi”.

Taarifa hiyo nyeti ilichapishwabila hata kufanyiwa utafiti wa kuhoji

vyanzo mbalimbali kama vile polisiau hospitali ili kuweza kuthibitishamadai hayo.

Uandishi wa namna unaonyeshadhahiri jinsi ya vyombo vya habarivinavyoweza kuwa mateka wapropaganda za mikutano ya kampeniambayo ni mara chache kukosamambo kama hayo.

Wakati wagombea wanatumiapropaganda kwa ajili ya kunadi serazao, ni wajibu wa waandishi wahabari kuchuja habari kwakutofautisha propaganda na habariza kweli.

Gazeti hilo hilo la Tanzania Daimala Septemba 13 lilichapisha taarifailiyokusudiwa kumdhihaki mgombeaurais wa Chama Cha Mapinduzi DkJohn Magufuli iliyobeba kichwa chahabari: Magufuli waache waliokufawalale salama.

Taarifa hiyo ilenga kumkejeli DkMagufuli wakati alipotembeleakaburi la Baba wa Taifa, MwalimuJulius Nyerere katika kijiji chaButiama.

Maoni yaliyomo katika taarifa hiyoni kwamba Dk Magufuli hawezikuubadilisha au kuufumua mfumouliopo wa utawala chini ya Chamacha Mapinduzi.

Katika taaluma ya uandishi wahabari, tahariri au makala za maonini lazima zizingatie kanuni zauandishi unaolenga kujenga badalaya kubomoa.

Matamshi ya chukikwenye kampeniyaripotiwa bilatahadhari

Darubini ya Uchaguzi 201512

Kuimarisha weledi wa vyombo vya habari juu ya kuripoti habari za uchaguzi Tanzania

Habari nyingi za uchaguzikwa visiwa vya Unguja naPemba kwa mwaka huu,

zinahusu ushindani wa vyama vyaCCM na Chama cha Wananchi(CUF).

Magazeti mengi yanayochapishwaTanzania Bara kama vile Daily News,The Guardian, The Citizen, HabariLeo, Nipashe, Mwananchi, Uhuru,Tanzania Daima, Mtanzania, RaiaTanzania, Jambo Leo na Majiraambayo yamekuwa yakifuatiliaharakati za uchagauzi wa Zanzibaryamesheheni taarifa za CCM na CUF.

Gazeti la Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, Zanzibar Leo ambalo ndilochanzo kikubwa cha habari visiwanihumo limejinasibu zaidi na taarifa zawagombea wa CCM na kutoa nafasindogo sana kwa CUF na vyamavingine vya upinzani.

Kwa mujibu wa Ripoti yaUfuatiliaji wa Habari za Uchaguzi yamwanzoni mwa Septemba, ZanzibarLeo lilikuwa na taarifa 88 kuhusuuchaguzi na kati ya hizo taarifa 29zilihusumgombea wa CCM wakatichama pinzani cha CUF kilikuwa nataarifa 12 tu.

Chama cha Demokrasia naMaendelo (CHADEMA) kilikuwa nataarifa 6 wakati vyama vingine,zikiwemo tume za Uchaguzi za ZECna NEC, viligawana asilimia iliyobaki.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, gazetila Zanzibar Leo lilimshambuliammoja wa viongozi wa kundi laUKAWA kwa kuandika kuwa:Sumaye kaenda UKAWA kuletamabadiliko au kuongeza giza?

Katika kipindi cha wiki ya pili yaSeptemba, Zanzibar Leo iliandikataarifa 79 zinazohusu uchaguziambapo taarifa 33 zilihusu CCM naCUF ilikuwa na 11 tu.

Kampeni za Chadema, kama ilivyokwa vyama vingine na tume za

uchaguzi, hazikupewa kipaumbele.Katika kipindi cha hicho cha

Septemba 11 hadi 17 magazetimengi ya Tanzania Barahayakuandika habari nyingi kuhusuZanzibar. Kati ya magazeti 12yanayofuatiliwa katika Mradi waUfuatiliaji wa Habari za Uchaguzi nihabari na picha 68 tu zilizohusuuchaguzi wa 2015.

Kati ya magazetiyaliyochunguzwa, gazeti la DailyNews liliongoza kwa kuwa na taarifa14 likifuatiwa na The Citizen naHabari Leo.

Kwa mujibu wa Ripoti yaUfuatiliaji wa Habari za Uchaguzi yaSeptemba 11 hadi 17, habari nyingiza uchaguzi kutoka Zanzibarzilichapishwa kwenye kurasa zandani za magazeti ya Tanzania Bara.Taarifa 21 zilichapishwa ukurasa wakwanza.

Kwa upande wa redio natelevisheni, vyombo hivyo viliandikahabari zenye kuzingatia misingi yataaluma zilizohusu chama pinzanicha CUF.

Mfano bayana ni ule wa Septemba9 wakati CUF ilipozindua kampenizake za uchaguzi ambapo ZBC Radioilitangaza mara tatu tukio hilowakati ZBC TV nayo ilitoakipaumbele kwa uzinduzi huo.

Pamoja na hayo, ZBC TV ilitoanafasi kubwa kwa kipindi maalumcha CUF kunadi ilani yake na serazake za maendeleo. Hata hivyo, halihiyo haikutokea kwa wagombeawawili wa urais wa Jamhuri yaMuungano, Dk John Magufuli waCCM na Edward Lowassa waCHADEMA.

Mfano halisi ni ule wa Septemba 6ambapo ZBC TV ilitangaza taarifanne zilizomhusu Dk John Magufuliwa CCM wakati taarifa moja ilimhusuEdward Lowassa wa Chadema.

Ushindani wa CCM,CUF watawala habariza uchaguzi Zanzibar

likapachikwa.Kufanya hivyo ni ukiukwaji wa

kanuni za Mamlaka yaMawasiliano Tanzania (TCRA)kuhusu vyombo vya habari vyaelektroniki wakati wa uchaguzi.

Kufuatana na kanuni hizovyombo vya habari vya elektronikivinakatazwa kurusha matangazoya kisiasa ya vyama vya siasawakati ikirusha vipindi vya mojakwa moja au vile vilivyorekodiwavinavyohusiana na uchaguzi.

Mtangazaji aliomba radhibaadae kwa tangazo hilo akisemawanatambua vilirushwa kwamakosa.

Kutoka Ukurasa 8

Star TV yatopeakukipigia debeChama chaMapinduzi

ZBC Radio na TV zazingatia weledi