MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Kwanza: UtaratibU Wa KUandaa Mazingira
YaliYosheheni Machapisho
Moduli ya Mwalimu
Moduli ya Mwalimu 2
Moduli ya Mwalimu 3
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Kwanza: UtaratibU Wa KUandaa Mazingira
YaliYosheheni Machapisho
Moduli ya Mwalimu
Moduli ya Mwalimu 4
Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:
Wizara ya elimu na Mafunzo ya Ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma
Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa eQUip-tanzania
Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:
C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora c.c.U ndala C.C.U Kasulu
C.C.U Kabanga c.c.U bundaC.C.U Tarime
c.c.U shinyangaC.C.U Mpwapwa
Moduli ya Mwalimu 5
Maelekezo na taswira katika moduli
Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:
Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.
Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.
Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.
Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.
Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.
Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.
6Mwongozo wa Kitaifa wa Ujuzi wa Uongozi Mahiri Katika Shule - Tanzania
Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule kwa walimu wa madarasa ya mwanzo
Moduli ya Kwanza: Utaratibu Wa Kuandaa Mazingira Yaliyosheheni Machapisho
MAUDHUI YA MODULI:
Moduli hii inamsaidia mwalimu kuandaa mazingira yaliyosheheni machapisho katika darasa na kuanzisha utaratibu wa kufundisha kwa kurudia rudia ili kuimarisha uwezo wa wanafunzi kujifunza kusoma kwa ufanisi.
DHANA KUU:
Mazingira yaliyosheheni machapisho: Humaanisha darasa lenye picha, kadi za maneno, majina ya wanafunzi, chati ya alfabeti, michoro na machapisho mengine yanayofanana na hayo. Mazingira yaliyosheheni machapisho ni muhimu kwa sababu wanafunzi wanahitaji kuona herufi na maneno mara kwa mara ili wajifunze kusoma kwa ufanisi.
MALENGO YA MODULI:
Baada ya kumaliza moduli hii kila mwalimu ataweza:• Kuandaa utaratibu wa kufundisha kwa kurudiarudia ili kuwajengea wanafunzi tabia ya
kujisomea.• Kubainisha vifaa muhimu vya kuandaa ili darasa liwe na zana zinazotosheleza.• Kuwezesha ujifunzaji wa kusoma Kiswahili kwa kutumia mbinu rahisi kama vile ”ujumbe wa
kila asubuhi”, ”herufi ya siku” na ”wimbo wa alfabeti”.
MAANDALIZI YA KIPINDI:
Mara zote uwe na Moduli yako ya Mafunzo ya Walimu Kazini na kalamu
TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI:
1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama inavyoonekana katika picha 2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki wote waonane na kuongea pamoja 3. Kuwa huru kuuliza maswali kama hujaelewa 4. Kuwa wa msaada kwa wenzako 5. Kuwa mbunifu na fikiria jinsi dhana unazojifunzazinahusiana na darasa lako 6. Weka simu yako katika hali ya mtetemo
Moduli ya Mwalimu 7
UTANGULIZI
Chunguza chumba (dakika 15)
Kwa kushirikiana na mwenzako tazama sehemu ya madarasa mawili hapa chini.
Darasa A Darasa B
Jadili maswali yafuatayo pamoja na mwenzako na andika majibu:
Umegundua nini kuhusu madarasa haya? Andika mambo yanayofanana? Andika mambo yanayotofautiana?
Yanayofanana: Yanayotofautiana:
Unafikiri darasa lipi linamwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujifunza kusoma kwa ufanisi? Kwa nini unafikiri hivyo?
Moduli ya Mwalimu 8
Wanafunzi hujifunza kusoma kwa haraka wanapokuwa kwenye mazingira yaliyosheheni machapisho kama vile vitabu, chati ya alfabeti, kadi za herufi darasani. Kwa kadri wanavyoona machapisho kwa wingi kila siku ndivyo akili zao hutaka kujifunza kusoma mambo mengi zaidi.
Darasa lenye ‘mazingira yaliyosheheni machapisho’ ni darasa linalotosheleza mahitaji ya wanafunzi katika kuona na kujifunza maudhui yaliyokusudiwa. Mazingira yaliyosheheni machapisho yana manufaa yafuatayo: 1) Huchochea stadi ya kuongea, kusikiliza, kusoma na kuandika kwa uhalisi; 2) Huwavutia wanafunzi kwa sababu ya matumizi ya rangi ambayo hufanya herufi na maneno yaliyoumbwa vizuri kupendeza ; 3) Darasa lenyewe huwa zana ya kufundishia; 4) Ni rahisi kulitumia kulingana na utaratibu wa darasa.
Kubandika majina ya vitu darasani, kutundika chati ya alfabeti na kuandika taarifa mbalimbali ubaoni ni njia muhimu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza msamiati mwingi zaidi. Darasa lenye kadi nyingi za maneno na picha huwawezesha wanafunzi kujizoesha kuhusianisha herufi moja moja na utamkwaji wake, muunganiko wa herufi na utamkwaji wake, na pia maneno na maana zake. Hii hutokea wanafunzi wanapoangalia kadi na picha hizo katika kila kona ya darasa au wanapoelekezwa na mwalimu ambaye hutumia kadi na picha hizo za kufundishia na kujifunzia.
Kujenga mazoea ya kutumia zana hizi, kunaimarisha kujifunza usomaji halisi wa kila siku na matumizi mbalimbali ya herufi na maandishi darasani. Kwa mfano, endapo mwalimu atabandika chati ya alfabeti darasani anaweza kuitumia kuimbisha wimbo wa alfabeti na kumtaka mwanafunzi aoneshe herufi zinazoimbwa, au akatumia maneno yaliyobandikwa darasani yakasaidia katika kusoma maneno mengine kama hayo kwenye vitabu.
Kujifunza kusoma kwa ufanisi ni muhimu sana kwa ajili ya mafanikio ya baadaye. Kwa sababu hiyo, mwalimu anapaswa kuhakikisha wanafunzi wanatumia muda wao mwingi inavyowezekana katika madarasa ya mwanzo kuona maandishi mengi, kubaini maneno mapya na kuandika wenyewe. Uzoefu unaonesha kuwa ufundishaji wa jumla wa herufi za alfabeti na dhana za maandishi darasani hautoshelezi. Ikumbukwe kuwa kila mwanafunzi anajifunza kwa uwezo unaotofautiana. Kwa hivyo, kila mmoja apewe fursa ya kutosha kujifunza kwa kuzingatia uwezo wake.
Unaweza kufanya mengi kuleta mabadiliko ya haraka na rahisi katika mazingira ya darasani yaliyosheheni machapisho ili kuendeleza ujifunzaji wa wanafunzi. Fanya jitihada zote kuhakikisha kuwa darasa lako lina “mazingira yaliyosheheni machapisho,” yaani darasa zima liwe limejaa picha, kadi za maneno, majina ya wanafunzi, chati ya alfabeti, michoro na machapisho mengine yanayofanana na hayo.
Jadiliana katika kikundi (dakika 10)1
1. Kwa kuzingatia matini uliyosoma hapo juu, taja ni sehemu gani ya matini ambayo unafikiri ni muhimu, haieleweki au ni mpya kwako?
1. Mwalimu mmoja anaanza kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha aya anamwita mwalimu mwingine kwa jina asome aya inayofuata.
2. Wakati unaposoma:
- Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu
- Weka alama ya (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo
- Weka mduara katika maneno ambayo ni mapya.
DHANA KUU
Umuhimu wa Mazingira Yaliyosheheni Machapisho (dakika 15)
Moduli ya Mwalimu 9
Fikiri peke yako kisha washirikishe washiriki katika kikundi (dakika 10)
1. Fafanua kwa mifano dhana ya mazingira yaliyosheheni machapisho :
2. Taja njia tatu (3) unazoweza kutumia ili kulifanya darasa lako lisheheni machapisho:
a)
b)
c)
3. Jadili umuhimu wa mazingira yaliyosheheni machapisho:
ZOEZI
Kujenga utaratibu wa kufundisha na kijifunza katika mazingira ya darasa yaliyosheheni machapisho (dakika 25)
Ni muhimu kuwa na taratibu zinazoongoza utendaji darasani. Taratibu hizi zinaweza kujengwa kwa kurudia rudia shughuli wanazofanya walimu na wanafunzi. Shughuli hizo zaweza kuwa maandalizi ya awali, kusalimiana, chemsha bongo, maswali na majibu na tathmini. Taratibu za darasani zinazojirudia rudia huweza kuwasaidia wanafunzi kuimarisha stadi ya kuzungumza na kuandika. Kwa mfano, mwalimu anaweza kutumia salamu ya maandishi ubaoni badala ya kuzungumza. Salamu hii huitwa ‘Ujumbe wa Siku’ kama inavyofafanuliwa hapa chini
Ujumbe wa siku
Ujumbe wa siku ni wazo ambalo mwalimu huandika ubaoni kwa wanafunzi siku inapoanza. Ujumbe unaweza kuundwa na sentensi ambazo hutoa ujumbe wa:1. salamu2. Picha ya jumla kuhusu shughuli za siku3. Maelezo ya maudhui ya somo linalokusudiwa katika kipindi husika4. Swali linalohusu tukio muhimu lililotokea jana
Moduli ya Mwalimu 10
5. Swali linalohusu tukio muhimu linalotarajiwa 6. Dhana au jambo lenye kufurahisha ambalo limetendeka
Utaratibu wa kuandika ujumbe wa siku
Mwalimu unatakiwa kuandika ujumbe wa siku kabla wanafunzi hawajaingia darasani. Kwa wanafunzi wa darasa la kwanza ambao hawajajua kusoma, mwalimu unatakiwa kusoma ujumbe wa asubuhi kwa kuonesha maneno unayoyasoma kwa kutumia ncha kionesheo. Wakati unasoma, onesha kwa vitendo taratibu za ku-soma ambazo ni 1) kusoma kwa kuanzia kushoto kwenda kulia; 2) kuanzia juu kushuka chini.
Ufuatao ni mfano wa Ujumbe wa siku:
Njia nyingine ya kufundisha utaratibu zinazojirudiarudia ambao unaweza kuimarisha stadi ya kuzungumza na kuandika ni ufundishaji wa ‘Herufi ya Siku’ ’
Herufi ya siku
Fanya kazi hii kwa dakika 5-10 kila siku kulingana na uwezo wa wanafunzi wako ili kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya kubaini herufi. Endelea na utaratibu huu unaojirudia rudia hadi utakapomaliza herufi zote.
1. Andika herufi za siku ubaoni.
2. Andika neno ambalo herufi ya siku inaanza mwanzo wa neno, mwisho wa neno na katikati ya neno (Tumia maneno ambayo yanafahamika vizuri kwa wanafunzi).
3. Wagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi 3-5 kisha waongoze kundika maneno mengi yenye herufi ya siku kadri wanavyoweza. Kama darasa lina wanafunzi wengi, waongoze wanafunzi kufanya kazi na jirani aliye upande wa kushoto au kulia ili wasitumie muda mrefu kutengeneza makundi.
4. Kwa darasa la kwanza waongoze wanafunzi kubungua bongo maneno ambayo herufi ya mwanzo inawakilisha herufi ya siku.
5. Waongoze wanafunzi wa darasa la 2 na la 3 kuandika maneno ambayo yanaanza na herufi ya siku.
6. Kama una muda wa ziada, waongoze wanafunzi waje mbele na kuandika maneno sahihi ubaoni kama haya.
7. Anza na maneno yenye silabi mbili kwa darasa la kwanza na kisha maneno yenye kuundwa na silabi tatu kwa darasa la pili
Hamjambo watoto wazuri.Leo ni Jumatatu, siku ya kwanza ya juma.
Leo katika somo la Kiswahili tutajifunza kusoma herufi ’m’.Kisha tutajifunza kusoma maneno mapya.
Karibu tufurahie somo la leo.
Moduli ya Mwalimu 11
Njia nyingine inayojirudia rudia katika ufundishaji darasani ambayo inaweza kuimarisha stadi ya kuzungumza kwa wanafunzi ni wimbo wa alfabeti.
Wimbo wa Alfabeti
Kuimba wimbo wa alfabeti ni tendo la kufurahisha ambalo huweza kuwa rahisi katika kulifanya liwe la kujirudia rudia. Ni muhimu wakati unapoimba wimbo pamoja na wanafunzi, tamka kwa usahihi majina na sauti ya herufi ili wanafunzi wahamasike na kukuiga. Ni muhimu pia kuonyesha kila herufi kama unavyoiimba. Ni vema kuandika herufi ubaoni ili iwe rahisi kuonesha ni herufi gani wanayoimba.. Jaribu kufuatilia mabadiliko baada ya tendo hili.
1. Simama mbele ya chati ya alfabeti au andika herufi ubaoni.
2. Imba wimbo wa alfabeti pamoja na wanafunzi.
3. Tumia fimbo au kionesheo/kilichochongoka kuonyesha kila herufi unayoiimba
4. Imba tena wimbo, safari hii badilisha kasi. Kwa muda imba polepole na muda mwingine imba kwa haraka
5. Mwite mwanafunzi yeyote aje mbele kuliongoza darasa kuimba kwa njia ileile.
6. Mwelekeze mwanafunzi anayeimba kuonesha kila herufi anayoiimba.
Sasa ni wakati wa kujifunza taratibu hizi kwa kutumia igizo dhima.
Igizo (dakika 20)
Kila mwalimu atachagua utaratibu mmoja kati ya tatu tuliojifunza katika moduli hii ambao ni ‘ujumbe wa siku, ‘herufi ya siku’ na ‘wimbo wa alfabeti’. Utakuwa na dakika 10 za kuandaa igizo dhima ambapo wewe utakuwa mwalimu na washiriki wenzako watakuwa wanafunzi wa darasa la 1-3
Mwalimu atakayechagua utaratibu wa ‘Ujumbe wa siku’ lazima afikiri ujumbe mpya ambao utaandikwa ubaoni na utasomwa kwa pamoja (mwalimu na wanafunzi).
Mwalimu atakayechagua ‘herufi ya siku’ lazima abainishe maneno ambayo yanaanza na herufi ya siku, yanaishia naherufi ya siku na katikati ya neno kuna herufi ya siku.
Mwalimu atakayechagua wimbo wa alfabeti lazima aandike herufi ubaoni na kuzionesha herufi wakati wanafunzi wanaimba wimbo wa alfabeti.
Neno linaloanza na herufi ’a’
andazi
Neno linaloishia na herufi ’a’
baba
Bainisha herufi ’a’ katika neno
nazi
Moduli ya Mwalimu 12
Jadiliana katika kundi kubwa (dakika 5)
1. Je, ni wakati gani utaratibu uliochagua hapo juu unaweza kuwa muhimu zaidi darasani kwa-ko? (Utaratibu huu unaweza kuwa tofautina ule uliochaguliwa na mwalimu mwenzako).
2. Unawezaje kuboresha taratibu hizi na kuzitumia darasani?
KUPANGA MKAKATI
Kuandaa ‘Kipindi cha Kusoma na Kuandika’ (dakika 15)
Katika kuimarisha uwezo wa wanafunzi kujifunza kusoma na kuandika, ni muhimu mwalimu kuwa na mpango unaomwezesha kutumia maarifa mapya aliyojifunza wakati wa mafunzo ya walimu kazini kwa vitendo. Aidha ni muhimu kwa wanafunzi kupata muda zaidi wa kujifunza kusoma na kuandika. Kwa mantiki hii, ni muhimu kwa mwalimu kuandaa kipindi cha saa moja cha kusoma na kuandika mara moja kwa wiki. Kwa darasa la kwanza na la pili inaweza kuwa rahisi kupanga kipindi cha kujifunza kusoma na kuandika, ila kwa darasa la tatu ni vema kumshirikisha mwalimu mkuu na mwalimu wa taaluma ili kutoleta mkanganyiko katika ratiba ya masomo.
Soma kwa makini kanuni za kufundisha darasani hapo chini na kisha panga namna nzuri utakavyozitekeleza wakati wa kipindi cha ‘kusoma na kuandika’
Matumizi ya kanuni ya kwanza: Wimbo wa alfabeti
Utangulizi:
1. Andika herufi za alfabeti kwenye ubao
2. Uliza maswali rahisi yanayohusu alfabeti. Kwa mfano kuna herufi ngapi kwenye alfabeti? Ni herufi ipi ya mwanzo au ya mwisho? Ni herufi gani inayotangulia kabla ya herufi ‘m’? Herufi ipi inayotangulia kabla ya herufi ‘d’? Herufi ipi inafuata baada ya herufi ‘s’?
Vitendo:
3. Imba wimbo wa alfabeti pamoja na wanafunzi. Tumia kionesheo ili kuonesha kila herufi inayoimbwa. Kumbuka kutamka herufi kwa uwazi. Imba wimbo tena ila mara hii imba kwa haraka kidogo. Kisha badilisha utaratibu kwa kuimba pole pole na wakati mwingine imba kwa haraka. Ita mwanafunzi mmoja kusimama mbele ya darasa na aimbe wimbo wa alfabeti kwa kufuata utaratibu ulioanza nao. Kumbuka kuwaongoza wanafunzi kuonesha herufi wanayoitamka wakati wa kuimba wimbo.
Upimaji:
4. Futa herufi ubaoni na kisha waambie wanafunzi waandike herufi katika daftari zao za mazoezi (Kwa watoto wa darasa la kwanza wanaweza kuanza kuandika hewani, kisha kwenye mchanga baada ya hapo kwenye daftari zao.
5. Zunguka katika darasa kukagua wanafunzi wanavyoandika herufi kwenye daftari zao na kuwapa msaada wale wanaopata changamoto ya kuandika.
6. Andika orodha ya alfabeti ubaoni . Anza na herufi ‘a’ kisha chagua mwanafunzi mmoja mmoja kuandika herufi moja ya alfabeti.
7. Toa msaada kwa wanafunzi wanaopata ugumu wa kufanya zoezi hili.
Moduli ya Mwalimu 13
Matumizi ya kanunu ya pili: Ujumbe wa siku
Utangulizi:
1. Andika ujumbe wa siku kabla ya wanafunzi hawajaingia darasani
2. Kwa ujumla unaanza na salaam,kisha kutaja jina la siku, hali ya hewa ya siku hiyo na wakati mwingine unaweza kuanza kwa kuzungumzia tukio maalumu kwa mfano jaribio au ugeni wa mtu maarufu hapo shuleni.
Vitendo:
3. Mara baada ya wanafunzi kuketi waambie kuangalia ujumbe wa asubuhi ulioandikwa ubaoni
4. Waambie wanafunzi kila mmoja amulize jirani yake kama kuna neno katika ujumbe wa siku analoweza kulitambua.
5. Waulize wanafunzi kushirikishana maneno wanayoyatambua.
6. Wasomee ujumbe wa siku wanafunzi kwa sauti lakini polepole. Tumia kidole kuonesha maneno unayoya-soma kwenye ujumbe wa siku.
7. Soma ujumbe wa asubuhi kwa pamoja na wanafunzi huku ukionesha kila neno linalosomwa
Upimaji:
8. Rudia kusoma ujumbe wa siku. Wakati huu chunguza mwanafunzi anayepata ugumu wa kubashiri neno linalofuata wakati wa kusoma ujumbe wa asubuhi.
Jadili na mwenzako (dakika 15)
Ukiwa na mshiriki mwenzako, jadilianeni jinsi mnavyoweza kuingiza taratibu hizi za kufundisha katika andalio lako la somo na katika kipindi cha wiki cha kusoma na kuandika. Onesha kwa vitendo namna utakavyoweza kutumia kwa ufanisi taratibu hizi kwa darasa la kwanza, la pili, na la tatu. Kisha wasilisha mawazo yako kwenye kikundi.
Moduli ya Mwalimu 14
Mwisho (dakika 10)
Jibu maswali yafuatayo
Mada ya kipindi:
Ni kwa namna gani umenufaika na malengo ya somo? Kipi kimekusaidia?
Ni mambo gani utapenda kujaribu kwenye darasa lako ndani ya mwezi mmoja ujao?
Kipi umekipenda katika kipindi cha leo?
Je kuna lolote linaloweza kufanyika kwa ajili ya kuboresha kipindi kijacho?
Andika taarifa ya kipindi kijacho:
Mada:
Tarehe na Muda:
Mahali:
Moduli ya Mwalimu 15
Kupima Utendaji Kazi (dakika 5)
Tafadhali tafakari jinsi mratibu wa MWK alivyofanya kazi leo. Jaza fomu ifuatayo kwa ajili ya tathmini yako. Fomu hii itakusanywa na Timu ya Wilaya ya MWK kwa ajili ya kuwasaidia waratibu wa MWK.
Mwongozo wa Usahihishaji kwa ajili ya Waratibu wa MWK:Alama 0:
Hajaweza kabisa
Alama 1:
Ameweza kidogo
Alama 2:
Ameweza kiasi cha kuridhisha
Alama 3:
Ameweza vizuri sana Mratibu wa MWK hajaweza kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kidogo kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya kwa kiwango cha kuridhisha yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya vizuri sana yale yaliyoorodheshwa
Yale yaliyofanywa wakati wa kipindi cha MWK:
0 1 2 31. Maandalizi: Mratibu wa MWK amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri
moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia
2. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu
3. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika
4. Ufundishaji na ushauri: Mratibu wa MWK anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini MWK ni muhimu kwetu
5. Ufundishaji na ushauri : Mratibu wa MWK anatoa ushirikiano – anafuatilia maendeleo yetu kujua kama tunatumia mbinu mpya darasani na anatusaidia pale anapoona tuna tatizo
Alama za jumla:
/15 x 100% = ________
Moduli ya Mwalimu 16
Moduli ya Mwalimu 17
Moduli ya Mwalimu 18
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Pili:Usimamizi Fanisi wa Darasa
Moduli ya Mwalimu
Moduli ya Mwalimu 2
Moduli ya Mwalimu 3
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Pili:Usimamizi Fanisi wa Darasa
Moduli ya Mwalimu
Moduli ya Mwalimu 4
Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:
wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma
Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa EQUIP-Tanzania
Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:
C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.U ndala C.C.U Kasulu
C.C.U Kabanga C.C.U BundaC.C.U Tarime
C.C.U shinyangaC.C.U Mpwapwa
Moduli ya Mwalimu 5
Maelekezo na taswira katika moduli
Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:
Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.
Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.
Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.
Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.
Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.
Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.
Moduli ya Mwalimu 6
Moduli ya Pili: Usimamizi Fanisi wa Darasa MAUDHUI YA MODULI: Moduli hii ni kuhusu usimamizi fanisi wa darasa. Kwako mwalimu, inamaanisha kujifunza mbinu mbalimbali za kuwa na mazingira rafiki darasani pamoja na njia ambazo walimu hutumia kuwafanya wanafunzi waelekeze fikra zao katika kujifunza, wasikilize na kushiriki kikamilifu katika kujifunza wakiwa darasani. DHANA KUU:
Usimamizi fanisi wa darasa: mbinu na njia mbalimbali ambazo walimu wanaweza kutumia kuwafanya wanafunzi waelekeze fikra zao katika kujifunza, kusikiliza na kushiriki kikamilifu katika kujifunza darasani.
Mazingira rafiki: mazingira hapa yanaweza kuwa mahali pa kuishi au kujifunzia. Mazingira rafiki ni hali ya kutokuwa na vitisho, hofu, chuki au adhabu, hasa ya kuchapa fimbo, kuzaba makofi, kupiga konzi, kufinya au kuvuta masikio. Mazingira rafiki yanaboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa sababu wanafunzi wanapata fursa ya kujieleza, wanaweza kujiamini na kuaminiana.
MALENGO YA MODULI: Hadi mwisho wa moduli hii, washiriki waweze:
Kuelewa maana ya “Usimamizi fanisi wa darasa” na umuhimu wa kufanya hivyo; Kubaini angalau mbinu kati ya 4 hadi 5 zinazowasaidia walimu kuwafanya wanafunzi waweze kuzingatia
kinachofundishwa darasani, kusikiliza na kushiriki katika kujifunza, hasa kwa madarasa yenye wanafunzi wengi;
Kufanya mazoezi ya mbinu rahisi za kuyaweka mazingira ya darasa yawe rafiki na kuweza kuzitumia mbinu hizo wakiwa madarasani.
MAANDALIZI YA KIPINDI: Mara zote uwe na Moduli yako ya Mafunzo ya Walimu Kazini na kalamu
TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI:
1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama inavyoonekana katika picha
2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki wote waonane na kuongea pamoja
3. Kuwa huru kuuliza maswali kama hujaelewa 4. Kuwa wa msaada kwa wenzako 5. Kuwa mbunifu na fikiria jinsi dhana unazojifunzazinahusiana
na darasa lako 6. Weka simu yako katika hali ya mtetemo
Weka simu yako katika hali ya mtetemo
Moduli ya Mwalimu 7
TAFAKARI Katika moduli iliyopita ulifanya kwa vitendo mada iliyohusiana na uanziswaji wa kanuni katika madarasa yaliyosheheni machapisho hususan matumizi ya ujumbe wa siku, herufi ya siku na kuimba wimbo wa alfabeti. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa kufundisha maudhui ya moduli hiyo darasani kwako
Andika peke yako (dakika 5) Tafadhali andika kwenye visanduku mafanikio na changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutekeleza mikakati hii katika darasa lako.
Mafanikio (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)
Changamoto
(Elezea utaratibu uliotumia na fafanua changamoto zake)
Jadiliana katika kikundi (dakika 10)
Shirikisha wenzako kwenye kundi mojawapo ya uzoefu huo. Kwa kila changamoto, pendekeza namna ya kukabiliana nayo. Wakati wa majadiliano, andika ufumbuzi unaoendana na changamoto ulizobainisha.
Njia Muhimu za Ufumbuzi (Mawazo muhimu mahususi kwa wenzetu)
Moduli ya Mwalimu 8
UTANGULIZI Zoezi binafsi la kujikumbusha (dakika 5)
Ukiwa peke yako soma maelezo yafuatayo na andika kama unakubali au hukubali. Tafadhali jibu kulingana na uelewa wako. Hutakiwi kumshirikisha mwenzako majibu yako na hakuna atakayekuhukumu kutokana na majibu uliyotoa.
Maelezo Nakubali/Sikubali Haiwezekani kuwafanya wanafunzi kwenye darasa kubwa wakakusikiliza na kuwa kimya bila ya kuwachapa (au kuwatishia kuchapa)
Kukiwa na wanafunzi wengi darasani si rahisi kuunda makundi haraka na bila ya kelele
Ikibainika kuwa wanafunzi wamedanganya, kuiba au kufanya jambo baya, lazima waonywe kwa kuchapwa, la sivyo watarudia tena
Kama wanafunzi watakosa umakini darasani, kuwachapa ndiyo njia pekee ya kuwafanya wawe makini darasani
Kutembea na fimbo katika maeneo ya shule ni sawa tu kwani inawafanya wanafunzi wawe na adabu (hata kama sitaitumia)
Wanafunzi watawaheshimu walimu wao ikiwa wanawaogopa
Kuandika Tafakuri Binafsi (dakika 10)
Baada ya kumaliza zoezi hili, tafadhali jaza fomu ifuatayo kwa kuzingatia yafuatayo: 1) Kumbuka miaka ya nyuma ulipokuwa mwanafunzi wa shule ya msingi 2) Tafadhali orodhesha adhabu zote ulizowahi kupata, kama vile kuchapwa fimbo, kuzabwa makofi,
kuvutwa masikio, kuchuchumaa, kulala na kujinyanyua kwa mikono (push up), nk. 3) Tafadhali taja sababu zilizokufanya upate hiyo adhabu (na kama hakukuwa na sababu yoyote andika pia) 4) Tafadhali andika ulivyojisikia baada ya kupata hizo adhabu. Tafadhali sema ukweli (je zilikusaidia? Je
zilikufanya uogope, uwe na hasira au mwenye huzuni?) 5) Baada ya kumaliza, jadili mawazo yako katika kikundi.
Ni adhabu zipi ulipewa ulipokuwa
shule ya msingi? Kwanini ulipewa adhabu hizo? Ulijisikiaje baada ya kuadhibiwa
Moduli ya Mwalimu 9
1. Mwalimu mmoja anaanza kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha aya anamwita mwalimu mwingine kwa jina asome aya inayofuata.
2. Wakati unaposoma: -‐Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu -‐Weka alama ya (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo -‐Weka mduara katika maneno ambayo ni mapya.
DHANA KUU
Mbinu fanisi za kusimamia darasa (dakika 20)
Utafiti unaonyesha kuwa kuchapa viboko kunaweza kuwa na athari mbaya kwa wanafunzi (kumbuka jinsi ulivyojisikia baada ya kuadhibiwa ulipokuwa mdogo). Kwa mfano,
1) Kunasababisha madhara ya kimwili, kiakili na kihisia; 2) kunamfanya mwanafunzi awachukie au awaogope walimu wake, kitendo kinachopunguza uwezo wao wa
kujifunza; 3) Wanafunzi hawawezi kujirekebisha kutokana na makosa yao, badala yake wanajifunza mbinu za kukwepa
adhabu; 4) Hofu ya wasichana kuadhibiwa, pamoja na kudhalilishwa na walimu na wanafunzi wenzao wa kiume,
huwafanya washindwe kujieleza vizuri darasani. Hali hii ya wasichana ya kutokuwa wepesi wa kujieleza darasani ndio mara nyingi huwafanya waonekane wameumbwa wenye aibu au wapole.
5) Huwafanya wavulana wenye uwezo mdogo darasani wasitoe ushirikiano darasani (hali inayowafanya wazidi kuchapwa) au kuwa watoro/kuacha masomo (ili kuachana kabisa na vichapo zaidi)
Kwa kuzingatia matatizo haya, walimu wanakuwa na wakati mgumu sana kwa kuwa wanakabiliwa na madarasa yenye wanafunzi wengi kuliko uwezo wao huku wakipata msaada kidogo. Walimu wengi wanahisi kuwa mazingira haya magumu ndiyo huwalazimisha waamue kuwachapa wanafunzi. Mwaka 2010, walimu 65 kutoka mkoa wa Arusha walihojiwa kuhusu maoni yao juu ya adhabu ya viboko. Walimu wengi waliohojiwa walieleza kuwa hawapendi kuchapa, lakini hawakuwa na njia nyingine zaidi ya kuchapa. Kwa mfano mwalimu Dora kutoka shule iliyoko maeneo ya vijijini alisema, “Sipendi kuwachapa kwa kuwa lengo si kuwachapa. Lengo ni kuwaelimisha na kuwafanya waelewe. Lakini kutokana na darasa kuwa na wanafunzi wengi, inakuwa vigumu kuwadhibiti, ndio maana wakati mwingine nalazimika kutumia fimbo.” Maelezo haya yanadhihirisha ugumu walimu wanaokabiliana nao kwa kuwa hawapendi kutumia adhabu ya kuchapa viboko ila wanalazimika kutumia adhabu hiyo kwa ajili ya kutawala darasa. Na Mwalimu Grace kutoka shule iliyoko nje ya mji alieleza,
“Serikali inatuzuia kutumia fimbo, hata hivyo tunaendelea kuwachapa hata kama hairuhusiwi. Tumezuiwa kabisa kuchapa. Lakini bila kuwachapa watoto hawasikii.” Kuna tafsiri tofauti za walimu wakuu kuhusu sheria ya adhabu ya viboko. Baadhi wanaifuata na kuwazuia walimu kuchapa wanafunzi, lakini wapo wengine wanawaruhusu waendelee kuwachapa wanafunzi. Walimu wakuu wengi wapo njia panda. Hii inadhihirisha ugumu ambao walimu wanakabiliana nao – wanajua kabisa hawapendi kuchapa au hatakiwi kuchapa lakini bado wanaona ndio njia pekee ya kutumia kwa ajili ya kuweka nidhamu ndani ya darasa. Mwalimu Amani kutoka shule iliyo nje ya mji alisema:
Moduli ya Mwalimu 10
« Najaribu kuwaambia wanafunzi wangu, tafadhali ninapokuwa humu darasani nikifundisha, sipendi kumwona mwanafunzi akiongea, sipendi kumwona mwanafunzi anayetembea huku na kule … pengine nafundisha hisabati halafu wewe unasoma Kiswahili. Sipendi kabisa tabia hiyo. Unatakiwa kusikiliza kwa makini kwa sababu baada ya kipindi nitawauliza maswali. Hamtaweza kufanya vizuri maswali nitakayowapa kwa sababu hamkunisikiliza vizuri wakati nafundisha. Na hicho ndicho ninachochukia sana. Ndio maana wakati mwingi nawachapa fimbo. » Hii inaonyesha jinsi inavyotokea kwa mwalimu hadi kulazimika kutumia adhabu kwa nia ya kuwasaidia wanafunzi wake, lakini bado hawamsikii, wanaongea darasani, wanazunguka huku na kule ndani ya darasa, au kufanya zoezi la somo jingine. Mwalimu Omari aliongelea kuhusu kuwachapa wanafunzi ili wawe na tabia nzuri ambayo itawafanya wakubalike na jamii. Hii adhabu ya kuchapa ilikuja kwa lengo la kuwaadhibu wanaochelewa shule, walio na sare chafu au wasio na madaftari ya somo husika au vifaa vya kujifunzia. Kwa kauli yake mwalimu Omari, « Tunawanyoosha tu wanafunzi kwa kuwachapa fimbo moja moja mkononi. Hii itawafanya wasirudie tena makosa kama hayo. » Nukuu hizi zote zinadhihirisha kuwa hata kama walimu hawapendi kuchapa, wengi hulazimika kufanya hivyo. Adhabu ya kuchapa hutoa suluhisho la haraka na jepesi la kuwafanya wanafunzi wawe na adabu, lakini inaweza kusababisha matokeo mabaya hapo baadaye (kama vile tabia ya wanafunzi kukwepa masomo, kuchukia masomo, walimu au tabia yoyote mbaya). Walimu wasiopenda kutumia adhabu hii hujikuta wakichoka kimwili na kiakili. Lakini huenda hii inatokea kwa sababu walimu hawajui njia nyingine za kuwawezesha kudhibiti nidhamu ya darasa, kuwafanya wanafunzi wakae kimya, wanafunzi wawe wasikivu, au kuzuia uchelewaji. Huenda walimu wangekuwa na mbinu nyingine za kuweka mazingira rafiki ya madarasa yao, na zikathibitika kuwa na ufanisi, wasingekimbilia kutumia sana adhabu ya kuchapa.
Jadiliana katika kikundi (dakika 10)
1) Ni mambo gani katika matini ya hapo juu ambayo unaona ni ya muhimu, hayaeleweki au mapya?
2) Je unaweza kuhusianisha kile walichosema walimu waliohojiwa na maisha yako? Kama ndiyo, je ni katika hali zipi?
3) Kama ungepata mbinu nyingine mbali ya kuchapa, je utapenda au hutapenda kuzitumia? Kwanini utapenda? Kwanini hutapenda?
ZOEZI
Chunguza jedwali lifuatalo, kisha shirikiana na mwenzako kuoanisha kila tatizo na ufumbuzi wake (dakika 20)
Tafadhali zingatia kuwa matatizo mengine yanaweza kuwa na majibu zaidi ya moja, kwa hiyo andikeni majibu yote mnayohisi ni sahihi kwa tatizo husika. Pia kama kuna njia nyingine kwa ajili ya kutatua kila tatizo, tafadhali andika njia hizo. Baada ya kumaliza, washirikishe majibu yenu wenzenu kwenye kundi.
Moduli ya Mwalimu 11
MATATIZO UFUMBUZI WA MATATIZO
1. Darasa ni kubwa na ni vigumu kuwafanya wanafunzi wawe wasikivu, na walio tayari kujifunza.
A. Mwalimu anaweza kuanzisha mchezo kwa kuwaambia wanafunzi: “Nikiinua mkono, mnyamaze na muinue mikono yenu ”. Wanafunzi wote wataanza kuinua mikono na wale wa mwisho (wanaoongea au ambao hawajawa tayari) watajisikia vibaya. Kasha watafuata wanavyofanya wenzao.
B. Wanafunzi hujibu vizuri maswali yenye manufaa kwao. Tumia dakika 15
kuwauliza wanafunzi ni tabia zipi wanadhani ni njema; kisha wasaidie wakubaliane (kama vile kuwa tayari kusikiliza, kufanya mazoezi ya somo jingine, kutocheza darasani, n.k.). Waambie kuwa atakayeweza kuzingatia vyote hivyo atakuwa ‘Mwanafunzi bora wa siku’, ukimaanisha kuwa kesho yake utamtangaza mwanafunzi bora wa siku na kumvisha nishani au alama ya ushindi (unaweza kutengeneza shada kwa kutumia karatasi na uzi). Ukiwa unachagua mwanafunzi bora wa siku ni vema kuwachagua wale wanaohitaji
motisha na kuhamasishwa waendelee kubadilika.
C. Tembea darasani huku ukifundisha halafu simama pembeni ya wanafunzi wanaoongea. Simama pembeni yao halafu weka mikono yako juu ya mabega yao huku ukiendelea kufundisha. Hii itawafanya wanafunzi wajue kuwa unajua wanachokifanya na hivyo wataacha kuongea.
D. Ukiona wanafunzi waIioko nyuma ya darasa wanaongea na si wasikivu wahamishie mbele kwa muda na wabadilishane na waliokaa mbele ya darasa.
Njia zinazoweza kutatua: Kwa mfano, A
Njia nyingine:
2. Wakati nafundisha kuna wanafunzi wanaongea, hasa wanaokaa nyuma ya darasa.
Njia zinazoweza kutatua:__________
Njia nyingine:
3. Kuna wanafunzi wengi ndani ya darasa na hivyo inakuwa vigumu kuunda vikundi kwa muda mfupi na kwa utulivu.
Moduli ya Mwalimu 12
Njia zinazoweza kutatua:___________
E. Tumia dakika 15 kuwapanga katika vikundi. Waweke katika vikundi kadiri ya mahitaji tofauti (kwa mfano kundi la kusoma pamoja kitabu, kundi la kuwachanganya wenye uwezo tofauti), na waelekeze wachague kiongozi. Waambie kila kundi lichague jina lake (kwa mfano jina la mnyama, matunda nk). Waambie ukifika wakati wa makundi itabidi wajikusanye kadiri ya makundi (kiongozi wao atawasimamia). Waambie kuwa ni mashindano ya kuona kundi lipi litakuwa la kwanza kujipanga mapema zaidi. Baada ya makundi kuwa tayari watangazie washindi watatu wa mwanzo, andika majina yao ubaoni na wanafunzi nwenzao wawapigie makofi.
alichofanya haikuwa sahihi, fafanua ili mwanafunzi aelewa kuwa alichofanya haukuwa uamuzi sahihi huku ukijiridhisha kuwa mazingira ya nje ya shule hayachangii mwanafunzi kuwa na tatizo hilo la nidhamu. Hatua ya pili, mwambie kuwa kwa kosa alilofanya hataweza kwenda kupumzika na wenzake wakati wa mapumziko badala yake atafanya tafakari aidha kwa maandishi au kwa maneno kwanini alichokifanya ilikuwa ni utovu wa nidhamu na atafanya nini asirudie kosa hilo tena.
kwenye kundi ameonyesha tabia mbaya, alama za kundi zitapunguzwa. Waruhusu wanafunzi waorodheshe mifano mingine ya ‘tabia mbaya’ (kwa mfano, mwanafunzi si mtulivu, anaongea wakati wa kipindi, au anafanya kazi ya
Njia nyingine:
4. Akibainika mwanafunzi akidanganya, akiiba, au kufanya jambo fulani vibaya. Ipi ni njia nzuri ya kumuadhibu ili ajue alichofanya ni kibaya?
Njia zinazoweza kutatua:___________
Njia nyingine:
5. Kuna wanafunzi wanaochelewa kuja shuleni, wakiwa wachafu au hawana vifaa vya kujifunzia kama vile madaftari na kalamu. Ninafanyaje kuzuia tabia hii isijirudie?
F. Kwa wanafunzi wenye matatizo makubwa ya kinidhamu unaweza kutumia mbinu inayoitwa ‘muda wa tafakari’. Hatua ya kwanza unaongea na mwanafunzi kwanini anafikiri kuwa
G. Wanafunzi watashiriki vizuri katika somo lako kama utalifanya liwe na mvuto. Jaribu kutumia michezo – wanafunzi wanaweza kuwa wasikivu kama watapata nafasi ya kucheza. Ni muhimu pia kuwachagua wale ambao wanaonyesha kutokuwa wasikivu washiriki kwenye michezo.
H. Ligawanye darasa katika makundi kama una darasa lenye wanafunzi wengi. Kama una safu tatu za madawati basi unda kundi kwa kila safu. Waache wanafunzi watoe majina ya makundi yao. Watangazie kuwa kila kundi lina alama 100 na waambie kuwa kama kuna mwanafunzi toka
Moduli ya Mwalimu 13
Njia zinazoweza kutatua:___________
somo jingine). Endelea kupunguza alama wakati unafundisha na baada ya kipindi tangaza kundi lililoshinda
I. Kama wanafunzi wanachelewa kuja darasani au wanakuja wakiwa hawajajiandaa, kwanza kabisa waulize kwanini wamechelewa au hawajajiandaa. Kama kuna tatizo kubwa jaribu kuwapa ushauri. Kama hawana sababu ya maana, waambie kuwa unawapa onyo mara mbili kabla hawajawekwa kwenye ‘kifungo cha ndani’ (ukimaanisha kuwa hawataweza kwenda mapumziko). Ukiona wanarudi mara ya tatu, jaribu adhabu ya ‘kifungo cha ndani’ (tazama njia namba F).
Njia nyingine:
Jadiliana katika kikundi (dakika 10)
1) Je unafikiri njia hizo zinaweza kusaidia vya kutosha? Kwa nini zinasaidia? Kwa nini hazisaidii? 2) Njia ipi inafaa? Ipi haifai? Na kwanini? 3) Njia zipi utapenda kuzijaribu darasani kwako? Utaziboreshaje? 4) Unafikiri mwalimu mkuu anaweza kutumia mbinu hizi? Kama hawezi, kwanini?
TATHMINI BINAFSI
Tathmini Binafsi ya Mbinu za Kusimamia Darasa (dakika 5)
ANGALIZO: Tathmini hii ni binafsi hulazimiki kumshirikisha mshiriki yeyote. Ni njia ya kutathmini uwezo wako wa kubainisha maeneo ya kuboresha ili kuimarisha mbinu za usimamizi wa darasa.
Mbinu fanisi za kusimamia darasa Sielewi Naelewa lakini huwa sifanyi
Huwa nafanya lakini nahitaji kuboresha zaidi
Nafanya vizuri sana
Natumia ishara (kama vile kumkodoloIea macho, kusimama karibu na mwanafunzi, kunyoosha mkono) kuwafanya wanafunzi wawe wasikivu.
Kwa mwanafunzi mwenye tatizo kubwa la kinidhamu ninapanga kuwa na muda wa tafakari wakati wa mapumziko .
Napanga kuwa na mchezo darasani ili kulifanya somo langu liwe la kuvutia
Natumia motisha chanya kuwafanya wanafunzi wangu wawe na nidhamu
Moduli ya Mwalimu 14
Mawazo kuhusu Usimamizi wa Darasa (dakika 5) Jaza tena chati ifuatayo ambayo uliijaza wakati wa kujikumbusha. Linganisha majibu yako ya mwanzo
wakati wa zoezi la kujikumbusha na majibu yako ya sasa. Je majibu yako yamebadilika?
Maelezo Nakubali/ Sikubali Haiwezekani kuwafanya wanafunzi kwenye darasa kubwa wakakusikiliza na kuwa kimya bila ya kuwachapa (au kuwatishia kuchapa).
Kukiwa na wanafunzi wengi darasani si rahisi kuunda makundi haraka na bila ya kelele .
Ikibainika kuwa wanafunzi wamedanganya, kuiba au kufanya jambo baya, lazima waonywe kwa kuchapwa, la sivyo watarudia tena.
Kama wanafunzi watakosa umakini darasani, kuwachapa ndiyo njia pekee ya kuwafanya wawe makini darasani.
Kutembea na fimbo katika maeneo ya shule ni sawa tu kwani inawafanya wanafunzi wawe na adabu (hata kama sitaitumia).
Wanafunzi watawaheshimu walimu wao ikiwa wanawaogopa.
KUANDAA MPANGO KAZI
Kupanga ‘Kipindi cha Kusoma na Kuandika’ (dakika 10)
Katika kuimarisha uwezo wa wanafunzi kujifunza kusoma na kuandika, ni muhimu mwalimu kuwa na mpango unaomwezesha kutumia maarifa mapya aliyojifunza wakati wa mafunzo ya walimu kazini kwa vitendo. Aidha ni muhimu kwa wanafunzi kuwa na muda zaidi wa kujifunza kusoma na kuandika. Kwa mantiki hii, ni muhimu kwa mwalimu kuandaa kipindi cha saa moja cha kusoma na kuandika mara moja kwa wiki. Ingawa kazi zifuatazo hazina uhusiano wa moja kwa moja ila mbinu zifuatazo zinaweza kutumika kusimamia darasa lolote na katika somo lolote. Aidha, zitakuwa na msaada wakati kwa kufundisha kusoma. Ni vema kuandaa namna utakavyoingiza mbinu hizi wakati wa kipindi cha wiki cha kusoma na kuandika. Matumizi ya mbinu ya kwanza: Uundaji shirikishi wa kanuni za darasani 1. Andika kanuni za darasani ubaoni. 2. Jadili na wanafunzi umuhimu wa kuwa na kanuni za darasa ambapo kila mwanafunzi atashiriki na kujifunza
kutoka kwa wengine. 3. Waulize wanafunzi ni aina gani ya kanuni wanafikiri ni muhimu. Ungependa ushirikiane na wenzako kwa namna
gani? Ungependa kushirikiana na mwalimu wako kwa namna gani? Ungependa mazingira ya darasani yawe katika hali gani?
4. Waongoze wanafunzi kujibu maswali 5. Andika ubaoni majibu yao 6. Kama baadhi ya wanafunzi wanapata ugumu kujibu maswali waulize kwa kutumia mifano na ikiwezekana wape
ushauri wako: Fikiri kabla ya kutenda Zingatia muda
Moduli ya Mwalimu 15
Shirikiana – Lakini omba unapotaka kutumia kitu cha mwanafunzi mwingine Kuwa msikivu mwenzako anapoongea Weka mazingira ya darasa katika hali ya usafi
7. Baada ya kubungua bongo kuhusu kanuni za darasa na wanafunzi, wape muda mchache wa kusoma kwa sauti. 8. Fafanua umuhimu wa wanafunzi wote kuridhia kanuni za darasani. 9. Baada ya kila mmoja kuridhia andika kanuni kwenye ubao wa darasa au andika kwenye karatasi na unaweza
kuwaonesha wanafunzi unapotaka kuwakumbusha kuhusu kanuni za darasa Matumizi ya mbinu ya pili: Kusimamia vikundi 1. Ligawe darasa katika vikundi, kila safu inaweza kuunda kikundi. 2. Waambie kila kikundi kichague jina la kikundi (kama vile rangi, majina ya viongozi mashuhuri, matunda au
wanyama) 3. Watangazie kuwa kila kikundi kinazo alama 10 za kuanzia. 4. Andika jina la kila kikundi ubaoni na weka alama kumi chini ya kila jina la kikundi 5. Waambie wanafunzi kuwa ikiwa mmoja wenu katika kikundi akitenda kosa la kinidhamu alama moja itatolewa
kwenye alama 10. 6. Jadili na wanafunzi maana ya nidhamu isiyofaa (mfano, mwanafunzi anaongea bila ruhusa wakati wa somo,
mwanafunzi anawasumbua wenzake wakati wa somo, au siyo msikivu wakati mwalimu anafundisha 7. Waambie wanafunzi wachangie kwa kutoa mifano maana ya neno ‘nidhamu isiyofaa’. 8. Punguza alama kwa wasio na nidhamu wakati unapofundisha; na mwisho wa kipindi watangazie wanafunzi ni
kikundi kipi kimeshinda kwa kubaki na alama nyingi . 9. Kikundi kilichoshinda kinaweza kupata upendeleo wa kutoka mapema kwenda mapumziko au kupewa majukumu
ya kufanya darasani kama vile kuwa kiongozi wa darasa n.k.
Jadili na mwenzako (dakika 15)
Kwa kushirikiana na mwenzako jadili namna unavyoweza kuingiza mbinu za kusimamia darasa katika andalio la somo kwa ajili ya kipindi cha wiki cha kusoma na kuandika. Andika kwenye daftari lako namna utakavyotumia mbinu hizi kwa darasa lako (Darasa la kwanza, darasa la pili, darasa la tatu). ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________
___________________________________________________________________________
Moduli ya Mwalimu 16
Mwisho (dakika 5) Jibu maswali yafuatayo
Mada ya kipindi:
Ni kwa namna gani umenufaika na malengo ya somo? Kipi kimekusaidia?
Ni mambo gani utapenda kujaribu kwenye darasa lako ndani ya mwezi mmoja ujao?
Kipi umekipenda katika kipindi cha leo?
Je kuna lolote linaloweza kufanyika kwa ajili ya kuboresha kipindi kijacho?
Andika taarifa ya kipindi kijacho:
Mada:
Tarehe na Muda:
Mahali:
Moduli ya Mwalimu 17
Kupima Utendaji Kazi (dakika 5)
Tafadhali tafakari jinsi mratibu wa MWK alivyofanya kazi leo. Jaza fomu ifuatayo kwa ajili ya tathmini yako. Fomu hii itakusanywa na Timu ya Wilaya ya MWK kwa ajili ya kuwasaidia waratibu wa MWK. Mwongozo wa Usahihishaji kwa ajili ya Waratibu wa MWK:
Alama 0:
Hajaweza kabisa
Alama 1:
Ameweza kidogo
Alama 2:
Ameweza kiasi cha kuridhisha
Alama 3:
Ameweza vizuri sana
Mratibu wa MWK hajaweza kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kidogo kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya kwa kiwango cha kuridhisha yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya vizuri sana yale yaliyoorodheshwa
Yale yaliyofanywa wakati wa kipindi cha MWK:
0
1
2
3
1. Maandalizi: Maratibu wa MWK amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia
2. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu
3. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika
4. Ufundishaji na ushauri: Mratibu wa MWK anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini MWK ni muhimu kwetu
5. Ufundishaji na ushauri : Mratibu wa MWK anatoa ushirikiano – anafuatilia maendeleo yetu kujua kama tunatumia mbinu mpya darasani na anatusaidia pale anapoona tuna tatizo
Alama za jumla: /15 x 100% = ________
Moduli ya Mwalimu 18
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Tatu: TaThmini ya Wanafunzi na msaada kWa Wanafunzi Wanaojifunza kWa shida
Moduli ya Mwalimu
Moduli ya Mwalimu 2
Moduli ya Mwalimu 3
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Tatu: TaThmini ya Wanafunzi na msaada kWa Wanafunzi Wanaojifunza kWa shida
Moduli ya Mwalimu
Moduli ya Mwalimu 4
Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:
Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma
Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa EQuiP-Tanzania
Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:
C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.u ndala C.C.U Kasulu
C.C.U Kabanga C.C.u BundaC.C.U Tarime
C.C.u shinyangaC.C.U Mpwapwa
Moduli ya Mwalimu 5
Maelekezo na taswira katika moduli
Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:
Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.
Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.
Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.
Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.
Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.
Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.
Moduli ya Mwalimu 6
Moduli ya Tatu: Tathmini ya Wanafunzi na Msaada kwa Wanafunzi Wanaojifunza kwa Shida
MAUDHUI YA MODULI: Moduli hii inamwongoza mwalimu kutathmini kwa haraka kiwango cha kujifunza cha wanafunzi wakati wa somo ili kupima kwa kiasi gani wanafunzi wanafikia malengo ya somo. Vilevile inajadili, mwalimu afanye nini iwapo wanafunzi wanashindwa kuelewa dhana mpya. DHANA KUU:
Tathmini – mchakato wa kupima uelewa wa wanafunzi katika somo au dhana. Inaweza kufanywa wakati wote wa somo au mwisho wa kipindi au kwa muda maalumu.
Utofautishaji – kurekebisha sehemu ya somo ili ilingane na uwezo tofauti wa wanafunzi katika kujifunza.
MALENGO YA MODULI: Washiriki wakifika mwishoni mwa moduli hii, waweze:
Kupanga na kutoa tathmini rahisi ya shughuli za wanafunzi ambayo itasaidia kupata uelewa na ufahamu wa wanafunzi
Kutekeleza mikakati ya kusaidia wanafunzi walio na matatizo ya kujifunza
MAANDALIZI YA KIPINDI: Tafuta changarawe au jiwedogo uje nalo katika kipindi.
UTARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI:
1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama inavyoonekana katika picha
2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki wote waonane na kuongea pamoja
3. Kuwa huru kuuliza maswali kama hujaelewa 4. Kuwa wa msaada kwa wenzako
Kuwa mbunifu na fikiria jinsi dhana unazojifunza zinahusiana na darasa lako
5. Weka simu yako katika hali ya mtetemo
• Mara zote uwe na Moduli yako ya Mafunzo ya Walimu Kazini na kalamu• Tafuta changarawe au jiwe dogo uje nalo katika kipindi
Moduli ya Mwalimu 7
TAFAKARI Kipindi kilichopita tulijifunza kuhusu mikakati ya usimamizi fanisi wa darasa. Sasa kila mmoja aandike jambo moja alilofanikiwa na moja ambalo lilikuwa changamoto katika kutekeleza mikakati hiyo darasani wakati wa vipindi vya kusoma na kuandika.
Andika peke yako (dakika 5) Tafadhali andika kwenye visanduku mafanikio na changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutekeleza mikakati hii katika darasa lako.
Jadiliana katika kikundi (dakika 10) Shirikisha wenzako kwenye kundi mojawapo ya uzoefu huo. Kwa kila changamoto, jaribu kutoa suluhisho lako kwa ajili ya kutatua changamoto za
wenzako. Wakati wa majadiliano, andika ufumbuzi unaoendana na changamoto ulizobainisha.
Ufumbuzi Unaowezekana (Mawazo muhimu kwa wenzetu)
Mafanikio (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)
Changamoto (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua changamoto zake)
Moduli ya Mwalimu 8
UTANGULIZI
Zoezi la Kuchangamsha (dakika 10)
Kalamu na Changarawe: Weka kalamu na changarawe yako juu ya meza yako. Sikiliza kauli zinazosomwa na mwezeshaji wako.
Kama kauli ni ya kweli kamata kalamu yako na uinyanyue juu (tazama picha hapo chini). Kama kauli sio ya kweli kamata changarawe yako uinyanyue juu . (tazama picha hapo chini)
�
Fikiri –Wawili wawili – Shirikishana (dakika 10) Jadili maswali yafuatayo na mwenzako. Baadaye tutashirikishana katika vikundi.
1. Katika zoezi hili mlitakiwa kufanya nini? 2. Mratibu wa Mafunzo anaweza kupima nini? 3. Kazi hii inaweza kuwa na manufaa kwa mwalimu? Kwanini? 4. Je, unaweza kuliboresha zoezi hili lifae kutumika darasani kwako?
Moduli ya Mwalimu 9
1. Mwalimu mmoja anaanza kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha aya anamwita mwalimu mwingine kwa jina asome aya inayofuata.
2. Wakati unaposoma: -‐Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu -‐Weka alama ya (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo -‐Weka mduara katika maneno ambayo ni mapya.
DHANA KUU
Umuhimu wa tathmini endelevu wakati wa kufundisha (dakika 10)
Tathmini ya wanafunzi inasaidia walimu kujua kama wanafunzi wamefikia lengo lililowekwa la kusoma na kuandika. Kama wanafunzi hawajafikia lengo ina maana kwamba bado hawajaelewa yaliyofundishwa katika somo hilo. Vilevile tathmini ya wanafunzi inasaidia walimu kuchukua hatua ili kuweza kujiandaa vyema zaidi na kuandaa vipindi muhimu vya kupitia yale waliyofundisha.
Je kutathmini wanafunzi kunamsaidiaje mwalimu?
Walimu wanaweza: -‐ Kufahamu kama wanafunzi wameweza kufikia
lengo la somo; -‐ Kuthibitisha ufahamu wa wanafunzi katika somo; -‐ Kuthibitisha jinsi wanafunzi wanavyofanikiwa na
kwa kiwango gani; -‐ Kupima idadi ya wanafunzi wanaofahamu dhana
zilizofundishwa na idadi ya wale wanaohitaji mazoezi na msaada zaidi.
-‐ Kuandaa masomo ya kufundisha kwa wakati ujao.
Je, tathmini zinamsaidiaje mwanafunzi?
Wanafunzi wanaweza: -‐ Kufahamu ni makosa gani wanayofanya; -‐ Kupima uelewa na ufahamu wao wenyewe na
kutambua maeneo wanayohitaji msaada ; -‐ Kuinua ubora na kasi ya kuelewa dhana
zinazofundishwa. -‐ Kujijengea hali ya kujiamini kulingana na uwezo
wao; -‐ Kusaidia wenzao wenye matatizo ya kujifunza .
Tathmini za Wanafunzi siyo lazima ziwe za kufanya majaribio ya kuandika kwenye karatasi mwishoni mwa kila sura ya kitabu cha kiada. Tathmini za mwanafunzi zinaweza na zinapaswa kufanyika wakati wote kwa kila somo unalofundisha. Kuna aina kuu mbili za tathmini unazoweza kutumia wakati wa kufundisha:
Moduli ya Mwalimu 10
TATHMINI-‐UFAFANUZI
Tathmini Endelevu
Ni mchakato wanaoutumia walimu wakati wa kufundisha ili kupata mrejesho wa kuwezesha kurekebisha ufundishaji unaoendelea ili kuinua uwezo wa wanafunzi kufikia malengo ya kujifunza.
Tathmini Tamati
Shughuli rasmi za tathmini ambazo zinaonesha hatua waliyofikia wanafunzi katika kipindi maalumu
Baada ya kupima kiwango cha wanafunzi cha kujifunza kutokana na tathmini endelevu, walimu wanaweza kurekebisha mikakati yao ya ufundishaji kulingana na mahitaji. Mfano, ikiwa tathmini endelevu inaonesha kuwa wanafunzi hawaelewi dhana fulani, inabidi mwalimu ajaribu kuelezea dhana hiyo kwa kutumia njia nyingine au atumie mifano mingine mipya. Vilevile mwalimu anaweza kutumia tathmini endelevu kubaini wanafunzi wenye shida zaidi katika kujifunza na kuwapa msaada stahiki.
Jadiliana katika kikundi kikubwa (dakika 5)
Ni sehemu gani katika matini ya hapo juu ambayo unaona ni ya muhimu, haieleweki au mpya?
Zoezi (dakika 5) Zungushia duara aina ya tathmini iliyo sahihi (tathmini endelevu, tathmini tamati, au zote mbili)
kulingana na maelezo ya aina za tathmini katika jedwali hapo chini. Mara baada ya kuzungushia duara, ukiwa katika kikundi, jadili majibu na kutoa maelezo ya kina zaidi.
Maelezo ya aina za Tathmini Aina ya Tathmini
1) Inatathmini rasmi uwezo/maarifa kwa kipindi maalumu (mfano: mwishoni mwa sura au mwishoni mwa nusu mhula n.k)
Tathmini Endelevu
Tathmini ya Tamati
Zote mbili
2) Inawapa walimu taswira ya ufahamu wa wanafunzi wakati wote wa somo.
Tathmini Endelevu
Tathmini ya Tamati
Zote mbili
3) Inawapa wanafunzi fursa ya kuonesha ufahamu wao. Tathmini Endelevu
Tathmini ya Tamati
Zote mbili
ZOEZI
Mikakati ya Tathmini Endelevu (dakika 10)
Kuna njia nyingi za haraka za kutathmini ujifunzaji wa wanafunzi wakati somo linaendelea. Ifuatayo ni mikakati minne ambayo unaweza kutumia hata katika madarasa makubwa:
ZOEZI
Moduli ya Mwalimu 11
Kalamu na Changarawe-‐ Waambie wanafunzi kila mmoja aje na changarawe moja darasani. Waambie waweke kalamu zao na changarawe katika madawati yao. Waambie wanafunzi kuwa utasoma kauli zinazotokana na somo unalofundisha. Kama wanafikiri kauli hiyo ni ya kweli, washike kalamu zao mkononi na kuinua juu. Kama wanafikiri kuwa usemi huo siyo kweli, wachukue changarawe zao na wainue juu. Mfano, baada ya kujifunza siku za juma, unaweza kutengeneza kauli ifuatayo: “Jumatano ni siku ya kwanza ya juma”. Kama ilivyo katika shughuli uliyofanya mwanzoni mwa moduli, aina hii ya mkakati wa tathmini inasaidia kupima kama wanafunzi wanaelewa dhana ambazo umekuwa ukifundisha.
Mchezo wa kulala-‐ Waambie wanafunzi waweke viganja vya mikono yao usoni na wainamishe vichwa vyao kwenye madawati wakiwa wamefumba macho kama vile wamelala (waambie wasifumbue macho!) Waambie wanafunzi utatamka semi ambazo zinauhusiano na somo unalofundisha. Kama wanafikiri kauli hiyo ni ya kweli, wainue mikono yao (wakiwa wameweka vichwa vyao chini). Kama wanafikiri kuwa usemi huo siyo kweli, wasiinue mikono yao. Mchezo wa kulala unafanana na ule wa Kalamu na Changarawe, lakini mchezo huu unawapa wanafunzi fursa ya kujibu kwa uaminifu bila kuangalia wenzao kupata jibu sahihi.
Mchezo wa Nioneshe -‐ Kuhakiki kama wanafunzi wanaelewa unachofundisha, waambie wanafunzi kuwa utauliza swali la haraka na wanatakiwa kuandika jibu katika karatasi (au nyuma ya daftari zao). Wakimaliza wainue karatasi zao juu uzione. Mfano, ikiwa unafundisha silabi, unaweza kuuliza, “Andika silabi ba." Kisha wanafunzi wakuoneshe majibu yao. Unaweza kuendelea na mchezo huu kwa kusema, “Sasa andika silabi bo”
Okota kwa Kubahatisha Wanafunzi waandike majina yao katika vitu vya kudumu kama vile, vipande vya
makasha (kutoka makasha yaliyotupwa), kifuniko cha chupa au hata kipande cha jiwe kilicho na uso laini. Weka vitu vyote katika mkoba, kasha au ndoo na uwe navyo katika kila somo. Wakati unapouliza swali, chomoa kwa kubahatisha kitu kimojawapo kutoka katika mkoba, kasha au ndoo na mwanafunzi ambae jina lake lipo katika kitu hicho ajibu swali. Mbinu hii inasaidia kuchagua wanaojibu kwa njia ya kubahatisha. Hii ina maana kuwa wanafunzi ambao wananyoosha mikono mara kwa mara hawatawali majadiliano ya darasani (na tathmini). Vilevile inasaidia kupata majibu zaidi ya yale
ya ndio au hapana.
Igizo (dakika 20)
Kila mwalimu achague mojawapo kati ya mikakati minne ya tathmini endelevu iliyoelezwa hapo juu (Kalamu na Changarawe, Mchezo wa Kulala, mchezo wa Nioneshe na Kuokota kwa Kubahatisha). Kila mwalimu aandae igizo dhima ambapo yeye ni mwalimu na walimu wengine ni wanafunzi wake. Tumia mkakati wako wa tathmini uliochagua kutathmini ujifunzaji wa wanafunzi katika mada unayofundisha katika somo la Kiswahili, kama vile, herufi, rangi, siku za juma au mada nyingine katika muhtasari. Mfano, kama ukichagua kutathmini wanafunzi kuhusu uelewa wao wa rangi na umechagua kutumia mkakati wa Mchezo wa Kulala, andika semi ambazo ni kweli au siyo kweli ambazo wanafunzi wanaweza kuchagua jibu (kama vile, ‘majani ya mti ni ya zambarau’). Una dakika 10 kujiandaa. Baada ya hapo kila mwalimu ataonesha igizo lake kwa kupokezana.
Moduli ya Mwalimu 12
Fikiri –Wawili wawili-‐ Shirikishana (dakika 5)
Ni kwa namna gani kila mkakati umesaidia kutathmini uelewa wa wanafunzi? Utawezaje kutekeleza mikakati hii darasani kwako? Kwa namna gani utaitumia hiyo mikakati? Kuna mikakati mingine ya tathmini endelevu ambayo imekujia kichwani kwako wakati ukiwa sehemu ya igizo
dhima?
Mikakati ya Kusaidia Wanafunzi Wanaopata Shida Kujifunza (dakika 15)
Unapotathmini wanafunzi wakati wote wa somo, unaweza kuona wanafunzi wengi ambao hawajaelewa dhana fulani. Katika hali kama hii inabidi ufundishe upya maudhui ya mada husika, utumie njia bora zaidi ya kuelezea maudhui hayo au kutoa mifano zaidi. Hata hivyo, pamoja na kwamba wanafunzi wengi watakuwa wamefikia malengo yaliyowekwa, bado wapo wanafunzi wachache ambao watakuwa na shida ya kujifunza. Unatakiwa kuhakikisha kuwa wanafunzi hawa wanaopata shida kujifunza wanakuwa na mwelekeo chanya na hawakati tamaa pamoja na kwamba wako nyuma ya wenzao. Ifuatayo ni mikakati ya kusaidia wanafunzi wanaopata shida kujifunza:
Kazi Zilizotofautishwa: Kama unafahamu kwamba mwanafunzi anayepata shida kujifunza hataweza kukamilisha zoezi, panga marekebisho rahisi katika ufundishaji wako ili wanafunzi wa aina hii waweze kukamilisha kazi wanazopewa. Mfano, Kama wanafunzi wa Darasa la 2 wanaandika matini kuhusu walichofanya mwisho wa juma, wanafunzi wanaopata shida kujifunza wanaweza kuchora picha kwanza na baadaye wajikite tu katika kuandika maneno ya msingi, ‘kaka,’ kuku’, ‘chipsi’.
Wawili Wawili Kimkakati-‐ Wanafunzi wanaopata shida kujifunza, mara nyingi hujifunza kujenga stadi zao kutoka kwa wenzao ambao wako mbele katika kujifunza. Kuweka mkakati wa kuchagua mwenzao anayeweza kusaidia mwanafunzi anayepata shida kujifunza, ni fursa nzuri ya kuwapa msaada binafsi ambao wasingeupata wakiwa katika darasa kubwa. Mfano, baada ya mwanafunzi anayepata shida kujifunza kuandika maneno ya msingi kuhusu mwisho wa juma (kaka, kuku, chipsi), mwenzake anaweza kumsaidia kuandika maneno yaliyorukwa kukamilisha sentensi (‘Kaka yangu amepika kuku na chipsi’).
Mpangilio wa Kukaa-‐ Wakati mwingine wanafunzi wanaopata shida katika somo, utakuta wana uono hafifu. Jaribu kuweka wanafunzi wa aina hii mbele ya darasa kupunguza vikwazo na kuwarahisishia kuona maudhui ya somo na vifaa. Hakikisha unawaambia wanafunzi kwamba, kukaa mbele ya darasa ni upendeleo na siyo kwa sababu ya kutoelewa. .
Msaada wa ziada-‐ Ikiwa darasa linafanya mazoezi binafsi, unaweza kutoa msaada wa ziada wa pamoja kwa wanafunzi wengi kwa kuwaketisha karibu karibu. Mfano, waketishe wanafunzi wenye shida ya kujifunza mbele ya darasa (kwa mara nyingine waeleze kwamba ni upendeleo) ili kuwapa msaada wa karibu wanapofanya mazoezi.
Moduli ya Mwalimu 13
Muda wa kusubiri-‐unapowaita wanafunzi wenye shida ya kujifunza kujibu maswali darasani, wape muda mrefu wa kufikiria maswali. Unaweza kuhesabu kichwani mwako taratibu kuanzia moja hadi tano kuhakikisha kuwa umetoa muda wa kutosha wa kufikiria na kutoa jibu. Mara nyingi ni vigumu mwalimu kutoa muda huu wa kusubiri, lakini unaweza kuwa wa thamani. Vile vile ni muhimu kufafanua maswali au kuwapa maelekezo zaidi. Ni muhimu kwa wanafunzi wenye shida ya kujifunza kukuza uwezo wa kujiamini. Hakikisha unawasaidia kufikia jibu sahihi.
Jadili katika kikundi (dakika 5)
Kwa wastani, kuna wanafunzi wangapi wanaopata shida ya kujifunza darasani kwako? Unafikiri ni mikakati ipi kati ya hiyo inaweza kuwasaidia kufanya vizuri?
Je, kuna mikakati mingine unayoweza kutumia kusaidia wanafunzi wanaopata shida kujifunza? Jadiliana na walimu wenzako.
TATHMINI BINAFSI
Andika (dakika 5)
Tafadhali kamilisha tathmini binafsi ifuatayo. Weka X katika nafasi husika kuonesha kwa kiasi gani unatumia mkakati huo KATIKA DARASA LAKO. ZINGATIA: Tathmini hii binafsi ni ya kwako mwenyewe (huhitaji kumshirikisha mtu yeyote) na ni njia ya kujichunguza kuona uwezo ulionao na ni maeneo gani unahitaji kujiimarisha katika utendaji wako.
Tathmini na Mikakati ya Kusaidia Sielewi Naelewa lakini sifanyi
Nafanya lakini naweza
kufanya vizuri zadi
Nafanya vizuri sana
Natengeneza na kutoa aina mbalimbali za tathmini tamati kufuatilia uelewa wa wanafunzi.
Natengeneza na kutoa aina mbalimbali za tathmini endelezi kufuatilia uelewa wa wanafunzi.
Narekebisha ufundishaji wangu kulingana na matokeo ya tathmini na ninarudia kufundisha maudhui ya mada inapobidi.
Natoa muda wa ziada wa kusubiri kwa wanafunzi wanaopata shida kujifunza wakati wanapojibu maswali au wanapokamilisha kazi.
Najitahidi kujenga uwezo wa kujiamini wa wanafunzi wanaopata shida ya kujifunza ili wasijione ni wajinga.
Wakati wa kuuliza maswali darasani, nachagua wanafunzi tofauti tofauti na siyo lazima wale wanaonyoosha mikono yao kwanza.
Nabaini wanafunzi wanaopata shida kujifunza na kuweka mikakati ya kuwasaidia.
Moduli ya Mwalimu 14
KUPANGA MKAKATI
Kupanga ‘Kipindi cha Kusoma na Kuandika’ (dakika 15)
Ili kuimarisha uwezo wa wanafunzi wa kusoma, ni muhimu walimu waweze kutumia mbinu mpya za kusoma na kuandika ambazo wamejifunza katika MWK. Vile vile ni muhimu wanafunzi wapate muda maalumu wa kusoma. Hii ndiyo maana ni muhimu kuwa na kipindi cha kusoma na kuandika mara moja kwa juma (kando ya kipindi cha Kiswahili). Pamoja na kuwa shughuli zinazofuata hazina uhusiano mahususi katika kusoma na kuandika (zinaweza kutumika kutathmini na kusaidia wanafunzi katika darasa lolote na somo lolote) lakini zitasaidia katika kufundisha wanafunzi kusoma. Tafadhali jaribu kutumia shughuli hizi katika kipindi chako cha kusoma na kuandika.
Kitendo cha Matumizi #1: Tathmini ya Kuokota kwa Kubahatisha Maandalizi
1) Kabla ya siku ya somo, waagize wanafunzi walete vitu vidogo vilivyoandikwa majina yao (kifuniko cha chupa, kipande cha kasha, au kipande cha jiwe chenye uso laini). Vitu vya kudumu vinaweza kutumika mwaka mzima lakini karatasi zinaweza kutumika vile vile.
2) Tafuta mkoba, kasha au ndoo kwa ajili ya kuwekea vitu vya wanafunzi. 3) Tayarisha orodha ya maswali ya kutathmini ujifunzaji wa wanafunzi katika mada ambayo unafundisha au
ambayo umeifundisha karibuni. Jiandae kuuliza wanafunzi maswali yapatayo 10-‐20.
Kitendo Muhimu cha Ufundishaji
1) Waambie wanafunzi kwamba kutakuwa na mapitio ya kujifunza. Waeleze kuwa utaokota jina kwa kubahatisha, na mwanafunzi mwenye jina hilo lazima ajibu swali atakalopewa. Wasisitizie kuwa yeyote anaweza kuitwa jina kwa hivyo wasikilize kwa makini wakati wote.
2) Anza kitendo, lakini hakikisha unawapa wanafunzi sekunde chache za kusubiri kabla ya kujibu swali. Kama wanashindwa kupata jibu, angalia kama unaweza kuwadokezea ili wafikie jibu sahihi. Vile vile unaweza kuchagua mwanafunzi mwingine adokeze jibu. .
3) Baada ya swali, tumia dakika chache kuelezea jibu sahihi. Hii ni nafasi nyingine ya kujifunza maudhui kwa wanafunzi wanaopata shida kujifunza.
Matendo
1) Katika vikundi vidogo (au dawati kwa dawati) wanafunzi wafanye kwa pamoja kitendo cha kuokota kwa kubahatisha. Kila mmoja aandike jina lake katika kikaratasi. Baada ya hapo wanabadilishana kuwa ‘mwalimu’ na kuokota jina la kujibu mojawapo ya maswali ya mapitio. Wanaweza kurudia maswali ya mwalimu au kufikiria maswali yao mengine ya mapitio.
2) Zunguka darasani kufuatilia wanafunzi. Weka kumbukumbu ya mada ambazo zinaonekana zina utata kwa wanafunzi wengi na ambazo zitahitaji kufundishwa upya.
KUPANGA MKAKATI
Moduli ya Mwalimu 15
Kitendo cha Matumizi # 2: Wawili wawili Kimkakati Maandalizi
1) Waambie wanafunzi kwamba, lengo la somo la leo ni kuwafanya wanafunzi kufanya kazi katika jozi (wawili wawili) na mwenzake ambaye hawafahamiani vizuri. Lengo lingine ni kujenga timu nzuri ambapo mmoja wao anaweza kusaidia mwenzake inapohitajika.
2) Mwalimu utaanza mchakato wa kuwaweka wanafunzi wawili wawili. Anza kwa kuwaweka mbele ya darasa wanafunzi wanaopata shida kujifunza. Hii itahakikisha kwamba, wanaona ubao vizuri na kusikia maelezo vizuri. Baada ya hapa, waweke pia wanafunzi wanaojiweza mbele ya darasa na kuhakikisha kila jozi ina mwanafunzi anayejiweza na mwanafunzi ambaye anapata shida kujifunza.
3) Baada ya kupata jozi hizo, wanafunzi wengine wakae katika jozi na wenzao ambao hawafahamiani vizuri au kukaa pamoja.
4) Waeleze wanafunzi wote kwamba, lengo ni kusaidia wenzao wakati wa somo. Hata hivyo, wawasaidie wenzao pale inapohitajika.
Kitendo muhimu cha ufundishaji:
1) Waambie wanafunzi kwamba, utafundisha mtoto wa shule ya awali kupiga mswaki meno yake. Kwa hivyo itabidi utoe maelekezo fasaha na kueleza namna ya kufanya kwa usahihi.
2) Waambie wanafunzi kwamba, hatua ya kwanza wakati wa kupiga mswaki meno yako ni kuchukua mswaki. Kisha andika sentensi hiyo katika ubao wakati unasema kila neno unavyoendelea kuandika. Mfano:
3) Waulize wanafunzi wakueleze hatua inayofuata. Andika hatua hiyo ubaoni.
4) Endelea kuuliza wanafunzi hatua inayofuata na andika kila hatua katika ubao. 5) Baada ya kuandika hatua zote katika ubao, soma maandiko hayo kwa sauti mbele ya darasa wakati huo huo unaonesha kila neno unalosoma. Matendo Binafsi
1) Wanafunzi wa Darasa la 1: Waambie wanafunzi wasome maelekezo katika ubao pamoja na wenzao katika jozi. Baada ya hapo watachora picha kwa kila hatua (Mfano, picha ya kwanza itaonesha mtoto akichukua mswaki). Waambie wanafunzi kwamba, wanaweza kuwaomba wenzao kuwasaidia kuelewa hatua yeyote iliyoandikwa katika ubao kama hawawezi kusoma ubaoni au hawakumbuki.
2) Darasa la 2: Futa neno moja katika kila sentensi. Waambie wanafunzi waandike upya maelekezo katika
madaftari yao na kuweka maneno yanayokosekana. Waambie wanafunzi kwamba, wanaweza kuomba msaada kwa wenzao katika jozi kuandika au kukumbuka maneno yeyote ambayo yanawatatiza.
3) Darasa la 3: Futa hatua zote. Waambie wanafunzi waandike upya maelekezo wanayoyakumbuka.
Waambie wanafunzi kwamba wanaweza kuomba msaada kwa wenzao katika jozi kukumbuka hatua yeyote au kutamka herufi moja moja katika neno lolote.
2. Weka dawa ya mswaki katika mswaki.
1. Chukua mswaki
Moduli ya Mwalimu 16
Jadili na mwenzako (dakika 15)
Wewe na mwenzako, jadili namna unavyoweza kuingiza vitendo hivyo viwili katika andalio lako la somo katika vipindi viwili vijavyo vya kusoma na kuandika. Tafadhali andika mawazo yako, hasa namna utakavyotumia vitendo hivyo kulingana na kiwango cha darasa lako ( darasa la 1, 2 au 3). Baada ya majadiliano, wasilisha katika kikundi cha wote. _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________________________
Mwisho (dakika 5)
Jibu maswali yafuatayo mwenyewe. Mada ya kipindi cha mafunzo: Ni kwa namna gani umenufaika na malengo ya somo? Kipi kimekusaidia? Ni mambo gani utapenda kujaribu kwenye darasa lako ndani ya mwezi mmoja ujao? Kipi umekipenda katika kipindi cha leo cha mafunzo? Je kuna lolote linaloweza kufanyika kwa ajili ya kuboresha kipindi kijacho cha mafunzo?
Moduli ya Mwalimu 17
Andika taarifa ya kipindi kijacho :
Mada:
Tarehe na Muda:
Mahali:
Kupima Utendaji Kazi (dakika 5)
Tafadhali tafakari jinsi mratibu wa MWK alivyofanya kazi leo. Jaza fomu ifuatayo kwa ajili ya kumbukumbu ya upimaji wako. Fomu hii itakusanywa na Timu ya Wilaya ya MWK kwa ajili ya kuwasaidia waratibu wa MWK. Mwongozo wa kutoa alama kupima utendaji kazi wa Waratibu wa MWK: Alama 0: Hajaweza kabisa
Alama 1: Ameweza kidogo
Alama 2: Ameweza kiasi cha kuridhisha
Alama 3: Ameweza vizuri sana
Mratibu wa MWK hajaweza kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kidogo kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya kwa kiwango cha kuridhisha yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya vizuri sana yale yaliyoorodheshwa
Kazi zilizotekelezwa wakati wa kipindi cha Mafunzo Kazini:
0 1
2
3
1. Maandalizi: Mratibu wa mafunzo amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia
2. Uwezeshaji: Mratibu wa mafunzo anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu
3. Uwezeshaji: Mratibu wa mafunzo anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika
4. Kuelekeza na kushauri: Mratibu wa mafunzo anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini mafunzo kazini ni muhimu kwetu
5. Kuelekezana kushauri : Mratibu wa mafunzo anatoa ushirikiano – anafuatilia maendeleo yetu kujua kama tunatumia mbinu mpya darasani na anatusaidia pale anapoona tuna tatizo
Alama za jumla: /15 x 100% = ________
Moduli ya Mwalimu 18
Moduli ya Mwalimu 20
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Nne: Kuongeza usawa wa
Kijinsia na ushiriKi
Moduli ya Walimu
Moduli ya Mwalimu 2
Moduli ya Mwalimu 3
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO
Moduli ya Nne: Kuongeza usawa wa
Kijinsia na ushiriKi
Moduli ya Walimu
Moduli ya Mwalimu 4
Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:
wizara ya elimu na Mafunzo ya ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma
Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa EQUIP-Tanzania
Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:
C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.u ndala C.C.U Kasulu
C.C.U Kabanga C.C.u BundaC.C.U Tarime
C.C.u shinyangaC.C.U Mpwapwa
Moduli ya Mwalimu 5
Maelekezo na taswira katika moduli
Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:
Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.
Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.
Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.
Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.
Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.
Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.
Moduli ya Mwalimu 6
Moduli ya Nne: Kuongeza Usawa wa Kijinsia na Ushiriki
MAUDHUI YA MODULI: Moduli hii inamwelekeza mwalimu ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia jinsia. Walimu wanaozingatia jinsia wanasahihisha kwa vitendo kuegemea upande mmoja wa jinsia na ubaguzi wa kijinsia darasani. Mfano, wanahakikisha kwamba lugha inayotumika haichochei mwelekeo hasi wa kijinsia, wavulana hawatawali darasa na vifaa vya kufundishia na kujifunzia havina masuala ya kijinsia ambayo ni ya mazoea. Moduli hii itamsaidia mwalimu kutumia misingi ya usawa wa kijinsia ili wanafunzi wote wapate fursa sawa za kujifunza kufikia kiwango chao cha juu. DHANA KUU: Usawa wa kijinsia: Kutoa huduma kwa usawa, matumizi ya vifaa kwa usawa na kutoa fursa sawa kwa
wasichana na wavulana. Katika utoaji wa elimu inahusu kuhakikisha kwamba wasichana na wavulana wanapata fursa sawa kuandikishwa shuleni, wanafundishwa kwa usawa na wanapata vifaa na fursa zingine za kielimu kwa usawa.
Ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia jinsia: Hii inahusu walimu kusahihisha kwa vitendo kuegemea upande mmoja wa kijinsia na ubaguzi wa kijinsia ili kuhakikisha usawa wa kijinsia kupitia mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji.
Ushiriki wa wanafunzi: Wanafunzi kushirikishwa kikamilifu katika kutoa mrejesho na taarifa kwa walimu.
MALENGO YA MODULI: Mwisho wa moduli hii, walimu wawe wameweza:
kueleza namna jinsia inavyoweza kuathiri ujifunzaji kubainisha maeneo ya ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia jinsia Kutumia mbinu za kufundishia ambazo zinawafanya wanafunzi wote kushiriki vizuri, hasa katika madarasa
makubwa.
MAANDALIZI YA KIPINDI: Mara zote uwe na Moduli yako ya Mafunzo ya Walimu Kazini na kalamu TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI:
1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama inavyoonekana katika picha
2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki wote waonane na kuongea pamoja
3. Kuwa huru kuuliza maswali kama hujaelewa 4. Kuwa wa msaada kwa wenzako 5. Kuwa mbunifu na fikiria jinsi dhana unazojifunza
zinahusiana na darasa lako 6. Weka simu yako katika hali ya mtetemo
Moduli ya Mwalimu 7
TAFAKARI Kipindi kilichopita tulijifunza kuhusu mikakati ya Tathmini fanisi ya Wanafunzi. Muda huu kila mmoja aandike jambo moja alilofanikiwa na moja ambalo lilikuwa changamoto katika kutekeleza mikakati hiyo darasani wakati wa vipindi vya kusoma na kuandika.
Andika peke yako (dakika 5) Tafadhali andika kwenye kisanduku mafanikio na changamoto ulizopata wakati wa kutumia mbinu hizo darasani kwako.
Jadiliana katika kikundi (dakika 10) Elezea mojawapo ya uzoefu huo kwenye kundi. Kwa kila changamoto, jaribu kutoa ufumbuzi wako kwa ajili ya kutatua changamoto za
wenzako. Wakati wa majadiliano, andika ufumbuzi unaoendana na changamoto ulizobainisha.
Ufumbuzi Unaowezekana (Mawazo muhimu kwa wenzetu)
Mafanikio (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)
(Elezea utar
Moduli ya Mwalimu 8
UTANGULIZI
Fikiri –Wawili wawili – Shirikishana (dakika 15)
Mawazo kuhusu majukumu ya wanaume na wanawake katika jamii yanaweza kuchochewa na taswira katika vitabu vya kiada. Angalia picha zifuatazo ambazo zimechukuliwa katika kitabu kimoja cha kiada na angalia shughuli au mwonekano wa jinsia. Kisha jibu maswali yanayofuata chini yake.
1. Wanaume wana majukumu gani? 2. Wanawake wana majukumu gani? 3. Mazoea gani ya kijinsia yanayooneshwa? 4. Unafikiri ni muhimu kubadilisha vielelezo hivi? Kwa namna gani?
Moduli ya Mwalimu 9
1. Mwalimu mmoja anaanza kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha aya anamwita mwalimu mwingine kwa jina asome aya inayofuata.
2. Wakati unaposoma: -‐Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu -‐Weka alama ya (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo -‐Weka mduara katika maneno ambayo ni mapya.
DHANA KUU Ufundishaji na Ujifunzaji Unaozingatia Jinsia (dakika 15)
Uchunguzi wa utendaji darasani unaonesha kwamba, ufundishaji na ujifunzaji kwa kiasi kikubwa umeegemea upande mmoja wa jinsia. Walimu wengi wanatumia njia na mbinu ambazo haziwapi wasichana na wavulana fursa sawa kushiriki. Vile vile walimu wanatumia vifaa vya kufundishia na kujifunzia ambavyo vinaendeleza mazoea ya kijinsia. Kutokana na hali hii. Kuna haja ya kufanya haraka kuanzisha ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia jinsia.
Jinsia inahusu uhusiano na majukukumu ya wanawake na wanaume ambayo yamepangwa na jamii. Majukumu haya yamekuwa yakirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Pamoja na kwamba urithi huu unabidi kuthaminiwa, lakini ni muhimu majukumu ya kijinsia yasiingilie ujifunzaji wa watoto. Mawazo ambayo hayahojiwi kama vile, ‘wasichana ni mahiri katika usafi’ au ‘wavulana ni mahiri katika michezo,” yanaweza kukatisha tamaa mojawapo ya jinsia kushiriki hata kabla ya shughuli kuanza. Vile vile watoto wanaweza kufanyiwa mzaha kwa kufanya vizuri katika jambo ambalo ‘limehifadhiwa ‘kwa ajili ya upande mmoja wa jinsia. Zifuatazo ni dhana ambazo zinatumika sana wakati wa kujadili masuala ya jinsia:
1. Ubaguzi wa kijinsia: Kuwanyima fursa na haki au kutoa upendeleo kwa watu kulingana na jinsia yao.
2. Mazoea ya Kijinsia: Kuweka taswira mara kwa mara ya wanawake au wanaume wakiwa katika majukumu ya kijadi au mgawanyo wa kazi (katika vyombo vya habari, mazungumzo, utani au vitabu). Katika vitabu vya kiada vya wanafunzi, kwa mfano, wanawake wanaonekana kama wafanya usafi, walezi na wauguzi, na wanaume wanaonekana kama madereva, madakatari na viongozi.
3. Usawa wa kijinsia: Kutoa huduma kwa usawa, matumizi ya vifaa kwa usawa na kutoa fursa sawa kwa wasichana na wavulana. Katika utoaji wa elimu inahusu kuhakikisha kwamba wasichana na wavulana wanapata fursa sawa kuandikishwa shuleni, wanafundishwa kwa usawa na wanapata vifaa na fursa zingine za kielimu kwa usawa.
4. Ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia jinsia: Hii inahusu walimu kusahihisha kwa vitendo kuegemea upande mmoja wa kijinsia na ubaguzi wa kijinsia ili kuhakikisha usawa wa kijinsia kupitia mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji.
Katika darasa ambalo linazingatia jinsia, wavulana na wasichana wanahudumiwa kwa usawa, wanapewa fursa sawa za kujieleza na kushiriki kikamilifu. Walimu wanaozingatia jinsia wanahakikisha kwamba vifaa vya kujifunzia wanavyopewa au mazoezi yanahaririwa ili kurudisha usawa wa kijinsia. Mfano, wakati wa kuandika maswali ya zoezi, walimu wanaozingatia jinsia wanapinga mazoea ya kijinsia kwa kuandika, ‘Kaka anapika’ badala ya ‘Mama anapika’. Zaidi ya yote, walimu wanaozingatia jinsia wanahakikisha shughuli za darasani kama vile kazi za vikundi
Moduli ya Mwalimu 10
na majadiliano yanaongozwa kwa usawa kati ya wavulana na wasichana.
Jadiliana katika kikundi kikubwa (dakika 10)
1. Sehemu zipi za matini uliyosoma ni muhimu, haieleweki au ni mpya? 2. Unafikiri unatumia njia za kufundishia na kujifunzia zinazozingatia jinsia? 3. Unawezaje kufanya ufundishaji na ujifunzaji uzingatie jinsia zaidi?
Mshirikishe mwenzako katika kuoanisha hali ya ufundishaji na mikakati ya uwajibikaji wa kijinsia kwa kujaza kwenye karatasi ya maswali na majibu (dakika 15)
. Jihadhari, wakati mwingine kuna majibu zaidi ya moja. . Pia, kama kuna njia nyingine kwa ajili ya kutatua tatizo mojawapo, tafadhali andika njia hizo. Baada ya kumaliza, Kila kikundi cha watu wawili kisome majibu katika darasa
Hali ya Ufundishaji Mikakati ya Uwajibikaji wa kijinsia
1. Mpangilio wa darasa Njia zinazoweza kutatua:____ Njia nyingine:
A. Epuka misemo ambayo itawafanya wavulan au wasichana
kujisikia wao ni bora au duni kuliko wengine. Mfano, wavulana wasifanywe kujisikia wanaposhindwa michezo wanakuwa kama wasichana au wasichana wanaoongea kwa sauti kubwa au wanaopenda kuongoza wasikatishwe tamaa kufanya hivyo.
B. Kuwa msikivu kwa mahitaji yanayogusa hisia za wanafunzi. Weka ‘sanduku la matatizo’ katika dawati lako. Au, waeleze wanafunzi wako kwamba wanaweza kukuona wakati wowote wakijisikia hawakutendewa haki.
C. Hakikisha kwamba wasichana na wavulana wanapata fursa sawa ya kukaa mbele ya darasa, hasa wasichana wenye aibu ambao wanaweza kuhitaji msaada kuweza kushiriki vizuri katika somo.
D. Panga wavulana na wasichana kwa kupokezana unapowapa majukumu kama vile, , kiranja wa darasa, kiranja mkuu, kiranja wa zamu n.k
E. Tumia mifano na mazoezi ambayo yanapinga mazoea ya kijinsia. (mfano, ‘Baba anasafisha nyumba’).
2. Usafi wa darasa Njia zinazoweza kutatua:____ Njia nyingine:
3. Kuepuka kukuza ubaguzi wa kijinsia Njia zinazoweza kutatua:____ Njia nyingine:
4. Kuwahamasisha wanafunzi kuwaheshimu wenzao, walimu na jamii nzima
Njia zinazoweza kutatua:____ Njia nyingine:
Moduli ya Mwalimu 11
5. Wavulana na wasichana kupewa fursa sawa za majukumu ya uongozi
Njia zinazoweza kutatua:____ Njia nyingine:
F. Unapoona mvulana anamnyanyasa msichana, mwalimu anaweza kuonesha kuguswa na suala hilo kwa kumrudi mhalifu lakini hakikisha darasa zima linaona umuhimu wa heshima. Mfano, mwalimu anaweza kusisitiza kwamba wavulana na wasichana ni sawa na hivyo ni lazima waheshimiane.
G. Hakikisha wasichana na wavulana wanafanya usafi kama
timu, au wanapeana zamu mara kwa mara kati ya jinsia. Wape hamasa wavulana na wasichana kuweka darasa lao safi. .
H. Kuwa makini na masuala ya kijinsia yaliyowekwa kwa mazoea katika vitabu vya kiada na kuwafanya wanafunzi nao kutambua uwepo wa mazoea hayo. Kisha jadili jinsi mambo haya yanavyoweza kuathiri uelewa wetu wa uwezo wa wavulana na wasichana.
6. Kuhakikisha kwamba wanafunzi wanatoa taarifa ya uchokozi unaohusisha unyanyasaji wa kijinsia kwa walimu na uongozi wa shule
Njia zinazoweza kutatua:____ Njia nyingine:
Jadiliana katika kikundi kikubwa (dakika 10)
1. Kati ya hizi ni ipi ambayo unajisikia kujiamini kutekeleza au ambayo umeshatekeleza? 2. Kati ya hizi ni ipi ina changamoto zaidi, au itahitaji msaada kutoka katika uongozi? Gani? bainisha 3. Ni mikakati ipi ambayo unafikiri walimu wote wanapaswa waitekaleze? 4. Je, inawezekana kujadili na walimu wote? Lini?
VITENDO
Kuhakikisha Usawa wa Kijinsia na Ushiriki wa Wanafunzi (dakika 5)
Kupendelea sauti ya wanafunzi wote, mawazo yao na ushiriki wao darasani ni muhimu. Kama kundi moja la wanafunzi halihamasishwi kushiriki, utu wao na hamasa yao pamoja na ujifunzaji wao vinadidimia. Walimu wanaweza kutumia mikakati shirikishi ambayo itasaidia wanafunzi wote kushiriki na kujisikia kuthaminiwa. Mikakati hii inahusisha, kazi za wanafunzi wawiliwawli , maigizo dhima, na majadiliano katika vikundi. Pamoja na kwamba mikakati hii inaongeza ushiriki, lakini hakuna hata mkakati mmojawapo ambao ni kwa ajili kuzingatia jinsia. Katika hali hii wavulana wana uwezekano wa kutawala mchakato wa kujifunza na kuwatenga wasichana. Kwa hivyo, ni muhimu walimu kuhakikisha kwamba mikakati shirikishi inajali pia jinsia. Mfano:
1. Toa mazoezi ambayo yatahamasisha wanafunzi, hasa wasichana kuwa na hamasa na kuwa na malengo. 2. Wape hamasa wasichana na wavulana kuwasilisha kazi zao katika makundi. 3. Hakikisha makundi yote yana mchanganyiko wa wasichana na wavulana. 4. Hakikisha wavulana na wasichana wanashiriki kama wanakikundi na viongozi wa vikundi. . 5. Toa nafasi sawa kwa wasichana na wavulana kujibu maswali. 6. Ongeza ari kwa wote, wavulana na wasichana. 7. Tunga maswali na mifano ambayo inaakisi usawa wa kijinsia-‐ tumia uwakilishi wa wasichana na wavulana
katika muktadha na majukumu anuwai. .
Moduli ya Mwalimu 12
Jadili na mwenzako (dakika 15)
Hapa chini kuna mikakati mitatu ambayo imekusudiwa kuwafanya wanafunzi washiriki kikamilifu kwa vitendo katika masomo. Katika jozi, soma mikakati hiyo na fikiri namna utakavyohakikisha kwamba kitendo hicho kinazingatia jinsia. Unaweza kutumia mawazo yaliyopo hapo juu au ukafikiria ya kwako.
1. Fikiri-‐ Wawiliwawili-‐ shirikishana: Uliza swali kwa wanafunzi na waache kwanza wafikirie wenyewe, kisha washirikiane na jirani yao katika kujadili majibu yao. Wakati wanafunzi wanajadili mwalimu anazunguka darasani na kusikiliza kutoelewana na kutoa maswali ya ziada inapobidi. Baada ya hapo, mwalimu anachagua baadhi ya wanafunzi kuwasilisha majibu yao.
Utachukua hatua gani kuhakikisha kwamba majadiliano yanazingatia jinsia? __________________
_____________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________
2. Igizo dhima: Wanafunzi wanaigiza jambo ambalo linaonesha kujifunza. Mfano, ikiwa unafundisha kusalimiana, wanafunzi wanatengeneza igizo fupi kwa kusalimia kwa usahihi. Kama unafundisha rangi, wanafunzi wanaweza kufanya kazi pamoja kutengeneza wimbo unaohusu rangi.
Utachukua hatua gani kuhakikisha kwamba maigizo yanazingatia jinsia? ___________________ _____________________________________________________________________________________ _____________________________________________________________________________________
3. Michezo ya Darasa zima: Michezo inasaidia sana katika vitendo vya kujifunza vya darasa zima ambavyo vinaweza kutumika kama muda wa kujifunza na kufurahisha. Mfano wa mchezo wa darasa zima unaitwa, ‘Mwalimu Anasema.’ Katika mchezo huu, mwanafunzi mmoja anasimama mbele ya darasa kama kiongozi na kutoa maelekezo kwa kikundi. . Mfano, ‘Mwalimu anasema inua mkono wako.’ Mwalimu anasema chora herufi B hewani kwa kidole chako.’ Wanafunzi wanafuata maelekezo ya kiongozi. Hata hivyo, kama kiongozi haanzi na maelekezo ya ‘Mwalimu anasema’ basi wanafunzi hawafuati maelekezo ya kiongozi. Mfano, kama kiongozi akisema, ‘Msalimie rafiki yako,’ wanafunzi hawasalimiani. Kama mwanafunzi anafanya kitendo bila ya maelekezo ya ‘Mwalimu anasema’ mwanafunzi huyo anakaa chini. Wanafunzi watakaobaki wamesimama ndio washindi.
Utachukua hatua gani kuhakikisha kwamba michezo ya darasa zima inazingatia jinsia?____________________ ___________________________________________________________________________________
Moduli ya Mwalimu 13
TATHMINI BINAFSI
Tathmini Binafsi ya Mikakati inayozingatia Jinsia (dakika 5) Baada ya kujifunza kujali jinsia, tafadhali kamilisha tathmini binafsi ifuatayo. Weka alama ya X katika
nafasi husika kuonesha kwa kiwango gani unatumia mkakati huo katika darasa lako.
ZINGATIA: Tathmini hii binafsi ni ya kwako mwenyewe (huhitaji kumshirikisha mtu yeyote) na ni njia ya kujichunguza kuona uwezo ulionao na ni maeneo gani unahitaji kujiimarisha katika utendaji wako.
Mikakati inayozingatia Jinsia 0 1 2 3
Nahakikisha kwamba wasichana na wavulana wanapata fursa sawa katika majukumu ya uongozi.
Nawapa wasichana na wavulana wajibu kwa usawa. (rejea mkakati wa kwanza hapo juu)
Nahakikisha kwamba wanafunzi wanatoa taarifa za kunyanyaswa au kuonewa, zikiwemo zile za kijinsia.
Nahakikisha kwamba darasa linasafishwa na wasichana na wavulana.
Naepuka kuendeleza mazoea ya kijinsia.
Nawahamasisha wanafunzi kuheshimu wenzao, walimu na wanajumuiya wote. .
Moduli ya Mwalimu 14
KUANDAA MPANGO KAZI
Kuandaa ‘Kipindi cha Kusoma na Kuandika’(dakika 15)
Ili kuimarisha uwezo wa wanafunzi wa kusoma, ni muhimu walimu waweze kutumia mbinu mpya za kusoma na kuandika ambazo wamejifunza katika MWK. Vile vile ni muhimu wanafunzi wapate muda maalumu wa kusoma. Ndiyo maana ni muhimu kuwa na kipindi cha kusoma na kuandika mara moja kwa juma (kando ya kipindi cha Kiswahili). Pamoja na kuwa shughuli zinazofuata hazina uhusiano mahususi katika kusoma na kuandika (zinaweza kutumika kutathmini na kusaidia wanafunzi katika darasa lolote na somo lolote) lakini zitasaidia katika kufundisha wanafunzi kusoma. Tafadhali jaribu kutumia shughuli hizi katika kipindi chako cha kusoma na kuandika.
KITENDO CHA MATUMIZI #1: NITAKAPOKUWA MKUBWA
1. Kwa kutumia mkakati wa Fikiri-‐ Wawiliwawili-‐ Shirikishana, waulize wanafunzi wanataka kuwa nani watakapokua. Sisitiza ukweli kwamba wavulana na wasichana wanaweza kufanya kazi yeyote ya kitaalam.
2. Wakati wanafunzi wanashirikishana majibu, andika ndoto zao za kazi katika ubao. 3. Kisha waeleze wanafunzi kuwa wataandika hadithi ya ndoto zao za kazi. 4. Andika sentensi ya mfano katika ubao kuonesha aina ya sentensi wanayopaswa kuandika. Hakikisha
sentensi ya mfano inazingatia jinsia na inakazia wazo la wasichana kuwa na kazi ya kifahari. Mfano,
Juma atakuwa mpishi.
Amina atakuwa rais
5. Kisha elekeza wanafunzi kuanza kuandika. Darasa la 1 wanaweza kuchora picha za ndoto zao za kazi na pengine wakaandika neno, fungu la maneno au sentensi kuhusu picha hiyo. Wanafunzi wa Darasa la 2 na 3 wanaweza kuandika sentensi moja au zaidi kuhusu ndoto zao za kazi na pengine kwa nini wanataka kufanya kazi hiyo.
6. Mwisho wa somo, wasichana na wavulana wasimame na kusoma sentensi zao kwa sauti au kuonesha michoro yao kwa wenzao.
KITENDO CHA MATUMIZI #2: MWALIMU ANASEMA
Kitendo hiki ni cha darasa zima kushiriki katika mchezo ambao unaweza kutumiwa wakati wa somo la msamiati, wakati wa kupitia upya, utendaji na vitendo vya tathmini
1. Waambie wanafunzi kwamba watacheza mchezo unaoitwa ‘Mwalimu anasema.’ 2. Waeleze kanuni kwa kusema ‘Mchezo huu sio rahisi, unahitaji kusikiliza kwa MAKINI. 3. Onyesha jinsi ya kufanya kwa kusema ‘Mwalimu anasema shika sikio lako’ – kisha shika sikio lako. Inayofuata,
‘Mwalimu anasema inua mkono wako’ –kisha inua mkono wako. Mwisho, sema ‘Shika aridhini’ – onesha itakavyokuwa ukiwa umesimama tuli.
4. Eleza kwamba kama ulisema ‘shika kidole cha mguu’ badala ya ‘Mwalimu anasema shika kidole cha mguuni’ ….wanafunzi hawapaswi kushika kidole chao cha mguuni. Wanapaswa kusimama na kungojea maelekezo mengine.
5. Fanya majaribio kuona kwamba kila mmoja ameelewa na yupo tayari kucheza. 6. Cheza ‘Mwalimu anasema’ kwa kutumia msamiati unaohusu viungo vya mwili (Uso, midomo, pua, nywele,
mkono, bega, tumbo, mguu, kanyagio, kidole cha mguuni….) 7. Waalike wanafunzi kucheza mchezo ‘Mwalimu anasema’ katika vikundi vidogo vya wanafunzi 4, mahali
ambapo kila mwanafunzi atapata nafasi ya kucheza nafasi ya kiongozi na wengine wamfuate. 8. Zunguka kwenye chumba kusaidia vikundi vidogo.
Moduli ya Mwalimu 15
Jadili na mwenzako (dakika 15)
Wewe na mwenzako, jadili namna unavyoweza kuingiza vitendo hivyo viwili katika andalio lako la somo katika vipindi viwili vijavyo vya kusoma na kuandika. Tafadhali andika mawazo yako, hasa namna utakavyotohoa vitendo hivyo kulingana na kiwango cha darasa lako (darasa la 1, 2 au 3). Baada ya majadiliano, wasilisha katika kikundi cha wote. _________________________________________________________________________ _________________________________________________________________________ _________________________________________________________________________ _________________________________________________________________________ _________________________________________________________________________ _________________________________________________________________________
______________________________________________________________________________________________ _________________________________________________________________________
_________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________________
______________________________________________________________________________________________
______________________________________________________________________________________________
Moduli ya Mwalimu 16
Mwisho (dakika 5) Jibu maswali yafuatayo
Mada ya kipindi:
Ni kwa namna gani umenufaika na malengo ya somo? Kipi kimekusaidia?
Ni mambo gani utapenda kujaribu kwenye darasa lako ndani ya mwezi mmoja ujao?
Kipi umekipenda katika kipindi cha leo?
Je kuna lolote linaloweza kufanyika kwa ajili ya kuboresha kipindi kijacho?
Moduli ya Mwalimu 17
Andika taarifa ya kipindi kijacho:
Mada:
Tarehe na Muda:
Mahali:
Kupima Utendaji Kazi (dakika 5)
Tafadhali tafakari jinsi mratibu wa MWK alivyofanya kazi leo. Jaza fomu ifuatayo kwa ajili ya tathmini yako. Fomu hii itakusanywa na Timu ya Wilaya ya MWK kwa ajili ya kuwasaidia waratibu wa MWK. Mwongozo wa Usahihishaji kwa ajili ya Waratibu wa MWK:
Alama 0:
Hajaweza kabisa
Alama 1:
Ameweza kidogo
Alama 2:
Ameweza kiasi cha kuridhisha
Alama 3:
Ameweza vizuri sana
Mratibu wa MWK hajaweza kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kidogo kufanya yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya kwa kiwango cha kuridhisha yale yaliyoorodheshwa
Mratibu wa MWK ameweza kufanya vizuri sana yale yaliyoorodheshwa
Yale yaliyofanywa wakati wa kipindi cha MWK:
0
1
2
3
1. Maandalizi: Mratibu wa MWK amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia
2. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu
3. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika
4. Ufundishaji na ushauri: Mratibu wa MWK anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini MWK ni muhimu kwetu
5. Ufundishaji na ushauri : Mratibu wa MWK anatoa ushirikiano – anafuatilia maendeleo yetu kujua kama tunatumia mbinu mpya darasani na anatusaidia pale anapoona tuna tatizo
Alama za jumla: /15 x 100% = ________
Moduli ya Mwalimu 18