Uchomaji bora wa makaa «Namna gani kuyatengeneza makaa
mengi zaidi ?»
Projet Makala«Gérer durablement la ressource bois énergie»
Sote turudishe pori
Guide pratique
Kitabu ya projet Makala
Guide Pratique ya Projet Makala 1
Uchomaji bora wa makaa
Utayarishaji wa jiko unapashwa kuanza sasa hivi ili kuiacha mti
kukauka mwezi mmoja ao miwili
Alama muhimu za kipekee kwa ajili ya uchomaji bora wa makaa ndizo :
Kukausha mti utakaotumiwa kwa makaa mbele ya mwezi mmoja •(ukarasa 2 na 3),Kuheshimu kanuni za ujenzi wa jiko bora (ukarasa 4 mpaka 15),•Kufuatilia siku kwa siku kwa kuongoza vema kazi ya uchomaji wa •makaa ndani ya jiko (ukarasa 16 mpaka 21).
Lengo la mtengeneza – makaa nikupata matokeo zaidi ndani ya kazi na uchomaji huo huo.Na lengo la wote nikupunguza ushambulizi wa miti ndani ya maeneo yanayo patikana kando kando ya miji mikuu, kwani uchomaji bora wa makaawasaidiakutokatamitimingikwakufikiakiwangochamakaainayohitajika.
Shabaa ya kuboresha uchomaji wa makaa ni kuyatengeneza makaa mengi zaidi kwa kadiri ya miti iliyotumiwa. Kuyafuata maoni yaliyo ongezewa na uzoezi wa mchoma – makaa yatarahisisha mara na mara kuyafikiamatokeomazuri.
Guide Pratique ya Projet Makala 2
Kwa kurahisisha shina kutoa miti mingine, nitaukata mti
wangu kwa urefu wa sentimeta kumi (10 cm) toka chini
Ukataji wa miti
10 à 15 cmmax
Guide Pratique ya Projet Makala 3
UkaUshaji wa mti
Kwa jiko nzuri la makaa mengi, inabidi kukausha mti muda wa
mwezi mmoja ao miwili....
....na sehemu nene zapashwa kupasuliwa kwa
kuukausha kwa ndani
Guide Pratique ya Projet Makala 4
maandalizi ya kiwanja
Nasafisha kiwanja kwa kurahisisha kazi
Uwanja wa kazi wapashwa kusawanishwa
na kuachwa wazi kwa kutumika bila mashaka
Guide Pratique ya Projet Makala 5
kUsimikwa na maelezo ya jiko
Jiko langu lapashwa kuelekeya ngambo ya upepo
mkali
Urefu
Upepo mkali
Guide Pratique ya Projet Makala 6
kUsimika reli
Kama udongo ni mwinchi ao mwenye kuregea, nitaweka
vizuwizi chini ya reli ili yasitumbukie ndani ya udongo
jiko likipakizwa
Ili upepo uzunguke vema chini ya jiko, nitazipanga reli*
nyororo kila sentimeta 50 (50 cm)
* Reli : Mti wa sentimeta 8 ao 10 za unene, unaotiwa chini ya jiko juu ya sentimeta 50 ya udongo unaosawanishwa, unaonyoka
Guide Pratique ya Projet Makala 7
maandalizi ya matUndU
Si vema tundu liwe pana sana, inaombwa kutoboa
kwa upanga
Nitayafunika matundu kwa matawi ili udongo
usiyafunike tena
Guide Pratique ya Projet Makala 8
majengo ya jiko la shimoni
Udongo ukiwa mwenyi mchanga na nikiwa na miti ama mbao nyingi, naweza chimba shimo la sentimeta
40 ao 50 chini undongoni kwa kupunguza urefu wa jiko
Shimo 40 à 50 cm
Upepo mkali
Guide Pratique ya Projet Makala 9
Utayarishaji wa matUndU ya jiko la shimo
Nachimba mifereji midogo midogo itakayo faa kwa
matundu
Natambulisha mwisho wa kila mfereji ili niweze
kufungua kila tundu majengo ya jiko yatakapo
kuwa yamemalizika (cf. page15)
Guide Pratique ya Projet Makala 10
Ujenzi wa kitanda
Lazima kitanda kinyoroke, kiwe kimefungwa vizuri bila
nafasi wazi
Hutumia miti yenye kunyoroka na iwe yenye
unene wa sentimeta 4 ao 5
Guide Pratique ya Projet Makala 11
maUnganisho ya jiko kipindi cha kwanza (étape1)
Naunganisha miti vizuri bila kuacha fasi wazi.
Miti minene yawekwa kati kati ya jiko
Kwa kila sehemu, nafasi wazi zapashwa kujazwa na
vifungo*
* Vifungo ni miti mifupi na nyembamba ifaayo kwa kujaza nafasi wazi ndani ya jiko
Guide Pratique ya Projet Makala 12
maUnganisho ya jiko kipindi cha pili (étape 2)
Maunganisho yangu ni nzuri na sawan na hayana na fasi wazi
Miti minene inapasuliwa na
kuwekwa kati kati
Guide Pratique ya Projet Makala 13
UfUnikaji
Nalifunika jiko lote kwa majani
Navika ngambo zote za jiko na majani yenye
kusimama
Guide Pratique ya Projet Makala 14
jalada
Napandisha kuta za udongo kando kando ya majani
Namwanga udongo kwa upana wa sentimeta 40 juu ya paa la jiko kwa
kulifunika kikamilifu
Guide Pratique ya Projet Makala 15
UfUnUzi wa matUndU
Na ninaondoa ikihitajika udongo kwa upanga
Likiwa ni jiko la shimo, nachimba kwa uwima kwa
kuyafunua matundu
Naondoa ulinzi wa matawi
Guide Pratique ya Projet Makala 16
Ukongaji
Naondoa udongo na majani mahali pa kuwashia moto ngambo ingine ya upepo
Natumia kaa la moto uliokongwa pembeni ya jiko
Guide Pratique ya Projet Makala 17
UchUngaji wa jiko kipindi cha 1 sikU za mwanzo
Moshi ni wa kawaida pia mweupe , moto wasonga polepole ndani ya jiko, nasaidia mara moja ao mara mbili kwa siku kwa kuongoza uchomaji
Moshi ni mwingi, moto ni mkali sana jikoni, inabidi kufunga kidogo tundu
Guide Pratique ya Projet Makala 18
UchUngaji wa jiko kipindi cha 2fUngeni mahali pote moto waweza kUponyokea na
pUlizeni zaidi baadaye
Tundu zote zapashwa kufungwa, umbalimbali na hayo makaa yatawaka
na kuteketea
Kwa usalama wangu, natumia fimbo kwa kutembea vizuri juu ya
paa la jiko
Guide Pratique ya Projet Makala 19
UchUngaji wa jiko kipindi cha 3Uongozaji wa Uchomaji
Uchomaji umekwisha na nusu ya urefu wa jiko imepunguka. Nafunga matundu ya pembeni kwa kuzuia
makaa kuungua na kuteketea.
Guide Pratique ya Projet Makala 20
UfUngaji wa jiko
Jiko halitoi moshi tena, ucho-maji wa makaa umekwisha, ni
sherti kuzifunga
Yafaa kuhoma vizuri kwa kufunga
nyufu zote
Guide Pratique ya Projet Makala 21
kUyapakUa makaa
Likishapoa (siku moja kisha ufungaji), fungueni jiko kwa kuyaweka makaa
chini kwenyi hewa
Ni vema kutumika asubui mapema wala mangaribi kwa kuyaona makaa ambayo yakiwaka bado. Yakiwa yakingali nawaka nayazimisha kwa
udongo mpaka yapoe
Guide Pratique ya Projet Makala 22
kUpakiza mfUkoni
Nahakikisha ya kwamba makaa yamepoa na yamepata baridi ka-bisa, nayatenganisha na udongo na uchafu wowote ili usipakiziwe
mfukoni pamoja na makaa
Guide Pratique ya Projet Makala 23
kUboresha Uchomaji wa makaa wafaidia msitU na Uchomaji
Sasa naukausha mti wangu na kufuatilia vizuri jiko, na utoaji wangu
wa makaa umeongezeka zaidi
Na bila kuikata miti mingi mno !
François Pinta (1); Dieudonné Kalala (2); Emilien Dubiez (2); Adelaïde Larzillière (2); Jean-Noël Marien (3) :
(1) Cirad UR Biomasse énergie, 73 av. Jean-François Breton34398 Montpellier - France
[email protected] (2) Cirad dep ES, UR 36, c/o FHS Kinshasa Gombe – RDC
[email protected] [email protected] [email protected]
(3) Cirad dep ES, UR 36, Baillarguet - Montpellier – France [email protected]
Projet Makala :57 Av. des sénégalais – Gombe – Kinshasa – RDCSite web: http://makala.cirad.fr Publication janvier 2012
Projet Makala ina pata usaidizi wa pesa kutokea umoja wa ulaya kufatana na mapatano ya usaidizi DCI-ENV/2008/151-384, kwa njia ya pesa 21 04 01, kunamba EuropeAid/126201/C/ACT/Multi.
Mafaa ya projet niku leta swali, yaku ongezeka kwa maitaji yakuendelea na kutoku linda vema mali ya pori naku ongeza ku dumu namna yaku pata miti ya makala ku RDC, hata ku africa ya kati.
Ukomo kubwa ya projet ni kusaidia ku chunga miti ya makala mambo yaku leta koni kwa miji miwili ya RDC na moja ya Congo-brazza, kwa njia yaku tengeneza zaidi ku linda pori (yakawaida na yaku panda) na ushurti wa kubadilisha kwa kuongeza katika maisha ya wanainchi.
Hiyi kitabu ina fanyiwa na usaidizi wa pesa ya umoja wa ulaya.Mambo ya ndani ya kitabu hiyi inahushu tu na waandishi wenyeji na hayawezi
kuangalia mambo yanayohushu wenyeji wa umoja wa ulaya.