Transcript
Page 1: TAARIFA KWA UMMA - Tanzania Revenue Authority · 2018-02-06 · BENKI ZILIZOIDHINISHWA KUPOKEA MALIPO YA KODI Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuutarifu Umma kwamba, Benki

BENKI ZILIZOIDHINISHWA KUPOKEA MALIPO YA KODIMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuutarifu Umma kwamba, Benki za Biashara zifuatazo ndizo zilizoidhinishwa na TRA kupitia utaratibu wa zabuni kwa

ajili ya kukusanya mapato kwa niaba ya Serikali.

Hivyo, Umma unashauriwa kuzitumia benki hizo kama wakusanyaji walioidhinishwa kupitia Mfumo wa Malipo baina ya Benki (TISS) na kupelekwa

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na Mfumo wa Malipo ya Kodi kupitia Benki (Tax Bank).

Benki nyingine zozote ambazo hazijaorodheshwa hapa chini, haziruhusiwi kukusanya kodi ya Serikali kwa namna yoyote ile. Malipo yoyote yatakayofanyika

kupitia benki ambazo hazipo katika orodha hii, TRA haitahusika na ukosekanaji wa huduma kwa Mlipakodi. Zifuatazo ni benki zilizoingia mkataba na TRA;-

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi0800-780078 au 0800-750075

Barua pepe: [email protected]"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Benki za Biashara zisizo na mkataba na TRA zinapaswa kuacha mara moja kupokea malipo yoyote ya kodi au hamisho lolote kwenda akaunti za TRA

zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania. Kama kutakuwa na benki nyingine zozote zitakazoingia mkataba na TRA Umma utajulishwa kwa wakati.

Charles E. KichereKAMISHNA MKUU

TRA MAKAO MAKUUS.L.P 11491, DAR ES SALAAM

1. Azania Bank2. Amana Bank3. Tanzania Postal Bank4. TIB Corporate Bank5. KCB Bank (T) Ltd6. Commercial Bank of Africa7. NBC Ltd8. Citibank (T) Ltd9. CRDB Bank PLC10. Standard Chartered Bank11. UBL Bank (T) Ltd

12. Eco Bank (T) Ltd13. Equity Bank Tanzania Ltd14. Habib African Bank Ltd15. Exim Bank (T) Ltd16. Bank of Africa (T) Ltd17. I&M Bank (T) Ltd18. NMB PLC19. People's Bank of Zanzibar20. Maendeleo Bank PLC21. Diamond Trust Bank (T) Ltd22. United Bank of Africa

TAARIFA KWA UMMA

Top Related