Download - Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
1/21
| Zanzibar Daima Online | Toleo Nambari 07 | Novemba 2013 - Disemba 2013 | Toleo la bure
ONLINE
ZANZIBAR DAIMAUMOJA
WAKITA
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
2/21
A
2 Zanzibar Daima OnlineTAHARIRI
Ahmed Rajab
Ni Uungwana kumpa mtu haki
yake. Katika toleo hili tuna maka-la yenye kumpa haki yake Rais Ali Mo-
hamed Shein kwa msimamo wake wa
kuitetea Serikali ya Umoja wa Kitaifa
(SUK) na kumkinga Makamu wake wa
Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif
Hamadi, ambaye pia ni Katibu Mkuu
wa Chama cha Wananchi (CUF).
Si siri kwamba kuna baadhi ya Wa-
zanzibari ambao kila siku, usiku na
mchana, wanakula njama za kuihu-
jumu SUK. Wanaitwa wahafidhina
kwa sababu hawana siasa za kileo, za
kimaendeleo. Hawataki Serikali hiyo
ifanikiwe. Kwa hakika, hawataki Se-rikali hiyo iendelee kuishi. Wanataka
ife, leo kesho.
Wanaiombea Serikali hiyo mauti kwa
sababu wanaelewa vilivyo nini kina-
choweza kutokea Serikali hiyo ikifa au
hata ikisambaratika tu.
Wanachotaka wahafidhina hao, am-
bao ni wachache sana katika jamii
yetu, ni kuirejesha Zanzibar kule ili-
kotoka na tusikotaka kurudi. Wa-
nachotaka wao ni kuiona Zanzibar
ina machafuko, michirizi ya damu na
uhasama utaovifanya visiwa vyetuvisikalike. Hali hiyo ndiyo wanayoililia,
ndiyo wanayoitilia ubani irudi, tena
kwa haraka sana.
Hawataki kuiona Zanzibar yenye utu-
livu na amani hali ambazo ni mu-
himu kwa maendeleo. Hakuna taifa
linaloweza kuendelea ikiwa halina
utengamano, utulivu na hali ya amani.
Wahafidhina hao wachache, ambao
hatuchoki kuwaombea dua Mungu
awahidi, wana silaha kadhaa wana-
zozitumia ili kulifanikisha lengo lao.Silaha yao kubwa ni fitna. Kwanza
wanataka kuwafitinisha wabia kati-
ka SUK. Na wanaanza hukohuko juu
kuwagonganisha vichwa wakubwa
wa Serikali hiyo. Mishale yao ya fitna
wamekuwa wakiilenga kwa Maalim
Seif. Wanav yo ona wao ni kwamba ni
wao waliomweka Maalim Seif katika
kiti cha umakamu wa Rais.
Wanachosahau au wasichokijua ni
kwamba hii si Serikali iliyo mali yao.
Ni Serikali ya Wazanzibari wote.
Wala hii si Serikali inayoundwa nachama kimoja. Ni Serikali iliyoundwa
na vyama vyote viwili vikuu vilivy-
ochuana katika uchaguzi mkuu uliopi-
ta. Hivyo ndivyo Katiba ya Zanzibar
isemavyo baada ya kura ya maoni ya
2010 iliyoidhinisha kwa asilimia ku-
bwa uundwaji wa Serikali aina hiyo.
Mchezo walioupanga ni kumpaka
matope Maalim Seif na kumfitinisha
na Rais wake.
Matamshi ya Rais Shein alipozun-
gumza na waandishi wa habari hivi
majuzi yalikuwa na lengo la kuukatahuo mzizi wa fitna. Kwa hilo hatuna
budi ila kumpa heko Rais Shein. Tu-
nampa heko huku tukimsihi aendelee
kuwa na ujasiri wa kuushika uzi hu-
ohuo.
Wanaitumia pia fitna kujaribu kutu-
fitinisha sisi Wazanzibari wa kawa-
ida na kujaribu kutugawa baina ya
Wapemba na Waunguja. Watafurahi
wakituona tunapofoana macho na
kuchinjana.
Silaha nyingine inayotumiwa na hao
wanaojikakamua kutuletea balaani kuzipanda na kuzipalili mbegu za
chuki. Hawakuanza jana. Walianza
na chuki za kikabila. Sasa wameka-
mia kupalilia chuki kati ya Pemba na
Unguja ikiwa ni sehemu ya mkakati
wao niliokwishautaja wa kutugawa.
Bahati nzuri hakuna Mzanzibari mwe-
nye akili yake timamu anayewasikili-
za na kuwatia maanani wanapozun-
gumzia juu ya kuzitenganisha Pemba
na Unguja. Wengi wa Wazanzibari
wanawaona hawa wahafidhina kuwa
ni muflis wa kisiasa. Hawana lao jam-
bo. Na wenyewe wanajijuwa na ndiomaana wanatapatapa.
Silaha yao ya tatu ni kutumia vitisho.
Wanajaribu kumtisha kila mtu waki-
sahau kwamba enzi za kutishana zi-
mekwisha zamani Zanzibar. Hii tuliyo
nayo ni enzi ya siasa mpya na mwele-
keo mpya.
Hatusemi kwamba siasa zetu ni safi
safina wala hatusemi kwamba Se-
rikali tuliyo nayo imekamilika. La-
kini tunachosema na kukitambua ni
kwamba Wazanzibari kwa wingi wetu
tumeamua kuwa wamoja, kuziachasiasa za kutugawa na za kuturudisha
nyuma. Tunachotaka ni maendeleo na
ufanisi wetu sote bila ya kujali, kabila,
dini, itikadi za kisiasa au kisiwa gani
au kijiji gani tumetoka.
Inavyoonyesha ni kwamba Rais She-
in naye pia anayatambua haya na
ndio maana aliyasema aliyoyasema
alipokutana majuzi na waandishi wa
habari
Shein anatambua
tulikotoka na tuendako4
9
12
14
18
22
26
30
34
HABARI KUUShein awaangusha Wahafidhina.
NIONAVYO
Uroho wa Wanasiasa kujitajirisha.
NGURUMO LA MKAMA NDUMEDonge na Pemba ni moja na zitabaki hivyo.
MKEKA WA MWANA WA MWANAKama Zanzibar haiwezi kuchangia serikali Tatu,
Bara inachangiaje kwenye Serikali Mbili.
KAULI YA MWINYI MKUU
Shein astahili kuitwa Rais wa busara.
TUFUNGUE KITABUVuta nkuvute, kielelezo cha uandishi wa Kizanzibari
WARAKA KUTOKA BONNWazanzibari tujipange, mafuta yasije yakawa nuksi
kwetu.
BARZA YA JUMBA MARO
Dk. Mvungi ameikosa treni ya mwisho, ila tuko nae.
HEKAYA ZA ZANZIBARHadithi fupi ya meza fupa ya Ally Hilal.
Zanzibar DaimaOnline
YaliyomoMHARIRI MKUU
Ahmed RajabEmail: [email protected]
MHARIRI MSAIDIZIMohammed Ghassani
Email: [email protected]
MHARIRI MSANIFUHassan M Khamis
Email: [email protected]
MSIMAMIZI WA MAWASILIANOHassan M Khamis
WAANDISHIJabir Idrissa
Email: [email protected]
Othman MirajiEmail: [email protected]
Hamza RijalEmail: [email protected]
Mohamed AbdulrahmanEmail: [email protected]
Ally SalehEmail: a [email protected]
WASAMBAZAJImzalendo.net
zanzibardaima.netzanzibardaima/facebook
MATANGAZOHassan M Khamis
Simu: +44 7588550153Email: [email protected]
WASIALIANA [email protected]
JARIDA HILI HUCHAPISHWA NAZanzibar Daima Collective
233 Convent WaySouthallUB2 5UH
Nonnstr. 2553119 Bonn
Germany
www.zanzibardaima.net
Timu Yetu
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
3/21
PAGINATION 15
Zanzibar Daima Online4 Zanzibar Daima Online 5Zanzibar Daima Online
Zanzibar Daima Online
HABARI KUU
SHEIN AWAANGUSHA
WAHAFIDHINA
Wahafidhina ndani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar
wameangushwa puuu.
Haya yalitokea pale Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.
Ali Mohamed Shein, alipofanikiwa kuihami
serikali anayoongoza ya Umoja wa Kitaifa
dhidi ya njama zenye lengo la kuisambara-
tisha.
Dk. Shein katika hali iliyoonesha kuwa
anajua mitego ya siasa, alijibu kwa ufasa-
ha alipoulizwa anamchukulia vipi Makamu
wake wa Kwanza Maalim Seif Shariff Ham-
ad ambaye amekuwa akitoa kauli nzito
zilizoashiria kama ndio msimamo wa Seri-
kali kuhusu upatikanaji wa Katiba ya Muun-
gano Tanzania.
Suala hili limekuwa likitajwa mara kwa
mara na wahafidhina wakiwemo viongozi
wa Umoja wa Vijana wa CCM, kama uth-
ibitisho wa Maalim Seif kukiuka utaratibu
na walimtaka Rais amchukulie hatua kali za
kinidhamu.
Lakini Dk. Shein, mzaliwa wa Mkanyageni,Mkoa wa Kusini Pemba, alimhami Maalim
Seif kwa kusema kuwa kiongozi huyo ame-
kuwa akieleza msimamo wake binafsi kati-
ka suala hilo wala si msimamo wa Serikali
anayoiongoza.
Dk. Shein ambaye aliingia madarakani No-
vemba 3, 2010, alisema yeye na mawa-
ziri wake wanafanya kazi kwa pamoja na
kwa kuvumiliana ambapo kila linalofany-
wa na Serikali wanaliamua kwa pamoja na
wanafanya kazi kwa mshikamano mkub-
wa tofauti na ilivyotokea katika nchi nyingi
zilizounda Serikali kwa mfumo wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa.
Nchi zilizounda serikali ya mfumo huo kwa
Afrika ni pamoja na Zimbabwe ambako
ZANU-PF cha Robert Mugabe kimeunda
Serikali pamoja na Chama cha Movement
for Democratic Change (MDC) cha Morgan
Tsvangirai na Kenya ambako serikali hiyo il-
iundwa kama njia ya kuleta amani baada ya
machafuko ya uchaguzi mkuu wa Desemba
2007. Rais Mwai Kibaki ambaye amestaafu,aliunda Serikali ya ubia pamoja na Muunga-
no wa Upinzani chini ya Raila Odinga.
Dk. Shein anaongoza Serikali ya ushirikiano
yenye mawaziri kutoka chama chake cha
CCM na Chama cha Wananchi (CUF) vilivyo-
pata kura za wananchi siku ya uchaguzi Ok-
toba 31, 2010.
Alisema Serikali hiyo inafanya kazi vizuri li-
cha ya changamoto nyingi zinazoisibu; laki-
ni amesema kuwa mambo yanakuwa rahisi
kwa vile wanashauriana kwa pamoja bila ya
kujali itikadi za vyama vyao vya siasa vilivy-
owaingiza uongozini.
Dk. Shein alionesha ujasiri kiuongozi kwa
kumkingia kifua Maalim Seif Sharif Ham-
ad hata pale alipoulizwa atachukua hatua
gani dhidi ya kilichoelezwa kama kauli za
Makamu wake wa kwanza zinazoashiria
kuisemea serikali kuhusu msimamo wake
Na Jabir Idrissa Zanzibar
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
4/21
DONATE FOR PEMBA
A brief reminder about the Pemba Foundations crowdfunding campaign to introduce new cash
crops to the impoverished Zanzibar island of Pemba. We had a good start but are stuck at $1,225
-- only 11% of the goal, with 55 days left.
For those who have already contributed -- thanks again, and please pass along the link to friends
who might be interested.
For those who would like to contribute but havent got to it yet, please click on the link to the Indie-
gogo campaign page and then click on Contribute Now. Donations are by credit card in dollars, but
UK or other cards work. Your donation will be matched one-for one, so it will be worth double.
Donations are tax deductible in the US. You will be able to give anonymously if you wish.
Here is the link to the campaign page:
http://www.indiegogo.com/projects/a-passion-for-fruit
Many thanks.
John Angier
6
6 Zanzibar Daima Online 7
HABARI KUUZanzibar Daima Online
katika suala la upatikanaji wa katiba mpya
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema ni yeye tu mwenye wajibu wa
kikatiba kuisemea Serikali katika suala hilo;
wengine watachofanya ni kutoa misimamo
yao binafsi.Hakuna kiongozi yeyote wa kutoa msima-
mo wa Serikali isipokuwa mimi mwenyewe
Rais. Makamu wangu wote watatoa mi-
simamo yao kama viongozi binafsi katika
vyama vyao. Sina tatizo la kauli za Maalim
Seif; najua yeye ana haki ya kutoa msimamo
wake binafsi. Na mimi pia ninayo haki kama
hiyo. Lakini mimi ni Rais ndiye nitakayetoa
msimamo, sijafanya hivyo, alisema akijibu
swali lililoulizwa na mwandishi wa habari wa
gazeti la Zanzibar Leo, Mwantanga Ame.
Kumekuwa na shinikizo ndani ya CCM kum-
taka Rais Shein amchukulie hatua kali Maal-
im Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF,
kutokana na kile wanachodai wahafidhina
kuwa kutoa kauli za kuisemea Serikali huku
akimzidi mamlaka Makamu wa Pili, Balozi
Seif Ali Iddi, ambaye ndiye kiongozi wa Seri-
kali katika Baraza la Wawakilishi.
Wahafidhina wakiwemo viongozi waandam-
izi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UV-
CCM) wamekuwa wakimsukuma Rais wa
Zanzibar amfukuze kazi Maalim Seif kwa
kumtuhumu kuwa amekuwa akimtii zaidi
Rais Mstaafu Amani Abeid Karume kuliko
Rais aliyemteua.
Maalim Seif aliteuliwa na Dk. Shein kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa
marekebisho makubwa mwaka 2010, kabla
ya uchaguzi mkuu, kwa kujumuishwa ibara
zinazoweka wadhifa wa Makamu wawili wa
Rais kama wasaidizi wakuu wa Rais.
Mabadiliko hayo yaliidhinishwa katika mpan-
go mpana wa kuruhusu kuundwa kwa Seri-
kali ya Umoja wa Kitaifa baada ya uchagu-
zi, mpango uliowezeshwa na maafikiano ya
kujenga siasa za Maridhiano Zanzibar yal-
iyofikiwa na Maalim Seif na Amani Karume
alipokuwa rais.
Hatua hiyo ya Maridhiano waliifikia baada ya
kufanya majadiliano ya faragha tangu mwa-
ka 2009 kutokana na mpango ulioasisiwa na
Mzee Hassan Nassor Moyo akisaidiwa na
ile inayoitwa Kamati ya Maridhiano inayoju-
muisha makada watatu wa CCM na viongozi
waandamizi watatu wa CUF.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ni pigo
kubwa kwa wana-CCM wasiopenda mabadi-
liko, imekuwa ikikabiliana na majaribio mengi
ya kuisambaratisha.
Wahafidhina wamekuwa wakichochea vuru-
gu kwa kuzuia demokrasia kuenea huku
wakimtukana Maalim Seif hadharani kupi-
tia maandishi kwenye mbao za maskani
ya Muembekisonge na Kachorora. Matusi
mengine hutolewa kwenye majukwaa ya
mikutano ya hadhara ya chama hicho
http://http//www.indiegogo.com/projects/a-passion-for-fruithttp://http//www.indiegogo.com/projects/a-passion-for-fruit -
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
5/21
9Zanzibar Daima Online
NIONAVYO
Na Mohamed Abdulrahman Nionavyo
Uroho wa wanasiasa kujitajirisha
Rais Jose Albarto Mujica
Cardano wa Uruguay
Ukisema kama kuna nchi yenye Rais maskini duniani kuna watakaoangalia kwa jicho la
sadiki ukipenda, kuwa ni porojo tu na si wengi watakaokuamini. Sidhani kutokuamini
kwao kunatokana na dhana ya kuwa haiwezekani , lakini si katika wakati huu tulionao
,kwani uongozi umegeuka na kuwa jukwaa la kujitajirisha badala ya utumishi kwa umma. Hata
hivyo kweli ni kwamba kiongozi wa aina hiyo yupo. Naye ni Jose Alberto Mujica Cordano (ana-
tamkwa kihispania - Khose Mukhika), Rais wa Uruguay.
Mujica mwenye umri wa miaka 78 ,alishinda uchaguzi 2009 na akaingia madarakani Machi 1,
2010. Bwana huyo mpiganaji wa zamani wakati wa vita vya chini kwa chini dhidi ya utawala wa
kidikteta ,aliyejeruhiwa kwa risasi, kufungwa , kuteswa na polisi na kuwekwa gerezani kwa mia-
ka 14 , kabla ya kuteuliwa waziri katika serikali ya muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto
(2005-2008), hutoa asilimia 90 ya mshahara wa urais , dola za Marekani 12,000, kila mwezi kwa
jumuiya za misaada kuwasaidia masikini na wajasiri amali.
Anaishi katika nyumba yake mwenyewe kwenye kiunga kimoja cha mji mkuu Montevideo. Gari
anayoendesha ni aina ya Volkswagen Beatle ya miaka ya 1960 na wala hana walinzi. Nivmtu wa
ajabu anayewashangaza wengi katika ulimwengu wa Leo. Nasema katika ulimwengu wa leo kwa
sababu, kuna viongozi wal-
iotekeleza alau sehemu ya
walichohubiri na hasa kuhu-
siana na hili la kujitajirisha
wakitarajia watakaowafuata
baadaye wataendelea kuwa
ni dira kwa jamii. (Mfano
mmoja Mwalimu JuliusNyerere aliyeondoka madar-
akani baada ya miaka 27 bila
ya yeyote kuthubutu kum-
nyooshea kidole kwamba al-
itumia madaraka yake kuji-
tajirisha).
Leo hii mambo ni mengine.
Mbunge anaweza kuwa ta-
jiri katika kipindi cha miakamitano tu. Hugombea ubu-
nge kwa malengo ya ku-
jinufaisha binafsi na badala
ya bunge kuwa chombo ki-
kuu cha uwakilishi wa umma
limegeuka kuwa mahala pa
kula.
Ubinafsi Umetawala
Kinachokirihisha ni pale
wabunge na wawakilishi
wanapokuwa na moyo wa
kulalamika hadharani kuwa
mishahara yao haitoshi na
wanataka waongezewe. La
kukirihisha zaidi ni pale vi-
ongozi wa juu wanapokaa
kimya na kushindwa ku-
wakemea mabwana wakub-
wa.
Hivi karibuni kumeibuka ma-
dai ya wabunge kuwa msha-
hara hautoshi. Sambamba na
madai hayo ni zumari lililop-ulizwa na Spika wa bunge
la Muungano Anna Makinda
kuyaunga mkono madai hayo
. Akitoa mfano alisema yeye
binafsi amewahi kuende-
wa na wabunge watatu wa
zamani wakiomba msaada
kwa vile hali zao ni mbaya.
Ingawa hakutaja kiwangocha mishahara ya wabunge,
Makinda amegusia posho ya
vikao Shilingi 330,000 kwa
siku, Shilingi 30,000,000 za
shughuli za jimbo na Shilingi
72,000,000/= zikiwa kiinua
mgogo mbunge anapomal-
iza miaka 5.
Makinda amedai wabunge
wengi wanashindwa kukidhi
mahitaji yao katika mazingira
yaliopo sasa .
Spika amesema wabunge
wengi wanajuta kuwan-
ia ubunge na wangetam-
ani kurejea katika taaluma
zao. Sijui kama taaluma
hizo zingewapa marupuru-
pu na fedha wanazojikingia.
Kiroja cha mambo madak-
tari wamekuwa wakivutana
na serikali kuhusu misha-
hara na mazingira yao ka-
zini. Matatizo yao mpaka leo
hayajapatiwa suluhuhisho lakudumu.
Spika Makinda hajanis-
hangaza, Waswahili wanase-
ma .Mwamba ngoma hu-
vutia pande wake, kwani
marupurupu anayopata yeye
mwenyewe hayasemeki.
Wazanzibari hawana tafauti
Hoja hii inawagusa pia
wabunge wa Zanzibar ka-
tika bunge la Muungano na
hata wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi (BLW) . Hivi
tunapozingatia na kujiuliza
kuhusu kiwango cha fed-
ha anazojikingia mbunge
wa Zanzibar na mshahara
wa mfanyakazi wa kawaida
tunakuwa na majibu gani ?
Ni wafanyakazi wangapi wa
serikali wanaoweza kupa-
ta kiinua mgongo cha kiasi
hicho baada ya miaka 30 ya
utumishi, ukilinganisha na
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
6/21
10 Zanzibar Daima Online
10
tija za miaka mitano ya ubu-
nge ? Wabunge wangapi wal-
iotumia posho wanaolipwa
kushughulikia kweli matatizo
majimboni mwao ?
Kwa bahati mbaya ugonj-
wa huu hauko tu miongonimwa wabunge wa chama kin-
achotawala cha CCM bali hata
kwa wale wa vyama vya up-
inzani.
Sikio la kufa halisikii dawa
Zanzibar ina serikali ya ubia
na waliokuwa wapinzani sasa
nao wamo serikalini. Kwa ba-
hati mbaya lakini baadhi ya
waliokuwa wakiyalalamikia
sasa hayazungumzwi tena.
Ukihoji unaambiwa Waziri
anapaswa kuishi kulingana na
hadhi yake. Je, daktari hap-
aswi kuishi kulingana na hadhi
ya taaluma yake ?
Kwa kumbukumbu zangu ni
mwakilishi wa Mji mkongwe
Ismail Jussa peke yake ali-
yepinga kuongezwa masila-
hi ya wawakilishi,alipokuwa
akichangia katika kikao cha
bajeti ya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Juni 18 mwaka huu .
Lakini sikio la kufa halisikii
dawa. Mwanzoni mwa mwe-
zi wa Novemba, ilitangazwa
kwamba BLW limepandis-
ha posho ya vikao kutoka
Sh. 100,000 hadi Sh.150,000
kuanzia mwaka huu .
Wananchi wameanza kukata
tamaa na kutokuwa na ima-
ni na wanasiasa. Hata hivyo,wao pia wana wajibu mkub-
wa wa kujiletea mabadiliko.
Kwanza wanapaswa wata-
fakari ni kina nani wanaofaa
kuwawakilisha, kuwapigan-
ia na kuwaletea maendeleo.
Kuna matumaini Katiba mpya
huenda ikawa na kifungu ki-
takachoruhusu wagombea
binafsi. Hiyo itakuwa nafasi
muruwa ya kuwapima wanao-
faa kuwa viongozi bora.
Kiongozi anayewajibika kwa
umma
Rais Jose Mujica alipoamua
kugombea urais alishawishi-
wa na hali ngumu aliyoiona
wakikabiliana nayo walala
hoi. Alisahau umimi akawe-ka mbele utaifa. Hakukimbilia
utajiri bali uwajibikaji. Uamuzi
wake wa kutoa asilimia 90 ya
mshahara wake kila mwezi
kwa jumuiya za kiraia kwa ajili
ya miradi mbalimbali ya ku-
wasaidia masikini ni kielelezo
cha uadilifu anaopaswa kuwa
nao kiongozi . Uadilifu huo ni
wa kuwatetea, kuwasimamia
na kuwapigania waliomcha-
gua. Nikimnukuu, amesema
hivi: Mshahara wa mke wan-
gu ambaye tumejuana katika
siasa na ni Seneta unatutos-
ha, kwanini cha ziada tusitoekwa wengine.
Mujica anasema anashaji-
ishwa na falsafa ya utu, ya
kumheshimu na kumfikiria
binadamu mwengine na hasa
masikini.
Hadi miaka ya 1970 wakati
Mujica Rais wa 40 wa Uru-
guay akiwa gerezani sisi pia
tulikuwa nao viongozi wa aina
hiyo waliowajali na kujitolea
kuwatumikia raia , waliobakia
wakati wote kuwa sawa na
wengine.... gari na vazi la ka-
waida, viatu vya kanda tu na
hata nyumba ya kawaida na
waliokuwa karibu na umma
kuanzia majimboni hadi kitai-
fa, viongozi ambao umma naoulijivunia. Kama usemavyo
usemi wa kihispania Un
gobierno honrado, un pas de
primera Serikali yenye hes-
hima ni ile inayoliweka taifa
mbele. Je, wengi wa viongozi
na wanasiasa wa kwetu ni wa
aina gani ?
Barua za Wasomaji
Ni fakhari ya kila Mzanzibari wa kweli kuwa na watu we-nye upeo, misimamo na kauli thabit kama wewe auntRiziki. Hapana shaka wewe ni moja katika rizki kubwa kwa
taifa la ZANZIBAR. Jazaaka llah l kheir.
Mshirazi
Ahsante kwa makala yako murwa kabisa. Umenifurahishasana Sheikh Othman. Mungu akujaze kheir kwa hilo. LakiniAli Mrandazi, kwa uhakika, hatujui kama alikuwa walii wala la,
lakini kwa ulengo wangu ana alama na dalili za uwalii.
Tatizo Bwana Ali Saleh unalijua. Hapa petu wewe si mgeni wa siasa.Unajua kitu kinachopiganiwa hapa si utaifa bali ni matumbo kujaa. Sasahawa wahadimu wa pande hizi mbili, CUF na CCM, hawana mtafarukuisipokuwa wanatafuta mtu wamtie kati wamtoe kafara. Unawaona,Muamsho, waliwatumia CCM na CUF, baadaye, wamewatafutia gunia
wamewavisha. Usione wewe umebahatika na umepata hicho kijifupa, sihaba. Hawa CUF, walikupigisha vigongo hata nakukutilisha ndani wakatiwanyamunyamu hawa kukumbuka. Sasa wache wapige ngoma watacheza wenyewe, kubomoa rahisi kujenga kazi.
Nawe Bwana Ahmed Rajab una maoni mazuri na michango ndani yamajarida na mitandao mbalimbali ya k idunia, lakini wewe mchangowako wa kivitendo hatuuoni. Umekuwa kama Zanzibar. Wengine,wako ughaibuni, wana tuchochea, sisi wahadimu wanatuua, waowanakula raha ughaibuni. Tunasikia, wewe baada ya kustaafu umeonahapakaliki Zanzibar, umeomba uraia Kenya. Unajua hapa hapafai, sasakwa kuwa mwenzetu umealimka, ugemuiga mzee wetu almaruhum AliNabwa, aliyewaelimisha na kuwafunza mengi. Mungu amlipe mema naamughufiriye dhambi zake na amuondoshee adhabu ya kaburi. Na wewenjoo uwaelimishe, utarajie mema kwa Mungu. Muda huu wa mapumziko,
ya utu uzima, ikumbuke jamii yako iliyo dhulumika miaka 50. Na weweunajua mengi kuhusu Zanzibar, makomredi mana deni kwa Wazanzibari.
Ali Azani [email protected]
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
7/21
12 13
NGURUMO LA MKAMA NDUMEZanzibar Daima Online Zanzibar Daima Online
Wengine tutauchuku-lia mwezi huu waNovemba kuwa wa
aina yake visiwani Zanzi-bar kwa sababu ya matukiomawili, tunayoyaona ni mu-himu kwa maendeleo yakidemokrasia na kiutawalavisiwani humo.
Moja ni kujizoazoa kwaSerikali ya Mapinduzi (SMZ)na kuja juu dhidi ya vyombovya habari vitakavyotumiavibaya uhuru wa habari na
kuchapisha au kutangazahabari zenye lengo la ku-vuruga amani.
Hayo yalisemwa na wazirianayeshughulikia habari,Said Ali Mbarouk, katika kilekilichotajwa na vyombo vyahabari vya Tanzania kuwa nimkutano wa waziri huyo nawakuu wa vituo vya rediovya Zenj FM na Coconut FM,
vyote vya Zanzibar.Ujuu iliokuja nao SMZ katikahili ni kutoa onyo kwambaama vyombo hivyo viachekupandikiza mgawanyikowa Pemba na Unguja auvichukuliwe hatua kali. Hatu-
jui ukali wa hatua hizo kali,lakini mazoea ya serikalizetu yanatupa mwelekeowa makisio - vitapigwa faini,vitafungiwa, lakini havitape-lekwa mahakamani. Vikipe-lekwa mahakamani itakuwa
ni hatua nyengine kubwa yakupongezwa katika ukuajiwa demokrasia na utawalawa sheria nchini mwetu.
Isifahamike kwamba makalahaya yanapingana na onyohilo la Waziri Said. La hasha.Kwa hakika, yanakubaliananalo kabisa na yangelipendahata liongezwe nguvu zaidi,yaani sio tu vyombo hivyo
vikabiliane na adhabu iwapovikiendelea, bali viwajibikesasa kwa yale ambayo tayarivimeshayatangaza.
Ikiwa msingi wa kuchukuliwakwao hatua hapo baadayeni athari za matangazo yaodhidi ya Umoja wa Kitaifawa Wazanzibari, basi ta-yari umoja huo umeanzakuathiriwa. Sikiliza kauli zaviongozi wajiitao wa shehia,wazee na vijana wa Ungujakutoka Chama cha Mapin-
duzi (CCM) wakifoka hadimapovu kuwatoka dhidi yawatu wenye asili ya kisiwacha Pemba. Hapa nimewaitawajiitao na namaanishahivyo hivyo wajiitao waUnguja.
Hao niwaitao wajiitao waUnguja wanasikika wakita-mka kwamba Wapembahawapaswi kuendelea kuba-
kia kisiwani Unguja kamawanapingana na mfumo waMuungano wa Serikali Mbi-li uliopo sasa. Wasikie haowajiitao Waunguja waki-kumbusha mauaji yaliyofany-ika wakati wa Mapinduzi nawakiapa kwamba wako ta-yari kwa mapinduzi menginekama hayo ili kuweka heshi-
ma na adabu.Chuki, hasira na kisasikinaonekana wazi kwenyemaneno yao kama zioneka-navyo kwenye nyuso nadhamira zao. Kauli ya vita,damu, mauaji, majeruhi,unaweza kuihisi kwa mba-li. Makala haya yanadhanikwamba hatua zilipaswa ku-chukuliwa leo, mfano wa vileviongozi wa Uamsho walivyo-chukuliwa hatua na Serikali hiihii, ikiwa kweli Serikali ilikuwa
na haki ya kufanya vile wakatiule.
Ila kama panangojewa hadiwatu washikiane mapanga,kama ilivyotokea Rwandabaada ya Redio Intarahamwekutumika kuchochea mauajidhidi ya kabila la Watutsi naWahutu wenye msimamo wawastani, basi natusubiri uleuitwao kwetu pwani ushahi-di wa Kinyamwezi.
Nimeiita hatua hii ya sasa
ya Serikali kwamba imekujabaada ya kujizoazoa. Nakus-udia kwamba ni hatua nzuriiliyokuja baada ya Serikalikuchelewa sana na kuwa-chelea wakubwa. Paliku-wa pamezoeleka kwa walewanaojinasibisha na Mapin-duzi na Chama cha Mapindu-zi, hata kama ni mijitu mijahili,mijinga na mikatili, kuogope-wa na SMZ. Ni kituko, lakini
ndio ukweli kwamba Serikaliya Mapinduzi inawaogopawajinasibishao na Mapinduzi,hata kama hawana uwezowala njia za kupindua tena.
Si haba kwamba angalau kwamara ya kwanza hao wajina-sibishao na Mapinduzi nakwa hakika ukichungua his-
toria utawakuta wengi waohata hawakuhusika nayo sasa wanaambiwa kwambaZanzibar si yao mali yao, walayao peke yao.
Novemba hii pia itaingia tenakwenye historia ya mae-ndeleo ya kisiasa visiwaniZanzibar, kwani kwa maraya kwanza tangu kurudikwa mfumo wa vyama vingi,Serikali iliamua kusimamiahaki ya kisiasa ya kila raiakwa kukiruhusu Chama cha
Wananchi (CUF) kufanyasiasa za wazi k wenye jimbola Donge, ambalo kwa miakayote 20 na ushei ya siasa zavyama vingi wanasiasa wa-hafidhina wa chama tawalawamejenga mazingira ya ku-litenga na sehemu nyengineza Zanzibar kama kwambaDonge ni nchi pekee.
Nakumbuka mwaka 2005,kundi letu la wanahabarililipojikuta likilazimika kuripotirisasi na mabomu pale Ma-
honda baada ya polisi kuwa-zuia wana-CUF kwa maranyengine. Matokeo yake,yalikuwa majeruhi na mauaji.Uvunjwaji wa haki za binada-mu ukaendelea hata baada yahapo.
Lakini ukweli ni kwam-ba mambo yana zama nazamu. Ndivyo alivyosemaRais Mstaafu wa Zanzibar,
Dk. Salmin Amour Juma, sikuakitoa hotuba ya kusisimua
juu ya umoja wa Wazanzi-bari, Ikulu ya Mnazimmojakwenye mkesha wa Mwafakawa kwanza wa kisiasa kati yaCCM na CUF mwaka 1999.
Sasa zama zimebadili-ka na mabadiliko haya
yanawaumiza wanasiasa am-bao walivuta pumzi, walikulana walikunywa uhasama wakisiasa. Donge imefungukana kujiunga tena na sehemunyengine za Zanzibar.
Wala kujiunga huko si lazimakumaanishe kuiacha mkonoCCM na kuikumbatia CUF. Lahasha. Kunamaanisha kwam-ba sehemu hiyo nayo sasa ikotayari kusikiliza hoja na kuzip-ima ndani ya ardhi yake kishaikafanya uamuzi baada ya
kuzipokea hoja hizo. Wanao-taka kujiunga na CUF waka-fanya hivyo kwa mujibu wawalichoelewa na wanaotakakusalia CCM wakafanya hivyokwa mujibu huo huo. Lakini sikinyume chake.
Mantiki muhimu hapa nikwamba kubwa kuliko yoteDonge nayo ni Zanzibar, ime-kuwa hivyo na itakuwa hivyomilele. Kama ilivyo Pemba,kwa ujumla wake, ndivyo il-ivyo Donge kwa udhati wake.
Zote ni sehemu za Zanzibar,zimekuwa hivyo na zitabakihivyo milele.
Wale wanasiasa waliopiganiakuitenga Donge na Zanzibarna ambao sasa wanahubiriutengano wa Pemba na Un-guja, imekula kwao kwakutumia lugha ya vijana wakileo
Na Mohammed Ghassani Ngurumo la Mkama Ndume
Donge na Pemba nimoja na zitabaki hivyo
Ali Shamhuna Mwakilishi wa Donge
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
8/21
1514
MKEKA WA MWANA WA MWANA
Zanzibar Daima Online Zanzibar Daima Online
Kama Zanzibar haiwezi kuchangia Serikali Tatu,Tanzania Bara inachangiaje kwenye Serikali Mbili?
Hoja ya Mheshimiwa Awadhi
ina mapungufu mengi. Mo-
jawapo ni ikiwa kama hicho
anachokisema ni cha kweli,
basi kwa nini asipendekeze
serikali moja tu kabisa, maana
kwa vyovyote vile Zanzibar
inatakiwa ichangie kwenye
mfumo huu wa sasa uliopo na
kama haitaweza kuchangia
wakati huo, haiwezi kuchan-
gia sasa pia. Hii ni kuuambia
upande wa pili wa Muungano
kwamba umekuwa ukiibeba
Zanzibar sikuzote na sasa ...
Na Riziki Omar Mkeka wa Mwana wa Mwana
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Fedha
na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzi-
bar, Salmin Awadh Salmin, alisema hivi karibuni
kwamba Zanzibar haitakuwa na uwezo wa ku-
changia uendeshaji wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano kama muundo wake utakuwa wa
Serikali Tatu.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo wa jimbo la
Magomeni (CCM), Zanzibar haiwezi kuchang-
ia hata kwa asilimia 10. Hayo aliyazungumza
kwenye semina ya Wabunge wa Muungano
na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar mjini Dodoma Jumatatu ya tarehe 11
Novemba, 2013. Hoja yake kubwa ni kwam-
ba Zanzibar ina uchumi mdogo na, kwa hivyo,
mfumo wa sasa wa serikali mbili ndio unaofaa
katika kuudumisha Muungano.
Nimekuwa mbunge kwa mwaka wa nane huu,
nikiwakilisha maslahi ya Zanzibar kwenye
bunge la Muungano, na lazima niseme kauli ya
mtunga sheria mwenzangu huyu, Mzanzibari
mwenzangu, ilinikirihisha. Wakati mwengine
anasimama mtu kutokea upande wako wa
nchi, analisema neno, unatamani uingie chini ya
meza kukimbia aibu na fedheha. Huu ulikuwa ni
wakati mmojawapo kwangu.
Hoja ya Mheshimiwa Awadhi ina mapungufu
mengi. Mojawapo ni ikiwa kama hicho ana-
chokisema ni cha kweli, basi kwa nini asipende-
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
9/21
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
10/21
Dk. Shein astahili kuitwa
Rais wa Busara
KUMBE Rais wa Zanzibar, Dk. AliMohamed Shein, ana busara nyin-gi.
Daktari huyu wa binadamu, ninayem-fahamu kwa miaka 20 hivi tangu akiwaofisa mdogo katika k ilichokuwa Kiten-go cha Kudhibiti Ugonjwa wa Ukimwianashangaza.
Najua anapoamua kusema au kutenda,anaweza. Akatenda kwa kiwango usi-choweza kuamini. Tatizo kwa asili yake,hatabiriki. Labda upole wake unachan-gia. Nini maana yake?Pale unapomtarajia afikirie suala fulaninamna unavyoliona, usishangae aka-wa anafikiria tafauti. Anaweza kufikiriavingine kabisa na bado mkaendeleakujadiliana. Hana papara. Mtulivu kwe-likweli.
Wanasaikolojia wanasema tabia hii nimoja ya sifa za watu wenye akili nyingi.Sijiingizi kusema naye ana akili nyingi.Kwa muda mrefu sijakaa naye kujadili-ana lolote, nikapata kumpima.
Wiki iliyopita, alikutana na waandishiwa habari, wengine wakitoka Dar esSalaam kwa kugharimiwa na ofisi yake.
Sikubahatika kualikwa. Nin-geupata mwaliko, ningeu-daka kwa moyo mkunjufu.Ningehudhuria maana ninamaslaha makubwa na Zan-zibar. Kwa hivyo, ningepatamawili matatu ya kujifunza.Tunapojadili Zanzibar na sia-sa zake, ingenisaidia.Hata mwaka jana, ingawanilitarajia, baada ya ku-wasiliana na Mkurugenzi waMawasiliano Ikulu, HassanKhatib, sikualikwa. Ofisahuyu anajua zaidi kilichot-okea. Hilo ni historia leo,mkutano umepita. Kinacho-
endelea sasa ni watu kuta-fakari maelezo aliyoyatoaRais, maswali aliyoulizwa,na majibu aliyoyatoa. Kuto-kuwepo kwangu, walakini,hakuninyimi haki yangu yakuchambua aliyoyasema.Ndo ninachokifanya.
Dk. Shein amenikoshaalivyoihifadhi Serikali an-
ayoiongoza. Amefanikiwakuifichia matatizo yake kiu-tendaji. Aibu zake kitaswira.Ameifichia Serikali ya Umoja
wa Kitaifa (SUK) madhambiyake. Ameitetea vya kutoshaakisema inafanya kazi vizuri,kwa mshikamano imara nauvumilivu.Haya yanawasuta waha-fidhina wanaohangaikakuisambaratisha. Walitarajiaatashambulia. Wao waliami-ni atamsema na kumbomoaMaalim Seif Sharif Hamad,
mmoja wa wasaidizi wakewawili wakuu.
Maalim ni Makamu waKwanza wa Rais. Makamuwa pili, ni Balozi Seif Ali Iddiambaye pia ni kiongozi washughuli za Serikali katikaBaraza la Wawakilishi chombo cha kutunga sheriana chenye kuisimamia Seri-kali katika utendaji.Moja ya maswali aliyoulizwaDk. Shein lilihusu eneo hilila mwenendo wa Makamuwa Kwanza wa Rais, kuhusuKatiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano.Wahafidhina wanamchukuliavingine Maalim Seif. Wa-nambeza na kudhani sistahili yake kupewa wadhifahuu. Wanamwona kuwa nishawishi tu asiye na lolote.Kwao, Maalim Seif, hanamchango. Amejiingiza Seri-kalini. Wanadhani ile nafasi
NASEMA HIVI, DK. SHEIN ANABUSARA SANA. ANAJUA SIKUATAKAYOMBOMOA MA ALIMSEIF HADHARANI, NA HATAKWENYE BARAZA LA MAPIN-DUZI, ITAKUWA JAMBO KUB-WA.
18 19
Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar,
Maalim Seif Shariff Hamad
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein
Na Jabir Idrissa Kauli ya Mwinyi Mkuu
KAULI YA MWINYI MKUU
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
11/21
21HABARI KUUZanzibar Daima Online Zanzibar Daima Online20
si kumfukuza Maalim Seif.Hawa hawasomi Katiba yaZanzibar, hasa lile fungulililoweka nafasi yenyewe yaMakamu wa Kwanza. Si kati-ka asili zao kusoma. Maranyingi hukurupuka. Ndiomaana kila wanapofanyashambulio dhidi yake, hujik-uta wakiishia kupiga ngumibaharini. Hakuna mtikisikoila yale maji yanamwagikianyusoni mwao.
Mabao ya maskani yaMwembekisonge naKachorora yanaandikamaandishi ya kuthibitishamashambulizi dhidi ya Maa-lim Seif. Kazi yao kila wakatini hiyo tu ya kumsukumaakasirike. Wanakosea sana;hata mara moja kiongo-zi huyu hajababaishwa namashambulizi yao.
Na kule kubaki kwake imaraofisini, kubaki imara katikakumsaidia na kumshauriRais wanachukia. Kubakiimara katika kufanya kaziyake kwa ushujaa mkubwakunawatesa. Kwa upandemwingine, wanapomwonaanafanikiwa huku akizidikukijenga Chama cha Wa-nanchi (CUF) kilichomfikishahapo, wanaumia wahafidhi-na.
Ni pigo kubwa kwao kwanimashambulizi wanayomlen-gea yanawarudia. Hayam-pati na wanamkuta ametuliakama maji mtungini. Hatamara moja Maalim Seif haja-toa kauli ya kuwalenga wa-hafidhina. Yeye sanasana nikuelekeza wananchi kutuliawasichafue amani. Husematu Ndugu wananchi nawasi-
hi bakini watulivu, mt ayaonamengi makubwa yatatokeachini ya Serikali hii.
Dk. Shein anasema Serikaliinatekeleza majukumu yakekwa ufanisi na mshikama-no mkubwa. Ninamnukuu:Serikali yangu imefanikiwakudumu kwa miaka mitatusasa kutokana na kuvumil-iana na kufanya kazi kwapamoja bila ya kutangulizaitikadi za kisiasa.
Nchi nyingine zime-jaribu hili (mfumo huu waSerikali ya Umoja wa Ki-taifa) zimeshindwa, laki-ni sisi tumefanikiwa kwasababu tunavumiliana. Hililinahitaji stahamala kub-wa vinginevyo tutagawanambao na sitaki hili litokeekwenye uongozi wangu.
Aliyasema haya aliposukum-wa kusema anachukuliajekauli za Maalim Seif wakatihuu wa maandalizi ya kuan-dikwa Katiba mpya. Ni kweliMaalim Seif analizungum-zia kila wakati suala hili.Wao wahafidhina wanaonaanaisemea Serikali ilhali yeyesi rais. Walishasema am-fukuze.
Dk. Shein amesema yeyendo wa kutoa msimamo waSerikali. Hajafanya hivyona hawezi kufanya hivyokiongozi mwingine yeyotekatika Serikali anayoiongo-za. Si Makamu wa Kwanzawala wa Pili. Wao wanawe-za kutoa misimamo binafsiinayozingatia mielekeo yavyama vyao. Anasema hatanaye aweza kutoa maonikulingana na mtizamo wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Maalim Seif amesema sanakuhusu suala la Katiba. Am-etoa msimamo binafsi, mbalikabisa na wa CUF. AnatakaMuungano wa Mkataba naZanzibar yenye mamlaka ka-mili. Sera ya CUF ni ya kuwana muundo wa Muunganowenye Serikali tatu. Aliyase-ma hayo mbele ya Tume yaMabadiliko ya Katiba ya JajiJoseph Warioba. Maalim Seifanajiamini kwa kile ana-chokiamini.
Ona alivyomkingia kifuaMakamu mwenzake, BaloziSeif, alipojikuta ak ishambuli-wa na umma unaopendeleamabadiliko ya Muunganokwa kutaka Muungano waMkataba chini ya Serikali yaZanzibar yenye mamlakakamili.
Balozi Seif alitegwa naSerikali ya Muungano kwakuombwa kueleza ushirikiwa Zanzibar katika kujadilimapendekezo ya marekebi-sho ya Sheria ya Mabadilikoya Katiba. Alipoinuka aka-liambia Bunge kuwa Zan-zibar ilishirikishwa. Kumbe,Zanzibar ilipewa vifunguvinne tu vya mapendekezokati ya 12 vilivyopitishwaSeptemba 6 na Wabunge waCCM pekee pamoja na Au-gustine Mrema wa TanzaniaLabour Party (TLP).
Maalim Seif alimtetea Balozikuwa alijibu kwa kuangaliavifungu walivyovijadili Ser-ikalini. Hakujua wataalamuwa Wizara ya Sheria naKatiba na Ofisi ya Mwa-nasheria Mkuu wa Serikali
waliweka vifungu vingi zaidikatika Mswada, vikiwemo vileambavyo vina maslaha makub-wa na Zanzibar.
Nasema hivi, Dk. Shein anabusara sana. Anajua sikuatakayombomoa Maalim Seifhadharani, na hata kwenye
Baraza la Mapinduzi, itakuwajambo kubwa. Atakuwa ameji-umiza na kujimaliza. Atakuwaameondoka kwenye mstari.Atakuwa amejichongea. AnajuaSerikali ina deni kubwa kwawananchi. Anajua Serikali hai-
jatimiza ahadi zake.Dk. Shein anajua Maalim al-isema nini Bwawani siku ma-tokeo yalipotangazwa. Anajuaametimiza au hajatimiza yale.
Anajua Maalim Seif anasaidiakuwepo amani na utulivu nchi-ni. Anajua akimbeza ni hatarikwake. Wahafidhina wanasubi-ri hali hiyo itokee.
Watu hawa wamekuwa waki-taka Serikali ivunjike ili pazukebalaa. Siku zote imekuwa
ni imani yao kwamba kui-shi kwao kunategemea sanasiasa chafu, zilizojaa chuki,hasama na ubaguzi dhidi yawatu wa wasioipenda CCM nahasa Wazanzibari wenye asiliya Pemba ambao wanawa-ona kama wasiostahili kuwaWazanzibari.Wanapata shida leo kwa saba-bu vile viapo vyao kuwa Ikuluhataigusa kiongozi kutoka
Pemba vimefika mwisho kwakuwa Dk. Shein amezaliwaMkanyageni, Kusini Pemba.Hata Maalim Seif, Makamuwake wa Kwanza, ni mzaliwawa Mtambwe, Kaskazini Pem-ba. Wanatokea wapi?
Viapo hivi ni kama vile
walivyoapa wahafidhina waDonge kuwa kamwe MaalimSeif na CUF yake hawataingiaDonge kufanya mkutano wahadhara. Maalim ameingia naCUF yake ikafanya mkutanomkubwa Novemba 10, hukumzaliwa wa Donge na muasisiwa CUF, Machano Khamis Ali,ambaye ni Makamu Mwenyeki-ti, akihutubia
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
KAULI YA MWINYI MKUU
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
12/21
2322
TUFUNGUE KITABUZanzibar Daima Online Zanzibar Daima Online
Shafi Adam Shafi
TANBIHI: Uhakiki huu uliandikwa kwa
lugha ya Kiingereza naFLAVIA AIELLOTRAOREkwa jina la INVESTIGATING
TOPICS AND STYLE IN VUTA NKUVUTE BY
SHAFI ADAM SHAFI. Hapa tumeutafsiri
kwa minajili ya kuwapa wasomaji wetu
mtazamo wa wengine kwa fasihi ya
Kizanzibari.
Kwa miongo mingi
sasa, wahakiki wa
kazi za fasihi wame-
zisifu kazi za waandishi waKizanzibari kwa sifa tele.
Kwa mfano, akirejea riwaya
za Mohamed Suleiman Mo-
hamed, Said Ahmed Mo-
hamed na Shafi Adam Shafi,
M. M. Mulokozi aliandika
mwaka 1985: Maendeleo
muhimu kabisa, na pengine
ya kufurahisha sana, katika
kazi za fasihi za K iswahili ka-
tika miaka ya 1970 na 1980,ni kuibuka kwa Zanzibar
kama mtoaji bora kabisa wa
kazi za Kiswahili kuwahi ku-
tokea hadi sasa, na kiongozi
wa wazi wa riwaya za Kiswa-
hili katika siku zijazo.
Hisia kama hizi zinaelezewa
pia na R. Ohly ambaye, baa-
da ya kukumbana na riwaya
zilizoandikwa na waandishi
wa Kizanzibari na wale wa
Kitanzania na Kikenya bai-
na ya mwaka 1975 na 1981,amezielezea riwaya za Ki-
zanzibari kama changamoto
kubwa kwa uwezo wa kisa-
naa kwa waandishi wengine
wa Kiswahili.
Ingawa mnasaba uliotumi-
wa na Ohly unaweza kujadi-
lika kwa kujikita kwake na
kazi zilizotolewa Bara hasahadithi fupi fupi na kuwaa-
cha waandishi wenye vipaji
kama vile Eupluase Kezila-
habi au Claude Mungongo,
uhakiki wake bado umezu-
ngumzia sifa kuu za riwaya
za Kizanzibari, yaani kujikita
sana kwenye masuala ya ki-
historia na kijamii, pamoja na
utajiri wa lugha mwanana na
kutokufanya mzaha kwenyemasuala ya fani.
Sifa hizi za fani zinashabihi-
ana sana na riwaya ya Vuta
Nkuvute iliyoandikwa na
Shafi Adam Shafi na kuchap-
ishwa mwaka 1999, ambayo
ndiyo shughuliko la uhakiki
huu.
Waandishi wa Kizanzibari
mara kadhaa wamean-dika riwaya za kihistoria,
wakizikita simulizi zao kati-
ka zama za ukoloni ama za
kabla ya Mapinduzi visiwani
humo. Kufuatia hali hiyo,
matukio kwenye Vuta Nku-
vute nayo yanazungumzia
siku za mwisho mwisho za
ukoloni visiwani Zanzibar.
Mandhari ya riwaya hii ni
changamano sana, maisha
ya dhiki ya wahusika wakuu
yanachorwa kupitia matukio
kadhaa, wahusika wadogo,
matendo ya kuchangam-
sha, yote yanaunganishwa
na mapenzi ya uhuru na ku-
jutawala (KUJUTAWALA NI
NINI?), katika viwango taf-
auti vya maisha ya kibinafsi,kijamii na kisiasa, na hivyo
kuusafirisha ule moyo wa
Ujamaa katika muonekano
wa kilimwengu zaidi.
Hadithi yenyewe inaanza
kwa kumtambulisha mso-
maji kwa msichana wa Ki-
hindi, Yasmin, ambaye ku-
tokana na mila ya ndoa za
kupangwa na wazazi, anak-
wenda Mombasa na mume
wake, mfanyabiasharamzee, Bwana Raza. Lakini
Yasmin anaoneshwa kuwa
mtu asiye na furaha na mp-
weke na hatimaye anaasi na
kurudi nyumbani, Zanzibar.
Kutabiri matokeo ya makuzi
mabaya ni jambo maarufu
kwenye riwaya za Kiswahili,
ambapo kawaida waandishihuchora mashaka yale yale
yanayoathiri maisha ya vija-
na, hasa wa kike, ama kus-
hindwa hadi kufikia mauti
yao au mateso ya kiakili na
kimwili kama vile Rosa Mis-
tika au Asumini, au kukimbia
mazingira kandamizi kama
vile Maimuna na Yasmin,
ambapo mote hupelekea
maisha mapya kabisa.
Mara tu baada ya kurudi Zan-
zibar, Yasmin anakataliwa na
mjomba wake na anaomba
msaada wa shoga yake wa
pekee, Mwajumba, msicha-
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
13/21
2524 Zanzibar Daima OnlineTUFUNGUE KITABU
WATUHUMIWA MENO YA
TEMBO WAONGEZEKA
JESHI la Polisi Zanzibar li-mewakamata watuhumi-wa wengine watatu, waki-
wamo maofisa wawili wa
Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA) kituo cha Bandari Zan-
zibar kwa kuhusika na kash-
fa ya kupatikana kwa menoya tembo yenye thamani ya
mabilioni ya shilingi.
Kamishna wa Polisi Zanzi-
bar (CP) Mussa Ali Mussa,
amewataja maofisa hao wa
TRA waliokamatwa kuwa
ni Omari Hamad Ali (50) na
Mohammed Hija (48) ambao
wote wanafanya kazi katika
Bandari ya Zanzibar. Mtu-
humiwa mwingine ni kiba-
rua wa Mamlaka ya Bandari
Zanzibar, Haidar Ahmad Ab-
dallah (54).
Kukamatwa kwa watuhumi-wa hao kunaifanya idadi ya
watuhumiwa waliokamatwa
hadi sasa kwa kuhusika na
sakata hilo kufikia watano.
Kamishna Mussa amesema
watuhumiwa wengine wa-
wili ambao ni wafanyakazi
TANBIHI:
Habari hiiiliandikwana gazeti laTanzania Daimala tarehe 17
Inaendelea Uk. 40
na wa Kiswahili anayeishi
kwenye mitaa ya masikini
ya Ngambo, ambaye anam-
pokea kwa moyo wote.
Licha ya ukarimu wa Mwa-
juma, mama yake Yasmin
anakataa kumsamehe bin-
tiye sio tu kwa kuiabisha fa-
milia kwa kumuasi mumewe,
bali pia kwa kujichanganya
na Waswahili na hivyo ku-
vunja khulka ya jamii yake na
tafauti za kijamii na kitama-
duni zilizojikita sana kwenye
unyanyapaa wa sera za
kikoloni linapohusika suala la
mahusiano kati ya makabilayanayounda jamii kubwa ya
Kizanzibari.
Baada ya kukandamiz-
wa kwenye misuguano na
ubaguzi wa kijamii huko
alikokulia, Yasmin anapa-
ta ladha ya maisha mapya
wakati akiishi kwa Mwa-
juma, ambako anagunduamaisha yenye wasaa zaidi,
mukiwemo ulevi, klabu za
usiku na, zaidi ya yote, an-
apendana na kijana aitwaye
Denge.
Denge ni kijana msomi ali-
yerejea nyumbani akitokea
Ulaya akiwa hana chochote
zaidi ya digrii yake ya Kiru-
si na dhamira madhubuti ya
kuikomboa nchi yake kutoka
kwenye Himaya ya Mwing-
ereza. Yeye na marafiki zake
wanaandamwa na polisi kwa
kufanya propaganda ya ki-
siasa na kuingiza kwenye
nchi vitabu na magazeti
yaliyopigwa marufuku na
wakoloni.
Yasmin anajikuta akihusi-
ka moja kwa moja katika
mapambano kati ya kundi
la Denge na polisi, ambaowanajaribu kumlazimisha
amsaliti mpenzi wake mko-
munisti na kafiri, lakini
anaamua kuwasaidia wan-
aharakati hao, akiamini wa-
naandamwa kwa sababu tu
wanapigania uhuru.
Kama inavyoelezwa na
Denge katika ukurasa wa68 wa riwaya hii, serikali ya
Kiingereza ilijaribu kuwaten-
ganisha wapigania uhuru na
wafuasi wao kwa kutumia
sera ya wagawe uwatawale:
Sikiliza Sista, hawa wakolo-
ni na vijibwa vyao ni watu
wapumbavu kabisa, kwao
kila mtu ni koministi Ukid-
ai haki yako wewe koministi
Ukisema kweli wewe komin-
isti Ukipinga kutawaliwa
wewe koministi. Kila anaye-
dai haki kwao ni koministi,na sumu yao kubwa wanay-
oitumia ya kutaka kuten-
ganisha watu kama hao
na wananchi wenziwao ni
kusema kwamba watu hao
wanaowaita makoministl
hawaamini Mungu.
Mapambano ya daima kati ya
maafisa wa kikoloni na wap-
igania uhuru yanaipeleka ri-waya hii kwenye upeo wa ha-
dithi ya kusisimua, kurusha
roho na hekaya za kijasusi,
mtindo ambao uliletwa kwa
mara ya kwanza kwenye
riwaya za Kiswahili na Mo-
hamed Said Abdulla (Bwana
MSA), ingawa kwenye riwaya
hii polisi wamekuwa wahusi-
ka wabaya, wanaotumikiamaslahi ya kikoloni kibubusa.
Kama inavyoelezewa na Pazi
katika ukurasa wa 113, kati-
ka mapambano ya kuwania
uhuru, ni muhimu kutumia
hata njia zisizo za halali
kisheria
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
14/21
2726Zanzibar Daima Online
WARAKA KUTOKA BONNZanzibar Daima Online
Kutafuta mafuta Zanzibarkumeanza mwaka 1957, ilitarajiwakisima cha Chuwini peke yakekitachimbwa kufikia futi 12,000 ....
K
atika wiki mbili za mwanzo za mwe-
zi huu wa Novemba nilitembelea
Umoja wa Falme za Kiarabu. Lichaya kuizuru nchi hiyo mara kadhaa hapo ka-
bla, safari yangu ya mwishoni ilikuwa ndefu
kabisa kuwahi kuifanya na ya kwanza kukaa
na wenyeji walio Waimarati wa kindakinda-
ki, kama wanavojiita watu wa asili wa nchi
hiyo ilio ya muungano wa falme saba ndo-
gondogo.
Imarati, nchi yenye wahamiaji wengi wa Ki-
zanzibari, pia ni nchi yenye historia ya main-
giliano ya miaka na dahari na Zanzibar, ime-piga maendeleo makubwa katika miongo ya
miaka ya karibuni, hasa ya miundo mbinu.
Hivyo imekuwa ni kivutio kwa Wazanzibari
wengi kwenda kutafuta ajira. Wananchi we-
ngi katika miji ya Dubai, Abu Dhabi, al-Ain
na Ras al-Khaimah wanaishi katika neema
ambayo hata watu wa Ulaya wanawaonea
gere. Wafanya kazi hawatozwi kodi ya ma-
Syd.Khalifa akiikagua mitambo yakuchimba mafuta, Zanzibar. Pamojanaye ni M.M.Pennel Mkuu wa Kampuniya Shell.
Waziri Ramadhan AbdallahShaaban akibadilishana hatiiya makubaliano na Mwenyekitiwa Kampuni ya Shell
Wazanzibari tujipange, mafuta yasije yakawa nuksi kwetu
Na Othman Miraji Waraka kutoka Bonn
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
15/21
29Zanzibar Daima Online
28 Zanzibar Daima Online
pato, na serikali inatoa nafuu nyingi kwa
wananchi .
Familia nilikofikia ya watu watano, ukiwacha
watoto wanne, kila mmoja ana gari mbili za
fahari. Tulipoketi kula chakula, meza ilijaa
vyakula vinavoweza kuwashibisha watu 40.
Nilijiuzulu moyoni: kuna harusi? Kadiri asi-limia 60 ya vyakula vinabakia na hutupwa
mapipani. Sebuleni mazungumzo ya weny-
eji wangu yalikuwa tu juu ya likizo zao wa-
lipokuwa Marekani na Ulaya. Mikahawa ya
Kimarekani ya Macdonald na Kentucky ime-
furika katika miji ya Imarati. Vipindi vya te-
levisheni wanavoangalia wenyeji wangu ni
vya kutoka Marekani na Ulaya, ni nadra wao
kuangalia vya Kiarabu.
Nilivuta fikra hadi udogoni mwangu nika-
iona sura ya maduka ya tende, nguru, papa
na chumvi yaliosheheni wakati huo katika
mtaa wa Mchangani, Unguja mjini, pamoja
na suwela na hanide waliokuwa wanauzwa
Malindi. Vitu hivyo vilikuwa vinaletwa Zan-
zibar na mababu wa hawa Waimarati wa
sasa waliokuja katika majahazi yao ya Mu-
sim. Waliporejea makwao pale pepo za Mu-
sim zilipogeuka, watu hao walichukua bori-
ti kutoka Bara na bidhaa nyingine kutokeaZanzibar.
Mnamo muda wa kizazi kimoja tu, maisha
ya Waimarati yamebadilika kwa mshangao
mkubwa, na yote imetokana na utajiri wao
mkubwa wa mafuta ya petroli, k wa jina len-
gine dhahabu nyeusi. Watu hao hadi katika
miaka ya 1950 walikuwa wanaishi katika hali
ngumu, wengi majangwani katika mahema
na katika miji midogo pembezoni mwa Ghu-
ba, wakivua samaki na kula tende, maziwa
na nyama ya ngamia. Sasa wanakula kwa
wingi vyakula vya kutoka ngambo, nyama
kutoka Marekani na Australia inayowaonge-
zea uzito mwilini. Matokeo yake wanapatwana magonjwa ambayo hapo zamani yaliku-
wa nadra kusikika Arabuni.
Niliwauliza wenyeji wangu: Je, mmefikiria
vipi nchi yenu itakavyokuwa bila ya mafuta?
Walinijibu kwamba akiba yao ya mafuta ita-
bakia kwa zaidi ya miaka 100 ijayo. Hata wa-
najizuia kuchimba mafuta mingi hivi sasa ili
bei isiporomoke. Niliwaambia kwamba hata
kama mafuta yatabakia daima, lakini Wa-zungu na Wamarekani, wanaonunua mafu-
ta hayo kwa wingi, itafika wakati watafaulu
kujitosheleza na nishati mbadala ilio safi,
kama vile ile ya kutoka nguvu za jua, upepo
au maji ya moto chini ya ardhi. Walinijibu: Al-
lahu Qadeer -Mwenyezi Mungu ni mwenye
nguvu ya kufanya kila kitu. Kama alivowa-
pa utajiri wa mafuta hivi sasa , basi atawapa
utajiri mwingine pale mafuta yatakapokua
hayahitajiki. Hilo ni jibu la kujipa moyo tu. In-
asikitisha.
Mafuta, licha ya kurahisisha maisha ya watu
wa Uarabuni, neema hiyo nimeona ina ma-
tatizo na hasara zake pia. Raia wengi wa-
naupoteza utambulisho wao na utamaduni
wao, baadhi wameingiwa na kiburi cha kuwa
matajiri sana. Ukiwaona wanatoka kwe-
nye maduka makubwa ya Supermarkets,
wamebeba mifuko mikubwa iliojaa vyakula
chungu nzima vya aina mbalimbali, vitu vya
anasa - vingi ambavyo hata hawatavitumia
- ukiwaona kila mwezi wanabadilisha simu
za mikononi na kuchukua mpya zilizoingia
masokoni unajiuliza: wazimu huu wa ku-
tumbua na kutumbua fedha bila ya mipaka
mwisho wake ni nini?
Ni nchi za Ulaya, Marekani na sasa China zi-
naziuzia nchi za Kiarabu zilizo tajiri kwa ma-
futa bidhaa hizo. Cha kushangaza ni kwam-
ba ni raia wa nchi hizo za Ulaya na Marekani
wanaotambua sasa hasara ya kutumia na
kutumbua mali bila ya mipaka. Ulaya na Ma-
rekani sasa zinajifunza kupunguza matumi-zi, zinajizuia kutumia ovyo rasilmali na utajiri
wao, zikishikilia kwamba binadamu inabidi
aachane na mtindo wa kuishi kwa raha sana
ya kupita kiasi kwa gharama ya vizazi vija-
vyo. Serikali zinawahimiza raia wao wayahi-
fadhi mazingira kwa ajili ya uhai wa sayari
yetu hii ya dunia.
Nchi za Kiarabu zina akiba kubwa ya mafu-
ta, lakini hiyo haina maana kwamba mafutahayo yatumiwe ovyoovyo. Ukiona taa nyingi
zinazowaka ovyo usiku mzima mabarabara-
ni na maji ya chumvi mengi yanayogeuzwa
kuweza kunyunyuzia bustani unasikitishwa
na uchafuzi mkubwa wa ma zingira unaosa-
babishwa na moshi mchafu hewani. Bei ya
lita moja ya mafuta Abu Dhabi ni asilimia 14
tu ya bei mtu anayolipia akiwa Berlin,Ujeru-
mani.
Mwanadamu alitoka kutoka enzi ya ustaara-
bu wa kutumia mawe na kuingia katika enzi
ya ustarabu wa kutumia chuma, na hiyo si
kwa sababu mawe yalikwisha. Hasha. Ila tu
binadamu alitanabahi kwamba chuma ndio
njia ya kuboresha maisha yake. Na hivyo
ndivyo itakavokuwa pale mwanadamu ata-
kapoachana na mafuta, si kwamba mafuta
hayatakuweko, lakini kutakuwako mbadala
ulio bora.
Kuna habari nzuri kwamba si miaka mingi
kutoka sasa, Inshaallah, nchi yetu ya Zan-
zibar itakuwa mtoaji wa mafuta ya petroli.
Nahisi ni wakati sasa kwa Wazanzibari kuji-
tayarisha, kisaikolojia, juu ya ujio wa neemahiyo. Mafuta yameleta maendeleo kwa nchi
kadhaa, lakini utajiri huo kwa baadhi ya nchi
umeziletea madhara. Si tu tujifunze namna
ya kuyachimbua mafuta hayo na kutowa-
achia kila kitu wageni watufanyie, lakini pia
tupange tangu sasa namna ya kujiepusha
na hasara zilizopata nchi nyingine kutokana
na mafuta, kisaikolojia, kwa wananchi wao,
kimazingira, na kupanuka mizozo ya kijamii.
Tujue kutakuweko uchochezi wa kutoka njewa waroho watakaonyemelea kuupora uta-
jiri huo kwa kutugonganisha vichwa weny-
ewe kwa wenyewe Wazanzibari. Pia tuchu-
kue tahadhari juu ya kumomonyoka maadili
na tunu zetu, kwa kisingizio cha utandawazi
unaotokana na utajiri huo. Mafuta yawe ba-
raka na si nakama na balaa k wetu
WARAKA KUTOKA BONN
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
16/21
30 31Zanzibar Daima OnlineZanzibar Daima Online
Dk Mvungi ameikosatreni ya mwisho ilatuko naye
Watu wengi wamekuwa wakisikia
sifa nyingi mno za Dk Adri-
an Sengondo Hamis Mwarabu
Mvungi katika kipindi alichokuwa amejeru-
hiwa na wanaodhaniwa kuwa ni majambazilakini wamesikia zaidi baada ya kufa kwake.
Si ajabu watu wengi wanadhani hizo ni sifa
anazopewa tu kwa sababu ameshakufa
hasa kwa kuwa Waafrika na watu wenye
imani ya dini wanaamini kuwa maiti hasem-
wi vibaya. Lakini hiyo sio kweli hata kidogo.
Kwa hakika Dk Mvungi, aliyetimiza umri wa
miaka 61 siku moja kabla hajashambuli-
wa, alikuwa ni mtu mwema, mstahamilivu,
msikivu na hodari sana kwa watu.
Kama kuna njia ya kumwombea binadamu
wa kawaida apite njia nyepesi kuelekea kwa
Muumba wake, sisi wajumbe wa Tume am-
bao tumemjua Dr Mvungi tusingesita kufa-
nya hivyo. Kila mmoja wetu anaijua sifa ya
ukarimu wake pamoja na umbo kubwa am-
balo lingemfanya awe na kiburi cha maguvu.
Daktari huyu wa sheria aliyasabilia maisha
yake kwa watu. Alianza kwa ndugu zake na
jamaa zake. Si hasha moja ya matunda yake
ni padre anayesimamia kanisa la St Joseph
mjini Dar es salaam na utitiri wa nduguzeambao wengi wao wamehitimu hata elimu
ya juu.
Akajitolea kusimamia wachochole na wala-
lahoi kwa nguvu na elimu yake. Alianzia kwa
kuanzisha kituo cha kisheria cha kuwasaidia
wanyonge na baadaye alisukuma kuund-
wa Kituo cha Haki za Binadamu na Sheria
(LHRC) na kushirikiana nacho katika mambo
kadhaa pamoja na kubuni njia kadhaa za ku-
wasaidia watu wa tabaka hilo.
Ndipo mwombolezaji mmoja aliposema, Ni
kinyume cha mambo kwamba waliomuua ni
katika kundi la wanyonge ambao angeweza
kwenda Mahakamani kuwatetea. Lake ali-
jualo Mungu ni la shani zaidi.
Ratiba ya Dlk Mvungi ilikuwa ya ajabu sana.
Dk. Adrian SengondoHamis Mwarabu Mvungi
Daktari huyu wa sheriaaliyasabilia maisha yakekwa watu. Alianza kwandugu zake na jamaazake. Si hasha moja yamatunda yake ni padreanayesimamia kanisala St Joseph mjini Dar
es salaam na utitiri wanduguze ambao wengiwao wamehitimu hataelimu ya juu.
Barza ya Jumba MaroNa Ally Saleh
BARAZA YA JUMBA MARO
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
17/21
32 33Zanzibar Daima OnlineZanzibar Daima Online
Nayo hiyo ilitokana na muda mrefu wa ku-
jizoesha ambapo kila siku ya Mungu alikuwa
akifanya mchakamchaka, au saa 12 asubuhi
alikuwa ameshaanza kazi kama alivyoshu-
hudia mfanyakazi mwenzake wa South Law
Chambers aliyekutana naye siku hiyo ya ku-
zaliwa kwake tarehe 2 Novemba.
Kwenye taaluma Dk Mvungi, ambaye ali-
kuwa mwalimu wangu wa somo la Katiba
katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, haku-
wahi kufanikiwa kufikia uprofessa na miye
naamini ni kwa sababu alikosa muda kwa
vile kipindi kikubwa alikitumia akijitolea ku-
wasaidia watu.
Aliandika sana kuhusu haki za binadaamu na
mambo ya katiba na alitoa matamko mengi
ambayo ungeyasikia kama yalivyonukuli-
wa na LHRC ungetokwa na machozi. Alijaa
tamaa ya usawa, uchu wake, kiu ya mabadi-
liko lakini hasa alikuwa na ashiki ya usawa.
Alikuwa Mjamaa ndani ya moyo wake lak-
ini pia alikuwa yu tayari kwa mabadiliko ya
zama mpya. Na ndio maana akaona njia pe-
kee ni kuingia ndani ya mfumo na akajaribu
kugombea Urais mwaka 2000, lakini mfu-
mo ulimjibu vilivyo maana hata kura yake
mwenyewe katika k ituo alichopiga kura hai-kuonekana na kuhesabika.
Alikiri kushindwa katika ugombezi huo bila
ya kinyongo na akaona kunakomfaa katika
harakati hizi ni kuwa upande wa wananchi
na ndipo nguvu zake za kudai Katiba Mpya
zikawa za kasi, kina na nguvu zaidi.
Si katika waliochelewa hata huko nyuma.
Maana alianza pale mwaka 1992 NCCR-Ma-
geuzi ilipoanza kutokana na Watanzania
kuona haja ya mabadiliko ya Kikatiba.
Niliwahi binafsi kukutana naye katika Kama-
ti ya Katiba iliyoundwa na vyama mbalim-
bali vya siasa. Mimi nikaonekana nafaa ku-wemo humo tutengeneze Katiba ambayo
ingepelekwa Serikalini, lakini Serikali ilisema
wakati bado.
Rais Jakaya Kikwete wakati wa kuzindua
Tume ya Katiba mwaka jana alimdhiha-
ki Dk Mvungi kwa kumwambia alimkuta
amejifungia katika hoteli moja Bagamoyo
akitengeza Katiba. Akamwambia kwamba
sasa kuwamo katika Tume ya Katiba ni fur-
sa ya kutumia nguvu zake zote katika kazi
hii mpya.
Na kwa kweli sisi tulio ndani ya Tume tuna-
kiri alitumia nguvu zake zote. Alikuwa tayari
kufanya utafiti, kusoma makala ya ziada na
hata kujitolea kwa lolote lile. Alitoa sulu-
hu palipokwama, alitoa ushauri penye fun-
do alimradi alichotaka ni kwamba mwisho
Katiba ipatikane.
Nilibahatika kufanya naye kazi kwenye
Kamati iliyoaminiwa kuwa ngumu kuliko
zote katika Tume. Humo ndiko nilikomjua
zaidi na kustaladhi kufanya naye kazi. Kub-
wa ni kuwa alikuwa mtu wa maridhiano. Ali-
kuwa muda wote tayari kuuacha msimamo
wake pindi akishawishiwa na alitafuta sulu-
hu ili kuuridhia upande ulojisogeza.
Tulimtania sana na yeye alikuwa na utani
mwingi. Mimi sijawahi kufanya kazi katika
Tume ya Kitaifa yoyote ile, lakini nimeona
kazi katika Tume ya Katiba ilikuwa nyepesi
kwa sababu ndani yake pamekuwa na nafa-si ya ubinadamu na zaidi watu wote wame-
jifanya ni wa daraja moja na kwa hivyo
wamejenga ukuruba. Mmoja aliyekurubiwa
na kila mtu ni yeye Dk. Mvungi.
Aliwahi kusema kwamba angetamani kus-
hona suti ili aende katika Bunge la Katiba
kutetea andiko la Tume ambalo alifanya kila
njia liaminike na likubalike kwa sababu al-
ijua huo ni mchango wake muhimu na ali-
fanya kazi kana kwamba ndio kazi yake ya
mwisho.
Lakini hakuwahi kuivaa suti yake kama al-
ivyokosa kuendelea kuwemo katika Treni yaKatiba ambayo inaelekea kituo chake cha
mwisho. Ila wengi tunaamini japo hatutam-
wona tena atakuwa akitusubiri kusherehek-
ea na sisi Katiba Mpya katika zama mpya
za Tanzania ambazo wanawe na wanetu
wataishi nazo
Wanachama wa NCCR - Mageuzi wakiwa wamebebajeneza lilohifadhi mwili wa Kiongozi wao Marehemu
Mvungi, ambae pia alikuwa ni Mjumbe wa Tume yaMadiliko ya Katiba Mpya.
BARAZA YA JUMBA MARO
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
18/21
34 35
HEKAYA ZA Z ANZIBAR
Zanzibar Daima OnlineZanzibar Daima Online
MEZA FUPABila ya kubaini, chembe
ndogo ya wema
uipandayo ardhini, huenda
ikachipua na kutoa mti
mkubwa utakaoweza
kukupatia kivuli aukuwapatia wengine
wakati wa jua kali la
kiangazi.
Bila ya kubaini, chem-
be ndogo ya wema
uipandayo ardhini,
huenda ikachipua na kutoa
mti mkubwa utakaoweza
kukupatia kivuli au kuwap-atia wengine wakati wa jua
kali la kiangazi.
Ilikuwa ni safari ya mwendo
mkubwa, walikuwa ni vijana
watatu walioongozana kati-
ka kukitafuta kijiji ambacho
walipata kusikia kuwa aliishi
bibi mwenye historia nzima
ya nchi yao. Bibi aliyeishi mi-
aka mia mbili, ndiye pekeye
aliyeweza kutambua hali hal-
isi ya nchi yao. Sio kama hai-kuwepo historia, lakini histo-
ria iliyokuwepo ilipotoshwa
na kuwaziba macho vijana
waitwao kizazi kipya.
Walilkuwa ni vijana watatu
wenye umri kati ya miaka
ishirini hadi thelathini. Aliyekuwa mstari
wa mbele katika kuiandaa safari hii ali-
kuwa ni Miftaha, kijana jasiri asiyeogopa
kitu katika kuitafuta haki. Mwili wake ul-
ionekana dhaifu kutokana na wembamba
wake, alikuwa ni mweusi kidogo, hakuwamrefu sana ila wembamba wa umbile lake
ulimfanya aonekane mrefu wa kimo.
Wengine walikuwa ni Suheli na Maimuna.
Wanaume wawili na mwanamke mmoja.
Maimuna alikuwa ni ndugu yake Miftaha.
Bi. Msiri alifanana na jina lake. Moyo wake
uliyabeba mengi tena makubwa mithili ya
dunia au sawa na umri wake. Miaka mia
mbili kwa ulimwengu wa sasa utatolewa
kwenye vyombo vya habari na kuingiz-
wa katika kundi la watu wa maajabu. Huundio ulikuwa umri wa bibi huyu aliyeishi
katika kiijiji cha Maukio. Pamoja na umri
wake mkubwa, bibi huyu alikuwa na meno
yote thelathni na mbili, macho yake yali-
kuwa hayaoni tena vizuri lakini alikuwa na
uwezo wa kusikia kama mtoto mdogo, si
Hekaya za ZanzibarNa Ally Hilal
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
19/21
36 37Zanzibar Daima OnlineZanzibar Daima Online
rahisi kumsengenya ukiwa karibu yake.
Alikuwa anatembea kwa tabu sana, alitem-
bea kwa mkongojo wake uliochongwa vi-
zuri, ulichorwa nakshi nzuri za msumeno na
ulikuwa umeandikwa TUTAFIKAJE?
Bi Msiri aliishi kando na mto mkubwa ul-
iokuwepo katika bonde kubwa kijijini pale.
Maisha yake yalikuwa ya upweke tangu al-
ipokuwa na miaka ishirini baada ya kuipo-
teza familia yake yote katika hali tata hadi
leo hakuweza kuwaona tena.
Alikuwa mtu wa mwanzo kuhamia kijiji
hiki baada ya kukimbia mjini kwao na kuji-
tokomeza katika bonde hili. Aliishi kwa tabu
sana akiwa mafichoni huku ambako kuliku-wa mbali na mji aliotoka.
Miaka ilivyozidi kusonga mbele, nyumba zili-
sogea hadi kufika sehemu aliyoishi Bi Msiri.
Ni historia ndefu ambayo hakuna aliyeijua,
walioishi naye walikuwa hawajui chochote
kuhusu bibi huyu, walimuona kuwa ni bibi
wa kawaida tu asiyepungua umri wa miaka
themanini kutokana na muonekano wake
lakini hawakuujua umri halisi wa bibi huyu.Hakuwahi kuwa na rafiki wa karibu ambaye
aliweza kubadilishana naye mawazo zaidi
ya Bi Tausi aliyekuwa mkulima katika bonde
hili, alikuwa na shamba lake mwenyewe.
Linaweza likajengeka suali katika akili ya mtu
kuhusu bibi huyu aliyejitenga na watu kwa
miaka mingi na aliyebeba siri nzito moyoni
mwake, suali jengine ni kuwa vipi Miftaha
na wenzake waliujuwa uwepo wa bibi huyu
na kwa ajili gani waliamua kumtafuta.
Miftaha ni miongoni mwa vijana waliopata
elimu, alisoma hadi chuo kikuu nje ya nchi,
alibahatika kusomeshwa na serikali yake il-
iyokuwa madarakani kutokana na nafasi ya
baba yake, baba yake alikuwa mfuasi mkub-
wa wa chama kilichokuwepo madarakani,
hapakuwa na chama cha upinzani kwa sa-
babu serikali iliogopa kupingwa na kukosa
wafuasi iwapo wataendesha serikali yao
kinyume na wanavyotaka wananchi. Pamo-
ja na hayo wananchi wengi hawakukiunga
mkono chama hiki, walikipinga chini kwa
chini kwa kuhofia kukamatwa na kuishia
gerezani. Pamoja na kwamba Miftaha al-iishi kwa baba yake, baba yake alikuwa ni
mshauri wa raisi wa nchi, aliyajua mengi yal-
iyokuwa yakitendeka nchini, lakini watoto
wake wote wawili hawakukubaliana naye,
kila siku waligombana na baba yao. Licha ya
elimu yake, Miftaha hakuweza kupata na-
fasi za juu serikalini kama ilivyokusudiwa na
baba yake hapo awali, kusoma kwake nje
ilikuwa ni kuandaliwa ili aweze kuingizwa
katika mfumo wa serikali lakini alionekanana msimamo tofauti, kutokana na sababu
hiyo alibaki kuwa mwalimu wa skuli.
Siku moja alirudi mapema skuli kwa sababu
kichwa kilikuwa kinamuuma, ilikuwa ni jioni
saa kumi na moja kamili, alikutana na Bibi
mmoja aliyechoka sana, mguu wake uliku-
wa unavuja damu, alikuwa ametafunwa na
nyoka, ilikuwepo gari moja tu inayokuja ku-
toka kijiji alichoishi bibi huyu, ilikuja asubuhi
na kuondoka jioni, alikuwa ni Bi Tausi, rafiki
yake bi Msiri.
Miftaha alisimama na kusogea pembeni al-
ipokuwepo bibi huyu, alimuweka kwenye
kibao cha baiskeli yake na kumpeleka hos-
pitali.
Hakuna aliyemjali mgonjwa, kila mmoja ali-
jishuhulisha na kazi zake, baadhi ya waugu-
zi walimtazama mgonjwa wa Miftaha kwa
dharau bila ya kujali kuwa alikuwa katika hali
mbaya kwani sumu ya nyoka ilikuwa inazidi
kumuenea mwilini. Daktari wa zamu aliku-
wa amekaa nje anasoma kitabu cha riwaya.Miftaha alitoka hadi nje baada ya kuambi-
wa kuwa daktari wa zamu alikuwepo nje,
alimkuta daktari amewacha kitabu na sasa
anacheza karata na vijana wa mtaa. Ilimuu-
ma sana kumuona daktari anacheza karata
huku wagonjwa wakiumia bila ya matibabu,
alimsogelea daktari na kumwambia kuwa
kuna mgonjwa yuko hali mbaya.
Alipata majibu ya kukatisha tamaa.
Kijana mimi mwenyewe ni mgonjwa hapa,
au hujui kama na sisi madaktari ni wagonj-
wa na tiba yetu hatujaiona, vilio vyetu hav-
isikilikani maana tuna sauti ndogo, ila nyinyi
munataka tuvisikilize vilio vyenu, je vyetu
avisikilize nani?
Maneno haya alikuwa anayazungumza da-
ktari kumwambia Miftaha bila ya kumtaza-
ma aliyekuwa akizungumza naye.
Kwa hiyo unataka kunambia kuwa wagon-
jwa wetu tuwaache wafe?
Yule daktari aliendelea kucheza karata na
kumjibu Miftaha bila ya kumtazama usoni.
Kufa! Mh! Sasa wewe unafikiri mimi unay-
eniita daktari niko hai! Kwa lipi la kusema ni
uhai, mimi ni maiti k wenenda!
Muda ulizidi kupotea, Miftaha aliamua kuz-
itawanya karata na kuuharibu mchezo, vi-
jana waliokuwepo pale walipanda hasira na
karibia kumrukia Miftaha, muda wote huo
Daktari alikuwa hajamjua anayelumbananaye, alipoinua uso wake alimuona Maal-
im Miftaha ambaye alikuwa ni mwalimu
msaidizi wa skuli ya Mwendapole, alikuwa
ni mwalimu wa watoto wa daktari, alipojua
kuwa alikuwa ni mwalimu wa watoto wake
aliomba radhi kwa kudai kuwa alikuwa ha-
jamjua. Aliwatuliza vijana waliokuwa na ha-
sira na kutaka wamuache mwalimu.
Miftaha alitikisa kichwa na kuongozana nadaktari bila ya kumjibu kitu ingawa daktari
alijifanya mchangamfu kwa lengo la ku-
jizimuwa kwa maneno yake yaliyomkera
Miftaha.
Itaendelea.
HEKAYA ZA Z ANZIBAR
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
20/21
38 39Zanzibar Daima OnlineZanzibar Daima Online38
KALAMU YA BIN RAJAB
HOTELI MPYA YA NYOTA SABAKUFUNGULIWA MJI MKONGWE
Na Ahmed Rajab Kalamu ya Bin Rajab
Mapema mwakani hoteli mpya ita-
funguliwa Mji Mkongwe. Inase-
mekana kwamba hoteli hiyo ita-
kuwa na hadhi ya nyota saba. Ikiwa ni kweli
basi tunastahiki kujipigia makofi kwani niju-
avyo ni kwamba duniani kuna hoteli moja tu
yenye nyota saba; nayo imejibandika yeny-
ewe hadhi hiyo ya kuwa ya nyota saba.
Hiyo hoteli inayojigamba kwamba ni yenye
nyota saba ni hoteli ya Burj al Arab iliyo Du-
bai. Nijuavyo ni kuwa hata ya nyota sita iko
moja tu duniani, nayo ni Hoteli ya Fullerton
iliyoko Singapore.
Bila ya kujiingiza katika mabishano ya iwapo
ni kweli hoteli hiyo mpya ya Mji Mkongwe
itakuwa ya nyota saba ni sahihi nadhani tu-
kisema tu kwamba hoteli hiyo itakuwa ku-
bwa na ya kisasa. Mapambo na nakshi za
ndani ya hoteli ni za hali ya juu kabisa.
Hoteli hiyo itayofunguliwa mwakani Mji
Mkongwe itaendeshwa na Kundi la Ma-
Burj Al Arab
-
8/13/2019 Zanzibar Daima Online: Toleo la Saba
21/21
40 41KALAMU YA BIN RAJAB
Zanzibar Daima Online Zanzibar Daima Online
kampuni ya Melia yenye makao yake makuu
Uhispania. Kweli sio sisi tuliotoa fedha za
kuijenga kwa hivyo hatuwezi kusema kuwa
ni yetu lakini iko kwetu.
Hilo si fanikio dogo kwa sababu kampuni
hiyo ya Uhispania kuamua kujenga hoteli
aina hiyo Mji Mkongwe kunaashiria mengi
kuhusu Zanzibar.
Muhimu ni kwamba kampuni hiyo baada ya
kuipima na kuitathmini hali ya mambo ilivyo
Zanzibar imeona kwamba kuna usalama na
utulivu wa kutosha kisiwani humu wa kuha-
kikisha kwamba rasilmali yao wanayoileta
Zanzibar haitokuwa hatarini.
Walioijenga hoteli hiyo wanasema k wambaujenzi wake umefuata kanuni za kuuhifadhi
Mji Mkongwe ambao umetangazwa na Shi-
rika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (Unesco) kuwa ni moja ya Tu-
rathi za Dunia.
Hayo yote ni sawa. Lakini kuna mingine
yaliyo mazito pia yanayostahili kuzingatiwa
na waendeshaji wa hoteli hiyo ili isije ikawa
chanzo cha mfarakano baina ya wakazi wa
Unguja mjini, hasa wa Mji Mkongwe, na ho-
teli yenyewe.
Tunafahamu kwamba hoteli ya babu kubwa
kama hiyo itahitaji iwe na wafanyakazi we-
nye ujuzi mkubwa na uzoefu wa shughuli za
utalii. Tunatambua kwamba huenda tusiwe
na watu wa aina hiyo walio tayari kupatiwa
ajira hotelini humo.
Hata hivyo, tuna haki ya kuwauliza wakuu
wa hoteli hiyo iwapo wameandaa mkakati
wowote wa kuwafunza vijana wenyeji wa
Mji Mkongwe shughuli za utalii ili wawezenao kupatiwa ajira humo badala ya kuajiri-
wa watu kutoka nje ya Zanzibar.
Ikifanya hivyo basi hoteli hiyo itasaidia ku-
wapatia ajira vijana na hivyo kuwaingiza ka-
tika jamii badala ya kuwatenga na itasaidia
pia kuupiga vita umaskini na unyonyaji.
Mwaka 1999, Jumuiya ya Umoja wa Mataifa
ya Utalii Duniani (UNWTO) ilitunga kanuni za
maadili kuhusu utalii ambazo zinatakiwa zi-
fuatwe kote duniani. Kanuni hizo zina lengo
la kupunguza athari mbaya zinazopata nchi
na wana wa nchi, kutokana na shughuli za
utalii.
Kwa hakika, inatia moyo kuona kwamba
mahoteli duniani siku hizi yanajihusisha na
masala ya haki za binadamu na maadili ya
kufanyia biashara. Katika muda wa miaka
kumi iliyopita makampuni makubwa ya ho-
teli yamechukua hatua muhimu za kuziun-
ganisha sera za haki za binadamu na ku-ziingiza katika sera zao kuhusu maadili na
namna ya kufanya biashara.
Suala la maadili lina umuhimu mkubwa
katika nchi kama ya kwetu yenye kufuata
maadili ya Kiislamu. Utalii tunautaka lakini
hatuutaki ikiwa utakuwa unazikanyaga mila
zetu, dini yetu na ut amaduni wetu.
Hapo ndipo penye hatari. Na hatari inaweza
ikazuka mara moja iwapo hatuhakikishi ya
kwamba wageni wenye kuendesha shughuli
za utalii nchini mwetu hawendi kinyume na
maadili yetu. Miongoni mwa wanayopaswa
kuyafanya ni kuhakikisha kwamba haki za
binadamu zinaheshimiwa na kwamba wa-
toto wadogo wanapewa hifadhi na hawa-
tumiwi kwa shughuli za kifisadi, kama kwa
mfano za ngono, na wateja wa hoteli.
Wakuu wa hoteli hiyo, pamoja na nyingine-
zo zilizo Mji Mkongwe, wana wajibu wa ku-
angalia namna gani wanaweza kuwasaidiawenyeji wa Mji Mkongwe sio tu katika ku-
wapatia ajira lakini pia katika mambo min-
gine ili wahisi kwamba hizo hoteli kweli ni
sehemu ya jamii yao
wa Kampuni ya Uwakala wa Mizigo ya Is-
land Sea Food Limited, Mohammed Sule-
iman Mussa (45) na Juma Ali Makame (34),
walikamatwa siku ya tukio la kukamatwa
kwa meno hayo ya tembo kwenye Bandari
ya Zanzibar.
Tayari watuhumiwa hao wamesafirishwa
kwenda Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi. Pamoja
na mambo mengine, kusafirishwa kwa wa-
tuhumiwa hao kwenda jijini Dar es Salaam,
kunatokana na Zanzibar kutokuwa na sheria
maalumu inayohusu wanyamapori.
Maofisa wa Idara ya Wanyamapori nchini
leo wamekamilisha kazi ya kuhesabu na ku-
linganisha vipande 1,023 vya meno ya tem-
bo vilivyokamatwa juzi kwenye Bandari ya
Zanzibar na kubaini idadi ya tembo walio-
uawa kuwa ni 305.
Meno hao yenye uzito wa kilo 2,915 yenye
thamani ya dola 4,775,000 sawa na Sh
7,480,125,000 za Tanzania, yalikamatwa
Inatoka Uk. 25 WATUHUMIWA MENO YA TEMBO WAONGEZEKAjuzi yakiwa yamehifadhiwa katika magu-
nia 98 na kuwekwa kwenye kontena moja
la futi 40 lenye namba PCIU 857619/0 li-lilokuwa tayari kupakiwa kwenye meli ya
MV Kota Henning kupelekwa nchini Ufili-
pino kwa magendo.
Hadi sasa bado makachero wa Polisi wa
Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikia-
na na makachero wa Polisi Zanzibar, Idara
ya Wanyamapori makao makuu wanaen-
delea na upelelezi kuwabaini waliohusika
na kashfa hiyo.
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP)
Mussa Ali Mussa, alisema kuwa kazi ku-bwa iliyobaki ni kuhakikisha upelelezi wa
kina unafanyika ili kuwakamata wahusika
wa mtandao huo.
Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi bado li-
namsaka tajiri aliyewezesha mipango ya
kukusanywa na kusafirisha shehena hiyo
kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar ili ku-
safirishwa nje ya nchi