fataawa za wanachuoni (13)
DESCRIPTION
1 .·«·-|· .,··· Fataawa Za Wanachuoni [13] Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush © 2 Dibaji: Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo. Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faidaTRANSCRIPT
1
������� ���
Fataawa Za Wanachuoni
[13]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo ni hizi zifuatazo:
1. Kunywa Kwenye Kikombe Cha Dhahabu
2. Je, Ni Lazima Kwa Mke Kufanya Kazi Za Nyumbani?
3. Hukumu Ya Kusherehekea Krismasi Na Sikukuu Za Makafiri
4. Hukmu Ya Filamu Zinazolingania Katika Kheri Na Fadhila
5. Kufurahi Kwa Kufa Mwanachuoni IbnJibriyl
6. Anaekufa Huku Kaacha VitabuMbalimbali Vya Dini
7. Hatari Ya Mawasiliano Ya Wachumba
8. Jamaa´at-ut-Tabliygh Wanahitajia Jihaad
9. Kufasiri Vitabu Bila Ya Idhini Ya Mwandishi
10. Kunywa Katika Kikombe Cha Dhahabu
11. Swalat-ul-Kusuuf Msikitini Au Nyumbani?
12. Baba Hataki Kuswali Anadai Anajua Zaidi Yangu
13. Kumtembelea Mtu Ambaye Haswali
14. Habbat Sawdaa (Haba Soda) Ni Dawa Ya Kila Ugonjwa
15. Hukumu Ya Jina La ”al-Haadiy”
16. Je, Du´aa Hii Yatosheleza Du´aa Zingine Zote?
17. Je, Inajuzu Mwanamke Kuvaa Suruwali Pana Isiyobana?
18. Je Kumuona Mtume Usingizini Ni Bishara Njema?
19. Kuomba Wafu Ni Shirki Kubwa Au Ndogo?
20. Kumpa Mtu Jina La "Mwenye Kumjua Allaah"
21. Kupokea Zawadi Ya Pesa Za Haramu
22. Kupunguza Ndevu Au Kufukuzwa Kazini?
23. Kusomea Maji Ruqyah Kisha Kuyaoga
24. Msafiri Kujumuisha Swalah Ya Ijumaa Na ´Aswr
25. Tofauti Ya Sunnah Na Ada Ya Mtume (و��م ���� ��)
26. Upi Msimamo Wa Mwanamke Kwa Madu´aat Wapotevu?
27. Wale Wanaotumia Mantiki Na Falsafa Katika Hadiyth
28. Wanachuoni Wa Hedhi Na Nifasi
29. Wale Wanaokaa Na Ahl-ul-Bid´ah Wamelaaniwa
30. Neno "Jins-ul-´Amal" Limetoka Kwa Murji-ah
31. Mwanamke Kwenye Nifasi Akitwaharika Kabla Ya Siku Arubaini
32. Mwanamke Anaetaka Kuzaa Kapitwa Na Swalah Nyingi, Afanye
Nini?
4
33. Mishaary Raashiyd al-´Afaasy Na Anashiyd Zake
34. Kwa nini Mwanamke Hafai Kumuonesha Mwanamke
Wa Kikafiri Nywele Zake?
35. Kipote Kitakachookoka Na Moto
Wanachuoni waliomo ni hawa wafuatao:
1. ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
2. Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
3. Swaalih bin Swaalih bin Fawzaan
4. Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
5. Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
5
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1. Kunywa Kwenye Kikombe Cha Dhahabu
Swali:
Swali kutoka Ireland. Je, inajuzu kunywa kwenye chombo cha dhahabu?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Jibu hapana! Chombo cha dhahabu haijuzu kukinywiya humo kitu.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=itDh565ss1s
2. Je, Ni Lazima Kwa Mke Kufanya Kazi Za Nyumbani?
Swali:
Je, mwanamke ni lazima kupika na kutandika kitanda nyumbani kwa ajili ya
mume wake?
´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy:
Ada za kiarabu na za Waislamu wengine katika wanawake ni kwamba wao
ndio wanaofanya kazi mbalimbali katika manyumba yao; kama kufua nguo,
kuangalia watoto n,k. Hili ni jambo wanaliweza baina ya Waislamu na
waarabu. Hatotoka mwanamke katika hilo. Kuna Wanachuoni wanaosema
kwamba hana ulazima wa chochote katika makazi, bali lililo la wajibu kwake
ni ile sababu ya mwanamme kumuoa. Akifanya kazi hizo basi yuko na ujira
6
na kafuata Maswahabah wanawake wema [... sauiti imekatika ...] ufahamu
katika Dini.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=BkKE5lN0K2c
3. Hukumu Ya Kusherehekea Krismasi Na Sikukuu Za Makafiri
Swali:
Baadhi ya Waislamu wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa - yaani krismasi
kama wanavyoiita, tunaomba nasaha?
Imaam Ibn Baaz:
Haijuzu kwa Muislamu mwanamme na mwanamke kushirikiana na
Manaswara au Mayahudi au makundi mengine katika sikukuu zao. Ni wajibu
kuacha hilo kwa kuwa [Mtume yu wasema]:
"Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao."
Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katukataza kushirikiana nao,
kuchukua tabia zao. Ni juu ya muumini mwanamme na mwanamke
kujiepusha na hilo wala wasihudhurie katika sikukuu zao kwa chochote. Kwa
kuwa sikukuu zao zinakhalifu Shari´ah ya Allaah isitoshe ni maadui wa
Allaah. Kwa hiyo haijuzu kushiriki humo wala kusaidizana nao wala
kuwasaidia kwa lolote; si kwa [kunywa] hata chai, kahawa na kadhalika. Pia
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
�وى و� ��و�وا ��� ا� م وا�دوان و��و�وا ��� ا��ر� وا���
”Na saidianeni katika wema na uchaji Allaah. Wala msisaidiane katika
dhambi na uadui.” (05:02)
7
Kushirikiana na makafiri katika sikukuu zao ni aina ya kusaidiana katika
dhambi na uadui. Ni wajibu kwa Waislamu wote wanamme na wanamke
kuacha hilo. Wala mtu asidanganyike na wayafanyayo watu; bali ni wajibu
aangalie alifanyalo - Uislamu na yale iliyokuja nayo na atekeleza amri za
Allaah na Mtume Wake wala asidanganyike na mambo ya watu. Hakika watu
wengi hawajali na Shari´ah ya Allaah, kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall)
katika kitabu Chake kitukufu:
� وإن �ط+ أ( ر )ن '& ا%رض �#�"وك �ن ��ل
“Na ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya
Allaah.” (06:116)
و)� أ( ر ا����س و�و 1ر0ت �)ؤ)��ن
“Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.” (12:103)
Ni wajibu kutekeleza Shari´ah, haijuzu kuichukulia sahali. Muislamu hufanya
vitendo na kauli zake na za watu kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah za
Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa yataafikiana nayo
(Qur-aan na Sunnah) basi yatakubaliwa hata watu wakiyaacha. Na
wakiyakhalifu au wakayachukia watu, yatarudishwa (hayatokubaliwa) hata
watu wakiyafanya.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=O7jikWCbou0
4. Hukmu Ya Filamu Zinazolingania Katika Kheri Na Fadhila
Swali:
8
Huyu anauliza hukumu ya filamu ambazo zinalingania katika kheri na
fadhila?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kheri na fadhila bila ya filamu. Hawakuwa Salaf wakicheza filamu. Hizi ni
katika desturi ambazo zimetujia kutoka nje. Wala hatutumii filamu kwa
Da´wah. Si katika mfumo wa Da´wah kucheza filamu, kamwe.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa &
http://www.youtube.com/watch?v=axQeeDqdIbs
5. Kufurahi Kwa Kufa Mwanachuoni IbnJibriyl
Swali:
Baadhi ya wanafunzi walifurahi kwa kufa Shaykh Ibn Jibriyn (Rahimahu
Allaah). Je, kitendo hichi ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili halijuzu. Haijuzu kufurahi kwa kifo cha Waislamu wote kwa jumla.
Haijuzu kwa kuwa hili ni kashfa katika Uislamu. Tusemeje kwa kifo cha
mwanachuoni? Haijuzu hili kuwa wanafurahi kwa mauti ya mwanachuoni
katika Wanachuoni wa Kiislamu. Hili linatokana ima kwa ujinga au unafiki -
A´udhubi Allaah.
Chanzo: http://alfawzan.ws/node/2034
http://www.youtube.com/watch?v=uOWhuy9lQJc
9
Tarehe: 1430-08-18/2009-08-09
6. Anaekufa Huku Kaacha VitabuMbalimbali Vya Dini
Swali:
Muulizaji kutoka Ireland, je vitabu ambavyo vipo maktabah ni katika elimu
ambayo itakuja kumfaa mtu baada ya kufa kwake?
´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy:
Bila shaka, vitabu vya faida kama vya tafsiri, hadiyth, fiqh, syrah ya Mtume,
´aqiydah na vitabu vingine vya Kiislamu akifariki mtu na kukaja mtu baada
yake sawa ndugu au wengineo, hakika yuko na ujira mbele ya Allaah
(Tabaarak wa Ta´ala) kwa elimu ya manufaa aliyoacha.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=b-4Jbk_ySkU
7. Hatari Ya Mawasiliano Ya Wachumba
Swali:
Je, inajuzu kuwasiliana wawili wanaotaka kuchumbiana kwa idhini ya walii
wake (mwanamke)?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
10
Hili halitakiwi kuwa moja kwa moja (yaani bila mipaka). Kwa kuwa
wakiwasiliana baina yao, mawasiliano mengi hakuaminiki huenda kukatokea
mawasiliano ya vitendo. Baada ya mawasiliano ya vitendo la kufuatia ni
mawasiliano ya kimwili. Hiki ni kitu kimeshajaribiwa na ni maarufu.
"Hawi mwanamme na mwanamke ispokuwa Shaytwaan huwa watatu wao."
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=caM_dg_KkwM
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action
8. Jamaa´at-ut-Tabliygh Wanahitajia Jihaad
Swali:
Muulizaji kutoka Ufaransa anauliza. Ipi Tafsiyr ya kauli ya Allaah
(Subhaanahu wa Ta´ala):
8 �د�ون إ�� ا�6�ر و�5)رون ���)روف و�3�ون �(م أ)� �ن ا�)�(ر و��(ن )�
“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha
mema na unakataza maovu.” (03:104)
Vipi tutawaradi Jama´at-ut-Tabliygh ambao hutumia Aayah hii?
Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Jama´at-ut-Tabliygh wanahitaji (kupigwa) Jihaad. Jama´at-ut-Tabliygh ni
makhurafi, wanaitakidi Usufi. Muasisi wake alikuwa akikaa kwenye kaburi la
"Kankoohi" kiasi cha nusu saa nzima. Alikuwa akikaa na kusema "Allaah
kahudhuria." Anasema Allaah kahudhuria kwenye kaburi la mtu yule.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=caM_dg_KkwM
11
9. Kufasiri Vitabu Bila Ya Idhini Ya Mwandishi
Swali:
Ipi hukumu ya kufasiri (vitabu) bila ya kuomba idhini kwa wamiliki - yaani
mwandishi - kwa ajili ya biashara? Je, inajuzu kuuza na kununua vitabu hivi?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Kwa hakika haifai kwenda kinyume, inatakiwa kuomba idhini kwa
mwandishi au mmiliki. Wala haifai masuala yakawa vurugu. Vurugu
haipelekei kwenye chochote isipokuwa shari.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=7LfbMFmUK0I
10. Kunywa Katika Kikombe Cha Dhahabu
Swali:
Swali kutoka Ireland. Je, inajuzu kunywa kwenye chombo cha dhahabu?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Jibu hapana! Chombo cha dhahabu haijuzu kukinywiya humo kitu.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=7LfbMFmUK0I
12
11. Swalat-ul-Kusuuf Msikitini Au Nyumbani?
Swali:
Swalat-ul-Kusuuf (Swalah ya kupatwa jua au mwezi) inaswaliwa nyumbani
au Jamaa´ah Msikitini na ipi kauli yenye nguvu katika hili?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Swalat-ul-Kusuuf inaswaliwa Msikitini na inaswaliwa nyumbani. Wanawake
wanaiswali nyumbani na wanaume wanaiswali Msikitini.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=2_ieB2FuyMo
12. Baba Hataki Kuswali Anadai Anajua Zaidi Yangu
Swali:
Baba yake haswali na anapomnasihi anasema: "Mimi najua zaidi yako wewe."
Unaninasihi nini kuamiliana naye?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yaani hajui hata Swalah? Anajua zaidi yako wewe kisha hajui hata Swalah?
Huu ni ujinga mkubwa - A´udhubillaah. Au ni mjuzi mpotofu. Na ni juu yake
kuendelea nasaha naye akimukhofisha Allaah, akimukhofisha Allaah (´Azza
wa Jalla). Akikataa na yeye (mtoto) ni mwenye uwezo wa kuishi mwenyewe
13
afanye hivyo, lakini aendelee kuwasiliana naye kwa wema na Ihsaan. Hata
kama atakuwa anaishi nyumba nyingine.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=YvSIjQzHbwI
13. Kumtembelea Mtu Ambaye Haswali
Swali:
Niko na baba mdogo ambaye anavuta sigara na wala haswali Msikitini Swalah
ya Ijumaa tu na (Swalah) zilizobaki anaswali nyumbani kwake bila ya
kuhifadhi wakati. Je, ni wajibu kwangu kuwasiliana naye, kumtembelea na
kumtolea Salaam kwa kuwa anasema usininasihi wala usiongee na mimi kwa
nasaha kamwe?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana usimtembelei maadamu anasema maneno haya basi ni kafiri, wala
hakubali nasaha. Muache!
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=YvSIjQzHbwI
14. Habbat Sawdaa (Haba Soda) Ni Dawa Ya Kila Ugonjwa
Swali:
Habbat Sawdaa (haba soda) imethibiti katika chakula chake kitu kama athari
au Hadiyth Swahiyh, sisi tunasoma baadhi ya maongozo (tukaona hivyo)?
14
´Allaamah al-Fawzaan:
Imethibiti ya kuwa ina tiba ya kila ugonjwa isipokuwa mauti tu. Iko na dawa
kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama jinsi ya
kuitumia itatokana na mt. (Mtu) anaweza kuitumia kwenye kinywaji, chakula,
akaitumia wakati wa kula au akainywisha maji au mfano wa hayo.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=4el_PeDIkDE
15. Hukumu Ya Jina La ”al-Haadiy”
Swali:
Je, inajuzu kuitwa kwa jina la “al-Haadiy”?
´Allaamah al-Fawzaan:
´Abdul-Haadiy hili ndio maarufu. al-Haadiy pekee ni (Jina la) Allaah.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=v2lHcGsbT1o
16. Je, Du´aa Hii Yatosheleza Du´aa Zingine Zote?
Swali:
Je, inachukuliwa hii Du´aa ni kubwa na yatosheleza kwa Du´aa zingine zote
zilizobaki, nayo ni:
15
���� د ��� و��م و���دك ا�����ون ا���م إ�� أ���ك ن ��ر � ���ك ���ك
“Ewe Allaah mimi nakuomba katika ya kheri aliyokuomba nayo Mtume
Wako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waja Wako
wema.”
´Allaamah al-Fawzaan:
Du´aa hii ni kubwa lakini haitoshelezi Du´aa zilizobaki, bali kila Du´aa ajuazo
mtu aombe kwazo. Ni katika kujizidishia kheri wala asisimamie kwa
(kuomba) Du´aa moja tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
hakusimamia (kwa kuomba) Du´aa moja; bali alikuwa akiomba kwa hii mara
fulani, na wakati mwingine kwa hii.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=ewVV1GR-iEs
17. Je, Inajuzu Mwanamke Kuvaa Suruwali Pana Isiyobana?
Swali La Kwanza:
Ipi hukumu ya kuvaa suruwali kwa mwanamke? Na je, kuna tofauti ikiwa
pana au nyembamba?
´Allaamah al-Fawzaan:
Katika mji wetu si ada ya wanawake kuvaa suruwali, na wanawake wanavaa
kutokana na wavaavyo wanawake wa mji. Haijuzu khaswa kayika mji huu
(Saudi Arabia) kuvaa suruwali. Hata katika miji mingine, kwa kuwa suruwali
inabainisha mwili wa mwanamke wala haisitiri stara kamili. Na huenda fitina
ya suruwali ikawa kubwa. Kwa kuwa inadhihirisha yaliyomo ndani.
Mwanamke ajiepushe kuvaa suruwali, hususan katika mji huu kwa kuwa hii
16
si katika ada ya mji huu. Mwenye kuvaa mavazi yanayokwenda kinyume na
makubaliano (ya waislamu) basi yuko katika makemeo makali (kwa Mola
Wake).
Swali La Pili:
Vipi akivaa yuko nyumbani?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hata nyumbanni (haijuzu). Kwa kuwa ataanza kuivaa nyumbani kisha hatua
baada ya hatua ataanza kuivaa hata barabarani.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=165rIMROtGY
18. Je Kumuona Mtume Usingizini Ni Bishara Njema?
Swali:
Je, maono ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usingizini katika
umbo lake huchukuliwa ni bishara kwa yule aliyemuona au kwamba ni katika
watu wa Peponi?
Imaam Ibn Baaz:
Ikiwa mtu atamuona kwa sura yake kama ilivyotangulia basi ni kheri – In
Shaa Allaah - lakini haizingatiwi kuwa ni kuokoka, au mafanikio, uchaji
Allaah n,k. Kwa kuwa kuna waliomuona Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa
sallam) kipindi cha uhai wao makafiri na wanafiki na haikuwafaa kitu muono
huu. Alimuona Abu Jahl na akafa kwenye kufuru wakati aliuawa katika vita
17
vya Badr. Alimuona Ibn Rabiy´ah na Shaybah bin Rabiy´ah na wakauawa juu
ya ukafiri wao. Alimuona anko wake Abu Twaalib na akafa juu ya ukafiri.
Alimuona Abu Lahab na akafa juu ya ukafiri. Alimuona ´Abdullaah ibn
´Ubayd kiongozi wa wawanafiki na akafa juu ya ukafiri. Muono wa mtu
ambaye hapewi uzito katika uongofu wake au Uislamu wake au mafanikio
kwa watu wake; isipokuwa (yule) atayemuamini akamsadikisha na kumfuata
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yapewa uzito zaidi ikiwa
atamuona usingizini. Atayemuona usingizini naye ni muumini mchaji Allaah;
hutarajiwa kheri mtu huyo ikiwa atamuona kwa sura yake ya kweli. Ama
atayemuona na haamini Shari´ah yake na hafuati yale aliyokuja nayo, hakika
muono huu hautomfaa kitu bali ni hoja dhidi yake, sawa akimuona kihakika
au usingizini. Kama walivyomuona wale makafiri katika uhai wake Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na haikuwafikisha kumuamini bali
iliwazidishiwa kuwa wanyonge. Na Allaah Atukinde kwa hilo. Hali kadhalika
kwa yule atayemuona usingizini hamuamini wala hafuati yale aliyokuja nayo,
haitomfaa kitu muono huu bali itakuwa ni hoja dhidi yake.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=fudgl4fkrbc
19. Kuomba Wafu Ni Shirki Kubwa Au Ndogo?
Swali:
Ipi kauli za wanachuoni kwa yule anayetaka Du´aa kutoka kwa wafu? Je, hili
linaingia katika Shirki kubwa au ndogo?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Bila shaka hili ni katika Shirki kubwa. Kwa kuwa anaitakidi kama maiti
anamsikia. Na Allaah (Ta´ala) katwambia kuwa maiti hawasikii.
18
ن '& ا���ور و)� أ�ت �) )+ )�
”Wala wewe siwakuwasikilizisha walio makaburini.” (35:22)
Huyu anataka kutoka kwa wafu nini? Akiamini kuwa wanamsikia, pia
akiamini uwezo wao katika kitendo hichi, hii ni batili bali ni Shirki kubwa
inayomtoa mtu katika Uislamu. Anaeitakidi hivi ni (Shirki kubwa) inayomtoa
katika Uislamu.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=5Nu-mEnjAKo
20. Kumpa Mtu Jina La "Mwenye Kumjua Allaah"
Swali:
Inajuzu kutoa jina "Mwenye kumjua Allaah" kwa baadhi ya watu wema?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huku ni kumtakasa mtu. Mwenye kumjua Allaah huku ni kutakasa na hili ni
maarufu kwa Suufiyyah.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=V333ryRJB4A
21. Kupokea Zawadi Ya Pesa Za Haramu
Swali:
19
Je, inajuzu kupokea zawadi (inayotokana na) pesa za Haramu au
kuchanganyikana (nayo)?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Ni bora zaidi kutoikubali, bora zaidi kutoikubali.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=JpY4zl8Hl-s
22. Kupunguza Ndevu Au Kufukuzwa Kazini?
Swali:
Dada huyu anauliza mume wake anafanya kazi katika taasisi ya kutengeneza
pasta kama vile tambi na kadhalika, wamemuomba kupunguza ndevu zake ili
aweze (kuendelea) kufanya kazi. Je, inajuzu kwake kufanya hivyo na kama
hakufanya hivyo watamfukuza kazini?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Asiwatii, hichi ni kitu kimeumbwa fasi yake (kwa mwanamme), wala
asipunguze.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=r1yWnaIL2fM
23. Kusomea Maji Ruqyah Kisha Kuyaoga
20
Swali:
Mimi nasomea maji Ruqyah ya Kishari´ah halafu nayanywa na kuyaoga. Je, ni
sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna ubaya. Ni vizuri kuoga maji ya Ruqyah. Na Allaah Anajua Zaidi.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=UyxhG1FwOz0
24. Msafiri Kujumuisha Swalah Ya Ijumaa Na ´Aswr
Swali:
Je, msafiri siku ya Ijumaa anajumuisha mwa zile nyakati za mwanzo au
anachelewesha?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Msafiri siku ya Ijumaa akijiwa na wakati wa Ijumaa naye yuko katika safari,
anaweza kujumuisha (na ´Aswr). Sawa ikiwa ni wakati ule wa Ijumaa au
akichelewesha (hadi wakati wa Swalah ya ´Aswr]. Kwa kuwa hakuswali
Ijumaa. Ama kwa mfano anataka kuswali Ijumaa na kujumuisha na ´Aswr
hapana (haijuzu).
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=LnH8ZX-t8tE
21
25. Tofauti Ya Sunnah Na Ada Ya Mtume (و��م ���� ��)
Swali:
Ipi kipimo (kujua) Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa
kuwa watu wengi wamekuwa wakikazia katika mambo mengi na wanasema
na hili ni katika Sunnah; kwa mfano kuvaa kilemba, kuendesha farasi, nywele
ndefu. Na je, kila alichofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
inakuwa Sunnah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yako aina mbili:
1. Aina ya kwanza aliyoyafanya kwa minajili ya kuyaweka katika Shari´ah,
haya ni Sunnah ima ni (jambo) la wajibu au Mustahaba.
2. Ama aliyoyafanya kwa minajili (ilikuwa ni) ada yake; kama vile nguo,
kilemba, mavazi, kanzu, kikoi, haya ni katika ada yake na si ya Kiibaadah.
Nii ni ada yake.
Haya si Sunnah bali yanaingia katika mambo ya Mubaha na si katika mambo
ya Kiibaadah.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=OHuYbKOSAEg
26. Upi Msimamo Wa Mwanamke Kwa Madu´aat Wapotevu?
Swali:
Muulizaji mwanamke anauliza, upi msimamo wa mwanamke Muislamu
kutokana na Madu´aat (walinganiaji) wapotevu?
22
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwanamke na mwanaume msimamo wao ni kutoa nasaha katika jambo hili
na kukataza dhidi ya Madu´aat wapotevu na kutoa tahadhari (kwa watu)
dhidi yao, ili asije kudanganyika mwenye kudanganyika.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=HMN1UVyF6m8
27. Wale Wanaotumia Mantiki Na Falsafa Katika Hadiyth
Swali:
Mwenye kusema Hadiyth zinaweka dhana kuthibiti kwake - Hadiyth za
Ahaad wala hazichukui. Je, anaingia katika tishio la Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, anaingia katika tishio la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa
kuwa wana makusudio mabaya. Makusudio yao watangulize dalili za
kimantiki, na falsafa waziweke mahala pa Hadiyth. Haya ndio makusudio
yao. Wanasema dalili za kimantiki ndio za mwisho (kutegemewa), na dalili za
Hadiyth ni za kudhania. Wanatanguliza za kukata shauri (falsafa & mantiki)
kabla ya hizi za dhana (Hadiyth). Ni kinyume chake, Hadiyth ndio za mwisho
(baada ya Qur-aan) na kanuni za kimantiki ndio za kudhania. Kwa kuwa ni
fikra za kibinaadamu zinapatia na kukosea. Ama Sunnah hakosei (Mtume)
kamwe, ikiwa (ni Hadiyth) sahihi hakosei - yeye kalindwa na madhambi.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=0PyVOzLVFSM
23
28. Wanachuoni Wa Hedhi Na Nifasi
Swali:
Tunaomba uwanasihi baadhi ya wanafunzi au vijana wanaowafedhehesha
baadhi ya wanachuoni kwa kukusudia au bila ya kukusudia. Wanapoambiwa
kurejea kwa wanachuoni wakati wa fitina na mfarakano wanasema hawa
wanachuoni ni wanachuoni wa hedhi na nifasi. Hata mimi nilisikia hivyo
Shaykh. Tunaomba nasaha huenda ikaleta manufaa.
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Ni wajibu kwa mtu kumcha Allaah (´Azza wa Jalla) na asimdharau mtu
mwengine.
�3 ا��ذ�ن آ)�وا � � 6ر :وم ن :وم � � أن �(و�وا �� أ�" 3�م )� 6�را )�
”Enyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, huenda hao
wakawa bora kuliko wao.”(49:11)
Na mtu ahifadhi ulimi wake kwa kuwa ulimi ni kiungo hatari sana kwa mtu.
Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Mu´aadh bin
Jabal:
"Je, nikueleze kitu kinachomiliki vyote hivyo? Akasema "ndio ewe Mtume wa
Allaah." Akaushika ulimi wake na kusema: "Uhifadhi huu [ulimi]" Akasema
"Ewe Mtume wa Allaah kwani tutachukuliwa kwa yale tuyasemayo?" Hivyo
akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): Akukose mama yako ewe
Mu´aadh! Je kipi kitachowafanya watu kutupwa Motoni kwa nyuso zao
isipokuwa ni kwa sababu ya ndimi zao.”
Na mwanachuoni mwenye ujuzi wa hedhi na nifasi ni mwanachuoni katika
mipaka ya Allaah na Shari´ah miongoni mwa Shari´ah za Allaah. Na hedhi na
24
nifasi ni katika masuala magumu sana kwa wanafunzi kutokana na Ikhtilaaf
nyingi zilizomo humo. Na mwanachuoni kwa hilo ni mwanachuoni kigogo.
Mtu hasemi hilo kwa njia ya dharau. Hedhi na nifasi yanaingia humo mambo
mengi; kama ´Ibaadah, muda wa kusubiri, Talaka na mengineyo. Si jambo
sahali.
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarehe: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (74 B)
http://www.youtube.com/watch?v=toPN9LCFwi4
29. Wale Wanaokaa Na Ahl-ul-Bid´ah Wamelaaniwa
Swali:
Je, imewekwa katika Shari´ah kwa Muislamu mwenye msimamo kukaa,
kuwapenda na kufurahi na wafanya maasi na wale wenye kutumbukia
kwenye Bid´ah zisizokuwa kufuru wakati hawatumbukia katika haya
madhambi? Au ni wajibu kuwasusa kwa hali zote isipokuwa tu kama
atawakataza atapokutana nao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kuchanganyika na wafanya madhambi, washirikina, makafiri, wanafiki
linahitaji ufafanuzi. Ikiwa atachanganyika nao kwa ajili ya kuwalingania kwa
Allaah, kuwapa nasaha na kuwabainishia huku akitaraji huenda wakatubia na
kujirejea, hili limeamrishwa. Ni kulingania (Da´wah) kwa Allaah. Ama
kuchanganyika nao kwa ajili ya kuwa kijamii nao na kufurahi nao na
hawahukumu wala kuwakataza hili halijuzu. Hii ni njia ya Baniy ´Israaiyl
ambao wamelaaniwa na Allaah.
(��وا ��دون (?روا )ن ��& إ را<�ل ��� � �ن داوود و�� ��ن ا��ذ�ن (��وا � ا�ن )ر�م ذ�ك �)� 0�وا و��(ر '�وه ��<س )� (��وا �?�ون ����ھون �ن )"
25
”Walilaaniwa waliokufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa
Dawuud na wa ´Iysa mwana wa Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na
wakawa wanapindukia mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyokuwa
wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyokuwa wakiyafanya!”
(05:78-79)
Hii ndio sababu.
Mtu asiwe sawa na watu (kama hawa). Akiona maasi. Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam anasema):
"Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu mwache akiondoe (abadilishe) kwa
mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na
ikiwa hawezi basi kwa moyo wake. [Muslim]
Ukikikataza kwa moyo wako (yaani kuchukia) usikae nao. Jetenge nao mbali.
Na ukikaa nao, wewe hukuwakataza kwa moyo wako. Asli ni kwamba
hukumu ya kukaa na wafanya madhambi na wengineo wanaokwenda
kinyume, lina ufafanuzi. Yule mtu ambaye katika kuchanganyika nao kuna
maslahi ya kidini, kama kuwanasihi na kuwabainishia na kuwalingania kwa
Allaah - hili ni wajibu. Ama yule anayekaa nao, akala nao, akanywa nao na
akafurahi nao - huyu amelaaniwa kwa ulimi wa Dawuud na ´Iysa mwana wa
Maryam na Mtume Muhamad (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam).
Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Naapa mtaamrishana mema na kukatazana mabaya, na mtamzuia mfanya
madhambi na kumfanya ashikamane na haki. La sivyo Allaah Atazifanya
nyoyo zenu kuambatana nyote halafu Awalaani kama alivyowalaani."
Ni lazima kuweka tanbihi ya kitu kimoja. Kuwalingania kwa Allaah (Da´wah)
wafanya madhambi, washirikina na makafiri ni lazima kuwa na elimu. Ama
kwa mjinga, haiwezekani akachanganyika nao. Kwa kuwa hana elimu ya
kuwabainishia na kuwanasihi. Au anaweza kuwalingania kwa Allaah kwa
ujinga, halitozidisha isipokuwa shari. Ni wajibu mtu awe na elimu kwa kiasi
ambacho anaweza kuamrisha, kuwakataza na kuwafanyia Da´wah kwa
26
Allaah kwa Baswiyrah. Kumbukeni hili! Kwa yule asiyekuwa na elimu
asijiingize katika hili. Ajiweke mbali.
´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: http://alfawzan.ws/node/2033
http://www.youtube.com/watch?v=51_E7jpx4gY
Tarehe: 1430-08-17/2009-08-08
30. Neno "Jins-ul-´Amal" Limetoka Kwa Murji-ah
Swali:
Je, ni sahihi kauli: "Jins-ul-´Amal” ni lafdhi ya Bi´dah haikuwepo kwa Salaf; na
ni lafdhi ya utata yenye maana nyingi na ni bora kuiacha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hatujui neno hili katika maneno ya ´Ulamaa wetu na ´Ulamaa wa Salaf. Sijui
tofauti ya Jins-ul-´Amal na kitendo. Inasemwa "Kitendo" na si "Jins-us-´Amal".
Kunasemwa "Kitendo." Kitendo ni katika Imani. Imani ni kauli kwa ulimi na
Itikadi katika moyo na vitendo vya mwili, na hawakusema "Jins-ul-´Amal."
Lafdhi hii haina asili na huenda imetoka kwa Murji-ah.
´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: http://alfawzan.ws/node/2033
http://www.youtube.com/watch?v=yZ90SMogswA
Tarehe: 1430-08-17/2009-08-08
31. Mwanamke Kwenye Nifasi Akitwaharika Kabla Ya Siku Arubaini
27
Swali:
Je, damu baada ya (siku) arubaini kwa wenye nifasi huchukuliwa ni
Istihaadhah? Na vipi ikiwa atatwaharika kabla ya (siku) arubaini?
´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy:
Akitwaharika kamili (vizuri) mwanamke kabla ya siku arubaini, ni wajibu
kwake Swalah na Swawm kawaida kama wanawake wengine. Hata kama
itakuwa siku ishirini, hata chini ya hapo au zaidi huchukuliwa... wala
asiangalie siku arubaini. Na (damu) ikikatika siku arubaini na kutwaharika
(vizuri), na aghlabu huwa hivi kwa wanawake.
Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema nifasi siku arubaini,
kwa kuwa ndo huwa aghlabu kwa wanawake. Lakini anaweza kutwaharika
chini ya siku hizo, na damu inaweza kuendelea zaidi ya siku arubaini.
Ikiendelea kumtoka damu ndani ya siku arubaini, hukumu yake ni hukumu
ya wenye nifasi. Na ikiendelea zaidi ya siku arubaini, basi hiyo ni Istihaadhah
(damu ya ugonjwa). Na mwenye Istihaadhah hukumu yake ni kama hukumu
ya waliotwahara - ´Ibaadah n,k hatofautiani na waliotwahara katika
wanawake.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action
http://www.youtube.com/watch?v=lF3toS5rCtk
32. Mwanamke Anaetaka Kuzaa Kapitwa Na Swalah Nyingi, Afanye Nini?
Swali:
28
Muulizaji kutoka Ubeljiji, mwanamke alikwenda kwa daktari kwa ajili ya
kujifungua saa kumi asubuhi, na hakujifungua ila saa tisa kabla ya ´Aswr na
hajaswali Dhuhr. Je, ana madhambi na vipi atalipa faradhi hizi?
´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy:
Ikiwa katika muda huu tangu alipoenda kwa daktari na kujifungua alikuwa
akitokwa na damu au na kitu aina ya damu, hana juu yake kitu wala hafai
kuswali. Na kama alikuwa twahara hakutokwa na kitu, ni wajibu kwake
kulipa Swalah zilizompita naye alikuwa twahara.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action
http://www.youtube.com/watch?v=GNir-FntYRY
33. Mishaary Raashiyd al-´Afaasy Na Anashiyd Zake
Swali:
Ipi rai yenu, tunataka kutoka kwa Mishaary Raashiyd al-´Afaasy (dalili sahihi
za kuimba Anashiyd) katika Swahiyh al-Bukhaariy?
Shaykh Mahir Qahtwaaniy:
Hizi ni katika Bid´ah zake maarufu kwake, anataka kutumia Hadiyth za katika
al-Bukhaariy kwa kuimba kwake. Bila shaka ni mtu wa Bid´ah mpotofu. Ni
wajibu kujiepusha na njia zake ambazo hawakuwahi kuafikiana nazo Salaf.
Chanzo: http://youtu.be/_T3RcEBU8UE
29
34. Kwa nini Mwanamke Hafai Kumuonesha Mwanamke Wa Kikafiri Nywele Zake?
Swali:
Ipi dalili ya uwajibu wa mwanamke kufunika nywele zake mbele ya
wanawake wa kikafiri?
´Allaama Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy:
Dalili ni kuwa wanawake wa kikafiri mara nyingi wanafanya khiyana katika
amaanah. Huenda akaenda kusifia umbile la huyu mwanamke Muislamu
kwa mtu ajinabi, ikapelekea katika madhara. Ama kwa yule ambaye atakuwa
na wanawake makafiri ambao ni waaminifu, hakuna ubaya akaonesha uso
wake - khaswa ikiwa kumetokea dharurah.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action
35. Kipote Kitakachookoka Na Moto
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
"Kipote kitakachookolewa, Ahl-us-Sunnaah wal-Jamaa'ah, na wala
haitomfaidikisha mtu yeyote isipokuwa (kwa kufuata Manhaj/ufahamu) wa
Salafiyyah. Wale walioshikamana na njia ya Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) na Maswahabah zake."
Chanzo: http://youtu.be/qwkaa5CVljg
30
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.