fataawa za wanachuoni (21)

38
1 علماء ال فتاوىFataawa Za Wanachuoni [21] Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush ©

Upload: wanachuoni

Post on 16-Apr-2015

196 views

Category:

Documents


7 download

DESCRIPTION

Fataawa Za Wanachuoni (21)

TRANSCRIPT

Page 1: Fataawa Za Wanachuoni (21)

1

فتاوى العلماءFataawa Za Wanachuoni

[21]

Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

©

Page 2: Fataawa Za Wanachuoni (21)

2

Dibaji:

Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili

kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji

elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya

Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.

Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu

zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe

nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila

Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa

jumla.

Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana

Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo

Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta

aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa

kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.

Jazaakumu Allaahu Khayra

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na

Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

Page 3: Fataawa Za Wanachuoni (21)

3

Fataawa za wanachuoni: 1. Dalili Kuwa Muhammad Hassan Kapinda 2. Tovuti Ya al-Athar Inayodai Kwamba Shaykh al-Fawzaan Anawasapoti 3. Abu Ishaaq al-Huwayniy Yuko Pamoja Na Qutbiyyuun 4. Tovuti "Kull Salafiyuun" Inatosheleza Kumjua Ni Nani al-Halabiy 5. Shaykh al-Bura´iy Kuhusu Swaalih al-Munajjid Na Mukhtaar ash-Shanqiytwiy 6. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Chaneli Ya al-Athar Jordan 7. Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy Kuhusu Swaalih al-Munajjid Mmiliki Wa Tovuti Islamqa.info 8. Kuonya Watu Dhidi Ya Mtu Wa Bid´ah Kwa Kumtaja Jina 9. Kuwagawa Waislamu Kati Ya Walio Juu Ya Haki Na Wapotofu 10. Hukumu Ya Mwenye Kuwasifia Watu Wa Bid´ah 11. Mwenye Kuwasifia Au Kuwatetea Watu Wa Bid´ah Ni Katika Wao 12. Vipodozi Ndani Ya Hijaab 13. Qiyaamah 2012 14. Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy Kuhusu Swaalih al-Mughaamisiy 15. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Facebook, WhatsApp Na Twitter 16. ´Ariyfiy Anafuata Hawaa Zake 17. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Kuwaradi Wanaokhalifu Na Kosa La al-´Ariyfiy 18. Sayyid Qutwub Alikuwa Kaathirika Na Vitabu Vya Watu Wapotofu 19. Ibn Baaz Akisifia Jamaa´at-ut-Tabliygh Na al-Ikhwaan al-Muslimuun Kabla Ya Kufa Kwake 20. Kusoma Vitabu Bila Ya Wanachuoni Ni Upotevu 21. Asiyemfanyia Takfiyr Asiyeswali Ni Mtu Wa Bid´ah? 22. Vipi Wewe Ni Salafiy? 23. Ni Wanachuoni Wakuulizwa Wakati Wa Matukio Ya Khatari 24. Ususiaji Kwa Bidhaa Za Makafiri Kwa Mtu Mmoja Wawili Halinufaishi -1- 25. Mwenye Kumsema Shaykh Rabiy´ Ni Hizbiyyuun 26. al-Waadi´iy Kuhusu Vitabu Vya Shaykh al-Fawzaan Na Rabiy´ al-Madkhaliy 27. al-Waadi´iy Kuhusu Vitabu Vya Imaam Ibn´Uthaymiyn 28. Hii Ndio Sababu Ya Kutojuzu Kushiriki Katika Serikali 29. Ni Wajibu Kusaidiana Na Makundi Mengine 30. Shaykh al-Fawzaan Kuhusu Uvunjaji Wa Masanamu Bamiyan Na Taliban 31. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Anashiyd Za Malengo 32. Salafiyyah Inanufaisha Wote Na Haimdhuru Yeyote 33. Hivyo Utajua Kuwa Hizbiyyuun Hawajali Uislamu

Page 4: Fataawa Za Wanachuoni (21)

4

34. Shaykh Rabiy´ Ni Mwanachuoni Mkubwa Wa Hadiyth 35. Ikiwa Hizbiyyuun Watakwita Katika Mkutano Na Kujitolea 36. Serikali Inanufaika Kwa Da´wah Ya Ahl-us-Sunnah 37. Ahl-us-Sunnah Wanawapenda Maimamu Na Wanachuoni Wote 38. Baadhi Ya Sifa Za Kumjua Ni Nani Salafiy Wa Kweli

39. Kijakazi Alijua Mola Wake Alipo Tofauti Na Watu Wengi Wa Zama Hizi

40. Kumbadili Mtoto Nepi Kunavunja Wudhuu?

41. Kuna Uongo Mweupe Na Mweusi?

42. Mtu Avute Sigara Kwa Mkono Wa Kulia Au Wa Kushoto?

43. Kumpiga Mwanamke Ni Katika Tabia Mbaya

Wanachuoni waliomo:

1. Imaam Muhammad Naaswir-ud-iyn al-Albaaniy 2. Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz 3. ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy 4. ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy 5. ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy 6. ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan 7. Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy 8. Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Yahyaa al-Bura´iy 9. Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam 10. Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy:

Page 5: Fataawa Za Wanachuoni (21)

5

Bismillaahi Rahmaani Rahiym 1. Dalili Kuwa Muhammad Hassan Kapinda

Swali:

Je, huchukuliwa Muhammad Hassan ni mwanachuoni ambaye inaweza

kuchukuliwa elimu kutoka kwake, kwa vile alishiriki katika maandamano

Misri na akawachochea vijana kubadili hukumu, kama ilivyoonekana kwenye

chaneli ya kiarabu.

Shaykh Dr. ´Abdullaah al-Imaam:

Ikiwa ni kweli... mimi sijui chochote kuhusu Muhammad Hassan kwa

aliyomo. Sisi tuna khabari tu ya kwamba amepinda kidogo. Ikisihi kweli ya

kuwa ameshirika katika maandamano haya, hii ni dalili ya kwamba amepinda

na kuwa anakubaliana kufanya Khuruuj (uasi) kwa watawala. Na hili ni

katika jumla ya fitina na kupinda. Mpaka kufikia kiwango hichi ni kupinda

zaidi; kufanya Khuruuj pamoja na wanaoiba, wanaobaka, kutukana na

wanalaani. Kweli huyu ataitwa kuwa ni mwanachuoni? Kufanya Khuruuj na

watu aina hii pamoja na matendo haya, jarima na madhambi ni dalili

ionyeshayo kupinda kwake zaidi.

Wanachuoni wanaoruhusu kufanya uasi, hawaruhusu Waislamu kufanyiwa

hivi. Hivyo sasa, ni dhambi ipi Waislamu hawa wamefanya mpaka wao

wafanyiwe namna hii; waibiwe mali yao, wapigwe na kuuawa? Waislamu

wamefanya dhambi ipi? Hii ni dalili ionyeshayo kupinda kwake zaidi.

Tunamuomba Allaah kinga na fitina zilizo za dhahiri na zilizojificha. Leo

wanachuoni wa vikundi wao ndio wanasahilisha na wanajuzisha haya mambo

mabaya kama ya maandamano na upingaji. Huchukuliwa ni katika uasi wa

Haramu katika Shari´ah ya Allaah; sawa ikiitwa maandamano au upingaji.

Hukumu yake ni moja ya uasi ambayo ni maarufu katika historia.

Na mmekwishasikia ya kwamba wale wanaofanya uasi kwa mtawala wa

Kiislamu, hata kama atakuwa ni dhalimu, ni aina mbili ya watu:Kuna wenye

wanaowakufurisha Waislamu, na kuna wengine hawawakufurishi Waislamu

Page 6: Fataawa Za Wanachuoni (21)

6

wala hawamkufurishi mtawala ambaye ni dhalimu. Lakini anakuwa ni muasi

tu ambaye anataka kumiliki, nafasi n,k. Anakuwa moja katika watu hao

tuliotaja. Muhammad Hassan si katika wanaorejelewa katika elimu, wala

isichukuliwe kutoka kwake na wala si kiigizo, kutokana na aliyoyafanya. Hili

linatosha kutahadharisha dhidi yake.

Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=6171

2. Tovuti Ya al-Athar Inayodai Kwamba Shaykh al-Fawzaan Anawasapoti

Swali:

Kuna tovuti katika mtandao unaoitwa "al-Athar" na wanasema ya kwamba

uko na baadhi ya Fataawa umewasapoti Manhaj yao na wanasema ya

kwamba kuna watu wa Ghuluu (wachupao mipaka) na majina ya bandia

wanawapachika wanachuoni, na khaswa Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy. Je, una

taaliki yoyote?

´Allaamah al-Fawzaan:

Uongo leo umekuwa mwingi. Kunisemea uongo mimi na kwa wengine leo

imekuwa sana. Anaemnasibisha yeyote kauli au Fatwa, lazima athibitishe hilo

kwa saini ya aliefutu au kwa sauti yake; ima kwa saini au kwa sauti yake. Au

kuropoka tu ya kwamba, fulani kasema fulani katoa Fatwa hili lisikubaliwe.

Kwa kuwa uongo leo umekuwa mwingi na khaswa kuwasemea wanachuoni

na kwa watalawa, bali kwa watu wote. Wanawasingizia na kuwasemea

uongo. Yote haya ni katika shari.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=EEqvRKclu9c

Page 7: Fataawa Za Wanachuoni (21)

7

3. Abu Ishaaq al-Huwayniy Yuko Pamoja Na Qutbiyyuun

Swali:

Vipi hali za watu hawa na je, tuwasikilize duruus zao na kustafidi kutoka

kwao? Abu Ishaaq al-Huwayniy, Sa´iyd bin Musfir, Swaalih al-Mughaamisiy,

Swaalih al-Munajjid, Muhammad ash-Shanqiytwiy, Ibraahiym Shaqrah na

´Aliy bin Hasan [al-Halabiy].

Shaykh Yahyaa al-Bura´iy:

Ama kuhusiana na Abu Ishaaq al-Huwayniy huyu, kama inavyojulikana yuko

pamoja na Qutbiyyuun.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133766

4. Tovuti "Kull Salafiyuun" Inatosheleza Kumjua Ni Nani al-Halabiy

Shaykh al-Buraa´iy:

Ama kuhusiana na Ibraahiym Shaqrah na ´Aliy bin Hasan [al-Halabiy], sina

maelezo kuhusu Ibraahiym Shaqrah, hata hivyo kule kuwa kwake pamoja na

´Aliy bin Hasan, ´Aliy bin Hasan kishajidhihirisha yeye ni nani. Inatosha

kuona yeye ndiye yuko nyuma ya tovuti iitwayo "Kull Salafiyyuun" (ya

Salafiyyuun wote). Ingelifaa kuitwa ”Kull Mutasaaqitwiyn" (Ya wote

walioanguka) au ”Kull Halkaa" (Wote walioangamia). Ni Salafiyuun gani

aliyonao? Abul-Hasan, Muhammad Hassan, Adnaan ´Ar´uur, al-Maghraawiy

na mfano wa watu hawa. Hii ndio tovuti inayowajumuisha wote.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133766

Page 8: Fataawa Za Wanachuoni (21)

8

5. Shaykh al-Bura´iy Kuhusu Swaalih al-Munajjid Na Mukhtaar ash-Shanqiytwiy

Shaykh al-Buraa´iy:

Ama Swaalih al-Munajjid yuko pamoja na Qutbiyyuun. Mikanda yake ni ya

kielimu, lakini [sauti haisikiki]. Yuko pamoja na Qutbiyyuun. Muhammad [al-

Mukhtaar] ash-Shanqiytwiy ni Suufiy. Na yuko na ibara katika ibara za

Suufiyyah. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

anapoteremshiwa Wahyi anatoka katika umbile la kibinaadamu. Suufiyyah

kule wanampenda sana.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133766

6. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Chaneli Ya al-Athar Jordan

Swali:

Kumejitokeza chaneli Jordan iitwayo "Chaneli ya al-Athar". Wasimamizi wayo

wanasema ya kwamba umewasifia kwa chaneli hii. Je, hili ni sahihi?

´Allaamah al-Fawzaan:

Naapa ya kwamba mimi siwajui wala sijui chaneli yoyote. Lakini kusema

uongo leo imekuwa ni jambo bure kwa watu hawa. Wanaleta uongo na kuzua

uongo - A´udhubi Allaah. Hawasikii hata haya wala hamuogopi Allaah

(Ta´ala).

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=94uz8VRdsY4

Page 9: Fataawa Za Wanachuoni (21)

9

7. Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy Kuhusu Swaalih al-Munajjid Mmiliki Wa Tovuti Islamqa.info

Swali:

Nimesikia kutoka kwa baadhi ya Mashaykh, kama Shaykh Saliym al-Hilaaliy,

na Shaykh Usaamah al-Quusiy, kwamba Swaalih al-Munajjid kamili katika

Suruuriyyah. Mimi nataka kujua nini wanachosema wanachuoni wa Saudi

Arabia kuhusu mtu huyu pamoja na kuwa ni msyria anayeishi Saudi Arabia.

Shaykh Dr. `Ubayd al-Jaabiriy:

Mimi siwezi kuwasemea wanachuoni wa Saudi Arabia, kwa kuwa mimi

similiki hilo. Lakini nitaelezea vile nijuavyo mimi. Nataka kutoka kwako,

vijana wetu na mabanati zetu wasikilize na kufahamu yafuatayo. Nijuayo

kuhusu mtu huyu ni kama uliyosikia pia wewe kuhusu mtu huyu na kwamba

ni Qutbiy.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=hQbG-97gqSQ

8. Kuonya Watu Dhidi Ya Mtu Wa Bid´ah Kwa Kumtaja Jina

Swali:

Je, inajuzu kumtaja mtu wa Bid´ah kwa jina lake na kutahadharisha watu

dhidi yake?

´Allaamah Ahmad an-Najmiy:

Ndio inajuzu. Ikiwa mtu huyu amewafitinisha watu na akawa ni kiongozi wa

upotofu, hakuna ubaya ukasema.

Page 10: Fataawa Za Wanachuoni (21)

10

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=Qj2Fe0jjunQ

9. Kuwagawa Waislamu Kati Ya Walio Juu Ya Haki Na Wapotofu

Swali:

Siku hizi imekuwa vijana wengi wamekuwa ni wenye kugawanyika na

kutiana katika vikundi; tumekuwa tukisikia sasa migawanyiko mingi kwa

mfano: "Fulani ni Ikhwaaniy, Tabliygh, Suruuriy na Jaamiy na kadhalika." Na

ipi haki kwa migawanyo hii? Kugawanya watu kumekatazwa moja kwa moja

na je, ni katika Ikhtilaaf?

´Allaamah al-Fawzaan:

Kugawa ambako makusudio yake ni kukimbiza watu, kueneza chuki na

uadui, hili halijuzu. Ama kugawa ambako makusudio yake ni kubainisha ni

nani aliyekosa na aliye juu ya yaki, na ni nani aliye juu ya Manhaj sahihi na

asiyekuwa juu ya Manhaj sahihi, makusudio yake ni kutaka aliyekosa kurudu

katika usawa, [mgawanyo huu] ni sawa. Watu hawako sawa. Miongoni mwao

kuna makafiri, wanafiki, mafasiki, waasi na muumini. Na katika waumini

kuna ambao wana Imani kamili na kuna waumini wenye Imani dhaifu. Watu

hawako katika daraja moja. Na ikiwa makusudio ni kubainisha upotofu na

haki, hili ni sawa. Ama ikiwa makusudio ni kueneza uadui baina ya vijana wa

Kiislamu na baina ya Waislamu, hili ni jambo lisilojuzu. Na hii ni kazi ya

Shaytwaan na wasaidizi wa Shaytwaan.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=9UffUctwWo4

10. Hukumu Ya Mwenye Kuwasifia Watu Wa Bid´ah

Page 11: Fataawa Za Wanachuoni (21)

11

Swali:

Kuna mtu anawasifia Mubtadi´ah [watu wa Bid´ah] na anakataa maneno ya

wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kuhusu wao na anawaponda wanachuoni wa

Sunnah na kadhalika.

Shaykh Dr. Muhammad al-Madkhaliy:

Yule ambaye anawasifia Mubtadi´ah ni katika Mubtadi´ah bila ya shaka. Bali

ni katika walinganiaji wao. Shaykh wetu - Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz -

aliulizwa katika darsa:

"Yule ambaye anawasifia Mubtadi´ah, je huchukuliwa ni katika wao?"

Akasema "ndio, huyu bila ya shaka ni katika wao, bali ni mlinganiaji wao."

Mkanda huu unapatikana kwa sauti yake na umeandikwa pia. Hakuna shaka

ya hilo.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=GnSy-1P3VyU

11. Mwenye Kuwasifia Au Kuwatetea Watu Wa Bid´ah Ni Katika Wao

Swali:

Kuna mtu anawasifia Ahl-ul-Bid´ah [watu wa Bid´ah] na anawatetea. Je, ni

katika wao?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio, hili halina shaka. Mwenye kuwasifia na kuwatetea anaingia katika wao,

bali ni katika walinganiaji wao.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=s_3cUhGflsg

Page 12: Fataawa Za Wanachuoni (21)

12

12. Vipodozi Ndani Ya Hijaab

Swali:

Je, [mwanamke] anaweza kutoka kwa vipodozi? Na vipi ikiwa amevaa Hijaab,

inaruhusiwa kutoka nje kwa vipodozi?

Imaam al-Albaaniy:

"Haijuzu kwa mwanamke ambaye hana Hijaab, sembuse ambaye kavaa

Hijaab, kutumia vipodozi vya kikafiri, vipodozi vichafu. Tokea lini katika

vipodozi vya wanawake [wa Salaf], mlisikia kuna [vipodozi kama hivi] vya

jina ambalo Allaah Hakuteremsha chochote kuhusiana navyo; "maquillage"

(makeup).

Hili ni neno ambalo hatujui hata sisi wala baba zetu kabla, bali ni neno la

kigeni likitoa maelezo ya mapambo [vipodozi] vya wanawake wachafu wa

Ulaya. Mpaka kwa masikitiko makubwa, wanawake zetu wamejifananisha

nao [wanawake hao wa Ulaya] isipokuwa yule Aliyelindwa na Allaah.

Miongoni mwao ambao wanajipodoa kwa mapambo haya ambayo yameathiri

jamii ya Kiislamu, nayo ni "maquillage". Kwa hivyo haijuzu kwa mwanamke...

Na hili kwa hakika imekuwa ni katika mambo yanayoshangaza. Babarani

tunaona wanawake waliovaa Hijaab isiokuwa na ubaya - sisemi kama ni

Hijaab [ya kujieneza vizuri inayokubalika] Kishari´ah - Ishaarb au Khimaar

inafunika nywele zake, shingo lake na kadhalika, lakini kaweka poda na rangi

ya mdomoni usoni. Haifai namna hii! Kwa nini wanafanya hivi?

Ni moja ya mambo mawili: Ima ni ujinga wa kutokujua hukumu ya

Kishari´ah, au ni kuiga wanawake kwa wasiwasi wa Shaytwaan. Kwa ajili

hiyo, sisi kwanza tunawanasihi wanawake ambao wamepewa mtihani kwa

vipodozi hivi, pili tunawakumbusha walii [wasimamizi] wa wanawake; sawa

akiwa ni baba, mume au kaka. Kutokana na kuwa kasema Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam):

Page 13: Fataawa Za Wanachuoni (21)

13

"Kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja wenu ataulizwa kwa kile

alichokichunga. Mwanaume ni mchungaji na ataulizwa kwa alichokichunga."

Mpaka mwisho wa Hadiyth."

Na kuna mithali ya kiarabu isemayo:

"Farasi ni sehemu ya mpanda farasi."

Wewe mume wa mke, haijuzu kwako kumruhusu ukamuachia akatoka kwa

sura hii ambayo inawafitinisha wanaume tusiseme vijana. Na wewe

watakiwa... ewe mwanaume, eeh baba, ee kaka watakiwa kuwa ni mwenye

wivu sana. Kwa nini?

Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

"Hatoingia Peponi Duyyuuth."

Kwa nini [hatoingia Peponi]? Ni nani Duyyyuth? Ni yule ambaye hajali kwa

wanawake zake.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=li8Osag3eB8

13. Qiyaamah 2012

Swali:

Imeenea kwa watu wengi ulimwenguni ya kwamba Qiyaamah kitakuwa

mwaka wa 2012. Wanasema ni kwa madai ya watafiti, huu ni utafiti wa kisomi

uliofanywa.

´Allaamah al-Fawzaan:

Watu hawa wamekosa shughuli ya kufanya. Wameacha kujifunza elimu

yenye manufaa yenye maslahi na wao na kheri, na wamekuwa ni wenye

kujishughulisha na mambo ya kipuuzi. Ni jambo lisilowezekana kujua lini

Qiyaamah kitatokea kamwe. Ni Allaah (Ta´ala) pekee ndiye mwenye ujuzi wa

hilo. Na wala Hakumbainishia hili Malaika Wake, wala Mitume Wake wala

Page 14: Fataawa Za Wanachuoni (21)

14

kiumbe yeyote. Na kwa ajili hiyo, Jibriyl alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam), akamwambia "Nambie ni lini Qiyaamah?" Akasema

"Muulizwaji si mjuzi - naye ni Mtume Muhammad (´alayhis-Salaam) - kama

asivyo vile vile Muulizaji - naye ni Jibriyl." Si mimi wala wewe sote hatujui.Na

hakuna faida kwetu ya sisi kujua wakati Qiyaamah kitatokea. Faida yetu ni

sisi kufanya ´amali njema na kujiandaa kwa Qiyaamah hicho. Hii ndio faida

yetu. Ama wakati wa kutokea kwake, hili halina faida kwetu.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=2gw8C4yCvFw

14. Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy Kuhusu Swaalih al-Mughaamisiy

Swali:

Swaalih bin ´Awwaab al-Mughaamisiy; Imamu wa Msikiti wa Quba na ana

duruus katika Tafsiyr.

Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:

Mtu huyu ni mjinga. Siwanasihi kuchukua elimu kutoka kwake. Kwa kuwa

hakutakhasusi katika elimu ya Kishari´ah, kutokana na nilivyosikia. Hili ni

jambo la kwanza. Jambo la pili ni kwamba, mtu huyu analingania katika

Taswawwuf (Usufi). Na ninapata dalili ya hilo kisa cha marehemu kwenye

kaburi, na nimekiradi katika Sahab (sahab.net) kwa anuani "at-Taqriyraat al-

Mastuurah". Isnadi ya kisa hichi ni dhaifu. Kimepatikana kwa mwanachuoni

mmoja wa Taswawwuf al-Ghulaat. Na kuna mambo mabaya (katika kisa

hicho). Anaweza kukirejelea kwa mwenye kukitaka. Na nimefikiwa na

khabari ya kwamba anasema inajuzu kuacha kulingania katika Tawhiyd na

kuacha kukataza Shirki kwa ajili ya kutafuta Umoja. Kamtanguliwa kwa hili

na al-Qaradhwaawiy, na al-Qaradhwaawiy ni kiongozi ambaye kazama

kabisa kwenye upotofu, na hayuko katika uongofu. Ana mambo ya kufuru.

Lau mimi (´Ubayd) ningelikuwa na Imani kama hii ya al-Qaradhwaawiy,

ningekufuru. Kwa hivyo, ni lazima kutahadhari na huyu Swaalih bin

´Awwaab al-Mughaamisiy, Imamu wa Msikiti wa Quba, kama jinsi vilevile ni

Page 15: Fataawa Za Wanachuoni (21)

15

lazima kutahadhari na al-Qaradhwaawiy, na kuonya watu dhidi ya watu

hawa wawili.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=GTka_WL0bC4

15. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Facebook , WhatsApp Na Twitter

Swali:

Ipi hukumu ya programu hizi za Internet na njia za mawasiliano kama

WhatsApp, Twitter, Facebook au nyinginezo ambazo zimejumuisha mambo

mengi ndani yake na vipi tutawalea watoto wetu na vitu hivi?

´Allaamah al-Fawzaan:

Mtu anatakiwa kujiepushe nazo kadiri atakavyoweza. Mtu ajiepushe nazo na

kusalimika nazo. Kwa kuwa zinashawishi fikira zetu na zinatuathiri

tunapoona mambo haya ya kukejeli mambo ya Dini au kuwaponda

wanachuoni. Vikaja kumuathiri mtu na kumtatiza. Mtu ajiepushe nazo kadiri

na atakavyoweza. Mtu asiziingie isipokuwa kwa yule mwenye uwezo na

elimu na baswiyrah na anaweza kupambanua kati ya kheri na shari, na nia ya

kuingia kwake iwe ni kuchukua yale ya kheri na ayasambaze. Na

atahadharishe watu yale ambayo ataona ni ya shari na ayapige Radd. Namna

hii kutakuwa hakuna neno na ni kitendo kizuri. Pamoja na kwamba vina

khatari na ni vigumu kusalimika na fitinazilizo humo. Kwa hali yoyote,

kujiweka nazo mbali na kujiepusha nazo ni salama na ni bora zaidi.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=OxI3WyXtsZs

16. ´Ariyfiy Anafuata Hawaa Zake

Page 16: Fataawa Za Wanachuoni (21)

16

Swali:

Inanasibishwa kwa maimamu wawili Ibn Hajar na an-Nawawiy

(Rahimahumu Allaah) taaliki yao kwa Hadiyth:

"Msikilize na umtii mtawala, hata ikiwa atakupiga mgongo wako na

kuchukua mali yako."

Ya kwamba makusudio ya Hadiyth awe ni Khaliyfah muadilifu na awe

kamdhulumu mtu binafasi, asubiri ili kuepuka fitina.

´Allaamah Fawzaan:

Hadiyth ni kwa jumla. Na si kwa mtu binafsi. Hadiyth ya Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa jumla watu wote. Yule ambaye anaifasiri

kwa maana nyingine, mtu huyu ana hawaa. Anataka kuifasiri Hadiyth kwa

hawaa yake, matamanio yake na madhehebu yake. Wala Hadiyth haimsapoti.

Hadiyth ni kwa jumla himidi zote ni za Allaah. Na wala hatukupata haya

katika maneno ya an-Nawawiy. Niliangalia sikupata haya katika maneno ya

an-Nawawiy.

Muulizaji:

Baada ya kutafuta katika vitabu vya an-Nawawiy na Ibn Hajar hukupata hilo?

´Allaamah Fawzaan:

Ndio, mimi nilitafuta na wala sikupata hili.

Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14264

Chanzo: http://www.almokhtsar.com/node/52152

17. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Kuwaradi Wanaokhalifu Na Kosa La al-´Ariyfiy

Page 17: Fataawa Za Wanachuoni (21)

17

Swali:

Kumeenea katika kipindi cha mwisho, kwenye tovuti nyingi za Internet,

youtube na nyinginezo katika barnamiji na simu za mkononi kipande cha

sauti yako. Na watu wameandika anwani na muqaddimah katika kipanda

hichi, wakisema "Shaykh Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan anampiga Radd

Shaykh Muhammad al-´Ariyfiy na kwamba ni mtu anafuata hawaa." Ipi

nasaha yako kwa watu kama hawa ambao wanatahadharisha dhidi ya

Mashaykh na wanataka kuwagonbanisha. Na wanaandika ibara kama hizi

kwa baadhi ya Madu´aat. Na wanasema kuhusu baadhi ya Madu´aat ambao

Allaah Amejaalia kutumia wakati wao wote kuilinda Dini hii kubwa,

wanasema kuwa Shaykh fulani na Shaykh fulani ni Suufiy na Shaykh fulani

ni...

´Allaamah al-Fawzaan:

Ewe ndugu, sisi na wasiokuwa sisi katika wanachuoni tunawapiga Radd

wanaokwenda kinyume na tunabainisha kosa. Wala hawakusudii kumuweka

chini au kumuangusha mtu huyo, hawakusudii hili. Tunajilinda kwa Allaah

kwa hili. Wanachokusudia ni kubainisha haki. Hivyo, anapokosea mtu

hakuna neno akabainisha kosa lake na hilo halimpunguzii manzila yake,

isipokuwa ni tanbihi kwake na kusaidiana naye ili arudi katika haki. Afaidike

yeye na wafaidike wasomaji na wasikilizaji. Wala haliachwi kosa likaenea

kwa watu na wala hakuna kupakana mafuta katika jambo hili. Lazima

kubainisha haki na kuiweka wazi. Wala hakuna kupakana mafuta katika haki.

Na hili halimdhuru yule mwenye kupigwa Radd ikiwa ni katika wale wenye

kutengeneza ambao wanataka haki. Ama ikiwa hataki haki na anataka kubaki

katika hawaa yake, huyu hatuna juu yake hila.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=TFVDZey6bJE

18. Sayyid Qutwub Alikuwa Kaathirika Na Vitabu Vya Watu Wapotofu

Page 18: Fataawa Za Wanachuoni (21)

18

Swali:

Amesema mmoja wa wafikiriaji ya kwamba uongozi wa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ilikuwa ni tupu katika historia na kwamba waliomfanyia uasi ´Uthmaan walikuwa karibu na roho ya Kiislamu.

´Allaamah al-Fawzaan:

Haya yamesemwa katika baadhi ya vitabu. Yeye ndie aliyesema maneno haya. Aliathirika na aliyokuwa akisoma na kusikia katika vitabu vya watu wapotofu, ndo akawa ameandika kitabu hichi. Ikiwa ni kwa kukusudia, kosa ni kubwa. Na ikiwa ni kwa ujinga, Allaah Atusamehe sisi na yeye. Lakini kwa vyovyote hili ni kosa.

Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14100

19. Ibn Baaz Akisifia Jamaa´at-ut-Tabliygh Na al-Ikhwaan al-Muslimuun Kabla Ya Kufa Kwake Swali:

Wamedhihiri baadhi ya Madu´aat wanaosema ya kwamba Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kafariki naye anasifia na kunasihi watu na Jamaa´at-ut-Tabliygh na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Maneno haya ni kweli?

´Allaamah al-Fawzaan:

Maneno haya si sahihi. Na sisi tulikaa nae zaidi ya miaka kumi hatukumsikia akisifia isipokuwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, na akilingania katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Na akinasihi waliokosea katika makundi mengine warejee makosa yao, Tabliyghiyyuun na mengine. Haya ndio nijuayo kwa Shaykh wangu, Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah).

Page 19: Fataawa Za Wanachuoni (21)

19

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133663

20. Kusoma Vitabu Bila Ya Wanachuoni Ni Upotevu

Swali:

Inatosheleza katika kutafuta elimu kusoma vitabu na maelezoya maandiko ya wanachuoni bila ya kuhudhuria vikao vya wanachuoni.

´Allaamah al-Fawzaan:

Huu ni upotofu. Mwenye kuishia kwenye vitabu, hii njia potofu. Lazima kuwepo wanachuoni, lazima kuchukua elimu kutoka kwa wanachuoni. Ama vitabu ni njia tu. Ni kama mfano wa silaha. Je, unaweza kuitumia bila ya kujifunza jinsi ya kuitumia kwanza? Ni lazima kujifunza kwanza jinsi ya kuitumia silaha. Kutoka kwa wale wanaojua jinsi ya kutumia silaha. Wanachuoni ndio watakufunza jinsi ya wewe kutumia vitabu. Na wanajua kati ya vitabu vyenye manufaa na vya sahihi na visivyokuwa vya sahihi. Kwa kuwa vitabu vingi ni vitabu vya upotofu na vya shari. Hakuna avifanyiae utafiti na kuvisherehesha ila wanachuoni. Unaweza kusoma na kufahamu kimakosa. Ni kama mfano wa mtu aliyesoma katika "Swahiyh al-Bukhaariy", Hadiyth iko namna hii:

"al-Habbah as-Sawdaa´ ni dawa ya kila ugonjwa."

Kwa sababu ya kosa la uchapishaji akasoma:

"Nyoka mweusi (al-Hayyah as-Sawdaa´) ni dawa ya kila kitu."

Akaenda na kula nyoka mweusi akafariki. Kwa kuwa hakuwauliza wanachuoni. Ni wanachuoni ndio wanaojua yaliyo sahihi na yasiyo sahihi. Ni wao ndio wanaojua maana ya sahihi na maana ya kimakosa. Wao ndio wanajua mambo haya. Chukua kitabu katika vitabu vya matibabu na ukisome kisha ukawapasue watu na matumbo yao kwa kudai kuwa wewe ni daktari. Haiwezekani namna hii. Ikiwa hali ni namna hii katika matibabu, tusemeje kwa elimu, Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Lazima wawepo wanachuoni.

Page 20: Fataawa Za Wanachuoni (21)

20

Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls--14331112.mp3

21. Asiyemfanyia Takfiyr Asiyeswali Ni Mtu Wa Bid´ah?

Swali:

Je, wale wanaosema ya kwamba mwenye kuacha Swalah ni kufuru ndogo iliyo chini ya kufuru kubwa inayodumisha Motoni wanakuwa Mubtadi´ah?

´Allaamah al-Fawzaan:

Hapana, sio Mubtadi´ah. Hili limesemwa pia na baadhi ya wanachuoni maimamu. Lakini ni kosa. Dalili za sahihi zinatolea dalili ya kosa la kauli hii, bila ya kujali aliyeisema. Lakini haifikii kiwango cha kufuru au kuritadi.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133614

22. Vipi Wewe Ni Salafiy?

´Allaamah al-Fawzaan:

Allaah Anasema:

لونمنالأمهاجرين والسابقون و نصاروالذيناتبعوهم الأ سان والأ بإحأ

"Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (waliowasaida na kuwanusuru

Page 21: Fataawa Za Wanachuoni (21)

21

Muhaajiriyn katika wakaazi wa Madiynah), na wale waliowafuata kwa ihsaan... " (09:100)

Bi maana kufuata njia yao. Sio kwa madai tu na kusema "mimi ni Salafiy" na kwamba "mimi nafuata njia ya Salaf."

Ukimuuliza nini maana ya njia ya Salaf:

"Sijui, lakini mimi ni Salafiy."

Hivyo wewe sio Salafiy. Ikiwa hujui madhehebu ya Salaf wewe sio Salafiy. Vipi utakuwa pamoja na Salafiy na wewe hujui madhehebu yao?

سان والذين اتبعوهمبإحأ

"Na wale waliowafuata kwa ihsaan... " (09:100)

Ikiwa unataka kuwa katika madhehebu ya Salaf, jifunze madhehebu ya Salaf na yale waliomo, ili uweze kushikamana nayo bara bara.

Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls--14331112.mp3

23. Ni Wanachuoni Wakuulizwa Wakati Wa Matukio Ya Khatari

Swali:

Kuna kitu unataka kumwambia Shaykh wetu al-Albaaniy (Hafidhwahu Allaah)?

´Allaamah Mubqil al-Waadi´iy:

Shaykh al-Albaaniy (Hafidhwahu Allaah) sisi ndio wenye kuhitajia nasaha zake. Ninamuomba Allaah Al-´Adhwiym Amuhifadhi na Amlipe kwa yote aliyofanya kwa Sunnah, Uislamu na Waislamu. Ikiwa ana uwezo wa kukaa na wanafunzi hata angalau saa moja kwa siku. Na ikiwa hawezi, dhambi ni juu ya yule aliyemzuia. Kuna mtawala alimuomba al-Bukhaariy kumsomea kitabu

Page 22: Fataawa Za Wanachuoni (21)

22

"as-Swahiyh" na "at-Taariykh [al-Kabiyr]". Hivyo akasema hawezi kumtenganisha yeyote na elimu na angelimzuia kufunza, angelikuwa ni mwenye udhuru kwa Allaah. Sisi tunamwambia Shaykh wetu muheshimiwa (Hafidhwahu Allaah) ya kuwa, ikiwa amezuiwa kufunza, basi ni mwenye udhuru kwa Allaah. La sivyo, mimi namnasihi ajaalie kwa wanafunzi angalau saa moja nyumbani kwake au kwenye Msikiti. Na mimi nimeambiwa ya kwamba hawezi hilo. Wanafunzi leo wanahitajia wa kuwafunza vipi watalingania katika Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na vipi wataamiliana na serikali hii na jamii hii iliyoghafilika. Wanahitajia wanachuoni wajitokeze. Na ni wanachuoni ndio wanaoweka kila kitu katika nafasi yake inayostahiki. Walisema nini watu waliokuwa na pupa ya maisha haya wakati Qaaruun alipotoka?

مهفيزينتهقال فخرج نأياياليأتلنامثألما الذينيريدونالأحياة علىقوأ لذوحظ أوتيقارونإنه الد وقال عظيم ه الذينأوتوا ثواباللـ آمنوعملصالحا الأعلأمويألكمأ ابرون خيأرلمنأ الص وليلقاهاإل

"Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale wanaotaka (wanaopendelea na kufadhilisha) maisha ya dunia wakasema: “Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kubwa mno.” Na Wakasema wale waliopewa elimu: “Ole wenu! Thawabu za Allaah (Aakhirah) ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri".” (28:79-80)

Ni wajibu kwa wanachuoni kujitokeza kadiri na wanavyoweza na kukaa na kuwafunza ´Aawaam, wanafunzi na Madu´aat. Da´wah imekuwa leo ni kama mchezo bali mgawanyiko. Watu wamejisitiri nyuma ya jinala Da´wah na wakati huo huo wanalingania katika mgawanyiko na Uhizbiyyah. Wanachuoni wanatakiwa kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kujitokeza katika jamii kama ambavyo inatakikana kwa jamii kuchukua elimu kwa wanachuoni.

Hakika Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

ألواف اسأ ل رإنكنتمأ كأ لمون أهألالذ تعأ

"Basi waulize watu wenye Adh-Dhikri (wenye ujuzi na Tawraat na Injiyl) mkiwa hamjui." (21:07)

Pindi ni wakati wa uchaguzi ni wajibu kwa ´Awwaam kuwauliza wanachuoni. Pindi ni wakati wa kupiga kura ni wajibu kuwauliza wanachuoni. Pindi ni wakati wa migomo ni wajibu kuwauliza wanachuoni. Pindi mji unavamia mwingine ni wajibu kuwauliza wanachuoni. Inatakiwa kuwa namna hii. Wasiwaulize wajinga, wamwaga damu au Hizbiyyuun wanaotumia fursa yao katika Uhizbiy wao.

Page 23: Fataawa Za Wanachuoni (21)

23

Chanzo: http://www.olamayemen.net/default_ar.aspx?id=8354

24. Ususiaji Kwa Bidhaa Za Makafiri Kwa Mtu Mmoja Wawili Halinufaishi -1-

Swali:

Ipi hukumu ya kuwasusa makafiri wapiganaji katika mambo ya mubaha ili kudhoofisha nguvuzao kwa Waislamu?

´Allaamah al-Fawzaan:

Hii ni katika kazi ya mtawala. Akiona mtawala kususa bidhaazao na kufanya nao biashara, wanasuswa. Ama rai, sio katika kazi yao kuwasusa. Na wala hawatodhurika makafiri wakisuswa na mtu mmoja, kumi au ishirini. Hili haliwaduhuru. Lakini mji mzima ukiwasusa, hili bila ya shaka litawadhuru.

Chanzo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/Mowalat--1426-11-10_0.mp3

25. Mwenye Kumsema Shaykh Rabiy´ Ni Hizbiyyuun

Swali:

Wasemaje kwa hawa wanafunzi waliohitimu al-Madiynah wanaomsema Shaykh Rabiy´?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Page 24: Fataawa Za Wanachuoni (21)

24

Hawa watu wanaomsema muheshimiwa Shaykh Rabiy´ - Allaah Amjaze kheri kwani amekaa kwenye njia kwa Mubtadi´ah wengi - ni lazima awe Hizbiyuun, sawa ni katika al-Ikhwaan al-Muslimuun, Suuruuriyyuun au Hizbiyyuun wengine. Wanajidhuru wenyewe.

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=38

26. al-Waadi´iy Kuhusu Vitabu Vya Shaykh al-Fawzaan Na Rabiy´ al-Madkhaliy

Swali:

Unasemaje kwa vitabu vya Shaykh Swaalih al-Fawzaan na Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Ni vitabu vizuri vyenye faida. Allaah Awajaze kheri. Wana nafasi nzuri kwa Hizbiyyuun. Wanatakiwa kushukuriwa kwa hili. Tumejua vitu vingi ambavyo tulikuwa hatujui kwa sababu ya vitabu vya ndugu yetu Shaykh Rabiy´. Allaah Amjaze kheri. Kwa vyovyote, hawa waandishi wawili ni katika waandishi bora Saudi Arabia.

Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=3556&PageN=

27. al-Waadi´iy Kuhusu Vitabu Vya Imaam Ibn´Uthaymiyn

Swali:

Page 25: Fataawa Za Wanachuoni (21)

25

Baadhi ndugu wanasema vibaya kuhusu maelezo ya Shaykh Ibn ´Uthaymiyn. Wasemaje kwa maelezo yake na ipi nasaha yako kwa hawa vijana?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Kwa kweli mimi sijasoma kitu katika vitabu vya Shaykh ila kitu kidogo katika Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitwiyyah. Nilistaajabu sana kwa maelezo yake. Allaah Amjaze kheri. Hapa kwetu kunafunzwa maelezo haya na kitabu chake katika Usuul-ul-Fiqh, al-Qawaa´id al-Mutlaa, Sharh al-Usuul at-Thalaathah na Sharh Lum´at-il-I´tiqaad. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Kampa nguvu katika ´Aqiydah na Fiqh. Huenda akatumia dalili kwa kutumia baadhi ya Hadiyth dhaifu na kuzinyamazia. Sisi tunawanasihi ndugu zetu wastafidi katika vitabu vyake. Allaah Amjaze kheri.

Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=3540&PageN=

28. Hii Ndio Sababu Ya Kutojuzu Kushiriki Katika Serikali

Swali:

Je, inajuzu kushiriki katika ubunge?

Imaam al-Albaaniy:

Ikiwa ubunge hauhukumu kwa Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hatuonelei kujuzu kushiriki. Kwa kuwa ina maana mtu atashiriki katika kitu kisichohukumu na hukumu ya Allaah. Jambo lingine ni kuwa, katika baadhi ya miji wanatakikana wabunge waape kusaidia katiba ambayo haikujengeka juu ya Qur-aan na Sunnah. Inaweza kuwa imejengeka juu ya ishara, na si kwa uhakika. Katiba inakwenda kinyume sana na Shari´ah na tusiseme kanuni inayoifasiri. Hatuonelei mtu kusaidia katiba hizi na serikalihizi ambazo haziweki wazi kwamba zinahukumu kwa Shari´ah ya Allaah.

Page 26: Fataawa Za Wanachuoni (21)

26

Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy Chanzo: Fataawaa Juddah (19 A)

29. Ni Wajibu Kusaidiana Na Makundi Mengine

Imaam al-Albaaniy:

Baada ya makundi ya Kiislamu kujitokeza, jambo ambalo ni lenye kusitikiza, wanatakiwa wote kusaidiana lakini kwa sharti kusaidiana kwao iwe juu ya misingi sahihi ya Qur-aan, Sunnah na Manhaj ya Salaf-us-Swaalih. Yule atakayekataa kusaidiana na makundi mengine kwa kuwa hawataki kusaidiana kwa Manhaj hii sahihi, Qur-aan, Sunnah na kwa Manhaj ya Salaf-us-Swaalih, hivyo itakuwa haitakikani kusaidiana nao kwa kuwa wanakwenda kinyume naaliokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake baada yake. Kusaidiana ni jambo la wajibu na kugawanyika ni jambo la haramu.

Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy Chanzo: Fataawaa Juddah (20 B)

30. Shaykh al-Fawzaan Kuhusu Uvunjaji Wa Masanamu Bamiyan Na Taliban Swali:

Unasemaje kwa kitendo cha Taliban waliovunja masanamu? Je, kitendo chao ni sahihi kwa kuwa tunasikia baadhi ya watu wanasema wamefanya makosa?

´Allaamah al-Fawzaan:

Page 27: Fataawa Za Wanachuoni (21)

27

Hivi vinavyochongwa na masanamu vinatakiwa kuvunjwa. Ibraahiym (´alayhis-Swalaat was-Salaam) alifanya hivyo. Na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivyo alipouteka mji wa Makkah. Kuyavunja masanamu kwa mamlaka yanayoweza hilo ni jambo linalotakikana. Lakini kabla ya hilo, ni wajibu kubomoa manyumba yaliyo kwenye makaburi. Je, Taliban wamebomoa manyumba yaliyo kwenye makaburi? Ikiwa wamefanya hivyo na wakavunja masanamu, hili ni jambo zuri. Ama ikiwa wamevunja masanamu tu na hawakubomoa manyumba, watakuwa wamefanya kitu na wameacha ambacho ni kibaya kuliko masanamu.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=131494

31. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Anashiyd Za Malengo

Swali:

Ipi hukumu ya Qaswiydah, ambazo huitwa pia Anashiyd za malengo? Je, ni Bid´ah za matendo ya Suufiyyah au kuna ambazo ni za haramu na zinazojuzu?

´Allaamah al-Fawzaan:

Anashiyd ni katika nyimbo. Na katika nyimbo hakuna kitu kinachojuzu. Ni nyimbo. Isitoshe, ni katika Dini ya Suufiyyah wanajikurubisha nazo kwa Allaah. Au Dini ya Hizbiyuun wanaowachochea vijana kwa Qaswiydah na Anashiyd hizi. Hazina kheri. Kwa hali yoyote hazina kheri.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133247

32. Salafiyyah Inanufaisha Wote Na Haimdhuru Yeyote

Page 28: Fataawa Za Wanachuoni (21)

28

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Tunataraji wayemeni wakubali Salafiyyah. Ambayo ni Da´wah kutoka katika Kitabu cha Allaah na kwenda katika Kitabu cha Allaah na kutoka katika Sunnah za Mtume wa Allaah kwenda katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni Da´wah isiyokuwa na madhara kwa mtawala. Na wala haidhuru jamii. Da´wah inayomtengeneza mtawala na rai. Da´wah ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sisi hatuwaiti watu kutufuate. Mimi binafsi naona sio mtu wa kufuatwa. Na wala hatuwaiti watu pia watufuate kichwa mchunga. Kwa hakika kufuata kichwa mchunga ni haramu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

قليلا ما تذكرون اتبعوا ما أنزل إليكم من ربكم ول ت تبعوا من دونه أولياء

”Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake (Allaah), awliyaa (marafiki wapenzi, walinzi wanaokuamrisheni kufru, shirki). Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03)

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta´ala):

إن السمع والبصر والفؤاد كل أول ئك كان عنه مسئولا ت قف ما ليس لك به علم ول

”Na wala usiyafuate (kusema au kufanya) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo daima vitaulizwa (Siku ya Qiyaamah).” (17:36)

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=40

33. Hivyo Utajua Kuwa Hizbiyyuun Hawajali Uislamu ´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Mwishowe tutaweka wazi ukweli wa mambo na tufichue Hizbiyyuun. Na ni wajibu kwa wanachuoni wa Sunnah kubainisha hali za Hizbiyyuun. Hizbiyyuun hawa ambao wanachafua picha ya wanachuoni watukufu wanaolingania katika Dini ya Allaah. Nani kasema ya kwamba wanajali Uislamu? Lau wangelikuwa kweli wanajali Uislamu, basi wasingeliwaponda

Page 29: Fataawa Za Wanachuoni (21)

29

wanachuoni watukufu. Hawawapondi kwa jengine ila ni kwa sababu hawakubaliani kwa makundi makundi yao. Allaah Amjaze - Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy - kheri. Na hakulindwa na madhambi. Sisi hatusemi ya kwamba hakosei. Sote tunapatia na kukosea, na kuna mambo tusiyojua na tunayojua.

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=41

34. Shaykh Rabiy´ Ni Mwanachuoni Mkubwa Wa Hadiyth

Swali:

Kuna watu wanaomponda Shaykh Rabiy´ (Hafidhwahu Allaah) na Da´wah yake. Na kuna watu huku kwetu USA wanaofanya pia hivi. Nini unachojua kwa Shaykh na Da´wah yake?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Shaykh Rabiy´ (Hafidhwahu Allaah) nilimjua katika mji wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Shaykh ni katika wanachuoni wakubwa wa Hadiyth. Na ni katika watu wanaopenda Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanaolingania kwayo. Na ana vitabu vyenye thamani. Moja ya kitabu bora katika hivyo ni "Bayn al-Imaamayn; Muslimna ad-Daaraqutniy". Halafu nikasafiri kwenda Yemen. Akapata ujuzi wa Hizbiyuun wengi. Na baadhi yao walikuwa ni wanafunzi wenzake kama ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq. Shaykh Rabiy´ alikuwa katika al-Ikhwaan al-Muslimuun na ndio maana akajua makosa ya Sayyid Qutwub, Hasan al-Bannaa na waliyokuwemo wengi katika al-Ikhwaan al-Muslimuun. Kwa hivyo, akawa ameandika kitabu cha thamani. Ninamuomba Allaah Amjaze kheri.

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=41

Page 30: Fataawa Za Wanachuoni (21)

30

35. Ikiwa Hizbiyyuun Watakwita Katika Mkutano Na Kujitolea

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Hali kadhalika tunachukia Hizbiyyah ambao umewagawanya Waislamu. Na kufarakanisha Jamaa´ah yao. Na tunajua kuwa ni wadanganyifu. Ni wingi ulioje wanadanganya al-Ikhwaan al-Muslimuun? Wanasema ya kwamba wanataka mji wa Kiislamu. Ni mara ngapi nimeshawaambia kwenda kwao kinyume na Uislamu? Bali niliambiwa na baadhi ya ndugu watukufu jinsi walivyochagua mkristo katika jimbo moja la Amerika. Ninachotaka kusema enyi ndugu zangu, tafuteni na msome elimu yenye manufaa. Msipoteze wakati wenu katika mijadala.

at-Tirmidhiy kapokea katika "al-Jaamiy´" yake kupitia kwa Abu Umaamah ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kasema:

"Hawakupotea watu baada ya kuongoka isipokuwa walianza kujadili."

Kisha akasoma Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Kauliya Allaah (Ta´ala):

جدل بلأضربوه ما لكإل مخصمون قوأ همأ

"Hawakukupigia (mfano huo wa kulinganisha) isipokuwa tu kutaka kujadili. Bali wao ni watu makhasimu." (43:58)

Hivyo, tafuteni elimu yenye manufaa. Na ikiwa al-Ikhwaan al-Muslimuun watawaita katika mkutano waambieni tunamhimidi Allaah ambaye Katukinga kwa yale Aliyowapa mtihani kwayo. Na wakiwaita kujitolea [swadaaqah] waambieni ya kwamba mna mambo tunayojua wapi tutatumia pesa. Hakika kwa pesa hizo wanajenga manyumba makubwa San´aa'. Hali kadhalika watu wa shirika al-Hikmah na al-Ihsaan. Hali kadhalika Suuruuriyyah. Kuweni tahadhari na chungeni sana kwa watu wa makambi wanaofuata madhehebu na Hizbiyuun na badala yake tafuteni elimu yenye manufaa.

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=41

Page 31: Fataawa Za Wanachuoni (21)

31

36. Serikali Inanufaika Kwa Da´wah Ya Ahl-us-Sunnah

Yemen Times:

"Vipi mawasiliano yako na serikali? Na je, kuna ukandamizi wowote unaopata wewe binafsi, markazi yako au wanafunzi wako wanaotoka nje ya nchi na kuja kusoma kwako?"

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Serikali haina madhara yoyote kwa Da´wah yetu. Bali kinyume chake. Lau wangelielewa inawanufaisha wao. Tunawatahadharisha watu kumwaga damu ya Waislamu. Tunawatahadharisha watu kumfanyia uasi mtawala. Tunawatahadharisha kwa mapinduzi na migomo. Na hii ndio Dini yetu. Na si kwa ajili serikali iko juu yetu. Hii ndo Dini yetu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

"Mtu atakayewajia na anataka kufarakanisha na Umoja wenu, mkateni shingo yake yeyote awae."

Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Watapoahidiwa makhalifah wawili utiifu na usikivu, basi mkateni shingo yule wa mwisho wao."

Kisha isitoshe, sisi tunajitayarisha kuwa na subira. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn Mas´uud ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kasema:

"Kwa hakika mtakuja kuona [mtawala] anachukua vitu vya dunia na mambo msiyoyajua." Wakasema: "Watuamrisha nini, ewe Mtume wa Allaah?" Akajibu: "Wape haki iliyo juu yenu na nyinyi mumuombe Allaah haki yenu."

Akasema tena kuwaambia Answaar:

"Mtakuja kuona [mtawala] anavyochukua mambo ya kidunia baada yangu. Hivyo kuweni na subira mpaka mtapokutana na mimi katika hodhi."

Serikali wanawasaidia watu wengine kwa Misikiti ya Ahl-us-Sunnah. Na hili hutendeka sana. Linafanywa kwa jina la nchi. Wanakuja na kikosi katika Misikiti ya Ahl-us-Sunnah. Lakini sisi - In Shaa Allaah - tuna subira na tunahesabu thawabu kwa hili. Zawadi hii ni kutoka kwa Allaah (Subhaanahu

Page 32: Fataawa Za Wanachuoni (21)

32

wa Ta´ala). Na wakitutoa Misikitini tutafunza barabarani. Na hii huchukuliwa pia ni Da´wah. Watatuuliza kwa nini mnafunza nje barabarani wakati Msikiti huu uko karibu yenu? Tatizo ni kwamba hawatuachi tufunze humo. Tumejiyatarisha - In Shaa Allaah - kuwa na subira, hata kama haijuzu kwa serikali kuchukua Misikiti ya Ahl-us-Sunnah.

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=40

37. Ahl-us-Sunnah Wanawapenda Maimamu Na Wanachuoni Wote

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:

Sisi tuko na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isitoshe Ahl-us-Sunnah wanawapenda Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mapenzi ya Kidini. Na wanawapenda maimamu wa Hadiyth mapenzi ya Kidini. Na wanawapenda maimamu watukufu kama Imaam Ahmad, Imaam Maalik na Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahumu Allaah) mapenzi ya Kidini. Tofauti na wale wanaofuata madhehebu kichwa mchunga. Ukisoma vitabu vya historia, kama "al-Bidaayah wan-Nihaayah" cha Ibn Kathiyr utaona kulivyokuwa ugomvi na fitina Misikitini. Bali baya zaidi kuliko hili, katika al-Masjid al-Haraam kulikuwa kunaswali madhehebu manne kila mmoja na Swalah yake. Kila dhehebu lilikuwa na imamu wake na wanaswali nyuma yake. Waislamu walikuwa haswali Swalah moja kwa pamoja mpaka likandolewa katika muda ambao si mbali sana. Sisi Ahl-us-Sunnah - Alhamduli Allaah - tunawapenda wanachuoni wote. Na wala hatumfuati kichwa mchunga yeyote katika wao.

Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=41

38. Baadhi Ya Sifa Za Kumjua Ni Nani Salafiy Wa Kweli

Page 33: Fataawa Za Wanachuoni (21)

33

Swali:

Sisi ni kundi la vijana tunatatizika na jambo, kila kundi linatoa dalili ya Aayah

na Hadiyth ya kwamba ni Salafiyyah. Na sisi tumetatizika

tufanye nini?

´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:

Jambo la kwanza, angalieni hawa wanaodai kama wako na al-Walaa´ wal-

Baraa´. Mkiona wanawapenda Ahl-ul-Bid´ah, watakuwa wamejifedhehesha

tayari na kujulikana ni watu gani. Jambo la kwanza litakalowafedhehesha ni

mapenzi yao ya uongo kwa Manhaj ya Salaf, na mapenzi yao ya kihakika kwa

Ahl-ul-Bid´ah wad-Dhwalaal. Hili ni jambo la kwanza litakalowafedhehesha.

Isitoshe kuna jambo lingine la lazima, mafungamano yao na Salaf-us-Swaalih,

sawa katika mambo ya ´Aqiydah, ´Ibaadah, Halali na Haramu.

"Yule ambaye Allaah Anamtakia kheri, humpa ufahamu wa Dini."

Yule ambaye ataifahamu vyema Dini, ataona makosa ya watu hawa na

kupinda kwao katika kupenda kwao na kujiweka kwao mbali [kuchukia] na

katika mambo yao mengi ya kimsingi na Manhaj yao, na katika al-Walaa´ wal-

Baraa´. Kwa yule ambaye Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Kampa ufahamu

mzuri na Anamtakia kheri atajua. Kama walivyokuwa vijana wengi wa ki-

Salafiy, wataweza kupambanua baina ya Ahl-ul-Ahwaa na Ahl-ul-Haqq, na

Ahl-ul it-Tibaa´ na Ahl-ul Inhiraaf.

Chanzo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=355

39. Kijakazi Alijua Mola Wake Alipo Tofauti Na Watu Wengi Wa Zama Hizi

Imaam al-Albaaniy:

Page 34: Fataawa Za Wanachuoni (21)

34

Huu ndio upotofu wa wazi, kutokana na dalili zilizo wazi katika Qur-aan

zioneshazo ya kwamba Ar-Rahmaan Yuko juu ya ´Arshi Kastawaa. Na Kauli

ya Allaah:

العلى ربك اسم سبح

"Sabbih (tukuza) Jina la Mola wako Aliye juu kabisa." (87:01)

Na pindi Alipowasifu waja Wake waumini:

هم يخافون م من رب فوق ه

"Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao, na wanafanya yale

wanayoamrishwa." (16:50)

وح الملئ كة تعرج إ ليه والر

“Malaika na Roho (Jibrily) wanapanda Kwake.” (70 : 04)

Katakasika Allaah kwa wayasemayo madhalimu kutakasika ambako ni

kukubwa.

Katika Hadiyth Swahiyh:

"Alikuwepo Allaah na hapakuwa kitu pamoja Naye."

Ni mahali gani [Alikuwepo Allaah] mahali ambapo wamekusanyika watu

hawa walio kila mahali? Na khaswa mahali kama hizi kuna ambazo ni safi, na

kuna ambazo ni za najisi na chafu, vyoo, baa, sehemu za taka, sehemu za

wafanya uasherati na kadhalika. Vipi basi wasimtakasi Allaah (´Azza wa Jalla)

kwa kuwa kila mahali? Pamoja na kuwa Amesema katika Aayah nyingi kama

tulivyosema ya kwamba Yeye Yuko juu ya ´Arshi Yake Kastawaa. Na katika

Hadiyth Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

alimuuliza kijakazi ambaye bwana wake alikuwa anataka kumwacha huru:

Akamuuliza: "Yuko wapi Allaah?". [Kijakazi yule akajibu]: "Mbinguni".

Akamuuliza tena: "Ni nani mimi?". Akajibu: "Wewe ni Mtume wa Allaah".

Akamgeukia bwana wake na kumwambia: "Muache! Kwani kwa hakika ni

muuminah".

Kijakazi katika zama za Mtume alikuwa na Fiqh [katika Dini] zaidi kuliko

Fuqahaa wengi wa leo. Kwa kuwa ukiwauliza wengi katika watu hawa [Ahl-

ul-Bid´ah]: "Yuko wapi Allaah?" Watakujibu: "Yuko kila mahali".

Page 35: Fataawa Za Wanachuoni (21)

35

Mmoja katika majirani zangu anasema:

"Allaah Yuko katika kila kilichopo".

Masikini watu hawa. Vilivyopo vimeumbwa, na Alikuwepo Allaah na

hapakuwa kiumbe chochote. Hivyo, baada ya Mola Wetu kuumba viumbe,

Akageuka kuwa sehemu ya viumbe hawa - pamoja na

takataka/uchafuunaopatikana humo! [Kamwe!]. Ametakasika Allaah kwa

wasemayo madhalimu kutakasika kukubwa.

Chanzo: Silsilat al-Hudaa wan-Nuur 178

40. Kumbadili Mtoto Nepi Kunavunja Wudhuu?

Swali:

Wudhuu wa mama unatenguka pindi anapombadili nepi mtoto wake?

Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:

Wudhuu katika hali kama hii utakuwa umeamrishwa kwa njia ya upendeleo

na kupendekezwa, na sio kwa njia ya uwajibu na faradhi. Akitawadha tena

atapata ujira, na akitosheka kwa Wudhuu wa mara ya kwanza ataosha

mikono yake tu ikiwa kama alipatwa na kitu.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=rtQCHTjTQgg

41. Kuna Uongo Mweupe Na Mweusi?

Page 36: Fataawa Za Wanachuoni (21)

36

Swali:

Je, kuna uongo mweupe na mweusi?

´Allaamah al-Fawzaan:

Uongo wote ni mweusi na hakuna mweupe. Wote ni mweusi. Haujuzu,

isipokuwa katika hali tatu ambazo kazisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam). Uongo ili kupatanisha wawili waliogonbana, uongo kwa mume na

mke ili kutengeneza uhusiano wao au uongo ili kusamilika kutoka kwa

dhalimu - na hii ndo huitwa taawili. Mbali na hayo, uongo wote ni Haramu.

Na ni katika madhambi makubwa na haujuzu.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=N_caKhSkh5M

42. Mtu Avute Sigara Kwa Mkono Wa Kulia Au Wa Kushoto?

Swali:

Mtu avute sigara kwa mkono wa kulia au wa kushoto?

Imaam al-Albaaniy:

Hata mmoja katika yayo.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=lnF19WlksEY

43. Kumpiga Mwanamke Ni Katika Tabia Mbaya

Page 37: Fataawa Za Wanachuoni (21)

37

Shaykh Dr. Muhammad al-Madkhaliy:

Enyi ndugu! Kumpiga mwanamke, hata kama imeruhusiwa lakini sio kitu

kinachopendwa. Sio kitu kinachopendwa kwa wanaume watukufu, masharifu

wao na wabora wao. Na kwa ajili hii, kasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu

´anha):

"Hajawahi kumpiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke

kwa mkono wake wala mtumwa, wala kulipiza kisasi kwa ajili yake

mwenyewe, isipokuwa tu kunapovukwa mipaka ya Allaah, hapo hulipiza

kisasi kwa ajili ya Allaah."

Hakuwahi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumpiga

mwanamke. Kwa hivyo, kuwapiga wanawake ni jambo linalochukiza kwa

wanaume wenye akili, watukufu, masharifu, wenye fadhila na waliyo juu

katika wao. Hili ni jambo linalochukizwa kwao. Na kwa ajili hii, alisisitiza

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana hii [ya kutowapiga], pamoja

na kwamba imeruhusiwa. Akasema:

"Mmoja wenu asimpige mijeledi mwanamke wake kama anavyompiga

mijeledi mtumishi wake kisha (akataka) kulala nae."

Katika upokezi mwingine:

"... mwanzoni mwa siku kisha (akataka) kulala nae mwisho wa siku."

Vipi, kwa Jina la Allaah, utampiga na kumpa mijeledi kama unavyompiga

mtumwa kisha wataka aje katika kitanda chako? Hili haliwezekani. Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katahadharisha tabia kama hii mbaya.

Hata kama imeruhusiwa kumpa adabu mwanamke:

ت ي ظوهن نشوزهن تخافون والل ع ف ي واهجروهن فع بوهن المضاج واضر

"Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na

(wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe

wakishikilia uasi) wapigeni." (an-Nisaa 04 : 34)

[Allaah] Akafanya kupiga ndio iwe dawa ya mwisho. Pamoja na hivyo, kipigo

hichi kimefundishwa ni namna gani kwa wanachuoni; ya kwamba iwe ni pigo

khafifu ambacho hakitomvunja wala kumuachia jeraha. Usimpige

ukamuumiza jicho lake kisha jicho lake likatoka. Au ukampiga kwenye sikio

lake kiwambo chake kikaharibika. Hili halijuzu. Na kupiga kwenye uso ni

Page 38: Fataawa Za Wanachuoni (21)

38

Haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kalikataza. Pamoja na

hivyo, mahakamani unasikia daima mashtaka ya wanaume kuwapiga

wanawake; na hii ni tabia mbaya ambayo katahadharisha Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa hili mlilosikia:

"Mmoja wenu asimpige mijeledi mwanamke wake kama anavyompiga

mijeledi mtumishi wake au kama mja kisha (akataka) kulala nae."

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=ezWzgCQszpE

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na

Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.