habari ya mfumuko wa bei agosti 2015

3
MFUMUKO WA BEI WABAKI KUWA ASILIMIA 6.4 KAMA ILIVYOKUWA MWEZI JULAI, 2015 Na: Veronica Kazimoto, Dar es Salaam, 08 Septemba, 2015. Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015. “Tunaposema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ya mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi ya mwezi Julai, 2015 haimanishi kuwa bidhaa hazijapanda wala kushuka isipokuwa baadhi ya bidhaa zimepanda bei na nyingine kushuka ila kasi yake ya upandaji bei ndio imekuwa sawa na ile ya mwezi Julai, 2015,” amesema Kwesigabo. 1

Upload: ngabwe

Post on 12-Dec-2015

90 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: Habari Ya Mfumuko Wa Bei Agosti 2015

MFUMUKO WA BEI WABAKI KUWA ASILIMIA 6.4 KAMA ILIVYOKUWA MWEZI JULAI, 2015

Na: Veronica Kazimoto,Dar es Salaam,08 Septemba, 2015.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015.

“Tunaposema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ya mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi ya mwezi Julai, 2015 haimanishi kuwa bidhaa hazijapanda wala kushuka isipokuwa baadhi ya bidhaa zimepanda bei na nyingine kushuka ila kasi yake ya upandaji bei ndio imekuwa sawa na ile ya mwezi Julai, 2015,” amesema Kwesigabo.

Kwesigabo amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo, Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi kufikia 158.81 kwa mwezi Agosti, 2015 kutoka 149.31 mwezi Agosti, 2014. Kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula.

“Baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa asilimia 2.0, mafuta ya taa kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia 1.4, dizeli kwa asilimia 3.8 na petroli kwa asilimia 8.3,” amesema Kwesigabo.

1

Page 2: Habari Ya Mfumuko Wa Bei Agosti 2015

Kwa upande wa uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na Shilingi 62 na senti 98 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.

Aidha, Mfumuko wa Bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Akitolea mfano wa nchi za Kenya na Uganda, Mkurugenzi Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2015 nchini Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015.

MWISHO.

2