hotuba ya kuaganga na kuvunja bunge la kumi, 2015 - final.doc
TRANSCRIPT
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
1/104
1
HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO
KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA
KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE,
DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015
Mheshimiwa Spika;
Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha
kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu
na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi
imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia
nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze
kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini,
shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na
shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi
rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
2/104
2
mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama
salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari
hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika
uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza
kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa
kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake
wakipewa nafasi wanaweza.
Mheshimiwa Spika;
Niruhusu pia nitoe shukrani na pongezi zangu za dhati
kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kazi kubwa na nzuri
mliyoifanya. Mmetimiza ipasavyo wajibu wao wa Kikatiba
wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawashukurukwa ushirikiano wenu na msaada wenu. Ni ukweli ulio
wazi kuwa bila ya ninyi Wabunge wetu na Bunge hili,
tusingeweza kupata mafaniko na maendeleo tuliyoyapata.
Mmejijengea, nyinyi wenyewe na Bunge letu heshima kubwa
mbele ya wananchi. Mmeitendea haki demokrasia ya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
3/104
3
Tanzania na kuliletea heshima kubwa Bunge letu nchini,
kikanda na kimataifa.
Mheshimiwa Spika;
Tarehe 30 Desemba 2005 nilipozindua Bunge la Tisa
nilielezea mtazamo wangu kuhusu nchi yetu na kutaja
majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali ya Awamu
ya Nne. Nilisema tutatekeleza wajibu wetu na vipaumbele
hivyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Tarehe 16
Julai, 2010 wakati wa kuvunja Bunge hilo nilielezea
mafanikio tuliyopata na changamoto zilizotukabili katika
kipindi hicho. Tarehe 28 Novemba, 2010 wakati wa kuzindua
Bunge hili la Kumi niliainisha vipaumbele vya Serikali yaChama cha Mapinduzi katika kipindi changu cha pili cha
uongozi wa nchi yetu na kuahidi kuvitekeleza kwa ari zaidi,
nguvu zaidi na kasi zaidi. Kama ilivyo ada, leo tunafikia
mwisho wa uhai wa Bunge la Kumi, naomba kutumia fursa
hii kutoa mrejesho wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali
na yale mambo ambayo tuliahidi na kupanga kufanya.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
4/104
4
Umoja, Amani na Usalama
Mheshimiwa Spika;
Niliahidi kuwa katika kipindi cha uongozi wangu
nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa Tanzania
inaendelea kuwa nchi moja na watu wake wanaendelea
kuwa wamoja, wanaopendana na kushirikiana licha ya
tofauti zao za rangi, dini, makabila, mahali watokako, na
ufuasi wa vyama vya siasa. Pia, kwamba nchi yetu
itaendelea kuwa yenye amani, usalama na utulivu.
Leo tunapoagana, ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa
Tanzania na Watanzania tumebakia kuwa wamoja. Hata
hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na matukio ya hapana pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi
yetu na watu wake. Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta
chuki baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, baina ya Wakristo
na Waislamu na baina ya maeneo fulani ya nchi na wengine.
Bahati nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa
Serikali zetu mbili wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
5/104
5
na ushirikiano na viongozi wa dini na wa jamii na uelewa
wa wananchi, vimeliwezesha taifa letu kushinda
changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi
zimethibitisha ubora wa mazungumzo. Ni kweli kabisa
kwamba wanaozungumza hawagombani na
wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.
Mheshimiwa Spika;
Niruhusuni, nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara
nyingine viongozi wakuu wenzangu, Makamu wa Rais, Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchiwote kwa ushindi tulioupata katika kudumisha umoja wetu.
Hata hivyo, tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa
kwani watu wenye nia mbaya kwa nchi yetu au na umoja
wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba hawajafaulu.
Huenda wakajaribu tena. Tunachotakiwa kufanya ni
kuendelea kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
6/104
6
Muungano Wetu Umeimarika Zaidi
Mheshimiwa Spika;
Nafurahi kwamba namaliza kipindi changu cha
uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na kuuimarisha
Muungano wetu adhimu na adimu Barani Afrika.
Mtakumbuka kuwa katika hotuba yangu ya kufungua
Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa viongozi wa pande
zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi
wa Muungano wetu. Nafurahi kwamba jambo hili
limefanyika chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais,
akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara
na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamuyangu ya kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika
awamu hii.
Mafanikio yaliyopatikana ni makubwa. Masuala
mbalimbali ya zamani na mapya yamezungumzwa,
yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa mfano,
hadi mwaka 2005 zilikuwa zimebakia kero13za Muungano
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
7/104
7
zilizoainishwa na Tume ya Shelukindo, hivi sasa zimebaki
kero nne. Tayari ufumbuzi wa kero moja unakamilishwa
kiutawala na tatu zimeshughulikiwa kwa ukamilifu katika
Katiba Inayopendekezwa. Kama kura ya maoni ingekuwa
imefanyika na Katiba hiyo kupitishwa kungekuwa hakuna
kiporo cha kero za Tume ya Shelukindo. Lakini kwa vile
kura ya maoni haijafanyika ndiyo maana tunaendelea
kuzitaja. Hata hivyo, Serikali zetu mbili zimezungumza na
kukubaliana tutafute njia ya kumaliza suala la rasilimali ya
mafuta na gesi. Ndiyo maana katika Muswada wa Petroli
hoja ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ya kusimamia
uchimbaji wa mafuta na kumiliki mapato yake ilijumuishwa.Natoa shukrani nyingi kwa Bunge lako tukufu kwa
kupitisha Muswada huo. Moja ya kero kubwa katika
Muungano tumeimaliza.
Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
8/104
8
Mheshimiwa Spika;
Mtakumbuka kuwa nilizungumzia kusononeshwa
kwangu na mpasuko wa kisiasa uliokuwepo Zanzibar
wakati ule na kuelezea utayari wangu wa kusaidia
kuuondoa. Kama mjuavyo mazungumzo yalifanyika ndani
ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka
ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na
mpasuko wa kisiasa ukawa umepatiwa tiba. Matokeo ya
yote hayo ni kuwa mazingira ya kisiasa na kijamii
yamekuwa bora zaidi siku hizi kuliko ilivyokuwa kabla ya
hapo.
Ni matumaini yangu kuwa ndugu zetu wa Zanzibarwatayadumisha mafanikio haya ili waendelee kuishi kwa
amani, upendo na udugu. Natambua kuwepo kwa
changamoto za hapa na pale katika uendeshaji wa Serikali
hiyo. Jambo linalonipa faraja ni kuwa matatizo yenyewe
hayahusu muundo wa Serikali bali yanaletwa na watu
kupishana kauli au kutofautiana katika uendeshaji wa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
9/104
9
baadhi ya mambo. Mimi naamini hayo ni mambo
yanayoweza kumalizwa kwa wadau kukaa kitako na
kuzungumza kama ilivyokuwa kabla ya muafaka.
Amani na Usalama
Mheshimiwa Spika;
Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama kwa sababu
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea
kutimiza ipasavyo jukumu lake la kulinda uhuru na mipaka
ya nchi yetu. Katika kipindi hiki tumewekeza sana katika
kuliimarisha Jeshi letu kwa vifaa na zana za kisasa za kivita
na mafunzo. Tumeimarisha Kamandi za Nchi Kavu, Anga na
Majini. Utayari kivita wa jeshi letu ni mzuri tena wa hali ya juu. Weledi na nidhamu ya Wanajeshi wetu ni ya hali ya juu.
Tumeboresha maslahi na makazi ya wanajeshi kwa kujenga
nyumba mpya za kuishi. Utekelezaji wa mpango wa
kuwajengea nyumba10,000unaendelea vizuri. Hadi hivi
sasa nyumba6,064zinaendelea kujengwa nchi nzima na kati
yake nyumba3,096 zimekamilika. Namaliza kipindi changu
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
10/104
10
cha kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama kwa kujiamini kwamba “Tupo vizuri”. Pamoja na
hayo kazi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka 15 wa
kuimarisha JWTZ lazima iendelezwe ili kulifikisha Jeshi letu
pale tulipopakusudia.
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa ya
kupambana na uhalifu ili kulinda usalama wa maisha na
mali za watu waishio Tanzania. Mtakumbuka kuwa mwaka
2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi ya
ujambazi. Niliahidi wakati wa kampeni na katika hotuba
yangu Bungeni kwamba hatutawaacha majambaziwaendelee kutamba. Hali ile imedhibitiwa. Ingawaje
matukio ya ujambazi hayajaisha, lakini hayako kama
ilivyokuwa wakati ule.
Hali kadhalika, matukio ya uhalifu wa kuwania mali
yamepungua kutoka53,268 mwaka 2005 hadi43,808 mwaka
2014. Natoa pongezi nyingi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
11/104
11
kubwa na nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kufanya.
Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za
barabarani. Lazima tuendelee kuzitafutia muarobaini wake.
Niruhusuni niwatambue na kuwashukuru Inspekta Jenerali
(mstaafu) Omari Mahita, Inspekta Jenerali (mstaafu) Said
Mwema na Inspekta Jenerali Ernest Mangu aliyepo sasa kwa
uongozi wao mzuri.
Mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali
katika utakelezaji wa mpango wa maboresho ya Jeshi la
Polisi uliobuniwa wakati wa uongozi wa Ndugu Saidi
Mwema, IGP mstaafu. Jeshi la Polisi linaendelea
kuwezeshwa kwa zana, vifaa na mafunzo. Taratibuzimekamilika za kulipatia Jeshi hilo magari ya kutosha ili
kuongeza ufanisi.
Pia, tumeendelea kuboresha maslahi na mazingira ya
kuishi Maafisa na Askari. Kwa ajili hiyo tumekarabati
baadhi ya nyumba zilizopo, tumejenga nyumba kadhaa
mpya za ghorofa, za kawaida na mabweni. Mipango
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
12/104
12
imekamilika ya kuwezesha ujenzi wa nyumba 10,000
ambazo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa
nyumba za kuishi katika Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Spika;
Jeshi letu la Magereza nalo limeendelea kutekeleza
vizuri majukumu yake ya kulinda wafungwa na kurekebisha
tabia zao. Aidha, huduma za malazi, mavazi, chakula na
usafiri kwa wafungwa zimeendelea kuboreshwa.
Changamoto kubwa ni msongamano wa wafungwa
Magerezani. Naamini mipango ya kujenga magereza mapya
na kupanua yaliyopo ikitekelezwa tatizo litaisha. Aidha,
mpango wa maboresho ya Jeshi la Magereza ukikamilika nakutekelezwa, utaboresha mazingira ya kufanyia kazi na
kuishi maafisa na askari, hivyo kupandisha morali wao na
kuongeza ufanisi.
Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
13/104
13
Ahadi yangu ya kuanzisha upya utaratibu wa
kuchukua vijana wa mujibu wa Sheria katika Jeshi la
Kujenga Taifa imetimia. Mpaka hivi sasa vijana38,200
wamekwisha hitimu mafunzo hayo wakiwemo
Waheshimiwa Wabunge. Nawapongeza sana Waheshimiwa
Wabunge walioshiriki kwa kuongoza kwa mfano. Imesaidia
sana utaratibu huo kuanza upya bila vipingamizi. Ni
matumaini yangu kuwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa watakaa pamoja kujadili namna ya
kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zilizopo. Naamini
zinaweza kumalizwa, vijana wetu wakashiriki mafunzo bila
matatizo yoyote.
Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi cha miaka kumi hii tumetekeleza
dhamira yetu ya kujenga na kuimarisha utawala bora kwa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
14/104
14
sera, sheria, mifumo, taasisi na kwa rasilimali watu.
Tumefanya hivyo katika maeneo yote muhimu yakiwemo
yale yahusuyo haki za binadamu, demokrasia, mapambano
dhidi ya rushwa, maadili ya viongozi, ukusanyaji wa mapato
na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na mgawano
wa madaraka hati ya mihimili.
Bunge la Jamhuri ya Muungano
Mheshimiwa Spika;
Serikali imetimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili
mkuu wa dola wa Kutunga Sheria. Tulianzisha Mfuko wa
Bunge na kuongeza fedha katika bajeti ya Bunge toka
shilingi bilioni 30.58 mwaka 2005/06 hadishilingi bilioni173.76 mwaka 2015/16. Pia tumeanzisha Mfuko wa Jimbo ili
kuwawezesheni Wabunge kuchangia katika kutatua
changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi wa
majimbo yao. Bunge letu limetekeleza ipasavyo majukumu
yake kupitia Kamati zake za kudumu na pale ilipolazimu
Kamati teule zilizoundwa.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
15/104
15
Katika kipindi hiki miswada163 imepitishwa, maswali
ya msingi7,544 na ya nyongeza22,632 yameulizwa na
kujibiwa. Kamati teule 2 ziliundwa. Haya ni mafanikio
makubwa kwa Bunge letu. Bunge hili limefanya kazi kubwa
na kazi ya kutukuka. Michango na ushauri wake umekuwa
chachu ya baadhi ya hatua na mabadiliko ya kisera, kisheria
na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali. Kwa kweli mnastahili
pongezi nyingi. Huwezi kutaja mafanikio ya Serikali ya
Awamu ya Nne bila kutambua mchango wa Bunge hili.
Mchakato wa Katiba
Mheshimiwa Spika;
Kama sote tujuavyo, kupitia Sheria iliyotungwa naBunge hili, mwaka 2013 tulianzisha mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuipatia nchi yetu Katiba
mpya iliyo bora zaidi kuliko iliyopo sasa. Nafurahi kwamba
mchakato huo ulituwezesha kupata Katiba
Inayopendekezwa ambayo imekidhi matarajio hayo. Narudia
kutoa pongezi za dhati kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
16/104
16
na Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na nzuri
waliyofanya. Hatua iliyobaki ni Kura ya Maoni ambapo sote
tunasubiri maelekezo ya Tume ya Uchaguzi. Mimi naamini
iwapo itapitishwa, Katiba Inayopendekezwa itaimarisha
zaidi taifa letu.
Vyama vya Siasa
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumeshuhudia vyama vya siasa
vikiendelea kuimarika na kujijenga nchini. Idadi ya vyama
vya siasa imeongezeka kutoka18 hadi24. Vyama vya siasa
vimefanya shughuli zake kwa uhuru. Viongozi na
wanachama wao wamefanya mikutano mingi na hatamaandamano kote nchini. Baraza la Vyama vya Siasa na
TCD vimekuwa vyombo muhimu vilivyofanya kazi nzuri ya
kujenga ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.
Yamekuwa majukwaa muhimu ya mashauriano baina ya
vyama vya siasa kwa masuala mbalimbali. Matatizo na
changamoto nyingi zimeweza kupatiwa ufumbuzi. Ni
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
17/104
17
matumaini yangu kuwa vyombo hivi viwili vitaendelezwa
na kuimarishwa miaka ijayo.
Huu ni mwaka wa Uchaguzi, na vyama vya siasa ndiyo
wahusika wakuu. Ni matumaini yangu kuwa vyama vya
siasa vitaheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi. Hii
itasaidia kuwepo kwa utulivu na amani katika mchakato wa
uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu
Mheshimiwa Spika;
Habari kubwa hapa nchini sasa ni uchaguzi mkuu.
Tayari Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na ile ya Zanzibar
(ZEC) zimekwisha tangaza tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwa nisiku ya kufanyika uchaguzi mkuu. Maandalizi ya uchaguzi
huo yanaendelea vizuri. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inaendelea na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa
mfumo mpya wa teknolojia yaBiometric Voters Register (BVR).
Hadi sasa zoezi la uandikishaji limekamilika katika mikoa13
na linaendelea katika mikoa11 na katika mkoa wa Dar es
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
18/104
18
Salaam na Zanzibar uandikishaji unategemea kuanza mwezi
huu. Kwa taarifa za Tume ya Uchaguzi, tayari wamekwisha
andikisha hadi sasa wapiga kuramilioni 11 kati ya lengo la
kuandikisha wapiga kura kati yamilioni 21hadi 23.
Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu
wa kuiwezesha Tume kutimiza wajibu wake. Napenda
kuwahakikishia kuwa kila Mtanzania mwenye haki ya
kupiga kura atapata fursa ya kuandikishwa. Shime tuhimize
watu wajitokeze kujiandikisha ili wasikose haki yao hiyo.
Uhuru wa Habari Mheshimiwa Spika;
Mtakubaliana nami kuwa katika kipindi hiki uhuru wa
habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao umepanuka sana.
Tanzania kuna magazeti ya kila siku16 na kati ya hayo ya
Serikali ni2(Daily News, Habari Leo). Pia magazeti ya kila
wiki yapo62. Aidha, kuna vituo vya redio115 na vya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
19/104
19
televisheni29. Serikali haifanyi uhakiki wa habari kabla ya
kuchapishwa au kuandikwa. Tumeamua hivyo kwa imani
yangu kwamba ustawi wa demokrasia hutegemea sana
uhuru wa vyombo vya habari. Pili, kwa vile tunatambua
manufaa ya vyombo vya habari kuelimisha jamii,
kupambana na maovu na kuhimiza uwajibikaji.
Pamoja na hayo, hatukusita wala kuchelea kuchukua
hatua pale uhuru huo ulipotumiwa vibaya na kutishia
kuvuruga amani, umoja na usalama wa jamii au taifa. Au,
pale ambapo Sheria za nchi zimekiukwa. Huo ni wajibu
wetu wa kikatiba ambao mimi na wenzangu tuliapa
kuutimiza. Mheshimiwa Spika;
Katika kuongeza uwazi na mawasiliano na wananchi
mwaka 2007 tulianzisha tovuti ya wananchi. Tovuti hiyo
imeshapokea hoja117,243 na kati ya hizo zilizohusu Serikali
zilikuwa78,258 na zote zimeshughulikiwa.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
20/104
20
Katika kuboresha mfumo wa mawasiliano, Tanzania
imeshahama kutoka mfumo wa analogia na kuingia kwenye
mfumo wa digitali. Hii ni hatua kubwa muhimu kwa
maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Jambo ambalo
nasikitika kuwa hatukuweza kulikamilisha ni utungaji wa
Sheria ya Haki ya Upatikanaji wa Habari na Sheria ya
Vyombo vya Habari. Miswada imekamilika na kusomwa
mara ya kwanza hapa Bungeni lakini mchakato wake
haukuweza kufika mwisho. Tunawaachia wenzetu wajao
washughulike nayo katika Bunge la 11.
Vita dhidi ya Rushwa Mheshimiwa Spika;
Vita dhidi ya rushwa ni eneo jingine ambalo tulilivalia
njuga katika Awamu ya Nne. Tumepata mafanikio ya kutia
moyo katika mapambano dhidi ya rushwa ingawaje kazi
bado ni kubwa. Tumefanya mambo matatu. Kwanza,
tumetunga Sheria Na. 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
21/104
21
Kupambana na Rushwa ambayo imeongeza nguvu ya
mapambano dhidi ya uovu huu. Idadi ya makosa ya rushwa
iliongezwa kutoka4mpaka24 na wigo wa wakosaji pia, kwa
kuhusisha watu katika sekta binafsi. Mifumo ya upelelezi na
uendeshaji mashitaka nayo imeimarishwa.
Tumeunda chombo kipya TAKUKURU badala ya
TAKURU ambacho kimepewa majukumu ya kuzuia na
kupambana na rushwa badala ya kuzuia peke yake.
TAKUKURU imepewa mamlaka zaidi katika kuongoza
mapambano haya. Taasisi imeendelea kuimarishwa kwa
kuipatia zana na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na
rasilimali watu na mahitaji mengine. TumeiwezeshaTAKUKURU kufungua ofisi katika Mikoa na Wilaya zote.
Mheshimiwa Spika;
Maboresho haya yamewezesha idadi ya kesi za tuhuma
za rushwa zinazofikishwa mahakamani kuongezeka kutoka
kesi50mwaka 2005 hadi1,900mwaka 2014. Jumla ya
shilingi bilioni 87.8 ziliokolewa. Watumishi wa Serikali97
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
22/104
22
wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa na matumizi
mabaya ya ofisi zao baada ya ushahidi wa kijinai
kukosekana. Kwa upande wa kupambana na rushwa
kwenye shughuli za uchaguzi, tumetunga Sheria ya
Kudhibiti Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 ili
kutoa majibu ya kilio cha siku nyingi dhidi ya watu
wanaotumia fedha kununua kura.
Mapato na Matumizi ya Fedha na Mali za Serikali
Mheshimiwa Spika;
Nilieleza katika hotuba yangu ya Kuzindua Bunge la
Tisa tarehe 30 Desemba, 2005 kuwa tutatoa kipaumbele cha
juu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na nidhamu yamatumizi ya Serikali. Leo miaka kumi baadae ninaona
fahari tumepata mafanikio makubwa. Mapato ya Serikali
yameongezeka kutokashilingi bilioni 177.1 mwaka 2005
kwa mwezi hadi takriban shilingi bilioni 850. Hii
imewezesha bajeti ya Serikali kukua kutokatrilioni 4.13
mwaka 2005/2006 haditrilioni 22.49 mwaka 2015/2016.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
23/104
23
Isitoshe imetuwezesha kupunguza misaada na mikopo ya
washirika wa maendeleo kutokaasilimia 42 ya Bajeti ya
Serikali mwaka 2005 hadiasilimia 15 mwaka 2014/2015 na
tumejipa lengo la kushusha zaidi hadiasilimia 8 mwaka
huu wa fedha wa 2015/2016.
Mheshimiwa Spika;
Mafanikio haya yametokana hasa na kazi kubwa
tuliyoifanya ya kuimarisha Mamlaka ya Mapato ambao
wanastahili pongezi zetu nyingi. Bado naamini tunaweza
kufanya vizuri zaidi ya hivi, kama tukiongeza udhibiti kwa
mianya ya kupoteza mapato na kuimarisha zaidi TRA na
mamlaka nyingine za ukusanyaji mapato ya Serikali. Badoukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya kodi katika
Halmashauri za Wilaya na Miji na katika Wizara, Idara
zinazojitegemea na Wakala wa Serikali uko chini ya lengo.
Huku kuendelee kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
24/104
24
Kwa upande wa nidhamu ya matumizi ya fedha na
mali za Serikali tulielekeza nguvu zetu katika kuimarisha
utaratibu wa manunuzi Serikalini na ukaguzi wa hesabu za
Serikali. Kwa upande wa ununuzi wa bidhaa na huduma,
tumeendelea kuimarisha Sheria na Mamlaka ya Ununuzi wa
Umma ili iweze kuhakikisha kuwa kuna usimamizi thabiti
wa sheria hiyo na kanuni zake. Kama mjuavyo sehemu,
kubwa ya fedha za Serikali hutumiwa katika ununuzi wa
bidhaa na huduma, hivyo kuwepo usimamizi mzuri ni
jambo jema. Ukikosekana, wizi na rushwa hutawala.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za Serikali,
tumechukua hatua za makusudi za kuimarisha Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Tumetunga Sheria mpya inayoipa nguvu na uhuru zaidi
Ofisi hiyo. Aidha, tumewaongezea bajeti, vitendea kazi na
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
25/104
25
rasilimali watu. Ofisi8 za Mikoa zimejengwa na2
zinaendelea kujengwa.
Nafurahi kwamba maagizo yangu kwa viongozi na
watendaji katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhusu
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
kupewa uzito linazingatiwa. Taarifa hizo sasa zinasomwa,
zinajadiliwa na hatua kuchukuliwa kwa kasoro
zilizoonekana. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
imefanya kazi nzuri. Wezi na wabadhirifu wanaobainika
kuchukuliwa hatua za kisheria mara makosa
yanapogundulika. Kitaifa taarifa hiyo hujadiliwa Bungeni
kwa muda wa kutosha. Mheshimiwa Spika;
Niliamua pia kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali na kuwaweka Wakaguzi wa Ndani wote
wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka yake
na kuwajibika kwake. Ofisi hii imesaidia kuhakikisha sheria
na kanuni za matumizi ya fedha na mali ya umma
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
26/104
26
zinaheshimiwa. Pia, katika ufuatiliaji na utekelezaji wa
mapendekezo ya CAG. Uimarishaji wa ukaguzi wa ndani na
ule wa CAG umesaidia kuboresha hesabu za Serikali kuwa
nzuri zaidi siku hizi. Hati safi zimeongezeka na hati chafu
zinazidi kupungua Serikalini. Kwa mfano katika
Halmashauri za Wilaya na Miji, hati safi zimeongezeka
kutoka56 mwaka 2006 hadi150 mwaka 2014. Hati zenye
mashaka ni13 na hakuna Hati isiyoridhisha. Kazi ya
kuimarisha ukaguzi na nidhamu ya matumizi lazima
iendelezwe.
Maadili ya Viongozi wa Umma
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka 10 hii tumeimarisha mfumo wa
kusimamia maadili ya viongozi. Tumefanya hivyo kwa
kutambua kuwa maadili mema ni sifa ya msingi ya kiongozi
na huiletea heshima Serikali. Tumeendeleza Kamati ya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
27/104
27
Maadili na kuunda Baraza la Maadili kwa mujibu wa Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya 1995.
Tumepanua wigo na kwamba sasa mali za viongozi na
familia zao hutolewa taarifa na kiongozi katika Tamko la
Mali la kila mwaka. Hii inasaidia kuondoa uwezekano wa
kiongozi kuficha mali kwa mgongo wa mwenza wake au
mtoto.
Mheshimiwa Spika;
Kamati ya Maadili sasa si tu inapokea fomu na
kuzihifadhi, bali inafanya ukaguzi wa mali za viongozi na
kuzifuatilia. Kikwazo chao ni kupata rasilimali fedha. Hili
litazamwe zaidi. Pale inapoonekana kuna makosa yakimaadili wahusika hufikishwa kwenye Baraza la Maadili.
Sote tumeshuhudia kazi nzuri iliyofanywa na Baraza hilo
wakati wa sakata la Escrow. Bado kazi ya kuimarisha
Kamati ya Maadili kwa rasilimali fedha, vitendea kazi,
majengo ya ofisi na rasilimali watu haina budi kuendelezwa.
Muhimili wa Mahakama
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
28/104
28
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi cha miaka10 hii tumefanya jitihada
kubwa za kuimarisha mhimili wa Mahakama. Miongoni
mwa mambo mengine, tumefanya mambo muhimu kwa
madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa
jukumu lake la msingi la utoaji haki.
Kwanza, tumetenganisha shughuli za kutoa haki na za
utawala. Tumeunda Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya kushughulikia mambo ya fedha na utawala. Hivyo basi,
Wasajili wa Mahakama wanabaki na jukumu la kutoa haki.
Mpaka sasa mabadiliko haya yamekuwa ya manufaa
makubwa kwa Mahakama kwani yameboresha utekelezaji
wa majukumu katika Mahakama.Pili, tumeanzisha Mfuko
wa Mahakama ambao unaipa Mahakama uhuru katika
kuendesha shughuli zake. Sambamba na hilo tumeongeza
bajeti ya Mahakama kutokashilingi bilioni 36.6mwaka
2006/07 hadishilingi bilioni 87.6mwaka 2014/15. Jambo
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
29/104
29
linalohitaji kuboreshwa ni Hazina kutoa fedha kwa wakati ili
shughuli zifanyike kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Spika;
Jambo latatu,ni kwamba tumeongeza idadi ya Majaji
wa Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu Wakazi na
Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Lengo letu ni
kuongeza nguvukazi ya kusikiliza na kuamua mashauri.
Kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo
wameanza kuteuliwa watu wenye Shahada ya Sheria. Hivi
sasa itawawezesha watu wenye mashauri katika Mahakama
hizo kupata utetezi wa Mawakili. Kati ya mwaka 2005 na
2015 tumeongeza Majaji wa Rufani kutoka 8 mwaka 2005
hadi16, na Majaji wa Mahakama Kuu kutoka37 hadi81
katika kipindi hicho. Hali kadhalika, tumeongeza idadi ya
Majaji wanawake. Katika Mahakama ya Rufani wapo5na
katika Mahakama Kuu wapo32 na kufanya jumla yao kuwa
37. Hivi sasa tunao jumla ya Mahakimu Wakazi1,266 katika
ngazi zote za Mahakama. Kati ya hao534 sawa naasilimia
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
30/104
30
35 ni wanawake. Idadi ya Majaji na Mahakimu wanawake
hivi sasa ni kubwa kuliko wakati wowote uliopita.
Mheshimiwa Spika;
Kutokana na mipango mizuri iliyowekwa na Jaji Mkuu
Mohamed Chande Othman Mahakama zimepiga hatua
kubwa katika kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.
Majaji wamejiwekea malengo kwa kila Jaji asikilize na
kuamua mashauri yasiyopungua220 kwa mwaka na kila
Hakimu Mkazi mashauri250 na wale wa Mahakama ya
Mwanzo mashauri260 kwa mwaka. Kwa sababu hiyo,
kuanzia Julai, 2014 hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2015
yalifunguliwa mashauri177,586 na Mahakama ilisikiliza na
kuamua mashauri 179,962. Maana yake ni kuwa
zimesikilizwa zote na nyingine zilizobakia miaka ya nyuma.
Bila shaka kwa kasi hii sasa mrundikano wa kesi utabakia
kuwa historia katika kipindi kifupi kijacho. Nawapongeza
sana Majaji na Mahakimu kwa kazi nzuri waifanyayo.
Kwa upande wa ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu,
wamekamilisha ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu za
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
31/104
31
Divisheni ya Kazi pamoja na majengo ya Mahakama Kuu
Mikoa ya Shinyanga na Kagera. Aidha, majengo mawili ya
Mahakama za Wilaya na12 ya Mahakama za Mwanzo nayo
yamekamilika. Hivi sasa, ujenzi unaendelea wa majengo ya
Mahakama Kuu9 za mikoa iliyosalia, Mahakama za Wilaya
9 na za mwanzo25.
Maboresho ya Mfumo wa Utoaji Haki
Mheshimiwa Spika;
Jambo lingine ambalo tumefanya katika nia ya
kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na kupunguza malalamiko ya
wananchi na ucheleweshaji wa mashauri ni kutenganisha
kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na uendeshaji wamashtaka hayo Mahakamani. Polisi waliokuwa wanafanya
yote sasa watashughulikia upelelezi na ofisi ya Mkurugenzi
wa Mashtaka ndiyo inayoendesha mashauri. Tayari Ofisi za
Mkurugenzi wa Mashtaka zimekwishafunguliwa katika kila
Mkoa na sasa tunaenda wilayani. Aidha, tumeboresha Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa rasilimali watu,
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
32/104
32
vitendea kazi na fedha ili kuongeza ufanisi katika utendaji
wa ofisi hiyo muhimu sana. Kuna haja ya kuendelea
kuongezea rasilimali fedha na vitendea kazi ili ufanisi
uongezeke zaidi.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki, tumeimarisha Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora kwa kuiwezesha kwa nyenzo,
rasilimali fedha na watu. Tume sasa inafanya kazi katika
eneo lote la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kutokana na
utumiaji wa mfumo wa elektroniki malalamiko ya wananchi
mengi zaidi yanafikishwa kwenye Tume na mengiyanapatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, idadi ya malalamiko
yaliyowasilishwa Tume yameongezeka kutoka9,455mwaka
2006 hadi 25,921 mwaka 2014 na uwezo wa Tume
kushughulikia malalamiko kwa mwaka umeongezeka
kutoka malalamiko3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko
18,501 mwaka 2014.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
33/104
33
Utendaji Serikalini
Maeneo ya Utawala
Mheshimiwa Spika;
Kwa nia ya kusogeza huduma, mwaka 2010 tulianzisha
mikoa mipya4 ya Geita, Simiyu, Njombe na Katavina
wilaya mpya19. Pia,tulianzisha Halmashauri45, kata 1,432,
vijiji1,949, Mitaa1,379 na vitongoji8,777. Nimeamua
kuanzisha mkoa mpya wa Songwe kutoka mkoa wa Mbeya
na Wilayasita kama ifuatavyo: Tanganyika mkoani Katavi,
Kigamboni na Ubungo mkoani Dar es Salaam, Songwe
mkoani Mbeya, Kibiti mkoani Pwani na Malinyi mkoani
Morogoro. Najua tulikuwa na maombi mengi lakini kwasasa tufanye haya.
Maslahi ya Wafanyakazi
Mheshimiwa Spika;
Serikali ya Awamu ya Nne imelipa umuhimu wa juu
suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa Serikali. Karibu
kila mwaka tumekuwa tunaongeza kima cha chini cha
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
34/104
34
mshahara. Kwa sababu hiyo, kima cha chini cha mshahara
kimeongezeka kutokashilingi 65,000 mwaka 2005 hadi
shilingi 265,000 mwaka wa jana. Mwaka huu tumefikia
shilingi 300,000. Najua bado hakikidhi mahitaji lakini
ukilinganisha na tulikokuwa kipindi hiki tumeongeza sana
mishahara ya wafanyakazi. Vile vile, tumeendelea
kupunguza kodi ya mapato kwa mfululizo kutokaasilimia
18 mwaka 2005 hadiasilimia 11 mwaka huu. Dhamira yetu
ni kutaka kutoa nafuu zaidi kwa wafanyakazi. Vile vile,
tumewapandisha vyeo watumishi 233,876 na kulipa
malimbikizo ya watumishi422,348 ya kiasi chashilingi
bilioni 384.8. Mheshimiwa Spika;
Tumetekeleza sera ya ugatuaji wa madaraka kwa wilaya
jambo ambalo limelazimu kuongeza rasilimali fedha na watu
kwa Halmashauri za Wilaya na Miji. Kwa ajili hiyo ruzuku
kwa Halmashauri zetu imeongezeka kutokashilingi bilioni
780 mwaka 2005/2006 hadishillingi trilioni 4.69 mwaka
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
35/104
35
2015/2016. Aidha, tumeimarisha utumishi katika
Halmashauri kwa kuajiri watumishi wengi wa kada
mbalimbali.
Usawa wa kijinsia
Mheshimiwa Spika;
Mwaka 2005 niliahidi wakati wa kampeni na wakati wa
kuzindua Bunge la Tisa, kuwa tutaongeza ushiriki wa
wanawake katika shughuli na nyanja mbalimbali za maisha
ya watu wa nchi yetu ikiwemo nafasi za maamuzi. Ninyi na
mimi ni mashahidi kwamba tumetimiza ahadi hiyo. Idadi
ya Wabunge wanawake imeongezeka kutoka62mwaka 2005
hadi127.Hivi sasa hamsini kwa hamsini ni rasmi katikaKatiba Inayopendekezwa. Kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi yetu na Bunge letu tumepata Spika
mwanamke Mheshimiwa Anne Semamba Makinda.
Wanawake wameongezeka katika ngazi zote kuu za
uamuzi. Kwa mfano, tunao Mawaziri wanawake10, Naibu
Mawaziri wanawake5, Majaji wanawake37 na Wakuu wa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
36/104
36
Wilaya wanawake wako53. Kwa upande wa Makatibu
Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa,
Wakurugenzi Watendaji n.k. pia wameongezeka. Katika
elimu nako tuna usawa wa kijinsia kwa upande wa idadi ya
wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule za msingi na
sekondari. Katika vyuo vya elimu ya juu, idadi ya
wanafunzi wa kike imeongezeka kwa kasi kutoka10,039
mwaka 2005 hadi78,800 mwaka 2014.
Hali ya Uchumi
Mheshimiwa Spika;
Wakati ninaingia madarakani mwaka 2005 niliwaahidi
Watanzania wenzangu kuwa tutafanya kila tuwezalo
kujenga uchumi ulio imara na shirikishi. Hususan, nilisema
nitaendeleza sera za mageuzi ya kiuchumi na kuweka
misingi madhubuti ya kukuza uchumi, kuongeza ajira,
kuongeza Pato la Taifa na kupunguza umaskini. Katika
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
37/104
37
miaka kumi iliyopita tumeendelea kusimamia kwa kiwango
kizuri sera za uchumi jumla na sera za uchumi katika ngazi
ya chini zinazogusa wananchi wa kawaida.
Jitihada zetu hizo zimezaa matunda ya kutia moyo.
Katika kipindi hiki, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa
takriban asilimia 7. Nchi yetu ni miongoni mwa mataifa10
ya Afrika na20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa
kasi kubwa. Pato ghafi la Taifa limeongezeka zaidi ya mara
tatu kutokashilingi trilioni 14.1 mwaka 2005 hadi kufikia
trilioni 79.4mwaka 2014. Hivyo basi, pato la wastani la
Mtanzania nalo limeongezeka kutoka shilingi 441,030
mwaka 2005 hadishilingi 1,724,416 mwaka 2014. Mheshimiwa Spika;
Mauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za
Marekani bilioni 1.67 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani
bilioni 8.76 mwaka 2014 na kutunisha akiba yetu ya fedha
za kigeni na kutuwezesha kuagiza bidhaa na mahitaji ya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
38/104
38
nchi kutoka nje kwa kipindi cha miezi 4.1 kama
tulivyopanga. Mfumuko wa bei niasilimia 6.1.
Mheshimiwa Spika;
Kama mjuavyo, mwaka 2000 nchi yetu ilijiwekea Dira
ya Taifa ya Maendeleo ya hadi mwaka 2025. Mwaka 2010
tulitengeneza Mpango wa Muda Mrefu (Long Term
Perspective Plan) wa (2010 – 2025) wa kuongoza utekelezaji
wa Dira kwa miaka 15 iliyobaki. Tuligawa utekelezaji wake
katika Mipango mitatu ya Maendeleo ya Miaka Mitano kila
mmoja. Tuko katika hatua za mwisho za utekelezaji wa
Mpango wa Kwanza, (2011/12 – 2015/16) na kuandaa
mpango wa pili (2016/17 – 2021/22).Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
Mheshimiwa Spika;
Kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa Serikali
nilianzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Huu ni mfumo mpya wa kupanga, kufuatilia na kusimamia
utekelezaji wa malengo na shughuli za Serikali kwa nia ya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
39/104
39
kuhakikisha kuwa kilichokusudiwa kinafanyika, tena kwa
wakati. Tuliamua kuanza na sekta sita zaElimu, Nishati,
Kilimo, Uchukuzi, Maji na Mapato ya Serikali. Baadae
sekta ya afya na uboreshaji mazingira ya uwekezaji
ziliongezwa.
Katika kipindi hiki kifupi Mpango umethibitisha kuwa
wenye manufaa. Mambo katika sekta zilizojumuishwa katika
BRN yameanza kwenda vizuri. Changamoto yetu kubwa
imekuwa ni upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa wakati
kutoka Hazina. Kama changamoto hiyo isingekuwepo
mambo yangekuwa mazuri zaidi.
Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Spika;
Kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza
uchumi, kuzalisha ajira, kuongeza mapato na kupunguza
umaskini, Serikali yetu imekuwa inachukua hatua thabiti za
kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji wa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
40/104
40
ndani na nje kuchagua Tanzania kuwa nchi inayofaa
kuwekeza.
Mwaka 2010 tumetengeneza Sera na kutunga Sheria ya
Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public
Private Partnership—PPP). Lengo letu ni kuweka mazingira
mazuri kwa sekta binafsi kuvutika kushirikiana na Serikali
katika shughuli za kiuchumi na maendeleo. Faida kubwa ya
utaratibu huu ni kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwekeza
katika baadhi ya shughuli ambazo sekta binafsi inaweza
kubeba sehemu ya gharama. Hii siyo tu inaongeza kasi ya
maendeleo, bali kuiwezesha Serikali kuokoa fedha ambazo
inaweza kuzitumia kwa shughuli nyingine. Juhudi zetu za kuboresha mazingira ya uwekezaji
zinaendelea kuzaa matunda mema. Kati ya 2005 na 2014,
Kituo chetu cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi7,159
yenye thamani yaDola za Marekani bilioni 154.274. Kati ya
miradi hiyoasilimia 49.38 ni ya wawekezaji wa ndani,
asilimia 23.41 ni wawekezaji wa kutoka nje naasilimia 27.18
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
41/104
41
ni miradi ya ubia baina ya Watanzania na wawekezaji wa
kigeni. Ajira16,000 zilipatikana. Ukuaji huu wa uwekezaji
umeongeza mapato ya Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda na Biashara
Duniani (UNCTAD) ya mwaka 2015, Tanzania inaongoza
Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji. IlipataDola za
Marekani bilioni 2.142 sawa naasilimia 31.5 ya uwekezaji
wote katika Jumuiya yetu.
Sekta za Uzalishaji
Sekta ya Kilimo
Mheshimiwa Spika;Kuendeleza kilimo ilikuwa ni moja ya mambo
tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Shabaha yetu kuu ni kutaka
kuongeza tija ili uzalishaji uongezeke, wakulima wapate
mavuno mengi, masoko ya uhakika yawepo na bei iwe nzuri
ili mapato yao yaongezeke na umasikini uwapungukie. Vile
vile wao na taifa lijitosheleze kwa chakula.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
42/104
42
Kwa ajili hiyo mwaka 2006 tuliasisi Programu ya miaka
7 ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector
Development Programme—ASDP). Katika Programu hiyo,
matatizo yanayofanya tija na uzalishaji katika kilimo kuwa
mdogo yalitambuliwa na kutengenezewa mpango wa
kuyatatua. Serikali pia ilianzisha mikakati, programu na
mipango mingine ya kuongeza msukumo katika kuleta
mageuzi ya kilimo. Miongoni mwa hiyo ni mkakati wa
Kilimo Kwanza, Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika
Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mpango wa
Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP), Sera ya
Umwagiliaji tuliyoitunga mwaka 2010 na Programu yaMageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika.
Mheshimiwa Spika;
Pamoja na hayo, tumeongeza pia bajeti ya sekta ya
kilimo kutokashilingi bilioni 233.3 mwaka 2005/06 hadi
shilingi bilioni 1,084.7 mwaka 2014/15. Kuongezwa kwa
bajeti kumewezesha fedha za ruzuku ya mbolea na
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
43/104
43
pembejeo kuongezeka kutokashilingi bilioni 7.5mwaka
2005/06 hadishilingi bilioni 299.3 mwaka 2013/14.
Matrekta makubwa na madogo yameongezeka kutoka7,491
mwaka 2005 hadi16,412 mwaka 2014. Kwa sababu hiyo
matumizi ya jembe la mkono yamepungua kutokaasilimia
70 hadiasilimia 62. Tumeongeza maafisa ugani kutoka 3,379
mwaka 2005 hadi7,974 mwaka 2014.
Vituo vya utafiti wa kilimo tumeviongezea rasilimali
fedha, watu na vitendea kazi. Aidha, tumeanza safari ya
kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na kuhusisha sekta
binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika
kuzalisha mbegu. Aidha, tumeimarisha Wakala wa Mbegu(Agricultural Seed Agency – ASA) na kuongeza uzalishaji wa
mbegu bora kutoka tani10,477.17 mwaka 2005 hadi tani
32,340mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
Juhudi za Serikali kuendeleza kilimo zimezaa matunda
mazuri. Tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
44/104
44
chakula imeongezeka. Kwa upande wa mazao ya chakula
uzalishaji umeongezeka kutoka tanimilioni 9.66 mwaka
2005 hadi tanimilioni 16.01 mwaka 2014. Ongezeko hili
limeliwezesha taifa letu kujitosheleza kwa chakula kwa
asilimia 125 mwaka 2014 ikilinganishwa naasilimia 95
mwaka 2005. Uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara
umeongezeka toka tani427,738 mwaka 2005 hadi tani
569,054mwaka 2014 na uzalishaji wa mbegu za mafuta
umeongezeka karibu ya mara4 toka tani1,389.9 mwaka 2005
hadi tani5,545.6mwaka 2014. Aidha, uzalishaji wa matunda
nao umeongezeka toka tanimilioni 1.2mwaka 2005 hadi
tani milioni 4.4mwaka 2014 na maua toka tani5,862 haditani10,790.
Mheshimiwa Spika;
Upatikanaji wa masoko ya uhakika na bei nzuri kwa
mazao ya wakulima bado ni changamoto. Pia kuna tatizo la
upungufu wa maghala ya kuhifadhi mazao. Jitihada
zinaendelea kupata mkopo au wabia wa kujenga maghala ya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
45/104
45
kisasa nchi nzima. Programu ya Mageuzi na
Modenaizesheni ya Ushiriki ilianzishwa ili kutatua tatizo la
masoko. Aidha, tumeanza maandalizi ya kuanzisha soko la
bidhaa (Commodity Market Exchange) kwa nia hiyo hiyo.
Naamini misingi mizuri tuliyoijenga pamoja na kuenea kwa
SACCOS na kuanza kwa Benki ya Kilimo ikiendelezwa itatoa
mchango mkubwa katika kuongeza kasi ya mapinduzi ya
kilimo.
Mifugo
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa mifugo, dhamira yetu ilikuwa kuanzasafari ya kuleta mageuzi katika sekta hii. Safari hiyo
tumeianza kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya
Mifugo. Changamoto zinazochangia maendeleo duni ya
sekta hii zimeainishwa na kutengenezewa mkakati wa
utekelezaji. Katika kipindi hiki malambo1,008, majosho
2,364na maabara104za mifugo zimejengwa. Visima virefu
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
46/104
46
101 vimechimbwa, malambo 370 na majosho 499
yamekarabatiwa katika kipindi hiki cha miaka10.
Ukarabati na ujenzi wa majosho umeongeza idadi
kutoka 2,177 mwaka 2006 hadi3,637 mwaka 2015.
Tumeongeza Maofisa Ugani kutoka2,270 mwaka 2005 hadi
6,041 mwaka 2014. Kuhusu uhamilishaji, tumeongeza vituo
kutoka kituo1 mwaka 2005 hadi vituo8mwaka 2015 na
kuwezesha ng’ombe955,360 kuhamilishwa katika miaka 10
hii.
Mheshimiwa Spika;
Mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi
tuliyoyajenga yamewezesha viwanda vya kusindika nyama,maziwa na vyakula vya mifugo kuongezeka. Viwanda vya
kusindika maziwa vimeongezeka kutoka22 mwaka 2005
hadi74 mwaka 2015. Viwanda vya kuzalisha vyakula vya
mifugo vimeongezeka kutoka viwanda6mwaka 2005 hadi
80mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tanimilioni
1.4za vyakula hivyo kwa mwaka. Aidha viwanda na
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
47/104
47
machinjio ya kisasa9 vimejengwa katika kipindi hiki.
Usindikaji wa ngozi pia umeongezeka kutoka vipande
790,000mwaka 2005 hadi vipandemilioni 3.78 mwaka 2014.
Hivi sasa kwa mfano, uzalishaji wa malisho ya mifugo (hei)
umefikia marobota957,860 ikilinganishwa na marobota
178,100 mwaka 2005.
Safari yetu ya kuanza kuondoka kwenye uchungaji
kwenda kwenye ufugaji imeanza. Vijiji vingi vimeandaa
mipango ya matumizi bora ya ardhi na hivyo vimetenga
maeneo ya kilimo na ya ufugaji. Tuendelee kuhimiza vijiji
vyetu kutekeleza mipango hiyo ili wafugaji wapate maeneo
ya malisho mbali na mazao ya wakulima. Pia, tuhimizeuhamilishaji kama mlango wa kuingilia kwenye kuboresha
kosafu za mifugo yetu.
Uvuvi
Mheshimiwa Spika;
Wakati nazindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005
nilisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
48/104
48
kwenye kuendeleza sekta ya uvuvi. Katika kutekeleza hayo
tumefanya yafuatayo.Kwanza, nimeunda Wizara mpya ya
Mifugo na Uvuvi.Pili, tulifuta kodi ya zana za uvuvi ili
kuwawezesha wavuvi kupata zana bora na za kisasa kwa bei
nafuu zaidi.Tatu, tumeimarisha vyuo vya uvuvi na hivi sasa
vina uwezo wa kudahili wanafunzi1,215 ikilinganishwa na
wanafunzi 127 mwaka 2005. Hii imetuwezesha kuongeza
wagani wa uvuvi kutoka103 mwaka 2005 hadi540 mwaka
2014.Nne, tumeongeza sana juhudi za kupambana na uvuvi
haramu ili kutunza mazingira, mazalia ya samaki na kuzuia
kuvuliwa au kuuawa kwa samaki wadogo.
Tumeimarisha maabara ya Taifa ya Samaki paleNyegezi kwa vifaa vya kisasa na wataalamu ili iende na
wakati.Tano, tumeongeza msukumo wa kuhimiza ufugaji
wa samaki na kuwezesha mashamba ya samaki kuongezeka
kutoka13, 011 mwaka 2005 hadi20, 325 mwaka 2014.
Uvuvi haramu unapungua. Mapato ya sekta ya uvuvi
yameongezeka kutokashilingi bilioni 351.6 mwaka 2005
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
49/104
49
hadishilingi trilioni 1.8 mwaka 2013.Bado tuna kazi kubwa
ya kufanya katika sekta hii ili kuongeza tija na mapato ya
wavuvi na taifa.
Utalii
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa utalii, tumeendelea na jitihada za
kuiendeleza sekta hii muhimu. Tumeongeza kutangaza
vivutio vya utalii vya nchi yetu katika masoko makubwa
duniani. Sekta ya utalii imekua kwa wastani waasilimia 7.1
na imechangiaasilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.
Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii612, 754mwaka
2005 hadi watalii1,140,156 mwaka 2014. Idadi ya vitandakatika mahoteli imeongezeka kutoka15,828 hadi21,929.
Mapato pia yameongezeka kutoka Dola za Marekani
milioni 823.05 mwaka 2005 hadiDola za Marekani bilioni 2
mwaka 2014. Ajira za moja kwa moja zimeongezeka kutoka
32,673 hadi686,130 na zisizokuwa za moja kwa moja kutoka
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
50/104
50
165,883 hadi1,318,109. Haya ni mafanikio makubwa na ya
kujivunia.
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumekabiliana na tukio kubwa la
ujangili wa wanyamapori hasa wa ndovu kutokana na
kushamiri kwa biashara ya meno ya ndovu na bei kuwa
kubwa katika nchi za Mashariki ya Mbali. Vuguvugu la
ujangili lilifikia kiwango cha kutishia kumaliza ndovu nchini
na dunia nzima. Tukaamua kuchukua hatua za kuidhibiti
hali hiyo. Tumefanya operesheni tatu kukabiliana na tishio
hili. Yakwanza, iliendeshwa na Idara ya Wanyamapori na
Misitu wakishirikiana na TANAPA na NgorongoroConservation Area. Hii hasa ilihusu kupambana na ujangili
katika hifadhi na mapori ya Kaskazini mwa Tanzania.
Mafanikio makubwa yalipatikana.
Mheshimiwa Spika;
Operesheni yapili ni ile iliyohusisha Jeshi la Polisi
katika hifadhi na sehemu nyingine za Tanzania. Operesheni
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
51/104
51
Kipepeo kama ilivyoitwa nayo ilipata mafanikio. Na yatatu,
Operesheni Tokomeza iliyohusisha vyombo vyote vya ulinzi
na usalama. Pamoja na changamoto zake operesheni hizi
zimesaidia sana kupunguza kasi ya ujangili nchini. Matokeo
yake katika sensa ya ndovu iliyofanyika mara ya mwisho,
ukiacha Ruaha, hali katika hifadhi na mapori mengine ina
muelekeo mzuri.
Kuundwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA)
yenye mamlaka makubwa zaidi ya kusimamia sekta ya
wanyamapori nako kutaimarisha uhifadhi na mapambano
ya ujangili. Kwa mipango na program zilizopo Wizarani,
naamini mambo yatakuwa mazuri zaidi muda si mrefu.Viwanda
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka kumi hii, sekta ya viwanda imeendelea
kukua kwa kasi nzuri ya kutia moyo. Viwanda vikubwa, vya
kati na vidogo vimeongezeka kutoka11, 544 mwaka 2005
hadi viwanda51,224mwaka 2015. Kati ya mwaka 2005 na
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
52/104
52
2014 na miradi751 imepewa leseni za kudumu na BRELA ya
kuanzisha viwanda. Mchango wa sekta ya viwanda katika
Pato la Taifa umefikiaasilimia 7.3 mwaka 2014 kutoka
asilimia 6.8mwaka 2005. Mchango wa viwanda kwenye
mauzo ya nje umeongezeka kutokaasilimia 9.3 mwaka 2005
hadiasilimia 23.3 mwaka 2014.
Tunategemea ukuaji mkubwa wa viwanda katika
Mpango wa Pili wa maendeleo wa miaka5 kutokana na
misingi imara tuliyoijenga katika Mpango wa Kwanza.
Ujenzi wa kiwanda cha chuma kule Liganga na makaa ya
mawe cha Mchuchuma, unatarajiwa kuanza mwaka huu na
kiwanda cha kuchakata gesi pale Lindi unatarajiwa kuanza baada ya taratibu za kuwapatia ardhi zitakapokamilika.
Hivi ni viwanda vya msingi na mama ambavyo vitachochea
kasi ya ukuaji wa viwanda nchini na uchumi kwa jumla.
Madini
Mheshimiwa Spika ;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
53/104
53
Sekta ya Madini ndiyo ya pili baada ya utalii kwa
kuingiza fedha nyingi za kigeni. Kama nilivyoahidi, tulipitia
upya sera, sheria na mikataba ya madini iliyokuwepo na
kutengeneza sera na sheria mpya. Halikadhalika,
tulianzisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ambayo
hatimaye yalizaa marekebisho ya mikataba yao na hivyo
kuboresha maslahi ya taifa.
Kufuatia marekebisho hayo, makampuni husika ya
madini yanalipa kodi ya mapato. Bila ya hivyo huenda
mpaka leo yangekuwa hayajaanza kulipa kodi. Kutumika
kwa Sheria mpya ya Madini, viwango vipya vya mrahaba na
kupunguzwa kwa misamaha ya kodi vimeongeza mapato yaSerikali. Aidha, tuliunda Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA) ambao umewezesha kukagua mahesabu
ya migodi kuhusu uwekezaji na mauzo ya madini na
kuwawezesha TRA kutoza kodi stahiki kutoka kwa
makampuni hayo.
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
54/104
54
Mabadiliko haya pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji
katika sekta hii yamewezesha mchango wa sekta ya madini
katika Pato la Taifa kuongezeka kutokaasilimia 2.9 mwaka
2005 hadi kufikiaasilimia 3.5mwaka 2014. Thamani ya
mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka kutokaDola
za Marekani milioni 655.5 mwaka 2005 hadi kufikiaDola za
Marekani bilioni 1.794 mwezi Desemba 2014. Mambo
yangekuwa mazuri zaidi kama bei ya dhahabu isingeshuka
katika kipindi hiki.
Mheshimiwa Spika;
Serikali ilifanya uamuzi wa kulifufua na kuliwezeshaShirika letu la Madini (STAMICO) kuanza tena kazi ya
utafutaji na uchimbaji wa madini kupitia kampuni zake
tanzu. STAMICO kwa kupitia kampuni yake ya
STAMIGOLD imeanza kuzalisha dhahabu na kuuza nje.
Vilevile, tumejiunga na Mpango wa Uwazi wa Uvunaji wa
Maliasili (EITI) ambao umesaidia sana katika kuongeza
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
55/104
55
uwazi katika biashara ya madini na kusaidia katika
ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye makampuni ya
madini.
Katika kipindi hiki, migodi mitatu mipya ilianzishwa
nayo ni Migodi ya dhahabu wa Buzwagi (Shinyanga) na
New Luika (Mbeya) na mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka
(Ruvuma). Aidha, miradi mikubwa mingine 8
imeendelezwa na kufikia hatua ya kuanzisha mgodi
ukiwemo Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma), Mradi wa
Chuma Liganga na Mradi wa Makaa ya Mawe wa
Mchuchuma (Njombe). Pia, ajira rasmi kwenye migodi
mikubwa nchini imeongezeka kutoka waajiriwa 3,517mwaka 2005 hadi waajiriwa15,000 mwaka 2014. Hali
kadhalika, makampuni ya madini yameongeza unununzi wa
bidhaa na huduma hapa nchini (local procurement) kutoka
Dola za Marekani milioni 230.41mwaka 2005 hadiDola za
Marekani milioni 536.56 mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
56/104
56
Katika kipindi hiki pia, tumetengamaeneo 8 kwa ajili
ya wachimbaji wadogowadogo. Maeneo haya yamewezesha
wachimbaji wadogo kuchimba madini bila bughudha.
Aidha, Wizara imenunua mitambo miwili kwa ajili ya
uchorongaji wa miamba kusaidia utafiti wa madini kwa ajili
ya wachimbaji wadogo. Tumeanzisha mfuko wa
kuwakopesha wachimbaji wadogo pale Wizarani ili kutoa
fursa kwa wachimbaji wadogo kupata mikopo ya
kuendeleza shughuli zao.
Nishati
Mheshimiwa Spika;Wakati naanza kazi ya uongozi wa nchi yetu, Tanzania
ilikuwa inakabiliwa na ukame mkubwa uliosababisha
upungufu mkubwa wa chakula. Pia kulikuwa na upungufu
mkubwa wa umeme kwa sababu ya mabwawa ya kuzalisha
umeme kukosa maji ya kutosha. Serikali ililazimika kulisha
watu zaidi ya milioni3,776,000 na kukodisha mitambo ya
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
57/104
57
kuzalisha umeme. Kwa siku za usoni tuliamua kuchukua
hatua thabiti ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa
kutumia gesi asilia na vyanzo vingine kama vile makaa ya
mawe, mionzi ya jua na upepo.
Ujenzi umekamilika wa bomba la kusafirisha gesi
kutoka Mtwara na Songo Songo litakaloongeza kiasi cha gesi
kuja Dar es Salaam na kuwezesha uzalishaji wamegawati
3000 za umeme. Wakati huo huo kazi ya kujenga vituo vya
kufua umeme inaendelea pale Kinyerezi, Dar es Salaam.
Umeme huo utakidhi mahitaji ya umeme sasa na miaka
kadhaa ijayo.
Mheshimiwa Spika; Katika kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme Vijijini
(REA) ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri ya
kusambaza umeme kwa vijiji5,336 kati ya vijiji12,423 nchini.
Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa na ile ya
mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata umeme
kutokaasilimia 10 hadiasilimia 40 mwaka 2015. Uamuzi
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
58/104
58
uliofanywa katika Bajeti ya mwaka huu wa kukusanya fedha
kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta ya petroli,
utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini.
Gesi Asilia
Mheshimiwa Spika;
Tumepata mafanikio katika utafutaji wa mafuta na gesi
asilia. Kuanzia mwaka 2010 nchi yetu imepata bahati ya
ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi bahari kuu. Mpaka sasa
zimegundulika futi za ujazotrilioni 47.08.Ukijumlisha na
futi za ujazotrilioni 8 zilizogunduliwa takriban miaka 40
iliyopita kule Songo Songo na Msimbati jumla ya rasilimali
ya gesi asilia nchini ni futi za ujazotrilioni 55.08. Kazi yautafutaji inaendelea na wataalamu wanasema kuwa
Tanzania inaweza kuwa na akiba ya futi za ujazotrilioni 200.
Kiasi cha gesi kilichogunduliwa mpaka sasa ni kikubwa na
kufanya Tanzania kuwa mahala papya pa kuipatia dunia
nishati hii.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
59/104
59
Gesi asilia tuliyonayo ikisimamiwa na kutumiwa vizuri
itaiwezesha nchi yetu na watu wake kupata maendeleo
makubwa na kuondokana na umaskini. Ni fursa ya aina
yake ya kuipatia Serikali mapato makubwa na kuiwezesha
kutimiza kwa uhakika majukumu yake na mipango yake.
Lakini, ili hayo yaweze kufanyika hapana budi pawepo
usimamizi mzuri wa hatua zote muhimu za mnyororo wa
thamani: yaani utafutaji, uchimbaji, usafirishaji, uuzaji wa
gesi asilia na matumizi yake nchini kama nishati na mali
ghafi ya viwanda upande mmoja. Upande mwingine
inategemea sana matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na
rasilimali hiyo. Mheshimiwa Spika;
Ni kutokana na kutaka kuhakikisha kwamba mambo
yanakuwa hivyo ndiyo maana tumetunga Sera ya Gesi Asilia
na kuwasilisha katika Bunge hili ile Miswada miwili yaani
wa Sheria ya Petroli na ule wa Matumizi ya Mapato ya
Mafuta na Gesi. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
60/104
60
kuipitisha Miswada hii nami nitaitia saini mara
nitakapoletewa.
Usafirishaji na Uchukuzi
Barabara
Mheshimiwa Spika;
Serikali ya Awamu ya Nne, imetoa kipaumbele cha juu
kwa uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji na
uchukuzi nchini. Hii ni pamoja na barabara, reli, bandari,
usafiri wa majini na usafiri wa angani. Tumeendeleza kazi
ya kuongeza mtandao wa barabara za lami nchini kwa
mafanikio makubwa. Karibu barabara kuu zote nchini na
zile zinazounganisha mikoa zimekamilika kujengwa au kaziya ujenzi inaendelea. Kwa sababu hiyo hivi leo kutokea po
pote nchini kwenda Dar es salaam unafika siku hiyo hiyo,
tofauti na ilivyokuwa zamani watu walichukua zaidi ya siku
moja. Adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu wa
Mikoa ya Ziwa tumeimaliza.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
61/104
61
Katika mkakati wetu wa kupanua mtandao wa
barabara za lami nchini, tulitambua barabara za urefu wa
kilomita 11,474 za kujengwa kwa kiwango cha lami. Baadae
tuliongeza barabara nyingine na kufikishakilomita 17,742
katika mpango huo. Utekelezaji wake upo katika hatua
mbalimbali. Tayari ujenzi wakilomita 5,568 kwa upande wa
barabara kuu nakilomita 535kwa barabara za mijini
umekamilika. Ujenzi wa kilomita 3,873 unaendelea.
Upembuzi yakinifu na usanifu umekamilika kwa barabara
za urefu wakilometa 4,965 kinachosubiriwa ni kupatikana
fedha ujenzi uanze. Baadhi ya barabara hizo zimo katika
bajeti ya mwaka huu wa fedha. Barabara za urefu wakilometa 3,336 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu
wa kina.
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki pia, madaraja madogo7,200 na
makubwa12 yamejengwa na mengine16 yapo katika hatua
mbalimbali za ujenzi. Miongoni mwa madaraja makubwa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
62/104
62
yaliyokamilika ni daraja la Mto Malagalasi na yanayojengwa
ni daraja la Kigamboni na lile la Mto Kilombero. Madaraja
haya yalikuwa miongoni mwa matano yaliyopangwa
kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa
Miaka Mitano mara baada ya uhuru. Madaraja mawili yaani
la Kirumi lilijengwa mwaka 1985 na la Rufiji mwaka 2003.
Kwa upande wa vivuko, tumeongeza vipya15 na kufikisha
idadi ya28 kote nchini mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
Tumeongeza sana fedha katika mfuko wa barabarakutokashilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/06 hadishilingi
bilioni 866.63 mwaka 2015/16. Hii itasaidia katika
matengenezo ya barabara za lami tulizojenga na kujenga
nyingine mijini. Hali kadhalika itatumika kuimarisha
barabara za udongo na changarawe wilayani na vijijini
ziweze kupitika wakati wote. Katika kipindi hiki barabara
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
63/104
63
za changarawe zimeongezeka kutokakilometa 9,424hadi
kilometa 22,089.
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka kumi hii idadi ya vyombo vya moto yaani
magari, bajaji na pikipiki imeongezeka kutoka1,696,088
mwaka 2005 hadi3,313,254 hivi sasa. Ongezeko hili
linalotokana na hali ya kiuchumi ya watu wengi kuwa nzuri
limezua tatizo la msongamano wa magari katika miji mingi
nchini. Katika jiji la Dar es Salaam ambako tatizo ni kubwa
zaidi na Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali
kupunguza ukali wake. Tunapanua ukubwa wa baadhi ya
barabara, kujenga barabara za mzunguko (ring roads) nasasa tunaanza ujenzi wa barabara za juu ya nyingine
(flyovers). Tulianzisha matumizi ya treni katika reli za
TAZARA na TRC kusafirisha abiria. Hivi sasa reli hizo
zinasafirisha abiriamilioni 2,804,269 kwa mwaka ambao
wangehitaji daladala 253 kwa siku. Mpango mkubwa wa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
64/104
64
kuendeleza matumizi ya reli, Dar es Salaam umeandaliwa na
tumeanza kuutafutia fedha.
Usafiri wa Reli
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumetumia muda mwingi kutafuta
ufumbuzi wa matatizo yanayozikabili reli zetu za TAZARA
na TRC. Kimsingi reli hizo zimekuwa zinakabiliwa na
matatizo ya uchakavu wa miundombinu na uongozi na
uendeshaji usioridhisha. Kwa sababu ya matatizo hayo reli
hizi ambazo kila moja inaweza kusafirisha tanimilioni 5
kwa mwaka zinasafirisha kati yatani 200,000 na300,000tu.
Hivyo basi, mizigo mingi husafirishwa kwa barabara nakutishia uhai wa barabara ambazo tumezijenga kwa
gharama kubwa.
Kwa upande wa reli ya kati, uboreshaji wa reli kati ya
Dar es Salaam na Tabora unakaribia kukamilika na
utaendelea mpaka Kigoma na Mwanza. Wakati huo huo
mchakato wa ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
65/104
65
(standard gauge) unaendelea. Ujenzi unaweza kuanza
mwaka huu kutegemea kukamilika kwa majadiliano na
mabenki yaliyoonyesha utayari wa kutukopesha pesa za
ujenzi.
Mheshimiwa Spika;
Azma yetu ya kufufua reli ya TAZARA nayo
tumeiwekea mkakati. Sisi na Zambia tumekubaliana
kushirikiana kwa karibu katika kutafuta ufumbuzi wa
matatizo yanayoikabili reli yetu hiyo. Bahati nzuri marafiki
zetu wa China nao wamekubali kutusaidia katika mipango
yetu hiyo. Ni matumaini yangu kuwa safari hii tutapata
ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo yanayoathiri ufanisi wareli hii yenye umuhimu wa aina yake kwa uhai na ustawi wa
uchumi wa nchi zetu na watu wake.
Bandari
Mheshimiwa Spika;
Tumeboresha na kuimarisha huduma katika bandari ya
Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa. Mwaka 2014
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
66/104
66
bandari yetu ilihudumiatani milioni 14.4 ukilinganisha na
tani milioni 6.7 mwaka 2005. Mwaka huu inaweza kufikia
tanimilioni 18. Siku hizi huduma hutolewa kwasaa 24 na
kasi ya kupakua, kupakia na kutoa mizigo imeongezeka
sana na wizi umepungua sana. Hata wale walioacha
kuitumia bandari yetu wameanza kurudi.
Mheshimiwa Spika;
Kuanza kutumika kwa mfumo wa Single Custom’s
Territoryunaorahisisha upakuaji na upakiaji mizigo ya nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki kumeongeza zaidi ufanisi.
Tuko katika majadiliano na DRC na Zambia ambao nao
wameonyesha nia ya kuingia katika mfumo huu.Kuongezeka kwa usafirishaji wa mizigo inayopita
nchini kuna faida kwani sekta ya usafirishaji inachangia
zaidi yaasilimia 15 ya pato la taifa. Hali kadhalika, ujenzi
wa gati za 13 na14 katika bandari ya Dar es Salaam
unaotegemewa kuanza mwezi huu utawezesha huduma ya
makasha kuongezeka kutoka makasha600,000 hadi makasha
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
67/104
67
1,200,000. Mipango ya kuboresha bandari za Mtwara, Tanga
na zile zilizo kwenye Maziwa yetu makuu na ujenzi wa
bandari ya Bagamoyo zitaiwezesha Tanzania kunufaika na
fursa ya jiografia yake.
Usafiri wa Anga
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumefanya jitihada kubwa ya
kuwekeza kwenye ukarabati, upanuzi na ujenzi wa viwanja
vya ndege nchini. Tumekarabati Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao umeongeza uwezo
wa kuhudumia kutoka ndege7 hadi30 hivi sasa. Aidha
tunajenga jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo lenyeuwezo wa kuhudumia abiriamilioni 3.5. Ujenzi huo
unategemewa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kukamilika kwake kutauwezesha uwanja wa Kimataifa wa
Julius Nyerere kuhudumia abiriamilioni 6na ndege nyingi
zikiwemo ndege kubwa za kisasa za Airbus 380.
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
68/104
68
Vile vile, tumeufanyia ukarabati na upanuzi Uwanja wa
Kimataifa wa Kilimanjaro ambao ni muhimu sana kwa sekta
ya utalii ya ukanda wa kaskazini. Uwanja mpya wa ndege
wa Songwe kule Mbeya umekamilika na hivi sasa
unatumika. Hali kadhalika, tumeviboresha upya viwanja
vya ndege vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora,
Mwanza na Bukoba.
Ujenzi, upanuzi na ukarabati huu tulioufanya,
umechangia sana katika ongezeko kubwa la safari za ndege
na abiria nchini. Safari za ndege kuja nchini zimeongezeka
toka safari78 mwaka 2005 zilizokuwa zinatolewa na
kampuni 29 za usafiri wa ndege hadi safari175 zinazotolewana kampuni55mwaka 2014. Aidha, abiria wanaoondoka na
kuwasili katika viwanja vya ndege wameongezeka kutoka
2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria4,670,380mwaka 2013.
Siku hizi Watanzania wanaopanda ndege wanaongezeka
kwa kasi kubwa.
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
69/104
69
Jambo ambalo hatukuweza kufanikiwa ni lile la
kufufua Shirika letu la Ndege. Tumefanikiwa kulifanya lisife
lakini hatukuweza kulihuisha lirejee hata kwenye ile hali
yake ya zamani. Hata hivyo, fikra na mawazo kuhusu
mkakati wa kulijenga upya shirika hilo yapo. Kwa sasa
Menejimenti imepewa jukumu la kuandaa mpango wa
biashara unaoeleweka na unaokopesheka, kisha Serikali
itaona namna ya kulisaidia shirika.
Utabiri wa Hali ya Hewa
Mheshimiwa Spika;Sambamba na hayo, tumeboresha huduma za utabiri
wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa imepatiwa vifaa
vipya ambavyo vimeongeza ufanisi na usahihi wa utabiri
unaotolewa. Mwezi Februari 2014 Mamlaka hiyo ilipata cheti
cha utoaji wa huduma bora cha ISO na hivyo kuufanya
taarifa zake kutambuliwa kimataifa.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
70/104
70
Mawasiliano
Mheshimiwa Spika;
Tumepiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia ya
habari na mawasiliano. Tumejenga Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano wenye urefu wakilometa 7,560 unaounganisha
miji mikuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara isipokuwa mkoa
mpya wa Simiyu. Kwa Mikoa ya Unguja na Pemba, ujenzi
wake utakamilika mwezi ujao. Katika Awamu ya Pili, Mkoa
wa Simiyu na wilaya zote nchini zitaunganishwa.
Ujenzi wa mkongo huu umechangia katika kuongeza
ubora na kasi ya mawasiliano, na kushusha gharama za
mawasiliano. Kwa mfano, gharama za kupiga simuzimeshukakutoka shilingi 115 kwa dakika mwaka 2005
hadishilingi 34.92 mwaka 2014 na gharama za intaneti
zimeshuka kutoka wastani washilingi 36,000 kwa Gigabyte
moja mwaka 2005 hadi wastani washilingi 9,000 kwa
Gigabyte moja (GB 1) mwaka 2014. Hii imeshusha pia
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
71/104
71
gharama za biashara kwa kurahisisha mawasiliano na
malipo kati ya mabenki na kwa njia ya mtandao na simu.
Kwa upande wa laini za simu, zimeongezeka kutoka
lainimilioni 2.96mwaka 2005 hadimilioni 28mwaka 2014.
Watu wanaotumia intaneti wameongezeka tokamilioni 1.6
hadimilioni 9.3mwaka 2014. Kukua kwa mawasilino ya
simu kumewezesha watumiajimilioni 12.3 kupata huduma
ya fedha kupitia simu za mkononi. Kati ya Julai 2013 na
Aprili 2014 jumla ya miamalamilioni 972.6 ilifanyika yenye
thamani yashilingi trilioni 28. Huu ni wastani wa zaidi ya
shilingi trilioni 2 kwa mwezi na kufanya Tanzania
kuongoza duniani kwa huduma hii. Mheshimiwa Spika;
Tulitambua kuwa makampuni binafsi ya simu
hayapendi kuwekeza vijijini ambako biashara si kubwa kama
mijini. Kwa kutambua umuhimu wa huduma ya
mawasiliano kwa maendeleo, Serikali iliamua ibebe mzigo
huo. Kwa sababu hiyo tumeanzisha Mfuko wa Mawasiliano
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
72/104
72
kwa Wote (UCSAF) ambao utawezesha kata na vijiji vyote
nchini kufikiwa na huduma za mawasiliano. Mfuko huo
umekwisha wezesha jumla ya kata52 na vijiji314kufikiwa
na huduma hizo. Upelekaji wa huduma za mawasiliano
kupitia Mfuko huo zinaendelea kwa kata nyingine163 zenye
vijiji922, ambapo wananchimilioni 1.2 watanufaika.
Mheshimiwa Spika;
Tumechukua hatua ya kuhakikisha kuwa mianya ya
kodi inazibwa na kwamba makampuni yanalipa kodi stahiki
kwa kununua na kufunga mtambo wa Kusimamia
Mawasiliano ya simu nchini. Mtambo huo unaowezesha
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kukusanya takwimu halisiza mawasiliano yanayofanywa. Tangu kuanza kutumika kwa
mtambo huo, mwaka jana Serikali imeweza kukusanya
shilingi bilioni 24.6 ambazo vinginevyo zisingepatikana.
Aidha, tumekuwa nchi ya kwanza Afrika ya Mashariki
kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali. Karibu
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
73/104
73
tutakamilisha kwa mikoa yote. Tunazipokea nchi kadhaa
zinazokuja kujifunza kwetu juu ya uendeshaji wa zoezi hili.
Ardhi na Makazi
Mheshimiwa Spika;
Maisha bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na
kuboresha makazi ya watu. Sote tunafahamu kuwa makazi
ni hitajio la msingi la binadamu. Lengo letu la kuboresha
huduma za ardhi, nyumba na makazi limepata mafanikio
makubwa. Tumepeleka huduma za utawala wa ardhi karibu
zaidi na wananchi kwa kuanzisha Kanda nane za kusimamia
upangaji, upimaji na utoaji hatimiliki. Uamuzi huu
umepunguza lile tatizo la watu kuchelewa kupata hatimiliki. Toka 2006 hadi sasa jumla ya hati164,275zimetolewa,
vijiji10,500 vimepimwa na kati yake vijiji10,341 vimepatiwa
hatimiliki.
Mheshimiwa Spika;
Tumetunga Sheria kwa ajili ya kuwezesha upatatikanaji
wa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba. Sheria hizo ni
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
74/104
74
pamoja na Sheria ya Mikopo ya Nyumba (Mortage Finance)
na Sheria ya Kutambua Milki ya Sehemu ya jengo haswa
kwenye maghorofa (Unit Tittles Act) ya mwaka 2008. Sheria
hizi kwa ujumla wake zimewezesha watu wengi zaidi
kupata mikopo ya kujenga au kukarabati nyumba zao na
kuwawezesha watu kupata umiliki wa sehemu ya jengo.
Mabadiliko hayo pia yamewezesha sekta ya nyumba
kukua kwa kasi kubwa na majengo na nyumba za kisasa
kujengwa katika kipindi cha miaka 10 hii. Dar es Salaam ya
leo na ile ya 2005 ni tofauti kabisa. Shirika la Nyumba la
Taifa, Wakala wa Nyumba za Serikali, Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii nayo imefanya uwekezaji mkubwa sana katika ujenziwa nyumba katika kipindi hiki.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa watumishi wa serikali kuwa na
nyumba mwaka 2008 tulianzisha Mfuko wa Mkopo kwa
watumishi wa umma ambao hadi sasa umetoa mikopo ya
shilingi bilioni 5.4 kwa watumishi1,169. Pia, tumeanzisha
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
75/104
75
Kampuni ya Mikopo ya Nyumba kwa ajili ya watumishi wa
umma ambayo tayari imeanza kazi.
Mheshimiwa Spika;
Ninayo furaha kueleza kuwa makazi ya wananchi pia
yameendelea kuwa bora. Takwimu za Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka 2012, inaonyesha kuwa idadi ya nyumba
zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutokaasilimia 46
mwaka 2002 hadiasilimia 65 mwaka 2012. Kwa lugha
nyingine nyumba zilizoezekwa makuti na nyasi zimezidi
kupungua. Haya ni mafanikio makubwa ya kutia moyo na
hatua muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania.
Utafiti Mheshimiwa Spika;
Jambo lingine ambalo tumeliwekea msingi mzuri ni
eneo la utafiti. Hili ndilo eneo ambalo ilitalivusha taifa letu
kwenda katika maendeleo makubwa zaidi. Niliamua Serikali
ichukue hatua za makusudi za kufufua shughuli za utafiti
ambazo zilikuwa zinapita katika kipindi kigumu. Niliamua
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
76/104
76
kuwa Serikali ianze safari ya kutenga fedha za kutosha kwa
ajili ya utafiti. Tulianza nashilingi bilioni 10na kuendelea
kuongeza mwaka hadi mwaka na kufikashilingi bilioni 60
mwaka 2014, katika kipindi cha kujitahidi kufikiaasilimia 1
ya bajeti ya Serikali na hatimayeasilimia 1 ya pato la Taifa
kwa ajili ya shughuli za utafiti.
Mheshimiwa Spika;
Kwa kutumia kiasi hiki kidogo kilichopo wanasayansi
wetu 344 wamepata ufadhili wa masomo ya shahada ya
Uzamili na173 wa shahada ya Uzamivu. Miradi70 ya utafiti
imefadhiliwa, kati ya hiyo22 ni ya kilimo. Fedha hizi pia
zimewezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojiakuanzisha viatamizi vya teknohama ambavyo vimewezesha
vijana wetu kubuni na kuvumbua teknolojia zenye manufaa
kwa maendeleo ya jamii na taifa. Wamezalisha ajira na
kunufaisha watu wengi. Kampuni ya Max Malipo ni mfano
mmojawapo mzuri wa matokeo mazuri ya viatamizi hivi.
Huduma za Jamii
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
77/104
77
Elimu
Mheshimiwa Spika;
Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa mwaka
2005 nilisema kuwa, “ Hakuna Taifa lililopata maendeleo
bila kuendeleza elimu. Hivyo kuendeleza elimu nchini
itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Nne”.
Tumetimiza ahadi. Katika kipindi chote cha miaka kumi
bajeti ya sekta ya elimu ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko za
sekta nyingine zote. Mwaka huu 2015 bajeti ya elimu
imefikiashilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa nashilingi
bilioni 669.5 za mwaka 2005.
Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani
ya miaka 10 hii ni ya kutia moyo. Tumeongeza shule za
msingi kutoka14,257 mwaka 2005 hadi16,538 mwaka 2015
na wanafunzi wameongezeka kutoka 7,541,208 hadi
8,202,892. Upanuzi huu umewezeshaasilimia 98 ya watoto
wanostahili kupata elimu ya msingi sasa kuandikishwa.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
78/104
78
Kwa kushirikiana na wananchi na sekta binafsi
tumeongeza Shule za Sekondari kutoka Shule1,745 mwaka
2005 hadi Shule4,753mwaka 2015. Idadi ya wanafunzi
imeongezeka kutoka524,325 mwaka 2005 hadi1,804,056
mwaka 2015. Katika kipindi hiki pia vyuo vya Ufundi
vimeongezeka kutoka184mwaka 2005 hadi 744 mwaka 2015
na wanafunzi katika vyuo hivyo wameongezeka kutoka
40,059 hadi145,511 mwaka 2015. Haya ni mafanikio
makubwa sana.
Kwa nia ya kuongeza ubora wa elimu, tumechukua
hatua thabiti za kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu,
vitabu, maabara za sayansi na vifaa vya kujifunzia nakufundishia. Tumepanua mafunzo ya ualimu wa Cheti,
Stashahada na Shahada. Hii imetuwezesha kuongeza idadi
ya walimu wa Shule za Msingi kutoka135,013 mwaka 2005
hadi202,752 mwaka 2015, na walimu wa Shule za Sekondari
kutoka18,754 mwaka 2005 hadi88,908 mwaka 2015. Uhaba
wa walimu wa masomo ya sanaa si tatizo tena, tunao wa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
79/104
79
kutosha. Tuna upungufu wa walimu20,141wa masomo wa
sayansi na hisabati. Ninaamini, hata hivyo, kwa programu
za kusomesha walimu wa sayansi vyuoni zilizopo, katika
miaka michache ijayo tatizo hili nalo tutalipatia ufumbuzi.
Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dodoma, mwaka 2014
kimeanza kudahili wanafunzi5,000 wa ualimu wa masomo
ya sayansi.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa maabara za sayansi, katika shule za
sekondari za kata tayari maabara5,979 zimejengwa na
nyingine4,410ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Hivi sasa tunashughulikia upatikanaji na usambazaji wavifaa kwa matumizi ya maabara hizo. Kwa upande wa
vitabu tumeweza kuboresha upatikanaji wake kwa
mwanafunzi wa Shule za Msingi kutoka uwiano wa1:5
mwaka 2005 hadi1:3 mwaka 2015. Katika shule za sekondari
uwiano ni1:2ukilinganisha na 1:8 mwaka 2005.
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
80/104
80
Katika kipindi hiki pia tumeshuhudia upanuzi
mkubwa wa elimu ya juu nchini. Idadi ya vyuo vikuu
imeongezeka kutoka vyuo26 mwaka 2005 hadi52 mwaka
2015. Miongoni mwa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha
Dodoma na cha Nelson Mandela cha Arusha ambavyo
vimejengwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Tumeanza
mchakato wa kujenga Chuo Kikuu cha Julius Nyerere cha
Kilimo kule Butiama. Vyuo hivi ni fahari ya nchi yetu kwani
tumevijenga kwa fedha zetu wenyewe bila msaada kutoka
kwa wafadhili. Ongezeko la vyuo vikuu limefanya idadi ya
wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi40,719 mwaka
2005 hadi218,959mwaka 2014. Idadi ya wanafunziwanaonufaika na mikopo nayo imeongezeka kutoka
wanafunzi16,345 mwaka 2005 hadi wanafunzi99,590
mwaka huu.
Afya
Mheshimiwa Spika;
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
81/104
81
Tumepata mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa
kuboresha na kupanua huduma ya afya nchini. Tuliazimia
kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi watu kwa
kujenga vituo vya kutoa huduma ya afya vipya na
kuimarisha vilivyopo. Kati ya mwaka 2005 na 2014 vituo vya
kutolea huduma za afya2,175 vimejengwa. Kati yake
hospitali19, vituo vya afya 168 na zahanati1,883
zimejengwa.
Tumeimarisha hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa na Wilaya kwa
kuzipatia vifaa vya tiba na uchunguzi (MRI, CT Scan, X ray,
Ultra Sounds, Maabara n.k). Tumejenga maabara ya Taifa yaAfya ya Jamii ambayo inatumika kama maabara ya
Kimataifa ya Rufaa kwa nchi za SADC. Tumeimarisha
maabara za mikoa kwa majengo na vifaa vya kisasa vya
uchunguzi wa magonjwa. Maabara yetu ya Mbeya sasa ina
uwezo wa kubaini virusi vya Ebola jambo ambalo miezi
michache iliyopita tulikuwa tunapeleka sampuli Nairobi.
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
82/104
82
Hivi sasa hospitali za wilaya zinaweza kufanya uchunguzi
wa mwenendo wa figo na ini.
Mheshimiwa Spika;
Tumeboresha huduma ya Afya ya Kinywa katika
Hospitali ya Muhimbili kwa kufunga mashine26 za kisasa
za tiba ya meno na maabara ya kisasa ya kutengeneza meno
bandia. Pia tumeimarisha huduma ya afya ya kinywa kwa
kuweka vifaa vya tiba ya meno kwenye Halmashuri91. Hivi
sasa hospitali136, vituo vya afya63 na zahanati3 zinatoa
huduma hiyo nchini.
Tumeanza kupata mafanikio katika dhamira yetu ya
kujenga uwezo wetu wa ndani wa kuchunguza na kutibumaradhi ya figo, moyo, saratani na mishipa ya fahamu
ambayo tumekuwa tunapeleka wagonjwa wengi nje. Kwa
mfano, tangu Taasisi ya Moyo ianze kutoa huduma pale
Muhimbili wagonjwa 71,963 wamepatiwa matibabu
wakiwemo 692 waliofanyiwa upasuaji. Watu hao
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
83/104
83
wangepelekwa nje taifa lingelipa pesa nyingi. Uwezo wetu
utaongezeka sana hospitali ya Mloganzila itakapokamilika.
Mheshimiwa Spika;
Tumebadilisha utaratibu wa kusambaza dawa kutoka
Bohari ya Dawa. Tumeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba
kutokashilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadishilingi
bilioni 147 mwaka 2014. Idadi ya watu wanaonufaika na
Mfuko wa Afya ya Jamii na Mfuko wa Bima ya Afya
wameongezeka kutokaasilimia 3 mwaka 2005 hadiasilimia
19 mwaka 2014.
Katika kipindi hiki tumetoa msukumo mkubwa katika
kupambana na maradhi makubwa ya kuambukizayanayosababisha vifo vya watu wengi. Tumeendesha
kampeni ya kupambana na malaria nchi nzima kwa
kubadilisha dawa ya kutibu malaria na kugawa vyandarua
26,371329 kwa watoto chini ya miaka mitano, kwa akina
mama wajawazito na katika kila kaya. Aidha, tumepulizia
dawa ya kuua mbu ndani ya nyumba katika mikoa ya kanda
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
84/104
84
ya ziwa. Matokeo ya jitihada hizo ni kupungua kwa
maambukizi ya malaria kwaasilimia 51 na vifo kwa
asilimia 71. Baada ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua
viluwiluwi vya mbu pale Kibaha kuanza uzalishaji, safari ya
kutokomeza malaria hapa nchini ni ya uhakika.
Mheshimiwa Spika;
Juhudi zetu katika kupambana na ukimwi
zimewezesha kushuka kwa maambukizi ya ukimwi kutoka
asilimia 7.7mwaka2005 hadiasilimia 5.1 mwaka 2012.
Idadi ya watu waliopima virusi vya ukimwi imeongezeka
kutoka365,189 mwaka 2005 hadi25,468,564mwaka 2014.
Aidha, tumewezesha vituo5,244na asilimia 97 ya vituovyote vinavyotoa huduma ya uzazi kutoa huduma ya kuzia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mheshimiwa Spika;
Kati ya mwaka 2005 na 2014 tumeongeza udahili wa
wanafunzi katika vyuo vya afya kutoka3,025 mwaka 2005
hadi11,807 mwaka 2014. Katika kipindi hicho wataalamu wa
-
8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc
85/104
85
afya55,608 wameajiriwa. Aidha, tumeongeza ajira ya kada
mbalimbali za afya. Kwa sababu hiyo idadi ya madaktari
imeongezeka kutoka madaktari1,048 mwaka 2006 hadi
madaktari2,325 mwaka 2014. Halikadhalika, madaktari
wasaidizi wameongezeka kutoka1,223 hadi1,914, wauguzi
kutoka15,961hadi22,942 wataalamu wa Maabara kutoka
1,277 hadi2,378 mwaka 2014. Hivi sasa uwiano wa Daktari
kwa wagonjwa ni 1:6,666ikilinganishwa na 1:35,714 mwaka
2005. Na, uwiano wa Muuguzi kwa wagonjwa umeshuka
kutoka1:2,347 mwaka 2005 hadi1:2,008 mwaka huu.
Mheshimiwa Spika;
Tumeendesha kampeni ya kub