hotuba ya mhe wka uzinduzi wa bodi.pdf

7
1 HOTUBA YA MHE. GAUDENTIA KABAKA (MB), WAZIRI WA KAZI NA AJIRA KWENYE UZINDUZI WA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KATIKA UKUMBI WA WIZARA YA KAZI NA AJIRA TAREHE 4 SEPTEMBA, 2015 Bw. Eric Shitindi, Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira; Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti, Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi; Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi; Wakuu wa Idara na Vitengo hapa Wizarani Wizarani; Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA); Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF); Mwakilishi, Shirika la Kazi Duniani (ILO); Mwakilishi, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE); Mwakilishi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA); Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana; Habari za asubuhi!

Upload: ngabwe

Post on 25-Jan-2016

3.883 views

Category:

Documents


10 download

TRANSCRIPT

Page 1: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

1

HOTUBA YA MHE. GAUDENTIA KABAKA (MB), WAZIRI WA KAZI NA

AJIRA KWENYE UZINDUZI WA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA

FIDIA KWA WAFANYAKAZI KATIKA UKUMBI WA WIZARA YA KAZI

NA AJIRA TAREHE 4 SEPTEMBA, 2015

Bw. Eric Shitindi, Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira;

Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti, Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa

Fidia kwa Wafanyakazi;

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi;

Wakuu wa Idara na Vitengo hapa Wizarani Wizarani;

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya

Jamii (SSRA);

Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Fidia kwa

Wafanyakazi (WCF);

Mwakilishi, Shirika la Kazi Duniani (ILO);

Mwakilishi, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE);

Mwakilishi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA);

Wageni waalikwa;

Mabibi na Mabwana;

Habari za asubuhi!

Page 2: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

2

1. Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa

Rehema kwa kutujaalia uzima, nguvu na afya njema kwa kutuwezesha

kukutana hapa leo katika siku hii muhimu.

Aidha,napenda nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa

heshima kubwa mliyonipa ya kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika hafla

hii ya Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa

Wafanyakazi.

Pia, nitumie nafasi hii, kutoa pole kwako Mwenyekiti na kwa

Wajumbe wote kwa kufiwa na mmoja wenu aliyekuwa Mjumbe wa

Bodi ya Wadhamini ya ya Mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi

Marehemu Bw. Henry Nyamubi. Mungu amlaze mahala pema

peponi Amina.

2. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Napenda pia nitumie fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwako

wewe Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi ya Wadhanini ya

Mfuko wa Fidia kwa kuteuliwa kwenu kuwa wasimamizi wa shughuli za

Mfuko huu. Ninazo taarifa kwamba, pamoja na Uzinduzi kutokufanyika

kwa wakati, lakini kwa kutambua umuhimu, wa majukumu ya Bodi hii,

tayari mlikwishaanza utekelezaji wa majukumu yenu. Ninawapongeza

sana!

3. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008, imetungwa

kutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kupitwa na wakati kwa

Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 iliyotungwa toka Mwaka

Page 3: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

3

1949 na kufanyiwa marekebisho mengi hivyo kuleta ugumu katika

utekelezaji. Aidha, mafao yanayotolewa chini ya Sheria hii ya zamani ni

machache na viwango vya malipo ya Fidia ni vidogo sana na hivyo

kutokukidhi mahitaji ya sasa ya wafanyakazi pindi wanapoumia, kuugua

ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.

4. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Kuundwa kwa Mfuko wa Fidia ni hatua muhimu sana kwa nchi yetu

katika kupanua wigo wa Hifadhi ya Jamii nchini. Ujio wa Sheria Mpya ya

Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008 ni mkombozi si kwa

wafanyakazi pekee, bali hata kwa waajiri na Wananchi kwa ujumla. Hii

ni kutokana na sababu kwamba, kupitia Sheria Mpya ya Fidia kwa

Wafanyakazi, idadi ya mafao imeongezeka, viwango vya malipo Fidia

kwa wafanyakazi na wategemezi wao vitaboreshwa, na hata utaratibu

wa kushughulikia madai ya Fidia utaboreshwa. Tunatarajia kwamba

hata mchakato wa kufuatilia na kulipa fidia utakuwa rahisi na wa muda

mfupi zaidi kuliko ilivyo sasa.

5. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Kazi kubwa niliyopewa kwa siku ya leo ni kuzindua Bodi ya Wadhamini

ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, lakini naomba nitumie fursa hii

kueleza yafuatayo;

Page 4: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

4

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi imeundwa kwa

mujibu wa matakwa ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Fidia kwa

Wafanyakazi, Na. 20 ya Mwaka 2008, na inajumuisha wajumbe kutoka

Serikalini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Vyama vya

Wafanyakazi, Vyama vya Waajiri, OSHA, Benki Kuu, Taasisi za Elimu

ya Juu, pamoja na wawakilishi kutoka kwa watu wenye ulemavu

unaotokana na ajali ama magonjwa yanayotokana na kazi.

6. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Katibu Mkuu ameelezea kwa kifupi madhumuni ya kuanzisha Mfuko wa

Fidia pamoja na majukumu ya Mfuko. Mimi najielekeza kwenye

majukumu ya Bodi ya Wadhamini. Majukumu ya Bodi ya Wadhamini ya

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi yameainishwa bayana katika kifungu

cha 13 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na. 20 ya Mwaka 2008.

Majukumu hayo ni pamoja na:

(i) Kusimamia uendeshaji wa shughuli za Mfuko;

(ii) Kutengeneza, kutekeleza na kupitia Sera zinazohusiana na

Fidia kwa wafanyakazi kulingana na matakwa ya Sheria;

(iii) Kumshauri Mhe. Waziri wa Kazi kuhusu maswala yote

yanayohusu Fidia kwa wafanyakazi, marekebisho ya sheria ya

fidia kwa wafanyakazi , kanuni ama sheria nyingine

zinazohusiana na Sheria hii;

(iv) Kukuza mbinu za kuzuia ajali na magonjwa katika sehemu za

kazi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Afya na Usalama mahala

pa kazi (OSHA);

Page 5: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

5

(v) Kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa mwajiri, mfanyakazi na

wategemezi wao.

7. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Majukumu haya ni makubwa na muhimu sana kwa ustawi wa Mfuko.

Hivyo nina matumaini makubwa kwamba, mtatekeleza majukumu hayo

na mengine ambayo sikuyataja lakini yameelezwa katika Sheria husika

ili kuhakikisha kwamba, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unakidhi

matarajio ya wadau na kuleta tija na mahusiano mazuri sehemu za kazi.

Hamkuchaguliwa kuwa Wajumbe kwa bahati mbaya isipokuwa

tulizingatia sana sifa mlizonazo pamoja na uzoefu wenu. Hivyo,

tunaimani na nyinyi kwamba mtatumia weredi wenu kwa uadilifu katika

kutekeleza majukumu yenu.

8. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Taasisi mnayosimamia ni Sehemu ya Wizara ya Kazi na Ajira. Hivyo

nitumie nafasi hii kuwakaribisha sana kwenye familia ya Taasisi zilizo

chini ya Wizara ya Kazi na Ajira. Taasisi nyingine ambazo ziko chini ya

Wizara ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya

Jamii (SSRA), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Tija la Taifa

(NIP), Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), Wakala

wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) na Tume ya Usuluhishi na

Uamuzi (CMA), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Page 6: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

6

Ni matarajio yangu mtatekeleza majukumu yetu kwa Ushirikiano wa

karibu na Wizara pamoja na Taasisi nyingine kwa kuzingatia Sera,

Sheria, Kanuni na mikakati ya Wizara.

9. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Nafahamu kwamba zipo changamoto nyingi ambazo mfuko utakabiliana

nazo hasa katika siku hizi za mwanzoni. Changamoto hizo ni pamoja na

uelewa mdogo wa jamii kuhusu Mfuko huu, zoezi la kuwasajili waajiri

wote wa sekta ya Umma na binafsi Tanzania Bara na uendelevu wa

mfuko. Serikali kwa kushirikiana na wadau tutaendelea kuzikabili

changamoto hizo hatua kwa hatua ili kuhakikisha kwamba malengo

yaliyokusudiwa yanafikiwa.

Kazi kubwa iliyo mbele yenu ni kuhakikisha elimu na uhamasishaji

unafanyika ili kuwezesha wafanyakazi na Waajiri wengi wanashiriki na

kujiunga na mfuko huu.

10. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Kwa kumalizia napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa

maandalizi makubwa yaliyowezesha kufanikisha hafla hii, na

Page 7: HOTUBA YA MHE WKA UZINDUZI WA BODI.pdf

7

ninawashukuru wote mlioshiriki kwa namna moja ama nyingine

katika uzinduzi huu.

Baada ya kusema hayo machache, ninayo heshima kubwa kutamka

kwamba, BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA FIDIA KWA

WAFANYAKAZI imezinduliwa rasmi.

Asanteni kwa kunisikiliza