hotuba ya mheshimiwa dr. jakaya mrisho kikwete, rais … · 2015-07-10 · ya ccm na cuf na baina...

104
1 HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE, DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015 Mheshimiwa Spika; Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa. Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini, shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari

Upload: others

Post on 06-Feb-2020

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

1

HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO

KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA

TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA

KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA

MUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE,

DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015

Mheshimiwa Spika;

Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu

mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha

kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu

na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi

imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.

Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia

nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze

kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini,

shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na

shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi

rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari

Page 2: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

2

mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama

salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari

hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika

uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza

kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa

kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake

wakipewa nafasi wanaweza.

Mheshimiwa Spika;

Niruhusu pia nitoe shukrani na pongezi zangu za dhati

kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kazi kubwa na nzuri

mliyoifanya. Mmetimiza ipasavyo wajibu wao wa Kikatiba

wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawashukuru

kwa ushirikiano wenu na msaada wenu. Ni ukweli ulio

wazi kuwa bila ya ninyi Wabunge wetu na Bunge hili,

tusingeweza kupata mafaniko na maendeleo tuliyoyapata.

Mmejijengea, nyinyi wenyewe na Bunge letu heshima

kubwa mbele ya wananchi. Mmeitendea haki demokrasia

Page 3: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

3

ya Tanzania na kuliletea heshima kubwa Bunge letu nchini,

kikanda na kimataifa.

Mheshimiwa Spika;

Tarehe 30 Desemba 2005 nilipozindua Bunge la Tisa

nilielezea mtazamo wangu kuhusu nchi yetu na kutaja

majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali ya Awamu

ya Nne. Nilisema tutatekeleza wajibu wetu na vipaumbele

hivyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Tarehe 16

Julai, 2010 wakati wa kuvunja Bunge hilo nilielezea

mafanikio tuliyopata na changamoto zilizotukabili katika

kipindi hicho. Tarehe 28 Novemba, 2010 wakati wa

kuzindua Bunge hili la Kumi niliainisha vipaumbele vya

Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kipindi changu cha

pili cha uongozi wa nchi yetu na kuahidi kuvitekeleza kwa

ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Kama ilivyo ada, leo

tunafikia mwisho wa uhai wa Bunge la Kumi, naomba

kutumia fursa hii kutoa mrejesho wa utekelezaji wa

Page 4: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

4

majukumu ya Serikali na yale mambo ambayo tuliahidi na

kupanga kufanya.

Umoja, Amani na Usalama

Mheshimiwa Spika;

Niliahidi kuwa katika kipindi cha uongozi wangu

nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa Tanzania

inaendelea kuwa nchi moja na watu wake wanaendelea

kuwa wamoja, wanaopendana na kushirikiana licha ya

tofauti zao za rangi, dini, makabila, mahali watokako, na

ufuasi wa vyama vya siasa. Pia, kwamba nchi yetu

itaendelea kuwa yenye amani, usalama na utulivu.

Leo tunapoagana, ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa

Tanzania na Watanzania tumebakia kuwa wamoja. Hata

hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na matukio ya hapa

na pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi

yetu na watu wake. Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta

chuki baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, baina ya

Page 5: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

5

Wakristo na Waislamu na baina ya maeneo fulani ya nchi na

wengine.

Bahati nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa

Serikali zetu mbili wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja

na ushirikiano na viongozi wa dini na wa jamii na uelewa

wa wananchi, vimeliwezesha taifa letu kushinda

changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi

zimethibitisha ubora wa mazungumzo. Ni kweli kabisa

kwamba wanaozungumza hawagombani na

wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.

Mheshimiwa Spika;

Niruhusuni, nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara

nyingine viongozi wakuu wenzangu, Makamu wa Rais, Rais

wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu

wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais

Zanzibar, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchi

wote kwa ushindi tulioupata katika kudumisha umoja wetu.

Hata hivyo, tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa

Page 6: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

6

kwani watu wenye nia mbaya kwa nchi yetu au na umoja

wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba hawajafaulu.

Huenda wakajaribu tena. Tunachotakiwa kufanya ni

kuendelea kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.

Muungano Wetu Umeimarika Zaidi

Mheshimiwa Spika;

Nafurahi kwamba namaliza kipindi changu cha

uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na kuuimarisha

Muungano wetu adhimu na adimu Barani Afrika.

Mtakumbuka kuwa katika hotuba yangu ya kufungua

Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa viongozi wa pande

zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi

wa Muungano wetu. Nafurahi kwamba jambo hili

limefanyika chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais,

akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara

na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamu

yangu ya kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika

awamu hii.

Page 7: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

7

Mafanikio yaliyopatikana ni makubwa. Masuala

mbalimbali ya zamani na mapya yamezungumzwa,

yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa mfano,

hadi mwaka 2005 zilikuwa zimebakia kero 13 za Muungano

zilizoainishwa na Tume ya Shelukindo, hivi sasa zimebaki

kero nne. Tayari ufumbuzi wa kero moja unakamilishwa

kiutawala na tatu zimeshughulikiwa kwa ukamilifu katika

Katiba Inayopendekezwa. Kama kura ya maoni ingekuwa

imefanyika na Katiba hiyo kupitishwa kungekuwa hakuna

kiporo cha kero za Tume ya Shelukindo. Lakini kwa vile

kura ya maoni haijafanyika ndiyo maana tunaendelea

kuzitaja. Hata hivyo, Serikali zetu mbili zimezungumza na

kukubaliana tutafute njia ya kumaliza suala la rasilimali ya

mafuta na gesi. Ndiyo maana katika Muswada wa Petroli

hoja ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ya kusimamia

uchimbaji wa mafuta na kumiliki mapato yake ilijumuishwa.

Natoa shukrani nyingi kwa Bunge lako tukufu kwa

Page 8: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

8

kupitisha Muswada huo. Moja ya kero kubwa katika

Muungano tumeimaliza.

Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar

Mheshimiwa Spika;

Mtakumbuka kuwa nilizungumzia kusononeshwa

kwangu na mpasuko wa kisiasa uliokuwepo Zanzibar

wakati ule na kuelezea utayari wangu wa kusaidia

kuuondoa. Kama mjuavyo mazungumzo yalifanyika ndani

ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka

ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na

mpasuko wa kisiasa ukawa umepatiwa tiba. Matokeo ya

yote hayo ni kuwa mazingira ya kisiasa na kijamii

yamekuwa bora zaidi siku hizi kuliko ilivyokuwa kabla ya

hapo.

Ni matumaini yangu kuwa ndugu zetu wa Zanzibar

watayadumisha mafanikio haya ili waendelee kuishi kwa

Page 9: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

9

amani, upendo na udugu. Natambua kuwepo kwa

changamoto za hapa na pale katika uendeshaji wa Serikali

hiyo. Jambo linalonipa faraja ni kuwa matatizo yenyewe

hayahusu muundo wa Serikali bali yanaletwa na watu

kupishana kauli au kutofautiana katika uendeshaji wa

baadhi ya mambo. Mimi naamini hayo ni mambo

yanayoweza kumalizwa kwa wadau kukaa kitako na

kuzungumza kama ilivyokuwa kabla ya muafaka.

Amani na Usalama

Mheshimiwa Spika;

Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama kwa sababu

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea

kutimiza ipasavyo jukumu lake la kulinda uhuru na mipaka

ya nchi yetu. Katika kipindi hiki tumewekeza sana katika

kuliimarisha Jeshi letu kwa vifaa na zana za kisasa za kivita

na mafunzo. Tumeimarisha Kamandi za Nchi Kavu, Anga

na Majini. Utayari kivita wa jeshi letu ni mzuri tena wa hali

ya juu. Weledi na nidhamu ya Wanajeshi wetu ni ya hali ya

Page 10: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

10

juu. Tumeboresha maslahi na makazi ya wanajeshi kwa

kujenga nyumba mpya za kuishi. Utekelezaji wa mpango wa

kuwajengea nyumba 10,000 unaendelea vizuri. Hadi hivi

sasa nyumba 6,064 zinaendelea kujengwa nchi nzima na kati

yake nyumba 3,096 zimekamilika. Namaliza kipindi changu

cha kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na

Usalama kwa kujiamini kwamba “Tupo vizuri”. Pamoja na

hayo kazi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka 15 wa

kuimarisha JWTZ lazima iendelezwe ili kulifikisha Jeshi letu

pale tulipopakusudia.

Mheshimiwa Spika;

Katika miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa ya

kupambana na uhalifu ili kulinda usalama wa maisha na

mali za watu waishio Tanzania. Mtakumbuka kuwa mwaka

2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi

ya ujambazi. Niliahidi wakati wa kampeni na katika hotuba

yangu Bungeni kwamba hatutawaacha majambazi

waendelee kutamba. Hali ile imedhibitiwa. Ingawaje

Page 11: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

11

matukio ya ujambazi hayajaisha, lakini hayako kama

ilivyokuwa wakati ule.

Hali kadhalika, matukio ya uhalifu wa kuwania mali

yamepungua kutoka 53,268 mwaka 2005 hadi 43,808 mwaka

2014. Natoa pongezi nyingi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi

kubwa na nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kufanya.

Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za

barabarani. Lazima tuendelee kuzitafutia muarobaini wake.

Niruhusuni niwatambue na kuwashukuru Inspekta Jenerali

(mstaafu) Omari Mahita, Inspekta Jenerali (mstaafu) Said

Mwema na Inspekta Jenerali Ernest Mangu aliyepo sasa kwa

uongozi wao mzuri.

Mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali

katika utakelezaji wa mpango wa maboresho ya Jeshi la

Polisi uliobuniwa wakati wa uongozi wa Ndugu Saidi

Mwema, IGP mstaafu. Jeshi la Polisi linaendelea

kuwezeshwa kwa zana, vifaa na mafunzo. Taratibu

Page 12: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

12

zimekamilika za kulipatia Jeshi hilo magari ya kutosha ili

kuongeza ufanisi.

Pia, tumeendelea kuboresha maslahi na mazingira ya

kuishi Maafisa na Askari. Kwa ajili hiyo tumekarabati

baadhi ya nyumba zilizopo, tumejenga nyumba kadhaa

mpya za ghorofa, za kawaida na mabweni. Mipango

imekamilika ya kuwezesha ujenzi wa nyumba 10,000

ambazo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa

nyumba za kuishi katika Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Spika;

Jeshi letu la Magereza nalo limeendelea kutekeleza

vizuri majukumu yake ya kulinda wafungwa na

kurekebisha tabia zao. Aidha, huduma za malazi, mavazi,

chakula na usafiri kwa wafungwa zimeendelea kuboreshwa.

Changamoto kubwa ni msongamano wa wafungwa

Magerezani. Naamini mipango ya kujenga magereza mapya

na kupanua yaliyopo ikitekelezwa tatizo litaisha. Aidha,

mpango wa maboresho ya Jeshi la Magereza ukikamilika na

Page 13: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

13

kutekelezwa, utaboresha mazingira ya kufanyia kazi na

kuishi maafisa na askari, hivyo kupandisha morali wao na

kuongeza ufanisi.

Jeshi la Kujenga Taifa

Mheshimiwa Spika;

Ahadi yangu ya kuanzisha upya utaratibu wa

kuchukua vijana wa mujibu wa Sheria katika Jeshi la

Kujenga Taifa imetimia. Mpaka hivi sasa vijana 38,200

wamekwisha hitimu mafunzo hayo wakiwemo

Waheshimiwa Wabunge. Nawapongeza sana Waheshimiwa

Wabunge walioshiriki kwa kuongoza kwa mfano. Imesaidia

sana utaratibu huo kuanza upya bila vipingamizi. Ni

matumaini yangu kuwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ulinzi

na Jeshi la Kujenga Taifa watakaa pamoja kujadili namna ya

kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zilizopo. Naamini

zinaweza kumalizwa, vijana wetu wakashiriki mafunzo bila

matatizo yoyote.

Page 14: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

14

Utawala Bora

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi cha miaka kumi hii tumetekeleza

dhamira yetu ya kujenga na kuimarisha utawala bora kwa

sera, sheria, mifumo, taasisi na kwa rasilimali watu.

Tumefanya hivyo katika maeneo yote muhimu yakiwemo

yale yahusuyo haki za binadamu, demokrasia, mapambano

dhidi ya rushwa, maadili ya viongozi, ukusanyaji wa

mapato na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na

mgawano wa madaraka hati ya mihimili.

Bunge la Jamhuri ya Muungano

Mheshimiwa Spika;

Serikali imetimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili

mkuu wa dola wa Kutunga Sheria. Tulianzisha Mfuko wa

Bunge na kuongeza fedha katika bajeti ya Bunge toka

shilingi bilioni 30.58 mwaka 2005/06 hadi shilingi bilioni

173.76 mwaka 2015/16. Pia tumeanzisha Mfuko wa Jimbo ili

Page 15: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

15

kuwawezesheni Wabunge kuchangia katika kutatua

changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi wa

majimbo yao. Bunge letu limetekeleza ipasavyo majukumu

yake kupitia Kamati zake za kudumu na pale ilipolazimu

Kamati teule zilizoundwa.

Katika kipindi hiki miswada 163 imepitishwa, maswali

ya msingi 7,544 na ya nyongeza 22,632 yameulizwa na

kujibiwa. Kamati teule 2 ziliundwa. Haya ni mafanikio

makubwa kwa Bunge letu. Bunge hili limefanya kazi kubwa

na kazi ya kutukuka. Michango na ushauri wake umekuwa

chachu ya baadhi ya hatua na mabadiliko ya kisera, kisheria

na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali. Kwa kweli

mnastahili pongezi nyingi. Huwezi kutaja mafanikio ya

Serikali ya Awamu ya Nne bila kutambua mchango wa

Bunge hili.

Mchakato wa Katiba

Mheshimiwa Spika;

Page 16: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

16

Kama sote tujuavyo, kupitia Sheria iliyotungwa na

Bunge hili, mwaka 2013 tulianzisha mchakato wa

Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuipatia nchi yetu Katiba

mpya iliyo bora zaidi kuliko iliyopo sasa. Nafurahi kwamba

mchakato huo ulituwezesha kupata Katiba

Inayopendekezwa ambayo imekidhi matarajio hayo.

Narudia kutoa pongezi za dhati kwa Tume ya Mabadiliko

ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na

nzuri waliyofanya. Hatua iliyobaki ni Kura ya Maoni

ambapo sote tunasubiri maelekezo ya Tume ya Uchaguzi.

Mimi naamini iwapo itapitishwa, Katiba Inayopendekezwa

itaimarisha zaidi taifa letu.

Vyama vya Siasa

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki tumeshuhudia vyama vya siasa

vikiendelea kuimarika na kujijenga nchini. Idadi ya vyama

vya siasa imeongezeka kutoka 18 hadi 24. Vyama vya siasa

vimefanya shughuli zake kwa uhuru. Viongozi na

Page 17: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

17

wanachama wao wamefanya mikutano mingi na hata

maandamano kote nchini. Baraza la Vyama vya Siasa na

TCD vimekuwa vyombo muhimu vilivyofanya kazi nzuri ya

kujenga ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.

Yamekuwa majukwaa muhimu ya mashauriano baina ya

vyama vya siasa kwa masuala mbalimbali. Matatizo na

changamoto nyingi zimeweza kupatiwa ufumbuzi. Ni

matumaini yangu kuwa vyombo hivi viwili vitaendelezwa

na kuimarishwa miaka ijayo.

Huu ni mwaka wa Uchaguzi, na vyama vya siasa ndiyo

wahusika wakuu. Ni matumaini yangu kuwa vyama vya

siasa vitaheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi. Hii

itasaidia kuwepo kwa utulivu na amani katika mchakato wa

uchaguzi.

Uchaguzi Mkuu

Mheshimiwa Spika;

Habari kubwa hapa nchini sasa ni uchaguzi mkuu.

Tayari Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na ile ya Zanzibar

Page 18: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

18

(ZEC) zimekwisha tangaza tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwa ni

siku ya kufanyika uchaguzi mkuu. Maandalizi ya uchaguzi

huo yanaendelea vizuri. Tume ya Taifa ya Uchaguzi

inaendelea na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa

mfumo mpya wa teknolojia ya Biometric Voters Register

(BVR). Hadi sasa zoezi la uandikishaji limekamilika katika

mikoa 13 na linaendelea katika mikoa 11 na katika mkoa wa

Dar es Salaam na Zanzibar uandikishaji unategemea kuanza

mwezi huu. Kwa taarifa za Tume ya Uchaguzi, tayari

wamekwisha andikisha hadi sasa wapiga kura milioni 11

kati ya lengo la kuandikisha wapiga kura kati ya milioni 21

hadi 23.

Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu

wa kuiwezesha Tume kutimiza wajibu wake. Napenda

kuwahakikishia kuwa kila Mtanzania mwenye haki ya

kupiga kura atapata fursa ya kuandikishwa. Shime

tuhimize watu wajitokeze kujiandikisha ili wasikose haki

yao hiyo.

Page 19: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

19

Uhuru wa Habari

Mheshimiwa Spika;

Mtakubaliana nami kuwa katika kipindi hiki uhuru wa

habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao umepanuka

sana. Tanzania kuna magazeti ya kila siku 16 na kati ya hayo

ya Serikali ni 2 (Daily News, Habari Leo). Pia magazeti ya

kila wiki yapo 62. Aidha, kuna vituo vya redio 115 na vya

televisheni 29. Serikali haifanyi uhakiki wa habari kabla ya

kuchapishwa au kuandikwa. Tumeamua hivyo kwa imani

yangu kwamba ustawi wa demokrasia hutegemea sana

uhuru wa vyombo vya habari. Pili, kwa vile tunatambua

manufaa ya vyombo vya habari kuelimisha jamii,

kupambana na maovu na kuhimiza uwajibikaji.

Pamoja na hayo, hatukusita wala kuchelea kuchukua

hatua pale uhuru huo ulipotumiwa vibaya na kutishia

kuvuruga amani, umoja na usalama wa jamii au taifa. Au,

Page 20: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

20

pale ambapo Sheria za nchi zimekiukwa. Huo ni wajibu

wetu wa kikatiba ambao mimi na wenzangu tuliapa

kuutimiza.

Mheshimiwa Spika;

Katika kuongeza uwazi na mawasiliano na wananchi

mwaka 2007 tulianzisha tovuti ya wananchi. Tovuti hiyo

imeshapokea hoja 117,243 na kati ya hizo zilizohusu Serikali

zilikuwa 78,258 na zote zimeshughulikiwa.

Katika kuboresha mfumo wa mawasiliano, Tanzania

imeshahama kutoka mfumo wa analogia na kuingia kwenye

mfumo wa digitali. Hii ni hatua kubwa muhimu kwa

maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Jambo ambalo

nasikitika kuwa hatukuweza kulikamilisha ni utungaji wa

Sheria ya Haki ya Upatikanaji wa Habari na Sheria ya

Vyombo vya Habari. Miswada imekamilika na kusomwa

mara ya kwanza hapa Bungeni lakini mchakato wake

haukuweza kufika mwisho. Tunawaachia wenzetu wajao

washughulike nayo katika Bunge la 11.

Page 21: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

21

Vita dhidi ya Rushwa

Mheshimiwa Spika;

Vita dhidi ya rushwa ni eneo jingine ambalo tulilivalia

njuga katika Awamu ya Nne. Tumepata mafanikio ya kutia

moyo katika mapambano dhidi ya rushwa ingawaje kazi

bado ni kubwa. Tumefanya mambo matatu. Kwanza,

tumetunga Sheria Na. 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na

Kupambana na Rushwa ambayo imeongeza nguvu ya

mapambano dhidi ya uovu huu. Idadi ya makosa ya rushwa

iliongezwa kutoka 4 mpaka 24 na wigo wa wakosaji pia,

kwa kuhusisha watu katika sekta binafsi. Mifumo ya

upelelezi na uendeshaji mashitaka nayo imeimarishwa.

Tumeunda chombo kipya TAKUKURU badala ya

TAKURU ambacho kimepewa majukumu ya kuzuia na

kupambana na rushwa badala ya kuzuia peke yake.

TAKUKURU imepewa mamlaka zaidi katika kuongoza

mapambano haya. Taasisi imeendelea kuimarishwa kwa

Page 22: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

22

kuipatia zana na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na

rasilimali watu na mahitaji mengine. Tumeiwezesha

TAKUKURU kufungua ofisi katika Mikoa na Wilaya zote.

Mheshimiwa Spika;

Maboresho haya yamewezesha idadi ya kesi za tuhuma

za rushwa zinazofikishwa mahakamani kuongezeka kutoka

kesi 50 mwaka 2005 hadi 1,900 mwaka 2014. Jumla ya

shilingi bilioni 87.8 ziliokolewa. Watumishi wa Serikali 97

wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa na matumizi

mabaya ya ofisi zao baada ya ushahidi wa kijinai

kukosekana. Kwa upande wa kupambana na rushwa

kwenye shughuli za uchaguzi, tumetunga Sheria ya

Kudhibiti Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 ili

kutoa majibu ya kilio cha siku nyingi dhidi ya watu

wanaotumia fedha kununua kura.

Mapato na Matumizi ya Fedha na Mali za Serikali

Mheshimiwa Spika;

Page 23: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

23

Nilieleza katika hotuba yangu ya Kuzindua Bunge la

Tisa tarehe 30 Desemba, 2005 kuwa tutatoa kipaumbele cha

juu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na nidhamu ya

matumizi ya Serikali. Leo miaka kumi baadae ninaona

fahari tumepata mafanikio makubwa. Mapato ya Serikali

yameongezeka kutoka shilingi bilioni 177.1 mwaka 2005

kwa mwezi hadi takriban shilingi bilioni 850. Hii

imewezesha bajeti ya Serikali kukua kutoka trilioni 4.13

mwaka 2005/2006 hadi trilioni 22.49 mwaka 2015/2016.

Isitoshe imetuwezesha kupunguza misaada na mikopo ya

washirika wa maendeleo kutoka asilimia 42 ya Bajeti ya

Serikali mwaka 2005 hadi asilimia 15 mwaka 2014/2015 na

tumejipa lengo la kushusha zaidi hadi asilimia 8 mwaka

huu wa fedha wa 2015/2016.

Mheshimiwa Spika;

Mafanikio haya yametokana hasa na kazi kubwa

tuliyoifanya ya kuimarisha Mamlaka ya Mapato ambao

wanastahili pongezi zetu nyingi. Bado naamini tunaweza

Page 24: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

24

kufanya vizuri zaidi ya hivi, kama tukiongeza udhibiti kwa

mianya ya kupoteza mapato na kuimarisha zaidi TRA na

mamlaka nyingine za ukusanyaji mapato ya Serikali. Bado

ukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya kodi katika

Halmashauri za Wilaya na Miji na katika Wizara, Idara

zinazojitegemea na Wakala wa Serikali uko chini ya lengo.

Huku kuendelee kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika;

Kwa upande wa nidhamu ya matumizi ya fedha na

mali za Serikali tulielekeza nguvu zetu katika kuimarisha

utaratibu wa manunuzi Serikalini na ukaguzi wa hesabu za

Serikali. Kwa upande wa ununuzi wa bidhaa na huduma,

tumeendelea kuimarisha Sheria na Mamlaka ya Ununuzi wa

Umma ili iweze kuhakikisha kuwa kuna usimamizi thabiti

wa sheria hiyo na kanuni zake. Kama mjuavyo sehemu,

kubwa ya fedha za Serikali hutumiwa katika ununuzi wa

bidhaa na huduma, hivyo kuwepo usimamizi mzuri ni

jambo jema. Ukikosekana, wizi na rushwa hutawala.

Page 25: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

25

Mheshimiwa Spika;

Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za Serikali,

tumechukua hatua za makusudi za kuimarisha Ofisi ya

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Tumetunga Sheria mpya inayoipa nguvu na uhuru zaidi

Ofisi hiyo. Aidha, tumewaongezea bajeti, vitendea kazi na

rasilimali watu. Ofisi 8 za Mikoa zimejengwa na 2

zinaendelea kujengwa.

Nafurahi kwamba maagizo yangu kwa viongozi na

watendaji katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhusu

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za

Serikali kupewa uzito linazingatiwa. Taarifa hizo sasa

zinasomwa, zinajadiliwa na hatua kuchukuliwa kwa kasoro

zilizoonekana. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali

imefanya kazi nzuri. Wezi na wabadhirifu wanaobainika

kuchukuliwa hatua za kisheria mara makosa

Page 26: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

26

yanapogundulika. Kitaifa taarifa hiyo hujadiliwa Bungeni

kwa muda wa kutosha.

Mheshimiwa Spika;

Niliamua pia kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa

Ndani wa Serikali na kuwaweka Wakaguzi wa Ndani wote

wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka yake

na kuwajibika kwake. Ofisi hii imesaidia kuhakikisha sheria

na kanuni za matumizi ya fedha na mali ya umma

zinaheshimiwa. Pia, katika ufuatiliaji na utekelezaji wa

mapendekezo ya CAG. Uimarishaji wa ukaguzi wa ndani na

ule wa CAG umesaidia kuboresha hesabu za Serikali kuwa

nzuri zaidi siku hizi. Hati safi zimeongezeka na hati chafu

zinazidi kupungua Serikalini. Kwa mfano katika

Halmashauri za Wilaya na Miji, hati safi zimeongezeka

kutoka 56 mwaka 2006 hadi 150 mwaka 2014. Hati zenye

mashaka ni 13 na hakuna Hati isiyoridhisha. Kazi ya

kuimarisha ukaguzi na nidhamu ya matumizi lazima

iendelezwe.

Page 27: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

27

Maadili ya Viongozi wa Umma

Mheshimiwa Spika;

Katika miaka 10 hii tumeimarisha mfumo wa

kusimamia maadili ya viongozi. Tumefanya hivyo kwa

kutambua kuwa maadili mema ni sifa ya msingi ya kiongozi

na huiletea heshima Serikali. Tumeendeleza Kamati ya

Maadili na kuunda Baraza la Maadili kwa mujibu wa Sheria

ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya 1995.

Tumepanua wigo na kwamba sasa mali za viongozi na

familia zao hutolewa taarifa na kiongozi katika Tamko la

Mali la kila mwaka. Hii inasaidia kuondoa uwezekano wa

kiongozi kuficha mali kwa mgongo wa mwenza wake au

mtoto.

Mheshimiwa Spika;

Kamati ya Maadili sasa si tu inapokea fomu na

kuzihifadhi, bali inafanya ukaguzi wa mali za viongozi na

Page 28: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

28

kuzifuatilia. Kikwazo chao ni kupata rasilimali fedha. Hili

litazamwe zaidi. Pale inapoonekana kuna makosa ya

kimaadili wahusika hufikishwa kwenye Baraza la Maadili.

Sote tumeshuhudia kazi nzuri iliyofanywa na Baraza hilo

wakati wa sakata la Escrow. Bado kazi ya kuimarisha

Kamati ya Maadili kwa rasilimali fedha, vitendea kazi,

majengo ya ofisi na rasilimali watu haina budi kuendelezwa.

Muhimili wa Mahakama

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi cha miaka 10 hii tumefanya jitihada

kubwa za kuimarisha mhimili wa Mahakama. Miongoni

mwa mambo mengine, tumefanya mambo muhimu kwa

madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa

jukumu lake la msingi la utoaji haki.

Kwanza, tumetenganisha shughuli za kutoa haki na za

utawala. Tumeunda Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama

ya kushughulikia mambo ya fedha na utawala. Hivyo basi,

Wasajili wa Mahakama wanabaki na jukumu la kutoa haki.

Page 29: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

29

Mpaka sasa mabadiliko haya yamekuwa ya manufaa

makubwa kwa Mahakama kwani yameboresha utekelezaji

wa majukumu katika Mahakama. Pili, tumeanzisha Mfuko

wa Mahakama ambao unaipa Mahakama uhuru katika

kuendesha shughuli zake. Sambamba na hilo tumeongeza

bajeti ya Mahakama kutoka shilingi bilioni 36.6 mwaka

2006/07 hadi shilingi bilioni 87.6 mwaka 2014/15. Jambo

linalohitaji kuboreshwa ni Hazina kutoa fedha kwa wakati

ili shughuli zifanyike kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika;

Jambo la tatu, ni kwamba tumeongeza idadi ya Majaji

wa Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu Wakazi

na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Lengo letu ni

kuongeza nguvukazi ya kusikiliza na kuamua mashauri.

Kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo

wameanza kuteuliwa watu wenye Shahada ya Sheria. Hivi

sasa itawawezesha watu wenye mashauri katika Mahakama

hizo kupata utetezi wa Mawakili. Kati ya mwaka 2005 na

Page 30: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

30

2015 tumeongeza Majaji wa Rufani kutoka 8 mwaka 2005

hadi 16, na Majaji wa Mahakama Kuu kutoka 37 hadi 81

katika kipindi hicho. Hali kadhalika, tumeongeza idadi ya

Majaji wanawake. Katika Mahakama ya Rufani wapo 5 na

katika Mahakama Kuu wapo 32 na kufanya jumla yao kuwa

37. Hivi sasa tunao jumla ya Mahakimu Wakazi 1,266 katika

ngazi zote za Mahakama. Kati ya hao 534 sawa na asilimia

35 ni wanawake. Idadi ya Majaji na Mahakimu wanawake

hivi sasa ni kubwa kuliko wakati wowote uliopita.

Mheshimiwa Spika;

Kutokana na mipango mizuri iliyowekwa na Jaji Mkuu

Mohamed Chande Othman Mahakama zimepiga hatua

kubwa katika kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.

Majaji wamejiwekea malengo kwa kila Jaji asikilize na

kuamua mashauri yasiyopungua 220 kwa mwaka na kila

Hakimu Mkazi mashauri 250 na wale wa Mahakama ya

Mwanzo mashauri 260 kwa mwaka. Kwa sababu hiyo,

kuanzia Julai, 2014 hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2015

Page 31: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

31

yalifunguliwa mashauri 177,586 na Mahakama ilisikiliza na

kuamua mashauri 179,962. Maana yake ni kuwa

zimesikilizwa zote na nyingine zilizobakia miaka ya nyuma.

Bila shaka kwa kasi hii sasa mrundikano wa kesi utabakia

kuwa historia katika kipindi kifupi kijacho. Nawapongeza

sana Majaji na Mahakimu kwa kazi nzuri waifanyayo.

Kwa upande wa ujenzi wa majengo ya Mahakama

Kuu, wamekamilisha ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu za

Divisheni ya Kazi pamoja na majengo ya Mahakama Kuu

Mikoa ya Shinyanga na Kagera. Aidha, majengo mawili ya

Mahakama za Wilaya na 12 ya Mahakama za Mwanzo nayo

yamekamilika. Hivi sasa, ujenzi unaendelea wa majengo ya

Mahakama Kuu 9 za mikoa iliyosalia, Mahakama za Wilaya

9 na za mwanzo 25.

Maboresho ya Mfumo wa Utoaji Haki

Mheshimiwa Spika;

Jambo lingine ambalo tumefanya katika nia ya

kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na kupunguza malalamiko ya

Page 32: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

32

wananchi na ucheleweshaji wa mashauri ni kutenganisha

kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na uendeshaji wa

mashtaka hayo Mahakamani. Polisi waliokuwa wanafanya

yote sasa watashughulikia upelelezi na ofisi ya Mkurugenzi

wa Mashtaka ndiyo inayoendesha mashauri. Tayari Ofisi za

Mkurugenzi wa Mashtaka zimekwishafunguliwa katika kila

Mkoa na sasa tunaenda wilayani. Aidha, tumeboresha Ofisi

ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa rasilimali watu,

vitendea kazi na fedha ili kuongeza ufanisi katika utendaji

wa ofisi hiyo muhimu sana. Kuna haja ya kuendelea

kuongezea rasilimali fedha na vitendea kazi ili ufanisi

uongezeke zaidi.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki, tumeimarisha Tume ya Haki za

Binadamu na Utawala Bora kwa kuiwezesha kwa nyenzo,

rasilimali fedha na watu. Tume sasa inafanya kazi katika

eneo lote la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kutokana na

Page 33: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

33

utumiaji wa mfumo wa elektroniki malalamiko ya wananchi

mengi zaidi yanafikishwa kwenye Tume na mengi

yanapatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, idadi ya malalamiko

yaliyowasilishwa Tume yameongezeka kutoka 9,455

mwaka 2006 hadi 25,921 mwaka 2014 na uwezo wa Tume

kushughulikia malalamiko kwa mwaka umeongezeka

kutoka malalamiko 3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko

18,501 mwaka 2014.

Utendaji Serikalini

Maeneo ya Utawala

Mheshimiwa Spika;

Kwa nia ya kusogeza huduma, mwaka 2010 tulianzisha

mikoa mipya 4 ya Geita, Simiyu, Njombe na Katavi na

wilaya mpya 19. Pia, tulianzisha Halmashauri 45, kata 1,432,

vijiji 1,949, Mitaa 1,379 na vitongoji 8,777. Nimeamua

kuanzisha mkoa mpya wa Songwe kutoka mkoa wa Mbeya

na Wilaya sita kama ifuatavyo: Tanganyika mkoani Katavi,

Kigamboni na Ubungo mkoani Dar es Salaam, Songwe

Page 34: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

34

mkoani Mbeya, Kibiti mkoani Pwani na Malinyi mkoani

Morogoro. Najua tulikuwa na maombi mengi lakini kwa

sasa tufanye haya.

Maslahi ya Wafanyakazi

Mheshimiwa Spika;

Serikali ya Awamu ya Nne imelipa umuhimu wa juu

suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa Serikali. Karibu

kila mwaka tumekuwa tunaongeza kima cha chini cha

mshahara. Kwa sababu hiyo, kima cha chini cha mshahara

kimeongezeka kutoka shilingi 65,000 mwaka 2005 hadi

shilingi 265,000 mwaka wa jana. Mwaka huu tumefikia

shilingi 300,000. Najua bado hakikidhi mahitaji lakini

ukilinganisha na tulikokuwa kipindi hiki tumeongeza sana

mishahara ya wafanyakazi. Vile vile, tumeendelea

kupunguza kodi ya mapato kwa mfululizo kutoka asilimia

18 mwaka 2005 hadi asilimia 11 mwaka huu. Dhamira yetu

ni kutaka kutoa nafuu zaidi kwa wafanyakazi. Vile vile,

tumewapandisha vyeo watumishi 233,876 na kulipa

Page 35: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

35

malimbikizo ya watumishi 422,348 ya kiasi cha shilingi

bilioni 384.8.

Mheshimiwa Spika;

Tumetekeleza sera ya ugatuaji wa madaraka kwa

wilaya jambo ambalo limelazimu kuongeza rasilimali fedha

na watu kwa Halmashauri za Wilaya na Miji. Kwa ajili hiyo

ruzuku kwa Halmashauri zetu imeongezeka kutoka shilingi

bilioni 780 mwaka 2005/2006 hadi shillingi trilioni 4.69

mwaka 2015/2016. Aidha, tumeimarisha utumishi katika

Halmashauri kwa kuajiri watumishi wengi wa kada

mbalimbali.

Usawa wa kijinsia

Mheshimiwa Spika;

Mwaka 2005 niliahidi wakati wa kampeni na wakati wa

kuzindua Bunge la Tisa, kuwa tutaongeza ushiriki wa

wanawake katika shughuli na nyanja mbalimbali za maisha

ya watu wa nchi yetu ikiwemo nafasi za maamuzi. Ninyi na

mimi ni mashahidi kwamba tumetimiza ahadi hiyo. Idadi

Page 36: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

36

ya Wabunge wanawake imeongezeka kutoka 62 mwaka

2005 hadi 127. Hivi sasa hamsini kwa hamsini ni rasmi

katika Katiba Inayopendekezwa. Kwa mara ya kwanza

katika historia ya nchi yetu na Bunge letu tumepata Spika

mwanamke Mheshimiwa Anne Semamba Makinda.

Wanawake wameongezeka katika ngazi zote kuu za

uamuzi. Kwa mfano, tunao Mawaziri wanawake 10, Naibu

Mawaziri wanawake 5, Majaji wanawake 37 na Wakuu wa

Wilaya wanawake wako 53. Kwa upande wa Makatibu

Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa,

Wakurugenzi Watendaji n.k. pia wameongezeka. Katika

elimu nako tuna usawa wa kijinsia kwa upande wa idadi ya

wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule za msingi na

sekondari. Katika vyuo vya elimu ya juu, idadi ya

wanafunzi wa kike imeongezeka kwa kasi kutoka 10,039

mwaka 2005 hadi 78,800 mwaka 2014.

Page 37: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

37

Hali ya Uchumi

Mheshimiwa Spika;

Wakati ninaingia madarakani mwaka 2005 niliwaahidi

Watanzania wenzangu kuwa tutafanya kila tuwezalo

kujenga uchumi ulio imara na shirikishi. Hususan, nilisema

nitaendeleza sera za mageuzi ya kiuchumi na kuweka

misingi madhubuti ya kukuza uchumi, kuongeza ajira,

kuongeza Pato la Taifa na kupunguza umaskini. Katika

miaka kumi iliyopita tumeendelea kusimamia kwa kiwango

kizuri sera za uchumi jumla na sera za uchumi katika ngazi

ya chini zinazogusa wananchi wa kawaida.

Jitihada zetu hizo zimezaa matunda ya kutia moyo.

Katika kipindi hiki, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa

takriban asilimia 7. Nchi yetu ni miongoni mwa mataifa 10

ya Afrika na 20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa

kasi kubwa. Pato ghafi la Taifa limeongezeka zaidi ya mara

tatu kutoka shilingi trilioni 14.1 mwaka 2005 hadi kufikia

trilioni 79.4 mwaka 2014. Hivyo basi, pato la wastani la

Page 38: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

38

Mtanzania nalo limeongezeka kutoka shilingi 441,030

mwaka 2005 hadi shilingi 1,724,416 mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika;

Mauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za

Marekani bilioni 1.67 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani

bilioni 8.76 mwaka 2014 na kutunisha akiba yetu ya fedha

za kigeni na kutuwezesha kuagiza bidhaa na mahitaji ya

nchi kutoka nje kwa kipindi cha miezi 4.1 kama

tulivyopanga. Mfumuko wa bei ni asilimia 6.1.

Mheshimiwa Spika;

Kama mjuavyo, mwaka 2000 nchi yetu ilijiwekea Dira

ya Taifa ya Maendeleo ya hadi mwaka 2025. Mwaka 2010

tulitengeneza Mpango wa Muda Mrefu (Long Term

Perspective Plan) wa (2010 – 2025) wa kuongoza utekelezaji

wa Dira kwa miaka 15 iliyobaki. Tuligawa utekelezaji wake

katika Mipango mitatu ya Maendeleo ya Miaka Mitano kila

mmoja. Tuko katika hatua za mwisho za utekelezaji wa

Commented [A1]: Ni kwa mujibu wa economic survey, angalizo: takwimu zimewekwa kwenye dola milioni na sio dola bilioni

Page 39: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

39

Mpango wa Kwanza, (2011/12 – 2015/16) na kuandaa

mpango wa pili (2016/17 – 2021/22).

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa

Mheshimiwa Spika;

Kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa Serikali

nilianzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Huu ni mfumo mpya wa kupanga, kufuatilia na kusimamia

utekelezaji wa malengo na shughuli za Serikali kwa nia ya

kuhakikisha kuwa kilichokusudiwa kinafanyika, tena kwa

wakati. Tuliamua kuanza na sekta sita za Elimu, Nishati,

Kilimo, Uchukuzi, Maji na Mapato ya Serikali. Baadae

sekta ya afya na uboreshaji mazingira ya uwekezaji

ziliongezwa.

Katika kipindi hiki kifupi Mpango umethibitisha kuwa

wenye manufaa. Mambo katika sekta zilizojumuishwa

katika BRN yameanza kwenda vizuri. Changamoto yetu

kubwa imekuwa ni upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa

Page 40: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

40

wakati kutoka Hazina. Kama changamoto hiyo

isingekuwepo mambo yangekuwa mazuri zaidi.

Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji

Mheshimiwa Spika;

Kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza

uchumi, kuzalisha ajira, kuongeza mapato na kupunguza

umaskini, Serikali yetu imekuwa inachukua hatua thabiti za

kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji

wa ndani na nje kuchagua Tanzania kuwa nchi inayofaa

kuwekeza.

Mwaka 2010 tumetengeneza Sera na kutunga Sheria ya

Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public

Private Partnership—PPP). Lengo letu ni kuweka mazingira

mazuri kwa sekta binafsi kuvutika kushirikiana na Serikali

katika shughuli za kiuchumi na maendeleo. Faida kubwa ya

utaratibu huu ni kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwekeza

katika baadhi ya shughuli ambazo sekta binafsi inaweza

kubeba sehemu ya gharama. Hii siyo tu inaongeza kasi ya

Page 41: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

41

maendeleo, bali kuiwezesha Serikali kuokoa fedha ambazo

inaweza kuzitumia kwa shughuli nyingine.

Juhudi zetu za kuboresha mazingira ya uwekezaji

zinaendelea kuzaa matunda mema. Kati ya 2005 na 2014,

Kituo chetu cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi 7,159

yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 154.274. Kati ya

miradi hiyo asilimia 49.38 ni ya wawekezaji wa ndani,

asilimia 23.41 ni wawekezaji wa kutoka nje na asilimia 27.18

ni miradi ya ubia baina ya Watanzania na wawekezaji wa

kigeni. Ajira 16,000 zilipatikana. Ukuaji huu wa uwekezaji

umeongeza mapato ya Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na

Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda na Biashara

Duniani (UNCTAD) ya mwaka 2015, Tanzania inaongoza

Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji. Ilipata Dola za

Marekani bilioni 2.142 sawa na asilimia 31.5 ya uwekezaji

wote katika Jumuiya yetu.

Page 42: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

42

Sekta za Uzalishaji

Sekta ya Kilimo

Mheshimiwa Spika;

Kuendeleza kilimo ilikuwa ni moja ya mambo

tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Shabaha yetu kuu ni kutaka

kuongeza tija ili uzalishaji uongezeke, wakulima wapate

mavuno mengi, masoko ya uhakika yawepo na bei iwe nzuri

ili mapato yao yaongezeke na umasikini uwapungukie. Vile

vile wao na taifa lijitosheleze kwa chakula.

Kwa ajili hiyo mwaka 2006 tuliasisi Programu ya miaka

7 ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector

Development Programme—ASDP). Katika Programu hiyo,

matatizo yanayofanya tija na uzalishaji katika kilimo kuwa

mdogo yalitambuliwa na kutengenezewa mpango wa

kuyatatua. Serikali pia ilianzisha mikakati, programu na

mipango mingine ya kuongeza msukumo katika kuleta

mageuzi ya kilimo. Miongoni mwa hiyo ni mkakati wa

Kilimo Kwanza, Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika

Page 43: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

43

Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mpango wa

Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP), Sera ya

Umwagiliaji tuliyoitunga mwaka 2010 na Programu ya

Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika.

Mheshimiwa Spika;

Pamoja na hayo, tumeongeza pia bajeti ya sekta ya

kilimo kutoka shilingi bilioni 233.3 mwaka 2005/06 hadi

shilingi bilioni 1,084.7 mwaka 2014/15. Kuongezwa kwa

bajeti kumewezesha fedha za ruzuku ya mbolea na

pembejeo kuongezeka kutoka shilingi bilioni 7.5 mwaka

2005/06 hadi shilingi bilioni 299.3 mwaka 2013/14. Matrekta

makubwa na madogo yameongezeka kutoka 7,491 mwaka

2005 hadi 16,412 mwaka 2014. Kwa sababu hiyo matumizi

ya jembe la mkono yamepungua kutoka asilimia 70 hadi

asilimia 62. Tumeongeza maafisa ugani kutoka 3,379 mwaka

2005 hadi 7,974 mwaka 2014.

Vituo vya utafiti wa kilimo tumeviongezea rasilimali

fedha, watu na vitendea kazi. Aidha, tumeanza safari ya

Page 44: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

44

kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na kuhusisha sekta

binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika

kuzalisha mbegu. Aidha, tumeimarisha Wakala wa Mbegu

(Agricultural Seed Agency – ASA) na kuongeza uzalishaji

wa mbegu bora kutoka tani 10,477.17 mwaka 2005 hadi tani

32,340 mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika;

Juhudi za Serikali kuendeleza kilimo zimezaa matunda

mazuri. Tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na

chakula imeongezeka. Kwa upande wa mazao ya chakula

uzalishaji umeongezeka kutoka tani milioni 9.66 mwaka

2005 hadi tani milioni 16.01 mwaka 2014. Ongezeko hili

limeliwezesha taifa letu kujitosheleza kwa chakula kwa

asilimia 125 mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 95

mwaka 2005. Uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara

umeongezeka toka tani 427,738 mwaka 2005 hadi tani

569,054 mwaka 2014 na uzalishaji wa mbegu za mafuta

umeongezeka karibu ya mara 4 toka tani 1,389.9 mwaka

Page 45: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

45

2005 hadi tani 5,545.6 mwaka 2014. Aidha, uzalishaji wa

matunda nao umeongezeka toka tani milioni 1.2 mwaka

2005 hadi tani milioni 4.4 mwaka 2014 na maua toka tani

5,862 hadi tani 10,790.

Mheshimiwa Spika;

Upatikanaji wa masoko ya uhakika na bei nzuri kwa

mazao ya wakulima bado ni changamoto. Pia kuna tatizo la

upungufu wa maghala ya kuhifadhi mazao. Jitihada

zinaendelea kupata mkopo au wabia wa kujenga maghala

ya kisasa nchi nzima. Programu ya Mageuzi na

Modenaizesheni ya Ushiriki ilianzishwa ili kutatua tatizo la

masoko. Aidha, tumeanza maandalizi ya kuanzisha soko la

bidhaa (Commodity Market Exchange) kwa nia hiyo hiyo.

Naamini misingi mizuri tuliyoijenga pamoja na kuenea kwa

SACCOS na kuanza kwa Benki ya Kilimo ikiendelezwa

itatoa mchango mkubwa katika kuongeza kasi ya

mapinduzi ya kilimo.

Page 46: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

46

Mifugo

Mheshimiwa Spika;

Kwa upande wa mifugo, dhamira yetu ilikuwa kuanza

safari ya kuleta mageuzi katika sekta hii. Safari hiyo

tumeianza kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya

Mifugo. Changamoto zinazochangia maendeleo duni ya

sekta hii zimeainishwa na kutengenezewa mkakati wa

utekelezaji. Katika kipindi hiki malambo 1,008, majosho

2,364 na maabara 104 za mifugo zimejengwa. Visima virefu

101 vimechimbwa, malambo 370 na majosho 499

yamekarabatiwa katika kipindi hiki cha miaka 10.

Ukarabati na ujenzi wa majosho umeongeza idadi

kutoka 2,177 mwaka 2006 hadi 3,637 mwaka 2015.

Tumeongeza Maofisa Ugani kutoka 2,270 mwaka 2005 hadi

6,041 mwaka 2014. Kuhusu uhamilishaji, tumeongeza vituo

kutoka kituo 1 mwaka 2005 hadi vituo 8 mwaka 2015 na

kuwezesha ng’ombe 955,360 kuhamilishwa katika miaka 10

hii.

Page 47: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

47

Mheshimiwa Spika;

Mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi

tuliyoyajenga yamewezesha viwanda vya kusindika nyama,

maziwa na vyakula vya mifugo kuongezeka. Viwanda vya

kusindika maziwa vimeongezeka kutoka 22 mwaka 2005

hadi 74 mwaka 2015. Viwanda vya kuzalisha vyakula vya

mifugo vimeongezeka kutoka viwanda 6 mwaka 2005 hadi

80 mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tani milioni

1.4 za vyakula hivyo kwa mwaka. Aidha viwanda na

machinjio ya kisasa 9 vimejengwa katika kipindi hiki.

Usindikaji wa ngozi pia umeongezeka kutoka vipande

790,000 mwaka 2005 hadi vipande milioni 3.78 mwaka 2014.

Hivi sasa kwa mfano, uzalishaji wa malisho ya mifugo (hei)

umefikia marobota 957,860 ikilinganishwa na marobota

178,100 mwaka 2005.

Safari yetu ya kuanza kuondoka kwenye uchungaji

kwenda kwenye ufugaji imeanza. Vijiji vingi vimeandaa

mipango ya matumizi bora ya ardhi na hivyo vimetenga

Page 48: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

48

maeneo ya kilimo na ya ufugaji. Tuendelee kuhimiza vijiji

vyetu kutekeleza mipango hiyo ili wafugaji wapate maeneo

ya malisho mbali na mazao ya wakulima. Pia, tuhimize

uhamilishaji kama mlango wa kuingilia kwenye kuboresha

kosafu za mifugo yetu.

Uvuvi

Mheshimiwa Spika;

Wakati nazindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005

nilisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele

kwenye kuendeleza sekta ya uvuvi. Katika kutekeleza hayo

tumefanya yafuatayo. Kwanza, nimeunda Wizara mpya ya

Mifugo na Uvuvi. Pili, tulifuta kodi ya zana za uvuvi ili

kuwawezesha wavuvi kupata zana bora na za kisasa kwa

bei nafuu zaidi. Tatu, tumeimarisha vyuo vya uvuvi na hivi

sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi 1,215

ikilinganishwa na wanafunzi 127 mwaka 2005. Hii

imetuwezesha kuongeza wagani wa uvuvi kutoka 103

mwaka 2005 hadi 540 mwaka 2014. Nne, tumeongeza sana

Page 49: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

49

juhudi za kupambana na uvuvi haramu ili kutunza

mazingira, mazalia ya samaki na kuzuia kuvuliwa au

kuuawa kwa samaki wadogo.

Tumeimarisha maabara ya Taifa ya Samaki pale

Nyegezi kwa vifaa vya kisasa na wataalamu ili iende na

wakati. Tano, tumeongeza msukumo wa kuhimiza ufugaji

wa samaki na kuwezesha mashamba ya samaki kuongezeka

kutoka 13, 011 mwaka 2005 hadi 20, 325 mwaka 2014.

Uvuvi haramu unapungua. Mapato ya sekta ya uvuvi

yameongezeka kutoka shilingi bilioni 351.6 mwaka 2005

hadi shilingi trilioni 1.8 mwaka 2013. Bado tuna kazi kubwa

ya kufanya katika sekta hii ili kuongeza tija na mapato ya

wavuvi na taifa.

Utalii

Mheshimiwa Spika;

Kwa upande wa utalii, tumeendelea na jitihada za

kuiendeleza sekta hii muhimu. Tumeongeza kutangaza

vivutio vya utalii vya nchi yetu katika masoko makubwa

Page 50: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

50

duniani. Sekta ya utalii imekua kwa wastani wa asilimia 7.1

na imechangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.

Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii 612, 754 mwaka

2005 hadi watalii 1,140,156 mwaka 2014. Idadi ya vitanda

katika mahoteli imeongezeka kutoka 15,828 hadi 21,929.

Mapato pia yameongezeka kutoka Dola za Marekani

milioni 823.05 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani bilioni 2

mwaka 2014. Ajira za moja kwa moja zimeongezeka kutoka

32,673 hadi 686,130 na zisizokuwa za moja kwa moja kutoka

165,883 hadi 1,318,109. Haya ni mafanikio makubwa na ya

kujivunia.

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki tumekabiliana na tukio kubwa la

ujangili wa wanyamapori hasa wa ndovu kutokana na

kushamiri kwa biashara ya meno ya ndovu na bei kuwa

kubwa katika nchi za Mashariki ya Mbali. Vuguvugu la

ujangili lilifikia kiwango cha kutishia kumaliza ndovu

nchini na dunia nzima. Tukaamua kuchukua hatua za

Page 51: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

51

kuidhibiti hali hiyo. Tumefanya operesheni tatu kukabiliana

na tishio hili. Ya kwanza, iliendeshwa na Idara ya

Wanyamapori na Misitu wakishirikiana na TANAPA na

Ngorongoro Conservation Area. Hii hasa ilihusu

kupambana na ujangili katika hifadhi na mapori ya

Kaskazini mwa Tanzania. Mafanikio makubwa yalipatikana.

Mheshimiwa Spika;

Operesheni ya pili ni ile iliyohusisha Jeshi la Polisi

katika hifadhi na sehemu nyingine za Tanzania. Operesheni

Kipepeo kama ilivyoitwa nayo ilipata mafanikio. Na ya tatu,

Operesheni Tokomeza iliyohusisha vyombo vyote vya ulinzi

na usalama. Pamoja na changamoto zake operesheni hizi

zimesaidia sana kupunguza kasi ya ujangili nchini. Matokeo

yake katika sensa ya ndovu iliyofanyika mara ya mwisho,

ukiacha Ruaha, hali katika hifadhi na mapori mengine ina

muelekeo mzuri.

Kuundwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA)

yenye mamlaka makubwa zaidi ya kusimamia sekta ya

Page 52: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

52

wanyamapori nako kutaimarisha uhifadhi na mapambano

ya ujangili. Kwa mipango na program zilizopo Wizarani,

naamini mambo yatakuwa mazuri zaidi muda si mrefu.

Viwanda

Mheshimiwa Spika;

Katika miaka kumi hii, sekta ya viwanda imeendelea

kukua kwa kasi nzuri ya kutia moyo. Viwanda vikubwa,

vya kati na vidogo vimeongezeka kutoka 11, 544 mwaka

2005 hadi viwanda 51,224 mwaka 2015. Kati ya mwaka 2005

na 2014 na miradi 751 imepewa leseni za kudumu na BRELA

ya kuanzisha viwanda. Mchango wa sekta ya viwanda

katika Pato la Taifa umefikia asilimia 7.3 mwaka 2014

kutoka asilimia 6.8 mwaka 2005. Mchango wa viwanda

kwenye mauzo ya nje umeongezeka kutoka asilimia 9.3

mwaka 2005 hadi asilimia 23.3 mwaka 2014.

Tunategemea ukuaji mkubwa wa viwanda katika

Mpango wa Pili wa maendeleo wa miaka 5 kutokana na

misingi imara tuliyoijenga katika Mpango wa Kwanza.

Page 53: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

53

Ujenzi wa kiwanda cha chuma kule Liganga na makaa ya

mawe cha Mchuchuma, unatarajiwa kuanza mwaka huu na

kiwanda cha kuchakata gesi pale Lindi unatarajiwa kuanza

baada ya taratibu za kuwapatia ardhi zitakapokamilika.

Hivi ni viwanda vya msingi na mama ambavyo vitachochea

kasi ya ukuaji wa viwanda nchini na uchumi kwa jumla.

Madini

Mheshimiwa Spika;

Sekta ya Madini ndiyo ya pili baada ya utalii kwa

kuingiza fedha nyingi za kigeni. Kama nilivyoahidi, tulipitia

upya sera, sheria na mikataba ya madini iliyokuwepo na

kutengeneza sera na sheria mpya. Halikadhalika,

tulianzisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ambayo

hatimaye yalizaa marekebisho ya mikataba yao na hivyo

kuboresha maslahi ya taifa.

Kufuatia marekebisho hayo, makampuni husika ya

madini yanalipa kodi ya mapato. Bila ya hivyo huenda

mpaka leo yangekuwa hayajaanza kulipa kodi. Kutumika

Page 54: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

54

kwa Sheria mpya ya Madini, viwango vipya vya mrahaba na

kupunguzwa kwa misamaha ya kodi vimeongeza mapato ya

Serikali. Aidha, tuliunda Wakala wa Ukaguzi wa Madini

Tanzania (TMAA) ambao umewezesha kukagua mahesabu

ya migodi kuhusu uwekezaji na mauzo ya madini na

kuwawezesha TRA kutoza kodi stahiki kutoka kwa

makampuni hayo.

Mheshimiwa Spika;

Mabadiliko haya pamoja na kuongezeka kwa

uwekezaji katika sekta hii yamewezesha mchango wa sekta

ya madini katika Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia

2.9 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2014.

Thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka

kutoka Dola za Marekani milioni 655.5 mwaka 2005 hadi

kufikia Dola za Marekani bilioni 1.794 mwezi Desemba

2014. Mambo yangekuwa mazuri zaidi kama bei ya dhahabu

isingeshuka katika kipindi hiki.

Page 55: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

55

Mheshimiwa Spika;

Serikali ilifanya uamuzi wa kulifufua na kuliwezesha

Shirika letu la Madini (STAMICO) kuanza tena kazi ya

utafutaji na uchimbaji wa madini kupitia kampuni zake

tanzu. STAMICO kwa kupitia kampuni yake ya

STAMIGOLD imeanza kuzalisha dhahabu na kuuza nje.

Vilevile, tumejiunga na Mpango wa Uwazi wa Uvunaji wa

Maliasili (EITI) ambao umesaidia sana katika kuongeza

uwazi katika biashara ya madini na kusaidia katika

ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye makampuni ya

madini.

Katika kipindi hiki, migodi mitatu mipya ilianzishwa

nayo ni Migodi ya dhahabu wa Buzwagi (Shinyanga) na

New Luika (Mbeya) na mgodi wa makaa ya mawe wa

Ngaka (Ruvuma). Aidha, miradi mikubwa mingine 8

imeendelezwa na kufikia hatua ya kuanzisha mgodi

ukiwemo Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma), Mradi wa

Chuma Liganga na Mradi wa Makaa ya Mawe wa

Page 56: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

56

Mchuchuma (Njombe). Pia, ajira rasmi kwenye migodi

mikubwa nchini imeongezeka kutoka waajiriwa 3,517

mwaka 2005 hadi waajiriwa 15,000 mwaka 2014. Hali

kadhalika, makampuni ya madini yameongeza unununzi

wa bidhaa na huduma hapa nchini (local procurement)

kutoka Dola za Marekani milioni 230.41 mwaka 2005 hadi

Dola za Marekani milioni 536.56 mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki pia, tumetenga maeneo 8 kwa ajili

ya wachimbaji wadogowadogo. Maeneo haya yamewezesha

wachimbaji wadogo kuchimba madini bila bughudha.

Aidha, Wizara imenunua mitambo miwili kwa ajili ya

uchorongaji wa miamba kusaidia utafiti wa madini kwa ajili

ya wachimbaji wadogo. Tumeanzisha mfuko wa

kuwakopesha wachimbaji wadogo pale Wizarani ili kutoa

fursa kwa wachimbaji wadogo kupata mikopo ya

kuendeleza shughuli zao.

Page 57: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

57

Nishati

Mheshimiwa Spika;

Wakati naanza kazi ya uongozi wa nchi yetu, Tanzania

ilikuwa inakabiliwa na ukame mkubwa uliosababisha

upungufu mkubwa wa chakula. Pia kulikuwa na upungufu

mkubwa wa umeme kwa sababu ya mabwawa ya kuzalisha

umeme kukosa maji ya kutosha. Serikali ililazimika kulisha

watu zaidi ya milioni 3,776,000 na kukodisha mitambo ya

kuzalisha umeme. Kwa siku za usoni tuliamua kuchukua

hatua thabiti ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa

kutumia gesi asilia na vyanzo vingine kama vile makaa ya

mawe, mionzi ya jua na upepo.

Ujenzi umekamilika wa bomba la kusafirisha gesi

kutoka Mtwara na Songo Songo litakaloongeza kiasi cha gesi

kuja Dar es Salaam na kuwezesha uzalishaji wa megawati

3000 za umeme. Wakati huo huo kazi ya kujenga vituo vya

kufua umeme inaendelea pale Kinyerezi, Dar es Salaam.

Page 58: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

58

Umeme huo utakidhi mahitaji ya umeme sasa na miaka

kadhaa ijayo.

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme

Vijijini (REA) ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri ya

kusambaza umeme kwa vijiji 5,336 kati ya vijiji 12,423

nchini. Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa

na ile ya mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata

umeme kutoka asilimia 10 hadi asilimia 40 mwaka 2015.

Uamuzi uliofanywa katika Bajeti ya mwaka huu wa

kukusanya fedha kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta

ya petroli, utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza

umeme vijijini.

Gesi Asilia

Mheshimiwa Spika;

Tumepata mafanikio katika utafutaji wa mafuta na gesi

asilia. Kuanzia mwaka 2010 nchi yetu imepata bahati ya

ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi bahari kuu. Mpaka sasa

Page 59: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

59

zimegundulika futi za ujazo trilioni 47.08. Ukijumlisha na

futi za ujazo trilioni 8 zilizogunduliwa takriban miaka 40

iliyopita kule Songo Songo na Msimbati jumla ya rasilimali

ya gesi asilia nchini ni futi za ujazo trilioni 55.08. Kazi ya

utafutaji inaendelea na wataalamu wanasema kuwa

Tanzania inaweza kuwa na akiba ya futi za ujazo trilioni

200. Kiasi cha gesi kilichogunduliwa mpaka sasa ni

kikubwa na kufanya Tanzania kuwa mahala papya pa

kuipatia dunia nishati hii.

Gesi asilia tuliyonayo ikisimamiwa na kutumiwa vizuri

itaiwezesha nchi yetu na watu wake kupata maendeleo

makubwa na kuondokana na umaskini. Ni fursa ya aina

yake ya kuipatia Serikali mapato makubwa na kuiwezesha

kutimiza kwa uhakika majukumu yake na mipango yake.

Lakini, ili hayo yaweze kufanyika hapana budi pawepo

usimamizi mzuri wa hatua zote muhimu za mnyororo wa

thamani: yaani utafutaji, uchimbaji, usafirishaji, uuzaji wa

gesi asilia na matumizi yake nchini kama nishati na mali

Page 60: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

60

ghafi ya viwanda upande mmoja. Upande mwingine

inategemea sana matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na

rasilimali hiyo.

Mheshimiwa Spika;

Ni kutokana na kutaka kuhakikisha kwamba mambo

yanakuwa hivyo ndiyo maana tumetunga Sera ya Gesi

Asilia na kuwasilisha katika Bunge hili ile Miswada miwili

yaani wa Sheria ya Petroli na ule wa Matumizi ya Mapato ya

Mafuta na Gesi. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge

kwa kuipitisha Miswada hii nami nitaitia saini mara

nitakapoletewa.

Usafirishaji na Uchukuzi

Barabara

Mheshimiwa Spika;

Serikali ya Awamu ya Nne, imetoa kipaumbele cha juu

kwa uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji na

uchukuzi nchini. Hii ni pamoja na barabara, reli, bandari,

usafiri wa majini na usafiri wa angani. Tumeendeleza kazi

Page 61: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

61

ya kuongeza mtandao wa barabara za lami nchini kwa

mafanikio makubwa. Karibu barabara kuu zote nchini na

zile zinazounganisha mikoa zimekamilika kujengwa au kazi

ya ujenzi inaendelea. Kwa sababu hiyo hivi leo kutokea po

pote nchini kwenda Dar es salaam unafika siku hiyo hiyo,

tofauti na ilivyokuwa zamani watu walichukua zaidi ya siku

moja. Adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu wa

Mikoa ya Ziwa tumeimaliza.

Katika mkakati wetu wa kupanua mtandao wa

barabara za lami nchini, tulitambua barabara za urefu wa

kilomita 11,474 za kujengwa kwa kiwango cha lami. Baadae

tuliongeza barabara nyingine na kufikisha kilomita 17,742

katika mpango huo. Utekelezaji wake upo katika hatua

mbalimbali. Tayari ujenzi wa kilomita 5,568 kwa upande

wa barabara kuu na kilomita 535 kwa barabara za mijini

umekamilika. Ujenzi wa kilomita 3,873 unaendelea.

Upembuzi yakinifu na usanifu umekamilika kwa barabara

za urefu wa kilometa 4,965 kinachosubiriwa ni kupatikana

Page 62: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

62

fedha ujenzi uanze. Baadhi ya barabara hizo zimo katika

bajeti ya mwaka huu wa fedha. Barabara za urefu wa

kilometa 3,336 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu

wa kina.

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki pia, madaraja madogo 7,200 na

makubwa 12 yamejengwa na mengine 16 yapo katika hatua

mbalimbali za ujenzi. Miongoni mwa madaraja makubwa

yaliyokamilika ni daraja la Mto Malagalasi na yanayojengwa

ni daraja la Kigamboni na lile la Mto Kilombero. Madaraja

haya yalikuwa miongoni mwa matano yaliyopangwa

kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa

Miaka Mitano mara baada ya uhuru. Madaraja mawili yaani

la Kirumi lilijengwa mwaka 1985 na la Rufiji mwaka 2003.

Kwa upande wa vivuko, tumeongeza vipya 15 na kufikisha

idadi ya 28 kote nchini mwaka 2014.

Page 63: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

63

Mheshimiwa Spika;

Tumeongeza sana fedha katika mfuko wa barabara

kutoka shilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/06 hadi shilingi

bilioni 866.63 mwaka 2015/16. Hii itasaidia katika

matengenezo ya barabara za lami tulizojenga na kujenga

nyingine mijini. Hali kadhalika itatumika kuimarisha

barabara za udongo na changarawe wilayani na vijijini

ziweze kupitika wakati wote. Katika kipindi hiki barabara

za changarawe zimeongezeka kutoka kilometa 9,424 hadi

kilometa 22,089.

Mheshimiwa Spika;

Katika miaka kumi hii idadi ya vyombo vya moto yaani

magari, bajaji na pikipiki imeongezeka kutoka 1,696,088

mwaka 2005 hadi 3,313,254 hivi sasa. Ongezeko hili

linalotokana na hali ya kiuchumi ya watu wengi kuwa nzuri

limezua tatizo la msongamano wa magari katika miji mingi

nchini. Katika jiji la Dar es Salaam ambako tatizo ni kubwa

zaidi na Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali

Page 64: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

64

kupunguza ukali wake. Tunapanua ukubwa wa baadhi ya

barabara, kujenga barabara za mzunguko (ring roads) na

sasa tunaanza ujenzi wa barabara za juu ya nyingine

(flyovers). Tulianzisha matumizi ya treni katika reli za

TAZARA na TRC kusafirisha abiria. Hivi sasa reli hizo

zinasafirisha abiria milioni 2,804,269 kwa mwaka ambao

wangehitaji daladala 253 kwa siku. Mpango mkubwa wa

kuendeleza matumizi ya reli, Dar es Salaam umeandaliwa

na tumeanza kuutafutia fedha.

Usafiri wa Reli

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki tumetumia muda mwingi kutafuta

ufumbuzi wa matatizo yanayozikabili reli zetu za TAZARA

na TRC. Kimsingi reli hizo zimekuwa zinakabiliwa na

matatizo ya uchakavu wa miundombinu na uongozi na

uendeshaji usioridhisha. Kwa sababu ya matatizo hayo reli

hizi ambazo kila moja inaweza kusafirisha tani milioni 5

kwa mwaka zinasafirisha kati ya tani 200,000 na 300,000 tu.

Page 65: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

65

Hivyo basi, mizigo mingi husafirishwa kwa barabara na

kutishia uhai wa barabara ambazo tumezijenga kwa

gharama kubwa.

Kwa upande wa reli ya kati, uboreshaji wa reli kati ya

Dar es Salaam na Tabora unakaribia kukamilika na

utaendelea mpaka Kigoma na Mwanza. Wakati huo huo

mchakato wa ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa

(standard gauge) unaendelea. Ujenzi unaweza kuanza

mwaka huu kutegemea kukamilika kwa majadiliano na

mabenki yaliyoonyesha utayari wa kutukopesha pesa za

ujenzi.

Mheshimiwa Spika;

Azma yetu ya kufufua reli ya TAZARA nayo

tumeiwekea mkakati. Sisi na Zambia tumekubaliana

kushirikiana kwa karibu katika kutafuta ufumbuzi wa

matatizo yanayoikabili reli yetu hiyo. Bahati nzuri marafiki

zetu wa China nao wamekubali kutusaidia katika mipango

yetu hiyo. Ni matumaini yangu kuwa safari hii tutapata

Page 66: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

66

ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo yanayoathiri ufanisi

wa reli hii yenye umuhimu wa aina yake kwa uhai na

ustawi wa uchumi wa nchi zetu na watu wake.

Bandari

Mheshimiwa Spika;

Tumeboresha na kuimarisha huduma katika bandari ya

Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa. Mwaka 2014

bandari yetu ilihudumia tani milioni 14.4 ukilinganisha na

tani milioni 6.7 mwaka 2005. Mwaka huu inaweza kufikia

tani milioni 18. Siku hizi huduma hutolewa kwa saa 24 na

kasi ya kupakua, kupakia na kutoa mizigo imeongezeka

sana na wizi umepungua sana. Hata wale walioacha

kuitumia bandari yetu wameanza kurudi.

Mheshimiwa Spika;

Kuanza kutumika kwa mfumo wa Single Custom’s

Territory unaorahisisha upakuaji na upakiaji mizigo ya nchi

za Jumuiya ya Afrika Mashariki kumeongeza zaidi ufanisi.

Page 67: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

67

Tuko katika majadiliano na DRC na Zambia ambao nao

wameonyesha nia ya kuingia katika mfumo huu.

Kuongezeka kwa usafirishaji wa mizigo inayopita

nchini kuna faida kwani sekta ya usafirishaji inachangia

zaidi ya asilimia 15 ya pato la taifa. Hali kadhalika, ujenzi

wa gati za 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam

unaotegemewa kuanza mwezi huu utawezesha huduma ya

makasha kuongezeka kutoka makasha 600,000 hadi

makasha 1,200,000. Mipango ya kuboresha bandari za

Mtwara, Tanga na zile zilizo kwenye Maziwa yetu makuu

na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo zitaiwezesha Tanzania

kunufaika na fursa ya jiografia yake.

Usafiri wa Anga

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki tumefanya jitihada kubwa ya

kuwekeza kwenye ukarabati, upanuzi na ujenzi wa viwanja

vya ndege nchini. Tumekarabati Uwanja wa Ndege wa

Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao umeongeza uwezo

Page 68: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

68

wa kuhudumia kutoka ndege 7 hadi 30 hivi sasa. Aidha

tunajenga jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo lenye

uwezo wa kuhudumia abiria milioni 3.5. Ujenzi huo

unategemewa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

Kukamilika kwake kutauwezesha uwanja wa Kimataifa wa

Julius Nyerere kuhudumia abiria milioni 6 na ndege nyingi

zikiwemo ndege kubwa za kisasa za Airbus 380.

Mheshimiwa Spika;

Vile vile, tumeufanyia ukarabati na upanuzi Uwanja

wa Kimataifa wa Kilimanjaro ambao ni muhimu sana kwa

sekta ya utalii ya ukanda wa kaskazini. Uwanja mpya wa

ndege wa Songwe kule Mbeya umekamilika na hivi sasa

unatumika. Hali kadhalika, tumeviboresha upya viwanja

vya ndege vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora,

Mwanza na Bukoba.

Ujenzi, upanuzi na ukarabati huu tulioufanya,

umechangia sana katika ongezeko kubwa la safari za ndege

na abiria nchini. Safari za ndege kuja nchini zimeongezeka

Page 69: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

69

toka safari 78 mwaka 2005 zilizokuwa zinatolewa na

kampuni 29 za usafiri wa ndege hadi safari 175 zinazotolewa

na kampuni 55 mwaka 2014. Aidha, abiria wanaoondoka na

kuwasili katika viwanja vya ndege wameongezeka kutoka

2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka 2013.

Siku hizi Watanzania wanaopanda ndege wanaongezeka

kwa kasi kubwa.

Mheshimiwa Spika;

Jambo ambalo hatukuweza kufanikiwa ni lile la

kufufua Shirika letu la Ndege. Tumefanikiwa kulifanya lisife

lakini hatukuweza kulihuisha lirejee hata kwenye ile hali

yake ya zamani. Hata hivyo, fikra na mawazo kuhusu

mkakati wa kulijenga upya shirika hilo yapo. Kwa sasa

Menejimenti imepewa jukumu la kuandaa mpango wa

biashara unaoeleweka na unaokopesheka, kisha Serikali

itaona namna ya kulisaidia shirika.

Page 70: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

70

Utabiri wa Hali ya Hewa

Mheshimiwa Spika;

Sambamba na hayo, tumeboresha huduma za utabiri

wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa imepatiwa vifaa

vipya ambavyo vimeongeza ufanisi na usahihi wa utabiri

unaotolewa. Mwezi Februari 2014 Mamlaka hiyo ilipata

cheti cha utoaji wa huduma bora cha ISO na hivyo kuufanya

taarifa zake kutambuliwa kimataifa.

Mawasiliano

Mheshimiwa Spika;

Tumepiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia ya

habari na mawasiliano. Tumejenga Mkongo wa Taifa wa

Mawasiliano wenye urefu wa kilometa 7,560

unaounganisha miji mikuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara

isipokuwa mkoa mpya wa Simiyu. Kwa Mikoa ya Unguja na

Pemba, ujenzi wake utakamilika mwezi ujao. Katika Awamu

ya Pili, Mkoa wa Simiyu na wilaya zote nchini

zitaunganishwa.

Page 71: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

71

Ujenzi wa mkongo huu umechangia katika kuongeza

ubora na kasi ya mawasiliano, na kushusha gharama za

mawasiliano. Kwa mfano, gharama za kupiga simu

zimeshuka kutoka shilingi 115 kwa dakika mwaka 2005

hadi shilingi 34.92 mwaka 2014 na gharama za intaneti

zimeshuka kutoka wastani wa shilingi 36,000 kwa Gigabyte

moja mwaka 2005 hadi wastani wa shilingi 9,000 kwa

Gigabyte moja (GB 1) mwaka 2014. Hii imeshusha pia

gharama za biashara kwa kurahisisha mawasiliano na

malipo kati ya mabenki na kwa njia ya mtandao na simu.

Kwa upande wa laini za simu, zimeongezeka kutoka

laini milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 28 mwaka 2014.

Watu wanaotumia intaneti wameongezeka toka milioni 1.6

hadi milioni 9.3 mwaka 2014. Kukua kwa mawasilino ya

simu kumewezesha watumiaji milioni 12.3 kupata huduma

ya fedha kupitia simu za mkononi. Kati ya Julai 2013 na

Aprili 2014 jumla ya miamala milioni 972.6 ilifanyika yenye

thamani ya shilingi trilioni 28. Huu ni wastani wa zaidi ya

Page 72: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

72

shilingi trilioni 2 kwa mwezi na kufanya Tanzania

kuongoza duniani kwa huduma hii.

Mheshimiwa Spika;

Tulitambua kuwa makampuni binafsi ya simu

hayapendi kuwekeza vijijini ambako biashara si kubwa

kama mijini. Kwa kutambua umuhimu wa huduma ya

mawasiliano kwa maendeleo, Serikali iliamua ibebe mzigo

huo. Kwa sababu hiyo tumeanzisha Mfuko wa Mawasiliano

kwa Wote (UCSAF) ambao utawezesha kata na vijiji vyote

nchini kufikiwa na huduma za mawasiliano. Mfuko huo

umekwisha wezesha jumla ya kata 52 na vijiji 314 kufikiwa

na huduma hizo. Upelekaji wa huduma za mawasiliano

kupitia Mfuko huo zinaendelea kwa kata nyingine 163 zenye

vijiji 922, ambapo wananchi milioni 1.2 watanufaika.

Mheshimiwa Spika;

Tumechukua hatua ya kuhakikisha kuwa mianya ya

kodi inazibwa na kwamba makampuni yanalipa kodi stahiki

kwa kununua na kufunga mtambo wa Kusimamia

Page 73: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

73

Mawasiliano ya simu nchini. Mtambo huo unaowezesha

Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kukusanya takwimu

halisi za mawasiliano yanayofanywa. Tangu kuanza

kutumika kwa mtambo huo, mwaka jana Serikali imeweza

kukusanya shilingi bilioni 24.6 ambazo vinginevyo

zisingepatikana. Aidha, tumekuwa nchi ya kwanza Afrika

ya Mashariki kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda

digitali. Karibu tutakamilisha kwa mikoa yote. Tunazipokea

nchi kadhaa zinazokuja kujifunza kwetu juu ya uendeshaji

wa zoezi hili.

Ardhi na Makazi

Mheshimiwa Spika;

Maisha bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na

kuboresha makazi ya watu. Sote tunafahamu kuwa makazi

ni hitajio la msingi la binadamu. Lengo letu la kuboresha

huduma za ardhi, nyumba na makazi limepata mafanikio

makubwa. Tumepeleka huduma za utawala wa ardhi karibu

zaidi na wananchi kwa kuanzisha Kanda nane za

Page 74: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

74

kusimamia upangaji, upimaji na utoaji hatimiliki. Uamuzi

huu umepunguza lile tatizo la watu kuchelewa kupata hati

miliki. Toka 2006 hadi sasa jumla ya hati 164,275

zimetolewa, vijiji 10,500 vimepimwa na kati yake vijiji 10,341

vimepatiwa hatimiliki.

Mheshimiwa Spika;

Tumetunga Sheria kwa ajili ya kuwezesha upatatikanaji

wa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba. Sheria hizo ni

pamoja na Sheria ya Mikopo ya Nyumba (Mortage Finance)

na Sheria ya Kutambua Milki ya Sehemu ya jengo haswa

kwenye maghorofa (Unit Tittles Act) ya mwaka 2008. Sheria

hizi kwa ujumla wake zimewezesha watu wengi zaidi

kupata mikopo ya kujenga au kukarabati nyumba zao na

kuwawezesha watu kupata umiliki wa sehemu ya jengo.

Mabadiliko hayo pia yamewezesha sekta ya nyumba

kukua kwa kasi kubwa na majengo na nyumba za kisasa

kujengwa katika kipindi cha miaka 10 hii. Dar es Salaam ya

leo na ile ya 2005 ni tofauti kabisa. Shirika la Nyumba la

Page 75: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

75

Taifa, Wakala wa Nyumba za Serikali, Mifuko ya Hifadhi ya

Jamii nayo imefanya uwekezaji mkubwa sana katika ujenzi

wa nyumba katika kipindi hiki.

Mheshimiwa Spika;

Kwa upande wa watumishi wa serikali kuwa na

nyumba mwaka 2008 tulianzisha Mfuko wa Mkopo kwa

watumishi wa umma ambao hadi sasa umetoa mikopo ya

shilingi bilioni 5.4 kwa watumishi 1,169. Pia, tumeanzisha

Kampuni ya Mikopo ya Nyumba kwa ajili ya watumishi wa

umma ambayo tayari imeanza kazi.

Mheshimiwa Spika;

Ninayo furaha kueleza kuwa makazi ya wananchi pia

yameendelea kuwa bora. Takwimu za Sensa ya Watu na

Makazi ya Mwaka 2012, inaonyesha kuwa idadi ya nyumba

zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutoka asilimia 46

mwaka 2002 hadi asilimia 65 mwaka 2012. Kwa lugha

nyingine nyumba zilizoezekwa makuti na nyasi zimezidi

Page 76: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

76

kupungua. Haya ni mafanikio makubwa ya kutia moyo na

hatua muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania.

Utafiti

Mheshimiwa Spika;

Jambo lingine ambalo tumeliwekea msingi mzuri ni

eneo la utafiti. Hili ndilo eneo ambalo ilitalivusha taifa letu

kwenda katika maendeleo makubwa zaidi. Niliamua

Serikali ichukue hatua za makusudi za kufufua shughuli za

utafiti ambazo zilikuwa zinapita katika kipindi kigumu.

Niliamua kuwa Serikali ianze safari ya kutenga fedha za

kutosha kwa ajili ya utafiti. Tulianza na shilingi bilioni 10

na kuendelea kuongeza mwaka hadi mwaka na kufika

shilingi bilioni 60 mwaka 2014, katika kipindi cha kujitahidi

kufikia asilimia 1 ya bajeti ya Serikali na hatimaye asilimia 1

ya pato la Taifa kwa ajili ya shughuli za utafiti.

Mheshimiwa Spika;

Kwa kutumia kiasi hiki kidogo kilichopo wanasayansi

wetu 344 wamepata ufadhili wa masomo ya shahada ya

Page 77: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

77

Uzamili na 173 wa shahada ya Uzamivu. Miradi 70 ya

utafiti imefadhiliwa, kati ya hiyo 22 ni ya kilimo. Fedha hizi

pia zimewezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia

kuanzisha viatamizi vya teknohama ambavyo vimewezesha

vijana wetu kubuni na kuvumbua teknolojia zenye manufaa

kwa maendeleo ya jamii na taifa. Wamezalisha ajira na

kunufaisha watu wengi. Kampuni ya Max Malipo ni mfano

mmojawapo mzuri wa matokeo mazuri ya viatamizi hivi.

Huduma za Jamii

Elimu

Mheshimiwa Spika;

Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa

mwaka 2005 nilisema kuwa, “Hakuna Taifa lililopata

maendeleo bila kuendeleza elimu. Hivyo kuendeleza elimu

nchini itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya

Nne”. Tumetimiza ahadi. Katika kipindi chote cha miaka

kumi bajeti ya sekta ya elimu ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko

za sekta nyingine zote. Mwaka huu 2015 bajeti ya elimu

Page 78: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

78

imefikia shilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa na shilingi

bilioni 669.5 za mwaka 2005.

Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani

ya miaka 10 hii ni ya kutia moyo. Tumeongeza shule za

msingi kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,538 mwaka 2015

na wanafunzi wameongezeka kutoka 7,541,208 hadi

8,202,892. Upanuzi huu umewezesha asilimia 98 ya watoto

wanostahili kupata elimu ya msingi sasa kuandikishwa.

Kwa kushirikiana na wananchi na sekta binafsi

tumeongeza Shule za Sekondari kutoka Shule 1,745 mwaka

2005 hadi Shule 4,753 mwaka 2015. Idadi ya wanafunzi

imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056

mwaka 2015. Katika kipindi hiki pia vyuo vya Ufundi

vimeongezeka kutoka 184 mwaka 2005 hadi 744 mwaka

2015 na wanafunzi katika vyuo hivyo wameongezeka

kutoka 40,059 hadi 145,511 mwaka 2015. Haya ni mafanikio

makubwa sana.

Page 79: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

79

Kwa nia ya kuongeza ubora wa elimu, tumechukua

hatua thabiti za kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu,

vitabu, maabara za sayansi na vifaa vya kujifunzia na

kufundishia. Tumepanua mafunzo ya ualimu wa Cheti,

Stashahada na Shahada. Hii imetuwezesha kuongeza idadi

ya walimu wa Shule za Msingi kutoka 135,013 mwaka 2005

hadi 202,752 mwaka 2015, na walimu wa Shule za Sekondari

kutoka 18,754 mwaka 2005 hadi 88,908 mwaka 2015. Uhaba

wa walimu wa masomo ya sanaa si tatizo tena, tunao wa

kutosha. Tuna upungufu wa walimu 20,141 wa masomo wa

sayansi na hisabati. Ninaamini, hata hivyo, kwa programu

za kusomesha walimu wa sayansi vyuoni zilizopo, katika

miaka michache ijayo tatizo hili nalo tutalipatia ufumbuzi.

Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dodoma, mwaka 2014

kimeanza kudahili wanafunzi 5,000 wa ualimu wa masomo

ya sayansi.

Mheshimiwa Spika;

Page 80: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

80

Kwa upande wa maabara za sayansi, katika shule za

sekondari za kata tayari maabara 5,979 zimejengwa na

nyingine 4,410 ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.

Hivi sasa tunashughulikia upatikanaji na usambazaji wa

vifaa kwa matumizi ya maabara hizo. Kwa upande wa

vitabu tumeweza kuboresha upatikanaji wake kwa

mwanafunzi wa Shule za Msingi kutoka uwiano wa 1:5

mwaka 2005 hadi 1:3 mwaka 2015. Katika shule za sekondari

uwiano ni 1:2 ukilinganisha na 1:8 mwaka 2005.

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki pia tumeshuhudia upanuzi

mkubwa wa elimu ya juu nchini. Idadi ya vyuo vikuu

imeongezeka kutoka vyuo 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka

2015. Miongoni mwa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha

Dodoma na cha Nelson Mandela cha Arusha ambavyo

vimejengwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Tumeanza

mchakato wa kujenga Chuo Kikuu cha Julius Nyerere cha

Kilimo kule Butiama. Vyuo hivi ni fahari ya nchi yetu kwani

Page 81: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

81

tumevijenga kwa fedha zetu wenyewe bila msaada kutoka

kwa wafadhili. Ongezeko la vyuo vikuu limefanya idadi ya

wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi 40,719 mwaka

2005 hadi 218,959 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi

wanaonufaika na mikopo nayo imeongezeka kutoka

wanafunzi 16,345 mwaka 2005 hadi wanafunzi 99,590

mwaka huu.

Afya

Mheshimiwa Spika;

Tumepata mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa

kuboresha na kupanua huduma ya afya nchini. Tuliazimia

kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi watu kwa

kujenga vituo vya kutoa huduma ya afya vipya na

kuimarisha vilivyopo. Kati ya mwaka 2005 na 2014 vituo vya

kutolea huduma za afya 2,175 vimejengwa. Kati yake

hospitali 19, vituo vya afya 168 na zahanati 1,883

zimejengwa.

Page 82: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

82

Tumeimarisha hospitali ya Taifa ya Muhimbili,

Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa na Wilaya kwa

kuzipatia vifaa vya tiba na uchunguzi (MRI, CT Scan, X ray,

Ultra Sounds, Maabara n.k). Tumejenga maabara ya Taifa ya

Afya ya Jamii ambayo inatumika kama maabara ya

Kimataifa ya Rufaa kwa nchi za SADC. Tumeimarisha

maabara za mikoa kwa majengo na vifaa vya kisasa vya

uchunguzi wa magonjwa. Maabara yetu ya Mbeya sasa ina

uwezo wa kubaini virusi vya Ebola jambo ambalo miezi

michache iliyopita tulikuwa tunapeleka sampuli Nairobi.

Hivi sasa hospitali za wilaya zinaweza kufanya uchunguzi

wa mwenendo wa figo na ini.

Mheshimiwa Spika;

Tumeboresha huduma ya Afya ya Kinywa katika

Hospitali ya Muhimbili kwa kufunga mashine 26 za kisasa

za tiba ya meno na maabara ya kisasa ya kutengeneza meno

bandia. Pia tumeimarisha huduma ya afya ya kinywa kwa

kuweka vifaa vya tiba ya meno kwenye Halmashuri 91. Hivi

Page 83: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

83

sasa hospitali 136, vituo vya afya 63 na zahanati 3 zinatoa

huduma hiyo nchini.

Tumeanza kupata mafanikio katika dhamira yetu ya

kujenga uwezo wetu wa ndani wa kuchunguza na kutibu

maradhi ya figo, moyo, saratani na mishipa ya fahamu

ambayo tumekuwa tunapeleka wagonjwa wengi nje. Kwa

mfano, tangu Taasisi ya Moyo ianze kutoa huduma pale

Muhimbili wagonjwa 71,963 wamepatiwa matibabu

wakiwemo 692 waliofanyiwa upasuaji. Watu hao

wangepelekwa nje taifa lingelipa pesa nyingi. Uwezo wetu

utaongezeka sana hospitali ya Mloganzila itakapokamilika.

Mheshimiwa Spika;

Tumebadilisha utaratibu wa kusambaza dawa kutoka

Bohari ya Dawa. Tumeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba

kutoka shilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadi shilingi

bilioni 147 mwaka 2014. Idadi ya watu wanaonufaika na

Mfuko wa Afya ya Jamii na Mfuko wa Bima ya Afya

Page 84: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

84

wameongezeka kutoka asilimia 3 mwaka 2005 hadi asilimia

19 mwaka 2014.

Katika kipindi hiki tumetoa msukumo mkubwa katika

kupambana na maradhi makubwa ya kuambukiza

yanayosababisha vifo vya watu wengi. Tumeendesha

kampeni ya kupambana na malaria nchi nzima kwa

kubadilisha dawa ya kutibu malaria na kugawa vyandarua

26,371329 kwa watoto chini ya miaka mitano, kwa akina

mama wajawazito na katika kila kaya. Aidha, tumepulizia

dawa ya kuua mbu ndani ya nyumba katika mikoa ya kanda

ya ziwa. Matokeo ya jitihada hizo ni kupungua kwa

maambukizi ya malaria kwa asilimia 51 na vifo kwa

asilimia 71. Baada ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua

viluwiluwi vya mbu pale Kibaha kuanza uzalishaji, safari ya

kutokomeza malaria hapa nchini ni ya uhakika.

Mheshimiwa Spika;

Juhudi zetu katika kupambana na ukimwi

zimewezesha kushuka kwa maambukizi ya ukimwi kutoka

Page 85: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

85

asilimia 7.7 mwaka 2005 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012.

Idadi ya watu waliopima virusi vya ukimwi imeongezeka

kutoka 365,189 mwaka 2005 hadi 25,468,564 mwaka 2014.

Aidha, tumewezesha vituo 5,244 na asilimia 97 ya vituo

vyote vinavyotoa huduma ya uzazi kutoa huduma ya kuzia

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Mheshimiwa Spika;

Kati ya mwaka 2005 na 2014 tumeongeza udahili wa

wanafunzi katika vyuo vya afya kutoka 3,025 mwaka 2005

hadi 11,807 mwaka 2014. Katika kipindi hicho wataalamu

wa afya 55,608 wameajiriwa. Aidha, tumeongeza ajira ya

kada mbalimbali za afya. Kwa sababu hiyo idadi ya

madaktari imeongezeka kutoka madaktari 1,048 mwaka

2006 hadi madaktari 2,325 mwaka 2014. Halikadhalika,

madaktari wasaidizi wameongezeka kutoka 1,223 hadi

1,914, wauguzi kutoka 15,961 hadi 22,942 wataalamu wa

Maabara kutoka 1,277 hadi 2,378 mwaka 2014. Hivi sasa

uwiano wa Daktari kwa wagonjwa ni 1:6,666 ikilinganishwa

Page 86: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

86

na 1:35,714 mwaka 2005. Na, uwiano wa Muuguzi kwa

wagonjwa umeshuka kutoka 1:2,347 mwaka 2005 hadi

1:2,008 mwaka huu.

Mheshimiwa Spika;

Tumeendesha kampeni ya kuboresha lishe nchini na

kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Lishe (2011-2016). Kwa ajili

hiyo mwaka 2013 tulizindua Programu ya Uongezaji wa

Virutubishi. Matokeo ya jitihada zetu hizo yameanza

kuonekana. Udumavu umepungua toka asilimia 44 mwaka

2005 hadi asilimia 35 mwaka 2014 na uzito pungufu toka

asilimia 17 hadi asilimia 13.

Kwa jumla juhudi zetu za kuboresha huduma ya afya

zimezaa matunda ya kuridhisha. Wastani wa umri wa

kuishi wa Mtanzania umeongezeka toka miaka 49 mwaka

2005 hadi miaka 62 hivi sasa. Vifo vya watoto wachanga

vimepungua toka vifo 68 kwa kila vizazi hai 1000 hadi vifo

21 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2014. Vifo vya watoto

chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 112 kwa kila

Page 87: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

87

vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi vifo 54 kwa kila vizazi hai

1000 mwaka 2014, na vifo vya akinamama wajawazito

vimepungua toka vifo 578 kwa vizazi hai 100,000 hadi vifo

432 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2012. Haya ni mafanikio

ya kutia moyo ingawaje bado tunatakiwa kuendeleza juhudi

zaidi mara dufu ili vifo vipungue zaidi na zaidi.

Maji

Mheshimiwa Spika;

Serikali ya Awamu ya Nne imefanya juhudi kubwa

katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na

salama na usafi wa mazingira katika kipindi hiki.

Tumekamilisha miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa

8, Wilaya 6 na Miji midogo 2. Aidha, miradi katika miji

mingine 13 ya mikoa, 27 ya Wilaya na Miji midogo

inaendelea kutekelezwa. Utekelezaji wa miradi hii

umewezesha kiwango cha upatikanaji maji mijini kufikia

wastani wa asilimia 86 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia

73 mwaka 2005. Na kwa Vijijini imefikia asilimia 67.6

Page 88: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

88

Mwaka 2014 ukilinganisha na asilimia 53 mwaka 2005.

Tumevuka lengo letu la kuwapatia maji asilimia 65 ya

wakazi wa vijijini.

Aidha, miradi inayoendelea kutekelezwa hivi sasa

itakapokamilika katika mwaka huu wa fedha upatikanaji wa

maji mijini utafikia asilimia 90 ambalo ndilo lengo la Ilani ya

uchaguzi ya CCM. Vijijini inaweza kufikia asilimia 70

ambayo ni juu ya lengo la asilimia 65.

Aidha, tumeboresha huduma za uondoaji wa maji taka

katika miji ya Tanga, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa,

Songea, Tabora na Morogoro. Uboreshaji huu wa huduma

za utoaji wa maji taka ni mwanzo mzuri katika kuhakikisha

kwamba tunakuwa na mipango mizuri ya maji taka mijini.

Uwezeshaji wa Wananchi

Mheshimiwa Spika;

Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ilikuwa ni moja ya

dhima kuu ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005.

Katika kutekeleza dhamira hii, Serikali imeendeleza kwa

Page 89: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

89

mafanikio makubwa mifuko ya kutoa mikopo kwa vijana,

wanawake, wajasiriamali wadogo na kuanzisha fursa

nyingine mpya. Watu wengi wamenufaika na wao wenyewe

kuwa chachu ya kuzalisha ajira, kupunguza umasikini na

kuinua hali za maisha ya watu walioguswa na fursa

zilizopatikana.

Tumeiwezesha Benki ya Wanawake kuanza na

kuendelea kutoa huduma. Kama mjuavyo niliamua Serikali

ichangie mtaji wa mwanzo na inaendelea kuchangia mtaji

huo. Tayari Benki hiyo imeshakopesha watu 125,000 na kati

yao wanawake ni asilimia 82. Hali kadhalika, nilifanya

uamuzi wa makusudi wa kuifufua Benki ya Rasilimali (TIB).

Dhamira yangu ni kutaka iwepo Benki ya maendeleo

itakayotoa mikopo ya muda mrefu na wa kati kwa

wawekezaji wazawa. Hii itawezesha kuanzisha na

kuendesha shughuli za viwanda, madini, utalii na biashara

kwa urahisi.

Page 90: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

90

Tumeiwezesha Benki ya Rasilimali kwa mtaji, rasilimali

watu na vitendea kazi na kuifanya iwe moja ya benki ya

kutumainiwa nchini. TIB imeshatoa mikopo kwa

makampuni 365 yenye thamani ya shilingi bilioni 512.

Aidha, imetoa mikopo kwa miradi 201 yenye thamani ya

shilingi bilioni 156 kupitia dirisha dogo la kilimo. Natoa

pongezi maalum kwa viongozi na watumishi wa Benki ya

Rasilimali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya katika

kipindi hiki kifupi. Naomba waendelee na moyo huo kwa

maslahi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika;

Tumetimiza ahadi yetu ya kuimarisha ushirika nchini

kama nguzo kuu ya kuunganisha nguvu za wanyonge

kujiletea maendeleo. Katika kipindi hiki, idadi ya Vyama

vya Ushirika vya aina mbalimbali nchini imeongezeka

kutoka 5,832 mwaka 2005 hadi 9,604 mwaka 2015.

Kwa upande mwingine, Vyama vya Akiba na Mikopo

(SACCOS), vimeongezeka zaidi ya mara tatu kutoka vyama

Page 91: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

91

1,875 mwaka 2005 hadi 5,559 mwaka 2014. Akiba, hisa na

amana za wanachama zimeongezeka kwa zaidi ya mara

tano kutoka Shilingi bilioni 85.6 mwaka 2005/2016 hadi

Shilingi 463 bilioni mwaka 2014 na mikopo kwa

wanachama imekua mara 13 toka shilingi bilioni 65.7 hadi

shilingi bilioni 893 mwaka huu. Kwa hakika haya ni

mafanikio makubwa ya kujivunia. Watu wengi

wamewezeshwa kupunguza umasikini wao na wengine

kuondoka katika lindi la umasikini.

Sanaa na Michezo

Mheshimiwa Spika;

Niliahidi kusaidia kukuza michezo na sanaa nchini.

Kwa upande wa michezo niliahidi kuwa Serikali italipia

makocha. Nilitimiza ahadi yangu kwa michezo ya soka,

netiboli na ngumi. Kwa upande wa riadha tuliwapeleka

wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa

maandalizi ya mashindano ya kimataifa. Timu yetu ya taifa

ya soka haijafanya vizuri sana. Kwa upande wa soka

Commented [A2]: Source Baraza la Uwezeshaji

Page 92: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

92

tulianza kupata matumaini lakini baadae yakafifia. Timu

yetu ya taifa ya soka haijafanya vizuri sana pamoja na

kubadili makocha. Hata vilabu vyetu pia havifanyi vizuri.

Kwa kweli lazima Watanzania tukae chini na kujiuliza kwa

nini hatufanyi vizuri na tufanye nini tufanikiwe.

Mheshimiwa Spika;

Nilifanya uamuzi wa kurejesha michezo mashuleni

pamoja na mashindano ya michezo kwa shule za msingi na

sekondari (UMISHUMTA na UMISETA). Nia yetu ni kutaka

vipaji vya michezo vya vijana viibuliwe wakiwa bado

wadogo na kuendelezwa. Uamuzi huu umerejesha uhai na

matumaini kwamba siku za usoni tutaona matunda yake.

Kwa dhamira hiyo hiyo, kwa kushirikiana na Kampuni

ya Symbion Power na Klabu ya Soka ya Sunderland kituo

cha kuandaa wanamichezo wadogo kinajengwa pale

Kidongo Chekundu, Dar es Salaam. Kituo hiki kinatarajiwa

kuwa tayari ifikapo mwezi Septemba, 2015. Kikitumiwa

vizuri huenda ikawa ndiyo mwanzo wa safari ya uhakika ya

Page 93: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

93

kuendeleza soka hapa nchini. Tukifanikiwa Kidongo

Chekundu, vituo vingine kama hivyo vinaweza kuanzishwa

sehemu nyingine nchini na wadau mbalimbali.

Mheshimiwa Spika;

Tumepata mafanikio ya kuridhisha kwa upande wa

sanaa za filamu na muziki. Vijana wetu wa tasnia hizi

wamekuwa wanafanya vizuri kiasi kwamba leo hii Bongo

Flavor na Bongo Movie zimevuka mipaka ya Tanzania.

Zinaitangaza sanaa ya Tanzania, lugha ya Kiswahili pamoja

na nchi yetu. Vijana hawa wameitoa kimasomaso Tanzania

na kutufutia unyonge tunaopata kwenye michezo. Tasnia

hizi zimeajiri vijana wengi, wanalipa kodi na wanasaidia

sana katika kuhamasisha na kufikisha ujumbe kwa mambo

muhimu katika jamii.

Mheshimiwa Spika;

Kwa nia ya kutaka kuendeleza ujuzi, mbinu na maarifa

kwa wasanii wetu mwaka wa jana niligharimia timu ya

watu wazoefu wa fani za muziki na filamu kutoka Marekani

Page 94: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

94

kuja nchini kutoa mafunzo ya muda mfupi. Ninafanya

mipango waje tena kwani mafunzo ya mara kwa mara

yatawaimarisha wasanii wetu.

Kwa wasanii wa muziki niliwatimizia maombi yao ya

kutaka kuwa na mastering studio. Kwa wote nimefanya

jitihada kubwa ya kutafuta majawabu kwa tatizo sugu la

kupata malipo ya haki kwa kazi wazifanyazo. Tumetunga

Kanuni ambazo zimewezesha kazi za wasanii kutambuliwa

na kulindwa. Halikadhalika, tumeweza kuanza utaratibu

mpya wa kusambaza kazi za wasanii ambapo wao wenyewe

wana sauti nazo. Nitajitahidi katika kipindi kifupi

kilichobaki niyasukume kwa kasi masuala yaliyosalia ili

niwaache wasanii wetu mahali pazuri. Nataka wapate

malipo ya haki kwa vipaji vyao na jasho lao ili wainue hali

zao za maisha.

Page 95: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

95

Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Mheshimiwa Spika;

Wakati nalihutubia Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba

2005 niliahidi kwamba Serikali itafanya kila iwezalo

kuhakikisha Tanzania inakuwa na uhusiano mzuri na

mataifa mengine duniani, na mashirika ya kimataifa

na kikanda. Leo, miaka 10 baadae napenda

kuwahakikishia kuwa ahadi yetu tumeitekeleza, tena vizuri

kuliko tulivyotegemea. Tanzania ni rafiki wa kila nchi na

kila shirika la kanda na kimataifa. Hadhi yetu katika uso wa

kimataifa imepanda sana. Tunaheshimiwa, tunasikilizwa,

tunathaminiwa na kuaminiwa na mataifa makubwa na

madogo.

Katika kipindi hiki tumetembelewa na wageni wengi

mashuhuri kutoka mabara yote. Tumeweka historia kwa

kutembelewa mfululizo na Marais wawili wa Marekani

yaani Rais George W. Bush mwaka 2008 na Rais Barack

Obama mwaka 2013, na Marais wawili wa China Rais Hu

Page 96: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

96

Jintao mwaka 2009 na Rais Xi Jinping mwaka 2013. Pia

tulitembelewa na Wafalme, Marais, Mawaziri Wakuu na

Mawaziri kutoka nchi za Mabara yote duniani. Aidha,

tumetembelewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,

Rais wa Umoja wa Ulaya, Rais wa Benki ya Dunia n.k.

Tumeshirikishwa katika shughuli nyingi na mikutano

mingi. Nimepata fursa ya kushiriki katika mikutano

mbalimbali ya kimataifa pamoja na miwili ya G8

kuwakilisha Afrika. Nimewahi kushiriki na kupewa

dhamana ya uongozi katika kamati na Tume kadhaa za

Afrika na dunia. Nimewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa

Afrika (2008), Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za

Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mjumbe wa

Danish Africa Commission, Mwenyekiti wa ALMA. Hivi

karibuni nimeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja

wa Mataifa Kupendekeza Namna Bora kwa Dunia

Kushughulikia Majanga ya Afya.

Page 97: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

97

Mheshimiwa Spika;

Katika kipindi hiki tumefungua Balozi mpya 5 katika

nchi za Oman, Malaysia, Brazil, Uholanzi na Comoro. Hii

inafikisha idadi ya Balozi zetu kuwa 35. Pamoja na ufinyu

wa bajeti jitihada zimekuwa zinafanyika kuboresha huduma

kwa Balozi zetu na wanadiplomasia wetu. Tumejenga jengo

la Ubalozi New Delhi na kununua majengo ya ofisi ya kitega

uchumi Washington DC, New York na Ufaransa.

Tumeanzisha Kurugenzi ya Diaspora katika Wizara ya

Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ili

kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika

maendeleo ya nchi yetu.

Ushirikiano wa Kanda

Mheshimiwa Spika;

Tanzania imeendelea kuwa mwanachama mwaminifu

wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC, Umoja wa Afrika

na Umoja wa Mataifa. Tumepiga hatua kubwa katika

kuimarisha na kuendeleza utengamano wa Afrika

Page 98: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

98

Mashariki. Katika miaka 10 hii tumefanikiwa kukamilisha

utekelezaji wa Umoja wa Forodha tarehe 1 Januari, 2010 na

tarehe 1 Julai, 2010 tulianza utekelezaji wa Soko la Pamoja

ambao unaendelea hivi sasa. Tumetia saini Itifaki ya Umoja

wa Sarafu Novemba 2013 ambayo utekelezaji wake

unaendelea vizuri. Matunda ya utekelezaji wa utengamano

kiuchumi yameanza kuonekana. Kwa mfano, mauzo yetu

katika soko la Afrika Mashariki yameongezeka kutoka

bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 161

mwaka 2005 hadi bidhaa za Dola za Marekani bilioni 1.2

mwaka 2014. Uwekezaji nchini Tanzania kutoka nchi

wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki

umeongezeka toka miradi 35 yenye thamani ya Dola za

Marekani milioni 39.5 hadi miradi 244 yenye thamani ya

Dola za Marekani milion 676.5. Haya yote ni mafanikio

makubwa.

Mheshimiwa Spika;

Page 99: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

99

Kuhusu Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini Mwa

Afrika (SADC). Tumeendelea kushiriki kwa ukamilifu

katika shughuli za umoja huo. Tumeshiriki kwenye kutafuta

suluhisho la Visiwa vya Comoro, Madagascar, Zimbabwe na

DRC.

Salamu za Kuaga

Mheshimiwa Spika;

Tulipanga kufanya mengi na tumefanikiwa mengi,

lakini hatukuweza kuyamaliza yote kwa sababu ya

changamoto mbalimbali na kubwa zaidi ni uhaba wa

rasilimali fedha na wakati mwingine rasilimali watu na

vitendea kazi. Hata hivyo tumeweza kutekeleza zaidi ya

asilimia 88 ya ahadi zetu zilizomo kwenye Ilani za Uchaguzi

ya Chama cha Mapinduzi na mipango ya Serikali.

Siku moja nikiwa Marekani mwandishi mmoja wa

habari aliniuliza, je, utakapomaliza uongozi wako utapenda

Watanzania wakukumbuke kwa lipi? Nikamjibu, nitapenda

Watanzania waseme, “Rais Kikwete alitukuta kuleee! na

Page 100: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

100

sasa anatuacha hapa palipo juu”. Mimi na ninyi ni

mashahidi kuwa tulipo leo ni bora zaidi ya kule tulipokuwa

jana.

Changamoto za nchi haziishi kila siku zinaibuka mpya.

Kila ukimaliza moja inazaa changamoto nyingine. Hivyo

ndivyo ilivyokuwa kwa baba wa taifa ambaye naye

hakumaliza changamoto zote, ndivyo ilivyokuwa kwa Mzee

Mwinyi na hivyo ndivyo alivyoniachia Rais Mkapa. Nami

namwachia anayekuja, naye afanye yake na yatakayobakia

atamwachia atakayemfuatia. Jambo linalonipa faraja ni

kuwa nami nimetoa mchango wangu kwa maendeleo ya

nchi yetu na watu wake.

Shukrani

Mheshimiwa Spika;

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipokushukuru

Mheshimiwa Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal

kwa msaada wako, ushauri wako na ushirikiano wa karibu

ulionipatia katika kipindi hiki cha miaka 5. Nakutakia kila

Page 101: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

101

la heri katika maisha yako baada ya mimi na wewe

kumaliza kipindi chetu cha uongozi. Namshukuru Rais wa

Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, ambaye pia alikuwa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano katika kipindi

changu cha kwanza. Nakushukuru kwa ushirikiano wako

mkubwa, msaada wako na ushauri wako wa hekima na

busara ambao umewezesha mafanikio tuliyoyapata katika

kujenga nchi yetu na katika kuimarisha muungano wetu.

Kwa namna ya pekee namshukuru Mheshimiwa

Mizengo Kayanza Pinda, Waziri Mkuu na Kiongozi wa

shughuli za Serikali Bungeni kwa kazi nzuri na ya kutukuka

uliyoifanya katika kipindi cha miaka 8. Umepita katika

misukosuko mingi, na wakati mwingine umebebeshwa

lawama isiyokuwa yako. Daima umeonyesha ukomavu,

uimara na kutotetereka. Napenda pia kumtambua

Mheshimiwa Edward Lowassa ambaye katika kipindi kifupi

alichokuwa Waziri Mkuu alifanya kazi kubwa na nzuri.

Page 102: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

102

Nawashukuru pia Mawaziri, Manaibu Mawaziri,

Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa

Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Watendaji na

watumishi wote wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa

mchango wao katika kufanikisha majukumu ya Awamu ya

Nne. Mmenisaidia sana. Kwa kweli mafanikio haya

tunayozungumza leo yameletwa na juhudi zenu.

Nawashukuru viongozi wa dini, asasi za kiraia na

vyombo vya habari kwa kuniunga mkono mimi na Serikali

yangu na kwa mchango wenu muhimu. Nawaomba

muendelee kuilea amani ya nchi yetu na watu wake.

Nakishukuru Chama changu, Chama cha Mapinduzi

kwa kuniamini, kuniunga mkono na kunisaidia kwa karibu,

katika miaka yote hii kumi. Wakati wote CCM imekuwa

pamoja nami na Serikali. Kimetoa uongozi wa nchi na

kuisimamia Serikali kutekeleza Ilani.

Mwisho lakini sio mwisho wa umuhimu, naishukuru

sana familia yangu. Namshukuru mke wangu Bi. Salma

Page 103: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

103

Kikwete kwa mchango wake mkubwa ulionipa utulivu wa

kutekeleza majukumu yangu. Upo msemo kwamba, “kwa

kila mwanaume mwenye mafanikio, yuko mwanamke”,

nawaambia ni kweli. Shukrani zangu, pia, kwa wanangu na

wajukuu zangu kwa kunivumilia pale walipomkosa baba

yao na babu yao. Karibuni mambo yatakuwa tofauti

mtaniona mara kwa mara kiasi kuwa huenda mkanichoka.

Hitimisho

Mheshimiwa Spika;

Ninapoagana na Bunge letu natambua kuwa baadhi ya

Wabunge mnarudi kutetea viti vyenu nawatakia kila la

kheri. Nimewahi kuwa Mbunge, hivyo naelewa hofu na

mashaka mliyonayo. Mwenyezi Mungu awape utulivu na

subira. Nawatakia mapumziko mema kwa wale ambao

mmeamua kustaafu. Wale wanaogombea Urais waliomo

humu nawatakia kila la kheri, na nawashukuru kwa

kuonyesha nia ya kunipokea mzigo huu mzito.

Nawatakiwa heri katika matamanio yenu.

Page 104: HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS … · 2015-07-10 · ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na mpasuko

104

Kwa ndugu zangu Watanzania wenzangu,

nawashukuruni kwa kuniamini na kunichagua mara mbili

kuwa kiongozi wa nchi yetu. Nawashukuru kwa kuniunga

mkono wakati wote wa uongozi wangu. Mmenipa heshima

kubwa ambayo sitakaa nisahau maishani mwangu.

Ninamaliza kipindi changu cha uongozi nikiwa nawapenda

sana na nitaendelea kuwapenda mpaka siku Mwenyezi

Mungu atakaponiita. Nitawa-miss kama mtumishi na

kiongozi wenu mkuu lakini tutakutana kwa urahisi zaidi

nikiwa raia. Baada ya hotuba yangu ndefu, sasa natangaza

kuwa Bunge la 10 limevunjwa rasmi, lakini linabakia kuwa

hai mpaka tarehe itakayotangazwa rasmi kwenye Gazeti la

Serikali kwa mujibu wa Katiba.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Asanteni kwa kunisikiliza!