ijumaa | juni 28-julai 04 | 2019 habari taifa stars ......2019/06/03  · kumbe mchumba wa ngwea...

1
3 Ijumaa | Juni 28-Julai 04 | 2019 HABARI ZARI, MOBETO VITA MPYA! Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA M APEMA wiki hii Mbongo- Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alifunguka mengi kiasi cha kuibua vita mpya baina ya wanawake aliozaa nao, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mjasiriamali wa nchini Uganda na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto. Vita hiyo imeibuka baina ya mashabiki wa Zari na wale wa Mobeto baada ya Diamond kusema kuwa Mobeto ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Dylan ni mwelewa kwani baada ya kuachana kilichobaki anatoa matumizi ya mtoto kama baba licha ya hapo awali kusumbuana kidogo. Kwa upande wa Zari aliyezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan alisema hataki kuelewa kwamba wameachana kwani ‘ame-mblock’ kila sehemu ili asiweze kuwaona watoto wake wakati yeye ni baba mwelewa na anayewapenda watoto wake. “Kwenye suala la watoto niko makini sana, ninahakikisha chochote nitakachoweza kumfanyia, nimfanyie, kuhusu watoto wangu ni kwamba mama yao (Zari) alini-block, ikabidi nikae kimya, naamini hasira zake zitaisha siku moja, wa hapa (Mobeto) alinielewa japo mwanzo tulisumbuana kidogo,” alisema Diamond. Kutokana na maelezo hayo ya Diamond ilizuka vita ya maneno kwa pande hizo mbili yaani Timu Mobeto na Timu Zari ambapo walianza kupondeana huku wale wa Mobeto wakimtaka Zari akubali kuachika kama Mobeto alivyokubali na kukaa pembeni. TAIFA STARS YAMWEKA... Stori: ERICK EVARIST, IJUMAA D AR ES SALAAM: Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imemuweka njia panda mrembo wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ashindwe kujua asimame upande gani kati ya Taifa Stars na timu ya nchini kwao, Harambee Stars. Kwa mujibu wa chambuzi mbalimbali zilizofanywa na mitandao tofauti ya nchini Kenya, presha ya Tanasha itakuwa juu kabla na hata baada ya mechi iliyotarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia leo na kuzikutanisha timu hizo mbili. “Yaani kwa kweli Stars inamuweka mtegoni Tanasha maana anapaswa kumsapoti mpenzi wake na wakati huohuo Harambee ni timu ya kwao. “Bahati mbaya sana mechi hiyo ndiyo inatoa picha ya nani ana matumaini ya kusonga mbele, kwa vyovyote vile Tanasha hatakuwa na nguvu ya kushangilia ushindi wa Stars na pia hatakuwa na ujasiri wa kuufurahia sana ushindi wa Harambee,” ulichambua mmoja wa mitandao hiyo. Hata hivyo, licha ya maoni hayo kutikisa sana kwenye mitandao ya kijamii, Tanasha ameonekana kuwa kimya na mzito kuonesha upande wake wakati Diamond mara kadhaa ameonekana kujipambanua kwa kuiunga mkono Taifa Stars. Taifa Stars na Harambee Stars wanashiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Misri ambapo mataifa hayo mawili yapo katika moja la Kundi C. Katika kundi hilo, wapo pia na Senegal na Algeria ambao nao walitarajiwa kuumana mapema jana kabla ya Taifa Stars na Harambee Stars hawajapepetana mishale ya saa 5:00 usiku. Katika michezo ya awali, Taifa Stars ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal huku Harambee nayo ikiruhusu kichapo cha mabao kama hayohayo kutoka kwa Algeria. Kumbe mchumba wa Ngwea alisepa zake! M orogoro: Miaka sita baada ya kifo cha aliyekuwa staa wa muziki wa HipHop Bongo, Albert Mangweha ‘Ngwea’, imeelezwa kuwa aliyekuwa mchumba’ke, Misheily, raia wa Ufaransa alisepa miaka miwili baada ya kifo hicho. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, mama mzazi wa Ngwea, Denisia Magweha alisema kuwa, aliishi vizuri mno na Misheily, lakini tangu alipoondoka hakurejea. “Tuliishi vizuri sana na Misheily, alikuwa akinifariji sana na alikuwa na roho nzuri sana. “Alipoondoka alisema angerejea na kweli alikuwa akiwasiliana vizuri na dada zake Albert (Ngwea). “Lakini baadaye mawasiliano yalikatika na hatujui yupo wapi, kama anaweza kupata taarifa, ajue tu kwamba tunamkumbuka, tunaamini kuna siku atarejea,” alisema mama Ngwea na kumaliza maswali juu ya alipo Misheily. Ngwea aliyekuwa mkali wa freestyle Bongo alifariki dunia Mei 28, 2013 huko nchini Afrika Kusini ambapo kifo chake kiliibua utata mkubwa. Stori: DUNSTAN SHEKIDELE, IJUMAA Mbasha: Mimi na mwanangu ni vijana! Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA D AR ES SALAAM: Staa wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amefunguka kuwa anawashangaa wanaomsema vibaya anapojiachia na mwanaye, Elizabeth Emmanuel ‘Lizy’ na kwamba yeye na mwanaye ni vijana ndiyo maana wanafanya vitu vya ujana. Mbasha alisema kuwa, amekuwa akimuonesha upendo wa hali ya juu mwanaye huyo kwani wanakaribia kulingana kwa kuwa alimzaa mwaka 2004 yeye akiwa bado na umri mdogo. “Watu wanasema ooh...kwa nini ninakwenda kulala hotelini na mwanangu... kwani walitaka nikalale na nani? “Walitaka nikalale na vimada? Wengine wanahoji kulala hotelini, kwani walitaka tukalale gesti? “Mimi na mwanangu tunapendana na ndiyo maana ninampa mwanangu malezi bora ya baba,” alisema Mbasha ambaye hivi karibuni alitawala mitandaoni kutokana na pozi alizokuwa akiweka na mwanaye huyo wakiwa sehemu za kula bata.

Upload: others

Post on 10-Feb-2021

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 3Ijumaa | Juni 28-Julai 04 | 2019 HABARI

    ZARI, MOBETO

    VITA MPYA!Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

    MAPEMA wiki hii Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alifunguka mengi kiasi cha kuibua vita mpya baina ya wanawake aliozaa nao, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mjasiriamali wa nchini Uganda na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto.

    Vita hiyo imeibuka baina ya mashabiki wa Zari na wale wa Mobeto baada ya Diamond kusema kuwa Mobeto ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Dylan ni mwelewa kwani baada ya kuachana kilichobaki anatoa matumizi ya mtoto kama baba licha ya hapo awali kusumbuana kidogo.

    Kwa upande wa Zari aliyezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan alisema hataki kuelewa kwamba wameachana kwani ‘ame-mblock’ kila sehemu ili asiweze kuwaona watoto wake wakati yeye ni baba mwelewa na anayewapenda watoto wake.

    “Kwenye suala la watoto niko makini sana, ninahakikisha chochote nitakachoweza kumfanyia, nimfanyie, kuhusu watoto wangu ni kwamba mama yao (Zari) alini-block, ikabidi nikae kimya, naamini hasira zake zitaisha siku moja, wa hapa (Mobeto) alinielewa japo mwanzo tulisumbuana kidogo,” alisema Diamond.

    Kutokana na maelezo hayo ya Diamond ilizuka vita ya maneno kwa pande hizo mbili yaani Timu Mobeto na Timu Zari ambapo walianza kupondeana huku wale wa Mobeto wakimtaka Zari akubali kuachika kama Mobeto alivyokubali na kukaa pembeni.

    TAIFA STARS YAMWEKA...Stori: ERICK EVARIST, IJUMAA

    DAR ES SALAAM: Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imemuweka njia panda mrembo wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ashindwe kujua asimame upande gani kati ya Taifa Stars na timu ya nchini kwao, Harambee Stars.

    Kwa mujibu wa chambuzi mbalimbali zilizofanywa na mitandao tofauti ya nchini Kenya, presha ya Tanasha itakuwa juu kabla na hata baada ya mechi iliyotarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia leo na kuzikutanisha timu hizo mbili.

    “Yaani kwa kweli Stars inamuweka mtegoni Tanasha maana anapaswa kumsapoti mpenzi wake na wakati huohuo Harambee ni timu ya kwao.

    “Bahati mbaya sana mechi hiyo ndiyo inatoa picha ya nani ana matumaini ya kusonga mbele, kwa vyovyote vile Tanasha hatakuwa na nguvu ya kushangilia ushindi wa Stars na

    pia hatakuwa na ujasiri wa kuufurahia sana ushindi wa Harambee,” ulichambua mmoja wa mitandao hiyo.

    Hata hivyo, licha ya maoni hayo kutikisa sana kwenye mitandao ya kijamii, Tanasha ameonekana kuwa kimya na mzito kuonesha upande wake wakati Diamond mara kadhaa ameonekana kujipambanua kwa kuiunga mkono Taifa Stars.

    Taifa Stars na Harambee Stars wanashiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Misri ambapo mataifa hayo mawili yapo katika moja la Kundi C.

    Katika kundi hilo, wapo pia na Senegal na Algeria ambao nao walitarajiwa kuumana mapema jana kabla ya Taifa Stars na Harambee Stars hawajapepetana mishale ya saa 5:00 usiku.

    Katika michezo ya awali, Taifa Stars ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal huku Harambee nayo ikiruhusu kichapo cha mabao kama hayohayo kutoka kwa Algeria.

    Kumbe mchumba wa Ngwea alisepa zake!

    Morogoro: Miaka sita baada ya kifo cha aliyekuwa staa wa muziki wa HipHop Bongo, Albert Mangweha ‘Ngwea’, imeelezwa kuwa aliyekuwa mchumba’ke, Misheily, raia wa Ufaransa alisepa miaka miwili baada ya kifo hicho.

    Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, mama mzazi wa Ngwea, Denisia Magweha alisema kuwa, aliishi vizuri mno na Misheily, lakini tangu alipoondoka hakurejea.

    “Tuliishi vizuri sana na Misheily, alikuwa akinifariji sana na alikuwa na roho nzuri sana.

    “Alipoondoka alisema angerejea na kweli alikuwa akiwasiliana vizuri na dada zake Albert (Ngwea).

    “Lakini baadaye mawasiliano yalikatika na hatujui yupo wapi, kama anaweza kupata taarifa, ajue tu kwamba tunamkumbuka, tunaamini kuna siku atarejea,” alisema mama Ngwea na kumaliza maswali juu ya alipo Misheily.

    Ngwea aliyekuwa mkali wa freestyle Bongo alifariki dunia Mei 28, 2013 huko nchini Afrika Kusini ambapo kifo chake kiliibua utata mkubwa.

    Stori: DUNSTAN SHEKIDELE, IJUMAAMbasha: Mimi na mwanangu ni vijana!

    Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

    DAR ES SALAAM: Staa wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amefunguka kuwa anawashangaa wanaomsema vibaya anapojiachia na mwanaye, Elizabeth Emmanuel ‘Lizy’ na kwamba yeye na mwanaye ni vijana ndiyo maana wanafanya vitu vya ujana.

    Mbasha alisema kuwa, amekuwa akimuonesha upendo wa hali ya juu mwanaye huyo kwani wanakaribia kulingana kwa kuwa alimzaa mwaka 2004 yeye akiwa bado na umri mdogo.

    “Watu wanasema ooh...kwa nini ninakwenda kulala hotelini na mwanangu...kwani walitaka nikalale na nani?

    “Walitaka nikalale na vimada? Wengine wanahoji kulala hotelini, kwani walitaka tukalale gesti?

    “Mimi na mwanangu tunapendana na ndiyo maana ninampa mwanangu malezi bora ya baba,” alisema Mbasha ambaye hivi karibuni alitawala mitandaoni kutokana na pozi alizokuwa akiweka na mwanaye huyo wakiwa sehemu za kula bata.