imeandaliwa na fatuma semgaya kituo cha sheria na haki za binadamu

23
Mazingira ya Haki za Wanawake Tanzania na Mapendekezo ya Haki za Wanawake kwenye Katiba mpya . Imeandaliwa na Fatuma Semgaya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

Upload: dyani

Post on 11-Jan-2016

137 views

Category:

Documents


37 download

DESCRIPTION

Mazingira ya Haki za Wanawake Tanzania na Mapendekezo ya Haki za Wanawake kwenye Katiba mpya. Imeandaliwa na Fatuma Semgaya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Utangulizi. - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

PowerPoint Presentation

Mazingira ya Haki za Wanawake Tanzania na Mapendekezo ya Haki za Wanawake kwenye Katiba mpya.Imeandaliwa naFatuma SemgayaKituo cha Sheria na Haki za Binadamu.UtanguliziTanzania ni miongoni mwanchi za Afrika ambazo zimeridhia mikataba ya kimataifa mbalimbali ambazo zinawalinda wanawake kwa namna moja au nyingine.Ipo mikataba ya kimataifa na ya kibara tofauti tofauti inayo ainisha Haki za wanawake Kwa leo tunaangalia mazingira ya haki za Wanawake Tanzania,kuna sheria ambazo zinazowalinda wanawake Tanzania naHaki za Wanawake kwenye sheria za TanzaniaKatiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Ibara ya 12(usawa wa binadamu), Ibara ya 13 (Usawa mbele ya sheria - ubaguzi)Sheria ya ndoa, sura ya 29. Kifungu 66 (kinakataza kumchapa viboko mwenzi katika ndoa. Hivyo endapo mtu atamchapa mkewe ama mumewe ni kosa kisheria)Sheria ya Kuzuia Maambukizi ya Ukimwi(kulinda maambukizi ya kusudi, usiri wa taarifa)Sheria ya kuzuia Usafirishaji wa Watu ya mwaka 2008Haki za Wanawake.Sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 mabadiliko ya 1998 (k.130 ubakaji, k.135 shambulio la aibu, k.138 A-D unyanyasaji wa aina zote,k157 kufanyamapenzi kinyume cha maumbile, k.169A ukeketaji ). Pia kinaainisha aina nyingine za makosa kama Kupigana, kuumizana, k.89A kutoa vitisho, K.240 -243 mashambulioMazingira yanayopelekea ukiukwaji wa Haki za Wanawake TanzaniaVitendo vya ukatili wa Kijinsia kama ambavyo vilivyoainishwa kwenye Tamko la Umoja wa Mataifa la Uondoshaji wa Ukatili Dhidi ya Wanawake la mwaka 2005 ( the United Nations Declaration on the Elimination of Violence against Women (UNFPA, 2005)], limetafsiri Ukatili kumaanisha:

Kitendo chochote cha ukatili kuhusu jinsia, ambacho kinaweza kusababisha madhara/maumivu ama mateso ya kimwili au kisaikolojia kwa mwanamke, ikiwa ni pamoja na vitendo vya kutishia, kulazimisha, kunyima uhuru, bila kujali vimefanywa kisiri ama kwenye kadamnasi.

Vitendo ya ukatili kwa wanawake.Ukatili wa kutumia nguvu(kumpiga makofi, mateke, na kumchapa)-Ukatili wa kisaikolojia(kusema mambo yanayoKufanya kujisikia mdogo,kukunyanyasa, kukusimanga ) kulazimisha na kushinikiza kufanya naye mapenzi/tendo la ndoa

Inaendelea.Ukatili wa kiuchumi (kukunyima mahitaji muhimu na fedha za kujikimu, kukuzuia kufanyakazi)

Kukuweka chini yake (kukuweka mbali na ndugu au marafiki, kuchunguza mwenendo wako, kusimamia na kuzuia upatikanaji wako wa taarifa au msaada)Ukatili unaotokana na mila na desturi :Ukeketaji - Kitendo cha kukata kidogo au kuondoa kabisa sehemu ya uzazi ya mwanamke au msichana kwa sababu zozote zile.

Inaendelea.Ndoa za utotoni - ndoa inayofungwa ambayo mmoja wa wanandoa hajafikisha umri wa utu uzima, unaosababisha ashindwe kufanya maamuzi mwenyewe, juu ya afya yake ya uzazi, mwenzi wake, kumkosa kusoma, kipato. Hii ni moja ya sababu zinazosababisha ukatili kwa wanawake na pia ni ukatili.Utakasaji na kurithi wajaneMauaji ya vikongweUsafirishaji wa watu (wanawake na watoto)

Mapendekezo ya Haki za Wanawake kwenye KatibaBaada ya kuangalia sheria na mikataba ambayo inalinda haki za Wanawake Tanzania na mazingira yanayopelekea ukiukwaji wa Haki za Wanawake, mchakato wa Katiba ni nafasi muhimu ya kutoa mapendekezo ya kufanya mabadiliko katika Katiba mpya.Katiba ya sasa haijaelezea haki za Wanawake kwa upana wake kwahiyo tumeainisha mapendekezo yanayohusu haki za wanawake kwenye Katiba mpya.

Mapandekezo ya Jumla.

Katiba ya nchi lazima iainishe kwa ufasaha misingi yote ya Haki za Binadamu yaani (Kisiasa, kiraia, kiuchumi, na kijamii na kimaendeleo kuweka ulinzi madhubuti wa haki hizo.

Katiba iainishe na kutoa ulinzi wa haki za makundi hususani haki za wanawake na watoto

Inaendelea.Ionyeshe kuwa Mahakama zote zinaweza kusikiliza Mashauri ya uvunjwaji wa Haki za Binadamu.

Katiba iainishe kutokuwepo na muuingiliano wa mihimili ya dola yaani Mahakama, Serikali na Bunge.

Katiba iainishe kuwa mapato yatokanayo na Rasilimali za taifa yawanufaishe wananchi hasa maeneo yanayopatikana rasilimali hizoHAKI ZA KIJAMIIKatiba ianinishe kuwa watu wote wana haki ya kupata huduma bora za : Afya Maji Safi na Salama Elimu Makazi Bora .Kuwaka na utengwaji wa bajeti endelevu kwenye sekta za huduma mbalimbali za kijamii jamii.

Mwanamke kuthaminiwa na kupewa ulinzi wa utu na ubinadamu wake.

InaendeleaKuwalinda wanawake dhidi ya manyanyaso yote yakiwemo ya Kijinsia na kutoa adhabu kwa watendaji wa vitendo hivyo.

Kuondoa aina zote za Ubaguzi na unyanyasaji wa Kijinsia hasa kwa walemavu, wanawake na watoto

Kutungwa kwa sheria zinazomlinda mtu dhidi ya kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza ama kumdhalilisha.

HAKI ZA KISIASA:Kuwe na uwiano sawa wa Kijinsia asilimia 50/50 katika ngazi zote za maamuzi kama vile: - Bunge - Mahakama - Nafasi mbalimbali za uteuzi kama Makatibu wakuu, - mawaziri, - manaibu waziri, mabalozi n.k. - Madiwani Serikali za vijiji, miji na mitaaKuwepo na jitihada chanya za kurekebisha mfumo ili kuwa na usawa katika ngazi zote za maamuzi.

Serikali kutunga Sheria itakayo hakikisha kuwa wanawake wanashiriki bila ya Ubaguzi katika chaguzi zote.

Inaendelea..Katiba kuainisha kuwa kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa anachopenda.

Katiba kuainisha kuwa viongozi kutojilimbikizia mali wakati wa uongozi wao.Kuwepo na ukomo wa wabunge.

Mawaziri wachaguliwe kulingana na taaluma zao na vilevile wasichaguliwe kutokana na wabunge.

HAKI ZA KIUTAMADUNI:

Mwanamke kulindwa dhidi ya mila na desturi kandamizi na kuwepo kwa sheria za kumpa ulinzi mwanamke dhidi ya mila hizo.

Kuondoa na kubadilisha sheria zote za kibaguzi na kandamizi dhidi ya mwanamke zilizopo sasa mfano sheria ya mirathi, ndoa, sheria ya Uraia.

Kuweka ulinzi wa haki za Wazee dhidi ya Ubaguzi, mali na kunyanganywa

HAKI ZA KIUCHUMI:

Kutoa haki na kuhakikisha mwanamke anakuwa na haki ya kupata na kumiliki Rasilimali kama :Ardhi/UrithiMadiniMazao aliyolima mwenyewe.Pato lake

Katiba kutambua haki za wajane katika : - Kurithi mali - Kulea watoto wake. -Kuishi kwenye nyumba ya familia. -Haki ya kuolewa tena.

Inaendelea..Wanawake wapewe fursa na usawa katika ajira, na kuwa na uwiano wa ujira anaolipwa kati ya wanawake na wanaume.

Haki ya ulinzi kwa wanawake na kuwawekea mazingira mazuri kutokana na mahitaji yao.

Maliasili zote za nchi ziwe chini ya mamlaka ya wananchi ili Kuwepo na kuhifandhi na ulinzi kwa kutoweka wawekezaji wanyonyaji.

Inaendelea.Katiba iainishe kwa kuweka wazi mbele ya wananchi mikataba yote inayohusiana na uvunaji na matumizi ya Rasilimali za taifa .

Wananchi washirikishwe katika uwekezaji na umiliki wa ardhi ya umma na mamlaka yasiwe mikononi mwa rais tu.

HAKI ZA KIRAIA.Kuwepo kwa Mahakama ya kifamilia ili iweze kutatua matatizo ya kifamilia kwa haraka na wakati.

Katiba kuainisha haki ya watu kuwa na Uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zao.

Haki ya kupata taarifa kwa wakati kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za umma pamoja na mikataba yote iliyoingia baina ya serikali na wawekezaji.

Inaendelea..Katiba iainishe jukumu la serikali kutoa taarifa kwa wananchi.

Katiba iainishe kuwa watu wanastahili kuwa na Uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini.

Haki ya wanawake kushiriki katika shughuli za umma na kuweka jukumu kwa vyombo husika kuhakikisha ushiriki huo.

Kutoa jukumu kwa serikali kutekeleza mikataba ya kimataifa ya haki za Binadamu na haki za wanawake pindi inaporidhiwa na utekelezaji wa majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye mikataba hiyo.

HitimishoKwa kuhitimisha, tumeangalia sheria zinazolinda wanawake,na zinazowakandamiza wanawake ni jukumu letu sasa kutumia fursa tuliyonayo kupendekeza haki muhimu kuingia katika katiba mpya kwa kuangalia haki za msingi ambazo haziko kwenye katiba mpya.Pamoja tunaweza kulinda na Kutetea Haki za Wanawake