jamhuri ya muungano wa tanzania · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za...

54
i JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA MKANGA 1 MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI WA KIJIJI, KATA YA TANDANGONGORO, TARAFA YA NG’APA, MANISPAA YA LINDI, MKOA WA LINDI IMEFADHILIWA NA: SERIKALI YA NCHI YA NORWAY KUPITIA MRADI WA MKUHUMI KWA AJILI YA JAMII NA MAENDELEO YA MISITU UNAOTEKELEZWA NA TFCG NA MJUMITA JULAI, 2011

Upload: others

Post on 04-Feb-2020

17 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

i

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA MKANGA 1

MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI WA KIJIJI, KATA YA TANDANGONGORO, TARAFA YA NG’APA, MANISPAA

YA LINDI, MKOA WA LINDI

IMEFADHILIWA NA:

SERIKALI YA NCHI YA NORWAY KUPITIA MRADI WA MKUHUMI KWA AJILI YA

JAMII NA MAENDELEO YA MISITU UNAOTEKELEZWA NA TFCG NA MJUMITA

JULAI, 2011

Page 2: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

ii

MUHTASARI WA UTENDAJI

Kijiji cha Mkanga1 kipo katika Kata ya Tandangongoro Tarafa ya Ng’apa Manispaa ya Lindi Mkoa wa Lindi, eneo lake lipo kati ya jira 555385 na 564099 Mashariki na 8898270 na 8904654 Kaskazini. Kijiji cha Mkanga I ni miongoni mwa vijiji 134 vya Wilaya ya Lindi.

Ni kijiji cha asili na kina vitongoji vitatu (4) ambavyo ni Kilangalamatu, Mkanga juu, Mandanje na Mkanga chini. Kwa upande wa kaskazini kinapakana na kijiji cha Chikonji, mashariki kinapakana na kijiji cha Kineng`ene na Ng`apa, magharibi kinapakana na kijiji cha Mkombamosi na Nandambi, upande wa kusini kinapakana na kijiji cha Ng`apa na Nandambi. Kijiji kina ukubwa wa hekta 2475.24.

Kijiji cha Mkanga1 kinakabiliwa na matatizo yafuatayo: ukosefu wa zahanati, barabara inayopitika mwaka mzima, ukosefu wa maji safi na salama, upungufu wa madarasa, walimu na nyumba za walimu, ukosefu wa soko la kuuzia mazao, wanyama waharibifu wa mazao, ukosefu wa ofisi ya kijiji na ukosefu wa masjala ya ardhi ya kijiji.

Matatizo haya yanayowakabili wanakijiji wa Mkanga1 yanaweza kuisha iwapo fursa zilizopo ndani ya kijiji na nje ya kijiji zitatumika ipasavyo. Fursa zilizopo kijijini ni pamoja na ardhi ya kutosha na yenye rutuba, maeneo ya malisho, misitu ya asili, wataalam ngazi ya kijiji, uongozi, (serikali ya kijiji pamoja na Halmashauri ya kijiji), kamati mbalimbali za kijiji, maliasili na rasilimali za ardhi kama vile uoto, maji, udongo nguvu kazi n.k.

Matumizi bora endelevu yatasaidia kupunguza matatizo hayo, Sheria zitawezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya rasilimali za ardhi zilizopo kijijini. Sheria zinazohusika ni kama vile sheria za Ardhi, sheria za maji, sheria za misitu n.k. katika kutatua matatizo yanayo kikabili kijiji na kuwa na matumizi endelevu ya maliasili na rasilimali zilizopo.

Katika kijiji cha Mkanga1 wanakijiji wamependekeza matumizi ya ardhi yafuatayo:- Eneo la kilimo, eneo la vyanzo vya maji, eneo la makazi, miundombinu, eneo la msitu wa hifadhi, eneo la malisho na eneo la huduma za jamii.

Page 3: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

iii

SHUKURANI

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Timu ya Matumizi Bora ya Ardhi ya Wilaya (PLUM) na wataalam kutoka TFCG/MJUMITA wanatoa shukrani za dhati kwa mchakato wa kuwawezeha wananchi wa kijiji cha Mkanga1 kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji.

Mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji ni mojawapo ya misingi muhimu ya kuwawezesha wanakijiji kuwa na mafanikio ya uhakika katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii. Aidha, mpango huu ni nyenzo muhimu ambayo haina budi kutumika katika kufanikisha malengo ya matumizi na uhifadhi endelevu wa ardhi na rasilimali zake zote katika ngazi ya kijiji. Shukrani za pekee ziwaendee Timu ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi Wilaya ya Lindi pamoja wataaalam wa MKUHUMI ambao wamewezesha shughuli hii kuanza kama ilivyopangwa.

Wanakijiji wa kijiji cha Mkanga1 wameweza kutenga maeneo kwa matumizi mbalimbali ili waweze kutumia ardhi yao na maliasili zilizopo kwa ubora zaidi na uendelevu. Matarajio ni kwamba matatizo yanayowakabili wanakijijiji hivi sasa yanayohusiana na matumizi ya ardhi na maliasili zilizopo juu na chini yake, ikiwa ni pamoja na usalama wa miliki zao za ardhi, yatapungua au kuisha kabisa kutokana na utekelezaji wa mpango wao huu wa matumizi ya ardhi ya kijiji waliojiwekea. Na wataweza kuuhuisha mara kwa mara kadri haja na mahitaji yatakavyojitokeza.

Wawezeshaji waliofanikisha kuanzisha mchakato huu ni wafuatao:

Manace Nkuli, Abdallah Ndembo, Abdallah M. Mbinga, Ally Namila, Joyce Kazana na Ally Chimbuli toka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi na Manispaa ya Lindi.

Page 4: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

iv

YALIYOMO MUHTASARI WA UTENDAJI ................................................................................................................... ii

SHUKRANI ................................................................................................................................................. iii

UTANGULIZI ............................................................................................................................................ viii

SURA YA KWANZA ................................................................................................................................... 1

1. UTANGULIZI ....................................................................................................................................... 1

1.1 CHIMBUKO ................................................................................................................................. 1

1.2 MADHUMUNI .............................................................................................................................. 1

1.3 UTARATIBU ULIOTUMIKA ...................................................................................................... 1

SURA YA PILI ............................................................................................................................................. 2

2. TAARIFA ZA MSINGI ZA KIJIJI ....................................................................................................... 2

2.1 Mahali kijiji kilipo na historia...................................................................................................... 2

2.1.1 Mahali kijiji kilipo ................................................................................................................. 2

2.1.2 Historia ya kijiji .................................................................................................................... 2

2.2. Maumbile ya Nchi ....................................................................................................................... 2

2.2.1 Sura ya nchi na matiririsho ya maji .................................................................................. 2

2.2.2. Hali ya hewa ........................................................................................................................ 2

2.2.3. Jiolojia na udongo .............................................................................................................. 3

2.2.4 Uoto ...................................................................................................................................... 5

2.3. RASILIMALI ZA KIJIJI ............................................................................................................... 5

2.3.1. Ardhi ..................................................................................................................................... 5

2.3.2 Maji ....................................................................................................................................... 6

2.3.3. Misitu .................................................................................................................................... 6

2.3.4. Wanyamapori ...................................................................................................................... 7

2.3.5. Madini ................................................................................................................................... 7

2.3.6. Watu na utawala ...................................................................................................................... 7

2.4 HUDUMA ZA JAMII NA MIUNDOMBINU ............................................................................. 10

2.4.1 Elimu ................................................................................................................................... 10

Page 5: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

v

2.4.2. Afya ..................................................................................................................................... 10

2.4.3. Mawasiliano na uchukuzi ................................................................................................ 10

2.4.4. Nishati ................................................................................................................................ 10

2.5. MILIKI ZA ARDHI ..................................................................................................................... 10

2.5.1. Miliki na usimamizi wa ardhi ........................................................................................... 10

2.5.2. Upatikanaji wa ardhi ......................................................................................................... 11

SURA YA TATU ....................................................................................................................................... 12

3. MATUMIZI YA ARDHI YA SASA ................................................................................................... 12

3.1. KILIMO ....................................................................................................................................... 12

3.1.1. Mazao yanayolimwa ........................................................................................................ 13

3.1.2. Maeneo ya kilimo na ukubwa wake ............................................................................... 13

3.1.3. Mfumo wa kilimo ............................................................................................................... 13

3.1.4. Misimu ya kilimo ............................................................................................................... 13

3.1.5. Matumizi ya pembejeo za kilimo .................................................................................... 13

3.1.6. Zana za kilimo ................................................................................................................... 14

3.1.7. Viwango vya uzalishaji .................................................................................................... 14

3.1.8. Hifadhi ya mazao .............................................................................................................. 14

3.2. UFUGAJI ................................................................................................................................... 15

3.2.1 Aina ya mifugo na idadi yake .......................................................................................... 15

3.2.2. Maeneo ya malisho .......................................................................................................... 15

3.2.3. Mifumo ya ufugaji ............................................................................................................. 15

3.2.4. Magonjwa ya mifugo ........................................................................................................ 15

3.2.5. Huduma za miundombinu ya mifugo ............................................................................. 15

3.3. MISITU/MBUGA ZA WANYAMAPORI .................................................................................. 16

3.3.1. Aina na uendelezaji wa misitu ........................................................................................ 16

3.3.2. Matumizi ya misitu na miliki zake ................................................................................... 16

3.3.3. Mifumo ya uvunaji wa misitu ........................................................................................... 16

3.4. MAKAZI ...................................................................................................................................... 17

3.4.1. Ukubwa wa eneo la makazi ............................................................................................ 17

3.4.2. Vifaa vinavyotumika katika ujenzi na upatikanaji wake .............................................. 17

Page 6: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

vi

3.4.3. Mfumo wa nyumba ........................................................................................................... 17

3.4.4. Shughuli nyingine ndani ya eneo la makazi ................................................................. 18

3.5. Huduma za jamii na miundombinu ........................................................................................ 18

SURA YA NNE ......................................................................................................................................... 20

4. MATATIZO YA MSINGI YA KIJIJI FURSA, VIKWAZO NA MIKAKATI .................................... 20

4.1. Matatizo ya kijiji ......................................................................................................................... 20

4.2. FURSA ZILIZOPO .................................................................................................................... 23

4.3. VIKWAZO VILIVYOPO ............................................................................................................ 23

4.4. MIKAKATI YA KUTATUA MATATIZO YA KIJIJI ................................................................. 24

SURA YA TANO ....................................................................................................................................... 26

5. MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI ........................................................................................... 26

5.1. UTANGULIZI ............................................................................................................................. 26

5.2. MAHITAJI HALISI YA ARDHI KWA MATUMIZI MBALIMBALI ......................................... 26

5.2.1. Utangulizi ........................................................................................................................... 26

5.2.2. Mahitaji ya kuni ................................................................................................................. 28

5.2.3. Huduma za kijamii ............................................................................................................ 28

5.3 MAPENDEKEZO ...................................................................................................................... 29

5.3.1. Mgawanyo wa ardhi ......................................................................................................... 29

5.3.2 Upimaji wa maeneo.......................................................................................................... 32

5.3.3. Mpango wa kuendeleza maeneo yaliyotengwa ........................................................... 32

5.3.4. Kazi zitakazofuata ............................................................................................................ 33

SURA YA SITA ......................................................................................................................................... 34

6. RASIMU YA SHERIA NDOGO ...................................................................................................... 34

7. Adhabu ............................................................................................................................................... 40

8. Kupitishwa na kusainiwa ................................................................................................................. 41

ORODHA YA MAJEDWALI

Jedwali Na. 1 Aina za udongo na Mgawanyo wake kwa vitongoji na matumizi. ...................... 3

Jedwali Na 2. Aina kuu za udongo na matumizi yake .................................................................. 4

Page 7: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

vii

Jedwali Na. 3 Uoto wa asili na matumizi yake ............................................................................... 5

Jedwali Na. 4 Idadi ya watu katika kijiji cha Mkanga1 kwa jinsia ............................................... 7

Jedwali Na. 5 Matumizi ya sasa ya rasilimali za kijiji .................................................................. 12

Jedwali Na. 6 kalenda ya shughuli za kilimo ya kila mwaka ya kijiji cha Mkanga1 ................ 13

Jedwali Na. 7 uzalishaji wa mazao katika kijiji cha Mkanga1 .................................................... 14

Jedwali Na. 8 Idadi na aina ya mifugo katika kijiji cha Mkanga1 .............................................. 15

Jedwali Na. 9 Mpango kazi wa jamii kijiji cha Mkanga1. ............................................................ 21

Jedwali Na. 10 Matatizo, fursa, vikwazo na mikakati ................................................................. 24

Jedwali Na. 11: Mapendekezo ya mpango wa matumizi ya ardhi ............................................ 29

ORODHA YA RAMANI

MIPAKA YA KIUTAWALA KIJIJI CHA MKANGA1 ......................... Error! Bookmark not defined.

RAMANI YA KIJIJI CHA MKANGA1 MATUMIZI YA SASA YA ARDHI ................................... 19

RAMANI YA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI ................. 31

Page 8: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

viii

UTANGULIZI

Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Ardhi na Sheria za Ardhi (Sheria ya Ardhi na. 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Kijiji Na. 5 ya mwaka 1999) kila kijiji hakina budi kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa madhumuni ya kuwezesha usimamizi wa matumzi endelevu ya ardhi na maliasili na rasilimali zake zote. Hatua hii ni muhimu na ya lazima kwa sababu Watanzania walio wengi wanaishi vijijini na shughuli zao za kila siku za kiuchumi na kijamii ndio msingi wa kwanza wa maendeleo endelevu ya Taifa letu.

Aidha, Ofisi ya Makamu wa Rais imebaini kwamba hivi sasa kuna kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji. Kutokana na hali hii, imeandaa mkakati wa Taifa wa kuhifadhi Ardhi na Vyanzo vya Maji. Katika utekelezaji wa Mkakati mojawapo ya nyenzo muhimu zinazotumika kufanikisha malengo yanayokuMkanga1wa ni kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi inayofaa ngazi zote za utawala na usimamizi wa ardhi, ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa, kanda, taifa na kimataifa.

Kwa ngazi ya kimataifa.Tanzania imeridhia na itaendelea kuridhia Mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusiana na hifadhi ya mazingira ambayo kimsingi ni Mipango ya Kimataifa ya matumizi Bora ya Ardhi. Pia, Tume ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi inakamilisha Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi, na inaendelea na kuandaa pamoja na kuratibu maandalizi ya mipango ya wilaya, mikoa na kanda. Kwa kuwa ngazi ya kijiji ndipo mahali Watanzania wengi wanapoishi na ardhi ndio msingi mkuu wa maendeleo yao. Tume imeweka nguvu ya pekee katika kuwawezesha wanakijiji kuandaa na kurejea mipango ya vijiji vyao. Kuanzia mwaka wa fedha (2007/2008).

Tume imejiwekea mkakati wa kuwezesha angalau vijiji 500 kila mwaka katika wilaya mbalimbali. Kazi ambayo itafanyika sawia na kujenga uwezo wa Halmashauri za wilaya husika kwa kuunda timu ya PLUM na kuipatia mafunzo stahiki na kuimarisha taasisi zote za vijiji husika. Pamoja na jitihada za mamlaka nyigine katika kuwawezesha wanakijiji katika kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji vyao, ni matarajio ya Tume kwamba, baada ya muda si mrefu vijiji vyote vya Tanzania Bara; takriban 5130 watakuwa tayari wameandaa mipango yao ya matumizi bora ya ardhi.

Kijiji Mkanga1 ni miongoni mwa vijiji ambavyo vimechaguliwa katika Manispaa ya Lindi kuwa vya mwanzo katika mchakato huu wa kuwasaidia wanakijiji kuandaa na kurejea mipango ya matumizi bora ya Ardhi. Kijiji hiki kipo kata ya Tandangongoro, Tarafa ya Ng’apa wilaya ya Lindi,Mkoani Lindi.

Page 9: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

1

SURA YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI

1.1 CHIMBUKO

Kufuata kuwepo kwa kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji, uchakavu wa ardhi, kuongezeka kwa idadi ya watu, ongezeko la mahitaji kwa ajili ya matumizi mbalimbali na ongezeko la migogoro ya ardhi, Ofisi ya Makamu wa Rais, imeandaa Mkakati wa Taifa wa Kuhifadhi Ardhi na Vyanzo vya Maji. Katika kutekeleza mkakati huo, mojawapo ya nyenzo muhimu zinazotumika ni kuhakikisha kunakuwapo na mipango imara ya matumizi bora ya ardhi kwa kila kijiji. Kazi hii inafanyika kwa awamu kutegemea upatikanaji wa fedha na ufadhili; na zamu hii kijiji cha Mkanga1 kimeteuliwa kuwa miongoni mwa vijiji vya mwanzo kakita Manispaa ya Lindi.

1.2 MADHUMUNI Madhumuni ya utayarishaji wa mipango shirikishi ya Matumizi Bora ya Ardhi kwa kijiji cha Mkanga1 ni kama ifuatavyo:

Kuelimisha wanakijiji wa kijiji cha Mkanga1 juu ya umuhimu na nafasi ya mipango ya ardhi katika kusimamia rasilimali za Misitu na maliasili.

Kubainisha matatizo ya msingi yanayokabili kijiji hicho na fursa/nafasi waliyonayo wanakijiji kuweza kutatua matatizo hayo.

Kutoa elimu kuhusu sheria ya Ardhi ya vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 na sheria ya matumizi ya ardhi.

Kutayarisha mipango ya awali ya Matumizi Bora ya Ardhi kwa kuzingatia matakwa ya jamii (umma na watu binafsi)

Kuwawezesha wanakijiji kukubaliana aina mbalimbali za matumizi ya Ardhi na kuzitengea maeneo, kuyapima na kuyaingiza kwenye ramani.

Kutunga sheria ndogo za kutekelea makubaliano mbalimbali ya matumizi ya Ardhi.

Kupitishwa mpango wa matumizi ya ardhi na sheria ndogo na mkutano wa kijiji

1.3 UTARATIBU ULIOTUMIKA Hatua muhimu zilizofuatwa katika zoezi hili ni kama ifuatavyo:- (i) Kukusanya na kuchambua takwimu muhimu za kijiji (ii) Kubainisha matatizo ya msingi ya kijiji (iii) Kutayarisha mpango kazi wa jamii (iv) Kutayarisha mikakati ya kutatua matatizo yaliyobainishwa. (v) Kutayarisha mpango shirikishi wa matumizi ya ardhi wa kijiji (vi) Kutayarisha sheria ndogo (vii) Kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji (viii) Kupima maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali na

kuyaingiza kwenye ramani ya kijiji (ix) Kuandaa rasimu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji na ramani (i) Kuwasilisha mpango kwenye Halmashauri ya Wilaya ili upitishwe (ii) Kuwawasilisha mpango TUME ya Matumizi bora ya Ardhi

Page 10: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

2

SURA YA PILI

2. TAARIFA ZA MSINGI ZA KIJIJI

2.0 Mahali kijiji kilipo na historia

2.0.1 Mahali kijiji kilipo

Kijiji cha Mkanga1 kipo katika Kata ya Tandangongoro Tarafa ya Ng’apa Manispaa ya Lindi Mkoa wa Lindi, eneo lake lipo kati ya jira 564099 mashariki na 555385 magharibi na 8904654 kaskazini na 8898270 kusini. Kijiji cha Mkanga1 ni miongoni mwa vijiji 132 vya Manispaa ya Lindi. Kijiji ni cha kuhamia, kilisajiliwa mwaka 1974.

Kijiji hiki kina vitongoji vitatu (4) ambavyo ni Kilangalamatu, Mkanga juu, Mandanje na Mkanga chini. Kwa upande wa kaskazini kinapakana na kijiji cha Chikonji, mashariki kinapakana na kijiji cha Kineng`ene na Ng`apa, magharibi kinapakana na kijiji cha Mkombamosi na Nandambi, upande wa kusini kinapakana na kijiji cha Ng`apa na Nandambi. Kijiji kina ukubwa wa hekta 2475.24.

2.1.2 Historia ya kijiji

Kijiji cha Mkanga1 ni kijiji cha Asili ambacho watu wake ni wazawa wa kijiji hicho.

Vitongoji vya asili ni Lidoo na Ching`ong`o. Wazee waliokuwa wanaishi katika vitongoji

hivi ni Mzee Wakungwa na Mzee Naeya.

Mwaka 1974 wakati wa operation vijiji watu wote walijikusanya na kuishi pamoja katika

eneo ambalo lilikuwa limetawaliwa sana na majani ya kutengenezea ukili ambayo kwa

kimwera yanaitwa Mkanga na hivyo kufanya jina la kijiji kuitwa Mkanga1.

2.2. Maumbile ya Nchi

2.2.1 Sura ya nchi na matiririsho ya maji

2.2.1.1 Sura ya nchi (Physiography)

Maumbile ya kijiji cha Mkanga1 yamegawanyika katika makundi yafuatayo:- Tambarare, vilima, mabonde na vijito. Kutokana hali hii, kuna maeneo mengi ya mwinuko ambayo yanatumika kwa ajili ya kilimo na makazi.

2.2.1.2. Matiririsho ya maji

Katika kijiji cha Mkanga1 mtiririko wa maji yote ya mvua na vijito inakwenda katika bahari ya Hindi.

2.2.2. Hali ya hewa

Hali ya hewa ya kijiji cha Mkanga1 inafanana na hali ya hewa ya Wilaya ya Lindi vijijini katika vijiji vya Pwani ambapo kuna mvua za wastani wa mvua ni milimeta 750 hadi 1000 kwa mwaka. Kuna misimu miwili ya mvua, mvua za vuli na mvua za masika. Mvua za vuli huanza mwezi Novemba hadi Januari na vua za masika

Page 11: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

3

huanza mwezi Machi hadi Mei. Mwezi wa Juni hadi Julai ni majira ya baridi baada ya hapo mwezi Agosti hadi Novemba ni majira ya joto. Wastani wa hali joto kwa mwaka ni wastani wa sentigredi 24.0 na 28. Wastani wa unyevu katika hewa kila siku kwa mwaka ni asilimia 88. Kiwango cha mvua huzidi mvukizo mwezi Machi na Aprili. Hiki ndicho kipindi cha kuvuna mazao mashambani.

2.2.3. Jiolojia na udongo 2.2.3.1. Aina za miamba katika kijiji

Miamba aina ya Jurasiki yenye mawe ya aina mbalimbali imetawala katika kijiji cha Mkanga1

2.2.3.2 Aina kuu za udongo

Sehemu kubwa ya kijiji cha Mkanga1 ina udongo mwingi wa mchanga mweupe (50%) ambao umeenea katika vitongoji vya Mkanga1 shuleni na Kilolombwani. Udongo huu una kina kirefu lakini una rutuba kidogo na hupitisha maji kwa haraka. Udongo wa mfinyazi umeenea katika (30%) ya eneo la kijiji, una rutuba sana na unapatikana katika kitongoji cha umoja. Katika baadhi ya maeneo ya vitongoji vya Mkanga1 shuleni na Kilolombwani kuna aina ya udongo wa tifutifu ambao unmeenea katika (20%) ya eneo la kijiji. Aina za udongo katika kijiji cha Mkanga1 jiolojia ya udongo uliopo ni mchanganyiko wa udongo wa mfinyanzi, mchanga mweupe na tifutifu.

Jedwali Na. 1 Aina za udongo na Mgawanyo wake kwa vitongoji na matumizi.

Aina ya udongo Asilimia ya kijiji

%

Kiwango cha

rutuba

Mazao yanayostawi

zaidi

Vikwazo Vitongoji

Mchangamweusi

40 Nyingi Mahindi Ufuta Mbaazi Minazi Migomba Muhogo Mtama

Mgumu Mzito Mchwa

Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

Mchanga mweupe

24 Kidogo

Kunde Mbaazi Muhogo Karanga Korosho

Hautunzi maji Hautunzi mbolea Sisimizi

Kilangalamatu Mkanga juu Mkanga chini

Mfinyanzi

17 Kidogo

Mtama Ufuta Mahindi Mbaazi

Unanata Mgumu Mzito

Mandanje Mkanga chini

Udongo mwekundu 15 Nyingi Mahindi Muhogo Mtama Mbaazi Ufuta

Mgumu Sisimizi

Mandanje

Page 12: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

4

Minazi Migomba

Jasi 4 Hafifu Hakuna Kokoto Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Mei, 2011

JEDWALI NAMBA 2. AINA KUU ZA UDONGO NA MATUMIZI YAKE

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Mei, 2011

NA Aina ya udongo

Asilimia ya kijiji

%

Kiwango cha

rutuba

Mazao yanayostawi

zaidi

UZALISHWAJI KWA EKARI

VIKWAZO VITONGOJI

1

Mchanga mweusi

40 Nyingi Mahindi Ufuta Mbaazi Minazi Migomba Muhogo Mtama

- Gunia 4 - Gunia 4 - Gunia 6 - Gunia 21 - Matenga 40 - Viroba 30 - Gunia 4

Mgumu Mzito Mchwa

Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

2 Mchanga mweupe

24 Kidogo

Kunde Mbaazi Muhogo Karanga Korosho

- Gunia 3 - Gunia 4 - Viroba 60 - Gunia 6 - Gunia 6

- Gunia 6

Hautunzi maji Hautunzi mbolea Sisimizi

Kilangalamatu Mkanga juu Mkanga chini

3 Mfinyanzi

17 Kidogo

Mtama Ufuta Mahindi Mbaazi

- Gunia 5 - Gunia 3 - Gunia 3 - Gunia 4

Unanata Mgumu Mzito

Mandanje Mkanga chini

4 Udongo mwekundu

15 Nyingi Mahindi Muhogo Mtama Viazi Mbaazi Ufuta Minazi Migomba

- Gunia 4 - Viroba 30 - Gunia 4 - Viroba 30 - Gunia 6 - Gunia 4 - Gunia 24 - Tenga 50

Mgumu Sisimizi

Mandanje

5 Jasi 4 Hafifu Hakuna Hakuna

Kokoto Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje

Page 13: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

5

2.2.4 Uoto

Kijiji cha Mkanga1 kimefunikwa na misitu minene kwa sehemu kubwa, pamoja na vichaka na nyasi kidogo. Kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya upanuzi wa mashamba na mahitaji ya kuni, majengo na mbao uoto wa asili umebadilika. Upo pia uoto wa kupandwa ingawa kiasi ni kidogo ukilinganisha na uoto wa asili. Uoto huu umetawaliwa na mikorosho na minazi mashambani na katika maeneo ya makazi. Upandaji miti unafanyika pia katika maeneo ya taasisi kama vile shule. Aina mbalimbali za uoto na matumizi yake zimeanishwa katika jedwali hapo chini.

Jedwali Na. 3 Uoto wa asili na matumizi yake

Na

Aina ya

uoto

% eneo

la kijiji

vitongoji Aina ya miti Matumizi ya sasa

1 Msitu 70 Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje

Mvule,Msufi, Mninga,Mbambakofi, Mmang`unguli, Mmalala,Mtondo,Mtanga, Mmwidi,Mpweke,Mkala,Mtachi

Ujenzi wa nyumba, Mbao, mkaa, kamba,nishati na dawa

2 Vichaka na miti

20 Mkanga chini

Msufi, Mtanga, Mkala, Namng`uwa,Mtalawanda, Mpweke,Nang`ota, Mkwanga

Kujengea, nishati na dawa

3 Nyasi na majani

10 Kilangalamatu Mkanga chini

Usofu, Mabungo,Vitoro, Nambole,Kiano,Likulashaa, Lindatala,Liklova,Kiwawa, Ming`oko

Kuezekea nyumba,matunda, dawa na chakula

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Mei, 2011

2.3. RASILIMALI ZA KIJIJI

2.3.1. Ardhi

Katika kijiji cha Mkanga1 kuna aina moja ya ardhi nayo ni ardhi ya kijiji. Ardhi ya kijiji ina ukubwa wa hekta 2475.24; kati ya hizo hekta 790.8 zinahitajika kwa shughuli za kilimo, hekta 24.8 zinahitajika kwa ajili ya makazi. Hata hivyo hekta 1732 zinafaa kwa uhifadhi wa misitu sawa na asilimia 70 ya eneo lote la kijiji kwa kuwa eneo lisilo na msitu linatosha kwa kilimo, makazi, huduma za jamii na shughuli zingine.

Page 14: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

6

2.3.2 Maji

Rasilimali ya maji iliyopo katika kijiji cha Mkanga1 ni pamoja na mvua, na visima mbalimbali kama kisima cha Nachikalala katika kitongoji cha Mkanga juu, Mjangao, Mtandi, na Kwamtumba katika kitongoji cha Mandanje, Nangungwa na Rutende katika kitongoji cha Mkanga chini. Hata hivyo kijiji cha Mkanga1 kinauhaba wa maji baridi kwa ajili ya matumizi yao kwani visima vingi ni vya maji chumvi.

2.3.2.1. Maji ya mvua

Katika kijiji cha Mkanga1 kiasi cha maji ya mvua kwa mwaka hakijulikani. Aidha, mzunguko wa maji haya ni kama ufuatao: kiasi huzama ardhini na huvuja mpaka kwenye vilio maji chini ya ardhi na kusheheneza limbiko la maji ya chini ya ardhi, maji mengine hurudi katika anga hewa kupitia mchakato wa mvukizo, moja kwa moja au kupitia kwenye uoto na maji mengine hubaki juu ya ardhi katika mito.

2.3.2.2. Maji yaliyo juu ya ardhi

Kijiji cha Mkanga1 kinategemea zaidi maji yaliyo katika visima ambavyo vipo mbali sana kutoka katikati ya kijiji. Aidha, baadhi ya visima hukauka wakati wa kiangazi na kusababisha shida kubwa ya maji kijijini.

2.3.2.3. Maji yaliyo chini ya ardhi

Kwa mujibu wa tafiti za kijiolojia, na kihaidrolojia, ukanda kilipo kijiji cha Mkanga1 bado haifahamiki kiasi cha maji yaliyopo chini ya ardhi.

2.3.2.4. Usimamizi wa rasilimali maji

Katika kijiji cha Mkanga1, licha ya kutokuwepo shughuli za upimaji maji kihaidrolojia na kihaidrolojiolojia. Kama vile vipimo vya mvua, wingi na kina cha maji yaliyo juu ya ardhi na kina cha maji yaliyo chini ya ardhi kutoka kwenye uso wa ardhi. Kijiji cha Mkanga1 tayari kimeunda kamati ya maji na tayari wameanzisha mfuko wa maji.

2.3.2.5. Matumizi ya rasilimali majimaji

Matumizi makuu ya maji katika kijiji cha Mkanga1 ni pamoja na matumizi ya kawaida ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kunywa, kupikia, kufulia, kujengea na kumwagilia bustani wakati wa kiangazi.

2.3.3. Misitu

Katika kijiji cha Mkanga1 uoto wa asili unapungua hususani miti, kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika kijijini. Hivi sasa pamoja na kilimo cha kuhamahama, ukataji holela wa miti kwa ajili ya mbao, kujenga, unaendelea kwa kasi kiasi cha kufanya miti itoweke. Uoto huu unaweza kutoweka iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa kusimamia utunzaji wa uoto huu. Uoto uliopo wa asili unajumuisha aina mbalimbali za miti ambazo ni Mmalala, Ng’ungulu, Mbuyu, Mbambakofi, Mtondo, Mninga, Mvule, Ngongolo, Mitumbati, Misufi, Mtanga, Mvule, Mwindi, n. k.

Page 15: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

7

2.3.4. Wanyamapori

Katika kijiji cha Mkanga1 kuna aina mbalimbali ya wanyama pori, hii ni kutokana na misitu iliyopo. Wanyama waliopo ni wadogo wadogo kama nguruwe pori, mbawala na kima. Wanyama wakubwa wanao onekana kijijini hapo ni kama vile Nduvu n.k.

2.3.5. Madini

Katika kijiji cha Mkanga1 uchunguzi juu ya kuwepo kwa madini haujafanyika.

2.3.6. Watu na utawala

2.3.6.1. Idadi ya watu kijijini

Katika kijiji cha Mkanga1 idadi ya watu ni 798 ambao wanaume ni 400 na wanawake ni 398 idadi ya kaya ni 204.

2.3.6.2 Mchanganuo wa kijinsia.

Idadi kwa jinsia ya watu katika kijiji cha Mkanga1 ni kama inavyoonyeshwa katika jedwali namba 4.

Jedwali Na. 4 Idadi ya watu katika kijiji cha Mkanga1 kwa jinsia

Kitongoji Wanaume Wana

wake

Wazee Wa Toto Jumla Kaya

Kitongoji Me Ke Me Ke Me Ke

Kilangalamatu

37 41 10 11 104 108 311 92

Mkanga juu

25 24 8 6 53 51 166 36

Mandanje 22 29 11 7 59 52 180 43

Mkanga chini 19 20 5 6 41 44 141 32

JUMLA KUU 103 114 34 29 263 255 798 204

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Mei, 2011

2.3.6.3 Uhamaji na uhamiaji

Tathimini iliyofanywa na timu ya PLUM ya wilaya na wataalamu wa mradi wa MKUHUMI na VLUM na serikali ya kijiji inaonyesha kuwa wenyeji ni zaidi ya asilimia 70 na idadi kubwa ya wanakijiji ni waasili. Wageni wengi wapo katika vitongoji vya Mkanga1 shuleni na Kilolombwani. Kuhusu uhamaji na uhamiaji

Page 16: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

8

kijijini, kutokana na maelezo ya Halmashauri ya kijiji, kuna wanakijiji ambao kwa sababu mbalimbali huwa wanaamua kuhama kwenda kuishi kwenye maeneo mengine katika vijiji vingine au mijini ya ndani ya wilaya au sehemu nyingine za nchi, pia watu huhamia kijijini kutoka vijiji vingine au sehemu nyingine za nchi. Hata hivyo hakuna taarifa rasmi juu ya wahamiaj na wahamiaji.

2.3.6.4 Makadirio ya idadi ya watu kwa miaka ishirini ijayo

Makadirio ya idadi ya watu katika kipindi cha miaka ishirini ijayo, takwimu zinaonyesha kuwa Mei 2011 kijiji kina watu 798 ambao 400 ni wanaume na wanawake 398, na idadi ya kaya ni 204. Kwa mujibu wa sensa ya taifa ya mwaka 2002 ongezeko la idadi ya watu katika wilaya ni asilimia 1.3 kwa hiyo, ifikapo mwaka 2031 (baada ya kipindi cha miaka ishirini) inakadiriwa kwamba idadi ya watu katika kijiji itakuwa 988 na kaya zitakuwa ni 247.

2.3.6.5 Utawala wa kijiji

Kijiji kina serikali ambayo ina wajumbe 25. Serikali hiyo ambayo huchaguliwa kila baada ya miaka 5 kakzi yake kubwa ni kusimamia shughuli zote za kijiji zikiwemo shughuli za maendeleo na kijamii. Ili kutekeleza majukumu, Serikali ya kijiji imejipanga katika kamati za kudumu nazo ni:-

Kamati ya uchumi na fedha

Kamati ya huduma za jamii

Kamati ya mazingira

Aidha, Serikali ya kijiji imeunda kamati/timu za kusimamia majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na:-

Timu ya matumizi bora ya ardhi (VLUM)

Baraza la ardhi ya kijiji

Kamati ya maji

Kijiji kwa sasa hakina ofisi, hivyo ujenzi wa ofisi unahitajika.

Page 17: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

9

RAMANI YA KIJIJI CHA MKANGA 1 KUONYESHA MAHALI KILIPO

Page 18: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

10

2.4 HUDUMA ZA JAMII NA MIUNDOMBINU

Huduma za jamii zilizopo ni shule ya msingi Mkanga1, ghala, madrasa, fundi mwashi, fundi cherehani, misikiti, mgahawa, kiosk, waganga wa jadi, barabara, mashine ya kusaga, kilabu cha pombe, makaburi, kiwanja cha mpira.

2.4.1 Elimu

Kwa upande wa elimu kijiji cha Mkanga1 kina shule moja ya msingi ambayo hutumiwa na wakazi wote wa kijijini hapa.

2.4.2. Afya

Na kwa upande wa afya kijiji cha Mkanga1 hakina zahanati ya kijiji. Pia kuna baadhi ya wanakijiji hawana vyoo na wengine walionavyo havikidhi kanuni za afya hivyo wakati mwingine hali hii huweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama vile kuharisha na kipindupindu.

2.4.3. Mawasiliano na uchukuzi

Kuna barabara mbili zinazoingia katika kijiji cha Mkanga1, moja ni ile inayoingilia upande wa Nandambi na nyingine ni ile inayotoka Mtange kwenda Chikonji ambayo inachepuka kuingia Mkanga 1. Barabara zote hizi hupitika vizuri wakati wa kiangazi tu na hivyo kupelekea tatizo la usafiri wakati wa masika. Pia, kuna barabara / njia zisizo rasmi na zinazounganisha vitongoji zinazopitika kwa shida kwa gari hivyo zinahitaji kuboreshwa.

Katika kijiji cha Mkanga1 mtandao wa simu unaopatikana ni Zain hata hivyo kuna baadhi ya maeneo kijijini ambapo mitandao ya Zantel na Vodacom inapatikana na maeneo mengine hakuna mtandao unaopatikana, hivyo kufanya mawasiliano kijijini kuwa magumu.

2.4.4. Nishati

Nishati zinazotokana na visukuku mafuta ya taa na diseli) hutumika katika

kuwasha taa kwa matumizi ya nyumbani. Hata hivyo tegemeo kubwa la nishati

za asili katika kijiji hiki ni kuni. Aina nyingine ya nishati za asili zilizopo ni nguvu

ya joto la jua na nguvu za upepo ambazo hata hivyo hazitumiki kikamilifu.

Mathalani nguvu ya joto la jua hutumika tu kwa kukaushia mazao na nguo wakati

ingeweza pia kuzalisha umeme. Nishati ya upepo ingeweza kuasaidia kusukuma

maji kutoka chini ya ardhi kwa matumizi ya nyumbani, wanyama na bustani.

Tegemezi ya nishati ya kuni ni chanzo kikubwa cha kumalizika kwa misitu.

2.5. MILIKI ZA ARDHI

2.5.1. Miliki na usimamizi wa ardhi

Miliki za ardhi katika kijiji cha Mkanga1 ni za kimila. Sehemu kubwa ya kijiji

inamilikiwa na familia mojamoja au mtu mmoja mmoja. Maeneo ya matumizi ya

jumla ambayo ni pamoja na maeneo ya shule, misikiti, makaburi na viwanja vya

michezo yapo chini ya serikali ya kijiji.

Page 19: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

11

Wapo watu wachache wasiomiliki ardhi, hawa hukodisha au kuazima ardhi

wanayotumia. Familia zinazomiliki ardhi ni asilimia 95.

2.5.2. Upatikanaji wa ardhi

Watu wengi wamepata ardhi kwa kurithi au kugawiwa kutoka kwa serikali ya kijiji

na jamaa zao. Wastani wa ukubwa wa eneo la shamba ni ekari 3 kwa kila kaya.

Aidha, familia zinazomiliki ardhi kwa kugawiwa ni 12%, kwa kurithi 78%, kwa

kununua ni asilimia 3% na kuazima nia asilimia 7%.

Page 20: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

12

SURA YA TATU

3. MATUMIZI YA ARDHI YA SASA

Katika kijiji cha Mkanga1 matumizi ya ardhi yaliyopo ni pamoja na Kilimo,

Makazi, Uvunaji wa mazao ya misitu, huduma za jamii na miundo mbinu

(barabara, shule, na huduma za jamii na kiuchumi). Jedwali lifuatalo linaonyesha

shughuli kuu za kiuchumi katika kijiji cha Mkanga1

Jedwali Na. 5 Matumizi ya sasa ya rasilimali za kijiji

Na Aina ya mtumizi % ya kaya

zinazojihusis

ha

Mahali inapofanyika kijijini

Vitongoji husika % ya kijiji

1 Kilimo 100 Eneo la mwinuko, tambarare na mabondei

Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

40

2 Makazi 100 Eneo la mwinuko na tambarare

Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

1

3 Ufugaji 7 Maeneo ya mabondeni na kandokando ya makazi

Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

1

4 Makazi/Kilimo 33 Eneo la mwinuko na mabondeni

Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

21

5 Uvunaji wa mazao ya misitu

20 Msitu wa Mandanje, Lutende na Kilangalamatu

Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

50

5 Uhifadhi wa misitu 80 Misitu wa Lidoo Kilangalamatu Mkanga juu Mandanje Mkanga chini

35

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Mei, 2011

3.1. KILIMO

Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi na kijamii inayotegemewa na watu. Tathimini

iliyofanywa na timu ya PLUM na wataalamu wa mradi wa MKUHUMI kwa

kushirikiana na Halmashaui ya kijiji inaonyesha kwamba asilimia kubwa ya

wanakijiji ni wakulima ambao wengi wao hulima mazao ya chakula, na mengi ya

Page 21: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

13

mashamba haya yanalimwa kwa mtindo wa kuhamahama. Pia wapo wenye

mashamba ya kudumu ya mazao ya korosho na minazi.

3.1.1. Mazao yanayolimwa

Mazao makuu ya chakula ni mihogo, mtama, na mahindi. Mazao ya biashara ni

korosho na ufuta. Mazao ya nazi, kunde, mbaazi, karanga, hulimwa pia kama

mazao ya biashara na chakula.

3.1.2. Maeneo ya kilimo na ukubwa wake

Kwa ujumla katika kijiji cha Mkanga1 jumla ya hekta 2475.24 ambapo asilimia 40 zinatumika kwa kilimo. Sambamba na hayo asilimia 21 ni mchanganyiko wa makazi na kilimo.

3.1.3. Mfumo wa kilimo

Mfumo wa kilimo unaotumika Mkanga1 ni kilimo cha mseto kwa mazao yote.

Kilimo hiki ni matokeo ya ulimaji wa maeneo madogo na matumizi ya zana duni

za kilimo likiwemo jembe la mkono. Huduma ya ugani haipatikani japokuwa kuna

maofisa ugani katika ngazi ya kata; Wanakijiji walio wengi huhifadhi mazao

katika viroba, kese na darini kwakuwa kijijini hapo hakuna ghala.

3.1.4. Misimu ya kilimo

Katika kijiji cha Mkanga1 majira ya kilimo ni kama yalivyoainishwa katika jedwali

Na. 6 hapo chini.

Jedwali Na. 6 kalenda ya shughuli za kilimo ya kila mwaka ya kijiji cha Mkanga1

Na Shughuli 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12

1 Kuandaa mashamba

2 Kulima mashamba

3 Kupanda

4 Kupalilia

5 Kulinda wanyama

6 Kuvuna

7 Kuhifadhi mazao

8 Kula na kuuza

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Mei, 2011

3.1.5. Matumizi ya pembejeo za kilimo

Ukosefu wa pembejeo ni tatizo linalowakabili wanakijiji wa kijiji cha Mkanga1

ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za kilimo na ugani. Pembejeo za kilimo

hufuatwa Lindi mjini, umbali wa kilomita 34 toka kijijini. Hivyo kufanya watumiaji

wa pembejeo za kilimo kuwa wachache.

Page 22: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

14

3.1.6. Zana za kilimo

Jembe la mkono ndilo linaloongoza kuwa na watumiaji wengi zaidi. Matumizi ya

zana zingine kama wanyama kazi na trekta havitumiwi kutokana na wanakijiji

kuwa na uchumi duni hivyo kutokuwa na uwezo wa kukodi au kununua zana

hizo.

3.1.7. Viwango vya uzalishaji

Kwa ujumla uzalishaji wa mazao na hasa mazao ya chakula ni mdogo sana

ukilinganisha na mahitaji ya kaya kwa mwaka. Jedwali Na. 7 linaonyesha wastani

wa uzalishaji wa kila zao kwa mwaka kwa kila ekari.

Jedwali Na. 7 uzalishaji wa mazao katika kijiji cha Mkanga1

KITONGOJI Zao Wastani wa ekari

kwa kaya

Uzalishaji kwa ekari (Gunia)

Jumla ya

kaya

Jumla ya

ekari

Mazao kwa

mwaka (Gunia)

Kilangalamatu Mahindi 2 3 92 184 552

Mtama 1 2 35 35 70

Ufuta 1 1.5 70 70 105

Mbaazi 0.25 2 10 2.5 5

Korosho 6 6 3 18 108

Mkanga juu Mahindi 2 4 32 64 256

Mtama 1 4 6 6 24

Ufuta 1 3 32 32 96

Mbaazi 0.25 3 6 1.5 4.5

Mandanje Mahindi 2 4 43 86 344

Mtama 1 2 4 4 8

Ufuta 1 2 10 10 20

Mbaazi 0.25 3 21 5.25 15.75

Mkanga chini Mahindi 3 3 32 96 288

Mtama 4 5 32 128 640

Ufuta 1 3 16 16 48

Mbaazi 0.25 4 4 1 4

Chanzo: Serikali ya kijiji na mikutano ya vitongoji, 2011

3.1.8. Hifadhi ya mazao

Kutokana na riporti zilizopatikana katika kijiji cha Mkanga1 wanakijiji walio wengi

huhifadhi mazao katika vihenge na magunia. Hata hivyo ilidhihirisha kuwa

upatikanaji wa vifaa vya kuhifadhia mazao ni mgumu kidogo kutokana na umbali

wa vifaa hivyo vilipo.

Page 23: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

15

3.2. UFUGAJI

3.2.1 Aina ya mifugo na idadi yake

Katika kijiji cha Mkanga1 siyo shughuli kuu ya kijamii na kiuchumi. Mifugo iliyopo

ni mbuzi, bata na, kuku. Hata hivyo kuku ndio mifugo ambayo inawakimu

wanakijiji wa Mkanga1, kutumia kuku kama kitoweo na huuzwa. Takwimu za

mifugo zimeonyeshwa kwenye jendwali Na. 8

Jedwali Na. 8 Idadi na aina ya mifugo katika kijiji cha Mkanga1

Kitongoji Ng’ombe Mbuzi Kondoo Kuku Bata

Kilangalamatu 0 87 0 416 23

Mkanga juu 0 7 0 180 0

Mandanje 0 20 0 250 0

Mkanga chini 0 10 0 205 0

Jumla 0 124 0 2051 23

Chanzo: Serikali ya kijiji na mikutano ya vitongoji; mwezi Julai, 2011

3.2.2. Maeneo ya malisho

Hakuna eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya malisho na kuchungia mifugo; Pia

hakuna njia maalum za kupitishia mifugo. Wakati mwingine hali hii husababisha

mifugo kuingia mashambani na kula mazao hivyo kusababisha migogoro isiyo ya

lazima. Aidha, kutokana na kutokuwepo kwa lambo la kunyweshea mifugo

wafugaji wanalazimika kutumia mabeseni na ndoo kunyweshea mifugo yao maji.

Na kwa kuwa hakuna njia maalum za mifugo na kwa vile shughuli za kilimo ni

holela, pia hali hii wakati mwingine husababisha mifugo kuingia mashambani na

kuleta migogoro.

3.2.3. Mifumo ya ufugaji

Katika kijiji cha Mkanga1 hivi sasa kulingana na mifugo iliyopo hufungiwa

majumbani lakini wengine huachiwa na kuzunguka kijijini.

3.2.4. Magonjwa ya mifugo

Magonjwa ya mifugo yaliyopo kijijini hapa:- kuku ugonjwa mkubwa ni mdondo na

kideli, kwa upande wa mifugo aina ya, mbuzi magonjwa makuu ni homa ya

mapafu, minyoo na kuhara.

3.2.5. Huduma za miundombinu ya mifugo

Kutokana na kutokuwepo kwa maeneo ya mnada wa mifugo, wafugaji kwa

namna Fulani hawana uhuru wa kuuza mifugo yao na hulazimika kuuza kwa bei

ndogo kutokana na kutokuwepo kwa maeneo maalum ya kuuzia mifugo na

mazao yake.

Page 24: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

16

Pia kijiji hiki kinakabiliwa na ukosefu wa njia maalum za kupitishia mifugo. Wakati

mwingine hali hii husababisha mifugo kuingia mashambani na kula mazao hivyo

kusababisha migogoro isiyo ya lazima. Aidha, kutokana na kutokuwepo kwa

Lambo la kunyweshea mifugo, wafugaji wanalazimika kutumia mabeseni na

ndoo kunyweshea mifugo yao maji. Kijiji cha Mkanga1 hakina mtaalamu wa

mifugo hivyo tiba kama chanjo ya kuku na ushauri kwa wafugaji haipatikani

kijijini.

3.3. MISITU/MBUGA ZA WANYAMAPORI

3.3.1. Aina na uendelezaji wa misitu

Katika kijiji cha Mkanga1 uoto wa asili unapungua hususani miti, kutokana na

shughuli za kibinadamu zinazofanyika kijijini. Hivi sasa pamoja na kilimo cha

kuhamahama, ukataji holela wa miti kwa ajili ya mbao, kujenga, unaendelea kwa

kasi kiasi cha kufanya miti itoweke na vibakie vichaka tu. Uoto huu unaweza

kutoweka iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa kusimamia utunzaji wa uoto

huu. Uoto wa asili unajumuisha aina mbalimbali za miti ambazo ni Mmalala,

Ng’ungulu, Mbuyu, Mbambakofi, Mtondo, Mninga, Mvule, Ngongolo, Mitumbati,

Misufi, Mtanga, Mvule, Mwindi n.k.

Jitihada za uendeshaji rasilimali ya misitu katika kijiji cha Mkanga1 siyo ya

kuridhisha kwa kuwa baadhi ya wanakiji bado wanafyeka misitu kwa ajili ya

kilimo. Hali hii inatokana na kijiji kuwa bado na maeneo makubwa ya misitu.

Halmashauri ya kijiji inaombwa kuwepo kwa jitihada ya pekee ya Halmashauri ya

Wilaya ya kuwasaidia katika uendeshaji wa misitu katika eneo la kijiji vinginevyo

misitu itazidi kuteketezwa na kuisha. Aidha, katika kijiji tayari kuna kamati ya

mazingira inayosimamia mazingira pamoja na misitu.

3.3.2. Matumizi ya misitu na miliki zake

Katika kijiji cha Mkanga1 matumizi makubwa ya mazao ya misitu katika kijiji ni

pamoja na kuni, ujenzi (nyasi na miti), upasuaji wa mbao, dawa za miti shamba,

uchongaji wa vinu, dawa, malisho ya mifugo, matambiko, makazi ya wanyama,

ujenzi wa vyombo. Misitu yote iliyopo kijijini husimamiwa na Halmashauri ya kijiji.

3.3.3. Mifumo ya uvunaji wa misitu

Kwa ujumla, mfumo wa uvunaji wa misitu katika kijiji cha Mkanga1 ni holela

ambapo hakuna eneo la misitu ambalo limetengwa kwa ajili ya hifadhi na

matumizi ya kijiji. Hivyo hali hii inapelekea maeneo mengi ya misitu kuvamiwa na

kukatwa ovyo. Hivyo ni muhimu zaidi kwa kijiji kuwa na mpango wa matumizi

bora ya ardhi ili kunusuru kuteketea kwa uoto huo wa asili.

Page 25: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

17

Hivi sasa katika kijiji cha Mkanga1 hakuna eneo maalumu la misitu lililotengwa

kwa ajili ya uvunaji na hifadhi. Hali hii inachangia uvunaji holela wa mazao ya

misitu pamoja na ufyekaji kwa ajili ya kilimo na makazi.3.4. MAKAZI

3.4.1. Ukubwa wa eneo la makazi

Katika kijiji cha Mkanga1 kuna makazi ya aina mbili, Makazi msongamano na

makazi mashamba (makazi yapo katika eneo la mashamba) hasa katika kitongoji

cha Umoja. Na maeneo ya makazi msongamano yapo katika vitongoji vya

Kilangalamatu na Mkanga juu. Katika kijiji cha Mkanga1 makazi yana ukubwa wa

hekta 39.9

Aina ya nyumba

Katika kijiji cha Mkanga1 kuna aina mbalimbali za nyumba kama nyumba za miti

zilizokandikwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi na nyumba zilizojengwa kwa

matofali na kuezekwa kwa bati na zingine kwa nyasi. Hata hivyo Halmashauri

haikuwa na takwimu za nyumba hizo.

3.4.2. Vifaa vinavyotumika katika ujenzi na upatikanaji wake

Ni pamoja na miti ya kujenga na kupaulia, nyasi za kuezekea udongo wa

kukandikia /kufatulia matofali na kujengea, mbao kwa ajili ya kuezekea,

kutengenezea milango, madirisha na mabati ya kuezekea. Vifaa vya ujenzi

vinapatikana kijijini na mjini Lindi ambavyo ni saruji, mabati na nondo ambavyo

vyote ni ghali, hivyo wanakijiji wanatumia vifaa vinavyopatikana kijijini hivyo

kufanya nyumba zao kuwa za kiwango cha chini. Kutokana na maisha ya

Mkanga1 kuwa duni na gharama za ujenzi wa nyumba imara kuwa ghali kama

ufyatuaji na kuchoma matofali, ununuzi wa saruji, mawe mchanga na mbao,

hivyo wanakijiji wengi wanaishi kwenye nyumba duni ambazo wakati wa mvua

zinavuja, kutokana na kuezekwa kwa nyasi na pia nyumba hazina mwanga wa

kutosha kutokana na kutokuwa na madirisha au kuwa na madirisha madogo

sana.

3.4.3. Mfumo wa nyumba

Katika kijiji cha Mkanga1 aina za nyumba zifuatazo: nyumba za miti

zilizokandikwa udongo na kuezekwa kwa nyasi/makuti, nyumba zilizojengwa kwa

matofali ya udongo na kuezekwa kwa nyasi/makuti, nyumba zilizojengwa kwa

matofali ya udongo na kuezekwa kwa bati na nyumba zilizojengwa kwa tofali za

saruji na kuezekwa kwa bati. Hata hivyo Halmashauri ya kijiji cha Mkanga1

haikuwa na takwimu za nyumba hizi. Kwa upande wa upatikanaji wa viwanja;

Halmashauri ya kijiji cha Mkanga1 husimamia ugawaji wa viwanja kwa wananchi

wake hivyo huraisisha upatikanaji wa viwanja hivyo.

Katika kijiji cha Mkanga1 nyumba nyingi ni za udongo zilizoezekwa kwa nyasi na

nyingi hazikusakafiwa na hazina madirisha ya kupitishia hewa ya kutosha.

Wanakijiji walio wengi hawana kipato cha kutosha cha kuwawezesha kujenga

Page 26: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

18

nyumba bora; Pia, kutokana na kukosa elimu ya ujenzi wa nyumba kutokuwa na

madirisha yenye kupitisha hewa ya kutosha na nyumba nyingi hazina vyoo ni

mambo ambayo husababisha mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kama vile

kuhara.

3.4.4. Shughuli nyingine ndani ya eneo la makazi

Katika kijiji cha Mkanga1 shughuli za biashara ndogondogo kama magenge,

vioski, vilabu vya pombe, mashine za kusaga, zinafanyika katika eneo la makazi

ili kurahisisha upatikanaji wa mahitaji madogomadogo kwa wanakijiji. Hata hivyo

kuna uwanja wa mpira na viwanja vingine vidogo vidogo vya michezo kwa ajili ya

wanafunzi na watoto wadogo.

3.5. Huduma za jamii na miundombinu

Huduma za jamii zilizopo ni shule ya msingi Mkanga1 na misikiti. Barabara zote

ikiwa ni pamoja na ile inayoingia kijijini kupitia Kineng`ene toka kwenye barabara

itokayo Mtange kuelekea Chikonji na zote zinazounganisha vitongoji na zile

zinazounganisha kijiji na vijiji vingine haziko imara, hivyo kufanya mawasiliano

kuwa magumu. Pia kutokana na kutokuwepo minara ya mitandao ya simu katika

kijiji kunafanya mawasiliano ya simu kuwa magumu.

Page 27: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

19

RAMANI YA KIJIJI CHA MKANGA1 KUONYESHA MATUMIZI YA SASA YA ARDHI 2011

Page 28: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

20

SURA YA NNE

4.0 MATATIZO YA MSINGI YA KIJIJI FURSA, VIKWAZO NA MIKAKATI

4.1. Matatizo ya kijiji

Wakati wa kuandaa mpango huu wanakijiji walitanabaisha matatizo makuu

yafuatayo:-

Uzalishaji mdogo wa mazao. Hii inatokana na mapungufu yaliyopo katika

Nyanja ya kilimo ikiwa na pamoja na ukosefu wa pembejeo za kilimo,

matumizi duni ya zana za kilimo pamoja na viwadilifu, ukosefu wa mtaji

kwa wakulima ambapo karibu wakulima wote wanatumia jembe la mkono

kama zana za kilimo.

Uharibifu wa vyanzo vya maji na ukosefu wa vitalu vya miche ya miti. Hii

inatokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira na

vyanzo vya maji. Pia kutokuwapo na elimu juu ya uhifadhi wa vyanzo vya

maji umepelekea kutokea kwa uharibifu huo.

Barabara ziingiazo kijijini na na zile zinazounganisha kijiji na vijiji vingine

haziko imara hivyo kutopitika mwaka mzima na kufanya mawasiliano

kuwa magumu.

Kilimo cha kuhamahama na makazi holela.

Ukosefu wa zahanati

Ukosefu wa wanyama kazi na ukosefu wa nyama na maziwa.

Ukosefu wa ofisi ya serikali ya kijiji na ofisi ya masjala ya ardhi, hivyo

kufanya utunzaji wa kumbukumbu kuwa mgumu na kijiji kushindwa kupata

cheti na kutowa hati miliki za ardhi za kimila.

Page 29: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

21

MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MATUMIZI BORA YA ARDHI KWA

USHIRIKISHWAJI JAMII

Jedwali Na. 9 Mpango kazi wa jamii kijiji cha Mkanga1.

Na Lengo Shughuli Muda wa

utekelezaji

Wahusika kijijini

Wahusika nje

Mahitaji Matokeo

1 Kuwa na zahanati

- Kusafisha eneo la ujenzi - Kukusanya mawe, mchanga kokoto n.k. - Usanifu wa jengo

July, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya afya - Idara ya ujenzi - Wizara ya afya - Wizara ya ujenzi

- Fedha - Vifaa vya ujenzi (Cement, mawe, kokoto, mbao, nondo, bati n.k.) - Wataalam - Nguvukazi

- Kuwepo kwa zahanati ya kijiji - Kuwepo kwa huduma ya afya karibu

2 Kuwa na barabara inayopitika mwaka mzima

- Kusafisha eneo la ujenzi wa barabara - Kukusanya Vifaa vya ujenzi - Kutengeneza makaravati - Kuchimba mitaro ya maji

Augasti, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya ujenzi - Wizara ya ujenzi

- Fedha - Vifaa na mitambo mbalimbali ya ujenzi wa barabara - Wataalam na Nguvu kazi

Kuwa na barabara inayopitika mwaka mzima

3 Kuwa na maji safi na salama

- Kuainisha vyanzo vya maji - Kukusanya Vifaa vya ujenzi na mitambo - Kuchimba mitaro/visima

Septemba, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - Kamati ya maji - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya maji - Wizara ya Maji na umwagiliaji

- Fedha - Vifaa na mitambo - Nguvu kazi - Wataalam

Upatikanaji wa maji safi na salama kijijini

4 Kujenga madarasa

- Kusafisha eneo la ujenzi - Kukusanya Vifaa vya ujenzi -Ujenzi

Octoba, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - Kamati ya shule - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya Elimu - Idara ya ujenzi - Wizara ya Elimu

- Fedha - Vifaa vya ujenzi - Nguvu kazi - Wataalam

- Kuwa na madarasa ya kutosha

Page 30: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

22

5 Kujenga nyumba za walimu

- Kusafisha eneo la ujenzi - Kukusanya Vifaa vya ujenzi -Ujenzi

Novemba, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - Kamati ya shule - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya Elimu - Idara ya ujenzi - Wizara ya Elimu

- Fedha - Vifaa vya ujenzi - Nguvu kazi - Wataalam

- Kuwa na nyumba za walimu za kutosha

6 Kuwa na walimu wa Kutosha

-Mikutano ya H/Kijiji -Mikutano ya hadhara -Kuomba walimu H/Manispaa

July, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - Kamati ya shule - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya Elimu - Wizara ya Elimu

- Shajala - Fedha

- Kuwa na walimu wa kutosha

7 Kuwa na soko la kuuzia bidhaa

- Kusafisha eneo la ujenzi - Kukusanya Vifaa vya ujenzi -Ujenzi

Januari, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya Ujenzi - Idara ya ushirika na masoko - Wizara ya Ushirika na masoko

- Fedha - Vifaa vya ujenzi - Nguvu kazi - Wataalam

Kuwa na soko la kuuzia bidhaa kijijini

8

Udhibiti wa wanyama waharibifu mashambani

- Kuainisha wanyama waharibifu - Kutafuta vifaa vya kudhibiti wanyama waharibifu - Kuomba msaada wa kupewa utaalam wa kudhibiti wanyama waharibifu

Desemba, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - Kamati ya Maliasili - VLUM

- H/Manispaa - Wafadhili - Idara ya Maliasili

-Fedha - Vifaa - Nguvu kazi - Wataalam

Kupunguza tatizo la wanyama waharibifu

9 Kujenga ofisi ya kijiji na masjala ya ardhi

- Kusafisha eneo la ujenzi - Kukusanya mawe,

Februari, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - VLUM

- H/Manispaa -Wafadhili - Idara ya ujenzi

- Fedha - Vifaa vya ujenzi (Cement,

Kuwa na ofisi ya kijiji na masjala ya ardhi

Page 31: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

23

mchanga kokoto n.k. - Usanifu wa jengo

mawe , kokoto, mbao, nondo, bati n.k.) - Wataalam - Nguvu kazi

10 Kuwa na Mtaalam wa ugani

- Kufanya mikutano - Kuomba mtaalam wa ugani

Julai, 2011

- Wanakijiji - H/Kijiji - VLUM

- H/Manispaa -Wafadhili - Idara ya kilimo na mifugo

- Shajala - Fedha

- Kuwa na mtaalam wa ugani kijijini

Chanzo: Serikali ya kijiji na mikutano ya vitongoji mwezi Julai, 2011.

4.2. FURSA ZILIZOPO

Fursa zilizopo na zinazoweza kusaidia katika kutatua matatizo yanayowakabili

wanakijiji wa kijiji cha Mkanga1 ni pamoja na uwepo wa ardhi yenye rutuba kwa

ajili ya kilimo, wataalam wa kilimo na mifugo wa kata ingawa huduma zao

hazikidhi mahitaji. Nguvu kazi ipo ya kutosha hivyo kurahisisha uzalishaji wa

mazao, wasimamizi wa maeneo hayo (Halmashauri ya kijiji ipo, kamati ya

matumizi bora ya ardhi ipo na sheria ndogo za kusimamia matumizi bora y ardhi

zipo. Hata hivyo wanakijiji walitanabaisha kuwa fursa hizo zikitumika vizuri

zinaweza kusaidia katika utatuzi wa matatizo haya.

4.3. VIKWAZO VILIVYOPO

Wanakijiji wa kijiji cha Mkanga1 watanabaisha kwamba ingawa fursa zipo kijijini

lakini kuna vikwazo vinavyokwamisha utatuzi wa matatizo yanayowakabili

wanakijiji hao. Vikwazo vilivyotajwa ni pamoja na wanyama waharibifu, matumizi

ya pembejeo na zana duni za kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa

wataalamu wa kilimo na wanyamapori, ukosefu wa fedha, ukame, uchungaji

holela wa mifugo, ukosefu wa mbegu bora na pembejeo kwa ajili ya kilimo cha

kisasa, uharibifu wa mazingira hasa katika vyanzo vya maji na misitu, ukosefu

wa elimu juu ya uhifadhi wa mazingira na misitu, uhaba wa wataalamu wa

wanyamapori, ukataji miti ovyo, uchomaji wa mkaa, kilimo cha kuhamahama,

uchomaji moto misitu ovyo, kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi,

kukosekana kwa sheria ndogo kijijini ambazo zitatumika kulinda rasilimali husika

na kukosekana kwa elimu ya utumiaji wa mazingira.

Page 32: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

24

4.4. MIKAKATI YA KUTATUA MATATIZO YA KIJIJI

Jedwali Na. 10 Matatizo, fursa, vikwazo na mikakati

NA Matatizo Fursa Vikwazo

1 Ukosefu wa zahanati

- Eneo la ujenzi lipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Nguvu kazi ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - Kuwepo kwa vifaa vya ujenzi kama mawe, mchanga na mbao kijijini. - Idara ya ujenzi ipo - Idara ya afya ipo - Wizara ya ujenzi ipo - Wizara ya afya ipo

- Ukosefu wa fedha

2 Barabara mbovu - Barabara ya zamani ipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Nguvu kazi ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - Kuwepo kwa vifaa vya ujenzi kama mawe, mchanga na mbao kijijini. - Halmashauri ya manispaa ipo - Idara ya ujenzi ipo - Wizara ya ujenzi ipo

- Ukosefu wa fedha - Ukosefu wa mitambo

3 Ukosefu wa maji safi na salama

- Vyanzo vya maji vipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Nguvu kazi ipo - Kamati ya maji ipo - Mfuko wa maji upo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - H/Manispaa ipo - Idara ya maji ipo - Wizara ya maji na umwagiliaji ipo

- H/Manispaa kutotekeleza miradi inayoibuliwa - Ukosefu wa fedha - Ukosefu wa mitambo - Ugumu wa wanakijiji katika kuchangia Mfuko wa maji

4 Upungufu wa nyumba za walimu

- Eneo la ujenzi lipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Mafundi mwashi wapo - Nguvu kazi ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - Kuwepo kwa vifaa vya ujenzi kama mawe, mchanga na mbao kijijini. - Idara ya ujenzi ipo - Idara ya elimu ipo - Wizara ya ujenzi ipo - Wizara ya elimu ipo

- Ukosefu wa fedha

Page 33: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

25

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Julai, 2011

5 Uhaba wa walimu - Shule ya msingi ipo - Uwepo wa wanafunzi wa kutosha - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Kamati ya shule ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - Idara ya elimu ipo - Wizara ya elimu ipo

- H/Manispaa kutoleta Walimu wa kutosha - Walimu kuripoti na kukimbia kituo cha kazi - Upungufu wa nyumba Za walimu - Upungufu wa nyumba Za walimu - Ukosefu wa huduma muhimu kijijini

6 Ukosefu wa soko la kuuzia mazao

- Eneo la ujenzi lipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Nguvu kazi ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - Kuwepo kwa vifaa vya ujenzi kama mawe, mchanga na mbao kijijini. - Idara ya ujenzi ipo - Idara ya ushirika na masoko ipo - Wizara ya ujenzi ipo - Wizara ya ushirika na masoko ipo

- Ukosefu wa fedha

7 Wanyama waharibifu wa mazao

- H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Nguvu kazi ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - H/Manispaa ipo - Kitengo cha Maliasili kipo - Mradi wa MKUHUMI upo - Wizara ya Maliasili ipo

- Ukosefu wa zana za kufukuzia wanyama - Ukosefu wa utaalam wa kufukuza wanyama

8

Ukosefu wa ofisi ya serikali ya kijiji

- Eneo la ujenzi lipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Nguvu kazi ipo - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - Kuwepo kwa vifaa vya ujenzi kama mawe, mchanga na mbao kijijini. - H/Manispaa ipo - Idara ya ujenzi ipo - Idara ya utawala ipo - Wizara ya Miundombinu ipo

- Ukosefu wa fedha

9 Ukosefu wa wataalam wa ugani

- Ardhi ya kutosha na mashamba vipo - H/Kijiji ipo - Wanakijiji - Kamati ya matumizi bora ya ardhi ipo - H/Manispaa ipo - Idara ya kilimo na mifugo ipo - Wizara ya kilimo na mifugo ipo

- H/Manispaa kutoleta wataalam wa ugani - Uhaba wa wataalam wa ugani nchini

Page 34: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

26

SURA YA TANO

5.0 MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI

5.1. UTANGULIZI

Kuna hatua kuu 6 katika utayarishaji mipango ya matumizi bora ya ardhi (PLUM,

1998) Hatua hizo ni:-

HATUA YA 1: Maandalizi ngazi ya wilaya – kuunda timu ya PLUM na kuipa

Mafunzo

HATUA YA 2: PRA kijijini

HATUA YA 3: Upimaji zaidi – kuhakiki mipaka

HATUA YA 4: Utayarishaji rasimu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi

HATUA YA 5: Utarayarishaji na utekelezaji wa mipango ya kina ya

ya kuendeleza maeneo yaliyotengwa kwa matumizi

mbalimbali.

HATUA YA 6: Uimarishaji wa taasisi za kijiji ili ziweze kusimamia mipango

ya matumizi bora ya ardhi ya kijiji.

Kwa mujibu wa hatua hizo hapo juu, kazi ya utayarishaji mipango ya matumizi

bora ya Ardhi ya kijiji cha Mkanga1 imeishia hatua ya 4. Hata hivyo siyo kazi zote

zilizotakiwa kufanyika ndani ya hatua 1 – 4 zimekamilika, baadhi ya shughuli

ambazo hazikukamilika ni pamoja na kufungua masjala ya ardhi, kupima

mashamba na kuyasajili kwa kuanza kutoa hakimiliki za kimila.

5.2. MAHITAJI HALISI YA ARDHI KWA MATUMIZI MBALIMBALI

5.2.1. Utangulizi

Kwa jamii za wakulima wadogo na wachungaji waishio vijijini, shughuli zao

huziendesha kwa ajili ya kujikimu kwanza na mambo ya ziada au utajirisho

hufuata baadae; kimsingi hazipewi uzito mkubwa. Hali hii siyo tu imedumaza

maendeleo yao bali pia imechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira na

hasa katika miaka michache iliyopita ambapo Tanzania haikuwa na sheria za

Ardhi na matumizi yake. Aidha, hali hiyo ya kulima bila malengo a kukosekana

sheria ya kumbana mkulima vile vile imechangia kushamili kwa tabia ya kilimo na

uchungaji wa kuhamahama na hivyo kusasabisha uharibifu wa ardhi na rasilimali

zake. Kimsingi kuna, haja ya kuwapo malengo katika kuendesha kilimo na

ufugaji.

Katika sura hii ya tano, jaribio linafanyika kuweka malengo ya mkulima na

mfugaji kwa mtizamo wa uendeshaji shughuli zao kiuendelevu ili kuhakikisha

mahitaji ya msingi ya jamii husika yanapatikana na wakati huo athari kwa ardhi

na mazingira zinapunguzwa kwa viwango vinavyokubalika. Hii itawezekana

baada ya kubainisha mahitaji halisi ya ardhi kwa matumizi mbalimbali kwa

kuzingatia ukulima na ufugaji wa kisasa.

Page 35: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

27

Mahitaji ya wakulima na wachungaji ni ya aina mbili, kwanza kuzalisha chakula

chao na pili ni kupata fedha kutokana na mauzo ya mazao yao ili wapate fedha

ya kununua bidhaa muhimu wasizoweza kuzalisha wao wenyewe hususani

bidhaa za viwandani na huduma mbalimbali zinazolipiwa fedha taslimu mfano

tiba, michango ya kijamii na ada za shule.

5.2.1.1 Mahitaji ya mazao ya chakula

Mazao makuu ya chakula katika kijiji cha Mkanga1 ni mahindi, mtama na kunde.

Kitaalamu ukadiriaji wa mahitaji ya chakula katika kaya ni muhimu katika

kuhakikisha familia hasa za vijijini zinakuwa na chakula cha kutosheleza mahitaji

ya mwaka mzima. Kaya ikifahamu mahitaji yake itaweka mipango thabiti ya

uzalishaji kulingana na mahitaji ya chakula na matumizi mengine. Utafiti

uliofanywa na Taasisi ya chakula na lishe Tanzania umeonyesha kuwa wastani

wa mahitaji ya nishati kwa Mtanzania ni kilokalori 2360 kwa hiyo ukadiriaji wa

mahitaji ya chakula katika kila kaya kwa kila zao ni kama ilivyoainishwa hapa

chini:-

Ukadiriaji wa zao la mahindi; ili kupata nishati kilokalori 2360 mahitaji ya unga wa

dona yatakuwa kama ifuatavyo:-

Gramu 100 za unga wa dona zinatoa kilokalori 363, hivyo kilokalori 2360 ni sawa

na unga wa dona kiasi cha:-

2360 x Gramu 100 = Gramu 650 za unga wa dona

363

Kutokana na hesabu hiyo, mahitaji ya mtu mmoja kwa mwaka yatakuwa gramu 650 x siku 365 = gramu 237,250 ambazo ni sawa na kilo 237. Kwa kukadiria uzito wa gunia lenye kilogramu 100, kiasi hicho kitakuwa karibu sawa na magunia 2.37. Ukichukulia kuwa kaya moja inakuwa na jumla ya watu wanne (4) kwa hiyo kila kaya itahitaji magunia 9.5 ya kilogramu 100, kwa mwaka hesabu hii imeonyeshwa hapa chini:-

Mtu 1 anahitaji gunia 2.37 kwa mwaka, je kaya ya watu wanne itahitaji gunia ngapi?

Mtu 1 = 2.37 gunia

Watu 4 = X

X = 2.4 x 4 = 9.48 gunia kwa kaya au gunia 1934 2 kwa kaya 204 kwa kuwa wastani wa uzalishaji wa mahindi ni gunia 3 kwa ekari, hivyo kijiji kinahitaji ekari 644 kwa ajili ya zao la chakula kwa sasa na kwa miaka ishirini ijayo kijiji kinahitaji ekari 781 .

5.2.1.2 Mahitaji ya zao la biashara

Ufuta ni zao la biashara. Aidha, na kwa mujibu wa takwimu zilizofanya na Timu ya wilaya ya Matumizi bora ya ardhi na Kamati ya Matumizi bora ya ardhi ya kijiji

Page 36: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

28

pamoja na Serikali ya kijiji mahitaji ya fedha kwa ajili ya kununulia bidhaa na huduma wasizozalisha inakadiriwa kuwa 1,230,275/= kwa kaya kila mwaka. Kwakuwa bei ya ufuta kijijini hapo ni 1,000/= kwa kilo, hivyo kila kaya inahitajika kuzalisha kilo 1231 za ufuta ambazo ni sawa na gunia 16 za ufuta ( gunia la ufuta ni kilo 80). Hivyo ardhi itakayohitajika kwa zao la biashara ni ekari 5.3 kwa kaya au ekari 1088 kwa kaya zote kwa kuwa uzalishaji wa ufuta kijijini ni gunia 3 kwa ekari. Mahitaji kwa miaka ishirini ijayo ni ekari 1309

5.2.2. Mahitaji ya kuni

Kwa wastani mtu mmoja anahitaji kuni za ujazo wa mita 1.5 kwa mwaka. Hivyo mahitaji ya kuni hivi sasa (idadi ya kaya ni 204) ni mita za ujazo 1197 na baada ya miaka ishirini ni mita za ujazo 1482. Kwa kuwa ekari moja ya msitu inaweza kuzalisha kuni ujazo wa mita 1.8, hivyo eneo la msitu kwa ajili ya kuni linatakiwa kuwa ekari 824 kwa miaka ishirini ijayo.

5.2.3. Huduma za kijamii

Viwango vifuatavyo vya eneo la ardhi inashauriwa vitolewe kwa kila aina ya matumizi yanayohusu huduma za jamii. Viwango hivyo vimependekezwa kwenye mwongozo wa PLUM (1998)

MATUMIZI VIWANGO ENEO (ha)

Zahanati 5000m2 (0.5ha) 0.5 ha

Shule ya Msingi(wanafunzi)280-1120)1.2-4.5ha(zipo2) 9.0 ha

Shule ya Sekondari 2.5 – 5.0 ha 5.0 ha

Kiwanja cha michezo 10 ha 10.0 ha

Soko 0.5 – 1.5 ha 1.0 ha

Maduka 1.0 – 2.0 ha 2.0 ha

Majengo ya umma 0.32 – 1.5 ha 1.5 ha

Biashara na huduma 0.16 – 0.5 ha 0.5 ha

Maeneo ya dini 0.2 – 0.4 ha (kila dini) 2.0 ha

Makaburi 2.0 ha (kila kitongoji) 4.0 ha

Jumla 35.5 ha

Kwa sasa kati ya huduma zilizotajwa hapo juu kuna ambazo tayari zipo na zingine hazipo lakini inatarajiwa ifikapo mwaka 2031 huduma zote zitakuwapo kama zilivyoorodheshwa hapo kijijini.

Page 37: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

29

5.3 MAPENDEKEZO

5.3.1. Mgawanyo wa ardhi

Kutokana na mikutano ya ushirikishwaji jamii iliyofanywa na timu ya PLUM katika kijiji cha Mkanga1 wanakijiji walipendekeza matumizi ya ardhi kama ilivyoonyeshwa kwenye jendwali.

Jedwali Na. 11: Mapendekezo ya mpango wa matumizi ya ardhi

Na. Matumizi Mapendekezo Eneo la sasa Mabadiliko

ya Eneo

1. Makazi Nyumba zijengwe kwa mpangilio na kwa

mitaa na kila nyumba iwe na choo.

Ukubwa wa viwanja utakuwa robo ekari

kwa kaya.

Eneo kwa ajili ya makazi limependekezwa

kuongezeka kwa mita 200 kila upande toka

yalipo makazi ya sasa kwa kitongoji cha

Kilangalamatu na Mkanga juu. Kitongoji

cha Mkanga chini na Mandanje itakuwa ni

makazi mashamba.

2.

Mashamba (Kilimo)

Eneo la kilimo kwa kitongoji cha

Kilangalamatu limependekezwa kuanzia

mwishoni mwa makazi la sasa kuelekea

kusini mashariki hadi mMzee Mzalendo.

Kwa kitongoji cha Mkanga juu eneo la

kilimo limependekezwa kuanzia mwisho wa

shamba la Hassani Maarufu hadi mita 200

kabla ya mpaka wa msitu wa Lidoo. Eneo

la kilimo kwa Kitongoji cha Mkanga chini

linabaki vilevile. Eneo la kilimo kwa

kitongoji cha Mandanje linabaki vilevile hadi

mita 200 kabla ya kisima cha mjangao

3. Huduma za Jamii

Eneo kwa ajili ya huduma za jamii limependekezwa kuanzia mwishoni eneo la makazi la sasa kuelekea kusini magharibi hadi kwa Vayoyo

4. Msitu wa Hifadhi

Maeneo kwa ajili ya msitu wa Hifadhi

yamependekezwa katika misitu ya Lidoo

na Kilangalamatu. Msitu wa Lidoo utaishia

mpakani mwa shamba la Mzee Juma

Page 38: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

30

Ismail Tipe na ule wa Kilangalamatu

utaishia Ruaha.

6.

Eneo la

vyanzo vya

maji

Eneo la vyanzo vya maji limependekezwa

kuwa ni Mashine ya maji, Nanungwa,

Nachikalala na Rutende katika kitongoji cha

Mkanga1 chini, Nachikalala katika kitongoji

cha Mkanga juu. Mjangao, Mtandi na Kwa

mtumba katika kitongoji cha Mandanje.

7 Eneo la

Makaburi

Maeneo ya Makaburi yamependekezwa

kubaki palepale yalipoishia makaburi ya

sasa hadi mita 100 kwa kila kitongoji.

8 Eneo la

Matambiko

Eneo kwa ajili ya matambiko

limependekezwa kuwa palepale lilipo sasa

(Mandanje kwa Kalombe)

9 Makazi Nyumba zijengwe kwa mpangilio na kwa

mitaa na kila nyumba iwe na choo.

Ukubwa wa viwanja utakuwa robo ekari

kwa kaya.

Eneo kwa ajili ya makazi limependekezwa

kuongezeka kwa mita 200 kila upande toka

yalipo makazi ya sasa kwa kitongoji cha

Kilangalamatu na Mkanga juu. Kitongoji

cha Mkanga chini na Mandanje itakuwa ni

makazi mashamba.

Chanzo: Serikali ya Kijiji na Mikutano ya Vitongoji; mwezi Julai, 2011

Page 39: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

31

RAMANI YA KIJIJI CHA MKANGA 1 KUONYESHA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Page 40: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

32

5.3.2 Upimaji wa maeneo

Baada ya mapendekezo ya mgawanyo wa Ardhi ya kijiji kwa matumizi makuu (kilimo, makazi, hifadhi, malisho, huduma za jamii) kukubaliwa na kuidhinishwa na mkutano wa kijiji, shughuli inayofuata ni kuyapima maeneo hayo na kuyaingiza kwenye ramani ya kijiji kwa ajili ya kumbukumbu. Upimaji hufanyika kwa kutumia GPS (handheld GPS) lakini kabla ya kifaa hiki hakijatumika lazima kirekebishwe vipimo na kuwekwa katika mizania (calibration) ili kupunguza uwezekano wa kuapta vipimo visivyosahihi.Mpima pamoja na timu ya VLUM na wanakijiji watazungukia kila eneo lililotengwa na kuhakikisha vipimo vya kutosha kuingiza eneo hilo kwenye ramani vimechukuliwa na kila eneo panapochukuliwa kipimo alama ya kudumu (katani, minyaa, miti ya kuchipuka) inapandwa eneo hilo kwa ajili ya kumbukumbu ya wanakijiji husika.

Baada ya zoezi la hapo juu, inafuata kazi ya kuhakiki ukubwa wa maeneo hayo; hii inafanyika kwenye ramani. Mpima atahakikisha ukubwa wa maeneo yaliyopimwa unalingana na mapendekezo yaliyokubaliwa na wahusika.

Kimsingi kazi ya kupima maeneo na kuyaingiza kwenye ramani baada ya kupitishwa na mkutano wa kijiji ni hitimisho la awamu ya kwanza ya utayarishaji mipango ya matumizi bora ya ardhi. Hadi hatua hii kijiji kinakuwa na rasimu ya mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji. Ili mpango huu uweze kumpa mkulima faida tarajiwa ni lazima kuanzisha mchakato wa awamu ya pili ambayo inahusu utayarishaji wa mipango shirikishi ya kina ya kuendeleza maeneo yaliyotengwa kwa matumizi mbalimbali. Shughuli hii pamoja na kazi zitakazofuat ili kukamilisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji cha Mkanga1.

5.3.3. Mpango wa kuendeleza maeneo yaliyotengwa

Mipango ya matumizi bora ya ardhi haiishii kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi makuu mbalimbali, mfano, kilimo, makazi, malisho ya mifugo, vynzo vya maji, huduma za jamii n.k. utengaji maeneo peke yake hauongezi uzalishaji kwa namna yeyote ile, lazima zoezi hilo lifuatishwe na utayarishwaji mipango shirikishi ya kina ya kuendeleza maeneo yaliyotengwa (detailed management plans) kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa hiyo kila aina ya matumizi yaliyotengwa ardhi lazima yatayarishiwe mipango ya namna gani yatumike ili kuleta faida kubwa na endelevu. Kazi hii inatarajiwa ifanywe na Halmashauri ya wilaya (mwenye dhamana hiyo)0 kupitia idara zake, mfano Idara ya kilimo itayarishe mpango shirikishi wa kuendeleza eneo la mashamba Idara ya mifugo itayarishe mpango wa kuendeleza eneo la malisho, Ardhi ishughulikie eneo la makazi n.k.

Ni kupitia utekelezaji mipango ya kina ya kuendeleza maeneo, kama ilivyosemwa awali, uzalishaji unaweza kuongezeka na hifadhi ya ardhi na vyanzo vya maji kutaleta matokeo tarajiwa ambayo ni mkulima kuwa na maisha bora. Suala la mpango gani wa kuendeleza maeneo utayarishwe mwanzo litategemea na vyanzo vya fedha za kugharimia kazi hiyo na utashi wa jumuiya ya kijiji husika. Lakini katika hali ya kawaida suala la eneo la kilimo na eneo la malisho ya mifugo katika kijiji cha Mkanga1 ni ya kipaumbele na hivyo yanastahili kutayarishiwa mipango ya kina kwanza.

Page 41: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

33

5.3.4. Kazi zitakazofuata

Kazi zitakazofuata ni pamoja na;

Kujenga na kufungua masjala ya ardhi ya kijiji

Serikali ya kijiji mara baada ya kukamilisha ujeni wa masjala ya kijiji itawasiliana na bwana ardhi wa wilaa ili kupanga uzinduzi wa masjala hiyo.

Kuanza kazi ya upimaji maeneo ya umma na binafsi na kuyasajili

Mafunzo kwa uongozi wa kijiji jinsi ya kusimamia ardhi (utawala wa ardhi)

Mafunzo ya kina kwa uongozi jinsi ya kusimamia daftari la ardhi la kijiji

Kutoa mafunzo kwa baraza la ardhi la kijiji

Kazi zote zilizobakia kukamilisha hatua 1 – 4 za PLUM

Kuwasilisha mpango na sheria ndogo wilayani na wizarani ili upitishwe. Hii ni jukumu la serikali ya kijiji, VLUM na Bwana Ardhi wa wilaya.

Page 42: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

34

SURA YA SITA

6.0 RASIMU YA SHERIA NDOGO

Katika sehemu inayofuta hapa chini, jumuiya ya kijiji cha Mkanga1 imetayarisha sheria ndogo za kusaidia kufanikisha utekelezaji wa makubaliano waliyoyafikia kuhusu jinsi gani ardhi ya kijiji chau itumike kiuendelevu. Sheria ndogo hizi ambazo zinapitishwa na mkutano wa kijiji zitaanza kutumika baada ya kuidhinishwa na mamlaka husika kisheria.

RASIMU YA SHERIA NDOGO ZA KIJIJI CHA MKANGA1

(VILLAGE BY LAW)

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA YA KIJIJI) 1982 (NA.7 YA 1982)

Zimetungwa chini ya kifungu cha 163 – 167

1. Jina Sheria ndogo hizi zitaitwa sheria ndogo za Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi za kijiji cha Mkanga1 Wilaya ya Lindi na zitaanza kutumika mara zitakapoidhinishwa na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

2. Namba ya uandikishaji ya kijiji

Kijiji kimeandikishwa chini ya sheria ya kuandikishwa vijiji vya mwaka 1974 na kusajiliwa kwa namba LD/MK/339.

3. Tafsiri ya maneno yaliyotumika katika sheria ndogo hizi

“Serikali” maana yake ni Serikali ya Kijiji cha Muungano “Halmashauri ya Kijiji”

maana yake ni Halmashauri ya Kijiji cha Muungano iliyoundwa chini ya Sheria ya

Serikali za Mitaa (Tawala za wilaya) Na. 7 ya mwaka 1982.

“Mkutano wa Kijiji” maana yake ni Mkutano wa wanakijiji wa Mkanga1 uliotishwa na

kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Tawala za wilaya) Na. 7 ya

mwaka 1982.

“Kamati ya Usimamizi ya Matumizi ya Ardhi ya Kijiji” maana yake ni Kamati

iliyoundwa na Halmashauri ya Kijiji na kuidhinishwa na mkutano wa kijiji kuisaidia

kazi za usimamizi wa matumizi ya ardhi ya kijiji.

“Kamati ya Maliasili” maana yake ni Kamati iliyoundwa na wanakijiji na kuidhinshwa

na mkutano wa kijiji kuisaidia kazi za usimamizi wa misitu ya hifadhi ya kijiji.

“Huduma za jamii” Maana yake ni huduma za kijamii kama vile elimu, afya,

barabara, ibada na taasisi nyinginezo.ndani ya eneo la makazi ya pamoja.

Page 43: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

35

“Makazi” Maana yake ni maeneo yanayokaliwa na watu kwa kujengwa nyumba za

kuishi au biashara. Maeneo haya yana ukubwa wa robo ekari kwa kila kaya.

“Eneo la Kilimo (mashamba)” Maana yake ni eneo la uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

“Eneo la makazi mashamba” Maana yake ni eneo lenye makazi mtawanyiko na

linatumika kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. “Msitu”Maana yake ni mkusanyiko wa nyasi, vichaka vinene, miti ya asili na miti ya

kupandwa kwa matumizi mbalimbali.

“Msitu wa Hifadhi” Maana yake ni msitu uliotengwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya hifadhi ya mazingira na matumizi endelevu.

“Vyanzo vya Maji” Maana yake ni chemichemi, mito, visima, mabwawa, na

mabonde yenye maji.

“Eneo la malisho” Maana yake ni pori la miti na nyasi linaloweza kutumika kama malisho na/au manywesheo ya mifugo.

“Mgeni” Maana yake ni mtu asiye mkazi wa kijiji cha Mkanga1, awe Mtanzania au sio Mtanzania. “Mifugo” Maana yake ni wanyama wote wafugwao ambao huishi kwa kulamiti na nyasi, hii ni kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda n.k

4. Mahusiano ya mkutano wa kijiji, Halmashauri ya Kijiji na Kamati mbalimbali F. 24 – 26, 55 – 62 na 103 – 106 vya sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Na. 7 ya 1982 F. 107 – 109 – inatoa mamlaka kwa Halmashauri ya Kijiji kuteua na kuunda kamati kuisaidia kutekeleza majukumu yake, kadri itakavyoona inafaa.

5. Usimamizi na uendeshaji wa maeneo yaliyotengwa Usimamizi na uendeshaji wa maeneo yaliyopangwa na kutengwa utakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Eneo la Makazi

1. Ujenzi wa nyumba katika eneo la makazi sharti ufuate kanuni za afya bora na ujenzi wa nyumba za kudumu, nyumba zitajengwa kwa kufuata mitaa na kila nyumba sharti iwe na choo. Atakayebainika kutokuwa na choo nyumbani kwake atatozwa faini ya shilingi elfu kumi (10,000) na kulazimika kujenga choo.

2. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo lililotengwa kwa ajili ya makazi.

Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/- na kulipa fidia ya uharibifu uliotokana na moto huo au kupelekwa mahakamani.

3. Ni marufuku kulima katika eneo lililotengwa kwa ajili ya makazi na

atakayebainika kulima katika eneo lililotengwa kwa ajili ya makazi

Page 44: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

36

Halmashauri ya Kijiji itamwita na kumuelekeza kung`oa mazao yake. Akikaidi Halmashauri ya Kijiji itang`oa na muhusika atawajibika kulipa gharama za ung`oaji.

4. Ni marufuku kulisha mifugo katika eneo lililotengwa kwa ajili ya makazi. Atakaye bainika kulisha mifugo katika eneo hili atatozwa faini ya shilingi 5,000/- na kulipa fidia ya uharibifu uliofanywa na wanyama wake.

5. Kila kaya italazimika kufanyia usafi eneo linalozunguka nyumba yake pamoja na barabara zinazopita karibu na nyumba yake. Atakaye bainika kutofanya usafi eneo lake na eneo la barabara jirani na nyumba yake Halmashaurii ya kijiji itamwita na kumuagiza kufanya hivyo. Akikaidi atatozwa faini ya shilingi 2,000/- na kulazimika kufanya usafi maeneo hayo.

6. Ni marufuku kuacha kiwanja bila kukifanyia usafi au bila kukijenga kwa

muda wa miaka miwili (2) mfululizo. Atakayeacha kufanyia usafi kiwanja chake au kukiendeleza kwa muda huo, Halmashauri ya kijiji itamwita na kumwelekeza kufanyia usafi kiwanja chake na kukijenga. Akikaidi Halmashauri ya kijiji itamnyang’anya kiwanja hicho na kumpatia mtu mwingine atakayeweza kukiendeleza.

7. Kamati ya Usimamizi wa Ardhi ya kijiji (VLUM) na kamati ya Afya

vitasimamia uendelezaji wa maeneo haya kwa niaba ya Halmashauri ya kijiji.

(b) Eneo la kilimo (mashamba)

1. Uendelezaji wa maeneo haya uzingatie kanuni za kilimo bora, endelevu,

hifadhi ya ardhi na maji. 2. Ni marufuku kujenga katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kilimo na atakaebainika kujenga katika eneo hili Halmashauri ya Kijiji itamwita na kumuelekeza abomoe nyumba yake. Akikaidi H/kijiji itabomoa nyumba hiyo na muhusika atalazimika kulipa gharama za ubomoaji.

3. Mtu anaye miliki shamba ni lazima alihudumie kwa kulifanyia usafi ili kuzuia mashamba pori. Atakayeacha kuhudumia shamba lake kwa muda wa miaka mitatu (3) mfululizo Halmashauri ya kijiji itamwita na kumuagiza alifanyie usafi. Akikaidi Halmashauri ya kijiji itamnyang’anya na kumpatia mtu mwingine atakayeweza kulihudumia. 4. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo la kilimo, atakaebainika kuanzisha moto na kusababisha hasara yeyote atatozwa faini ya shilingi 50,000/- na kulipa fidia ya hasara itakayosababishwa na moto huo au kupelekwa mahakamani.

5. Ni marufuku kulisha mifugo katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kilimo. Atakaye bainika kulisha mifugo katika eneo hili atatozwa faini ya shilingi 10,000/- na kulipa fidia ya mazao yaliyoharibiwa na mifugo yake.

Page 45: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

37

6. Ni marufuku kuendesha kilimo cha kuhamahama nje ya eneo ambalo mkulima analimiliki kihalali. Atakaye bainika kufanya kilimo cha kuhamahama atatozwa faini ya shilingi 50,000/= na kulazimika kulima katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kilimo.

(c) Eneo la huduma za jamii 1. Huduma za jamii zitatengewa viwanja katika eneo lililoainishwa kadri zinavyohitajika. 2. Ni marufuku kujenga katika eneo lililotengwa kwa ajili ya huduma za jamii, atakaebainika kujenga katika eneo hili Halmashauri ya Kijiji itamwita na kumuelekeza abomoe nyumba yake. Akikaidi H/kijiji itabomoa nyumba hiyo na muhusika atalazimika kulipa gharama za ubomoaji.

3. Wakati bado sehemu za eneo hili hazijaendelezwa, ni marufuku kwa watu binafsi kupanda mazao ya kudumu katika eneo hili. Atakayebainika kupanda mazao ya kudumu katika eneo la huduma za jamii Halmashauri ya kijiji itamwita na kumuelekeza kung’oa mazao yake. Akikaidi Halmashauri ya kijiji itang’oa mazao hayo na muhusika atalazimika kulipia gharama za ung’oaji wa mazao yake. 4. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo lililotengwa kwa ajili ya huduma za jamii. Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/- na kulipa fidia ya uharibifu uliofanywa na moto huo au kupelekwa mahakamani.

(d) Eneo la Msitu wa hifadhi wa kijiji

1. Maeneo yaliyoainishwa yapimwe, yasajiliwe, kuendelezwa na kuhifadhiwa kama hifadhi za misitu na yatakuwa chini ya usimamizi, uangalizi na au umiliki wa Kamati ya Maliasili na Halmashauri ya Kijiji kwa niaba ya wanakijiji. 2. Ni marufuku kuingia ndani ya msitu wa hifadhi bila kibali. Mtu yeyote atakayebainika kuingia msituni akiwa na kifaa cha uvunaji bila kibali atatozwa faini ya shilingi 25,000/= na vifaa vya uvunaji alivyokamatwa navyo vitataifishwa. Mgeni atakayekutwa msituni bila kifaa cha uvunaji atatozwa faini ya shilingi 3,000/= wakati mwenyeji atatozwa faini ya shilingi 2,000/=

3. Ni marufuku kufanya utafiti au utalii katika msitu wa hifadhi bila kibali, atakaebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/= 4. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo lililotengwa kwa ajili ya msitu wa hifadhi. Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/- au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote viwili kwa pamoja.

Page 46: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

38

5. Ni marufuku kufanya uvunaji wa aina yeyote katika msitu wa hifadhi bila kibali. Atayekutwa anafanya uvunaji katika msitu wa hifadhi bila kibali, atatozwa faini ya shilingi 50,000/= kwa mbao na mkaa, shilingi 10,000/= kwa majengo na shilingi 5,000/= kwa fito, shilingi 4,000/= dawa za asili, shilingi 2,000/= kwa ming`oko,kuni na matunda. Aidha mazao yaliyovunwa na vifaa vya uvunaji alivyokamatwa navyo muharifu huyo vitataifishwa.

6. Atakaekamatwa na mazao ya misitu yasiyo na kibali atatozwa faini ya shilingi 30,000/= kwa mbao na mkaa, shilingi 20,000/= kwa majengo na shilingi 5,000/= kwa fito. Aidha mazao aliyokamatwa nayo na vifaa vya uvunaji alivyokamatwa navyo muharifu huyo vitataifishwa.

7. Ataekutwa anasafirisha mazao ya misitu bila kibali atatozwa faini ya shilingi 5,000 kwa anasafirisha kwa kichwa, shilingi 15,000/= kwa anayesafirisha kwa baiskeli na shilingi 40,000/= kwa anayesafirisha kwa gari. Aidha mazao aliyokamatwa nayo na vifaa vya uvunaji alivyokamatwa navyo muharifu huyo vitataifishwa.

8. Ni marufuku kulima au kujenga katika msitu wa hifadhi. Atakayebainika kulima au kujenga katika eneo la msitu wa hifadhi atatozwa faini ya shilingi 50,000/= na kuwajibika kung`oa mazao yake au kubomoa nyumba yake au kulipa gharama za ung`oaji wa mazao yake au ubomoaji wa nyumba yake. 9. Ni marufuku kulisha mifugo katika eneo lililotengwa kwa ajili ya msitu wa hifadhi. Atakaye bainika kulisha mifugo katika eneo hili atatozwa faini ya shilingi 20,000/= 10. Ni marufuku kuwinda wanyama katika maeneo ya msitu wa hifadhi bila kibali cha uwindaji kutoka kwa Afisa wanyama pori na kibali cha kuingia msituni kutoka kamati ya Maliasili au Halmashauri ya Kijiji, atakaebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya Tshs 50,000/= kwa watakaokutwa na bunduki, Tshs 10,000/= kwa silaha nyingine na wategaji mitego na Tshs. 4,000 kwa wanaokamata wanyama wadogo bila silaha. Aidha vifaa alivyokuwa anatumia kuwindia pamoja na kitoweo atakachokutwa nacho vitataifishwa.

11. Aidha itakuwa ni makosa kukiuka sheria ndogo zinazohusu msitu wa hifadhi zilizoainishwa katika mpango wa usimamizi wa msitu wa hifadhi wa Mkanga1

12. Halmashauri ya kijiji itahakikisha kuwepo kwa ulinzi muda wote katika hifadhi hizi.

13. Matumizi ya msitu wa hifadhi yatasimamiwa na Kamati ya Maliasili na Halmashauri ya kijiji kama ilivyoainishwa kwenye mpango wa usimamizi wa msitu wa hifadhi mkanga1 na sheria ndogo zake.

Page 47: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

39

14. Kamati ya Maliasili na Mazingira na Kamati ya Usimamizi wa Ardhi ya kijiji zitasimamia na kuendeleza maeneo haya kwa kushirikiana na Halmashauri ya kijiji. (e) Maeneo ya Hifadhi ya vyanzo vya maji 1. Ni marufuku kulima ndani ya mita 200 kutoka chanzo cha maji. Atakayebainika kulima katika eneo hilo atatozwa faini ya shilingi 10,000/= na kulazimika kung`oa mazao yake au kulipa gharama za ung`oaji wa mazao hayo. 2. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo lililotengwa kwa ajili ya vyanzo vya maji. Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/- au kupelekwa mahakamani. 3. Ni marufuku kujenga nyumba katika maeneo ya vyanzo vya maji. Atakaye bainika kujenga katika eneo hili serikali ya kijiji itamwita na kumuamuru kubomoa nyumba yake. Akikaidi H/kijiji itabomoa nyumba hiyo na muhusika atalazimika kulipia gharama za ubomoaji wa nyumba yake. 4. Ni marufuku kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo ya vyanzo vya maji. Shughuli za kibinadamu ni pamoja na kufua, kuoga, kuosha vyombo au kutupa uchafu. Atakaebainika kufanya shughuli yeyote kati ya hizo atatozwa faini ya Tshs. 2,000/=

5. Ni marufuku kuywesha mifugo katika eneo lililotengwa kwa ajili ya vyanzo vya maji. Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 5,000/- 6. Ni marufuku kuharibu mabango yaliyowekwa matangazo ya kutunza eneo la chanzo cha maji na mazingira. Atakayebainika kuharibu mabango atatozwa faini ya shilingi 5,000/- (f) Eneo la Malisho 1. Ni marufuku kulima au kujenga nyumba katika eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo. Atakaye bainika kujenga au kupanda mazao katika eneo hili serikali ya kijiji itamwita na kumuamuru kubomoa nyumba au kung’oa mazao yake. Akikaidi serikali ya kijiji itabomoa au kung’oa mazao yake na muhusika atalipia gharama za ubomoaji au ung’oaji wa mazao hayo. 2. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho. Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/- na kulipa fidia ya uharibifu uliosababishwa na moto huo au kupelekwa mahakamani. (g) Eneo kwa ajili ya Tambiko 1. Eneo hili lipo ndani ya msitu wa hifadhi wa Mkanga1 hivyo watu wataruhusiwa kuingia katika eneo la tambiko kwa kibali cha bure kutoka kamati ya Maliasili ya kijiji cha Mkanga1.

Page 48: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

40

(h) Eneo kwa ajili ya makaburi 1. Ni marufuku kulima au kujenga nyumba katika eneo lililotengwa kwa ajili ya makaburi. Atakayebainika kujenga au kupanda mazao katika eneo hili atatozwa faini ya Tshs 5,000/= na kulazimika kubomoa au kungo`a mazao yake, akikaidi Halmashauri ya kijiji itabomoa jingo hilo au kung`oa mazao hayo na muhusika kulipa gharama za ubomoaji wa jingo lake au ung`oaji mazao yake. 2. Ni marufuku kuanzisha moto katika eneo lililotengwa kwa ajili ya makaburi. Atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya shilingi 50,000/- au kupelekwa mahakamani. 6. Mabadiliko ya Matumizi ya Ardhi Mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika eneo lolote lililoainishwa yatafanyika tu kwa Halmashauri ya Kijiji kurejea (review) na kurekebisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji na kupata ridhaa ya mkuano wa kijiji.

7. Adhabu Mtu yeyote anayethibitisha kutenda kosa na kukiuka sheria ndogo hizi, atafikishwa mahakamani na akipatikanna na hatia atahukumiwa kulipa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini Tshs 50,000/=) kwa kila kosa, na kuamriwa kurekebisha/kurejesha katika hali ya awali eneo lililo haribiwa au kulipa fidia ya uharibifu uliofanyika au kifungo kisichozidi mwaka mmoja.

Page 49: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

41

8. Kupitishwa na kusainiwa Sheria ndogo hizi zimetungwa na Halmashauri ya kijiji cha Mkanga1

Tarehe ………………. na kuidhinishwa na mkutano wa kijiji cha Mkanga1

Tarehe ………………….

Zimesainiwa:

Sahihi …………………………. Sahihi …………………………..

Jina ……………………………. Jina ……………………………..

AFISA MTENDAJI WA MWENYEKITI WA SERIKALI YA

KIJIJI CHA MKANGA1 KIJIJI CHA MKANGA1.

Zimegongwa mhuri wa Halmashuri ya Kijiji cha Mkanga1. Sheria ndogo hizi zimepitishwa na kusainiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi. Tarehe: ……………………………..

Zianze kutumika tarehe: ………………………………………

Sahihi …………………………. Sahihi …………………………..

Jina ……………………………. Jina ……………………………..

MKURUGENZI WA MANISPAA MEYA WA MANISPAA

YA LINDI YA LINDI

………………………………….. ……………………………………… Zimegongwa mhuri wa Manispaa ya Lindi ……………..

Page 50: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

42

KIAMBATANISHO: MIHUTASARI YA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA MKANGA 1

Page 51: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

43

Page 52: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

44

Page 53: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

45

Page 54: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA · jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa halmashauri ya kijiji cha mkanga 1 mpango wa matumizi

46