jamhuri ya muungano wa tanzania wizara ya uchukuzi€¦ · kampuni ya ndege tanzania (atcl). dira...
TRANSCRIPT
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
TAARIFA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961 - 2011)
DESEMBA, 2011.
ii
YALIYOMO
1.0 MAELEZO YA UTANGULIZI KUTOKA KWA WAZIRI WA UCHUKUZI . 1
2.0 UJUMBE WA KATIBU MKUU - WIZARA YA UCHUKUZI ...................... …4
3.0 UTANGULIZI ...................................................................................................... 7
4.0 HISTORIA FUPI YA WIZARA YA UCHUKUZI ............................................. 7
5.0 DIRA NA DHAMIRA YA WIZARA ................................................................... 7
5.1 Dira........................................................................................................................ 7
5.2 Dhamira ................................................................................................................ 8
6.0 MUUNDO WA WIZARA YA UCHUKUZI ........................................................ 8
6.1 Taasisi zilizo chini ya Wizara ............................................................................... 8
6.1.1 Wakala .................................................................................................................. 8
6.1.2 Mamlaka za Udhibiti ............................................................................................ 8
6.1.3 Mabaraza .............................................................................................................. 8
6.1.4 Mashirika na Makampuni .................................................................................... 8
7.0 MAJUKUMU YA WIZARA YA UCHUKUZI ................................................... 9
8.0 MALENGO YA WIZARA YA UCHUKUZI ...................................................... 9
9.0 UONGOZI NA UTAWALA KUANZIA MWAKA 1961 – 2011 ....................... 10
10.0 SERA NA SHERIA............................................................................................. 22
11.0 SEKTA NDOGO ZILIZO CHINI YA WIZARA YA UCHUKUZI ........................ 23
9.1 USAFIRI WA NCHI KAVU.................................................................................. 23
9.1.1 Shirika la Reli Tanzania ......................................................................................... 23
9.1.2 Kuanzishwa kwa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO) ................. 26
9.1.3 Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ..................................... 28
9.2 USAFIRI/UCHUKUZI WA MAJINI ................................................................ 32
9.2.1 Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) .............................................................. 32
9.2.2 Kampuni ya Meli ya SINOTASHIP ................................................................... 43
9.2.3 Kampuni ya Huduma za Meli – MSCL ............................................................. 46
9.2.4 Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)........ 53
9.3 USAFIRI WA ANGA ......................................................................................... 57
9.3.1 Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) .............................................................. 57
9.3.2 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ............................................................ 62
iii
9.3.3 Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) .............................................................. 72
9.3.4 Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ............................................................... 74
9.4 VYUO VYA MAFUNZO CHINI YA WIZARA ............................................... 76
9.4.1 Chuo Cha Bahari Dar Es Salaam (DMI) ........................................................... 76
9.4.2 Chuo Cha Usafirishaji (NIT) .............................................................................. 84
9.5 HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI ....................................................... 87
1
1.0 MAELEZO YA UTANGULIZI KUTOKA KWA WAZIRI WA UCHUKUZI
Kipindi hiki tunapoadhimisha miaka 50 tangu tupate uhuru mwaka 1961, Taifa
linashuhudia mabadiliko makubwa ya kisera na kimuundo katika Sekta ya Uchukuzi na Hali ya
Hewa. Miundombinu mbalimbali na huduma za uchukuzi zimeboreka kwa kiasi kikubwa.
Mara baada ya kupata uhuru, Serikali ilifanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa
kuanzisha programu na mikakati mbalimbali yenye lengo la kufufua uchumi. Programu hizo ni
pamoja na programu ya kufufua uchumi (Economic Recovery Programme) na marekebisho ya
kimuundo na kimenejimenti (Structural Adjustment Programme). Kufuatia juhudi hizo, mwaka
1987, Serikali ilizindua Programu ya kufufua sekta ya uchukuzi (Transport Sector Recovery
Programme) ili iwe chachu katika juhudi za kufufua uchumi. Mabadiliko katika sekta ya
uchukuzi yalilenga kuboresha miundombinu na huduma za uchukuzi ili kusaidia utendaji wa
sekta nyingine za kiuchumi na kijamii.
Baadhi ya Programu zilizoanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya uchukuzi ni
pamoja na;
Programu ya kuboresha miundombinu na huduma za bandari (Port Modernization
Programme -1985),
Programu ya uboreshaji wa sekta ya uchukuzi (Transport Sector Recovery Proggramme
- 1987),
Programu ya kuboresha miundombinu na huduma za Reli (Railway Restructuring
Programme -1991), na
Programu ya kuboresha miundombinu na huduma za barabara (Integrated Roads
Programme - 1991).
Aidha, katika mwaka 1992, Serikali iliruhusu sekta binafsi kushiriki katika utoaji wa
huduma za ndani za uchukuzi kwa njia ya anga.
Juhudi nyingine zilizochukuliwa ni kubadili mfumo wa uendeshaji na uongozi wa Idara
na mashirika mbalimbali yenye majukumu ya kuendeleza Sekta za Uchukuzi na Hali ya Hewa
nchini. Kutokana na hatua hizi, ziliundwa taasisi mbalimbali za Umma ambazo zilisaidia
kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. Taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti
wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia
2
(TAZARA). Taasisi nyingine ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mamlaka ya Hali ya
Hewa (TMA) na Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA),
Vile vile jitihada za kuboresha usafirishaji na uchukuzi nazo zilifanywa kwa kuanzisha;
Kampuni Miliki ya Mali za Reli iliyokuwa TRC (RAHCO),
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL),
Kampuni ya uendelezaji wa uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO) na
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).
Dira ya Wizara ni kuwa na Miundombinu ya uchukuzi na Huduma za Uchukuzi na
Hali ya Hewa zenye ubora, salama, gharama nafuu na endelevu zinazochochea maendeleo ya
jamii kwa kuzingatia dira ya taifa ifikapo mwaka 2025.
Kutokana na dira ya wizara na ile ya taifa ya mwaka 2025, hali ya miundombinu na
huduma za uchukuzi bado hazijafikia viwango vya kukidhi mahitaji ya kiuchumi na kijamii. Ili
kuimarisha na kuboresha miundombinu na huduma za uchukuzi, Wizara ya Uchukuzi
imepanga kutekeleza yafuatayo;
Kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya uchukuzi.
Kushirikisha Sekta binafsi katika uwekezaji kupitia utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya
Umma na binafsi (PPP). Hatua hii itahusu kutafuta wawekezaji kwenye miundombinu
ya reli, viwanja vya ndege na bandari.
Kuboresha Rasilimali watu kwa kuimarisha vyuo vya mafunzo katika nyanja za Reli,
Anga, Majini na hali ya hewa.
Kuimarisha usalama wa abiria na mizigo katika vyombo vya uchukuzi.
Kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya uchukuzi. Hii ni pamoja na
utekelezaji wa Mpango Kamambe wa Sekta ya Reli, huduma za pamoja za utafutaji na
uokoaji, ushirikiano katika kupambana na matukio ya uharamia na uimarishaji wa
usalama wa usafiri wa Anga.
Kuimarisha huduma za reli ya Dar es Salaam - Tabora hadi Kigoma na Mwanza
pamoja na matawi yake,
Kujenga upya Reli ya Kati na matawi yake yote na kujenga reli mpya kutoka Isaka hadi
Kigali (Rwanda) na Musongati (Burundi) kwa kiwango cha kimataifa (Stndard Gauge),
Kukarabati na kuimarisha huduma za reli ya Tanga hadi Arusha,
Kuboresha reli ya Tanga hadi Arusha na kujenga reli mpya ya Arusha hadi Musoma
kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge)
Kuimarisha huduma za bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga,
Kujenga bandari mpya za Mbegani (Bagamoyo) na Mwambani (Tanga), na
Kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege
3
Katika kipindi cha miaka 50 ijayo, Serikali itahakikisha kuwa miundombinu na huduma za
uchukuzi zinaboreshwa ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka siku hadi siku. Lengo ni
kuhakikisha kuwa mifumo yote ya uchukuzi (Reli, Barabara, Anga, bandari na hali ya hewa)
inafanya kazi kwa kutegemeana na inakuwa na mtandao wa reli na usafiri wa anga
unaoiunganisha nchi nzima. Katika kufanya hayo, Sekta binafsi itashirikishwa kikamifu.
Kutokana na juhudi zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika katika kuboresha
miundombinu na huduma za uchukuzi tangu tupate uhuru, Sekta ya uchukuzi tunasema
TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE. Kwa pamoja,
tutafanikiwa.
Omari Rashid Nundu (Mb),
WAZIRI WA UCHUKUZI
Desemba, 2011
4
2.0 UJUMBE W AKA TIBU MKUU - WIZARA YA UCHUKUZI
Mwezi Desemba, 2011 nchi yetu inasherehekea miaka 50 ya
Uhuru wa Tanzania Bara. Sherehe hizo zinaambatana na kuainisha tulikotoka; mafanikio
yaliyopatikana na tuendako katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka shilingi bilioni 7.2 mwaka
1961 hadi kufikia shilingi trilioni 16.83 mwaka 2010. Ongezeko hili linachangiwanasektaya
Uchukuzi pamoja na sekta nyingine za kuichumi na kijamii.
Mchango wa sekta ya Uchukuzi katika pato la Taifa kwa mwaka 2010 pekee ni shilingi bilioni
853.53 sawa na asilimia 5.4 ya pato la Taifa. Kati ya mwaka 2005 na 2010 sekta ya Uchukuzi
imekua kwa wastani wa asilimia 6.4 na hivyo kuwa miongoni mwa sekta muhimu katika
kukuza uchumi wa Taifa letu.
Wakati wa Uhuru wa Tanzania Bara mwaka 1961, majukumu ya sekta ya uchukuzi yalikuwa
chini ya iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano, Umeme na Ujenzi. Kwa nyakati tofauti, majukumu
yasekta ya uchukuzi yamekuwa yakijumuishwa pamoja na sekta nyingine chini ya Wizara za
Usafirishaji, Kazi na Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mawasiliano na Ujenzi na
Miundombinu.
Baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kuingia madarakani katika kipindi chake cha pili,
Desemba, 2011, Wizara ya Miundombinu iligawanywa na kuundwa Wizara mpya za Uchukuzi
na ile yaUjenzi. Wizara ya Uchukuzi ina jukumu la kusimamia huduma na miundombinu ya
sekta ya Uchukuzi katika maeneo ya usafiri wa reli, usafiri wa majini, usafiri wa anga na
huduma za hali ya hewa
Majukumu ya Wizara ya Uchukuzi ni pamoja na kutunga sera zinazohusu sekta katika
masuala ya uchukuzi na hali ya hewa na kusimamia utekelezaji wake. Aidha, huratibu na
kusimamia shughuli za utoaji wa leseni na usalama wa usafiri wa anga. Pia Wizara inaendeleza
5
na inasimamia ujenzi wa miundombinu ya reli, viwanja vya ndege, bandari na hali ya hewa.
Wizara ya Uchukuzi inasimamia masuala ya ulinzi na usalama katika Sekta ya Uchukuzi;
kuendeleza rasilimali watu pamoja na kusimamia Idara za Serikali, Taasisi, Mashirika ya
Umma, Programu na Miradi.
Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita Wizara ya Uchukuzi imekuwa ikitekeleza
majukumu yake kwa kuzingatia Sera na Sheria za nchi, mipango na mikakati mbalimbali
ikiwemo MKUKUTA na Dira ya Taifa ya mwaka 2025.
Jitihada na mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya uchukuzi kwa miaka 50 iliyopita
ni pamoja na:
(i) Ujenzi wa Reli mpya kwenye maeneo ya:
Stesheni ya Ruvu - Mruazi (Kilometa 188) mwaka 1963,
Kilosa - Mikumi - Kidatu (kilometa 108) mwaka 1960-1965,
Kahe - Taveta (kilometa 18) mwaka 1984,
Manyoni - Singida (kilometa 115) mwaka 1985-1997.
(ii) Ujenzi wa reli ya Uhuru - TAZARA (kilometa 1,860; kwa upande wa Tanzania ni
km.975) mwaka 1970 - 1975. Reli hii inaanzia Dar es Salaam hadi New Kapiri
Mposhi, Zambia.
(iii) Ukarabati wa reli kati ya stesheni za Gulwe na Kilosa baada ya mafuriko,
(iv) Uimarishaji wa uwezo wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ili kutoa utabiri wa hali ya
hewa wa uhakika.
(v) Uanzishwaji wa vyuo vya mafunzo katika Sekta ya Uchukuzi. Vyuo hivyo ni Chuo cha
Bahari Dar es Salaam (DMI), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Hali ya
Hewa Kigoma, Chuo cha Reli Tabora, Chuo cha Usafiri wa Anga Dar es Salaam na
Chuo cha Bandari.
(vi) Ujenzi na upanuaji wa bandari za mwambao. Hii ni pamoja na kuongezeka kwa magati
kutoka 3 hadi 14 katika bandari ya Dar es Salaam; kuanzisha vituo 8 vya kuhifadhi
makasha nje ya bandari (ICDs).
(vii) Kuongezeka kwa shehena kupitia Bandari zetu kutoka tani milioni 1.2 mwaka 1961
hadi kufikia tani rnilioni 10.2 mwaka 2010.
(viii) Kuandaa na kuanza kutekeleza Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Uchukuzi(TSIP)
(ix) Kuongezeka kwa Viwanja vya Ndege vya Kimataifa nchini kutoka kimoja mwaka 1961
hadi vitatu mwaka 2011. Mwaka 1961 kulikuwa na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Dar es Salaam (hivi sasa Julius Nyerere International Airport - JNIA), Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Airport - KIA)
kilichojengwa mwaka 1971 na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe
ambacho kinatarajiwa kukamilika Desemba, 2011.
6
Pamoja na mafanikio mengi yaliyopatikana tangu Uhuru, Wizara ya Uchukuzi
imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake.
Changamoto hizo ni pamoja na uwezo mdogo wa kifedha kulinganisha na mahitaji halisi ya
miradi ya maendeleo, ajali mbalimbali ambazo zimepoteza maisha ya watu na mali, uchakavu
wa miundombinu ya reli na Bandari.
Katika kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana baada ya miaka 50 ya Uhuru,
Wizara imejiwekea malengo ya muda rnrefu kwa ajili ya kuendeleza sekta ya uchukuzi.
Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na kuendelea kutekeleza Mpango wa Uwekezaji wa Sekta
ya Uchukuzi (TSIP) ili kuboresha miundombinu ya reli, bandari na viwanja vya ndege. Lengo
la Mpango huu ni kupunguza umaskini na kuleta maendeleo; kuimarisha bandari za mwambao
na zile za maziwa makuu; kuimarisha huduma za uchukuzi wa anga na hali ya hewa nchini;
kuweka mazingira mazuri ya kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya uchukuzi;
uendelezaji wa matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali na
kuendeleza rasilimali watu ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika sekta.
Ni matarajio yangu kwamba katika kipindi cha miaka 50 ijayo Wizara ya Uchukuzi
itakuwa na miundombinu ya Uchukuzi ya kisasa inayoendeshwa kwa kutumia teknolojia ya
kisasa. Aidha, ni matumaini yangu pia kwamba watumishi wa Wizara ya Uchukuzi na
Watanzania kwa ujumla tutawajibika zaidi katika miaka 50 ijayo kwa nia ya kuijenga nchi kwa
manufaa yetu na vizazi vijavyo.
Tumethubutu, Tumeweza Tunazidi kusonga mbele
Mhandisi Omar A. Chambo
KATIBU MKUU
Desemba, 2011
7
2.0 UTANGULIZI
Tanzania Bara ilipata uhuru mwaka 1961. Mwaka 2011 Serikali imeazimia kusherehekea
miaka 50 ya Uhuru. Azma hiyo ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru ilitangazwa kwa
mara ya kwanza na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete wakati akitoa salamu za mwaka mpya 2011.
Taifa linasherehekea miaka 50 ya Uhuru wake huku likishuhudia mafanikio ya
maendeleo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Maendeleo haya ya
jumla yamechangiwa na michango ya sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sekta ya
Uchukuzi.
Nafasi ya Sekta ya Uchukuzi katika maendeleo ya nchi inaweza kufananishwa na damu
katika mwili wa binadamu. Sekta ya Uchukuzi huwezesha ukuaji wa shughuli za
kiuchumi na kijamii. Kwa mfano wakulima wanategemea mchango wa sekta ya uchukuzi
katika kusafirisha pembejeo katika maeneo yao ya kilimo na kusafirisha mazao ya kilimo
kutoka kwenye maeneo ya uzalishaji kwenda kwenye masoko; wafanyabiashara na
viwanda huhitaji kusafirisha bidhaa zao kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda kwa
watumiaji katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi; watalii huhitaji usafiri kuja
nchini na kwenda kwenye maeneo mbalimbali yenye vivutio vya kitalii nchini, usafiri
unahitajika kuwawezesha wananchi kupata huduma za kijamii kama elimu, afya, nk.
3.0 HISTORIA FUPI YA WIZARA YA UCHUKUZI
Wakati wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, shughuli za Sekta ya Uchukuzi zilikuwa chini ya
iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano, Umeme na Ujenzi. Kwa nyakati tofauti, shughuli za Sekta ya
Uchukuzi zimekuwa zikijumuishwa pamoja na Sekta nyingine kama inavyoonekana katika
Jedwali Na. 5.1.
Mnamo Disemba 2010 baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kuingia madarakani kwa kipindi chake
cha pili, Wizara ya Uchukuzi iliundwa. Wizara hii inahusika na usimamizi wa sekta za Uchukuzi na
Hali ya Hewa.
4.0 DIRA NA DHAMIRA YA WIZARA
4.1 Dira
Dira ya Wizara ya Uchukuzi ni kuwa na Miundombinu na Huduma za Uchukuzi na Hali ya Hewa
zenye ubora, salama, gharama nafuu na endelevu zinazochochea maendeleo ya jamii kwa
kuzingatia dira ya Taifa ifikapo mwaka 2025.
8
4.2 Dhamira
Dhamira ya Wizara ni kuwa na huduma na Miundombinu ya Uchukuzi, ambazo ni salama;
zinazotegemewa; zilizo na uwiano na ambazo zinakidhi mahitaji ya usafiri na uchukuzi katika
kiwango bora kwa bei nafuu na zinazoendana na mikakati ya Serikali ya maendeleo ya kiuchumi na
kijamii wakati huo huo zikiwa endelevu kiuchumi na kimazingira.
5.0 MUUNDO WA WIZARA YA UCHUKUZI
Wizara ya Uchukuzi ina Idara tano ambazo ni Idara za Utawala na Rasilimali Watu, Miundombinu
ya Uchukuzi, Huduma za Uchukuzi, Sera na Mipango, na Usalama na Mazingira. Aidha, Wizara
ina Vitengo sita ambavyo ni Uhasibu, Habari, Ununuzi, Ukaguzi wa Ndani, Sheria na TEHAMA.
5.1 Taasisi zilizo chini ya Wizara
5.1.1 Wakala
Wakala za Serikali ambazo zipo chini ya Wizara ni pamoja na Wakala wa Hali ya Hewa
(TMA), Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), na Wakala wa Viwanja vya Ndege
(TAA).
5.1.2 Mamlaka za Udhibiti
Ili kuhakikisha kuwa huduma za Uchukuzi zinatolewa kwa viwango na kwa kuzingatia
usalama, Serikali iliunda Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Usafiri
wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).
5.1.3 Mabaraza
i. Baraza la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi kavu na Majini
ii. Baraza la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Anga
5.1.4 Mashirika na Makampuni
Wizara ina Taasisi na Makampuni ambayo yanahusika na utekelezaji wa majukumu ya
Sekta. Taasisi na Makampuni hayo ni kama ifuatavyo:-
i. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA)
ii. Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL)
iii. Kampuni Miliki ya Raslimali za Reli (RAHCO)
iv. Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
v. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
9
vi. Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL)
vii. Kampuni ya Meli ya pamoja kati ya Serikali ya China na Tanzania
(SINOTASHIP)
viii. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
ix. Chuo cha Bahari Dar Es Salaam (DMI)
x. Chuo cha Hali ya Hewa (Kigoma)
xi. Kampuni ya Uendelezaji wa Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KADCO)
6.0 MAJUKUMU YA WIZARA YA UCHUKUZI
Kulingana na Hati (Instrument) iliyotolewa na Mhe. Rais kwa mujibu wa Katiba ya Nchi,
Wizara ya Uchukuzi imepewa majukumu ya kusimamia masuala yafuatayo:
i. Kutunga Sera zinazohusu Sekta katika masuala ya Uchukuzi na Hali ya Hewa na
kusimamia Utekelezaji wake.
ii. Kuratibu na kusimamia shughuli za Utoaji wa Leseni za usafirishaji.
iii. Kusimamia masuala ya Usalama wa usafiri wa Anga.
iv. Kusimamia masuala ya Usafiri na Uchukuzi wa Anga
v. Kuendeleza na kusimamia Viwanja vya Ndege (vikubwa na vidogo) na huduma
zake.
vi. Kuendeleza na kusimamia Miundombinu ya Reli na Huduma zake.
vii. Kuendeleza na kusimamia miundombinu ya Bandari na Huduma zake.
viii. Kusimamia masuala ya Ulinzi na Usalama katika Sekta ya Uchukuzi.
ix. Kuendeleza na kusimamia miundombinu ya Hali ya Hewa na Huduma zake.
x. Kuongeza tija (Utendaji kazi) na kuendeleza Rasilimali watu.
xi. Kusimamia Idara za Serikali, Taasisi, Mashirika ya Umma, Programu na Miradi
iliyo chini ya Wizara.
7.0 MALENGO YA WIZARA YA UCHUKUZI
Katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake, Wizara ilijiwekea malengo ya muda mrefu
kama ifuatavyo:
i. Kutayarisha na kutekeleza mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya Sekta ya
Uchukuzi ili kuboresha miundombinu ya reli, bandari na viwanja vya ndege kwa
lengo la kupunguza umasikini na kuleta maendeleo,
ii. Kuimarisha reli ili kuongeza uwezo wa uchukuzi wa shehena nchini na zile za nchi
jirani,
iii. Kuimarisha bandari za mwambao na zile za maziwa makuu
10
iv. Kutekeleza Mpango Kabambe wa Uendelezaji Bandari (Ports Masterplan) katika
maeneo muhimu ya kipaumbele katika uendelezaji wa bandari nchini.
v. Kuimarisha huduma za uchukuzi wa anga hasa viwanja vya ndege.
vi. Kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika
sekta.
vii. Kuendelea kushirikiana na taasisi husika katika kushughulikia masuala mtambuka
kama vile kampeni za kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI, uhifadhi
wa mazingira, masuala ya jinsia pamoja uendelezaji wa matumizi ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.
viii. Kuendeleza na kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini.
ix. Kuendeleza rasilimali watu ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
8.0 UONGOZI NA UTAWALA KUANZIA MWAKA 1961 – 2011
Mawaziri mbalimbali walipata fursa ya kuongoza Wizara hii tangu tupate uhuru mwaka
1961. Waziri wa kwanza wa Wizara ya Mawasiliano, Umeme na Ujenzi ambayo ilikuwa
na dhamana ya kusimamia shughuli za uchukuzi, alikuwa marehemu Amir Habib Jamal.
Mawaziri wengine ambao waliopata fursa ya kuiongoza Wizara hii wameoneshwa katika
Jedwali Na. 7.1. Aidha, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu
waliowahi kuwa katika wizara hii wameoneshwa kuanzia Jedwali Na. 7.2 hadi 7.4.
Jedwali Na.7.1: Wizara ya Uchukuzi ilivyokuwa inajulikana na Mawaziri waliowahi
kuiongoza Wizara tangu mwaka 1961 hadi 2011
S/N JINA JINA LA WIZARA KIPINDI
1. Amir Habib Jamal Mawasiliano, Umeme na Ujenzi 1959 - 1963
2. Job M. Lusinde Mawasiliano, Umeme na Ujenzi 1963 - 1965
3. Job M. Lusinde Usafirishaji, Kazi na Ujenzi 1965 - 1972
4. Alfred C. Tandau Mawasiliano na Uchukuzi 1972 - 1973
5. Job M. Lusinde Mawasiliano na Ujenzi 1973 - 1976
6. Amir H. Jamal Mawasiliano na Uchukuzi 1977 - 1979
7. Guntram A. M. Itatiro Mawasiliano na Ujenzi 1980 - 1981
11
8. Ibrahim Kaduma Mawasiliano na Uchukuzi 1981
9. Agustin Mwingira Mawasiliano na Uchukuzi 1982
9. Guntram A. M. Itatiro Mawasiliano na Uchukuzi 1981 - 1984
10. John. S. Malecela Mawasiliano na Uchukuzi 1984 - 1985
11. Steven Kibona Mawasiliano na Ujenzi 1986 - 1989
12. Mustafa Nyang‟anyi Mawasiliano na Ujenzi 1989 – 1990
13. Pius Ngw‟andu Uchukuzi 1990
14. Jackson Makweta Mawasiliano na Uchukuzi 1991 – 1992
15. Prof. Philemon Sarungi Mawasiliano na Uchukuzi 1993 - 1994
16. Nalaila Kiula Mawasiliano na Uchukuzi 1994 - 1995
17. William J. Kusila Mawasiliano na Uchukuzi 1995 - 1997
18. Ernest Nyanda Mawasiliano na Uchukuzi 1997 - 2000
19. Prof. Mark Mwandosya Mawasiliano na Uchukuzi 2000 - 2006
20. Basil P. Mramba Miundombinu 2006 - 2007
21. Andrew Chenge Miundombinu 2007 - 2008
22. Dkt.Shukuru J. Kawambwa Miundombinu 2008 - 2010
23. Omari R. Nundu Uchukuzi 2010 - hadi sasa
Jedwali Na.7.2: Manaibu Waziri waliopata fursa ya kuongoza Wizara 1961 – 2011
S/N JINA JINA LA WIZARA KIPINDI
1. Chifu E. A. Mang‟enya Mawasiliano, Umeme na Ujenzi 1963
2. John. A. Mhaville Mawasiliano na Ujenzi 1964
3. F.V. Mponji na
Alhaji Omari Muhaji Mawasiliano, Kazi na Ujenzi 1965 - 1967
4. F.V. Mponji na
Edward M. Sokoine Usafirishaji, Kazi na Ujenzi 1967 - 1968
12
5. Richard. S. Wambura Mawasiliano, Uchukuzi na Kazi 1969
6. Robert Ng‟itu Mawasiliano na Ujenzi 1973
7. Mustafa Nyang‟anyi Mawasiliano na Ujenzi 1974
8. Samwel J. Sitta Mawasiliano na Uchukuzi 1977
9. Edgar M. Majogo Mawasiliano na Uchukuzi 1978 -1979
10. Arcado D. Ntagazwa Mawasiliano na Ujenzi 1985 – 1987
11. Simai Pandu Makame Mawasiliano na Uchukuzi 1991- 1992
12. Capt.Ditopile Mzuzuri Mawasiliano na Uchukuzi 1993
13. Edgar M. Majogo Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi 1993 - 1995
14. Dkt. Maua Daftari Mawasiliano na Uchukuzi 1995 – 2005
15. Dkt. Maua Daftari na
Dkt.Makongoro Mahanga Miundombinu 2006 - 2008
16. Hezekiel N. Chibulunje Miundombinu 2008 - 2010
17. Athuman R. Mfutakamba Uchukuzi 2010 hadi sasa
Jedwali Na.7.3: Makatibu wakuu waliopata fursa ya kuongoza Wizara 1961 – 2011
S/N JINA JINA LA WIZARA KIPINDI
1. F. K. Burengelo Mawasiliano, Uchukuzi na Kazi 1962
2. Balozi Juma Maggidi Mawasiliano, Umeme na Ujenzi 1962 – 1965
3. Ainamansa E. Mbuya Usafirishaji, Kazi na Ujenzi 1965 - 1968
4. J. Sepeku Mawasiliano na Uchukuzi 1970
5. Daniel N. M. Mloka Mawasiliano na Ujenzi 1978 – 1979
6. Odira Ongara Mawasiliano na Uchukuzi 1979 – 1980
7. Richard Shenkunde Juma Mawasiliano na Uchukuzi 1980 –1983
8. Paul Justine Mkanga Mawasiliano na Uchukuzi 1983 - 1984
13
9. Odira Ongara Mawasiliano na Ujenzi 1984 – 1987
10. Paul Justine Mkanga Mawasiliano na Ujenzi 1987 – 1989
11. Dkt Felician Mujuni Mawasiliano na Ujenzi 1989 – 1990
12. Balozi Richard Maliki Mawasiliano na Uchukuzi 1990 – 1993
13. Dkt George Mlingwa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi 1993 – 1995
14. Salim M. Msoma Mawasiliano na Uchukuzi 1995 – 2005
15. John Kijazi Miundombinu 2005 – 2006
16. Dkt.Enos Bukuku Miundombinu 2006 – 2008
17. Mhandisi Omar A. Chambo Miundombinu 2008 - 2010
18. Mhandisi Omar A. Chambo Uchukuzi 2010 hadi sasa
Jedwali Na.7.4: Manaibu Makatibu wakuu waliopata fursa ya kuongoza Wizara
1. Mhandisi Omar A. Chambo Miundombinu 2006 - 2008
2. Ndg. Joyce Mapunjo Miundombinu 2008 - 2009
3. Balozi Harbert Mrango Miundombinu 2010
4. Ndg. John T. Mngodo Uchukuzi 2011 hadi sasa
14
Kielelezo 1: PICHA ZA VIONGOZI WA SASA WA WIZARA
Mhe. Omari R. Nundu (Mb.)
Waziri wa Uchukuzi
Mhe. Dkt. Athuman R. Mfutakamba (Mb.)
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Mhandisi Omar A. Chambo Ndg. John T. Mngodo
Katibu Mkuu Naibu Katibu Mkuu
15
Kielelezo 2: PICHA ZA MAWAZIRI WALIOWAHI KUONGOZA WIZARA
Amir H. Jamal
Job M. Lusinde
Wizara ya Mawasiliano, Umeme na Ujenzi
Wizara ya Mawasiliano, Umeme na Ujenzi
1959 - 1963
1963 - 1972
Alfred C. Tandau
Job M. Lusinde
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi
1972 - 1973
1973 - 1976
Amir H. Jamal
Guntram A.M Mtatiro
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi
1977 - 1979
1980 - 1981
16
Ibrahim Kaduma
Augustin Mwingira
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
1981
1982
Guntram A.M Mtatiro
John S. Malecela
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
1982- 1984
1984 - 1985
Steven Kibona
Mustafa Nyang'anyi
Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi
Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi
1985 - 1989
1989 - 1990
17
Pius Ngw'andu
Jackson Makweta
Wizara ya Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
1990
1991 - 1992
Prof. Philemon Sarungi
Nalaila Kiula
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
1993 - 1994
1994- 1995
William J. Kusila
Ernest Nyanda
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
1995- 1997
1997- 2000
18
Prof. Mark Mwandosya
Basil Mramba
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
Wizara ya Miundombinu
2000- 2006
2006 - 2007
Andrew Chenge
Dkt. Shukuru J. Kawambwa
Wizara ya Miundombinu
Wizara ya Miundombinu
2007 - 2008
2008- 2010
19
Kielelezo 3: PICHA ZA MANAIBU MAWAZIRI WALIOWAHI KUONGOZA
WIZARA
Chifu E. A Mang'enya John A. Mhavile
Wizara ya Mawasiliano,
Umeme na Ujenzi
Wizara ya Mawasiliano na
Ujenzi
1963 1964
F.V Mponji Alhaji Omari Muhaji
Wizara ya Mawasiliano, Kazi
na Ujenzi
Wizara ya Mawasiliano, Kazi
na Ujenzi
1965 - 1968 1965 - 1968
Edward M. Sokoine Richard S. Wambura
Wizara ya Usafirishaji, Kazi
na Ujenzi
Wizara ya Mawasiliano,
Uchukuzi na Kazi
1967 - 1968 1969
20
Robert Ng'itu Mustafa Nyang'anyi
Wizara ya Mawasiliano na
Ujenzi
Wizara ya Mawasiliano na
Ujenzi
1973 1974
Samwel J. Sitta Edgar M. Majogo
Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi
1977 1978 - 1979
Arcado D. Ntagazwa Edgar M. Majogo
Wizara ya Mawasiliano na
Ujenzi
Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi
1985 – 1987
1993 - 1995
21
Kapt. Ditopile U. Mzuzuri Dkt. Maua Daftari
Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi
Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi
1993 1995 - 2005
Dkt. Maua Daftari Dkt. Makongoro Mahanga
Wizara ya Miundombinu Wizara ya Miundombinu
2006 - 2008 2006 - 2008
Hezekiel N. Chibulunje
Wizara ya Miundombinu
2008 - 2010
22
9.0 SERA NA SHERIA
Tangu uhuru Serikali imeendelea kuandaa sera na sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha
huduma katika sekta hii ya uchukuzi. Sera na sheria hizo ni pamoja na;
i. Airports Service Charges (1962)
ii. The Transport Licensing Act (1973) ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1978,
1979, 1994, 1996, 1999, 2001, 2005 na 2009 ikiwa inatekelezwa na Central Traffic
Licensing na Regional Licensing Authorities.
iii. The Aerodromes (Licensing and Control) Act No. 1 of 1974
iv. Tanzania Railways Corporation Act No. 11 of 1977
v. Civil Aviation Act No. 13 of 1977 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002 na
2003.
vi. Meteorology Act 1978
vii. Sheria ya Bunge Na. 30 ya 1997 kuhusu uundwaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
viii. Sheria ya Bunge Na. 30 ya 1997 kuhusu uundwaji wa Mamlaka ya hali ya Hewa
Tanzania
ix. Sheria ya ya Bunge Na. 212 ya mwaka 1997 inayohusu uanzishwaji wa makampuni
iliyoanzisha MSC
x. Sheria ya Bunge Na. 9 ya mwaka 2001 iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri
wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)
xi. Sheria ya Bunge Na. 4 ya Mwaka 2002 (Railway Act No. 4 of 2002) kuhusu uanzishaji
wa Reli Assets Holding Company – (RAHCO)
xii. Sera ya Taifa ya Uchukuzi (2003)
xiii. Mamlaka ya Usafiri wa Usafiri wa Anga (TCAA) ilianzishwa upya kwa Sheria Na. 10
ya mwaka 2003 (Civil Aviation Authority Act 2003)
xiv. Sera ya Taifa ya Teknohama 2003
xv. Sheria ya Bunge Na. 17 ya mwaka 2004 kuhusu uanzishaji wa Mamlaka ya Usimamizi
wa Bandari Tanzania (TPA)
xvi. Sera ya Taifa ya Usalama Barabarani 2010
23
xvii. Sheria ya Bunge Na 4 ya mwaka 1975 kuhusu uanzishwaji wa TAZARA
10.0 SEKTA NDOGO ZILIZO CHINI YA WIZARA YA UCHUKUZI
10.1 USAFIRI WA NCHI KAVU
10.1.1 Shirika la Reli Tanzania
Uendelezaji wa Reli nchini ulianzishwa kwa mara ya kwanza wakati wa enzi za Utawala wa Kijerumani
mnamo miaka ya 1880, wakati reli ya kwanza ilipojengwa kutoka Tanga na kufika Mombo mwaka 1904.
Ujenzi wa reli hiyo uliendelea na kufika Moshi mwaka 1911, na baadaye Arusha katika mwaka 1929.
Ujenzi wa reli ya kati ulianzia Dar es salaam mnamo mwaka 1905 na kufika Morogoro mwaka 1907, na
baadaye kufika Mwanza mwaka 1926. Reli ya kutoka Tabora hadi Kigoma ilijengwa kati ya mwaka 1912
-1914. Mtandao wote wa reli kwa wakati huo uliendelea kumilikiwa na kuendeshwa na Serikali za
Kikoloni, hadi ilipofika Mwaka 1961, Tanganyika ilipojitawala.
Kama ilivyo katika nchi nyingi duniani, usafiri wa reli umeendelea kuwa nguzo muhimu ya kuwezesha na
kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara. Hii inatokana na ukweli kwamba usafiri wa reli ni wa gharama
nafuu sana ikilinganishwa na aina nyingine za usafiri, hususan kwa kusafirisha mizigo mikubwa kwa
umbali mrefu kuanzia kilometa 400 na zaidi.
Wakati wa Utawala wa Kijerumani, ujenzi wa reli ulifanywa kwa lengo kubwa la kusafirisha mali ghafi
kama katani, kahawa, pamba, madini na mbao ngumu n.k kwa ajili ya Soko la Ulaya. Malighafi hizi kwa
ujumla zilisafirishwa kutoka bara kuelekea pwani kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi. Kwa Upande
mwingine usafiri wa reli ulitumika kama njia rahisi ya kusafirisha bidhaa mbalimbali za viwandani kutoka
nje ya nchi, kwa ajili ya soko la hapa nchini.
Mwaka 1948 Reli ya Tanganyika (Tanganyika Railways) na huduma za Bandari ( Port services)
ziliungana na makampuni ya reli ya Kenya na Uganda na bandari kuwa “ East African Railways and
Harbours – (EAR& H)” . Wakati Tanzania, Kenya na Uganda zilipoanzisha Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) mwaka 1967, Shirika la reli la Afrika Mashariki (EARC) liliundwa kama nguzo
mojawapo ya msingi wa kiuchumi wa Jumuiya ya Afrika mashariki. Katika miaka ya sabini (70s), Shirika
la reli la Afrika Mashariki lilianza kufifia polepole kutokana na mahusiano kudorora na kila nchi ikawa
inajitegemea zaidi yenyewe nje ya Jumuiya. Sehemu ya reli ya Tanzania wakati mwingine ilikuwa
ikijulikana kama EAR (T) ilianza kutafuta vitendea kazi vyake na kujitegemea. Mwaka 1977, baada ya
kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania ilianzisha Shirika la Reli Tanzania ( Tanzania
Railways Corporation – TRC) kwa sheria ya Bunge Na. 11 ya mwaka 1977.
Mtandao wa Reli ya Kati uliopo hivi sasa una umbali wa jumla ya kilometa 2,707, kama unavyoanishwa
hapa chini.
Njia Kuu (Main Lines);-
Dar es Salaam –Tabora 840km
Tabora – Kigoma 411km
24
Tabora – Mwanza 379km
Tanga - Moshi - Arusha 438km
Ruvu Junction – Mruazi Junction 188km
Matawi (Branch Lines);-
Kilosa – Kidatu 108 km
Kaliua - Mpanda 210 km
Manyoni – Singida 115 km
Kahe –Taveta (Mpakani na Kenya) 18 km
Mtandao wa TRC uliopo unahudumia nchi nne zisizopakana na bahari. Nchi hizo ni Burundi, Rwanda,
Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Vile vile mtandao huu unaungana na ule wa Kenya
kupitia tawi la reli lenye urefu wa Kilometa 18 kutoka Kahe hadi Taveta.
Katika kipindi cha miaka hamsini (1961 – 2011) baada ya uhuru mafanikio kadhaa yameweza kupatikana
katika Sekta ya Reli kama yanavyoainishwa katika aya zifuatazo.
Ujenzi wa Reli mpya
i. Kujengwa kwa reli (kilometa 188) kutoka Stesheni ya Ruvu hadi Mruazi iliyoko katika njia ya
reli ya Tanga – Arusha, mwaka 1963.
ii. Kukamilika kwa ujenzi wa reli kati ya Kilosa - Mikumi – Kidatu (kilometa 108) mwaka 1960-
1965.
iii. Kukamilika kwa ujenzi wa reli (kilometa 18) kati ya Kahe – Taveta mwaka 1984.
iv. Ujenzi wa reli (kilometa 115) kati ya Manyoni – Singida mwaka 1985-1997.
Kuanzishwa kwa Shirika la Reli la Afrika Mashariki
Moja ya mafanikio makubwa ilikuwa ni kuanzishwa kwa Shirika la Reli la Afrika Mashariki, lililodumu
kwa miaka kumi (1967 – 1977), ambapo zilizokuwa nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda na
Tanzania) ziliweza kuendesha shughuli za reli katika mtandao mmoja wa reli, wenye upana wa mita moja
(meter gauge). Shirika hili lilivunjika mwaka 1977 kutokana na kutoelewana miongoni mwa nchi
wanachama.
Usafirishaji wa Mizigo na Abiria
Sekta ya reli iliendelea kuwa njia muhimu katika usafirishaji wa mizigo na abiria hapa nchini. Mfano
mwaka 1984 kati abiria 4,100,000 waliosafirishwa kwa njia zote za usafiri abiria 3,040,000 walisafirishwa
kwa reli, hii ikiwa ni sawa na asilimia 74. Katika mwaka huo pia, kati ya tani 1,030,000 za mizigo yote
iliyosafirishwa nchini, tani 910,000 zilisafirishwa kwa njia ya reli, hii ikiwa ni sawa na asilimia 89.
Katika mwaka 2002, Shirika la Reli (TRC) lilivunja rekodi kwa kusafirisha jumla ya tani 1,446,000 za
mizigo, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa tangu mwaka 1977 Shirika lilipoanzishwa. Jedwali 9.1(a)
na Jedwali 9.1(b) yafuatayo yanabainisha jinsi ambavyo sekta ya reli iliweza kuchangia, kuwezesha na
kuchochea shughuli za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo.
25
Jedwali Na 9.1 (a): Usafirishaji wa abiria TRC (Miaka ya 1970, 1980, 1990 na
2000)
Mwaka Idadi ya abiria wote Idadi ya abiria
waliosafirishwa kwa Treni
Asilimia
1976 (1970‟s) 2,660,333 2,197,912 83
1987(1980‟s) 2,154,000 1,485,000 69
1990(1990‟s) 2,486,142 1,714,000 69
2007(2000‟s) 585,310
Jedwali Na 9.1 (b): Usafirishaji wa mizigo TRC (Miaka ya 1970, 1980, 1990 na
2000)
Mwaka Kiasi cha mizigo yote
iliyosafirishwa nchini
(Tani)
Kiasi cha mizigo
iliyosafirishwa kwa
Treni (Tani)
Asilimia
1976 (1970‟s) 712,030 698,206 98
1987(1980‟s) 1,000,000 902,000 90
1990(1990‟s) 1,011,580 898,810 89
2007(2000‟s) 545,241
Ubinafsishaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Kama sehemu ya Mpango wa Taifa wa kubinafsisha Mashirika ya Umma, Shirika la Reli
Tanzania (TRC) lilibinafsishwa rasmi mnamo mwezi Septemba mwaka 2007, baada ya Serikali
ya Tanzania kuingia ubia na Kampuni ya RITES ya India, iliyokuwa imeshinda zabuni ya
kuendesha reli ya kati kwa kipindi cha miaka 25.
Ubinafsishaji huu ulisababisha kuundwa kwa Kampuni ya Reli Tanzania (Tanzania Railways
Ltd). Tanzania Railways Limited (TRL) ni Kampuni iliyoundwa na kumilikiwa kwa pamoja
kati ya Serikali ya Tanzania iliyomiliki asilimia 49 ya hisa na RITES iliyomiliki asilimia 51 ya
hisa. Kampuni ilianza kazi rasmi ya kuendesha reli ya kati mwezi Oktoba 2007, chini ya
menejimenti ya RITES.
26
Pamoja na Serikali kuingia ubia na Kampuni ya RITES kwa lengo la kuboresha usafiri wa reli
ya kati, TRL ilishindwa kabisa kufikia na kutimiza malengo yaliyowekwa na kutegemewa.
Hivyo, baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya Serikali na RITES, na baada ya
kukubaliana, Serikali iliamua kununua hisa asilimia 51 za RITES. Ili kuinusuru Kampuni ya
Reli (TRL), pamoja na huduma ya reli nchini, Serikali iliamua kuteua menejimenti ya mpito
kuendesha Kampuni, wakati utaratibu wa kumpata mwekezaji ukiendelea. Bodi ya
Wakurugenzi ya RITES ilijiuzulu tarehe 22 Julai, 2011 na kufuatia kujiuzulu huko shughuli za
TRL zilikabidhiwa rasmi kwa Menejimenti ya mpito tarehe 26 Julai, 2011.
10.1.2 Kuanzishwa kwa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO)
Kwa kupitia Sheria ya Reli Namba 4 ya mwaka 2002 na kama sehemu ya mchakato wa
ubinafsishaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Serikali iliamua kuanzisha Kampuni ya
Kusimamia na Kuendeleza Miundombinu na Rasilimali za Reli (RAHCO). Majukumu na kazi
za RAHCO ni pamoja na:
Kurithi majukumu ya iliyokuwa TRC ya utoaji wa huduma ya usafiri wa reli, ikiwa ni
pamoja na kurithi mali, haki na madeni ya TRC;
Kwa niaba ya Serikali Kusimamia, Kukuza na Kuendeleza Miundombinu ya Reli
Kuingia mikataba na makampuni mengine kwa njia za ukodishaji (concession), ubia,
ushirikishaji wa sekta binafsi n.k. katika kutoa huduma ya usafiri wa reli.
Kutafuta maeneo mapya ya ardhi (Estates) kwa ajili ya kuendeleza shughuli za reli
kama kujenga ICDs, maghala n.k.
Kuboresha miundombinu iliyopo ya reli ya kati ili kuhakikisha inapitika kwa kipindi
chote cha mwaka.
Kwa ujumla RAHCO ni mmiliki (Landlord) wa miundombinu ya Reli iliyokuwa inamilikiwa
na TRC na pia muendelezaji wa miundombinu ya Reli nchini wakati TRL ni muendeshaji
(Operator) wa huduma za reli.
Katika kutekeleza majumu yake baadhi ya kazi ambazo RAHCO imeendelea kutekeleza na
kufanikisha ni pamoja na:
Kuendelea na mchakato wa uendelezaji na ujenzi wa reli mpya kutoka Dar es Salaam -
Isaka – Kigali / Keza-Gitega-Musongati kwa kiwango cha kimataifa “Standard
Gauge”.
Kufanya matengenezo ya awali (restoration works) na kuendelea na matengenezo ya
kudumu (protection works) ya miundombinu ya reli iliyokuwa imeharibiwa vibaya na
mvua kati ya Stesheni za Kilosa na Gulwe mnamo miezi ya Disemba 2009 na Januari
2010. Baadhi ya kazi zinazoendelea kufanyika, ni pamoja na Kurekebisha mwelekeo
wa mto Mkondoa (River Training) kwa kutumia matuta, Kuimarisha kingo za tuta la
27
reli katika sehemu hatarishi kwa kutumia “gabioni”, Kuimarisha / kujenga madaraja
katika sehemu ya reli, Kuhamisha njia ya reli (diversion of route) ili ipite sehemu
salama n.k.
Kufidia wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya kujenga
miundombinu ya reli ili kugeuzia mabehewa (Marshalling yard) katika maeneo
yanayotegemewa kujengwa bandari ya Mwambani (Tanga) na Mbegani (Bagamoyo).
Kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya miradi mipya ya ujenzi wa reli kama mradi wa
reli ya kutoka Mwambani (Tanga) kupitia Arusha mpaka Musoma.
Eneo No. 3 km 289+575 kabla ya kutengenezwa Jan-2010
Eneo No. 3 km 289+575 Baada matengenezo Novemba -2010
Changamoto zinazoikabili Reli ya Kati:
28
Uchakavu wa miundombinu ya reli kwa nchi nzima. Mtandao wa reli ya kati uliopo
ulijengwa miaka mingi iliyopita, takribani miaka 100. Mtandao huu kwa sasa unahitaji
kuboreshwa, ikiwa ni pamoja na utandikaji wa reli nzito zaidi ili kuweza kuhimili na
kukidhi mahitaji ya sasa.
Uchakavu wa Injini, mabehewa na mitambo mbalimbali (Rolling stock).
Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya reli unaohitaji
fedha nyingi (capital intensive).
Idadi ndogo na kushuka kwa ubora wa injini za treni kwa sababu ya uchakavu.
Mipango ya RAHCO katika uboreshaji wa Miundombinu ya Reli katika miaka 50 ijayo
Mipango muhimu ya uboreshaji na uendelezaji wa huduma ya usafiri wa reli inayotegemewa
kutekelezwa katika kipindi cha miaka hamsini ijayo ni kama ifuatavyo:
i. Kuboresha kilometa 982 za njia ya reli kutoka Dar es salaam – Isaka ili kufikia kiwango
cha kimataifa (standard gauge) itakayokuwa na kiwango cha upana wa mm 1435 na
uzito wa ratili 120 kwa yadi,
ii. Kujenga kilometa 690 ya njia ya reli mpya kutoka Isaka – Kigali (Rwanda)/Keza-
Gitega-Musongati (Burundi) kwa kiwango cha upana wa mm 1435 na uzito wa ratili
120 kwa yadi kwa kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi.
iii. Kuboresha reli kutoka Isaka – Mwanza, Tabora- Kigoma na matawi ya Kidatu, Singida
na Mpanda kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge) itakayokuwa na upana wa
mm 1435 na uzito wa ratili 120 kwa yadi (Jumla ya kilometa 1,105)
iv. Kuboresha na kujenga reli ya kutoka Tanga (Mwambani) – Arusha – Musoma
(kilometa 938) kwa kiwango cha upana wa mm 1435 na uzito wa ratili 120 kwa yadi.
Hii itajumuisha pia kujenga matawi ya njia kwenda sehemu za Minjingu katika kiwanda
cha mbolea na Wosiwosi – Lake Natron panapotarajiwa kujengwa kiwanda cha
kuzalisha magadi.
v. Kujenga reli ya kutoka Mtwara – Songea mpaka Mbamba Bay na kuunganisha na
maeneo ya Liganga na Mchuchuma kunapotarajiwa kujengwa Migodi ya chuma na
makaa ya mawe.
vi. Kujenga reli kutoka eneo la Kidomole katika njia ya reli (Ruvu – Mruazi) kwenda eneo
la Bandari mpya ya Mbegani – Bagamoyo.
vii. Kuboresha na kujenga mtandao mzuri wa reli ndani ya Jiji la Dar es salaam kwa ajili ya
treni za abiria ili kupunguza msongamano.
10.1.3 Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
TAZARA imeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya TAZARA namba 23 ya mwaka 1975
iliyorekebishwa kwa sheria ya TAZARA namba 4 ya mwaka 1995 na inamilikiwa kwa uwiano
wa hisa hamsini kwa hamsini 50:50 baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na
Serikali ya Jamhuri ya Zambia.
29
TAZARA ilijengwa katika mwaka 1970 hadi mwaka 1975 na kuanza rasmi biashara ya
usafirishaji kwa treni za abiria na mizigo katika mwezi Julai, 1976. Serikali ya Jamhuri ya watu
wa China (PRC) ilifadhili ujenzi wa reli hii.
Mamlaka ya reli TAZARA huanzia katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania na huishia
katika mji wa New Kapiri Mposhi nchini Zambia ikiwa ni urefu wa umbali wa jumla ya km
1,860; upande wa Tanzania kuna umbali wa km 975 na kwa upande wa Zambia kuna umbali
wa km 885. TAZARA inasafirisha mizigo kati ya nchi ya Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC), Malawi na Bandari ya Dar es Salaam. Reli hii pia husafirisha mizigo ya ndani
ya nchi ya Tanzania, kati ya mikoa ya ukanda wa kusini na Dar es Salaam. TAZARA pia
hufanya biashara ya usafirishaji wa abiria wa ndani na wa kimataifa kwa treni zake za abiria
zinazofanya kazi kati ya Dar es Salaam na New Kapiri Mposhi. TAZARA imekuwa ikitoa
huduma ya treni maalum kwenda na kurudi kwenye mbuga za wanyama za „Sealous National
Park‟ kwa kadri ya mahitaji.
Usafirishaji wa abiria na mizigo – TAZARA
Takwimu za mafanikio katika usafirishaji wa mizigo na abiria kuanzia mwaka 1976/77 hadi
mwaka 2009/10 zimeoneshwa katika Jedwali Na.9.2 ambapo jumla ya tani za mizigo
26,998,477 zilizosafirishwa na jumla ya abiria 43,671,888 waliosafirishwa.
Jedwali Na 9.2: Tani za mizigo na idadi ya abiria waliosafirishwa kwa miaka ya 1976/77
hadi 2009/10
Mwa
ka
wa
fedha
Jumla
ya Tani
za
mizigo
zilizosaf
i rishwa
(tani)
Kati ya hizo
Mizigo
iliyosafir
ishwa ya
nchi
nyingine
Jumla ya
idadi ya
abiria
waliosafi
rishwa
(Watu)
Kwenda
nje ya
Zambia
Kuingi
a
ndani
ya
Zambi
a
Mizigo
ya
ndani
mkoa
wa
Zambia
Kwend
a nje
ya
Tanzan
ia
Kuingi
a
ndani
ya
Tanza
nia
Mizigo
ya
ndani
mkoa
wa
Tanzan
ia
(tani)
76/77 1134000 511000 418000 37000 - - 168000 - 826000
77/78 1273000 596000 425000 16000 - - 236000 - 1134000
78/79 924000 393000 271000 9000 - - 251000 - 1313000
79/80 790000 228000 204000 33000 - - 325000 - 1397000
80/81 752000 312000 235000 20000 - - 185000 - 1025000
81/82 797000 328000 263000 42000 - - 174000 - 987000
30
82/83 825000 392000 239000 42000 - - 152000 - 564000
83/84 973000 431000 492000 58000 - - 192000 - 1198000
84/85 1102000 491000 289000 55000 - - 267000 - 1080000
85/86 984000 402000 168000 61000 - - 306000 47000 1220000
86/87 1228000 483000 323000 57000 - - 310000 55000 1335000
87/88 1173000 419000 351000 52000 - - 291000 60000 1575000
88/89 1075000 370000 365000 55000 - - 245000 40000 1652000
89/90 996000 343000 261000 56000 - - 310000 26000 1681000
90/91 927000 349000 187000 62000 - - 285000 44000 1551000
91/92 963000 345000 165000 39000 - 91000 228000 95000 1888000
92/93 1079000 282000 399000 21000 37000 69000 96000 175000 2180000
93/94 647000 239000 85000 7000 21000 68000 88000 139000 1789000
94/95 641000 236000 124000 28000 34000 34000 96000 89000 1762000
95/96 663000 227000 64000 29000 100000 11000 144000 88000 1475000
96/97 555235 198291 61481 7334 26195 19144 137149 105641 1225487
97/98 631751 180890 88495 7708 26667 25918 220570 81503 1535814
98/99 616073 162256 27857 22050 38952 51412 229643 83903 1422138
99/00 633832 163559 65784 22599 26980 19476 226974 108460 1543297
00/01 608528 156082 45728 20092 15638 14731 228624 127633 1540682
01/02 577207 164682 79663 36345 10408 6203 155820 124086 1068287
02/03 613693 175975 107591 68313 15173 19675 108615 118351 1050612
03/04 610280 196567 55829 16168 26698 18277 183151 113590 929138
04/05 632478 166819 90631 14422 39093 45284 161180 115049 933439
05/06 601229 164209 97145 13727 43669 17124 136298 129057 889740
06/07 538530 153501 83740 8087 29066 8866 123188 132082 1090359
07/08 527620 170211 118984 11075 45307 16856 73393 91794 1047281
31
08/09 383055 112907 157932 2325 27033 5978 25861 53019 996548
09/10 522966 179032 114123 986 27287 8196 87997 105345 767066
Juml
a
2699847
7
972198
1
652298
3
1030231 590166 550140 644746
3
2347513 43671888
Chanzo: Vitabu vya Takwimu za TAZARA
Hali ya sasa ya Reli ya TAZARA
Reli ya TAZARA ina jumla ya Stesheni 93 ambapo 56 zipo upande wa Tanzania na 37 upande
wa Zambia.
Kwa upande wa matanuli (tunnels), reli ya TAZARA ina jumla ya matanuli 23 ambapo 12
yapo upande wa Tanzania na 1 lipo mpakani mwa Tanzania na Zambia. Tanuli refu kabisa lina
urefu wa km 1.8 na lipo kati ya Mrimba na Makambako. Aidha, katika eneo hili, ndani ya km
30 kuna jumla ya matanuli 9.
Reli ya TAZARA ina jumla ya madaraha 322 ambapo 274 yapo upande wa Tanzania na 48
upande wa Zambia. Daraja kunbwa kabisa lipo kati ya Mrimba na Makambako na lina urefu
wa mita 800 na kina cha mita 50.
Changamoto zinazoikabili Reli ya TAZARA
Sekta ya Reli imekuwa ikikabiliwa na changamoto zifuatazo:
Uchakavu wa miundombinu ya reli kwa nchi nzima. Mtandao wa reli ya kati uliopo
ulijengwa miaka mingi iliyopita, takribani miaka 100. Mtandao huu kwa sasa unahitaji
kuboreshwa, ikiwa ni pamoja na utandikaji wa reli nzito zaidi ili kuweza kuhimili na
kukidhi mahitaji ya sasa.
Uchakavu wa Injini, mabehewa na mitambo mbalimbali (Rolling stock).
Ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya reli unahitaji fedha nyingi (capital intensive).
Serikali inaendelea na mchakato wa kutafuta fedha kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na kuishirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya umma na
Sekta binafsi (Public Private Partnership – PPP).
Kurudisha imani kwa wateja walioamua kusafirisha mizigo yao kwa kutumia barabara
baada ya usafirishaji katika sekta ya reli kuzorota kwa muda mrefu.
Idadi ndogo na kushuka kwa ubora wa injini za treni kwa sababu ya uchakavu.
Kuongezeka kwa gharama za uendeshaji zinazochangiwa na kupanda kwa gharama za
mafuta na vipuri.
Tatizo la uhaba na uchakavu wa mawasiliano na ishara kwa treni.
Mipango ya uboreshaji wa sekta ya Reli katika miaka 50 ijayo
32
Mipango muhimu ya uboreshaji na uendelezaji wa huduma ya usafiri wa reli inategemewa
kutekelezwa katika kipindi cha miaka hamsini ijayo ni kama ifuatavyo:
viii. Kuboresha kilometa 982 za njia ya reli kutoka Dar es salaam – Isaka ili kufikia
kiwango cha kimataifa (standard gauge) itakayokuwa na kiwango cha upana wa
mm 1435 na uzito wa ratili 120 kwa yadi,
ix. Kujenga kilometa 690 ya njia ya reli mpya kutoka Isaka – Kigali (Rwanda)/Keza-
Gitega-Musongati (Burundi) kwa kiwango cha upana wa mm 1435 na uzito wa ratili
120 kwa yadi kwa kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi.
x. Kuboresha reli kutoka Isaka – Mwanza, Tabora- Kigoma na matawi ya Kidatu,
Singida na Mpanda kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge) itakayokuwa na
upana wa mm 1435 na uzito wa ratili 120 kwa yadi (Jumla ya kilometa 1,105)
xi. Kuboresha na kujenga reli ya kutoka Tanga (Mwambani) – Arusha – Musoma
(kilometa 938) kwa kiwango cha upana wa mm 1435 na uzito wa ratili 120 kwa
yadi. Hii itajumuisha pia kujenga matawi ya njia kwenda sehemu za Minjingu
katika kiwanda cha mbolea na Wosiwosi – Lake Natron panapotarajiwa kujengwa
kiwanda cha kuzalisha magadi.
xii. Kujenga reli ya kutoka Mtwara – Songea mpaka Mbamba Bay na kuunganisha na
maeneo ya Liganga na Mchuchuma kunapotarajiwa kujengwa Migodi ya chuma na
makaa ya mawe.
xiii. Kujenga reli kutoka eneo la Kidomole katika njia ya reli (Ruvu – Mruazi) kwenda
eneo la Bandari mpya ya Mbegani – Bagamoyo.
xiv. Kuboresha na kujenga mtandao mzuri wa reli ndani ya Jiji la Dar es salaam kwa
ajili ya treni za abiria ili kupunguza msongamano.
xv. Kuimarisha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa kuboresha
miundombinu ya reli.
xvi. Kuimarisha TAZARA ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vichwa vya treni, ukarabati
wa vichwa vya treni, ununuzi wa mabehewa ya mizigo, ukarabati wa Kreni za
mizigo, ukarabati wa Kreni za okoa, ununuzi wa malighafi ya utengenezaji wa
mataruma ya reli (Concrete sleepers) na vipuri vya mabehewa 1200 ya mizigo.
10.2 USAFIRI/UCHUKUZI WA MAJINI
10.2.1 Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
Bandari ni kiungo muhimu katika uchukuzi kati ya nchi kavu na majini na zaidi ya asilimia 85
ya biashara yote duniani husafirishwa kupitia sekta ya bandari. Tanzania ina ukanda wa bahari
wenye urefu wa kilomita 960 na bandari kuu tatu ambazo ni Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Pia ina maziwa makuu matatu ambayo yana bandari ambazo ni Mwanza, Bukoba, Musoma na
Kemondo katika ziwa Victoria; Kigoma na Kasanga katika Ziwa Tanganyika; na Itungi na
Mbambabay katika Ziwa Nyasa. Bandari zote ziko chini ya umiliki na usimamizi wa Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
33
Bandari za Tanzania ni tegemeo katika kuhudumia shehena ya Tanzania na nchi za jirani. Nchi
hizi ni pamoja na Burundi, Rwanda, Congo na Uganda ambazo hutumia reli ya kati (TRL), na
Zambia, DR Congo na Malawi zinazotumia reli ya TAZARA.
Historia Fupi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA)
Historia ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari inaanza mwaka 1893 wakati wa ujenzi wa reli
kutoka Tanga na Bandari ya Dar es Salaam mwaka 1905. Mwaka 1947 hadi 1967 mamlaka
hii ilijulikana kama “East African Railways and Harbours Corporation”. Mwaka 1967 hadi
1977 ilijulikana kama “The East African Harbours Corporation” na mwaka 1977 hadi 2005
kwa jina la “Tanzania Habours Authority - THA”. Mwaka 2004 Bunge la Tanzania lilipitisha
Sheria ya Bandari (Ports Act No. 17) iliyoanzisha Mamlaka mpya inayojulikana kama
“Tanzania Ports Authority - TPA”.
Shirika la Reli na Bandari Afrika Mashariki lililojulikana kama “The East African
Railways and Harbours Corporation (1947-1967)
Mwaka 1947, iliundwa taasisi/mamlaka rasmi iliyojulikana kama „The East African Railways
and Harbours Corporation” ilikuwa na jukumu la kuhudumia mifumo ya njia za reli pamoja
na bandari kwa nchi zilizokuwa makoloni ya Uingereza katika eneo la Afrika Mashariki (yaani
Kenya, Uganda na Tanganyika).
Uongozi wa „The East African Railways and Harbours Corporation‟ uliundwa mwaka 1948
baada ya kuvunjwa kwa uongozi wa mashirika makuu mawili yanayosimamia reli na bandari
eneo la Afrika Mashariki ambayo ni Shirika la Reli na Bandari kwa Kenya na Uganda (KUR)
na Shirika la Reli na Bandari kwa Tanganyika (TR).
Mapema katika miaka ya 1960, nchi tatu za Afrika Mashariki ziliingia mkataba wa ushirikiano
katika kumiliki vyombo vikuu vya usafirishaji kwa njia ya reli, huduma za barabara, huduma
za meli na bandari, huduma za anga, pamoja na karakana kuu zilizokuwa katika miji ya Dar es
Salaam na Nairobi.
Shirika la Bandari Afrika Mashariki lililojulikana kama “The East African Harbours
Corporation” (1967-1977)
Mwaka 1967 nchi tatu za Afrika Mashariki ziliunganisha nguvu na kuunda Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC). Hivyo, ikalazimu kuunda mamlaka mpya ya usimamizi wa bandari kwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye jukumu la kuendesha bandari kuu za Dar es Salaam,
Mombasa na bandari ya Tanga.
Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977. Mwaka 1976 mali na madeni ya Jumuiya
ziligawanywa baina ya nchi hizo tatu na kila nchi ilikuwa huru na yenye mamlaka ya kuhifadhi
34
mali zake. Tarehe 11 Februari 1977 Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Harbours
Authority) ilianzishwa.
Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Habour Authority - THA) mwaka 1977–2005
Mwaka 1998 THA iliwekwa kwenye orodha ya mashirika ya umma yaliyopangwa
kubinafsishwa (specified) na Serikali kupitia Tume ya Rais ya kurekebisha Mashirika ya
Umma (PSRC). Mwaka 2000, Kitengo cha Kontena kilibinafsishwa kwa TICTS ambayo
mwaka 2001 iliuza hisa kwa Kampuni ya HPH ya Hongkong.
Kati ya mwaka 2003 hadi 2004 Serikali ilifanya utafiti kuhusu kufungua milango ya biashara
(trade liberalization) katika sekta ya usafiri wa majini kwa kutumia kampuni ya „Marine‟
(RMG ya Uholanzi) ambayo ilipendekeza kutungwa Sheria mpya ya Bandari yaani “The Ports
Act No. 17” ambayo ilipitishwa na Bunge Novemba 2004, na kuunda Mamlaka
itakayosimamia bandari zote Tanzania. Mamlaka ilianza kazi zake rasmi Julai 1, 2006.
Mwezi Julai 2006, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania iliondolewa katika orodha ya
Mashirika ya kubinafsishwa yaani (de-specification). Sera ya Serikali ni kukodisha rasilimali
kwa waendeshaji binafsi na Serikali kuendelea kumiliki hisa zote (100%) chini ya mfumo wa
“Landlord Port Authority”.
Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi
Jukumu la utoaji wa huduma za bandari unashirikisha pia sekta binafsi na maeneo yafuatayo
yanaendeshwa na kampuni binafsi:
(i) Kitengo cha Kontena katika bandari ya Dar es Salaam ambacho kinaendeshwa na
Kampuni ya TICTS kwa mkataba wa miaka 25 (2000 – 2025);
(ii) Kitengo cha mizigo bandari ya Kigoma katika Ziwa Tanganyika ambacho
kinaendeshwa na Kampuni ya Gravimport ya Burundi chini ya Kampuni tanzu ya
MUAPI kwa mkataba wa miaka 5 (2008 – 2012);
(iii) Bandari ya Kasanga katika Ziwa Tanganyika ambayo inaendeshwa na Kampuni ya
Agro-Trucking ya Sumbawanga kwa mkataba wa mwaka 1 (Novemba 2010 – Oktoba
2011).
Nchi za jirani za Zambia, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, na
Malawi hupitisha mizigo yake katika bandari za Mamlaka. Makampuni tisa makubwa ya meli
ambayo ni East African Conference Lines, P&O Nedloyd, Maersk, Messina, MSC na Global
Container Line yanahudumiwa katika bandari za Mamlaka.
Matukio muhimu ya historia ya bandari ni kama ifuatavyo:
1901 Ujenzi wa sehemu ya kuundia majahazi Bandari ya Dar es Salaam
ulianza na baadaye ukaendelea mpaka Mwanza.
1912 Ujenzi wa bandari ya Kigoma ulianza
35
1914 Ujenzi wa bandari ya Tanga ulianza
1927 Chuo cha kusimamia shughuli za reli na huduma za bandari
kilichoitwa Tanzania Railways and Port Services Institution
kilianzishwa.
1954 Bandari ya Mtwara ilianza kujengwa
1950‟s Ujenzi wa bandari za Mwanza, Bukoba, Nansio, Musoma na Itungi
katika Ziwa Victoria na Ziwa Nyasa
1953 Upanuzi wa lango la bandari ya Dar es Salaam
1956 Ujenzi wa gati namba 1 mpaka 3 uliasha na gati hizo zikakabidhiwa na
mtoto wa Malkia wa Uingereza aitwaye Margaret.
1958 Ujenzi wa Kurasini Oli Jet (KOJ).
1967 Ujenzi wa Kituo cha Kuhifadhia Makasha kilichopo Ubungo.
1968 Ujenzi wa gati namba 4, 5 na 6.
1969 Shirika la Bandari la Afrika Mashariki lilianzishwa baada ya
kutenganisha Reli na Bandari.
1973 Kitengo cha mafuta cha Single Bouy Mouring (SBM) kilikabidhiwa
1977 Mamlaka ya Bandari (Tanzania Harbours Authority) ilianzishwa baada
ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
1978 Kukamilika kwa ujenzi wa gati namba 9, 10 na 11
1984 Kuanzishwa kwa Chuo cha Bandari kilichopo Dar es Salaam
1988 Gati namba 9, 10 na 11 zilibadilishwa na kuwa Kitengo rasmi cha
Makontena.
1989 Kukamilika kwa ujenzi wa Ghala la Nafaka bandari ya Dar es Salaam.
1998 Kina cha Mlango wa Bandari ya Dar es Salaam kiliongezwa kuruhusu
meli kuingia bandarini mchana na usiku.
1998 Mamlaka kuwekwa chini ya usimamizi wa PSRC (specified).
2000 Kitengo cha kontena kilikabidhiwa kwa mwendeshaji binafsi (TICTS).
2004 Sheria iliyounda Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
ilipitishwa ba Bunge kwa ajili ya kumiliki na kusimamia shughuli zote
za bandari za mwambao na maziwa.
2006 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania iliondolewa katika
orodha ya Mashirika ya yaliyoainishwa kubinafsishwa yaani „de-
specification‟.
2008 “Inland Container Depots” binafsi zilianza kutumika kuhudumia
shehena kontena bandari ya DSM.
2009 Mpango Mkakati wa kuendeleza bandari (Ports Master Plan) 2008 –
2028 ulikamilika.
2009 Serikali iliondoa Kipengele cha ukiritimba (Exclusivity) katika
kuhudumia makasha Bandari ya Dar es Salaam.
2010 Ukarabati wa kituo cha mafuta cha SPM (Single Point Mooring)
ulianza ili kukiwezesha kuhudumia mafuta ghafi na yaliyosafishwa.
2010 “Cargo Freight Stataions” (CFS) zilianza kuhudumia shehena ya
magari
Majukumu ya Mamalaka
36
Mamlaka imerithi majukumu ya iliyokuwa Mamlaka ya Bandari (THA) na kupewa majukumu
zaidi ya kumiliki na kuendeleza bandari zote nchini na zilizo katika Maziwa Makuu ambazo
zilikuwa zikiendeshwa na “Marine Services Company. Majukumu ya Mamlaka ni kama
yafuatayo:
(i) Kuendeleza Bandari (Develop)
(ii) Kuendesha shughuli za Bandari (Operate)
(iii) Kutangaza bandari kimasoko (Promote)
(iv) Kushirikisha na kusimamia sekta binafsi katika uendeshaji wa shughuli za bandari
(Landlord)
Hali ya Shehena
Kumekuwa na ongezeko kubwa la Shehena kupitia bandari za Mamlaka tangu wakati wa
UHURU mwaka 1961 hadi mwaka 2010. Shehena imeongezeka kutoka tani 1.185 milioni
mwaka 1961 hadi kufikia tani 9.624 milioni mwaka 2010.
Hali hii imechangiwa na kukua kwa uchumi katika nchi zinazotumia bandari zetu, uboreshaji
wa njia za usafirishaji kwa barabara na reli na kuongezeka kwa uwezo wa bandari zenyewe.
Shehena iliyopitia katika bandari zetu katika miaka ya 1961 ilikuwa ni ya kawaida iliyobebwa
na meli za kawaida zenye vifaa vya kupakua na kupakia. Hali hii ilibadilika baada ya
kuanzishwa kwa usafirishaji wa kontena katika miaka ya 1975 hadi hivi sasa. Mabadiliko haya
yamechangia shehena ya kontena kuongezeka kutoka kontena 46,507 zilizohudumiwa mwaka
1985 hadi kontena 425,181 mwaka 2010 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 9.3.
Jedwali Na. 9.3: Shehena iliyohudumiwa na Bandari za Mamlaka 1961-2010
.
Vifaa vya Kuhudumia Shehena
Mamlaka imewekeza zaidi ya dola milioni 500 pamoja na misaada kutoka Benki ya Dunia na
nchi mbalimbali za Ulaya katika kuendeleza miundombinu na manunuzi ya vifaa mbalimbali
kama yalivyoorodheshwa hapa chini:
(a) Magati na maeneo ya kuhifadhi mizigo
(b) Vifaa vya kupakia na kupakua mizigo
(c) Vifaa vya majini
(d) Majengo
MWAKA 1961 1985 1995 2005 2010
Shehena (tani) 1,185,000 1,262,820 4,583,407 6,794,773 9,623,550
Kontena (TEUs) - 46,507 99,708 249,310 425,181
37
Bandari imeongeza vifaa vya kuhudumia mizigo, sambamba na mabadiliko ya mfumo mzima
wa mabadiliko ya ubebaji mizigo. Usalama wa Bandari, pamoja na vifaa vya doria
umeimarishwa.
Bandari ya Dar es salaam
Bandari ya Dar es salaam ndiyo kubwa kuliko zote ikiwa na urefu wa kilomita 2.6 na upana wa
mita 500 na ina uwezo wa kuhudumia tani milioni 10.1 kwa mwaka. Bandari ina magati 11,
Gati Na. 1 - 7 zinahudumia shehena mchanganyiko na zinaendeshwa na Mamlaka. Gati Na. 8 -
11 zinahudumia shehena ya kontena na zimekodishwa kwa kampuni ya TICTS, Gati hizi zina
uwezo wa kuhudumia kontena 330,000 kwa mwaka. Vitengo vingine ni pamoja na kituo cha
kuhudumia mafuta (KOJ na SPM), kituo cha nafaka na karakana ndogo ya kukarabati meli,
Mashedi 10 ya mizigo, Kitengo cha kuhudumia meli za mwambao na Kitengo cha Nafaka
chenye uwezo wa kuhifadhi tani 30,000.
Lango Kuu la Bandari ya Dar es Salaam
Kabla ya Uhuru 1961, lango lilikuwa na uwezo wa kuingiza meli zenye urefu wa mita 145 –
175 na kina cha maji cha mita 7. Upanuzi wa lango ulifanyika mwaka 1998 ambapo kina
kilichimbwa hadi kufikia mita 10.5 na upana wa mita 140 kwa gharama ya Dola za Kimarekani
240 milioni. Hivi sasa lango linaruhusu meli zenye ukubwa usiozidi mita 234. Kutokana na
utekelezaji wa mradi wa kupanua na uwekaji wa taa katika lango kuu, pamoja na uchimbaji
ndani ya Bandari mwaka 1998, meli zinaweza kuingia usiku na mchana, ukubwa wa meli
umeongezeka hadi kufikia urefu wa mita 234/240 na kina cha maji kimeongezeka hadi kufikia
mita 10.5.
Uzito wa Meli na Vifaa
Uzito wa meli umeongezeka kutoka 18,000 DWT hadi 40,000 DWT. Vifaa vya kuhudumia
meli vimebadilika kutokana na mabadiliko ya meli na mizigo, kama vile ubebaji wa mizigo
kwenye kontena.
Changamoto zinazoikabili Bandari ya Dar es Salaam
Uwezo Mdogo wa Kuhudumia Meli Kubwa
Mabadiliko ya teknolojia yamesababisha meli kuongezeka ukubwa katika dhana ya “economies
of scales” ambapo kampuni nyingi za meli zimeshawishika kuzinunua. Meli hizi kubwa
zimelazimisha bandari nyingi kuongeza kina na upana wa milango ya bandari na kwenye
magati zinapofunga meli. Hivi sasa kuna meli za kizazi cha saba (7th generation) zenye uwezo
wa kuchukua kontena zaidi ya 10,000 kwa mara moja. Meli hizi zinahitaji bandari zenye kina
kinachozidi mita 15 na upana wa zaidi ya mita 240. Aidha, urefu wa gati unatakiwa uwe na
zaidi ya mita 300.
Meli kubwa zinaweza kufunga katika gati namba 7 - 11 tu ambapo gati namba 8 – 11
zinahudumia meli za kontena (kitengo kinachoendeshwa na kampuni ya TICTS). Hata hivyo
38
gati hizi zina urefu wa mita 180 kila moja na hivyo ni meli nne tu zinazoweza kufunga kwa
wakati mmoja badala ya meli tano.
Miundombinu Hafifu ya Reli na Barabara
Bandari ya Dar es Salaam inaunganishwa na masoko ya bara (hinterland) na nchi jirani kupitia
mtandao wa reli na barabara. Reli ya TRL inayoanzia bandari ya Dar es Salaam na ni tegemeo
kubwa katika usafirishaji wa mizigo ya nchi za DR Congo, Rwanda, na Burundi. Aidha reli ya
TAZARA inatumika kusafirisha mizigo ya Zambia na Malawi. Kutokana na utendaji hafifu wa
reli, mizigo mingi inasafirishwa kwa njia ya barabara. Kiwango cha uondoshaji wa mizigo
bandarini kwa njia ya reli kimeshuka na hivyo kuathiri uwezo wa bandari zetu kushindana
kikamilifu na bandari jirani katika kufikia masoko ya nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, Burundi, Rwanda na Uganda. Kwa mfano, shehena yote ya mafuta kuelekea nchi za
Rwanda, Malawi na DR Congo inasafirishwa kwa njia ya barabara.
Njia ya barabara ambayo ndiyo tegemeo kwa kusafirisha karibu asilimia 90 ya shehena
bandarini imeendelea kuathiriwa na gharama kubwa za uchukuzi, safari ndefu za njiani (Transit
times), uwezo mdogo wa kubeba mizigo mizito, na pia vikwazo vya njiani (Non tariff barriers).
Kwa mfano, inakadiriwa kuwa muda wa lori la mzigo kutoka Dar es Salaam kwenda DR
Congo na kurudi ni wastani wa siku 45 kutokana na vikwazo na urasimu mbalimbali njiani.
Hali hii itaendelea kuchangia katika kudumaza mtiririko mzima wa shehena na ufanisi wa
bandari kwa ujumla
Uondoshwaji wa mizigo ya hapa nchini pia unaathiriwa na msongamano wa magari katika
barabara za jiji, ubovu wa barabara zinazoingia na kutoka bandarini na zile zinazounganisha
bandari na vituo vya kuhifadhia kontena. Barabara hizi hazina taa na hivyo zinakwamisha
juhudi za bandari kutoa huduma masaa 24 kama ilivyo bandari nyingine.
Uwezo wa kuhudumia shehena ya Uganda na nchi za Maziwa Makuu umezidi kupungua
kutokana na uchache wa meli za mabehewa katika ziwa Victoria. Hivi sasa kuna meli moja tu
ya Tanzania, MV UMOJA ambayo husafirisha mizigo kutoka Port Bell hadi Mwanza.
Ushindani mkubwa kutoka bandari nyingine
Bandari za Mamlaka hususan bandari ya DSM inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka
bandari nyingine katika eneo hili kama vile bandari ya Mombasa nchini Kenya, Bandari
zilizoko nchini Msumbiji na Afrika Kusini. Shehena inayoshindaniwa ni kutoka nchini
Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Burundi, Rwanda na
sasa Sudani Kusini.
Kutokana na ushindani huu mkali, hata baadhi ya shehena ya Tanzania inapita bandari ya
Mombasa hasa shehena itokayo Kanda ya Ziwa (yaani Mwanza, Kagera, Shinyanga na Mara)
na mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania (Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Pia bandari zilizoko nchini Namibia na Angola zinalenga kuhudumia shehena katika ukanda
huu hasa ile ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Bandari ya Tanga
39
Bandari ya Tanga ilianza mwaka 1914 ambapo gati la kwanza la matishari lilijengwa na
mwaka 1952 gati lingine liliongezwa. Bandari ina kina kifupi na hivyo meli zinafunga nje ya
bandari (outer anchorage) na hivyo mizigo kupakiwa na kupakuliwa kwa kutumia pantoni.
Bandari ya Tanga ina gati mbili zenye jumla ya urefu wa mita 380 na kina kinafikia mita 2.5.
Mwaka 1970, gati lenye umbo la “L” lilijengwa kwa ajili ya kuhudumia shehena ya mbolea
kavu na ya majimaji. Utumiaji wa gati hili kwa ajili ya shehena ya mbolea ulisitishwa mnamo
mwaka 1990 kufuatia kufungwa kwa kiwanda cha mbolea cha Tanga.
Bandari ina vifaa vinavyotumika kuhudumia shehena ya mafuta yanayoingizwa kutoka nje ya
nchi ikiwa ni pamoja na boya lililounganishwa bomba la mafuta katika kina kifupi na kirefu
cha bandari. Bandari ina uwezo wa kuhudumia tani 500,000 kwa mwaka. Katika mwaka
2009/10, bandari ilihudumia tani 630,000, ikiwa ni zaidi ya uwezo wake kwa asilimia 26.
Changamoto za bandari ya Tanga
(i) Uwezo mdogo wa bandari kuhudumia meli kubwa.
(ii) Ufinyu wa maeneo ya kufanyia kazi (operational area). Bandari ina uhaba wa ardhi kwa
ajili ya upanuzi kwa kuwa maeneo jirani na bandari yanamilikiwa na kampuni na taasisi
nyingine.
(iii) Miundombinu ya barabara zinazoondosha mizigo bandarini ni hafifu.
(iv) Kusuasua kwa usafiri wa reli ambako kumedumaza maendeleo ya bandari. Hapo awali
Bandari ilikuwa inahudumia shehena ya mchanga kutoka migodi ya Kahama; Hivi sasa
shehena hii imepotea kutokana na usafiri wa reli kukoma.
(v) Kupungua sheheha ya viwanda kutokana na viwanda vingi kufungwa.
Bandari ya Mtwara
Bandari ya Mtwara ilianza mwaka 1954 ambapo gati mbili zilijengwa sanjari na reli ya
Nachingwea. Bandari ya Mtwara ilijengwa kwa madhumuni ya kuhudumia zao la korosho.
Hata hivyo reli ya Nachingwea iliondolewa mwaka 1963 kutokana na mradi wa kilimo cha
karanga kusitishwa. Bandari ina uwezo wa kuhudumia tani 400,000 kwa mwaka. Utendaji
wa bandari hivi sasa ni asilimia 25 tu ya uwezo wake.
Changamoto za Bandari ya Mtwara
Matatizo ya Bandari ya Mtwara ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji wa Bandari
ikilinganishwa na mapato. Bandari inategemea aina moja ya shehena ambayo ni Korosho.
Shehena ya korosho inaendelea kupungua kutokana na korosho inayobanguliwa hapa nchini
kufikia takribani asilimia 20 ikilinganishwa na asilimia 10 miaka ya nyuma. Korosho
iliyobanguliwa inasafirishwa kwa njia mbadala. Shehena nyingine iliyopungua ni pamoja na
Saruji kutoka Tanga na mafuta kutokana na uchache wa meli za mwambao.
Changamoto nyingine ya bandari ni pamoja na uwezo mdogo wa uondoshaji mizigo bandarini
kutokana na miundombinu hafifu ya usafirishaji.
40
Bandari ina fursa nzuri ya kuvutia wawekezaji kutokana na kuwepo eneo kubwa kwa ajili ya
upanuzi wa bandari. Mamlaka inamiliki hekta 2,600 kwa ajili ya upanuzi wa Bandari na
shughuli za EPZ. Matumizi ya bandari yanatarajiwa kuongezeka kutokana na miradi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
Vifaa vya ujenzi wa kiwanda cha Saruji na kiwanda cha Mbolea vinavyotarajiwa kuanza
kujengwa mwaka 2012;
Vifaa vya utafiti wa mafuta (off-shore exploration) katika bahari ya Hindi unaoendelea;
Shehena ya saruji na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya miradi ya ujenzi katika ukanda wa kusini;
na
Kauli mbiu ya Serikali ya ”Kilimo Kwanza” itaongeza uzalishaji wa mazao ya biashara
kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.
Bandari za Ziwa Victoria
Ujenzi wa Bandari za Mwanza, Bukoba, Nansio na Musoma ulianza miaka ya 1950. Bandari
hizi zinahudumia maeneo ambayo yana utajiri mkubwa wa kilimo na madini.
Changamoto Zinazokabili Bandari za Ziwa Victoria
Miundombinu ya kizamani, mfano matumizi ya „‟link span” ambayo yanategemea meli za
mabehewa. Shehena kati ya bandari za Mwanza na Port Bell nchini Uganda imepungua
kutokana na uchache wa meli za kubeba mabehewa (wagon ferries). Ukosefu wa
miundombinu ya kuhudumia shehena ya kontena umesababisha maendeleo ya bandari hizi
kudumaa. Aidha,
(a) Utendaji hafifu wa shirika la reli (TRL) pia umeathiri upatikanaji wa shehena;
(b) Wenye meli za abiria kutumia magati binafsi ziwani;
(c) Bandari zinajiendesha kwa hasara.
Bandari za Ziwa Tanganyika
Bandari kuu ni Kigoma ambayo ujenzi wake ulifanyika katika mwaka 1912 sanjari na ujenzi
wa reli ya kati. Gati la bandari ya Kasanga lilijengwa mwaka 1997. Kama zilivyo bandari
nyingine za maziwa, miundombinu yake imechakaa sana na hivyo inahitaji kuboreshwa.
Changamoto Zinazokabili Bandari za Ziwa Tanganyika
Matatizo ya bandari hizi ni pamoja na:
(a) Utendaji hafifu wa reli kati ya Dar es Salaam na Kigoma;
(b) Kutumika kwa gati binafsi ziwani;
(c) Miundombinu hafifu ya kuunganisha bandari na vyanzo vya shehena;
(d) Hali mbaya ya miundombinu ya bandari;
Miundombinu ya Bandari za Ziwa Nyasa
Bandari ya Itungi katika Ziwa Nyasa ilijengwa miaka ya 1950 sanjari na bandari nyingine
upande wa Malawi.
41
Changamoto zilizojitokeza katika utendaji wa Bandari ya Kyela ni pamoja na:
(a) Hali mbaya ya miundombinu ya bandari;
(b) Upungufu wa shehena ziendazo Malawi ikiwa ni pamoja na mbolea;
(c) Uhaba wa Meli zinazofanya kazi katika ziwa Nyasa.
(d) Gharama kubwa za uendeshaji wa bandari ukilinganisha na mapato.
Chuo Cha Bandari
Chuo cha Bandari kilichopo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kilianzishwa mwaka
1984. Madhumni ya kuanzishwa kwa Chuo hiki ilikuwa kutoa wataalamu wa kuendesha
shughuli za bandari. Chuo cha Bandari kama zilivyo idara nyingine za Mamlaka, kimekuwa
kikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo na mipango mkakati ya Mamlaka.
Katika kutekeleza mikakati hiyo, Chuo kinafanya yafuatayo:
(i) Kutoa mafunzo ya kuwaendeleza wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari katika fani zote
za shughuli za Bandari ili kuongeza tija na ufanisi. Katika kutekeleza jukumu hili Chuo
kinafanya kazi kwa karibu na Kurugenzi ya Utumishi na Bandari zote katika kubaini
mahitaji ya mafunzo na hatimaye kuandaa na kufundisha kozi zinazokidhi mahitaji
hayo;
(ii) Kutoa ushauri katika fani za uendeshaji wa bandari (Port Operations) na uendeshaji wa
vifaa vya bandari (Port Equipment Operations) kwa watu binafsi, makampuni,
mawakala wa meli, wadau wa Bandari na wale ambao wanafanya shughuli
zinazohusiana na Bandari;
(iii) Kubuni na kuendesha mafunzo yanayohusiana na biashara ya upakuzi na upakiaji
mizigo katika meli na huduma mbalimbali zinazohitajiwa na jamii;
(iv) Kufuatilia na kutathmini mafanikio ya mafunzo kwa wateja binafsi na wadau wa
biashara ya majini na kufanya mchanganuo wa soko la kozi zinazotolewa;
(v) Kufanya mahusiano na vyuo vya ndani na nje na kufanya ushirikiano wa kimafunzo ili
kuinua viwango vya kozi zinazotolewa;
(vi) Kuendeleza na kuinua viwango vya elimu vya wakufunzi na wafanyakazi wengine;
(vii) Kuhakikisha kuwa mafunzo na vyeti vinavotolewa na Chuo vinatambulika katika
biashara ya majini (maritime industry), na kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na
Taasisi za Kitaifa kama vile NACTE (National Council for Technical Education).
Mafanikio ya Chuo
Kuanzishwa kwa masomo ya jioni ili kukidhi mahitaji hasa ya wafanyakazi
wasioweza kuhudhuria vipindi vya asubuhi;
Kujiendesha kibiashara;
Kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi hadi kufikia 887 katika mwaka
2011;
Baadhi ya wakufunzi wamepata mafunzo yanayoendeshwa na UNCTAD na
wangine wanajiendeleza kufikia Shahada ya Uzamili (Masters).
42
MATARAJIO YA MAMLAKA KWA MIAKA 50 IJAYO
Mpango wa Kuendeleza Bandari ( Ports Master Plan)
Mamlaka imetayarisha Mpango kamambe wa kuendeleza bandari zote katika kipindi cha miaka
20 ijayo.
Jedwali Na. 9.4 “Ports Master Plan” imeainisha miradi kwa kila bandari kama ifuatavyo:
Bandari Mikakati
Bandari mpya (a) Bandari ya Mbegani, Bagamoyo
(b) Bandari ya Mwambani, Tanga.
Dar es Salaam (a) Ujenzi wa gati mbili za kuhudumia kontena yaani gati namba
13 na14.
(b) Kuongeza kina cha lango la bandari kufikia mita 12
(c) Kuongeza kina cha gati namba 1-7 hadi mita 12
(d) Ujenzi wa kituo cha mafuta cha SPM
(e) Kuongeza eneo la Kurasini kwa ajili ya shehena ya kichele,
ujenzi wa silo za mbolea na “conveyor system” kuunganisha
na silo.
(f) Ujenzi wa gati la RoRo kwa ajili meli za magari
(g) Ujenzi wa kituo cha mizigo Kisarawe
(h) Ujenzi wa gati za kontena eneo la vijibweni.
Tanga (a) Kuongeza maeneo kwa ajili ya upanuzi wa bandari
(b) Kuboresha vifaa vya kupakulia na kupakia mizigo
Mtwara (a) Kuboresha miundombinu ya Bandari ya iliyopo
(b) Ujenzi wa miundombinu itakayohudumia shehena
itakayozalishwa na miradi ya Ukanda wa maendeleo ya
Mtwara ( Mtwara Development Corridor)
(c) Kuendeleza bandari kama kituo cha kuhudumia shughuli za
utafiti wa mafuta na gesi (Oil and Gas Supply Base)
(d) Kuifanya bandari kuwa bandari huru (free port)
Bandari za Maziwa (a) Bandari ya Mwanza Kaskazini kuwa tengefu kwa ajili ya
kuhudumia abiria
(b) Bandari ya Mwanza Kusini kuendelezwa kwa ajili ya mizigo
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kitengo cha kontena
(c) Upanuzi wa bandari ya Kigoma
(d) Upanuzi wa Bandari ya Kasanga
43
(e) Ujenzi wa gati la Kiwira
(f) Kupata ardhi zaidi kwa ajili ya upanuzi wa bandari ya
Kigoma, Kiwira, Mbambabay na Musoma
(g) Ujenzi wa Magati katika ziwa Tanganyika (Kalya, Karema,
Kibirizi, Kirando, Lagosa na Kasanga
(h) Kuendeleza bandari ya Itungi
(i) Kujenga gati bandari ya Ndumbi
(j) Kujenga gati bandari ya Pangani
(k) Kujenga gati bandari ya Mafia
(l) Kujenga gati bandari ya Lindi
10.2.2 Kampuni ya Meli ya SINOTASHIP
Kampuni ya Ushirika wa usafirishaji mizigo kwa meli baina ya Tanzania na China ni ushirika
unaomiliki na kuendesha meli kwa asilimia hamsini kwa hamsini (50 kwa 50) ulio chini ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China. Wabia
waliopewa mamlaka ya umiliki wa Kampuni ni Wizara ya Uchukuzi Tanzania na Wizara ya
Mawasiliano ya China.
Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1967 kutokana na agizo la Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai
na Rais wa kwanza Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere. Kwa kipindi cha miaka 44,
SINOTASHIP imeimarisha urafiki na ushirikiano wa Tanzania na China na meli zake zinabeba
mamilioni ya tani za mizigo kati ya China na Tanzania, na kati ya nchi hizo mbili na nchi
nyingine duniani.
Ukubwa na Umiliki wa Meli na Ugharimiaji
Awali iliamuliwa kwamba SINOTASHIP ingemiliki na kuendesha meli nne za mizigo mikavu
ya kawaida. Kwa hiyo, serikali hizi mbili ziliwekeza paundi za Uingereza milioni 3 katika
kampuni, ambazo zote zililipwa na serikali ya China, nusu ya kiasi hicho kikitolewa kama
mkopo nafuu kwa serikali ya Tanzania. Mkopo huo haukuwa na riba na hivyo kutakiwa
kulipwa kwa awamu sawa za vipindi kumi baada ya kipindi cha nyongeza cha miaka kumi,
tangu malipo kufanyika.
Mipangilio ya Kiuendeshaji
Ofisi kuu ya SINOTASHIP ipo Dar es Salaam, Tanzania, na tawi la ofisi lipo Beijing, China.
Licha ya kumilikiwa na nchi mbili wabia, pia kampuni inasimamiwa na wajumbe kiushirika.
Bodi ya Wakurugenzi inaundwa na wajumbe sita, watatu kutoka kila upande na mjumbe
mmoja kati yao kutoka kila upande, akiwa kama mwenyekiti mwenza. Wakurugenzi Wakuu
wawili, mmoja kutoka kila upande, wakiongoza Utawala wa Ushirika kama Maofisa Watendaji
Wakuu wa kampuni.
Uendeshaji na Utendaji wa Shughuli
Kwa kipindi cha miaka 44 iliyopita, vyombo vya kampuni vimebeba zaidi ya tani milioni 8 za
mizigo hasa bidhaa zinazoingizwa ndani ya nchi na zile zinazouzwa nje ya nchi zikisafirishwa
44
kwa meli ndani na nje ya China, na Tanzania pia. Kibiashara SINOTASHIP imekuwa ikipata
faida kwa miaka yote, kwa sasa ina utajiri halisi wa takribani DOLA ZA MAREKANI
MILIONI 71. Mapato yaliyokusanywa na kuhifadhiwa yameisaidia kampuni kuboresha mali
zake mara tatu bila kutegemea fedha za ziada kutoka kwa wanahisa.
Kampuni pia imejitahidi kukuza na kutoa huduma za biashara ya kigeni baina ya China na
Tanzania. Aidha, SINOTASHIP iliandaa mafunzo kwa wataalamu wa usimamizi wa meli na
wataalamu wa melini hasa kwa upande wa Tanzania ambapo vijana wake wamenufaika kwa
kiasi kikubwa kwa kupata uwezo na ujuzi mpya.
Viashiria vya Mafanikio
Kuna viashiria vingi vilivyofanya SINOTASHIP iweze kudumu na kufanikiwa katika kipindi
cha miongo minne iliyopita. Viashiria hivyo ni pamoja na;
i. Tabia ya kujali na jitihada zinazofanywa na serikali zote mbili katika kampuni.
ii. Msaada mkubwa unaotolewa na kikundi cha COSCO kampuni ya usafirishaji mizigo
kwa meli inayomilikiwa na Serikali iliyopewa mamlaka na Wizara ya Mawasiliano ya
China kushughulikia usimamizi wa SINOTATHIP kwa upande wa China.
iii. Ubora wa hali ya juu wa usimamizi wa kitaalamu na wataalamu wa ufundi
waliowekwa kwenye ushirika na pande zote mbili umekuwa na uhakikisho wa kampuni
kusimamiwa vyema wakati wote.
iv. Ushirikiano mzuri na bidii kati ya wafanyakazi wa pande zote mbili za Tanzania na
China.
Changamoto zilizopo sasa
i. Utekaji nyara wa meli hasa katika bahari ya Hindi ambako kumefanya gharama za
uendeshaji kupanda kwa ajili ya kugharamia ulinzi baharini.
ii. Upungufu wa mizigo inayosafirishwa kwa meli duniani.
Uamuzi wa Kununua Meli kubwa mpya
Kutokana na kushindwa kupata meli nzuri za mtumba sokoni kwa kipindi cha miaka ya nyuma,
kampuni iliamua kwa mara ya kwanza katika historia yake, kutengeneza meli mbili mpya. Meli
ambazo zilikwishaagizwa kutoka karakana ya kutengeneza meli ya China, ni meli kubwa zenye
uwezo wa kubeba uzito mkubwa wa tani 57,000 na tani 34,000.
Kuletwa kwa meli hizi kutasaidia kuongeza uwezo wa safari za kampuni kwa sababu uwezo
wake wa kubeba utakuwa ni mara sita ya uwezo wa meli zilizokuwepo.
Ugharimiaji
45
Jumla ya uwekezaji katika meli mbili ni DOLA ZA MAREKANI MILIONI 73.1 ambapo 40%
inatoka kwenye fedha za kampuni. Salio la 60% ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China
baada ya kufikiria njia nyingine zote kama vile;
1. Kuita wanahisa kuchangia kiasi hicho kwa utaratibu wa asilimia hamsini kwa hamsini
(50 kwa 50). Njia hii ilikuwa si halisi kwa sababu ya matatizo ya sera na fedha kwa
upande wa Tanzania.
2. Kuomba upande wa China pekee kuchanga mchango wote wa hisa. Njia hii
haikushauriwa kwa sababu ingebadili kabisa muundo wa umiliki kwa kupunguza nguvu
ya uwekezaji wa Tanzania kwa zaidi ya asilimia 50.
Meli moja yenye uwezo wa tani 57,000 ililetwa mwezi Septemba 2009 na sasa inafanya kazi.
Meli ya pili yenye uwezo wa tani 34,000 inatarajiwa kuletwa mwezi Desemba 2011.
Mdororo wa Uchumi Duniani
Matokeo ya mdororo wa uchumi katika viwanda vya usafirishaji mizigo kwa Meli na vya
utengenezaji meli duniani yamekuwa mabaya zaidi baada ya soko la usafirishaji kwa meli
kuanguka kama ilivyooneshwa kwenye Baltic Dry Index (BDI) ambayo ilishuka kutoka 11,793
mwezi Mei 2008 mpaka kufikia 800 mwezi Novemba 2008. Hii ni hali tete kwa kampuni za
usafirishaji kwa meli ndogondogo na za kati kama SINOTASHIP.
Hata hivyo, wataalam wanatabiri kuwa tasnia ya usafiri wa meli utahimili masharti ya soko hili
dhaifu kwa kipindi cha mwaka 2009 na 2010.
Malengo ya Baadaye
Malengo ya kampuni yetu kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni kuongeza usafirishaji kufikia
takribani vyombo 20, makontena na vichukuzi vikubwa ikijumuisha matangi ya kubeba gesi
yenye uwezo wa kubeba tani 10,000 kila moja, ikizingatiwa kwamba kwa wakati huo
uchimbaji wa gesi katika mwambao wa kusini mwa Tanzania utakua kwa kiasi kikubwa.
Pia tunatarajia kuwa takribani asilimia 50 ya vyombo vya kampuni vitakuwa vikipeperusha
bendera ya Tanzania, kwa maana hiyo tunatengeneza nafasi za kazi zaidi kwa Maofisa na
wafanyakazi wengine kuajiriwa Melini.
46
MV Chang Shun Ii Bulk Carrier
Meli mpya yenye uwezo wa kubeba shehena ya tani 57,000
10.2.3 Kampuni ya Huduma za Meli – MSCL
Kampuni ya Huduma za Meli (Marine Services Company Limited – MSCL) ilianzishwa chini
ya Sheria ya Makampuni sura 212 mnamo tarehe 08/12/1997 kutokana na kilichokuwa kitengo
cha usafirishaji wa majini cha Shirika la Reli (TRC).
47
Baada ya kuanzishwa kwa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), mali zote zilizokuwa chini
ya kitengo cha usafiri majini cha TRC zilihamishiwa katika Kampuni hii mpya mnamo tarehe
21/06/1999 kupitia Gazeti la Serikali No. 125A. Kampuni ilianza kazi tarehe 01/08/1999 ikiwa
na mtaji wa meli 15 bila fedha yoyote.
Kampuni iliendelea kufanya kazi huku ikimiliki meli, bandari zote na miundombinu yake yote
katika maziwa makuu hadi tarehe 30/06/2006. Mnamo mwaka 2004, serikali ilianzisha
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kupitia sheria No. 17 ya 2004. Sheria iliyoanzisha
Mamlaka ya Bandari ilianza kutumika tarehe 01/07/2006.
Kutokana na mabadiliko haya baadhi ya mali za Kampuni ya Huduma za Meli ikiwemo
miundombinu yote ya kibandari, meli moja, majengo ya ofisi, karakana na vyelezo katika
maziwa yote makuu vilihamishiwa Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Aidha wafanyakazi 77 ikiwemo Menejimenti nzima ya Kampuni, nao walihamishiwa Mamlaka
ya Bandari. Mali za Kampuni ya Huduma za Meli zilihamishiwa TPA kwa GN No. 303 ya
tarehe 14/10/2005. Mabadiliko haya yalipunguza ukubwa na mali za Kampuni pamoja na
baadhi ya vyanzo vyake vya mapato.
Kampuni hii kwa sasa inaendesha jumla ya meli 14 za abiria na mizigo, ambapo meli 9 ziko
ziwa Victoria, 3 ziko ziwa Tanganyika na 2 ziwa Nyasa. Idadi hii ni baada ya meli moja
kuhamishiwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari. Jedwali Na. 9.3 inaonesha meli hizo kwa
kila ziwa.
Kampuni hii inaundwa na Matawi matatu yaani Tawi la Mwanza katika Ziwa Victoria; Tawi la
Kigoma katika Ziwa Tanganyika na Tawi la Kyela Katika Ziwa Nyasa. Makao Makuu ya
Kampuni yako Mwanza.
Shughuli kubwa za Kampuni hii ni kusafirisha abiria na mizigo katika maziwa yote matatu,
ikitoa huduma kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya mwambao wa maziwa haya na
katika visiwa, ndani ya nchi na nje ya nchi.
Vile vile Kampuni hii ni daraja katika shughuli za kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na
nchi jirani. Nchi za Uganda na Kenya katika Ziwa Victoria, Burundi, Mashariki ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na Zambia katika Ziwa Tanganyika, na Malawi katika Ziwa Nyasa.
Kutoa huduma bora, inayotegemewa, inayoaminika, inayotabirika, angalifu na yenye kujali
usalama kwa wateja wake katika maziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Kuwa kampuni ya usafirishaji katika maziwa iliyo na ushindani, yenye kutegemewa,
salama na itendayo kwa kuwalenga wateja wake siku zote.
Kufanya matengenezo ya mara kwa mara (preventive/routine maintenance) ya meli
zake kufuatana na miongozo iliyopo katika “Merchant Shipping Act”. Kuboresha
48
usalama wa abiria kwa kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kuokolea maisha melini
vinatosheleza mahitaji kulingana na idadi na wafanyakazi walioko melini.
Kampuni hii inaendelea kutekeleza makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi
(UNHCR) kwa kuwarudisha nyumbani Wakimbizi wa DRC toka Kigoma, Tanzania na
Mpulungu, Zambia kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Zoezi hili bado ni
endelevu.
Jedwali Na. 9.5 Uwezo wa Kila Meli na Mwaka wa Ujenzi kabla na Baada ya Uhuru
Jina la Meli Uwezo wa Ubebaji Mwaka Meli
Ilipojengwa Abiria Mzigo (Tani)
ZIWA VICTORIA
M.V. Victoria 1200 200 1960
M.V. Butiama 200 100 1980
M.V. Serengeti 593 350 1983
M.V. Clarias 293 10 1961
M.T. Nyangumi - (Mafuta) 350 1964
M.T. Ukerewe - 480 1983
M.L. Maindi - 120 1938
M.L. Wimbi - 120 1938
M.V. Umoja - 1200 1964
ZIWA TANGANYIKA
M.V. Liemba 600 200 1913
M.V. Mwongozo 800 80 1979
M.T. Sangara - (Mafuta) 350 1981
ZIWA NYASA
M.V. Iringa 139 5 1974
M.V. Songea 212 50 1973
Hali ya Uongozi na Utawala Kuanzia 1961
1976: Idara ya Usafirishaji Majini ilikuwa chini ya Mkurugenzi wa Usafirishaji Reli
ambayo makao makuu yake yalikuwa Nairobi – Kenya na hapa Tanzania
upande wa usafirishaji majini kitengo kilikuwa chini ya Mrakibu
Usafirishaji (District Traffic Superintendent – Mwanza) kitengo cha “Marine
Transport Officer – Mwanza” (Mwanza na Kigoma).
1977: Baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika kitengo cha Usafirishaji
majini kilibaki kikiendeshwa na Ofisi iliyokuwa ya Meneja Usafirishaji (CTM)
chini ya Warakibu wa Usafirishaji (Mwanza na Tabora) chini ya Marine
Transport Officer (MTO) Mwanza.
49
1977: Meli zilizokuwa za Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Railways) Ziwa
Victoria nyingi zilikamatwa zikabaki nchini Kenya – Kisumu nazo ni M.V.
Victoria, M.V. Umoja, M.T. Nyangumi, M.S. Usoga, M.V. Uhuru na
nyinginezo nyingi.
Meli tulizobaki nazo upande wa Tanzania Ziwa Victoria ni M.V. Clarias, M.S.
Buvuma na M.V. Ng‟ombe na S.S. Buganda. Kwa Ziwa Tanganyika tulibaki na
meli ya M.S. Liemba ikiwa kwenye matengenezo makubwa ya kubadilishwa
kutoka injini za mvuke (steam engine) kuwekewa injini za mafuta (Diesel
Engine). Kazi ilikamilika mwaka 1978 na kuanza kazi ya kuhudumia wananchi
wa mwambao wa Ziwa Tangnyika kwa upande wa Tanzania na baadaye
wananchi wa nchi za jirani za Burundi, Zaire na Zambia.
1978: Kurudishwa kwa meli 3 kutoka Kenya ambazo ni M.V. Victoria, M.T.
Nyangumi na M.V. Umoja.
1979: Ndiyo ujenzi wa meli zilizotoka Ubelgiji ulipoanza. Meli hizo ni: M.V. Bukoba
ilijengwa mwaka 1979, M.V. Butiama na M.T. Sangara zilijengwa mwaka 1980,
M.V. Mwongozo mwaka 1982 na M.T. Ukerewe mwaka 1983.
Kitengo cha uendeshaji meli, kwenye maziwa haya matatu (3); Ziwa Nyasa,
Tanganyika na Victoria ziliwekwa chini ya Meneja Usafirishaji. Reli (CTM)
kwa kuunda matawi matatu. Tawi la Mwanza chini ya cheo kipya
kilichojulikana kama Engineer Incharge – Lake Victoria, hivyo hivyo ilikuwa
kwa vituo vya Kyela na Kigoma.
1982: Shirika la Reli lilipata udhamini wa uendeshaji wa meli katika maziwa kutoka
Denmark kupitia DANIDA.
Uundwaji wa kitengo cha usafirishaji majini kiliondolewa kwa Meneja
Usafirishaji (CTM) Reli na kuanzishwa Idara iliyojulikana kama TRC MARINE
DIVISION chini ya Chief of Marine Operations (CMO), ambaye aliwajibika
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli.
1983: Zilizokuwa meli za TACOSHILI Ziwa Nyasa zilikabidhiwa Shirika la Reli kwa
kuziendesha na miundombinu yake yote. Meli hizo ni M.V. Iringa na M.V.
Songea.
1988: Pamoja na hayo yote kufanyika chini ya msaada wa DANIDA, yaliundwa
matawi matatu ambayo ni Mwanza, Kigoma na Kyela chini ya uongozi wa
District Marine Manager na vitengo kama vile Karakana, Ugavi na mengineyo.
Makao makuu yakiwa Dar-es-salaam. Katika kipindi hicho meli za M.V.
Serengeti na M.T. Linda zilijengwa kwa msaada wa DANIDA. Pia, katika
kipindi hicho meli za M.V. Victoria na M.V. Liemba zilifanyiwa matengenezo
makubwa ikiwa ni pamoja na kuwekewa mitambo mipya.
1996: Kampuni ya Huduma za Meli (Marine Services Company Limited – MSCL)
ilianzishwa chini ya Sheria ya Makampuni sura 212 mnamo tarehe 08/12/1997
kutokana na kilichokuwa kitengo cha usafirishaji wa majini cha Shirika la Reli
(TRC). Kutenganisha Shirika la Reli na kitengo cha usafirishaji wa majini na
50
kuanzishwa Kampuni mpya ya Huduma za Meli ilikuwa ni mwanzo wa
utekelezaji wa mkakati wa ubinafishwaji wa taasisi hizo mbili.
Ajali ya meli ya M.V. Bukoba
Tarehe 21 Mei, 1996 meli ya M.V. Bukoba ilipata ajali umbali wa kilometa 8 kutoka Bandari
ya Mwanza Kaskazini ikiwa njiani kutoka Bukoba. Athari za ajali ni pamoja maisha ya watu
kupotea, kuzama kwa chombo cha usafiri na hivyo kufanya baadhi ya njia kukosa chombo cha
kuhudumia, Wananchi walipoteza imani kwa Serikali na Shirika la Reli (TRC). Pia, ajali ya
M.V. Bukoba ilisababisha kuanzishwa Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi
Kavu (SUMATRA) na kuboreshwa kwa usalama wa usafiri wa majini. Kuna mpango wa
uokozi majini unaoandaliwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Meli ya M.V. Bukoba ikiwa inazama
Mara tu baada ya uhuru wa Tanzania, sera ilikuwa ni Serikali kuendesha na kusimamia usafiri
wa majini katika maziwa makuu. Sera hiyo iliendelea hadi mwaka 1995 ambapo Serikali
ilijitoa kabisa katika shughuli za biashara na hivyo kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji
binafsi kuwekeza katika shughuli mbalimbali za kibiashara zikiwemo usafiri wa majini.
Serikali imeweka mazingira mazuri na inakaribisha wawekezaji toka nje ya nchi na ndani ya
nchi kuwekeza katika eneo hili, yaani kununua meli nzuri zaidi ambazo zitakidhi vyema
mahitaji ya wasafiri katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
Shughuli kuu ya MSCL ni kutoa huduma ya usafirishaji majini kwa abiria na mizigo katika
Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Vile vile hujishughulisha na utengenezaji na
utunzaji wa vyombo vyake. Katika kutekeleza shughuli zake za kudhibiti na kiutawala, MSCL
imekuwa ikiweka maanani yafuatayo:
i. Malengo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
ii. Kipengele cha wajibu wa huduma kwa umma (Public Service Obligation) kwa watu
waishio kuzunguka maziwa hayo matatu ambao hawana njia mbadala za usafiri,
hususan, kuzunguka Maziwa ya Tanganyika na Nyasa, ambako huduma za usafiri ni
chache.
51
iii. Usalama, afya na ustawi wa jumla wa umma kwa kufanya shughuli zake katika njia
ambazo zinalinda mazingira kwa taratibu zilizofungamana na endelevu.
Tanzania imepitia mifumo miwili ya kisiasa tangu mwaka 1961. Mara tu baada ya uhuru
tulikuwa na mfumo wa ujamaa. Katika kipindi hicho meli zilitoa huduma kwa hasara na
serikali ilifidia hasara hiyo.
Katika ulinzi, meli zimetoa michango mbalimbali katika ulinzi wa nchi. Kwa mfano, meli ya
M.V. Victoria ilisafirisha zaidi ya wanajeshi 2,000 wa Tanzania kutoka Mwanza kwenda
Uganda katika Ziwa Victoria ili kufanikisha vita ya kumuondoa madarakani nduli Idd Amin.
Meli hii pia ilitumika kuwarudisha wanajeshi Tanzania.
Meli ya M.V. Umoja ilisafirisha vifaa vya kijeshi kama vile vifaru na wanajeshi kwenda
Uganda wakati vya vita hivyo. Pia meli ya M.T. Nyangumi ilisafirisha mafuta ya kuendeshea
vifaa mbalimbali wakati wa vita hivyo.
Katika kipindi hiki cha soko huria, Kampuni imekuwa ikijiendesha kibiashara kwa kutumia
mapato yanayotokana na usafirishaji wa abiria na mizigo.
Mafanikio Yaliyopatikana Hadi Sasa
i) Kampuni imeendelea kuzifanyia matengenezo makubwa na yale ya kawaida meli
ambazo ni chakavu.
ii) Kampuni imeendelea kufanya ukarabati mkubwa (Rehabilitation) na kuboresha hali
ya meli zake ili kuziongezea maisha na uhakika wa kufanya safari zake salama.
iii) Kuongeza na kuimarisha hali ya usalama wa meli zake kwa kuboresha vifaa vya
usalama, kusisitiza uangalifu wa utendaji kazini, kuepusha ulevi na kuelimisha
wananchi (wasafiri) matumizi sahihi ya vifaa vya usalama ndani ya meli zetu.
iv) Kuzifanyia ukaguzi kila mwaka kupitia Mkaguzi wa Serikali na kufuata miongozo ya
Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa uendeshaji salama.
v) Kampuni imekuwa ikiziwekea bima meli zote dhidi ya matukio yoyote yasiyotarajiwa
ikiwa ni pamoja na abiria na mizigo pamoja na wafanyakazi melini.
vi) Kupanua soko la meli za Kampuni kupitia matangazo redioni na katika majarida
mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
vii) Kukuza na kuboresha huduma kwa wateja (Customer Care) ambao ndiyo msingi wa
kuboresha soko.
viii) Uongozi wa Kampuni kwa kutambua kuwa uwezo wa serikali kugharamia miradi
yote una ukomo, tuliandaa andiko la mradi wa ukarabati wa meli za Kampuni na
52
ujenzi wa meli mpya na kulisambaza kwa washirika wa maendeleo (development
partners).
Serikali ya Denmark, kupitia Shirika lake la maendeleo “DANIDA” ilionesha utayari kutoa
fedha za kugharamia mradi na tayari upembuzi yakinifu umefanyika na ripoti yake iko kwenye
hatua za mwisho. Aidha, serikali ya Ujerumani imeonesha utayari wa kugharamia matengenezo
makubwa ya kuboresha meli ya M.V. Liemba.
Changamoto
Kampuni ya Huduma za Meli inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo:
i) Meli nyingi kuwa za zamani sana na kuwa chakavu na hivyo kuchukua sehemu
kubwa ya mapato yapatikanayo katika kufanya matengenezo ya mara kwa mara na
pia kusababisha ongezeko la matumizi ya mafuta.
ii) Kupanda kwa bei za vipuri vinavyohitajika kuzifanyia matengenezo meli zetu
ambavyo vinapatikana nje ya nchi.
iii) Ushindani wa kibiashara na vyombo binafsi katika usafirishaji katika barabara
zinazozunguka maziwa yetu.
iv) Gharama na kodi zilizowekwa na Serikali kama ushuru wa mafuta, gharama za
matumizi ya maji ya Ziwa, ushuru wa Serikali za mitaa, na gharama za Mamlaka ya
Uthibiti wa Vyombo vya Majini na Nchi Kavu (SUMATRA).
v) Maslahi madogo kwa watumishi ikiwa ni mishahara na posho mbalimbali ambazo
zinafanya baadhi ya watumishi kukimbilia kwa washindani wetu kwa visingizio vya
kufuata maslahi bora zaidi.
vi) Kuzorota kwa utendaji wa reli katika kusafirisha abiria na mizigo wakati wa kipindi
cha mpito kuelekea ubinafsishaji kuliathiri sana utendaji wa meli zetu.
vii) Kupungua kwa kina cha maji katika maziwa yetu kuliathiri uwezo wa upakiaji wa
mzigo katika kiwango kinachohitajika na vile vile kuathiri usalama wa meli zetu.
viii) Kuchakaa kwa miundombinu ya kibandari katika maziwa yetu na sehemu nyingine
kutokuwepo kabisa, kumeathiri utendaji wa meli zetu katika kubeba abiria na mizigo.
ix) Kutokuimarika kwa hali ya kisiasa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo ambako kumeendelea kukwaza shughuli za kibiashara na usafirishaji wa
abiria.
x) Majukumu ya kuendelea kutoa huduma katika maeneo ambayo Kampuni inafanya
uendeshaji kwa hasara (Public Obligation) bila kupata ruzuku yoyote kutoka
Serikalini.
53
Matarajio ya Kampuni
i. Kujiendesha kwa uwezo wote tulio nao ifikapo mwaka 2013.
ii. Kutoa huduma zenye ongezeko la thamani.
iii. Kuajiri na kubakiza watumishi stadi katika soko la sasa.
iv. Kuongeza mapato ya shughuli kwa zaidi ya 50% ifikapo mwisho wa mwaka
2013.
v. Kutoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo kwa usalama, uhakika na kwa bei
nafuu.
vi. Kuwekeza kwenye miradi ambayo inalenga kupunguza gharama za uendeshaji
na kuboresha huduma.
10.2.4 Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ilianzishwa kwa Sheria ya
Bunge Na.9 ya mwaka 2001. Mamlaka ilianza kazi mwaka 2004 na kupewa jukumu la
kudhibiti usafiri wa Nchi Kavu na Majini. Mamlaka hii iliundwa kufuatia kufutwa kwa Shirika
la kudhibiti shehena (TCFB), na kuunganishwa na Mamlaka ya Leseni za Usafirishaji (CTLA),
hivyo kuundwa kwa chombo kijulikanacho kama SUMATRA. Utekelezaji wa majukumu ya
Mamlaka ulianza mwezi Novemba, 2004 baada ya Serikali kukamilisha uundwaji wa Bodi na
uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu.
Mamlaka inaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi na shughuli za kila siku za Mamlaka
zinasimamiwa na Mkurugenzi Mkuu. Mamlaka ina ofisi katika mikoa kumi na tano ya
Tanzania Bara ikiwemo Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Kagera,
Rukwa, Kigoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Tabora, Mara, Arusha na Iringa. Aidha, ili
kusogeza huduma karibu na wananchi, Mamlaka ina Waratibu Wateule kutoka ofisi za
Makatibu Tawala katika mikoa ambayo Mamlaka haijafungua ofisi zake. Lengo ni kuwa na
ofisi katika mikoa yote ya Tanzania Bara ifikapo mwaka 2013.
Majukumu ya Mamlaka kwa mujibu wa sheria iliyounda SUMATRA na kwa mujibu wa Sheria
za Sekta ni:
Kuhimiza na kukuza ushindani na ufanisi katika soko la usafirishaji wa nchi kavu na
majini, kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma,
Kulinda na kujenga mazingira ya kuvutia kwa watoa huduma,
Kuendeleza na kuhakikisha kuwa huduma za usafirishaji zinakidhi mahitaji ya
watumiaji ikiwa ni pamoja na wenye kipato cha chini na wasiojiweza,
Kuwaelimisha watumiaji wa huduma za usafiri na Wananchi kwa ujumla kuhusu
huduma zinazotolewa na sekta na kuhakikisha kwamba watoa huduma na watumiaji
wanalinda na kutunza mazingira.
54
Majukumu ya Mamlaka kwa Mujibu wa Sheria za Sekta
(a) Usafiri kwa Njia ya barabara - kutoa leseni za usafirishaji kwa magari ya abiria
kuanzia saba na kuendelea na magari ya mizigo.
(b) Bandari na Usafiri Majini - kuweka na kusimamia viwango na masharti ya
huduma ili kuleta ufanisi katika utendaji, ushindani na huduma bora;
(c) Ulinzi na Usalama wa usafiri Majini - kusimamia ulinzi na usalama wa vyombo
vya usafiri majini na pia kulinda mazingira.
(d) Reli: kudhibiti usalama wa reli.
Mamlaka inafanya kazi kwa misingi na maadili ya udhibiti, uwazi, ushirikishwaji, wepesi wa
kutambua mabadiliko (flexibility), uwajibikaji (accountability) na kutokuwa ubaguzi (non-
discrimination).
Mafanikio ya SUMATRA
Tangu kuanzishwa kwake Mamlaka kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imepata mafanikio
mengi ikiwa ni pamoja na:
Kukabiliana na ajali za barabarani,
i. Mamlaka ilifanya Utafiti wa kina kuhusu ajali za barabarani kwa kutumia
mshauri mwelekezi (Consultant) na kuonekana kuwa asilimia 76% ya ajali zote
za barabarani Tanzania Bara zinasababishwa na madereva. Kwa kutumia
mapendekezo ya utafiti huo utaratibu wa mabasi ya abiria kuanza kutumia “log
book” umeanzishwa ili kuratibu mwendo kasi wa mabasi hayo.
ii. Mamlaka imekuwa ikihakikisha kwamba wenye mabasi wanakuwa na nyaraka
muhimu ikiwa ni pamoja na hati za ukaguzi wa gari/magari (Vehicle Inspection
Report) kutoka Jeshi la Polisi na hati ya bima (insurance cover) kabla ya
kupewa leseni.
iii. Mamlaka imekuwa ikipanga ratiba ya safari za mabasi ya abiria zinazozingatia
mwendo salama barabarani na kusimamia masharti ya ratiba na leseni ikiwa ni
pamoja na madereva kufuata muda uliopangwa kwenye ratiba na kutembeza
basi kwenye njia zilizoidhinishwa na Mamlaka.
iv. Mamlaka imekuwa ikiweka utaratibu wa kuwa na madereva wawili kwa mabasi
yanayosafiri kwa muda unaozidi saa 12 na kutoa elimu kwa umma kupitia
vipindi vya redio na matangazo ya mara kwa mara katika vyombo vya habari
ikisisitiza umuhimu wa matumizi salama ya barabara.
Juhudi za kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar-es-Salaam
i. Kuondoa mabasi madogo (vipanya) na kuingiza mabasi makubwa;
Mamlaka ilikwishaanza juhudi za kupunguza matumizi ya mabasi madogo
55
(vipanya) kwa kutotoa leseni mpya kwa mabasi hayo kutoa huduma katikati ya
Jiji tangu Julai, 2006. Mabasi madogo kwa hivi sasa yanatoa huduma
pembezoni mwa Jiji na hivyo kuboresha upatikanaji wa usafiri katika maeneo
hayo. Aidha, kuondolewa kwa mabasi madogo kutoa huduma katikati ya Jiji
kumehamasisha uingizaji wa mabasi makubwa ya kutoa huduma ya usafiri wa
umma Jijini na kuongeza ubora wa huduma hii. Idadi ya mabasi makubwa
ikilinganishwa na mabasi madogo katika kipindi cha mwaka 2006 hadi mwaka
2010 imeainishwa katika jedwali hapa chini.
Jedwali Na: 9.6 Idadi ya mabasi makubwa na madogo ilivyokuwa Dar es
Salaam kwa kipindi cha Julai 2006 hadi Julai 2010
Mwaka Mabasi madogo Mabasi makubwa
Julai 2006 3,382 1,273
Julai 2008 2,978 2,002
Julai 2009 2,212 2,779
Julai 2010 1,747 4,182
Chanzo: SUMATRA
Changamoto Zinazoikabili Mamlaka
i. Ajali za barabarani: Pamoja na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa serikali
kwa kushirikiana Mamlaka na wadau wengine, ajali za barabarani zimeendelea
kuongezeka. Hali ya ajali barabarani ni kama ilivyoonyeshwa katika jedwali
namba 2 na kielelezo namba 1 hapa chini.
Jedwali Na.9.7: Ajali za Barabarani: Mwaka 2005 - 2010
Mwaka 2005 2006 2007 2008 2009 2010
Ajali 16,388 17,039 17,753 20,615 22,739 24,665
Ongezeko
%
4 4 16 10 8.5
Chanzo: Polisi Usalama Barabarani
56
Chati Na: 9.1 .Idadi ya Ajali za Barabarani
ii. Uharamia katika baharí ya Hindi: pamoja na kuwa na kituo cha kisasa cha
mawasiliano cha uokoaji na utafutaji katika bandari ya DSM, uwezo mdogo wa
kuitikia na kutoa msaada haraka pindi taarifa za majanga zitolewapo bado ni
changamoto.
iii. Usalama wa vyombo vidogo vya usafiri majini: kumekuwa na ugumu wa
wamiliki wa vyombo vidogo vya majini kuitikia wito ili vyombo vyao
vikaguliwe.
iv. Miundombinu duni ya barabara: maeneo yenye miundombinu duni ya
barabara katika miji hukumbwa na tatizo la ubora na uhaba wa huduma za
usafiri. Imekuwa ni jambo la kawaida kwa maeneo yenye miundombinu hafifu
kuhudumiwa na vyombo vya usafiri ambavyo ni duni ama /chakavu huku
watumiaji wakilazimika kulipia huduma kwa bei ya juu.
v. Uchakavu wa miundombinu ya reli na wizi wa vifaa vya reli: uchakavu wa
miundombinu ya reli na wizi wa vifaa vya reli kwa kiwango kikubwa unaathiri
hali ya usalama na ulinzi wa reli.
57
Matarajio Kwa Miaka 50 Ijayo
Matarajio ya Mamlaka kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni kutatua changamoto
zinazoikabili sasa ili kuboresha utoaji wa huduma kufikia viwango bora kama ilivyo
katika mataifa yaliyoendelea. Ili kufikia matarajio hayo ni jitihada za makusudi
zinahitajika ili kuendeleza na kuboresha matandao wa miundombinu nchini
ikijumuisha; reli, bandari na usafiri majini na barabara.
Kwa kuwa Mamlaka ni mdhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini inatarajia kufanya
yafuatayo;
i. Kushirikiana na vyombo ya usalama hapa nchini na nje katika kukabiliana na
majanga mbalimbali yanayogusa usafiri wa majini na nchi kavu. Hii itajumuisha
kuwa na vifaa vya kisasa vya mawasiliano (ambapo huduma ya udhibiti inaweza
kufanywa mikoani ikisimamiwa na mtu akiwa DSM
ii. Kuimarisha ofisi kwa ajili ya kutoa huduma katika ngazi ya chini (Wilaya au
Kata) na kujenga uwezo wa kitaaluma kwa watumishi ili kusimamia udhibiti
kwa ufanisi zaidi.
10.3 USAFIRI WA ANGA
10.3.1 Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)
Kabla ya Uhuru, kuanzia mwaka 1948 nchi za Kenya, Tanganyika, Uganda na visiwa vya
Zanzibar zilikuwa chini ya utawala wa Uingereza, ambazo baadhi ya shughuli za kiuchumi
zilikuwa zikifanywa kwa pamoja chini ya East African High Commission. Moja ya shughuli
hizo ni masuala ya Usafiri wa Anga.
Tangu wakati huo, shughuli nyingi za usafiri wa anga zilikuwa zikifanywa kwa pamoja kwa
sababu mtawala wa eneo hilo lote alikuwa ni Muingereza. Kwa hali halisi, ushirikiano wa nchi
hizi ulianza kabla ya mwaka 1948.
Hatua ya kwanza kabisa zilianza mwaka 1943 wakati wa Mkutano mkuu wa magavana wa
Afrika Mashariki ulioteua kamati kuandaa mpango wa maendeleo ya mawasiliano baada ya
vita kuu ya kwanza ya dunia.
Lakini kimsingi, shughuli za usafiri wa anga, hasa za kibiashara zilianza tangu mwaka 1929
wakati huo kukiwa na shirika la ndege la Wilson ambalo lilianzishwa na Florence Wilson.
Shirika hilo lilivunjika mwaka 1939 vita kuu ya pili ya dunia ilipoanza na kutumika kama
Kikosi cha Jeshi la Anga la Mfalme wa Uingereza.
58
Baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961, East African High Commission
ilivunjwa na kuanzishwa East African Common Services Organisation. Moja ya idara yake
katika organizesheni hii ilikuwa ni Kurugenzi ya Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki (East
African Directorate of Civil Aviation).
Majukumu ya Kurugenzi hii yalikuwa ni kutoa huduma za uongozaji ndege, huduma za
mawasiliano, utoaji leseni, usajili wa ndege, utafutaji na uokoaji ndege zinapopotea na kupata
ajali, utoaji leseni kwa mashirika ya ndege, uchunguzi wa ajali za ndege na utoaji wa taarifa za
anga.
Makao Makuu ya kurugenzi hii yalikuwa Nairobi, Kenya ambako Mkurugenzi Mkuu alikuwa
na ofisi zake na nchi zilikuwa na ofisi ambazo zilikuwa zikimsaidia Mkurugenzi Mkuu. Kituo
Kikuu cha kuongozea ndege nacho kilikuwa Nairobi.
Usimamizi wa viwanja vya ndege ulikuwa chini ya Serikali zenyewe, hazikuwa chini ya
Kurugenzi za Usafiri wa Anga. Shughuli na majukumu ya Kurugenzi hii yaliendelea hadi
mwaka 1967 wakati mataifa haya yalipoamua kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Baada ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, shughuli za usafiri wa
anga ziliendelea kuwa chini ya Kurugenzi ya Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki. Ingawa
Kurugenzi hii ilikuwa ikifanya shughuli za kiufundi katika masuala ya usafiri wa anga, utoaji
wa huduma za matengenezo na uangalizi wa viwanja, zimamoto zilibaki kuwa ni jukumu la
serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kulingana na sheria ya Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki, Kurugenzi hii ilikuwa chini ya
bodi ambayo ilikuwa na mwenyekiti aliyekuwa akiteuliwa na Jumuiya, Mkurugenzi Mkuu na
Wakurugenzi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Makao Makuu
yalikuwa Nairobi, Kenya. Chini yake kulikuwa na Wakurugenzi watatu kutoka nchi tatu
wanachama wa jumuiya wakiwakirisha nchi zao na ambao pia ofisi zilikuwa katika nchi zake,
Dar es Salaam- Tanzania, Nairobi- Kenya na Entebbe- Uganda. Mtanzania wa kwanza kuwa
Mkurugenzi wa Usafiri wa Anga Tanzania alikuwa Lot Mollel.
Ofisi ya Nairobi ilikuwa inawajibika kusimamia shughuli zote zinazohusu masuala ya usafiri
wa anga kama uongozaji wa ndege, ikisimamia pia shughuli za ajira na mafunzo.
Katika kipindi hiki, Watanzania mbalimbali walifunzwa na kupata ujuzi katika masuala ya
urubani, uhandisi wa ndege, uongozaji ndege na nyinginezo zinazohusiana na shughuli za anga.
Mitambo mbalimbali pia iliwekwa katika vituo mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mawasiliano
kati ya marubani na waongoza ndege na pia utoaji wa taarifa mbalimbali, ingawa kimsingi
kituo kikubwa zaidi cha kuongozea ndege kilikuwa Nairobi.
59
Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 nchi zote zililazimika
kubadilisha muundo wa Kurugenzi hiyo ambayo kwa upande wa Tanzania ilikuwa sasa
Kurugenzi ya Usafiri wa Anga Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Lot Mollel.
Majukumu yote ambayo Kurugenzi ya Afrika Mashariki ilikuwa ikiyafanya sasa yalihamia
Tanzania na hivyo kuwa na mamlaka ya kufanya shughuli zao wenyewe chini ya Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi. Hata hivyo kutokana na unyeti wa masuala ya usafiri wa anga, anga
la Tanzania liliendelea kusimamiwa chini ya kituo cha kuongozea ndege cha Nairobi kwa
miezi kadhaa hadi Serikali ilipojiweka sawa.
Hii ilitokana na ukweli kwamba kituo kikuu cha kuongozea ndege kilikuwa Nairobi, hivyo
serikali ilipaswa kwanza kuweka kituo chake. Kituo kiliwekwa Dar es Salaam na kilifungwa
vifaa vyote muhimu vilivyokifanya kuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano na vituo vingine
vyote nchini na vituo vingine vikuu nje ya mipaka ya Tanzania.
Kurugenzi hii ilianzishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1977 mbayo ilikuwa chini ya Bodi
iliyokuwa na wajibu wa kumshauri Waziri anayehusika na masuala mbalimbali yahusuyo
usafiri wa anga nchini. Mkurugenzi Mkuu ni mmoja wa wajumbe katika bodi hiyo ambaye
alikuwa akiingia kwa wadhifa wake wakati wajumbe wengine walikuwa wakiteuliwa na
Waziri. Chini ya sheria hii, Kurugenzi ilipewa mamlaka ya kusimamia shughuli zote za usafiri
wa anga kama ilivyokuwa wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kutokana na mageuzi ya kiuchumi na kimifumo, Kurugenzi hii ilibadilika na kuwa Wakala wa
serikali mwaka 1997, lengo likiwa kuipa madaraka ya kufanya maamuzi na kazi zake kwa
haraka na ufasaha. Kuanzia wakati huo ikabadilishwa jina na kuitwa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga. Kazi zake ziliendelea kuwa zile zile na Mkurugenzi Mkuu wa kwanza chini ya Mamlaka
hii alikuwa Mhandisi Bibi Margaret Munyagi.
Mageuzi haya yalileta mabadiliko zaidi kwani mwaka 2003, Mamlaka ilipewa uhuru zaidi
chini ya Sheria ya kuanzishwa Mamlaka ya mwaka 2003, Wizara ikijiondoa katika shughuli za
utendaji ikibaki kuisimamia sera zaidi. Mkurugenzi Mkuu wake aliendelea kuwa Mhandisi Bibi
Margaret Munyagi hadi mwaka 2010 alipostaafu kwa mujibu wa sheria.
Tangu uhuru mwaka 1961, kumekuwa na maendeleo ya kutosha wa upande wa Mamlaka
katika kusimamia na kujishughulisha na majukumu yake kama ilivyoanishwa katika sheria na
pia kama ilivyoanishwa katika Mkataba wa Chicago chini ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa
Anga Duniani (ICAO).
Tangu wakati huo, kumekuwa na maendeleo mengi, kuanzia katika mafunzo kwa Watanzania
ambao walikuwa wachache wakati ule hadi hivi sasa ambapo wataalam wote waliopo kwa sasa
ni matunda ya serikali kuwasomesha na kuwapata madaraka kufanya kazi walizotakiwa
kufanya.
Udhitibi wa Usalama wa Anga
Kiwango cha udhibiti wa usalama wa anga ni kikubwa hadi sasa, na Tanzania ni moja ya anga
ambalo inajulikana kuwa ni salama kuliko anga nyingine nyingi za Afrika. Ni ajali chache
zimetokea katika eneo hilo ikilinganishwa na maeneo mengine mbalimbali ya Afrika, hasa
60
ikizingatiwa kwamba kutokana na takwimu za ICAO, Afrika ni bara linaoongoza kwa kuwa na
ajali nyingi za ndege.
Haya yote yamewezekana kutokana na utaratibu wa Mamlaka kuendelea kufanya ukaguzi na
utoaji vyeti kwa ndege, makampuni ya ndege, viwanja vya ndege na kutoa mitihani kwa
marubani na wahandisi.
Hivi sasa Mamlaka imekamilisha kuandaa Kanuni za Mfuko wa Mafunzo kwa ajili ya
marubani na wahandisi wa ndege uliowekwa kwa sheria namba 10 ya TCAA ya 2003 kwa ajili
ya kukabiliana na uhaba wa wataalamu katika sekta baada ya serikali kwa kipindi kirefu
kusitisha mafunzo kwa wataalam wake kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyolikabili taifa.
Mafanikio mengine ni kukamilishwa kwa uanishaji wa kanuni za usafiri wa anga kwenye
Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuboresha usalama, siyo tu katika anga la Tanzania, bali pia
katika anga la jirani zetu katika eneo la Afrika Mashariki.
Uanzishwaji wa Wakala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kusimamia Usalama wa Usafiri
wa Anga ni moja ya mafanikio ambayo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru serikali
imefanikiwa kuianzisha. Lengo la wakala hii ni kuendeleza rekodi safi ya nchi katika suala la
kuwa na anga salama kwa sababu chini ya wakala hii, nchi za Afrika Mashariki zitaunganisha
utaalam wa usalama wa anga na hivyo kuwa na nguvu zaidi katika kusimamia usalama na
kuepusha ajali. Mkurugenzi wake wa kwanza ambaye bado anaendelea na wadhifa huo ni
Mtanzania, Bw. Mtesigwa Maugo.
Udhibiti wa Biashara na Uchumi
Idadi ya watoa huduma ya usafiri wa anga wenye leseni imeongezeka kiasi kikubwa hivi sasa
wamefikia 34. Zamani tulikuwa na shirika moja tu la ndege, ATC, lakini hivi sasa baada ya
kufungua masoko, tumekuwa na mashirika mengi zaidi ya ndege ambayo yanatoa huduma za
usafirishaji abiria ndani na nje ya nchi.
Mashirika na Makampuni ya ndege kutoka nje nayo yanazidi kuongeza huduma za usafiri wa
anga nchini. Hivi sasa mashirika ya Kimataifa yanayotoa huduma nchini yapo zaidi ya 22.
Idadi ya marubani wazalendo imeongezeka tangu kupata uhuru na hivyo kufanya kazi katika
mashirika mbalimbali ya ndege, si ndani tu ya Tanzania, bali wapo pia marubani watanzania
ambao wanafanya kazi nje ya nchi katika mashirika mbalimbali ya ndege.
Idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga kuja na kuondoka katika viwanja inaendelea
kuongezeka. Hadi hivi sasa, kwa mwaka zaidi ya abiria milioni 4 wanatumia usafiri huu.
Uongozaji Ndege
Kuanzishwa kwa Chuo cha Waongoza ndege Tanzania (Civil Aviation Training College -
CATC) ambacho hadi sasa kimetoa karibu waongoza ndege wote wanaofanya kazi katika vituo
mbalimbali vya kuongozea ndege ndani na nje ya nchi. Chuo hiki pia kinatoa mafunzo kwa
waongoza ndege wengine kutoka nje ya Tanzania hata kwenda nje ya nchi kutoa mafunzo kwa
maombi mbalimbali kutoka katika nchi hizo. Chuo hiki kimekuwa msaada mkubwa kwa
serikali kwa sababu kimesaidia kupunguza matumizi ya fedha nyingi za kigeni ambazo serikali
ingetoa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalam wapya wanaoingia katika fani hii muhimu.
61
Mamlaka ya Usafiri wa Anga imeendelea na mpango wake wa uwekaji wa mitambo ya kisasa
katika vituo mbalimbali na ubadilishaji wa mitambo chakavu ya kuongozea ndege katika
maeneo mengi ya nchi kama Songea, Arusha, Kigoma na Tanga. Moja ya maeneo ambayo
teknolojia inakwenda kasi na kuathiri utendaji ni katika usafiri wa anga, lakini pamoja na hali
hiyo, serikali imeweza kwenda na wakati kwa kuweza kubadilisha mifumo mbalimbali ya
mawasiliano na mitambo kiasi cha kuweza kuendana na matakwa na kanuni za ICAO.
Ubadilishaji wa mitambo ya mawasiliano ya VSAT wa SADC umekamilika na sasa mitambo
ya kisasa zaidi imeshasimikwa na inafanya kazi. VSAT pia imeunganishwa na mtandao wa
mawasiliano wa nchi za Kaskazini mwa Afrika (NAFISAT VSAT).
Mamlaka pia imeweza kuweka mitambo ya kisasa ya kungozea ndege (VOR/DME) na wa
mwisho umewekwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar na katika Kiwanja
cha Mwanza.
Rada ya kuongozea ndege ambayo ilifungwa katika Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA) ni moja ya mitambo muhimu ambayo kwa kiasi kikubwa inasaidia kuingiza mapato na
pia kuhakikisha kwamba usalama katika anga letu unaimarika.
Kujengwa jengo la Makao Makuu ya Mamlaka lililokamilika hivi karibuni ambalo
limewezesha wafanyakazi wote wa Makao Makuu kufanyakazi pamoja na pia kuwarahisishia
wateja kupata huduma zote sehemu mmoja kwa wakati mmoja.
Malengo ya Mamlaka katika kipindi cha miaka 50 ijayo
Malengo ya Mamlaka yapo kwenye makundi makubwa yafuatayo:-
(a) Usalama (Safety and Security)
Pamoja na kuhakikisha usalama (safety and security), kwa kufanya juhudi za makusudi
kuzuia matatizo, Mamlaka kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama yetu zitaweka
utaratibu wa kutumia wataalam kwa pamoja. Hatua hii itaenda sambamba na kuongeza
idadi ya wataalam katika fani za uhandisi na urubani. Aidha, ili kutunza mazingira na
kupunguza usumbufu, mifumo mizima ya utoaji moshi (engine emissions) na kelele
(noise pollution) itaboreshwa.
(b) Uongozaji Ndege
Mitambo yote itabadilishwa ili itumie teknolojia ya “digital” kwa njia ya satelaiti.
Mitambo ya Automatic Dependent Survaillance – Broadcast (ADS-B), yenye uwezo wa
kusambaa nchi nzima. Aidha, mawasiliano ya uongozaji ndege yataendelea kuboreshwa
kwa kutumia mfumo wa kisasa wenye ufanisi (Performance Based Navigation). Pia
matumizi ya anga yataboreshwa kwa kushirikiana na nchi za EAC, SADC na hatimaye
Afrika nzima.
(c) Chuo cha Mafunzo ya Usalama wa Anga
Chuo cha Usalama wa Anga kitaendelea kuimarishwa kwa kuwa na majengo yake
yenyewe na kuweza kujitegemea. Mafunzo ya wakufunzi yataimarishwa ili kukidhi
kiwango cha elimu ya juu cha kitaifa na kimataifa. Chuo kinategemewa kupanua wigo
62
wake kwa kutoa mafunzo ya Urubani, uhandisi wa ndege na huduma za uendeshaji
ndege (Flight Operations). Mitambo ya mafunzo (simulators) itaendelea kuwekwa
kulingana na teknolojia ya kisasa.
(d) Ukuaji wa Sekta
Ukuaji wa idadi ya abiria na huduma za ndege unategemea zaidi ukuaji wa uchumi.
Inakadiriwa kuwa, abiria wataongezeka kutoka abiria 3,027,512 mwaka 2010 hadi
abiria 55,767,238 mwaka 2050 hili likiwa ongezeko la 1,742%. Aidha, safari za ndege
zinategemewa kuongezeka kutoka safari 181,240 hadi safari 3,334,816, likiwa ni
ongezeko la 1,740%, katika kipindi hicho.
10.3.2 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA)
Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru wake tarehe 9 Desemba, 1961, serikali ya
Tanganyika ilirithi miundo ya uendeshaji wa viwanja vya ndege kutoka kwa serikali ya
kikoloni ya Mwingereza. Viwanja vya ndege vilikuwa chini ya „Public Works
Department (PWD)”, muundo ambao uliendelea hadi miaka ya 1970. Muundo huu
ulibadilika mwaka 1970 wakati serikali ilipounda Wizara ya Mawasiliano na Kazi
(Ministry of Communication and Works) na viwanja vya ndege vikaendelea kuwa chini
ya Wizara hii.
Mkurugenzi wa kwanza wa Viwanja vya Ndege aliteuliwa rasmi tarehe 01/07/1974
akiwa chini ya Wizara ya Mawasiliano, Usafirishaji, Nishati na Kazi. Viwanja vya
Ndege viliendelea kuwa ni kitengo tu cha Idara ya Barabara na Viwanja vya Ndege
(Department of Roads and Aerodromes).
Historia ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inaanzia mwaka 1974
ilipoundwa kama Kitengo chini ya Idara ya Barabara na Viwanja vya Ndege katika
Wizara ya Ujenzi. Mwaka 1980, ikawa Idara kamili chini ya Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi. Kati ya mwaka 1980 hadi 1999, Idara hii ilipita katika
miundo kadhaa sambamba na mabadiliko mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika katika
Wizara ya Mawasiliano na Wizara ya Ujenzi.
TAA ilianzishwa tarehe 29 Novemba, 1999 na kuzinduliwa rasmi mnamo tarehe 03
Desemba, 1999 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali.
Viwanja vya ndege vilivyorithiwa kutoka kwa utawala wa Mwingereza vilikuwa ni
sabini (70) ikiwa ni pamoja na Kiwanja cha Kimataifa cha Dar es Salaam amabacho
kwa sasa kinajulikana kama Kiwanja Cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Baada ya
Uhuru, Serikali ilijenga kiwanja cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) ambacho
kilifunguliwa mwaka 1971. Hivi sasa, Serikali inakamalisha ujenzi wa Kiwanja cha pili
cha Kimataifa cha Songwe mkoani Mbeya.
63
Hali ya Viwanja kwa Wakati Huo
Viwanja vya lami vilikuwa kumi na mbili (12) ambavyo ni; Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Mtwara , Tanga, Kigoma, Tabora,
Moshi, Iringa na Musoma. Viwanja vingine vilikuwa vya changarawe na nyasi.
Maelezo ya kila kiwanja ni kama ifuatavyo:
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar Es Salaam (DIA).
Kwa mujibu wa mapokezi ambayo si rahisi kupata maandiko yanayoweza kuthibitisha
usahihi na tarehe zake, Kiwanja cha ndege cha kwanza katika Jiji la Dar es Salaam,
kilikuwa ni cha maji “sea port”. Kiwanja hiki kilikuwa kwenye sehemu ya bahari
iliyopo kati ya Ferry na pwani ya karibu na Kanisa Kuu la Mt. Joseph. Jengo lake la
abiria (Terminal) lilikuwa jirani na Ardhi House. Kiwanja hicho kilianza wakati wa
mkoloni, na kilihamishiwa barabara ya Kilwa karibu na Uwanja wa Taifa kikiitwa
Kiwanja cha Ndege cha Mkeja. .
Kiwanja cha kisasa cha Kimataifa cha Dar es Salaam kilijengwa eneo la Ukonga
mwaka 1954. Jiwe la msingi la kiwanja la Jengo la abiria (Terminal I) liliwekwa na
Right Hon. A.T. Lennox Boyd P.C. MP ambaye alikuwa ni „Secretary of State for
colonies” tarehe 16 Oktoba, 1954. Kiwanja cha ndege cha Mkeja (Kilwa Road)
kilifungwa mwaka 1954, Wakati huo Gavana wa Tanganyika alikuwa ni Sir Edward
Twining.
Kiwanja cha Kimataifa cha Dar es Salaam kiliendeshwa na “East African Airways”
ambalo lilikuwa ni shirika la ndege la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, na hata
Menejimenti yake ilikuwa chini ya “Station Manager” wa East African Airways.
Wafanyakazi wake, Marshallers, Security, Porters na Cleaners walikuwa chini ya
Station Manager wa East African Airways.
Shughuli za usanifu na ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal II) la Kiwanja Cha
Ndege cha kimataifa cha Dar es Salaam zilihusisha ujenzi wa majengo ya mnara wa
kuongozea ndege (Control Tower), radar, huduma za hali ya hewa (meteorlogical
services); barabara za kuruka na kutua ndege (runways), njia za viunganishi (taxiways)
na mitambo ya kuongoza ndege (Air Navigational Aids). Jiwe la msingi la kiwanja
hicho liliwekwa na Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere tarehe 16 Oktoba, 1982.
Shughuli za usanifu na maandalizi ya ujenzi wa Terminal II ulianza tangu mwaka 1979
na kukamilishwa Oktoba, 1984. Fedha za uwekezaji katika mradi huu zilipatikana
kutoka serikali ya Ufaransa wakati wakandarasi walikuwa ni kampuni ya kifaransa ya
Bouygues na wahandisi washauri walitoka “Airport de Paris”.
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA)
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro kilijengwa na Mkandarasi wa
Kiitaliano tangu mwaka 1969 mpaka 1971 chini ya usimamizi wa Idara ya Barabara na
Viwanja vya Ndege. Katika ujenzi huo, mwaka 1969 kazi iliyofanywa ni ya uchoraji na
64
usanifu wa michoro ya kiwanja. Aidha ujenzi halisi ulianza mwanzoni mwa mwaka
1970.
Mwaka 1998, Serikali iliingia mkataba wa kubinafsisha Kiwanja cha Ndege cha KIA
kwa kampuni ya “Kilimanjaro Airports Development Limited” (KADCO) chini ya
ubinasishaji huo, Serikali ilimiliki asilimia 24 ya hisa katika kampuni hiyo. Wabia
wengine waliokuwa na hisa katika kampuni hiyo ni Mott McDonald asilimia 41.4,
SAIF asilimia 30 na Interconsult asilimia 4.6.
Kutokana na sababu mbalimbali, mwaka 2010 Serikali iliamua kukirudisha Kiwanja
kwa kuvunja Mkataba uliokuwepo na kampuni za Mott McDonald na SAIF.
Kiwanja cha Ndege cha Mwanza
Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kilijengwa mwaka 1946 kikiwa kwenye kitongoji cha
Butuja kwa sasa kinajulikana kama Sabasaba kilometa saba (7) kutoka mjini kwenye
barabara ya Makongoro au Airport. Kiwanja hiki kilikuwa kinamilikiwa na kampuni ya
machimbo ya madini ya Mwadui Diamond Mines. Mmiliki wa kiwanja hiki yaani Sir
Williamson alikitumia kiwanja hiki kwa ajili ya kusafirisha almasi kwenda Uingereza
kupitia Nairobi Kenya.
Mwaka 1954 Serikali ya mkoloni ikishirikiana na Sir Williamson waliamua
kukihamisha kiwanja hiki na kujengwa sehemu ijulikanayo kama Kisaka mahali kilipo
sasa.
Serikali ya Tanganyika ilikabidhiwa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza mwaka 1961.
Huduma za matengenezo ya kiwanja zilikuwa zikifanywa na Idara ya Ujenzi wakati
huo ikiitwa PWD (Public Works Department). Usafi wa Runway ulifanyika kwa
kutumia ng‟ombe maksai waliokuwa wakikokota fagio la kufagilia runway mara moja
kwa wiki.
Mwaka 1972 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikipanua kiwanja hiki na
kampuni ya “Mouldad & Rose” ilipewa kandarasi ya kukipanua tena na kukiongezea
urefu kutoka mita 2,000 hadi mita 3,000 ikiwa ni pamoja na kujenga “service road”.
Mradi huu ulisimama mwaka 1978 kutokana na vita kati ya Tanzania na Uganda
(Kagera).
Mwaka 1990 Kiwanja kiliendelea kuboreshwa ambapo majengo kadhaa yalijengwa
kama kituo cha kisasa cha Zimamoto na Uokoaji, msingi wa mnara wa kuongozea
ndege (Control Tower), Ofisi za Hali ya Hewa (MET), upanuzi wa maegesho ya ndege
na ujenzi wa majengo mbalimbali ya ofisi. Miongoni mwa wahandisi waliosimamia
miradi hii ikiwa chini ya Wizara ya Ujenzi ni pamoja na Inj. Prosper F. H. Tesha
65
ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
baada ya kuundwa mwaka 1999.
Kiwanja cha Ndege cha Mwanza ni miongoni mwa viwanja vikubwa vya ndani (Major
Domestic Airports), ambacho kinahudumia ndege nyingi za ndani na nje ya Tanzania.
Safari nyingi za ndege za abiria ni kati ya Mwanza na Dar es Salaam, Arusha, Bukoba
Kigoma, Geita, Shinyanga Zanzibar, Kilimanjaro na Mpanda. Wakati safari za nje ya
nchi ni Nairobi, Entebbe, Bujumbura, Mombasa, Kisumu na Kigali. Kiwanja hiki kina
barabara ya kurukia ndege ya lami yenye urefu wa kilomita 3.3 na upana wa mita 45,
maegesho ya ndege manne (4) ambayo ni „Terminal apron, Cargo apron, Military apron
na Isolation area‟.
Kiwanja cha Ndege cha Arusha
Kiwanja cha Ndege cha Arusha kilianzishwa mwaka 1954 kama mali ya mtu binafsi
chini ya mzungu aliyekuwa anajulikana kwa jina la Colonel Aggrey, ambaye alikuwa
akimiliki mashamba ya mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ngano. Wakati huo
“runway” ya Kiwanja hiki ilikuwa inatoka Kaskazini kuelekea Kusini, tofauti runway
na iliyopo sasa ambapo „runway‟ inatoka Mashariki kuelekea Magharibi. Kiwanja kipo
kilomita saba (7) Magharibi kutoka katikati ya mji wa Arusha, kikiwa na eneo la hekari
129.96 zenye hati miliki.
Miaka ya 1960 Bwana Aggrey aliamua kumilikisha mali zake zote kwa Serikali, ikiwa
ni pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Arusha, ambapo kilikabidhiwa kwa Wizara ya
Kilimo, Idara ya Kilimo Anga, ambapo Serikali ilinunua Ndege ndogo za umwagiliaji
zikawa zinatumika kumwagilia dawa kwenye mashamba ya NAFCO huko Mbulu.
Katikati ya miaka ya 70 alitokea mfanyabiashara aliyekuwa anajulikana kwa jina la
Gerry Hunt, ambaye alinunua ndege chakavu za serikali akazikarabati, na kuzileta
Arusha, akaanza kuziendesha kibiashara kwa kubeba abiria na kuwapeleka sehemu
mbalimbali na hasa kwenye mbuga za wanyama. Miaka ya 1990 mahitaji ya safari za
ndege yaliongezeka na hivyo kuanzisha safari za Dar es Salaam na Zanzibar ambapo
makampuni kadhaa ya ndege za kukodi yakazaliwa na hatimaye kukawa na ndege za
ratiba maalum ikiwa ni pamoja na ndege za ATCL.
Kiwanja cha Ndege cha Mtwara
Kiwanja cha ndege cha Mtwara kilijengwa mwaka 1952/53. Kiwanja hiki ni cha tabaka
la lami na kina barabara mbili za kutua na kuruka ndege (2 runways), moja ni ya nyasi
na nyingine ni ya lami (R/way 01/19 na 08/26). Kiwanja cha ndege cha Mtwara kina
urefu wa mita 2258 na upana wa mita 30 (lami) na “runway” ya nyasi ina urefu wa mita
1158 na upana wa mita 30.
66
Kiwanja cha ndege cha Mtwara ni miongoni mwa viwanja vikubwa vinavyomilikiwa na
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Kiwanja cha ndege kina uwezo wa
kuhudumia ndege zenye uzito wa kilogram 56470 na kinapata ndege 50 kwa mwezi.
Kiwanja cha ndege cha Mtwara kilipata umaarufu sana wakati wa kusafirisha shaba
kutoka Lusaka (Zambia) kuja bandari ya Mtwara ili isafirishwe kuja Dar es Salaam.
Wakati Shirika la Ndege la Afrika Mashariki linafanya kazi, kiwanja cha ndege
kilikuwa kiungo kikubwa kati ya Maputo, visiwa vya Shelisheli na Dar es salaam. Kwa
upande wa Msumbiji (Maputo), kiwanja hiki kilitumika sana wakati wa vita ya harakati
za kupata uhuru wa nchi hiyo.
Kiwanja cha Ndege cha Lake Manyara
Kiwanja cha ndege cha Lake Manyara kilijengwa mwaka 1960 kikiwa mali ya mzungu
aliyejenga hoteli ya kitalii iliyojulikana kwa jina la Lake Manyara. Mzungu huyo
alikuwa anaitwa Dougras na alipewa eneo hilo na wananchi wenyeji.
Barabara ya kiwanja cha ndege cha Lake Manyara ni ya changarawe yenye urefu wa
mita 1221 na upana wa mita 23. Kiwanja hiki kinatumiwa sana na ndege za kitalii
zinazotoka Arusha, Dar es salaam, Zanzibar na Kilimanjaro. Wakati wa Shirika la
Ndege la Afrika Mashariki, Kiwanja hiki kilitumika kwa ajili ya kupokea ndege moja
kwa moja toka nje ya nchi (entry point).
Kiwanja cha Ndege cha Songea
Kiwanja cha ndege cha Songea kilianzishwa na raia wa Uingereza aliyeitwa Robert kwa
matumizi binafsi mwaka 1952. Mwaka 1960 kiwanja kilikabidhiwa kwa serikali
kikiwa cha vumbi. Kati ya mwaka 1974 na 1980 kiwanja hiki kilibadilishwa na kuwa
cha lami, kazi iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi chini ya usimamizi wa Mhandisi
Kambona. Kiwanja hiki kina uwezo wa kuhudumia ndege aina ya Fokker 50.
Kiwanja cha Ndege cha Tanga
Kiwanja cha ndege cha Tanga kilijengwa mwaka 1930 na serikali ya kikoloni kwa ajili
ya kurahisisha usafiri wa kwenda kukagua mashamba yao ya mkonge yaliyoko Lugoba,
Amboni, Kogome na Sakura. Kabla ya kujengwa kwa kiwanja hiki, wamiliki hao
walikuwa wanatumia “Air strip” iliyojulikana kama Mnyanjani nje kidogo ya mji wa
Tanga. Kiwanja cha Ndege cha Tanga kilifunguliwa rasmi mwaka 1942 baada ya
kuwekwa tabaka la lami.
67
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Kiwanja cha Ndege cha Tanga, kilitumiwa na
ndege za majeshi ya Waingereza yaliyokuwa yakipigana na majeshi ya Wajerumani.
Hivyo, huduma ya safari za kiraia hazikuwepo kabisa.
Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Kiwanja cha Ndege cha Tanga kilipata
umaarufu mkubwa kwani kilikuwa kiungo kati ya Tanzania (Tanganyika), Kenya na
Uganda.Wakati huo kulikuwa na Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (EAA)
lililokuwa linafanya safari zake kati ya Nairobi, Mombasa, Dar es Salaam na Zanzibar.
Wakati huo kiwanja cha ndege cha Tanga kilikuwa kinapata ndege hata nyakati za
usiku.
Kiwanja cha Ndege cha Kigoma
Kiwanja cha ndege cha Kigoma kilijengwa na mkoloni (Mwingereza) mwaka 1954.
Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, kiwanja hiki kiliendeshwa na Idara ya
Kazi (Public Works Department – PWD).
Madhumuni ya kuanzishwa kwa kiwanja hicho wakati wa ukololoni yalikuwa ni
kurahisisha usafiri wa anga kati ya Kigoma na miji mingine ya Tanganyika na
Usafirishaji wa barua, mizigo ya posta na vifurushi.
Mwaka 1982 njia ya kutua/kuruka ndege (runway) pamoja na majengo mawili ya abiria
yalikamilika na hivyo kukifanya kiwanja cha ndege cha Kigoma kutumika kikamilifu.
Barabara ya kuruka na kutua ndege ya Kigoma ina urefu wa mita 1767 na upana wa
mita 30. Aidha kiwanja kina uwezo wa kuhudumia ndege yenye uzito wa tani 21.
Kiwanja cha Ndege cha Dodoma
Kiwanja cha ndege cha Dodoma ni miongoni mwa viwanja vya Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege Tanzania ambacho uhudumia zaidi Viongozi wa Kitaifa baada ya Makao
Makuu ya nchi kuhamishiwa Dodoma. Kiwanja hiki kilijengwa mwaka 1948 kikiwa na
urefu wa chini ya mita 100 ulioiwezesha ndege aina ya C. 206 (Cesna 206) kutua na
kuruka na lengo kuu likiwa ni kutoa huduma kwa vile Mkoa wa Dodoma upo katikati
ya Afrika Kusini na Misri.
Mahali panapoegeshwa magari ya Zimamoto (kwa sasa) ndipo kilipokuwa kituo cha
kuongozea ndege (control tower). Waanzilishi wa kiwanja hiki ni kanisa la Angalikana
kwa ajili ya kutoa misaada baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Ujenzi wa barabara ya
kiwanja hiki haukujengwa kwa mara moja ulikuwa ukiongezwa kidogo kidogo.
Kiwanja hiki kilipata umaarufu sana mwaka 1974 Serikali ilipoamua kuwa Makao
Makuu ya Chama na Serikali yawe Dodoma. Hivyo kiwanja kiliboreshwa na kuwa na
uwezo wa kupokea ndege yenye uzito wa tani 36 na kina Runway ya lami yenye
68
urefu wa mita 2042 na upana mita 30. Aidha mwaka 1973-1974, Kiwanja hiki
kiliwekwa tabaka la lami chini ya usimamizi wa Mhandisi Mtetemela akisaidiwa na
Mazengo.
Kiwanja cha Ndege cha Tabora
Kiwanja cha kwanza kujengwa nchini Tanzania (wakati ule Tanganyika) kilikuwa ni
kiwanja cha ndege cha Tabora ambacho kilijengwa mwaka 1939. Kilijengwa wakati
huo kwa ajili ya kuunganisha makoloni ya uingereza kutoka kusini Rhodesia na Kenya
hadi Uingereza. Kiwanja hiki kilitumika sana wakati wa vita kuu ya pili ya dunia (1939
-1945) kwa ajili ya ndege za kivita kutoka Afrika Kusini kwenda Ethiopia kupigana na
Wataliano.
Kiwanja cha Ndege cha Musoma
Kiwanja cha ndege cha Musoma kina barabara ya kutua na kuruka ndege yenye urefu
wa mita 1600 na upana wa mita 33. Kiwanja cha ndege cha Musoma kina hudumia
wastani wa ndege 40 kwa mwezi. Kiwanja hiki kilifunguliwa tarehe 01/01/1950 na
kilitumika zaidi kwa ndege ndogo kwa kuwa wakati huo wa ufunguzi kilikuwa ni
“airstrip”.
Kiwanja cha Ndege cha Lindi
Kiwanja cha ndege cha Lindi kilibuniwa na utawala wa kikoloni wa kiingereza mwaka
1924. Kiwanja hiki kina barabara za kutua/kuruka ndege mbili (2) nazo ni 16/34 yenye
urefu wa mita 1847 na upana wa mita 46.
Mwaka 1933 kiwanja hiki kilianzishwa rasmi kwa ajili ya matumizi ya kijeshi.
Kutokana na kubadilika kwa muelekeo wa upepo mara kwa mara kulisababisha
kujengwa kwa “runway” mbili (2) za kutua/kuruka ndege hivyo kuwa na “runway” sita
(6) za Changarawe. Aidha eneo la maegesho ya ndege (apron) lina uwezo wa kuegesha
ndege tano (5) kwa wakati mmoja zenye uzito wa tani 20.
Kukosekana kwa matengenezo ya mara kwa mara (preventive maintenance) kwa
kipindi kirefu, runway zote zimekuwa za nyasi isipokuwa mita 300 za “Threshold and
Touchdown” ya barabara 04/22 na eneo la maegesho. Kiwanja cha ndege cha Lndi
kilitumika wakati wa vita kuu ya pili ya dunia kikiwa ni kiwanja pekee chenye barabara
nyingi za kutua/kuruka ndege.
69
Majukumu
Kama ilivyoelezwa katika Tangazo la Gazeti la Serikali la kuunda Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege Taanzania (G.N Number 404 la mwaka 1999), chini ya Kifungu cha 3.2 cha
tangazo hilo la Serikali, majukumu ya TAA yameainishwa kama ifuatavyo:-
Kuendesha, kusimamia, kutunza na kuendeleza viwanja vya ndege
vinavyomilikiwa na Serikali.
Kutoa huduma bora na salama katika kuwahudumia abiria, ndege na mizigo pale
usafiri wa anga unapotumika ili kujenga taswira nzuri ya nchi kwa mataifa
mengine duniani.
Kutoa ushauri wa kiufundi kwa Serikali katika masuala yanayohusu uendelezaji
wa viwanja vya ndege.
Kuhakikisha kwamba sera za Serikali, kanuni na taratibu zinazohusiana na
masuala ya viwanja vya ndege yanatekelezwa kwa viwango vya kimataifa.
Kuishauri Serikali katika masuala ya kitaifa na kimataifa yanayohusu
usimamiaji wa viwanja vya ndege pamoja na kanuni, ada na tozo zinazoendana
na utoaji wa huduma hiyo.
Kuunga mkono maendeleo ya kitaifa na kiuchumi kwa kuhakikisha
kunakuwepo miundombinu na huduma muhimu.
Malengo
Sambamba na Kifungu 2.1, malengo mkakati ya TAA ni kama yalivyoainishwa katika
kifungu cha 3.3 cha tangazo hilo la Serikali kama ifuatavyo:
Kupata ziada ya mapato dhidi ya matumizi katika kutekeleza Sera ya Taifa
ya Usafirishaji pamoja na kutekeleza malengo mkakati mengine ya
Mamlaka.
Kuboresha utoaji wa huduma katika viwanja vya ndege kupitia mipango
madhubuti ya kuendeleza na kutunza miundombinu.
Kujenga nguvukazi madhubuti na yenye uwezo kitaaluma kupitia sera na
kanuni husika za utumishi.
Kutekeleza matakwa ya kufuata viwango vya kimataifa vinayohusiana na
masuala ya usalama na mfumo wa habari.
Kuongeza mbinu za upatikanaji wa mapato kwa kuvutia vitega uchumi vya
ziada katika viwanja vya ndege.
Katika utekelezaji wa majukumu yake, TAA kama Wakala wa Serikali inasimamiwa na
Bodi ya Ushauri ya Wizara (Ministerial Advisory Board) ambayo kwa mujibu wa
kifungu cha 3.4 cha Tangazo hilo la Serikali, Bodi hiyo hutakiwa kila mara kufuatilia
na kupima utendaji wa TAA katika masuala ya kuboresha viwango vya huduma
zitolewazo pamoja na masuala mengine ya usimamizi wa kifedha na uendeshaji.
70
Mafanikio Yaliyopatikana Hadi Sasa
(a) Tangu tulipopata uhuru, Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam
kiliendelea kukua mwaka hadi mwaka na kuweza kuhudumia abiria laki tano
kwa mwaka (500,000) hadi ilipofika mwaka 1982.
(b) Kutokana na ukuaji huo wa abiria, ililazimu kujengwa kwa Jengo Jipya la
Abiria (Terminal II) lenye uwezo wa kuhudumia hadi abiria wapatao 1,500,000
kwa mwaka. Jengo hilo Jipya lilianza kujengwa mwaka 1979 na kuanza
kutumika mwaka 1984.
(c) Ujenzi wa kiwanja cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) ulianza mwaka 1969
na kukamilika 1971 kikiwa na uwezo wa kuhudumia hadi abiria 500,000 kwa
mwaka. Kiwanja hiki kilijengwa kwa madhumuni ya kukuza utalii katika Kanda
ya Kaskazini.
(d) Viwanja vingi vilifanyiwa matengenezo ya lami kwenye njia ya kuruka na kutua
ndege (runway & apron) kama vile Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa,
Songea na Arusha.
(e) Kushirikisha wadau katika umiliki na uendeshaji wa viwanja kwa mfano;
KIA kinaendeshwa na kampuni ya KADCO,
Seronera kinaendeshwa na TANAPA,
Liwale kinaendeshwa na Idara ya Wanyama Pori, Wizara ya Maliasili na
Utalii,
Mbalizi kilikabidhiwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Geita kilikabidhiwa kampuni ya AshantiAnglogold - Mgodi wa Geita,
Morogoro kinaendeshwa na kampuni ya tumbaku ya TTLC,
Sao Hill kinaendeshwa na kampuni ya Mufindi Paper Mills na,
Mkwaja kinaendeshwa na TANAPA.
Changamoto Zilizojitokeza
i. Kuvunjika kwa “East African Airways” ambako kulipelekea viwanja vingi
kukosa ndege baada ya ndege zilizokuwa zinatumika aina ya “Dakota” (DC 3)
kubakia Kenya.
ii. Ndege zilizotumika na ATC aina ya Fokker Friendship (F27) zilikuwa ni chache
na zilihitaji runway ndefu zaidi ya kutua/kuruka, wakati viwanja vingi vya
71
mikoani na wilayani vilijengwa kwa ajili ya ndege ya Dakota ambayo ilihitaji
runway fupi. Hivyo viwanja vingi vilikosa huduma za ndege.
iii. Kukosekana kwa Kampuni kubwa ya ndege (Strong National Carrier)
kumechangia kiwanja cha JNIA kutokuwa kitovu (hub) cha kuunganishia ndege
kama ilivyokuwa enzi za “East African Airways”.
iv. Uhaba wa mameneja na wahandisi wa viwanja vya ndege ulipelekea usimamizi
wa viwanja kuwa chini ya Regional /District Engineers.
v. Uangalizi mdogo na ukosefu wa hatimiliki, ulipelekea baadhi ya viwanja
kuvamiwa na makazi ya watu (Encroachment). Baadhi ya viwanja vilifungwa
kwa kukosa usalama (mfano Newala na Oldean) kwa vile kulijengwa majengo
kwenye maeneo ya „approach‟ na “runway strips”.
vi. Makampuni ya ndege yalikosa fedha za kigeni kutoka Benki Kuu ya Tanzania
(BOT) kwa mauzo ya tiketi zilizonunuliwa kwa shilingi hapa Tanzania. Hivyo,
Mashirika mengi yalifunga ofisi na safari zao hapa nchini k.m. TRANS
WORLD AIRLINE, SABENA, PAKISTANI, LUFTHANSA, SCANDINAVIA
na mengine mengi.
vii. Mwamko na maandalizi ya kukabiliana na matukio ya kiusalama yalikuwa
madogo sana. Matukio ya utekaji nyara uliofanywa na magaidi wa hapa nchini
yalifanyika mara mbili na kuharibu sifa ya usalama wa viwanja vyetu.
Kukosekana kwa vifaa vya kufanyia kazi hasa upande wa ukaguzi wa abiria na
mizigo, kama mwongozo wa International Civil Aviation Organization (ICAO).
Kazi hii ilifanywa kwa mikono (hand search).
viii. Matukio ya kigaidi ya Septemba 11 nchini Marekani (New York), yalisababisha
kubadilisha mifumo ya usalama kuanzia vifaa vipya, kuajiriwa kwa maafisa
usalama wengi zaidi, mafunzo na taratibu mpya za kukabiliana na matishio
mbalimbali ya ugaidi. Hivyo gharama za uendeshaji ziliongezeka sana na nafasi
za kumbi za abiria zilipunguzwa kwa kufungwa mitambo ya ukaguzi.
ix. Ujenzi wa makazi kwenye maeneo ya viwanja vya ndege ambao unasababisha
ugumu katika juhudi za maendeleo ya upanuzi wa miundombinu mbalimbali
inayohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa viwanja,
x. Upungufu wa makandarasi, wahandisi wazalendo kwenye fani ya viwanja vya
ndege.
xi. Kukua na mabadiliko ya kasi katika matumizi ya teknolojia ya usafiri wa anga
duniani ambayo yanahitaji uwezo mkubwa wa uwekezaji katika miundombinu
na huduma za viwanja vya ndege.
72
Matarajio ya TAA katika Miaka 50 ijayo
Mpango Mkakati wa Uendelezaji wa Viwanja vya ndege katika miaka 50 ijayo na uendeshaji
wa viwanja vya ndege itazingatia yafuatayo:
(a) Viwanja vyote katika majiji na vilivyopakana na nchi jirani, vipanuliwe na
kuboreshwa ili kuwezesha kutua na kuruka ndege aina ya B737 au inayolingana na
hiyo na vitoe huduma masaa 24.
(b) Viwanja vilivyopo mikoani viboreshwe na kupanulia ili viweze kuhudumia Ndege
yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 50 na viweze kutoa huduma masaa 24.
(c) Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi /Umma (PPP) katika kuendesha, kuendeleza na
kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege.
(d) Mkakati wa kuufanya Wakala wetu kuwa Mamlaka kamili (Full Authority) tofauti
na ilivyo sasa.
Katika mpango wa Serikali wa “Transport Sector Investment Programme”, (TSIP), viwanja
vya ndege 16 vimepata kipaumbele katika mpango huo wa kitaifa viwanja hivyo ni JNIA,
Arusha, Mwanza, Lake Manyara, Mafia, Mtwara, Tabora, Bukoba, Dodoma, Kigoma, Moshi,
Shinyanga, Musoma, Tanga, Singida, na Songwe. TSIP inatekelezwa kupitia “Medium Term
Expenditure Framework (MTEF).
Katika jitihada za kutekeleza dira, dhima na malengo ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania inatekeleza majukumu yake hayo kwa kutumia Mpango Mkakati wa Kati (wa miaka
3) na Mpango Kazi (wa mwaka 1). Aidha katika utekelezaji wa Mpango kazi, utajumuisha pia
mipango taraji ya kibiashara pamoja na Bajeti ya mwaka husika.
Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) chini ya mpango huu zimeshaandaa
mpango mkakati na upembuzi yakinifu kwa ajili ya viwanja vya ndege ambayo vinakuza
shughuli za kitalii. Mchakato huo unaendelea kushughulikiwa
10.3.3 Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL)
Shirika la Ndege Tanzania (ATC) lilianzishwa Machi 10, 1977 chini ya sheria ya Mashirika ya
Umma ya mwaka 1969 baada ya kuvunjwa lililokuwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki
ambalo lilikuwa ni ushirikiano wa nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.
Uendeshaji ulianza rasmi mwezi Juni 1,1977.
Shirika lilianza kutoa huduma kwa kutumia ndege tatu, moja aina za DC-9 na mbili aina ya
Foker Friendships F27.
Serikali ilinunua ndege nyingine aina ya Boeing B737-200 Combi (mbili), Foker Friendships
(mbili) na Twin Otters (nne).
73
Hadi kufikia mwaka 2002 ATC ilikuwa na ndege moja aina ya B737-200 na nyingine ya
kukodi ya B737-300.
Aidha ATC iliwekeza katika shughuli nyingine za kutoa huduma viwanjani kwa kununua hisa
asilimia 45 za kampuni ya DAHACO -ambayo kwa sasa inaitwa SWISSPORT, asilimia 50 za
kampuni ya Tanzania Airport Catering Company Ltd na asilimia 15 za kampuni ya African
Join Air Services Company.
Kwa sasa shirika la ndege la Tanzania linamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja. Aidha,
shirika limebaki na ndege mbili aina ya Q-400 dash 8. Ndege moja inafanya kazi na nyingine
ipo kwenye matengenezo.
Makao Makuu ya Shirika la Ndege yako makutano ya barabara ya Ohio na „Garden Avenue‟
Dar es Salaam. Shirika lina „Hangar‟ moja ambayo iko katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere.
Ubinafsishwaji wa Shirika la Ndege la Tanzania
Katika kutekeleza Sera ya Serikali ya ubinafsishwaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika
uendeshaji wa mashirika ya umma ya mwaka 2002, Serikali ilikuwa na asilimia 49 ya hisa zake
kwa Shirika la Ndege la Afika ya Kusini (SAA) na uendeshaji wa shirika hili ulipewa shirika la
Ndege la Afrika ya Kusini. Zoezi la ubinafsishwaji lilipekelekea kuundwa upya kwa Kampuni
ya Ndege ya Tanzania (ATCL).
Baada ya ubinafsishwaji kampuni ilikuwa na haki (rights) za kufanya safari za nje katika miji
ya Entebbe, Nairobi, Kigali, Bujumbura, Kinshasa, Addis Ababa, Harare, Lusaka, Luanda,
Mauritius, Gaborone , London, Mumbai, Rome na mingineyo. Kutokana na uchache wa ndege,
kampuni ilitoa huduma kwenye miji ya Afrika ya Kusini, Entebbe, Nairobi na Visiwa vya
Komoro katika mji ya Hahaya na Afrika ya Kusini katika mji wa Johannesburg, kama
inavyoonyeshwa kwenye jedwali Na.9.7 hapo chini.
Kwa safari za ndani, kampuni ilikuwa na haki ya kutoa huduma katika miji ifuatayo; Kilwa,
Mafia, Pemba, Sumbawanga, Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora na mingneyo. Kutokana na
uchache wa ndege, kwa Tanzania Kampuni iliweza kuhudumia miji ifuatayo; Mwanza,
Kilimanjaro, Mtwara na Zanzibar.
Kampuni ilitoa huduma kwa kutumia ndege mbili ambazo ni Boeing B737-200 ambayo
ilikuwa mali ya shirika na Boieng B737-300 ambayo ilikodishwa.
74
Jedwali Na 9.7: Safari za Ndege mbili Boeing 737 kwa mwaka 2002
Na Njia Kupitia Miruko kwa Wiki
1 DAR/JRO/DAR DCT 7
2 DAR/MWZ/DAR DCT 7
3 DAR/MYW/DAR DCT 3
4 DAR/JNB/DAR DCT 3
5 DAR/NBO/DAR DCT 3
6 DAR/EBB/DAR JRO 3
7 DAR/ZNZ/DAR DCT 7
Ili kuhakikisha kampuni mpya ya ATCL inafanikiwa katika uendeshaji wake, Serikali ya
Tanzania ilichukua madeni yote yaliyokuwa ya ATC. Kampuni mpya ya ATCL ilianza bila
madeni kwenye mizania yake. Serikali ilianzisha shirika jingine lililosimamia madeni na mali
ambazo zilikuwa hazihusiki mojamoja kwa uendeshaji wa shirika jipya.
Nia ya Serikali ilikuwa ni kuifanya kampuni ya ndege kuwa imara na kutoa huduma bora za
ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, baada ubinafsishaji na uundwaji mpya, kampuni ilishindwa
kukua na kuanza kujiendesha kwa hasara. Hali hii ileta mzigo wa madeni kwa ATCL na
Serikali iliamua kuvunja ubia kati ATCL na SAA mwaka 2006 kwa kununua hisa asilimia 49
zilizokuwa zinamilikiwa na SAA.
Baada ya kuvunjika kwa ubia, Serikali iliendelea na mikakati ya kuifufua kampuni hiyo.
Mikakati hiyo iliwezesha kampuni kuanza kutoa huduma zake mwanzoni mwa mwezi
Novemba, 2011.
10.3.4 Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA)
Historia ya Wakala wa Ndege za Serikali
Kabla ya Uhuru wa Tanganyika, kulikuwa na Kitengo cha Ndege za Serikali chenye Historia
ndefu. Kitengo hiki kilianzishwa mwaka 1930 kama kitengo maalum cha Jeshi la Anga la
Kifalme (R.A.F) kikiwa na jukumu la kupima ramani na kuwasafirisha viongozi wa kikoloni
waliopewa dhamana ya kutawala na kuendesha Tanganyika. Baada ya vita vya pili vya dunia,
Serikali ya kikoloni iliunda Kitengo cha Kiraia na kukipangia majukumu hayo hayo. Kitengo
hicho kipya kiliendelea kutumia marubani na mafundi wa jeshi walioachishwa kazi
kukiendesha.
Mwishoni mwa miaka 1960 shughuli za upimaji ramani kwa ndege ulisitishwa hivyo kufanya
Kitengo kuwa cha Usafiri wa ndege wa Serikali (TGFU) chini ya Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi. Kitengo hicho kilipewa Marubani na mafundi wazalendo kutoka Jeshi la Wananchi
ambao waliongezeka kadiri walivyoendelea kupatikana.
Mwaka 1974, Serikali ilinunua ndege moja kubwa aina ya HS 748 na mbili ndogo za kisasa
aina ya Beechcraft King Air 100 na kuongeza ufanisi wa huduma kwa Serikali na chama.
Aidha, 1978 Serikali iliongeza ndege moja kubwa aina ya Jet, Fokker 28 iliyokiwezesha
kitengo hiki kuendelea kutoa huduma kwenda popote barani Afrika na Ulaya. Ndege hii ndio
75
iliyowahudumia Marais wote wastaafu yaani Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Baba wa
Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere, Mhe. Ali Hassani Mwinyi Rais wa awamu ya pili wa Tanzania
na Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya Tatu wa Tanzania. Ndege hii pia
inamhudumia Rais wa awamu ya nne wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Ndege
mbili(2) aina ya Beechcraft King Air 100 ziliuzwa mwaka 1984 na kununuliwa ndege
nyingine mbili (2) aina ya Aero Turbo Commander 690 ambazo hazikukaa sana kwani zote
mbili ziliuzwa. Mwaka 1992 Serikali ilinunua ndege nyingine aina ya Fokker 50 kuwa mbadala
wa HS 748. Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 50 na kutua viwanja hata vya udongo. Ni
chombo kinachosaidia sana kutoa huduma ya ndege kwa Rais pamoja na viongozi wakuu wa
Serikali. Kwa miaka mingi tegemeo la Serikali la Usafiri wa Anga limekuwa ni vyombo hivi
viwili tu Fokker 28 na Fokker 50.
Mwaka 2004 Serikali ilinunua ndege mpya ya kisasa aina ya Gulfstream G550. Ndege hii ina
uwezo wa kuruka dunia nzima, inasaidia kusafirisha viongozi wakuu wa kitaifa masafa marefu
popote ulimwenguni kwa usalama wa hali ya juu na kwa gharama nafuu zaidi. Aidha pia kuna
ndege ndogo ya watu 7 aina ya PA 31, Navajo tuliyoirithi kutoka TCAA.
Kuanzishwa kwa Wakala wa Ndege za Serikali
Wakala wa Ndege za Serikali ni Wakala chini ya Sheria ya Wakala namba 30 ya mwaka 1997,
ulianzishwa tarehe 17 Mei, 2002 ili kusafirisha Viongozi Wakuu wa nchi pamoja na Viongozi
wengine wa Serikali.
Wakala una wajibu wa:
i. Kutoa huduma ya Usafiri wa Anga kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa na wageni wa
Kitaifa.
ii. Kutunza, kuongeza na kuendesha vyombo kwa kiwango cha Kimataifa
iii. Kuboresha Menejimenti ya Wakala.
Katika kutekeleza wajibu wake, Wakala una majukumu ya:
i. Kumhudumia Mhe Rais, Viongozi Wakuu wa Kitaifa na wageni mashuhuri wa Taifa
letu.
ii. Kuhakikisha kuwa vyombo hivyo (ndege na karakana) vinatunzwa pamoja na
kutengenezwa kwa kiwango cha juu cha Kimataifa.
iii. Kuendesha vyombo hivi kwa kuzingatia Sheria na viwango vinavyokubalika Kimataifa.
iv. Kuendelea na uboreshaji wa Menejimenti ya Wakala wa nia ya kuongeza ufanisi katika
kutoa huduma.
v. Kushauri Serikali juu ya vyombo hivi kila mara inapohitajika.
Mafanikio
76
i. Wakala umeweza kuendelea kutoa huduma kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa na
Serikali.
ii. Kuhakikisha uzima wa ndege zote nne (4).
iii. Kuweza kusimamia matengenezo ya ndege zote nne (4), matengenezo makubwa na ya
kawaida.
iv. Wakala umeweza kuwapeleka watumishi kwenye mafunzo kulingana na taaluma zao ili
kuboresha utendaji wa kazi.
Matarajio ya Wakala
i. Kununua ndege kubwa moja na helikopta kwa ajili ya Viongozi Wakuu wa
Kitaifa.
ii. Kudumisha na kuboresha usalama na ubora wa huduma zetu kwa kufuata
taratibu zilizopo kwenye mkataba wa huduma kwa mteja.
iii. Kuendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi yakiwemo maslahi ya
watumishi kulingana na uwezo wa Mamlaka.
iv. Matumizi mazuri ya rasilimali zilizopo, watu, teknolojia ya kisasa, mbinu za
kisasa na fursa mbalimbali ili kujiletea maendeleo ya haraka.
v. Kufanya ukarabati mkubwa wa karakana ya Ndege za Serikali pamoja na ofisi
ili ndege zote ziwe zinaegeshwa humo kwa usalama zaidi.
vi. Kuendelea kuelimisha umma wa Tanzania kuhusu wajibu na majukumu ya
Wakala ili wananchi wapate kufahamu Wakala wa Ndege za Serikali.
vii. Ununuzi wa vyombo vya ukarabati wa majengo na vifaa na uboreshaji wa
nyenzo za kufanyia kazi.
viii. Kuendelea kuwapa watumishi mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuboresha
utoaji wa huduma ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia duniani.
ix. Kuendelea kulinda mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka tisa na
kukamilisha malengo ambayo Mamlaka imejipangia.
x. Kuboresha ukusanyaji wa mapato, pamoja na kuimarisha nidhamu ya matumizi
ya fedha.
xi. Kuendeleza mapambano na maambukizi ya ukimwi kwa watumishi wa Wakala.
10.4 VYUO VYA MAFUNZO CHINI YA WIZARA
10.4.1 Chuo Cha Bahari Dar Es Salaam (DMI)
Chuo cha Bahari (DMI) kina wajibu wa kutoa elimu na mafunzo ya mambo
yanayohusiana na shughuli za bahari (Maritime Sector). Chuo hiki kilianzishwa kwa
77
sheria ya Bunge Na.22 ya mwaka 1991 (Act No 22 of 1991). Hata hivyo historia ya
DMI inakwenda nyuma zaidi hadi tarehe 3 July 1978 ilipokuwa ni kitengo kidogo
kilichojulikana kama DMTU kilichoanzishwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya
mabaharia kulingana na mahitaji ya Kampuni ya Meli Mwambao Tanzania
(TACOSHILI) wakati huo.
DMI ina ithibati (Accreditation) ya ‟National Council for Technical Education
(NACTE), „Association of Business Managers and Administrators‟ (ABMA-UK) na
„Chartered Institute of Logistics and Transport‟ (CILT-UK).
Chuo kinatambuliwa na Mamlaka na Taasisi mbalimbali kama SUMATRA, Wizara ya
Uchukuzi, Kampuni ya Ukaguzi ya Det Norske Veritas (DNV) ya Norway. Vilevile
DMI ina uhusiano wa kitaalam katika masuala ya usalama baharini na Kampuni ya
„Viking-Liferafts AS‟ ya Dernmark na Kampuni ya Jotron AS ya Norway. Pia chuo
kina uhusiano wa kitaaluma na:
i. Chuo Kikuu cha Aaresund-Norway - AUC
ii. Chuo Kikuu cha Dalian cha China - DMU
iii. Chuo Kikuu cha Bahari Shanghai cha China - SMU
iv. Chuo Kikuu Kishiriki cha Hangesund cha Norway -HUC
v. Taasisi ya Bahari na Uvuvi ya Namibia - NAMFI
Kufuatia kiwango cha ubora wa elimu inayotolewa na Chuo hiki kutambuliwa
kimataifa, udahili wa wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi kama Comoro, Namibia,
Uganda na Kenya(taja) umeongezeka sana baada ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuingia kwenye orodha ya ubora (White list) ya Shirika la Kimataifa
linalosimamia shughuli za Bahari duniani (IMO ) mwaka 2003.
Tanzania inatekeleza kikamilifu mkataba wa kimataifa wa mafunzo ya Mabaharia wa
mwaka 1978 kama ulivyorejewa mwaka 1995 (STCW 78 as amended in 1995).
Utekelezaji huo unawapa nafasi wahitimu wa DMI kufanya kazi nje na ndani ya nchi na
hivyo kuongeza uwezo wa Serikali katika mikakati yake ya kuongeza ajira.
Vilevile Chuo kimeweza kuanzisha mfumo wa viwango vya ubora (Quality Standards
System) na kukaguliwa na Shirika la Kimataifa katika ukaguzi wa ubora katika mambo
ya bahari na kutunukiwa hati ya ubora ya ISO- 9001/2000 na Shirika la Kimataifa la
Det Norske Veritas (DNV).
Majukumu ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam
Majukumu ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam ni kutayarisha wataalamu katika Nyanja
mbalimbali ili kusimamia na kuendesha sekta ya bahari. Chuo kinatoa Wataalamu kwa
gharama nafuu na kwa idadi kubwa ikilinganishwa na gharama ya kusomesha
wataalamu hao nje ya nchi. Kozi zinazotolewa na chuo hiki ni:
78
Ukarabati wa meli ( Ship Repair)
Kuendesha meli
Kuendesha shughuli za bandari na container terminal
Mafunzo kwa Watendaji wa Hifadhi za wanyama pori
Mafunzo kwa Watendaji wa Uvunaji maliasili baharini
Mafunzo kwa Waratibu usafirishaji shehena na huduma za meli (Freight
Forwarders, Shipping agents na ships handlers)
Chuo pia kinatoa mafunzo Maalumu kwa taasisi za Jeshi la Wananchi, Polisi na
Uvuvi.
Uongozi na Utawala wa Chuo
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1978, Chuo cha Bahari Dar es Salaam kimepitia utawala wa
wakuu mbalimbali. Kama inavyoelezea historia ya chuo, chuo kilianzishwa kwa msaada wa
Serikali ya Norway, na mkuu wa Chuo wa kwanza alikuwa ni raia kutoka nchi ya Norway
(Ona Jedwali Na. 9.8).
Baada ya kuanzishwa mwaka 1991 na kutambuliwa rasmi kama chuo cha Bahari (DMI),
uongozi wa chuo ulisimamiwa na bodi ya kwanza iliyoundwa mwaka 1992, chini ya
Mwenyekiti Mr.Peter Mtandu. Kikianzishwa kama sehemu ya iliyokuwa Kampuni ya Meli ya
Mwambao (TACOSHILI), na chuo kilikuwa na Idara mbili:
i. Idara ya Usafirishaji wa Majini
ii. Idara ya Uhandisi na Teknolojia.
Mbali ya kuwa kila moja ya Idara hizi ilikuwa inaongozwa na kiongozi wake (Course Leader),
pia Idara hizi zilikuwa katika maeneo tofauti ambapo idara ya Usafirishaji wa Majini ilikuwa
ipo Ubungo katika majengo ya Chuo Cha Usafirishaji (NIT) na Idara ya Uhandisi na
Teknolojia ikiwa katika eneo la TACOSHILI.
Mwaka 1989 Idara ya Usafirishaji ilihamishwa kutoka Ubungo na kuja katika jengo la
TACOSHILI na kuziweka Idara zote katika jengo moja. Mwaka 1991, Chuo kilihamia katika
jengo lililokuwa linatumiwa na kitengo cha Ugavi (Supplies Department) cha Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari ya Tanzania.
Jedwali Na 9.8: Wakuu waliokiongoza chuo kuanzia mwaka 1988.
Jina la Mkuu wa Chuo Kuanzia
Mwaka
Mpaka
Mwaka
Uraia wa Mkuu wa
Chuo
1. Capt. Peder Solem 1988 1992 Mnorway
2. Capt Tim Harris 1992 1994 Mwingereza
3. Mr. Nil Nes 1994 1995 Mnorway
79
4. Mr. Fabian Ninalwo 1995 2000 Mtanzania
5. Mhandisi Thomas J.Mayagilo 2000 2009 Mtanzania
6. Capt S.A. Mkali 2010 Hadi sasa Mtanzania
Udahili wa wanafunzi
Kozi ndefu, kozi za ujuzi na za jioni
Idadi ya wanafunzi waliodahiliwa katika Chuo cha Bahari chuoni imekuwa ikiongezeka kila
mwaka. Udahili wa wanafunzi wa kozi ndefu umekuwa ukiongezeka hasa baada ya wanafunzi
wa Stashahada ya Juu kupata udhamini wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu. Pia
udahili wa wanafunzi wa kozi za jioni umekuwa ukiongezeka kila mwaka kama
unavyooneshwa katika Chati ifuatayo.
80
DMI ilidahili wanafunzi wa kozi ndefu wapatao 428 mwaka 2009/2010 na wanafunzi 480
mwaka 2010/2011. Udahili huu unaonesha kuwa wanafunzi wamekuwa wakiongezeka kila
mwaka, hali inayoashiria hitaji la kuwa na vyumba vya madarasa, vifaa vya kufundishia na
rasilimali watu ili kuendana na ongezeko hilo.
Kozi fupi
Ili kuzuia kutokea kwa ajali za meli zinazoweza kusababisha hasara kubwa, Chuo kinaendesha
kozi fupi ili kuwawezesha wafanyakazi melini na katika bandari kujikinga na kuchukua hatua
za tahadhari pindi ajali zinapotokea.
Chati 2: Udahili wa wanafunzi wa kozi mbalimbli
81
Kumekuwa na ongezeko la wanafunzi waliodahiliwa takribani kila mwaka ukiacha mbali
upungufu uliojiotokeza mwaka 2009/2010
Wahitimu
Katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010 Chuo kimedahili wanafunzi 1,540 wa kozi ndefu na
wanafunzi 25,051 wa kozi fupi. Jumla ya wanafunzi waliodahiriwa ni 26,591.
Jedwali Na: 9.9 Kuonyesha Idadi ya Wahitimu wa Kozi ndefu kuanzia mwaka 1986 – 2006
Nchi Idadi ya Wahitimu
Watanzania 379
Wamalawi 8
Waganda 12
Wacomoro 1
Jumla 400
Jedwali Na. 9.10: Kuonyesha Idadi ya Wahitimu wa Kozi ndefu kuanzia mwaka 2006 –
2010
Nchi Idadi ya Wahitimu
Watanzania 1485
Wakenya 71
Waganda 22
Chati 3: Udahili wa wanafunzi wa kozi fupi
82
Wacomoro 40
Wanamibia 2
Jumla 1620
Huduma na Ushauri wa kitaalamu
Katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010 meli 54 zimefanyiwa ukaguzi, Meli 1
imetathiminiwa ili kujua thamani yake, na uchunguzi wa matukio ya ajali kwa vyombo vya
majini ulifanyika katika meli 2. Kupitia kituo cha Liferaft (servicing of life-saving appliances)
kinachoshughulika na vifaa vya kujiokolea, jumla ya vifaa vya kujiokolea 589 vimefanyiwa
ukarabati mdogo na mkubwa, vilevile vifaa vya zima moto vipatavyo 1,049 vimehudumiwa.
Changamoto
i. Kuboresha miundombinu
ii. Kusomesha Wakufunzi kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na Shahada ya udaktari
iii. Kufanya tafiti katika sekta ya bahari
iv. Kuandaa na kupitia upya mitaala ya kozi mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko.
Kuanzisha kozi za Shahada ya Kwanza
Uchumi endelevu wa taifa lolote lile hutegemea elimu na ujuzi walionao watu wake pamoja na
nyenzo za kufanyia kazi. Kwa kuzingatia umuhimu huo wa rasilimali watu, Chuo kupitia
uhusiano wetu kitaaluma na Chuo Kikuu cha Dalian – China tumekubaliana tuanze na kozi
moja ngazi ya shahada ya kwanza ili kupata kada ya wahitimu ambao wataweza kuchangia
katika kuendeleza Sekta. Kozi hiyo ni Port and Logistics Management.
Chuo pia kimeandaa mitaala ambayo imeshapita NACTE (National Council for Technical
Education) kwa kuhakikiwa na kupata ithibati. Mitaala hiyo ni katika ngazi ya Shahada ya
kwanza ( Degree):
i. Marine Engineering Technology
ii. Nautical Science (Maritime Transport Management)
Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi
Chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) kinayo fursa kubwa katika kutoa kozi mbalimbali
zinazopatikana katika ukanda wa bahari kama utafutaji na uchumbaji wa mafuta na gesi.
83
Taaluma hii mpaka sasa haitolewi hapa nchini japokuwa Tanzania ina rasilimali hiyo ya mafuta
na gesi. DMI kwa kushirikiana na International Marine Institute of Memorial University (MI)
cha Canada inaweza kuendesha kozi fupi na ndefu zinazohusiana na utafutaji na uchimbaji wa
mafuta (Petroleum Technology) hapa nchini baada ya kusaini makubaliano (MoU). Mafunzo
hayo yatatoa mwanya wa kuwa na wataalam katika maeneo yafuatayo:-
i. Dynamic positioning
ii. Anchor handling
iii. Off-shore safety
Taaluma hii itapunguza utegemezi wa wataalam kutoka nje ya nchi na pia kuepuka kusomesha
wataalamu nje ya nchi kwa gharama kubwa. Kwa taarifa, sehemu ya mazungumzo ya suala hili
ilifanyika hapa nchini wakati ndugu Glenn Blackwood ambaye ni Mkurugenzi na Mkuu wa
Chuo Kikuu cha MI (Executive Director and CEO) na ndugu Bill Chislett ambaye ni
Mkurugenzi wakati walipotembelea DMI na kupendekeza DMI itembelee Canada ili kuona na
kukamilisha ushirikiano huo wa kitaaluma.
Kuanzisha Mafunzo ya Cadetship
Kozi hii inaanzishwa mwaka huu (2011/2012) ili kuweza kupata wanafunzi watakaoingia
katika kozi za shahada ya kwanza. Wanafunzi hawa watakapohitimu watakuwa na sifa
zinazohitajika katika soko la ajira katika sekta ya bahari. Sekta hii ya bahari, kwa taarifa ya
IMO litakuwa na uhaba wa mabaharia wapatao 83,900 ifikapo 2012. Hivyo DMI inayo nia ya
dhati na mipango madhubuti katika kuhakikisha kwamba wahitimu wake wanafaidika na fursa
hii kwa kujaza nafasi hizo za ajira, kitaifa na kimataifa.
Matarajio ya Miaka 50 Ijayo
Kwa sababu ya kukua kwa Sayansi na Teknolojia, Chuo kimejipanga kutoa programu ambazo
zinakidhi mahitaji ya nchi na yale ya kimataifa. Chuo pia kinatarajia kufundisha Shahada
(Degree) katika maeneo yafuatayo:-
i. Maritime Economics and Management,
ii. Port and Shipping Administration,
iii. Naval Architecture and Shipbuilding,
iv. Marine Electronics and Electro-technology,
v. Maritime Law.
vi. Computer Science
Matarajio ya Chuo kwa miaka 50 ijayo yamegawanyika katika maeneo mbalimbali. Katika
orodha ya matarajio ya chuo katika kipindi cha miaka 50 kuanzia sasa, chuo kinakusudia
84
kuongeza idadi ya wanafunzi kuweza kufikia wanafunzi 10,000 kwa mwaka. Sambamba na
hilo, chuo kinakusudia kupanua miundombinu itakayofanikisha azma hiyo.
Chuo kinakusudia katika kipindi hicho kuzitumia eka 500 za ardhi ambazo zimepatikana
katika maeneo ya Mkuranga kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa ikiwa ni pamoja
na mabweni, maabara, uwanja wa michezo wa kisasa utakaoweza kuingizia chuo mapato.
Ongezeko la idadi ya wanafunzi litaambatana na kuongeza Kitivo na idara ili kukidhi
mahitaji ya idadi hiyo kubwa ya wanafunzi.
Chuo kinakusudia kukuza ushirikiano uliopo na makampuni na taasisi mbalimbali na pia
kupanua wigo wa ushirikiano na makampuni zaidi. Matarajio zaidi yanalenga kufanikisha
Chuo kuwa na hadhi ya Chuo kikuu kamili.
10.4.2 Chuo Cha Usafirishaji (NIT)
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kilianzishwa rasmi mwaka 1975 kama Idara ya Serikali
chini ya Shirika la Taifa la Uchukuzi kwa madhumuni ya kutoa mafunzo katika Sekta ya
Usafirishaji na Uchukuzi. Mwaka 1982, Chuo kilipanda hadhi na kuwa Chuo cha Elimu ya
Juu chini ya sheria ya Bunge Na.24 ya mwaka 1982 (The National Institute of Transport
Act No.24 ya 1982). Kwa sheria hiyo, Chuo kilipewa uwezo kamili wa kisheria na
madaraka ya kuendesha shughuli zake ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na mafunzo,
kufanya tafiti na elekezi katika fani mbalimbali za Usafirishaji, Uchukuzi na Mawasiliano
chini ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi.
Mafanikio Yaliyopatikana
Katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru, Chuo katika kutekeleza mipango na mikakati yake
kimeweza kupata mafanikio yafuatayo:
Ithibati na “Chartered Institute of Logistics and Transport ( CILT International –
UK)”
Mwaka 2006/2007, Chuo kilipata ithibati “Chartered Institute of Logistics and Transport”
ya Uingereza na kuweza kufundisha na kudahili kozi za kimataifa za uchukuzi na
usafirishaji kuanzia ngazi ya Astashahada hadi Stashahada ya Juu. Hii imekiwezesha chuo
kuweza kutambulika kimataifa.
Ithibati na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Katika mwaka 2008/2009, Chuo kimepata ithibati (accreditation) kamili kutoka Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika ngazi ya Nane (NTA level 8) - ya Muundo wa
Tuzo (Awards) hilo. Hii imekiwezesha Chuo kuanza kutoa taaluma katika ngazi ya
85
Shahada ya kwanza (Degree) na kufuta rasmi utoaji wa taaluma katika ngazi ya Stashahada
ya Juu ikilinganishwa na kutoa taaluma katika ngazi ya Stashahada ya Juu mara tu
kilipoanzishwa.
Kutoa Mafunzo Katika Mfumo wa Ufanisi Competence Based Education and
Training (CBET)
Chuo kimeweza kutoa mafunzo ya ufanisi „Competence Based Education and Training
(CBET)‟ hadi shahada ya kwanza (NTA level 8). Hii imekiwezesha Chuo kutoa wahitimu
ambao watakidhi soko la ajira.
Ongezeko la Programu na wadahili wa Kozi ndefu
Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kimeweza kuongeza programu zake kutoka kozi
ndefu mbili (2) ambazo zilikuwa Stashahada ya Juu Uongozi katika Usafirishaji na
Stashahada ya Kawaida ya Uhandisi Magari mwaka 1975/76 hadi kufikia programu tisa (9)
kwa mwaka 2010/11 ambazo ni; Shahada ya Lojistiki na Menejimenti ya Usafirishaji,
Shahada ya Upokeaji na upelekaji Shehena, Shahada ya Uhandisi Magari, Stashahada ya
Kawaida ya Upokeaji na Upelekaji Shehena, Stashahada ya kawaida ya Uhandisi Magari,
Stashahada ya Kawaida ya Lojistiki na Menejimenti ya Usafirishaji, Stashahada ya
Kimataifa ya Lojistiki na Ushafirishaji, Stashahada ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano na Astashahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kutokana na kuongezeka kwa programu, idadi ya wanafunzi waliodahili kozi ndefu
iliongezeka kutoka wanafunzi 32 mwaka 1975/76 hadi kufikia wanafunzi 288 katika
mwaka 2010/11 ambapo ni ongezeko la wanafunzi 256. Aidha, chuo kimeweza kuongeza
idadi ya wanafunzi wa kozi mbali mbali kutoka wanafunzi 32 mwaka 1975/76 hadi kufikia
wanafunzi 585 katika mwaka 2010/11. Hili ni ongezeko la wanafunzi 553.
Ongezeko la Programu za Kozi Fupi za Udereva na Ukaguzi Magari.
Chuo kimeendelea kuendesha kozi fupi za kuanzia siku moja hadi miezi sita. Mwaka
1975/76, Chuo kilikuwa na kozi fupi tatu ambapo zimeongezeka hadi kufikia kozi fupi 14
mwaka 2010/11 ambazo ni ; Udereva Mahiri Daraja la Kwanza, Udereva Mahiri Daraja la
Pili, Udereva wa Magari ya Viongozi, Udereva wa Magari ya Abiria, Udereva wa
Kujihami, Udereva wa Magari ya Mizigo, Udereva Mwandamizi, Maafisa Usafirishaji,
Ualimu wa Madereva, Udereva wa Pikipiki, Semina kwa Askari wa Usalama Barabarani
Tanzania Bara na Visiwani, Mfumo wa Udhibiti wa Menejimenti ya Usafirishaji,
Utengenezaji wa Injini za Dizeli na Ukaguzi wa Magari na Utahini wa Madereva.
Katika kipindi hicho zaidi ya washiriki 23,333 walishiriki katika kozi mbali mbali za
udereva na ukaguzi wa magari.
Ongezeko la Miundombinu
Wakati kilipoanzishwa chuo kilikuwa na jengo moja la Utawala ambalo lina madarasa nane
(8), ofisi za watumishi kumi na moja (11) pamoja maktaba yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 56 kwa wakati mmoja. Vile vile chuo kilikuwa na mabweni mawili (2) yenye
86
uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 tu . Katika kipindi hiki, Chuo kimeweza kuongeza
madarasa saba (7) na ofisi za watumishi ishirini na moja (21). Katika hatua nyingine ya
kuongeza miundombinu ya chuo, mwaka wa 2007/2008, Chuo kilianza rasmi
ujenzi wa kituo cha rasilimali mafunzo na jengo la ghorofa sita(6) lenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi mia tano (500) kwa wakati. Jengo hilo litakuwa na maktaba ya kisasa,
maabara za kompyuta, kumbi za mihadhara na mikutano, madarasa, ofisi za watumishi,
maabara za modeli za kufundishia, kitengo cha maandiko, machapisho na kurudufu.
Ushirikiano na Vyuo Vingine
Chuo kimeendelea kuimarisha ushirikiano na vyuo vingine kama vile Chuo Kikuu cha
“Leeds Metropolitan” cha Uingereza (Ushirikiano ulianza mwaka 2004). Vyuo vingine ni
pamoja na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Vyuo
vingine vya Elimu ya Juu vilivyopo hapa nchini. Vyuo na mashirika mengine ya nje ni
pamoja na kuingia makubaliano na ''Berlin University of Technology '' ya Ujerumani,
''International Supply Chain Management Consultant'' ''TRANSAID” vya Uingereza na
''Nigeria Institute of Transport Technology''.
Ongezeko la Vifaa vya Kufundishia
Chuo kimeweza kuongeza vifaa vya kufundishia kama vitabu rejea katika maktaba kufikia
10,000, magari ya kufundishia - “Bus” aina ya Marcopolo – Scania lenye uwezo wa kubeba
abiria 59 kwa ajili ya mafunzo ya madereva wa magari ya abiria, Basi aina ya TATA, vifaa
vya Karakana na kompyuta 71 pamoja na ''Digital Projector'' saba (7).
Kufanya Tafiti na kutoa Ushauri Elekezi
Chuo kimeendelea kufanya tafiti na elekezi mbali mbali katika sekta ya usafirishaji,
uchukuzi na nyinginezo. Jumla ya tafiti 20 na elekezi 18 zimefanyika ambazo zimetoa
ufumbuzi na ushauri katika Serikali, Mashirika na jamii kwa ujumla.
Ongezeko la Utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Chuo kimeongeza utumiaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika kufundishia na
utendaji kazi. Kwa sasa Chuo kina maabara tatu (3) za kompyuta na kupata “Software” kwa
ajili ya utunzaji wa taarifa za wanafunzi inayoitwa “Students Academic Records
Information System” (SARIS).
Changamoto
Pamoja na mafanikio makubwa ambayo Chuo kimeyapata tangu kupatikana kwa uhuru,
Chuo kimepata changamoto nyingi ambazo zimeathiri utekelezaji wa majukumu ya msingi
kwa ufanisi. Changamoto hizo ni pamoja na:-
a. Vifaa Vya Kufundishia
87
Chuo kinakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kufundishia ikizingatiwa kuwa
chuo kinatoa mafunzo ya ufanisi '' Competence Based Education'' ambayo
yanaenda sanjari na vitendo. Vifaa hivi ni pamoja na vitabu vya rejea kwa ajili
ya maktaba, magari ya kufundishia, vifaa vya karakana, 'Simulators', 'training
models', barabara za mafunzo n.k.
b. Miundombinu
Kwa ujumla hali ya miundombinu ya madarasa, ofisi za wahadhili, watumishi,
mabweni, uzio wa kuzungukia chuo na barabara za ndani si ya kuridhisha na
hivyo kuleta changamoto katika ufundishaji.
c. Tatizo la Umeme
Chuo kinakabiliwa na tatizo la umeme ambao husababishwa na umeme mdogo
(Low Voltage). Tatizo hili linatokana na kupanuka kwa chuo na ongezeko la
matumizi ya umeme.
d. Tatizo la Maji
Chuo kinakabiliwa na tatizo kubwa la maji ambalo husababisha upungufu wa
maji katika matumizi ya chuo. Hii inatokana na upungufu wa maji kutoka
DAWASCO na kisima kilichokuwepo kuchakaa.
Matarajio ya Chuo kwa Miaka 50 Ijayo
Kuendelea na utoaji wa mafunzo bora ya taaluma za lojistiki, upokeaji na
uondoshaji mizigo, usafirishaji, ufundi na mawasiliano kwa ukanda wa Afrika
Mashariki, Kati na dunia nzima kwa jumla.
Kuanzisha utoaji wa mafunzo kwa kiwango cha Uzamili na Uzamivu katika
taaluma za lojistiki, upokeaji na uondoshaji mizigo, usafirishaji, ufundi,
mawasiliano utawala wa rasilimali watu na nyinginezo.
Kuwa na sura ya Kimataifa kwa ubora wa taaluma itolewayo itakayowavutia
washiriki wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi kwa kuboresha mitaala ya
kufundishia ili kuongeza kiwango cha ubora wa wahitimu sanjari na mabadiliko
ya sayansi na teknolojia.
Kuanzisha vituo vya mafunzo katika kanda zote za Tanzania Bara na Visiwani.
Kuongeza idadi ya wahadhiri, watumishi na vitendea kazi.
Kuongeza vifaa vya kufundishia kwa lengo la kutoa mafuzo bora ya vitendo.
Kuwa kitovu cha kufanya utafiti na kukusanya takwimu zitakazosaidia kutoa
suluhu ya matatizo ya Menejimenti ya usafiri nchini, hususan katika miji yetu na
nchi za jirani.
Kuwa Taasisi inayoaminika na kushauri jamii na Serikali kwa ujumla kuhusiana
na masuala ya kitaalam ya Sekta na hivyo kufanywa kitovu cha taarifa muhimu
zinazohusu na Sekta ya Uchukuzi.
10.5 HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI
Huduma za hali ya hewa nchini zilianza kutolewa mwaka 1929 chini ya Taasisi ya Hali ya
Hewa ya Uingereza iliyojulikana kama British East Africa Meteorological Services (BEAMS).
Katika kipindi husika vituo viwili vya hali ya hewa vilijengwa Kazeh Hill huko Tabora na
Chukwani Zanzibar ambapo makao makuu ya taasisi hii yalikuwa Tabora. Taasisi hiyo ilikuwa
88
na majukumu ya kutoa huduma za hali ya hewa kwa nchi za Kenya, Tanganyika, Zanzibar na
Rhodesia ya Kaskazini (sasa Zambia). Baadaye Taasisi hiyo iliitwa British East African
Meteorological Department (BEAMD) chini ya British East African High Commission kwa
nchi za Kenya, Tanganyika, Uganda na Zanzibar.
Baada ya kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni (WMO) mnamo mwaka
1951, huduma za hali ya hewa duniani ziliimarika ambapo mwaka 1963 British East African
High Commision ilibadilishwa muundo na kuwa East African Common Services Organisation
(EACSO) ambapo BEAMD ilibadilika na kuwa East African Meteorological Department
(EAMD) iliyokuwa na jukumu la kuhudumia nchi tatu za Afrika Mashariki yaani; Kenya,
Uganda na Tanzania. Makao makuu ya BEAMD na EAMD yalikuwa Kabete, Kenya na
baadaye yakahamishiwa Nairobi, Kenya. Mwaka 1967 EACSO ilibadilika na kuwa East
African Community (EAC). Taasisi ya Hali ya Hewa nayo ilipata muundo mpya lakini
iliendelea kuitwa EAMD na makao yake makuu kuwa huko Nairobi, Kenya.
Mwaka 1977, baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, huduma za hali ya
hewa nchini zilikuwa chini ya Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi kama Idara ya Serikali. Idara
Kuu ya Hali ya Hewa (Directorate of Meteorology (DoM)) ilianzishwa rasmi 1978 kwa Sheria
namba 6 ya mwaka huo.
Idara Kuu ya Hali ya Hewa ilibadilishwa na kuwa Wakala wa Serikali mnamo mwaka 1999
kwa Sheria namba 30 ya Executive Agencies (Act) na ikaitwa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania. Mabadiliko hayo yalilenga kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa vile wakala
uliongezewa uwezo wa kufanya baadhi ya maamuzi ya kiutendaji.
Historia ya Ofisi Kuu za Hali ya Hewa Tanzania
Tanzania kulikuwa na ofisi ndogo na ya kiutawala zaidi kwa vile shughuli za hali ya hewa
hazikuwa nyingi na makao makuu yalikuwa Nairobi, Kenya. Shughuli zilianza kupanuka baada
ya Uhuru na ofisi za hali ya hewa zilikuwa katika jengo la Avalon Building, Sokoine Drive.
Mnamo mwaka 1966, Jumuiya ya Africa Mashariki (EAC) ilijenga makao makuu yake
Sokoine Drive kwenye jengo la EAC Building ambalo sasa linaitwa Mapato House. EAMD
Tanzania na baadaye DoM walikuwa ghorofa ya 6 katika jengo hilo. Kutokana na kupanuka
kwa shughuli zake, EAC ilijenga ofisi nyingine kwa ajili ya EAMD na Directorate of Civil
Aviation (DCA) kanda ya Tanzania katika eneo la Sokoine Drive karibu na Posta ya zamani.
Kwa bahati mbaya wakati EAC ilipovunjika mwaka 1977 jengo hilo halikuwa limekamilika na
1978 lilichukuliwa na Wizara ya Maji na Nishati.
Shughuli za DoM zilizidi kupanuka na majukumu yaliyokuwa yakifanyika makao makuu
Nairobi yalianza kufanyika hapa nchini kwa hiyo kukawa na uhitaji mkubwa wa ofisi. Shughuli
nyingi za makao makuu ya DoM zilitawanyika katika majengo ya EAC Building (Mapato
House), Tancot House Building, Dar es Salaaam Airport na Revenue (TRA) Samora Avenue.
Katika kutatua tatizo hili, Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilihamia katika jengo la Ubungo
Plaza mwaka 2004.
Historia ya Utabiri wa hali ya hewa Tanzania
89
Utabiri wa hali ya hewa ulianzishwa na mwana sayansi wa Uingereza, Lewis Richardson
mwaka 1926 ambapo aligundua kuwa mifumo ya hali ya hewa inafuata kanuni za hesabu na
fizikia. Kabla ya 1961, utabiri wa hali ya hewa nchini ulikuwa unafanyika katika viwanja vya
ndege.
Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilianzishwa National Meteorological
Centre iliyokuwa na jukumu la kutoa utabiri wa hali ya hewa nchini. Katika kipindi hicho,
utabiri uliokuwa unatolewa ulikuwa wa muda mfupi wa saa sita kutokana na uwezo mdogo wa
teknolojia iliyokuwa inatumika wakati huo.
Mnamo miaka ya 1990, utabiri wa hali ya hewa kwa kutumia mifumo ya modeli za hesabu
(Numerial Weather Prediction) na picha za satellite ilianza kutumika nchini. Mifumo hii
imeimarisha huduma za utabiri wa saa sita na kuwa wa saa 24, siku kumi na msimu. Aidha,
mifumo hiyo imerahisisha kazi ya kuandaa utabiri nchini.
Historia ya mfumo wa ubadilishanaji wa taarifa za hali ya hewa Tanzania
Ili kuweza kutabiri hali ya hewa nchini na pia kubadilishana na nchi nyingine kwa ajili ya
usalama wa binadamu na mali zao lazima nchi zote zibadilishane taarifa na takwimu za hali ya
hewa. Kabla ya uhuru, mfumo wa mawasiliano ulitumia mikanda na mapigo maalum ya sauti
(Torn tape’ na „morse code) katika ubadilishanaji wa taarifa za hali ya hewa.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inatumia njia mbili za kukusanya na kubadilishana taarifa na
takwimu za hali ya hewa. Mfumo wa kwanza ni ule wa WMO wa Global Telecommunications
System (GTS) na mwingine ni ule mahsusi kwa ajili ya Usalama wa Usafiri wa Anga uitwao
Aeronautical Fixed Telecommunications Network (AFTN) wa ICAO.
Katika kipindi cha 1971 – 1981, mfumo wa mawasiliano ulitegemea „land-line Teletype (LLT)‟
kwa kiasi kikubwa na simu za mezani ambapo Shirika la Posta na Simu ndio lililokuwa
likisimamia kwa uhakika wa mawasiliano. Aidha, mifumo ya mawasiliano ya „Facsmile’
ilitumika ambapo taarifa zilikuwa zinabadilishwa kupitia „Line Teletype (LTT), Telexes, Radio
Teletype (RTT)‟ pamoja na kutumia radio za „High Frequency (HF)‟.
Kuanzia miaka ya 1990, mifumo ya mawasiliano iliboreshwa na kuanza kutumia Premicel,
tovuti, Transmet, Radio Telephone (SSB), VSAT, SADIS, Retim Synergie na Microwave link.
Aidha, maendeleo ya kisayansi duniani yamekuwa yakiendelea kuboresha mifumo ya
mawasiliano ya hali ya hewa.
Ramani iliyopo hapa chini inaonesha mifumo ya mawasiliano inayotumika kubadilishana data
za hali ya hewa toka vituo mbalimbali nchini kwenda kituo kikuu cha utabiri kilichopo Dar es
Salaam. Aidha, data hizo hupelekwa kituo cha kanda – Nairobi.
90
Historia ya usambazaji wa taarifa za hali ya hewa Tanzania
Tangu mwaka 1961, mfumo wa utoaji wa taarifa za hali ya hewa, ulikuwa unalenga kuboresha
huduma za usafiri wa anga maeneo maalum na majini, kilimo cha mazao ya biashara pamoja na
tahadhari. Njia kuu ya utoaji habari kipindi hicho ilikuwa ni vyombo vya habari ikiwa ni
pamoja na magazeti na radio. Magazeti haya yalikuwa hayawafikii walengwa kwa kiasi
kikubwa hasa vijijini na radio zilizokuwepo wakati huo zilikuwa hazisikiki nchi nzima na pia
sio walengwa wote waliweza kumiliki Radio. Kwa hivi sasa, Mamlaka imefanikiwa kuboresha
ufikishaji wa taarifa za hali ya hewa kwa walengwa kwa kuongeza idadi ya vyombo vya habari
ikiwemo radio, tovuti, magazeti na televisheni.
Madhumuni ya kutoa huduma za hali ya hewa
Kabla ya uhuru huduma za hali ya hewa zilikuwa zinatolewa kwa ajili ya kukidhi matakwa ya
Wakoloni ikiwemo kufanikisha safari za ndege za Ulaya na Afrika ya Kusini. Aidha, huduma
za hali ya hewa zililenga katika kutoa huduma kwa sekta ya kilimo cha mazao ya biashara
(Groundnut scheme-Nachingwea na Kongwa).
Baada ya uhuru, majukumu ya utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini yaliongezeka na
huduma ziliboreshwa ili kukidhi mahitaji ya jamii na kuchangia katika ukuaji wa sekta za
kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania hasa sekta ya usafiri wa anga.
91
Mwaka 1999, Serikali ilifanya mabadiliko kwa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa kuwa
Wakala wa Hali ya Hewa yenye majukumu yafuatayo:-
Kuanzisha na kuendesha vituo vya hali ya hewa ili kupata takwimu na taarifa za hali ya
hewa kwa ajili ya kutoa huduma za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi
na kijamii.
Kutoa utabiri wa hali ya hewa wa kila siku, muda wa kati (siku 10) na wa msimu na
kutoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa na kuhakikisha taarifa hizi zinawafikia
walengwa katika muda muafaka.
Kutoa huduma za hali ya hewa kwa sekta za kilimo, usafiri na uchukuzi, miundombinu,
maji, nishati, mazingira, utalii, nk
Kufuatilia na kufanya utafiti wa kisayansi kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi
(Climate change) nchini.
Kushirikiana na taasisi za kimataifa na nchi nyingine katika kubadilishana takwimu na
taarifa za hali ya hewa, hususani majanga ya asili kama ukame na vimbunga kwa ajili
ya kutoa tahadhari.
Sekta ya hali ya hewa ina jukumu la kuendeleza na kutunza mtandao wa vituo vya
kupima na kuangaza hali ya hewa ili kukidhi makubaliano ya kimataifa ya
kubadilishana taarifa hizo na nchi nyingine. Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi
(climate change) yanahitaji ushirikiano wa kimataifa. Mamlaka ina jukumu la kufuatilia
na kupima kisayansi mabadiliko ya hali ya hewa nchini.
Kufanya utafiti na kutoa mafunzo ya fani ya hali ya hewa kwa kushirikiana na vyuo vya
ndani na nje ya nchi.
Kushirikiana na taasisi za kanda na za kimataifa zinazojihusisha na shughuli za hali ya
hewa kama vile Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC);
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).
Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru
Upanuzi wa mtandao wa Vituo vya kupima hali ya hewa nchini.
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na Kituo Kikuu kimoja tu cha Dar es salaam
kilichokuwa kinafanya kazi kwa saa ishirini na nne (24). Kwa sasa Tanzania ina vituo vikuu 28
vya kupima hali ya hewa vinavyopima kwa saa 24.
Vituo vya kupima mvua
Upimaji mvua ulianza 1892 wakati Tanganyika ikiwa chini ya utawala wa Kijerumani. Wakati
huo upimaji mvua ulikuwa ni wa kujitolea na haukuwa na malipo.
Serikali ya Kikoloni ilijenga vituo 1074 vya kupima mvua na lengo kuu lilikuwa ni kukuza
kilimo cha mazao ya biashara. Baada ya uhuru, Serikali iliendeleza na kuongeza mtandao wa
vituo hivi na kufikia 2043. Katika miaka ya 1960 hadi 1980, vituo vilipungua hadi kufikia 1200
kutokana na kupungua kwa bajeti ya kuhudumia shughuli za hali ya hewa nchini. Kwa
kutambua umuhimu wa taarifa na takwimu za mvua, Mamlaka kuanzia miaka ya 1990
92
ilianzisha mpango wa kuwalipa posho wapimaji mvua wachache wanaofanya vizuri na mpango
ukazaa matunda ambapo mpaka sasa vituo vimeongezeka na kufikia 1600.
Vituo vya hali ya hewa Mahsusi kwa Kilimo (Agromet stations)
Wakati wa ukoloni kulikuwa na vituo sita (6) tu vya hali ya hewa mahsusi kwa kilimo
(agrometeolojia). Baada ya uhuru, Serikali kwa kutambua mchango wa Sekta ya Kilimo
ambayo ndiyo mhimili mkuu wa uchumi wa Tanzania ilifanya jitihada za kujenga vituo zaidi 7
na kuongeza idadi ya vituo hivyo kufikia 13.
Vituo vya Rada za hali ya hewa
Wakati tunapata uhuru, tulikuwa tunamiliki vituo viwili vya rada za hali ya hewa zilizokuwa
Dar es Salaam na KIA, lakini kutokana na mabadiliko ya Teknolojia, Rada hizi zilipitwa na
wakati hivyo, hazitumiki tena. Kwa sasa Mamlaka imekamilisha ujenzi wa kituo cha Rada ya
Hali ya Hewa kilichopo Dar es salaam na taratibu za ununuzi wa rada ya pili itakayofungwa
Mwanza zinaendelea.
Vituo vya kupima hali ya hewa ya anga za juu (Radiosonde Stations)
Baada ya uhuru tulianzisha vituo vya Radiosondes Dar es Salaam na Tabora na baadaye
tuliongeza vituo vingine huko Kigoma na Mtwara kupitia mradi wa FINNIDA (1988–1992).
Hata hivyo, kutokana na kubadilika kwa teknolojia, mitambo ya vituo hivi ilipitwa na wakati
ikawa haitumiki tena. Kwa sasa Mamlaka imefufua kituo cha Dar es Salaam kwa kufunga
mtambo mwingine wa kisasa.
Wafanyakazi na Mafunzo
Wafanyakazi
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961, Taasisi ya Hali ya Hewa kwa nchi zote za Afrika ya
Mashariki ilikuwa na wafanyakazi 330 kati yao wanasayansi walikuwa 14 na hakukuwa na
watabiri (forecasters) wazalendo. Kwa sasa huduma za hali ya hewa zinatolewa na TMA iliyo
chini ya Wizara ya Uchukuzi yenye wafanyakazi 570 kati yao wanasayansi ni 407 wanawake
wakiwa ni asilimia 20 ya wanasayansi waliopo. Aidha, kwa hivi sasa wako watabiri 82
miongoni mwa hao wanawake ni 26.
Mafunzo
Tangu enzi za ukoloni, mafunzo ya taaluma ya hali ya hewa katika ngazi zote yamekuwa
yakipatikana nje ya nchi. Mnamo mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Serikali ilianzisha Chuo cha Hali ya Hewa Dar es Salaam na baadaye mwaka
1981 kuhamishiwa Kigoma ili kupunguza gharama ya kuwapeleka wanafunzi katika elimu ya
awali nje ya nchi. Mnamo mwaka 1999, Chuo kilianza kutoa mafunzo ya kati ya watabiri
(Class III) na mwaka 2002 kilianzisha mafunzo ya stashahada ya utabiri (Forecasting) hapa Dar
es Salaam na baadae kuhamishiwa Kigoma.
93
Mpaka sasa, Mamlaka ina wafanyakazi wenye shahada wapatao 92 wanawake wakiwa ni 22.
Wafanyakazi wenye shahada ya kwanza wakiwa 62 wanawake 14, shahada ya pili wakiwa 24
wanawake 7 na shahada ya tatu wakiwa 6 mwanamke mmoja.
Mifumo ya Utabiri
Baada ya mwaka 1961, Mamlaka haikuwa na mfumo wa utabiri kwa kutumia Numerical
Weather Prediction Models, NWP hadi ilipofika miaka ya 1990 ambapo utabiri wa aina hii
ulianza kutumika toka vituo vikuu vya utabiri kupitia tovuti. Mpaka kufikia mwaka 1994,
Mamlaka ilianzisha mfumo wa utabiri wa NWP na imeendelea kuuboresha mfumo huo mpaka
sasa.
Hadi kufikia mwaka 2011, Mamlaka imekuwa na mafanikio makubwa katika upatikanaji wa
taarifa mbalimbali za hali ya hewa katika satelaiti ambazo zimewekwa angani na kuangalia
eneo moja la dunia (geostationary satellites).
Kutokana na kuongezeka kwa mtandao wa vituo nchini, Mamlaka imekuwa ikitoa utabiri wa
kila siku, siku kumi, mwezi na msimu kwa usahihi na kuaminika katika kiwango cha
kuridhisha ukilinganisha na miaka 50 iliyopita.
Mifumo ya usambazaji wa taarifa za hali ya hewa
Mamlaka imeweza kuanzisha studio ya hali ya hewa inayotumika kuandaa utabiri wa hali ya
hewa kwa ajili ya kuutangaza kwenye luninga. Pia imefungua tovuti yake (www.meteo.go.tz)
kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma zake. Hapo awali, utabiri wa hali ya hewa ulikuwa
unatolewa kupitia redio na magazeti. Mabadiliko ya utoaji wa taarifa yaliambatana moja kwa
moja na mabadiliko makubwa ya kisayansi na kiteknolojia katika vifaa vya mawasiliano
ambapo serikali ilichangia kwa kiasi kikubwa ikiwemo uundwaji wa sera mbalimbali za
vyombo vya mawasiliano nchini. Vyombo vya habari vimekuwa vikiongezeka ambapo
Mamlaka ilianza kutoa taarifa zake kupitia Televisheni moja mwaka 1995 na hadi kufikia sasa
kuna magazeti 5, radio 11, Televisheni 6.
Mfumo wa kuhifadhi taarifa za hali ya hewa
Wakati wa uhuru 1961, takwimu zote za hali ya hewa zilikuwa zikihifadhiwa Nairobi ambapo
mnamo mwaka 1972, kiasi kikubwa cha takwimu hizo zililetwa nchini. Idara Kuu ya Hali ya
Hewa nchini ilikuwa ikizihifadhi taarifa na takwimu za hali ya hewa katika mifumo ya
makabrasha, magnetic tapes na punch-cards. Mnamo mwaka 1990, Idara Kuu ya Hali ya Hewa
ilifanya mabadiliko katika kuhifadhi na kuchambua taarifa na takwimu za hali ya hewa kwa
kuanza kutumia teknolojia ya kompyuta. Teknolojia hiyo ya kuchambua na kuhifadhi takwimu
kupitia kompyuta inayoitwa CLICOM ilianza kutumika 1990. Shughuli ya ubadilishaji na
uhifadhi wa taarifa na takwimu za hali ya hewa ni kubwa kutokana na wingi wa takwimu za
hali ya hewa zilizopo kuanzia mwaka 1892 na inaendelea hadi sasa.
94
Changamoto katika utoaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania
Kutokuwepo kwa Sera na Sheria ya Hali ya Hewa
Upungufu wa vituo na vifaa vya kupimia hali ya hewa
Gharama kubwa za kununua na kuendesha mitambo ya hali ya hewa.
Mabadiliko ya hali ya hewa duniani (Climate Change) yanayosababisha changamoto
katika kutoa utabiri.
Upungufu wa wataalam wa hali ya hewa.
Ufinyu wa bajeti.
Kutokuwa na jengo la Kituo Kikuu cha Utabiri.
Uchakavu wa Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma
Matarajio katika miaka 50 ijayo
Mamlaka ina mikakati ya muda mrefu ya kuboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji ya
huduma za hali ya hewa nchini ambayo yameongezeka kutokana na kukua kwa sekta
mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Mikakati hiyo ni pamoja na:-
Kuongeza idadi ya vituo vinavyopima taarifa zote za hali ya hewa kutoka 27 hadi
kufikia 70. Pia kununua mitambo 100 ya kupima taarifa za hali ya hewa inayojiendesha
yenyewe.
95
Kuwa na vituo saba Dar es Salaam, Kigoma, Mwanza, Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya,
Mtwara vya rada nchi nzima. Katika utekelezaji wa mradi huo tayari ufungaji wa rada
moja umekamilika na taratibu za ununuzi wa rada ya pili zinaendelea. Kukamilika kwa
mradi huo kutaimarisha shughuli za utabiri wa hali ya hewa pamoja na tahadhari dhidi
ya matukio ya hali mbaya ya hewa.
Kuongeza idadi ya vituo vya hali ya hewa mahsusi kwa kilimo kutoka 13 vilivyopo sasa
na kufikia ishirini (20) ili kukidhi mahitaji ya sekta ya kilimo.
Kuongeza vituo 900 vya kupima mvua na kuviimarisha vilivyopo ili kufikia vituo
2,500. Aidha Mamlaka ina mpango wa kununua vifaa 2,500 vyenye uwezo wa kupima
mvua vyenyewe (Automatic raingauges) ili kufikia malengo ya kuwa na vituo 5,000
nchi nzima.
Kuboresha Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma na kuanzisha mafunzo ya shahada, uzamili
na uzamivu ya Hali ya hewa hapa nchini.
Kuboresha mfumo wa mawasiliano ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia
ya ubadilishaji wa taarifa za Hali ya Hewa duniani.