jamhuri ya muungano ya tanzania ofisi ya rais tawala … ya ukaguzi wa... · v) ujenzi wa vyumba 8...
TRANSCRIPT
JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA DAR ES SALAAM
TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZWA NA MAMLAKA
ZA SERIKALI ZA MITAA HADI KUFIKIA ROBO YA TATU KWA KIPINDI CHA MWAKA
2016/17
Imetayarishwa na:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
3 Barabara ya Rashid Kawawa,
S. L. P. 5429
12880 DAR ES SALAAM. Mei, 2017
YALIYOMO UK.
1. UTANGULIZI: … … … … …… … … … … … 1
2. TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI
ZA MKOA WA DAR ES SALAAM … … … … … … … 1
3. CHANGAMOTO ZA JUMLA ZILIZOJITOKEZA WAKATI WA UKAGUZI WA
MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI NA USHAURI ULIOTOLEWA … 4
4. VIAMBATISHO: … … … … … … … … … 8
4.1 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA KINONDONI … … … … … … 8
4.2 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA UBUNGO … … … … … … … 25
4.3 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA ILALA … … … … … … … 50
4.4 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA TEMEKE … … … … … … … 92
4.5 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA KIGAMBONI … … … … … … 106
4.6 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
JIJI LA DAR ES SALAAM … … … … … … … 131
4.7 ORODHA YA WALIOSHIRIKI KATIKA UKAGUZI WA MIRADI YA
MAENDELEO … … … … … … … … 136
1.0 UTANGULIZI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ilifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Halmashauri za Manispaa zote za mkoa hadi kufikia robo ya tatu kwa
kipindi cha mwaka 2016/2017. Ukaguzi huo ulianza tarehe 25 Aprili hadi tarehe 25 Mei,
2017. Jumla ya miradi 62 ilitembelewa kwa mchanganuo ufuatao: Kinondoni miradi 15,
Ubungo miradi 11, Ilala miradi 15, Temeke miradi 11, Kigamboni miradi 8 na Halmashauri
ya Jiji miradi 2. Miradi iliyotembelewa katika Halmashauri ni pamoja na miradi ya sekta za
Barabara, Maji, Elimu, Afya, Usafi/Usafishaji, Ukarabati wa majengo ya Serikali na Masoko.
Katika kutembelea miradi hiyo, Timu ya Ukaguzi iliongozana na Katibu Tawala wa Mkoa na
shughuli zote za ukaguzi ziliratibiwa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na
Uratibu.
Nyaraka zilizohitajika wakati wa ukaguzi ni pamoja na:-
a) Mpango wa bajeti na Mpango Kazi (Action Plan) ya Halmashauri kwa mwaka
2016/2017,
b) Mkataba na michoro kwa kila miradi iliyokaguliwa,
c) Taarifa za utekelezaji kwa mwaka 2016/2017 hadi kufikia Machi, 2017 kwa kila
miradi (Physical & Financial), na
d) Historia ya mradi husika kutoka kwa msimamizi.
Ukaguzi wa miradi ya maendeleo ulianza katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
tarehe 25 Aprili, 2017 na kumalizika katika Halmashauriya ya Jiji la Dar es Salaam tarehe
25 Mei, 2017. Tarehe za ukaguzi kwa kila Halmashauri zipo kwenye maelezo ya kila
Halmashauri husika.
2.0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA KINONDONI
Utangulizi.
Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri hii ulianza tarehe 25 hadi 27 Aprili,
2017. Shughuli za Ukaguzi zilianza kwa Mchumi wa Manispaa kutoa taarifa kwa ufupi ya
miradi itakayotembelewa kwa kuelezea lengo la kila mradi, tarehe ya kuanza na
kukamilisha mradi, gharama za mradi na fedha zilizotolewa na zilizotumika. Jumla ya miradi
15 ya maendeleo ilitembelewa ambayo ni kama ifuatavyo:-
i) Ujenzi wa mradi wa Maji Makongo Mbuyuni
ii) Ujenzi wa madarasa 12 Shule ya Sekondari Mivumoni Kata ya Wazo
iii) Ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa Shule ya Sekondari Kondo Kata ya Kunduchi
iv) Upanuzi wa wadi ya Wazazi katika Zahanati ya Kijitonyama katika Kata ya
Kijitonyama
v) Ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa Shule ya Msingi Bunju A katika Kata ya Bunju
vi) Ujenzi wa machinjio ya Kuku awamu ya pili katika Kata ya Kawe
vii) Ukamilishaji wa ujenzi wa Soko la Kisiwani katika Kata ya Makumbusho
viii) Ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete katika
Kata ya Kijitonyama
ix) Ujenzi wa Wodi ya Wazazi Hospitali ya Mabwepande awamu ya kwanza
x) Ujenzi wa Tanuru ya kuchomea taka katika Zahanati ya Boko
xi) Ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala
xii) Ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa Shule ya Sekondari ya Mzimuni awamu ya
kwanza katika Kata ya Mzimuni
xiii) Ukaguzi wa barabara ya Arsenal kwa magoti
xiv) Ukaguzi wa barabara ya Polisi Mabatini
xv) Ukaguzi wa barabara ya Magomeni – Sinza
2.1 Ujenzi wa Tanki la Maji Makongo Juu - Mtaa wa Mbuyuni
Utangulizi
Mradi wa Maji Makongo Mbuyuni upo katika Kata ya Makongo Juu Mtaa wa Mbuyuni.
Lengo la mradi ni kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Makongo
Mbuyuni. Mradi ulianza Februari, 2016 na ulikamilika Agosti, 2016. Mkandarasi aliyejenga
mradi huu ni M/S EDGE POINT Company Ltd na JV REMO (T) Ltd. Kiasi kilichotengwa kwa
ajili ya ujenzi wa mradi ni Tsh. 195,980,000 183 na kiasi kilichotolewa ni Tsh.
183,190,068.00.
a) Utekelezaji
Mradi umekamilika na unatoa huduma ya maji kwa Wananchi wa Makongo Mbuyuni.Awali
kilichimbwa kisima chenye urefu wa mita 100.Ujenzi umejumuisha Tanki lenye ujazo wa lita
40,000 lenye uwezo wa kuhudumia watu 7,200, vituo vya kuchotea maji (DP’s) 14,ufungaji
wa Pampu na mtandao wa mabomba yenye urefu wa Km 2.567. Aidha, kuna Kamati ya
maji yenye wajumbe wanane (8)
b) Changamoto
Changamoto zinazokabili mradi huu ni upatikanaji wa maeneo ya ujenzi wa miundombinu
ya maji.
c) Maoni
Hatua stahiki ya kuchukua ni kushirikisha wananchi katika hatua zote za mradi kuanzia
wakati wa kubuni mradi, kuandaa mpango wa utekelezaji na ujenzi wa mradi na usimamizi
wa matumizi ya mradi.
Picha Na.1: Ujenzi wa Tanki la Maji lenye ujazo wa lita 40,000 katika mradi wa maji Makongo- Mbuyuni
2.2 UJENZI WA VYUMBA VINNE VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI
SALMA KIKWETE.
Utangulizi:
Mradi huu wa ujenzi wa madarasa unajengwa kwa thamani
ya Sh. 68,000,000 sawa na sh. 17,000,000 kwa chumba. Mpaka sasa ujenzi umefikia hatua
za ukamilishaji (rangi, sakafu na vyumba vya usalama).
Ujenzi huu ni mpango wa kupunguza uhaba wa vyumba 10 vinavyotakiwa hapa shuleni
a) Utekelezaji:
Mkataba wa ujenzi kati ya shule na ‘local fundi’ ulifanyika mnamo tarehe 24/01/2017 na
ujenzi ulianza mara moja. Ujenzi ulitakiwa uwe umekamilika majuma matano baada ya
kusainiwa mkataba 28/02/2017). Uongozi wa shule unamshukuru Mkuu wa Wilaya,
Mkurugenzi na uongozi wa Halmashauri kwa ujumla kwa kuwaletea mradi huu. Hata hivyo
mradi ulishindwa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali lakini kubwa
ikiwa ni ucheleweshaji wa idhini ya malipo. Fundi aliomba muda wa nyongeza mpaka
tarehe 20/04/2017 ingawa bado hajaweza kukamilisha ulipaji kutokana na changamoto za
kitaalam zinazokwamisha ulipwaji wa fedha kulingana na mahitaji halisi ya kazi. Mnamo
tarehe 25/4/2017 kamati ya ujenzi ilikutana kwa dharura kujadili changamoto hizo na kuja
na mapendekezo halisi ya kuwezesha kukamilisha mradi.
- Kupitia upya BOQ ili kufanya marekebisho kulingana na hali halisi iliyojitokeza kazini
(omition or addition)
- Kupewa BOQ ya bei elekezi ili iweze kukwamua tatizo hilo.
Ujenzi utaendelea pindi mambo hayo mawili yatakapofanyiwa kazi.
Mpaka sasa ujenzi umefanyika kwa viwango vilivyowekwa na Idara ya Ujenzi.
b) Changamoto:
Changamoto tulizokutana nazo mpaka sasa ni mbili;
i) Maelezo yasiyokamilika toka idara ya ujenzi hasa katika suala la ujazaji wa gharama
katika BOQ hali ambayo imesababisa upotevu wa muda.
ii) Ucheleweshwaji wa idhini ya malipo (certificate) hali ambayo imesababisha usubufu
mkubwa na upotevu wa muda.
c) Maoni
Ushauri uliotolewa na Timu ya Mkoa ni kuwa wasimamizi (Idara ya Elimu na Uhandisi)
kufanya kazi kwa uwazi na ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo kwa wakati
na kiwango kilichokusudiwa.
1.3 MRADI WA UJENZI WA JENGO LA WAZAZI (MARTENITY BLOCK) KATA YA
MABWEPANDE.
Utangulizi
Mradi huu ulianza rasmi tarehe 04/8/2016 ukilenga kujenga Jengo la Wazazi na Hospitali
ya Kanda (Zonal Hospital) ikitarajiwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD),
wagonjwa wa kulazwa na huduma zote zitakiwazo katika ngazi ya Hospitali.
Mradi huu ulipangwa kugharamia kiasi cha Tshs. 974,997,704.40 ili kuweza
kukamilika kwa kuanza kutoa huduma zote kwa wananchi.
a) Utekelezaji
i) Ujenzi wa mradi wa Jengo la Wazazi Kata ya Mabwepande.
kwa Awamu ya kwanza umekamilika.
ii) Wakati mradi huu ukiendelea kutekelezwa, huduma zinaendelea kutolewa kwenye jengo
la zamani ambalo hutoa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) ambapo Wananchi
wapatao 19,234 kutoka sehemu mbalimbali za Kata ya Mabwepande pamoja na
wananchi waliopata mafuriko mwaka 2011-2012 hupata huduma katika Hospitali hii.
b) Changamoto.
i) Stoo ya dawa inahitajika kufanyiwa mgawanyo (partition) ili kupata chumba cha
kuhifadhi dawa na kutolea dawa.
ii) Hakuna chumba cha mapokezi na kuchukulia kadi kwa wagonjwa.
iii) Hakuna sehemu ya kupimia watoto.
iv) Hakuna “Incinerator” ya kuchomea taka
v) Ukosefu wa chumba cha kujifungulia katika jengo hili.
c) Maoni
Mradi huu ni muhimu sana, hivyo Halmashauri iukamilishe haraka ili wananchi wapate
huduma zote za afya zilizopo katika hadhi ya Hospitali
Picha Na.2: Jengo la linalojengwa la Wazazi (Martenity Block) Kata ya Mabwepande.
Picha Na.3: Sehemu ya kupandia (ramp) kwa kutumia “wheel chair” wodi ya wazazi katika Hospitali ya
Mabwepande
1.4. MRADI WA UJENZI WA WODI YA WAZAZI KATIKA ZAHANATI YA
KIJITONYAMA
Utangulizi
Zahanati ya Kijitonyama ilianza kujengwa rasmi mnamo mwaka 1978 na kuanza kutoa
huduma mwaka 1979 chini ya ufadhili wa Serikali ya Canada.
Kutokana na ongezeko la mahitaji ya huduma za Afya katika katika eneo hili, Zahanati ya
Kijitonyama ilipata mfadhili ambaye MDH (Management and Development of Health), na
alikubali kusaidia kufanya ukarabati mkubwa na upanuzi wa wodi ya jengo la wazazi
kituoni. Mradi ulianza Mwezi Machi 2016, na kukamilika mwezi Juni 2016.
Jengo hili la wazazi lina sehemu kuu tatu:-
i) Sehemu ya wajawazito kusubiri kabla ya kujifungua (Ante Natal Care)
ii) Chumba cha kujifungulia (Labour Room)
iii) Chumba cha uangalizi baada ya kujifungua (Post Natal Care)
Jengo hili la kisasa la wazazi limegharimu kiasi cha Tshs. 155,700,000 (Milioni Mia Moja
hamsini na tano na laki saba), ambapo MDH wamechangia Tsh. 120,000,000/= kwa ajili ya
ukarabati na Halmashauri imechangia Tsh. 35,700,000/= kwa ajili ya ununuzi wa vifa tiba.
Jengo lilikabidhiwa kwa Manispaa rasmi Desemba 2016. Huduma katika jengo hili lilianza
kutolewa mwezi Desemba 2016, ambapo Jumla ya wajawazito 73 wamepokelewa na
kupata huduma salama ya kujifungua pasipo na matatizo yoyote hadi sasa.
a) Utekelezaji
i) Manispaa kwa kushirikiana na wadau ina mpango wa kuiendeleza zahanati hii
kupanda hadhi na kuwa kituo cha afya (Urban Health Center)
ii) Kujenga chumba cha upasuaji ili kuweza kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa
kina mama wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
b) Changamoto
i) Hakuna tanuru yenye vigezo vinavyotakiwa ya kuchomea taka “Incinerator”
ii) Hakuna chumba cha upasuaji “Theatre”
iii) Idadi ya Vitanda kwa kinamama wajawazito havitoshi
c) Maoni
i) Manispaa wajenge tanuru ya kuchomea taka “Incinerator” kwani iliyopo haifai na
haikidhi vigezo.
ii) Kujenga chumba cha upasuaji “theatre” kwa ajili ya kusaidia upasuaji wa dharura.
iii) Kuingiza kwenye bajeti ujenzi wa Hospitali ya Kisasa kwa usanifu wa ghorofa.
Picha Na.4: ujenzi wa Wodi ya Wazai katika Zahanati ya Kijitonyama
1.4. MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI KWA WAZAZI KATIKA
HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Utangulizi
Hospitali ya Mwananyamala ilianza kama kituo cha kutolea huduma za afya ya mama na
mtoto (MCH) mwezi Julai 1973. Na kupandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Novemba, 2010. Kwa sasa Hospitali hii inahudumia wakazi wa Manispaa ya Kinondoni na
Manispaa zingine ikiwemo Manispaa ya Ubungo pamoja na wale wanaotoka Wilaya
nyingine za Tanzania. Kwa wiki wanatibu takribani wagonjwa 15,000.
Hospitali inatoa huduma za uzazi kwa akina mama kati ya 100 hadi 120 kwa siku, kati yao
akinamama 8-10 wanahitaji huduma za upasuaji wa dharura kila siku, na kwa wiki idadi ya
akinamama wanaohitaji huduma za upasuaji ni kati ya 58 hadi 60.
Jengo hili la upasuaji ni sehemu ya utatuzi wa changamoto za ufinyu wa nafasi za kulaza
wagonjwa pamoja na uchache wa vyumba vya upasuaji, lakini pia lina mazingira mazuri na
ya kisasa kwa ajili ya kutolea huduma kwa mama na watoto.
a) Utekelezaji
i) Ujenzi wa jengo umekamilika na Idara ya Afya ya Manispaa tayari imekwisha agiza
vifaa vya upasuaji kutoka Bohari Kuu ya Dawa na malipo yamekwisha fanyika
ambapo baadhi vimeletwa na vingine wanatarajia kuvipokea mwanzoni mwa mwezi
Juni, 2017. Vifaa hivi vimegharimu kiasi cha Tshs.182, 691,344/=.
ii) Ujenzi wa jengo hili umegharimu Tsh. 302,128,001/= kwa ufadhili wa GSM kupitia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda. Jengo hili linatarajia
kuanza kutumika kuanzia mwezi Juni, 2017 wakati vifaa vyote vitakapofika.
iii) Ujenzi wa jengo hili umefanyika kwa takribani miezi kumi, kuanzia tarehe 13 Machi,
2016 na kukamilika mwishoni mwa mwaka 2016 na kuzinduliwa tarehe 29 Januari,
2017.
Picha Na.5: Kibao kinachoonesha ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala
Picha Na.6: Jengo la upasuaji katika hospiatali ya Mwananyamala
b) Changamoto
i) Jengo halina viyoyozi
ii) Jengo halina Masinki ya kunawia na kufulia na kuoshea vifaa
iii) Pia hakuna makabati ya kutunzia vifaa
iv) Hakuna Meza
c) Maoni
i) Mkurugenzi ajitahidi kununua vifaa vyote ambavyo havipo katika jengo la upasuaji
(theatre).
ii) Hospitali ianzishe “fast track” kwa wagonjwa ambao wanapenda kutibiwa kwa
uchangiaji kwani inaweza kuongeza mapato ya Hospitali.
1.5 MRADI WA UJENZI WA VYUMBA 5 VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI
MZIMUNI
Utangulizi
Mradi wa ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa Shule ya Sekondari Mzimuni ni utekelezaji wa mradi
huu awamu ya pili. Mradi ulifunguliwa kwa uwekaji wa jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam ambapo wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni tarehe 10 Januari, 2016. Lengo
la mradi huu ni kuwa na Shule ya Sekondari katika Kata ya Mzimuni. Kata ya Mzimuni itaweza
kupata shule ya Sekondari ambayo itaondoa usumbufu wa Wanafunzi wanaomaliza shule za msingi
na kwenda kusoma Kata za mbali.
a) Utekelezaji
Mkataba wa ujenzi ulisainiwa mwezi Desemba, 2016 na makubaliano ya mkataba ni kuanza kazi
tarehe 06 Desemba, 2016. Ujenzi ulitarajiwa kukamilishwa tarehe 07 Aprili, 2017. Mkandarasi
aliyepewa kazi ya ujenzi ni Nyakwe Constuction kwa gharama ya Sh. 246,621,740.00. Hadi siku ya
ukaguzi fedha aliyolipwa ni Sh. 104,000,000. Ujenzi umefikia hatua ya kumimina zege katika
ghorofa ya kwanza.
b) Changamoto
Ujenzi umesimama kutokana na nyaya za umeme kupia katika eneo la ujenzi ambapo mwendelezo
wa ujenzi wa kuta utakwamishwa na nyaya hizo.
c) Maoni
i) Mwalimu Mkuu wa Shule kuwasiliana na TANESCO ili kuondoa nguzo ya umeme
inayokwamisha ujenzi.
ii) Mkurugenzi wa Halmashauri awezeshe kufanyika kwa haraka kuhamisha nguzo ya
umeme ili ujenzi uweze kuendelea
Picha Na.7: Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mzimuni iliyozinduliwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
tangu Januari, 2016.
Picha Na.8: Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mzimuni ikionesha nyaya za umeme zilizokatisha katika eneo la
ujenzi.
1.6 MRADI WA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA KINONDONI - DMDP
Utangulizi
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ni miongoni mwa Halmashauri za Manispaa tatu za
Mkoa wa Dar es Salaam zinazotekeleza Mradi wa kuboresha Miundombinu katika Jiji la Dar
es Salaam kupitia fedha za Serikali kupitia mkopo wa Benki ya Dunia ujulikanao kama “Dar
es Salaam Metropolitan Development Project – DMDP). Halmashauri za Manispaa nyingine
zinazotekeleza mradi huu wa DMDP ni Ilala na Kinondoni.
Mpango huu una maeneo makuu manne ambayo ni:
i) Ukosefu wa Miundombinu
ii) Kuinua makazi ya watu wenye vipato vidogo (upgrading in low income
communities)
iii) Kujenga uwezo (Institutional Strengthening and Capacity Building)
iv) Kusaidia usimamizi katika utekelezaji na Tathmini (Implementation Support and
Monitoriong & Evaluation)
a) Utekelezaji
Mtaalam Mshauri M/S Guff Engineering amekamilisha mapitio ya usanifu na kutengeneza
nyaraka za zabuni kwa miradi ya mafungu matatu (3 package):-
Fungu la I: Barabara za Sokoni – Makumbusho - Km. 1.45, MMK – Km. 0.9, Nzasa – Km.
1.25, Viwandani – Km. 1.68, TANESCO – Soko la Samaki – Km. 1.58.
Fungu la II: Barabara za Makanya – Km.5.1, Tandale –Kisiwa – Km 0.8, Kilimani – Km.1.3,
Simu 2000 – Km. 1.3, Kilongawima Km. 1.8 na Makumbusho CBD) – Km. 0.9.
Fungu la III: Barabara za External Km. 1,65, Kisukuru Km. 1.9, Korogwe – Kilungule – Km.
2.88, Maji ya Chumvi – Kilungule Km. 2.85.
Katika utekelezaji wa kazi hizi, fungu la kwanza ambalo halikuwa na ulipaji wa fidia
linaendelela na ujenzi, ambapo Manispaa ya Kinondoni iliingia Mkataba na Kampuni ya
Estim kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami kuanzia tarehe
18/01/2017 kwa muda wa mwaka mmoja. Kazi ambayo imefanyika ni uwekaji wa lami
barabara ya Sokoni – Makumbusho uumbaji wa tuta kwa barabara za viwandani Km. 1.68
na TANESCO Soko la Samaki Km. 1.58. Aidha, fungu la II na III linahitaji fidia.
b) Changamoto
Kuchelewa ulipaji wa fidia kwa baadhi ya nyumba ili kupisha mradi kuanza.
C) Maoni
Halmashauri kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kulipia fidia kwa maeneo ambayo mradi
unapita ili mradi uweze kuanza.
2.0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA UBUNGO .
UTANGULIZI.
Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Ubungo ulianza tarehe 03 hadi 05 Mei,
2017 ambapo jumla ya miradi 11 ilitembelewa. Ifuatayo ni taarifa ya kila mradi uliotembelewa
ikiwa inaonesha utangulizi, utekelezaji, mafanikio, changamoto na maoni.
2.1. Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Riverside – Kibangu kwa kiwango cha lami
Utangulizi.
Mradi upo katika Kata ya Ubungo Mtaa wa Kibangu. Mradi huu ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe.
John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati
alipotembelea eneo hilo na kukuta hali mbaya ya barabara katika Kata hii. Kukamilika kwa
barabara hii kutaondoa tatizo la usafiri na kuboresha miundombinu ya barabara.
a) Utekelezaji
Kipande cha barabara kilichotengenezwa kwa kiwango cha lami kina urefu Km. 1. Mradi
umekamilika kwa asilimia 100. Kiasi cha fedha kilichotengwa na kutumika ni Sh.
1,200,000,000.00 fedha ambazo ni msaada wa Mhe. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Halmashauri imetenga katika bajeti ya mwaka
2017/18 kiasi cha Sh. 600,000,000.00 kwa ajili ya kuendeleza kujenga barabara hiyo (km 0.5)
likiwa ni ombi la wananchi wa maeneo hayo.
b) Mafanikio
Kukamilika kwa mradi huu wa barabara yenye urefu wa Km 1 kumerahisisha shughuli za
usafiri na usafirishaji kwa wakazi wa maeneo ya Kibangu, Riverside, Makoka n.k. Pia usumbufu
wa kuharibikiwa na vyombo vya usafiri kwa sababu ya ubovu wa barabara umepungua.
c) Changamoto
i) Maji ya mvua yanayokusanywa kwenye mifereji iliyotengenezwa kando ya barabara
yameelekezwa kwenye makazi ya watu.
ii) Uwepo wa nyumba za wakazi kwenye eneo la barabara ambao inatarajiwa
kuendelezwa.
d) Maoni
i) Timu ya ukaguzi ilishauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuwapongeza wakazi wa
Kibangu ambao walitoa maeneo yao wakati wa kupanua barabara bila kulipwa fidia
ii) Mkurugenzi atume wataalam kufanya tathmini ya nyumba mbili kwa ajili ya kulipa fidia
ili ujenzi wa kipande cha Km 0.5 uweze kufanyika.
Picha Na.1: Ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Riverside Kibangu (1 Km) – Kata ya Ubungo
Picha Na. 2: Nyumba zinazotakiwa kufanyiwa tathmini na kulipwa fidia ili kukamilisha
ujenzi wa barabara ya (River side – Kibangu yenye urefu wa 0.5 Km)
2.2 Ujenzi wa Choo Matundu 12 Shule ya Sekondari Saranga Kata ya Saranga
Utangulizi
Katika kuimarisha suala la usafi katika Kata ya Saranga hasa kwenye shule ya sekondari
ya Saranga, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo iliazimia kujenga matundu 12 ya vyoo
yaliyogharimu kiasi cha sh. Milioni 32
a) Utekelezaji
Ujenzi wa choo hicho umekamilika lakini usanifu uliotumika ni mbovu kwa sababu vyoo
vya desin ya kuchimba shimo chini na kuta kujengwa juu, vimekuwa vikibomoka kwa
kutitia chini. Mfano wa vyoo hivi vilivyotitia vipo katika shule za msingi za
Malambamawili na Bunju ‘B’ (katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni).
b) Mafanikio
Ujenzi wa vyoo hivyo umekamilika na vinatumika.
c) Changamoto
i) Hakuna milango kwa ajili ya kuimarisha ulinzi pindi wanafunzi wanapokuwa
nyumbani
ii) Choo kimejengwa kwa usanifu ambao si salama sana kwa mipango ya muda mrefu
(Vyoo vingi vinavyojengwa kama hivi huwa vinadidimia mfano wa vyoo
vilivyobomoka ni pamoja na choo cha shule ya msingi Malambamawili (Picha Uk .
iii) Hakuna chumba cha kubadilishia nguo/pedi kwa wasichana wanapokuwa hedhi
iv) Hakuna sehemu ya kunawia mikono kwa wanafunzi baada ya kutoka chooni.
d) Maoni
i) Usanifu wa ujenzi wa vyoo ubadilishwe ili kuepusha madhara pindi choo hicho
kitakapotitia pamoja na kuokoa gharama zisizo za lazima
ii) Walimu wahusika na suala la afya na mazingira shuleni wahakikishe shule inakuwa
na vibuyu mchirizi au waige “best practice” ya shule ya msingi Kibamba, pamoja na
kuweka mazingira kwa ajili ya wanafunzi wa kike kubadilishia pedi.
Picha Na. 3.Ujenzi wa matundu 12 ya choo katika shule ya Sekondari Saranga
Picha Na. 4: Ujenzi wa matundu 12 ya choo katika shule ya Sekondari Saranga
2.3 Ujenzi vyumba 8 vya madarasa katika Shule ya Msingi Temboni
Utangulizi
Katika shule ya Msingi Temboni upo uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa. Lengo
la mradi huu wa Ujenzi vyumba 8 vya madarasa ni kupunguza msongamano wa
wanafunzi madarasani ambao wanakaa takribani 130 hadi 170 katika darasa moja.
a) Utekelezaji
Ujenzi wa vyumba vitano (5) umekamilika na ujenzi wa vyumba vitatu (3) haujaanza
mpaka wakazi wa eneo hilo walipwe fidia
b) Mafanikio
Wanafunzi wameanza kutumia vyumba vya madarasa 5 yaliyokamilika hivyo kupunguza
msongamano wa wanafuzni hadi kufikia wanafunzi 70 – 80 kwa darasa.
c) Changamoto
i) Mwinuko wa eneo la mwisho wa veranda ambao hauna vyuma vya vizuizi.
ii) Sakafu ya darasa moja haitoi maji nje kwa kutiririsha.
iii) Mbao za kuandikia baadhi haziko katika ubora unaostahili na pia Ash-board haipo.
iv) Vyoo vinajengwa kwa usanifu wa “ shimo chini Jengo juu”- vyoo hivi mara nyingi
vinaleta athari na havidumu kwa muda mrefu (Mfano choo cha shule ya msingi
Malambamawili)
d) Maoni
i) Vizuizi viwekwe ili wanafunzi wasianguke.
ii) Kuboresha sakafu na mbao za kuandikia pamoja na marekebisho mengine.
Picha Na. 5: Ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa katika shule ya Msingi Temboni
Picha Na. 6: Ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa katika shule ya Msingi Temboni
34
Picha Na. 7: Ujenzi wa matundu ya choo unaoendelea katika shule ya Msingi Temboni
Picha Na. 7: Ujenzi wa matundu ya choo unaoendelea katika shule ya Msingi Temboni
35
2.4 Ujenzi vyumba 8 vya madarasa katika Shule ya Msingi Malambamawili
Utangulizi
Kufuatia tatizo la uhaba wa madarasa katika shule msingi Malambamawili
kutokana na wingi wa wanafunzi katika eneo hilo, Halmashauri Mama ya
Manispaa ya Ubungo ambayo ni Kinondoni ilikuja na mpango wa kuanzisha
shule mpya ambapo madarasa 8 kati ya 10 yaliyopangwa kujengwa
yamekamilika. Mpango huu ulianza katika kipindi cha mwaka wa fedha
2015/16 na kukamilika mwaka 2016/17 kwa jumla ya Sh. Milioni 178. Aidha,
shule hiyo inapendekezwa kuitwa shule ya msingi Bwawani kulingana na
mazingira ya ki-jiografia ya mahali ilipo.
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika lakini madarasa hayana ‘ceilingboard’ na vyoo pia hakuna
b) Mafanikio
i) Ujenzi umekamilika na unatumika vile vile inatarajiwa kuwa shule mpya
mara baada ya taratibu za usajili zitakapokamilika. Imependekezwa iitwe
shule ya msingi Bwawani kulingana na hali ya ki-jiografia ya mahali
ilipojengwa.
ii) Kukamilika kwa madarasa hayo kumesaidia kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo wanaofikia 3,754 (Darasa la I-VII).
c) Changamoto
i) Uhaba mkubwa wa vyoo kwa kuwa Matundu 8 kati ya 12 yametitia. ii) Ceiling board hakuna na “ash chalk” haikuwekwa. iii) Hakuna sehemu ya kunawia mikono wanafunzi baada ya kutoka chooni.
d) Maoni
i) Itengwe bajeti ya choo kabla shule haijaanza. ii) Ujenzi wa vyoo uzingatie miundombinu ya wasichana waliopevuka na
walemavu
iii) Mbao za kuandikia ziwekewe “ash chalks” na madarasa hayo yawekewe
dari ili usikivu uwepo kati ya mwalimu na mwanafunzi pindi hata mvua
itakapokuwa inanyesha.
iv) Usanifu wa ujenzi wa vyoo ubadilishwe tunapendekeza ujenzi huo uwe
unatenganisha shimo na mahali vyoo vilipo (Shimo liwe mbali na jengo la
vyoo). Mfano mzuri (Best practice) ni vyoo vya shule ya msingi
Lubakaya Kata ya Msongola katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
36
Picha Na. 8: inaonesha hali halisi ya choo kilichotitia katika shule ya Msingi Malambamawili
Picha Na. 9: Mfano wa Usanifu wa ujenzi wa vyoo ukionesha jengo lenye matundu ya vyoo
kujengwa mbali na shimo (Septic tank) - katika shule ya Msingi Lubakaya- Ilala
37
Picha Na. 10: Ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa katika shule ya Msingi Malambamawili
2.5 Ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo
Utangulizi
Kuanzishwa kwa maeneo mapya ya kiutawala kumeupa msukumo mkoa
wa Dar es Salaam kufanya jitihada za kupata maeneo kwa ajili ya ujenzi
wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya. Hivyo, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
imekwishatwaa eneo Mbezi Ruguruni kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ili kurahisisha shughuli za kiutendaji na pia kuepusha gharama
za kupanga/ kukodi ofisi zinazofanyika sasa.
a) Utekelezaji
i) Eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 3,509 limepatikana lakini ujenzi
bado haujaanza
ii) Eneo hilo lipo Mbezi Ruguruni Block (A) 341.
iii) Yamefanyika maandalizi ya Hati kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa gharama za Sh. 480,000.
b) Mafanikio
i) Kutwaa eneo na kulipa fidia kwa wakazi.
ii) Kuna fedha kiasi cha Sh. Milioni 500 zimekwishapatikana kwa ajili ya
kuanza hatua za awali za ujenzi.
38
c) Changamoto
Wananchi kuendelea kuwepo katika eneo la mradi licha ya kuwa fidia
walikwishalipwa.
d) Maoni
i) Halmashauri ihakikishe wananchi waliolipwa fidia wanapewa taarifa
mapema waondoke kabla ujenzi haujaanza ili kuondoa usumbufu.
ii) Fedha zilizokwishapatikana zitumike kwa shughuli iliyopangwa na
thamani yake ionekane.
Picha Na. 11: inaonesha ramani (Hati) ya eneo ambalo Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo itajengwa
39
Picha Na. 12: inaonesha mkazi aliyelipwa fidia katika eneo ambalo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo lakini
bado hajapewa taarifa ya kuondoka.
2.6 Ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo
Utangulizi
Uhitaji wa kujenga Ofisi za Wakurugenzi kwa lengo la kusogeza huduma
kwa jamii kumefuatia baada ya kuanzishwa kwa maeneo mapya ya
kiutawala katika Mkoa wa Dar es Salaam. Ili kutekeleza azma hiyo
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imefanikiwa kutwaa ardhi yenye
ukubwa wa Hekta 1.64 sawa na ekari 4 ambayo imekwishapimwa na
uondoshwaji wa vichaka katika eneo hilo umefanyika. Eneo hilo lipo katika
Kitalu Na.1 (A) 348. Mbezi Luguluni.
a) Utekelezaji
Eneo limepatikana lakini ujenzi bado haujaanza
b) Mafanikio
i) Eneo limepatikana kwenye Kitalu Na.1 (A) 348, na limekwishapimwa
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
ii) Maandalizi ya hati yamefanyika kwa gharama za sh. milioni 1.9
iii) Zoezi la kuondoa vichaka katika eneo la mradi limefanyika.
iv) Halmashauri kufanikiwa kutenga kiasi cha Sh. billion 2 kwa bajeti ya
mwaka 2017/18 kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo kati ya hizo Sh. bilioni
40
1.2 zinatokana na mapato ya ndani na Sh. milioni 800 ni za Ruzuku
kutoka Serikali Kuu.
c) Changamoto
Kuchelewa kupata hati kwa kuwa utaratibu wa ujenzi hauwezi kuanza
kabla ya kupata hati.
d) Maoni
Kwa kuwa Hati imekwishapatikana Mkurugenzi ahakikishe Michoro ya
ujenzi inapatikana haraka ili ujenzi uanze kwa sababu kukamilika kwa
Mradi huu, kutasaidia kuimarisha utendaji kazi wa Watumishi katika kutoa
huduma kwa jamii pamoja na kuokoa gharama kubwa zinazotumika sasa
hivi kwa kukodi/kupanga ofisi.
2.7 Ujenzi vyumba 3 vya madarasa katika Shule ya Msingi Msakuzi
Utangulizi
Katika kuongeza miundombinu ya kusomea na kupunguza tatizo la uhaba wa
vyumba vya madarasa, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeendelea na
ufuatiliaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali
(zilizoanzishwa na Halmashauri ya Kinondoni) ikiwemo hii ya Msakuzi. Ujenzi
huo ulianza katika mwaka wa fedha 2015/16 na kukamilika mwaka 2016/17
na umegharimu kiasi cha Sh. milioni 63.
a) Utekelezaji
Mradi umekamilika na umekabidhiwa kwa Mkurugenzi tarehe 04/04/2017 na
Mkandarasi aliyejenga ni M/S Kachima Limited
b) mafanikio
i) Kukamilika kwa madarasa hayo kumesaidia kupunguza msongamano wa
wanafunzi 829 waliokuwa wanatumia vyumba vinne (4) tu vya madarasa.
ii) Kukamilika kwa mradi huo kumewezesha shule kuwa na vyumba saba (7)
vya madarasa.
iii) Wanafunzi wa masomo ya awali nao wamepata darasa la kujifunzia.
c) Changamoto
i) Mradi hauridhishi kwa kuwa una mapungufu mengi ikiwemo rangi
iliyopakwa ukutani ikiguswa inafutika,
ii) Madirisha hayana nyavu kwa ajili ya ulinzi
iii) Sakafu iliyowekwa haiko kwenye kiwango kinachotakiwa, iliyowekwa ni
rafu na siyo ya kioo
iv) Sehemu ya kuwekea chaki (Ashboard) katika mbao haipo
41
v) Choo chenye jumla ya matundu 12 kinachotumika ni chakavu hasa
sehemu ya velanda
vi) Hakuna huduma ya kunawa mikono wanafunzi wanapotoka chooni.
d) Maoni
Halmashauri ihakikishe Mkandarasi kabla hajamalizia kasoro zilizojitokeza asilipwe fedha zake za “rentantion”, malipo yafanyike baada ya kukamilisha kazi.
Picha Na. 13: Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya Msingi Msakuzi
2.8 Ujenzi wa vyumba sita (6) na kimoja cha walimu wa shule ya
Sekondari Matosa
Utangulizi
Madarasa hayo yamejengwa kwa lengo lile lile la kukabiliana na uhaba wa
vyumba vya madarasa. Ujenzi huu wa kama ilivyo miradi mingi katika
Halmashauri ya Ubungo ilianzishwa na Halmashauri mama ya Kinondoni.
Ujenzi huu uligharimu kiasi cha Sh. milioni 150 kikiwa kimehusisha ujenzi wa
chumba kimoja ambacho kitatumika kama ofisi ya walimu.
a) Utekelezaji
42
Ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa umekamilika (kwa mujibu wa
Mkandarasi wa Halmashauri) kwa sababu siku hiyo ya Ukaguzi timu ya Mkoa
haikuweza kufika katika eneo la mradi kutokana na changamoto ya barabara
kuharibiwa na mvua.
b) Mafanikio
Wanafunzi kupata madarasa ya kujifunzia
c) Changamoto
Kutokana na changamoto ya barabara, timu ya ukaguzi haikuweza kufika
kuona hali halisi ya ujenzi wa nyumba hiyo.
d) Maoni
i) Miundombinu ya barabara hiyo iboreshwe ili iwe inapitika hata kipindi cha
mvua
ii) Halmashauri ipitie maoni yaliyotolewa kwenye kaguzi zingine za miradi ya
shule ili kuona kama na shule hiyo ya Matosa ina mapungufu ya namna
hiyo, na endapo yatakuwepo basi yafanyiwe kazi.
iii) Timu ya Mkoa itahakikisha inatoa kipaumbele kwa kufanya ukaguzi
kwenye miradi ambayo haikuweza kukaguliwa kwa kipindi hiki kutokana
na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.
2.9 Mradi wa Soko la Mabibo (Mahakama ya ndizi) Kata ya Mabibo
Utangulizi
Soko la Mabibo linalojulikana kwa jina la “Mahakama ya ndizi” lililopo katika
Kata ya Mabibo kwa muda mrefu limekuwa likisimamiwa na Kampuni binafsi
ya “Maji moto” kabla ya Wilaya ya Ubungo haijaanzishwa. Hata hivyo, wazo
la kutaka soko hilo lisimamiwe na Serikali lilikuja baada ya kuanzishwa kwa
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambapo kwa uongozi wao kupitia kwa
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo (Mh. Hamphrey Polepole ambaye kwa sasa ni
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Taifa) ulifanya
juhudi ambazo zilisaidia soko hilo kuwa chini ya usimamizi wa Manispaa. Vile
vile umiliki wa eneo la soko hilo haujawa chini ya Manispaa kwa sababu eneo
hili ni la Kiwanda cha nguo cha Urafiki. Hapo awali Halmashauri ilikuwa
ikipata takribani kiasi cha sh. milioni 3 kama mapato yanayotokana na soko
hili kila mwezi tofauti na sasa hivi pato la mwezi ni kati ya Sh. Milioni 70-80
kwa mwezi.
43
a) Utekelezaji
Juhudi zilizofanyika ni pamoja na kuhakikisha Soko linasimamiwa na
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jambo ambalo limefanikiwa.
b) Mafanikio
i) Kufanikiwa kudhibiti suala la upotevu wa mapato
ii) Kuongeza mapato ya Halmashauri kutoka wastani wa shilingi milioni 3
hadi shilingi milioni 70 au 80 kwa mwezi.
iii) Kufanikiwa kusisitiza matumizi ya mashine za ki-ilektroniki katika
kukusanya mapato
c) Changamoto
i) Bado eneo la soko lipo kwenye umiliki wa kiwanda cha nguo cha Urafiki.
ii) Miundombinu ya soko hilo ni mibovu mfano kipindi cha mvua kunakuwa
na matope hali inayosababisha kuongezeka kwa uchafu na hivyo
kutowavutia wateja.
iii) Maji bado ni kero kwa kuwa eneo hili linahitaji maji kwa ajili ya kuimarisha
hali ya usafi
d) Maoni
i) Miundombinu ya soko hilo iboreshwe ili kuongeza tija kwa watumiaji kwa
vipindi vyote vya misimu ya mwaka.
ii) Wakati Mkoa unachukua wazo la kufanya mazungumzo na uongozi wa
Kiwanda cha Urafiki, pia Halmashauri ihakikishe inamkumbusha suala hilo
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mh. Hamphrey
Polepole kwa kuwa aliahidi kufuatilia suala hili hata baada ya kupewa
Wadhifa huo wa ngazi ya Kitaifa.
iii) Halmashauri isijihusishe na masuala ya kamati za masoko kwa sababu
zimekuwa ndicho chanzo cha migogoro, rushwa na hata ubadhilifu wa
mapato.
44
Picha Na. 14: inaonesha hali halisi ya miundombinu katika soko la Mabibo (Mahakama ya ndizi)
2.10 Ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa katika Shule ya Msingi
Kawawa
Utangulizi
Shule ya msingi Kawawa ina jumla ya wanafunzi wapatao 3,000 ambao wamekuwa wakisoma kwa shida sana kutokana na uchache wa vyumba vya madarasa. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilipanga kujenga madarasa 5 ili kupunguza kero hiyo. Hata hivyo, kuanzishwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kumesaidia kusimamia kwa ukaribu miradi iliyoanzishwa na Halmashauri ya Kinondoni ambayo sasa imo ndani ya Manispaa ya Ubungo ukimwemo mradi huu wa madarasa 5. Ujenzi wa madarasa hayo ulijengwa na Local fundi kwa gharama ya sh. Milioni 85. Mradi ulianzishwa kipindi cha bajeti ya mwaka 2015/2016 na kukamilika mwaka 2016/17.
a) Utekelezaji Maradasa manne (4) kati ya matano (5) yaliyokuwepo kwenye mpango yamekamilika na yanaridhisha.
b) Mafanikio Kukamilika kwa vyumba 4 vya madarasa kumesaidia wanafunzi kupata mahali pa kusomea na hivyo kupunguza msongamano madarasani
c) Changamoto Mapungufu yaliyopo ni kutokuwepo kwa wavu ‘wire mesh’ madirishani na ‘Ashboard’
d) Maoni
Mapungufu yaliyojitokeza yanatakiwa yarekebishwe haraka kabla tatizo
halijawa kubwa
45
Picha Na. 15: inaonesha ujenzi vyumba 5 vya madarasa katika shule ya Msingi Kawawa
2.11 Ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa shule ya Msingi
Kibamba
Utangulizi
Shule ya msingi Kibamba ipo katika Kata ya Kibamba katika Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo. Ujenzi wa madarasa 2 shule ya hiyo ni
mwendelezo wa juhudi za kukabiliana na tatizo la uhaba wa madarasa ili
kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira stahiki. Mradi huu wa
madarasa mawili (2) ulianza kipindi cha mwaka 2015/16 na kukamilika
kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 kwa kutumia mapato ya ndani ya
Halmashauri.
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na jumla ya sh. milioni 34 zilitumika kwa ujenzi huo.
b) Mafanikio
Vyumba hivyo vya madarasa vimesaidia kupunguza msongamano wa
wanafuzi japo si kwa kiwango kinachotakiwa.
c) Changamoto
i) Kuna mapungufu ya paa pamoja na sakafu kutokuwa imara.
ii) Ofisi ya walimu iliyojengwa kwa nguvu za kamati ya shule na walimu
haijakamilika kwa kuwa haina choo.
d) Maoni
i) Mapungufu yaliyojitokeza yarekekebishwe.
ii) Maelekezo yametolewa kuwa ofisi ikamilishwe kwa kutumia fedha za
Malipo ya Halmashauri.
46
Picha Na. 16: inaonesha ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya Msingi Kibamba
Picha Na. 17: inaonesha vibuyu chirizi na hatua za kunawa mikono baada ya kutoka chooni
katika shule ya Msingi Kibamba.
47
4.0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
MANISPAA YA ILALA
UTANGULIZI
Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Ilala ulianza tarehe 09 hadi 11
Mei, 2017. Hata hivyo, pamoja na miradi 12 iliyopendekezwa na Halmashauri kuikagua,
Sekretarieti ya Mkoa ilipendekeza mradi mwingine wa ujenzi wa shule ya msingi
Magorofani iliyopo Gongo la Mboto Jeshini na hivyo kufanya jumla ya miradi
iliyokaguliwa kufikia 13. Ifuatayo ni taarifa ya kila mradi uliotembelewa ikiwa inaonesha
mafanikio, changamoto na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo.
4.1 Ujenzi wa Shule Mpya ya Yangeyange (Vyumba 10 vya Madarasa na
Matundu 10 Ya Vyoo)
Utangulizi
Shule ya Msingi Yangeyange ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na
tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa. Mradi huo unahusisha pia
ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kwa gharama ya Sh. Milioni 190 ambazo ni
fedha za ndani za Halmashauri.
a) Utekelezaji
Ujenzi wa vyumba 8 umekamilika chini ya usimamizi wa uongozi wa shule ya
msingi Msongola na ujenzi wa vyumba 2 upo katika hatua za awali za
mandalizi.
b) Mafanikio
Kukamilika kwa ujenzi wa madarasa 8 ya shule hiyo kumesaidia sana
wanafunzi wengi kupata mahali pa kujifunzia ikiwa ni pamoja na kuipunguzia
mzigo shule ya msingi ya Msongola. Hadi sasa mradi unahudumia wanafunzi
1,544 wa darasa la I-VI, na walimu wapo 23. Pia shule ilipata msaada wa
kuchimbiwa kisima cha maji kwa ufadhili wa Ubalozi wa Kuwait.
c) Changamoto
Pamoja na mafanikio hayo pia kuna kasoro zifuatazo katika shule hiyo:- i) Sakafu imeonekana kutokuwa imara kwani imeanza kulika. ii) Huduma ya kunawa mikono haitoshelezi kwani lipo ‘sink’ moja tu la
kunawia mikono wakati wanafunzi wanapotoka chooni. iii) Hakuna chumba maalum cha kubadilishia nguo/pedi wasichana hasa wale
waliokwisha vunja ungo. iv) Eneo la shule lipo katika hatari ya kuvamiwa na majirani, eneo lipimwe na
kuwekewa mipaka v) Mbao za kufundishia ni ndogo na hazina ‘ash board’.
48
vi) Usimamizi wa ujenzi wa mradi huo ulikuwa si wa kuridhisha.
d) Maoni
i) Mapungufu yaliyoonekana yafanyiwe kazi haraka kabla tatizo halijawa
kubwa ili kuepusha gharama za ziada za ukarabati.
ii) Wahandisi wafuatilie utekelezaji unaofanyika mashuleni
iii) Kuwe na mawasiliano baina ya Idara ya Mipango na Uhandisi ili kujua
fedha zinazotengwa kwenye miradi ya shule
iv) Maafisa elimu wa Manispaa wahakikishe Walimu wa shule hiyo
wanazingatia suala la usafi shuleni hapo ikiwa ni pamoja na uwekaji wa
vibuyu chirizi kwa ajili ya kunawia mikono wanafunzi ili kuepuka
magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara na kipindupindu.
Picha Na. 1: Moja ya jengo la vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Yangeyange.
49
Picha Na. 2: Choo chenye matundu 10 kilichojengwa katika shule ya msingi Yangeyange
4.2 Ujenzi wa Shule ya Msingi Ukonga (Magorofani) Utangulizi Mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Magorofani ulianzishwa ili kuweza
kukabililiana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya
msingi Gongo la Mboto Jeshini. Ujenzi huo uligharimu jumla ya Sh. Milioni
323.
a) Utekelezaji
Madarasa yamekamilika na yalianza kutumika kuanzia mwezi Januari, 2017
ambapo hadi sasa jumla ya wanafunzi 1,583 wa darasa la I-VII wanayatumia.
Awali wanafunzi hao walikuwa katika shule nyingine ya Gongo la Mboto
Jeshini. Aidha, katika shule hiyo kuna kisima cha maji ambacho kinasaidia
kuyafanya mazingira ya shule hiyo kuwa mazuri.
b) Mafanikio
Mradi unaridhisha na ulianza kutumika kuanzia Januari, 2017 hadi sasa kuna
jumla ya wanafunzi 1,583 wa darasa la I-VII.
Pia kuna kisima cha maji ambacho kinasaidia kuweka mazingira ya shule kuwa mazuri.
c) Changamoto i) Kuna kasoro ndogo ndogo tu za kiujenzi kama vile mwinuko mkukwa
kwenye kingo za madarasa ambazo zinaweza kusababisha wanafunzi
kuanguka
ii) Mbao za kufundishia hazina kiwekeo cha chaki “ash board”
50
d) Maoni
Sehemu zilizoinuka ziwekewe kingo za kuzuia wanafunzi/walimu kuanguka
pamoja na kuweka “ash board” kwenye madarasa yasiyonazo.
Picha Na. 4: Sehemu ya baraza la shule ya msingi magorofani ambayo imeinuka kupita kiasi
51
Picha Na. 5: Vyumba vya madarasa vilivyojengwa katika shule ya msingi Magorofani
4.3 Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Chanika
a) Utangulizi
Ujenzi wa Hospitali ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya cha Chanika katika
kata ya Chanika unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea Kusini
kupitia Shirika la Koica. Mradi huo unahusisha ujenzi wa wodi zenye vitanda 160
ikiwemo antenatal (kabla ya kujifungua), labour ward (chumba cha kujifungulia),
postnatal (baada ya kujifungua) vyumba vya upasuaji viwili, vyumba vya
uangalizi maalum vitatu (intensive care units), chumba cha uangalizi wa watoto
(neonatal care room) vyumba kwa ajili ya uchunguzi na vipimo mbali mbali vya X
ray, ultra sound na maabara. Sambamba na hilo, kuna ujenzi wa nyumba za
watumishi 12 katika jengo ghorofa 3 ambapo watakaa watumishi muhimu
wanaohitajika muda wote katika kutoa huduma, kutakuwa na ununuzi wa gari la
wagonjwa (Ambulance) ili kuimarisha huduma ya rufaa kwa wagonjwa. Ujenzi
wa Mradi ulianza mwezi wa Februari 2016 na unakabidhiwa June 2017 na mradi
una thamani ya shillingi Billioni 8.8
b) Utekelezaji
i) Ujenzi wa Hospitali umekamilika kwa asilimia 96%, ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa majengo na kuweka sakafu, kuunganisha mifumo ya umeme,
maji safi na maji taka pia kazi ya ufungaji wa vifaa tiba ikiwemo x-ray,
ultra sound, vifaa vya maabara, theatre, mashine za kufua na masinki ya
vyoo. Aidha, ununuzi wa samani za Hospitali kama meza, kabati, na viti
52
unaendelea. Pia kazi ya kusafisha na kuweka sakafu eneo la maegesho ya
magari inaendelea.
ii) Ujenzi wa nyumba 12 za watumishi katika jengo la ghorofa la sakafu 3
umekamilika na ununuzi wa samani za nyumba unaendelea.
c) Mafanikio:
i) Kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia sana kutoa huduma za afya kwa
akina Mama na Watoto waliopo maeneo ya jirani na kata ya Chanika na
hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiasi kikubwa.
ii) Hospitali hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa akina mama
wanaokwenda kupata huduma za afya katika hospitali zingine za Mkoa wa
Dar es Salaam hasa katika hospitali ya Amana.
iii) Huduma za upasuaji zitafanyika kwa wakati hivyo kupunguza maumivu na
vifo vilivyokuwa vinatokea kwa wajawazito na watoto wenye matatizo
iv) kutoa huduma katika mazingira bora na vifaa bora kutaongeza ari na
motisha kwa watoa huduma hivyo kuleta ufanisi na maboresho katika
huduma
v) Halmashauri imekwishapata eneo kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho ya
Magari na fidia tayari imekwishalipwa.
d) Changamoto
i) Kuna ufinyu wa eneo la kuegeshea magari na kukosekana kwa uzio
ii) Samani za hospitali hiyo hazijakamilika ili ianze kutoa huduma.
e) Maoni
i) Halmashauri iweke mpango wa kujenga uzio pamoja na kuharakisha zoezi
la ununuzi wa samani za hospitali hiyo ili huduma zianze kutolewa.
ii) Pia Halmashauri ijenge maeneo ya maegesho ya magari kwenye eneo
lililokwishapatikana.
53
.
Picha Na. 8: Katibu Tawala wa Mkoa akikagua jinsi vifaa vya Hospitali ya Mama na Mtoto-Chanika
vinavyofanya kazi.
Picha Na.6: Eneo mojawapo la wazi
(Corridow) katika hospitali ya
‘Mama na Mtoto Chanika’
Picha Na. 7: Hiki ni chumba mojawapo cha kuhudumia
wagonjwa/wajawazito
54
Picha Na. 11: Hili ni Wodi litakalotumika kuwalaza wagonjwa (Mama na Mtoto) katika Hospitali ya
Chanika.
Picha Na. 9: Hiki ni moja kati ya vifaa
ambavyo vitatumika kutoa huduma
maalumu kwa watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati “Pre-mature babies”
Picha Na. 10: Hii ni moja kati sehemu ambazo
mgonjwa anafanyiwa uchunguzi kwa njia za kisasa
55
4.4 Ujenzi wa Vyumba 10 vya Madarasa Ya Shule Ya Msingi Mafanikio
Utangulizi
Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mafanikio ulianza
kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na kukamilika 2016/2017 lengo likiwa
la kukabiliana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika
Halmashauri.
a) Utekelezaji
Jumla ya vyumba vya madarasa 10 vimekamilika na vimegharimu kiasi
cha Sh. Milioni 210.
b) Mafanikio:
Mradi unatumika na unawahudumia wanafunzi 1,208 kuanzia darasa la I-
VII na kuna walimu 15.
c) Changamoto
i) Kuna mgogoro wa ardhi na hivyo inahitajika fidia kwa baadhi ya
watu/majirani.
ii) Mapungufu ya ubao wa kufundishia (ash board, na ubao kuwa mdogo) na
sakafu siyo imara
iii) Kutokuwepo huduma ya umeme kwa ajili ya kusukuma maji.
d) Maoni
i) Kupima ardhi na kutoa fidia zinazohitajika.
ii) Kufuatilia umeme ili utumike katika huduma mbalimbali shuleni.
iii) Kufanya maboresho ya mbao za kufundishia.
56
Picha Na.12: inaonesha jengo mojawapo la vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi
Mafanikio
4.5 Ujenzi wa Mradi na Usambazaji wa Maji Pugu- Bangulo
Utangulizi
Ujenzi wa Mradi wa maji Pugu- Bangulo ulianza 1/08/2015 na kukamilika
8/05/2017. Mkandarasi aliyejenga mradi huo ni MS Gwantwa Contractors Ltd.
Mradi huo haukukamilika mapema kwasababu ya umeme kuchelewa
kuunganishwa katika eneo la mradi.
a) Utekelezaji
Mradi umekamilika ingawaje bado kuna mapungufu ya rangi ya nyumba ya
pampu ambayo yanahitaji marekebisho. Mradi umegharimu kiasi cha Sh.
152,929,000.00
57
b) Mafanikio
Kukamilika kwa mradi huu kunanufaisha wananchi wapatao 1,800 wa Mtaa
wa Pugu-Bangulo kupata maji safi na salama kwa wastani wa kuchota ndoo 3
za lita 20 kwa siku.
c) Changamoto
i) Mradi ulichelewa kwa umeme kukamilika kwa sababu ya kuchelewa
kuunganishiwa umeme kutoka TANESCO,
ii) Kusimamishwa kwa ujenzi wa nyumba ya kuwashia pampu ya maji “Pump
House”na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwa eneo hilo ni la Wizara
hiyo.
iii) Rangi iliyotumika kwenye uzio wa ‘pump house’ haina kiwango cha
kuridhisha. Aidha rangi haiendani na rangi inayotumika katika masuala ya
maji ambayo ni blue na nyeupe
d) Maoni
i) Changamoto ya umeme na kibali cha kuomba eneo la nyumba ya pampu
zilikwishatatuliwa
ii) Rangi irudiwe (ibadilishwe) na pia pawepo na mipango ya kupata nishati
mbadala kama vile jenereta ili wananchi wasikose huduma hiyo muhimu
pindi umeme wa TANESCO unapokatika.
iii) Kuwepo na kamati ya maji ili kuufanya mradi uwe endelevu.
Picha Na. 13: Marekebisho ya ukuta/uzio wa ‘pump house’ katika kisima cha maji Pugu-Bangulo
58
Picha Na. 14: Tanki la maji la ujazo wa lita 50,000 eneo la Pugu-Bangulo katika Kata ya Pugu.
4.6 Matengenezo ya Barabara ya Mombasa Moshi- Bar kwa Kiwango
cha Lami
Utangulizi
Matengenezo ya barabara hii yalifanyika mahsusi kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wakazi wa Majohe, Kipunguni, Kivule na maeneo mengine ya jimbo la Ukonga kuingia barabara kuu ya Pugu. Mradi huu ulianza 22/02/2016 na kukamilika 21/01/2017.
a) Utekelezaji
Mradi haujakamilika kwa sababu bado vituo vya kupakilia na kushushia abiria
“Bus bays” havijakamilika
59
b) Mafanikio
Kukamilika kwa barabara hii kumerahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wakazi wa Majohe, Kipunguni, Kivule na maeneo mengine ya Jimbo la Ukonga kuingia barabara kuu ya Pugu
c) Changamoto
i) Kuchelewa kuondoa miundombinu ya mawasiliano (nguzo za simu na umeme),
mabomba ya maji na ndani ya eneo la mradi.
ii) Uhamishwaji wa miundombinu hiyo ulihitaji gharama ambazo hazikutengwa na
Halmashauri
iii) Hakuna vituo vya kushushia/kupakilia abiria “Bus Bays”
d) Maoni
i) Ni vyema kuwe na upembuzi yakinifu kwanza kabla ya mradi kuanza ili
kuondoa tatizo la kazi za ziada “additional works.”
ii) Wahandisi wametakiwa kuhakikisha “Bus Bays” zinajengwa haraka.
60
Picha Na. 15 : Hii ni barabara ya Mombasa –Moshibar
iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Picha Na. 16: Mfereji wa maji ya mvua uliojengwa kwenye
barabara ya Mombasa-Moshibar
61
4.7 UJENZI WA VYUMBA 5 VYA MADARASA –KIMANGA SEKONDARI
Utangulizi
Uamuzi wa kujenga vyumba 5 vya madarasa ni juhudi za Halmashauri katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa. Mradi huo ulienda sambamba na ujenzi wa matundu 27 ya vyoo na Mjenzi ni ‘Local Fundi’ na gharama za mradi ni Sh. Milioni 120.
a) Utekelezaji
Ujenzi wa vyumba vya madarasa 5 pamoja na samani tayari vimekamilika
ispokuwa vyoo vipo kwenye hatua ya umaliziaji.
b) Mafanikio
Shule inatarajiwa kuchukua wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza kutoka
katika shule waliyokuwa wanasoma kwa muda. Mradi unatarajiwa
kukamilishwa tarehe 28/5/2017. Viti na meza 200 vipo tayari kwa ajili ya
wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na shule hiyo.
c) Changamoto
i) Ubao wa kuandikia kutokuwa na urefu wa kutosha pamoja na ‘Ash board’ ii) Hakuna nyumba ya Mkuu wa shule atakayeteuliwa ikizingatiwa kuwa ni
shule mpya. iii) Shule bado haina hati – hiyo iliyopo ni ya Bodi ya Wakandarasi iv) Vyoo havijakamilika
d) Maoni
Halmashauri ifanye yafuatayo:- i) Maboresho ya ubao, ukamilishaji wa vyoo, kufanya tathmini ya nyumba
iliyopo shuleni kwa ajili ya makazi ya atakayekuwa Mkuu wa shule , au endapo ukarabati utakuwa na gharama kubwa, ushauri ni kuijenga upya
ii) Kufuatilia hati ya kiwanja kutoka bodi ya wakandarasi na kuibadilisha.
62
Picha Na. 17: Huu ni mwonekano wa Jengo la vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari
Kimanga
4.8 UJENZI WA BARABARA YA TABATA ST. MARY’S KWA KIWANGO
CHA LAMI
Utangulizi
Ujenzi wa barabara hii ya Tabata St.Mary’s ni marudio ya ujenzi wa awali
ambao haukuwa imara na hivyo kusababisha barabara hiyo kutodumu
kwa muda mrefu kwa sababu ya kukosa usimamizi thabiti. Mradi huu
ulianza tarehe 28/11/2012 na kukamilika tarehe 13/03/2017 na
umetekelezwa kwa muda mrefu kutokana na sababu iliyoelezwa.
a) Utekelezaji
Matengenezo ya barabara hiyo yamekamilika kwa kiwango cha zege na
lami ngumu pia ujenzi umehusisha Culvert pamoja na mifereji ya
kuondolea maji ya mvua.
b) Mafanikio
Kuimarika kwa miundombinu ya barabara ili kurahisisha shughuli za usafiri
na usafirishaji kwa wakazi wa Tabata, Segerea, Kisukuru na maeneo
mengine kuingia barabara ya Mandela.
63
c) Changamoto
i) Kuna changamoto ya mifereji kuziba kutokana na uchafu pamoja na nyasi zilizoota ndani na pembezoni mwa mifereji hiyo
ii) Road shoulder hazijawekewa lami, zimebaki udongo hivyo kuweza kuchimbika kwa sababu ya maji ya mvua.
d) Maoni
i) Halmashauri kwa kutumia sheria ndogo ndogo (by-laws) za usafi inatakiwa iwahamasishe viongozi wa Serikali za Mitaa kuhimiza suala la usafi katika maeneo hayo
ii) Mkandarasi aweke lami katika road shoulder kama ilivyo katika mkataba
Picha Na. 19: Barabara ya Tabata St. Mary’s iliyojengwa
kwa kiwango cha lami
Picha Na. 18: Nyasi zilizoota kwenye
Mfereji wa maji katika barabara ya
Tabata St. Mary’s
64
4.9 Matengenezo ya barabara ya Vingunguti –Barakuda kwa kiwango
cha lami
Utangulizi
Kama ilivyo kwa barabara ya Tabata St.Mary’s, barabara hii ya Vingunguti –Barakuda imerudiwa baada ya ujenzi wa awali kutokuwa wa ufanisi. Ujenzi huo awali ulitekelezwa na Mkandarasi Patty Enterplan Ltd na baadaye alisimamishwa na akapewa Mkandarasi Del Monte (T) Ltd.
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na gharama za mradi zilikuwa Sh. 1,478,757,133.33 na mpaka mradi unakamilika kiasi cha Sh. 1,333,421,118.00 kilitumika.
b) Mafanikio
Kuimarisha miundombinu ya barabara ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wananchi na vilevile kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu ya Nyerere kwa Wakazi wa Segerea, Tabata, Kimara, Mbezi na sehemu zinginezo.
c) Changamoto
Kiwango cha maji ya ardhini (under ground water table) katika eneo hilo kuwa juu. Hali hiyo ilisababisha barabara hiyo kuharibika mapema baada ya Mkandarasi wa mwanzo kumaliza kazi yake.
d) Maoni
i) Halmashauri ione umuhimu wa kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study) kabla ujenzi haujafanyika pamoja na kuwa na Washauri katika ujenzi.
ii) Usanifu ‘Design” uliotumika kujenga mahali pengine ukafanikiwa usitumike kila mahali bila kufanya upembuzi yakinifu kwa kuwa hali ya ki-jiografia hutofautiana kutoka eneo moja na jingine.
65
Picha Na. 20: Ujenzi wa barabara ya Vingunguti – Barakuda kwa kiwango cha lami.
4.10 Ujenzi wa Culvert–Barabaray Kinyerezi- Bonyokwa.
Utangulizi:
Mradi huu wa Ujenzi wa Culvert katika barabara ya Kinyerezi- Bonyokwa ulianza tarehe 18/03/2015 na kukamilika 02/02/2017.Ucheleweshwaji wa kukamilika kwa ujenzi huo ni kutokana na TANROADS kuchelewa kutoa michoro, na vile vile vifaa vya ujenzi kutoka kwa Mkandarasi M/S Engineering & Construction Co. Ltd vilicheleweshwa.
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na unatumika pia ujenzi umehusisha (box culvert) daraja la chuma lenye uwezo wa kuhimili uzito wa tani 7
66
b) Mafanikio
Kuimarisha miundombinu ya barabara kumesaidia kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji hasa kwa wakazi wa Kinyerezi, Bonyokwa, Kimara, Mbezi na sehemu nyingine
c) Changamoto
i) Wizi wa sehemu za vyuma vilivyounganishwa katika daraja hilo
ii) Magari yasiyotakiwa (yenye zaidi ya uzito wa tani 7) kupita katika daraja
hilo.
d) Maoni
i) Pawepo na usimamizi madhubuti pamoja kutoa elimu kwa wakazi wa eneo
hilo juu ya umuhimu wa daraja hilo
ii) Kutoza faini kwa watakaothubutu kupitisha magari na mitambo yoyote
isiyoruhusiwa kisheria.
Picha Na. 21: Hii ni alama inayoonesha uzito
sahihi wa magari yanayotakiwa kupita
katika daraja la Kinyerezi-Bonyokwa
Picha Na. 22: Hili ni box culvert
(daraja la chuma) barabara ya
Kinyerezi -Bonyokwa
67
4.11 Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi (Madarasa 16) Lubakaya na
Matundu 31 ya Vyoo
Utangulizi
Kimsingi shule ya msingi Lubakaya ilianzishwa kwa lengo la kuimarisha
miundombinu ya sekta ya elimu katika Kata ya Msongola. Ujenzi huo
ulianza na kukamilika ndani ya kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.
Ujenzi huo ulienda sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo 31 ambapo
mradi wote uligharimu kiasi cha sh. Milioni 374. Kati ya madarasa hayo
16, madarasa 8 yalijengwa kwa Mpango wa Performance for Results (P4R)
na 8 yalijengwa kwa fedha za makusanyo ya ndani ya Halmashauri.
a) Utekelezaji
Ujenzi wa mradi huu umekamilika ukiwa umetekelezwa na Local Fundi’s –
wanaounda umoja wao unaoitwa (Kijiji Construction).
b) Mafanikio
i) Kukamilika kwa shule hiyo kumeimarisha miundombinu ya Sekta ya Elimu pamoja na kuwawezesha wanafunzi wapatao 1,316 kupata madarasa ya kusomea, na hivyo kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Msongola.
ii) Vyoo vilivyojengwa katika shule hiyo vinaridhisha kwa sababu vimejengwa kwa usanifu kuchimba shimo pembeni na jengo.
c) Changamoto
i) Shule haina maji kwa sababu ya kukosa umeme licha ya kuwa ilipata msaada wa kisima kutoka kwa Wafadhili wa Kuwait. Hali hii inapelekea wanafunzi wa shule hiyo kuja na maji yao kutoka kwenye makazi yao bila kujua hali halisi ya usalama wake.
ii) Shule hiyo haina uzio hali ambayo itasababisha uvamizi wa eneo na wizi wa vifaa.
d) Maoni
i) Utatuzi wa muda mrefu ni kuweka umeme katika shule hiyo kwa kuwa tatizo ni kupatikana kwa gharama za kununulia transfoma.
ii) Utatuzi wa muda mfupi imeshauriwa uongozi wa shule hiyo kufanya utaratibu wa kuvuna maji ya mvua ambayo yangeweza kusaidia katika kuboresha shughuli za usafi wa mazingira pamoja na watoto kunawa. wanavyotoka chooni.
iii) Eneo la shule lipimwe na mipango ya kuweka uzio ifanyike ili kuepuka migogoro inayojitokeza.
69
Picha Na. 24: Haya ni majengo ya vyoo yaliyojengwa katika
shule ya msingi Lubakaya
Picha Na. 25: Hili ni moja kati ya mashimo ya
vyoo katika shule ya Msingi Lubakaya
70
4.12 Ukarabati wa Soko la Buguruni
Utangulizi
Kwa kifupi Soko la Buguruni lilianzishwa mnamo mwaka 1978 likiwa lina
wafanyabiashara takribani 500 ambao walikuwa wauzaji wa rejareja. Kadri
miaka ilivyozidi kwenda na kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu
yamekuwa yakifanyika maboresho mbalimbali ya kupandisha hadhi ya soko ili
kukidhi mahitaji na ubora kwa watumiaji.Adiha, Halmashauri katika
kutekeleza agizo la Serikali lilitolewa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jaffo (MB.) lililohusu
ujenzi/uboreshaji wa masoko nchini, walianza kutekeleza agizo hilo kwa
kuhakikisha masoko yanapimwa na kufanya maboresho yanayostahili.
a) Utekelezaji
i. Zoezi la upimaji wa Soko limefanyika na hatua za ujenzi wa mabanda
umekamilika kwa hatua za upauaji.
ii. Hati bado haijapatikana
iii. Bado ile dhana ya kuondoa bidhaa kutoka chini ya ardhi na kuziweka
juu ya vizimba/ meza haijafanyika.
b) Mafanikio
i) Eneo la soko tayari limepimwa jambo ambalo litasaidia Halmashauri kujua mipaka na uhalali wa umiliki wake.
ii) Halmashauri kuweka kipaumbele cha kuboresha masoko yake likiwemo soko la Buguruni ambalo litakuwa la kisasa zaidi.
c) Changamoto
i) Kiasi cha makusanyo kwa mwezi ni Sh. 34,910,000, (milioni thelathini na nne laki tisa na kumi elfu) kilichotajwa hakilingani na ukubwa wa soko hilo kwa maana ya makadirio ya idadi ya wauzaji na wanunuzi wanaokuwepo katika soko hilo kila siku. Wastani wa wafanyabiashara kwa siku ni 3,000 na kiwango cha chini ni Tshs. 500/=
ii) Takwimu ya wauzaji wa bidhaa iliyotajwa kuwepo sokoni hapo hailingani na hali halisi iliyoonekana sokoni hapo.
iii) Hakuna maeneo ya maegesho ya magari. iv) Miundombinu ya vyoo ni mibovu licha ya kuwa inaingiza makusanyo
mengi.
71
d) Maoni
Halmashauri ihakikishe kwamba:-
i) Inasimamia masoko yenyewe kwa kuingia mkataba na wafanyabiashara
moja kwa moja bila kuruhusu mambo ya kamati za masoko. Mfano mzuri
ni kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia soko
linalojulikana kama mahakama ya ndizi (Mabibo) ambapo wakati
lilipokuwa linaendeshwa na watu binafsi, Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni (kwa kipindi hicho) ilikuwa ikipata takribani Sh. milioni 3 kwa
mwezi. Kwa sasa lipo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo na makusanyo kwa mwezi ni kati ya Sh. Milioni 70 hadi 80 kwa
mwezi.
ii) Inahimiza matumizi ya Electronic Fiscal Devices (EFDs) katika
ukusanyaji wa mapato.
iii) Inafanya sensa ili kupata takwimu sahihi ya wafanyabiashara pamoja na
kufanya tathimini ya viwango vyao vya ushuru katika soko hilo.
iv) Inaimarisha usafi na mazingira hususan suala la vyoo kwa usalama wa
afya za watu waliopo katika soko hilo lakini pia kwa wakazi wote wa Jiji la
Dar es Salaam.
v) Inafuatilia hati ya eneo la soko hilo.
74
4.13 UJENZI WA MRADI WA MAJI KIPUNGUNI ‘B’
Utangulizi
i) Ujenzi wa mradi wa maji katika eneo la Kata ya Kipunguni ulianza tarehe 14/07/2014 na kukamilika tarehe 10/05/2017. Kama ilivyo miradi mingine, ujenzi huo pia haukukamilika kwa wakati kutokana na kuchelewa kupata msamaha wa kodi ya vifaa kutoka TRA na ucheleweshwaji wa kuondosha miundombinu iliyokuwepo awali na taasisi husika.
a) Utekelezaji
i) Ujenzi umekamilika isipokuwa Kamati ya maji bado. ii) Ujenzi umejumuisha kisima cha maji chenye urefu wa mita 120, Tanki la
lita 250,000, vituo vya kuchotea maji (DP's) 12, nyumba ya Pampu (Pump house), ufungaji wa Pampu, matenki 3 ya kuvuna maji ya mvua (rain water harvesting tanks) na mtanadao wa mabomba yenye urefu wa Km 9.057 na kufunga transfoma.
b) Mafanikio
i) Mradi umekamilika na hivyo utasaidia wakazi wa Mitaa ya Kipunguni ‘B’ na Mji Mpya na maeneo mengine kupata maji safi na salama (zaidi ya 6000 watapata huduma ya maji)
ii) Kufanikiwa kutatua changamoto zilizokuwa zikichelewesha ujenzi wa mradi kama vile kuchelewa kupewa msamaha wa kodi kutoka TRA na uondoshwaji wa miundombinu ya mabomba iliyokuwepo awali.
c) Changamoto
i) Umeme mdogo unaotokana na kuchelewa kuunganishiwa Umeme na TANESCO licha ya kuwa Mkandarasi alikwishalipia Transfoma ya kuongeza nguvu ya umeme.
ii) Kuchelewa kuunda Kamati ya maji.
d) Maoni
i) Ufuatiliaji wa upatikanaji wa umeme wa kutosha ufanyike. ii) Uundaji wa Kamati za maji uwe unafuata utaratibu yaani miezi 6 kabla ya
mradi kukamilika. iii) Uundaji wa Kamati hiyo ufanyike haraka ili mradi huu uanze kuwanufaisha
wananchi kwa usimamizi thabiti.
75
5. 0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE
UTANGULIZI
Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke ulianza tarehe 16 hadi 17 Mei, 2017. Shughuli za ukaguzi zilianza
kwa kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na baada ya hapo
kupata taarifa kwa ufupi ya miradi itakayotembelewa. Mchumi wa
Manispaa alielezea miradi ambayo itatembelewa, lengo la kila mradi,
tarehe ya kuanza na kukamilisha mradi, gharama za mradi, fedha
zilizotolewa na zilizotumika. Jumla ya miradi 11 ya maendeleo
ilitembelewa ambayo imeorodheshwa hapo chini:-
i) Ujenzi wa Jengo la ghorofa 1 kwa ajili ya Ofisi ya DMDP Manispaa ya Temeke
ii) Ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shule ya sekondari Kibasila iii) Ujenzi wa vyumba 15 vya madarasa katika shule ya Msingi Rufu iv) Ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa katika shule ya Msingi Mbande Kata
ya Chamazi v) Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule ya Msingi Majimatitu
Kata ya Chamazi vi) Ujenzi wa Zahanati charambe iliyopo Kata ya Charambe vii) Ujenzi wa Shule ya Sekondari kidato cha V-VI katika Kata ya Kibonde
Maji. viii) Ujenzi wa barabara ya Kijichi- Nasaco yenye KM 1.2 ix) Ujenzi wa choo matundu 3 katika eneo la soka la buza lililopo Kata ya
Buza x) Ukarabati wa mfereji wa Evareti Chang’ombe Polisi kata ya
Temeke. xi) Ujenzi wa Mabanda 4 (manne) ya biashara katika soko la Temeke
Stereo
76
4.1: Ujenzi wa Jengo la Ghorofa Moja kwa Ajili ya Ofisi ya Dar
es Salaam Metropolitian Development Programme (DMDP)
Manispaa ya Temeke
Utangulizi
Mradi huu umeanza tarehe 15 Februari, 2017 na unatarajia kukamilika
tarehe14 Februari, 2018 lengo la Mradi ni kuimarisha miundombinu hasa
ujenzi wa barabara.
a) Utekelezaji
Mpaka sasa ujenzi wa Fremu, Bimu, nguzo na Slabu vimekamilika na
sasa jengo lipo hatua za umaliziaji.
b) Changamoto
- Manispaa haina Wataalam wa maabara hiyo
c) Maoni
i) Halmashauri ifundishe Wataalam wa Maabara ili pindi hao
Wafadhili wakiondoka halmashauri iweze kuendelea na kazi
hiyo.
ii) Maabara hiyo itangazwe ili ijulikane
iii) Halmashauri inashauriwa kumalizia Maghorofa mawili
yaliyobaki kwani Wafadhili hao wanajenga ghorofa 1
wakati msingi wake ni ya ghoropha 3
Picha Na.1 Mradi wa ujenzi wa ofisi ya DMDP ghorofa 1
77
4.2 Ujenzi wa Vyumba Vinne vya Madarasa Shule ya Sekondari Kibasila
Utangulizi
Ujenzi wa majengo hayo umelenga kuboresha elimu na kupunguza
uhaba wa madarasa shuleni hapo ambapo shule ina jumla ya
wanafunzi 1,343 kuanzia kidato cha I-VI na walimu 86.
a) Utekezaji
i) Vyumba vinne vimejengwa na vimepauliwa
ii) Huduma ya maji ipo na watoto wananawa mikono
b) Changamoto
i) Mradi bado haujapigwa plasta,
ii) ubao wa kufundishia haujawekwa, silling board, milango, sakafu na
wiremesh za madirishani hazijawekwa
iii) Malipo yamefanyika kwa asilimia 25 tu ya mradi inayogharimu sh. Milioni
themanini
(80,000,000/=).
iv) Miti ya miarobaini imepandwa mingi ambayo inahatarisha majengo
kuharibiwa na mizizi
c) Maoni
i) Malipo yafanyike kwa asilimia 100 ya mradi inayogharimu Sh.
Milioni themanini (80,000,000/=) ili madarasa yaanze
kutumika.
ii) Maelekezo yametolewa kuhakikisha kuwa ukamilishaji unafuata
vigezo
iii) Miti hiyo ya miarobaini iondolewe inaweza kuharibu miundo
mbinu ya majengo.
78
Picha na.2: Mradi wa ujenzi wa Madarasa manne shule ya Sekondari Kibasila
4.3 Ujenzi wa Vyumba 15 vya Madarasa Katika Shule ya Msingi Rufu
Utangulizi
Shule hii ni mpya ina darasa la Awali, la Kwanza, na la Pili ikiwa na jumla ya wanafunzi 741 na walimu 13. Ujenzi wa vyumba 15 vya madarasa katika shule ya msingi Rufu unaendelea (5 vinajengwa na Halmashauri na 10 vinajengwa na TATOA (Tanzania Truck Owners Associations) iliyokuwa imetafutwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadick. a) Utekelezaji
i) Kwa sasa vyumba 3 tu vimekamilika na vinatumika. ii) Mradi unaotekelezwa na TATOA umesimama kwa kukosa
mawasiliano na wafadhili. Aidha, mradi upo katika hatua tofauti, vyumba 4 vimepauliwa, 3 havijapauliwa lakini vimepigwa plasta na 3 havijapauliwa wala havina plasta.
iii) Mradi wa ujenzi wa vyumba 5 wa Halmashauri vipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji.
iv) Shule ina maji yaliyofadhiliwa na shirika la UNICEF
b) Changamoto
i) Vyumba vilivyopauliwa vinazidi kuharibika wakati mahitaji yangalipo
ii) Ash board hazijawekwa katika vyumba 5 vinavyokamilishwa.
79
iii) Hakuna huduma ya kunawa mikono japo maji yapo iv) Vyoo havina milango na vipo barabarani Walimu hawana Ofisi
c) Maoni
i) Halmashauri imeelekezwa na timu ya ukaguzi ya Mkoa kufuata utaratibu wa ujenzi kwa kufuata vigezo sahihi.
ii) Kufanya mawasiliano na TATOA ili ikiwezekana wamalizie majengo hayo.
iii) Halmashauri ikamilishe majengo hayo kwa kipato cha ndani (Own Source)
iv) Huduma ya wanafunzi kunawa mikono baada ya kutoka chooni izingatiwe.
v) Vyoo vitengenezewe milango
Picha na.4: Mradi wa madarasa 5 yanayofadhiliwa na Manispaa, Shule Msingi Rufu
80
Picha na.5: Mradi wa madarasa 10 Shule ya Msingi Rufu yaliyojengwa na shirika la TATOA ambayo
hayajakamilika
4.4 Ujenzi wa Vyumba 5 vya Madarasa Katika Shule ya Msingi Mbande Kata ya Chamazi
Utangulizi
Mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mbande upo katika kata ya Chamazi kweye mtaa wa Mbande. Kutekelezwa kwa mradi huu ni juhudi za Halmashauri katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa vyumba vya vya madarasa linalosababisha msongamano wa wanafunzi kwenye vyumba vichache vilivyopo. Shule ina wanafunzi 6,274 kuanzia darasa la I-VII. na Walimu 90, vyumba vya madarasa ni 38, matundu ya vyoo 20 yanayotumika na 20 yanayojengwa.
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika ila bado rangi,wiremesh na sakafu
b) Changamoto
i) Ukamilishaji umesisitizwa
ii) Bado fedha za kukamilisha ujenzi
iii) Hakuna Ofisi ya Walimu
iv) Vyoo vya Walemavu ni vya kizamani
c) Maoni
i) Marekebisho yafanywe kwenye ubao
ii) Pia fedha zilizopelekwa shuleni zifuatiliwe
81
iii) Ofisi ya Walimu ijengwe ili kuboresha ufanisi wa kufundisha ili
kupata ubora wa elimu
iv) Vyoo vya Walemavu viboreshwe.
4.5 Ujenzi wa Vyumba Kumi vya Madarasa Katika Shule ya Msingi Majimatitu Iliyopo Kata ya Chamazi.
Utangulizi
Ujenzi wa vyumba 11 shule ya msingi Maji matitu umesaidia kupunguza uhaba wa madarasa kwani shule ina jumla ya wanafunzi 6,798 , Walimu 98 , madarasa 42 na matundu ya vyoo 42. Shule ina kisima cha DAWASCO.
a) Utekelezaji
-Ujenzi umekamilika
b) Changamoto
i) Madirisha hayana “wire mesh”
ii) Hakuna maji kwa sababu shule haina umeme wa kutosha
kupandisha maji
iii) Hakuna ofisi ya Walimu
iv) Walimu hawatoshi ni wachache
c) Maoni
i) Madirisha yawekewe nyavu
ii) Idara ya Mipango kwa kushirikiana na TANESCO itatue tatizo kwa
kuipatia shule umeme wa kutosha kusukuma maji
iii) Ofisi ijengwe na Halmashauri iongeze idadi ya Waalimu
82
Picha na.7: Mradi wa ujenzi wa madarasa 10 S/M Majimatitu
4.6 Ujenzi wa Zahanati Charambe Iliyopo Kata ya Charambe
Utangulizi
Katika kuboresha huduma za afya hasa kwa wakazi wa kata ya
Charambe, Halmashauri ilipanga kuanzisha ujenzi wa Zahanati katika
Kata hiyo. Mpango huu unatekelezwa kwa mapato ya ndani (Own source)
ya Halmashauri. Ujenzi wa Zahanati hiyo utasaidia kuhudumia wananchi
wa Charambe wanaosafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya Afya.
a) Utekelezaji
Mradi upo katika hatua ya ukamilishaji
b) Changamoto
i) “Ramp” kwa ajili ya walemavu hazijawekwa
ii) Eneo halijapimwa
iii) hakuna maji
iv) Eneo halina uzio
v) Hakuna mfereji wa kutoa maji ya mvua nje ya zahanati
c) Maoni
i) “Ramp” za walemavu zijengwe
ii) Eneo lipimwe
iii) Eneo liwekewe uzio
iv) Manispaa ifanye utaratibu wa kuvuta maji hadi kwenye
zahanati hiyo.
83
v) Ghata ziwekwe kwa ajili ya kuvuna maji
vi) Mfereji wa kutoa maji nje uwekwe.
Picha Na 8: Mradi wa ujenzi wa Zahanati Charambe
4.7 Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kidato Cha V-VI Katika Kata
ya Kibonde Maji.
Utangulizi
Ujenzi wa vyumba 14 vya shule ya A level Mbagala sekondari unaendelea
ambapo mradi ulianza 2014/2015. Hii ni shule ya ghorofa 2, itakamilika
Septemba 2017 na itakuwa na maabara 2. Mkandarasi wa kwanza
alikuwa Mchina wakavunja mkataba akapatikana mkandarasi mwingine
ambaye anaendelea kujenga ambapo gharama za Mradi ni billion 1.2 na
amelipwa milioni 120 kama malipo ya gharama za awali.
a) Utekelezaji Hardcore, groundbeam na slabu ya chini vimekamilika. Column zote zimemiminwa kwa sasa kazi ya block work kwa sakafu ya chini inaendelea na inakadiriwa kufika asilimia 50. b) Changamoto
i) Ujenzi bado unaendelea kutokana na mvua kuwa nyingi magari
hayafiki eneo la mradi kupeleka vifaa vya ujenzi hasa mchanga na kokoto.
ii) Eneo halijapimwa na hakuna maji.
84
iii) Maabara 2 hazitoshi kwa wanafunzi wa mchepuo wa sayansi. iv) Mkondo wa maji unahitaji kutafutiwa njia muafaka, v) Eneo halijapimwa. vi) Mkandarasi anasuasua.
C) Maoni
i) Manispaa kwa kutumia idara ya ardhi ipime eneo hilo. ii) Manispaa kuongeza maabara moja zaidi
iii) Kuondoa mkondo wa maji unaopita eneo la ujenzi wa shule ili
kuepuka uharibifu wa miundo mbinu ya shule.
iv) Mkandarasi aonyeshe Mpango kazi wake ili kuondokana na
kusuasua kwake
Picha na. 9: Mradi wa ujenzi wa S/Sekondari Mbagala
8. Ujenzi wa barabara ya Kijichi - NASACO yenye KM 1.2 Utangulizi
Mradi huu ulianza kujengwa Julai 2015 na ulitarajiwa kukamilika Disemba 2015 na Mkandarasi anayetekeleza mradi huu ni CASCO. Mradi huu unajengwa kupitia fedha za ndani za Halmashauri (Own Source), ulichelewa kukamilika kutokana na upatikanaji wa fedha.Barabara ina jumla ya urefu wa Km 1.2, urefu wa awali ukiwa mita 905. Gharama ya jumla ya mradi ni Tsh. 904,000,000/-. Kuna nyongeza ya mita 300 anazoendelea kujenga Mkandarasi itakayogharimu Tsh. 330,000,000/- . a) Utekelezaji
i) Ujenzi umekamilika mita 905 kiwango cha lami na mitaro pande zote
85
ii) Kazi ya nyongeza inaendelea b) Changamoto
i) Kipande kilichoongezewa hakijakamilika ili barabara ianze kutumika
ii) Mabega (shoulders) za barabara ukamilishaji wake hayajajengwa vizuri kwanio zinamomonyoka.
iii) Wananchi wanaendelea na shughuli ya uchimbaji mchanga katika sehemu ya Karavati la juu hali itakayopelekea kuleta uharibifu katika barabara hiyo
iv) Maji yametuama katika mtaro kutokana na kuingiliwa na taka mbalimbali na nyingi.
d) Maoni
i) Wahandisi waendelee kusimamia kwa ukaribu ilikukamilisha sehemu iliyobaki
ii) Mabega (sholders) za barabara zimaliziwe vizuri kuweka uimara wa barabara
iii) Mifereji isafishwe mara kwa mara kuepusha maji kuingia barabarani na kuharibu barabara (Watendaji wa mtaa watumike)
iv) Wanaochimba mchanga wasitishwe na kufuatiliwa v) Mwenyekiti wa Mtaa aweke ulinzi kwa ajili ya wachafuzi wa
mifereji na wachimba mchanga pia waweke Sheria ndogo ili kuwezesha utekelezaji.
86
Picha na.10: Ujenzi wa Mradi wa barabara ya Kijichi –Nasaco ambayo shoulder zake ukamilishaji wake hazijajengwa vizuri
4.9 UJENZI WA CHOO MATUNDU 3 KATIKA ENEO LA SOKA LA BUZA LILILOPO KATA YA BUZA Utangulizi
Choo hicho kitasaidia kutoa huduma kwa wafanya biashara na kimejengwa na fedha za Halmashauri pia kitaongeza pato la Taifa na Halmashauri kwani kitakuwa choo cha kulipia. a) Utekelezaji
i) Ujenzi wa choo cha Buza kipo hatua ya ukamilishaji ii) Taratibu za malipo ya mwisho zinaendelea
b) Changamoto
i) Choo hakina ”ceiling board” ii) Choo hakijakamilika kwa wakati kwani kilitakiwa kikamilike
Septemba, 2016 sasa kinatarajiwa kuisha Julai 2017 iii) Soko halina wafanya biashara wa kutosha
87
c) Maoni
i) Kutafuta fedha kwa ajili ya ceiling board ii) Itafutwe mbinu ya kuhakikisha watu/Wafanyabiashara wanaenda
kufanyia biashara zao sokoni badala ya pembezoni mwa barabara
Picha na.11: Mradi wa ujenzi wa choo soko la Buza
4.10. UKARABATI WA MFEREJI WA EVARETI CHANG’OMBE POLISI KATA YA TEMEKE Utangulizi
Mfereji huo umekarabatiwa ili kupitisha maji sehemu moja yaliyokuwa yanatawanyika.
a) Utekelezaji i) Mfereji umekarabatiwa ii) Ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua kwa kuchimba, kufunga waya,
kuweka changarawe, kujenga mfereji, kusuka vikapu vya mawe, kujenga kalvati na kazi ya ujenzi umekamilika.
b) Changamoto i. Barabara ya juu ya karavati hilo halijajengwa vizuri ii. Mkandarasi hajalipwa mpaka leo na anaendelea kudai fedha zake
c) Maoni i) Barabara iwekewe karavati na ijengwe kwa fedha za ndani za
Halmashauri.
ii) Mkandarasi alipwe fedha zake baada ya kukamilisha kazi.
88
Picha na.12: Mradi wa ukarabati wa mfereji Chang’ombe Polisi
4.11. UJENZI WA MABANDA MANNE YA BIASHARA KATIKA SOKO LA TEMEKE STEREO Utangulizi
Lengo la mradi ni upanuaji wa biashara ili kuongeza kipato cha wafanya biashara na Serikali. Mradi huu umeanza tarehe 17 Machi, 2016 na utakamilika tarehe 17 Juni, 2016 na mkandarasi ni MASUFIN'S GENERAL CO. LTD
a) Utekelezaji i) Mabanda 3 ya kuuza bidhaa yamekamilika na banda 1 la
machinjio ya kuku limekamilika ii) Mabanda yanatumika
b) Changamoto i) Hakuna sakafu kwenye mabanda hayo ii) Biashara nyingi zinauziwa chini iii) Takwimu sahihi za wafanyabiashara hazipo kwani wamiliki
wanaofahamika ni wale wapangishaji wa zamani.
c) Maoni i. Kutafuta fedha kwa ajili kwa kuweka sakafu ya zege ii. Wauzaji wa Chakula watafutiwe meza na mabanda ya kuuzia iii. Manispaa iepuke uwepo wa kamati ya soko ili kuepuka matumizi
mabaya ya fedha. iv. Utafiti wa kupata takwimu sahihi za wafanyabiashara ufanyike ili
kujua ni kiasi gan cha fedha kwa siku na kwa mwezi kitakusanywa.
89
Picha na.13: Mradi wa ujenzi wa mabanda 4 ya biashara soko la Temeke Stereo
Maoni ya jumla ya ufuatiliaji yaliyotolewa ya miradi ya Temeke
Timu ya ukaguzi ilitoa maoni ya jumla kama ifuatavyo:-
i) Fedha zinapotumwa shuleni, taarifa itolewe katika idara zote ili miradi
ifuatiliwe kwa utaratibu na kwa viwango vinavyotakiwa.
ii) Ujenzi wa vyumba vya madarasa uendane na ujenzi wa vyoo na Ofisi za
Walimu.
iii) Suala la afya na usafi wa mazingira shuleni hasa maeneo ya kunawa
mikono lipewe kipaumbele.
iv) Kupima maeneo ya shule ili kuepusha migogoro.
v) Kuanza utaratibu wa kuchimba kisima na kutengeneza mifumo ya
kukusanya/kuvunia maji ya mvua shuleni.
vi) Wakandarasi ambao hawajalipwa fedha zao walipwe kwa wakati.
vii) Kugawa shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi na kuzisajili
viii) Miradi ya shule inayojengwa na Local fundi Wahandisi wa
Halmashauri waisimamie kwa umakini maana wanapojenga
wakikosea wahandisi ndio watakaowajibika kwani hawana mikataba
nao kama ya Wakandarasi.
90
TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
UTANGULIZI
Ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
ulifanyika tarehe 23 na 24 Mei, 2017. Jumla ya miradi nane ya maendeleo
ilikaguliwa. Ifuatayo ni taarifa ya kila mradi.
5.1 Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa Shule ya Msingi Bohari
Utangulizi
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inaendelea kutekeleza Miradi ambayo
ilianzishwa na Halmashauri mama ya Temeke ukiwemo mradi huu wa ujenzi wa
vyumba 3 vya madarasa. Shule ina jumla ya wanafunzi 413 wa kuanzia darasa
la I hadi VII. Ujenzi umekemilka na madarasa yanatumika. Fedha hizi imetolewa
kwa msaada (Mfuko) wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambapo Mkandarasi ni ‘Local Fundi’
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na unatumika.
b) Changamoto i) Eneo la shule halijapimwa
ii) Ngazi za kuingia na kutokea madarasani zipo sehemu moja tu hivyo
kusababisha msongamano wa wanafunzi
iii) Ukubwa wa ubao hauridhishi (ni mdogo)
iv) Darasa la awali wanasomea nje
v) Vyoo vinavyotumika vimeanza vinaonesha kuanza kutitia
vi) Kuna mgogoro wa mipaka ya shule kati ya Wananchi na uongozi wa
shule
vii) Sakafu siyo imara hali inayopelekea kuanza kubomoka
viii) Vitasa na milango iliyowekwa siyo imara (sub standard)
c) Maoni i) Halmashauri ijitahidi kupima eneo la shule haraka na kuonesha
mchoro wa madarasa ya shule
ii) Kujenga ngazi upande wa pili kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum
iii) Kuongeza ukubwa wa ubao
iv) Kuongeza ujenzi wa madarasa ili darasa la awali wapate chumba cha
kusomea
91
v) Kufanya ukarabati vyooni na kutenga choo maalumu kwa wasichana
wenye uhitaji.
vi) Halmashauri ijitahidi Kutatua mgogogro wa ardhi uliopo kati ya
mwananchi na Shule
vii) Kufanya ukarabati wa baadhi ya madarasa
5.2 UJENZI WA VYUMBA 2 VYA MADARASA SHULE YA MSINGI
MWONGOZO
Utangulizi
a) Utekelezaji
Shule ina jumla ya wanafunzi 11,235. Ujenzi wa vyumba 2 vya
madarasa umekamilika na vinatumika.
b) Changamoto
i) Kutokuwapo kwa ngazi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (ramp)
ii) Wavu uliowekwa kwenye madirisha ni dhaifu (sub-standard) iii) Shule haina madarasa ya kutosha iv) Kuwapo kwa nyumba ya mwalimu ambayo haijamaliziwa kwa muda
mrefu tangu mwaka 2012 v) Kutokuwapo kwa “Ash board” kwa ajili ya kuweka/kupokea unga wa
chaki vi) Kutofanya ukarabati vyooni na uchache wa matundu ya vyoo vii) Eneo la shule bado halijapimwa viii) Ushirikishwaji wa mradi ni mdogo kwani walimu wengine hawaujui mradi. Mradi unajulikana na Mwalimu Mkuu.
c) Maoni
i) Kujenga ngazi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ii) Kurekebisha waya kwenye madirisha. Uliowekwa ni dhaifu. iii) Kujenga madarasa mengine ili kuweza kuchukua madawati yaliyopo nje
ya madarasa iv) Kumalizia ujenzi wa nyuma za walimu zilizojengwa mwaka 2012 bila
kukamilika. v) Kujenga Ash board kwa ajili ya kupokea chaki vi) Kufanya ukarabati vyooni na kujenga matundu mengine ya vyoo
ambavyo vitatenganisha matundu ya vyoo na mashimo yake vii) Kufanya upimaji wa eneo la shule ili kuondoa migogoro. viii) Kufanya ushirikishwaji wa miradi ya maendeleo kati ya Halmashauri na
wanufaika
92
5.3 UJENZI WA SHULE MPYA YA MSINGI MIKENGE KATA YA
KIMBIJI
a) Utekelezaji
Shule ina jumla ya wanafunzi 69. Mradi unafadhiliwa na Mdau (Abdallah
Salim) pamoja na nguvu za wananchi. Ujenzi wa madarasa matatu na
ofisi moja ya mwalimu upo hatua ya umaliziaji bado kuweka Ceiling
Board, milango, mbao za kuandikia na kupaka rangi.
b) Changamoto
i) Eneo la shule halijapimwa japo lilitolewa na mdau. ii) Hakuna mkataba wowote kati ya Mfadhili na Halmashauri iii) Hakuna mchoro wa kusaidia ujenzi wa madarasa yatakayoendelea
kujengwa iv) Hakuna jenereta kwa ajili ya kusukuma maji pamoja na kwamba maji
yapo shuleni. v) Shule bado haijapatiwa usajili japo Serikali imepeleka walimu vi) Kutokuwapo kwa ngazi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum vii) Hakuna milango kwenye vyoo 4
c) Maoni
i) Halmashauri kupima eneo la shule ii) Kuwapo Mkataba kati ya Mfadhili na Halmashauri iii) Kuwapo kwa michoro ya majengo ya Elimu inayokubalika iv) Kuweka “Ceilinga board”, milango, mbao za kuandikia na kupaka rangi ili
kuwapo na mazingira mazuri ya kujifunzia v) Kununua jenereta kwa ajili ya kusukuma maji shuleni vi) Kujenga ngazi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum vii) Kuweka milango kwenye vyoo 4
5.4 Ujenzi wa mradi wa Maji kisarawe II - Mwasonga
a) Utekelezaji
Ujenzi wa ‘Riser’ ya mita sita kwa ajili ya kuweka tanki lenye ujazo wa lita
elfu ishirini, ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji, kukarabati nyumba na
kununua pump zimeshakamilika. Mradi huu bado haujaanza kutumika
kutokana na kutoshirikiana kati ya Halmashauri, Kamati ya Maji na
Mkandarasi. Aidha, huu ni mradi mmojawapo ya miradi iliyokuwa
inatekelezwa na Halmashauri ya manispaa ya Temeke na kuhamishiwa
Kigamboni bila fedha.
b) Changamoto
i) Kutokamilika kwa mradi kwa wakati. Mradi huu una kipindi kirefu ambacho ni zaidi ya miaka mitatu;
93
ii) Kuna Ushirikiano mdogo uliopo kati ya kamati ya Maji, Wataalam wa Halmshauri na Mkandarasi
iii) Baadhi ya vituo vya kuchotea maji kutotoa maji na kusababisha wananchi kukataa kuupokea mradi.
c) Maoni
i) Halmshauri kuakikisha mradi unakamilika haraka iwezekanavyo ii) Ushirikiano na uwazi kati ya kamati ya maji, wataalam wa Halmashauri
na Mkandarasi uharakishwe ili kumaliza tofauti zilizopo. iii) Kuhakikisha vituo vya kuchotea maji (DPs) 15 zinatoa maji kama mradi
ulivyosanifiwa iv) Pawepo ushirikiano wa kutosha kati ya Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke na Kigamboni ili kuhakikisha mradi unakamilika. Makabithiano yawe bayana.
5.5 Ujenzi wa jengo la wazazi zahanati ya kisarawe II
a) Utekelezaji
Mradi huu ulianza rasmi mwaka 2012 na jengo kukamilika mwaka 2016
na vifaa tiba vilipatikana mwaka 2017. Ujenzi huu umefadhiliwa na Water
Com (Said Munifu). Jengo hili ni kwa ajili ya wodi ya wazazi, kuhudumia
mama waja wazito katika kata ya Kisarawe II ili kuwapunguzia akina
mama umbali mrefu kwenda kujifungua katika vituo vya mbali. Jengo
limegawanywa katika vyumba vitatu ambapo chumba I ni Wodi ya waja
wazito (Antenatal ward), chumba II ni Wodi ya kujifungulia (Labour
ward) na chumba cha III ni Wodi ya waliojifungua (Post Natal)
b) Changamoto
i) Shimo dogo maalum (Placenta pit) kwa ajili ya kuweka kondo la uzazi
baada ya mama kujifungua ni dogo sana kwani lililopo harufu inaweza
kurudi ndani.
ii) Hakuna “incinerator” za kuchomea taka ngumu iii) Vitanda havitoshelezi kulala wazazi masaaa 24 ya uangalizi. iv) Kutokuwapo kwa “heater” kwa ajili ya mama wajawazito kupata maji ya
moto ya kuoga kabla na baada ya kujifungua. v) Usafi wa wodi hauridhishi vi) Waya wa kutolea umeme kutoka kwenye jengo la zahanati kuingia
kwenye wodi ya wazazi ni mdogo sana (hauna kiwango).
c) Maoni
i. Kuongeza ukubwa wa ‘Placenta Pit’ ii. Kujenga incinerator za kuchomea taka ngumu iii. Kuongeza vitanda viwili na vifaa tiba k.m. tray maalum za kujifungulia. iv. Kufanya uangalizi wa mama na mtoto kwa masaa 24 v. Kufanya usafi wa labour word na itumike ipasanyo vi. Kuweka heater kwa ajili ya mama wajawazito kupata maji ya moto ya
kuoga kabla na baada ya kujifungua.
94
vii. Kutumia condwit kuingiza umeme wa uhakika katika jengo la wazazi viii. Utaratibu wa makabidhiano kati ta Mdau na Halmashauri ufanyike ix. Kufanya ushirikiano kati ya Mfadhili na Halmashauri ili kuwepo kwa
ubora wa miradi
5.6 Ujenzi wa madarasa 2 Shule ya msingi Kisiwani
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na madarasa yanatumika. Ujenzi umefanywa kwa
nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri
b) Changamoto
i. Kutokuwapo kwa waya kwenye madirisha yaliyojengwa na wananchi
ii. Kutokuwapo Ash board kwenye mbao za madarasa
iii. Ufinyu wa matundu ya vyoo
iv. Upungufu wa madarasa
v. Kutokuwapo ofisi ya waalimu ambao kwa sasa wanatumia darasa
vi. Baadhi ya maeneo rangi haijamaliziwa inavyotakiwa
vii. Kuwapo kwa nyumba za walimu mbili ambazo hazijamaliziwa kwa muda
mrefu (nyumba zilijengwa mwaka 2012)
viii. Kutokuwapo kwa ngazi (ramph) kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum
ix. Hakuna vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum
c) Maoni
i. Kuweka waya kwenye madirisha yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi ii. Kuweka Ash board kwa ajili ya kupokea chaki iii. Kuongeza matundu ya vyoo ili kukabiliana na uhaba uliopo iv. Kujenga madarasa mengine ili kutatua upungufu wa madarasa uliopo v. Kujenga Ofisi ya Waalimu ambao wanatumia darasa kama Ofisi vi. Kumalizia kupaka rangi katika sehemu ya juu ya madarasa vii. Kumalizia ujenzi wa nyumba za waalimu mbili za muda mrefu viii. Kujenga ngazi (ramph) vyooni kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum
5.7 Ujenzi wa mfereji wa dharura wa maji na
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na mradi unatumika
b) Changamoto
i. Baadhi ya maeneo ya mradi kutitia
ii. Kutokuwapo kingo zinazoweza kusaidia usalama wa wananchi (mfefreji
una kina kifefu kiasi kwamba mtu akitumbukia kwa bahati mbaya
atavunjika vibaya).
95
iii. Kuwapo kwa nyufa katika baadhi ya maeneo ndani ya mfereji.
iv. Kutokuwapo kwa sehemu ambazo wananchi wanaiweza kupita (mfereji
umejengwa bila kuzingatia kuwa kuna watu wenye nyumba na
wanafanya biashara pembeni.
c) Maoni
i) Kufanya marekebisho ya sehemu zinazotitia
ii) Kujenga kingo ili kuimarisha usalama wa wananchi
iii) Kufanya ukarabati katika mfereji (kuziba nyufa)
iv) Kujenga sehemu za kupitia wananchi/ wafanya biashara.
5.8 Mradi wa Maji katika Shule ya Msingi Kijaka
a) Utekelezaji.
Mradi umetekelezwa na Ufadhili wa Watu wa Kuwait. Aidha, mradi huo
umeshaanza kutumika
b) Changamoto
i) Wataalam wa Halmashauri kutoshiriki katika utekelezaji;
ii) Kutokuwepo (distribution point) katika eneo la shule. Maji hayafiki chooni
iii) Kuwapo kwa tanki dogo la lita 2000 ambalo halikidhi mahitaji ya shule
iv) Kuwapo kwa matundu machache ya vyoo. Lipo tundu moja tu la choo
v) Uhaba wa vyumba vya madarasa hali inayopelekea darasa la tatu na la
tano kutumia chumba kimoja
c) Maoni
i) Wataalam wa Halmashauri kushiriki kikamilifu katika Utekelezaji wa Miradi ya
maendeleo;
ii) Kujenga (distribution point) katika eneo la shule
iii) Kujenga tanki kubwa ili kukidhi mahitaji ya shule na majirani
iv) Kujenga matundu ya vyoo ili kukabiliana na upungufu uliopo
v) Kujenga vyumba vya madarasa ili kila darasa liwe na chumba cha kujifunzia
vi) Halmashauri kufanya usimammizi wa miradi ya wafadhili na kutoa ushauri
wa kitaalam
vii) Idara ya Elimu ishirikiane na idara ya Maji katika ujenzi wa miradi ya maji ya
wafadhili mbalimbali ili kujenga mradi bora.
96
TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
UTANGULIZI
Ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kigamboni ulifanyika tarehe 23 na 24 Mei, 2017. Jumla ya miradi nane ya
maendeleo ilikaguliwa. Ifuatayo ni taarifa ya kila mradi.
5.9 UJENZI WA VYUMBA 3 VYA MADARASA SHULE YA MSINGI
BOHARI
Utangulizi
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inaendelea kutekeleza Miradi
ambayo ilianzishwa na Halmashauri mama ya Temeke ukiwemo mradi
huu wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa. Shule ina jumla ya wanafunzi
413 wa kuanzia darasa la I hadi VII. Ujenzi umekemilka na madarasa
yanatumika. Fedha hizi imetolewa kwa msaada (Mfuko) wa Mh. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mkandarasi ni ‘Local Fundi’
d) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na unatumika.
e) Changamoto
ix) Eneo la shule halijapimwa
x) Ngazi za kuingia na kutokea madarasani zipo sehemu moja tu hivyo
kusababisha msongamano wa wanafunzi
xi) Ukubwa wa ubao hauridhishi (ni mdogo)
xii) Darasa la awali wanasomea nje
xiii) Vyoo vinavyotumika vimeanza vinaonesha kuanza kutitia
xiv) Kuna mgogoro wa mipaka ya shule kati ya Wananchi na uongozi wa
shule
xv) Sakafu siyo imara hali inayopelekea kuanza kubomoka
xvi) Vitasa na milango iliyowekwa siyo imara (sub standard)
b) Maoni
i. Halmashauri ijitahidi kupima eneo la shule haraka na kuonesha mchoro
wa madarasa ya shule
ii. Kujenga ngazi upande wa pili kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum
iii. Kuongeza ukubwa wa ubao
iv. Kuongeza ujenzi wa madarasa ili darasa la awali wapate chumba cha
kusomea
97
v. Kufanya ukarabati vyooni na kutenga choo maalumu kwa wasichana
wenye uhitaji.
vi. Halmashauri ijitahidi kutatua mgogogro wa ardhi uliopo kati ya
mwananchi na Shule
vii. Kufanya ukarabati wa baadhi ya madarasa
5.10 UJENZI WA VYUMBA 2 VYA MADARASA SHULE YA MSINGI
MWONGOZO
d) Utekelezaji
Shule ina jumla ya wanafunzi 11,235. Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa
umekamilika na vinatumika.
e) Changamoto
ix) Kutokuwapo kwa ngazi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (ramp)
x) Wavu uliowekwa kwenye madirisha ni dhaifu (sub-standard) xi) Shule haina madarasa ya kutosha xii) Kuwapo kwa nyumba ya mwalimu ambayo haijamaliziwa kwa muda
mrefu tangu mwaka 2012 xiii) Kutokuwapo kwa “Ash board” kwa ajili ya kuweka/kupokea unga wa
chaki xiv) Kutofanya ukarabati vyooni na uchache wa matundu ya vyoo xv) Eneo la shule bado halijapimwa
Ushirikishwaji wa mradi ni mdogo kwani walimu wengine hawaujui mradi. Mradi unajulikana na Mwalimu Mkuu.
f) Maoni
ix) Kujenga ngazi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum x) Kurekebisha waya kwenye madirisha. Uliowekwa ni dhaifu. xi) Kujenga madarasa mengine ili kuweza kuchukua madawati yaliyopo nje
ya madarasa xii) Kumalizia ujenzi wa nyuma za walimu zilizojengwa mwaka 2012 bila
kukamilika. xiii) Kujenga Ash board kwa ajili ya kupokea chaki
xiv) Kufanya ukarabati vyooni na kujenga matundu mengine ya vyoo ambavyo vitatenganisha matundu ya vyoo na mashimo yake
xv) Kufanya upimaji wa eneo la shule ili kuondoa migogoro. xvi) Kufanya ushirikishwaji wa miradi ya maendeleo kati ya Halmashauri na
wanufaika
98
5.11 UJENZI WA SHULE MPYA YA MSINGI MIKENGE KATA YA
KIMBIJI
a) Utekelezaji
Shule ina jumla ya wanafunzi 69. Mradi unafadhiliwa na Mdau (Abdallah
Salim) pamoja na nguvu za wananchi. Ujenzi wa madarasa matatu na
ofisi moja ya mwalimu upo hatua ya umaliziaji bado kuweka Ceiling
Board, milango, mbao za kuandikia na kupaka rangi.
b) Changamoto
viii) Eneo la shule halijapimwa japo lilitolewa na mdau. ix) Hakuna mkataba wowote kati ya Mfadhili na Halmashauri x) Hakuna mchoro wa kusaidia ujenzi wa madarasa yatakayoendelea
kujengwa xi) Hakuna jenereta kwa ajili ya kusukuma maji pamoja na kwamba maji
yapo shuleni. xii) Shule bado haijapatiwa usajili japo Serikali imepeleka walimu xiii) Kutokuwapo kwa ngazi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum xiv) Hakuna milango kwenye vyoo 4
c) Maoni
viii) Halmashauri kupima eneo la shule ix) Kuwapo Mkataba kati ya Mfadhili na Halmashauri x) Kuwapo kwa michoro ya majengo ya Elimu inayokubalika xi) Kuweka “Ceilinga board”, milango, mbao za kuandikia na kupaka rangi ili
kuwapo na mazingira mazuri ya kujifunzia xii) Kununua jenereta kwa ajili ya kusukuma maji shuleni xiii) Kujenga ngazi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum xiv) Kuweka milango kwenye vyoo 4
5.12 Ujenzi wa mradi wa Maji kisarawe II - Mwasonga
d) Utekelezaji
Ujenzi wa ‘Riser’ ya mita sita kwa ajili ya kuweka tanki lenye ujazo wa lita
elfu ishirini, ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji, kukarabati nyumba na
kununua pump zimeshakamilika. Mradi huu bado haujaanza kutumika
kutokana na kutoshirikiana kati ya Halmashauri, Kamati ya Maji na
Mkandarasi. Aidha, huu ni mradi mmojawapo ya miradi iliyokuwa
inatekelezwa na Halmashauri ya manispaa ya Temeke na kuhamishiwa
Kigamboni bila fedha.
99
e) Changamoto
j) Kutokamilika kwa mradi kwa wakati. Mradi huu una kipindi kirefu ambacho ni zaidi ya miaka mitatu;
vii) Kuna Ushirikiano mdogo uliopo kati ya kamati ya Maji, Wataalam wa Halmshauri na Mkandarasi
viii) Baadhi ya vituo vya kuchotea maji kutotoa maji na kusababisha wananchi kukataa kuupokea mradi.
f) Maoni
v) Halmshauri kuakikisha mradi unakamilika haraka iwezekanavyo vi) Ushirikiano na uwazi kati ya kamati ya maji, wataalam wa Halmashauri
na Mkandarasi uharakishwe ili kumaliza tofauti zilizopo. vii) Kuhakikisha vituo vya kuchotea maji (DPs) 15 zinatoa maji kama mradi
ulivyosanifiwa viii) Pawepo ushirikiano wa kutosha kati ya Halmashauri ya Manispaa
ya Temeke na Kigamboni ili kuhakikisha mradi unakamilika. Makabithiano
yawe bayana.
5.13 Ujenzi wa jengo la wazazi zahanati ya kisarawe II
a) Utekelezaji
Mradi huu ulianza rasmi mwaka 2012 na jengo kukamilika mwaka 2016
na vifaa tiba vilipatikana mwaka 2017. Ujenzi huu umefadhiliwa na Water
Com (Said Munifu). Jengo hili ni kwa ajili ya wodi ya wazazi, kuhudumia
mama waja wazito katika kata ya Kisarawe II ili kuwapunguzia akina
mama umbali mrefu kwenda kujifungua katika vituo vya mbali. Jengo
limegawanywa katika vyumba vitatu ambapo chumba I ni Wodi ya waja
wazito(Antenatal ward), chumba II ni Wodi ya kujifungulia (Labour ward)
na chumba cha III ni Wodi ya waliojifungua (Post Natal)
b) Changamoto
ii) Shimo dogo maalum (Placenta pit) kwa ajili ya kuweka kondo la uzazi
baada ya mama kujifungua ni dogo sana kwani lililopo harufu inaweza
kurudi ndani.
ii) Hakuna “incinerator” za kuchomea taka ngumu iii) Vitanda havitoshelezi kulala wazazi masaaa 24 ya uangalizi.
ix) Kutokuwapo kwa “heater” kwa ajili ya mama wajawazito kupata maji ya moto ya kuoga kabla na baada ya kujifungua.
x) Usafi wa wodi hauridhishi xi) Waya wa kutolea umeme kutoka kwenye jengo la zahanati kuingia
kwenye wodi ya wazazi ni mdogo sana (hauna kiwango).
100
c) Maoni
i. Kuongeza ukubwa wa ‘Placenta Pit’ ii. Kujenga incinerator za kuchomea taka ngumu iii. Kuongeza vitanda viwili na vifaa tiba k.m. tray maalum za kujifungulia.
iv. Kufanya uangalizi wa mama na mtoto kwa masaa 24 v. Kufanya usafi wa labour word na itumike ipasanyo vi. Kuweka heater kwa ajili ya mama wajawazito kupata maji ya moto ya
kuoga kabla na baada ya kujifungua.
vii. Kutumia condwit kuingiza umeme wa uhakika katika jengo la wazazi
viii. Utaratibu wa makabidhiano kati ta Mdau na Halmashauri ufanyike
ix. Kufanya ushirikiano kati ya Mfadhili na Halmashauri ili kuwepo kwa ubora
wa miradi
5.14 Ujenzi wa madarasa 2 Shule ya msingi Kisiwani
a) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na madarasa yanatumika. Ujenzi umefanywa kwa
nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri
b) Changamoto
x. Kutokuwapo kwa waya kwenye madirisha yaliyojengwa na wananchi
xi. Kutokuwapo Ash board kwenye mbao za madarasa
xii. Ufinyu wa matundu ya vyoo
xiii. Upungufu wa madarasa
xiv. Kutokuwapo ofisi ya waalimu ambao kwa sasa wanatumia darasa
xv. Baadhi ya maeneo rangi haijamaliziwa inavyotakiwa
xvi. Kuwapo kwa nyumba za walimu mbili ambazo hazijamaliziwa kwa muda
mrefu (nyumba zilijengwa mwaka 2012)
xvii. Kutokuwapo kwa ngazi (ramph) kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum
xviii. Hakuna vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum
c) Maoni
ix. Kuweka waya kwenye madirisha yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi
x. Kuweka Ash board kwa ajili ya kupokea chaki
xi. Kuongeza matundu ya vyoo ili kukabiliana na uhaba uliopo
xii. Kujenga madarasa mengine ili kutatua upungufu wa madarasa uliopo
xiii. Kujenga Ofisi ya Waalimu ambao wanatumia darasa kama Ofisi
101
xiv. Kumalizia kupaka rangi katika sehemu ya juu ya madarasa
xv. Kumalizia ujenzi wa nyumba za waalimu mbili za muda mrefu
xvi. Kujenga ngazi (ramph) vyooni kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum
5.15 Ujenzi wa mfereji wa dharura wa maji na
d) Utekelezaji
Ujenzi umekamilika na mradi unatumika
e) Changamoto
v. Baadhi ya maeneo ya mradi kutitia
vi. Kutokuwapo kingo zinazoweza kusaidia usalama wa wananchi (mfefreji
una kina kifefu kiasi kwamba mtu akitumbukia kwa bahati mbaya
atavunjika vibaya).
vii. Kuwapo kwa nyufa katika baadhi ya maeneo ndani ya mfereji.
viii. Kutokuwapo kwa sehemu ambazo wananchi wanaiweza kupita (mfereji
umejengwa bila kuzingatia kuwa kuna watu wenye nyumba na
wanafanya biashara pembeni.
f) Maoni
v) Kufanya marekebisho ya sehemu zinazotitia
vi) Kujenga kingo ili kuimarisha usalama wa wananchi
vii) Kufanya ukarabati katika mfereji (kuziba nyufa)
viii) Kujenga sehemu za kupitia wananchi/ wafanya biashara.
5.16 Mradi wa Maji katika Shule ya Msingi Kijaka
a) Utekelezaji.
Mradi umetekelezwa na Ufadhili wa Watu wa Kuwait. Aidha, mradi huo
umeshaanza kutumika
b) Changamoto
vi) Wataalam wa Halmashauri kutoshiriki katika utekelezaji;
vii) Kutokuwepo (distribution point) katika eneo la shule. Maji hayafiki chooni
viii) Kuwapo kwa tanki dogo la lita 2000 ambalo halikidhi mahitaji ya shule
ix) Kuwapo kwa matundu machache ya vyoo. Lipo tundu moja tu la choo
x) Uhaba wa vyumba vya madarasa hali inayopelekea darasa la tatu na la
tano kutumia chumba kimoja
102
c) Maoni
viii) Wataalam wa Halmashauri kushiriki kikamilifu katika Utekelezaji
wa Miradi ya maendeleo;
ix) Kujenga (distribution point) katika eneo la shule
x) Kujenga tanki kubwa ili kukidhi mahitaji ya shule na majirani
xi) Kujenga matundu ya vyoo ili kukabiliana na upungufu uliopo
xii) Kujenga vyumba vya madarasa ili kila darasa liwe na chumba cha
kujifunzia
xiii) Halmashauri kufanya usimammizi wa miradi ya wafadhili na kutoa
ushauri wa kitaalam
xiv) Idara ya Elimu ishirikiane na idara ya Maji katika ujenzi wa miradi
ya maji ya wafadhili mbalimbali ili kujenga mradi bora.
103
Ujenzi wa jengo la wazazi zahanati ya kisarawe II.
Vitanda vya kujifungulia kina mama katika zahanati ya kisarawe II.
105
Kisima na Pump za Mradi wa maji wa Kisarawe II
Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya msingi Kisiwani
107
Ujenzi wa shule ya mpya ya msingi Mikenge Kata ya Kimbiji
Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Mwongozo
108
6.0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA
JIJI LA DAR ES SALAAM
5.1 Ukarabati wa ukumbi wa Karimjee:
Utangulizi:
Timu ya ukaguzi ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilitembelea miradi ya
maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
tarehe 26 Mei, 2017. Miradi iliyotembelewa ilikuwa ni ukarabati wa
ukumbi wa Karimjee na Ukarabati wa Miundombinu wa Kituo Kikuu cha
mabasi Ubungo.
a) Utekelezaji:
Shughuli zilizofanyika katika ukarabati wa ukumbi wa Karimjee zilikuwa ni
kubomoa, kujenga na kurekebisha sehemu zote chakavu kama vile
madirisha, milango kuziba sehemu za bati zinazovuja, kuweka celling
zilizoharibika, kukarabati mfumo wa maji, kukarabati mfumo wa vyoo,
kufunga viti vya kukalia na kuweka zulia jekundu na kupaka kuta rangi.
Kazi ya ukarabati ipo hatua ya mwisho kukamilika.
b) Changamoto
Maeneo mengine ambayo hayakuwa katika makisio ambayo ni
machakavu kujitokeza kwa ajili ya ukarabati hivyo kuongeza gharama za
ziada na muda wa ukarabati.
c) Maoni
i) Upembuzi yakinifu uwe unafanyika kabla ya kufanya makisio ili
kuepuka gharama za ziada.
ii) Umaliziaji wa maeneo mengine ufanyike kwa umakini ili kuhakikisha
upakaji rangi hauathiri maeneo ambayo hayatakiwi kuchafuliwa na rangi
mfano vishikio vya taa, matundu ya kutolea hewa na nakshi iliyowekwa
kwenye madirisha.
iii) Maamuzi ya kulipa gharama za ziada yafanyike haraka ilikukamilisha
mradi kwa wakati.
109
Picha Na.1: Upakaji rangi, uwekaji wa viti vya kukalia na karpeti katika
ukumbi wa mikutano Karimjee.
6.2 Ukarabati wa maegesho ya mabasi katika kituo cha Ubungo
a) Utekelezaji
Kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo kinahudumia wasafiri wa kuingia na
kutoka mikoani na nchi za jirani ya Tanzania. Inakadiriwa zaidi ya watu
500 wanaingia na kutoka kila siku, hivyo wanahitaji kupata huduma
mbalimbali ikiwa ni pamoja na miundombinu rafiki ya maegesho ya
mabasi, sehemu za kupumzikia abiria, huduma za vyoo na huduma za
afya.
i) Ukarabati unaendelea kufanyika katika baadhi ya maeneo ya
maegesho. Nusu ya sehemu ya maegesho imekamilika
ii) Taa za usalama ndani ya Kituo zimewekwa
iii) Ukarabati wa vyoo vya umma umefanyika
b) Changamoto
i) Eneo kuwa na uwanda wa maji (water table) ulio wa juu na kufanya ukarabati kuwa ngumu.
ii) Mvua zinazoendelea kunyesha zimefanya ujenzi kuchelewa kukamilika kwa wakati
110
iii) Bado maeneo mengi ya ukarabati hayajafanyiwa ukarabati iv) Kuwepo kwa mashimo katika njia za maegesho ya magari hivyo
kusababaisha kutuama kwa maji.
c) Maoni
i) Ukarabati uharakishwe kwani wingi wa magari yanayotumia
maegesho haya yatasababisha uharibifu wa kuwa mkubwa zaidi
hivyo kuongeza gharama.
Picha Na.2: Maeneo ambayo bado hayajakarabatiwa eneo la maegesho
ya mabasi kituo kikuu cha Ubungo.
ii) Kituo kina sehemu ambayo inaweza kutumika kuweka Zahanati.
Halmashauri ya Jiji na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakae
wazungumze wajue namna ya kuanzisha Zahanati katika kituo cha
Mabasi Ubungo
iii) Huduma ya choo iboreshwe ili pawepona vyoo vingi zaidi
111
iv) Halmashauri ifanye maamuzi haraka na kutoa fedha kwa kazi
zilizoongezeka
Picha Na.3: Maeneo ambayo bado hayajakarabatiwa eneo la maegesho ya mabasi
kituoni.
63
ORODHA YA WALIOSHIRIKI KATIKA UGAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZWA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZA MKOA WA DAR ES SALAAM HADI KUFIKIA ROBO YA TATU YA
MWAKA 2016/17
NA. JINA CHEO
1. Theresia Mmbando Katibu Tawala wa Mkoa
2. Yokobety N. Malisa Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu
3. Edward A. Otieno Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji
4. Mary P. Assey Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Serikali za Mitaa
5. Michael Ole Mungaya Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu
6. Lawrence Malangwa Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu
7. Eng. Elizabet Kingu Katibu Tawala Msaidizi Maji
8. Mbaraka M. Kumenya Afisa Ugavi Mkuu
9. Rogasian E. Kimaryo Mchumi Mkuu
10. Upendo Charles Afisa TEHAMA Mwandamizi
11. Athumani Mayunga Mchumi
12. Oble F. Mongi Mtakwimu
13. Given Sure Afisa Maendeleo ya Jamii
14. Esterine Sephania Afisa Maendeleo ya Jamii
15. Issaya Mngurumi Mshauri Sekretarieti Ya Mkoa
16. Josephat N. Shehemba Mhandisi Ujenzi
17. Gilbert Bakula Mkadiriaji Majengo
18. Gratius Haule Mhandisi Maji
19. Eng. Mussa Natty Mshauri Sekretarieti Ya Mkoa
20. Bernadetha Thomas Afisa Elimu Mkuu
21. Jumanne Ndaigeze Afisa Biashara Mkuu
22. Hilda Kigoda Msanifu Ramani
23. Vicenti Mseti Mhasibu
24. Forunatus M. Kagoro Mshauri Sekretarieti ya Mkoa
25. Sister Mathew Katibu wa Afya Mkoa
26. Ackim Mwaikasu Afisa Afya
27. Mussa B. Abdallah Mhandisi Maji
28. Mambo Gunze Afisa Ugavi
29. Damsoni Mlashani Afisa Ugavi