jarida litolewalo na; banana investments ltd · mhariri mkuu 0717 350 971 emanuel nevava mjumbe...

8
HALIUZWI Toleo la 21 April - June TOLEO NAMBA 21 HALIUZWI APRIL— JUNE Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd

Upload: others

Post on 29-Aug-2019

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

TOLEO NAMBA 21 HALIUZWI APRIL— JUNE

Jarida litolewalo na;

Banana Investments Ltd

Page 2: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

2 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

BODI YA WAHARIRI

Beatha Anthony

Mhariri Mkuu

0717 350 971

Emanuel Nevava

Mjumbe

0756 601 830

Augustine Minja

Mwenyekiti

078 5451 004

Gerald Lyimo

Mjumbe

SALAMU ZA MHARIRI

YALIYOMO

WATU NA MATUKIO

Ilikua ni siku ya Alhamis tarehe 5/5/2011 yalisikika

matatumbeta katika kijiji cha Oloirien, pale Bi Tecla aki-

tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari wa Golden Rose ambapo wazazi wake alikua wamemuan-

dalia tafrija kwa ajili ya kumuaga kwenda kuanza maisha

ya kifamilia na Bw. Godbless Msuya wa Moshi. Baada ya sherehe hizo

siku ya Jumamosi tarehe

7/5/2011 ilifanyika ibada ya ndoa takatifu katika kanisa la

KKKT CKMC Moshi na

kufuatiwa na sherehe zilizo-

fanyika ukumbu wa chuo cha Ushirika hukohuko Moshi.

Bwana harusi ni Af-

isa masoko wa TBL na Bibi harusi ni Afisa Ugavi wa Ba-

nana Investments Ltd.

Imeandikwa na

Beatha Anthony.

Ni mara nyingine tena toleo la Mbiu ya Banana li-

natoka na kwa habari mbalimbali. Toleo hili

tumeweka habari kutoka mikoa mbalimbali ambayo

kampuni yetu inasambaza bidhaa zake. Hii ni

kuonyesha kwamba kampuni inawajali wateja wake

wote popote pale walipo. Tungependa sana kupokea

makala kutoka kwa wateja wetu. Pia tunashauri

kwamba makala hizo ziwe fupi na pia kwa namna

moja au nyingine zihusiane na kampuni.

Kwa wale wateja wetu ambao wataandika makala

yao wazitume kwa kupitia magereva wetu wa

Mauzo au wasambazaji. Pia unaweza kuleta hapa

kiwandani na ukakabidhi mapokezi.

Makala itakayochapishwa kwenye jarida mwandishi

atalipwa kiasi cha shilingi 10,000/=.

Tunatumia tena nafasi hii kuwakarisha katika kam-

puni ya Banana Investments Ltd watengenezaji na

wasambazaji wa mvinyo halisi wa Ndizi.

Kwa mawasiliano zaidi tumia namba za simu

zilizopo ukurasa wa mwisho wa Jarida hili.

1.MAONI YA MHARIRI…………………………………….02

2. HABARI KUTOKA SINGIDA …………………………...02

3. BANANA SPORTS CLUB YAJIPANGA UPYA ………..03

4. KAMPUNI YABORESHA MASOKO…………………….03

5. SAFARI YANGU YA LOLIONDO……………………….03

6. KAMPUNI YASHIRIKI MEI MOSI 2011………………...04

7. BOHARI MPYA YAFUNGULIWA MOROGORO ……...05

8 HABARI HUTOKA BOHARI YA DSM…………………..05

9. MPANGO WA KAMPUNI KUSAFISHA MAJI TAKA… 06

10. DONDOO MUHIMU ZA UNYAJI WA VILEO ……….. 06

11. AJIRA MPYA NGUVU MPYA…………………………..07

12. Y’S MEN ARUSHA WAPOKEA UGENI KUTOKA

GENEVA……………………………………………………...07

BI TECLA EDUARD, AFISA UGAVI APATA MWENZA

Page 3: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

3 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

Miongoni mwa wanafalsafa maarufu duniani ni Mgiriki Socrates.

Kwa wale wanaosoma na kufuatilia maisha ya wanafalsafa wa kale hapa duniani, huenda watakuwa wanajua kuhusu ndoa ya

mwanafalsafa huyu maarufu.

Wanaofuatilia maisha ya wanafalsafa hao watakubaliana nami kuhusu mke wa Socrates. Watu au wenzake Socrates walipokuwa

wanamuuliza kuhusu mke wake, wakitegemea kusikia akila-

lamika, kwa sababu mama huyu alikuwa na ghubu sana, hawa-

kusikia malalamiko yoyote. Badala yake aliwauliza, ‘mnataka

kujua yukoje kwa kulinganisha na nini? Ni hivi, iwe ni kwa watu,

maeneo, hali, matukio, na hata hisia zetu vyote hivyo havina

maana yenye kulingana kwa watu wote. Vyote hivyo ni vizuri au

vibaya kwa viwango kwa kutegemea tunavilinganisha na nini.

Hebu tuchukue vikombe vya aina moja, kama kimoja kimeben-

duka, tunaweza kusema hakiko kamili. Ni rahisi kusema hivyo

kwa sababu, tuna mahali pa kulinganisha, ambapo ni kwenye vile

vikombe vingine vizima. Kwa binadamu hali ni tofauti kabisa,

kwa sababu wote ni tofauti.

Hebu fikiria kuhusu tukio fulani kwenye maisha yako. Lakini

bado kuna swali, kwa kulinganisha na tukio lipi? Kila tukio lina-

tokea mahali pake, muda wake na kwa sababu fulani ili maisha

yaendelee kuwepo. Kwa nini kama ni hivyo udhani tukio fulani ni baya au zuri? Huu ubaya au uzuri ni kwa kulinganisha na tukio

lipi wakati kila tukio lina mahali, muda,na sababu ya kutokea

kwake?

Tunaambiwa kwamba kila jambo ambalo linaingia kwenye

mfumo wetu wa kufikiri ni vizuri au vema likawa limepimwa

kwa mujibu wa tafsiri zetu ambazo hazipaswi kutuumiza. Unaona

jambo ambalo linataka kukuumiza kihisia, ni kwa nini usijiulize

kama jambo hilo ni baya, ni kwa kulinganisha na lipi?

Kumbuka ni lazima kuwe na mahali ambapo tunasimama ili

kupima uzuri au ubaya wa jambo kwa kulinganisha na mengine,

ambayo kwa kawaida hayatarajiwi kubadilika.

Kama yanabadilika, basi ni vigumu kusema kuwa ni mabaya au

mazuri, kwani hatuna mahali pa kuyalinganisha. Kama vikombe

vinavyofanana kabatini vingekuwa wakati mwingine kimoja ki-

nakuwa kirefu kingine kifupi au kinabadilika rangi, tusingeweza kuvilinganisha pia. Binadamu kila mmoja ana haiba yake, kila

mmoja ni yeye kwa tabia, mienendo na hata miili.

Na, Peter Mapunda.

Baada ya kimya kirefu sasa ile Club maarufu ya

Banana imeanza kujipanga upya ili kuendeleza

shughuli za michezo na utalii wa ndani na nje ya

nchi.

Ili kuhakikisha kuwa mipango yake yote

inafanikiwa Club hiyo inatarajia kufanya uchaguzi

wa viongozi katika ngazi za Mwenyekiti, Katibu,

Mweka hazina na wajumbe wane.

Viongozi hao wanatarajiwa kuwa wabunifu hasa

kwa kuanzisha miradi itakayoongeza kipato cha

Vlubu na kukusanya ada za wanachama kwa wa-

kati.

Pia Club hii inatarajia kuingia ubia na Club ya

Genuine Sports Club iliyopo maeneo ya Kijenge

Backdad kwaajili ya kufanya mazoezi ya viungo

ya kunyanyua vyuma na Aerobics.

Wanachama wanaombwa kuwa tayari kulipa ada

zao za mwezi ili kuwezesha mipango yote hii.

Imeandikwa na

Adrian Anthony

BANANA SPORTS CLUB YAJIPANGA UPYA KAMPUNI YADHAMIRIA KUBORESHA MASOKO

Katika kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, kampuni imesogeza

huduma zake kwa karibu zaidi katika mikoa ya Kilimanjaro,

Manyara na Dodoma.

Hii ni pamoja na kuajiri wawakilishi wa masoko katika

mikoa hiyo. Wawakilishi hao ambao wameanza kazi ya rasmi mwezi wa tano, 2011 pamoja na mambo mengine wa-

tasikiliza na kutatua matatizo mbalimbali ya wateja, watatoa

fursa kwa wateja wapya watakaokua tayari kufanya biashara na kampuni yetu pia kuhakikisha kwamba bidhaa zetu zi-

nafika kwa wateja kwa wakati unaotakiwa.

Wawakilishi hao ni

1. MANYARA

Patrice B. Menda - Namba ya simu 0754 299529

0785 945067

2. DODOMA

Denis Kessy- Namba ya simu 0713 778958

0762 966988

3. KILIMANJARO

Tumaini A Mungete Namba ya simu 0754 299529

0688 299529

0715 229529 Kwa wateja wetu waliopo maeneo hayo wawasiliane na

hawa wawakilishi ili waweze kupata huduma kwa haraka

zaidi.

Imeandikwa na

Emanuel Nevava

NI M’BAYA KWA KULINGANISHWA NA NINI HASA?” Kuna mengi tusiyoyajua!

Page 4: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

4 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

KAMPUNI YASHIRIKI MAONESHO SIKUU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI

Kampuni ya Banana Investments Ltd imekua iki-

shiriki maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi za

Mei Mosi kwa miaka mingi. Na kila mwaka huibuka

na ushindi mnono. Mwaka huu vilevile kampuni

imejinyakulia makombe mawili ikiwa ni pamoja na

mashindano ya maandamano ya miguu na naonesho

ya bidhaa kwenye maandamano ya magari.

Katika kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanapon-

geza uongozi wa kampuni uliandaa tafrija fupi iliyo-

fanyika katika ukumbi wa kampuni mara baada ya

sherehe ya uwanjani. Karika tafrija hiyo ambayo ili-

jumuisha wafanyakazi tu, mkurugenzi mkuu alitoa

hotuba fupi akiwashukuru wafanyakazi wote kwa

moyo wao wa utendaji pamoja na kushiriki katika

maonesho hayo. Pia aliahidi kuwa kampuni

itaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wafanya-

kazi kwa uaminifu na kuomba pia wafanyakazi won-

yeshe uzalendo na uaminifu katika kufanya kazi za

kampuni. Pia aliwatakia sherehe njema ingawa na

yeye pia alikuwepo mpaka mwisho wa tafrija.

Baada ya hotuba ya Mkurugenzi mtendaji wafanya-

kazi waliendelea kupata chakula na vinywaji na

baadae lilipigwa disco la nguvu na Dj Rogaa.

Sherehe iliisha salama na kila mfanyakazi kurejea

nyumbani.

Imeandikwa na

Beatha Anthony

Maandamono ya Magari yakiongozwa na Pikipiki za kampuni

Magari ya Maonesho ya kampuni yakipita mbele ya mkuu wa

Mkoa yakiwa yamepambwa vizuri.

Mkurugenzi msaidizi akikabidhiwa ngao ya ushindi na mkuu

wa Mkoa.

Wafanyakazi wakiburudika na kinywaji na Muziki.

Page 5: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

5 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

Maendeleo ni hatua. Banana Investsments Ltd imepiga

hatua moja kati ya hatua nyingi, ya kufungua bohari

mjini Morogoro ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa

wateja wake. Bohari hii ipo maeneo ya Kihonda Ma-

gorofani Polyester Club mkabala na Carmel/Kanisa

Katoliki.

Wateja wa mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani sasa

watahudumiwa vizuri kutokana na uwepo wa bohari

hii. Kampuni inakaribisha maoni, ushauri na mawa-

kala maeneo ya Turiani, Kilosa, Ifakara, Morogoro

vijijini, na Mahenge. Wasiliana na afisa masoko Mi-

chael Emanuel kwa maelezo zaidi.

Fika ofisini au: Simu:

0713791119/0788791119/0759980851

Email: [email protected]

RAHA: RAHISI: HALISI. BIDHAA BORA YA BANANA

INVESTMENTS LTD - ARUSHA

BOHARI MPYA YAFUNGULIWA MOROGORO

HABARI KUTOKA SINGIDA

Picha: Jengo ambalo linatumika kama bohari kabla

ya marekebisho. Polyester Club Kihonda.

Baada ya kampuni kuanzisha utaratibu wa kutoa huduma

mojakwa moja kwa wateja wake, sasa wananchi wa Mkoa

wa Singida wanafurahia huduma hiyo kwani wanapata bid-

haa yetu hususani Raha kwa bei nzuri inayo wawezesha

kupata faida nono.

Kampuni kwa kushirikiana na wasambazaji

wake wanefanya upatikanaji wa kinywaji cha RAHA ku-

wepo na pia kuhakikisha kwamba bei yake inamuwezesha

hata mwananchi ya kawaida kuweza kununua.

Kampuni kupitia muwakilishi wake aliyeko

mkoani Singida Ndg Frank Joseph Urio inakaribisha

ushauri,maoni, kutoka kwa wateja mbalimbali katika

kuboresha biashara yake kwa faida ya wateja na kampuni

kwa ujumla. Mwakilishi wetu sasa anapatikana kwenye

ofisi iliyoko eneo la Shule ya Msingi Mughanga chumba

namba 23, Au wasiliana nae kwa simu namba 0754

607715, 0786 607718.

Imeandikwa na

Frank Joseph Urio

TANZIA

Kampuni ya Banana Investments Ltd unasikitika kutan-

gaza vifo vya wafanyakazi wawili wafuatao:-

Bi. Editha Joachim alifariki tarehe 03.02.2011 na

kuzikwa tarehe 08.02.2011 nyumbani kwake Moshono - Arusha. Bi Editha ali-

yekuwa anafanya kazi katika Idara ya

Uzalishaji ameacha mtoto mmoja na waju-

kuu wawili. Mungu ailaze roho ya Mare-

hemu Editha mahala pema peponi Amina.

Bw. Uhuru Kawiche alifariki tarehe 15.05.2011 na

kuzikwa tarehe 19.05.2011 nyumbani kwake Marangu

Mamba mkoa wa Kilimanjaro. Bw.

Uhuru alikuwa anafanya kazi katika

Idara ya Uzalishaji. Bw. Uhuru ameacha

mke pamoja na watoto. Mungu ailaze roho ya Marehemu Uhuru mahala pema

peponi Amina.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA

BWANA LIHIMIDIWE

Imeandikwa na Joan Mrema

Page 6: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

6 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

DONDOO MUHIMU ZA UNYWAJI SALAMA WA KILEO “ALCOHOL”

Kileo ni kitu chochote kinacholevya kilicho katika

mfumo wa bia, mvinyo, ama spirits. Jamii yote

duniani iwe Africa, Ulaya, Asia na hata Amerika, ime-

kuwa na aina yake ya kileo kulingana na utamaduni

wake. Wengi wameathirika kutokana na kutozingatia

njia nzuri za unywaji salama. Umri wako unaruhusu?

Kama una miaka chini ya miaka 18, USIJARIBU NA

ACHA KILEO. Hapa chini ni dondoo muhimu ku-

husu unywaji ulio salama:

Uhalali wa kinywaji chenyewe; Kila kinywaji kina

utaalamu wake unaokubalika kwa mnywaji ku-

toka kwa mamlaka husika. Tanzania tuna mam-

laka inayoitwa TBS-hawa ni wataalamu wa vi-

wango nchini na TFDA ni wataalamu wa vya-

kula na madawa. Kinywaji chako hakikisha ki-

meruhusiwa na kupewa nembo ya TBS kwa

usalama wa afya yako

Fahamu kiwango chako. Kama wewe ni mnywaji wa

Raha kwa mfano, kwanini leo unywe Raha + bia

+ viroba? Ni hatari kuzidisha kiwango cha kileo.

Kwa sababu huwezi kubaini kiasi ulichokunya

kwa urahisi.

Daima zingatia chakula kwanza kabla ya kileo/

pombe. Watalamu wanashauri ule vyakula

vyenye protini mfano nyama, samaki, jibini

’cheese’ kwa kuwa vyenyewe vinauwezo wa ku-

punguza kasi ya kileo kuingia katika mzunguko

wa damu kukuepusha na madhara.

Kubali kinywaji pale ukitakapo. Wengi wetu tume-

kuwa wataalamu wa ofa ya hapa na pale hata

kama mtu umetoka hospitalini leo ukiambiwa

“ebwana karibu tule vitu”, unavamia kileo. Je

nafsi yako ipo tayari? Kumbuka nafsi yako ni

muhimu sana kwenye maamuzi.

Epa kileo kama unatumia Dawa. Kama unaumwa na

unatumia dawa, acha kileo. Kama kuna umu-

himu sana wa kunywa, omba ushauri kwa

mtaalamu wa afya kwanza.

Epa unywaji ukiwa na njaa na kwenye joto kali

(juani). Wataalamu wanasema utapata kizungu-

zungu, udhaifu/legea, na kupoteza “mood” hali

iitwayo hypoglycemia,

Zingatia usalama wa maisha yako na wengine bara-

barani. Kama unajua utaendesha chombo cha

moto (gari, pikipiki hata baiskeli)

Zingatia unywaji wa maji. Kama ulipata kileo kiwe

kingi ama kidogo, shurti unywe maji mengi.

Unywaji wa kileo husababisha upotevu wa maji

mwilini kwa njia ya mkojo hivyo ukaribishaji wa

mning’inio “hang over” na kuumwa sana ki-

chwa. Dawa yake ni maji

Mwisho zingatia uchumi wako. Tunajua kuwa unap-

enda kunywa ila sasa uchumi wako unaruhusu?

Kinywaji unachotaka kunywa unamudu

kukinunua? Au unataka kunywa kwa mkopo,

upigwe, au kupewa ‘ofa’ daima huku familia

yako ikidhalilika?

Imeandikwa ma

Michael Massawe - Deport Incharge

Simu: 0713791119/0788791119/0759980851

Email: [email protected]

Morogoro

Page 7: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

7 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

Bw. Eliabu Joram –Machine Operator Bw. Eliabu ana cheti cha Technician in Mechanical Engineering

kutoka chuo cha Ufundi Arusha (ATC). Pia ame-

hitimu kidato cha IV katika shule ya Iyunga

Technical Secondary School. Ana uzoefu wa mi-aka 3 katika taasisi mbalimbali

Bw. Marko Andongolile – Machine Technician Bw. Marko ana Diploma ya Mechanical Engi-

neering katika chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Pia amehitimu kidato cha IV katika shule ya

Ifunda Technical iliyopo Iringa. Ana uzoefu

katika kazi hii kwa zaidi ya miaka 3 katika taasisi

mbalimbali.

Bw. Mohamed H. Luhindi – Auditing Technician Bw. Mohamed ana cheti cha Accountancy

Technician (ATEC II) kutoka National Board of

Accountancy and Auditing (NBAA). Pia na

Stashahada ya Elimu kutoka chuo cha Ualimu

Dar es Salaam. Na amehitimu kidato cha VI

katika shule ya Sekondari Union Islamic na

kidato cha IV katika shule ya Same Sekondari.

Bw. Tumaini A. Mungete – Marketing De-

velopment

Supervisor (Kilimanjaro Region) Bw. Tumaini ana Stashahada ya Biashara na utawala katika chuo cha Biashara (CBE). Pia

amehitimu kidato cha VI Kolila High School

Moshi na kidato cha IV Highlands Secondary

iliyoko Iringa. Ana uzoefu wa miaka 10 katika

taasisi mbalimbali.

Bw. Denis F. Kessy – Marketing Development

Supervisor (Dodoma Region) Bw. Denis ana Shahada ya juu ya biashara na

mahesabu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Pia amehitimu kidato cha VI Minaki High School

na kidato cha IV Uru Seminary.

Bw. Patrice M. Melley – Marketing Development Supervisor

(Manyara region) Bw. Patrice ana cheti cha Biashara katika chuo

cha Uchira Business College na cheti cha Auto

mechanics grade two VETA Dar es Salaam. Pia

amehitimu kidato cha IV Sarwatt Secondary

School na anao uzoefu wa miaka 10 katika

taasisi mbalimbali

.

AJIRA MPYA, NGUVU MPYA KAMPUNI YA BANANA

Y’S MEN ARUSHA WAPATA UGENI KUTOKA GENEVA

Klabu ya kimataifa ya Y’s Men imeendelea kujipatia umaarufu

mjini Arusha kutokana na shuhuli zao ya kijamii wanazofanya

kupitia wanachama wake waliopo mkoani hapo. Mnamo tarehe

12/04/2011 Klabu ya Y’s Men Arusha walipata ugeni mkubwa

kutoka makao makuu ya Taasisi hiyo iliyopo Geneva. Ugeni huo ulikua ni Mr Takao Nishimura ambae ni mtendaji mkuu wa

taasisi hiyo.

Pamoja na mambo mengine Mr Takao alitembelea kiwanda cha

kuzalisha Net aina ya Olyset cha A to Z ambao wanatengeneza

net zinazisambazwa na Y’s Men hii ni kufanikisha project ya

Y’s Men ya kuzuia Malaria (Roll Back Malaria). Pia katika

kuonyesha utendaji wake Mr Takao alishirikiana na wanachama wa Y’s Men wa Arusha kupanda miti katika eneo

la Mlima suye. Baadaye wanachama waliandaa chakula cha

jioni katika mgahawa wa Albero uliopo barabara ya Haille Sil-

las na kubadilishana mawazo na mgeni huyo.

Vilevile vijana hawakubaki nyuma kwani waliweza kutuma

muwakilishi katika Mkutano wa Jimbo la Y’s Men la kanda ya

Africa, kusini Mashariki. iliyofanyika Kitwe, Zambia na pia

walipokea ugeni kutoka Geneva ambae ni mtendaji mkuu Y’s

Youth Mami Hashikazi raia wa Japan. Katka Mkutano huu

Tanzania iliwakilishwa na Willy Kwayu wa Club ya Arusha.

Kutokana na changamoto zilizoonekana wakati wa mazun-

gunzo na wakeni hao Club ya Y’s Men Arusha pamoja na

Y’s Youth wamejipanga imara ili kuhakikisha wanatoa

huduma kwa jamii kulingana na mungu alivyowajalia.

Pia wanajipanga kuendesha mafunzo kuhusu TB na vilevile

kufungua rasmi club ya Y’s Youth ya Moshi. Kwa wale wata-

kaopenda kujiunga wawaliliane na Rais wa Club hiyo ambae ni

Miss Lucy Tesha Mob +255716395497 kwa upande wa vijana

na Mr Shanell Kavishe Mob +255717157128.

Na Beatha Anthon Mr Takao akipanda mti katika maeneo ya Mlima Suye.

Page 8: Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd · Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 ... pale Bi Tecla aki-tokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari

8 HALIUZWI

Toleo la 21 April - June

Makao Makuu Kiwanja Na. 311, Kitalu jj Oloirien Village, P. O. Box 10123, Arusha TANZANIA S i m u : +255754224440,+255272506475 E-mail: [email protected] .banana.co.tz

Dar es Salaam Depot Ubungo Kibangu, S. L. P. 79407, Dar es Sa-laam TANZANIA Simu: +255 222 774 276, +255 756 707 983 Email: [email protected]

Tanga Depot Barabara ya 4, S. L. P. 5150, Tanga TANZANIA Simu: +255 272 646 134

Email:

[email protected]. tz

Tunawakaribisha wafanyabiashara kujiunga na Kampuni yetu ya Banana Investments Ltd kusambaza kinywaji chetu kwenye mikoa am-bayo RAHA haijafika. Hali ya sasa katika usambazaji wa mvinyo wa Raha upo kama unavyoonyesha hapo juu kwenye Ramani

Morogoro Deport

Kihonda Area Simu +255713791119

+255788791119

+255759980851

Email:

[email protected]