je, mwalimu mzuri - twaweza teacher...21 22 kwa sababu tunakuwa waoga na wakimya na tunapoteza...
TRANSCRIPT
Je,
Mwalimu mzuri
ana sifa zipi?
Hakuna unyanyasaji
hapa!
TRV-Bk3
Jishindie kompyuta
ndani!
1 2
Baba, nani shujaa wako?
Shujaa?!Unamaanisha nini?
Shuleni tumeambiwa tuandike insha juu watu tunaowachukulia kama mifano ya kuigwa...wa kwako ni nani?
Mh! Hassan, wa kwangu ni mwalimu aliyenifundisha darasa la tano.
Mwalimu! Kwanini?
Alinisaidia sana kila niliposhindwa kuelewa...
3 4
...alikuwa mpole na hakuwa na ubaguzi.
Kweli?
Ndiyo, lakini alikuwa na msimamo sana!
Alitarajia nisome kwa bidii, hakuwa na msamaha kwa hilo.
Nilijitahidi kumheshimu siku zote!
Alinifanya niamini kuwa naweza kufanikisha chochote!
Kweli? Wakati mwingine waalimu wangu wananifanya nijione mjinga!
5 6
Hata mimi walimu wangu wengi walinitenda hayo, na ndio maana nilimpenda sana Mwalimu Jonathan.
Aliniheshimu siku zote.
Aliwahi kukuchapa bakora?
Oh! Nilichapwa na wengine, lakini mwalimu Jonathan hakuwahi kutumia kiboko.
Kweli?Kamwe hakuwahi. Nilijisikia vizuri siku zote kwenda kumuona, nilimwamini!
!"#$%&"'"%natamani mwalimu Jonathan angekuwa anafundisha shuleni kwetu!
7 8
Shule nzuri zina waalimu
wazuri kama
mwalimu Jonathan!
Mwalimu mzuri anaweza
kuwasaidia wanafunzi kukuza
uwezo wao!
9 10
Kwahiyo, Mwalimu mzuri ana sifa gani?
Mwalimu mzuri ana sifa nyingi...
Anatumia ubunifu katika kufundisha.
Anaelewa tunavyojifunza
Anahamasisha nidhamu inayojenga
Anatujali.
Anajivunia shule yetu.
Kutana na
walimu wetu
wazuri
11 12
Walimu wazuri ni kama mwalimu wangu.
MwalimuFortunata anatumia ubunifu anapotufundisha!
Anasisitiza uwezo wa kujieleza...
Jaribu rangi hii...
...anahimiza udadisi
()"*+*+%,*"#-+.+%/"0+*1+%hayastawi vizuri hapa?
13 14
...ananihimiza kuuliza maswali
Kwanini baadhi ya mimea inabadilika rangi na kuwa ya kahawia.
!!!"#$%&'%()($*+,"-,+,
Je, ni kwa sababu jua ni kali sana?
Au pengine hakuna maji ya kutosha?
...kujaribu mambo mapya
Oh, vitabu vipya! Sijawahi kuvisoma
na kujifunza kutokana na makosa
Ningejua ningeomba /2""1"%-,3+#-+"%vitabu
15 16
Mwalimu wako ni mzuri.
Mwalimu wangu, Mwalimu Shamim, ni mwalimu mzuri pia! Anaelewa namna tunavyojifunza!
Anaelewa kuwa, walimu hufanya mambo mengi zaidi ya kufundisha.
Unamaanisha nini?
17 18
Sikiliza, siku hizi wanafunzi wengi hujifunza kwa kukariri tu
Walimu wanategemea katika uandishi wa notisi nyingi.
Mwalimu analenga katika kutupatia taarifa,
Na sio namna taarifa hizo zinavyopokelewa
19 20
Mwalimu
anaamini kuwa
kama mwana‐
funzi haelewi,
au ameshindwa
mtihani, ni kwa
sababu hasomi
vya kutosha.
Mwalimu anapokasirika,
Wanafunzi hawa ni wavivu!
Hawaheshimu ufundishaji wangu!
Walimu wanaweza kutumia vitisho na aibu kwa wanafunzi kwa lengo la kuwahamasisha.
Hii inatuathiri kujifunza kwetu!
Kivipi?
21 22
Kwa sababu tunakuwa waoga na wakimya na tunapoteza mwamko wa kujifunza. Tunaanza kuamini kuwa sisi si wanafunzi wazuri.
Na hilo linaathiri hata maisha yetu ya baadae!
Kama huwezi kujifunza hii namna mpya ya kutunza /"042"',%%/5"-"%-,#-+"%wiki ijayo…
Siwezi kujifunza, sina uwezo kabisa!
Mwalimu mzuri anafahamu kwamba kujifunza ni zaidi ya kukariri!
Mwalimu mzuri anatusaidia kujua nini cha kufanya na taarifa...na sio kuzihifadhi tu katika akili zetu.
23 24
Mwalimu mzuri anatusaidia kujifunza katika hatua nne.
TAARIFA
Kuzielewa
Kuzichanganua
!"#$%&'%$
Kuzitumia
Kwanza, tunahitaji kuielewa taarifa.
Pili, tunahitaji kuzichanganua.
Kama ndizi 10 zinauzwa shilingi 300, ndizi 1 itauzwa shilingi ngapi?
tunahitaji kulinganisha na kile tunachokifahamu
tayari,
= Tsh. 300/=
= Tsh. 300/= = Tsh.?/=
25 26
Nataka ndizi 6, itakuwa shilingi ngapi?
Na kuchagua kile kinacholeta maana.
Ndizi 10 ni shilingi 300,
lakini nitakupa nusu kwa shilingi 200 tu.
Ninunue au?
.#/&0$/&"#1(/#2($%&/#'/(
Je kila mtu anauza ndizi kwa bei hiyo?
Nikitoa shilingi 150 nitapata ndizi ngapi?
Na kugundua maana ya taarifa hii
Kama nina shilingi 500, je nitanunua ndizi ngapi?
= Tsh. 300/= = Tsh. 400/=
27 28
Mwisho, tunahitaji kutumia ufahamu wetu
Ninahitaji kiasi gani cha fedha kila wiki kama ninataka kununua ndizi 10 kila siku? Tsh. 300/= x 7 = ?
Kuchukua tulichojifunza
Ningekuwa na akiba ya pesa kiasi gani kama ningenunua ndizi 5 kila siku badala ya 10? Ningezitumia pesa kwa ajili ya nini?
SOKONI
Na tafakari nini cha kufanya na hiyo pesa
29 30
Kujifunza ni
mchakato
unaohitaji
ujuzi.
Elewa
Changanua
(&'%$)
Tumia
Mwalimu mzuri ni yule anayesaidia wanafunzi kukuza stadi zinazohitajika katika hatua zote nne.
31 32
Hiyo ni namna bora ya kujifunza!
Ngoja nikwambie kuhusu mwalimu wangu, Mwalimu Jimmy...
Ni mwalimu mzuri kwasababu anasisitiza nidhamu inayojenga
Mwalimu Jimmy hachapi viboko kabisa!
33 34
Anatusaidia kujifunza kutokana na makosa
Unajisikiaje mtu anapoiba vitabu vyako? Utasomaje?
Anatufundisha kufanya maamuzi mazuri
Kwa sababu anajali maendeleo yetu
35 36
Na tunapofanya makosa, mwalimu Jimmy anatumia busara kutuelewesha tulichokosea
Stella, utawaomba msamaha wenzako kwa usumbufu, na nitahamisha kiti chako kuja hapa mbele.
Kamwe haogopeshi wala kudhalilisha mtu.
Unazidi kufaulu, insha yako ilikuwa nzuri sana!
Ana sheria na taratibu thabiti
Nategemea nyote mfuate taratibu hizi. Zinaeleweka?
SHERIA ZA DARASANI
1.Wahi mapema2.Heshimu wenzako3.Malizia mazoezi ya ziada - Asante! -
Na tunapovunja sheria, tunajua matokeo yake.
Stella, umechelewesha -"6+%7"-8%94*":%;"#-+.+%unazifahamu taratibu!
Ndiyo mwalimu, nitabaki baada ya muda wa shule na kuimalizia.
37 38
Mwalimu wenu ni mzuri
Ngoja nikwambie juu ya mwalimu wangu. Mwalimu Harriet, ni mwalimu mzuri pia!
Mwalimu Harriet ni mwalimu mzuri kwa sababu anajivunia shule yetu!
Anajivunia mazingira ya shule
TUPA TAKA HAPA
39 40
...na kazi yake pia.
ChetiMWALIMU BORA
MWALIMU HARRIETH
...ana uwezo mkubwa na daimahujiongezea ujuzi,
...anatafuta habari kila mahali,
Habari
...na kutumia akili yake kila wakati,
41 42
...anatoa mawazo yake na kujishughulisha darasani,
...kwenye utawala wa shule,
MKUU WA
SHULE Siku ya Michezo
Karibuni wazazi!
...kwa wazazi pia,
pamoja na jamii nzima!
43 44
!"#%2"*"<Mwalimu, Ahmed ni mwalimu mzuri pia. Ananijali!
Anatenga muda kwa ajili yangu. Anasikiliza matatizo yangu.
Pole Hassan! Kuna tatizo ="*+>%;?88%8#2+*+%,*+4@464:
Huwa anajitahidi kunisaidia
Unajisikiaje?
45 46
Yeye huwa hahamasishi mafanikio tu, bali juhudi pia!
Vizuri sana, Hassan! Unakumbuka muhula uliopita ulikuwa wa 22!
Matokeo ya Mitihani
Ananiheshimu...
Hassan, chukua hiki kitabu. Ninaamini utakirudisha.
Anapenda nifaulu...
Kazana! Unaweza!
47 48
Na anafurahia mafanikio yangu. Mwalimu Ahmed ni mfano bora wa kuigwa!
Kazi nzuri sana vijana!
Natamani niwe kama Mwalimu Ahmed nikiwa mkubwa.
49 50
Waalimu wazuri ni mashujaa wetu!!!!
51 52
Shule Nzuri ina Waalimu Wazuri!
Tunafundisha kwa ubunifu.
Tunaelewa jinsi wanafunzi wanavyopaswa kujifunza.
Tunahimiza nidhamu isiyo ya uoga.
Tunajivunia shule yetu!
Tunajali wanafunzi wetu!
Je, shule yenu ina Waalimu makini?
53 54
Je, utafanya nini ili kuwa mwalimu mzuri?
A%!"+1+"%)"*"B,*6+%-"9+-"%/,1"%)"%baada ya masomo!
A%C"*"B,*6+%)")4%3+5",/'4@4%37"-8$
A%D"/"2+20"%/"2)"@+$
A%E".+',%-,9,/+"%/'+*,%*7+*=+*4%6"+1+%ya mihadhara!
A%E+B,*64%/"/'8%/"57"$%
A%F*"*"%*"%)"6"6+$
A%C"58*=464%)"*"B,*6+%/"."%wanapojitahidi!
A%G2+9,/+4%-+'8-8$
A%G)4%/B"*8%)"%-,+=)"$
A%!0+.+-+20"%*"%?"1+@+%*"%)4*6"-8%kuhusu uzoefu wako wa kazi!
Namna ya kutumia kijitabu
hiki:
A%% F.810420"%2+B"%6"%/)"@+/,%'8."A%% H)"/'+4%."#-+%7"-8%",%/)"@+/,%%% mwenzio aandae orodha kama hiyo na kisha ifananishe na ya kwako. A%% !8/"%-+?+9"',%0+-+%5"/8?"%% % na walimu wengine au wanafunzi shuleni. Kisha jadili jinsi mwalimu bora anapaswa kuwa namna gani.%A% C""@+/,I%28/4*+%2404/,%/8?"%% % ya kijitabu hiki kila wiki wakati wa mkutano waalimu kisha jadilini jinsi ya kutekeleza mapendekezo haya.%A%% E"1+@+*+%J0"*="/898%6+*"68)46"%% % kujitokeza katika kufanikisha malengo haya. Kisha andaeni mbinu zinazoweza kusaidia kutatua hizo changamoto.%A%% C"*"B,*6+I%28/4*+%2404/,%/8?"%%% ya kijitabu hiki kila wiki pamoja na % ."#-+%64*,:%(+20"%?".+',*+% kubainisha waalimu wazuri katika shule yenu.
HJ08."?+%I%/".J89+'"2+/"K7"088:J8/
55 56
Toa maoni, shiriki na jishindie kompyuta!
Msomaji, Serikali yako inataka kukusikia! Shiriki kwa kutuma maoni yako. Mawazo yako yanaweza kuboresha huduma kwa jamii na utawala bora. Pia, hii itakuza ushirikiano kati ya wananchi na Serikali. Maoni yako yatahusiana na mafunzo uliyopata kupitia kitabu hiki. Kigezo cha kupata washindi ni ubunifu au wazo jipya.
Kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka 2012, maoni ya wanafunzi yatakayotumwa kupitia shule zao yatashindanishwa. Maoni kumi bora yatachaguliwa na yatachapishwa kwenye vitabu pamoja na tovuti. Kila shule itakayoshinda itapata kompyuta ndogo mbili ﴾laptops﴿.
Zawadi:
H)+208%)"%/"8*+%7"-8%)4-"%9"".+B"%6"-8I%
a﴿ Tareheb﴿ Majina kamili, umri wako na jina la shule/taasisic﴿ Jinsia Mwanaume/Mwanamked﴿ Anuani ﴾SLP﴿ kamili, makazi ﴾Kata, Wilaya, na Mkoa﴿e﴿ Simu yako na/au Barua pepe ﴾kama unayo﴿.
Unangoja nini! Shiriki basi kwa njia zifuatazo. L,/"%-)"I
M% &".,"I%FNO%P-,@,Q%!:R:O%STUV%W".%42%!"@""/M% &".,"%5454I%8=5K+-,@,:=8:96%au % %% %%%%%%%854*=8396K=/"+@:J8/M% L83,9+I%www.wananchi.go.tz
Fikiria. Paza Sauti. Twaweza!
Vibokohavina nafasihapa!
Mfano bora zaidi wa
kuigwa!
Hakuna unyanyasaji
hapa!
WAALIMU
(+9"',%0+-+%-+/4"*1"@+)"%*"I
Jadili na wenzio ulichojifunza humu ",%20+.+-+%/?"1"@"%-,5+9+"I
Twaweza_Nisisi
Twaweza Tanzania
www.twaweza.org www.raisingvoices.org