kanuni za imani za kanisa la kitume la kimataifa · 2 anuani ya makao makuu ya kanisa la kitume la...

54
Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa

Upload: phamdien

Post on 02-Mar-2019

386 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

Kanuni za Imani

za Kanisa la Kitume la Kimataifa

Page 2: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

2

Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa

S.L.P 4442

Addis Ababa, Ethiopia

S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

Page 3: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

3

YALIYOMO Utangulizi …………………………………………………………………………...4 Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa Kanuni ya 1: Biblia Takatifu …………………………………………………. 5 Kanuni ya 2: Mungu Mmoja wa Kweli Baba wa Wote …………..….7 Kanuni ya 3: Mwana wa Mungu …………………………………………...9 Kanuni ya 4: Roho Mtakatifu ……………………………………………….16 Kanuni ya 5: Jina la Bwana Linalookoa ………………………………..18 Kanuni ya 6: Mwito wa Wokovu kwa Ulimwengu ……………….. 20 Kanuni ya 7: Neema …………………………………………………………..21 Kanuni ya 8: Uumbaji wa Mwanadamu na Kuanguka Kwake …..23 Kanuni ya 9: Kuzaliwa Upya ………………………………………………..25 9:1 Toba ………………………………………………………………..28 9:2 Ubatizo kwa Maji ……………………………………………….30 9:3 Ubatizo kwa Roho Mtakatifu ……………………………….32 Kanuni ya 10: Kanisa ………………………………………………………….36 Kanuni ya 11: Huduma ya Kuwekelewa Mikono …………………….39 Kanuni ya 12: Uponyaji na Baraka za Mungu ………………………..42 Kanuni ya 13: Urejesho wa Walioanguka Kupitia Toba …………..43 Kanuni ya 14: Dhamiri ………………………………………………………..44 Kanuni ya 15: Utakatifu ……………………………………………………..45 Kanuni ya 16: Chakula cha Bwana / Meza ya Bwana …………....46 Kanuni ya 17: Kuoshwa/Kutawadha Miguu ………………………….48 Kanuni ya 18: Ndoa na Talaka …………………………………………….49 Kanuni ya 19: Sadaka na Zaka …………………………………………….50 Kanuni ya 20: Utawala ……………………………………………………...51 Kanuni ya 21: MWito Mkuu ………..……………………………………….52 Kanuni ya 22: Kunyakuliwa kwa Wateule …………………...………..53 Kanuni ya 23: Hukumu ya Mwisho ……………………………………….54

Page 4: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

4

Utangulizi “Akawaambia, ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya” (Luka 24:46-48). Haya ni maneno yaliyosemwa na Bwana Yesu Kristo kwa wanafunzi wake wa kwanza baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.

Kabla ya kupaa kwake aliahidi, “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi (Matendo 1:8).

“Imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yuda 3) ilizinduliwa siku ya Pentekoste na ujumbe wa Mtume Petro chini ya upako na uwezo wa Roho Mtakatifu (Matendo 2:14-47). Ilikuwa ni kwa Mtume huu kwamba Bwana Yesu Kristo aliahidi kumpa funguo za ufalme wa mbinguni (Mathayo 16:15-19).

Maandiko yafuatayo yanadhihirisha kwa dhati mamlaka ya mafundisho ya mitume wa Bwana Yesu Kristo (Mathayo 10:40; Luka 10:16; Yohana 15:16; 17:18-20; Marko 16:15; Luka 24:44-45; Matendo 10:39-42; Wagalatia 1:8-12; 1 Wakorintho 3:10-11; 2 Wakorintho 4:3-4; 1 Yohana 4:6; 1 Yohana 1:1-4; Waefeso 2:20; Ufunuo 21:14).

Kanisa la Kitume la Kimataifa linaamini na kufuata kikamilifu mafundisho na mazoea ya waandishi wa Biblia, manabii na mitume ambao wamefanya muhtasari katika kanuni ya imani ifuatayo:

Page 5: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

5

Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa

Kanuni ya 1

Biblia Takatifu Biblia inadai kuwa mwandishi wake ni Mungu. Ni neno lake lililopuliziwa. Umoja kamili na maelewano wa vitabu 66 vya Biblia unashuhudia msukumo wa Uungu (Isaya 34:16; 2 Petro 1:19-21, Yoshua 1:7-9; Mithali 22:20-21).

Kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, Biblia inathibitisha uhakika wake mwenyewe (Mithali 30:5-6; Ufunuo 22:18-19; Kumbukumbu la Torati 4:2).

Madhumuni ya msingi ya maandiko ni kudhihirisha Mungu mmoja wa Kweli wa milele, Baba wa viumbe vyote, na kuonyesha wanadamu njia ya wokovu (Yohana 20:31; Mathayo 22:29).

Hakuna wokovu nje ya Neno la Mungu lililoandikwa.

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.” (2 Timotheo 3:16).

Neno la Mungu ni uzima, uponyaji na chakula kwa ajili ya nafsi (Kumbukumbu la Torati 8:3; Mithali 4:20-22; Mithali 22:19-21; Yohana 6:63, 68; Zaburi 107:20; Kutoka 15:26; Matendo 5:20; Yeremia 15:16; Ezekieli 3:1-3; Mathayo 4:1-10).

Page 6: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

6

Kunukuu Biblia yenyewe: “Hakuna unabii katika maandiko upatao kutafsiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa hapo awali kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2 Petro 1:20-21).

Ufahamu wa maandiko unahitaji mwongozo wa roho wa Mungu (Luka 24:45; 1 Yohana 2:27; Zaburi 119:18, Isaya 28:9-11; Waefeso 4:11-12; 1 Wakorintho 12:1-28; Yakobo 3:1-2; Matendo 18:24-28; Matendo 8:29-35; Isaya 30:20-21; Yohana 14:26; Wagalatia 1:6-12; Yoshua 1:6-9; 1 Timotheo 4:13; Wakolosai 1:24-29; 1 Wakoritho 4:1-2; 2:9-14; Waefeso 3:1-6).

Page 7: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

7

Kanuni ya 2

Mungu Mmoja wa Kweli Aliye Baba wa Wote Kuna Mungu Mmoja tu wa Kweli na wa Milele, ambaye ni Roho na Neno, Muumba wa mbingu na nchi na viumbe vyote. Imani kwamba kuna Mungu mmoja tu inaendeshwa katika Maandiko Matakatifu ya Maagano yote mawili (Kumbukumbu la Torati 6:4; Marko 12:29; Kumbukumbu la Torati 4:9-24; 32:39-40; 1 Timotheo 6:15-16; Zaburi 33:6; Yohana 4:24; Zaburi 139:7-8; Isaya 66:1-2; Yeremia 23:23; Isaya 45:5-6; 48:12-13; Yakobo 2:19).

Hakuna Mungu mwingine badala yake, kabla au baada Yake, wala kama Yeye, na Yeye ni Mwokozi wa pekee (Isaya 43:10-12; 44:6-8, 24; 45:21-24; 46:8-9; 25:6-9; 1 Samweli 2:2; Isaya 40:18).

Mwanadamu aliye na kikomo hawezi kumfahamu Mungu asiye na mipaka na kuweka pamoja ufafanuzi kamili wa Muumba wake. Hata hivyo, sifa za Mungu au ukamilifu wake unajulikana kwetu sisi kwa njia ya ufunuo. Mungu asiyechunguzika humfunulia mwanadamu (Ayubu 26:14; Isaya 45:15), na orodha hii haiwezi kukamilika. Kwa kawaida anajulikana kama wa Milele (Zaburi 90:2; Mwanzo 21:33; Waebrania 13:8), mwenye mamlaka (Isaya 10:13-14), Mtakatifu (Mambo ya Walawi 11:44; Zaburi 99:3, 59; Isaya 40:25; Habakuki 1:12; Yohana 17:11; 1 Petro 1:15; Ufunuo 4:8; 1 Yohana 1:5); Asiyebadilika (Malaki 3:6; Yakobo 1:17), wa Milele (1 Wafalme 8:27; Matendo 17:24-28, Ayubu 36:26), Upendo (1 Yohana 4:8), Mwenyezi (Mwanzo 17:1, Kutoka 6:3; 2

Page 8: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

8

Wakorintho 6:18; Ufunuo 1:8; 19:6), aliye kila mahali (Zaburi 139:7-11; Yohana 3:13), mwenye maarifa (Matendo 15:18; Waefeso 1:11; Zaburi 135:6; Yohana 16:4; Waefeso 1:14), na Kweli (Yohana 17:3; Tito 1:2; Warumi 3:4; Waebrania 6:18; 1 Yohana 5:20-21).

Maandiko yanatukumbusha: “Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu?” (Malaki 2:10).

Nabii Isaya alitabiri, “Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake” (Isaya 25:9). Mlango wa wokovu ulifunguliwa kwa wanadamu wakati “Katika utimilifu wa wakati,” Mungu asiyeonekana na asiyegawanyika alijidhihirisha katika Mwana, kama “mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Isaya 7:13-14; 8:8; 9:6; 12:1-6; 53; 59:16-17; 52:5-7; Zaburi 118:22-24; Danieli 9:24; Waebrania 1:1:1-3; Wakolosai 1:12-15). Lile lililokuwako tangu mwanzo, Neno la uzima, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa (1 Yohana 1:1-4). Mungu Mmoja wa kweli alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake (2 Wakorintho 5:19; 1 Timotheo 3:16; Yohana 1:1, 14; 1 Timotheo 2:5; 1 Wakorintho 8:5-6; Mathayo 1:20-23; Luka 1:35; Warumi 9:5; Ufunuo 1:5-8, 17-18).

Maandiko yanatangaza, “Naye BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zekaria 14:9; Isaya 44:6; Ufunuo 1:8; 19:1-15; 21:3-7).

Page 9: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

9

Kanuni ya 3

Mwana wa Mungu Kuanzia na Mwanzo 3:15 hadi mwisho wa Agano la Kale, ahadi ya kinabii ya kuja kwa Mkombozi inabadilishana na tangazo la Mungu mwenyewe kuwa Yeye ndiye Mwokozi wa pekee. Biblia inatangaza kwamba Mungu “. . . Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia” (Isaya 59:16). Ukweli kwamba wokovu ni wa Mungu pekee unasisitizwa katika Maandiko kama Isaya 43:11: “Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi” (tazama pia Isaya 52:5-6; Zaburi 2:2-3). Wokovu wake unaenea duniani kote: “Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine. Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa” (Isaya 45:22-23; tazama Wafilipi 2:6-11; Isaya 7:13-14; Warumi 14:10-12).

Katika Injili yake, mtume Yohana alinukuu Yesu akisema, “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3; tazama pia 1 Yohana 5:20). Biblia inazungumzia “siri ya Mungu, yaani, Kristo; ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika” (Wakolosai 2:2-3). Ni madai ya Yesu mwenyewe kwamba “Hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia” (Luka 10:22; 1 Petro 2:6-7; Isaya 28:16).

Page 10: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

10

Kweli, “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” (Yohana 1:18). Hakika, ilichukua ufunuo kutoka kwa Mungu kwa Mtume Petro kuweza kutangaza, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai” (Mathayo 16:16-17).

Biblia inatangaza kwamba “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu . . . Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; (nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba;) amejaa neema na kweli” (Yohana 1:1-14; tazama Yohana 6:33-68).

Pia ni mafundisho wazi ya Biblia kuwa “Mungu alidhihirishwa katika mwili” (1 Timotheo 3:16). Mungu ambaye alidhihirishwa katika mwili hakuwa mwingine ila Mungu Baba Mwenyewe (Yohana 14:7-11).

Imeandikwa kwamba “Kila . . . wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia” (2 Yohana 1:9).

Yesu ni Mwana pekee wa Mungu (Yohana 1:14; 1:18; 3:16).

Bwana akasema, “Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa” (Zaburi 2:7). Na sauti kutoka mbinguni ilithibitisha, “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe” (Luka 3:22).

Kuzaliwa na bikira, ilitangazwa na Bwana kupitia nabii Isaya, ni kazi ya miujiza ya Roho Mtakatifu (Isaya 7:14,

Page 11: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

11

9:6; Luka 1:35; Isaya 53:1; Yeremia 31:22; Zaburi 118:23).

Jina Emanueli, lililotolewa na nabii kwa mtoto aliyezaliwa na bikira Mariamu, linatafsiriwa katika Agano Jipya kama "Mungu pamoja nasi" (Mathayo 1:21-23).

Yesu alisema kwamba Yeye “aliyeshuka kutoka mbinguni,” “Nalitoka kwa Baba,” na kwamba Yeye “ni wa juu; si wa ulimwengu huu” (Yohana 3:13, 31; 8:23-24; 16:28; 17:8),

Mtume Yohana aliandika, “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.” (1 Yohana 1:1-3).

Mwana wa Mungu alitangaza kwamba Yeye ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni na kuwa mkate ambao atatoa kwa ajili ya maisha ya ulimwengu ulikuwa mwili wake (Yohana 6:33, 45-51).

Mtume Paulo alibaini kuwa, “Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni” (1 Wakorintho 15:47).

Page 12: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

12

Mwili wa mbinguni ambao Mungu alidhihirishwa ndani yake uliandaliwa na Nafsi yake kwa ajili ya kazi ya maridhiano na ukombozi wa mwanadamu (Isaya 43:10-11; Isaya 53; Yeremia 31:22; Yohana 1:14; Wakolosai 2:9; 1 Wakorintho 15:47-49; Warumi 9:4-5; Waebrania 8:1-2). Biblia inatangaza kwamba, “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake” (2 Wakorintho 5:19).

Kulingana na Maandiko, “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu . . . Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:5-7, 10; Yohana 1:1-3, 9; 1 Yohana 4:3).

Mungu alinunua kanisa lake kwa damu Yake mwenyewe (Matendo 20:28; Warumi 8:3; 5:11; Ufunuo 1:5). Na Yesu alitangaza, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi” (Mathayo 26:28). Ukombozi wa roho ni wa thamani sana kwamba hakuna mbadala mwingine wa damu ya Mungu mwenyewe unaweza kuchukua dhambi za ulimwengu (Waebrania 7:26-28; Mathayo 20:28; Waebrania 9:11-12, 24-28; Zaburi 49:7-8). Kuna hatari katika kuaibisha Kristo na agano iliyoidhinishwa kwa damu Yake takatifu (Waebrania 10:29; Warumi 1:18, 12-23, 25).

Page 13: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

13

Maana imeandikwa, “Mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:10; 12:22). Maandiko pia yanasema, “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa” (1 Petro 3:18).

Hivyo, Mwana wa Mungu ni mwili ambao Mungu, Baba wa milele, ambaye ni Neno na Roho, alijidhihirisha nao ili kuharibu kazi za shetani na kutuokoa sisi kutoka katika nguvu za giza (Wakolosai 1:12-22; Yohana 1:1, 14; 1 Timotheo 3:16; 1 John 3:1-2, 5, 8; Wagalatia 1:3,4). Maana imeandikwa, “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Wakolosai 2:9).

Kristo aliitwa, “Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29). “Mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo” (1 Petro 1:10-11) ni mada kuu ya kati ya Maandiko (Isaya 53; Danieli 9:24, 26). Mtume Paulo aliandika, “Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu” (2 Timotheo 1:10-11) Akizungumza juu ya injili hii, alisisitiza “Nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, . . . ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko” (1 Wakorintho 15:1, 3-4; Wakolosai 1:23; Yohana 10:17-18).

Page 14: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

14

Kama Agano la Kale na Yesu Mwenyewe ilivyotabiriwa, Yesu alifufuka katika wafu siku ya tatu, bila kuona mauti, “Amemeza mauti hata milele;” (Mathayo 16:21; Yohana 2:19, 21; Luka 24:26, 46; Mathayo 28:5-9; Matendo 2:22-32; 13:29-37; 17:31; Warumi 1:3-4; 1 Wakorintho 15:12-22; 1 Petro 1:3-5; Isaya 25:7-8; 53: 10-12; 26:19).

Akizungumza juu ya Baba kwa wayahudi, Yesu aliwaonya, “Msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu” (Yohana 8:21-24)

Yesu alisema, “. . . Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. . . Aliyeniona mimi amemwona Baba; . . . Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe” (Yohana 14:6-11).

Mafundisho ya mitume pia yanakubaliana na madai ya Yesu: “Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.” Mungu ametupa uzima wa milele kwa njia ya Mwana Wake (1 Yohana 5:11-12; Yohana 3:16; 1 Yohana 5:20;

Page 15: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

15

Wakolosai 2:9; 1 Timotheo 3:16; Yohana 1:1-14; 1 Yohana 1:1-4; 2 Wakorintho 5:19; Waebrania 1:2-8; Wakolosai 1:15; Warumi 9:4-5).

Maandiko yanatuonya, “Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia” (1 Yohana 2:23).

Bila shaka, Bwana Yesu Kristo ndiye Mungu wa kweli pekee, Baba wa milele (Isaya 9:6), “Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1:8) na Muumba wa ulimwengu (Wakolosai 1:17; Waebrania 1:2; Yohana 1:1-3).

Katika ujumbe wake kwa kanisa Bwana Yesu Kristo alisema, “Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu” (Ufunuo 1:8, 17-18; Yohana 10:17-18).

Page 16: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

16

Kanuni ya 4

Roho Mtakatifu

Katika vitabu vya Agano la Kale, Sheria, Manabii na Maandiko ya Agano Jipya yanaungana kutoa msingi wa somo: kuna Mungu mmoja wa milele, ambaye ni Roho (Mwanzo 1:2; 3:8; Kumbukumbu la Torati 4:12, 15:19; Zaburi 139:7-8; Isaya 40:12-15, 18, 21-22, 25; Yohana 4:24).

Mafundisho ya Agano la Kale kuhusu Roho wa Bwana hutoa historia ya mafundisho ya Kikristo kuhusu Roho Mtakatifu, yalivyoelezwa katika Agano Jipya.

Mungu Mwenyezi, Muumba wa ulimwengu wote ambaye amekiri, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu” (Isaya 66:1), na “Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? . . .” (Yeremia 23:24) alijitambua hapo awali kwa mababu wa Israeli kama asiyeonekana, aliye kila mahali, Roho wa milele (Isaya 44:6-7; 45:5-6; 46:9; 48:12-13).

Viumbe vilifanywa hai kwa pumzi ya Mungu Baba (Zaburi 33:6; Ayubu 33:4; 34:14, 15), kwa kuwa Roho Mtakatifu ni pumzi ya Mungu ambayo hutiririka kutoka kwa nafsi yake na kuwapa viumbe vyote uhai. Katika kitabu cha Mwanzo, alipulizia mwanadamu pumzi yake ya uhai (Mwanzo 2:7). Bwana, aliye Roho, ni uzima wa milele kwa ufafanuzi (Yohana 1:1-4; 1 Yohana 1:1-3). Mungu hadumishwi na uhai nje ya nafsi Yake (Isaya 40:13-14; 45:10-11). Katika kumbukumbu zote za Biblia, Roho wa Mungu kamwe haonekani kama mwenye asili tofauti kutoka kwa Mungu. Roho

Page 17: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

17

wa Mungu ni pumzi yake itoayo uhai, uwepo wake binafsi na kimsingi Mungu Baba katika matendo kwa njia zenye nguvu na za ajabu. Yeye ni chanzo cha maisha kisicho na mwisho na amejieleza mwenyewe kama, “chemchemi ya maji ya uzima” (Yeremia 2:13), ambaye ameahidi kumwaga roho yake juu ya uzao wa Yakobo (Isaya 44:1-6; 59:21; 32:15).

Ilitabiriwa kwamba Mungu angeweza kubadili wanadamu katika siku za Agano Jipya kwa kuweka Roho wake Mtakatifu ndani yao, ili wapate kutembea katika njia Zake na kushika amri zake (Yeremia 31:31-34; Ezekieli 36:25-27). Hayo yalikuwa matumaini ya siku za mwisho, na haya yalikuwa matumaini ambayo Wakristo walikuwa wameona yakitimia kupitia ufufuo na kupaa kwa Yesu (Yoeli 2:28, 29; Matendo 2). Roho Mtakatifu, baada ya kumwagwa siku ya Pentekoste, alianza kuleta utakatifu katika watu wa Mungu (tazama Kanuni 9.3).

Page 18: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

18

Kanuni ya 5

Jina Linalookoa la Bwana

Kuwasilisha Agano lake Jipya, Mungu ambaye amekiri, “Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi” (Isaya 43:11; 45:20-21) alijidhihirisha katika mwili kwa ukombozi wa mwanadamu (Yohana 1:1-14; 1 Timotheo 3:16), na kuwa Imanueli, “Mungu pamoja nasi” (Isaya 7:14). Jambo hili lilifanyika wakati wa kutimiza Maandiko, Kristo alizaliwa na bikira Mariamu na akapewa jina la Yesu kwa kuwa, “yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21-23). Jina hilo, ambalo pia aliitwa “BWANA ni haki yetu” na nabii Yeremia (Yeremia 23:6), kwa hakika lilikuwa jina la Bwana mwenyewe linalookoa (Isaya 9:6; Mithali 30:2-4; Yohana 3:13; Isaya 52:6; 12:2-4; 62:2; Matendo 15:14-17; Malaki 1:11). Kwa maana imeandikwa, “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake” (2 Wakorintho 5:19; tazama Yohana 1:1, 14; Wakolosai 2:9; 1 Timotheo 3:16). Na kwa usahihi, Yesu mwenyewe alibainisha:

“Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu” (Yohana 5:43).

“Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu” (Yohana 17:6).

“Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo” (Yohana 17:26).

Rekodi katika Injili ya Mmoja atakayekuja kwa jina la Bwana na ufalme Wake (Marko 11:9-10) inarudia maneno ya unabii katika Zaburi 118:22-26, Mika 5:4, Zekaria 9:9 ambayo inalenga kwa Mungu, wokovu wetu.

Page 19: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

19

Kwa upatanifu na unabii wa Isaya, Agano Jipya inatangaza, “. . . Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba” (Wafilipi 2:9-11; Isaya 45:22-25). Chanzo cha mafundisho ya ukombozi, ambayo ni kiini cha imani ya Kikristo, ilikuwa kukiri Yesu Kristo kama Mtakatifu pekee wa Israeli wa Agano la Kale. Ufunuo wa jina la Mungu Baba linalookoa ni chanzo cha mafundisho ya wokovu ya Agano Jipya kama inavyosisitizwa na maandiko yafuatayo: “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Manabii, Bwana Yesu mwenyewe, na Mitume walishuhudia kwamba kuondolewa kwa dhambi ni kwa jina la Yesu, na kwamba wale ambao wanaamini ndani yake na kutii mafundisho ya kitume walipokea uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yohana 1:12; pia Luka 24:46; Matendo 2:38-39; Wagalatia 3:26-29; 1 Petro 1:23-25; 1 Yohana 2:12; Matendo 10:43; 1 Wakorintho 6:11). Kama wanafunzi wa Kristo (Wakristo), tunahimizwa kutumia jina hili takatifu la Mungu Baba katika sala, shukrani, kuabudu, na sifa: “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye” (Wakolosai 3:17; tazama Wafilipi 2:9-11; Yohana 14:13; 15:16; 16:23, 24, 26, Mathayo 6:9). Ubatizo katika jina la Yesu ni kuivua asili ya kale ya mwili wa mavumbi na dhambi zake zote na kuvaa utu mpya, ambaye ni Kristo (Wagalatia 3:27; Waefeso 4:22-24; Waefeso 2:1-3; Wakolosai 3:9-10; 2 Petro 1:4).

Page 20: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

20

Kanuni ya 6

Mwito wa Ulimwengu Kwa Wokovu

Mafundisho ya Wokovu ni mada maalum katika Maandiko. Inahusiana na wanadamu wote bila ubaguzi (Mathayo 22:9, 14; Warumi 10:12; Isaya 45:22; Isaya 55:1; Yohana 7:37; 1 Timotheo 2:4; Ufunuo 22:17), na kiini chake ni Bwana wetu Yesu Kristo. Yohana Mbatizaji alitangaza, “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29; tazama Yohana 3:1-15; 1 Timotheo 1:15-17; 2:6; Waebrania 2:9; 1 Yohana 2:2). Kutokana na mtazamo wa Mungu, wokovu unajumlisha kazi yote ya Mungu katika kuleta watu kutoka hukumu hadi kwa haki, na kutoka mauti hadi uzima wa milele, na kutoka kutengwa na kuchukuliwa kama watoto (Waefeso 1:4). Kwamba wokovu umetolewa kwa watu wote, hata kama mtu ataupokea au ataukataa, jambo hili linaonyesha kuwa Bwana Mungu afurahii kufa kwake mtu mwovu; (Ezekieli 18:25; 33:11) na hapendi mtu ye yote apotee (2 Petro 3: 9) Jambo hilo ni wazi katika amri ya mwisho ya Kristo (Matendo 1:8; Marko 16:8-20; Mathayo 24:9-14; tazama Isaya 45:5-13; Yeremia 1:4-19; Isaya 60; 61:1-9; 45:22-23; 66:18-19; 2 Wakorintho 5:14, 18-20).

Page 21: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

21

Kanuni ya 7

Neema

Neno “Neema” lina maana ya upendeleo usiostahili, au zawadi ya bure. Ni huruma usiostahili (Yeremia 9:23-24; Yohana 1:14-29; Waefeso 2:8), ushawishi wa Uungu juu ya moyo wa wale ambao wamepewa. Neema ya Mungu imedhihirishwa ili kuokoa na ikapewa wale ambao watakuwa wanyenyekevu mbele za Mungu na kuikubali kwa imani (Waefeso 2:8; Zaburi 34:18; Tito 2:11-12, Yakobo 4:6; 1 Petro 5:5).

Neema inatajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia katika Mwanzo 6: 8 ambapo ilitolewa kwa mtu mwenye haki, Nuhu, katika mfumo wa onyo ya hukumu inayokuja (Waebrania 11:7). Hii neema (ya ushawishi wa uungu ambayo ilionya kuhusu kuja kwa hukumu) ingekuwa haifai kwa Nuhu kama hangeamini onyo kuwa ilikuwa ni ya kweli na kwenda kwa hofu ili apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo, ni muhimu neema iambatane na imani, ambayo iinaonyeshwa kwa kutii. Nuhu aliokolewa kwa neema kwa njia ya imani (Waefeso 2:8-9). Kujenga kwake kwa safina haikuwa wokovu wake kwa matendo, lakini, kwa utii wake kwa neema, ambayo ni jibu sahihi ili neema ipate kuokoa. Huu ni “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1 Petro 3:20-21).

Bila ya ushawishi wa uungu wa neema moyoni, mtu hana njia yoyote ya kutii Injili kwa imani na kuokolewa (Matendo 18:27). Injili yenyewe ni ufunuo wa Uungu, na ni ushahidi wa neema ya Mungu (Matendo 20:24; Tito 2:11). Ili injili ambayo ilihubiriwa na

Page 22: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

22

mitume kuokoa, ni lazima ipokelewe na kuheshimiwa (1 Wakorintho 15:1-4; Warumi 6:16-18). Upatikanaji wa neema (kutumia neema katika hali zetu) inaweza tu kupatikana kwa imani (Waefeso 2:8), ambayo imeonyeshwa kupitia kwa matendo ya utiifu (Warumi 6:16-18; 16:25-26; Yakobo 2:18-26).

Kitendo cha kuja mbele za Mungu kwa moyo mnyenyekevu ili ubatizwe katika maji, au kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu, inaweza kuchukuliwa na baadhi kuwa matendo ya haki yetu wenyewe (Isaya 59:6; Waefeso 2:9; Tito 3:5; Warumi 10:3), hata hivyo, Biblia inaonyesha wazi tofauti kati ya matendo ya sheria na utii wa imani (Wagalatia 2:16; 3:1-14). Warumi 14:23 huenda mbali zaidi kwa kusema “...Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.” Ubatizo kwa maji, ubatizo wa Roho Mtakatifu, Jina la Yesu na damu yake, Neno la Mungu - haya yote ni zawadi ya neema ambayo haiwezi kununuliwa kwa bei (1 Petro 1:18-19, 23; 3:18-21; 2 Petro 1:2-3; Ezekieli 36:25-29; Mathayo 7:21-23; Warumi 10:3-8), inaweza tu kupokelewa na sisi na kutumika katika hali yetu kwa njia ya imani, ambayo ni dhihirisho letu kwa kutii neema (Yakobo 2:14-26).

Page 23: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

23

Kanuni ya 8

Uumbaji wa Mwanadamu na Kuanguka Kwake

Rekodi ya Biblia inatupa taarifa ya pekee iliyo sahihi kuhusu chanzo cha mwanadamu. Kwa mujibu wa simulizi la kitabu cha Mwanzo, “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7).

Adamu tangu awali alichukuliwa afananishwe na mfano wa Kristo (Warumi 8:29) Wakati Mungu, kwa wakati wake, alidhihirishwa katika mwili (Yohana 1:1-14; Waebrania 1:1-13), “Mfano wake usioonekana” kwa hakika ulionekana katika Kristo, ambaye ndani yake “unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Wakolosai 2:9; 1:15-16). Kwa hivyo, siri ya uumbaji wa mwanadamu ni picha kamili ya hatima ya mwanadamu ni wazi tu ikichukuliwa katika marejeo na masharti ya Agano Jipya (1 Petro 1:10-12). Kwa maana, mtu wa kwanza, Adamu, aliyeumbwa kutoka kwa mavumbi ya nchi, ambaye tangu awali Mungu alikuwa ameamua awe kiumbe cha milele katika sura na mfano wa Kristo, kushiriki tunda la “mti wa ujuzi wa mema na mabaya” (Mwanzo 2:17; 1 Wakorintho 15:47).

Maelezo ya kuanguka kwa mwanadamu katika Mwanzo sura ya tatu imethibitishwa katika Agano Jipya (1 Wakorintho 15:21-22; 1 Timotheo 2:14; Warumi 5:12-21). Dhambi ya Adamu huathiri jamii nzima ya binadamu. Kuanguka kuliathiri binadamu wote, na

Page 24: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

24

kuleta upotovu na mauti ya milele (Waefeso 2:1, 3; Warumi 3:9-10, 23; Wagalatia 3:22; Wakolosai 2:13; Zaburi 51:5).

Tunafahamu kutoka kwa maandiko kwamba Mungu, katika maarifa yake, alijua kuwa mwanadamu, kwa sababu ya udhaifu na asili yake ya dunia, angeshindwa na majaribu na kuvunja amri zake, kwa kuwa Biblia inazungumzia kuhusu “Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia” (Ufunuo 13:8). Kwa hiyo, Mungu alitimiza kama alivyoagiza hapo mbele mpango wake mkuu wa ukombozi kupitia kifo cha Mwana Wake, Yesu Kristo (Mwanzo 3:15; Warumi 8:1-3, 29, 30; Waefeso 1:4-12; Tito 3:4-8; Waebrania 1:1-3).

Page 25: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

25

Kanuni ya 9

Kuzaliwa Upya

Kristo, mwenyewe ni mwanzilishi na mwenye kutimiza imani yetu; alikuwa wa kwanza kueleza masharti ya kuingia katika ufalme wa Mungu kwa kuifunua siri ya kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:1-8). Akifundisha Nikodemo umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili, Yesu alisema, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” (Yohana 3:5).

Mafundisho ya Yesu na Mitume wake yalionyesha Kuzaliwa Upya ambayo hatimaye ingeweza kubadilisha wana wa Adamu katika "mfano na sura ya Mungu", ya kweli na kufanya uwezekano wa mpito kutoka asili iharibikayo, kwa asili ya dhambi iliyorithiwa kutoka kwa Kuanguka, kwa hali isiyoharibika ambayo ilikuwa tangu asili wafananishwe na Mungu (Warumi 8:29-30; Yohana 3:3-8; Yohana 1:12; Tito 3:3-5; 1 Petro 1:23-25; 1 Wakorintho 15:45-50; Wagalatia 3:26-29; 2 Wakorintho 5:17-18; Wakolosai 2:10-14. Hii ndiyo sababu Biblia inatangaza, “Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake” (Yakobo 1:18).

Biblia inatangaza kwamba Injili kwa mara ya kwanza ilihubiriwa na Mungu kwa Ibrahimu na kwamba, “ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake”, kubainisha kwamba hii "mbegu" ya kuzaliwa upya kwa kweli ni Kristo (Wagalatia 3:8, 16).

Maana imeandikwa, “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa

Page 26: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

26

kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:11-12). Sharti la Kuzaliwa Upya kwa maji na roho ni imani katika ufunuo wa injili ya Yesu Kristo (Marko 16:15-16; Matendo 8: 36-37). Wakati mtu amepokea injili, ni lazima aingie katika, au "kusimama katika", ahadi kwa kutii injili ili kuokolewa (1 Wakorintho 15:1-2). Mfano wa kwanza wa Biblia ulianzishwa katika siku ya Pentekoste wakati Petro alihubiria watu wote waliokuwapo (Matendo 2:14-36). Kuhubiri kwa Petro kulianza kwa kuchochea na kusababisha swali, “Tutendeje, ndugu zetu? (Matendo 2:37). Petro alijibu kwa amri ya Matendo 2:38:

“Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Hii ilikuwa ni amri ambayo mtu anatakiwa kufuata ili kuzaliwa mara ya pili, au "kuokolewa", ikiwa ataipokea na kutii (Matendo 2:40). Wale ambao kwa furaha hupokea neno, walitii kwa kubatizwa (kuzaliwa kwa maji), na kupokea Roho Mtakatifu (kuzaliwa kwa roho) waongezewe kwa mwili wa kanisa ambao Yesu Kristo ni Mwokozi (Matendo 2:41, 47; 1 Wakorintho 12:13; Waefeso 5:23, tazama pia Warumi 6: 16-18; 16: 25-26). Uzoefu wa “kuzaliwa tena” huanza mchakato wa mabadiliko katika mfano wa Kristo (2 Wakorintho 3:18; Waebrania 6:1-2).

Ni Mkristo tu aliyezaliwa tena anaweza kuhusiana na maandiko kama haya:

“Kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba” (Wakolosai 3:9-10)

Page 27: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

27

“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi” (Warumi 8:29).

“Lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo” (1 Yohana 3:2).

“Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele” (1 Petro 1:23).

“. . . tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu . . .” (Wafilipi 3:20-21).

“Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni” (1 Wakorintho 15:49).

Page 28: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

28

9.1

Toba

Maneno ya kwanza ya Yesu yaliyoandikwa katika injili ya Marko yalikuwa, “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili” (Marko 1:15). Kabla ya kupaa kwake, Bwana aliwaambia wanafunzi wake “mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu” (Luka 24:47).

Biblia inatangaza kwamba Mungu “anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu” (Matendo 17:30) na kwamba yeye “hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (2 Petro 3:9). Mitume waliomba kwa bidii, “twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu” (2 Wakorintho 5:20). Toba ni hatua ya kwanza ya ukombozi (Matendo 2:38) na inahitaji tendo la uhakika na makusudi, kwa upande wa mwenye dhambi, kugeuka kutoka mapenzi yake na kutoka kwa maisha yake ya awali ya dhambi.

Namna mbalimbali za toba zimetajwa katika Maandiko:

Matendo yanayopatana na kutubu yanatarajiwa kutoka kwa yule anayetaka kuokolewa (Matendo 26:20; Mathayo 3:7-12).

Ni kugeuka kutoka kuabudu sanamu kwa Mungu mmoja wa kweli aliye hai (1 Wathesalonike 1:10; Matendo 26:20).

Page 29: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

29

Ni kifo kwa kutenda dhambi, kwa “Kusulibiwa pamoja na Kristo” (Warumi 2:6-7; Wagalatia 2:20; 1 Petro 2:24) ama vifisheni viungo vyenu (Wakolosai 3:3-5; Warumi 8:9-14).

Toba ni sawa na kuacha dhambi (Kumbukumbu la Torati 7:1-5; Ayubu 22:21-23; Isaya 1:16; Yohana 5:14; Yohana 5:11; Warumi 6:2-4; 1 Wathesalonike 4:3).

Kukiri na ukombozi ni faradhi zimeunganika (Mithali 28:13; Luka 3:12-14; Mathayo 5:23-26; Yohana 4:15-20).

“Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu” (2 Wakorintho 7:10).

Toba inatolewa na Mungu haina ubaguzi. Katika Matendo 11:15-18, akinukuu kipindi cha Cornelius, mtume Petro alisema, “Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.” Ni kwa kupitia wakala wa Roho Mtakatifu hatia ya dhambi huja, kutuvutia kwa Yesu Kristo na kutuwezesha kuamini na kutubu, na kufanya tuwe na uwezo wa kuwa Wakristo.

Muujiza wa kuzaliwa upya kwa maji na Roho unaweza tu kufanyika katika maisha ya mwenye dhambi anayetubu kwa kweli. Toba kwa kweli ni kipengele muhimu cha amri ya Matendo 2:38.

Page 30: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

30

9.2 Kubatizwa Kwa Maji

Kabla ya kupaa kwake, Bwana wetu Yesu Kristo aliwaamuru, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” (Marko 16:15-16), kufanya ubatizo kuwa muhimu kabisa kwa wote ambao wanataka kuokolewa. Yesu alitangaza kwamba “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5).

Katika kitabu cha Matendo, kutoka kwa vipindi vyote vya ubatizo vinavyoelezea jinsi Agizo Kuu ilivyotekelezwa katika kanisa la kwanza, inaweza kuhitimishwa kwa urahisi kwamba "kuzaliwa kwa maji" kwa kweli hugunduliwa katika waumini wanaotubu, na kwa imani, kujiwasilisha wenyewe kwa ubatizo wa maji kwa kuzamisha kwa jina la Yesu Kristo ili wapate ondoleo la dhambi (Matendo 2:37-41; 8:12-18, 26-39; 9:1-9; 22:16; 10:42-48; 11:13, 14; 16:30-34; 15:3; 19:1-7). Hii pia ni sambamba na mafundisho ya nyaraka (Warumi 6:3-8; Wagalatia 3:27-29; Wakolosai 2:10-13; Tito 3:4-7; 1 Petro 3:20-21). Aina kadhaa na vivuli, ikiwa ni pamoja na unabii wa kimasiya ukielekeza kwa ubatizo katika mpango wa kizazi cha Agano Jipya, zinapatikana katika Agano la Kale (Ezekieli 36:25-26; 37:1-14; Mika 7:18-20; Zakaria 13:1; Yeremia 31:31-34; Isaya 53; Zaburi 74:13-14).

Nabii Ezekiel, hasa, alizungumzia “maji safi” ambayo ingeweza kuondoa uchafu wote na sanamu kwa kuambatana na ahadi ya moyo mpya na roho mpya kwa watu wa Mungu (Ezekieli 36:25-27) Mtume Paulo alitoa ufunuo kwamba agano la tohara ambalo

Page 31: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

31

Mungu alifanya na Ibrahimu halikuwa lingine ila kivuli cha ubatizo wa kuzaliwa upya unaoletwa na Agano Jipya, kwa kuzingatia kifo cha upatanisho, kuzikwa na ufufuo wa Kristo (Wagalatia 3:8, 16, 29; Wakolosai 2:11). Mtume Petro aliandika, “wokovu wa roho zenu. Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi” kufanya dokezo kwa matumaini ya unabii wa Masiya (1 Petro 1:9-12).

Mtume Paulo anaelezea kuwa katika uzoefu wa Kuzaliwa Upya, aina ya upasuaji wa kiroho hufanyika wakati “mtu wa kale amezikwa pamoja na Kristo katika ubatizo” (Wakolosai 2:12; Warumi 6:3-4). Alitangaza, “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo” (Wakolosai 2:11; Warumi 6:6-7). Tamko la Nabii Mika, “atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari” (Mika 7:19), kwa hakika inazungumzia kuzikwa pamoja na Kristo katika ubatizo kwa ondoleo la dhambi (tazama Zaburi 74:12-13). Biblia inasema kwamba Kristo alikuja kwa mwili, damu na maji kwa ajili ya upatanisho wa mwisho (1 Yohana 4:3; 1 Yohana 5:6; Ufunuo 1:5; 5:9). Kukamilisha picha, Paulo anaendelea, Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27). Hii kwa hakika ilionekana na Isaya alipotabiri kuhusu vazi la wokovu na vazi la haki (Isaya 61:10).

Page 32: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

32

9.3 Kubatizwa kwa Roho Mtakatifu

Yohana Mbatizaji alitayarisha njia ya Bwana, akibatiza kwa maji kama ishara ya toba. Akitangaza ufalme ujao, alitangaza kwamba Yesu “yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Mathayo 3:11; Marko 1:8; Luka 3:16; Yohana 1:33).

Yesu pia aliahidi ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa wanafunzi wake akisema, “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu” (Matendo 1:8) (tazama Yohana 7:37-39; 14:26; 15:26; 16:7-15; Luka 24:49; Matendo 1:5). Yesu alieleza kuzaliwa kwa Roho kuwa hitaji muhimu ya kuingia katika ufalme wa Mungu (Yohana 3:5-8; tazama Tito 3:4-8).

Manabii wa kale walikuwa wakiongozwa na Mungu walitabiri siku za mwisho na kumiminwa kwa pumzi ya Mungu Mwenyewe (Roho) kwa mtu, na kusababisha moyo wake kutamani njia ya Mungu, na kumwezesha kuitunza (Yoeli 2:28-32; Ezekieli 36:25-27; Isaya 28:9-13; Zekaria 10:1). Tumaini hili la unabii ulitimia siku ya Pentekoste wakati wanafunzi wa Kristo, wakajazwa Roho Mtakatifu, “wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka” (Matendo 2:1-4, 16-18). Siku hiyo, Mtume Petro alitangaza kwamba yeyote angetubu, na kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo atapokea kipawa cha Roho Mtakatifu (Matendo 2:38). Hata kama Roho Mtakatifu amemiminwa juu ya watu wengi, haimaanishi kwamba Roho Mtakatifu amekuwa wengi kwa idadi, au mashirika mengi. Biblia inasema, “Kwa maana katika Roho

Page 33: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

33

mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, . . . nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja” (1 Wakorintho 12:13).

Maandiko yanatangaza kwamba, “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu”, ili kupitia kwake “tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Wagalatia 3:13-14).

Yesu alikufa ili atukomboe na kutupanga katika familia ya Mungu. Kwa sababu sisi ni watoto wa Mungu, Yeye alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, na kutuwezesha sisi kuita “Aba, yaani, Baba” (Wagalatia 4:5; 6; Waefeso 1:5; Warumi 8:15-17). Kwa sitiari hii ya “kupanga”, waandishi wa Agano Jipya walitumia maneno tofauti kuelezea masuala mbalimbali ya kazi hii ya hakikisho (1 Wathesalonike 1:5) ambayo imekamilishwa katika moyo wa muumini na Roho Mtakatifu. Ni “muhuri” (Waefeso 1:13), “bidii” au ahadi ya maisha kamili yajayo. (2 Wakorintho 1:22; Waefeso 1:14; 2 Wakorintho 5:5; Waebrania 6:5).

Roho ya Mungu huwajia waumini ili kutengeneza ubora wa maisha ndani yao ambayo hawangeweza kupata kwa nguvu zao wenyewe. Baada ya kutuhakikishia uwana wetu, Roho huanza kuzalisha ndani yetu tabia na neema ya familia ambayo tumekubaliwa ndani yake. Ni Roho wa uhuru (2 Wakorintho 3:17; Wagalatia 3:10-14), Roho wa nguvu (2 Timotheo 1:7). Kwa hakika, kwa Roho wake, Mungu ametupa uwezo wa kutimiza mahitaji katika sheria Yake. Siyo tu kwamba “hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu,” lakini “sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti” (Warumi 8:1-2). Tumehamasishwa na Maandiko kwamba Mungu anatenda kazi “ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema” (Wafilipi 2:13). Tunda la Roho ni sifa ya maisha ya

Page 34: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

34

muumini mpya ndani ya Kristo (Wagalatia 5:22). Mungu wetu mtakatifu anatuhitaji sisi, kama watu Wake, kuwa watakatifu lakini pia anatuwezesha kutimiza mwito wake wa utakatifu kwa kutupatia Roho Mtakatifu (1 Wathesalonike 4:7, 8).

Biblia pia inatuambia kwamba mtu ambaye amezaliwa kwa maji na Roho “amevaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba” (Wakolosai 3:10; 2 Wakorintho 5:17). Kutoka kuzaliwa upya anaibuka mtu mpya ndani ya Kristo ambaye lazima ajihesabu mwenyewe “kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu” (Warumi 6:11). Biblia inatangaza, “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake,” na kwamba waumini waliozaliwa mara ya pili ni "kamili ndani Yake " (Warumi 8:29; Wakolosai 2:10).

Ni kwa Roho Mtakatifu katika umoja wa mwili wa kanisa na karama za Roho husambazwa miongoni mwa waumini wake kupitia kwa kazi yake ipasavyo ya nguvu za Mungu (1 Wakorintho 12:1-11; Waefeso 3: 7; 4: 3-16 ). Karama za Roho hutolewa kwa kila muumini ili apate kuwa imara katika mwili, na kwamba mwili uweze kupata faida kutoka kwa kila muumini (Warumi 1:11-12; 12:6-8; 1 Wakorintho 7:7; 1 Wakorintho 12:7). Karama za roho ambazo zimetajwa katika Maandiko ni kama ifuatavyo: kuonya, kutoa, huruma, neno la hekima, neno la maarifa, imani, uponyaji, matendo ya miujiza, unabii, kupambanua roho, aina za lugha na tafsiri za lugha (1 Wakorintho 12:7-11; Warumi 12:6-8). Pia kuna vipawa vya huduma vilivyozungumziwa juu yake katika Biblia: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu, wasaidizi na serikali (1 Wakorintho 12:28; Waefeso 4:8-15). Vipawa hivi

Page 35: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

35

vinafaa kutumiwa kwa hekima kwa njia ya utaratibu (1 Wakorintho 14:12-33). Maandiko yanampa changamoto muumini kuchochea kipawa chake alichopewa kwa kuwekewa mikono, si kukipuuza bali kuhudumia mmoja kwa mwingine kama mawakili wema wa vipawa vilivyotolewa kwa neema (1 Timotheo 4:14; 2 Timotheo 1:6-7; 1 Petro 4:10-11).

Page 36: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

36

Kanuni ya 10

Kanisa

Siku ile Mtume Petro alitangaza, kupitia ufunuo wa Mungu, Kristo kuwa Mwana wa Mungu (tazama Kanuni ya 3), Yesu alitangaza kwamba, juu ya ufunuo huo huo, atalijenga Kanisa Lake, wala milango ya kuzimu haitalishinda. Kisha aliahidi funguo za Ufalme wa mbinguni kwa chombo chake kiteule, Petro (Mathayo 16:16-19).

Kuzaliwa kwa kanisa kulifanyika “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste” (Matendo 2:1-4; Yoeli 2:28-32; Luka 24:44-49). Chini ya nguvu za Roho Mtakatifu, katika imani, watu walitii amri muhimu ya ukombozi ya Mtume Petro, iliyoandikwa katika Matendo 2:38-39 kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo na kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa njia hii, Mungu alianza kuteuwa watu wake kwa jina lake (Matendo 15:14-18), kutimiza mpango wake wa uungu aliokuwa ameteua hapo awali (Waefeso 1:3-11; 2:1-14; Waebrania 11:39-40; Yohana 10:16).

Wakati Kristo alikufa msalabani (Waebrania 13:11-12), pazia la hekalu la Yerusalemu likapasuka kutoka juu hadi chini (Mathayo 27:51). Ilikuwa ni mwanzo wa kutimia kwa maneno ya Yesu, “Livunjeni hekalu hi l i , nami katika s iku tatu nitalisimamisha.” (Yohana 2:19-21; Matendo 7:48-50). Kwa kumwaga damu yake ya thamani (Matendo 20:28), amri zake zote za damu za Agano la Kale zilimalizika (Waebrania 7:27; 9:11-12; 10:14). Utaratibu mpya ulikuwa umeingia (Waebrania 7:19), njia mpya (Matendo 9:2; Waebrania 10:11-20; Yohana 14:6),

Page 37: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

37

upatikanaji mpya na ulio hai wa Mungu ulikuwa umefunguliwa kwa njia ya ukuhani wa Kristo (Waebrania 8:1-2; 10:19-22; 12:22-24; 1 Petro 2:9). Siku za hekalu zilikuwa zimekwisha. Mungu alikuwa ametayarisha makaazi yake ya milele, ambayo ni kanisa, mwili wa Kristo, unaoundwa na waumini waliozaliwa mara ya pili (Warumi 12:4-5; 1 Wakorintho 6:15; 12:12-27). Kuzaliwa huku ni kwa mbegu isiyoharibika (1 Petro 1:23-25; Wagalatia 3:27-29), na washirika wa tabia yake ya kimungu (2 Petro 1:4), zimefanywa kamili katika Yeye (Wakolosai 2:10). Biblia inatangaza kwamba kanisa la Mungu aliye hai limenunuliwa kwa damu yake mwenyewe (Matendo 20:28). Wakristo waliozaliwa mara ya pili “ni viungo vya mwili wake” (Waefeso 5:30). Biblia inaonyesha kwamba kanisa ni kiumbe cha Mungu kipya katika Kristo, ambacho kitatangaza "hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi" kwa “falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho” (Waefeso 3:10; Wakolosai 3:15; 1 Petro 2:9-10).

“Israeli wa Mungu” (Wagalatia 6:15-16) wanaendelea kuitwa kutoka katika kila kabila, lugha, taifa, na jamii (Ufunuo 5:9-10) “katika ufalme wa Mwana wa pendo lake” (Wakolosai 1:13. Biblia inaamuru, “Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana . . .” (2 Wakorintho 6:17; Matendo 2:40; Ufunuo 18:4).

Sitiari mbalimbali zinatumika katika Agano Jipya kuelezea kanisa, ya wakati wote “Iklezia”, na kwa pamoja, kuwasilisha asili ya kipekee ya kanisa:

Mwili wa Kristo (Waefeso 1:22-23; 5:23-27, 30; Wakolosai 1:18; 2:10, 19; 1 Wakorintho 12:11-14; Wakolosai 3:9-11; Matendo 2:42).

Page 38: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

38

Hekalu la Mungu (Matendo 7:48-49; Yohana 2:19, 21; 1 Wakorintho 3:16; 6:19-20; Ufunuo 21:3; Mathayo 18:20; 1 Petro 2:9).

Bibi Harusi wa Kristo (Mwanzo 2:18-25; Yohana 3:6; 1:12-14; Waefeso 5:30; Yohana 3:29; 2 Wakorintho 1:3; Waefeso 5:22-27; Ufunuo 22:17; 19:7-8; Wakolosai 2:10-14; 1 Yohana 3:1-3; Wafilipi 3:20-21; Hosea 2:19-20, 23; 3:1-5)

Watoto wa Mungu (Waefeso 3:8-9; Wakolosai 1:26-27; Yohana 3:3; 5-7; Warumi 8:29; Waefeso 1:5; 1 Yohana 5:1; Yohana 1:12-13; Waefeso 1:5; 2 Wakorintho 6:18; Yeremia 31:33-34; 2 Samweli 7:12-16; 1 Yohana 3:9; 1 Petro 1:23; 1 Yohana 3:1; 2 Wakorintho 6:16).

Page 39: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

39

Kanuni ya 11

Huduma ya Kuwekelewa Mikono

Kuwekelewa mikono inasemekana kuwa moja ya kanuni za msingi ambazo Mkristo aliyekomaa hujenga maisha yake juu yake (Waebrania 6:1-2). Ni kanuni ya msingi ya mafundisho ya Kristo kwa ajili ya utendaji kazi wa Roho katika Kanisa. Kuwekewa mikono hasa hutumika kwa ajili ya ubadilishanaji, utekelezaji na kupasha kazi ya Roho Mtakatifu kupitia uongozi wa uwakilishi katika mwili wa Kristo. Ni kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu na onyesho la nguvu za Mungu na kusudi la mwanadamu kwa mujibu wa madhumuni ya uungu wa Mungu takatifu inayopatikana katika Neno lake Takatifu.

Biblia inatupa shughuli nne muhimu mbalimbali za kuwekewa mikono:

Kwa ajili ya kuhamisha baraka za vizazi na za ahadi. Rekodi ya kwanza katika Biblia ya kuwekewa mikono hupatikana katika Mwanzo 48:8-20 ambapo Israeli alibariki Efraimu na Manase, wana wa Yusufu. Katika baraka hii Israeli aliomba “. . . na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka . . .” Hii ilikuwa baraka za vizazi ambazo zilitumika kuendeleza heshima ya mtu binafsi ambayo alikuwa ameingia katika agano na Mungu. Katika Hesabu 27:18-20 tunajifunza kwamba baadhi ya heshima ya Musa iliwekwa juu ya Yoshua kwa kuwekewa mikono na Musa, ili baada ya kifo cha Musa, Yoshua alionekana

Page 40: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

40

kuwa “amejaa roho ya hekima” (Kumbukumbu la Torati 34:9). Ni muhimu pia kutambua kuwa Yesu aliweka mikono yake juu ya kile kizazi kilichofuata, na kwenda umbali wa kuwakataza kuzuia zoezi hilo (Mathayo 19:13-15; Marko 10:13-16).

Kwa ajili ya kuhamisha mamlaka iliyokabidhiwa aliyeteuliwa katika utawala wa kanisa. Hii ni uhamisho wa wajibu, (Hesabu 8:10-14; Waebrania 5:1-4, 8:3; matendo 6:1-6) kitendo cha kutenga au kuwekwa wakfu kwa ajili ya Bwana, wale watakaotumiwa na Bwana kwa kusudi lake kuu. Walawi waliwekwa wakfu “ili wawe wenye kufanya utumishi wa BWANA.” Kadhalika katika kanisa la kwanza wakati wao wa kufunga, “Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.” (Matendo 13:1-4). Kitendo hiki kwa kawaida kinajulikana kama kuwekwa wakfu kwa kazi takatifu au kazi kuu (Marko 3:13-19; Yohana 15:16; Matendo 1:20-26; 6:1-6; 14:21-23; Tito 1:5-9), na imehifadhiwa kwa ajili ya wale walio katika nafasi za uongozi na mamlaka ya kimungu (Luka 10:2-3, 16-20; Yohana 17:16-20; 20:21-23). Ni lazima ieleweke kwamba hekima ni hitaji wakati wa kutumia mamlaka hii kutoka kwa Mungu (1 Timotheo 5:22)

Kwa ajili ya Kupasha karama muhimu za kiroho. Kupasha kwa karama za Roho, na hasa, kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu alikuja na kuwekewa mikono ya mitume, au huduma (Matendo 8:14-19; 19:6; 1Timotheo 4:13-14; Warumi 1:11; 2Timotheo 1:6-7).

Page 41: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

41

Kwa ajili ya kupewa nguvu za Mungu za uponyaji na kwa wote wanaoamini. Uponyaji wa wagonjwa kwa kuwekewa mikono ilianzishwa na Bwana wetu Yesu mapema katika huduma yake na ikawa mazoezi yake ya kawaida (Marko 6:5, 12-13; 7:32-35; 16:18; Luka 4:40; 13:11-13). Nguvu hizi zilizopewa sio tu Mitume Kumi na Wawili alipokuwa akiwatuma (Mathayo 10:1-8; Marko 3:14-15; Luka 9:1-2), lakini pia zilipewa wale sabini waliotumwa wawili wawili (Luka 10:1-9) na kisha kwa wote miongoni mwa wazee wa kanisa (Marko 16:17-18; Matendo 28:8; Yakobo 5:14-15).

Page 42: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

42

Kanuni ya 12

Uponyaji na Baraka za Mungu

Biblia inatangaza kwamba Yesu Kristo, kwa mapigo na michubuko yake, na kwa njia ya mateso yake, amechukua maumivu na udhaifu wetu (Isaya 53:4-5; Mathayo 8:16-17; 11: 5-6; 12:28; 1 Petro 2:24; Kutoka 15:26; 23:25). Kupitia kifo chake msalabani, ametuokoa kutoka katika dhambi na kutuweka huru kutoka kifo cha milele (1 Wakorintho 1:18; 15: 55-57; Wagalatia 1: 4; 3:13; Waefeso 2; Isaya 53: 1-10; Isaya 61). Biblia inatuhakikishia, kuwa ni kwa ajili yetu, ingawa alikuwa tajiri, Yesu akawa maskini, alipata mateso na kuwa uchi, ili tuweze, sisi wafuasi wake, kwa umaskini wake tupate kuwa tajiri na kuishi maisha ya heri katika dunia hii (Mathayo 8: 20; 2 Wakorintho 8: 9; Marko 10:29-31). Njia pekee ambayo tunaweza kupokea baraka hizi zote ni kama sisi tutapokea neno lake kwa imani (Zaburi 107: 20)

Page 43: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

43

Kanuni ya 13

Urejesho wa Walioanguka Kupitia Toba

Toba ina maana ya kujuta kabisa na kugeuka kutoka dhambi, kufa kutoka kwa uchafu wa dunia hii na mapenzi ya dhambi. Kama baada ya mtu kuzaliwa kwa maji na kwa Roho, na yeye aanguke katika dhambi, mtu huyo anaweza kurejeshwa kama yeye atatubu dhambi zake kwa uaminifu. Bila kujali jinsi dhambi yake inaweza kuonekana kuwa nzito, dhambi zake husamehewa papo hapo anaporejea katika toba. Maana imeandikwa katika 1 Yohana 1:7-9, “. . . na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote . . . Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” Waebrania 8:12 inasema, “. . . Na dhambi zao sitazikumbuka tena.” Pia katika Ezekieli 18:21-32, kifungu cha 28 kinasema, “Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.” (Pia tazama Luka 7:36-50; 13:3-5; 15:1-32; 18:35-43; 22:54-65; 1 Yohana 2:1-3; Ezra 10:11-12; Mithali 28:13; Yeremia 3:13; Yoeli 2:12; Matendo 8:21-23; Yohana 8:1-11; Waebrania 9:14; 10:10-25).

Page 44: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

44

Kanuni ya 14

Dhamiri

Neno la Mungu linathibitisha kwetu kwamba wakati mtu anatii Injili ya Yesu Kristo, yeye hufanywa kuwa haki na kupewa dhamiri njema ambayo itamwezesha kuweka sheria ya Mungu (Warumi 2:2-16; 1 Yohana 3:19-22). Kwa hiyo, anapaswa kujiondoa kutoka kwa chochote ambacho kitaletea shida dhamiri yake. Kama yeye ataenda kinyume cha dhamiri yake, maandiko yanatangaza kwamba ni dhambi (Warumi 9:1; 13:5; 2 Wakorintho 1:12; 8:7; Waebrania 9:14; 13:18; Matendo 23:1; 24:16; 1 Timotheo 1:5, 19; 3:9; 1 Petro 2:19-23; 3:16; Mwanzo 42:21; Yohana 8:7-9). Kwa hiyo, watakatifu wanapaswa kusikiliza na kutii dhamiri yao ambayo huwatia moyo kuishi maisha safi na ya utakatifu

Page 45: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

45

Kanuni ya 15

Utakatifu

Utakatifu ni sifa ya Mungu. Kwa kuwa tumekuwa watoto wa Mungu kupitia kuzaliwa upya, Roho wake huleta utakatifu wake ndani yetu. Kwa kuwa miili yetu ni hekalu ya Mungu, iliojawa na Roho Mtakatifu, ni lazima tujiepushe na yale ambayo ni chukizo kwa Mungu na ambayo itanajisi au kudhuru miili yetu na roho.

Waefeso 1:4 inashuhudia, “kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi kwa ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.” Kwa hiyo, tunaamini kwamba tunapaswa kutofuata namna ya dunia hii aidha katika miili yetu (jinsi tunavyovalia na kujiweka wenyewe), au maisha yetu (mienendo yetu) (2 Wakorintho 6:14-18; 7:1; 1 Wakorintho 3:14-17; 6:19-20; 1 Petro 1:13-16; 2:9-10; 3:1-18; Waefeso 4:17-32; 5:1-33; Kutoka 22:5; Wakolosai 3:1-25; Mathayo 5:48; Waebrania 12:14; 1 Timotheo 2:8-12; Ayubu 22:21-30; Isaya 3:1-26; Kumbukumbu la Torati 28; Mambo ya Walawi 19:1-4; Ezekieli 44:9-24).

Page 46: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

46

Kanuni ya 16

Chakula cha Bwana/Meza yaBwana

Wale ambao wanakubali kama kweli, kuwa Kristo Yesu ni Neno lililofanyika mwili (Yohana 1:1, 14), wanaamini alikufa kwa ajili ya kuondolewa kwa dhambi zao, na wamezaliwa kwa maji na kwa Roho (Yohana 3:3-7; Matendo 2:37-41), na kumvaa Kristo (Wagalatia 3:27), watakuwa washiriki wa Chakula cha Bwana ili kushuhudia kifo chake.

Biblia iko wazi kwamba inawezekana kuwe na ushiriki wa Chakula cha Bwana, au "Ushirika" kwa njia isiyostahili (1 Wakorintho 11:29) na inatoa sababu kadhaa za kujiepusha na ushirika. Wale ambao hawajapata mfano wa Kristo kwa kutii Injili, ambao bado hawajavaa Kristo katika ubatizo, hawapaswi kushiriki katika ushirika. Hii ni kwa sababu ushirika unawakilisha kuungana kwa viungo vya mwili wa Kristo, ni lazima tuwe wa mwili wake na Roho ili kuunganishwa naye (1 Wakorintho 6:15 -17; 12:13-20; Waefeso 5:30). Wale ambao hawana uelewa kamili wa siri ya mwili wa Kristo na damu hawastahili kushiriki katika ushirika. Hii ni kwa sababu hawajabaini mwili wa Bwana (Yohana 6:48-51; 8: 21-24; 1 Wakorintho 11:29), hawaelewi wanajiunganisha na nini. Wale ambao hawajajichunguza wenyewe hawawezi kuwa sehemu ya ushirika huu mtakatifu, kwa sababu hawajakuwa makini kujihukumu wenyewe, hasa kwa kuzingatia kile wanachotaka kushiriki (1 Wakorintho 11:28-31). Kwa sababu baadhi wamechukua ushirika kwa njia isiyostahili, Biblia inatoa maelezo kwa kusema, “wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala” (1 Wakorintho 11:23-34).

Page 47: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

47

Kwa hivyo tunachukua tahadhari na onyo la neno la Mungu ili kuepuka kuleta hukumu ya Mungu juu yetu. (Warumi 15:4; 1 Wakorintho 10:1-22; 2 Timotheo 3:16-17). Kwa sababu hizi, tunaamini kwamba kanisa inapaswa kutoa onyo kali kwa kuhubiri kwamba mtu aliye na ugomvi na mwingine, anapaswa kwanza kutubu au kufanya haki na Mungu na mtu ambaye wametofautiana.

Tunaepuka kushiriki meza ya Bwana mara nyingi mno, na hivyo kupunguza hatari ya kupatwa na mtazamo wa kawaida dhidi ya sakramenti hii na kuleta hukumu ya Mungu juu ya wale ambao wanaweza kushiriki kwa njia isiyostahili (Mathayo 5:23-26; 26:26-29; Yohana 6:35-63; 1 Wakorintho 5:6-8; 10:14-22).

Page 48: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

48

Kanuni ya 17

Kuosha/Kutawadha Miguu

Kama vile Bwana wetu na Mwokozi, Yesu Kristo kabla ya karamu ya mwisho, alijinyenyekeza na kuosha miguu za wanafunzi wake, sisi pia, kwa kuelewa na imani iliyojengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, tunapaswa kujinyenyekeza na kupata tohara ya moyo (Yeremia 4:4; Waefeso 2:19-22; Wafilipi 2:5-8). Ni lazima tunyenyekee na kutawadha miguu ninyi kwa ninyi, bila kudharau mtu yeyote, awe mdogo au mkubwa, na kwa sababu ni wajibu wa watakatifu, tufanye hivyo kwa upendo na unyenyekevu (Mwanzo 18:3; 19:2). Bwana alituagiza akisema, “imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi” na “Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda” (Yohana 13:3-17).

Page 49: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

49

Kanuni ya 18

Ndoa na Talaka Waebrania 13:4 inasema, “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.” Ili kuokolewa kutoka hukumu ya Jehanamu, Biblia inaamuru uaminifu, ikiruhusu mwanamke mmoja kwa mwanamume mmoja na mwanamume mmoja kwa mwanamke mmoja. Kwa hiyo, ndoa yoyote ambayo ni kinyume cha kanuni hii ni ndoa najisi ambayo ni kinyume cha sheria za Mungu. Ni jambo la muhimu sana kwa kanisa kuheshimu neno la Mungu, kwani kitu chochote kinyume cha neno lake kitavunja ufunuo wa uhusiano wa Mungu na kanisa na pia kuleta madhara kwa jamii na familia. Kanisa halitafanya wala kutoa idhini kwa, ndoa mbili (mitala) kati ya watakatifu, wala kwa ndoa ya jinsia moja, (Mambo ya Walawi 18:22; 20:13; Kumbukumbu la Torati 23:17; Warumi 1:26-27; 1 Wakorintho 6:9) wala kanisa halitapendelea mpango wa aina hii katika jamii kwa kuwa Kristo ana bibi mmoja tu (Waefeso 5:23-32), kanisa, na Yeye ni mwaminifu kwake.

Kwa sababu kitendo cha talaka ni chukizo na maovu machoni pa Mungu (Malaki 2:14-16), isipokuwa ni kwa sababu ya usherati, mtu yeyote atakayeanzisha talaka hatafikiriwa kuwa Mkristo, lakini kafiri. Wale ambao hutoa talaka kwa sababu isiyo ya uasherati wataishi bila kuolewa, au wafanye amani na kupatanishwa (Mathayo 19: 3-9; Waefeso 5: 22-23; 1 Wakorintho 7:10-11, 39.)

Hata hivyo, Biblia inatoa nafasi katika kesi ya mke au mume ambaye si muumini kuondoka. Katika kesi kama hiyo, muumini hana wajibu wa kukaa katika muungano (1 Wakorintho 7:15).

Page 50: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

50

Kanuni ya 19

Sadaka na Zaka

Biblia inatuonya waziwazi kutoa kwa serikali mali ipasayo kwa serikali na kwa Mungu mali ipasayo kwa Mungu. Kwa hiyo, wale ambao hawatashiriki katika kanuni ya uwakili wa Biblia wamelaaniwa na Mungu (Malaki 3:7-12), kwa sababu wao ni waasi wa Utawala wa Mungu na ufalme wa dunia hii. Tunaamini kwamba wale ambao wanaamini neno la Mungu na kumtumikia Mungu mmoja wa kweli watapokea baraka maradufu (Marko 12:14-17; Mithali 3:1-10; Kumbukumbu la Torati 8:18; 12:5-6; 16:16 -17; Warumi 13:1-7; 1 Wakorintho 9; Luka 8:1-3; Mathayo 25:34-36).

Katika 2 Wakorintho sura ya tisa, tunasoma katika mstari wa sita, “Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.” Kifungu cha tisa kinaendelea, “Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele” (2 Wakorintho 9:6-15; Kumbukumbu la Torati 26:1-19).

Page 51: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

51

Kanuni ya 20

Serikali

Warumi 13:4 inasema, “. . . kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.” Kanuni na sheria za serikali ya dunia hii zimetoka kwa Mungu, na kila nafsi inapaswa kuwa chini ya nguvu hizo kwa sababu wao wamewekwa mahali pale na Mungu.

Hili amani iwe tele katika dunia hii na sisi tuwe na uwezo wa kuishi kimya kimya na kwa utulivu katika uhuru, ni lazima tuombee viongozi wetu kwa bidii na pia viongozi wote duniani kote wenye mamlaka (1 Petro 2:13-14, 17; Ezekieli 24:21; Mhubiri 8:1-5; 10:20; Tito 3:1; Mathayo 17:27; Kutoka 22:28; 1 Samweli 24:5-7; Matendo 23:5; Mithali 25:5).

Tazama pia marejeo yafuatayo ya maandiko matakatifu ambayo yanahusiana na kuombea viongozi wetu: 1 Timotheo 2:1-4; 1 Wafalme 13:6; 2 Wafalme 19:1-37; 2 Mambo ya Nyakati 19:32; 20:23; 33:10-13; Ezra 8:21-23; Danieli 9:3-23; Esta 4-9).

Page 52: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

52

Kanuni ya 21

Mwito Mkuu

Bwana wetu Yesu Kristo ametupa mwito mkuu, “. . . Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Kwa hiyo kama alivyo tupata kuwa waaminifu, ni lazima tumkiri yeye kwa ulimwengu, si kuwapendeza watu, lakini kumpendeza Mungu aichunguzaye mioyo yetu.

Kanisa imepewa changamoto ya kuhubiri injili mpaka mwisho (kifo), ili kuwakomboa wale ambao wanavutwa kwa mauti ya milele (kifo cha pili), na kuokoa wale ambao wako tayari kuuawa kwa upanga wa dhambi. Kama ni mateso, njaa, au kiu, kuhesabu mambo hayo kama si kitu, ni lazima tumfanyie Mungu kazi zaidi ya jinsi tulivyowahi kufanya tukitembea kuelekea siku za usoni (1 Wathesalinike 2:9; Ufunuo 2:10-11; 21:8; Marko 16:8-17; Mathayo 5:11-12; 10:16-39; Mathayo 25; 28:17-20; Mithali 24:11-13; Yohana 15:13-14; 2 Timotheo 4:1-8; 1 Petro 2:9; Wafilipi 1:15-30; 2 Wakorintho 6:3-10; 1 Wakorintho 9:16-17; Warumi 1:16; Luka 24:47-49; Matendo 1:8; Danieli 12:3).

Page 53: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

53

Kanuni ya 22

Kufufuliwa au Kunyakuliwa kwa Waumini

Wale ambao wamezaliwa kwa maji na kwa Roho kwa jina la Yesu kulingana na Matendo 2:38; Yohana 1:12-13; 3:1-6; Tito 3:4-8; Wakolosai 2:11-14; Wagalatia 3:26-27, ambao wamekufa kwa uchafu na dhambi za dunia hii, ambao wanatembea katika maisha mapya, ambayo wamejawa na upendo na umoja, watakatifu (wana wa Mungu) ambao ni Kanisa (mwili wa Kristo), wataungana na Kristo wakati atakapochagua. Kwa sababu ndani yao wana Roho huyo wa Mungu ambaye alimfufua Kristo, tunaamini kwamba miili yao ya binadamu itabadilishwa wakati yeye atarudi kumeza kifo na kuchukua bibi yake (Warumi 8:11; 1 Wakorintho 15:50-57).

Tukiishi maisha matakatifu, tutembee kwa upendo na kubakia hai hadi kuja kwake Bwana, kwa hakika hatutazuia wala kutanguliza hao wamelala (peponi), lakini tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu (1 Wathesalonike 4:13-18; Ufunuo 3:10-12; Wafilipi 3:20-21; Yuda 14-15; Zakaria 14:5-9; Ufunuo 19:7-8; Danieli 7:27; 9:27).

Page 54: Kanuni za Imani za Kanisa la Kitume la Kimataifa · 2 Anuani ya Makao Makuu ya Kanisa la Kitume la Kimataifa S.L.P 4442 Addis Ababa, Ethiopia S.L.P 102174 - 00101 Nairobi, Kenya

54

Kanuni ya 23

Hukumu ya Mwisho

Siku imeteuliwa ambapo dunia nzima itahukumiwa (Zaburi 96:13; Matendo 17:31). Yesu Kristo mwenyewe ataketi kwenye kiti cha utukufu wake (Mathayo 25:31-32; Ufunuo 20:11-15), ambapo mbele yake nafsi zote lazima zitasimama (Warumi 14:10; 2 Wakorintho 5:10). Siri za watu wote, walio hai na waliokufa watahukumiwa kulingana na injili ambayo Mitume walihubiri (Warumi 2:16; 2 Timotheo 4:1; 1 Petro 4:5; Matendo 10:42). Tukio hili pia linajulikana kama hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe (Ufunuo 20:11-15).