kijitabu cha uchambuzi wa biblia...juu ya kubadili mzozo na daniel l. buttry [2]$ $ yaliyomo...

49
[1] KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry

Upload: others

Post on 31-Jan-2020

29 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[1]    

KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA

JUU YA

KUBADILI MZOZO

NA

Daniel L. Buttry

Page 2: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[2]    

YALIYOMO

Utangulizi

Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha

Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya Tamaduni Nyingi

Jinsi ya kutumia Kijitabu hiki

Sehemu ya 1: Ukaguzi wa Mzozo

Awamu ya 1: Mzozo Kama Eneo Takatifu (Kutoka 2.23-4.17)

Awamu ya 2: Kuongezeka kwa Mzozo (Mwanzo 3.8-13; 4.1-16; 4.19-24; 10.8-12)

Awamu ya 3: Mzozo wa Kifamilia (Mwanzo 25.19-34; 26.34-28.9)

Awamu ya 4: Safari ya Maridhiano (Mwanzo 28.10-33.20; 35.27-29)

Sehemu ya 2: Utatuzi wa Mzozo

Awamu ya 5: Mzozo Juu ya Kutoelewana (Yoshua 22.10-34)

Awamu ya 6: Mpatanishi Jasiri (1 Samueli 25.1-35)

Awamu ya 7: Mzozo Juu ya Maadili ya Kidini (Matendo ya Mitume 15.1-15)

Awamu ya 8: Kutafuta Suluhu Usioegemea Upande Wowote (Hesabu 32.1-33)

Awamu ya 9: Isipowezekana (Matendo ya Mitume 15.36-41)

Sehemu ya 3: Katikati na Ukingo

Awamu ya 10: Mzozo Katika kila Kikundi (Matendo ya Mitume 6.1-7)

Awamu ya 11: Kutafuta Sauti ya kila mmoja (Esta 4.1-17)

Awamu ya 12: Mama aliyekasirishwa na mwenye huzuni (2 Samueli 21.1-14)

Sehemu ya 4: Mipango ya mabadiliko bila Vita

Awamu ya 13: Kupenda Adui Kupitia Mipango ya mabadiliko (Matayo 5.38-48)

Awamu ya 14: Kulisha Adui (2 Wafalme 6.8-23)

Awamu ya 15: Kutotii iliyo Takatifu (Kutoka 1.15-22)

Awamu ya 16: Matendo ya Kuigiza Yenye Maana ya Ndani (Luk 19.38-44; Isaya 20.1-6;

Yeremia 32.1-15)

Awamu ya 17: Kushinda Maovu kwa Wema (Warumi 12.9-21)

Vitabu Vilivyatumiwa Kupata Habari

Orodha Fupi ya Vitabu

   

Page 3: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[3]    

UTANGULIZI:

Yesu alisema, “Heri wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu” (Matayo 5.9) Watafutao amani

hujitoza katika mzozo kwa kujitolea ili kuleta wema wa Mungu katika hali hii, hata iwe mbaya kiasi

gani.. Leo tamko “kubadilisha mzozo” imetumika kueleza mikondo yote ambapo watu na mataifa

wanatafuta kuweka mienendo yakujengayo na pia kuweka taasisi katika jamii badala ya uharibifu na

masikitiko ya vita na mizozo ya umma. Kubadilishwa kwa mzozo inajumuisha kukabiliana na maovu

bila vita, kuweka haki, kujadili maagano, kujenga amani na kuunda maridhiano. Kama Wakristo

tunaamini kuwa Yesu aliwaamuru wafuasi wake kuleta suluhu kwa mizozo, kwani wao ni wana wa

Mungu kwa kuonyesha kujali na kuwa na huruma kwa watu wanaopitia matezo katika mzozo kama

vile Mungu alitoa mfano kupitia Kristo.

Kijitabu hiki kimetayarishwa kuwezesha na kuupa uwezo kazi ya Wakristo ya kujenga amani kama

mtu binafsi au kama washiriki wote. Biblia ni kifaa chetu cha kutoa maelezo zaidi, ni mwongozo wa

kuongoza fikra na matendo yetu. Masomo haya yatasaidia wachungaji na walimu kuongoza wafuasi

wao kujifunza kutoka kwa Biblia “ mambo yaletayo amani” (angalia Luka 19.42)

Kijitabu hiki kinatupa vifungu vya Biblia vya kusoma na kinasisitiza vipeo vitakavyoambiwa

wanafunzi. Kijitabu hiki pia kinatoa mwelekeo kwa mbinu za masomo ambazo zinachangia

pakubwa katika mafunzo kwa washiriki wa uchambuzi wa Biblia. Njia nyingi za kuendesha

uchambuzi wa Biblia katika mazingira ya kanisa zinapunguza kiwango ambacho watu wanakumbuka

na hivyo kupunguza uzito wa mafunzo hayo kwa maisha yao ya kila siku. Kijitabu hiki kinatupa

mbinu ambayo itahusisha wanafunzi kikamilifu katika mkondo wa mafunzo ambapo wanafunzi

watakumbuka mengi ya waliyofunzwa na kubadilishwa katika mbinu zao za kukumbana na mzozo.

Amani na vita ndivyo maudhui makuu katika Biblia. Kijitabu hiki hakijajaribu kutoa masomo ya

mambo hayo katika Biblia kwa ukamilifu. Kuna vitabu vingi katika maktaba ya vyuo vya Biblia kwa

wale wangependa kusoma zaidi. Orodha ya vitabu katika tamati mwa kijitabu hiki ni nzuri kwa somo

kama hilo. Bali masomo haya yametolewa kuwatayarisha na kuwezesha Wakristo na makanisa

kujihusisha vyema katika mizozo karibu nao kwa njia zitakazoleta uponyaji, matumaini na

maridhiano. Kijitabu hiki kimeelekezwa kusaidia kubadilisha mizozo na kujenga amani kwa njia za

ukweli kupitia mtazamo na masomo yaliyopatikana kupitia Maandiko.

UCHAMBUZI WA BIBLIA KWA KUSHIRIKI

Kwa mara nyingi, uchambuzi wa biblia umefanywa kwa njia ambayo mwalimu ndiye anaonekana

kana kwamba ana ujumbe wote ulio kamilifu wa kupewa wanafunzi tu. Mwalimu ni kama chupa ya

maji ambayo humwagwa kwa vikombe vitupu vya wanafunzi. Uchambuzi ni mkondo moja, kutoka

Page 4: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[4]    

kwa mwalimu hadi kwa wanafunzi .Katika mbinu hii, wakati mwingine mwalimu huruhusu maswali

kutoka kwa wanafunzi na hujibu moja kwa moja au wakati mwingine wanafunzi hujadiliana

miongoni mwao,lakini mwalimu ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho kwa yale wanafunzi

wamejadili kuwa ni hivyo au la.

Kwa mara nyingi hii huenda ikawa njia bora kwa masomo ya kawaida, lakini kijitabu hiki cha

uchambuzi wa biblia kinaelezea mbinu nyingine tofauti, mbinu inayoshirikisha sana wote

wanaohusika au wanaosoma..

Mbinu inayoelezwa katika kijitabu hiki kinatia moyo wanaotumia kuchukua jukumu la masomo yao.

Wanahusika moja kwa moja kutambua yale biblia inasema. Mbinu hii hualika wote wanaotumia

wawe walimu pia, kila mmoja ana uwezo wa kuchangia katika masomo ya kikundi kisima.

Utafiti uliofanywa kuonyesha ni jinsi gani wanafunzi huelewa wanachofunzwa darasani

umeonyesha kuwa watu hukumbuka karibu asilimia 10% ya kile wamesoma, asilimia 20% ya kile

wamesikia. Kwa hiyo njia hii ya kuhadhiri na kusoma kazi ya ziada inayotumiwa kila mara ina

kiwango kidogo sana ya kuifadhi kile mtu amesoma. Tunakumbuka asilimia 30% ya kile tumeona na

asilimia 50% ya kile tumeona na kusikia. Hivyo basi utumizi wa vifaa vinavyotumia uwezo wetu wa

kuona na kusikia, kama vile kuandika ubaoni au jikaratasi ama kutumia vipande vidogo vya

makaratasi vyenye ujumbe maalum ikiwemo kuigiza huongeza mafanikio ya somo

Watu hukumbuka 70% ya waliojadili na wengine na hutoa nafasi kwa wanafunzi kukutana pamoja

kuhusu ujumbe waliofunzwa na hivyo kuongeza kiwango cha ujumbe wanaokumbuka. Kwa

kuongezea zaidi, 80% ya kile watu huvumbua wao wenyewe ndiyo kinakumbukwa kuliko kile

wanaambiwa na mwalimu. Hivyo basi huwapa watu nafasi ya kujihusisha moja kwa moja katika

kugundua ni mbinu muhimu ya mafunzo iletayo mafanikio kuliko uhadhiri. Watu watakaofunza

wengine ujumbe huu hukumbuka 95% ya wanachosoma. Katika uchambuzi wa Biblia, hii hufanyika

kwa kuwapa vikundi nafasi ya kuelezana habari na vilevile kuhimiza washiriki kuwa walimu katika

mazingira mengine.

Watu hijifinza kupitia mbinu mbalimbali. Mbinu moja ni kujifunza kwa kutazama tukitumia macho

yetu. Kuandika kwenye ubao, mapango, vijikaratasi na video; hivi vyote hutumia macho kama njia

ya kufikia akilini. Wakati mwingine lugha yetu husababisha kutokea kwa mbinu ya kujifunza kwa

kutazama kutokana na maswali kama “umeona chenye ninamaanisha?”

Mafunzo ya kusikia yanatumia masikio yetu. Uhadhiri ni mfumo mmoja ya mafunzo ya kusikia.

Kusimulia hadithi na kusoma kwa sauti pia ni mafunzo ya kuskia.” Katika lugha tunaweza kutumia

matamshi kama “hicho kinajitokeza vipi kwako?”

Page 5: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[5]    

Mafunzo ya matendo yanahusisha miili yetu, kusongasonga na kuhisi kwa kushika. Masonyuso au

ishara inayokusudiwa kuleta ujumbe wa mdomo, pia kusongasonga kwa watu katika mafunzo-hayo

yote yanaleta Mafunzo ya Matendo Matendo yafanyao watu kutoka kwenye viti vyao na kufanya

miili yao kusonga husababisha njia ya mafunzo ya matendo. Mazoezi na mchezo wa kuigiza hufanya

watu kuhusika kimwili. Lugha inaweza kusababisha mafunzo ya matendo kwa matamshi kama

“maoni hayo yanakufanya uendelee mbele?”

Mafunzo ya hisia yanahusisha wanafunzi kwa undani kabisa. Kando ya hadithi kuhusisha kusikia na

kusema, kwa mara nyingi uhusisha hisia ya wasikilizaji. Kutakuwa na utambulizi wa hisia..

Ushuhuda ya mtu kuhusu aliyoyapitia katika maisha yake yanaweza kusisimua moyo wake na kuleta

hisia katika mkondo wa masomo. Makumbusho ya mambo watu walipitia maishani kupitia kuigiza

yanaanzisha mafunzo ya hisia. Lugha inaweza kusisimua mafunzo ya hisia kwa matamshi kama “una

hisia kwa hiyo?” Sote tunaweza kujifunza kwa njia moja ya mbinu hizi, ijapokuwa kama hatuna

mojawapo ya hisia hizi, lakini kwa kawaida kila mtu ana mbinu moja au mawili ambayo ni njia zake

za kufunzwa vizuri kuliko wengine.

Katika kikundi chochote kile kuna wanafunzi ambao mbinu yao ya mafunzo inawezakuwa katika

moja ya hizi mbinu. Kwa mwalimu, changamoto ni kutoa mbinu nyingi za mafunzo ikiwemo

kutumia mbinu zote nne katika sehemu moja katika mkondo wa elimu. Kutumia mbinu nyingi katika

mafunzo yanatuelekeza zaidi mioyoni na akilini mwa mwanafunzi.

VIFAA VYA MAFUNZO

ü Kutazama, Kusikiza, Matendo na Hisia

ü Ubao, Kuhadithia, Kuigiza na Ushuhuda

ü Vibandiko, Kusoma kwa Sauti, Kuiga na Hadithi

ü Ubao, Mazoezi ya Uhadhiri na Video

ü Kanda, Ishara na Kuimba

ü Maonyesho, Kuimba, Michezo na Kuigza

ü Video, Kusikza na Kuacha kuiga

ü Vijikaratasi, Lugha, Viti na Mazoezi

ü Kutazama, Lugha na Kuimba kwa Hisia.

ü Lugha ya Masonyuso

ü Kusongasonga

ü Lugha

Page 6: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[6]    

Kwa kiongozi wa uchambuzi wa biblia, kuongea, kuandika maandishi makubwa ili wote waone,

kutumia viashiria, kutoa makaratasi ya matumizi, kuwapanga watu kuhama kutoka gundi ndogo hadi

kubwa na kurudi magundi yao ya hapo awali, kuigiza hadithi, kuhadithia, kuwapa fursa watu kueleza

hadithi zao wenyewe zinazo kubaliana na hadithi za Biblia, hivi vyote hufanya mafunzo kueleweka

zaidi.

Toleo hili lina mipangilio ya mafunzo inayohimiza matumizi ya njia nyingi na kushirikisha

wanafunzi. Kiongozi wa uchambuzi wa Biblia anahimizwa kutumia jinsi ilivyo au kubadili mipango

ya uchambuzi wa Biblia kulingana na mahitaji ya kikundi.

Kuongeza uigizaji au kubadili kiwango cha kikundi kinaweza kuongeza utajiri wa mafunzo kwa

washiriki wako. Kushirikisha kila mtu katika mafunzo yaweza kuleta mambo ya kuduwaza kutoka

kwenye vikundi.Washiriki katika vikundi wanaweza kutambua mafunzo mengine kando na yale

yaliyokusudiwa. Mitazamo hayo mipya na matumizi ni vya maana kwani Biblia ina mengi ya

kutufunza kuliko ufahamu wa mwalimu yeyote.

Utumizi wa “wakati mafunzo yanafaa” kutoa nje hekima ya kikundi kupitia mtindo wa kushirikisha

inaweza kuwapa fursa watu kujifunza mengi kuliko “mitazamo ya mafunzo” yaliyoandikwa kwenye

tamati ya kila awamu. Kuwa na mpango maalum na kuwa na uwazi kwa kila hali na mitazamo ya

kikundi, mwalimu anaweza kuongoza uchambuzi wa Biblia ambayo ni ya kufurahisha na ya kuleta

mabadiliko.

(Ujumbe wa jinsi watu hujifunza na kukumbuka na mtindo ya kujifinza yametolewa kutoka

“Training for Change, 1501 Cherry Street, Philadelphia, Pennsylvania,

19102 USA.” Tufuti: www.TrainingForChange.org)

UCHAMBUZI WA BIBLIA KATIKA MUKTADHA WA TAMADUNI MBALI MBALI

Punde tunapochambua Biblia tunakutana na tamaduni tofauti. Hakuna mtu yeyote kati yetu ambaye

amewahi kuishi katika tamaduni zilizo ndani ya Biblia kwani tulitengwa nao na maumbile ya dunia,

nyakati na lugha. Zaidi ya hayo, hamna utamaduni moja ya kibibliaMaandiko ya Biblia inashirikisha

miaka yanayozidi miaka 2,000 na tamaduni za Kiebrania na Kiyahudi yamekuwa yakibadilika katika

karne hizo.

Orodha ya tamaduni za kibiblia ni kama utamaduni wa Waebraniaa wa kuhamahama, utamaduni wa

mashambani au vijiji vya makabila ya Israeli hapo mwanzo, utamaduni wa wafalme wa Kidaudi

uliyokuwa katika miji mikubwa, utamaduni wa Wayahudi waliyo kuwa matekani iliyoundwa

kutokana na dini badala ya mahali wanatoka, utamaduni wa makabila nyingi kati ya Wagiriki na

Warumi ni baadhi ya tamaduni zilizotajwa kwenye Biblia.

Page 7: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[7]    

Hadithi za Biblia zina lengo kamili kama vile hadithi zote za kibinadamu zilivyo. Zimejitokeza

kulingana na mazingira katika nyakati hizo, kwa wakati mwingine inahusisha tamaduni ya baadaye

inayotusimulia hadithi iliyofanyika hapo awali au utamaduni tofauti. Tunaposoma hadithi hizo za

zamani, tusiyatumie amri za Mungu au taswira kwa wakati wetu au mahali tupo vile ilivyo. Bali

tunafaa kujiweka katika mazingira ya tamaduni hizo ili tushike msimamo, tabia na mabadiliko ya

kiroho iliyojitokeza wazi katika tamaduni hiyo.

Walimu waliopitia mashule ya Biblia wanafaa kutoa kutoka mafunzo yao kuhusu tamaduni za Biblia.

Kama mwalimu anawezakupata vitabu vya historia ya Biblia aidha kutoka kwa maktaba ya mashule

ya Biblia au mchungji aliye karibu, basi utafiti dogo kuhusu historia na mazingira ya tamaduni ya

hadithi inaweza kufanya kazi hiyo kuwa na mistari mingi ya Biblia.

Punde somo la hadithi au mafunzo ya biblia yameeleweka katika mazingira yao kamili, tunatwaa

msimamo, tabia na mabadiliko ya kiroho katika mazingira za tamaduni zetu za kawaida. Tunajiuliza

maswali ya jinsi msimamo, maadili na tabia za kiroho ya zile nyakati zingechukua mfumo ipi leo

katika mazingira ya tamaduni zetu.

Msimamo iyo hiyo inaweza kuchukua mfumo tofauti katika tamaduni tofauti. Kwa mfano, mafunzo

kuhusu “nguo zinazostahili kuvaliwa” yawezakuleta hisia tofauti kulingana na jinsi sheria ya

tamaduni inavyotambua nguo zinazostahili.

Hii jinsi ya kusoma na kutafsiri muktadha tamaduni tofauti za Bilia ni nzuri sana katika kusoma

kuhusu mzozo na jinsi ya kubadili mzozo. Mizozo nyingi yana habari kamili ya shida na mambo kati

ya pande zote zinazozozana. Yawezekana kuwa shida hizo hatuyajui na tunaziacha na kukimbilia

mistari ya Biblia ambayo ni rahisi kufahamu. Kuchukua wakati mwingi katika vifungu, kutumia

uigizaji ili kutumia hisia na akilia zetu katika mapito hayo ya kitambo na ni ya kibinaadamu yaweza

kusaidia kufunua kisa ambacho kwa mara ya kwanza kinaonekana kigumu na kinaduwaza.

Ili kuendesha uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya tamaduni tofauti, tujiulize maswali

yafuatayo:

1. Je, ni nini kilikuwa kinatendeka katika kisa hicho cha Bilia?

2. Mambo hayo yalikuwa na maana gani kwa waathiriwa?

3. Mafunzo gani ya kiroho, ikiwemo mizozo na maridhiano waliyojifunza kuptia mambo hayo?

4. Mafunzo hayo ya kiroho yana maana gani katika maudhui yetu?

5. Ni nini tunaweza kufanya katika maisha yetu, mizozano yetu, uhusiano kati yetu, ambayo itafanya

mafunzo hayo kuwa vitendo?

Page 8: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[8]    

Hatuwezi kwa ukamilifu kutafsiri tamaduni za Biblia moja kwa moja hadi tamaduni zetu, lakini

twaweza kugundua kile Mungu anatueleza siku hizi. Katika jitihada zetu kujiingiza katika hadithi za

Biblia tunaona Mungu akiingia katika hadithi zetu kwa njia mpya.

JINSI YA KUTUMIA KIJITABU HIKI CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA

Kijitabu hiki chaweza kutumiwa kama kosi kuu ya kusoma au kusoma mojawapo ya taarifa

uliyopewa hapa.

Kwa kila sehemu ya uchambuzi, mwalimu anapaswa kusoma taarifa mara kadhaa. Maandiko ya

utangulizi yaweza toa usaidizi aidha kwa kuelewa baadhi za tamaduni na lugha au maudhui yote ya

hadithi katika Biblia.

Uliza maswali kuhusu muktadha wa tamaduni mbali mbali kutoka Biblia kulingana na muktadha

wako. Pitia maswali yote ya kila awamu katika kijitabu hiki.

Tilia maanani “vidokezi muhimu” na “mtazamo wa somo.” Mtazamo wa somo linatoa mambo

ambayo yamekuwa ya fanaka katika kazi ya kutafuta amani. Rudia kusoma taarifa ukiwa na maswali

pamoja na vidokezi akilini. Uwe na uhakika kuwa unajua hadithi na maudhui yake.

Chagua mbinu utakayotumia katika somo. Uwe huru kuongeza au kutumia jinsi ilivyo ratiba ya somo

kulingana na uzoefu wako au mahitaji cha kikundi.. Waza njia za kuongeza kiwango cha kushirikisha

kila mmoja katika vikundi vyote katika mafunzo ukitumia vifaa na mbinu za kufunza tofauti tofauti

kusaidia kila mbinu ya mafunzo.

Unapofundisha wanafunzi wako, utilie manani baadhi ya vipeo ambavyo vinahitaji kushughulikiwa

sana katika somo. Kama kikundi hicho kitataja vipeo hivyo kutokana na kusoma Biblia, unaweza

kuvisisitiza kwa kuvitaja tena na tena. Kama kikundi hakitataja, waweza kuvitaja baadaye, kwa

mfano, kuuliza maswali ili kuwafanya kufikiria vile inavyo kusudiwa. Si vyema kuvitaja vipeohivyo

muhimu tamati mwa somo, bali litajwe wakati ufaao katika mashauriano ya vikundi.

Uwape washiriki wote nafasi ya kubuni vipeo vingi ikiwemo baadhi ya vitu usiyoyaona au

kuyatambua.Kwa hakika, tarajia kikundi kutambua baadhi ya mitazamo, maarifa au nji ya kutumia

mafunzo ya Biblia ambayo wewe au mwandishi wa kijitabu hiki hawakuyatarajia. Hivi ni vizuri

maana wewe unaweza kuwa mwalimu na vilivile mwanafunzi! Kubali, himiza, sifu na kushukuru

washiriki wa vikundi kwa hekima waliyoleta katika somo hili.

Nyingi ya awamu yanahitaji vikundi vidogo vidogo. Baadhi ya awamu hizi yanahitaji kuigizwa.

Chumba cha kuendesha shughuli hii inafaa kupangwa kwa njia itakayorahisisha vitendo hivi. Viti

ambavyo vinaweza kuhamishwa kwa urahisi vinafaa. Vinaweza kupangwa kwa mtindo wa duara au

nusu duara ili michezo ya kuigiza yafanyike katikati na wote wapate kuona. Viti vinaweza

Page 9: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[9]    

kugawanywa kwa vikundi vidogo vitatu au vinne na baadaye kuvirejeshwa punde darasa lote

linakusanyika tena. Omba kabla ya kuanza matayarisho na kabla darasa kuanza. Wewe sio mwalimu

kamili bali ni Roho Mtakatifu.

Wajibu wako ni kuwa mtumishi wa Roho Mtakatifu kufunua akili na mioyo ya wanafunzi kwa yale

Roho Mtakatifu amewakusudia katika maandiko, kujua na kukua. Roho Mtakatifu ataleta “wakati

ufaao kwa mafunzo” ikiwemo nyakati zile sizizopangwa na ya kustaajabisha. Kuwa wazi kwa

vipawa vya Mungu katika nyakati hizo.

Anayefunza hupata mafunzo nyingi, kwa hivyo kuwa tayari kufunzwa na Mungu!

Page 10: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[10]    

SEHEMU YA 1:

UKAGUZI WA MZOZO

Awamu ya 1: Mzozo kama Eneo Takatifu (Kutoka 2.23-4.17)

Awamu ya 2: Kuongezeka kwa Mzozo (Mwanzo 3.8-13; 4.1-6; 4.19-24; 10.8-12)

Awamu ya 3: Mzozo wa Kifamiliai (Mwanzo 25.19-34; 26.34-28.9)

Awamu ya 4: Safari ya kupata maridhiano (Mwanzo 28.10-33.20; 35.27-29)

AWAMU YA 1

MZOZO KAMA ENEO TAKATIFU

KIFUNGU: Kutoka 2.23-4.17

HAPO NYUMA:

Jamii ya Yakobo walihamia Misri ili kujiepusha na ukame uliokuwa kule Kanani na kwa wakati huo

mwanake alikuwa mkubwa sana katika afisi ya Farao. Kwa miongo na karne nyingi uongozi wa

Yosefu ulisahauliwa kule Misri. Uongozi upya wa kifalme ulianzishwa kule Misiri bila uhusiano na

Yosefu au umaarufu wake.

Baadaye wafarao wa Ufalme wa Misri mpya wakatia matekani Waebrania wote. Hofu kuhusu

kuongezeka kwa idadi ya Waebrania ulizuka na ikawabidi Farao kuanzisha masharti makali sana

kwao.

Baada ya jaribio la kuwafanya wakunga kuwaua watoto wa kiume wa Waebrania wakati wa

kuzaliwa kutibuka (angalia awamu ya 15 ulioangazwa na Kutoka 1:15-22), Farao aliamuru watoto

wote wa kiume wa Waebrania kuuwawa. Mamake Musa alimweka ndani ya kikapu na kumficha

kando ya mto. Bintiye Farao alipata mtoto yule na kumlea katika mazingira ya kifalme.

Kama mwanamme, Musa alihisi mzigo wa watu wake. Alishuhudia mmisri ambaye ni kiongozi wa

watumwa akimpika mtumwa wa kiebrania. Musa alimuua yule Mmisri na kuuficha mwili wake.

Muda mfupi baadaye Musa aliingilia vita iliyokuwa kati ya Waebrania wawili, na kumbe walijua

kwamba Musa alimuua Mmisri. . Farao alipata habari kuhusu mauaji yale na akajaribu kumkamata

Musa. Musa alitorokea Midiani, mji uliokuwa Uarabuni, lakini uliopanuliwa kujumuisha miji yote ya

Sinai.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Anza somo kwa kuandika neno “MZOZO” kwenye ubao au jikaratasi. Uliza darasa: ni maneno, hisia

au michoro gani inawajia akilini wakifikiria juu ya “mzozo”? Yaandike maneno na sentensi zao

kwenye ubao au karatasi. Alika watu kuongezea ile orodha methali au misemo juu ya mzozo

Page 11: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[11]    

Uwape watu muda mwingi ya kufikiri. Wakati kikundi kimetoa orodha nzuri, uwaambie wasome

orodha nzima. Huenda utasoma kila neno, sentensi na msemo. Uliza kikundi ni nini waligundua juu

ya ile orodha. Katika kila hali, orodha inaweza kuwa na maneno yaonekanayo mabaya. Maneno

mazuri yanaweza kuwa kwenye orodha ile na ungetaka kuyatambua. Kuna maneno mazuri

yatakayopatikana kutokana na kupitia mzozo.

Halafu yaandike maneno haya: “Eneo Takatifu” juu ya orodha. Uliza washiriki: maneno “Eneo

Takatifu” yana maana gani?

Ni jinsi gani mzozo waweza kutambuliwa kama Eneo Takatifu? Kuna yeyote anayejua ni wapi

maneno “Eneo Taatifu” yanapatikana kwanza Bibliani? Kama mwanafunzi atatambua kisa cha Musa

karibu na ule msitu uliyokuwa ukiteketea, alika mwanafunzi huyo kueleza kisa hicho kadiri ajuavyo.

Kama hamna, fafanua kisa hicho kwa ufupi kuhusu Musa kuona msitu ukiteketea, kuukaribia, na

kusikia sauti ikisema, “vua viatu vyako, kwa maana eneo uliyosimama ni Eneo Takatifu” Uwambie

darasa kuvua viatu vyao kwa kipindi chote cha Uchambuzi wa Biblia. Uwe kielelezo kwao kwa

kuvua viatu vyako. Gawa darasa kwa vikundi vya watu 5 au 6. Uwaambie wasome kisa hicho kwa

muda wa dakika 20, wakijibu maswali haya: ni maudhui gani madogo au makubwa wa mzozo kwa

kisa hiki? (huenda watapaswa kurejelea aya ya 2) Musa alijifunza nini kuhusu Mungu? Musa

alijifunza ninin kujihusu? Musa alijifunza nini kuhusu wengine (Farao, Aroni, Waebrania)? Baada ya

uchambuzi wa vikundi vidogo, uwakutanishe darasa lote tena. Alika kikundi kimoja kutoa jibu lao

kwa swali la kwanza.

Alika vikundi vile vingine kutoa maoni yeyote yatakayo ongezea kile kilichosemwa na kikundi cha

kwanza. Alika kikundi kingine kujibu swali la pili, ukikubali maoni kutoka kwa vikundi ambavyo

wanataka kutoa maoni. Endelea vivyo hivyo kwa maswali yote manne. Toa maoni kuhusu ufunuo

unaotendeka kwenye Eneo Takatifu. Tuonavyo katika kifungu hiki, katikati mwa mzozo mkali, Musa

alijifunza kuhusu Mungu, kujihusu na kuhusu wengine.

Katika mizozo yetu, tunapata ufunuo au mitazamo mipya kutuhusu, kuhusu wengine na kuhusu

Mungu. Mitazamo hiyo mipya, ambayo huenda yamewezekana kupitia masahibu ya mzozo,

inatusaidia kukua kama watu au jamii. Halafu uwaulize walivyohisi kusoma Biblia ikiwa viatu vyao

vimevuliwa. Wengine huenda walifurahia tendo hilo. Wengine wanaweza kuhisi vibaya. Ikiwa mtu

atalalamika kuwa alihisi vibya kuvua viatu vyake, uliza darasa kama kuna mwingine alihisi vile

aweka mkono wake juu. (Hisi huru kuinua mkono wako!) Eleza kuhusu mzozo jinsi inatufanya tuhisi

vibaya, ukirejelea orodha uliyoundwa mwanzo wa awamu. Na mzozo huenda ikawa “eneo takatifu”

ambalo tunajifunza mengi kutuhusu, kuhusu wengine na kuhusu Mungu. Chora “Eneo La Raha”

(angalia picha iliyo mwisho wa awamu hii). Hatujifunzi mengi tukiwa kwa Eneo la Raha kwa sababu

Page 12: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[12]    

kila kitu ki rahisi na salama. Pia, hatujifunzi mengi tukiwa Eneo la Tahadhari. Katika Eneo la

Tahadhari tunakabiliwa na hatari na hofu. Kwa mara nyingi tunaacha mambo mengine na kujizuia

badala ya kukubali ujumbe mpya. Eneo bila Raha ni eneo nzuri ya kujifunza kwa maana tuna

changamoto tele, tuko macho, na huenda tumetishwa kiasi cha kutupa nguvu.

Hatujatosheka, kwa hivyo tunatafuta njia mpya ya kukabiliana na masahibu yaliyo mbele yetu. Kwa

mara nyingi mzozo hutuondoa kutoka eneo letu la raha. Baadhi ya mizozo hutupeleka kwenye eneo

la tahadhari ambapo tunahisi kuhatarishwa. Lakini tukikabiliana na mizozo yetu kwa ustadi na

ubunifu, tutaweza kuifanya iwe eneo bila raha ambapo tunajifunza na kukua.

Eneo Bila Raha ni Eneo Takatifu. darasa kuunda vikundi vya watu wawili au watatu. Uwaalike

kuelezeana mambo mengine matatu wamepokea kutokana na mizozo katika maisha yao- labda

mtazamo, ujuzi, nafasi, rafiki. Halafu waelezeane jambo moja wangependa kupokea kupitia mzozo

wanaoshuhudia kwa sasa. Kabla kumaliza awamu itisha kila kikundi kitu kimoja au vitu viwili

walichopata kwa kupitia mzozo.

VIPEO MUHIMU:

* Ingawa nyingi ya uzoefu wetu na mzozo yanazua huzuni na kuleta matokeo mabaya, mna mambo

mazuri yapatikanayo mzozo. Watu wataelewana vizuri. Shida zaweza kutuleta uwezo na moyo ili

kuleta suluhu ya kutendeka kwa kila mtu aliyehusika. Tunaweza kukua kwa kupitia changamoto za

mzozo. Mtazamo ya somo: mzozo inaweza kuwa na mchango bora ambayo tunaweza kujenga zaidi

* Kwa mara nyingi Wakristo husema vile Mungu huwa nao wakati wanapitia magumu. Biblia

huongea juu ya Mungu kuwa “ngao” yetu au “mlinzi” wetu au juu ya baraka kwa yule

“atakayeshinda”. Haya yote ni picha za mzozo. Mungu anajua kila mzozo. Kwa hakika, tunaweza

kusema kuwa wokovu ni kitovu cha ubunifu, upendo, ukomboaji na hukumu ya Mungu katika mzozo

baina ya Mungu na binadamu. Ikiwa yote haya ni sehemu ya imani yetu, tunapaswa kutambua

kwamba mizozo katika familia, jamii, makanisa na mataifa inayotukumba pia ni sehemu imeingiliwa

na Mungu. Mungu ako nasi katika mzozo kwa kutenda, kutuongoza, kutufunza, kutuweka huru,

kututia motisha na mengine mengi. Mtazamo wa somo: mizozo yetu yote inaweza kuwa Eneo

Takatifu ambapo tunakutana na Mungu na kubadilishwa katika mkutano huo.

* Ukubwa wa kukua na kujifunza kwetu hutokea katika mazingira ambayo sisi tumepata motisha

kujiona kwa ndani kabisa na kung’ang’ana na maswali na changamoto. Mzozo unaweza kuwa

mwalimu mkuu wa kututoa kwenye Eneo la Raha hadi hali ambapo tunataka kujifunza na kukua ili

tuyafikie suluhu dhabiti. Pia katika elimu, kujifunza zaidi hakutokani na kuwapa wanafunzi majibu

lakini kuwapa maswali ambayo yatawapa changamoto kufikiria sana, kutangamana na kugundua

Page 13: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[13]    

hekima pamoja. Mtazamo wa somo: mafunzo hutokea vizuri katika Eneo bila Raha, ikiwemo

kutohisi vizuri iletwayo na mzozo.

MCHORO WA ENEO LA RAHA

Eneo la Raha

Eneo Bila raha

Eneo la tahadhari

Page 14: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[14]    

AWAMU YA 2

KUONGEZEKA KWA MZOZO

VIFUNGU: Mwanzo 3.8-13; 4.1-16; 4.19-24; 10.8-12

HAPO NYUMA:

Aya za kwanza katika kitabu cha Mwanzo zinatupa picha ya hali ilivyokuwa hapo mwanzo ya

mwanadamu. Habari ya uumbaji wa dunia inafuatiliwa na habari ya kuanguka kwa mwanadamu

(“kuanguka” kwa mwanadamu kutoka ile uhusiano wa karibu na Mungu hadikutotii, dhambi na

kifo). Mzozo unazuka haraka kati ya Hawa na mumewe. Katika kila kisa kinachofuata inaonekana

kwamba uzito wa mzozo unaongezeka ikijumuisha kutokea rabsha kwa ghafla.

Katika Mwanzo 10 Nimrodi aliitwa “mtu mwenye nguvu” maneno yanayoashiria kuwa alikuwa

kiongozi katili. Jina la Nimrodi linahusishwa na miungu ya wababiloni na mfalme wa Asiria wa

kwanza kuongoza Babiloni.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Gawa darasa kuwa vikundi vine, ukiwapa kila kikundi moja ya vifungu vifuatavyo:

Mwanzo 4.1-16

Mwanzo 4.19-24

Mwanzo 10.8-12

Uliza kila kikundi kutazama mzozo katika kifungu walichopewa na kujibu maswali katika somo lao:

Mzozo uliopo ni lipi nal inahusisha akina nani?

Nini ilileta mzozo kuzuka?

Ilishughulikiwa vipi?

Mzozo ulipanuka vipi?

Matokeo yake?

Kikundi walichopewa kushughulikia habari ya Nimrodi katika Mwanzo 10 wanapaswa kufikiria

zaidi kuhusu kinachoendelea na matokeo inayohusu mzozo. Punde vikundi vinavunjwa, kiongozi cha

kikundi kilichopewa Mwanzo 10 kueleza habari kuhusu Nimrodi iliyopewa katika hapo nyuma.

Uliza ni maneno yapi mapya yamejitokeza kwa binadamu ambayo yanahusiana na mzozo kutokana

na kuongezeka kwa umaarufu wa Nimrodi kama kiongozi wa kwanza ya ufalme? Ufalme wake

ungeundwa vipi?

Uwape kila kikundi dakika 15 kusoma na kujadili vifungu hivyo. Kila kikundi kije na mchezo mfupi

wa kuigiza kupitisha habari au maudhui iliyo katika kifungu kama wanaweza. Halafu uwape kila

Page 15: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[15]    

kikundi kuripoti habari kwa kufuata orodha ilivyo katika Biblia. Wakati kipindi cha Michezo ya

kuigiza na kuripoti kimeisha uliza vikundi vyote maswali yafuatayo:

Ni vipi mzozo unayoptia unaonekana kuzidi? Hatua zipi tofauti zinazoleta kuongezeka kwa mzozo?

Mmoja asome Mwanzo 6.11-13. Habari ya Nuhu inatendeka kati ya habari ya Lameki na Nimrodi.

Hii inasema nini kuhusu mbinu ya Lameki ya kukabiliana na mzozo katika uhusiano kati yake na

binadamu na kati yake na Mungu?

Vifungu hivi vinaleta picha gani kuhusu asili ya mzozo katika maisha yako na katika shughuli za

kimataifa. Kuna mafunzo yanayojitokeza kutokana na kulinganisha hivi?

Katika mjadala mwalimu anaweza kutoa habari kutoka kwa vipeo Muhimu kuelezea zaidi baadhi ya

njia habari hizi za kale zinatumiwa katika kukabiliana na mzozo.

VIPEO MUHIMU:

* John Paul Lederach katika “Mediation Taining Manual” iliyotolewa na Mennonite Conciliatio

Service inaeleza hatua saba ya kubadilisha mzozo:

1. Utatuzi wa shida ambapo vikundi havisikizani bali wanaelezana shida hilo.

2.Kubadilisha kutoka hali ya kutosikizana hadi tofauti za kibinafsi; mtu huyo anaonekana kama

shida.

3.Kuongezeka kwa mambo-kutoka jambo fulani hadi jumla, kutoka jambo moja hadi mambo mengi.

4. Kuzungumza na wengine juu ya mtu aliye kwenye mzozo badala ya kuzungumza na aliyeathiriwa

moja kwa moja

5. Majibizano na kuongezeka –jicho kwa jicho.

6. Uadui kuongezeka zaidi

7. Uaribifu kwa maadili ya jamii (kwa mfano talaka, kugawanyika kwa kanisa, vita vya umma na

mengine)

Mzozo ikizidi kuendelea kupitia hizi hatua kutakuwa na rabsha nyingi, upungufu wa kuaminika,

upungufu wa kupokezana habari na upungufu wa kukutana uso kwa uso.

Katika habari kutoka kitabu cha Mwanzo tunaona Adamu na Hawa wakiwa katika hatua ya pili

ambapo Adamu anawalaumu Hawa na Mungu kwa ile shida. Kaini pia alikuwa katika hatua ya pili

akimuona Abeli kama shida, lakini akarukia upesi hatua ya saba na kujiua.

Lameki alibakia hatua za 5, 6 na 7 akijikabiliana mara nyingi. Mtazamo wa somo: Mzozo

usiokabiliwa kikamilifu huelekea kuwa mbaya zaidi.

Page 16: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[16]    

* Katika Nimrodi tunaona kuchipuka kwa mifumo ya utawala wa kifalme wenye nguvu. Utawala

wenye nguvu ni hali ambapo mtu mmoja au kundi la watu wajitwalia uongozi ambayo inatumiwa

kutisha au kutukana wengine.

Bibliani kote, uongozi wa kimabafu ni ya shida sana, hata uangalie utawala wa Farao au matamanio

ya Samueli kutaka kuanzisha utawala wa kifalme mle Israeli (angalia 1Samueli 8). Mwisho wa

utawala wa kimabafu inaonekana katika Ufunuo wa Yohana 13 ambapo Ufalme wa Warumi

uliyoteza Wakristu inaelezwa kuwa ni ya kishetani.

Kinyume na mtazamo wa Ufunuo wa Yohana kwa utawala au serikali wa kidunia kuwa ni wa

kishetani, Paulo katika Warumi 13. 1-7 anatoa mtazamo wake wa serikali kuwa umewekwa na

Mungu kuzuia jamii kutokana na watu wabaya. Kila serikali ya kidunia ina mchanganyiko wa

kuwekwa na Mungu na pia kuwekwa na kishetani. Serikali zingine zinaonyesha matendo ya

kishetani katika tabia zao zinazoharibu, ilhali serikali zingine zinajali sana hali ya maisha ya wale

walio chini yao.

Mtazamo wa somo: mara nyingi, njia ya kutatua mizozo imewekwa kwenye taasisi, kwa hivyo ni

changamoto kwa wakristo kufahamu uwezo wa mamlaka ili kuweza kubadilisha mizozo za kisiasa au

za kijamii

 

Page 17: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[17]    

AWAMU YA 3

MZOZO WA NYUMBANI

KIFUNGU: Mwanzo 25.19-34; 26.34-28.9

HAPO NYUMA:

Isaka na Rebeka walikwa wafukaji wa kuhamahama waliyoishi mji wa Kanani. Abrahamu babake

Isaka alikwa amesafiri kutoka miji yenye rotuba, kutoka miji ya Uri na Harani, chini hadi Kanaani.

Walikwa wafukaji wa kondoo na mbuzi.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Historia ya Yakobo na Esau ni ndefu katika maandiko, hivyo vifungu vya Biblia vingesomwa kabla

wakati wa masomo au darasa. Somo hili linagawa habari hii kuwili: “Jinsi ya Kuingia kwenye

ugomvi” na “Jinsi ya Kuridhiana” Vifupisho vya habari hizi zaweza kuandikwa na kutumiwa badala

ya vifungu vya Biblia darasani, ijapokuwa ni vyema kuhimiza darasa kusoma vifungu hivyo kabla ili

wawe na ufahamu wa habari hiyo.

Gawa darasa hadi vikundi vinne. Uwape kila kikundi majawapo ya hawa wahusika: Yakobo, Esau,

Isaka na Rebeka. Kila kikundi kitachagua mmoja wao kuwakilisha kikundi chao kama mhusika

mbele ya darasa. Kwa kila kikundi, soma habari kwenye ufupisho au vifungu vyote kwa sauti. Halafu

kikundi kijadili na kujibu maswahili yafuatayo yanayohusu nafasi ya mhusika waliyopewa:

* Je, unafikri ni hisia zipi mhusika alipitia nayo kwenye habari kwa wakati tofauti?

* Je, ni mambo gani mhusika alikumbana nayo, na ni njia zipi maoni yake yanajitokeza?

* Je, ni jinsi gani mhusika alitetea au anaweza kutetea matendo yake?

Wape muda wa dakika 20 hivi wa kusoma na kujadili. Halafu leta darasa pamoja kwa mahojiano ya

kuiga mhusika, ukimualika yule anayachukua nafasi ya mhusika fulani katika biblia, aje mbele au

katikati ya darasa kutoka kila kikundi. Alika kila mhusika kuwasilisha maoni yake kuhusu mzozo wa

kifamilia. Anzia mhusika yeyote au unaweza kuwapanga (kwa mfano: Isaka, Rebeka, Esau, Yakobo)

Mpe kila mhusika dakika chache kueleza maoni yake, halafu waulize kila mhusika maswali zaidi ya

kindani, kama vile (tumia majina kamili ya wahusika, siyo majina ya washiriki) “Esau, kwa nini

ulipeana haki yako ya mzaliwa wa kwanza kwa supu tu?”

“Yakobo, wengine watasema kuwa ulitumia mateso ya nduguyo kujinufaisha-utajitetea vipi dhidi ya

shutma hizi?”

“Isaka, uliacha uongozi wa familia yako kwa kuruhusu mzozo kati ya wanao kuendelea bila utatuzi

wako kama mzazi?”

“Rebeka, kwa kupendelea Yakobo dhidi ya Esau, je ulichangia katika kudhorora kwa tabia na

mienendo yake Yakobo?”

Page 18: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[18]    

Uliza darasa lote iwapo kuna mtu ana swali au maswali kwa mhusika yeyote.

Unaweza kuuliza wahusika kujibu maswali, kama :

Ni nani ana mamlaka makuu nyumbani? Je, ni kwa njia zipi unahisi mamlaka hayo?

Matarajio yako gani yalikuwa dhidi ya watu wengine wa jamii katika hali hii?.Matarajio hayo

yalifikiwa au hayakufikiwa vipi?

Shukuru washiriki wote walioshiriki. Halafu alika darasa lote kusaidia kutambua:

Ni mamabo yepi yaliyotokea haraka katika mizozo zile?

Ni mambo yepi ya kindani yalitokea katika zile mizozo?

Ni hisia zipi zilizowakumba wahusika tofauti katika habari?

Ni maamuzi yepi ya wahusika yaliyochangia kuzambaratika na kufanya hali kuwa ngumu zaidi?

Ni maamuzi yepi mbadala kila mhusika angechukua ambaye yangepunguza kiwango cha

mzozo?(andika orodha ya maamuzi mbadala amabayo yametolewa na vikundi)

Ni muundo au vikezo vipi vya kitamaduni unaweza kutambua ambavyo vingezambaratisha au

kupunguza mzozo?

Ni maswala gani tunaweza kupata kutokana na mzozo unaoendelea sasa, katika hii familia ya kale?

Waulize watu wajikumbushe mzozo ambao unawakabili na waeleze uamuzi ambao wamefanya, bila

kujali kama itakuwa bora au mbaya.

Je, kuna maamuzi ambayo wamefanya yanayoweza kupeleka mzozo kuelekea kupatikana kwa

suluhisho? Waulize watu wasimulie kutoka kwa mafikira yao baadhi ya suluhisho ambayo inaweza

kuleta mapatano mazuri katika mzozano.

Tengeneza orodha ya maoni yaliyotolewa. Funga na ombi kimya kuhusu hii kwa kila mtu darasani.

Kipindi kifuatacho kitaangazia hatua zilizochukuliwa na familia hii kuelekea maridhiano.

VIPEO MUHIMU

* Mizozo ina viwango viwili. Kiwango cha kwanza kinahusu muktadha. Katika hadithi hii, Sababu

ya mzozo kati ya Yakobo na Esau ni kutokana na haki ya mzaliwa wa kwanza na baraka zake.

Kiwango kingine kinatokana na uhusiano. Esau alikuwa katika uhusiano mbaya wa kushindana.

Wazazi wao pia walikuwa wamegawanyika, huku kila mzazi akimpendelea mmoja wa wanao.Wakati

mwingi mzozo hutokana na visababu, lakini kutopatana katika uhusiano wao ulizidisha mzozo zaidi.

Hivyo basi visababu na uhusiano inastahili kutambuliwa ili kuelewa kinachoendelea katika mzozo,

na yote yanafaa kupewa kipaumbele kama mzozo unapaswa kutatuliwa kwa njia kamilifu.

Mtazamo wa somo: Tuangalie visababu na mahusiano wakati tunapotazamia kutatua mzozo.

Page 19: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[19]    

*Katika hali mbalimbali za mzozo kuna wakati mtu anaweza akafanya mzozo uendelee zaidi au

kuisuluhisha. Kila mhusika alichukua hatua ambayo ilifanya mzozo kuendelea na kuwa mgumu

zaidi. Hakuna mfumo katika mizozo yetu ambayo mwisho inatarajiwa kuwa mbaya zaidi.

Lakini wote wanaohusika katika mzozo hufanya uamuzi. Maamuzi haya yanaweza yakafanya mzozo

kusuluishwa au kuendelea zaidi. Maamuzi yanaweza yakasababisha shida zingine na kuzidisha

uadui, au maamuzi yanayofungua mawasiliano na kuleta njia mpya za kusulihisha shida. Maamuzi

mengi yanafanywa ili kuuwezesha kuzidisha mzozo.

Hivyo basi hatua nyingi nzuri huitaji kufanywa ili kusuluhisha mzozo hatua kwa hatua. Tunapaswa

kuchukua jukumu la maamuzi yetu katika mazingira ya mzozano.

Mtazamo wa somo: Angalia kwa makini suluhisho kabla ya kuingilia mzozo na uchukue matokeo ya

uamuzi wako.

AWAMU YA 3:

HAPO NYUMA

Yakabo na Esau sehemu ya 1: Jinsi mzozo ulivyoanza.Kwa miaka ishirini baada ya kuoana, Isaka na

Rebeka hawakubarikiwa kupata watoto. Isaka alimwombea Rebeka, kisha Rebeka alichukua mimba,

mapacha, kwa kuwa Mungu alijibu maombi ya Isaka. Lakini watoto walipigana tumboni mwa

Rebeka sana hadi akaona uchungu mwingi na kufadhaika “ikiwa ni hivi mbona niishi?”

Rebeka akaombea ujauzito wake uliokuwa wa taabu. Mungu akamwambia yeye kuwa mataifa

mawili yako tumboni mwake, watu wawili watakaotengana. Mwingine atakuwa mkuu, na mkubwa

atamtumikia yule mdogo. Wakati wa kijifungua ulipofika, aliyetangulia alikuwa mweupe na alikuwa

na nywele nyingi na akaitwa Esau. Nduguye akafuata huku akimshika kisikino chake Esau, naye

akaitwa Yakobo, maana yake “anayeshika kisikino.”

Wakati watoto hao walipokua, Esau akawa anayependa kwenda mwituni na akawa mwindaji hodari.

Lakini Yakobo akawa mpole na kukaa nyumbani. Isaka alipendezwa sana na Esau, lakini Rebeka

alimpenda Yakobo. Siku moja, Esau alifika toka mawindoni huku amehisi njaa. Yakobo alikuwa

akipika chakula. Esau akamwomba supu, lakini Yakobo akamwambia Esau, “Kwanza nipe haki yako

ya mzaliwa wa kwanza” ( Haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya faida au zawadi ya kuwa kifungua

mimba mvulana, pamoja na haki ya kupewa urithi kubwa). Kwa hakika Esau, kwa ajili ya njaa,

hakujali hayo akasema karibu afe kwa njaa, hivyo basi haki ya mzaliwa wa kwanza itamsaida na

nini? Lakini Yakobo alisisitiza kwa Esau aape, na Esau akaapa, kwa hivyo akapeana haki yake ya

mzaliwa wa kwanza kwa nduguye mdogo. Yakobo hivyo basi akampa Esau supu, mkate na kinywaji.

Aliposhiba, akaondoka akaenda zake.

Page 20: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[20]    

Alipofikia utu uzima, Esau akaoa wanawake wawili wakanani. Wanawake hawa wakafanya maisha

ya Rebeka na Isaka kuwa mgumu na uchungu sana. Kwa hivyo kulikuwa na mzozo mwingi sana

katika familia hiyo.

Isaka alipokuwa mzee, na karibu kuwa kipofu, akamwambia Esau kuwa aende mawindoni alete

chakula na kumwandalia baba yake. Na Isaka atambariki mwanawe Esau kama baba yake mzazi

kabla hajalala. Rebeka alimsikia, na baada ya Esau kuondoka kwenda mawindoni, wakakula njama

na Yakobo. Akamwambia Yakabo achinje wana mbuzi wawili ili yeye Rebeka amwandalie Isaka

chakula kitamu, halafu Yakobo apokee baraka badala ya Esau. Lakini Yakobo alilalama kuwa hata

ingawa baba yake Isaka alikuwa kipofu, atajua kwa kuwa Esau ana nywele mwilini kote ilhali yeye

Yakobo ana ngozi laini, kwa hivyo atalaaniwa na baba yake badala ya kumbariki. Lakini Rebeka

akamwambia Yakobo kuwa acha laana imwendee yeye mwenyewe Rebeka, bali tu atii yale

anamwambia. Kwa hivyo Yakobo akachinja wale wanambuzi, na Rebeka akaanda chakula.

Akachukuwa mavazi mazuri ya Esau na kumvalisha Yakobo. Akachukua ngozi ya wale mbuzi na

kuvalisha mikono na kufungia shingo ya Yakobo, halafu akampatia chakula ampelekee babake Isaka.

Yakobo akamwendea babake akisema kuwa yeye ni Esau na kumpa yeye chakula. Isaka alishangaa

kwa nini Esau amefika mapema mno, lakini Yakobo akajibu kwa upole kuwa Mungu ndiye

amemwezesha. Lakini Isaka bado alikuwa na tashwishi na hajaamini, akamwita mwanawe karibu.

Akamgusa mikono ya Yakobo na akasema, “Sauti ni ya Yakobo, lakini mikono ni ya Esau”. Tena

akauliza kinagaubaga, “Wewe kweli ni mwanangu Esau?” “Ndiyo ni mimi” Yakobo akamdanganya,

hivyo basi Isaka akala. Alipomaliza kula akambusu Yakobo na kusikia harufu ya mwituni iliyokuwa

katika nguo ya Yakobo. Isaka sasa akampa Yakobo baraka, akidhani kuwa ni Esau. Alimbariki kuwa

atakuwa bwana na mkuu dhidi ya nduguye, na yeyote atakayemlaani Yakobo atalaaniwa, na wote

watakaombariki watabarikiwa.

Pindi tu Yakobo alipoondoka, Esau alifika kutoka mawindoni. Aliandaa chakula na kumpelekea

babake. Walipogundua udanganyifu wa Yakobo, walivunjika moyo. Isaka alitetemeka sana huku

akumwelezea Esau kuwa tayari amepeana baraka zake. Esau alilia sana kwa uchungu, huku akimsihi

babake ambariki. Lakini Isaka akamjibu kuwa ameshamfanya Yakobo kuwa mkuu.Esau alilalamika

kuwa Yakobo sasa amemdanganya na kumfadhaisha mara ya pili. Kwanza kwa haki yake ya

mzaliwa wa kwanza na sasa kwa Baraka zake. Akamlilia babake na kumwomba ambariki. Hatimaye

Isaka akasema kuwa Esau ataishi kwa upanga na kumtumikia nduguyo Yakobo, lakini mwishowe

atalivunja mzigo kutoka kwa shingo ya nduguyo.

Kutoka wakati huo, Esau alijawa na chuki dhidi ya nduguyo Yakobo, lakini hakutaka kumwaibisha

babake mzazi aliyekuwa mzee. Hivyo basi aliasimia kuweka hasira yake hadi atakapofariki babake,

Page 21: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[21]    

na maombolezo kuisha ndipo atalipisha. Lakini alitembea huku na huku akitangaza mpango wake wa

kumuua Yakobo. Vitisho vyake vilimfikia mamake Rebeka ambaye alipanga kumtorokesha Yakobo

kwenda nchi ya mbali ya Harani kwenda kuishi na mjombake Labani, nduguyo Rebeka. Alifaulu

kumsihi Isaka amruhusu Yakobo kwenda, huku akitumia ndoa ya Esau ya wanawake wakanani kama

kisingizio- akisema kuwa ni bora Yakobo aende ndiyo apate mwanamke kutoka kwa watu wao,

kupitia Labani, mmoja wa jamii yao. Isaka akambariki Yakobo aende Harani na kumpata mwanamke

ambaye si mkanani.

Esau akagundua kuwa wanawake wake wa kabila 21inguine la wakanani walikuwa tatizo kwa baba

yake, hivyo basi akamwoa shangaziye, msichana wa Ismaeli

(Sehemu hii ya hadithi imetolewa Mwanzo 35.19-34; 26.34-28.9)

 

Page 22: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[22]    

AWAMU YA 4

SAFARI YA MARIDHIANO

KIFUNGU: Mwanzo 28.10-33.20; 35.27-29

HAPO NYUMA:

Isaka na Rebeka walikuwa wafugaji wa kuhamahama,na walikuwa wakiishi Kanani. Ibrahimu baba

yake Isaka alisafiri kutoka eneo lililokuwa na rotuba sana, katika nchi ya Uria na Harani, na

kuteremka hadi Kanani. Walikuwa wakifuga kondoo na mbuzi. Katika sehemu ya 1, mzozo baina ya

Yakobo na Esau ulianza kabla wao kuzaliwa, ulianzia tumboni, na hatimaye ikaendelea kuzidi baada

ya wao kuzaliwa na jinsi wao walipokua. Yakobo anamfanya Esau kuuza haki yake ya mzaliwa wa

kwanza ili apate supu. Badaaye, Yakobo tena anamwibia nduguyo baraka zake kutoka kwa baba yao.

Esau anagadhabika sana kwa uchungu mwingi na kuzongwa na hasira na chuki mpaka anatishia

kumuua nduguyo. Yakobo anatorokea kwa mjombake Labani huko Harani kwa madhumuni ya

kupata mke.

MKONDO WA MASOMO NA MASWALI:

Hadithi hii imechukua vifungu vingi katika kitabu cha mwanzo, kwa hivyo huenda ikawa wa msaada

ukiwapa wanafunzi sehemu hii wasome mapema kabla ya wakati wa darasa. Ufupisho wa hadithi

hii inafuata baada ya maandishi ya awamu. Ufupisho huu unaweza kuandikwa na kusomwa na

wahusika katika vikundi vyao wakati wa darasa au kabla darasa kukutana.

Gawa wahusika katika vikundi, na uwape muda wa dakika thelathini hivi wajadili na kufikiria

kuhusu hadithi yenyewe, huku wakitumia maswali yafuatayo;

Ni mambo gani Yakobo aliyapitia ambayo hatimaye yalimfanya kubadili nia na mawazo yake dhidi

ya nduguye Esau?

Ni kwa njia upi mambo hayo aliyoyapitia yalibadilisha nia yake?

Ni juhudi gani Yakobo alichukua ambayo yalizaidia kuleta utangaano na uwiano na nduguyo?

Nini matokeo ya juhudi hizo?Ni nini kilibadilika ndani ya Esau, na kwa nini? Ni nini Esau alifanya

ambayo ilisaidia kuleta maridhiano?

Waite vikundi walete ripoti vyao. Kwa awamu, waulize kila kikundi kueleza tukio moja tu waliopitia

katika maisha ya Yakobo iliyombadilisha, na ni jinsi gani Yakobo alibadilika. Zunguka kila kikundi

hadi pointi zote ambazo zimeletwa na kila kikundi zisikizwe na darasa nzima.

Tumia mbinu iyo hiyo ili kupata juhudi amabazo Yakobo alichukua ili kufikia maridhano. Na nini

kilibadilika katika maisha ya Esau, na ni nini haswa Esau angefanya;

Halafu sasa uliza: Ni juhudi gani au ni nini mnaona katika hadithi hii kama vifaa vya maridhiano,

ambavyo tunaweza tumia kwa mizozo zinazotukumba maishani?

Page 23: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[23]    

Alika darasa kukumbuka na kufikiri kuhusu mzozo waliotafakari juma lililopita. Je kuna njia au

juhudi kuelekea maridhiano zinazijitokeza katika uchambuzi huu, ambayo tunaweza kuweka katika

mukthada wa mzozo huo? Ruhusu muda wa kutafakari kwa kimya na maombi.

VIPEO MUHIMU:

Ni kiasi gani au kiwango gani juhudi ya Yakobo ya kutafuta uwiano ilikuwa ya kiroho na kuhusisha

Mungu? Tazama kwanzia wakati aliona maono ya malaika ngazini wakielekea mbinguni, na kupitia

kupigana usiku kucha. Sehemu kubwa ya kutafuta uwiano na Maridhiano, inatokana na mtu binafsi,

kujirudia na kujifahamu kuwa sisi ni nani ( Tazama kuwa Yakobo alilazimishwa kusema jina lake-

alikumbana na kukaribia maisha yake ya kale ya ulaghai), ndipo akapokea neema na akajitolea

kutenda kulingana na maagizo ya Mungu. Matokeo ya kujirudia na kubadilika kindani kwa Yakobo

ilikuwa pia ni kukubali majukumu ya matendo yake, pamoja na kukubali majukumu kwa kurudisha

na kukuza uhusiano ambayo uliharibiwa, kuzoroteshwa na kubomolewa kwa matendo yake.

Mtazamo wa funzo: Maridhiano huanzia ndani ya mtu binafsi na hujitokeza nje kwa kujali wengine.

* Maridhiano hujumisha hatari.Yakobo hakuwa na uhakika kuwa Esau atamkubali. Pengine Yakobo

angeuawa, lakini alijitolea mhanga licha ya kufahamu kuwa Esau angeweza kumfanyia chochote,

akanyenyekea, akasema ukweli na akatubu. Hatutachukua majukumu kwa matendo ya wengine.

Lakini tutakubali mjukumu kwa maamuzi yetu, pamoja na kuanzisha juhudi za maridhiano,

tutachukua jukumu kwa lolote ambalo laweza tokea katika juhudi hizo.

Mtazamo wa somo: maridhiano kwa mzozo mkali si rahisi kupatikana bila mtu au kwa wakati

mwingine kila mtu wakichukua hatari kurejesha uhusiano.

* Yakobo alihisi kiwango fulani cha maridhiano na baba mkwe wake Labani kabla kukutana na

Esau. Yeye mwenyewe alihisi na kuona jinsi ilikuwa uchungu mno kudanganywa au kulaghaiwa

(Jinsi Esau alihisi alipotendewa hivyo naye Yakobo).Alikumbana na hasira ya Labani kwa

kudanganywa. Yakobo na Labani walizungumzia mzozo wao na hisia zao. Hatimaye walifikia

mapatano na wakakubaliana, hivyo basi wangeweza kuishi kwa amani na kuimarisha uhusiano wao

wa kifamilia. Hayo yote yalimwandaa Yakobo kwa safari ya maridhiano makuu na nduguye

waliyotengana naye kabisa kitambo..

Mtazamo wa somo: Ukifaulu kubadilisha mzozo, utapata mazoezi ambayo itajenga uwezo wako na

utaweza kubadilisha mizozo mengine maishani.

AWAMU YA 4

YAKOBO NA ESAU, SEHEMU YA PILI: SAFRI YA KUPATA MARIDHIANO

HAPO NYUMA:

Page 24: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[24]    

Yakobo aliondoka na kuacha familia yake kwa juhudi la kukwepa vitisho vya Esau na akaamua pia

aende ajitafutie mke miongoni mwa watu was huko Harani.

Usiku moja Yakobo alilala akiwa safarini na akaanza kuota. Aliota kuwa aliona ngazi ndefu

lililokuwa likiunganisha dunia na mbingu huku malaika wakienda juu na chini ya ile ngazi. Mungu

akajitokeza kando yake na kumkumbusha lile agano walilokuwa wamefanya na Abrahamu pamoja

na Isaka, kwamba wazao wa Yakobo watakuwa taifa kuu na kwamba wataridhi ardhi aliyokuwa

amelala, na kuwa wanao watakuwa baraka kwa mataifa yote.

Mungu akaahidi kuwa na Yakobo popote aendapo na kumrejesha tena kwenye ile ardhi. Yakobo

alipoamka, alijawa na hofu. Alijihisi amekuwa kwa nyumba ya Mungu na kwenye mlango wa

mbunguni.nAliamua kujenga madhabau mahali pale na kuliita Betheli (“Nyumba ya Bwana”).

Yakobo alipofika Harani, walipendana na Raheli, mwanawe mjombake Laban.

Akafanya agano na Laban kuwa atakuwa mjakazi wake kwa muda wa miaka 7, lakini Laban

akafanya njama na kumwoza Yakobo bintiye mkubwa Leah wakati wa harusi. Yakobo akangoja

miaka mengine 7 ili kumwoa Raheli. Yakobo akajitayarisha kurejea Kaanani na kwa miaka mengine

6 akafanya kazi na kusanya mifugo kama malipo yake kutoka Laban. Akatumia mtindo mpya wa

kuwazalisha mifugo ili kuongeza idadi ya mbuzi pamoja na kondoo wake.

Laban alikasirika sana alipogundua lile njama, hivyo basi Yakobo akakwepa kwa siri pamoja na

mkewe, wanawe na mifugo wake. Laban akamwandama lakini katika ndoto Mungu akamuonya

Laban jinsi anavyopaswa kuhusu jinsi anafaa kuhusiana na Yakobo. Laban alipomfikia, yeye na

Yakobo wakaongea jinsi walivyokuwa wamekwasana na kutoaminiana naye. Yakobo akasema hisia

zake ya hofu na usaliti aliyopata kwa miaka yote aliyokuwa amemtumikia Laban.

Laban akasemezana na Yakobo kwamba wake wa Yakobo ni binti zake na watoto wake ni wajukuu

wake. Wote wawili wakafanya agano wasiumizane na Yakobo atawachunga vizuri wanawake na

watoto wake. Laban akawabusu binti zake na wajukuu wake, na akaondoka. Yakobo akaelekea

Kaanani.

Akatuma wajumbe kwa Esau kumjulisha kurudi kwake akisema kuwa alitarajia kupokelewa na

kubalika kutoka kwa nduguye. Wajumbe wakarejea na onyo kuwa Esau anakuja na wanaume 400

kumkabili. Hii ikamtia Yakobo wasiwasi. Kwanza akachukua hatua ya kuwagawanya familia na

mifugo wake akitarajia kwamba kikundi moja kingenusurika.

Kisha akaomba apate kunusurika. Akajihisi kuwa hakuhitaji tena upendo na uaminifu wa mungu.

Akahofia tisho la Esau na akatumainia agano la mungu kwake. Yakobo akabadilisha mtindo.

Akatuma mbele kikundi kikubwa cha mifugo kama zawadi kutoka kwa zizi lake na wajakazi wakiwa

na ujumbe maalum kwa Esau. Yakobo alitarajia kupoesha hasira ya nduguye, ili apate kukubali

Page 25: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[25]    

kuona uso wake na kumkubali yeye. Yakobo basi akawatuma familia yake ikiwemo watoto wake

kuvuga mto kuelekea Kaanani.

Yakobo alikuwa pekee yake. Kisha mtu akaja na akaanza kupigna na Yakobo hadi kulipokucha.

Wakati Yule mtu alipozidiwa, akamgonga Yakobo kwenye kiuno, na akamvunja. Yakobo hata hivyo

hakumwachilia hadi mtu yule akaamua kumbariki. Mtu yule akamwulizia jina lake. Yakobo akasema

jina lake, inamaana “anayeshika kisigino” Kisha yule mtu akamwambia jina lake si “Yakobo,” tena,

lakini litakuwa “Israeli” linalomaanisha kuwa “Yule alipigana na mungu”. Yakobo akauliza jina la

yule mtu lakini hakupata jibu.

Mtu yule alipota kwa ghafla, na Yakobo akasema,” hakika nimeonaMungu uso kwa uso na maisha

yangu bado imelindwa”. Akaendelea na safari yake huku akichechema kwa kuwa nyonga yake

ilijeruhiwa.

Yakobo alimwona Esau akija na wanaume 400. Yakobo akajitokeza mbele ya familia yake na kupiga

magoti na kuinama. Esau alikimbia mbio na kumkumbatia.Wakabusiana na kulia. Esau alitazama

familia kubwa ya Yakobo na akatambulishwa .Esau akaulizia kuhusu zawadi zote alizotumiwa, na

Yakobo akamjibu kuwa anatumai atakubali. Lakini Esau akamjibu Yakobo kuwa yeye ana mali ya

kutosha na hayahitaji mengine kutoka kwake. Yakobo akamwambia Esau achukue zawadi zake, kwa

kuwa katika nafsi yake, alipoona nduguye ni kana kwamba aliona uso wa Mungu. Mungu alikuwa

amemnehemisha sana, na aliona nehema hiyo kwa Esau. Hatimaye Esau akapokea zawadi hiyo.

Wakaendelea na safari yao pamoja Yakobo akionyesha unyenyekevo na shukrani ilhali Esau

akionyesha ukarimu. Yakobo akaishi Kanani. Na Isaka alipofariki, ndugu hawa wawili walimzika

baba yao pamoja.

(Sehemu hii ya hadithi limetolewa Mwanzo 28.10-33.20; 35.27-29)

Page 26: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[26]    

SEHEMU YA 2

UTATUZI WA MZOZO

Awamu ya 5: mzozo kutokana na kutoelewana (Yoshua 22.10-34)

Awamu ya 6: Mpatanishi jasiri (1 Samweli 25.1-35)

Awamu ya 7: mzozo kutokana na imani za kidini (Matendo ya Mitume 15.1-35)

Awamu ya 8: kutafuta suluhisho linalokubaliwa na pande zote (Hesabu 31.1-33)

Awamu ya 9: Isipowezekana (Matendo ya Mitume 15.36-41)

AWAMU YA 5

MZOZO KUTOKANA NA KUTOELEWANA

KIFUNGU: Yoshua 22.10-34

HAPO NYUMA:

Wakati wana wa Israeli walipopigana vita ili kumiliki Kanani, kabila zote 12 walihusika. Lakini

kabila za Rubeni na Gadi na nusu ya kabila za Manase walikuwa wameamua kuishi eneo la

mashariki mwa Yordani eneo la Yasa na Kiledi. Hesabu32 (angalia somo lililoko sehemu ya 8)

inaelezea jinsi makabila ya Rubeni, Gadi na Manase chini ya Musa walikuwa wamekubaliana

kuhusika katika vita vya kugomboa Kanani kabla ya kuishi eneo la mashariki. Katika Yoshua 22.1-9

Yoshua atangaza kuwa vita vimeisha na ukombozi wa Kanani umekamilika, na anawaruhusu hao

makabila mawili kwenda kujenga nyumba zao na kuishi mashariki mwa Yordani.

Hali ya maisha na uzoefu wa Israeli umetajwa katika somo hili. Kuelewa yale matukio ya kwanza

kidogo ni muhimu ili kusaidia kuelewa malalamishi ya makabila waliyokuwa wakiishi magharibi

mwa Yordani. Mstari wa 17.inanena kuhusu “dhambi za Peori”. Hii inaashiria ile habari imeandikwa

katika Hesabu 25.1-9, ambapo Wana wa Israeli walishiriki katika kuabudu miungu mingine kama

vile baali. Watu wapatao 24,000 walifariki kwa ugonjwa iliyotokana na hukumu ya Mungu kwa

kuwa watu waliabudu miungu mingine.

Mstari wa 20 inanena kuhusu “Achani mwana wa Zeraia”. Hadithi ya Achani inapatikana Yoshua 7.

Achani aliviiba baadhi ya vitu vilivyopatikana baada ya ukuta wa Yeriko kubomolewa akalichukua

vingine ambavyo vingemtolea Mungu kama dhabihu. Kwa sababu hiyo, wana wa Israeli walishindwa

katika vita iliofuata katika Ai. Mungu akawaeleza kuwa jamii yote imeadhibiwa kwa sababu ya kosa

ya mtu mmoja ambaye hakumtolea Mungu dhabihu kutakana na yale vitu walipata baada kuvamia

Yeriko. Achani alipatikana na hatia, na kilichopatikana kilizikwa katika hema yake. Hatimaye

Achani aliuawa kwa makosa yake ili atakaze jamii yote kutokana na matendo yake.

Page 27: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[27]    

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Njia moja moja ya kusoma kifungu ni kugawanyika katika vikundi vidogo, kusoma na kujadiliana

katika vikundi, huku wakitumia maswali hayo kuongoza somo lao.Wape muda wa dakika 40 hivi ili

kila kikundi kijadiliane. Hatimaye ualika kikundi kimoja kiripoti au kieleze darasa kile walichosoma.

Waambie vikundi vingine waeleza wamepata nini kutokana na somo bila kusema hadithi yote.

Vikundi vyote zvitakapomaliza, kiongozi anaweza kueleza pointi ambazo huenda zilisahauliwa na

kukamilisha kwa ufupi.

Maswali yatakayotumiwa na vikundi katika somo lao:

Huu mzozo ulikuwa juu ya nini? Ni nini haswa ilileta mzozo kwa haraka? Ni nini kero au lalama za

pande zote?

Ni mambo gani yanazidisha mzozo? Ni nini Wana wa Israeli waliyo chini ya Finae wanafanya

ambacho ni cha kusaidia? Ni nini anachofanya au anachosema Finea ambacho si cha faida sana

katika kusuluhisha mzozo?

Ni nini wanachofanya akina kabila la Rubenii, Gadi na nusu ya kabila la Manase (au wakaaji wa

Mashariki) ambacho ni cha faida? Na ni nini wanachofanya wao tena ambacho si wa msaada katika

kusuluhisha mzozo?

Ni hali gani ya kipekee au ni mambo gani ya kipekee yaliyosaidia kuleta suluhisho?

Suluhisho ilikuwa nini?

Suluhisho liliweza kufikiwa kivipi?

Suluhisho hilo lilipokelewaje na wao waliokuwa wamezozana?

Ni nini vikundi hao waliokuwa wamezozana walifanya ili maagano yao yawe rasmi?

Njia nyingine ya kupanga somo hili ni kuchagua vikundi vitatu visome huku kila kikundi kina

sehemu ya kushughulikia. Kikundi cha kwanza watajishughulisha na makabila ya mashariki (Rubeni,

Gadi na kabila nusu ya Manase) Kikundi cha pili watajishughulisha na makabila ya magharibi (chini

ya uongozi wa Finea) Kila kikundi kitasoma habari yenyewe huku wakizingatia na kutilia mkazo ile

sehemu ya makabila wamepewa. Wanafaa kugundua, je ni nini malalamishi au kero ya makabila

hayo, na pia maoni ya makabila hayo. Ni jinsi gani makabila hayo walionyesha na kuelezea mahitaji

yao. Kila kikundi kitachagua mmoja wao atakayewawakilisha katika mchezo wa kuigiza.

Kikundi cha tatu kitakuwa wapatanishi. Watachunguza kwa makini mambo fulani katika kila

kikundi, wakijaribu kufahamu eneo la mapatano. Watamchagua mmoja wao kuwa mpatanishi baina

ya vikundi katika mchezo wa kuigiza.

Wape vikundi muda wa dakika 30 wasome somo lenyewe na kujiandaa kwa nafasi zao

watakazohusika katika mchezo wa kuigiza.

Page 28: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[28]    

Halafu uwaalike wale wamechaguliwa kama wasemaji waje mbele wafanye mchezo wenyewe.

Mpatanishi ndiye ataongoza mazungumzo baina ya vikundi viwili, huku akialika kila kikundi

kujieleza.

Kikundi cha tatu kinaweza kuwa mpatanishi. Watasoma mienendo kati ya vikundi wakijaribu

kutambua sehemu ya masikilizano. Katika mchezo wa kuigiza, chagua mmoja awe mpatanishi kati

ya vikundi walio kkatika mchezo wa kuigiza.

Uwape vikundi dakika 30 kusoma kifungu ili wajitayarishe kwa majukumu yao. Halafu uwaalike

wasemaji katikati mwa au mbele ya darasa kufanya majukumu yao. Mpatanishi atasimamia

maongezi kati ya vikundi akialika kila upande kuelezea habari yao.

Mpatinishi anafaa kusaidia kila kikundi kutambua mashaka yao, vivutio na mahitaji na pia

akiwasaidia kutafuta sehemu moja ya masikilizano. Halafu mpatanishi atajaribu kuwafanya

wakubaliane kwa agano ambalo linaguza mahitaji yao. Hii haitakuwa na mshindi, bali suluhu sawa

kwa wote.

Kufuatana na mchezo huo wa kuigiza, uliza darasa lote kulinganisha suluhu iliyotokea kwa mchezo

wa kuigiza na suluhu iliyotekea kwenye Biblia. Ni kipi ambacho kinapendwa sana na kila upande

kilichopatwa na suluhu zilizopatwa.

Funga awamu kwa kuwaalika darasa kuunda upya vikundi vyenye watu wawili au watatu. Uwaalike

kufanya mazoezi kwa kufikiria mzozo wanaopitia kwa sasa na mtu amabapo hawajataja hofu au

shaka iliyo kati yao. Uwaambie washiriki kusema vizuri hofu au shaka wanao. Halafu wasikilizaji

wanaweza kualika anayeongea ikiwa wanataka kufikiria kiundani kama kuna lolote chini au nyuma

ya hofu hilo ambalo litatufahamisha hatari iliyomo kwenya mzozo.

VIPEO MUHIMU:

*Ni rahisi sana kulaumu wengine kwa kile tunachohofia , lakini pengine hofu yetu isiwe na msingi .

Waliokuwa wakiishi Mashariki walihofia kuwa huenda waliokuwa wakiishi magharibi hatimaye

watawatenga wao na familia ya Israeli kwa sababu ya mto Yordani. Waliokuwa wakiishi Magharibi

vile vile walilaumu wale waliishi Mashariki kwa hofu yao ya hukumu ya Mungu kutokana na tabia

yao wenyewe ya kutotii agano. Hakuna kikundi kilichojaribu kuchunguza lawama zao dhidi ya

wengine kwa kuzungumza na kikundi kingine kabla ya kulalamika kwa hofu yao.

Wana Mashariki walijenga madhabau bila kuhusisha au kuzungumza na wana Magharibi juu ya hofu

yao au kutoa sababu ya vitendo vyao.

Wana Magharibi walipanga vita bila kuzungumza kwanza na wana Mashariki kuhusu ni nini kitendo

chao cha kujenga madhabau kilimaanisha.

Kwa hekima kubwa, Finea alizungumza kabla vita kuanza.

Page 29: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[29]    

Mtazamo wa somo: Zungumza kwanza ili uone ikiwa malalamishi na hofu yako ina msingi!

* Mambo ya mawwasiliano yanajitokeza katika hadithi:

-Ni muhimu kugundua na kuzungumzia hofu na mambo yanayosumbua mtu binafsi jinsi

ilivyofanywa na Finea alipozungumzia malalamishi yake kuhusu hukumu ya Mungu kwa jamii

nzima iliyoonekana kama si ya haki kwao.

Lakini Finea alianza na lugha ya shutuma (angalia mstari wa 16). Lugha ya “Wewe” ambayo ni ya

kushtumu huenda ikasisimua jibu ya upingamizi. Lugha ya “Mimi” ni lugha ambayo watu hutumia

wanapoeleza hofu yao, mashaka yao au kuumiza kwao hufungua mazungumzo zaidi kwa vikundi

vyote. Lugha ya “Mimi” ni lugha ambayo inaalika maelezo zaidi, uaminifu na nafasi ya kutafuta

suluhisho badala ya kuongeza upingamizi inayotenganisha vikundi vyote zaidi.

- Maoni ya kipekee kinachozingatia kile kikundi kingine (kama kile kilichotolewa na Finea katika

mstari wa 19) kitaweza kufungua mazungumzo na kuelekeza suluhisho la kufaa na linalokubalika na

pande zote mbili.

-Weka nia yenu wazi ( kama vile makabila ya Mashariki walifanya katika mstari wa 24-27) ili kile

kikundi kingine kiweze kuelewa mawazo na hisia zenu zilizowafanya kutenda hivyo.

* Hakikisha kuwa unafuatilia maagano yawe rasmi na ya kueleweka ( kama vile kuwapa ripoti ya

wana wa Israeli wote kilichojiri na kupea jina madhabau”Mshahidi” angalia mstari wa 32-34)

* Mara nyingi katika vikundi vinavyozozana, kila upande hufikiri kuwa wao ndio wanastahili

kushinda na wengine kushindwa. Mtindo huu wa kushughulikia mzozo hufanya kikundi kimoja

kishinde na kingine kisifaulu.

Kupitia mazungumzo na maoni ya kila kikundi, jawabu lisiloegemea popote au suluhisho la kudumu

inaweza kupatikana. Vikundi vyote vinaweza vikapata kushinda lakini sio kwa gharama ya upande

mwingine kushindwa. Katika hadithi hii Wanamashariki walikuwa na kumbukumbu ili kuonyesha

mapatano yao na watu wa Waebrania kutoka magharibi mwa Yordani. Jamii ya magharibi walipewa

hakikisho ya uaminifu kwa dini ikiwemo wale waliohamia mashariki mwa Yordani.

Mtazamo wa somo: Tutafuta “suluhisho usioegemea upande wowote”. Hii itafanya kila mmoja

ajisikie vizuri kuhusu utatuzi wa mgogoro huo kuliko kupatikana na suluhisho la kuupa upande

mmoja ushindi.

 

Page 30: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[30]    

SEHEMU YA 6

MPATANISHI JASIRI

KIFUNGU: 1 Samueli 25.1-35

HAPO NYUMA:

Daudi alikuwa akiishi maisHa ya utumwa kule jangwani kwa sababu mfalme Saulo alikuwa na nia ya

kumwangamiza. Daudi akakusanya kikundi la wanajeshi na wanasheria pamoja. Wakakuwa pale

wakitegemea walichotafuta, walichoomba na walichopata kupitia mabavu.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Gawa darasa kwa vikundi vidogo vidogo ili kusoma na kufafanua ufahamu kupitia maswali

yafuatayo. Waruhusu vikundi kufanya huku kusemezana pamoja kwa dakika 30. Kisha uteue kikundi

kimoja kije kitoe ripoti ya walichojadiliana. Kisha uulize vikundi vingine wasirudie yaliyosemwa

bali watoe mtazamo wao kulingana na ufahamu. Vikundi vyote vitakapomaliza kusema maoni yao,

kiongozi aseme hoja zozote ambazo huenda yalisahaulika na kisha baadaye kutoa maono ya mwisho.

Maswali ya vikundi yatakayotumiwa kwa somo:

Taja wahusika wakuu katita masimulizi haya. Je, ni sifa gani iliyojitokeza kutoka kwa kila mhusika/

kutoka kwa kundi la kila mhusika?

Ni yepi yaliyojitokeza kwenye sehemu ya mgogoro? Ni hatua gani iliyochukuliwa na kila mhusika ili

kutafuta suluhisho?

Ni nani alichukua hatua ya kuelekeza mgogoro kuelekea kwa kutafuta amani? Je, hatua yao

ilibadilishaje sifa ya wengine?

Nani alitoa nini katika mazungumzo haya? Nani alifaidika na nini katika utatuzi huo?

Kama njia nyingine ya mbadala, kikundi kimoja kinaweza kupewa hadithi hii awali na kuulizwa

waigize matukio ya wahusika mbalimbali kwenye masimulizi. Baada ya kuigiza, mwalimu anaweza

akauliza vikundi maswali.

Waulize vikundi waseme sehemu ambayo mogogoro hutokea kila mara kama vile: kati ya mme na

mke, kati ya wanafunzi, kati ya wanajamii, watoto wanaocheza, wafanyi kazi, na wafanya kazi na

waajiri wao, afisa wa serikali na wananchi n.k. katika kila kikundi ni nani anaweza akateuliwa kama

mpatanishi ili kusaidia kutatua kwa njia rasmi? Je, kuna watu wanaoweza wakateuliwa kusaidia

kutatua? Ni sifa gani wapatinishi wanapaswa kuwa nao.?

Umwalike mmoja wa wanafunzi kuelezea walichopitia katika kutatua mzozo. Baada ya habari

kuelezwa, uliza kikundi kitambue hatua amabayo ilitumiwa kupata suluhu katika pande zote

zinazozozana. Pia, utambua sifa za mpatanishi zilizosaidia kuleta suluhu.

VIPEO MUHIMU:

Page 31: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[31]    

* Mtumishi Yule mdogo kwa umri katika mistari 14-17 alichangia sana katika kutatua mzozo huu.

Hakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko katika mzozo huo kati ya Nabali na Daudi. Lakini alijua

kuwa Abigaili ni mwanamke mwenye hekima na inabidi awafikie hao wanaozozana. Ingawa alifanya

jambo dogo, alifanya chenye angeweza kufanya.

Mtazamo wa somo: Fanya chenye unaweza ambacho kinaweza kubadili mkondo wa mzozo.

* Abigaili, kwa hekima zake, alijiweka kwa mtazamo na mapendeleo yake Daudi ili kuonyesha kuwa

mna umuhimu wa kupata suluhu katika mzozo huo (angalia mistari ya 30, 31). Alimuashria kuwa

itakuwa vyema kama mfalme wakati wa usoni kama hatakuwa muuaji katika kipindi chake cha

uongozi.

Mtazamo wa somo: kupata suluhu husaidia kupata mahitaji mapendeleo na maadili ya upande ule

mwingine ili kuunda suluhu litakalotendeka na inajumuisha vivutio vya upande ule mwingine.

 

Page 32: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[32]    

AWAMU YA 7

MZOZO JUU YA MAADILI YA DINI

KIFUNGU: Matendo 15.1-35

HAPO NYUMA:

Wakristo wa kwanza waliku wayahudi au Watu wa Mataifa waliyogeuzwa kuwa mayahudi na

baadaye wakawa wafuazi wa Yesu. Habari Njema ilipokuwa ikienea, Watu wengi wa Mataifa

waligeuzwa kuwa wafuasi wa Kristo, hasa safari ya kiunjilisti ya Paulo na Barnaba ilipoanza katika

mkusanyiko wa Wakristo kule Antiokia.

Swali likaja: je, mtu wa mataifa anapaswa kuwa mfuasi wa kidini ya wayahudi ili awe Mkristo? Je,

dini ya Kikristo ni sehemu ya dini Wayahudi au ni imani mpya inayojaza pengo kati ya Wayahudi na

Watu wa Mataifa? Je, ni sifa zipi za kidini na maadili zinazoelezea imani hii mpya? Kutahiriwa kwa

wanaume ilikuwa ni agano ambalo lilikuwa ni njia ya kujiunga na jamii ya Wayahudi, kwa hivyo huu

ulileta pengo la kujadili kama hili litahitajika kwa mteule mpya wa Mtu wa Mataifa au la. Haya

ndiyo maswali viongozi wa kanisa la kwanza walifikiri walipokuwa wakikutana katika mkutano

uliotajwa katika Matendo 15.

Wafarisayo wanatajwa katika mstari wa 15, lakini wanatambuliwa kama “waamini”. Hawa walikuwa

wafuasi wa tamaduni ya Wafarisayo ambao waligeuzwa na kuwa wafuasi wa Yesu (angalia

Nikodemo katika Yoana 3 kama mfano). Walikuwa na mtazamo wa juu sana wa sheria ya Musa na

wakisisitiza maoni yao kuwa kila manaume aliyegeuzwa atahiriwe. Katika mstari wa 7-11 Petero

anatusimulia habari iliyoelezwa kwa ufasaha katika Matendo 10.1-11.8 Kornelio, aliyekuwa mtu wa

mataifa na nyumba yake yote, aligeuka kuwa Wakristo. Walipokea Roho Mtakatifu kama vile

Mitume na Wafuasi wengine walivyopokea siku ya Pentekosti. Habari ya Kornelio ilikuwa ni

mwanzo wa matukio kwa kanisa la Kwanza na inaelezwa mara nyingi katika kitabu cha Matendo.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Darasa ligawanywe kwa vikundi vidogo kusoma na kujadili habari wakiwa na maswali yafuatayo

yatakayowaongoza katika somo lao. Uwape vikundi dakika 40 kufanya kazi hiyo pamoja. Halafu

alika kikundi kimoja kueleza walichojifunza. Himiza vikundi vingine kutoeleza tena habari hiyo yote

badala yake waeleze mtazamo waliopata. Baada ya vikundi vyote kumaliza, kiongozi anaweza kuleta

vipeo vingine huenda vilisahauliwa na kutoa ufupisho wa kumalizia.

Maswali ambayo yatatumiwa na vikundi katika somo lao:

Je, mzozo inahusu nini? Je, ni jambo lipi lilitokea kwa haraka? Je, nini mashaka ya pande zote mbili?

Gundua waliyomo kwenye mzozo. (Mwalimu anauwezo wa kutoa habari inayohusu kutahiriwa

katika kanisa la kwanza au la ikitegemea ufahamu wa darasa wa Biblia.)

Page 33: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[33]    

Je, mzozo umefika kiwango kipi ili kitajwe? Je, ni nini ulisababisha kufika kiwango hicho? Je, nini

kilitiwa maanani katika kutatua mzozo huu? Je, ni mienendo ipi ilijaribu kuleta suluhu? Je, ni suluhu

upi ulipatikana? Je, vipi wahusika wa mzozo walichukulia suluhisho hilo?

VIPEO MUHIMU:

* Wakati wa mabadiliko Katika mjadala ni pale Petero alisimulia habari ya Kornelio halafu Paulo na

Barnaba wakasimulia safari yao ya umisionari. Kabla ya hapo kulikuwa na “mjadala mkubwa”

(angalia mstari wa 7). Katika mzozo unayohusu maadili, ni vigumu kwa upande wowote

kuwashawishi wale wengine wakitumia uwezo wao wa kupinga au kutaja mistari ya maandiko.

Badala yake, kupingana inaweza endelea bila mwisho na kwa mara nyingine huleta mgawanyiko

zaidi. Habari za mtu binafsi zaweza badilisha mazingira ya mjadala. Habari inaondoa mjadala wote

kutoka kwenye fikra hadi ukweli wa mambo katika maisha yetu. Kuna njia nyingi ukweli unasikika

na unaonekana katika habari, kitu ambacho ni rahisi kutambuliwa na kuheshimiwa hata kama habari

hiyo inatoka sehemu tofauti katika maisha na penye msikilizaji yupo. Habari inaunda sehemu sawa

katika ubinadamu, na kwa habari hii kupata Mungu akitenda kwa njia zisizotarajiwa.

Mtazamo wa somo: tumia habari za watu kuwafanya wahusika katika mzozo kuelewana, kukuza

heshima baina yao hata ingawa wanatofautiana pakubwa, na kufungua njia mpya ya kufikiri ambayo

itakubali ukweli unaojitokeza katika habari.

* Baada ya agano kupatikana, kikao kikatangaza agano kwa kuandika waraka uliyopelekwa na

wakilishi wawili hadi makanisa ya Watu wa Mataifa (mistari ya 22-23). Suluhisho la mzozo

ukipatikana, ni vyema kutafuta njia ya kutangaza agano hilo. Agano lilioandikwa inaweza kuwa wa

msaada ili kila mhusika anajua ni nini walikubaliana.

Mtazamo wa somo: Tangaza agano au fanya liwe rasmi.

* Ingawa kutahiriwa hakuhitajiki kwa mteule mpya wa Watu wa Mataifa, kikao kilitaka wateule

kukomesha usherati na “kukoma kutoka damu” (Je, hii inamaanisha kukoma kuua au kula

kisichouliwa kwa njia unofaa? Wasomi wengi wanaamini kuwamatamshi hayo yalimaanisha

kustawisha sheria za zinazokubalika juu ya chakula), na wasishiriki katika kuabudu miungu mingine

kwa kula nyama iliyopewa miungu. Kama hayo ndiyo maadili mema tuliyopewa na kanisa la kwanza

kuonyesha imani yao, hata katika Agano la Pili tunapata mjadala unaoanza kuuliza maadili hayo

yalimaanisha nini. Katika Warumi 14 na 1 Korinto 8, jambo hili linaguzwa na Mtume Paulo kwa njia

inyoonyesha ugumu wa kuishi kwa kuamini mambo fulani ya tamaduni.

Katika utamaduni ambao hawakuwa na kiumbe cha kuabudu, jambo hilo kubwa haina maana. Imani

kwa Kristo itaonekana katika madili mengine. Jambo la kutilia maanani hapa ni kuwa katika mizozo

nyingi agano linaweza kukaa kwa muda fulani, lakini uzoefu na kufikiri zaidi linaweza hitaji kuunda

Page 34: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[34]    

tena maelewano yalioleta agano au agano lenyewe. Mabadiliko kwa muktadha wa utamaduni au

maendeleo tofauti za kihistoria zaweza fanya mambo ya hapo kitambo kusiwe na umuhimu lakini

kutoa mambo mengine yanayohitaji kujadiliwa.

Mtazamo wa somo: suluhu katika mizozo nyingi ni hatua njiani na zawezahitaji kuundwa tena katika

matukio mapya.

 

Page 35: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[35]    

AWAMU YA 8

KUTAFUTA SULUHISHO USIOEGEMEA UPANDE WOWOTE

KIFUNGU: Hesabu 32.1-33

HAPO NYUMA:

Wana wa Israeli walikuwa wamemaliza safari yao nyikani ya miaka 40 baada ya kutoka Misri.

Walikuwa wakikaribia nchi ya Kanani kutoka mashariki wakiendelea hadi Yordani. Katika Hesabu

21 habari inaelezwa kuhusu kushindwa kwa wafalme wa Waamori, Sihoni na Ogu ambao walitawala

Mashariki ya Yordani. Sehemu hiyo ilikuwa chini ya Wana wa Israeli ambao walikuwa

wamesimama tayari kuvamia nchi ya Kanani.

MKODO WA SOMO NA MASWALI:

Gawa darasa kwa vikundi vidogo kusoma na kujadili habari na kusoma maswali yafuatayo. Uwape

dakika 30 kufanya kazi hiyo pamoja. Halafu alika kikundi kimoja kueleza walichojifunza. Halafu

alika kikundi kimoja kueleza walichojifunza. Himiza vikundi vingine kutoeleza tena habari hiyo yote

badala yake waeleze mtazamo waliopata. Baada ya vikundi vyote kumaliza, kiongozi anaweza kuleta

vipeo vingine huenda vilisahauliwa na kutoa ufupisho wa kumalizia.

Maswali vikundi vitatumia katika somo:

Je, ni wahusika wepi wamo kwenye mzozo?

Je, ni vivutio vipi na mahtaji yapi ya kila kikundi?

Je, nini hofu gani inaweza kuadhiri mapendeleo na mtazamo ya mhusika wowote?

Je, suluhisho ipi ilipatikana? Je, suluhisho hili linatimiza mahitaji na mapendeleo ya vikundi vyote

viwili vipi? Je, unafikiri ni nini kilichochangia kupatikanan kwa suluhu hili?

VIPEO MUHIMU:

* Mizozo mingi yaweza kuwa na ushindani mkali: kwa upande mmoja kushinda lingine lazima

kishindwe. Hapo awali, Wana wa Reubeni na Wana wa Gadi walisimama sehemu moja ilhali Musa

akiwa sehemu ile nyingine wakikabiliana. Tukianagalia mahitaji na mapendeleo ya vikundi hivyo

viwili (Wana wa Reubeni na Wana wa Gadi walitaka shamba nzuri ya kulisha wanyama wao na

makabila wengine wakitaka kujihami kuvamia) suluhisho lilipatikana ambapo wote walipata

walichotaka. Huu ndiyo inaitwa “ushindi usioegemea upande wowote”. Suluhisho halikuwa hapo

awali msimamo uliotajwa hapo mwanzo, bali ilijitokeza punde mahitaji na mapendeleo

yalipotambuliwa.

*Musa alisema maoni makali kuhusu Wana wa Reubeni na Wana wa Gadi hapo mwanzoni (mstari

wa 14). Wana wa Reubeni na Wana wa Gadi walijibu kwa kutoa pendeleo lililotia maanani mahitaji

yake Musa.

Page 36: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[36]    

Mtazamo wa somo: kutambua na kukubali mapendeleo ya haki ya wahusika wote itasaidia kuleta

suluhu inayokubalika.

 

Page 37: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[37]    

AWAMU YA 9

ISIPOTENDEKA

VIFUNGU: Matendo 15.36-41

HAPO NYUMA:

Paulo, aliyeitwa Saulo hapo awali, na Barnaba walikuwa pamoja katika kazi ya Mungu mle Antiokia.

(Matendo 11.25-26). Kutoka Antiokia walitumwa pamoja kwa safari ya umisionari (Matendo 13.1-

3). Mwanamume mdogo kwa umri aliyeitwa Yohana Marko aliwafuata (Matendo 13.5), lakini

aliwaacha na kurudi nyumbani mapema katika safari (Matendo 13.13). Sababu ya Yohana Marko

kurudi hayakutajwa.

Paulo na Barnaba walitoka kwenye Kikao cha Yerusalemu ambapo kazi yao kwa Watu wa Matafa

ilikubaliwa na kanisa lote.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Gawa darasa kuwa vikundi vitatu. Kikundi kimoja kitasoma habari na kuelewa msimamo wa

Barnaba. Kikundi cha pili kitasoma habari na kufahamu msimamo wa Paulo. Kikindi cha tatu

kitatafakari kuhusu msimamo wa mtu mwingine au kikundi kingine kingechukua. Kwa wanaosoma

juu ya Paulo na Barnaba, maswali haya ni muhimu: je, nini kilikuwa kiini cha hali hiyo? Ni maadili

ipi unayofikiria yalichangia kufanya hisia hizi kuwa za ndani kabisa katika mzozo huu?

Kwa kikundi cha katikati: je, nini maadili na hofu iliyokuwa kati ya Paulo na Barnaba? Ni suluhu ipi

inaweza kutimiza hofu zao? Suluhisho hilo linaweza kuelezwa vipi ili wote wakubali?

Uwape dakika 15 ya kusoma na kujadili. Kila kikundi kitachagua msemaji aweze kuigiza. (Kikundi

kilichopewa Barnaba chaweza kuchagua mmoja wao kuwa Yahana Marko). Anza mchezo kwa Paulo

na Barnaba wakijadili wakienda kazi ya umisionari kwigine na kusema msimamo wao juu ya Yohana

Marko. Uwaache kujadili jambo hilo kwa dakika chache. Halafu alike mtu mwingine kutoka kwenye

kikundi cha katikati kuingilia mchezo huo aweza kuwasaidia kuwapa suluhu. Mchezo uendelee hadi

ubunifu unaonekana kupungua au wahusika hawajui wanakoelekea.

Fupisha mchezo huo. Uliza kile kikundi kikubwa kipi kilichotendeka? Tambua misimamo ya Paulo

na Barnaba katika Mzozo huo. Tambua maadili muhimu. Ni jukumu lipi mtu wa katikati alitenda?

Kwa mfano, mtu huyo alikuwa na uwezo na mwenye kuelekeza au kuuliza akiwasaidia wale wengine

kutafuta suluhisho lao wenyewe? Ni nani yule alitoka kikundi cha katikati alitenda lililofanya

ilivyokusudiwa? Nini hakikufanyika? Ni mambo gani yalitambuliwa kujulikana kwote? Suluhisho

lilipatikana lilikubaliwa na wote?

Ni mafunzo yepi vikundi vinaweza kupatikana na zoezi hili? Ni vipi mkondo huu laweza kuleta

mabadiliko maishani mwetu? Alika wanachama wa vikundi kueleza habari ya mtu aliyetenda kazi

Page 38: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[38]    

hiyo ya upatanishi katika mzozo waliopitia. Baada ya kusikia habari hii, uliza darasa kutaja

mitazamo na matendo yaliyochukuliwa na mpatinishi ambayo ilisaidia kugeuza mzozo?

VIPEO MUHIMU:

*Suluhisho katika Matendo 15.39 ya Paulo kuchukua Sila na kwenda njia moja na Barnaba kuchukua

Yohana Marko na kwenda njia nyingine ingeweza kuleta agano ya kuongeza kazi ya umisionari na

kutengeneza vikundi sawa kwa kazi ya Mungu. Lakini hamna kinachoashiria katika Maandiko ya

njia moja au nyingine kuhusu kama walitengana kwa njia ya maridhiano au la. Sentensi iliyopo ni

kuwa mzozo huo ulikuwa “kali sana”.

Mtazamo wa somo: utengano unaoheshimiwa waweza kuwa suluhisho kwa mizozo mengine, ingawa

kutengana yaweza kuashiria kukosekanaan kwa maridhiano.

* Hatujui kilichojiri baadaye baina ya Barnaba na Yohana Marko. Huenda yule kijana alibadilika

kutoka mwenye Paulo alitamani awe, yaaminika kwa sababu ya kuhimizwa na kushauriwa na

Barnaba. Baadaye Yohana Marko aliandika Kitabu cha Marko. Zaidi, Paulo anamuagiza Timotheo

kumleta Marko pamoja naye “kwa maana alikuwa mtumishi mwema wa kunisaidia” (2 Timotheo

4.11). kitu muhimu kilitendeka ambacho kilibadilisha maoni ya Paulo juu ya Marko!

Mtazamo wa somo: tunaweza kuona au kupitia mzozo kipindi kimoja kinachozusha moyo, lakini

hiyo haitakuwa mwisho wa habari! Zaidi matukio yanaweza kutokea ambayo yatapeleka hali kutoka

hali mbaya hadi nzuri kwa waliohusika.

Page 39: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[39]    

SEHEMU YA 3

KATIKATI NA UKINGO

Awamu ya 10: Mzozo Katika kila Kikundi (Matendo ya Mitume 6.1-7)

Awamu ya 11: Kutafuta Sauti Yako (Esta 4.1-17)

Awamu ya 12: Mama Aliyekasirishwa na Mwenye Huzuni (2 Samueli 21.1-14)

AWAMU YA 10

MZOZO KATIKA KILA KIKUNDI

KIFUNGU: Matendo 6.1-7

HAPO NYUMA:

Vifungu vya kwanza vya Matendo ya Mitume vinaeleza kuhusu maisha ya kanisa changa baada ya

Yesu Kristo kupaa mbinguni. Roho Mtakatifu iliwajia wanafunzi siku ya Pentekosti, jinsi imeelezwa

katika Matendo ya Mitume kifungu cha 2.

Wafuasi wa Yesu Kristo waliongezeka kwa ghafla. Wengi wao walikuwa Wayahudi waliozungumza

Kiaramu kilichotokana na Kiebrania, wakati mwingine walikuwa wakiitwa “Waebrania” .Wageni

wapya waliojumuika na jamii hii walitoka maeneo ya mbali, walikuja Yerusalemu kwa shughuli za

kidini- hija au pengine walikuja kwa biashara. Walisikia injili wakati wa Pentekosti au muda mfupi

baadaye na wakawa wafuasi wa Yesu. Watu hawa walikuwa wayahudi pia, lakini walikuwa baadhi

ya wayahudi walioishi nje ya Uyahudi, wale walikuwa wametawanyika katika karne nyingi baada

kuanguka kwa Yerusalemu mnamo mwaka wa 586 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.( Waliokuwa

wakiishi nje ya Uyahudi inamaanisha Wayahudi au watu wengine waliotawanyika na kutapakaa

mbali na nchi zao).Walikuwa wameishi miji mbalimbali katika Kaskazini mwa Afrika, Kusini mwa

Ulaya, Mashariki ya kati na Magharibi mwa Asia. Waliongea Kigiriki kama lugha yao ya kawaida,

lugha iliyotumiwa sana na watu wote katika enzi hizo. Kwa hivyo katika Yerusalemu, watu hawa

kutoka nje ya Uyahudi walioamini na kuwa wafuasi wa Yesu waliitwa “Wayunani” kwa kuwa

waliongea Kigiriki.

Baada ya Pentekosti, jamii kipya cha waumini walianza kugawa na kutumia vitu vyao pamoja huku

wakisaidia waliokuwa na mahitaji na waliopungukiwa (Matendo ya Mitume 2.44-45 na 4.32-37).

Wengi wao waliuza mashamba yao na vitu vyao vingine walivyovimiliki. Fedha walizopata walipatia

Mitume ili kugawia waliokuwa na upungufu au mahitaji.

Page 40: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[40]    

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Kabla ya kusoma sehemu ifuatayo, toa maelezo mafupi kuhusu “tawala” na “ukingo“ au kutengwa na

kufinywa katika kikundi. Ikiwezekana, ukiwa na muda unaweza fanya mazoezi yafuatayo ili

kujiandaa kwa kipindi cha uchambuzi wa biblia.

Uwaambie wahusika au wanafunzi wavumbe macho na kukumbuka wakati ambapo walihisi kuwa

walikuwa kando - hawakuwa na ushawishi wowote na kikundi kilichokuwa na mamlaka . Wape

moyo au wasizitizie wakumbuke wakiwa kimya kilichosemwa, ni kitu gani kilichofanywa ama

kilichotendeka. Walihisi vipi? Waliitikiaje?Walihisi vipi kuhusu kuitikia kwao?Uliza vile kikundi

maalum au mtu mkuu alivyokuwa kwa maoni yao. Kama wangekuwa na ujumbe ambao

wangeuwasilisha kwa yule kiongozi wa kikundi hicho au kwa kikundi kizima bila kujulikana,ni nini

wangesema?

Alika watu kujadiliana katika vikundi vya watu 3 au 4 kwa dakika chache, wasiseme hadithi fulani,

lakini waelezee jinsi walihisi walipowekwa kando au walipotengwa, waeleze jinsi kikundi cha

katikati kilivyokuwa, na ni nini wataambia kikundi cha kati kama maoni yao kutoka kando au

kutokana na kufinyiliwa kando.

Halafu sanya majibu ya darasa nzima dhidi ya majadiliano haya. Mtu hujihisi vipi akiwa kando,

katikati huonekana vipi, na ni nini wataambia watu wa katikati kutoka kando.

Wakati majibu yote yamekusanywa na kuandikwa kwenye karatasi au ubao, ambia vikundi vyote

kuwa una “habari mbaya” na “habari njema” kwao. Habari mbaya ni kuwa, kila mmoja darasani

pamoja na mwalimu, ni yale mambo wamesema kuhusu katikati. Sisi sote tuko katikati kwa wakati

fulani, na ni hivi ndivyo tunavyoonekana kama tuko katikati kwa wale wako kando. Hata hivyo,

habari njema ni kuwa sisi sote tunaweza kubadilisha matendo yetu kutokana na kile tumejifunza

tukiwa kando. Tunaweza kusikiliza kama watu wa katikati sauti zetu wenyewe tukiwa kama watu wa

kando. Tunaweza kufanya kulingana na ile changamoto tuliyowapa wale wa katikati wawe, na

kutekeleza hii kutoka mtazamo wetu tukiwa kando .

Habari ya somo hili kinatoa mifano ya baadhi ya watu wanoajaribu kutenda wema kwa nafasi zao,

wakiwa katika au kando.

Gawa watu katika vikundi vidogo ili wasome na wajadili Matendo ya Mitume 6.1-7, huku wakitumia

maswali yafuatayo kuongoza majadiliano yao. Wape vikundi dakika 20 hivi kujadiliana pamoja.

Halafu alika kikundi kimoja kuripoti walichosoma . Uwaulize vikundi vingine wasiseme historia yote

bali tu watoe maoni yao dhidi ya fungu. Watakapomaliza, kiongozi wao anaweza kueleza pointi

zingine ambazo labda zilisahauliwa, na kumalizia na ufupisho.

Page 41: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[41]    

Maswali ya kutumia katika vikundi vidogo vya uchambuzi:

Vitaje vikundi vilivyohusika katika mzozo. Ni nini ilikuwa suala la hapo kwa hapo?

Ni nini mashaka ya pande zote?

Ni kikundi gani tunaweza kutambua kama imo “katikati” mwa jamii ? na ni kwa nini?

Ni kikundi gani tunaweza sema ni ya “kando”, ama iliyo ukingo wa jamii? Walihisi vipi kuwa

kando?

Kikundi cha Katikati kilikuwa na ufahamu wa kiwango gani kwa mambo kikundi cha kando

walikuwa wakipitia? Kiwango hicho cha ufahamu kilibadilika vipi?

Ni kwa njia gani maamuzi yaliyofanywa yaliathiri Katikati na Ukingo. Majina yote ya watu saba

yaliyochaguliwa yalikuwa majina ya Kigiriki. Haya yanaashiria kitu kuhusu mafikiano

yaliyopatikana? Kulikuwa na watu wengine ukingoni ambao hawakuwa katika suluhisho?

Ni nini unaona kama tashwishi kwa wale hawakuwa katika suluhisho?

Ni njia gani zingine, kama zipo, ambazo uamuzi uliofanywa haikushughulikia mahitaji ya wale wa

katikati na wa kando?

Ni nini ilifanywa na wale wa kando iliyosaidia?

Ni nini ilifanywa na wale wa katikati iliyosaidia?

VIPEO MUHIMU:

* Huenda njia bora ya kuelewa mabadiliko ya mzozo katika hadithi hii ni kupitia “katikati” na

“kando”. Katikati ni sehemu ya kikundi ambacho ndicho huweka masharti, sheria,desturi na

tamaduni ambazo hufuatwa na kikundi chote. Kikundi cha kati huenda kikawa ni wengi katika

kikundi, ingawa si lazima. Pia kikundi cha kati huenda wakawa ni wachache katika idadi, lakini

bado wana ushawishi mkubwa wa kuamrisha vitu vitendwe kulingana na matakwa yao katika

kikundi. Vivutio vya katikati ndivyo kikundi kizima kinaheshimu na kuchukua kama vivutio vya

kikundi kizima. Katikati huenda ikawa kikundi kinachoongoza au kilicho na mamlaka ama kilicho na

ushawishi mkubwa wa kitamaduni, wakati mwingine huenda wakawa ni kikundi fulani cha kikabila

kilicho na uongozi au mamlaka na tamaduni yao hufuatwa. Huenda wakawa ni wazazi katika familia,

uongozi katika kanisa, uongozi wa chuo cha masomo au taasisi. Kando ni watu au vikundi vya watu

ambao wako na maadili ambayo, tamaduni ambazo na mienendo ambayo ni mibadala kwa wale wa

katikati. Kila kikundi kina katikati na kando, kwanzia kile kikundi kidogo katika shule au kanisa

Page 42: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[42]    

mpaka vikundi vya mataifa. Watu wanaweza kuwa “katikati” kwa sehemu fulani na katika sehemu

nyingine wakawa “kando”.

Zaidi ya hayo, mtu anaweza kuwa “katikati” kwa njia moja katika kikundi fulani na “kando” kwa

njia nyingine katika kikundi kilekile ( kwa mfano, mwanamke aliyesoma-mpaka chuo, akiwa kikundi

cha kanisa anaweza kuwa “katikati” kwa sababu ya masomo yake na vilevile anaweza kuwa

“kando” kwa ajili ya jinsia yake). Kila mmoja wetu ana uzoefu wa kuwa “katikati” katika hali moja

na “kando” katika hali nyingine.

Mtazamo wa somo: Tunaweza kujifunza kusikiliza na kutenda haki zaidi wakati tupo “katikati”

kutokana na kile tulichopitia tukiwa “kando”.

* “Katikati” haifahamu haki zake wala cheo chao. “Katikati” hajui kile “kando” kinapitia. Hata hivyo

kikundi cha kando kinafahamu sana imani na mienendo yao wenyewe na cha katikati, kwa kuwa kila

mara lazima wao watii na watende kulingana na matakwa ya kikundi cha katikati wanaoongoza na

kutoa amri inayotumika na kikundi cha kando.

Wakristo Waebrania, wakiwemo Mitume hawakufahamu mateso ambayo akina mama wajane

walipitia. Hatujui kabisa ni jinsi gani mateso ya kukataliwa na kutengwa kwa wajane wa Kiyunani

yalifikia mitume. Pengine wao walilalamika moja kwa moja. Labda kiongozi wao alileta

malalamishi.

Pengine palikuwepo na Mwebrania mmoja aliyeona mateso hayo na kuripoti kwa mitume. Hata

hivyo ilifanyika, mitume hawakusifu wala kukashifu aliyeleta ujumbe huo, bali walisikiliza na

kushughulikia vilivyo ili kunusuru hali. Kusikiliza ni hatua bora ya kwanza ya kumudu kutojali na

kutofahamu wa “katikati”.

Mtazamo wa somo: Hatua ya kwanza bora na ya kujenga ambayo kikundi cha katikati kinaweza

kufanya katika mzozo ni kusikiliza!

* Ikiwa mzozo inahusisha ukosefu wa haki kutokana na ulegevu wa taasisi za umma, kama ilivyo

katika habari hii, ni lazima pia mabadiliko ya taasisi za umma yajumuishwe katika suluhusho la

mzozo. Katika hadithi ya Matendo ya Mitume 6, wajane wa Kiyunani walinyimwa mgao wa chakula.

Kwa hiyo, mabadiliko yalijumuisha kuundwa kwa kamati kanisani ili kushughulikia msaada wa

wasiojiweza na pia kuwapa uwezo waliokataliwa kwa kuwa sasa mambo ni mapya.

Wote ambao waliongoza au kusimamia mpango huu mpya ni Wayunani ambao hawakuwa

wanajaliwa.

Mtazamo wa somo: Inafaa kuhusisha “kando” katika kutafuta suluhisho la haki kama njia moja ya

kusuluhisha mizozo iliyojikita katika ukosefu wa haki.

Page 43: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[43]    

* Baada ya mzozo huo kusuluhishwa, mstari wa 7 inatueleza jinsi uinjilisti ilivyopanuka kwa kazi.

Mzozo huchukua nguvu nyingi mno ya jamii, mzozo itakaposuluhishwa, nguvu iliyoelekezwa katika

mizozo inabadilishwa na kutumika katika kazi zingine za kujenga.

Mtazamo wa somo: Kunawiri kwa uinjilisti unatokana na kusuluhisha mizozo kwa njia bora kanisani.

 

Page 44: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[44]    

AWAMU YA 11

KUTAFUTA SAUTI YAKO

FUNGU: Esta 4.1-17

HAPO NYUMA

Wayahudi walikuwa wametawanyika kote baada ya kuangushwa kwa Yerusalemu mnamo 586 kabla

ya kuzaliwa kwa Kristo. Kundi kubwa la Wayahudi walichukuliwa matekani kule Babiloni.

Hatimaye Wana wa Uajemi wakafamia Babiloni, wakaanzisha na kuimarisha ufalme uliyounga

mkono vikudi mbalimbali vya kidini. Mfalme wa Uajemi, Koreshi, aliwaruhusu Wayahudi chini ya

Esra na Nehemia kurejea Yerusalemu ili kuijenga tena. Wayahudi wengi waliamua kusalia Uajemi

Kitabu cha Esta kinaeleza hadithi ya jamii ya Wayahudi waliokuwa Uajemi. Esta alikuwa malkia wa

mfalme Ahasuero. Mjombake Esta Mordeikai alilitoboa njama iliyopangwa ya kuua mfalme.

Mordeikai alikataa kumwinamia Hamani aliyekuwa na tamaa nyingi ya uongozi na hila nyingi kwa

Wayahudi. Alikuwa afisa wa karibu na mfalme. Kwa sababu ya hasira na chuki dhidi ya Mordeikai,

Hamani alipanga njama ya kuchinjwa na kumalizwa kwa Wayahudi wote. Kwa hiyo alipanga madai

ya uongo dhidi ya Wayahudi na kumpelekea mfalme ili aagize kuchinjwa kwa Wayahudi.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Unaweza kuandaa mchezo wa kuigiza fupi mapema kidogo na wahusika wanne ambao watachukua

nafasi za Mordeikai, Esta, kijakazi wa Esta na Hathaki. Hao wanne wanafaa wasome hadihthi

yenyewe mapema na kujiandaa kuambia darasa hadithi yenyewe kwa njia ya kuigiza.

Mchezo wa kuigiza utakapomalizika, darasa linaweza kujadili maswali yafuatayo kwa vikundi

vidogo vidogo au wakiwa kama darasa nzima. Darasa nzima laweza kusoma kitabu cha Esta yote

kabla ya somo.

Mchezo wa kuigiza usipowezekana kufanywa, gawa darasa katika vikundi vidogo ili wajadili babari

wakitumia maswali yafuatoyo ili kuongoza somo yao. Uwaruhusu vikundi muda wa dakika 30-35

hivi wajadaliane. Halafu alika kikundi kimoja kiripoti walichosoma. Uliza yale makundi mengine

kutoa maoni yao kutokana na walichosoma, bila kusimulia hadithi yote ya fungu. Wakati ambapo

makundi yote yamemaliza, kiongozi wao anaweza kueleza chochote ambacho haikusemwa huku

akimalizia.

Maswali ya kutumiwa na vikundi au darasa lote:

Mordeikai na Esta walihisi vipi waliposika habari ya kuangamizwa kwa Wayahudi?

Ni nini ilikuwa hatari iliyowakumba wao kama Wayahudi katika jamii hii?

Ni kwa njia gani Esta alikuwa katika hatari licha ya kuwa kama mamlaka nyingi ya malkia?

Page 45: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[45]    

Ukikumbuka majadiliano ya “katikati” na “ukingo” ( au katikati na kando) katika somo la Mitume 6,

ni changamoto zipi Esta na Mordeikai walikumbana nazo ndani yao kama watu wa kando au

waliotengwa sana, katika hadithi hii?

Wao walifanya nini ili kuimarisha jitihada zao ili kubadilisha mzozo huu hatari?

Ni jinsi gani Mordeikai alimfanya Esta kushughulika?

Ni nini Mordeikai aliamini juu ya nafasi maishani ya kuchukua ili kuleta mabadiliko? Ikiwa tutawaza

au kufikiri kama yeye, wazo kama hili litawezaje kuathiri jinsi tunavyokaa na watu na kutatua

mzozo?

Ni mzaada gani Esta alitafuta kwa matendo yake? Mzaada huu ulimsaidia yeye kivipi?

Maombi yake yaliweza kujenga umoja kati ya jamii Wayaudi kivipi?

Matendo ya Esta yalikuwa kutotii wa umma? Esta alifanyaje ili kuvutia huruma na uwazi wa mfalme

kwa uwito wake? (Esta 5.1-3 huonyesha vile Esta alianza kujipanga kumwendea mfalme)

Uliza darasa ikiwa wamewahi kuhisi kuwa wao ndio watu maalum kwa wakati maalum kwa mahali

maalum ambao walistahili kuitikia mzozo au changamoto kwa njia maalum ama ya kipekee na

muhimu? Hali ilikuwa nini? Ulihisi vipi? Ulifanya au ulisema nini? Unaona kama uko katika hali

hivi sasa ambayo huenda ikawa ni wewe ndiye uko na nafasi ya kipekee ya kutenda ili kuleta

mabadiliko ya kujenga katika mzozo?

Alika wahusika waunde vikundi vya watu 2 au 3 kuzungumzia mambo kama hayo na changamoto

miongoni mwao. Ikiwa kuna yeyote katika kikundi anayepitia hali kama hii, inayohitaji vitendo

vishirikishi kwa sasa, ombeaneni kama vile Esta alivyojumuisha maombi ya jamii yake kuupa uwezo

matendo yake.

VIPEO MUHIMU:

* Esta, kwa ujasiri mkuu alihatarisha maisha yake na kuongea mbele ya mfalme. Alipanga kwa

uangalifu jinsi atakavyomwendea mfalme ili ombi lake lipate kusikizwa. Mordeikai akachukua

kitendo cha umma kwa kulia na kuomboleza kwa maangamizi makuu yanayokuja na kuchinjwa

kuliyowagodolea macho. Hata ingawa Mordeikai binafsi hangeweza kuwafikia wenye maamuzi,

lakini alijiandaa kwa kujipanga, kusanya habari (kama vile nakala ya amri ya mfalme), na kujiweka

katika sehemu ambayo matendo yake yataonekana.

Mtazamo wa somo: Mpango mzuri, ujasiri wa kujihatarisha na kujitolea kabisa ni viungo muhimu

vya kubadilisha mzozo.

* Jambo ambalo ni gumu sana kufanya kwa wale wako kando ni kupata sauti yao na kuongea, haswa

wanapohisi kuwa wanahatarishwa. Walio madarakani, wa katikati, mara nyingi hawafahamu shida

Page 46: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[46]    

ambazo matendo yao yanaleta kama vile ilivyokuwa na mfalme Ahasuero. Wengine wanaweza kuwa

katili moja kwa moja jinsi alivyokuwa Hamani.

Esta alistahili kufahamu kwa undani kilichokuwa karibu kutendekea watu wake na kuwa na

changamoto ya kujihatarisha, kwa kuwa ilikuwa ni yeye tu aliyekuwa katika nafasi ya kuwafikia

wenye maamuzi.

Mtazamo wa somo: Kutafuta njia ya kufanya waliotengwa kuongea ukweli juu ya yale yanayofanyika

, ni muhimu sana kwa kubadilisha mzozo.

Page 47: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[47]    

AWAMU YA 12

MAMA ALIYEKASIRISHWA NA MWENYE HUZUNI

FUNGU: 2 Samweli 21.1-14

HAPO NYUMA:

Wakati wana wa Israeli waliposhinda Kanani, Wenyeji wa Gibeoni walifanya maagano kwa njia ya

ujanja na wana wa Israeli. Habari hii inapatikana Yoshua 9.3-27. Yoshua alifanya maagano na

Wenyeji wa Gibeoni, kuwaruhusu wao waishi, agano hili lilionekana takatifu,na ambalo

halingevunjwa. Kwa hakika, kulikuwa na mauaji ya Wenyeji wa Gibeoni chini ya utawala wa

mfalme Sauli.

Sauli alikuwa na wana watatu, akiwemo Yonatani rafikiye Daudi, ambao waliuliwa badaye na

Wafilisti. Daudi akawa mfalme na mlinzi wa Mefiboshethi mwanawe Yonatani, aliyekuwa mlemavu.

Rispa, suria wa Sauli aliyekuwa hai alikuwa ametumiwa hapo mbeleni kama mmiliki ikiashiria

mvutano wa mamlaka wa kisisa uliokuwa ukiongezeka baina ya mwana wa Sauli Ishbosheti na

jemedari wake Abneri (tazama 2 Samweli 3.6-11). Ifikapo hadithi iliyo 2 Samweli 21, Daudi ana

madaraka tele na anamiliki ufalme wake kabisa, hii ikiwa baada ya kustahimili vita vingi vya

kujiimarisha na migomo nyingi.

MKONDO WA SOMO NA MASWALI:

Watu wagawanyike katika vikundi vidogo ili wasome na kujadili habari wakitumia maswali

yafuatayo kuongoza mjadala wao. Ruhusu dakika 30 hivi ili kikundi kijadili pekee yao. Baada ya

hayo, alika kikundi kimoja kuripoti walichosoma. Uliza vile vikundi vingine, bila kurudia kusema

hadithi nzima bali kuelezea mtazamo wamepata kutoka habari. Wakati ambapo vikundi vyote

vimemaliza, kiongozi wao anaweza kusema yale pengine yamesahauliwa na kisha kumalizia.

Maswali ya kutumika katika vile vikundi vidogo:

Chanzo cha vita kati ya Sauli na Wenyeji wa Gibeoni hakijaripotiwa katika Biblia, ila tu katika

kumbukumbu cha kifungu hiki. Je ni kitu gani unadhani kilifanyika? ( Wenyeji wa Gibeoni walikuwa

wameahidiwa usalama katika Israeli katika Yoshua 9) Ushawishi gani Daudi alifanya ili

awafurahishe Wenyeji wa Gibeoni? Ni nani angeteseka katika kutokea kwa vita tena kwa upya

wakati huu? Je, kuna dalili yoyote ya kuonyesha kuwa watu hawa walihusika katika mwanzo wa vita

hivi? Kwa nini Wenyeji wa Gibeoni na Daudi kuhisi kuwa kitendo kama hicho kitafanya hali kuwa

“bora”? Ni jinsi gani Daudi yuko kwenye kikundi chaa katikati katika hadithi hii? Na yeye Daudi

anachukulia vipi na wale watu wa kando?

Rispa ni nani? Rispa yu vipi katika “ukingo” wa hadithi hii?Ni hatua zipi alizichukua?Hiki kilikuwa

kitendo cha uma?alitenda zaidi kuliko kulilia alichopoteza?chagua lke ni tofauti kivipi na chaguo la

Page 48: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[48]    

Mikali , mama Yule mwingine katika habari? Unafikiri ni mambo gai kindani Rispa angekumbana

nayo ili kutenda alivyofanya? Unafikiri nini kilimpa uwezo na ujasiri kwa tendo lake?

Kitendo cha Rispa kilikuwa na athari zipi? Ni vipi Daudi kama mtu wa “katikati” alijibu Rispa kama

mtu wa “ukingo”? Hii inaonyesha nini kuhusu Daudi, aliyepeana wanaume hao kuuwawa, kuzika

maiti zao kwa hadhi ya ufalme? Mungu yu wapi katika habari hii? Kwani Mungu anachukulia mzaha

makubaliano yaliyofanyika kati ya wenyeji Gibeoni na Daudi? Ni baraka zipi zilijia nchi? Ni vipi

dini imetumiwa kueneza vitendo vya kisiasa”

Baada ya ripoti za vikundi, uliza yeyote awaze mfano wa kisasa kama Rispa, unaweza kuzungumzia

habari za wamama waliohamasisha kutenda sababu ya vurugu didhi ya watoto wao (angalia hapa

chini). Ligawe darasa kwa vikundi vya watu wawili au watatu kujadidli jinsi Rispa angesimama

kama angukuwa siku hizi. Angekuwa na nani? Angefanya nini?

VIPEO MUHIMU:

* Daudi aliwafayanya jamii ya Sauli kama dhabihu akiwa kwenye utawala. Alikuwa amezingatia

kikamilifu kutatua shida ya kisiasa ya wenyeji wa Gibeoni, na pia akilinda kiti chake kutokana na

hatari ya wafuasi wa mfalme aliyemtangulia, yaani Sauli. Daudi hakufikiria ahari ya mauaji yake

kwa wamama ya waliokufa au kutokuwa na hatia kwa waliotolewa kama dhabihu kwa sababu ya

manufaa ya siasa. Kunyimwa kwa haki kwa mara nyingi ni upofu wa walio kwenye “katikati” kwa

maadili, mahitaji na mashaka ya walio “ukingoni”.

Mikali hakuchukua hatua yeyote kukabiliana na dhuluma, kwa hivyo alibakia asionekane, yaani

“ukingo” usiosikika. Rispa alitoa nje dhuluma kwa vile ilivyokuwa, huku akikataa kumkubali

matendo ya Daudi aliye “katikati”. Alifanya dhuluma zinazopitiwa na wale wa “ukingo” kiwe wazi

kabisa.

Mtazamo wa somo: Walio “katikati”, kwa mara nyingi, huteza walio “ukingoni”, kwa hiyo

inwalazimu wale walio “ukingoni” kujisimamia na kuupa changamoto hali matendo kisicho na haki.

* Wamama wakati mwingine wamepanga kupinga, hata katika uso wa vurugu, upuuzaji wa haki za

kibinadamu zinazohatarisha maisha ya watoto wao. Mifano mitatu yananawiri zaidi:

Wamama wa Plaza Del Mayo kule Ajentina uliopangwa katika miaka ya 1970 katika “vita vichafu”

vya nchi hiyo. Kumi maelfu ya vijana “walipoea” huku wakikamatwa na wanajeshi. Hawakuonekana

tena. Watu waliwawa na kuzikwa bila kujua idadi yao au wengine waliangushwa kwa helikoptta hadi

kwenye bahari. Wakati wamama hawakupata maelezo ya kupote kwa watoto wao, wakajipanga.

Wakawa na mkesha kila wiki katika jiji kuu, wakibeba picha za watoto wao waliopotea. Katika hali

hii ngumu wakaendelea na matendo yao na wakawa sauti ya ukombozi uliyokomesha utawala wa

kuogofya wa kijeshi.

Page 49: KIJITABU CHA UCHAMBUZI WA BIBLIA...JUU YA KUBADILI MZOZO NA Daniel L. Buttry [2]$ $ YALIYOMO Utangulizi Uchambuzi wa Biblia kwa kushirikisha Uchambuzi wa Biblia katika muktadha ya

[49]    

Wamama wa Waliopotea kule El Salvador walipanga kuukaza serikari kuwapa habari ya majamaa

wao waliopotea. Wakawa mmoja ya sauti dhabiti iliyokomesha vita katika nchi hiyo.

Wamama wa Naga Mothers Association walianza kama wamama wa kushughulikia jamii mle

Nagaland Kazkazini Mashariki mwa India. Walianza kwenda kwenye maksi ya wananjeshi wa India

na vituo vya polisi wakisanya miili ya watu wa Naga waliowawa katika vita tangu mwaka 1955.

Hamna aliye na uwezo wa kuitisha miili hizo kwa sababu ya kuhofia mateso ya polisi. Wamama hao

walizika miili hizo vizuri kamam ttamaduni, hku wakiwafunga na vitambaa vipya. Wakati idadi ya

Naga wliowawa ilizidi kuongezeka, wakapasa sauti zao wakikabilianana katika vitendo vya kisisasa

kwa ajili ya kukoma kwa vurugu hiyo. Wamama wa Naga Mothers Association imekuwa sauti ya

haki za binadamu na amani.

Mtazamo wa somo: nguvu ya upendo wa mama inaweza kuwa na nguvu ya kupata haki na amani

akikabiliwa na hatari za vurugu dhidi ya wanao.

* Matendo ya Rispa yalikuwa ya kutangaza uwazi kwa muda mrefu. Akawa na mkesha tangu

mavuno ya shayiri mpaka mvua iliponyesha (msatri wa 10), kutoka Oktoba hadi Mei hivi. Alifanya

kifo cha wanawe kuwa wazi kwa wana wa Israeli. Alipowasili Daudi na kumsika wanawe Rispa,

vitendo vyake Daudi vilikuwa vya uwazi. Alikuwa akibadilisha sera zake kinaganaga, huku akifanya

kitendo cha toba kutokana na ushuhuda wa Rispa.

Mtazamo wa somo: Vitendo vya wazi visivyo na vurugu wakati mwingine hubadilisha nyoyo au sera

za wenye nguvu

* Maelewano ya Kisiasa baina ya Dauidi na wana wa Gibeoni yalivalishwa lugha ya kidini. Vijana

wa kiume saba walichinjwa “mbele ya Bwana” (mstari wa 6 na 9). Hata ingawa katika historia

yenyewe Mungu aliwakumbusha shida ya awali ya mauaji makuu ambayo haijasuluhishwa ya wana

wa Gibeoni, iliyotekelezwa na Sauli kama chanzo cha njaa (mstari 1), Mungu hajibu mauji ya wana

wa Gibeoni yaliyotekelezwa na Sauli kwa kuondoa njaa. Kinachoonekana kimasomaso ni kuwa

matendo ya Daudi hayakuwa mapenzi ya Mungu. Lakini Daudi alipotubu mbele ya umma kwa kuja

kumzika kwa heshima wanawe Rispa, baada ya Rispa kukaa macho kwa miezi kadhaa huku akitoboa

uozo wa vurugu za kisiasa, ndiposa Mungu akaubariki nchi.

Mtazamo wa somo: Baraka za Mungu hailetwi na kuzidi kwa vurugu, bali inaletwa na kumalizwa

kwa vurugu za kila mara.