kitabu cha marafiki wa elimu handbook.pdf4 kitabu cha mara˜ki wa elimu mojawapo ya kushiriki katika...

32

Upload: others

Post on 10-Jan-2020

49 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Marafiki wa Elimu 1

Page 2: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Marafiki wa Elimu2

Page 3: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu i

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu

Page 4: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimuii

Waandaaji: Pius Makomelelo, Joyce Mkina, Naomi Mwakilembe, Honoratus Swai na Agness Mangweha

Wachangiaji: Robert Mihayo, Elisante Kitulo

Mhariri: Elizabeth Missokia

Mchoraji: Marco Tibasima

Toleo la Nane

© HakiElimu, 2013

SLP 79401, Dar es SalaamSimu (022) 2151852/3, Faksi (022) 2152449Barua pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

ISBN: 978-9987-18-038-7

Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa minajili isiyo ya kibiashara; ilimradi chanzo cha sehemu iliyonakiliwa kinaonyeshwa na nakala kutumwa kwa HakiElimu.

Page 5: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 1

Tutatokomeza ziro kwa kupanga na kusimamia utelekelezaji

makini wa mipango ya kuboresha elimu katika kila

shule, pia kwa kuwawezesha na kuwasimamia walimu kufanya kazi; na kwa kuwashirikisha

wananchi kutambua thamani ya elimu na wajibu wao.

Page 6: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu2

Utangulizi

Karibu! Hongera kwa kuwa Rafiki wa Elimu. Wewe ni mmoja wa wanaharakati wengi ambao wanajali elimu na demokrasia Tanzania! Ni wajibu wako kushiriki kikamilifu kuleta mabadiliko!

Kitabu hiki kimetengenezwa kwa ajili ya Marafiki wa Elimu kama rejea katika shughuli zao za kila siku. Kinatoa maelezo mafupi kuhusu Harakati za Marafiki wa Elimu ili kupanua uelewa wa walengwa kuhusu historia, madhumuni na uendeshaji wa Harakati hizi. Pia kinatoa maelezo kuhusu haki na wajibu wa Rafiki wa Elimu katika Harakati.

Tunataraji kwamba kitabu hiki kitajibu maswali mengi ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu Harakati za Marafiki wa Elimu na kukutia hamasa zaidi kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma ya elimu nchini. Kama una maswali zaidi kuhusu Harakati hizi tafadhali wasiliana nasi, tutajitahidi kukujibu. Vilevile kama una maoni ya kuboresha kitabu hiki tafadhali tuandikie.

HakiElimu ni nini?HakiElimu ni shirika la hiari linalolenga kuona jamii yenye uwazi, inayozingatia haki, demokrasia na inatoa elimu bora kwa wote. Linafanya hivyo kwa kuwezesha jamii kupata habari, kubadili shule na uundaji wa sera, kuchochea ubunifu wa mijadala ya umma, kufanya utafiti yakinifu, uchambuzi wa sera na kushirikiana na wadau ili kuendeleza manufaa ya pamoja kwa kuzingatia haki ya jamii. HakiElimu inawasaidia wananchi kujua haki na wajibu wao kwa kuwapa taarifa mbalimbali ili waweze kuchukua hatua za kuboresha elimu.

Anuani yetu ni:Harakati za Marafiki wa Elimuc/o HakiElimu739 Mathuradas StreetUpangaSLP 79401Dar es SalaamSimu (022) 2151852 / 3Faksi (022) 2152449Barua pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

Page 7: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 3

Harakati za Mara�ki wa Elimu ni nini?

Harakati ni nini? Ni jitihada za kimapinduzi zinazofanywa na watu kwa lengo la kubadilisha kabisa jambo fulani.

Harakati za Mara�ki wa Elimu ni nini? Ni Harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu kwa lengo la kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa programu mbalimbali za maendeleo ya elimu. Kufikia mwezi Julai 2012, Harakati hizi zilikuwa na wanachama takribani 36,000 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.

Sera na mipango mbalimbali ikiwemo Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Sekondari (MMES) inasisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake. Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini.

Harakati za Marafiki wa Elimu zinalenga kukuza ushiriki wa wananchi katika michakato mbalimbali ya kuboresha elimu na demokrasia. Madhumuni ya Harakati hizi ni kuwawezesha watanzania kuleta mabadiliko katika elimu. HakiElimu ni mraghabishi tu wa Harakati hizi na anayewajibika kukupa taarifa mbalimbali, lakini mtendaji mkuu ni wewe Rafiki. Unapaswa kutambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii, kuchukizwa na hali duni ya utoaji wa elimu katika eneo na taifa lako kwa ujumla, na kuelewa nafasi uliyonayo katika kuchagiza mabadiliko.

Kwa ujumla, watanzania bila kujali nafasi walizonazo katika jamii wana wajibu wa kuboresha elimu na demokrasia nchini kwa kushiriki kikamilifu katika masuala na michakato mbalimbali ya maamuzi yenye kuathiri kwa namna moja au nyingine utoaji wa huduma ya elimu kwa watu wote. Njia

Madhumuni ya Harakati za Mara�ki wa Elimu niKuwezesha Watanzania kuleta mabadiliko katika elimu.

Page 8: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu4

mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu kujiunga na Harakati hizi ili uchangie kuongeza ufanisi juu ya utoaji wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

Harakati za Mara�ki wa Elimu:

nZitatoa maelezo ya kiutendaji kwa watu wanaojali kuhusu elimu nchini Tanzania,

nZitasaidia kupeleka maoni na kero za Marafiki kwa vyombo na mamlaka husika,

nZitawaunganisha Marafiki ili kuweza kubadili shule ziweze kutoa elimu bora kwa wote,

nZitawapa Marafiki fursa ya kupata habari mbalimbali kuhusu elimu na demokrasia.

nZitaongeza uelewa wa wananchi juu ya kinachoendelea nchini kuhusiana na elimu na kupanua mijadala inayolenga kuboresha elimu na demokrasia.

Harakati za Marafiki wa Elimu pia zitakupa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu na watu wengine wanaojali elimu na demokrasia. Tutakupa anwani za Marafiki wengine kwa lengo la kukuunganisha nao uweze kujifunza uzoefu na stadi mbalimbali kutoka kwao na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha kwamba kila mtoto anafurahia kupata elimu ya msingi yenye ubora.

Dira ni kwamba Mara�ki wa Elimu

watashirikiana kutambua,

kufuatilia na kushawishi

mwelekeo wa elimu nchini Tanzania.

Page 9: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 5

Nani anaweza kuwa Ra�ki wa Elimu?

Mtu yeyote anaweza kuwa Rafiki wa Elimu! Hakuna masharti. Unaweza kuwa kijana au mzee, mwanamke au mwanaume, mwenye ulemavu au asiye na ulemavu, aliye nje au ndani ya shule. Licha ya watu binafsi, vilevile tunakaribisha maombi kutoka kwa wanafunzi, wazazi pia na walimu wanashauriwa kujiunga. Wanawake na wasichana wanakaribishwa kujiunga kwa wingi kwani ushiriki wao una umuhimu wa kipekee katika kusukuma gurudumu la maendeleo ukizingatia kundi hili kihistoria limeachwa pembeni katika ngazi mbalimbali za maamuzi kwa muda mrefu.

Hata hivyo, tunawashauri Marafiki popote walipo kuunda vikundi kabla au hata baada ya kujiunga na Harakati hizi.

Kwa nini tunashauri Mara�ki kuanzisha vikundi?

Changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya elimu zinahitaji nguvu ya pamoja kuweza kuzitatua. Kwa kadri harakati za Marafiki wa Elimu zinavyozidi kukua, tunashauri Marafiki kuunganisha nguvu pamoja ili kuongeza nguvu kukabiliana na changamoto zinazojitokeza. Makundi haya yanaweza kuanzishwa katika ngazi za vijiji, vitongoji, kata, wilaya, hata mkoa kwa lengo la kuimarisha ushiriki wao katika kukabiliana na changamoto zinazokwamisha maendeleo. Umoja huu utawezesha washiriki kubadilishana taarifa, utaalamu na mbinu za kiutendaji. Utawapa sauti ndani ya jamii inayoweza kusaidia kuleta mabadiliko na kuongeza uwajibikaji. Aidha, umoja huu ni nafasi muhimu kufanikisha mijadala ya wazi kuchagiza ushiriki hai wa wananchi katika maamuzi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya elimu katika maeneo yao na taifa kwa ujumla.

Page 10: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu6

Kikundi cha Mara�ki wa Elimu wanaohamasisha elimu kwa mtoto wa kike.

Marafiki wa Elimu wa vijiji vya Kitunguluma, Mbalimbali, na Koleli wilayani Serengeti wana kikundi chao cha pamoja wanachokiita KIMKO. Kikundi hiki pamoja na shughuli nyingine kinapigania elimu kwa mtoto wa kike ambayo kwa muda mrefu ni tatizo katika maeneo ya jamii ya Wakurya. Kikundi kinaendesha kampeni dhidi ya mila iliyopitwa na wakati ya ukeketaji na ndoa katika umri mdogo kama njia ya kuondokana na mila hii kandamizi ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kutoandikishwa au kuacha shule kwa watoto wengi wa kike. Kikundi pia huendesha harambee kupata fedha kwa ajili ya kusomesha watoto wa kike waishio katika mazingira magumu. Kinafuatilia pia kuona watoto wa kike wanaenda shule bila kubugudhiwa na wazazi wao wenye tamaa ya mali. Aidha, kikundi kimeanzisha maktaba ya jamii kwa lengo la kukuza mwamko wa wananchi na jamii juu ya umuhimu wa elimu. Tangu kilipoanzishwa mwaka 2003 kikundi kimefanikiwa kuleta mapinduzi ya kifikra kwa jamii ya kata ya Machochwe. Sasa watoto wengi wa kike wanaenda shule na kufanikiwa kumaliza elimu katika madaraja mbalimbali. Huu ni mchango wao mkubwa katika kuboresha taaluma na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya elimu ndani ya shule na jamii husika.

Kama Rafiki wa Elimu unaweza kubadilishana mawazo na uzoefu na wenzako na pia kuwajulisha kuhusu Harakati za Marafiki wa Elimu. Kwa nini usiwashawishi kujiunga na Harakati? Kwa nini usiwashauri Marafiki wenzako katika jamii yako, kijiji, mtaa, kata, wilaya hata mkoa kuunda umoja utakaokuwa na nguvu kuchangia na kuchagiza uwajibikaji wa pamoja kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya elimu nchini? Inawezekana, wengine wamefanya hivyo wakafanikiwa na sasa wanasonga mbele.

Kama Rafiki wa Elimu unaweza kutarajia kuwa mmoja wa wanaharakati wakubwa waliojitolea kuboresha elimu na demokrasia nchini Tanzania. Kwa kujiunga na Marafiki wa Elimu utaonesha kuwa unajali na kwamba unataka kuleta mabadiliko.

Kwa namna yoyote ile Harakati za Marafiki wa Elimu hazina uhusiano wa moja kwa moja na masuala ya kisiasa, rangi ya mtu au dini. Wala harakati hizi siyo za unyanyasaji wa kidini, ubaguzi wa rangi, kijinsia au imani. Badala yake zinazingatia utekelezaji wa mojawapo ya misingi mikuu ya haki za binadamu, kuwa kila mtu ana haki ya kupata elimu.

Page 11: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 7

Nikijiunga na harakati za Mara�ki wa Elimu usajili wangu utadumu kwa muda gani?

Hakuna muda maalum wa kuwa katika Harakati za Marafiki wa Elimu. Unapojiunga katika Harakati hizi unaweza kuwepo kwa kipindi chochote kile hadi hapo utakapoamua mwenyewe kujitoa. Maswali ya msingi ya kujiuliza kama Rafiki wa Elimu ni je umefanya nini kusaidia kuboresha elimu tangu ulipojiunga? Umechangia kwa kiasi gani kukuza au kuimarisha Harakati za Marafiki wa Elimu? HakiElimu kila mara itatathmini kutambua ushiriki wa kila Rafiki katika Harakati na kuwasiliana naye kujua utayari wake kuendelea na Harakati. Angalizo: Kisheria watoto walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kutia saini katika fomu ya kujiunga na Harakati za Marafiki wa Elimu. Wazazi au walezi wao wanapaswa kutia saini kwa niaba ya watoto wanaojiunga. Utaratibu huu unawahusu pia wenye mtindio wa ubongo.

Ungana na wananchi na viongozi wako wa serikali ya mtaa kuleta mabadiliko!

Katika Harakati za Marafiki wa Elimu, Rafiki ndiye anayekuwa chachu ya kuleta mabadiliko. Hii ina maana kuwa ni juu yako kuleta mabadiliko! Tunatambua wazi kuwa Marafiki wamezungukwa na wananchi wengi ambao pengine kwa utashi wao hawajaamua kujiunga na Harakati hizi lakini wanapenda kujua nini kinaendelea kwenye sekta ya elimu na wako tayari kushiriki. Ni juu ya Rafiki kutumia nafasi yake kuihabarisha jamii juu ya umuhimu wa elimu na kuichagiza kushiriki katika michakato ya kuleta mabadiliko. Aidha, Rafiki wa Elimu anatakiwa kufanya kazi sambamba na juhudi zinazofanywa na viongozi wa serikali za mitaa. Ushirikiano ni wa muhimu kwa pande zote. Ueleweshe uongozi kwa nini unahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ya shule. Tambulisha Harakati zinalenga kuleta nini katika jamii. Ni vizuri sana kupata baraka za viongozi wako na kufanya nao kazi kuchagiza mabadiliko chanya na uwajibikaji.

Page 12: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu8

Ikiwa unahitaji msaada au ushauri unaweza kuwasiliana na Marafiki wa Elimu wengine, HakiElimu au wadau wengine katika sekta ya elimu.

Unachoweza Kufanya katika Jamii Yako ili Kuleta Mabadiliko ya Elimu

Kama Rafiki wa Elimu kuna mbinu nyingi unazoweza kutumia kuleta mabadiliko katika jamii yako. Tuna mapendekezo machache; lakini kumbuka kuna njia nyingi zaidi unazoweza kutumia kama nafasi yako kuwa katika mchakato huu wa kuleta mabadiliko chanya katika elimu na demokrasia hapa nchini Tanzania.

§Jadili na wengine suala linalohusu elimu.Je, kuna kero zinazokugusa katika jamii au shuleni kwako? Ni kero gani hizo? Je, kero hizo zinaathiri vipi jamii yako? Je, kuna taarifa iliyochapishwa gazetini, kutangazwa redioni au mada uliyosoma kwenye machapisho ya HakiElimu? Je, kuna mtu mwenye wazo au pendekezo juu ya suala lililojadiliwa? Ongelea suala hili katika mikusanyiko ya kawaida na kwenye mikutano na jumuiya. Amueni kwa pamoja ni hatua gani mnazoweza kuchukua kuleta mabadiliko. Tuambieni kuhusu mafanikio yenu na changamoto.

§Ungana na Mara�ki wa Elimu wengine katika eneo lako. Kwa kujumuika pamoja na Marafiki wengine mnaweza kujadili kero na mawazo yenu na watu wengine wanaojali elimu. Mtakapojadili ni vyema mawazo hayo mkayafikisha kwa mamlaka husika au vyombo vya habari. Sehemu zingine Marafiki hukaribisha viongozi na vyombo vya habari wakati wa mijadala yao. Ni vizuri kuanza kutatua kero hizo kuanzia ngazi mlipo.

§Anzisha midahalo Ujadili namna jamii inavyoshiriki katika uendeshaji wa shule yako. Je, watu wanafahamu ni nani mwenye jukumu la uendeshaji wa shule? Je, watu wanajisikia kwamba wana sauti? Kwa nini usiwaulize vijana wanafikiri

Page 13: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 9

nini? Mkaribishe kiongozi kutoka Serikali za Mitaa au mwandishi wa habari. Washirikishe Marafiki wengine, wadau mbalimbali wa elimu au HakiElimu katika matokeo ya majadiliano yenu. Tunaweza kujumuisha maoni yenu katika jarida letu la SautiElimu au machapisho mengine.

§Ongea na Kamati ya Shule yako au walimu. Je, wana mtazamo gani juu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) au Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES)? Waulize kuhusu kazi zao.Wanapenda nini? Ni yapi wangependa kuboresha? Wanakwazwa na nini katika kutekeleza majukumu yao? Fursa zipi ambazo zikitumika zinaweza kuleta tija kwa maendeleo ya shule? Jadili maoni yenu na wengine katika jumuiya na ishauri Kamati ya Shule. Je, kuna njia rahisi mnazoweza kupendekeza kutatua matatizo yao? Tafuta namna ambavyo jumuiya yako ingeweza kuwasaidia. Pale inapobidi pigania kuingia kwenye Kamati ya Shule utoe mchango wako wa maendeleo ya shule moja kwa moja.

§Hudhuria kwenye mikutano ya Serikali za Mitaa. Changia hoja na maoni ya jinsi ya kuboresha elimu. Ni haki ya kila mwananchi kujua kuhusu mapato na matumizi ya fedha katika kitongoji, kijiji au mtaa. Kila mwananchi ana haki ya kuuliza kuhusu daftari la matumizi na mapato ili aweze kulikagua na kuuliza pale atakapokuwa haelewi. Kwa kuzingatia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni haki ya raia wa Tanzania kutoa maoni, kupata habari na kusikilizwa.

§Wezesha jamii yako kupata taarifaJitahidi kuanzisha na kuendeleza maktaba za jamii katika eneo lako. Pia hamasisha matumizi ya mbao za matangazo na mijadala ya wazi katika kupashana habari. Matumizi ya vyombo vya habari kama vile redio, televisheni na magazeti ni nyenzo nzuri pia katika suala la upashanaji habari. Vitumie kwa faida ya umma. Anza kidogo kidogo kwa kuwashirikisha viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla. Wengine wameweza, wewe je?

Page 14: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu10

§Wezesha shule yako kuwa ya mfano wa kuigwaHamasisha uandikishaji na mahudhurio ya watoto shule. Jenga mahusiano mazuri kati ya wazazi/wanajamii na uongozi wa shule. Hamasisha uanzishaji wa vilabu vya masomo na mabaraza ya wanafunzi ili kuboresha taaluma na demokrasia ndani ya shule. Hamasisha wazazi kuchangia kwa hali na mali shughuli za maendeleo ya shule. Shiriki kutatua migogoro ya shule.

§Fuatilia shughuli za maendeleo ya shuleNi haki ya msingi kwa raia wa Tanzania kupewa au kutoa taarifa (Ibara namba 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Ni vizuri kuwa karibu na uongozi wa shule kujua takwimu na hali nzima ya maendeleo ya shule. Pima kwa kiasi gani shule yako imefanikiwa katika uandikishaji na mahudhurio ya watoto shule, ufaulu katika mitihani, uwepo na utendaji wa walimu, hali ya miundombinu ya shule yaani madarasa, nyumba za walimu, vyoo na kadhalika. Pia pima hatua iliyofikiwa kwa kuzingatia maelekezo ya kisera mfano kiasi cha fedha za ruzuku kinachofika shule. Kumbuka kuwa kila mtoto anatakiwa kupata shilingi za kitanzania 10,000 kwa mwaka kwa shule za msingi (MMEM II), na shilingi 25,000 kwa shule za sekondari (MMES II). Chumba kimoja cha darasa kinatakiwa kuwa na wanafunzi 40; mwalimu mmoja anatakiwa kuhudumia wanafunzi 40; tundu moja la choo linatakiwa kuhudumia watoto 25 wa kiume na 20 wa kike. Kitabu kimoja kinatakiwa kisomwe na mtoto 1.

Page 15: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 11

Mara�ki mvumi wajenga maktaba ya jamii

Wazo lilianza kwa kutumia machapisho wanayopata kutoka HakiElimu yawafikie na wananchi wengine wasio Marafiki wa Elimu. Mchango mdogo mdogo wa machapisho kutoka wanachama wa kundi la Marafiki wa Elimu Mvumi ukazaa huduma ya maktaba. Taratibu huduma hii ikazidi kukua siku hadi siku, kwa msaada wa machapisho kutoka kwa wadau mbalimbali idadi ya vitabu ikaongezeka. Hatimaye wanachama wakaona umuhimu wa kujenga kituo cha maktaba jambo ambalo wamefanikiwa na sasa kijiji kina maktaba ya jamii inayohudumia wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wengine wa elimu.

 

Maktaba ya Jamii Mvumi 2008  20082008   Maktaba ya Jamii Mvumi-2012 Maktaba ya jamii mvumi 2008 Maktaba ya jamii mvumi-2012

Page 16: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu12

Inatupasa tuwathamini walimu

Na Theodora Malata, Dar es Salaam

Ni muda mrefu sasa tangu tuanze kusikia malalamiko na vitisho vya migomo ya walimu inayosababishwa na madeni na malimbikizo ya mishahara yao. Malalamiko hayo yamekuwa kama ‘kelele za chura’ ambazo hazimzuii ng’ombe kunywa maji kwani si leo wala jana tangu malalamiko hayo yaanze, lakini yanaonekana kutojaliwa na mwajiri wao ambaye ni serikali

Inasikitisha walimu wanapodharauliwa huku Serikali hiyo hiyo ikiongeza jitihada za kujenga shule kila kata. Shule hizo zitahitaji walimu, Je ni walimu gani mnaowahitaji huku hamuwajali? Ni elimu gani tunayoitaka huku chanzo cha elimu bora tukikidharau?

Fani ya ualimu imekuwa ni ya kudharauliwa siyo na serikali tu bali na jamii kwa ujumla na hii ni kwa sababu tu serikali haioneshi mshikamano wowote na walimu hao wala kusikiliza malalamiko yao. Hapo hapo wanafunzi wakifeli mitihani yao watu wa kwanza kuwalaumu ni walimu. Je walimu hao watafundisha bila kuwezeshwa?

Elimu bora itabaki kama ndoto kila siku katika maisha yetu kama hatutowajali walimu hawa. Kama serikali itaendelea kutotoa ushirikiano wowote basi wanafunzi ambao ndio serikali ya kesho itaathirika, Tutapata wapi viongozi bora? Walimu wawe ni watu wa kuthaminiwa.

Chanzo: Barua toka kwa Ra�ki wa Elimu

§Iulize Kamati ya Shule yako na Mwalimu Mkuu kuhusu bajeti ya shule.

Mapato ya shule ni kiasi gani? Mapato yalitumikaje mwaka uliopita? Mwaka huu je? Salio ni kiasi gani? Litatumika vipi? Taarifa za mapato na matumizi zimeandikwa vipi? Jamii yako itapataje taarifa hizo? Kama Rafiki wa Elimu huna haja ya kuwa na kitambulisho kwa ajili ya kutembelea shule au kuongea na kamati ya shule. Kumbuka kuwa kupata taarifa ni haki ya msingi ya kila binadamu hivyo tumia haki hiyo.

Page 17: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 13

§Wasiliana na mashirika yanayojishughulisha na elimu katika eneo lako. Je, kuna Asasi Zisizo za Kiserikali (AZISE) au mashirika mengine yanayoshughulikia elimu katika eneo lako? Uliza wanafanya nini. Kwa kukutana mnaweza kupata nafasi ya kujifunza na kusaidiana. Mnaweza pia kuibua masuala muhimu na kutafuta jinsi ya kuboresha elimu kwa pamoja.

§Andika baruaKwa watu unaopenda wapate ujumbe wako. Wanaweza kuwa Mwalimu Mkuu, Mratibu wa Elimu, Afisa Elimu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya au Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Unaweza pia kumwandikia Rais wa Nchi. Rais amefungua Idara ya Mawasiliano kupokea maoni ya wananchi: andika SLP 9120 Dar es Salaam, barua pepe [email protected], Simu (022) 2116913. Waeleze unafikiri nini kuhusu elimu katika jumuiya yako.

§Omba machapisho Kutoka serikalini na AZISE uyasambaze katika jumuiya yako. Katika kitabu hiki zipo baadhi tu ya anwani za mashirika kwa ajili ya kukusaidia wewe kupata taarifa utakazohitaji. Unapotaka kuwasiliana na mashirika hayo unaweza kuandika anwani yao moja kwa moja bila kupitia HakiElimu. Kwa njia hiyo utapata majibu kwa haraka zaidi.

§Waulize wanafunzi kuhusu shule yao. Nini uzoefu wao? Ni matatizo yapi yanayowakabili? Ni mambo yapi wanayoyapenda kuhusu shule? Ni yapi wangependa yabadilike? Sikiliza maoni yao uone jinsi utakavyowasaidia. Saidia kuwasilisha maoni yao kwa watu walio katika nafasi ya kufanya maamuzi.

Tunawashauri Marafiki wa Elimu kuunda vikundi vya majadiliano kujadili kuhusu namna ya kuboresha elimu katika jamii. Marafiki wanaweza pia kuunda mtandao wa mawasiliano kwa njia ya tovuti yaani kuwa na anwani pepe ambayo kila Rafiki anaweza kufungua na kupata ujumbe kutoka kwa Marafiki wengine.

Page 18: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu14

Kama una mifano mingine tafadhali jadili na Marafiki wa Elimu wengine na pia HakiElimu.

Mara�ki wa Elimu Dodoma (MED) washirikiana na Asasi ya Oxfam kuimarisha mabaraza ya wanafunzi shuleni DodomaKikundi cha Marafiki Dodoma kimeweka mikakati ya kuhakikisha shule katika manispaa ya Dodoma zinaanzisha mabaraza ya wanafunzi ili kuimarisha demokrasia na ushiriki wa wanafunzi katika maamuzi ngazi ya shule. Kwa kushirikiana na Asasi ya Oxfam GB kikundi kimefanikiwa kuanzisha mabaraza katika shule 4 za sekondari na 2 za msingi.

Aidha, kikundi kimepata ufadhili kutoka Asasi ya Oxfam wa kiasi cha paundi 36,000 za Uingereza kuweza kuendesha shughuli zake. Hivi karibuni kimepokea vitabu vya thamani ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya kusambaza katika shule za msingi wilayani Chamwino.

Mahusiano na Asasi au wadau mengine husaidia kuongeza kasi ya kuleta mabadiliko kama walivyofanya Marafiki hawa wa Dodoma.

Majukumu ya HakiElimu ni yapi?

HakiElimu ni mraghabishi tu wa Harakati za Marafiki wa Elimu. Hiyo maana yake ni kuwa sisi si viongozi ambao mtawajibika kwetu. Badala yake tutakuwa tukitoa msaada ili muweze kushiriki kikamilifu katika michakato ya kuboresha elimu kwa njia ambazo mnaamini na sisi pia tunaamini kuwa ni muhimu. Jukumu la HakiElimu ni kuhamasisha, kusisimua na kufikiria hatua mbalimbali ambazo Rafiki anaweza kuchukua ili kuleta mabadiliko katika elimu na demokrasia. Ni juu yako kuamua jinsi utakavyoboresha elimu katika jumuiya yako. Nguvu ya harakati inategemea watu binafsi na vikundi vyao na siyo matendo na shughuli za waraghabishi! Ongoza, HakiElimu tutakuunga mkono.

Baadhi ya Viongozi wa Mabaraza ya Wanafunzi Dodoma

Page 19: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 15

Tutatekeleza hayo kwa:

§Kukutumia kila toleo la jarida la SautiElimuSautiElimu huchapishwa mara mbili kwa mwaka. Jarida lina mpangilio unaosomeka kwa urahisi. SautiElimu imesanifiwa kuvuta hisia za msomaji. Kila toleo litakuwa na mada tofauti inayohusiana na elimu na demokrasia. Kuna sehemu ya barua ambapo unaweza kutoa maoni yako na nyingine ambayo itaelezea shughuli za Harakati za Marafiki wa Elimu. Tunakukaribisha kutoa michango kwa njia ya makala, picha na michoro. Pia tueleze jinsi ya kuboresha gazeti hilo.

§Kutunza orodha ya washiriki wa harakati na anwani zaoTutakuwa na orodha ya Marafiki wa Elimu na anwani zao. Orodha hiyo itatumika kwa ajili ya mawasiliano ya wanaharakati wote. Hata hivyo, usitutegemee sisi pekee kufanya mawasiliano! Kama utapenda kuchangia mawazo yako na wengine tujulishe na tutakupatia anwani za washiriki katika mkoa wako, wilaya, mji au kijiji kilichopo karibu nawe. Ikiwa anwani yako imebadilika tafadhali tujulishe ili tuweze pia kuibadilisha katika kumbukumbu zetu.

§Kuchangia maoni na kero zakoJe, ungependa kuboreshaje elimu? Nini mapendekezo yako katika kuleta mabadiliko? Ni kero zipi ungependa kujadili na wenzio? Usibaki nazo mwenyewe. Ongea na wengine katika jumuiya yako. Tuma maoni na kero zako moja kwa moja kwa vyombo vya habari.

Tunaweza pia kukusaidia kuchangia maoni yako kwa mapana zaidi na Marafiki wa Elimu wengine, mashirika mengine yanayojali masuala ya elimu, Serikali na watunga sera za elimu, au kukuunganisha nao moja kwa moja.

 

 

Page 20: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu16

Tunaweza pia kukuunganisha na vyombo vya habari ili uweze kuandika habari kuhusu shughuli mnazofanya. Tunaweza kufanya hivyo kwa njia tofauti. Tunaweza kukuunganisha na mwandishi wa habari au unaweza kuandika barua na tukaituma kwenye magazeti mbalimbali kwa niaba yako. Ikiwa umewasiliana na vyombo vya habari kama vile kuandika barua katika magazeti tafadhali tujulishe. Pia tutumie nakala ya barua uliyotuma pamoja na nakala ya kipande cha gazeti lililoichapisha barua hiyo ili tuweze kuwashirikisha Marafiki wengine.

Usiishie kutuambia sisi tu! Jadili na washiriki wengine wa Harakati za Marafiki wa Elimu na jumuiya yenu!

§Kukupa taarifa kuhusu masuala ya ElimuJe, ungependa kufahamu sera ya Serikali kuhusu elimu ya msingi au sekondari? Tutajitahidi kukusaidia.

Tunaweza kukutumia nakala za sera husika, mipango na nyaraka za Serikali. Tunaweza kukutumia nakala za habari za magazetini kuhusu masuala ya elimu na matukio maalum. Wakati mwingine tunaweza kukupa taarifa za mikutano muhimu ya elimu.

Tunaweza pia kukupa taarifa za matukioyahusuyo elimu yanayotokea kupitia jarida la SautiElimu na kwa njia ya barua.

Kama kuna mambo muhimu ambayo tumesahau tujulishe! Tuambie pia ni njia zipi tunazoweza kutumia ili kubadilishana habari vyema! Tuko hapa kwa ajili yako!

Dhumuni lamachapisho hayoni kuchocheamidahalo namajadilianokuhusu elimuna demokrasia.

Page 21: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 17

§Kukupa machapisho yetu na taarifa nyingineHakiElimu inachapisha vitabu na taarifa nyingine kwa ajili ya jumuiya, shule, wasomi, taasisi za maendeleo na jamii kwa ujumla. Lengo la machapisho hayo ni kuchochea midahalo na majadiliano kuhusu elimu na demokrasia.

Kama Marafiki wa Elimu, mnaweza kutumia machapisho hayo kujielimisha na kuibua majadiliano katika jumuiya yenu.

Kama Rafiki wa Elimu utapata baadhi ya machapisho katika kifungashi cha habari. Kama utapenda kuwashawishi wengine kupata machapisho au kusambaza nakala zaidi wewe mwenyewe soma kipengele kinachofuata. Ili kupata machapisho mengine tuliyonayo wasiliana nasi kwa anwani iliyoandikwa hapo chini.

HakiElimu haina utaratibu wa kutumia mawakala katika usambazaji wa machapisho. Mtu yeyote anaweza kusambaza machapisho kwa ridhaa yake mwenyewe. Vilevile hatutoi usafiri wala malipo yoyote kwa ajili ya usambazaji.

Jinsi ya kupata machapisho ya HakiElimu

Watu binafsi wanaweza kuomba nakala moja yakila chapisho bure.

Idadi ndogo ya ziada pia inaweza kutolewa bure. Hata hivyo, utahitajika kutoa maelezo ya sababu za kutaka machapisho ya ziada na namna utakavyoyatumia.

Mashirika yanaweza kuomba nakala tatu za kila chapisho bure.

Maombi kwa ajili ya nakala za ziada yaambatane na maelezo ya kina kuhusu sababu za kuomba na kueleza yatatumikaje.

Page 22: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu18

Kwa mashirika ambayo yanaweza kumudu gharama yataombwa kufidia gharama za posta, matayarisho na uchapishaji. Wakati mwingine, gharama hizo zinaweza kuondolewa kulingana na uwezo wa kifedha wa mashirika yenyewe. Mashirika yatakayoomba kupunguziwa gharama yatatakiwa kutoa maelezo ya kwanini wasilipie.

Machapisho mengine ya HakiElimu yanaweza pia kupatikana katika tovuti www.hakielimu.org bila gharama yoyote.9

Kwa maelezo zaidi tuandikie:

Machapisho HakiElimuSLP 79401, Dar es SalaamSimu (022) 2151852 / 3

Faksi (022) 2152449Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.hakielimu.org

HakiElimu imetengeneza tovuti kutoa taarifa kuhusu shughuli mbalimbali na kukupa nafasi ya kutoa maoni yako juu ya masuala ya elimu. Kuna ukurasa maalum kwa ajili ya taarifa za Marafiki wa Elimu. Ukiwa unaweza kupata mtandao wa intaneti (internet) soma maelezo zaidi sasa! Iwapo utapenda tuchapishe habari kuhusu shughuli zenu tujulishe na tutaangalia uwezekano.

Ni yapi tusiyoweza kufanya.

HakiElimu ipo kwa ajili ya kusaidia juhudi zako kwa kadri ya uwezo wetu. Lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya. Ni vyema kuyaweka wazi kuanzia awali.

Page 23: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 19

Hatuwezi:§Kulipia karo ya shule, kununua sare, vitabu, kutoa usafiri, wala kudhamini

gharama zozote za mwanafunzi§Kulipia gharama za mafunzo kwa walimu§Kusaidia ujenzi wa shule wala ukarabati§Kulipia posho au gharama nyingine za mikutano, semina au warsha

mtakayoamua kufanya katika jumuiya yenu§Kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya watu binafsi, kikundi cha Marafiki au

mashirika§Kutoa vitambulisho kwa Marafiki wa Elimu§Kufungua matawi mikoani. Hii ni kwa sababu HakiElimu ni shirika

dogo na haliwezi kuifikia nchi nzima kwa njia hiyo. Shirika linachofanya ni kuwawezesha watu kuleta mabadiliko pale walipo kwa kuwatumia machapisho yenye habari mbalimbali za elimu na kuwaunganisha Marafiki wa Elimu na mashirika mbalimbali hapa nchini ili kupata habari zaidi. Pia HakiElimu inatumia redio na televisheni kupeleka ujumbe ambao unawafikia wananchi karibu nchi nzima kwa mara moja.

§Kuendesha warsha au semina kama njia kuu ya kuleta mabadiliko. Zipo njia nyingine bora za kuleta maendeleo. HakiElimu inazingatia zaidi upashanaji wa habari na midahalo ya umma iliyo wazi na ambayo huweza kufanyika mahali popote ikishirikisha watu wengi zaidi kutoa maoni.

Haki na wajibu wa Ra�ki wa Elimu

Kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila raia ana haki ya kupata au kutoa taarifa ili mradi asivunje sheria

§Rafiki wa Elimu ana haki ya kuitisha mikutano na kujadiliana katika vikundi ili mradi majadiliano hayo yasiende kinyume na sheria za nchi.

§Rafiki wa Elimu kama mwananchi mwingine yeyote ana haki ya kuchaguliwa katika kamati ya shule kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Pia ana haki ya kushiriki katika mikutano kama vile mikutano ya kijiji au mitaa. Katika mikutano hiyo Rafiki ana haki ya kuuliza maswali na kupata majibu kwa niaba yake mwenyewe na si kwa niaba ya HakiElimu.

Page 24: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu20

§Rafiki ana haki ya kuunda kikundi na kuomba usajili wa kikundi hicho kwa kutumia nembo ya Marafiki wa Elimu. Marafiki watakaopenda kusajili vikundi vyao wanaweza kupata ushauri kutoka HakiElimu au taasisi iliyo karibu nao kuhusu namna ya kuomba usajili.

§Rafiki wa Elimu atakayependa kupata taarifa kuhusu maendeleo ya elimu katika jamii yake anaweza kufanya hivyo kwa kufuata taratibu zilizowekwa. Kwa mfano Rafiki anaweza kuonana na kamati ya shule kwa kufuata taratibu zilizowekwa na shule husika bila kuingilia ratiba ya masomo.

§Ni wajibu wa Rafiki wa Elimu kujenga uhusiano mzuri na kutumia kauli nzuri katika mawasiliano na uongozi wa shule, kijiji/mtaa na ngazi nyingine mbalimbali, pamoja na wananchi wengine.

§Ni wajibu wa Rafiki wa Elimu kufahamu ngazi za uongozi na kuwa na taarifa za kutosha kuhusu kamati ya shule, kijiji na kamati ya maendeleo ya kata, wilaya na hata taifa.

§Rafiki ana wajibu wa kuzifahamu na kufuata sheria za nchi na hapaswi kufanya shughuli yoyote kinyume cha sheria za nchi. Ikiwa ataenda kinyume cha sheria za nchi anaweza kupata matatizo na hata kushitakiwa kisheria.

Darasa likiwa limesheheni watoto katika shule ya Msingi Mtendeni Tabora

Page 25: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 21

Uhusiano kati ya Ra�ki wa Elimu na HakiElimu ukoje?

Marafiki wa Elimu ni Harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuona haki ya kupata elimu bora inakuwepo Tanzania. Shughuli za harakati zitafanywa na Marafiki. HakiElimu ni mraghabishi tu. Tutakupa taarifa mbalimbali, lakini mtendaji mkuu ni wewe Rafiki.

Ukiwa katika harakati za Marafiki wa Elimu ni muhimu kukumbuka kwamba wewe si mwanachama wala mwakilishi wa HakiElimu. Hii ina maana kwamba madai au matamshi utakayotoa yanawakilisha maoni yako binafsi na si ya HakiElimu. Hii haimaanishi kwamba hatutakubaliana nawe, pengine mara nyingi tutakubaliana! Kumbuka kuwa wewe ni ‘ Rafiki wa Elimu’. Si sahihi kusema wewe ni ‘mwanachama wa HakiElimu’ wala ‘ Rafiki wa HakiElimu’. Bali ni sahihi kusema wewe ni ‘ Rafiki wa Elimu’ au mwanaharakati katika Harakati za Marafiki wa Elimu. Rafiki wa Elimu anaweza kuwa Rafiki wa HakiElimu kwa kuzingatia mantiki ya mahusiano ya kazi tunazofanya bila kuondoa maana halisi ya dhana nzima ya Rafiki wa Elimu.

Watu binafsi, vikundi na wengine watakaojiunga na Harakati za Marafiki wa Elimu watawajibika kwa shughuli zao. Matendo yao yatafanyika kwa niaba yao wenyewe na si kwa namna yoyote au wakati wowote kwa niaba ya HakiElimu.

HakiElimu haitawajibika kisheria kwa namna yoyote kutokana na vitendo vya Marafiki wa Elimu watakaodai kufanya kazi kwa niaba ya HakiElimu.11

Mara�ki wa Elimu ni watu wanaojali na wenye nia ya kuona haki ya kupata elimu bora inakuwepoTanzania. Kama ilivyobainishwa awali, HakiElimu ni Mraghabishi tu wa harakati hizi.

Page 26: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu22

Orodha ya vyombo vya habari

Tumeorodhesha anuani mbalimbali za vyombo vya habari tukiamini kuwa wewe kama Rafiki wa Elimu utakuwa na kero, changamoto na maoni mbalimbali ambayo ungependa yatoke kwenye vyombo vya habari. Ikiwa una anuani za vyombo vya habari vingine ambavyo unadhani ungependa wengine wavifahamu, tafadhali tujulishe.

Chombo cha habari Namba ya faksi Namba ya simu Sanduku la Posta

BBC, Dsm 2127911 2127911/5 79545 DSMBusiness Times 2150987; 2115025 2118378/9 71439 DSMChangamoto 2126502 2126602 12137 DSMClouds FM 2124649 2123919 31513 DSMDaily News 2135239/2112881 2116074; 2110595 9033 DSMDTV/CTN/Channel 10

2113112 2116342 19045 DSM

East Africa Radio 2775915 2775916 21122 DSMGlobal Publishers Limited

2773356 2773357 7534 DSM

HabariLeo 2135239/2112881 2110595/2123063/2127491/3

9033 DSM

Ikulu 2113425 2116913 9120 DSMITV / Radio One 2775915 2775916 31042 DSMJamboLeo 2137684 2137681 3209 DSMIdara ya Habari Maelezo

2113814 2122771 9142 DSM

Majira 2115025 2118377/9 71439 DSMMtanzania 2460030; 2123186 2461459; 2460029 78235 DSMMwanaHalisi 2760560 2760560 67311 DSMMwananchi 2450881; 2450886;

24508732450875-6/8 19754 DSM

Nipashe 2700146 2700735/7 31042 DSM

Page 27: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 23

Radio Mlimani 2700239 2700236 4067 DSMRadio Uhuru 2182369 2181700 9221 DSMRai 2460030; 2123186 2461459; 2460029 78235 DSMRaia Mwema 2401311 2401310 8560 DSMRTD 2865577 2860760/5;

2865564;749191 DSM

Sauti Huru 21610 DSMStar TV/Radio Free Africa

028-2500713; 2136834;2666681

028-2503262; 21368342666834

1732 Mwanza; 6404 DSM

Taifa Tanzania 0789-050051; 715-424741

13412 DSM

Tanzania Daima 2126234 2126232 15261 DSM�e African 2460030; 2123186 2461459; 2460029 78235 DSM�e East African 2115566 2119657/8 8101 DSM�e Citizen 2450881; 2450886;

24508732450875-6/8 19754 DSM

�e Express 2182659 2182665 20588 DSM�e Guardian 2773582 2700735/7 31042 DSMTBC 2700011 2700466;

2700062,3231519 DSM

Victoria FM 028-2622944 028-2622091; 0755-205875

942 MUSOMA

Voice of Tabora 0773-361371; 0733-361371

84 TABORA

Wapo Radio FM 2851265 2851265 76837 DSM

Chombo cha habari Namba ya faksi Namba ya simu Sanduku la Posta

Page 28: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu24

Orodha ya Asasi Barua pepe Namba ya simu

Sanduku la Posta

ActioAid [email protected] +255222700596 21496 DSMAide et Action Aea.dar@aide-et-

action.or.tz+255222760018 76339 DSM

Children’s Book Project

+255222760750 78245 DSM

Legal and HumanRights Centre

[email protected]

+255222118354 75254 DSM

Mwalimu NyerereFoundation

[email protected]

+255222772718 71000 DSM

Oxfam GM [email protected] +255222772718 10962 DSMPlan International Tanzania.co@plan-

international.org+255222601576 3517 DSM

Mwanza Policy Initiative

2472 MWZ

Farm Africa [email protected]

+255272548042 15335 ARS

HakiKazi Catalyst [email protected]

+255272509860 781 ARS

Maarifa ni Ufunguo Action for Democracy and Local Governance (ADLG)

[email protected] +255272500298 15102 ARS

Chrisiatn Council of Tanzania

+255754388882 1631 MWZ

Forum Syd +255714414940 1454 DomKaribu Tanzania +255282501228 11850

MWZKilimanjaro Education Network

[email protected] +255754999115 10069 Moshi

Page 29: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 25

Policy Forum [email protected] +255222780200 38486 DSMTGNP [email protected] +255222443450 8921 DSMHakiArdhi [email protected] +255222771362 75885 DSM

Orodha ya Asasi Barua pepe Namba ya simu

Sanduku la Posta

Page 30: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Marafiki wa Elimu26

Shule nyingi za msingi, hazina madawati, watoto wanakaa chini na tena kwenye sakafu iliyochimbuka ovyo. Darasa moja wanasoma watoto

zaidi ya mia moja na hamsini, mapaa yanavuja mvua ikinyesha, walimu wanahaha kwa kuhama kuokoa vitabu visilowe, kuta zimepasuka ovyo

kiasi cha kuhatarisha maisha ya watoto wetu. Tundu moja la choo linatumiwa na wanafunzi zaidi ya 70.

Marafiki wa limu tunaweza kuleta mabadiliko katika shule zetu kwa kushirikiana kikamilifu na kamati za shule, wabunge, viongozi wa serikali

za mitaa, wananchi, maafisa elimu pamoja na madiwani.Simama imara; tetea shule yako!

Page 31: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu 27

“Mwaka huu [2012]kumejitokeza malalamiko mengi katikashule za msingi na sekondari kwa wanafunzi kutokujua

kusoma, kuhesabu na kuandika kwa kuwawalikosa msingi mzuri kielimu kuanzia ngazi ya awali na chekechea”

Majira 18/06/2012.

Ra�ki wa Elimu unawezakuhamasisha jamii ili ipeleke watoto elimu ya awali!

Page 32: Kitabu cha Marafiki wa Elimu Handbook.pdf4 Kitabu cha Mara˜ki wa Elimu mojawapo ya kushiriki katika hili ni kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu. Unakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Kitabu cha Mara�ki wa Elimu28

www.facebook.com/hakielimuwww.youtube.com/hakielimutz

www.twitter.com/hakielimu

 Tafakari nasi kuhusu ELIMU

kupitia: