kuwait
TRANSCRIPT
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: [email protected] pepe: [email protected] : www.foreign.go.tzNukushi: 255-22-2116600
20 KIVUKONI FRONT, P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM, Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania kufungua Ubalozi nchini Kuwait
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufungua
Ubalozi nchini Kuwait kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa
fedha wa 2014/2015.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) alipokutana na
Mtukufu Sheikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah, Naibu Waziri Mkuu
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait nchini Kuwait
siku ya Jumanne tarehe 14 Aprili, 2015.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wawili walisifu ushirikiano
uliopo baina ya nchi hizi mbili ambao ni wa kidugu na unalenga
kuwanufaisha wananchi wa nchi hizi.
“Kwa kufungua ofisi za Ubalozi, Kuwait ushirikiano huu wa kidugu
utaongezeka kwenye nyanja zote muhimu na utazaa matunda
yatakayo wanufaisha watu wetu, kwa nchi hizi mbili” alisisitiza
Waziri Membe katika mazungumzo yake na kiongozi huyo.
Kwa upande wa Kuwait, Serikali yao ilifungua ubalozi nchini
Tanzania Februari 2015 na Mhe. Jassem Ibrahim Al Najem kuwa
Balozi wake wa kwanza nchini Tanzania, mwenye makazi yake
Jijini Dar es salaam.
Aidha, kwa sasa Tanzania inawakilishwa nchini Kuwait kupitia
Ubalozi wake uliopo Riyadh, Saudi Arabia.
Katika mkutano huo, Mtukufu Sabah Al-Khalid Al Sabah alisifu
jitihada za Tanzania kwenye kulinda na kuleta amani Barani Afrika
hasusan kwenye maeneo yenye migogoro. Alisema kuwa Serikali
yake itaendelea kushirikiana na Tanzania sio tu kwenye maeneo
muhimu ya maendeleo lakini pia hata kwenye ulinzi wa amani
kwani ndio changamoto kubwa inayoikabili dunia kwa sasa.
Kuhusu misaada Barani Afrika, viongozi hao walijadili suala la
uratibu wa misaada mbalimbali ya Serikali ya Kuwait Barani humo
ambapo waliangalia uwezekano wa kuanzisha kituo maalum
nchini Tanzania kwa ajili ya kusimamia shughuli za uratibu wa
misaada hiyo.
Kwa sasa Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo –
Kuwait Fund- imetoa Dola za Kimarekani Bilioni moja kwenye
Umoja wa Afrika kwa ajili ya usalama wa chakula Barani Afrika.
Awali Waziri Membe alikutana na Mhe. Abdulwahab A. Al-Bader,
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na kumshukuru
kwa misaada mbalimbali ya kimaendeleo wanayoendelea kuitoa
nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Aidha Waziri Membe alielezea kuwa maandalizi ya miradi mitano
ya umwagiliaji nchini Tanzania ambayo inayofadhiliwa na mfuko
huo yamekamilika, na kwamba sasa iko tayari kuanza. Aidha
Waziri Membe na Mhe. Al-Bader walizungumzia uwezekano wa
mfuko huo kuikopesha Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) ili iweze
kuendesha shughuli zake kikamilifu.
Waziri Membe yuko nchini Kuwait kwa ziara ya siku moja na
anatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Oman. Ujumbe wa
Mhe. Membe nchini Kuwait unamjumuisha Bw. Peter Noni,
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Uwekezaji Tanzania, Balozi Simba
Yahya, Mkuregenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Mindi Kasiga,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo
ya Nje.
-Mwisho-
Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam15 Aprili 2015.