leif packalØn na katti ka-batembo · 2012. 12. 17. · mwanamke na sheria mpya ya ardhi. hadithi...

30
Komiki -hadithi kwa njia ya michoro Leif Packalén na Katti Ka-Batembo

Upload: others

Post on 26-Jan-2021

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Komiki -hadithi kwanjia ya michoroLeif Packalén na Katti Ka-Batembo

  • UtanguliziMatumizi ya vielelezo vya michoro katika kuelimisha yamekuwapo kwa mudamrefu na umuhimu wake unafahamika. Michoro au picha hupeleka ujumbe kwaharaka na kueleweka kwa urahisi hata kwa watu ambao uwezo wao wa kusomani mdogo.

    Hivi karibuni matumizi ya michoro yameongezeka zaidi na hasa kwa kutumiahadithi zenye michoro yaani komiki. Hadithi kwa njia ya michoro au komiki zinauwezo mkubwa wa kupeleka ujumbe kwa walengwa kwa kuwa huburudisha nakusisimua na hasa hadithi zenyewe zitkiwa zinahusu walengwa wenyewe. Pia nimuhimu iwapo mchoraji wa hadithi hizi atakuwa anatokana na jamii yenyewekwa kuwa anayafahamu mazingira na mila na desturi za walengwa.

    Komiki zimekuwa zikitumika kwa muda sasa kwa lengo la kuburudisha na hasakatika magazeti ya mzaha kuanzia miaka ya tisini baada ya kuwepo uhuru wamagazeti. Hata hivyo matumizi ya komiki si kwa lengo la kuburudisha tu balizinaweza kutumika kama zana muhimu ya kuelimisha jamii masuala mbalimbalikama vile afya, elimu ya mazingira, uchumi, kilimo na kadhalika.

    Mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO vikundi na taasisi mbalimbali huwa naprogramu za mafunzo katika kueneza ujumbe husika kwa kutumia zanambalimbali. Baadhi ya mashirika hivi sasa yameanza kuona umuhimu wamatumizi ya hadithi za michoro. Hata hivyo si watu wengi wanafahamuumuhimu wa komiki au jinsi ya utayarishaji wa hadithi hizi na hasa kwa kuwazinahusisha michoro wengi huhofia kuwa hawajui kuchora.

    Lengo la kijitabu hiki ni kutoa mwongozo kwa watumishi na wadau mbalimbaliwa mashirika yasiyo ya kiserikali, vikudi vya kijamii na taasisi jinsi yakutayarisha hadithi za michoro yaani komiki na jmatumizi yake kwa lengo lakuelimisha. Huhitaji kuwa mchoraji stadi kutayarisha hadithi hizi balilililomuhimu ni ujumbe utakaowasilishwa na michoro yako.

    Katika kijitabu hiki tutaonyesha baadhi ya michoro iliyotayarishwa na watukutoka mashirika yasiyo ya kiserikali ambao si wachoraji stadi lakiniwameweza kutoa ujumbe wenye kueleweka zaidi kwa njia ya komiki.

    Ni matumaini yetu kuwa kijitabu hiki kitakuwa ni msaada mkubwa kwa woteambaao wamekuwa wakifikiria kuanza kutumia komiki katika kueneza ujumbe.

  • Mpango wa kazi kwa ufupi

    Buni hadithi na kuigawa katikapeneli

    Futa maandishi yasiyo muhimu

    Chora kwa ukamilifu katikakaratasi nzuri na kupiga mistariya peneli

    Piga mistari ya kuandikia nakuandika maandishi

    Chora michoro ya wahusikakatika hadithi kwa kalamu yarisasi

    Malizia kwa kutia wino mweusina kufuta penseli, hadithi ikotayari

    1

  • Peneli ya kwanza:Hii lazima ionesheutangulizi na mahalipa tukio.

    Peneli ya tatu:Hadithi inachukuamwelekeo wenyekuvutia na

    Peneli ya nne: Hadithiinaisha na yote aliyopatamsomaji yanahitimishwa.Msisimuko katika hadithihusaidia msomaji kuelewa

    Jina la mtunzi liwekwehapa, kama mmojaalitunga na mwingineakachora ni lazimamajina yate mawili

    Peneli ya pili:Hapa hadithi

    Kichwa cha habari: Unawezakuweka maelezo kama vilejina la mhusika au madailiyopo katika hadithi

    Komiki: hadithi zinazosimuliwa kwa mfululizo wa michoro

    iv2

  • Hadithi hii inayohusu “ULEVI” ilitungwa na kuchorwa na D. Pongothai kutoka India, inasimuliakisa cha mwanamme aliyekuja na chupa ya pombe nyumbani kwake, baada ya kuinywaanaanza kuvuta sigara huku amelala kitandani na hatimaye kuuguza nyumba. Hadithi yote

    Komiki ni simulizi za taswira

    v3

  • Komiki kimsingi ni taswira

    Katika hadithi hii inayohusu UKIMWIpeneli ya kwanza mwanamke anaonekanakugundua kitu katika mkoba wa mmewake na peneli ya pili mwanamkeanamwonyesha kitu hicho mme wake. Bilakutaja kitu chenyewe msomsji anatambuakuwa ni pakiti ya kondomu kwa kuonamaandishi juu ya hiyo pakiti.

    Mfano kutoka hadithi inayohusu mgawanyo wa kazi kulingana na jinsia; Wanaume wanaaonekanawakinywa pombe na kupiga gumzo wakati mama anaandaa chakula cha jioni na kulea watotobaadaya kazi zote za mchana.

    Hapa mtu anayeshukiwa kwa wizi wa kuku anaonekanaa anakimbia na kuku amemshikamkononi. Mama aliyeibiwa kuku wake anaomba msaada na mtu mmoja mwenye nguvuanajiandaa kumdhibiti mtuhumiwa.

    Komiki lazima zitumie lugha ya vitendo, nyuso na taswira kwa ajili ya kutoa mvuto navionjo vingine katika hadithi ili kufikisha ujumbe kadiri iwezekanavyo. kanuni ni:Simulia kwa kuonesha.

    4

  • Komiki husomwa kutoka kushoto kwenda kulia.Msururu mmoja wa peneli huitwa (strip) mfululizo

    Komiki inapochapiswa katika sehemundogo yenye msururu wa mfululizo wapeneli, msururu wa juu ndio husomwakwanza.

    Utaratibu ni kwamba usomaji huanziakushoto na kuelekea kulia kisha juuhalafu nchini.

    Utaratibu wa usomaji ndani ya peneli moja ni huo huo kwanza husomwa kutoka kushoto kwenda kuliana kama hii haiwezekani basi yaweza kuwa kutoka juu kwenda chini.

    Kwa lugha kama Kiarabu ambapo usomaji huanzia kulia kwenda kushoto basi na komiki hufuatautaratibu wa maandishi.

    Mpango wa usomaji

    5

  • Katika peneli hii kilakitu kinaonekana,sura ya kijiji, jengo lakiliniki, daktari na

    Katika peneli hii watuwanaonekana kwa ukamilifu.Bango, daktari na manesivinatujulisha kuwa hapa ni

    Katika peneli hii robo tatutu ya urefu waoinaonekana. Mtu wamwisho haonekani vizuri.

    Shingoni na uso tu. Kwamchoro huu unaweza kuoneshasehemu za uso vizuri na hisia

    Sehemu ya juu yawahusika tundiyo inayoonekana. Hapasura ya eneo walilopo

    Sehemu ya juu ya mtummoja tu ndioinayoonekana. Msisitizohapa ni mtu anayeonekanatu ndiye anayeongea.

    Michoro katika peneli

    6

  • Kuchora uso kwa kutumia maumbo mbalimbaliJapokuwa watu wana sura tofauti lakini sura aina mbalimbali zinawezakuchorwa kutokana na umbo aina moja kwa kutofautisha macho, nywele, pua nk.Hapa kuna mifano michache jinsi ya kutofautisha uso wa msichana na mvulana

    Hatua ya Hatua ya

    Hatua ya Hatua ya

    Hatua ya Hatua ya

    Hatua ya Hatua ya

    7

  • Mifano zaidi ya kuchora sura mbalimbali kwa kutumia umbo moja la mviringo.

    8

  • Sura pia zinaweza kuchukua maumbo tofauti. Hii hapa mifano zaidi ya kuchora surambalimbali kwa kutumia umbo la yai, embe na kibuyu.

    Hatua ya -1 Hatua ya -2

    Sura mbili tofauti zilizochorwakutokana na umbo la yai. Katikasura ya pili yai limegeuzwa juu

    Sura ya kijana kutokana naumbo la embe.

    Sura ya mwanamke mnenekutokana na umbo la yai.

    Sura ya mwanamme mwenyendevu nyingi na kibandikokutokana na umbo la kibuyu.

    Hatua ya -1

    Hatua ya -1

    Hatua ya -1

    Hatua ya -1

    Hatua ya -2

    Hatua ya -2

    Hatua ya -2

    Hatua ya -2

    9

  • Kuchora mtu kwa kutumia maumbo njitiIli kuchora umbo kamili la binadamu njia rahisi ni kuanza na umbo njiti. Hii hurahisishakukadiria kimo na mkao wa mtu unayetaka kuchora kulingana na kitendoanachofanya.

    Kimo halisi cha mtu mzima huwamara saba ya urefu wa kichwa.Kimo cha mtoto mkubwa kiasi nimara tano ya urefu wa kichwachake. Na urefu wa mtotomdogo anayeaanza kutembea nimara tatu ya kichwa chake.

    Michoro njiti katika mkao na vitendo mbalimbali

    Kwa kuangalia michoro hii ya njiti unaweza kujua ni kitendo gani kinafanyika

    10

  • Kubadili umbo njiti kuwa umbo kamiliHatua inayofuatia baada kuchora umbo njiti ni kulipa umbile kamili kwa kuchora mstarikufuatia umbo hilo.

    Hatua ya -1

    Hatua ya -1

    Hatua ya -1 Hatua ya -2

    Hatua ya -2

    Hatua ya -2

    11

  • Hisia za mhusika katika hadithi lazima zionekane kutoka usoni, Maelezo ya nyuso yanawezakutofautishwa kwa kubadilisha mdomo, macho na nyuso, hii hapa mifano michache.

    Uso wenye tabasamu

    Uso wenye furaha

    Uso wenye kiburi Uso wenye hofu

    Uso wa mlevi Uso wenye kufikiria

    Uso wenye shaka

    Uso wenye aibu

    Uso wenye mshangao

    Uso wenye huzuni Uso wenye hasira

    Uso uliochoka

    Maelezo ya nyuso

    12

  • MAANDISHI MAZUNGUMZO

    U F U N G U Z I

    Kwanza pigamistari, Kishaandika maandishikwa penseli.

    Kisha chora puto(baloon) na kuoneshakuzunguuka maandishiukiacha nafasi yakutosha kutoka puto

    Halafu andikamaandishi kwawino na kumaliziana mistari ya puto.

    Futa penseli.Sasa kazi ni safina yenyekusomeka.

    Mkono (pointer)unaweza kuwa mrefukadri inavyohitajika.

    Puto linaweza kuwa naumbo kulingana namuundo wa maneno.

    Maneno yenye msisitizoyaandikwe kwa wino mzito.

    Maputo yanaweza kuwa na umbo lolote muhimuyasibane maandishi na mkono wake uelekeze kwayule, anayeongea au anaefikiria.

    Maelezo ya utangilizi lazima yawe ya kwanzakusomwa. Hii ina maana ni bora kuyawekakwenye kona ya juu ya kushoto katika peneli,kisanduku cha maneno mara nyingi ni chamstatili

    Maandishi

    Mkono wa puto lenye manenoya kufikiria huchorwa kwamiviringo midogomidogo.

    13

  • Chora mistari yote kwakalamu ya wino mweusi.

    Futa alama zote za penseli.

    Jaza wino mweusi sehemuzinazohitajika kwa kalamu

    Ukipenda weka mapambozaidi pale panapostahili

    Tumia wino mweusi tu! Kama utatumia rangi ya kijivu au hafifu mchoro hautapendezaukipigwa fotokopi.

    Kwanza chora kwa penselinyepesi kisha mistari yakuandikia, mwisho andikaherufi.

    1 2 3

    4 5

    Kutia wino

    14

  • Mwendo na sauti ya kudunda Mwendo wa kasi. Angalia gari liko juu namagurudumu yanaonekana yakiwa umbo la yai hukuyamelalia mbele.

    Mkono ukipunga taratibu.Sauti ya gari baada kupiga breki angalia bodi la gari

    Maumivu yanaweza kuoneshwa kwa kuvimbishana kuweka alama za mistari midogo midogo nanyota zikinururika kutoka sehenmu iliyoumia.

    Mzunguko wa feni huoneshwa kwamistari kuizunguka.

    Sauti ya muziki huoneshwa kwa kuchoraalama za muziki na mistari ikichomozakutoka redioni.

    Mistari ya mawimbi huoneshaharufu.

    Sauti, mwendo, harufu, n.k.Unapohitaji kuashiria sauti, mwendo au mtingisiko, harufu n.k.unaweza kutumia ainatofauti ya alama katika mchoro. Alama hizi lazima ziwe rahisi kuelezeka kwa msomaji.Hivyo ukichora kitu kipya jaribu kuonesha kwa rafiki zako wachache kwanza kuonakama kinaeleweka, Hapa kuna mifano michache.

    15

  • Wazo la komiki za mabango ya ukutani ni kuunganishwa karatasi mbili za A4 ilikupatabango moja dogo. Pande zote mbili zenye muundo na vipimo namna mojahuunganishwa huku peneli za juu na chini zikitazamana, Hii inakupa muundo wa bangokama ilivyo hapa chini.

    Vipande vyote viwili viunganishwe kwa gundi vikipishana kwa vipimo vya milimita 5-10.

    Kama una mashine ya fotokopi yenye kutoa karatasi wa A3 unawezakutengeza bango lenye ukubwa wa A2 kwa kutumia vizuri (miraba )kama ilivyo katika mfano wa A4 hapo juu, ikikuzwa kwa asilimia 140mara mbili.

    vipimo:

    Hadithi za komiki za ukutani

    16

  • Katika hadithi ya bango la ukutani kuna nafasi urefu wa sentimita 4 juu na chini ya peneli, katikasehemu ya juu unaweza kuandika kichwa cha habari na hata nembo. Katika sehemu ya chiniyanaweza kuwekwa maelezo zaidi kuhusu shirika linalotumia mabango kama vile anuani, n.k.Unaweza kuitumia nafasi hiyo pia kwa kuweka kauli mbiu.

    Mfululizo hapa chini umeundwa kwa kufuata michoro ya bango iliyopunguzwa kwa asilimia 50. Hii ninjia nyingine ya kuiweka hadithi ileile katika chapisho kama vile kipeperushi.

    N e m b o

    maelezoyamchapishaji

    jina lamtayarishajii

    Kichwa chahabari

    Imetolewa na.......S.L.P. Dar es Salaam

    17

  • Mifano ifuatayo ni hadithi za komiki zinazoweza kutumika kama mabango ya ukutani.Komiki hizi zilitayarishwa na washiriki wa warsha ya uchoraji kwa watumishi wamashirika yasiyo ya kiserikali iliyoandaliwa na World Comics Finland kwa ushirikiano naT A N G O

    Hadithi kuhusu haki ya mirathi iliyotungwa na kuchorwa na Bi Naomi Makota kutoka Shirika la WomenAdvancement Trust lililopo Dar es Salaam.

    18

  • Mwanamke na Sheria mpya ya ardhi. Hadithi hii imetungwa na kuchorwa na Bi Grace Daffa kutokaWomen’s Legal Aid Centre (WLAC), Dar es Salaam.

    19

  • 1. Chagua ukubwa wa peneli kwa ajili ya hadithi yako, Eneo katika A4 ni milimita 148 kwa 105mm kama utaacha nafasi ya milimita 10 kila upande, ukubwa wa peneli zako utakuwa milimita139 x 85. Hapa kuna mifano michache jinsi nafasi hizi zinavyoweza kutumika.

    Huu ni ukubwa wa mwisho, unakupanafasi nzuri kuweka puto upande wajuu wa peneli.

    Peneli hii ni ndogo kidogo na inawezakutumika pale unapohitaji kuwekamaelezo kwa chini .

    Jinsi ya kutumianafasi ya ukurasa.

    Katika ukurasa wakwanza jina la hadithilazima litokee.

    Inashauriwa kila marakutumia sehemu ya juukwa kuweka maneno yamazungumzo

    Kutengeneza kijitabu cha kurasa 8

    20

  • 1.Ukubwa sahihi wa peneli2.Ukubwa uliokuzwa kwa asilimia141% (A4-A3

    2.Vipimo vya peneli: Iwapounataka kuchora katika karatasikubwa kumbuka kuwa na vipimosahihi . (A4 kwenda A3 ni asilimia70%), hivyo ukichora katikaukubwa wa milimita 119 x 183unatakiwa upunguze kwa aslimia70% kabla ya kuunganisha hadithiyako kwa ajili ya kuchapisha.

    3 .Chora hadithi yako

    4.Kata peneli na kuziunganishajuu ya karatasi ya ukubwa wa A4kwa mpango uliooneshwa hapachini.

    Acha nafasi ya milimita 10 kutokakila upande na nafasi ya kati iwemilimita 20.

    5. Rudufu (piga fotokopi) karatasi zote mbili ulizounganishakatika karatasi moja. Hakikisha pande zipo sahihi. Ukishapigafotokopi upande mmoja acha karatasi ipoe kabla hujapigaupande wa pili. Hii husaidia karatasi kutogandamana.

    21

  • 6. Kunja ukurasa namba 1 ukiwa juu naukurasa 8ukiwa pembeni mwake

    7. Kunja tena kiasi ukurasa namba 1peke yake ndio unabaki juu.

    8. Shona kwa mashine kubwa ya stepula katikati

    9. Kata chini kwa kisu ili zifunguke

    Kijitabu chako kiko tayari

    ......au unaweza kutumia mkasi

    22

  • Katika paneli fupi kiasi unaweza kuwekamaelezo au tafsiri ya chini ya peneli kamainahitajika kufanya.

    85mm

    85mm

    85mm

    85mm

    120mm

    64mm

    64mm

    110mm

    Kijitabu chenye kurasa 8 kilichopigwa fotokopina kukunjwa kutoka kurasa ya A4

    Hivi ni vipimo vya paneli vinavyopendekezwa,kama unataka kuacha nafasi ya maelezo aupeneli mbili kila ukurasa, ukubwa usizidimilimita 85 kwa 130, ambapo unatakiwa kuachanafasi ya milimita 10 pembeni mwa karatasi. Hiiinatosha kuachia nafasi wakati wa kupigafotokopi isije kukata mchoro

    23

  • Waweza kutengeneza kijitabukidogo cha kurasa 12 kwa kupigafotokopi pande zote mbili zakaratasi yenye ukubwa wa A4ukiwa na peneli katika mpangokama inavyooneshwa hapa.

    Kisha kata kurasa nakuziunganisha. Zishone kwamashine ya stepula na uzikunje

    Ni kijitabu kwa gharama yakaratasi moja iliyopigwa fotokopipande mbili.

    Vipimo vinaoneshwa katikamchoro huu.

    vipimo:

    kata kurasa

    mbele nyuma

    zishone pamoja ....kunja na kijitabu kiko tayari

    Kutengeneza kijitabu cha kurasa 12

    85 mm

    10 mm

    78 mm

    297 mm

    20 mm

    1 2

    1 0 3

    8 5

    1 2 11

    4 9

    6 7

    24

  • Kijitabu cha mkunjo wa kinanda (kodiani)Kijitabu cha mkunjo wa kinanda hutengenezwa kutoka karatasi ya ukubwa wa A3iliyopigwa fotokopi). Hadithi ni ya peneli 8. Kijitabu hukunjwa kama kinanda chakodiani kutoka karatasi ya A3 iliyogawanywa safu 4 zilizo sawa kila safu ikiwa nahadhithi kamilifu. Chini mfano uliotengenezwa kwa kutumia hadithi iliyochorwa na S.Fransis kutoka shirika la VCDS Tamil Nadu India inayohusu ndoa. Ukubwa wa kijitabuni milimita 74, urefu na upana milimita 52.5

    sehemu ya mchoro iliyokuzwa

    Ukubwa michoro ni kati yamilimita 60-65 na upana nimilimita 38, yatengemea kamaunahitaji kuweka maelezochini ya michoro

    Unaweza kuchora mchoromkubwa na kuupunguzawakati wa kurudufu kwa kuwaukichora ukubwa ulio sawamichoro huwa midogo sana.

    Kijitabu cha kinanda kinafaazaidi kwa kuwa ni kidogo nakinaweza kutumika kwamasuala nyeti

    Maelezo jinsi ya kukunja yapoukurasa ufuatao.

    25

  • Kukunja Kijitabu cha kinanda

    xxviii26

  • 27

  • Mwongozo huu umetolewa na Chama cha Wachoraji Komiki Tanzania kijulikanachokama Tanzania Popular Media Association (TAPOMA) kwa kushirikiana na Chama chaKomiki Finland (World Comics Finland).

    TAPOMA ni chama cha Wachoraji kilichosajiliwa rasmi kama Shirika lisilo la kiserikalitangu mwaka 1994. Madhumuni makuu ya TAPOMA ni kuendeleza matumizi ya hadithiza michoro yaani komiki kama njia ya mawasiliano katika shughuli mbalimbali zamaendeleo. Tangu kuanzishwa kwake TAPOMA imeendesha warsha mbalimbali zawachoraji kwa kushirikiana na vyama vya Finnish Tanzania Friendship Society na WorldComics Finland kwa msaada wa serikali ya Finland.

    Hivi karibuni TAPOMA kwa kushirikiana na World Comics waliendesha warsha yauchoraji wa komiki kwa watumishi na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyowanachama wa TANGO ambao si wachoraji yaani grassroot comics. Baadhi ya kazizilizotokana na warsha hiyo zimeoneshwa kama mfano katika mwongozo huu.

    World Comics Finland ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa nchini Finland nawachoraji wa komiki pamoja na wanaharakati wa misaada ya kujitolea mwaka 1997.Shirika hili hili lina wanachama na washiriki sehemu mbalimbali duniani.

    World Comics huandaa warsha za komiki, kozi, mihadhara, maonesho, n.k. ili kukuzamatumizi ya komiki kama njia ya mawasiliano. Mpaka sasa World Comics ina ushirikianona Tanzania, Msumbiji, Kenya, Morocco, na India. Pia imeshawaalika wasanii kutokaTanzania, Ghana, Nigeria na Cuba katika matamasha mbalimbali huko Finland.

    Tanzania Popular Media Associatiation (TAPOMA)S.L.P. 14894 Dar es Salaambaruapepe: [email protected]

    World Comics-FinlandVanamontie 4 E 156, 03150, Vantaa, Finlandsimu: +358-9-8736751baruapepe: [email protected]: www.worldcomics.fi