mabehewa 25 yakubebea kokoto yanafanya kazi kama kawaida na hayakufichwa!

2
KAMPUNI YA RELI TANZANIA-TRL TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE) Mabehewa 25 yakubebea kokoto yanafanya kazi kama kawaida na hayakufichwa! Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unachukua fursa hii kukanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mabehewa 25 ya kubeba kokoto ( Ballast Hopper Bogies- BHB) yamefichwa na uongozi wa kampuni kwa vile ni mabovu. Taarifa zilizotolewa sio za kweli na zina lengo la kuwapotosha wananchi bila ya sababu zozote za msingi. Aidha jambo linalostaajabisha zaidi ni pale mwandishi mwenye ujuzi mkubwa kitaaluma anaposhindwa kutafiti upande wa pili wa habari husika na badala yake anaamua kuandika taarifa ambayo ni ya upande mmoja na mwishoni kuishia kuupotosha umma. Habari kuhusu mabehewa ya kokoto imetolewa mara kadhaa na baadhi ya vyombo vya habari. Kwa sababu zisizojulikana, kila mara habari hii inapotoshwa na imekuwa haitolewi kwa usahihi na mara nyingi imekuwa ikichanganywa na habari zisizohusiana na mabehewa haya na hivyo kuuchanganya umma. Madhumuni ya taarifa hii ni kufafanua kilichotokea kuhusu mabehewa haya ya kokoto. Mabehewa 25 ya kokoto yaliagizwa na TRL kutoka kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Ltd (HEIL) ya India, kupitia mchakato wa zabuni ya ushindani wa kimataifa (International Competitive Bidding). Mabehewa haya yaliwasili nchini na kupokelewa yote kwa pamoja Julai 24, 2014. 1

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 01-Oct-2015

7.043 views

Category:

Documents


6 download

DESCRIPTION

Mabehewa 25 yakubebea kokoto yanafanya kazi kama kawaida na hayakufichwa!

TRANSCRIPT

KAMPUNI YA RELI TANZANIA-TRL

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

Mabehewa 25 yakubebea kokoto yanafanya kazikama kawaida na hayakufichwa!Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL unachukua fursa hii kukanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mabehewa 25 ya kubeba kokoto ( Ballast Hopper Bogies-BHB) yamefichwa na uongozi wa kampuni kwa vile ni mabovu. Taarifa zilizotolewa sio za kweli na zina lengo la kuwapotosha wananchi bila ya sababu zozote za msingi. Aidha jambo linalostaajabisha zaidi ni pale mwandishi mwenye ujuzi mkubwa kitaaluma anaposhindwa kutafiti upande wa pili wa habari husika na badala yake anaamua kuandika taarifa ambayo ni ya upande mmoja na mwishoni kuishia kuupotosha umma.

Habari kuhusu mabehewa ya kokoto imetolewa mara kadhaa na baadhi ya vyombo vya habari. Kwa sababu zisizojulikana, kila mara habari hii inapotoshwa na imekuwa haitolewi kwa usahihi na mara nyingi imekuwa ikichanganywa na habari zisizohusiana na mabehewa haya na hivyo kuuchanganya umma. Madhumuni ya taarifa hii ni kufafanua kilichotokea kuhusu mabehewa haya ya kokoto. Mabehewa 25 ya kokoto yaliagizwa na TRL kutoka kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Ltd (HEIL) ya India, kupitia mchakato wa zabuni ya ushindani wa kimataifa (International Competitive Bidding). Mabehewa haya yaliwasili nchini na kupokelewa yote kwa pamoja Julai 24, 2014.

Mkataba ulioingiwa kati ya TRL na HEIL una vipengele vinavyotaka mabehewa kufanyiwa majaribio (commissioning) yanapofika Tanzania na kuwepo na muda wa uangalizi (warranty period) wa miezi 24. Vipengele hivi vinamtaka mtengenezaji (HEIL) kurekebisha kasoro zote zitakazojitokeza wakati mabehewa yanafanyiwa majaribo pamoja na zile zitakazojitokeza wakati wa muda wa uangalizi. Marekebisho haya yanatakiwa kufanywa kwa gharama za mtengenezaji (HEIL).Ni kweli kuwa mabehewa haya yalipofika nchini yaliwekwa kwenye utaratibu wa kufanyiwa majaribio kwa kupelekwa stesheni ya TURA, ambako upo mgodi wa kokoto, ili kuyapakia kokoto na kwenda kuzimwaga kwenye njia ya reli. Hata hivyo wakati wa kufungua milango ili kumwaga kokoto zilijitokeza kasoro kwenye baadhi ya mabehewa kwani pini zinazoshikilia milango zilikatika. Baada ya kasoro hizi kujitokeza mabehewa yote yalirudishwa Dare s salaam na HEIL waliarifiwa na kutakiwa kuzirekebisha kasoro hizo pamoja na zingine zilizoonekana wakati wa ukaguzi kama mkataba unavyotaka.Kazi ya kurekebisha kasoro zote zilizoonekana kwenye mabehewa yote 25 imekwishakamilika. Tuandikapo taarifa hii mabehewa yote 25 hayapo tena Dare es Salaam kwani yamepelekwa Tura kwenda kupakia kokoto ili kuzisambaza sehemu mbalimbali za njia ya reli. Hivyo si kweli kwamba mabehewa haya yameondolewa Dar es Salaam kwa nia ya kuyaficha kwani kazi ya mabehewa haya haipo hapa Dar es Salaam bali ni huko yalikopelekwa.

Uongozi wa TRL unawashauri Waandishi wa Habari kutumia fursa ya falsafa yetu ya uongozi wa milango wazi ili kuwasiliana nasi wakati wowote ili muweze kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayowafikia na hatimae muweze kuwapasha wananchi habari zilizofanyiwa utafiti.Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba yaMkurugenzi Mtendaji,

Mhandisi Kipallo KisamfuDar es Salaam Aprili 10, 20151