mafunzo ya ujasiriamali

36

Click here to load reader

Upload: kaka-sule

Post on 16-Apr-2017

17.097 views

Category:

Documents


104 download

TRANSCRIPT

Page 1: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Training of Trainers (TOT)

ISLAMIC HELP TANZANIA

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Page 2: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

MUONGOZO CHINI YA

Page 3: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Mkusanyaji na Mwandishi: SELEMAN ABDALLAH;ISLAMIC HELP TANZANIA- 2012-03-06Email: [email protected], /

[email protected]

Phone: +255689131400 or 0754 371115

Page 4: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• UTANGULIZI• DHANA YA UWEZESHAJI KIUCHUMI• DHANA YA UJASIRIA MALI• Dhana ya ujumla ya ujasiriamali:• Sehemu ya Pili: Mjasiriamali• HAJA YA UJASIRIAMALI: Kwanini tunahitaji kuusoma

Ujasiriamali?• UMUHIMU WA UJASIRIAMALI.• Dhana ya biashara• UISLAMU NA BIASHARA• FAIDA ZA BIASHARA.• ADABU ZA BIASHARA KIISLAMU

Page 5: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA BIASHARA• MPANGO WA BIASHARA NA MRADI• ANDIKO LA MRADI (Project Proposal)• MPANGILIO WA BIASHARA (Business Plan)• MPANGO WA MASOKO (Market Plan)• UTUNZAJI KUMBUKUMBU KATIKA BIASHARA• UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU• UMAKINI KATIKA GHARAMA ZA BIASHARA• CHANGAMOTO ZA BIASHARA.• MBINU ZA BIASHARA• BIASAHARA NA FAMILIA:

Page 6: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

UTANGULIZI

•  Uchumi ni sekta ambayo huchochea kwa namna moja au nyingine maendeleo ya mwanaadamu

• Biashara ni moja ya sehemu kuu ya uchumi na maiongiliano makuu ya uchumi hupatikana kwa kupitia biashara,miradi na kwa ujumla Ujasiriamali.

• Kufanya ujasiriamali ni moja katika njia za kujipatia kipato na jitihada ilizungumzwa na dini

Page 7: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Kujipatia riziki ya halali ni jambo linalomfurahisha sana Mola na hili limedhihirishwa katika hadithi na mafundisho ya mtume (saw), hadithi iliyopokelewa na At-twabaraniy: -

• inayosema “Kutafuta chumo la halali ni Wajibu kwa kila muislamu”

Page 8: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Kwa kuzingatia haya pamoja na uhitaji wa dhana hii kuna changamoto juu ya ufahamu na ujuzi maalumu juu ya Biashara, miradi na ujasiriamali katika ujumla wake.

• Ujasiriamali ni ujuzi kama zilivyo tasnia nyingine, lazima usomwe na kufunzwa kila anayetaka ufanisi wake na matunda yake.

Page 9: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Dhana inayojengeka miongoni mwa jamii kuwa ujasiriamali ni swala la kipaji cha kuzaliwa nacho, kurithi au kujulikana pasi na elimu ni dhana potofu inayowakwamisha wale wanaotaka kuchukua hatua kuufanyia kazi ujasiriamali.

• Mjasirimali mmoja anasema maneno yafuatayo: “Mengi katika usikiayo kuhusu ujasiriamali sio sahihi.

Si uchawi; si mazingaombwe; na hauna lihusianalo na maumbile, ni nidhamu na, kama nidhamu nyingine, Inawezekana kwa kusomwa.” Peter F. Drucker

Page 10: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

DHANA YA UWEZESHAJI KIUCHUMI

• Katika maisha yeyote ya wanaadamu uchumi ni sehemu kubwa ya maisha yao kwa kuwapatia njia na fursa za maisha.

• Dhana hii ni mahimu kufanyiwa jitihada na njia za kuikwamua ili kuleta tija na muonekano wa ubora katika ngazi ya jamii.

• Kujikwamua kiuchumi ni hatua ya kufanya jitihada na michakato mbalimbali ili kuboresha mapato na kuinua ufanisi wa matokeo yanayotazamiwa kutokana na uchumi.

Page 11: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Sehemu kubwa ya ufanisi katika mchakato wa kujikwamua na kujikomboa kichumi unapatika kwa jamii kujihusisha na mpango wa Ujasiriamali.

• Ujasiriamali husaidia kipato cha mwanajamii na kutoa mchango mkubwa katika sehemu au mahali anapopatikana.

Page 12: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

DHANA YA UJASIRIAMALI

Page 13: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Sehemu ya Kwanza: Maana ya Ujasiriamali:

Ujasiriamali:• Ni utekelezaji au utendaji ambao mtu

anapanga, anafanya, anasimamia na kuendesha na kukisia mashaka au hatari kwa kuthubutu kufanya jambo la kiuchumi au kijamii ua biashara.

Page 14: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Maana ya Ujasiriamali• Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili

ambayo ni UJASIRI na MALI. Hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na: -

• Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;

• Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na

• Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.

Page 15: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Ujasiriamali: ni utashi juu ya kufanya kitu; ni njia ya kufikiria, kufikia na kufanya jambo au kitu fulani.

• Ujasiriamali ni mchakato ambapo mtu anachukua hatua kutumia fursa bila kujali hali ya rasilimali alizonazo

Page 16: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

“Ni mchakato ambapo mtu anafanisi, kusimamia, kuandaa na kuratibu ubunifu, uboreshaji na uvumbuzi, kujenga thamani na uthamini unaompa faida au kutoa

manufaa na kuzingatia na kujenga ukuaji na upekee wa tahmani kwa jamii inayomzunguka”

Kuutafsiri Ujasiriamali

Mjasiriamali

UBUNIFU

Kuunda kundi/TaasisiKujenga

Thamani

Kujenga Faida

Kukua

Upekee

MCHAKATO

Page 17: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Sehemu ya Pili: Mjasiriamali

• Mtu ambaye “anathubutu kufanya,” Jambo, vitendo au mradi wenye manufaa”.

• “Aliyechochewa au mwenye vichocheo vya kuendelea kiuchumi kwa kutafuta na kubuni njia mpya za kujikwamua na kufanya mambo”.

• “Mjasiriamali kwa tafsiri ya Drucker, ni ahamishae rasilimali kutoka eneo lenye uzalishaji mdogo na kupeleka katika eneo lenye uzalishaji mkubwa na mavuno (mengi).

Page 18: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

HAJA YA UJASIRIAMALI: Malengo ya Kujifunza: Kuweza kuanzisha na kumiliki kitega

uchumi: Hapa kitega uchumi (enterprise) inamaanisha swala lolote la kiuchumi au kijamii aidha biashara au mradi wa faida.

Kusaka fursa za kijamii: Ujasiriamali unajenga ushawishi wa kuyabadili matatizo kuwa fursa hasa katika jamii.

Page 19: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Malengo ya Kujifunza:

• Uelewa na uhabarisho wakibiashara: Kuelewa biashara katika maono mapana,

• Kuabadili utashi wakimaisha ndani ya kazi na ajira: Hutoa moyo wa utegemezi binafsi/ uhuru kwa kupitia kujijenga uwezo.

• Ajira Binafsi: Kwa kupitia ujasiriamali ni rahisi kupata ajira na kujisimamia mwenyewe.

• Ubora wa maisha: Kuanzisha biashara kunampa fursa muasisi kuwa na baadhi ya uchaguzi juu ya lini, wapi,na nani, na vipi ufanye kazi.

Page 20: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI
Page 21: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Faida za kuwa Majsiriamali

• Husaidia kubadili fikra za vijana, utashi na mtazamo juu ya uzoefu wa jamii au hali ya kazi za jamii kama masoko, maradhi, na maswala ya ajira.

• Husaidia utambuzi binafsi na kukuza akili.• Huchochea kutumia rasilimali kwa

ukamilifu na fursa zinazopatika katika jamii na mzingira yetu.

Page 22: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Faida …….

• Ujasiriamali ni alama ya maendeleo ya miradi na umakini, kujituma na mafanikio katika biashara

• Mapinduzi ya ujasiriamali ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo.

• Ujasiriamali huweza kuathiri hali yetu ya baadae kwa njia nyingi kama: – Kuboresha ubunifu wa fursa : Mafano Simu ndogo

rahisi kubeba zilizounganishwa na faksi na Komputa ndogo aina za Laptop huweza kubadili gari, treni, au mapokezi ya ndege kuwa ofisi.:

Page 23: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Dhana ya biashara-Business• Biashara ni matendo ambayo

humuhusisha mtu katika kununua na kuuza huduma au bidhaa kwa lengo la kupata faida.

• Biashara ni pamoja na hali ya kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalamu, wito na makubaliano ya kipekee yenye lengo la kibiashara kwa nia ya kupata faida.

Page 24: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Mambo ya kuzingatia katika uazishaji wa biashara:

• Katika kuamua aina ya biashara unayotaka kufanya tafadhali zingatia vigezo vifuatavyo,

• Namna ya upatikanaji wa bidhaa hiyo au huduma unayoitarajia kuiuza au kuitoa.

• Idadi ya washindani wanaouza ama kuitoa bidhaa hiyo.

• Matakwa ya wateja katika eneo husika na idadi yao.

• Gharama za uendeshaji wa biashara husika.

Page 25: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Mambo ya kuzingatia……

• Taratibu mbalimbali za ulipaji ada na kodi mbalimbali.

• Hali ya hewa ya eneo husika.• Hali halisi katika eneo la biashara, angalia

mwenendo wa maisha ya wakazi katika eneo husika mfano, amani na utulivu, vita, mfumuko wa bei, n.k.

Page 26: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA

• Ni ukweli ulio wazi kuwa si kila anayeuza au mfanyabiashara ndogo ndogo ni mjasiriamali.

• Imekuwa ni 'fashion' kwa sasa nchini tangu nchi ijiunge katika mfumo unoangozwa na soko kwa kila muuzaji wa bidhaa na mtoaji wa huduma kujiita mjasiriamali.

Page 27: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Kwa ufupi mjasiriamali ni mtu yeyote ambaye haogopi kuweka mipango na kushindwa, tofauti na mfanyabiashara yeye huwa na mtazamo wa kuwekeza kwa ajili ya faida pekee.• Mjasiriamali mhimili wake mkuu ni ubunifu

• Kuzalishwa wa bidhaa mpya, njia mpya za uzalishaji kugunduliwa, kutafutwa kawa masoko mapya na utumiaji wa rasilimali zinazomzunguka.

Page 28: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Misingi ya Ujasiriamali

1. Elimu juu ya ujasiriamali na kujifunza; ni muhimu kwa kila anayejihusisha na dhana ya ujasiriamali akaujua ujasiriamali na sikuchukulia kuwa ni jambo ala kuiga ama kunakili kutoka kwa watu waliofanikiwa au wanaojihusisha na ujasiriamali, kujifunza huku kuwe kwa nadharia na vitendo.

2. Ubunifu na uvumbuzi: Majasiramali haswa ni yule anaeyekuwa na kubuni vyanzo na mbinu mbalimbali za kuboresha utendaji wake

Page 29: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

3. Kukua na kupanuka: ni muhimu mjasiriamali akue na kutanuka kimaslahi na si kuwa katika hali moja tua kila mara, anapaswa kutanuka kimtaji,kiutendaji na kimahusiano, hili huboresha huduma na uwanda wake wa malengo. Hivyo ni muhimu pia majaisiriamali kuwa mtu wa mipango na kuwa na uelekeo Fulani anaotakaa kufikia sehemu Fulani.

4. Kujaribu na kudhamiria: Mjasiiramali si mtu wakuaogopa kutenda apindia aionapoa fursa na kuitathmini kuwa ianpaswa kuendewa. Hivyo si muoga katika kujaribu

Page 30: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Maeneo ya kutengeneza mtandao wako kama mjasiriamali;

Washindani wako: Biashara ni ushindani lakini sio uadui.Kama

unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio ni vizuri sana ukawajua washindani wako wa kibiashara.

• Mshindani wako anaweza kukufaa pia.• Anaweza kuzidiwa na kazi akakusukumia

zingine.Jitambulishe,jenga uhusiano mzuri wa kibiashara.

Page 31: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Vyombo vya Habari: • Kama mjasiriamali,ni muhimu ukajuana na

watu wanaoendesha au hata kumiliki vyombo hivi vya habari.

• Na zaidi angalia vile ambavyo vipo karibu zaidi na eneo lako la ujasiriamali.

• Kutangaza na kupata taarifa.

Page 32: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO): • Mjasiriamali makini ni yule ambaye

anadhamiria kuisaidia jamii yake kwa njia moja au nyingine

• Isitoshe jamii iliyo bora,iwe kiafya,kielimu nk ni wateja wako wazuri wa siku za mbeleni.

Page 33: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

05/03/2023 ISLAMIC HELP TANZANIA

DHANA POTOFU JUU YA UJASIRIAMALI NA BIASHARA

Page 34: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

• Hujihusisha na ujasiriamali tu• Ni mtu anayejihusisha na Biashara Ndogo

tu• Ni mtu asiye na Elimu• Ni kamari na kubahatisha• Ujasiriamali unazaliwa nao• Inahitaji mawazo makubwa• Ni kazi rahisi

Page 35: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Haruna Zakharia, Said Bakhresa, Reginald Mengi, Ambassador Said and Gulam Dewji

Page 36: MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Mfano wa kuigwa: