matukio muhimu ya teknolojia – maoni ya wakemia

2
MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA Kemia na wahandisi kemia wametoa mchango mkubwa sana katika masuala ya chakula na kilimo kwa kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao pamoja na matumizi ya vyakula vyenye virutubisho. Mwishoni mwa karne za 19 na 20 asilimia kubwa ya majiko yetu yalijaa mavuno ya vyakula kutoka katika ghala za kuhifadhia vyakula vya mizizi, bustani ama mashamba ya kienyeji; siagi iliyotengenezwa kutoka katika maziwa safi, mayai kutoka katika kuku waliofugwa upenuni, mboga kutoka katika bustani, nyama iliyohifadhiwa kutoka katika sanduku la barafu na kupikwa kwa mkaa wa mawe au kuni. Katika karne iliyopita tumeshuhudia mbadiliko makubwa sana juu ya namna ya kupata vyakula vyetu, uzalishaji zaidi katika mashamba yetu na urahisi wa kupatikana kwa vyakula pamoja na maji. Wakulima wa kisasa wameweza kutumia kemikali kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo. Matumizi ya mbolea na dawa za kuulia wadudu waharibifu wa mazao yamepelekea mavuno kupatikana kwa wingi na kwa uhakika zaidi. Jamii imefaidika na teknolojia mpya ambayo imechangia katika kuboresha ladha, umbo, upatikanaji wake pamoja na wingi wa virutubisho kutoka katika vyakula hivyo. Maendeleo na mafanikio haya katika kemia yamesaidia sana kulisha ulimwengu unaoendelea kwa kasi ya ongezeko la watu. IV.1. Mbolea na Virutubisho vya Udongo Mbolea za Naitrojeni Mpango wa Haber-Bosch Ubora wa mbolea za kemikali Mapinduzi ya Kijani na mimea ya kupandishia (chotara) IV.3. Utengenezaji, Uhifadhi na Usalama wa vyakula Sakarini na Vikolezo utamu Vitamini na madini Hatua za uhifadhi na uzalishaji. Usalama wa vyakula na ubora wake IV.2. Uhifadhi wa Mazao na Udhibiti wa wadudu waharibifu Mpango wa Bordeaux na dawa za kuondosha ukungu/kuvu DDT na dawa za kuulia wadudu Tiba/Uhifadhi wa wanyama Matunzo/Uhifadhi wa mashamba IV.4. Uhifadhi wa Chakula Hifadhi katika vyakula Mafriji (jokofu) na kloroflorokaboni Majiko ya Maikrowevu Maji safi na salama IV. CHAKULA NA KILIMO

Upload: kiona

Post on 14-Jan-2016

129 views

Category:

Documents


2 download

DESCRIPTION

IV. CHAKULA NA KILIMO. - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

Page 1: MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA

Kemia na wahandisi kemia wametoa mchango mkubwa sana katika masuala ya chakula na kilimo kwa kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao pamoja na matumizi ya vyakula vyenye virutubisho. Mwishoni mwa karne za 19 na 20 asilimia kubwa ya majiko yetu yalijaa mavuno ya vyakula kutoka katika ghala za kuhifadhia vyakula vya mizizi, bustani ama mashamba ya kienyeji; siagi iliyotengenezwa kutoka katika maziwa safi, mayai kutoka katika kuku waliofugwa upenuni, mboga kutoka katika bustani, nyama iliyohifadhiwa kutoka katika sanduku la barafu na kupikwa kwa mkaa wa mawe au kuni.Katika karne iliyopita tumeshuhudia mbadiliko makubwa sana juu ya namna ya kupata vyakula vyetu, uzalishaji zaidi katika mashamba yetu na urahisi wa kupatikana kwa vyakula pamoja na maji. Wakulima wa kisasa wameweza kutumia kemikali kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo. Matumizi ya mbolea na dawa za kuulia wadudu waharibifu wa mazao yamepelekea mavuno kupatikana kwa wingi na kwa uhakika zaidi. Jamii imefaidika na teknolojia mpya ambayo imechangia katika kuboresha ladha, umbo, upatikanaji wake pamoja na wingi wa virutubisho kutoka katika vyakula hivyo. Maendeleo na mafanikio haya katika kemia yamesaidia sana kulisha ulimwengu unaoendelea kwa kasi ya ongezeko la watu.

IV.1. Mbolea na Virutubisho vya Udongo Mbolea za Naitrojeni Mpango wa Haber-Bosch Ubora wa mbolea za kemikali Mapinduzi ya Kijani na mimea ya kupandishia (chotara)

IV.3. Utengenezaji, Uhifadhi na Usalama wa vyakula Sakarini na Vikolezo utamu Vitamini na madini Hatua za uhifadhi na uzalishaji. Usalama wa vyakula na ubora wake

IV.2. Uhifadhi wa Mazao na Udhibiti wa wadudu waharibifu Mpango wa Bordeaux na dawa za kuondosha ukungu/kuvu DDT na dawa za kuulia wadudu Tiba/Uhifadhi wa wanyama Matunzo/Uhifadhi wa mashamba

IV.4. Uhifadhi wa Chakula Hifadhi katika vyakula Mafriji (jokofu) na kloroflorokaboni Majiko ya Maikrowevu Maji safi na salama

IV. CHAKULA NA KILIMO

Page 2: MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA

IV. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – CHAKULA NA KILIMO

Matukio

1881 Mwanasayansi wa Kifaransa Louis Pasteur agundua tiba ya kimeta kwa kondoo na nguruwe mwitu.

1883 Mkemia wa Kidenish Johan Gustav Kjeldahl aboresha njia za kugundua kiwango cha naitrojeni katika vitu/mazao asilia.

1884 Mwanasanysi wa Kifaransa Pierre M. A. Millardet agundua mchanganyo wa Bordeaux kupambana na kuvu/ukungu katika mashamba ya mizabibu.

1901 John F. Quenny, mwanzilishi wa Kampuni ya Monsanto inayotengeneza Saccharin.

1913 Wakemia wa Kijerumani, Fritz Haber na Carl Bosch waboresha uzalishaji wa kiwango kikubwa cha ammonia kwa matumizi ya viwandani.

1913 Elmer V. McCollum na Marguerite David wagundua Vitamin A katika samli na kiini cha yai.

1918 Kampuni ya Kelvinator yazindua kwa mara ya kwanza friji (jokofu) kwa matumizi ya kawaida.

1933 Maziwa yenye viongezo vya Vitamin D yaanza kuuzwa.

1939 Mwanakemia wa Uswissi Paul Mueller agundua matumizi ya DDT, dawa ya kuangamiza wadudu waharibifu.

1943 Wanakemia wa Idara ya Kilimo nchini Marekani yazindua dawa ya kupuliza aerosol kwa kuua vijidudu na matumizi ya mashambani.

1953 Saran wrap kwaajili ya matumizi ya kawaida yaanzishwa na kampuni ya Dow.

1964 ‘Mapinduzi ya Kijani’: Mpango wa mimea ya kupandishia (chotara) na matumizi ya mbolea za maji maji zimesaidia kuondosha tatizo la lishe kwa nchi.

1972 Matumizi ya DDT yapigwa marufuku nchini Marekani (ikiwa nchi ya kwanza duniani, Hungary imepiga marufuku 1968).

1974 Monsanto yagundua dawa ya kuua magugu.

1990 Usanii katika chakula kwa kuchanganya virutubisho vya lishe na chembe-chembe za madawa zaanza kupata umaarufu.

Louis Pasteur akidunga sindano

wanyama.

Kipimo cha Kjelhahl cha kugundua kiwango cha

naitrojeni katika vitu/mazao asilia

Pierre M. A. Millardet

Kasha asilia la Sakarini (Saccharin)

Kiini cha yai chenye vitamin A

Friji (jokofu) la kawaida la Kelvinator

Kasha asilia la kufungia DDT

Maziwa yakiwa na viongezo vya

vitamin D

Bango-ujumbe la Monsanto