mbora wa manabii - seal of prophets

33
1 MBORA MBORA MBORA MBORA MBORA WA WA WA WA WA MAN MAN MAN MAN MANABII ABII ABII ABII ABII HADHRAT MIRZA TAHIR AHMAD AHMADIYYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA

Upload: dinhkiet

Post on 20-Dec-2016

339 views

Category:

Documents


6 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

1

MBORAMBORAMBORAMBORAMBORA

WAWAWAWAWA

MANMANMANMANMANABIIABIIABIIABIIABII

HADHRAT MIRZA TAHIR AHMAD

AHMADIYYA MUSLIM JAMAATTANZANIA

Page 2: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

2

MBORA WA MANABII

Mwandishi: Hadhrat Mirza Tahir Ahmad -Khalifatul Masih IV.

© Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania

Chapa ya kwanza: April 2000. Nakala 3000

Kimeenezwa naAhmadiyya Muslim JamaatP. O. Box 376Dar us SalaamTanzania

Kimechapwa naAhmadiyya Printing PressP. O. Box 376Simu: 051 - 110473 Fax: 051 - 121744Dar us SalammTanzania.

Page 3: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

3

Mheshimiwa Meya wa mji wa Hounslow, waheshimiwaWabunge, na wageni wengine watukufu. Sisi twaichukulia hiikuwa hafla takatifu kwa sababu ya lile jambo litakalozungumzwahapa. Hii ni heshima kubwa kwangu mimi bali nafurahi sanakuongea nanyi juu ya jambo hili ninalolipenda mno.

Mwanzoni, nimesoma mbele yenu Kalima Shahada. Kishanikasoma Sura ya kwanza ya Qur'an Tukufu na aya moja yaSura iitwayo Al-Kahf. Kalima Shahada niliyoisoma ilikuwa ileiliyorefushwa zaidi ya ile Kalima Shahada inayojulikana kwakawaida. Hii inazo sehemu mbili; ya kwanza; Allah ni Mmoja,hapana Mungu ila Allah; na sehemu nyingine ni Muhammad niMtumishi Wake, mja na Mtume. Mkazo ni juu ya kuwa yeye yumja kabla ya kuendelea mbele kumchukulia kuwa Mtume.

Ile Kalima Shahada fupi ndiyo iliyokuwa machoni pa BwanaGibbon wakati yeye alipoituhumu. Bwana Bosworth aliandikajuu yake kama ifuatavyo:

Linakaribia sana kuwa pia jambo geni ya kwamba BwanaGibbon, ambaye kwa jumla kamsema Muhammadkikamilifu, awe aanze kwa kusema, 'Dini yaMuhammad ni ukweli mmoja asilia na uwongo mmojaulio wa lazima - Yupo Mungu Mmoja na Muhammad niMtume Wake.'

Bwana Smith anazidi kuliendeleza jambo hili kwa kusema:Haukuwa, jinsi mimi nilivyojaribu kuonyesha, uwongokwake yeye Muhammad au kwa wafuasi wake; kamaingelikuwa hivyo, dini ya Muhammad isingelikuwaimejitokeza jinsi ilivyofanya, wala kuwa vile ilivyo leohii.

Page 4: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

4

Twamshukuru Bwana Smith kwa kuhifadhi picha nzuri yamisimamo ya Kimagharibi kuihusu Islam, na hususan kumhusuMwanzilishi Mtakatifu wa Islam, Mtume Muhammad amani iwejuu yake. Yeye analizungumzia jambo hili sehemu mbili katikahistoria nami hapa namnukuu:

Mnamo karne chache za awali za Dini ya Muhammad,Ukristo haukuweza kuthubutu kushutumu wala kuelezea;uliweza tu kutetemeka na kutii. Lakini Waislamuwalipokuwa wamepata ushindi wao wa mara ya kwanzakatikati ya Ufaransa yale mataifa yaliyokuwayakiwaogopa, yalirudi nyuma kama kundi lango'mbe lifanyavyo wakati mwingine pale yule mbwammoja aliyekuwa akiwatimua mbio anaposimamishwa;na ingawaje wao hawakujaribu kupigana, waliwezaangalau kuwasingizia wale maadui zao waliokuwawakitoroka.

Sasa inafuata mifano ya masingizio kama alivyoandika BwanaSmith, yeye anasema:

Katika visa vya Turpino, vilivyonukuliwa na BwanaRenan, Muhammad mkomeshaji shupavu wa ibada zamasanamu, amejigeuza sanamu la dhababu, na, chini yajina Maumet, yasemekana amekuwa mwabudiwa hukoCadiz.

Kisha anasema:Yeye (Muhammad) ndiye Dajjali, mtu wa dhambi,mwenye kijipembe, nami sijui kinginecho minghairiyake; wala sidhani ya kuwa hadi kufikia katikati ya karneya kumi na nane mwandishi hata mmoja, isipokuwa ajabuya yule Myahudi Maimonides, anamchukulia(Muhammad) kinyume na kuwa yu mzushi mkubwa nani nabii bandia.

Ili kuzidi kulipanua jambo hili, yeye anaendelea kusema:

Page 5: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

5

Visa vya Bafomet, vilivyokuwa vya kawaida katika karneya kumi na nne na kumi na tano, vinamnasibisha yeyekila kosa, kama Waathanasia walivyomfanyiaArius. 'Yeye ni fasiki, mwizi wa ngamia, Kadinaliambaye baada ya kutofaulu kupata shahada za matamanioya kila Kadinali, hubuni dini mpya ili kujilipizia kisasinduguze'.

Hukaa pa wazi 'Motoni'.

Bwana Dante anamtia ndani ya kundi lake la tisamiongoni mwa wapandao mbegu za ugomvi wa kidini.

Kwa upande wa viongozi wa Matengenezo, Muhammad,amani iwe juu yake, mletaji mkubwa zaidi wamatengenezo, hashirikishwi vilivyo, na ile chuki yaodhidi yake, kama lilivyokuwa pengine jambo lakutazamiwa, yaonekana yenye kubadilikabadilika kamaujuzi wao. Lutha haridhiki ya kuwa yeye (Muhammad)si mwovu kuliko Leo; naye Melancthon anamwaminikuwa ndiye Yajuja na Majuja, au pengine hao, yeye niwote wawili.

Kwa bahati mbaya, ukurasa huu wa kuhuzunisha wenyemasingizio na maoni yaliyokithiri ya chuki dhidi ya MwanzilishiMtakatifu wa Islam hayakukoma. Hata hivyo twayaonamabadiliko katika upepo ambao umemleta mmoja wa waandishimashuhuri juu ya Islam toka Uingereza, ambaye ndiye BwanaCarlyle. Yeye alianzisha zama mpya za njia za kuichukulia Is-lam. Katika zile zama za giza la chuki yeye alikuwa mtu wahuku wa kwanza mwenye ujasiri na utu kutukuza sifa za MtumeMuhammad, amani iwe juu yake, na alikuwa ishara ya kwanzakuashiria ujaji wa majira mapya.

Baada ya Bwana Carlyle mambo yalianza kubadilika, lakini

Page 6: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

6

hayakuishilizia kuwa ni mtindo, badala yake likabakia tu kuwajambo lililokatizwa. Tunaona ya kwamba katika historia nzimaya kumlaumu Mtume Muhammad, amani iwe juu yake,palikuwepo na wanachuoni waliorejelea misimamo yao ya kale,huku akizaliwa Salman Rushdie hapa na pale. Kuzaliwa kwamtu kama Salman Rushdie sio jambo geni katika historia yaukinzani wa kidini; wahusiana sana na ujinga, utovu wauvumilivu ni kitu anachokijua sana mwanadamu.

Hebu sasa nimgeukie Bwana Carlyle. Katika kitabu chakemashuhuri na kwa baadhi ya watu ni kitabu chake 'kilaumiwa'kwa jina 'Heroes and Hero Worship (yaani Mashujaa na Ibadaya Mashujaa) yeye anasema:

Lahaula, fikira sampuli hiyo zasikitisha sana ikiwatutaupata ujuzi wa cho chote katika viumbe halisi waMwenyezi Mungu. Hebu tusiziamini kabisa. Zaonyeshaupoozaji wa kiroho wa kuhuzunisha sana nazo zilikuwamauti ya uhai wa roho za watu. Mawazo ya utovu waMwenyezi Mungu ulio mkubwa zaidi ya huo miminadhani hayajapata kuhubiriwa humu ardhini. Eti ayarialianzisha dini. Kwa nini, ayari hawezi kujenga nyumbaya matofali kama hazizingatii kihalisi asili za saruji,udongo uliochomwa na cho chote kingine anachokifanyiakazi, basi hiyo anayoijenga si nyumba bali ni lundo latakataka. Haitadumu kwa karne kumi na mbili nakukaliwa na (watu) milioni mia moja na thamanini.Itabomoka kwa mara moja.

Kisha anasema:Masingizio ambayo juhudi kabambe zimemlundikia mtuhuyu yalikuwa yenye kutufedhehesha sisi wenyewe paletu Bwana Pocock alipomdadisi Bwana Grotiousakimwuliza: Li wapi thibitisho la ile hadithi ya njiwamzoeshwa kudonoa mbaazi sikioni pa MtumeMuhammad na kuonekana kuwa ni malaika. Bwana

Page 7: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

7

Grotious akimjibu alimtangazia akisema hapakuwa nathibitisho. Huu ndio wakati wenyewe wa kuyatupiliambali hayo yote.

Kwa maoni yangu, kiini hasa, na kipengele muhimu zaidikatika Kalima ni hili neno Abd, lenye maana ya mja, yule mjamwaminifu kwa Bwana wake kiasi hiki kwamba neno hili pialina maana ya kuwa mtumishi mtiifu mwaminifu. Leo nimeamuakutoongea juu ya bishara za Mtume Muhammad amani iwe juuyake, lakini nizungumzie utu wake kama mja, akiwa mtumishitu wa Mwenyezi Mungu na kama mtu mpole aliyepitisha maishayake yote miongoni mwa nduguze, wafuasi wake na maaduikama mtu mwaminifu.

Kwa minajili hii mimi nimechagua sehemu kadha za maishayake yenyewe na tutazikariri pamoja nanyi, ili muweze kuamuayeye alikuwa ni mtu wa aina gani.

Mimi nilisema kwamba kuwa Abdu ilikuwa muhimu kwasababu naamini kwamba kile kipengele cha utume daimakinapingwa. Upande mmoja wa mtume u wazi kumwelekeaMwenyezi Mungu, na kulifanya jambo gumu kwa watu wakawaida kuamini au kukataa ukweli wake. Huu upande uliozidisana kutoeleweka hulifanya jambo gumu kwao wao kukipigapicha kimawazo kitu wasichoweza kukishirikia abadan; lakinikama mwanadamu kila mdai (utume) anaweza akaamuliwavyema tena sawasawa na kila mtu. Ikiwa mtu huyo nimwaminifu haiwezekani kwake kuwa Mtume bandia.

Nitaanzia na dondoo za wanachuoni wa kimagharibi nami kwamara nyingine namnukuu Bwana Bosworth Smith:

Muhammad alikuwa na urefu wa wastani na mwenyemwili madhubuti; kichwa chake kilikuwa kikubwa najuu ya paji lake kubwa la uso, na juu ya miinuko

Page 8: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

8

myembamba ya nyusi zake palipita mshipa mmoja wadamu, ambao, alipokasirika, uligeuka kuwa mweusi nakuonekana ukipuma. Ilikuwa nadra kwake yeyekukasirika, sina budi kuwaambieni. Macho yake yalikuwana weusi wa mkaa na makali kwa nuru yake; nywele zakezilijikunja kwa kiasi; na ndevu ndefu, ambazokama wa-mashariki wengine, alikuwa akizipapasapapasaalipokuwa akitafakari, viliutilia fora uzuri wasura yake. Mwendo wake ulikuwa wa haraka tena thabiti,'kama mwenye kushuka toka mlimani'.

Bwana Bosworth anaandika juu ya tabia yake kwa manenoyafuatayo:

Yeye alikuwa msema machache ..... na mwaminifu.Walimwita 'Al-Amyn', Mwaminifu. Uchungaji wake wamifugo wa mwajiri wake; safari zake za Syria; labdaurafiki wake wa muda mfupi kule na Sergius au Bahira,Mmonaki wa kihistoria; nadhiri yake mashuhuri yakuwatononesha wadhulumiwa; kuajiriwa kwake naKhadija katika kazi ya biashara, na kufunga ndoa nayebaadaye takriban ndiyo matukio pekee ya ki-nje yenyekustahili kukumbukwa katika maisha yake ya hapomwanzoni.

Akielezea maisha yake ya hapo mwanzoni Bwana Carlyleanatuambia:

Bali toka mapema maishani yeye alikuwaametambulikana kuwa mtu mwenye kuwaza sana,wenzake walimwita Al-Amin, mwaminifu, msema kwelitena thabiti, mwaminifu kwa alilosema na alilotenda.Waliona kwamba yeye daima alimaanisha kitu fulani.Kidogo mnyamavu katika maongezi, mnyamavu kabisa

Page 9: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

9

pasipo na la kuzungumziwa lakini msema ilivyo sawa,mwenye hekima, mkweli alipopata kuzungumza, daimaakitoa ufafanuzi wa jambo lenyewe. Na hii ndiyo ainaya pekee ya uzungumzaji inayopasa kuzungumzwa.Maisha mazima tunamkuta aliyechukuliwa kwa jumlakuwa mtu thabiti, mkweli, mchukulia mambo kwa dhati,mnyofu na hata hivyo mpole, mkunjufu, mwenye tabiaya kirafiki, mcheshi, hata kushiriki katika kicheko chawengi. Wako watu ambao kicheko chao si cha kweli kamakisivyokuwa kweli kila kitu kuwahusu wao. Mtu husikiahabari za uzuri wa Muhammad, uso wake mzuri,ulioonekana wa busara na uaminifu, rangi yake ya majiya kunde nyekundunyekundu, macho meusi makali,macho karibu yafanane na ule mshipa wa paji la uso wakeuliokuwa ukifura kwa weusi alipokasirika.

Yeye alikuwa ameishi miongoni mwa watu wake kwa mudawa miaka arubaini kabla hajainuliwa na Mwenyezi Mungukuwa Mtume. Hata wakanushi wakali wa tabia yake hawaweziwakaonyesha doa lolote katika maisha yake hadi kufikia umriule. Wala hapana kutafautiana au kutopatana miongoni mwawanahistoria juu ya ukweli huu. Mambo yakiwa hivyo Qur'anTukufu ikawatambia wale waliomkana kwa kusema.

Hakika mimi nimeishi nanyi maisha yangu yote kabla ya hayo.Kwa nini hamtumii akili zenu. Je, hamwoni ya kwamba mtualiyeishi miaka arubaini ya maisha yasiyokuwa na dosari kwaghafla hawezi akageuka kuwa mtukutu wa kupindukia ardhini.Ambaye hakupata kabisa kusema uwongo kuwahusu wanadamuwenzake angelithubutuje kusema uwongo kumhusu Mwumbawake, aliye Mungu aliyempenda sana.

Hadhrat Khadija aliishatajwa hapo mapema kama mwajiriwake. Ndiye aliyekuwa yule bibi tajiri aliyemtuma safari

Page 10: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

10

mbalimbali za kibiashara hadi nchini Syria. Daima alionekanaakiwa mwenye kufaulu katika shughuli hizi. Lakini miminaamini ilikuwepo sehemu moja ya biashara hii ambayo ndiyoiliyofaulu kupita zote, lakini kwa kawaida huwa haitajwi. BiKhadija mwishowe alipoolewa naye, yeye alikuwa mtu mwenyeumri wa miaka ishirini na mitano, ilhali Bi Khadija mwenyewealikuwa tayari ameisha toka ujanani na kuingia makamoni. Lichaya tofauti hii ya umri, Bi Khadija alipopendekeza posa yakealikubali, na akaishi naye kwa miaka mingine ishirini na mitano.Baada ya ndoa hii kufanyika, huku akimfahamu heshima yake,Bi Khadija alimkabidhi rasilimali yake yote na akampatia kilaalichokuwa nacho. Ile biashara niliyoitaja kuwa ya heshimazaidi, yenye shani zaidi na iliyofaulu zaidi, ilikuwa hii. Baadaya kupokea utajiri ule wote wa mali yeye aliwagawia maskinikila kitu, bila ya kujibakizia hata hela moja. Hii pia ni sifa kubwakwa Bi Khadija, ambaye akiwa mwanamke tajiri zaidi waUarabuni, kwa ghafla akawa mmoja wa maskini wake wakubwa,wala hakunung'unika hata kidogo; akiishi mwisho mzima wamaisha yake na Mtume Muhammad amani iwe juu yake, kwauaminifu mkubwa kabisa. Alimpenda mtu aliyekuwa badohajaondokea kuwa Mtume. Hata hivyo, haukuwa uzuri wa suraya mtu yule bali uzuri wake wa kindani, wa kumetameta kamalulu, ndio uliompendeza. Jambo hili lilibainika zamaMwanzilishi Mtakatifu wa Islam alipopokea wahyi wake waawali toka kwa Mwenyezi Mungu. Yeye alishtushwa sana nanguvu ya wahyi ule hivi kwamba alirudi nyumbani akitetemekakana kwamba alikaribia kushikwa na homa. Bi Khadijaalimdhania yu karibu kuwa mgonjwa na akamfunika blanketi.Baadaye, Mtume Muhammad amani iwe juu yake, akamwelezeakile kisa kilichokuwa kimempata cha malaika kumjia katika suraya mtu na kumwamuru asome. Alipojihofia yeye mwenywe;huku akiwa ameshtuka nafsi nzima hakuweza kutambuakilichokuwa kikitendeka kwake. Baada ya kusikia habari hiiHadhrat Khadija, r.a., alimjibu akimwambia:

Page 11: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

11

Mimi nimekujua kwa muda na najua wewehuyashughulikia maslahi ya wanyonge na kuhuzunikiadhiki zao. Wewe u mtu abebaye taabu za walewalioelemewa na uzito wa mateso. Wayarejesha tenamaadili yaliyokuwa yametoweka ardhini. Wewe u mpolemwenye huruma kwa jamaa na unauchukulia udugu kwanjia iliyo bora zaidi. Wewe u mkweli na daima umekuwahivyo. Basi angeliwezaje Mwenyezi Mungukukuangamiza. Mimi nayaamini hayo uliyonena.

Ulikuwa ni ule usafi wa yule mja wa ndani yakeuliomsadikishia mkewe kwamba yeye alikuwa kweli Nabii.katika hali hiyo akawa wa kwanza kumwamini MwanzilishiMtakatifu wa Islam na akatambua kwamba haikuwezekana kwamtu mkweli kuondokea kuwa nabii bandia.

Bwana Bosworth amekielezea kisa hiki kwa maneno yakemwenyewe naye anasema:

Khadija akamgeukia na akasema:Allah hatakufedhehesha. Si wewe umekuwa mwenyekuwapenda nduguzo, mpole kwa jirani zako, mhisani kwamaskini, mtimiza ahadi na mtetea kweli daima.

Kinyume na maoni ya Hadhrat Khadija, r.a., maoni ya marafikizake wote yaligeuka ghafla baada ya yeye kujitangaza kuwaMtume toka kwa Mwenyezi Mungu. Wale waliokuwawakimwita Al-Amin, mwaminifu kupita wote; waliokwendakwake kuamuliwa ugomvi wao; waliomwamini kabisa nakumfahamu kuwa mtu mnyofu, walianza kumlaumu kwauwongo wa aina mbaya zaidi. Bwana Bosworth anakariri hayamaoni ya watu wa Makka, baada ya tangazo la Nabii Muhammadamani iwe juu yake la kuwa mteule toka kwa Mwenyezi Mungu,kwa maneno yafuatayo:

Page 12: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

12

Huyoo anakwenda zake mtoto wa Abdullah mwenyeuzungumzaji wake wa mbingu. Walimwita mtazamanyota, mshairi mwehu. Babake mdogo alimdhihaki nasehemu iliyokuwa kubwa zaidi ya wenyeji wakampuuzakwa dharau ambayo ni lazima ilikuwa isiyovumilika sanakwake yeye kuliko mateso ya kidhahiri.

Kisha anatuambia kwamba wenyeji wa Makka wakajaribumbinu za vishawishi na maafikiano, hongo na hata vitisho(inavyotambulikana katika kauli hii ya Mtume Muhammadamani iwe juu yake):

Wakinikabili na kuliweka jua juu ya mkono wangu wakuume na mwezi juu ya mkono wangu wa kushoto, naMungu akiniamuru mimi sitaitangua imani yangu.

Hii siyo kauli au nia ya mzushi, kaandika Bwana Bosworth.

Yeye alikuwa mtu mpole penye kila uhusiano na watu naalikuwa kwa hakika, mnyenyekevu kwake Mwenyezi Mungu.Alikuwa mpole hata kwa wale waliokuwa wamemkubali kuwayu Nabii wa Mungu. Safari moja huko Madina, baada ya kuwayeye tayari ameisha kuambiwa na Mwenyezi Mungu kwambaalikuwa Muhuri wa Manabii, hii ikiwa na maana kwamna yeyendiyealiyekuwa mbora zaidi miongoni mwao, mmoja wamasahaba zake alibishana na bwana mmoja aliyekuwaakimheshimu sana Nabii Yunus, amani iwe juu yake. Yulesahaba wa Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam alisema kwambaNabii Muhammad, amani iwe juu yake alikuwa mbora zaidi,huku yule mwingine akisema kwamba Nabii Yunus amani iwejuu yake ndiye aliyekuwa bora zaidi. Ubishi huu uliporipotiwakwa Mtukutu Mtume amani iwe juu yake yeye akatamkaakisema: "Msinitangaze ubora wangu kuliko Yunus, mwanawa Muta, kwa sababu ni kinyume na heshima za uhusiano wawanadamu kuendelea kujigambia ubora wa viongozi wenu dhidi

Page 13: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

13

ya viongozi wa wengine. Jambo la ubora wa mmoja kulikomweingine ni swali la kuamuliwa na Mwenyezi Mungu, siokitu cha kujivunia. Huo ndio ujumbe tuliopewa, ambao kwabahati mbaya umesahauliwa na Waislamu wengi hivi leo.

Kisa kama hiki kilifanyika baina ya Myahudi na Mwislamukuhusu swala la ubora baina ya Nabii Muhammad na NabiiMusa, amani iwe juu yao. Yule Mwislamu akakasirishwa sanana tabia ya ufidhuli ya Myahudi yule na hata akamzaba kibao.Huyu Myahudi akaenda kwa Mtume Mtukufu amani iwe juuyake na akanung'unika. Yule sahaba mhusika akagombezwa sanana Mtume Mtukufu amani iwe juu yake, ambaye alikariri tenamaneno yale yale aliyoyatumia katika kile kisa kingine cha hapombeleni, akisema: Msinitangulize kuwa bora kuliko Musa.Akaendelea kusimulia mambo bora ya Nabii Musa amani iwejuu yake na akamsifu kwa njia iliyolainisha sononeko za moyowa yule Myahudi.

Ziko habari za yeye kusimama usiku kucha, akiomba msamahawa Allah. Masahaba zake waliona kwamba miguu yake ilikuwaikifura kwa sababu ya muda mrefu wa kusimama katika sala.Hawakuwa wamepata kumwona akitenda dhambi nawalimwamini kuwa mtu safi kuliko wote ardhini. Hilililiwashangaza. Wakamwuliza: kwa nini Ewe Mtume waMwenyezi Mungu, kuomba msamaha kwa Allah. Akawajibuakisema: je, nisimshukuru Mungu wangu kwa fadhili zotealizonijaalia. Safari nyingine wakati swala hili hili la msamahana uchaji Mungu wa mtu lilipokuwa likijadiliwa, MtumeMtukufu amani iwe juu yake, aliwaambia masahaba zake yakwamba hapana mtu ardhini atakaye samehewa kwa sababu yavitendo vyake vizuri. Ni rehema ya Allah ambayo mwishowehuokoa kutoka nira ya madhambi na ndiyo itakayosababishauingiaji wa peponi. Maelezo haya yaliwashangaza na mmojawao akauliza akisema: Ewe Mtume wa Mungu, wewe

Page 14: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

14

hutasamehewa kwa ucha-Mungu wako na vitendo vyako vizuri?La, hata mimi. Nitasamehewa tu kwa rehema ya Mwenyezi Mungu.Kila kitu ni chake, hapana kilicho chetu. Cho chote kile alichotujaalia,tunakitumia na kukitumikisha kadri ya ujuzi wetu na uwezo wetu.Hata mtu mnyofu, aliyepitisha maisha yake yote akitenda vitendovizuri, hatasamehewa kwa sababu ya vitendo vyake. Vile fursa nzurinzuri alizopewa na Mwenyezi Mungu.

Tabia yake ya kutotaka makuu haikuwa na mipaka. Alipokuwaakiketi na wafuasi wake, akivaa nguo za kawaida, akila chakula kilekile walichokuwa wakila, yeye hakuketi mahali maalumu. Mara nyingiwalipata kukosea ni nani aliyekuwa Mwanzilishi Mtakatifu wa Is-lam, amani iwe juu yake. Hadhrat Abu Bakar, Mungu awe radhinaye, baadaye alikuja kuwa Khalifa wa Kwanza wa Islam, alikuwamzee kumshinda na huenda alikuwa na ndevu ndefu zaidi, sina hakika,haya ni makisio yangu tu, lakini kitu fulani umboni mwake kiliwafanyabaadhi ya wageni wamwite Mtume wa Mungu. Naye kwa njia yastaha alikuwa akimgeukia Mtume Mtukufu, amani iwe juu yake, nakuwaongoza kwake.

Safari moja Hadhrat Umar, r.a., aliyekuja kuwa Khalifa wa Pili waIslam, aliomba ruhusa aende akatimize ibada ya Umra; hii ni ziarafupi mjini Makka sawa na Haji. Mtume Mtukufu wa Islam amaniiwe juu yake alimtazama na akatamka akisema: Naam nenda,kaitimize ibada ya Umra na tafadhali usinisahau katika maombi yako.Hii ndiyo iliyokuwa hali ya kutojitakia makuu ya yule mtu, ambayemaombi yake aliyategemea kila Mwislamu, hivi kwamba alikuwaakimtafadhalisha mmoja wa watumishi wake amkumbuke katikamaombi yake.

Maisha yake mazima alishiriki katika kila aina ya dhiki zilizowakabiliWaislamu kwa jumla. Katika Vita vya Handaki anafahamika kuwaaliyedhikika kwa njaa pamoja na wengine.

Page 15: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

15

Zilipogawanywa sehemu za kulichimba handaki lenyewe, yeyehakuachwa kando na akachangia fungu lake kuchapa kazi. sa-fari moja sahaba mmoja alimwona Mtume Mtukufu, amani iwejuu yake katika hali isiyovumilika. Akasema sahaba huyu: Sikuya vita vya Handaki, nilimwona Mtume Mtukufu akisombaudongo uliokuwa umeufunikiza weupe wa tumbo lake. Alikuwaakisema: Bila ya wewe Ee Mola wangu tusingeliweza kupatamwongozo, wala kutoa sadaka, wala kuomba; tafadhalitumiminie utulivu na uiimarishe miguu yetu tutakapomkabiliadui. Hakika watu wametudhulumu lakini kamwe hatukukatatamaa ikiwa watajaribu kututesa kwa sababu yako Wewe.

Hadhrat Jabir r.a., anasimulia kwamba walikuwa wakichimbasiku za Vita vya Handaki na wakakuta jiwe kubwa.Wakamripotia Mtume Mtukufu amani iwe juu yake. Alipoinukawakaona jiwe limefungwa juu ya tumbo lake; alikuwa hajakulacho chote kwa muda wa siku tatu. Ni desturi ya Kiarabu kufungajiwe namna hii unapoteseka kwa njaa ya kukithiri, huenda hayoyalipunguza ukali wa njaa. Katika hadithi nyingine ya kisa hichohicho, twakuta kwamba kila sahaba wa Mtume Mtukufualifungia jiwe juu ya tumbo lake, lakini shati la Mtume Mtukufulilipoinuka, wakaona tumbo lake limefungiwa mawe mawili.Alipomwona katika hali hii Hadhrat Jabir hakuweza kuivumiliatena. Akamwomba ruhusa na kwenda eneo la akina mama,akamwita mkewe na kumwuliza kama alikuwa na chochote chakutabaruku. Yule mama akamjibu ya kwamba nyumbanialikuwemo mbuzi na unga pia. Hapo Hadhrat Jabir r.a.,akamwambia mkewe amchinje yule mbuzi kwani alikuwaamwemwona Mtume Mtukufu katika hali isiyovumilika asilani.

Huyo ndiye aliyekuwa yule mtu, Nabii Muhammad, amaniiwe juu yake, ambaye daima alipata taabu pamoja na watumishiwake. Hapakuwepo na tafauti yoyote ile. Kinyume chake, tokahadithi nyingi juu ya jambo hili tunaweza tukaamini kwamba

Page 16: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

16

yeye aliteseka zaidi.

Alikuwa ni mtu asiyetishika, bila woga ambaye hakusitakuikabili hatari ana kwa ana. Katika maisha yake alipigana vitavingi vya kujihami, ingawaje yeye hakupata hata mara mojakuanzisha vita vya uchokozi. Kwa kawaida yeye alionekanakatika zile sehemu hatari zaidi vitani, ambapo mapiganoyangeliwaka kama moto. Yaripotiwa na msimuliaji mmoja yakwamba Mtume Mtukufu alipotakikana katika uwanja wa vita,basi wao wangelimtafuta katika lile eneo la vita ambapomapambano yalipamba moto zaidi na yeye daima angelikuwakatikati yake. Safari moja mjini Madina, ule mji aliohamia baadaya miaka kumi na mitatu ya mateso mjini Makka, usiku wamanane watu walisikia vishindo vya kugutusha. Katika sikuzile yalihofiwa mashambulio toka pande zote, kwa hivyo watuwaliwaandaa farasi wao na wakaenda kupeleleza. Badala yakewakamkuta Mtume Mtukufu amani iwe juu yake toka upandeule akiwa juu ya farasi asokuwa na tandiko. Yeye alikuwaameenda peke yake, kwa haraka, hata bila ya kumtandika farasiwake. Akawaambia haikuweko hatari nao wanaweza wakarudikwao majumbani.

Siku moja alipokuwa safarini, ikiwa siku ya joto kali, alikuwaakijipumzisha chini ya kivuli cha mti. Bedui mmoja, aliyetokanana waabuduo masanamu, akajionea nafasi yake kwa vile MtumeMtukufu kajitenga peke yake. Basi akaushika upanga wa MtumeMtukufu amani iwe juu yake, na akamwamsha huku akimkejeliakimwabia: Nani atakaye kuokoa mikononi mwangu EweMtume wa Mungu. Mtume Mtukufu akajibu Mungu wangu. Hilijibu fupi likamtisha huyu mtu kiasi hiki kwamba mikono yakeikatetemeka na upanga ukajidondokea chini. Sasa MtumeMtukufu akauchukua ule upanga na kamwuliza yule mtuakimwambia: Ni nani atakaye kuokoa nami? Kwa ghafla mamboyakiwa yamegeuka, mtu huyu aliweza tu kusema kwamba ni

Page 17: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

17

jinsi gani Mtukufu Mtume Muhammad amani iwe juu yake,alivyokuwa mtu mpole na mrehemevu na akamwomba nusraya maisha yake. Mtume Mtukufu akatamka akisema: Ole wako,hata hukujifunza somo; alikuwa ni Mungu aliyeniokoa dhidiyako. Mtu huyu alisamehewa kwa hakika. Mtume Mtukufualikuwa mtu mwenye moyo wa huruma sana.

Siku hizi misikiti imekuwa mwahali mwa mikwaruzanoduniani kote. Mapenzi juu ya misikiti moyoni mwa MtumeMtukufu amani iwe juu yake, yalikuwa yamefurika kiasi hikikwamba ni jambo lisilofikirika kwa mtu mwingine yeyotekuupenda msikiti kiasi hicho. Safari moja Bedui mmoja asokuwaMwislamu alikuja kutembea Madina na akapatiwa malazimsikitini. Siku zile na hata leo hii katika baadhi ya sehemu zadunia, misikiti yatumiwa kama nyumba za wageni. Pakiwamahali pa ibada misikiti huwekwa katika hali ya usafi, hataviatu haviruhusiwi ndani. Lakini mtu huyu, kwa sababu yakutojua, alianza kutabawali mahali pale pale watu waliposali nakusujudu. Na haja hii ndogo ilifanyika akiwepo Mtume Mtukufuna masahaba zake. Baadhi ya masahaba zake wakamhamakiakutaka kumpiga mtu huyu mwenye kuudhi lakini wakakatazwamara moja na Mtume Mtukufu. walinasihiwa wasimghasi wakatianapojisaidia, Alipomaliza haja yake Mtume Mtukufu akaitishandoo ya maji na yeye mwenyewe akapasafisha mahali pale.Kisha akawageukia masahaba zake na akawaambia: Ninyihamkuinuliwa na Mungu kuwapatia watu shida. Daimakumbukeni ya kwamba mlienuliwa kuwaletea wanadamu faraja.

Safari moja ujumbe mmoja wa Wakristo kutokea eneo laNajran ulifika mjini Madina kwa mjadala wa mada za tofautibaina ya Islam na Ukristo. Wakakaa Madina siku tatu.Walipokuwa wakijadiliana ndani ya msikiti wa Mtume Mtukufu,wakati wa sala yao ukafika. Wakamwomba Mtume Mtukufuruhusa waende zao nje kwa minajili ya kusali sala yao. Mtume

Page 18: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

18

Mtukufu amani iwe juu yake akasema kwamba msikiti ulikuwapia mahali pa ibada, na wanakaribishwa kusali mle, nao wakasalimle msikitini. Muda si muda wakafika msikitini baadhi yamasahaba na wakawaona wale Wakristo wakiabudu wakielekeamashariki; tofauti kabisa na wanakoelekea Waislamu katika salazao. Wakasogea mbele kupinga jambo hili, lakini yeye kwauthabiti akawakataza wasiwabughudhi Wakristo wale naakatamka akisema: Mimi nimewaruhusu kwa sababu hii ninyumba ya Mungu, na hapana mwenye haki ya kumkatazayeyote yule mwenye kumwabudu Mungu katika mahali palipowakfu kwa minajili ya ibada.

Safari moja ujumbe toka makao ya watawa wa Kikristo yaSt. Catherine waliandika tangazo lililosema kwamba makao yaoyapatiwe ulinzi wakati Islam itakapopata ushindi katika sehemuzile za dunia. Mtume Mtukufu mara moja akalikubali ombi laona akaandika amri za kulitekeleza. Nifahamuvyo mimi nikwamba amri hizi bado zinahifadhiwa nchini Uturuki. Amrizenyewe zinasema hivi: Haimpasi yeyote kuingilia rasilimaliza Makao ya watawa, wala sanamu ya msalaba au kitu chochotekinachowakilisha dini yao. Na visidhuriwe kwa njia yoyoteiwayo. Yeyote atakayelipuuza jambo hili hatakuwa mmoja wetu.

Mengi yanasemwa juu ya chuki iliyopo baina ya Waislamuna Wayahudi. Ingawaje yale makabila ya Wayahudi mjiniMadina na pembezoni mwake yalimpinga vikali NabiiMuhammad, moyo wake kumhusu Myahudi kamwehaukuathirika. Safari moja alikuwa ameketi na masahaba zakewakati yalipopitia karibu yao maandamano ya mazishi,akasimama kutoa heshima zake, Mtu mmoja akatamka akisemakwamba maiti yenyewe ilikuwa ya Myahudi. Mtume Mtukufuakajibu: Je, mtu huyu hakupewa uhai na Mwenyezi Mungu? Je,yeye hakuwa kiumbe cha Mungu? Kumbukeni, katika yalemambo yaliyo ya kawaida kwa mwanadamu, ni sharti tuonyeshe

Page 19: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

19

heshima, bila kujali dini ya mtu, taifa au imani. Huu ndio ujumbewa Islam, haukufundishwa tu wakati wa Mtume Mtukufu baliulitimizwa kwa dhati katika kila jiha.

Yeye alikuwa mtu mwenye mapenzi yaliyochanganyikanakimaridadi na upole. Aliwapenda watoto, hata aliwaheshimu.Baada ya Mtume Mtukufu kufariki, mmoja wa masahaba zakesafari moja alipita kati ya kundi la watoto na akawaamkiaAssalaamu Alaikum yaani amani iwe juu yenu. Wao walikuwabado chipukizi na walishangaa kwamba mzee mwenyekuheshimiwa sana, tena sahaba wa Mwanzilishi Mtakatifu waIslam aliwatangulia katika kuwatolea maamkizi ya Kiislamu.Yeye akawaambia ni kwa nini alifanya hivyo na akasema: Mimidaima nilimwona Mwanzilishi Mtakatifu akifanya hivyo hivyo,yalikuwa ni mazoea yake kuwa wa kwanza kusema AssalaamuAlaikum, hata kwa watoto.

Hadhrat Anas Osama bin Zaid, Mungu awe radhi naye,anasimulia ya kwamba alipokuwa mtoto, aliinuliwa na MtumeMtukufu na akakalishwa juu ya goti lake moja, kisha MtumeMtukufu akamkalisha mjukuu wake Hassan juu ya goti lakejingine, na huku akiwakumbatia wote wawili akimwambiaMwenyezi Mungu: Ewe Mola wangu kawaonyeshe huruma jinsininavyowaonyesha huruma. Kisa hiki kilimpatia athariisiyofutika Hadhrat Osama bin Zaid aliyekiripoti huku machoziyakimlengalenga.

Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam alikuwa na ucheshi wenyekupendeza sana. Alizoea kuwatania watoto ili kuwachekeshakwa njia rahisi. Lakini utani wake haungelimuudhi yeyote.Tunazo ripoti nyingi za utani wake kwa watoto na wakatimwingine kwa watu wazima pia. Safari moja mama mmojamzee alimtafadhalisha ya kwamba aombe kwa minajili yakusamehewa kwake na Allah. Katika kumjibu kwake Mtume

Page 20: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

20

Mtukufu akasema kwamba hapana mtu mzee atakayeingiaPeponi. Bila shaka yule mama alishtuka aliposikia hayo. LakiniMtume Mtukufu alitabasamu na akatamka akisema kwambayeyote yule aingiaye Peponi hufanywa kijana. Uchekeshaji wakeulikuwa wa hekima na wa kupendeza, ambao daima ulitumiwajuu ya msingi wa mapenzi; wala si kwa nia ya kudharau.

Yeye alikuwa mshikilia uadilifu halisi tena mtimilifu. Hatahivyo nafsini mwake tunaiona sifa hii yake ikienda samabambana majaaliwa yake ya kuwa na huruma halisi. Katika vita vyaBadr ambapo makafiri walienda kuivamia Madina, ami yakemmoja alipokuwa akipigana upande wa makafiri, alitiwambaroni na Waislamu. Sawa na mahabusu wengine mikono namiguu yake vilifungiwa kwenye nguzo msikitini. Katika sikuzile hazikuwako jela, kwa hivyo misikiti ikatumiwa badala yake.Ikatokea kwamba mtu fulani alikuwa amewakaza kambamahabusu hawa kwa nguvu sana. Mtume Mtukufu, ambayemaskani yake yalikaribiana na msikiti, hakuweza kupata usingiziusiku ule. Yasemekana kwamba hakupata utulivu na akawamwenye kugeukageuka ubavu huu na ule kitandani mwake.Masahaba zake wakagunduwa na wakamuuliza ni ninikilichokuwa kikimuhangaisha. Akawajibu akiwaambia kwambaalikuwa akimsikia ami yake akilia huko msikitini. Hapo mtummoja akaenda kuzilegeza zile kamba alizofungiwa BwanaAbbas. Baada ya muda Mtume Mtukufu hakusikia tena kwikwizozote, akapata wasiwasi na akadadisi akisema mbona kwikwizimeisha. Mtu mmoja akajibu kwamba kamba zake BwanaAbbas zilikuwa zimelegezwa. Mtume. Mtukufu akasema; Kamammemfanyia hivyo Abbas basi mfanyieni vivyo hivyo kilamahabusu. Hivi ndivyo uadilifu wake ulivyoongezea hurumayake.

Safari moja binti wa chifu mmoja Mwarabu mashuhurialishikwa akiiba, alikuwa akiitwa Fatima, kama vile bintiye

Page 21: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

21

Mtume Mtukufu. Jambo hili lilikuwa likibishaniwa nje yanyumba ya Mtume Mtukufu na baadhi ya watu walitakaahurumiwe kwa vile yeye alikuwa bintiye chifu mwenye uwezosana. Wakambembeleza Hadhrat Osama bin Zaid. r.a., aliyekuwamwana wa mtumwa wa zamani wa Mtume Mtukufu, aendeakaombe msamaha kwa niaba yake. Kijana huyu alikuwa badohajaifahamu vyema tabia ya Mtume Mtukufu na akaendakumwombea msichana yule msamaha. Hili lilikuwa mojawapoya yale matukio ya nadra ambapo ule mshipa wa paji la uso waMtume Mtukufu ulikuwa mweusi, akasema: una maana ganikwa kumtakia msamha. Mimi bila shaka ningelifanya vileMwenyezi Mungu anitakavyo nifanye hata kama angelikuwabinti yangu Fatima aliyefanya uhalifu huu.

Mtume Mtukufu wakati mmoja alikuwa na pesa za Myahudi.Yule Myahudi akafikiria kwamba wakati wa kulipwa pesa zileulikuwa tayari umeishapita, kumbe ulikuwa bado haujapita.Akamwendea Mtume Mtukufu na kumdai pesa zake akitumialugha mbaya sana, na akalaumu akisema kwamba watu wa kabilala Quraishi wote walikuwa kundi moja la wasoio kopeshekaambao kamwe hawatimizi ahadi zao. Hadhrat Umar r.a., ambayepia alikuwepo pale alikasirika sana na akataka kumchomaupanga wake. Mtume Mtukufu, akamzuia Hadhrat Umar ambayesasa alikuwa ameisha msema mabaya yule Myahudi na penginealikuwa karibu kumchapa kofi, na akasema; Ewe Umar,ungelitenda tofauti na hivyo. Kwanza ungeliniambianilikumbuke deni na nilipe wakati wake, kisha ungelimwambiaawe na huruma anapodai mali yake na awahurumie wadeni wake.Kisha Mtume Mtukufu akamgeukia sahaba wake mwingine naakasema: Bado zimesalia siku tatu, mimi najua hatujakiuka sikuya miadi, lakini wewe mlipe chochote anachodai na umpatienyongeza kwa sababu ya ukali wa Umar. Hii ndiyo iliyokuwatabia yake baada ya yeye kutusiwa kidhahiri mbele ya masahabazake. Uadilifu wake ulikuwa wa kileleni. Ulikuwa uadilifu wa

Page 22: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

22

kupindukia, usiofungamana kwa vyovyote vile na uaminifuwake, kabila au dini yake.

Leo hii uhusiano wa Wayahudi na Waislamu ni kitukinachoeleweka visivyo na ipo haja ya kukisahihisha. Miminitakariri baadhi ya mifano toka kwa uhusiano wa MtumeMtukufu na Wayahudi kwani ni sharti tuige desturi yake katikauwanja huu; msimamo wowote unaokwenda kinyume haunabudi kukataliwa mbali. Mtume Mtukufu wa Islam amani iwejuu yake alikuwa amejenga picha katika umma ya kuwa mtumwadilifu kabisa. Hata kama ilikuwapo mikwaruzano baina yaWaislamu na Wayahudi au baina ya Waislamu na waabuduomasanamu, wangelitafuta uamuzi wake. Katika kesi mojainaripotiwa kwamba kipande kimoja cha ardhi kilikuwakikibishaniwa na Mwislamu na Myahudi. Wao wakamwendeaMtume Mtukufu na kumtaka hukumu yake. Mtume Mtukufukwanza akamtaka mlalamishi Mwislamu atoe dalili zake. YuleMwislamu akasema kwamba yeye hakuwa na mashahidi, lakinialikuwa akisema kweli sawa na ahadi. Mtume Mtukufuhakumjali na akamwambia yule Myahudi aape kwa jina laMungu ikiwa kweli ardhi ile ilikuwa yake. Yule Mwislamuakapinga na akasema: Ewe Mtume wa Mungu, huyu ataapakiuwongo. Si jambo kubwa kwake yeye kudanganya kwa sababuya kipande cha ardhi. Mtume Mtukufu akajibu akisema: Hapananjia nyingine ya kuamulia jambo hili, kama yeye ataapa basiardhi itakuwa yake. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Safari moja msafara mmoja mdogo ulitembelea eneo laKhaibar palipokuwa mahali penye kukaliwa na kabila moja laWayahudi kwa jina la Bani-Nazir. Watu hawa mbeleniwalifukuzwa toka Madina na sasa walikuwa wamelifanya eneohili kuwa makao yao; lakini hiyo ni habari nyingine. Eneo hilisasa lilikuwa ngome ya Wayahudi na tokea hapo lilikuwalikikaliwa nao peke yao. Ule msafara wa kibiashara toka

Page 23: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

23

miongoni mwa Waislamu ulipozuru Khaibar, mfanya biasharammoja wao aliuliwa. Wakamwendea Mtume Mtukufu nawakapendekeza kwamba kosa la mauaji yale liwekwe juu yaWayahudi wa eneo lile, na wote kwa pamoja wadaiwe fidia.Mtume Mtukufu akasema: Je, mnao ushahidi wowote wa huyumtu kuuawa na Myahudi. Wakajibu wakisema: Hapana shahidilakini ni sharti muuaji awe mmoja wao; hapana mtu mwingineaishiye kule. Mtume Mtukufu akasema: Njia ya pekee iliyoponi kwamba Wayahudi wale ni sharti waape kwambahawakufanya mauaji haya. Wayahudi wakafanya hivyo nawakaondolewa hatia ya mauaji yale. Lakini hata hivyo, kwaamri ya Mtume Mtukufu, jamaa wa marehemu aliyeuawawalilipwa fidia toka hazina ya serikali. Katika dhati yake twaonahuruma ikiambatana na uadilifu wake kwa njia ya kuvutia nayenye kuafiki zaidi, ambayo kusema kweli inakuwa furahakubwa kujitazamia.

Yeye pia alikuwa mwenye huruma kwa watumishi wake nawatumwa wake. Swala la utumwa ni wazo linaloeleweka vibayasana upande huu wa magharibi. Mimi sitalifanyia swala hiliufafanuzi wowote, lakini ninawahakikishieni ya kwamba tunayonjia moja tu halali inayotajwa katika Qur'an Tukufu, ambayokwayo watumwa wanaweza wakahodhiwa. Hii imo katika suraAl-Anfal, aya ya sitini na nane. Aya hii yasema kwamba njia yapekee ya kuwafanya wanadamu kuwa watumwa ni katika vitavikali mno, sio eti katika mashambulio ya hapa na pale. Katikasiku zile haukuwepo utaratibu wa kambi za wafungwa wa kivita,kwa hivyo mateka wa vita wangeligawiwa nyumba mbalimbali.Pia twaona ya kwamba Qur'an Tukufu yapendekeza njia nyingiza kupata uhuru kwa minajili ya wafungwa wa kivita. Zipo ayanyingi juu ya jambo hili, hivi kwamba baada ya kuzisoma,yashangaza ungeliwezaje utumwa kuja kuchukuliwa na Waislamwa leo kama jambo linalohalalishwa na Qur'an Tukufu. Ziponjia nyingi za kujipatia uhuru kiasi hiki kwamba sawa na

Page 24: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

24

Qur'an Tukufu na sunna ya Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam,s.a.w., endapo mfungwa wa kivita hakombolewi kwa fidia yakulipwa na nduguze, na hana njia nyingine ya kujipatia uhuru,anaweza akaenda katika mahakama ya Kiislamu na kutakaaachiliwe mara moja, kwa hili sharti ya kwamba atajichumiakipato kulipia kidogo kidogo bei yoyote inayochukuliwa kuwandiyo thamani ya ukombozi wake. Amri hizi za Qur'an Tukufuzilifuatwa kwa dhati wakati Mtume Mtukufu. Wakati mwinginemaelfu ya wafungwa yalikombolewa kwa siku moja. Kwasababu ya yale yaliyotendeka siku zilizopita na pia kwa kuwahizo zilikuwa nyakati za taabu, badhi ya watumwa walirithiwana watu na wakaendelea kutumika majumbani. Mtume Mtukufumara kwa mara aliwanasihi Waislam kwamba wawahurumiechambileche ndugu zao wa damu. Tunakuta vikihadithiwa visavingi vya aina hii; kwa mfano, wakati bwana na mtumwa wakewalipokwenda kununua vitu, mwenye duka hakuwezakuwatafautisha. Safari moja Hadhrat Ali r.a. aliyekuwa Khalifawa Nne wa Islam baada ya Mtume Mtukufu, alikwenda dukanina akaitisha mavazi mawili yaliyofanana. Mwenye dukaakampendekezea anunue mavazi ya rangi zinazotafautiana. Yeyeakajibu akisema: Bwana wangu ameniambia niwatendeewatumwa wangu kama ndugu zangu wa damu. Hivyo basi,chochote ninachovaa, nitamvalisha hicho hicho mtumwa wangu.

Hadhrat Abu Masud Badri r.a. anasimulia akisema kwamba:Nilikuwa nikimjadili mtumwa niliposikia sauti nyuma yanguikiniambia: Jihadhari ewe Abu Masud. Nilikuwa nimekasirikahivi kwamba sikutambua sauti yenyewe hadi msemajialiponikaribia na nikagundua kumbe alikuwa Mtume Mtukufuna alikuwa akisema: Jihadhari ewe Abu Masud, Allah ana uwezojuu yako kuliko ulio nao juu ya mtumwa huyu; nami nikajibunikisema: ewe Mtume wa Allah, mimi namwachilia huru nipateradhi ya Allah. Mtume Mtukufu akasema: Kama usingelifanyahivyo basi ungelikugusa moto (wa Jahannamu).

Page 25: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

25

Hadhrat Zaid, r.a. hutajwa mara nyingi katika historia ya Is-lam kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mtumwa pekee kupatakuishi na Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam. Anasimulia akisema:Nilipokuwa nikimtumikia Mtume Mtukufu, mimi nilifanyamakosa mengi, lakini yeye hakupata kunikaripia, hata mara moja.Hakupata kunilaumu, achilia mbali swala la kunipiga.Wakatiwa zama za Madina, baba na ami ya Hadhrat Zaid walipatahabari kwamba yeye alikuwa mtumishi wa MwanzilishiMtakatifu wa Islam. Basi wakafika mjini Madina na wakamsihiMtume Mtukufu kwamba amwachilie huru. Akawajibu akisema:Bila shaka mimi nitafanya hivyo lakini kwa nini hamumuuliziyeye? Ni mtu huru. Kama anataka kukaa hapa mimi siwezinikamshurutisha aondoke. Hapo Mtume Mtukufu akajinyamaziawakati Hadhrat Zaid alipoletwa mbele za baba yake na ami yake.Ukawa mkutano wa machozi ya furaha kwani walikuwawakikutana baada ya muda mrefu. Wakamtaka Hadhrat Zaidarudi kwao. Yeye akawajibu akiwaambia: Kama chaguo nilangu, basi mimi sitarejea nyumbani kwetu kwa sababunimegundua mtu ninayempenda zaidi ya baba yangu, mamayangu, ami yangu na mtu mwinginewe humu ulimwenguni.Kusikia hivyo Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam akatoka nao nje,na mbele za watu ambao yeye mwenyewe alikuwa amewaita;akatangaza akisema: Namtangaza Zaid kutokuwa tena mtumwa.sasa yeye yu mtu huru. Aidha natangaza kwamba nitamtendeakama mwanangu, na tokea sasa awe akijulikana kama Zaid binMuhammad.

Sasa nitageukia upande mwingine wa utu wa MtumeMuhammad, kama bwana, kama baba na kama jamaa. Kuwahusuwanawake, yeye alitenda kwa wema na huruma hivi kwambahusikii ukali wowote toka kwake. Ingawaje zipo ripoti zaHadhrat Aisha r.a., na wakeze wengine kumkasirikia; yeyeharipotiwi hata mara moja kuwa alipata kuwarukia kwa ukalikwa vyo vyote vile. Hadhrat Aisha r.a. anasimulia kwamba

Page 26: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

26

alimsaidia kazi zake za nyumbani; haya yote yakiwa ni ziada yawajibu wake kwa wanadamu wote kama Nabii wa Mungu.Akajishonea nguo zake; akajirekebishia viatu vyake; akajitekeamaji na wala hakutaka msaada katika mambo haya. Upande huuwa tabia yake uliwapendeza sana masahaba zake. Baada ya kifochake sahaba wake mmoja, alipokuwa akiendesha farasi,aliangusha mjeledi wake. Kijana mmoja akakimbia kwendakumwokotea mjeledi wake lakini yeye kasema: Uache, tafadhali,hebu nishuke chini nikauokote mimi mwenyewe kwa sababumaisha yangu yote nimemuona Mwanzilishi Mtakatifu wa Is-lam hakutegemea wengine; hakumsumbua mtu mwinginekumfanyia kazi zake.

Tandiko lake laelezewa na Hadhrat Aisha, r.a. kuwa jifuko langozi lililojazwa majani. Anasema: Hakupata kula mkate wangano kwa siku tatu mfululizo. Zilikuwepo nyakati ambazo mieziiliweza kupita bila ya sisi kula nyama wala mkate, badala yaketuliyaruzuku matumbo yetu tende na maziwa, isipokuwa penginezawadi isiyotazamiwa ambapo mtu angelichinja kondoo nakutuletea nyama. Hadhrat Umar r.a. anasimulia kwamba:Nilikwenda kwenye chumba kidogo alimokuwa akikaaMwanzilishi Mtakatifu wa Islam. Alikuwa amelalia mkeka wamajani makavu uliokuwa mparuzi kiasi hiki kwamba ubavuuliolalia mkeka ule niliona ukijaa miparuzo. Nikakitupia jichokile chumba na kilikuwa kitupu, hamkuwemo na chochoteminghairi ya ndoo ya maji na kidubwana kimoja au viwili. Miminilimfahamu kuwa mpenzi mkubwa zaidi wa Mwenyezi Mungu,mja aliyekifikia kilele cha utu wema. Kulinganisha hukukukanihuzunisha kiasi hiki kwamba nikaanza kulia. MtumeMtukufu akanigeukia na akasema: Umar waumwa na nini?Nikasema: Ewe Mtume wa Mungu, Mwenyezi Mungu,anakupenda sana; wewe ndiwe mbora wa alivyoviumba; lakinihata hivyo nakuona ukidhikika sana jinsi hii. Huna kitanda chakufaa. Huna cho chote cha kupambia nyumba yako; hamna

Page 27: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

27

cho chote. Mtume Mtukufu akatabasamu na akatamka akasema:Umar, je, wewe ungelipendelea vitu vya kidunia vya maishahaya kuliko vile tunavyowekewa na Mwenyezi Mungu katikamaisha yajayo. Hadhrat Umar akajibu kwamba bila shaka vilevinavyokuja ndivyo bora zaidi, na mazungumzo yakakomeahapo.

Hiki kilikuwa kisa kidogo tu, lakini je, mzushi angeliwezakufanya hivyo? Kwa nini watu hutunga uwongo? Kwa minajiliya nini? Je, ni kwa ajili ya kuishi maisha ya dhiki na machungukama hayo, na kwa ajili ya kushiriki katika shida za zama zaopamwe na watumishi wao waaminifu. Kama hayo ni kweli, basiukweli wenyewe unakuwa hauna maana; kila kitu katikamwanadamu hapo kinakuwa bandia.

Yeye aliwahurumia hata wanyama. Siku moja alipokuwasafarini alimsikia ndege mdogo akitoa kelele za mahangaiko.Akawageukia masahaba zake na kuwauliza ni kitu ganikilichokuwa amefanyiwa ndege yule. Mmoja wao akajibuakisema kwamba alikuwa amempokonya mayai yake mawili.Mtume Mtukufu akasema: Yarudishe. Katika hadithi nyingineya kisa hicho hicho yasemekana ni makinda wawili wala siomayai yalikuwa yamechukuliwa, na Mtume Mtukufuakawaambia masahaba zake kwamba mama na asisononeshwejuu ya watoto wake. Hili halikuwa jambo la ndege na makinda,bali lilikuwa swala la utu wa watu maishani.

Mtume Mtukufu safari moja aliwasimulia masahaba zake kisakimoja akisema: Mtu aliyekuwa na kiu jangwani, aligunduakisima kilichojaa maji. Akaingia kisimani na akanywa maji yakumtosha. Alipotoka, akamwona mbwa akitweta kwa kiu;pengine alikaribia kufa. Yule mtu akarudi kisimani na akachotamaji kwa viatu vyake, akavishikilia vizuri kwa meno yakeakatoka kisimani, hapo akamnywesha maji yule mbwa.

Page 28: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

28

Mwanzilishi Mtakatifu akaendelea kuelezea akisema: MwenyeziMungu ameniambia, mtu yule alisamehewa madhambi yake yoteya hapo kabla. Katika hadithi nyingine juu ya kisa hikiyasemekana ni mwanamke malaya aliyefanya hivyo. Maishayake mazima yalijaa madhambi. Lakini akasamehewa mbele yaMwenyezi Mungu kwa sababu ya kitendo cha kumhurumiamnyama.

Mmoja wa masahaba zake alimwuliza ya kwamba je, watapatathawabu kwa sababu ya vitendo vya kuwahurumia wanyama.Akasema: Naam, wanyama wale wote wenye maini chepechepe.Neno hili 'chepechepe katika Kiarabu hutumiwa kuonyeshawororo na uwezo wa kushtuka upesi. Mimi nimelitumia vilelilivyo lakini tafsiri yake ni ya mnyama ye yote ambaye kwavyo vyote vile ni mwepesi wa kushtuka, awe akitendewa huruma,na Mwenyezi Mungu atalipa thawabu kwa vitendo vyote vyahuruma namna hiyo.

Safari moja alimwona mtu akimkama mbuzi na akawa nawasiwasi wasije wanambuzi kutobakiziwa cho chote.Aliwakataza masahaba zake wasiuwe hivi hivi, ndege yeyoteau mnyama. Akasema: Mtaulizwa na Mwenyezi Mungu juu yakuua hivi hivi tu wala bila sababu nzuri. Alipoulizwa na ni sababuipi inayoweza ikawa nzuri, alijibu akisema: Kama mnahitajinyama, basi ueni. Kisha akawakumbusha ya kwamba hata katikakuua wasije wakakosa huruma: Ueni kwa njia ambayo kwayomnyama atapata maumivu kidogo inavyowezekana. Baadhi yaWanajumuiya wananiuliza kama ile njia ya kisasa ya kuuamnyama ni ya Kiislam; yaani kwanza kumziraisha mnyama nakisha kumchinja. Mimi nasema hiyo ndiyo hasa njia ya Kiislamu.Sikubaliani na wale wanachuoni wa Kiislamu, wanaosemakwamba njia hii haikufahamiwa na Islam ya hapo awali. Lakinivifaa hivi vinavyosaidia kuwapunguzia wanyama machunguhavikuwa vikipatikana siku zile. Hili agizo ya kwamba hata

Page 29: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

29

katika kuua onyesheni huruma, hata hivyo, lilitolewa naMwanzilishi Mtakatifu wa Islam mwenyewe.

Sasa naligeukia lile swali la leo lenye kujadiliwa vikali; swalala kufuru. Kokote ninakotembelea ulimwengu, swali hilihuniandama. Naulizwa ya kwamba je, wasemaje juu ya fatwaya Khomeni ya kifo cha Salman Rushdie. Mimi huwaambiakwamba Islam niijuayo, niliyojifunza toka kwa MwanzilishiMtakatifu wa Islam, yatuambia kwamba hamna adhabu yoyoteile dhidi ya kufuru. Sio swala la kifo au kitu kinginecho.Miongoni mwa mambo mengine, mimi hukariri hususan kisahiki kilichotokea maishani mwa Mtume Mtukufu; pia kimetajwakwa ufupi ndani ya Qur'an Tukufu. Kabla ya kufika kwa MtumeMtukufu huko Madina, mtu mmoja alikuwa akiinukia kwamaoni ya watu wote kuwa kama kiongozi wa makabila yote namakundi ya kidini. Alikuwa akiitwa Abdullah bin Ubayy binSalul. Baada ya kuwasili Mtume Mtukufu mambo yakabadilikapole pole na badala yake yeye kwa kauli moja akakubaliwaawe kiongozi wa Madina. Japokuwa tofauti zilikuwepo, lakinikwa hakika, wake yeye ndio uliokuwa uongozi wenye mamlaka.Jambo hili likamfanya Abdullah bin Ubayy bin Salul awe mwivukupindukia. Akawa yu mwenye kufichua moto wa sonono zakekwa njia hii au ile. Tabia yake ilikuwa ya aina ambayo kwayoWaislam wengine walimfahamu kuwa 'Mkuu wa Wanafiki'.Safari moja akiwa njiani toka vita ambavyo kwa jumlahavikufaulu, na wapiganaji wote walikuwa wachovu sana tenawalioudhika; mtu huyu Abdullah bin Ubayy bin Salul, akaonasasa ndio uliokuwa wakati wa kujilipizia kisasi. Miongoni mwawenzake fulani yeye akatangaza akisema kwamba watakaporudiMadina, mheshimiwa miongoni mwao, atamfukuzilia mbalimnyonge zaidi miongoni mwao. Kauli hii ilikuwa wazi na kilammoja alijua alichokimaanisha. Hadhrat Umar, r.a., baada yakupata habari hii alimwomba Mtume Mtukufu ruhusa amuuliembali mtu huyu; akasema kwamba Mtume Mtukufu karushiwa

Page 30: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

30

matusi wasiyoweza kuyavumilia. Lakini Mtume Mtukufuhakuruhusu adhabu yoyote. Inaripotiwa kwamba mwanaweAbdullah bin Ubayy bin Salul, aliyeitwa Julabi Ubayy bin Salul,naye pia alifika mbele ya Mtume Mtukufu na akasema: EweMtume wa Mungu, pengine kama ukimruhusu mtu mwingineamuue baba yangu, mimi nikiwa mwanawe, huenda nikawa nakinyongo. Baadaye katika wakati usiotazamiwa, huendanikajaribu kujilipizia baba yangu na kumuua muuaji wake, nahivyo kutenda dhambi kubwa. Baba yangu anastahili adhabuhii kwa matusi aliyokutusi, kwa hivyo tafadhali niruhusunimuulie mbali. Mtume Mtukufu akatabasamu na akasema: La,hasha, hapana adhabu. Wakarejea mjini Madina na kwa miakamingi mtu huyu akaishi kwa amani chini ya ulinzi kamili waMwanzilishi Mtakatifu wa Islam, aliyekuwa amemtukana.Alipofariki, Mtume Mtukufu akaamua kusalisha sala yake yajeneza. Hili halikuvumilika kwa baadhi ya masahaba zake.Hadhrat Umar r.a. anasimulia kwamba yeye alijaribu kumzuiana kasema: Si huyu ni mkubwa wa wanafiki. Huyu siye yuleambaye kumhusu yeye Mungu kasema kwamba hata kamaukimwombea msamaha mara sabini, hatasamehewa. Basi kwanini, Ewe Mtume wa Mungu, uliye mpokeaji wa Wahyi huuwote, umeamua kusalisha sala yake ya jeneza. Jibu lilikuwa:Umar, simama kando. Ningelikuwa nayo matumaini kwambaMwenyezi Mungu angelimsamehe kama nikimwombea zaidi yamara sabini, mimi ningelifanya hivyo. Hiyo ndiyo iliyokuwatabia ya Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam. Alikuwa mtu mwenyehuruma tele; mtu mwenye msimamo; mtu aliyeishi maisha yaukweli na si kinginecho ila ukweli.

Alipoona kwamba siku za kurudi kwa Bwana wake MtakatifuAllah zilikuwa zimewadia, aliwahutubia Waislam. Hii ilikuwahalaiki kubwa zaidi aliyopata kuihutubia. Hafla yenyewe ilikuwaHaji ya mwisho; inayojulikana pia kama Hijja-tul-Wida. Katikahotuba ile, ujumbe wake ulikwa kwa minajili ya wanadamu wote

Page 31: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

31

na kwa wakati wote ujao. Aliwahutubia kama "Enyi wanadamu",hakusema Enyi Waislam lakini akasema: Enyi wanadamu, ninyinyote mko sawa. Mwarabu si bora kuliko asiyekuwa Mwarabu,mtu mweupe si bora kuliko mweusi. Watu wote, wawe ni wataifa au kabila gani, na wawe wanashikilia madaraka gani, wakosawa. Ubora wowote unaoweza kufikiriwa ni ucha-Mungu wamtu. Mwishowe akasema: Hebu niambieni kama nimeufikishaujumbe. Wote wakajibu kwa sauti moja wakisema: Naam, EweMtume wa Mungu, kwa kweli ujumbe umeufikisha. Akasema:sasa nipeni ahadi kwamba mtazidi kuusambaza ujumbe huu kwawanadamu wote, pembe zote za ulimwengu. Yeyote aliyepo hapani sharti aendelee kufikisha ujumbe huu kwa hao wasiokuwepohapa na kazi hii ni sharti iendelee hadi mwisho wa ulimwengu.

Ubaguzi wa kitaifa ni swala linalojadiliwa vikali leo hii.Ingawaje mataifa mengi yaliyostaarabika yatakanusha kuwepokwa jambo hili, uzoefu wangu baada ya kusafiri maeneo mengi,waonyesha kwamba ubaguzi huu wapatikana katika kila taifana katika kila sehemu ya ulimwengu. Hili si tu swala la mweupekujiona mbora kuliko mweusi, bali mweusi naye pia kujiona naubora wa kuwa na nia ya kujilipizia kisasi dhidi ya weupe. Badondilo jambo la chini kwa chini lililo hatari zaidi katika fikara zakibinadamu na vihimizo. Chini ya maagizo bayana ya MtumeMtukufu, mimi nawafikishieni ujumbe wa usawa wa wanadamu.Sisi sote tukiwa viumbe wa Mungu, tukiwa na chimbuko moja,twawezaje kujiruhusu kuporomoka kwenye kiwango ambapotunatawaliwa na maswala ya ubora wa wanadamu kulikowanadamu wengine.

Ulipokaribia wakati wake wa kuyatoka maisha haya,alihiyarishwa na Mwenyezi Mungu ama arudi kwake au apateziada ya miaka katika maisha haya ya ardhini. Yeye jibu lakelilikuwa: Firifiqil Allah; Napendelea kurudi kwa Mola wanguMtukufu. Haya pia ndiyo yaliyokuwa maneno yake ya mwisho

Page 32: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

32

aliyotamka kabla ya kuingia maisha ya akhera.

Kama mnamwona kuwa yu mwongo basi bila shaka alikuwanabii bandia. Kama si hivyo basi mimi ninawezanikawahakikishieni kwamba hapana mtu mkweli awezayeakaambulia kuwa Nabii mwongo. Haiwezekani kabisa. Ni ufinyuwa fikara za mwanadamu unaovifanya vitu viwe tofauti na vilevilivyo. Ni mwanadamu ageuzaye ukweli kuwa uwongo nahekaya. Baadhi ya hekaya hubuniwa kwa mshabaha wa upendo;juhudi yenyewe ikimalizikia kutukuza daraja la mwanadamuhadi lile linalokiuka hilo, wakati mwingine hadi kufikia darajala Mungu. Jambo hili limekuwa likitendeka katika dini zilizonyingi zaidi ulimwenguni. Halikadhali tunaiona mandhari iliyokinyume na hakika. Mtume Muhammad s.a.w. aligeuzwa kuwahekaya ya chuki kwa karne nyingi na tabia hii isiyokubalikabado haijakoma. Tafadhalini mnapowahukumu watu,msiwahukumu katika misingi ya hekaya, wahukumuni juu yamisingi ya hali yao ilivyo kwa hakika.

Allah na awabarikini nyote na amani iwe juu yenu. Ahsanteni

Page 33: Mbora wa Manabii - Seal of Prophets

33

SEAL OF THE PROPHETSSwahili Translation

This book was first published as an address delivered by TheHead of the Ahmadiyya Muslim Jamaat at Hounslaw London.The address was shortly tries to clearup some misconceptionsabout the Holy Prophet's life.On the other side the address tries to furnish the true picture ofthe Holy Prophet's life before and after his claim as the Prophetsent by Allah.The address concludes to say that with all these good and noblecharacters of The Holy Founder of Islam it is impossible forhim to be a False Prophet.