mem 84 online.pdf

Upload: jackson-m-audiface

Post on 10-Jan-2016

22.633 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Habari za nisHati &madini

    Toleo No. 84 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 11 - 17, 2015

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

    Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

    Wabunge Soma habari Uk. 2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

    Ni marufuku watoto kumiliki leseni za madini - Serikali

    Wataalam Nishati, Madini, wapigwa msasa Mifumo ya Biashara ya Jotoardhi Soma

    habari Uk. 3

    UK2

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Masolla (aliyesimama), akifungua semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Wengine pichani ni wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Kutoka kushoto ni Placid Kabyemera, Juma Masoud, Mhandisi Nuru Shabani, Mhandisi Gabriel Senge na Tantao Tantao.

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Veronica Simba -Singida

    Imeelezwa kuwa ni marufuku kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa kama wabia wa umiliki wa leseni za madini za aina yoyote hapa nchini.

    Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo wa madini mkoani Singida kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao ujulikanao kama OMCTP (Online Mining Cadastre Transactional Portal.)

    Sheria hairuhusu kutoa leseni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kwa wale watakaobainika kutoa taarifa zisizo za kweli kwa kuwaandikisha watoto walio chini ya umri husika kama wabia wa umiliki wa leseni za madini, watachukuliwa hatua kali za kisheria, alisema Mhandisi Shabani.

    Aidha, Mhandisi Shabani aliwataka washiriki wa semina hiyo na watanzania wote kwa ujumla kufahamu kuwa ni Wizara ya Nishati na Madini pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutoa leseni za madini za aina zote hapa nchini.

    Alitoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya washiriki wa semina kuuliza iwapo kuna mamlaka nyingine nchini zinazoruhusiwa kisheria kutoa leseni za madini.

    Kuna baadhi ya watu au vikundi vya watu au taasisi ambazo zimekuwa zikiingilia zoezi la utoaji wa leseni za madini kwa baadhi ya waombaji nchini. Naamini wanafanya hivyo kwa kutokujua sheria, hivyo ni vyema watu wote wafahamu kuwa hakuna mamlaka nyingine hapa nchini yenye ruhusa ya kutoa leseni za madini kisheria isipokuwa Wizara ya Nishati na Madini pekee, alisisitiza.

    Mhandisi Shabani aliwataka wananchi hasa wamiliki halali wa leseni za madini wanaokumbana na matatizo ya kutotendewa haki kwa kuzuiliwa kuendesha shughuli zao katika maeneo yao kisheria, kutoa taarifa kwa ofisi za madini zilizopo karibu nao ili waweze kupatiwa msaada kwa kufuata sheria.

    Pia, aliwaasa wachimbaji madini wadogo na wamiliki wa leseni pamoja na wananchi wote hususani viongozi wa vijiji, halmashauri na taasisi mbalimbali, kuisoma na kuifahamu Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ili kuepusha migogoro mbalimbali inayotokea kuhusiana na shughuli za uchimbaji wa madini.

    Semina iliyofanyika Singida kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao, ni mwendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima chini ya Wizara ya Nishati na Madini kwa lengo la kuongeza uwazi na kuboresha zaidi huduma za sekta ya madini.

    Ni marufuku watoto kumiliki leseni za madini - SerikaliSehemu ya washiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao iliyofanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Semina hiyo ni mwendelezo wa zoezi la utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchi nzima kuhusu matumizi ya huduma hiyo mpya.

    Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP) kwa Wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 5, mwaka huu mjini Singida.

    Mshiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao, akiuliza maswali wakati wa semina hiyo. Semina ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu.

    Viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mkoani Singida walioshiriki katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao. Wa tatu kutoka kulia (Waliokaa kwenye viti) ni Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati Singida na Kulia kwake ni Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani. Semina ilifanyika Septemba 5, mwaka huu.

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    Five Pillars oF reForms

    KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

    Bodi ya uhariri Mhariri MkUU: Badra Masoud

    MSaNifU: Essy OgundeWaaNdiShi: Veronica Simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    increase eFFiciencyQUality delivery

    oF Goods/servicesatisFaction oF

    tHe clientsatisFaction oF

    BUsiness Partners

    satisFaction oF sHareHolders

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Ni marufuku watoto kumiliki leseni za madini

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Wataalam Nishati, Madini, wapigwa msasa kuhusu Mifumo ya Biashara ya Jotoardhi

    Na Johary Kachwamba, Dar es Salaam

    Imeelezwa kuwa elimu kuhusu mifumo ya kibiashara ya mvuke utokanao na nishati ya jotoardhi ina manufaa

    kwa Taifa kwani itasaidia kujenga uelewa kuhusu utaratibu unaoweza kutumika katika kupanga bei ikiwemo kudhibiti biashara ya jotoardhi.

    Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja Mkuu wa Kampuni inayoshughulikia Nishati ya Jotoardhi Tanzania

    (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe wakati akifungua warsha ya siku tatu iliyofanyika hivi karibuni ambapo ilishirikisha wataalam kutoka TGDC, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wizara ya Nishati na Madini iliyohusu mifumo ya biashara ya jotoardhi.

    Mhandisi Njombe alisema elimu kwa ajili ya mifumo ya kibiashara katika nishati hiyo ni muhimu kwa wadau mbalimbali kwani inawawezesha kuwekeza na kuwa na mchango mkubwa katika sekta ya nishati.

    Akielezea lengo la warsha hiyo Mhandisi Njombe alisema kuwa ni kuwapa wadau mbalimbali uelewa mzuri kuhusu mifumo mizuri ya kibiashara ambayo itasaidia Tanzania na jamii kwa ujumla kunufaika na nishati hiyo, lengo likiwa ni kupata faida

    kwa Serikali na kuweza kutumia faida hiyo kusaidia jamii ya Watanzania.

    Wakati huohuo akizungumza katika warsha hiyo, mtaalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Anastas Mbawala alisema EWURA kama mdau mkubwa wa nishati hiyo, mwaka jana iliingia katika maandalizi ya mifumo ambayo itasaidia kudhibiti biashara ya umeme utokanao na jotoardhi.

    Alisema moja ya majukumu waliyopewa na Wizara ya Nishati na Madini katika maandalizi hayo lilikuwa ni pamoja na kuandaa mikataba elekezi inayohusiana na nishati ya jotoardhi.

    Ni wakati muafaka sasa kwa wataalam kutoka nje kuipitia mikataba yetu elekezi na kutoa maoni ili kufanyiwa maboresho kabla ya kuanza kutumika,alisema Mhandisi Mbawala

    Sekta ya Madini imekuwa ikikua kwa kasi tangu mwaka 1992 na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Kutokana na ukuaji wa sekta hiyo wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wamekuwa wakiwekeza kwa wingi katika sekta ya madini kupitia uchimbaji wa madini. Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikitunga na kusimamia sera na sheria mbalimbali za madini ili uchimbaji madini nchini uwe na manufaa kwa nchi bila kuleta athari katika jamii na mazingira yake.

    Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, zimeweka wazi suala la kuzuia umilikishaji wa leseni na ajira kwa watoto.

    Kumekuwepo na taarifa kuhusu matukio ya watoto wenye umri chini ya miaka 18 kujihusisha na uchimbaji wa madini katika baadhi ya maeneo nchini badala ya kuhudhuria shuleni hivyo kuchangia kiwango cha elimu kushuka katika maeneo husika.

    Sheria ya madini ya mwaka 2010 kifungu Namba 8 kinazuia mtu mwenye umri chini ya miaka 18 kujihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini.

    Hivi karibuni akizungumza katika semina ya wachimbaji wa madini mkoani Singida kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao ujulikanao kama OMCTP (Online Mining Cadastre Transactional Portal.), mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani alieleza kuwa ni marufuku kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa kama wabia wa umiliki wa leseni za madini za aina yoyote hapa nchini.

    Alifafanua kuwa sheria hairuhusu kutoa leseni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kusisitiza kuwa kwa wale watakaobainika kutoa taarifa zisizo za kweli kwa kuwaandikisha watoto walio chini ya umri husika kama wabia wa umiliki wa leseni za madini, watachukuliwa hatua kali za kisheria.

    Tunachukua fursa hii kuwaomba wamiliki wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini katika maeneo yenye madini kutowahusisha watoto wenye umri chini ya miaka 18 katika shughuli za uchimbaji madini.

    Ieleweke kwamba, watoto hawa ni taifa la kesho hivyo kuwashirikisha katika shughuli za madini badala ya kusoma ni kuwanyima haki yao ya msingi.

    Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe akichangia mada katika warsha kuhusu mifumo mbalimbali ya biashara kwa soko la jotoardhi. Warsha hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 2 4 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Mnaotaka leseni za madini jisajilini kwenye mfumo mpya SerikaliNa Veronica Simba - Shinyanga

    Serikali imewataka wananchi wote wenye malengo ya kumiliki leseni za madini nchini kujisajili katika mfumo mpya wa huduma

    za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao.

    Wito huo ulitolewa hivi karibuni mjini Shinyanga na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani wakati wa Semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni hai za madini kuhusu matumizi ya mfumo huo mpya wa utoaji leseni za madini.

    Mhandisi Shabani alisema kuwa mfumo husika umeweka mazingira wezeshi kwa mtu yeyote mwenye leseni hai na hata yule asiye na leseni kuweza kujisajili.

    Hivyo, tunawashauri wale wote wenye malengo ya kumiliki leseni za madini siku zijazo wasisubiri,

    bali wajisajili kwenye mfumo huu mpya ili mfumo uwatambue na wakati watakapotaka kuomba leseni, itakuwa rahisi kwao kwani watapaswa tu kukamilisha sehemu iliyobaki ya usajili ambayo ni maombi ya leseni, alisisitiza.

    Akizungumzia faida za kujisajili kwenye mfumo huo mpya wakati huu badala ya kusubiri mpaka pale watakapotaka kuomba leseni, Mhandisi Shabani alisema pamoja na mambo mengine, itasaidia kupunguza gharama za usajili.

    Tukumbuke kwamba gharama za usajili kwenye mfumo huu zitakuwa zikibadilika kulingana na hali halisi ya gharama za maisha, hivyo kwa atakayeweza kujisajili muda huu atatumia gharama nafuu zaidi, alisema.

    Aidha, akitoa ufafanuzi kwa swali lililoulizwa na mmoja wa washiriki wa semina, kuhusu changamoto kwa wale wasioweza kutumia kompyuta, kutokana na mfumo husika kuwa katika mtandao,

    Mhandisi Shabani aliwataka wamiliki wa leseni kuondoa hofu kwani Sheria ya Madini inamruhusu mmiliki au mwombaji wa leseni za madini kuwa na Wakala anayeweza kusimamia kazi zake.

    Unaweza kuteua Wakala ambaye ni mwanao, rafiki yako, jirani yako au mtu yeyote unayemwamini ili aweze kusimamia kazi zako. Hivyo basi, tunashauri kuwa kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kutumia kompyuta watafute mawakala wenye sifa za kuweza kusimamia shughuli zao, alifafanua.

    Vilevile, Mhandisi Shabani alisema kuwa kwa wale ambao hawawezi kutumia kompyuta na hawataki kuteua mawakala wa kusimamia kazi zao, Wizara imeweka utaratibu wa kutoa huduma hiyo katika ofisi zote za madini nchini.

    Alisema kuwa kila Ofisi ina Dawati ambalo lina Maofisa wanaofanya kazi maalum ya

    kutoa huduma ya kuwasajili wateja wanaohitaji huduma hiyo isipokuwa akatahadharisha kuwa kwa upande wa malipo, mteja atatakiwa kufanya malipo kupitia simu yake ya mkononi.

    Awali, akifungua Semina hiyo, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi, Humphrey Mmbando aliwataka washiriki kuhakikisha wanaufahamu mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP) kwani ni wale tu watakaosajiliwa kwenye mfumo husika ndiyo watakaotambuliwa kisheria na kupata haki zote za msingi.

    Zoezi la utoaji semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini linaendeshwa na wizara ya nishati na madini nchi nzima ambapo mkoani Shinyanga wachimbaji zaidi ya 60 wamepatiwa mafunzo hayo.

    Mtaalamu kutoka Kitengo cha Leseni cha Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani, akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP) kwa wachimbaji wa madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga.

    Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kati Magharibi, Humphrey Mmbando akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala muhimu yaliyojitokeza wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP). Semina hiyo ilifanyika Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa nchi nzima kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini. Wengine pichani (mstari wa mbele) ni baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Madini Shinyanga.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Wachimbaji Madini Mpwapwa wapewa semina ya matumizi ya OMCTPNa Samwel Mtuwa - Dodoma

    Wizara ya Nishati na Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Dodoma hivi karibuni ilitoa

    semina elekezi kuhusu utumaji wa maombi ya leseni za madini kwa njia ya mtandao ( Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) kwa wachimbaji wadogo kutoka katika vijiji vya Kibakwe , Chogola, Winza, Gulwe, Tambi, na Magai Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

    Semina hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Afya wilayani Mpwapwa ililenga kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo katika kutuma maombi ya leseni za madini kwa njia mtandao.

    Akizungumza na MEM Bulletin Afisa Madini Mkazi Dodoma , Silimu Mtigile alisema Wizara kupitia kitengo cha huduma za leseni za madini ilizindua mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao ili kuweza kutoa huduma kwa haraka, kuongeza uwazi na kumwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe.

    Silimu alisema kuwa mfumo

    huu una faida mbalimbali kwa mmiliki wa leseni ya madini kama vile kumwezesha kuwasilisha maombi mapya, kuhuisha leseni yake , kufanya malipo kupitia mtandao , kurudisha leseni , kuongeza au kupunguza ukubwa wa leseni kulingana na mahitaji yake.

    Aliendelea kusema kuwa mfumo huu wa OMCTP unatumika katika aina tano za leseni za madini ambazo ni leseni za utafutaji mdogo wa madini , leseni za uchimbaji mdogo wa madini , leseni za utafutaji mkubwa wa madini , leseni za uchimbaji wa kati wa madini na leseni za uchimbaji mkubwa wa madini .

    Akizungumzia kuhusu matumizi ya mfumo huu, Silimu alisema kuwa mfumo huu unahusisha wamiliki wawili tu ambao ni Afisa wa leseni ambaye atakuwa na uwezo wa kuhakiki leseni za mteja , kusajili na kurekebisha taarifa za mteja na mmiliki wa leseni ambaye atakuwa na uwezo wa kusimamia leseni zake na kufuatilia taarifa za leseni yake na kufanya malipo yeyote anayodaiwa kwa njia ya simu au kadi maalum ya malipo (smart card).

    Aliongeza kuwa mfumo huu pia utamwezesha mteja kufanya

    maombi mapya na kuwasilisha taarifa za madini ikiwa ni pamoja na kuhamisha leseni husika.

    Aliendelea kusema kuwa kulingana na teknolojia itumikayo katika mfumo wa OMCTP , mtumiaji atatakiwa kuwa na barua pepe yaani (E-mail) kwa ajili ya kuingiza taarifa zake pamoja na namba za simu ya mkononi ambayo ni muhimu kwa ajili ya kupata taarifa za leseni na kufanya malipo anayodaiwa.

    Akielezea kuhusu hatua za kusajiliwa, Silimu alieleza kuwa ili mmiliki wa leseni aweze kusajiliwa anatakiwa kujaza fomu maalumu ya usajili, pamoja na kuwa na kitambulisho kinachokubalika kisheria mfano kitambulisho cha mpiga kura ,leseni ya udereva,hati ya kusafiria, utambulisho wa mlipa kodi(Tin Namba) au kitambulisho chochote cha mfuko wa hifadhi ya jamii .

    Alisisitiza kuwa kwa upande wa mwakilishi wa kampuni inayomiliki leseni, mwombaji atatakiwa awe na nyaraka kama za mmiliki binafsi wa leseni pamoja barua ya utambulisho wa kisheria kutoka kwa mmiliki wa kampuni, cheti cha usajili wa kampuni na anwani za mawasiliano kama vile barua pepe

    na namba ya simu ya mkononi.Akizungumzia kuhusu

    kuunganishwa na mifumo mingine Silimu alisema kuwa, mfumo huu una uwezo wa kumuunganisha mmiliki wa leseni na mifumo mingine ya taasisi nyingine kama vile Mmlaka ya Mapato (TRA), benki na mfumo ya vitambulisho vya kitaifa.

    Akielezea matarajio katika mfumo huu Silimu alisema mfumo huu utawezesha kuwepo kwa takwimu sahihi za maombi ya leseni, kuepusha migogoro katika muingiliano wa viwanja , kuongezeka uwazi katika sekta ya madini , maombi ya leseni za madini kufanyiwa kazi kwa haraka kwa kuzingatia sheria na waombaji wote wa leseni kufanya maombi kupitia njia ya mtandao.

    Mnamo Juni 8, 2015 Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao ili kuongeza uwazi na kumwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe , mfumo huu ni rahisi kutumia na upo chini ya sheria ya Madini ya mwaka 2010 kwa kuzingatia kanuni na taratibu zake.

    Afisa Madini Mkazi Dodoma Mhandisi Silimu Mtigile , akitoa semina kwa wachimbaji wadogo mkoani Dodoma kuhusu mfumo mpya wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal ; OMCTP) Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa wachimbaji madini uelewa wa matumizi ya huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao.

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    MATUKIO KATIKA PICHA

    Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Cradle Resources, Davey Grant akimkabidhi zawadi ya picha Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja baada ya kutembelea ofisi za kampuni hiyo mjini Perth Australia wakati wa mkutano wa Africadownunder 2015 uliofanyika hivi karibuni. Kampuni ya Cradle Resorces itafanya shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Songwe Mkoani Mbeya lililokuwa likimilikiwa na Gereza la Songwe pamoja na kujenga upya miundombinu ya gereza hilo ili kutumika kwa matumizi mengine ya kijamii baada ya gereza hilo kuhamishwa.

    Ujumbe wa Wizara ya Nishati na Madini ukiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa kampuni ya Cradle Resource, mara baada ya kukabidhiwa zawadi walipotembelea ofisi ya kampuni hiyo mjini Perth nchini Australia. Katikati ni Kamishna wa Madini Mhandisi Paul Masanja (aliyeshika picha), kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deudatus Kinawiro aliyeambatana na ujumbe huo na kulia kwa Kamishna Masanja ni Mhandisi Salim Salim.

    Mhandisi wa Migodi Assa Mwakilembe (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji ya Cradle Resources, Davey Grant zawadi ya sanamu ya ndege iliyotengezwa kutokana na moja ya madini yanayopatikana nchini baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini, mjini Perth nchini Australia wakati wa mkutano wa Africadownunder 2015

    Mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Juma Masoud akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa wakati wa Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP). Semina hiyo ilifanyika Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara husika kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini kote.

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    MATUKIO KATIKA PICHA

    Baadhi ya Vijana ambao ni wamiliki wa leseni za madini mkoani Shinyanga wakiwa katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining cadaster Transactional Portal OMCTP) yanayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini nchi nzima. Kutoka Kushoto ni Juma Swalehe, Steven Ngonyani, Salum Abdallah na Meshack Daniel. Mafunzo hayo kwa mkoa wa Shinyanga, yamefanyika Septemba 9, 2015.

    Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Erick Mkoma, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Madini Kanda ya kati Magharibi iliyoko mjini Shinyanga. Wengine pichani ni Juma Masoud (katikati) na Mhandisi Nuru Shabani (Kulia). Wataalam hawa Septemba 9, 2015 walitoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini mkoani Shinyanga kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandano (Online Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP).

    Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja katika warsha kuhusu mifumo mbalimbali ya biashara kwa soko la jotoardhi. Warsha hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 2 4 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.

    Mtaalam kutoka Shirika linaloshughulikia masuala ya Jotoardhi Afrika Mashariki (EAGER), John Heath akisisitiza jambo katika warsha kuhusu mifumo mbalimbali ya biashara kwa soko la jotoardhi. Warsha hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 2 4 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Tanzania yashiriki katika mkutano wa baraza la kisekta kuhusu nishati Afrika Mashariki NA Mwandishi Wetu

    Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini inashiriki katika mkutano wa Baraza la Kisekta kuhusu nishati Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha kuanzia

    tarehe 7 hadi 11 Septemba 2015 mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa

    Kamishna wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Hosea Mbise mkutano huo unajumuisha wataalamu kutoka katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika

    Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.

    Lengo la mkutano huo ni kutathmini utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Kisekta pamoja na masula mengine muhimu katika sekta ndogo tatu za nishati hususani nishati jadidifu na matumizi bora ya nishati; mafuta na gesi, pamoja na umeme.

    Shughuli za mkutano huo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Wataalam, Makatibu Wakuu na Mawaziri.

    Kamishna wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise.

    Na Mwandishi Wetu, Bangkok

    Maonesho ya 56 ya vito na usonara yameanza kwa kishindo jijini Bangkok, Thailand huku Tanzania ikiwa imengara kutokana

    na madini ya Tanzanite kuzalishwa katika nchi ya Tanzania pekee duniani.

    Maonesho ya kimataifa ya vito na usonara yameanza rasmi tarehe 10 hadi 14 ambapo hufanyika kila mwaka nchini Thailand na kukutanisha wauzaji na wanunuzi wa madini ya vito na usonara duniani.

    Katika maonesho hayo ambapo wachimbaji na wauzaji wa madini wanashiriki ili kujitangaza pamoja na kutafuta masoko ya madini yao kwa sasa na katika siku zijazo ambapo wanunuzi wengi wamejitokeza na kutaka kujua utaratibu wa kuweza kununua madini hususan ya vito mbalimbali yanayopatikana Tanzania.

    Wanunuzi hao wengi wamejitokeza kutoka katika nchi za Brazil, Canada, India, Thailand, Hongkong na Marekani ambapo pia wameahidi kushiriki katika maonesho ya kimataifa ya vito ambayo yatafanyika mjini Arusha.

    Lengo la Tanzania kushiriki maonesho hayo nchini Thailand ni kutangaza madini ya vito mbalimbali yaliyopo nchini ikiwamo Tanzanite ambayo inapatikana Tanzania pekee katika eneo la Mererani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.

    Aidha, ziara hiyo pia inatoa fursa kubwa kwa Taifa la Tanzania hususan katika sekta ya Madini kuvutia wanunuzi mbalimbali duniani wanaoshiriki maonesho ya Bangkok kuja pia Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya vito yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha kununua madini ya vito na kuufanya mji wa Arusha kuwa kituo

    kikubwa cha madini ya vito katika bara la Afrika.

    Ni dhahiri kwamba maonesho hayo ya vito Bangkok ni jitihada za serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini hususan Idara ya Madini kuwatafutia masoko wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hasa wale wadogo.

    Katika maonesho hayo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hasa ya vito wanapata mawasiliano kwa wanunuzi mbalimbali wa kimataifa badala ya kuwatumia madalali ili kuweza kuuza madini yao kwa wanunuzi walengwa na kuuza madini kwa bei nzuri na hatimaye kupata faida maradufu.

    Maonesho hayo ya vito yanatoa fursa pia kwa sekta nyingine kujitangaza pamoja na kuitangaza Tanzania duniani mathalani sekta ya utalii ambapo madini ya vito yanakwenda pia na ujumbe wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwamo mbuga za wanyama pamoja na mlima wa Kilimanjaro.

    Tanzanite yaingarisha Tanzania katika maonesho ya vito Bankok

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA RUZUKU AWAMU YA PILI KWA WACHIMBAJI WADOGO

    Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini inaendelea kutekeleza azma yake ya kuwawezesha wachimbaji wadogo nchini kimtaji na kiteknolojia ili waweze kuongeza tija na ufanisi

    katika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini. Moja ya hatua iliyochukuliwa na Serikali ni kuwapatia ruzuku. Awamu ya Kwanza ya utoaji ruzuku ilifanyika Aprili, 2014 ambapo jumla ya Dola za Marekani 511,000 zilitolewa kwa wachimbaji wadogo 11.

    Utaratibu uliotumika kupokea maombi ya Ruzuku Awamu ya Kwanza ulikuwa ni: waombaji kupeleka maombi yao moja kwa moja Benki ya TIB; Benki ya TIB kuchuja majina ya waombaji ili kubaki na majina machache ya waombaji wenye sifa; Kamati ya Tathmini (Screening Team) kuundwa na Wizara ili kupitia na kuhakiki uhalali wa maombi yaliyovuka mchujo wa kwanza na hivyo kupata majina ya wale wanaopendekezwa kupewa ruzuku; majina hayo kupelekwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kwa ridhaa; TIB kusaini mikataba na washindi; na hatimaye ruzuku kutolewa kwa washindi.

    Kutokana na uzoefu tulioupata wakati wa kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Utoaji Ruzuku, utaratibu mpya wa utoaji ruzuku ulianzishwa kwa ajili ya Ruzuku Awamu ya Pili. Utaratibu huo unahusisha hatua zifuatazo: maombi kuwasilishwa kwa Maafisa Madini mikoani ambao kimsingi ndio wanawafahamu vyema waombaji; Maafisa Madini Kanda kuhakiki maombi husika na kutoa mapendekezo kwa Kamishna wa Madini kwa kuzingatia hali halisi ya mradi unaoombewa ruzuku na kiasi cha fedha zilizoombwa; Kamishna wa Madini kufanya uhakiki zaidi wa maombi yaliyopokelewa; Kamati ya Tathmini (Screening Team) kuundwa ili kupitia maombi yote kwa kuzingatia Mwongozo wa Utoaji Ruzuku Awamu ya Pili; mapendekezo ya Screening Team kuwasilishwa kwa Kamishna wa Madini; Kamishna wa Madini kufanya uhakiki wa mwisho wa majina ya washindi kwa kushirikiana na Maafisa Madini Kanda; mapendekezo ya majina ya washindi kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu - Wizara ya Nishati na Madini kwa ridhaa; na majina ya washindi wa ruzuku kupelekwa TIB kwa ajili ya kusaini mikataba kabla ya ruzuku kutolewa.

    Tangazo kwa umma la kuanza kupokea maombi ya Ruzuku Awamu ya Pili lilitolewa na Wizara tarehe 23 Februari, 2015 ambapo waombaji walitakiwa kuwasilisha maombi yao kwa Maafisa Madini mikoani kabla ya tarehe 27 Machi, 2015. Jumla ya maombi 750 yalipokelewa kupitia Ofisi za Madini

    mikoani ambapo jumla ya fedha zilizoombwa ni Shilingi 122,140,013,986. Fedha iliyopo kwa ajili ya Ruzuku Awamu ya Pili ni Shilingi 7,200,000,000 sawa na asilimia 6 tu ya kiasi cha fedha kinachotakiwa kutolewa kwa waombaji wote.

    Kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika, jumla ya wachimbaji wadogo 111 wameshinda kupatiwa ruzuku katika Awamu ya Pili ambapo jumla ya Shilingi 7,194,500,000 zitatolewa. Majina ya washindi yametolewa katika Taarifa hii. Wahusika watajulishwa rasmi kwa barua na kupewa maelekezo mahsusi kuhusiana na zoezi hilo.

    Ruzuku Awamu ya Pili imetolewa kwa kuzingatia idadi ya maombi yaliyopokelewa katika kila Kanda, jumla ya fedha iliyoombwa, na ukubwa na Kanda husika. Kwa kuzingatia utaratibu huo, Kanda ya Mashariki yenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga imetoa washindi 13; Kanda ya Kati yenye mikoa ya Singida na Dodoma imetoa washindi 10; Kanda ya Kati Magharibi yenye mikoa ya Shinyanga na Tabora imetoa washindi 9; Kanda ya Ziwa Victoria Mashariki yenye mikoa ya Mara na Simiyu imetoa washindi 10; Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi yenye mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera imetoa washindi 11; Kanda ya Ziwa Nyasa yenye mikoa ya Ruvuma na Njombe imetoa washindi 6; Kanda ya Kaskazini yenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara imetoa washindi 12; Kanda ya Kusini yenye mikoa ya Mtwara na Lindi imetoa washindi 18; Kanda ya Kusini Magharibi yenye mikoa ya Mbeya na Iringa imetoa washindi 10; na Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma imetoa washindi 12.

    Pia, tathmini iliyofanyika ya maombi ya ruzuku imesaidia kuwapata wachimbaji wadogo 179 ambao wamekidhi vigezo vya kupatiwa ruzuku lakini hawataweza kupata ruzuku katika Awamu hii ya Pili kutokana na ukosefu wa fedha. Serikali itaendelea kutoa ruzuku kwa washindi hao ambao wapo kwenye orodha ya akiba kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

    Tunawapongeza wote walioshinda kupewa ruzuku Awamu ya Pili na tunawahimiza kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

    Imetolewa na:KAIMU KATIBU MKUUWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    03/9/2015

    ORODHA YA MAJINA YA WASHINDI WA RUZUKU AWAMU YA PILI

    4

    ORODHA YA MAJINA YA WASHINDI WA RUZUKU AWAMU YA PILI

    Kanda ya Mashariki Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Jumanne Maro Mokili PML 0021889

    2. Raha Kikoba Group Morogoro

    MAMA LISHE

    3. Kilosa Mining Company Ltd

    PML 0016998

    4. Rehema Enteprises Leseni ya Biashara 5. M/S Steven Petro

    Fataki PML 010645

    6. Bishagazi Yakhub Mgimbwa

    PML 0003227

    7. Msengo Mining Co. Ld PML 003335 8. Abdallah Juma Said

    /Kiwakoki Group PML011436EZ

    9. Salim Seif Kirungi PML 008718 EZ

    10. Kunjelo Ngombale Mwiru

    PML 004239 EZ

    11. Manyangwa Company Ltd & Partners

    PML 006668 EZ

    12. Ramadhani Mohamedi Hamisi

    PML 002423 EZ

    13. ABM Equipment Services Ltd

    PML 004063 EZ

    Kanda ya Kati Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Aminika Gold Mine

    Cooperative Society PML003808CZ

    2. Elizabeth Shango PML006944 3. Kikundi cha Amani HC/CBO/074 4. Emanuel Mbasha PML004647CZ

    5. Yusufu Mwandami Gwayaka

    PML006891

    6. Ernest Mshumbusi Kato PML003365 7. Bakary H. Kahinda &

    Partners PML003198CZ

    8. Valence Ngabani PML006956CZ

    9. Beda Mughusi Kitiku PML0016359 10. Yusufu Daudi

    Semuguruka PML0017498

    5

    Kanda ya Kati Magharibi Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Erick Sunday

    Byaruhanga & Partners PML000797CWZ

    2. Samwel Mchele Chitalilo na Mwenzake

    PML001078CWZ

    3. Nyangalata Mining Cooperative Society LTD

    PML000794CWZ

    4. Kasi Mpya Gold Miners Cooperative Society LTD

    PML0014673CWZ

    5. Jamal Ally Radman & Partners

    PML000748CWZ

    6. Shigitwa Gold Mine Cooperative Society LTD

    PML001445CWZ

    7. Kash Daud Gacha Biashara (Karakana) 8. Joseph Sala Sagayi PML0000772 9. Abdallah Sadiki Msumeno

    Kawika PML0004323

    Kanda ya Ziwa Victoria Mashariki Na.

    Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Josephat Muniko Mwita PML002321 2. Naigoti Gold Mines Limited PML001899 3. Virginia Mkandala &

    Samson Gesase PML000851

    4. Juma Mabura Salt Mining PLM 000826 5. Nyorogore Miners Co-

    operative Society Limited PML000022

    6. Pathane Tanzania Limited PML00232

    7. Nemco Quality Product PML 3061 8. Mwangaza Mining Co-

    operative Society Ltd PML000978

    9. Magunga Mining Co-operative Society Ltd

    PML00119

    10 Dorica Kitamara PML002728

    Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi Na.

    Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Inuka Geita Town CBO 163 2. Mgusu Miners Cooperative

    Society LTD PML00043LZW

    3. Epson Limited B-01710612 4. M/S Isamilo Miners Saccos

    LTD 001044LZ

    5. Thomas Lugangira PML 0013109 6. Adamu Ally Horoma Leseni ya Uchenjuaji 7. Adam Mohamed Mahamud PML5996 8. Amad Issa PML16792

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    5

    Kanda ya Kati Magharibi Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Erick Sunday

    Byaruhanga & Partners PML000797CWZ

    2. Samwel Mchele Chitalilo na Mwenzake

    PML001078CWZ

    3. Nyangalata Mining Cooperative Society LTD

    PML000794CWZ

    4. Kasi Mpya Gold Miners Cooperative Society LTD

    PML0014673CWZ

    5. Jamal Ally Radman & Partners

    PML000748CWZ

    6. Shigitwa Gold Mine Cooperative Society LTD

    PML001445CWZ

    7. Kash Daud Gacha Biashara (Karakana) 8. Joseph Sala Sagayi PML0000772 9. Abdallah Sadiki Msumeno

    Kawika PML0004323

    Kanda ya Ziwa Victoria Mashariki Na.

    Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Josephat Muniko Mwita PML002321 2. Naigoti Gold Mines Limited PML001899 3. Virginia Mkandala &

    Samson Gesase PML000851

    4. Juma Mabura Salt Mining PLM 000826 5. Nyorogore Miners Co-

    operative Society Limited PML000022

    6. Pathane Tanzania Limited PML00232

    7. Nemco Quality Product PML 3061 8. Mwangaza Mining Co-

    operative Society Ltd PML000978

    9. Magunga Mining Co-operative Society Ltd

    PML00119

    10 Dorica Kitamara PML002728

    Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi Na.

    Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Inuka Geita Town CBO 163 2. Mgusu Miners Cooperative

    Society LTD PML00043LZW

    3. Epson Limited B-01710612 4. M/S Isamilo Miners Saccos

    LTD 001044LZ

    5. Thomas Lugangira PML 0013109 6. Adamu Ally Horoma Leseni ya Uchenjuaji 7. Adam Mohamed Mahamud PML5996 8. Amad Issa PML16792

    6

    9. James Mulela & PTNS PML1084 10. Kikundi Cha

    Nyanghomango PML001039LVW

    11. Christopher M. Kadeo PML00261

    Kanda ya Ziwa Nyasa

    Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Menas Mbunda Andoya PML004116SZ 2. Isaya Boniface Mhagama PML0004051SZ 3. John D. Njau PML0009911SZ 4. Kilelevana PML000195SWZ 5. Johnson Kenneth

    Nchimbi PML000004SZ

    6. Deograsias V. Tarimo PML003619SW

    Kanda ya Kaskazini Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Pili Mzuri Mughamba PML0010037

    2. Joseph Naaman PML 001830NZ 3. Paul K. Tarimo PML002468NZ 4. Rose Justo Swai PML001690NZ 5. Vuasu Ar Co. PML000622NZ 6. G & T International

    Limited PML002289NZ

    7. Menner Alfred Msofe PML000623NZ 8. Uwami Youth Group Muungano wa 13 PMLS 9. Charles Qwari Agent For

    Kijiji Cha Gendabi PML000436NZ

    10. Pili Hussein Mpondo PML002892NZ 11. Manyara Mining Co. Ltd PML001051NZ 12. Suzie Dida Kennedy Lapidary License

    Kanda ya Kusini Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Umoja wa Vijana

    Uchimbaji Madini PML003597SZ

    2. Salumu Juma Mohamed PML001278SZ

    3. Ahamadi Saidi Samli PML002163SZ 4. Kenneth Edward Nipepe PM004477SZ 5. Salum Mohamedi Kitenge PML0002994 6. Mohamed S. Mshangani PM000129SZ 7. Mohamed Abdurahmani

    Abood PML004631SZ

    8. Mishindo Salt Works PML004351SZ 9. Omary Ally Issa PML000203SZ 10. Mohamed Ally Zubery PML003878SZ 11. Hamad Ahmad Abdallah PML004642SZ 12. Abdallah Ally Esmail PML004427SZ 13. Ally Esmail Ally PML004311SZ 14. Issa Ajaly PM004214SZ 15. Haji Rashidi Chijinga PM000196SZ 16. Mwinyimkuu Seleman PML0003294SZ

    7

    Dalali & Ptn 17. Salama Saidi Bakiri Leseni ya mama ntilie 18. Mohamed Nassoro

    Khalfani PML004312SZ

    Kanda ya Kusini Magharibi Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Ernest O. Mgogo PML0001922SWZ 2. Wikangulu Investment PML0000940SWZ 3. Ben Elias PML000365SWZ 4. Mwanaidi O. Sembo PML0005SWZ 5. Gervas Maganga PML0000915 6. Ephraim G. Malesa PML 0000732 7. Ihanzutwa Gold Mine Ltd PML000490SWZ 8. Aidan A. Msigwa PML00061SWZ 9. Mbeya Quarry Associate Ltd PML00372 10. Jose H. Musyani PML0011131SWZ

    Kanda ya Magharibi Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Aifola Investment Co. Ltd PML 001699WZ

    2. Augustino James Ruronona & Partners

    PML 001624 WZ

    3. Pius Kipeche 10295

    4. Amri Chande & Sospeter Ernest

    PML 0002234

    5. Shija Sombi & Part PML0000130

    6. Tani Maarufu Idd PML 001745 WZ

    7. Said Selemani Sanyeo PML000237WZ

    8. Rhoda J. Simtenda PM L000465WZ

    9. Josephat Gwanchele PML 0013003WZ

    10. Makidongo Mining Co. Ltd PML001499WZ

    11. Yona Ntimba Dyamvunye PML 000239

    12. Mlele Resources PML 0000131WZ

    ORODHA YA MAJINA YA WASHINDI WA RUZUKU AWAMU YA PILI

    6

    9. James Mulela & PTNS PML1084 10. Kikundi Cha

    Nyanghomango PML001039LVW

    11. Christopher M. Kadeo PML00261

    Kanda ya Ziwa Nyasa

    Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi

    1. Menas Mbunda Andoya PML004116SZ 2. Isaya Boniface Mhagama PML0004051SZ 3. John D. Njau PML0009911SZ 4. Kilelevana PML000195SWZ 5. Johnson Kenneth

    Nchimbi PML000004SZ

    6. Deograsias V. Tarimo PML003619SW

    Kanda ya Kaskazini Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Pili Mzuri Mughamba PML0010037

    2. Joseph Naaman PML 001830NZ 3. Paul K. Tarimo PML002468NZ 4. Rose Justo Swai PML001690NZ 5. Vuasu Ar Co. PML000622NZ 6. G & T International

    Limited PML002289NZ

    7. Menner Alfred Msofe PML000623NZ 8. Uwami Youth Group Muungano wa 13 PMLS 9. Charles Qwari Agent For

    Kijiji Cha Gendabi PML000436NZ

    10. Pili Hussein Mpondo PML002892NZ 11. Manyara Mining Co. Ltd PML001051NZ 12. Suzie Dida Kennedy Lapidary License

    Kanda ya Kusini Na. Jina Namba ya Leseni/Mradi 1. Umoja wa Vijana

    Uchimbaji Madini PML003597SZ

    2. Salumu Juma Mohamed PML001278SZ

    3. Ahamadi Saidi Samli PML002163SZ 4. Kenneth Edward Nipepe PM004477SZ 5. Salum Mohamedi Kitenge PML0002994 6. Mohamed S. Mshangani PM000129SZ 7. Mohamed Abdurahmani

    Abood PML004631SZ

    8. Mishindo Salt Works PML004351SZ 9. Omary Ally Issa PML000203SZ 10. Mohamed Ally Zubery PML003878SZ 11. Hamad Ahmad Abdallah PML004642SZ 12. Abdallah Ally Esmail PML004427SZ 13. Ally Esmail Ally PML004311SZ 14. Issa Ajaly PM004214SZ 15. Haji Rashidi Chijinga PM000196SZ 16. Mwinyimkuu Seleman PML0003294SZ

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA TANSORT KWA MWAKA 2014/15

    TANSORT ni kitengo cha uchambuzi na uthamini wa madini ya almasi na vito chini ya Wizara ya Nishati na Madini. Uchambuzi na uthamini unaofanywa na kitengo unalenga kuwezesha ukokotoaji sahihi wa mrabaha wa Serikali kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Vifungu vya 87, 88 na 89.

    Uthamini wa almasi na vito ulifanyika katika ofisi zifuatazo: KandayamasharikiDaresSalaam Kandayakaskazini-Arusha Kandayakatimagharibi-Shinyanga KandayaZiwaNyasa-Songea MakaomakuuyawizaraMEMQH AntwerpUbelgiji;Usimamiziwamauzo

    ya WDL

    MALENGO YA BAJETI 2014/15

    Katika mwaka wa fedha wa 2014/15, Kitengo kililenga kushirikiana na Idara, Vitengo na Taasisi zinazohusika na sekta ya madini katika kuiwezesha Wizara kutekeleza jukumu la Kuboresha usimamizi na uendelezaji rasilimali za Madini kwa manufaa ya Taifa.

    MAJUKUMU YA KITENGO

    1. Kuchambua na kuthamini madini ya almasi na vito vya rangi pamoja na kutoa huduma za Kijemolojia;

    2. Kusimamia mauzo ya almasi na vito pamoja na kufanya tafiti za masoko na bei za madini hayo kwenye masoko ya kimataifa;

    3. Kupata vitendea kazi vya kutosha, kujenga uwezo wa Kitengo kiutendaji na kulipa mishahara na stahili za watumishi wa Kitengo ipasavyo.

    MATOKEO YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2014/15

    A. ALMASI Carat 237,196.21za almasi zenye thamani

    ya Dola za Kimarekani milioni 69.22 zilithaminishwa;

    MrabahauliokusanywanaSerikalikutokanana kazi hiyo ni Dola za Kimarekani milioni 3.46 sawa na Shilingi bilioni 6.30 za Kitanzania;

    Minada 6 ya mauzo ya almasi zaWDLilisimamiwa huko Antwerp Ubelgiji;

    Thamini9zilifanyikakatikakampuniyaElHillal Minerals Ltd;

    Thamini 36 zilifanyika kwa kampuninyingine 14 zinazojihusisha na biashara ya almasi.

    B. VITO VYA RANGI Kilogramu milioni 2.28 za madini ya

    mapambo (Ornamental stones), Gramu milioni 2.00 za madini ya vito ghafi (rough gemstones) na carat 479,688 za madini ya vito vilivyochongwa yalithaminiwa;

    Madini hayo yalithaminiwa kwa Dola zaKimarekani milioni 49.16;

    Serikali ilikusanya Mrabaha wa Shilingibilioni 2.97;

    Thamini1630zilifanyikakatikamakampuni149 ya madini ya vito.

    Masoko9yaKimataifa yaalmasinavitoduniani yalifatiishwa;

    HongKong(2),Bangkok,Antwerp(2),LasVegas, Colombo, and Arusha (2).

    Kitengokilichapishamatoleo3yabeielekeziza almasi na vito;

    Uelimishaji umma ulifanyika katikaMaonesho ya Sabasaba, Nanenane na Wiki ya Utumishi wa umma.

    MAFANIKIO

    Wastaniwa bei ya almasi yetu umepandakwa 2% toka US$/ct 285.54 (2013/14) hadi US$/ct 291.83 katika soko la dunia;

    Mauzo ya almasi yalipanda kwa 12% ki-uzito na 14% kwa thamani ikilinganishwa na 2013/14; hivyo kusababisha makusanyo ya mrabaha kupanda kwa 14%;

    SeminayaIIIyakilamwakayawajemolojiailifanyika kwa mafanikio huko Bagamoyo Pwani.

    CHANGAMOTO

    Kutokuwepo jengoau sehemumahsusi yakufanyia biashara ya madini ya thamani kubwa hapa nchini;

    Kutokuwepokwasatellitecenterszamauzoya madini ya vito hususan sehemu za uchimbaji wa madini hayo;

    Ukwepaji wa kodi na tozo za Serikali nautoroshwaji wa madini ya vito hasa miongoni mwa wazalishaji na wafanyabiashara wadogo wa madini ya vito hususani Tanzanite.

  • 12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

    providingGEO-SCIENTIFIC INVESTIGATIONS COUNTRYWIDE.Geological Survey of Tanzania (GST)offers among others, ground geophysical surveys using the following:

    Our clients are guaranteed with quality services.

    Electromagnetic Survey (EM) Magnetic Survey

    0DJQHWLFPHWKRG (OHFWURPDJQHWLFPHWKRG(0 (OHFWULFDOPHWKRG,QGXFHG3RODUL]DWLRQDQG5HVLVWLYLW\ 5DGLRPHWULFPHWKRG8UDQLXPWKRULXPDQG3RWDVVLXP *UDYLW\PHWKRG %RUHKROHORJJLQJ

    Expect More, Pay Less.

    Name: Geological Survey of Tanzania Address: P. O. Box 903, Dodoma - Tanzania

    Physical Address: 8 Kikuyu AvenueTel: +255 26 2323020 / Fax: +255 26 2323020

    Email: [email protected] / Website: www.gst.go.tzWeb portal: www.gims-tanzania.com

    0ore than 80 Years

    GEO

    LOGI

    CAL SU

    RVEY OF TANZANIA

    GST

    0LQHUDOH[SORUDWLRQILUPVPLQHUVFRQVWUXFWLRQDQGZDWHUGULOOLQJFRPSDQLHVand other related earth resource stakeholders need not to survey the countrys vast land but they are encouraged to consult (at the one stop geo-scientific centre) the Geological Survey of Tanzania for guidance.

    7KHDJHQF\LVXQGHUWKH0LQLVWU\RI(QHUJ\DQG0LQHUDOVZLWKLWVPDLQRIILFHcentered in Capital Town of Tanzania - Dodoma.

    ContactInformation: