mem 97 final.pdf

7
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 97 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Desemba 11 - 17, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Soma habari Uk. 2 Almasi Adimu ya Pinki Yauzwa USD 10,050,000 KUMEKUCHA!!!! Nishati na Madini: PROF. SOSPETER MUHONGO DK. MEDARD KALEMANI n Ni Prof. Muhongo na Dkt. Kalemani

Upload: othman-michuzi

Post on 16-Jul-2016

158 views

Category:

Documents


5 download

TRANSCRIPT

Page 1: MEM 97 FINAL.pdf

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 97 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Desemba 11 - 17, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Soma habari

Uk. 2Almasi Adimu ya Pinki Yauzwa USD 10,050,000

KUMEKUCHA!!!! Nishati na Madini:

PROF. SOSPETER MUHONGO DK. MEDARD KALEMANI

n Ni Prof. Muhongo na Dkt. Kalemani

Page 2: MEM 97 FINAL.pdf

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Asteria Muhozya naTeresia Mhagama

Almasi Adimu ya rangi ya Pinki iliyochimbwa nchini mwezi Novemba, 2015, katika mgodi wa Williamson unaomilikiwa

na Kampuni ya Dhahabu ya Petra Diamond Mwadui, Shinyanga, imeuzwa katika mnada jijini Antwerp Ubelgiji kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 10,050,000.

Kampuni ya Madini ya Petra iliuza Almasi hiyo Adimu ya Pinki yenye uzito wa carat 23.16, tarehe 9 Disemba, 2015, kwa kampuni ya Golden Yellow Diamonds ambayo ilinunua kwa niaba ya Kampuni ya M.A Anavi Diamond, kampuni kongwe inayoongoza katika kutengeneza almasi zenye ukubwa na rangi za kipekee.

Katika mauzo hayo ambayo pia yalishuhudiwa na Afisa Mthamini Mwandamizi kutoka Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini, kampuni ya Petra iliuza almasii hiyo kwa kiasi cha Dola za Marekani 433,938 kwa kila carat, ikiwemo kubakiwa na riba ya asilimia 20 ya mauzo.

Akizungumza baada ya mauzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Petra, Johan Dippenaar, alisema kuwa, “Matokeo ya mauzo haya yanaendelea kuthibitisha kuwa soko la almasii za rangi zenye ubora wa juu inabaki kuwa imara. Almasi yenye ukubwa huu ni nadra sana kupatikana lakini Williamson inajulikana kwa kuzalisha madini ya aina hiyo kwa vipindi tofauti,” alisema Dippenaar.

Taarifa kutoka kampuni hiyo imeeleza kuwa, Almasi ya rangi ya Pinki ya kwanza kuzalishwa katika mgodi wa Williamson ilipatikana mwaka 1947 ambapo inatajwa kuwa ya pekee kuwahi kutokea ikiwa na uzito wa carat 54. Mmiliki wa mgodi kwa kipindi hicho, alikuwa Mjiolojia raia wa Canada, Dkt. John Williams ambaye alitoa Almasi hiyo kama zawadi ya harusi kwa Malkia Elizabeth wa Uingereza.

Nchini Tanzania, Kampuni ya Petra, ni pekee inayozalisha madini ya almasi ambapo inamiliki eneo la kiasi cha hekta 146 Mwadui Shinyanga. Mbali na Tanzania, Kampuni hiyo inamiliki migodi minne katika nchi ya Afrika Kusini, vilevile inaendesha mpango wa utafiti katika nchi ya Botswana.

Almasi za mgodi wa Williamson na almasi nyingine kutoka nchi mbalimbali duniani huuzwa katika mnada wa madini hayo uliopo jijini Antwerp, nchini Ubelgiji. Vilevile, mgodi huo huzalisha almasi zenye ubora wa hali ya juu zinazofikia wastani wa thamani ya Dola za Marekani 298 kwa karat moja kama ilivyoshuhudiwa katika mwaka wa fedha 2015.

Almasi Adimu ya Pinki iliyochimbwa Tanzania yauzwa USD 10,050,000

Almasi ya Pinki

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAHADHARI YA UTAPELIWIZARA YA NISHATI NA MADINI INAWATAARIFU WANANCHI KUJIHADHARI NA WATU WANAOTUMIA JINA LA KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI MHANDISI OMAR CHAMBO KUTAPELI WANANCHI NA WATUMISHI KATIKA TAASISI ZA SERIKALI.

WATU HAO WAMEKUWA WAKIWAPIGIA SIMU BAADHI YA WATUMISHI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NA TAASISI ZAKE WAKIJITAMBULISHA KWA JINA LA MHANDISI OMAR CHAMBO NA KUTOA MAAGIZO MBALIMBALI ILI YAFANYIWE UTEKELEZAJI.

VILEVILE WATU HAO HUTOA MAAGIZO YA KUTUMIWA FEDHA KWA NJIA YA SIMU, NA MOJA YA NAMBA INAYOTUMIKA NI 0676 856 862.

TUNATOA ONYO KALI KWA WATU WANAOTUMIA VIBAYA JINA LA MHANDISI OMAR CHAMBO KUWA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

IMETOLEWA NA;KITENGO CHA MAWASILIANO,

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Page 3: MEM 97 FINAL.pdf

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

TahaririMEM

Na Badra Masoud

FIVE PILLARS OF REFORMS

KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

BODI YA UHARIRI

MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Lucas Gordon

WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

OF GOODS/SERVICE

SATISFACTION OF THE CLIENT

SATISFACTION OF BUSINESS PARTNERS

SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Hongera Prof. Muhongo na Dkt. Kalemani

Karibuni tuchape kazi!

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Mawaziri Wateule Nishati na Madini

Kwa hakika tumepokea kwa furaha kubwa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Dk. Medard Kalemani kuwa Naibu wa Wizara yetu.

Uteuzi wa Profesa Muhongo na Dk. Kalemani unatokana na weledi wao katika Sekta za Nishati na Madini kwani walishawahi kufanya kazi katika Wizara hii na matokeo chanya yalionekana.

Prof. Muhongo aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini kuanzia mwaka 2012 hadi mwazoni mwa mwaka 2015 ambapo alifanya mambo mengi yenye tija bila kusahau alivyosimamia utekelezaji wa upelekaji umeme vijijini pamoja na kuhakikisha TANESCO inawahudumia wananchi ipasavyo hadi kufikia kupewa jina la utani la “Mzee wa nguzo”.

Kama hiyo haitoshi Profesa Muhongo alisimamia na kufuatilia kwa karibu matatizo ya wachimbaji wadogo na hatimaye kuanzisha utaratibu wa kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwapatia ruzuku ili waweze kujikwamua na lindi la umasikini kwa kuchimba kisasa kwa kutumia zana bora za uchimbaji madini.

Dk. Medard Kalemani pia alifanya kazi kubwa akiwa Wizara hii ya Nishati na Madini wakati akiwa Mwanasheria wa Wizara ambapo aliwezesha mchakato wa upatikanaji wa Sheria za Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia, Sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi asilia na sheria za mafuta zote za mwaka 2015.

Hakika Rais John Pombe Magufuli hakufanya kosa hata kidogo kuwateua kwani uwezo mnao, uzoefu mnao halikadhalika Wizara hii ya Nishati na Madini mnaifahamu vizuri na hakuna mahali kokote mnaweza kudanganywa.

Hivyo, sisi watendaji wa Wizara hii tunawapa pongezi kubwa na tunawakaribisha sana tushirikiane kuchapa kazi kwani uwezo tunao, sababu tunazo na nia tunayo ya kuwatumikia Watanzania.

Tunawatakia kila la kheri Prof. Muhongo na Dkt. Kalemani katika kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini kwani Watanzania wana matarajio makubwa kwa Serikali iliyopo madarakani katika kuwatatulia kero na changamoto zinazowakabili.

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli Wiki hii amefanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri ambao wataongoza Serikali ya Awamu ya

Tano katika Sekta mbalimbali ambapo katika Wizara ya Nishati na Madini amemteua Prof. Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Dkt. Medard Kalemani kuwa Naibu wake.

Kwa wanaofuatilia utendaji na historia ya Prof. Muhongo ni kiongozi mwadilifu, mwaminifu na mpenda kazi anayezifahamu vyema sekta za Nishati na Madini.

Hakuna shaka juu ya utendaji wa Profesa Muhongo kwani kati ya mwaka 2012 hadi mwanzoni mwa mwaka 2015 alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini alielekeza, kuanzisha na kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imeleta tija kubwa katika sekta hizo mbili za Nishati na Madini.

Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana chini yake ni uhamishaji wa umiliki wa Mgodi wa Biharamulo (Tulawaka) uliokuwa ukimilikiwa na African Barrick Gold (ABG) kuwa chini ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa asilimia 100 na kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB ambayo sasa imefikia awamu ya Tatu.

Vilevile, aliweka kipaumbele katika utekelezaji wa Mradi wa uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I (MW 150) ambao umeshaanza kuingiza umeme katika gridi ya Taifa, na kuongeza kasi ya

usambazaji umeme vijijini .Masuala mengine aliyoyasimamia ni

ujenzi wa bomba kubwa la gesi lenye uwezo wa kusafirisha gesi asilia kiasi cha futi za ujazo milioni 784 kwa siku kwa kiwango cha juu bila mkandamizo (compression) kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam lenye lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilomita 477 ambalo limeenda sambamba na kukamilika kwa mitambo ya kusafisha gesi hiyo iliyojengwa katika eneo la Madimba mkoani Mtwara na Songosongo mkoani Lindi.

Halikadhalika, Naibu Waziri ambaye ni Dk. Medard Kalemani; kabla ya kuingia katika siasa alikuwa ni Mkurugenzi wa Sheria katika Wizara ya Nishati na Madini aliyezingatia uadilifu, kupenda kazi na kuhakikisha kuwa masuala anayoyasimamia yanatekelezwa kwa ufanisi.

Dkt. Kalemani aliiongoza Wizara katika kufanikisha masuala mbalimbali ya kisheria kubwa ikiwa ni mchango wake katika upatikanaji wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania; Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi Asilia, na sheria ya mafuta zote za Mwaka 2015 ambazo zinaiwezesha serikali kuisimamia vyema tasnia ya uziduaji nchini.

Kutokana na uwezo walionao Prof. Muhongo na Dkt. Kalemani hakuna shaka kwamba Wizara ya Nishati na Madini imepata viongozi hodari na shupavu katika kuongoza na kusimamia sekta za Nishati na Madini ili ziweze kukuza uchumi wa Taifa letu.

Waziri Mteule wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kulia) alipozindua mkuo wa kwanza wa dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Biharamulo mwaka 2014.(picha kutoka Maktaba).

Page 4: MEM 97 FINAL.pdf

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Remija Salvatory na Nuru Mwasampeta

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo amewaagiza Madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama kuandaa

utaratibu wa kuwawezesha wahanga wa Mgodi wa Nyangalata kwenda Hospitali za rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya zao.

Mhandisi Chambo aliyasema hayo alipowatembelea wahanga hao waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na ajali ya kufukiwa na kifusi na kufanikiwa kuokolewa

baada ya kuishi chini ya ardhi kwa siku 41 katika Mgodi wa Nyangalata mkoani Shinyanga.

Katibu Mkuu alitoa maagizo hayo baada ya mmoja wa wahanga hao, Joseph Buruge kueleza kuwa ingawa ngozi za wachimbaji hao zinaonekana kuimarika lakini bado kuna tatizo la vijipele vidogo vidogo mwilini ambavyo baada ya muda hutoa usaha hivyo aliomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kutibu tatizo hilo.

“Kwa kweli Mheshimiwa tunaendelea vizuri na matibabu na tunawashukuru madaktari na wauguzi wote wanaotuhudumia na tunaishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa misaada na huduma walizotoa, lakini

kwa sababu umekuja Mheshimiwa tuna maombi yetu ambayo tunaomba Serikari iweze kutusaidia sisi wahanga wote” , alisema Buruge.

Buruge alisema kuwa pamoja na kuwa afya zao kuimarika lakini bado kuna viashiria ambavyo si vizuri kwa sababu ya kula magome ya miti na wadudu chini ya mgodi hivyo wanahitaji uchunguzi kwani magome ya miti yalikuwa yakiwalevya kama wamekunywa pombe kali hivyo ni vyema uchunguzi ukafanyika ili kujua kama magome hayo yalikuwa na sumu na athari zake katika miili yao.

Pamoja na hayo, wameomba pia kufanyika kwa uchunguzi wa tumbo kwa kuwa maji machafu waliyokuwa

wakinywa chini ya mgodi yalikuwa na kemikali kwani yalikuwa yamechanganyika na baruti hivyo ni vema kufahamu baruti iliwaathiri kiasi gani.

Baada ya maombi hayo, Mhandisi Chambo aliwaahidi wahanga hao kuwa ataendelea kufanya mawasiliano na Madaktari wa Hospitali hiyo ili kuhakikisha majibu ya maombi yao yanafanyiwa kazi kwa wakati. Aidha aliwahakikishia kuwa vipimo vyote wanavyotakiwa kufanyiwa vitagharamiwa na Serikali.

Alipotakiwa kuelezea taratibu za kuwahamishia wahanga hao katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Robert Rwebagira alisema kuwa wahanga hao wanahitajika kwenda Hospitali kubwa ya Muhimbili kwani wataweza kupata huduma zote ambazo zitachukua si chini ya miezi Sita.

Alisema kuwa huduma za awali walizopatiwa wahanga hao zilikuwa ni kuangalia miili yao (Physical treatment) na sasa wanahitaji matibabu ya kisaikolojia na kiakili ambayo yatapatikana katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba aliahidi kushirikiana bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa pamoja na Hospitali hiyo ili kuhakikisha kuwa wahanga hao wanapata huduma stahiki kwa wakati.

Wahanga Watano wa mgodi wa Nyangalata waliopokelewa katika hospitali ya wilaya ya Kahama tarehe 16/11/2015 ni Amos Muhongo, Joseph Buruge, Msafiri Gerard, Chacha Wambura na Onyiwa Kaiwao ambaye kwa sasa ni marehemu.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo akimsikiliza Joseph Buruge (mhanga) wakati alipowatembelea wahanga wa mgodi wa Nyangalata katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Meneja wa mgodi wa SHIGOMICO, Amos Elias Mbaga akiwa mbele ya ya shimo la mgodi lililofunika wafanyakazi sita waliokolewa wakiwa hai baada ya kukaa siku 41

Mhandisi omar Chambo akimjulia hali mmoja wa wahanga wa Nyangalata Amosi Muhongo mara baada ya kuwatembelea wahanga hao wodini katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Serikali yaahidi vipimo zaidi wahanga Nyangalata

Page 5: MEM 97 FINAL.pdf

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Nuru Mwasampeta na Remija Salvatory

Wa c h i m b a j i w a d o g o katika eneo la Nyangalata m k o a n i

Shinyanga wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kuwawezesha kwa kuwapatia ruzuku iliyoanza kutolewa na Serikali tangu mwaka 2013.

Hayo yalielezwa na Amos Mbaga, Meneja Mkuu wa kampuni ya SHIGOMICO, ambayo inachimba madini ya dhahabu katika eneo hilo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo pamoja na wataalamu mbalimbali walipofika katika eneo hilo ili kuzungumza na wachimbaji wadogo.

Alieleza kuwa wachimbaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini pamoja na vifaa vya usalama na uokoaji.

“Pamoja na hayo leseni za madini zitumike kama dhamana ya kupata mikopo mbalimbali katika taasisi za kifedha kwani leseni hizi zina

gharama na thamani kubwa,” alisema Mbaga.

Alisema kuwa uwezeshaji wa wachimbaji hao utaongeza mapato ya Serikali kwani wachimbaji wadogo hulipa serikalini asilimia Nne ya mapato wanayopata katika madini hayo ambayo huchangia uendelezaji wa sekta mbalimbali ikiwemo afya, miundombinu na elimu.

Vilevile wachimbaji hao waliiomba Wizara kutoa elimu kuhusu usalama wa migodi, mbinu za kisasa za uchimbaji madini na uokoaji wakati maafa yanapotokea.

Mbaga alisema kuwa kwa sasa Serikali kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na utoaji wa elimu ya usalama kwa wachimbaji wadogo ya OSE (Organisation of Safety Education) na SHILEMA (Shinyanga Regional Mining Association) yanaendelea kutoa elimu hiyo kwa wachimbaji wadogo katika mgodi wa Kalole na wataendelea katika migodi mingine.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampuni ya SHIGOMICO, Hamza Tandiko alisema kuwa Ruzuku inayotolewa

kwa wachimbaji wadogo ikiongezeka itasaidia vikundi vya wachimbaji hao kupata zana za kisasa za uchimbaji madini zitakazoongeza tija katika shughuli zao na kupunguza hatari katika migodi zinazotokana na matumizi ya zana duni kwenye uchimbaji madini nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar chambo aliyezungukwa na wachimbaji wadogo wa madini wa Mwanshina mjini Nzega akiwasikiliza na kufikia uamuzi wa kuwafukuza kazi viongozi wa wachimbaji hao baada ya kupokea malalamiko mengi dhidi yao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo akizungumza na wachimbaji wadogo waliokusanyika mara baada ya kuwasili katika eneo Nyangalata mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa kampuni ya SHIGOMICO Hamza Tandiko akizungumza jambo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa Nishati na madini Mhandisi Omar Chambo ili aweze kuzungumza na wachimbaji wadogo wa Nyangalata mkoani Shinyanga.

Chambo awasimamisha kazi viongozi Wachimbaji Wadogo

Wachimbaji Wadogo waomba Ruzuku

Nuru Mwasampeta na Remija Salvatory

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo, amewasimamisha

kazi viongozi wa kikundi cha wachimbaji wadogo wa mgodi wa dhahabu wa Mwanshina katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora kutokana na kuwepo kwa malalamiko dhidi yao.

Katibu Mkuu alichukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi Mwenyekiti, Katibu na Meneja wa mgodi huo wakati wa ziara yake mgodini hapo ambapo wachimbaji hao wadogo walimueleza kuwa viongozi hao wamekuwa wakitumia mamlaka yao vibaya.

Wachimbaji hao walieleza

kuwa viongozi wa mgodi walikuwa hawajali nguvu kazi na gharama ya uwekezaji inayotumiwa na wachimbaji hao na badala yake walijali katika kugawana faida tu.

“Kuna kodi ambazo ni kero kwetu kwa mfano, tunanunua mifuko ya mawe kwa gharama kubwa ya shilingi 25,000 na kila tunaponunua mifuko 10, mifuko 3 kati ya hiyo hutozwa kama ushuru na viongozi na sisi tunabakiwa na mifuko Saba. Vilevile, kuna kodi nyingine hutolewa kila tunapoenda kuchenjua dhahabu ambapo nusu ya mifuko hutozwa kama ushuru wa uchenjuaji,” alisema mmoja wa wachimbaji wadogo.

Vilevile, Wachimbaji hao waliongeza kuwa viongozi hao huwatoza kodi ya shilingi 2,000 pamoja na mfuko mmoja wa mawe ikiwa ni kodi ya maafa ambayo hata hivyo walilalamikia

kuwa haiwanufaishi kama inavyotakiwa.

Baada ya kusikia malalamiko hayo Katibu Mkuu alichukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi viongozi hao na kuagiza kupelekwa katika vyombo vya Dola ili mapato waliyokusanya isivyo halali katika mgodi huo yarejeshwe kwa wahusika na serikali ipate mapato yake stahiki.

Aidha, Mhandisi Chambo aliahidi kuwa wachimbaji hao wadogo watapewa maeneo ya uchimbaji madini ambapo watachimba madini hayo bila kubughudhiwa na mtu yeyote.

Viongozi wa mgodi wa Mwanshina waliosimamishwa kazi na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ni Juma James (Mwenyekiti) Samwel Nhindilo (Katibu) na Masumbuko Jumanne, Meneja wa mgodi huo.

Page 6: MEM 97 FINAL.pdf

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa (mwenye jezi) pamoja na viongozi wa wizara na Tanesco mara baada ya kumaliza mazungumzo mafupi yaliyofanyika katika ofisi ya mkuu huyo wa Wilaya kabla ya kuwatembelea waathirika wa Nyangalata waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Kampuni yaishukuru Wizara kufanikisha uokoaji NyangalataRemija Salvatory na Nuru Mwasampeta

Mw e n y e k i t i wa kampuni ya uchimbaji madini ya

SHIGOMOCO na Msimamizi wa shughuli za uchimbaji katika eneo la Nyangalata, Hamza Tandiko ameishukuru na kuipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano ilioutoa katika zoezi la uokoaji wachimbaji wadogo waliofukiwa katika mgodi wa dhahabu wa Nyangalata mkoani Shinyanga, tarehe 5 Oktoba 2015.

Hamza alitoa pongezi hizo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo alipotembelea eneo hilo ili kuzungumza na wachimbaji wadogo pamoja na kuwaona wahanga waliookolewa katika maafa ya mgodi huo ambao walilazwa katika hospitali ya wilaya Kahama.

“Tunashukuru kwa jinsi Serikali ilivyopambana kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi ule wanaokolewa, Afisa Madini Mkazi na Timu kutoka wizarani, Uongozi wa Mkoa na Wilaya tulikuwa nao katika kufanikisha zoezi la uokoaji,” alisema Hamza.

Aidha, Mchimbaji mwingine mdogo katika eneo hilo, Musa Jacob alisema kuwa Serikali ilishirikiana nao katika masuala mbalimbali ikiwemo usafiri, kugharamia matibabu na matunzo ya wahanga waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Robert Rwebangira alisema kuwa tarehe 16 Novemba, 2015 walipokea wahanga watano ambao ni Amos Muhongo, Joseph Buruge, Msafiri Gerard, Chacha Wambura na Onyiwa Kaiwao ambaye kwa sasa ni marehemu.

“ Hali zao zilikuwa dhoofu, walikuwa wakilalamika miili

kuchoka, hawakuwa na uwezo wa kusimama wenyewe wala kukaa, walikuwa na vidonda sehemu mbalimbali za miili yao, uzito ulikuwa umepungua, mfumo wa upumuaji na mzunguko wa damu haukuwa sawasawa, na mfumo wa misuli na mifupa ulikuwa umeathirika kwa kuwa viungo havikuwa na uwezo wa kujikunja,” alieleza Dkt. Rwebangira.

Alisema kuwa baada ya wahanga hao kupata matibabu mbalimbali ikiwemo kuwapa vyakula laini, kuwaongezea oksijeni, na mazoezi mepesi kwa sasa wanaweza kuruhusiwa kurudi nyumbani. Hata hivyo alieleza kuwa hospitali imewasiliana na wadau wengine wakiwemo Serikali na viongozi wa mgodi ili kuhakikisha wachimbaji hao wanaendelea kuhudumiwa huko watakapokuwa.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi, Amos Mbaga alisema kuwa pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha uchimbaji mdogo wa madini unakuwa wenye tija, lakini bado wanahitaji elimu zaidi ya masuala mbalimbali ikiwemo usalama, na uwekezaji.

Meneja Mkuu wa SHIGOMICO, Amos Mbaga akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo (wa pili kushoto) eneo ambalo wahanga wa Nyangalata walifukiwa na kifusi

Katibu wa SHIGOMICO akieleza jinsi kifusi kilivyokuwa kikishuka katika mgodi wa Nyangalata na kusababisha maafa ya kufukia waokoaji 6 waliokamilisha zoezi la kuokoa wachimbaji wadogo wanne waliokuwa wamefukiwa kabla yao.

Page 7: MEM 97 FINAL.pdf

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

 

Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

Tanzanite , Ruby, Sapphire , Tsavori te , Rhodol i te , Spessart i te , Tourmaline,

Chrysobery l na Almasi yanatarajiwa kuvutia

Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini; na zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

ulimwenguni

Jisajili na Ushiriki Sasa!!!

Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF Simu: +255 784352299 or +255 767106773

Barua pepe: [email protected]

:ama Ofisi za Madini za Kanda

Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)

Wafanyakazi 362 STAMIGOLD wapima ukimwiNa Jacqueline Mattowo-STAMIGOLD

Kila ifikapo tarehe 1 Desemba Mataifa mbalimbali huadhimisha siku ya UKIMWI duniani ikiwa ni siku maalumu ya kutathmini

mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo iliyofanyika kwa muda wa mwaka mzima pia kukumbuka kama sehemu ya jamii kupanga mikakati endelevu ya kuzuia maambukizi mapya, kuzuia unyanyapaa na kukabiliana na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

Mgodini Biharamulo harakati za kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani zilianza mwanzoni mwa mwezi Novemba ambapo Wafanyakazi na Wakandarasi wanaofanya kazi mgodini hapo walijitokeza kupata ushauri nasaha pamoja na kupima virusi vya UKIMWI kwa hiyari kwa lengo la kutambua afya zao, vile vile, kuingia katika bahati nasibu ya maadhimisho ya Siku ya ukimwi Duniani” ili kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo jokofu.

Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo Mhandisi Dennis Sebugwao ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mara baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa bahati nasibu aliwapongeza wafanyakazi kwa kujitokeza kwa wingi kufahamu afya zao ambapo mwaka huu

ilielezwa kuwa jumla ya wafanyakazi 362 walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI kwa hiyari ikilinganishwa na 230 waliojitokeza mwaka 2014.

“Kwa mujibu wa Madaktari idadi ya watu walioathirika mgodini imeongezeka kwa asilimia 4 katika watu 362 waliopima kwa mwaka huu hivyo ninaomba mwaka ujao asilimia hii isiongezeke kwa kuhakikisha kila mmoja anailinda afya yake ili kuzuia maambukizi mapya. Ni vyema kila mmoja kujitahidi kufahamu afya yake ili kama umeathirika uweze kuishi kwa kuzingatia ushauri wa Daktari ukizingatia kuwa hapa mgodini hakuna unyanyapaa wa aina yoyote kwa waathirika na ikitokea haujaathirika uzidi kujilinda zaidi dhidi ya maambukizi,” alieleza Mhandisi Sebugwao.

Kupitia risala ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Daktari wa kliniki ya mgodi, Kiangi Mbwambo alieleza kuwa Siku ya UKIMWI duniani ni siku maalumu inayokumbusha na kutoa uhalisia wa hali ya ugonjwa wa UKIMWI duniani, kitaifa na hata kwa watumishi wa STAMIGOLD.

“UKIMWI bado ni tishio na ni ugonjwa usio na tiba kamilifu mpaka sasa. Mwaka huu takwimu zinaonyesha kupungua kwa maambukizi mapya duniani na hata nchini. Hii ni kutokana na watu wengi kuwa na ufahamu kuhusu UKIMWI, kujitokeza kupima kwa hiari na pia kuongeza umakini katika kujikinga kupata maambukizi

ya VVU. Tanzania maambukizi mapya yamepungua kutoka asilimia 7 hadi 5.4. Kwa hapa mgodini, maambukizi bado ni tatizo hivyo kila mmoja wetu ana jukumu la kuijali na kuilinda afya yake,”alisisitiza Dkt. Mbwambo.

Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani mgodini hapo pia yalihusisha ugawaji dawa za magonjwa mbalimbali kwa hospitali za vijiji vya Mavota na Mkunkwa pamoja na ugawaji wa vitanda vitatu na magodoro kwa ajili ya

wodi za hospitali ya Mkunkwa ambapo awali kina mama wajawazito walikuwa wakijifungulia sakafuni.

Vilevile, mgodi ulitoa shilingi 200,000 kusaidia uendeshaji wa kikundi cha JUKU kinachoundwa na wanachama 70 wanaoishi kwa matumaini baada ya kuathirika na VVU kutoka katika vijiji vya Mavota na Mkunkwa ambapo kikundi hicho hutoa huduma majumbani kwa waathirika pamoja na ushauri nasaha kwa wanajamii.

Meneja Maendeleo endelevu mgodi wa STAMIGOLD Korodias Shoo (katikati), akikabidhi dawa na vitanda kwa hospitali ya Mkunkwa. Anaepokea ni Mwenyekiti wa kamati ya hospitali hiyo na wenye fulana za rangi ya bluu ni wanachama kikundi cha JUKU.