mem_bulletin_58.pdf

9
Bulletin News Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] http://www.mem.go.tz HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No.58 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Machi 13-19, 2015 Wizara yavipatia vijiji 10 umeme jua wa Makontena - Uk7 Soma habari Uk.2 UTOROSHWAJI TANZANITE Serikali yaimarisha ulinzi Merelani Serikali yaimarisha ulinzi Merelani Kamishna wa Madini nchini Mhandisi Paul Masanja (kulia) akielezea mikakati iliyowekwa na Serikali katika kuimarisha ulinzi katika machimbo ya Merelani. Picha pembeni ni baadhi ya waajiriwa katika moja ya migodi mikubwa nchini. k

Upload: jackson-m-audiface

Post on 18-Nov-2015

17.129 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No.58 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Machi 13-19, 2015

    Wizara yavipatia vijiji 10 umeme jua wa Makontena-Uk7

    Soma habari Uk. 2

    UTOROSHWAJI TANZANITE

    Serikali yaimarisha ulinzi Merelani Serikali yaimarisha ulinzi Merelani Kamishna wa Madini nchini Mhandisi Paul Masanja (kulia) akielezea mikakati iliyowekwa na Serikali katika kuimarisha ulinzi katika machimbo ya Merelani. Picha pembeni ni baadhi ya waajiriwa katika moja ya migodi mikubwa nchini.

    k

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Serikali yaimarisha ulinzi utoroshwaji madini Tanzanite nchini Masanja

    Na Greyson Mwase, Arusha

    Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja, amese-ma kuwa, Serikali imejipanga kuimari-

    sha ulinzi ndani ya machimbo ya Tanzanite yaliyopo Merelani ka-tika wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.

    Mhandisi Masanja aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Ku-dumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika kikao cha Kamati hiyo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wanaosimamia Sekta ya Madini kilichofanyika ji-jini Arusha.

    Mhandisi Masanja alisema kuwa, katika hatua ya awali, Seri-kali ilijenga uzio wenye urefu wa kilomita 10 kwa gharama ya shilingi milioni 300 na kuongeza kuwa, bado serikali ina mpango wa kujenga vibanda kwa ajili ya walinzi ili kupunguza wachimbaji haramu kuingia ndani ya maeneo ya uchimbaji wa madini hayo na kutoroka na Tanzanite.

    Alisema pamoja na kuima-risha ulinzi kwenye maeneo ya mgodi, Serikali imepanga ku-jenga kituo kikubwa kwa ajili ya biashara ya madini ya vito ki-takachojulikana kwa jina la Ma-dini House ambapo kutafanyika biashara ya madini hali itakay-opunguza utoroshwaji wa madini yanayopelekwa nje ya nchi.

    Aidha, alisema kuwa, kituo hi-cho kitakuwa na mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa madini kwani kitakuwa na ofisi zote za serikali za usimamizi wa biasha-ra ya madini, wafanyabiashara, mabenki na sehemu za kutunzia madini ambazo zitakuwa na pass-word maalum itakayomwezesha mfanyabiashara kuweka na kutoa

    mzigo wake kwa usalama. Pia aliongeza kuwa, kituo hi-

    cho kitakuwa na sehemu ambayo helikopta itatua na kumwezesha mfanyabiashara wa madini kusa-firisha mzigo wake hadi kiwanja cha ndege kwa usalama.

    Kutokana na tatizo la watu wengi kutapeliwa kwasababu ya kufanya biashara ya madini ka-tika maeneo yasiyofaa na wen-gine kutofahamu mahali yana-popatikana madini, uwepo wa kituo maalum cha uuzaji wa ma-dini kitasaidia kuondoa utapeli na hivyo serikali kupata mapato stahiki kutokana na biashara ya madini,alisema Masanja.

    Vilevile, aliongeza kuwa, kamati ya usalama kwa kushiriki-ana na mkuu wa wilaya ya Siman-jiro na kituo cha polisi imechangia kuimarishwa kwa ulinzi katika eneo la mgodi na kusisitiza kuwa, bado serikali inabuni njia ny-inyine zaidi za kisasa kwa ajili ya kudhibiti utoroshwaji wa madini

    ya Tanzanite nje ya nchi.Akielezea changamoto ka-

    tika eneo la Merelani Mhandisi Masanja alisema, kumekuwepo na migogoro ya kugombea ardhi na kutokuzingatia sheria na kanuni za uchimbaji madini hali inayopele-kea ajali za mara kwa mara mgo-dini.

    Kule kwenye eneo la mgo-di kuna uchimbaji hatari unao-fanyika chini kwa chini ambapo wamejiwekea utaratibu wa kuwa, mchimbaji anapokutana na mwen-zake kwenye mkondo wa madini chini ya ardhi, anatakiwa kurudi nyuma hatua kumi lakini bado kumekuwepo na changamoto ya wachimbaji kuvamia maeneo wa-nayohisi madini yapo bila kuzinga-tia kanuni za uchimbaji madini, alisisitiza Mhandisi Masanja

    Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na maeneo ya uchimbaji kuwa madogo na kuongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya migogoro ali-

    washauri wachimbaji wadogo kuunda umoja kwa kuunganisha maeneo yao na kuomba leseni ya pamoja hali itakayowaongezea ki-pato huku ikipunguza migogoro isiyo ya lazima.

    Kwa mfano iwapo wachim-baji wataungana na kuomba leseni ya pamoja na kuchimba madini, kila mchimbaji ana uhakika wa kupata faida ya shilingi milioni 500 kwa mwaka, alisema Mhandisi Masanja

    Wakichangia kwa nyakati to-fauti wajumbe wa Kamati ya Ku-dumu ya Bunge ya Nishati na Ma-dini waliitaka Serikali kuongeza juhudi zaidi katika usimamizi wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na suala la ulinzi kwenye migodi hususan katika eneo la Merelani.

    Akichangia hoja katika kikao hicho mjumbe wa Kamati ya Ku-dumu ya Bunge ya Nishati na Ma-dini ambaye ni Mbunge wa Singida (Viti Maalum CCM) Martha Mla-ta alisema kuwa mbali na kuimari-

    sha ulinzi katika eneo la Merelani kwa kuweka uzio na vibanda kwa ajili ya walinzi, vitambulisho kwa ajili ya wachimbaji wa mgodini vinatakiwa kutengenezwa vikiwa na majina ya makampuni wanay-ochimba madini.

    Alisema kufanya hivyo, kuta-punguza wimbi la wachimbaji haramu na wahamiaji wanaoingia katika maeneo hayo na kutoroka na madini hayo.

    Mlata alisisitiza kuwa makam-puni yanayoshindwa kulipa kodi kwa kisingizio cha kupata hasara yasivumiliwe kamwe , ikiweze-kana yanyanganywe leseni za madini.

    Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Richard Ndassa alisema kuwa mwarobaini wa utoroshwaji wa madini ya Tanzanite unaweza kupatikana kwa kujenga ukuta mkubwa, imara na kuitaka Seri-kali kuwa na mikakati zaidi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika eneo la Merelani.

    Ndassa alisema kuwa suala la usimamizi wa Sekta ya Madini halihitaji siasa, na kuwataka wa-jumbe wa kamati hiyo kuwa wa-zalendo badala ya kuweka siasa zaidi kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini.

    Madini ya Tanzanite yanapa-tikana Tanzania, hivyo ni vyema kuhakikisha madini haya yana-lindwa kwa nguvu zote pamoja na usimamizi wake usiongezwe na siasa, alisema Ndassa.

    Watendaji wa taasisi wali-oshiriki kikao hicho ni kutoka Shirika la Umeme Nchini (TA-NESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Wakala wa Uk-aguzi wa Madini Nchini (TMAA) na Wakala wa Udhibiti wa Hudu-ma za Nishati na Maji (EWURA), ambapo Kamati hiyo ilipokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi na kutoa maazimio na mapendekezo mbalimbambali.

    Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa inasomwa na Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja (hayupo pichani)

    Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mubaba wakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wanawake mgodi wa STAMIGOLD wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka.

    Wafanyakazi wanawake mgodi wa STAMIGOLD wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wasichana wa Shule ya Msingi Mubaba

    WANAWAKE STAMIGOLD

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Mwandishi Wetu, Geita

    Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene amewaagiza maafisa ma-dini wote nchini kutoa leseni za madini ya ujenzi

    kwa vijiji ili waweze kuchimba madini husika na kuweza kunufaika na uwepo wa madini hayo katika maeneo yao.

    Simbachawene amesema hayo mkoa-ni Geita wakati akizungumza na watendaji wa mkoa huo akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekele-zwa na Wizara ya Nishati na Madini.

    Simbachawene amesema ugawaji wa leseni hizo za madini ya ujenzi zitaondoa migogoro baina ya wachimbaji na wanavi-jiji wa eneo husika.

    Amesema haiwezekani wazawa wa maeneo yanayopatikana madini ya ujenzi kama mawe, kokoto na mchanga washindwe kutumia rasilimali hiyo kwa madai ya kuwa kuna mtu anamiliki eneo hilo kutoka nje ya eneo husika.

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVE PILLARS OF REFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Essy Ogunde

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James

    na Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

    OF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OF THE CLIENT

    SATISFACTION OF BUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Hongera Wizara kwa umeme Jua wa Makontena

    Moja ya habari ya kutia matumaini iliyoandikwa katika Jarida la Wiki hii ni kuwa Wizara ya Nishati na Madini imeviunganishia umeme jumla ya Vijiji 10 vilivyo katika Wilaya za Kongwa, Mlele na Uyui, mkoani Dodoma, kupitia Mradi wa makontena ya kuzalisha umeme unaotokana na jua.

    Imeelezwa kuwa mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, upo katika hatua ya majaribio na un-alenga kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa Gridi ya Taifa katika sehemu mbalimbali nchini.

    Katika kutekeleza mradi huo, Wizara ya Nishati na Madini wiki hii, ilisaini makubaliano ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Mradi huo na Kampuni ya Elektro-Merl ya nchini Austria ambayo ndiyo ilileta na kufunga makontena 14 ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme kwenye nyumba zilizoko katika vijiji husika.

    Tumeelezwa kuwa wananchi waliounganishiwa umeme huo wa jua, watapata huduma hiyo bure kwa kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ambayo ni ya matazamio.

    Pia imeelezwa kuwa baada ya miaka miwili, kuanzia tarehe wal-iyosaini makubaliano, wananchi wa vijiji husika wataanza kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kama betri na paneli vinavyotumika katika mradi huo, ambavyo vina ukomo wake.

    Akielezea mradi huo, Ofisa wa Wizara aliyefika kushuhudia utiaji saini makubaliano ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi, Paul Kiwele alisema kuwa awali Wizara ilifanya tathmini ya kucha-gua vijiji kwa ajili ya majaribio ya mradi huo ambapo vigezo mbalim-bali vilitumika.

    Kiwele alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na Kijiji husika kuwa mbali na gridi ya Taifa, kutokuwa katika mpango wa kufikiwa na miradi ya umeme ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivi karibuni.

    Alitaja vigezo vingine kuwa ni nyumba za Kijiji husika kuwa ka-ribu pamoja na uwepo wa matumizi ya kiwango cha umeme utakao-zalishwa.

    Alieleza kuwa mradi huo wa majaribio, ulilenga kupata mikoa mi-tatu tofauti ili uzoefu utakaopatikana katika mikoa hiyo utumike ka-tika uendelezaji wa teknolojia husika katika maeneo mengine ya nchi.

    Katika makontena hayo ya umeme jua, wananchi watafaidika kwa namna mbali ikiwemo kuunganisha mashine ndogo ndogo za kusaga, kuchomelea, kuranda na kuchana mbao na hivyo kujiendeleza kiu-chumi.

    Baadhi ya wananchi wa vijiji husika hawakusita kuonesha furaha yao ya kupata huduma hiyo ya umeme na hakika waliishukuru na kuipongeza Serikali kwa ubunifu huo wa kuwapelekea wananchi hao umeme wa jua ili nao waweze kunufaika kwa namna mbalimbali ku-tokana na uwepo wa nishati hiyo muhimu.

    Ninaishukuru sana Wizara ya Nishati na Madini kuona mata-tizo yetu na kusikia kilio chetu. Imekuwa kama ndoto. Umeme huu umeniwezesha kuendesha biashara ya saluni kwa njia ya kisasa ka-bisa. Situmii tena Mkasi kunyoa wateja wangu kama hapo awali. Sasa ninatumia mashine za kunyolea na ninapata wateja wengi, hivyo kuboresha kipato changu na maisha yangu kwa ujumla, alisema Lazaro Kutamika, mkazi wa Kijiji cha Lobilo, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.

    Maneno hayo ya shukrani ya Bwana Lazaro Kutamika hakika yanaongeza chachu kwa watendaji wetu ya kuendelea kubuni miradi mbalimbali ambayo itawawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kuweza kufaidika na nishati hii muhimu ya umeme.

    Narudia kusema tena, hongera Wizara ya Nishati na Madini kwa mradi huu wa majaribio ambao umeshaanza kuonyesha mafanikio.

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Maafisa Madini waagizwa kutoa leseni za madini ya ujenzi kwa Vijiji

    Waziri wa Nishati na Madini, George simbachawene akipiga makofi mara baada ya kuzindua rasmi nyumba 18 ambazo mgodi wa dhahabu wa Geita umezijenga kwa ajili ya makazi ya kaya 1000 katika kijiji cha Ihalahala mkoani Geita.

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni mbili na milioni 213 iliyotolewa na Mgodi wa dhahabu wa Geita kama tozo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa Geita.

    Mmoja wa wananchi ambaye amefaidika na nyumba zilizojengwa na mgodi wa Geita katika kijiji cha Ihalahala mkoani Geita, akitoa salam za shukrani kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani) mara baada ya Waziri kuzindua rasmi nyumba hizo ambazo zitafaidisha kaya 1000 katika kijiji hicho.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa (Viti Maalum CCM) Jimbo la Singida, Martha Mlata (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Dkt. Miganda Manyahi (kulia), jijini Arusha kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi ya umeme. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inafanya ziara katika miradi ya umeme mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kuona hatua ya utekelezaji miradi hiyo pamoja na kuzungumza na watendaji.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda (kulia) mara baada ya Kamati hiyo kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya kupokea taarifa ya Mkoa kabla ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya umeme.

    Mgawo wa umeme Arusha kumalizika Juni

    Meneja Mradi wa Kusambaza Umeme , Mhandisi Florence Gwangombe (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa (kulia) mara baada ya kamati hiyo kuwasili kwenye eneo la mradi huo ili kujionea maendeleo ya utekelezwaji wake.

    Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB, Pal Aberg (kushoto) akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro.

    Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini , baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) , na baadhi ya watendaji wa Wizaraya Nishati na Madini wakitembelea eneo la kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Njiro nje kidogo ya jiji la Arusha.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa (wa kumi na moja kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kukamilisha ziara yake katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha KIA kilichopo mkoani Kilimanjaro.

    Na Greyson Mwase, ArushaMeneja Mradi wa Kusambaza Umeme unaojulika-na kwa jina la Electricity V unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Florence Gwangombe, amesema kuwa, tatizo la umeme kuka-tika mara kwa mara mkoani Arusha litakwisha mwezi Juni mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo katika eneo la Njiro, nje kidogo ya jiji la Arusha.

    Mhandisi Gwangombe aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ili-yofanya ziara katika kituo hicho ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuishauri serikali kuhusu usimamizi wake.

    Alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika jiji la Arusha, wateja wapya wapatao 30,000 kuungan-ishiwa umeme.

    Akifafanua kuhusu mradi huo, Mhandisi Gwangombe alisema kuwa, mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa mkopo wa kiasi cha shilingi za kitanzania 72,588, 506,400, unahusisha ujenzi wa njia za umeme yenye urefu wa kilomita 480 za msongo wa kilovolti 33 na ufungaji wa transfoma 102 za kusambaza umeme zenye ukubwa wa 33/0.4 kV.

    Alisema pia mradi huo unahusisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme vya Ilala, Sokoine katika mkoa wa Dar es Salaam na upanuzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Njiro.

    Aliongeza kuwa mradi unatekelezwa na Mkandar-asi National Contracting Company, ambaye alishinda

    zabuni ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha na mkandarasi Eltel Networks TE AB ambaye alishinda zabuni ya ujenzi na ukarabati wa mifumo ya kusam-bazia umeme katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

    Akielezea kuhusu ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Njiro, Mhandisi Gwangombe alisema kazi zinazoendelea katika kituo hicho ni pamoja na ufungaji wa transfoma mbili na ufungaji wa mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuendesha na kulinda mifumo ya umeme.

    Aliongeza kuwa, uagizaji na utengenezaji wa vifaa umekamilika kwa asilimia 85, kazi za ujenzi zime-kamilika kwa asilimia 76 pamoja na kumalizika kwa kufunga na kuunganisha vifaa na mifumo ya umeme.

    Alisisitiza kuwa, mradi huo unategemewa kuongeza ukuaji wa uchumi katika mkoa wa Arusha pamoja na mikoa mingine ikiwemo Shinyanga na Mwanza kwani utachochea ukuaji wa viwanda vido-go vidogo na biashara katika maeneo husika pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.

    Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba ali-iambia Kamati ya Bunge kuwa ongezeko la wateja wa kawaida na viwanda lilisababisha ongezeko la kasi ya matumizi kufikia Megawati 70 hali iliyopelekea shirika kuboresha na kujenga vituo vya kupoozea na kusam-bazia umeme.

    Mhandisi Mramba alisema, Shirika limeamua kufanya mapinduzi katika sekta ya umeme kwa ku-hakikisha linashirikiana na wawekezaji mbalimbali na wataalamu wake katika ujenzi wa vituo vya kuzalisha na kusambaza umeme ili kuzalisha nishati ya umeme ya kutosha na ya uhakika.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James Mataragio (katikati), akiongea jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (kulia) pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini waliohudhuria Mkutano wa Saba wa Mafuta, uliofanyika mjini Kigali, Rwanda. Kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri, Mhandisi Robert Dulle.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage akieleza masuala mbalimbali kuhusu sekta ya nishati nchini zikiwemo fursa za uwekezaji wakati wa mkutano wa Saba wa Mafuta uliofanyika hivi karibuni mjini Kigali, Rwanda.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) (wa kwanza mbele) Michael Mwanda, baadhi ya Maofisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na wadau mbalimbali wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa Saba wa Mafuta, uliofanyika mjini Kigali, Rwanda.

    Mwenyekiti wa Kijiji cha Lobelo kilichoko Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, Alex Ngulele (mwenye kofia), akitoa shukrani kwa Maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wataalam kutoka Kampuni ya Elektro Merl kwa kufungiwa umeme katika Kijiji chake.

    MATUKIO KATIKA PICHAKamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja (kushoto) akielezea mikakati iliyowekwa na Serikali katika kuimarisha ulinzi katika machimbo ya Merelani mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani). Kamati hiyo ilikutana na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) jijini Arusha, ili kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi na kutoa maazimio.

    Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Singida (Viti Maalum CCM) Martha Malata akisisitiza jambo wakati Kamati hiyo ilikutana na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na Taasisi zake , ili kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi na kutoa maazimio.

    Taa ikiwaka ndani ya nyumba ya Stephano Manzo, mkazi wa Kijiji cha Silale, wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma. Nyumba hii ni miongoni mwa kaya zilizounganishiwa huduma ya umeme kupitia mradi wa makontena ya umeme wa jua.

    Taa zilizofungwa mtaani/barabarani katika Vijiji vya Lobilo la Silale, wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma. Taa hizi zinazotumia umeme wa jua na ni sehemu ya mradi wa makontena ya umeme wa jua.

    u

    u

    u

    u

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mradi Mkubwa wa Upepo Singida kutumia Dola milioni 132

    Na Greyson Mwase, Singida

    Mkuu wa Kitengo cha Mi-u n d o m -binu na

    Nishati kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Pascal Malesa amesema kuwa serikali inatarajia kutumia kiasi cha Dola za Marekani Milioni 132 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 50 utakaotokana na nishati ya upepo ifikapo mape-ma mwaka 2016.

    Malesa aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipofanya ziara ya kutembelea mradi huo unaojengwa katika eneo la Kisesile nje kidogo ya mji wa Singida.

    Alisema mradi huo unatekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Maen-deleo la Taifa (NDC) lenye hisa asilimia 60, Shirika la Umeme Nchi-ni (Tanesco) asilimia 20 na kampuni ya Power Pool East Africa Lim-ited yenye asilimia 20 ya hisa chini ya kampuni

    ya ubia iitwayo Geo Wind Power Tanzania Limited (Geo Wind) il-iyoundwa mwaka 2011.

    Malesa alieleza kuwa, gharama hizo zinahusisha utekelezaji wa mradi awamu ya kwanza ambazo ni kwa ajili ya kuzalisha mega-wati 50, ujenzi wa msongo wa umeme wa kiasi cha kilovolti 220 kwa umbali wa kilomita 12 na kuunganisha kwe-nye gridi ya taifa.

    Alisema fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China na kuongeza kuwa hivi sasa NDC inafuatilia mkopo huo chini ya udhamini wa Serikali kupitia Wizara ya Fed-ha.

    Akielezea matarajio ya mradi Malesa alise-ma mara baada ya ku-kamilika, mradi huo utaimarisha uwezo wa Gridi ya Taifa kwani utazalisha umeme wa uhakika.

    Alisema mradi utaingiza Dola za Mare-kani milioni 23.2 kwa mwaka kutokana na mauzo ya umeme na ku-toa ajira zipatazo 2,200 na kusisitiza kuwa, mra-di utalipa kodi mbal-imbali serikalini ikiwa ni pamoja na Kodi ya

    Ongezeko la Pato (VAT) na nyinginezo.

    Akielezea suala la fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo Malesa alisema kuwa jumla ya shilingi milioni 418 zililipwa kama fidia kwa wakazi waliopisha mradi huo katika awa-mu mbili tofauti.

    Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndas-sa, aliitaka serikali ku-harakisha mchakato wa mkopo kutoka Benki ya Exim ili mradi huo uanze mara moja na mkoa wa Singida uweze kunufaika na mradi huo.

    Ndassa alisema kuwa, mbali na uwezo wa kuzalisha megawati 50, mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi megawati 300 kiasi ambacho ni kikubwa kwenye Gridi ya Taifa.

    Alisema mbali na kupunguza tatizo la mgawo wa umeme, mradi huo pia utapele-kea punguzo la bei ya umeme kutoka shilingi za kitanzania senti 30 ya awali hadi senti 13 na hivyo kuchangia kwe-nye ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa (katikati) akisisitiza jambo katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya upepo lililopo Kisesile wilayani Singida Mjini mara kamati hiyo ilipotembelea mradi huo ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na watendaji wa eneo hilo.

    Kuzalisha megawati 50 , ajira 2,200

    UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    CHINA SCHOLARSHIP OPPORTUNITIES FOR 20151. INTRODUCTION

    Applications are invited from qualified Tanzanians to apply for postgraduate studies in the one of Chinas best Oil and Gas Studies, the China University of Geosciences (Wuhan).

    Sponsorship will be in the fields of oil and gas. The scholarships will be processed in collaboration with the Embassy of China in Tanzania and will be awarded to the best twenty two (22) candidates.

    2. ELIGIBILITY (a) Applicants must be holders of Bachelors degree in Earth Sciences or Engineering from recog-nized universities; (b) Masters Degree and Ph.D. applicants should not be older than 35 and 40 years respectively; and (c) Applicants will be required to pay for a ticket to China; other costs will be paid by the Government of China.

    3. MODE OF APPLICATION

    3.1 Interested applicants should write a letter of application to The Permanent Secretary of the Min-istry of Energy and Minerals in which they should state their academic and practical background in the fields of gas and oil; level of studies they wish to pursue (Masters or Ph.D.); why they should be offered the scholarship; and how they will use their knowledge for the benefit of the nation. 3.2 Application for admission can be conducted online through http://www.csc.edu.cn/laihua or http://www.campuschina.org .3.3 All applications should be addressed to:

    Permanent Secretary, Ministry of Energy and Minerals, P.O. Box 2000, Dar es Salaam. 3.4 Applications must be attached with:

    a) Two copies of application forms printed from online applications;b) Two original sets of Letter of Recommendation; c) Two photocopies of academic transcripts of the most advanced studies (notarized photo-copy); d) Two photocopies of Diploma of the Most Advanced Studies (notarized photocopy); e) Two photocopies of Foreigner Physical Examination Form; f) Two photocopies of Blood Test Report; g) Two copies of Study Plan in China; h) Two copies of Birth Certificate; i) Reliable contacts: postal address and telephone numbers; j) A detailed Curriculum Vitae (CV); k) Copies of Form IV and VI National Examination Certificates; and l) One recent passport size photograph.

    Note: 3.5 All the above mentioned full package of application documents should be arranged in two complete sets and use paper DIN A4.3.6 Testimonials/ provisional results/ statements of results will not be accepted. 3.7 Applicants who are employed in the Public Service should route their applications through their respective employers; and 3.8 Any application without relevant documents shall not be considered.

    3.5. Closing Date: 20th March, 2015. 3.6. Notification: Shortlisted applicants will be notified by 10th April, 2015.

    Permanent Secretary Ministry of Energy and Minerals 5 Samora Machel Avenuee P. O. Box 2000, 11474 Dar es Salaam E-Mail: [email protected] Website: www.mem.go.tz

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    http://www.mem.go.tz

    nNi vilivyo mbali na gridi ya Taifa nKutumia bure kwa miaka miwili Na Veronica Simba Dodoma

    Jumla ya Vijiji 10 katika Wilaya za Kong-wa, Mlele na Uyui, mkoani Dodoma, vimeunganishiwa umeme kupitia Mradi wa makontena ya kuzalisha umeme un-aotokana na jua.

    Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, upo katika hatua ya majaribio na unalenga kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa gridi ya Taifa.

    Wizara ya Nishati na Madini wiki hii, ili-saini makubaliano ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Mradi huo na Kampuni ya Elektro-Merl ya nchini Austria ambayo ndiyo ilileta na kufunga makontena 14 ya umeme wa jua pamo-ja na mfumo wa usambazaji umeme kwenye ny-umba zilizoko katika vijiji husika.

    Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwe-bangira alisema wananchi waliounganishiwa umeme huo wa jua, watapata huduma hiyo bure kwa kipindi cha miaka miwili ya mwanzo am-bayo ni ya matazamio.

    Alisema kuwa, baada ya miaka miwili, kuanzia tarehe waliyosaini makubaliano, wa-nanchi wa vijiji husika wataanza kuchangia fed-ha kidogo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalim-bali kama betri na paneli vinavyotumika katika mradi huo, ambavyo vina ukomo wake.

    Vifaa hivi vina gharama kubwa sana, hivyo inabidi kuwa na utaratibu wa kukusanya fedha za kutosha ili kuweza kununua vifaa vingine pin-di vifaa vilivyopo vinapofikia ukomo wake wa kutumika. Hivyo kila mwananchi anayetumia huduma hii inabidi achangie gharama, alisema Mhandisi Rwebangira.

    Aidha, aliongeza kuwa, ili kuhakikisha mradi unatoa matokeo yaliyotarajiwa, inabidi uendeshwe na mtu au kampuni yenye utaalamu wa masuala mbalimbali ya umeme ikiwemo mitambo ya umeme jua pamoja na uzoefu na ufahamu wa kutosha kuhusu mitambo ya aina hiyo.

    Hivyo, kila baada ya miaka miwili, ukiacha kipindi cha majaribio ambapo mradi utakuwa chini ya Wizara, atachaguliwa mtaalamu au kampuni kupitia njia ya ushindani ambaye atalipwa kwa utaratibu utakaokubaliwa katika mkataba, alisema Rwebangira.

    Kwa upande wake, Ofisa wa Wizara ali-yefika kushuhudia utiaji saini makubaliano ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi, Paul Kiwele alisema Wizara ilifanya tathmini ya kuchagua vijiji kwa ajili ya majaribio ya mradi huo ambapo vigezo mbalimbali vilitumika.

    Kiwele alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamo-ja na Kijiji husika kuwa mbali na gridi ya Taifa, kutokuwa katika mpango wa kufikiwa na miradi ya umeme ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivi karibuni.

    Alitaja vigezo vingine kuwa ni nyumba za

    Kijiji husika kuwa karibu pamoja na uwepo wa matumizi ya kiwango cha umeme utakaozal-ishwa.

    Aidha, kwa kuwa mradi huu ni wa majar-ibio, ililengwa kupata mikoa mitatu tofauti ili uzoefu utakaopatikana utumike katika uende-lezaji teknolojia hii katika maeneo mengine ya nchi, alisema.

    Naye, Mtaalam kutoka Kampuni ya Elek-tro Merl, Mhandisi Hannes Merl akizungum-zia mkataba uliosainiwa na Wizara pamoja na Kampuni yake, Januari mwaka jana, alisema mbali na kufunga makontena 14 ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme, mkataba pia ulihusisha ufungaji wa nyaya, taa, swichi na soketi moja kwa kila nyumba iliyofiki-wa.

    Mhandisi Merl alisema kila kontena lina uwezo wa kuzalisha kWp 13.75 ambapo kila nyumba ya makazi na huduma za biashara zim-etengewa Wati 250 na taasisi za kijamii zimet-engewa Wati 500.

    Aliongeza kuwa, wananchi wanaweza ku-unganisha mashine ndogo ndogo za kusaga, ku-chomelea, kuranda na kuchana mbao pamoja na nyinginezo kutoka katika makontena hayo hivyo kunufaika na shughuli za kiuchumi.

    Pia, Mhandisi Merl alisema mradi umetoa jokofu kwa kila zahanati na vituo vya afya vili-vyopo katika vijiji vinavyonufaika na mradi huo. Aidha, alisema kuwa mradi umefunga taa za mitaani kwa kila kijiji kilichonufaika na mradi husika.

    Kwa upande wao, baadhi ya wananchi ka-tika vijiji vilivyonufaika na mradi huo wa ma-kontena ya umeme wa jua, waliishukuru na kui-pongeza Serikali kwa wazo zuri la kuwapelekea wananchi hao umeme wa jua ili nao waweze kunufaika kwa namna mbalimbali kutokana na uwepo wa nishati hiyo muhimu.

    Ninaishukuru sana Wizara ya Nishati na Madini kuona matatizo yetu na kusikia kilio che-tu. Imekuwa kama ndoto. Umeme huu umeni-wezesha kuendesha biashara ya saluni kwa njia ya kisasa kabisa. Situmii tena Mkasi kunyoa wateja wangu kama hapo awali. Sasa ninatumia mashine za kunyolea na ninapata wateja wengi, hivyo kuboresha kipato changu na maisha yangu kwa ujumla, alisema Lazaro Kutamika, mkazi wa Kijiji cha Lobilo, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.

    Wizara ya Nishati na Madini imekuwa iki-tumia mbinu mbalimbali katika jitihada za ku-wafikishia wananchi huduma ya umeme. Kwa kupitia mradi huo wa makontena ya kuzalisha umeme kutokana na jua, Serikali inafanya ma-jaribio ya kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa gridi ya Taifa kwa kutumia teknolojia husika.

    Vijiji vilivyonufaika na mradi huo kwa awa-mu ya kwanza ni pamoja na Lobilo, Leganga, Ngutoto na Silale vya mkoa wa Dodoma. Ving-ine ni Tura, Loya na Lutende vilivyoko mkoa wa Tabora. Aidha, kwa mkoa wa Katavi, vijiji vili-vyonufaika ni Nsenkwa, Mapili na Ilunde.

    Wizara yavipatia vijiji 10 umeme jua wa Makontena

    Baadhi ya watalaam kutoka Kampuni ya Elektro Merl ya nchini Austria ambao walileta na kufunga makontena ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme kwa vijiji 10 vilivyo mbali na gridi ya taifa, pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakikagua moja ya makontena ya umeme wa jua katika Kijiji cha Lobilo, wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma hivi karibuni.

    Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya Elektro Merl, wakijadiliana namna

    ya kuboresha mradi wa makontena ya umeme wa jua - awamu ya pili, baada ya kukamilika kwa

    awamu ya kwanza. Mradi huo unalenga kuwapatia umeme wananchi wa vijiji vilivyo mbali na gridi

    ya taifa na tayari, vijiji 10 vimenufaika kupitia mradi huo.

    Baadhi ya nyumba za wananchi katika Vijiji vya Lobilo na Silale, wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma, ambazo zimeunganishiwa na huduma ya umeme wa jua kupitia makontena maalum.

    Makontena ya umeme wa jua yaliyopo katika Vijiji vya Lobilo na Silale, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Makontena haya ni sehemu ya Mradi unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ambapo upo katika hatua ya majaribio na unalenga kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa gridi ya Taifa.

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Jacqueline Mattowo

    Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongela hivi karibuni ameipongeza

    Kampuni ya uzalishaji dhaha-bu ya STAMIGOLD kupitia mgodi wake wa Biharamulo

    kwa kuwa ndio mgodi pekee unaoendeshwa na kusimamiwa na watanzania hapa nchini na kufanya vizuri katika uzalishaji hivyo aliahidi kutoa ushiriki-ano kwa Kampuni ili kuweza kutimiza malengo yake na ku-leta sifa na tija kwa taifa.

    Pongezi hizo zilitolewa wakati Meneja Mkuu wa Mgo-di wa Biharamulo Mhandisi Dennis Sebugwao alipofika ka-

    tika ofisi ya Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Kagera kwa nia ya kujitambulisha na kuelezea shughuli mbalimbali zinazo-fanywa na mgodi wa Bihara-mulo ambao ni mgodi pekee wa dhahabu katika mkoa wa Kagera.

    Mhandisi Sebugwao alieleza kuwa mgodi umekuwa ukisimamiwa na kuendeshwa na wataalamu wa kitanzania

    waliopo katika vitengo mbalim-bali mgodini tangu mgodi ul-ipokabidhiwa kutoka kwa Kam-puni ya African Barrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka 2013 na umeendelea kufanya vi-zuri ingawa bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ufinyu wa mtaji wa kuende-sha mgodi.

    Mbali na kuelezea shughuli zi-nazofanywa na mgodi, mafanikio pamoja na changamoto zilizopo, Mhandisi Sebugwao pia alim-weleza Mkuu wa Mkoa mpango wa mgodi wa kusaidia kupun-guza tatizo la uhaba wa madawati katika mkoa wa Kagera ambapo tayari madawati 1000 yamek-wisha tolewa katika shule za msingi zenye upungufu ndani ya wilaya ya Biharamulo na kuahidi kufikisha madawati mengine 500 katika shule za mkoani Kagera zenye upungufu wa madawati.

    Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa mbali na kutoa pongezi aliahidi kutoa ushirikiano kwa mgodi huo na kueleza kuwa STAMIGOLD imekuwa ni dira kwa watanzania wote kwa kuo-nyesha kuwa watanzania wana uwezo wa kuendesha migodi bila kutegemea wataalam kutoka nje ya nchi.

    Kila mtu anao wajibu wa kutimiza majukumu na wajibu wake ili kufikia malengo mliyoji-

    wekea na mkoa upo pamoja nanyi na tutatoa ushirikiano wa namna yeyote ile kwani hii ni nafasi pekee ambayo mmepewa kuonyesha dunia nzima kuwa watanzania tunaweza na mkiweza kudhibiti-sha hilo hata pale mgodi utakapo-fungwa mtaaminiwa na kupewa miradi mingine muisimamie, na hii itaondoa ile dhana potofu ya kushindwa kwani watanzania walio wengi wamejijengea tabia ya kushindwa kabla hata ya kuanza kufanya jamboalisisitiza Mkuu wa Mkoa.

    Aliiasa STAMIGOLD ku-tumia teknolojia mbalimbali za kisasa katika shughuli zake ili kufikia malengo yake na kutafuta namna ya kukabiliana na changa-moto walizonazo pamoja na ku-fanikisha malengo waliyojiwekea badala ya kubaki na mifumo ya kizamani ambayo itachelewesha maendeleo.

    Watendaji wa STAMIGOLD walioambatana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Biharamulo ni pamoja na Meneja wa Maen-deleo Endelevu, Korodias Shoo, Meneja Utawala na Fedha, Enea Minga, Mrakibu wa Ulinzi, Lute-ni Mstaafu Rueshwa Katakweba, Msimamizi wa Mawasiliano Jac-queline Mattowo pamoja na Msi-mamizi wa ulinzi SUMA JKT, Meja Cresentious Magori.

    MKUU WA MKOA KAGERA AIPONGEZA STAMIGOLD

    Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela katikati (mwenye shati la kitenge) na Meneja mkuu wa mgodi wa Biharamulo Mhandisi Dennis Sebugwao (wa kwanza kulia)Wakiwa katika picha ya pamoja nje za ofisi ya mkuu wa mkoa mara baada ya mkutano . wengine katika picha ni viongozi wa vitengo mbalimbali kutoka mgodini.

    n Ni kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalamu wa kitanzania

    Na Rhoda James, Dar Salaam

    Kampuni za One Planet Africa na WarnerCom (T) zimeonesha nia ya ku-wekeza katika uzalishaji wa umeme unaotokana

    na jua nchini. Hayo yalibainika mwishoni mwa

    wiki wakati watendaji wa kampuni hizo walipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madi-ni (Madini), Charles Kitwanga, wiza-rani, kwa lengo la kujadili uwekezaji wa kampuni hizo katika uzalishaji wa umeme jua mkoani Shinyanga.

    Wakizungumza katika kikao hi-cho, Mkurugenzi wa One Planet Africa, John Wood na Mkurugenzi Mkuu wa WarnerCom,Mark Buy-amba walieleza kuwa, tayari kampuni hizo zimepata eneo la ukubwa wa ekari 15,000 wilayani Kishapu Mkoa-ni Shinyanga.

    Tunazo fedha, na uzoefu wa ku-tumia teknolojia hii kuzalisha umeme utokanao na jua, tunaahidi kufanya

    vizuri katika kufanikisha zoezi hili wakati tutakapoanza uzalishaji, alisema John.

    Aidha, Wood alisema kuwa, kam-puni hizo imelenga kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150, jambo ambalo litaongeza upatikanaji wa umeme kwa Shirika la Umeme Tan-zania (Tanesco) na hivyo wananchi kunufaika na huduma hiyo.

    Vilevile, Wood aliongeza kuwa, mradi huo utakapoanza unatarajia kutoa ajira za kudumu zipatazo 50 hadi 100 wakati ajira za muda zina-tarajia kuwa 400 hadi 600.

    Naye, Naibu Waziri Kitwanga al-izisisitiza kampuni hizo kujenga ma-husiano mazuri na wananchi wanao-zunguka maeneo yao ya uwekezaji ili kuziwezesha kuendesha shughuli zao kikamilifu bila kuwepo migogoro baina yao na wananchi.

    Aidha, Kitwanga aliongeza kuhu-su umuhimu wa kampuni hizo kuzin-gatia utoaji wa huduma za jamii ka-tika maeneo yanayozunguka maeneo ya uwekezaji ikiwemo kujenga shule, zahanati na miundombinu ya bara-bara.

    Kampuni zaonesha nia kuzalisha umeme wa Jua Kishapu

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (katikati), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa One Planet Africa John Wood (wa kwanza kushoto kwa waziri) wakati wa kikao ambapo kampuni za One Planet Africa na Warner Com (T) zimeonesha nia kuwekeza katika uzalishaji umeme unaotokana na jua. Wengine katika picha ni wawakilishi wa kampuni hizo na watendaji wa wizara.

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    EOI No. ME/008/2014-2015/HQ/C/3for

    Provision of consultancy services for conducting MEM service delivery survey (SDS) and self assessment (SA) exercise.

    Expression of InterestDate: 9th March, 2015

    1. This invitation for expression of interest follows the General Procurement Notice (GPN) which appeared in Daily News Issue no. 0856-3812 dated 17th July, 2014.

    2. The Government of the United Republic of Tanzania has set aside funds for the operation of the Ministry of Energy and Minerals during the financial year 2014/2015. It is intended that part of the proceeds of the fund will be used to cover eligible payment under the contract for the Provision of consultancy services for conducting MEM service delivery survey (SDS) and self assessment (SA) exercise.

    3. The Ministry of Energy and Minerals now invites eligible firms to indicate their interest in providing the services which include Provision of consultancy services for conducting MEM service delivery survey (SDS) and self assessment (SA) exercise.

    4. Interested firms must provide information indicating that they are qualified to perform the services by submit-ting consultants profile, description of similar assignments, experience in similar conditions, availability of appropriate skills among staff, etc. Consultants may associate to enhance their qualifications.

    5. A consultant will be selected in accordance with the procedures set out in the Public Procurement Act No. 7 of 2011 and the Public Procurement Regulations, 2013 Government Notice No. 446 (hereinafter called Procure-ment Regulations).

    6. Selection will be conducted through Consultant qualification selection (CQS) procedures specified in the Public Procurement Regulations.

    7. Interested eligible consultants may obtain further information from the office of the Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Energy and Minerals (MEM) 5 Samora Avenue, 6th Floor, Room No. 10 Wing B 11474 Dar es salaam, Tanzania from 8:30am to 3:30pm on Monday to Friday inclusive except on public holidays.

    8. Expressions of Interest (EoI) must be delivered to the address below Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Energy and Minerals (MEM) 5 Samora Avenue, 6th Floor, Room No. 10 Wing B 11474 Dar es salaam, Tanzania at or before Monday 23rd March, 2015 10:00am.

    9. Late Expressions of Interest shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.

    Permanent Secretary,Ministry of Energy and Minerals (MEM) 5 Samora Avenue, 6th Floor, Room No. 10 Wing B 11474

    Dar es salaam, Tanzania

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    AWAMU YA PILI YA KUKARIBISHA MAOMBI YA KUPATA RUZUKU KWA WACHIMBAJI WADOGO

    WA MADINI NCHINI Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini chini ya Mradi Endelevu wa Usimamizi wa Rasilimali Madini (SMMRP) inakaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya Pili kwa wachimbaji wadogo nchini. Malengo ya ruzuku (a)Kuendeleza uchimbaji mdogo ili uwe na tija; (b)Kuwakwamua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuongeza Pato la Taifa; (c)Kuendeleza mkakati wa kurasimisha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini ; na (d)Kutoa mitaji ili kusaidia ukuaji wa tasnia ya uchimbaji mdogo wa madini na uongezaji thamani ya

    madini wenye Matokeo Makubwa Sasa. Namna ya kuomba

    Waombaji wafike kwenye Ofisi za madini zilizopo mikoani kwa ajili ya kuchukua fomu, kuzijaza na ku-wasilisha fomu hizo zikiwa zimejazwa kikamilifu na viambatanisho vyake kwenye Ofisi mwombaji alipochukulia fomu. Fomu zitaanza kutolewa tarehe 1 Machi, 2015 na mwisho wa kurudisha fomu kwa ajili ya ruzuku awamu ya pili ni saa 9:30 Alasiri tarehe 27 Machi, 2015. Utoaji wa Taarifa Kwa Waombaji

    Baada ya mchakato wa kuchambua maombi kukamilika, mwombaji atajulishwa kwa maandishi kuhusu kukubaliwa au kukataliwa kupitia anuani yake. Mchakato mzima wa utoaji ruzuku utakuwa wa uwazi na bila upendeleo. Imetolewa na

    Mhandisi Ngosi C. X. Mwihava KAIMU KATIBU MKUU

    Fikisheni Mahakamani wanaotoza zaidi ya Sh.177, 000/ - Ndassa

    Na Greyson Mwase, Bahi - Dodoma

    Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ni-shati na Madini, Richard Ndassa

    amewaambia wakazi wa kata ya Ibihwa iliyopo wilayani Bahi mkoani Dodoma kuwa, gharama za kuunganishiwa huduma ya umeme zimeshuka hadi shilingi 177,000 na iwapo watatozwa zaidi ya kiwango hicho, na watumishi wasio waamini-fu, wana haki ya kuwafikisha mbele ya vyombo vya kisheria.

    Ndassa alisema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ni-shati na Madini ilipotembelea wilaya ya Bahi kwa lengo la kukagua miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.

    Ndassa alisema kuwa, Seri-kali imekuwa ikijitahidi kupunguza gharama za kuunganishiwa umeme hasa maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kuhakikisha kila mwananchi anapata nishati hiyo muhimu na kujiletea maendeleo.

    Alisema kuwa, Serikali ka-tika kuhakikisha kila mwananchi anaondokana na umasikini, Serikali kupitia REA iliamua kupunguza

    gharama za kuunganishiwa umeme kwa wananchi wanaoishi vijijini ili waweze kupiga hatua kimaendeleo, na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiandaa na uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

    Iwapo atatokea mtumishi na kuwatoza gharama zaidi ya ile inayohitajika kulipwa kisheria, basi mna haki ya kumfikisha polisi ili afunguliwe mashtaka, alisema Ndassa

    Aliendelea kusema kuwa, umefika wakati wa watanzania kuchangamkia fursa mbalim-bali zinazojitokeza mara baada ya kukamilika kwa miradi ya umeme kwa kuwa umeme ndio kitovu cha ukuaji wa uchumi katika nchi yoyote.

    Kuna vijiji ambayo vimeshaan-za kunufaika na huduma ya umeme, nawasihi muanzishe viwanda vidogo vidogo vya kukoboa nafaka, kukamua mafuta ya alizeti ili ku-jiongezea kipato, alisema Ndassa.

    Naye, Mtendaji wa Kata, Jeni-pha William alisema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme ya REA Awamu ya Pili pamekuwepo na changamoto ya vijiji vingine ku-rukwa hali inayopelekea wananchi wachache kupata umeme.

    Akifafanua jinsi Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lilivyoji-panga kukabiliana na changamoto hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Me-

    Moja ya mnara kwa ajili ya njia kuu ya umeme ikiwa chini ya ujenzi unaosimamiwa na kampuni ya Jyoti Structures Limited kutoka India. Nguzo moja inagharimu shilingi milioni 200.

    neja wa Tanesco Dodoma, Zakayo Temu alisema kuwa, kazi ya kujenga miudombinu ya umeme chini ya REA Awamu ya Pili imekuwa ikifanywa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na uwiano na mikoa mingine.

    Alisema kuwa, vijiji hivyo vilivyokosa umeme vimewekwa katika mpango wa fedha wa mwaka ujao.

    Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (kulia) akiieleza Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida hadi Shinyanga inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili. Kamati ya Bunge imefanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na wananchi