mheshimiwa pinda hakupinda bali wanasheria wamecheua

3
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA Mwananchi Na Prof. Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Ujenzi wa dhana potofu ndani ya akili na mioyo ya wana sheria ndicho chanzo cha kulaumu hadi kufikia kutamka bayana kumshitaki Waziri Mkuu Mizengo Pinda juu ya Kauli yake aliyoitoa Bungeni ikidaiwa kwenda kinyume na Haki za Binadamu. Lakini kabla wanasheria hao hawajacheua kauli zao hizo ingekuwa vyema wangefanya tathmini ya Jeshi la Polisi Kimuundo na Utendaji Kazi wake. Jeshi la Polisi liliundwa kama moja ya njia za kujenga Ukoloni ambapo utawala wa Waingereza uliendeleza Tarakibu ya Ireland (Royal Irish Constabulary Model) iliyokuwa tofauti na Tarakibu ya Kiingereza (Metropolitan Model) lengo kubwa ilikuwa ni kusimamia Sheria za Kijeshi (Paramilitary Law and Order) ingawa baadaye lilisimamia Usalama wa Raia lenye mamlaka ya kulinda kutokea kwa makosa ya jinai kwa faida ya Jamii. Tarakibu ya Ireland ilihamia India na kuboreshwa kisha kusambaa kwenye Makoloni mengine ikiwemo Afrika ya Mashariki. Hata hivyo, kuwepo kwa jeshi la kitaalamu kulikuwa ni kulinda Ubepari kwa ajili ya kutafuta masoko mapya na rasilimali mbalimbali. Jeshi la Kikoloni liliwajibika kwa Watawala, kuifanya jamii iheshimu utawala uliokuwepo likijengwa kwa utaratibu wa Amri kutoka vyeo vya juu hadi chini kiutawala (pecking order). Ingawa wakati wa Tanganyika Jeshi lilikuwa likijengwa kwa kulinda sekta za mazao yaliyomilikiwa na wageni, wakulima wazawa, na kutawala kupitia kwenye Utawala wa Asili chini ya Machifu na kwa upande fulani chini ya Maafisa wa Kikoloni. Baadaye Jeshi hilo lilikuwa chini ya utawala wa wilaya ambao ulifanya pia kazi ya Mahakama. Afisa wa Wilaya alikuwa ndiye Kiongozi wa Polisi, Hakimu na Afisa Mkuu wa Magereza. Kufuatia Muundo wa Vyama vya Wafanyakazi na Waafrika kuukataa utawala wa kikoloni, Jeshi la Polisi lilifanyiwa mabadiliko na kuimarishwa kijeshi zaidi. Hata hivyo kufuatia kuundwa kwa TANU Wakoloni waliacha kutumia Jeshi katika hadhi ya kijeshi isipokuwa pale tu migomo inapotokea kwa kile kilichoitwa “Police Motorized Companies” kilichorithiwa baadaye na Kitengo cha kutuliza ghasia (FFU). Kitengo hiki hapo awali kilitumika wakati wa migomo ya wafanyakazi na wakati wa Operasheni Vijiji na kuwaondoa Wabarabaig kwenye eneo lililotolewa kwa NAFCO; aidha lilitumika kwa wanafunzi wa chuo kikuu miaka ya sabini wakati wa migomo ya Akivaga na wakati Fulani kutuliza ghasia za wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mwaka 1986. Aidha, Jeshi hilo limetumika kutuliza ghasia kwenye Msikiti wa Mwembechai Magomeni Mwaka 1993, Uchaguzi wa Zanzibar Miaka ya 2000 na 2005 na maeneo mengi yakiwepo yale ya mjini Arusha hivi karibuni. Kwa Mujibu wa Sheria ya Polisi Sura ya 322 kifungu Na 5 neno “Force” kwa maana ya Jeshi la Polisi kinabainisha kuwa Jeshi la Polisi; litatumika ndani na mahala popote pa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kulinda amani, kusimamia sheria na Kanuni, kuzuia na

Upload: prof-handley-mpoki-mafwenga

Post on 11-Jan-2017

97 views

Category:

Documents


13 download

TRANSCRIPT

Page 1: MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA

MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA

Mwananchi

Na Prof. Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM

(taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

Ujenzi wa dhana potofu ndani ya akili na mioyo ya wana sheria ndicho chanzo cha kulaumu hadi

kufikia kutamka bayana kumshitaki Waziri Mkuu Mizengo Pinda juu ya Kauli yake aliyoitoa

Bungeni ikidaiwa kwenda kinyume na Haki za Binadamu. Lakini kabla wanasheria hao

hawajacheua kauli zao hizo ingekuwa vyema wangefanya tathmini ya Jeshi la Polisi Kimuundo na

Utendaji Kazi wake.

Jeshi la Polisi liliundwa kama moja ya njia za kujenga Ukoloni ambapo utawala wa Waingereza

uliendeleza Tarakibu ya Ireland (Royal Irish Constabulary Model) iliyokuwa tofauti na Tarakibu

ya Kiingereza (Metropolitan Model) lengo kubwa ilikuwa ni kusimamia Sheria za Kijeshi

(Paramilitary Law and Order) ingawa baadaye lilisimamia Usalama wa Raia lenye mamlaka ya

kulinda kutokea kwa makosa ya jinai kwa faida ya Jamii. Tarakibu ya Ireland ilihamia India na

kuboreshwa kisha kusambaa kwenye Makoloni mengine ikiwemo Afrika ya Mashariki. Hata

hivyo, kuwepo kwa jeshi la kitaalamu kulikuwa ni kulinda Ubepari kwa ajili ya kutafuta masoko

mapya na rasilimali mbalimbali.

Jeshi la Kikoloni liliwajibika kwa Watawala, kuifanya jamii iheshimu utawala uliokuwepo

likijengwa kwa utaratibu wa Amri kutoka vyeo vya juu hadi chini kiutawala (pecking order).

Ingawa wakati wa Tanganyika Jeshi lilikuwa likijengwa kwa kulinda sekta za mazao

yaliyomilikiwa na wageni, wakulima wazawa, na kutawala kupitia kwenye Utawala wa Asili chini

ya Machifu na kwa upande fulani chini ya Maafisa wa Kikoloni. Baadaye Jeshi hilo lilikuwa chini

ya utawala wa wilaya ambao ulifanya pia kazi ya Mahakama. Afisa wa Wilaya alikuwa ndiye

Kiongozi wa Polisi, Hakimu na Afisa Mkuu wa Magereza.

Kufuatia Muundo wa Vyama vya Wafanyakazi na Waafrika kuukataa utawala wa kikoloni, Jeshi la

Polisi lilifanyiwa mabadiliko na kuimarishwa kijeshi zaidi. Hata hivyo kufuatia kuundwa kwa

TANU Wakoloni waliacha kutumia Jeshi katika hadhi ya kijeshi isipokuwa pale tu migomo

inapotokea kwa kile kilichoitwa “Police Motorized Companies” kilichorithiwa baadaye na Kitengo

cha kutuliza ghasia (FFU). Kitengo hiki hapo awali kilitumika wakati wa migomo ya wafanyakazi

na wakati wa Operasheni Vijiji na kuwaondoa Wabarabaig kwenye eneo lililotolewa kwa NAFCO;

aidha lilitumika kwa wanafunzi wa chuo kikuu miaka ya sabini wakati wa migomo ya Akivaga na

wakati Fulani kutuliza ghasia za wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mwaka 1986.

Aidha, Jeshi hilo limetumika kutuliza ghasia kwenye Msikiti wa Mwembechai Magomeni Mwaka

1993, Uchaguzi wa Zanzibar Miaka ya 2000 na 2005 na maeneo mengi yakiwepo yale ya mjini

Arusha hivi karibuni.

Kwa Mujibu wa Sheria ya Polisi Sura ya 322 kifungu Na 5 neno “Force” kwa maana ya Jeshi la

Polisi kinabainisha kuwa “Jeshi la Polisi; litatumika ndani na mahala popote pa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania kwa lengo la kulinda amani, kusimamia sheria na Kanuni, kuzuia na

Page 2: MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA

kutafiti jinai, kulinda wahalifu, na kulinda mali na litatumika kwa ajili ya kazi zote zilizobainishwa

na watapaswa kuwa na silaha”.

Polisi wanapambana na kazi ngumu na ya hatari ambayo ni lazima udhibiti wa fujo ufanyike, na

hivyo kazi zao lazima ziwe na upinzani kutoka kwa jamii kwa vile kuna baadhi ya watu hawaridhii

kukamatwa, hivyo nguvu shurti itumike. Ukosekanaji wa nguvu umesababisha Polisi kuuwawa,

kuumia na kukosa heshima kwa wananchi na hivyo kuacha kundi la wanaofanyiwa uharifu kukosa

kinga na haki zao. Hata hivyo, nguvu inatakiwa kuwa ndogo (minimum force) katika kufikia

malengo yaliyopo; Kabla ya kutumia nguvu polisi wanapaswa kushawishi, kutumia nguvu bila

silaha, kutumia nguvu na silaha zisizo za hatari, nguvu kwa kutumia silaha zenye madhara, na

mwisho huwa ni nguvu iliyokithiri. Hata hivyo zipo silaha zilizobainishwa kutegemeana na

matukio ya uhalifu kama vile fimbo za polisi, minyororo, pingu, mbwa, bunduki, mabomu ya

machozi nk. Aidha, Polisi hawapaswi kutumia nguvu iliyokithiri hadi kufikia kuua au kuumiza

wahalifu na yapo maeneo maalum ya mwili ambayo polisi anapaswa kupiga bila kuathiri afya ya

mharifu hata angekuwa Jambazi, ingawa ipo pia nafasi kwa Polisi kujilinda (self-defence) dhidi ya

hali inayohatarisha maisha yake na hivyo kulazimika kuua bila kukusudia. Pengine hapa watu wa

haki za Binadamu wamechelewa kwani walipaswa kuhangaikia matukio ya watanzania ambao

Polisi wamekuwa wakienda kinyume na taratibu (kama yapo) na mchakato wa kutumia

nguvu(kama upo) kuliko kushupalia kauli ya Waziri Mkuu iliyojikita kwenye taratibu za kutumia

nguvu kisheria (minimum force procedure).

Polisi wanayo haki ya kutumia nguvu kwa dhana ya kuzuia uhalifu na chini ya Utawala wa Sheria

ni Nguvu ile tu muhimu inayohitajika (necessary force); na inapotumika kwa mtu ni ile ambayo ni

stahiki na muhimu kutegemeana na mazingira (reasonable and necessary force). Sheria ya Kutumia

Nguvu (Use of Force Doctrine) inatumiwa na Jeshi la Polisi ili kuweka hali ya usalama na

kuioanisha na mahitaji ya maadili kwa ajili ya kulinda haki na maisha ya wanaohatarisha amani na

wanaohisiwa kufanya hivyo. Na iwapo jamii inaumia itaashiria kuwa Polisi alikuwa akijilinda na

mtu akifa katika tukio inahalalishwa kuwa ni mauaji halali (justifiable homicide). Moja ya Kazi

kubwa ya Dola ni kulinda raia wake dhidi ya hatari za ndani na nje ya nchi ili wananchi wajisikie

wako salama wakati wote. Hii ndiyo inayowafanya wananchi wawe na imani na nchi yao. Ukosefu

wa Nchi kushindwa kulinda Sheria na Kanuni na kutokuwepo kwa usalama wa maisha na mali ya

raia unaweza kusababisha fujo.

Kauli ya Mhe Waziri Mkuu ni ya Ujumla zaidi haikubainisha ni kipigo au nguvu ipi itumike kwani

Sheria zipo zinazobainisha nguvu gani itumike. Wakuu wa Jeshi la Polisi tokea enzi za ukoloni

hadi sasa ndiyo wenye dhamana ya kutoa amri ya kutumia Nguvu; kwa upande wa Waziri Mkuu

inabaki kuwa Ushauri au Agizo na siyo Amri. 1Ni kazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kupokea agizo

na kulitolea Amri kwa Mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi Sura ya 322 Kifungu Na 7(1)(2)

ikisomwa pamoja na Kifungu Na 8 (1) na Kanuni zake (Code of Conducts) na huwa na sura

1Viongozi Wa Polisi Wakati wa Ukoloni Hadi Uhuru na Orodha ya IJP toka Uhuru, Wakati Wa Muungano

hadi sasa

(1916 – 1920 Major S.T. Davis). (1920 – 1929 E.F. Brown) (1929 – 1933 G.H. Kiram) (1933 – 1942F.A.B. Nicholl) (1942 – 1949E.B. Birthray) (1949 – 1951W.A. Muller) (1951 – 1958 R.E. Fouler) (1958 – 1962 G.S. Wilson) ( 1962 – 1964 E.N. Shaidi) (1964 – 1970 Elangwa N. Shaidi) (1970 – 1973 Hamza Azizi) (7/8/1973 –Aug 1975 Samweli H. Pundugu) (8/8/1975 – Nov 1980 Philemon N. Mgaya) (2/11/1980 – 30/11/1984 Solomoni Liani)(1/12/1984 – 3/5/1996 Harun G. Mahundi)( 4/5/1996 – 2/3/2006 Omar I. Mahita) (3/3/2006 Hadi sasa Saidi A. Mwema)

Page 3: MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA

iliyotofauti katika utekelezaji wake. Kwa Waziri Mkuu huwa ni “Ideological Order” na kwa IGP

huwa ni “Coercive Force Order”.