mwongozo wa choo cha vetiva - echocommunity · 2019. 12. 12. · mwongozo wa choo cha vetiva vile...

17
Mwongozo wa choo cha Vetiva Vile mtu yeyote anaweza unda na kutumia choo chake wakati wowote kwa kutumia nayasi ya vetiva. Matumizi ya nyasi ya vetiva yachukuliwa pahala pa utumiaji wa choo cha kuchimbiwa,huleta ufaraga/ficha siri na kuifanya choo cha watu/usaha kuumbuka kwa haraka.Nyasi kwa jina jiji vilivile zinaweza tumiwa katika mahali penye baridi au ukali wa mazingira ambapo vetiva hazikui. Utafsiri wa hivi punde wa mwongozo huu unaweza patikana kwa: http://www.healthy-mind-body.com/humanitarian/vetiver_latrine.html 1

Upload: others

Post on 19-Feb-2021

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Mwongozo wa choo cha VetivaVile mtu yeyote anaweza unda na kutumia choo chake wakati wowote kwa kutumia

    nayasi ya vetiva.

    Matumizi ya nyasi ya vetiva yachukuliwa pahala pa utumiaji wa choo cha kuchimbiwa,huleta ufaraga/ficha siri na kuifanya choo cha watu/usaha kuumbuka kwa haraka.Nyasi kwa jina jiji vilivile zinaweza tumiwa katika mahali penye baridi au ukali wa mazingira ambapo vetiva hazikui.

    Utafsiri wa hivi punde wa mwongozo huu unaweza patikana kwa:http://www.healthy-mind-body.com/humanitarian/vetiver_latrine.html

    1

    http://www.healthy-mind-body.com/humanitarian/vetiver_latrine.html

  • Umuhimu: Sio ghali kama vyoo vya kawaida (ni dola 25-50) ishirini na tano hadi hamsini badala ya (dola

    mia tano (500). Hupatikana kirahisi kuliko choo cha miinuko,mwangaza na ufaraga unaweza ongezwa

    kulingana na mahitaji. Huweza kujengwa kwa urahizi hata katika mashinani. Mizizi ya nyazi ya vetiva huongezea nguvu ukuta wa choo Mzingi wake wa saruji huweza kubebwa na kutumiwa pahali pengine ikiwa choo kimejaa. Nyazi za vetiva huleta mandhari ya siri maluum na vilevile vinaweza katwa kwa matumizi

    mengine kama(Kuwakisha moto,chakula cha mifugo,kuunda mbolea,kuunda vikapu,kuezeka nyumba,kutumiwa kwenye ujenzi wa kuta…nakadhalika).

    Mizizi ya vetiva hunyonya na kusaidia kwenye uozo wa taka za choo hivyo kupunguza uchafufuzi wa mazingira.

    Hujengwa kwa urahizi kwa hivyo yeyote mwenye mahitaji hayo anaweza jijengea. Hujisafisha na kujikarabati yenyewe,msingi wake hukubalia maji ya mvua kuingia kwa shimo

    hivyo basi kuosha na vile vile kurutubisha mizizi ya nyasi kuota tena.

    Udhaifu Wake: Nyasi hizi zinamahitaji ambazo ni lazima zitimizwe: 1)Unyunyizaji wa maji ikiwa nyasi

    zimepandwa wakati wa kiangazi; 2)Mahali amabapo haina jua sana; 3)Kuzuia wanyama wasiharibu hadi zitakapokuwa timamu.

    Vetiva huchukua takribani msimu 1-2 (Mmoja hadi miwili) ya upanzi kukomaa na kutumiwa vilivyo.

    Sheria ya usafi wa uma zinaweza zuia utumiaji wa choo cha vetva.

    Nyasi ya vetiva huzuia mmomonyoko hata katikahali mbaya.Picha hii huonyesha jinsi nyasi hii

    inavyoshika udongo kwa nguvu wakati wammonyoko na kando yake ambapo hapana nyasi

    hizi humomonyoka na kusombwa.

    Mzizi ya vetiva huwa na mashiko yanguvu mchangani kwa vile huenda futi 4-5

    (nne hadi tano) chini ya ardhi.Picha hiihuonyesha kiwambo cha vetiva (matawi na

    kati ishakatwa) baada ya kungolewa nawatu watatu kwa kutumia jembe na mbao

    kuinulia.

    2

  • Pahali Pa UjenziVipengele vinne muhimu kizingatiwa wakati wa ujenzi wa choo cha vetiva.

    1. Jua: Vetiva hupenda jua kwa kipimo kila siku.Ikiwa eneo hilo lina kichaka basi muhimu kufweka/kukata matawi mengineyo.

    2. Uchafuzi: Ni vyema uchafu wa choo kubaki salama kwenye shimo.Uangalifu hutakakikana ili uchafu huo usipate upenyu na kuingia katika maji masafi ya kunywa au kwenye mito.Vyoo hivi vinafaavijengewe upande wa chini wa bonde mbali na miito na chemichemi za maji.Vyoo unafaa view mita 30kutoka kwenye vianzo vya maji.Vyoo vile vile vinafaa view mita 2 kutoka ardhini kuinuka juu.Hii inazuia upenyu wa uchafu majini wakati wa mvua nyingi/gharika.

    3. Utumiaji Wa Karibu: Choo lazima kiwe karibu na makao ya familia ili hata mtu mgonjwa aweze kukifikia hata kama ni usiku,lakini mbali kidogo ili nzi wasiweze kusafirisha uchafu nyumbani.Kiuweka choo mita sita (6) mabli na nyumba ni masafa unaokubalika kikamilifu.

    4. Ushawazishaji: Ushawazishaji wa msingi wa choo hutakikana timamu.

    3

  • UsafiMagonjwa mengine husabishiwa na viini vinavyoishi kwenya kinyaa na huweza kusambazwa kupitia midomoni.Njia za kawaida za usambazaji,nzi,mikononi na chakula.Mseto wa utumiaji wa safi,vyoo vilivyojengwa vizuri na kunvya mikono vizuri huweza kuzuia uambukizaji na kundeleza afya nzuri.

    Ujenzi Wa Choo Cha Kuchimbwa

    Pahali: Chimbe choo chako kwenye sehemu thabiti huku pande zake mbili ziwe umbo la mstatili ili ipunguze uwezekano wa kuporomoka.Umbo lake kwenda chini na upande huweza tofautiana.Jedwali la hapo chini linaweza kutuonyesha jinsi uteuzi muhimu hutekelezwa.Ikiwa msingi wa choo utasafirishwa kutoka mahali moja hadi nyingine basi msingi huo uwe wa mdwara utafaa zaidi.Ikiwa choo hicho kitadumu mahala pake hapo,basi mtindo wa mraba utatumiwa/unafaa zaidi.Msingi hiyo miwili husaidianyasi ya vetiva kua vyema na kuongezea nguvu choo chake.

    4

  • Round Square

    Umuhimu:1) Choo chenye udwara huwa na kuta zenye

    nguvu tele. Vitu2) Vifaa vichache tu vitahitajika kuunda slabi

    yake.3) Slabi hiyo vilevile huwa rahisi kuhamisha

    kwani huweza kubingirishwa kwa haraka.

    Umuhimu:1) Choo kama hiki huwa na maisha marefu ya

    utumizi kuliko cha mstatitili.2) Na pia slabi yake huwa rahizi kujenga.

    Udhaifu Wake:1) Slabi ya mraba huwa ngumu kutengeza.2) Slabi dwari ni nypesi kushinda ya mraba.

    Udhaifu Wake:1) Slabi ya mraba huwa ngumu kuhamisha

    kwani zingine huwa na uzito wa kilo 200.2) Vifaa vingi hutumika katika ujenzi wake na

    kwa hivyo ni ghali.3) Choo cha mraba pia haidumu sana.

    Urefu na upana was shimo huweza badilishwa kulingana na mahitaji.Shimo yenye upana wa mita 1 na mita 2.3 kwa kina huweza kutumiwa na familia ya watu sita kwa muda wa miaka mitano.Ikiwa upana wa shimo itabadilishwa,lazima kiwango cha msingi wake kubatilishwa pia.Sakafu yake yapasa kuwa sentimita 20 pana kuliko shimo yenyewe. Usajili huu hutumiwa kwa ongezeko la ½(nusu mita) ya shimo ambalo hujazwa kwa mchanga ukimalizwa.Hii hufanywa ili kuzuia uchafuzi wa mchanga.Ili kujua vyema urefu wa matumizi ya choo chako,kadiria matumizi hivi kwamba kila mja/mtu hutumia kiwango upana wa kiubika 0.6 kila mwaka.Hilo litaongezeka mpaka kubiki 0.1 ikiwa watumizi wa choo hizo watajisafisha kwa kutumia bidhaa ghusi kama mabaki ya mahindi na mawe.Hesabu hii ni ya choo cha kawaida.Hata hivyo choo cha vetiva kinaweza dumu zaidi kwani mizizi yake huozesha chemichemi hizo.Utafiti unaonyesha kuwa choo chenyw kimo cha 1.2 huweza kudumu kwa muda wa karibu mwaka.

    Kukadiria Utumishi Wa Choo

    Matarajio ya matumizi: watu watu 6*0.06 kiubiki mita *miaka 5=1.8 kubiki mita

    Matumizi ya choo: Mita 1*mita 1*1.8 mita (2.3 mita-0.5 mita)=1.8 kubiki mita

    Ikiwa upana wa choo itabadilishwa,huna budi pia kubadilisha kiwango cha slabi na nguzo zake.Slabi iwe sentimita 20 kuzidi upand wa shimo,na nguzo za choo pia ziwe sentimita 70 zaidi ya shimo.

    Sakafu Ya Choo:Sakafu ya choo huweza kuundwa kwa: Mchanga vipimo vitatu,kokoto vipimo vitatu,saruji mfuko moja.Bidhaa hivi vinaweza kupatikana mashinani.Kokoto iwe saisi ndogo,mchanga isiwe na uchafu na mawe.Aina ya waya ya meshi hutumika kutenganisha mchanga na uchafu.Mkorogo huu huweza kubadilishwa kulingana na maeneo na pia uwepo wa bidhaa hizi mashinani.Kwa mfano unaweza kuwa na mkorogo wa mchanga vipimo viwili,kokoto vipimo vine na saruji moja.Pia unakubaliwa vipimo vine vya mchanga, vipimo viwili vya kokoto na mfuko moja wa saruji.Mikorogo

    5

  • kama huu huongezewa maji kulingana na matumizi.Kadiria ndoo tatu za maji na vile vile katika usafishaji wa vyombo vya kazi.Slabi hii na nguzo zinaweza undwa kwa umbo mbalimbali kwa kutumia miti iliyowekwa sakafuni.Kazaslabi hii kwa kutumia nguzo 3/8 vile ilivyochorwa kwenye mchoro wa picha.Ukimaliza nguzo hizo za nyaya hukunjwa vyema ndani ya slabi ili pasiwe na chuma/waya yoyote nje.Kabla ya kuumwaga mkorogo wa saruji,mawe ndogo ndogo zinaweza kutumiwa katika kuinua nguzo yenyewe pahali pake.Shimo ya choo utengenezwa kwa kuta na kuubana kwa jiwe ama chombo cha plastiki.Shimo lenyewe isiwekubwa wa sentimita 25 pande zote.Kipimo hiki huhakikishia hata motto mdogo usalama wake.Ondoa kifuniko cha sakafu baada ya masaa matatu,hata hivyo unaweza kutandazia maganda ya miti,mchanga,karatasi ya plastiki juu ili kuufanya saruji ukauke polepole.Ijapokuwa wajenzi wengine hutumia sakafu hii baada ya siku 6,slabi dhabiti huachwa hadi siku 21.Baada ya udhabiti wa slabi,unaweza hamishwa kufunikia shimo ya choo na kuekeza mawe kando kando kote ili choo chako kisiporomoke chini.Ikiwa unahitaji kiti cha choo,basi unaweza tumia saruji pamoja na tafali au mti.Hakikisha kuwa shimo ya choo imefunikwa kila wakati kuzuia nzi wasiingie.Kifuniko cha choo kinaseza tengenezwa kwa kutumia mbao lakini mtindo huu haidumu kama ya saruji.Ni muhimu kifuniko hiki kifungwe na kufunguliwa kwa kutumia mguu,hii huzuia uasambazaji na uchafuzi wa mikono.Miti isiyooza kwa haraka ama bamboo inaweza tumika kutengeneza slabi.Miti hii huchongwa sambamba halafu mkorogo wa saruji kutandazwa juu yake.Mbinu hii si ghali kutengeneza lakini haidumu kuliko saruji na vilevile haiwezi kuhamishwa kwingine kwa matumizi.

    Vifaa vya ujenzi wa slabi-vifaa vya kutumiwa tena

    Miti 4,sentita 5*sentimita 10(2*4s) kila moja mita 1.2 ambao hutumiwa kujengea slabi ya saruji.Glasi moja nyepesi wa sentimita 6.3,urefu wake 377 sentimita kwa utunzi wa slabi.Miti mitatu(3), sentimita 5*10(2*4s) kila mita 1.8 kusaidia kwenye nguzo.Mbao nne za vipimo 5 kwa 10 sentimita (2*4) kwa 40*30 sentimitaGlasi ndogo moja ya kipimo cha 6.3 sentimita kuwekewa slabi.Mbao moja kilichokatwa kwa mfano wa kitumbuo cha ufunguo kwa slabi.Ikiwa hakipatikani basin doo ndogo cha kipimo cha sentimita 25 huweza kutika.Kijiko cha saruji na shepeo hutumiwa kwa saruji.Vifaa vya usafishaji kama vile plastiki wa kuzuia uchafu kwenye saruji.Msumeno wa kukata vyuma.Jembe ndogo,shepeo na vyuma vya uchimbajiVisikiki kama msumari,nyundo na kisebusebu hutajika

    Orodha ya vifaa- vinavyotumika mara moja tu

    Nyasi za vetiva hamsini ( vetiva vidogovidogo)Vyuma/ vidhibiti viwili vya vipimo vya 9.5 milimitaSaruji mfuko moja wa uzani wa kilo 50Ndoo tatu za maji (kutumiwa kukoroga na usafishaji wa vyombo)Ndoo tatu za mchangaNdoo tatu za kokoto

    6

  • Choo nzuri chenye ukuta sambamba. Tumia mguu wala sio mkono kwa kuufungwakifuniko cha choo.

    Utengenezaji wa slabi kwa kutumia vindoo na mbao.Ndoo hii ni kubwa sana,ni kama sentimita 30badala ya sentimita 25.

    7

  • 8

  • 9

  • 10

  • Jinsi Ya Kupanda Vetiva

    Panda nyasi hii sentimeta 10-15 kwenye mistari tatu zinazofuatana kuzunguka choo chako.Mistari hiyoiwe sentimeta 30-40 kutoka moja hadi nyingine.Acha sehemu ndoo cha kuingia/kama mlango.Kutoka katika ukuta wa choo ,acha sentimeta 30 kabla ya kupanda nyasi hii,kwani kufanya hivyo itafanya mizizi yake kushika chini vizuri.Panga ununuzi wa vetva 50 ikiwa utafwata muundo huu.Ni vizuri kupanda wakati wa vua ili kuepuka unyunyuzaji maji.Maji taka za nyumba huweza kutumiwa katika shnguli hii.Tumia mbolea kwenye upanzi wako.Ikiwa kuna kiangazi unaweza ongezea nyasi zingine,matawi maganda na mbao kuwa vizuizi vya jua.Pia unafaa kuchunga wanyama wasiharibu vetva wakati huo hadi labda baada ya miezi (4-6).

    Vetiver latrine with newly planted slips, notice that the slips are planted right next to the slab and will not interfere with the slab as the roots grow down vertically and not horizontally.

    Utunzi Wa VetivaKwa msimu wa mwaka moja vetiva zitakua kwa pamoja na kuunda kichaka .Nyasi hizi zinaweza katwakwa matumizi mbalimbali.Wakati wa kukatwa hakikisha umeacha sehemu ya kama sentimita 30 kutoka ardhini.Nyasi hii hutumiwa kulisha wanyama moja kwa moja au kama sileji.Pia huweza kuwa kukarabitiwa na kutumiwa kama kuni kwenye upishi na hautoi moshi,hutumiwa kutengneza vyombo,wezekaji wa nyumba.

    11

  • Usafisaji Na Utunzi Wa Choo

    Ni vyema kuhakikisha usafi wa sakafu ya choo chako kwa kutumia sabuni na maji pekee wala sio didha za klorini..Hii ni muhimu kwa kuwa kitatunza mizizi ya vetiva.Ikiwa sakafu hii haina paa,basi maji ya mvua itasaidia katika usafishaji kwani maji yataingia moja kwa moja kutoka kwa slabi hadi kwenye shimo la choo.Ukarabati wa kila mara ni buhimu kuzuia uporomokaji wa choo.Katika nchi ya Haiti,takribani vyoo 365 za vetiva zilizojengwa mashinani,ni mbili (2) ambayo ni asilimia 0.5 peke zilizobomoka kulinganana utafiti uliofanywa miaka miwili unusu(2.5) iliyopita.Njia moja nyeti ya kuzuia vyoo kuporomoka kando na kuvijenga kwenye pahala thabiti ni upanzi wa vetiva na kuiacha ishikamane.Njia ya pili ni kukagua dalili za awali za mmomonyoko.Dalili za kuonyesha kuwa choo kitaporomoka huonekana mapema hivyo basi inaweza zuiliwa.Ikiwa nyufa zimeonekana,ziba kwa mchanga/au maganda ya miti halafu pandia vetiva juu yake.Mzizi ya vetiva hudhibiti mashimo na kuzuia uporomokaji.Ikiwa nyufa ni kubwa sana basi shimo nyingine ni lazima ichimbwe na slabi kuhamishwa huko.

    Choo cha vetiva kilichokomaa na chenye useri auufaraga.

    Choo chenye upenyu wa mwangaza napaipu ya kutoa harufu.

    Urudiaji wa matumizi:

    Wakati shimo la choo kimejaa,sakafu yake ya saruji/slabi pia na nyasi ya vetiva huhamishiwa pahala pengine.Chimba chini kando yam mea wa vetiva,zitoe zikiwa zimeshikana,chonga mizizi na uache sentimita kumi na tano (15) matawi uyachonge kwa sentimita (15-20) na pia uzigawe kwenye vitatu vitatu hadi vitano(3-5) kwa kutumia upanga au vyombo kama jembe shoka.Rudia upansi wake vile ulivyo fanya katika choo cha mwanzo.Choo cha kwanza kifunikwe kwa mchanga nusi mita(1/2) mahala hapo panaweza limwa baada ya miaka miwili au mti wa matunda inaweza pandwa hapo mara moja.

    12

  • Vetiva zilizopandwa kwa mstari Vetiva zilizopandwa chini mno.

    Ukarabati

    Utunzi:

    kuibadilisha/kukarabati,uhamazisho itakuwa muhimu ili wazo hili la choo kama hiki kikubaliwa na jamii wenye itikadi na imani mbalimbali.Kijumba kinaweza jengwa juu ya slabi kuleta upekee Fulani.Pia kifaa kama kiti cha choo kinaweza jengwa juu ya shimo ya kukalia.Shimo ya inchi 4 inaweza achwa ili kuleta mwangaza.Ikiwa kumejengwa nyumba hii,bomba ya kuputisha harufu mbaya huwekwa na kupitishwa kwa paa.Ni vyema nyaya itumiwe kwenye bomba hizi kuzuia nzi na wadudu wengine kuingia chooni.Kwa mawaidha ya ziada juu ya ujenzi wa vyoo hivi na vile vinapambwa wasiliana na mtandao wa: http://www.clean-water-for-laymen.com/privy-privacy-shelter.html.

    Nyasi ya jiji:

    Kwenye mahali pasipopatikana nyasi ya vetiva,choo hiki kinaweza jengwa kwa kutumia nyasi ya jiji.Vetiva hukua vyema kwenye maeneo ya joto na hukua katika tropiki pekee.Nyasi ya jiji hata hivyo huweza vumulia baridi/joto na pia udongo wenye chumvi.Mzizi yake huzagaa kote na kama vetiva hudhibiti udongo.Kwa hivyo nyasi ya jiji huwa mbadala nzuri ya vetiva ikitakikana.Nyasi hii pia huzuia mmomonyoko wa ardhi/udongo kama vile vetiva.

    13

    http://www.clean-water-for-laymen.com/privy-privacy-shelter.html

  • Mzizi ya nyasi ya jiji vilivile huzuia mmmonyoko kama vile vetiva

    Udwara Wa Ndizi:

    Ukarabati mwingine muhimu ni uongezaji wa miche ya ndizi kwenye udwara/mzunguko wa choo cha vetiva.Jamii hukubali kukitunza choo cha cha vetiva ikiwa ina mimea ya matunda yanayowakidhi.Panda miche mitano ya ndizi kwa safu na kuacha nafasi inayootakikana kando ya vetiva.Mti wa papai pia huweza pandwa katkati ya ndizi na kuacha nafasi ya kuingia chooni.Mimea hiihunyunyiziwa maji hadi itakapokua vyema hasa wakati wa kiangazi.Ijapokuwa sio hatari kula matunda kutoka kwa miti hii,hata hivyo si salama kupanda mboga karibu na choo kwa sababu ya uasambazaji wa uchafu.

    14

  • 15

  • Mbegu Za Paipai Kama Kizuizi Na Pia Tiba:

    Wadudu/viini vya utumbo ni jambo la kawaida kote hata katika nchini zilizoendelea. Kando na kuonyesha dalili mbalimbali tumboni kama upungufu wa uzani,pia zinweza fanya mtu kupoteza fikra ama kuwa na kiarusi.Ikiwa miti hii itapandwa karibu ,basi mbegu zake zitatumika kama dawa za minyoo.Kumeza vijiko vine ndogo vya mbegu mbichi au vijiko viwili vya mbegu vilivyokauka kutoa tiba kamili kwa watu wazima na watoto.Mbegu hizi zinauchacha Fulani kwa wengine.Wale wanaoweza kumeza mzima bila kuzisiaga mdomoni ndio njia rahisi.Kwa watoto au wasioweza kuzimeza ,basi mbegu hizi hukaushwa, husiagwa na kuchanganywa na sukari au asali,ama siagi.Mbinu hii huzuia uakali wake.Dawa hii huweza tumiwa mara moja kwa mwezi na huzuia minyoo tumboni.Lakini mkorogo huu usitumiwe sana/nyinyi kwani husababisha udhaifu wa mbegu mwilini.Kwa watoto au wasioweza kuzimeza mzima ,basi mbegu hizi hukaushwa,husiagwa na kuchanganywa na sukari au asali,ama siagi.Mbinu hii huzuia ukali wake.Dawa hii huweza tumiwa mara moja kwa mwezi na huzuia minyoo tumboni.Lakini mkorogo huu usitumiwe sana/nyingi kwani husababisha udhaifu wa mbegu mwilini.Kwa maeneo ambayo paipai hukuzwa na vyakula hupeanwa shuleni kwa watoto,njia hii ya tiba huwezajaribiwa ili kiimarisha afywa na masomo ya wanafunzi kwa gharama ndogo sana.

    Papaya ukwa huu hutoa mavuno 3 ya matibabu ya antiparastic

    16

  • Marejeleo:

    1. Okeniyi J, Ogunlesi T, Oyelami O, Adeyemi L; 2007; Effectiveness of dried Carica papaya seeds against human intestinal parasitosis; Journal of Medicinal Food; 10(1): 194-196.

    Mapokeshi:

    1) Owen Lee (www.vetiverlatrine.org); Mhasisi wa mwongoza wa vyoo vya vetiva pamoja na picha zao.

    2) TVNI (The Vetiver Network International, www.vetiver.com); Mhasisi wa vetiva pamoja na jiji na picha zao.

    3) Dale Rachmeler, PhD ([email protected]); Mhariri wa mwongozo.

    4) Roger Gietzen, MD (www.healthy-mind-body.com & [email protected]); Mhasisi pamoja na wahariri wote katika kazi hii na picha zao.

    5) Kwa ruhusa ya uchapishaji wa mwnogozo huutafadhali wasiliana na; Mr Daniel O Simba @ [email protected],ama ; www.imanigroupkenya.org.

    Hatimiliki:

    © 2016 Roger Gietzen, MD. Haki zote zimehifadhiwa.Uchapishaji huu uwe huru kwa yeyote ulimwenguni mzima.Usambaji mahali popote unaruhusiwa na kwa njia yoyote ile hata ya mtandao ni bora tu iwe ni bure/bila malipo.Shughuli hii isiwe ya kibiashara au kipata faida Roger Gietzen, MD ([email protected]).

    17

    mailto:[email protected]:[email protected],amamailto:[email protected]://www.healthy-mind-body.com/mailto:[email protected]://www.vetiver.com/http://www.vetiverlatrine.org/