namna ya kuombea ndoto zilizogusa maisha yakomalango mengine ni ndoto. ukisoma biblia utaona malango...

32
NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA OTTU-MBEYA NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO Kutoka tarehe 10/10/16 hadi 16/10/16 1

Upload: others

Post on 04-Mar-2021

7 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA OTTU-MBEYA

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Kutoka tarehe 10/10/16 hadi 16/10/16

1

Page 2: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

SIKU YA KWANZA

TAR 10-OCTOBER -2016

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

Katika hali ya kawaida masomo haya si rahisi sana kuyapata. Na Mungu aliponiruhusu kuanza kufundisha si somo ambalonililichangamkia sana kuanza kufundisha na sikuwa na uhakika sana juu ya upokeaji wa watu wa somo hili.

Na tutaendelea vizuri kadri Mungu atakavyokuwa ananiambia.

JAMBO LA KWANZA; Usidharau au usipuuzie ndoto uliyoota

Ni kwa sababu ndoto ni lango la Kiroho ambalo Mungu na Shetani wanalitumia kumfikia mwanadamu. Katika Ulimwengu wa roho kuna ukuta ambao Mungu aliuweka ambao ni mbingu na nchi, na baada ya dhambi kuingia ilitengeneza ukuta kati ya Mungu na mwanadamu. Ndipo Mungu alitengeneza njia za mawasiliano kwa njia ya malango na miongoni mwa malango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana.

Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo Mwanzo katika Mwanzo 1:1 ina maana aliukata umilele na alifungua lango la Muda. Yesu ni alfa na Omega yaani Mwanzo na mwisho. Japo yeye hana mwanzo na mwisho. Ili aweze kutusaidia kutembea katika muda, ukiweza kujua namna bora ya kutembea katika muda utakuwa umefaulu sana katika hali ya kimwili na Kiroho.

Ndoto ni langoMfano wa kwanza

Mwanzo 41:1-7 “Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini.

Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! *Ni ndoto tu”

Farao alipoamka akasema kumbe ni ndoto tu. Ina maana alikuwa ameidharau lakini bado ilimletea mfadhaiko. Angalia mstari wa nane, ndoto ya pili aliyoota ya masuke ndiyo iliyomletea mahangaiko sana na kumfanya atafute waganga na wachawi. Lakini hawakuweza kumsaidia, na nisawa na watu wengine ambao wakiota ndoto wanapambana kwenye ndotona wakijakungundua kumbe ilikuwa ni ndoto wanaona afadhali na hawafuatilii na hata wakifutalia hawajui waombeje kwa sababu hata kujua maana yake inakuwa ni shida.

Farao angeweza kupuuzia na gharama yake ingekuwa ni kubwa sana. Na Yusufu ndiyo aliweza kutafsiri ndoto yake baada ya waganga na wachawi kushindwa. Na kupuuzia ndoto ile kungefanya Dunia nzima kwenda vizuri sana kwa miaka 7 na baada ya hapo miaka 7 mingine wangepitia kipindi kigumu sana. Na watu wangejiuliza mbona Mungu hujasema na sisi kumbe aliwaambia.

Mwanzo 41:53-57 “Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya Misri, ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri palikuwa na chakula. Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote”

Yusufu mume wake Mariam alipewa maelezo kwenye ndoto mara nne na alitii, fikiria angepuuzia ingekuaje?

2

Page 3: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Mfano wa pili

Ayubu 33:14-19 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni*, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake”

Kazi ya ndoto ni kuyafunua masikio yako ya ndani ili waweze kuondoka kwenye makusudia yao yasiyo ya kimungu ndani yao. Na pia kuweza kuwaondoa kwenye mafundisho yasiyo sahihi.

Mfano, Kuna mtu mmoja alinisimulia, alipookoka si unajua kunakuwa na mto wa kutafuta chakula na alikuwa anasali hapana pale, na alikuwa anasali kanisani kwake na akitoka pale alikuwa anaenda na mahali pengine na pengine. Hata katikati ya wiki utakuta anaenda kanisa hili na lile ilia pate mafundisho. Sasa alikutana na kanisa moja akaona limechangamka sana na aliazima kuhamia pale moja kwa moja. Usiku aliota ndoto kuwa Yule mchungaji yupo kwenye njia na watu wanamfuata, mara baada ya muda kidogo akawaona wameingia kwenye majani na mchungaji akiwa mbele, na yeye mwenyewe akawa anawafuata kwa nyuma sasa kabla nae hajaingia kwenye majani akaamka usingizini. Baada ya hapo alijua kuwa ni Mungu anamuambia kuwa asihamie lile kanisa.

Ukiangalia tena Ayubu 33 : 17-19, Mungu anamuondoa mtu kwenye kiburi na kwenye mapenzi yako. Maana kuna watu wanakuwa na kiburi moyoni mwao na wanaanza kuona wao ndio wao na kuna baadhi ya mambo ya kumuuliza Mungu na mengine sio ya kumuuliza Mungu. Kwa sababu hiyo wanakuwa na vikundi vyao na vinakuwa vitovu vya nidhamu na wanakuwa na misimamo yao na kuona hiyo ndio bora sana na hata wanapoteza maana ya wokovu kwa sababu wanakuwa a kiburi sana. Mungu hutumia ndoto ili kuwatoa kwenye mapenzi yao na kuwarudisha kwenye njia nzuri. Kwa hiyo Mungu anatumia ndoto kufikia nafsi ya mtu na mwili wa mtu.

Kumbukumbu 13:1-4 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni nakushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye”

Hesabu 12:6 “Kisha akawaambia, sikilizeni basi maneno yangu, akiwapo nabii kati yenu mimi Bwana nitajifunua kwake katika maono nitasema naye”

Aliyeumba lango la ndoto ni Mungu mwenyeshe na shetani anaiga maana yeye hajaumba kitu, bali anatumia malango yaliyoko. Na malango haya yaliumbwa kwa ajili yetu na biblia inasema tunatakiwa tumiliki malango ya adui. Na sisi kazi yetu ni kuyajua hao malango na kudhibiti shetani asipite hapo.

Mungu anaweza akasema na watumishi wake kwa ndoto, na pia ukitaka kujua ulichoota kwenye ndoto haijalishi kimetokea kiasi gani bali angali matokeo yake maana kama yanakupeleka karibu na Mungu ni sawa ila kama yanakutoa nje ya Mungu basi ujue si ya Mungu hata kama yanatokea kwa ishara kubwa sana na za kutisha, ila kama zinakutoa mbali na Mungu kaa mbali nazo.

Unakuta watu wanajipa vyeo na kuona kuwa ni Mungu kawapa hizo ndoto. Na wakiota ndoto zikitokea katika maisha yao wanasema mimi Bwana nikiota ndoto huwa zinatokea. Na hawaangali mwisho wao, kwa mfano Mungu kakuonesha jambo baya na wewe unaanza kusema kuna hili na litatokea lakini lengo la Mungu kukuonesha doto hiyo ni ili ujue na uweze kuomba ili kupangua hicho kinachotarajiwa kutokea ulichoota.

Watu wengi huwa wanafuata miujiza na ona baada ya miujiza kuomba kwao kunapotea sana, na wanaanza kuwa wazito wa kusoma neno la Bwana. Na hata wakisoma hawaelezi. *Muuujiza ni kwa ajili ya Mungu na sio wako ni kwa ajili ni kwa ajili ya Mungu. Wana wa Israel walikula Mana jangwani na walipovuka kwenda kanani Mungu aliwaambia washike jembe walime.

3

Page 4: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Mungu aliwaelekeza kwenye maji machungu ili ajifunue kama Yehova Rafa, muujiza umebeba ujumbe, muujiza una sauti ndani, na ndio maana Mungu alikuwa anarudia tena ili waweze kusikia tena.

Ndio maana biblia inasema haijalishi ndoto unayoota ila cheki matokeo yake, au kama umepewa unabii au muujiza isikupe shida ukitokea ila cheki mwisho wake yaani matokeo yake. Ukiona inakupeleka mbali na Mungu wako ujue kuna shida Fulani.

Shetani akija kama shetani inaweza ikawa ni rahisi sana kumjua ila sasa anachofanya anakuja kama malaika wa Nuru lengo lake ni kukupotosha kwa hiyo kuwa makini sana usiamini kila kitu* kama unafuata huo msimamo ulioupata ambao shetani kauleta unakuleta kwenye kiburi na ndio maana na Mungu nae anatumia ndoto ili kukuondoa kwenye hayo makusudi yako yaliyo nje ya mapenzi ya Mungu.

Pia ukipuuzia ndoto ya shetani itakugharimu sana. Kuna watu hawatembei kwenye msimamo wa kanisa la Laiodokia unaosema kumbuka ulipoanguka ukatabu na usipofanya hivyo basi Yesu atakuja kukiondoa kile Kinara chako. Na ujue kuondolewa Kinara ni gharama kubwa sana.

Jambo la Kwanza, Jambo unaloota linaweza kujitokeza kwenye nafsi, kwenye mwili wako na nafsi yako Likiwa na maelekezo na ukayafuata utaona matokeo yake katika maisha yako. Kama ilivyokuwa kwa Farao, Ayubu na katika Kumbukumbu la Torati.

Baada ya kuona ndoto na nimesoma ndoto nyingi na wengi hawazilewi na shida kubwa sana niliyoiona ni namba ya kuziombea hizo ndoto.

Na mwingine kwa kutokuwajibika anajipachika cheo kuwa kila nikiota ndoto huwa zinatokea, ila hajui kuwa Mungu anataka upangue hiyo ndoto na badala yake wewe unaanza kutangaza.

MIFANO YA NDOTO MBALI MBALI

01.Kuna mama mmoja mume wake aliota ndoto anakula bui bui na baada ya siku chache alipatwa na kikohozi ambacho alikuwa haponi na alitafuta kila dawa hakupona na alisikia kuwa tunafundisha semina hizi ndipo akaandika ndoto yake akiomba msaada.

02. Mwingine aliota ndoto ya kugongwa na Nyoka, na katika ndoto aliona katika ndoto kuwa kidole chake kinatoa damu, na aliposhtuka usingizini aliona kweli kidole chake kitoa damu. Na Maisha yake yaliporomoka saa hiyo hiyo.

03.Mwingine aliota ndoto anagombana na mwenzie kwenye ndoto na huyo mwenzie alimng? ata mkono na alipoamka aliona alama kwenye mkono wake,

04.Mwingine aliota ndoto kuwa kuna mtu kaja kwenye ndoto alipokuwa amelala na baada ya kupita muda kidogo alienda hospitali na alikutwa na uvimbe tumboni.

05.Na mwingine aliota kang? atwa na nyoka kwenye mkono wake wenye pete ya ndoa. Na Baada ya hapo aliona anapata maumivu na akaamua kumuachia yule nyoka kwenye ndoto. Baada ya muda kidogo ndoa yake ilivurugika. Na tulipokuwa tunaomba alikuwa anatusikiliza kwenye redio tukiomba alitapika kitu cheupe.

Wangapi hapa huwa wanaota ndoto wanakula kwenye ndoto? Na wengine hawajui maana yake ni nini. 1 Wakorintho 10: 15-22 “Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja”

kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si

4

Page 5: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

Lazima ucheki vizuri unakula nini

1. Chakula kwenye ndoto inawezeka kabisa ni ushirika wa kimaagano, kati ya mwotaji wa ndoto na hao aliowaota kwenye ndoto na wanaunganishwa na ndoto hiyo na madhabahu iliyobeba ndoto hivyo na madhabahu iliyobeba agano husika.

Damu ni uhai, hunapelekwa na kunywa kwenye ndoto wengi huwa wanashiriki hivi na kutokujua kuwa wanashiriki aganobila wao kujua.

Na matokeo yake unaanza kuwa mzito kutoa sadaka, kwa sababu maeneo yote ambayo watu wanatoa sadaka kwa mizimu au miungu. Wanaanza kuwa wazito kutoa sadaka kwa Mungu wetu. Ila sasa watu hao hao ukiwaita kwenye kikao cha harusi ona hela watakazo toa utashangaa sana. Hali ya kiroho ya mwotaji wa ndoto anaanza kuwa mzito kumtumia Mungu.

Ndoto inakujulisha kwa kuna agano la kurithi. Ivi unajua kuwa Ibrahimu alifunga agano kwenye ndoto na Mungu fuatilia Kwenye Mwanzo 15:1-21”Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjiaAbramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu,Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini,nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimilikinyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtualiyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyuhatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiyeatakayekurithi.Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni,kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu.Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hilikuwa haki. Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuletakutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua yakwamba nitairithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, nambuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wamiaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili,akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndegehakuwapasua.Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramuakawafukuza. Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshikaAbramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika yakwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyoyake, watawatumikia watu wale, nao watateswamuda wa miaka mia nne.Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu;baadaye watatoka na mali mengiLakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani,utazikwa katika uzee mwema.Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimiauovu wa Waamori bado.Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru yamoshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vilevipande vya nyamaSiku ile Bwana akafanya agano na Abramu,akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mtowa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, naMyebusi.”kwa hiyo agano linaweza fungwa kwenye ndoto.

Unajua kwanini wana Israel walipoabudu ndama walitoa sadaka ya Amani na miungu mingine, wanafanya hilo agano na wanashiriki na Ibada ya miungu mingine. Na vitu vya ndoto ni halisi kabisa. Na kwanza kutumika kwenye ndoto Petro, aliona katika maono kwa njia hiyo ndipo alianza kuhubiri injili kwa mataifa.

MFANO

5

Page 6: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Sitasahau siku moja nilikuwa na Maswali, niliyokuwa namuuliza Mungu kuhusu baba yangu. Na Mungu alitumia ndoto kunijibu na siku moja usiku niliota ndoto ya kuwa nimeenda hotelini, na baada ya muda kidogo nikamwona mhubiri mmoja wa marekani anakula chakula. Nikamwambia yule mhudumu niletee chauka pale alipokaa yule mhubiri na nilisogea pale alipo na nikavuta kiti nikakaa pale pale. Na akainuka na nikamuona ni baba yangu. Alimaliza kula na sahani yake ikawa imesha chakula na akanipa vijiko alivyokuwa anavitumia kula chakula. Na nikasikia sauiti ikaniambia nitakushibisha kwa wingi wa siku. na neno hili unalipata Zaburi 91:16 “Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu na ndipo nilielewa kuwa baba yangu aliomba kwa Mungu kuwa aondoke kwa sababu alibakiza miaka mitatu tuliyokubaliana.”

NOTE Kitu cha muhimu kujua ni kuwa si kila mara ukitokewa na watu waliokufa kwenye ndoto ina maana ni shetani. Na angalia anakumabia nini, Yesu alipokuwa anaomba alitokewa na Musa na Elia wakati walikuwa wamekufa.Tutafanya zoezi hapa na kuombea watu wote waliokula chakula kwenye ndoto.

SIKU YA PILI

6

Page 7: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

TAR 11-OCTOBER -2016

SOMO; NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

kama unatusikiliza kwa mara ya kwanza mimi naitwa mwalimu Christopher mwakasege nikifundisha kutoka Mbeya semina yenye kichwa kinachosema "NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO"karibu tushirikiane kwa pamoja.

Jana nilikwambia namna ambavyo nilipata shida wakati nimeokoka na naskia kiu ndani yangu ya kumtumikia Mungu na mara kwa mara nilipata kumsikia Mungu akizungumza nami kwa njia ya ndoto juu ya Utumishi alioweka ndani yangu.

Ilinipa shida sana na nikaamua kutafuta zaidi mafundisho juu ya ndoto sehemu mbali mbali toka katika vitabu vya kidini na vile vya kidunia LAKINI havikunisaidia sana mpaka ROHO MTAKATIFU ALIPOANZA KUNIFUNDISHA.

na nilikwambia somo kama hili halikua katika mipango yangu ya kufundisha ingawa nimekua nikijifunza kwa muda mrefu sana tangu miaka ya 80 nilipoitwa kwenye huduma LAKINI MUNGU AKASEMA NAMI NIPATE KUFUNDISHA kwa watu ingawa kabla ilikua vigumu sana kufundisha kutokana na mwitikio wa watu lakini nilikua najaribu kumfundisha mtu mmoja mmoja au baadhi ya watu ambao walikua wanashida Na wanaota ndoto lakini hawapati majibu au tafsiri ya ndotohizo.

Pia wakati naanza huduma nilikua na kiu mno ya kumtumikia Mungu na ilitokea ndani yangu hali ya kutaka kuacha kazi serikalini nikamtumikie Mungu kiasi cha kwamba sa nyingine naingia ofisini na kazi zipo lakini sijisikii kufanya ila nataka nikahubiri au kuombea wagonjwa na saa nyingine nilikua nikienda hospitalini kwa rafiki angu na kumwambia kama unaona kuna mgonjwa na ugonjwa wake sio wa matibabu ya kiganga nipo nje namsubiri nipate kumuombe.

KUNA SIKU wakati wa usiku nikaota ndoto ambayo niko ng'ambo ya mto na kuna watu wengine wako upande wa pili lakini kuna wigo wamewekewa hawaruhusiwi kuvuka apo alafu ghafla nikamuona mtu amevaa nguo nyeusi mwili mzma na amejifunga kitambaa cheusi akiniambia vuka tu nenda upande wa pili...vuka tu...vuka tu...Nami nikawa namjibu siwezi kuvuka mpaka nimeona pakukanyaga...halafu badae likatokea jiwe nikasema sasa naweza kuvuka na nilipovuka nikakuta nipo kwenye chumba kikubwa pekeangu halafu kuna nyoka mkubwa usawa wa urefu wangu afu chumba icho kimefungwa sioni pakutoka baada ya mda fulani nikaona kuna mtu ametokea na kuvunja ukuta wa kile chumba na nikapita.

NILIPOAMKA NIKAJUA KUWA ILIKUA SIO MPANGO WA MUNGU MIMI KUACHA KAZI MUDA HUO.

Bwana Yesu asifiwe!!kwa hiyo sio kila msukumo wa kuacha kazi na kumtumika Mungu unatoka kwa Mungu saa nyingine unatoka kwa shetani na ndiyo maana unatakiwa ujifunze kutofautisha msukumo toka kwa Mungu na ule toka kwa adui.

ZINGATIA JAMBO HILI; shetani akishindwa kukuzuia kuanza safari atakuzuia kuendelea na safari.

hebu tusogee mbele kidogo; Jana tuliangalia Jambo la kwanza ambalo unatakiwa kujua kuhusu ndoto linalosema; USIIDHARAU WALA KUIPUUZIA NDOTO ULIYOOTA MAANA NDOTO NI LANGO MOJA WAPO LA KIROHO AMBALO MUNGU NA shetani WANALITUMIA KUMFIKIA MWANADAMU.

JAMBO LA PILI; ambalo nataka tujifunze siku ya leo ni kwamba VIJUE VYANZO VYA NDOTO NA KUVIOMBEA IPASAVYO.

VYANZO VYA NDOTO;

(1) NDOTO KUTOKA KWA MUNGU.

-Daniel 2:21-28

, matendo 2:17

kumbuka jambo hili sio kila ndoto unayoota imetoka kwa shetani wala sio kila ndoto unayoota imetoka kwa Mungu.

7

Page 8: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

(2)SHETANI AU NDOTO KUTOKA KWA SHETANI.

shetani nae anaouwezo wa kuleta ndoto.

Kumbukumbu 13:1-4

?usifurahie tu matendo ya mtumishi cheki na matunda yake.usifurahie tu miujiza ya mtumishi angalia matokeo ya miujiza hiyo..kama ni yanakutenga na Mungu na kukusogeza karibu zaidi na mtumishi uwe na uhakika sio utumishi toka kwa Mungu.

(3)NDOTO KUTOKA KWENYE MAZINGIRA YA SHUGHULI NYINGI.

Mhubiri 5;3

(4) NDOTO KUTOKA KWENYE HALI YA KIROHO YA MAHALI ULIPOLALA.

Mwanzo 28:10-19, Mwanzo 13:2-4.

Yakobo aliota ndoto mahali alipolala palipokua na madhabau aliyoijenga babu yake mzee ibrahimu kama tunavojua ibrahimu alikua na tabia ya kumjengea Mungu aliyehai madhabau maeneo mbalimbali.

Betheli ni eneo ambalo lilikua na madhabau ya Mungu aliyehai kwa hiyo liliunganishwa na mbingu ndiyo maana Yakobo aliota ndoto akiona malaika wakipenda na kushuka.

KUMBUKA; kujua kwako chanzo cha ndoto ni muhimu sana katika kukusaidia katika kuomba juu ya jambo hilo.

Sasa uyo ni yakobo alilala mahali ambapo paliunganishwa na mbingu umewahi jiuliza umelala sehemu yenye umiliki au maagano na miungu mingine.

HEBU TUANGALIE CHANZO KIMOJA KIMOJA NA NAMNA YA KUOMBA.

(1) NDOTO KUTOKA KWA MUNGU.

Omba Mungu akusaidie kusikia kama kile kitu kimetoka kwa Mungu. (Omba upate kusikia na kuelewa kama kweli jambo hilo limetoka kwa Mungu)

Ayubu 33:14-15

Mwanzo 41;1,4,5,32

unapoona ndoto inajirudia mara mbili ni kwasababu neno hilo Mungu amerithibitisha na atalitimiza upesi.

Pia tambua ndani ya ndoto kuna muda uliomo ndani ya ndoto.

Daniel4:27-33.

Farao alipewa miaka saba.

Nebukadneza alipewa ndoto yenye miezi kumi na mbili ndani yake.

Mke wa pilato aliota ndoto ambayo ilikua chini ya masaa kumi na mbili.

(2) CHANZO KUTOKA KWA SHETANI.

kumbukumbu 13:1-4, kutoka 12:21-23

Ombi; Jifunze kuomba langi la ndoto katika ulimwengu wa roho lifunikwe na damu ya Yesu.

(3)CHANZO CHA SHUGHULI NYINGI.

Luka 8:5-15.

8

Page 9: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

kama umewahi ota unapita njia kuna miba basi katika jambo hili utapata kujua maana yake.

Maisha ya mwanadamu yameumbwa na yameratibiwa katika ulimwengu wa roho na Mungu hata kabla ya kutokea.

Haitoshi tu utembee kwenye njia na Bwana Bali hadi atua ziongozwe na Bwana.

OMBI;jifunze kumwomba Mungu akupangilie siku na aongoze siku yako.

(4)CHANZO CHA NNE;HALI YA KIROHO YA MAHALI UNAPOLALA.

OMBI:Jifunze kuombea hali ya kiroho ya mahali unapolala.

Yakobo alilala kwenye ardhi ambayo inamilikiwa na Mungu.kuna maeneo au nyumba ambazo zina milikiwa na miungu na mapepo.

Biblia inaeleza wazi sehemu yoyote ambayo ni ukiwa au haijakaliwa na mtu kwa mda mrefu inakua makazi ya mapepo na majini alafu nawe unaingia umo unaanza kuabudu na kuishi bila kuombea eneo hilo kwanza ghafla unashangaa wanakwambia aisee mbona umeingia nyumbani kwetu.

Mungu alipo tufundisha mambo haya tumekua tukiomba kila mahali tunapolala ata kama tumefika na kuchoka sana.

kuna mwaka nilipata kushiriki katika mkutano wa uchumi marekani na ulikua unafanyika mahali ambapo ni jirani na kijiji ambacho kina kampuni ya HOLLYWOOD...Na tukapangiwa hoteli yenye jina la Hollywood njee ya ile hoteli mtaani kuna mambo yalikua yanafanyika ambayo sio ya kimungu. nikamuuliza Roho mtakatifu naombaje juu ya eneo hili akanambia usiombee chochote ila JIFUNIKE KWA DAMU YA YESU.

WARUMI 8;26

Swali; Umejuaje Chanzo cha ndoto na unaombaje juu ya chanzo cha ndoto husika.

jibu; WARUMI 8:26__Roho mwenyewe hutusaidia udhaifu wetu maana hatujui kuomba jinsi ipasavyo.

KABLA YA KUOMBA; OMBA NAMNA YA KUOMBEA JAMBO.Omba Mungu akupe namna ya kuombea jambo.

omba kwa kunena kwa lugha.

KUMBUKA; Udhaifu wetu haupo katika kuomba upo katika kuomba jinsi ipasavyo.

Ndio maana unatakiwa ujazwe Roho mtakatifu na apete kukupa kunena kaa lugha iliuweze kuomba.

SIKU YA TATU

9

Page 10: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

TAR 12-OCTOBER -2016

SOMO; NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

kati ya vitu vilivyonisumbua kwa mda mrefu sana ni kwanini Mungu awatume katika mji ambao alikua hana mpango nao wanaisrael wapate kupita mahali. Kama Mungu alikua hana shida na mji wa yeriko kwanini aliwapeleka watu wake waishi katika mji asio utaka. kwanini asiwapitishe wanaisrael katika njia nyingine.

kilichomfanya Mungu aende yeriko ni Rahabu...Rahabu alikua muhimu sana kwa Mungu kiasi cha kutomruhusu aendelee kwenye ukahaba au aangamie na yeriko.

Rahabu alikua muhimu sana kiasi cha kwamba Mungu alikua tayari kutuma malaika wake kwa ajili ya Rahabu.

Inawezekana nimekuja hapa mbeya lakini si kwajili ya kila mtu__Kuna uwezekano kabisa semina hii ikawa inamhusu mtu ambaye ni Rahabu.

Mungu anataka ujue haijalishi shetani amekuchafua kiasi gani...haijalishi ukahaba umekubana kiasi gani lakini yupo Mungu aliemtuma Yesu kwajili ya kukutoa huko.

Haijalishi shetani ameweka ukuta kiasi gani unaokuzuia kuja kwa Yesu lakini kama Mungu amekukusudia anaouwezo wa kubomoa huo ukuta...haijalishi ni ukuta wa dini,ukuta wa dhambi Mungu anaouwezo wa kukutoa katika ukuta huo.

Kama mbele yako ni kuzuri zaidi VITA YAKO itakua kubwa zaidi.

Kama Mbele ya paulo ni kukubwa mno ni lazima mapito ya paulo na kubanwa kwa paulo na shetani ni kukubwa zaidi.

Haijalishi saizi hautamaniki wala haijalishi hakuna anayekukumbuka lakini yupo Mungu ambae atakukumbuka.

ebu niendelee na somo langu;

JAMBO LA TATU;N'GOA KILICHOPANDIKIZWA NA SHETANI NDANI YAKO KWA NJIA YA NDOTO NA UPATE KUONDOA NA MADHARA YAKE.

Ayubu 4:12-16,Ayubu33;14-15,Daniel.7:1

Ni mistari inayozungumzia juu ya ndoto.au maono ya usiku ambayo kwa jina lingine tunaweza ita Ndoto.

MAENEO YALIYOGUSWA NA NDOTO ALIYOOTA AYUBU.

1)Mawazo yaliingia ndani yake ambayo yalikuja kama neno.

2) iligusa kusikia kwake.

Lango la ndoto liko kwenye nafsi.

3) Mstari wa 14. Roho ya hofu ilidondoka ndani yake na ikamfanya kutetemeka

4)Ndoto iligusa mifupa na mifupa yake ikaanza kupata matatizo.

Mtu huyu alipoamka asubuhi ni lazima hakua vizuri. hakua na ujasiri tena...alikua na shida

Katika mawazo yake maana ndani yake yaliingia mawazo ambayo hakua nayo.

KAMA KUNA VITU VYA ADUI AMBAVYO NDOTO IMEWEKA NDANI YAKO USIVIONEE HURUMA VIN'GOE.

Siku moja nilikua mjini daresalam na huwa sina desturi ya kutoka nje ya gari kama mara kwa mara.na nilipotoka nje ya gari karibu na hospitali siku hiyo nikakutana na mama na mtoto wake akiwa anachechemea na wakanisimamisha wakanisalimia kama kawaida Bwana asifiwe mwalimu nikasema amina! Nikauliza kunatatizo gani akasema binti yangu

10

Page 11: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

anaumwa na akanielezea mguu ule aliumia kwenye ndoto alipoota anapiga mpira wa miguu ndotoni...nikamuliza yule binti unataka kupona akasema ndio nikang'oa vile vitu ambavyo shetani amepanda kupitia ndoto na akawa mzima mda huo huo.

Mwingine nilipata kukutana nae alinambia alianguka kwenye ndoto na baada ya kuanguka kila akiamka ule mguu unakua na kidonda. Nikamuombea na kung'oa mapandikizo yote ya shetani aliyopanda kwenye ndoto ghafla akawa mzima.

Sasa usipojua namna ya kushughulika na vitu kama hivi unaweza ukazunguka hospitali na mwisho wakakwambia kansa lakini sio kansa.

Kumpiga mbu aliyekuuma mwenye maralia hakuondoi maralia ndani yako ni lazima ujue pia namna ya kushughulika na maralia pia iliyoingia.

USHUHUDA; nimeota ndoto jana usiku nipo kwenye kundi na katika hilo kundi la maombi nikaona mume wangu akiniparua macho yangu na baada ya kuamka macho yangu yanauma na yana uvimbe na zaidi mume wangu ameniacha na kuuza vitu vyote...UNAMSAIDIAJE MTU KAMA HUYU???-USIPOJUA KITU KILICHO NYUMA YA SHIDA HII NI VIGUMU SANA KUMSAIDIA HUYU MAMA.

Isaya29:8 ,waebrania 12:22-24

Ni mistari inayozungumzia mtu anayeota ndoto...huyu mtu ameota ndoto anakula na alipoamka hamna kitu.

ndoto yake ilienda kugusa nafsi yake moja kwa moja.

Shetani akitaka kuleta vita na watu wa Mungu anatumia njia ya ndoto mara unaamka unahasira na watumishi wa Mungu,unaamka unachukia kanisa, unaamka unaanza kuuchukia wokovu.LAKINI tatizo ni nini...tatizo ni NAFSI YAKE IMEBANWA KWA NJIA YA NDOTO juu ya kazi ya Mungu na mlima sayuni wa Bwana.

Msichana mmoja baada ya kuokoka alikuja kwangu kuniambia baba naomba unisamehe akasema kabla ya kuokoka niliweka agano na shetani kuwa nitakuua kwa njia yoyote ile..kuna siku ulikua hotelin tukaamua tutumie njia ya chakula kukuua ndani ya dakika tano tukaweka sumu kwenye chakula lakini tulishtuka baada ya dakika tano haufi tukakimbia.siku nyingine tuliamua kukuua kwa njia ya ajali tukakuona uko pekeako na tukaamua tuombe rift ilitukuue akaja askari kutuombea rift akakuta gari limejaa lakini ukashangaa maana gari lilikua tupu kwahiyo tukashindwa kukuua

adui anapandikiza hasira ndani ya watu na huwa anatumia njia ya ndoto kupanda hasira ndani ya watu.

Tulikua njombe wiki iliyopita na Roho mtakatifu akaniambia kua kuna watu ambao kupitia ndoto kuna roho ya kuchukia biblia

MAMBO UNAYOTAKIWA KUFANYA UNAPOKUTANA NA HALI YA NDOTO KAMA HIYO:

(1)LAZIMA UOMBE TOBA KWA KILICHO SABABISHA LANGO LA NDOTO LIKAFUNGUKA NA SHETANI AKALITUMIA KUPITISHA MAMBO YAKE.

TOBA INAFANYA MAMBO MAWILI

Toba itaondoa uhalali wa shetani kisheria wa kuendelea kukusumbua.

Toba inampa Mungu uhalali wa kukupigania.haijalishi shetani anakudai kitu gani lakini ipo damu ya Yesu ambayo inafuta kila kosa na kila deni.

(2 )NG'OA ROHO ILIYOONGIA NDANI YAKO.

Kwenye isaya kuna roho ya hasira iliyoingia ndani yake.

(3)OMBA UPONYAJI WA MADHARA YALIYOTOKEA.

Ombea na mifupa ipate kupona.

11

Page 12: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Ombea madhara yaliyo achiliwa ndani yako kwenye hiyo ndoto yapate kutoka.

(4)KAMA UJAOKOKA OKOKA.

kama unaota ndoto za namna hiyo na ujaokoka mpe Yesu maisha yako.

Yesu sio wa wakristo wala biblia sio ya wakristo Yesu ni wawote na Biblia ni ya wote.

Suala la Yesu ni la watu wote...na swala la wokovu ni la watu wote kama ambavyo suala la ndoto ni la watu wote uwe unaenda mbinguni au jehanamu lazima uote ndoto.

(5)KAMA UMEOKOKA NA UKAOTA NDOTO ZA NAMNA HIYO OMBA MUNGU AKUPE MAANDIKO AU NENO ILI LIKUSAFISHIENJIA YA KUKUONGOZA.

jinsi gani kijana aisafishe njia yake kwa kutii akilishika neno lako...Zaburi 119;

12

Page 13: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

SIKU YA NNE

TAR 13-OCTOBER -2016

SOMO; NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

JAMBO LA NNE LA KUZINGATIA; Kuombea tafsiri ya ndoto husika kusikusahaurishe kuombea Ujumbe ulio bebe ndoto hiyo.

Mambo Matatu ya kukumbuka

Lengo la kuletewa ndoto ni kuletewa ujumbe.

Ayubu 33:14-15

Mungu anatumia njia moja wapo ya ndoto kusema na mtu au watu kutelemsha ujumbe

Pia fahamu. Hata kama chanzo cha ndoto sio Mungu, Mungu bado anaweza kutumia hiyo ndoto kukusaidia kwa kutumia ujumbe wa ndoto hiyo hiyo.

Torati 13:1-4

UKIFATILIA NDOTO VIZURI UTAGUNDUA VITU VIFWATAVYO?

1: Kuna ndoto zilizo beba vitu vinavyoitaji tafsiri ili upate ujumbe ndani yake. Mwanzo 40:5-23 Kuna ndoto zinavitu ndaniyake ambavyo unaitaji utafsiri kwanza ndio utaweza kupata ujumbe ndani yake.

2: Kuna Ndoto ambazo zilizobeba vitu ndani yake ambayo maana yake ipo wazi havihitaji tafsiri ili kupata ujumbe wake Mathayo 1:18-24

Kuna ndoto nyingine haziitaji tafsisi vitu vilivyo ndani yake vipo wazi kabisa na ujumbe upo wazi

3: Kuna ndoto nyinge ambazo zina ujumbe peke yake hazijabeba vitu vingine zaidi ya ujumbe. Mathayo 2:12,22

Kuna Doto zipo tofauti tofauti lazima uombe Mungu akusaidie katika kuzielewa.

2: Omba Mungu akupe kufaham ujumbe wa ndoto, usiishie kufaham tafsiri yake peke yake. Daniel 4:4-19,27

Ulicho kiona ndani ya ndoto ni kibaya lakin kinaweza kugeuzwa.

Usiishie tuu kutafuta tafsiri ya hiyo ndoto na kujua maana yake ila ombea kujua maana ya ujumbe uliobebwa na hiyo Ndoto.

3; Usipofanya Maombi ipasavyo ili ujue namna ya kushugurikia ujumbe wa ndoto ipasavyo, ujumbe huo unaweza kugeuka kuwa jaribu kwako.

Kama umeota watu wamevaa nguo nyeupe na wewe unawafata ila wao wanakukimbia basi jua ya kuwa Muda wako wa kufa umefika au umekaribia na Mungu anataka utengeneze ukiwa duniani (uokoke) kabla ya muda wako haujafika. Maanavazi jeupe ni vazi la wokovu.

KWA NINI MUHIMU KUFATILIA UJUMBE WA NDOTO??

Ni kwa sababu ndani ya ujumbe uliomo ndani ya ndoto kuna taarifa ndani yake ili kukuandaa au kukuepusha na yaliopo mbele yako.

Mfano kutoka ktk Biblia kwa Yusufu mwana wa Yakobo.

13

Page 14: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Maisha ya Yusufu yalijengwa ndani ya ndoto saba nakati ya hizo ndoto mbili aliota yeye, nne alitafsiri na moja ilikuwa inajieleza yenyewe.

Ndoto ya kwanza na ya pili aliota mwenyewe.

Mwanzo 37:5-11

Ndoto ya tatu mnyweshaji wa Faraho aliyekuwa gerezani.

Ndoto ya ya nne ni ya mwokaji mikate wa Faraho aliyekuwa gerezani.

Ndoto ya mbili zilizo fatta aliota faraho kwa usiku mmoja. Mwanzo 41,45

Ndoto ya saba ni ya baba yake Yusufu ambaye ni Yakobo. Mwanzo 46:1-5

Linganisha na Zaburi 105:17-21

KUMBUKA. Usipojua kuombea ipasavyo ujumbe uliopo dani ya ndoto ahadi inageuka jaribu.

Ujumbe uliopo ndani ya ndoto iliyo toka kwa Mungu ni neno lake Mungu kwako.

Kuna ndoto ambazo Mungu atakupa, na ujumbe wake unaweza ukawa na maagizo ya kuweza kusubiri kwa muda mrefu ilihiyo ndoto iweze kutimia.

Kuna wakati ambapo watu wanakufanyia fujo ktk maisha yako ila sio tuu kwa sababu wanakuchukia ila ni kwa sababu wanawinda ndoto yako isije timia katika maisha yako.

Sio kila ndoto utatakayo ota unatakiwa kuwaambia ndugu zako au watu maana hao wanaweza kuwa adui kwako na wanaweza kukukasirikia, bali kuwa unaliombe tu.

Ndoto ambayo Mungu atakuotesha katika maisha yako lazima tuu itimie juu ya Maisha yako haijalishi unapitia magumu kiasi gani.

Hautakiwi kuwa na kinyongo juu ya ndugu zako au wale wanaokuchukia kwa kuota kwako.

Hautakiwi kumkasirikia Mungu wako pale unapokuwa unasubiri ndoto yako kutimia.

Kama wewe ni mwana wa Mungu na umepitia mateso mengi na majaribu unaweza kumwomba Mungu akayafipisha hayomateso yako, wewe mtegemee Mungu.

VITU AMBAVYO VINAWEZA KUKUSAIDIA KUSUBIRI NDOTO YAKO

1.Hakikisha ndani ya ndoto umepata Ujumbe (neno la Bwana lililopo ndani yake).

Maana yake utalipata kwa kutafuta ujumbe hutalipata kwa kutafuta tafsiri peke yake.

2.Uhusiano wako na Mungu uchukuwe nafasi ya kwanza katika Maisha yako. Kuwa na Neno la Mungu ndani yako maanalitakuwa ni chakula cha kukusaidia pale utakapo pitia mahali pagumu katika maisha yako. Unapopata neno la Bwana na ukalichukua kuwa lako binafsi hilo neno linageuka kukuandaa kwa ajili ya maisha yako ya baada na kuwa nuru , uponyaji juu ya maisha yako.Unapo anza kuomba juu ya ndoto zako mwombe Mungu akupe tafsiri ya neno kutoka kwenye Biblia kwa maana hakuna ndoto utakayo ota isiwe na tafsiri yake hata kama iyo ndoto imetoka kwa shetani.

3. Uhusiano wako na watu wanaokuzunguka. Kama Mungu amekubebesha kitu katika maisha yako huitaji kugombana na watu kwa maana nafasi ambayo Mungu amekuandalia ni ya muhimu sana kuliko kugombana na watu.

4. Nguvu za Mungu zitakazo kawa juu yako

Mithali 24:10 Ukisikia kuchoka au kukata tamaa siku ya jaribu au taabu wakati unasubiri wakati wa Bwana basi jua Nguvu zako ni chache. Nguvu ni Roho Mtakatifu ndani yako. Unapokuwa upo kwenye jaribu unatumia Nguvu nyingi sana ndani

14

Page 15: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

yako hivyo unatakiwa uhakikishe unapata nguvu mpya. USIKATE TAMAA.Usikate tamaa maana wewe unaweza kuwakatisha au kuwasimamisha watu wengine wanao kuzunguka.

Mwl alifanya maombi kwa wale walio kata tamaa ili Nguvu za Mungu zishuke ndani yao kwa upya

15

Page 16: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

SIKU YA TANO

TAR 14-OCTOBER -2016

SOMO; NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

Kama ni mara yako ya kwanza unasikiliza masomo haya, nimekwenda kwa siku nne, na sina namna ya kurudi nyuma jitahidi pata kanda na sikiliza na kusikiliza hata kama ulikuwepo tokea awali pia pata kanda za masomo haya. Haya si masomo unaweza pata kirahisi sana maana si rahisi sana kufundishwa makanisani. Pia unaweza tembelea www.mwakasege.org kwa ajili ya kupata maelekezo wapi utapata kanda hizi hata kama uko mbali

Tuendelee na somo letu.

SUMMARY

1 Usidharau wala usipuuzie ndoto uliyoota kwa maana ndoto ni lango mojawapo la kiroho

2 Vijue vyanzo vya ndoto na jua namna ya kuviombea ipasavyo.

3 Ng’oa kilichopandikizwa na shetani kupitia ndoto na madhara yake.

4 Kuombea tafsiri ya ndoto kusikuzuie kuombea na ujumbe wa ndoto husika.

5 Ombea Fikra zako zikwamuliwe mahali zilipokwamishwa kupitia ndoto ulizoota.

Kabla sijaenda mbali Zaidi kwanza tutazame maana ya maneno haya mawili muhimu.

Fikra ni mkusanyiko na mtirirko wa mawazo yanayotengenenza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu.

Kufikiri maana yake ni akili za mtu kulifanyia kazi wazo lilioingia akilini mwake.

VITU VITATU MUHIMU UNAHITAJI KUVIJUA

1.Fikra zinauwezo wa kutengeneza aina ya maisha na kiwango chake

Mithali 23:7a “Maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, na kuna tafsiri zingine zinasema.”

Maana atafakarivyo

Maana awazavyo

Maana afikirivyo

Kwahiyo aina ya maisha uliyonayo ni matokeo ya unavyotakari.

Ili kujua kutafakari au kufikiri kwa mtu angalia aina ya maisha, maana nikihitaji kujua unatafakari nini maishani mwako au unafikiri nini maishani mwako naangalia aina ya maisha unayoishi ndiyo tutajua unachotafakari. Biblia inasema aonavyo nafsini mwake, haijazungumzia kuona mwili au rohoni bali inazungumzia kuona nafsini. Katika uumbaji wa Mungu, Mungu aliumba roho kwanza na ndipo akaumba mwili na alipopulizia pumzi ndipo mtu akawa nafsi hai. Kwa hiyo kwa itifaki ya Mungu uumbaji unaanza na Roho unakuja mwili alafu nafsi. Kwa hiyo mtu ni roho anayo nafsi anaishi kwenye mwili. Sasa kaz ya nafsi ni kutafsiri kutoka kwenye roho kwenda kwenye mwili na kutoka kwenye mwili kwenda kwenye roho. Nafsi yako ikivurugwa unakuwa na hali ngumu sana. Ndio maana Daudi alisema nafsi yangu mhimidi Bwana ina maana nafsi yake ndiyo inatakiwa imhimidi Bwana na sio mwili au roho.

Na Pia Zaburi 84:2 “Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.”

16

Page 17: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Mwili unaenda kwa kuona, na Roho inaenda kwa Imani kwa hiyo nafsi kazi yake ni kutafsiri yaani kutoa kwenye imani na kuleta kuona halisi kwa njia ya mwili. Kwa sababu kwenye nafsi kuna akili za kufanya kile kilichonekana kwa imani kiwe halisi kabisa. Lengo la Mungu ni kumfanya mwandamu aweze kuishi kwenye ulimwengu wa roho na wa kimwili kwa wakati mmoja.

Ndiyo maana ni mwanadamu peke yake mwenye sifa ya kuishi katika ulimwengu wa mwili au wa roho. Hata Mungu akihitaji kuwa Duniani ni lazima avae mwili huu wa damu na nyama. Utanielewa kwanini Yesu ilibidi aje katika ulimwengu huu achukue mwili kwa Mariam. Mungu mwenyewe ndiye kapewa hadhi hii ,malaika hawana na hadhi hii ya kumwingia mwanadamu. Ndio maana hata shetani nae anatuma mapepo na kuwaingia watu. Maana ili uweze kufanya kazi katika ulimwengu huu mwili unahitajika sana. Bila mwili hamna kinachoendelea hapa duniani.

Dhambi ilipoingia iliua roho na mwili ukawa uanenda kivyake na roho ilipoteza mahusiano na mamlaka yake ndiyo maandiko yanasema roho I radhi lakini mwili ni dhaifu. Hii ni kwa sababu ya dhambi ilivuruga utaratibu wote . Dhambi ni uasi hii unaipata kutoka 1 Yohana 3:4 “Maana ya uasi ni kwenda kinyume cha., kwa hiyo baada ya dhambi kuingia nafsi ikawa inafanya kazi kinyume cha mapenzi ya Mungu”.

Nafsi ilipewa jukumu la kutengeneza aina ya maisha na viwango vyake sawasawa na neno la Mungu linavyotaka. Hili somo la Fikra ni pan asana, Tafuta kanda za Dar es Salaam za Sept Mwaka huu, hili somo la Fikra nilifundisha kwa siku nane, na sikumaliza ooh Hii ni siri muhimu sana unahitaji kujua.

2.Mungu au shetani wanatumia ndoto ili kugusa fikra za mtu

MFANO 01

Mathayo 1:18-20.”Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.”

Biblia inasema alipokuwa anafikri hayo aliota ndoto, rudia tena mstari huu hadi uone ninachotaka uone hapa Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Yaani alipokuwa anafikiria kumwacha Mariam kwa siri ndipo alipoota ndoto usiku wakati amelala. Sasa hii ndoto ilikuja kujibu alichokuwa anafikiria. Na nimekuambia kufikiria ni kulifanyia kazi wazo lililoingia akilini mwako na wazo alilokuwa nalo ni la kumuacha Mariam. Ina maana wazo lililoingia liliweka msimamo Fulani ndani yake wa kumuacha Mariamu, ndiyo maana Mungu ilibidi aweke na mstari kabisa ili kuwa ni yeye ‘Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,’ (Isaya 7:14) “Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; (Mathayo1:23-24).”

Kwa sababu kwa hali ya kawaida ni ngumu kuamin kuwa ni kwa uweza wa roho mtakatifu ndiye kafanya Mariam apate ujauzito maana hili suala ni jipya na halijawahi kuokea hata siku moja.

kwa sababu Yusufu alijua kuwa kama atasema ile mimba siyo ya kwake lazima Mariam angeuawa kwa kawaida ya Dini ya Kiyahudi. Sasa ile kuona Mariamu asiuawe Yusufu aliazimia kutoroka ili akubali kubeba ile aibu ionekane ni yeye aliyempamimba. Na wakati anawaza hayo ndipo Malaika akamtokea katika ndoto. Na asante Yesu alitii ile ndoto, sasa fikiria asingetii ile ndoto na angesema hii ni ndoto tu kama Farao alivyosema unafikiria ingekuwaje.

Hapa ndipo utaelewa ile Ayubu 33:14-19 ‘’ Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;.”

17

Page 18: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Soma pole pole hiyo mistari hasa niliyowekewa nyota na Linganisha na Mathayo 1:18-20 .”Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.”

Kwa hiyo unaweza ukawa unawaza juu ya jambo Fulani na usiku ukaota ndoto na fuatilia vizuri hiyo ndoto iliyokuja maana usiishie tu kupata tasfir yake bali na ujumbe maana ujumbe utakupa cha kufanya, na hutua zake ambazo unatakiwa uzifuate. Na kipingele hiki naona msisitizo sana ni kuwa soma kwa kupata maarifa masomo haya

Tuko pamoja mpaka hapo? Kama hujaelewa rudia tena soma hadi uone kitu Mungu anataka uone, kama bado nyunyiza damu ya Yesu katika somo hili na Yesu afungue Fikra zako uweze kuelewa. Ooh Mungu wangu akupe kuelewa afunue akili zako ili uweze kuelewa maandiko haya.

Sasa suala la umuoe nani au uolewe na nani ni suala la akili yako na nafsi yako siyo suala la Roho yako

Ngumu eeeh ngoja nikupe mfano

Kuna wakati Fulani dada mmoja alikuja nyumbani kwetu akatukuta mimi na mke wangu alikuja nyumbani kutushirikisha suala la yeye kuolewa na akatuletea na jina la huyo kijana, maana alisema naomba mnisaidie kuomba kwa Mungu kwa sababu mimi nimejaribu kufikiria ila naona kama sielewi hivi. Basi tukamwambia sawa tutaomba. Basi haikumalizika wiki usiku mmoja niliota ndoto nikaona yule dada na yule kijana wako nyumba moja tayari na baada ya muda yule kijana aliondoka bila taarifa. Basi nikaomba Mungu anipe tafsiri na ujumbe.

Tafsiri Yule msichana tayari alikuwa kafanya maamuzi tayari ya kuolewa na kijana na ndio maana nilmuona yupo kwenye nyumba moja na kijana. Lakini ni kuwa ile ndoa yake anayotaka kuingia haitadumu kwa muda mrefu.

Ujumbe Yule Kijana sio wa kwake kwa hiyo inabidi aachane nae tu.

Baada ya kumuambia hivyo yule msichana akasema jamani naomba mniombee tu. Bassi baada ya hapo alioondoka hatukumuona tena na tulipomuona alikuwa tayari na kadi ya harusi ya kuolewa na Yule kijana. Na sisi tulisema alichosema Mungu ni hiki basi kwa kuwa wewe umeamua basi sisi tutakusndikiza tu. Ila ujue gharama iko, Basi wakaoona na wakazaa na mtoto baada ya muda kidogo Yule kijana alitoweka Nyumbani bila maelezo. Sawa sawa na ile ndoto niliyoota.

Kijana sikia kuwa makini sana kwa sababu unakuta akili yako inaanza kuishi na mtu tayari wakati mkiwa wachumba bado na unaishi nae miaka kadhaa ijayo akilini na sasa ghafla unaota ndoto Mungu anakuambia sio yeye ghafla na wewe unaanza kupata tabu kidogo. Sikuambii kuwa hamna dhoruba katika ndoa hata kwa watendaji wa neno. neno la Mungu liko wazi kabisa linasema kuwa dhoruba itakuja kwa kila mtu ila sasa mwisho wake itakuaje, hapo ndipo pana tofauti kati ya kuwa mtendaji wa neno na asiyekuwa mtendaji wa neno

Mfano kidogo alioupata Yusufu na jaribu gumu kuliko unavyofikiri maana ni jambo zito sana alilolipitia Yusufu. Inahitaji sana hekima ya Mungu na kuwa mtii wa kile Mungu anataka kukuambia. Fikiria Yusufu angetoroka pole pole ingekuaje kwa Mariam. Lazima angeuawa na je kama angeuawa Yesu angezaliwa wapi? Ooh kijana mtii Mungu katika maamuzi yako.

Sikiliza msichana akija kijana kwako anataka kukuoa na una Yesu moyoni awe tayari kukuchukua wewe na Yesu wako na asiseme mweke Yesu wako pembeni. Gharama ya kuingia kwenye ndoa bila Yesu ni gharama kubwa saba. Heri Kijana akaePembeni lakini Yesu wako abaki. Na ndio maana watu wengi wakitaka kuolewa/kuoa Mungu anasema nao kwa njia ya ndoto na hawajui

MFANO WA 02

Daniel 4:2,5,19 “Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu, Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha. Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.”

18

Page 19: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Ndoto iliyoingia ilitengeneza msimamo Fulani na Daniel alipopewa hiyo ndoto nae pia ilimfadhaisha. Lakini Mungu alikuwa anafuatilia msimamo wa Nebukadreza baada ya kumpa ujumbe wake. Lakini cha ajabu Nebukadreza hakukubaliana ili kubadilisha msimamo wake lakini hakubadilisha na alikuwa na allowance ya miezi 12 ili yamkini afanye toba hakufanya Toba na hata Daniel nae hakumuombea Toba kwa Mungu na ona matokeo yake aligeuzwa Fikra zake akawa kama Mnyama kwa Nyakati 7.

Mungu au shetani wanatumia ndoto kugusa maisha ya mtu

Mithali 3:1-5 “Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe.”

Mungu katuruhusu kutumia akili zetu na sio kuzitegemea ila kuzitumia aaah ni ruksa kabisa lakini kuweka tegemo kwake ndio makosa. Akili ziko kwenye nafsi, na jua kuwa akili hazikuumbwa ili zifanye kazi peke yake ila zinatakiwa ndani yake ziwe na ufahamu wa Kimungu ili kuweza kuishi maisha ambayo Mungu anataka. 2 Wakorintho 4:3-4 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”

Ibilisi ndio anapokuwa anawinda maisha yako anakuja moja kwa moja fikra zako na kuzipofusha. Na sababu ya yeye kuzipofusha ni kwa ajili yake ili usione fikra zake mbaya zikiingia. 2 Wakorintho 2:11 “Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. Shetani alipoenda kwa Hawa aliingia kwenye Fikra zake na akazipofusha na ndipo aliweza kumdanganya. Maana biblia inasema 2 Wakorintho 11:3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.”

Pia angalia Warumi 1:28 ‘’ Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Kwa hiyo ukimkataa Mungu katika fahamu zako ujue kuwa atakuacha ufuate mambo yasiyofaa na gharama yake ni kubwa sana.”

Mungu hulituma neno lake, na mawazo yake Isaya 55:8, 11 “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”

Kwa hiyo kuna uhusiano kati ya neno na njia na njia maana yake ni mkakati wa kukutoa mahali ulipo kwenda mahali pengine yaani hatua ndio maana neno linasema hatua za mtu zaimarishwa na Bwana Mithali 19:6, Zaburi 37:23.

3.Ndoto inaweza kutumika kufanya fikra zako kufungwa au kufunguliwa maisha yako

Daniel 4:31-37 “Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele. kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili .”

Daniel 4:15-16 “Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake.”

SASA ONA TAFSIRI YA NDOTO.

Daniel 5:18 “Hapa unapata tafsiri ya ndoto aliyoota Nebukadreza. Na ukiunganisha na Daniel 4 ni ushuhuda wa Nebukadreza jinsi alivyopita kwa miaka 7 alipokuwa Mnyama na ufalme wake kurejeshwa. Alikuwa amenyang’anywa

19

Page 20: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

ufalme wake na Mungu. Na Mungu ndiye aliyempa ufalme Nebukadreza lakini yeye alienda kinyume na yeye alieuziliwa kwa amri ya walinzi lakini aliyemtoa ni Mungu mwenyewe. “

Baada ya kupewa ufalme alianza kujiona yeye ndiyo yeye na akawa anafanya mambo kama yeye anavyojisikia. Lakini Mungu aliyempa alimuezua na hakuishia hapo aliondoa na ufahamu wake akawa kama Mnyama. Na kwa kuwa alimkataa Mungu katika fahamu zake basi Mungu akaziondoa aakili zake na kamauacha afuate akili zake zisizofaa. Kipindi cha miaka 7 kilisimamisha kabisa maisha yake na zilimpa aina Fulani ya maisha na kwa kuwa alipewa allowance ya miezi 12 ili yamkini afanye toba hakufanya Toba, na baada ya meiz 12 kupita ndipo alipoezuliwa maana ule muda ulikuwa umepita wa kufanya Toba.

Swali Je aina ya maisha unayoishi au kiwango cha maisha unayoishi ndicho Mungu alikukusudia. Kama sio ukigundua kuwa sio hicho basi ujue kuwa fahamu zako zinakurudia kwa sababu umegundua ila kama hujui basi fahamu zako zimekamatwa

Ni kweli kabisa umeokoka na mbinguni utaenda ila cheki maisha yako yamechakaa, na hawa watu wakikutazama na ukijifananisha nao huna tofauti n tofauti yako ni kuwa una Yesu moyoni. Sasa ni kazi yako kujua kuona agano la Mungu linasemaje na je unayoyasoma yapo wenye maisha yako?

Sasa chukulia wewe ni Nebukadreza na umeota kuna pingu na kisiki kimekatwa. Na kwa kuwa hujui maana yake nini na chakufanya hujui unajikuta unakemea kuanzia asubuh hadi jion kwa sababu hujui kuwa ulitakiwa utubu maana hujajizoeza kuomba tafsiri kwa Mungu ili akusaidie kujua maana ya ujumbe wa ndoto unakuta ndoto hiyo umeshindwa kudaka kilichoka ndani na maisha yako yanakuwa magumu sana.

Pia kwa kuwa hujui unakuta umeota ndoto mbuzi kafungwa kwenye mti nakamba, na wewe unajua ni mbuzi kawaida kumbe ni wewe umefungwa ni sawa na Nebukadreza hakujua sawa sawa maana ya ile ndoto na hakutilia maanani na onaalipelekwa msituni.

Sasa kama hutaki kufuata mfumo wa Kimungu itakuwa hasara sana kwako, na ndio maana unaweza ukawa na fedha lakiniukawa mlevi na unaweza ukawa na akili sana lakini bado maisha yako yakawa mabovu bila Mungu akili yako haina faida, ni sawa na injini ya Petroli ukaweka Diesel uwe na uhakika tu kuwa haifiki mbali.

UTAFANYAJE KUJUAKUWA UFAHAMU WAKO UMEHARIBIKA NA UNAHITAJI KWENDA HOSPITALI YA MUNGU

Tutatumia mfano wa Nebukadreza.

1.Alipoteza kujitambua kwa miaka 7

Ndipo aligundua kuwa Fahamu zake zilipotea ndipo alijua. Ukiona maisha yako hayafai kuishi ujue kuwa unahitaji kwenda kwa Mungu ili akusaidie maana kipimo cha maisha yako ni agano.

2 Cheki watu wanaokuzunguka wakati huu na husaidiki japo wanajithaidi kukusaidia husaidiki

Nebukadreza unadhani ndugu zake walikuwa hawammpendi, tena kiongozi wa nchi unadhani ilikuwa ni rahisi tu kwenda msituni. Lazima walimsaidia ila waliona hasaidiki na wakaamua kumuacha aende porini. Na ni sawa na wewe unakuta watu wamekukariri kuwa yule yule mwenye matatizo kaja tena.

3 Cheki waliozoea kukutembelea tena wako wapi

maana biblia inasema utajiri huleta marafiki. Lakini ona ufahamu wa Nebukadreza ulipopotea ulipoteza na marafiki na uliporudi watu wote waliokuwa wanamzunguka fahamu zao wote wailirudi.

Yamkini angejua wakati Mungu alipozungumza nae kwa njia ya ndoto lakini alipuuzia, na gharama yake ilikuwa ni Kubwa sana.

Ukisoma waebrania 4:1-4 Kikwazo cha wana wa Israel kwenda Misri ilikuwa ni kwenye Fikra zao maana unaweza ukawa na imani na ni sawa kabisa lakini ukishindwa kuchanganya imani yako na Fikra zako unaweza ukaishia jangwani na kanani yako huwezi fika.

20

Page 21: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Watu wengi ndoto zao zimekufa kwa kushindwa kuchanga Fikra yaani kutumia akili zao na Imani zao Na ukimkaribisha Mungu atakusaidia sana maishani mwako na Mungu atakuletea fahamu kwa upya na kukubadilisha.

Nakumbuka nyakati zile Mungu ananionesha kuwa ntakuwa nahubiri kwenye uwanja wa mpira kama hivi ilikuwa ni ngumu sana kuamini maana kupata tu watu 100 ilikuwa ni kazi na nikaona nisomee uchungaji na Mungu alinitoa kwenye nia yangu mbaya maana nilikuwa sina mpango wa kuwalea ila nilikuwa ntafuta watu.

ooh ni neema iloje mtu wa MUNGU, Nebukadreza alipewa miez 12 ili aombe lakini hakuomba na Daniel pia nae hakumuombea Toba Nebukadreza. Leo neema ipo hapa shikilia hili wingu omba kwa Mungu,

Baada ya hapo Mwl alituongoza kwenye maombi mazuri sana wewe fanya kwa imani omba na naamini Mungu atakupa hitaji lako ng’ang’ana na Mungu wako. Kumbuka kuombea semina hizi na njia ambazo Mungu anazitumia kukufikia. Ubarikiwe sana.

21

Page 22: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

SIKU YA SITA

TAR 15-OCTOBER -2016

SOMO; NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

Kazi ya Mungu ukiifanya kunakuwajibika ndani yake, yaani si kwamba wewe unaeifanya hiyo kazi unastahili sana au uko sahihi sana kuliko wengine hapana bali ni neema yake tu Mungu. Somo hili ni kwa ajili ya kujenga uhusiano wako na Mungu na sio ndoto tu.

Jana nilizungumza na wewe jambo la Tano la Jambo la 5 Ombea Fikra zako zikwamuliwe mahali zilipokishwa au kwama

Katika pointi hii ya tano tuliangalia vipengelee kadha wa kadha ngoja nikukumbushe kwa uchache

1 .Fikra zinauwezo wa kuetengeneza aina ya maisha na kiwango chake

Na tuliangalia Mstari wa Mithali 23:7a

2 Mungu au shetani wanatumia ndoto ili kugusa fikra za mtu

Tuliangalia mfano wa Yusufu aliyemlea Yesu na Nebukadreza

3. Ndoto inaweza kutumika kufanya fikra zako kufungwa au kufunguliwa maisha yako

Yaani hapa huwa muda mwingine ninapokuja kufundisha huwa nakuja na Karamu yaani kuna vitu Roho Mtakatifu ananiambia hapa ili nikasome na nifuatilie.

4.Ndoto inaweza kutumika kuweka ndani ya Fikra zako umuhimu wa kujua namna ya kujiandaa ipasavyo ili kupata maarifa yanayohitajika katika hatua iliyopo kwa ajili ya maisha yako ya wakati ujao

Soma kwa Upya kitabu cha Mwanzo 41:1-46 . Ila mimi nitasoma kwa kuruka ruka Kidogo

Kumbuka haya mambo matatu katika hii mistari tutakayoisoma ya Mwanzo 41.

A) Ndoto (Mwanzo 41:1-7)

b) Tafsiri (Mwanzo 41:25-31)

c) Ujumbe (Mwanzo 41: 32-36)

A NDOTO ALIYO OTA FARAO

Mwanzo 41:1-7” Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.”

Ukiisoma vizuri hapo utaona hizi ndoto alizoota Farao moja ya ng’ombe nyingine ya masuke. Jitahidi twende pamoja ili tuelewane. Na ukiendela kusoma mistari inayofuata utaona ya kuwa Farao alianza kupata mahangaiko na kuanza kutafutawaganga na wachawi ili wamsaidie kutafsiri ndoto hizi na walishindwa hadi alipoitwa Yusufu.

B TAFSIRI YA NDOTO YA FARAO

Mwanzo 41:35-31” Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Na wale

22

Page 23: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana”

C UJUMBE WA NDOTO YA FARAO

Mwanzo 41:32-36” Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa.”

Na ukienda ndani Zaidi kuanzia Mwanzo 41:39-4 .”hapa unapata maandalizi ya maisha ya baadae yaani miake 7 ile ya njaa. Baada ya ujumbe ilitakiwa jambo la kufanya, na baada ya kupewa ujumbe tunaona mambo kadhaa hapa ngoja tuliangalie jambo moja moja.“

i) Tafsiri ya ndoto za Farao zilibeba taarifa halisi ya chakula kwa Taifa zima na dunia nzima iliyokuwa inafahamika kwa wakati ule kwa miaka 14

ii) Ujumbe wa Ndoto za Farao zilibeba msisitizo kwa Farao Kutumia vizuri miaka 7 ya shibe ili kujiandaa na miaka 7 ya njaa

( a). Si kila wakati utapata tafsiri katika ujumbe wa ndoto. Kuna ndoto zinakuja na ujumbe moja kwa moja na ukienda kwenye biblia unaona mistari iko wazi kabisa. Na kuna ndoto zingine zina ujumbe na hazihitaji tafsiri bali zina ujumbe moja kwa moja. Msisitizo wa ndoto sio tafsiri bali ni ujumbe

Haijalishi ndoto imetoka wapi kwa Mungu au Shetani mwenye uhalali wa kutoa Tafsiri ni Roho Mtakatifu , usiende kwa mganga au bali Roho Mtakatifu atakupa cha kufanya juu ya hiyo ndoto hata kama ni ya shetani nayo bado Mungu ndiye atakuambia maana yake nini na ufanye endapo kama shetani anataka kuingilia maisha yako na Mungu ni Mwaminifu atakusaidia.

Msisitizo wa leo ni kuwa ndoto inaweza kutokea mara mbili na inaweza isifanane kwenye tafsiri ila inaweza ikawa na ujumbe mmoja, ndio maana Roho Mtakatifu atakusisitiza kufuatilia hiyo ndoto, na kwa kuwa imetokea mara mbili ni kuwa wajiandae kwa kuwa Mungu ataitimiza upesi.

Na isingekuwa hii mistari na msisitizo wake basi tungejua. Kwa sababu kama Mungu anaweza leta kipindi cha ukame si tunaweza omba kwa Mungu kuwa Baba tunaomba tuepushie hii njaa/huo ukame au aiweke mbali. Lakini inatakiwa tumfahamu Mungu kutoka Kona tofauti tofauti na sio moja tu

Ndio maana ukisoma biblia utaona Maserafi katika kiti cha enzi ukisoma katika Kitabu cha Isaya alipokufa mfalme uzia anaposema alimuona Bwana. Maserafi wakawa wanasema utukufu utukufu kwa sababu kila mmoja alikuwa anamuona Mungu kwa namna ambayo hawajawahi kumuona hata siku moja. Na kila mmoja alikuwa anatamani mwenzie aweze kuona alichoona, lakini kila mtu aliona kwa tofauti sana.

Hakuna mtu anaweza kumjua Mungu kabisa, bali tunajua kwa sehemu na Mungu kila siku ni mpya na haijalishi nasoma biblia kila siku nimemaliza yote lakini narudia tena kusoma na Napata kitu fresh kabisa na kipya na Zaidi sana ninapokufundisha kuliko ninavyosoma kwa ajili yangu mwenyewe. Mungu kila siku ni mpya.

Ili uishi vizuri kipindi kijacho unahitaji kujiandaa au kuandaa maandalizi yake katika kipindi hiki cha sasa kwa sababu maandalizi yanatakiwa katika kipindi hiki cha sasa ili kuweza kuishi katika kipindi kijacho

Kama umekuwa ukinisikiliza nimekuwa nasisitiza sana katika kipindi hiki cha uwingi kuwa ndicho kipindi cha kuandaa kwa ajili ya kesho. Ukiona upo kwenye uwingi kuwa makini hiyo ni fursa nzuri sana ya kutengeneza mambo yako yajayo kwa kutumia kipindi hicho.

23

Page 24: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

(c) Hekima ya Mungu inahitajika leo ili kuunganisha roho na akili za mtu ili awe na maarifa ya kujiandaa ipasavyo kwa ajiliya Kesho akiwa kwenye nafasi aliyopo leo

Mwanzo 41:8,33 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo. Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri

KATIKA MISTARI HII KUNA VITU VINNE NATAKA UONE

1.Roho Kufadhaika

2.Akili

3.Hekima

4.Nafasi/cheo ambacho/ambayo ataitumia kuwa na maamuzi juu ya kipato kwa ajili ya kuweka akiba.

Roho ya Mtu bila akili kushiriki si rahisi kuweka akiba leo kwa ajili yake kesho, na hekima ya Mungu inakupa mtazamo wa kuweka akiba sawa sawa na mipango ya Mungu juu ya maisha yao.

Mithali 30:24-25 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu;Lakini hujiwekea chakula wakati wa harI.”

Mithali 6:6-11 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.”

Chungu ni wadudu wanaoishi katika nchi za baridi na hujiwekea akiba kabla kipindi cha baridi hakijafika. Na wanayafanya yote haya bila ya kuwa na kiongozi ndio maana biblia inasema hawana akida na hujiendesha wenyewe. Maana yake Mungu anasema hata yeye katupa hii hekima ya kuweza kutunza akiba. Ila sasa Mnyama anaitumia ila ni shida kwa mwanadamu kuitumia hekima hii.

Ndio maana biblia inasema ewe mvivu tafakari njia zake/ mikakati yake ili upate hekima yaani andaa maisha ya kesho kwakutumia leo yako. Maana maisha yanaandaliwa katika kipindi cha shibe na sio njaa na ndio maana hata Silaha huwa inaandaliwa katika kipindi cha Amani na sio kipindi cha vita. Akili zako ziko kwenye nafsi na kazi yake ni kutumia wazo linaloingia kwa ajili ya kuweka akiba ya maisha ya baadae.

Uvivu wa kufikiri kwa ajili ya kesho yako biblia inasema umasikini utakujia ghafla kwa sababu hukujua kujipanga mapema. Na ndio maana unaona mtu amekuwa yuko vizuri sana akiwa kazini au akiwa anafanya biashara endapo biashara yake ikiyumba kidogo tu unaona ile taabu anayoipitia na namna Uchumi wake unavyoyumba. Kukosa akiba ni matokeo ya uvivu wa kufikiria na Mungu kamuweka chungu kwenye maandiko ili akusaidie kuweza kuzungumza na wewe ili ujue unahitaji hekima hii ya kuweka akiba.

(d) Muhimu kujali muda wa leo na matumizi yake katika kupata maarifa leo yanayohitajika kujiandaa leo kwa ajili ya kesho

Swala la muda na matumizi yake kazungumza kwa kifupi sana ila kwa kirefu Zaidi kazungumzia suala la maarifa yanayohitajika katika kipindi cha shibe kwa ajili ya kipindi njaa. Nataka nikufundishe kwenye suala la matumizi ya muda wa kuweka akiba, usiweke akiba bila kupiga mahesabu ya muda. Maana akiba itaisha na bado wewe utakuwa na uhitaji.

Weka akiba yako kwa muda maalumu yaani akiba yako iendane na muda utakaoihitaji. Kwa mfano kwa habari ya taifa la misri akiba ilihitajika kwa miaka 7 na Mungu aliweka msisitizo sana katika jambo hili na ndio maana alisema na akiba ilindwe (Mwanzo 41:35) Sasa ile hali ya kuja kuishi kwa miaka 7 ya njaa ilihitaji sehemu ya tano yaani 20% ya mavuno ya mwaka mmoja. Na hili jambo la mifuko hifadhi ya jamii ya kutunza asilimia 20% ya mshahara wa mtu ilitoka hapa. Wengine hawajui ona. Kuna mfumo miwili ya uchangiaji yaani 10% ya mwajiri na 10% ya mwajiriwa au 15% mwajiri na 5%

24

Page 25: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

mwajiriwa. Sasa ukijumlisha unapata 20% haya mambo yametoka kwenye biblia na sheria ya kuweka akiba nayo imetoka kwenye biblia (Mwanzo 41:35) aliposema na chakula kilindwe ina maana akiba nayo ilindwe na ilindwe kivipi ni kwa sheria

Ile akiba yao ilihitaji asilimia 20% tu ya mavuno ya mwaka na kuweka kwenye ghala za kitaifa na matumizi yake yangetosha mwaka mzima. Pia maarifa yalihitajika sana kuweza kuweka mambo sawa yaani takwimu kujua ni kweli mavuno yaliyotunzwa yamekuwa 20% kweli au sio na kuhakikisha maghala yamejengwa, kuhakikisha kuna watu wa kusimamia hili jambo pia kuhakikisha kuna vitu vya kutunza nafaka ili isiharibike. Kwa hiyo halikuwa ni jambo dogo kabisa lilikuwa linahitaji maarifa makubwa sana na hekima ya hali ya juu sana. Kwa sababu pesa ilihitajika kutengwa kwa ajili ya kufanya jambo hili si unajua lazima kama kulikuwa na vikao vilikuwa vya moto sana maana unakuta mna mambo mengi sana. Watu wanasema hatuna dawa, mdawati, elimu, barabara alafu wewe unawaambia kutunza chakula wanaweza sema Mungu mwenyewe anajua, maana najua sio wote walielewa kwa hiyo ndio maana hekima ilihitajika sana, usione ilikuwa kazi rahisi kwa Yusufu ilikuwa ni ngumu sana.

Yusufu hakuwa mvivu wa kufikiri na yeye ilibidi afikiri kwa niaba ya taifa zima juu ya kesho yao. Kwa sababu hata wewe hata kama unajiongoza wewe mwenyewe jifunze kufikiria juu ya kesho yako weka mipango yako ya mbele miaka mingi ijayo na anza kuitekeleza mmoja mmoja. Nilikuwa mkoa mmoja kiongozi mmoja alinijia alisema Mwakasege umenipiga ngumi za uso nikasema kwanini alisema uliposema. Kiongozi hauruhusiwi kuishi kama watu wengine au kufikiri kama watu wengine, wewe unatakiwa uishi mbele yao yaani wao kabla hawajafika kesho wewe uwe tayari umefika kesho. Majukumu ya kiongozi sio kuwauliza wananchi wanahitaji nini ina maana ukiwa hivyo hauna haja ya kuwa kiongozi. kiongozi ni lazima uwe na uwezo wa kuona mbele kuliko watu unaowaongoza.

Nilikuwa nasoma ushuhuda mmoja wa kijiji Fulani hivi nchini Brazil na viongozi wa pale walipoenda kuwauliza wananchi kuwa wanahitaji nini na wananchi walisema ngoja tufikirie kwanza na baada ya muda kidogo wakasema wanahitaji kiwanja cha mpira. Wakati huo huo walikuwa hawana shule na hospitali. Na ukiwa kama kiongozi unahitaji kujua kuwa hawa watu japo wanahitaji kiwanja cha mpira hawawezi kucheza mpira bila kuwa na Afya. Kwa hiyo unapeleka hospitali kwanza na shule ndipo unapeleka kiwanja cha mpira. Maana huwezi kuwa kiongozi na ukamfurahisha kila mtu, maana wapo tu watakao kuchukia.

Watu wa Misri walikuwa wavivu wa kufikiria, kipindi cha shibe kilipoisha walisema hawana chakula, sasa swali ni kuwa walikuwa wapi wakati serikali yao inaweka akiba ya chakula kwani wao walikuwa hawaoni? Njaa imeingia ndipo wanatakambegu ya kwenda kupanda maana wao walikuwa na akiba ya pesa na wanyama na zilipoisha biblia inasema Yusufu aliwahamisha akawaweka kwenye matuo kwa sababu alinunua ardhi yao yote. Na hata alipowaweka kwenye matuo nako bado aliwapa mbegu kwa kuwauzia.

Mwanzo 47:14- 26 “Yusufu akakusanya fedha zote zilizoonekana katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kanaani, kwa nafaka waliyoinunua. Yusufu akazileta zile fedha nyumbani mwa Farao. Fedha zote zilipokwisha katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kanaani, Wamisri wote walimjia Yusufu, wakisema, Tupe sisi chakula, kwa nini tufe mbele ya macho yako? Maana fedha zetu zimekwisha. Yusufu akasema, Toeni wanyama wenu, nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu,kama fedha zenu zimekwisha. Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng'ombe, na badala ya punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule. Na mwaka ule ulipokwisha wakamjia mwaka wa pili, wakamwambia, Hatumfichi bwana wetu ya kwamba fedha zetu zimekwisha, na makundi ya wanyama ni mali ya bwana wetu, hakikusalia kitu mbele ya bwana wetu, ila miili yetu na nchi zetu. Kwa nini tufe mbele ya macho yako, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu kwa chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumwa wa Farao; kisha utupe mbegu, tuishi wala tusife, wala nchi yetu isipotee

Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri; maana Wamisri waliuza kila mtu shamba lake; kwa sababu njaa ilikuwa imewazidi sana, nchi ikawa mali yake Farao. Akawahamisha hao watu, akawaweka katika miji, tangu upande huu wa Misrihata upande huu. Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao. Yusufu akawaambia watu, Angalieni, nimewanunua leo, ninyi, na nchi yenu, kuwa mali ya Farao; basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi. Itakuwa wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu. Wakasema, Umetulinda hai, na tuone kibali

25

Page 26: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao. Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo,ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao”

Hii ni habari ya ajabu sana maana Tunaona pia kodi kuanzishwa kwa sababu alisema ‘’ Itakuwa wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano’’ sehemu ya tano maana yake ni asilimia 20 na sehemu ya nne ni 80% kwa hiyo kodi hapandipo ilipozaliwa ilitakiwa watoe 20% ya mapato yao kama kodi.

ndipo kodi ilipozaliwa. Yaani walipangiwa hata mfumo wa kuishi wewe soma hiihabari pole pole na Roho Mtakatifu akisaidie kupata cha kuona.

Nazungumza na wewe ni kitu gani kinakufanya uwe na akiba kubwa ya mkaa kuliko chakula. Ndiyo una stoo sasa ona una madebe mangapi ya chakula, unaweza sema mimi natunza hela ya kununua chakula si hata wamisri walitunza hela ila sasa ziliwasaidia nini katika kipindi cha njaa? Bado hazikutosha. Utumie muda vizuri kwa ajili ya kutunza chakula nyumbani kwako. Na jambo hili lilimlazimu Mungu kuzungumza na mtu katika ndoto na ndio maana unaona watu wengi wanaota ndoto wanarudi shule au wako shule Mungu anakurudisha tena nyuma ni sawa umemaliza chuo kikuu sawa ila una akili kama za Primary. Na mwingine anarudishwa kazini na Mungu anasema maandalizi hayako vizuri na anasema je ukifukuzwa kazi utaishije?

Au Mungu anazungumza na wewe kwa njia ya ndoto kuwa umefeli mtihani au unapitiliza mlango au uko kazini na wewe unacheza cheza tu Mungu anakuambia kuwa tumia muda vizuri muda wako usicheze cheze na muda.

Kuna kijana mmoja nilipokuwa mkoa mmoja alikuja na kusema baba kwa kweli sielewi maana sasanimeshuka kidogo na maksi zangu zimekwenda chini na sijui nifanyeje maana mara ya kwanza nilikuwa vizuri sana ila sasa nimejaribu hata kuongeza bidi lakini bado nashuka kila siku. Hapo hapo nikuwa namuuliza Roho Mtakatifu kujua shida ni nini aliniambia kuwa shida ni siku moja alinyolewa nywele kwenye ndoto. Nikamuuliza kijana ulinyolewa nywele kwenye ndoto akasema ndiyo nilinyolewa kwenye ndoto alisema ndiyo na mahali aliponyolewa nywele hazijaota mpaka leo. Alikamatwa ufahamukupitia kwenye nywele zake. Na ndio maana biblia inasema nywele ni utukufu na ndio maana wale wazee huwa wanatakanywele za kwanza za mtoto na huzipeleka kwenye mizimu ha mtoto yule akikua mapepo yanaanza kumfuatilia na huweza hata kumuadhibu endapo atakiuka masharti yao. Kwa hiyo ukiota ndoto upo kwa kinyozi fikiri mara mbali.

Vitu vingine ni vigumu kuelewa ila unakuta tunaposma baadhi ya ndoto huwa tunashangaa maana kuna zingine ziko straightforward na unaona na mstari kwenye biblia lakini unakuta mtu haoni. Muda mwingine unakuta tayari ndoto nimeshaitolea ufafanuzi lakini bado mtu anauliza ina maana hakuelewa nilipokuwa natoa ufafanuzi hapa madhabahuni na unajua tu huyu mtu anahitaji maombi.

MUDA WA SHULE

Daniel 1:1-5” Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, NebukadrezaBwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake. Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana Vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.”

Kazi ya shule ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya kesho. Sasa ile kazi aliyokuwa anahitaji Nebukadreza ilikuwa tayari chini ya wachawi na waganga na alikuwa bado hajapata watendaji kazi wa kubadili zile nafasi zao. Kwa hiyo ilitakiwa akina Daniel na wenzao waweze kuandaliwa vizuri kwa ajili ya kuchukua nafasi hizo. Na walipewa maarifa kwa miaka 3 kwa ajili ya kuja kukaa kwenye ikulu ya mfalme.

Shule inatoa maarifa yanayohitajika kwa wakati Fulani ndio maana utona kuna kozi ya mwaka 1, miaka 2 au miaka 3 au 5 kwa ajili ya kutoa maarifa maalumu. Kwa hiyo maandalizi yalihitajika ili kuweza kuwandaa lakini ilitakiwa kwanza wawe na msingi yaani elimu ndiyo maana waliotuandalia mitaala ya elimu walijua kabisa huwezi toka primary alafu uende chuo kikuu, kuna ngazi za elimu inabidi upite kwanza alafu ndipo uweze kwenda chuo kikuu. Ndio maana sekondari ni miaka 4

26

Page 27: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

na high school ni miaka 2 na chuo ni miaka 3 au 4 au 5 au 7 kutegemea na kozi unayosoma. Huu ni wakati wako wa shibe usicheze na muda huo shikilia omba Mungu akusaidie kuutumia vizuri huo muda maana huo ndio utakuja kujenga maishayako ya baadae na biblia inasema msike sana Elimu usimwache aende zake maana huo ndio uzima wako.

Nebukadreza aliwachagua hao watu na akawapa maarifa na Daniel na wenzake walipata nafasi ila sasa wale wenzao maana lazima darasani walikuwa wengi na hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kufanya kazi ikulu ya Nebukadreza. Na muda wao ulipotea na Ile miaka mitatu ya akina Daniel chuo iliwasaida kwa muda mrefu sana na waliyatumia katika kipindi cha Nebukadreza, Dario na Koreshi. Lakini yalikuwa ni maarifa ya miaka 3 waliyoyapata ndiyo yaliyodumu kwa Zaidi ya vipindi vitatu.

Kiongozi Fulani alinipigia na alisema Mwakasege nilikuwa nasikiliza semina yako uliyosema kuwa soma ili kupata maarifa na sio elimu. Alinisimulia kuwa alikuwa na mwekezaji mmoja hapa nchini na alihitaji watu wa kufanya kazi na sisi tuliendakuongea nae ili aajiri vijana wetu waliomaliza hapa nchini, lakini yeye ataajiri mchanganyiko. Yule mwekezaji alichagua vijana mchanganyiko, wengine form four na wengine form six na wengine chuo kikuu. Basi baada ya mwaka mmoja kuna sehemu aliondoa wa form four akabakiza wa chuo kikuu, na pengine alitoa wa chuo kikuu na akabakiza form six na form four. Basi wale wa chuo kikuu wakaanza kulalamika kuwa kwanini umetuacha sisi, yule mtu alisema neno gumu kidogo MIMI SIAJIRI CHETI, AU ELIMU BALI NAAJIRI UTENDAJI KAZI YAANI MAARIFA

Akina Daniel walimkaribisha Mungu katika maandalizi yao na ndio maana aliwasaidia katika kupata kazi, ukiamua kumuweka Mungu katika fahamu zako au akili zako na katika kipindi chako cha maandalizi huwezi kosa kazi. Mungu anakuandaa kwa ajili ya kukupa kazi na uwe na uhakika lazima kazi utapata. Ndio maana inamlazimu Mungu kukusemshakwa njia ya ndoto baadhi ya mambo na kukuonesha kuwa uko shuleni na unafanya mtihani na muda mwingine anakuonesha na aina ya mtihani yaani hapo anakuonesha kuwa Fikra zako zimekwama mahali inabidi zinasuliwe

KUNA AINA MBILI ZA MITIHANI

1.Mtihani wa darasani na kwa ajili ya kupima elimu uliyoipata baada ya masomo uliyosoma

2.Mtihani wa interview (usaili) Kwa ajili ya kupata kazi, ina maana unapima maarifa uliyoyapata baada ya kumaliza elimu. Hii haifanani maana unakuta mtu katoka interview anasema Bwana hawa watu wameuliza swali ambalo hata ambalo sikusoma. Swala sio kusoma walikuwa wanapima je una maarifa ya kukutosha kufanya ile kazi wanayoihitaji.

MFANO WA DAUDI

Daudi alipakwa mafuta mara tatu

Nyumbani kwa baba yake Yese Samwel alipomfuata Nyumbani kwao

Alipokuwa Hebroni ili awe mfalme wa Yuda

Wazee wa Israel walipompa ufalme wa kuwa Mfalme wa Israel yote

Sasa Daudi alitawala Israel kwa muda wa miaka yote 40 lakini miaka 40 inahesabiwa kuanzia pale alipokuwa amaenza kutawala Yuda. Sasa swali ni je katika kipindi cha upako wa kwanza kwanini hakihesabiki? Ina maana ule upako ulikuwa kwa ajili ya maandalizi.

Upako wa Maandalizi ni kwa ajili ya kumuandaa mtu, hiki ni kipindi muhimu sana kwa mtu maana unaona daktari huyu anakutibu kwa dk tano tu maana anajua wewe una kazi nyingi sana za kujenga taifa na hata hataki kupoteza muda wako lakini yeye ilimchukua miaka 7 kujifunza. Au yule daktari wa meno ilimchukua miaka 5 kujua kutibu meno na ukapona unaanza kusema “Loli unganga uju nnunu mwee likabhabhapo nu kubhabhapo” Maana yake ni kuwa Huyu daktari ni bingwa/mzuri sana kwa sababu sijapata hata maumimivu) lakini yeye huyo imemgharimu miaka 5 kujua kukutibu.

Hivi unajua kitu unachojifunza hapa kwa lisaa limoja mimi nimetumia Zaidi ya masaa 4 -5 hadi sita ili kuandaa na ina maana yale masaa manne au matano kwangu yanakuwa blocked kwa sababu ni ya maandalizi. Na muda mwingine

27

Page 28: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

wananikaribisha kuwa karibu siku moja Kansan kwetu, uje ufundishe ile siku moja ya kujifunza wewe itanichukua siku 3 au nne kujiandaa. Kwa hiyo kuna sehemy siendi si kwa sababu sina somo bali ni kuwa sina muda wa kutosha kujiandaa.

Nazungumza na wewe vitu vigumu kidogo tumia vizuri ule muda wa maandalizi na rasilimali zake. Unapopata pesa ina maana hiyo ni miaka ya shibe yaani uwingi tumia vizuri weka akiba fanya hela yako izalishe. Na ukikosa akiba usiende kwaMungu kutafuta msaada kwanza maana msaada ni mzuri kwa kitambo na ukizidi sana utakulemaza. Kwa hiyo anza na Toba ili Mungu anapokupa msaada akupe na mbegu pia na kuzifanya Fikra zako zifikiri.

Tunaenda kufanya maombi hapa

Unahitaji kutafuta kanda ya leo maana ina vitu vizuri sana na itakusaidia san sana. Hizi summary ni sehemu tu ya kukujulisha kilichokuwa kinaendelea uwanjani. Ukiwezapata pata Kanda hii. Kama uko mbali tembelea www.mwakasege.org kupata maelezo au kuwasiliana na huduma ya MANA kujua namna ya Kupata Kanda

Miaka ile ya 80 wito ulikuwa unawaka sana ndani yangu na nikajua kumtumikia Mungu ni kwenye uimbaji basi nikajiunga na kwaya na mwalimu aliniuliza naimba sauti ya ngapi nikamwambia sauti ya….

Basi akanipa zoez dogo na kuimba na kwa kweli nadhan hata yeye alishindwa kuniambia ukweli kuwa ile sauti yako sijailewa kwa sababu sauti ilkuwa inapanda na kushuka mara naimba base mara sauti ndogo basi akasema jaribu sauti ya kwanza. Nikajaribu mara akanihamisha sauti ya nne, nako nikaona sifit kwa sababu niliona kuna watu wabase nzuri kuliko ya kwangu. Basi nikahamaia kwa wapiga vyombo nako niliona wako watalaamu kunishinda. Basi nikaanza kupiga mabati (crash) na nilitunga hata style yangu ya kupiga. Na niliota ndoto kuwa napelekwa shule ya kuimba na ndipo niligundua kuwa nako kuimba kunahitaji kujifunza. Sasa nina nyimbo kadhaa nimetunza ili wasije wakaniibia na ziko kadhaa ntatoa albamu yangu na nikiona haitoshi ntaweka na tenzi kidogo

Baada ya hapo yalifanyika maombi sana ya kuombea watu wote wanaopata shida kwenye shule hasa vijana. Na hakika nguvu ya Mungu ilionekana sana pale uwanjani.Ili semina hizi ziwe msaada kwakohakikisha unaokoka na unamjua Mungukama hujaokoka hakikisha unaokoka maana huu ndio mtaji mkubwa sana. Fanya maamuzi hayo leo na ukishaokoka soma somo la utangulizi kwenye link hapo chini na jiunge na waliokoka walioko kansani kwako.

SIKU YA SABA

TAR 16-OCTOBER -2016

SOMO; NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO.

28

Page 29: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

LENGO LA SOMO; NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

Najua leo kuna wengine ni siku yao ya kwanza kuja kwenye semina kwa sababu mbali mbali hawakuweza kufika ila jitahidipata kanda za masomo haya. Na unaponunua kanda hizi usiende na wazo na kununua au iwe ni kitabu au ni nyimbo za watumishi wa Mungu maana huwezi linganisha thamani ya pesa yako na kilichoko ndani. Tunafanya hivi ili kupanua wigo sio kwa ajili ya kupata faida. Kanda hizi ni chakula chukua sikiliza na kusikiliza. Kama uko mbali tembelea www.mwakasege.org utapata maelezo ya namna ya kupata kanda na vitabu.

SUMMARY YA MAMBO TULIYOJIFUNZA KWENYE SEMINA.

1 Usidharau wala usipuuzie ndoto uliyoota kwa maana ndoto ni lango mojawapo la kiroho

2 Vijue vyanzo vya ndoto na jua namna ya kuviombea ipasavyo.

3 Ng’oa kilichopandikizwa na shetani kupitia ndoto na madhara yake.

4 Kuombea tafsiri ya ndoto kusikuzuie kuombea na ujumbe wa ndoto husika.

5 Ombea Fikra zako zikwamuliwe mahali zilipokwamishwa kupitia ndoto ulizoota.

6.Tumia uhusiano wa neno na Roho Mtakatifu ukusaidie kuombea ndoto ipasavyo.

LEO TUTANGALIA JAMBO LA 6 TUMIA UHUSIANO WA NENO NA ROHO MTAKATIFU UKUSAIDIE KUOMBEA NDOTO IPASAVYO

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Warumi 8:26-27 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”

Kutumia uhusiano wa neno na Roho Mtakatifu. Kama unataka kuomba vizuri inabidi neno la Mungu likae kwa wingi ndaniyako. Na inategemea sana ngazi uliyopo huo mstari wa Yohana 15:7 inabidi uombe tofauti kidogo ili uweze kutembea kwenye mapenzi ya Mungu. Mungu anaweza akakupa kitu unachokitaka lakini kuwa makini sana. Maana wana wa Israel walipewa Nyama na walikondeshwa Roho zao. Maana hata huku mjini watu wanasema mtoto akililia wembe…., MALIZIA HAPO

Kuna wengine wamepewa vitu wanavyovitaka lakini ni nje ya mapenzi ya Mungu kwa lugha ya kiingereza tungesema kunaPerfect will of God na Permissive will of God. Yaani hii Permissive will of God ni kwa kuruhusiwa na Mungu lakini sio mapenzi ya Mungu. Na wa perfect will of God na huyu wa Permissive will of God hawawezi kuwa sawa hata kidogo.

Na nakumbuka mwaka Fulani tukiwa tunaandaa semina ya Dodoma. Na tulikuwa tunaomba Mungu Fanya hiki fanya hiki na Mungu anafanya. Na wakati ule tulikuwa hatuna mahema kama hivi tulikuwa tunafanya semina ndani ya kanisa. Basi tuliwaambia wenzetu wafanye maombi sana juu ya semina ile na walifunga na kuomba kwa ajili ya semina kwa miez kadhaa na kila ijumaa walikuwa wanafanya mkesha wa maombi. Basi na mimi na Mke wangu tuliwahi kwenda Dodoma ili tungane nao kwenye mkesha. Basi tuliomba sana na wenzetu walijitahidi kwa kweli. Sasa iliwadia siku ya Semina hiyo sikuilikuwa ngumu kweli maana nilikuwa naonekana kama naongea peke yangu alafu najiuliza kama watu wamenielewa kwelinikawa naongea alafu naona neno lile kama linanirudia mwenyewe. Ilikuwa ngumu kweli kweli basi nikaita watu kuokoka na walitoka, nilijua hawatatoka kwa sababu sikuwa na uhakika kama wamenielewa.

Baada ya pale nikamwambia mke wangu kuwa kwa kweli mimi siombi tena, maana haiwezekani tuombe kiasi kile na kufunga kwa siku zote vile alafu semina iwe ngumu vile yaani kama niko peke yangu maana hata ule uwepo wa Bwana haupo. Basi moyo wangu uliumia sana na nilisema mimi siombi tena siku iliyofuata mke wangu aliniamsha twende kuomba nilimuombia mimi siendi ila nilisema nitakusindikiza tu basi tulipofika Kansan asubuh akafungua mlango akashuka ndani ya gari na alienda Kansan. Mimi nikavuta kiti ndani ya gari nikaka. Sikuenda kuomba, basi mke wangu alirudi tulirudi pale mahali tulipofikia. Na mchana niliomba chakula nikala na sikufunga tena. Zilipobaki dakika kidogo kabla ya kwenda semina nilimwambia Bwana Yesu unakitu cha kuzungumza na watu wako akanipa na niliandika. Siku ile

29

Page 30: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

ilishuka nguvu kubwa sana ya Mungu pale katika semina. vIlipofika jion nilipomaliza semina nilishangaa sana maana sikuomba lakini nguvu iliyoshuka pale ilikuwa ni kubwa sana. Nikamuuliza Mungu sasa ndio nini Mungu alisema neno lango katika Yohana 12:26 “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo”. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu na alisema kuwa nikikutuma kufanya semina inabidi uje kwangu kuomba au kuuliza kuwa mimi Mungu ninataka kufanya nini kwenye hii semina, na sio ambavyo wewe unataka kwenye hii semina.

Biblia inasema pale nilipo ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa na sio sisi tulipo na Mungu atakuwa. Kuwa makini hapo biblia haijipingi maana mwingine atasema Mathayo 18:20 “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”. Sasa hukusanyiki wewe upendavyo maana ile kazi ya kufundisha au kuhubiri ni lazima Mungu awe amekutuma na kasema biblia iko wazi kabisa Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo Pale alipo Yesu ndipo utakuwa kumtumikia. Ina maana mwenye kukualika kutumika ni Mungu na inabidi ufanye vile yeye apendavyo maana biblia inasema Mathayo 7:21” Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Kwa hiyo ile kusema mnasema Bwana Bwana na mjisahau kuwa mnafanya mapenzi ya Mungu si kweli. Kwa hiyo usipendekumpangia Mungu mambo ya kufanya bali yeye ndiye akupangie wewe maana yeye ndiye mwenye kazi. (Haya maelezo mwalimu hakuongea na hakuweka mistari hii nimeweka baada ya kupata msisitizo ndani yangu kwa ajili ya kutoa ufafanuzi nilipokuwa naandika

Na ndio maana nilikupa tahadhari mapema katika Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.” Nilisema usiombe lolote bali omba kulingana na mapenzi ya Mungu Na Biblia hiyo hiyo imesema Yakobo 4:3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. _ Na 1 Yohana 5:14-15 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.”

Hata Ibrahimu aliomba kuwa Ishmael abarikiwe na ni kweli alibarikiwa nje ya agano, na si watu wengi wanajua tofauti ya kati ya Baraka za agano na Baraka zilizo nje ya agano. Ishmael hakupewa ardhi bali Isaka alipata ardhi. Hivyo ukiota ndoto na usikimbilie tu kuomba bali tafuta uhusiano kati ya neno na Roho Mtakatifu ili upate msaada.

Neno na Roho vinafanya kazi kwa pamoja na neno bila Roho Mtakatifu halina msaada kwa sababu katika uumbaji wa Mungu Roho alitulia juu ya maji na Mungu alipokuwa anasema na kuwe Nuru ndipo Roho alikuwa anenda kutenda. Angalia Mwanzo 1:2-3 “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru Lakini ukiangalia kwa habari za kuzaliwa kwa Yesu biblia inasema kuwa neno alitangulia na Roho akafuata”. Angalia Luka 1:30-35 “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu”. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu

Hapa unaona neno kutangulia yaani kuwa atapata Mimba na ona Mariam alipouliza itakuje ndipo Malaika alisema ‘’ RohoMtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli kwa hiyo neno + Roho Mtakatifu =Matokeo.Kwa maana Roho Mtakatifu na neno wanafanya kazi pamoja sasa watu wengi hata hawajui kwanini wanakuwa wazito kusoma biblia sasa sijui wanaombaje kwa sababu kuwa na nguvu za Mungu bila neno ni sawa sawa na gari lina kila kitu lakini halina taa maana neno la Mungu ni taa.

Na unajua kwanini huwezi kusoma biblia ni kwa sababu hujapangia muda. Kitu ambacho hakina thamani kwako huoni umuhimu wa kukipangia muda. Maana natamani sana watu wawe kama watu wa Beroya wakichunguza chunguza maandiko maana natamani na wao wafuatilie kwenye biblia.

Ivi umewahi jiuliza kwanini Yesu aingie gharama ya katukalisha hapa kwenye hema anataka tukae kama darasa ili tujifunze neno na Mungu. Lakini sasa unakuta mtu haji kwa mkao wa kujifunza bali anasubiri saa ngapi aombewe. Lakini ujue hapa ni semina sio mkutano kwa hiyo kaa mkao wa kujifunza.

30

Page 31: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

Je sasa ukifika mahali pa kisiwa cha Patmo utafanyaje maana utakuwa peke yako na sasa utamtafuta nani maana hata simu unakuta hauna ya kuwapigia wapendwa. Sasa Unaweza kusoma biblia kila mwaka maana kuna vitabu vya kuongoza mwongozo wa kusoma biblia kwa mwaka mzima au kwenye simu yako kuna application za kukuongoza namna ya kusoma biblia kwa mwaka mzima. Sasa jiulize ni muda gani unakaa whatsapp au sehemu nyingine na ni muda gani unasoma nenola Bwana, hata kwenye simu yako unaweza weka biblia yako na ukaisoma kila siku.

Mungu alisema na mimi katika ndoto nyingi sana. Nilipokuwa Form Six katika Sekondary ya Mkwawa na sikuelewa maanayake ni nini. Niliota ndoto nikiwa mwisho wa Dunia na watu waliokuwa wanapona ndio waliokuwa wanapita kwenye nyumba niliyokuwamo. Hapo ndipo nilipojua kuwa nimepewa kazi ya kutangaza habari za Mwisho wa Dunia.

Pia nikiwa SUA wakati ule ni sehemu ya chuo kikuu cha Dar es Salaam. Niliota ndoto mtu mmoja mrefu amakuja na nguo nyeupe na amekuja na kitu cheupe cha Duara na ilikuwa na kishikizo, na mara alisema duniani mna dhambi nyingi mara akaondoka nacho. na Kwa kweli hii ndoto nilishindwa kuvumilia ilibidi niende kwa mganga na rafiki yangu na pikipiki. Na Mganga kidogo apatie tu na nilipomsimulia ile ndoto alisema alisema kweli aliyekuja ni Malaika na kuna Baraka anataka akupe sasa tatizo sio duniani kuna dhambi bali ni wewe unadhambi nyingi sana. Na nilimuuliza sasa ndio natubu vipi alinipa utaratibu wa dini ya kwao namna wanavyofanya aliniandikia na ile sala ya toba na akaniambia niikariri. Sasa nilipokuja kuokoka ndipo nilielewa kuwa lile jiwe jeupe lilikuwa ni nini Ufunuo 2:17 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea”

Nazungumza na wewe umuhimu wa kuweza kutazama uhusiano wako na Yesu na utumishi na maana ni muhimu sana kujua kuwa si kila nguvu ni za Mungu na si kila mtu anayekujia kwenye ndoto amevaa vazi jeupe ni malaika maana hata shetani nae hujifanya malaika wa Nuru. 2 Wakorintho 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Nakuambia vitu vya muhimu na vya kukusaidia ukiona ndoto inakupeleka mbali au inakuondoa karibu na Yesu wako chekivizuri. Maana si vyote vya kuamini bali fuatilia maandiko.

NDOTO NYINGINE

Niliota ndoto nyingine kuna kanisa moja lipo kwenye kijiji Fulani na katikati yake kuna migomba na niliona kuna mchungaji mmoja na kaingia kila akihubiri katika lile kanisa watu wanakufa, na akihubiri tena theluthi nyingine wanakufa na baada ya hapo akatoka. Na akavua joho basi mimi nikaingia nikasema kwa jina la Yesu amka, nikaamka na wakaamka na nikasema kwa jina la Yesu waliamka tena. Na hadi waliamka wote na hapo ndipo wito wangu nilijua ni kwa ajili ya kanisa yaani kulifufua kanisa la Mungu.

NDOTO NYINGINE

Niliota nipo kwenye Bustani moja na ghafla nikamuona Yesu amenitokea na kaja na taji na ghalfa akaja kwenye benchi nililokaa na ghafla akanichukua juu na akienda juu na mimi nikawa naenda juu sasa na tazama nguo kubwa nyeupe ikanishukia na ikanifunika hadi chini. Basi nilipofika nikamkuta mke wangu yupo kwenye uwanja na watu wengi sana uwanjani na anasema tulikuwa tunakusubiri.

Na nilipokuja kusoma kwenye biblia kuwa ndipo nilielewa iliposema Luka 24:49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu na nilijua mke wangu ndiye mwenye uwezo wa kuwakusanya watu na nilianza kumuombea kwa namna ya tofauti sana. Na hadi leo yeye ndiye mratibu wangu mkuu wa wa semina zote.”

Kwa hiyo unapopata ndoto nenda kwa Mungu yaani jizoeze kuomba tafsiri kwa Mungu ili akupe maana ya hizo ndoto kama Daniel alivyofanya. Daniel 2:16-17 “Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake”

Usifanye kosa kama la Yusufu la kuwasimulia ndugu zake maana si wote watafurahia hiyo ndoto yako bali nenda kwa Mungu ili akupe cha kufanya kama walivyoambiwa akina Daniel na wenzake.

31

Page 32: NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKOmalango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. Muda ni lango, Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo

NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO

MFANO

Kuna dada mmoja nilipokuwa mkoa mmoja akasema baba naomba nisaidie. Kuna mwanaume mmoja alitaka kunioa na yeye anamke tayari ya Yeye na alisema kwa mujibu wa dini ya kwao wanaruhisiwa kuona wanawake wengi. Na yule dada aliniambia kuwa yeye alimkataa na alimuambia kuwa yeye kaokoka. Basi yule mwanaume alianza kumuingilia kwa njia ya ndoto. Nilimuuliza unapolala huwa unaomba alisema ndiyo naomba sasa tena najifunika kwa damu ya Yesu. Basi nikasema ngoja na mimi niombe niliomba kwa njia hizi tano

1. Niliomba kwa damu ya Yesu kutenganisha muunganiko wa kipepo kati ya lango la ndoto na viungo vya uzazi vya yule msichana.

2. Nilikemea lile pepo lililokuwa linakuja na ile sura ya mtu kwa ajili ya kumtesa Yule msichana.

3. Uponyaji kwa ajili ya madhara yaliyompata yule msichana.

4. Kufanga milango na kuzuia asioteshe tena zile ndoto

5. Ulinzi wa Damu ya Yesu ili aolewe na atakapoolewa aolewe vizuri kwa muda wa Mungu utakapofika.

Na baada ya muda alikuja kuniambia kuwa baba ile hali haijajitokeza tena. Na ila aliniuliza swali kuwa je wewe ndiyo umeombaje maana na mimi nimeomba kwa damu ya Yesu hiyo hiyo na sijapata majibu sasa wewe ndiyo umeombaje. Nilimuambia shida hapa msichana ni Imani yaani sio kwamba umeokoka basi damu ya Yesu inaweza kufanya kazi bali bali kuwa na imani yaani kuwa na uhakika wa kile unachokitarajia katika imani yako.

Kuna mtu mmoja pia aliniambia kuwa Mwakasege ninaota ndoto nazini na wanyama, ni kweli nilielewa kuwa kuna agano lipo na Pia mwingine aliniambia kuwa aliota ndoto nyoka kapita katika tumbo lake nilijua kuwa kizazi chake kilikabidhiwa kwa miungu mingine. Maana yake usiposhughulika na ndoto hizi mara baada ya muda utakuwa unapata wachumba na bila sababu za msingi unakuta wanakuacha. Na wengine wanaota wanazini na majini hata hawajui maana yake nini Mambo ya Walawi 17:7 “Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi”

TAFSIRI YAKE

Usherati wa Kiroho ni Mbaya sana maana ukiachia hivi mara utajiona una mimba na mara unanyonyesha watoto na hali yako inaanza kuwa mbaya sana. Kwa hiyo Damu ya Yesu inaweza pangua kabisa hivyo vitu na kukufanya kuwa safi.

Pia mtu mmoja aliniambia kuwa aliota mbwa kalala kwenye kiatanda chake na mwingine aliota kwenye kitanda chake yeye ni mwanaume wako watatu yaani yeye na mke wake na mwanaume mwingine. Mwingine pia aliniambia kuwa kaota ndoto kuwa Wanawake wawili wamelala kwenye kitanda pamoja na mume wake na hakujua cha kufanya.

Kwa hiyo ni muhimu sana kujua namna Damu ya Yesu inavyofanya kazi fuatilia somo hili la Damu ya Yesu katika tovuti pamoja na kwenye Ukurusa wa Facebook wa Mwalimu. Na ukilijua hili neno utakuwa umepata kitu kikubwa sana. MaanaShetani anafurahia sana watu wasijue neno la Mungu.

Zoezi shika kidole chako cha ndoa na Mwalimu aliomba sana kuhusu mapepo yaliyokamata vidole vya ndoa na hakika nguvu ya Mungu ilishuka kwa nguvu kubwa sana sana na kutufungua. Na Mwalimu aliachilia sana Baraka kwa watu wote walikuwepo kwenye semina. Hata wewe huko huko Pokea Baraka za Mungu. Na Ubarikiwe sana sana na tuzidi kumshukuru sana Mungu kwa huduma ya MANA na watenda kazi wote Mungu awabariki sana. Hebu tamka neno la Baraka kwa Hawa watu maana wanajitoa sana sana. Hadi mafundisho haya tunayapata bure kabisa… ni neema sana sanakwa Mungu basi tuituime vizuri sa

Prepared by DISMARK NISALILE MWAKASEGE with assistance of MANA Ministry

0657 531 444

32