nasari za miche - world agroforestry...

52
Regional Land Management Unit (RELMA) TECHNICAL PAMPHLET No. 3 Nasari za miche Mwongozo wa wenye nasari kwenye vitongoji vya miji Caleb Basweti

Upload: others

Post on 17-Jan-2020

9 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

Regional Land Management Unit (RELMA)

TECHNICAL PAMPHLET No. 3

Nasari za miche Mwongozo wa wenye nasari kwenye vitongoji vya miji

Caleb Basweti

Page 2: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

RELMA Technical Pamphlet (TP) series

Enclosures to protect and conserveAichi Kitalyi, Alphonse Musili, Jorge Suazo and Frederick Ogutu. 2002. TP No. 2. ISBN 9966-896-54-6Puonjruok e gero deche mag pi e dala mar KusaJohnson Ouko and Alex Oduor. 1999. TP No. 1. ISBN 9966-896-48-1

Page 3: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

i

Nasari za micheMwongozo wa wenye nasari za kibinafsi

Caleb Basweti

Regional Land Management Unit (RELMA)

Page 4: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

ii

Published byRegional Land Management Unit (RELMA)/Sida, ICRAF House, GigiriP.O. Box 63403, Nairobi 00619, Kenya

© 2003 Regional Land Management Unit (RELMA), Swedish International Develop-ment Cooperation Agency (Sida)

EditingKimunya Mugo and Wainaina Kiganya

Editor of RELMA series of publicationsAnna K Lindqvist/RELMA

Design and layoutKimunya Mugo

IllustrationsCover photo top: Jonathan MuriukiCover photo bottom: Hannah Jaenicke

Drawings: James Mugo

Cataloguing-in-Publication dataNasari za miche: Mwongozo wa wenye nasari za kibinafsi. 2003. RELMA TechnicalPamphlet series No. 3. Nairobi, Kenya: Regional Land Management Unit (RELMA),Swedish International Development Cooperation Agency (Sida). 43 p. + vi p.

ISBN 9966-896-68-6

The content of this field guide may be reproduced without special permission. However,acknowledgement of the source is requested. View expressed in the RELMA series ofpublications are those of the authors and do not necessarily reflect the views ofRELMA/Sida.

Printed in Dubai by AG Printing & Publishing Ltd, Kenya Tel: +254 20 4446560/4449775Email: [email protected]

Page 5: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

iii

YaliyomoForeword ....................................................................... vUtangulizi .................................................................... vi

1. Utangulizi ................................................................. 1Nasari ni nini? ................................................................................. 1Lengo la nasari za miche ............................................................... 1Umuhimu wa nasari za miche ....................................................... 1Uanzishaji wa nasari ....................................................................... 1Usimamizi wa nasari ...................................................................... 2

2. Kutayarisha nasari ..................................................... 3Aina za nasari ................................................................................. 4Ubora wa udongo wa bustani la miche ........................................ 4Kuongezea viumbe vya manufaa .................................................. 5

3. Uzalishaji wa miti ...................................................... 6Mbegu zilizopandwa ...................................................................... 6Mbegu zilizodondoka kutoka kwenye mti .................................. 13Uzalishaji miche usiotumia mbegu ............................................. 13

4. Njia za ukuzaji miche ................................................ 15Kukuza miche kwenye ardhi tupu ............................................... 15Kukuza miche ndani ya mifuko na mikebe ................................ 17

5. Ulezi bora wa miche ................................................... 19Kuhamisha miche ......................................................................... 19Kunyunyiza maji .......................................................................... 21Kivuli ............................................................................................ 24Kupunguza mizizi ......................................................................... 27Kupalilia ....................................................................................... 28Kuifanya mimea kuwa thabiti na kuisafirisha ............................. 28

6. Wadudu na magonjwa miche kwenye bustano ............... 30Usafi wa bustani ya miche ........................................................... 30Kuepushia miche madhara katika bustani .................................. 31Jinsi ya kuzuia magonjwa katika bustani la miche ..................... 35

Page 6: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

iv

Kuzuia na kuangamiza wadudu waharibifu na magonjwa ........ 37

7. Upandaji wa miche shambani ...................................... 38

8. Soko ........................................................................ 39

9. Hitimisho: mambo muhimu ya kuzingatia .................... 40Rekodi ........................................................................................... 40Kuwahudumia wateja .................................................................. 40Wenzako wanakuza nini? ............................................................. 40Kutangaza nasari ......................................................................... 41Kupakia miche ...................................................................... 41Kupatia wateja sampuli za bure ........................................... 41Kushirikiana na wenzako ..................................................... 41

Wasahihishaji........................................................ 42

Page 7: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

v

ForewordThe urban and peri-urban population in many developing countries israpidly increasing and it is projected that by 2015 the urban populationwill equal the rural one. A new dimension of food and fodder insecurityis foreseen to accompany this increase. The urban population will bemainly supplied with food from the countryside, which is a great marketopportunity for the rural farmers. The rate of food and fodder productionproduced in the urban/peri-urban areas will increase. Agroforestrytechnologies can contribute to increased food and fodder productionand minimize the risks associated with small-scale agriculture, especiallyin the peri-urban setting. However, quite a number of rural farmers buytheir tree and shrub seedlings in the urban areas.

The preparation of this field guide was proposed after the publicationof the Tree nursery trade in urban and peri-urban areas (RELMA Working PaperNo. 13). This paper contained results of a survey of 39 nurseries inNairobi and Kiambu Districts, Kenya.

The purpose of this guide is to share basic knowledge required for theeffective management of urban and peri-urban nurseries. Anyonereading it will quickly understand and learn the practical requirementfor the establishment of nurseries. RELMA has had a goal to producefield guides in local languages for easy reading by the intended users.This guide provides such an opportunity.

Åke BarklundDirector, RELMA

Page 8: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

vi

UtanguliziIdadi ya watu kwenye miji na viunga vyake katika nchi zinzoendeleainaongezeka kasi na yakisiwa kwamba kufika mwaka 2015, idadi yawatu mijini itakuwa sawa na ya wakazi wa mashambani. Yabashiriwaongezeko hilo bila shaka litasababisha uhaba wa chakula na malisho yamifugo. Teknolojia za kukuza miti pamoja na chakula inaweza kuchangiakatika kuongeza kiasi cha chakula na pia malisho. Kadhalika,zitapunguza madhara ambayo huhusishwa na kilimo na vijishambavidogo, hasa katika maeneo ya mitaa ya miji.

Uandalizi wa mwongozo huu wa kutumiwa nyanjani ulipendekezwakufuatia kuchapishwa kwa Tree nursery trade in urban and peri-urban areas(RELMA Workinng Paper No 13). Hati hii ilishirikisha matokeo ya uchunguziwa nasari 39 katika Wilaya za Kiambu na Nairobi, Kenya.

Madhumuni ya mwongozo huu ni kutoa maelezo ya kimsingi ambayoyanahitajika kwa usimamizi kamili wa nasari za miche katika miji naviungani vyake. Yeyote anayeusoma ataelewa haraka na pia kujifunzamambo anayohitaji kufanya ili kuanzisha nasari. limekuwa ni lengo laRELMA kutoa miongozo ya nyanjani kwa lugha za kiasili inayowezakusomeka kwa urahisi na jamii zinazolengwa. Mwongozo huu unatoamojawapo ya nafasi hizo.

Åke BarklundMkurugenzi, RELMA

Page 9: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

1

1. UtanguliziNasari ni nini?Ni mahali ambapo miche ya miti hukuzwa na kutunzwa vizuri kabla yakuhamishwa na kupandwa mashambani au mahali popote inapohitajika.Idadi ya miche inayokuzwa hulingana na mahitaji yake na yale ya soko.

Lengo la nasari za micheLengo la kuanzisha nasari za miche ni kukuza aina ya miti na kwa kiasikinachohitajika. Kadhalika, huhakikisha kwamba mimea inayokuzwa niya kiwango na hali nzuri iwezayo kupandwa kila inakohitajika, na hasakatika msimu wa mvua.

Umuhimu wa nasari za miche• Nasari huinua hali ya maisha ya binadamu na mazingira kwa

jumla;• Hutoa nafasi za kazi kwa watu wengi, iwe ni katika nasari za

kibinafsi, za serikali na za mashirika mbali mbali yanayohusikana upandaji wa miti;• Miche iliyokomaa huuzwa na kuwapatia wakuzaji na wafanya

kazi wao mapato;• Miti husafisha hewa, husaidia kuhifadhi maji, kuzuia

mmomonyoko wa udongo na huwapatia makao wanyama wengiwa pori;• Miti hutupatia kuni, mbao, dawa, chakula cha mifugo na

matunda; na• Miti hugeuza sura za miji na kuifanya kuwa maridadi.

Uanzishaji wa nasariKuna mambo kadhaa muhimu ya kuzingatia kabla hujaanzisha nasari:

• Maji ni muhimu sana kwa ukuzaji wa miche na inafaa nasari iwekaribu na maji safi na ya kutosha. Epuka utumiaji wa maji yenyechumvi;

Page 10: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

2

• Udongo bora wenye rutuba na kiwango kifaacho cha kushikiliana kuachilia maji;• Nasari haifai kuwa mahali ambapo maji husimama na iwapo

yatakwama, itakubidi uchimbe mitaro ya kuyaondoa. Mahalapenye mteremko mdogo uwezao kuruhusu maji kuteremka bilakusababisha mmomonyoko wa udongo panafaa;• Pawe na mwangaza wa kutosha na kivuli cha kukinga miche

kutokana na miale ya jua, hasa wakati wa kiangazi;• Vifaa vya kazi kama vile mifuko, jembe, makasi, panga na

kadhalika vinavyotumiwa kurekebisha hali ya udongo; ns• Mbolea na fatalaiza.

Usimamizi wa nasari• Nasari ikiwa karibu na mahala ambapo miti inahitajika,

itapunguza gharama za usafirishaji• Nasari inafaa kuwa mahala ambapo wateja na wafanya kazi

watafika kwa urahisi• Ukubwa wa nasari utategemea idadi ya miche inayohitajika;• Kiwango cha mifuko ya kukuza inayotumika;• Muda ambao miche ya miti tofauti huchukua

Page 11: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

3

2. Kutayarisha nasariKuna aina mbili za nasari za kupandia miche:

Nasari zilizoinuka (raised beds) zinafaa mahala penye mvua yakutosha na ambapo maji yatateremka kwa urahisi

Nasari nyingine huchimbiwa chini (sunken beds), na hasa katikasehemu zenye mvua haba ama zisizo na maji ya kutosha

Bustani hizi huwa na upana wa mita moja na urefu wa mita moja au zaidikulingana na mahitaji yako. Nafasi kutoka kwa kitanda kimoja hadi kingineni sentimita 60.

Mifuko ya aina mbali mbali, na hasa ya nailoni, hutumiwa kwa wingi kwakukuzia miche. Mifuko hii hupatikana kwa urahisi na kwa saizi tofauti.Hutobolewa upande wa chini ili kupatia mizizi hewa ya kutosha na piakupitishia maji udongo ukilowa.

Page 12: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

4

Aina za nasariNjia mwafaka ya kubainisha aina za nasari ni kulinganisha wamilikajiwake na lengo lao. Nasari zinaweza kuwa kubwa au ndogo kulingana naidadi ya miche inayokuzwa. Aina hizi ni:

Nasari za utafiti zinamilikiwa na mashirika ya utafiti kwa madhumuniya kufanyia uchunguzi wa kisayansi, kama vile Taasisi ya Utafiti wa Misitu(KEFRI), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (KARI) au World Agroforestry Centre(ICRAF).

Nasari za kijamii hupatikana mashambani na pia katika miji mbalimbali. Lengo lake ni kukuza miche ya mahitaji ya kijamii, kibinafsi amaya kutumika kwa mradi fulani. Aina mbili kuu za nasari kwenye kundi hilini:

Nasari za kibinafsi ambazo kwa kawaida huwa zimeanzishwa nakumilikiwa na mtu mmoja.

Nasari za vikundi huanzishwa na kumilikiwa na watu wawili au zaidi.

Ubora wa udongo wa bustani la micheUkuaji bora wa miche kwenye bustani hutegemea hasa hali ya udongounaotumika kwa kupanda. Mmea wenye mizizi thabiti na kwenye udongowenye rutuba utastahimili kwa urahisi mazingira magumu, kama vileudongo usio na rutuba na maeneo yasiyo na maji ya kutosha. Hivyo basi,ni wazi kwamba afya na uthabiti wa mizizi hazitegemei hali ya mmea, ilaudongo unaotumika.

Udongo bora wa bustani la miche unahitaji kuwa:• Mwepesi na uwezao kubebwa kwa urahisi;• Na uwezo wa kushikilia mbegu kikamilifu;• Hauna kwekwe ama mbegu za magugu na magonjwa;• Unapitisha maji kwa urahisi hata yakiwa mengi;• Unapitisha hewa ya kutosha na kwa urahisi kwenye mizizi;• Thabiti na usiopata miatuka ukikauka; na• Uwe na lishe ya kutosha kwa mimea.

Page 13: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

5

Udongo kinamu (clay soil) 1 2 2

Udongo wa hali ya kadri (loam) 1 1 1

Udongo wa mwepesi (changarawe) 1 0 1

Aina ya udongo ulio kwenyenasari

Udongo Changarawe Mbolea asili

Viwango vya mchanganyiko

• Usiwe na chumvi nyingi kupindukia• Haubadilishi hali yake ukimwagiliwa maji.

Mara kwa mara, udongo unaotumiwa na wenye bustani za miche wengihauridhishi kamwe. Ili kuimarisha hali ya udongo dhaifu, unahitajikuchanganywa na changarawe au mbolea kuzingatia viwango maalumu.Vipimo hivi huwa ni tofauti na hulingana na aina ya udongo na miche.

Kuongezea viumbe vya manufaaJamii nyingi za miti huwa na uhusiano spesheli ambao ni wa manufaa katiya mizizi na viumbe maalum viitwavyo rhizobium na mycorrhiza.

Kwa kawaida, uhusiano huu huwa na manufaa kwani husaidia mti kutumiamaji na chakula vizuri, hukinga mizizi kutokana na magonjwa, na husaidiakuchanganya hewa ya nitrojeni kupitia kwa mizizi na hivyo udongo rutuba.

Ukikuza miti kwa mara ya kwanza, kama vile calliandra au leucaena, nimuhimu kuongezea kwenye mizizi viumbe vifaavyo vya aina ya rhizobium.Ukosefu wa viumbe hivi huifanya miti kubadilika rangi na kuwa yamanjano, na hutumia rutuba kwenye udongo bila kuiongezea kamainavyokusudiwa. Kadhalika, huwa inakua pole pole na mara nyingine hufaikihamishwa kutoka kwenye nasari na kupandwa mahala pengine. Njiarahisi ya kuhakikisha kuwepo kwa viumbe wenye manufaa, ni kutumiaudongo kutoka kwenye aina hii ya miti na kuuchanganya na udongounaotumiwa katika bustani. Maafisa wa kilimo wa nyanjani huwa naviumbe hawa na unaweza kuwasiliana nao.

Page 14: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

6

3. Uzalishaji wa mitiMbegu zilizopandwaMbegu ndizo njia kuu ya kujipatia miche

Jinsi ya kupata mbegu

Unaweza kupata mbegu za miti:• Kutoka katika taasisi za utafiti, kama vile vile KEFRI, ICRAF na

FORI, ambapo kuna wataalamu wanaohakikisha mbeguzinazopatikana katika mashirika hayo ni bora na za hali ya juuwakizingatia kanuni za kitaalamu za ukusanyaji, utayarishaji nauchunguzi.• Kwa kujikusanyia kutoka mashambani, misituni ama mahala po

pote penye mbegu za miti unayohitaji. Baadhi ya wakuzaji wamiche ya miti wana ujuzi wa kutambua mbegu za kufaa lakiniwengine hawana.• Kutoka kwa wafanya biashara. La muhimu ni kuepuka kupata

mbegu duni kutoka wafanya biashara walaghai.

Ubora na ukusanyaji wa mbegu

Ubora wa miche utategemea kiwango cha mbegu na pia asili yake.Kadhalika, mbegu hulingana na matumizi ya mmea unaohusika. Kwamfano yaweza kuwa ni miti ya kutengenezea mbao, matunda, malisho yamifugo au dawa.

Ni muhimu kuhakikisha umekusanya mbegu za kutosha na kuziweka alamaiwapo unanuia kuzihifadhi. Mbegu zilizokomaa ndizo humea haraka.Iwapo unakusanya mbegu, unashauriwa kuzitafuta kutoka kwa zaidi yamiti 30 iliyo katika umbali wa mita 100 kati ya mti mmoja na mwingine.Kadhalika, hakikisha kwamba zaidi ya nusu ya mbegu ulizokusanyazimekomaa.

Ukinunua mbegu, unaweza kuchunguza zimetolewa kutoka kwa mitimingapi na wapi. Ili kupata miche ya miti ya hali ya juu, unashauriwakutumia mbegu kutoka katika maeneo tofauti.

Page 15: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

7

Ukinunua mbegu, hakikisha umepata maelezo yafuatayo:• Asili yake• Jina la kawaida na la kisayansi la mimea husika• Tarehe ya kukusanywa• Nambari ya fungu la mbegu hizo• Maeneo na hali ambako zinafaa kupandwa• Asilimia ya kiasi kinachoota kutoka kwa mbegu ambazo

zinapandwa• Usafi• Jinsi ya kuzitayarisha mbegu kabla ya kuzipanda

Kuhifadhi mbegu

Mbegu nyingi zinazotolewa ndani ya matunda zinahitaji kutolewa nakuoshwa vizuri kisha zipandwe mara moja. Mbegu zinaweza kuharibikamatunda yakishambuliwa na vijani vyembamba vinavyoota, hasa mahalikwenye umajimaji. Ndiposa unashauriwa kuhakikisha mbegu hiziunazipanda haraka iwezekanavyo.

Ikiwa mbegu zimefunikwa kwa maganda kama vile maharagwe, ziachezichipue zenyewe mahali penye kivuli kidogo.

Matunda mengine yana sehemu ya nje ngumu na huhitaji kukaushwamahali ambapo hapana jua kali, kisha kupasuliwa taratibu ili kutoa mbegu.Unapozikausha kwa jua, hakikisha haziungui na hivyo basi kuziharibu.

Iwapo baada ya kukusanya mbegu hunuii kuzipanda mara moja,unashauriwa kuzihifadhi vizuri mahali penye hewa ya kutosha. Unawezakuzihifadhi ndani ya gunia, chungu ama kifaa kingine cho chote ambachokitawezesha mbegu kupata hewa ya kutosha na kuzikinga na vijanivyembamba vinavyoota, hasa mahali kwenye umajimaji. Kuna pia mbeguzinazoweza kuhifadhiwa katika friji. Unashauriwa kukagua kila marambegu ulizohifadhi ili kuondoa zinazoharibika na kuhakikisha hazivamiwina wadudu waharibifu.

Muda wa kuhifadhi mbegu hutegemea aina ya mmea. Kuna mbeguzinazoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu, ilhali nyingine hupoteza uwezo

Page 16: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

8

wa kuota zikihifadhiwa kwa muda mrefu. Ukihifadhi mbegu kwa muda,tuseme kama wa mwezi mmoja au zaidi, ni muhimu kuthibitisha ni kiasigani kitaota zikipandwa. Unafaa kufanya majaribio kwa kuchukua kiasicha mbegu na kuzipanda. Zikiota, hesabu idadi ya zilizomea na uilinganishena ya ulizozipanda. Kwa kufanya hivyo, utaweza kujua kwa hakika kiasicha mbegu unachohitaji kupanda. Kwa mfano, mbegu 25 zikiota kati ya100 ulizozipanda, itakubidi upande mbegu nne kwa kila chombo. Jaribiohili litakuokolea muda na rasilmali.

Unaweza pia kupanda mbegu kadhaa za majaribio ili kuthibitishazinachukua muda gani kuchipuka. Kadhalika, jaribio hili litakuwezeshakuamua ni mbinu ipi ya upandaji itafaa.

Kutayarisha mbegu

Utayarishaji wa mbegu kabla hazijapandwa unahusisha:• Kutoa mbegu kutoka kwenye matunda• Kuzikausha• Kuzisafisha• Kuzipakia kulingana na ukubwa au uzito• Kuondoa zile mbovu

Zitoe mbegu kutoka kwenyemaganda yake.

Page 17: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

9

Zioshe mbegu zile ili uondoe uchafuwowote usiotakikana.

Kisha, zikaushe mbegu zile.

Baada ya kukauka,zitenganishe mbegu nzurikutoka kwa zile zilizodhoofika.

Zihifadhi mbegu ndani yamikebe, makaratasi aumagunia. Hakikisha kwambambegu zimehifadhiwa mahalapalipo pakavu na penye giza.

Page 18: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

10

Mbinu za kuandaa mbegu kabla ya kupanda

Maji baridi

Kuna mbegu ambazo unaweza kuzitia katika maji baridi kwa kati ya masaa12 na 48. Kisha, zikaushe mbegu zile kwenye kivuli.

Maji moto

Chemsha maji.

Tia mbegu ndani ya maji yamoto kwa dakika mbili.

Page 19: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

11

Zitoe mbegu kutoka kwenyemaji moto.

Tia mbegu ndani ya chombokingine.

Ongeza maji baridi nakuziacha mbegu ndani kwasiku mbili.

Page 20: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

12

Vifaa vingine

Visu na msasa (sandpaper) hutumiwa kutayarisha mbegu. Hakikisha usiharibusehemu ambako mzizi hutokea. Kata mbegu kidogo kwa kisu, ama uipasuekwa kutumia kijiti, au uikwaruze kwa msasa. Ikiwa mbegu ni ndogo, iwekekaratasi ya kupiga msasa kwenye kuta za ndani za chupa ama kikombe,mwaga mbegu ndani kisha utingishe kwa haraka chombo hicho.

Iweke sandpaper kwenye kutaza ndani za chombo

Tingisa mbegu ndani ya chombochenye sandpaper.

Kata mbegu kwa kisu. Kwaruza mbegu ukitumiasandpaper.

Page 21: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

13

Mbegu zilizodondoka kutoka kwenye mtiKuna baadhi ya miti ambayo hudondoa mbegu. Baadhi ya mbegu hizohuanguka chini na kuchipuka baadaye. Miche (wildlings) inayomea inawezakukusanywa na kuhamishiwa nasari ili kutunzwa ipasavyo. Kadhalika,miche hiyo yaweza kuuzwa au kupandwa inakohitajika pindi ikikusanywa.

Miche hii ambayo kwa kawaida isipotunzwa itaishia kuwa magugu, nimuhimu hasa kwa ukuzaji wa miti ambayo haijulikani ni lini hutoa mbeguama mimea ambayo mbegu zake ni haba. Miche ya miti mingi ya kiasili,kama vile Prunus africana, hupatikana kwa njia hii.

Uzalishaji miche usiotumia mbeguHuu ni uzalishaji wa miche kwa kutumia matawi, mashina ama mizizi yamimea inayohitajika (vegetative propagation). Mbegu hazitumiki katika mbinuhii. Lengo kuu ni kuendeleza uzalishaji wa mimea ya hali ya juu na piainayostahimili hali ngumu, hasa za anga. Kadhalika, ni mbinu muafakaya kusambaza uzuri wa mmea mmoja hadi mwingine. Njia kuu ambazohutumiwa ni kama zifwatazo.

Vitawi (cuttings)

Hivi ni viungo vinavyokatwa kutoka kwenye mizizi, majani ama matawiya mti ili kupandwa na kutupatia mmea mpya. Mifano ya mimeainayokuzwa kwa njia hii ni bouganvillea na gliricidia.

Mfano wa kitawi.

Page 22: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

14

Pandikiza (grafting)

Kwa kutumia mbinu hii, kijitawi cha mtihutiwa katika shina la mti mwingine. Mfanowa miti ambayo huzalishwa kwa njia hii nimaembe na avokado.

Lengo la kupandikiza ni:• Kupunguza muda wa mti

kukomaa (kutoa maua, matundana mbegu);• Kuimarisha hali na kiwango cha

miti inayozalishwa;Mfano wa kipandikiza.

• Kuzalisha miti ambayo si rahisi kuotesha mbegu ama kuikuzakutumia mbinu nyingine;• Kutambua magonjwa ya bakteria; na• Kuipatia uhai mpya miti iliyozeeka kwa kuiunganisha na mmea

mchanga ambao utasaidia kuimarisha hali yake na hivyo basikuongeza manufaa yake.

Kadhalika, chipuko la mmea linaweza kuunganishwa kutoka kwenye mmeawa mti wa jamii moja hadi nyingine (budding), kama vile michungwa namidimu

Kuotesha mizizi katika matawi au shina (layering/marcotting)

Tawi ama shina linaweza kukunjwa na sehemu yake moja kufunikwamchangani na baada ya kuota mizizi linakatwa kutoka kwenye mti asiliaili kuupata mmea mwingine. Kadhalika, kuna mimea mingine yenye shinana matawi magumu na haiwezi kukunjwa kwa urahisi. Unaweza kutumiahomoni, udongo ama vumbi la mbao na kuzirundika kwenye sehemu yatawi ambapo unanuia kuotesha mizizi (marcotting).

Aina nyingine za uoteshaji mizizi kwenye matawi ama mashina ni moundlayering au stooling.

Page 23: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

15

4. Njia za ukuzaji micheKuna njia mbili za kukuza miche:

• Ardhini; na• Ndani ya mifuko

Hata hivyo, kabla hujaamua njia utakayoitumia, ni muhimu kufahamumatumizi ya mti unaohusika na pia mahitaji ya wateja wako

Kuna miti ambayo huota kwa urahisi, kama vile eucalyptus na kei apple.Mimea hii ninaweza kupandwa kutumia njia yo yote kati ya zilizotajwahapo awali.

Iwapo mbegu za mmea unaonuia kuupanda hazipatikani kwa urahisi,zinahitaji utunzaji maalumu na ni ghali, njia muafaka ya kuziotesha nikuzipanda ardhini ili zitunzwe vizuri kabla kuhamishwa na kupandwakwingineko.

Shimo la kupanda mbegu hutegemea saizi ya wa mbegu. Mbegu kubwahuhitaji shimo refu kwenda chini kuliko la mbegu ndogo.

Kukuza miche kwenye ardhi tupuNjia hii huonekana kuwa rahisi kwa kukuza miche kuliko nyingine zote.Huhitaji kiasi kidogo cha udongo na miche husafirishwa kwa urahisi. Hatahivyo, mbinu hii ina matatizo mengi, hasa yanayohusiana na rutuba nautunzaji. Udongo ukitumika kwa miaka mingi kukuzia miche, rutuba yakehupungua na kusababisha kuzorota kwa mimea inayopandwa. Kadhalika,miche iking’olewa, isafirishwe na kupandwa mahala pengine, mizizihuharibiwa na huenda ikasababisha mche kufa.

Ili kuitunza ardhi tupu inayotumika kila mara, unashauriwa kupanda michechini ya 200 katika kila eneo la mita moja mraba ili hupunguzamng’ang’anio wa rasilmali kama vile maji, mwangaza na chakula kati yamiche.

Kadhalika, unaweza kutumia mbolea au fatalaiza katika kila msimu ili

Page 24: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

16

kuongeza rutuba. Unaweza kupanda miche kwa msimu mmoja, kishakuiacha bustani wazi katika msimu unaofuata ili kuupatia udongo nafasiya kurejesha rutuba. Baada ya kung’oa miche, itumbukize ndani ya utopewa udongo, kisha ifunge kwa karatasi au gazeti lenye majimaji. Wakati wausafirishaji, iweke kwenye kivuli na uikinge na upepo

Ni muhimu kuipanda miche mara moja baada ya kuing’oa. Chimba shimorefu kwenda chini na uhakikishe mizizi imenyooka vizuri kuelekea chini.Bustani za miche zikiwa mashambani huwa hazihitaji rasilmali nyingi.

Kukuza miche kwenye ardhi tupu.

Faida za miche ambayo imekuza ardhini:• Mtu mmoja anaweza kubeba maelfu ya miche kuelekea

shambani• Gharama ndogo ikilinganishwa na ya upandaji wa miche

kwenye mifuko; na• Shimo la kupanda huwa mdogo likilinganishwa na la mche ulio

ndani ya mfuko

Hasara za miche ambayo imekuza ardhi:• Upungufu wa chakula kwenye udongo• Miche hukua polepole baada ya kupandwa shambani• Miche mingi hufa baada ya kupandwa shambani• Huwa na mng’ang’anio wa mwangaza, chakula na maji miche

ikiwa chini ya kivuli cha miti

Page 25: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

17

Kukuza miche ndani ya mifuko na mikebeMifuko ya plastiki ndiyo itumiwayo sana kukuzia miche katika nchizinazoendelea. Huwa ina mashimo upande wa chini kwa ajili ya kupitishiamaji yakiwa mengi ndani ya udongo na pia kuwezesha mizizi kupumua.Ikiwa mfuko huna mashimo, unaweza kuyatoboa wewe mwenyewe. Mifukohii hupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Huwa kuna hatari ya mizizi kwenda kombo ikifika mwisho wa mfuko nakuanza kuingia ardhini. Miche ikisafirishwa, mizizi ya mimea kama hiyohuharibiwa.

Hali ya mche uliopandwa ndani ya mfuko hutegemea hali ya udongo,wala sio ukubwa wa mfuko. Udongo ukiwa wa hali ya juu, ni vyema kutumiamifuko midogo, ukiwa wa hali ya chini, utahitaji mifuko mikubwa. Utunzajibora wa bustani la miche hufanikishwa kwa kutumia udongo wenye rutuba.Udongo unaweza kuimarishwa kwa kutumia mbolea ama fatalaiza.

Utumiaji wa mifuko midogo humsaidia mwenye bustani ama mkulimakwa sababu:

• Unahitaji kiasi kidogo cha udongo.• Hurahisisha ubebaji na usafirishaji.

Anayepanda miche anaweza pia kutumia vifaa vya plastiki vilivyotumikavya mafuta ya kupikia ya Kimbo ama Kasuku, na pia pakiti za maziwa.La muhimu zaidi kuzingatwa ni urefu wa chombo, wala si upana wake.

Page 26: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

18

Mkebe Pakiti ya maziwa

Mfuko wa nailoni Chungu cha plastiki

Page 27: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

19

5. Ulezi bora wa micheChochote kichanga kinahitaji malezi bora ili kukua vizuri na kustahimiliugumu wa kimazingira. Miche yenye afya na iliyotunzwa vyema hutegemeauadilifu wa mtunza nasari, na pia utendaji wake wa kazi. Yafuatayo nimuhimu kwa ukuzaji wa miche:

Kuhamisha micheKuhamisha miche kutoka mahali ambapo imeoteshwa na kuipanda kwenyechombo au mahali kunaweza kuiharibu mizizi. Kuna kanuni zinazofaakuzingatiwa unapoung’oa mche, hasa kwenye bustani ambapo kuna idadikubwa ya miche, ili kupunguza kuharibiwa kwa mimea mingi. Nazo ni:

• Unashauriwa kuitupilia mbali miche dhaifu na iliyovamiwa namagonjwa ya mimea.• Hamisha mche mara tu baada ya mzizi wa kwanza kutokeza au

mche ukiwa bado mdogo (kipimo cha chini ya sentimita tano).• Inyunyuzie miche maji usiku unaotangulia siku unayopanga

kuiong’oa na uhakikishe maji yamepenya kabisa kwenye udongo.• Hakikisha umetayarisha mahali pa kuipanda kabla hujaing’oa.

Iweka miche uliyoing’oa mahala penye kivuli.• Inyunyuzie miche maji tena saa moja kabla hujaing’oa na masaa

baada ya kung’olewa.• Wakati wa kiangazi, unashauriwa kuing’oa miche nyakati za

asubuhi ama jioni.• Weka miche ndani ya maji unapoing’oa kwenye kitalu.

Tumia kijiti au ama chombo cha kuchoteamchanga ili kuulegeza udongo uliokandokando ya miche.

Page 28: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

20

Lijaze shimo udongo ukianzia chini,kisha uupatie mche maji.

Toa miche kutoka kwenyeudongo kwa kushika matawiya kwanza au ya chini –usishike shina.

Tengeneza mashimo ya kupandaukitumia kijiti na uhakikishe yanaupana na urefu tosha wa kwendachini.

Iunganishe mizizi yote na kuhakikishaimenyooka kuelekea chini unapoipanda.

Page 29: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

21

Njia zisizofaa ambazo hutumiwa mara kwa mara kung’oa miche ni:• Kungoja mpaka miche iwe mikubwa na kuwa na mizizi mirefu.• Kung’oa miche kutoka kwenye udongo mkavu na baadaye

kuinyunyizia maji.• Kutengeneza kivuli baada ya kung’oa miche.• Kung’oa miche wakati wa kiangazi ama jua likiwa kali.• Kung’oa na kupanda miche ambayo imeharibika.• Kung’oa mche ukiwa umelishika shina, hali ambayo yaweza

kuuharibu mche.• Kubeba miche mkononi au kwa chombo bila maji.• Kutengeneza shimo kwa kutumia kidole – shimo huwa ndogo

sana.• Mizizi kujikunja na kuelekea juu badala ya kuinyoosha ielekee

chini ikiwa shimoni.• Kuacha mifuko ya hewa karibu na mizizi baada ya kupanda kwa

sababu ya kutoushindili na kuutandaza udongo vizuri. Hali hiihuifanya miche kunyauka na hatimaye kufa.

Kunyunyiza majiKuwepo kwa maji ni muhimu kwa ukuzaji wa mimea bora. Asilimia 90 yamche huwa ni maji. Miti inapopandwa ndani ya vyombo, huwa na udongokidogo. Kadhalika huwa haina uwezo wa kupeleka au kupenyeza mizizichini ya ardhi kutafuta maji. Kiwango cha maji yanayonyunyuziwa mchehutegemea na umri wa mche, hali ya anga na aina ya udongo.

Maji ya kutosha na ya kutegemewa ni muhimu kwa bustani la miche. Majiyenye chumvi nyingi, madini, mafuta ama yaliyochafuliwa na dawa mbalimbali zinazotumiwa shambani, yanafaa kuepukwa.

Wasaa wa kunyunyuzia miche maji

Utunzaji bora wa bustani la miche unahusu kuangalia hali ya maji katikamajani ili ujue ni wakati gani utanyunyuza maji. Majani ni lazima yaweimara. Unafaa kuitunza vyema mimea na kuhakikisha inapata maji yakutosha kila udongo ukikauka kidogo.

Page 30: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

22

Nyunyiza maji asubuhi ama jioni wakati kiwango cha joto kimepungua namiale ya jua si mikali. Jua likiwa kali, mimea hupoteza maji mengi kupitiakwa majani kuliko inavyopata kwa kunyunyuziwa. Mimea inayopotezamaji mengi hukua kwa shida. Matone ya maji kwenye majani jua likiwakali yaweza kuharibu majani.

Udongo wa aina ya changarawe hupoteza maji haraka kuliko udongo wakawaida na kwa hivyo huhitaji maji mara kwa mara. Hata hivyo, udongoulio na mfinyanzi mwingi wakati unapokauka, huwa mgumu na hupasuka.Hii inaweza kukata mizizi kufanya mmea kukua pole pole au kufa.

Bustani ikiwa mahali penye jua ama kuanzishwa wakati wa kiangazi,itakuwa ikihitaji maji mengi. Vile vile, ikiwa kwenye kivuli, itahitaji kiasikidogo cha maji. Usiweke mimea kwenye kivuli kwa muda mrefu ili uokoemaji. Ni vyema kubadilisha kivuli mara kwa mara ili kuiimarisha hali yamimea.

Maji yakizidi an kupungua sana, mmea huharibika. Ili mimea iwe mizuri,maji na hewa katika mizizi ziwe za kiwango kifaacho. Maji yakiwa mengikwenye huinyima mizizi uwezo wa kupumua. Kadhalika, hufanya shinakuoza na kuleta wadudu waharibifu kwenye udongo.

Jinsi ya kunyunyiza maji

Ili kutunza vyema bustani ya miche, inafaa kuhakikisha kila sehemu yaudongo imepata maji.

Kuna njia nyingi za kunyunyuzia mimea maji, kama vile kutumia paipukutoka kwenye mfereji ama kutumia chombo cha kuchote maji. Njia hizombili ni nafuu ingawa hazifai kwa mimea ya aina zote. Ni kawaidaunaponyunyuza maji, baadhi ya mimea inapata maji ya kutosha na minginekiasi kidogo. Kwa mfano, mimea iliyo kwenye mistari ya mwisho ama kandokando haipati maji ya kutosha ikilinganishwa na iliyo katikati. Ni jukumula kila mtunza bustani la miche kuhahakikisha kwamba kila mmea umepatamaji ya kutosha.

Mimea inahitaji kunyunyuziwa maji taratibu na kwa njia inayohakikishayamepenya kwenye mizizi, wala sio kwa njia ambayo itazifukua mbegu

Page 31: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

23

ama kuing’oa mimea kutoka udongoni.

Mfereji wenye kifaa cha kunyunyiza maji kinachozunguka (sprayer nozzle)ni kifaa bora kwa mimea yako, kwani hakipotezi maji, ni rahisi kukitumiana hutoa maji kulingana na mahitaji yako.

Ni muhimu kunyunyuzia miche maji safi. Kiwango cha maji kinachohitajikakwa miche hutegemea umri wake. Kwa utunzaji bora wa bustani ya micheunahitaji:

• Kuangalia hali ya maji katika miche kila wakati ili ujue ni liniutanyunyuza maji

• Kunyunyiza maji asubuhi au jioni• Kunyunyiza maji ya kutosha katika udongo wala si kwenye

majani• Kunyunyiza maji taratibu na kuhakikisha yameingia ndani ya

udongo hadi chini ya mizizi• Kutumia mfereji wenye kifaa cha kunyunyizia maji

kinachozunguka ukiwa na uwezo• Kupunguza maji unayonyunyuzia miche kwa muda wa kama

wiki nne kabla ya kuihamisha na kuipanda, kwa mfano,shambani

• Kunyunyiza maji vizuri siku moja kabla ya kuisafirisha miche nakuipanda mahali pengine

• Kufunika miche kwa karatasi ya nailoni unapoisafirisha iliuikinge isikauke

Vyombo vya kunyunyiza maji.

Page 32: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

24

Mbinu zisizofaa za kutunza bustani za miche na zinazotumika sana ni:• Kunyunyiza maji kulingana na ratiba iliyowekwa hata kama

udongo una maji ya kutosha• Kunyunyizia majani maji badala ya udongo• Kunyunyiza maji wakati wa mchana• Kunyunyiza maji maji haraka haraka na kuyanyima nafasi ya

kuingia ndani ya udongo• Kutumia kidole gumba kuzuia maji ya mfereji yasitoke mengi

unaponyunyizia miche

KivuliMiche katika bustani hukingwa kutokana na mazingira mabaya hadi ipateuwezo wa kukabiliana nayo. Kivuli ni mbinu kukinga miti kutokana nahali hii kwani:

• Huzuia maji kupotea kutoka kwenye udongo• Hupunguza kasi ya maji kupotea kupitia kwa matawi• Hupunguza kiasi cha joto katika mti na udongo• Kiasi cha kivuli hupunguzwa kulingana na umri wa miche

Nyunyuza maji kwenye udongo na wala si kwenye majani.

Page 33: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

25

Kubadilisha kivuli

Mimea mingi inapoota huhitaji kivuli cha kati ya asilimia 40 na 50, ingawakuna baadhi yake ambayo huhitaji kivuli zaidi ama hata kidogo kulikokiwango hiki. Kivuli hupunguzwa kulingana na vile miche inavyokua.

Miezi miwili kabla miche haijahamishwa na kupandwa nyanjani, kivulihuondolewa kabisa au miche inahamishiwa mahali penye jua bila kivulichochote.

Utunzaji bora wa bustani ya miche unahusu kushughulikia kiwango chakivuli pamoja na kiasi cha maji. Miche inayokua kwenye kivuli kingi huhitajimaji kidogo kuliko iliyo penye jua. Ni jambo la kawaida, ingawa halifai,kuacha miche kwenye kivuli kwa wakati wote miche ikiwa nasari.

Mimea inayopandwa kwenye kivuli kingi:• Hukua pole pole, au ikiwa mirefu na dhaifu yenye shina

jembamba• Hupata magonjwa na hushambuliwa na wadudu kwa urahisi• Huharibiwa na jua kwa urahisi ikitolewa nasari na kupandwa

nyanjani• Matawi hupoteza rangi yake ya kijani kibichi

Aina za kivuli

Miti

Miti inapendelewa na wengi kwa vile ni nafuu na rahisi kutunza. Ingawahutoa mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watunzaji wa nasari, maranyingi huwa inapatia bustani kivuli kingi. Inafaa uhakikishe kuwa kivulicha miti hakifuniki bustani yote na kuzuia miche kupata mwangaza wowote mchana kutwa.

Neti (shade cloth)

Hupatikana kwa gredi tofauti na huzuia kati ya asilimia 30 na 95 yamwangaza kupenya. Miche ikiwa michanga huhitaji kivuli kingi cha katiya asilimia 60 na 80 ikilinganishwa na iliyokomaa, ambayo kwa kawaidahuhitaji kivuli cha kati ya asilimia 30 na 40. Neti itumiwayo kutoa kivulikwa kawaida huzuia nusu ya joto la jua kupenya.

Page 34: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

26

c) Nyasi

Nyasi kavu hutumika sana. Unapaswa kuepuka kutumia nyasi ambazobado hazijakauka kwa sababu huweza kuleta magojwa na waduduwaharibifu.

Unaweza kutumia pia majani na matawi ya mianzi (bamboo).

Mti.

Neti.

Page 35: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

27

Urefu wa kivuli

Urefu kati ya kivuli na mimea inayokingwa kutokana na miale ya jua nimuhimu kwa ukuaji bora wa miche. Kivuli kikiwa karibu hudhoofishamiche na kutatiza shughuli muhimu za wafanya kazi kufanya kazi kamavile kupalilia au kunyunyizia maji. Urefu wa kati ya mita moja na mbilibaina ya kivuli na miche au nasari unafaa.

Kupunguza miziziLengo huwa ni kuzuia mizizi isienee ardhini miche ikiwa bado ndani yamifuko. Tendo hili:

• Huzuia miche kupata mizizi ya kati iliyo thabiti kabla yakuhamishiwa njanjani:

• Hupunguza tatizo la kuondoa miche kutoka nasari na piamadhara yawezayo kutokea ikipelekwa kupandwa; na

• Huwezesha miche au miti michanga kuwa na mizizi ya kutoshana thabiti

Kuna njia tofauti za kupunguza mizizi:• Kukata mizizi ambayo imejitokezea nje ya mfuko kwa makasi au

kisu;• Kuinua-inua mifuko kila wakati (baada ya wiki mbili); na• Kuweka miche juu ya kitanda kilichoinuka.

Nyasi.

Page 36: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

28

KupaliliaKwekwe hudhoofisha nasari kuifanya isiridhishe wala kupendeza, huletamng’ang’anio wa maji, mwanga na chakula kati ya magugu hayo na miche,huwa makazi ya wadudu waharibifu na viyoga (fungi), virusi, bakteria naviini vinginevyo viletavyo magonjwa. Kwekwe zikirefuka na kukomaa huwangumu kung’olewa. Kadhalika, huharibu mizizi ya miche na hata mmeawote. Bustani inapaswa kupaliliwa kwekwe zikiwa bado changa.

Kuifanya mimea kuwa thabiti na kuisafirishaIli kuifanya mimea iwe thabiti na kuizoesha kwa taratibu hali halisi yanyanjani, kiwango cha kivuli na kiasi cha maji hupunguzwa kwa muda wakama wiki nne kabla ya miche kuhamishwa. Wakati huu, unawezakunyunyizia miche maji kila siku ya pili. Kwa kufanya hivi, huwaunaitayarisha mimea kukabiliana na hali mpya nyanjani na labda tofautiambapo yawezekana kuwa maji na kivuli hazitoshi. Hakikisha micheinapata maji vizuri siku inayotangulia wakati wa kuing’oa. Hii huepushiamiche kupoteza maji wakati inaposafirishwa, na hasa joto likiwa jingi,uharibifu unaotokana na upepo, au vitu vingine. Kama miche inasafirishwakwa gari lililo wazi, unafaa kuikinga kwa kuifunika kwa karatasi ya nailoni.

Jinsi ya kuifunika miche wakati inaposafirishwa.

Page 37: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

29

6. Wadudu na magonjwa michekwenye bustanoUsafi wa bustani ya micheLengo la kila mwenye bustani ya miche ni kuwa na miti bora na yenyeafya nzuri. Kutunza bustani za miche na kudumisha usafi hakuna maanakutumia dawa za sumu au ghali za kumaliza magugu na kuua waduduwaharibifu. La muhimu ni kutumia kemikali kwa njia ambayo haitakudhuruwewe au mazingira, na wakati huo huo kuimarisha usafi.

Kuna mbinu mbili za kimsingi zinazotumiwa kutunza bustani za michekiafya. Mbinu hizi zimefafanuluwa hapa chini.

Kuzuia

Mambo muhimu katika mbinu hii ni utumiaji mzuri wa mbolea, upandajimiti inayokabiliana na magonjwa, kuifanya miche kuwa migumu kwawakati unaofaa, kudumisha usafi wa bustani ya miche, na kuwafunzawafanya kazi kuhusu umuhimu wa usafi.

Kuondolea mbali na kuponya

Utumiaji wa kemikali, joto, kukata na kutupa sehemu ya mti au kuung’oana kuutoa kwenye nasari mmea uliovamiwa na maradhi.

Mbinu hizi mbili za kimsingi zinaweza kutumiwa pamoja kukabiliana namagonjwa na wadudu waharibifu kwa njia ambayo haidhuru mazao walakuathiri mazingira.

Madhara yatokanayo na hali za kimaumbile, kama vile:• Joto au baridi• Kiangazi au maji kwenye udongo kuwa mengi kupindukia

Madhara yaweza kusababishwa pia na:• Virusi• Kwekwe• Tete au nematoda, kwa mfano minyoo mviringo

Page 38: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

30

Usafi wa vyombo vinavyotumiwa kwenye bustani ya michena mahali pa kufanyia kazi ni muhimu.

• Wadudu• Viyoga• Ndege na wanyama

Kuepushia miche madhara katika bustaniMagonjwa huingia kwenye bustani za miche kupitia:

• Vyombo, visu, makasi, mahali pa kufanyia kazi, na vinginevyo• Magugu na wadudu• Udongo• Maji• Kinachopandwa kama vile mbegu, sehemu za mti

zinazopandwa, kwa mfano vitawi• Mavazi ya wageni na wafanya kazi

Magugu na wadudu

Ondoa magugu kutoka kwenye bustani ya miche kwa sababu baadhi yakehuwa makao ya wadudu au vijidudu ambavyo huleta magonjwa kwa miche

Ili uzuie mchwa kuharibu miti, vipake vigingi mafuta. Ilinde miche kotokanana wadudu wanaosababisha au kueneza magonjwa.

Page 39: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

31

Udongo

Magonjwa yanaweza kuenezwa kwenye bustani kupitia kwa udongo.Bustani ambapo mbegu hupandwa ardhini, wala si katika karatasi, huwana wadudu na bakteria nyingi zinazosababisha magonjwa, hasa wakatiudongo huo umetumika kwa muda mrefu bila kubadilishwa. Ni vizurikuhamisha bustani ya miche kila mara kutoka eneo moja kwenda jingineau kutumia udongo mpya.

Zifuatazo ni baadhi ya mbinu ambazo hutumika kuua viini katika udongo:

Utumiaji wa kemikali au dawa za viyoga (fungicide)

Nyunyizia dawa kwenye nasariukifuata maelezo uliyopewa. Mfano wadawa hizi ni Basamid.

Changanya udongo na dawa vyema.

Page 40: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

32

Nyunyizia maji kwenye udongompaka yapenye kabisa.

Funika nasari ukitumia karatasi yanailoni.

Hakikisha karatasihaitapeperushwa na upepo.

Page 41: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

33

Miale ya jua na mvuke

Njia ya pili ni kutegemeamiale ya jua wakati wakiangazi kabla msimu wamvua haujaanza.

Nyunyizia udongo maji yakutosha.

Funika nasari ukitumiakaratasi ya plastiki.

Udongo utakuwa tayarikutumiwa baada ya wikimoja.

Njia ya tatu ni ya kuchoma majani namatawi juu ya nasari.

Moto huu utaua bakteria na magonjwayaliyo kwenye udongo.

Kuchoma majani na matawi

Maji ya kunyunyizia

Maji ya kunyunyizia mimea kwa kawaida hutoka kwenye bwawa, kisimaau tangi lenye maji ya mvua. Maji haya ambayo huwa yametulia hutoanafasi ya viyoga kukua na kuzaana. Kwa mfano, Pythium na Phytophthoraambavyo husababisha ugonjwa wa miche kunyauka na kufa ghafla. Njiarahisi ya kukabiliana na tatizo hili ni kutia kiasi kidogo cha Jik katika majihayo. Kifuniko kimoja cha chupa ya Jik kinatosha kila mtungi wa maji yalita 20. Yaache kwa dakika 30 ili kuangamiza viyoga hatari.

Page 42: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

34

Mimea inayopandwa

Vipandikizi na vitawi (scions, rootstocks na cuttings) vinaweza kuwa makao yawadudu au magonjwa kwenye bustani la miche. Sehemu hizi ni lazimaziwe thabiti ili kuepuka magonjwa.

Miti yenye magonjwa kwenye bustani inafaa kuondolewa na kuchomwabadala ya kutengenezwa mbolea. Utumiaji wa miti au mabaki ya mitiyenye magonjwa kutengeneza mbolea unakubalika tu iwapo kiwango chajoto cha mbolea hiyo kitakuwa zaidi ya digrii 60 sentigredi kwa siku kadhaaili iiangamize hayo magonjwa.

Mavazi

Mara nyingi magonjwa huingizwa na kuenezwa kwenye bustani bila kujuakupitia kwa viatu au mavazi. Ili kukabiliana na tatizo hili, ye yote anayeingiakwenye bustani ya miche anahitaji mavazi na viatu maalumu. Kadhalika,kijidimbwi chenye maji yaliyotiwa Jik katika kiingilio ili yeyote anapoingiakwa bustani aogeshe viatu, kinaweza kuzuia uingizaji wa viini vya magonjwakwenye bustani.

Tia kifuniko kimoja cha Jik kwenye lita 20 za maji.

Page 43: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

35

Jinsi ya kuzuia magonjwa katika bustani la micheHali ya afya ya mmea

Mimea ambayo ina afya nzuri, mbolea na maji ya kutosha huwezakukabiliana na viumbe waharibifu. Hata hivyo, epuka uwekaji wa mboleanyingi, hasa nitrogeni, ambayo hulemaza mimea na kuifanya kuvutiawadudu wafyonzao ‘maji’ kutoka kwa mmea, kama vile aphids na psylids

Idadi ya mimea

Jiepushe kupanda mbegu nyingi pamoja au kutoacha nafasi ya kutoshakati ya miche kwenye vitalu vya bustani. Magonjwa huenea haraka katikahali hii na miche huwa minyonge na mirefu na huwa rahisi kupatwa namagonjwa.

Dipu leyenye Jik katika kiingilio cha bustani.

Miche mingi zaidi.

Page 44: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

36

Miche michache zaidi.

Miche katika kiwango cha kadri.

Kuufanya mche kuwa mgumu

Kuufanya mche kuwa mgumu kwa wakati mzuri huupatia nguvu na afyanzuri. Miche hii inaweza kukabili ushambulizi wa wadudu waharibifu namagonjwa. Pia, inaweza kustahimili hali duni ya hewa.

Miti inayokabiliana na magonjwa au wadudu waharibifu

Ikiwezekana, panda miti ambayo haishambuliwi na magonjwa au wadudu.Kwa mfano, matunda ya jamii ya machungwa na malimau yasipandwepenye aphids wengi kwani huwa wanasababisha ugonjwa wa citrus greeningambao ni vigumu kutibu.

Usafi wakati wa kuunganisha sehemu za mti

Unapotafuta sehemu za mti utakazotumia, unafaa kuwa mwangalifu nakutoa kiungo cha mti ulio na afya na chakula cha kutosha. Kisu na makasini lazima viwe safi ili kuepuka kueneza magonjwa. Baada ya kuunganishammea mmoja na mwinginne, vioshe vifaa unavyotumia kabla ya kuendeleana mche wa pili.

Page 45: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

37

Kuzuia na kuangamiza wadudu waharibifu namagonjwaMatatizo ya magonjwa na wadudu waharibifu katika nasari mara nyingihuletwa na utunzaji duni kama vile:

• Kutonyunyizia maji au kukosa kabisa kunyunyizia maji;• Kutumia mbegu zenye magonjwa, wadudu na vifaa chafu;• Nasari kuwa mahali pabaya au penye mazingira mabaya;• Miche kukosa lishe inayofaa;• Ukosefu, utengenezaji na utumiaji mbaya wa mbolea; na• Kutopalilia.

Hatua zifuatazo ni muhimu kwa uzuiaji:• Tumia mbegu na vifaa safi;• Tumia mbolea;• Zungushia nasari miti ambayo itafukuza wadudu;• Panda aina tofauti za miti/miche;• Punguza upepo mkali kwa kupanda miti kulizunguka eneo la

nasari;• Palilia vizuri;• nyunyizia miche maji ya kutosha na kikamilifu;• Ondoa na uangamize miche migonjwa; na• Uzingatie usafi wa nasari na vyombo vinavyotumika.

Ugonjwa hatari kwa nasari wa dumping off huletwa na viyoga. Husababishambegu kuoza kabla hazijaota, kuoza kwa mizizi na mche kufa ghafla.Kuzuia ugonjwa huu unafaa:

• Kubadilisha udongo au mchanganyiko wake baada ya mudafulani;• Kutonyunyizia maji kupita kiasi;• Kuondoa na kutupa miche ambayo imepatwa na ugonjwa;• Kuwa na hewa ya kutosha;• Mchanganyiko wa udongo uweze kupitisha maji;• Miche isikaribiane sana ili iweze kupaliliwa; na• Kupunguza kiwango cha nitrojeni katika mchanga kwa

kupunguza kiwango cha mbolea

Page 46: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

38

7. Upandaji wa miche shambaniMiti hupandwa katika misimu ya mvua. Yatayarishe mashimo kabla yamsimu wa mvua kuanza. Ili upate miti inayokua haraka na ya kupendeza,lazima shimo liwe na upana na urefu wa kutosha. Unapochimba shimo,usichanganye udongo wa juu wenye rutuba na ule wa chini usio na rutubaau wenye rutuba kidogo. Kisha changanya udongo wa juu na mboleaiwapo huridhishwi na kiwango cha rutuba. Mchanganyiko huu ndioutakuwa wa kwanza kuwekwa kwenye shimo wakati wa kupanda mche ilimizizi iwe na chakula cha kutosha. Kumbuka, shimo la kupanda mti sikama lile la kupanda maharagwe au sukumawiki.

Vile vile, kumbuka kuwa kila mti una mahala ambapo kukua vizuri; mingineinahitaji kupandwa eneo la juu, chini ama penye maji mengi. Somamashauri ya mti huo, uliza mtaalamu, au thibitisha ya kwamba mti huounakuzwa kwenye mazingira hayo.

Iwapo mahali pa kupanda haparidhishi, changanya udongo na mbolea.

Kuweka mche shimoni:• Kutegemea kiwango cha mche, kwanza, weka udongo au ule

mchanganyiko wenye rotuba ujaze nusu au, thuluthi mbili zashimo;

• Kama mche umo ndani ya mfuko, bandua karatasi/mfuko kwauangalifu;

• Uweke mche shimoni na ujaze udongo mpaka kwenye kiwangoambapo mmea ulikuwa umefunikwa na udongo wa nasari

• Baada ya kupanda, tengeneza kizuia maji ukitumia udongoulioinuka kulizunguka shina ili mizizi iwe na maji kwa mudamrefu.

Page 47: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

39

8. SokoKuanzisha na kutunza bustani ya miche ni kazi inayohitaji uangalifumkubwa, kwani mimea inayokuzwa mwishowe husaidia katika kutunzamazingira na pia kuwaletea wahusika. Nasari ndipo mahali pa kuzalishana kukuza miti kulingana na mahitaji yako. Ni muhimu kwa mwenyebustani kujitayarisha kikamilifu kabla ya kuanzisha nasari.

Kuna mambo kadhaa ya muhimu yanayohitaji kuzingatiwa na mwenyenasari ili aweze kujinufaisha, kuimarisha mazingira na uchumi wa nchi.Mwenye nasari ni lazima aelewe vyema ni aina gani ya miche inahitajikakatika eneo lake; na mahitaji ya wateja wake.

Katika nasari za kibiashara, ni muhimu mwenye nasari kuwa na habari zamabadiliko ya soko la miche, na kuweza kujibu maswali yafuatayo:

• Ni miche ya aina gani inayohitajika?• Ni kiasi kipi cha miche kinachohitajika? Rekodi za misimu

iliyopita zitasaidia kuyatayarisha mahitaji yote ya miche kwamsimu ujao.• Wateja watatoka wapi?• Wateja hawa watahitaji miche lini, na kiasi gani?

Ikiwa miche ni ya matumizi ya nyumbani, panda mimea inayotoshelezamahitaji yako. Iwapo miche itabakia kwenye nasari baada ya mahitaji yakokutoshelezwa, iuze ya ziada ama uwagawie majirani na watu wengine.

Ni vyema kuwa na habari kamili kuhusu aina tofauti za miti inayowezakupandwa, ile ambayo mbegu zake hazinapatikana kwa urahisi lakinizinahitajika sana. Maelezo haya yatakuwezesha kupanga, kuvuna aukuagiza mbegu zinazohitajika ili zipandwe wakati ufaao. Kwa mfano, mitiinayotumika kulisha ng’ombe kama vile calliandra, leucaena na mforsadi (mul-berry) na ile itumikayo kuzungusha nyua za nyumba, kwa mfano kai appleinahitajika kwa kiasi kingi kwa wakati mmoja. Kwa hivyo ni lazima mpangomwafaka uwepo kutafuta mbegu kwa wingi kwa vile hununuliwa kwa wingina mteja mmoja.

Page 48: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

40

9. Hitimisho: mambo muhimu yakuzingatia

RekodiUnahitaji rekodi kukuwezesha:

• Kujua ni miti ya aina gani inayohitajika zaidi katika soko na lini.Ukiwa na rekodi, utajua ni miti gani itakayokuletea pato nzuri.Kadhalika, unaweza kupanda miti kulingana na mahitaji yawateja wako.• Kutambua kiasi kinachohitajika katika nyakati tofauti na kwa bei

gani. Itakubidi uwe ukiweka rekodi ya miche yote uuzayo.• Kupanga jinsi ya kuitunza miche, muda ambao inachukua

katika nasari, gharama za kuikuza na pato unalotarajia. Nimuhimu kulinganisha gharama zako za ukuzaji na zile zawenzako.• Kuamua ni bei gani itakayokupatia faida ya haja.• Kuwafahamu wateja wako, wanakotoka na kinachowavutia

katika nasari yako ama huduma unayowapatia.• Kujua ni wapi pengine ambapo wateja hununua miche.

Kuwahudumia wateja• Unashauriwa usiwakasirishe wateja. Kadhalika, hakikisha

kwamba unapawatia miche bora na iwapo huna, unawatafutiakutoka kwa wakuzaji wenzako. Huduma bora itawafanya watejawawe na imani nawe na kukuhakikishia pato la kudumu.• Timiza matakwa ya wateja

Wenzako wanakuza nini?Tembelea nasari nyingine ili kujifunza na kupata maarifa zaidi kuhusushughuli hii.

Page 49: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

41

Kutangaza nasari• Ni muhimukutumia kila mbinu kutangaza nasari yako na aina

ya miti unayokuza. Unaweza kuweka maelezo hayo kwenyemabango karibu na nasari ama hata kuchapisha karatasi zakuwapatia wateja.• Unaweza pia kujaribu kutumia mbinu tofauti za kuuza miche,

kama vile kuipeleka sokoni ama kuiweka kando ya njia mahalaambapo wapitaji wataiona kwa urahisi

Kupakia micheHakikisha unawapakia wateja miche kwa njia inayoridhisha na kupendeza.

Kupatia wateja sampuli za bureKila ukipata miti mipya, ni muhimu kuitangaza kwa wateja wako kwakuwapatia mimea miwili ama mitatu ya bure wakaifanyie majaribio.Kadhalika, unaweza kuwapasha kila mara habari muhimu kuhusu mimeamipya unayopata, kama vile matumizi na utunzaji wake.

Kushirikiana na wenzakoMuungano na ushirikiano wa wenye nasari husaidia kupashana habari nakubadilishana mawazo katika nyanja hii. Kadhalika, wakuzaji michewanaweza kushirikiana kuinua kiwango cha huduma kwa wateja wao.

Page 50: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

42

WasahihishajiWataalamu kadhaa walifanya mkutano ili mwongozo huu uwsahihishwena uimarishwe, shukurani kwao. Nao ni:

Charles Kamure, Nursery ownerP.O. Box 1067, Kikuyu

D. N. Magichu, Nursery ownerP.O. Box 5, Limuru

Francis Muiruri Ngugi, Development AgentP.O. Box 5, LimuruTel: +254 66 71457E-mail: [email protected]

James Mugo, ArtistP.O. Box 295, KikuyuTel +254 733 940214E-mail: [email protected]

Joseph Kihanya Mwaura, Nursery ownerP.O. Box 222 Kiambu

Josphat Ndoria Njuraita, Extension ServicesP.O. Box 104, LimuruTel +254 66 71070/ 71158/71533 Fax +254 66 71335E-mail: [email protected]

Kaigua Peter Ngatho, Nursery ownerP.O. Box 5, LimuruTel +254 66 71457

Page 51: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

43

Kimunya Mugo, Facilitator/EditorAssistant Information OfficerRegional Land Management UnitP.O. Box 63403, Nairobi 00619Tel +254 20 524419 Fax +254 20 524401E-mail: [email protected]

Salome W. Angaine, Extension ServicesP.O. Box 30513, NairobiTel +254 733 823045

Titus Kasamba Ndunda, Extension ServicesP.O. Box 74414, NairobiTel +254 20 512833 Fax +254 20 512501E-mail: [email protected]

Wainainah Kiganya, EditorP.O. Box 3315 , Nairobi 00506Tel +254 722 833631/ +254 20 32088441 Fax +254 20 213946E-mail: [email protected]

Page 52: Nasari za miche - World Agroforestry Centreold.worldagroforestry.org/downloads/Publications/PDFS/le...katika msimu wa mvua. Umuhimu wa nasari za miche • Nasari huinua hali ya maisha

The Swedish International Development Cooperation Agency (Sida) has supported rural development programmes in eastern Africa since the 1960s. Through its Regional Land Management Unit (RELMA), Sida promotes initiatives to strengthen small-scale land users in

order to enhance food security and reduce poverty.

RELMA, the successor of Regional Soil Conservation Unit (RSCU), is based in Nairobi and operates mainly in six eastern and southern African countries: Eritrea, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Uganda and Zambia. RELMA’s goal in the region is to improve livelihoods of small-scale land users and

enhance food security for all households. In pursuit of this goal, RELMA promotes environmentally sustainable, socially and economically viable farming and marketing systems, and supports policies that favour small-scale land users.

RELMA organizes, on a regional level, training courses, workshops and study tours. It also gives technical advice, facilitates exchange of expertise and produces information material for the dissemination of new knowledge, techniques and approaches. A variety of reports, handbooks,

posters and other information materials are published and distributed in the region on non-profi t making basis.

About this book The preparation of this fi eld guide was proposed after the publication of the Tree nursery

trade in urban and peri-urban areas, RELMA Working Paper No. 13. This paper contained results of a survey of 39 nurseries in Nairobi and Kiambu Districts, Kenya.

The urban and peri-urban population in many developing countries is rapidly increasing and it is projected that by 2015 the urban population will equal the rural one. The rate of food and fodder production produced in the urban/peri-urban areas will increase.

The purpose of this guide is to share the basic knowledge required for the effective management of urban and peri-urban nurseries. Anyone reading it will quickly understand and learn the practical requirement for the establishment of nurseries. RELMA has had a goal to produce fi eld guides in local languages for easy reading by the intended users. This guide provides such an opportunity.

ISBN 6699 896 68 6

Regional Land Management Unit (RELMA), ICRAF Building, Gigiri, P. O. Box 63403, Nairobi, KenyaTel: (+254 2) 52 44 00, 52 44 18, 52 25 75, Fax: (+254 2) 52 44 01, E-mail: [email protected]

www.relma.org

SWEDISH INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION AGENCY