nguruwe ni mnyama mwenye faida

10
Prepeared by hebron venance UFUGAJI WA NGURUWE Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa. Katika nchi nyingi zinazo endelea ikiwemo Tanzania kiasi kikubwa cha nyama kinatokana na wanyama wenye matumbo Zaidi ya moja kama ng’ombe, mbuzi, kondoo, nk. Kutokana na kukua na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu kunaumuhimu mkubwa wa mabadiliko ya vyanzo vya nyama ili kuweza kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya ongezeko hilo la watu. Moja ya chazo kizuri na kinacho weza kupunguza uhaba wa nyama kwa muda mfupi ni pamoja na nguruwe ambao wanakuwa kwa muda mfupi, wanatupatia protini nyingi, gharama zake za uzalishaji si kubwa sana kwani wanatumia aina nyingi za vyakula kulingana na mazingira husika na pia wanaweza kuzaliana kwa vingi kwa muda mfupi. Mfano nguruwe anaweza kufikisha kilo 90-120 akifugwa vizuri ndani ya miezi sita(6) na hivyo tayari kwa kuchinjwa kwaajili ya nyama, na kwa mzao mmoja anaweza kuzaa vitoto 9-14 ambapo kwa mwaka anazaa mara mbili hivyo twaweza kupata vitoto 14-24 kwa mwaka.

Upload: hebron-venance

Post on 12-Apr-2017

645 views

Category:

Documents


9 download

TRANSCRIPT

Page 1: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

UFUGAJI WA NGURUWE

Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa. Katika nchi nyingi zinazo

endelea ikiwemo Tanzania kiasi kikubwa cha nyama kinatokana na wanyama wenye matumbo Zaidi ya moja kama

ng’ombe, mbuzi, kondoo, nk. Kutokana na kukua na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu kunaumuhimu

mkubwa wa mabadiliko ya vyanzo vya nyama ili kuweza kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya ongezeko hilo la

watu. Moja ya chazo kizuri na kinacho weza kupunguza uhaba wa nyama kwa muda mfupi ni pamoja na nguruwe

ambao wanakuwa kwa muda mfupi, wanatupatia protini nyingi, gharama zake za uzalishaji si kubwa sana kwani

wanatumia aina nyingi za vyakula kulingana na mazingira husika na pia wanaweza kuzaliana kwa vingi kwa muda

mfupi. Mfano nguruwe anaweza kufikisha kilo 90-120 akifugwa vizuri ndani ya miezi sita(6) na hivyo tayari kwa

kuchinjwa kwaajili ya nyama, na kwa mzao mmoja anaweza kuzaa vitoto 9-14 ambapo kwa mwaka anazaa mara

mbili hivyo twaweza kupata vitoto 14-24 kwa mwaka.

Page 2: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa

matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi

kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha

miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.

Ufugaji

Kwa kawaida nguruwe wanafugwa na watu wa kada zote, wafugaji wadogo wadogo na hata wakubwa. Aina hii ya

ufugaji huweza kumpatia mkulima kipato pamoja na lishe kwa familia, na hauhitaji gharama kubwa.

AINA ZA NGURUWE

Hampshire (USA)

Wana rangi ya dhahabu – nyeusi na msitari mweupe kuzunguka mabega.

Mdomo mfupi,masiko makubwa na yametazama nyuma.

Wana ngozi ngumu na rangi ya kahawia.

Wanakua haraka, nyama pana na mabega mapana

Ni wapole

Page 3: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

Landrace (Denmark)

Ni weupe na miili yao ni mikubwa

Masiko yaliyo anguka na yametazama mbele

Mdomo mrefu na ulionyooka

Wanazaa vizuri na vitoto vinakua kwa haraka

Wanatoa nyama nzuri

Wanavumilia mazingira magumu na wanahitaji matunzo mazuri.

Page 4: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

LARGE WHITE / YORKSHIRE(Yorkshire, England)

Masikio yaliyo simama, uso mpana na umebonyea ndani na mabega makubwa na mapana

Wanaathiriwa na jua na wanaweza kuvumilia kwa muda mfupi

Wanazaa vizuri na watoto wanakua haraka

Wana miili mirefu na wanatoa protini kwa wingi

SADDLEBACK, England (Essex and Wessex)

Wana rangi nyeusi na mabaka meupe kuzunguka mabega na miguu ya mbele.

uso mrefu na ulio nyooka

Masikio yaliyo anguka

Saizi ya kati

Wanauwezo mzuri wa kulea vitoto

Wazuri kwa kuwafugia nje

Page 5: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

NGURUWE WA KIENYEJI

Ndio wanao patikana kwa kiasi kikubwa nchini

Wanakua polepole na wanadumaa

Uzaaji mdogo (5 paka 6 vitoto kwa mzao mmoja)

Wanavumilia mlo mbovu, magonjwa na wadudu.

Wakiwa wamekua huwa na miili midogo

Wanastahimili joto kali na jua

Midomo yao imenyooka na miguu yenye ncha kali

Rangi ya ngozi inaweza kuwa nyeusi au nyeusi yenye mabaka

UCHAGUZI WA MBEGU BORA YA NGURUWE Tabia nzuri za nguruwe wa mbegu.

Uwezo mkubwa wa kuzaa.

Anaye sitahimili magojwa na hali ya hewa ya mazingira husika

Uwezo mzuri wa kukibadilisha chakula na kufanya nyama nzuri inayo pendwa na watu.

Uwezo mzuri wa kulea watoto.

Aina ya nguruwe.

Isiwe na magonjwa ya kurithi.

Awe na miguu imara na yenye nguvu

Awe angalau na matiti yasiyo pungua 12 na yawe na mpangilio mzuri.

Mrefu na awe na misuli imara.

Page 6: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

MIFUMO MBALI MBALI YA UFUGAJI WA NGURUWE

KUFUGIA NJE (KUWACHIA HURU)

Ni ufugaji wa kieneji wenye gharama ndogo na idadi ya nguruwe jike wanaofugwa wanaweza kuwa 1-3.

Mfumo huu unaendeshwa aidha kwa kuto wapatia chakula cha ziada wanyama wanapo toka kuzunguka

zunguka nje au hupewa chakula kisicho na ubora.

Ni mfumo wa ufugaji usio na mpangilio maalumu.

Nguruwe wa kienyeji ndio wanaofugwa kwa kiasi kikubwa na huwa wanachiwa huru kuzunguka.

Ukuaji na uzalishaji wake ni mdogo ukiambatana na vifo vingi

Wanyama huwa na wadudu wengi katika miili yao

Mara nyingi ni kwaajili ya kuipatia familia mahitaji yao. Ni rahisi kwa nguruwe kupata magonjwa na

wadudu.

NUSU NDANI NUSU NJE

Nguruwe wanafungiwa kwenye mabanda nyuma ya makazi na mara nyingine wanaruhusiwa kutoka nje.

Wanalisha mabaki ya jikoni, mboga na masalia mengine kama pumba.

Matunzo ya kawaida

Mavuno madogo na kiasi kikubwa cha vifo

Nguruwe wano fugwa ni wale wa kienyeji na chotara

Mavuno ni makubwa kwa kiasi ukilinganisha na wale wanao fungwa kwa kuachiwa huru.

KUFUGIA NDANI

ni ufugaji wa kisasa ambapo wanyama wanafungiwa ndani na hawaruhusiwi kutoka nje

uzalishaji kwaajili ya biashara mkulima huwa na nguruwe kuanzia hamsini na kuendelea

chakula kinacho tumika ni bora na huwa chakula cha kununuliwa.

mabanda mazuri na yenye nafasi ya kutosha

matunzo makubwa yanayopelekea mavuno mazuri

nguruwe si rahisi kupata magonjwa na wadudu.

mara nyingi nguruwe wa kigeni na wa kienyeji wanaofanya vizuri

masoko ni mabucha ya kawaida (kienyeji)

Page 7: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

Picha hapo juu inaonyesha ufugaji wa nguruwe kwa kuwachia nje (picha 1) na kufugia ndani kwa ujumla

bila kuwaachia nje (picha 2).

Picha hapo juu inaonyesha mfumo wa ufugaji wa nguruwe kwa kuwachia huru au kuwafungia nje.

UJENZI WA BANDA LA NGURUWE

Sehemu ya kujenga banda la nguruwe.

• Eneo liwe linafikika kwa urahisi.

• Iwe ni sehemu ambayo haituamishi maji.

• Iwe nisehemu ambayo iko mbali kidogo na makazi ya watu.

• Liwe ni eneo ambalo halipigwi na mionzi ya jua moja kwa moja)

• Eneo liwe na maji ya kutosha kwaajili ya usafi wa mabanda

Ujenzi wa banda bora la nguruwe

• Inashauliwa banda la nguruwe liwe na 25 sentimita za urefu; 1.5 mita za mraba kwa nguruwe mmoja mkubwa

ambaye ni jike na banda liwe limeezekwa.

Page 8: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

• Eneo la kutosha kwaajili ya maji ya kunywa, chakula na kufanya usafi

• Unapo jenga zingatia mwelekeo wa upepo ili kusaidia mzunguko wa hewa ndani ya banda.

• Banda bora ni lile lililo ezekwa kwa nyasi au mianzi ili kupunguza joto ndani. Endapo banda litaezekwa kwa

bati upande wa juu wa bati unatakiwa upakwe rangi nyeupe na kuta zake lazima ziwe ndefu (2.4-3.0m kwenda

juu na 1.8-2.1m kutoka chini) ili kusaidia mzunguko wa hewa kwenye banda

• Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa vifaa nafuu. Unaweza kutumia mchanga na simenti

kuweka sakafu, ama ukatumia udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kuweka sakafu. Ukubwa wa banda

unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10

wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.

ZINGATIA: Usafi ni muhimu katika banda ili kuepuka magonjwa.

Picha hapo juu inaonyesha Mabanda ya nguruwe yanavyo onekana kwa ndani

Picha hapo juu ni banda la nguruwe linavyo onekana kwa nje.

Page 9: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

Malisho

Ulishaji wa nguruwe ni rahisi kwa kuwa wanakula aina mbalimbali za vyakula kulingana na mazingira

wanayofugwa. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali, na pia hulishwa kwa kutumia

masalia ya nafaka (pumba). Unaweza kuwalisha kwa kutumia mashudu na pumba. Pia unaweza kuwalisha kwa

kutumia mabaki ya jikoni.

Kuzaliana

Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe

mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 9 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula

cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo

mazuri, baada ya miezi 6-8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 90-120 na wanaweza kuuzwa.

Matunzo

Baada ya nguruwe kuzaa siku ya kwanza asipewe kitu chochote ila apewe maji ya kutosha, baada ya hapo

anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto

wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili

toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi

mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.

MAGONJWA YANAYOATHIRI NGURUWE

Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima

kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija.

Ugonjwa wa miguu na midomo

Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa

mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka

sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.

Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja.

Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.

Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu

magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.

Homa ya Nguruwe (Swine fever)

Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya nguruwe huenea kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya

nguruwe, na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamu na hauambukizwi kwa binadamu.

Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa

mekundu.

Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni

kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.

Page 10: Nguruwe ni mnyama mwenye faida

Prepeared by hebron venance

Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au

Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.

Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)

Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na

kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi

na gesi inayotokana na madawa makali.

Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama

sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.

Kimeta (Anthrax)

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa

wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka

mingi.

Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio

karibu nawe.

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.

Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini

Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa

Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.