pendekezo kuhusu kuzuia unyonyaji dhidi ya wasanii katika biashara ya miito(ringback tones)
TRANSCRIPT
-
7/30/2019 Pendekezo Kuhusu Kuzuia Unyonyaji Dhidi Ya Wasanii Katika Biashara Ya Miito(Ringback Tones)
1/3
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI
DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO
(RING BACK TONES)
Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara
Kuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama
miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi
binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko
haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo
kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la
USIRIlipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo
Wizara ya Viwanda na Biashara.
USIRI
Biashara hii ya Ring Back Tones (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network
providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao nao
huingia mikataba na Wasanii (Content Creators).
Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo
Network providers na Content Providers kuwa watu pekee wenye taarifa zote za
biashara hii. Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake
-
7/30/2019 Pendekezo Kuhusu Kuzuia Unyonyaji Dhidi Ya Wasanii Katika Biashara Ya Miito(Ringback Tones)
2/3
mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au content
nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii. Wachuuzi (Content Providers) nao
hawatoi taarifa za mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa wasanii
kuwasainisha mikataba inayowanyonya. Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi
cha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake. Hivi sasa biashara hii
inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.
Suluhisho:
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha
makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya
simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules). Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa
taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)
UNYONYAJI
Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii wamekuwa wakinyonywa kimapato.
Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake
(wimbo) katika mwezi (downloads).
Lakini mapato yatokanayo na subscriptions ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku
msanii hapati chochote. Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja
kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za downloads na
ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na
Kampuni za Simu.
-
7/30/2019 Pendekezo Kuhusu Kuzuia Unyonyaji Dhidi Ya Wasanii Katika Biashara Ya Miito(Ringback Tones)
3/3
Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public
Performances) na hivyo copyright Association ya Marekani imeweka kiwango cha
chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia
10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.
SULUHISHO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi
za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama performance na kwamba Kampuni
za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya mapato ghafi, ambapo asimilia 10%
itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi na Ulinzi wa kazi
za Wasanii.
HITIMISHO
Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya Ring Back Tones na mgawo
wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta
tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni
(Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013
Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini
Dodoma, 13 Mei 2013.