press release - mabadiliko ya wajumbe mei 2016
TRANSCRIPT
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA
Simu: +255 026 23222761-5 Fax No. +255 026 2322624 E-mail: [email protected]
Ofisi ya Bunge, S.L.P. 941,
DODOMA
TAARIFA KWA UMMA _________
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko mengine ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia maombi ya baadhi ya Wabunge pamoja na mahitaji mapya yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli za Kamati za Bunge.
Mabadiliko haya yamefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 116(3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili 2016 na yamehusisha maeneo manne ambayo ni:
• Kuhamishwa kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati,
• Kualikwa kwa baadhi ya wajumbe katika Kamati ya Bajeti,
• Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge kuondolewa pamoja na
• Uteuzi wa wajumbe wapya katika kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge
Mabadiliko haya ya wajumbe kwenye kamati yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa kamati na nafasi zao imeambatishwa.
Imetolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge DODOMA 26 Mei, 2016.
1.0 WANAOHAMISHWA KAMATI
Na JINA LA MBUNGE
KAMATI ALIYOKWEPO
AWALI
KAMATI ANAYOHAMIA
1. Mhe. Ezekiel Magoyo Maige, Mb.
Nishati na Madini
PAC
2. Mhe. Allan Joseph Kiula, Mb.
Mambo ya Nje, Ulinzi na usalaama
PAC
3. Mhe. Omary Tebweta Mgumba, Mb.
Sheria Ndogo PAC
4. Mhe. Rhoda Rdward Kunchela, Mb.
Masuala ya UKIMWI
PAC
5. Mhe. Joseph George Kakunda, Mb.
PIC PAC
6. Mhe. Ahmed Ally Salum, Mb.
PAC Huduma na Maendeleo ya Jamii
7. Mhe. Neema William Mgaya, Mb.
Huduma na Maendeleo ya Jamii
Ardhi, maliasili na Utalii
8.
Mhe. Salma Mohamed Mwassa, Mb.
Bajeti Ardhi, Maliasili na Utalii
2.0 WAJUMBE WAALIKWA KATIKA KAMATI
NA. JINA LA MBUNGE KAMATI ALIYOPO
HADHI YA UJUMBE
1. Mh. Andrew John Chenge, Mb.
Sheria Ndogo Mwalikwa
2. Mhe. Joseph Roman Selasini, Mb.
LAAC Mwalikwa
3. Mhe. Dkt Dalali Peter Kafumu, Mb.
Viwanda, Biashara na Mazingira
Mwalikwa
4. Mhe. Japhet Ngalilonga Hasunga, Mb.
PAC Mwalikwa
5. Mhe. Albert Obama Ntabaliba, Mb.
PIC Mwalikwa
6. Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mb.
Huduma na Maendeleo ya Jamii
Mwalikwa
3.0 WALIOONDOLEWA KATIKA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA
YA BUNGE 1. Mhe. Dkt. Haji Hussein Mponda, Mb. 2. Mhe. Najma Murtaza Giga, Mb.
4.0 WANAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE 1. Mhe. Asha Abdalla Juma, Mb. 2. Mhe. Emmanuel Mwakasaka, Mb. 3. Mhe. Augustino Manyanda Masele, Mb.