republic of kenya ministry of health unachohitaji … · mfumo wa kinga ya mwili. chembechembe za...

44
K E N C O K e n y a n N e t w o r k o f C a n c e r O r g a n i s a t i o n s MINISTRY OF HEALTH REPUBLIC OF KENYA UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU SARATANI KWA MATUMIZI YA WAGONJWA NA WAUGUZI

Upload: others

Post on 29-Aug-2019

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

KENCOKenyan Network of

Cancer Organisations

MINISTRY OF HEALTH

REPUBLIC OF KENYA

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU SARATANI KWA MATUMIZI YA WAGONJWA NA WAUGUZI

Page 2: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi
Page 3: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Unachohitaji Kujua Kuhusu Saratani Kwa matumizi ya wagonjwa na wauguzI

DIBAJI Kijitabu hiki kimeandaliwa na Wizara ya Afya ya Kenya pamoja na Johns Hopkins Centre for

Communications Programs, kwa usaidizi kutoka kwa American Cancer Society.

Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya ya Kenya, Kenyatta National Hospital, Moi Teaching and Referral Hospital, Aga Khan Hospital pamoja na Kenya Network of Cancer Organizations (KENCO) ambao pia

walitoa muongozo wa kiufundi na kusaidia katika usanifishaji wa maelezo ya kijitabu hiki kuambatana na utafiti mpana katika wagonjwa wa saratani na wahudumu wao wa afya.

Maelezo yaliyopo kwenye chati za saratani na muigo wa maelezo yaliyoopolewa kutoka kwa American Cancer Society. Baadhi ya maelezo kuhusu hali ya maisha pamoja na lishe yaliopolewa

kutoka kwa MacMillan Cancer Support, na taasisi ya U.S. National Cancer Institute. Waliohusika katika ruwaza na usanifishaji wa muundo walikuwa ni Avocado Design Studio.

© American Cancer Society, 2016.

Page 4: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Saratani ni Nini?

n Seli za kawaida zinajiongeza na kujizidisha kwa utaratibu mzuri. Saratani hutokea ikiwa seli hizo zinaanza kujiongeza bila mpangilio maalum.

n Seli zenye saratani huendelea kukua na kuunda seli mpya bila kikomo. Hali hii huupatia mwili wakati mgumu sana wa kufanya kazi jinsi inavyofaa

n KUELEZA SELI NI NINI: Seli ni sehemu ndogo zaidi katika mwili wa binadamu ambayo hutekeleza majukumu yote yanayohitajika ili aishi. Kwa kuwaida, seli huwa ni chembechembe ndogo zaidi zisizoonekana kwa macho ila tu kwa kutumia hadubini.

1

Page 5: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

SELI ZA KAWAIDA

SELI YA SARATANI KUONGEZEA MARA DUFU UVIMBE UNAOSAMBAA

Saratani ni nini? 1

Page 6: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mambo ya Kimsingi Kuhusu Saratani

n Saratani si ugonjwa wa aina moja tu, kuna aina nyingi za saratani.n Saratani inaweza kuanzia katika sehemu yoyote ya mwili. n Saratani inaweza kusambaa hadi katika sehemu nyinginezo za mwili, aidha

kupitia kwa mifumo ya limfu au mishipa ya damu na inapofanya hivyo huitwa metastasis.

n Saratani hutofautiana kutokana na jinsi inavyokua na kusambaa mwilini, na jinsi inavyopimwa na kutibiwa.

2

Page 7: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mambo ya Kimsingi Kuhusu Saratani

MGAWANYIKO WA VIUNGO MBALI MBALI

UVIMBE WA AWALI

2

Page 8: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Saratani Maarufu Nchini Kenya

3

n KWA WANAUME

- Saratani ya Kibofu- Saratani ya umio - Saratani ya

mishipa ya damu na limfu

- Saratani ya tumbo- Satani ya bawasili

au utumbo (njia ya haja kubwa)

n KWA WANAWAKE:

- Saratani ya njia ya uzazi

- Saratani ya matiti- Saratani ya umio- Saratani ya tumbo- Saratani ya

mishipa ya damu na limfu

n KWA WATOTO:

- Limfoma- Saratani ya Damu

(Leukemia)- Uvimbekatikafigo- Uvimbe katika

macho - Saratani ya mifupa

Page 9: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Saratani Maarufu Nchini Kenya 3

SARATANI YA NJIA YA UZAZI

SARATANI YA MISHIPA YA DAMU NA LIMFU

SARATANI YA UMIO

SARATANI YA KIBOFU

SARATANI YA TUMBO

SARATANI YA BAWASILI AU

UTUMBO SARATANI YA MATITI

Page 10: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Je, Uvimbe Ndani ya Mwili (Tumor) ni Nini?

n Saratani nyingi hufanya uvimbe unaoitwa (tumor) au seli yenye kitufe.n Uvimbe ambao si saratani huitwa “benign”. n Uvimbe ambao ni saratani huitwa “malignant” au uvimbe wenye kijicho.n Madaktari huchukua sehemu ndogo ya uvimbe huo na kuichunguza ili

kubaini iwapo ni saratani. Hatua hii huitwa bayopsia. Bayopsia nyingi hufanywa kwa kutumia sindano ndogo.

n Kuna aina fulani fuluni za saratani, kama vile Saratani ya damu (Leukemia) ambazo hazifanyi uvimbe. Hukua kwenye damu ama katika seli nyinginezo za mwili.

4

Page 11: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

SELI ZA KAWAIDA

SELI ZINAZOSAMBAA

Je, Uvimbe Ndani ya Mwili (Tumor) ni Nini?

Uvimbe ndani ya mwili Utambuzi wa ugonjwa

4

Page 12: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mbona Iwe Mimi?

n Iwapo unajiuliza swali “Nilikosea wapi?” au “Mbona ikawa mimi?” hauko peke yako.

n Unafaa ujue kwamba saratani si adhabu kwa mienendo yako ya hapo awali. Wala haisababishwi na mizengwe au nguvu zozote za giza kama vile uchawi.

n Saratani ni ugonjwa unaoweza kuathiri mtu yeyote, mahali popote, katika nchi yoyote ile, na wakati wowote.

n Saratani si kosa lako. Zingatia kujitunza vizuri sasa.

5

Page 13: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mbona Iwe Mimi? 5Saratani unaweza kuathiri mtu yeyote Saratani haisababishwi na uchawi

Page 14: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Athari Zinazoambatana na Saratani

n Kwa hakika, madaktari hawajui kinachosababisha saratani. n Tunajua kwamba kuna vitu vinavyoitwa ‘ hali ya kuzua hatari’ ambayo

huathiri uwezekano wako wa kushikwa na magonjwa. n Baadhi ya hali hatari za saratani zinaweza kubadilishwa lakini nyingine

haziwezi. Hali hatari ambazo haziwezi kubadilishwa zinahusisha umri wako, jinsia yako, na historia ya familia yako.

n Hali zinazoweza kubadilishwa ni mambo unayofanya, kama vile iwapo unatumia tumbaku au pombe, aina ya chakula unachokula, na kiwango cha mazoezi unayofanya. Hali nyingine zinazozua hatari zinahusiana na vitu vilivyomo kwenye mazingira ambayo husababisha saratani.

6

Page 15: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Athari Zinazoambatana na Saratani 6

SodaSODA

wine

KIWANGO CHA MAZOEZI POMBE

VYAKULAUNAVYOKULA

TUMBAKU

UCHAFUZI WAMAZINGIRA

Page 16: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Dalili na Ishara za Ugonjwa

n Dalili ni ishara inayoonyesha kwamba kuna kasoro mwilini mwako.

n Matibabu hufanya kazi vizuri saratani inapogunduliwa mapema – ikiwa bado changa na uwezekano wake wa kusambaa hadi sehemu nyinginezozamwilinifinyu.

n Dalili za kawaida za saratani huwa ni pamoja na:- Kupungua kwa uzani

kusikoelezeka chanzo chake ni nini

- Maumivu- Mabadiliko ya ngozi- Joto jingi mwilini- Uchovu wa kila mara- Kuvuja damu kupita kiasi

n Saratani nyingi hazionyeshi dalili hadizinapofikiakiwangochajuunazinaweza tu kutambuliwa mapema kupitia ukaguzi.

Kumbuka sio kila mara dalili hizi humaanisha mtu aliye nazo ana saratani kwani zinaweza kuwa

dalili za magonjwa mengine tofauti.

7

Page 17: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Dalili na Ishara za Ugonjwa

Maumivu Mabadiliko ya ngozi

Joto jingi mwilini Uchovu wa kila mara Kuvuja damu kupita kiasi

Upunguaji wa uzani

7

Page 18: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Itikadi Zinazotumiwa Sana Ambazo ni za Uongo

n Saratani huambukizwa.n Saratani hutibiwa kwa dawa za kienyeji.n Si kweli kwamba hakuna kinachoweza kufanywa ili kuzuia kusambaa kwa

saratani mwilini.n Mjamzito aliye na saratani huzaa mtoto mwenye saratani.n Saratani ni ugonjwa wa wazee au matajiri pekee.n Saratani ni hukumu ya kifo.

8

Page 19: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Itikadi Zinazotumiwa Sana Ambazo ni za Uongo

UONGO!

8

Page 20: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Viwango vya saratani

n Viwango hivi hutuonyesha jinsi na ambavyo saratani imesambaa kutoka ilikoanzia mwilini.

n Saratani nyingi huwa na viwango vinne.n Ufahamu wa viwango vya saratani husaidia daktari kuamua ni aina gani ya

matibabu yanayofaa na jinsi matibabu hayo yanavyoweza kutekelezwa na jinsi yanavyoweza kufanya kazi vizuri.

n Kama kawaida, kiwango cha chini (kama vile kiwango cha 1 au 2) humaanisha kuwa saratani haijasambaa sana mwilini.

n Ngazi ya juu (kama vile 3 au 4) humaanisha saratani imeenea zaidi. Hatua ya 4 ndiyo ya juu zaidi.

9

Page 21: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Ngazi za Saratani

KIWANGO CHA 0 Uvimbe katika kiungo Fulani

ndani ya mwili – saratani ikiwa

inaanza.

KIWANGO CHA 1Saratani

imeguduliwa katika kiungo

kimoja.

KIWANGO CHA 2Uvimbe unakua kwa kiasi, lakini mahala pamoja.

KIWANGO CHA 3Saratani imesambaa na kuwa

mafundo ya limfu na bila shaka kuvurugamkusanyiko

wa seli mwilini.

KIWANGO CHA 4saratani imesambaa katika sehemu nyingine za mwili.

Hapa inakaribia kufikia kiwango cha juu sana.

MSHIPA WA DAMU

FUNDO LA LIMFU

FUNDO LA LIMFU LIKIWANA SELI ZENYE SARATANI

AMBAZO ZIMESAMBAA KATIKA

KIUNGO FULANI CHA MWILI

9

Page 22: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Matibabu

n Matibabu yake yanaweza kuwa ya kutibu, kudhibiti, au kutibu matatizo yanayoisababisha.

n Matibabu maarufu ya saratani ni kufanyiwa upasuaji, kufanyiwa tiba ya kuchomwa (kemotherapi) na tiba ya miale yaani (radiation).

n Mtu anayeugua saratani huenda akahitaji mojawapo wa tiba hizi au aina zote na mara nyingi huduma kadhaa za matibabu huenda zikahitajika.

n Aina ya matibabu ambayo daktari wako atapendekeza itategemea:

- Aina ya saratani uliyo nayo;- Ngazi ya saratani;- Umri wako, hali ya afya kwa

jumla, na mahitaji ya mtu binafsi.

n Hakikisha kwamba unapata matibabu yako kutoka kwa kituo cha afya kinachojulikana vyema katika utoaji wa huduma za saratani.

10

Page 23: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Matibabu 10

Page 24: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Je, Upasuaji wa Saratani ni Nini?

n Baadhi ya Saratani zinaweza kuondolowa kupitia upasuaji.n Upasuaji unafaa kutumika katika eneo zenye uvimbe ambao haujasambaa

katika viungo vingine mwilini.n Upasuaji unaweza kutumika kutibu saratani, ama kutibu matatizo

mengine yaliyosababishwa na saratani hiyo.n Muulize Daktari wako sababu kamili ya upasuaji huo.

11

Page 25: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

11Je, Upasuaji wa Saratani ni Nini?

Page 26: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Kemo ni Nini?

n Kemo hutumia dawa zenye nguvu ili kuua seli za saratani.n Kwa kawaida, dawa hizo huingizwa kwenye mishipa ya damu kupitia

chubu na sindano.n Baadhi ya dawa za kemo huweza kumezwa kama vidonge ama dawa ya

maji.n Kemo hutolewa kutibu saratani, au kumsaidia mgonjwa kuishi maisha

marefu zaidi au kumsaidia apate afueni.n Kemo hutumika kwa wagonjwa mbalimbali kwa kusudi mbali mbali.

Muulize muuguzi wako ni kusudi la kupewa tiba ya kemo.

12

Page 27: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

12Kemo ni Nini?

Page 28: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Je, Tiba ya Miale ni Nini?

n Tiba inayotumia miale huwa ni matumizi ya miale ili kuua seli za saratani.n Vifaa maalum hutuma dozi kali za miale ili kumaliza saratani.n Miale hiyo pia inaweza kuathiri seli za kawaida zinazokaribiana na seli za

saratani. Lakini seli za kawaida zinaweza kujikarabati zenyewe na seli za saratani haziwezi kufanya hivyo.

n Tiba ya miale haina joto na pia haina uchungu.n Tiba ya miale inaweza kutumika kutibu saratani, au kuzuia kukua kwa

saratani.n Muulize muuguzi wako wa afya ni kwa nini unapewa tiba ya miale.

13

Page 29: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

13Je, Tiba ya Miale ni Nini?

Page 30: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Madhara Andamizi ya Matibabu

n Kila matibabu yanaweza kuwa na athari zake.

n Baadhi yanaweza kuwa makali na mengine mepesi, lakini madhara mengi andamizi ya matibabu mengi ya saratani yanaweza kutibiwa.

- Kuchafuka roho na kutapika;- Kukosa hamu ya chakula; - Kunyonyoka nywele kwa muda;- Vidonda vya mdomo;- Hatari kubwa ya kupata

maambukizi;

- Kuvuja damu au kuchubuka kila unapojeruhiwa au kukatwa kidogo;

- Upungufu wa damu (kutokana na kupungua kwa seli nyekundu za damu), hali inayoweza kusababisha uchovu, kupumua kwa shida, ngozi iliyopauka, na dalili nyinginezo;

- Mwasho wa ngozi;- Uchovu wa kila mara.

n Madhara mengi andamizi humalizika baada ya kukamilika kwa matibabu.

n Madhara mengi ya saratani yanaweza kutibiwa.

14

Page 31: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Madhara Andamizi ya Matibabu

Kunyonyoka nywele Makovu kinywani Mwasho wa ngozi

14

Page 32: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Je, Nitaishi?

n Zipo sababu nyingi zinazoathiri urefu wa maisha atakayoishi mwathiriwa wa saratani.

- Aina ya saratani na mahali ilipo mwilini mwako; - Kiwangoambachosaratanihiyoimefikia; - Hali ya seli zenye saratani; - Umri wako na hali yako ya afya kabla ya

kupata saratani; - Jinsi mwili unavyoitikia matibabu.n Saratani nyingi zinaweza kutibiwa. n Ni vigumu sana kubashiri muda ambao mtu

anayeugua saratani ataishi.

Yanayompasa kujua mhudumu wa afya : Kuwa tayari kwa mazungumzo

halisi yanayohusu mgonjwa anayeugua

saratani..

15

Page 33: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Je, Nitaishi?

COMMUNITYCLINICJe,

Nitaishi?

15

Page 34: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mapendekezo ya Lishe Wakati wa Matibabu

n Ulaji wa chakula kinachofaa kabla, wakati na baada ya matibabu, unaweza kukuwezesha kuhisi vizuri na kuongeza nguvu mwilini.

n PROTENI (NYAMA NA VIBADALA VYAKE): mimea jamii ya maharagwe, nayama ya ndege (k.m. kuku), nyama nyepesi, mayai, samaki, dagaa, bidhaa za maziwa, njugu na simsim na siagi.

n MAFUTA: - Asili nzuri ya mafuta ni: mafuta ya mboga kama vile yanayotokana na mahindi machanga,simsim, ufuta na

njugu. - Mlo mzuri haufai kuwa na mafuta yaliyotengenezwa kutokana na wanyama. - Jaribu kupunguza ulaji wa mafuta yabisi (yaliyogandamanishwa), kama vile siagi na mafuta yabisi ya kupikia.

Mafuta kama haya yanaweza kupatikana katika vitafunio na vyakula vya kuokwa.n STACHI (VYAKULA VYENYE WANGA): Aina za matunda, mboga za majani na nafaka. Mifani bora ni kama:

mahindi, mchele, maharage, viazi, mawele, mhogo, ngano, viazi mbatata, mtama, ndizi mbichi, pasta na nafaka.

n VITAMINI NA VIRUTUBISHI VYA MADINI: Vitamini na madini hutekeleza jukumu muhimu katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini.

16

Page 35: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mapendekezo ya Lishe Wakati wa Matibabu

YOGURT

MIZIZI

NAFAKA

MBOGA

MAHARAGWE NA NJUGU

MATUNDA

MAJANI

SAMAKI NA KUKU

NYAMA

YOGURTMAZIWA

KEKI

Wakati Mwingine

Vipimo Wastani vyakila siku hadi kila wiki

Mara kwa mara, angalau mara mbili kwa wiki

Pangilia kila mlo utumievyakula hivi

MAFUTA

16

Page 36: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Maji

n Maji au vinywaji ni muhimu kwa afya. Unafaa unywe angalau gilasi nane za vinywaji kila siku.

n Unaweza kuhitaji vyakula vya rojo-rojo zaidi iwapo unatapika, unaendesha, au hata ukiwa umepunguza kiasi cha chakula unachokula.

n Unaweza kuhitaji vinywaji zaidi hasa unapopokea matibabu ya kemo.

n Unafaa uepukane na vinywaji vilivyowekwa sukari kabla ya kuuzwa, pamoja na pombe.

17

Page 37: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Maji

121

2

3

4

56

7

8

9

10

11

17

Page 38: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mapendekezo ya Mazoezi

n Shughuli za kutumia nguvu hukufanya kuwa imara. Zinaweza kusaidia kupunguza mzongo wa mawazo, jakamoyo, uchovu wa kila mara, kitefutefu, shida wakati wa haja kubwa inayotokana na upungufu wa maji mwilini. Zinaweza kuimarisha hamu yako ya chakula.

n Ratiba na aina ya mazoezi yatategemea hali ya kila mgonjwa. Mazoezi hayo yafaa kuwa ni jambo unalopenda kufanya.

n Unapaswa kutambua hali ya mwili wako na upumzike unapohitajika kufanya hivyo. Huu si wakati wa kujilazimisha kufanya mazoezi.

18

Page 39: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mapendekezo ya Mazoezi

Kufanya kazi Kuruka kamba Kucheza

18

Page 40: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mikakati ya Kuizoea Hali Mpya

n Waambiemarafikipamojanafamilia yako kuhusu saratani yako punde tu unapogundua kwamba unayo.

n Wafahamishe kwamba hauwezi kuwaambukiza. Waeleze kwamba unaendelea kupata matibabu ili kuimarisha afya yako.

n Waruhusumarafikinafamiliawakokukusaidia, na wafahamishe aina ya msaada unaohitaji.

n Kuna makundi mengi ya kuhimizana pia (mwelekeze mgonjwa na muuguzi wa afya kwenye kijitabu).

n Baadhi ya tiba badala huenda zikapunguza aina fulani ya dalili za saratani, kupunguza athari za matibabu, au kuimarisha hali yako ya afya. Lakini tiba za miti shamba na waganga huenda zikawa hatari kwa afya yako. Kila mara wasiliana na daktari wako au muuguzi kabla ya kutafuta tiba hizo.

19

Page 41: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Mikakati ya Kuizoea Hali Mpya 19

Page 42: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Haki za mgonjwa

20

n Haki zako kama mgonjwa ni pamoja na:

- Haki ya kupata matibabu.- Haki ya kupata matibabu ya dharura

katika kituo chochote cha afya.- Haki ya kukataa matibabu.- Haki ya kudumisha siri.- Haki ya kufahamishwa ili kukubali

matibabu.- Haki ya kupata maelezo. - Haki ya kutibiwa kwa heshima na

taadhima.- Haki ya kutafuta maoni tofauti ya

kimatibabu.- Haki ya kulalamika.

n Majukumu yako kama mgonjwa ni pamoja na:

- Kujishughulikia mwenyewe kuishi maisha bora kwa afya yako

- Kuwa na mtazamo chanya kuhusu afya na maisha yako

- Kuheshimu haki za watu wengine na kuepuka kuhatarisha maisha na afya yao

- Kuwapa habari zifaazo na sahihi wahudumu wa afya, ili kuwawezesha kukufanyia ukaguzi, matibabu na ushauri ufaao.

- Chunga stakabadhi zako za afya ulizonazo- Ili kutimiza ratiba ya kuonana na daktari,

chunga masaa na iwapo itakuwa vigumu kufikakwawakatiufaaowasilianamapemana mhudumu wako wa afya

- Ili kuzingatia maagizo, zingatia na wala usitumia vibaya madawa au matibabu uliyopewa.

Page 43: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi

Haki za mgonjwa 20

Page 44: REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi