ripoti ya kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu …2. ndg. othman ali haji - katibu 3. ndg. asha...
TRANSCRIPT
1
RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA NA KUDHIBITI
HESABU ZA SERIKALI NA MASHIRIKA (P.A.C) YA BARAZA LA
WAWAKILISHI ZANZIBAR, 2014/2015
SEHEMU YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Kufuatia Mhe. Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Utumishi wa Umma na Utalawa Bora, Mhe.
Haji Omar Kheir, kuwasilisha ripoti mbili za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ambazo ni Ripoti ya
Ukaguzi wa Hesabu kwa Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na Ripoti ya Ukaguzi Yakinifu kwa Miradi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, zote za mwaka 2011/2012 katika kikao cha Bajeti ya mwaka 2013/2014, na kwa
kuzingatia kuwa, Kamati ilizifanyia kazi ripoti hizo bila ya kuzimaliza na hatimae ilitoa
taarifa yake mwaka jana.
Kwa kuzingatia uwasilishwaji mwengine wa ripoti mbili za Ukaguzi wa Hesabu kwa
Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ripoti ya Ukaguzi
Yakinifu kwa Miradi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, za mwaka 2012/2013,
kupitia kwa Mhe. Waziri, Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini wa Wizara ya Nchi, Afisi ya
Rais, Ikulu na Utawala Bora, katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi wa mwezi wa
Oktoba 2014, Kamati pia ilikabidhiwa ripoti hizo na kutakiwa kuendelea nazo na hatimae,
itoe taarifa yake katika Mkutano huu wa Baraza, Machi/Aprili, 2015 kwa ripoti zote nne.
1.1 WAJUMBE NA SEKRETARIETI YA KAMATI
Kwa mwaka 2014/2015, Kamati inaundwa na Wajumbe 8 na Sekretarieti kama ifuatavyo:
1. Mhe. Omar Ali Shehe - Mwenyekiti.
2. Mhe. Fatma Mbarouk Said - Makamo Mwenyekiti.
3. Mhe. Mbarouk Wadi Mussa (Mtando) - Mjumbe
4. Mhe. Mwanajuma Faki Mdachi - Mjumbe
5. Mhe. Rufai Said Rufai - Mjumbe
6. Mhe. Salim Abdalla Hamad - Mjumbe
7. Mhe. Salma Mussa Bilali - Mjumbe
8. Mhe. Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
Sekretarieti ya Kamati iliongozwa na Makatibu wa Kamati, Afisa wa Afisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Maofisa kutoka Wizara ya Fedha kama wafuatao:-
1. Ndg. Nasra Awadh Salmin - Katibu
2. Ndg. Othman Ali Haji - Katibu
3. Ndg. Asha Foum Makame - Afisa Sera, Wizara ya Fedha.
4. Ndg. Hurina Said Mohamed - Afisa Bajeti, Wizara ya Fedha
5. Ndg. Khalid Bakar Hamrani - Afisa Sera, Wizara ya Fedha
6. Ndg. Mfaume Mohamed Mfaume - Afisa wa Afisi ya Mdhibiti
1.2 REJEA ZA KAMATI
Kwa mwaka 2013/2014, Kamati ilifuatilia ripoti nne za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali ambazo ndio rejea za Kamati. Ripoti zenyewe ni hizi zifuatazo:
2
Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu kwa Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2011/2012.
Ripoti ya Ukaguzi Yakinifu kwa Miradi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, ya mwaka 2011/2012.
Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu kwa Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2012/2013.
Ripoti ya Ukaguzi Yakinifu kwa Miradi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, ya mwaka 2012/2013.
1.3 UTARATIBU WA KAZI ZA KAMATI
Kamati imefanya kazi kwa utaratibu wa kawaida kama unavyoelekezwa na kanuni ya 108(7)
ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi toleo la 2012, juu ya uwezo wa Kamati kujipangia kazi
zake baada ya kushauriana na Spika. Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ilikutana na
Wizara na Taasisi za Serikali zilizohusika na kazi, na hatimae Kamati ilifanya ziara katika
maeneo mbali mbali kushuhudia uhalisia wa maelezo ya Wizara, Taasisi husika ama hoja ya
ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu. Aidha, Kamati kwa kuzingatia haja iliyokuwepo,
ilifanya ziara katika maeneo husika na baadae ilifanya mijadala ya hoja mbali mbali.
1.4 UPEO WA RIPOTI
Pamoja na kuzifanyia kazi ripoti nne za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kama
tulivyoeleza awali, kwa mwaka 2014/2015 na kwa kuzingatiwa kuwa, ripoti nne hizo
zimejumuisha Ukaguzi Maalum wa Viinua Mgongo, Ukaguzi Yakinifu wa Miradi mbali
mbali ya Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali, Ukaguzi Maalum wa Mazingira na
Ukaguzi wa kawaida wa Hesabu za Serikali kwa miaka ya 2011/2012 na 2012/2013. Aidha,
Kamati imeshindwa kuyafanyia kazi maeneo yafuatayo ya ripori hizo:
Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu kwa Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya SMZ,
kwa mwaka 2011/2012
Ukaguzi wa Viinua Mgongo kwa Baadhi ya Taasisi kama zifuatazo (uk-19, Hoja
Namba 14.2)
Wizara ya Kilimo na Maliasili
Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM)
Kikosi cha Valantia (KVZ)
Kikosi cha Zimamoto na Uokozi
Wizara ya Afya
Wizara ya Fedha
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Ripoti ya Ukaguzi Yakinifu kwa Miradi ya Maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2012/2013
Taarifa ya Ukaguzi wa Mazingira - Pemba
Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu kwa Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya SMZ,
kwa mwaka 2012/2013
3
WIZARA YA NCHI (OR) TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
Jeshi la Kujenga Uchumi
Chuo cha Mafunzo
Kikosi cha KMKM
Kikosi cha Zimamoto na Uokozi
Kikosi cha Valantia
Ofisi ya Kadi za Utambulisho
Mkoa wa Mjini Magharibi
Mkoa wa Kusini Unguja
Mkoa wa Kusini Pemba
Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A”
Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi
Halmashauri ya Wilaya ya Kusini
WIZARA YA NCHI OFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Baraza la Wawakilishi
Tume ya Uchaguzi
WIZARA YA NCHI OFISI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS
Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Tume ya UKIMWI
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Wizara ya Katiba na Sheria
Mahkama Kuu
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
Tume ya Kurekebisha Sheria
WIZARA YA ARDHI, MAKAAZI, MAJI NA NISHATI
Wizara Ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO
Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo
Kamisheni ya Utalii
MASHIRIKA YA UMMA
Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu
Pamoja na taarifa hii kuelezwa katika ripoti hii, Kamati ilimuarifu Mhe. Spika wa Baraza la
Wawakilishi kuhusiana na uwezekano mdogo wa kumalizwa kwa kazi hizo kupitia barua ya
tarehe 04 Febuari, 2015 yenye kumbu kumbu namba BLW/K.10/2 VOL.VII/49 ambayo pia
imenakiliwa kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi, ili kama Afisi ya Baraza la Wawakilishi
itaona ipo haja ya kumalizwa kwa kazi zote hizo ama nusu yake, iongeze muda wa ziada
kwa Kamati ili mapema kabla ya kutoa ripoti yake, kazi hizo ziweze kufanywa na taarifa
yake iweze kupatikana pamoja na taarifa hii. Hata hivyo, hadi tunaandika taarifa hii,
hakukuwa na majibu yoyote ya barua hiyo wala hakukuwa na muda wowote ulioengezwa,
pamoja na makubaliano ya Baraza hili kwa Kamati ya P.A.C kuongezewa muda wa kazi.
4
1.5 MUUNDO WA RIPOTI
Ripoti hii ina sehemu tatu, Utangulizi, Maudhui na Hitimisho. Utangulizi umejumuisha
Utangulizi, Wajumbe wa Kamati na Sekretarieti, Rejea za Kamati, Utaratibu wa Kazi za
Kamati, Upeo na Muundo wa ripoti. Maudhui ya Ripoti yamejumuisha; Ripoti ya Ukaguzi
wa Hesabu kwa Mawizara, Mashirika na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya
mwaka 2011/2012; Ripoti ya Ukaguzi Yakinifu kwa Miradi ya Taasisi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, ya mwaka 2011/2012; Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu kwa Mawizara,
Mashirika na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2012/2013 na Ripoti
ya Ukaguzi Yakinifu kwa Miradi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ya
mwaka 2012/2013.
Katika kila ripoti tulizozitaja hapo juu, zimegusia mambo manne ambayo ni Hoja ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kama maudhui yake yalivyoripotiwa katika ripoti
tulizozitaja hapo juu, Majibu ya Wizara au Taasisi husika, Uchunguzi wa Kamati na mwisho
ni Mapendekezo ya Kamati.
Isipokuwa, katika ufafanuzi wa hoja za Ukaguzi Maalum wa Viinua Mgongo, mapendekezo
ya Kamati yamejumuishwa kwa hoja zote.
SEHEMU YA PILI
MAUDHUI YA RIPOTI
UFAFANUZI WA HOJA MBALI MBALI ZILIZOFANYIWA
KAZI NA KAMATI
RIPOTI YA UKAGUZI WA HESABU KWA MAWIZARA, MASHIRIKA NA
TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
2.0 UKAGUZI MAALUM WA VIINUA MGONGO
Ukaguzi huu ulifanyika kwa miaka miwili, baina ya mwaka 2010 hadi Machi 2012, kwa
kupitia baadhi ya majalada na kubainika kasoro mbali mbali zikiwemo; kuongezwa kwa
muda wa utumishi wa mstaafu, kuongezwa mshahara wa mwisho ambao hutumiwa
kutayarisha malipo ya viinua mgongo na mstaafu kulipwa mara mbili kinyume na utaratibu.
Ukaguzi umebaini kuwa, kasoro hizi zimejitokeza zaidi katika Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano mara tu yalipofanywa mabadiliko ya mshahara mwezi wa Oktoba 2011. Aidha,
kasoro nyengine zimeonekana katika Chuo cha Mafunzo, Mkoa wa Mjini Magharibi, Wizara
ya Kilimo na Maliasili, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Kikosi Maalum cha Kuzuia
Magendo, Kikosi cha Valantia, Kikosi cha Zimamoto na Uokozi na Jeshi la Kujenga
Uchumi.
Kwa upande wa kuifanyia kazi hoja hii, Kamati ilianza mahojiano yake tokea mwaka
2013/2014 ilipokutana na Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa hoja mbali mbali
zilizotokana na ripoti ya ukaguzi, na kuelezwa kuwa, hoja hii ingepaswa zaidi kufanywa kwa
kukutana na Wizara ya Fedha na taasisi mbali mbali zilizohusika. Hivyo, katika mwaka huu,
Kamati iliifanyia kazi hoja hii katika ratiba ya awali kwa kuipangia Wizara ya Fedha, lakini
kabla ya kazi, ilifanya kikao na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ambapo
Kamati ilipatiwa ufafanuzi pamoja na Mkuu wa Utawala wa Afisi ya Baraza la Wawakilishi
5
na kubainika kuwa, hoja ingestahiki kufanyiwa kazi kwa Taasisi zilizohusika, ambapo
wakati huo Kamati ilifanya marekebisho ya ratiba na kutokana na uchache wa muda, Kamati
haikuweza kukutana na kila taasisi zilizotajwa katika ripoti, isipokuwa imefanikiwa
kukutana na taasisi zote muhimu zilizotajwa zaidi katika hoja hizo ambazo ni hizi zifuatazo:
2.1 CHUO CHA MAFUNZO
Hoja Namba 14.2 Ukaguzi Maalum kupitia mafaili 8 yaliyohusika na ukaguzi
Ukaguzi uliyapitia mafaili manane ya Chuo na kubaini kasoro za kuongezwa kwa muda wa
utumishi wa mstaafu, kuongezwa mshahara wa mwisho ambao hutumiwa kutayarisha malipo
ya viinua mgongo na mstaafu kulipwa mara mbili kinyume na utaratibu.
Majibu ya Chuo
Kwa bahati mafaili hayo hayakutaja wafanyakazi halisi waliohusika na ukaguzi, na hivyo
inakua tabu kuyatambua moja kwa moja. Waliomba Kamati iwapatie muda wa ziada
kuyatafuta na kuyatambua mafaili hayo na walileta taarifa za wastaafu 47 kwa mwaka
2010/2011.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imekubaliana na Chuo kuwa, hoja hii haikutaja wastaafu waliohusika na ukaguzi
moja kwa moja na hivyo inakuwa tabu kuwatambua wastaafu wanaotakiwa, pamoja na
ukweli kwamba, Chuo kilikabidhi kwa Kamati idadi kubwa zaidi ya wastaafu 47, badala ya
wastaafu 8 kama walivyoripotiwa. Aidha, Kamati kabla ya kukutana na Chuo kuhusiana na
hoja hii ilimtaka Afisa Mkaguzi anaefuatana na Kamati kufuatilia majina ya wastaafu hao
katika Afisi yake ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu, lakini alishindwa kupata majina
hayo na hivyo Kamati haikuwa na uhakika wa wastaafu waliohusika isipokuwa kwa
kutegemea majibu sahihi ya Taasisi husika.
Hoja Namba 14.2.1 Kuongezeka kwa malipo ya viinua mgongo, Tsh. 35,899,595
Ukaguzi umebaini kuwepo wastaafu watatu wa chuo walioongezewa mishahara yao kinyume
na taratibu, kwa lengo la kupata viinua mgongo vikubwa ambavyo hawastahiki kulipwa
kulingana na mishahara yao halisi. Wastaafu hao ni Ndg. Jaffar Silima Jaffar, Ndg. Abdu
Makame Vuai na Ndg. Rahma Mgeni Mzee.
Majibu ya Chuo
Chuo kinakubali kuwa na wastaafu wawili tu na sio watatu kama walivyoripotiwa. Ndg.
Jaffar Silima Jaffar na Ndg. Abdu ndio wastaafu halali, lakini Ndg. Rahma Mgeni Mzee, sio
mfanyakazi wao na hawakuwa na taarufa zozote za utumishi wake. Kuhusiana na wastaafu
hao wawili, Chuo kililazimika kuwastaafisha kutokana na maradhi na baada ya kupata
ushauri wa bodi ya madaktari kwa kutoweza kwao kuendelea na kazi.
Walipostaafu waliwalipa viinua vyao mgongo kwa kuzingatia mshahara halali na halisi wa
mwisho wa mwezi, na sio kweli kwamba Chuo kimewazidishia, lakini ni Afisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ndio iliyofanya hivyo na yenye dhamana ya kujibu suala hilo,
kwani viinua mgongo vyote vilipitiwa na Afisi hii na kuhakikiwa.
Kwa mfano, mshahara uliofanyiwa malipo kwa Ndg. Jaffar ni Tsh. 63,200 na Ndg. Abdu
Makame amefanyiwa kiinua mgongo kwa mshahara halali wa mwezi ambao ni Tsh. 61,400
na sio vyenginevyo.
6
Aidha, Chuo kilikataa kuwalipa viinua mgongo wastaafu hao, na baada ya wao kulalamika
kwa barua, Chuo kilimuandikia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuomba muongozo
wao, lakini kwa bahati hadi wanaripoti kwa Kamati, hawakujibiwa barua zao.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha na maelezo ya Chuo kuwa Ndg. Rahma Mgeni Mzee sio mfanyakazi
wao baada ya kupata taarifa za hakika kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Fedha anaefuatana na
Kamati kuwa ni mstaafu wa Wizara ya Afya, na namba yake ya ajira ilikuwa 7105481 na
tarehe 22/3/2012 ndipo Mdhibiti alitoa barua ya mafao yake ya kiinua mgongo aliyolipwa ni
Tsh. 11,024,000/-.
Kuhusiana na taarifa za Ndg. Jaffar na Ndg. Abdu, Kamati ilipoangalia fomu za malipo
zilizotayarishwa na Chuo, ilijiridhisha kuwa, malipo halali waliyoombewa wastaafu hayo ni
mishahara yao ya mwisho kama walivyoeleza Chuo, kuwa Ndg. Jaffar ni Tsh. 63,200 na
Ndg. Abdu Tsh. 61,400, lakini kwa kuzingatia taarifa zao za mishahara (Service Record)
zinaonesha kuwa mshahara wa mwisho wa Ndg. Jaffar ulikuwa Tsh. 93,000/-(badala ya Tsh.
63,200/-) na Ndg. Abdu ni Tsh. 103,000/- (badala ya Tsh. 61,400/-).
Hata hivyo, suala hili halikuweza kuthibitishwa zaidi kwa Kamati kushindwa kupata fomu
kamili zilizotoka Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na hata barua za
kuthibitisha malipo ya wastaafu hao. Aidha, kwa kuzingatia maelezo ya Afisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu katika kikao cha pamoja cha kupata uelewa wa hoja hii kuwa
Afisi ya Mdhibiti tayari ilipogundua mapungufu ya baadhi ya watendaji wake ilichukua
hatua na hivyo, hawana lolote la kusema ama kushirikishwa katika suala hili na kwa kuwa
Kamati ilikosa mashirikiano ya moja kwa moja kwa ufafanuzi kamili wa hoja hii, Kamati
pamoja na uchache wa muda, haikuweza kufuatilia kwa kina suala hili.
Hoja Namba 14.2.2 Wastaafu kulipwa mafao mara mbili, kinyume na utaratibu.
Ukaguzi umebaini kuwepo kwa tatizo la mstaafu, Ndg. Abdu Vuai Makame kulipwa kiinua
mgongo mara mbili kinyume na utaratibu. Mkataba wake wa ajira unaonesha ameanza kazi
tarehe 18/4/1994 na kumaliza tarehe 9/4/2002. Barua ya tarehe 24/7/2008 kutoka kwa
Kamishna wa Chuo inathibitisha kulipwa kiinua mgongo mara mbili baada ya kukatishwa
mkataba wa kazi ingawa alikuwa akidai malipo ya pencheni tu.
Aidha, barua ya tarehe 12/10/2006 kuliyotoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara wa Nchi (OR)
Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ kwenda kwa msaafu na barua ya tarehe 01/08/2008
kutoka kwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo kwenda kwa mstaafu zote zinaeleza wazi
kuwa mstaafu alikuwa hastahiki kupata pencheni kutokana na muda wake wa utumishi.
Katika hatua nyengine ukaguzi umebaini kwamba, mstaafu huyo aliombewa malipo ya
kiinua mgongo kutoka Chuo cha Mafunzo kupitia barua ya tarehe 8/03/2012 yenye kumbu
kumbu namba MF/G.2/Vol.VI/2012 na analipwa kiinua mgongo kwa mara ya pili kupitia
hundi namba 112416 yenye thamani ya Tsh. 8,065,200
Majibu ya Chuo
Chuo kimemlipa kiinua mgongo mara moja tu kwa mshahara wa Tsh. 61,400 na hakijawahi
kulipa pencheni kwa mstaafu huyo, zaidi ya kupokea malalamiko yake ya kulipwa pencheni
ambapo Chuo iliyakataa na mwishowe kuomba muongozo wa kisheria na kihatua kutoka
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ambapo hawajawahi kujibiwa barua yao.
Aidha, Mkaguzi aliegemeza hoja zake kwa kuangalia barua tu bila ya kufanya mahojiano ya
kina na kupatiwa ufafanuzi sahihi wa hoja hizo.
7
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepitia barua hizo zilizonukuliwa na hoja ya ukaguzi lakini haijajiridhisha kwamba,
Chuo cha Mafunzo kimelipa mara mbili kiinua mgongo cha Ndg. Abdu Vuai Makame.
Aidha, Kamati imejiridhisha kwamba, Chuo kiliomba ufafanuzi wa haki ya mstaafu huyo
kulipwa pencheni, lakini hakukuwa na majibu kutoka Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu.
2.2 AFISI YA MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Hoja Namba 14.2 Ukaguzi Maalum kupitia mafaili 5 yaliyohusika na ukaguzi
Katika Afisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, ukaguzi umeyapitia mafaili matano na kubaini
kasoro za kuongezwa kwa muda wa utumishi wa mstaafu, kuongezwa mshahara wa mwisho
ambao hutumiwa kutayarisha malipo ya viinua mgongo na mstaafu kulipwa mara mbili
kinyume na utaratibu.
Majibu ya Afisi ya Mkoa
Mafaili matano yaliyohusika na ukaguzi ni ya Ndg. Pili Salum Said, Ndg. Rehema Mwinyi
Zubeir, Ndg. Idrisa Iddi Siwamoja, Ndg. Salum Haji Haji na Ndg. Nassir Ali Kombo.
Watumishi wote hao wamekaguliwa lakini kasoro zilizoelezwa zilipatikana kwa mtumishi
mmoja tu, Ndg. Pili Salum Said, ambapo kwa upande wa Afisi, haukubaliani na hoja za
ukaguzi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, kasoro zilizoelezwa na ukaguzi zinamhusu Ndg. Pili, ambapo
hoja yake itafafanuliwa katika hoja inayofuata baadae. Kuhusiana na wastaafu wanne
waliobakia, Kamati imekagua mafaili yao na kujiridhisha kuwa hayakuwa na tatizo.
Hoja Namba 14.2.2 Wastaafu kulipwa mafao mara mbili, kinyume na utaratibu
Ukaguzi umebaini kuwepo kwa kasoro ya mstaafu, Ndg. Pili Salum Saidi kulipwa kiinua
mgongo mara mbili kinyume na utaratibu. Aidha, kwa mujibu wa Mkataba wake wa kuingia
kazini, ameanza kazi tarehe 02/08/1999 na kumaliza utumishi wake tarehe 2/12/2011.
Kutokana na utaratibu wa ulipaji wa kiinua mgongo, wastaafu walioajiriwa baada ya mwezi
wa sita mwaka 1998, walitakiwa kulipwa na kupokelea mafao yao ya uzeeni katika Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na sio Hazina. Hata hivyo, ukaguzi umebaini kwamba
Ndg. Pili alilipwa kiinua mgongo ZSSF kwa hundi namba 100144 yenye thamani ya Tsh.
3,137,391 na pia amelipwa Hazina kwa hundi namba 048665 yenye thamani ya Tsh.
8,210,400 ambapo hakustahiki kulipwa.
Majibu ya Ofisi ya Mkoa
Ofisi haina uhakika wa suala hilo lakini inawezekana limefanyika au halikufanyika kwani
alipostaafu Ndg. Pili Ofisi ilitakiwa na ilitayarisha fomu za kiinua mgongo kwa utaratibu
uliowekwa na kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa ajili ya
kufanyiwa uchunguzi wa kisheria kama taratibu zilivyo.
Fomu ya kiinua mgongo kwa Ndg. Pili iliyotayarishwa na Ofisi ya Mkoa inaonesha malipo
ya Tsh. 2,906,107.60/- kwa mujibu wa „formula‟ iliyotumika baada ya masahihisho ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu imeonekana imekosewa na usahihi wake ukafanywa
na Mkaguzi kuwa Tsh. 3,907,200, ambapo Ofisi hii haikuwa na pingamizi dhidi ya
masahihisho hayo na ndiyo yaliyolipwa. Ofisi inashauri Kamati ifuatilie suala hili kwa
8
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, kwa kuwa ndie aliehusika na nyongeza hiyo na
anajua usahihi wake. Pia Kamati ifuatile Wizara ya Fedha au Mfuko wa ZSSF.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepitia faili la mstaafu huyu na kujiridhisha kuwa mshahara wake wa mwisho
ulikuwa Tsh. 132,000/- na ndio uliofanyiwa hesabu za kiinua mgongo chake na Ofisi ya
Mkoa. Pia, Ndg. Pili alizaliwa tarehe 2/12/1951 na ameajiriwa tarehe 9/7/1999 na kustaafu
kwa miaka 60, tarehe 2/12/2011, hivyo hakukuwa na muda wa ziada ya malipo yake.
Hata hivyo, kasoro kubwa iliyobainika na Kamati ni mstaafu huyo kufanyiwa hesabu ya
miezi 148 na sio 144 ambapo Afisa Utumishi alikiri mbele ya Kamati kukosea hesabu hizo,
ingawa anashangazwa na Ofisi ya Mdhibiti kukubali ziada ya miezi hiyo, na kuidhinisha
malipo zaidi. Vile vile, Kamati haikupata uthibitisho wa fomu ya malipo au barua kutoka
Afisi ya Mdhibiti inayoonesha kima halisi na fomula iliyotumika kumlipa mstaafu huyu, na
Kamati imejiridhisha kuwa, udhaifu ulioonekana katika hoja hii, Afisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu inahusika kwa namna moja ama nyengine.
2.3 JESHI LA KUJENGA UCHUMI (J.K.U)
Hoja Namba 14.2 Ukaguzi Maalum kupitia mafaili 8 yaliyohusika na ukaguzi
Ukaguzi uliyapitia mafaili manane ya J.K.U na kubaini kasoro za kuongezwa kwa muda wa
utumishi wa mstaafu, kuongezwa mshahara wa mwisho ambao hutumiwa kutayarisha malipo
ya viinua mgongo na mstaafu kulipwa mara mbili kinyume na utaratibu.
Majibu ya J.K.U
Ni kweli majalada yaliyohusika na ukaguzi yalikuwa manne, lakini ni majalada matatu
ambayo yalionekana na kasoro zilizohusika na hoja. Mafaili hayo ni ya wastaafu, Ndg.
Abdalla Moh‟d Khamis, Ndg. Kombo Adeeti Othman na Ndg. Zakia Abdalla Sleiman na
Uongozi wa J.K.U haukubaliani kuhusika na hoja za ukaguzi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeyapitia mafaili yote manane yaliyohusika na hoja hii na kujiridhisha kuwa, ni
mafaili ya wastaafu watatu ndio yaliyohusika na hoja.
Hoja Namba 14.2.1 Kuongezeka kwa malipo ya viinua mgongo, Tsh. 35,899,595
Ukaguzi umebaini kuwepo wastaafu watatu wa J.K.U walioongezewa mishahara yao
kinyume na taratibu kwa lengo la kupata viinua mgongo vikubwa ambavyo hawastahiki
kulipwa kulingana na mishahara yao halisi. Wastaafu hao ni Ndg. Abdalla Moh‟d Khamis,
Ndg. Ndg. Kombo Adeeti Othman na Ndg. Zakia Abdalla Sleiman.
Majibu ya J.K.U
J.K.U hawakubalini kuhusika na hoja hiyo na badala yake anaehusika ni Afisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu. Kwa mfano, mstaafu Ndg. Abdalla Moh‟d Khamis, fomu
iliyotayarishwa ya kiinua mgongo chake na J.K.U inaonesha alistahiki kulipwa kiinua
mgongo cha Tsh. 20,013,600 lakini baada ya kuiwasilisha faili la mstaafu huyo kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, ndipo walipoelekezwa kwamba, mstaafu anatakiwa
alipwe Tsh. 21,627,600 kama inavyothibitika katika barua ya tarehe 06/02/2012 yenye
kumbu kumbu namba AUD/G.18/2/WF/VOL.XIV/41.
9
Mstaafu, Ndg. Kombo Adeeti Othman fomu ya kiinua mgongo iliyotayarishwa na JKU kuwa
cha Tsh. 30,727,200 lakini baada ya kuiwasilisha faili la mstaafu huyo kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, ndipo walipoelekezwa kulipa Tsh. 32,792,200 kama
inavyothibitika katika barua ya tarehe 06/02/2012 yenye kumbu kumbu namba
AUD/G.18/2/WF/VOL.XIV/41.
Vile vile kwa mstaafu Ndg. Zakia Abdalla Sleiman, inathibitishwa kupitia fomu ya kiinua
mgongo iliyotayarishwa na J.K.U kuwa alistahiki kulipwa Tsh. 11,625,600 lakini baada ya
kuiwasilisha faili la mstaafu huyo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, ndipo
walipoelekezwa kwamba, mstaafu anatakiwa alipwe Tsh. 13,238,400 kama inavyothibitika
katika barua ya tarehe 06/02/2012 yenye kumbu kumbu namba
AUD/G.18/2/WF/VOL.XIV/41.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepitia mafaili ya wastaafu hao pamoja na fomu zao za malipo ya viinua mgongo
vilivyotayarishwa na J.K.U na kuzipitia barua zilizotoka Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu kama zilivyonukuliwa hapo juu na kujiridhisha usahihi wa maelezo ya
J.K.U. Hata hivyo, Kamati imehitaji uthibitisho wa malipo ya wastaafu hawa kwa mujibu wa
hesabu zilizotoka Afisi ya Mkaguzi Mkuu, lakini haikuweza kupatiwa. Aidha, J.K.U
wameshindwa kuwasilisha mbele ya Kamati fomu za malipo zilizotayarishwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, kwa kueleza kuwa hawakuwahi kupewa, ingawa ni haki na
kitaratibu kupewa fomu hizo.
2.4 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
Hoja Namba 14.2 Ukaguzi Maalum kupitia mafaili 22 yaliyohusika na ukaguzi.
Ukaguzi uliyapitia mafaili 22 ya Wizara na kubaini kasoro za kuongezwa kwa muda wa
utumishi wa mstaafu, kuongezwa mshahara wa mwisho ambao hutumiwa kutayarisha malipo
ya viinua mgongo na mstaafu kulipwa mara mbili kinyume na utaratibu.
Majibu ya Wizara
Kati ya majalada 22 yaliyofanyiwa ukaguzi, Wizara imefanikiwa kuyapata 18, lakini kwa
bahati hakukuwa na kasoro yoyote iliyoelezwa katika ripoti ya ukaguzi. Kwa mfano mstaafu
Ndg. Batuli Masoud, Ndg. Safia Ali na Ndg. Moh‟d Ali walirekebishiwa mishahara yao kwa
toleo la Serikali namba OR/UUU/M.140/1/VOL.I/58 la tarehe 17 Oktoba 2011, likitoka kwa
Katibu Mkuu (OR) Utumishi wa Umma Zanzibar. Ndg. Safia alilipwa kwa mshahara wa
Tsh. 231,000/- kwenye vocha ya mshahara wa mwisho, wakati kweye „salary register folio‟
kwa bahati mbaya umerekodiwa Tsh. 230,000/-
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka uthibitisho wa toleo hilo na kupatiwa, ambalo linahusu marekebisho ya
mishahara. Kuhusiana na mstaafu Ndg. Safia Ali, Kamati imejiridhisha kuwa kalipwa kwa
mshahara wa Tsh. 230,000/- badala ya Tsh. 231,000/ ambazo ndizo mshahara halisi
aliostahiki kulipwa, na Kamati ikaridhika na maelezo kuwa Wizara ilikosea kumfanyia
hesabu, lakini tayari malalamiko yake yameshafikishwa sehemu inayohusika na yanafanyiwa
kazi.
Ndg. Batuli Masoud Juma kwa mujibu wa „salary register‟ alilipwa kwa mshahara wa Tsh.
254,000/- badala ya Tsh. 106,426 kama ilivyoelezwa na Wizara na kwa bahati Wizara
imekiri usahihi huo.
10
Aidha, Ndg. Moh‟d Ali Abdalla alilipwa kwa Tsh. 229,000/- tofauti na ilivyoelezwa na
Wizara kuwa kalipwa kwa Tsh. 377,000/. Hata hivyo, ili kujiridhisha na usahihi wa
kiwango gani hasa kimelipwa kwa mishahara ya wastaafu hao, Kamati imeitaka Wizara
kuwasilisha kwa Kamati, fomu za viinua mgongo kutoka kwao kwenda kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ama kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kwenda kwa
Wizara, ambapo fomu hizo nazo zilithibitisha malipo ya wastaafu hao kama tulivyoeleza
hapo juu.
2.5 WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Hoja Namba 14.2 Ukaguzi Maalum kupitia mafaili 22 yaliyohusika na ukaguzi.
Ukaguzi uliyapitia mafaili 69 ya Wizara na kubaini kasoro za kuongezwa kwa muda wa
utumishi wa mstaafu, kuongezwa mshahara wa mwisho ambao hutumiwa kutayarisha malipo
ya viinua mgongo na mstaafu kulipwa mara mbili kinyume na utaratibu.
Majibu ya Wizara
Wizara katika kipindi cha Disemba 2011 na Febuari 2012, ilistaafisha kisheria baada ya
kutimia muda wao kustaafu kwa wafanyakazi wake 16 kwa upande wa Unguja na Pemba 37.
Kati ya wafanyakazi hao 53 waliotengenezewa mafao yao, ilibainika wafanyakazi 12
walitengenezewa mafao yao kwa makosa. Baada ya kugundua hilo, Watendaji wa Wizara
walifuatilia suala hilo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kutaka kujua
ukweli wa suala hilo walipowasiliana na watendaji wa Afisi ya Mdhibiti, waligundua kuwa
kosa hilo limefanyika kweli na wafanyakazi wawili kati ya hao 12 walikuwa wameshapokea
malipo hayo na waliwataka warejeshe fedha hizo kwa haraka.
Pamoja na kuwa watendaji wa Wizara ndio waliogundua kasoro hizo, watendaji wa Afisi ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu walimuandikia barua Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kumjuulisha juu ya suala hilo ambae nae alichukua
hatua za kuiandikia Wizara yao.
Wizara ilichukua hatua za kuwasimamisha kazi wafanyakazi wanne, mmoja wa Makao
Makuu na wengine watatu wa Ofisi Kuu Pemba. Aidha, Wizara iliunda Kamati Maalum ya
kuchunguza suala hilo na kutoa mapendekezo kwa uongozi wa Wizara ambao uliyafanyia
kazi mapendekezo hayo. Hivyo, wafanyakazi waliobainika kushiriki katika suala hili,
walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa makosa waliyoyafanya kama Sheria ya
Utumishi wa Umma ya mwaka 2011 inavyoelekeza.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha juu ya usahihi wa taarifa za Wizara kuwa chanzo halisi cha
udanganyifu uliofanyika kupitia viinua mgongo ni Ndg. Mgeni Ramadhan Suwed, mmoja
kati ya wastaafu katika mwaka uliofanyiwa ukaguzi. Ndg. Mgeni alistahiki kupokea kiinua
mgongo cha Tsh. 10,708,800 lakini wakati anakwenda kupokea kiinua chake mgongo
alitakiwa kulipwa Tsh. 21,964,800, na aliyesimamia malipo hayo ni Afisa Utumishi
aliyekuwepo wakati huo Ndg. Ali Hassan.
Dg. Mgeni kwa uchamunu wake na uaminifu aliokuwa nao, alieleza kuwa hastahiki fedha
hizo, lakini alinasihiwa sana na Ndg. Ali achukue kwani mgao huo (wa ziada ya kiinua
mgongo halali) pia unalipwa (kinyume na taratibu) kwa Mkurugenzi wa masuala ya
Utumishi, Ndg. Rajab Uweje. Hali hii ilimpelekea Ndg. Mgeni kufika kwa Mkurugenzi
Uweje na kumueleza hali ilivyo, lakini kwa bahati Ndg. Uweje akamhakikishia kuwa yeye
11
hayumo katika udanganyifu huo na hana mgao wowote, na ndipo alipoanza kulifikisha suala
hilo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na hatimae suala hilo likafuatiliwa kama
ilivyoelezwa na Wizara.
Kamati pia imejiridhisha kuwa, suala hili lilifanywa zaidi na Afisa huyo Utumishi wa Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano, lakini kwa mashirikiano ya karibu na kuhusika kwa
baadhi ya Maofisa wa Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu pamoja na baadhi ya
Maofisa wa Wizara ya Fedha.
Hoja Namba 14.2.1 Kuongezeka kwa malipo ya viinua mgongo, Tsh. 35,899,595
Ukaguzi umebaini kuwepo wastaafu watano wa Wizara, waliongezewa mishahara yao
kiyume na taratibu kwa lengo la kupata viinua mgongo vikubwa ambavyo hawastahiki
kulipwa kulingana na mishahara yao halisi. Wastaafu wenyewe ni hawa wafuatao:
Nam Jina Malipo ya
awali
yaliyopangwa
kulipwa
Malipo
yaliyostahiki
kulipwa
Tofauti
1. Mgeni Ramadhan
Suwed
21,964,800 10,708,800 11,256,000
2. Moh‟d Ismail Moh‟d 20,428,800 10,188,800 10,240,000
3. Ibrahim Elius Kilundira 725,578 248,769.60 476,808
4. Khamis Ali Kombo 5,224,892.40 4,979,277 245,615
5. Ali Haji Mcha 5,046,263.60 4,912,292 133,972
Majibu ya Wizara
Wizara inakiri juu ya ukweli wa hoja hii na wao waliwahi kuwalipa Ndg. Mgeni na Ndg.
Moh‟d Ismail, lakini baada ya kugundua mwenyewe na kwa khiari yake, Ndg. Mgeni
alizirejesha fedha hizo na kwa hivyo, alilipwa fedha alizostahiki na fedha za ziada alizolipwa
Tsh. 11,256,000/- zilirejeshwa Wizara y Fedha kwenye akaunti namba 9928161504.
Ndg. Moh‟d Ismail alilipwa Tsh. 20,428,800 kwa makosa, wakati anastahiki kulipwa Tsh.
10,240,000/. Hatua ambazo Wizara ilizichukua baada ya kugundua ilimwita na kumtaka
arejeshe fedha za ziada alizolipwa kwa makosa. Kwa bahati alikuwa tayari ameshazitumia
zote na Wizara ilimtaka azirejeshe fedha hizo na Ndg. Moh‟d aliahidi kuzirejesha mara tu
atakapozipata. Kwa hivi sasa mhusika amesimamishwa kulipwa pencheni ya kila mwezi
kufidia deni hilo.
Aidha, wastaafu waliobakia wote walilipwa viinua vyao mgongo sahihi wala hakukuwa na
udanganyifu wowote uliotokea, baada ya kufanyiwa uhakiki hesabu za awali ambazo kweli
hapo mwazo zilikosewa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeridhishwa na majibu ya Wizara kuhusiana na ukweli wa hoja hii. Na
imejiridhisha kuwa, kasoro zilizojitokeza zilichangiwa na kusababishwa na Afisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Wizara ya Fedha.
12
Hoja Namba 14.2.3 Malipo ya Viinua Mgongo yaliyobainika kuwa na udanganyifu
ambayo hayakuwahi kulipwa, Tsh. 48,570,917
Fedha hizo ni ziada ya fedha ambazo zilitarajiwa zilipwe kwa wastaafu mbali mbali, lakini
kutokana na kasoro iliyobainika ya kuongezwa muda wa utumishi wa wastaafu hao, fedha
hizo hazijawahi kulipwa.
Nam Jina Malipo ya
awali
yaliyopangwa
kulipwa
Malipo
yaliyostahiki
kulipwa
Tofauti
1. Fasihi Mtumweni Ali 12,000,000 7,000,000 5,000,000
2. Bogo Isabu Khamis 12,304,000 6,592,600 5,712,000
3. Jongo Juma Mtwana 12,672,000 7,392,000 5,280,000
4. Mzee Khamis Mzee 11,857,200 5,492,833 6,364,367
5. Simai Makame Pandu 11,785,600 6,705,600 5,080,000
6. Kassim Haji Ameir 19,401,200 10,389,400 9,011,800
7. Fatma Rashid Said 12,000,000 7,336,000 6,136,000
8. Hamad Saleh Hamad 12,240,000 7,140,000 5,100,000
9. Ramadhan Khatib Ali 2,678,250 319,500 2,358,750
JUMLA KUU 106,938,850 58,367,933 48,570,917
Majibu ya Wizara
Kama walivyoeleza awali kuwa, wastaafu hao hawakuwahi kulipwa kwa udanganyifu
kutokana na juhudi za Wizara yenyewe baada ya kugundua kupitia kwa Mstaafu mwaminifu,
Ndg. Mgeni na kulifanyia kazi suala hili ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za
kinidhamu waliohusika.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeridhishwa na usahihi wa maelezo ya Wizara ispokuwa imehoji juu ya Wizara
kutowachukulia hatua za kijinai watendaji wake waliohusika, wakati suala hili sio tu la
kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu wakati kosa lililofanyika linahusika na wizi na
kuvunja uaminifu.
Mapendekezo ya Kamati (kwa hoja zote zinazohusiana na Ukaguzi wa Kiinua
Mgongo)
Ni kweli Kamati imejiridhisha kuwepo kwa udanganyifu uliotajwa katika ripoti ya Mkaguzi
kuhusiana na suala zima la Viinua Mgongo na udanganyifu huo ulitokea baina ya Maofisa
Utumishi wa Taasisi husika kwa mashirikiano na Maofisa wa Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali na Wizara ya Fedha. Hivyo, Kamati inapendekeza ifuatavyo:
Wale wote waliohusika na udanganyifu huo wachukuliwe hatua za kinidhamu na
kisheria.
Serikali iimarishe „database‟ ya wafanyakazi, ili iwe rahisi kuzipata taarifa za
wafanyakazi wote.
Serikali iunde Kamati Maalum ya kufuatilia hatua sahihi zilizochukuliwa na Afisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
dhidi ya watendaji wao waliohusika na udanganyifu huo na ambao tayari
walikwishachukuliwa hatua kabla ya ukaguzi wa Kamati ya P.A.C.
13
Kamati inamshauri Mdhibiti kuweka wazi taarifa za hoja anazoziripoti, ili ziwe ni
taarifa za wazi na kujitosheleza na kuiwezesha Kamati kuzifuatilia hoja hizo kwa
urahisi.
3.0 UKAGUZI WA HESABU WA MAWIZARA NA TAASISI ZA SERIKALI
KWA MWAKA 2011/2012
3.1 WIZARA YA FEDHA
Hoja Namba 15.1 Matokeo ya Hesabu za mwisho wa mwaka.
Taarifa za mapato na matumizi.
Wizara ya Fedha iliidhinishiwa kukusanya Tsh. 248,260,661,000 kwa mwaka 2011/2012.
Hadi kufikia Juni 2012, mapato yaliyokusanywa yalikuwa Tsh. 286,962,675,000.44 ambayo
ni sawa na asilimia 115 ya makadirio.
Kwa upande wa matumizi ya kawaida, fedha zilizoainishwa ni Tsh. 47,020,000,000/- na
fedha halisi zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 33,912,500,000/- ikiwa ni pungufu ya Tsh.
13,107,500,000 sawa na asilimia 27.9 ya makadirio. Aidha, matumizi ya maendeleo, Wizara
iliidhinishiwa kutumia Tsh. 7,240,000,000/-, lakini mwisho wa mwaka ulipofika, fedha
zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 6,144,663,000, sawa na asilimia 85 ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Taarifa za makisio ya makusanyo ni sahihi, isipokuwa taarifa ya fedha zilizopatikana
hazikuwa Tsh. 286,962,675,000.44 na usahihi ni Tsh. 240,339,913,699.44. Kufanikiwa
kuongeza makusanyo kunatokana na kupata baadhi ya mapato ambapo vyanzo vyake
havikukadiriwa kukusanywa katika upangaji wa bajeti.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji sababu zinazopelekea Wizara hii kuvuka lengo la makusanyo wakati Wizara
nyengine na taasisi za Serikali hazifikii, wakati kwa kiasi kikubwa makisio yao ya
makusanyo yanaongozwa na Wizara hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuwa na vigezo sahihi vya makusanyo ya mapato, ili Taasisi zote
ziwe na rikodi nzuri za kiwango cha mafanikio ya makusanyo halisi.
Hoja Namba 15.4 Malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu), Tsh.
295,977,000
Fedha hizo zimelipwa kwa matumizi mbali mbali lakini vielelezo husika havikupatikana kwa
ukaguzi, na hivyo, uhalali wa malipo hayo haukuweza kuthibitishwa.
Majibu ya Wizara
Ni kweli wakati wa ukaguzi vielelezo hivyo havikuwepo kutokana na matumizi husika
yanayohusu safari za viongozi kuwa na taratibu tofauti na safari za kawaida. Hata hivyo,
wakati Mkaguzi anafanya mkutano wa kuingia na kutoka (entry and exit meeting), Wizara
ilimuandikia kuwa vielelezo vipo, arudi kwa ajili ya ukaguzi. Lakini Mkaguzi huyo hajaja
hadi leo Kamati ipofika kwa ukaguzi wake.
14
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka ushahidi wa maandishi wa barua ambayo Wizara iliiandikia Afisi ya
Mkaguzi kuhusiana na vielelezo hivyo, ambapo Wizara haikuweza kutoa kwa maelezo kuwa
waliwasiliana kwa mazungumzo tu, bila ya maandishi. Hata hivyo, Kamati imejiridhisha
kuwa matumizi hayo yalihusu viongozi wa Kitaifa ambapo taarifa za safari zao huwa siri
kwa maslahi ya usalama, lakini haikubaliani kukiukwa kwa sheria kwa sababu hiyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuzingatia sheria kwa matumizi ya fedha za Serikali pamoja na
matumizi hayo kuwahusu viongozi wa kitaifa.
3.2 WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO
Hoja Namba 15.2 Ujenzi wa uzio wa maeneo ya Chumbuni na Bungi, Tsh.
474,810,000
Ukaguzi umebaini kuwa Wizara ya Fedha imefanya malipo ya fedha hizo kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kupitia Kitengo cha Madeni ya Serikali
(Public Debt) kwa hati namba P/D 05/11/2011 yenye hundi namba 048084 ya tarehe 2
Novemba, 2011 na katika malipo hayo, Tsh. 281,041,000 ni kwa ajili ya ujenzi wa uzio
eneo la Chumbuni na Tsh. 193,769,000 kwa ajili ya ujenzi wa uzio eneo la Bungi.
Aidha, ukaguzi umebaini kuwa, fedha zilizotumika katika ujenzi huo hazilingani na hali
halisi ya uzio huo. Wizara ilijenga uzio kwa kutumia waya (senyenge) wakati fedha
zilizoingizwa zilikuwa na uwezo wa kujenga ukuta utakaokuwa madhubuti na utakaodumu
kwa muda mrefu.
Majibu ya Wizara
Ni kweli fedha hizo ziliingizwa na kutumiwa kwa ujenzi wa uzio wa waya kama
ulivyolelezwa, lakini sio sahihi kuwa fedha hizo zingelitosha kujengea uzio wa ukuta. Eneo
la Chumbuni lina ukubwa wa hekta 17 na lenye mzunguko wa kilomita 3.5 sawa na mita
3500. Aidha, makisio ya Wakandarasi walio wengi walioandikiwa kutoa makisio ya kazi
hiyo walithibitisha kuwa, ujenzi wa ukuta wa tofali ungeligharimu Tsh. 640,500,000/-,
gharama ambazo bado hazijajumuisha kazi za uwekaji wa msingi, uwekaji wa zege kwenye
nguzo na usafishaji wa eneo husika.
Eneo la Bungi linaukubwa wa hekta 14 na mzunguko wa mita 2700, ambapo ujenzi wa ukuta
ungeligharimu Tsh. 494,100,000/, gharama ambazo hazijajumuisha uchimbaji wa msingi,
uwekaji wa zege kwenye nguzo na usafishaji wa eneo. Aidha, gharama za ukuta kama huo
wenye mzunguko wa kilomita 3.5 kwa ujenzi wa kuta za zege unahitaji Tsh. 300,000 kwa
mita moja ya mraba na kwa kuzidisha mita za mraba 8,100, zitakuwa Tsh. 2,430,000,000/-,
na sio kama zilivyoelezwa na Mkaguzi.
Kuhusiana na taratibu za kupatikana kwa mjenzi, Wizara imetumia kifungu cha 146(3) cha
Kanuni ya Manunuzi na 67(1)(ii) na kutumia Idara ya Majenzi ya Serikali kwa kufuata
kifungu cha 63 cha Kanuni za Manunuzi.
Sababu kuu za ujenzi huo ni wa uharaka wa kuondoshwa mnara wa redio medium wave ni
kunusuru hatari iliyotolewa na Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ya mnara huo
uliokuwepo Chumbuni, kuhatarisha urukaji na utuaji wa ndege za Kimataifa, hali ambayo
ingelipelekea kuanguka kwa uchumi na kudhoofika kwa sekta ya utalii Zanzibar.
15
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, msingi wa ujenzi huo ni barua ya tarehe 17 Machi, 2011
kutoka Mamlaka ya TCAA na baada ya kupokelewa kwa barua hiyo, Idara ya Habari kwa
muongozo wa Wizara ilipeleka Waraka Serikalini na kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu
wa kufuatilia suala hilo ambapo baada ya utafiti, walipeleka taarifa yao Baraza la Mapinduzi
na kuangizwa kuhamishiwa kwa mnara huo, kujengwa uzio wa Chumbuni na eneo jipya
lililohamishiwa mnara huo, Bungi pamoja na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na walinzi
huko Bungi, kama Kamati ilivyojiridhisha kupitia barua ya tarehe 11/08/2011 yenye kumbu
kumbu namba BLM/30/M/C.6/VOL.VI/13. Na ndipo Wizara ya Habari ilitekeleza ujenzi
huo kufuatia agizo hilo.
Pamoja na usahihi wa ujenzi wa uzio kufuatia kupokea maelekezo ya Baraza la Mapinduzi,
kwa mujibu wa gharama zilizoainishwa katika barua husika, Kamati hairidhishwi na
kutokuwepo kwa juhudi zozote za kujengwa ukuta wa matofali, ambao ndio madhubuti, na
inaamini ujenzi wa uzio hautafikia lengo, kwa kukosa umadhubuti, pamoja na usahihi kuwa,
ukuta wa tofali una gharama kubwa kuliko wa senyenge.
Kuhusiana na hatua za kisheria zilizofuatwa kwa ujenzi huo, Kamati imehoji iwapo njia hiyo
ilipata idhini ya Bodi ya Zabuni kama inavyoelezwa na kifungu cha 32 cha Sheria ya
Manunuzi na iwapo ilifuatiliwa na Kamati ya Tathmini kama inavyotakiwa kuundwa na
kutekeleza majukumu yake kisheria, mambo ambayo kwa ujumla wake yametekelezwa na
Kamati ya Wataalamu iliyoundwa.
Pia, kifungu cha 67 kilichotumiwa na Wizara kinahusiana na bidhaa „goods‟ na sio kazi za
ujenzi husika, na hivyo, bado haikidhi kuthibitisha kuwa, taratibu sahihi za manunuzi
zimefuatwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuzingatia sana ujenzi utakaodumu kwa muda mrefu na sio kufanya
matumizi ambayo kudumu kwake ni kwa muda mfupi. Aidha, Kamati inaishauri Wizara
kufuata ipasavyo taratibu za manunuzi katika matumizi yoyote ya fedha za Serikali.
Hoja Namba 15.3 Ujenzi wa nyumba pamoja na kutengeneza mnara wa matangazo
eneo la Bungi, Tsh. 1,021,790,000
Ukaguzi umebaini kuwa Wizara ya Fedha imefanya malipo ya fedha hizo kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kupitia Kitengo cha Madeni ya Serikali
(Public Debt) kwa hati namba P/D 05/11/2011 yenye hundi namba 048084 ya tarehe 2
Novemba 2011 na hati namba P/D 23/12 yenye hundi namba 048335.
Ukaguzi umebaini kuwa, kazi za ujenzi wa mnara huo zilifanyika kwa kuhamisha vifaa vya
mnara wa zamani uliokuwepo Chumbuni na kuupeleka Bungi. Aidha, ukaguzi umebaini hata
gharama za kutengeneza mnara ni kubwa, kwani fedha hizo zimeingizwa na kutumika kwa
kujenga mnara mpya kwa kutumia vifaa vipya.
Majibu ya Wizara
Sio kweli kuwa Tsh. 398,000,000 ambazo zimeainishiwa kutumika kwa kuhamishia mnara
huo zingelitosha kujengea mnara mpya wa redio wa medium wave. Kuna tofauti kubwa ya
ujenzi wa mnara huo na minara mengine ya redio za FM, mawasiliano ya simu au kuongozea
meli. Mnara huo uliohamishiwa Bungi, una urefu wa mita 150 na ulijengwa 1971 na
16
kampuni ya Hurish Tower Co. Ltd ya Ujerumani kwa USD 1,527,000 na mnara kama huo
haupo popote Afrika ya Mashariki na Kati.
Sweden kwa mfano mwaka 1985 walijenga kwa sawa na gharama USD 3,125,000. Hivyo,
Tsh. 398,000,000 hazingelitosha kujenga mnara mpya. Hata hivyo, Wizara imetafuta vifaa
vingi vipya vinavyohusu usimamizi wa mnara huo isipokuwa viunzi (sections) 21 vyenye
urefu wa mita 7 kila kimoja, ndivyo vilivyorejeshwa wakati wa kuusimamisha tena.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imezingatia hoja hii ya ukaguzi lakini imeshindwa moja kwa moja kulinganisha na
bei halisi ya mnara mpya, ambapo ripoti haijaonesha mlingano wa bei hiyo. Aidha,
ilipohitaji kuelezwa bei ya mnara mpya kama huo, ilielezwa na Wizara kuwa ungeligharimu
kwa bilioni 2 na nusu.
Aidha, pamoja na kuelezwa kuwa fedha zilizotumika katika hoja hii ni Tsh. 1,021,790,000
lakini ripoti hiyo inathibitisha kuwa, Tsh. 398,000,000 zimetumika kwa ajili ya kuhamishia
mnara kutoka Chumbuni hadi Bungi, na Tsh. 623,790,000 zimetumika kwa ujenzi wa
nyumba za wafanyakazi na walinzi eneo la Bungi, lakini ukaguzi haukuhoji matumizi ya
ujenzi wa nyumba, jambo ambalo lilipaswa nalo kutolewa ufafanuzi wake.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Afisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu kutoa ufafanuzi wa
kutosha katika ripoti zake na anapohoji ukubwa wa gharama za suala lolote, ni vyema
akaainisha gharama ndogo zilizofanyiwa utafiti wa kitaalamu.
3.3 WIZARA YA NCHI (OR) TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA
S.M.Z
3.3.1 KIKOSI CHA VALANTIA
Hoja Namba 20.1 Hesabu za mwisho wa mwaka
Taarifa za mapato na matumizi
Kwa mwaka 2011/2012, Kikosi kiliidhinishiwa kutumia Tsh. 2,802,616,659 kwa kazi za
kawaida na fedha halisi iliyoingizwa ni Tsh. 2,802,616,659, sawa na 100% ya makadirio.
Kwa upande wa matumizi ya maendeleo, Kikosi kiliidhinishiwa kutumia Tsh. 100,000,000
na fedha halisi zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 90,000,000 sawa na wastani wa 90% ya
makadirio.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati imetaka kujua iwapo kuna athari zozote zilizopatikana kwa Kikosi kushindwa
kuingiziwa Tsh. 10,000,000 kwa kazi za maendeleo, na Kikosi kilithibitisha kuathirika
katika baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kushindwa kukamilisha ujenzi wa
mesi yao. Hata hivyo, Kamati imetaka kujua iwapo ujenzi huo umefuata taratibu za kisheria
na kuelezwa kuwa, msimamizi wa Ujenzi huo anatoka katika Kikosi cha Zimamoto na
Uokozi, na kwa hatua hiyo Kikosi kimefuata taratibu za sheria.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Kikosi kutafuta Mjenzi na Mshauri Elekezi wa Ujenzi kwa kuzingatia
Sheria ya Manunuzi na Ugavi na sio kuzingatia urahisi na uhusiano wa kikosi kimoja na
chengine.
17
Hoja Namba 20.2 Malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu), Tsh.
90,000,000
Fedha hizo zimetumika kwa matumizi mbali mbali lakini vielelezo havikupatikana kwa
ukaguzi.
Majibu ya Kikosi
Ni kweli wakati wa ukaguzi vielelezo hivyo havikupatikana. Na Kikosi kilipotambua kasoro
hiyo, walijikuta tayari wamesharipotiwa katika ripoti ya Mkaguzi. Hata hivyo, juhudi
waliyoichukua ni kwenda Ofisini bila ya kuwa na maandishi yoyote ya barua.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati haikuridhika na hoja ya Kikosi, na kwa mujibu wa Kanuni za Fedha, kutokuwa na
risiti mara tu matumizi ya fedha za Serikali yanapofanyika, ni kosa la kisheria. Aidha,
majibu ya Kikosi kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu, hayakufuata taratibu. Hata
hivyo, Kamati imeshuhudia kuwepo kwa vielelezo hivyo, lakini haiwezi kukubaliana na
ilichokifanya Kikosi wala haikuwa na uwezo wa kufanya ukaguzi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Kikosi kufuata ipasavyo Sheria na Kanuni za Fedha wakati inapotumia
fedha za Serikali.
Hoja Namba 20.3 Malimbikizo ya madeni, Tsh.252,625,000
Fedha hizo zinadaiwa na wafanyabiashara pamoja na taasisi mbali mbali kwa ajili ya utowaji
wa huduma kwa Kikosi, lakini madeni hayo ni ya muda mrefu na kuwepo kwake ni kwenda
kinyume na mfumo sahihi wa kiuhasibu unaotambua mapato na matumizi kwa fedha taslim
ambao unatumika kwa Mawizara ya Serikali.
Majibu ya Kikosi
Ni kweli walikuwa na madeni hayo kwa muda mrefu, lakini tayari yamechukuliwa hatua ya
kulipwa, ingawa bado hayajamalizika. Kwa mfano deni la Regalia, Kikosi kimepokea barua
kutoka Wizarani kuwa tayari ameshalipwa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka kuthibitishiwa kwa kupewa barua ya malipo hayo ya deni la Regalia, lakini
Kikosi kimeshindwa kuthibitisha kwa barua. Aidha, Kamati imetaka ushahidi mwengine
wowote wa kulipwa kwa deni hilo, ambao nao haukuweza kupatikana, zaidi ya Kikosi
kuahidi kufuatilia Wizarani na kuijuulisha Kamati.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Kikosi kuhakikisha kuwa kinafuatilia madeni yake kwa uhakika na
kinayalipa kama yanavyotakiwa.
Hoja Namba 20.4 Taarifa ya ukusanyaji wa mapato
Kikosi kinatoa huduma ya ulinzi kwa taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi na kujipatia
mapato, lakini taratibu za ukusanyaji wa mapato hayo hazifuatwi kisheria. Aidha, kasoro
zilizopo katika ukusanyaji huo ni kukosekana kwa vitabu vya stakabadhi za mapato,
kutotayarishwa kwa daftari la fedha taslim (Cash Book) na kutokuwepo kwa hesabu ya
mapato ya Kikosi.
18
Vile vile Kikosi hakikufungua hesabu juu ya ukusanyaji wa mapato yake ya ndani na
kupelekea uvujaji wa mapato na matumizi mabaya ya fedha za Umma. Aidha, ukaguzi
umeshindwa kupata taarifa za mapato na matumizi kutokana na kutayarishwa kwa daftari la
mapato na matumizi, ambalo lingelitoa taarifa za fedha zilizokusanywa na zilizotumiwa. Pia
ukaguzi umebaini Tsh. 64,674,000 zimekusanywa lakini taarifa za fedha iliyowasilishwa
kwa ukaguzi ilikuwa ni Tsh. 6,270,000, huku tofauti ya Tsh. 58,404,000/- hazijuulikani
taarifa zake.
Majibu ya Kikosi
Ni kweli taarifa za Mdhibiti na takriban taarifa zote za mapato zimebaki Kikosini. Aidha,
kuhusiana na risiti zinazotumiwa na Kikosi kwa ajili ya malipo, hapo awali zilikuwa za
Kikosi lakini kasoro hiyo imerekebishwa na hivi sasa wanatumia risiti za Serikali.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji hali ilivyo sasa ya utowaji wa huduma kwa Kikosi na kuelezwa kuwa,
Kikosi kinatoa huduma kwa taasisi za Serikali pekee na wala hakitoi huduma za ulinzi kwa
watu binafsi. Kuhusiana na hoja, Kamati imejiridhisha kuwepo kwa kasoro zilizoelezwa na
Mdhibiti.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imewataka Viongozi wa Kikosi kufanya marekebisho ya haraka kwa kufungua
akaunti kwa mujibu wa sheria ili mapato yote yanayokusanywa yaingizwe katika akaunti
hiyo, kutumia risiti za Serikali kwa kukusanya mapato na kuwa na daftari kama
alivyoelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
Hoja Namba 20.5 Matumizi yaliyofanyika kinyume na vifungu, Tsh. 21,529,660
Kuna baadhi ya malipo yamefanyika kinyume na vifungu vilivyoidhinishwa na Baraza la
Wawakilishi, huku taratibu za uhaulishaji hazikufuatwa kinyume na maelekezo ya Sheria.
Majibu ya Kikosi
Ni kweli wamefanya uhaulishaji kinyume na kufuata taratibu za Sheria kutokana na taratibu
hizo zinachukua muda mrefu na zina urasimu mwingi. Hata hivyo, Kikosi kimefanya kosa
hilo kwa kutokujua lakini sasa wamesharekebisha kasoro hizo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwua, Kikosi kimeshindwa kufuata taratibu za uhaulishaji kama
zinavyoelekezwa na Sheria na kupelekea kwa Kikosi kufanya matumizi kinyume na
maelekezo ya Baraza la Wawakilishi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imekitaka Kikosi kufuata ipasavyo Sheria za uhaulishaji ili kuepuka kufanya
matumizi kinyume na makusudio.
3.4 OFISI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS
Hoja Namba 49.1 Hesabu za Mwisho wa mwaka. Taarifa kuhusu mapato na
matumizi ya kazi za kawaida na kazi za maendeleo
Mapato yanayotokana na ada za hifadhi mazingira na ada za ukaguzi wa mazingira,
yalikadiriwa kukusanywa kwa Wizara hii Tsh. 9,000,000 kwa mwaka 2011/2012, lakini
mapato yaliyopatikana ni Tsh. 5,978,000 sawa na 66.4 asilimia ya makadirio. Matumizi ya
19
kazi za kawaida ni Tsh. 1,493,000,000 lakini matumizi halisi yalikuwa Tsh. 1,830,250,655
sawa na asilimia 122.6 ya makadirio.
Aidha, kwa upande wa matumizi ya maendeleo, Ofisi ilikadiriwa kutumia Tsh. 155,000,000,
lakini matumizi halisi yalikuwa Tsh. 140,000,000/- sawa na asilimia 90.3 ya makadirio.
Majibu ya Ofisi
Baada ya kueleza vyanzo vyao vya mapato, Ofisi ilieleza kuwa haikuridhika kama
ilivyokuwa kwa Kamati, hawajaridhika na kasi ndogo ya ukusanyaji wa mapato. Wizara
itakabiliana na changamoto hii kwa kupitia Sheria mpya ya Mazingira iliyopitishwa karibuni
na Baraza la Wawakilishi.
Kuhusu matumizi ya kawaida, Ofisi ilisema yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa
kima cha mshahara, na athari za kutokamilika kwa bajeti ya matumizi ya maendeleo
kumeathiri shughuli kadhaa, ikiwa ni pamoja na kulazimika kukatisha matumizi ya gari
Pemba pamoja na matumizi mengine.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwa kuzingatia uhaba wa mapato kuwa, miradi mingi inayotakiwa
kufanyiwa ukaguzi wa kimazingira huwa haifanyiwi. Aidha, Kamati inahoji Serikali kuwa
na miradi mingi wakati mmoja ambayo inashindwa kutekelezeka, na kwa nini kusiwe na
miradi michache ambayo utekelezaji wake utakuwa fanisi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Ofisi kuangalia zaidi suala la ukaguzi wa kimazingira kwa miradi mbali
mbali inayopitishwa na Serikali na kulifanya hilo pia kwa azma ya kuongeza mapato. Aidha,
kuhusiana na suala zima la uandaaji na utekelezaji wa miradi, Kamati inaishauri Serikali
kuwa na miradi michache inayotekelezeka kuliko kuwa na miradi mingi ambayo inaachwa
njiani.
3.4.1 TUME YA UKIMWI
Hoja Namba 50.1 Hesabu za Mwisho wa mwaka. Taarifa ya matumizi ya kazi za
kawaida na kazi za maendeleo.
Kwa mwaka 2011/2012, Tume ilikadiriwa kutumia Tsh. 472,000,000 kwa kazi za kawaida
na fedha halisi iliyoingizwa ni Tsh. 518,535,274 sawa na asilimia 109.9 ya makadirio.
Kwa upande wa matumizi ya maendeleo, Tume ilikadiriwa kutumia Tsh. 90,000,000 na
fedha hizo hizo zimeingizwa na kutumika, sawa na asilimia 100.
Majibu ya Tume
Ongezeo la matumizi ya kazi za kawaida linatokana na kuongezwa kwa mishahara.
Ongezeko hilo lilikuwa ni la Tsh. 6,083,414.00 kwa mwezi.
Uchunguzi wa Kamati
Ongezeko la matumizi ya kazi za kawaida linalotokana na ongezeko la mishahara,
limeshuhudiwa kujirejea katika Taasisi mbali mbali za Serikali, na hili linatokana zaidi na
Serikali kutoainisha matumizi hayo katika bajeti husika, huku ikifahamu wazi kuwa, katika
mwaka kunakuwa na ongezeko la mishahara.
Mapendekezo ya Kamati
20
Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha inajipanga mapema katika ongezeko la mishahara,
ambalo takriban huathiri matumizi ya kazi za kawaida za taasisi zake.
3.5 OFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS
Hoja Namba 13.1 Uwasilishaji wa hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi
Kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Fedha namba 12 ya mwaka 2005, inakitaka taasisi zote za
Serikali zitayarishe na kufunga hesabu zao za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi. Hata hivyo,
uwasilishaji huo usizidi tarehe 30 ya mwezi wa Septemba ya kila mwaka, lakini Ofisi hii
imechelewa kwa kuwasilisha hesabu zao tarehe 3 Octoba, 2012.
Majibu ya Ofisi
Ni kweli Ofisi ilichelewa kuwasilisha hesabu hizo kwa wakati, lakini sasa wamechukua
hatua za kutorejea tena kosa hilo, na tokea lilipotokezea awali, kasoro hiyo haikutokezea
tena katika miaka iliyofuata.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imesikitishwa na Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kuchelewa kuwasilisha hesabu
zao za mwisho wa mwaka kwa wakati, kutokana na umuhimu wa Ofisi hii kuwa kioo kwa
taasisi nyengine za Serikali.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, kufanya haraka marekebisho ya kasoro
hii, kwani Ofisi hii ndio kioo na kigezo kwa taasisi nyengine za Serikali.
Hoja Namba 51.1 Hesabu za Mwisho wa mwaka
Taarifa kuhusu mapato na matumizi ya kazi za kawaida na kazi za maendeleo
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais imekusanya Tsh. 9,374,100 na matumizi ya kawaida
yalikadiriwa kuwa Tsh. 2,611,000,000 na fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh.
3,118,818,842 sawa na asilimia 119.4 ya makadirio. Aidha, kwa upande wa matumizi ya
maendeleo, Ofisi ilikadiriwa kutumia Tsh. 715,000,000, na fedha zote hizo ziliingizwa na
kutumiwa, sawa na asilimia 100 ya makadirio.
Majibu ya Ofisi
Makusanyo hayakuwa makubwa kutokana na mapato yake kutegemea huduma za uchapaji
zinazotolewa chini ya Idara ya Uchapaji, ambapo mashine za uchapaji zimechakaa. Hata
hivyo, makusanyo hayo yameongezeka kutokana na kuhamishiwa kiwanda hicho Maruhubi
na kuwepo kwa baadhi ya vifaa vipya vya uchapaji. Aidha, kazi ya mwanzo ni kuchapisha
bajeti za Serikali, hali inayopelekea kuokoa fedha nyingi za Serikali.
Kuhusiana na ongezeko la matumizi ya kawaida, linatokana na ongezeko la mishahara
ambayo hapo wakati wa kuandaa bajeti haikuweza kuzingatiwa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati haikukubaliana na maelezo ya Ofisi kwa kuzingatia makusanyo ya mwaka
2010/2011 ambayo yalikuwa 18%, mwaka 2011/2012 ni 17% na mwaka 2012/2013
yalikuwa 43%, hali ambayo haioneshi hoja ya uchakavu wa mitambo kuwa hoja madhubuti,
huku Kamati inaona ni kukosekana kwa mipango madhubuti ya ukusanyaji wa mapato.
21
Aidha, Kamati imehoji juu ya malipo yanayofanywa na taasisi za Serikali zinazopatiwa
huduma katika Idara ya Upigaji Chapa, na Ofisi ilijibu kuwa, fedha zote kwa ajili ya bajeti
kwa kuchapisha vitabu vya bajeti zinafikia Tsh. 74,000,000/- . Aidha, Ofisi huiandikia
Wizara ya Fedha kwa taasisi zote za Serikali ambazo hazilipi, ili wakatwe moja kwa moja
katika bajeti zao.
Pia, kuhusiana na ongezeko la matumizi, Kamati inahoji kwa nini taasisi hizi zisiandae
nyongeza husika tokea wakati wa kuandaa bajeti, na kushindwa kufanya hivyo hupelekea
ongezeko kubwa la matumizi kinyume na idhini ya nyongeza hiyo kufahamika.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kuhakikisha inakuwa na fedha za
kutosha za matengenezo ya mashine za uchapishaji. Aidha, Kamati inaishauri Serikali
kuangalia uwezekano wa kuipa Idara ya Uchapaji mamlaka kamili ya kujiendesha
kibiashara. Vile vile, Kamati inaishauri Serikali kuwa na mipango mizuri yenye kufahamika
kwa mwaka mzima, ili kuepusha kuongezeka kwa matumizi kwa sababu ya mishahara.
3.5.1 IDARA YA MAAFA
Hoja Namba 51.2.1 Malipo ya fidia kwa waathirika wa ajali ya MV. Spice Islander 1.
Malipo ya fidia kwa waathirika wa ajali ya Mv. Islander, kati ya 1429 waliofariki na 941
waliopona, walilipwa Tsh. 1,267,661,287 kwa ajili ya fidia. Hata hivyo, katika ulipaji huo,
kuna kasoro kadhaa zilijitokeza ambazo ni fomu za malipo kukosa namba, kutumika tarehe
moja tu wakati ulipaji uliendelea kwa zaidi ya miezi mitatu, kukosekana kwa idadi sahihi ya
wanaopaswa kulipwa fidia hiyo, kutofanywa marejesho ya fedha ilobakia baada ya ulipaji
huo kufanyika, kukosekana kwa baadhi ya sahihi za waliopokea fedha hizo na kutokuwa na
idadi sawa ya walioathirika katika maafa hayo na kupelekea hadi leo hii kuna baadhi ya watu
wanakwenda kudai fedha hizo.
Majibu ya Ofisi
Idadi halisi ya maathirika inatofautiana katika orodha tatu tofauti. Mara tu ilipotokea ajali,
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais iliwataka Masheha wa Shehia zote kuwasilisha majina ya
walioathirika na baadae kuyakabidhi kwa Wakuu wa Wilaya. Kulikuwa na orodha ya pili
ambayo waathirika walipewa kujaza na kuziwasilisha Wizarani na orodha ya tatu ni ile
iliyopatikana kutokana na Tume iliyoundwa na Mhe. Rais ambayo inasema waliohai ni 941
na waliofariki ni 1529 na kufanya idadi yote kuwa waathirika 2470, ambao Ofisi inaamini
ndio sahihi zaidi.
Aidha, walipopata orodha ya Tume wamezunguuka Wilaya zote na kuwalipa waathirika.
Kati ya waliohai 941, waliowapata ni 640 tu na kati ya 1529 waliofariki, waliwapata 1328 tu,
ila walitangaza katika vyombo vya habari, na kwa malalamiko yaliyoletwa kwa waliohai 53,
wamewalipa 14.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imezipitia fomu zilizowasilishwa na Ofisi hii na kugundua kuwa hazikuwa na
nambari. Kuhusiana na kutumiwa kwa tarehe moja, Kamati imeihoji Ofisi na kueleza kuwa,
wao walitumia orodha, kwa mtu ambae hakulipwa tarehe ya siku, alilipwa kwa tarehe
iliyofuata.
22
Aidha, malipo ya fidia kwa waliofariki ilikuwa Tsh. 550,000/- na waliohai ilikuwa Tsh.
412,500/-. Na kwa upande wa Pemba, walilipa kwa mkupoa mmoja na „cheque‟ ilisainiwa
siku moja ila uvunjaji wa „cheque‟ hiyo ulifanywa siku tofauti.
Ofisi inakiri kuwa, wakati alipokuja Mkaguzi hakukuwa na baadhi ya marejesho kwa baadhi
ya Wilaya, ila sasa marejesho hayo yapo, hali inayoipelekea Kamati kuthibitisha usahihi wa
hoja ya Mdhibiti. Vile vile, Kamati imehoji kukosekana kwa baadhi ya sahihi, ambapo
ilielezwa kuwa baadhi ya waliohusika na malipo hawajui kusaini na hivyo kutilishwa dole
gumba. Aidha, Kamati imeelezwa kuwa, fedha iliyobakia imependekezwa kubakia katika
akaunti ya Idara ya Maafa kwa kusaidia matukio mbali mbali ya maafa kwa namna
yanavyojitokeza. Aidha, Tsh. 100,000,000 zimetengwa kwa ujenzi wa fance ya eneo
walikozikwa waliofariki, ili iwe kumbu kumbu na eneo tengefu kuwazika wengineo. Hivyo,
fedha zote zilizochangwa ni Tsh. 1,256,603,688/, fedha zilizotumika kwa malipo mbali
mbali ya fidia ni Tsh. 1,107,975,000/- na fedha zilizobakia ni Tsh. 148,628,688/-.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuwa makini na masuala ya malipo ya fidia kwa matukio mbali
mbali, kwa kuwa na utambulisho sahihi wa wanaostahiki kulipwa fidia hiyo, lakini pia
ihakikishe fedha za michango ya namna kama hiyo zinalipwa na kuwafikia walengwa.
3.5.2 TUME YA UCHAGUZI
Hoja Namba 52.1 Hesabu za Mwisho wa mwaka. Taarifa kuhusu matumizi ya kazi za
kawaida za Tume ya Uchaguzi
Tume ya Uchaguzi ilikadiriwa kutumia jumla ya Tsh. 761,000,000 kwa kazi za kawaida kwa
mwaka 2012/2013. Aidha, hadi kufikia Juni 2013, Tume iliingiziwa Tsh. 910,506,569 kwa
kazi hizo za kawaida na kufanya nyongeza ya fedha hizo za matumizi kuwa Tsh.
149,506,569.
Majibu ya Tume
Ni kweli fedha hizo ndizo zilizoingizwa na kutumiwa, huku kukiwa na nyongeza iliyotajwa.
Nyongeza hiyo imesababishwa na kuongezeka kwa mabadiliko ya viwango vya mishahara
kwa wafanyakazi mbali mbali wa Tume.
Uchunguzi wa Kamati
Kwa mwaka huu, Kamati imeshuhudia taasisi mbali mbali za Serikali zikiwa na ongezeko la
matumizi ya fedha walizoomba katika Baraza la Wawakilishi. Aidha, Kamati imekuwa
inashuhudia majibu hayo hayo ya kuongezeka kwa matumizi hayo kutokana na ongezeko la
mishahara. Hata hivyo, Kamati inashangazwa sana na Serikali kwa kutoona mabadiliko hayo
na kuzingatiwa mapema katika bajeti za taasisi hizo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuangalia mapema mabadiliko ya mishahara katika bajeti ya
mwaka, kabla ya kutangazwa kwa mabadiliko hayo, ili kuweka sawa taarifa za hesabu.
3.6 WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO
Hoja Namba 60.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012 na 2012/2013
Taarifa ya Mapato na Matumizi:
23
Jumla ya Tsh. 30,000,000 zilikadiriwa kukusanywa kwa mwaka 2011/2012, na mwaka
ulipomalizika Wizara ilikusanya Tsh. 33,583,600 ambayo ni sawa na asilimia 112 ya
makadirio, ikiwa ni ongezeko la Tsh. 3,583,600 sawa na asilimia 12 ya makadirio.
Aidha, matumizi ya kazi za kawaida, yalikuwa Tsh.2,362,000,000/- na fedha halisi
zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 2,327,069,314, sawa na asilimia 98.5 ya makadirio,
ikiwa ni pungufu ya Tsh. 34,930,686 sawa na asilimia 1.5 ya makadirio. Aidha, matumizi ya
maendeleo, Wizara iliidhinishiwa kutumia Tsh. 300,000,000/-, lakini mwisho wa mwaka
ulipofika, fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 298,985,100 sawa na asilimia
99.76 ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa Wizara hii limetokana na ufuatiliaji mzuri wa
vianzio vya mapato ikiwemo vituo vya mafuta na kuzikagua mizani za wafanyabiashara.
Uchunguzi wa Kamati
Katika kufanya uchunguzi wa suala hili, Kamati ilibaini kuwa ukusanyaji wa mapato wa
Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko hauridhishi kwa kuwa inaonekana kuna vianzio
vyengine vya mapato havijafikiwa. Aidha, Kamati iliwataka Wizara kuwasilisha vianzio
vyao vya mapato kwa Kamati, lakini hadi tunaandika taarifa hii, taarifa hiyo haijapatikana
kwa Kamati.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuongeza mikakati ya ukusanyaji wa mapato na ifanye matumizi
kwa kuzingatia mahitaji halisi ya Wizara na taratibu za kisheria. Aidha, Kamati inazitaka
taasisi za Serikali kuheshimu maelekezo ya Kamati ya kupatiwa taarifa mbali mbali
inazozihitaji.
Hoja Namba 60.2 Malipo yasiyokuwa na Vielelezo (Nyaraka Pungufu Tsh.
46,018,985)
Fedha hizo zimelipwa kwa matumizi mbali mbali lakini vielelezo husika havikupatikana kwa
ukaguzi, kinyume na taratibu za kisheria. Hali ambayo haikuweza kuthibitisha uhalali wa
malipo hayo. Malipo hayo yaligawika katika hesabu mbili, ya kawaida kwa Tsh. 46,018,985
alizolipwa Harisini Enterprises kwa ajili ya ukarabati wa banda la maonesho ya saba saba
Dar es Salaam na hesabu ya maendeleo ya Tsh. 140,855,100 alizolipwa Cris and
Infrastructure Solution Ltd kwa ajili ya utafiti wa kuifanya Zanzibar kuwa bandari kuu.
Majibu ya Wizara
Wizara iliieleza Kamati hii kuwa kwa upande wa hesabu za kawaida, kasoro hiyo
imesharekebishwa kwa kuwa malipo hayo hivi sasa yamelipwa kwa mujibu wa vielelezo
husika. Aidha, kuhusiana na Hesabu ya Maendeleo Wizara ilikiri kuwa ni kweli wakati wa
ukaguzi kielelezo cha ithibati cha uhaulishaji fedha (Bank Transfer) hakikuwepo. Hali hii
ilitokana na utaratibu uliotumika wa kumlipa Mshauri Elekezi ambapo Wizara ya Fedha
ilifanya uhaulishaji huo moja kwa moja na kusawazisha katika bajeti ya Wizara ya Bishara,
Viwanda na Masoko kwa kukata uhaulishaji uliofanyika katika matumizi ya eneo husika.
Hivyo, risiti kwa ajili ya ithibati hiyo ilikuwepo Wizara ya Fedha na tayari Wizara hii
imeshapokea nakala ya ithibati.
24
Uchunguzi wa Kamati
Katika kufuatilia hoja hii Kamati ya PAC imebaini kuwa kasoro hii imejitokeza kwa kuwa
Kampuni iliyopewa shughuli hii ilishindwa kuwasilisha nyaraka husika kwa wakati. Ingawa
Wizara ilikuwa inahitaji kukarabatiwa banda la maonyesho ya sabasaba kwa uharaka, hata
hivyo, Wizara haikupaswa kuilipa Kampuni hii fedha za awamu ya pili kwa kuwa Kampuni
ilishindwa kutoa nyaraka kwa malipo ya awali yaliyofanyika jambo ambalo limeondosha
uaminifu wake.
Aidha, Kamati hii imebaini kuwa upatikanaji wa Mshauri Elekezi haukufuata taratibu za
kisheria. Suala hili hulitia mashaka Kamati hii na kuhisi kuwa kuna mchezo mchafu
ulifanyika wakati zoezi hili linafanyika. Aidha, kuhusiana na hesabu ya maendeleo Kamati
iliridhika na majibu yaliyotolewa na Wizara kuhusiana na suala hili.
Mapendekezo ya Kamati:
Kamati imeitaka Wizara kuwa wabunifu pamoja na kutafuta wataalamu ili iweze
kukusanya mapato mengi zaidi.
Waendelee kutoa taaluma kwa wananchi juu ya umuhimu wa kukaguliwa mizani
wanazozitumia katika shughuli zao za biashara.
Watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa Sheria za nchi.
Mengineyo
Kamati ilielezwa kuwa Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) limeanza kutekeleza shughuli
zake, hata hivyo, kutokana na ukosefu wa maabara (Laboratory) Shirika hili hupeleka bidhaa
zake kwa ajili ya kuangaliwa ubora wa viwango katika Shirika la Viwango la Tanzania
(TBS). Hivyo basi, Kamati hii inaitaka Serikali iliongezee nguvu Shirika la ZBS, ili
kuhakikisha kuwa Shirika linatekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kamati inaishauri Serikali kuipa mamlaka ya kushughulikia vibali vya kuingizwa gari
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano badala ya Mamlaka ya Kukusanya Mapato (TRA)
na kuwa Taasisi hii ndio hasa inayohusika na masuala ya usafiri.
Kwa upande wa ZBS, Kamati ilishauri kuwa iajiri Kampuni itakayoshughulikia masuala ya
ubora wa viwango kwa bidhaa za hapa nchini ili kuongeza mapato ya nchi.
Vile vile, Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kuwa Shirika hili muhimu linapewa
kipaumbele kwani Sheria yake imeanzishwa tokea mwaka 2011 lakini utekelezaji wake bado
unasuasua.
3.7 WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA
USHIRIKA
Hoja Namba 63.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Mapato na Matumizi
Wizara iliidhinishiwa kukusanya Tsh. 68,500,000 kwa mwaka 2011/2012. Hadi kufikia Juni
2012, mapato yaliyokusanywa yalikuwa Tsh. 123,277,000 ambayo ni sawa na asilimia 180
ya makadirio.
Kwa upande wa matumizi ya kawaida, fedha zilizoainishwa ni Tsh. 1,545,000,000/- na fedha
halisi zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 1,939,037,749/- sawa na asilimia 122.5 ya
makadirio. Aidha, matumizi ya maendeleo, Wizara iliidhinishiwa kutumia Tsh. 90,000,000/-,
lakini mwisho wa mwaka ulipofika, fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh.
25
70,000,000, sawa na asilimia 77.8 ya makadirio, kukiwa na upungufu wa Tsh.20,000,000
sawa na asilimia 22.2 ya makadirio.
Majibu wa Wizara:
Wizara hii iliieleza Kamati kuwa ongezeko la mapato hayo limetokana na kuongezeka kwa
idadi ya Vyama vya Ushirika vilivyoandikishwa, uchunguzi wa vibali vya katika Hoteli na
sehemu mbali mbali.
Aidha, walizidi kueleza kuwa kupanga makadirio ya mapato kuna changamoto kubwa kwani
kunategemea mazingira ya wakati; kwa mfano katika mwaka uliopita walikusanya fedha
nyingi kwenye eneo la vibali vya kazi (Work Permit), lakini mwaka uliofata walishindwa
kufikia malengo kutokana na malalamiko yaliyotolewa juu ya ongezeko la fedha katika eneo
hili. Ongezeko la matumizi ya kazi za kawaida limetokana na Serikali kupandisha mishahara
ya watendaji wake.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na maelezo hayo ya Wizara, Kamati hii inaona kuwa bado kuna changamoto
Serikalini katika kupanga makadirio ya mapato.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuwa makini wakati wa kuandaa makadirio hayo. Kwani
imefahamika wazi kuwa, nyongeza hiyo ya mishahara huwa haionekani katika bajeti za
Wizara na taasisi zake, inapopitishwa na Baraza.
3.7.1 IDARA YA MIKOPO
Hoja Namba 63.2.1 Malimbikizo ya madeni ambayo hayajalipwa ya (JK na AK) hadi
kufikia tarehe 30 juni, 2012 tsh. 877,877,910.6
Idara imekopesha fedha hizo kwa ajili ya watu binafsi SACCOS na vikundi mbali mbali vya
kiuchumi, lakini hadi kufikia 30 Juni, 2012, jumla ya Tsh. 740,197,007.09 zilikopeshwa
bado hazijarejeshwa. Fedha hizo zimekopeshwa kwa mikoa yote ya Unguja na Pemba.
Majibu ya Wizara
Wizara iliieleza Kamati kuwa usimamizi wa Mfuko huo ulikuwa na changamoto ambazo
ziliathiri urejeshaji wa mikopo iliyotolewa. Changamoto hizo ni kama zifuatazo;
i. Mfuko wa AK na JK ulikuwa ukiendeshwa na Taasisi mbili yaani Benki ya Watu wa
Zanzibar na Wizara inayohusika na masuala ya uwezeshaji. Hata hivyo, Benki ya
Watu wa Zanzibar ndio iliyokuwa na jukumu la utoaji wa mikopo pamoja na
ufuatiliaji wake wakati jukumu la Idara ya Mikopo lilikuwa ni kuratibu na
kuhakikisha mikopo inawafika wananchi wote waliostahiki;
ii. Kulikuwa na upungufu wa vitendea kazi, hasa usafiri kwa Idara ya Mikopo; na
iii. Tatizo la kuhamahama kwa wakopaji bila ya kutoa taarifa kwa Masheha wa Shehia
zao.
Ingawa jukumu la Idara ya Mikopo lilikuwa ni kuratibu tu, hata hivyo baada ya kubaini
kuwa kuna tatizo la ucheleweshaji wa malipo ya mikopo hiyo, ilikubaliana na Uongozi wa
Benki kusaidia ufuatiliaji na ukusanyaji wa fedha hizo.
26
Tangu zoezi hilo lilivyoanza deni lililobaki ni kama ifuatavyo;-
MKOA DENI LILILOBAKI HADI SEPT, 2014
Mkoa wa Kaskazini Unguja Tsh. 104,954,619.50
Mkoa wa Kusini Unguja Tsh. 69,019,483.45
Mkoa wa Mjini/Magharibi Tsh. 277,804,214.24
Mkoa wa Kaskazini Pemba Tsh. 114,227,335.65
Mkoa wa Kusini Pemba Tsh. 110,126,947.70
JUMLA = Tsh. 676,132,600.54
Walizidi kueleza kuwa hivi sasa fedha zote zilizokuwa kwenye Mfuko wa JK/AK
zimejumuishwa kwenye Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambao ulizinduliwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mnamo mwezi wa Disemba,
2013.
Katika mwezi wa Septemba, 2014 Wizara hii ilipokea kutoka PBZ jumla ya Tsh.
600,000,000.00 zilizokuwa kwenye Mfuko huo pamoja na orodha ya wadaiwa ambao
hawajamaliza madeni yao. Hivyo, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana,
Wanawake na Watoto inaendelea kufuatilia madeni hayo.
Mapendekezo ya Kamati
Kwa kuwa deni lililobaki ni kubwa na kwa kuwa wadaiwa wakilipa madeni yao, fedha
zitakazopatikana zitawawezesha wananchi wengine kupata mikopo hiyo, Kamati hii
inaishauri Wizara kuendelea kufuatilia madeni hayo na kuwachukulia hatua wale wote
ambao hawatolipa madeni yao.
3.8 WIZARA YA NCHI (OR) UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
Hoja Namba 43.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Matumizi ya kawaida na maendeleo
Iliyokuwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka
2011/2012 ilikadiriwa kutumia Tsh. 1,997,000,000 kwa kazi za kawaida na fedha halisi
zilizoidhinishwa na kutumika ni Tsh. 2,180,494,994 sawa na asilimia 109.3 ya makadirio,
kukiwa na ongezeko la Tsh. 183,494,994 sawa na asilimia 9.3 makadirio. Aidha, matumizi
ya kazi za maendeleo yalikisiwa kuwa Tsh. 360,000,000 na fedha hizo hizo ziliingizwa na
kutumiwa, sawa na asilimia 100 ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Taarifa hizo ni sahihi na kuhusiana na matumizi ya maendeleo, Wizara ilikuwa na shughuli
mbali mbali za utekelezaji wa miradi iliyohusika, ikiwa ni pamoja na utungaji wa Sheria za
Utumishi wa Umma na kanuni zake, miradi ambayo hapo awali ilikuwa inategemea „World
Bank‟ lakini hivi sasa Wizara inapata fedha kutoka Serikalini pekee. Hivyo, Wizara
inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa wafadhili wa mradi huu isipokuwa Serikali.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati imehoji muda mrefu wa utekelezaji miradi ya Wizara na kuamini kuhusiana na
kukosa wafadhili kuwa, suala hilo lingestahiki kufanywa na Serikali na sio kutegemea
Wafadhili.
27
Hoja Namba 43.2 Malipo yaliyofanywa kinyume na utaratibu, Tsh. 89,232,000
Fedha hizo zimelipwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Utawala wa Umma (IPA), lakini
stakabadhi zinazoonesha kupokelewa kwa malipo hayo hazikubaliki kwa mujibu wa Sheria.
Majibu ya Wizara
Suala hili liliwahi kujitokeza kwa mkandarasi wa ujenzi wa Chuo hicho (Chuo cha Mafunzo)
ila tatizo hilo liliwahi kuelezwa kwa Chuo cha Mafunzo kuhusiana na kasoro ya risiti
wanazotoa kuthibitisha mapokezi ya fedha za umma.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati inafahamu kuwa bado baadhi ya Vikosi vya SMZ vinatumia stakabadhi zao badala
ya stakabadhi za Serikali na Kamati imekuwa inalitolea taarifa suala hili takriban kila
mwaka.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo cha Mafunzo kutumia risiti za Serikali, kwa huduma wanazozitoa
kwa taasisi za Serikali na watu binafsi.
3.8.1 IDARA YA NYARAKA
Hoja Namba 43.3.1 Kuwepo kwa nyumba binafsi ndani ya uzio wa Idara
Ukaguzi umebaini kuwepo kwa nyumba ya mtu binafsi ambae hutumia mlango mkubwa wa
Idara ya Nyaraka ili aweze kufika ndani ya nyumba yake. Tatizo hili husababisha mlango wa
Idara kuwa wazi kwa muda mrefu kwa matumizi ya mtu binafsi. Hali hii hupelekea
kudhoofika kwa mfumo mzima wa kiusalama wa mali na nyaraka muhimu za Serikali. Suala
hili ni la muda mrefu linahitaji kutafutiwa ufumbuzi.
Majibu ya Wizara (Idara)
Ni kweli hoja hiyo na Idara kwa mashirikiano na Wizara wamechukua hatua kubwa na ya
muda mrefu kulieleza suala hilo na kulitafutia ufumbuzi, lakini hakuna mafanikio yoyote
yaliyopatikana. Nyumba hiyo imo ndani ya eneo hilo kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Mmiliki
wa nyumba hiyo amekubali kuondoka hapo kwa kulipwa Tsh. 800,000,000 fedha ambazo ni
nyingi sana na hazina uhalisia wa thamani ya nyumba yake hiyo.
Aidha, pendekezo jengine ni mwenye nyumba atumie mlango wa mbele uliopo katika
barabara kuu ya Kilimani iendayo Uwanja wa Ndege na geti la nyuma lizibwe, lakini kwa
bahati mwenye nyumba hajaridhia au imegwe sehemu ya ardhi ya aneo la Idara ili kujenga
ukuta utakaowacha nafasi ya upana wa kupandisha gari yake, lakini bado pendekezo hili
linahitaji ushauri zaidi wa kitaalamu. Hata hivyo, Wizara inawasiliana na Wizara ya ardhi ili
kuwasilikiliza ushauri wao kuhusiana na suala hili.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati inaamini suala hili bado Serikali haijawa tayari kulifanyia kazi. Kama inaathirika
kweli, ina uwezo wa kulifanyia kazi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
28
3.9 WIZARA YA USTAWI WA JAMII MAENDELEO YA VIJANA
WANAWAKE NA WATOTO
Hoja Namba 13.1 na 12 Uwasilishaji wa Hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya
ukaguzi (mwaka 2011/2012 na 2012/2013)
Kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Fedha namba 12 ya mwaka 2005, inakitaka taasisi zote za
Serikali zitayarishe na kufunga hesabu zao za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi. Hata hivyo,
uwasilishaji huo usizidi tarehe 30 ya mwezi wa Septemba ya kila mwaka, lakini Wizara hii
ilichelewa kwa kuwasilisha 01/10 kwa miaka yote miwili, mwaka wa 2011/2012 na
2012/2013.
Majibu ya Wizara
Mhasibu wa Wizara aliieleza Kamati kuwa, ripoti zote mbili ziliwasilishwa Masjala ya
Wizara kabla ya tarehe iliyotajwa na ukaguzi. Kwa mfano, ripoti ya mwaka 2011/2012
iliwasilishwa kwa Mdhibiti kama saa 9 hivi, lakini watendaji wao walipofika Ofisini hapo
kwa Mdhibiti walikuta Ofisi imeshafungwa na walimkuta mlinzi aliyewaambia warudi nayo
na waende siku ya pili yake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji sababu zilizowapelekea Wizara kuchelewa hadi siku ya mwisho ambayo
ndiyo imetajwa kisheria, na kuelezwa kuwa, kulikuwa na mafunzo mafupi kutoka kwa
Mhasibu Mkuu wa Serikali, na hivyo walisubiri mafunzo hayo. Hata hivyo, Kamati
imejiridhisha kwamba, Wizara hawakuwajibika ipasavyo kwa kuandaa na kuwasilisha
hesabu zao kwa wakati na matokeo yake kuripotiwa usahihi wa kuchelewa kwao.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kurekebisha kasoro hiyo kwa miaka inayofuata.
Hoja Namba 64.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo
Wizara iliidhinishiwa kufanya matumizi ya kawaida ya Tsh. 1,540,000,000 na fedha halisi
zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 1,754,310,000 sawa na asilimia 114 ya makadirio, ikiwa
ni ongezeko la Tsh. 214,310,000 sawa na ongezeko la asilimia 14 ya makadirio. Aidha,
matumizi ya maendeleo, Wizara iliidhinishiwa kutumia Tsh. 230,000,000/-, lakini mwisho
wa mwaka ulipofika, fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh.224,450,000, sawa na
asilimia 97.6 ya makadirio, kukiwa na upungufu wa Tsh. 5,550,000 sawa na asilimia 2.4 ya
makadirio.
Majibu ya Wizara
Wizara hii iliieleza Kamati kuwa ongezeko la matumizi haya yametokana na kupandishwa
mishahara ya watendaji. Pia Kamati ilielezwa na Wizara kuwa upungufu wa fedha hizo
umetokana na Wizara ya Fedha kwa kuingiza fedha kinyume na makadirio ya Wizara hii.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa kasoro ya uingizaji wa fedha ilisababishwa na Wizara ya Fedha
na inasikitishwa na utoaji wa fedha hizo kwa kutokuzingatia vipaumbele vya Wizara na
majukumu ama nafasi yao katika ujenzi wa taifa.
29
Mapendekezo ya Kamati
Ingawa bajeti ya nchi hii ni „cash budget‟ bado Kamati inaitaka Serikali kuziingizia Taasisi
zake fedha za matumizi kwa mujibu wa makadirio ya Taasisi hizo hasa ikizingatiwa kuwa
Wizara ya Fedha ndio inayotoa ukomo „ceiling‟ ya makadirio hayo.
Hoja Namba 64.2 Malipo yasiokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu) Tsh. 5,152,000
Fedha hizo zimelipwa kwa matumizi mbali mbali lakini vielelezo vyake havikupatikana kwa
ukaguzi, kitendo ambacho kinakwenda kinyume na sheria ya Fedha na Kanuni zake.
Majibu ya Wizara
Vielelezo vyote vya matumizi yaliyotajwa kwenye hoja hii ikiwa ni pamoja na stakabadhi za
malipo vimeonekana baadae, isipokuwa kwamba hakukuwa na mawasiliano ya maandishi
baina ya Wizara husika na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kufuatia kasoro hiyo Kamati ya Uongozi ya Wizara ilitoa maagizo yafuatayo kwa watendaji
wa Wizara hii:
i. Kujenga utamaduni wa kudai stakabadhi za malipo mara tu malipo yanapofanyika;
ii. Kuviimarisha Vitendo vya Manunuzi na Ukaguzi wa ndani ili viweze kutekeleza
majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa sheria;
iii. Kuimarisha mashirikiano ya kikazi kati ya Kitengo vya Manunuzi, Ukaguzi wa
Ndani na Uhasibu ili kuwe na uratibu mzuri wa masuala ya manunuzi;
iv. Ripoti za Ukaguzi wa Ndani zifanyiwe kazi ipasavyo ili kurekebisha kasoro
zinazojitokeza;
v. Wizara isimamie utaratibu wa kukagua “voucher; kabla ya malipo ili kuepuka hoja
zisizokuwa za lazima wakati wa ukaguzi;
vi. Uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu uimarishwe, ikiwa pamoja na Vitengo vya
Uhasibu na Ununuzi kuweka namna bora ya uwekaji wa kumbu kumbu ili
kurahisisha shughuli za ukaguzi;
vii. Kamati ya Uchunguzi ihakikishe inafuatilia kwa karibu masuala yote yanayohusu
hesabu za Wizara na Kumshauri Katibu Mkuu ipasavyo, pamoja na kuhakikisha
kuwa inapatiwa na kupitia ripoti kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Wakaguzi
wa Hesabu;
viii. Idara ya Uendeshaji na Utumishi iandae mafunzo kwa Wakurugenzi wote na Maafisa
Waandamizi wa Wizara juu ya sheria na kanuni za manunuzi na usimamizi wa fedha;
na
ix. Kuvitumia ipasavyo vikao vya “Entry Meeting” na “Exit Meeting” vinavyoitishwa na
wakaguzi ili kuepusha hoja zisizokuwa za msingi.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa, Wizara haikufuata taratibu katika kuhifadhi vielelezo
vilivyotakiwa katika matumizi haya, kama Sheria ya Fedha ya mwaka 2005 inavyoelekeza.
Hivyo, Kamati inaitaka Wizara kufuata taratibu za kisheria inapofanya matumizi ya fedha za
Umma.
3.10. WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
3.10.1 OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA 2011/2012
30
Hoja Namba 13.1: Uwasilishaji wa Hesabu kwa ajili ya Ukaguzi
Ukaguzi umebaini kuwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka haikuwasilisha hesabu za
mwaka, zinazojumuisha Mapato na Matumizi kama vifungu vya 24(2) na 8 vya Sheria ya
Fedha Namba 12/2005 vinavyoelekeza.
Majibu ya Ofisi
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ilikiri kosa la kutowasilisha hesabu kwa ajili ya ukaguzi
kwa kuwa Mhasibu aliyekuwepo wakati ule hakuwajibika ipasavyo katika kutekeleza
majukumu yake. Baada ya kupata Mhasibu mpya tatizo hilo limeondoka na kwa kuthibitisha
hilo katika mwaka wa fedha 2012/2013 Ofisi hii iliwasilisha hesabu hizo kwa wakati.
Uchunguzi wa Kamati:
Kamati ya P.A.C ilikubaliana na maelezo yaliyotolewa na Ofisi na hasa ikizingatiwa kuwa
kwa mwaka wa fedha uliofuata Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka iliwasilisha hesabu zake
kwa wakati.
Mapendekezo ya Kamati:
Kamati imewashauri Watendaji kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kama sheria
za nchi zinavyoelekeza.
Hoja Namba 46.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Matumizi ya Kazi za Kawaida na Maendeleo
Ukaguzi umebaini kuwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ilitumia kwa kazi za kawaida
ongezeko la Tsh. 115,044,697/- sawa na asilimia 14.9 ya makadirio, kutokana na kukadiriwa
kutumia Tsh. 774,000,000 na hatimae ilipofikia Juni 2012, ilitumia Tsh. 889,044,697 sawa
na asilimia 114.9 ya makadirio. Kwa kazi za kawaida, ukaguzi umebaini kuwa Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka ilitumia kwa kazi za maendeleo asilimia 100 ya makadirio ambazo
ni Tsh. 250,000,000.
Majibu ya Ofisi
Ofisi hii imeongeza matumizi ya ziada kwa kazi za kawaida kutokana na ongezeko la
mishahara na posho kwa watendaji. Ingawa kulikuwa na ongezeko hilo bado mishahara ya
Watendaji wa Ofisi hii ni midogo ukiliganisha na uzito wa majukumu yao. Jambo hili
linapelekea watendaji wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuhama na kuisababishia Ofisi
hii kukosa watendaji waandamizi. Kuhusiana na tatizo ililolipata Ofisi kutokana na
kutokamilika kwa bajeti ya matumizi, Ofisi imeiarifu Kamati kuathiriwa kwa shughuli zake
mbali mbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kuitumia Ofisi yao ya Makunduchi kwa kukosa
fedha, kama ilivyo tatizo la kutopewa OC kwa wakati.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ya PAC ilikubaliana na maelezo yaliyotolewa na Ofisi hii. Hii ni kutokana na kuwa
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka imebakiwa na mtendaji mmoja tu kati ya watendaji
waanzilishi wa Ofisi hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuyazingatia upya maslahi ya Watendaji wa Ofisi hii ili
wasiendelee kuhama ovyo pamoja na kuwaepusha kutenda vitendo viovu ikiwemo kupokea
rushwa.
31
Hoja Namba 46.2 Malimbikizo ya Madeni Tsh. 93,637,950
Fedha hizo zinadaiwa na wafanyabiashara na taasisi mbali mbali kwa kutoa huduma zao kwa
Ofisi. Ukaguzi umebaini kuwa, madeni hayo ni ya muda mrefu na kuwepo kwake ni
kinyume na mfumo sahihi wa kiuhasibu unaotambua mapato na matumizi kwa fedha taslim
ambao unatumiwa na Mawizara ya Serikali.
Majibu ya Ofisi
Ni kweli Ofisi kutokana na kazi zake na umuhimu wa kazi zake imebidi iingie katika madeni
hayo. Hii ni kutokana na ufinyu wa bajeti inayotengewa Ofisi hii. Hata hivyo, Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka imejitahidi kupunguza madeni hayo ingawa imeshindwa
kuyamaliza lakini kila hali inaporuhusu inajitahidi kupunguza kulipa madeni hayo kwa kiasi
kikubwa. Afisi hii hivi sasa imeondoa utaratibu wa kununua kwa mkopo na badala yake
imeamua kununua kwa fedha taslimu.
Jadweli lifuatalo linaonesha madeni yaliyosalia;
S/NO. MDAI MAELEZO KIASI KILICHOSALIA
1. Al Hilal Work Shop Ununuzi wa AC Tsh. 1,125,000
2. Majid Store Ununuzi wa Stationaries Tsh. 1,395,000
3. Masomo Book Shop Ununuzi wa Magazeti Tsh. 2,694,720
4. Masomo Book Shop Ununuzi wa Dictionary Tsh. 140,000
5. Penguin Refrigarator Matengenezo ya
Viyoyozi
Tsh. 349,000
6. Patel Import Export Ununuzi wa Mashine Tsh.290,000
7. Fire Rescue Force Ukaguzi wa Usalama wa
Moto
Tsh. 840,000
8. Moh‟d Ngweshani Ununuzi wa Vifaa vya
Gari
Tsh. 260,000
9. Omar S. Mtwana Kutengeneza Samani Tsh. 698,800
10. Abdulrahman Khamis
Juma
Matengenezo ya
Nyumba ya Naibu
Mkurugenzi wa
Mashtaka
Tsh. 6,800,000
11. Ramadhan S.
Abdallah
Utengenezaji wa Meza
na Viti
Tsh. 2,514,000
12. KMKM Ujenzi wa Jengo la
Maktaba
Tsh. 36,000,000
13. Hassan & Sons Ununuzi wa Vipasola Tsh. 4,000,000
14. Arkam Household
and Office Furniture
Ununuzi wa Samani Tsh. 2,800,000
JUMLA YA DENI LILILOSALIA NI TSH. 59,906,520
Uchunguzi wa Kamati
Tatizo kubwa la madeni la Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka linachangiwa na bajeti ndogo
wanayopatiwa na Serikali. Kamati imeelezwa kuwa, OC huingizwa kati kati ya mwezi na
hukabidhiwa katika mazingira magumu, hali inayokwamisha na kukosesha ufanisi wa
utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hasa inapokuja Mahakama ya Rufani, kwa Ofisi
kushindwa kupata fedha za kutosha za maandalizi ya kesi zake mbele ya Mahakama hiyo.
32
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuangalia kipaumbele cha kuwapa fedha kamili Ofisi hii ili iweze
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.
3.10.2 AFISI YA MRAJIS MKUU WA SERIKALI (WAKALA WA USAJILI WA
BIASHARA NA MALI)
Hoja Namba 44.3.1 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 29,984,800
Fedha hizo zinadaiwa na wafanya biashara pamoja na taasisi mbali mbali kwa ajili ya
utowaji wa huduma tofauti kwa Afisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali, lakini ukaguzi umebaini
kuwa madeni hayo ni ya muda mrefu na kuwepo kwake ni kinyume na mfumo sahihi wa
kiuhasibu unaotambua mapato na matumizi kwa fedha taslmi ambao unatumika kwa
Mawizara ya Serikali. Aidha, madeni hayo yanatokana na Tsh. 6,000,000 kwa ajili ya
uchapaji wa fomu za kuhaulisha, Tsh. 18,000,000 kuhusiana na uchapishaji wa vyeti vya
uzazi na Tsh. 5,984,800 kwa ununuzi wa zulia
Majibu ya Afisi
Ni kweli deni hilo lilikuwepo, ila sasa tayari Afisi imeshalipa. Aidha, deni la Tsh. 6,000,000
halikuwa halali kutokana na ukweli kuwa, hawakuzihitaji fomu hizo kutokana na suala la
uhaulishaji kuhamishiwa kwa Bodi ya Uhaulishaji wa Ardhi. Vile vile deni la Tsh. 5,984,800
ambalo kimsingi lingelipaswa lilipwe na Wizara ya Fedha kwa kuwa suala la ununuzi wa
zulia lilihitajika kutokana na kuhamishiwa kutoka jengo lao la awali la Mambo Msiige, hadi
jengo la sasa la zamani la Benki ya Watu wa Zanzibar. Hata hivyo, hivi sasa wamekubaliana
kuwa deni hilo litalipwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwepo Afisi imeshawasiliana na Idara ya Uchapaji kuhusiana na deni hilo
wanalosema hawalikubali, na kuelezwa na Afisi hii kuwa, deni hilo lilikuja baada ya miaka
miwili tokea walipowataka wawafanyie fomu hizo kwa Idara kuleta barua yenye „Invoice‟ ya
deni hilo. Aidha, Kamati imewataka Afisi wathibitishe iwapo nao walijibu kwa barua na
kuelezwa kuwa hawana hakina kama walijibu kwa barua, ila mawasiliano yalikuwepo baina
yao.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati iliitaka Afisi kuandika barua kwa Idara ya ya Upigaji Chapa kuwaeleza kuhusiana na
deni hilo na nakla ya barua hiyo iwasilishwe kwa Kamati.
Aidha, Kamati inaitaka Wizara au hata Afisi ihakikishe deni lililobakia la ununuzi wa zulia
linalipwa.
3.11 WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI
Hoja Namba 65.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Makadirio ya Mapato na Matumizi
Mapato yaliyokadiriwa kukusanywa na Wizara hii kwa mwaka 2011/2012 ni Tsh.
240,000,000 na fedha halisi iliyokusanywa ni Tsh. 539,752,000 sawa na asilimia 225 ya
makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 299,752,000 sawa na asilimia 125 ya makadirio.
Aidha, Wizara iliidhinishiwa kufanya matumizi ya kawaida ya Tsh. 6,923,000,000 na fedha
halisi zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 8,456,604,481 sawa na asilimia 122.2 ya
makadirio, ikiwa ni ongezeko la Tsh.1,533,604,481 sawa na oasilimia 22.2 ya makadirio.
Vile vile, matumizi ya maendeleo, yaliidhinishiwa kwa Tsh. 3,600,000,000/-, lakini fedha
33
zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 3,313,552,544, sawa na asilimia 92 ya makadirio,
kukiwa na upungufu wa Tsh. 286,447,456 sawa na asilimia 8 ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Wizara hii iliieleza Kamati kuwa ongezeko la mapato hayo yametokana na kufanyika kwa
mapitio kwa vianzio vyake pamoja na Wizara kubaini mashamba mapya ya mikarafuu na
minazi baada ya kupata taarifa kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati na hatimae
mashamba hayo kukodishwa kwa wananchi. Aidha, Wizara iliongeza bei kwa baadhi ya
vianzio vyake.
Majibu wa Wizara
Kamati ya PAC ilielezwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kuwa, Wizara hii ililazimika
kutumia zaidi ya makadirio iliyokadiriwa kutokana na ongezeko la mishahara na maposho ya
Watendaji wake baada ya Serikali kuongeza mishahara hiyo.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati hii iliridhika na majibu ya Wizara, hata hivyo, pamoja na kuridhika kwake imeitaka
Wizara kuendelea kuchukua juhudi za makusudi za kufuatilia mashamba ya Serikali ili
kuweza kujua idadi halisi ya mashamba yake jambo ambalo litasaidia kuongezeka kwa
mapato ya nchi.
Aidha, Kamati imeitaka Wizara kuzalisha miche mbali mbali ya mazao kwa kutafuta miche
bora ili kuepusha hasara za makusudi.
Pia, imeitaka Wizara kuwachukulia hatua wale wote wanaohujumu miti ya mikarafuu ili
kulinda hadhi ya mazao hayo
Hoja Namba 65.2 Mali hazikuoneshwa katika hesabu za mwaka Tsh. 29,886,000
Ukaguzi umebaini kuwepo kwa vyombo/magari ambayo yanamilikiwa na Wizara, lakini
hayakuoneshwa katika hesabu za mwaka (Financial Statement) wakati kufanya hivyo
kunaweza kusababisha upotevu wa mali za Serikali pia ni kwenda kinyume na Sheria na
Kanuni za ufungaji wa hesabu.
Majibu ya Wizara
Wizara hii ilikiri kwamba kuna baadhi ya vifaa, vyombo ambavyo vinamilikiwa na Wizara
havikuoneshwa katika Ripoti ya Hesabu za Fedha (Financial Statement) ya mwaka
2011/2012. Kadhia hii imechangiwa na kasoro ya uwekaji wa kumbukumbu, hata hivyo
hatua madhubuti tayari zimechukuliwa kwa kufanya mapitio ya vifaa vyote na kuviingiza
katika vitabu vya kumbukumbu (Asset Registry). Pamoja na hatua hiyo, Wizara imejipanga
kuwajengea uwezo watendaji wake wanaohusika na uwekaji wa kumbukumbu na usimamizi
madhubuti wa fedha na mali za Serikali kwa kuwapatia mafunzo.
Vile vile, Wizara ya Kilimo na Maliasili iliieleza Kamati kuwa gari aina ya Toyota Land
Cruiser SMZ 6927 haipo katika mamlaka yake na hivi sasa ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais na inatumiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo. Kitendo hiki
kimetokea baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Ndg.
Islam Seif kuhamishiwa katika Ofisi hiyo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati katika kufuatilia suala hili imebaini kuwa vifaa hivyo ni kweli vimeingizwa baada ya
ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanyika. Hata hivyo,
34
uingizwaji huo unakabiliwa na baadhi ya kasoro kama vile vifaa kukosa thamani halisi
nakadhalika.
Aidha, Kamati imebaini kuwa Serikali inazivunja sheria tulizozitunga wenyewe. Hii ni
kutokana na agizo la Katibu Mkuu Kiongozi Ndg. Abdulhamid Yahya Mzee la kuwataka
watendaji wa Wizara hii kuipeleka gari katika Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais bila ya
kuwepo kumbukumbu yoyote ya barua inayoonesha kuhamishiwa gari hilo katika Ofisi hiyo.
Vile vile, katika majibu ya Wizara, Kamati ilibaini kuwa kuna upungufu wa vespa moja
ukilinganisha na idadi ya vespa zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti.
Mapendekezo ya Kamati
Taasisi za Serikali zijitahidi kufuata sheria za nchi ili kuepusha kasoro zisizo za lazima.
Aidha, Wizara ya Kilimo na Maliasili ihakikishe kuwa kunakuwepo na kumbukumbu rasmi
zinazothibitisha kuwa gari aina ya Toyota Land Cruiser SMZ 6927 haipo katika mamlaka
yake na badala yake ipo chini mamlaka ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
3.12 WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Hoja Namba 57.2 Vifaa ambavyo havikuingizwa katika daftari la ghalani, Tsh.
61,717,700
Fedha hizo zimetumika kwa kununua vifaa mbali mbali kwa matumiszi ya Ofisi, lakini vifaa
hivyo havikuingizwa kwenye daftari la vifaa vya ghalani ili kuweza kuthibitisha uhalali wa
mapokezi pamoja na matumizi yake, kinyume na kanuni ya 198 ya Kanuni za Fedha za
mwaka 2005.
Majibu ya Wizara
Wizara inathibitisha kuwa vifaa vyote vyenye thamani iliyotajwa katika hoja hii,
vilinunuliwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na vifaa hivyo vimeingizwa katika
daftari la ghalani. Aidha, fedha zote hizo zimetumika kwa usahihi na vifaa vyote
vimesharikodiwa katika daftari la ghalani na lipo tayari kwa ukaguzi wa Kamati.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa hoja ya Mkaguzi inasimama katika usahihi wake, hata kama
Wizara itafanya masawazisho baada ya ukaguzi huo. Vile vile Kamati imejiridhisha baada ya
kuzipitia hati za malipo kuwemo na kasoro nyingi za kihesabu ikiwa ni pamoja na hati hizo
za malipo kukosa vielelezo vilivyokamilika, kama vile ilivyokuwa kwa baadhi ya risiti
zilizoambatanishwa kutokuwa na sifa zinazokubalika, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa
namba ya usajili wa ZRB (Tin Number) na pia baadhi ya hati hizo za malipo hazina saini ya
Afisa Mhasibu.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kufuata taratibu za kuingiza taarifa za vifaa wanavyovinunua katika
daftari la ghalani. Aidha, Kamati inaitaka Wizara kufuata Sheria katika matumizi ya fedha za
Serikali, ikiwa ni pamoja na kufanya manunuzi kwa mujibu wa taratibu za Kisheria.
Hoja Namba 57.3.1 Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa
Pwani (MACEMP), Fedha zilizotumika kinyume na malengo, Tsh. 136,000,000
Tsh. 216,000,000 ziliingizwa kwa ajili ya kuendesha shughuli za mradi wa usimamizi wa
mazingira ya bahari na ukanda wa pwani kwa kipindi cha mwaka 2011/2012. Ukaguzi
35
umebaini kuwa Tsh. 136,000,000 hazikutumika kwa lengo lililokusudiwa, hali iliyopelekea
malengo yaliyokusudiwa kutofikiwa.
Majibu ya Wizara
Mradi ulifanya matumizi ya fedha kwa mujibu wa malengo yaliyopangwa na mradi ulipokea
fedha hizo kutoka Wizarani kwa hati namba M10/1/2012 yenye thamani ya Tsh. 56,000,000,
kwa hati namba M20/2/2012 yenye thamani ya Tsh. 38,000,000 na hati namba M26/3/2012
yenye thamani ya Tsh. 42,000,000 ambazo zote zinafanya jumla ya Tsh. 136,000,000.
Aidha, Tsh. 56,000,000 zilitumika kwa ujenzi wa msingi wa jengo la ghorofa tatu la Ofisi ya
Wizara hii, badala ya ghorofa moja iliyokuwa katika bajeti ya awali na mchango kwa
„Marine Legacy Fund,‟ fedha ambazo ni mchango wa Serikali. Hivyo Tsh. 36,000,000
zilitumika kwa ujenzi wa jengo la Wizara, Unguja na Tsh. 20,000,000 zilitumika kama
mchango wa „Marine Legacy Fund‟ iliyoanzishwa, ili fedha hizo zitumike kuendeleza kazi
zilizofanywa na mradi wa MACEMP baada ya mradi kumalizika na sio Mamlaka ya Bahari
Kuu, kama ilivyoelezwa na Mkaguzi.
Vile vile, Tsh. 38,000,000 zilitumika kwa mgawanyo wa matumizi ya Tsh. 21,500,000
kutumika kwa ujenzi wa jengo la Wizara Unguja na Tsh. 16,500,000 kununuliwa samani za
majengo ya Wizara, Unguja na Pemba.
Katika matumizi ya Tsh. 42,000,000, jumla ya Tsh. 16,000,000 ilikuwa ni mchango wa
Serikali kwa ajili ya kuanzisha „Marine Legacy Fund‟, Tsh. 17,000,000 zilitumika kwa
manunuzi ya mashine na boti kwa ajili ya Idara ya Uvuvi (MCS) na Tsh. 9,998,966
zilitumika kwa ununuzi wa mafuta yaliyopelekwa Idara ya Uvuvi kwa ajili ya Doria.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na majibu ya Wizara, Kamati imekubaliana kuwa, kwa hoja hii ilivyo na majibu ya
Wizara yakitofautiana na maelekezo ya Mkaguzi, ni vyema Kamati ipatiwe ufafanuzi wa
kina kuhusu mradi huu na namna fedha zake zilivyotumika na sio kupata majibu ya jumla
jumla kama yalivyotolewa. Hivyo, pamoja na taarifa hizo zinazohitajika kwa Kamati,
Kamati pia imeelekeza kupatiwa maelezo ya Mradi kwa ukamilifu na ushahidi wa vielelezo
kwa kila maelezo yatakayotolewa, na baada ya kupatikana taarifa hizo, yawasilishwe kwa
Kamati. Hata hivyo, hadi tunaandika taarifa hii, maelekezo hayo ya Kamati yalikuwa bado
hayajatekelezwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuheshimu maelekezo ya Kamati kwa kuipatia taarifa inazozihitaji.
Aidha, Kamati inahitaji muda zaidi wa kuifanyia kazi hoja hii na kutoa taarifa yake.
3.13 AFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI –
BLM
Hoja Namba 17.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Matumizi ya kawaida na maendeleo
Afisi iliidhinishiwa kufanya matumizi ya kawaida ya Tsh. 964,913,351 na fedha halisi
zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 964,997,151 sawa na asilimia 100 ya makadirio.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Katika kufuatilia hoja Kamati haikupata mashirikiano mazuri kutoka kwa Afisi husika
ingawa baadhi ya watendaji walihudhuria kikao hicho. Hii ni kutokana na kuwa Naibu
36
Katibu Mkuu Ndg. Salmin Amour Abdalla ambaye ni Afisa Masuul alikuwa safarini na
alishindwa kutoa taarifa mbele ya Kamati hii. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg. Salum
Maulid Kibanzi, aliishauri Kamati hii kutoa majibu ya Afisi hiyo kwa niaba ya Naibu Katibu
Mkuu, hata hivyo, Kamati ya PAC iliukataa ushauri huo kwa kuwa Ndg. Salum sio Afisa
Mas ul wa Afisi hiyo. Baada ya majadiliano makubwa Kamati iliamua kupokea taarifa ya
Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora ingawa ratiba ya kazi ya siku hiyo, ilikuwa inaigusa
moja kwa moja Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Pamoja na kuwasilishwa kwa taarifa hiyo Kamati ya PAC iligundua kuwa Afisi hiyo
haikuwa na maandalizi mazuri kwani takriban masuala mengi yaliyoulizwa yalikosa majibu
ya uhakika na hivyo Kamati iliitaka Afisi hii kuwasilisha taarifa zake kwa maandishi kwa
yale maeneo ambayo yalikosa majibu. Kwa masikitiko makubwa hadi tunawasilisha taarifa
hii hakuna taarifa yoyote iliyowasilishwa mbele ya Kamati.
Kwa msingi huo hoja hiyo haikujibika, hivyo maafisa wanaohusika wafike mbele ya Kamati
kwa kujibu hoja hizo.
TAARIFA YA UKAGUZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA MAMLAKA ZA
SERIKALI, KWA MWAKA 2011/2012
4.0 MAMLAKA YA MAJI (ZAWA)
Hoja Namba 74.1 Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi
na uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Mamlaka ya Maji ilikuwa na mali za mpito za 6,462,608,268 na
dhima za mpito za 393,629,848 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 6,068,978,420 na uwezo wa
kulipa dhima kwa ratio ya 16.4:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wengi
wa Malmaka na ikishauriwa kuongeza kukusanya mapato kutoka kwa wadaiwa.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 10,793,844,809 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 15,653,307,963 na hivyo kuendeshwa kwa hasara ya Tsh. 4,859,463,154
ambayo imepanda kwa tofauti ya Tsh. 392,305,263 sawa na 8.8% kwa mwaka
ikilinganishwa na mwaka 2010/2011.
Majibu ya Mamlaka
Wameupokea ushauri wa kuongeza mapato kwa kuongeza wigo wa ukusanyaji kupitia
wateja wakubwa kwa kuwafungia mita pamoja na wateja mbali mbali wanaopata huduma ya
maji. Aidha, imejipanga kuwaondoa katika orodha wateja wasiopata huduma ya maji katika
orodha ya wateja wanaotakiwa kulipia huduma hiyo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imegundua kuwa Mamlaka bado haijachukua hatua madhubuti za kukusanya mapato
kwa wateja wakubwa ikiwa ni pamoja na kuwafungia mita za matumizi ya maji, ingawa
imeanza kuchukua hatua hizo. Aidha, bado Mamlaka haijaweza kuwapatia wananchi wote
huduma ya maji.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kutekeleza kwa vitendo kwa kuwaondoa wananchi
wasiopata huduma ya maji katika orodha ya wateja wanaotakiwa kulipia huduma
hiyo.
37
Kamati inawapongeza kwa kuchukua hatua za kuwakatia huduma ya maji wateja
wote ambao hawalipii maji na kuwataka waendeleze kuchukua hatua hizo na hata
taasisi za Serikali ambazo hazilipii huduma hiyo.
Kamati inaishauri Serikali kuisaidia Mamlaka katika kulipia deni la umeme.
Mamlaka liwe na mipango madhubuti ya kukusanya mapato, ili kuwa na uwezo wa
kujiendelesha.
Hoja Namba 74.2 Wadaiwa wa Mamlaka kwa deni la Tsh. 8,784,017,613.82
Ukaguzi umebaini kuwa, Mamlaka inadai watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutoa
huduma ya maji bila ya kulipwa, kinyume na Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 na kanuni za
Mamlaka za mwaka 2007.
Majibu ya Mamlaka
Kweli deni hilo limetokana na tokea kuanzishwa kwa Mamlaka. Hata hivyo, hivi sasa
wamechukua hatua ya kulipunguza deni hilo kwa kuchukua hatua mbali mbali za kuwakatia
maji wateja wasiolipa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imegundua kuwa, tatizo la Mamlaka kutofunga mita kwa wateja wake wote
wanaopata huduma ya maji, ikiwa ni pamoja na wateja wakubwa kunachangia sana
kulimbikizwa kwa madeni hayo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kuharakisha ufungaji wa mita kwa wateja wake na kuchukua hatua
za kuwakatia huduma ya maji wateja wote wenye madeni. Aidha, Kamati inaishauri Serikali
kulipa deni la umeme inalodaiwa Mamlaka.
4.1 SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA
Hoja Namba 76.1 Uwezo wa Shirika kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Shirika lilikuwa na mali za mpito za 331,420,988.90 na dhima za
mpito za 326,189,256.08 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 5,231,732.90 na uwezo wa kulipa
dhima kwa ratio ya 1.01:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa deni la benki na deni la
taasisi nyengine.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 3,535,594,558.59 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 2,731,354,038.59 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh. 804,240,520
ambayo imepanda kwa tofauti ya Tsh. 498,187,980.89 sawa na 163% kwa mwaka
ikilinganishwa na mwaka 2010/2011.
Majibu ya Shirika
Sababu kubwa iliyopelekea hali hiyo ni kulazimika kulipa madeni ya USD 150,000 kwa
Benki ya Watu wa Zanzibar na USD 65,000 walilokuwa wanadaiwa na GAPCO. Hata hivyo,
hivi sasa Shirika halina madeni ya namna hiyo , ila madeni ya mzunguko tu.
Kuhusiana na kupunguza gharama, Shirika limechukua hatua za kurekebisha muundo wake
kwa kuwapa kazi hiyo Chuo cha Uongozi wa Fedha kilichopo Chwaka kwa ajili ya kufanya
uchunguzi wa Shirika kujiendesha kibiashara, kuandaa mpango wa Shirika kujiendesha
kibiashara na kutayarisha mpango mkakati wa Shirika kwa miaka minne. Hata hivyo, Shirika
bado halijakabidhiwa ripoti hiyo.
38
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, Shirika linadaiwa na Shirika la Bandari fedha nyingi na ni
deni la muda mrefu na limethibitishwa na Shirika la Bandari wakati Kamati ilipofika katika
Shirika hilo, ingawa wakati wa mjadala na Shirika la Meli uongozi wake ulieleza kuwa
hakuna uthibitisho wa deni hilo.
Kamati imehitaji kufanya ukaguzi angalau wa stakabadhi za karibuni za Shirika hili
kuwalipa Benki ya Watu wa Zanzibar, ingawaje mpaka tunaandika ripoti hii, hakuna
uthibitisho ulioletwa mbele ya Kamati. Aidha, Kamati ilipohitaji taarifa za matumizi ya
Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi cha Shirika, imeelezwa kukutana kwake mara 4 kwa
mwaka kwa vikao vya kawaida lakini kuna zaidi ya vikao hivyo vinavyofanyika kwa njia ya
dharura na wajumbe wake wanafanya ziara ndani na nje ya Tanzania.
Mapendekezo ya Kamati
Shirika lisimamie ipasavyo ushauri wa kupunguza gharama za matumizi hasa katika
uendeshaji wa shughuli za Bodi ya Wakurugenzi kwa kupunguza wingi wa vikao na safari
zisizo za lazima.
Hoja Namba 76. 2 Kuajiriwa kwa Mfanyakazi wa Kigeni
Shirika limemuajiri Mfanyakazi wa Kigeni Ndg. Abdalla Moh‟d Mwakidudu kutoka Kenya
kwa mshahara wa USD 1,000 kwa mwezi. Mfanyakazi huyo ameajiriwa bila ya kuwepo
kibali cha ukaazi na kutokuwepo kwa ruhusa ya ajira yake kutoka Idara ya Kazi, aidha,
mshahara wake haukatwi kodi ya mapato.
Majibu ya Shirika
Ni kweli Shirika limeajiri mfanyakazi huyo kutokana na kuwa na matatizo ya breakdown ya
mara kwa mara katika meli zake na wamefanya hivyo ili kupunguza gharama za
matengenezo yake kutokana na kukosa mtaalamu wa aina hiyo hapa Tanzania. Shirika
limefunga mkataba na mfanyakazi huyo na tayari wameshachukua hatua za kumtaka alipe
kodi Serikalini.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imegundua kuwa, wafanyakazi hao sio mmoja kama ilivyoelezwa na ripoti ya
Ukaguzi, bali ni watatu ambao ni Ndg. Peter Oguti Wanyama, Ndg. Thomas Msemwa na
Ndg. Abdalla Moh‟d Mwakidudu.
Kamati imejiridhisha kupitia vocha zao za malipo kwamba sasa wanakwatwa kodi na pia
barua ya kuombewa kibali cha kazi kupitia barua ya tarehe 24/04/2014.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inayataka Mashirika ya Serikali kutoa kipaumbele zaidi kwa wafanyakazi wazalendo
na ikibidi kuajiriwa wageni, basi ni lazima wafuate ipasavyo taratibu za kisheria.
4.2 SHIRIKA LA BANDARI
Hoja Namba 75.1 Uwezo wa Shirika kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Shirika lilikuwa na mali za mpito za 10,089,038,751.26 na dhima
za mpito za 1,993,582,704.80 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 8,095,456,046.46 na uwezo wa
kulipa dhima kwa ratio ya 5:1, hali iliyochangiwa zaidi na uwekaji wa fedha benki katika
muda maalum (fixed deposit).
39
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 15,714,578,510.11 na
matumizi yake yalikuwa Tsh. 14,742,721,238.21 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh.
971,857,271.90 ambayo ni ongezeko la Tsh. 842,518,310.04 wastani wa 651 kwa mwaka.
Majibu ya Shirika
Katika kuhakikisha Shirika linaongeza mapato, juhudi mbali mbali zimechukuliwa ikiwa ni
pamoja na kudhibiti vianzio vya mapato. Shirika limefanya mapitio ya viwango vya tozo
(tariff) na kutoza kwa mujibu wa wakati, ambapo viwango hivyo vipya vimesaidia sana
kuongeza mapato.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalishauri Shirika kuongeza juhudi ya makusanyo na kupunguza gharama za
uendeshaji, ili liweze kujiendesha kwa faida.
Hoja Namba 75.1.1 Wadaiwa wa Shirika kwa Taasisi za Serikali, Tsh. 464,465,927 na
USD 843,756.82
Fedha hizo zinadaiwa na Shirika kwa Taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na Kampuni na
watu binafsi kwa huduma mbali mbali zilizotolewa na Shirika, lakini madeni hayo
hayajalipwa kwa muda mrefu sasa.
Majibu ya Shirika
Madeni hayo ni ya muda mrefu na baadhi yao hayana vielelezo vya kuyathibitisha.
Waliandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, tarehe 30/07/2013 yenye kumbu
kumbu namba ZPC/MYS/C.16/VOL III/147, kuomba muongozo wa kisheria kwa ufutwaji
wake, lakini hawakupata majibu yoyote. Aidha, kwa kupitia Makamo wa Pili, waliweka
miadi ya kuonana nae na kujaribu kuwaandikia baadhi ya wadaiwa ikiwa ni pamoja na
KMKM, ila hakuna mafanikio.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha juu ya hatua walizozichukua Shirika katika kutafuta hatua za kusafisha
madeni hayo. Aidha, Kamati pia nayo ilichukua hatua ya kuishauri Serikali kuhusiana na
ufutwaji wa madeni ya namna hiyo kisheria, lakini mpaka leo hakuna hatua zilizochukuliwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuchukua hatua za makusudi na haraka kuyawasilisha madeni
yasiyolipika na ya muda mrefu Barazani kwa hatua za kuyafuta kabla ya Kikao cha Bajeti.
Hoja Namba 75.2 Ukiukwaji wa Sheria na Muongozo wa Manunuzi, Tsh.
856,264,185.92
Lishirika limefanya manunuzi ya vitu mbali mbali kwa matumizi ya Shirika lakini manunuzi
hayo hayajafuata taratibu za Sheria na muongozo wa manunuzi, kinyume na kifungu cha
6(1) na 73 cha Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2005.
Majibu ya Shirika
Fedha hizo zimetumika kwa matengenezo ya „burgee‟ kubwa na wamevinunua vifaa vya
matengenezo yake kutoka Damen Shipyards, Kampuni ambayo ndiyo iliyotengeneza burgee
hiyo na wamefanya hivyo kwa sababu ni kampuni hii pekee ndiyo iliyohusika na burgee
hiyo.
40
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imesikiliza hoja za Shirika na imeridhika kuwepo haja ya kununuliwa vifaa hivyo
kutoka Damen Shipyards, lakini Shirika linapaswa kufuata taratibu za kisheria ambazo nazo
zinaruhusu kwa mazingira maalumu kufanywa ununuzi kutoka kwa Kampuni ama mtoa
huduma mmoja. Aidha, kutokana na kuvunjwa kwa taratibu za sheria katika ununuzi huo,
Kamati haikuridhishwa na hatua hiyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Shirika lifuate taratibu za kisheria katika kutumia fedha za umma.
Hoja Namba 75.3 Malipo yaliyofanywa kinyume na utaratibu , Tsh. 56,891,500
Fedha hizo zimelipwa kwa matumizi mbali mbali ya Shirika, lakini stakabadhi
zilizothibitisha kupokea malipo hayo hazikubaliki kwa mujibu wa Sheria.
Majibu ya Shirika
Shirika halioni kuwepo kwa kosa lolote katika stakabadhi hizo ambazo zinatoka Sami
Trader, ambaye katika risiti zake zimo Tin Numbers na Namba za ZRB kuonesha kuwa
mfanya biashara huyu analipa kodi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati nayo imezipitia risiti hizo na kujiridhisha kuwa, zimo tin namba 104-704-603 na
namba za ZRB, ambazo ni ZRB/03/LCA/271.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inapendekeza kuwa hoja hii ifutwe.
4.3 BODI YA MAPATO YA ZANZIBAR (ZRB)
Hoja Namba 82.1 Uwezo wa Bodi kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
Uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Bodi ilikuwa na mali za mpito za 546,302,494 na dhima za mpito
za 208,718,033 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 337,584,461 na uwezo wa kulipa dhima kwa
ratio ya 2.6:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa pamoja na salio la benki na
hivyo ni faraja kwa Bodi.
Mapato ya Bodi kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 5,495,692,118 na matumizi yake
yalikuwa Tsh. 4,691,543,773 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh. 804,148,345 ambayo
imeshuka kwa tofauti ya Tsh. 277,976,439 sawa na 25.7% kwa mwaka ikilinganishwa na
mwaka 2010/2011.
Majibu ya Bodi
Kuhusiana na takwimu zilizoelezwa na Mdhibiti kuhusiana na uwezo wa Bodi kujiendesha,
zinahitaji kupatiwa usahihi wake kwa kuwa Bodi imeeleza kuwa hazina usahihi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imesikiliza maelezo ya Bodi na kumtaka Afisa wa Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali anaefuatana na Kamati kulifuatilia zaidi suala hili ili lipatiwe
usahihi wake.
41
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inamshauri Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu kutayarisha vyema taarifa zake
ili ziweze kueleweka kwa wepesi na usahihi na Kamati iweze kuzifanyia kazi kwa uhakika.
Hoja Namba 82.2 Malipo ya ziada kwa ujenzi wa jengo jipya la Mazizini, Tsh.
2,387,492,229.85
Bodi ilifunga Mkataba na China Railways Co. Ltd kwa barua yenye kumbu kumbu namba
ZRB/C.3/VOL.1/48 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo, huku bei ya ujenzi mpaka kukamilika
kwake ni Tsh. 6,216,820,414.69 kwa muda wa wiki 104 tokea tarehe ya kuanza kazi,
10/07/2009. Aidha, mpaka ilipofikia mwisho wa mwaka 2012, Bodi imeshalipa Tsh.
8,604,312,644.54 ikiwa ni ongezeko la Tsh. 2,387,492,229.85 zaidi ya makubaliano ya
mwanzo ya mkataba wa ujenzi ambapo bado malipo hayo yataendelea kulipwa katika
mwaka wa fedha 2012/2013 na kuongezeka kwa gharama za ujenzi.
Majibu ya Bodi
Uongozi wa Bodi ulilazimika kujenga jengo la Afisi zake katika eneo la Kilimani kwa
thamani ya Tsh. 6,488,171,072, na taratibu zote za tenda zilikuwa zimekamilika. Hata hivyo,
Mshauri Mwelekezi alishauri ujenzi huo usifanyike hapo kutokana na kupitishwa kwa mtaro
mkubwa wa kuondosha maji ya mvua, hatua iliyopeleka Serikali kupatiwa kiwanja chengine
Mazizini.
Hatua hii ililazimu kufanywa marekebisho katika ujenzi wa Mazizini kwa kuongeza ghorofa
moja katika sehemu ya nyuma ya jengo, kubadilisha „structure‟ za „patrons‟ (material and
designs) tofauti na mchoro wa awali, kubadilisha mfumo wa umeme, kuongeza na mambo
mengine.
Hivyo, ni kweli kuna ongezeko la Tsh. 2,387,492,229.85 na kufanya gharama hizo kuwa
Tsh. 8,604,312,644.45 badala ya Tsh. 6,216,820,414 zilizokisiwa awali kwa ujenzi
uliotarajiwa kufanyika Kilimani. Aidha, kiwango cha malipo alichokwishalipwa Mjenzi ni
Tsh. 8,392,755,072.87 na fedha zilizosalia kulipwa hadi kukabidhiwa jengo ni Tsh.
211,557,571.57 na Uongozi wa Bodi uliwasiliana na Bodi ya Wakurugenzi kuhusiana na
mabadiliko hayo ili kupata idhini iliyotakiwa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji taratibu za sheria ya manunuzi kama zimefuatwa katika upatikanaji wa
Mshauri Mwelekezi na Mjenzi. Na kwa upande wa upatikanaji wa Mshauri Mwenyekezi,
Ndg. Ramadhan Mussa Bakar (Rama China), Kamati imejiridhisha kwamba, haukufuatwa
utaratibu kwa sababu yeye sio Kampuni bali alielezwa kama mtu binafsi. Aidha, Kamati
imejiridhisha kuwa, Ndg. Rama China alikuwemo katika Kamati ya Tathmini na amealikwa
kama mataalamu wala sio kwamba, amepatikana kwa taratibu za kisheria kama Mshauri
Mwelekezi na badala yake, Bodi imetafuta Mtaalamu Mwelekezi mwengine.
Kuhusiana na ujenzi, Kamati ilihitaji kupatiwa Mkataba wa Mkandarasi wa ujenzi wa
Kilimani na taratibu za kupatikana kwake.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati iliutaka Uongozi wa Bodi kufuatilia ipasavyo Sheria na Kanuni za manunuzi, ili
kuepusha hasara kwa Serikali. Aidha, Kamati inaishauri Serikali kuwa makini na Washauri
Elekezi wa kigeni ambao baadhi yao huwa sio waaminifu na hushirikiana na Mjenzi katika
kuhujumu fedha za Umma.
42
Hoja Namba 82.3 Vifaa vya Tsh. 21,529,000 ambavyo havikuingizwa katika Daftari
la ghalani.
Fedha hizo zimetumika kwa ununuzi wa vifaa mbali mbali lakini havikuingizwa katika
daftari la ghalani na kupelekea kushindwa kuthibitishwa uhalali wake.
Majibu ya Bodi
Ni kweli vifaa hivyo havikuingizwa kutokana na haja ya kuepuka gharama kwa kampuni
mbili tofauti kwa ajili ya ununuzi na kufanya „installation‟. Bodi iliona ni vyema kutumia
kampuni moja itakayofanya kazi zote mbili chini ya „guarantee‟ ya vifaa walivyowauzia,
kwani kampuni hizo ndizo zilizotumika kwa baadhi ya maeneo ya ujenzi.
Pia vifaa hivyo havikuingizwa katika daftari kutokana na uharaka uliojitokeza kwa wakati
huo ili kupata vifaa vitakavyosaidia kukwamua changamoto za dharura zilizojitokeza kipindi
hicho.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na fedha za ununuzi wa vifaa hivyo kupewa Mjenzi, vifaa hivyo vinatakiwa
kurikodiwa katika daftari la ghalani kama taratibu zilivyo, na zaidi kwa kuzingatia kuwa,hati
ya malipo iliyohusika na matumizi ya fedha hizo imejitegemea na ile iliyohusika na malipo
kwa Mjenzi.
Aidha, Kamati imejiridhisha kwamba, Bodi haikutekeleza maelekezo ya sheria kwa
kutofuata taratibu za manunuzi za matumizi ya fedha hizo na zaidi kwa kitendo cha Bodi
kumpa mjenzi huyo fedha zilizohusika na hoja hii, bila ya wao wenyewe kununua vifaa
hivyo na kumpatia mjenzi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati iliitaka Bodi kuzingatia sheria za manunuzi kwa matumizi yote ya fedha za Serikali.
Hoja Namba 82.4 malipo yasiyokuwa na vielelezo (Nyaraka pungufu) za Tsh.
915,788,712
Fedha hizo zimetumika kwa mahitaji mbali mbali ya Bodi, lakini vielelezo vya kuthibitisha
matumizi yake vimekosekana wakati wa ukaguzi.
Majibu ya Bodi
Viongozi wa Bodi wamekiri kuwa, wakati wa ukaguzi vielelezo hivyo havikuwepo na
vilikuwa „misplaced‟ lakini ilipofika Kamati vilipatikana na Kamati kuombwa kuvikagua na
kujiridhisha juu ya usahihi wake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati haikuona haja ya kuvipitia na kuvikagua vielelezo hivyo, kwani Sheria ya Fedha na
Kanuni zake zinaelekeza kupatikana kwa vielelezo vya matumizi ya fedha za Serikali, mara
tu matumizi ya fedha hizo yanapofanyika.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuchukua hatua stahiki kama ilivyoelezwa katika Sheria na Kanuni
za Fedha za Umma za mwaka 2005.
Hoja Namba 82.5 Kitengo cha Magendo
Sheria Namba 36 ya Kodi ya Mafuta inamtaka mtu aliyekamatwa akijihusisha na upitishaji
ama uletaji wa mafuta kinyume na Sheria, awajibike kulipa faini isiyopungua Tsh. 1,000,000
43
na isiyozidi Tsh. 10,000,000 ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafirishaji na uwekaji
wa mafuta hayo, sambamba na utaifishwaji wa vyombo vilivyotumika kusafirishia mafuta
hayo.
Aidha, Ukaguzi ulibaini Kitengo hiki cha Magendo kilikamata vyombo mbali mbali katika
mwaka 2012 lakini vielelezo vinaonesha utaifishwaji wa vyombo hivyo havikupatikana kwa
ukaguzi.
Majibu ya Bodi
Ni kweli MV. Mashallah na MV. Burak 1 na Burak 2 pamoja na gari la mafuta (Tanker)
viliwahi kukamatwa na Bodi vikiwa vimepakia mafuta ya magendo na mafuta
yaliyokuwemo kwenye vyombo hivyo yalitaifishwa na kuuzwa. Hatua ya utaifishaji wa
mafuta yaliyokamatwa ilichukuliwa kwa sababu utaratibu upo na unaeleweka, lakini kwa
upande wa utaifishaji wa vyombo haikuchukuliwa, kutokana na changamoto zake zikiwa ni
pamoja na kukosekana kwa utaratibu wa kufuatwa katika utaifishaji wa vyombo vya aina
hiyo na bado wananchi, ikiwia ni pamoja na taasisi za Serikali na za watu binafsi, bado
hawajapewa taaluma ya kutosha kuhusiana na matakwa ya Sheria ya mafuta, Zanzibar na
utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika kufanya biashara ya mafuta na nishati pamoja na athari
za biashara ya magendo.
Hata hivyo, Bodi imetayarisha utaratibu unaotakiwa wa kuondoa changamoto hizo kwa
kutayarisha utaratibu wa kufuatwa katika utaifishaji wa vyombo hivyo na kujipanga upya ili
kutoa elimu ya kisheria na utaratibu utakaotumika katika utaifishaji wake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati inachukulia hoja za Bodi kama za kujitetea zaidi na hazikusudii kutekeleza
majukumu yao waliyopangiwa kisheria. Aidha, Kamati imehoji iwapo ZRB inatumia kanuni
zozote katika kuendesha zoezi la kukamata mafuta ya magendo na kuelezwa kuwa, kanuni
zimeshatungwa ila zinasubiri saini ya Mhe. Waziri kwa ajili ya kuwa na nguvu kisheria.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeitaka Bodi kufuata taratibu za ukamataji kisheria na kuharakisha utiwaji saini wa
kanuni zao ili waweze kuzitumia katika majukumu yao.
4.4 MAMLAKA YA VITEGA UCHUMI ZANZIBAR (ZIPA)
Hoja Namba 13 Kuwasilisha hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi
Mamlaka imeshindwa kuwasilisha hesabu zake za mwisho wa mwaka kwa Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu na hivyo ameshindwa kutoa taarifa za ukaguzi za Taasisi hii.
Majibu ya Mamlaka
Hawakuweza kufunga hesabu kwa sababu hawana thamani ya mali zote na ili uweze
kufunga hesabu ni lazima ujue thamani ya mali zako zote. Wamewasiliana na Chuo cha
Ardhi kilichopo Tanzania Bara kwa ajili ya kuwafungia hesabu, lakini chuo hicho kilihitaji
Tsh. 30,000,000/ fedha ambazo ni nyingi na hawakuwa nazo. Aidha, wameshindwa hata
kupata muongozo kutoka Wizara ya Fedha ya Zanzibar juu ya ufungaji wa hesabu zao,
wakati Taasisi hii ni tofauti na Taasisi nyengine za Serikali.
44
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, Mamlaka imeshindwa kufunga hesabu za mwaka wa
2011/2012, ingawaje ilipofanya ukaguzi wa mwaka uliofuata, ilithibitisha kwamba, hesabu
hizo zimefungwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imekemea tabia ya Mkurugenzi kushindwa kufunga hesabu kwa kusingizio cha
kutopata muongozo wa Wizara ya Fedha wakati muongozo huo ulikwisha toka zamani.
Kamati inamtaka Mkurugenzi wa Mamlaka kurekebisha kasoro hii.
4.5 CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)
Hoja Namba 72.1 Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi
na uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Chuo kilikuwa na mali za mpito za 943,877,359 na dhima za mpito
za 112,138,600 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 831,738,759 na uwezo wa kulipa dhima kwa
ratio ya 8.4:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa pamoja na salio la benki
kwa hesabu za Chuo.
Aidha, kwa upande wa uwezo wa kujiendesha, ukaguzi umepima mapato ya Chuo kwa
mwaka 2011/2012 ambayo yalikuwa ni Tsh. 6,340,907,560 na matumizi yalikuwa Tsh.
6,785,849,432, huku kukiwa na upungufu wa Tsh. 444,941,872 ya matumizi ukilinganisha
na mapato.
Majibu ya Chuo
Ni kweli kama ilivyoelezwa na ukaguzi kuhusiana na mali za mpito ambazo zinajumuisha
akiba ya Chuo Benki, madeni ya ada za wanafunzi na madeni ya mikopo ya wafanyakazi.
Kuhusu uwezo wa kulipa kuwa mkubwa kuliko kiwango cha kawaida (cha 2:1), hali hii
imechangiwa na kuwa na salio la kiwango kikubwa wakati wa kifunga hesabu kutokana na
fedha za mradi. Kwa mfano Tsh. 783,354,609.23 kama akiba katika hesabu za benki za
Chuo, kati ya hizo, Tsh. 445,845,500 zilikuwa za mradi wa Sayansi na Teknolojia
unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, Tsh. 69,576,096 zilikuwa ni za mradi wa „Building
Stronger Universities‟ unaofadhiliwa na Serikali ya Denmark na Tsh. 118,317,692 zilikuwa
ni mfuko maalum kwa ajili ya wanataaluma wa Chuo.
Kuhusiana na taarifa za mapato na matumizi, Chuo kiutaratibu kinatakiwa kioneshe mapato
yake yote kilichoyakusanya kwa mwaka unaohusika kutoka katika vyanzo vyake vyote,
ambavyo ni Ruzuku (Serikalini), mapato ya misaada au fedha za miradi na mapato
yaliyozalishwa na Chuo. Na matumizi nayo pia wanapaswa kuyaonesha na kuyajumuisha
katika vyanzo vya mapato vya Chuo.
Aidha, ukubwa wa matumizi umetokana na kutekeleza kazi za miradi kwa mwaka
2011/2012 kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na pesa walizozipokea. Ziada ya matumizi
ilitekelezwa kwa fedha zilizoletwa na kubaki katika mwaka wa fedha 2010/2011.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka kufahamu iwapo hali ya upungufu ingeliendelea na kuelezwa kuwa, Chuo
kimejipanga kuongeza mapato yao kwa kuimarisha ukusanyaji wa ada za wanafunzi,
kuanzisha program za elimu kwa jamii, kushajihisha mafunzo ya Kiswahili kwa wageni na
kuwashajihisha wafanyakazi kuandaa miradi mbali mbali.
45
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imekitaka Chuo kuchukua juhudi ya kuhakikisha kinaongeza mapato ili kukidhi
mahitaji yake.
Hoja Namba 72.1.1 Malipo yaliyofanywa kinyume na kanuni na taratibu za
manunuzi, Tsh. 74,084,000
Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa gari ya Makamu Mkuu wa Chuo, lakini
ununuzi huo haukufuata Sheria wala kanuni ya manunuzi.
Majibu ya Chuo
Ni kweli wamefanya matumizi ya fedha hizo kwa kununua gari kama ilivyoelezwa na ripoti,
lakini wamefuata taratibu za manunuzi kwa kutumia njia ya „Single Source‟, kama
inavyoelezwa na kifungu cha 38 cha Sheria ya Manunuzi.
Uchunguzi wa Kamati
Kifungu cha 38 kinachoelezea „Direct Procurement method‟, kinashurutisha kutumiwa njia
hii kwa kuwepo dharura ya kutolazimika kupatikana washindani zaidi ya mmoja katika
manunuzi, ikiwa ni pamoja na bidhaa inayonunuliwa kuwa haipatikani zaidi ya muuzaji
mmoja, kuwepo kwa haraka ya manunuzi yake ambayo haikupangwa kabla na masharti
mengine ambayo Chuo hawakuyafuata wala hawakuwa na sababu ya kulazimika kutumia
njia hii. Hata hivyo, wakati Kamati inakagua hati iliyohusika na manunuzi hayo, imegundua
kuwa Chuo kimetafuta wauzaji watatu, na kuchagua mmoja. Hivyo, fedha hizo ni nyingi na
walilazimika kufuata taratibu za tenda, angalau kufanya „quotation‟ kwa njia ya tenda, na
njia hiyo kupata idhini ya Bodi ya Zabuni, vitu ambavyo havikufanyika.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kufuata kikamilifu taratibu za manunuzi.
4.6 CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA
Hoja Namba 70.1 Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha.
Chuo cha Uongozi wa Fedha kwa mwaka 2011/2012, kilikuwa na mali za mpito zenye
thamani ya Tsh. 956,583,572 na dhima za mpito za 63,900,594 kwa bakaa la thamani ya Tsh.
892,682,978 na uwezo wa kulipa dhima kwa ratio ya 15:1, hali iliyochangiwa zaidi na
kuwepo kwa wadaiwa pamoja na salio la benki kwa hesabu za Chuo.
Mapato ya Chuo kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 2,802,282,653 na matumizi yake
yalikuwa Tsh. 1,681,555,319 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh. 1,120,727,333 ambayo
imeshuka kutoka Tsh. 1,409,434,625 kwa mwaka 2010/2011.
Majibu ya Chuo
Chuo hiki ni taasisi inayotoa huduma kwa umma na haifanyi biashara, hivyo haiwezi
kufanya faida. Fedha inayobakia katika akaunti yao, huwa wanaifanyia kazi katika maeneo
mengine. Aidha, kuhusiana na kuongezeka kwa dhima za mpito inatokana na mikato na wao
hawalipi mpaka wapate ruzuku. Pia wana deni ZSSF, ambapo hawawezi kulipa mpaka
waingiziwe fedha na Serikali, jambo linalowafanya wasubiri hiyo ruzuku kutoka Serikalini
ambayo kwa kawaida huchelewa.
46
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji kuongezeka kwa dhima za mpito kwa mwaka 2011/2012 ukilinganisha na
mwaka 2010/2011, ambapo ilielezwa inatokana na deni walilokuwa wanadaiwa na China
Railways Jang Chang Engineering Ltd kutokana na ujenzi wa dahalia ya wanafunzi. Aidha,
kwa mwaka huo, pamoja na juhudi walizozichukua Wizara ya Fedha, bado walikuwa
wanawadai milioni 500 za ada ya wanafunzi wanaolipiwa na Wizara hiyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imekitaka Chuo kuongeza kasi na umakini katika kukusanya mapato hasa kwa
kufuatilia ada za wanafunzi na kuhakikisha wanalipia gharama zinazowakabili.
Hoja Namba 70.1.1 Mfuko wa Mchango wa Wafanyakazi wa Chuo (ZIFA Deposit
Fund)
Wafanyakazi wa Chuo hukatwa mishahara yao ya kila mwezi na fedha hizo huhifadhiwa
katika hesabu ya Chuo. Idadi ya fedha hizo haikuwa inakaguliwa kutokana na kukosekana
kwa kumbu kumbu zinazohusiana na michango hiyo. Aidha, kuendelea kutumika hesabu ya
Chuo kwa kuingiza na kutoa fedha zinazotokana na michango ya wafanyakazi, kunaweza
kusababisha mwanya na upotevu wa fedha za Chuo na kupelekea kutokujua idadi halisi ya
fedha za Chuo na fedha za michango ya wafanyakazi.
Majibu ya Chuo
Ni kweli mchango huo upo ambapo walimu huchangia Tsh. 5000 na wafanyakazi wengine
huchangia Tsh. 3000 kwa mwezi, fedha ambazo zinawasaidia wafanyakazi wenyewe wakati
wanapopata mitihani ikiwa ni pamoja na majanga. Fedha hizo pia hugawana kwa mwaka
sawa sawa bila ya tofauti ya michango waliyoitoa.
Chuo kimechukua hatua za kupeleka nyaraka zao za Mfuko kwa Mkurugenzi anaehusika na
SACCOS, ili waunde SACCOS ya Chuo, lakini walielekezwa kuwa na mtaji usiopungua
Milioni 20, hali iliyopelekea ugumu wa kuanzisha SACCOS yao.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, Chuo kimeanzisha akaunti hiyo kwa nia njema na fedha hizo
zina msaada mkubwa kwa wafanyakazi wote wa Chuo. Hata hivyo, kuzichanganya fedha
hizo na account ya Chuo huenda kukaleta matatizo.
Kwa ajili ya kujiridhisha juu ya fedha hizo, Kamati ilihitaji kupatiwa taarifa za mikato
ambazo zililetwa na kukaguliwa na Kamati.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakishauri Chuo kutafuta utaratibu wa kuihifadhi fedha inayopatikana katika
michango ama mikato hiyo ya wafanyakazi, ili kuepusha utata ambao ungeliweza kujitokeza.
4.7 MAMLAKA YA KUSIMAMIA UVUVI WA BAHARI KUU
Hoja Namba 73.1.1 Kuwasilisha hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi
Mamlaka imechelewa kuwasilisha hesabu zake za mwisho wa mwaka kwa Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu, kinyume na maelekezo ya Sheria ya Fedha za Mwaka ya mwaka
2005.
47
Majibu ya Mamlaka
Mamlaka imekiri kuchelewesha hesabu hizo kutokana na tatizo la uchache wa wafanyakazi
wenye uwezo wa kufunga hesabu zao, na huku ikizingatiwa kuwa Mamlaka imeazishwa
karibuni, mwaka 2010.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na majibu ya Mamlaka, Kamati imehoji iwapo hesabu hizo kwa mwaka uliofuata
(2012/2013) zimewasilishwa kwa wakati na kuelezwa kuwa, pia imechelewa ingawa kwa
mwezi mmoja.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeitaka Mamlaka kurekebisha kasoro hiyo kwa haraka.
Hoja Namba 73.1 Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi
na uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Mamlaka ya Maji ilikuwa na mali za mpito za 2,386,660,778 na
dhima za mpito za 24,536,873 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 2,362,123,906 na uwezo wa
kulipa dhima kwa ratio ya 97.2:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa salio kubwa
benki, la Tsh. 2,385,780,364 kwa hesabu za Mamlaka.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 2,337,056,151 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 539,443,728 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh. 1,797,612,422.
Majibu ya Mamlaka
Mamlaka haina dhima kubwa za mpito kutokana na kwamba Mamlaka imeanzishwa
karibuni na haina madeni makubwa. Kwa mfano, wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika
Mamlaka wameazimwa kutoka Wizara zinazohusika na Uvuvi, Tanzania Bara na Zanzibar,
hali inayofanya pia wasiwe na dhima ya kodi inayotokana na mishahara (payee).
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na majibu yao, Kamati ilitaka kufahamu kuhusu utaratibu wa vikao vya Bodi ya
Wakarugenzi ya Mamlaka, na ilielezwa kwamba, vikao hivyo havijawahi kuitishwa zaidi ya
vinne na hivyo hakuna matumizi makubwa ya vikao hivyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeitaka Mamlaka kufanya vizuri zaidi katika uwiyano wa mali na dhima zao za
mpito, pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji na kuinua ufanisi, ili uwezo wa
Mamlaka uendelee kukua.
Hoja Namba 73.2 Malipo yasiyokuwa na vielelezo, Tsh. 178,460,370 na Pound 8,354
Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya matumizi mbali mbali ya Mamlaka, lakini vielelezo vya
kuthbiitisha uhalali wa matumizi hayo havikupatikana kwa ukaguzi.
Majibu ya Mamlaka
Wakati wa ukaguzi vielelezo hivyo vilikuwepo na suala hili lilisababishwa na Mkaguzi
aliyekuja kufanya ukaguzi, hakuangalia mafaili yote, wakati mafaili hayo yalikuwepo na
walipogundua ilikuwa tayari Mdhibiti huyo ameshaandika ripoti yake.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na majibu hayo, Kamati haiwezi kukubaliana moja kwa moja na Mamlaka, kwa
sababu kwa kawaida ukaguzi hufanywa kwa kutolewa taarifa mapema na mashirikiano ya
48
moja kwa moja, baina ya Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na Taasisi
inayohusika na ukaguzi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeishauri Mamlaka kutekeleza vyema majukumu yake ili iweze kutoa taarifa kwa
wakati pale zinapohitajika.
4.8 BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (P.B.Z)
Hoja Namba 71.1 Kuwasilisha hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi
Benki imeshindwa kuwasilisha hesabu zake za mwisho wa mwaka kwa Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu na hivyo ameshindwa kutoa taarifa za ukaguzi za Taasisi hii.
Majibu ya Benki
Benki inafunga hesabu zake kila mwisho wa mwaka, kwa kuzingatia taratibu na maelekezo
ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ila tatizo lilikuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
alikua hahusishwi katika ukaguzi huo, wakati yeye Kikatiba na Sheria za Zanzibar ndie
mwenye mamlaka ya ukaguzi au kwa idhini yake.
Hata hivyo, tatizo hilo kwa mwaka 2012/2013 litakua limeshaondoka kwa sababu Serikali
kupitia Wizara ya Fedha imeshalishughulikia suala hili, kwa ukaguzi kufanywa kwa idhini
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Mkaguzi atakaepewa kazi hiyo atatoa mashirikiano kwa
Maofisa wa Afisi hii.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati inakiri kupokea taarifa hiyo kutoka Afisi ya Mdhibiti na Serikali yenyewe na
imepongeza hatua hizo ambazo Kamati ililisimamia suala hilo kwa miaka ya nyuma.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kutoa mashirikiano makubwa kwa Taasisi hizi kwa kila mmoja
kutekeleza majukumu yake Kikatiba na Kisheria ili kuweza kupata ufanisi zaidi.
4.9 SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI
Hoja Namba 66.1 Uwezo wa Shirika kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Shirika la Magazeti kwa mwaka 2011/2012, ilikuwa na mali za mpito za 383,326,865 na
dhima za mpito za 30,725,405 kwa bakaa ilikuwa na thamani ya Tsh. 352,601,460 na uwezo
wa kulipa dhima kwa ratio ya 12:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wengi
wa Shirika pamoja na salio la benki.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 788,358,419 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 838,874,818, hali iliyopelekea kuendeshwa kwa hasara ya
Tsh.50,516,399 ambapo mwaka wa 2010/2011, Shirika liliendeshwa kwa hasara ya Tsh.
55,981,988, ingawaje imepungua kidogo kwa Tsh. 5,465,589.
Majibu ya Shirika
Shirika limekiri taarifa hiyo na kueleza kuwa, deni kubwa linatokana na gharama za
uchapishaji wa magazeti, kwa sababu mpaka leo Zanzibar haina kiwanda na mashine ya
49
kuchapisha magazeti ya rangi, hali inayolifanya Shirika kupeleka magazeti yake
kuchapishwa Dar es Salaam ambako ni ghali sana.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwapo Shirika lina mkakati wowote wa kuondokana na tatizo la uchapishaji
huo na kuelezwa kuwa Shirika limekuwa likiandika mradi kwa kila mwaka na kuupeleka
Serikalini, lakini hilo bado halijafanikiwa.
Hata hivyo, hivi sasa Shirika limeamua kuiuza kwa Wafadhili miradi hiyo lakini nalo bado
halijafanikiwa. Shirika pia limezungumza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar
(ZSSF) kwa ajili ya kupatiwa mkopo wa Milioni 800 kwa ajili ya ununuzi wa mtambo wa
rangi wa kuchapisha magazeti, ambapo mtambo mpya haupungui Bilioni 2. Hata hivyo,
suala hili la kupatiwa mkopo huo linahitaji udhamini wa Serikali.
Kamati inahoji juu ya matumizi ya Tsh. 800 milioni kwa ununuzi wa mitambo iliyotumika,
ikizingatiwa pia Serikali sasa haitakiwi kununua vifaa ama mitambo kama hiyo iliyotumika.
Aidha, kuhusiana na uwezo wake wa kujiendesha, Kamati imepata maelezo na imeridhika
kwamba, Serikali imelianzisha Shirika hilo bila ya kulipatia nyenzo kamili za kufanyia kazi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imelitaka Shirika kufanya ununuzi wa mitambo mipya ya rangi kwa ajili ya
uchapishaji wa magazeti, lakini inaitaka Serikali na Shirika kusimamia kwa makini na kwa
misingi ya Sheria suala zima la ununuzi wa mitambo inayotakiwa na Shirika.
Hoja Namba 66.1.1 Kukosekana kwa mchanganuo wa samani (Assets) zenye thamani
ya Tsh. 443,845,155
Fedha hizo zimeoneshwa katika taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka za Shirika, bila ya
kuwepo mchanganuo wa orodha ya samani hizo, kinyume na taratibu za kufunga hesabu.
Majibu ya Shirika
Shirika limekiri kukosekana kwa mchanganuo huo wakati wa ufungaji wa hesabu hizo,
kasoro ambayo tayari wameshairekebisha.
Uchunguzi wa Kamati
Maelekezo ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2005 na kanuni zake, zinaelekeza kuorodheshwa
kwa mchanganuo huo, katika taarifa za hesabu zinazotakiwa kuwasilishwa kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu. Kukosekana wakati wa hesabu ni kwenda kinyume na
maelekezo ya sheria.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inautaka uongozi wa Shirika kuwa makini wakati wa kufunga hesabu, kwa
kuhakikisha taarifa zote zinazotakiwa katika hesabu hizo zinapatikana kwa wakati.
Hoja Namba 66.1.2 Madeni kwa Taasisi za Serikali, Tsh. 323,925,000
Fedha hizo zinadaiwa na Shirika kwa taasisi mbali mbali za Serikali kwa huduma za mauzo
ya magazeti pamoja na matangazo yaliyochapishwa katika gazeti la Zanzibar Leo. Fedha
hizo bado hazijalipwa.
Majibu ya Shirika
Shirika limechukua hatua mbali mbali kudai kulipwa kwa madeni hayo ikiwa ni pamoja na
kuziandikia taasisi zenye madeni, hatua ambazo zimeleta mafanikio kwa kupunguzwa kwa
50
deni hilo, ambapo kwa sasa deni hilo limeshalipwa Tsh. 103,773,000 na limebakia
220,152,000/-. Aidha, Shirika wamelipeleka suala hilo Serikalini na Katibu Mkuu Kiongozi
aliwaandikia Makatibu Wakuu wanaohusika na deni kuwataka walipe madeni yao, hatua
ambayo ilileta mafanikio japo kwa kiasi kidogo.
Uchunguzi wa Kamati
Shirika limekuwa linatoa huduma kwa taasisi za Serikali bila ya kulipwa na hatimae deni
hilo huwa kubwa, kutokana na kukosekana kwa utaratibu imara wa Shirika kusimamia
malipo ya huduma wanayoitoa, na hatimae huwepo na ugumu mkubwa wa kudai madeni
hayo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kulisaidia Shirika katika kusimamia madeni yake, ili fedha
zinazodaiwa na taasisi za Serikali ziweze kulipwa. Na kama taasisi hizo zitashindwa kulipa
kwa khiari, basi zikatwe katika bajeti zao.
Hoja Namba 66.2 Gharama za uchapishaji, Tsh. 313,612,866
Kwa kawaida Shirika linapatiwa ruzuku ya Tsh 238,799,240 ili kukidhi kulipa mishahara ya
wafanyakazi wake. hata hivyo, ukaguzi umebaini kuwa, kutokana na gharama za uchapishaji
kuwa kubwa, Shirika linalazimika kukopa ruzuku hiyo na kuitumia kwa ajili ya uchapishaji
wa gazeti hilo na kuathiri ulipaji wa mishahara. Aidha, Shirika linalazimika kuwa na ukosefu
wa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za Shirika kwa wakati unaotakiwa na kusababisha
wafanyakazi kutopata mishahara yao kwa wakati.
Majibu ya Shirika
Suala hilo halijawahi wala halitaweza kufanyika kutokana na utaratibu wa mishahara ya
wafanyakazi kuingizwa moja kwa moja benki na wafanyakazi huchukua fedha hizo kupitia
akaunti zao, wala hazipitii katika Shirika.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imemtaka Afisa Mdhibiti anaefuatana na Kamati kufuatilia zaidi suala hili, ili
uhakika wake uweze kupatikana.
Mapendekezo ya Kamati.
Kamati inahitaji muda zaidi na uhakika zaidi wa taarifa hii, ili iweze kuifuatilia kwa uhakika
wake.
4.10 SHIRIKA LA UTALII
Hoja Namba 68.1 Uwezo wa Shirika kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Shirika lilikuwa na mali za mpito za 62,262,419 na dhima za mpito
za 31,500,000 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 30,500,000 na uwezo wa kulipa dhima kwa
ratio ya 2:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wengi wa Shirika.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 107,523,000 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 180,879,549 na hivyo kuendeshwa kwa hasara ya Tsh. 73,356,549.
Majibu ya Shirika
Wanakubaliana na maelezo ya ripoti, na hatua zilizochukuliwa na Serikali ni kulivunja
Shirika hilo, kupitia kikao cha Baraza la Mapinduzi cha tarehe 14/03/2013. Aidha, mali za
51
Shirika zimeshakabidhiwa Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mitaji ya Umma na taarifa ya
kufungwa kwa Shirika hilo ilitolewa katika Baraza la Wawakilishi kupitia hotuba ya Bajeti
ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo ya mwaka 2013/2014.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeandika barua Serikali kutaka uthibitisho wa kuvunjwa kwa Shirika hilo, na
kuthibitishiwa kuwa limevunjwa kwa mujibu wa taraitub za Sheria.
Mapendekezo ya Kamati.
Kamati haikuweza kuendelea na hoja zilizobakia za Shirika kutokana na kutokuwepo kwake.
Aidha, Kamati inaitaka Serikali kuwa makini na uvunjaji wa Mashirika kwa kuzingatia
taratibu zilizopo na kuchunga upotevu wa mali za Mashirika hayo, ambapo bila ya
kusimamiwa ipasavyo, upotevu huo utatokea.
4.11 HOTELI YA BWAWANI
Hoja Namba 67.1 Uwezo wa Hoteli kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Mali za Mpito za Hoteli ya Bwawani kwa mwaka 2011/2012,zilifikia thamani ya Tsh.
356,429,176.65 na dhima za mpito zikifikia thamani ya Tsh. 37,975,888.38 na hivyo kufanya
hali halisi ya mali za mpito kuwa Tsh. 318,453,287.80 kwa ratio ya 9.38:1, hali
iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa pamoja na salio la benki Tsh. 240,436,414.68
kwa mwaka 2011/2012, fedha ambazo zingeliweza kutumika kwa kuiendeleza hoteli kwa
uwekezaji na kupunguza tatizo la upungufu wa mishahara ya wafanyakazi limaloikabili
hoteli kwa muda mrefu.
Aidha, Hoteli imekuwa na mapato ya Tsh. 1,100,632,772 na matumizi yakawa Tsh.
1,059,818,300.73 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 40,814,471.27.
Majibu ya Hoteli
Uongozi wa hoteli umechukua hatua mbali mbali za kudai madeni kwa watu na taasisi mbali
mbali za Serikali na binafsi, hatua ambayo imesaidia sana kupunguza kwa kiasi kikubwa
kwa madeni hayo. Kwa upande wa uwezo wa kujiendesha, uongozi umechukua hatua za
kudhibiti vianzio vya mapato viliopo na kubuni vipya. Aidha, uongozi ulipitia viwango
vinavyotozwa kwa huduma mbali mbali na kubaini vingi vyao vimepitwa na wakati na kwa
kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, viwango hivyo
vimerekebishwa kwa kuendana na wakati.
Uchunguzi wa Kamati
Taasisi nyingi za Serikali zinazodaiwa na Hoteli huwa hazilipi huduma wanazopatiwa na
kuifanya hoteli kama sehemu inayotolewa huduma bure. Kamati imejiridhisha kwamba,
Wizara yenyewe ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo inadaiwa Tsh. 17,520,640 kwa
muda mrefu na wala hailipi. Hali hii inaifanya Kamati iamini kuwa, Wizara hii inaifanya
Hoteli kama kitega uchumi chake bila ya malipo yoyote ya huduma inayopatiwa. Aidha,
Kamati imepewa taaria ya barua mbali mbali zilizoandikwa na Hoteli kwa wadaiwa wake
kuwataka walipe madeni yao. Kamati imeridhishwa na hatua hiyo, lakini bado haitoshi kuwa
njia pekee ya kudai.
52
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuangalia na kufanya maamuzi sahihi ya hatima ya Hoteli
ama iwe Shirika linalojitegemea, Idara iliyo chini ya Wizara au vyenginevyo, kuliko
hali iliyopo sasa.
Hoteli iundiwe chombo cha usimamizi wake badala ya kuwa chini ya Wizara.
Wizara ilipe deni inalodaiwa na Hoteli hii haraka iwezekanavyo ili Hoteli iweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Hoteli ichukue hatua za kisheria kwa wadaiwa wote ambao hawatalipa madeni yao
badala ya kuwaandikia barua pekee.
Hoja Namba 67.1.1 Kukosekana kwa Mchanganuo wa samani (Assets) zenye thamani
ya Tsh. 6,137,266,383
Fedha hizo zimeoneshwa katika taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka bila ya kuwepo
mchanganuo wa orodha ya samani za hoteli, kinyume na taratibu za ufungaji wa hesabu za
Serikali.
Majibu ya Hoteli
Ni kweli wameshindwa kuwasilisha mchanganuo huo katika ufungaji wao wa hesabu
waliouwasilisha kwa Mdhibiti, ingawaje taarifa hizo zipo.
Uchunguzi wa Kamati
Kutowasilisha mchanganuo huo ni kwenda kinyume na maelekezo ya Sheria na Kamati
haikubaliani na hoja za Hoteli za kuzipitia taarifa hizo wakati Sheria imeelekeza
kuwasilishwa kwake wakati wa ufungaji wa hesabu. Aidha, Kamati imeendelea kuhoji
kuhusu Cheo cha Kaimu Meneja wa Hoteli, ambae zaidi ya miaka mitatu sasa anaendelea
kukaimu nafasi hiyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inautaka uongozi wa Hoteli ufanye marekebisho ya mara moja kwa kasoro za
kuwasilisha mchanganuo wa samani wakati wa uwasilishaji wa hesabu za mwisho wa
mwaka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.
Aidha, kuhusiana na cheo cha Meneja, Kamati inaendelea na ushauri wake kwa Serikali
kufanya maamuzi ya haraka kuhusiana na mstakabali wa Hoteli.
4.12 MFUKO WA HIFADHI YA JAMII (ZSSF)
Hoja Namba 13.1 Uwasilishaji wa hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi
Kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Fedha namba 12 ya mwaka 2005, kinazitaka taasisi zote za
Serikali zitayarishe na kufunga hesabu zao za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi. Hata hivyo,
uwasilishaji huo usizidi tarehe 30 ya mwezi wa Septemba ya kila mwaka, lakini Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii haukuwasilisha hesabu zao kwa ukaguzi.
Majibu ya Mfuko
Mfuko ulikuwa haukaguliwi na Mdhibiti kutokana na wakati huo ulikuwa unakaguliwa moja
kwa moja na wakaguzi wa nje. Hivyo, sio sahihi kuelezwa kwamba haukuwasilisha kabisa,
badala yake ulichelewa kuwasilisha.
53
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka kujiridhisha iwapo Mfuko ulichelewa kuwasilisha na sio haukuwasilisha
kabisa kama ilivyoelezwa katika ripoti ya ukaguzi na kupatiwa ushahidi unaothibitisha
kuchelewa huko.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeridhika kwamba, Mfuko ulichelewa kwasilisha hesabu zake na kasoro hiyo sasa
imesharekebishwa.
4.13 CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII
Hoja Namba 69.1 Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Chuo cha Maendeleo ya Utalii kilikuwa na mali za mpito za
221,549,527.39 na hakikua na dhima za mpito, huku hali halisi ya mali za mpito ilikuwa ni
Tsh. 221,549,527.39. Hali hii inaonesha kuwa, mali za mpito ni kubwa kutokana na
kutokuwepo kwa dhima za mpito, hali iliyochangiwa na kuwepo kwa wadaiwa pamoja na
salio la benki kwa hesabu za Chuo.
Aidha, mapato ya Chuo kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni 892,902,429 na matumizi yake
ni Tsh. 748,345,046 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 144,557,383 ambayo
imeongezeka kwa tofauti ya Tsh. 134,312,716.90 sawa na 1311%.
Majibu ya Chuo
Sababu zilizopelekea hali hiyo ni kujipanga kwa Chuo kwa kutofautisha fedha za makusanyo
na fedha za ruzuku na kuzisimamia vizuri. Aidha, Chuo kimechukua hatua za makusudi
kupunguza matumizi ambayo sio ya lazima. Pia Chuo kimechukua hatua za kuboresha
huduma za Chuo kwa wanafunzi. Na kuhusiana na madeni, Chuo kilichukua hatua mbali
mbali za kulipa madeni hayo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji sababu zilizopelekea mafanikio hayo, na kuelezwa zaidi juhudi za
Mkurugenzi baada ya kufika katika Chuo hicho, akisaidiana na watendaji wengine.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakipongeza Chuo kwa maendeleo yake na kukitaka kuendelea na juhudi za
kuimarisha uwezo wake.
Hoja Namba 69.1.1 Kukosekana kwa mchanganuo wa samani (Assets) wa Tsh.
1,302,887,070
Fedha hizo zimeoneshwa katika taarifa za mwaka za Chuo, bila ya kuwepo mchanganuo wa
orodha ya samani za Chuo, kitendo ambacho kinapingana na maelekezo ya Sheria na taratibu
za ukaguzi na ufungaji wa Hesabu za mwaka.
Majibu ya Chuo
Ni kweli hilo lilikuwa tatizo wakati wa ufungaji wa hesabu za mwaka 2011/2012, lakini sasa
tayari wamesharekebisha kasoro hii kwa mwaka 2012/2013.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imefanya rejea ya maoni ya Ukaguzi yanayohusiana na Chuo, ambayo hayaoneshi
sura halisi na sahihi kufuatana na vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa, na pamoja na
54
kasoro nyengine, imesababishwa pia na kutoambatanishwa kwa mchanganuo huo katika
taarifa za hesabu.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kurekebisha mara moja kasoro hiyo, ili kukidhi matakwa ya Sheria
pamoja na kuweka vizuri hesabu zake kwa mujibu wa vigezo vya ukaguzi wa kitaifa na
kimataifa.
Hoja Namba 69.1.2 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 113,694,750
Fedha hizo ni deni la wanafunzi wa fani mbali mbali katika Chuo, ambalo hadi ukaguzi
unafanyika, ilikuwa bado halijalipwa.
Majibu ya Chuo
Ni kweli kulikuwa na deni hilo. Hata hivyo, Kamati hii ilipokuja mwaka uliopita iliwataka
wafuatilie madeni hayo na uongozi umefanya hivyo ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo
kwa wanaowadai, kufuatilia makazini, kwa wale ambao tayari wameshaajiriwa na hatua
nyengine, na kufanikiwa deni hilo kupungua na kufikia Tsh. 86,686,000/-.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, katika ufuatiliaji wa madeni hayo, Chuo hakiwajui wanafunzi
wote waliosoma na kudaiwa na hawana mawasiliano nao ya moja kwa moja.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuendelea na juhudi na kuchukua hatua zaidi kuhakikisha deni hilo
linalipwa lote.
4.14 MAMLAKA YA UWANJA WA NDEGE
Hoja Namba 78.1 Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi
na uwezo wa kujiendesha
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa mwaka 2011/2012, ilikuwa na mali za mpito za
989,929,435 na dhima za mpito za 496,752,012 na hali halisi ya mali hizo kuwa Tsh.
493,177,423, sawa na ratio ya 2:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wengi
wa Mamlaka na salio la benki.
Kwa upande wa mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh.
2,275,561,428 na matumizi yake yalikuwa Tsh. 1,418,307,282 na hivyo kuendeshwa kwa
faida ya Tsh. 857,254,146.
Majibu ya Mamlaka
Mamlaka haifanyi biashara bali inatoa huduma, na kwa maana hii, haingeweza kufanya
faida. Aidha, Mamlaka ni wakala wa Serikali na fedha zote wanazozikusanya wanazipeleka
Serikalini na hali ya Mamlaka inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku. Wameiomba Serikali
kwa muda mrefu sasa kupatiwa mgao wa wanachokikusanya, lakini hakuna mafanikio
yoyote.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeridhika kwamba, utekelezaji wa Sheria inayoanzisha Mamlaka unaiwezesha
Mamlaka kujinasua na hali waliyonayo sasa na kufikia hali wanayoitarajia.
55
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kutekeleza ushauri waliopewa na Mdhibiti ya kuongeza juhudi ya
ukusanyaji na usimamizi wa vyanzo vyake vya mapato. Vile vile, Kamati inaishauri Serikali
kuipatia mgao wa fedha Mamlaka ili iweze kujienedesha kwa ufanisi
Hoja Namba 78.1.1 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 73,285,940 na USD 273,317
Fedha hizo zinadaiwa na Mamlaka kwa wafanyabiashara na taasisi mbali mbali kutokana na
huduma walizowapatia, ambapo hadi ukaguzi unamalizika, fedha hizo bado hazijalipwa.
Majibu ya Mamlaka
Ni kweli Mamlaka inadai deni hilo na wamechukua hatua za kudai fedha hizo na kufanikiwa
kupungua. Utaratibu wanaoutumia ni kuwapelekea Ankara (Bill) wadaiwa wake wote tarehe
5 baada ya kutoa huduma, ambapo malipo hufanyika ndani ya siku 25 katika mwezi. Aidha,
kwa juhudi hizo, Mamlaka imelipunguza deni hilo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwapo mikataba inayohusika na huduma wanazozitoa Mamlaka, kama tayari
imesharekebishwa kama ilivyoelekezwa na Baraza la Wawakilishi. Aidha, imeipitia na
kujiridhisha kwamba, imerekebishwa katika eneo zaidi la kodi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka iendelee kufuatilia madeni yake ili kuhakikisha kuwa, wateja wote
wanaopatiwa huduma wanalipa ipasavyo kodi zao na wale ambao wanaendelea wachukuliwe
hatua za kisheria kwa mujibu wa mikataba yao.
Hoja Namba 78.2 Malipo yasiyokuwa na Vielelezo, Tsh. 11,200,000
Mamlaka imemlipa Moral Architectural and Engineering Consultancy Ltd kwa ajili ya
usimamizi wa Shopping Complex. Aidha, hadi ukaguzi unakamilika, ujenzi huo haujaanza
na hakukuwa na maelezo yoyote juu ya kuwepo uwezekano wa kufanyika kwa ujenzi huo.
Majibu ya Mamlaka
Ujenzi huo umefanywa na Msamaria mwema aliejitolea kujenga kwa kutumia fedha zake,
bila ya Mamlaka kutoa fedha yoyote. Aidha, baada ya kukamilika kwa ujenzi, Msamaria
huyo atakusanya 70% na Mamlaka 30%, na baada ya Msamaria mwema kurejesha fedha
zake za ujenzi, majengo hayo yatakuwa ya Mamlaka.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imefanya ziara katika eneo linalohusika na kugundua kuwa, ujenzi huo haukuwa
„Shopping Complex‟ bali ni ujenzi wa Ofisi mbali mbali zilizokodishwa kwa taasisi binafsi.
Ujenzi huo ulijengwa na Kampuni ya ASB Engineering na Mshauri wake ni Ndg. Abdu
Jindi, aliyechora ramani. Pamoja na msaada walioupata Mamlaka, Kamati imeona ujenzi huo
sio wa muda mrefu, kutokana na kuwa wa chini, wakati ingestahiki kujengwa kwa ghorofa
Aidha, kuhusiana na fedha Tsh. 11,200,000 zilizolipwa kwa Moral Architectural and
Engineering Consultancy Ltd, Kamati imejiridhisha kutumika bila ya vielelezo na zimelipwa
kwa Kampuni hiyo kwa ajili ya michoro na kutayarisha BOQ, kazi ambayo haikuiendeleza
na kuikamilisha.
56
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kuhakikisha inatumia vizuri rasilimali zake kwa malengo ya muda
mrefu. Aidha, kuhusiana na fedha ambazo hazina vielelezo, Kamati inaitaka Mamlaka
kurekebisha mara moja kasoro hizo.
4.15 CHUO CHA UTAWALA WA UMMA
Hoja Namba 77.1 Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Chuo kilikuwa na mali za mpito za thamani ya Tsh. 406,206,983 kwa mwaka 2011/2012,
bila ya kuwa na dhima za mpito, hali iliyopelekea salio ama mali halisi za mpito kuwa Tsh.
406,206,983 hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa na salio la benki la chuo.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 1,397,161,548 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 935,745,286 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 444,036,762.
Majibu ya Chuo
Ni kweli mpaka sasa hawana dhima, na mapato yao yanatokana na ada za wanafunzi wa fani
mbali mbali wanaosoma Chuoni hapo. Malipo ya ada hufanyika kwa njia ya hundi na fedha
taslim kupitia Benki ya Watu wa Zanzibar. Aidha, Chuo kinaiomba Serikali kuwamalizia
jengo la chuoni hapo kwa ajili ya kujiendesha kwa ufanisi zaidi.
Kuhusiana na deni kwa taasisi zinazoleta wafanyakazi wao kwa mafunzo, Uongozi wa Chuo
umefanya juhudi za kufuatilia ulipwaji wa madeni hayo, na mpaka sasa taasisi zote zimelipa
isipokuwa Mahakama.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, taasisi nyingi za Serikali zenye wanafunzi katika Chuo hiki,
zinahitaji msukumo ili waweze kulipa madeni yao.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato yake kupitia ada za
wanafunzi na kuzifuatilia kwa karibu taasisi zote zenye wanafunzi, ili kuhakikisha madeni
yote yanalipwa ipasavyo.
Hoja Namba 77.1.1 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 383,140,250
Fedha hizo zinadaiwa na Chuo cha Utawala wa Umma, kwa wanafunzi na taasisi mbali
mbali kutokana na huduma walizowapatia. Deni hilo halijalipwa
Majibu ya Chuo
Ni kweli kulikuwa na malimbikizo hayo ya madeni. Hata hivyo, baada ya kuchukua juhudi
wamefanikiwa kuondosha deni hilo kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao, na hivyo, deni
hilo sasa halipo tena.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji juu ya wanafunzi wanaoakhirisha masomo katika semista husika, wakati
tayari wameshatumia huduma za Chuo angalau kwa mwezi mmoja au miwili, na kukitaka
Chuo kuwa makini sana na wanafunzi wa aina hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imepongeza juhudi zilizochukuliwa za kufuatilia na hatimae kulipwa kwa madeni
hayo na kuzitaka taasisi nyengine, hasa Vyuo, ziige mfano huu.
57
4.16 CHUO CHA UANDISHI WA HABARI
Hoja Namba 79.1 Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2011/2012, Chuo kilikuwa na mali za mpito za 27,511,413 bila ya kuwa na
dhima za mpito, hali iliyopelekea bakaa kuwa kama mali za mpito. Hali hii imesababishwa
na kutokuwepo kwa madeni.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2011/2012 yalikuwa ni Tsh. 389,962,342 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 356,777,719.
Majibu ya Chuo
Ni kweli Chuo hakikuwa na dhima za mpito kwa mwaka 2011/2012 na kilichowasaidia
kuwa na mali za mpito ni ongezeko la wanafunzi 30. Aidha, kuhusiana na matumizi, Chuo
kilitumia Tsh. 356,777,719 badala ya Tsh. 395,458,994 zilizorikodiwa awali.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwapo Chuo kinamiliki jengo ambalo sasa ndio kipo Chuo chenyewe na
kujibiwa kuwa, jengo hilo sio mali ya Chuo na wao wanatumia ghorofa mbili, huku ghorofa
ya tatu ikitumiwa na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali. Katika mahojiano ya Chuo
kuhusiana na mali, Kamati ilifahamishwa kwamba, Chuo kilinunua gari kwa Tsh.
39,000,000 lakini utaratibu wa manunuzi kama Sheria inavyoelekeza, haukufuatwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeutaka uongozi wa Chuo kuwa makini wakati wa kutumia fedha za umma kwa
kufuata ipasavyo Sheria zinazohusika.
Hoja Namba 79.1.1 Kukosekana kwa mchangauo wa samani (Assets) zenye thamani
ya Tsh. 119,460,550
Fedha hizo zimeoneshwa katika taarifa ya hesabu za mwaka za Chuo, lakini mchanganuo wa
orodha ya samani husika haukuwepo katika taarifa za hesabu za Chuo, kinyume na
maelekezo na matakwa ya Sheria zinazohusiana na ukaguzi na Sheria ya Fedha.
Majibu ya Chuo
Ni kweli wakati wa ukaguzi, mchanganuo huo haukuwemo katika taarifa ya hesabu za Chuo,
lakini kwa mwaka uliofuata walirekebisha kasoro hiyo.
Uchunguzi wa Kamati
Tatizo hili limeripotiwa sana kwa Vyuo, na majibu yake yamekuwa yanafanana.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kurekebisha kasoro hiyo kwa kutorejea tena kasoro iliyojitokeza.
4.17 CHUO CHA KILIMO, KIZIMBANI
Hoja Namba 13.1 Uwasilishaji wa Hesabu za mwisho wa mwaka kwa ukaguzi.
Chuo cha Kilimo Kizimbani kimeshindwa kuwasilisha hesabu zake za mwisho wa mwaka
wa 2011/2012, kinyume na maelekezo ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2005.
58
Majibu ya Chuo
Chuo kilishindwa kufunga hesabu zake, lakini kasoro hiyo tayari imeshafanyiwa kazi kwa
mwaka uliofuata. Aidha, kwa kawaida, baada ya Chuo kufunga hesabu zake, kwanza kabla
ya kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, huziwasilisha kwanza kwa
Baraza la Chuo, ili wapate idhini ya kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwapo Chuo kimeshakuwa na Daftari la kuhifadhia vifaa na kugundua kuwa,
daftari hilo halijahifadhiwa kwa pamoja, ni karatasi tu zilizowekwa pamoja. Hata hivyo,
Kamati iliwataka Chuo ndani ya wiki mbili kutayarisha Daftari hilo, ambalo baada ya muda
huo waliweza kulikabidhi kwa Kamati.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kufahamu kuwa, Sheria ya Fedha ya mwaka 2005 inawataka
wafunge na kuwasilisha hesabu zao za mwisho wa mwaka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali, suala ambalo haliwezi kuwekewa kipingamizi cha hesabu hizo
kwanza kukabidhiwa kwa Baraza la Chuo.
Hoja Namba 80.1 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 2,350,000
Fedha hizo ni deni la wanafunzi wa fani mbali mbali katika Chuo, lakini hadi ukaguzi
unamalizika, deni hilo lilikuwa halijalipwa.
Majibu ya Chuo
Chuo kinakiri kuwepo kwa deni hilo wakati wa ukaguzi, lakini wamefanya juhudi ya
kulifuatilia na wakati ilipofika Kamati, ni wanafunzi wawili pekee walibakia kuwa na deni.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji wanafunzi ambao wameacha Chuo huku wakiwa wanadaiwa, mbali na
wanafunzi wanaodaiwa baada ya kuhitimu Chuo, na kuelezwa kuwa wapo baadhi ya
wanafunzi huakhirisha kwa sababu za msingi, kiasi ambacho kuwadai inakuwa tabu. Aidha,
Kamati imezipitia risiti za malipo na kujiridhisha kuwa zipo sawa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuwa makini na kulichukulia kwa uzito wake suala la wanafunzi
wanaokatisha masomo, huku wakiwa hawajalipa miezi ambayo wamepata huduma hiyo,
ingawaje hawakuwahi kumaliza mitihani yao ya mihula husika.
4.18 SHIRIKA LA MAGARI
Hoja Namba 83.1 Rasilimali za Shirika kukodishwa bila ya kuzingatia thamani
halisi ya fedha
Ukaguzi umebaini kwamba, Shirika linamiliki majengo mbali mbali ambayo yamekodishwa
kwa mashirika mbali mbali na watu binafsi, lakini ukodishwaji huo haukuzingatia thamani
halisi ya majengo hayo kibiashara na muda wa ukodishwaji kwa lengo la kuleta tija kwa
Shirika kwa mujibu wa upandaji na ushukaji wa thamani ya fedha. Kwa mfano, benki ya
NMB imekodishwa jengo kwa miaka 33 tokea tarehe 31/12/2008, kwa mkataba kuanza kazi
tarehe 01/10/2008 hadi 30/09/2041, huku NMB wakilipa Tsh. 37,280.52 kwa mwaka.
Benki ya Posta imekodishwa jengo kwa mkataba wa tarehe 27/11/2007 kwa Tsh. 31,188,000
kwa mwaka, huku Mkataba huo ukimtaka Mkodishwaji kulipa kodi ya miaka miwili kwa
59
mwaka wa mwanzo na kodi inayofuata kulipa kila mwaka, kwa sharti la ongezeko la asilimia
10 kila baada ya mwaka kuwa muda wote anaohitaji kulitumia jengo.
Ghala la Shirika liliopo Mchangani limekodishwa kwa Ndg. Bakia Ally Suleiman tarehe
9/2/2011 kwa malipo ya Tsh. 1,793,000 kwa mwaka. Tatizo zaidi ni kuwa, Mkodishwaji
amefariki na sasa linatumiwa na Ndg. Abubakar Pass Kajore na mkataba ulimalizika Januari
2012, bila ya kuingia mkataba mwengine, na hivyo Ndg. Abubakar anaendelea kulitumia
ghala hilo bila ya kulipa.
Majibu ya Shirika
Ni kweli wakati wa ukaguzi, majengo hayo yalikuwa yamekodishwa kwa kiwango kidogo
cha fedha , kutokana na hali mbaya na uchakavu wake. Hata hivyo, hivi sasa tatizo hilo
limesharekebishwa na bei zimefanyiwa marekebisho na ziko sawa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji mkataba wa Postal Bank na kugundua kuwa, hakuna marekebisho yoyote
yaliyofanywa. Aidha, Mkaguzi alishindwa kuupata mkataba wa benki hii kutokana na kuisha
muda. Kuhusiana na ghala, Kamati ilielezwa kuwa baada ya kumaliza muda wa ukodishwaji
kwa Ndg. Bakia Ally Suleiman, limerudi kwao na sasa wamekodisha kwa miaka miwili Tsh.
74,580.48.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Shirika kuhakikisha inafuatilia ipasavyo kodi za majengo yake kwa kufanya
marekebisho ya mikataba ili iendane na thamani halisi ya fedha kwa mujibu wa wakati
tulonao na sehemu ambayo majengo hayo yalipo.
Hoja Namba 83.2 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 95,461,728
Fedha hizo zinadaiwa na Shirika la Biashara ya Magari kwa taasisi mbali mbali za Serikali
na watu binafsi, lakini hadi ukaguzi unakamilika, madeni hayo yalikuwa bado hayajalipwa
wakati yameshakaa muda mrefu.
Majibu ya Shirika
Ni kweli madeni hayo ni ya muda mrefu, mengine tokea Shirika lilipokuwa Bizanje. Aidha,
madeni ya taasisi nyingi yameshindwa kulipwa kutokana na baadhi yao kukosa vielelezo vya
ushahidi wa kuwepo kwake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeshuhudia kuwa madeni hayo ni ya muda mrefu kutokana na sababu mbali mbali
ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa usimamizi imara wa huduma iliyokuwa inatolewa na
Shirika kwa taasisi na watu mbali mbali. Aidha, ni kweli kuwa, baadhi ya vielelezo hasa vya
madeni ya muda mrefu sana, havipo kwenye Shirika kiasi ya kukwamisha juhudi za
kufuatilia ulipwaji wa madeni hayo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Shirika kuendelea kufuatilia madeni yake, ili kuongeza uwezo wa Shirika.
4.19 MAMLAKA YA MAFUNZO YA AMALI
Hoja Namba 54.6.1 Ruzuku ya Tsh. 60,000,000
Fedha hizo zikiwa ni ruzuku kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, hazikuingizwa
katika taarifa za hesabu za Mamlaka za mwisho wa mwaka, kinyume na taratibu za
60
utayarishaji wa taarifa za hesabu, hali ambayo pia hupelekea taarifa za hesabu kutokuwa
sahihi. Fedha hizo zimelipwa kwa Mamlaka kupitia hundi namba 395303 ya tarehe
28/5/2012.
Majibu ya Mamlaka
Ni kweli viongozi wa Mamlaka wanakiri kutokea kwa kasoro hiyo, isipokuwa tayari
wamesharekebisha na kuahidi kutotokea tena kwa kasoro hiyo. Fedha hizo zimetumika na
uthibitisho wa vocha zake upo, isipokuwa kosa lililotokea ni la kibinaadamu.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilipohoji sababu za msingi zilizopelea kasoro hiyo, imeelezwa kuwa ni sababu za
kibinaadamu. Aidha, Kamati imetaka kufahamu elimu ya Mhasibu wa Mamlaka, lakini kwa
bahati Mhasibu aliyepo sasa mwenye kiwango cha „Master‟ hakuwa yeye wakati Mamlaka
ilipokaguliwa.
Aidha, Kamati imejiridhisha pia, kosa hilo limejitokeza kutokana na kufungwa hesabu za
mwisho wa mwaka bila ya kukaguliwa na Mkaguzi wa Ndani wa Mamlaka, ambae iwapo
angeliona kasoro hizo mapema, angeliijuulisha Mamlaka inavyostahiki. Aidha, Kamati
imejiridhisha kurekebishwa kwa kasoro hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia „cash book‟ na
kuiona ipo sawa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kuhakikisha inarekebisha kasoro hiyo isitokezee tena.
Hoja Namba 54.6.2 Matumizi yaliyofanyika kinyume na vifungu husika, Tsh.
42,650,155
Fedha hizo zimetumika kinyume na vifungu vilivyoidhinishwa , kitendo ambacho kinakiuka
kanuni 41(4) ya Kanuni za Fedha za mwaka 2005.
Majibu ya Mamlaka
Ni kweli wamefanya matumizi hayo kinyume na vifungu vilivyoidhinishwa na Bodi ya
Mamlaka, isipokuwa matumizi hayo hayakuzidi bajeti ya Mamlaka na yamefuata taratibu
zote za kisheria. Imefahamishwa kuwa, pamoja na Mamlaka kupokea ruzuku Serikalini,
Mamlaka ina vituo vyake vya mafunzo ya amali vilivyopo Mwanakwerekwe, Mkokotoni na
Vitongoji, ambapo wamepewa idhini ya matumizi madogo madogo kwa usimamizi wa
Mkurugenzi.
Hapo mwanzo fedha hizo walikuwa hawazioneshi katika MTEF, ila sasa tayari
wamesharekebisha kasoro hiyo na fedha hizo za mapato zinaonekana katika MTEF na jumla
yake kuu ndio wanayoipangia matumizi. Aidha, fedha hizo zilitakiwa zipatiwe idhini ya
Bodi ya Mamlaka, ila viongozi wa Mamlaka wanakiri kasoro hiyo na tayari sasa kosa hilo
wameshalirekebisha.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na Mamlaka kushindwa kufanya matumizi kinyume na vifungu vilivyoidhinishwa na
Bodi, Kamati imejiridhisha kuwepo kwa tatizo kubwa la Wizara ya Fedha kutokutoa fedha
kwa wakati kwa taasisi husika, ili hatimae taasisi husika zipate muda mzuri wa kuzitumia
fedha hizo kwa kufuata taratibu za kisheria.
61
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kurekebisha kasoro iliyobainika na kutorejea tena katika kufanya
kasoro hizo. Aidha, Kamati inaishauri Serikali, kupitia Wizara ya Fedha, kuhakikisha taasisi
zote za Serikali zinapatiwa fedha katika muda muafaka, ili taratibu za kisheria ziweze
kufuatwa ipasavyo.
Hoja Namba 54.6.3 Matumizi ya Ununuzi wa vifaa ambavyo havijapokelewa, Tsh.
46,960,800
Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya manunuzi ya vifaa mbali mbali kwa matumizi ya vituo
vya Mamlaka vya Mwanakwerekwe na Mkokotoni, lakini hadi ukaguzi unakamilika vifaa
hivyo havikuonekana katika vituo husika na mapokezi ya vifaa hivyo hayakuonekana katika
kumbu kumbu ya vituo hivyo.
Majibu ya Mamlaka
Uongozi wa Mamlaka unakubaliana na hoja za Mkaguzi kwamba, baadhi ya taratibu
zimekiukwa kutokana na baadhi ya vifaa kupokelewa moja kwa moja na wakuu wa vituo,
lakini havikuingizwa katika daftari la ghalani. Tatizo hili limesababishwa na ugeni na hamu
ya kuvipata vifaa hivyo baada ya kuviomba kwa mufa mrefu. Uongozi unahakikisha
kwamba, vifaa hivyo vimenunuliwa na vilitumika kama vilivyokusudiwa. Aidha, wakati
huo, Mamlaka haikuwa na stoo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilipohoji kuhusiana na upokelewaji wa vifaa hivyo kama umerikodiwa katika
„delivery note‟ ilijiridhisha kwamba, vifaa hivyo vinaonekana kupokelewa lakini
havijaingizwa katika „store ledger‟ na kulelezwa kuwa tatizo kama hili pia lipo Vitongoji.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inawataka Mamlaka kufuata utaratibu kama ulivyoelezwa katika Sheria.
Hoja Namba 54.6.4 Malipo ya Tsh. 58,320,800 yaliyofanywa kinyume cha Kanuni na
taratibu za manunuzi
Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbali mbali lakini ununuzi wake
haukufuata taratibu za zabuni, wakati thamani ya fedha hizo zinazidi kiwango kinachotakiwa
kuitishwa zabuni kwa mujibu wa Sheria.
Majibu ya Mamlaka
Ni kweli Mamlaka ilifanya manunuzi hayo kinyume na Sheria, kutokana na kutokuwepo
kwa Bodi ya Zabuni wakati huo. Aidha, vifaa hivyo vilivyonunuliwa ni vya mitihani na
Mamlaka inalazimika kuvinunua kwa muuzaji (supplier) mmoja ambae aliwahi kutoa
huduma kama hizo hapo awali. Hata hivyo, Mamlaka imesharekebisha kasoro hiyo.
Uchunguzi wa Kamati
Baada ya kujiridhisha kukiukwa kwa taratibu za manunuzi, Kamati imehitaji kupatiwa hati
za malipo ya fedha hizo na ilijiridhisha kwamba yalikuwa yanafanyika kidogo kidogo kwa
mujibu wa upatikanaji wa fedha. Aidha, Kamati pia imegundua kutokuwepo kwa maombi ya
fedha hizo kutoka kwa mtumiaji (user department) ndani ya Mamlaka, kosa ambalo Kamati
imeelezwa kuwa limesharekebishwa.
62
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kufuata taratibu za kisheria katika manunuzi ya vifaa
vinavyohitajika.
Hoja Namba 54.6.5 Upotevu wa vitabu vya risiti
Mamlaka imechapisha vitabu vya risiti kwa ajili ya kukusanya mapato ya fedha kwa vituo
vyake mbali mbali. Kituo cha Mkokotoni vimepelekwa vitabu 40, vyenye risiti namba 6001
hadi 8000 kupitia barua yenye kumbu kumbu namba P33/MMA/18/42/VOL.I ya tarehe 31
Mei 2011, huku ukaguzi ukishindwa kuviona vitabu viwili vya risiti nambari 6701-6750 na
6901 – 6950, hali iliyopelekea kushindwa kupatikana ufafanuzi wa makusanyo ya fedha
kupitia vitabu hivyo.
Majibu ya Mamlaka
Ni kweli wakati wa ukaguzi vitabu hivyo havikuonekana kutokana na Mkuu wa Kituo hicho
kustaafu na aliviweka katika sehemu ambayo wao hawakuijua, ila baada ya kuvitafuta kwa
zaidi ya mwezi mmoja baada ya ukaguzi, ndipo walipoviona.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji utaratibu wa malipo katika Mamlaka, na kuelezwa kuwa wanafunzi
wanalipia Benki na baada ya kupewa „pay in slip‟ ndio Mamlaka hutoa risiti.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeitaka Mamlaka ifuate taratibu za kisheria katika kuweka kumbu kumbu zao.
4.20 AFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI
Hoja Namba 13.1 Uwasilishaji wa Hesabu kwa ajili ya Ukaguzi
Ukaguzi umebaini kuwa Afisi ya Mtakwimu Mkuu haikuwasilisha hesabu za mwaka,
zinazojumuisha Mapato na Matumizi kama vifungu vya 24(2) na 8 vya Sheria ya Fedha
Namba 12/2005 vinavyoelekeza.
Majibu ya Mtakwimu Mkuu
Afisi ya Mtakwimu Mkuu iliieleza Kamati kuwa haikuwasilisha hesabu hizo kwa kuwa
tangu Afisi hii inaanzishwa ilikuwa inawasilisha taarifa zake za hezabu kupitia Wizara ya
Fedha, isipokuwa kwamba ilipofika mwaka 2011 walipata agizo la kuandaa hesabu hizo
kupitia Ripoti ya Mdhibiti kwa kuwa ni taasisi inayojitegemea.
Kwa kuwa agizo hilo lilitolewa kipindi ambacho hesabu za mwaka zilikuwa zishawasilishwa
Afisi hii ililazimika kuwasilisha kwa wakati mmoja taarifa zake za mwaka wa fedha
2011/2012 na 2012/2013 mnamo mwezi wa Septemba, 2013.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ya PAC iliitaka Afisi hii kuthibitisha kauli yake hiyo kwa kuonesha nyaraka
zinazothibitisha maelezo yake hayo na baada ya kufanya hivyo Kamati ilikubaliana nayo na
kuifuta hoja hiyo ingawa kwa mwaka fedha 2012/2013 Afisi ya Mtakwimu Mkuu
haikuorodheshwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti kama imewasilisha taarifa za hesabu kwa
wakati au la.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati iliisisitiza Afisi hii kujitahidi kuwasilisha taarifa za hesabu kama Sheria
inavyoelekeza.
63
Mengineyo
Kamati ilitaka kuona namna Afisi hii inavyoingiziwa fedha za matumizi ya kawaida na
maendeleo. Katika kufuatilia hili Kamati hii ilibaini kuwa uingizwaji wa fedha za matumizi
ya kawaida sio mbaya sana kinyume na upande wa kazi za maendeleo.
Aidha, Kamati ya PAC imebaini kuwa makadirio ya fedha kila mwaka yanashuka jambo
ambalo litadhoofisha utendaji wa Afisi hii.
WIZARA NA TAASISI MBALI MBALI ZA SERIKALI-PEMBA
5.0 KAMISHENI YA WAKFU NA MALI YA AMANA
Hoja Namba 44.2.1 Kiwango kidogo cha fedha za kodi za milango mbali mbali ya
Wakfu
Kamisheni inakodisha milango ya biashara kwa wafanya biashara mbali mbali lakini
kiwango cha kodi kinachotozwa ni kidogo kulingana na hali halisi ya thamani ya milango
hiyo katika maeneo hayo. Hali inayowapelekea Kamisheni kukosa mapato yanayostahiki.
Majibu ya Kamisheni
Milango hiyo ilikuwa katika hali mbaya sana ya ubovu na uchakavu na haikuwa ikileta faida
kwa Kamisheni wala wanufaika wa wakfu hiyo. Na kwa kuwa hakukuwa na fedha za
kuijenga upya, Kamisheni ilikubaliana na wapangaji wawekeze katika nyakfu hizo kwa
kutanguliza kima kikubwa cha fedha ili ijengwe kisha wapangishwe kwa mikataba nafuu na
ya muda mrefu, ambapo wanajilipa theluthi mbili na kulipa kodi theluthi moja, na utaratibu
huu ni maarufu katika utunzaji wa nyaraka ulimwenguni kote kwani kinachozingatiwa ni
wanufaika wa sasa na kutunza mali yenyewe ya wakfu ili idumu na iwe sadakatul jariya kwa
wajao.
Aidha, bei hizo huwa zinapitiwa na kupangwa upya kwa kila unapomalizika mkataba wa
miaka mitano kwa kuzingatia hali ya soko na kima alichowekeza mtumiaji. Hivyo, viwango
hivyo vilifanyiwa marekebisho mwaka 2012 na wale ambao mikataba yao haijamalizika,
Kamisheni itairekebisha kwa kuongeza kodi watakapopewa mikataba mipya.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehitaji kupatiwa chanzo cha kuharibika kwa nyumba hiyo ya wakfu na kuelezwa
kuwa imetokana na kuungua moto. Kamati ilipohoji iwapo kulikuwa na taarifa rasmi ya
Polisi au Kikosi cha Zimamoto kuhusiana na moto huo, ilishindwa kupata uthibitisho huo
zaidi ya kuelezwa kuwa, walipofika wao moto huo ulikuwa umeshazimwa.
Vile vile, Kamati imekosa uthibitisho wowote wa kuhusiana na hatua zilizochukuliwa katika
jengo hilo zaidi ya kuelezwa kuwa walimtafuta Engineer Bwana Suleiman Omar Hamad kwa
usimamizi wa ujenzi huo, lakini Kamati ilipohitaji uthibitisho wa upatikanaji wake ambapo
kwa mujibu wa mkataba alilipwa Tsh. 500,000/-, Kamati ilikosa uthibitisho wa upatikanaji
wake kisheria, lakini pia uthibitisho wa kupokea fedha hizo alizolipwa haukuweza
kupatikana kwa Kamati.
Hata hivyo, Kamati ilipofanya ziara katika maeneo hayo, ilishuhudia tofauti ya bei ya
milango kwa mnasaba wa hata eneo ilipo na ukubwa wake.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Kamisheni kuwa makini inaposhughulikia suala la ujenzi, kwani kama
hakutakuwa na usimamizi imara, watu wasiokuwa waaminifu watatumia mwanya huo na
kuifanya Kamisheni ishindwe kutimiza majukumu yake.
64
MASHIRIKA YA SERIKALI - TANZANIA BARA
6.0 SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA (ZSTC), TAWI LA DAR ES SALAAM
Hoja Namba 84.1.1 Rasilimali za Shirika
Nyumba ya Sinza
Shirika linamiliki nyumba namba 82 katika eneo la Sinza ambayo imekodishwa kwa Ndg.
Ramadhan Mwita kwa kodi ya Tsh. 500,000 kwa mwezi ni sawa na Tsh. 6,000,000 kwa
mwaka. Ukaguzi umebaini kuwa nyumba hiyo hairidhishi kutokana na kutofanyiwa
ukarabati kwa muda mrefu.
Majibu ya Shirika
Ni kweli hoja hiyo na Shirika linakiri kuwa kihalisia nyumba hiyo hairidhishi. Iwapo
inanyensha mvua, majo yote yanakwenda na kutuwama katika nyumba hiyo. Hata hivyo,
Shirika limechukuwa hatua ya kuamua kuivunja nyumba hiyo na kujenga jengo la ghorofa
tano kutokana na masharti ya ujenzi katika eneo hilo ni jengo lisilozidi ghorofa hizo tano,
vyenginevyo wangelizidisha zaidi ya ghorofa hizo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji gharama za kukodisha Tsh. 500,000 kama zina tija ukizingatia nyumba
pamoja na ubovu na uchakavu wake, kwa mazingira ya eneo la Sinza ingelikuwa na soko
zaidi, na kuelezwa ni kodi ya takriban miaka miwili sasa na hapo mwazo waliikodisha kwa
Shirika la Bima kwa Tsh. 350,000/- na kwa sasa hawana mpango wa kuzidisha kodi
kutokana na uchakavu wake na kutuwama kwa maji ya mvua.
Aidha, Kamati imeelezwa zaidi kuwa, mvua inaponyesha na maji kutuwama, wapangaji
hulazimika kuhama kwa takriban miezi mitatu na zaidi kipindi cha mvua za masika na
baadae Shirika hulazimika kutafuta gari la kufyonza maji ili maji hayo yaondoke.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeridhika kwamba, jengo hilo linahitaji matengenezo ya haraka na kwa kuwa
Shirika lina azma ya kujenga jengo jengine la ghorofa tano, ni vyema ujenzi huo ukaanza
mara moja ili kuepusha hasara inayoendelea kupatikana.
Kamati inalikumbusha Shirika kufanya ujenzi huo kwa kufuata taratibu za Sheria, ili
kuepuka kujengwa chini ya kiwango na kupoteza fedha za Serikali.
Tawi la Dar es Salaam
Ukaguzi umebaini kuwa, tawi la Shirika la Dar es Salaam halionekani kuwa na tija kwa
Shirika. Kuendelea kuwepo kwa tawi hilo ni kuongeza gharama za uendeshaji ambapo kuna
wafanyakazi wawili wanaoendesha shughuli za tawi hilo ambapo hulazimika kulipa gharama
za kukodi nyumba kwa ajili ya Ofisi na ghala kwa Tsh. 4,131,298 kwa mwezi ambapo ni
sawa na Tsh. 49,575,576 kwa mwaka.
Majibu ya Shirika
Tawi la Dar es Salaam ni sehemu ya Shirika na kwa sasa Shirika limo katika mageuzi
makubwa. Katika kuhakikisha tawi hilo linaleta tija, jambo la msingi ni kuhakikisha Shirika
linauziwa jengo liliopo tawi hilo kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa, ambapo walifanya
juhudi ya kumuomba Makamo wa Pili wa Rais kuwasaidia kuwaomba Serikali ya Jamhuri
ya Muungano kuuziwa jengo hilo kwa Shirika.
Aidha, Shirika lilikiomba Chuo cha Utawala wa Fedha, Chwaka kulifanyia utafiti wa
kitaalamu (study) tawi hilo la Dar es Salaam, ili kujua faida na hasara ya kuwa na tawi hilo
na tayari Chuo kimeshakuja na kuliona na wanaendelea na kazi.
65
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilitaka kujiridhisha na kuthibitishiwa juhudi za kuomba kuuziwa kwa jengo hilo na
kupatiwa barua ya tarehe 29/12/2014 yenye kumbu kumbu namba SBT/BLW/52/36 VOL.III
inayotoa uthibitisho wa ufuatiliaji wa kuuziwa jengo hilo, ambapo uchambuzi wake ni huu
ufuatao.
Mnamo tarehe 16 August, 2004 Meneja wa Tawi Dar es Salaam, Ndg. Said M. Khamis
alimuandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda, Masoko na Utalii yenye
kumbu kumbu namba ZSTC/DSM/36 VOL.2 kupendekeza hatua za kuuziwa kwa jengo hilo
ili Shirika, tawi la Dar es Salaam liweze kujitanua kibiashara kwa kuweza kupunguza
gharama za kodi zinazopanda mwaka hadi mwaka, na kopi ya barua hiyo ikapelekwa kwa
Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi na
Shirika la Nyumba la Taifa.
Tarehe 19 Augosti 2004, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda, Masoko na Utalii
alimuandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi yenye
kumbu kumbu namba WBVMU/M.120/C6 VOL.II/14 kumuomba kama Wizara, kuuziwa
kwa jengo hilo, na nakla ya barua hiyo ikapelekwa kwa Meneja Mkuu wa Shirika.
Mnamo tarehe 19 March 2009, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Utalii, Biashara na
Uwekezaji alimuandikia barua Meneja Mkuu wa Shirika yenye kumbu kumbu namba
WUBU/B.70/C2 VOL.IV/152 kumtaka afuatilie suala la kuuziwa kwa jengo hilo kwa
Shirika.
Tarehe 22 Oktoba 2010, Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji Zanzibar alimuandikia
barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ya Tanzania kumkukumbusha
juhudi alizofanya za kumuandikia barua kabla na watendaji wa Wizara pamoja na Shirika
kufuatilia suala la kuuziwa kwa jengo hilo kwa Shirika, bila ya kupata majibu yoyote.
Waziri huyo huyo mnamo tarehe 1/11/2012 alimuandikia barua nyengine Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makaazi yenye kumbu kumbu namba WBVU/M.120/C.8/43
akiomba kwa mara nyengine tena kuuziwa kwa jengo hilo huku akieleza gharama inazopata
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Shirika lakini hakuna mafanikio yoyote
yaliyofikiwa.
Kama hii haitoshi, Makamo wa Pili wa Rais, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alimuandikia barua
nyengine Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi yenye kumbu kumbu namba
OMPR/MASH/TS.35/1 ya tarehe 26 Agosti 2013, kukumbushia barua zilizopita za Serikali
na kulalamikia tabia ya kutopata majibu yoyote na kueleza umuhimu wa jengo hilo kuuziwa
Shirika na nakla ya barua hiyo ikitumwa kwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko ya
Zanzibar na Mkurugenzi wa Shirika. Lakini hadi leo hakuna mafanikio yoyote.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeridhika kuwa Shirika limechukua hatua na juhudi za kutosha kuomba kuuziwa
jengo hilo lakini inashangazwa sana na Serikali ya Muungano kupitia Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makaazi kukaa kimya na kuonesha dharau kubwa kwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, jambo ambalo halikupaswa kufanywa.
Kamati inaitaka Serikali kusafiri hadi Tanzania bara kuonana na Mhe. Rais kuhusiana na
suala hili, ambae huenda akawa hajui kilichoendelea muda wote huo.
66
RIPOTI YA UKAGUZI WA HESABU KWA MAWIZARA, MASHIRIKA NA
TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
7.0 WIZARA NA TAASISI MBALI MBALI ZA SERIKALI
7.1 WIZARA YA FEDHA
Hoja Namba 19.1 Matokeo ya Hesabu za mwisho wa mwaka. Taarifa za mapato na
matumizi
Taarifa za mapato za Wizara ya Fedha za mwaka 2012/2013, zinathibitisha kuwa ilikadiriwa
kukusanya Tsh. 553,400,000/-, na ulipotimia mwaka, Wizara ilifanikiwa kukusanya Tsh.
956,918,000/. Kwa upande wa matumizi ya kawaida, fedha zilizoainishwa ni Tsh.
39,584,000,000/- na fedha halisi zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 37,277,912,000/- kukiwa
na upungufu ya Tsh. 2,306,088,000 sawa na asilimia 6 ya makadirio. Aidha, matumizi ya
maendeleo, Wizara iliidhinishiwa kutumia Tsh. 8,325,000,000/-, lakini mwisho wa mwaka
ulipofika, fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 6,144,663,000, sawa na asilimia 74
ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Taarifa za makisio ya makusanyo za mwaka huu haziko sawa, kwani inashindwa kujua kama
ni ya Wizara au ya Serikali, ukizingatia taarifa ya mwaka 2011/2012, ambapo makisio ya
makusanyo yaliyooneshwa katika taarifa yanathibitika kuwa ni ya Serikali kwa ujumla wake.
Uchunguzi wa Kamati
Ili kujiridhisha maelezo ya Wizara, Kamati ilihitaji ufafanuzi kutoka kwa Afisa Mdhibiti
aliefuatana na Kamati na kukubaliana kuwa, taarifa hizo hazioneshi uhalisia wa makusanyo
yaliyokusudiwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Afisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali,
kufafanua kwa uwazi na usahihi taarifa za ripoti zake, ili ziweze kufanyiwa kazi
kiurahisi na Kamati.
Kamati inaishauri Serikali kuwa na vigezo sahihi vya makusanyo ya mapato, ili
Taasisi zote ziwe na rikodi nzuri za kiwango cha mafanikio ya makusanyo halisi.
7.2 WIZARA YA AFYA
Hoja Namba 25.1.1 Matokeo ya hesabu za Mwisho wa Mwaka
Taarifa za mapato na matumizi
Wizara ya Afya ilikadiriwa kukusanya Tsh. 995,500,000 kwa mwaka 2012/2013, fedha
ambazo hazikuweza kufikiwa kama ilivyokisiwa kwa kukusanywa Tsh. 581,123,624 sawa na
asilimia 58.4 ya makadirio, kukiwa na upungufu wa Tsh. 414,376,376, sawa na asilimia 41.6
ya makadirio.
Aidha, matumizi ya kazi za kawaida yalikuwa Tsh. 18,229,000,000, na kutokana na hali
halisi ya kuingiziwa fedha hizo kwa ukamilifu wake, Wizara ilitumia kama ilivyokadiriwa.
Vile vile kwa kazi za maendeleo, Wizara ilikadiriwa kutumia Tsh. 21,982,205,000 kutoka
kwa Wahisani wa Maendeleo na Serikali, lakini fedha halisi iliyoingizwa na kutumika,
ilikuwa Tsh. 4,070,854,400.
67
Majibu ya Wizara
Wizara inakiri hesabu hizo, ambapo uchache wa mapato kinyume na makadirio unatokana na
kuondoshwa kwa michango ya mama wajawazito. Aidha, kwa matumizi ya kawaida, Wizara
inashukuru kwa kupata asilimia mia moja, ingawaje hesabu hiyo inaakisi zaidi fedha za nje
ya nchi kwa matibabu, huku Wizara ikikosa fedha za matumizi kwa vifungu vyengine.
Aidha, kutokana na kukosa bajeti kamili ya maendeleo, Wizara imeshindwa kutekeleza
baadhi ya miradi kwa ukamilifu wake, kwa mfano, imeathirika katika mradi wa kupandisha
hadhi hospitali ya Mnazi mmoja na hospitali zilizotakiwa kuwa za Wilaya kutoka „Cottage‟
na kwa upande wa Mradi wa ujenzi wa jengo la Kitengo cha Macho, wameshindwa
kukarabati jengo hilo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imelipokea suala la usafirishwaji wa wagonjwa nje ye nchi kwa upekee, ambalo
linahitaji kuangaliwa tena, kwani Wizara huonekana inaingiziwa fedha hizo, wakati gharama
za usafirishaji na posho la kujikimu kwa watumishi wa Serikali, lingeliweza kufanywa na
Wizara ama Taasisi husika, huku Wizara ikabaki na jukumu la kugharamia matibabu tu.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuzingatia kipaumbele cha Wizara hii ya Afya kwa
kuingizia fedha kamili za matumizi ya kawaida na maendeleo.
Kamati inaishauri Serikali kupitia Wizara ya Fedha, kuzitaka Wizara na Taasisi za
Serikali, zitayarishe bajeti itakayoonesha malipo ya nauli na posho la kujikimu kwa
watumishi na viongozi mbali mbali wa Wizara na Taasisi husika, wanaosafirishwa
nje ya nchi kwa matibabu, huku jukumu la Wizara likabaki katika kugharamia
matibabu pekee.
Hoja Namba 25.1.2 Malipo yaliyofanywa kinyume na kanuni na taratibu za
manunuzi, Tsh. 54,425,500
Fedha hizo zimetumika kwa ununuzi wa madawa ya wodi ya wazazi, Unguja na Pemba,
lakini manunuzi hayo hayakufuata taratibu za kisheria.
Majibu ya Wizara
Dawa zilizonunuliwa kwa fedha hizo ni za kuwasaidia kina mama wajawazito na watoto.
Dawa hizo hununuliwa kila muda zinapopatikana fedha kwa awamu na sio kwa mara moja.
Vile vile hufuata taratibu za manunuzi ambapo kiwango kinachozidi USD 10,000 huitishwa
tenda na manununzi chini ya kiwango hicho hufuata utaratibu wa manunuzi kwa kuwasilisha
„Qoutation‟ na Kampuni yenye kiwango kidogo ndio wanayoitumia kununua dawa hizo.
Hivyo, Wizara imenunua dawa hizo kwa kutumia „Invoice System‟ kwa kufuata utaratibu wa
manunuzi.
Uchunguzi wa Kamati
Kwa kuzingatia fedha iliyotengwa kufanya manunuzi husika, Wizara haikuwa na sababu ya
kuzitumia fedha hizo kidogo kidogo (instalment) kwa lengo la kukwepa kufuata taratibu za
kisheria. Na kwa kuwa Wizara hutakiwa kuwa na Mpango wa Manunuzi, ambayo huonesha
matumizi ya fedha hizo kwa pamoja, kutumia kidogo kidogo kwa lengo hilo, haiifanyi
ulazima wa wa kufuatwa Sheria kubatilika.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuhakikisha inafanya manunuzi kwa kufuata taratibu za kisheria.
68
7.3 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
Hoja Namba 24.1.1 Matokeo ya hesabu za Mwisho wa Mwaka
Taarifa za mapato na matumizi
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ilikadiriwa kutumia Tsh. 71,050,000,000 kwa kazi za
kawaida kwa mwaka 2012/2013. Aidha, Wizara iliingiziwa na kutumia Tsh. 67,698,946,000
sawa na wastani wa asilimia 95, kukiwa na upungufu wa bajeti kamili ya Tsh. 3,351,054,000
sawa na asilimia 5 ya makadirio. Kwa matumizi ya kazi za maendeleo, Wizara ilikadiriwa
kutumia Tsh. 5,1000,000,000, lakini hali halisi ya uingizwaji na utumiaji wa fedha hizo
unaonesha kuwa ni Tsh. 3,016,700,000 sawa na asilimia 59 ya makadirio, kukiwa na
upungufu wa Tsh. 2,083,300,000 sawa na asilimia 41 ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Ni kweli fedha hizo zimeingizwa na kutumika na athari zilizopatikana kwa upungufu wa
fedha za kawaida, ni kukosekana kwa vifaa vya kufanyia mitihani. Wizara pia ilipanga
kununua kompyuta kwa skuli za sayansi na kupelekea kushindwa kununua kompyuta hizo
kwa mwaka 2012/2013 na matokeo yake wamenunua kwa mwaka huu wa fedha. Wizara ina
limbikizo la deni linalotokana na ada ya mitihani ya Form IV na hawakuweza kulipa kwa
mwaka huo na wamelazimika kulibeba kwa miaka iliyofuata na sasa limeshafikia Tsh.
998,000,000/-
Kwa upande wa matumizi ya kazi za maendeleo, Wizara imeathirika katika maeneo mbali
mbali kwa kukosa bajeti kamili, ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa mradi wa
uimarishaji wa maktaba na kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa ukarabati wa taasisi
ya Karume pamoja na ujenzi wa msingi wa dahalia ya skuli ya sekondari ya Kengeja.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeelezwa kwamba, Wizara ya Fedha ina taarifa nyingi rasmi za madeni ya Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Amali, pamoja na kupokea mabadiliko ya mshahara na
malimbikizo yake kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma
kuhusu suala hilo na hakuna hatua ilizozichukuwa au kama ipo, basi hatua zilizochukuliwa
ni za kiwango kidogo na haziridhishi. Kwa mfano tokea 2012, Wizara ya Elimu Pemba
hakujafanyika mabadiliko ya mshahara wakati barua zimeshafika Wizara ya Fedha mapema.
Aidha, Wizara inakabiliwa na tatizo la kuchelewa kulipwa kwa walimu wanaosimamia
mitihani, huku Wizara ikitoa taarifa mapema za maombi hayo Wizara ya Fedha. Pia Kamati
imetaka ufafanuzi wa mradi wa usambazaji wa madawati katika Skuli za Zanzibar na
kuelezwa kuwa, Wizara inapewa kasma ya bilioni 2 kwa mwaka, lakini fedha wanayopata ni
milioni 300 pekee.
Kamati imesikitishwa na taarifa hii kutokana na fedha ya usambazaji wa madawati wakati
Serikali ilipandisha kodi ya Tsh. 1,000 kwa wasafiri wa njia ya boti wanaokwenda Dar es
Salaam, ili yanunuliwe madawati.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuwaingizia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, fedha zote
zinazotokana na kodi hiyo ili Wizara iweze kutekeleza malengo yaliyokusudiwa.
69
7.4 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
7.4.1 OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA
Hoja Namba 20.5.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Matumizi ya Kazi za Kawaida na Maendeleo
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ilikadiriwa kutumia kwa kazi za kawaida, Tsh.
979,000,000 kwa kazi za kawaida kwa mwaka 2012/2013. Aidha, fedha halisi zilizoingiziwa
na kutumia Tsh. 978,546,000 sawa na wastani wa asilimia 100 ya makadirio. Kwa matumizi
ya kazi za maendeleo, Wizara ilikadiriwa kutumia Tsh. 250,000,000, na fedha hizo hizo
ndizo zilizoingizwa na kutumika, sawa na asilimia 100 ya makadirio.
Majibu ya Ofisi
Ni kweli taarifa hizo na Ofisi imeshukuru kwa kuingiziwa lakini bado Ofisi inakabiliwa na
tatizo la mishahara na posho kwa watendaji. Ofisi pia inaendelea na tatizo la
kucheleweshewa kuingiziwa fedha za OC kiasi cha kukwamisha shughuli zake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepokea taarifa ya Ofisi kwa masikitiko makubwa na kuishangaa Serikali
kushindwa kutoa kipaumbele cha matumizi na mgawanyo wa fedha kwa Ofisi hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuzingatia mahitaji ya Ofisi hii na kuipatia fedha kwa wakati na
kwa ukamilifu, ili itekeleze majukumu yake kwa ufanisi.
7.4.2 KAMISHENI YA WAKFU NA MALI YA AMANA
Hoja Namba 20.2.1 Malimbikizo ya madeni kwenye nyumba za wakfu na mali ya
amana, Tsh. 205,125,700
Kumekuwa na ugumu kwa wananchi kulipia kodi ya upangaji katika nyumba za wakfu,
jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada za Serikali katika ushughulikiaji wa nyumba hizo
kutokana na kuhitaji matengenezo tofauti na yanayohitaji gharama kubwa. Hivyo, fedha
zinazodaiwa kwa wapangaji hao ni Tsh. 205,125,700 na bado hazijalipwa na inashauriwa
kuandaliwa utaratibu wa kuwafanya wapangaji walipie kodi kwa wakati.
Majibu ya Kamisheni
Taarifa hiyo ni kweli, ingawaje Kamisheni imeshachukua hatua mbali mbali kama
ilivyoshauriwa na Mkaguzi. Miongoni mwa hatua hizo utoaji wa elimu juu ya dhana na
malengo ya wakfu, kuimarisha kumbu kumbu kwa kufanya uhakiki na kutambua wenye
madeni kila baada ya miezi sita, kukamilisha sulhu ya mzozo uliobuka baada ya
kupandishwa kwa kodi, kutayarisha na kuzifanyia kazi kanuni zilizotolewa kupitia Gazeti la
tarehe 9 Juni 2014, kuunda kikosi kazi cha watu watano kwa kufuatilia madeni na
kuwapangia baadhi ya watendaji kazi ya kudumu ya ukaguzi wa nyumba. Aidha, sasa deni
hilo la Tsh. 205,125,700 limelipwa na kubaki Tsh. 72,554,500/-
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji sababu zinazowapelekea wapangaji kutolipa wakati mikataba yao inaeleza
wanatakiwa kulipa. Aidha, kwa nini Kamisheni isiwachukulie hatua za kuwapeleka
Mahakamani ili kuwalazimisha kulipa. Kamati imefurahishwa na juhudi zilizochukuliwa na
Kamisheni za kupunguza deni, lakini imesikitishwa sana na baadhi ya wapangaji 31 ambao
hawajalipa kabisa na kuonesha dharau dhidi ya Kamisheni. Pia Kamati ilihitaji kupatiwa
70
majina ya wapangaji waliokuwa hawakujaza mikataba mwaka 2014, na tarehe 24/02/2015
iliwasilishwa kwa Kamati orodha ya wapangaji 33 kupitia barua yenye kumbu kumbu namba
KWNMA/BW/85/VOL.I/11 inayoonesha majina yao, nyumba waliyopanfa na mtaa ambao
ipo nyumba husika.
Aidha, Kamati imehoji mkataba wa Aga Khan wa kukodishwa „Old Dispensary‟ kwa
gharama ndogo kabisa ya Tsh. 1,000 kwa mwezi tena kwa kodi ya miaka 80, wakati sheria
imeipa uwezo wa kuvunjwa kwa mikataba ya aina hiyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Kamisheni kuhakikisha kuwa wapangaji 31 waliobainika kuwa hawajalipa
kabisa wafikishwe Mahakamani ili waweze kulipa madeni yao. Kuhusiana na wapangaji
ambao bado hawakujaza mikataba, Kamisheni inatakiwa kuhakikisha wapangaji hao
wanajaza mikata kwa mujibu wa Sheria, ili iweze kusimamia ipasvyo nyumba wanazokaa
wapangaji hao. Aidha, kuhusiana na mkataba wa Aga Khan, Kamati imeitaka Kamisheni
kulifuatilia suala hilo kwa hatua za kisheria.
Hoja Namba 20.2.2 Kuchukuliwa kwa shamba la wakfu.
Ukaguzi umebaini kuwa, shamba la wakfu la Ndg. Hamoud Ahmed liliopo Mfenesini
Unguja, limechukuliwa na watu mbali mbali kwa ajili ya shughuli za kilimo na kujenga
nyumba za kuishi, bila ya kibali kutoka kwa Kamisheni. Kamisheni inashauriwa kuchukua
hatua za kuyapitia mashamba ya wakfu pamoja na kuhakikisha kwamba, kunakuwa na
udhibiti mzuri wa mashamba hayo.
Majibu ya Kamisheni
Kamisheni imefanya uhakiki na uchambuzi wa kiutafiti kuhusiana na mashamba ya wakfu
juu ya namna bora ya kurejeshwa kwa mashamba ya wakfu na moja kati ya mambo
yaliyobainika ni kuwepo kwa utashi wa kisiasa (political will), kwani wakati Kamisheni
inaanzishwa mwaka 1980, mashamba ya wakfu yalikuwa tayari yameshavamiwa.
Shamba linalohusika na hoja hii liliasisiwa kuwa wakfu wa mawali (freed slave) mwaka
1875 na asili yake lilikuwa Saateni kwa Abass Hussein. Mwaka 1953 Serikali ya Zanzibar
ililichukua shamba hilo na kubadilishana na shamba la Mfenesini ambalo kwa sasa
limevamiwa kwa makaazi ya watu na shughuli za kilimo kwa zaidi ya miaka 40.
Hata hivyo, Kamisheni imechukua hatua za kufanya uhakiki na upembuzi wa wanufaika
pamoja na vikao tokea mwaka 2011 na wanufaika wa shamba na wanaolitumia. Pia
Kamisheni ilitoa barua tarehe 21/3/2013 kuwataka waliojenga nyumba za muda wahame na
wanaofanya shughuli za kilimo waendelee lakini wakati wowote wakitakiwa kuhama wasije
kudai fidia na uongozi wa Jimbo la Mfenesini kumuomba Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria
kusitisha utekelezaji wa amri kwa muda ili kuliangalia upya suala hilo na kuomba Serikalini,
wakfu huo ufidiwe shamba jengine, ingawaje mazungumzo bado yanaendelea na kikao cha
mwisho kilitarajiwa kufanyika tarehe 7/11/2014.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na ufafanuzi huo, Kamati pia imeelezwa kuwa, wenye wakfu walikwishaongea na
Muzdalifa Charitable Association kwa ajili ya kujengwa chuo cha ufundi na dahalia, lakini
bado suala hilo lipo katika ngazi ya Wizara.
71
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali pamoja na Kamisheni ya Wakfu kuharakisha kulitatua na
kulipatia mustakbali mwema suala hili kwa haraka.
7.5 WIZARA YA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA,
WANAWAKE NA WATOTO
Hoja Namba 28.1.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa za matumizi ya kawaida na maendeleo
Wizara ilikadiriwa kutumia Tsh. 2,066,396,041 kwa kazi za kawaida kwa mwaka 2012/2013.
Aidha, Wizara iliingiziwa na kutumia Tsh. 2,034,175,011 sawa na wastani wa asilimia 98,
ikiwe ni upungufu wa Tsh. 32,221,030 sawa na asilimia 2 ya makadirio. Kwa matumizi ya
kazi za maendeleo, Wizara ilikadiriwa kutumia Tsh. 1,506,600,000, lakini hali halisi ya
uingizwaji na utumiaji wa fedha hizo unaonesha kuwa ni Tsh. 571,088,782 sawa na asilimia
38 ya makadirio, kukiwa na upungufu wa Tsh. 935,511,218 sawa na asilimia 62 ya
makadirio.
Majibu ya Wizara
Ni kweli kwamba Wizara hii iliingiziwa fedha hizo zikiwa na mapungufu hayo, hata hivyo,
Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto haina hatua za
kuchukua kwa kuwa inategemea kuingiziwa fedha kutoka Wizara ya Fedha. Kuhusiana na
nyongeza ya matumizi ya kazi za kawaida, Wizara imepata nyongeza hiyo kutokana na
nyongeza ya mishahara.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati hii imebaini kuwa ingawa kuna upungufu wa uingizwaji wa fedha za matumizi kwa
kazi za kawaida katika mwaka huu wa fedha, hata hivyo upungufu huo sio mkubwa sana
ukilinganisha na uingizwaji wa fedha kwa matumizi ya kazi za maendeleo. Hii ni kutokana
na kuwa kwa upande wa matumizi ya kazi za maendeleo kuna upungufu wa asilimia 62 ya
makadirio.
Mapendekezo ya Kamati
Serikali ifanye juhudi ya kuingiza kwa ukamilifu bajeti za Wizara na taasisi zake, ili Wizara
na taasisi hizo ziweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
7.6 WIZARA YA NCHI (OR) KAZI NA UTUMISHI WA UMMA
Hoja Namba 43.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2011/2012
Taarifa ya Matumizi ya kawaida na maendeleo
Makusanyo ya Wizara yalikadiriwa kuwa Tsh. 93,000,000 kwa mwaka 2012/2013 na hali
halisi ya makusanyo yalikuwa Tsh. 137,786,787. Kwa upande wa matumizi, Wizara
ilikadiriwa kutumia Tsh. 2,324,277,000 kwa kazi za kawaida na fedha halisi zilizoidhinishwa
na kutumika ni Tsh. 2,125,771,199. Aidha, matumizi ya kazi za maendeleo yalikisiwa kuwa
Tsh. 2,067,602,896 na fedha hizo hizo ziliingizwa na kutumiwa zilikuwa Tsh. 513,053,744.
Majibu ya Wizara
Taarifa hizo ni sahihi na kuhusiana na matumizi ya maendeleo, Wizara ilikuwa na shughuli
mbali mbali za utekelezaji wa miradi iliyohusika, ikiwa ni pamoja na utungaji wa Sheria za
Utumishi wa Umma na kanuni zake, miradi ambayo hapo awali ilikuwa inategemea „World
72
Bank‟ lakini hivi sasa Wizara inapata fedha kutoka Serikalini pekee. Hivyo, Wizara
inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa wafadhili wa mradi huu isipokuwa Serikali.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati imehoji muda mrefu wa utekelezaji miradi ya Wizara na kuamini kuhusiana na
kukosa wafadhili kuwa, suala hilo lingestahiki kufanywa na Serikali na sio kutegemea
Wafadhili.
Hoja Namba 16.1.2 malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu), Tsh.
15,519,500
Fedha hizo zimelipwa kwa matumizi mbali mbali lakini vielelezo husika havikupatikana kwa
ukaguzi, kinyume na kanuni ya 95(4) ya Kanuni za Fedha za mwaka 2005 na kwa hali hii,
uhalali wa malipo haukuweza kuthibitishwa na Mkaguzi.
Majibu ya Wizara
Ni kweli wakati wa ukaguzi vielelezo hivyo havikuwepo, lakini hivi sasa tayari vipo tayari
kwa kukaguliwa na Kamati.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati inafahamu usahihi wa hoja ya Mkaguzi na maelezo ya Wizara hayawezi kufuta
maelekezo ya Sheria ya kupatikana kwa vielelezo hivyo, mara tu fedha za Serikali
zinapotumiwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara irekebishe kasoro hiyo.
7.6.1 KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA
Hoja Namba 16.2.1 Taarifa ya Matumizi ya Kazi za Kawaida
Kamisheni ya Utumishi wa Umma ilikadiriwa kutumia Tsh. 856,484,000 kwa kazi za
kawaida kwa mwaka 2012/2013 na fedha halisi zilizopatikana na kutumika ni Tsh.
420,673,177, sawa na asilimia 49.12 ya makadirio, ikiwa kuna upungufu wa Tsh.
435,810,823 sawa na asilimia 50.88 ya makadirio.
Majibu ya Kamisheni
Ni kweli fedha hizo zimeingizwa na kutumika na athari kubwa zilizopatikana kwa
Kamisheni kutopatiwa fedha zote za makisio ya matumizi ni kushindwa kutekeleza
majukumu yake kisheria, ikiwa ni pamoja na kushindwa kutowa elimu ya Sheria za
Utumishi wa Umma na kutofanya shughuli mbali mbali. Kamisheni pia imeshindwa kutoa
uwezeshaji wa Miongozo ya Utumishi wa Umma na kufanya tathmini kwa taasisi mbali
mbali za Umma.
Aidha, Kamisheni haikuweza kununua gari iliyopanga kuinunua kwa Makamishna kwa ajili
ya kutembelea sehemu mbali mbali za umma na zaidi kwa hivi sasa ununuzi wa gari
hauhesabiki kuwa ni sehemu ya matumizi ya maendeleo, hivyo hulazimika kutumia OC kwa
matumizi hayo.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na maelezo ya Kamisheni, Kamati imejiridhisha kuwa Kamisheni inakabiliwa na
tatizo la kutokuwa na watendaji wa kutosha kwa kazi zake, jambo ambalo linawanyima pia
73
fursa ya kuomba miradi ya maendeleo. Aidha, Kamisheni haina jengo lake na ililonalo sasa
linawagharimu USD 500 kwa kila mwezi kuwalipa Shirika la Bandari wamiliki wa jengo
hilo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuiwezesha Kamisheni kimatumizi na kuwapa miradi ya maendeleo
ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Hoja Namba 12. Uwasilishaji wa hesabu za mwisho wa mwaka kwa ukaguzi
Pamoja na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Fedha kuzitaka taasisi zote za Serikali
kuwasilisha hesabu zao za mwisho wa mwaka, Kamisheni imechelewa kwa kuwasilisha
tarehe 01/10/2013 kinyume na maelekezo ya Sheria ya kuwasilishwa hesabu hizo si zaidi ya
tarehe 30/09 ya kila mwaka.
Majibu ya Kamisheni
Si kweli kuwa Kamisheni imewasilisha hesabu zake tarehe iliyotajwa na mkaguzi na badala
yake imewahi na imewasilisha kwa wakati.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilitaka kuthibitishiwa ukweli wa maelezo ya Kamisheni na kwa kupitia „Despatch‟,
ilijiridhisha kuwa waliwasilisha tarehe 30/09/2013 kupitia barua yenye kumbu kumbu namba
OR/KUU/F.47/VOL.1/010.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inapendekeza hoja hii ifutwe.
7.7 WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI
Hoja Namba 21.1.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Makadirio ya Mapato na Matumizi
Tsh. 426,000,000 zilikadiriwa kukusanywa kwa mwaka 2012/2013 na Wizara ya Kilimo na
Maliasili, na ulipotimia mwaka, Wizara ilifanikiwa kukusanya Tsh. 550,216,660 sawa na
asilimia 129 ya makadirio, ikiwa ni ongezeko la Tsh. 124,216,660 sawa na asilimia 29 ya
makadirio.
Kwa upande wa matumizi ya kawaida, fedha zilizoidhinishwa ni Tsh. 11,488,810,589/- na
fedha halisi zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 11,219,744,188/- sawa na asilimia 98 ya
makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 269,006,401 sawa na asilimia 2 ya makadirio. Aidha,
matumizi ya maendeleo, Wizara iliidhinishiwa kutumia Tsh. 11,507,116,000/-, lakini
mwisho wa mwaka ulipofika, fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 3,250,832,104,
sawa na asilimia 28 ya makadirio, kukiwa na upungufu wa Tsh. 8,256,283,896 sawa na
asilimia 72 ya makadirio.
Majibu ya Wizara:
Wizara iliieleza Kamati kuwa ongezeko la mapato hayo yametokana na juhudi kubwa
zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara hii za kufuatilia vianzio vyake vya mapato. Aidha,
Wizara ilikiri kuingiziwa fedha zikiwa na upungufu. Hata hivyo, ilieleza kuwa tatizo hilo
limetokea Wizara ya Fedha kwani ndio taasisi yenye mamlaka ya kutoa fedha kwa Zanzibar.
Kutokana na upungufu huo Wizara ilishindwa kutekeleza baadhi ya shughuli zake kama
ilivyojipangia.
74
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imebaini kuwa makisio ya mapato kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ni madogo
ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa kwa mwaka 2011/2012. Kutokana na hilo Kamati
hii ilielezwa kuwa Wizara haikuanzia kupanga kwenye makusanyo waliyoyapata katika
mwaka wa fedha 2011/2012 ambayo ni Tsh. 539,752,000.00 kwa kuwa katika mwaka
uliofuata mzao wa karafuu haukuwa mzuri. Kitendo hiki kimesababishwa na baadhi ya
wananchi kuikata mikarafuu jambo ambalo hupelekea mikarafuu kuwa michache na hivyo
kukosa mapato.
Kamati ya PAC haikukubaliana moja kwa moja na majibu hayo hasa ikizingatiwa kuwa
katika mwaka huo wa fedha (2012/2013) Wizara hii pia ilikusanya mapato kwa ongezeko la
Tsh.10,464,660.00.
Vile vile, Kamati imebaini kuwa uingizwaji wa fedha za maendeleo kwa Wizara hii sio wa
kuridhisha hata kidogo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Wizara hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kupitia Wizara ya Fedha kuhakikisha wanaipatia Wizara kiwango
kamili cha makisio ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Kwa upande wa
mapato, Kamati inaishauri Wizara kuongeza juhudi ya kukusanya, ili mapato ya Serikali kwa
ujumla yaweze kupatikana kwa uhakika.
7.8 WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Hoja Namba 23.1.1 Taarifa ya Mapato na Matumizi
Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilikadiriwa kukusanya Tsh. 213,000,000 kwa mwaka
2012/2013, na fedha halisi ya makusanyo hayo zilikuwa Tsh. 157,115,000 sawa na asilimia
74 ya makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 55,885,000 sawa na asilimia 26 ya makadirio.
Matumizi ya kawaida kwa Wizara hii, yalikadiriwa kuwa Tsh. 3,042,068,389, lakini fedha
halisi zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 3,007,524,535, sawa na asilimia 99 ya
makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 34,543,854, sawa na asilimia 1 ya makadirio. Aidha,
matumizi ya maendeleo ya Wizara, yalikadiriwa kuwa Tsh. 1,029,960,000, ingawa fedha
halisi zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 382,731,790 sawa na asilimia 37.2 ya
makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 647,228,210 sawa na asilimia 62.8 ya makadirio.
Majibu ya Wizara
Wizara inakusanya mapato yake kupitia Idara nne kati ya Idara sita zilizomo katika Wizara
hii. Sababu kuu ya kushindwa kufikia malengo ya makusanyo yaliyokusudiwa kwa mwaka
huu, inaokana na makusanyo yanayohusiana na Bahari Kuu, sasa yanakusanywa na
Mamlaka ya Bahari Kuu, ambayo hapo kabla yalizingatiwa kama mapato yanayokusanywa
na Wizara hii.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji sababu iliyotolewa na Wizara kuhusiana na makusanyo ya mapato, kwa
kuitaka kutoa maelezo ya sababu zilizowapelekea kuijumuisha Mamlaka ya Bahari Kuu
katika makisio ya mapato yao, wakati walijua kuwa haiko tena chini ya Wizara hii na
kuelezwa kuwa, wakati wa makisio ya mapato hayo, hawakujua kama ingeliondoshwa chini
ya Wizara na kuwa inajitegemea.
75
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuhakikisha inaongeza juhudi za makusanyo ya mapato sambamba
na kufanya matumizi ya fedha zinazopatiwa kwa mujibu wa Sheria. Aidha, Wizara
inashauriwa kuwa na uhakika wa makisio ya mapato kwa uhakika wa vyanzo vyake vya
mapato.
Hoja Namba 23.1.2 Vifaa ambavyo havikuingizwa katika daftari la ghalani, Tsh.
19,918,450
Ukaguzi umebaini kufanyika kwa malipo kwa kununua vifaa mbali mbali kwa matumizi ya
Ofisi, lakini vifaa hivyo havikuingizwa kwenye daftari la vifaa vya ghalani ili kuweza
kuthbitisha uhalali wa mapokezi pamoja na matumizi yake, kinyume na kanuni ya 168 ya
Kanuni za Fedha za mwaka 2005.
Majibu ya Wizara
Wizara inathibitisha kuwa vifaa vyote vyenye thamani iliyotajwa katika hoja hii,
vilinunuliwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na vifaa hivyo vimeingizwa katika
daftari la ghalani. Aidha, fedha zote hizo zimetumika kwa usahihi na vifaa vyote
vimesharikodiwa katika daftari la ghalani na lipo tayari kwa ukaguzi wa Kamati.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na majibu ya Wizara, Kamati imehoji sababu zilizopelekea kutokaguliwa wakati wa
ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, ambapo Kamati inathibitisha kuwa, kwa
kutokaguliwa wakati wa ukaguzi ni wazi kuwa Sheria tayari ilikuwa imeshavunjwa. Pamoja
na hayo, Kamati ilipoangalia baadhi ya hati za malipo zinazohusika, imegundua baadhi ya
kasoro ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa maombi ya Katibu Mkuu wa Wizara kumuomba
fedha Mhasibu wa Wizara, badala ya yeye Afisa Mhasibu kuombwa fedha hizo. Aidha,
baadhi ya malipo hayakuombwa matumizi yake na Kitengo cha Mtumiaji, au Afisa mweye
hamitaji ya vifaa hivyo.
Vile vile baadhi ya hati hizo za malipo hazina vielelezo vilivyokamilika, kama vile
ilivyokuwa kwa baadhi ya risiti zilizoambatanishwa kutokuwa na sifa zinazokubalika, ikiwa
ni pamoja na kukosekana kwa namba ya usajili wa ZRB (Tin Number) na pia baadhi ya hati
hizo za malipo hazina saini ya Afisa Mhasibu.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kufuata taratibu za kuingiza taarifa za vifaa wanavyovinunua katika
daftari la ghalani. Aidha, Kamati inaitaka Wizara kufuata Sheria katika matumizi ya fedha za
Serikali, ikiwa ni pamoja na kufanya manunuzi kwa mujibu wa taratibu za Kisheria.
7.9 AFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI –
BLM
Hoja Namba 17.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Matumizi
Afisi iliidhinishiwa matumizi ya kawaida, ya Tsh. 3,750,000,000/- na fedha halisi
zilizoingizwa na kutumiwa ni Tsh. 3,102,320,000/- sawa na asilimia 83 ya makadirio, ikiwa
ni upungufu wa Tsh. 647,680,000 sawa na asilimia 17 ya makadirio. Aidha, matumizi ya
maendeleo, yaliidhinishwa kwa Tsh. 3,922,400,000/-, lakini mwisho wa mwaka ulipofika,
fedha zilizoingizwa na kutumika zilikuwa Tsh. 3,967,590,000, sawa na asilimia 100 ya
makadirio.
76
Uchunguzi wa Kamati
Katika kufuatilia hoja ya Kamati haikupata mashirikiano mazuri kutoka kwa Afisi husika
ingawa baadhi ya watendaji walihudhuria kikao hicho. Hii ni kutokana na kuwa Naibu
Katibu Mkuu Ndg. Salmin Amour Abdalla ambaye ni Afisa Masuul alikuwa safarini na
alishindwa kutoa taarifa mbele ya Kamati hii. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg. Salum
Maulid Kibanzi, aliishauri Kamati hii kutoa majibu ya Afisi hiyo kwa niaba ya Naibu Katibu
Mkuu. Hata hivyo, Kamati ya PAC iliukataa ushauri huo kwa kuwa Ndg. Salum sio Afisa
Masuul wa Afisi hiyo. Baada ya majadiliano makubwa Kamati iliamua kupokea taarifa ya
Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora ingawa ratiba ya kazi ya siku hiyo ilikuwa inaigusa
moja kwa moja Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Pamoja na kuwasilishwa kwa taarifa hiyo Kamati ya PAC iligundua kuwa Afisi hiyo
haikuwa na maandalizi mazuri kwani takriban masuala mengi yaliyoulizwa yalikosa majibu
ya uhakika na hivyo Kamati iliitaka Afisi hii kuwasilisha taaifa zake kwa maandishi kwa
yale maeneo ambayo yalikosa majibu. Kwa masikitiko makubwa hadi tunawasilisha taarifa
hii hakuna taarifa yoyote iliyowasilishwa mbele ya Kamati.
Kwa msingi huo, hoja hii imebaki kama ilivyo na wahusika wanapaswa kufika mbele ya
Kamati ya PAC kuwasilisha majibu ya hoja hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakemea kitendo cha Afisa Mhasibu kutofika mbele ya Kamati, wakati Kamati
imeshatoa barua za kazi kwa Maofisa hao.
7.10 OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ.
7.10.1 TAARIFA ZA MIKOA, HALMASHAURI NA MABARAZA YA MIJI-
UNGUJA
7.10.2 MKOA WA KASKAZINI
Hoja Namba 15.9:1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Matumizi ya Kawaida
Kwa mwaka 2012/2013 Mkoa uliidhinishiwa kutumia Tsh. 1,108,400,000 kwa kazi za
kawaida ingawaje fedha zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 1,001,832,354 sawa na asilimia
90 ya makadirio ikiwa ni upungufu wa Tsh. 106,567,646 sawa na asilimia 10 ya makadirio.
Aidha, taarifa za fedha za maendeleo zinaonesha kuwa ziliingizwa Tsh. 60,000,000 ambazo
ndizo zilizokadiriwa.
Majibu ya Mkoa
Ni kweli taarifa hizo za ukaguzi wa hesabu ya matumizi ya kawaida, na athari kubwa
iliyopatikana kwa Mkoa kutokana na kushindwa kupata fedha hizo ni pamoja na kushindwa
kujenga ukuta wa Ofisi ya Mkoa na kujenga Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambayo ingelijengwa
kwa fedha za O.C. Aidha kuhusiana na fedha za maendeleo, Mkoa haukupata fedha za
maendeleo kwa mwaka 2012/2013 na fedha zilizoainishwa katika ripoti ya ukaguzi ni za
mwaka 2011/2012.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji juu ya usahihi wa majibu ya Mkoa na yale ya ripoti ya ukaguzi kuhusiana na
fedha za maendeleo, na kuhitaji kupatiwa „finantial statement‟ ambayo baada ya kuletwa na
kuipitia, Kamati ilijiridhisha kuwa, ripoti ya ukaguzi imekosewa na majibu ya Ofisi ya Mkoa
yapo sahihi. Aidha, Kamati pia imeshtushwa na taarifa ya Ofisi ya Wilaya kujengwa kupitia
77
O.C za Mkoa na kuelezwa kuwa, baada ya Ofisi ya Mkoa kuona fedha za maendeleo
zimekatwa, ndipo walipoomba fedha hizo kupitia O.C.
Hata hivyo, Kamati ilipopitia bajeti ya Ofisi kwa mwaka huu, ilijiridhisha kuombwa Tsh.
30,000,000 kwa ajili ya ujenzi huo, lakini Ofisi ilieleza baadae kuwa, fedha hizo
hazikuingizwa zote na ndipo walipolazimika kukata kutoka O.C. Aidha, Kamati imetaka
kupatiwa „finantial statement‟ ya Ofisi ambayo Afisa Tawala na Mhasibu wa Ofisi hii
walishindwa kuiwasilisha kwa Kamati na hivyo, Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa
majibu ya Mkoa kuhusiana na fedha za ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Ofisi ya Mkoa kuwa makini na matumizi ya fedha za Ofisi kwa namna
ambayo imeidhinishwa na kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi. Kitendo cha kutumia fedha
za O.C kwa ujenzi usiokudiwa bila ya kufuata taratibu za uhaulishaji, ni kukiuka Sheria.
Hoja Namba 15.9.2 Vifaa ambavyo havikuingizwa katika daftari la ghalani, Tsh.
14,180,000
Fedha hizo zimetumika kwa ununuzi wa vifaa mbali mbali kwa matumizi ya Ofisi, lakini
vifaa hivyo havikuingizwa kwenye daftari la vifaa vya ghalani ili kuweza kuthibitisha uhalali
wa mapokezi pamoja na matumizi yake, kinyume na kanuni ya 198 ya Kanuni za Fedha za
mwaka 2005.
Majibu ya Wizara
Ni kweli wakati wa ukaguzi hawakuingiza vifaa hivyo katika daftari. Hata hivyo, kasoro
hiyo sasa imesharekebishwa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji matumizi ya vifaa hivyo pamoja na kujiridhisha kuwa, hoja ya Mkaguzi iko
sahihi. Katika mahojiano hayo, Kamati ilipitia hati mbali mbali za malipo na kujiridhisha
kukiukwa kwa taratibu mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kukosekana barua za maombi ya
fedha kwa Afisa Mhasibu na hata maombi ya vifaa hivyo kutoka kwa watumiaji, jambo
ambalo linatia shaka juu ya ufuataji wa taratibu za manunuzi. Aidha, hati hizo hazioneshi
kuwa vifaa vilivyonunuliwa vimerikodiwa na hata uingizwaji wa vifaa hivyo katika daftari,
hauko sahihi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Wizara kuipatia Mkaguzi wa Ndani Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini, ili
aweze kuisaidia Ofisi kurekebisha kasoro mbali mbali zinazoendelea kufanyika Ofisini hapo.
7.10.3 BARAZA LA MANISPAA
Hoja Namba 15.12.1 Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kazi za Kawaida na
Maendeleo
Baraza la Manispaa lilikadiriwa kukusanya Tsh. 3,193,965,000 na mapato halisi
yaliyokusanywa yalikuwa Tsh. 2,839,200,094 sawa asilimia 89 ya makadirio, ikiwa ni
upungufu wa Tsh. 354,764,906 sawa asilimia 11 ya makadirio. Matumizi ya kazi za kawaida
yalikidiriwa kuwa Tsh. 4,300,409,302 na matumizi halisi yalikuwa Tsh. 2,890,440,095 sawa
na asilimia 67 ya makadirio, ikiwa ni pungufu ya Tsh. 1,409,969,207 sawa na asilimia 23 ya
makadirio.
78
Kwa upande wa matumizi ya maendeleo makisio yalikuwa Tsh. 369,407,302 na fedha halisi
zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 59,039,500, sawa na asilimia 16 ya makadirio, ikiwa ni
upungufu wa Tsh. 310,367,802 sawa na asilimia 84 ya makadirio.
Majibu ya Baraza
Sababu kubwa iliyolifanya Baraza kushindwa kupata makisio halisi waliyoyakisia
kunatokana na kukosea kupanga makusanyo hayo, kushuka kwa vyanzo vya mapato
kutokana na sababu mbali mbali, mapungufu ya kisheria na kutegemea leseni za biashara
lakini maduka mengi hivi sasa wanakata leseni zao ZRB, Wizara ya Biashara, Viwanda na
Masoko na maeneo mengine. Hii ni kutokana na Baraza kukata leseni ndogo ndogo za
200,000 hadi 300,000 na leseni kubwa, wananchi hukimbilia ZRB. Na tatizo hilo lipo kwa
mkanganyiko wa Sheria kuwa kila taasisi kati ya hizi zinatumia Sheria zenye kutoa mamlaka
tofauti ya makusanyo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepokea sababu hizo na kuhoji uhalisia wa makusanyo hayo na makisio na
kuelezwa kuwa, kuongezeka kwake kunatokana zaidi na agizo la Mhe. Waziri
anaeshughulikia Tawala za Mikoa kwa kuwataka lazima wafikie makusanyo ya bilioni 5,
wakati uwezo wa Baraza hauwezi kufikia makusanyo hayo, na hakuna vyanzo vyovyote
vipya vilivyoongezeka kinyume na vyanzo vilivyokuwepo kabla.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Baraza kuongeza juhudi katika makusanyo na lifanye matumizi yake kwa
kufuata taratibu za Sheria. Aidha, makisio ya makusanyo yawe halisi ili yaweze kufikiwa,
kuliko kukisia bila ya kuangalia uwezo halisi wa Baraza.
Hoja Namba 15.2.2 Malipo kwa ajili ya usafi, Tsh. 5,200,000
Baraza limefanya malipo ya usafi kwa kikundi cha Muwata, lakini makubaliano au mkataba
wa kazi hiyo haukuambatanishwa na kuweza kupatikana kwa ukaguzi na hivyo, Mkaguzi
ameshindwa kujua uhalali wa malipo hayo.
Majibu ya Baraza
Muwawata ni kikundi cha Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania chenye namba ya
usajili S.A 17184 iliyotolewa tarehe 27/12/2010 chini ya Sheria ya Usajili wa Jumuiya
(Society Act), Cap 337 (R.E 2002) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na namba ya
usajili 934 ya tarehe 6/4/2011 chini ya Sheria ya Usajili wa Jumuiya (Society Act) namba 6
ya mwaka 1995 ya Zanzibar.
Kikundi hiki kiliomba na kupewa kazi ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo ndogo za
usafi na utunzaji wa mji na waliingia mkataba wa makubaliano na Baraza la Manispaa kwa
muda wa miezi mitatu kuanzia tarehe 01/06 hadi 31/08/2012. Kasoro iliyojitokeza ni
kutoambatanishwa mkataba huo katika kila hati ya malipo. Hata hivyo, Baraza linathibitisha
kwamba, mkataba huo upo na upo tayari kwa ukaguzi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji kwa nini mkataba huo ambao ndio sasa unawasilishwa kwa Kamati,
haukuwepo wakati wa ukaguzi na kuelezwa kuwa, ulikuwepo katika hati za malipo ya awali
ambao ulikuwa ni mwisho wa mwaka (tarehe 1/6/2012), hivyo kasoro ilikuwa ni
kutoambatanishwa na hazi hizo za malipo. Hata hivyo, Kamati inatia mashaka majibu haya
79
kwa sababu Mkaguzi hufanya kazi yake kwa mashirikiano makubwa na taasisi anayoikagua
na huwepo katika taasisi husika si chini ya wiki mbili za ukaguzi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Baraza la Manispaa kutoa mashirikiano mazuri na wakaguzi kwa kuwapatia
taarifa wanazozihitaji.
Hoja Namba 15.12.3 Malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu), Tsh.
8,500,000
Fedha hizo zimetumika kwa matumizi mbali mbali lakini vielelezo husika havikupatikana
kwa ukaguzi, kinyume na kanuni ya 95(4) ya Kanuni za Fedha za mwaka 2005. Malipo hayo
ni kama ifuatavyo:
Hati
namba
Fedha
zilizolipwa
Aliyelipwa Maelezo
20/2 2,000,000 Pili Saidi
Ramadhani
Malipo ya usafi kwa mwezi wa
Januari 2013
21/2 2,000,000 Zacedy Malipo ya usafi kwa mwezi wa
Januari 2013
47/2 4,500,000 Mkurugenzi wa
Baraza la Manispaa
Fedha za maendeleo kwa wadi
tisa za Manispaa
Majibu ya Baraza
Ni kweli vielelezo hivyo vimekosekana kutokana na uhalisia na mazingira maalum ya
matumizi ya fedha hizo. Kwa mfano fedha zilizolipwa Ndg. Pili Saidi ni kwa ajili ya kikundi
cha usafi cha Glittering Volunteer Group kwa ajili ya huduma ya usafi, lakini kikundi hicho
hakikuwa na risiti wala akaunti ya benki na ndio maana akalipwa Mwakilishi wao.
Fedha za Zacedy nazo ni kama za awali, ni za kikundi za ZACEDY kwa ajili ya huduma ya
usafi, ambapo stakabadhi ilikuwepo lakini kwa bahati mbaya haikuambatanishwa na hati ya
malipo wakati ukaguzi unafanyika. Aidha, Tsh. 4,500,000 ni fedha za maendeleo kwa wadi
tisa ambazo wamepewa Waheshimiwa Madiwani ambapo kwa kuzingatia matumizi ya fedha
hizi, baadhi ya Waheshimiwa hawarejeshi marejesho kwa wakati. Hata hivyo, Baraza
linaendelea kutoa elimu kwa Waheshimiwa, ili waweze kutekeleza maelekezo ya Sheria.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na hoja za Baraza kuhusiana na hali halisi ya marejesho ya vielelezo vinavyohusiana
na hoja hii, Kamati haikubaliani kukiuikwa kwa Sheria kwa sababu hizo. Aidha, Kamati
imefanya mapitio ya hati za malipo zilizoelezwa kuwa vielelezo vyake vimekamilika wakati
wa kazi za Kamati na kujiridhisha kuwa kuna kasoro mbali mbali ikiwa ni pamoja na malipo
ya Tsh. 4,500,000 hayana risiti za malipo wala hati ya kuthbitisha malipo husika, na
Waheshimiwa Madiwani wamefanya wao maombi moja kwa moja kwa Mkurugenzi, badala
ya maombi yao kuombwa na watendaji wa Baraza.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Baraza kufuata taratibu za Sheria ya Fedha na Kanuni zake kwa kufanya
matumizi ya fedha za Umma kwa kufuata taratibu za matumizi yake na uthibitisho wa
vielelezo sahihi vya matumizi ya fedha hizo.
80
Mengineyo yaliyojitokeza
Kamati imehoji Mradi wa ZUSP na kuelezwa kuwa una matatizo mengi katika utekelezaji
wake na Waheshimiwa Madiwani wa Baraza wamesema hawashirikishwi katika
utekelezwaji na upangaji wake. Hivyo, Kamati inahitaji kupata taarifa za kina kuhusiana na
mradi huu, namna ulivyoanza na utekelezaji wake pamoja na gharama zake.
Aidha, Kamati inaishauri Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, kufanya ukaguzi
wa mradi huu kwa sababu umeshakuwa na malalamiko mengi kutoka taasisi mbali mbali
zilizohusika na mradi huo.
7.10.4 HALMASHAURI YA WILAYA YA KASKAZINI “B”
Hoja Namba 17.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Makadirio ya Mapato na Matumizi
Taarifa ya mapato ya Halmashauri inaonesha kukadiriwa kukusanywa Tsh. 100,000,000 kwa
mwaka 2012/2013, ingawaje fedha halisi iliyokusanywa ni Tsh. 212,204,768 sawa na
asilimia 212 ya makadirio, ikiwa ni ongezeko la Tsh. 112,204,768 sawa na asilimia 12 ya
makadirio.
Matumizi ya kawaida, yalikadiriwa kuwa Tsh. 188,810,000 na fedha halisi zilizoingizwa na
kutumiwa ni Tsh. 211,000,100 sawa na asilimia 112 ya makadirio, ikiwa ni upungufu wa
Tsh. 22,190,100 sawa na asilimia 112 ya makadirio, ikiwa ni pungufu ya Tsh. 22,190,100
sawa na asilimia 12 ya makadirio.
Majibu ya Halmashauri
Halmashauri ilikadiriwa kukusanya Tsh. 275,600,000 na sio Tsh. 100,000,000 kama
ilivyoelezwa na Mkaguzi. Hadi kufikia Juni, 2013, fedha zilizokusanywa zilikuwa Tsh.
212,204,768, sawa na asilimia 78.20 ya makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 63,395,232,
sawa na asilimia 21.80 ya makadirio.
Matumizi yaliyokadiriwa kwa Halmashauri yalikuwa Tsh. 265,860,000 kwa kazi za kawaida
na za maendeleo na sio 188,810,000 kama ilivyoelezwa na ripoti ya ukaguzi. Aidha, Tsh.
211,000,100 zilitumika kwa kazi za maendeleo sawa na asilimia 79 ya makadirio, ikiwa ni
upungufu wa Tsh. 54,860,000 sawa na asilimia 20 ya makadirio.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na majibu ya Halmashauri, Kamati imehoji sababu zilizopelekea kushindwa kufikia
makisio ya makusanyo na kuelezwa kunatokana na kuwepo kwa mvua na kuadimika kwa
saruji, kulipekea kutopata mapato mengi, ikizingatiwa Halmashauri inategemea chanzo cha
mapato kupitia uchimbaji wa mchanga.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Halmashauri kuongeza vyanzo vya mapato, kwani kutegemea chanzo
kimoja tu tena kwa kinachotegemea mashamba ya watu binafsi kwa ajili ya uchimbaji wa
mchanga sio uhakika wa makusanyo ya mapato.
Hoja Namba 15.5.2 Kukosekana kwa kumbu kumbu za vifaa vilivyonunuliwa kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya wananchi, Tsh. 10,500,000
Fedha hizo zimetumika kwa ununuzi wa vifaa mbali mbali, kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi ya wananchi ya Halmashauri, lakini ukaguzi umeshindwa kupatiwa kumbu kumbu za
upokeaji, utoaji na utumiaji wa vifaa hivyo, kinyume na kanuni ya fedha ya 198 ya Kanuni
za Fedha za mwaka 2005.
81
Majibu ya Halmashauri
Ni kweli kuwepo kwa upungufu huo katika uwekaji wa vifaa, hili linatokana na vifaa hivyo
kukabidhiwa moja kwa moja kwa waheshimiwa Madiwani na Kamati zao za Wadi kwa ajili
ya matumizi kutokana na mahitaji ya jamii kwa mazingira yao ya wakati huo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa, matumizi ya vifaa hivyo ni kwa matumizi ya miradi ya
wananchi inayosimamiwa na Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri hiyo, na hivyo
kutaka kujua taratibu zinazotumika katika maombi ya matumizi hayo. Aidha Kamati
ilipofanya ukaguzi wa hati za malipo ya matumizi hayo, ilijiridhisha kuwa, baadhi ya hati
hizo hazina barua za maombi ya Waheshimiwa Madiwani hao. Pia hati hizo zinakosa saini
ya Afisa Mhasibu, ili kuthibitisha uhalali wa matumiz yaliyofanyika.
Aidha, kuhusiana na vifaa kuingizwa katika daftari, Kamati imejiridhisha kuwa, baadhi ya
vifaa tayari vimesharikodiwa katika daftari la ghalani, lakini vifaa vyengine bado
havijarikodiwa. Aidha, uingizwaji na utokaji wa vifaa hivyo hauoneshi usahihi na namna ya
vifaa hivyo vilivyotumika.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Halmashauri kuzingatia taratibu na maelekezo ya Sheria kwa kuingiza vifaa
katika daftari linalohusika. Aidha, Kamati inaitaka Halmashauri kuzingatia maelekezo ya
Sheria na Kanuni za Fedha kwa matumizi ya fedha za umma na khasa wanazopatiwa
Waheshimiwa Madiwani kwa miradi ya wananchi.
7.10.5 HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI
Hoja namba 15.17.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kazi za Kawaida
Halmashauri ilikadiriwa kukusanya mapato yake kwa ongezeko la Tsh. 200,000,000 kwa
mwaka 2012/2013 na fedha halisi iliyokusanywa ilikuwa Tsh. 167,979,183 sawa na asilimia
84 ya makadirio, kwa upungufu wa Tsh. 32,020,817 sawa na asilimia 16 ya makadirio.
Aidha, ilikadiriwa kutumia Tsh. 200,000,000 kwa kazi za kawaida na hatimae iliweza
kutumia Tsh. 161,383,499 sawa na asilimia 80 ya makadirio, kwa upungufu wa Tsh.
38,616,501 sawa na asilimia 19 ya makadirio.
Majibu ya Halmashauri
Mapato yalipungua katika kifungu namba 1200 ambacho kinakusanyiwa ada ya mauziano ya
Ushuru wa Forodha. Hali hii imesababishwa na Halmashauri kutaka kujiepusha na migogoro
ya ardhi kama alivyoagiza Mhe. Rais katika semina elekezi ya tarehe 4-5 Julai 2012.
Kifungu hiki kilikadiriwa kukusanya Tsh. 68,780,500 na kimeweza kukusanya Tsh.
17,219,000. Aidha, kulikuwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi wenye taaluma na
vitendea kazi na vyanzo vingi havina uhakika kutokana na kukosekana kwa takwimu sahihi,
jambo ambalo hivi sasa linafanyiwa kazi. Hivyo, na matumizi ya kazi za kawadia ya
Halmashauri nayo yaliathirika kwa namna hii.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa, pamoja na makisio ya makusanyo yanayofanywa na
Halmashauri zetu, makusanyo hayo hayafanywi kwa uhakika wa vyanzo vya mapato na
82
takwimu halisi ya uwezekano wa hakika wa kukusanywa kwake, hali inayopelekea kuwepo
kwa pengo kubwa baina ya makisio na uhalisia wa mapato.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Halmashauri iongeze juhudi za makusanyo kwa kufanya utafiti na kuwa na
taarifa za vyanzo vyake vya mapato kabla ya kufanya makisio, ili kuepusha kuwepo kwa
tofauti kubwa sana ya makisio ya makusanyo na uhalisia wake baada ya mwaka kukamilika.
Hoja Namba 15.17.2 Kukosekana kwa kumbu kumbu za vifaa vilivyonunuliwa kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya wananchi, Tsh. 12,345,000
Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbali mbali kwa utekelezaji wa miradi
ya wananchi Wilaya ya Kati, lakini ukaguzi umeshindwa kupatiwa kumbu kumbu za
upokeaji, utoaji na utumiaji wa vifaa hivyo, kinyume na kanuni ya 198 ya Kanuni za Fedha
za mwaka 2005.
Majibu ya Halmashauri
Ni kweli Halmashauri ilifanya manunuzi ya vifaa hivyo vilivyotajwa na kweli kumbu kumbu
zake zilikosekana wakati wa ukaguzi, lakini marekebisho yamefanywa na sasa kumbu
kumbu zote zipo kamili na zipo tayari kwa ukaguzi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa, Halmashauri imekiri makosa yake, lakini hali hii haiifanyi
Kamati kuwavua makosa Halmashauri kwa sababu tu kumbu kumbu zilizokosekana wakati
wa ukaguzi sasa zipo tayari kwa Kamati. Kamati inasimamia Sheria kuwa ilikiukwa na
Halmashauri kwa kukosekana kwa kumbu kumbu hizo wakati wa ukaguzi.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Halmashauri kufanya marekebisho ya kasoro hii kwani haitoi sura nzuri kwa
utendaji wake.
WIZARA NA TAASISI MBALI MBALI ZA SERIKALI-PEMBA
8.0 OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ.
8.1 TAARIFA ZA MIKOA, HALMASHAURI NA MABARAZA YA MIJI-
PEMBA
8.1.1 MKOA WA KASKAZINI
Hoja Namba 15.11:1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Matumizi ya Kawaida
Kwa mwaka 2012/2013 Mkoa uliidhinishiwa kutumia Tsh. 1,254,010,723 kwa kazi za
kawaida ingawaje fedha zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 1,240,816,897 sawa na asilimia
99 ya makadirio ikiwa ni upungufu wa Tsh. 13,193,826 sawa na asilimia 1 ya makadirio.
Majibu ya Mkoa
Afisi hii iliidhinishiwa kutumia jumla ya Tsh. 1,384,000,000 kwa ajili ya matumizi ya kazi
za kawaida. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa mishahara ya watendaji Afisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini ililazimika kuomba kuidhinishiwa fedha za ziada ambazo ni
Tsh. 19,220,000 na kufanya fungu la mishahara na maposho kufikia Tsh. 581,220,000 badala
ya 562,000,000 ilizoidhinishiwa hapo kabla.
83
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imebaini kuwa kuna mgongano wa taarifa juu ya ongezeko la matumizi ya fedha
baina ya Ripoti ya Mdhibiti na taarifa ya Mkoa iliyowasilishwa mbele ya Kamati. Aidha,
Kamati imebaini kuwa Mabaraza ya Miji hayaoneshi mapato yao yote ndani ya bajeti zao
zinazowasilishwa mbele ya Baraza la Wawakilishi. Kitendo hiki kimekitia mashaka Kamati
na hata kudhania kuwa baadhi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya matumizi ya
Mabaraza ya Miji hupotea mikononi mwa wachache.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inayataka Mabaraza ya Miji kuonesha mapato yao yote wanayoyapata wakati wa
uwasilishwaji wa bajeti ndani ya Baraza la Wawakilishi.
Kamati inazitaka Taasisi za Serikali kutoa mashirikiano mazuri na taarifa sahihi kwa
wakaguzi, ili kuepusha usumbufu wa taarifa moja ya Taasisi kutofautiana na
inayowasilishwa kwa Mkaguzi.
Aidha, Kamati inaitaka Serikali kuacha tabia ya kuzishurutisha Taasisi zake kutumia fedha
za matumizi mengineyo kwa ajili ya kulipia mishahara ya watendaji wake endapo itaongeza
mishahara ili Taasisi hizo ziweze kutekeleza vyema majukumu yake.
Hoja Namba 15.11.2: Uchelewaji wa ujenzi wa ukuta (fence) Ofisi ya Wilaya Ndogo
Kojani kwa gharama ya Tsh. 83,308,500
Fedha hizo zimetumika kwa ujenzi wa ukuta wa ofisi ya ilaya ndogo Kojani ambapo ujenzi
wa ukuta huo ulichukua muda mrefu kumalizika na kazi iliyofanyika haikidhi viwango na
gharama zilizotumika. Aidha, mkataba wa ujenzi ulifungwa 2007 baina ya Mkoa wa
Kaskazini Pemba na El-Shally Construction Corperative Society tarehe 25/05/2007 ambapo
mkandarasi alitakiwa kujenga ukuta huo kwa muda wa mwaka mmoja kwa makubaliano ya
gharama ya Tsh. 83,308,500 ambapo Tsh. 81,500,000 zililipwa kwa mkandarasi huyo kwa
vpindi tofauti.
Mkandarasi alitakiwa kukamilisha ujenzi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe
ya mkataba, kutositisha kuendelea na ujenzi hata kama fedha za malipo zitachelewa na
kuzingatia vigezo vya ubora wa ujenzi huo. Aidha, baada ya ukaguzi kuufuatilia ujenzi huo,
mapungufu yafuatayo yalibainika:
Taratibu za kumpata mkandarasi hazikufuata sheria za manunuzi.
Ujenzi wa ukuta ulianza mwaka 2009 na kukabidhiwa Septemba 2013.
Hali halisi haioneshi ubora na umadhubuti wa ukuta huo, kwani baadhi ya
kuta tayari zimeshaanza kupasuka, baadhi ya sehemu za madirisha
zimeharibika na sehemu ya mbele ya ukuta huo haukukamilika.
Fedha zilizotumika hazilingani na hali halisi ya ukuta huo, na
Mkoa wa Kaskazini Pemba umeshindwa kuchukua hatua dhidi ya mkandarasi
huyo baada ya kukiuka makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba.
Majibu ya Mkoa
Taratibu za kumpata mkandarasi hazikufuata Sheria za Manunuzi No. 9 ya mwaka
2005
Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini – Pemba baada ya kupokea agizo la kujenga ukuta kutoka kwa
Waziri aliehusika na tawala za mikoa, ilimuandikia barua yenye kumbukumbu Namba
MKP/J.1/8/VOL.11/30 ya tarehe 15 Februari, 2007 Mjenzi wa ukuta huo ambaye ni El –
Sahaly Construction Cooperative Society iliyopo Wete na kumtaka kuandika barua ya ombi
la kukubali kujenga ukuta huo pamoja na kuambatanisha gharama za ujenzi huo. Mjenzi
84
alilichukulia hatua suala hilo kama alivyoombwa na mnamo tarehe 2 Machi, 2007 Afisi ya
Mkuu wa Mkoa ilipokea barua ya Mjenzi inayokubali kujenga ukuta huo kwa gharama za
Tsh. 83,308,500. Baada ya mjenzi kukubali ombi hilo Afisi ya Mkoa ilifunga mkataba na
mjenzi tarehe 25 Mei, 2007 na kukubaliana kujenga ukuta huo ndani ya kipindi cha mwaka
mmoja.
Ujenzi wa Ukuta ulianza mwaka 2009 na kukabidhiwa Septemba, 2013
Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini – Pemba haikukubaliana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa ujenzi wa ukuta ulianza mwaka 2009, isipokuwa kwamba
ujenzi huo ulianza mwaka 2007 mara baada ya kufunga mkataba. Ingawa ujenzi wa ukuta
ulianza mwaka 2007 Mjenzi alianza kulipwa fedha zake kwa awamu kuanzia mwaka 2012
hadi mwezi Agosti, 2013. Hii ni kutokana na uhaba wa fedha unaoukabili Mkoa huu.
Hali halisi haioneshi ubora na umadhubuti wa ukuta huo kwani baadhi ya kuta tayari
zimeanza kupasuka, baadhi ya sehemu ya madirisha zimeshaharibika na sehemu ya
mbele ya ukuta huo haikukamilika.
Nyufa ilizojitokeza ni nyufa ndogo ndogo za kawaida, hii ni kutokana na mazingira ya hali
ya hewa ya eneo husika. Aidha, wakati ukaguzi unafanyika ni miaka sita tokea ukuta huo
ulipojengwa.
Pia, Afisi ya Mkoa haikukubaliana na madai ya Mdhibiti kuwa sehemu ya madirisha
zimeshaharibika. Hii ni kutokana na kuwa ukuta huo haukutiwa madirisha bali umewekwa
venti. Baadhi ya venti hizo zimeharibika kutokana na watoto kucheza na kuparamia ukuta
kwa kuwa jengo la Afisi hii lipo karibu na uwanja wa mpira.
Ama kwa upande wa sehemu ya mbele Afisi ya Mkoa ilieleza kuwa sehemu hiyo
imekamilika kinyume na ilivyodaiwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali.
Fedha zilizotumika hazilingani na hali halisi ya ukuta huo
Afisi ya Mkoa wa Kaskazini – Pemba ilikiri kuwa fedha zilizotumika hazilingani na hali
halisi ya ukuta huo kutokana na sababu zifuatazo;-
i. Ujenzi wa kwenye visiwa hususan kisiwa cha Kojani ni tofauti na ujenzi wa sehemu
nyengine zisizo za visiwa. Hii ni kutokana na kuwa vifaa vya ujenzi inabidi
visafirishwe kwa njia ya gari baadae kwa dau na hatimae vibebwe kwa kichwa hadi
katika eneo husika.
ii. Wakati ujenzi unafanyika hakukuwa na maji kwenye jengo na ililazimika maji hayo
kuchukuliwa ng‟ambo ya pili ya kisiwa.
Mkoa wa Kaskazini Pemba umeshindwa kuchukua hatua dhidi ya Mkandarasi huyo
baada ya kukiuka makubaliano yaliyomo ndani ya Mkataba
Afisi ya Mkoa ilishindwa kumchukulia hatua Mjenzi kwa kuwa Afisi yenyewe ilishindwa
kufuata matakwa ya mkataba kama vile kushindwa kumlipa Mjenzi kwa wakati.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati ya PAC haikuridhika na ujenzi wa ukuta wa Wilaya Ndogo Kojani kama
ilivyoelezwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Kutokana na
kutoridhishwa kwake huko Kamati imeutaka Mkoa huu kufuata Sheria za nchi
zinavyoelekeza juu ya mambo mbali mbali ikiwemo ujenzi wa majengo, ununuzi wa vifaa
nakadhalika.
85
Mengineyo
Kamati inawataka viongozi wa Taasisi za Serikali kuziheshimu ratiba za kazi za Kamati ili
Kamati hizo ziweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na hasa ikizingatiwa kuwa Kamati
za Baraza la Wawakilishi hutekeleza majukumu yake ndani ya kipindi maalum. Kamati ya
PAC inatoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni kushindwa kuhudhuria
kikao cha Kamati kutokana na ziara ya Mheshimiwa Waziri, Wizara ya Nchi, (AR), Tawala
za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, kitendo hiki kilikikosesha Kamati kupata taarifa za
Wilaya hiyo.
Aidha, Kamati ya PAC ilisikitishwa sana na kitendo cha Mahkama cha kuchelewa kutoa
maamuzi ya kesi ya Kituo cha Mafuta kinachomilikiwa na Mkoa huu na hasa ikizingatia
kuwa Mkodishwaji anaendelea kunufaika na kituo wakati Mkoa wa Kaskazini Pemba ndie
mmiliki wa Kituo na hanufaiki na chochote tokea mwaka 2013.
8.1.2 BARAZA LA MJI WETE
Hoja namba 15.13.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kazi za Kawaida
Ukaguzi umebaini kuwa Baraza la Mji Wete lilikusanya mapato yake kwa ongezeko la Tsh.
1,100,000 sawa na asilimia 2 ya makadirio. Aidha, imetumia kwa kazi za kawaida ongezeko
la Tsh. 700,000 sawa na asilimia 1 ya makadirio.
Majibu ya Baraza la Mji Wete
Baraza la Mji Wete liliiieleza Kamati kwamba kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikisia
kukusanya jumla ya Tsh. 50,125,000/- na sio Tsh. 53,200,000 kama ilivyoripotiwa na Ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2012/2013. Hivyo, hadi
kufikia Juni, 2013 Baraza hili lilikusanya jumla ya Tsh. 55,578,641 ikiwa ni ongezeko la
Tsh. 5,453,641.
Ama kwa upande wa matumizi ya kazi za kawaida na maendeleo Baraza la Mji Wetet
liliomba idhini ya matumizi ya ziada ya Tsh. 5,453,641 kinyume na ilivyoripotiwa na
Mdhibiti.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na maelezo yaliyotolewa na Watendaji na Waheshimiwa Madiwani wa Baraza la Mji
Wete, Kamati ya P.A.C haikukubaliana na kauli hiyo. Hii ni kutokana na kuwa Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kawaida huwasilisha taarifa ya Hoja
hiyo na Baraza la Mji Wete haikuchukua hatua yoyote kuhusiana na Hoja hiyo.
Sambamba na hilo, katika kufuatilia matumizi ya kazi za maendeleo yaliyofanywa na Baraza
hili, Kamati ya PAC ilibaini kuwa ukarabati wa Ukumbi wa Jamhuri Hall haukufuata
taratibu za Sheria, pia Kamati haikuridhika na kiwango cha gharama ambacho kimetumika
(thamani ya matumizi halisi ya fedha hayakufikiwa). Vile vile, Kamati hii imegundua
kwamba Kamati ya Ujenzi ya Baraza la Mji Wete haikupata fursa ya kuupitia mkataba wa
ujenzi wa ukumbi huo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Mapendekezo ya Kamati:
Kwa kuwa Baraza la Madiwani ndio lenye dhamana na utendaji wa Baraza la Mji
Kisheria.
Kamati ya PAC imewataka Watendaji wa Baraza hili kuwapatia mafunzo kuhusiana
na Sheria ya Manunuzi Waheshimiwa Madiwani ili waweze kuyasimamia vyema
majukumu yao.
86
Katika kuliongezea mapato Baraza hili, Kamati inaishauri Serikali kuifanyia
ukarabati bandari ya Wete ambayo ni kipindi kirefu haitumiki.
Mengineyo
Baraza la Mji Wete halifuati taratibu za kazi katika kutekeleza majukumu yake, jambo hili
limeipelekea Kamati hii kushindwa kupata baadhi ya nyaraka ikiwemo „Financial Statement‟
kwa kuwa Mhasibu aliyekuwepo hivi sasa hakukabidhiwa afisi rasmi na Mhasibu aliyepita
ingawa Mhasibu huyo aliondoka kwa ajili ya kwenda matibabuni nchini India.
Pia, Kamati ya PAC ilishindwa kupata taarifa za kiutendaji kwa kina kwa kuwa watendaji
waliokuwepo wakati Kamati inafanya shughuli zake ni wapya. Kwa kuwa mtendaji
aliyekuwa madarakani ndiye anayepaswa kujibu suala lolote kuhusiana na nafasi yake
aliyokuwepo, Kamati inawashauri watendaji kuchukua jitihada za makusudi za kufuatilia
masuala mbali mbali yaliyomo chini ya dhamana yake ili kuepusha migongano isiyo ya
lazima.
8.1.3 HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAKE CHAKE
Hoja Namba 15.19.1 Hesabu za mwisho wa mwaka, 2012/2013
Taarifa za mapato na matumizi
Kwa mwaka 2012/2013, makadirio ya makusanyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chake
Chake ilikua ni kukusanya Tsh. 33,217,860.17 na ilipofika Juni 2013, iliweza kukusanya
Tsh. 33,217,860.17 ikiwa ni sawa na asilimia 100 ya makadirio.
Kwa matumizi ya kazi za kawaida na maendeleo, Halmashauri hii ilikadiriwa kutumia Tsh.
33,217,860.17 na ilipofika Juni 2013, ilitumia Tsh. 33,217,860.17 sawa na asilimia 100 ya
makadirio.
Majibu ya Halmashauri
Halmashauri ya Wilaya ya Chake Chake iliieleza Kamati kuwa Makadirio ya bajeti
yaliyooneshwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti yanatofautiana na makadirio ambayo
Halmashauri hii inayafahamu. Aidha, matumizi yaliyofanywa na Halmashauri ambayo
yameripotiwa na Mdhibiti yanatofautiana na kumbukumbu za mahesabu walizokuwa nazo
Halmashauri. Jadweli liliopo chini linaonesha mchanganuo huo;
Maelezo Taarifa ya Halmashauri kwa
Mwaka wa fedha 2012/2013
Ripoti ya Mdhibiti kwa
Mwaka wa fedha 2012/2013
Makadirio ya
bajeti
Tsh. 36,000,000.00 Tsh. 33,217,860.17
Mapato
yaliyopatikana
Tsh. 33,217,860.17 Tsh. 33,217,860.17
Matumizi
yaliyofanyika
Tsh. 32,963,650.00 Tsh. 33,217,860.17
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilihitaji kuangalia matumizi yaliyofanyika na imebaini kwamba Ripoti ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imetoa taarifa zisizokuwa sahihi.
Aidha, Kamati ya PAC imebaini kuwa baadhi ya malipo (matumizi) yanafanywa kinyume na
utaratibu kwa mfano; fundi ameomba kazi ya kuweka vitasa vya milangoni tarehe 28 Agosti,
2012 wakati ombi la kununuliwa vitasa hivyo limefanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Pia, barua
za safari za kikazi kwa mtu mmoja zimeandikwa tarehe moja ingawa ni safari mbali mbali
nakadhalika.
87
Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeitaka Halmashauri ya Wilaya ya Chake Chake kutekeleza majukumu yake kama
Sheria zinavyoelekeza.
Aidha, Kamati ya PAC inaitaka tena Serikali kutoa elimu na semina kwa Waheshimiwa
Madiwani ili wafahamu majukumu yao.
Mengineyo na Mapendekezo ya Kamati
Kamati ya PAC imeishauri Serikali kuzishirikisha Halmashauri za Wilaya kwenye Miradi ya
TASAF hususan katika ujenzi wa masoko ili kuziwezesha Halmashauri hizo kuongeza
mapato yake sambamba na kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Kamati imeshauri hili baada
ya kubaini kuwa baadhi ya masoko yaliyojengwa na TASAF kama vile Soko la Wesha
mapato yake yanasimamiwa na wananchi wenyewe. Kitendo hiki kimeifanya Halmashauri
hii kupewa asilimia 20 tu ya mapato yanayopatikana kwa mwezi na baadhi ya miezi
hawapewi chochote. Kiwango hicho cha fedha kinatofautiana kutoka Tsh. 40,000.00 hadi
Tsh. 100,000.00 hutegemea mapato yaliyokusanywa. Kwa kuwa Halmashauri hii haina
mtendaji wake anayesimamia ukusanyaji wa mapato hayo, Halmashauri haina uhakika na
kiwango halisi cha fedha inachopewa.
Aidha, Kamati imeitaka Halmashauri ya Wilaya ya Chake Chake pamoja na uhaba wa
watendaji unaoukabili kuteua mtendaji atakaefuatilia ukusanyaji wa mapato katika Soko la
Wesha ili kuwa na uhakika wa mapato inayopatiwa.
Kwa kuwa Halmashauri hii inakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo ya kuchukuliwa
rasilimali zake kama vile kifusi bila ya kupata kipato chochote na matatizo mengi
mengineyo, Kamati hii imeitaka Wizara ya Nchi (AR), Tawala za Mikoa na Idara Maalum za
SMZ kukaa pamoja na Afisi za Mikoa na Wilaya ili kutatua matatizo hayo.
8.2 WIZARA YA AFYA
Hoja Namba 25.2.1 Malimbikizo ya madeni ya shilingi 302,499,575
Fedha hizo zinadaiwa na wafanyakazi na taasisi za Serikali na bado madeni hayo hayalipwa
hadi ukaguzi unafanyika. Kufanya hivyo ni kinyume na mfumo sahihi wa kiuhasibu wa
IPSAS unaotambua mapato na matumizi kwa fedha taslmi na iaathiri bajeti ya miaka
inayofuata.
Majibu ya Wizara: Wizara ya Afya imekiri kuwepo kwa malimbikizo ya madeni hayo na uwezo wa Wizara hii
kulipa madeni hayo ni mdogo kutokana na bajeti ndogo sana wanayopatiwa ukilinganisha na
hali halisi ya mahitaji yake kwa mwaka pamoja na upatikanaji mdogo wa fedha. Kwa mfano
kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Wizara hii ilikadiriwa kutumia jumla ya Tsh.
563,000,000.00 na hadi kufikia Juni, 2013 ilipokea jumla ya Tsh. 307,884,649.00 sawa na
asilimia 55 ya makadirio.
Hata hivyo, Wizara imechukua juhudi ya kulipa madeni hayo na hadi kufikia mwezi wa
Oktoba, 2014 inadaiwa kama ifuatavyo;
S/No. AINA YA DENI DENI HALISI
1. Umeme kwa hospitali tano za Pemba Tsh. 343,190,924.00
2. Maji kwa hospitali tano za Pemba Tsh. 16,620,000.00
3. Call za Madaktari Tsh. 47,980,000.00
4. Likizo za wafanyakazi Tsh. 39,900,000.00
JUMLA Tsh. 447,690,924.00
88
Uchunguzi wa Kamati Ingawa Wizara ya Afya – Pemba imejaribu kulipa madeni hayo, hata hivyo, kiwango
kilichobaki ni kikubwa mno.
Aidha, Kamati ya PAC baada ya kuwahoji baadhi ya watendaji wanaodai fedha zao za likizo
imebani kuwa watendaji wa Taasisi hiyo hawana taaluma ya kutosha kuhusiana na stahiki
zao.
Mapendekezo ya Kamati:
Kwa kuwa deni la umeme ni kubwa sana, na kwa kuwa Wizara ya Afya haina uwezo
wa kulipa deni hilo kutokana na udogo wa bajeti yake, na kwa kuwa Shirika la
Umeme linahitaji kulipwa fedha hizo ili liweze kujiendesha, Kamati ya PAC
inaishauri Serikali kulibeba deni hilo ili lilipwe kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina.
Kwa kuwa Hospitali zinalipa Tsh. 20,000.00 kwa mwezi kwa ajili ya malipo ya maji,
ingawa wakati mwengine huduma hiyo ya maji huwa haipatikani, Kamati imeishauri
Wizara hii kuomba kufungiwa mita za maji ili walipe gharama hizo kwa mujibu wa
matumizi yao.
Mamlaka ya Maji Zanzibar kuweka viwango tofauti vya fedha kati ya wale wanaotoa
huduma na watumiaji wa kawaida.
Ingawa fedha zinazoingizwa ni kidogo, hata hivyo, Kamati imeitaka Wizara hii
kuwalipa kwa wakati fedha za call madaktari kwa lengo la kuwatia moyo na
kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Wizara ya Afya iwapatie taaluma watendaji wake juu ya stahili zao ili kuondosha
malalamiko yasiyo ya lazima.
8.3 WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Hoja Namba 27.2.1 Malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu) shilingi
18,520,000.00
Fedha hizo zimelipwa kwa matumizi mbali mbali, lakini vielelezo vyake havikupatikana kwa
ukaguzi, jambo ambalo linakwenda kinyume na kanuni ya 95(4) ya Kanuni za Fedha za
mwaka 2005.
Majibu ya Wizara
Ni kweli kwamba baadhi ya vocha hizo zilikosa stakabadhi (receipts), ingawa kulikuwa na
sahihi za wapokeaji wa malipo hayo wakati Mkaguzi alipofanya marejeo ya hoja zake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ya P.A.C imegundua kuwa hoja hiyo imeibuka baada ya Wizara ya Mindombinu na
Mawasiliano kukubali kuviajiri vikundi ambavyo havikuwa na usajili wala akaunti. Jambo
hili limepelekea vikundi hivyo kukosa stakabadhi ya malipo ingawa hutumiwa sana na
Wizara ya Kilimo na Maliasili kupitia Idara ya Misitu.
Katika kujiridhisha kama ni kweli vikundi hivyo vilitafutwa na Idara ya Misitu, Kamati
iliomba kupatiwa barua ya maombi iliyotumwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kwenda
kwa Idara ya Misitu, hata hivyo, Kamati ilishindwa kupata ushahidi wa suala hilo na
kuelezwa kuwa mawasiliano hayo yalifanywa kwa njia ya mdomo.
Sambamba na hilo, Kamati imebaini kuwa mikataba iliyofungwa baina ya vikundi
vilivyopanda miti na Wizara hii imewekwa saini na Msaidizi Mhasibu badala ya Mkuu wa
Taasisi jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
89
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kufuata sheria za manunuzi katika matumizi ya fedha
zinazoidhinishwa kwake.
Hoja Namba 27.2.2 Magari machakavu ambayo hayafanyi kazi kwa muda mrefu
Ukaguzi umebaini kuwepo kwa magari 10 yanayomilikiwa na Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano Pemba, ambayo ni chakavu na hayafanyi kazi kwa muda mrefu. Magari hayo
yanahitaji matengenezo kwani kila yakiendelea kukaa bila ya kutengenezwa yanaendelea
kuharibika na kuna uwezekano wa kufa kabisa. Kuendelea kukaa kwa magari hayo bila ya
kuchukuliwa hatua muafaka, kunaweza kusababisha hasara kwa Serikali. Ukaguzi unashauri
hatua muafaka zichukuliwe kuhusiana na magari hayo.
Majibu ya Wizara
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilikiri kuwa wakati wa ukaguzi yalikuwepo magari
machakavu Afisini hapo. Hata hivyo, magari hayo pamoja na vifaa vyengine vichakavu
vimeshauzwa na Idara ya Uhakiki Mali. Ingawa magari hayo na vifaa hivyo vilikuwa mali za
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Wizara hii haijui gharama halisi ya mali hizo kwa
kuwa zoezi la uuzwaji wa mali hizo lilisimamiwa na Idara ya Uhakiki Mali.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati iliridhika na majibu ya Wizara hii kwa hoja ya pili, na kwa upande wa hoja ya
kwanza Kamati ya PAC haikuridhika na majibu ya Wizara na imeitaka Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ili
kuepusha dhana ovu kwa watendaji wake. Kwa mfano, kuwepo na mawasiliano rasmi ya
maandishi baina ya Taasisi za Serikali na sio kutekeleza majukumu yake kwa njia ya
mdomo.
9.0 MASHIRIKA NA MAMLAKA MBALI MBALI ZA SERIKALI
9.1 BODI YA MAPATO
Hoja Namba 48.1 Taarifa ya Mapato na Matumizi kufuatia ufungaji wa Hesabu za
Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Bodi ilikadiriwa kukusanya Tsh. 7,397,684,066 kwa mwaka 2012/2013 na ulipomalizika
mwaka, ilikusanya Tsh. 7,358,500,788 sawa na asilimia 99.5 ya makadirio. Aidha, Bodi
ilikadiriwa kutumia Tsh. 5,616,214,100 kwa kazi za kawaida, na ilipofika tarehe 30 Juni,
2013, fedha zilizoingizwa na kutumika ni Tsh.6,061,166,430, sawa na asilimia 108 ya
makadirio, ikiwa ni ongezeko la Tsh. 444,952,330, sawa na asilimia 48 ya makadirio.
Majibu ya Bodi
Pamoja na maelezo hayo ya ukaguzi, taarifa sahihi za makadirio ya makusanyo kwa Bodi
yalikuwa Tsh. 162.02 bilioni na makusanyo halisi ni Tsh. 141.71 bilioni sawa na asilimia
87.46 ya makadirio. Aidha, matumizi yalikadiriwa kuwa Tsh. 7.358 bilioni na hali halisi ya
matumizi kwa kazi za kawaida yalikuwa bilioni 5.77 na Tsh. 1.39 bilioni kwa kazi za
maendeleo.
Tatizo kubwa lililipelekea kutofikia malengo ya makusanyo ni kushamiri kwa biashara ya
magendo ya mafuta, kuwepo kwa uwajibikaji mdogo kwa walipa kodi, kukosekana kwa
taaluma maalum kwa wafanyakazi wa Bodi, kukosa ufadhili kwa utekelezaji wa Mpango
Mkuu wa Miaka Mitano na viwango vidogo vya kutozea kodi kwa mfumo wa „package‟ kwa
hoteli kubwa zenye hadhi ya juu (transfer prising).
90
Hata hivyo, Bodi inafanya juhudi za kuzishinda changamoto hizo kwa mikakati mbali mbali
ikiwa ni pamoja na kushirikiana na taasisi na vyombo vyengine kukabiliana na biashara ya
magendo ya mafuta, kuandaa mfumo wa kompyuta utakaosaidia kuhakikisha kuwa wanatoa
risiti wakati wa mauzo na kuimarisha elimu kwa walipa kodi na wananchi kwa ujumla kwa
lengo la kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwapo kuna utaratibu maalum na viegezo maalum vilivyowekwa katika
makisio ya makusanyo ya Bodi na kujiridhisha kuwa, makisio hayo hufanywa tu zaidi kwa
kuzingatia mafanikio yaliyofikiwa mwaka uliopita. Aidha, Kamati imejiridhisha kuwa,
kutokuwepo kwa mfumo wa utoaji wa risiti za electroniki kunachangia upotevu wa mapato,
na wakati sasa umefika kwa Serikali kuanzisha mfumo huo na zaidi mahotelini, ambako kwa
kushindwa kuwa na mfumo huo, kuna upotevu mkubwa wa mapato yatokanayo na kodi.
Kamati pia imeelezwa kuwa, kuna tatizo kubwa la kuwepo taasisi mbili (ZRB na TRA)
Zanzibar zinazokusanya kodi mbili ambazo zinategemeana katika kupata taarifa sahihi za
makusanyo ya aina moja. Ni vyema Serikali ikaliangalia hili kwa umakini na kulitafutia
ufumbuzi.
Mapendekezo ya Kamati
Serikali iagalie upya vigezo vya kufanya makisio ya makusanyo ili viwe wazi na kufahamika
kwa taasisi zake zote. Aidha, Kamati inaishauri Bodi kusimamia ipasavyo mikakati ya
kukusanya kodi ili izidi kuongeza mapato.
Uwezo wa Bodi kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa kujiendesha
Bodi ya Mapato kwa mwaka 2012/2013 ilikuwa na mali za mpito za thamani ya Tsh.
711,733,044.73, huku dhima za mpito zikiwa na thamani ya Tsh. 35,619,191, huku hali
halisi ya mali za mpito zikiwa na thamani ya Tsh. 676,113,853.73 sawa na 20:1, hali
iliyotokana na kuwepo kwa wadaiwa wengi kwa hivyo ni faraja kwa Bodi. Mapato ya
Mamlaka yalikuwa ni Tsh. 7,358,500,788.15 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
6,061,166,429.72 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa ya Tsh. 1,297,334,358.43.
Majibu ya Bodi
Taarifa ni kweli na Bodi inaendelea na mikakati yake ya kuongeza mapato ya makusanyo na
kupunguza gharama za matumizi, ili iendelee kupata faida na kutekeleza kwa ufanisi
majukumu yake.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaipongeza Bodi kwa juhudi inazozichukua na kuitaka kukusanya mapato zaidi.
9.2 MAMLAKA YA UKUZAJI VITEGA UCHUMI ZANZIBAR (ZIPA)
Hoja Namba 47.1 Taarifa ya Mapato na Matumizi kufuatia ufungaji wa Hesabu za
Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Mamlaka imekadiriwa kukusanya Tsh. 371,762,500 kwa mwaka 2012/2013 na ulipomalizika
mwaka, Mamlaka iliweza kukusanya Tsh. 397,837,675 sawa na asilimia 107 ya makadirio,
kukiwa na ongezeko la Tsh. 26,075,175, sawa na asilimia 7 ya makadirio. Aidha, Mamlaka
ilikadiriwa kutumia Tsh. 776,174,312 kwa kazi za kawaida, na ilipofika tarehe 30 Juni, 2013,
fedha zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 452,134,513, sawa na asilimia 58 ya makadirio,
ikiwa ni pungufu ya Tsh.324,039,799, sawa na asilimia 42 ya makadirio.
91
Majibu ya Mamlaka
Makadirio ya Mamlaka yaliangalia zaidi vyanzo vya ndani na fedha za ruzuku kutoka
Serikalini. Ni kweli mwaka huu walikuwa na mafanikio ya makusanyo, ingawaje mara
nyingi huanguka kwa makusanyo kutokana na kuanguka kwa shughuli za biashara kwa
wawekezaji.
Aidha, mwaka huu waliweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutokana na kupata taarifa
ya Kampuni ya Zalu kuuza hisa zake kwa kampuni nyengine, ingawaje suala kama hili
halitokezei mara kwa mara.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji iwapo Mamlaka inafahamu suala la kuahamishwa kwa hisa za Kampuni ya
Zanteli, kufuatia pia kuelezwa kwamba, Kampuni zinazofika katika Mamlaka kufuatia kuuza
hisa, ni ile ambayo miradi yake imeidhinishwa na Mamlaka.
Aidha, Mamlaka imeeleza kutojua chochote kuhusiana na Kampuni ya Zanteli. Vile vile,
Mamlaka wameeleza kuwa, wajibu wa Mamlaka ni kurahishisha kwa Kampuni yoyote
inayotaka kuekeza Zanzibar, kuikabidhi kampuni hiyo kwa taasisi ya Serikali inayosimamia
uwekezaji wa kampuni hiyo na kuhakikisha miradi inaendelea na kutoa msaada kutoka hali
moja ya uekezaji kwenda katika hali bora zaidi ya kampuni hiyo.
Kuhusiana na matumizi ya kawaida kuwa chini ya makadirio, Kamati ilihoji athari
zilizopatikana kutokana na kutotimia kwa makadirio na kuelezwa athari hizo ni pamoja na
kushindwa kufanya utafiti, kushindwa kufanya makongamano ya kutoa elimu mbali mbali
ikiwa ni pamoja na kushindwa kurusha vipindi vya redio, kusita kwa ujenzi wa Afisi ya
Mamlaka Pemba, kushindwa kufanya matengenezo ya mitaro na kushindwa kutengeneza
maghala.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuwa wazi katika taarifa zake na ubia wa Kampuni ya Zanteli, ili
taasisi zake nyengine zinazohusika na uwekezaji ziwe na taarifa za kutosha na za uhakika ili
kukuza uekezaji nchini. Aidha, Kamati inaitaka Serikali kuhakikisha inatoa fedha kamili kwa
Mamlaka, ili iweze kutekeleza miradi na shughuli zake ilizojipangia kwa mwaka.
Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa
kujiendesha
Kwa mwaka 2012/2013, Mamlaka ilikuwa na mali za mpito za thamani ya Tsh.
16,073,005,717.54, huku dhima za mpito zikiwa na thamani ya Tsh. 445,997,822.13, huku
hali halisi ya mali za mpito zikiwa na thamani ya Tsh. 15,627,007,895.41 sawa na 36.04:1,
hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa pamoja na salio la benki. Mapato ya
Mamlaka yalikuwa ni Tsh. 1,578,185,942.42 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
2,191,039,830.69 na hivyo kuendeshwa kwa hasara kwa Tsh. 612,853,888.27.
Majibu ya Mamlaka
Mamlaka ni Wakala wa Serikali na sio Shirika la biashara kwamba lingefanya faida. Aidha,
tokea kuanzishwa kwa Mamlaka, Mfuko wa Mamlaka haujawahi angalau kupata fedha za
kutosha za kufanyia shughuli zake za msingi kama zilivyoelezwa katika Sheria, hivyo
haijapata kuwa na ziada. Aidha, ni sahihi kuwa Mamlaka haikufikia malengo yake kwa
mujibu wa mipango yake na makadirio ya mapato.
92
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji suala zima la kuimarika kwa mipango ya maendeleo kama inavyotarajiwa
kusimamiwa na Mamlaka, na kuelezwa tatizo kubwa la nchi yetu ni kutokuwepo kwa
muendelezo wa mipango ya maendeleo (sustainability of development policy). Mfano
unatolewa kwa Waziri wa Fedha anapofuta msamaha wa kodi Fulani, bila ya kuwashirikisha
Mamlaka kunaleta tatizo na kurudisha nyuma maendeleo ya Mamlaka na Taifa.
Aidha, Kamati imesikitishwa sana na taarifa ya Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya
Mamlaka kwa baadhi ya vifungu vyake, huku viongozi wa Mamlaka hiyo wakiwa hawana
taarifa wala hawakushirikishwa katika mabadiliko hayo. Aidha, mfano unatolewa wa
kufanya marekebisho ya Sheria ya Fedha (Appropriation Bill) bila ya kufanya marekebisho
ya Sheria ya Uekezaji inayosimamiwa na Mamlaka, ni kufanya mambo kinyume nyume.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuwa na mipango endelevu ya maendeleo na kuachana na sera ya
kila kiongozi kuja na mipango yake ya maendeleo. Aidha, Kamati inaitaka Serikali
kuzishirikisha taasisi zinazohusika na usimamizi wa Sheria na sio kuzifanyia marekebisho
Sheria bila ya kuwashirikisha watendaji wakuu wa taasisi hizo.
9.3 MAMLAKA YA MAJI (ZAWA)
Hoja Namba 45.1 Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Mamlaka ya Maji ilikuwa na mali za mpito zenye thamani ya Tsh. 6,920,333,649.63 na
dhima za mpito za 1,644,718,751.84 kwa mwaka 2012/2013 na kufanya uwezo halisi wa
mali za mpito kuwa Tsh. 5,275,614,897.79 kwa uwezo wa kulipa dhima 4.2:1,
kulikochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wengi wa Malmaka na ikishauriwa kuongeza
kukusanya mapato kutoka kwa wadaiwa.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa ni Tsh. 11,282,646,495.08 na
matumizi yake yalikuwa Tsh. 12,772,002,960.03 na hivyo kuendeshwa kwa hasara ya Tsh.
1,489,356,464.95, ingawaje imepungua ukilinganisha na mwaka 2011/2012, iliyokuwa Tsh.
4,859,463,154. Aidha, juhudi za makusudi zinahitajika za kuongeza ukusanyaji wa mapato
na kupunguza gharama za uendeshaji.
Majibu ya Mamlaka
Mamlaka inakubaliana na ushauri wa kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato kutoka
kwa wadaiwa na miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kutoa elimu kwa wananchi kupitia
vyombo vya habari na kufanya mikutano na wadau. Mamlaka pia imeanzisha zoezi maalum
la siku ya Alhamis kutoa huduma za maji ikiwa ni pamoja na kuwakatia huduma wale wote
wenye madeni zaidi ya miezi mitatu.
Mamlaka pia inaendelea na zoezi la uingizwaji wa taarifa za wateja katika mfumo wa kumbu
kumbu za Mamlaka (SBM), ili kuweza kuwajua wateja wepi wanaopata huduma ya maji na
wasiopata. Mamlaka inaendelea kuwafungia mita hususan katika maeneo ya utalii, ili
kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji uwezo wa Mamlaka katika uhalisia wake na kuelezwa kuwa, bado Mamlaka
inasua sua kutokana na kuelemewa na madeni ambapo hivi sasa ina deni lifikalo Bilioni 1.8,
na kuna matarajio makubwa ya kuongezeka kwa deni hilo. Kamati pia imejiridhisha kuwepo
93
kwa deni kubwa linalodaiwa na Shirika la Umeme dhidi ya Mamlaka na hali inayoikabili
Mamlaka kushindwa kuviendeleza visima na miradi yake mbali mbali ya uchimbaji wa
visima, kutokana na ukubwa wa gharama za umeme.
Aidha, Kamati imeelezwa kuwa Mamlaka hivi sasa ina visima 250 Unguja na Pemba,
ambapo ufanisi wake haupatikani kutokana na gharama za umeme. Aidha, deni la visima
hivyo inafikia milioni 400 kwa mwezi na kwa kujumuisha visima vipya vilivyochimbwa
lakini vimeshindikana kuendeshwa kwa kukosekana kwa uwezo wa kulipia huduma ya
umeme, gharama zake kwa mwezi zinatarajiwa kufikia milioni 500 hadi 600.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka iendelee na juhudi za kukusanya mapato na kupunguza gharama
za uendeshaji kwa kuiwezesha kujiendesha kwa faida.
9.4 MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE
Taarifa ya Mapato na Matumizi kufuatia ufungaji wa Hesabu za Mwisho wa Mwaka
2012/2013
Makusanyo ya Mamlaka kwa mwaka 2012/2013, yalikadiriwa kufikia 3,526,205,437, lakini
uhalisia wa makusanyo hayo ulikuwa Tsh. 3,431,996,398 sawa na asilimia 97 ya makadirio,
ikiwa kuna upungufu wa Tsh. 94,658,288 sawa na asilimia 3 ya makadirio.
Aidha, kwa ajili ya kuendesha shughuli za kawaida, Mamlaka ilikadiriwa kutumia Tsh.
3,526,654,686 na ulipotimia mwaka wa fedha, Mamlaka ilikwishatumia Tsh. 3,355,307,887,
sawa na asilimia 95 ya makadirio, ikiwa ni pungufu ya Tsh. 3,183,961,088 sawa na asilimia
5 ya makadirio.
Majibu ya Mamlaka
Mapato ya Mamlaka yanaathirika sana na huduma wanazozitoa ambazo zinastahiki kubebwa
na Serikali. Kwa mfano, Mamlaka inalipa 20,000,000/- kila mwezi kuwalipa KVZ kwa kutoa
huduma ya ulinzi ili kuwazuia watu wasichote mchanga na ulinzi mwengine unaohusika,
wakati jukumu hilo lingebebwa na Serikali. Aidha, Mamlaka inategemea mapato pekee ya
„airport service charge‟ ambayo ni wastani wa bilioni 12 kwa mwaka na ndio hizo hizo ni
mapato ya Serikali kuu.
Uzoefu walionao, „airport service charges‟ inayokusanywa na Bodi ya Mapato ya Tanzania
(TRA), kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Julius K. Nyerere, Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege ya Tanzania inarejeshewa asilimia 70 ya makusanyo hayo. Aidha, kwa
upande wa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, wa nchi ya Uganda na Kenya, Mamlaka za
Viwanja vya ndege hizo hupewa asilimia 100 ya makusanyo, kinyume na inavyofanyika
Zanzibar.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kuwa, Serikali bado haijawa tayari kuiacha kodi hii ya huduma ya
uwanja wa ndege moja kwa moja kwa Mamlaka, kutokana na Serikali yenyewe kutegemea
sana mapato hayo. Hata hivyo, kama tu Serikali ingeliangalia huduma bora zitakazopatikana
kutokana na kodi hiyo kusimamiwa na Mamlaka na huku faida ya maendeleo yake ikawa
ndio mafanikio ya Serikali, basi uchumi wa nchi ungelikuwa kwa kiwango kikubwa.
94
Mapendekezo ya Kamati
Serikali iiwezeshe Mamlaka katika ukusanyaji wa mapato kwa kuwaongezea kiwango cha
mapato ya kodi ya uwanja wa ndege kwa Mamlaka, ili baada ya miaka miwili ijayo, kodi
hiyo moja kwa moja iwe kwa Mamlaka.
Uwezo wa Mamlaka kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa
kujiendesha
Kwa mwaka wa 2012/2013, Mamlaka ilikuwa na mali za mpito zenye thamani ya Tsh.
1,260,183,373 na dhima za mpito zilikuwa na thamani ya 680,743,469 na kufanya uwezo
halisi wa mali za mpito kuwa Tsh. 579,439,904 kwa uwezo wa kulipa dhima 1.9:1, hali
iliyochangiwa na kuwepo kwa wadaiwa na salio la benki.
Taarifa ya mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa ni Tsh. 3,696,097,369 na
matumizi yalifikia Tsh. 5,764,876,672, hali iliyoifanya Mamlaka kuendeshwa kwa hasara ya
Tsh. 2,068,779,303, hasara ambayo inaweza kupungua iwapo Mamlaka itaongeza juhudi ya
ukusanyaji wa mapato na kupunguza gharama za uedeshaji.
Majibu ya Mamlaka
Mamlaka inatoa huduma kulingana na viwango vinavyotambulika na taasisi za kimataifa.
Kwa ujumla, Mamlaka ina mali za kudumu zenye thamani kubwa ambapo kwa mujibu wa
taratibu za kihasibu zimeoneshwa kama sehemu ya matumizi. Yaani, kwa mwaka huu,
uchakavu wa mali za kudumu ulifikia thamani ya Tsh. 2,650,041,479, ambapo gharama hizo
hazina uhalisia wa fedha bali ni njia ya kuweka kumbu kumbu za kimahesabu. Hivyo, kwa
kuzingatia gharama hizo za uchakavu na hasara iliyooneshwa katika ripoti, ya Tsh.
2,068,779,303, ni sawa kusema kuwa, Mamlaka ina ziada ya Tsh. 536,262,176.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji kwa Mamlaka kutoeleza ufafanuzi huo wakati wa ukaguzi, na hatimae
imekubaliana na Mamlaka kuwa, maelezo halisi ya taarifa hii ni kuonesha uhalisia wa
kimahesabu kwa Mamlaka.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kutoa ufafanuzi wa
kutosha katika ripoti kuhusiana na suala zima la uwezo wa Mashirika kumudu kulipa dhima
zao za muda mfupi na uwezo wa kujiendesha.
Hoja Namba 46.2 Malimbikizo ya Madeni, Tsh. 680,743,469
Fedha hizo zinadaiwa na wafanyabiashara, wafanyakazi pamoja na taasisi mbali mbali kwa
ajili ya utowaji wa huduma tofauti katika Mamlaka, deni ambalo limerithiwa kutoka Idara ya
Anga, ambalo hadi kuanzishwa kwa Mamlaka halijalipwa hadi sasa.
Majibu ya Mamlaka
Kweli madeni hayo ni ya muda mrefu. Aidha, deni la Tsh. 30,000,000 ni la TCAA kwa ajili
ya mafunzo ya wafanyakazi wa Mamlaka kutoka chuo cha Aviation CATC, deni ambalo
litalipwa mwaka wa fedha 2014/2015. Deni la Tsh. 34,018,986 ni la „salary in area‟ na hapo
awali lilikuwa kubwa sana lakini limelipwa na lililobaki litalipwa katika mwaka wa fedha
2014/2015. Aidha, deli lilobakia la Tsh. 467,333,708 ni deni endelevu la Shirika la Umeme
(ZECO), ambalo Mamlaka imelirithi kutoka Idara ya Anga. Deni hilo hadi Disemba 2014
lilikuwa Tsh. 639,643,389.40 ambapo Mamlaka imekubaliana na ZECO kupunguzwa kwa
95
deni hilo kwa kila mwezi na ilipofikia Januari 2015, Mamlaka ilikwishalipunguza na kufikia
Tsh. 204,767,433.54.
Uchunguzi wa Kamati
Suala la madeni linahitaji kuekewa mikakati madhubuti ukizingatia kuwa, hakuna bajeti
inayowekwa kwa ulipaji huo, lakini ni jukumu la kila taasisi yenye madeni kuyalipa madeni
hayo, isipokuwa kwa yale madeni ambayo yangestahiki kubebwa na Wizara ya Fedha.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Mamlaka kukamilisha malipo ya deni lililobakia.
9.5 CHUO CHA UTAWALA WA UMMA
Hoja Namba 50.1 Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha.
Chuo cha Utawala wa Umma kilikuwa na mali za mpito zenye thamani ya Tsh.
968,455,883.58 kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 na hakukuwa na dhima za mpito, hali
iliyopelekea uwezo halisi ya mali za mpito kuwa na thamani ya Tsh.968,455,883.58 na
hivyo, mali za mpito kuwa kubwa kutokana na kutokuwepo kwa dhima za mpito.
Taarifa hizi pia zinaonesha mapato ya Chuo kuwa Tsh. 2,233,792,500 na matumizi yake
yakawa ni Tsh. 1,577,708,549.62, hali inayoonesha kuwa Chuo kinaendeshwa kwa bakaa ya
Tsh. 656,083,950.38, huku Chuo kikishauriwa kuongeza juhudi ya makusanyo na usimamizi
wa vyanzo vyake vya mapato.
Majibu ya Chuo
Suala la madeni yanayoikabili Chuo yanasababishwa zaidi na wanafunzi wanaochelewa
kulipia gharama za masomo kwa wakati unaotakiwa. Kwa kuzingatia sera ya Chuo na
Serikali ya kuwasaidia wanafunzi wanyonge kuweza kupata elimu, Chuo kinawasaidia
wanafunzi kwa kuhakikisha wanalipa madeni yao bila ya kuwazuilia kufanya mitihani.
Inapofikia mwanafunzi amelipa kidogo, Chuo kinamruhusu kufanya mitihani ila huzuia
matokeo yake na akishindwa kulipa, basi hatua ya mwisho ni kumzuia kupata cheti chake
mpaka amalize kulipa fedha zote.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji kuhusiana na nafasi ya Chuo kumueleza Mkaguzi wakati wa ukaguzi
kuhusiana na hali halisi inayowakabili na kuelezwa kuwa, Mkaguzi kwa kawaida huangalia
Ankara za malipo (invoice) na kuzihesabu kama deni.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuongeza makusanyo ya mapato kwa kudhibiti ipasavyo uvujaji
wake.
Hoja Namba 50.2 Udhaifu katika ukusanyaji wa mapato
Chuo kilianzisha mfumo wa malipo ya ada za wanafunzi kulipiwa benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) kupitia akaunti namba 021103000578 kuanzia tarehe 1/7/2012, ambapo
baada ya malipo mwanafunzi hupatiwa stakabadhi ya benki (pay in slip) na kuikabidhi
Chuoni kwa kupewa risiti.
Hata hivyo, ukaguzi umebaini kuwa baadhi ya wanafunzi walikuwa wanalipa bila ya kufuata
utaratibu huo kwa kumlipa Mshika Fedha wa Chuo, hali iliyokipelekea Chuo kukosa
96
mapato. Aidha, ukaguzi umeshindwa kupata kiasi kamili cha fedha zilizopotea kutokana na
kukosa kumbukumbu za ukusanyaji wa mapato hayo, ambapo baadhi ya stakabadhi ziliweza
kupatikana na kujulikana fedha zilizokusanywa, lakini baadhi yao hazikuweza kupatikana na
kupelekea ukaguzi kushindwa kujua kiasi halisi cha fedha zilizokusanywa. Aidha,
kushindwa kwa ukaguzi kuendelea kulifuatilia suala hili, kunatokana na iliyokuwa Wizara ya
Nchi(OR) Utumishi wa Umma na Utawala Bora huingilia kati kadhia hiyo na baadhi ya
kumbu kumbu za mahesabu kuchukuliwa na Wizara husika ambapo ni kinyume na taratibu
za sheria ya fedha, kifungu namba 67(1) ya mwaka 2005.
Majibu ya Chuo
Wizara haijaingilia kati suala hilo ambalo ni Uongozi wa Chuo ulikuwa wa mwanzo
kugundua udhaifu huo na ililifikisha suala hilo kwa Bodi ya Chuo na kushauriwa
kuliwasilisha kwa Wizara kwa ajili ya ushauri na hatua zinazofaa. Chuo kiligundua udhaifu
huo baada ya kuwataka wanafunzi kuleta uthibitisho wa malipo, ambapo walileta risiti
zisizokubaliwa, ambazo kwa kiasi kikubwa zimefanana sana na risiti za Serikali wanazotoa
Chuo kutoka Wizara ya Fedha.
Baada ya kugundua, Chuo kilimpa fursa ya kujieleza Mshika Fedha huyo, Ndg. Hafidh Ali
Hassan kwa njia ya mazungumzo na maandishi na baada ya kujiridhisha kwamba, Ndg.
Hafidh amehusika, Chuo kilimpa likizo ya lazima la miezi mitatu kwa kumlipa nusu
mshahara na kuendelea na uchunguzi, kupitia barua ya tarehe 8/4/2013 yenye kumbu kumbu
namba IPA/OPF/H.18131/C/.
Chuo baadae kilitoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mhasibu Mkuu wa
Serikali tarehe 9/4/2013 kuhusiana na kadhia hiyo na kutokana na ushauri wa Baraza la
Chuo, hatua iliyofuata ni kumuagiza Mhusika kuzilipa fedha zote alizopokea kwa wanafunzi
kinyume na taratibu na Chuo kiliziwasilisha benki. Aidha, Mhusika alitekeleza agizo hilo
hadi kufikia Januari 2015 akiwa ameshalipa Tsh. 55,095,000/- sawa na asilimia 89% ya
fedha alizopokea (ambazo ni Tsh. 61,395,000/-) na fedha zilizobaki aliendelea kukatwa
katika mshahara wake kwa kiwango cha Tsh. 79,000/- kila mwezi.
Chuo kilitekeleza ushauri wa Baraza la Chuo na Wizara ya kwa kumrejesha Mhusika
Utumishi na kwa kipindi hiki, anaendelea na kazi katika kitengo cha Kalamazoo. Sambamba
na hilo, kadhia ya Ndg. Hafidh inashughulikiwa na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na
Uhujumu wa Uchumi Zanzibar.
Kuhusiana na hatua za kuimarisha Kitengo cha Fedha, Chuo kimeimarisha wafanyakazi wa
Kitengo hicho, wakiwemo Wahasibu watatu na Washika Fedha wawili, ambapo awali
Kitengo kilikuwa na Mhasibu mmoja pekee na Washika Fedha wawili. Vile vile Kitengo
kina kompyuta tatu na zote zimeunganishwa na mitandao inayoweza kugundua uwepo wa
stakabadhi bandia na udanganyifu.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na hatua ilizochukua Chuo, suala hili linaonekana lina mtandao mkubwa ambao
unapaswa kushughulikiwa ipasavyo na Serikali. Aidha, kulionekana kuwepo kwa udhaifu wa
udhibiti wa ndani, na Chuo kinatakiwa kuchukua hatua madhubuti zaidi katika kudhibiti
udanganyifu utakaoweza kutokea.
97
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuchukua hatua za kudhibiti uvujaji wa fedha kwa kupitia risiti feki
zinazotumiwa na baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu. Aidha, hatua madhubuti za
kisheria ziendelee kuchukuliwa kwa Mhusika, ili iwe funzo wa watu wengine.
Hoja Namba 50.3 Madeni ya wanafunzi, Tsh. 611,743,863
Fedha hizo deni la wanafunzi 1555 wa fani mbali mbali katika Chuo ambazo hazijalipwa na
wanafunzi hao. Hali hii inatokana na Uongozi wa Chuo kutokuwa na usimamizi madhubuti
wa ukusanyaji wa mapato yanayotkna na huduma mbali mbali zinazotolewa na Chuo.
Majibu ya Chuo
Ni kweli Chuo kina madeni hayo, ingawaje sasa kimechukua hatua madhubuti kuhakikisha
wanafunzi hawezi kumaliza masomo na kupewa cheti, bila ya kulipa deni lake lote.
Uchunguzi wa Kamati
Vyuo vingi vya Serikali vinakabiliwa na tatizo la malumbukizo ya madeni kutokana na vyuo
hivyo kujikita zaidi katika kutoa huduma na kuwasaidia wananchi wengi wenye kipato
kidogo. Pamoja na hali hii kuonekana kuwasaidia wananchi wengi, Serikali na Uongozi wa
vyuo husika, bado vina jukumu la kusimamia ukusanyaji wa malipo, ili vyuo hivyo viweze
kujiendesha.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuhakikisha kuwa madeni hayo yanalipwa na yanapungua kila
mwaka na hatimae yamalizike kabisa.
9.6 CHUO CHA UANDISHI WA HABARI
Hoja Namba 51.1 Matokeo ya Hesabu za Mwisho wa Mwaka.
Taarifa za mapato na matumizi
Tsh. 80,800,000 zilikadiriwa kukusanywa na Chuo cha Uandishi wa Habari kwa mwaka
2012/2013, ambapo hali halisi ya makusanyo hayo yalikuwa Tsh. 105,710,000, sawa na
asilimia 131 ya makadirio ya makusanyo. Kwa upande wa matumizi ya kazi za kawaida,
Chuo kilikadiriwa kutumia Tsh. 305,000,000 na kuingiziwa Tsh. 216,000,000, sawa na
asilimia 71 ya makadio.
Majibu ya Chuo
Vyanzo vya mapato ni vile vile, lakini nyongeza ya makusanyo imetokana na ongezeko la
wanafunzi kwa mwaka 2012/2013. Hata hivyo, Chuo kinapanga kuongeza wanafunzi na
kufikia 600, lakini wanakabiliwa na tatizo la sehemu ya kuwaweka. Kuhusiana na gharama
za matumizi, Chuo kinatumia zaidi fedha zake kwa mitihani na gharama za Bodi, ambapo
kitendo cha kuwa na idadi kubwa ya walimu wa muda (part time), kinawalazimu kutumia
fedha nyingi, ili waweze kutoa elimu Chuoni hapo.
Kuhusiana na hasara ya Chuo, hali hiyo inatokana na utaratibu wa ufungaji wa hesabu
ambao unaelekeza kuzingatia kuingiza uchakavu wa thamani ya mali zilizopo katika taasisi
husika yaani (Depraciation) ambazo kwa kawaida huwa sio fedha taslim katika matumizi
(Non cash expenses). Kwa msingi huo, Chuo hakikutumia kwa hasara kwa mujibu wa
makusanyo na matumizi, ila hasara kama hiyo katika mahesabu huonekana kadri Chuo
kinapokuwa kinaongeza mali za mpito mwaka hadi mwaka kwa kuwa thamani za aina hiyo
hushuka.
98
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imeridhishwa na juhudi za Chuo kuongeza idadi ya wanafunzi, lakini mabadiliko
hayo yaende sambamba na majengo ya kuwawezesha wanafunzi hao kusoma bila ya
usumbufu. Aidha, Kamati imejiridhisha kwamba, jengo walilonalo Chuo hivi sasa
wanatakiwa kuhama na jengo watakalohamia liliopo Kilimani Bar, ni dogo wala halitakidhi
mahitaji halisi ya Chuo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Chuo kutafuta mkopo Benki ya Kiislamu ya PBZ, kwa ajili ya kupata
mkopo utakaowawezesha kujenga majengo ya kisasa katika kiwanja cha Chuo kilichopo
Tunguu.
Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa kujiendesha.
Kwa mwaka 2012/2013, Chuo kilikuwa na mali za mpito za 26,972,422.50, bila ya kuwa na
dhima za mpito, hali iliyopelekea hali halisi ya mali za mpito kuwa sawa na mali zenyewe za
mpito, kutokana na kutokuwepo kwa madeni.
Mapato ya Chuo yalifikia Tsh. 358,335,000 na matumizi yake yakawa Tsh. 385,555,266, na
kukifanya Chuo kuendeshwa kwa upungufu wa Tsh. 27,220,266 na kumfanya Mkaguzi
ashauri kuongezwa kwa makusanyo na kuchukua hatua za kupunguza gharama za
uendeshaji.
Majibu ya Chuo
Pamoja na maelezo ya ripoti ya Mdhibiti, ni vyema ikafahamika kuwa, Chuo ni Taasisi ya
Serikali kinachotoa huduma na hivyo, hakina dhamira ya kupata faida. Hata hivyo, gharama
za matumizi kuzidi mapato, kunatokana na kushuka kwa thamani ya vifaa mwaka hadi
mwaka.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na ukweli kwamba, Chuo kama Taasisi ya Serikali huwa haifanyi faida, kuanzishwa
kwake kunatakiwa kukiwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi, jambo ambalo
halitaweza kupatikana iwapo uwezo wa Chuo utapungua mwaka hadi mwaka.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji zisizo za
lazima, ili kiweze kujiendesha na kutoa huduma bora iliyokusudiwa.
9.7 SHIRIKA LA BANDARI
Hoja Namba 38.1 Uwezo wa Bodi kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
Uwezo wa kujiendesha
Mali za mpito za thamani ya Tsh. 11,400,359,862.80 na dhima za mpito za thamani ya Tsh.
644,309,782.86 hufanya hali halisi ya mali za mpito kwa Shirika kuwa Tsh.
10,756,050,079.94 kwa mwaka 2012/2013, ambayo ni sawa na uwezo wa ration ya 18:1.
Mapato ya Shirika yalikuwa Tsh. 18,825,503,482.22 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
16,454,104,373.42 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 2,371,399,108.8, hali hii
itaimarika, iwapo Shirika litasimamia vyanzo vyake vya mapato na kupunguza gharama za
uendeshaji.
99
Majibu ya Shirika
Jumla ya Tsh. 1,140,420,886 zilikadiriwa kukusanywa kwa mwaka 2012/2013, lakini fedha
halisi zilizokusanywa zilikuwa Tsh. 606,747,899.72 sawa na asilimia 53.20 ya makadirio.
Sababu kubwa iliyopelekea kutofikia lengo lililokusudiwa ni kwa Shirika kuandaa makadirio
makubwa kuliko hali halisi ilivyokuwa katika mwaka huo na kulitokana na viashiria mbali
mbali ikiwemo matarajio ya biashara kulingana na mwenendo pamoja na mabadiliko ya
thamani za sarafu mbali mbali zikilinganishwa na shilingi ya Kitanzania.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na juhudi za Shirika, Kamati imeendelea kujishuhudia tatizo la madeni ya muda
mrefu yanayoikabili Shirika, ambapo Kamati ilielezwa kuwa, hatua ambazo sasa zimefikiwa
na Shirika ni kushughulikiwa suala hili na Afisi ya Mwanasheria Mkuu kwa lengo la
kutafutwa taratibu za kutumika ili suala hilo liwasilishwe Baraza la Wawakilishi kwa hatua
za kufutwa.
Kuhusiana na vyanzo vya mapato vya Shirika, Kamati imehoji sababu zinanazokwamisha
kujengwa bandari mpya ya Mpiga Duri, kutaendelea kuzorotesha makusanyo ya Shirika na
wakati umefika kwa Serikali kutoa kauli ya kuanza kwa ujenzi wa bandari hiyo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kuharakisha taratibu za kuanza ujenzi wa bandari mpya ya Mpiga
Duri, ili kulifanya Shirika liongeze juhudi za makusanyo ya mapato na kuwa na uwezo
kamili wa kujiendesha. Kuhusiana na madeni ya muda mrefu ya Shirika, Kamati inaendelea
kuishangaa Serikali kwa kuchukua muda mrefu bila ya madeni hayo kuwasilishwa Barazani
kwa hatua za kufutwa, ikizingatiwa kuwa, Kamati ilifanya jihudi kubwa miaka iliyopita
kuhusiana na madeni ya namna kama hii, lakini bado Serikali haijafikia muafaka wa ufutwaji
wa madeni hayo. Inapendekezwa hatua ziharakishwe ili madeni yasiyolipika yafutwe
kisheria.
9.8 SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA
Hoja Namba 36.1 Uwezo wa Bodi kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
Uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2012/2013, Shirika ilikuwa na mali za mpito za 151,850,572.7 na dhima za
mpito za 362,603,018.32 na kulifanya Shirika kuwa na hali halisi ya mali za mpito kwa
upungufu wa Tsh. 210,752,445.62 kwa ratio ya 0.42:1, hali iliyosababishwa na kuwepo kwa
deni la benki na madeni ya taasisi nyengine.
Mapato ya Shirika yalikuwa Tsh. 5,607,945,958.83 kwa mwaka 2012/2013 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 4,805,425,292.36 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh.
802,520,666.47 ambayo imepungua kwa Tsh. 1,719,853.53 sawa na asilimia 0.2 kwa
mwaka. Hali hii itaimarika, iwapo Shirika litasimamia vyanzo vyake vya mapato na
kupunguza gharama za uendeshaji.
Majibu ya Shirika
Sababu kubwa ya kupungua kwa faida na kulifanya Shirika kujiendesha kunatokana na
uchakavu wa meli za Shirika. Kwa mfano Shirika lilizipeleka meli hizo chelezoni, hali
iliyolifanya Shirika kuathiriwa sana kiutendaji kwa sababu meli hizo zinapokuwepo
chelezoni, Shirika huwa halipati mapato yoyote ya kodi na ipomaliza kufanyiwa
matengenezo, Shirika hulazimika kutafuta mkodishwaji mwengine kwa ajili ya kuendelea
kujipatia mapato. Kwa ujumla, tatizo hili halitamaliza iwapo Shirika halitapata meli mpya,
kwa sababu meli walizonazo sasa tayari muda wake wa kufanya kazi umeshamaliza. Kwa
100
mfano, meli hizi zina umri wa miaka 34, wakati umri halisi ulitakiwa usizidi miaka 20
mpaka 25.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji ufuatiliaji wa meli mpya ya Serikali na kwa nini Shirika limetumia mapato
yake kwa kuwasafirisha Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano wakati tayari bajeti ya ununuzi huo tayari imeshakatwa kutoka kwa Wizara na
Taasisi zote za Serikali.
Kamati pia imehoji ununuzi wa majereta mawili ambayo yameshatumika (second hand)
kununuliwa Singapore kwa USD 158,640, kwa mnasaba wa matumizi ya Shirika kama
umefuata taratibu za kisheria na kujiridhisha kwamba, ununuzi huo haukufuata taratibu za
kisheria kwa kukosekana Bodi ya Zabuni inayotakiwa kuundwa kwa mujibu wa Sheria,
ingawa kulifanyika vikao, kwa mfano, tarehe 7/8/2012, lakini kikao hicho hakina sifa ya
kuwa Bodi ya Zabuni.
Aidha, Bodi ya Wakurugenzi imechukua jukumu la kuidhinisha manunuzi ya majenereta
hayo, ambapo kazi hiyo inatakiwa kufanywa na Bodi ya Zabuni. Pia, hakukuwa na Kamati
yoyote ya tathmini iliyohusika na ununuzi wa majereta hayo, kinyume na taratibu za
kisheria.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inalitaka Shirika kuhakikisha matumizi yake yanakwenda sambamba na Sheria na
kufuata ipasavyo ushauri ya Mkaguzi wa kudhibiti matumizi yake na kuongeza makusanyo.
9.9 SHIRIKA LA UMEME (ZECO)
Kwa mwaka 2012/2013, Shirika ilikuwa na mali za mpito za 32,674,896,553 na dhima za
mpito za 45,641,826,646 na kulifanya Shirika kuwa na hali halisi ya mali za mpito kwa
upungufu wa Tsh. 12,966,930,093 kwa ratio ya 0.72:1, hali iliyosababishwa na kuwepo kwa
deni la benki na madeni ya taasisi nyengine.
Mapato ya Shirika yalikuwa Tsh. 15,965,004,949 kwa mwaka 2012/2013 na matumizi yake
yalikuwa Tsh. 18,218,538,557 na hivyo kuendeshwa kwa hasara ya Tsh. 2,253,533,608. Hali
hii inayoonesha haja kubwa ya Shirika kufanya juhudi za kupunguza gharama za uendeshaji
na kufuatilia wadaiwa mbali mbali wa Shirika ikiwezo taasisi za Serikali pamoja na watu
binafsi.
Hoja Namba 31.2 Wadaiwa ambao hawakuingizwa katika hesabu za mwaka (Financial
Statement), Tsh. 39,971,226
Ukaguzi umebaini Shirika limeshindwa kuingiza madeni ya wateja wanaodaiwa ambao
wamepata huduma za umeme katika hesabu ya mwaka ulioishia Juni, 2013 zilizowasilishwa
kwa ajili ya ukaguzi. Aidha orodha hiyo inaonesha idadi ya wateja 64 hawajaingizwa katika
hesabu ya mwaka.
Hoja Namba 31.3 Malimbikizo ya madeni, Tsh. 13,687,263,487.83
Fedha hizo zinadaiwa na Shirika kwa taasisi mbali mbali za Serikali. Ukaguzi umebaini
kuwa, madeni hayo ni ya muda mrefu na hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa juu ya
taasisi za Serikali za kulipa madeni hayo kwa wakati, hali inayopelekea Shirika kushindwa
kujiendesha kutokana na fedha hizo kubakia katika mikono ya wadaiwa.
101
Uchunguzi wa Kamati
Kamati haikufanya kazi na Shirika hili kwa kuwa tayari ilifanya kazi zinazohusiana na
udhaifu wa Shirika katika mwaka 2012/2013 kufuatia Hoja Binafsi ya Mhe. Hija Hassan
Hija ya kuundwa Kamati Teule ya kufuatilia Shirika hilo kwa rejea zilizotolewa, ambayo
hatimae kazi hiyo ya kufuatilia hoja hizo ilifanyiwa kazi na Kamati na kutoa ripoti yake
Barazani, ambayo hadi leo haijafanyiwa kazi kama ilivyopendekezwa na Kamati.
Hata hivyo, Kamati ilifanya kazi na taasisi zilizotajwa kuhusika na madeni hayo kwa upande
wa Pemba, ambazo zilikuwa Mamlaka ya Maji (ZAWA), Wizara ya Afya, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo na Mahakama Kuu. Katika kufanya kazi na taasisi hizo,
Kamati iliwakutanisha na muwakilishi wa Shirika na kujiridhisha juu ya usahihi wa hoja hii
na taasisi zote ambazo zilikuwa hajizalikamilisha malipo ya madeni hayo, Kamati ilizitaka
zikamilishe madeni.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Serikali kufahamu kuwa, kasoro na udhaifu uliogundulika na Kamati hii
wakati ilipowasilisha ripoti yake ya Uchunguzi Maalum kwa Shirika hili, bado unaendelea
na utaendelea iwapo Serikali haitochukua hatua madhubuti za kutekeleza mapendekezo ya
Kamati hii kuhusiana na Shirika hili.
9.10 SHIRIKA LA BIMA
Shirika la Bima la Zanzibar halikuwa na hoja yoyote katika ripoti nne za Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za mwaka 2011/2012 na 2012/2013. Hata hivyo, kutokana na
mamlaka ya Kamati kama yanavyoelezwa na kifungu cha 118(2)(c) ya kanuni za Baraza la
Wawakilishi, toleo la 2012, Kamati imefanya ziara ya tawi la Shirika la Bima, Dar es
Salaam, Dodoma na Mbeya na ufafanuzi wake ni kama ufuatao:
Shirika la Bima Kanda ya Pwani (Dar es Salaam)
Shirika limefanikiwa kuongeza wigo wa biashara kwa kutanua huduma zake ikiwa ni pamoja
na kuongeza ofisi katika sehemu mbali mbali za Tanzania, ambapo Pemba mwaka 1985,
Kanda ya Pwani (Dar es Salaam) mwaka 2000, Kanda ya Ziwa Mwanza 2003, kanda ya
kaskazini, Arusha 2004, kanda ya nyanda za juu kusini, 2009, kanda ya Dodoma mwaka
2010 na kanda ya kusini Mtwara mwaka 2013.
Shirika pia limefanikiwa kuongeza mapato kupitia ofisi zake mbali mbali ambapo kwa
upande wa kanda ya pwani, Shirika kwa mwaka 2011 ilikusanya Tsh. 4,368,777,692/-,
mwaka 2012 ilikuwa Tsh. 4,032,934,917 na mwaka 2013 iliongezeka na kufikia Tsh.
5,185,146,746/-. Hata hivyo, Shirika linakabiliwa na changamoto nyingi ambapo kwa
upande wa kanda hii, pamoja na changamoto nyengine, Shirika halina ofisi yake mwenyewe
na hutumia kiasi kikubwa cha fedha kulipia kodi za ofisi zote za kanda hii na sehemu
nyengine Tanzania bara, ambapo kodi hizo ni kubwa na huongezeka mwaka hadi mwaka.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka kufahamu sababu zilizopelekea Shirika kutoonekana katika ripoti ya
Mkaguzi kwa miaka takriban miwili sasa na kuelezwa kuwa Shirika linafunga hesabu zake
kila mwisho wa mwaka lakini na Uongozi wa Shirika unashangaa kutokuwemo katika taarifa
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kamati imehoji iwapo Shirika linalipia mgao Serikalini na kuelezwa kuwa, Serikali inadaiwa
zaidi ya 250 milioni na Shirika na Shirika limeshaiandikia Serikali kuomba kufidia mgao
huo kwa kusamehe deni hilo ili Shirika lisilipe gawiyo kwa mwaka 2012/2013.
102
Kamati pia imejiridhisha kuwa, Serikali haikati bima kwa majengo yake, magari na hata
wafanyakazi wake, huku Mashirika pekee yanayokata bima kwa wafanyakazi wao ni Shirika
la Umeme na Shirika la Bandari ya Zanzibar, na hali mbaya zaidi Pemba, ambapo Serikali
haikati bima yoyote hata kwa magari ya Serikali kwa taasisi zake za Pemba, mpaka Shirika
lifanye ukaguzi maalum.
Kamati pia imeridhika na hatua za Shirika kuanzisha Bima inayofuata taratibu za Kiislamu
(Islamic Insuarence) ambapo tayari Shirika limeshalipitisha suala hilo katika Bodi yake ya
Wakurugenzi na sasa limo katika hatua za kufikishwa Bungeni.
Kamati imeshikitishwa na hatua zisizoridhisha za Kamisheni ya Utumishi kuzorotesha
„scheme of service‟ ya Shirika na kupelekea mishahara ya wafanyakazi wa Shirika
kutofanyiwa kazi na kuboreshwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaushauri uongozi wa Shirika kanda ya pwani kuongeza wigo wa kuhifadhi fedha
zao katika Benki ya Watu wa Zanzibar, ili kukuza biashara baina ya taasisi hizi za Serikali.
Aidha, Kamati inaitaka Serikali kukata bima za majengo na vyombo vyake mbali mbali vya
moto, pamoja na wafanyakazi wake.
Serikali isimamie Kamisheni ya Utumishi kushughulikia maslahi ya Shirika, kwani kinyume
chake kutaondosha motisha ya kufanya kazi kwa kujituma na kupunguza mapato ya Shirika.
Shirika la Bima Kanda ya Kati-Dodoma
Kanda ya Kati Dodoma inajumuisha mikoa wa Dodoma na wilaya zake, Tabora na wilaya
zake, Morogoro na wilaya zake, Singida na wilaya zake na baadhi ya maeneo katika mipaka
ya wilaya ya Kiteto. Kanda hii ina wafanyakazi wanne na imeanza biashara mwezi Mei 2011
na imefanikiwa kukusanya Tsh. 116,997,000 mwaka 2011, Tsh. 320,707,000/- mwaka 2012,
Tsh. 355,980,000 mwaka 2012 na Januari hadi Septemba ya mwaka 2014, imeweza
kukusanya Tsh. 324,758,000. Aidha, Kanda hii inashirikiana na Mawakala na Madalali
mbali mbali wanaopatikana Dodoma na maeneo mbali mbali ya mikoa ya jirani.
Pamoja na mafanikio hayo, Ofisi ya Shirika kanda ya Kati inakabiliwa na changamoto
kadhaa ikiwa ni pamoja na ugumu wa kuanzishwa kwa mawakala wapya ili kukuza biashara
kutokana na mji wa Dodoma kutokuwa na watu wengi wenye sifa ya kuruhusiwa na
Kamishna wa Bima kufungua Ofisi ya uwakala wa bima kama matakwa ya Sheria ya bima
yanavyohitaji. Aidha, soko la bima limeingiliwa na makampuni binafsi yasiyofuata kanuni
zilizopo kwa kutoa bima kwa bei ya chini sana kinyume na makubaliano na mikataba ya
mashirika ya bima.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imetaka kujua iwapo kanda hii inafanya juhudi za kutoa huduma kwa taasisi za
Serikali zilizopo Dodoma na kuelezwa kuwa, wamefanya juhudi ya kuonana na viongozi wa
Chuo Kikuu cha Dodoma, ingawaje bado wanahitaji nguvu za Kamati na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kufanikisha hilo.
Pamoja na tatizo la ukosefu wa ofisi, Kamati imeridhishwa na juhudi zinazofanywa na
uongozi wa kanda na kushuhudia majengo tofauti ambayo yanaweza kupatikana kwa
kuuziwa Shirika, iwapo kutakuwa na umakini na juhudi za makusudi za kupatikana ofisi
hiyo ya kudumu.
103
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri kanda hii kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa taasisi mbali mbali za
Serikali zilizopo katika kanda hiyo. Aidha, Kamati inaushauri uongozi wa Shirika pamoja na
Serikali kununua jengo eneo litakaloonekana linafaa mjini Dodoma, kwa ajili ya kupatikana
ofisi ya kudumu ya Shirika.
Shirika la Bima Kanda ya Kusini-Mbeya
Ofisi ya nyanda za juu kusini, ilianzishwa rasmi mwezi July 2009 ikiwa na watendaji watatu
na sasa ina watendaji watano. Eneo hili la nyanda za juu kusini, lina mikoa ya Iringa,
Rvuma, Mbeya, Rukwa, Njombe na Katavi. Hali halisi ya makusanyo ya kanda hii kwa
mwaka 2010 ni Tsh. 723,554,746.50, mwaka 2011 ilikuwa Tsh. 911,398,481, mwaka 2012
iliongezeka kwa kufikia Tsh. 1,078,599,545 na kwa mwaka 2013 ni Tsh. 1,376,923,860.
Makusanyo ya kanda kwa mwezi Januari hadi Disemba 2014 yalikisiwa kuwa Tsh.
1,562,990,000/- na yameongezeka hadi kuwa Tsh. 2,036,107,038/- ikiwa ni ziada ya Tsh.
473,117,038/-. Matumizi kwa mwaka huo yalikisiwa kuwa Tsh 156,379,956/- kwa kazi za
kawaida, na halisi ikawa Tsh. 97,303,115.50 na Ofisi ya kanda imelipa Tsh. 256,654,023.30
kwa kulipia ujira wa mawakala.
Kanda hii ya kusini ni muhimu sana kwa mapato ya Shirika. Kwa mfano mwaka 2014,
Shirika la Bima la Zanzibar lilikusanya bilioni 17.7 ambapo, Kanda hii ilichangia kwa
asilimia 12.
Miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili kanda hii ya kusini ni „incentives‟ za
wafanyakazi. Ukimchukua Meneja wa Tawi na kumlinganisha na Mameneja wa mashirika
mengine binafsi na wafanyakazi wote kwa ujumla, kuna tofauti kubwa ambayo kama Shirika
na Serikali hawatolishughulikia kwa kupandisha maslahi yao, ni wazi kuwa, wafanyakazi
hao wanaweza kuchukuliwa na kuajiriwa na makampuni hayo. Hivyo, ni vyema Kamisheni
ya Utumishi wa Umma ikaharikisha maslahi ya watendaji wa Shirika, ili kuwatia moyo na
kuwawezesha kufanya kazi kwa bidii.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji juhudi za kanda za kuongeza makusanyo baina ya mwaka juzi na mwaka
uliopita na kuelezwa kuwa zinatokana na watendaji binafsi na mawakala wao kwa kufungua
mikataba mipya na kujitangaza kwa takriban wateja wote. Aidha, mabadiliko ya tozo ya
bima (tariff) iliyoanza mwaka jana, imewasaidia sana kuongeza mapato na kufanya juhudi ya
kudhibiti matumizi.
Kuhusiana na Kanda kukosa madalali na kuwa na mawakala pekee, Kamati imeelezwa kuwa
bado Mbeya watu hawajatanua wigo wa udalali wa bima lakini Kanda ina azma ya kuwanao
iwapo watatimiza masharti na vigezo vinavyotakiwa kuwa navyo. Kamati pia imehoji
kuhusiana na bima ya moto kwa wafanyabiashara mbali mbali na kuelezwa kuwa, kutokana
na wateja wengi kuhamia katika mabenki na kwa kuwa wao bado hawajaingia katika
makubaliano na mabenki maalum, kunachangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kupata wateja
wa bima hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaushauri uongozi wa Kanda ya Kusini na Shirika kwa ujumla kuingia mahusiano
na mabenki ikiwa ni pamoja na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ili kutanua wigo wa
kutoa huduma ya bima ya moto kwa wafanyabiashara mbali mbali. Aidha, Kamisheni ya
Utumishi wa Umma ishughulikie „scheme of services‟ ya Shirika la Bima la Zanzibar, kwa
lengo la kufanya marekebisho ya mishahara yao ili kuwajengea motisha wa kufanya kazi
kwa kujituma na kuongeza mapato ya Shirika.
104
9.11 SHIRIKA LA BIASHARA YA MAGARI
Hoja Namba 40.1 Matokeo ya Hesabu za mwisho wa mwaka. Taarifa za mapato na
matumizi
Shirika lilikadiriwa kukusanya Tsh. 673,548,183 kwa mwaka 2012/2013. Aidha, mwisho wa
mwaka ulipokamilika, Shirika lilifanikiwa kukusanya Tsh. 334,572,992, sawa na asilimia 50
ya makadirio, kukiwa na upungufu wa Tsh. 338,975,191 sawa na asilimia 50 ya makadirio.
Vile vile, Shirika lilikadiriwa kutumia Tsh. 603,276,210, lakini fedha haisi zilizoingizwa na
kutumiwa ni Tsh. 315,719,151, sawa na asilimia 61 ya makadirio.
Majibu ya Wizara ya Fedha na Shirika
Taarifa hizo ziko sawa, lakini wanapenda kuijuulisha Kamati kuwa, Shirika hilo sasa
limeshafungwan adhamana ya mali zake zipo katika Idara ya Uhakikimali iliyo chini ya
Wizara ya Fedha. Aidha, Serikali imetekeleza ushauri wa Mkaguzi unaopatikana katika
ripoti ya Ukaugi wa Hesabu ya mwaka huu (2012/2013), ukurasa wa 104.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imyari limeshafungwa na mali zake zinasimamiwa chini ya udhamini wa Wizara ya
Fedha kupitia Idara ya Uhakiki mali na wafanyakazi wake wameshapelekwa katika taasisi
mbali mbali za Serikali, kwa ajili ya kuendelea na utumishi wao.
Mapendekezo ya Kamati
Pamoja na Sheria ya Uekezaji wa Umma, Namba 4 ya mwaka 2002, kumpa Mhe. Rais
uwezo mkubwa wa kuvunja Mashirika ya Umma kwa amri ya kuyavunja, Kamati inaishauri
Serikali kutoa taarifa rasmi Baraza la Wawakilishi na kwa Kamati zinazohusika na Shirika
hilo, ili kuwe na uwazi na ufahamu wa kina juu ya kuvunjwa kwa Mashirika hayo.
9.12 SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI ZANZIBAR
Hoja Namba 32.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Mapato na Matumizi
Shirika lilikadiriwa kukusanya Tsh. 500,000,000 kwa mwaka 2012/2013, lakini
kilichokusanywa halisi ni Tsh. 404,454,233 sawa na asilimia 81 ya makadirio, kukiwa na
upungufu wa Tsh. 95,545,767 sawa na asilimia 19 ya makadirio. Kwa upande wa matumizi,
Shirikalilikadiriwa kutumia kwa shughuli zake za kawaida, Tsh. 856,000,000 na fedha halisi
iliyoingizwa na kutumika ilikuwa Tsh. 598,280,421 sawa na asilimia 70 ya makadirio,
kukiwa na upungufu wa Tsh. 257,719,579 sawa na asilimia 30 ya makadirio.
Majibu ya Shirika
Ni kweli kuwa gharama za uchapaji ni kubwa na Shirika hulazimika kutumia zaidi ya
asilimia 70 ambazo ni sawa na Tsh. 334,974,490 kwa mwaka 2012/2013 na katika gharama
hizo pesa za makusanyo zilizotumiwa kwa matumizi hayo ni Tsh. 186,000,000.
Vile vile Tsh. 317,176,870 za ruzuku kwa mwaka 2011/2012 zilitumika kulipia gharama za
uchapishaji magazeti ambapo Tsh. 129,889,363 za makusanyo zilitumiwa katika gharama za
uchapishaji wa magazeti ya kila siku ya Zanzibar Leo, ambalo hugharamia zaidi ya Tsh.
36,000,000 kwa mwezi na Tsh. 432,000,000 kwa mwaka na gazeti la kila wiki la „Zaspoti‟
ambalo hugharimu Tsh. 42,000,000 kwa mwaka, malipo yake hupitia mapato ya Shirika kwa
vile hayatoshelezi, hata kama ruzuku itapatikana yote ambapo jambo hilo limetokana na
bajeti hiyo ya ruzuku kupangwa kwa mujibu wa ukomo (ceiling) ambayo Shirika limepewa
na Serikali ambayo hupatikana kwa asilimia ndogo na si kwa uhakika. Hali hii itaendelea
mpaka pale Shirika litakapopatiwa mitambo yake ya kuchapishia magazeti.
105
Kuhusiana na posho la wafanyakazi halimo katika kuongeza gharama, kwani ni jambo la
kawaida kwa taasisi zinazozalisha magazeti duniani kutokana na maumbile ya kazi zenyewe
ambazo hazina muda maalum wala mapumziko kutokana na kuwa kazi ya kila siku. Na
hivyo, wafanyakazi hulazimika kuwepo kazini zaidi ya muda wa kawaida na haiwezekani
kuwapangia zamu.
Upungufu wa ukusanyaji wa mapato kwa Shirika hili umetokana na kutokuwa na kiwango
maalum cha uchapishaji wa magazeti, yaani, uchapishaji unategemea na kipindi wakati
wengine wanachapisha nakala nyingi na wakati mwengine nakala kidogo.
Aidha, walizidi kueleza kuwa kwa kawaida Mashirika ya Magazeti hupata faida kubwa
kutokana na matangazo yanayotangazwa, ingawa kwa Shirika hili mambo ni kinyume kwani
kuna taasisi nyingi hutoa matangazo yao bila ya kuyalipia kwa wakati, jambo ambalo
linalipelekea Shirika hili kushindwa kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi unaotakiwa.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati ya PAC ilishindwa kufuatilia majibu ya hoja hizi kama ilivyopangwa baada ya
Watendaji wa Shirika hili kushindwa kutoa maelezo sahihi. Tatizo hili limejitokeza baada ya
watendaji wa Shirika la Magazeti kutoa majibu tofauti kwenye hoja, jambo ambalo
limeipelekea Kamati kushindwa kujua lipi jibu sahihi kati ya majibu hayo. Pamoja na hayo
walishindwa kujibu baadhi ya hoja za Wajumbe wa Kamati walizozihoji. Hatua hii imefikia
kwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika Ndg. Nasima kutokuwa na taarifa za kutosha
kuhusiana na Shirika analolikaimu.
Kutokana na kasoro hizo Kamati hii imehisi ni vyema ikatoa muda zaidi kwa Shirika ili
liweze kujiandaa vyema na hatimae kuwasilisha taarifa sahihi mbele ya Kamati kwa manufaa
ya Shirika na taifa kwa ujumla. Hata hivyo, Shirika liliwasilisha majibu yake tarehe
11/12/2014 kupitia barua yenye kumbu kumbu namba SMS/U/H/I/VOL.I/08, lakini majibu
hayo hayawezi kuchukuliwa sahihi bila ya kukaa tena na kujadiliana na Kamati. Hivyo,
Kamati hii haikubahatika kukutana tena na Shirika hili kutokana na majukumu mengi
iliyokuwa nayo. Kwa msingi huo, hoja za Shirika la Magazeti zimebaki kama zilivyo.
9.13 HOTELI YA BWAWANI
Hoja Namba 34.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Mapato na Matumizi
Ukaguzi umebaini kuwa Hoteli ya Bwawani ilikusanya mapato yake kwa upungufu wa Tsh.
73,046,378 sawa na asilimia 8 ya makadirio. Kwa upande wa matumizi, Hoteli ya Bwawani
iliingiziwa na kutumia jumla ya Tsh. 817,905,841 kwa kazi za kawaida ikiwa ni upungufu
wa Tsh. 8,261,675 sawa na asilimia 1 ya makadirio.
Majibu ya Hoteli
Hoteli ya Bawawani iliieleza Kamati kuwa upungufu huo wa ukusanyaji wa mapato
umetokea kutokana na uhaba wa wageni wanaofika hotelini kwa kuwa jengo la hoteli
linaendelea na ukarabati.
Walizidi kueleza kuwa ingawa hoteli hii inaendelea na ukarabati bado makisio ya ukusanyaji
wa mapato yameongezeka kutokana na mikakati waliojiwekea ikiwa ni pamoja na kufuatilia
madeni wanayodai. Katika kuthibitisha hili walizitaja baadhi ya Taasisi ambazo zilikuwa
zinadaiwa na Hoteli na hivi sasa zimepunguza kulipa madeni yao hayo na nyengine
zimekamilisha deni. Jadweli lifuatalo linaonesha namna baadhi ya Taasisi hizo zilivyolipa
madeni hayo;
106
S/NO. JINA LA TAASISI KIWANGO CHA
FEDHA
ALICHOKUWA
ANADAIWA
KIWANGO CHA
FEDHA
ANACHODAIWA
1. Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo
Tsh. 2,340,648 -
2. Wizara ya Fedha Tsh. 12,437,200 -
3. Wizara ya Afya (Daktari wa
Kichina)
Tsh. 50,615,000 Tsh. 24,215,000
4. Hammy & Distributor Tsh. 3,360,000 -
5. National Marketing Co. Tsh. 75,000,000 -
6. Break Enterprise Tsh. 3,360,000 -
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ya PAC imesikitishwa sana na mwenendo wa uendeshaji wa Hoteli hii. Hii ni
kutokana na kuwa baadhi ya Taasisi za Serikali, Wanasiasa na Watendaji wa Serikali
huitumia Hoteli ya Bwawani kinyume na utaratibu. Jambo hili litapelekea Hoteli hii
kushindwa kujiendesha kutokana na ukosefu wa mapato.
Kutokana na kasoro hiyo, Kamati hii imebaini kuwa baadhi ya Taasisi za Serikali hutumia
fedha zao kinyume na walivyoidhinishiwa na Baraza la Wawakilishi
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inazitaka Taasisi zote pamoja na watu wote wanaodaiwa na Hoteli hii kuchukua
juhudi za makusudi za kulipa madeni yao ili kuiwezesha Hoteli ya Bwawani kutekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Uwezo wa Hoteli ya Bwawani kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa
kujiendesha
Kwa mwaka 2012/2013, Hoteli ilikuwa na mali za mpito za Tsh. 488,785,177.16 na dhima
za mpito za Tsh. 20,171,218 kwa bakaa la thamani ya Tsh. 468,613,959.16 na uwezo wa
kulipa dhima kwa ratio ya 24.2:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wa Tsh.
325,091,753 pamoja na salio la benki la Tsh. 163,693,424.16 kwa mwaka 2012/2013.
Mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa ni Tsh. 1,136,279,917 na matumizi
yake yalikuwa Tsh. 986,417,431 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 149,862,486.
Majibu ya Hoteli
Ni kweli kwamba Hoteli ni taasisi inayojiendesha kibiashara hivyo ni lazima itakuwa ina
wadaiwa. Katika kufuatilia madeni hayo Uongozi wa Hoteli imeunda Kamati ya Watu saba
ambao jukumu lao ni kuhakikisha wanafuatilia madeni ya Hoteli ili Hoteli iweze kutatua
tatizo la upungufu la mishahara kwa wafanyakazi wake ambalo linaikabili hivi sasa. Jumla
ya fedha inazodai ni Tsh. 325,091,753.
Pamoja na juhudi hizo Uongozi wa Hoteli imewasilisha tatizo hilo Wizara ya Fedha ili
kusaidiwa kulitafutia ufumbuzi suala hili na Wizara ya Fedha imekubali kushirikiana nao.
Aidha, kwa kipindi kirefu Hoteli ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za
uendeshaji kibiashara. Kutokana na hilo Hoteli imechukua juhudi za makusudi ikiwa ni
pamoja na kudhibiti vianzio vya mapato na kudhibiti gharama za matumizi ya hoteli.
Aidha, Hoteli ilipitia viwango vinavyotozwa kwa huduma mbali mbali na kubaini viwango
vingi kati hivyo kuwa inahitaji kuongezwa. Hivyo, Hoteli kwa kushirikiana na Wizara ya
107
Habari, Utamauni, Utalii na Michezo ilifanya mapitio ya viwango hivyo ili viendane na
wakati hatua ambayo itaongeza mapato ya Hoteli.
Mchanganuo wenyewe ni kama ifuatavyo;
S/NO. JINA LA UKUMBI BEI YA ZAMANI BEI YA SASA
1. Salama Hall – Promotion na
Biashara
Tsh. 1,000,000 Tsh.1,500,000
2. Salama Hall – Harusi na
Mahafali
Tsh. 600,000 Tsh. 1,000,000
3. Café Changu Restaurant -
Promotion na Biashara
Tsh. 500,000 Tsh. 1,000,000
4. Café Changu Restaurant –
Harusi na Mahafali
Tsh. 200,000 Tsh. 300,000
5. Roof Top – Semina Tsh. 200,000 Tsh. 300,000
6. Conference Hall above
Pemba Bar – Semina
Tsh. 250,000 Tsh. 300,000
Uchunguzi wa Kamati Kamati inaitaka Hoteli kuendelea kufuatilia madeni yake kwa inaowadai, pamoja na juhudi
walioionesha ya kuwasiliana kwa njia ya barua kwa wadaiwa, Kamati imejiridhisha kuwa,
taasisi nyingi za Serikali hazichukui hatua za kufuatilia madeni yao kisheria, hali
inayozifanya taasisi hizo kushindwa kusimamia ipasavyo mapato yake na kuendelea kutoa
huduma bila ya kulipwa chochote. Hivyo, Hoteli ichukue hatua za kisheria mbali na
kuandika barua, kwa wadaiwa wote watakaoshindwa kulipia madeni yao.
Mapendekezo ya Kamati
Serikali itoe toleo maalum kwa taasisi zake kutumia kumbi za Hoteli hii endapo zitakuwa na
shughuli kama vile semina, makongamano nakadhalika, jambo hili litalisaidia Hoteli kupata
mapato zaidi.
Aidha, inazitaka Taasisi za Serikali kulipia gharama za ukodishwaji wa kumbi kwa wakati ili
Hoteli iweze kutekeleza majukumu yake bila ya usumbufu wowote.
Hoja Namba 34.2 Kukosekana kwa mikataba kwa wasambazaji wa chakula
(Suppliers) Tsh. 27,139,300
Fedha hizo zilitumika kwa ununuzi wa vyakula kwa ajili ya wageni wa Hoteli ya Bwawani
kwa kununua bidhaa mbali mbali kwa ajili ya huduma za Hoteli bila ya kuwepo mikataba
maalum kuhusiana na manunuzi hayo, wakati kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kifungu
cha 73 cha Sheria Namba 9 ya mwaka 2005.
Majibu ya Hoteli
Hoteli ya Bwawani ilikiri kutokufunga mikataba na wasambazaji wa vyakula, hii ni kutokana
na kuwa Hoteli kwa kupitia Serikali Kuu katika kipindi hicho chote imo katika mikakati ya
kutaka kumpa Mwekezaji ili kuiendeleza. Kutokana na malengo hayo Hoteli ilishindwa
kufunga mikataba ili kuepusha kujakutozwa fidia endapo itakatisha mikataba hiyo wakati
zoezi hilo litakapofanikiwa.
Kufuatia hoja hiyo ya Mdhibiti, Uongozi wa Hoteli umo katika mikakati ya kuwamalizia
madeni yao watoa huduma hiyo na baadae kutangaza zabuni kwa kumpata mzabuni ambae
atakaekidhi vigezo vyote kwa mujibu wa sheria.
108
Uchunguzi wa Kamati Kamati ya PAC haiungi mkono suala la Hoteli hiyo kupewa Mwekazaji kutokana na uzoefu
uliopatikana kwa Hoteli hiyo kupewa Mwekezaji.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Hoteli kuwa na utamaduni wa kutoa zabuni kwa zile huduma
inazozihitaji ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Vile vile, Kamati hii inaishauri Serikali kuendelea kuwaendeleza wafanyakazi wa
Hoteli ili waje wafaidike na ajira zao endapo Serikali atabaki kwenye msimamo wake
wa kuipatia Mwekezaji Hoteli hii.
Ili kulinda ajira za wananchi wake, Kamati ya PAC imeishauri Serikali kuwa
miongoni mwa masharti ya kupatiwa hoteli hiyo Mwekezaji huyo iwe ni uhakikisha
kuwa anawapa kipaombele watendaji wa Hoteli hii kwani mtu mwenye uzoefu
anaweza kufanya kazi nzuri kuliko mtu mwenye elimu kubwa.
9.14 MFUKO WA HIFADHI YA JAMII (ZSSF)
Hoja Namba 33.1 Uwezo wa Mfuko kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka 2012/2013, Mfuko ulikuwa na mali za mpito za Tsh. 5,950,764,431 na dhima
za mpito za Tsh. 141,637,269,148 kwa hasara ya Tsh. 135,686,504,717 na uwezo wa kulipa
dhima kwa ratio ya 0.04:1, hali iliyochangiwa zaidi na kuwepo kwa wadaiwa wengi wa
Mfuko.
Mapato ya Mfuko yalikuwa ni Tsh. 41,272,755,594 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
10,360,040,228 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 30,912,715,366.
Majibu ya Mfuko
Hesabu za dhima za mpito zimekosewa katika taarifa ya ukaguzi hali inayoonesha pia
maelezo yaliyotolewa hayana usahihi. Usahihi wa dhima kwa mwaka 2012/2013 ni Tsh.
310,159,732.81 na hali halisi ya mali za mpito ni Tsh. 5,640,604,699.00 na hivyo uwezo wa
kulipa dhima ni 19,186,128.36. aidha, kuhusiana na uwezo wa kujiendesha, uongozi wa
Mfuko umeeleza kuwa, Mfuko haufanyi faida na ziada yote inayopatikana inapelekwa moja
kwa moja kwa wanachama wake na wamefanikiwa kuwa na ongezeko kubwa kutokana na
kupunguza gharama za vikao vya bodi ya Wakurugenzi na kwa watendaji wa Mfuko. Pia
Mfuko umeongeza ufanisi wa kuwasomesha wafanyakazi wake, kiasi ya kufanya kazi kwa
juhudi kubwa ya kuendeleza Mfuko.
Uchunguzi wa Kamati
Kufuatia marekebisho yaliyoelezwa, Kamati ilimtaka Afisa Mkaguzi anaefuatana na Kamati
kutoa usahihi wa maelezo ya Mfuko na taarifa ya Mkaguzi na kueleza kuwa, anakubaliana
na maelezo ya Mfuko na kilichoandikwa katika taarifa ya ukaguzi kilikosewa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inamshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar, kuandaa
vyema taarifa zake kwa usahihi, ili kuiwezesha Kamati kutekeleza vyema majukumu yake.
109
9.15 SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA (ZSTC)
Hoja Namba 12 Uwasilishaji wa hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi
Kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Fedha namba 12 ya mwaka 2005, inakitaka taasisi zote za
Serikali zitayarishe na kufunga hesabu zao za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi. Hata hivyo,
uwasilishaji huo usizidi tarehe 30 ya mwezi wa Septemba ya kila mwaka, lakini Shirika
lilichelewa kwa kuwasilisha 9/04/2013.
Majibu ya Shirika
Shirika la Biashara la Taifa liliieleza Kamati kuwa linafunga hesabu za mwisho wa mwaka
katika mwezi wa Juni tofauti na Mashirika mengine. Pamoja na kufunga hesabu katika
mwezi huo limekiri kuwa limechelewa kufunga hesabu zake kutokana na mageuzi ya
kiutendaji i.e linabadilisha mfumo wa kiutendaji kutoka „manual‟ na kutumia „computer‟.
Hata hivyo, wameiahidi Kamati kuwa watajitahidi kufunga hesabu zao mapema ili
kuzipeleka kunakostahiki na kufanyiwa kazi kama ilivyotarajiwa.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ya PAC imebaini kuwa muda wa ufungaji wa hesabu za mwaka kwa Mashirika ya
Umma unatofautiana, jambo ambalo linaweza likaikosesha Serikali kujua mapato yake halisi
katika mwaka husika.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati ya PAC ililitaka Shirika kujitahidi kufunga hesabu za mwaka na kuziwasilisha kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama sheria inavyoelekeza.
Aidha, Kamati hii inaishauri Serikali kuwa na mfumo mmoja wa ufungaji wa hesabu kwa
Taasisi zake zote ili kujua mapato halisi ya nchi.
Hoja Namba 39.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013.
Taarifa ya Mapato na matumizi
Shirika la Biashara la Taifa lilikadiriwa kukusanya Tsh. 53,808,214,000 katika kipindi cha
mwaka 2012/2013, lakini hadi kufikia Juni 2013 lilikusanya jumla ya Tsh. 32,932,176,,000
sawa na asilimia 61 ya makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 20,876,038,0020 sawa na
asilimia 39 ya makadirio. Aidha, Shirika liliidhinishiwa kutumia Tsh. 53,753,050,000 na
kuingiziwa na kutumia Tsh. 32,535,901,100 sawa na asilimia 61 ya makadirio, ikiwa ni
pungufu ya Tsh. 21,217,148,900 sawa na asilimia 39 ya makadirio.
Majibu ya Shirika
Shirika lilikabiliwa na upungufu wa ukusanyaji wa mapato kwa mwaka huo, kutokana na
mzao wa karafuu kwa mwaka huo kuwa ni mdogo. Hii ni kutokana na kuwa kwa kawaida
mzao wa karafuu mwaka mmoja unakuwa mkubwa lakini mwaka unaofuata unakuwa
mdogo.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ya PAC iliridhika na majibu ya Shirika kwa upande wa ukusanyaji wa mapato. Ama
kwa matumizi ya kazi za kawaida, Kamati hii imebaini kuwa Shirika la Biashara la Taifa
hutumia fedha nyingi kwa ajili ya kukilipa Kikosi Kazi „Task Force‟ kilichoundwa kwa ajili
ya zoezi la ukamataji wa karafuu za magendo wakati katika zoezi hilo Shirika halinufaiki na
chochote ingawa Shirika lenyewe linahisi zoezi hilo lina tija.
110
Aidha, Kamati ya PAC imeshangazwa na kitendo cha Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM)
kulipwa fedha kwa kazi ya kuzuia magendo hayo ya karafuu kwa kuwa lengo kuu la
kuundwa kwa Kikosi hicho ni kuzuia magendo ndani ya nchi.
Sambamba na hilo, Kamati hii imebaini kuwa fedha zinazotumika kwa ajili ya Kikosi Kazi
hukabidhiwa kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko na Shirika na huwa hazikaguliwi
na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kitendo ambacho kimekitia mashaka
Kamati hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati hii inamshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuzikagua fedha
hizo kwa kuwa fedha zinazotumika ni nyingi. Kwa mfano; katika mwaka wa fedha
2012/2013 jumla ya Tsh, 420,000,000 zilitumika kwa ajili ya zoezi la ukamataji wa magendo
ya karafuu.
Ingawa Kikosi Kazi kipo kwa mujibu wa Sheria , Kamati ya PAC inawataka wakuu wa
Kikosi Kazi hicho kusitisha malipo kwa KMKM kwa kuwa kinatimiza jukumu lake kisheria.
9.16 SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA ZANZIBAR (ZBC)
Hoja Namba 37.1 Taarifa ya Mapato na Matumizi kufuatia ufungaji wa Hesabu za
Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Shirika la ZBC lilikadiriwa kukusanya Tsh. 280,700,000 na makusanyo halisi yalikuwa Tsh.
210,326,283 sawa na asilimia 75 ya makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 70,373,717, sawa
na asilimia 25 ya makadirio. Aidha, matumizi ya kawaida yalikuwa Tsh. 2,016,224,000 na
fedha halisi zilizopatikana kwa matumizi zilikuwa Tsh. 1,611,857,366 sawa na asilimia 80
ya makadirio na upungufu wa Tsh. 404,366,634 sawa na asilimia 20 ya makadirio.
Majibu ya Shirika
Upungufu wa kutofikia makisio ya makusanyo unategemea na vyanzo vya mapato ya Shirika
kupungua kutokana na kukisia na kutegemea chanzo kimoja ambacho huathiri vyanzo
vyengine. Kwa mfano vipindi vya Baraza la Wawakilishi wanapotumia muda mwingi
takriban siku nzima kurusha vikao vya Baraza, huathiri kwa kukosa kurusha matangazo
mengine na hivyo hukosa biashara.
Shirika pia lina chanzo chengine ambacho ni minara ila kwa sasa makampuni mengi ina
minara hiyo. Na kuna taasisi zikikodi minara hiyo hazilipi wala haziingiliki, kwa mfano
Idara ya Usalama, Polisi. Hata hivyo, Shirika linajipanga kuwa na mikataba na taasisi hizo.
Aidha, changamoto nyengine ni kuzimwa kwa umeme kwa ghafla, kwani hukimbiza wateja
wa minara hiyo.
Kwa upande wa matumizi, Shirika linakabiliwa na ukata mkubwa na udogo wa mishahara ya
wataalamu wake kulipwa mishahara midogo, kwani hupunguza ari ya kufanya kazi kwa
kujituma.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imesikitishwa na taarifa ya udogo ya mishahara kwa wafanyakazi wa Shirika na hata
suala zima la kurushwa kwa vipindi vya Baraza la Wawakilishi bila ya malipo, wakati
Shirika linakosa uwezo wa kutoa huduma na kujipatia mapato katika wakati huo.
Mapendekezo ya Kamati
Baraza la Wawakilishi litenge bajeti ya huduma ya matangazo wanayopatiwa na Shirika na
ni vyema Baraza likanunua na kufunga mitambo yake ambayo itasaidia hata kuwepo kwa
111
„storage’ ya vikao vya Baraza. Aidha, Serikali iangalie kwa karibu mishahara ya
wafanyakazi wa Shirika ili kuwaendeleza na kuwabakisha katika kulihudumia Shirika.
Uwezo wa Shirika kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa
kujiendesha
Kwa mwaka wa 2012/2013, Shirika lilikuwa na mali za mpito zenye thamani ya Tsh.
63,690,000 na dhima za mpito za Tsh. 587,727,614 na hali halisi ya uwezo wa kulipa dhima
za mpito kuwa 0.11:1, ambapo uwiyano wa mali za mpito ni mdogo kuliko dhima za mpito,
hali iliyosababishwa na kuwepo kwa deni kubwa.
Taarifa ya mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa ni Tsh. 1,557,350,432 na
matumizi yalifikia Tsh.2,173,966,466 hali iliyoifanya Mamlaka kuendeshwa kwa hasara ya
Tsh. 616,616,034 kuonesha kuwepo uwezekano wa kuongezeka kwa hasara iwapo Shirika
halitochukua juhudi za makusudi za kupunguza gharama za uedeshaji.
Majibu ya Shirika
Deni kubwa wanalokabiliwa ni la Shirika la Umeme ambalo walilirithi kutoka Sauti ya
Tanzania Zanzibar na Televisheni ya Zanzibar, ambapo kila mara Shirika la Umeme
limekuwa linahoji na kutaka kulipwa. Shirika limejaribu kulilipa lakini kwa kiwango kidogo.
Shirika limechukua hatua ya kuwaomba viongozi mbali mbali kusamehewa kwa deni hilo,
lakini hakuna mafanikio, nab ado wanashauri ama deni hilo lilipwe na Serikali au lifutwe.
Uchunguzi wa Kamati
Kama zilivyo taasisi nyingi za Serikali, zimekuwa na deni kubwa la umeme ambalo huwa
mzigo mzito na kushindwa kulilipa. Kamati imejiridhisha kwamba, Shirika lilimuandikia
Mhe. Rais barua ya tarehe 23 May 2004 yenye kumbu kumbu namba ZBC/MUM/VOL.II
iliyoandikwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kuomba ifuatiliwe ahadi ya Mhe. Rais ya
kusamehewa deni hilo.
Mapendekezo ya Kamati
Shirika liendelee kuchukua juhudi ya kufuatilia deni lake na kwa nafasi ya Kamati inaiomba
Serikali kutafakari namna ya kulilipa deni hilo ambalo limekuwa mzigo mzito kwa Shirika.
9.17 CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)
Hoja 43.1 Hesabu za Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Taarifa ya Mapato na Matumizi
Kwa mwaka 2012/2013 Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kilikadiriwa kukusanya jumla
ya Tsh. 6,936,252,920 hadi kufikia 30 Juni, 2013 kilifanikiwa kukusanya Tsh.
6,510,873,906 sawa na asilimia 94 ya makadirio ikiwa ni upungufu wa Tsh. 425,379,019
sawa na asilimia 6 ya makadirio. Aidha, kwa mwaka 2012/2013 Chuo hiki uliidhinishiwa
kutumia Tsh. 7,232,044,940 kwa kazi za kawaida ingawaje fedha zilizoingizwa na kutumika
ni Tsh. 6,527,987,637 sawa na asilimia 90 ya makadirio ikiwa ni upungufu wa Tsh.
704,057,303 sawa na asilimia 10 ya makadirio.
Majibu ya Chuo
Ni kweli kwamba kuna upungufu wa ukusanyaji wa mapato katika mwaka huo wa fedha. Hii
ni kutokana na upungufu wa Ruzuku kutoka Serikalini kwa asilimia 13, ambapo Chuo
kilitarajia kuingiziwa Ruzuku ya Tsh. 4,200,000,000.00 na badala yake kiliingiziwa jumla ya
Tsh. 3,646,331,000.00. Hata hivyo, vianzio vyengine vya mapato vilizidi malengo. Kamati
ya PAC ilielezwa na Chuo kuwa upungufu huo umetokea zaidi kwenye kipengele cha
112
mishahara na matumizi mengineyo ambapo chimbuko lake ni kupatikana na upungufu kwa
fedha za Ruzuku.
Walizidi kueleza kuwa Chuo kilitumia zaidi kwa asilimia 10 kwenye fedha za misaada, hii ni
kutokana na utekelezaji wa miradi kwa kiwango kikubwa kwa kuwa fedha hizo zilikuwepo
tayari.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilishtushwa na majibu ya Chuo ya upungufu wa mishahara kwa watendaji wake na
kuomba maelezo zaidi, ambapo ilijibiwa kuwa upungufu huo wa mishahara umetokana na
kuwepo kwa nafasi wazi (vacant posts) pamoja na kuwepo kwa Wahadhiri wa muda „Part
timer Lecturers‟ ambao malipo yao hutokana na fedha nyengine za mapato ya Chuo ukiacha
Ruzuku. Jambo ambalo hupelekea Chuo kushindwa kutekeleza baadhi ya shughuli ambazo
kimejipangia.
Aidha, Kamati imebaini kuwa Chuo hakiingiziwi fedha za matumizi ya kazi za Maendeleo
ingawa Chuo kinashirikiana na Serikali kutafuta washirika wa maendeleo.
Mapendekezo ya Kamati
Serikali ijitahidi kukipatia Chuo Ruzuku iliyokadiriwa ili kiweze kutekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Serikali iwapatie Chuo hiki fedha za matumizi ya kazi za maendeleo kwa kuwa Chuo
kina mahitaji mengi kama vile ofisi ya kituo kinachohusiana na shughuli za
wanafunzi „student center‟, ofisi kwa watendaji, duka nakadhalika.
Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na Uwezo wa kujiendesha.
Mali za mpito za thamani ya Tsh. 1,223,541,312.43 na dhima za mpito za thamani ya Tsh.
73,572,882.20 hufanya hali halisi ya mali za mpito kwa Shirika kuwa Tsh. 1,149,968,430.23
kwa mwaka 2012/2013, ambayo ni sawa na uwezo wa ration ya 16:1.
Mapato ya Shirika yalikuwa Tsh. 6,510,873,906.48 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
6,527,987,637.39 na hivyo kuendeshwa kwa hasara ya Tsh. 17,113,730.91, mwendo huo wa
hesabu hizo unaonesha kuwepo kwa uwezekano wa kupunguka kwa hasara iwapo Chuo
kitachukua juhudi za makusudi za kupunguza gharama za uendeshaji.
Majibu ya Chuo
Ni kweli kwamba mali za mpito zinazidi dhima ya mpito kwa kuwa mali za mpito
zinajumuisha Akiba za Benki, madeni ya ada za wanafunzi na madeni ya mikopo ya
wafanyakazi.
Aidha, uwezo wa kulipa umeonekana mkubwa kutokana na kiwango kikubwa cha salio
wakati wa kufunga hesabu kilichotokana na fedha za miradi ambapo, kwenye hesabu za
Benki kulikuwa na Tsh. 745,883,984.43. Aidha, hesabu za mapato na matumizi inaonesha
kuwa mapato yamezidiwa na matumizi kutokana na kutekeleza kazi za miradi kwa fedha
ambayo Chuo imeipokea kipindi cha nyuma.
Pia, Chuo kilizidi kueleza kuwa kiutaratibu kilitakiwa kwenye matumizi kijumuishe pia na
gharama za uchakavu wa mali za kudumu ambapo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 gharama
hizo zilikuwa ni Tsh. 315,395,814.48.
Kiujumla Uongozi wa Chuo unazingatia sana matumizi ya Chuo, na umekuwa ukichukua
jitihada mbali mbali kuhakikisha kwamba matumizi yanafanywa kwa kuzingatia bajeti na
kazi zinaendana na Mpango Mkakati.
113
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati:
Kamati imeridhika na majibu yaliyotolewa na Chuo hiki na inaiomba Serikali kukitengea
fedha za matumizi ya maendeleo Chuo, ili kiweze kufikia malengo yake kilichojipangia
ikiwa ni pamoja na kuongeza majengo ya madarasa hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya vijana
wanaoomba nafasi za mafunzo Chuoni hapo hukosa nafasi za kujiunga na masomo kutokana
na ufinyu wa madarasa.
9.18 CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR
Hoja Namba 42.1 Hesabu za Mwaka 2012/2013
Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na Uwezo wa kujiendesha.
Mali za mpito za thamani ya Tsh. 1,002,066,951.54 na dhima za mpito za thamani ya Tsh.
39,023,967.70 hufanya hali halisi ya mali za mpito kwa Shirika kuwa Tsh. 963,042,983.84
kwa mwaka 2012/2013, ambayo ni sawa na uwezo wa ration ya 26:1. Kwa takwimu hizo,
uwiyano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha na dhima za mpito, hali iliyochangiwa
zaidi na kuwepo kwa wadaiwa pamoja na salio la benki kwa hesabu za Chuo.
Mapato ya Shirika yalikuwa Tsh. 3,517,210,714.18 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
2,559,665,672.8 na hivyo kuendeshwa kwa faida ya Tsh. 957,545,041.38, mwendo huo wa
hesabu hizo unaonesha kuwepo kwa uwezekano wa kuzidi kushuka kwa faida iwapo Chuo
hakitachukua juhudi za makusudi za kupunguza gharama za uendeshaji, sambamba na
kuwepo kwa mipango imara ya ukusanyaji wa mapato, kwa sababu takwimu zinaonesha
kwamba faida ya Chuo imeshuka kutoka Tsh. 1,120,727,333 kwa mwaka 2011/2012 hadi
kufikia Tsh. 957,545,041.38 kwa mwaka 2012/2013 ikiwa ni upungufu wa Tsh.
163,182,291.62 sawa na wastani wa asilimia 15 kwa mwaka, kwani upungufu huo
umetokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji ikiwemo gharama za kukodi majengo
ya watu binafsi.
Majibu ya Chuo
Chuo cha Uongozi wa Fedha kimeieleza Kamati ya PAC kuwa hakikubaliani na maelezo
yaliyotolewa kwenye Ripoti ya Mdhibiti kwa kuwa Mapato ya Chuo yaliongezeka kwa
asilimia 25 ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita, ongezeko hilo limechangiwa na
kuongezeka kwa mapato mengineyo kwa asilimia 48.2, kuongezeka kwa Ruzuku kutoka
Serikalini asilimia 47.2, kuongezeka kwa ada za wanafunzi asilimia 9.4 na kuongezeka kwa
fedha za maendeleo asilimia 6.3.
Aidha, gharama za matumizi zimeongezeka kwa asilimia 54.4, ongezeko hili
limesababishwa na kuongezeka kwa gharama za matunzo ya majengo na magari kwa
asilimia 157. Kwa upande wa majengo gharama zimeongezeka kutokana na uchimbaji wa
mashimo ya maji machafu na mfumo wake katika dahalia ya Chuo. Ama kwa upande wa
magari gharama imeongezeka kutokana na kuanza kuyakatia bima kubwa „Comprehensive‟
magari ya Chuo.
Walizidi kueleza kuwa kuongezeka kwa matumizi ya gharama za usafiri, malazi na chakula
kwa asilimia 94.8, kwa walimu wanasomeshwa na Chuo katika Shahada ya Uzamivu (PhD)
na Uzamili katika nje ya nchi.
Pia, gharama za uendeshaji zimechangia kuongezeka kwa matumizi kwa asilimia 67.7.
Gharama hizo zimeshababishwa na kuanza kulipa riba (Interest) ya shilingi 236,174,220.46
kwa ajili ya mkopo kutoka ZSSF uliotumika kwa ujenzi wa dahalia.
114
Sambamba na hayo, kodi ya magari na madarasa ambayo imeongezeka kwa asilimia 10%
ukilinganisha na mwaka uliopita imechangia kuongezeka kwa matumizi ya Chuo. Aidha,
kuongezeka kwa huduma kwa mfano; kuwepo kwa dahalia, Chuo kimeanza kulipia huduma
za usafi na ulinzi kwa kampuni binafsi baada ya Bodi ya Chuo kushauri huduma hizi
zitolewe na kampuni binafsi ili kuweka uwiano wa walimu na wafanyakazi wengine kama
vyombo vya udhibiti wa ubora wa vyuo unavyotakiwa. Jadweli lifuatalo linaonesha namna
Mapato na Matumizi ya Chuo yalivyokuwa katika miaka husika.
Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 - 2012/2013
2011/2012 2012/2013 Ongezeko/Upungufu
Mapato
Ruzuku, Ada ya
Masomo na Mapato
mengineyo
2,802,282,653.00 3,517,210,714.18 25.51
Matumizi
Mishahara na Posho 753,594,036.20 1,004,013,525.50 33.23
Gharama za
Uendeshaji
546,448,205.08 916,419,017.17 67.70
Gharama
Usafiri,Malazi na
Chakula
53,634,939.25 104,480,309.00 94.80
Matunzo ya
Majengo na Magari
63,286,060.00 162,852,090.00 157.33
Ziada ghafi 1,416,963,240.53 2,187,764,941.67 54.40
Ziada/Upungufu
baada ya kutoa
Uchakavu
1,120,727,333.02 957,545,041.38 (14.56)
Mapato Kwa Wanafunzi Waliokodishiwa Madarasa Nje ya Chuo
2011/2012 2012/2013
Mapato kwa wanafunzi waliokodiwa madarasa 445,350,000.00 400,050,000.00
Kodi 61,830,000.00 64,890,000.00
Mapato Halisi 383,520,000.00 335,160,000.00
Jadweli ilinaonesha gharama na mapato ya kukodi kwa madarasa ambayo yako nje ya chuo,
Katika mwaka wa fedha 2012/2013, uendeshaji wa mafunzo katika sehemu za kukodi
madarasa nje chuo kimeweza kuongeza mapato yaliyosaidia kutekeleza shughuli za mipango
yake. Chuo kiliweza kukusanya mapato ya jumla ya TZS 400,050,000 ikilinganishwa na
gharama ya TZS 64,890,000 na kukiwezesha Chuo kupata mapato halisi ya TZS
335,160,000.
Kwa hivyo, takwimu hizi hazioneshi kuwa zimeleta upungufu katika mapato ya Chuo kwa
kukodi majengo binafsi. Kwani Chuo kisingeweza kutoa mafunzo hayo katika majengo
yake, aidha, kupata fedha za zaidi ya milioni 335.
Gharama za uendeshaji zimekuwa zikiongezeka sambamba na kuongezeka kwa kutanuka
kwa shughuli za chuo zikiwemo za kuongezeka kwa programu mpya za masomo. Katika
115
mwaka wa fedha 2015/2016 Chuo kimejipanga kuangalia kupunguza gharama za uendeshaji
bila kuathiri utekelezaji wa majukumu ya Chuo kama ilivyotajwa katika sheria.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati ya PAC iliridhika na majibu yaliyotolewa na Chuo na pamoja na mambo mengine
ilibaini na kupendekeza yafuatayo;
Kitendo cha wanafunzi kutokukaa katika dahalia za Chuo na badala yake kukodi
katika nyumba za watu binafsi kunakikosesha mapato Chuo. Hivyo, Kamati hii
inawashauri wanafunzi wa Chuo hicho kutumia dahalia za Chuo kwa usalama wao
na mali zao pamoja na kukipatia Chuo mapato.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar hutoa asilimia tofauti ya fedha kwa fani
moja. Kwa mfano; kijana aliyeomba kusoma fani ya Teknohama na Uhasibu
(Computer with Accounting) ambaye amejiunga na Chuo cha Zanzibar basi hulipwa
asilimia ndogo ukilinganisha na kijana aliyeomba fani hiyo hiyo katika Chuo cha
Tanzania Bara. Jambo hili hupelekea vijana wengi wa Kizanzibari kuomba Vyuo vya
Tanzania Bara ili wapate fedha nzuri na kuvikosesha nafasi Vyuo vya Zanzibar.
Kutokana na changamoto hiyo Kamati ya PAC inaishauri Bodi hii kulifikiria kwa
makini suala hili ili Vyuo vya Zanzibar viweze kudahili wanafunzi kwa mujibu wa
uwezo wao na hatimae kupata mapato ambayo yatachochea kufikia malengo
waliyoyakusudia.
Kwa kuwa Chuo hiki kinadaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)
kutokana na ujenzi uliofanyika, na kwa kuwa Chuo hakina uwezo wa kulipa deni
hilo, Kamati ya PAC inaishauri Serikali kulilipa deni hilo ili Chuo kiweze kutekeleza
shughuli zake ipasavyo.
9.19 CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII
Hoja Namba 41.1 Taarifa ya Mapato na Matumizi kufuatia ufungaji wa Hesabu za
Mwisho wa Mwaka 2012/2013
Chuo kilikadiriwa kwa 2012/2013 kukusanya Tsh. 262,000,000 na makusanyo halisi
yalikuwa Tsh. 295,000,700, sawa na asilimia 113 ya makadirio. Aidha, kwa ajili ya
kuendesha shughuli za kawaida, Chuo kilikadiriwa kutumia Tsh. 420,000,000 na ulipotimia
mwaka wa fedha, Chuo kiliidhinishiwa na kutumia Tsh. 382,635,777 sawa na asilimia 91 ya
makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 37,364,223 sawa na asilimia 9 ya makadirio, ikiwa ni
upungufu wa Tsh. 37,364,223 sawa na asilimia 9 ya makadirio.
Majibu ya Chuo
Matumizi ya fedha hizo yalikusudiwa kuendelea kujenga uzio wa Chuo, ununuzi wa samani
na ujenzi wa vibanda vya kusomea. Pia kufundishia walimu katika ngazi ya shahada ya
kwanza na afisa katika ngazi ya shahada ya pili. Chuo vile vile kilijipanga kutumia fedha
hizo kwa kushiriki mikutano mbali mbali ndani na nje ya Zanzibar na kuonesha shughuli
mbali mbali zinazotolewa na Chuo kwa wanafunzi katika wilaya za Zanzibar.
Pamoja na malengo hayo, kutokana na kutopatikana kwa ukamilifu fedha hizo, Chuo
kimeendelea kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo, kushindwa kutayarisha sera mbali
mbali za Chuo, kama vile sera ya mafunzo na sera ya fedha. Aidha, kushindwa kutayarisha
kanuni zinazosimamia wafanya kazi, wanafunzi, fedha, mitihani na utumishi, kama vile pia
walivyoshindwa kufanya marekebisho ya maslahi kwa wafanyakazi yakiwemo mishahara.
116
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji msaada wanaupata Chuo kutoka NAUFIC wakisaidiwa mafunzo na masomo
kupitia NACTE lakini fedha na msaada wanaoupata hawauoneshi katika bajeti yao. Pamoja
na Chuo kueleza kuwa fedha hizo zinatoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kamati
imeeleza bado ipo haja ya kuoneshwa katika bajeti ya Chuo ili ziweze kufuatiliwa.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inakitaka Chuo kuonesha fedha na misaada wanayoipata kupitia NAUFIC na
NACTE, katika bajeti na hesabu zake za mwisho wa mwaka, ili iweze kutambuliwa na
kufanyiwa ukaguzi.
Uwezo wa Chuo kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na uwezo wa kujiendesha
Kwa mwaka wa 2012/2013, Chuo kilikuwa na mali za mpito zenye thamani ya Tsh.
315,048,240 na hawakuwa na dhima za mpito na kufanya uwezo halisi wa mali za mpito
kuwa na mali zenyewe, hali iliyochangiwa na kuwepo kwa wadaiwa na salio la benki.
Taarifa ya mapato ya Mamlaka kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa ni Tsh. 839,993,714 na
matumizi yalifikia Tsh. 796,871,499 hali iliyoifanya Mamlaka kuendeshwa kwa faida ya
Tsh. 43,122,215 na kuonesha kuwepo uwezekano wa kuongezeka kwa faida iwapo Chuo
kitaongeza juhudi ya kusimamia vyanzo vyake vya mapato na kupunguza gharama za
uedeshaji.
Majibu ya Chuo
Pamoja na maelezo ya ukaguzi, Chuo kinataraji kuongezeka kwa gharama za matumizi yake
kutokana na wanahitajika kutumia fedha kwa matumizi na kudumisha jengo lao walilonalo
sasa ambalo wamefunga huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na intaneti kuvutia
ukodishwaji na watu wanaokodi waweze kutumia intaneti. Aidha, Chuo kinakabiliwa na deni
la huduma ya umeme kutoka Shirika la Umeme.
Kuhusiana na uwezo wa kujiendesha utaongezeka iwapo kitapokea tenda za „catering‟
kutoka taasisi mbali mbali za Serikali, jambo ambalo hivi sasa wamelikosa khasa kutoka
Baraza la Mapinduzi ambapo hapo awali walikuwa wanatoa huduma kwao.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati pamoja na majibu ya Chuo imejiridhisha kuwa, Chuo kinatakiwa kuongeza juhudi ya
kukusanya malipo ya madeni yake inayowadai wanafunzi mbali mbali waliosoma Chuoni
hapo ambao bado wanadaiwa.
Kamati imesikitishwa na taarifa kuwa Baraza la Mapinduzi limekatisha huduma yake ya
vyakula na viburidhaji kutoka Chuoni hapo wakati ni njia moja ya taasisi moja ya Serikali
kuisaidia nyengine.
Mapendekezo ya Kamati
Chuo kinatakiwa kuendelea kuchukua juhudi za kudai madeni yake inayowadai wanafunzi
mbali mbali waliosoma na ambao hawajalipa madeni yao. Aidha, Kamati inaitaka Baraza la
Mapinduzi na taasisi za Serikali kwa ujumla kuzingatia sana kupatiwa huduma za „catering‟
kutoka Chuoni hapo.
9.20 BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (P.B.Z)
Hoja Namba 49.1 Uwezo wa Benki kumudu kulipa dhima zake za muda mfupi na
Uwezo wa kujiendesha
117
Mali za mpito za thamani ya Tsh. 257,538,000,000 na dhima za mpito za thamani ya Tsh.
260,074,000,000 hufanya hali halisi ya mali za mpito kwa Benki kuwa Tsh. 2,536,000,000
kwa mwaka 2012/2013, ambayo ni sawa na uwezo wa reshio‟ ya 0.990:1.
Mapato ya Benki yalikuwa Tsh. 28,224,473,000 na matumizi yake yalikuwa Tsh.
23,293,494,000 na hivyo kuendeshwa kwa bakaa la Tsh. 4,930,979,000. Aidha, mwenendo
wa hesabu hizo unaonesha kuwepo kwa uwezekano wa kuongezeka kwa faida iwapo Benki
itaendelea kuimarisha huduma na kupunguza gharama za uendeshaji.
Majibu ya Benki
Uongozi wa Benki hauna shaka na takwimu zilizotumika, lakini kutokana na mifumo ya
kihesabu ya kibenki, hakuna taarifa inayoelezea hali halisi ya uwiano wa mali za mpito
(current assets) na dhima za mpito (current liabilities). Kwa hivyo, ni vigumu kutoa uwiano
wa ukwasi (current ratio). Hali inayothibitisha kuwa, mtindo wa uwasilishwaji wa mahesabu
ya kibenki ni tofauti na mtindo unaotumika kuwasilisha mahesabu yasiyokuwa ya kibenki.
Kwa hivyo kuanisha uchambuzi wa mahesabu ya mitindo tofauti isingelikuwa sahihi.
Uongozi wa Benki unapendekeza kuwa, ingekuwa ni vyema kufanya uchambuzi wa
mahesabu ya kibenki katika kupima (liquidity) kwa kutotumia uwiano wa ukwasi (current
ratio) kwa sababu, vipo vigezo maalum vinavyopima ukwasi katika mabenki. Aidha,
mabenki hupimwa kwa namna mbili kuu; mali zenye ukwasi wa haraka (liquid assets) dhidi
ya jumla ya mali zote za taasisi (Total assets). Na aina ya pili mali zenye ukwasi zilizopo
(Available Liquid assets) dhidi ya dhima zitazohitajika kulipwa wakati wowote (Demand
liabilities).
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepokea maelekezo ya Benki na imekuwa elimu kubwa kwa Kamati. Baada ya
maelezo yao, Kamati ilimtaka Afisa Mkaguzi anaefuatana na Kamati kutoa maelezo yoyote
kuhusiana na ripoti ya Afisi yake na usahihi wa maelekezo ya Benki, ambae alikubaliana
kuwa maelezo hayo ya Benki ni sahihi na yeye atayachukua na kuyawasilisha Afisini kwake.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuongeza uelewa na
ufahamu wa namna ya mabenki yanavyofunga hesabu zao na vipimo vya mali na dhima za
mpito za mabenki husika.
Tawi la Dar es Salaam
Kwa mwaka 2012/2013, Benki haikuwa na hoja yoyote katika ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu, lakini kwa kuzingatia mamlaka ya Kamati ya kuchunguza kwa namna
yoyote inayoona inafaa hesabu zote za Serikali na taasisi zake, Kamati imetembelea Benki
ya Watu wa Zanzibar, Tawi la Dar es Salaam na kupata ufafanuzi wa masuala mbali mbali
kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya Benki.
Kama ilivyoripotiwa katika ripoti zilizopita za Kamati, Benki imefungua matawi mawili Dar
es Salaam tokea mwaka 2011. Tawi liliopo Kariakoo kati ya mtaa wa Mkunguni na Swahili
linatoa huduma za kawaida za kibenki na jengine liliopo mtaa wa Lumumba na Mahiwa
hutoa huduma za Kiislamu. Uanziswaji wa matawi haya ni miongoni mwa malengo
yaliyomo kwenye Mpango Mkakati wa Kibiashara (Business Plan) wa Benki 2008-2011.
Madhumuni ya kufungua matawi hayo ni kuingia ushindani wa soko dogo la wateja na
Benki, kuwafuata wateja wake waliopo na wanaokuja Tanzania bara kibiashara, kikazi,
kimasomo na wanaopita ambao huhitaji huduma za Benki, kutanua wigo wa wateja wa
Tanzania bara na kuongeza „market share‟ na kutimiza malengo ya kutoa huduma bora kwa
wananchi wote.
118
Matawi haya yana wafanyakazi 30, 16 ni wa tawi linalotoa huduma za kawaida za kibenki na
14 wa tawi linalotoa huduma za Kiislamu. Miongoni mwao, wafanyakazi 16 ni wanaume na
14 ni wanawake. Pia Benki imeajiri kampuni za kutoa huduma za usafi, ulinzi, askari jeshi la
Polisi na kampuni ya kuchukua na kupeleka fedha. Aidha, Benki inaendelea na kukabiliana
na changamoto iliyopo kwa wananchi walio wengi juu ya kuzifahamu huduma za Kiislamu
zinazotolewa na Benki.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imepongeza juhudi za Benki na kufarajika kuelezwa kuwa, tawi la huduma za
Kiislamu limejipanga na tayari limeshaanzisha kutoa mikopo kwa wanafunzi mbali mbali
wanaojiunga na Vyuo Vikuu nchini. Kamati imehoji utanuzi kama huu wa matawi mbali
mbali ya Benki Tanzania bara na kuelezwa kuwa, Benki imejipanga kuongeza matawi yake
katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara, ikiwa ni pamoja na Mwanza na Arusha.
Kamati imesikitishwa na huduma za ulinzi zinazotolewa na Jeshi la Polisi kwani pamoja na
kulipwa na Benki na pamoja na askari wanaokuwa lindo usiku kugaiwa fedha kama motisha,
baadhi ya askari hao wamekuwa na tabia ya kukimbia kulinda na kumwacha askari mmoja
peke yake masaa 24 na siku nyengine hawaji kabisa, hali ambayo inahatarisha usalama wa
benki.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inautaka Uongozi wa Benki kukaa tena pamoja na Mkuu wa Polisi kwa ajili ya
kuzungumzia tena suala la huduma zao za ulinzi wanazozitoa kwa Benki. Aidha, Benki
iongeze juhudi katika kutekeleza mipango yake, ili kujiongezea mafanikio.
RIPOTI YA UKAGUZI YAKINIFU KWA MIRADI NA MAENDELEO YA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
10.0 WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI
Hoja Namba 10.1 Mradi wa Mpango wa Kuendeleza Huduma za Kilimo
(Agricultural Service Support Program-ASSP)
Mradi huu wa kuendeleza Huduma za Kilimo (Agricultural Service Support Program-
ASSP)ni mradi unaotoa huduma kwa wananchi, uliofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Mkopo kutoka Shirika la Kimataifa (IFAD) pamoja na nguvu za wananchi.
Malengo yake ni kuimarisha upatikanaji na utumiaji wa elimu na maendeleo ya kilimo kwa
wananchi wa vijijini pamoja na kushajiisha upatikanaji wa akiba ya chakula na kuongeza
pato la wananchi.
Mradi uliidhinishiwa kutumia Tsh. 805,845,452 lakini fedha zilizoingizwa na kutumika ni
Tsh. 680,354,274.92 sawa na wastani wa asilimia 84, hali inayoonesha upungufu wa
Tsh.125, 491,177.08, sawa na asilimia 16 ya makadirio.
Ukaguzi unashauri kuharakishwa uingizwaji wa fedha na utekelezwaji wa malengo
yaliyopangwa ili kuepuka uwezekano wa kuongezeka gharama kwa baadhi ya shughuli na
manunuzi ya vifaa vilivyokusudiwa.
Maelezo ya Wizara
Wizara inakiri mapungufu hayo ya fedha, lakini yametokana na wafadhili wa mradi
kutoingiza fedha kwa ukamilifu na kwa wakati, ikiwa ni pamoja na IFAD na Serikali. Hata
hivyo, Wizara inachukua juhudi za kuondosha kasoro nyengine za utekelezaji wa mradi huu
kwa ujumla, ili kusiwe na upungufu wowote.
119
Uchunguzi wa Kamati
Kwa muda mrefu hoja hii hujirejea katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
na kwa ujumla majibu yanayojibiwa yanakuwa ya jumla jumla. Aidha, hata ripoti za ukaguzi
hazitoi ufafanuzi mkubwa na wa wazi kuhusiana na hoja hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Wizara kutoa majibu ya kina kuhusiana na hoja hii, ili iweze kufanyiwa
kazi na Kamati. aidha, Kamati inamshauri Mkaguzi kuendelea kufuatilia hoja hii kwa undani
na taarifa zake ziwe wazi na kufahamika, hasa katika maeneo yenye kasoro, ili kuwe na
wepesi wa ufuatiliaji wake.
Hoja Namba 10.2 Kuhusiana na Mpango wa Kuendeleza Huduma Sekta ya Ufugaji
(Agricultural Support Development Program-Livestock/ASDP-L)
Mradi huu wa kuendeleza Huduma sekta ya ufugaji ni mradi unaotoa huduma kwa wananchi,
uliofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mkopo kutoka Shirika la Kimataifa
(IFAD) pamoja na nguvu za wananchi.
Malengo yake ni kuimarisha uwezo na kipato cha wafugaji wadogo wadogo; Kushajiisha
upatikanaji wa huduma za maendeleo kwa wafugaji wadogo wadogo na Kuimarisha
miundombinu ya masoko kwa wafugaji wadogo wadogo.
Kwa mwaka 2011/2012 mradi huu ulikadiriwa kupokea Tsh. 1,190,272,666 na fedha halisi
zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 1,393,833,583 sawa na wastani asilimia 117 ya makadirio,
ikiwa ni ongezeko la Tsh. 203,560,917 ya makadirio.
Maelezo ya Wizara
Wizara inakiri mapungufu hayo ya fedha, lakini yametokana na wafadhili wa mradi
kutoingiza fedha kwa ukamilifu na kwa wakati, ikiwa ni pamoja na IFAD na Serikali. Hata
hivyo, Wizara inachukua juhudi za kuondosha kasoro nyengine za utekelezaji wa mradi huu
kwa ujumla, ili kusiwe na upungufu wowote.
Uchunguzi wa Kamati
Kwa muda mrefu hoja hii hujirejea katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
na kwa ujumla majibu yanayojibiwa yanakuwa ya jumla jumla. Aidha, hata ripoti za ukaguzi
hazitoi ufafanuzi mkubwa na wa wazi kuhusiana na hoja hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Wizara kutoa majibu ya kina kuhusiana na hoja hii, ili iweze kufanyiwa
kazi na Kamati. aidha, Kamati inamshauri Mkaguzi kuendelea kufuatilia hoja hii kwa undani
na taarifa zake ziwe wazi na kufahamika, hasa katika maeneo yenye kasoro, ili kuwe na
wepesi wa ufuatiliaji wake.
10.1 WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Hoja Namba 11.2 Mradi wa ukarabati wa jengo la Beit el Ajaib, Zanzibar.
Mradi huu ulifandhiliwa na MACEMP na ulianza tarehe 16 Septemba 2010, ambapo Serikali
ilitiliana mkataba na Lucky Construction Ltd, ya Dar es Salaam, mkataba wenye namba
DFMRZ/MACEMP/CW/REH.2/10 na thamani ya mradi huo hadi unakamilika ni Tsh.
249,409,400. Aidha, Tsh. 83,202,633 zimetumika katika mwaka huu wa fedha na ukaguzi
umebaini kasoro ya kukosekana ubora wa ukarabati wa jengo hilo, ukilinganisha na fedha
zilizotumika. Vile vile, ukaguzi umebaini kasoro zifuatazo:
120
Mkataba kushindwa kuonesha na kuthibitisha tarehe ya kuanza na kumalizika kwa
ujenzi huo.
Sehemu ya jengo bado haijakamilika kulingana na hati ya makisio ya ujenzi (BOQ),
hivyo kupelekea maji ya mvua kuingia ndani.
Utiaji wa umeme haujakamilika na kupelekea maharibiko makubwa katika baadhi ya
sehemu za ndani ya jumba hilo.
Baadhi ya sehemu zilizojengwa tayari zimeshaanguka chini.
Kengele ya usalama (security alarm) yenye thamani ya Tsh. 5,000,000 haijafungwa.
Taa za dharura zenye thamani ya Tsh. 500,000,000 bado hazijafungwa.
Power Generator 3 phase 380/50 KV na vifaa vyake vyenye thamani ya Tsh.
35,000,000 bado hazijafungwa.
Majibu ya Wizara
Wizara haikubaliani na maelezo ya ukaguzi na usahihi wa majibu ya hoja hii ni kuwa,
Mkataba uliofungwa unaonesha tarehe na maelezo ya kuanza na kumalizika ujenzi kama
inavyooneshwa katika mkataba husika. Na kuhusiana na kutokamilika kwa jengo kulingana
na makisio ya ujenzi (BOQ) na kupekeleka kukosekana baadhi ya athari, hii inatokana
kwamba, wakati wa ukaguzi, Mkandarasi basdo alikuwa anaendelea na kazi. Hata hivyo,
kazi hiyo ilisitishwa bada ya kuporomoka sehemu ya nyuma ya jengo hilo, na kupelekea
masuala yaliyobaki ya ujenzi kusitishwa pamoja na malipo yaliyobaki ya Tsh. 166,197,767
kama ripoti ya Mshauri Mwelekezi inavyoonesha.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati ilihoji juu ya taratibu za manunuzi kwa kuhoji namna alivyopatikana Mshauri
Elekezi na Mkandarasi wa ujenzi na kujiridhisha kuwa, Wizara ilitangaza zabuni tarehe
11/06/2010 na 12/06/2010 na kampuni 3 ziliingia katika zabuni hiyo ambapo Kampuni ya
Lucky ndio iliyopewa kazi hiyo. Na kwa upande wa Mshauri Elekezi walitoa zabuni kama
Mshauri Elekezi binafsi. Kuhusiana na hali halisi ya jengo hilo, Kamati ilijiridhisha kuwa
tayari liliporomoka, na Mamlaka ya Mji Mkongwe ilitoa taarifa ya kusitishwa kwa ukarabati
wake, huku Tsh. 83,202,633 tayari zilikwishalipwa kwa Mjenzi na tayari ameshazitumia kwa
ukarabati uliofanyika.
Kamati imejiridhisha kuwa Mkataba wa ujenzi ulisainiwa tarehe 16/09/2010 na ujenzi
ulitakiwa uanze baada ya wiki mbili kutokea kusainiwa kwa mkataba na mkataba huo huo
unaonesha ujenzi ungelimalizika baada ya miezi 10 ya kuanza kwa ujenzi na jengo hilo
liliporomoka tarehe 1/12/2012, hali hii iliithibitishia Kamati kuwa, jengo liliporomoka muda
mrefu baada ya ujenzi, kinyume na Mkataba ulivyoelekeza.
Kamati pia ilijiridhisha kuwa, Mshauri Elekezi alitoa taarifa yake kwa Wizara kuhusiana na
hali hiyo, na Kamati iliarifiwa kuwepo kwa ripoti ya hali ya jengo kabla ya kufanyiwa
ukarabati, lakini Kamati haikuweza kupatiwa kwa kuelezwa kuwa haikuwepo wakati kikao
kinafanyika. Hata hivyo, Kamati imeelezwa kuwa Mradi huu ulikuwa na wadau sita wa
Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na Wizara yenyewe, Tawala za Mikoa, Mamlaka ya Mji
Mkongwe, Wizara inayoshughulikia Utalii, Wizara inayoshughulikia mambo ya kale na
Idara yenyewe ya Uvuvi. Aidha, ilielezwa kuwa, Idara hii ya Uvuvi ilikuwa inatekeleza
maagizo ya Wizara na taasisi hizo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuwa makini katika kufanya ukarabati wa majengo yake na zaidi
haya ya zamani. Hata hivyo, Kamati nayo imeridhika, pamoja na sababu zilizoelezwa kuwa,
ukarabati wa jengo hilo haulingani na fedha zilizotumika.
121
RIPOTI YA UKAGUZI YAKINIFU KWA MIRADI NA MAENDELEO YA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
11.0 WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI
Hoja Namba 10.1 Mradi wa Mpango wa Kuendeleza Huduma za Kilimo
(Agricultural Service Support Program-ASSP)
Mradi huu wa kuendeleza Huduma za Kilimo (Agricultural Service Support Program-
ASSP)ni mradi unaotoa huduma kwa wananchi, uliofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Mkopo kutoka Shirika la Kimataifa (IFAD) pamoja na nguvu za wananchi.
Malengo yake ni kuimarisha upatikanaji na utumiaji wa elimu na maendeleo ya kilimo kwa
wananchi wa vijijini pamoja na kushajiisha upatikanaji wa akiba ya chakula na kuongeza
pato la wananchi.
Mradi uliidhinishiwa kutumia Tsh. 807,534,540 lakini fedha zilizoingizwa na kutumika ni
Tsh. 762,134,868.59 sawa na wastani wa asilimia 94, hali inayoonesha upungufu wa
Tsh.45,599,671.41 sawa na asilimia 6 ya makadirio.
Maelezo ya Wizara
Wizara inakiri mapungufu hayo ya fedha, lakini yametokana na wafadhili wa mradi
kutoingiza fedha kwa ukamilifu na kwa wakati, ikiwa ni pamoja na IFAD na Serikali. Hata
hivyo, Wizara inachukua juhudi za kuondosha kasoro nyengine za utekelezaji wa mradi huu
kwa ujumla, ili kusiwe na upungufu wowote.
Uchunguzi wa Kamati
Kwa muda mrefu hoja hii hujirejea katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
na kwa ujumla majibu yanayojibiwa yanakuwa ya jumla jumla. Aidha, hata ripoti za ukaguzi
hazitoi ufafanuzi mkubwa na wa wazi kuhusiana na hoja hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Wizara kutoa majibu ya kina kuhusiana na hoja hii, ili iweze kufanyiwa
kazi na Kamati. aidha, Kamati inamshauri Mkaguzi kuendelea kufuatilia hoja hii kwa undani
na taarifa zake ziwe wazi na kufahamika, hasa katika maeneo yenye kasoro, ili kuwe na
wepesi wa ufuatiliaji wake.
Hoja Namba 10.2 Kuhusiana na Mpango wa Kuendeleza Huduma Sekta ya Ufugaji
(Agricultural Support Development Program-Livestock/ASDP-L)
Mradi huu wa kuendeleza Huduma sekta ya ufugaji ni mradi unaotoa huduma kwa wananchi,
uliofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mkopo kutoka Shirika la Kimataifa
(IFAD) pamoja na nguvu za wananchi.
Malengo yake ni kuimarisha uwezo na kipato cha wafugaji wadogo wadogo; Kushajiisha
upatikanaji wa huduma za maendeleo kwa wafugaji wadogo wadogo na Kuimarisha
miundombinu ya masoko kwa wafugaji wadogo wadogo.
Kwa mwaka 2012/2013 mradi huu ulikadiriwa kupokea Tsh. 1,354,441,157 na ilipofikia
mwisho wa mwaka, fedha zilizoingizwa ni Tsh. 1,311,145,526.15, sawa na asilimia 97 ya
makadirio, ikiwa ni pungufu ya Tsh. 43, 295,630.85 sawa na asilimia 3 ya makadirio.
Maelezo ya Wizara
Wizara inakiri mapungufu hayo ya fedha, lakini yametokana na wafadhili wa mradi
kutoingiza fedha kwa ukamilifu na kwa wakati, ikiwa ni pamoja na IFAD na Serikali. Hata
122
hivyo, Wizara inachukua juhudi za kuondosha kasoro nyengine za utekelezaji wa mradi huu
kwa ujumla, ili kusiwe na upungufu wowote.
Uchunguzi wa Kamati
Kwa muda mrefu hoja hii hujirejea katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
na kwa ujumla majibu yanayojibiwa yanakuwa ya jumla jumla. Aidha, hata ripoti za ukaguzi
hazitoi ufafanuzi mkubwa na wa wazi kuhusiana na hoja hii.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Wizara kutoa majibu ya kina kuhusiana na hoja hii, ili iweze kufanyiwa
kazi na Kamati. aidha, Kamati inamshauri Mkaguzi kuendelea kufuatilia hoja hii kwa undani
na taarifa zake ziwe wazi na kufahamika, hasa katika maeneo yenye kasoro, ili kuwe na
wepesi wa ufuatiliaji wake.
11.1 WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Hoja Namba 11.1 Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Mifugo
Kwa mwaka 2012/2013 Wizara ilikadiriwa Tsh. 200,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa
ujenzi wa chinjio jipya eneo la Kisakasaka. Hadi kufikia Juni 30, 2013, fedha zilizoingizwa
ni Tsh. 17,537,700, sawa na asilimia 9 ya makadirio.
Ukaguzi umebaini kuwa mradi huo haukuweza kutekelezwa kutokana na kutoingiziwa fedha
zilizokadiriwa kwa ajili ya ujenzi wa chinjio jipya katika eneo la Kisakasaka. Wakaguzi
walitembelea eneo hilo na kutoona ujenzi wowote uliofanyika. Pia, imebainika kuwepo kwa
matumizi yaliyofanyika kwa baadhi ya shughuli za ujenzi wa chinjio hilo kwa malipo ya
uchoraji wa ramani, malipo kwa Mshauri Mwelekezi (Consultant) na malipo ya ujenzi.
Majibu ya Wizara
Fedha halisi zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 16,527,700 na sio Tsh. 17,537,700 kama
ilivyoripotiwa na Mkaguzi. Kuhusiana na maelezo ya kushindwa kutekelezwa mradi huo
kutokana na kutoingizwa fedha ni sahihi, na Wizara ilimuajiri Mshauri Mwelekezi kwa ajili
ya michoro tu, ingawaje walianza kwa hatua ya upimaji na ufuatiliaji wake. kwa ujumla,
mradi haukuweza kutekelezwa kutokana na kutopatikana kwa fedha.
Uchunguzi wa Kamati
Pamoja na kutoingizwa kwa fedha hizo, Kamati imehoji iwapo Wizara ina hatimiliki ya eneo
hilo la mradi na kuelezwa kuwa waliandika barua kwenda Wizara ya Ardhi kwa ajili ya
malipo ya hatimiliki hiyo. Hata hivyo, Kamati ilipokagua hati za malipo hayo, ilijiridhisha
kuwa yamekosekana maombi ya mahitaji yake. Aidha, hati namba 9/11 na 26/11 yenye
thamani ya Tsh. 1,500,000/- haina risiti wakati fedha zimelipwa kwa Wizara ya Ardhi,
Makaazi, Maji na Nishati nayo ni taasisi ya Serikali, bila ya shaka lazima itoe risiti.
Vile vile hati namba 10/3 ya tarehe 15/1/2013 haina saini ya Afisa Masuuli wala maombi
maombi ya fedha hizo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuhakikisha inafuata ipasavyo Sheria katika matumizi ya fedha za
Serikali.
123
Hoja Namba 11.2 Mradi wa kudhibiti maradhi ya kichaa cha mbwa (Rabies Control
Project)
Mradi huu ulianza rasmi Agosti 2005 na unafadhiliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya
kuwalinda wanyama (World Society for the Protection of Animals-WSPA) ambayo makao
makuu yake yapo nchini Uiengereza. Jumuiya hiyo imejitolea kuufadhili mradi huu kwa
kugharamia matumizi yote yanayohitajika katika mradi huu kwa kushirikiana na Serikali.
Mradi huu unatarajiwa kumalizika Disemba 2016.
Lengo la mradi ni kudhibiti na hatimae kutokomeza kichaa cha mbwa kwa lengo la
kutokomeza maambukizi ya kichaa kwa binaadamu pamoja na kuongeza muamko kwa
wafugaji ili kujali afya za wanyama wao.
Kwa mwaka 2012/2013 mradi huu ulikadiriwa kupokea Tsh. 158,166,790 kutoka kwa
Washirika wa Maendeleo wa WSPA kwa lengo la kudhibiti maradhi ya kichaa cha mbwa na
ilipofikia mwisho wa mwaka, Tsh. 158,166,790 ziliingizwa na kutumika, sawa na asilimia
100 ya makadirio.
Aidha, kwa upande wa mchango wa Serikali, mradi huu ulikadiriwa kupokea Tsh.
80,000,000 na fedha halisi zilizoingizwa na kutumika ni Tsh. 13,000,000 sawa na asilimia 16
ya makadirio, ikiwa ni upungufu wa Tsh. 67,000,000 sawa na asilimia 84 ya makadirio.
Ukaguzi uliweza kutathmini hali halisi ya utekelezaji wa mradi huu kama ifuatavyo:
Namba Utekelezaji Idadi ya mbwa Idadi ya paka
1. Waliochanjwa 14731 3989
2. Waliofungwa uzazi 560 617
3. Waliopatiwa dawa za minyoo 5318 369
4. Waliotibiwa maradhi ya aina
mbali mbali
1454 320
5. Waliokingwa na kupe 2212 256
Jumla 24275 5551
Aidha, ukaguzi umebaini kasoro zifuatazo katika utekelezaji wa mradi huo:
Baadhi ya wananchi wengi hushindwa kuwadhibiti mbwa wao kwa ajili ya
kuwapeleka na kupata huduma za matibabu.
Mbwa wanaozurura ovyo hata inapotumika mitego kwa lengo la kuwadhibiti
inakuwa ni vigumu kupatikana.
Baadhi ya wafugaji bado hawajaona umuhimu wa kupeleka mbwa wao katika chanjo
kutokana na kukosa taaluma.
Majibu ya Wizara
Changomoto hizo zipo na zinasababishwa na sababu mbali mbali. Kwa mfano kuhusiana na
wananchi kushindwa kuwadhibiti mbwa wao, pamoja na sababu nyengine kunachangiwa na
kutofahamu wafugaji kwamba wao ndio wenye dhamana ya mbwa wao. Hivyo
wanalazimika kuwalisha, kuwapatia makaazi na huduma nyengine. Aidha, kuzurura kwa
mbwa kunatokana zaidi na wamiliki wao kushindwa kuwadhibiti na kuwapa huduma
zinazotakiwa.
Vile vile kuna dhana potofu kwa wafugaji wengi, kwa mfano wengi wao huamini kuwa,
mbwa wanapochanjwa ni kuwafunga uzazi wakati sio kweli. Hata hivyo, Wizara inaendelea
kuzikabili changamoto hizo kwa kuendelea kuwaelimisha wafugaji na wananchi wote kwa
ujumla.
124
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji mradi huu kuwa ni wa mbwa katika asili yake, lakini pia umehusisha paka
na kuelezwa kuwa, wanyama haswa waliokusudiwa ni mbwa lakini na paka pia wanaingia
katika lengo moja. Hiyo ni kwa sababu, kichaa cha mbwa pia kinaambukizwa kwa wanyama
wengine, ikiwa ni pamoja na paka.
Aidha, Kamati imeitaka Wizara kutayarisha na kuwasilisha kwa Kamati fedha zilizotumika
kwa mbwa na paka na mambo yaliyoikwaza Wizara kufikia malengo kwa kukosa fedha
katika bajeti yao ya mradi huu. Hata hivyo, Kamati haijawasilisha kwa Kamati taarifa hizo.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kusimamia utekelezaji wa miradi kwa kufuata taratibu za Sheria na
kuheshimu maelekezo ya Kamati ya kukabidhi taarifa mbali mbali zinazohitajika na Kamati.
11.2 WIZARA YA ARDHI, MAKAAZI, MAJI NA NISHATI-PEMBA
Hoja Namba 13.1 Kutochukuliwa hatua ya utekelezaji wa ukarabati wa nyumba za
Maendeleo-Wete
Jumla ya Tsh. 110,080,000 ziliingizwa kwa ajili ya ukarabati wa jumba namba 4 lilioko
Wete Mtemani,Pemba. Ukaguzi umebaini kwamba, fedha hizo zilizoingizwa zilitumika kwa
matumizi mengine badala ya kufanya ukarabati wa jengo hilo. Jengo hilo lilikusudiwa
kufanyiwa ukarabati tangu mwaka 2011/2012 na fedha za ukarabati huo ziliingizwa na
kutumika kwa matumizi mengineyo kama ilivyoripotiwa katika ripoti ya ukaguzi ya mwaka
2011/2012. Jengo hilo limeshaanza kuporomoka na kusababisha hatari kwa wanaoishi
pamoja na wapita njia.
Aidha, ukaguzi unashauri hatua muafaka zichukuliwe ili kumaliza tatizo hilo kwa
kuyakarabati majengo ambayo yapo katika katika hali mbaya.
Majibu ya Wizara
Fedha hizo Tsh. 110,080,000/- zilitengwa kwa ajili ya shughuli zote za Idara ya Nyumba
Pemba ikiwa ni pamoja na matengenezo ya nyumba zote za Serikali (Nyumba za maendeleo,
za vijiji na za kutaifishwa) kwa Pemba nzima. Aidha, fedha zilizopatikana ni Tsh.
62,881,644 na zimetumika kwa ukarabati wa nyumba za maendeleo Block No.5 iliyoko
Mtemani Wete, nyumba Namba T. 17B iliyoko Kilimatinde Chake, matengenezo ya makaro
na mitandao ya maji machafu katika nyumba za maendeleo Micheweni, Machomanne Chake
na Mkoani na matengenezo ya nyumba Namba T.67 iliyopo Tibirinzi Chake Chake.
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imejiridhisha kwamba, hoja hii tayari imesharipotiwa mwaka uliopita na Kamati
ilifanya tena ziara katika eneo hilo la Mtemani na kushudia hali mbaya ya uchakavu wa
majengo hayo, bila ya kufanyiwa ukarabati wowote, pamoja na kuwahi kuahidiwa na Wizara
kuwa yatafanyiwa marekebisho.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaendelea kuitaka Wizara kufanya marekebisho majengo hayo sambamba na
Kamati kuitaka Serikali iipe fedha Wizara ili iweze kuyakarabati majengo hayo.
125
11.3 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
Hoja Namba 12.1 Mradi wa uimarishaji wa elimu ya Lazima (Zanzibar Basic
Education Improvement Project (ZABEIP))
Mradi huu unaoshughulikia huduma za elimu kwa ajili ya maendeleo ya elimu Zanzibar,
umehusika na ujenzi wa Maskuli, kutoa huduma za maabara, huduma za maktaba na huduma
nyenginezo. Mradi ni wa miaka mitano (Juni 2008 hadi Juni 2013) na umeripotiwa na
Kamati tokea uanze kutolewa taarifa zake katika ripoti ya ukaguzi na kwa mwaka wa
2012/2013, ukaguzi uliendelea kuuzungumzia kuwa umeonesha mafanikio makubwa kwa
wastani wa asilimia 90 ya utekelezaji wake wa awamu ya mwisho na kwa hivyo,
umefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwani majengo mengi ya skuli za sekondari kwa Unguja na
Pemba yamekamilika na tayari yameshaanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma ya elimu
kwa wanafunzi wa sekondari, na hali halisi iliyooneshwa katika ripoti hiyo ni skuli za
sekondari za Kiembe Samaki, Mpendae, Faraja, Forodhani, Hamamni, Tumekuja, Fidel
Castro, Uweleni na Utaani.
Majibu ya Wizara
Ni kweli taarifa za ukaguzi kuhusiana na mradi huo, na kuhusiana na skuli tatu za Kombeni,
Paje Mtule na Paje, ambazo Kamati iliziripoti kuwa wakandarasi wake walikimbia mwaka
uliopita, tayari ujenzi wake umefikia asilimia 99. Ujenzi wa skuli hizo ulichelewa kutokana
na mkandarasi aliyeanza ujenzi wake (Electrics International Limited) kushindwa
kuzimaliza.
Wizara iliamua kukatisha mkataba wake na kazi iliyobakia kumalizwa na Wakandarasi
wengine watatu ambao ni; Zeccon Company Ltd (kwa Skuli ya Kombeni Sekondari) kwa
Tsh. 296,850,000/; Quality Builders Contractor (kwa Skuli ya Sekondari ya Tunguu) kwa
Tsh. 299,061,360 na Rans Company Litd (kwa skuli ya Sekondari ya Paje Mtule) kwa Tsh.
299,943,000/- na jumla ya fedha zilizotumika kwa ujenzi huo ni Tsh. 895,854,360/-
Aidha, fedha zote hizo zilitolewa na Serikali na zimelipwa mwezi Oktoba 2014. Kwa upande
wa skuli za Kombeni na Tunguu zimeanza kutumika mwezi Septemba 2014 na skuli ya Paje
Mtule imeanza kutumika mwezi Januari 2015. Jambo jengine la msingi ni kuwa, Mkandarasi
aliyeshindwa awali (Electrics International Limited), hakukubaliana na uamuzi wa
kumalizwa kazi iliyomshinda kwa kupewa makampuni mengine na hivyo, amepeleka kesi
Mahakamani ambayo mpaka sasa bado haijatolewa uamuzi na anadai kulipwa fedha
zilizobakia kukamilisha ujenzi, ambazo ni Tsh. 152,741,412.12/-
Uchunguzi wa Kamati
Kamati imehoji sababu zilizopelekea Wizara kushindwa kumpeleka Mahakamani
mkandarasi huyo Electrics International Limited, ambae kwa makusudi amevunja mkataba
walioingia nao na Kamati ililishauri hilo awali, na kuelezwa kuwa, suala hilo halikuwa
uamuzi wa Wizara moja kwa moja kwani ni Serikali ndiyo iliyowapa maagizo ya kukaa
pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa lengo la kufungua kesi dhidi ya Mkandarasi
huyo, lakini kabla ya kumaliza, ndipo waliposhtukia mkandarasi huyo alitangulia kufungua
kesi hiyo.
Kamati imehoji taratibu zilizotumika kuwapata wajenzi hao waliomaliza skuli hizo na
ikizingatiwa kuwa fedha zilizotumika ni nyingi na kuelezwa kuwa, Wizara imezingatia
uteuzi wa wakandarasi ambao tayari wameshafanyakazi nao katika maskuli mengine.
126
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaitaka Wizara kuzingatia taratibu za Sheria inapofanya ujenzi na matumizi ya
fedha za Umma.
11.4 WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO
11.4.1 JENGO LA KAMISHENI YA UTALII PEMBA
Hoja Namba 14.2 Jengo la Kamisheni ya Utalii Pemba, kutofanyiwa matengenezo
kwa muda mrefu
Kamisheni ya Utalii Pemba inamiliki jengo lililonunuliwa kutoka kwa Ndg. Ali Abeid Nassir
kwa Tsh. 30,000,000 tangu mwaka 1992 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Utalii,
Pemba. Ukaguzi umebaini kwamba, jengo hilo bado halijafanyiwa matengenezo yoyote kwa
kipindi kirefu tokea liliponunuliwa. Kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda
mrefu, Kamisheni inaendelea kukodi jengo kwa matumizi ya Ofisi kwa muda mrefu na
kutumia gharama kubwa.
Majibu ya Kamisheni
Ni kweli kwamba jengo hilo halijafanyiwa matengenezo tokea liliponunuliwa na Kamisheni
ya Utalii na bado Kamisheni inaendelea kukodi jengo tokea mwaka 1992. Hii ni kutokana na
kuwa Wizara ilikusudia kupata tathmini ya kitaalamu juu ya hali halisi ya jengo lilivyo kwa
vile msingi wake umeshakaa karibu miaka 20.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Kamisheni kuiandikia barua Wizara ya
Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati mnamo tarehe 31 Mei, 2012 ili kuomba kufanyiwa tathmini
jengo hilo liliopo Chachani. Hata hivyo, hakukuwa na majibu yoyote ya barua hiyo na
mnamo tarehe 23 Aprili, 2013 Kamisheni ya Utalii iliiandikia tena barua ya ukumbusho
Wizara hiyo na tarehe 27 Februari, 2014 Kamisheni ilipokea barua kutoka Wizara ya Ardhi,
Makaazi, Maji na Nishati inayotoa maelekezo na ushauri baada ya kufanywa ukaguzi wa
kitaalamu kuwa ni vyema jengo hilo livunjwe na kujengwa upya badala ya kuliendeleza.
Kutokana na ushauri na maelekezo hayo Kamisheni ya Utalii imeona ni vyema kutafuta M-
bia wa kulijenga jengo hilo kutokana na ugumu wa upatikanaji wa fedha kutoka Hazina na
hivi sasa juhudi za kutafuta M-bia huyo zinaendelea.
Uchunguzi na Mapendekezo ya Kamati
Kamati imeunga mkono ushauri na maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Ardhi, Makaazi,
Maji na Nishati. Hata hivyo, imesikitishwa na kitendo cha Wizara hiyo cha kuchukua muda
mrefu kutoa ushauri na maelekezo hayo.
Kwa mnasaba huo, Kamati ya PAC inaishauri Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati
kuchukua hatua za haraka pale inapopelekewa jambo kwa kuwa Wizara hii ndio Taasisi
pekee inayotegemewa na Serikali kutoa ushauri na maelekezo juu ya majengo yake.
Vile vile, Kamati hii imeridhika na maamuzi ya Kamisheni ya Utalii ya kuendelea kutafuta
M-bia wa kujenga jengo hilo. Hii ni kutokana na kuwa Kamisheni inazalisha mapato mengi
lakini fedha zote inazokusanya huwasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina na hakuna
mgao wowote wanaoupata katika mapato hayo zaidi ya kupewa Ruzuku. Hivyo, ni vigumu
kwa Kamisheni kuweza kujenga jengo hilo kwa nguvu zake mwenyewe.
127
11.4.2 UTUNZAJI NA UDHIBITI WA MAENEO YA KIHISTORIA (WIZARA YA
HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO-PEMBA)
Hoja Namba 14.2 Utunzaji na Udhibiti wa Maeneo ya Kihistoria
Ukaguzi umebaini kuwa baadhi ya sehemu za kihistoria ambazo ni vivutio vya wageni wa
ndani na nje, utunzaji na udhibiti wa maeneo hayo hauridhishi. Baadhi ya maeneo
yaliyokaguliwa ni magofu ya Rasi Mkumbuu, magofu ya Mkamandume Pujini, magofu ya
Chwaka Tumbe na magofu ya Jambangome Wambaa.
Kukosekana kwa utunzaji na udhibiti wa maeneo hayo kunaweza kusababisha uvamizi
pamoja na uharibifu na matumizi mabaya katika maeneo hayo. Aidha, maeneo hayo
hayajawekewa alama za utambulisho na kuonesha kwamba ni maeneo ambayo yako katika
hifadhi za kihistoria. Hali hii inaweza kupelekea kukosekana kwa mapato yatokanayo na
wageni wanaotembelea maeneo hayo muhimu ya kihistoria.
Mkaguzi anashauri hatua muafaka zichukuliwe ili kunusuru maeneo hayo ya kihistoria kwa
kuyaendeleza, kuyafanyia matengenezo, kuyawekea alama za utambulisho na kuweka
wataalamu wa uhifadhi wa historia, walinzi na wahudumu kwa ajili ya kuhifadhi, kutoa
huduma pamoja na kutoa maelezo kwa wageni wa ndani na nje wanaotembelea maeneo
hayo.
Majibu ya Wizara
Mabango
Wizara na Kamisheni ya Utalii imekiri kuwa hali ya Mabango iliyopo hivi sasa hairidhishi,
hii ni kutokana na gharama kubwa za kuyashughulikia Mabango hayo ambapo bango moja
kubwa linagharimu Tsh. 350,000.00 na Bango dogo Tsh. 300,000.00 wakati Mabango yote
ni 50 ambayo yatagharimu Tsh. 17,000,000.00. Mabango hayo yanahitaji kila baada ya
mwaka mmoja kuandikwa tena upya kutokana na kuharibika kwa mvua na kuwa kjaribu na
bahari.
Walizidi kueleza kuwa katika kuhami hali hiyo Kamisheni ina mpango wa kutayarisha
Mabango mapya ambayo yatatumia saruji. Ujenzi wa Mabango hayo utagharimu Tsh.
40,000,000.00.
Utunzaji wa maeneo
Utunzaji wa maeneo ya Kihistoria ni suala muhimu ambalo linahitaji nyenzo za kutosha
katika kuyatunza na kuyashughulikia maeneo hayo. Kwa sasa Idara ina wafanyakazi saba tu
ambao ndio wanaohudumia maeneo hayo 45 ya Kihistoria yaliyopo Pemba. Idadi hiyo ya
wafanyakazi ni ndogo sana na haikidhi haja. Hata hivyo, jitihada za kuajiri wafanyakazi
wapya zinachukuliwa ambapo nafasi 10 zimeshaombwa Idara ya Utumishi Serikalini ili
kuziba upungufu huo.
Kutokana na kasoro hiyo wameeleza kuwa Idara inachukua juhudi za makusudi za kuyaweka
maeneo hayo katika hali ya usafi, isipokuwa kwamba juhudi hizo zinakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa fedha hivyo, kasi ya kuyafanyia matengenezo maeneo hayo sio
kubwa sana.
Alama za maeneo
Alama katika maeneo ya Kihistoria zinafahamika kwa kuwa maeneo yote mipaka yake
imetangazwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Baadhi ya alama hizo zimo kwenye maeneo
husika isipokuwa kwamba alama za maeneo mengine zimeondolewa na wananchi
wanaolima katika maeneo hayo.
Aidha, tayari wameshapeleka maombi ya kupatiwa hati miliki ingawa hadi hivi sasa hati hizo
hazijapatikana.
128
Nyumba za Ofisi katika maeneo ya kihistoria
Nyumba zilizopo katika maeneo ya Kihistoria zilijengwa kwa msaada wa Mradi wa TASAF
na MACEMP ambapo zilikabidhiwa Kamati za Jamii zilizoundwa na TASAF. Baada ya
Mradi wa MACEMP kumaliza muda wake nyumba hizo zimekabidhiwa Wizara na wakati
Mdhibiti anafanya ukaguzi maeneo hayo, nyumba hizo zilikuwa bado zipo chini ya udhibiti
wa Kamati za Jamii. Kwa sasa Idara imeanza kuzisimamia nyumba hizo na kuziweka katika
hali ya usafi.
Panga la Watoro
Panga la Watoro bado lipo chini ya udhibiti wa Serikali na liko huru kwa wananchi na
wageni kwenda kuliona wakati wowote. Pango hilo lipo karibu sana na ufukwe wa bahari,
ambapo mipaka aliyopewa Mwekezaji wa Hoteli ya Manta mita 20 kutoka ufukwe wa bahari
haingiliani kabisa na eneo la pango hilo.
Aidha, kwa upande wa kusini kwa Mwekezaji huyo ipo njia maalum ya wapitao kwa miguu
wanaohitaji kwenda katika pango hilo bila ya kupita ndani ya Hoteli hiyo.
Uchunguzi wa Kamati
Katika kufuatilia hoja hii Kamati ya PAC imeunga mkono maelezo yaliyotolewa na Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia Ripoti yake ya Ukaguzi Yakinifu. Hii ni
kutokana na kuwa Wizara na Idara inayohusika na masuala ya Hifadhi ya maeneo ya
kihistoria, imeshindwa kusimamia vyema maeneo ya kihistoria kwa ujumla na kupelekea
baadhi ya sehemu za kihistoria kuanza kutoweka kwa mfano; katika eneo la Mkamandume
kisima kimeanza kuporomoka, ngazi ambazo zilikuwa zinatumika katika eneo hilo
zimejifukia, msikiti upo kwenye eneo la shamba la mtu binafsi nakadhalika.
Aidha, Kamati pia ilisikitika kwa taarifa kwamba, mmiliki wa hoteli iliyo karibu na pango la
Watoro, Kigomasha analitumia pango hilo kama sehemu yake na kujipatia makusanyo ya
fedha kwa wageni wanaofika hotelini hapo, lakini yote haya ni kwa sababu Wizara
imeshindwa kuyashughulikia maeneo hayo ya kihistoria.
Mapendekezo ya Kamati
Kamati inaishauri Serikali kuiwezesha kifedha Wizara ili iweze kuyatunza maeneo ya
kihistoria.
Wizara ifanye juhudi ambazo zipo katika uwezo wake katika kuhakikisha maeneo
hayo yanalindwa na kuhifadhiwa, ili iwe rahisi kuyaimarisha mara tu watakapopata
fedha.
SEHEMU YA TATU
HITIMISHO
Sehemu hii ya Ripoti inahusiana na Maoni ya Kamati na Mapendekezo yake kwa Baraza la
Wawakilishi, ili iiagize Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kutekeleza yale yote ambayo
Kamati imeyapendekeza. Kwa ujumla, Ripoti yetu inatofautiana sana na ripoti za Kawaida
za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi. Kwa Kamati hizo inakuwa rahisi sana
kupendekeza Mapendekezo yote ya Kamati katika sehemu moja, lakini kwa kuwa Kamati ya
P.A.C inachunguza hoja moja baada ya moja inayotokana na Ripoti ya Mdhibiti na
Mkauguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, inakuwa kwa namna yoyote ile, lazima
mapendekezo ya Kamati yawe katika baada ya ufafanuzi wa Hoja husika.
129
Hii ina maana kwamba, katika ripoti hii tumeeleza vitu vinne kwa takriban kila hoja. Jambo
la kwanza tumeitaja Hoja yenyewe na kutoa maelezo yake kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu alivyofanya katika Ripoti zake ; jambo la pili tulieleza maelezo ya Wizara.
Sehemu hii inamaanisha majibu yote ya Wizara iliyojibu mbele ya Kamati kuhusiana na
Hoja ya Mdhibiti. Maelezo ya tatu ni Uchunguzi wa Kamati. Sehemu hii inahusiana na
uchambuzi na ufafanuzi wa Kamati kuifafanua hoja ya Mdhibiti kwa namna ilivyokuwa
inaifanyia kazi na kwa kuzingatia uchunguzi wake mbele ya Taasisi husika ; na maelezo ya
mwisho ni Mapendekezo ya Kamati. Hapa panahusiana na maagizo na mapendekezo ya
Kamati kuhusiana na hoja ya Mdhibiti na Majibu yaliyotolewa na Taasisi husika.
Hivyo basi, katika kuifanyia kazi ripoti hii, mapendekezo ya Kamati yote yanapatikana
katika ripoti yenyewe na katika sehemu hii ya tatu ya Hitimisho, Kamati inaliomba Baraza la
Wawakilishi, iiagize Serikali kutekeleza maoni yote ya Kamati kama yalivyo katika ripoti
hii.
Baada ya maelezo hayo, Kamati inapenda kutoa shukurani za dhati kwa Wizara, Mashirika
na Taasisi zote za Serikali kwa mashikiano makubwa waliyoyaonesha wakati wote wa kazi
za Kamati. Shukurani pia ziwafikie Watendaji wote wa Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu kwa mashirkiano mazuri waliyoipa Kamati wakati wote, aidha Kamati inatoa
shukurani za pekee kwa Afisi hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Afisi ya Baraza la Wawakilishi, na Taasisi zote
zilizohusika kwa kuiandalia mafunzo kuhusu mada mbali mbali yanayohusiana na
majukumu yake, kwa lengo la kuiwezesha kutekeleza vyema majuku hayo.